Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 6 Sitting 10 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 115 2022-02-14

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Njika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kujenga Vyuo vya VETA katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha kwa lengo la kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini. Kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 25 na Mikoa 4 ukiwemo Mkoa wa Simiyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu na maeneo mengine, wananchi wa Meatu wanashauriwa kutumia Vyuo vya VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo jirani kwa ajili ya kupata elimu na mafunzo ya ufundi. Nakushukuru.