Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 5 Sitting 4 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 48 2021-11-05

Name

Cosato David Chumi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafinga Mjini

Primary Question

MHE.COSATO D. CHUMI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatoa GN kuwezesha Mradi wa Regrow kuanza rasmi katika eneo la Kihesa?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa maliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa tangazo la awali la siku 90 la nia ya kubadilisha matumizi ya sehemu ya eneo la Msitu wa Kihesa Kilolo, tarehe 9 Julai, 2021. Siku 90 tayari zimekwisha, hivyo Serikali imepanga kutoa GN ya Msitu wa Kihesa, Kilolo mwezi Novemba, 2021. Naomba kuwasilisha.