Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 5 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 18 2021-11-03

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Jimbo la Kilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali kupitia fedha za Mkopo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imetenga shilingi bilioni 46.94 kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa 253, ambapo magari 195 yenye thamani ya shilingi bilioni 35.1 yatanunuliwa kwa ajili ya halmashauri zote 184, ambapo kupitia magari hayo Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi itapatiwa gari moja la wagonjwa. Ahsante sana. (Makofi)