Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 3 Sitting 59 Finance and Planning Wizara ya Fedha na Mipango 498 2021-06-25

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, Serikali imejipangaje kutatua changamoto ya msongamano wa magari yanayovuka kuelekea nchi jirani kupitia mpaka wa Tunduma?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto ya msongamano wa magari katika Kituo cha Forodha Tunduma. Hatua hizo ni pamoja na kutekeleza mpango wa kurasimisha utaratibu wa kubadilishana taarifa za mizigo kati ya Dar es Salaam na Nakonde, Zambia; kuendelea kutoa huduma za forodha kwa muda wa saa 24; kuimarisha mifumo ya TEHAMA ya pande mbili ili kuwezesha taarifa za mizigo inayotoka katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia kusomana kwa wakati; na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa makubaliano baina ya pande mbili ya Januari, 2020 kuhusu mkakati wa kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na ujenzi wa maeneo ya maegesho ya magari kwa upande wa Zambia.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Zambia zitaendelea kuimarisha utendaji wa taasisi zote zinazohusika na shughuli za forodha katika Kituo cha Tunduma, pamoja na kuboresha mifumo ya TEHAMA na miundombinu ya barabara ili kukabiliana na changamoto ya msongamano wa magari.