Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 45 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 378 2019-06-13

Name

Vedastus Mathayo Manyinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Mjini

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE (K.n.y. MHE. VEDASTUS M. MANYINYI) aliuliza:-

Licha ya kazi nzuri ya waendesha bodaboda ya kurahisisha usafiri na kupunguza tatizo ya ajira bado ziko changamoto mbalimbali wanazosababisha kama ajali za mara kwa mara pamoja na wizi.

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza tatizo hilo?

(b) Je, Serikali haioni umuhimu wa kutofautisha adhabu ya waendesha bodaboda na ile ya magari makubwa kulingana na vipato vyao?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, vipo vyanzo vikuu vitatu vinavyosababisha ajali za barabarani hapa nchini. Vyanzo hivyo ni makosa ya kibinadamu ambayo kuchangia kwa asilimia 76, ubovu wa magari asilimia 16 na mazingira ya barabara huchangia kwa asilimia nane. Makosa ya kibinadamu ni pamoja na uendeshaji wa kizembe/hatari, mwendo kasi, ulevi, uzembe wa wapanda pikipiki, uzembe wa wapanda baiskeli, uzembe wa watembea kwa miguu na sababu nyinginezo kama hizo.

Mheshimiwa Spika, aidha Serikali kupitia Jeshi la Polisi iimekuwa ikitoa elimu kwa waendesha bodaboda namna nzuri ya utumiaji wa pikipiki ikiwa ni pamoja na kuvaa kofia ngumu, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa leseni za waendesha bodaboda ili kupunguza wale waendeshaji wasio na leseni ambao wanaweza kusababisha ajali.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekwishaliona hilo na kwamba kuna hatua mbalimbali zinaendelea kufanyika ili hatimaye adhabu zitofautiane kati ya waendesha bodaboda na wale wa magari makubwa.