Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 38 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 323 2019-05-29

Name

Haji Khatib Kai

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Micheweni

Primary Question

MHE. HAJI KHATIB KAI aliuliza:-

Je, ni sifa gani anastahili kuwa nazo Askari Polisi ili aweze kuteuliwa kuwa OCD?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khatib Haji Kai Mbunge wa Micheweni kama ifuatavyo;-

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa muundo wa maendeleo ya Utumishi wa Maaifa wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi ili Afisa aweze kuwa OCD ni lazima awe na sifa zifatazo;

• Awe na cheo cha Mrakibu Muandamizi wa Polisi.

• Awe na uwezo wa kuongoza ikiwa ni pamoja na kusimamia, kuratibu kazi za Maafisa, Wakaguzi na Askari walio chini yake kusimamia nidhamu katika himaya yake, kubuni na kuandaa mikakati ya ulinzi na usalama katika himaya yake.

• Awe na uwezo wa kufanya uamuzi, kutatua changamoto mbalimbali za kazi kuanzisha na kudumisha mahusiano mazuri na wananchi, pamoja na watendaji wengine wa Serikali na Taasisi zingine zilizo katika himaya yake na,

• Endapo kuna upungufu wa Maafisa wenye cheo cha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Afisa mwenye cheo cha Mrakibu wa Polisi anaweza kupewa madaraka ya kuwa OCD ili mradi awe na uzoefu na uwezo wa kuongoza.