Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 37 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 314 2019-05-28

Name

Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. SAADA MKUYA SALUM aliuliza:-

Kumekuwa na vitendo vya mauaji ya mara kwa mara kwa upande wa Zanzibar katika siku za hivi karibuni; mauaji hayo yanatokana na aidha kuuwawa kwa wanaoshukiwa kuwa ni wezi au mauaji mengine hayajulikani chanzo chake.

(a) Je, Serikali imeshafanya tathmini ya hali hiyo?

(b) Je, ni washukiwa wangapi kwa kipindi cha karibuni ambao wametiwa hatiani kutokana na vitendo vya mauaji kwa upande wa Zanzibar?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI aliji:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Saada Mkuya, Mbunge wa Welezo lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa kukijitokeza mauaji ya aina mbalimbali yakiwemo yale ya wananchi kujichukulia sheria mkononi baada ya kuchukizwa na vitendo vifanywavyo na watu wanaowaua. Hali hii ni kosa kisheria na Serikali imeshafanya tathmini ya kutosha ambapo kwa kipindi cha Juni, 2016 hadi Juni, 2017 jumla ya watu 34 waliuawa, 29 kati yao waliuawa kwa kutuhumiwa wizi, mmoja kwa tuhuma za ushirikina, wawili kwa tuhuma za wivu wa mapenzi na watatu kwa migogoro ya ardhi. Thathmini hii ya Serikali inakwenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi ili wasijichukulie sheria mikononi na badala yake wawafikishe watuhumiwa mbele ya vyombo vya sheria ili kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya watuhumiwa 33 wamekamatwa kwa tuhuma za mauaji na kesi 36 zimefunguliwa na zipo katika hatua mbalimbali mahakamani na baadhi zikiwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.