Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 18 Sitting 4 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 40 2020-01-31

Name

Mgeni Jadi Kadika

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MGENI JADI KADIKA aliuliza:-

Utandawazi umechangia sana vijana kupoteza maadili:-

Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kwa vijana wetu kuwekewa umri maalum wa kutumia mitandao ili kupunguza mmomonyoko wa maadili?

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli utandawazi umechangia sana katika kuleta mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa kwa jamii zetu hususan vijana kupitia intanenti, mitandao ya kijamii na maudhui ya nje kupitia muziki na filamu. Ndiyo sababu ya Serikali kuja na Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrime) ya mwaka 2015 na Kanuni za Maudhui ya Mtandao na Maudhui ya Redio na Runinga za mwaka 2018 ambazo zimepigiwa sana kelele ndani ya Bunge hili Tukufu kuwa zinaua uhuru.

Mheshimiwa Spika, wazazi na familia kwa ujumla ndio walezi wa kwanza wenye jukumu la kumlea mtoto kuanzia hatua ya awali na hufuatiwa na Taasisi za elimu ya awali, msingi, sekondari hadi elimu ya juu ambao huwaelimisha kwa maneno na vitendo watoto na vijana hususan utambuzi wa mambo mema na mabaya, yanayofaa na yasiyofaa. Baada ya hatua hizi kupita ndipo wajibu mkubwa wa Serikali unajitokeza.