Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 session 13 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 04 2018-11-06

Name

Lolesia Jeremia Maselle Bukwimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBAaliuliza:-
Je ni lini Serikali itapeleka gari la wagonjwa kwenye Kituo cha Afya Bukoli?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina gari saba zinazotoa huduma kwa wagonjwa (ambulance). Gari tano zinatoa huduma katika Vituo vya Afya vya Katoro, Nzera na Chikobe ambavyo vimeanza kutoa huduma za upasuaji. Gari mbili zinatoa huduma katika vituo vya afya vinavyobaki kikiwemo Bukoli ambacho kipo katika ukarabati ili kukiwezesha kutoa huduma za upasuaji. Halmashauri inashauriwa kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa gari za wagonjwa kulingana na mahitaji.