Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 11 Sitting 50 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 425 2018-06-13

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Mwese?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnamo tarehe 7 Mei, 2018, Serikali ilipeleka jumla ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya kujenga chumba cha mionzi (x-ray), nyumba ya mtumishi, maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Kituo cha Afya cha Mwese katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2018.