Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 7 Sitting 26 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 210 2017-05-16

Name

Eng. Atashasta Justus Nditiye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE aliuliza:-
Kwa muda wa zaidi ya miaka miwili, Hospitali ya Wilaya ya Kibondo haina mganga wa meno licha ya hospitali hiyo kuhudumia wagonjwa wengi kwa sasa ikiwemo wakimbizi kutoka nchini jirani ya Burundi:-
Je, ni lini Serikali itapeleka mtaalam wa meno katika hospitali hiyo?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Injinia Atashasta Justus Nditiye, Mbunge wa Muhambwe, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekwishapeleka mtaalam wa meno (Daktari Msaidizi wa Meno) tangu tarehe 12/4/2016. Kwa sasa yupo katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo na anaendelea kutoa huduma kwa wagonjwa.