Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 61 2024-02-02

Name

Salim Alaudin Hasham

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulanga

Primary Question

MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza:-

Je, lini serikali itajenga skimu za umwagiliaji katika Jimbo la Ulanga?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Salim Alaudin Hasham, Mbunge wa Ulanga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) inaendelea kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Skimu za Euga, Ulanga, hekta 440, Minepa, Ulanga, hekta1,800 na Lupilo, Ulanga, hekta 3,000. Mara baada ya zoezi la upembuzi yakiniffu kukamilika skimu hizi zitaanza kujengwa kulingana na upatikanaji wa fedha.