Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 2 Planning and Investment Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji 20 2024-04-03

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaachia maeneo yaliyotwaliwa na EPZA ambayo hayapo kwenye mipango ya matumizi ili wananchi wayatumie?

Name

Prof. Kitila Alexander Mkumbo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ubungo

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya EPZA imetwaa maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuanzisha Kanda Maalum za Kiuchumi. Maeneo hayo yapo katika hatua mbalimbali za utwaaji na uendelezaji. Katika kuendeleza maeneo hayo Mamlaka huandaa Mpango Kabambe ili kuainisha matumizi mbalimbali ya maeneo hayo. Hivyo, maeneo yaliyotwaliwa na EPZA bado yapo kwenye mpango wa matumizi yaliyokusudiwa.