Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 38 Industries and Trade Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara 341 2022-06-06

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Viwanda vya Mbolea nchini ili Wakulima waongeze tija?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA, alijibu: -

Mheshimwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Athuman Almas Maige, Mbunge wa Tabora Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na Mpango wa Kuratibu Uwekezaji wa Viwanda vya Mbolea Nchini. Matokeo ya uratibu huo ni pamoja na Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu na ujenzi unaoendelea wa Kiwanda cha Mbolea cha Itracom Fertilizer Limited, Jijini Dodoma. Nakushukuru.