Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 38 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 340 2022-06-06

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: -

Je, ni vijana wangapi wamepata nafasi za masomo nje ya nchi kwa mwaka 2015 - 2020 na kati yao ni wangapi wanatoka Zanzibar?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimwa Naibu Spika, kwa mwaka 2015 - 2021, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar iliratibu ufadhili wa masomo katika Nchi za Uingereza, Hangaria, China, Morocco, Misri, Algeria, Urusi, Ujerumani, Msumbiji, Thailand, Mauritius, Iran na Indonesia. Watanzania walionufaika na ufadhili huo ni 856 ambapo kati yao wanaume ni 609 sawa na 71.1% na wanawake 247 sawa na 28.9%.

Mheshimwa Naibu Spika, nafasi za ufadhili wa masomo nje ya nchi hutolewa pasipo kujali mwombaji anatoka upande upi wa Muungano.

Mheshimwa Naibu Spika, nakushukuru sana.