Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 38 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 335 2022-06-06

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka shilingi milioni 500 ya ujenzi wa Kituo cha Afya Namiungo na shilingi milioni 200 ya Kituo cha Afya cha Nakayaya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Zidadu Kungu, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Nakayaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kujenga Vituo vya Afya kwenye Kata za kimkakati kwa awamu ikiwemo Kata ya Namiungo. Ahsante.