Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 37 Foreign Affairs and International Cooperation Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 328 2022-06-03

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Pakistan?

Name

Amber. Mbarouk Nassor Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza kufanya utafiti wa kuangalia uwezekano wa kufungua Ubalozi nchini Pakistan. Utafiti huo unahusisha kuangalia faida za kiuchumi zilizopo nchini humo ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo ikiwa ni pamoja na kuainisha gharama za ufunguzi wa Ubalozi huo na uendeshaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.