Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Daniel Nicodemus Nsanzugwako (55 total)

Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nakushukuru ingawa muda ni mchache niseme mawili tu ya haraka haraka.
Kwanza, Waheshimiwa Wabunge leo tuna taarifa hizi kumi na zote hizi zinazungumzia mapendekezo ya Bunge hili. Kwa hiyo, nilikuwa nafikiri ni vyema ungetuongoza kwamba kama walivyosema wenzetu kwenye Kamati ya Uwekezaji ukurasa wa 49 kwamba ni vyema maazimio haya, mengine ni mazito sana, kwa mfano mambo yaliyozungumzwa kuhusu Bandari ya Dar es Salaam kama ni ya kweli basi yataisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sio hiyo tu wewe mwenyewe kwa sababu ni mahiri kuongoza Bunge hili ningeomba sana haya yote maazimio Waheshimiwa Wabunge tukubaliane yasiachiwe kwa Katibu wa Bunge; sisi wenyewe Wabunge tuunde Kamati yetu ndogo ya kuratibu mambo haya ni mambo mazito sana, vinginevyo yatakuwa hayana maana haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukumbushane kidogo, Mabunge mengine yanafanya hivyo kwamba kazi hii tunayoifanya ni kazi muhimu ya Kikatiba; ni kazi yetu kabisa ya msingi ya kuishauri Serikali na kuisimamia, lazima mambo ya msingi yalimo humu pengine si yote, lakini yale ya msingi lazima yadadavuliwe, yaandikwe vizuri na Serikali tuitake ije na majibu na kalenda yake ya utekelezaji, vinginevyo itakuwa ni hadithi tu, mambo ni mengi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengi yamezungumzwa humo ndani, ushauri wangu nakubaliana na wenzetu wa Kamati ya Uwekezaji kama walivyoainisha kwamba tuunde Kamati Ndogo na wewe Mheshimiwa Chenge utuongoze tuunde Kamati Ndogo itakayosimamia mambo haya kwa kuwa ni mambo makubwa na mazito sana ambayo haiwezi kuachiwa Ofisi ya Katibu peke yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ningependa niliseme kwa muda uliobaki kidogo huu nizungumzie suala la PPP. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda anahangaika sana, hongera. Kaza buti, lazima ufanye promotion na lazima uendelee kufanya promotion.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ushauri wangu ni kwamba, ili upate pesa lazima utumie pesa; waswahili wanasema ili ule lazima uliwe, ndiyo maana yake. (Kicheko)
Kwa hiyo, nilikuwa naomba hii private sekta tuisaidie, yenyewe haiwezi kunyanyuka; private sector duniani kote inasaidiwa kukua ili hatimaye iweze kuzalisha wafanyabiashara na walipe kodi na hatimaye kodi hiyo ndio inakuja kusaidia Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa mambo mengine yanatisha ukiyasoma humu ndani, kwa mfano kama kesi imeamuliwa ni kwa nini wenzetu wa Maliasili hawatekelezi haya yaliyoamuliwa na Mahakama? Kwa nini Serikali hamfanyi? Tunapotaze shilingi bilioni 10 wakati kesi imeamuliwa na Serikali imeshinda? Hakafu wakati huo tunaambiwa fedha hazipo, fedha si ndizo hizi? Ten billion mnai-surrender namna gani wakati kuna court ruling? Wale matajiri kama hawataki kakamateni mali zao tupate ten billion yetu. Sasa mengine humu ndani yanazungumzwa kwa kweli yanatia uchungu sana. Tunatafuta fedha tuna shida ya fedha ya miradi ya maendeleo fedha zingine zimeachiwa kwa matajiri na sababu iliyotolewa humu kwamba eti hakuna Bodi ya Tanzania National Parks, alah! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi bodi hiyo iundwe haraka sana na ndio mambo ambayo sisi kama Bunge lazima tusimame kidete na tuitake Serikali iunde hiyo bodi tuokoe ten billion yetu na hilo linakuwa halina mjadala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala mwisho ni la kilimo. Mimi tafsiri yangu ya viwanda ni viwanda vya kilimo, vya mifugo na vya sekta ya uvuvi. Hivi viwanda vya Wachina Waturuki, Waingereza na wengine wanakuja kutusaidia tu lakini the basic industry ni lazima itokane na kilimo chetu, kilimo, wafugaji na wavuvi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusa yako nizungumzie habari ya wawekezaji; ndugu Mwijage tembea na wawekezaji mfukoni kama wapo walete kwetu tutawapa maeneo ya kufanya shughuli zao.
Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nami nikupe pole kwa yaliyotokea maana mimi nipo karibu nao hapa, nilisikia minong‟ono yao tangu mapema. Tunakushukuru kwa uvumilivu wako mkubwa maana kwa kweli waliamua kufanya vurugu ambayo wala haikuwa na msingi wowote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna moja nilitaka kulisema lakini lingenoga kama wangekuwepo. Nataka niwakumbushe Wabunge wa CCM kwamba hii Serikali ni yetu sisi na sisi ndiyo wenye ajenda, wao hawana cha kupoteza hawa. Nilikuwa nafikiri ni vyema na sisi tukalifahamu vizuri jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana kuna Mbunge mmoja amezungumza ningependa angekuwepo rafiki yangu yule kwamba Wabunge wanajikombakomba, jambo hili limenikera sana. Hatuwezi kujikomba Serikali ni ya kwetu sisi. Rais huyu anatokana na Chama cha Mapinduzi ndiye anakuwa ni Rais wa Watanzania wote. Kwa hiyo, Serikali hii ni ya Chama cha Mapinduzi of course inafanya kazi kwa wananchi wote. Ndugu zangu Mawaziri mlioteuliwa na Mheshimiwa Magufuli msonge mbele kwani ajenda iliyopo mbele yetu ni kubwa na tusipepese macho. Twende kwa malengo yetu ili tuwe na cha kusema mwaka 2020 vinginevyo wenzetu hawa kwa msingi mkubwa hawana cha kupoteza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee naomba niwashukuru wananchi wa Kasulu Mjini kwa kuniamini, kwa kunituma kuja hapa na kwa kunirudisha Bungeni. Walinipeleka likizo lakini wameamua wao wenyewe kwa mapenzi yao nirudi hapa. Nami nawahakikishia kwamba sitawaangusha na nawashukuru wananchi wa Kasulu kwa kuchagua Madiwani wengi wa CCM na kura nyingi za Mheshimiwa Rais. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hotuba hii kwa maoni yangu, ningeshauri sana hotuba hii iwe ni input kwenye Mpango wetu wa Maendeleo kwa sababu imegusa kila kitu ambacho wananchi wanakilalamikia. Ukurasa wa 6 Mheshimiwa Rais amezungumzia vitendo vya rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Ukienda ukurasa 12 anazungumza hayo hayo lakini anahitimisha ukurasa wa 25 ana-quote maneno ya Mwalimu Nyerere miaka ya 1980 ambaye alisema hivi:- “Rushwa na ufisadi havina budi kushughulikiwa bila huruma kwa sababu naamini wakati wa amani, rushwa na ufisadi ni adui mkubwa wa ustawi wa jamii na ni adui mkubwa kuliko hata wakati wa vita.” Hayo ni maneno ya Mwalimu Nyerere.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 6, 11, 12 na 25, Mheshimiwa Rais ameonekana kukerwa sana na vitendo vya rushwa na wizi. Lazima tumsaidie kwa nguvu zetu zote kupiga vita rushwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nitoe mfano tu, katika kipindi cha mwaka 2012 - 2015, miaka mitatu tu, sisi wenzenu wa Halmashauri ya Kasulu, kwa mujibu wa ripoti ya CAG, tuliibiwa fedha shilingi bilioni 5.9 na wakati huo, ndiyo nataka na rafiki zangu wangesikiliza, waliokuwa Wabunge wa Majimbo yote mawili, Jimbo la Kasulu Mjini na Jimbo la Vijijini walikuwa ni wapinzani hawa. Wizi uliopitiliza, wizi uliotamalaki umetokea wakati wapinzani hawa wanasimamia Halmashauri yetu ila kule tumewashinda, tumewashughulikia vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naona Waziri wa TAMISEMI simuoni hapa, niombe kwa Waziri Mkuu, yale majizi yaliyotuibia kule Kasulu bado yapo. Wengine wamehamishwa, wengine wamestaafu na wengine eti wamepewa likizo za kustaafu. Tunaomba sana, Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI, bahati nzuri tumepata nyaraka muhimu sana za wote waliohusika, nitazipeleka kwa Waziri Mkuu ili majizi haya yashughulikiwe na mkondo wa sheria uchukue nafasi yake na yale yatakayotiwa hatiani hakika tuyapeleke jela pengine kule magereza ndipo ambapo wanastahili kuishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nimefarijika Mwanasheria Mkuu wa Serikali amenidokeza kwamba kumbe sheria ya kufilisi mali bado iko, haya majizi yanayotuibia nafikiri wakati sasa umefika, kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali sheria hiyo isimamiwe vizuri haya majizi tuyafilisi jamani haya. Wanaiba, wanafungwa wanarudi, tuyafilisi majizi haya ili nchi yetu iendelee kuwa na ustawi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo Mheshimiwa Rais amelizungumza na aliliona kama ni kero kote alikopita ni tatizo la maji. Maana ni ukweli usiopingika kwamba wanawake wa nchi hii ndiyo wametupa utawala huu na wanawake hawa ndiyo wanateka maji. Nafikiri wakati umefika kwa kweli wanawake hawa tuwape faraja ya kuwaondolea mzigo wa kuteka maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kule kwetu Kasulu sisi hatuna shida ya vyanzo vya maji na Waziri wa Maji analijua hili. Vyanzo tunavyo, shida ni kuviendeleza tu ili kuongeza mtandao wa maji katika Mji wa Kasulu ili hatimaye katika kata zinazozunguka Mji wa Kasulu ziweze kupata maji ya kutosha. Vyanzo tunavyo, tunahitaji fedha wala si nyingi sana ili tuweze kuwa na mtandao mkubwa wa maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 11 Mheshimiwa Rais amezungumzia na ametukumbusha juu ya nia na sera za CCM za kujenga barabara za lami kuunganisha mkoa na mkoa. Hili jambo ni la kisera wala siyo la utashi wa mtu, barabara ya kuunganisha mkoa na mkoa ni kipaumbele cha Serikali ya CCM. Waziri wa Fedha unalijua suala hili vizuri, sisi barabara ya Kigoma – Nyakanazi haina mbadala kwa sababu inatuunganisha na Mkoa wa Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga. Barabara hii kwetu haina mbadala. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nilidokeze kidogo tu ni suala hili la ujenzi wa reli, tumeshalizungumza sana.
Mimi ni muumini katika uchumi wa reli, bila nchi kuwa na reli hakuna kitu kinachoitwa kukuza uchumi. Huwezi kukuza uchumi au ukafikiria kuingia katika uchumi wa kati kama huna railway system. Hilo naliamini kabisa kwa nguvu zangu zote na Waziri wa Fedha bila shaka na yeye anaamini hivyo. Tutizame reli ya kati kwa jicho la kwenda kubeba mzigo ulioko Kongo ya Mashariki. Kule Kongo ya Mashariki kuna tani milioni tatu za shaba zinataka kwenda Ulaya na njia muafaka na nyepesi ni kupita reli ya kati, bandari ya Dar es Salaam na mwisho kwenye masoko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni wakimbizi. Jambo la wakimbizi sisi kwetu ni jambo kubwa na sisi wenzenu wa Mkoa wa Kigoma tumebeba dhamana ya kubeba wakimbizi hawa. Tuna wakimbizi kutoka Kongo, Rwanda, Burundi na kusema kweli tuna wakimbizi kutoka Somalia. Wote hawa wako katika Mkoa wa Kigoma. (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hotuba ya Rais kwa asilimia mia moja kwa mia moja. Nashukuru sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DANIEL N. NSANZUGWAKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia hoja ya Mapendekezo ya Mpango, nikisoma pamoja na mwongozo wake wa kuandaa bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze tu kwa kusema katika Bunge hili kwamba katika utamaduni wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Muswada kuwasilishwa mezani au na Waziri wa Serikali au na Mbunge na Muswada huu au hoja hii ikatolewa ni jambo la kawaida sana, ni jambo ambalo ni la kawaida kabisa na wala hakuna kitu ambacho ni cha ajabu. Nataka tuweke rekodi hizo kwa sababu yaliyotokea katika siku mbili ilionekana kama ni kitu kikubwa, lakini kumbe ni jambo la kawaida.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nitajikita katika mambo makubwa matatu, nitajielekeza katika miradi ya Kitaifa ya kimkakati. Bila shaka huwezi kuzungumzia kukuza uchumi kama huwezi ukazungumzia miradi ya kimkakati. Miradi ya kimkakati tafsiri yake ni kwamba ni miradi ambayo ikitekelezwa itausukuma uchumi ule uweze kuzalisha mambo mengi zaidi na uweze kuzalisha fedha ziweze kutekeleza mambo mengi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika miradi ya kimkakati, kabla sijaendelea na jambo hilo naomba ukurasa wa tisa wa Mpango, tufanye marekebisho kidogo. Katika yale maeneo yanayolima kahawa, nimeona yametajwa pale katika ukurasa wa tisa, wamesema katika Wilaya za Moshi, Mbinga, Bukoba, Mbozi na Tarime, kana kwamba ndiyo zinalima kahawa peke yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuweke rekodi sawasawa, kwa takwimu za Tanzania Coffee Board, Mkoa ambao unatoa kahawa ya arabika bora katika nchi za Afrika Mashariki ni pamoja na Mkoa wa Kigoma. Kwa hiyo, naomba katika mpango ule katika ile miche ya kahawa, ijumuishe pia Wilaya ya Kigoma na Wilaya ya Kasulu ambako tunalima arabika ya kiwango cha juu kabisa na zaidi ya hapo hata TaCRI wana kitalu kikubwa sana cha kuzalisha miche zaidi ya 1,000,000 pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miradi ya kimkakati, niungane na wasemaji waliopita kuzungumzia suala la reli ya kati. Naona kuna confusion kidogo hapa, hivi tukisema reli ya kati maana yake nini? Reli ya kati maana yake ni kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tabora, Kigoma na unakuja branch ya Tabora kwenda Mwanza ndiyo reli ya kati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muktadha wa Mpango huu, reli ya kati ni pamoja na mchepuko kutoka Isaka pale Kahama kwenda Keza, Keza iko kwenye mpaka wetu na Rwanda na pia mchepuko wa kutoka Uvinza kwenda Msongati ya Burundi na pia mchepuko wa Kaliua, Mpanda kwenda Kalema bandarini na mchepuko wa Dodoma kwenda Singida, hiyo ndiyo reli ya kati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli tunataka tuwe na uchumi wa viwanda, kama kweli tunataka nchi yetu ibadilike ingie katika uchumi wa kati, lazima tujenge reli. Sasa shida inakuwa pesa tunapata wapi, gharama ni kubwa kwa awamu kwanza tunahitaji takriba dola bilioni 7.6. Hii siyo fedha nyingi, nchi hii ni kubwa, tunakwenda kukopa, tuna marafiki wetu wa maendeleo, kuna Wachina na Wajapani wanatuamini na sisi tunawaamini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwamba hatuna fedha za kujenga reli, hatutaki kuisikia katika Bunge hili. Tunataka Serikali ije na mkakati mahsusi, mkakati wa msingi kabisa wa kwenda kukopa fedha hizi kwa Serikali ya Watu wa China, kwa Serikali ya Wajapani tujenge reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge, bila ya kuwa na reli, tunacheza ngoma. Haiwezekani mizigo yote, makontena yote, mafuta yote yapite kwenye barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, ni nchi yetu pekee ambayo mizigo mizito inapita kwenye barabara. Matokeo yake barabara hizi zinaharibika sana, inajengwa barabara ya kukaa miaka 30, uhai wake unakuwa ni miaka mitatu, minne, barabara inakuwa imeharibika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge tukubaliane, Waziri wa Fedha usipokuja na mkakati wa kujenga reli ya kati ikiwa na michepuko niliyoitaja, Isaka, Keza kwenda kubeba mzigo wa nickel, Uvinza - Msongati kwenda kwa ndugu zetu wa Burundi kuchukua mzigo wa Congo; mchepuko wa Kaliua, Mpanda - Kalema kwenda bandari ya Momba katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kuchukua mzigo wa Lumbumbashi.
Tunaomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha, utakapokuja na Mpango huo bila hiyo reli ya kati hatuwezi kuelewana katika Bunge na nitaomba Waheshimiwa Wabunge tusimame kidete kumwambia arejeshe Mpango huo mpaka atuwekee reli ya kati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani miaka zaidi ya ishirini tunazungumza reli ya kati, lakini haijengwi, haiwezekani? Wenzetu Kenya wameanza kujenga Mombasa kwenda Kigali, kwa nini sisi hatujengi, kwa nini hatuanzi, utasikia tumekarabati kilomita 176 za latiri 80, hatutaki kusikia lugha hiyo na nchi yetu si maskini, ina rasilimali za kutosha, tunaweza tukazikopea kujenga reli ya kati na michepuko niliyoitaja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya kati maana yake hizo reli zinakwenda kwenye mali, ukichepuka Isaka kwenda Keza, unakwenda kwenye nickel nyingi sana, tani milioni kwa mamilioni. Bandari ya Uvinza kwenda Msongati hiyo inapita Kasulu hiyo, Shunga - Kasulu, kwenda Burundi - Msongati maana yake ni madini ya nickel yaliyopo Burundi na mzigo ulioko Congo ya Mashariki. Isitoshe bila kujenga reli ya kati kwa standard gauge, tutaua bandari ya Dar es Salaam, bandari ya Dar es Salaam kwa miaka michache ijayo itakuwa haina mzigo, tutaua bandari ya Mwanza, tutaua bandari ya Kigoma na tutaua bandari ya Kalema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba sana, Waziri wa Fedha, bila kuja na mkakati mahususi wa reli hii, kwa tafsiri hiyo, tutashawishiana Wabunge wote tukuombe urudi tena mpaka uje na hoja mahususi ya kujenga reli ya kati. Bila reli ya kati hakuna uchumi wa viwanda, bila reli ya kati hakuna nchi kwenda kwenye pato la kati, kwa nini tuendelee kujiharibia wenyewe, wakati tunaweza tukatenda haya na yakafanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie ni maeneo wezeshi kwa maendeleo ya viwanda. Soma kwenye Mpango hapa, tumezungumzia juu ya nishati, reli na barabara. Nimefurahi kusikia kwamba washirika wetu wa Maendeleo wametupatia fedha kwa ajili ya kujenga gridi ya Taifa kutoka Geita sasa kuja Nyakanazi, Kwilingi na Kakonko, Mkoa wa Kigoma. Ningefikiri kupitia kwa Washirika wetu wa Maendeleo hao hao, tungeendeleza hiyo grid sasa, ile western grid, ile corridor kutoka Kakonko iende Kibondo, Kasulu, Kigoma na Katavi. Hatimaye iweze kuja ku-link na Tabora, tuweze kuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni la msingi sana na la kisera na liko kwenye Ilani yetu ni barabara ya Kigoma – Kidahwe - Nyakanazi. Hii barabara ni barabara ya kihistoria, imesemwa kwa miaka zaidi ya 20 sasa na bahati nzuri mkandarasi yuko site pale. Yule mkandarasi nimepata habari, alikuwa ananiambia Waziri wa Uchukuzi hapa kwamba wamempa fedha kidogo ili aendelee. Sasa tunaomba barabara hiyo ni barabara ya kimkakati kwa sababu inatuunganisha na mikoa mitano ya nchi hii; inatuunganisha Kigoma - Kagera, Kigoma - Mwanza, Kigoma - Geita, na Kigoma - Shinyanga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo barabara ni muhimu sana. Tunamwomba Waziri wa Fedha, aje na mkakati sasa wa kuimalizia barabara hiyo. Na huyo mkandarasi ambaye yuko site, basi tunamwomba aendelee ili barabara hiyo ikamilike. Si hiyo tu, sisi tunaotoka Kigoma, hiyo barabara ndiyo siasa za Kigoma na tunasema barabara ya Nyakanazi kipindi hiki, ndio wakati wake na niseme tu kwamba tutaomba sana barabara hii ijengwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nami nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza naipongeza sana Serikali kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya na hasa hii dhana ya kuwajibika Serikalini, ni dhana muhimu sana. Haya majitu yasiyowajibika wala msirudi nyuma, yaendelee kutumbuliwa ili yapotee kabisa! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaendelea, napenda nimrudishe Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa ukurasa wa 28. Ukurasa wa 28 kuna mambo ya nyongeza ambayo Mheshimiwa Waziri ameyasoma, kwenye kitabu hayapo. Yapo kumi nimeyasikia; moja mpaka kumi. Ulikwenda moja, tisa, kumi. Naomba yale kumi ya namna ya utekelezaji wa mkakati, ayaandike tuyapate. Ni ya msingi sana, nilimsikia vizuri sana kwa sababu nilikuwa hapa. Hilo ni ombi katika hotuba hii nzuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, nina mambo mawili ya haraka haraka, la kwanza naomba nijielekeze ukurasa wa 15 ambapo Tanzania imekuwa ikipoteza uwezo wake wa kushindana kibiashara.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia zile takwimu, zinatisha kidogo, kwamba kuanzia mwaka 2012 tumekuwa tunashindwa kuvutia mitaji ya ndani na ya nje na mbaya zaidi mwaka 2016 inatarajiwa tutakuwa nchi ya 139 katika nchi 186 katika kuvutia mitaji ya ndani na nje.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri, katika mkakati mzima wa kutekeleza Mpango wetu mzuri wa miaka mitano inayokuja, ni muhimu sasa Serikali na Wizara tukajua ni kwa nini hasa tumeshindwa kuvutia wawekezaji? Ni kwa nini hasa tumeshindwa kuvutia mitaji ya ndani? Tatizo ni nini? Ni urasimu kwenye vyombo vyetu huko TIC au tatizo ni nini hasa?
Mheshimiwa Naibu Spika, lazima iwepo sababu ambayo inafanya nchi yetu ishindwe. Katika nchi 186 kwa mujibu wa vigezo vya World Bank, tunapokuwa nchi ya 140, ni sawa na kuwa nyuma kabisa. Kwa hiyo, nawiwa kusema kwamba ni vyema Serikali yote ikae kuelewa kwa nini tumeshindwa kuvutia mitaji ya ndani na nje na ukizingatia mpango mzima kwa kiwango kikubwa, umetamka kwamba utashirikisha sekta binafsi?
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo ningependa kusema ni kilimo ambalo wenzangu wamelisemea, lakini niseme eneo dogo tu, kwenye Benki ya Kilimo. Mheshimiwa Waziri wa Fedha atakubaliana nami kwamba kama kweli tunataka kuwa nchi ya viwanda kwa dhati kabisa, ni lazima tuweke nguvu kubwa sana kwenye Sekta ya Kilimo.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya nyenzo za kukuza Sekta ya Kilimo ni pamoja na Benki hii ya Kilimo. Kwa mujibu wa hotuba hii, Benki ya Kilimo haina mtaji na kama inao ni kidogo sana. Ina Shilingi bilioni 60 tu, ukiachilia mbali kwamba Benki hiyo iko Dar es Salaam na wamekuja kwenye Kamati yetu tumewashauri kwamba wajitofautishe ili ikibidi sasa wahamie katika maeneo ya uzalishaji ili iwe Benki ambayo kweli ni kioo, ni Benki ya Wakulima na hakika isiwe Benki iliyoko Dar es Salaam.
Mheshimiwa Naibu Spika, nina ushauri mmoja kwa Serikali na hasa Wizara ya Fedha, hatuwezi kuendelea kama ilivyokuwa mwaka wa 2015 kwamba Benki ya Kilimo haina mtaji, lakini wenzao wa TIB, Alhamdullah wana angalau Shilingi bilioni 212. Benki ya Kilimo ambayo tunaitarajia isaidie wakulima ili wazalishe, hatimaye nchi iingie kwenye nchi ya viwanda na viwanda vingi viwe vya kuchakata mazao ya kilimo, bado Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kuna haja kubwa kama Serikali mwangalie namna nzuri ya kuwezesha Benki hii ya Kilimo iweze kufanya kazi zake.
Mheshimiwa Naibu Spika, zipo njia nyingi. Kwa mfano, kama wenzetu wa DANIDA waliweza ku-support CRDB na mnaona ilipofika, kama wenzetu wa DANIDA waliweza ku-support PASS kule Morogoro na mnaona PASS ilipofika, kwa nini Mashirika rafiki na nchi rafiki pengine zenye masharti rafiki msizihusishe katika mkakati mzima wa kuiwezesha Benki ya Kilimo kupata mtaji unaoeleweka? Nina hakika mkifanya hivyo Benki hii itasambaa katika maeneo mbalimbali katika nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, niweke angalizo; hatuwezi kuzungumza nchi ya viwanda kama hatuwezi kuwezesha Sekta ya Kilimo. Hilo ni lazima tukubaliane kabisa na bado kuna matatizo makubwa hata kwenye bajeti ya Sekta ya Kilimo. Mheshimiwa Waziri unajua kwamba bajeti ya pembejeo iko chini sana. Sasa kama bajeti ya pembejeo ipo chini sana kwa maana ya mbolea, mbegu, viatilifu, tafsiri yake ni kwamba hiki kilimo tunachotaka baadaye iwe ndiyo nguvu ya kujenga viwanda vya ndani, hiyo azma inaweza ikashindwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ushauri wangu sincerely kabisa ni kwamba lazima tuangalie namna nzuri ya kutoa fedha za kutosha kwenye eneo la pembejeo na hasa mbolea. Kwa takwimu za wenzetu wa Wizara ya Kilimo ni kwamba hata uzalishaji wa chakula mwaka 2015 ulishuka kwa takribani tani 500,000. Ni dhahiri tukienda katika mfumo huu ambapo hata fedha za pembejeo za kilimo zimeshuka, tafsiri yake ni kwamba uzalishaji wa mazao ya kilimo utakuwa chini and consequently itakuwa ni ngumu sana kupata mazao ya kutosha kumudu viwanda vyetu vya ndani na hatimaye tuweze kuboresha maisha ya watu wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo limenivutia sana ni hii miradi ya kipaumbele hasa reli ya kati. Naomba Serikali ifahamu kabisa tukisema reli ya kati, maana yake ni reli inayoanzia Kigoma inaishia Dar es Salaam, ndiyo reli ya kati na ndiyo jina lake. Mwanzo wa reli ni Kigoma na mwisho wa reli ni Dar es Salaam. Msingi wake ni mmoja tu, kwamba hii reli kule Kigoma itakuwa ni mkakati wa ku-tape kutoka nchi ya Kongo Mashariki ambako kuna shaba nyingi sana, zinc nyingi sana na mbao nyingi sana!
Mheshimiwa Naibu Spika, takwimu zinaonesha kwamba mzigo ulioko Mashariki ya DRC ni takribani tani milioni nne na hizo zinaweza kufika kwenye bandari na kwenda kwenye masoko nje ya nchi kupitia reli ya kati. Reli ya kati maana yake ni Kigoma - Dar es Salaam. Matawi yake ndiyo Tabora - Mwanza, Tabora – Kaliua – Mpanda na sasa hii mpya ya Uvinza – Msongati.
Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo tafsiri ni muhimu sana ili tuelewane vizuri. Kwa sababu bila kuwa na tafsiri hiyo, tafsiri yake ni kwamba ule mkakati wa tani milioni nne za Kongo ya Mashariki, hautaweza kupita Bandari ya Dar es Salaam. Sincerely nashauri hata ujenzi wa reli ya kati kwa standard gauge uanzie Kigoma kwa ku-tape mali iliyoko DRC halafu reli hiyo itoke Kigoma ndiyo ijengwe kuelekea Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine la mwisho ni utafiti. Nimesoma kwenye kitabu cha hotuba, Mheshimiwa Waziri wa Fedha umeanisha vizuri sana umuhimu wa utafiti, lakini liko jambo moja linahitaji uelewa tu wa jumla. Kwa nini Taasisi zetu za Utafiti, ili zipate fedha za Utafiti lazima eti zikashindanie COSTECH? Ni mambo ya ajabu kabisa haya! Nina hakika haya mambo ndiyo Mheshimiwa Magufuli hataki hata kuyasikia!
Mheshimiwa Naibu Spika, watafiti wako Ilonga, Uyole, Mlingano, lakini eti fedha za utafiti zinapelekwa COSTECH wakazishindanie ndiyo ziende kwenye Taasisi za Utafiti, kwa nini? Hivi unahitaji kwenda shule kulijua hili? Kwa nini pesa hizi zisiende kwenye utafiti moja kwa moja? Kwanza itapunguza urasimu na itapunguza muda wa fedha kutoka Hazina na kufikia Vyuo vya Utafiti.
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, nakualika Mheshimiwa Waziri wa Fedha, utembelee Kituo cha Utafiti cha Cholima kilichoko Dakawa. Hicho ndiyo kituo ambacho ni known kwa utafiti wa mpunga. Waheshimiwa Wabunge, kama tukiendelea hivi bila utafiti kwenye Kituo hicho nchi hii tutakosa mchele kwa miaka michache ijayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati yetu tumekwenda pale, tumekuta mambo ya ajabu sana! Hawa watu wana miaka mitatu hawajapata fedha kwa ajili ya utafiti. Fedha kidogo waliyoipata, eti wanashindanishwa na COSTECH! Mimi sielewi! Wala haikuingia kwenye kichwa changu hata kidogo, kwamba watafiti, wasomi wazuri, Watanzania hawa wanaanza tenda, ku-lobby kule COSTECH ili wapate fedha kuendesha utafiti kwenye Vyuo vyao.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali mjue wazi kabisa kwamba Vyuo vya Utafiti hasa kwa mazao ya kilimo vinajulikana; vipo Uyole, Naliendele, Ilonga, Ukiriguru, Mlingano, Seriani na kadhalika. Wapelekeeni fedha hao moja kwa moja, ni wataalam na wasomi wazuri katika jambo hili. Kupitisha hizi fedha COSTECH ni kupoteza wakati tu na kuweka urasimu ambao hauna sababu. (Makofi)
Mwisho kabisa naomba nami kwa namna ya pekee niwashukuru wapigakura wangu wa Kasulu Mjini kwa kuniwezesha kurudi Bungeni, maana haya mambo ni mazito!
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuwashukuru, naomba nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii na naunga mkono hoja. Mkakati ni mzuri na msonge mbele. Ahsanteni sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUNGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kwa namna ya pekee nikushukuru wewe mwenyewe binafsi kwa namna ambavyo unatuongoza katika kikao hiki kwamba Wabunge tunahitajiana na Muungano wetu huu ni muungano wa watu wa sehemu zote mbili na lazima wote tuvumiliane, tuheshimiane na tupendane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaanza kusema ninachotaka kusema naomba kwanza nioneshe masikitiko yangu kabisa kwa Wizara hii. Mheshimiwa Waziri nilikuwa nasoma hotuba yako yote, katika maeneo yaliyoathirika na ujio wa Wakimbizi Mkoa wa Kigoma tangu mwaka 1958 tumepokea Wakimbizi, lakini hotuba yote hii ya Ofisi ya Makamu wa Rais, hakuna hata sentensi moja inazungumzia uharibifu wa mazingira uliosababishwa na ujio wa Wakimbizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imenishangaza sana na Mheshimiwa Waziri sijui nina hakika ulisahau maana huwezi kufanya hivyo. Waheshimiwa Wabunge, Mkoa wa Kigoma tuna mazingira ya peke yetu kabisa, hayafanani na mahali pengine. Ujio wa Wakimbizi tumechukua dhima hii kwa niaba ya Taifa letu, lakini naona juhudi zinazofanywa na Serikali ni juhudi hafifu katika hatua zote za kukabiliana na uharibifu wa mazingira ambao umefanywa na ujio wa wakimbizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sina haja ya kushika mshahara wa Waziri baadaye ingawaje nimejiandaa kuukamata, ningependa nipate maelezo ni kitu gani kama Serikali inafanya kwa mazingira ambayo yameharibika kwa miaka 40 iliyopita na iko mito ambayo iko mbioni kupotea, Mheshimiwa Waziri wewe unajua Mto Makere sasa hivi umepotea, ule mto hautumiki tena. Chepechepe ya Malagarasi ambayo ni ardhi oevu na imetamkwa na UNESCO iko katika hatari ya kupotea kwa sababu ya harakati za binadamu na nyingi zikisababishwa na wakimbizi.
Ningeomba Mheshimiwa Waziri wakati unahitimisha hotuba yako ili tusigombanie mshahara wako ueleze ni hatua gani za makusudi zimefanywa kwa Mkoa wa Kigoma, Mkoa wote tumeathirika katika jambo hili, uhalifu ni mwingi, ujambazi ni mwingi, maradhi ya kuambukiza ni mengi kwa sababu ya ujio wa wakimbizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu ni shahidi, juzi ulikuwa Kigoma umeona mambo ya ajabu katika makambi ya wakimbizi, tunaomba jambo hili Mheshimiwa Waziri utueleze hatua gani zimefanyika katika ku-mitigate janga na mazingira vis-a-vis ujio wa wakimbizi katika Mkoa wa Kigoma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kwa ruhusa yako niliseme kidogo ni hili la Muungano. Hili jambo linazungmzwa, nina bahati nzuri nilishiriki katika harakati za muafaka tu, nilishiriki najua harakati zake. Mheshimiwa Waziri, CCM tumeshinda Uchaguzi Zanzibar, CCM tumeshinda Bara, lazima sasa wakati umefika Chama cha Mapinduzi na Serikali zetu mbili tufungue milango ya mazungumzo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo ya kisiasa hayaondolewi na uchaguzi, migogoro ya Kijeshi haiondolewi na uchaguzi, migogoro ya kiusalama haiondolewi na uchaguzi, migogoro ya kiusalama ya kisiasa inaondolewa na mazungumzo. Tufungue milango tuzungumze. Sisi ndiyo wa kupoteza, wana CCM ndiyo wenye mali, hawa wenzetu hawana mali sisi ndiyo tuna dhima ya kulinda mali hii. Nina hakika na naamini bila kutia mashaka kabisa kwamba hatuwezi kuiacha Zanzibar kama ilivyo, lazima tuzungumze ili hatimaye Muungano huu uweze kuwa na hatima ambayo itatusaidia kusonga mbele. Muungano tunauhitaji sana, acha kunipotosha wewe hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa niliseme ni athari pana za mazingira. Nitoe ushauri kwa Mheshimiwa Waziri, nchi yetu inakabiliwa na jangwa na wewe umeeleza vizuri kwenye kitabu chako. Nchi yetu inaathiriwa na kuzurura ovyo kwa mifugo kila pembe za nchi yetu. Wakati umefika jambo hili la uharibifu wa mazingira, jambo hili la nchi yetu kuingia katika athari na hatari ya jangwa haliwezi kuondolewa na Wizara moja, ni vizuri Ofisi ya Makamu wa Rais, iongoze harakati hizi za kukaa pamoja ili jambo hili lipate suluhu ya kudumu ili wakulima na wafugaji sasa watulie na athari hizi za tabianchi ziweze kutazamwa kwa ujumla wake kama Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo ni makubwa sana kila mahali kuna shida, naamini kabisa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano mnaweza kuwa ndiyo vinara, mkasikia will kuhakikisha kwamba tatizo hili la mazingira mnatazama kwa ujumla wake kama Serikali na kamwe siyo Wizara moja moja kama ambavyo tunaiona inatokea sasa hivi, kuna migogoro katika maeneo mengi sana na yote inatishia uhai wa mazingira ya Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo umelizungumza katika ukurasa wa 41, Mheshimiwa Waziri umezungumza kwamba kuna mwongozo umeutoa wa elimu ya hifadhi ya mazingira, ingekuwa vizuri hizo nakala 1,050 ambazo umesema zimesambazwa basi nakala chache Wabunge tuko siyo chini ya 400, Wabunge wote tupate nakala ya huo mwongozo wa elimu ya mazingira kama ulivyoeleza kwamba mmeusambaza katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo muhimu sana ili na Waheshimiwa Wabunge waweze kufanya kazi hii katika maeneo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, niwaombe wenzetu wa NEMC, katika hotuba yako umezungumza majukumu makubwa sana ya NEMC, ukaguzi wa viwanda, ukaguzi wa majosho, ukaguzi katika hifadhi zetu za wanyama, ukaguzi wa mahoteli. Naomba kupitia kwako wawekezaji wengi wanalalamikia muda mwingi ambao unatumiwa na NEMC katika ukaguzi wao, matokeo yake wawekezaji wengi wamekuwa wakinung‟unika sana na manung‟uniko yao ni pamoja na urasimu usiokuwa na sababu kabisa za wenzetu wa NEMC.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizungumza na wenzetu wa NEMC wako wasomi wazuri tu wakiongozwa na Dkt. Baya, ni wazuri sana, shida yao ni rasilimali fedha, rasilimali watu. Huwezi ukazungumzia uwekezaji wenye nguvu kama taasisi hizi zinazopaswa ku-facilitate uwekezaji bado ni dhaifu. Wenzetu wa NEMC wapeni nguvu, waongezeeni fedha ili kaguzi zao katika miradi mbalimbali ya uwekezaji uweze kwenda na iende kwa wakati. Kuchelewa unajua wawekezaji hawa lengo lao kubwa ni wakati, haiwezekani mtu anajenga kiwanda chake au hoteli anahitaji miezi mitatu ya ukaguzi, anawasubiri NEMC, anajenga service station anahitaji miezi mitatu, minne kusubiri NEMC haiwezekani! Tumezungumza nao wanasema shida yao kubwa ni resources, hawana fedha za kutosha na waongezewe wataalam wa kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, nitaunga mkono hoja hii kama nitasikia hatua ambazo zinafanyika za ku-mitigate masuala ya wakimbizi katika Mkoa wa Kigoma. Kwa hiyo, na-reserve jambo hili la kuunga mkono hoja hii mpaka nitakapopata maelezo mazuri kuhusu hatua ambazo zinafanyika kwa Mkoa wa Kigoma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru na sina haja ya kugombana na Waziri kwenye mshahara wake, nitaunga mkono nitakaporidhika na maelezo yake. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nami nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kusema machache. Niseme kwamba niko kwenye Kamati ya Kilimo, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri tunaendelea kukupa hongera kwa kazi yako nzuri na timu yako. Hata hivyo, nina machache ambayo ningependa tuweke record sawasawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hiki kitabu cha Mheshimiwa Waziri ni record, kina kumbukumbu, nimekisoma chote. Ukurasa wa 116 kinaainisha msaada wa chakula uliotolewa; ameainisha baadhi ya Wilaya. Kwa takwimu hizi, tafisiri yake ni kwamba, takriban asilimia 65 ya nchi yetu ina upungufu wa chakula. Kitu ambacho ningependa tuweke record sawasawa, humu ndani Mheshimiwa Waziri unasema kuna msaada wa chakula mmepeleka kwa Wakimbizi. Sasa nataka tuweke record sawasawa, siku hizi NFRA ndiyo inalisha wakimbizi wetu au ni suala la UNHCR? Naomba tuweke record vizuri kwenye vitabu vyetu hivi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia bullet inayofuata umesema tumetoa msaada wa chakula Southern Sudan. Sasa tumerudi kwenye enzi za Mzee Nyerere za ukombozi wa Bara la Afrika? Kwamba sisi tunaanza kuwalisha watu wa Southern Sudan?
Mheshimiwa Naibu Spika, nilidhani kule Southern Sudan tunakwenda kuuza nafaka zetu, kwasababu kuna fedha za UNHCR! Nilihisi vilevile kwenye makambi ya wakimbizi NFRA inakwenda kuuza chakula kule ili tupate fedha, tena fedha za kigeni kwa sababu haya Mashirika ya Kimataifa yana fedha za kigeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuweke record sawasawa, huo msaada unaosema unapeleka Southern Sudan ni msaada wa namna gani? Hao wakimbizi to my knowledge ni kwamba hawahitaji NFRA, wao wanalishwa kupitia fedha za UNHCR. Pengine Mheshimiwa Waziri kwa taarifa yako tu, sisi kwenye RCC tumeshakubaliana kwamba RC atakuja kwako kuomba kibali ili Mashirika ya Wakimbizi yanunue chakula katika Mkoa wa Kigoma ambacho kinazalishwa na wananchi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hilo tumeshakubaliana kwenye RCC na nasikia eti mpaka waje waombe kibali kwa Waziri. Mahindi ya kwetu, kuyauza NHCR hatuwezi mpaka tuje tuombe kibali kwenye Wizara. Nadhani hayo ni baadhi ya mambo ambayo yanahitaji kurekebishwa katika mfumo wa huu utawala wa nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo ningependa niliseme, Mheshimiwa Waziri tumeshazungumza suala la uzalishaji wa mbegu na suala la Bugaga. Nimekupa options mbili; hili shamba la Bugaga maarufu shamba la Wajapani; shamba la mbegu tulilitoa kwa ASA. Huu ni mwaka wa nane limeachwa kuwa shamba pori. Sisi tumewapa option tu, kama hili shamba hamlihitaji turudishieni Halmashauri. Turudishieni shamba letu! Haiwezekani! Uhaba wa kuzalisha mbegu ni mkubwa, lakini huu ni mwaka wa nane, shamba limekaa, lina miundombinu ya umwagiliaji lakini halitumiki! Kama wenzetu wa ASA wameshindwa Mheshimiwa Waziri na Wizara yako imeshindwa kulitumia, tunaomba shamba letu mturudishie. Wala hatuna ugomvi na hilo, tutalitumia wenyewe na tuna uwezo wa kulitumia.
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine kwa kweli ni kwamba na Waheshimiwa Wabunge wote mtuunge mkono, tumuunge mkono Waziri tuhakikishe fedha za pembejeo zinaongezeka. Hatuwezi kuzungumzia uchumi wa viwanda wakati hatujatafsiri kibajeti kusaidia Sekta ya Kilimo, haiwezekani! Naomba Waheshimiwa Wabunge wote tushikamane wakati utakapofika tuhakikishe sekta hii inaongezewa fedha; fedha za mbolea, fedha za madawa na kadhalika na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa niliseme ni mbolea hii ya Mijingu. Mheshimiwa Waziri kuna maeneo mengi, mbolea hii ya Mijingu ambayo inazalishwa katika nchi yetu, wananchi hawaelewi vizuri, wanailalamikia! Kwa nini Wizara msije clearly na wewe Mheshimiwa Waziri na watalaam wako mkaeleza exactly utajiri wa mbolea hii ili wananchi waelewe? Kwa sababu mbolea hii inazalishwa nchini, tungekuwa na fursa ya kuitumia zaidi. Ni muhimu kabisa wananchi hawa waelewe contents za mbolea hii na umuhimu wa mbolea hii. Maeneo mengine mbolea hii watu wanaikataa, lakini Serikali imekaa kimya haisemi jambo lolote. Tokeni nje muisemee mbolea hii kwa sababu inazalishwa hapa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, ni kumkumbusha tu Mheshimiwa Waziri na Watalaam wake wananisikia, kuna mtu mmoja amezunguza jambo hili; katika nchi yetu mikoa mitatu inayopata mvua za uhakiki inajulikana na ni Mikoa mitatu tu!
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miaka 40 iliyopita mikoa yenye mvua za uhakika, udongo wa rutuba ni mikoa mitatu tu. Mkoa wa kwanza ni Kagera, hakuna uwekezaji wa maana umefanyika wa kilimo kule; Mkoa wa pili ni Kigoma, hakuna uwekezaji wa maana wa kilimo umefanyika kule; Mkoa wa tatu ni Katavi. Sasa mnahangaika, mnawekeza maeneo ambayo hayana mvua, hayana udongo wenye rutuba, ni kitu gani mnafanya Mheshimiwa Waziri? Mkae kama Serikali, hii Mikoa ambayo tuna comperative advantage, tuweze kuwekeza kwa nguvu zetu zote katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, pale Kasulu tuna Chuo cha Kilimo. Kile Chuo kilikuwa cha World Bank baadaye World Bank wakakiacha, sasa kimerudi. Tunaomba kupitia kwako Mheshimiwa Waziri na wananchi wa Kasulu wamenituma jambo hili, tunakiomba kiwe ni sehemu ya mlingano, sehemu ambayo…
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja hii lakini Mheshimiwa Mwigulu nadhani tumeelewana vizuri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami kwa namna ya pekee nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Naomba kwanza nianze kwa kukupa hongera nyingi sana Profesa Ndalichako na timu yako, mnafanya kazi nzuri, hongereni sana. Hiyo ni tafsiri kabisa kwamba akina mama wenye ujuzi, mnaweza, hongereni sana! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wizara hii, niseme tu kwamba Mheshimiwa Waziri unafahamu kwamba asilimia 68 ya Civil Service ya nchi hii ni Walimu. Kwa hiyo, zaidi ya Watumishi wa Serikali hii ni Walimu. 68 percent ndiyo Civil Service ya nchi hii. Tafadhali sana! Wewe Mheshimiwa Waziri, Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Utumishi, kaeni pamoja kuhakikisha kwamba Walimu hawa tunawapa kipaumbele cha kwanza. Bila wao hakuna nchi hii. Sisi wote tuko hapa kwa sababu tulisoma, kwa sababu tulifundishwa na Walimu hawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bila shaka kila mmoja anafahamu kwamba Walimu hawa wana changamoto nyingi sana. Shule zetu nyingi hazina nyumba za Walimu, shule nyingi hazina madarasa ya kutosha, Halmashauri zetu zinahangaika kushoto na kulia. Naomba, wakati umefika, Serikali yenyewe itafute fedha popote itakapopata fedha hizo, kujumuika na Halmashauri zetu ili miundombinu ya elimu iweze kuwa rafiki na hakika shule zetu ziweze kuboreka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, ambalo napenda kulisema, ni hili jambo la ada elekezi. Mimi huwa sielewi vizuri, labda Mheshimiwa Waziri atanifafanulia. Hivi ada elekezi ambazo mng‟ang‟ana na hao wenye shule, hizi shule siyo mali ya Serikali! Hizi shule ni mali ya watu binafsi. Mmekaa nao? Mmezungumza nao? Mmelewana? Maana yake haya ni kama mtu mwenye mali yako, halafu anakuja mtu mwingine anasema basi weka ada elekezi. Kila mmoja anajua nchi hii, miaka ya 1980 na 1990, watoto wetu walikuwa wakienda Kenya, Uganda na Malawi kusoma. Sasa wenye mitaji yao wameanzisha shule hizi, tunaanza kuja na ada elekezi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu na ushauri wangu kwa Serikali, kaeni na wamiliki wa shule hizi, ni mali zao, mwasikililize, Serikali ifanye facilitation tu. Hakuna sababu ya kugombana na hawa watu. Tunataka watoto wetu wakasome tena Kenya? Wakasome Uganda? Ni muhimu sana ada elekezi hizi mkubaliane na wamiliki wa shule, zile shule ni mali yao na kamwe siyo mali ya Serikali; na tumeshatoka huko ambako mali zilikuwa za Serikali, shule zilikuwa za Serikali; sasa shuke hizi ni za watu binafsi. Naomba sana jambo hili Mheshimiwa Waziri, wewe ni mahiri, wewe mwenyewe ni Mwalimu, mkae mliangalie vizuri mkubaliane na hawa wamiliki wa shule na muafaka upatikane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hakika mkizungumza na wamiliki wa shule, wana uelewa, wamewekeza fedha zao nina hakika mtafika mahali kwenye middle ground ambapo hata kama ni ada elekezi basi ni rafiki kwa wamiliki wa shule na kwamba pia watafanya biashara pamoja na kwamba elimu kwa kweli kwa kiwango kikubwa ni huduma zaidi kuliko biashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda niliseme ni haya mafao na malipo ya Walimu, kwa mfano, Walimu katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Walimu katika Mkoa wa Kigoma, wamekuwa na malimbikizo mengi sana. Nimepata taarifa kwamba juzi wamelipwa, eti madai yao fedha iliyohakikiwa wameletewa asilimia 13 tu basi. Sasa anayefanya uhakiki ni nani huyo? Hawa Walimu ni kipaumbele. Naomba sana Walimu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Walimu wa Kasulu Mjini na Halmashauri wahakikiwe vizuri. Unafanyaje uhakiki unakuja na ten percent ya uhakiki! Ni kitu ambacho hakikubaliki. Ingekuwa angalau 40 percent, 50 percent unaweza ukaelewa, ten percent, 13 percent ya madai yao yaliyohakikiwa, hilo ni dhahiri kabisa kwamba kuna mahali kuna tatizo na tatizo tusiliruhusu likachafua Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imeanza kwa matumaini makubwa kwa Watanzania hawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda nilizungumze, sisi Mkoa wa Kigoma, tumeanza kujenga a grand High School, Shule ya Sayansi. Maana yake Waheshimiwa Wabunge mnafahamu kwamba Mwanasayansi aliyepata tuzo ya Nobel katika nchi hii, anatoka Mkoa wa Kigoma. Tumeanza kwa juhudi zetu wenyewe, tumejenga a ground high school, shule ya sayansi. Imejengwa pale Kasulu, tumejichangisha wenyewe, mkoa mzima tumepata karibu shilingi milioni 600 na tumeanza kujenga shule pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana Wizara nayo, wewe Mheshimiwa Mama Ndalichako ni mdau, nawe kama Wizara na Serikali kwa ujumla mwangalie namna nzuri ya kusaidia juhudi za watu wa Kasulu na watu wa Kigoma ili hatimaye ile grand high school baadaye tuibadilishe iwe Chuo Kikuu. Kitakuwa Chuo Kikuu cha kwanza cha sayansi. Nina hakika kwa uwezo wa vijana wa Kigoma, kitatoa wanasayansi walio bora na walio mahiri sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi hiyo imeshaanza na wenzetu wa SUMA JKT wametupa ushirikiano mzuri sana, ndio wanatujengea eneo hili. Nasi Halmashauri ya Mji wa Kasulu tumetoa eneo bila fidia, eneo la ekari 115 nami Mbunge wao nimetumia kila lililokuwa ndani ya uwezo wangu, kuhakikisha kwamba eneo lile limepimwa na linamilikiwa kihalali sasa na Halmashauri na Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya ujenzi wa Grand High School. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho nizungumzie ujenzi wa makitaba. Sisi pale katika Mji wa Kasulu tumejenga maktaba. Kipindi kile nikiwa Mbunge mwaka 2005 tulijenga maktaba kwa kushirikiana na wenzetu wa Tanzania National Parks. Tumejenga jingo kubwa, lina gorofa mbili. Jengo lile limegota, nafikiri ni wakati muafaka umefika sasa Wizara na Serikali mwingilie kati mtupe nguvu, mtusaidie ili jengo lile sasa lianze kufanya kazi. Malengo na madhumuni ni kufanya maktaba ile kiwe ni kituo cha elimu katika Mji wa Kasulu na ni mji ambao unakua kwa haraka sana kama miji mingine inavyokua katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba nizungumzie suala la ukaguzi wa shule. Mheshimiwa Waziri, shule hazikaguliwi. Waheshimiwa Wabunge shule za Sekondri na za Msingi hazikaguliwi. Sasa shule hazikugaliwi…
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, naunga mkono hoja hii, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii. Hata hivyo nianze na kuchangia machache katika sekta hii ya elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Wizara na Serikali kuzifanya High Schools zote nchi nzima ziwe chini ya Wizara ya elimu na TAMISEMI ibaki na Primary Schools na „O‟ Level Secondary Schools tu. Hii itasaidia sana Halmashauri za Wilaya na Miji yetu kujikita zaidi kuboresha shule tajwa hapo juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya 2006/2007 Serikali iliamua kwa maksudi kusaidia Mikoa, ambayo ipo nyuma kielimu. Mikoa hiyo ni pamoja na Kigoma, Singida, Mtwara, Lindi na Katavi. Mikoa hii ilikuwa inapata fedha za ziada kila mwaka shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia kujenga madarasa, mabweni ya wasichana na nyumba za walimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha hizi zilisaidia sana na kwa Mkoa wa Kigoma hali ilianza kubadilika, ajabu ni kwamba, baadaye 2011/2012 fedha hizo zilisitishwa!
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashauri sana fedha hiyo, irejeshwe ili Mikoa iliyobaki nyuma kielimu iweze angalau kupiga hatua. Huu ulikuwa mpango maalum ni lazima Serikali iangalie hali hii ili kuweka uwiano mzuri katika nchi yetu na baina ya Mikoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitengo cha Ukaguzi wa Shule; kitengo hiki kimezorota sana na sehemu nyingine shule za msingi na sekondari hazikaguliwi kabisa! Ni vizuri kitengo hiki kiwe kitengo huru na kisimamiwe na Wizara moja kwa moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu malipo ya Walimu katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu; malipo ya walimu yahakikiwe vizuri na walipwe stahili zao za matibabu, likizo, likizo ya uzazi, kupanda vyeo na kadhalika. Walimu wengi wanalalamika sana, Wizara ya Elimu na TAMISEMI harakisheni uhakiki ili walimu hawa walipwe fedha zao mapema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la Ujenzi wa Maktaba ya Wilaya Kasulu; Halmashauri ya Mji wa Kasulu tulijenga jengo la maktaba lenye ukubwa wa ghorofa mbili. Tulishirikisha wadau mbalimbali wa elimu kama vile TANAPA na UNHCR tukafika ujenzi wa asilimia 65. Tafadhali Wizara au Serikali saidieni juhudi za wananchi hawa, tupeni nguvu. Tukipata shilingi milioni 200 zitasaidia sana kukamilisha jengo hili na litaanza kutumika. Ni matarajio yetu mwaka 2016/2017, Wizara itaangalia namna njema ya kufanikisha na kukamilisha mradi huu muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ujenzi wa Kasulu Science Grand School; Mkoa wa Kigoma wenye Halmashauri Nane tumeanza mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Sayansi. Mkoa wa Kigoma ulianza kazi hii kutuma Suma JKT, kazi imeanza na hadi sasa shilingi milioni 600 zimetumika. Tunaomba Serikali na Wizara ya Elimu isaidie mradi huu muhimu kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma. Tumeanza tusaidieni kukamilisha ndoto yetu ya kujenga shule hii muhimu ya sayansi. Matarajio yetu ni kwamba, shule hii baadaye tutaifanya ni Chuo Kikuu cha Sayansi na kitaitwa Kigoma University of Science and Technology.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Kasulu tumetoa eneo la ekari 115 kwa ajili ya ujenzi wa shule hii. Eneo hili limepimwa na sasa tuna – process hati ya kumiliki ardhi hiyo. Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Kigoma tumeanza, tunahitaji msaada wa Wizara ya Elimu ili ndoto yetu iweze kukamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa namna ya pekee kabisa, naomba niwape hongera sana Mawaziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Simbachawene na Mheshimiwa Kairuki na Naibu Waziri, bado ni vijana na mna nguvu, tunataraji mtakimbia na kasi hii na mtafika. Pia kwa namna pekee naomba nimshukuru sana Katibu Mkuu wa Wizara yenu ni mtu msikivu sana, Alhaji Iyombe, kila ukienda ofisini kwake ni mtu wa msaada sana. Alhaji Iyombe kama unanisikia hongera sana kwa utulivu wako na utu uzima wako, endelea kulea vijana hawa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa na machache ya kuzungumzia. La kwanza ni utawala bora. Wakati Mheshimiwa Bashe anachangia alizungumzia habari ya majizi ambayo yanahama kutoka halmashauri moja kwenda nyingine. Mheshimiwa Waziri Mkuu maadam uko hapa nikukumbushe jambo moja kwamba moja ya majizi makubwa nililokuletea lilipelekwa Nzega kutoka Kasulu.
Mheshimiwa Simbachawene liko tatizo kubwa la wizi uliotokea pale Kasulu wa shilingi bilioni 5.9 kati ya mwaka 2013/2015 na haya majizi bado yanatembea tu na mengine yamehamishwa. Mheshimiwa Waziri Mkuu katika yale majizi yaliyokubuhu, moja ya majizi yale lilitoka Kasulu likaenda Nzega na kule Nzega nimeambiwa amestaafu baada ya kutuibia pesa nyingi sana. Haiwezekani! Huyu mtu lazima atafutwe na afikishwe kwenye mikono ya sheria.
Kwa hiyo, kusema kwamba Nzega ilikuwa ni dumping ground nadhani ni kweli maana hata hilo jizi lililokubuhu lilitoka Kasulu likapelekwa Nzega. Mheshimiwa Waziri Mkuu mtusaidie majitu haya yakamatwe yafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo napenda kulizungumzia alilisema Mheshimiwa Makamba siku anachangia bajeti ya Waziri Mkuu, juu ya utawala bora. Mheshimiwa Simbachawene tuna Halmashauri zaidi ya 34 zinaongozwa na wapinzani wetu kwa maana kwamba baada ya matokeo ya uchaguzi walichaguliwa na wanaziongoza. Nawashauri sana, hizi Halmashauri ambazo zinaongozwa na wapinzani na hizi zinazoongozwa na wana CCM zenye wapinzani wengi vilevile, kuna haja kabisa ya kuzipangia mkakati wa mafunzo maalum vinginevyo hazitatawalika, wataishia kwenye ubishi tu, ndio ni zote, hazitatawalika hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, siku ile Mheshimiwa Makamba alisema jambo la msingi kwamba chama cha siasa kikishinda uchaguzi kinaunda Serikali, ni kweli na ndiyo utamaduni wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Siyo kuunda Serikali tu, kinaanza kutekeleza ilani yake ya uchaguzi na hakiishii hapo lazima kipate space ya kutawala na wapinzani wetu lazima watupe nafasi ya kutawala, hilo halina ubishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, equally the same, chama tawala nacho lazima kijue kwamba kuna nafasi ya wapinzani katika demokrasia na hiyo space lazima iwepo. Space hiyo Mheshimiwa Simbachawene haiwezi kutoka mbinguni lazima hawa watu wawe trained. Halmashauri 34 zinaongozwa na wapinzani per se lakini ziko nyingine kama 14 hivi zina wapinzani wengi kwa maana kwamba unakuta CCM tumezidi mmoja, wawili, watatu au wanne, kwa sababu ya dhana nzima ya utawala bora lazima kuwe na special program kupitia TAMISEMI kuwajengea uwezo vyama na Halmashauri zote hizi na hasa hizi ambazo zinaongozwa na CCM kwa wingi na hizi ambazo zinaongozwa na wapinzani.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu wa Kambi ya Upinzani niwakumbushe kitu kimoja, opposition maana yake ni kuikumbusha Serikali ya siku isilale usingizi.
Ndiyo utamaduni huo lakini na ninyi kwa sababu mlishindwa uchaguzi mkuu lazima mtoe space ya kutawala kwa watu walioshinda na hilo hatubishani. Mimi sikuwepo siku mbili hizi nimeshukuru sana leo kuona wapinzani wanachangia ndiyo demokrasia hiyo. Ile kukimbia hupati kitu unaposema unatusaidia sisi tujue unachosema, unachofikiri lakini mkikaa kimya mlikuwa mnatunyima haki yetu.
MBUNGE FULANI: Eeeeh.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Ndiyo na mlikuwa mnafanya vibaya, lakini sasa nashukuru busara zimeingia, mmewasomesha wameelewa na tutakwenda vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu ambalo napenda nilizungumzie ni mipango miji. Mheshimiwa Simbachawene unazungumza kwenye hotuba yako upangaji wa miji na kwamba umeisha-identify miji 600, hiyo miji yenyewe iliyopo haina Maafisa wa Ardhi, Maafisa Mipango Miji na haina Valuers. Sasa niulize, hivi kuna tatizo gani la kuajiri moja kwa moja toka kwenye vyuo vyetu vya ardhi wataalam hawa wakaenda kwenye Halmashauri zetu ili kuzuia miji holela? Hili ni jambo muhimu sana, Waziri wa Ardhi uko hapa hebu mshirikiane na TAMISEMI muweze kuondoa tatizo hili. Huwezi kuzungumzia kupanga miji kama huwezi kuwa na wataalam ambao kazi yao ni kupanga miji hii. Jambo hili linawezekana na mnaweza mkalifanyia kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la nne ni nyumba za walimu. Nadhani walimu wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba kama kuna shida kubwa iliyopo kwenye halmashauri zetu ni nyumba za walimu jamani, walimu hawana nyumba za kukaa, kabisa. Unashangaa sasa kila Halmashauri inakuwa na utaratibu wake wa kuweka kwenye bajeti nyumba 5, 10, 12. Nilikuwa naangalia kwenye kitabu hiki cha TAMISEMI kwenye development, Mheshimiwa Simbachawene una karibu shilingi trilioni moja kwa ajili ya development. Hebu Mheshimiwa Simbachawene hizi fedha za development katika eneo la nyumba za walimu kwa nini ...
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa muda umeisha.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia sekta hii muhimu sana ya uchukuzi, barabara, reli na kadhalika. Kwanza niwape hongera sana timu ya Profesa na mwenzake kwa kazi mnayoifanya.
Mheshimiwa Spika, nataka nijielekeze katika mambo matatu. Suala la kwanza ni suala la kisera. Tumeshakubaliana na kwa mujibu wa Sera za Chama cha Mapinduzi kwamba tutajenga barabara za lami kuunganisha mkoa na mkoa, ndivyo tulivyokubaliana. Nilikuwa najaribu kuangalia hotuba ya Mheshimiwa Waziri, hiyo sera hamuizingatii. Mnaanza kuhamisha rasilimali na resources kuhangaika na barabara za Kata kwenda Kata na Wilaya kwenda Wilaya. Kwa nini tusianze kujenga barabara za kuunganisha mikoa kwa mikoa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa mfano sisi Mkoa wa Kigoma, nashukuru nimeona kuna juhudi inafanyika kwa barabara yetu ya Tabora – Kigoma kwamba kuna vipande vipande bado vinafanyiwa kazi na nimeona kuna mweleko mzuri. Hopefully flow ya fedha itakwenda vizuri ili barabara ile ikamilike; lakini bado sisi hatujaunganishwa na Tabora, hatujaunganishwa na Katavi, haijaunganishwa na Kagera, haijaunganishwa na Mwanza, haijaunganishwa na Shinyanga. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa napenda Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha anieleze, kwa nini wanatapanya resources wakati tumeshakubaliana kwamba mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano iunganishwe kwanza kabla ya maeneo mengine? Hilo ni jambo muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, nizungumzie suala la uwiano. Jamani hii nchi ni yetu wote. Hakuna wa Tanzania bora kuliko Watanzania wengine, Watanzania wote ni sawasawa. Ukiangalia mtandao wa barabara za TANROADS na unaweza ukaenda tu ukapata picha ukurasa 279, ukiangalia zile barabara za changarawe kwa mfano, inakupa picha ya moja kwa moja kwamba kuna mikoa ambayo ina mtandao mkubwa kuliko mikoa mingine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri, ni mpya katika awamu hii na bahati nzuri Jimbo lake ni Ikulu, hana Jimbo la uchaguzi, naomba waanze kwenda na utaratibu kuwe na uwiano, ikibidi wa-employ concept ya slow match na quick match. Wale waliotangulia sana, wasubiri wenzao. Haiwezekani unakuwa na mkoa una mtandao wa kilometa 300 wengine wana mtandao wa kilomita 600 wengine 900 wengine 800; that is very unfair. Twende kwa utaratibu mzuri (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hiyo, sisi Mkoa wa Kigoma tumeomba barabara kupandishwa hadhi kutoka barabara za Wilaya, Halmashauri, kuwa barabara za Mkoa kwa maana ya TANROADS. Tunaomba Mheshimiwa Waziri alizingatie hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa mfano kule Kasulu kuna barabara muhimu sana, inatuunganisha kati ya Kasulu, Kabanga, Msambala, inakwenda Mwanga mpaka Wilaya mpya ya Buhigwe, kwenda border yetu na Burundi. Barabara hiyo tunaomba, Mheshimiwa Waziri kwa kibali chake tumeshapitisha kwenye RCC, inangoja timu yake ile na Kamati yake ili barabara hiyo waweze kuipandisha hadhi. Tutaomba sana! Siyo hiyo tu, ziko barabara tatu, nne za Mkoa wa Kigoma ambazo tumeomba zipandishwe hadhi na hiyo tafsiri yake itatuongezea mtandao wa barabara angalau za changarawe. Hilo lilikuwa la kwanza.
Mheshimiwa Spika, la pili, ni barababara yetu ya kihistoria ya muda mrefu nimeona imetengewa fedha, shilingi bilioni 70 Kidahwe – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi, Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 32 ameeleza vizuri kwamba kipande cha Kidahwe – Kasulu kuna mkandarasi yuko pale na kimetengewa fedha; na kipande cha Kabingo - Nyakanazi, nacho kimetengewa fedha, lakini hapo katikati, kuna kilometa zaidi ya 200 za Kabingo – Kibondo – Kasulu - Manyovu Border na Burundi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri ameandika kwenye kitabu chake kwamba kilometa 258, amezungumza kwenye kitabu chake kwamba hiyo inafadhiliwa na fedha za African Development Bank. Sasa tungependa kujua, ameishia hapo tu na akaweka na nukta kubwa, maana yake nini? Hizo barabara zinaanza lini? Kwenye vitabu vyake vyote viwili haonyeshi bajeti au hizo fedha za ADB zitatoka lini na ni kiasi gani kwa barabara hiyo?
Mheshimiwa Spika, hiyo maana yake nini? Maana yake ni kwamba, hiyo barabara kubwa ya kihistoria ya Kigoma - Kidahwe - Nyakanazi itakuwa haijakamilika, kama hicho kipande hakijakamilika, sisi tunaotoka Kidahwe, Kasulu itakuwa imekamilika. Nilimshukuru Mheshimiwa Waziri, nilimwona akiwa Kijiji cha Kasangezi anahangaika na barabara ile. Yule Mkandarasi juzi nimemuuliza mwenyewe akaniambia amepewa fedha. Hiyo ni assuarance ya watu wa Kigoma, kwamba hiyo barabara ya kihistoria sasa inajengwa. Tunaomba flow ya fedha iendelee, barabara hiyo ni muhimu sana, kwa sababu ni barabara ya kihistoria na ni barabara ya siku nyingi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini sambamba na hilo naomba pia nizungumzie barabara ambayo ameitaja kwenye kitabu chake, hii barabara ya Sumbawanga - Mpanda - Nyakanazi, shilingi bilioni 77. Sasa nataka kujua Mheshimiwa Waziri, hii barabara maana yake kutoka Sumbawanga ukaja mpaka Katavi - Mpanda, ukaja mpaka Uvinza - Border, ukaja mpaka Kanyani - Kasulu kwenda Nyakanazi, hiyo ni barabara ndefu sana. Tunaomba sana Mheshimiwa Waziri tuelewe, hizi fedha ambazo wamezitenga, shilingi bilioni 77 zinajenga sekta ipi? Maana yake ukitoka Mpanda mpaka Uvinza, unazungumza habari ya kilometa 600 ni mbali sana! Sasa napenda kujua, hizo shilingi bilioni 77.5 zinajenga sekta ipi katika barabara hiyo?
Mheshimiwa Spika, nakumbuka kulikuwa na mkakati wa kujenga barabara itoke Katavi kwa maana ya Mpanda kuja Uvinza border, ije mpaka Kanyani - Kasulu - Nyakanazi inakuwa ina-link ile barabara. Sasa tungependa kujua hizi fedha huyo mkandarasi atakuwa anaanzia wapi, anaanzia Kanyani kwenda Uvinza au anaanzia Uvinza kwenda Mpanda, kwa maana ya Mkoa wa Katavi? Mheshimiwa Waziri ningependa kuelewa kwa sababu hiyo ni barabara ndefu sana na inapewa jina refu sana, kilometa zaidi ya 600, ni barabara ndefu na ningeomba kupata maelezo ya kutosha.
Mheshimiwa Spika, jambo lingine dogo tu, kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 75 amezungumza ujenzi wa block train kwenda Kigoma na Mwanza kwa kuhudumia wafanyabiashara wa Kigoma – Mwanza – Tabora – DRC - Burundi - Uganda na kadhalika. Amezungumza habari ya vichwa vya treni, kuundwa. Yeye unajua Kiswahili; yeye ni mtu wa Zanzibar, kuundwa maana yake nini? Wanaunda vichwa vya treni au wananunua vichwa vya treni? Sijui kama ni lugha maana wanazungumza kuunda vichwa vya treni, sasa kuunda maana yake nini? Kama wanaviunda, basi napenda clarity tu, labda ni lugha, lakini ninachojua kama wanachozungumza ni kununua vichwa vya treni naweza nikaelewa. Naomba hilo jambo aliweke makini.
Mheshimiwa Spika, ukurasa 72 nafikiri nayo ni error, anazungumza habari ya ujenzi wa reli ya Arusha – Musoma, lakini anazungumza habari ya matawi yake ya Tabora – Mwanza. Mheshimiwa Waziri hiyo jiografia imekosewa; hakuna ujenzi wa reli ya Arusha – Musoma ukawa na matawi ya Tabora kwenda Mwanza. Halafu anazungumza habari ya tawi la kwenda Minjingu na matawi ya kwenda Engaruka, angalieni jiografia hiyo msije mkajichanganya katika utekelezaji wa miradii hii ya reli, hiyo iko ukurasa wa 72.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, juhudi ni nzuri, Mheshimiwa Waziri endelea, tuna matumaini makubwa na naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi na hongera kwa Waziri, Profesa Mbarawa na Naibu Waziri wake na timu nzima ya Wizara. Mmeanza vizuri, endeleeni kwa kasi hiyo hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache kuhusu barabara ya Kidahwe - Kasulu kilometa 50, fedha shilingi bilioni 19.3. Kutoka Kidahwe hadi Kasulu Mjini ni kilometa 60; je, ina maana kilometa 10 zinazobakia zitajengwa lini? Ni vizuri barabara yote ya Kidahwe - Kasulu, kilometa 60, zikajengwa pamoja bila kuacha kiporo au kipande hicho; tafadhali Wizara angalieni jambo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kasulu – Kibondo – Kabingo na Kasulu – Manyovu, Mheshimiwa Waziri umesema itakuwa financed na ADB kama sehemu ya mkakati wa Sekretarieti ya EAC. Ni vizuri tukajua time frame ya ujenzi wa barabara hii, ni barabara ndefu, kilometa 2,258; tafadhali Wizara pamoja na Wizara ya Fedha muipe kipaumbele barabara hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kupandisha hadhi barabara za Mkoa wa Kigoma. Mheshimiwa Waziri, Mkoa wa Kigoma ni kati ya mikoa yenye mtandao mdogo kabisa wa barabara za mikoa (Regional Roads). Tafadhali, pandisha au toa idhini ya kupandishwa barabara zifuatazo kuwa barabara za mkoa:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kasulu – Kabanga – Msambara – Mwaufa – Mganza hadi Herujuu; barabara ya Nkundutsi – Malamba – Muhunga – Herujuu; barabara ya Buhigwe – Muyama – Kasumo – Mwanga – Mganza – Herujuu. Barabara hizi zina sifa na kitakuwa kichocheo za kukuza uchumi na zina sifa zote stahili kupandishwa hadhi kuwa Regional Roads.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii. Hata hivyo, nashauri niseme machache.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana Wilaya ya Kasulu kuanzisha Baraza la Ardhi tangu mwezi Aprili, 2016. Nashauri basi wataalam hao wafike haraka Kasulu ili Baraza lianze kazi mara moja. Ni hatua nzuri yenye manufaa kwa Wilaya za Kasulu na Buhigwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upo uhaba mkubwa sana wa Maafisa Ardhi na Maafisa Mpango Miji. Ni vizuri Serikali iliangalie jambo hili ili wahitimu wa vyuo vyetu vya ardhi waajiriwe moja kwa moja bila kusubiri nafasi hizo eti zitangazwe, ni jambo muhimu sana. Kama walimu wanaajiriwa moja kwa moja, kwa nini isiwe hivyo kwa wapimaji wa ardhi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara sasa iongeze hoja hii Serikalini ili mwaka huu shida hii kwenye Halmashauri, Wilaya, Manispaa na Miji imalizike. Kasulu Town Council ina uhaba mkubwa wa upimaji ardhi, valuers na Afisa Mipango miji yupo mmoja. Hatuna muda wa kusubiri, wakati ni sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu zoezi hili hati za ardhi za kimila limefanyika nchi nzima, Wilaya ya Kasulu na hasa vijiji vinavyounda Halmashauri ya Mji bado hati hazijatolewa, licha ya baadhi ya vijiji kupimwa. Ni muhimu sasa zoezi la kutoa hati za kimila lihamie Wilaya ya Kasulu na hasa vijiji vya Nyumbigwa, Mhunga, Malumba Herujuu, Karanga, Mpanza na Masambara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Kasulu (Kasulu Town Council) tumetenga ardhi, viwanja kwa ajili ya wawekezaji wa nyumba na hasa nyumba za gharama nafuu za NHC. Tafadhali kupitia kwa Mheshimiwa Waziri, aagize NHC waje sasa Kasulu, soko ni zuri kwa sababu sasa Kasulu ina Halmashauri mbili; Kasulu DC na Kasulu TC, nyumba zinahitajika sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mahitaji ya nyumba za walimu na waganga ni kubwa, mfano Wilaya ya Kasulu, Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya Wilaya, mahitaji ya nyumba ni zaidi ya nyumba 2000. Kwa nini NHC wasiagizwe kufanya kazi hiyo badala ya Halmashauri ya Wilaya kujenga nyumba chache chache kwa kipindi kirefu? Hii inaweza kufanywa kwa uamuzi wa Serikali na hasa Wizara yako ili NHC wasijikite mijini tu na waelekezwe kupeleka nguvu maeneo ya vijijini wakajenge nyumba za gharama nafuu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa namna ya pekee naomba niwape hongera nyingi sana Waziri na Naibu Waziri na timu nzima ya wenzetu wa Wizara ya Maliasili. Naomba pia niwape hongera za dhati kabisa Mhifadhi Mkuu na Wahifadhi wa Gombe na Mahale National Parks kule Kigoma, wanafanya kazi nzuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijasema ninachotaka kusema, mimi hii Kampuni ya Green Miles naifahamu, nilikuwa kwenye Tume ya Wanyamapori. Kama haya yanayosemwa na Kambi ya Upinzani ni ya kweli, basi lipo tatizo kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo kampuni ya Green Miles tulii-disqualify nikiwa kwenye Tume kwa sababu ilikosa sifa. Nafikiri ni mambo ambayo Wizara mnaweza mkakaa na wenzenu mkayafanyia kazi vizuri kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri. Moja ya disqualification yao waliidanganya Tume kipindi kile na kwa kweli tukawa-disqualify. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wizara na wataalam wenu mkae chini ikibidi mwende kule kwenye eneo lenyewe muweze kujiridhisha na hali halisi iliyopo pale. Maana yake nakumbuka Waziri wa Maliasili aliyepita hiyo kampuni aliinyang‟anya leseni kwa kukosa sifa. Sasa nasema haya mambo yako ndani ya Wizara, mnaweza mkaangalia namna ya kufanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie juu ya ikolojia ya Kigosi Moyowosi. Hii ikolojia Kigosi Moyowosi inaanzia Mkoa wa Shinyanga eneo la Bukombe inakuja Kibondo inakwenda Kasulu mpaka Uvinza. Naomba niseme eneo hili limevamiwa na mifugo wengi sana na kusema ukweli linatishia uhai wa Mto Malagarasi na siyo Mto Malagarasi tu inatishia hata chepechepe (wet land area) ya Mto Malagarasi na hakika inatishia uwepo wa Ziwa Tanganyika. Nadhani ni jambo muhimu sana Serikali ikae na kuangalia namna njema na nzuri ya kuwaondoa hawa wafugaji na kuwatafutia maeneo mengine ya kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme siyo jambo jema sana Mheshimiwa Waziri mkaanza kuwa na utamaduni wa kuua ng‟ombe kwa risasi, hilo jambo linatufedhehesha sana kwa kweli. Kama nchi kunakuwa na makosa yamefanyika basi nchi hii ni ya kiistaarabu yatatuliwe kistaarabu. Wafugaji hawa waelekezwe, waondoshwe kwenye hifadhi, wasiharibu mazingira yetu, lakini kitendo cha kuua ng‟ombe, kupiga risasi ng‟ombe kinaturudisha kwenye ujima kwa kweli siyo ustaarabu wa leo. Naomba hilo jambo lizingatiwe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika ikolojia hiyo hiyo ya Moyowosi kuna msitu mashuhuri sana unaitwa Msitu wa Makere Kusini maarufu kama Pori la Kagera Nkanda. Hilo pori lilikuwa gazetted mwaka 1954, Septemba, nina hakika Wabunge wengi mlikuwa hamjazaliwa kwa sababu hata mimi mwenyewe nilikuwa sijazaliwa. Eneo hilo lilikuwa halina watu kipindi hicho lakini sasa hivi limejaa watu na kuna misuguano mikubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naangalia hotuba ya Waziri inazungumzia juu ya usimamizi wa misitu na Wakala kufanya mapitio, ukurasa wa 59 wa hotuba yake. Katika hilo eneo la Kagera Nkanda lenye wanavijiji wengi kuna migongano ya wakulima na hawa wenzetu wa TFS. Naomba mipaka ile ya mwaka 1954 iweze kuhuishwa hawa wakulima wapate maeneo yao ya kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia napenda nimuarifu Profesa kwamba ikolojia ile haitishiwi na kilimo cha wananchi wale wa vijiji vya Wilaya ya Kasulu bali ikolojia ile inatishiwa na mifugo mingi toka nchi jirani na mifugo mingi inayoingia katika eneo lile bila utaratibu. Tafadhali sana, kama alivyobainisha ukurasa wa 59 wa hotuba yake, naomba mipaka ile ihuishwe vizuri, tena wametumia neno zuri soroveya. Tunaomba usoroveya huo mkaurudie upya ili yale maeneo ambayo wananchi wameyalima kwa muda mrefu waendelee kuyatumia bila kuwasumbua. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hawa wenzetu wa TFS wamekuwa ni walaji rushwa, wanasumbua watu wetu na kusema kweli hakuna tija hata kidogo. Mheshimiwa Waziri naomba hilo alizingatie na nimeshazungumza naye. Wananchi wetu wa vijiji vinavyozunguka pori lile wamekuwa wakilima pale kwa miaka 20 iliyopita na tumewazuia sisi kama Halmashauri wasikate miti wanalima kilimo rafiki. Kwa hiyo, ni muhimu sana Profesa akatoa maelekezo hawa watu wa TFS wasiwasumbue waendelee kujikimu kupata maisha yao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo Mheshimiwa Waziri ningeomba Sheria ya Misitu Na.14 itazamwe upya kwani imepitwa na wakati.
Nchi hii ina watu wengi sasa, kabla watu hawakuwa wengi kiasi hiki. Ni vyema sheria hii ingeangaliwa na kusema kweli yale maeneo ambayo yamekosa sifa, yako maeneo Profesa yamekosa sifa kwa mfano mapori ya akiba na open area wapewe wananchi wakiwemo wafugaji tupunguze migogoro hii ambayo kama Taifa inatufedhehesha kwa kweli. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe mfano mmoja mdogo, kwa mfano eneo la wazi la Wembere lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 10,000 limepoteza sifa, hakuna mnyama tena, wananchi wanakatakata mikaa mle lakini hawa watu wa maliasili wanazuia watu kufanya shughuli zao. Maeneo kama hayo mngeyahuisha tukapunguza migogoro hii ya wakulima na wafugaji ili watu wafanye shughuli zao kwa sababu yale maeneo hayana sifa tena ya uhifadhi na yako mengi tu mkifanya tathmini mtagundua hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo napenda nilizungumzie ni kuhusu Sekta ya Utalii. Ukisoma hotuba ya Waziri ukurasa wa 81 unazungumza Wizara na World Bank kuandaa mpango mkakati wa kuendeleza utalii, ni jambo jema, lakini hawajaeleza time frame ya huo mpango mkakati wao. Ukurasa wa 89 umezungumzia kuainisha vivutio vya utalii nchini na wametaja Mikoa ya Mwanza, Mara, Kigoma, Geita na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu kwa Wizara, nilidhani kuanza kubainisha vivutio vya utalii pamoja na vivutio vya utamaduni ingekuwa ni input kwenye mpango mkakati wa Wizara. Kipi kinaanza, bila shaka unaanza mpango mkakati kabla ya kuzungumzia habari ya vivutio na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 81 na 89 wa hotuba ya Wizara, naomba wautazame upya ili kuleta maana zaidi kwamba lazima uanze na mpango mkakati halafu vivutio vya utalii katika Mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara na kadhalika pamoja na culture tourism ziwe ni input kwenye mpango mkakati wenu. Bila shaka kama mnafanya kazi hiyo na World Bank ingekuwa jambo la busara sana basi mpango mkakati huo uwe na time frame na mtueleze katika mpango mkakati huo mmeandaa kufanya mambo gani.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri baada ya mpango mkakati kukamilika, basi tu kwa mahusiano mema na Wabunge wenzake, Waziri atuletee mpango mkakati huo tuuone ili tuweze kuwasadia baadhi ya mambo ambayo tunafikiri yanafaa kuwemo katika mkakati huo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho ambalo napenda niliseme kwa ujumla wake kwa Mheshimiwa Waziri, ni kutangaza utalii.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo hasa Kagera Nkanda, naunga mkono hoja hii. Ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nami naomba kwa namna ya pekee nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niseme machache. Mengi yameshasemwa, nami nitakuwa na machache kabisa. Naomba pia, Waziri wa Fedha, Ndugu Mpango na Naibu wake na timu yake niwape hongera kwa kazi. Changamoto bado ni kubwa kwa sababu ndiyo tumeanza bajeti. Kwa hiyo, tumeanza vizuri, nina hakika tutakwenda katika muktadha huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kabla sijaanza kusema ninayotaka kusema, nikuombe wewe mwenyewe kitu kimoja. Wewe Naibu Spika sasa hivi ndio mkubwa wa Bunge hili, nawe hakuna mashaka kabisa, uwezo wako tumeuona wote hauna mashaka hata chembe! Uwezo wako ni mkubwa, lakini wewe ni mkubwa wa taasisi hii sasa. Hivi Waheshimiwa Wabunge wa CCM naomba niwaulize swali moja, hivi sisi tukiwasamehe hawa tunakosa nini? Naomba mnisaidie tu, wewe ndio mkubwa wa mhimili huu; hivi Wapinzani hawa ambao wanakuonea wewe bila sababu, tukiwasamehe tunakosa kitu gani? Sisi ni Chama kikubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba, hatuna mashaka nawe, uwezo wako ni mkubwa, linda mhimili huu. Kamati ya Uongozi mkutane, Mama Naibu Spika una uwezo mkubwa, tuwahurumie hawa; wewe ni Mkristo, unasali; tuwahurumie hawa. Nami nina hakika, maana leo ukiwauliza kwa nini wametoka, sababu hawana, lakini na sisi tuulizane sisi tunapata faida gani wao kutoka hawa? Mnijibu swali, tunapata faida gani? (Kelele)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba unilinde, hoja yangu mimi nasema, sisi ni Chama kikubwa, tuna maslahi mapana ya kufanya, tuna kazi ya kufanya. Nakuomba kama Mkuu wa mhimili huu, mkae tumalize stalemate hii, haitusaidii kama Chama. Hayo yalikuwa ni mawazo yangu mimi. (Kelele)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hata kama halipendezi, lazima lisemwe. (Kelele/Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa niliseme, nataka nijielekeze kwenye kitabu hiki cha Kamati ya Mheshimiwa Mama Hawa, Kamati ya Bajeti. Waheshimiwa Wabunge, ukurasa wa 28 na 29 wa Kitabu hiki cha Kamati, Kamati ya wenzetu wa Bajeti wananung‟unika, wanasema Serikali haijasikiliza maoni ya Wabunge. Yameandikwa humu ndani, naomba ninukuu;
“Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwa Kamati ya Bajeti katika utekelezaji wa bajeti hii kwa kiasi kikubwa Serikali haikuzingatia maoni na majukumu ya Kamati ya Bunge ya Bajeti. Masuala la kibajeti ambayo ni ya kisheria Kamati hii imeona Serikali inayapuuza. Bunge linataka kufanywa kama rubber stamp kwa kuidhinisha bajeti ya Serikali.”
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba, narudia tena maneno yangu, wewe ni mkuu wa mhimili huu, linda hadhi ya Bunge. Kama liko tatizo limetokea kwenye Kamati ya Bajeti, ni vizuri kabisa Serikali wakae na Kamati ya Bajeti waelewane. Kwa sababu, Kamati ya Bajeti ndiyo inatusemea sisi Waheshimiwa Wabunge. Sisi wote hatuwezi kuwa kwenye Kamati ya Bajeti. Haiwezekani tuwe na Serikali ambayo haipokei ushauri wa Kamati ya Bajeti. Haiwezekani, mhimili huu tutauharibu, tutauvunjia heshima na Bunge ni chombo cha heshima.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba, yako mambo mengi yamezungumzwa na wenzetu wa Kamati ya Bajeti, hayapendezi. Wanalalamika! Haiwezekani Bunge letu sisi wenyewe, Bunge la Chama cha Mapinduzi wasisikie maoni ya Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, haiwezekani! Nakuomba jambo hili ulichukulie kwa uzito unaofaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 29 wa maoni ya Kamati hii wanasema, utaratibu wa Kikanuni wa kupokea hoja wakati wa kujadili bajeti umekaa vibaya.
Mheshimiwa Naibu Spika, wewe ni mwanasheria mzuri, tafadhali tuongoze vizuri. Hii Kanuni kama imekaa vibaya, tuiangalie upya ili Bunge liwe na maana katika upitishaji wa bajeti ya Serikali, vinginevyo tutakuwa rubber stamp tu.

TAARIFA....

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpe Taarifa kaka yangu Mheshimiwa Daniel Nsanzugwanko kwa kutumia Kanuni ya 68(7) kwamba humu ndani hakuna Mbunge wa Upinzani aliyefukuzwa na Naibu Spika. Kwa hiyo, kusema Naibu Spika uwasamehe, ni kuondoa ukweli kwamba walioadhibiwa wameadhibiwa na Bunge zima na siyo Naibu Spika. Hawa waliotoka, wameondolewa na Mwenyekiti wao wa Chama, nami wameniomba niwatetee na ndiyo maana nimesema pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba ulinde muda wangu. Hiyo hoja anayoizungumza Mheshimiwa Lusinde naikubali, wala sina matatizo nayo. Hoja yangu ni kwamba, sisi ni Chama kikubwa, ndiyo chenye ajenda. Hata hao wakitoka mwaka mzima hawana cha kupoteza hawa. Sisi ndio tuna ajenda yetu, ndiyo hoja yangu tu iko hapo. (Kelele/Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tafadhali muda wangu ulindwe. Nilikuwa nazungumzia juu ya Kanuni ambapo wewe ni Mtaalam, jambo hilo mlizingatie.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba pia nizungumzie makato ya pensheni. Nimesikiliza maoni yakitolewa hapa, lakini naomba tu niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge na Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Wabunge sio Watumishi wa Serikali. Sisi Wabunge hatuna pensheni. Hatuna hata Bima ya Afya, ukimaliza miaka mitano ndiyo imetoka, haupo tena.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi sielewi hata kidogo msingi kabisa wa kukata pensheni ya Wabunge, siuoni hata kidogo. Sababu zitakuwa ni nyingi. Kwa mujibu wa utaratibu, pensheni yenyewe ni kama posho tu. Pensheni siyo malipo ya moja kwa moja, ni kale kapesa unapewa kwamba Mbunge wewe kajikimu baada ya kazi yako ya miaka mitano. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mheshimiwa Waziri wa Fedha anakakata panga, kama alivyosema kijana hapa ili iweje? Waheshimiwa Wabunge, jambo hili halikubaliki kwa sababu, kwanza ni la kibaguzi. Kama hoja ni hiyo, ili Wabunge tuwe fair kwa mujibu wa ile Sheria ya Mwaka 1999 ya Political Pensioners Act, basi wale wote waliotajwa kwenye Act ile waorodheshwe tulipe kodi kama tunataka kuwa fair. Kwa nini Serikali wana-single out Waheshimiwa Wabunge tu? Hakuna sababu ya msingi. Labda Mheshimiwa Waziri atakapokuja atueleze hoja ya msingi, kwa nini wanafikiri ni Wabunge tu ndio wawe liable kwa kukatwa pesa hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vinginevyo jambo hili mrudi kwenye Kamati ya Bajeti. Hata kwenye Kamati ya Bajeti nao wanashangaa, wanalilalamikia vilevile. Hatuwezi kuwa na Bunge ambalo Wabunge hawasikilizwi, haiwezekani; na sauti ya Wabunge iko kwenye Kamati zao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili hata Mheshimiwa Mama Hawa Ghasia kasema kwenye kitabu chake; hata Kamati ya Bajeti hawalijui jambo hili, Serikali wanalitoa wapi? Kwa hiyo, bado naamini kabisa, kama walivyosema wenzangu, bado kukata posho ya Wabunge hawa wakimaliza miaka yao mitano siyo sahihi na ni jambo ambalo halikubaliki, wakalitazame upya kwenye Kamati ya Bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa niliseme, limesemwa sana hili la biashara ya utalii. Mheshimiwa Waziri wala huhitaji mtu kwenda shule kuliona. Wapinzani wetu wakubwa wa biashara hii ni Kenya; wapinzani wetu wa biashara hii ni Rwanda; wapinzani wetu wa biashara hii ni Uganda; wote wameondoa VAT, wewe unaitoa wapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, biashara hii tukiweka VAT maana yake watalii hawatakuja. Kama hawatakuja maana yake tutapata hasara. Tukipata hasara, hata hayo mapato ya Serikali yatashuka bila shaka. Kwa hiyo, naomba hii VAT kwenye biashara ya utalii ni jambo ambalo halikubaliki wala halina msingi wowote katika mazingira haya ya ushindani.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa niliseme ni hizi milioni 50 kwa kila kijiji. Ushauri wangu kwa Serikali, tujifunze kutokana na mamilioni ya JK. Tujifunze kutokana na experience ya mamilioni ya JK. Bahati nzuri kipindi kile nilikuwa Serikalini, zile fedha hazikuwa na impact yoyote, ni kwa sababu zilitumika vibaya. Sasa na hizi fedha shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa muktadha huu kwamba tukafungue SACCOS ziende kwenye vijiji hazitakuwa na impact iliyokusudiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mmoja alizungumza jana jambo hili, ni vyema fedha hizi tukaangalia namna nzuri ya kuzitumia, hata kama maana yake ni kwenda ku-push on kwenye mbolea, kwenye viuatilifu na madawa ya mifugo ili wananchi hawa kama ni mkulima apate mbolea kwa bei ya Coca Cola. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, fedha hizi, vijiji viko vingi sana. Jimboni kwangu au Wilaya ya Kasulu kuna vijiji 108, mara milioni 50 ni takriban shilingi bilioni tano. Hizo shilingi bilioni tano ukizishusha kwenye pembejeo za kilimo, watu watakwenda kununua mbolea kama wanavyonunua Coca Cola na shida itakwisha. Tutakwenda kuwaeleza na jambo hili litakuwa na maana zaidi kuliko hivi tunavyofikiria eti kwenda kufungua SACCOS katika maeneo haya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho nizungumzie miradi ya kipaumbele. Miradi ya kipaumbele ambayo imezungumzwa ni pamoja na barabara zetu muhimu; Bandari ya Dar es Salaam, Reli ya Kati, Barabara ya Kidahwe – Nyakanazi. Sasa Mheshimiwa Waziri atakapokuwa ana-wind up ningependa kuelewa vizuri status ya hii miradi ya East Africa; miradi hii ya Afrika Mashariki ambayo katika ile barabara ya Kidahwe – Nyakanazi kuna portion ya kwenda Manyovu na kuna portion ya Kabingo – Kasulu ambayo inakuwa financed na East Africa. Napenda kujua status yake ili tuweze kwenda vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, ni dhahiri naunga mkono hoja kwa sababu ndiyo wanaanza, lakini mshirikiane na Kamati ya Bajeti. Serikali msiwe peke yenu. Nawashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Naomba kwa namna ya pekee kabisa nikupe hongera sana Balozi Mahiga na Naibu wako. Na kweli tuwape hongera sana Mabalozi wetu wanaofanya kazi nchi za nje katika mazingira magumu. Wengine wanafanya kazi katika mazingira ambayo sio rafiki sana, hawana vitendea kazi, hawana staff wa kutosha, lakini wameendelea kufanya kazi kwa moyo mmoja, tunawapongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilikuwa naomba nianze na hili moja na Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba ulisikie hili. Lipo tatizo, nilikuwa nafikiri ni muhimu Wabunge wote wa Chama cha Mapinduzi, Wabunge wa Upinzani, tuwe na mafunzo maalum ya diplomasia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kama ni ya siku mbili, siku tatu. Unajua Mheshimiwa Msigwa kuna mambo mengine hayasemwi hadharani. Kuna mambo mengine hayasemwi hadharani na kuna mambo mengine yanasemwa hadharani. Katika utamaduni wa diplomasia kuna mambo ambayo unaweza ukayasema tu hadharani na mengine yanazungumzwa ndani, under camera. Kwa hiyo, niombe, huko ndani nyuma kulikuwa na utamaduni huu kwamba Bunge linakaa, Balozi Mahiga na uzoefu wako unakuja na wenzako mnatupiga shule sawasawa, tunaelewa. Hata makatazo mnatueleza kwamba hiki usifanye na hiki ufanye. Maana haitoshi tu kwamba, wewe ni Mbunge unakwenda kukutana na Mabalozi, unakutana nao kuzungumza kitu gani? Kuna mambo mengine ambayo yanagusa uhai wa Taifa letu yana namna yake ya kuyazungumza na hata Bunge la mwaka 2005, Bunge la mwaka 2000 yote yalifanyika mafunzo yaliendeshwa na Wabunge walifundishwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge kujifunza hakuishi, unaweza ukakaa unasema sema maneno hapa kwa sababu tu pengine hujui vizuri au unafikiri kila kitu lazima kisemwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa Mheshimiwa Balozi nikurudishe kwenye kitabu chako ukurasa wa 118, nianze na kuzungumzia ujenzi wa Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja na pia nimeona imeambana na kipeperushi hiki hapa ambacho kinazungumzia Vituo vya Pamoja na Utoaji wa Huduma Mipakani. Naomba nikukumbushe tu, umeorodhesha vituo saba, lakini katika kipeperushi hiki umeongezea habari ya Vituo vya Kasumulu kule Songwe, Malawi na Mtambaswala na kwenye border ya Tanzania na Msumbiji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba nikukumbushe kitu kimoja kwamba kuna vituo muhimu sana umevisahau. Kuna kituo muhimu sana cha forodha, kiko kwenye mpaka wetu wa Burundi, sehemu ya Manyovu na Burundi, ni border post ya muda mrefu sana na Serikali ya Tanzania kimkakati ilishajenga barabara ya lami kutoka bandari ya Kigoma mpaka kwenye border na wenzetu wamejenga barabara ya lami kuanzia border pale kwenda Bujumbura. Sasa kituo kile ni cha siku nyingi sana, sasa katika orodha hii sikioni. Nilikuwa nafikiri kama sio oversight basi mkiongeze na kiweze kupewa fedha kikarabatiwe vizuri. Mpaka wa Manyovu ni mpaka wa siku nyingi na ni mpaka wa kihistoria. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo kingine cha forodha, ambacho umekisahau Mheshimiwa Waziri ni Kituo cha Forodha cha Mabamba na Burundi ni Kituo cha Forodha cha muda mrefu, kiko katika Wilaya ya Kibondo, hiyo Manyovu iko Wilaya ya Buhigwe. Nilikuwa naomba katika vituo vile ambavyo vinahitajiwa kufanyiwa ukarabati, Mheshimiwa Waziri ni vyema mkavitazama vituo hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba, swali langu la pili Mheshimiwa Waziri, naomba Balozi unisaidie utakapokuwa unahitimisha, ni vigezo gani mnavitumia tunapoanzisha Ubalozi mpya? Ningependa kujua vigezo, ambavyo vinatumika kwa mfano, mimi mpaka leo sielewi ni kwa nini hatuna Ubalozi Seoul - Korea ya Kusini? (Makofi)
Mheshmiwa Mwenyekiti, nchi ya Burundi ina Ubalozi pale, nchi ya Zambia ina Ubalozi pale. Niliishi pale Seoul, kwa nini sisi Tanzania hatuna Ubalozi pale? Na mnajua wenzetu Wakorea hawa na katika diplomasia ya kiuchumi ndiyo wametujengea Daraja la Malagarasi.
Mheshmiwa Mwenyekiti, mtu akikuuliza moja ya vitu halisi vya kuonyesha ni kwamba Daraja la Mto Malagarasi na viunga vyake limejengwa kwa sababu ya ushirikiano ulioanzia Foreing Affairs kwa kweli na ni jitihada za Mheshimiwa Kikwete akiwa Waziri wa Foreign Affairs, ambaye alizungumza na wenzetu wale, hatimaye tukapa daraja lile. Sielewi kwa nini hatuna Ubalozi pale. Seoul - Korea ya Kusini mnajua ni nchi, ambayo imepiga hatua kubwa katika TEHAMA, katika ujenzi, katika kilimo, ni muhimu Mheshimiwa Waziri utakapohitimisha unieleze ni kwa nini hatuna ofisi pale Seoul?
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, ambalo ningependa niliseme ni kuhusu Wakimbizi. Sisi Mkoa wa Kigoma tumepokea wakimbizi tangu uhuru, lakini bado wakimbizi wanaingia katika nchi zetu. Nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri kupitia ofisi yako pale ofisini kwako kwenye Foreign Services anzisheni kitengo cha wakimbizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu kitengo cha wakimbizi kilichopo Mambo ya Ndani kina deal na usalama zaidi wa wakimbizi. Lakini sisi ambao tumeathirika na ujio wa wakimbizi, ambao Mabalozi wengi wanakuja Kigoma pale, Mabalozi wengi wanakuja Kasulu pale, Mabalozi wengi wanakwenda Kibondo pale hatuna namna ambayo tuna kiunganishi cha kwamba Mabalozi hawa sasa wanaokuja kuhudumia wakimbizi kuwe na jitihada maalum hasa ya kusaidia maeneo, ambayo yameathirika na ujio wa wakimbizi.
Mheshimiwa Balozi, mwezi Januari nilibahatika kukutana na Mabalozi sita waliokuja kutembelea kambi za wakimbizi, tumezungumza mengi sana nikahisi ni wakati sasa kwenye ofisi yako au ofisi yako muwe na uhusianao wa karibu kati ya Kitengo cha Wakimbizi Mambo ya Ndani na Kitengo cha Wakimbizi katika ofisi zako ambacho kitakuwa kina-raise masuala haya na hasa huduma kwa maeneo ambayo yameathirika na ujio wa wakimbizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho nizungumzie suala la migogoro. Alisema ndugu yangu mmoja suala la Kongo, Mheshimiwa Balozi Mahiga, lazima tuilinde Kongo ya Mashariki, lazima tuilinde DRC kimkakati, wale ni partners wetu katika biashara. Kwa sababu tuna askari wetu kule ambao wanafanya kazi nzuri sana na nimwombe Waziri wa Ulinzi wale askari wasitoke Kongo wanatufanyia kazi nzuri sana, naomba tuilinde DRC kimkakati kama partners wetu wa kibiashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naunga mkono kwamba wakati umefika pale Lubumbashi angalau tuwe na Ofisi ndogo ya Kibalozi kwa ajili ya kulinda maslahi yetu kama nchi. Ile ni nchi kubwa, nchi yenye utajiri mkubwa na kusema kweli tunaweza tukanufaika nayo kwa msingi huo, naomba uyazingatie hayo.
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Nsanzugwanko.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii. Hata hivyo, niseme machache. Kwanza, nianze na suala la usalama. Katika nchi za maziwa makubwa hali ya usalama ni tete sana, hali siyo shwari katika nchi nyingi za majirani. Kenya hali siyo nzuri; Uchaguzi Mkuu wa mwaka kesho nchini humo inatia shaka kama usalama utakuwepo. Ukabila nchini Kenya sasa ni kidonda ndugu. Hatari iliyopo ni kutengeneza wakimbizi na wengi watakimbilia Tanzania. Tanzania ichukue jukumu la usuluhishi na upatanishi ili tuwe salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepeleka vijana (Askari) kurejesha amani Kongo; ni jambo jema sana. Tuilinde Kongo kimkakati kama mbia wetu wa biashara na Foreign Service. Anzisheni Ofisi ndogo ya biashara pale Lubumbashi ili tulinde maslahi yetu ya kiuchumi na kibiashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu Mgogoro wa Burundi na Usuluhishi. Juhudi zinazoendelea pale Arusha ni njema sana. Ni vizuri katika usuluhishi ule pia, washirikishwe Viongozi wa Dini hasa Wakristo na Waislamu. Haya ni makundi mahususi ambayo yanaweza kusaidia kuwezesha mawasiliano na maelewano. Zaidi usuluhishi huo pia, ushirikishe Baraza la Wazee (Council of Elders) ambalo linaweza kuundwa na Elders waliopo katika Mkoa wa Kigoma na Wilaya za Biharamulo na Ngara. Tamaduni za maeneo hayo zinafanana sana na hali/mazingira yaliyopo Burundi, hata lugha yetu ni moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Kutangaza Lugha yetu ya Kiswahili kilichopo Addis Ababa, Ethiopia, kimeendelezwa kiasi gani? Kimeleta ajira ngapi kwa vijana wetu? Tunataka Kiswahili kiwe bidhaa tena bidhaa ambayo itatuongezea mapato kama Taifa. Kwa nini hadi sasa Kiswahili hakitumiki kama lugha rasmi ya EAC? Tatizo ni nini? We have to promote Kiswahili now.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni watumishi wangapi wa vyeo vya juu wameajiriwa pale Head Quarters iliyopo Arusha? Ni watumishi wangapi wa vyeo vya kati walioajiriwa na EAC Head Quarters pale Arusha? Watumishi wa vyeo vya chini/operating staff, wahudumu/drivers ni wangapi? Nataka kujua pia tunavyonufaika na EAC kuwapo katika ardhi ya Tanzania kiajira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna protocol yoyote katika nchi wanachama za kuhakikisha demokrasia inakua na kustawi katika Jumuiya hii? Kitendo cha kung‟ang‟ania madaraka kwa Viongozi katika Jumuiya hii ni hatari sana, kitaua ustawi wa jamii na uhuru wa watu wetu. Tanzania must take lead; tuzungumze, tushauri na tuongoze juhudi hizi za kujenga demokrasia hii ambayo ni changa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono jitihada zinazofanyika katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa 2016/2017 hadi 2020/2021, mkakati ni mzuri uelekeo unatoa picha kubwa ya matumaini.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya kwanza, Utekelezaji wa Miradi ya Kipaumbele kama Taifa; Ushauri, miradi ya kielelezo itekelezwe kwa umakini kama Taifa, we need action and not words. Miradi ya Reli ya Kati, Kanda Maalum za Kiuchumi, Bagamoyo, Kigoma, Mtwara na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, Bandari ya Kidahwe-Nyakanazi na Manyovu, Kasulu; miradi hii ni muhimu sana itekelezwe hata kama ni kukopa fedha kutoka nje au ndani, imepangwa vizuri itekelezwe kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya pili, ukurasa wa 28; Hotuba ya Mheshimiwa Waziri, Kikosi Kazi cha Maboresho ya Kodi kiangalie vyanzo vipya vya mapato (New Tax Revenues) mfano, angalieni Economic za Uvuvi wa Bahari Kuu, tunaambiwa ni eneo lenye kuweza kuchangia pato kubwa la Taifa hili. Uzoefu wa nchi za Singapore, Thailand na Austria unatoa rejea sahihi kabisa. Tuwekeze huko, tununue meli ya uvuvi na tuboreshe gati namba Sita, ambayo imetolewa na Mamlaka ya Bandari (TPA), kama bandari yetu kituo cha kupokea mavuno hayo ya Bahari Kuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Taasisi za Umma ambazo Serikali inamiliki hisa zake ukurasa wa 43 hadi 44 wa hotuba ya Waziri; taasisi za Tipper, PUMA Energy, Kilombero Sugar ni taasisi ambazo Serikali yetu ina hisa, lazima tuwekeze huko. Taasisi za Tipper na PUMA Energy ambako Serikali ina asilimia 50 ni maeneo ambayo yakisimamiwa vema na Serikali kuweka nguvu yanaweza kuongeza pato la Taifa letu. Kampuni hizo zipewe support ili zizalishe mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, ushiriki wa sekta binafsi kupitia PPP; Mheshimiwa Waziri, dhana hii inafahamika vizuri Serikalini? Ipo wapi miradi ya PPP mfano, ujenzi wa barabara ya Chalinze- Dar es Salaam wako wapi sekta binafsi? Ushiriki mdogo wa sekta binafsi kutokana na Mazingira yasiyowezeshi ya uwekezaji, angalieni upya vikwazo vinavyokwamisha ushiriki wa private sector, tatizo lazima libainishwe na lipatiwe dawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 40 kupitia upya ada, ushuru na tozo ili kuzirekebisha ziendane na maendeleo na ustawi wa jamii. Kikosi kazi kiangalie tozo kwenye pamba, kahawa, tumbaku, mkonge, chai na kadhalika ili mazao haya yalimwe kwa tija bora zaidi kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja hii.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nakushukuru. Mimi nitakuwa na machache tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja nataka tuweke angalizo kuhusu hifadhi zetu na mifugo. Waheshimiwa Wabunge tusipokuwa makini baada ya miaka michache tutakuwa hakuna wildlife nchi hii. Hii ya wafugaji kung’ang’ania kwenye hifadhi zetu eti tu kwa sababu bwana mkubwa alisema msitoke, hii siyo sahihi jamani. This country tuta-wipe-up wildlife yote ya nchi hii. Nadhani hoja ya msingi ambayo nafikiri Serikali ingekwenda kuifanyia kazi ni ile Tume ya Waziri Mkuu ya zile Wizara tano ziharakishe kufanya zoezi lile ili yale maeneo ambayo yamekosa sifa ya uhifadhi ndiyo mifugo ihamishiwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Ngorogoro hamjui mkakati uliopo wa Wakenya hapa, wanataka kui-suffocate Ngorongoro hatimaye tuiue Serengeti ili wabaki na advantage ya Masai Mara ya Kenya. Nilikuwa naweka tu angalizo ili tuweze kuelewana vizuri na watu wa maliasili nadhani jambo hili hatuwezi kulifumbia macho, tusipokuwa makini baada ya miaka michache nchi hii itakuwa haina maliasili wala haitakuwa na wanyamapori au watapungua sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie suala la tozo. Ukiangalia taarifa ya Kamati yetu ya Bajeti inazungumzia kwamba tozo hizi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 kwamba hizi tozo zimeondolewa. Mimi nipo kwenye Kamati ya Kilimo na Mifugo, hizi tozo hazijaondolewa na taarifa niliyonayo ni kwamba Waziri wa Biashara anahangaika kutafuta namna gani ya kuziondoa, sasa hizi taarifa zingine zinakuwa hazina uhalisia. Tozo za mazao, tozo ya Bodi ya Pamba, Bodi ya Kahawa, Bodi ya Korosho kidogo wameangalia, lakini Bodi ya Chai bado na mazao mengine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri nikikubaliana na mapendekezo ya Kamati hii ya kilimo madam tunakwenda kwenye bajeti tunaomba tozo hizi Mheshimiwa Waziri wa Fedha, hizi tozo futeni. Waziri Mramba alizifuta hizi sijui kwa nini zinarudishwa. Wale wenye kumbukumbu tozo hizi ziliitwa kodi za kero, kodi za mazao na zikaondolewa, sasa leo kwa nini zishiondolewe? Nafikiri hilo ni jambo muhimu kwa sababu tunajenga na tunakwenda kwenye bajeti ni vema tozo za mazao ya biashara zikaondolewa ili wakulima waweze kuuza mazao yao na hatimaye wapate kipato chao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalopenda kuzungumzia ni upatikanaji wa mbegu, Waziri wa Kilimo unajua kwamba nchi hii hatuna mbegu, hata mbegu za mazao ya chakula zinazozalishwa nchini ni asilimia 35 mpaka asilimia 40, mbegu nyingi zinatoka nje ya nchi yetu. Zinatoka Zimbabwe na Kenya. Ushauri wangu kwa Serikali kama tulivyosema kwenye Kamati yetu ya Kilimo haiwezekani tuzungumzie uchumi wa viwanda wakati hatuna hata mbegu za mazao yetu wenyewe ambayo hatimaye ndiyo zitatengeneza hivi viwanda vya agro industries. Sasa suala la mbegu ni la msingi sana na nilikuwa naomba wenzetu wa Serikali mkaliangalie hasa kwa sababu tunajenga upya bajeti yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la upatikanaji wa mbolea limezungumzwa. Labda niseme Waheshimiwa Wabunge wananchi wetu wengi wanaishi vijijini na wananchi wetu wengi ni wakulima. Hawa wananchi wetu bado kuna shida ya upatikanaji wa mbolea. Kwa mfano, takwimu za mwaka jana huu mwaka tunaoumaliza sasa, ni kaya 378 tu ambazo zimepata pembejeo nchi nzima ambayo ni sawa sawa na asilimia 0.06 ya wakulima, sasa huu kama siyo mchezo wa kuigiza ni kitu gani? Hatuna mbolea, hakuna mbegu halafu unakuja kuzungumzia uchumi wa viwanda, viwanda vipi hivyo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda tunavyovifikiria lazima viwe ni viwanda ambavyo vitaajiri watu wetu wengi vijijini na viwanda hivyo ni viwanda vya mazao ya kilimo pamoja na michikichi. Kwa hiyo, hili ni jambo ambalo ni jambo la msingi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la uzalishaji wa mbegu Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Waziri wa Uwekezaji na Waziri wa Mambo ya Ndani jengeni mkakati wa kuzalisha mbegu kupitia Magereza yetu. Jeshi la Magereza Waziri wa Mambo ya Ndani jana umelisema vizuri tu, nina hakika wenzetu wa Magereza wana mashamba makubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na mkakati maalum ambao umejengwa kibajeti, nina hakika tunaweza tukazalisha mbegu zetu wenyewe na zikatosheleza. Maeneo kama Magereza, JKT na hata watu binafsi wanaweza wakafanya kazi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo langu la mwisho ni hii food for thought wenzetu wa Serikali mkalitizame. Kwa maoni yangu na maoni ya watu wengi kwenye Kamati yetu ya Kilimo jamani hii Wizara ya Kilimo ni kubwa sana, hii Wizara ina vitu vingi sana. Ushauri wangu kwa Serikali muangalie namna nzuri ya kumshauri bwana mkubwa hii Wizara muundo wake utazamwe upya. Maana yake una mifugo una kilimo, uvuvi, ushirika, masoko na taasisi zaidi ya 60 chini ya Wizara moja.
Kwa hiyo, nilikuwa nashauri sincerely kabisa, wenzetu wa Serikali mkakae mliangalie hili mumshauri bwana mkubwa namna anavyoweza kuhuisha huu muundo ili uweze kuwa na tija kwa sababu Wizara hii kwa kweli ni Wizara mama. Wizara hii ndiyo roho ya Taifa letu kwa sababu ndiyo inaajiri watu wengi na ni tegemeo la maisha ya Watanzania walio wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa ni huu Mfuko wa Maji ambao umesemwa sana na kwenye Kamati tulikwenda mbali zaidi tukasema ni vizuri hata hizo fedha zinazotolewa tuwe tunajua ni kiasi gani cha mafuta yameuzwa. Kwa sababu msingi wa Mfuko wa Maji ni hizi fedha zimezungushiwa wigo wake ili zikaondoe tatizo la maji katika maeneo yetu vijijini. Kumekuwa na kuchechemea kidogo kwa Serikali. Tunataka kujua exactly ni kiasi gani ambacho Mfuko wa Maji unapaswa kupata, siyo ku-remit kwenda Wizarani. Mapato halisi ya Mfuko wa Maji lazima yajulikane kwa sababu ni kauli ya Bunge hili, tuli- ring fence zile fedha kwa ajili ya kwenda kuondoa matatizo ya maji katika maeneo yetu ya vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mengine nimeyasema jana, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana kwa kwa kunipa nafasi hii na naunga mkono mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimwa Mwenyekiti ahsante, ningejua kama Mheshimiwa Zitto ana utamu huu ningempa hizo dakika tatu lakini ngoja niendelee. Hilo la mwendelezo ni la msingi sana kwamba amemteua Kamishna na mimi nimesikia kwenye redio wakati nakuja, ni jambo jema kwamba sasa kuna chombo maalum kinashughulikia dawa za kulevya ni jambo jema sana. Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo mambo mawili tu ya kwa haraka. La kwanza, ukurasa wa 35 wa kitabu hiki cha repoti kinazungumzia Sera ya Mambo ya Nchi za Nje kwamba mpaka sasa tunavyozungumza Sera ya Mambo ya Nchi za Nje inayotumika ni sera ya mwaka 2001. Nafikiri wasemeji waliopita akiwemo Mheshimiwa Zitto nimemsikia na Mheshimiwa Bashe akizungumza shida iko hapo. Kwa mujibu wa repoti hiyo ukurasa wa 35 wanasema sera mpya na mapitio ya sera hiyo ya mambo ya nchi za nje inayozingatia diplomasia ya kiuchumi na mapana yake bado haijafanyiwa kazi. Mimi nilikuwa nafikiria Waheshimiwa Wabunge hapo ndipo kwenye shida. Tuiombe Serikali kama ni kalenda ya miezi sita, ya mwaka mmoja basi wenzetu wa Mambo ya Nchi za Nje wawe wametuletea sera hiyo ambayo inafanyiwa mapitio tangu mwaka 2001, haiwezekani sera ifanyiwe mapitio tangu mwaka 2001 mpaka leo. Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala haya ya kuzingatia diplomasia ya uchumi ndiyo masuala ya msingi ya sera mpya ambayo kila siku tunaisema lakini kwa mujibu wa taarifa ya wenzetu wa Kamati na ndugu yangu Mheshimiwa Balozi Adadi mmefanya kazi nzuri sana kuikumbusha Serikali kwamba lazima tuipe time frame. Kama ni miezi sita, kama ni mwaka mmoja watuletee sera hiyo ambayo imefanyiwa mapitio inayozingatia diplomasia ya kiuchumi. Hoja yangu ya pili nimeshangaa kidogo na Waziri wa Ulinzi uko hapa nimeshangaa kidogo. Ukurasa wa 30 wa repoti hii wanasema, hatuna Sera ya Ulinzi, hilo jambo limenishtua Waheshimiwa Wabunge, kama hatuna sera ya ulinzi tumepelekaje askari wetu Congo, Darfur, Lebanon na kwingineko? Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nipate maelezo wakati Mwenyekiti unahitimisha ni kwa nini hakuna sera...
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa muda wako umeisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kabla sijasema mengi, kwanza niunge mkono hoja hii ambayo imeletwa mbele yetu toka Ofisi ya Waziri Mkuu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa na machache sana, lakini moja kubwa naomba tu kwa namna ya pekee niwapongeze wenzetu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri na watendaji wake, timu nzima ya Serikali, mmefanya kazi nzuri sana na hasa hii kazi ya kurejesha nidhamu Serikalini,
hongereni sana. Hili ni jambo jema na kila mmoja anaona tofauti iliyokuwepo siku za nyuma na siku za sasa hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bado niendelee kuwashauri, kama ilivyo kazi yetu Wabunge ni kuwashauri Serikali, kwamba tunaomba utaratibu huu wa nidhamu ya watumishi wa Serikali ujikite katika kulinda misingi ya sheria. Tafadhalini sana, endelezeni nidhamu ya watumishi wa umma, tuwaheshimu watumishi wa umma kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa namna ya pekee naipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kumaliza ligi hii ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya ya kuwaweka ndani watumishi wa umma hovyo hovyo. Kwa kweli juhudi zimekuwa nzuri, sasa tunaona mashindano haya hayapo tena, maana huko nyuma ilikuwa Mkuu wa Mkoa akijisikia, Mkuu wa Wilaya akijisikia anaweza kumweka ndani ofisa yeyote wa Serikali bila utaratibu. Tunashukuru sana, jambo hili wenzetu wa Utumishi, TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu mmelisimamia vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee, Mheshimiwa Simbachawene najua amefanya vizuri katika jambo hili, na tunakupongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya. Lazima Wakuu wetu wa Wilaya na Mikoa wafuate sheria kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo napenda nilisemee limeainishwa ukurasa wa 31 na 32 wa hotuba ya Waziri Mkuu ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge. Tunaishukuru sana Serikali kwa jitihada hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwakumbushe, Mheshimiwa Jenista, reli ya kati tafsiri yake ni reli inayotoka Kigoma kwenda Dar es Salaam ikiwa na matawi ya kutoka Tabora kwenda Mwanza na matawi kutoka Kaliua kwenda Mpanda, ndiyo reli ya kati hiyo. Sasa nimeona kwenye kitabu cha Waziri Mkuu, kuna juhudi kubwa zimefanyika katika ujenzi wa reli ya kati na hususan kuanza kufanya feasibility studies katika matawi haya ya reli ya kati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwashauri kwamba ili reli hii iweze kuwa ya kiuchumi, maadamu inaanza kujengwa kwa kiwango cha standard gauge ni vizuri reli hii ikatoka Dar es Salaam ikaenda Kigoma kwa sababu ya mzigo mkubwa, tani milioni nne zilizoko katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambayo zinahitaji njia kwenda kwenye masoko ya Kimataifa. Tusipofanya hivyo, tutajikuta mbele ya safari, hii reli haitakuwa na faida za kiuchumi mbali na kusafirisha abiria peke yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda niliseme ni uwiano wa maendeleo katika Mikoa yetu. Waheshimiwa Mawaziri mlioko hapa nadhani Waziri wa TAMISEMI unanisikia, nchi yetu hii ina mikoa takribani 25.
Uwiano wa Mikoa hii umetofautiana katika sekta mbalimbali, ni vyema sasa Serikali yenyewe kama ambavyo mwaka wa 2016 mlitupa takwimu za hali ya umaskini katika nchi yetu tukawa na utaratibu wa kuiinua mikoa ambayo iko nyuma, mikoa hiyo iko nyuma kwa sababu za kihistoria tu. Mikoa kama Kigoma, Dodoma, Singida, Katavi, iko nyuma kwa sababu za kihistoria. Ni jukumu la Serikali kuweka uwiano sawa wa mikoa hii katika sekta mbalimbali kama elimu, maji, afya, kilimo, barabara na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo mengine yana nafuu kidogo na maeneo mengine yana shida kubwa sana na wananchi wote hawa ni Watanzania hawa hawa.
Kwa mfano, Mkoa wetu wa Kigoma mpaka leo bado ni mkoa haujaunganishwa na Tabora kikamilifu, haujaunganishwa na Katavi, haujaunganishwa na Geita, haujaunganishwa na Kagera, haujaunganishwa na Shinyanga, hali ni mbaya sana.
Sasa naomba sana TAMISEMI mko hapa, Ofisi ya Waziri Mkuu, angalieni uwiano ambao una afya katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania hawa wana haki sawa. Maeneo mengine yana unafuu na mengine yana shida kubwa. Kwa hiyo, naomba kama ushauri Serikalini kwamba ni muhimu sana kuweka uwiano wa maendeleo katika mikoa ya nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa niishauri Serikali ni suala la kilimo. Katika nchi yetu kuna maeneo yanapata mvua, Mwenyezi Mungu ameyabariki tu, yanapata mvua za kutosha na tunalo tatizo kubwa sana hata la kuzalisha mbegu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu kwa kweli kwa miaka yote hii, miaka 50 ya uhuru sasa hatuwezei kujitosheleza hata kwa mbegu za mazao ya nafaka. Nilikuwa nafikiri ni wakati muafaka wenzetu wa kilimo na Serikali, yale maeneo yanayopata mvua za kutosha kwa mwaka mzima tuyape kipaumbele ili tuweze kuzalisha mbegu za kutosha ili tujitosheleze kwa mbegu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonesha kwamba mpaka sasa nchi yetu tunazalisha mbegu asilimia 40 ya mbegu zilizobaki zinatoka nchi jirani kama Kenya, Zimbabwe na mataifa mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho nizungumzie juu ya umeme wa Malagarasi. Niwapongeze wenzetu wa nishati wamefanya kazi kubwa na taarifa niliyonayo ni kwamba wenzetu wa Benki ya Dunia na African Development Bank wametoa fedha kwa ajili ya kuanza kujenga umeme wa
Malagarasi. Huo umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya watu wa Kigoma na ni dhahiri umeme huo utaingizwa pia kwenye Gridi ya Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa nizungumzie suala la maji, maji ni uhai na ni dhahiri kwamba maeneo yenye vyanzo vya maji vingi na mikoa ambayo ina vyanzo vya maji vingi tu sasa kwa sababu ya matatizo ya tabia ya nchi, uharibifu wa mazingira, naishauri Serikali
kwamba wakati umefika maeneo yenye vyanzo vya maji tuyalinde, kuwe na mkakati wa kitaifa wa kulinda vyanzo vya maji. Kwa mfano, katika Mkoa wa Kigoma, katika Wilaya ya Kasulu peke yake tuna vyanzo vya maji takribani 600 ambavyo havikatiki mwaka mzima. Vyanzo hivi vinapeleka maji yake katika Mto Malagarasi kwa kiwango kikubwa na maji hayo hatimaye yanakwenda kwenye Ziwa Tanganyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna huu mpango kabambe wa kupeleka maji Malagarasi, Urambo, Kaliua na kwingineko kama hakuna mkakati endelevu wa Serikali nina hakika tutafika mahali maji ya Mto Malagarasi yatakuwa hayatutoshi, hayataweza kuzalisha umeme na kufanya
shughuli za kilimo. Kwa hiyo, nashauri strongly kabisa kwamba wenzetu wa Serikali hata kama ni mwakani tuleteeni a comprehensive plan ya kulinda vyanzo vya maji. Iko mikoa yenye vyanzo vingi, Morogoro wana vyanzo vingi, Katavi wana vyanzo vingi tuwe na mpango mkakati kabisa kitaifa wa kulinda vyanzo vya maji katika maeneo ambayo maji hayakauki mwaka mzima. Ni kweli yako maeneo yenye shida lakini tukiwa na mkakati endelevu nina hakika maji haya hatimaye yatatusaidia sisi wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, Mheshimiwa Simbachawene ulitembelea Kigoma, ulitumwa na Mheshimiwa Rais kule Kigoma…
Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii. Hata hivyo nina machache ya kuchangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya uharibifu mkubwa wa mazingira ulisababishwa na ujio wa maelefu ya wakimbizi toka Burundi, DRC na Rwanda. Ujio huu umesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira katika Wilaya ya Kasulu, Kibondo na Kakonko, idadi ya wakimbizi sasa ni zaidi ya 600,000. Ajabu ni kwamba katika hotuba yote ya Waziri hakuna hata mistari wala aya inayoelezea uharibifu huo wakati madhara yake kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma ni makubwa sana. Naishauri Serikali/Wizara ije na mpango maalum wa kuhifadhi mazingira na au kufufua maeneo yaliyoharibika sana na ujio wa wakimbizi. Mfano:
(i) Mto Makere umekufa na kukauka kabisa
(ii) Misitu katika vijiji imekatwa sana na kuharibiwa kabisa
(iii) Vyanzo vya maji (water resources) nyingi zimeharibika kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, “we need comprehensive program to restore the environment on area hosting refugees and communities hosting refugees in Kigoma”
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkakati wa kuhifadhi vyanzo vya maji katika Wilaya ya Kasulu na hasa vyanzo vilivyopo Kasulu Mjini. Katika eneo la Kasulu Mjini tuna vyanzo zaidi ya
200. Naomba jitihada za pamoja za Serikali/Wizara na Halmashauri ya Mji kulinda vyanzo vya maji ambavyo hatimaye hupeleka/hutiririsha maji yake katika Ziwa Tanganyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana hatua ya Waziri kutuma wataalam wa Maji na Mazingira kuja Wilaya ya Kasulu kufanya “study Project on that one”. Hatua ni njema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Taifa wa Mazingira; nashauri tozo zinazotozwa na TFS na migodi iliyopo nchini angalau asilimia 25% ya tozo hizo zipelekwe kwenye Mfuko huo ili kulinda Mazingira ya Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mwaka 2015/206 – TFS walikusanya zaidi ya shiligi billioni 50 ingekuwa busara sana kama 25% ya fedha hizi zingepelekwa kwenye mfuko huo. Tozo toka mgodini ni fedha nyingi sana na kwa hali ilivyo sasa hakuna hata senti inayopelekwa kwenye mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inaweza kuleta pendekezo la sheria Bungeni ili sheria hiyo tuitunge haraka sana kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nakushukuru kwa kunipa nafasi hii na nianze kwa kuwapa hongera sana Waziri, Naibu Waziri na timu yako ya wahandisi mlioko Wizarani na wahandisi walioko TANROADS, mnafanya kazi nzuri hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitakuwa na machache sana. Mheshimiwa Waziri mimi nataka kukukumbusha tu suala la kisera kwanza. Alikuwa anatukumbusha Ndugu Chenge mchana hapa, ujenzi wa barabara za nchi hii zinahitajika kila mahali sana kabisa na nchi yetu bahati nzuri ni kubwa. Naomba tujirejeshe kwenye sera ya ujenzi wa barabara hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulishakubaliana kwa mujibu wa Sera ya CCM ya miaka 20 kwamba tutajenga barabara za kuunganisha mkoa na mkoa, tungejielekeza katika maeneo hayo. Kuna mikoa ambayo imeunganishwa tayari na kuna mikoa mingine haijaunganishwa. Na fedha ambazo mnatenga kwenye bajeti ni kidogo mno, sasa sungura mdogo lakini fedha mnatapanya na baadhi ya maeneo kusema kweli hayana umuhimu wa kiuchumi leo. Kuna Mkoa kama Katavi kwa mfano, Mkoa wa Katavi haujaunganishwa na Kigoma, Mkoa wa Kigoma haujaunganishwa na Geita, Mkoa wa Kigoma haujaunganishwa na Shinyanga, Mkoa wa Kigoma haujaunganishwa na Tabora ingawa kuna juhudi hizo kidogo za kilomita chache, Mkoa wa Kigoma haujaunganishwa na Kagera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na Mheshimiwa Waziri wewe umetembea mpaka pale Kasangezi nilikuona siku ile, yale ndiyo maeneo ambayo yanazalisha chakula kingi. Sisi ndiyo tunalisha migodi mingi iliyoko ukanda wa ziwa. Naomba mjirejeshe kwenye sera tuweze kufanya haya mambo kwa utaratibu, otherwise kila mahali barabara, uwezo huo kwa mara moja hatuna. Mheshimiwa Waziri wewe unajua barabara ya Kigoma - Nyakanazi huu ni mwaka wa 20 barabara haikamiliki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipande cha kutoka Kidahwe mpaka Kasulu kilometa 50 huu mwaka wa tisa haikamiliki. Sasa nimeona kwenye bajeti yako umetenga bilioni 19, lakini umesema hizo ni za Kidahwe – Kasulu hizo ni za Kabingo – Nyakanazi na unazungumza kwenye hotuba yako unasema katika fedha hizo hizo ni za upembuzi yakinifu na kuandaa ujenzi wa barabara ya Manyovu – Kasulu – Kibondo – Kakonko, na unasema ni za maandilizi ya ujenzi. Sasa nilikuwa nakuomba hizi shilingi bilioni 19 ni ngapi zinajenga barabara ya Kidahwe tujue Kasulu na ngapi zinatoka Kabingo ziende Nyakanazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi sielewi kabisa jambo hili. Hili jambo mkilifanya kisera tutafanikiwa, tutaanza na barabara ambazo zina umuhimu kiuchumi si kujenga kila mahali kwa mara moja. Nilikuwa naomba hilo liwe la kwanza Mheshimiwa Waziri, nikurejeshe kwenye sera na wewe bahati nzuri umekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya muda mrefu, hili jambo unapaswa kulisimamia wewe, hili ni jambo muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hapo hapo nilishazungumza na Mheshimiwa Waziri nilikwenda ofisini kwake zaidi ya mara moja, kwamba hii barabara ya Kidahwe - Kasulu haifiki Kasulu Mjini inaishia Nyumbigwa au Kanyani karibu na njia panda ya kwenda Uvinza kwenda barabara ya Katavi. Naomba kwa sababu mkandarasi yuko site inakuwa ni vigumu sana kuja kum-mobilize baadaye apatikane kwa kilometa nane zile za kuja Kasulu Mjini, itachukua muda mwingine mrefu. Maadamu mkandarasi yuko site ingekuwa ni vizuri basi kuwe na addendum au nyongeza ya mazungumzo ili aongeze kile kipande cha kilometa nane ile barabara itoke Kidahwe ifike Kasulu Mjini. Hilo naomba sana ulizingatie na liko ndani ya uwezo wako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nalizungumza, na nisipolizungumza kila mmoja atanishangaa, ni hii reli ya kati. Waziri Mbarawa, reli ya kati msiipotoshe, reli ya kati inatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam si vinginevyo. Lakini zaidi ya hayo faida ya reli ya kati hasa standard gauge ni kwenda kubeba mzigo mkubwa na mzito.

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri leo hata Mheshimiwa Rais wakati anazungumza na vijana wa UDOM hilo kalizungumza kwamba tunajenga standard gauge kwa ajili ya kubeba mizigo mizito ili barabara zetu ziwe salama. Sasa economics zake ziko hivi, ukitoka Dar es Salaam ukaenda mpaka Tabora, Isaka, Keza, Msongati na Kigali ni mbali zaidi kuliko kutoka Dar es Salaam ukaja Uvinza, ukaenda Msongati, ukaenda Bandari ya Kigoma tofauti yake ni kilometa 700, hizo ni economics tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, uking’ang’ania hii route mnayotaka kuichukua mnakwenda kuinufaisha nchi ya Rwanda, maana Kigali wanataka ile hub itoke Isaka pale iende Keza, iende Kigali - Msongati na Msongati ni South East ya Burundi. Msongati ambako kuna deposit ya nickel, coal, cobalt na copper iko karibu na Mkoa wa Kigoma, ni South East.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ile reli ikitoka Msongati – Uvinza ni karibu na Bandari ya Kigoma ni karibu na kwenda Bandari ya Dar es Salaam, hizo ni economics tu. Msihangaike na hiyo route ya mbali, tuanze na hii route ya karibu kwenye mzigo, kwenye mali na andiko la economics of geography inatueleza kwamba (na liko pale TRL, aliandika Bwana Karavina akiwa Mkurugenzi pale TRL) kwamba mzigo ulioko DRC ndiyo uatakofanya reli ya kati ya standard gauge iwe na maana kiuchumi, ni tani milioni 40.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi nashangaa eti mnaanza upembuzi yakinifu kutoka Tabora mnakwenda Shinyanga, kubeba samaki? Hizi reli ni za kiuchumi hizi. Dhamira nzuri ya Mheshimiwa Rais ya kujenga reli ya standard gauge itusaidie kuokoa na barabara zingine hizi ambazo zinaharibiwa kwa kubeba mizigo mizito. Tafadhali sana mjielekeze kwenye historia ya mambo haya. Sasa sina haja ya kuzungumzia habari ya reli ya kati kwa sababu nadhani hiyo imeingia, ni economics tu. Bashe amezungumza asubuhi, tuma watu wako basi wafanye hizo cost benefit analysis tuone ni wapi kuna nafuu ya kiuchumi zaidi na tuna ushindani zaidi kuliko sehemu nyingine, simple.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa nilisemee kidogo, nimesoma kwenye taarifa ya Kamati kwamba Shirika la ATCL ambalo tumelifufua kwa juhudi kubwa na kila mmoja ananufaika nalo kwamba si mwachama wa IATA. Sasa swali dogo tu, kwa nini si mwanachama wa IATA na kama sio mwanachama wa IATA maana yake nini kiusalama? Kwa sababu tusifanye mambo tumefumba macho, exactly!

Mheshimiwa Naibu Spika, IATA ni Shirika la Usalama la Anga la Dunia, sasa Air Tanzania nimesoma kwenye paragraph moja kwamba ATCL sasa sio member wa IATA, kwanini sio member wa IATA? Sasa juhudi zote hizi, zinakuja ndege kubwa, tunataka kwenda China, twende Marekani, lazima tuwe member wa IATA kwa sababu masuala ya kiusalama na masuala mengine ya anga.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho ambalo ningependa nizungumzie; Mheshimiwa Waziri tunaomba utupe comfort hii barabara ya Manyovu ambayo unasema ni barabara ya East Africa chini ya NEPAD ufadhili wa African Development Bank inafanyiwa upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nataka kujua, bila shaka kuna time frame upembuzi yakinifu unaisha lini na ujenzi huu unaisha lini? Kwa sababu tayari kuna problem kwamba tayari kutoka Manyovu kuja Kasulu Mjini nyumba zimewekwa alama “X” kwamba watu watalipwa fidia. Sasa hebu mtueleze, na mimi ningeshauri strongly Mheshimiwa Waziri kwamba mna wataalam wengi pale, tuwe na vita ambavyo vinajulikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi ukifanya upembuzi yakinifu maana yake ni miaka kumi? Lazima kuna time frame yake; kama ni miaka miwili ama ni mwaka mmoja tuweze kujua. Ningependa Mheshimiwa Waziri utakapokuja kuhitimisha utueleze barabara ya Manyovu - Kasulu - Kibondo
- Kabingo huo upembuzi yakinifu utakuwa umekamilika lini na lini barabara hiyo itaanza kujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa kabla kengele haijalia, nizungumzie kipande kidogo hiki cha Kanyani kwenda Uvinza hadi Katavi. Hicho kipande Mheshimiwa Waziri au Naibu wako amepita pale, kile kipande kinatoka Nyumbigwa pale ambapo ndiyo Kanyani zamani, mnaita ni barabara eti ya Nyakanazi kwenda mpaka Tunduma, mimi sielewi hii! Ile barabara inatoka pale Kanyani inakwenda Rungwe mpya, inakwenda Basazi inakwenda Uvinza, inakwenda Mishamo inakwenda Mpanda Stalike. Barabara ile ni muhimu sana kwa sababu ukijenga hii barabara ya Kidahwe - Kasulu kwenda Nyakanazi ile ndiyo roop ya kwenda Mkoa wa Katavi, ni barabara muhimu sana inayotuunganisha sisi na Mkoa wa Katavi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri tafadhali sana zingatia hayo zirejeshe kwenye sera.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa sababu mmeanza vizuri. Nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali kuzingatia mambo muhimu yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa Reli ya Kati; Dar es Salaam – Kigoma ndiyo Reli ya Kati. Matawi yake ni Tabora – Mwanza; Kaliua – Mpanda - Kasanga Port, Uvinza - Msongati (Burundi) na Isaka - Keza. Uchumi wa reli na hasa reli ya standard gauge ni kubeba mzigo mzito, siyo kubeba samaki wala abiria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali dhamira ya ujenzi wa reli ya kati izingatie msingi wa uchumi. Mzigo zaidi ya tani milioni 40 zipo nchi jirani ya DRC na zaidi ya mzigo tani milioni 10 zipo kwenye deposit ya Msongati katika Province ya Kusini Mashariki mwa Burundi. Mzigo upo DRC na sasa Burundi; na njia rahisi ya kwenda bandarini ipo kupitia Kigoma
- Dar es Slaam. Economic of Geography zizingatiwe. Matawi yaliyobaki ya Tabora/Mwanza na Isaka –Keza yasubiri! Iwe Second lot.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kidahwe – Kasulu - Kikondo na Nyakanazi, speed ya ujenzi wake inatia shaka sana. Kipande cha kilometa 50 cha Kidahwe - Nyumbigwa kimetumia sasa miaka saba. Naomba sana Serikali iharakishe ujenzi huo. Aidha, kutoka Nyumbigwa hadi Kasulu Mjini ni kilometa 9 - 10 hivi. Nashauri Mkandarasi aongezewe hizo kilometa 9 - 10 ili barabara hiyo ifike Kasulu Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Manyovu – Kasulu – Kibondo – Kabingo, usanifu wake na ujenzi wake unaanza lini? Tusubiri kwa miaka mingapi? Ishirini tena ijayo!

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa ya Kamati inaonesha Shirika letu la ATCL siyo mwanachama wa AITA. Je, taarifa hizi ni za kweli? Kama ni kweli, nini maana yake hasa kiusalama?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ushauri uzingatiwe na Serikali itoe majibu yaliyo sahihi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa namna ya pekee kwa kweli niwape hongera sana Waziri wa Maliasili na Naibu wake, lakini pia na watendaji wote ambao kwa kweli wamefika mahali wamesaidia sana ujangili kushuka kwa kiwango kikubwa, hongereni sana kwa kupunguza ujangili katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo mambo mawili tu na ningeomba niyaseme kama ifuatavyo; kwanza ningependa kuzungumzia suala la msitu wa Taifa wa Makere Kusuni maarufu kama Kagera Nkanda. Msitu huu una ukubwa wa hekta 97,000 na msitu huu Waziri unanisikia msitu huu ulikuwa gazetted mwaka 1954 wakati eneo lile lilikuwa halina watu kwa kweli, sasa maeneo haya watu wameongezeka vijiji vimeongezeka na sasa watu wanasumbuliwa kujua mipaka halisi ya eneo lile na maeneo ya vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba sana Mheshimiwa Waziri na timu yako hasa wenzako wa TFS na juzi nilipata bahati kuzungumza hata na Dkt. Silayo kuhusu jambo hili, kwamba ni wakati umefika mkaweke mipaka upya, mka-re-map eneo lile kwa sababu watu wameongezeka na kama alivyosema jana Profesa Tibaijuka hapa jamani mazingira yamebadilika huwezi kuwa na mipaka ya 1954 leo ni miaka 60 ukasema mambo yatabaki yale yale, hawa wananchi wameongezeka na lazima utaingia kwenye maeneo kufanya shughuli zao za kujitafutia kipato na uchumi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri hili jambo tumelisema na ilishakuja Tume yako kule Kasulu tukalizungumza sana jambo hili, ningeomba sana suala la Kagera Nkanda lifikie mwisho na kwa kweli wananchi waweze kupata maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Pia niseme kwamba popote itakavyokuwa juzi Mkurugenzi wa Wanyamapori alikuwa anatupa habari ya genesis ya biblia, lakini tukubaliane pia kwamba hakuna mahali popote kwenye biblia pamesemwa kwamba sasa viumbe hivi vya wanyamapori na misitu vitakuwa badala ya binadamu, la hasha! Lazima binadamu awe mbele kwa sababu wameumbwa na Mwenyezi Mungu kuweza kutumia rasilimali hizi.

Suala la Kagera Nkanda Mheshimiwa Waziri ninaomba na wenzako wa TFS lifike mwisho, mka-re-map mipaka ile, sisi hatuna shida na uhifadhi, lakini mka-re-map mipaka ile ili watu waweze sasa kupata maeneo ambayo wanaweza kuyatumia kwa kilimo na ninasema tena mwaka 1954 lile eneo lilikuwa halina watu kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ningependa niliseme ni suala la la eneo oevu la Malagarasi, maarufu kama Malagarasi wetland. Eneo hili liko kwenye uhifadhi wa dunia chini ya UNESCO, chini ya Ramsar site, eneo hili linaharibika.

Mheshimiwa Waziri wale ng’ombe mliowafukuza kule Geita, ng’ombe waliotoka Burigi wamehamia kwenye chepechepe ya Malagarasi, sasa unataka tupoteze Mto Malagarasi? Kwetu watu wa Kigoma na watu hata Geita wenyewe, Malagarasi ni ikolojia ambayo ni muhimu sana kwa maisha ya watu wetu naomba sana maadam hii wetland ya Malagarasi, eneo oevu ama chepechepe la Malagarasi lipo chini ya Ramsar site, chini ya uhifadhi ya dunia, kwa nini lisilindwe kwa nguvu zote, kwa nguvu ya pamoja kati ya UNESCO, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara yako, maeneo haya tunayaacha yanaharibika na baadaye athari zake ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupotea kwa wetland ya Malagarasi maana yake ni kupotea kwa Ziwa Tanganyika, kupotea kwa Ziwa Tanganyika unajua madhara yake itakuwa ni makubwa sana. Hivyo nilikuwa naomba sana maeneo ambayo yametengwa, maeneo ambayo yametangazwa kidunia nina hakika, Wizara na Serikali mnaweza ku-join hands na watu wa UNESCO maeneo haya yakalindwa ili yaweze kuendelea kuwepokwa sababu binadamu lazima pia waendelee kuwepo.

Mwenyekiti baada ya kusema hayo mawili muhimu niliyokuwa nayo naomba niseme jambo moja la mbuga la Mahale na Gombe National Parks, hizi ni mbuga mpya, hizi ni mbuga virgin kabisa, nafikiri kupitia…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii. Hata hivyo, nitoe ushauri kwa Serikali na Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulinda na kuhifadhi eneo oevu la River Malagarasi. Eneo hili ni Ramsar Site chini ya udhamini wa UNESCO. Eneo hili limevamiwa na ng’ombe wengi ambao baadhi yao ni wale walioondoshwa huku Burigi Pori la Akiba na Kimisi. Ng’ombe hawa wanahatarisha uhai wa Mto Malagarasi. Chukueni hatua haraka bila kuchelewa ili kuokoa rasilimali hii muhimu kwa Taifa na kimataifa. Bila Mto Malagarasi hakuna Ziwa Tanganyika na bila Ziwa Tanganyika hakuna Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo la Msitu wa Taifa wa Makere Kusini maarufu Kagera Nkanda lenye ukubwa wa hekta 97,000; Wilaya ya Kasulu tumeomba hekta 20,000 - 25,000 ili wananchi wapate eneo la kilimo na kufanya shughuli za kufuga nyuki na wanyama wengine. Tunahitaji sasa eneo hili lipimwe upya ili kuhuisha mipaka ya wakoloni (Waingereza) ambao walitangaza msitu huo mwaka 1954. Zaidi ya miaka 60 haiwezekani mambo yawe yale yale wakati idadi ya wakazi imeongezeka mara kumi. Baada ya re- mapping hiyo hali ya amani na utulivu itarejea baina ya wananchi na Serikali yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mbuga ya Hifadhi ya Gombe na Mahale zilizopo Mkoani Kigoma; mbuga hizi ni mpya, ardhi ni mpya na miundombinu yake ni mipya. Juhudi kubwa lazima ifanywe ili kutangaza vivutio vya pekee vya sokwe wanaopatikana katika mbuga hizo mbili katika nchi yetu. TTB wafanye kazi ya kutangaza vivutio hivi kwa juhudi kubwa. TTB wanaweza hata kutumia mbinu ya PPP/TTB Joint initiative. Taasisi ya Jane Godall watafiti wa sokwe Kigoma wanaweza kushirikishwa pia. Jengeni upya wa fikra katika tasnia hii ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivutio vipya vya utalii vilivyopo katika Mkoa wa Kigoma ambavyo vinahitaji kutangazwa na TTB pamoja na TANAPA ni pamoja na:-

(i) Njia ya watumwa ya Kigoma/Ujiji - Tabora - Dodoma - Morogoro hadi Bagamoyo. Hiki ni kivutio kikubwa sana kama kitakuwa promoted na developed. Njia hii ipo kihistoria, kazi ni kuwa na mkakati wa muda mrefu na dhamira ya dhati ya Wizara hii na TTB, tuanze sasa.

(ii) Makumbusho ya Dkt. Livingstone alipokutana na Dkt. Henry Morton Stanley 1871. Jengo la makumbusho lipo limejengwa, likamilike ili lianze kazi. Utendaji kazi wake lazima uende sambamba na promotion ya kivutio hiki. Nina hakika eneo hili linaweza kuingiza mapato mengi Serikalini.

(iii) Cultural tourism - Kigoma is rich in cultural activities lets promote this area. Tuanze sambamba na kutangaza mbuga zetu za Gombe na Mahale.

(iv) Ziwa Tanganyika na fukwe zake, hiki nacho ni kivutio kikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TTB amkeni sasa, njooni na mikakati endelevu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii na mimi. Kwa namna ya pekee naomba nianze kwa kuwatia shime na kuwapa hongera kubwa sana wewe Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wako, Makatibu Wakuu watatu maana ndiyo Wizara yenye Makatibu Wakuu watatu, hongereni sana kwa kazi pamoja na wataalam walio katika Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni Wizara kubwa na ningeshauri, Mheshimiwa Jenista wewe ni co-ordinator wa mambo ya Serikali Bungeni. Hii Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni Wizara kubwa sana, mshauri Mheshimiwa Rais aangelie upya muundo wa Wizara hii. Ni Wizara yenye mambo makubwa na yanayogusa watu wetu kwa asilima zaidi ya
75. Ni Wizara yenye mifugo, kilimo, uvuvi pamoja na taasisi 130 chini yake, lakini ni Wizara moja na ina Waziri mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nafikiri kwamba wakati umefika kwa Bunge hili kupitia kwenu Baraza la Mawaziri mumshauri Mheshimiwa Rais wakati mnakunywa naye chai aangalie namna bora ya kui-restructure. Wizara hii ni kubwa mno na hata kwenye Kamati sisi tunapata shida kweli kwa sababu ina mambo mengi sana na mambo yote yanagusa maslahi ya wananchi wetu ambao ndio wapiga kura wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hilo pia nitoe pongezi nyingi kwa wataalam wetu, Waheshimiwa Wabunge sijui mmeangalia ukurasa wa 42, wataalam wetu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wamepata Tuzo ya African Union kwa kuandika mradi ambao umewezesha Wizara yetu kupata shilingi bilioni 44. Mheshimiwa Waziri hongera sana na wataalam wako, na mimi ningedhani sasa pengine hii ndiyo iwe trend.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo mna wataalam wengi sana, mna wasomi wengi sana, kuna Makatibu Wakuu wataalam wazuri kabisa, nilikuwa nafikiri hii ndiyo iwe trend sasa kwamba kwenye mashindano kama haya ambayo yanatolewa na AU, hizi nazo ni fursa nyingine za kutuongezea fedha kwenye sekta ya kilimo, hongereni sana kwa kupata shilingi bilioni 44 ambazo zimepatikana kwa kushinda Award ya Global Agriculture and Food Security; watalaam wa Wizara hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa niliseme, jana Mheshimiwa Waziri Mwijage amelisemeaa vizuri, kwamba Serikali hii ni moja maana kuna baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanafikiri Serikali hii ni Serikali ya vipande vipande, kwamba kuna Serikali Wizara ya Fedha, kuna Serikali Wizara ya Kilimo, kuna Serikali Wizara ya TAMISEMI. Serikali ni moja, na kwa ushahidi aliouonesha jana Waziri Mheshimiwa Mwijage na wewe ulioutoa leo umefanya vizuri sana kuondoa tozo zilizokuwa kero kwa wakulima wetu, hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye kahawa, mimi natoka katika zone ambayo pia tunalima kahawa; tumeshukuru sana hizi tozo 17 ambazo zilikuwa ni kero kwa wakulima wetu, na nina hakika zitasaidia sana kuongeza morally ya kuendeleza zao letu la kahawa. Sasa nina mambo mawili, matatu ya ushauri kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza ni kuhusu upatikanaji wa mbolea. Mheshimiwa Waziri tumezungumza sana kwenye Kamati, bahati nzuri mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimo. Hili tumelizungumza sana, juu ya umuhimu wa upatikanaji wa mbolea na Serikali mmekuja na mkakati wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja, sisi Wabunge wote tunawaunga mkono kwa asilimia 100. Zoezi hili ni zuri, mbolea hii itatusaidia sana. Jambo ambalo ningeomba tu kulisisitiza ni yale mambo ambayo Mheshimiwa Waziri tuliyazungumza kwenye Kamati ambayo ni muhimu kuyazingatia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, jana nimemsikia Waziri Muhongo anatuhamasisha kuhusu ujenzi wa Kiwanda chetu cha Mbolea kule Lindi na Mtwara, lakini uko ukweli Waheshimiwa Wabunge kwamba kiwanda hiki kimekuwa kinahujumiwa na taarifa hizi ni za uhakika. Sasa nikutie shime Mheshimiwa Waziri wewe na timu yako, wataalam wako wa Tanzania Fertilizers Regulatory Authority wana uwezo mkubwa sana, wasimamie zoezi hili la ununuzi wa mbolea kwa pamoja ili hatimaye bei ya mbolea iweze kushuka na iweze kupatikana katika maeneo mengi ya Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niweke angalizo dogo tu, kwenye ununuzi wa pamoja kuna changamoto zake kama ambavyo zilikuwepo kwenye ununuzi wa pamoja wa mafuta. Ziko changamoto nyingi na moja ya changamoto kubwa ni hujuma, lazima kutakuwa na watu wenye Makampuni yao watakuwa wanataka kuhujumu effort hii ya kuanzisha bulk procurement. Nikuombe Mheshimiwa Waziri, mambo ya msingi ya kuzingatia iwe ni pamoja na ku-mitigate hizo hujuma, hiyo ni muhimu sana ili isitokee hata siku moja katika nchi yetu tukakosa mbolea eti kwa sababu utaratibu huu wa kununua mbolea kwa pamoja umekuwa na matatizo na umeshindwa kusambaza mbolea katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni matumaini yetu kwamba utaratibu huu wa kununua mbolea kwa pamoja utasaidia mbolea ipatikane kwa bei ya chini kama ilivyo ndoto yetu ya awali, kwamba tungependa mbolea hii ipatikane nchi nzima kama ilivyo Cocacola au vocha ya simu. Nina hakika, Mheshimiwa Waziri bahati nzuri tumeyazungumza kwa kirefu kwenye Kamati kwamba haya yote mtayazingatia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa kushauri na nimelisema sana Mheshimiwa Waziri ni kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika Mikoa inayopata mvua ya kutosha na Mikoa hiyo siyo mingine ni Mkoa wa Katavi, Mkoa wa Kigoma na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kagera. Haya ni maeneo ambayo yana fursa kubwa sana kwa sababu jiografia yake inaruhusu na tumeshazungumza sana, ni matumaini yangu kwamba jambo hili utalizingatia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ametufariji sana juu ya migogoro ya ardhi ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi pamoja na Mamlaka, Hifadhi za Misitu na Hifadhi za Wanyamapori. Mimi niombe jambo moja, Mheshimiwa Waziri wewe katika jambo hili ni mdau mkuwa sana, jambo hili sasa limalizike. Yale maeneo ambayo yamekosa sifa ya uhifadhi yarejeshwe kwa wananchi ili wayatumie, msing’ang’anie maeneo ambayo hayana faida kwa wananchi wetu. Mheshimiwa Waziri wewe unajua pale kwetu Kasulu kuna hifadhi ya msitu wa Kagera Nkanda, msitu ulioko Makere Kusini, watu wanasumbuka, eneo lenyewe limeshakosa hadhi ya uhifadhi kwa kweli. Ni vizuri maeneo kama haya kama ambavyo tumekuwa tukishauri maeneo yarejeshwe kwa wananchi wayatumie kwa shughuli za kilimo ili waweze kujikimu kwa maisha yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu upataikanaji wa mbegu. Mheshimiwa Waziri nikukumbushe kwamba kuna shamba kubwa la Bugaga, nitapata comfort sana kama utakapokuja ku-wind up utanieleza namna gani mnajipanga kutumia shamba la Bugaga lenye hekta zaidi ya 1,000. Shamba lile ni kubwa sana, limekaa tu, liko idle. Sisi Halmashauri tulilitoa kwa ajili ya kuzalisha mbegu, lakini shamba hili limekaa halitumiki na kama Wizara hamuwezi kulitumia basi nimeshakwambia siku zote mturejeshee kwenye Halmashauri sisi tulitumie kadiri tutakavyoona inafaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu Mawakala wa Mbolea kwa masimu wa 2016/2017. Mheshimiwa Waziri umeshatueleza na wadau wamekuja wamezungumza na Waziri Mkuu pia, mmeahidi kuwalipa mawakala wale waliohakikiwa katika kipindi cha mwezi
mmoja, fanyeni zoezi limalizike. Wale mawakala wa mbolea ambao makaratasi yao yako vizuri, ambao hawana matatizo basi walipwe fedha zao, na wale wenye matatizo ndio wasubiri; lakini wale ambao mikataba yao iko vizuri, wamesambaza mbolea kwa wakulima wetu walipwe fedha zao ili kuweza kupunguza tatizo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo linguine, nimeshazungumza a wewe ni kuhusu Chuo cha Kilimo cha Mbondo, tafadhali sana angalia namna bora ya kuweza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Basi nakushukuru Mheshimiwa Waziri naomba uzingatie Mbondo, ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, nashukuru nami kwa kunipa nafasi hii. Kwanza naanza kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa. Wale mnaokumbuka, kwa miaka 10, 15 iliyopita, hii ni hotuba ya pili kwa ubora. Hotuba ya kwanza ni ile ya wakati ule wa Mzee Mkapa aliyotoa Mzee Mramba kufuta kodi, Nuisance Taxes kama mnakumbuka mliokuwepo.

Mheshimiwa Spika, hotuba hii kwa ubora wake imejikita kuondoa matatizo na mizigo kwa wakulima wetu na watu wa kipato cha chini. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mpango hongera sana, kama nilivyokwambia siku ile, ulikuwa kwenye form vizuri na ulifanya kazi nzuri, hongera, tena hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine bila kusahau, unakumbuka wewe na mimi tulikwenda North Mara kipindi kile kwenye vurugu ya Mto Tigite wakati kuna zile tuhuma kwamba yale maji ya Mto Tigite yameua watu wengi sana kule. Naomba kwa namna ya pekee Waheshimiwa Wabunge wote kazi ambayo ameifanya jana Mheshimiwa Mzee Magufuli ni kazi ya peke yake kabisa. Unaibiwa, sasa ametokea jasiri kusema jamani tunaibiwa, tusiibiwe, huyo amekuwa mbaya? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema, nawe tumekusikia jana uliona ile nguvu iliyokuwepo pale, mmefanya kazi nzuri sana, hongereni. Tunaibiwa na kama alivyosema Mbunge mmoja, sasa basi, tusiibiwe tena. Maana mtu kama anakuibia, kwanza anakudharau. Nasi tunasema hao Wazungu waliokuwa wanatuibia, sasa basi tumeona. Tumsaidie Mheshimiwa Rais, rasilimali za Taifa tuzilinde. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wewe utakuwa shahidi yangu, wala siyo madini tu, wewe unajua ni maeneo chungu nzima. Ile spirit kwamba sasa tupitie maeneo yote yenye fedha, yanayozalisha fedha katika nchi yetu, tuyapitie yote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilibahatika mwaka 2009, niliongoza Kamati Ndogo kwenda Mwadui, tukiwa na Mheshimiwa Mzee Shellukindo kama mnakumbuka. Tulipofika pale Mwadui, Williamson Diamond, tuliyoyakuta pale ni mambo ya aibu. Wale De Beers wamekopea shares zetu kule London bila sisi wenyewe kujua. Tulikuwa na Mbunge wakati ule Bwana Mpendazoe, alikuwa ni Board Member kwenye ile group ya Williamson Diamond. Wanasema walikwenda London pale wakakuta hisa zilishauzwa na Serikali haijui.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nami nakubaliana nawe kuunda Tume Ndogo kwenda Mwadui pale kuona. Ni uchafu uliopitiliza kwamba shares zetu za Serikali ya Tanzania ndizo De Beers alikwenda kukopea na kuanzisha migodi, Niger na Namibia. Mambo ya aibu kabisa! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii vita ni kubwa, nina hakika Mheshimiwa Rais peke yake haiwezi. Ni lazima tumuunge mkono kama Bunge, tusimame pamoja kulinda rasilimali za Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nitakuwa na machache tu. La kwanza, nianze na miradi ya kipaumbele. Mheshimiwa Waziri tangu bajeti iliyopita na bajeti hii tumezungumzia habari ya miradi ya vipaumbele. Mimi nataka nijikite kwenye miradi hii ya kipaumbele; nianze na mradi wa kujenga reli ya kati. Tumeanza vizuri, lakini bado tunawakumbusha na hasa wenzetu wa Hazina ambao ndio mnatoa fedha na kumshauri Mheshimiwa Rais, endeleeni kumkumbusha kwamba hii reli ya kati itakuwa na faida kubwa zaidi kama itaanza kwenda Kigoma kabla ya kwenda matawi mengine; na sababu ziko wazi; ni za kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kule Kigoma ndiyo kuna mzigo ambao utaifanya reli hiyo iwe na faida kiuchumi. Mzigo uko Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ya Mashariki. Hilo tumelisema sana. Sasa kwa sababu kuna mkakati huo, nashauri, wakati anatafutwa Mkandarasi wa kujenga tawi la Tabora kwenda Mwanza, wakati huo huo atafutwe Mkandarasi kujenga tawi la kwenda Kigoma ili tuwahi ule mzigo wa DRC ambao utaifanya hii reli ya kati iwe na maana kiuchumi. Mzigo mkubwa uko DRC na kila mmoja anafahamu. Siyo DRC tu, hata hii Msongati ya Burundi ambapo kuna nickel nyingi, maana yake ni karibu zaidi na Bandari ya Kigoma, ni karibu kabisa na Station ya Uvinza ambayo iko katika Mkoa wa Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo napenda nilisemee, Mheshimiwa Waziri alikwenda Korea ya Kusini wakasaini mradi unaoitwa North West Grid ambao unatoka Mbeya – Sumbawanga – Katavi – Kigoma – Nyakanazi.

Mheshimiwa Spika, sasa napenda wakati Mheshimiwa Waziri anajumuisha na kwenye kitabu chake ameuzungumza mradi huu, napenda kujua vizuri, huo mradi unaanza lini? Unaanzia wapi? Kwa sababu kutoka Tunduma pale mpaka Nyakanazi ni kilometa zaidi ya 2,000. Ni dhahiri kabisa kwamba huo mradi utakuwa na maana kama utakuwa hauna Wakandarasi wengi, mmoja atokee Tunduma aje Sumbawanga, aje Katavi na pengine mwingine atoke Nyakanazi kuja Kigoma. Nina hakika kama ni Mkandarasi mmoja itachukua miaka mingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia habari ya uchumi wa viwanda, maana yake ni pamoja na kuwa na umeme wa viwandani. Maana huu umeme wa REA ni mzuri, lakini ni dhahiri kwamba ni umeme ambao hauimarishi viwanda kwa sababu siyo umeme mwingi sana. Kwa hiyo, napenda sana kujua hilo kwa sababu yeye mwenyewe alisaini mkataba ule pale Korea Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo napenda nilisisitize kwenye Mpango wa Kipaumbele ni pamoja na barabara. Kwanza hongera kwa barabara hii ya Tabora. Sisi tukisikia barabara ya kwenda Tabora, maana yake hiyo barabara inakwenda Kigoma.

Mheshimiwa Spika, tumeshukuru sana hii barabara ya Chaya – Nyahua, imepata fedha, tumeshukuru sana, maana yake inakwenda mpaka Kigoma. Tunashukuru pia kwamba juhudi ziko kubwa na tumeshapata fedha kujenga kipande cha Daraja la Malagarasi kwenda Uvinza kwa fedha za Kuwait Fund. Sisi kwetu ni faraja kubwa sana. Napenda hiyo juhudi iunganishwe na ujenzi wa barabara ya kimkakati ya kutoka Kigoma kwenda Nyakanazi. Barabara hiyo imetengewa fedha, lakini fedha kidogo sana, shilingi bilioni
19. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikurejeshe, Sera ya Ujenzi wa Barabara za nchi hii, tumeshakubaliana huko nyuma, Sera ya Ujenzi wa Barabara na Sera ya Chama cha Mapinduzi kwamba tutaunganisha mikoa na mikoa. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, waende kwenye misingi ya Sera ile kwamba mikoa ambayo haijaunganishwa na mikoa iwe ndiyo kipaumbele Waheshimiwa Wabunge. Mkoa wa Kigoma haujaunganishwa na Katavi, haujaunganishwa na Geita, haujaunganishwa na Kagera na pia haujaunganishwa na Shinyanga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lazima twende kwenye misingi hiyo. Hizi barabara nyingine za Wilaya kwa Wilaya, Tarafa kwa Tarafa, Kijiji kwa Kijiji zisubiri kwanza. Kwa sababu nchi hii lazima ufanye equalization, lazima Keki ya Taifa tunufaike nayo wote. Kama tunasema tunajenga kuunganisha mikoa kwa mikoa basi, iwe ndiyo kipaumbele na iwe ndiyo mtazamo wa Hazina na uwe ndiyo mtazamo wa Serikali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho nizungumze habari ya vyeti fake, Mheshimiwa Waziri wa Utumishi yuko hapa. Nashauri tu, kazi nzuri sana imefanyika kubaini vyeti fake, lakini waende sambamba na kufanya kitu kinaitwa performance audit. Kuwa na cheti halali hakufanyi mtu awe bora. Ndiyo ile hadithi kwamba afadhali kuwa na cheti fake kuliko kuwa na akili fake. Fanyeni performance audit ya Watumishi wa Umma hawa tuweze kujua kwamba hawa watu kweli wana manufaa na wana tija katika uendeshaji wa shughuli zetu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, la mwisho kabisa, pia nipendekeze jambo moja tu kuomba Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mazingira kwa Mheshimiwa Makamba pale na Wizara ya Maji, waje na mkakati comprehensive wa namna ya kulinda mito yetu katika nchi hii. Mito inakauka, Ruaha iko threaten, Malagarasi iko threaten. Naomba sana, mje na kitu comprehensive kwa ajili ya kulinda mito mikubwa hii ili tuweze kuendelea kuwa na rasilimali za maji.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii na nasema ahsante sana kwa kunipa nafasi hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante. Mbunge wa Msalala amenifurahisha anasema nchi inaibiwa kwa hiyo kama nchi inaibiwa, basi lazima tuzuie isiibiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naunga mkono hoja hii na nimpongeze Waziri Dkt. Mpango na Naibu wake hongera sana wanafanya kazi kubwa. Pia niwapongeze wataalam kwenye Wizara yake, Gavana wa Central Bank Profesa Ndulu wanafanya kazi nzuri hasa katika mazingira haya mapya ambayo muda wote tumekuwa tukiibiwa na watu wengi wamekuwa hawalipi kodi. Dkt. Mpango wako vizuri hongera, wachape kazi, changamoto ni nyingi lakini huo ndiyo mwendo. Mzee Mwinyi Rais wa Awamu ya Pili alisema kwamba “kila zama zina kitabu chake” sasa zama hizi ni mpya lazima tucheze ngoma kadri inavyopigwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo mawili tu ya haraka haraka, kwanza; Mheshimiwa Waziri namkumbusha ujenzi wa Ofisi za TRA – Kasulu, kwa maana kwamba huduma za TRA pale Kasulu ili mtu akafanye registration ya gari akitoka Kakonko, Kibondo, Buhigwe na Kasulu anasafiri kwenda Kigoma. Bosi wa TRA pale anasema shida yao ni mashine kwamba kuna mkubwa mmoja alikuwa haja-release mashine zile kwenda pale Kasulu ili wawe wanafanya registration ya magari. Nimepata taarifa sasa hivi kwamba registration ya TIN-number wameanza last week, hilo ni jambo jema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Waziri nimkumbushe kwamba Halmashauri ya Mji wa Kasulu tumeshawapa kiwanja TRA, tunaomba wajenge Ofisi sasa. Wanapanga kwenye vijumba vya hovyo hovyo pale, wakati nina uhakika TRA wana uwezo wa kujenga Ofisi pale. Tunataka Ofisi ya TRA tumewapa kiwanja, tunaomba wajenge Kasulu kwa Wilaya zote nne ambazo zinazunguka eneo lile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hilo, niseme lingine dogo, Waziri naomba alisikie hili, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimo tulikuwa na semina na watu wa SADC na watu wa IFAD na wafadhili wengine, wamelalamika sana wanasema Serikali, Wizara ya Mheshimiwa Waziri, Hazina hawataki kupokea fedha za msaada wa kilimo. Wote tukatazamana tuliokuwepo pale. Wamelaumu kitu kinaitwa Kamati inayopitia madeni sijui kwamba imejaa urasimu, siyo rafiki, sasa tukajiuliza wote, Mwenyekiti wangu ataniunga mkono yule pale ni kitu gani hiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu, hebu wakakae na hawa partners wetu, ni kitu gani ambacho kiko Hazina pale mpaka kinasema hawa marafiki zetu wanaotaka kutusaidia kwenye sekta ya kilimo hizo fedha hawazitaki kuzipokea. Actually underline wamesema hawataki kupokea fedha zao na wakaenda mbali zaidi wakasema IFAD wana miradi mitatu, hawataki kupokea fedha zao, World Bank wana miradi mitatu ya kilimo, hawataki kupokea fedha zao, NORAD wana mradi mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliokuwepo pale tukaanza kushangaa pale. Ni kitu gani kinatokea Hazina, fedha za support, zingine ni msaada unakuja, ni kitu gani pale Hazina kinaleta urasimu huo? Tunakwenda mbali zaidi Mheshimiwa Waziri wanalaumu baadhi ya Watendaji wake kwamba wamejaa urasimu na wanatupotezea fedha nyingi katika sekta ya kilimo. Nimelisema hili kwa sababu jana limezungumzwa na wenyewe waliokuwepo pale hebu wawe pro-active basi, fedha zinazokuja wazipokee tuweze kuchapa mwendo kusaidia sekta ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine dogo ni hili, kwenye kitabu ukurasa wa 89 Mheshimiwa Waziri amesema moja ya majukumu kwa mwaka 2017/2018 ya Benki ya Kilimo ni kuwasaidia na kuwawezesha wakulima wadogo. Waziri atakapokuja kuhitimisha atueleze hao wakulima wadogo ni wa wapi watakaowawezesha, watawawezeshaje wakati Benki yenyewe ndiyo hiyo? Wao jana walikuwepo kwenye semina hiyo, walikuwepo watu wa Tanzania Agricultural Bank, nao wanasema wana shida ya fedha. Ningependa hilo nalo Mheshimiwa Waziri aliweke sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja, Waziri chapeni mwendo na wakati ndiyo huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsanteni sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mimi nitakuwa na mambo machache sana. Mheshimiwa Waziri Balozi Mahiga wewe ni Waziri mzoefu nina uhakika yote yaliyosemwa utatuonyesha njia, namna ya kutoka hapa tulikofika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo mawili; katika hotuba yote hii, Mheshimiwa Balozi Mahiga hujaweka hata sentensi moja kuhusu wakimbizi (refugees). Katika Mkoa wa Kigoma tumekuwa na wakimbizi tangu miaka ya 1960 na nilidhani kupitia diplomasia yetu hii ya mahusiano na majirani zetu, ni wakati muafaka sasa kwamba wakimbizi hawa wangerudi kwao. Wewe unajua, Mkoa wa Kigoma una raia zaidi ya nusu milioni wanaotokea katika Jamhuri ya Congo, Burundi na Rwanda. Leo DRC mambo siyo mabaya sana Kusini mwa DRC, watu wao hawa wangeweza kwenda kuhifadhiwa katika DRC na makambi yakawa ndani ya DRC, hivyo hivyo kwa Burundi na Rwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kwa sababu muda wenyewe ni mdogo, nizungumzie juu ya huu mpango kabambe wa UN. Naomba unisikilize. Mpango kabambe wa UN wa kusaidia maeneo yaliyoathirika na ujio wa wakimbizi (Refugee Hosting Area Program). Wewe na Wizara yako na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mna uwezo mkubwa mkakaa na hawa UNHCR mkaja na program ya kusaidia maeneo ambayo tumekaa na wakimbizi kwa miaka zaidi ya 60 in this country.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana muda wenyewe ni mdogo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natumaini kwamba mtatoa majibu yanayofaa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami kama ilivyo ada nianze kwa kuwapa hongera sana Ofisi ya Waziri Mkuu na timu yake kwa kazi wanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niwapongeze Serikali kupitia kwa Waziri Mkuchika kwa tangazo lake la asubuhi. Limetufariji sana kwa sababu maeneo mengi yalikuwa na shida, wenzetu wa Serikali hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo mawili tu. La kwanza bahati nzuri nimeliandika kulipeleka kwa Mawaziri na watalaam ni kuhusu uraia. Nchi hii wananchi walio wengi wanaishi kwenye mipaka ya Taifa hili na katika mipaka ya Taifa hili upo Mkoa unaitwa Mkoa wa Kigoma. Sisi tumekuwa wahanga wakubwa wa ubaguzi wa waziwazi kabisa. Tumekuwa ni wahanga wa madhila na maonevu ambayo hayamithiliki kupitia wenzetu wa Idara ya Uhamiaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu aje atueleze hawa wananchi wa Kigoma ambao wanasumbuliwa kwa sababu ya au maumbile yao, au sura zao, au lugha yao, kwa nini kila mara wanaambiwa wao siyo raia? Tunajua iko mikoa mingi, lakini jambo hili kwa Mkoa wa Kigoma limekithiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, leo kumetokea tukio la ajabu kabisa. Kuna mwananchi amekamatwa anaambiwa aende na wazazi wake wote wawili Uhamiaji wakati sisi tunajua kabisa ni mzaliwa wa pale pale. Haya madhila ni makubwa sana na tungeomba kwa kweli yatolewe ufafanuzi mzuri. Inawezekana pengine wenzetu wa Uhamiaji wamekosa tu weledi wa kutenda kazi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, litakuwa jambo la msingi sana wenzetu wa Serikali jambo hili wakilitazama na kwa kweli lipate ufumbuzi. Mbona hatusikii mambo haya kwenye mipaka mingine ya nchi hii kama Tanga, Mbeya au Kilimanjaro ni Mkoa wa Kigoma tu kwa nini? Hili jambo linatukera sana ningeomba lipatiwe majibu ya moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nitapitia ukurasa wa 44 wa hotuba ya Waziri Mkuu ambapo anazungumzia barabara na amebainisha wazi kabisa kwamba barabara zitakazojengwa zitakuwa na urefu wa kilomita 1,760. Sasa nina ushauri tu, katika barabara zinazopangwa kujengwa, najua Serikali ni moja jambo hili ningeweza nikalizungumza kwenye sekta ya ujenzi na kama alivyosema rafiki yangu Mheshimiwa Mgimwa pale, Waziri Mkuu ndiyo Kiranja wa Mawaziri wote, nataka nimpe angalizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi hii barabara ndefu kuliko zote ambayo haijajengwa kwa miaka 20 ni barabara inayoitwa Kigoma – Kasulu – Kibondo - Nyakanazi. Naomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati umefika barabara hii sasa ipewe kipaumbele. Kwa mfano, barabara hii ya Iringa - Dodoma imekuja sasa wakati barabara ya Nyakanazi ilikuwepo haijamalizika. Barabara ya Dar es Salaam - Mtwara imekuja sasa wakati barabara hii ya Nyakanazi - Kigoma haijakamilika. Barabara ya Singida - Minjingu imekuja sasa wakati barabara ya Kigoma - Nyakanazi bado haijajengwa kwa lami. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua mahitaji ya barabara ni muhimu sana katika nchi yetu, lakini barabara hii ndefu kuliko zote ambayo imesanifiwa miaka 20 iliyopita hata vipande vyake vya Kasulu - Kidahwe na Kabingo - Nyakanazi bado havijakamilika, wakandarasi wanadai fedha zao. Nimekuwa nikishangaa kupitia Wizara ya Ujenzi, wakandarasi hao walioko site kila wakiomba fedha zao wanalipwa kidogo kidogo na barabara hizi zimechukua muda mrefu sana takribani miaka 20 barabara haimaliziki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ipo hapa inasikia, tunaomba barabara hii ipewe kipaumbele vinginevyo tutachukua hatua ambazo hazipendezi sana kwa sababu hatuwezi kuona kabisa keki ya Taifa inagawiwa kwa ubaguzi wa dhahiri kabisa, kwa maana kwamba kuna maeneo mengine yanapewa kipaumbele na kujengewa barabara za lami na maeneo mengine yanaambiwa yasubiri.
Tumesubiri…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ndassa umerudi, jiandae Mheshimiwa Chuachua.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wangu bado.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Nianze kwa kuwapa hongera Profesa na timu yake, Makatibu wake Wakuu, Engineer Nyamuhanga, Injinia Chamuriho na Injinia Sasabo kwa kazi nzuri. Vilevile niwape hongera Naibu wake wawili, Engineer Nditiye na Mhasibu na mbobezi ndugu yangu Mheshimiwa Kwandikwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache tu kwa sababu hii ni Kamati yangu, mambo mengi tumeshazungumza kwenye Kamati. Nianze na barabara ya Kidahwe – Kasulu – Nyakanazi. Nimkumbushe Mheshimiwa Waziri tu kwamba barabara hii ina miaka 26 tangu imefanyiwa upembuzi yakinifu na detail design, barabara haijengwi. Kwa taarifa tu ni kwamba ndiyo barabara ndefu ambayo haijawa paved for the last 26 years, ni barabara sasa ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo – Kabingo - Nyakanazi. Najua ziko juhudi zinazofanyika lakini quick match ndiyo tunayoitaka kuliko hii slow match.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa barabara hizi mbili za Kabingo -Nyakanazi na Kidahwe - Kasulu kwa kweli tunaomba zimekaa sana, zina miaka tisa sasa, hawa wakandarasi wanadai fedha wamalize zile barabara. Mheshimiwa Waziri haiingi akilini mkandarasi anadai shilingi bilioni 11 analipwa shilingi bilioni moja analipa diesel tu basi kazi inasimama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, on a serious note nimshauri Mheshimiwa Waziri na timu yake, wafanye inventory ya barabara hizi, zile barabara ambazo zilianza na zina wakandarasi zikamilike kwanza kuliko barabara zilizoanza hazikamiliki, zinakuja barabara za katikati zinakamilika, hatuna sababu ya kuzitaja hapa kwa sababu kila mmoja anahitaji barabara. Naomba sana Mawaziri wapo hapo wafanye inventory ya barabara hizi, barabara zilizoanza zenye wakandarasi zikamilike ili tupige hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa 227 unazungumzia habari ya kitu kinachoitwa Lake Tanganyika Roads under Lake Tanganyika Transport Program. Sasa Lake Tanganyika ni mikoa mitatu tu Mkoa wa Kigoma, Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Rukwa. Napenda watakapokuja kuhitimisha tujue ni barabara zipi hizi ambazo zimetengewa shilingi milioni 200 kwenye bajeti hii, ukurasa 227. Tusije tukawa tunazungumza barabara kumbe ni ya kwenda Chaguru au barabara ya Ilagala kwenda Kalya kumbe iko chini ya programu nyingine ambayo wanaita Lake Tanganyika Roads Program.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda niliseme na hili limenishangaza kidogo, nadhani wenzangu kwenye Kamati watakubaliana na mimi tulijadili sana, ujenzi wa hii reli ya standard gauge. Naona zimetengwa shilingi bilioni 100 kuanzia Isaka kwenda Rusumo, hiyo inatoka wapi? Nilidhani hoja ya sasa ingekuwa ni kuanzia Makotopora kwenda Tabora ili hatimaye reli hiyo iwe na maana ya kiuchumi uliokusudiwa. Sasa hii hoja ya kuanzia Isaka kwenda Rusumo eti kwa sababu mnajenga na Rwanda maana yake nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie vipaumbele vyetu na kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati yetu tunataka reli hii iwe na manufaa zaidi kwa Watanzania kuliko majirani. Majirani watanufaika baada ya kuwa Watanzania tumeanza kunufaika zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niweke msisitizo, reli hii jina lake ni Dar es Salaam – Kigoma, ndiyo reli ya kati na ndiyo tafsiri yake. Sijui kwa nini tafsiri hii imekuwa ikipotoshwa na nashangaa sasa hiki kipande cha kutoka Isaka kwenda Rusumo wanakipa kipaumbele shilingi bilioni 100 wakati kipande cha Tabora – Dodoma bado. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nishukuru ujenzi wa uwanja wa ndege, jengo la abiria, nimeona shilingi bilioni mbili kwenye kitabu cha hotuba ya Waziri. Napenda atakapokuja kuhitimisha hoja yake maeneo mengine ameeleza status mkandarasi amepatikana, lakini sisi imetengwa shilingi bilioni 2.3 lakini hawaelezi status ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma ambao naona ni jengo la abiria na maingiliano yake. Kwa hiyo, napenda atakapokuja kuhitimisha Waziri atueleze status ya ujenzi wa kiwanja hicho umefikia wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni mawasiliano. Tumeshapeleka kwa Mheshimiwa Waziri orodha ya vijiji ambavyo havina minara, sasa huu mwezi wa nne. Tunataka tuone minara inajengwa, nadhani ndiyo hoja ya sasa. Hatuwezi kuzungumzia habari ya mawasiliano wakati maeneo mengine hayana mawasiliano.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Nianze kwa kuunga mkono hoja hii lakini nitakuwa na mambo ya ushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais ambaye ameondoa tatizo la miaka 20 kwenye Msitu wa Makere Kusini, maarufu kama Kagera Nkanda. Tatizo limekwisha, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais alikuja na ameliondoa tatizo lile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoomba Mheshimiwa Waziri mipaka mipya imewekwa, eneo ambalo Mheshimiwa Rais amelitoa kwa wakulima wa Wilaya ya Kasulu linajulikana, tunaomba askari wa wanyamapori waheshimu mipaka iliyowekwa sasa. Eneo lile hatukupewa na Wizara kwa sababu Wizara kwa miaka 20 imeshindwa, tumepewa na Mheshimiwa Rais. Kwa kweli, alipotutembelea nilimnong’oneza jambo hilo akalielewa. Sifa ya Mzee yule jambo akilielewa na akaliamini anatoa uamuzi. Kwa hiyo, tunaomba sana mipaka mipya sasa iheshimiwe ili Kagera Nkanda watu waishi kwa amani na wafanye shughuli zao za kilimo bila usumbufu wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hilo la shukrani kwa Mheshimiwa Rais, nina jambo ningetaka AG anisikilize. Hili jambo nataka nili-address kwa AG kwa sababu ndiyo Mshauri wa Mambo ya Sheria katika Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hotuba hizi, hii ya Wizara na hotuba ya Kamati ni mbingu na ardhi, ni vitu viwili tofauti. Wenzetu hawa wamekuja na mambo mahsusi ambayo ni lazima yafanyike kuboresha tasnia ya uhifadhi na utalii lakini hapa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri hakuna mkakati mahsusi unaoonekana humu ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hilo kwa AG na more serious ukurasa wa 16 na 17, hawa Wabunge wenzetu 24 ambao wamechambua bajeti hii, Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa AG, wameeleza vifungu ambavyo vimekosewa kisheria na matamko ambayo yanaathiri tasnia ya uwindaji.

Labda ni-declare interest, mwaka 2013 nilikuwa kwenye Kamati ya Kumshauri Waziri juu ya Ugawaji wa Vitalu hivi, nimetembea mapori yote najua kinachoendelea huko na tulitoa mapendekezo. Sasa Mheshimiwa AG nakuja, sheria zimevunjwa, hivi sheria ikivunjwa maana yake ni nini? Ndiyo hoja yangu. Mheshimiwa Mwenyekiti na wewe ni Mwanasheria utanisadia, sheria imevunjwa maana yake ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa Wabunge 24 wanasema, labda nisome, ‘Kamati inaitaka Serikali kurejesha utulivu katika tasnia hii ya uwindaji na kuondoa au kuhuisha barua yake ya ugawaji wa vitalu ya tarehe 16 Januari, 2017’. Hii tasnia tunaiua wenyewe kwa sababu Waziri wewe huna powers za kukiuka sheria. Nashangaa Wizara hii ina watu makini sana, una Katibu Mkuu makini sana, vipi mnavunja sheria? Hawa wawekezaji kwenye tasnia ya uwindaji wa kitaalii mnawauwa, mnawa-frustrate, hawafanyi kazi na wamewekeza fedha nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli on a serious note napenda AG kwa kweli alieleze Bunge hili sheria ikikiukwa katika misingi kama hii na Wabunge 24 hawa wanasema aaah, hii haiko sawa. Maana yake ni wawili au Mheshimiwa Waziri aje hapa aseme jamani ile barua ya tarehe 16 nakwenda kuifuta kwa sababu haiko kisheria ili wawekezaji wale wawe na amani katika tasnia ya uwindaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa tu, tasnia hii ya uwindaji ni muhimu sana na inatuingizia fedha nyingi sana. Nimeshuhudia jambo hili tena wakati huo tunafanya kazi na TRA hata baadhi ya watu waliokuwa hawalipi kodi tulishauri sana watu wale wafuatiliwe walipe kodi. Mheshimiwa Waziri tunakuomba sana, alisema Mheshimiwa Msigwa asubuhi umeanza kutulia, muendelee kutulia, tasnia hii ni muhimu sana sana, sana. Hawa wawekezaji hawa wana maslahi ya kulinda na tunawahitaji tupate fedha. Ni muhimu sana Mheshimiwa Waziri jambo hilo lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hilo la uvunjaji wa sheria na unaweza ukaiona katika ukurasa 16 na 17 wa kitabu cha Kamati halafu Wizara kwenye hotuba ukurasa wa 18. Tena Mheshimiwa Waziri mwenye anakiri anasema kwa kutambua umuhimu wa tasnia hii ya uwindaji wa kitalii na kukuza uchumi wa nchi yetu, Wizara kupitia TAWA inaendelea kurekebisha muundo na utaratibu wa kugawa vitalu vya uwindaji. Hatua hiyo inahitaji mabadiliko ya Sheria ya Wanyamapori ambayo inafanyiwa kazi, Waziri mwenyewe amekiri hapa bado inafanyiwa kazi. Sasa mnatoaje matamko ambayo yanawa-frustrate wawekezaji? Hiyo pesa ya kigeni tunapata wapi? Ni mambo ambayo lazima tuyaangalie haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda nilizungumzie ni promotion drive ya Mbuga za Gombe, Mahale na Katavi kwa sababu ya corridor ile moja. Mheshimiwa Waziri humu sioni kabisa hata sentensi moja inazungumzia habari ya promotion drive ya Gombe na Mahale. Nimeona Katavi kidogo lakini Gombe na Mahale sioni. Mbuga hizi ni unique sana, ziko kwenye mwambao wa Ziwa Tanzanganyika. Ni mbuga ambazo ni tofauti na Serengeti na Ngorongoro, ni unique. Ningeshauri strongly Mheshimiwa Waziri na wataalam muwe na mkakati mahsusi wa corridor ile ya Katavi, Mahale na Gombe National Parks, ni utalii mzuri sana. Hata wataalam wengi wa sayansi wanakwenda sana kwenye maeneo yale kwa ajili ya scientific research ambazo nazo zinatuingizia fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingineambalo napenda niliseme, uhifadhi unahitaji mito. Ukizungumza Ruaha National Parks unazungumzia Mto Ruaha, ukizungumzia Gombe, Mahale, Kigosi, Moyowosi unazungumzia Mto Malagarasi. Ukizungumzia habari ya Kilombero, Serengeti unazungumzia Grumeti, ukizungumza habari ya Ugara Game Controlled Area unazungumzia Mto Ugara. Nashauri, Serikali ni moja, Wizara mkae pamoja Waziri wa Maliasili na Utalii, Waziri wa Maji na Waziri wa Mazingira, mje na strategy ya pamoja kulinda mito hii. Hii mito Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla isipokuwepo hakuna uhifadhi.

Hawa wanyama wote watatoweka. Naomba hilo mlichukue muweze kuwa na strategy ya pamoja kuweza kulinda mito mikubwa hii ambayo hakika ndiyo inalisha kwenye National Parks zetu, Games Controlled Areas na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni ushauri tulioutoa mwaka 2013 ambao unazungumzia mapori ambayo yamekosa sifa ya uhifadhi kupewa wafugaji. Hilo tumelizungumza tangu 2013 leo ni 2018 na mapori hayo yapo mengi. Kwa mfano, open area ya Wembere mnaiweka ya kazi gani wapeni wafugaji wafugie mifugo yao pale. Ile hifadhi Mheshimiwa Waziri imeshapoteza sifa ya uhifadhi tangu mwaka 2013. Yako maeneo mengi huko Ruafi katika Mkoa wa Katavi hata maeneo ya Kigosi Moyowosi ukiacha Njingwe 1 na Njingwe II maeneo mengine yote yameshakosa sifa za uhifadhi ni vema maeneo hayo wapewe wafugaji wayatumie kwa sheria ambazo zitakuwa zimewekwa ili mambo yaweze kwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa ni suala la Ngorongoro. Hivi Ngorongoro tunaitaka kweli Mheshimiwa Waziri. Huu mgogoro wa Loliondo hauishi. Nilimsikia Mbunge wa Arusha anazungumzia habari ya kumalizika mgogoro wa Loliondo haujaisha ule bado unaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo kubwa kabisa kuliko yote ni co-existence ya wafugaji wa Kimasai wale na wildlife, hivi vitu haviwezi kwenda pamoja mazingira yamebadilika. Zamani zile walikuwa Wamasai 8,000 tu leo hii Loliondo wako Wamasai maelfu kwa maelfu. Ile ikolojia haiwezi ku-sustain tena, tutapoteza Ngorongoro kama hatua mahsusi hazitachukuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tumekwenda Ngorongoro pale …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa namna ya pekee niunge mkono hoja hii na mapendekezo ya Waziri wa Fedha. Hata hivyo, naomba niwape hongera nyingi sana Waziri wa Fedha na timu yake kwa kazi nzuri wanayoifanya na hasa sera hizi za kodi za kuja na mkakati wa kulinda viwanda vya ndani na kuchochea uwekezaji katika Taifa letu, hilo ni jambo jema, hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba pia kuwapa hongera sana wenzetu wa TRA kwa kubadilisha mtazamo (attitudes), wameanza kuwa tax friendly kwa walipa kodi. Ni kitu chema sana na Ndugu Kichere na wenzake hongereni kwa kazi nzuri, songeni mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hili la mfumo mpya wa stempu za kodi za kielektroniki. Kwanza ni jambo jema, kama alivyosema ndugu yangu yule wa Kwimba na Mheshimiwa Waziri nadhani cha msingi hapa hebu rudini kwenye meza tena muangalie hizo economics zake, haya yanayozungumzwa yana ukweli kiasi gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia ni vyema Watanzania tusiogope mambo mapya. Mzee Dkt. Kikwete aliwahi kutueleza hapa kwamba ili ule lazima uliwe. Kwa hiyo, utaratibu huo wa stempu za kielectroniki uendelee lakini nimwombe tu Waziri wa Fedha na wenzake, warudi kwenye meza ya mazungumzo (drawing board) waangalie economics zake hizo. Hicho kinachosemwa kwamba watatupiga sana ni kitu cha kweli ili wajiridhishe na jambo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina ushauri katika suala hili la mifumo ya kutoza kodi. Wakati kampuni hiyo inafanya kazi hizi mngeifungamanisha na kampuni ya Kitanzania, hii Kampuni ya Maxicom Africa, hawa ni Watanzania, ni Waafrika wanaofanya kazi nzuri. Wamekubalika Uganda, Zambia, Rwanda na Kenya kwa washindani wetu wakubwa wa kibiashara. Kwa hiyo, ingekuwa jambo jema kwa miaka hii mitano muwafungamanishe na hii local company ili baadaye kazi hii iweze kufanywa na kampuni ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nitakuwa na machache tu. Jambo ambalo napenda niliseme ni nidhamu ya kibajeti. Pamoja na mambo mazuri haya ambayo yamekuja kwenye bajeti hii ambayo ameyaainisha na mengine akayazungumza hata kwenye hali ya uchumi, nizungumzie nidhamu ya utekelezaji wa bajeti, hili ni jambo kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 29 Mheshimiwa Waziri mwenyewe amebainisha kwamba kipaumbele kitakuwa ni ukamilishaji wa miradi inayoendelea. Sasa nimwombe sana miradi mipya isimame kwanza tukamilishe miradi ya kielelezo ambayo imekwama ili tuwe na
consistency.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini siyo hilo tu, kwenye hotuba pia ameainisha juu ya Waraka wa Hazina Na. 01 wa mwaka 2018/2019 ambapo anawaagiza Maafisa Masuuli wote watenge fedha za kutosha kwenye miradi inayoendelea. Narudia tena, miradi inayoendelea kabla ya kuanza mingine mipya. Sasa ipo miradi tunaijua ya kielelezo, miradi ya kipaumbele tangu bajeti ya mwaka jana, hiyo miradi haijakamilika. Moja ya miradi hiyo muhimu ni miradi hii ya barabara ya kuunganisha mkoa na mkoa mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika nchi yetu mikoa ambayo haijaunganishwa kati ya mkoa mmoja na mwingine ni pamoja na Mkoa wa Kigoma. Mkoa wa Kigoma haujaunganishwa na Tabora, Katavi, Mwanza wala Shinyanga. Niombe sana kupitia Waraka Na. 01 aliouainisha Waziri kwenye hotuba yake katika ukurasa wa 29 basi miradi hii ambayo ina wakandarasi tayari kwenye maeneo mbalimbali ipewe kipaumbele na fedha ili ikamilike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimkumbushe Mheshimiwa Waziri barabara muhimu sana katika nchi hii inayoitwa ya Kigoma – Kidahwe – Nyakanazi, hiyo ni barabara ya kielelezo imekaa miaka 20, bajeti zinakuja zinatoka barabara hii haijakamilika. Nimwombe Mheshimiwa Waziri naye aache legacy sasa kwamba barabara hii muhimu na kubwa katika nchi yetu inayotoka Kigoma - Nyakanazi haijakamilika. Nashauri Waziri akae na TANROADS na Katibu Mkuu wa Hazina, barabara hii ipewe fedha kwa sababu ni muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo napenda nilizungumze ni umeme. Umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya viwanda na hata hizi juhudi zinazofanywa za kujenga Stiegler’s Gorge maana yake umeme huu utaingizwa kwenye Gridi ya Taifa. Mimi nataka nimkumbushe Waziri kuna mikoa iko off grid na inahitaji kuendelea kiviwanda na moja ya mikoa hiyo ni pamoja na Mikoa wa Kigoma na Katavi. Napenda sana Mheshimiwa Waziri atakapokuja atueleze ule mkakati ambao Waziri wa Fedha mwenyewe alikwenda Korea kusaini pesa kwa ajili ya kitu kinachoitwa North West Grid, umeishia wapi? Kwa mradi ule Mikoa ya Geita, Kigoma, Katavi na Rukwa ingeunganishwa kwa Gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya hayo, sisi ambao tuko off grid kuna Mradi mkubwa wa Kielelezo wa Malagarasi Hydro Power ambao una uwezo wa kuzalisha megawati 45. Naomba nimueleze Mheshimiwa Waziri wa Fedha, mradi huu ni muhimu sana na hii mikoa ambayo sisi tuko off grid lazima tupate treatment sawasawa kama mikoa ambayo ipo kwenye Gridi ya Taifa. Haiingii akilini mikoa ambayo ipo kwenye Gridi ya Taifa inanufaika na umeme mwingi wa kiviwanda lakini kuna mikoa ipo off grid. Bahati nzuri sana sisi Mkoa wa Kigoma tuna umeme wetu huu wa Malagarasi wa megawati 45.4, nina uhakika umeme huu utasaidia sana pia kuchochea maendeleo ya viwanda katika Mkoa wa Kigoma na maeneo ya jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naomba nizungumzie uimarishaji wa ushirikiano na washirika wa maendeleo. Liko jambo ambalo ningependa Mheshimiwa Waziri atueleze, washirika wa maendeleo, Jumuiya ya Nchi za Ulaya, USAID na World Bank wana malalamiko makubwa na wamekuja kwenye Kamati zetu kutueleza kwamba Serikali mpaka tarehe 12 Juni kulikuwa na fedha shilingi bilioni 700 ambazo ni sawa na USD milioni 300, Serikali imeshindwa kusaini MoU. Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ni kitu gani hiki? Naomba aje atueleze tatizo liko wapi? Mfumo wa majadiliano ni wa kimkakati, kisera na kisiasa, zungumzeni na watu hawa tupate fedha hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, naunga mkono hoja lakini Waziri aje atueleze juu ya jambo hili muhimu sana, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Natumaini nina dakika kumi leo. Nami kama walivyosema Waheshimiwa Wabunge wenzangu nianze kwa kuwapongeza sana wenzetu katika Wizara hii muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nikiitazama TAMISEMI kama Serikali ndani ya Serikali yenyewe. Mheshimiwa Jafo na timu yake hongera sana kwa kazi nzuri, yeye na Naibu Mawaziri wake, Katibu Mkuu wake, Alhaji Iyombe, wanafanya kazi nzuri sana na Naibu Makatibu Wakuu, mama Zainab na Naibu mwingine anayeshughulikia masuala ya elimu, hongera sana kwa kazi nzuri na kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nianze haraka haraka na hili la hili la takwimu. Ukiangalia hotuba ya Mheshimiwa Jafo ukurasa wa 58, anazungumzia habari ya program ya kuijengea uwezo miji 18, ameitaja pale. Katika ile miji 18 aliyoitaja sikuona Mji wa Kasulu kwa sababu baadhi ya miji aliyoitaja imesajiliwa sanjari na Miji wa Kasulu na Mji wa Kasulu ni mji wa siku nyingi sana. Kwa hiyo, naomba sana katika kumbukumbu zao waweke Mji wa Kasulu katika program ile kwa sababu miji ambayo imesajiliwa pamoja na Mji wa Kasulu wameiainisha pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 59, Mheshimiwa Jafo amezungumzia juu ya kitu kinachoitwa program ya kuendeleza miji 18; bahati nzuri ile miji hakuitaja na amezungumzia habari ya kuboresha na kupanga na uandaaji wa mipango ya master plan katika miji. Ni kweli jambo la kupanga miji yetu ni jambo la msingi sana ili miji yetu isiharibike. Sasa ile miji hakuitaja pale, sasa sikuelewa kama hiyo miji ndiyo ile miji 18 au ni miji mingine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa 115, ameendelea kusisitiza juu ya program ya ujenzi wa barabara za kuimarisha miji 18. Sasa hoja yangu iko hivi; ukurasa wa 58 anazungumza miji 18, ukurasa wa 59 anazungumza miji 18, ukurasa 115 anazungumza miji 18. Sasa nataka kujua ni miji ipi hiyo? Ni hiyo hiyo? Kama miji ni hiyohiyo pengine wanatumia criteria gani kwamba mji huu tunaupanga na mji huu tunauboresha na huu mji tunajenga barabara zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kabisa kwamba hoja hii inahusu halmashauri za miji na si halmashauri za vijiji; na pale ukurasa wa 59 amekiri kwamba takribani billioni tisini na moja zitatumika kwa kazi hiyo. Sasa naomba sana; Mji wa Kasulu ni mji wa siku nyingi uko mpakani mwa nchi yetu na ni mji uliosajiliwa tangu mwaka 1974, ni mji wa siku nyingi sana; usiachwe kuingizwa kwenye Town Authority ambayo imefanywa sanjari na miji mingine kama Bariadi, Geita na Korogwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba sana, ule ni mjini wa siku nyingi, naomba watuingize kwenye program na hasa hizi program mbili, hii ya kupanga miji (master plans) na hii ya kuboresha miji, kwa maana ya kujenga barabara za mijini. Hilo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nijielekeze alikoishia rafiki yangu huyu, kuhusu hoja ya Walimu. Nichukue line kwamba kwa Walimu lipo tatizo kubwa la msingi, wana madai mengi sana. Labda nitoe mfano, Walimu wa shule ya msingi katika Mji wa Kasulu wanadai malimbikizo yao tangu Juni, 2016, shilingi milioni mia tatu tisini na sita, almost milioni mia nne, hawajalipwa. Fedha za likizo, masomo, matibabu, uhamisho, kujikimu na kadhalika. Kama alivyosema ndugu yangu Ryoba pale, hawa Walimu wanakuwa hawana incentive jamani, matokeo yake ni lazima elimu itashuka tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa najaribu kuangalia ile hoja aliyokuwa anaijenga Rais wetu Mstaafu Mzee Mkapa ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu elimu, lakini yako mambo hata kabla ya mjadala huo tunaweza tukaanza nayo. Huwezi kuwa na Mwalimu anadai matibabu yake tangu Juni, 2016 hajalipwa, hiyo ni kwa msingi.

Mheshimiwa Spika, ukija sekondari kwa sekondari zilizopo katika Mji wa Kasulu wana madai yao ya shilingi bilioni sabini, hawajalipwa hawa. Kama anavyosema mwalimu aliyetangulia hapa, kuna Walimu wa sayansi humu hawana incentives hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nafikiri, nadhani Mheshimiwa Kakunda ndiye anayeshughulikia sekta hii, kuna mambo ambayo wanaweza wakayafanya sasa ambayo nina hakika kama Walimu wakilipwa mafao ambayo ni stahili zao nina hakika kabisa suala zima hili la elimu tunaweza tukapiga hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, pamoja na shida zote hizi niwapongeze sana Walimu nchini, niwapongeze Walimu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, wanafanya kazi kubwa sana katika mazingira magumu. Nafikiri wakati umefika kabisa Waheshimiwa Mawaziri wote wawili, wa Utumishi na TAMISEMI kwa kweli kuangalia namna ya kuwapa incentives watu hawa, wanafanya kazi kubwa iliyotukuka. Watu hawa kwa kweli ndio wanaolea Taifa letu pamoja na mazingira yote magumu wanayokumbana nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu ambalo ningependa niliseme ni kuhusu suala la afya. Nakushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja Kasulu na bahati nzuri alinikuta tukamtembeza, tunamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri Kandege. Ushauri wake tuliuzingatia na kile Kituo cha Afya alichokitembelea cha Kiganamo kinakaribia kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo nilimweleza jambo moja mahsusi kabisa, sisi katika mji ule tumepata kituo kimoja cha afya na Mji wa Kasulu una wakazi 270,000, yaani Kasulu Mjini na viunga vyake. Naomba sana. Viko vituo vya afya tumeanza kujenga katika Kata za Murufiti, Heru Juu pamoja na Muhunga, tunaomba sasa nguvu ya Serikali ijumuike na nguvu ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema kweli mimi hata Mfuko wangu wa Jimbo nimeu-surrender kwa kazi hiyo ili akinamama hawa wasipate shida kusafiri kilometa 30 mpaka 35 kufuata huduma katika maeneo ya kutolea huduma Kasulu Mjini, naomba sana.

Mheshimiwa Mwenyeketi, kuhusu sekta ya afya, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumzia masuala ya kujenga vituo vya afya; jambo jema sana, jambo lenye afya jambo lenye akili kabisa. Hata hivyo, sikuona hata sentensi moja waliyozungumzia kukarabati hospitali za wilaya kongwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ziko hospitali za siku za nyingi, kwa mfano Wilaya kama za Kasulu, Kibondo zina hospitali za siku nyingi na hizo hospital zimekuwa ndizo zinazotoa huduma kwa kweli; na zimekuwa zikitoa huduma hata kwa halmashauri za jirani ambazo hazina hospitali ambazo ndizo wanazijengea sasa hivi. Kwa mfano Hospitali ya Wilaya Kasulu ambayo ndiyo ya Mji wa Kasulu inatoa huduma Buhigwe, Kasulu DC pamoja na Uvinza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo bado ni hospitali ya siku nyingi. Nafikiri kuliko tu kutuachia ile CDG Mheshimiwa Waziri ambayo inatusaidia kwenda kurabati kuwe na program maalum kama ilivyofanyika 2009 ya kukarabati hospitali za Mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnakumbuka, Waziri wa Afya atakuwa anakumbuka na TAMISEMI watakumbuka walitoa takriban milioni mia sita kwa hospitali nyingi za mikoa kwa ajili ya ukarabati. Ziko hospitali za wilaya, nina hakika ziko wilaya nyingi ambazo zina hospitali kongwe ambazo zinahitaji ukarabati na wangekuwa na special program kwa ajili ya kazi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Waganga na Madakrati, nalo hili wangeliangalia kwa umakini sana, hasa kwa mikoa ile ambayo ni disadvantaged, mikoa ya pembezoni, mikoa yenye shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimweleze Mheshimiwa Waziri, sisi watu wa Kigoma referral hospital yetu ipo Bugando-Mwanza ukiacha ile regional hospital…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja naomba Mheshimiwa Jafo ayatilie maanani yote niliyozungumza. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali Wizara ya Maji na Umwagiliaji 2018/2019
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, na mimi kwa namna ya pekee naomba kwa kweli kuwapa hongera nyingi sana Waziri Engineer Kamwelwe, Naibu wako Waziri, Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Engineer Kalobero na Wakurugenzi wote wakiongozwa na ndugu Mafuru mnafanya kazi nzuri, hongereni sana. Mnafanya kazi katika mazingira magumu na kwa kweli ukiangalia taarifa ya Kamati na hotuba ya bajeti kwa kiwango kikubwa mmefanyia kazi zile shilingi bilioni 158 za Mfuko wa Maji ambazo zimekuwa ring fenced, hongereni sana kwa kazi nzuri ambayo mmefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa kwenye Kamati ya Maji kipindi kilichopita, najua uwekezaji mliouweka ni mkubwa sana katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam. Mmefanya kazi kubwa sana, miradi mikubwa mliyowekeza sasa muisimamie iweze kukamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze na suala la takwimu, katika ukurasa 214 na 215 kwenye skimu za umwagiliaji na katika skimu zilizoko katika Mkoa wa Kigoma kuna skimu moja muhimu sana hamkuiweka pale, nafikiri ni oversight, Skimu ya Maji ya Msambala ni muhimu sana pale na iko katika Mji wa Kasulu. Ninaomba kwenye kumbukumbu zenu muiweke sikuiona humu na inawezekana katika mfumo wa kibajeti na yenyewe mkawa mmeisahau, nilikuwa nakumbusha tu jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, nianze na fedha za India, miradi ya miji 17 ambayo umeitaja kwenye kitabu chako. Naomba Mheshimiwa Waziri najua juhudi zinakwenda, Serikali imeshapiga hatua kubwa kuhusu fedha za mkopo kutoka Serikali ya India kwa miji ile 17 na miji hiyo 17 ni pamoja na Mji wa Kasulu. Kwenye kitabu chako hiki cha hotuba umeeleza kwamba, itakwenda kwa phases, kuna phase one Zanzibar na miji mingine mitatu/minne, halafu phase two na miji mingine iliyobaki. Sasa sikuelewa logic kama mradi wa maji unatekelezwa Zanzibar au unatekelezwa Njombe unazuia vipi mradi wa Kasulu usitekelezwe?

Mheshimiwa Spika, sikuelewa logic sikuiona hata kidogo, kwa hiyo nilikuwa nafikiri good practise kwa sababu hii miradi tumeisubiri muda mrefu na itakuwa na fedha za kutosha, hii miradi ingeanza simultaneously. Kama unatekelezwa Zanzibar, unatekelezwa Makambako na utekelezwe na Kasulu kwa wakati huo huo kwa sababu wahandisi tunao wa kutosha wa kufanya kazi hii. Sikuona logic ya kuanza kuweka kwa phase kwamba hii ni phase one na phase two, maana kwa tafsiri hii ni kwamba phase two sisi pamoja na Mji wa Kasulu itabidi tusubiri miaka mingine mitatu minne tungoje phase. Kwa hiyo, nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri utakapokuja hapa uweze kuliweka vizuri na wataalam wako wananisikiliza. Tunataka miradi hii, tumeisubiri sana, ianze mara moja katika maeneo yote kwa sababu kuna wakandarasi na wahandisi wengi wa kutosha. Nilifikiri nianze na jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa kulisema kwa sauti kubwa kwa kweli ni kukushukuru sana. Waziri ninakushukuru sana wewe na timu yako, mmefanya kazi kubwa sana. Katika Jimbo langu nimepokea shilingi bilioni 1.3 kwa kweli zimefanya kazi kubwa sana. Tumejenga chanzo kipya cha maji katika Mji wa Kasulu ambacho hakikuwepo katika eneo la Kimobwa, Kijiji cha Heru Juu chenye wakazi zaidi ya 15,000 sasa wanapata maji safi na salama. Kijiji cha Muhunga mradi unakwenda vizuri, tunahitaji fedha nadhani watakuwa wameshakuletea certificate ili uweze kutupa fedha nyingine kukamilisha mradi ule, kazi ni nzuri na tunawashukuru sana.

Mheshimiwa Spika, again kwenye kitabu chako hiki kuna miradi ambayo imetengewa fedha, nimeona kijiji cha Muganza, nimeona mradi wa maji Marumba unaendelea, kuna miradi Mheshimiwa Waziri ile nimekuwa nikisema sana kwenye Wizara yako, miradi ya siku nyingi, kule kwetu ilianzishwa na watu wa NORAD Water Project. Kuna miradi ya siku nyingi sana na jambo hili nimeshazungumza na hata na Katibu Mkuu wako na Ndugu Kalobero. Tuna mradi mkubwa sana wa Kijiji cha Ruhita - Kanazi ni miradi wa siku nyingi inahitaji tu kufanyiwa rehabilitation. Ninafikiri mwaka huu wa fedha ungetafuta fedha, mradi huu ni muhimu sana unahudumia vijiji vitatu kwa mara moja, unahudumia zaidi ya wakazi 50,000 katika vijiji vile. Kwa sababu system ipo ni suala la kupeleka wataalam na kuangalia namna bora ya ku-rehabilitate ili hatimaye wakazi hawa waweze kupata maji.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa nikukumbushe Mheshimiwa Waziri ni mradi wetu mkubwa wa maji unaofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji chini ya BTC. Ule ni mradi mkubwa sana kwa watu wa Kigoma, una-cover Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma, unaanzia Kigoma, Kasulu, Kibondo mpaka Kakonko. Ule mradi inaonekana umekwama na nimezungumza na RAS ananiambia tatizo kubwa ni kwamba Serikali ya Ubelgiji inataka procurement procedures zifuate Sheria ya Ubelgiji ya Procurement, haikuingia kwenye kichwa changu Mheshimiwa Waziri, wewe mwenyewe kwa juhudi zako umeshafanya mawasiliano na watu wa Kigoma, nilikuwa nafikiri kuna haja ya ku-fast track jambo hili. Ule mradi tuna uhitaji sana, fedha zipo, Waziri wa Fedha ameshasaini ile Financial Agreement tayari, kwa hiyo tuna fedha zetu kupitia Serikali ya Ubelgiji ambazo zinahitaji fast tracking na control ya aina fulani ili mradi ule uanze.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani mradi wa maji usubiri miaka miwili kufanyiwa procurement, it is just too long. Ni muda mrefu sana na wananchi hawa wanataka maji. Huu mradi wa Ubelgiji pale Kasulu Mjini ni muhimu sana kwetu kwa sababu una-cover vijiji vitatu, Vijiji vya Nyasha, Nyatale na Kijiji cha Kigondo ni vijiji vyenye wakazi wengi sana ningependa sana miradi hii Mheshimiwa Waziri ikamilike.

Mheshimiwa Spika, najua muda hautoshi nizungumzie pia suala hili la kulinda vyanzo vya maji. Hili jambo hata mwaka jana nimelisema. Nakushauri Mheshimiwa Waziri wa Maji wewe na mwenzako wa Mazingira hata Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Kigwangalla, muangalie njia nzuri ya ile mito mikubwa tuliyonayo katika nchi hii. Nimeona kwenye kitabu chako kuna mito michache ume-identify hapa ukurasa 107. Ukiangalia ukurasa wa 107 kuna mito umeitaja pale, lakini mito hiyo hamjautaja Mto Malagarasi wala hamjataja Mto Kilombero na nimeshangaa sana hata Mto Rufiji hamkuutaja nimeshangaa kidogo. Hiyo ni mito mikubwa sana, mmetaja Ruaha, Wami, Ruvu na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu naomba Serikali nzima mkae chini na muangalie namna ya kulinda mito hii mikubwa. Katika nchi hii mito mikubwa ni mito 14 tu, mito mikubwa sana. Mnahitaji kufanya kama mlivyofanya kwa Ruaha Mkuu mito hii ilindwe kwa sababu ina uhakika wa maji na pengine hii ya kufikiria kwamba maji yatatoka tu Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria pengine itakuwa si sawa sana, wakati kuna mito mikubwa 14 katika nchi hii ambayo tunaweza tukailinda. Kama Serikali mkawa na strategy kabisa ya kulinda mito hii ambayo tunataka iendelee kuwepo kwa manufaa ya vizazi vijavyo ni jambo la muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho niwakumbushe tu tulitembelea miradi mikubwa sana mmewekeza katika Jiji la Dar es Salaam. Tumetembelea Ruvu Juu, Ruvu Chini lakini unakumbuka Mheshimiwa Waziri watu wa DAWASCO na DAWASA wakati ule kabla ya hizi fikra za kuwaunganisha walikuwa na changamoto zao nyingi sana, baadhi ya miradi ilikuwa haijakamilika. Miradi ya Changanyikeni, Salasala, miradi mikubwa sana. Kujenga matenki makubwa sana kwa ajili ya kuondoa shida ya maji katika Jiji la Dar es Salaam. Nilikuwa nashauri strongly uwekezaji ule uliowekwa katika Jiji la Dar es Salaam na Mheshimiwa John Mnyika hiyo kamati ndiyo tulikuwa wote pamoja uwekezaji ni mkubwa sana umewekezwa katika miradi ile. Ilikuwa ni matumaini yangu kwamba Wizara kwa kushirikiana na DAWASCO off course na DAWASA miradi ile ni mikubwa sana ikamilike kwa wakati ili kuondoa shida ya maji kabisa katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nilikuwa namkumbusha ndugu yangu Mheshimiwa Mnyika kwamba tulikuwa naye kwenye Kamati ya Maji, hakuna uwekezaji mkubwa kama uwekezaji uliofanyika katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa namkumbusha tu. Nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Hata hivyo, naomba kwa ruhusa yako kabla sijasema ninayotaka kusema, nitoe shukrani za dhati kabisa kwako wewe mwenyewe, Katibu wa Bunge na timu yenu ya wafanyakazi wa Bunge kwa jinsi mlivyokuja kutufariji huko Kakonko. Wewe mwenyewe umesafiri kilometa 816 hadi Kakonko, tunakushukuru sana. Umeonesha mapenzi makubwa sana na kwa kweli familia inashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee pia naomba niwashukuru Wabunge wote, lakini hasa wale Wabunge 27 waliokuja Kakonko pale, tunawashukuru sana kwa kuja Kakonko, kwa kuja kutuhani.

Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako nimeagizwa pia na familia ya marehemu kwako wewe mwenyewe, mengine nitakwambia tukiwa faragha, lakini mama yake mzazi, kaka zake na mke wake wanashukuru sana, sana kwa kazi iliyofanywa na Bunge, kwa jitihada iliyofanywa na Bunge hadi kufikisha mwili wa marehemu Mheshimiwa Bilago nyumbani kwao. Tunasema ahsante sana na Mungu awape nguvu na afya tele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa niende kwa Wizara, kwanza, naunga mkono hoja hii, hoja muhimu sana. Pia niwape hongera ya kazi Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango na Naibu wake Mheshimiwa Dkt. Kijaji; Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu na timu yote ya Wizara bila kumsahau Mkurugenzi Mtendaji wa TRA wanafanya kazi nzuri, hongereni sana, mazingira haya ni mapya, wachape mwendo, tuko vizuri na wao wako vizuri. Sisi Wabunge wengi tunawapa hongera ya kazi, tunawatakia kazi njema katika mazingira haya mapya, hakuna kukata tamaa, ni kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nina machache, nina mambo matatu hivi, nitakuwa na hili la Wazabuni, nitazungumzia TRA Kasulu, nitazungumzia miradi ya PPP na mwisho kama muda utaniruhusu nitazungumzia soko la bidhaa, commodity exchange market katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na hili la malipo ya Wazabuni, nashauri sincerely hili jambo nimesoma kwenye kitabu cha Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 24 mpaka 26 amezungumzia malipo ya wazabuni. Hata hivyo, lipo tatizo kubwa kati ya madai ya Wazabuni, muda wanaotoa huduma zao, uhakiki wa madeni haya na hadi hawa watu kulipwa jamani.

Mheshimiwa Spika, hivi inawezekanaje Mzabuni analisha shule zetu za sekondari na zingine za msingi hizi za shule maalum, anawezaje kukaa anadai Serikali miezi 11? Huu uhakiki maana yake nini? Nafikiri wenzetu wa Wizara ya Fedha hii waichukue k ama changamoto, hawa suppliers wetu waki-supply, nitoe mfano tu mdogo, kwa sababu kuna wapiga kura wangu walitoka Kasulu, Buhigwe na Kibondo kuja hapa na nikakutana nao; wanadai TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, Katibu Mkuu wa TAMISEMI amewaandikia Hazina madai mbalimbali ambayo yameshahakikiwa. Madai hasa hasa ya Wazabuni wa elimu na wiki jana hiyo barua mwenyewe nimebahatika kuiona kwa sababu ilikuwa ni pressure kubwa sana. Inawezekanaje Mzabuni adai Serikali miezi 11. Naomba sana kupitia Wizara hii na wenzake Serikalini, warekebishe utaratibu, kweli wafanye uhakiki, tujiridhishe kwamba madeni haya ni halali, lakini Wazabuni wenye madeni halali walipwe kwa wakati jamani. Inachukua muda mrefu sana, sana.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano katika Jimbo langu la Kasulu peke yake Wazabuni wanayodai elimu, wanadai elimu zaidi ya shilingi milioni 500 na wamesubiri zaidi ya miezi kumi na kwa bahati nzuri kile kitabu cha madai mwenyewe nimekiona. Naomba sana wenzetu wa elimu mjaribu ku-fast track, wafanye uhakiki kweli, tujiridhishe na madeni, lakini hatimaye madeni haya yalipwe.

Mheshimiwa Spika, halikadhalika madeni ya Mawakala wa mbolea. Hilo limekuwa sasa ni kizungumkuti. Mawakala hawa tangu niko Kamati ya Kilimo miaka miwli iliyopita tuliletewa orodha na orodha ilikuwa inahakikiwa basi tuombe Mheshimiwa Waziri wale ambao wameridhika kwamba wana madai halali ya pembejeo walipwe basi fedha zao.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nazungumzia juu ya hawa wazabuni ambao wame-supply mbolea. Nakumbuka tangu kwenye Kamati ya Kilimo limejadiliwa jambo hili na Waziri wa alituletea orodha ya wanaodai, lakini kukawa kwamba linafanyiwa uhakiki. Ni jambo jema, lazima tujue nani hasa tunamlipa, lakini wale waliohakikiwa tafadhali sana, wale ambao wamejiridhisha kwamba hawa ni wadai halali walipwe fedha zao, muda umekuwa mwingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii sintofahamu ya Mabenki kuwatisha, kuuza mali zao, nadhani haijengi heshima ya Serikali, nina uhakika wala hata haijengi heshima ya Chama cha Mapinduzi. Naomba sana, wazabuni halali walio-supply huduma ya pembejeo na kadhalika walipwe baada ya kuwa wamefanya uhakiki na kuwe na timeframe kwamba wazabuni hao wanalipwa kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, la pili, ni jambo kidogo ambalo liko local, sisi Mkoa wa Kigoma, Wilaya ya Kibondo na Kakonko, Wilaya ya Kasulu na Buhigwe hatuna ofisi za TRA. Naomba kupitia kwa Mheshimiwa Waziri sina uhakika kama anaijua Buhigwe, Kasulu na Kibondo iliko sina uhakika. Haiwezekani TRA waendelee kukaa kwenye vijumba vya kupanga panga…

SPIKA: Mheshimiwa Nsanzugwanko huna uhakika kama Mheshimiwa Waziri anapajua Buhigwe?

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, eehhh! Maana yake angekuwa anapajua pengine angekuwa ameshajenga Ofisi ya TRA, ndivyo ninavyofikiri hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sana watujengee Ofisi za TRA angalau wenzetu wa Wilaya ya Kakonko na Kibondo wanaweza kuwa na TRA moja pale Kibondo wakai-share na sisi Kasulu na Buhigwe tukawa pia na Ofisi ya TRA.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri anajua sisi Halmashauri ya Mji wa Kasulu tumeshatoa Kiwanja bure kwa ajili ya kujenga Ofisi za TRA. Sasa kile kiwanja kinakuwa chaka, kinakuwa pori, ningeshauri sana kupitia yeye na Mkurugenzi Mtendaji wa TRA nadhani ananisikia hapa watujengee Ofisi ya kisasa ya TRA. Mji wa Kasulu na Mji wa Kibondo ni miji inayokua kwa haraka sana, inahitaji huduma za kibiashara.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, ambalo napenda nilisemee ni hii miradi ya PPP; nimesoma kwenye kitabu cha bajeti, umezungumzia PPP karibu kurasa tatu, lakini katika maelezo ya Waziri haoneshi exactly ni mradi gani wa PPP ambao Serikali ume-finalize sasa unatekelezwa hakuna hata mmoja, ni maelezo tu.

Mheshimiwa Spika, Sheria ya PPP tangu tumeitunga ndani ya Bunge hili ni zaidi ya miaka 10 sasa. Sasa ningependa pengine Waziri atakapokuja atueleze ni miradi ipi hasa wamei-finalize ya PPP ambayo inakwenda kutekelezwa na pengine ikibidi pia waitofautishe kati ya miradi ya huduma na miradi ya uzalishaji. Nawiwa sana hii PPP tungejielekeza kwenye miradi ya kilimo na ufugaji maeneo ambayo tuna uhakika yatazalisha fedha ili tuweze kupata fedha zingine.

Mheshimiwa Spika, la mwisho ambalo ningependa nilisemee, ni hii commodity exchange market. Waziri ameileza sana ukurasa wa 63 mpaka ukurasa wa 65, hili ni jambo geni. Kwanza ningeomba kupitia kwako pengine Wabunge wote tungepitishwa kwenye somo hili, hii stock exchange ni kitu gani? Kuna maelezo mengi sana pale na baadhi ya Makampuni ambayo yamekuwa registered kwa ajili ya kuhudumia hii commodity exchange.

Mheshimiwa Spika, ni vyema Wabunge wenyewe tungepata semina kubwa tukaelewa maana ya jambo hili. Ni jambo kubwa sana na nchi zingine zinatumia jambo hili kwa ufanisi mkubwa sana, lakini hapa bado ni kitu kipya, sisi wenyewe Wabunge hatukielewi vizuri, ningeshauri kupitia kwako tuwe na semina ya Bunge zima kuhusu hiki kitu kinachoitwa commodity exchange market. Ni kitu muhimu sana, lakini sina uhakika kama kinafahamika vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, kwa sababu Wizara hii ya fedha ndiyo wanagawa rasilimali fedha, naomba niendelee kuwakumbusha na hili nitalisema sana hata kwenye bajeti kuu, miradi ile ambayo tumeshaanza nayo itekelezwe, ikamilike.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nyakanazi ile uliyopita kutoka Airport mpaka Kakonko ndiyo inaitwa barabara ya Nyakanazi, umeiona, hipitiki. Sasa kwa sababu nakumbuka tangu mwaka jana ni moja ya miradi ya vielelezo.

Miradi ya vielelezo naomba itekelezwe.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja hii.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, I hope nina dakika 10?

MWENYEKITI: Wewe sema ukichoka utaniambia. (Kicheko)

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Sawa, nilitaka kuwa na uhakika nisikukwaze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwanza niwape hongera sana wenzetu wa Serikali hususani Wizara hii ya Miundombinu ambayo ni Wizara kubwa, niwape hongera Waziri, Naibu Mawaziri na watendaji wake wote kwenye Wizara hiyo. Kazi ni nzuri mnayoifanya lakini bado naamini wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitajikita kwenye mambo machache sana, la kwanza nianze na Wizara hii ya Miundombinu. Hii Wizara ni Wizara kubwa sana, hii ni Wizara ambayo ina taasisi zaidi ya 120, ni taasisi ambayo inasimamia mambo muhimu sana, na kusema kweli ni taasisi ambayo ndiyo kama mishipa ya damu kwenye uchumi wetu. Ukizungumza barabara ipo miundombinu, ukizungumza reli ipo miundombinu, bandari, mawasiliano, viwanja vya ndege, posta na simu, majengo, vivuko nchini, hali ya hewa na kadhalika bado yote haya yako chini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niombe wenzetu wa Serikali mko hapa, hii Wizara ni kubwa sana. Pamoja na uwezo mkubwa walio nao Waheshimiwa Waziri na Naibu Mawaziri wa Wizara hii na Makatibu wao Wakuu bado ni jambo jema kama Mheshimiwa Rais ikimpendeza Mheshimiwa Rais Magufuli afanye kama tulivyoshauri kwenye Wizara ya Kilimo na Mifugo na kama alivyofanya kwenye Wizara ya Biashara na Viwanda. Aitenganishe Wizara hii ili kuwe na Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu Wizara hii ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa maoni yangu ni kwamba inafika mahali hata watendaji wanakuwa hawawezi kufuatilia mambo yote katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niende kwenye jambo mahususi, hilo lilikuwa la jumla sana, nalo ni hili la ujenzi wa reli. Tunajenga reli ya Standard Gauge, jambo jema sana kwa uchumi wa nchi yetu; lakini niombe sana wenzetu na Mheshimiwa Waziri wa Fedha huko hapa, pendekezo lililopo ukurasa wa 31 ni pendekezo la msingi sana, kwamba ujenzi wa reli huu tunaouzungumza utakuwa na maana kiuchumi kama njia hii itajielekeza katika hiyo njia ya Tabora, Kigoma na Msongati na sababu zake wala huitaji kwenda shule kuzijua. Ni kwa sababu wenzetu wa DRC Mashariki yake na Kusini Mashariki yake wana mzigo mkubwa wana mzigo mzito ambao unahitaji kupita kwenye reli, ndizo economics zake tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na Waheshimiwa Wabunge reli msingi wake si kubeba bianadamu, reli msingi wake ni kubeba mizigo tena mizigo mizito. Hii dhana ya kwamba utatoka Dodoma utakwenda Dar es Salaam na mchicha wako na mayai yako ni mambo ya kizamani haya. Reli ni ya kiuchumi, tunaomba wenzetu wasimamizi Serikalini wakubaliane na agizo la ukurasa wa 31, tujikite eneo ambalo reli hii inakwenda kubeba mzigo mzito na huko si kwingine, ni Mashariki ya Demokrasia ya Congo na Kusini Mashariki ya Congo. Kwa maana ya kwamba reli hiyo ikitoka Tabora ikaenda Kigoma ikapata branch kwenda Msongati, kwa maana ya Uvinza kwenda Msongati - Burundi na nyingine ikaenda Kigoma - Lake Tanganyika mpaka Congo. Maana yake ni kwamba mzigo huo ambao una kisiwa kuwa zaidi ya tani milioni nne kwa mwaka utafanya reli hiyo iwe ni ya kiuchumi zaidi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa niliseme ni reli ya TAZARA. Mimi ni mjumbe wa Kamati hii ya Miundombinu, hili jambo la reli tumelizungumza sana. Reli ya TAZARA au reli ya uhuru kuna mambo ambayo hayaeleweki vizuri, hii reli imefilisika. Ziko taarifa kwenye magazeti tumezisoma na nyingine zikimnukuu Mheshimiwa Waziri kuhusu namna wanavyoshughulikia jambo hili la TAZARA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba lazima mkataba huu wa TAZARA wautazame upya. Reli ya TAZARA inakufa na tunaambiwa sasa kuna wakodishaji eti wameanza kukodisha reli yetu ya TAZARA na ningependa pengine wakati wa kipindi cha bajeti kinachokuja Mheshimiwa Waziri wa Fedha mtueleze vizuri kwamba hii reli mnaikodisha kwa akina nani na kwa gharama gani, maana mahusiano yaliyokuwepo kati yetu na Zambia wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere na Mzee Kaunda yamebadilika sana. Kuna haja sasa kuanza kuitazama kiuchumi zaidi reli hii ya TAZARA na kuanza kuitazama kwa maslahi ya Tanzania zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa nilizungumzie ni viwanja vya ndege na ndege za ATCL. Hivi viwanja vya ndege ni vya kimkakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na nilikuwa napenda niseme tu labda, kwamba nimekuwa Mkurugenzi kwenye Kampuni ya PUMA Energy kwa miaka saba. Ile Kampuni ya PUMA Energy ni Kampuni ya Serikali, kwa maana ya asilimia 50 za kampuni ile ni za Serikali. Kwenye viwanja vya ndege na mauzo ya mafuta ya ndege katika soko la SADC, PUMA Energy ina asilimia 86.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumza na Mheshimiwa Waziri namwambia PUMA Energy ina asilimia 50 za Serikali tena za kihistoria Mheshimiwa Waziri akawa haelewi vizuri. Mheshimiwa Waziri wa Fedha hili liko kwako, huyu ni ng’ombe wa maziwa, kama alivyokuwa anaita Mheshimiwa Mwijage, huyu ni ng’ombe wa maziwa tumpe majani, tumtunze ili tuendelee kukamua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara ya ndege, si ndege zetu, hata ndege za majirani zetu na kampuni nyingine zinahitaji kuwa na uhakika wa mafuta yao na Kampuni ya PUMA Energy kwa miaka zaidi ya 13 sasa wameshikilia hilo soko vizuri na sisi kama Serikali tunapata asilimia 50 ya mauzo yao. Ni jambo jema na tunaomba sana wenzetu wa Serikali, Mheshimiwa Waziri wa Fedha hilo jaribio la kuwatishia kampuni yenu wenyewe asilimia 50 eti kulinyima leseni ni jambo ambalo naona kama ni aibu kidogo. Ni vyema mjiridhishe na ukweli wa mambo haya ili muweze kujua ni kitu gani mnachokizungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa nilizungumzie ni kuhusu kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo la TEHAMA, jambo la mawasiliano ni jambo muhimu sana, ni jambo mtambuka. Ni maoni yangu kabisa kwamba kazi inayofanywa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) hoja hii ya TEHAMA sasa ihame iende shuleni na kwenye vyuo; dunia imebadilika, dunia ni ya mawasiliano, dunia ni ya mitandao. Ushauri wangu kwa Serikali, ingekuwa ni jambo jema sana sasa Mamlaka hii ya Mawasiliano tuihuishe tui-link na vyuo vyetu na shule zetu ili sasa suala la kujifunza juu ya mitandao na TEHAMA katika shule zetu liwe jambo la msingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningependa nilizungumzie suala la barabara. Iko sera ya dhahiri ya barabara; kwamba sera yetu ya ujenzi wa barabara kama ilivyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ni kuunganisha mikoa na mikoa. Hata hivyo bado kuna mikoa michache katika nchi yetu haijaunganishwa kwa mujibu wa sera hiyo ya barabara. Mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Kigoma na Mkoa wa Katai. Tunawaomba wenzetu wa Wizara ya Ujenzi acheni kuanzisha miradi mipya, kamilisheni miradi ambayo mmeshaianza ili barabara hizi zikamilike. Haingiii akilini wanaanza miradi mipya wakati miradi ya zamani bado haijakamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii barabara toka Nyakanazi mpaka Kabingo huko Kakonko ina mwaka wa kumi haijakamilika, leo hii barabara kutoka Kidahwe kuja Kasulu ina mwaka wa 11 haijakamilika, acheni kuanzisha miradi mipya tukamilishe miradi iliyopo. Tunaishukuru Serikali na wewe Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa jitihada mlizozifanya kupitia wenzetu wa African Development Bank kwa mradi mkubwa wa barabara kutoka Kabingo – Kibondo – Kasulu mpaka Maruku kwenda Burundi. Ni juhudi kubwa nzuri lakini tunaomba zisimamiwe ili kazi hiyo iishe. Ni kilometa 261 na kwa kawaida tunadhani ndani ya miaka mitatu/minne au mitano inaweza ikawa imekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine katika ujenzi wa miundombinu ni suala la umeme. Ningependa kujua, maana umeme nao ni miundombinu vilevile, ningependa kujua ujenzi wa Hydro ya Malagarasi umefikia wapi ambao hatimaye umetuingiza kwenye mpango huo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, najua muda wangu unakimbia, ni kuhusu jambo ambalo limezungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara na kuna Mheshimiwa Mbunge mmoja amelizungumza na mimi pia napenda kuliunga mkono. Tumeambiwa, kwa mujibu wa report ya Kamati, kwamba kuna viwanda 156 vilibinafsishwa, viwanda kama 50/56 vinafanya kazi na viwanda vingine 100 havifanyi kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninashawishika kukubaliana kwamba kuna haja sasa Bunge hili liunde Kamati Maalum, si lazima iwe Kamati Teule, iundwe Kamati Maalum isaidiane na wenzetu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ili tuweze kujua hivi viwanda 100 plus vilivyobinafsishwa hatima yake ni nini? Otherwise itabaki ni wimbo tu kila siku viwanda, viwanda ambavyo havifanyi kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo Tume ikiundwa inakuwa ya Kibunge tu wala si lazima iwe teule. Iwe Tume Maalum ambayo itakuwa na Waheshimiwa Wabunge wenzetu wachache pamoja na wenzetu wa Kamati ya Biashara na Viwanda, wapitie viwanda hivyo 100 plus ambavyo vimebinafsishwa lakini havifanyi kazi. Vinginevyo huu ni mwaka wa tatu, ni hadithi kila siku, kwamba viwanda, viwanda, lakini viwanda vyenyewe havifanyi kazi kama ambavyo tungetarajia vifanye kazi viweze kuingiza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ningependa kuzungumzia huu mradi wa chuma wa Liganga na Mchuchuma. Sisi wachache ambao tumebahatika kufika pale, ukifika Liganga, Mchuchuma na pale Mbamba Bay utaona Mwenyezi alikuwa na makusudi yake. Liganga ni mlima, mlima wote wa Liganga umejaa chuma, chini ya mlima ule kuna mto mkubwa. Ukienda kilometa 32 ukitoka Ludewa unakutana na eneo linaitwa Mchuchuma. Mchuchuma ni mto mkubwa sana na eneo lote la Mto limejaa makaa ya mawe, ni kama Mwenyezi Mungu alisema ninawapa makaa ya mawe mpate moto wa kuyayeyusha na maji ya Mto Mchuchuma uweze kupoza chuma chenu hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, ukienda Kusini Mashariki kuna Bandari ya Mbamba Bay, ni kama triangle una chuma, una makaa ya mawe na una bandari ya Mbamba Bay. Sasa kwa nini Serikali hamchukui hatua za makusudi …. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
Azimio la Bunge la Kuridhia Ubadilishaji Hadhi Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika – Orugundu kuwa Hifadhi za Taifa
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, nami nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza nianze kwa kuunga mkono hoja hii muhimu sana. Hata hivyo, nina mambo mawili. La kwanza ni kuwakumbusha wenzetu kwamba mapori haya ya Burigi na Biharamulo yako jirani na Mkoa wa Kigoma na pori letu mashuhuri sana la Kigosi Moyowosi. Nilitarajia katika kufanya Burigi, Biharamulo ziwe National Parks na Kigosi Moyowosi ingekuwa National Park kwa sababu haya mapori yanategemeana na yako jirani sana. Isitoshe katika Pori la Kigosi Moyowosi kuna eneo la Ramsar site, eneo chepechepe ambalo kwa kweli kwa wenzetu wa UNESCO wameshalitangaza kama ni urithi wa dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilitarajia kwa muktadha huu na kwa dhamira hii njema kwamba Burigi, Biharamulo inge- incorporate na Kigosi Moyowosi National Park kwa sababu ikolojia ile ni moja sisi tunatoka maeneo yale tunafahamu. Hofu yangu ni nini sasa? Endapo Kigosi Moyowosi mtaiacha tafsiri yake ni kwamba wale majangili na watu wabaya wataacha Burigi na Biharamulo National Parks watashuka huku, ni kushuka tu pale, kwa sababu kutoka Biharamulo kuja Kigosi Moyowosi ni chini ya kilomita 60, ni jirani sana. Kwa hiyo, angalizo langu kwa nia njema hiihii, naomba sana Mheshimiwa Waziri na timu yako hata ikiwapendeza basi Kigosi Moyowosi na Malagarasi wet land iwe chini ya uangalizi wa TANAPA vinginevyo yale maeneo yanaharibika sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni kulinda Mto Malagarasi. Mto huu jiografia yake ilivyo unapita katikati ya Pori la Kigosi Moyowosi na umeharibika sana kwani umevamiwa sana. Kwa hiyo, nasema tena ni hoja njema sana, ni jambo jema sana tena isitoshe limechelewa kwa sababu mimi nimewahi kuhudumu kwenye Tume ya Wanyamapori katika mambo tuliyoyapendekeza miaka ya 2013 ilikuwa ni kufanya mapori haya yote yawe National Park ili kupunguza uhalifu, ujangili na kadhalika. Ombi langu na angalizo langu kwa Serikali ni kwamba angalieni namna bora sasa ya kuilinda Kigosi Moyowosi kwa sababu wewe Spika ni Mhifadhi ni ikolojia ile ile tu na wanyama ni wale wale tu, mkibana huku Biharamulo maana yake uhalifu utashuka Kigosi Moyowosi. Kwa hiyo, angalizo langu kwa Serikali lilikuwa ni hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nadhani Mheshimiwa Waziri anakumbuka kwamba wale ndege wasiopatikana popote duniani mwezi wa Juni na Julai wanakwenda Kigosi Moyowosi. Uwanja wa Ndege wa Kigosi Moyowosi ulijengwa na wawekezaji, kwa hiyo, Uwanja wa Ndege wa Chato utasaidia sana kwani watalii watatoka Chato wanashuka kwa ndege na ni dakika 20 au 15 wanakuja Uwanja wa Ndege wa Kigosi Moyowosi. Ule uwanja wa ndege bado upo na ni uwanja muhimu sana. Kwa hiyo, maeneo haya ni mazuri sana kwa ajili ya ku-promote utalii katika Taifa letu. Nina hakika kupandisha hadhi mapori haya na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Chato eneo lile sasa litaimarika katika tasnia hii ya utalii.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, nilitaka niongezee hayo kwa ajili ya umuhimu wa Kigosi Moyowosi. Ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. DANIEL N. NSANZUGWAKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Labda nianze moja kwa moja kwa kuwapa hongera sana viongozi katika Wizara hii, Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, na makanda wote wa Jeshi la Polisi hongereni sana. Lakini kwa namna ya pekee na chukua nafasi hii kumpongeza RPC wa Mkoa wa Kigoma ndugu Otieno na ma-OCD wake kwa kazi kubwa wanayoifanya kule Kigoma ukizingatia Kigoma ni Mkoa wa mpakani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri na wewe binafsi nikushukuru kwa kufanya ziara katika Mkoa wa Kigoma na hasa Wilaya ya Kasulu ulikuja tukakutembeza maeneo mbalimbali ukaenda mpaka Kitanga ukashuhudia mauaji yaliyotokea hongera kwa kazi, na karibu sana katika Mkoa wetu wa Kigoma.

Labda Mheshimiwa Waziri nikukumbushe jambo moja, Mkoa wa Kigoma unapakana na nchi nne ndiyo mkoa pekee katika nchi hii ambao unapakana na nchi nne, unapakana na Zambia upande wa maji, unapakana na Congo DRC, tunapakana na Burundi na Rwanda. Na nchi zote hizo Mheshimiwa Waziri unajuwa ukiacha tu nchi ya Zambia nchi zilizobaki DRC, Burundi na Rwanda hali yake ya usalama si shwari sana hali ni tete.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wabunge wa Mkoa wa Kigoma tumekaa na wewe zaidi ya mara moja tukikuomba utumie mamlaka yako kwa mujibu wa instrument uliyonayo, uyatamke maeneo yenye uhalifu mkubwa ili yaweze kuwa na kikosi maalum cha polisi au mnahita kama Rorya ya Tarime ile Kanda Maalum ya Kipolisi. Na Mheshimiwa Waziri tunakusisitiza Kanda hii inaweza ikawa ni enclave ya Ngara, Biharamuro, Kakonko, Kibondo, Kasulu, na maeneo ya Buhigwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri unaposema hali ya usalama katika nchi yetu ni nzuri tena unaweka nzuri sana sisi wakazi wa maeneo yale tuna sema hali si shwari. Utekaji ni mwingi, ujambazi ni mwingi na tunaomba kabisa kabisa Mheshimiwa Waziri jambo hili mlipe kipaumbele. Nina hakika eneo hili likiongezewa rasilimali tukawa na Kanda Maalumu la Jeshi la Polisi na polisi wengine wakaendelea kuwepo katika maeneo yao hali ya usalama inaweza ikawa ni nzuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyozungumza hivi na Waziri unajuwa utekaji unaendelea katika maeneo ya Kakonko, maeneo ya Biharamuro, maeneo ya Nyakanazi, maeneo ya Kasulu, maeneo ya Kibondo na ule mpaka wetu ni mkubwa sana. Mheshimiwa Waziri ule mpaka unajuwa ni zaidi ya kilomita elfu 2000 kwa hiyo, ni muhimu sana Kanda hiyo Maalum ukaanza kufikiria na ningependa uje utueleze humu ndani mnajipangaje kuweza kupunguza uwalifu katika maeneo yale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ningependa nilisemehe ni upungufu wa askari katika Mkoa wa Kigoma, taarifa nilizonazo na wewe unazo kwamba Mkoa wa Kigoma unaupungufu wa askari kati ya 120 mpaka 150 na wewe Waziri unajuwa, wakimbizi wote wa nchi yetu wapo katika Mkoa wa Kigoma. Wakimbizi wapo Kasulu, wakimbizi wapo Kibondo, wakimbizi wapo Kakonko lakini kuna upungufu mkubwa sana wa askari pamoja na vitendea kazi. Sasa mtu yeyote mwenye akili angeweza kudhani kwa sababu Mkoa wa Kigoma upo mpakani unapakana na nchi nne hatupaswi kuwa na uhaba wa askari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haina maana unakuwa na askari wengi katikati ya nchi, unakuwa na askari wengi Dodoma, unakuwa na askari wengi Singida, unakuwa na askari wengi Tabora, unakuwa na askari wengi Shinyanga, wakati ujafunga mpaka, tafsiri yake ni nini? Tafsiri yake ni kwamba ualifu na wahalifu na silaha sinatoka nje ya nchi, zinapitia Kigoma kuingia kati kati hasa kwa akili ya kawaida nilidhani na nina amini wewe Mheshimiwa Waziri na timu yako na RPC ananisikia, RPC Sirro ananisikia haiwezekani Mkoa ambao kama shield yetu ndiyo ngome yetu tuhangaike..

MBUNGE FULANI: IGP Sirro umesema RPC.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWAKO: IGP Sirro ndiyo, aah IGP Sirro ni mtani wangu angeelewa tu hivyo hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, IGP Sirro ananisikiliza haina maana nasema tena inakuwa na askari wengi katikati ya nchi, lakini kwenye mpaka ambao unaingiza silaha haramu unawakimbizi haramu, una watu chungu mzima kumeachwa wazi. Nadhani busara ya kawaida ya polisi ingetumika na wewe Mheshimiwa Waziri kwamba tufunge mpaka, ule mpaka ni mrefu sana silaha zinaingia kutoka Burundi, silaha zinaingia kutoka Rwanda, silaha zinaingia kutoka Kongo na ndiyo zinapita katikati ya nchi yetu. Sasa Mheshimiwa Waziri uioni kama ni busara kawaida tu? Ukaanza kusini mpaka kule of couse ulivyosema mkisheana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, ingawaje wanajeshi wengi walioko katika detach zile wao wanasema wanakazi yao maalum. Lakini mshirikiane kwa karibu ili mpaka ule uweze kuwa salama na wananchi wa maeneo yale tuweze kuhishi kwa amani na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo ningependa nilisemehe na msema kweli mpenzi wa Mungu nimeshangaa kwenye kitabu chako hata hukugusia ujenzi wa barracks niliokwenda kukutembeza, Mheshimiwa Waziri tumekunywa chai pale Kasulu tukaenda kutembea wewe na mimi tukaenda kwenye barracks za Kasulu. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barracks ya Kasulu ile inauwezo wa kuifadhi familia za askari zaidi ya 50 tumekwenda pale sasa nimeshangaa kwenye kitabu chako hiki hata kugusia katika miradi inayoendelea na cha ajabu Mheshimiwa Waziri zile nyumba zimejengwa pia kwa msaada wa Jeshi la Polisi, Magereza wameshiriki pale na jambo hili hata Kamanda IGP Sirro nimewai kumueleza una-priority gani kama uwezi kuhifadhi askari katika maeneo ya mipakani, kwenye kitabu chako not even a mention hata kutamka tu umeona barracks hili mambo ya ajabu haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unasema unajenga nyumba tano Kigoma, Kigoma mjini unajenga nyumba tano tunazungumzia maeneo ambayo yamekithiri kwa uhalifu, hawa askari wanakaa mitaani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kitabu chako kabisa uelezi hata kutaja kwamba umetembelea barracks ile na wewe mwenyewe umeona zile blocks zile ni kubwa ni nyingi. Sasa nimeshangaa sana Mheshimiwa Waziri ningependa kwa kweli nipate maelezo kwanini? Unless ukutambua ile nguvu iliyofanyika pale kuna nguvu ya wafanyabiashara, kuna nguvu ya wananchi, kuna nguvu ya Magereza, kuna nguvu ya polisi nimeshangaa sana Mheshimiwa Waziri kwenye mpango wa maendeleo 2019/2020 hata kutaja kwamba kuna barracks inajengwa umesahau kutaja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo ningependa nilizungumze ni uhamiaji tunashukuru sana Kamanda wa Uhamiaji, Kamanda wa uhamiaji tunamshukuru na wenzake na timu yake zile harassment za kutambua watu kwa sura zimepungua sana angalau zimeanza kutumia weledi. Na sisi Mheshimiwa Waziri kupitia kwako niwashukuru sana wenzetu wa uhamiaji ule umbumbu wa kutambua watu kwa sura zao eti kutambua watu kwa rafudhi zao kwa kweli vituko vile vimepungua kwa kiwango kikubwa, tunaomba waendeleze weledi, wahamiaji haramu watambuliwe kwa namna ambayo ni ya kisayansi zaidi kuliko kuangalia sura zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake sura za watu wa Congo, sura za watu wa Zambia, sura za watu wa Burundi na Rwanda zinafanana.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWAKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hiyo lakini naomba hayo yote yazingatiwe Mwenyekiti nashukuru ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza nianze kwa kuwapa pole familia ya Mzee Mengi na Watanzania wote kwa kuondokewa na Ndugu Mengi. Kwetu sisi watu wa Kigoma huyu alikuwa Shemeji yetu kwa hiyo tunatoa pole nyingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba kwa namna ya pekee pia Mheshimiwa Waziri wewe nikupongeze Injinia Kamwelwe na Manaibu wako Injinia Nditiye na Mhasibu aliyebobea Ndugu Kwandikwa, Makatibu Wakuu wote, Architect Mwakalinga ambaye ni mgeni kwenye Wizara ameanza vizuri, anafanyakazi vizuri na Makatibu Wakuu wenzake Ndugu Chamliho na wenzake Mama Sasabo na Jimmy Yonasi wote tunawapongeza kwa kazi nzuri ya kusimamia wenzao katika maeneo hayo. Wizara mko vizuri, Mheshimiwa Waziri mko vizuri, tunawapongeza Watendaji wote kwa maeneo yote, maeneo ya anga, maeneo ya barabara, maeneo ya majini, mawasiliano kwa kweli wako vizuri watendaji, cha msingi ni kuwatia moyo. (Makofi)

Mheshimiwa mwenyekiti, nitakuwa na mambo machache kwa sababu hii ni Kamati yangu na mambo mengi tumeyadadavua kwenye Kamati. Ningependa tu mambo matatu ya haraka haraka:-

(i) Mheshimiwa Waziri asubuhi nilikuuliza swali kuhusu SGR; sisi tunaoelewa vizuri mambo haya, ujenzi wa standard gauge ni mradi wa msingi sana, sana, ndiyo roho ya Nchi, ndiyo roho ya uchumi wa Taifa hili. Nimekuuliza moja ya matawi yake ni kutoka Uvinza kupita Kasulu kwenda Msongati na hatimae Uvira ya Congo kuchukua mzigo mkubwa ulioko katika Jamhuri ya Congo. Ukanijibu kwamba nisiwahishe shughuli kwamba iko kwenye hotuba yako. Kwenye hotuba yako nimeangalia hakuna hata msitari umezungumzia juu ya hilo tawi la SGR. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri nikukumbushe tu na watendaji wako; reli hii ya SGR tunayoijenga ambayo ni uamuzi wa busara sana wa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ni mradi mzuri sana sana. Lakini faida yake, kazi yake ni kubeba mizigo mizito na mizigo mizito mingi Mheshimiwa Waziri kwa takwimu zilizopo, mzigo mkubwa katika nchi zinazotuzunguka uko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ni matumaini yangu kwamba Mheshimiwa Waziri utakapokuja hapa utatuleza hili tawi la Uvinza-Msongati kwenda mpaka Uvira ya Congo mtaanza lini hata angalau basi hata upembuzi yakinifu wa njia hiyo maana hatimaye tunataka SGR hii iwe na maana pana ya kiuchumi kwa Taifa letu.

(ii) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo ningependa lizungumze na hili tunalizungumza siku zote ni barabara; Sera ya barabara inajulikana, Mheshimiwa Waziri nikukumbushe tu na Watendaji wako kwamba Sera yetu ya barabara hasa barabara kuu ni kuunganisha Makao Makuu ya Mikoa na Makao Makuu ya Mikoa. Waziri unajua na watendaji wako wanajua kwamba katika Mikoa mitatu ambayo haijaunganishwa Makao Makuu kwa barabara za lami ni pamoja na Mkoa wa Kigoma, Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Katavi unaotoka wewe nakumbushwa hapa na Mkoa wa Morogoro kwa maana Morogoro na Lindi. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri najua ziko juhudi kubwa sana zinafanywa kutuunganisha sisi na Tabora, ziko juhudi zinafanywa kutuunganisha sisi na Mkoa wa Katavi, ziko juhudi kubwa zinafanywa kutuunganisha sisi na Mkoa wa Kagera pamoja na Shinyanga yake lakini bado bado speed ni ndogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hotuba yako Mheshimiwa Waziri, ukiangalia barabara kwa mfano ya Nyakanazi hiki kipande cha Nyakanazi kuja mpaka Kabingo, barabara imeanza kujengwa kwa miaka kumi lakini mpaka sasa ni asilimia 60 tu basi ya utekelezaji wake na hoja iliyoko hapa Mheshimiwa Waziri ni kwamba mkandarasi yuko site lakini anasema hana fedha. Ushauri wangu kwako na kwa Wizara na kwa Serikali, hamna sababu ya kuanzisha miradi mipya kama miradi ambayo tayari ina Wakandarasi haisogei kwenda mbele kwa sababu ya uhaba wa fedha, kupanga ni kuchangua Mheshimiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ambayo imeshaanza ina wakandarasi, miradi hii ikamilike ndio tuanze na miradi mingine haina maana kuwa miradi nusu nusu viporo kila pahala wakati haikamiliki, haiwezekani barabara ya Nyakanazi, Kabingo miaka 10 asilimia 60. Halikadhalika barabara ya Kidahwe kuja Kasulu kidogo umepiga ahatua asilimia 70 lakini miaka 10 unajenga kilometa 63 tafsiri yake ni kwamba kila mwaka unajenga kilometa tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali na hasa kwa Wizara na Mheshimiwa Waziri naomba hili ulichukue seriously niwaombe sana nasema tena hakuna sababu ya kuanzisha miradi mipya kama iliyopo haijatekelezeka, inakuwa haina maana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu kuna juhudi kubwa ya fedha za African Development Bank kwa barabara ya Kabingo, Kibondo, Kasuli Manyovu ni juhudi kubwa na leo kama kumbukumbu zangu ziko sahihi leo tarehe 9 zabuni zimefunguliwa kuwapata wakandarasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matumaini yangu kwamba sasa mradi huuutasogea kwenda mbele na haitakuwa tena hadithi kama ambavyo tumezoea, na sisi watu wa Mkoa wa Kigoma tumekuwa tuna mashaka kila mara miradi inaanzishwa lakini inasuasua sana katika ukamilishwaji wake. Nikuombe Mheshimiwa Waziri tumechoka kusubiri watu wa Kigoma wanataka miradi hii ikamilike na wanufaike nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo ningependa nilizungumze ni bandari ya Katosho najua kuna juhudi zinaendelea kujenga bandari ile tunataka pia mkandarasi yule nasikia ameshapatikana mkandarasi lakini mpaka leo hakuna ambacho kinaendelea mpaka sasa hivi ni matumaini yangu kwamba ile bandari ya nchi kavu imeshalipiwa fidia ni matarajio yangu kwamba sasa mkandarasi ataingia kazini na bandari ile iweze kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikukumbushe Mheshimiwa Waziri ujenzi wa airport ya Kigoma kupitia fedha za European Investment Bank taarifa tulizonazo sisi watu wa Kigoma na kupitia kwenye vikao vya RCC ni kwamba mkandarasi ameshapatikana tangu mwaka 2018 lakini bado hajakabidhiwa eneo la kufanya kazi, matatizo yaliyokuwepo mara ya makaburi yameshakamilika yameshakwisha nafikiri ni jukumu la Wizara sasa kufanyia a thorough follower up ili mradi ule sasa uanze na taarifa tulizonazo ni kwamba wenzetu wa European Investment Bank tayari hawana kikwazo sasa baada ya kuwa mgogoro uliokuwepo umekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kidogo pia kuhusu bandari ya Dar es Salaam na bandari ya Mtwara. Tulibahatika kutembelea bandari hizi nikuombe Mheshimiwa Waziri jilidhishe na matatizo tuliyoyaona katika bandari ya Mtwara na matatizo ya kiutendaji tuliyoyaona katika bandari ya Dar es Salaam, dawa ya tatizo ni kuliondoa sio kujificha kwenye kichaka na hii tabia ambayo imeanza kuzuka ukisema jambo basi watu wanasema huyu bwana kahongwa kapewa fedha msitafute vichaka vya kujifichia kuna matatizo ya kimkataba katika bandari ya Dar es Salaam, matatizo haya mkae chini kaa na watendaji wako Engineer Kakoko yupo na wenzake mkae mezani muyamalize matatizo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona matatizo ya usanifu kule Mtwara kaeni na wataalam, kaeni na Engineers waliopo muweze kuyaondoa matatizo haya. Na kama hii dhana ya kuanza kufikiri kwamba kila likisemwa jambo basi mtu amehongwa linakuwa kwa kweli ni kujipofusha sisi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ningezungumzia kuhusu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na hiyo kampuni ya PUMA Energy Tanzania. Mheshimiwa Waziri nakupa nakushauri tu pata muda wa kuifahamu kampuni hii ya PUMA Energy nimekuwa Mkurugenzi kwenye kampuni miaka saba na nilikuwa ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi, hii ni kampuni ya Serikali asilimia 50 za PUMA Energy ni Serikali ya Tanzania na ni hisa za kihostoria. Hizi hisa alipewa mwalimu Nyerere mwaka 1966 na Malikia wa Uingereza lakini napata shaka kwamba Mheshimiwa Waziri huelewi vizuri kwamba hii kampuni ya PUMA ni kampuni ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshauri sana Mheshimiwa Waziri una TR, kuna watu wa HAZINA kaeni chini hii kampuni ni ya kwetu imelipa dividend kwa miaka minane mfululizo. Sasa taarifa nilizonazo ni kwamba ina vikwazo vingi sana na Mheshimiwa Waziri umeonesha kutoipenda kampuni hii, sasa nikuishauri tu kwamba usimchukie mtoto wako kaa na Mamlaka, kaa na TR muweze kuelewa vizuri juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nikukumbushe tu Mheshimiwa Waziri naunga mkono hoja hii lakini niseme jambo moja kwa ruhusa yako nusu dakika tu kwamba ahadi zinatolewa na viongozi kuna ahadi zimetolewa 2017 hazijatekelezwa na kuna ahadi zimetolewa 2019…

MWENYEKITI: Ahsante mengine muandikie.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Niombe sana Mheshimiwa Waziri jambo hili. Naunga mkono hoja hii. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi naomba niwape hongera sana wenzetu wa Serikali kwa mpango wao huu waliotuletea hapa. Nianze kwa kuwapongeza watu wa Wizara ya Kilimo na biashara, leo tarehe 11 yale madai yote ya korosho yamelipwa na wakulima sisi; na mimi mkulima; kupitia cashew nut payments code 704 imelipwa, kwa hiyo, ahadi ya Mheshimiwa Rais Magufuli imetekelezeka hongereni sana na sisi wakulima tunaendelea kukaza mwendo, Hasunga hongereni sana kwa kazi ilikuwa ni kitu kabisa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nina mambo machache, nina mawili tu. Kwanza nilitaka nirejee maneno yako uliyoyasema asubuhi kuhusu China; ulivyosema nimekusikia vizuri. Kama nimekuelewa vizuri nadhani Mbunge yeyote mwenye maarifa amekuelewa vizuri, na bila shaka Serikali imeelewa vizuri. Kwasababu China inapaswa iwe ndicho chanzo chetu cha mtaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Lakini ni kwanini mpaka sasa, tunapozungumza, hata TAZARA iliyojengwa na Mwalimu Nyerere ina mgogoro mkubwa sana. Ni mahali gani tumeshindwa kuzungumza na Wachina hawa tukaelewana wakati wachina hawa kihistoria kwa kweli ni ndugu zetu na kuna maelewano ya kihistoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu wewe pia ni kiongozi wetu humu mimi napata hisia kwamba tuwashawishi viongozi wetu wakubwa wakatembelee China, ili kama kuna kitu hakieleweki wakakifungue wakubwa hawa. Wachina hawa tunaweza tukawatumia vizuri na wangeweza kutusaidia kwa mambo mengi, hasa masuala haya ya kimtaji kwa sababu uchumi wetu ndio unajijenga, unahitaji ku-stabilize, vinginevyo naona kama tutapata shida. Hii kukopa kwenye benki, fanya hiki inatuletea shida kubwa sana. Ni vyema twende China tukazungumze nao, tukakope mkopo mkubwa na wamuda mrefu ili kuweza kukwamua masuala haya tunayotaka kuyafanya katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, nafikiri hoja yako ya asubuhi imenikuna sana; nawe kwasababu mnakaa na wakubwa mnakunywa kahawa nadhani kuna haja ya kuipeleka na kwao kule waweze kuielewa vizuri; umetueleza kitu kizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ningependa niliseme pia amelizunguza ndugu yangu Mwakajoka hapa. Waziri wa Fedha fursa hazitusubiri, fursa zipo kesho hazipo. Nasema hivi kwa sababu; nizungumzie suala ya reli ya kati kwa mfano, SGR inayojengwa ni kitu chema sana, Rais Dkt. John Pombe Magufuli huyu ameamua uwamuzi wa busara kabisa kutujengea reli ya kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini reli hii ni mradi mkubwa na manufaa yake ni ya muda mrefu kidogo. Hii reli itakuwa na manufaa ya kiuchumi kama itafika Kigoma kwa ajili ya kuchukuwa mzigo mzito uliopo mashariki mwa DRC. Reli hii itakuwa na faida tawi lake hili la kutoka Tabora Kaliua kwende Kalema mpaka Kasanga Port kwa ajili ya kutape mzigo uliopo kusini mashariki ya DRC.

Mhimiwa Mwenyekiti, majirani zetu wote fursa wanayoitazama ni hiyo hiyo. Utasikia ooo! leo hii mzigo mkubwa unaopita bandari ya Dar es Salaam ni wa nchi ya Uganda! Zipo taarifa ambazo ninauhakika nazo kabisa; asilimia 60 wa ule mzigo unatoka Mashariki Kaskazini ya DRC ambao wangeweza kuja kutumia Bandari yetu ya Kigoma na wakaja kutumia Bandari yetu ya Kasanga kwenye Ziwa Tanganyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu yangu Mheshimiwa Keissy amezungumza Bandari ya Kigoma leo tunachozungumza, na Waziri wa Fedha unajua; kwamba Bandari ya Kigoma Modernization ya Kigoma pot kuna pakeji ya msaada kutoka Jamhuri ya watu wa Japan. Hata hivyo mradi ule umekwama na sababu zake za kukwama ni vikwazo eti! Wanadaiwa mitambo yao walipe kodi za TRA. Wale wajapani walikuwa negotiation na Serikali huu ni mwezi wa saba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi ningependa kujua kwakweli, on a serious note, ni kitu gani kimekwamisha modernization ya Port ya Kigoma ilhali wenzetu Wajapani wapo tayari kutusaidia ku-modernization bandari ile kwa maslahi mapana ya uchumi wa nchi yetu. Kwamba mzigo sasa utoke ngambo ya pili ya DRC uje Bandari ya Kigoma uje kwenye reli ya SGR itakayojengwa kupeleka mzigo nchi za China na mashariki ya mbali; hilo ni jambo ambalo ningependa tuendelee kulizungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii zana ya majirani zetu, sina haya ya kuwataja, kujenga barabara kujenga reli na matawi yake wanakuja kudhohofisha, maana tutakuwa tunapokea mizigo kutoka nchi ya tatu. Origin, nchi ya pili na sisi tunakuwa nchi ya tatu ilhali tuna fursa ya kuja moja kwa moja sisi kutoka DRC na kuja katika nchi ya Tanzania; fursa hizi mziangalie. Nina matumaini kule hazina mtakaa chini na wataalamu mliangalie kwa mapana na marefu haya; mumshauri Mheshimiwa Rais juu ya jambo hili sasa, jambo hili maslahi yake ni mapana sana kwa taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni kuhusu ndege. Tulikuwa wote wakati tunapokea Dreamliner, nadhani wewe ni shahidi na wote mliokuwepo, kwamba kilikuwa ni kitu chema mno, kitu ambacho kila mmoja alifurahi. Dreamliner inatoka Marekani inatumia masaa 16 kufika Dar es Salaam, non stop na kila kitu kinafanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu iko hivi; Mheshimiwa Waziri wa Fedha ununuzi wa ndege ni jambo jema mno, jambo jema sana. Hata hivyo ndege hizi lazima tuzifungamanishe mambo mengine, ndege hizi lazima tuzifungamanishe na wenzetu wa utalii ili ndege hizi ziweze kuwa na faida. Vinginevyo ndege peke yake hizi zitafika mahali itakwenda Mumbai haina abiria wa kutosha, itakwenda Guangzhou haina abiria wa kutosha. Kwa hiyo kuna haja wenzetu wa Serikali hasa Wizara ya Fedha wazungumze na mashirika rafiki kama vile Precision Air, Rwanda Air, na zimbambwe Airway, na sisi Dar es Salaam iwe hub katika International travel, vinginevyo ndege hizi zitakosa biashara inayotarajiwa.

Mheshimiwe Mwenyekiti, ndege tuliyopanda siku ile ukiiangalia inabeba abiria 260 non stop Dar es Salaam Guangzhou, non stop Dar es Salaam mpaka Mombai. Sasa ndege hizi sisi wenyewe hatuwezi lazima tufikiri kibiashara; kwamba abiria kutoka Lubumbashi, Lusaka, Lilongwe, Bunjumbura na Entebe wanakuja Dar es Salaam halafu Dar es Salaam, halafu Dar es Salaam ndiyo inakuwa ndiyo kitivo na eneo la hub. Kama ilivyo Dubai, sisi lazima tuwe Dubai nyingine katika nchi za maziwa makubwa ili ndege zetu ziweze kuwa na faida kubwa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa na li-link na hili hili…

MWENYEKITI: Pia katika hilo hili hawa Lubumbashi Waziri wa Uchukuzi akumbuke kujenga hoteli ya watu wa transit haraka sana, endelea Mheshimiwa.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa kabisa, ahsante sana; na hilo unalolisema, ukiangalia tulichowekeza kwenye ujenzi wa rada tuna rada nne zinafanya kazi. Viwanja vya ndege vyetu vingi havina taa za usiku na matokeo yake ndege zetu nyingi zinafanya kazi mchana usiku hazifanyi kazi; na abiria kutoka Goma Congo kutoka Bukavu; na kwa wale wasiojua, Mji wa Bukavu ni mkubwa kama Dar es Salaam, ni miji mikubwa sana hii. Hawa watu wangeweza kuwa wanakuja kwa ndege za kusafiri mpaka usiku. Tafsiri yake ni kwamba Bandari ya Kigoma sasa ijengewe facility ya ndege kutua usiku ili ndege zifanye usiku na mchana ili ndege zetu kubwa zile ziweze kuwa na faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa rada, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere, terminal III uweke na ndege hizi tumetumia takribani tirioni 2.7. Sasa lazima wenzetu wa hazina mfikiri kibiashara, muwe na mpango wa muda mfupi, muda wa kati na hakika tuwe na mpango wa muda mrefu kwa sababu hizi ni fursa, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kafungua fursa, hizi ndege wenzetu wanashangaa. Juzi nilikuwa nazungumza nabalozi mmoja wa nchi jirani akawa ananiuliza ninyi mmewezaje; nikamwambia hiyo ni Magulification of Africa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo haya ni makubwa, na wenzetu wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi, Mama Kairuki, wa uwekezaji, muanze kufikiri kibiashara. Juzi nimefurahi kusikia Waziri wetu wa biashara alikuwa China, nimefurahi sana, alikuwa anatueleza mambo ya kule China. Mawaziri msafiri msikae ndani. Ndege asiposafiri hawezi kujua mtama umekomaa wapi; na kadiri Mawaziri mnavyosafiri mnakuwa wa kisasa zaidi na namnakuwa mnaifahamu dunia zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwa leo nilifikiri nizungumze hayo, nakushukuru, ahsante sana.
Azimio la Kuridhia Itifaki ya Kinga na Maslahi ya Kidiplomasia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (The East Africa Community Protocol on Information and Communication Technology)
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza nashukuru nianze kwa kusema kwamba sisi Kamati yetu ya Miundombinu tumechambua sana Itifaki hii na naunga mkono Itifaki hii kwa niaba ya wenzangu kwenye Kamati kwa sababu ni kitu chema sana, chema kabisa, ila nina mambo mawili tu madogo sana na maadamu Waziri wa Mambo ya Nje yuko hapa kwa kweli hoja hii ningeilekeza kwake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, part two ya Protocol hii inasema kwamba ili Protocol hii ifanye kazi lazima nchi wanachama wote waridhie na mpaka sasa tumepewa taarifa toka Serikali ni nchi tatu tu zimesharidhia Protocol hii kwa maana ya Kenya, Uganda na Rwanda, Burundi bado Southern Sudan bado na kadhi hati yake ni kwamba Protocol hii haitafanya kazi mpaka members stance hawa wawe wamesaini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilikuwa naomba kwa sababu ni kitu chema sana hiki, kwa kweli ni chema kiuchumi kwa Tanzania nilikuwa naomba nipate maelezo ya Serikali kupitia Secretariat ya Afrika Mashariki, Waziri wa Foreign Affairs kwa kweli mfanye jambo hili haraka kidogo ili wenzetu wa Burundi nao wasaini na wenzetu wa Southern Sudan nao wasaini ili Protocol hii iweze kuwa, iweze kuwa na maana iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili faida yake ya pili nyingine kubwa sana ni Mkongo wa Taifa nadhani Waziri wa Fedha utakubaliana na mimi kabisa kwamba Mkongo wa Taifa sasa ni chanzo kingine kizuri sana cha mapato ya Serikali na Mkongo huu tayari umeunganishwa na Burundi na nchi ya Kenya, sasa kwa sababu ni kitu chema na tunafanya biashara ya ki-digital na wenzetu katika nchi jirani hizi ni vyema kabisa wenzetu wa Wizara hasa Foreign Affairs jambo hili mlipe kipaumbele sisi kwetu ni kibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitizame zaidi Protocol hii kibiashara ili hatimaye Mkongo huu wa Taifa tuweze kuuendesha kibiashara zaidi na hasa masoko yetu yakiwa ni nchi za jirani, la mwisho faida nyingine ya Itifaki hii.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa muda wetu ndiyo huo.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono Itifaki hii. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii; nami nitakuwa na mambo matatu tu. Nitazungumzia grid ya Taifa kwa mikoa ya Kigoma na Katavi, nitanzungumizia mradi wa Stiegler’s Gorge maarufu mradi wa umeme Rufiji halafu nitanzungumzia mradi wa densification, ujazilizaji baada ya ufanisi katika mikoa hii minane ambayo imekamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Mheshimiwa Waziri nikupe hongera sana kwa kazi, wewe na Naibu wako mnafanyakazi nzuri mnazunguka nchi yetu vizuri sana na mnafanya kazi nzuri sana. Kwa hiyo wewe na timu yako TANESCO, REA, TPDC mnafanya kazi nzuri sana hongereni sana sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na mradi huu wa grid ya taifa kwa Mkoa ya Kigoma na Mikoa ya Katavi. Katika nchi yetu ni mikoa miwili ambayo haijaunganishwa kwenye grid ya taifa; lakini nashukuru kupitia hotuba yako ya leo umezungumzia juhudi kubwa iliyopo ya kuunganisha Mikoa ya Kigoma na Katavi kwenye grid ya taifa. Ombi langu la msisitizo wangu kwako na ushauri kwa Serikali ni mikoa miwili tu imebaki kuunganishwa kwenye grid ya taifa.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nsanzugwanko kuna taarifa.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika nampa taarifa mzungumzaji anasema mikoa miwili sijui Rukwa ameisahauje? Si mkoa? Ni Wilaya ya Rukwa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nsanzugwanko unaipokea taarifa hiyo.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, sina hakika na Rukwa kwa sababu Rukwa wanapata umeme kutoka Zambia sasa sina hakika sana, nami napenda nizungumze vitu nina hakika navyo. Ambayo nina hakika ni Mkoa wa Kigoma na Mkoa wa Katavi, wenzetu wa Rukwa wanapata kidogo kutoka Zambia.

Mheshimiwa Naibu Spika, na hoja yangu ni dogo tu, kwa kuwa kuna shughuli mnafanya ya kuunganisha mikoa hii miwili, Mheshimiwa Waziri na timu yako niwaombe muipe priority mikoa hii. Bila kunganisha kwenye grid ya taifa ni impossible, haiwezekani, haiwezeikani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tunavyofahamu kwamba umeme ni roho ya uchumi, umeme ni maisha; kwa hiyo nikuombe Mheshimiwa Waziri mikoa hii miwili sasa kwa mujibu wa hotuba yako hapa ipeni priority, ipeni kipaumbele iweze kuunganisha na gridi ya taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya yangu ya pili ni Rufiji Stiegler’s Gorge. Mradi huu wa Stiegler’s Gorge ni muhimu sana kwa taifa, ni mradi ambao wala hatupaswi kujadiliana; huwezi kuwa na nchi ambayo haina umeme

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nimebahatika kwenda kutembelea bwawa la Aswan Dam kule Misri. Roho na ujeuri wa nchi ya Misri ni Bwawa la Aswan, wanapata umeme mwingi sana. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri tunakuunga mkono kwa nguvu zetu zote, Watanzania tupo nyuma yako, tupate umeme mwingi na wa kutosha. Kwa hiyo mradi muhimu sana, mradi wa kiuchumi, Mheshimiwa Waziri songambele taifa lipo nyuma yenu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu ya tatu ni huu mradi wa kujaziliza maeneo ambayo yana umeme. Mheshimiwa Waziri umefika Kigoma mara tatu sasa, tulizindua REA three kule Lusesa; tunashukuru sana kwa hotuba yako nzuri uliyoitoa. Baadaye ulikuja mpaka Luhita kule kwangu, umefanya kazi kubwa, hongera sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kuna huu mradi wa densification program au mradi wa kujaziliza maeneo yaliyobaki. Nimesoma kwenye hotuba yako Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 65 unasema kuna mikoa ile minane ambayo imakamilika; sasa nilikuwa naomba hii mikoa miwili ambayo tumechelewa kupata umeme wa REA II na REA III bado inasuasua. Nikuombe sana katika hii awamu inayokuja round two basi Mkoa wa Kigoma na Mkoa wa Katavi; nasisitiza mikoa hii miwili kwa sababu ni special kwa sababu ni mikoa ambayo haiunganishwa na grid ya taifa. Nikuombe katika hii pragramu ya densification mkoa wa Kigoma na mkoa wa katavi uipe kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho; lipo jambo mahususi kabisa. Umeme unaohudumia Wilaya mpya ya Buhigwe unatoka mjini Kasulu. Sasa vipo vijiji na maeneo ambayo watu wanatazama umeme na umepita kwenye maeneo yao. Nikuombe Mheshimiwa Waziri jambo hili nimeshakueleza, nikuombe ulipe kibaumbele. Yale maeneo ambayo umeme umepita katika vijiji vyao wasije wakahujumu miundombinu yetu, nakuomba sana maeneo hayo yaweze kupata umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja hii muhimu sana, nasema ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, ahsante nashukuru kwa kunipa nafasi hii nitakuwa na machache.

Mheshimiwa Spika, la kwanza kabla sijasahau ningependa Mheshimiwa Waziri wa Fedha atakapokuja atueleze zile kodi zinazodaiwa (tax refund) kwa mwaka mmoja kwa sababu kuna mashirika mengi na baadhi ya mashirika ni yale hata Serikali yenyewe ina hisa, lakini wanadai tax refund. Ningependa Waziri aje na figure atueleze angalau kodi ambayo TRA wanapaswa kui-refund kwa wafanyabiashara na makampuni ni kiasi kadhaa. Kwa hiyo, nilikuwa naomba hilo kabla sijasahau.

Mheshimiwa Spika, nina mawili madogo tu, la kwanza ningependa sana sana hayo yaliyozungumzwa jambo ni moja ni menejimenti ya uchumi wa nchi yetu. Bahati nzuri Waziri wa Fedha na Naibu wake ni wataalam wa masuala haya, ukisikiliza michango ya Wabunge yote hata Wapinzani wetu walivyosema ni kwamba lipo tatizo la msingi la economic management ya uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, hili jambo ushauri wangu mambo ni mengi na nchi ni kubwa. Nchi hii lazima tu-source talent za wenye uwezo mkubwa. Kuna watu wana uwezo mkubwa katika nchi yetu. Watu kama akina Profesa Ndulu kwa mfano, natoa mfano watu kama wakina Mafuru yule aliyekuwa TR kwa mfano na wengine wengi wapo wengi ndani ya CCM na nje ya CCM. Watu ambao tunaweza tukawafanya kama think tank ya nchi yetu wakamsaidia Waziri wa Fedha katika ku-manage uchumi wa nchi hii yako mambo mengi, mengi ambayo nina hakika yangetuletea fedha nyingi sana katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, maana hapa shida ni kwamba uchumi ni mdogo, sungura ni mdogo lakini bado vipo vyanzo vingi sana fedha ambavyo havijaguswa, kwa mfano, chukua item moja uvuvi wa bahari kuu, alikuja mtaalam mmoja kutoka Zanzibar, alikuwa Mzanzibar mwenye maarifa mengi sana wakati nipo Kamati ya Kilimo na Mifugo. Alitupitisha kwenye uchumi wa bahari kuu, alitushawishi kabisa kwamba kile ni chanzo ambacho hakijaguswa kabisa. Kwa sababu kuna nchi zinaendeshwa kwa kodi ya uvuvi wa baharini Seychelles, Maldives ni nchi ambazo zitegemea uchumi wa bahari kuu, lakini sisi hatuzungumzi na hata kwenye kitabu husikii kama Waziri wa Fedha anazungumza kama kuna source revenue nyingine muhimu sana ambayo imejificha kwenye bahari yetu.

Mheshimiwa Spika, ningeshauri sincerely bado kabisa kwamba Waziri wa Fedha una mamlaka kwa mujibu wa instrument yako unda timu ya wataalam, wazee kama kina Mzee Ndulu wakushauri mambo ya msingi yakufanya.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ningependa nizungumze ni haya mashirika na makapuni ambayo Serikali zina hisa. Tuchukue mfano hivi Kampuni kama Kilombero Sugar Company, kama TPC, Kampuni kama Puma Energy hivi Serikali ina maximize hisa zake zilizopo kule? Ni mambo ya kujiuliza tu. Sisi tulitembelea wakati nipo Kamati ya Kilimo tulitembea Kilombero Sugar Company, tukakuta pale kuna hisa kubwa za Serikali; 25% ya hisa za Kilombero Sugar Company ni za Serikali. Ukienda TPC 30% ni za Serikali na ukienda Puma Energy 50% ni za Serikali, lakini kweli Serikali ina maximize?

Mheshimiwa Spika, nafikiri wakati umefika Msajili wa Hazina ifanye kazi yake kwa umakini mkubwa ili mashirika haya ambayo Serikali iliwekeza hisa zake yaweze kuwa faida. Mheshimiwa Waziri Mpango naamini ile dividend ya bilioni ya tano/bilioni saba/bilioni mbili/milioni 500 ni kidogo mno. Naamini kabisa haya mashirika na yapo mengi kweli kweli yapo mengi tunapata kidogo sana ukilingaisha na investment ya hisa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukianga dividend ambayo inalipwa njoo kwenye kodi malipo ya kodi, njoo kwenye ajira na Mheshimiwa Jenista wewe ni Waziri wa Ajira, jambo lingine kubwa katika nchi yetu ni suala la ajira jamani. Suala la employment ni jambo kubwa sana, ni jambo kubwa, vijana wanatoka vyuo vikuu na wote tunaona kwamba ni mambo ya kawaida.

Kwa hiyo, mashirika hayo mwenyekiti yapo mengi yapo zaidi ya 200 na mimi na hakika bado mchango wake kwa uchumi wa Taifa letu, mchango wake kwa pato letu, mchango wake kwenye Mfuko wa Hazina bado ni kidogo ni kidogo ni kidogo sana.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ningependa nilizungumze ni jambo la TRA. Nashukuru nah ii tunamshukuru Mheshimiwa Rais mwenye ndio ameingilia kati kwamba TRA wawe marafiki wa wafanyabiashara, otherwise ilikuwa imefika mahali sasa TRA kazi yao ni kuwinda wafanyabiashara. Na rafiki yangu ana kiwanda kule Arusha alifuatwa na bunduki na polisi wakachukua computer zake na maskini ya Mungu akaamua kuacha biashara ame- reallocate amekwenda Jinja nchini Uganda.

Mheshimiwa Spika, sasa angalau tunaona TRA wameanza angalau kuwa marafiki wa wafanyabiashara, hiyo inatutia moyo na TRA sasa waende na trend hiyo, kwamba kazi ya TRA iwe ni ya kukusanya kodi na kamwe wasiwe maadui wa wafanyabiashara na wewe responsible kwa wafanyabiashara, wawasikilize wafanyabiashara, bila wafanyabiashara hawa kusaidia uchumi wa nchi hii tutapata matatizo na hatuwezi kujidai kwamba nchi itakwenda yenyewe bila kuwa na private sector na bila kuwa na hawa wafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa nitoe angalizo kwa Wizara ni matumizi makubwa ya Serikali. Ninaamini bado Serikali ina matumizi ya hovyo na makubwa sana. Kwa mfano, hivi nchi maskini kama hii nchi inayoendelea kama hii inawezaje ku-afford misaada ya Serikali inanunua magari ya kifahari ndio wanayotumia watendaji wetu ambapo maskini wanapaswa watumie magari ya kawaida kabisa. Unakuta gari shangingi, Vx 8, DFP iko Kasulu kule, mambo ya ajabu kabisa haya.

Mheshimiwa Spika, huko nyuma ilikuwa mkazo na trend ni matumizi ya Serikali hovyo ya Serikali ili fedha nyingi kama anavyosema Mheshimiwa Rais Magufuli tuzipeleke kwa watu tukajenge vituo vya afya tukajenge shule zetu na kadhalika na kadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Waziri bado yapo matumizi ya hovyo ya magari ya anasa kabisa ambayo hajapaswi kuwepo katika nchi yetu. Ukienda Uganda na nilibahatika kwenda Uganda mwaka jana tulikweda kwenye ziara ya wakimbizi. Ukienda Uganda hawana trend hiyo, hiyo luxury hiyo wameshaiacha. Hatusemi watembee na baiskeli Mheshimiwa Jenista no, no hoja sio hiyo, hiyo ni kupotosha hivi kwa mfano una mpaje Regional Manager wa TANROADS shanging Vx 8 why?

Mheshimiwa Spika, Regional Manager wa TANROADS kwa nini usimpe a good pickup car akikuta bango la barabara limeanguka, akatoka kwenye gari yake, akachukua bango lake, akaweka kwenye gari yake nimetoa mfano mgodo tu. Kwanini umpe Vx 8 nani ana service gari ile? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, hoja ya msingi ni kwamba Mheshimiwa Waziri nenda kaangalie kwenye archives yako bado matumizi ya hovyo ya Serikali ni makubwa sana na Serikali ina kazi nyingi sana za kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho nikukumbushe Mheshimiwa Waziri, sisi Halmshauri ya Mji wa Kasulu tumeshatoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya TRA, kwa maana ya Buhigwe na Kasulu tumetoa kiwanja bure kwa TRA kujenga ofisi zake na mwaka wa jana uliniahidi kwamba TRA wataanza kujenga ofisi pale na kile kiwanja tumewapa bure, sasa mambo mawili au mnajenga au hamjengi turudishieni kiwanja chetu tukitumie kwa mtumizi mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimshauri Waziri wa fedha afanye ziara katika Wilaya ya Buhigwe na Kasulu ajionee hali halisi yamambo yalivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada kusema hayo nakushukuru naunga mkono hoja hii, ahsante sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na mimi nianze kwa kweli moja kwa moja kwa kuwapa hongera sana Waziri Mpango na timu yako wewe na Naibu na timu yako yote ya Wizara Katibu Mkuu na wenzako wote, mmefaya kazi nzuri sana. Bajeti hii imekuwa ni bajeti ya kibiashara, imekuwa ni bajeti ambayo inajielekeza kwenye uwekezaji mkubwa, ni bajeti ya Watanzania. Hongera sana Dkt. Mpango mmeonesha uwezo mkubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kabla sijasahau, nianze na hili ambalo limeainishwa kwenye kitabu cha Kamati ya Bajeti ukurasa wa 60, haya madeni ya walimu. Nafikiri kama nchi sasa lazima tukubaliane kuna madeni ya walimu shilingi bilioni 61, kuna kujenga Ofisi za Kibalozi na kuendelea kukamilisha maboma ya shule.

Kwa maoni yangu na ushauri wangu ni kwamba lazima tuchague kimojawapo, kipi kinaanza na ushauri wangu sincerely kabisa Waziri wa Fedha anza kupunguza madeni ya walimu. Walimu hawa ndiyo kila kitu. Ofisi za Kibalozi zinaweza zikatusubiri kidogo lakini madai ya walimu kama ambavyo yameainishwa kwenye kitabu hiki cha Kamati ya Bajeti nafikiri Mheshimiwa Waziri Mpango ni muhimu sana. Tuwalipe walimu hawa madeni yao yaliyohakikiwa. Hata kule kwangu Kasulu Mji na Kasulu Vijijini kuna shida ya walimu ambao wanadai madeni yao ya muda mrefu na hawajalipwa, nilikuwa nafikiri nianze na hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo Mheshimiwa Waziri wa Fedha nikiendelea kuwapa pongezi kubwa ni huu mkakati wenu kama tulivyochangia kwenye hotuba mwanzo kujielekeza kwenye maeneo ya kutafuta fedha yaani vyanzo vya mapato. Mimi nimefarijika sana kwamba sasa mnajielekeza kwenye uvuvi wa Bahari Kuu ambao kuna ushahidi wa kila aina kwamba baadhi ya nchi zinaendesha mambo yake kwa kutumia fedha ambazo wanapata kwenye uvuvi wa Bahari Kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia niwapongeze sana kupitia kwako na timu yako kwamba sasa TRA wamezuiliwa kufunga biashara. Mimi nashauri na nadhani Mheshimiwa Waziri muende mbali zaidi, ile migogoro inayoendelea ndani ya TRA kati ya wafanyabiashara na TRA na baadhi ya mashauri (kesi) ziko kwenye Tax Tribunal unaweza kupitia mamlaka uliyonayo wakarejea kwenye meza ya mazungumzo. Yako maeneo nina ushahidi kabisa wanabishana kati ya wafanyabiashara na TRA. Mfanyabiashara amekubali kulipa shilingi bilioni mbili, TRA wanang’ang’ania alipe shilingi bilioni sita na wanapelekana kwenye Tax Tribunal.

Ushauri wangu sincerely nilikuwa nafikiri Mheshimiwa Waziri unaweza ukaenda mbali zaidi sasa kwamba mashauri yale ambayo bado hayajaamuliwa, yarejeshwe kwenye meza wazungumze kati ya TRA na wafanyabiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu niko kwenye vipaumbele, kwenye kitabu chako Mheshimiwa Waziri umeainisha vizuri juu ya vipaumbele utaviwekea mkazo. Mimi ni mkulima na ninapenda kilimo. Ningependa nizungumzie eneo la kilimo mambo mawili; kwanza suala la mbegu. Mheshimiwa Waziri wa Fedha, nchi hii tunajitosheleza kwa mbegu za nafaka kwa maana ya mahindi, maharage, mtama na mpunga kwa asilimia 32 tu.

Sasa nilikuwa nakuomba sana kama ulivyoeleza kwenye mkakati wako wa kibajeti tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda ambao msingi wake ni kilimo, basi tuboreshe eneo hili la mbegu. Mheshimiwa Waziri, Serikali ni moja, tuna JKT sasa, Magereza, Wakala wa Mbegu na Vyuo vya Utafiti tuelekeze fedha nyingi kwenye utafiti ili tuweze kupata mazao ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge, juzi tu Mheshimiwa Rais ametuonesha kitu kipya kabisa, alipokwenda Zimbabwe tumepata soko la mahindi karibu tani 800,000 huu ni ushahidi kabisa kwamba Mheshimiwa Waziri tuelekeze nguvu huko ili hatimaye mazao ya nafaka nayo yawe ni mazao ya kiuchumi, mazao kwa ajili ya kuuza kwenye masoko yetu ya nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine Mheshimiwa Waziri wa Fedha ambalo ningependa nilizungumzie, ulizungumza siku ile ya hotuba yako unahitimisha ulishukuru juu ya kikosi kazi cha kodi sasa sielewi labda unaweza ukalieleza vizuri zaidi kwanini kikosi kazi cha kodi hicho hicho kisiwe basi ni kikosikazi cha kusaidia uwekezaji na menejimenti ya uchumi. Siku ile nilikutajia baadhi ya watu ambao mimi nawafahamu nilifanya nao kazi wenye maarifa makubwa kabisa, nikamtaja Profesa Ndullu, ni mtu mwenye uwezo mkubwa, nikamtaja Ndugu Mafuru aliekuwa TR lakini bado kuna watu kama Dkt. Kimei aliyekuwa Mkurugenzi wa CRDB hawa ni watu wenye maarifa makubwa sana, watumie watu hawa tutoke hapa tulipo. Kupunguza umaskini kutoka asilimia 28 kuja asilimia 26 nadhani Waheshimiwa Wabunge mtakubaliana na mimi kwamba hiyo kasi ni ndogo sana. Ni vyema tujikite watu wenye maarifa watusaidie katika maeneo ambayo nina hakika tunaweza tukajikwamua.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mheshimiwa Waziri kwa muktadha hu huo haya mazao muhimu nimemsikia sana ndugu yangu Ndassa amezungumza vizuri sana zao la pamba, hayo mazao ya kimkakati, zao la pamba, korosho, kahawa na chai, Mheshimiwa Waziri hayo mazao yanaanguka/yanaporomoka. Ushauri wangu kikosi kazi hicho hicho wataalam wanaokusaidia Mheshimiwa Waziri basi wakae chini waangalie ni kwa nini pamba inaanguka sasa hivi, ni kwa nini korosho tunaingia kwenye migogoro mikubwa sana. Ni kwa nini kahawa inaanguka vilevile katika masoko yetu. Nafikiri mambo hayo yatatusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuema hayo, nina mawili madogo ya mwisho; la mwisho ni ujenzi wa reli ya SGR. Mimi Mbunge wa Kigoma nisipozungumza SGR hakuna atakayenielewa. Mheshimiwa Waziri, naendelea kukusisitiza katika mikakati endelevu na bahati nzuri juzi Rais wa Congo/Rais wa DRC Mheshimiwa Tshisekedi amezungumza juu ya biashara. Huwezi ukafanya biashara na Congo kama huwezi kujenga SGR kwenda Kigoma. Lile tawi la Tabora – Kigoma kwa maoni yangu tulipe kipaumbele kwa sababu fedha nyingi na mzigo mkubwa uko Congo ya Mashariki ambapo msigo ukifika Kigoma utaingia kwenye tishari na utavuka kwenda DRC Congo. Pia usisahau ile Nickel ilioko Msongati ya Burundi ni tawi lile la kutoka Uvinza kupita Kasulu kwenda mpaka Msongati ya Burundi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nafikiri tujielekeze kiuchumi, kibiashara na hayo ni maeneo ambayo yana mzingo mkubwa na mzigo mkubwa huo ndiyo utakaosaidia uchumi wetu na kujenga matawi mengine ya reli na mambo mengine ya kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa nizungumzie suala la... na hili nalisema sana, mikoa ambayo iko nyuma nchi hii ina mikoa minne iko nyuma kuliko mikoa mingine yote na sababu za kuwa nyuma si kwamba wale watu ni watu wajinga, la hasha! Ni watu wenye maarifa lakini wamekwazwa na madhila ya historia. Mikoa hiyo ni Kigoma, Katavi, Singida na Rukwa. Nilitarajia Mheshimiwa Waziri kuliko kugawa rasilimali tu pro rata tunaita, kwa watu wote sawa, nafikiri wakati umefika nammshauri Mheshimiwa Rais Magufuli ana uelewa mkubwa katika masuala haya kwamba ile mikoa ambayo iko nyuma kwa sababu za kihistoria nashauri kabisa Mikoa ile ipewe upendeleo maalum na upendeleo huo maana yake slow match na quick match. Ile mikoa iliyoko nyuma na yenyewe iweze kuwa katika usawa na mikoa mingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa ni Gridi ya Taifa; mikoa miwili bado Mheshimiwa Waziri wa Fedha haijaungwa kwenye Gridi ya Taifa. Ni muhimu sana mikoa hii ya Kigoma na Katavi nayo ifanane na mikoa mingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja hii na nasisitiza hotuba hii/bajeti hii ni ya msingi sana. Imejikita kwenye maeneo ya msingi kabisa. Hongereni na chapeni kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja hii. Waziri na timu yake hongereni sana kwa kazi. Ninayo mambo machache ya kuishauri Serikali na Wizara hii.

(a) Wazo la eti wasichana wanaopata mimba, warejeshwe shuleni ni dhahiri halina mashiko na halina msingi. Hatuwezi kuanza karne hii eti kuhamasisha watoto wa kike akipata mimba arejeshwe shuleni. Hii haikubaliki, haifai na kama Bunge tusishabikie jambo ambalo madhara yake ni makubwa sana. Tuendelee kupiga vita tabia ya zinaa mashuleni.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, vitabu vya kufundishia visivyo na ubora ambavyo vimeshasambazwa mashuleni kwa mamilioni:-

(i) Vitabu hivyo vyenye makosa viondolewe mashuleni haraka iwezekanavyo.

(ii) Waliohusika na ujinga huo wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kuwastaafisha kazi zao hata ikibidi kuwafukuza. Ni jambo la aibu sana kwa Serikali yetu na kwa Chama chetu cha Mapinduzi.

(iii) Fedha na gharama iliyotumika kuchapisha vitabu hivyo ilipwe na wahusika haraka sana ikiwa ni pamoja kuwafilisi mali wanazomiliki ambazo zitakuwa zimepatikana kwa wizi na udanganyifu huo.

(iv) Walioviandika vitabu hivyo na makampuni yao wasipewe kazi hiyo tena. Wasipewe tender tena za kuandika na kuchapisha vitabu.

(c) Chuo cha FDC Kasulu; chuo hiki ni kikongwe sana na kimechakaa, kilijengwa mwaka 1974. Ninaomba sana chuo hiki kiwemo katika vile vyuo kumi vitakavyofanyiwa ukarabati, kama hotuba ya Waziri ilivyobainisha ukurasa wa 93 – 94. Mkoa wa Kigoma upo nyuma sana kielimu na hata kiufundi. Kigoma na hususani Kasulu tuna kila sababu ya chuo chetu kuongezewa ubora wake wa miundombinu.

(d) Kuhusu maktaba ya Wilaya ya Kasulu; ninaomba sana Wizara ya Elimu iangalie uwezekano wa kukamilisha jengo lenye ghorofa moja la maktaba ya Wilaya ya Kasulu ambalo lilianza kujengwa 2007 kwa nguvu za Mbunge wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu. Jengo hilo linahitaji vifaa vifuatavyo:-

(i) Finishing ya Ndani (milango, ceilings, gates na kadhalika).

(ii) Kuboresha mazingira ya nje ikiwemo kujenga uzio wa tofali ili kuimarisha eneo hilo.

(iii) Gharama ya takribani shilingi milioni 200 - 300 inaweza kabisa kukamilisha jengo hilo na likaanza kutumika. Wizara isaidie nguvu na juhudi ambazo tayari Wilaya imefanya.

(e) Kusaidia kukamilisha maabara za sayansi zilizopo katika Mji wa Kasulu. Majengo ya maabara katika shule zetu nyingi za sekondari zipo katika hatua mbalimbali kuanzia asilimia 40 hadi 70 za ujenzi. Wizara kwa kutumia fursa mbalimbali kama vile P4R Programs na Equip Tanzania Projects inayotekelezwa katika Mkoa wa Kigoma. Ni vizuri juhudi za pamoja kati ya Wizara na Halmashauri zetu tuwe na mpango wa kukamilisha maabara hizi, ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hongera kwa kazi, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Hata hivyo, nitoe ushauri ufuatao:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara/Serikali ije Bungeni na mpango mkakati (strategic plan) wa kuhifadhi vyanzo vya maji nchini. Nchi hii ina mito, maziwa na hata mabwawa madogo ya asili. Ni vizuri Serikali ikafikiria namna bora ya kuhifadhi vyanzo vya maji. Mfano, Mkoa wa Kigoma una vyanzo zaidi ya 1,000. Serikali ije na mpango shirikishi ambao utazishirikisha Mamlaka na Halmashauri zetu ili kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji ambavyo vinaharibiwa kwa kasi ya ajabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa maji utakaofadhiliwa na Serikali ya India kwa USD 500, kati ya miji itakayonufaika na fedha hizo ni pamoja na Mji wa Kasulu. Nashauri sana process hii iharakishwe ili wananchi wetu wanufaike na huduma ya maji. Aidha, katika Mji wa Kasulu, maji yaliyopo/yanayotoka ni machafu na yamejaa tope. Tafadhali Wizara ije na mpango wa dharura kwa ajili ya maji katika Mji wa Kasulu. Maji ni machafu, Wizara chukueni hatua za dharura.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ya maji ya muda mrefu katika Wilaya ya Kasulu iliyoanza miaka ya 1980, mfano Mradi wa Maji wa Ruhita (Ruhita Water Scheme 1984) ni mradi wa siku nyingi. Nashauri Wizara itume wataalam wa maji waende Wilaya ya Kasulu wasaidiane na Halmashauri ya Mji wa Kasulu (Kasulu TC) ili Miradi ya Maji ya Ruhata, Kanazi, Mrufiti na Msambara itazamwe upya hatimaye mkakati wa rehabilitation uanze/uandaliwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja ya Wizara hii, hata hivyo nina ushauri kwa Serikali kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, issue ya wakimbizi katika Mkoa wa Kigoma tangu tupate uhuru, Mkoa wetu wa Kigoma umekuwa ndiyo makazi ya wakimbizi watokao DRC, Burundi, Rwanda. Ni vizuri sasa Serikali yetu ikaanza mkakati wa kuwarejesha wakimbizi hawa kwao, kwa kiwango kikubwa DRC ipo salama katika maeneo mengi, kwa nini raia wao waliopo Nyarugusu mkoani Kigoma wasirejeshwe kwao na/ au kulindwa katika nchi yao? Kwa nini makambi haya yasifunguliwe ndani ya nchi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, athari za wakimbizi ni nyingi sana ikiwa ni pamoja na usalama wa wanavijiji wetu, kusambaziwa maradhi mengi ikiwemo maradhi hatari ya Ebora na mengine mengi, Kigoma sasa inahitaji utulivu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jumuiya ya Kimataifa kusaidia maeneo yaliyoathirika na ujio wa wakimbizi katika Mkoa wa Kigoma, lazima Serikali sasa ibuni na ije na mkakati wa namna bora wa kusaidia wananchi wa Kigoma ambao wamehifadhi wakimbizi tangu enzi ya Uhuru miaka ya 1960. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kusaidiana na Wizara ya Mambo ya Ndani kaeni pamoja ili mjenge programu ya aina hii; “Refugees Host Area Program” Mheshimiwa Waziri do something on Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii, hata hivyo nitoe ushauri na maoni yangu katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinzi na usalama page 56. Idara ya Uhamiaji na matendo ya unyanyasaji wa raia hasa wanaoishi katika mipaka ya nchi yetu na hasa wananchi wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma. Imekuwa ni desturi hasa kwa wenzetu wa Idara ya Uhamiaji kushika watu, kunyanyasa watu eti kwa sababu ni wahamiaji haramu au uraia wao unatia mashaka. Niombe sana Ofisi ya Waziri Mkuu itoe maelekezo ya kiutawala juu ya mwenendo wa Idara ya Uhamiaji na hasa katika Mkoa wetu wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo yafuatayo yazingatiwe; heshima kwa wanachi wa Kigoma na kamwe watu wasitambuliwe kwa sura zao, lugha zao na maumbile yao. Weledi utawale na ikibidi mafunzo zaidi ya utambuzi wa nani ni raia na nani si raia yafanyike kwa uharaka. Baadhi ya wananchi wa Kigoma wanaamriwa na Idara ya Uhamiaji wapeleke vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wao na babu zao. Mambo ambayo ni vigumu sana kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara kadhaa ni kuendeleza unyanyasaji na usumbufu kwa wananchi wa Kigoma, Kasulu, Kibondo Kakonko na Uvinza. Aidha, kwa nini shida hii iwe zaidi kwa Mkoa wa Kigoma ilhali mikoa mingi ya mpakani hatusikii. Viongozi wa kisiasa, dini wanaharakati na hata wasanii mashuhuri wanatoka katika Mkoa wa Kigoma kudhaniwa na kuhisiwa siyo raia, jambo hili linatia simanzi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo matukio ya hovyo ambayo viongozi mbalimbali watokao Mkoa wa Kigoma wameitwa uhamiaji kwa mahojiano na wengine hata kupelekwa kolokoloni kwa sababu tu ya kuwa wenyeji wa Kigoma. Tafadhali haki itendeke kwa wote na mtindo wa sasa wa kukomoana, vitisho na hata kuoneana ifike mwisho, watu wetu wa Kigoma wanajihisi ni raia daraja la pili. Jambo ambalo siyo sahihi, raia wetu wote wapo sawa katika nchi yetu, tusitengeneze matabaka bila sababu za msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakimbizi na wahamiaji haramu watambuliwe, naomba sana Serikali na hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu ifanye kazi ya kuwatambua wakimbizi, wahamiaji haramu na wahalifu ili watofautishwe na raia wema na wakazi wa Mkoa wa Kigoma. Wakimbizi wetu wa DRC na Burundi zipo tamaduni tunazofanana, tamaduni hizo zisiwe sababu ya watu wetu kudhaniwa ni wakimbizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu vizuri juhudi za Serikali yetu, lakini Mkoa wa Kigoma kupokea wakimbizi isiwe laana, tunapokea wakimbizi kwa niaba ya Taifa lote, vitendea kazi kwa Idara ya Uhamiaji na Polisi changamoto ya vifaa vya kazi na wanafanya kazi katika Idara hizi mbili katika eneo lenye wakimbizi ni tatizo kubwa. Idadi ya Maofisa na Maaskari iongezwe, magari ya doria yaongezwe, malipo ya motisha kwa wafanyakazi wa Idara hizi yatazamwe upya na yaongezwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii.
Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja hii. Hata hivyo nina ushauri kwa Wizara kwa mambo yafuatayo:-

(i) Barabara ya Kidahwe – Kasulu (kilometa 63); barabara hii imeanza yapata sasa miaka 13 haijakamilika na ujenzi wake ni takribani asilimia 30 tu. Tatizo kubwa ni kwa sababu barabara hii pamoja na kipande cha Kabingo/ Nyakanazi (kilometa 50) hazipewi kipaumbele kabisa. Tafadhali namwomba Waziri a-fast track process ya kujenga barabara hizi kama sehemu ya barabara kubwa ya Kidahwe – Nyakanazi. Sisi wananchi wa Kigoma sasa tumechoka kusubiri barabara hii. Kwa maoni yangu juhudi zinazoendelea ni njema lakini muda ni jambo la msingi sana. Haiwezekani tusubiri zaidi ya miaka 26 barabara hii.

(ii) Barabara za Lake Tanganyika chini ya Lake Tanganyika Transport Programme (LTTP/FS&DD), hizi ni barabara zipi na zina urefu gani?

(iii) Barabara ya Kasulu – Manyovu, chini ya mpango wa barabara za Afrika ya Mashariki inaanza kujengwa lini? Timeline yake ikoje? Tusubiri tena miaka mingapi?

(iv) Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Standard Gauge; juhudi zinazofanyika kujenga reli hii ni za msingi sana, Dar es Salaam - Morogoro na Morogoro - Makutupora kazi inaendelea vyema. Ajabu ni shilingi bilioni 100 kutengwa kwa ajili ya Isaka – Rusumo - Kigali. Mantiki ya kibiashara na kiuchumi ya kuanza kujenga kipande hiki ni nini hasa? Je, ni kuisaidia nchi ya Rwanda kupata reli au ni kuifanya Kigali iwe business hub ya nchi za Maziwa Makubwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, binafsi siungi mkono kabisa ujenzi wa kipande hiki kwa sasa kabla ya kujenga kipande cha Dodoma - Tabora. Pesa hiyo shilingi bilioni 100 ihamishwe na ipangwe kujenga kipande cha Dodoma - Tabora. We have to be strategic and forward looking. Tukifanya makosa shida na adhabu yake ni kubwa sana. Reli ni uchumi mpana.

(v) Mawasiliano vijijini na mijini; minara ya simu sehemu mbalimbali za nchi yetu ipo vizuri. Hata hivyo, baadhi ya maeneo ya Kata ya Muhunga, Kijiji cha Marumba mawasiliano ni taabu sana. Ili upate network yakubidi upande mti au usimame juu ya kichuguu. Aidha, katika Kijiji cha Karunga, Kata ya Heru Juu mtandao unasumbua sana.

KIJIJI KATA JIMBO WILAYA
Karunga Heru Juu Kasulu Mjini Kasulu
Marumba Muhunga Kasulu Mji ni Kasulu
Mwanga Mganza Kasulu Mji ni Kasulu

Tafadhali sana wenzetu wa Mawasiliano kwa Wote wafanye juhudi ili kuondokana na usumbufu huu kwa wananchi wetu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mambo yafuatayo yazingatiwe hasa katika Mkoa wa Kigoma na Jimbo la Kasulu Mjini.:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la umaliziaji wa nyumba za Polisi Kasulu Mjini zipo Blocks nne zinazohitajika kukamilishwa ujenzi wake. Nyumba hizi zina uwezo wa kuishi zaidi ya familia 20 za Askari Polisi. Tafadhali kamilisheni nyumba hizo kwani ni muhimu sana kwa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi. Barua ya mchanganuo nimeiwasilisha kwa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa hatua zaidi tangu mwaka 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo umuhimu wa kuongeza idadi ya Askari katika Wilaya ya Kasulu ambayo ni kubwa na ina changamoto nyingi sana, pamoja na kuwa na Kambi kubwa ya Wakimbizi ya Nyarungusa. Wilaya inastahili kupewa kipaumbele cha Askari na vitendea kazi vingine kama magari ya doria na motisha kwa Askari hawa. Wilaya ya Kasulu ni tofauti kabisa na Wilaya nyingine kwa sababu zake za kijiografia na idadi kubwa ya watu. Kasulu pekee ina idadi ya wakazi zaidi ya 800,000 hadi milioni moja sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kigoma ni Mkoa uliopo mpakani na nchi jirani za DRC, Burundi na Zambia kwa upande wa Kusini. Watu tumeingiliwa sana tangu miaka ya uhuru 1961, wakati idara ya uhamiaji wanafanya doria zao za kusaka wahamiaji haramu, wakimbizi wa wageni wakazi. Naomba sana yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Idara itumie weledi zaidi kuliko hisia, watu watambuliwe kwa hoja na siyo kwa sura zao au lugha zao za asili; Idara itumie viongozi wa Serikali waliopo katika maeneo na kamwe Maafisa hawa wasivamie watu barabarani, sokoni na kwenye nyumba za starehe; Wageni wakazi na wahamiaji haramu wanaweza kufichuliwa na viongozi wa Serikali za Mitaa katika sehemu zao;

Vizuizi barabarani siku za masoko na gulio siku ya minada kamwe zisitumike kunyanyasa raia halali wa Taifa hili kwa sababu tu wanaishi mpakani mwa nchi yetu;

Vitendo vya rushwa, uonevu na unyanyasaji kamwe visipewe nafasi katika misako ya Idara hii ya Uhamiaji;

Makamanda wa Wilaya na Vituo wawasimamie vijana wao kutenda haki na kwa mujibu wa sheria zetu; na Pia Idara ya Uhamiaji Kasulu wapewe vifaa vya kazi, mfano magari na vitendea kazi vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Magereza linafanya kazi njema sana katika mazingira magumu. Jeshi hili kule Kasulu wapewe vitendea kazi ikiwemo nyumba za kuishi. Pia Wizara iboreshe makazi ya Askari wa Jeshi hili ili ubora wa Jeshi hili uonekane dhahiri mbele ya Jamii. Jengo la Magereza Wilaya ya Kasulu ni jengo la siku nyingi sana tangu Wakoloni wa Kijerumani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jengo hili lipo katika Mji wa Kasulu. Nashauri strongly Magereza haya yahamishiwe nje ya Mji wa Kasulu. Maeneo yapo mengi; maeneo ya Tarafa ya Makele yanafaa sana kujenga gereza la kisasa. Magereza ya sasa yaliyopo yanaweza kuendelea kutumika kwa ajili ya mahabusu tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii ya Waziri. Hata hivyo, ninayo machache ya kushauri; ni dhahiri bila kutunza mazingira nchi yetu itapata matatizo mengi na makubwa. Mkoa wa Kigoma na hasa Halmashauri ya Mji Kasulu ulibahatika kutembelewa na timu ya wataalam wa mazingira na vyanzo vya maji. Timu hii ilimaliza kazi na kutoa ripoti yake mwaka 2017. Kazi kubwa iliyofanyika ni pamoja na kutembelea vyanzo vya maji vilivyopo Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Vyanzo kadhaa vilifanyiwa tathmini na utafiti wa kina baada ya taarifa ile ya kitaalam niliamini kwamba hatua za utekelezaji zimechukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona hotuba yako ya Bajeti 2019/2020, ukurasa wa 83 (xi) kwamba moja ya kazi zitakazotekelezwa mwaka huu ni kupitia miradi iliyowasilishwa na wadau ili ipate wafadhili wa Mfuko wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Je mradi wa ulinzi wa vyanzo vya maji zaidi ya 25 katikaHalimashauri ya Kasulu Mjini ni sehemu ya mkakati huu? Naomba Wizara yako ifahamu kwamba maji yanayotiririka kutoka uwanda wa juu wa Heru Juu, Buhigwe maji hayo hatimaye hutiririka hadi Ziwa Tanganyika. Ulinzi wa vyanzo hivi si tu kwamba ni muhimu ni jambo la lazima, tafadhali hatua sasa zichukuliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinzi wa ardhi oevu ya Malagarasi; eneo hili maarufu Malagarasi wetland linahitaji kulindwa. Eneo hili kwa kiasi kikubwa linakumbwa na uvamizi wa ng’ombe wengi kutoka baadhi ya maeneo ya nchi yetu na wakati fulani nchi jirani. Eneo hili la Ramsar Site litapotea, urithi wetu utapotea na rasilimali hii itaangamia pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri Wizara ya Maliasili na Utalii, TAMISEMI, Mambo ya Ndani na Wizara hii waje na mpango mkakati wa kulinda eneo hili, lisipolindwa ndani ya miaka mitano mpaka saba shida itakuwa haiwezi kurekebishika tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatakie Wizara hii kazi njema katika kulinda mazingira ambayo ni uhai wa Taifa letu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii. Hongera nyingi kwa Waziri, Naibu Waziri na timu yote ya Wataalam wa Wizara. Mambo ya msingi:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, Wizara ifanye fast track ya miradi ya kuunga Mkoa wa Kigoma kwenye gridi ya Taifa:-

(a) Tabora-Kigoma na Nyakanazi-Kigoma. Miradi hii ni muhimu sana, vinginevyo Mkoa wa Kigoma utabaki nyuma kama ilivyo sasa, lazima tuonyeshe tofauti.

(b) Mradi wa Malagarasi Hydro Power MW 45.4; mradi huu ni muhimu sana kwa nchi na Mkoa wa Kigoma, kupata MW 45.4 ku-feed kwenye grid ni kitu kizuri na muhimu sana. Ushauri wangu kwa Wizara ni kwamba wapeni kipaumbele mradi huu, tumeusubiri sana. Hoja ya upungufu wa fedha haina nguvu ya kimkakati, ikibidi tukope fedha tujenge mradi huu, ni muhimu sana.

(c) Malipo ya fidia; Malagarasi na Kidahwe itakapojengwa sub-station ya grid. Walipeni fedha hizi haraka ili kazi ianze kwa jinsi ratiba ya utekelezaji ilivyopangwa. Miradi hii kwa Kigoma si tu ni muhimu, hii ndiyo roho ya mkoa wetu.

Mheshimiwa Spika, pili, REA lll Kigoma, Kasulu, Buhigwe, Uvinza na Mradi huu ulizinduliwa kule Rusesa, Kasulu DC mwaka jana 2018. Speed ya mradi huu ni ndogo sana, mkandarasi aongeze nguvu. Tangu uzinduzi ule, maeneo mengi hata vifaa havijapelekwa yaani nguzo, nyaya na kadhalika. Tafadhali kasi iongezeke.

Mheshimiwa Spika, tatu, mradi wa ujazilizaji wa maeneo (densification round two). Halmashauri ya Mji wa Kasulu-TC, kata nyingi zaidi ya tisa zilipata umeme wa REA ll, tatizo/shida ni kwamba, maeneo karibu yote umeme umefika sehemu moja tu. Mfano umeme umefika sokoni, umeme umefika Ofisi ya Mtendaji na kadhalika. Umeme haujafika kwenye mitaa, vitongoji walipo wananchi wetu wengi. Nishauri strongly, Mkoa wa Kigoma sasa uingizwe kwenye huu mradi wa ujazilizi hasa katika Mji wetu wa Kasulu. Ikiwa ni heshima kwa Serikali mikoa iliyopata shida ya kuanza REA lll basi ipate nafuu ya kupata mradi huu.

Mheshimiwa Spika, Kijiji/Kata ya Mrufiti, kata hii ilisahaulika wakati wa survey, nilimshauri Regional Manager TANESCO Kigoma akiingize kijiji hiki ambacho pia ni kata ili iende sambamba na maeneo ambayo yamefanyiwa survey ya Kigondo, Muhunga, Ruhita, Ngumbigwa na sasa Mrufiti. Hii ni muhimu sana ili wananchi hawa wasionekane wametengwa kwa sasa. Maeneo yote ya jirani yamefanyiwa survey hiyo, hii ya kusema Mrufiti isubiri phase two ya survey iondoke. Wananchi hawa wanataka umeme leo.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii labda kwa kuanza ningeanza na hili la Mheshimiwa dada yangu Saada, kwa sababu ni Mjumbe wa Kamati hii, na yeye alikuwa mwalikwa kwenye Kamati hii. Na kama kuna mambo tuliyajadili mle lilikuwa ni suala hili la consumers wa facility hii ni pamoja na Serikali ya Zanzibar na tulichokiona siku iliyofuata walikuja Senior Officers toka ofisi ya Makamu wa Rais wa Zanzibar na Senior Council toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Sasa nitapenda kujua labla kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali tunaposema Mamlaka ya Zanzibar tuna maana gani? Kwa sababu kwenye Kamati tulielewa kuwa mkishakuwa na Senior Council toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na ukawa na Senior officers toka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, maana yake ni una uwakilishi wa Serikali ya Zanzibar. Sasa baadaye Mwanasheria atakuja kuidefine vizuri… (Makofi)

T A A R I F A

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, umenisemea kwamba, mimi nataka Authority ndiyo itueleze kwa sababu najua Mamlaka ya kusema na kuyadadavua haya ni Authority ambayo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hiyo nilikuwa nalifahamu vizuri sana, na bado nasisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali uje utusaidie ku-define mamlaka hiyo maana yake nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache, nitazungumzia LATRA, La kwanza, nianze hili suala ambalo
Mheshimiwa Waziri limezungumzwa na wenzetu wa Kambi ya Upinzani juu ya Powers za Board na decision ya Board tulivyokubaliana na Serikali ni kwamba decision ya Board haitakuwa kama ya Mahakama Kuu, no! Tafsiri tuliyopewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kwamba decision ya Board enforcement yake ndio itakuwa enforcement kama vile decision imetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Kwa hiyo, kuna tofauti kubwa sana hapa, kwa hiyo na bado decision ya Board mtu anaweza akakata rufaa kwa maana ya ku-appeal kwenye FCC tulizungumza vizuri, hatukubaliana na Serikali juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo tunaomba sana Serikali walizingatie na tumelijadili sana kwenye Kamati kuna ni suala la Ukaguzi wa magari. Suala la ukaguzi wa magari tuliwaeleza kwamba uko duniani, suala la kukagua magari sio la trafiki Polisi, sio kazi ya trafiki Polisi hata kidogo. Na best practice ni kwamba mamlaka kama hii tunayoiunda sasa ndio iwe na duty ya kukagua magari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na wala sio tu, uko duniani hata kutoa leseni sasa sio kazi ya Trafiki Polisi, Trafiki Polisi kazi yake ni enforcement barabarani, kwa hiyo tukasema haya mambo kwa sababu ndio tunayaanza kuyajenga hii Mamlaka ya LATRA inayokuja badala ya SUMATRA ichukue majukumu hayo professionally kukagua magari na kama alivyosema dada yangu pale hii biashara magari yanakaguliwa asubuhi wasafiri wako ndani ya gari, mambo ya kizamani sana, kama gari inakaguliwa ikaguliwe siku moja kabla au siku mbili kabla kwa ajili ya safari zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo tulilizungumza kwa kishindo sana, ni hili la magari mwisho mpaka saa nne usiku, tukasema Dunia inabadilika na tunakwenda kwenye Uchumi wa kati, Uchumi wa Viwanda, huwezi kutembeza magari mtu anatoka Kigoma, anatoka Bukoba anakuja kuishia Morogoro Chalinze, eti muda umefika saa nne hawezi Dar es Salaam, mambo ya kizamani haya, na tumelizungumza na kuomba Serikali mkakae mlitafsiri hili. Mtu anasafiri all the way toka Bukoba anaishia Chalinze eti, kwa sababu hawezi kufika Dar es Salaam kwa sababu ni saa nne imefika, tukasema mambo haya mkayaangalie vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo lilizungumzwa kwa Kiwango kikubwa sana ni adhabu, penalty tulizungumza kwa kirefu sana, jambo hili, kwamba penalty peke yake zimekuwa kubwa na nyingi sana, hazijibu hoja, ya kutii Sheria. Tulifikiri suala zima pia la elimu kwa wamiliki na watumiaji wa vyombo hivi ni jambo litakuwa la msingi sana na kamwe faini kubwa kubwa haziwezi kujibu tatizo la uvunjaji wa Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa na machache kuhusu LATRA na mambo mengi nashukuru hata wenzetu wa upinzani wamekubali mambo mengi tulikubaliana na Serikali, na ndiyo maana hata ukiangalia schedule of amendment ya Serikali ina page tano. Muswada tumeujadili sana na tunashukuru Serikali mambo mengi waliyaona na wakayachukua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda uliobaki nizungumzie kidogo suala hili la Hali ya Hewa, Muswada huu wa Hali ya Hewa ulikuwa misingi yake ilikuwa mikubwa ni minne, msingi wa kwanza ilikuwa ni control ya quality ya vifaa vinavyotumika kupima hali ya Hewa.

MWENYEKITI: Endelea tu.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante, ilikuwa msingi ilikuwa mambo manne, la kwanza ilikuwa ni Controller quality ya vifaa vya kupimia Hali ya Hewa kwamba vifaa hivi, lazima viwe na ubora unaokubalika kimataifa, ilikuwa ndiyo msingi wa kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi wa pili, ilikuwa ni accuracy ya taarifa zile kwamba wenzetu wa Meteorological Authority sasa wawe ndiyo Mamlaka ambayo inatoa taarifa za uhakika katika masuala haya ya Hali ya Hewa. Na by the way tuliambiwa kwamba Tanzania ni member wa World Meteorological Board kwa hiyo nje ya Tanzania na Wataalamu wetu ni wajumbe kwenye International Meteorological Board kwa hiyo nchi yetu inatambulika kwa ubora wa vifaa vyake na Wataalam wake katika tasnia hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na msingi wa tatu ulikuwa ni kuondoa uholela wa kutoa taarifa nashukuru nalo limekuwa taken on board kwamba wale waganga wa Kienyeji nimeona liko kwenye marekebisho ya Sheria wale watabiri wa kienyeji hawatahusika na Sheria hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu la nne, ilikuwa ni best practice haiwezekani tu Dick and Harry anatoka anatoa taarifa za hali ya hewa itakuwa hatari, tukasema kuwe na chombo Technical Professional ambacho kitakuwa kinaweza kutoa hali ya hewa. Sasa kwa ruhusa yako jambo moja tu dogo ambalo kidogo tulikuwa tunaomba Serikali.

MWENYEKITI: Nilikupa dakika tano tu ambazo ndiyo halali yako … kwa hiyo malizia..

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa, tulisema watumiaji consumers wakubwa wa Meteorological facility ni pamoja na Umma, Mashamba makubwa, Watafiti, Vyuo vya Elimu ya Juu, pamoja na Serikali yenyewe. Tukasema masuala haya kuna haja sasa kwenye Kanuni, mambo yaelezwe vizuri na kwamba Kanuni hizo zitakapokuwa zimetungwa washirikishwe wadau ili Muswada huu, uweze kuwa na maana iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kuchangiwa hayo kwa muda ulionipa, nakushukuru ahsante. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018
MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii labda kwa kuanza ningeanza na hili la Mheshimiwa dada yangu Saada, kwa sababu ni Mjumbe wa Kamati hii, na yeye alikuwa mwalikwa kwenye Kamati hii. Na kama kuna mambo tuliyajadili mle lilikuwa ni suala hili la consumers wa facility hii ni pamoja na Serikali ya Zanzibar na tulichokiona siku iliyofuata walikuja Senior Officers toka ofisi ya Makamu wa Rais wa Zanzibar na Senior Council toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Sasa nitapenda kujua labla kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali tunaposema Mamlaka ya Zanzibar tuna maana gani? Kwa sababu kwenye Kamati tulielewa kuwa mkishakuwa na Senior Council toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na ukawa na Senior officers toka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, maana yake ni una uwakilishi wa Serikali ya Zanzibar. Sasa baadaye Mwanasheria atakuja kuidefine vizuri… (Makofi)

T A A R I F A

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, umenisemea kwamba, mimi nataka Authority ndiyo itueleze kwa sababu najua Mamlaka ya kusema na kuyadadavua haya ni Authority ambayo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hiyo nilikuwa nalifahamu vizuri sana, na bado nasisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali uje utusaidie ku-define mamlaka hiyo maana yake nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache, nitazungumzia LATRA, La kwanza, nianze hili suala ambalo
Mheshimiwa Waziri limezungumzwa na wenzetu wa Kambi ya Upinzani juu ya Powers za Board na decision ya Board tulivyokubaliana na Serikali ni kwamba decision ya Board haitakuwa kama ya Mahakama Kuu, no! Tafsiri tuliyopewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kwamba decision ya Board enforcement yake ndio itakuwa enforcement kama vile decision imetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Kwa hiyo, kuna tofauti kubwa sana hapa, kwa hiyo na bado decision ya Board mtu anaweza akakata rufaa kwa maana ya ku-appeal kwenye FCC tulizungumza vizuri, hatukubaliana na Serikali juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo tunaomba sana Serikali walizingatie na tumelijadili sana kwenye Kamati kuna ni suala la Ukaguzi wa magari. Suala la ukaguzi wa magari tuliwaeleza kwamba uko duniani, suala la kukagua magari sio la trafiki Polisi, sio kazi ya trafiki Polisi hata kidogo. Na best practice ni kwamba mamlaka kama hii tunayoiunda sasa ndio iwe na duty ya kukagua magari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na wala sio tu, uko duniani hata kutoa leseni sasa sio kazi ya Trafiki Polisi, Trafiki Polisi kazi yake ni enforcement barabarani, kwa hiyo tukasema haya mambo kwa sababu ndio tunayaanza kuyajenga hii Mamlaka ya LATRA inayokuja badala ya SUMATRA ichukue majukumu hayo professionally kukagua magari na kama alivyosema dada yangu pale hii biashara magari yanakaguliwa asubuhi wasafiri wako ndani ya gari, mambo ya kizamani sana, kama gari inakaguliwa ikaguliwe siku moja kabla au siku mbili kabla kwa ajili ya safari zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo tulilizungumza kwa kishindo sana, ni hili la magari mwisho mpaka saa nne usiku, tukasema Dunia inabadilika na tunakwenda kwenye Uchumi wa kati, Uchumi wa Viwanda, huwezi kutembeza magari mtu anatoka Kigoma, anatoka Bukoba anakuja kuishia Morogoro Chalinze, eti muda umefika saa nne hawezi Dar es Salaam, mambo ya kizamani haya, na tumelizungumza na kuomba Serikali mkakae mlitafsiri hili. Mtu anasafiri all the way toka Bukoba anaishia Chalinze eti, kwa sababu hawezi kufika Dar es Salaam kwa sababu ni saa nne imefika, tukasema mambo haya mkayaangalie vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo lilizungumzwa kwa Kiwango kikubwa sana ni adhabu, penalty tulizungumza kwa kirefu sana, jambo hili, kwamba penalty peke yake zimekuwa kubwa na nyingi sana, hazijibu hoja, ya kutii Sheria. Tulifikiri suala zima pia la elimu kwa wamiliki na watumiaji wa vyombo hivi ni jambo litakuwa la msingi sana na kamwe faini kubwa kubwa haziwezi kujibu tatizo la uvunjaji wa Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa na machache kuhusu LATRA na mambo mengi nashukuru hata wenzetu wa upinzani wamekubali mambo mengi tulikubaliana na Serikali, na ndiyo maana hata ukiangalia schedule of amendment ya Serikali ina page tano. Muswada tumeujadili sana na tunashukuru Serikali mambo mengi waliyaona na wakayachukua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda uliobaki nizungumzie kidogo suala hili la Hali ya Hewa, Muswada huu wa Hali ya Hewa ulikuwa misingi yake ilikuwa mikubwa ni minne, msingi wa kwanza ilikuwa ni control ya quality ya vifaa vinavyotumika kupima hali ya Hewa.

MWENYEKITI: Endelea tu.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante, ilikuwa msingi ilikuwa mambo manne, la kwanza ilikuwa ni Controller quality ya vifaa vya kupimia Hali ya Hewa kwamba vifaa hivi, lazima viwe na ubora unaokubalika kimataifa, ilikuwa ndiyo msingi wa kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi wa pili, ilikuwa ni accuracy ya taarifa zile kwamba wenzetu wa Meteorological Authority sasa wawe ndiyo Mamlaka ambayo inatoa taarifa za uhakika katika masuala haya ya Hali ya Hewa. Na by the way tuliambiwa kwamba Tanzania ni member wa World Meteorological Board kwa hiyo nje ya Tanzania na Wataalamu wetu ni wajumbe kwenye International Meteorological Board kwa hiyo nchi yetu inatambulika kwa ubora wa vifaa vyake na Wataalam wake katika tasnia hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na msingi wa tatu ulikuwa ni kuondoa uholela wa kutoa taarifa nashukuru nalo limekuwa taken on board kwamba wale waganga wa Kienyeji nimeona liko kwenye marekebisho ya Sheria wale watabiri wa kienyeji hawatahusika na Sheria hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu la nne, ilikuwa ni best practice haiwezekani tu Dick and Harry anatoka anatoa taarifa za hali ya hewa itakuwa hatari, tukasema kuwe na chombo Technical Professional ambacho kitakuwa kinaweza kutoa hali ya hewa. Sasa kwa ruhusa yako jambo moja tu dogo ambalo kidogo tulikuwa tunaomba Serikali.

MWENYEKITI: Nilikupa dakika tano tu ambazo ndiyo halali yako … kwa hiyo malizia..

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa, tulisema watumiaji consumers wakubwa wa Meteorological facility ni pamoja na Umma, Mashamba makubwa, Watafiti, Vyuo vya Elimu ya Juu, pamoja na Serikali yenyewe. Tukasema masuala haya kuna haja sasa kwenye Kanuni, mambo yaelezwe vizuri na kwamba Kanuni hizo zitakapokuwa zimetungwa washirikishwe wadau ili Muswada huu, uweze kuwa na maana iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kuchangiwa hayo kwa muda ulionipa, nakushukuru ahsante. (Makofi)