Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Richard Phillip Mbogo (62 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza niipongeze Serikali kwa kuleta haya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2016/2017. Wamejitahidi sana kuweza kuoanisha na nimpongeze Waziri wa Fedha na Mipango na timu yake kwa kiujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika huu Mpango naomba nichangie maeneo machache kwa sababu ya muda. Jambo la kwanza ambalo ningependa nishauri, ili tuweze kuwa na maendeleo katika huu mwaka mmoja, tuendelee kupunguza urasimu uliopo katika maeneo mbalimbali, ambayo ndiyo yanaongeza kipato cha Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ambayo imeshaanza kufanyika bandarini, TRA na kwenye border zetu kama Tunduma, Kyela, Namanga kote huko tuendelee kufanyia kazi. Pia Mamlaka husika kama ya mazingira na yenyewe pia iendelee kuangalia muda ambao wana-process vibali mpaka mtu anapata kuweza kufanya shughuli ambayo ameiomba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niingie eneo lingine ambalo ni suala zima la uchumi. Ili uchumi uweze kukua kuna vigezo mbalimbali, lakini kuna michango ambayo inachangia kukua kwa uchumi na vipato vyetu. Tumeangalia kipato kimekuwa mpaka kimefikia shilingi 1,700,000/=, ni hatua nzuri ya kuonesha kwamba uchumi umekuwa, lakini kuna sekta hambazo hazikufanya vizuri katika kipindi kilichopita na hasa upande wa kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweza kufikia 3.4%, na lengo lilikuwa ni 6% na upande wa kilimo ndio eneo ambalo limeajiri zaidi ya watu 70%. Sasa tunaomba kwenye huu Mpango wa mwaka mmoja 2016/2017 na katika bajeti, Serikali iangalie matatizo yaliyojiri, tukafikia 3.4%, badala ya 6% na iweze kurekebisha na hasa ni katika fursa mbalimbali na pembejeo ambazo wakulima hawapati ipasavyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine katika Mpango huu tumezungumzia kuboresha fursa upande wa viwanda, lakini hatujagusa upande wa viwanda vidogo vidogo. Sehemu kubwa ambayo naiona bado elimu ya ujasiriamali kwa watu wetu haijafika ipasavyo na wafanyakazi wa Halmashauri hasa Maafisa Biashara, wanatakiwa waifanye kazi hiyo ili watu wetu wajue na wapate hizo fursa za kufungua biashara ndogo ndogo na hizi ziendane kutokana na maeneo husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, katika kuongeza mapato, ni Taasisi za Serikali, zamani tuliona Jeshi la Magereza likiwa ni mojawapo likijishughulisha na uzalishaji, mazao ya biashara na mazao ya chakula. Hata hivyo, sehemu nyingi sana sasa hivi za Magereza hayazalishi, sasa tatizo liko wapi? Liangaliwe na wenyewe waingie katika kuchangia kwenye pato, tunawagharamia sana Magereza lakini uingizaji ni mdogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la mapato na kukuza uchumi na swali leo limeulizwa na Mheshimiwa Risala ni utalii, mbuga ya Katavi, Ruaha, Udzungwa, Mikumi ni sehemu ambazo haziangaliwi na kupewa kipaumbele. Matatizo ambayo yameoneshwa tunaomba Serikali kupitia Wizara zake, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja ziangalie kwenye bajeti hii ya mwaka 2016/2017, kuboresha miundombinu ambayo inakwenda kwenye hizi mbuga ili tuweze kuongeza kipato, pamoja na kuzitangaza. Kwa hiyo, tunaingia gharama lakini Serikali itaingiza fedha kwa kupitia watalii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja nyingine napenda niizungumzie tena, ni kuhusu mashirika ya umma. Tumekuwa na mashirika ya umma ambayo yanaendelea kuitia hasara Serikali, hayajiendeshi kibiashara. Namuunga mkono Mbunge wa Kigoma Mjini, Mheshimiwa Zitto, suala la Air Tanzania liangaliwe, retrenchment ifanyike, watu waingie kwenye mikataba ya ajira mipya, wapunguzwe wafanyakazi na tuweze kwenda kibiashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na yote tunayozungumza hapa, lazima turejee kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, tuone kitu gani ambacho kimeandikwa na tuangalie utekelezaji. Katika ilani ya Chama cha Mapinduzi tumeahidi kutengeneza reli katika kiwango cha Kimataifa, standard gauge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, katika haya mapendekezo gharama za upembuzi yakinifu, reli mpya kuanzia Mpanda kwenda Kalema na kukarabati kuanzia Kaliua mpaka Mpanda, iingie na iwemo na reli ya kuanzia Uvinza kwenda Burundi na yenyewe iingie iwemo katika upembuzi yakinifu kwa mwaka huu 2016/2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini iwe hivyo? Kwa sababu tayari nchi ya Burundi ina uhitaji wa haraka na wenzetu wa Kongo na wenyewe kwa habari ambazo sina hakika wameshaanza kutengeneza reli ya kuja Ziwa Tanganyika ili mizigo ipitie Kalema. Sasa sisi kwa upande watu tuanze kazi haraka iwezekanavyo na tunamwomba Mheshimiwa Waziri iingie katika bajeti hii, huu upembuzi yakinifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika ripoti ya miaka mitano iliyopita ya maendeleo, tulisema tutajenga reli kilometa 2,707. Mwaka huu wa mwisho tulisema tutajenga kilometa 197, lakini tumeweza kujenga kilometa 150. Tuangalie ni wapi tulikwama, tatizo ni fedha au tatizo ni utawala? Tunaomba reli yetu ya kati iwekewe kipaumbele, iweze kutengenezwa katika kiwango cha Kimataifa na ili tuweze kuingiza mapato kutokana na mizigo ya ndani pamoja na mizigo ya nchi jirani. Hilo nalo liingie katika huu mwaka 2016/2017 na lionyeshwe kwa kutajwa kilometa zitakazotengenezwa na maeneo wapi mpaka wapi na isiwe tu nadharia inayotaja idadi bila kujua na maeneo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nichangie kwenye suala zima la elimu. Tumeelezwa kwamba kutokana na mafunzo ya kiujumla kusomesha watu, lakini kuna Kanda nyingine hakuna Vyuo Vikuu. Tanzania ukanda wa Mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa ukanda ule pia hakuna Vyuo Vikuu. Sasa katika kugawa rasilimali kijografia na yenyewe tuangalie tuweze kupata Chuo Kikuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba vilevile niongezee katika suala zima la miundombinu. Tumeeleza fursa Tanzania ni nyingi na lazima kuwe na viwezeshi, kiwezeshi kimojawapo pia ni kuboresha miundombinu ili wawekezaji waweze kufika. Hata hivyo, katika sehemu nyingi barabara hatuna na hasa Mkoa wa Katavi. Tuna fursa nyingi, tuna madini, gesi, mafuta, lakini barabara hakuna. Barabara ya kuunganisha kutoka Uvinza kuja Mpanda tunaomba ianze na iingie kwenye bajeti hii na pia tuweze kupewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii na naunga mkono na naomba yote niliyopendekeza yafanyiwe kazi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nimshukuru Mungu kwa nafasi hii na pia nimpongeze Waziri na timu yake kwa kazi ambayo wameweza kuifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwanza na Mamlaka ya Mapato (TRA), suala la EFD. Niliwahi kuzungumza ndani ya Bunge hili kwamba TRA katika kudhibiti mapato na kuweka uwazi, Serikali ilianzisha EFDs na ESDs, lakini kilichopo ni kwamba tuna matatizo ya kimtandao kwenye hizi mashine, kwa hiyo tunaomba TRA iweze kuangalia. Katika uhasibu tunajua katika kurekebisha mahesabu ya kiuhasibu unatoa credit note au debit note, sasa hizi signatures hazichukui taarifa za marekebisho ya kiuhasibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine lililopo TRA, tunapata malalamiko sana kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu wanavyofanya makadirio. Wenyewe wako ofisini lakini na mteja mwenyewe ndio anajikadiria kama anavyotakiwa kufanya, lakini wanakadiriwa kwenye hali ya juu tofauti na uhalisia wa biashara walizonazo. Kwa hiyo, tunaomba TRA waangalie ikiwezekana waangalie na hali halisi ya biashara mtu anayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya majukumu ya Wizara hii ni kufuatilia mapato, lakini tunaomba, bajeti ya mwaka jana tumezungumza, kuna ripoti nyingi na Kamati ziliundwa na Bunge hili huko nyuma na maarufu sana ripoti ya Mheshimiwa Chenge, kuna Chenge One na Chenge Two. Sasa hizi mpaka sasa hivi kama Wizara wamefanyia kazi kiasi gani? Tunaomba Wizara zote kwa ujumla ziweze kufanya mawasilisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusuukusanyaji wa
property tax ni majukumu ya TRA, lakini nimeangalia katika website katika ripoti yao makusanyo wameweka mwezi Novemba, 2016 tu, sasa je, mpaka sasa hivi wamekusanya kiasi gani, tutaomba Waziri wakati wa majumuisho utueleze upande aw property tax TRA wameweza kufanikisha kiasi gani kwenye makusanyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ukiangalia kwenye ripoti za TRA kuna maeneo VAT baadhi ya categories sijaona wameripoti makusanyo, je, hatuna makampuni yanayo-fall kwenye hizo categories? Kwa mfano electrical products, alluminium, motor vehicle spares and bicycle, sijaona kwenye VAT on local, hawajaripoti. Kwa hiyo, tutaomba tupate kujua nini wanachotarajia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna uandaaji wa mahesabu, TRA wakija kukagua kuna wakati wanahitaji ushahidi wa risiti, lakini sasa hivi dunia imekuwa inaenda kimtandao zaidi. Kwa mfano, unaweza kulipia umeme, kununua airtime kwa kutumia Tigo Pesa, M Pesa, sasa unavyoandika mahesabu yako unaweka reference ipi ambapo yeye staff wa TRA atakuja aridhike kwamba kweli muamala huu uliufanya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaomba Waziri haya malipo ya sasa hivi ya miamala kwenye gharama zetu za uendeshaji atueleze Serikali wataridhika kwa maandishi yoyote ambayo mtu atasema alilipa kwa Tigo Pesa, M Pesa, Halopesa au Airtel Money au kwa njia nyingine za kibenki kwa njia ya simu, kwa hiyo tutaomba utueleze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mafao, watumishi wa Posta walipandishiwa mafao toka shilingi 50,000 mpaka 100,000 Julai, mwaka 2015 lakini kuna baadhi mpaka sasa hawajaanza kulipwa. Waziri, tutaomba majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la PPRA, tuna Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2011, kuna kipengele cha 77(4) mambo ya liquidated damage na ukienda kwenye regulation ya mwaka 2013 naomba PPRA watupe mwongozo mzuri, wanavyoandaa zile Standard Tender Documents kwenye general conditions zinatofautiana kabisa juu ya liquidated damage na sheria mama pamoja na kanuni. Kwa hiyo, tutaomba Mheshimiwa Waziri tutahitaji majibu kwa nini zinatofautiana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nachangia bajeti ya Wizara ya Kilimo, nilizungumzia kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Serikali mpaka sasa haijaongeza mtaji, Mheshimiwa Waziri tutaomba utuambie ni lini Serikali itaongeza mtaji kulingana na maazimio ambayo yamekuwa yakizungumzwa huko nyuma. Pia hii Benki ya Maendeleo ya Kilimo ndiyo ambayo itasaidia mtaji kwa wakulima na tunajua asilimia 67 ya wananchi wanajishughulisha na kilimo, sasa malengo ya hii Benki ya Maendeleo ya Kilimo ni yapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa na juhudi miaka yote, tulikuwa na CRDB, haikufanya vizuri matokeo yake imekuwa benki ya kibiashara. Huko nyuma baada ya uhuru tulikuwa na Agricultural Credit Agency iliweza kutoa matrekta. Sasa leo hii benki hii ya kwetu na niliangalia kwenye website yao kwamba wanapata fedha kutoka African Development Bank, je, wamekwishapata hizo fedha? Kwa mfano, Jimboni kwangu nina wakulima wa tumbaku, wanatarajia wakope fedha kwa ajili ya shughuli zao katika riba ambayo itakuwa ni ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie pia kuhusu Tanzania Investment Bank, hii inamilikiwa na Serikali, ni kweli kuna benki kama NMB Serikali ina asilimia 31 ya hisa lakini je, taasisi nyingine za Serikali zinashawishiwa vipi kwenda kufungua akaunti huku TIB ili waongeze mzunguko wa fedha na ndiyo benki ambayo inasaidia hata mashirika yetu. Kwa mfano TRL wamekopeshwa fedha na TIB wameweza kuinua operations zao. Kwa hiyo, ni jinsi gani sasa pia taasisi nyingine za Serikali ziweke fedha zao TIB na pia na yenyewe iweze kukua kama ambavyo tunasisitiza upande wa NMB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba Waziri pia atakapokuja, katika kitabu chake amezungumzia kuhusu mitaji inayozidi, nafikiri hizi ni taasisi mbalimbali za Serikali ambazo sasa hivi zinapeleka fedha zake BOT baada ya kuondoa zile gharama sasa ni mitaji inayozidi. Mpaka Machi, wameweza kupeleka ziada shilingi bilioni 182 ambayo ni sawa na asilimia 24.1 lakini malengo ikiwa ni shilingi bilioni 756, tuna upungufu wa shilingi bilioni 574.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba hii mitaji inayozidi tumezungumza humu tunaomba tulenge kwenye maji. Tuweke kwenye upande wa maji ili Wizara ya Maji na Umwagiliaji ipate vyanzo vingine vya fedha yenye uhakika kwenye hii mitaji inayozidi, iende kwenye maji ambacho ndicho kigezo kikubwa ambacho wananchi wetu wanataka kukiona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijikite kwenye madeni ya huduma mbalimbali pamoja na watumishi. Kumekuwa na malalamiko sana, wafanyabiasara wengi wanadai Wizara zetu miaka mitano, miaka minne, mpaka sasa hawajalipwa. Sasa Serikali kulipa haya madeni ya ndani tutaomba Waziri utuambie una mkakati gani juu ya kulipa madeni ya ndani? Kuna watu wamefanyakazi walikopa, wamekuwa-charged riba, kuna wengine wamepeleka mpaka kwenye Mahakama ya Kibiashara, Serikali ina-charge interest, sasa hizi gharama za Serikali kuendelea kuchajiwa riba kwenye haya madeni, Serikali ina mpango gani wa kulipa haya madeni ya ndani ili na mzunguko wa fedha katika nchi yetu uweze kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkaguzi wa Mahesabu ya Serikali (CAG). CAG amefanya kazi nzuri sana na ameweza kutoa ripoti mbalimbali na vitabu tumeviona. Mimi tu nitoe ushauri kwa upande wa Ofisi wa CAG, kuna baadhi ya watendaji katika auditing yao nimewahi kuwauliza, nilikuwa kwenye Kamati ya LAAC, wakati wa audit tunajua audit is all about analytical review, kuna baadhi ya watendaji hawafanya analytical review na ndiyo audit inapo-base hapo. Unaweza kulinganisha, ukilinganisha tu mahesabu ya miaka miwili/mitatu na maongezeko, pale unaweza kujua kwamba hapa kuna upungufu kiasi gani au udhaifu kiasi gani, kwa hiyo niombe Ofisi ya CAG hili waweze kuliangalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa upande wa Ofisi ya CAG teknolojia ya sasa hivi ime-advance, kampuni nyingi za auditing kama KPMG, PWC, Deloitte & Touche na wengine, wameweza ku-advance kwenye technology wana-audit, wanasambaza mafaili, sasa na hii Ofisi yetu ya NAO na yenyewe huku Serikali itoe fedha ya kutosha na kwa wakati ili wapate training na kuwekeza kwenye technology. Kwa hiyo, uwezeshaji upande wa Ofisi ya CAG uendelee kuwezeshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafunzo pia kwa wakaguzi wetu, kwa mfano upande wa Halmashauri wanakagua miradi ya maendeleo, wanajua kusoma vizuri BOQ (Bill of Quantities), wanajua kulinganisha? Kuna mahali unakuta kuna variation unakuta Ofisi ya CAG know how inakuwa haipo, tunaomba waweze kupata mafunzo kwenye hayo maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, today I am too very faster. Jambo lingine naomba nirudi upande wa TRA, huko nyuma mtu alikuwa akisimamisha biashara anaambiwa andika barua, lakini sasa hivi wanasema sheria ilikuwa haisemi vile, lakini ndani ya Taasisi hiyo ya TRA wanakwambia unatakiwa ulete nil return, halafu mtu anaku-penalize karibu shilingi milioni 15, shilingi milioni 20 na mtu hakufanyabiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaomba huku TRA kama mtu hakufanya biashara na mlimbwambia aandike barua, leo hii mnamwambia alitakiwa alete nil return, how come ofisi hiyo inatoa maelekezo mawili? Basi hawa watu wasamehewe, kama Waziri kwa mamlaka yako tutaomba utoe maagizo watu ambao hawakufanya biashara na leo hii wanakuwa assessed kodi pamoja na interest na ma- penalty waweze kusamehewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Kwanza nianze kwa kuipongeza Serikali kwa namna ambavyo wameweza kufanya kazi vizuri na hasa Mheshimiwa Rais kwa sababu katika hotuba ya Waziri ameweza kutueleza mambo 10 ambayo kimsingi Mheshimiwa Rais ameweza kuyafanya vizuri kabisa.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na kwenye Kitabu cha Hotuba ya Waziri ya mapendekezo ya bajeti. Kwa upande wa mapato ya ndani amezungumzia kwamba kuna changamoto ambazo zimekuwepo au matatizo ambapo yamepelekea makusanyo yetu ya ndani hatufikii malengo katika utekelezaji wa bajeti ya 2017/2018 ambayo makusanyo ya ndani trillioni 19.9 lakini kwa mpaka Aprili tumekusanya trilioni 14 na point; ila ukichukulia miezi miwili mpaka kufikia mwezi Juni huu tarehe 30 tunaweza kufikia labda kwenye trilioni 16.

Mheshimiwa Spika, katika matatizo ambayo ameweza kuyaeleza la kwanza ni suala la ukwepaji kodi. Ningependa matatizo ambayo ameyaeleza yote, ukwepaji kodi, sekta isiyo rasmi ambayo haijaweza kurasimishwa, mazingira siyo rafiki, masuala ya EFD, udhaifu katika kuvuna maliasili na utegemezi wa mashirika ya umma, kiujumla haya matatizo Mheshimiwa Waziri hajatueleza sasa haya matatizo anaenda kutatua kwa njia gani; ningeomba Serikali itusaidie.

Mheshimiwa Spika, naomba nichangie kwenye suala kwanza la ukwepaji kodi. Siku zote Serikali imekuwa ikifuatilia na inaweka jitihada mbalimbali na hasa kwenye TEHAMA lakini bado kuna udhaifu sana katika maeneo hayo. Kwa hiyo tuombe Serikali iangalie kwa undani na kikubwa zaidi katika kuweza kudhibiti ni suala la kuwa na takwimu. Bila kuwa na takwimu huwezi ukaingia kwenye namna bora ya kudhibiti. Kwa mfano, tumekuwa tukipata malalamiko kwenye suala la flow meter kwa upande wa mafuta, kwamba kumekuwa na wizi sana na Serikali inapoteza sana mapato.

Mheshimiwa Spika, ningeomba hebu Serikali ijaribu kuangalia; kwa mfano tukiweka kwenye hizi kodi kwa upande wa mafuta twende kwa capacity ya meli kama inabeba lita 10,000 au lita milioni mbili basi tuchaji kodi kutokana na capacity ya meli ambavyo imeleta hayo mafuta. Kwa hiyo mtu akibeba under capacity au full capacity itamlazimisha aijaze meli yote mafuta na sisi tu-base kule na kwa hiyo huu wizi unaotokea kwenye flow meter tutakuwa tumeukwepa.

Mheshimiwa Spika, tuna suala la sekta isiyo rasmi, hawa Machinga; mwaka jana Serikali iliahidi kwamba itafanya usajili na vitambulisho watapewa na tuweze kuweka tozo; na Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba utekelezaji wake bado ni hafifu. Sasa je, ni lini itafanyika kwa haraka ili sekta isiyo rasmi iweze kuchangia katika mapato ya Serikali na tuweze kukidhi katika kufanya kazi za maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kuna suala la EFD’s; mwanzoni kwa juhudi za Mheshimiwa Rais aliwahi kuibua kwamba kuna watu walikuwa wanacheza na hizi EFD’s ripoti haziendi TRA, wanatoa risiti na wanaiba pesa nyingi. Je, Serikali kwa sasa hivi ina mkakati upi wa kuhakikisha kwamba record za hizi EFD’s zinasoma huko katika mitambo yetu ya TRA na ziko sahihi? Je, wamewahi kulinganisha na kama kuna utofauti wowote umetokea nini ambacho kimeweza kufanyika ili kuweza kuboresha ukwepaji wa mapato?

Mheshimiwa Spika, kwenye halmashauri zetu tunatumia PoS lakini maeneo mengine hizi PoS hazitumi ripoti katika mfumo, ni eneo lile ambalo tayari lina udhaifu. Kwa hiyo watu wanakusanya ripoti haziingii katika mfumo na wanasingizia network. Kwa hiyo hapa ni mahali ambapo tunapoteza mapato, tumeona kwamba tunadhibiti lakini bado tunatakiwa tuongeze juhudi katika kusimamia.

Mheshimiwa Spika, kuna udhaifu katika uvunaji wa maliasili, kama ni udhaifu je, ni udhaifu wa mfumo, tatizo ni mfumo au tatizo ni watendaji? Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri aje atueleze kuhusu haya udhaifu katika uvunaji wa maliasili na tumepoteza mapato, tatizo ni mfumo au tatizo ni watendaji.

Mheshimiwa Spika, kuna suala la mashirika. Waziri amesisitiza sana kwamba Ofisi ya Hazina itasimamia mashirika ambayo Serikali inapata gawio. Niombe tu, kwamba juzi hapa Mheshimiwa Rais ameteua Msajili wa Hazina, basi staff waongezwe katika hiyo ofisi na kuweza kusimamia vyema ili Serikali ipate mapato ambayo hayatokani na kodi kutokana na hisa zilizokuwa kwenye makampuni au na mashirika mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, vile vile ipo pia chini ya Kamati yako ya Uwekezaji wa mitaji ya Umma (PIC). PIC inahitaji ipate muda mzuri ambao wa tofauti ili kuweza kusimamia hayo mashirika 270 na tuweze kuishauri Serikali namna bora ambavyo itaweza kuongeza zaidi mapato yasiyotokana na kodi kutokana na hizi dividend za sehemu mbalimbali. Kwa hiyo tutaomba Kamati yako ya PIC uiwezeshe zaidi kwa muda ili iweze kufanya kazi ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mabadiliko mbalimbali ya sheria ambayo Waziri aliyapendekeza katika hotuba yake. Kwanza kuna suala la tozo kwenye mvinyo HS code 2206.00.90. Mvinyo unaotokana na ndizi mwanzoni walikuwa hawa hawalipi, lakini sasa mapendekezo kwa lita moja watalipa Sh.200.

Mheshimiwa Spika, baada ya kupiga vita suala la viroba watu wetu ambao walikuwa wanatumia zaidi viroba wamehamia kwenye banana wine ambayo ni very cheap lakini imewekewa tozo ambayo ni kubwa ukilinganisha na kwa lita. Kwa hiyo, tutaomba Waziri uone namna ya kuipunguza hii badala ya Sh.200 iwe ndogo ambayo itaweza kukidhi, kwa sababu hizi banana wine zinauzwa Sh.2,000/= elfu moja na, tofauti na hizi zingine ambazo zinauzwa karibuni Sh.8,000/= mpaka Sh.12,000/=, Sh.15,000/=. Kwa hiyo hii tutaomba, nami naweza kuweka hata schedule of amendment tutakavyoweza kukubaliana.

Mheshimiwa Spika, kwenye mabadiliko ya kodi kuna suala la asilimia 10. Awali mapendekezo wameweka tu kwamba ni youth and women, lakini tulikuwa tuna vijana, wanawake na walemavu, kwa hiyo ilikuwa ni four, four, two. Kwa hiyo nitaomba hii ibadilishwe iendane na haya mapendekezo kama ilivyokuwa awali.

Mheshimiwa Spika, pia tulifanya mabadiliko ya produce cess, mwaka jana kutoka asilimia tano mpaka tatu. Hii imepunguza sana mapato kwenye halmashauri zetu ambapo kwa mfano wanunuzi wa tumbaku halmashauri mapato yameshuka. Sasa kwa nini wasiangalie kwa sababu haijamfaidisha mkulima na imefaidisha zaidi hawa wanunuzi wa haya mazao kama ya tumbaku.

Mheshimiwa Spika, vile vile katika mabadiliko ya sheria hapa kwenye Amendment of Local Government Finances Act, clause 35; kwamba corporate entity ambayo ina-produce hizi agricultural crops na hai-add value ndiyo ambayo itaenda kulipa zile produce cess. Hata hivyo, tuna wakulima ambao wengine wakubwa hawapo kwenye corporate, sasa hawa wanaenda kuchangia vipi katika kuweza kulipia mapato? Mtu anaweza akawa analima takribani heka 500, heka 200; sasa hapa wamesema tu ni corporate na mtu hayuko kwenye corporate. Hilo eneo nalo ni bora kuangalia.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni kwamba katika hotuba yake Mheshimiwa Waziri alizungumzia kuhusu balance of payment (Urari). Tumeona kwamba tunaagiza sana ngano nje na mafuta ya kula na tumeona kwamba katika hotuba yake mwaka mmoja wameweza kuongeza tozo kwenye mafuta ya kula ili tuweze ku-promote zaidi ukulima wetu wa ndani. Hata hivyo, naona tatizo hapa, kwamba ni jinsi gani tunawezesha na kuvutia wakulima wakubwa ambao watakuwa kwenye economies of scale na wanalima kwenye large scale ili tuweze kupunguza ulipaji wa fedha zetu za kigeni nje kwa ajili ya kuagiza malighafi za ngano na mafuta ya kula.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusiana na mambo mazuri ambayo Mheshimiwa Rais ameyafanya. Sisi Mkoa wa Kigoma na Mkoa wa Katavi umeme awamu wa tatu REA III bado mpaka tunavyozungumza hivi haujaingia; na tunamwangusha sana Mheshimiwa Rais kwa sababu ya matatizo ambayo yametokea katika tender ambazo zimekuwepo, kesi inapigwa dana dana kila siku. Wananchi wetu wanaendelea kuulizia kuhusu huu umeme. Kwa hiyo niombe Serikali ifikie mahali sasa jambo hili liweze kukamilishwa na wananchi wakaweza kupata huduma ya umeme ambayo tayari tunaitegemea sana kwa maendeleo yetu.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii. Kwanza namshukuru Mungu na pia nishukuru Wabunge wote kwa salamu za pole mlizotupatia wakati tulipofiwa na mama yetu mzazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nipongeze Serikali kwa kazi kubwa ambayo wamefanya na pia Waziri, Mheshimiwa Jafo, unafanya kazi kubwa sana pamoja na mzee wangu Mheshimiwa Mkuchika, unatumikia vyema chini ya Ofisi ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niguse suala dogo ambalo alikuwa anachangia rafiki yangu Mheshimiwa Heche kuhusiana na Mkuu wa Mkoa kuingilia kati utendaji wa Halmashauri katika Jimbo lake. Ukienda kwenye sheria, wanaotumia Wakuu wa Mikoa, The Regional Administration Act, 1997 kipengele cha 5(3) naomba ninukuu, “For the purpose of this section it shall be the duty of the Regional Commissioner to facilitate and assist local government authorities in the region to undertake and discharge their responsibilities by providing and securing the enabling environment for the successful performance by them of their duties and functions.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkuu wa Mkoa ndio mwakilishi wa Rais katika Mkoa na sheria imempa mamlaka ya kuingilia ili kuona kwamba performance ya Halmashauri inafanyika. Kwa hiyo, kitendo kilichofanyika ni chema na Halmashauri yake inapata service levy kutoka kwenye mgodi 1.5 billion. Wanapata corporate social responsibility shilingi bilioni tano. Kwa hiyo, kama kuna hali ya kifisadi ambayo imefanyika na tume iliundwa, kwa hiyo, ni sahihi kuhakikisha kwamba anadhibiti matumizi ya fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya suala hilo, naomba niingie kwenye suala letu la Mkoa wa Katavi. Bajeti ya TARURA…

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Bajeti ya TARURA…

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. RICHARD P. MBOGO: …tumepangiwa shilingi bilioni 3.6.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe…

MHE. RICHARD P. MBOGO: Tumepangiwa shilingi bilioni 3.6.

MHE. JOHN W. HECHE: Samahani tuvumiliane. Nina haki ya kutoa taarifa.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti hiyo…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbogo, tafadhali dakika moja.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Tusikilizane. Mheshimiwa Mbogo, subiri. Sasa nyie mnaongea, huyu mtu anatoa taarifa.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Bado ni ndogo sana bajeti hiyo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbogo, subiri kidogo.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, umenipa nafasi ya kutoa taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche ongea wewe siyo wenzako. Wewe ndio unatakiwa utoe taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimetulia nakusikiliza wewe.

MWENYEKITI: Haya sema hiyo taarifa.

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu ni hii; na iwe very clear. Sisi hatujakataa Mkuu wa Mkoa kuchunguza, kufanya chochote kwenye Halmashauri. Tunachokataa ni kuzuia vikao vya wananchi vi-deliberate kwenye issues za maendeleo ya wananchi. Ndicho tunachokataa. Hana sheria inayompa mamlaka hayo ya kuingilia na kujigeuza Pay Master General, hakuna sheria inasema hivyo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbogo, taarifa hiyo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama vikao vinakaa halafu havitendi haki ipasavyo, akizuia ni sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee, muda wangu naomba uulinde, utanipa na bonus.

MWENYEKITI: Endelea.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumzia kuhusu TARURA; kwa Mkoa wa Katavi tumepangiwa bilioni 3.6, ni fedha ambayo haitoshi. Tuna mtandao wa barabara kilometa 2,563 lakini ambazo zilihakikiwa na ile tume ni kwenye 2,400 na kitu, tofauti ni ndogo sana. Hata hivyo, katika mtandao huu kilometa 24 ndiyo ni lami ambayo ni asilimia moja, kilometa 511 ambayo ni asilimia 20 ndiyo barabara ya changarawe na kilometa 2,027 ambayo ni asilimia 79 katika Mkoa mzima wa Katavi ni za udongo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamoto hii ya ufinyu wa bajeti ambayo tunatengewa Mkoa wa Katavi, naomba sana Mheshimiwa Waziri Jafo na watendaji wa TARURA na kama wako humu ndani naomba walichukue hili; randama hii wakaiboreshe watuongezee iwe angalau bilioni tano. Kwa sababu Mkoa wa Katavi tunatunza mazingira, tuna mvua nyingi tunapeleka maji Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa na kadhalika, sasa barabara hizi kipindi cha masika hazipitiki. Kwa hiyo tunaomba tuongezewe toka bilioni 3.6 ifike angalau bilioni tano. Ilishangaza sana, kuna halmashauri karibuni 11 zinazidi mkoa mzima, kwa hiyo tunaomba suala hili Mheshimiwa Waziri Jafo na timu yake na watendaji wa TARURA walifanyie kazi, bajeti sio Biblia, bajeti sio Msahafu inaweza ikaboreshwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kuhusiana na mapato kwenye halmashauri zetu. Halmashauri za Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Nsimbo ambayo tunalima tumbaku pamoja na Chunya, kampuni za ununuzi wa tumbaku zimegoma kutulipa tozo kutokana na kudai fedha zao za marejesho ya VAT (VAT refund). Kwa hiyo, tuombe kama wahusika wa Wizara ya Fedha na wa TAMISEMI watusaidie ili tuweze kupata fedha na tutekeleze miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie suala la utawala bora; hii Sheria ya Regional Administration Act ya 1997 imewapa madaraka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuweza kutoa amri ya kumkamata mtu. Kuna wakati mwingine utekelezaji wake umekuwa hauendani na sheria inavyosema. Niombe Waziri wa Utawala Bora pamoja na Serikali kiujumla na tunajua muda mrefu semina zimetolewa, mafunzo na maonyo mbalimbali kwa watendaji wetu watekeleze sheria hii ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mfano mzuri, naomba ku-declare kabisa, nina mzee wangu anaitwa Ernest Wamryoma alikamatwa tarehe 24, Machi akiwa anatetea ardhi yake aliyoshinda Mahakama Kuu ya Ardhi na Mahakama Kuu ya Ardhi Kikatiba, Ibara ya 107A(1) ndiyo chombo chenye kutenda haki. Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mheshimiwa Sara Msafiri hajamtendea haki mzee Ernest Wamryoma kwa kumyanyasa na ameshinda Mahakama Kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Lukuvi, katika masuluhisho yake ya matatizo ya ardhi huwa anasema jambo lolote ambalo limeamuliwa na mahakama lisiletwe kwenye ofisi yake. Sasa niombe Waziri, Ofisi ya Rais suala la Utawala Bora, naomba asaidie Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aache kumsumbua huyu mzee, kashinda Mahakama Kuu na aliyemshinda alikuwa amemkaribisha tu, aache mahakama ambavyo imekwishaamua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Uchaguzi wa Vijiji na Serikali za Mitaa mwaka huu. Sasa kwa Nsimbo tuna Makazi ya Wakimbizi ya Katumba, tuombe mtoe mwongozo jinsi gani ambavyo kutokana na hadhi ya makazi ipo Katumba, Mishamo na Ulyankulu, namna gani uchaguzi wa vijiji utakwenda kufanyika na tuna sheria ya upande wa Wizara ya Mambo ya Ndani kuhusiana na wakimbizi ambapo tayari bado maeneo haya yako chini yao. Kwa hiyo tuombe tupate mwongozo jinsi gani uchaguzi utakwenda kufanyika kwenye maeneo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusiana na madeni ya watumishi; ukiangalia hesabu za halmashauri utakuta kuna receivable, wanadai na kuna payable wanadaiwa na watumishi kutokana na maslahi yao mbalimbali, hususan uhamisho na madaraja waliyopanda. Kwa hiyo tuombe watumishi wetu katika halmashauri Serikali itoe fedha ili waweze kulipwa malimbikizo yao ambayo yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni kuhusiana na uchangiaji wa jana wa kaka yangu, Mheshimiwa Mchungaji Msigwa, alizungumzia consequences kwenye SGR, kwenye ndege, kwenye Stiegler’s Gorge. Uwekezaji wowote una return on investment; Air Tanzania ita-promote utalii na kuanzia baada ya miaka minne ijayo itakuwa inafanya kwa faida, hizo ndiyo positive consequences. Kwenye SGR tutakwenda kunyanyua uchumi wa nchi yetu kwa kubeba mizigo toka kwenye nchi za jirani ambazo ni landlocked; Burundi, Rwanda, Kongo na Zaire. Kwa hiyo uchumi wa nchi utaongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye umeme, umeme wa maji ndiyo umeme ambao ni nafuu kuliko umeme wowote duniani. Naibu Waziri wakati anajibu swali la gesi kaeleza gharama ya gesi ni dola 5.1, kwa hiyo utaona jinsi gani kwamba umeme wa gesi uko juu kuliko ambavyo utakuwa umeme wa maji. Kwa hiyo consequences za maamuzi ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeyafanya ni positive kwa ajili ya wananchi wake na maendeleo ya taifa kiujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nimshukuru Mungu kwa kupata nafasi ya kuchangia, lakini pia niipongeze Serikali kiujumla kwa kazi ambayo wamefanya tangu walipoingia madarakani mpaka leo hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia upande wa TAMISEMI tunaelewa kabisa bajeti ya TAMISEMI ni trilioni sita ambayo ni wastani wa asilimia 20.4 ya bajeti nzima ya Serikali. Kwa hiyo, inaonesha ni jinsi gani TAMISEMI imebeba mambo mengi ambayo yanafanya huduma za jamii na mambo yote kwa karibu sana na wananchi wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo kuna mambo ambayo ningependa kuchangia katika kuishauri TAMISEMI. Jambo la kwanza upande wa kilimo; mwaka jana wakati wa kampeni Mheshimiwa Rais aliahidi kushughulikia masuala ya wakulima kulipwa fedha zao taslimu badala ya kuendelea kukopwa na Vyama vya Misingi na hawa mawakala wa mazao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tuiombe sasa, kwa kupitia Wizara yetu hii wamkumbushe au Wizara yenyewe ichukue wajibu wa kuliona suala hili kwa kushirikiana kiujumla katika Serikali waone wanalichukulia vipi. Tumekuwa na matatizo ya ruzuku, Serikali imejitoa, kwa namna nyingine tunaweza kusema maana bei za pembejeo zilipanda karibu mara mbili, sasa watu wetu wanakwenda kufanikiwa vipi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine katika masuala ya wakulima ni bajeti ambayo tunaomba iongezwe na mpango bora wa matumizi ya ardhi ili wakulima wetu waweze kupata maeneno mazuri yenye rutuba na kuweza kufanikisha masuala yote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la elimu. Binafsi Jimbo langu la Nsimbo hatuna A-level, kwa hiyo, katika maombi yetu kwenye hii Bajeti tunahitaji tuwe na A-level maana shule za sekondari tunazo takribani tano. Kwa hiyo, tunaomba tupate hiyo sekondari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba aliyotoa Mheshimiwa Waziri ameonyesha tuna vijiji vingi na vingi havina zahanati; mojawapo ni vijiji vilivyopo katika Jimbo la Nsimbo na tukizingatia kwamba Jimbo langu ni moja ya Jimbo ambalo lilikuwa lina makazi ya wakimbizi wanaotoka nchi jirani ya Burundi, kwa hiyo, huduma za kijamii zinahitaji kuboreshwa zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika yote hayo kuna jambo ambalo ni zuri sana na ni la muhimu katika maisha ya wananchi, ni kuhusu maji. Halmashauri yangu ilikuwa na bajeti mara ya kwanza shilingi bilioni 1.6 ya miradi ya maji. Serikali ilivyoshusha ceiling ikaenda shilingi milioni 703. Takribani wiki moja iliyopita ceiling imetoka shilingi bilioni 16 imeenda shilingi bilioni 14. Tumepewa ceiling mpya na ceiling hii inalingana na bajeti ya mwaka huu wa fedha 2015/2016. Maana yake hatuwezi kuajiri, hatuna miradi ya maendeleo ambayo mwaka huu haijatimizwa, imeingia kwenye bajeti mpya ya mwaka 2016/2017. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali bora tupunguze fedha za maendeleo katika maeneo kidogo kama ya barabara na sehemu nyingine, lakini sehemu muhimu ya maji tuweze kuongeza fedha ili wananchi wetu wapate maji kwa sababu maji ni muhimu sana na ukikosa maji hayana mbadala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie suala zima ambalo lipo katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri kuhusu mawakala kuondolewa asilimia 100 muda siyo mrefu ujao. Naomba ni-declare interest kwamba nina uzoefu kidogo katika eneo hilo, mimi mwenyewe ni wakala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la dhana ya kuweka mawakala ilikuwa ni kudhibiti mapato ambapo watumishi wa Halmashauri zetu walikuwa wanayapoteza kwa njia mbalimbali; aidha, kwa kuwa na vitabu hewa au kubadilisha zile nakala kutoweka copy, ndiyo maana Serikali iliamua kuweka mawakala. Pia tumeona kwamba kuna tatizo katika kuweka mawakala hawa na kutumia hizi electronic machine, tumeona Mtwara na Arusha kulingana na kwa hotuba ya Mheshimiwa Waziri imeonesha improvement kubwa kwamba mapato yameweza kuongezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto iliyopo kuna baadhi ya aina ya ushuru zitaleta shida sana. Kwa mfano, ule ushuru mdogo mdogo kwenye masoko, utatuletea taabu sana, maana yake itabidi tuongeze rasilimali watu kwa ajili ya kukusanya. Tuna ushuru mwingine wa mazao ya asili ya misitu, mazao ya biashara, mazao ya chakula na movement ya yale mazao, ndiyo maana katika hizi Halmashauri kuna mageti yanayofanya kazi saa 24, siku saba kwa wiki, mwezi mzima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maana yake, Halmashauri itabidi iajiri na tukiajiri zaidi watu tunaongeza gharama za staff, ndiyo hiyo mishahara na gharama nyingine ambazo zinahusiana na watumishi. Kwa hiyo, tuishauri Serikali, tunaunga mkono wazo hili, lakini tunaomba maeneo mengine ambayo kuna changamoto ya ukusanyaji, basi tuendelee kutumia mawakala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna mfano dhahiri; kuna baadhi ya maeneo tumepeleka watumishi wetu wamekwenda kukusanya, unakuta makusanyo yanakuja tofauti na wakala alivyokuwepo. Kwa hiyo, japokuwa tutatumia hizi electronic machine, lakini tuangalie namna ya kuimarisha udhibiti wetu wa ndani yaani internal control, lazima tuimarishe. Yawezekana ushuru wa shilingi 5,000 mtu akamkatia shilingi 2,000; lakini kwa sababu ni ya kielektroniki na imejisajili kule TRA, sasa sisi tutaona tumedhibiti lakini kumbe kuna njia nyingine ambayo tutaendelea kuporwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la kiutendaji katika Halmashauri. Mfumo wa kuandaa hizi bajeti kwenye Halmashauri yetu unatuongezea gharama na tunashindwa kuboresha huduma za jamii. Mfano mzuri, Halmashauri yangu mwezi Februari posho za kulala nje na movement zote katika kuandaa hii bajeti wametumia shilingi milioni 29. Sasa Serikali imewekeza katika Mkongo wa Taifa, tuangalie katika kutumia teknolojia na katika movement za Halmashauri zote 181 ambapo wote wanakuja Dar es Salaam ndiyo wapewe zile ceiling, wanaingia gharama kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama uongozi wa Mkoa ndiyo huo wenyewe ulete zile Bajeti na Serikali itoe zile ceiling ambazo ndiyo zenye ukomo. Maana leo inatoa ceiling ya kwanza, siku nyingine tena ceiling ya pili, kwa hiyo, tunakuwa na movement nyingi za watumishi wetu kuja Dar es Salaam. Kwa hiyo, tunaomba sana Serikali ikitoa ceiling iwe imetoa ili watu wasiwe wanakuja Dar es Salaam mara kwa mara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la kanuni za kudumu za Halmashauri, kwani zimekuwa zinakingana na miongozo inayotolewa na TAMISEMI. Kwa mfano, kuna mwongozo ulitoka takribani mwaka uliopita au mwaka juzi, unaelekeza Kamati za kudumu katika Halmashauri kama tatu, lakini kanuni inataja Kamati zote tano ni za kudumu. Sasa kipi kinafuatwa; kanuni za kudumu zilizopo au ni miongozo? Kwa hiyo, tuone ni jinsi gani iweze kuboreshwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni kuhusu fedha za majimbo zinagawanywa kwa kufuata masuala ya umaskini, idadi ya watu na ukubwa wa eneo. Kuna majimbo mengine ni makubwa lakini yana idadi ndogo ya watu, kwa hiyo, uwiano hapa hauendani kabisa. Bora tuondoe suala la ukubwa wa jimbo, tutumie idadi ya watu, hali ya umaskini ili kuwe na uwiano mzuri kwa kugawana hii rasilimali. Njia nzuri, tutumie hata ile weighted average ili Majimbo yetu yapate fedha kulingana na hali halisi iliyopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja na tunaomba sana bajeti yetu na kikubwa zaidi Halmashauri yangu ipandishwe bajeti yake kutoka shilingi bilioni 14 mpaka shilingi bilioni 18 ili tuweze kukidhi mahitaji katika Jimbo. Ahsante sana.
Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Kwanza nimshukuru Mungu kwa namna ya pekee ambavyo ametujalia mpaka tupo hapa na uhai tulionao.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, naomba niwashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Nsimbo kutoka Mkoa wa Katavi, kwa jinsi walivyoniamini. Nilivyowaeleza kwamba nitawatumikia, kazi tumekwishaianza, naomba waendelee kuniamini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, imesheheni mambo mazuri sana. Kwanza tukiangalia huduma za jamii na matatizo na kero ambazo zinazunguka jamii zote za Watanzania. Mimi namuunga mkono kwa hatua ambazo amechukua kuanza kushughulikia kero zetu, naamini Serikali anayoiongoza itafanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naamini kwamba Mheshimiwa Rais atafanikiwa kwa sababu amelenga pia kuongeza mapato na kupunguza matumizi. Mtanzania yeyote mfanyabiashara huwa haitaji kupata hasara katika biashara anayoifanya. Siku zote ataangalia mauzo yaongezeke na apunguze gharama. Mheshimiwa Rais wetu ameliangalia hilo ili aweze kuboresha na kupeleka fedha nyingi kwenye miradi. Mimi namuunga mkono mapato yaongezeke na matumizi yapungue na sisi Wabunge tutaendelea kumshauri maeneo mengi ambayo yatakuwa na upotevu wa fedha ili ziweze kuongezeka na wananchi wetu waweze kufaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu la Nsimbo limezungukwa na kero nyingi sana. Kwanza, wananchi wangu zaidi ya 80% au 90% ni wakulima wa mazao ya biashara na mazao ya chakula. Ndiyo maana mkoa wetu ni moja ya mikoa inayotoa chakula kingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna matatizo ya ardhi kuchoka sana, maeneo mengi tumekuwa hatupati mazao ipasavyo. Pia kuna tatizo la pembejeo na tunamwomba Waziri wa Kilimo katika ile ziara yake ya Tabora afike mpaka Mkoa wa Katavi ili aweze kuliangalia suala hili. Tunajua Naibu Waziri alipita lakini ratiba yake ikuruhusu pia kukanyaga na Jimbo la Nsimbo. Wakulima wa tumbaku wanapata taabu sana, kodi ziko nyingi, makato mengi, mikopo unamlipia hata yule ambaye hakuhusu. Kwa hiyo, tunaomba awaangalie sana wakulima. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu la Nsimbo ni jipya, kuna kata zimeongezeka na mojawapo ni kata ambazo zilikuwa ni makazi ya wakimbizi lakini Serikali ya Awamu ya Nne ilitoa uraia na mwaka jana wamepiga kura, tumepata Madiwani. Hata hivyo, zile kata zina mahitaji mengi sana. Kwanza, bado ziko kwenye hadhi ya Mkuu wa Makazi, kwa hiyo sheria iliyopo pale ni ya Mkuu wa Makazi, utendaji wa Halmashauri pale ndani umekuwa hauendi ipasavyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimwombe Waziri wa TAMISEMI kaka yangu Mheshimiwa Simbachawene, awasiliane na Waziri wa Mambo ya Ndani, kata au maeneo yaliyokuwa makazi ya wakimbizi ya Katumba, Mishamo na Bulyanhulu tuangalie jinsi gani hadhi za makazi ya wakimbizi zinafutwa yabakie kuwa maeneo huru ya raia. Wale raia ambao hawajapata uraia, nimkumbushe Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni aliahidi kwamba suala hili litashughulikiwa haraka ili waweze kupewa uraia.
Kwa hiyo, tunaomba sana ahadi ya Mheshimiwa Rais itekelezwe wale ambao bado wapate uraia na makazi hayo ya wakimbizi hadhi yake ya ukimbizi iondoke ibakie eneo huru.
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu lina kata 12 tuna vituo vya afya viwili tu na zahanati ni chache mno, vijiji vingi havina zahanati. Kwa hiyo, taabu ya huduma kwa mama zangu ambao ndio mara nyingi wanahitaji huduma za afya, imekuwa ni shida. Vilevile Jimbo langu la Nsimbo, sekondari ya juu hakuna na sekondari za kawaida ziko chache mno na tuna kata mpya. Kwa hiyo, tunaomba Serikali katika bajeti hii iliangalie kwa jicho zuri kabisa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunakumbwa na shida ya miundombinu na Jimbo la pili baada ya Mheshimiwa Rais kufungua kampeni mwaka jana lilikuwa ni la Nsimbo baada ya Jimbo la Mpanda Vijijini. Nilimwomba barabara kutokea Kanoge – Mnyake - Msaginya na aliahidi itatengenezwa kwa fedha za ndani. Nami nitamwomba Waziri ndugu yangu Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa anisaidie liingie kwenye bajeti ya mwaka huu 2016/2017.
Mheshimiwa Naibu Spika, yako mambo mengi, tunashukuru Serikali ya Awamu ya Nne, alhamdulillah imetupa majimbo, Halmashauri na pia umeme. Nimshukuru Mheshimiwa Profesa Muhongo kwa umeme wa vijijini, kata nne zimepata umeme lakini pia tupate umeme kwenye kata zilizobakia. Vilevile Halmashauri yangu inahitaji Wakuu wa Idara, kati ya Wakuu wa Idara 19 waliopo ni nane tu wengine wanakaimu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Rais, naomba tuangalie suala la viwanda ambalo lipo hata kwenye Mpango wa Miaka Mitano, tumesahau pia kuangalia viwanda vidogo vidogo. Kuna maeneo mengi ambayo tunahitaji viwanda vidogo vidogo, kama dada yangu Mheshimiwa Hasna alivyochangia jana kuhusu Kigoma kwa lile zao ambalo linatengeneza sabuni, basi tuangalie viwanda vidogo vidogo kulingana na maeneo yetu tulipo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba nichangie suala la bandari, kuna mpango wa Serikali wa kujenga bandari ya Bagamoyo lakini tujue faida na hasara zitakuwaje katika uchumi wa nchi yetu. Tukiweka mwekezaji maana yake mpaka arudishe gharama yake, tuangalie na bandari tuliyonayo tutakosa mapato kiasi gani? Tunaiomba Serikali iangalie suala hili kwa jicho la karibu zaidi.
Katika hotuba ya Mheshimiwa Rais alizungumzia Air Tanzania. Air Tanzania kwa muda mrefu imekuwa inaenda kwa ufadhili wa Serikali, ndege moja gharama kubwa za uendeshaji. Serikali imepanga kununua ndege nyingine mbili kwa katika Mpango wake wa Miaka Mitano. Tusiende kihasara, ni bora watumishi waliopo walipwe, waende wakaanze maisha mapya tubakize wafanyakazi wachache ili Air Tanzania ifanye kazi kibiashara na kwa faida. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la kodi kwa wastaafu, mtu amefanya kazi miaka 30, miaka 20 analipia kodi, lakini anakuja kwenye mafao ya kustaafu pia napo anakatwa kodi na hata TRA ukiuliza formula sahihi hakuna mahali ambapo pamenyooka kuhusiana na kodi hii. Kwa hiyo, tunaomba Serikali iwasamehe wastaafu kodi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Serikali, miundombinu kwenye jimbo langu ni shida na sasa hivi Mto Koga umejaa na kuna watu wamepoteza maisha. Kwa hiyo, tunaomba reli yetu kama ilivyoahidiwa treni ipite wakati wote, fedha za dharura zije, barabara ziweze kupitika, Mkoa wa Katavi tumekuwa kama tuko kisiwani. Kwa hiyo, tunaomba sana Serikali kwa kupitia Wizara mtuangalie. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia ni kuwa ajira ni kitu muhimu kwa watu wote. Kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi tuliahidi kwamba Serikali italeta mikopo (revolving fund) ya jumla ya shilingi milioni 50. Kwa hiyo, tunaomba utaratibu uandaliwe haraka, mfuko huo uanzishwe tuupitishe ili watu wetu waweze kupata mikopo na kufanya kazi ambazo zitawasaidia katika kunyanyua uchumi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye ajira jimbo langu lina wachimbaji wadogo wa dhahabu lakini Serikali imewapeleka Kaparamsenga kwenye copper. Hiyo haina msaada na sasa hivi kuna mwombaji mpya Kijani Investment kwa eneo lililokuwa linamilikiwa na GBA.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Serikali iachie wachimbaji wadogo wadogo eneo hilo, ni kilometa kumi tu kutoka Mpanda Mjini. Bahati nzuri ndugu yangu, kaka yangu, Mheshimiwa Profesa Muhongo barua imekuja ofisini kwako ya Chama cha Wachimbaji wadogo wadogo, wakiliomba hilo eneo wapewe wao badala ya kampuni mpya ya Kijani Investment. Maana wao hawana uwezo wa kwenda kuchimba copper, mashapo hayo ya copper hawawezi, inahitaji uwekezaji mkubwa sana. Kwa hiyo, tunaomba waachiwe sehemu ambayo wataweza kupata fedha kidogo kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao, dhahabu ni rahisi kuliko copper.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia niiombe Serikali, Halmashauri zetu zinapewa ceilling ya bajeti lakini Serikali huwa haiangalii mahitaji husika ya kila halmashari. Kwa hiyo, Serikali ifanye upembuzi mzuri ili hizi ceilling za bajeti inazotoa iangalie na uhalisia wa mahitaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Rais, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napongeza Mawaziri na Watendaji wote katika Wizara kwa kuwasilisha hotuba ya makisio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ubora wa elimu na ualimu. Tumeshuhudia zaidi ya miaka kumi mitaala mingi ikifanyiwa mabadiliko ambayo yameleta shida kwa wananchi kwani ubora wake umeshuka ukilinganisha na miaka ya nyuma. Vilevile kozi ya ualimu imekuwa haizingatii viwango hasa vyuo vya watu binafsi. Walimu katika shule za Serikali na binafsi hawazingatii taratibu na kanuni katika utendaji hivyo Wizara iangalie namna ya kuboresha kanuni ziendane na wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi. Katika hotuba ya Waziri hakutaja Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha Msaginya kilichopo Halmashauri ya Wilaya Nsimbo, Mkoa wa Katavi. Taarifa za hivi karibuni ni kuwa kimehamishwa toka Wizara ya Afya. Chuo hiki kina matatizo mengi kuanzia rasilimali watu, miundombinu na madeni ya wakandarasi ambao wamesimama kazi kwa sababu hawajalipwa. Hivyo tunaomba Wizara ifanye malipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mafunzo kwa vitendo. Katika kuongeza ujuzi wa wanafunzi, tunashauri Wizara iboreshe mwongozo wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa kuanzia mwaka wa kwanza kushiriki mafunzo haya ili kuwajengea uwezo mzuri wa kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi ya Mikopo. Wizara inahitaji kuboresha utendaji wa Bodi ya Mikopo na hasa kuwawekea malengo kwa kukusanya madeni toka kwa wanafunzi ambao wanadaiwa. Pia muda wa kulipa upunguzwe tena kwa kuwa fedha inahitajika kusaidia wengine na kuondoa mzigo kwa Serikali kutoa fedha kila mara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mitihara elimu ya juu. Ili kuboresha elimu ya vyuo vikuu nchini tunashauri Wizara itoe mwongozo juu ya mitahara (course outline) zenye kuendana na hali ya sasa na pia ziwe zenye ubora na kufanana ili shahada, stashahada zipate ubora duniani.
kusahihisha uwe unashirikisha mtu zaidi ya mmoja (panel) kuondoa rushwa za aina mbalimbali kwa wanafunzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ruzuku vyuo binafsi vya ufundi. Tunashauri Serikali iangalie namna ya kutoa ruzuku kwa vyuo binafsi vya ufundi ili kuviwezesha kutoa elimu bora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, mapato, kutokana na ongezeko la mapato shilingi trilioni tatu nukta nne kuna haja ya Serikali kuangalia maeneo mengi zaidi ili kuongeza mapato kama ifuatavyo:-
(i) Kupitia upya tozo mbalimbali zisizo za kodi katika Serikali na Taasisi zake ambazo hazijapandishwa kwa muda mrefu.
(ii) Kushawisha Kampuni nyingi kuandaa mahesabu badala ya kuwa katika mlipa kodi asiyeandaa hesabu.
(iii) Kufuatilia aina zote za kodi kuwa zinatumika ipasavyo. Mfano stamp duty on contracts. Kodi hii kampuni nyingi hazilipi.
(iv) Ripoti ya kuboresha mapato “CHENGE ONE AND TWO” itumike ipasavyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo; Serikali itoe kipaumbele zaidi katika kilimo kwani mchango wake ni mdogo wa asilimia 2.9 wakati lengo ni asilimia sita hivyo suala la pembejeo lipewe kipaumbele hususani ruzuku ili kilimo cha jembe la mkono kiondoke kama ilivyoahidi Serikali. Tumbaku bado tuna tozo nyingi na mkulima ananyonywa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, tozo katika mafuta sh. 50, tunaomba Serikali iweke sh. 50 kwa lita ili kukidhi mahitaji ya wananchi juu ya maji vijijini na zahanati kwa kuwa uwezo wa halmashauri nyingi ni mdogo hivyo bajeti ya 2017/2018 Serikali ikubali ombi hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya Bunge, kutokana na changamoto za utendaji 2016/2017 tunahitaji Waziri ahakikishe kuwa bajeti ya shughuli za Bunge iongezwe kwa kiasi kikubwa kukidhi shughuli za Bunge kwa mujibu wa katiba angalau 130 bilioni.
Mheshimiwa Naibu Spika, miradi inayoendelea, Serikali ihakikishe miradi hii inakamilika ili kupunguza gharama. Tunaomba barabara ya Sumbawanga-Mpanda, Manyoni-Itigi-Tabora na Sitalime-Mpanda zikamilike 2017/2018. Pia Shirika la Reli lipewe pesa kuboresha mabehewa na ofisi ili usafiri utumike mwaka mzima hata masika.
Mheshimiwa Naibu Spika, mikataba ya msamaha; tunaunga mkono hoja ya kupitia upya mikataba hii ya msamaha wa kodi na kuwezesha Serikali kuongeza mapato pia kusaidia zaidi wakulima kufanya kilimo cha kisasa.
Mheshimiwa Mweyekiti, ubia katika uwekezaji; zoezi la uwekezaji katika ubia lipewe muda maalum ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi hususani wawekezaji wa ndani wenye uwezo wapewe kipaumbele.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu pamoja na watendaji wote katika Wizara hii ya Fedha kwa kuandaa muelekeo huu ambao ndio dira ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka unaokuja wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilivyopitia hotuba ya Waziri cha kwanza naomba nianze kugusia changamoto ambazo ameweza kuzielezea, lakini pia niipongeze Serikali kwa kuweza kukusanya mapato haya ya ndani kwa wastani wa asilimia 88.7 ambapo ni muelekeo mzuri sana katika utekelezaji wa bajeti. Ni kweli kabisa moja ya changamoto ambayo Waziri alieleza ni kuhusiana na tozo katika sekta isiyo rasmi imechangia kiasi kiasi fulani kwenye kushusha mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii tumeiona pia hata katika halmashauri zetu kwamba, kile kiwango ambacho ni fixed wanacholipa ukikilinganisha kwa siku ni kidogo tofauti na hela ambayo imezoeleka. Kwa hiyo, nitoe ushauri kwamba, Serikali ijaribu kuangalia namna bora ambayo itaenda kutumika katika kutoza sekta isiyo rasmi kwa sababu wanatofautiana madaraja kutokana na biashara wanazofanya na faida ambazo wanapata. Kwa hiyo, kuweka rate moja kwa watu wote hii nafikiri tuibadilishe tuangalie aina ya biashara na tuwe na rate tofauti tofauti angalau sasa hii itatusogeza pale ambapo tulikuwepo kuliko tunashuka chini. Niipongeze Serikali kwa kurasimisha bandari bubu, kama ilivyoelezwa na pia kuendelea kudhibiti uvujaji wa mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo mwelekeo wa huu mpango umezungumzia masuala ya bajeti ambapo ni mapato na matumizi. Kwenye matumizi to matumizi ya maendeleo na ya kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nianze na suala la mapato yanayotokana na kodi, tumeona kwamba, Serikali iendelee kudhibiti hasa kwenye ukusanyaji wa kodi upande wa import tax ambapo bado kwa mfano juzijuzi tumeona kwamba, wizi wa bomba la mafuta kwenda kwenye ma-tank unafanyika. Sasa kama hiyo tu wananchi humu mtaani wanafanya wizi kama huo maana yake ni nini? Hiyo hata maeneo mengine Serikali itakuwa bado inaibiwa kwa hiyo, tuisihi sana Serikali iendelee kudhibiti. Na hicho tutaweza kufikia malengo ya mapato yetu ambayo yanatokana na kodi, lakini vilevile tuendelee kutanua tax base, ili tuweze kuongeza wigo huu ambao utasaidia kuongeza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kodi nyingine ambazo zinakusanywa na TRA kwa mfano Property Tax. Nikiangalia bado hatukusanyi vile inavyopaswa kwa sababu, tukichukua takwimu za nyumba zote ambazo ziko nchi nzima tulinganishe na mapato ambayo yamekusanywa lazima utaona uwiano hauendani. Niiombe TRA kwa sababu tuna watendaji wa kata, tuna watendaji wa mitaa, hebu tuwatumie katika kupata takwimu na kusaidia kufuatilia ukusanyaji wa mapato angalau kwa-commission ambayo itawa-motivate kuweza kukusanya sehemu zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja sambamba na hilo kuna kodi la zuwio kwa wapangaji, withholding Tax on the Rent. Kwa mfano inawezekana hata humu Wabunge wapo ambao wamepangisha watu nyumba, lakini uliza ni nani ambaye amelipa Withholding Tax, hakuna. Kwa hiyo, wengi zaidi wanaolipa ni wa Kariakoo na maeneo ya mijini ambako tu official ndio wanalipa Withholding Tax, lakini huku mitaani hii haikusanywi vile inavyopaswa. Kwa hiyo, niombe tutumie pia watendaji wetu wa mitaa, wa vijiji, wa kata katika kuchukua takwimu ni nyumba ngapi zinapangishwa, zina wapangaji, ili wakati mtu analipa kodi basi tuweze kukata hiyo kodi ya zuwio na TRA iweze kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mapato ambayo hayatokani na kodi. Katika makisio ya mapato haya mwaka wa fedha 2019/2020 makisio yalikuwa ni trilioni tatu bilioni 178 milioni 922. Lakini kilichonishangaza makisio kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa mapato yasiyotokana na kodi yanayokusanywa na mashirika, taasisi na Wizara makisio yametoka kutoka hii trilioni 3.1 kwenda trilioni 2.7; sasa nitaomba waziri atueleze tunajua sawa hatujafikia malengo kamili, lakini kwa nini makisio haya yameshuka wakati Bunge na Serikali tunaendelea kuhimiza kwenye taasisi na mashirika ya Serikali kuendelea kutoa magawio kwa mujibu wa sheria ambayo TR ndizo ambazo anasimamia? Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri tutaomba uangalie hili na uweze kutupa mrejesho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine pia katika kuboresha mapato haya tukiangalia kuna tozo mbalimbali za Serikali nyingine hazijabadilika zina miaka zaidi ya 10 nyingine ni zaidi ya miaka 20. Sasa ni wakati muafaka wa Serikali ku-review hizi rates sambamba na kutengeneza takwimu. Kwa mfano tu tozo ya mtu ambaye anaenda kuchukua Loss Report Police unalipa shilingi 500, hii 500 ina miaka mingapi ipo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuangalia, lakini tunajua sambamba Sera ya Mapato ya Ndani inazungumzia suala la kuhuisha na kupunguza tozo na ada, lakini kuna wakati lazima tuangalie kuna nyingine tunashusha, lakini nyingine tuangalie namna bora ya kuweza kuzipandisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niingie kwenye Sera ya Mapato ya ndani; cha kwanza Mheshimiwa Waziri ameeleza ni kuboresha mazingira ya kufanya biashara, hii ni kusema iende sambamba na uwekezaji. Kwa hiyo, niiombe Serikali iendelee kuhimiza watendaji ndani ya Serikali waendelee kufanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu, ili wafanyabiashara waendelee kufanya biashara kama ipasavyo, kuwa na kauli nzuri pamoja na malengo mahususi ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sambamba na hilo kuna suala la miradi ya kimkakati. Tuliweza kuboresha sheria ya ubia kati ya sekta za umma pamoja na sekta binafsi – PPP. Hebu Serikali iajaribu kuangalia kutengeneza mfumo mzuri ili twende kwenye PPP baadhi ya miradi na hapo tutaipunguzia mzigo Serikali kwenye uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kenye nishati ya gesi asilia kuna mikataba ile ya uwekezaji kwenye gesi imeshatengenezwa modal ambayo ndio inatumika mtu akitaka kuwekeza kwenye gesi asilia (PSA – Production Sharing Agreement). Kwa nini na huku kwenye PPP tusitengeneze modal ambayo itakuwa ina-guide katika kuingia hiyo mikataba ambapo itasababisha sasa watu kutokuingia mikataba ambayo itakuwa ni mibovu na haitanufaisha Taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lile suala ambalo Mheshimiwa Rais anahimiza suala la win-win situation tulitengenezee modal ambayo itakuwa ni guidance ambayo itatuongoza kuingia kwenye PPP. Kwa mfano hapa umekusanya asilimia 88 tumekosa asilimia kama 12. Je, hii 12 tungekuwa kwenye PPP maana yake ingeenda kusaida katika hiyo miradi ya kimkakati kwa mfano, kuna hii Liganga na Mchuchuma ambayo tunajua kwamba, ni mradi ambao utanyanyua viwanda vingi sana hapa Tanzania na ujenzi wa reli kutoka Mtwara mpaka huko Ruvuma. Sasa tupitie na tuwe engaged tusiogope, utawala bora umeboreshwa, tumeamka, tumejua kuangalia namna bora ya mikataba mbalimbali ambayo Serikali inaingia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusiana na suala la kilimo. Kilimo kinachangia asilimia 28 kwenye pato la Taifa, lakini bado tija yake ni ndogo. Tumezalisha tani milioni 16.8 lakini ukiangalia ule wastani kwa hekta uzalishaji bado uko chini sana. Kwanini iko hivyo, hatuna mbegu bora, pembejeo bado ni hafifu, jembe la mkono linaendelea kutumika, tulikuwa na kauli mbiu ya kilimo kwanza, sasa tukiongeza uzalishaji maana yake na Serikali itaongeza mapato kwa sababu, uzalishaji wenye tija ni huu wa kuwa kwamba, unakuwa na yield nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sambamba na hilo kuna uvuvi wa bahari kuu. Na wewe umewahi kuwa kwenye kamati ukaandaa ripoti Serikali namna gani itaongeza mapato; tuna Ripoti ile ya Chenge I na Chenge II, angalau tufikie zaidi ya trilioni 1.7 sasa hebu Serikali ijikite kwenye uvuvi wa bahari kuu. Ni kwamba, hawa samaki tunaachia nchi nyingine ndio wanawavuna, wanauza, sisi tunakosa mapato; nimeona kwamba, Serikali imefanya upembuzi yakinifu kwenye ujenzi wa bandari ya uvuvi, lakini sasa tuongeze kasi katika utekelezaji wa mradi huu ambayo itakuwa imewaongezea ma…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Asante sana Mheshimiwa Richard Mbogo kwa mchango wako mzuri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. RICHARD S. MBOGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi, kwanza nianze kumshukuru Mungu na niombe tu watanzania tuendelee kumwomba aendelee kutuepusha na hili janga ambalo linasumbua dunia la Covid 19.

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo naomba nipongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi nzuri ambayo anaifanya ya kumsaidia Mheshimiwa Rais kwenye kazi ya kuendeleza nchi yetu na watanzania kiujumla. Pia naomba niwapongeze mawaziri wote watatu Waziri mwenyewe Mheshimiwa Jenista na Manaibu Mheshimiwa Anthony na dada yangu Ikupa na watendaji wote makatibu wakuu na watendaji wote chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, ni vyema tuseme kwa hii miaka mitano Waziri Mkuu kwenye hotuba yake ameweza kueleza vyema kila sekta na kila wizara kwa maana nyingine ni jinsi gani ambavyo tumeweza kufanya kazi katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni kufatisha mpango wa maendeleo pamoja na ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo inaelekeza nini kifanyike kwa wananchi. Kwa hiyo, naipongeza sana Serikali kwa namna ambavyo wamefanya kazi kubwa sana ndani ya miaka mitano na takwimu zinajionyesha kwa vitu ambavyo vimefanyika vingi na vya thamani kubwa tofauti na miaka iliyopita ikiwa ni mabadiliko yaliyotokana na uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kueleza hilo naomba nianze na suala la majanga ambayo yametokea kwenye nchi hii. Mwaka huu 2020 na tangu mwaka jana 2019 Tanzania tumebarikiwa kuwa na mvua nyingi sana ambazo kwa miaka hii mitano kwa kweli haijapata kutokea. Kwa hiyo, mafuriko ambayo yametokea Rufiji kwa Mheshimiwa Mchengerwa na pia hata sisi Mkoa wa Katavi kuna baadhi ya maeneo yalipata mafuriko lakini siyo makubwa kama haya na yamepelekea baadhi ya nyumba za wananchi kuweza kubomoka.

Mheshimiwa Spika, pia Mheshimiwa Waziri Mkuu natumainia taarifa imefika ofisi kwako sasa hivi usafiri wa njia ya reli haupo kwenye Wilaya Mpanda, au Mkoa wa Katavi kutokana na tuta la Mto Ugala takribani mita 120 kubomoka baada ya kuwa mto umejaa sana na mvua zilivyo nyingi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hiyo wito wa wananchi wa Mkoa wa Katavi wanaomba kwenye fedha za dharura na vyanzo vingine chini ya Wizara kwamba punde tu baada ya kuwa mvua zimesimama basi tuta liimarishwe kwa kuwa midomo mingi ambayo itaweza kupitisha maji na madhara haya yasitokee tena kwa masika zinazofata. Kwa hiyo, hiki ni kilio kikubwa sana kwa wananchi wa Katavi tunakumbuka miaka ya nyuma tumewahi kukulilia sana kuhusu njia hii ya reli ni msaada mkubwa sana kwa Mkoa wetu wa Katavi. Tunalima pamba, tunalima mazao ya chakula, Mkoa wa Katavi ni moja ya mikoa ile minne inayotoa sana chakula na kulisha nchi hii pia tunalima tumbaku sasa ubebaji wa haya mazao unahitaji sana hii njia ya reli na ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu na uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Katavi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kimsingi sasa hivi Mheshimiwa Waziri Mkuu njia zinazotumika kutoka nje ya Mkoa wa Katavi ni kupitia Sumbawanga kuja Mbeya na kupitia Uvinza kuja Kigoma kuja Tabora. Ni hizo tu kwa hiyo, njia ya reli haipo nah ii njia ya kuja Tabora Sikonge na kwenye pale kwenye daraja la mto Ukoga na lenyewe limefungwa muda mrefu kutokana na kujaa sana na kuhatarisha maisha ya wananchi. Kwa hiyo, pia tunashukuru Mheshimiwa Rais mwaka jana alivyohimiza Air Tanzania na inafanya mara tatu kwa wiki na yenyewe pia ni njia ya usafiri inayotumika. Lakini hizi njia kuu mbili ni muhimu sana kwa Mkoa wa Katavi kwa hiyo tunaomba sana kwenye fedha za dharura mtuangalie tuweze kutengeneza hili tuta kwenye mto Ugana.

Mheshimiwa Spika, kuna suala la uwezeshaji. Kwenye hotuba yako Mheshimiwa Waziri Mkuu umezungumza vizuri na hatua ambazo zimeweza kuchukuliwa na lakini pia kupitia halmashauri zetu na majiji na manispaa wametekeleza vyema kupeleka fedha zile zinazotengwa kutoka kwenye mapato ya hizi halmashauri mapato ya ndani asilimia 10 ambayo inaenda kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Spika, nikianza na vijana tunajua rika la vijana mwisho ni miaka 35 lakini changamoto ambayo tumekutana nayo ni kwamba kuna watu wanazidi umri huo kwa hiyo wanakuwa hawako kwenye sifa za kuunda vikundi na kupata mikopo hii. Sasa tunajua mna vyanzo takribani taasisi 19 ambazo zinafanya uwezeshaji na ukopeshaji katika nchi hii lakini kwenye hili la vyanzo vya halmashauri kwenye asilimia 10 ya mapato ya ndani tuliondoa pia riba ambayo mmeweka sana unafuu. Kwa hiyo, tuombe sasa Serikali tuangalie Mheshimiwa Waziri Mkuu ile mifuko iliyo chini ya Ofisi yako ni namna gani sasa iende ikasaidie kundi la wanaume ambako wanakuwa hawako kwenye kundi la vijana ambao wamezidi miaka 35.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndio hao ambao wanakwama kwa sasa hivi kuwa na sifa ya kuweza kukopeshwa. Kwa hiyo, kama ule mfuko wa self na hii mifuko mingine ambayo ni ya kuwezesha vijana basi tunaomba tuongeze aidha tuongeze rika angalau tuweke kwamba vijana na watu wenye umri wa kati ambao labda wanafika hata miaka 50 hii itasaidia sana na ndio kizazi hichi ambacho ndio cha uzalishaji ni kinachangia sana kwenye pato la Taifa. Kwa hiyo tunaomba marekebisho ya sera hii au sheria ili tuongeze umri kwa upande wa vijana tuwabebe na watu wanaofkisha mpaka umri wa miaka 50 au la tuwezeshwe kwenye mifuko mingine na iende kukopesha bila riba.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine kwenye uwezeshaji hapa hapa kuna halmashauri ambazo zina mapato ambayo yako chini sana ni chini ya bilioni moja. Kwa hiyo, kile kiwango ambacho kinakuwa na uhitaji pia hakitoshi, kwa hiyo, tunahitaji sana hii mifuko pia iendelee.

Mheshimiwa Spika, pia kuna suala la vikundi sasa hivi tunaambiwa idadi ya vikundi imeongezwa kutoka watu 5 mpaka 10 sasa imekuwa inaweka mkanganyiko kwa wananchi kwa sababu wingi wao pia ile fedha wanayokopeshwa ni ndogo halafu wanakuwa wako wengi na wengi hawana biashara ya pamoja wanachukua halafu wanagawana. Kwa hiyo, hiki kiwango kilichoongezwa cha watu 10 tunaomba kipunguzwe na angalau pia tuangalie sheria hii kama kuna uwezekano wa kukopeshwa mtu mmoja pia na yenyewe pia iweze kuangaliwa na ambayo itasadia sana. Kwa mfano kwa watu wenye ulemavu kuna wengine wana ulemavu viungo vinatofautiana na aina ya kazi ya kufanya. Kwa hiyo, watu wenye ulemavu iangaliwe kukopeshwa mtu mmoja mmoja kwa sababu wengine kuna kijiji wako wachache na aina ya ulemavu na kufanya biashara kila mmoja inatofautiana.

Mheshimiwa Spika, kuna suala la uwekezaji, liko chini pia ya ofisi ya Waziri Mkuu lakini naomba turejee kwenye suala la tafiti mbalimbali na kwa nini tulikuwa tuna SIDO na kwa nini tulikuwa tuna TIRDO. Mpaka sasa hivi SIDO na TIRDO zimefanya, malengo yake wamefanya kwa asilimia gani kwa nini wamefeli na kama wamefeli tunawakwamua vipi ili waende mbele. Maana tunapozungumzia uwekezaji lazima tuangalie na taasisi ambazo zinaenda kusaidia uwekezaji hususani watu wa ndani na viwanda vikiwepo tunasaidia pia kutumia fedha zetu za kigeni ambazo tunazo kwa ajili ya manunuzi mengi kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni suala la ajira. Tunaona kwenye kilimo tunaajiri watu wengi lakini ile kada ya vijana bado hatujachukulia vyema kwenye upande wa kilimo. Uwezeshaji wa mitaji, uwezeshaji wa elimu na ujuzi na uzoefu bado upo kwa kiwango cha chini kwa hiyo tuombe Serikali kwa mfano PAMATEC wana matrekta mengi sana pale na wana mkataba lakini namna gani ya kuyatoa moja ya nyenzo za kuwasaidia watu kwenye kilimo bado linasuasua. Kwa hiyo, tuombe Waziri Mkuu uliingilie hili matrekta yako pale wana mkataba na mzalishaji wa Poland kwa hiyo, hawajatimiza ile kiwango ili sasa kiwanda kiweze kujengwa hapa Tanzania. Kwa hiyo, tunaomba uingilie kati na uweze kusaidia suala hilo.

Mheshimiwa Spika, la mwisho ambalo niligusie ni kuhusiana na Corona kama wenzetu ambavyo wamechangia Wabunge. Tunaomba sasa Serikali kwenye maeneo ya mikusanyiko kwenye vyomboo vya usafiri kabla abiria hawajaingia basi vipulizwe dawa na kikifika kipulizwe dawa pia stand zote kwa sababu zina mageti kwa nini maafisa wetu wa afya wasiwepo pale kama wanawapima kama sisi vile Wabunge tunavyoingia hapa ndani na tunapimwa. Ukienda Stand ya Ubungo, stand ya Usamvu zote hizo tuongeze usimamizi wa hali ya juu.

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. RICHARD P. MBOGO:Mheshimiwa Spika, nashukuru naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii na pia namshukuru Mungu kwa namna ya pekee ambavyo tumeweza kufika siku ya leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naunga mkono mabadiliko ya kuleta hii sheria na kuifuta kampuni ya TTCL na kuanzisha Shirika kwa sababu hii imelenga changamoto zilizokuwepo kwa ufanyaji kazi wa kampuni na imelenga changamoto zilizokuwepo katika ubinafsishaji kwa ujumla. Kwa hiyo, niipongeze sana Serikali kwa namna ya pekee ambavyo imeona sasa ni wakati muafaka kurudisha hili shirika na kutokana na umuhimu wake wa kuwa na shirika letu la mawasiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna baadhi ya nchi bado zina mashirika ya mawasiliano kwa mfano China, mpaka sasa hawaruhusu code share yaani muungano na kampuni nyingine za simu nje ya nchi ya China. Yote hii imelenga
kuimarisha usalama wa nchi yao, kukuza uchumi kama ambavyo kazi zimeainishwa za kampuni za hili shirika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, China kwa sasa hivi hata social media wanaangalia jinsi gani ya kuzidhibiti na hata mitandao kwa mfano kama whatsapp. Sasa yote hii inalenga kwenye mambo mazuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na michango hiyo, naomba niendelee na maeneo mengine, kuhusiana na composition ya Bodi, napendekeza angalau aongezeke mtu mmoja na kwa upande wa Zanzibar wawe wanatoka watu wawili. Vilevile katika uteuzi sifa za hawa Board Members ziweze kuangaliwa kiufasaha zaidi na angalau hata kwenye kanuni ambazo zitatungwa na Waziri mhusika basi sifa za members ziboreshwe angalau sasa kwa sababu shirika letu liko nchi nzima na tumeshakuwa na changamoto kule nyuma katika utendaji wake, mpaka ikasababisha hatua zilizochukuliwa na Mheshimiwa Rais katika kulifufua, basi tuwe na Bodi ambayo itakuwa ni nzuri na inafanya kazi vizuri, recruitment ya hawa Board Members kama kutakuwa na uwezekano tuweke taasisi ya tofauti (independent organ) iweze kufanya interview na ku–recruit bodi ambayo itakuwa ni nzuri kuliko kuwa chini ya Waziri. Kama itawapendeza Serikali, nitaomba ikae namna hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kifungu cha 22(1)(a) katika masurufu ya vyanzo vya mapato vya hili Shirika la Mawasiliano, kifungu cha (1) kinazungumzia kwamba Bunge linaweza likatenga fedha kwa ajili ya kazi za shirika hili. Kwa sababu tunajua mawasiliano ni moja ya sehemu ambazo kwenye mwaka wa fedha uliopita kwa mfano 2016/2017 zilichangia karibuni asilimia 17 kwenye kukuza uchumi na hata pato la Taifa hizi kampuni za simu tunaona ni maeneo ambayo mapato yapo kama tutakuwa na mkakati mzuri na uongozi na bodi zitafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama itapendeza tu-delete Kifungu cha 22(1)(a) shirika likajitegee asilimia 100 bila kupata ruzuku yoyote kutoka Serikalini ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kwa sababu vifungu vinavyofuata vinaruhusu kukopa basi wakawe kibiashara zaidi waweze kukopa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mojawapo ya sheria zilizopitishwa na Bunge lako Tukufu ni makampuni ya simu kujisajili kwenye soko la hisa. Kwa hiyo, tungeomba kutokana na mchakato ambao unaendelea na performance ya TTCL, najua sasa itahamishwa kwenda kwenye shirika, basi na mchakato wa kwenda kwenye soko la hisa uweze kufanywa na tuingie huko ili kuendelea kuweka uwazi. Kwa sababu sasa mahesabu, utendaji vitakuwa wazi kwenye public kwa hiyo hii itasaidia sana kulenga kwenye ufanisi wa Shirika letu hili la Mawasiliano. Kwa hiyo, nitaomba Serikali walichukue hilo na muweze kuifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kifungu cha 28 kwenye suala la kuhamisha mali na madeni kutoka kwenye kampuni inayofutwa na sasa tunakwenda kwenye shirika tungepata kwa sasa hivi hii TTCL ambayo sasa inaenda kufutwa kama kampuni hali yake ya ufanyaji biashara ikoje, wana-operate kwenye loss, wana operate kwenye faida na status za madeni zikoje maana ukienda kuangalia kwenye balance sheet utaweza kujua.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba sana katika kuhamisha mali hizi, uthamani na kuthamini madeni pamoja na mali zinazohamishwa ufanyike kiufasaha na najua tulipitisha Sheria ya mambo ya Valuers na Valuation mwaka jana, basi tuzingatie sana tupate valuers wazuri ili tunavyohamisha hizi mali na madeni, kwa mfano kama madeni haya third party confirmation ifanyike. Lazima tuthibitishe kwa wale wanaotudai kwamba kweli kiwango hiki ndicho tunachodaiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababu tumeshakuwa na changamoto nyingi kwenye kampuni ambayo ilikuwa ina nature ya shirika ya kuwa kwamba huenda kuna madeni hewa au wadaiwa hewa, kwa hiyo, ni suala la kuthibitisha. Kwa hiyo, tuhamishe vitu ambavyo vimebeba value ile halisi kwa ajili ya kwenda kwenye shirika letu ili lisije likabeba mizigo ambayo siyo ya kwake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefurahi kuona pia katika kifungu mmezingatia kwamba mtabeba masuala ya waajiriwa wote, kwenye kifungu hiki cha 31, terms zao zilivyo sasa hivi, masurufu yote ya watumishi yanabebwa yanaenda kwenye shirika na hapo ndiyo huwa msingi mzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, ningependekeza kama wanaweza kuongeza kipengele, sasa hivi najua watumishi wengi ni wa mkataba wa muda mrefu, wale permanent employees basi tuone kama wanaweza wakaruhusu na kama kuna mikataba ya hiari kwa hii kampuni sasa hivi kwa wale ambao wangependa kustaafu wakaanze maisha yao waruhusiwe lakini ni lazima waangalie pia na potential ya mtu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mtu mwingine anaweza akawa anaomba kustaafu lakini ni potential kwa mfano Idara ya Ufundi, Idara ya Mitambo ndiyo sehemu ya operation ndiyo production area, huko lazima tuangalie, lakini maeneo mengine katika kupunguza mizigo kwenda kwenye shirika, sasa hivi kampuni iangalie watu wenye hiari ya kustaafu iwaruhusu wastaafu, walipwe masurufu yao, basi tunavyoingia kwenye upande wa shirika na kama tunaleta ajira mpya tulete ajira pia za kudumu na hata zile za mkataba ili tuwe na soko huru.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kwa upande wa watumishi tuna changamoto kidogo, makampuni mengine ya simu kwa mfano Vodacom, Tigo, ulipaji wa wale key personnel’s na hasa upande wa operation masurufu yao wanalipwa vizuri zaidi kuliko watu walioko ndani ya TTCL. Kwa hiyo, unaweza kukuta kwenye hili shirika tunalolianzisha tutakuwa tunaajiri watu baada ya mwaka mmoja, miezi sita wanaacha kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tuangalie tuje kuwa na mishahara ambayo inaendana vizuri na soko ili
wataalam wetu ambao tutakuwa nao wakiingia na ndiyo wataalam wetu wasiondoke haraka. Kwa hiyo, ile labour turnover iwe ndogo kuliko kwa sasa hivi sidhani kama wana- maintain sana kutokana na malipo yao hayalingani na kampuni zingine za ushindani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangie kuhusu hii TTCL Pesa Limited, kwa sababu tuna-adapt kila kitu na katika vyanzo vya mapato vikubwa vya makampuni ni mambo ya miamala ya kipesa. Kwa hiyo, tuzingatie sana, hii TTCL Pesa Limited iendelee lakini usimamizi wake uwe wa hali ya juu kuhakikisha kwamba tunafanya kazi kwa faida na hakuna frauds.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine nimeona kwamba Bodi itaandaa Annual Report baada ya kufunga mahesabu miezi sita, lakini litakuwa ni shirika ambalo litakaguliwa. Sasa hii miezi sita sidhani kama inatosha, kuna miezi mitatu kama tunavyo-adapt katika Taasisi za Serikali ya kuandaa mahesabu, miezi mitatu Mkaguzi afanye kazi, kwa hiyo miezi sita hii haitoshi kwamba ripoti tayari amepewa Waziri. Kwa hiyo, angalau ingesema kwamba baada ya miezi sita Bodi inaweza ikawasilisha ripoti za ukaguzi kwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kwamba, tayari sisi nchi yetu tuna Mkonga wa Taifa na nina matumaini kwamba utakuwa chini ya shirika hili. Kwa hiyo, tuone matumizi mazuri na katika kuongeza vipato Halmashauri zote ziwe connected na huo Mkonga wa Taifa na unaendelea kusambazwa nchi nzima. Basi ufanisi wa kuuza data wa shirika hili la mawasiliano tuharakishe pia na Mkonga wa Taifa kuweza kutumika. Sasa hivi mawasiliano nasikia tunaenda kwenye 5G, tulikuwa 3G, tumeenda 4G, 5G inakuja, sasa tuangalie jinsi gani pia ambavyo tunaweza kwenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, tubadilishe tabia (attitude), ule ufanyaji kazi wa kimazoea kama ilivyokuwa shirika, imekuwa kampuni, tukibadilisha attitude ya watumishi na utendaji wa shirika kiujumla iwe na kimtazamo sasa wako kwenye ushindani, ufanisi wao na ufanyaji kazi wao utakuwa ni mzuri sana na mantiki ya kuvunja kampuni na kwenda kwenye shirika sasa tunatarajia italeja tija katika nchi yetu na tunatarajia Treasury Registrar ataweza kupata mgao wake wa faida kwa Shirika letu hili la Mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nashukuru sana kwa nafasi hii na naunga mkono mabadiliko ya sheria hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kupata nafasi hii. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Waziri na timu yake kwa kuweza kuandaa bajeti na kusimamia Wizara kiujumla. Kwa sababu dakika ni tano, naomba kwa ufupi tu nisemee kwanza suala la wachimbaji wadogo wa madini ambao wapo katika Jimbo langu la Nsimbo, Mkoa wa Katavi.
Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo haya kuna watu wanaopewa leseni ambazo ni ndogo (Primary Mining License), wamekuwa wakishirikiana vizuri na wananchi katika uchimbaji wa madini, lakini pale inapotokea mtu anapopanda daraja anaenda leseni kubwa, (Mining License - ML) anakuwa sasa na masharti magumu ya kushirikiana na wananchi katika uchimbaji wa madini. Hii imepelekea kuwa na mgogoro mkubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna mfano mzuri, mwaka huu imetokea Kampuni ya Sambaru, imeweza kuingia kwenye mgogoro na wananchi wa Kijiji cha Ibindi mpaka ikahatarisha amani. Sasa ombi langu kwa Mheshimiwa Waziri; tuna takriban vijiji 10 ambavyo wananchi hawa ndipo wanapata kipato. Tunaomba maeneo haya yawe ni kwa ajili ya wachimbaji wadogo tu na tusiweke uchimbaji mkubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini tunasema hivi? Maeneo haya yapo kilometa 15 mpaka 20 kutokea mjini na ndiko ambako inapatikana dhahabu.
Watu wanachimba na uchimbaji wao mdogo mdogo na wanaweza kukidhi maisha yao ya kila siku; kulipa ada na vitu mbalimbali katika maisha. Sasa tukiwekea namna hii, itakuwa inapelekea mgogoro na kuhatarisha amani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile katika mlolongo mzima wa kazi za Wizara, tumewahi kupata taarifa, kuna ule ufadhili wa World Bank kwenye kusaidia wachimbaji wadogo wadogo tu, ufadhili takriban Dola milioni nne. Sasa katika vile vituo saba vya mfano, namwomba Mheshimiwa Waziri Profesa Muhongo, maeneo ya Jimbo la Nsimbo yawe ni moja ya Kituo cha mfano katika hivyo vituo saba ambavyo vitapata msaada wa Benki ya Dunia katika huo ufadhili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile wachimbaji wadogo wana malalamiko kuhusiana na gharama za upande wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Gharama kwa hekta moja ni takriban sh. 1,500,000/= kwa mtu ambaye ameingia kufanya machimbo maeneo ya hifadhi ya misitu. Wakati huo huo, kwa hekta moja kwa upande wa madini, analipia sh. 80,000/=. Sasa imekuwa inawawia ngumu kuweza kukidhi hizi gharama.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba Wizara hizi mbili zikae kwa pamoja ziweze kuona namna gani hizi gharama zinapunguzwa ziendane na uhalisia wa uharibifu unaotokana na uchimbaji. Ni mara kumi zaidi watu wachajiwe kulingana na miti ambayo imeharibika kuliko kuchukua tu eneo wakati watu wengine wanachimba hata miti mingi anakuwa hajaikata. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vile vile nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa awamu ya II ya REA. Nashukuru Jimbo langu Kata nne zimeweza kupata umeme, lakini bado Kata nane. Kwa hiyo, naomba katika hii Awamu ya Tatu, ule upembuzi yakinifu ambao tayari umeshafanyika, wasiruke vijiji. Maana kuna vijiji vingine wamepitisha umeme lakini hawakuweka zile transformer na wenyewe waweze kufaidika na umeme huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natoa pongezi kwa Waziri na timu yake kwa hotuba nzuri ya bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mazingira ni Mtambuka, suala la mazingira ni muhimu sana katika utunzaji na faida zake, vilevile umuhimu katika maisha ya wanadamu. Wizara takribani nne zinaingiliana katika utunzaji na usimamizi wa mazingira; TAMISEMI, Maliasili na Utalii, Ardhi, Maji na Mazingira. Hivyo basi, usimamizi katika maeneo mengi umekuwa hafifu kutokana na fedha, rasilimali watu, vitendea kazi pia Wizara kukosa wawakilishi katika maeneo mengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, naiomba Serikali ifanye mpango ambao utakuwa unaweka mawasiliano mazuri ambayo yatakuwa na tija. Mfano, mabonde ya maziwa mbalimbali hayana usimamizi wa moja kwa moja kwenye vyanzo vyote vya mabonde kwa kuwa ofisi za mabonde zipo Kikanda na Halmashauri nyingi hazisimamii mabonde hayo. Tunahitaji Wizara zote hizi kuwa na uhusiano wenye tija.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Upandaji Miti, katika Halmashauri zetu zimeweza kutii maagizo ya kutenga fedha kwa ajili ya upandaji miti, tatizo ambalo litakuwa mbele yetu ni upatikanaji wa fedha za kutekeleza bajeti hiyo, vilevile usimamizi wa kuhakikisha miti inakuwa mfano mzuri, ni wakulima wa Tumbaku ambao upatiwa fedha ili kupewa miti, wengi wao huwa hawatilii maanani kuhakikisha miti inapandwa na kukua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ruzuku katika nishati, ili kuendelea kulinda mazingira ni muhimu kwa Serikali kuweka ruzuku katika nishati mbadala ambazo zitakuwa zinalinda mazingira, mfano matumizi ya gesi, nishati ya jua kuokoa au kupunguza matumizi ya mkaa ambao unapelekea ukataji mkubwa wa miti.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwapongeze viongozi wote wa Wizara ya Nishati na Madini katika kufanikisha uandaaji mzuri wa hotuba ya bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Nishati na Madini ni muhimu katika mpango wa Serikali wa maendeleo na kufanikisha nchi yetu kuwa ya viwanda, kwa kuwa nishati ni kiungo muhimu katika viwanda vyetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, REA; kwanza naomba Waziri aendelee kuwa imara katika Wizara hii na kuwezesha umeme vijijini kufikia malengo. Katika Jimbo la Nsimbo Mkoani Katavi, jimbo lina kata 12, lakini kata nne tu ndiyo zilizopata umeme wa REA. Sambamba na hilo, umeme umepita Kijiji cha Kapalala bila kuwekewa transformer. Tunashauri Wizara ikamilishe umeme katika kijiji hicho tukizingatia kuna wananchi wahitaji. Vile vile, tunahitaji, majibu ya Waziri ni lini kata zilizobaki nane zitakamilika kupata umeme?
Mheshimiwa Naibu Spika, gridi ya Taifa; Mkoa wa Katavi ni moja ya mikoa hapa Tanzania, ambayo haina umeme wa uhakika, yaani wa gridi ya Taifa. Hivyo, tunatumia umeme wa jenereta ambazo zilitolewa Shinyanga na tayari ni chakavu hazifanyi kazi kulingana na uwezo. Hivyo basi, tunahitaji Serikali ikague umeme uliopo Wilaya jirani ya Kaliua kwa kuwa ni jirani sana na Jimbo la Nsimbo. Hivyo, tunahitaji kauli ya Serikali ni lini itafanya upembuzi yakinifu wa kuleta umeme Jimbo la Nsimbo kupitia Kata ya Ugala?
Mheshimiwa Naibu Spika, madini; mradi wa wachimbaji wadogo wa Benki ya Dunia, Jimbo la Nsimbo ni mojawapo lina vijiji 11 ndani ya kata sita zina wachimbaji wadogo. Hivyo, tunaomba Serikali kuchagua maeneo ya mfano kati ya hayo saba. Naomba na Jimbo la Nsimbo tuna sehemu mbalimbali. Kwa mantiki hiyo, tunaomba Mheshimiwa Waziri atoe tamko la Nsimbo kuwa kati ya vituo saba vya mfano.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la wachimbaji wadogo; wachimbaji wadogo, ambao wana uwezo wa kuwa na leseni, waweze kupata leseni kwa mujibu wa Sheria (Primary Licence) na waweze kurahisisha wananchi wasio na leseni kuchimba katika maeneo yao na kuweza kuuza dhahabu na kupata mapato kuwasaidia kujikimu wao na familia zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Wizara ikitoa leseni kubwa mining licence (ML) wenye uhalali huo wanakataza wananchi kuchimba. Mfano mzuri ni kampuni ya SAMBARU, Kata ya Ibindi iliingia katika mgogoro na wananchi na hali siyo shwari. Pia, eneo la Dirifu, Kata ya Magamba nako kulitokea vurugu Januari, 2016. Kwa mantiki hiyo, tunahitaji Serikali kutoa tamko vijiji vifuatavyo viwe kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Jimbo la Nsimbo, Kata ya Machimbi, Kijiji cha Katisunga na Kapanda; Kata ya Ibindi, Kijiji cha Ibindi, Kapandamu na Kasherami; Kata ya Sitalike, Kijiji cha Mtisi; Kata ya Urwira, Kijiji cha Urwira, Usense; na Kata ya Itenka, Kijiji cha Msangama. Jimbo la Mpanda Mjini, Kata ya Magamba, Kijiji cha Dirifu Society.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni muhimu sana maeneo ya vijiji hivyo kuwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo kwa kuwa eneo la awali ni Wilaya ya Tanganyika, eneo la Kipalamsenga, ambako kuna madini zaidi ya aina ya shaba. (Copper)
Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za maliasili kwa wachimbaji madini utafutaji wa madini kuna wakati wananchi au kampuni huingia katika hifadhi za misitu. Wananchi hutozwa gharama za uharibifu wa misitu. Tatizo lililopo ni tozo zipo kwa ukubwa wa eneo badala ya kuangalia idadi ya miti na kupelekea watu wengi kushindwa kumudu gharama hizo. Hivyo, tunaomba, Wizara hizi mbili zikae pamoja na kuangalia gharama hizo, zipitiwe upya.
Mheshimiwa Naibu Spika, utafiti wa mafuta Lake Tanganyika kwa kuzingatia maendeleo ya nchi tunahitaji Serikali kupitia Wizara isaidie utafiti wa mafuta katika eneo la Ziwa Tanganyika. Hivyo, taarifa ni muhimu nasi wananchi kujua maendeleo ya utafiti huo na vyema kuwasilisha Bungeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maelezo hayo juu, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Hifadhi ya Katavi ni muhimu sana, inatakiwa kuwekewa mkakati wa kuboresha miundombinu kwani barabara ni chache. Pia hakuna sehemu za huduma kwa watalii kama simu, hoteli za hadhi ya nyota tano, barabara za ndani na visima vya upepo kukabiliana na ukame.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendeleza ujirani mwema (corporate social responsibility), hifadhi za Taifa husaidia kero mbalimbali. Hivyo basi, Hifadhi ya Katavi ina mpango wa kuchimba visima vitatu vya maji ambapo wananchi wanatakiwa kuchangia 30% ya gharama. Tunaomba Serikali ibebe mzigo/gharama zote za mradi ili kumsaidia mkulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania Tourism Board inahitaji fedha za kutosha ili kuweza kufanya kazi ya kutangaza utalii wa aina zote uliopo katika nchi yetu. Serikali lazima ihakikishe kuwa inatoa pesa kama sera ilivyo ambapo 3% ya mapato ya TANAPA na Mamlaka ya Ngorongoro yawe yanawasilishwa ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma za utalii. Tanzania imekuwa na kiwango cha chini cha huduma katika utalii kutokana na kutokuwa na package nzuri kulingana na uwezo wa watu mbalimbali. Hivyo, TANAPA na Serikali ni muhimu kuhakikisha kuwa watoa huduma wanakuwa na elimu na uwezo wa kutosha pia kuwe na standard zinazofuatwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hifadhi za misitu; maeneo mengi ya Tanzania yamevamiwa na wafugaji hivyo tunahitaji Serikali kufanya mpango bora wa matumizi ya ardhi na kudhibiti uharibifu wa misitu. Hivyo, Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza maeneo kiasi ili kuondoa migogoro. Mfano Halmashauri ya Nsimbo tunahitaji maeneo katika Kata za Ugala, Sitalike, Kange na Kapalala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa kutengeneza hotuba nzuri na pia na taasisi yake kiujumla, wameweza kutupatia makabrasha ambayo yatakuwa ni msaada kwetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalo ningependa kulichangia ni masuala mazima ya kuhusu vijiji. Vijiji vyetu ambavyo vilitangazwa mwaka 1974 tuna matatizo ya mipaka; tunaomba Mheshimiwa Waziri kwa kupitia Halmashauri zetu na taasisi zilizopo mipaka mingi kwa sasa hivi haijulikani, kwa hiyo, kumekuwa na uingiliano na matumizi ya kilimo. Hii inasababisha mpaka wananchi wetu wanapata matatizo. Kwa mfano, katika Halmashauri ya Jimbo la Nsimbo, Mkoa wa Katavi, eneo la kwenda Kata ya Ugala limekuwa na matatizo sana ya kujua mipaka ya kijiji iliishia wapi! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika upande wa ardhi tunajua wamefanya kazi yao na wanafanya vizuri, lakini kuna mamlaka ambazo wanaingiliana! Tutahitaji waweze kukaa kwa pamoja ili tu wapate ufafanuzi na wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuishi. Mamlaka ya Hifadhi ya Misitu; tunahitaji wawe na mawasiliano ya karibu ili mipaka ambayo Mamlaka hii ya Hifadhi ya Misitu ambayo inaitoa na wakihusisha pia na Wizara ya Ardhi kwa kupitia hizi Halmashauri zetu waweze kuwa pamoja kwa sababu, sehemu nyingi kumetokea mkanganyiko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa jinsi anavyoshughulikia migogoro. Halmashauri yangu na mimi binafsi nitaleta maombi, tumekuwa na migogoro kutokana na idadi ya watu kuongezeka. Maeneo mengi ya nchi ya Tanzania yamekuwa sasa hivi yanavamiwa kwa sababu ya ongezeko la watu. Watu wameongezeka na hasa wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano Halmashauri ya Jimbo la Nsimbo maeneo mengi yameingiliwa na hasa ya hifadhi za misitu, ardhi imekuwa ni haba. Sasa kuna mpango ambao Mheshimiwa Waziri ameuzungumza wa matumizi bora ya ardhi, lakini tuna tatizo la bajeti katika hizi Halmashauri zetu. Sasa tungeomba kwa upande wa Wizara waweze kusaidia, kwa kuwa wanaweza kupata mafungu aidha, kupitia taasisi nyinginezo. Tunajua kwenye bajeti itakuwa haitoshi, lakini kama Waziri anavyotumia jitihada kuwapata wafadhili mbalimbali, ili fedha ipatikane kwa ajili ya huu mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa sababu, kuna maelekezo mengi ametoa kwamba Halmashauri zetu ziweze kupima maeneo, lakini shida ni bajeti iko finyu kwelikweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, bajeti ya mwaka 2016/2017 ni shilingi bilioni 14 na bajeti inayoishia 2015/2016 ni shilingi bilioni 14, kwa hiyo, hatujapiga hatua! Matokeo yake ni kwamba, miradi mingi haiwezi kuja kufanyika. Sasa kama Wizara itaweza kusaidia Halmashauri zetu kwa kupata fedha sehemu nyingine, litakuwa ni jambo bora zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni masuala ya utapeli kuhusu viwanja vyetu. Tunaomba Wizara iangalie mpango ambao utakuwa ni mzuri kwa watu wanaohitaji kununua au kuuza viwanja. Ni kweli, Wizara inatoa huduma mtu akitaka kufanya searching anafanya na anaona jina kabisa pale, Mheshimiwa Richard Philipo Mbogo, lakini kuna tatizo Hati hizi zinavyotoka hazina picha moja kwa moja, sasa zingeweza kuboreshwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na kesi nyingi sana za watu wametapeliwa kuhusu uuzaji wa nyumba au viwanja katika maeneo mengi sana ya nchi yetu. Sasa tuombe Wizara itengeneze mpango mzuri ambao utasaidia kupunguza watu kutapeliwa na ndio maana ukipita sehemu nyingi mijini unakuta imeandikwa “Nyumba Haiuzwi” kwa sababu, watu wengi tayari wameshaingia katika hali ya utapeli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, Wizara imeweka suala la TEHAMA, maana yake hutumia teknolojia katika kupata taarifa zake na kufanya kazi sehemu mbalimbali. Kwa sababu, sehemu nyingi Mkongo wa Taifa bado haujaanza kufanya kazi, basi tunaomba Serikali iweze kuhakikisha kwamba, Mkongo huu unafanya kazi ili tuweze kuhakikisha kwamba, Halmashauri zetu zinakidhi mahitaji ambayo Wizara inaweza kuagiza katika Hotuba ya Waziri ambayo ameitoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia naomba sasa kwa upande wa Wizara tuongezewe huduma mikoani, watu waweze kupata Hati. Tuna makazi mengi ya vijiji, watu wengi hawana Hati, kwa hiyo, ikitokea pale mtu anahitaji dhamana Mahakamani, anahitaji apate mkopo, watu wengi hawana Hati. Kwa hiyo, tutaomba zile gharama kwa upande wa vijijini zishushwe ili watu waweze kupata Hati na hata hizo za category karibu tatu ambazo ameweza kuzieleza Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache, naunga mkono hoja na naomba Wizara iendelee kutimiza wajibu wa Serikali. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kwa hotuba nzuri yenye kusheheni mambo mazuri na taarifa kwa umma. MUVI, imefanya wilaya na mikoa saba tu hivyo basi ni muhimu kuongeza wilaya nyingine na hasa Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Mpanda katika Halmashauri ya Nsimbo.

Mheshimiwa Naibu Spika, NEDF. Mfuko huu bado haujasaidia wajasiriamali kwa kuwa bajeti ni ndogo hivyo Serikali itoe kipaumbele kwa kuongeza mtaji ili wananchi wakope.

Mheshimiwa Naibu Spika, Maafisa Biashara katika Halmashauri. Bado hatujaona jinsi Maafisa Biashara katika Halmashauri wanavyotumika kuendeleza kazi za Wizara katika Halmashauri zetu, hivyo basi Sekretarieti ya Mkoa inafaa kupewa majukumu ya kuendeleza masuala ya viwanda katika mkoa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza Mawaziri na watendaji wa Wizara kwa maandalizi na kuwasilisha bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Hifadhi ya Taifa ya Katavi katika Mkoa wa Katavi upande wa Kaskazini inapakana na Kijiji cha Sitalike lakini kwa mujibu wa mipaka sehemu ya kijiji ipo eneo la hifadhi. Hivyo, tunaomba mpaka urudishwe nyuma mpaka ng‟ambo ya Mto Katuma kwa kuwa wananchi hapo wanaishi tangu miaka ya 1990.
Mheshimiwa Mwenyekiti, TANAPA inahitaji kuwa na ujirani mwema yaani tunaomba sehemu ya Mto Katuma iruhusiwe wananchi kuvuna samaki angalau eneo lenye urefu wa kilometa tano ili kuwezesha wananchi kupata vitoweo na pia kuondoa ugomvi. Hivi karibuni vijana watatu walikamatwa eneo la mto na walipigwa sana na kuumizwa ambapo hali zao siyo nzuri. Jambo hili lilipelekea wananchi kutaka kuchukua hatua zinazopelekea kuvunja amani kati ya watumishi na wafugaji. Kwa mantiki hiyo, tunaitaka Serikali itoe tamko la watumishi wa TANAPA kufuata taratibu, kanuni na sheria katika utendaji wao ili kuondoa hali ya kuvunja amani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu promosheni ya hifadhi, kwa muda mrefu sana Serikali imekuwa ikitangaza sana baadhi ya hifadhi maarufu na kubwa hapa nchini bila kuhusisha pia hifadhi ambazo zinahitaji kutangazwa sana. Mfano mzuri ndege zetu zinabeba majina ya hifadhi kubwa. Tunahitaji Mbuga ya Katavi kuboreshwa na kutangazwa ili kupata watalii kwa kuwa uwanja wa ndege upo. Vilevile miundombinu na huduma nyingine ziboreshewe zaidi kama zilivyo sehemu nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujangili, Serikali imekuwa na juhudi kubwa zaidi kupambana na ujangili lakini uhalifu huo bado unaendelea. Tunahitaji Serikali iboreshe mbinu za kukabiliana na wahalifu. Watumishi wa TANAPA wameonekana kuhusika, hivyo utaratibu wa kuwahamisha utumike na kuwafuatilia mienendo yao. Pia Serikali lazima ifuatilie taarifa zinazotolewa na vyombo vingine vya usalama. Vilevile maeneo yanayozunguka Hifadhi za Taifa yawe yanachunguzwa mara kwa mara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hifadhi ya misitu na pori la akiba. Nchi yetu imekuwa na ongezeko la watu kila mwaka, vilevile nchi yetu ilipokea wakimbizi kutoka jirani za Burundi, Rwanda na Congo DRC hivyo kuhitaji maeneo. Vilevile baadhi ya maeneo ya nchi yamekuwa na ufinyu wa maeneo yenye rutuba na nyasi za kulisha mifugo na wafugaji na wakulima kuhamia maeneo mengine. Athari zilizotokea ni uvamizi wa maeneo ya hifadhi za misitu na mapori ya akiba. Vilevile migogoro imekuwa mingi. Pia tatizo la zana za kilimo imepelekea watu kutafuta maeneo mapya ya kulima. Athari imekuwa wananchi kuchomeana nyumba na kufyeka mazao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na athari hizo tunaishauri Serikali iongeze kusimamia sheria husika kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Taifa kwa kuwa rushwa imekuwa tatizo. Pili, ufugaji bora kwa kulima nyasi zinazokaa muda mrefu. Serikali ipange matumizi bora ya ardhi kwa kutoa fedha za kupima maeneo. Serikali ipunguze maeneo ya hifadhi ambayo tayari yamevamiwa muda mrefu, zaidi ya miaka 20.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la vitalu vya uwindaji, kwa kupitia utaratibu wa sheria, wahitaji au kampuni zinaomba na kupata leseni za uwindaji kwa mfumo wa vitalu lakini tatizo lililopo ni taarifa kamili za mapato na uvunaji unaofanywa na kampuni zenye leseni. Hivyo, kuna umuhimu wa Serikali kuangalia upya mfumo wa vitalu kwa takwimu za kifedha na idadi ya wanyama. Vilevile vitalu vifanyiwe uchunguzi katika kudhibiti ujangili wa nyara za Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tozo za misitu; Wizara imekuwa na tozo mbalimbali za mazao ya misitu lakini tozo kwenye mbao ni kubwa. Vilevile wachimbaji wadogo wa madini wanatozwa ada kubwa kwa hekta moja shilingi 1,400,000 ambayo haiendani na ukubwa na uharibifu. Hivyo tunaomba Serikali tozo ziendane na miti inayokatwa katika eneo husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Memorandum of Understanding, Serikali ya Tanzania mwaka 2015 ilisaini mkataba kudhibiti biashara ya magendo kati ya Tanzania na Kenya na kuokoa fedha nyingi. Hivyo tunaomba Serikali iangalie upya MoU na nchi nyingine pia hata za mbali ili kuokoa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napongeza Wizara na Serikali kwa kuwasilisha hotuba na utekelezaji wa miradi 2016/2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, mgao wa bajeti za Halmashauri. Ukifuatilia mgao wa bajeti kwenda katika Halmashauri kwa vyanzo vya ndani unahitaji marekebisho kwa uhitaji na matatizo ya kila Halmashauri hayakuzingatiwa ipasavyo. Mfano Nsimbo, 34% ya watu ndiyo wanaopata maji. Hivyo basi, tunashauri Wizara igawe Sh.1,000,000,000 kwa kila Halmashauri ambapo itakuwa Sh.185,000,000,000 kwa idadi ya Halmashauri 185.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia mgao huo, kila Halmashauri itaweza kutatua kwa kiasi matatizo ya maji. Baada ya mgao huo, ndipo Wizara iongeze kwa kila Halmashauri kulingana na miradi mikubwa na kero za maji kwa eneo husika. Vilevile ni muhimu kwa Wizara kuangalia idadi ya watu ambao hawapati huduma ya maji na kuwapatia mgao ambao utatatua kwa kiasi tatizo la maji kwenye eneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Maji ya 2002 iliyoeleza kwamba wananchi wapate maji ndani ya mita 400 bado ufanisi wake haujaonekana. Hivyo, sera hii ifanyiwe utafiti na kuwe na kigezo cha kugawa fedha kwa Halmashauri ambazo hazijafikia malengo ya Sera ya Maji, kigezo cha mita 400.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mfuko wa Maji Vijijini. Ni muhimu sana Serikali kuboresha Mfuko wa Maji Vijijini kwa kuwa ndiyo maeneo ambayo wananchi wanateseka sana kwani ndiyo ambao hawapati maji. Hivyo basi Sh.50 kwa kila lita katika mafuta iongezwe na fedha ipatikane kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya maji vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya umwagiliaji. Serikali ifanye ufuatiliaji wa miradi ya umwagiliaji. Mfano Mradi wa Kijiji cha Katambike, Kata ya Ugala, Halmashauri ya Nsimbo - Katavi mpaka sasa bado haujaanza kufanya kazi na haujakamilika. Hivyo, tunaomba Serikali ifanye haraka kumalizia mradi huo ili wananchi wafaidike.

Mheshimiwa Naibu Spika, vizibo vya umwagiliaji. Serikali ikamilishe kizibo cha Mwamkuli katika Manispaa ya Mpanda. Pia Serikali iendeleze vizibo vile ambavyo vimejengwa na watu binafsi ili wananchi wa Kata ya Itenka ambao wanalima zao la mpunga waweze kufaidika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwanza nimshukuru Mungu kwa kupata hii nafasi, lakini pia naomba kuchukua nafasi hii nikupongeze Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uimara na tunaomba Mungu aendelee kukujalia kwa afya njema ili uendelee kukalia hicho kiti na kusimamia kanuni na sheria mbalimbali na Chama cha Mapinduzi hakikufanya kosa kukupendekeza kwa kuwa hiyo ni fani yako na unaitendea haki.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niipongeze bajeti, ni bajeti nzuri ina muelekeo mzuri kwa kuongeza pande wa Maendeleo na tumefikia asilimia 40 na vilevile imezidi kwa trilioni saba bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016; kwa hiyo tunategemea kupata mambo mazuri.
Pamoja na kuiunga mkono bajeti kuna mambo machache ambayo ningependa kuchangia na zaidi nianze na suala la kodi kwenye masuala ya Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, binafsi siungi mkono hii hoja ya kuondoa msamaha kwa Wabunge kwa sababu Serikali iliangalia kwa mantiki kabisa mwaka ambao iliweza kuwapa Wabunge na viongozi wengine msamaha wa kodi waliona kuna maana.
Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia kwa mujibu wa Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wabunge ndio chombo kikubwa katika Jamhuri ambacho kina wajibu wa kusimamia na kuishauri Serikali. Kwa hiyo, na tuko hapa kwa niaba ya wananchi, kwa hiyo unapomuongezea gharama Mbunge ni sawa na unamuongezea gharama mwananchi. Kwa hiyo, tunaomba sana sasa Serikali tuko kwenye hiki chombo, tunaisimamia Serikali; kwa hiyo, tunaomba hili kusudio liweze kuondolewa maana kupitisha haya marekebisho ya hii sheria ni sawa na mtu umepanda kwenye mti unakata tawi ambalo umekalia mwenyewe, sasa sidhani kama Wabunge tutaweza kuiunga mkono hoja hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kwenye kodi (Capital Gain Tax) kwenye mambo ya hisa, Serikali tuna soko la hisa na moja ya faida kubwa ya kuwa na soko la hisa ni kuweka uwazi katika makampuni ambayo yameingia pale, na makampuni ambayo yako pale kwenye soko la hisa yanatoa mahesabu yao kwa uwazi, utendaji wao wa kazi. Kwa hiyo, wananchama ambao ndiyo wale wenye hisa wakati wa kuuza zile share zao kuna faida wanayoipata kwa utofauti wa bei ya kununua na kuuza. Sasa kwa kusudio la Serikali kutoza kodi liangalie suala zima la kwamba tuhamasishe uwekezaji.
Kwa hiyo, niishauri Serikali tuangalie namna ambayo ya kutoza kodi kwenye hii faida mtu anapouza zile hisa zake ambayo itakuwa inaudhibiti mzuri. Ukichukua mtu amenunua share mwaka mmoja uliopita amekuja ameuza leo sasa ile bei aliyonunulia kumbukumbu nani anakuwa ameitunza?
Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri ningeshauri kwamba kwa sasa hivi share zikiuzwa inachukuliwa asilimia mbili ambapo broker anapata asilimia yake, soko la hisa linapata na capital market wanapata mgao wao. Sasa Serikali iangalie namna kwenye hii asilimia mbili tuongeze labda tupeleke asilimia tatu, asilimia moja ndiyo iwe kipato ambacho kinaenda kuingia upande wa Serikali badala ya kuweka kodi ambayo kui-manage kwake itakuwa inasumbua.
Mheshimiwa Naibu Spika, uzuri mkubwa katika watu ambao wapo kwenye masoko ya hisa wanatuwezesha kuongeza ufanisi, natoa makampuni zaidi ya 20 hatujafikia wenzetu kama Wakenya wana makampuni 62. Kwa hiyo, tuhamasishe makampuni mengi zaidi yaweze kuingia kwenye Soko la Hisa ili kuwe na utandawazi na Serikali iweze kukusanya kodi zake zote ipasavyo. Kwa hiyo, tutaomba sana Serikali namna ya kutoza hapa tuongeze asilimia hii mbili inayotozwa sasa hivi badala ya kuangalia kodi ambayo itakuwa kui-manage kwake pale itakuwa ni kazi ngumu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumezungumzia kuondoa au kufuta baadhi ya tozo kwenye mazao ya kilimo. Tunaomba Serikali iangalie kwa umakini kwa sababu kuna maeneo ambayo Halmashauri zetu ndipo wanapopatia kodi. Lakini vilevile kuna kodi na tozo ambazo haziingii kwenye Serikali au kwenye hizi Halmashauri zinaenda kwenye Vyama vya Msingi na wakulima wamekuwa wakilalamikia sana. Kwa hiyo, ninaunga mkono kuondoa zile kodi ambazo hazina tija zinaongeza gharama kwa wakulima na hasa zinakuwa zinafaidisha tu vyama vya msingi na makampuni mengine ambayo yananunua hayo mazao ya biashara.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini zaidi ya hapo tungependa kwamba katika hotuba ya Waziri hatukuona upande wa tumbaku kwamba ameweka ni tozo zipi ambazo zinapendekezwa kuondolewa. Wakati Wabunge tumeshazungumzia sana kwenye upande wa tumbaku kuna gharama nyingi, wakulima wanapata taabu kwenye bei na hizo tozo mbalimbali, kwa hiyo tunaomba ziweze kuangaliwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la maji, sera ya maji ilianza mwaka 1991 ikafeli, 2002 ikaboreshwa lakini ukiangalia mtiririko wa bajeti upande wa maji ndiyo una asilimia ndogo sana.
Kwa hiyo, nashauri angalau tuweke kati ya shilingi 20 kwa lita mpaka 50 ili tuweze kupata nakuunda mfuko wa maji tuweze kuboresha maji zaidi kwa wananchi ambao wengi wanakuwa na tabu kwenye kupata huduma ya maji na sera ya maji vijijini bado haijafikiwa ukamilifu wa zile mita 400.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la VAT kwenye upande wa Bima, Serikali inakusudia kuondoa VAT kwenye Bima upande wa ndege, lakini tujaribu kuangalia ni soko ambalo halina ushindani na je, kuondoka kwake kuondoa huu msamaha kuondoa VAT kwenye hizi bima upande wa ndege tunaathiri vipi mapato yetu na ni soko ambalo halina ushindani kwa hiyo, tutakuwa hatuna kwamba tunavutia zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitoa fedha na cealing kwa Halmashauri zetu, lakini tuombe mwaka ujao wa fedha Halmashauri ziangalie bajeti zao tukiangalia kiutawala Halmashauri ndizo zenye wajibu mkubwa wa kusimamia huko chini kwa sekta zote, lakini wanapangiwa kiasi kidogo kwa hiyo upande wa maendeleo kwa Halmashauri ambao ndiyo tunaangalia wapi tuna mapendekezo zaidi tunakuwa tunazuiwa na ukomo wa bajeti. Kwa hiyo, niombe Mheshimiwa Waziri Halmashauri zetu kwa mwaka ujao wa fedha ziweze kuangaliwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwanza nimshukuru Mungu kwa namna pekee ametujalia mpaka muda huu tuna afya njema. Naomba tu niseme mimi ni mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na naanza kuchangia kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza naomba Serikali iiangalie Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwanza kwa masuala ya bajeti. Tulisema na wenzangu wamesema basi ni wakati muafaka sasa kushughulikia suala hili. Waziri wa Fedha aliahidi mwezi Disemba ataangalia utekelezaji na ataongeza fedha kulingana na kazi zinavyoenda. Tunaomba ahadi hiyo ikifika Disemba wakati wa kupitia bajeti aliangalie. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Ofisi ya CAG kwa kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanya, tumeona matunda yake kwani wameibua hoja nyingi, kwa hiyo tunawapongeza sana. Pamoja na pongezi hizi tunahitaji Ofisi ya CAG iboreshwe zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa vikao vya briefing vya kupitia hoja zao ambazo wamezikagua na wamezileta kwenye Kamati tuliweza kugundua upungufu mdogo mdogo aidha ni wa wafanyakazi au mfumo, hili tutaomba aliangalie. Kwa mfano, kuna wakati tuliwahi kuwauliza maofisa wanaotoka CAG, kwenye auditing kuna kitu kinaitwa analytical review, una-check movement, una-analyze kati ya mwaka wa fedha huu na mwaka wa fedha hata miwili, mitatu iliyopita. Hiyo ndiyo auditing ambayo inafanyika tukaona kwamba hii Ofisi ya CAG ni kama vile inafanya kazi kama internal auditor badala ya external auditor. Kwa sababu uki-check movement ya accounts mbalimbali hiyo ndiyo audit japokuwa utaenda kwenye item na ukapata zile schedule na utaangalia utajiridhisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunahitaji wa-improve maeneo mbalimbali kwenye audit procedures, audit technique na audit plan ili waweze kwenda vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika utendaji wa Ofisi ya CAG tunajua wanaangalia muhtasari wa vikao vya Kamati za Fedha za Halmashauri zetu, lakini inabidi waongeze juhudi kwa sababu kwenye Kamati hizi za Fedha na Mipango ndipo mahali ambapo maoni mengi yanatolewa kuhusiana na matumizi mbalimbali ya fedha za Halmashauri. Kwa hiyo, tunaomba waongeze sana juhudi kwenye kuangalia muhtasari wa vikao vya Kamati vya Fedha na Mipango.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tukizihoji Halmashauri mbalimbali tuligundua kuna upungufu kwenye mfumo wa kihasibu kwa kutumia computer (EPICOR). Maoni yangu ni kwamba Serikali iangalie mfumo huu wa EPICOR tangu tumekuwa nao kwa miaka yote hii umetusaidia nini? Kama hauna msaada wowote ambao umeutoa kwa nini tusipate mfumo mwingine wa kihasibu kwa kutumia computer? Kwa sababu kumekuwa na upungufu mbalimbali, modules nyingi zimekuwa hazifanyi kazi na maeneo mengine kweli Halmashauri wanakuwa hawajawekewa mfumo huu, lakini ile link pamoja na platform zingine za kiuhasibu na za report zimekuwa hazifanyi kazi vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ifanye upembuzi yakinifu kuangalia upungufu ulioko kwenye EPICOR. Dunia ya sasa hivi ina mifumo mingi ya accounting package ambayo inakuwa ni strong hata internal control yake inakuwa ni strong, huwezi uka-temper data. Kwa hiyo, tuhame kutoka kwenye EPICOR twende kwenye software zingine ambazo zitakuwa na msaada kwenye Serikali yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona maeneo mengi pia kama TAMISEMI haijaweza kukamilisha ufungaji wa EPICOR na wakati huo huo kwenye Halmashauri zetu kumekuwa na tatizo la mtu mmoja ndiyo anakuwa mtu wa EPICOR tu watu wengine wanakuwa hawajifunzi pale pale ndani. Kwa hiyo, hilo nalo Waziri wa TAMISEMI aangalie, kwenye Halmashauri isiwe anategemewa mtu mmoja kama atahama au atakufa au atakuwa anaumwa mambo mengine yatakuwa yamelala.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni upande wa Hazina, miradi mingi haijatekelezwa kwa sababu fedha zimekuwa hazipelekwi kwa wakati au zimepelekwa kiasi. Kwa hiyo, tumuombe Waziri wa Fedha akaangalie commitment ambazo zimefanywa na Halmashauri zetu, wengi walishatoa GPN wapelekewe fedha ili miradi ya maendeleo iweze kufanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo napenda kuchangia ni upande wa Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa. Wakati wa vikao vyetu Katibu Tawala wa Mkoa wameji-commit kwenda kuhakikisha kwamba Halmashauri zinafanya kazi ipasavyo.
Kwa hiyo, tumuombe Waziri wa TAMISEMI akahakikishe kwamba anawakumbusha, maana Wakurugenzi wengi wameahidi kushughulikia ule upungufu ulioonekana na wengi wameahidi kwa maandishi. Tuombe Ofisi ya Katibu Tawala ya Mkoa kuhakikisha kwamba anazisimamia hizi Halmashauri ipasavyo ili hata masuala mengine CAG anakuwa anapunguziwa kazi kwa sababu wao wapo kila siku na wana watumishi katika ngazi ya Mkoa wenye fani mbalimbali na wanaweza kusimamia hizi Halmashauri ndani ya Mkoa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni deni la 10% ambapo Halmashauri zinatakiwa zitenge fedha kwa ajili ya kukopesha vijana na akina mama ili waweze kupata mikopo ambayo riba yake ni nafuu sana. Tatizo ambalo tumeligundua fedha hizi hazina akaunti maalum benki, kwa hiyo, zinakuwa kwenye pool moja na Halmashauri zetu pale OC zinapochelewa wanatumia fedha hizi. Kwa hiyo, niombe Waziri wa TAMISEMI alichukue hili, apeleke mwongozo waidhinishe Halmashauri ili ziweze kufungua account bank ziwe maalum kwa ajili ya kuweka hizi fedha za 10% baada ya kuwa wamezikusanya ili kuongeza udhibiti wa kutokutumia kwenye matumizi mengine. (Makofi)
Jambo lingine ni suala zima la Kamati za Bunge kuwa na ufinyu wa bajeti. Tunaelewa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 63, wajibu wa Bunge ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali na kupitia hizi Kamati tunakuwa tunaisimamia Serikali lakini fedha zimetengwa kwa kiasi kidogo na hatukamilishi kazi. Kwa hiyo, tutakuwa tuna-save kumi lakini kwa usimamizi ambao hatuufanyi tunapoteza mia. Kwa hiyo, niiombe Serikali kwenye mapendekezo ya mpango tulichangia hivyo na Waziri wa Fedha ahakikishe kwamba bajeti ya Bunge isiwe chini ya 20% ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2015/2016. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo napenda kuchangia ni kuhusu operesheni za Halmashauri zetu. Makusanyo ya ndani yana mgawanyo kwa mujibu wa kanuni na sheria, kuna 60% iende kwenye miradi ya maendeleo, 20% maeneo mengine na 10% kwa vijana na akina mama. Niombe Ofisi ya CAG ikasimamie sana mgawanyo wa hizi fedha wanazokusanya wenyewe (own source) kulingana na sheria ili tuhakikishe kwamba miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri zetu na kwa wananchi wetu hasa maeneo ya afya, elimu na maji inafanyika kwa fedha za ndani.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie tu kwa kuunga mkono ripoti ya Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na niombe Serikali ikatekeleze mapendekezo yote ambayo yameonyeshwa mule ndani na sisi kama Kamati ihakikishe kwamba tunapata mrejesho. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa hii nafasi. Nami kwanza nianze kuunga mkono hoja ya Kamati hii ambayo report yake ni nzuri kweli kweli na imesheheni mambo mazuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nianze kwa kuchangia upande wa Mfuko wa kusaidia Kaya masikini (TASAF). Mfuko huu tunamaoni kwamba uendelee kuwepo. Uendelee kuwepo kwa misingi kwamba sisi ni Wabunge, tumezunguka, tumefanya ziara maeneo mbalimbali, wazee bado wanalilia uwepo wa pension. Sasa kama wazee tu wanalilia walipwe pension kwa ajili ya kuwasidia sasa je, hizi kaya masikini kwanini tuziondoe? Kwa hiyo tunaomba sana Serikali huu mfuko uendelee kuwepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la msingi ni kuboresha, katika kupitia majina kila baada ya miaka mitatu ikibidi iwe miaka miwili, kwa sababu kumekuwa na changamoto za maeneo mbalimbali, Watendaji wetu kule chini wanakuwa wanachakachua majina wanaweka watu ambao hawana sifa za kufaidika na huu mfuko. Katika kuboresha, badala tu ya kuangalia kutoa fedha, tuone jinsi gani tutoe fedha kiasi na tutoe hata shughuli ndogondogo kama za ufugaji wa aina mbalimbali wa ndege au wanyama ili ziweze kuwaongezea kipato. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili lililozungumzwa kwenye ripoti ya Kamati ni kuhusu fomu za maadili, Watumishi wengi wa Serikali kwa mujibu wa sheria tunatakiwa tujaze fomu za maadili, lakini kwenye ripoti ya Kamati humu wamehimiza kuhusu TEHAMA. Serikali iangalie jinsi gani TEHAMA iweze kutumika ili tuweze kupunguza gharama na kuwa na ufanisi pia kwenda na wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, uwasilishaji wa fomu za maadili Wabunge wengi waliweza kusafiri tena kurudi kuzileta fomu kwenye Kanda, Watumishi wa Serikali wamesafiri kwenda kwenye Kanda kuwasilisha fomu, ilikuwa ni gharama magari ya Serikali yametumika na fedha za Serikali. Kwa hiyo, tuombe sasa tupate mfumo wa kuwasilisha hizi ripoti kimtandao – web based reporting. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nichangie kuhusu utawala bora. Kweli Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wameteuliwa na Mheshimiwa Rais katika kutekeleza na kumsaidia, lakini tuombe wajaribu kuangalia ile sheria inayowaruhusu kutoa amri mbalimbali kama vile amri za kukamata. Ni makosa gani ambayo yanapaswa kuingia kwenye hiyo amri ya masaa 48 ya kuweza kukamatwa. Kwa hiyo, yaangaliwe ni makosa ya aina gani, kwa sababu sheria ilitungwa na wana mamlaka hiyo ya kuitumia basi waende kwenye Kanuni na kuangalia ni makosa ya aina gani, hatubezi utendaji wao bali tunaunga mkono wanavyofanya kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili litakuwa sambamba pia na masuala ya kiutawala kwa upande wa utumishi. Tumesikia kauli mbalimbali, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa anamshusha mtu cheo au anamfukuza kazi badala ya kufuata taratibu za kiutumishi katika kuchukua hatua hizo. Kwa hiyo, tuombe sana Serikali wayaangalie makosa ambayo yamekwishafanyika kwa kipindi hiki na Waziri husika afanye utaratibu wa kutoa barua au mwongozo ambao utaweza kusaidia utendaji wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo tunapenda sana katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ni mfuko ule wa kuwakopesha vijana na akinamama kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri zetu. Ufuatiliaji umekuwa ni hafifu sana, OC ziende kwa wakati ili mapato yetu ya ndani yaweze kutengwa. Inatakiwa asilimia 60 iende kwenye miradi ya mendeleo. Ndani ya asilimia 60, asilimia 10 ni kwa ajili ya vijana na akinamama. Sasa Halmashauri nyingi mpaka sasa hivi ukiwauliza miezi hii sita wametenga kiasi gani utakuta hakuna Halmashauri ambayo imeshatenga zaidi ya hata asilimia 20.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba OC ziende ili mapato ya ndani yote yasitumike kwenye shughuli za kila siku na vijana wetu na akinamama waweze kukopeshwa fedha na ndiyo utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu Tume ya Utumishi ya Walimu. Tume hii imeanzishwa na kwa mujibu wa Kamati kuna changamoto sana kwenye upande wa bajeti na baadhi ya sheria na kanuni zinazoongoza. Tujaribu kuangalia kwanza mfumo. Tume hii sasa hivi inavyofanya kazi kwenye Wilaya kuna zile Kamati za kinidhamu, kwa hiyo kama Wilaya ina Halmashauri mbili au tatu sasa ushughulikiaji wa ile Kamati unakuwa ni mgumu kidogo kwa sababu ya composition ya Wajumbe wa ile Kamati wanatoka sehemu mbalimbali na ruzuku fedha zinakuwa hazipatikani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshauri mfumo huu uende kihalmashauri na Mkurugenzi azifadhili hizi Kamati za nidhamu za Walimu kwa ajili ya ufanyaji kazi. Kama zitakutana mara tatu kwa mwaka au mara mbili ili kuwa na mapitio kabla ya bajeti na baada ya bajeti na Walimu wanapata promotion mbalimbali. Pia coordination ndiyo itaenda vizuri kati ya TAMISEMI na Utumishi kuhusu upandaji wa madaraja ya Walimu, mambo ya kinidhamu ndiyo yataenda vizuri. Kwa hiyo, tunaomba Tume hii Sheria ibadilishwe ambayo itakuwa inaweza kuongoza katika kuhakikisha kwamba Walimu wetu, maslahi yao na kesi zao ambazo zimekuwa ni nyingi na ndiyo ajira kubwa ya Halmashauri au upande wa TAMISEMI idadi kubwa ni Walimu. Kwa hiyo, ni muhimu sana tuweze kubadilisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho tungeomba sasa upande wa Serikali kuhakikisha kwamba Halmashauri zetu zinalenga kwenye kufuatilia promotion au madaraja ya Walimu na mishahara yao ibadilishwe na iendane na bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja ya Kamati hii. Ahsante sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nianze kumshukuru Mungu wote tupo salama mpaka siku ya leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niipongeze Serikali kwa namna ya pekee ambavyo wameweza kunyanyua kiwango cha ukusanyaji wa mapato yanayotokana na kodi na yale ambayo hayatokani na kodi, tunapongeza sana. Tukiangalia miezi hii sita ya mwanzo TRA wameweza kukusanya 7.2 trillion ukilinganisha na miezi sita kama mwaka wa fedha uliopita 6.4. Kwa hiyo, ni hatua nzuri na Mheshimiwa Rais aendelee na juhudi hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini upande wa Halmashauri zetu zimefanya vibaya kidogo. Wamekusanya shilingi bilioni 117 ambayo ni sawa na asilimia kama 70, sababu ni zipi? Bado tuna vyanzo vichache vya mapato au kuondolewa kwa property tax na kukusanywa kwa upande wa TRA? Kwa hiyo, tungeomba Serikali waweze kuangalia suala hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tatizo lililopo pia ni haya mapato ya Halmashauri jinsi gani yanapelekwa kwenye miradi ya maendeleo. Halmashauri nyingi kutokana na uhaba wa OC wanatumia fedha zote na kwenye miradi ya maendeleo haziendi. Kwa hiyo, Serikali ifanye tathmini ya hii miezi sita, mapato ya ndani kila Halmashauri ilikuwa ni ngapi na kulingana na sheria ya asilimia 60 kwenda kwenye miradi ya maendeleo wamepeleka asilimia ngapi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niipongeze Kamati kwa kazi nzuri sana ambayo wameifanya. Wametoa maoni na tunaomba Serikali iyachukue. Kwanza tukianza na pendekezo la kujenga zahanati kwa Serikali kutoa shilingi bilioni 30, ni muhimu sana. Tuna vijiji karibu 12,800 sina takwimu za haraka sidhani kama vijiji zaidi ya asilimia 60 vina zahanati. Halmashauri yangu nina vijiji 59 lakini zahanati zipo kwenye vijiji 17 tu na ukiangalia uwezo wa Halmashauri nyingi kuweza kukamilisha masuala haya ni ngumu. Kwa hiyo, tuombe Serikali hiyo shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati kwenye bajeti ya 2017/2018 waiweke. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Kamati imeiomba Serikali kuongeza tozo kwenye mafuta kwa ajili ya Mfuko wa Maji. Sera ya Maji ya mwaka 2012 inasema kwamba wananchi watapata maji ndani ya mita 400 lakini mfano kwenye Jimbo langu mtu anakwenda kufuata maji mpaka kilometa tatu, ni tofauti na sera. Sasa tukishaitunga sera ni lazima tuweke mipango ya kuweza kuitekeleza. Mipango yenyewe ndiyo hayo maoni ya Kamati tuongeze kwenye mafuta kutoka sh. 50 mpaka sh. 100.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge la bajeti ya 2016/2017 tulihimiza sana hapa ndani, lakini Serikali haikuchukua ikasema tutaangalia bajeti hii, sasa bajeti hii tunaomba msiangalie basi mkubaliane na maoni ya sisi Wabunge ili tukatatue matatizo ya maji vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo langu asilimia 34 ya wananchi ndiyo wanaopata maji safi na salama. Kwa hiyo, ni jinsi gani tutaweza kutatua hili tatizo la maji, tuongeze hii shilingi 50 na tunaomba sana hiki kilio mkisikie. Kwa kufanya hivyo ndiyo utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwani wananchi wana kilio sana na maji na sisi Wabunge tunasema tukitatua tatizo la maji hata 2020 mtatuona tena humu ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi tumeahidi kutoa shilingi milioni 50 na Serikali imekubaliana, wametenga kwenye bajeti shilingi bilioni 59. Hata hivyo mpaka sasa hivi ule mpango mzima wa jinsi gani huu mfuko utaendeshwa ili tuondokane na yale matatizo ya awali yaliyotukumba kwa zile fedha maarufu zikiitwa za JK ambazo watu waliona ni za bure na hata hizi shilingi milioni 50 wananchi kule wanafikiria ni za bure, hapana! Tunaomba tuwaambie wananchi hii itakuwa ni revolving fund, mnakopa kwa riba iliyo ndogo ili na wengine waweze kukopa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali iangalie uwezekano wa kwenda angalau kata chache kwa kila Jimbo. Kupeleka shilingi milioni 50 kwenye kila kijiji itahitaji fedha nyingi sana. Sasa hivi tukiangalia makusanyo ya ndani ya Halmashauri, zile asilimia 10 kwa ajili ya vijana na akinamama wanaojitokeza kukopa hawakopi kwa kiasi kingi. Kwa hiyo, hata hii shilingi milioni 50 kwa kuwa itahitajika hela nyingi na makusanyo yetu hayatoshelezi kama bajeti ilivyo, basi tuangalie kata chache ziwe kama za mfano tuguse kila Jimbo angalau hata kata mbili shilingi milioni hamsini hamsini ndiyo tuanze kama mfano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wengi wamezungumzia kuhusu mapato. Naomba nichangie, zile ripoti, Chenge I na II bado Serikali irudi mle ikapekue. Suala la deep sea fishing hatujalisikia na masuala mengine. Kwa hiyo, tunaomba sana kwenye hii bajeti, Waziri wa Fedha na Kamati ya Bajeti mrudi kwenye ile ripoti ya Chenge I na II muangalie maeneo yote ya mapato ambayo yalielezwa ambayo yatasaidia katika bajeti yetu. Mwelekeo wa bajeti ni shilingi trilioni 32, tunatoka kwenye shilingi trilioni 29. Sawa, mmeweka vyanzo vingine pale lakini muangalie jinsi gani tunaweza tukafika hata shilingi trilioni 34 kutokana na vyanzo vingine vipya vya mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wamelalamika kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye utalii, basi Serikali ifanye utafiti, je, kweli hii kodi ambayo imewekwa kwenye auxiliary services za watalii imepunguzwa kwa kiasi gani ili watu wapate uelewa? Nafikiri wakati Waziri Mkuu anafunga Bunge, naomba Waziri wa Maliasili na Utalii ampe hiyo taarifa aweze kuisoma hapa tupate uelewa zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara imeshazungumzwa upande wa transit goods, tumeweka VAT ambayo imeleta mgogoro sana na mizigo yetu mpaka kupungua. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais jinsi alivyoweza kujenga mahusiano na viongozi wa nchi jirani na sasa biashara imeanza kurudi na tumeona kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala ya kilimo kama ndiyo Uti wa Mgongo na asilimia 70 ya ajira. Tunaomba ruzuku iongezwe na pembejeo zije kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo ambalo bado hatujaona ni jinsi gani tunaweza kupata fedha ni upande wa mifugo. Tuweke blocks za ulishaji na watozwe. Kwa hiyo, Serikali iangalie suala hili na tupunguze migogoro hii ya wakulima na wafugaji na tuone ni kwa jinsi gani tunaweza kupata mapato kutoka kwenye mifugo, hili ni eneo ambalo bado hatujaliweka sawa. Tunatoza mifugo tu inapouzwa mnadani lakini kwa kila siku inavyokuwepo na uharibifu wa mazingira kama tunavyoelewa, tuangalie tunawekaje tozo katika mifugo ili tuweze kuongeza mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kamati wameeleza suala la utawala wa Kibunge kwamba Bunge sasa litakuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Wabunge na Kamati nyingi hazikuweza kwenda kukagua miradi ikiwa ni sehemu ya kuisimamia Serikali kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 63 kwamba Bunge tuna wajibu wa kutunga sheria na kuisimamia Serikali. Sasa tunavyoenda kama Kamati kukagua miradi ya Serikali ndipo tunapoisimamia. Kamati nyingi hazijafanya safari na maslahi ya kiujumla kwa mfano, je, Mbunge anatakiwa akakae hoteli ya nyota ngapi? Kwa hiyo, tuangalie maslahi ya Wabunge na gharama kiujumla katika kufanya kazi zao za kuweza kuisimamia Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyokagua miradi ndiyo tunatia chachu kwa watumishi wetu kule, wakisikia Kamati inakuja ndipo utaona mambo mengi yanakwenda mbiombio wanakimbizana. Tunapotoa maagizo inasaidia sana katika kutekeleza miradi na ndipo tunaleta tija kwa wananchi ili waweze kujua kwamba Serikali yao sasa imewaletea miradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho naomba niseme kwamba, tunaenda nchi ya viwanda lakini tunaomba Serikali iangalie uwiano. Siku za nyuma Hayati Mwalimu Nyerere alijaribu kuangalia uwiano wa Kikanda kuweka viwanda ili kuweka usawa katika ajira. Kwa mfano, Mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora, Chunya wanalima tumbaku. Je, hatuna haja Serikali ikashawishi NSSF au PPF, hii Mifuko ya Jamii wakaingia ubia na Vyama vyetu vya Msingi kutoa mchango wao kwa kujenga kiwanda Tabora ili …
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Kwanza
nianze kwa kuunga mkono hoja za Kamati zote mbili, Kamati ya Mindombinu na Kamati ya
Nishati na Madini.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kwa haraka, hoja yangu ya kwanza ni kutoa
msisitizo kwa Serikali juhudi ambazo wameonyesha katika vipande vingine upande wa reli
kwenda kwenye standard gauge basi wasisahau na reli yetu ya Mpanda ambapo inaanza
kuchepuka kutokea Kaliua kwenda mpaka Mpanda na vilevile reli kufanyiwa usanifu kutokea
Mpanda mpaka Karema, upande wa Karema tunatarajia kuwa na bandari ambapo pana
upana mdogo katika Ziwa Tanganyika na upande wa pili wa nchi yetu ya jirani ya DRC.
Mheshimiwa Naibu Spika, umuhimu wa hizi reli pamoja na bandari kule Karema ni
kupitisha mizigo, sasa na tunaona nchi nyingi ambazo hazina bandari (landlocked conutries),
tutumie hiyo fursa ili tuweze kuongeza mapato katika bandari yetu. Taarifa ya Kamati
imeonyesha jinsi gani mizigo kwenye bandari imeweza kushuka kwa asilimia 0.1 na sehemu
nyingine asilimia 5.2, kwa hiyo tuombe sana Serikali iangalie reli upande wa Wilaya ya Mpanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uwanja wetu wa ndege wa Mpanda, uwanja wa
ndege wa Mpanda hauna gari la zimamoto, hamna mkandarasi wa mafuta, kwa hiyo tunahitaji
Serikali iweze kushawishi hivyo vitu. Tuna Mbuga ya Katavi ambapo ni moja ya maeneo ya
mbuga ambayo wanasema ni very virgin, wanyama wana asili sana, ukienda Mbuga ya Katavi
utaona asili yao ukishuka kwenye gari samba anakimbia, tofauti na maeneo mengine kama
Serengeti. Kwa hiyo, uwanja wa ndege huu ni muhimu sana kwa ajili ya utalii kwenye Mbuga
yetu ya Katavi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala la mawasiliano tunahitaji kampuni za simu
ziendelee kuimarisha mawasiliano, na hasa Kampuni ya Halotel ambayo ilianzia vijijini, maeneo
yetu mengi tuna matatizo ya mawasiliano. Ukiwa unasafiri kutoka Mpanda kuja Tabora kuna
maeneo ya katikati unatembea kilometa karibu 90 hakuna mawasiliano, sasa inapotokea
dharura yoyote na dunia sasa hivi iko kwenye kiganja, kwa hiyo, tunaomba Serikali iendelee.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la SUMATRA, mamlaka hii ipo lakini usimamizi wa bei
bado ni hafifu sana. Tumepata kero nyingi kwenye ziara tulizozifanya, kwa mfano watu wetu
wanaotoka Mpanda kwenda Ugala wote wanachajiwa shilingi 5,000 lakini katikati hapa kuna
sehemu wanatakiwa walipe shilingi 2,000, shilingi 3,000 na shilingi 4,000 lakini wote wanalipa bei
moja. Kwa hiyo, SUMATRA wasiwe wanasubiri malalamiko ya wananchi, wawe wanafanya
testing ya hizi control zao zinafanyaje kazi na wachukulie hatua watu wenye vyombo hivi vya
usafiri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hapohapo kwenye mawasiliano, TCRA watusaidie
Halmashauri zetu, na ningeomba mwongozo wa Serikali, hii minara inakuwa na rekodi ya
mawasiliano yamefanyika katika lile eneo na yale mapato ambayo yametokana na kampuni
za simu kwenye mnara husika.
Sasa ile service levy haya makampuni wanalipa wapi? Kwa hiyo, unakuta Halmashauri
zetu hazipati mapato toka kwenye makampuni ya mawasiliano kwa sababu ya mawasiliano au
muunganiko katika ya TCRA na Halmashauri kidogo uko tofauti.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikienda kwenye madini, tumekuwa na changamoto kwa
wachimbaji, wamekuwa na migogoro na watu ambao wamepewa leseni. Kwa mfano kwenye
Jimbo langu la Nsimbo, eneo la Kijani Investment imekuwa ni mgogoro, Kampuni ya Sambaru
imekuwa ni mgogoro wanasema hakuna muhtasari, sasa shida iliyopo ni nini, tungeomba
Serikali itenge maeneo kwa ajili ya watu ambao hawana leseni, watu leo anaamua akachimbe
anunue unga au alipe ada na yawe chini ya uongozi wa kijiji ndiyo uweze kusimamia. Tukifanya
hivyo tutaondoa migogoro kwenye haya maeneo ya watu ambao wanakuwa na leseni.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile upatikanaji wa service levy toka kwenye makampuni
haya yanayochimba yenye leseni ndogo (PML) na leseni kubwa, rekodi zao haziko sahihi kwa
hiyo, Halmashauri zetu hazipati service levy. Kwa hiyo, nashauri Serikali iangalie fixed amount
kulingana na aina ya leseni na sehemu nyingine iwe ya kiasilimia.
Mheshimiwa Naibu Spika, niombe upande wa nishati, REA III, kwa Mkoa wetu wa Katavi
vijiji 74 haviko kwenye huu mpango wa sasa hivi, kati ya vijiji 191 tumepewa vijiji 117 na ni mkoa
wa pembezoni ambao ulisahaulika sana kimaendeleo. Kwa hiyo, tunaomba vijiji 74 viongezwe
na wakandarasi waongezewe mikataba yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, tunaomba Serikali iendelee kutoa ushirikiano kwa
kampuni inayofanya utafiti wa mafuta Ziwa Tanganyika na pia gesi na maeneo mengine ya
madini katika Mkoa wa Katavi na mikoa jirani.
Mheshimiwa Naibu Spika, basi baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja za Kamati
hizi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Kwanza nimshukuru Mungu kwa kuweza kutufikisha siku hii ya leo. Binafsi naomba nimpongeze Waziri Mkuu na timu yake na Mawaziri wote kwa jinsi ambavyo wameshirikiana naye katika kuandaa bajeti hii. Naomba nimpongeze Mheshimiwa Jenista Mhagama na Naibu Waziri, Mheshimiwa Mavunde kwa kushiriki vyema kwenye bajeti hii pamoja na uwashaji wa mwenge Kitaifa kwenye Mkoa wetu wa Katavi. Wametupa ushirikiano wa hali ya juu, tumekwenda nao na wamefanya kazi kubwa kwa kweli tunawapa pongezi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kidogo nigusie kwenye hotuba ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Mbowe. Kuna mahali alizungumzia kwamba bajeti ya Serikali ni ya kisiasa, kwamba ina vyanzo hewa vya mapato. Naomba alichukue hili, yeye
hotuba yake ndiyo ya kisiasa kwa sababu kwenye hotuba yake ile amesema kwamba Serikali kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 iliweka chanzo cha kodi kwenye kiinua mgongo cha Wabunge wakati kodi hiyo itakwenda kutozwa mwaka 2020. Naomba nimwambie kwamba yeye ndiyo amefanya kisiasa, sio sahihi. Nakumbuka mwaka jana nilileta schedule of amendment kwenye eneo hili na Kanuni ilifuatwa, kulikuwa hakuna financial implication kwenye masuala ya kodi kwenye kiinua mgongo cha Wabunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, kwenye bajeti hii ya Ofisi ya Waziri Mkuu ameweza kuzungumzia kwa kina kuhusu uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. Naunga mkono, wameweza kutoa shilingi bilioni 1.5 kwa vijana kutoka kwenye ofisi yake na takribani shilingi bilioni 4.6 kwa upande wa mapato ya ndani kwenye Halmashauri zetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tatizo ninaloliona ni Halmashauri nyingi kutotimiza ile kanuni inayoelekeza kutoa asilimia tano kwa vijana na asilimia tano kwa akina mama. Kwa hiyo, niombe sasa ili tuweze kufikia kuwawezesha wananchi wetu kufanya shughuli za kiuchumi, Serikali iweke msisitizo kwenye kuhimiza Wakurugenzi na kuwasimamia ili waweze kuhakikisha kwamba fedha hizi zinakwenda, maana Halmashauri nyingi maombi yapo lakini watu hawajapewa hizo fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia yale mafunzo ambayo yaliweza kutolewa chini ya Ofisi hii ya Waziri Mkuu kupitia VETA, Don Bosco, tunaomba yawe endelevu na hapa ndipo itakapokwenda kutusaidia katika kujenga ajira maana kuna watu wameweza kupata mafunzo haya na cheti. Naomba Serikali, Halmashauri zetu tuna mwongozo tunapeleka magari yetu kwa mfano TEMESA, lakini utaangalia gharama ile ambayo Halmashauri zinalipa kule TEMESA kwa baadhi ya huduma ni ghali sana. Kwa hiyo, tuombe sasa Serikali kwa mafunzo haya ambayo yanaendeshwa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu tuweke ajira za mikataba kwa watu ambao wamepata mafunzo ya ufundi ili tuwe na mafundi wetu katika Halmashauri tupunguze gharama ambazo zinakuwa hazina tija kwa upande wetu, tukiwezesha vijana tayari tumejenga suala la ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni migogoro. Ofisi ya Waziri Mkuu hili liko chini yenu kuna CMA na Mabaraza ya Wafanyakazi lakini kuna matatizo ya watumishi wanakuwa wanahamishwa bila tija tu kwa malalamiko ya baadhi ya viongozi. Utakuta kiongozi eneo moja tu
analalamika kwa makosa ambayo mtu anaweza akasahihishwa basi anahamishwa, kwa hiyo, tunaongeza gharama kwa Halmashauri na ndiyo tunazidi kuweka madeni upande wetu wa Serikali kwa uhamisho ambao hauna tija. Tunakumbuka wakati Mheshimiwa Rais alivyoapishwa
alisema kwamba hatamhamisha mtu, mtu atakuwa anachukuliwa hatua za kinidhamu kwenye eneo ambalo yuko. Sasa tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu itoe mwongozo kwa Wakurugenzi wasifanye uhamisho ambao hauna maslahi ya kihalmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni la Bunge letu hili. Wabunge wamechangia, tumeona kwamba kuna ongezeko la bajeti karibu shilingi bilioni 21. Napenda kujua, kwa mwelekeo mpaka mwisho kuna upungufu wa shilingi bilioni 21 na gharama nyingine za msingi ambazo Serikali
iliweza kuziomba na kuziahirisha, je, hii bajeti ya sasa hivi ya shilingi bilioni 121 kweli inakidhi? Kwa hiyo, tuangalie zile gharama nyingine, kwa mfano, ile wiki ya kwanza kutokana na Kanuni tarehe 11 Machi hatukuweza kufika, je, ile gharama imekuwa-incorporated kwenye hiyo shilingi bilioni 21? Kwa hiyo, tunaomba kwa misingi ya Katiba kama Bunge tunaofanya hiyo kazi bajeti hii iweze kuangaliwa kwa undani zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuongelea kuhusu walemavu. Ofisi ya Waziri Mkuu ina wajibu huo na sheria ipo ya mwaka 2010, Sheria Na. 9 na kuna Mabaraza ya Walemavu katika ngazi ya Kitaifa, Mkoa mpaka kwenye Kata. Je, nani mwenye wajibu wa kuhakikisha kwamba Mabaraza ya Walemavu kwenye Kata na Wilaya yanafanya kazi na kanuni zake zipo? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama inavyofanya kazi TASAF basi na walemavu wawe na mfuko wao tuweze kuwawezesha iwe ni sehemu ya ruzuku na isiwe mkopo ambao una riba na wapewe mafunzo kulingana na ulemavu mtu alionao ili aweze kufanya kazi yoyote ile. Siku moja redioni nilisikia mtu mwenye ulemavu wa macho anampima mtu na anashona nguo. Kwa hiyo, tunahitaji sana tuwaendeleze ili waweze kuondoka kutoka kwenye utegemezi. Kwa hiyo, tuombe sasa Ofisi ya Waziri Mkuu huu mfuko kama haupo basi muuanzishe na angalau hata kabla Bunge hili halijamalizika tuweze kuupata. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la Mifuko ya Jamii. Mwaka 2012 tuliweka sheria ya kuzuia lile fao la kujitoa lakini sina uhakika, ila ni kwamba NSSF japokuwa hii sheria ilikuwa inazuia waliweza kuendelea kutoa fao la kujitoa. Nchi yetu tunahitaji hii mifuko ya hifadhi ya jamii iweze kusaidia katika kuleta viwanda na tumeona maelekezo kwenye randama humu kuna karibu mikoa 14 ambayo mifuko ya jamii inaelekezwa kwenye kuwekeza. Maoni yangu kwa sababu kuna mwingine anakuwa ameachishwa kazi na hana uhakika wa kupata kazi basi Serikali iangalie angalau katika lile fao la kujitoa ama akate asilimia 25 ya akiba mtu aliyonayo au theluthi moja yule mtu aweze kupewa ili katika kipindi cha mpito wakati anatafuta kazi ziweze kumsaidia katika kuendeleza maisha aliyonayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye upande wa kisekta tunajua tuna Wizara zinahusika na haya mambo ya kisekta, upande wa viwanda, lakini nizungumzie kuhusu barabara ambayo kwenye bajeti hii ipo, ya Mpanda - Tabora kwa kiwango cha lami. Tender zilitangazwa lakini mpaka sasa hatujafahamu ni watu gani wamekwishapewa hizo tender kutokana na marekebisho ya mkandarasi mshauri. Kwa hiyo, tuombe watu wa TANROADS watuharakishie. Sisi tukifanya ziara kule wananchi wanatuuliza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Mpanda mpaka Tabora lini unaanza? Sasa kama fedha ipo tulishapata toka ADB kwa nini watendaji wetu wa TANROADS Makao Makuu wanachelewesha kurekebisha hiyo BOQ ili kazi ziweze kuwa awarded? Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye upande wa kilimo tumeona taarifa kwenye mpango, kilimo kimekuwa kimekua kwa asilimia 2.9 tofauti na malengo ya asilimia sita. Sasa tatizo ni nini na hapa ndiyo ajira kubwa ya wananchi wetu ilipo. Kwa mfano, Jimbo langu la Nsimbo asilimia 90 ya wananchi wangu ni wakulima wanalenga zaidi kwenye shughuli hii ya upande wa kilimo.
Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa maliasili, tuna Mbuga yetu ya Katavi, tunahitaji miundombinu iboreshwe na huduma ya Bombardier ya ATCL ianze ili watalii waje. Tuna viboko, Ziwa la Katavi, twiga mweupe ambaye atakuwa ndiyo kivutio zaidi kwa watalii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono bajeti hii ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Ahsante.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali kwa kuongeza bajeti tangu iingie madarakani na Mawaziri kufanya kazi kwa bidii na umakini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Msanginya kikiwa chini ya Wizara ya Afya kiliingia mkataba na Mkandarasi wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Chuo hicho, lakini mpaka sasa ujenzi umesimama na Mkandarasi hajalipwa kwa kazi za awali. Pia miundombinu mingi bado ni chakavu sana. Hivyo Serikali inaombwa kuangalia na kutatua kero hizo kwa kuongeza bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatoa wito kwa Serikali kulipa deni hili na kazi ikamilike ili huduma ziboreshwe na vijana wapate elimu bora na kuwasaidia katika maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma za Bima ya Afya kwa hospitali binafsi nyingi hazijaingia mkataba, hivyo kutowapa fursa wanachama wa NHIF kufaidika na huduma hiyo. Hivyo basi, Serikali itoe mwongozo kwa hospitali zote binafsi kupokea Bima za NHIF. Vilevile namna ya kuhudumia wateja wa NHIF iwe bora zaidi kwa kuwa wateja wa NHIF hupewa Wauguzi wachache na kuathiri muda wa kupata huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kuathiri mila, desturi na imani zetu, Serikali haina budi sasa kuleta Sheria ya Ndoa ya 1971 iboreshwe ili kurekebisha umri wa mtoto kuolewa na kuoa iwe miaka 18. Kwa kuwa miaka ya sasa, elimu kwa watoto angalau idadi kubwa wanafika kidato cha nne, kwa nini tuondoe haki ya watoto kupata elimu ya sekondari ukizingatia kuwa sekondari takriban kila kata zipo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, nchi haina dini, hivyo imani za watu wachache zisizuiwe haki za watoto kupata elimu na kuondokana na mimba zenye kuhatarisha maisha yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Rufaa katika nchi zipo kikanda ili kusaidia mikoa yote, lakini Kanda ya Magharibi hatujaona katika hotuba ya bajeti. Hivyo, tunashauri Mkoa wa Katavi uwe na Hospitali ya Rufaa kwa Kanda ya Magharibi kukidhi Mikoa ya Katavi, Kigoma, Tabora na Rukwa pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua Wizara ya Afya haiwajibiki moja kwa moja, lakini kwa kupitia wafadhili mbalimbali na kutimiza sera mbalimbali hususan kupunguza vifo vya mama na mtoto, Halmashauri ya Nsimbo bado tunahitaji gari la wagonjwa kutokana na moja lililopo kuwa halikidhi mahitaji, sababu ya eneo lilivyo la Jimbo la Nsimbo na pia miundombinu mibovu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Saratani ya Ocean road inahitaji kutanua huduma zake kwenye Hospitali za Rufaa kila kanda na kuwa na watumishi wanaowajibika moja kwa moja ili kusogeza huduma karibu kwa wananchi kwa kuwa ugonjwa wa Saratani umekuwa tatizo kubwa hasa kwa akina mama (cancer ya uzazi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtaji wa Benki ya Wanawake bado kuongezwa kwa kiasi cha kukidhi haja za wanawake, nchi nzima, hivyo tunashauri Serikali iongeze mtaji kama tulivyotoa tangu mwaka jana bajeti ya 2016/2017. Vile vile Halmashauri nyingi hazijatumia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, hivyo basi Wizara itoe taarifa kwa Wakurugenzi ili fedha zitoke na wanawake watumie fursa ya kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu na huduma za lishe ni muhimu sana ili kuondoa udumavu kwa watoto. Hivyo Wizara isimamie Halmashauri zote kuhakikisha zinatoa elimu na kusimamia lishe kwa watoto kwa kuhakikisha wazazi wanachangia gharama za lishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri alitoa taarifa nyakati tofauti kuwa mikoa tisa itapata Madaktari bingwa na Mkoa wa Katavi ukiwemo. Sasa zoezi hili limefikia wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nawapongeza Waziri na Naibu, pia watendaji wote katika Wizara kwa kazi nzuri na makini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kuchangia kuhusu makazi ya wakimbizi. Serikali ilipokea wakimbizi kutoka Burundi na kufufua makambi ya Katumba na Mishamo (Mpanda) na Ulyankulu (Tabora) na mwaka 2009 walianza kupewa uraia, lakini kwa sasa bado watu wachache hawajapata uraia. Wito kwa Serikali ni kuwataka Umoja wa Mataifa kufadhili maeneo hayo katika huduma za jamii mfano afya, elimu, barabara na uchumi kwa kuwa maeneo hayo yalikuwa yanafadhiliwa na UN. Hivyo ni muhimu nchi ambazo zimeathirika kwa namna moja au nyingine na kupokea wakimbizi basi UN izisaidie kama wanavyofanya kwa nchi zingine.

Tunaomba kauli ya Waziri ni lini Serikali itaibana UN kufadhili makazi ya Katumba (Mpanda - Katavi) kwani kwa sasa wametoa ambulance moja na kukarabati Kituo cha Afya Katumba, kituo ambacho bado hakitoshi kabisa kwa wananchi zaidi ya 60,000 waliopo Katumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kuhusu huduma za Konseli Miji ya Biashara. Tunajua kwa Serikali imefungua Balozi nchi ambazo tunafanya nazo biashara lakini mfano China Ubalozi upo Beijing, lakini Mji wa Biashara ni Guangzhou ambao upo mbali sana toka Beijing. Kwa hiyo, ni muhimu kuwa na huduma za konseli kwa watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, nizungumzie suala zima la kuimarisha amani. Tunazidi kutoa wito kwa Wizara kuongeza juhudi za kuimarisha amani kwa nchi jirani za Burundi, Kongo, Rwanda na Uganda ili kupunguza kuingia kwa wakimbizi ambao wanaathari nyingi katika jamii yetu kiutamauni, kiuchumi, ujambazi, wizi wa nyara na silaha haramu. Hivyo, Tume zilizoundwa ziendelee kuimarishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, ni kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuna nyanja nne za ushirikiano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Changamoto zilizopo katika maeneo mawili tunazikabili vipi na tunajiandaa vipi kwa maeneo ambayo bado kuingia katika ushirikiano? Vilevile Serikali iendeleze kushirikisha Wabunge wa EAC kama nchi katika kujenga hoja na kusimamia vema maslahi ya nchi. Nawasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi hii. Kwanza nimshukuru Mungu na pia nimpongeze Waziri kwa uwasilishaji mzuri pamoja na Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuchangia suala la shule za msingi na sekondari kwa ujumla wake upande wa sanaa, michezo na utamaduni. Sijui kama ni sera imebadilika au ni kipi kilichotokea tofauti na miaka ya nyuma, shule zetu za msingi tulikuwa tunafundishwa michezo, sanaa, utamaduni na muziki. Hii ilikuwa inatujenga mpaka hata leo hii wengine tunaweza kuimba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ilikuwa inasaidia kwa mtu ambaye anaendelea kusoma mpaka chuo kikuu anaenda kusomea muziki na kuna kozi zingine kwa mfano kama physical education, mtu anasomea muziki somo lingine la kufundishia. Kwa hiyo, atatoka ni mwanamuziki lakini pia anakuwa na somo la kufundishia. Msingi unakuwa umejengwa kuanzia shule ya msingi na tuna vyuo vingine ambavyo vilikuwa vinatoa diploma kwa mfano kule Mwanza (Butimba) watu wamesoma sanaa.

Kwa hiyo, tuombe Waziri atakavyokuja ajaribu kutuelekeza kwamba ni jinsi gani ataweza kurudisha kwenye shule zetu za msingi na sekondari jambo hili ambalo lilikuwa linatusaidia katika kukuza hivi vipaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Wizara hii tunaoanisha na utalii, kwa misingi ipi? Tunavyowakuza watu waka-perfom nje ya nchi, kama walivyokuwa akina Filbert Bayi na wengine, tukiangalia nchi za Kenya, Ethiopia watu ambao wanaweza kufanya hizi mbio za marathon kama akina Haile Gebrselassie wameingia mpaka kwenye matangazo, wanatangaza nchi yao, wameingiza mapato ya ndani katika nchi yao kwa kuleta fedha za kigeni. Sasa na sisi Wizara hii itakuwa ni moja ya Wizara ambazo zitaweza kuukuza utalii katika nchi yetu kwa watu kufanya kazi nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyikiti, kwa upande wa sanaa kwa mfano tulikuwa na Marehemu Kanumba aliweza kufanya collaboration na Wanaigeria, imeenda, sasa hizi tuna mwanamuziki Diamond anafanya collaboration na wanamuziki mbalimbali mpaka Marekani na huko kwingine. Kwa hiyo, Wizara hii inakuza utalii ni muhimu sana kwenye pato letu la nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine dunia sasa hivi imekuwa kwenye kiganja, teknolojia imekua. Ni jinsi gani Wizara inachukua ukuaji wa teknolojia katika kudhibiti mambo mbalimbali pamoja na kuongeza mapato. Kwa mfano, sasa kupitia simu zetu (smart phone), ukiingia youtube utaangalia wimbo umekuwa viewed labda mara milioni 900. Kwa mfano wimbo wa Diamond Mdogo mdogo ukiingia youtube sasa hivi viewers wame-view kwa milioni 900 karibuni na laki tatu. Je, kama Serikali kwa kupitia hii mitandao, tuna njia gani ya kuongeza mapato katika maeneo hayo? Sasa hivi watu wana-create application mbalimbali ambapo unaweza ukaingia uka-download na ukapata miziki mbalimbali, je, Serikali kupitia hizi applications tunaweza kufanyaje ili tuweze kuongeza mapato? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu ukuzaji wa mapato. Tukiangalia mchanganuo wa makusanyo ya maduhui, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ndio limeingiza shilingi 70,560,000 katika mapato ya kiujumla haya ya shilingi bilioni 36, kwa hiyo ni asilimia ndogo mno. Je, hawa viongozi wa Baraza la Michezo wana mkakati gani kuhakikisha kwamba wanapandisha mapato? Mapato haya ni madogo tatizo ni nini? Tuna poor internal control au vyanzo vingi vya mapato havifuatiliwi? Kwa hiyo, tutaomba Mheshimiwa Waziri wakati anahitimisha angalau awe na majibu ya jinsi gani BMT waweze kukuza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni ukuzaji wa vipaji, hizi academy. Tunamshukuru Mheshimiwa Jakaya Kikwete pale Kidongo Chekundu Dar es Salaam aliweza kuweka ile academy. Je, kwa ujumla wake tukienda kikanda, tuna mkakati gani angalau kikanda tukawa na ukuzaji wa
vipaji ili vijana wetu katika michezo ya aina mbalimbali mfano riadha, tufe, mikuki, netball, basketball yote ili tuweze kwenda kimataifa. Leo hii mimi ukanipeleka nikawe mwanamchezo mzuri wa football siwezi kuwa lakini mtoto mdogo kuanzia miaka mitano diyo wanatakiwa wajifunze. Sasa hivi ukiangalia mtoto wa Ronaldo anacheza mpira mzuri, yuko kwenye shule na ni academy, mzazi wake anamlipia na atakuwa mchezaji mzuri, ataingiza pato lake binafsi na la nchi. Sasa hizi academy kama Wizara kwa kushirikiana na vyama mbalimbali vya michezo mje mtuambie mkakati gani ambao mnaolenga kuweza kukuza michezo nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la sheria mbalimbali zilizoko katika Wizara. Mara ya mwisho ziliboreshwa lini ili kuendana na uhalisia wa hali halisi ya dunia ilivyo sasa hivi? Kwa hiyo, tutaomba Mheshimiwa Waziri upungufu wowote ulioko kwenye sheria mbalimbali hata hizi za haki miliki ambazo wasanii wengi wanalalamikia zije kwa ajili ya maboresho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sikufuatilia kwa ukaribu, tutaomba kujua ile mikakati ya vazi la Taifa na tamaduni mbalimbali lilifikia wapi? Nakumbuka mwaka jana ilizungumziwa lakini imefikia wapi kwamba hili ndilo vazi la Mtanzania ambaye akivaa hivi unajua ametoka Tanzania. Wenzetu Wahindi ukiona tu lile vazi unajua hili la Kihindi, ukimwona Mnaigeria unajua vazi la Kinaigeria na nchi zingine sasa na sisi Tanzania identity yetu katika utamaduni ni ipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho lakini siyo dogo, ni jinsi gani tunavyo-link Wizara na Halmashauri zetu za Wilaya, Manispaa na Majiji kupitia Idara za Utamaduni. Nashauri wapewe vifaa angalau pikipiki kwa ajili ya kuzunguka katika maeneo mbalimbali ili wafanye kazi zao kiufanisi. Ukiangalia Maafisa Utamaduni ni moja ya idara ambazo katika Halmashauri hazina vifaa kabisa, Wabunge tukienda tunataka kuendesha ligi inabidi umtafutie usafiri ili ndio akazunguke huko vijijini na vijijini tuna vijana wanamichezo wengi kweli kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hukitimisha tu naomba sana michezo upande wa shule za msingi na sekondari tuirudishe ili vijana wetu waweze kukuza vipaji na ni njia ya afya mojawapo, ukiangalia sasa hivi Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ametoa wito kwa watumishi kufanya mazoezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naomba niipongeze Serikali kwa namna ya pekee ambavyo imekuwa ikitenda kazi na kutekeleza ahadi mbalimbali zilizoko kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, binafsi katika Jimbo la Nsimbo 97% ni wakulima, 3% ni watumishi ambao ni kada upande wa walimu na huduma ya afya. Kwa maana hii ni kwamba, Wilaya hii inagusa sana Jimbo la Nsimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo langu la Nsimbo 55% ya mapato ya ndani yanatokana na zao la Tumbaku, lakini tumekuwa na changamoto na nimshukuru Waziri kuna tozo amezipunguza hapa, lakini katika hizi tozo kumi, tozo nne zinagusa wakulima, tozo sita zinagusa makampuni.

Sasa Mheshimiwa Waziri, hizi tozo zinazogusa makampuni kwa tani 60,000 ambazo haya makampuni wanatarajia kununua, ukichukua average cost per ton na hiki alichokipunguza is very minor. Hai-promote katika wakulima kupata bei nzuri kwa haya makampuni kununua Tumbaku; kutoka 4,000 mpaka 2,000 na hizi 4,000 nyingine alizofuta. Kwa hiyo, nakuomba Mheshimiwa Waziri uliangalie tena, libakie la wakulima, la makampuni liondoke kwa sababu hai-promote kwenye bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, wakati wa Mkutano wa Wadau wa Tumbaku, Morogoro, mwaka 2016 Desemba, Mheshimiwa Waziri aliahidi kwamba suala la bei na kuna sheria ambazo zitakuja, tutaweza kuzibadilisha hapa ndani. Sasa tutaomba wakati wa majumuisho atuambie ni lini zinakuja?

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kumekuwa na malalamiko sana kwa upande wa wakulima kuhusiana na ukaguzi unaofanywa na COASCO. Hii COASCO iangaliwe, kwa sababu ukiangalia tija yao katika ukaguzi wa vitabu vya mahesabu vya vyama vya msingi bado kuna mahali wanapita wanatoa Hati Safi lakini badaye unakuta kuna ufujaji wa pesa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri angalia WETCU Tabora. Waziri Mkuu kafanya ziara, ameibua, kasimamisha watendaji na Bodi, lakini rudi nyuma kwenye ripoti za COASCO. Kwa hiyo, COASCO iangaliwe kama uongozi ubadilishwe, mfumo na utendaji wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoangalia zao la Tumbaku tuangalie na mazingira. Ni zao ambalo linahitaji sana miti. Mmetoa mabanio kidogo ya kisasa, lakini pia makampuni yanaenda yanashusha kiwango cha kununua. Ukiangalia katika hotuba ya Waziri, mwaka wa fedha 2015/2016 kwa tumbaku ni 60,691 na takwimu hiyo hiyo ikaenda 2016/2017, lakini 2017/2018 itakuwa 55,900. Kwa hiyo, kiwango kinashuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa watu masikini ambao ni wakulima waliozoea kulima tumbaku, wanahitaji zao mbadala. Kwa nini tunahitaji zao mbadala? Tayari nchi imeamua kuwa ya viwanda. Tatizo kwenye tumbaku limeshaonekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaiomba Wizara, ile mapping ya mazao nchi nzima kwa kila Wilaya yanastawi mazao gani? Tuweze kugawiwa tuwape wananchi wetu wapate mazao mbadala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona tuna demand ya viwanda. General Tyre sasa hivi raw materials anatoa wapi? Bakhresa anatengeneza juice, raw materials nyingi inatoka nje ya nchi, kwa nini yasitoke humu humu? Kuna maeneo mengine watu hawana uelewa kwamba hapa ninaweza nikalima zao gani kwa sababu tangu mkoloni mtu amezaliwa, tangu mababu analima mazao hayo na watu wanaendelea hivyo hivyo. Kwa hiyo, Wizara kwa kupitia Halmashauri zetu, itoe hizo takwimu na sisi wanasiasa, Wabunge na Madiwani tusaidie kuelimisha wananchi. Hii itasaidia viwanda vipya vinavyokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna viwanda vya zamani vinavyohitaji raw materials na wengi wananunua kutoka nje na matokeo yake pesa nyingi ya kigeni tunazitumia kuagiza malighafi kwa ajili ya viwanda badala ya kwamba tuwekeze kwenye kilimo zaidi, tupunguze pesa ya kigeni kwenda nje ili balance of payment iendelee kuwa positive na ndiyo uchumi ambavyo unaenda unakua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna suala limezungumziwa hapa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge, kuhusu utafiti, mambo ya research, nami niungane mkono nao. Mwaka 2016 tumepitisha hapa Bungeni The Tanzania Agriculture Research Institute Act, 2016 na tumepitisha The Tanzania Fishers Research Institute Act, 2016. Kuna Bodi zinatakiwa ziundwe kwenye hizi institutes, je, mpaka sasa hivi zimekwishaundwa na kazi zimeanza? Kwa sababu inawezekana zile nyadhifa za Rais bado hajakumbushwa kuweza kuteua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba Mheshimiwa Waziri utatupa mrejesho wa hizi sheria mbili tulizopitisha na hizi Bodi kama zimeanza kazi na faida yake ni ipi? Kwa sababu tunajua, moja ya majukumu ya Bodi kama Agriculture Research Institute, ni kuishauri Serikali katika national policies, laws na regulations mbalimbali kwenye mambo ya Kilimo. Sasa badala ya kukaa tunalalamika hapa mambo ya research na sheria tumeshatunga, ni suala ambapo mnatakiwa Wizara sasa ndiyo mkimbie badala ya kutembea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna suala la pembejeo. Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini mvua zinawahi kuanzia mwezi wa kumi. Serikali ijaribu kuangalia kwamba pembejeo hizi zije kwa wakati, na pia ruzuku iwepo. Serikali imekuwa na jitihada kubwa sana tangu Uhuru. Nilikuwa naangalia Hansard swali la mwaka 1963 liloulizwa na Marehemu Philipo Mbogo, kwamba ni lini Serikali italeta matrekta na majibu ya Serikali, ilikuwa kwamba kwa kupitia Agriculture Credit Agency watapeleka matrekta Mpanda by that time.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mikakati hii tangu baada ya Uhuru ya kunyanyua kilimo, tukaja Benki ya CRDB hatukuifanyia vizuri, matokeo yake Benki ya CRDB imekuwa benki ya kibiashara badala ya kusadia vyama vya ushirika na wakulima. Sasa hivi tuna Tanzania Agriculture Development Bank. Mtaji ni mdogo, wakulima wetu kule kwenye vyama vya msingi wanakopa kwenye benki ya biashara, wanatozwa riba kubwa, lakini benki mahususi ambayo imeanzishwa kwa ajili ya kilimo, bado haiwasaidii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malengo, kama ilivyokufa CRDB imekuwa benki ya kibiashara isije na hii Benki ya Maendeleo ya Kilimo na yenyewe ikaangukia vile. Kuna uwiano kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara, kuna ile kitu inaitwa MUVI (Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini). Wakulima wanafundishwa, wanapewa mbegu bora, Kwa Nsimbo lini watakuja? Mawasiliano kati ya Wizara ya Viwanda na Kilimo yako wapi?

Pia katika tafiti tuangalie, tunaenda kwenye nchi ya viwanda, kuna writeup ya Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akichukua Doctorate alifanya writeup kwa kuangalia utomvu kwenye mabibo ya korosho jinsi gani yanaweza kutumika katika kuondoa kutu. Kwa hiyo, ni moja ya vitu ambavyo tunaweza tukaviangalia na vikatusaidia katika nchi yetu kuweze kuendeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nigusie kuhusu umwagiliaji. Tunaishi kwa kudra za Mwenyenzi Mungu, tunategemea mvua. Mikoa kati hapa mwaka huu imekosa mvua. Sisi kule tumebahatika, kwa nini tusiende kwenye umwagiliaji? Tunatumia maji kwa ajili ya kunywa. Maji ya Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Mto Malagarasi. Kwa nini tusiende kwenye kilimo cha umwagiliaji? Tunavyoleta maji huku kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya domestic, kwa nini tusitengeneze na mabwawa yakatumika kwa umwagiliaji? Nile inalisha huko Ethiopia na Misri.
Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa hii nafasi. Kwanza nitoe tu hoja kwamba Wabunge na Bunge zima tuunge mkono hizi hoja mbili ambazo zimewasilishwa ya kuhusu Bonde na hili la Amani na Usalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na hili Azimio la Bonde la Songwe, napendekeza kwamba kwa ujumla wetu tuangalie umuhimu wa haya mabonde. Sehemu kubwa, watu bado hawajatambua kwamba umuhimu wa bonde uko kwa kiasi gani katika nchi, tunaangalia kuyalinda mabonde kwa kwanza kuangalia vyanzo vyetu vya haya mabonde ne mito yote. Tumekuwa na sehemeu kubwa sna ya uharibifu wa mazingira ambapo imepelekea mtu wa chini hafaidiki tofauti na mtu wa juu, kwa lugha nyepesi ya kigeni wanaita upstream na downstream users. Sasa kwa kuweka huu mkataba kati ya nchi mbili tunaona kwamba kutakuwa na usawa katika utumiaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala zima la Bonde hili pia linakwenda kutujengea ushirikiano mzuri kati ya nchi hizi mbili, kati ya Malawi na Tanzania, kwa hapo nyuma kuna maneno yalishapita ya mtaani ambayo yalikuwa siyo mazuri lakini tunatumaini sasa kwa Mkataba huu ambao umesainiwa na matumizi haya ya bonde na faida zake zote ambazo zimeelezwa na Waziri mwenye dhamana, tunatumaini kwamba tutafaidika kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, faida ya kwanza ambayo nimeiona kwanza ni ushirikiano ambapo tutakuwa kwa pamoja na ukiangalia katika mipaka yetu watu wanafanana tamaduni na lugha, kwa hiyo ushirikiano utaendelea kuimarika.

Lingine ambalo naona litakuwepo ni suala zima la kiusalama. Nchi mbili mnapokuwa mmeshirikiana katika shughuli za kiuchumi kama hili ambalo tumesaini maana yake tutakuwa na uelewa wa pamoja, tutakuwa na usalama kati ya nchi na nchi, kwa hiyo, tunapongeza sana Serikali kwa kufanya hii jitihada.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho ningesema ni kwamba tuhusishe pia Wizara yenye dhamana upande wa Mazingira, iendelee kupitia Sheria zake za Mazingira kuendelea kulinda vyanzo vyote ambavyo vinakwenda kwenye hili bonde, tumeona kwamba nchi sasa hivi imezungukwa sana na shughuli za kiuchumi ambazo hazizingatii sana Sheria ya Mazingira, ile mita 60 kutoka kwenye kingo za mito, mita 500 kutoka kwenye vyanzo vya maji na Serikali imekuwa inahimiza sana. Kwa hiyo, naomba sana Wizara inayohusika na mazingira waendelee kulinda haya mabonde yote katika nchi yetu ili vizazi na vizazi ambavyo vinafuatia viweze kufaidika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hii nita-comment kidogo kwenye Commission, tuombe Wizara inayohusika iangalie Commission ambayo imeundwa, waangalie matatizo ambayo yamewahikutokea, kwa mfano TAZARA ambapo kwenye upande wa reli kati ya Tanzania na Zambia, waangalie changamoto zilizopo upande wa TAZARA na upande wa huku sasa hii Commission ambayo imeundwa zisiweze kujirudia na utendaji wake uwe wenye tija na ufanisi. Kwa hiyo, tunaomba sana na hata staffing yenyewe izingatie kama mkataba vile ulivyo na namna bora ambayo wataona ni ya kuboresha na itapendeza zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeelezwa faida nyingi na mimi napendezwa sana kuona kwamba litajengwa bwawa na tutaweza ku-control mafuriko ambayo huwa yanatokea na tutaweza kupata umeme, shughuli za kiuchumi zitaweza kufanyika. Naunga mkono na naomba Wabunge wote tuunge mkono Azimio hili ambalo ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuzungumzia Azimio hili la bonde la Mto Songwe, naomba nigusie pia na kuhusiana na kuridhia Itifaki, Amani na Usalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kiujumla Tanzania ni nchi ambayo ilijengwa kwa misingi mizuri na hasa Rais wetu wa kwanza, Hayati Julius Kambarage Nyerere alitengeneza amani kubwa sana katika nchi yetu ya Tanzania na vitu vingi aliweza kuviondoa. Kwa mfano; aliondoa utawala wa Kichifu ikapelekea nchi inakuwa inatawalika vizuri, ukabila vyote hivyo vimekuwa vimesaidia sana Tanzania tumekuwa na amani.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nchi yetu Tanzania ilipokea sana Wakimbizi kutoka nchi za jirani ambazo ni Congo, Burundi, Rwanda yote yalitokea kwa sababu wenzetu hawakuwa na amani. Sasa kwa misingi ya maazimio haya ambayo yanaletwa na tayari tuko kwenye Umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maana yake tutajikita kwenye haya maazimio ambayo yatakuwa yamesainiwa kwa ajili ya amani na usalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu wanapokuwa hawana amani matatizo yale yanaleta migogoro katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuja kwa wakimbizi, imetokea matukio wamekamatwa na silaha katika Kambi za Wakimbizi na wengine matukio ya kiujambazi, sasa kwa minajili hiyo kwa kulinda amani itatusaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengi ya nchi za jirani kuna Tume zimewahi kuundwa, kuna mojawapo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekuwa Mwenyekiti, Hayati Nelson Mandela amewahi kuwa Mwenyekiti, marehemu Hayati Mwalimu Nyerere amewahi kuwa Mwenyekiti katika kusuluhisha nchi za jirani kwa kutokuwa na amani. Nchi nyingi duniani zinasumbuliwa na masuala ya ugaidi, kwa hiyo tunavyokuwa na umoja kama Jumuiya ya Afrika Mashariki, tutaweka msimamo wa kulinda amani na wananchi wake wote watakuwa kwenye hali ya utulivu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja zote hizi mbili na nawashawishi Wabunge wote tuziunge mkono. Ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RICHARD P. MBOGO:Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa nafasi ambayo anatupatia na pili kwanza niunge mkono hoja ya bajeti hii ambayo Waziri amewasalisha nawapongeza kwa uwasilishaji mzuri, na pia kwa Waziri kuwa flexible na comments za Wabunge pamona na wadau mbalimbali ambao umeweka ndani ya bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nitakuwa sina furaha kama nisipompongeza Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna ya pekee ambavyo amekuwa na jitihada katika kuendeleza Nchi hii, tumeona katika hotuba kuna maeneo ambayo yamepewa msukumo wa kipekee ambao ni msukumo tunasema wa Mheshimiwa Rais. Tukianzia na ujenzi wa reli ya standard gage, ni msukumo wa Rais, ufufuaji wa Shirika la Ndege la Air Tanzania nimeshangaa sana kuona baadhi ya Wabunge na hasa rafiki zangu kule wanakandya juu ya kufufua Air Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani nchi yoyote ambayo inataka kukuza utalii lazima usafiri wa ndani uimarishwe, Ethiopia kuanzia mwaka 1963 waliweza kuanzisha Shirika la Ndege na wamelisimamia mpaka leo limekua na Addis Ababa ndiyo hub ya dunia nzima na wanaweza kukuza uchumi wao na sasa hivi wameongezea maeneo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona juhudi za Rais pia kwenye Mchuchuma na Liganga. Tunaomba Serikali muangalie huyu mwekezaji ambaye yuko tayari kutoa huu mtaji tuharakishe aweke fidia kwa wananchi kazi ianze. Tukipata chuma pamoja na umeme tutapunguza gharama ya uendeshaji wa Shirika la TANESCO maana sehemu nyingine ambako hakuna gridi ya Taifa wanatumia majenereta na uendeshaji wa mafuta ni mgumu ndiyo maana kila siku tunataka bei zipande na inakuwa ni gharama kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengine ya uwekezaji na pia kwenye gesi ya kimiminika ambako Serikali imewekea mkazo yote ni maeneo ambayo ya msukumo wa kipekee ambayo bajeti hii imewapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo naomba nizungumzie kuhusu tozo ya shilingi 40 ambayo tumeweka kwenye mafuta. Mheshimiwa Waziri kama itakupendeza tubadilishe tu jina, hii tuite tu tozo kwa ajili ya Mfuko wa Maji Vijijini. Kwa nini nasema hivyo? Mwaka jana tulikulilia sana kuhusu Mfuko wa Maji Vijijini, lakini ukasema tusiongeze kwenye mafuta kwa mwaka jana wa fedha ambao tulikuwa tunaujadili 2016/17. Basi mwaka huu hii shilingi 40 iwe ring fenced kwenda kwenye maji ili makusanyo ya fedha hizi moja kwa moja tuwe na cash flow inayotosha kwa ajili ya maji vijijini na ile bajeti ambayo tumeikubali mliyoishusha ya Wizara ya Maji kutoka shilingi bilioni 900 mpaka shilingi bilioni 600 lakini kwa Wabunge wote tulisema kwamba bajeti hii ikamilike kwa asilimia 100. Sasa ili iweze kukamilika kwa asilimia 100 bajeti ya shilingi milioni 600 lazima tuwe na chanzo cha uhakika.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba kwenye mabadiliko ya Sheria yako kwenye Finance Bill ambayo utaileta hii tuiwekee amendment na mimi nitakusaidia ku- lodge schedule of amendment ili fedha hii iwe ring fenced kwenye maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo naomba nije kwenye tozo ambazo zinahusu Halmashauri. Tunajua nia kabisa ya Serikali ni kuondoa mzigo kwa wakulima, lakini naomba tu nikumbushe Bunge lako ni kwamba Halmashauri zilianzishwa kwa mujibu wa Katiba, Ibara 145 na 146 ni kwa ajili ya kushughulikia wananchi wetu huku chini. Sasa zimeathirika kwa namna tatu, namna ya kwanza kwa kubadilisha Sheria namba 290 ambapo tozo ya mazao inashusha kutoka asilimia tano mpaka tatu na mbili kwa mazao ya chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aina ya pili ambayo Halmashauri zinaathirika ni kutokana na baadhi ya makusanyo kuchukuliwa na TRA ambapo ni mabango na property tax. Aina ya tatu, Halmashauri zinaathirika kwa mapato yao ya ndani ni kutokana na namna ya ujazo ambapo umeweka kwamba chini ya tani moja mtu asiweze kutozwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikianzia kwenye tozo. Mfano Halmashauri yangu ya Nsimbo asilimia 50 ya makusanyo tunapata kutoka kwenye zao la tumbaku. Kwenye bajeti hii 2017/2018 kwenye tumbaku tunatarajia kupata milioni 440 ambapo fedha hii tulikuwa tunatarajia kwamba iingie kwenye miradi ya maendeleo. Sheria mnaijua kabisa, makusanyo ya ndani na asilimia 60 inapelekwa kwenye miradi ya maendeleo na ndani ya asilimia 60 kuna ile asilimia tano ya vijana na akina mama. Kwa hiyo, kwa kupunguza haya makusanyo ya Halmashauri na kwenye bajeti yetu hapa Halmashauri zetu ni shilingi bilioni 687 matokeo yake hizi zinaenda kushuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tutaomba Waziri atuambie compensation ya hizi Halmashauri kutokana na kuathirika kwa mabadiliko ya sheria namna ya kutoza wana- compensate kiasi gani. Mimi nitaomba Mheshimiwa Waziri, kabla hatujaenda kwenye schedule of amendment na tukakubaliana kukubali mabadiliko yako au kuyakataa, tutaomba comfort yako ni jinsi gani Serikali inaenda kufidia Halmashauri zetu ambazo zinaathirika. Halmashauri nyingi hasa za vijijini wanategemea hizi tozo. Kwa mfano ukienda hapa Gairo ni mazao tu, hamna dhahabu hamna nini, wanategemea mazao haya. Ukienda Vwawa – Mbozi wanakusanya karibuni bilioni tatu, ni kwenye mazao, ukienda Nsimbo na Halmashauri nyingi. Sasa hapa Serikali naomba mjiandae, bila comfort kwakweli tutakutana kwenye schedule of amendment. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kuhusu kilimo, Serikali ina nia nzuri kabisa.Tumeona tozo mbalimbali zimepunguzwa kwenye aina mbalimbali za mazao lakini kwenye mbegu Mheshimiwa Waziri hatujaona! Hujafuta VAT ili mbegu inayozalishwa humu ndani nchini iweze kushindana na ile ambayo inatoka nje ya nchi. Vile vile kwenye kilimo Mheshimiwa Waziri bado Benki yetu ya Maendeleo ya Kilimo hujaiongezea mtaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la utalii; bajeti yako na tunajua nia kabisa ya Serikali ku-promote utalii lakini pia bado tunahitaji tuone juhudi zaidi ili utalii wetu uweze kufidia suala la mapato ndani ya bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kuhusu madini. Nashukuru sana umeongeza baadhi ya tozo kwenye madini, lakini watu wenye leseni za madini primary license, mining license they are always doing false declaration on their revenue. Hawasemi ukweli juu ya mapato, kwa hiyo Serikali ione namna gani ili soko liwe huru watu waje pale wauze kwa uhuru na Serikali iweze kupata mapato. Leo hii muulize mtu hata mwenye leseni sehemu zote za madini au leseni ndogo PML au ML, waulize kwa mwaka wanaingiza ngapi? Hawakuambii ukweli lakini tunaona maisha yao yanavyokwenda na Serikali tupate mapato. Mimi tu Halmashauri ya Nsimbo service levy hatupati! Wananunua, wanauza kimya kimya/kisiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niombe tena kuzungumzia kuhusu Benki Kuu ya Tanzania. Benki Kuu ya Tanzania inatanua huduma kanda mbalimbali. Tunaomba Kanda ya Magharibi Benki Kuu ijengwe tawi pale Katavi. Ukiangali Katavi pale kiusalama ni mbali na Ziwa Tanganyika na nchi zinazotuzunguka za majirani. Kwa hiyo, tawi la Benki Kuu lije lijengwe pale Katavi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu kodi kwenye mafuta ya ndege. Umeongeza kodi kwenye mafuta ya ndege ne tunajua kila ndege inamaximum takeover weight kwa hiyo tutawafanya kwamba wasiweke mafuta mengi hapa kwetu wanaenda kujaza sehemu nyingine hasa ndege za transit kwa hiyo tunaomba kodi hii Waziri aisimamishe kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kwa upande wa Serikali yetu, bajeti yetu ya trilioni 31 kodi ni trilioni 17. Nimuombe Waziri, hapa TRA wamejifunga kitanzi. Ongezeko la mpaka Juni tunatarajia mtakusanya trilioni 14.2; lakini kwenye bajeti 2017/18 makusanyo ya kodi ni trilioni 17. Sasa mnaenda kufanyaje ili ongezeko la trilioni mbili na ushee liweze kupatikana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa fursa, kwanza naunga mkono hoja za Kamati mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule binafsi kukaririsha watoto; ni ukweli dhahiri kabisa wamiliki wa shule binafsi wa mtindo wa kufanya udahili wa watoto wanaojiunga na pia katika mitihani yao wameweka kiwango cha ufaulu na wastani ni 75/100. Suala hili sio haki kwa watoto ambao huenda mazingira au uwezo wake wasiweze kufikia ufaulu huo, hivyo watoto wanakaririshwa darasa na umri wao unazidi kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, suala la Serikali kutoa mwongozo shule binafsi kutokaririsha watoto naunga mkono kwani hakuna mzazi asiyependa mtoto wake kufaulu. Kwa hiyo, Serikali iendelee na msimamo huo ili haki ya kikatiba itendeke kwa watoto wenye uwezo mdogo. Serikali imeweka mtihani maalum ya kupima watoto kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madeni yaliyorithiwa toka Wizara ya Afya yameenda Elimu; kuna baadhi ya vyuo vya mafunzo kwa jamii vimehamishiwa Wizara ya Elimu ambapo awali ilikuwa chini ya Wizara ya Afya, mfano Chuo cha Msaginya, Katavi; kuna kazi za ukarabati, mkandarasi hajamaliza miaka miwili imepita wala Serikali haijamlipa. Hivyo, Serikali iangalie madeni pia fedha za uendeshaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upimaji UKIMWI; Sheria ya UKIMWI inamtaka mama mjamzito kupima kwa lazima ambapo imetekelezwa kwa kiasi kikubwa lakini kwa wenza wa mama wajawazito sheria bado haijawataka wao kwa lazima kupima VVU. Hivyo kuna hoja sheria iboreshwe ili wenza wao nao wapimwe kwa lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikundi cha jamii kingine ambacho ni muhimu sana sheria iwatambue kupima kwa lazima, Serikali iangalie wanafunzi wanaotaraji kujiunga na Elimu ya Vyuo Vikuu ili kulinda maambukizi mapya.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwa sababu muda ni mchache sana nitakwenda haraka haraka. Kwanza naomba nimpongeze Waziri na Manaibu wake wote wawili na watendaji katika wizara kwa jinsi wanavyofanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni tunashukuru Serikali kwa kujenga barabara ya Sumbawanga – Kizi- Kibaoni lakini kipande cha Kizi- Lyambalamfipa- Stalike ambacho ni kabla hujafika Hifadhi ya Taifa ya Wanyama ya Katavi kina kilometa 35.5, tunaomba Waziri atuambie ni lini ataiweka kwenye bajeti?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, katika barabara hiyo ambayo imeshajengwa na imekamilika ya Stalike – Mpanda bado kuna wananchi ambao bado wanadai fidia. Sasa tutaomba Waziri atuambie katika bajeti hii kiasi gani ataenda kuwalipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru na kwenye kitabu nimeona barabara yetu ya kutoka Mpanda – Inyonga – Ipole – Sikonge – Tabora kilometa 346 na tayari wakandarasi wameanza mobilization. Sasa kwa sisi watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kuna fidia ya utility facilities yaani matenki ya kuhifadhi maji ambapo yapo mawili yanaenda kubomolewa, lakini kwa taarifa ambazo sio rasmi, kuna shilingi milioni 162 tu ambazo zipo katika mkataba ambazo haziendani na gharama halisi ya haya matenki ambayo tunatakiwa kufidiwa. Kwa hiyo, tutaomba Serikali iangalie uhalisia wa gharama za haya matenki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la reli, treni yetu ya kutoka Tabora mpaka Mpanda, njia yake kwa kipindi hiki cha masika inasumbua sana, hapa siku tatu zilizopita wananchi wamelala siku mbili kati ya Kaliua na kilometa 60 kutokana na mvua na kokoto kuondoka. Kwa hiyo, tunaomba katika bajeti hii na ukarabati ufanyike kwa umakini na pia mabehewa yaweze kuongezwa kutokana na hasa kipindi cha kiangazi abiria wanakuwa ni wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile wananchi pia wapo tayari kuachia maeneo ambayo yanamilikiwa na shirika letu la reli lakini upimaji wa ardhi mpya ulichelewa kwa hiyo tutaomba hisani ya Serikali watuvumilie kidogo wakati wananchi wanajenga maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la TAZARA, kiuongozi tunaona Serikali ilete sheria iweze kuboreshwa ili angalau tuwe na kupeana miaka mitatu mitatu katika kuongoza shirika hili na lifanye kiufanisi zaidi na kwa faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la TTCL, TTCL tumebadilisha sheria mwaka jana. Sasa niombe Wizara na Kampuni ya TTCL wakimbie na wasitembee. Walianzisha code yao 0732 lakini idadi ya wateja wao imekwishashuka na sidhani kama kuna watu wengi sana wanaotumia simu za mkononi za TTCL. Sasa kwa kuwa mkongo wa Taifa upo chini yao, wakimbie; amekuja juzi Halotel lakini ana wateja wengi, kwa nini TTCL bado anatambaa. Kwa hiyo, Serikali na uongozi mzima wa TTCL waje watueleze kwamba watafanya nini ili shirika liweze kufanya kazi kwa faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la TCRA, Halmashauri zetu nchi nzima kuna minara ambayo kampuni za simu zina- operate na sasa hivi wameweka kampuni moja na haya makampuni ya simu yanapanga, sasa tunatakiwa tupate service levy kutokana na mapato ambayo wanaingiza katika kila eneo. Kwa hiyo, tuombe kama inashindikana basi service levy inayotoka TCRA iingie na iwe ring fenced labda kwenye Wizara ya Afya kwa ajili ya kusaidia vifo vya mama na mtoto kama inashindikana kila Halmashauri kuweza kupata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la vivuko, tunaona kwamba katika barabara nyingi hakuna hizi underground crossing. Kwa mfano tu ukichukua eneo la NARCO ilitakiwa kuwe na kivuko cha chini ili wanyama waweze kupitishwa, sasa kwa nini TANROAD katika ku-design barabara maeneo mengine wasiweke vivuko vya kupita chini ili tuondoe ajali ambazo wananchi wetu na mifugo wanagongwa na hii itasaidia usalama kati ya wanyama na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho ni kuhusu ATCL, tunaipongeza Serikali kwa hatua kubwa, nimeona mchangiaji mmoja alisema kwamba kuwe na ndege za kampuni tofauti italeta changamoto kwenye suala la kuwa na hizi anga…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi moja kwa moja niseme tu kwanza naunga mkono hoja ya kupitisha hili azimio kwa ajili ya makubaliano ya Paris kuhusu kuboresha utekelezaji wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo ningependa kuchangia kwanza tukubaliane na hili Azimio kwa sababu tuna faida nyingi ambazo Mheshimiwa Waziri ameweza kuzieleza kama nchi ambavyo tunaweza kufaidika; la kwanza ni mkakati wa kutekeleza utunzaji wa mazingira, upatikanaji wa fedha, masuala ya kuweza kupanda miti ambayo itaweza kunyonya gesijoto, lakini kikubwa ni kwamba uhai wa mwanadamu upo kwenye mazingira, duniani nchi zote tunafanya shughuli za kimaendeleo lakini tunaangalia na uhai wa kwetu sisi wanadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ongezeko la joto duniani lina athari nyingi sana kama ambavyo tumeweza kuelezwa pamoja ikiwa ni uchafuzi wa mazingira, kuleta ukame, magonjwa, uharibifu wa miundombinu na mambo mengine mengi sasa kwa misingi hiyo tunavyokubali azimio hili na kila nchi kuweza kutaekeleza ili Azimio katika kusimamia kutunza mazingira tutaenda kuonyesha kwamba uhai wetu sisi wanadamu utakuwa na uhakika wa kuwepo na kuishi.

Sasa kutokana na vifungu mbalimbali vya makubaliano ambavyo vimeweza kuelezwa ningependa kama nchi kwa sababu haya ni mabadiliko yamepitishwa mwaka 2016 basi tuombe kwenye mabadiliko ambayo yatakayofuata mbeleni katika haya maazimio tusisitizwe sana kwenye nchi ambazo zinachangia katika uharibifu na kuleta joto duniani ziweke vipengele ambavyo vitahakikisha kwamba wanatekeleza utoaji wa fedha kwa ajili ya nchi zinazoendelea katika kutunza mazingira.

Mheshimiwa Naibu spika, hilo litakuwa ni jambo la umuhimu sana katika kuzibana hizi nchi na pia katika mawasilisho imeonekana kuna baadhi ya nchi ambazo zinakuwa haziko tayari zikiangalia kwamba zenyewe zinaathirika zaidi katika shughuli zao za kiuchumi kutokana na kubanwa kwenye shughuli zao.

Kwa hiyo, tuombe katika maazimio mbeleni huko marekebisho ambayo yatafanyika tuone namna ya kuzibana hizi nchi na hasa hizi nchi ambazo tena zilizoendelea zinazoshindana zaidi na zinakuwa zinapinga maazimio kama haya basi tuone namna ya kuzibana ili ziweze kutekeleza kwa namna ambayo na sisi ambao ndio nchi maskini tunaoendelea na ndio ambao wengi tunaotunza mazingira na dunia angalau inakuwa ya ina uhakika kwamba tutaendelea kuishi duniani kwa sababu ya nchi hizi ambazo tunazoendelea ambazo tunatunza mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano Tanzania asilimia 30 ya nchi yetu iko kwenye uhifadhi kwa hiyo, tuna uhakika wa kuendelea kutunza na dunia ikapata nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuangalia upande wa kimataifa naomba nije kwa upande wa kama nchi Tanzania, tunajua tunazo sheria, tuna sera, na tuna uongozi, lakini ni kwa namna gani tunasimamia hizi sera upande wa mazingira na tunasimamia sheria zetu ili ziweze kutunza mazingira tumeona changamoto sehemu mbalimbali za nchi yetu kumekuwa na uharibifu mkubwa sana wa mazingira na hasa kufanya kazi za maendeleo kutoka kwenye kingo za mito kama sheria inavyosema mita 60 na mita 500 kutoka kwenye vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Naibu spika, lakini kuna wamiliki wa mabonde, tunayo TAMISEMI na tunayo Wizara husika ila usimamizi katika maeneo mbalimbali huku hafifu mno matokeo yake shughuli za kibinadamu, za mifugo, za kulima wamekuwa wanaingia mpaka maeneo ya vyanzo vya maji na kingo za mito kwa hiyo inapelekea kuharibu mazingira, na kwa misingi hiyo changamoto mojawapo ninayoiona ni uwezeshaji wa Halmashauri zetu kupitia hii Wizara jinsi gani wanazishikisha katika kusimamia na kikubwa pia tunashindwa kuwatumia namna fulani sijapenda kuielewa Wakuu wetu wa Wilaya ambao ni Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama katika Wilaya kwanza hawana OC za kutosha kuweza kuzunguka na kusimamia vizuri watendaji walio chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niombe Serikali tuangalie namna gani tunaongezea OC Wakuu wetu wa Wilaya waweze kusimamia Halmashauri zetu katika kulinda mazingira na kijumla maana imekuwa ni changamoto na mpaka maeneo mengine Wakuu wetu wa Wilaya hawana vyombo vya usafiri vya kutosha au vingine vimechakaa na havifai katika utendaji wa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la kiuongozi kiujumla jinsi gani tunashirikisha kuanzia Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Kitongoji katika kulinda mazingira elimu je, wanayo na inatumika ipasavyo kwa hiyo tuombe tena Wizara tuone namna gani tunawashirikisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la nishati katika matumizi ya kawaida ya nyumbani mambo ya kupikia mkaa na kuni ndio vinatumika kwa asilimia 98 na je, mkakati wa Serikali katika kulinda mazingira nishati mbadala kwenye matumizi ya nyumbani mkakati uko namna gani, matumizi ya mkaa kwa mfano Jiji la Dar es Salaam ndio linaloongoza katika nchi hii je nishati mbadala iko vipi, tuna taasisi za Serikali sasa hivi wananchi wengi na wataalam wengi wanatengeneza biogas kwa kupitia taka na vyanzo vingine na wanatumia kwenye matumizi ya nyumbani kwa ajili ya kupikia, sasa mkakati wa Wizara hii husika kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais hili fungu linalopatikana toka kwenye nchi wahisani wanaotoa kwa ajili ya kutunza mazingira watenge kwa ajili ya kuelemisha na kufundisha na watu kuwawezesha kutumia biogas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa mfano unaweza ukaanza na taasisi kama Magereza, taasisi hizi kama vyuo vikuu, mashule watengeneze biogas kwa ajili ya kupikia. Hizi shule za bweni maana yake wanapikia wanafunzi chakula je, wanatumia nishati gani? Pia tukienda kwenye shughuli za kilimo kwa mfano mazao ya biashara kama tumbaku sasa hivi wakulima wanakausha tumbaku, wanakata miti sawa Serikali imeleta mabanio ambayo kidogo yanatumia kuni zile ndogo ndogo chache, lakini wengine hawatekelezi je tuna nishati mbadala tuache kukata miti?

Kwa hiyo, niombe sana Serikali kupitia hii Wizara waje watueleze biogas na nishati mbadala tuachane na mkaa na kuni katika kupikia ambayo ndio inayokata miti sana katika nchi yetu namna gani tunaenda kuwezesha kwa kupitia haya mafungu yanayotoka kwenye nchi zilizoendelea zinazotoa kwa ajili ya kusaidia kupunguza athari za ongezeko la joto humu duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia niombe sasa kwa upande wa hizi halmashauri mlizilazimishsa kwamba Serikali ilisema kila Halmashauri ipande miti 1,500,000 na waliweka kwenye bajeti sasa utekelezaji mpaka sasa hivi kila halmashauri wamepanda miti mingapi hiyo utakuta ni hafifu na watu hata wakipewa ile miti, je, wanaisimamia wanahakikisha kwamba na inakua kwa hiyo, usimamizi katika upande wa mazingira tuone namna gani tunaongeza juhudi ili tuhakikishe kwamba utekelezaji wake wa haya maagizo tunayotoa yanasimamiwa ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ni Wizara ya maliasili na utalii ina maeneo mengi yaliweza kuathirika kutokana na watu kuvamia kwa shughuli za kilimo mbalimbali lakini je, tunahusisha vipi kuingia ubia na halmashauri zetu kupanda miti rafiki kama ilivyo katika maeneo mengine kwa mfano kama mazao ya korosho ili tuweze kuboresha hayo maeneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, na la mwisho ni elimu tumesema kwamba tupande miti ambayo itaenda kunyonya gesi je, hii miti tunayowaambia wataalamu wetu huko na wananchi wetu tunawaelimisha kwamba miti hii mnayopanda ndio ambayo itaenda kunyonya gesi elimu hiyo inatolewa na kwa kiasi gani inatolewa na fedha za kusaidia kutoa elimu Halmashauri zetu tunazozipata.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja na nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze kiujumla Serikali na hususani Waziri Mkuu ambaye amewasilisha hii bajeti pamoja na timu yake Mheshimiwa Jenista na Manaibu Mawaziri kwa kutukuka kwenye kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nianze kwenye eno moja ambalo watu wengi na hasa upande wa pili kule wanaona uwekezaji kwenye miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli, ununuzi wa ndege na kazi nyingine ambazo Serikali ya Chama cha Mapainduzi inafanya, wanaona kwamba mpangilio wa rasilimali haukuwa sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe tu mfano, Wabunge waliopo hapa ndani wengi wamekopa pesa, wamewekeza katika kujenga ma-guest (guest houses), kujenga nyumba za kupangisha, magari, wanafanya biashara ili wapate faida na wafanye shughuli zingine. Kwa hiyo, kwa upande wa Serikali kuweza kununua ndege na kuboresha usafiri wa ndege ndani ya nchi yetu inasaidia na sekta zingine, mojawapo tutapata faida. Ili tuweze kuongeza mapato ya Serikali lazima tuboresha usafiri wa ndege ili na watalii wetu waweze kufika maeneo mbalimbali ya nchi. Kama vile Mkoa wetu wa Katavi tuna Mbuga ya Katavi, Nyanda za Juu Kusini vipo vituo vingi tu lakini tatizo ni miundombinu ya kuwafikisha watalii wetu na wananchi mbalimbali. Pia usafiri wa ndege unasaidia mtu unakuwa in efficiency unakwenda kwa wakati na wengi mnapanda ndege kama vile Fastjet ilivyoingia na kubadilisha mind za watu kwamba usafiri wa ndege si ghali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika masuala ya reli; ukiangalia kwa mfano treni inayotoka Tabora kwenda Mpanda inatumia lita 1000, sasa tukiboresha hii njia na kutumia umeme maana yake gharama za uendeshaji itashuka na matokeo yake nauli zitakuwa nafuu na usafirishaji wa mizigo kwa hiyo itakwenda kukuza uchumi. Kwa hiyo, mnapoona kwamba mikakati ya Serikali inafanyika katika maeneo mbalimbali ni mtambuka na kusaidia sekta zingine na kushusha gharama. Kwa hiyo, ni kazi nzuri ambayo inafanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tunajua chini ya Ofisi ya Waziri MKuu wanashughulika na Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu nitagusa hayo maeneo kama ifuatavyo:-

Ningependa sana niunganishe upande wa kazi pamoja na vijana. Tunajua kabisa asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na wengi wanahitaji kuweza kupata ajira na maeneo mengi kwa mfano Jimbo la Nsimbo asilimia 95 ya wananchi wanashughulika na kilimo. Sasa ningeomba kwa upande wa Serikali tujaribu kuangalia kwenye sekta ambazo zinatoa ajira kubwa upande wa kilimo. Ni jinsi gani tutahusisha kuboresha kilimo katika nyendo zake pamoja na hali ya hewa kwa sababu tunategemea tu mvua moja, sasa namna gani tutalima mara mbili na kuongeza hayo maeneo ili tuendelee kuboresha upande wa ajira.

Mheshimiwa Mwneyekiti, sambamba na kilimo, tunajua kaulimbiu ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika hii Awamu Tano ni kwenda kwenye nchi ya viwanda, sasa malighafi ya viwanda tulivyonavyo inahitaji pia malighafi kutoka upande wa kilimo. Sasa hivi viwandani vinavyohitaji malighafi za upande wa kilimo tunahakikisha kwamba tunafanya nini. Kwa sasa hivi tuna viwanda vingi vinavyotumia malighafi kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano ukienda kwenye ngano, mafuta ya kula. Tuchukue tu mfano Bakhressa ambaye anatoa ngano na tunapata unga, sasa asilimia kubwa ya malighafi ya Bakhressa inatoka nje ya nchi, sasa kwa kiasi gani tunakwenda kuwavutia wawekezaji upande wa kilimo na kuwashawishi wananchi wetu waweze kulima hizi kwa ajili ya viwanda ambavyo tayari vinatumia malighafi za kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwa upande wa mafuta ya kula, asilimia kubwa tunaagiza kutoka nje. Ni jinsi gani tutapunguza uagizaji wa mafuta kutoka nje na tuweze kujenga zidia ajira zetu upande wa vijana na wananchi katika Tanzania yetu. Kwa hiyo, tuombe Serikali huu mkakati unakwenda kwa namna gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la upande wa umeme vijijini. Bahati mbaya hatuwezi kuingiliana kwenye kuzungumzia mihimili, lakini naomba tu tuseme Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Kigoma kwa umeme vijijini, Mkandarasi kesi iko mahakamani kila siku inasomwa haijaanza kusikilizwa. Sasa ni lini itakamilika ili wananchi waingie kwenye kupata huduma ya umeme kama ilivyo azma ya Serikali? Kwa hiyo kwa namna nyingine basi na mhimili mwingine uone jinsi gani ya kuharakisha hiyo kesi ili miradi ya maendeleo kwa upande wa umeme vijijini ikatekelezwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tozo mwaka jana tuliibadilishia sheria na tuliweza kutoa tozo na kuweka nafuu chini ya tani moja, lakini tulisahau kwenye bidhaa ambazo hazidumu kwa muda mrefu (perishable goods). Sasa ni jinsi gani utaitoa shambani ukaitunze nyumbani kama vile nyanya, hoho, mboga mboga? Hapa tulipasahau kupaangalia. Sasa tumekuwa nachangamoto kwa wakulima wanakuwa wanatuhoji kutokana na kauli na maelekezo ya Serikali kutokutoza chini ya tani moja unapotoka Halmashauri moja kwenda Halmashauri nyingine.

Mheshimiwa Mwenytkiti, tatizo tulilonalo ni kwenye mboga mboga na bidhaa nyingine ambazo hazidumu (perishable goods). Kwa hiyo, Serikali naomba mliangalie, na nashukuru Mheshimiwa Jafo nimeshamtaarifu na barua nimeshamwandikia, basi lishughulikiwe kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu walemavu; kama Sheria Namba 9 ya mwaka 2010 ilivyo, kuna Mabaraza ya Kata nao wawezeshwe katika ile asilimia 10 ambayo inakwenda kwa vijana, akina mama pamoja na walemavu asilimia mbili. Tuwe na uwezeshaji wa miradi ya moja kwa moja kwa ajili ya kusaidia walemavu ili waweze kujiongezea kipato na waache utegemezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsanye, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, upgrading of Sumbawanga – Namanyere–Mpanda Road, package 3; Kizi – Lyambalyamfipa – Sitalike Section 86.5 kilometres.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanikiwa kwa asilimia kubwa package I & II na sasa wananchi wanatumia barabara hizo, lakini package III bado haijatengewa fedha katika mwaka wa fedha 2018/2019 kiwango cha lami ambapo kilometa 35.5 kati ya kilometa 86.5 hazipo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi. Naomba Waziri atuambie wananchi wa Katavi ni lini fedha zitatengwa kwa ajili ya kipande hicho cha kilometa 35.5?

Mheshimiwa Naibu Spika, kupandishwa hadhi barabara ya Katumba Complex II (Msaginya – Mnyaki – Kanoge kilometa 21) Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo (Katavi). TARURA wameomba barabara hii ipande hadhi kuwa chini ya TANROADS kwa kuwa ni muhimu sana na ni kiunganishi cha barabara mbili zinazotoka nje ya Mkoa wa Katavi ambazo ni Mpanda – Ugala – Ulyankulu, Kaliua – Kahama kilometa 457 na Mpanda – Ipele – Tabora (kilometa 346).

Mheshimiwa Naibu Spika, reli Mpanda – Tabora, bado hali ni mbaya sana njia ya reli Mpanda – Tabora hususani kipande cha Kaliua – Mpanda, mpaka abiria walilala njiani siku mbili baada ya mvua kufanya uharibifu, ilikuwa tarehe 18/04/2018 waliondoka Tabora na walifika Mpanda tarehe 20/04/2018 saa 12 asubuhi. TRL inaombwa kuongeza ukarabati wa njia kwa kuwa ni tegemeo la wananchi na kusafirisha mazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, inakabiliwa na changamoto kubwa ya mawasiliano katika kata za Ugala, Litapunguza, Kamage, Katumba, Uvaira, Nsimbo, Mtapenda, Kapalala, Machimboni, Itanka, Ibindi na Sitalike. Tunaomba sana Serikali kuboresha mawasiliano katika kata tajwa hapo juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Soko la Hisa kwa Kampuni za Simu, Bunge lako lilipitisha sheria inayozilazimu kampuni zote za simu kujiunga na soko la hisa, lakini mpaka sasa Vodacom ndio pekee wameshajiunga. Je, ni lini kampuni nyingine zikiwemo TTCL watatekeleza matakwa ya sheria? Kwa kuwa bado kampuni zingine kutekeleza; je, sheria inasema vipi juu ya hatua za kuchukuliwa kwa kutotii sheria hizo?

Mheshimiwa Naibu Spika, fidia ya matenki ya maji, mkataba wa mkandarasi Mpanda – Ipole – Tabora, anatakiwa kufidia matenki mawili ambayo thamani yake zaidi ya milioni 250 lakini fidia iliyopo ni ndogo haizidi milioni 150; kwa hiyo tunaiomba Serikali iangalie upya fidia hiyo na ikiwezekana Halmashauri ya Nsimbo ipewe fedha moja kwa moja ili ijenge yenyewe miundombinu ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, service levy V/s TCRA; Kampuni za Simu zinaingiza mapato kutokana na minara hivyo kutokana na sheria za Serikali za Mitaa wanatakiwa kutoza service levy ya asilimia 6.3 ya mapato. Tunaomba TCRA wasimamie utaratibu mzuri ili kila Halmashauri inufaike na minara iliyopo katika eneo lao au Serikali ifanye ring fence ya service levy kutoka katika kampuni zote na pato hili kuwekwa Wizara ya Afya ili kusaidia kazi za kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, fidia barabara ya Sitalike - Mpanda; bado kuna wananchi wanadai hawajalipwa na Serikali, tunaomba ifanye malipo haraka.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa pongezi kwa umahiri wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli pamoja na Waziri, Mheshimiwa Engineer Kamwelwe kwa umahiri wake katika kusimamia kazi za Wizara na miradi yake ili kumtua mama ndoo.

Pia pongezi kwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi wa Maji Vijijini na Mijijini na watendaji wote katika Wizara. Pia pongezi kwa Wizara kubadili utaratibu wa malipo kwa hati kutumwa Wizarani badala ya kupeleka pesa katika Halmashauri ambazo ziliweza kubadilishwa matumizi au miradi kuchelewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mabonde ya maji; Mamlaka ya Mabonde bado yana changamoto za watumishi katika maeneo yanayotakiwa kusimamiwa ipasavyo. Hivyo nashauri Wizara ya Maji iangalie itahusisha vipi Halmashauri au Manispaa kusimamia kwa kutoa fedha za usimamizi ili kulinda vyanzo vya maji ambavyo vinavamiwa sana na wafugaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu banio katika Mto Katuma na Mto Mpanda Mkoa wa Katavi; Wilaya ya Mpanda, Kata za Itenka, Kakese na Mwanamkulu zinalima sana zao la mpunga hivyo kuna haja ya kupata skimu ya umwagiliaji ili kilimo kifanyike mara mbili kwa mwaka. Pia kuwekea mabanio ya kusambaza maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu chanzo Ziwa Tanganyika, Mkoa wa Katavi bado unategemea vyanzo ambavyo si vya uhakika, mfano, Manispaa ya Mpanda wanapata maji kutoka Ikorongo chanzo ambacho hakikidhi mahitaji. Hivyo tunaomba Wizara ifanye upembuzi yakinifu kwa ajili ya kutoa maji Ziwa Tanganyika na kutumika Wilaya mbili yaani Tanganyika na Mpanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la madeni ya miradi ya maji katika Halmashauri, kampuni ya kizalendo ya Kahama ilikopesha wakandarasi katika Halmashauri takribani kumi ikiwemo ya Nkasi ambayo kuna utata wa mkataba na vigezo ambapo kampuni mbili zinadaiwa takribani shilingi bilioni mbili. Naomba Serikali iingilie kati mgogoro huo ili kampuni hiyo iweze kulipwa madeni. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kwanza kuongelea Bodi ya Mikopo. Ili kuweka tija na kuondoa malalamiko ya mara kwa mara ya mikopo kwa wanachuo, nashauri Serikali izingatie suala la Bodi ya Mikopo kuwa na revolving fund ambapo fedha hizo zisiwekwe Mfuko Mkuu ili Bodi iweze kuwekeza na kutunisha mfuko ambao utasaidia kuchangia gharama za kuendesha taasisi na baadae Serikali itaondoka katika kutoa fedha kuwezesha Bodi hii. Hivyo basi, Serikali itoe fedha kwa Bodi na kuwezesha revolving fund kufanya kazi ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri Bodi iwe chini ya Wizara ya Fedha. Kwa kuwa Bodi inahusika na masuala ya fedha ni vema ikawa chini ya Wizara ya Fedha ili kupata msaada zaidi wa kitaalamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mashirika ya misaada, kwa kuwa kuna taasisi nyingi za kiraia na mashirika ya kimataifa ambayo yanahusika kusaidia masuala ya elimu na ufadhili, je, Bodi ya Mikopo inashirikiana vipi na taasisi hizi ili misaada pia ipitie kwao kwa watu wenye uhitaji maalum?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili napenda kuongelea kuhusu sera, sheria na kanuni. Sheria iliyopo ni ya tangu mwaka 1979 ambapo imekuwa ikifanyiwa marekebisho nyakati mbalimbali, lakini sera zake bado hazijafanyiwa maboresho ili kuendana na sheria. Nashauri Serikali ipitie upya sera zake ili zikidhi mahitaji ya sasa kwa kushirikisha wadau wa elimu na ndipo sheria iboreshwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni kuhusu mitaala, kumekuwa na mabadiliko katika mitaala, nashauri Serikali iangalie ufanisi wa mitaala kwani mabadiliko yamekuwa hayakidhi uhitaji na kumekuwa na mkanganyiko kwa watumiaji. Hivyo, nashauri Serikali isimamie mitaala na vitabu ambavyo vitakuwa muhimu kwa watoto shuleni kulingana na umri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nne ni kuhusu usajili wa shule za Serikali. Serikali ina wajibu mkubwa kutoa elimu nchini na sasa elimu bure. Tatizo ni kuwa TAMISEMI bado ina changamoto ya bajeti na kuhusisha wananchi kujenga miundmbinu ya shule na watoto wa vijijini ndiyo wanapata shida kufika shule zilizo mbali kati ya kilometa sita mpaka 14. Tatizo kubwa na vigezo vya usajili na kusababisha shule zinazojengwa na wananchi kukosa sifa. Nashauri Serikali ipunguze masharti kwa shule za Serikali, iwe angalau na vyumba vinne, matundu sita ya choo, nyumba moja na ofisi moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tano ni vyuo vya elimu na shule za mazoezi. Tanzania kwa sasa vyuo vya ualimu vipo vingi kwa ngazi za cheti, diploma na shahada lakini wahitimu wanaotoka shule au vyuo hivyo wamekuwa hawana uwezo wa kuridhisha katika utaalam, ujuzi na maarifa. Hivyo, nashauri Serikali itoe mwongozo kila chuo kikuu kiwe na shule ya mazoezi mfano mzuri ni wahitimu wa DUCE wapo vizuri sana kwa kuwa wana shule ya mazoezi. Mpango huo unaweza pia kushushwa ngazi za chini yaani diploma na cheti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sita ni kukariri darasa. Nashauri mfumo uboreshwe ili kusaidia watoto kufaulu pia kuwezesha kuendelea na masomo. Jambo la kuangalia ni kwa kiasi gani mitaala hii inachangia watoto kukariri darasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pongezi kwa Serikali na Wizara na watendaji kwa kazi wanazoendelea kufanya.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Nishati
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza nianze kuunga mkono hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati. Naomba niende moja kwa moja kwenye jambo ambalo lina manufaa makubwa kwa nchi yetu lakini baadhi ya wachangiaji wamekuwa kidogo wanapotosha wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia miundombinu, tukianza na reli, mkoloni alivyojenga reli kuanzia Dar es Salaam mpaka Kigoma na Mwanza alisafisha miti na walivyojenga barabara walisafisha miti. Kwa hiyo, unavyotengeneza miundombinu yoyote kwa manufaa ya wananchi lazima utagusa mazingira. Kwa misingi hiyo, ujenzi wa Bwawa la Stiegler’s Gorge linagusa mazingira lakini kwa asilimia tatu ya eneo lote la Selous. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia kwenda kwenye nchi ya viwanda kama wenzangu ambavyo wameweza kuzungumza, lazima tuwe na umeme wa uhakika na vyanzo mbadala ambavyo ni zaidi ya kimoja. Nitaomba nijikite kidogo kwenye faida za kuwa na hili bwawa. Jambo la kwanza, Wabunge wengi wamezungumzia kuhusu TANESCO kufanya biashara kwa hasara, lakini hawajajiuliza kwa nini imefanya kwa hasara. Kwanza, ni nafuu ambayo imewekwa kwa wananchi kwa bei ambayo haiendani na soko na gharama za uzalishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu cha Waziri ukiangalia upande wa kuzalisha unit za umeme kwa kutumia maji ndiyo wenye bei nafuu, kwa shilingi za Kitanzania 36 kwa unit, kwa dola ni dola 1.63. Katika umeme tunaoutumia kwa sasa hivi wa megawatt 1,517 ni asilimia 37 tu inatokana na maji. Kwa hiyo, niombe Serikali huu mpango tunauunga mkono endeleeni, msiangalie nini watu wanasema, angalieni matakwa ambayo yalianzishwa na Baba wa Taifa tangu mwaka 1972. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna faida ya ajira, maji hayo pia yatatumika kwa ajili ya matumizi ya majumbani. Wananchi na Wabunge wengi wa Mtwara na Lindi walikuwa wanazungumzia kutoa maji kutoka Mto Rufiji kupeleka Mtwara na Lindi, hii itakuwa ni suluhisho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakuwa na uvuvi na sasa hivi tuna teknolojia ya kuwa na zile cage za uvuvi. Ziwa Victoria ipo, watu wanaotoka Musoma na Mwanza wanajua na wavuvi hapa wapo, itakuwepo. Tutakuwa na utalii, katika ujenzi watu wanaenda China wanatembea kwenye ule mlima wanaangalia lakini hapa pia tutakuwa na utalii wa ndani na nje tutaweza kuvutia na tutaongeza mapato ya ndani na GDP yetu itapanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Kilimo
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza ambalo napenda nimuachie Waziri pamoja na Wizara yake waje watuambie nchi yenye fursa kama Tanzania ambayo tunaweza tukuwa tunauza chakula nje ya nchi kwa nini bado tunaagiza chakula kutoka nje? Baada ya hapo naanza kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya Waziri, ukurasa wa 19 ameelezea vipaumbele nane ambavyo Wizara yake imekuwa ikifanya utekelezaji wa haya majukumu. Cha kwanza sikigusi, nagusa cha pili kwamba kuongeza kilimo chenye tija kwa kuongeza upatikanaji na utumiaji wa pembejeo za kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pembejeo kwa upande wa kilimo katika nchi yetu ya Tanzania bado ni hafifu sana. Niwapongeze kwa maamuzi ya ununuzi wa mbolea kwa pamoja (bulk procurement) lakini changamoto kubwa kwenye suala hili ni kufikisha mbolea kwa wakulima wetu kwa wakati kulingana na eneo husika na msimu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Oktoba Mkoa wetu wa Katavi tunaanza kazi za kilimo. Watu wa tumbaku wanaanza kufulia mbegu Julai kuelekea wa Agosti, ikinyesha tu mvua ya kwanza Oktoba wanaanza kupanda. Mazao yote ambayo tunalima ndani ya Mkoa wa Katavi tukianzia tumbaku, mahindi na mpunga utaratibu ni huo. Sasa kama mbolea ya kupandia inachelewa na kilimo chetu tunaenda kwa kudra za Mwenyezi Mungu kwa kutegemea mvua matokeo ni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika wasilisho la Wizara kwenye semina walieleza kwamba wamefanya saving nafikiri zaidi ya shilingi bilioni 9 kwenye ununuzi wa mbolea kwa pamoja (bulk procurement). Huku kwenye ununuzi wa mbolea kama Wizara mlifanya saving lakini wakulima wamepata hasara kwa sababu mbolea ilichelewa, by the time wanaweka ile mbolea mvua ikaondoka, wiki mbili hakuna mvua, kwa hiyo mazao yalidumaa, hawajaweza kuvuna ipasavyo. Mbolea waliyoweka haikuyeyuka kuingia ardhini kwa sababu mvua haikuwepo, tatizo mlichelewesha mbolea. Tuombe Wizara siyo mpaka Mkuu wa nchi aseme ndipo sasa na nyie mkimbizane mpaka na magari ya jeshi kufikisha mbolea kwa wakulima ambao sasa wanapata hasara, hili ni eneo ambalo linaajiri asilimia 70 ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu zana za kilimo, tumeona kuna mifuko ya ukopeshaji lakini pia juhudi hii inabidi iongezwe. Iliwahi kutolewa kauli hapa na Serikali kwamba jembe la mkono litaenda kukaa makumbusho, sasa utekelezaji wa kauli hii umefikia wapi? Kwa hiyo, tutaomba Waziri utuambie kwenye zana za kilimo ni lini jembe la mkono litaondoka na tuingie kwenye zana ambazo tutafanya kilimo chenye tija na kuzalisha zaidi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala la viuatilifu na wadudu. Tunajua mna changamoto kubwa katika eneo hili lakini maandalizi ya kukabiliana na hawa wadudu yasiwe ya zimamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala la mbegu sasa hivi zinawachanganya wakulima wetu. Kuna nyingine zina ubora mzuri na nyingine hazina. Ukishavuna mazao yakikauka bado yanawahi kubunguliwa tofauti na zile mbegu za zamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naenda kwenye upande wa zao la tumbaku. Makampuni ya tumbaku yamekuwa kama ndiyo wenye maamuzi katika nchi hii. Walishusha kutoka tani 60,000 mpaka tani 55,000 na bahati mbaya uzalishaji ukazidi kiwango na wakulima wetu walihangaika na bei mpaka mbolea zililowa na maji na matokeo yake waliuza mpaka Dola 0.6 kwa kilo kwa sababu ubora umeshashuka, tumbaku zilikaa muda mrefu. Tuombe Serikali watengeneze makubaliano ambayo yatakuwa yananufaisha wananchi hata kama kiwango cha uzalishaji kimezidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kwenye tumbaku kwa Wilaya yetu ya Mpanda kampuni ya TLTC imetoa barua ikisema inakusudia kusitisha ununuzi wa tumbaku kwa kisingizo kwamba go-down limejengwa ndani eneo la railway na ni kweli ni eneo la railway na wanatakiwa waliondoe na pili, ni masuala ya kiuongozi kutotimiza matakwa yanatotakiwa. Bodi ya Tumbaku inayo barua, huu wasiwasi wa wakulima wetu kwenye ununuzi wa tumbaku tutaomba kauli ya Waziri ni kweli TLTC mnakubali wasitishe ununuzi? Kama mnakubali ni kampuni gani mbadala itaenda kununua tumbaku katika Wilaya ya Mpanda?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana pia Waziri alikuja na mapendekezo ya kushusha produce cess kutoka 5% - 3% lakini haijamfaidisha mkulima kwenye haya mazao ya kibiashara kama tumbaku. Punguzo hili limeenda kutupunguzia mapato kwenye Halmashauri zetu na haijamgusa mkulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikuombe Mheshimiwa Waziri aje atuambie ni utafiti upi wa kina ambao wameufanya na kwa nini wasirudishe kwa upande wa wanunuzi kuwa 5% kwa sababu mkulima haijamfaidisha. Zile za leseni na kadhalika ambazo mliwapunguzia zibaki kama zilivyo lakini hii ya ununuzi wa haya mazao ya biashara kama tumbaku warudi kwenye 5%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Benki ya Maendeleo ya Wakulima. Chanzo cha CRDB kinafanana na hii TADB. CRDB ilivyoanzishwa ilikuwa kwa ajili ya kusaidia kilimo na vyama vya ushirika lakini imeenda imekuwa benki ya kibiashara. Kwa mfano, wakulima wa tumbaku wanakopa kutoka kwenye mabenki kwa riba ambayo ipo juu na kuanzishwa kwa benki hii ni chachu kwenye kutoa mikopo upande wa kilimo. Ni kwa kiwango gani mpaka sasa wameshatoa mikopo kwenye mazao ya aina mbalimbali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la SAGCOT. Nimeona kwenye hotuba wanataka waitanue pia ukanda mwingine lakini huu Ukanda wa Kusini SAGCOT imekamilika na kufanya kazi kwa kiasi gani? Hebu njooni Mkoa wa Katavi, ile mikoa ilikuwa ni big four sasa hivi ni big six kwa sababu imegawanyika Njombe na Iringa, Katavi na Rukwa. Kwa hiyo, SAGCOT ikamilishe kwanza Nyanda za Juu Kusini ndipo waende kwenye ukanda mwingine na tuweze kuongeza tija na uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la kufanya utafiti. Baadhi ya Wabunge wamelalamika kwamba mazao yanaanzishwa sehemu zingine, kama korosho imeanzishwa nchi nzima, maeneo mengi wamechukua wamepanda na haijakua na pamba inatanuliwa maeneo mengine. Mwaka juzi tulipitisha sheria ya mambo ya utafiti na kwenye bajeti nimeona mmetenga shilingi bilioni 1.4, utekelezaji wa fedha hizi za kufanya utafiti uko kwa namna gani ili tunapotawanya haya mazao tuwe na uhakika kwamba yataenda kukua na kuongeza uzalishaji? Mheshimiwa Waziri akija kuhitimisha tutaomba majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Jimbo la Nsimbo tumeanzisha zao la pamba na tupo kwenye mikakati ya kwenda kulikuza. Kwa hiyo, tunaomba ile Bodi husika ipitie pia maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hii Kampuni yetu ya Mbolea TFC. TFC ipo chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji lakini kazi kubwa za mbolea wanazofanya zinahusiana na Wizara ya Kilimo. Kwa nini Serikali kiutawala na kiutendaji, japokuwa ni kampuni, basi iwe chini ya Wizara ya Kilimo? Kama tunalaumu kwamba kuna upungufu kwenye utendaji basi anayehusika na usimamizi na usambazaji wa mbolea ambaye ni Wizara ya Kilimo aisimamie hii Kampuni ya Mbolea (TFC).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Tano imelenga kwenye kuwa nchi ya viwanda na mikakati iliyopo sasa hivi vile viwanda ambavyo tunaenda kuvilisha malighafi kwa kupitia shughuli zetu za kilimo, je, tunazi-link vipi hizi sekta zote ili tuwe na tija na kufanikisha malengo kwa wakati? Naomba Waziri atuambie katika mazao ya aina mbili tu, mafuta ya kula ambayo yamekuwa na mgogoro…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri wake na watendaji wote katika Wizara ya Fedha na Mipango, kwa kazi ambazo wameendelea kuifanya. Jambo la kwanza ambalo niende nalo kwanza nimpongeze Mheshimiwa Rais, Dkt. Pombe John Magufuli kwa hotuba yake ya jana ambapo amegusia Benki ya Wakulima jinsi gani inavyofanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka huu tukijadili bajeti ya Wizara ya Kilimo na hata mwaka 2017 nilitoa angalizo kwamba miaka ya 1980 tuliwahi kuanzisha Benki ya Wakulima ambayo sasa hivi ndiyo inaitwa CRDB lakini matokeo yake ikahama kwenye lengo na imekuwa benki ya biashara.

Sasa angalizo hilo jana Mheshimiwa Rais amelielezea vizuri kabisa na hii benki iliyoko sasa hivi tuliyoifufua TIDB iende kule mikoani na kila Mkoa na fedha ziende. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuliona hili na kulisimamia kwa ukaribu kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niguse kidogo jambo moja la 1.5 trillion ambalo linazungumziwa na wenzetu. Kimsingi kama umekusanya shilingi 200 ukatumia shilingi 190 unabaki na shilingi 10. Kwa hiyo, ni kuuliza hiyo shilingi 10 imekaa wapi? Kimsingi CAG katika ripoti yake hakusema hii 1.5 trillion haipo, sio hoja. Alieleza tu mapato na matumizi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika hii fedha kuna nyingine inatokana na kitu kinaitwa IPSA Accruals. Kwa wale wahasibu wanajua. Kuna Accounting Principles; kuna going concern, kuna monitory unit, historical cost, matching concept, accounting period consistency.

Mheshimiwa Spika, sasa ili kuweza ku-meet ile accounting principles kwa mfano ya matching kwamba umeuza Juni, uripoti Juni; umeuza Machi, uripoti Machi; ndiyo maana zimewekwa hizi accruals kwamba haya ni mapato tarajiwa katika mwaka wa fedha huu, kwa hiyo, unai-record ingawa fedha yake taslimu itaingia mwaka unaofuata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na mimi nazungumza nimeifanyia kazi, mimi ni mhasibu. Nime-practice pale Swissport Tanzania, mizigo ambayo imekuja na haijatoka, tulikuwa tunafanya accruals kutokana na kanuni za TRA kwamba mizigo baada ya siku 21 inaenda kupigwa mnada. Kwa hiyo, mnachukua ya miezi miwili mnafanya accruals, mna-record katika mapato, yanaingia kwenye mwaka wa fedha husika halafu amortize mwaka unaofuata. Kwa hiyo, mkitaka shule ya accruals nje.

Mheshimiwa Spika, naomba niende kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina. Ofisi ya Msajili wa Hazina ni muhimu sana. Tuna mashirika na makampuni takribani 270 yanayosimamiwa na hii ofisi. Kimsingi nimeona katika utekelezaji wa bajeti wamepewa fedha ndogo sana asilima 17 tu katika mafungu ambayo tunaenda kupitisha. Sasa uwekezaji uliofanywa na Serikali ni karibuni shilingi trilioni 47, kwa mali zote ambazo Serikali imewekeza katika haya mashirika.

Kwa hiyo, naomba utendaji wa TR uangaliwe kwa kupewa fedha na kuwezeshwa ili waende wakasimamie vizuri. Wakisimamia, maana yake uwekezaji ambao umefanywa na Serikali tutaiona ile return on investment. Kama kuna mashirika yanafanya kwa hasara watasimamia. Naomba pia wapewe fedha ili wawekeze katika mfumo wa kisasa wa TEHAMA, wasitoke physically, watengeneze mfumo wa kuripoti kila mwezi wanaona, ripoti zinaingizwa tu world based, kama mtu yupo Arusha, Bukoba au Mbeya, anaingia kwenye internet anaweka ripoti. Mtu wa Hazina aliyepo Dar es Salaam au Dodoma hapa ana-view na assess na ameweka criteria zake pale anaangalia kwamba performance imekaaje na anachukua hatua haraka.

Mheshimiwa Spika, kingine kwa upande wa ile asilimia 15 ya gross iangaliwe. Kuna mashirika mengine ambayo siyo ya kibiashara, kwa hiyo, yanakusanya na bajeti yao ya uendeshaji ni ndogo. Kwa hiyo, sheria iboreshwe zaidi ili mapato yao yaje yaingie kwenye Serikali na yasaidie katika miradi yetu mbalimbali ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine kuna Kampuni ya UTT PID inayohusiana na miradi ya maendeleo ya miundombinu, nimeona kwenye kitabu na hotuba ya Waziri kwamba wanapima maeneo mbalimbali kama Dodoma sijui Bukoba mtakaba na TPA.

Mheshimiwa Spika, naomba nimwambie Mheshimiwa Waziri kwamba hawa ITT PID they are dying. Mwaka 2017/ 2018 a half year performance wana loss ya 131 million. Kwa hiyo, inaenda kula reserves za nyuma. Wana receivable za almost eight billion. Kwenye five billion wapo watu mbalimbali. Are they collectable? Kwa hiyo, angalia hii. Aidha ufanye compulsory wind-up au voluntary wind-up, usiendelee kupata hasara na mtaji ambao umeshaingia kwa Serikali utaenda utaliwa wote. Hii receivable mkifanya provision, imekula reserve yote ya nyuma.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na wastaafu, jana liliulizwa swali na Mheshimiwa Lucy na akasema kwamba ni kweli kuna watu wanalipwa shilingi 50,000. Naomba nithibitishe, ni kweli kuna watu wanalipwa shilingi 50,000, mmojawapo ni Augustino Mbalamwezi mwenye Pf. No. 613667 Check No. 27850. Huyu alikuwa Mtumishi wa Posta tangu East Africa analipwa shilingi 50,000, yeye halipwi shilingi 100,000. Kwa hiyo, naomba Wizara na wanasikia, wamlipe arreas zake zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la Dar es Salaam Stock Exchange (DSE), hivi sheria inasemaje kama Bunge limepitisha sheria kwamba Makampuni ya Simu na taasisi nyingine zisajiliwe DSE na mpaka leo hazijasajiliwa, sheria inasemaje? Tumeona kwamba Makampuni ya Simu yanatakiwa yasajiliwe. Vodacom ndiyo ameshaingia, hao wengine mpaka leo kwa nini hawajaingia DSE? Sasa DSE hana meno au ndiyo Wizara kwamba haina meno? Kwa hiyo, tutaomba uje utueleze kwa nini imetokea hivyo?

Mheshimiwa Spika, kuna suala la fedha za ruzuku. Mwezi wa Pili mwaka huu TAMISEMI waliita Wakurugenzi, Maafisa Mipango na Wenyeviti wa Halmashauri waka-review bajeti kwamba waelekeze miradi ya kimkakati ambayo itafanyika na itakamilika na kwamba fedha za ruzuku zitakuja. Mpaka tunavyozungumza hivi, fedha za ruzuku hazijaenda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba Mheshimiwa Waziri atuambie, kwa nini hajatekeleza angalau kwa asilimia 50? Tumeaminisha wananchi kwamba tutajenga kituo cha afya, tutajenga sekondari, tutaboresha matundu ya vyoo kwa fedha hizi za ruzuku, lakini mpaka leo hii hata asilimia 50 hazijaenda na mwaka wa fedha ndiyo huu unaishia. Tutaomba utupe hayo majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la kurasimisha sekta zisizo rasmi. Katika hotuba ya bajeti ya mwaka 2017 wakati wa bajeti yako ya mwaka 2017/2018 ulieleza vizuri kabisa kwamba watasajiliwa, watapewa vitambulisho na TRA itaenda kukusanya kodi. Sasa huu mchakato wa kutoa vitambulisho na kutambulika hii sekta isiyo rasmi, ndogo ndogo lakini ni nyingi, utapata mapato huko na utaongeza. Utekelezaji wake mpaka leo umefikia wapi? Tunaona Kariakoo imejaa Machinga, utaratibu mzuri hauonekani, barabara zimefungwa kwa biashara, hata hapo Dodoma pale Nyerere Square kila jioni watu wanafanya biashara. Sasa hawa, ni ndogo ndogo wakitoa, lakini utaingiza mapato. Hebu Mheshimiwa Waziri atuambie imefikia wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la hii Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, wengi wamezungumza na ninaomba tu kwamba hebu tuone kutoka kwenye…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali na Wizara kwa kuendeleza vyema kulinda usalama na raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitabumbilisho vya Taifa (NIDA), zoezi la kuandikisha watu na kupata vitambulisho vya Taifa linaendelea katika mikoa mbalimbali nchini, lakini changamoto iliyopo ni uhaba wa fedha za kuendeshea zoezi mpaka inalazimu Madiwani, Wabunge na Watendaji wa Wilaya, Kata na Vijiji kuchanga pesa kusaidia chakula na malazi jambo ambalo linaweza kuathiri utendaji na mazingira hayo yanaweza weka ushawishi wa watendaji kutoa utambulisho kwa watu wasio na sifa yaani njia ya rushwa kutokana na malipo ya makarani kuwa madogo yaani shilingi elfu kumi kwa siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uendeshaji zoezi kwa kata ni ngumu kutokana na kata nyingine ni kubwa inaleta usumbufu kwa wazee, wagonjwa, mama wajawazito, hivyo zoezi liwe linazingatia umbali kati ya kijiji na kijiji ndani ya kata. Tunahitaji Waziri atoe tamko la namna bora ya kuendesha na pia upatikanaji wa vifaa na fedha ikiwemo magari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Madeni ya Askari Polisi katika TRC, jeshi la polisi hutumika na Shirika la Reli katika escort za treni na mkataba ni kuwa walipwe posho lakini kuna madai ya muda mrefu kati ya Askari na TRC mpaka kupelekea kufungua kesi Dodoma Mahakama Kuu. Naomba Serikali ifanye mazungumzo na TRC ili kuwe na malipo kwa wakati na madeni ya nyuma yalipwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Polisi Nsimbo, Halmashauri ya Nsimbo Kituo cha Polisi ambacho bado hakina vifaa vya kutosha kuanzia gari, pikipiki na hifadhi ya silaha. Tunaomba Wizara isaidie vifaa hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za barabarani, sheria zinazosimamiwa na Jeshi la Polisi juu ya makosa ya barabarani zinaingiliana na Wizara ya Ujenzi kupitia TANROAD hivyo ni vyema Serikali ikafanya sheria hizo ziwe chini ya Wizara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuni za Sheria za Barabarani, wananchi wengi hawazijui kanuni hizi. Mfano makosa ya gari na dereva, makosa kati ya mmiliki na Dereva mwajiriwa. Sheria iboreshwe ili kosa la Dereva lisiwe la mmiliki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza natoa pongezi nyingi kwa Waziri na Naibu Mawaziri kwa utendaji na ushirikiano wao kufanikisha malengo ya Serikali. Pili, nampongeza Mheshimiwa Rais Joseph Pombe Magufuli kwa uthubutu wake wa kulinda maliasili za Taifa ili nchi na vizazi vijavyo viweze kufaidi. Mheshimiwa Rais amefanya mabadiliko katika Sheria za Madini pia sheria mpya za Permanent Sovereignty na Unconscionable Terms ambazo zitasaidia kupitia mikataba isiyokuwa na tija kwa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tatizo la maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambao wanahangaika sana kutafuta kipato. Hivyo, Serikali ifanye mpango wa kuwa na maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na watambuliwe kwa kusajiliwa na wapewe leseni za bei nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilisimamisha utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji wadogo miaka miwili imepita. Fedha hizo zilikuwa zinasaidia wananchi na kuwainua kiuchumi. Hivyo, tunaomba Serikali irudishe ruzuku hiyo na kuweka mpango mzuri ambao utanufaisha wachimbaji wadogo nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ufadhili wa uchimbaji bora kwa vituo saba. Tangu 2016 Serikali ilitoa taarifa kuwa kutakuwa na vituo saba vya mfano ili kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na moja ya kituo hicho ni Ibindi, Jimbo la Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, Katavi. Tunaomba kauli ya Serikali mpango huu wa World Bank utafanikiwa lini? Je, Serikali ina mkakati gani wa kuuendeleza?

Mheshimiwa Naibu Spika, service levy za councils na soko huru. Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, kila aina ya biashara katika Halmashauri wanatakiwa kulipa service levy, lakini changamoto iliyopo ni usiri wa mauzo kwa wafanyabiashara wa madini ambapo huwa hakuna uwazi katika kununua na kuuza inapelekea Serikali kupoteza mapato. Hivyo basi, nashauri Serikali ianzishe soko huru kwa maeneo yote ili Serikali ipate mapato pia Serikali za Mitaa zipate service levy. Halmashauri ya Nsimbo ina wachimbaji wadogo wengi 98% ambao hawana uwazi na Halmashauri inapoteza mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, ugawaji maeneo kwa kigezo cha aina ya madini. Mkoa wa Katavi maeneo mengi yana madini aina tofauti tofauti, ukanda wa Wilaya Tanganyika ndio umepangwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo lakini ukanda huo zaidi ni madini ya shaba ndiyo yanapatikana kwa wingi lakini Wilaya ya Mpanda, Jimbo la Nsimbo ndiyo kuna dhahabu, hivyo eneo hilo linafaa kutengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuboresha sheria, sera na kanuni ili kufikia malengo. Serikali iendelee kuboresha sheria, sera na kanuni kwa kuzingatia pande zote za kulinda maliasili na uwekezaji kuendelea kukua.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Serikali iongeze kasi katika kutekeleza uwekezaji wa mashine ya uchenjuaji (smelter) ili kuokoa upotevu wa maliasili na kuongeza ajira nchini. Waziri atoe taarifa uwekezaji wa smelter umefikia wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, shukrani kwa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mungu mpo salama. Natoa pole kwa Wabunge wote kutokana na matukio na ajali ya power bank. Natoa pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Jafo, Mheshimiwa Waziri Mkuchika na Makatibu Wakuu wote na Watendaji kwa kazi nzuri ya kusimamia Halmashauri nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2017 Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290 ambapo uzito ndani ya tani moja hakuna tozo unaposafirisha kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine. Pia katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mheshimiwa Rais waliweza kueleza nafuu hiyo, lakini mwongozo au sheria hiyo haikuzingatia mazao yanayodumu katika muda mfupi (perishable goods) ambayo mkulima hawezi kuhifadhi na inamlazimu kupeleka sokoni moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali katika hitimisho la bajeti itoe tamko juu ya tozo kwenye mboga mboga (perishable goods) kwa kuwa wakulima wengi wa Jimbo la Nsimbo wanasafirisha kwa kiwango chini ya tani moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona maeneo mengine wanategemea perishable goods kama own source kubwa. Basi, nashauri mtu mwenye mzigo chini ya kilo 50 asilipe ushuru ili kutoa nafuu kwa wakulima wadogo wadogo. Pia produce cess 3% on value inavyotozwa na Halmashauri, ipo tofauti na sheria kwani Councils wanatoza fixed amount mfano shilingi 1,000/= kwa tenga, lakini ukitathimini kwa bei ya soko inakuwa chini ya shilingi 1,000/=. Serikali pia iangalie eneo hilo ingawa kwa kudhibiti fixed charge, itasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watumishi wa Serikali hususan Walimu wanadai pesa nyingi ingawa Serikali hivi karibuni ililipa kiasi. Kwa mfano Walimu wa Mkoa wa Katavi kwa madeni yasiyo ya mshahara wanadai kiasi cha shilingi bilioni 1.3. Naomba Serikali ifanye tena malipo ya madeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mkoa wa Katavi kuna madai ya kupanda madaraja mfano mwaka 2016, Februari Tume ya Utumishi ya Walimu ilitoa barua lakini kufikia Novemba, 2016 Walimu waliambiwa warejeshe barua hizo. Mpaka sasa hakuna waliopanda, lakini kwa wale wachache ambao hawakutii agizo hilo walipanda madaraja. Tunaomba Serikali iangalie Walimu hawa ili wapande madaraja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile wapo Walimu ambao wanatakiwa kupanda mishahara, lakini bado Lawson haiwatambui ingawa Halmashauri zimeshawasilisha madai yote Utumishi, naomba Mheshimiwa Waziri ashughulikie maombi hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TARURA, wazo la kuanzisha TARURA ni jema, lakini mgao wa road fund kwa uwiano wa 3:7 na TANROADS bado hauna tija kwa kuanzishwa kwa TARURA. Kuna ongezeko la gharama za utawala ambazo zinapunguza fedha za maendeleo. Ukiangalia hiyo asilimia 30 itakuwa imepungua; fedha za maendeleo inaenda asilimia 20 na nyingine utawala. Hivyo mgao na uwe uwiano wa 4:6 TARURA Vs TANROADS ili fedha za maendeleo zibaki kama ilivyokuwa kabla ya kuanzisha TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAMISEMI ilifanya kikao na madeni, Afisa Mipango na Wenyeviti wa Halmashauri 2018, Februari mwishoni ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha miradi inafanyika kwa ukamilifu na kutumia chini ya fedha za ruzuku. Tunaomba Serikali itoe fedha angalau asilimia 50 ili miradi iliyorekebishwa katika bajeti. Halmashauri zilifanya mawasilisho upya Machi, 2018. Kwa kutoa fedha kiasi itawezesha Halmashauri zianze kutekeleza miradi ya maendeleo iliyo chini ya LGCDG.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Halmashauri nyingi nchini zina Wakuu wa Idara ambao wamekaimu kwa muda mrefu. Aidha, kutokana na kutotimiza masharti au uzembe katika mchakato wa kuthibitisha. Naomba Serikali iangalie upya vigezo vya Utumishi kama Wakuu wa Idara mfano kupunguza miaka saba mpaka mitano, ikiendana sambamba na kupandisha cheo. Hii itasaidia watumishi kufanya kazi kwa hali na mori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Jimbo haina uwezo mkubwa na kati ya Kata 12 tuna Vituo vya Afya vitatu tu. Hivyo kwa kuwa mwaka 2018/2019 hatuna mgao wa Hospitali ya Wilaya, basi tunaomba msaada wa fedha kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Kapalala, chini ya Kijiji cha Songambele ambapo kituo hicho cha afya kitasaidia jumla ya Kata nne ambazo ni Kapalala, Nsimbo, Urwira na Mtapenda. Tunaomba sana Serikali itupatie msaada huo wakati tunasubiri bajeti ijayo kwa Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishukuru sana Serikali kwa kutupatia gari la wagonjwa (ambulance) Maruti Suzuki, itasaidia kwa kiasi changamoto ya usafiri. Hivyo basi, tunaomba tena gari la wagonjwa aina ya Land Cruiser Hardtop, ambalo linaendana na mazingira ya msingi kwani miundombinu bado mibovu sana na pia matukio ya vifo vya mama na mtoto bado yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Nsimbo bado ina uhaba mkubwa wa Walimu na Watumishi wa Idara ya Fedha. Tunaomba TAMISEMI katika ajira za Walimu zinazokuja mwangalie Halmashauri ya Nsimbo. Pia Wahasibu hawatoshi mpaka inapelekea kutofanya kazi kwa ufanisi katika kusimamia mapato ya Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TEHAMA, Serikali imefanya kazi nzuri katika TEHAMA upande wa kukusanya mapato, lakini changamoto iliyopo ni kwenye POS, hakuna udhibiti wa kutosha kwa kuwa mtozaji ndiyo anachagua aina ya tozo na idadi za bidhaa. Hivyo, upotevu wa mapato bado upo. Nashauri Serikali ihimize Halmashauri ziwe na takwimu ili kulinganisha na makusanyo halisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Jafo kwa kuweza kutoa kwa Nsimbo fedha za Kituo cha Afya na

ambulance, pia fedha za Equip, P4R, TEA, Shule za Msingi na nyingine nyingi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mungu mpo salama. Natoa pole kwa Wabunge wote kutokana na matukio na ajali ya power bank. Natoa pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Jafo, Mheshimiwa Waziri Mkuchika na Makatibu Wakuu wote na Watendaji kwa kazi nzuri ya kusimamia Halmashauri nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2017 Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290 ambapo uzito ndani ya tani moja hakuna tozo unaposafirisha kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine. Pia katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mheshimiwa Rais waliweza kueleza nafuu hiyo, lakini mwongozo au sheria hiyo haikuzingatia mazao yanayodumu katika muda mfupi (perishable goods) ambayo mkulima hawezi kuhifadhi na inamlazimu kupeleka sokoni moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali katika hitimisho la bajeti itoe tamko juu ya tozo kwenye mboga mboga (perishable goods) kwa kuwa wakulima wengi wa Jimbo la Nsimbo wanasafirisha kwa kiwango chini ya tani moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona maeneo mengine wanategemea perishable goods kama own source kubwa. Basi, nashauri mtu mwenye mzigo chini ya kilo 50 asilipe ushuru ili kutoa nafuu kwa wakulima wadogo wadogo. Pia produce cess 3% on value inavyotozwa na Halmashauri, ipo tofauti na sheria kwani Councils wanatoza fixed amount mfano shilingi 1,000/= kwa tenga, lakini ukitathimini kwa bei ya soko inakuwa chini ya shilingi 1,000/=. Serikali pia iangalie eneo hilo ingawa kwa kudhibiti fixed charge, itasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watumishi wa Serikali hususan Walimu wanadai pesa nyingi ingawa Serikali hivi karibuni ililipa kiasi. Kwa mfano Walimu wa Mkoa wa Katavi kwa madeni yasiyo ya mshahara wanadai kiasi cha shilingi bilioni 1.3. Naomba Serikali ifanye tena malipo ya madeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mkoa wa Katavi kuna madai ya kupanda madaraja mfano mwaka 2016, Februari Tume ya Utumishi ya Walimu ilitoa barua lakini kufikia Novemba, 2016 Walimu waliambiwa warejeshe barua hizo. Mpaka sasa hakuna waliopanda, lakini kwa wale wachache ambao hawakutii agizo hilo walipanda madaraja. Tunaomba Serikali iangalie Walimu hawa ili wapande madaraja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile wapo Walimu ambao wanatakiwa kupanda mishahara, lakini bado Lawson haiwatambui ingawa Halmashauri zimeshawasilisha madai yote Utumishi, naomba Mheshimiwa Waziri ashughulikie maombi hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TARURA, wazo la kuanzisha TARURA ni jema, lakini mgao wa road fund kwa uwiano wa 3:7 na TANROADS bado hauna tija kwa kuanzishwa kwa TARURA. Kuna ongezeko la gharama za utawala ambazo zinapunguza fedha za maendeleo. Ukiangalia hiyo asilimia 30 itakuwa imepungua; fedha za maendeleo inaenda asilimia 20 na nyingine utawala. Hivyo mgao na uwe uwiano wa 4:6 TARURA Vs TANROADS ili fedha za maendeleo zibaki kama ilivyokuwa kabla ya kuanzisha TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAMISEMI ilifanya kikao na madeni, Afisa Mipango na Wenyeviti wa Halmashauri 2018, Februari mwishoni ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha miradi inafanyika kwa ukamilifu na kutumia chini ya fedha za ruzuku. Tunaomba Serikali itoe fedha angalau asilimia 50 ili miradi iliyorekebishwa katika bajeti. Halmashauri zilifanya mawasilisho upya Machi, 2018. Kwa kutoa fedha kiasi itawezesha Halmashauri zianze kutekeleza miradi ya maendeleo iliyo chini ya LGCDG.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Halmashauri nyingi nchini zina Wakuu wa Idara ambao wamekaimu kwa muda mrefu. Aidha, kutokana na kutotimiza masharti au uzembe katika mchakato wa kuthibitisha. Naomba Serikali iangalie upya vigezo vya Utumishi kama Wakuu wa Idara mfano kupunguza miaka saba mpaka mitano, ikiendana sambamba na kupandisha cheo. Hii itasaidia watumishi kufanya kazi kwa hali na mori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Jimbo haina uwezo mkubwa na kati ya Kata 12 tuna Vituo vya Afya vitatu tu. Hivyo kwa kuwa mwaka 2018/2019 hatuna mgao wa Hospitali ya Wilaya, basi tunaomba msaada wa fedha kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Kapalala, chini ya Kijiji cha Songambele ambapo kituo hicho cha afya kitasaidia jumla ya Kata nne ambazo ni Kapalala, Nsimbo, Urwira na Mtapenda. Tunaomba sana Serikali itupatie msaada huo wakati tunasubiri bajeti ijayo kwa Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishukuru sana Serikali kwa kutupatia gari la wagonjwa (ambulance) Maruti Suzuki, itasaidia kwa kiasi changamoto ya usafiri. Hivyo basi, tunaomba tena gari la wagonjwa aina ya Land Cruiser Hardtop, ambalo linaendana na mazingira ya msingi kwani miundombinu bado mibovu sana na pia matukio ya vifo vya mama na mtoto bado yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Nsimbo bado ina uhaba mkubwa wa Walimu na Watumishi wa Idara ya Fedha. Tunaomba TAMISEMI katika ajira za Walimu zinazokuja mwangalie Halmashauri ya Nsimbo. Pia Wahasibu hawatoshi mpaka inapelekea kutofanya kazi kwa ufanisi katika kusimamia mapato ya Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TEHAMA, Serikali imefanya kazi nzuri katika TEHAMA upande wa kukusanya mapato, lakini changamoto iliyopo ni kwenye POS, hakuna udhibiti wa kutosha kwa kuwa mtozaji ndiyo anachagua aina ya tozo na idadi za bidhaa. Hivyo, upotevu wa mapato bado upo. Nashauri Serikali ihimize Halmashauri ziwe na takwimu ili kulinganisha na makusanyo halisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Jafo kwa kuweza kutoa kwa Nsimbo fedha za Kituo cha Afya na

ambulance, pia fedha za Equip, P4R, TEA, Shule za Msingi na nyingine nyingi.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi, napenda niipongeze Serikali na Waziri pamoja na timu yake nzima kwa namna wameweza kuandaa mpango huu na niseme tu katika changamoto ambazo amezieleza kutokana na utekelezeji wa mpango amekwa wazi na sisi kama Wabunge tunahitaji kumsaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili uweze kutekeleza mpango au bajeti tunaangalia mapato na matumizi, na katika upande wa mapato ili kuweza kuongeza mapato maana yake utaongeza bei au rate, utaongeza ushalishaji au utaongeza vyanzo vipya vya mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nianze na masuala ya kodi, kwanza niombe Serikali au Wizara husika ule muda wa makampuni au taasisi mbalimbali kupitia malimbikizo ya madeni ya riba kwenye kodi badala ya tarehe 30 Novemba muuongeze na watembelee makampuni mbalimbali ili watu waitikie na walipe malimbikizo ya kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna suala la kuongeza bei kwenye maeneo mbalimbali mara nyingi mwezi Juni kwenye Finance Bill ndio tunaletewa maeneo ya mapendekezo. Lakini ningependeza kipindi hiki cha mpango hebu Waziri awe anatupa maeneo anayotarajia kuongeza ili tuwe na nafasi nzuri ya kuweza kushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba kwa namna ya pekee kabisa tuumie Watanzania lakini tupate huduma, naomba tuongezee shilingi 50 kwenye kila lita ya mafuta ili iende kwenye maji. Kwa sababu gani napendekeza, miradi ya maji ikishatengenezwa maintenance inaachiwa kwenye jumuiya ya watumia maji watabaki wana-maintain wenyewe, tofauti na Road Fund kila mwaka zinatoka fedha za ukarabati lakini mradi wa maji ikisha tengenezwa COWOSO ndio inakuwa na wajibu wa ku-maintain kwa hiyo kama Serikali tukiruhusu hii shilingi 50 tukaongeza ikaenda kwenye maji itasaidia kwenye miradi ya maji ambayo ndio changamoto kubwa ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulifanya mabadiliko sheria ya fedha produce cess tukashusha kutoka asilimia tano kwenda asilimia tatu, lakini kimsingi kwenye mazao ya biashara kama tumbaku hatujamnufaisha mkulima kwa hiyo hii tumenufaisha mnunuzi. Kwa hiyo niombe Serikali muone namna gani vya ku-review hii punguzo kutoka asilimia tano kwenda asilimia tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni kuhusu sevice levy. Halmashauri nyingi hazipati service levy kutoka kwa wa wakandarasi wanaotengeneza barabara ambao wapo chni TARURA na chini ya TANROADS kwa hiyo mapato kwenye halmashuri hayakuwa hayafikii malengo vilevile kampuni za simu ambazo zimeweka minara sehemu mbalimbali nchini bado Halmshauri zetu hazipati mapato upande ya service levy. Kwa hiyo tunaomba kama Serikali muweze kuangalia maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awamu hii ya tano tunapongeza sana kwamba tutakuwa na uchumi upande wa viwanda, lakini kuna viwanda hapa Tanzania kuna viwanda vinalishwa kwa 90%; 75% kutoka nje ya nchi. sasa kama Serikali nini mkakati kwa mfano kwenye ngano Bakhresa 95% anaingiza toka nje, sasa tuna mkakati upi wa kuweza kuwezesha akapata malighafi hizi toka Tanzania ambapo tutatengeneza ajira humu ndani tutakusanya mapato ya kodi mbalimbali, sasa nini kifanyike tutaomba Serikali ingalie na upande hata wa mafuta 75% tunaingiza kutoka nje. Kwa hiyo, dola ambazo tunalipa kwenda nje ni nyingi kuliko tunazoziingiza kutokana na export, kwa hiyo balance payment inakuwa ni negative, kwa hiyo hii inatuathiri uchumi wetu.

Kwa hiyo, tunaomba pia kwenye upande wa kilimo wananchi wengi wanatumia jembe la mkono. Sasa ni lini tutawatoa hii benki yetu ambayo tumeanzisha kwa ajili ya kuendeleza kilimo inaenda kusaidia namna gani maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye upande wa Balozi zetu, nchi nyingi duniani tuna Balozi nyingi lakini ni jinsi gani kama kama Serikali tunazitumia hizi Balozi kwenye kupata wawekezaji na kuangalia fursa zilizopo kwenye nchi mbalimbali duniani. Tumeona Balozi nyingi hatujapata taarifa yake kamili lakini hatuzitumii vizuri na hata Balozi zingine zinahitaji taarifa toka huku nchi hazibiwi kwa wakati miezi miwili/miezi mitatu kwa hiyo tutumie vizuri hizi Balozi tuweze kukuza uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti,kuna suala la sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, mwaka juzi ilipitishwa na mwaka jana wakati wa bajeti ilitoa taarifa kwamba watapewa vitambulisho watambulike na waingie kwenye kuchangia kwa maana kwamba walipe kodi, sasa changamoto Waziri ameileza kwenye kitabu chake kwamba imekuwa ni ngumu, sidhani kama sisi wanadamu au Serikali ikiamua jambo linaweza likashindikana.

Kwa hiyo, tukiweka vitambulisho na maeneo husika na hata wale wanaotembea kama vitambulisho wataweza pia kuhusishwa vyema nakuweza kulipa kodi na staiki zingine zote za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala ya mashirika ya Serikali ambapo yana zaidi ya 50% na mengine chini 50%. Kuna kampuni kama TTCL inahitaji udhama wa concession loan, inahitaji Serikali iweze kusaidia kuwekeza. Mchango karibuni na Serikali dora 231,000 sasa ni lini Serikali itaoa fedha kwa Kampuni ya TTCL ili ingie kwenye ushindani, ipate faida na Serikali ipate gawio kama ambalo ndilo kusudio. Na ATCL tunashukuru shirika limefufuliwa vizuri lakini ATCL inahitaji jicho zaidi, ipate discount kwenye government bill kwa mfano land fees, mambo ya navigation wapunguziwe kama nation flag ili waweze kukua zaidi na zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la utalii kama ni Tanzania tuna vivutio vingi je, ni lini mchango wa utalii utaongezeka kwa kiasi kikubwa katika kukuza pato la Taifa. Tunaona nchi za wenzetu wanapata mapato mengi kwenye utalii lakini vivutio ni chache sana. Sasa tuombe Wizara ya Maliasili ya na Utalii kwa kushirikiana kwa ujumla kama kuna msaada wa Wabunge, msaada wa maeneo mbalimbali watuoneshe mkakati utalii utaenda kuongeza mapato kwa kiasi kikubwa na nchi ambazo watalii wengi wanapatikana tufanye mawasiliano...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi, kwanza naomba nipongeze Wajumbe wenzangu wa Kamati ya PIC kwa kazi nzuri ambayo wameifanya ya kuweza kuishauri Serikali katika utendaji kiujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na jambo la kwanza ya masuala machache ambayo yamejitokeza hapa ndani; kwanza kuna mchangiaji mmoja ameeleza hajui tofauti ya revenue na tozo, lakini naomba tutambue kwamba tuna mapato ya aina mbili katika bajeti yetu ya Serikali. Tuna mapato yanayotokana na kodi na tuna mapato ambayo hayatokani na kodi. Kwa hiyo, unavyotuambui revenue na utambui tozo nazo ni revenue ni mapato kwa hiyo tusiwe tunachanganya kidogo masuala haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine limejitokeza suala la kwamba faida kutoka Serikali inayopata katika uwekezaji kwenye taasisi na baadhi ya mashirika ya umma imepungua kutoka bilioni 800 na ushehe mpaka bilioni 600. Serikali katika hizi taasisi na mashirika ya umma ambapo imewekeza inapata aina mbili za mapato; kuna mapato ghafi ambayo ni 15% kutoka kwenye mauzo na pia kuna mapato yanayotokana na gawio baada gawio la kwenye faida yaani dividend. (Makofi)

Sasa baada ya kutoa haya unakuta bado kuna masalia ya ziada yamebaki, kwa hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ambayo ni 70% inachukuliwa na Hazina na 30% inabaki inaendelea kwa ajili ya kuendelea hayo mashirika kufanya uwekezaji. kwa hiyo kushuka kutoka bilioni 800 mpaka bilioni 600 ilitokana na kwamba kulikuwa na malimbikizo ya miaka ya nyuma kulikuwa na cummulative figure retained earnings ndiyo ambayo ilichukuliwa na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo alilisemea rafiki yangu Mheshimiwa Silinde ni kuhusiana na miradi ya maji. Mwaka jana tumepitisha bajeti ya maji takribani bilioni 673 ambayo ni ya miradi ya maendeleo katika hizi bilioni 673; shilingi bilioni 443 zinatokana na mapato ya ndani na zinazobaki zinatokana na mikopo pamoja na ruzuku za wafadhili mbalimbali yaani fedha za nje. Sasa kwenye hizo shilingi bilioni 443 hapo ndani pia tuna mfuko wa maji ambapo una bilioni 158 na siyo ile bilioni 249 aliyoisema na katika hiyo bilioni 158 Serikali imeshatoa bilioni 67 ambayo ni sawasawa na 43% ambayo imeshapatikana. Na wengi katika Halmashauri zetu tunajua kabisa miradi ya maji inatekelezwa na Halmashauri zinatuma certificate Wizarani ikishatuma certificate Wizarani ndipo Serikali inapeleka pesa na hatua hii ilichukuliwa kwa sababu fedha zilikuwa zinaliwa na miradi haitekelezwi kwa wakati, ndiyo maana Serikali ilibadilisha utaratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala lingine ambalo limeweza kuzungumziwa ni kuhusiana na masuala ya madeni. Ndugu zangu tunajua taasisi ya kufanya kazi kuna madeni na sisi kwenye Kamati yetu tumekuwa tukisisitiza sana ulipaji wa madeni na pia katika kuongeza mitaji baadhi ya taasisi na mojawapo ambapo tunaiona katika ulipaji wa madeni yasipolipwa kwa wakati kulingana na kanuni za kiuhasibu zinavyohitaji lazima ufanye provision for doubtful debts yaani unafanya in payment ya receivable kwamba endapo isipokusanywa tutakuwa na gharama ya hasara kiasi gani, kwa hiyo, tumekuwa tukisisitiza kwenye jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumzia hapo naomba nirudi kwenye usimamizi Ofisi ya Treasury Register (TR). Serikali kama tulivyosema awali kuna mapato yanayotokana na kodi na mapato ambayo hayatokani na kodi katika moja ya mapato ambayo hayatokani na kodi ni kutoka Ofisi ya TR. Sasa ili aweze tuweze kuongeza mapato ambayo hayatokani na kodi maana yake tukaboreshe usimamizi wa hiyo Ofisi ya TR na katika kuboresha ofisi hii kimsingi haya makampuni/taasisi zote ziko nchi nzima na watumishi wako kwenye kama 105 maana yake ni kada mbalimbali wa chini mpaka wa juu. Sasa niombe Serikali ikaweze kumwezesha TR kibajeti ili akawekeze kwenye TEHAMA na kwamba kila mwezi mashirika yote haya report zao za mahesabu za kila mwezi wanaziingiza katika mfumo ambapo mtu amekaa ofisini kwake kama ni Mwanza kama ni Mbeya anaingizwa kwenye mfumo ofisi ya TR kutokea Dodoma Makao hapa wana monitor. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna reporting system inaitwa work based reporting kwa hiyo inatumika ile na mna- control mashirika yetu na makampuni ya nje yana-control dunia nzima kwa kupitia mfumo na hii itamsaidia TR.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na sisi kama Kamati ya PIC ili tuweze tukasimamie vizuri haya mashirika tunahitaji kufanya kazi kwa ukaribu vizuri kabisa na Ofisi ya TR. Sasa ni vyema tukaboresha namna ya kiutawala Ofisi ya TR kuwasiliana na Bunge, TR awasiliane moja kwa moja na Bunge maana mlolongo wa kupitia kwa Katibu Mkuu halafu ndiyo ije kwa Mheshimiwa Waziri halafu ndiyo ije sasa Ofisi ya Bunge tumekuwa na mawasiliano yanachelewa na maamuzi pengine yanachelewa. Wajumbe wanahitaji kuchangia uwezo semina hazifanyiki, Wajumbe wanahitaji kwenye kukagua miradi tumealikwa hatujaenda kwa sababu ya mawasiliano. Kwa hiyo, tunaomba TR apewe madaraka ya moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ili tuweze kuongeza ufanisi katika taasisi na mashirika yote haya tunahitaji TR akazingatie sheria; 60% ya gharama ikaende kuzingatiwa na kuweza kusimamia na tukifanya hivyo tutaondoa uwalakini wa mashirika ambayo yatakuwa yanafanya biashara au kazi kwa hasara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Kamati yetu tumesisitiza uongezaji wa mitaji na tunapongeza sana Serikali kwa kufufua Shirika la Air Tanzania. Nina imani kabisa miaka mitanomitatu ijayo au minne Air Tanzania itaanza kufanya kazi kwa faida kwa sababu uwekezaji huu ambao umefanywa na Serikali tutaenda kuongeza biashara, abiria wengi watabebwa na ndipo ambapo gharama zitaenda zinashuka ukilinganisha na mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na pia kama wachangiaji wengine walivyosema kwamba kwa kufufua Air Tanzania tutaenda na kuboresha sekta zingine ambazo ni sekta kubwa sana ya utalii, tutaenda kuongeza ajira na maeneo mengine ya Tanzania yatafikika. Kwa mfano Mkoa wetu wa Katavi tuna Mbuga ya Katavi ambayo ni nzuri sana na wanyama wakubwa wazuri sana, lakini ni kwamba Air Tanzania ikifika kule na uwanja wa ndege upo tutaongeza watalii wakuja kutalii kwenye nchi yetu na mapato ya Serikali yataongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile shirika letu la Air Tanzania hebu kwenye kulinyanyua tulipe discount kwenye baadhi ya charge Serikali kwa mfano charge za airport, landing fee, kwenye charge cha TCIAA tuwape discount. Na pia TTCL wanahitaji mtaji wa dola kama 230,000 kama mchango wa Serikali ili iweze kushindana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natoa pongezi kwa Serikali kwa kuendelea kuimarisha elimu nchini. Pongezi kwa Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Maendeleo Msaginya (Katavi) ni muhimu sana kwa kuelimisha vijana katika sekta mbalimbali kuanzia watoto wenye elimu ya msingi. Chuo hiki kimepata ajali ya kuungua moto mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Hivyo, tunaomba Serikali kupitia Wizara kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili kwa kuwa watoto wanaishi katika mazingira magumu sana. Hivyo, tunaomba uwezeshaji ufanyike kwa haraka. Uongozi wa chuo umeshaleta barua Wizarani kwa taarifa na utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania imekuwa kinara katika kutoa elimu isiyo na mfumo rasmi (non-formal education). Tunayo UPE na Elimu ya Watu Wazima na nyinginezo, napenda kupata maoni ya Serikali, je, mpango upi uliopo wa kuboresha elimu hii? Pia Serikali imetenga kiasi gani kwa ajili ya mfumo huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Teachers’ Professional imepitishwa lakini bado inahitaji maboresho yafuatayo: Moja, uteuzi wa regional and district representative. Katika sheria uteuzi unafanywa na Waziri wa Elimu. Nashauri uteuzi ufanywe na registrar kwa kushirikiana na bodi. Pili, Teachers’ Professional haina mamlaka ya kuhakiki walimu na taaluma zao, hivyo mitaala iwe inapitiwa na Bodi ya Teachers’ Professional ili kuhakikisha wahitimu ni watu wenye sifa zinazotakiwa, kama professional bodies nyingine zinavyofanya, mfano Uhasibu, Sheria (Law School) na Manunuzi. Tatu, utunzi wa kanuni uzingatiwe kwa wakati ili kuharakisha utekelezaji wa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaomba Serikali iendelee kukarabati shule kongwe za msingi katika Halmashauri ya Nsimbo; Songambele, Isinde, Ikolongo, Katambike, Mtapenda, Isanjandugu na Uruwira.
Muswada wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini wa Mwaka 2016
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwanza namshukuru Mungu kwa siku ya leo, lakini pia naipongeza Serikali kwa ujumla na hasa Wizara husika kwa kuweza kuwasilisha muswada huu. Mazuri mengi ambayo tutafaidika kwenye muswada huu yameelezwa ikiwa ni mambo ya fidia, watu kufanya kiutaalam, mambo ya mikopo, wawekezaji na kupunguza utapeli kwa ujumla. Naipongeza sana Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Waziri Mkuu alifanya ziara Mkoa wa Katavi na Rukwa, aliweza kutatua kero ya ardhi kuhusu utapeli wa wanakijiji waliokuwa wanatapeliwa. Pamoja na hayo kuna masuala madogo ambayo naomba Mheshimiwa Waziri akija aweze kutupa ufafanuzi au kuelewa kwa kina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni ukataji wa rufaa kama ambavyo ameeleza kwenye hotuba yake, lakini kwa haraka haraka sijaona kifungu cha kisheria ambacho kinamwezesha mtu aliyefanyiwa thamani au kuthaminiwa kwamba atakitumia kwa ajili ya kukata rufaa na endapo hajaridhika na Mthamini Mkuu hiyo rufaa yake anaweza kuipeleka wapi? Tutaomba Mheshimiwa Waziri aweze kutufafanulia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile endepo Mthaminiwa atakuwa haridhiki na uthamini uliofanywa na Serikali, je, kuna uwezekano wa kumweka Mthamini wa binafsi (independentvaluer) halafu iingie kwenye Bodi? Hilo nalo Mheshimiwa Waziri tutaomba utusaidie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika muswada huu Kifungua cha 25 kinazungumzia adhabu kwa lugha nyepesi tuiite vishoka, lakini pia ukienda Kifungu cha 62 kwenye masharti ya jumla kinazungumzia adhabu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Kifungu cha 25 kwamba mtu atapewa adhabu kati ya shilingi milioni tano mpaka shilingi milioni 20 ikiwa ni mtu, lakini kama ni kampuni ni shilingi milioni 20. Ukienda kwenye masharti ya jumla Kifungu cha 62 kinazungumzia adhabu itakuwa kima cha juu ni Shilingi milioni tano au kifungo cha miaka miwili au vyote kwa pamoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naona hivi vifungu viwili kama vinaoana kutokana na makosa; kwa sababu kifungu cha 25 ni mtu ambaye hana cheti; lakini ukienda kifungu cha 62 ni mtu ambaye anafanya kazi, mtu ambaye hajasajiliwa, kwa hiyo, wanafanana na wanaoana kwamba mtu ambaye hajasajiliwa ni sawa sawa na mtu ambaye hana cheti. Kwa hiyo, hizi hesabu tusiwe na double standard na kuondoa katika maamuzi ya mahakama kutokuweka mazingira ya rushwa, basi adhabu iwe ya aina moja kati ya kifungu cha 25 na 62.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu taarifa ya utekelezaji, kwamba Bodi ikishafanya kazi yake baada ya mwaka, itatakiwa ndani ya miezi mitatu itengeneze taarifa ya utekelezaji. Sasa katika kifungu cha 61 inaelekeza Bodindani ya miezi minne wapeleke taarifa kwa Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Waziri copy ataipeleka katika Bunge, ikiwa Bunge maana yake ni Kamati husika. Sasa wasiwasi wangu ni kwamba taarifa hii itakuwa ni taarifa ambayo haijakaguliwa na Mkaguzi wetu, CAG.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nashauri kwenye kifungu hiki, taarifa iende kwa Mheshimiwa Waziri wakati imekwishakaguliwa ili anavyoileta katika Bunge iwe ni taarifa ambayo imeshapita kwa Mkaguzi Mkuu. Ukiangalia zile timing ni mwezi Septemba na mpaka mwezi wa tatu ambapo Mkaguzi Mkuu anatoa taarifa zake. Kwa hiyo, hilo nalo tutaomba Mheshimiwa Waziri aweze kuliangalia, ikiwezekana basi alete schedule of amendments nyingine baada ya mapendekezo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kifungu cha 57, inazungumzia masuala ya adhabu. Sasa kuna lugha pale imenitatiza kidogo, inasema Bodi itakavyoona. Kwa hiyo, tumeacha uhuru,Bodi iangalie ni adhabu kiasi gani. Sasa ni bora kwamba Waziri atakapotengeneza kanuni kwa kurejea kifungu hiki cha 57, aangalie ni adhabu gani ambazo Bodi itaweza kuzitoa kuliko kuacha mazingira yaBodi kufanya uamuzi wakati kosa limetokea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu kingine ambacho ningependa kuchangia ni kifungu cha 49 kwamba Mthamini anavyoandika report anatakiwa aandike sababu za kufanya huo uthamini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni bora Waziri katika upande wa zile kanuni aoanishe hizo sababu, tuwe na sababu ambazo ni standard ili watu wetu wanavyoandika hizi report za huu uthamini ambao wameufanya, mtu asitoe sababu zake na lugha zake ambazo zinakuwa hazieleweki; tuwe tayari na sababu zionyeshwe kwenye kanuni ambazo zitakuwa ni standard.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu wengi tunahitaji kuchangia, nishukuru kwa leo, ni hayo tu. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa hii nafasi. Kwanza naomba nianze kwa kuunga mkono hoja, pili naomba niipongeze sana Serikali kwa kuitendea haki Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo na nchi kwa ujumla. Pia nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu Profesa Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Kalobelo na watendaji wote ndani ya hii Wizara ya Maji kwa namna ambavyo wanatekeleza majukumu ya Serikali, na sisi Waheshimiwa Wabunge wanatupokea Wizarani, wanatusikiliza na kutekeleza yale ambayo tumeyaomba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ninaomba niipongeze Serikali kwa kuuweka Mji wa Mpanda katika fedha za mkopo wa kutoka nchi ya India, takriban zaidi ya milioni 500, yaani kwenye fedha za dola. Ninatumaini maji yakifika katika Mji wa Mpanda yatafika pia na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na kuhusiana na changamoto ambayo Mheshimiwa Waziri alizieleza katika hotuba yake ya bajeti. Changamoto ya kwanza ambayo aliieleza ni kuhusiana na utekelezaji wa miradi ambao haujafanyika kutokana na changamoto ya kifedha, kutopata kwa wakati au kwa uchache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Serikali isikilize kwa makini na ilichukue jambo hili. Haiingii akilini, sisi Waheshimiwa Wabunge tunawakilisha vijiji takribani vijiji elfu kumi na mbili mia nane na kitu, ndio tunawakilisha hivyo vijiji; na ndio ambao tunajua changamoto zilizoko katika maeneo yetu ya jimbo na vijiji vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi kule wanapenda sana na watafurahi sana kama watapata maji, katika mikutano yetu hakuna mkutano ambako utakwenda usipewe kero ya maji; akina mma hadi wanalia, na inatia uchungu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, malengo ya 2020 kwa vijijini ni kwamba tufike asilimia 85, ni jambo ambalo tumebakisha miezi tisa ya utekelezaji, hatuwezi kufika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niungane na Waheshimiwa Wabunge wote na Kamati kwa ujumla; kwamba kuongeza fedha ambayo itakuwa ring fenced iingie kwenye Mfuko wa Maji ili kutunisha na tuwe na fedha ya uhakika ya kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo ya maji; aidha kwenye mafuta au kwenye mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano uchukue asilimia kati ya 2 mpaka 5 anapo-recharge kwenye aidha MB za internet au kwenye muda wa maongezi tutapata fedha za kutosha, kilio kina wenyewe, hatuwezi kutegemea zaidi mikopo na misaada kutoka nje ya nchi, lazima tujikamue sisi wenyewe. kuna watu wanasema hapa kuongeza tozo hizi unaongeza mziko kwa wanachi. Hivi nyumba yako ikivuja jirani atakutengenezea? Lazima tufanye sisi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninaiomba Serikali, Juni 2016 tulihitimisha bajeti, lililalamikiwa sana, Juni, 2017 lilisemwa sana, Juni 2018 limesemwa sana. Hebu ifike mahali tulikubali, jinsi gani wananchi wetu wanavyoteseka, wanatoka saa tisa, saa kumi kuchota maji ya kwenye madimbwi; wanakoswakoswa kuliwa na fisi na simba; sisi ndio tunajua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Serikali ilichukue, kama kuonesha u-serious wa jambo hili, wananchi wanavyoumia na sisi ndio tunaowawakilisha, ndio tunawasikiliza, kama kuna namna ya kuonesha kwamba liko serious kweli kweli; kama ukisema kutembea uchi humu ndani niko tayari kutembea uchi kuonesha kwamba liko serious; I am ready. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Abraham aliambiwa atoe sadaka akamtoa mwanaye isaka baadaye akaambiwa chinja kondoo huyu hapa. Kama kuna namna yoyote ya kutoa sadaka ili kuonesha kwamba jambo hili lina umuhimu sana mtuambie tufanye; lakini tunaomba Serikali, tozo hii ni ya umuhimu kuliko jambo lolote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijijini tunachukua asilimia 65 ya wananchi walioko vijijini, watu takriban milioni 25, Mheshimiwa Waziri umeandika kwenye hotuba yako, lakini ndio watu wanaoongoza kwa kuteseka kupata maji safi na salama. Mfano mzuri Halmashauri ya Nsimbo, as I speak now 41 percent ndio wanaopata maji safi na salama, 41 percent. Bilioni 351 asilimia 51 tunaisoma kwa sababu tuliikopa kwa wakandarasi kufanya certificates zikawa Wizarani, ndizo zimelipwa, hiki ndicho kilichofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio kwamba tumepeleka pesa, utaratibu kwa ajili ya kudhibiti (control) na ndugu yangu Mheshimiwa Musukuma alichangia kwamba tukiongeza fedha ndiyo upigaji unaongezeka, no! Serikali imebadilisha utaratibu, una-design mradi unaleta wizarani wana-approve unarudisha, unatangaza ndio unapata mkandarasi anafanya. Sasa hivi mmesema kwamba akifanya kazi work execution ya 30 percent ndiyo u-raise certificate, fedha inapigwa wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya RAS lazima ikakague ndiyo certificate ije wizarani na wizarani wanarudi maeneo mengine wanaenda wanakagua ndiyo wana-release fedha kwenda kwenye halmashauri. Sasa upigaji, sawa upigaji unaweza ukawepo hao ni binadamu lakini not to that extent kama ilivyokuwa kule nyuma. Niombe sana maji ni uhai na maji ni siasa, let us do everything lakini kwenye maji please the government accept this fifty or other charges. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la usanifu wa miradi; tu-improve kwenye usanifu wa miradi. kuna mahali mtu ana- design mradi tumeshakutana kwenye Kamati ya LAAC, mradi umeenda kwenye mlima halafu tena tuna-raise up maji yakishindwa kwenda ni hoja. Mkandarasi anajenga according to the line na wengine wanapendekeza force account kwenye miradi ya maji, naomba niseme not everything unaweza kufanya kwa force account. Tumefanya kwa vituo vya afya lakini technicalities nyingine kwenye maji huwezi ukatumia force account; mambo ya reversion, pressure na nini, utaokota tu mtu barabarani aje ajenge kama kwenye nyumba, haiewezekani, hatuwezi kufanya kitu kwa force account. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuna ahadi ya Serikali kwenye Jimbo la Nsimbo, alivyokuja Waziri Mkuu katika Mkoa wa Katavi, Serikali iliahidi kutoa maji Kolongo kuleta Katumba lakini pia maji Kolongo yapo Nsimbo yanalisha manispaa hatunywi hata tone. Kata ya Mtapenda iliahidiwa maji, naambiwa kwenye kanadarasi iliyopo sasa hivi haipo, kwa nini. wananchi wamesema hawataruhusu maji kupita Mtapenda kwenda Ilembo. Kwa hiyo, naomba wizara muhakikishe Kata ya Mtapenda inakuwepo na tenki la zamani lipo na ni kilometa nne tu na ndiyo njia hiyo hiyo. maji hayatapita Mtapenda ya Ikolongo kwenda sehemu yoyote lazima Mtapenda wanywe maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la wataalam; hii ni changamoto na Waziri amesema lakini tuombe muendelee kuwajengea uwezo na tukisema mtaalam huyu ana-dilly-dully na nishukuru tu tumeanzisha RUWASA, tumeondoa ukiritimba kidogo kwenye manunuzi. Nimewahi kuingilia manunuzi kwenye halmashauri yangu, Mkurugenzi akawa na wasiwasi na nini na nini, tukasema what’s for? Tumevunja mkataba wa kwanza na huu, watu wanatumia hela zao certificate mpaka wizarani ndio watu walipwe, tuwe na mkandarasi ambaye yupo committed kwa hiyo ndio kidogo ikaenda. Kwa hiyo, ukiritimba huu naipongeza sasa Serikali kuanzisha RUWASA kwa hiyo, tunatumainia sasa kasi tunayoisifu kwenye TARURA, sasa ndio itaenda kwenye RUWASA, natumainia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, RUWASA ili iweze kufanya kazi kama tunavyosifu TANROAD na TARURA, lazima wawe na cash flow ya kutosha kwa hiyo naomba mruhusu sana hii tozo ya 50 kwenye mafuta au twende kwenye mawasiliano. Hilo ndilo ambalo tutaliunga mkono na tutakubaliana wote kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukubwa wa bajeti sio tija, tija ni utoaji wa…

MWENYEKITI: Malizia!

MHE. RICHARD P. MBOGO: tija ni utoaji wa fedha. Bajeti ya wizara hata ikiwa bilioni 450 lakini 100 percent zinapatikana, tunatekeleza miradi ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niombe mamlaka zote ambazo zinakusanya fedha vizuri, ziondoke kwenye huu mgao, mgao tupewe halmashauri za vijijini ambazo hatuna mamlaka na hatukusanyi fedha. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, asante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza nianze kumpongeza Waziri wa hii Wizara, Mheshimiwa Hasunga na Manaibu wako, Omary na Innocent na Watendaji wote katika Wizara hii ya Kilimo kwa kazi ambazo mnazifanya ili kuweza kuwanyanyua Watanzania ambao ndio wengi wako kwenye ajira hiyo kwa asilimia 65 kama ulivyoweza kueleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mchango wangu nianze kujielekeza kwenye zao la tumbaku pamoja na mazao mengine ya biashara. Kama wachangiaji wengine ambavyo wameweza kusema, kwenye tumbaku. uzalishaji unaenda unashushwa na wanunuzi, mpaka sasa imefikia tani 50,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi kushusha huku kunatokana na soko ambalo wenyewe ndiyo wanalijua, lakini linaathiri sana wakulima wetu, ambao wameshaingia katika hiki Kilimo, lakini sambamba na ushushaji wa uzalishaji; hivi karibuni nilikuwa na swali la msingi tarehe 30 Aprili, kuhusiana na tozo kwa hawa wanunuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka juzi 2017 tulifanya mabadiliko ya sheria tulikuwa na Amendment of the Local Government Finance Act, (Cap 290) tuliweza kushusha produce cess kutoka asilimia tano mpaka tatu. Kwa kiwango hicho ambacho tulishusha maana yake ni nini? Tulitoa discount ya asilimia 40; na hii imepelekea kushusha mapato kwenye halmashauri zetu kwa sababu hii ni produce cess iko kwa buyer. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kushuka huko kwa mapato imesababisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zetu umekuwa ni hafifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niiombe Serikali, mlisema kwamba mtafanya utafiti, haihitaji tuangalie utafiti, sisi tumeshafanya. Kwanza discount tu ya asimilia 40 hata kama uzalishaji uko pale pale, tayari mapato yameshuka, kwa hiyo tumeathirika na vitu viwili.

Mheshimimiwa Mwenyekiti, lakini pia, bado makampuni yanayonunua tumbaku katika Mkoa wa Katavi, tukienda Mbeya, Chunya pamoja na Ruvuma Kampuni ya Premium imegoma kulipa tozo hizi kwa sababu wanaidai Serikali kwenye marejesho ya VAT refund (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na tangu mwaka jana tumekuwa tukifatilia, sasa tuombe Serikali ije na tamko ni lini, Kampuni hii italipwa, na uhakiki tunajua kufanyika ni rahisi, ili halmashauri zetu na vyama vya msingi viweze kulipwa, maana haya tuna payables na receivables sasa na wao kwa kweli wamesimamia mahali ambapo wako sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusiana na masoko ya mazao ya wakulima, mazao ya chakula na mazao ya biashara. Mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, Mbeya mpaka Ruvuma tumekuwa tunazalisha sana mazao na hususan mahindi. Kuna vikwazo vilitokea, hasa kwenye ufungaji wa mipaka; na takwimu hapa wameonesha kwamba tuna ziada, na mkulima ambaye anahangaika ananunua Mbolea, analima hatimaye anahitaji apate bei nzuri ambayo atakuwa na fedha, na aweze kukidhi mahitaji yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iweke wazi mipaka watu waweze kuuza; na kama ilivyoelezwa na Waheshimiwa Wabunge wengine, kwamba kuna sehemu nyingi na hususan kwenye nchi jirani ya Congo DRC. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la uzalishaji wa tija. Serikali ije ituambie, kwa nini tuna uagizaji mkubwa wa malighafi za viwanda kwenye mafuta na ngano? Kwa nini tunaingia ngano asilimia 95 na tano, ndiyo ambayo inanunuliwa hapa Tanzania? Kwa nini iko hivyo na tunavuka kwenda wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la utafiti. TARI iwezeshwe ili waweze kufanya utafiti; kama ni mbegu tuwe na mbegu zilizo bora, na mazao. Kwa mfano mahindi mengine sasa hivi ukishavuna baada ya mwezi mmoja tu yanaanza kubunguliwa. Sasa hebu twende na utafiti wa kutumia hizi taasisi zetu ambazo zipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni kuhusiana na kilimo cha mara mbili katika mwaka, yaani cha umwagiliaji. Tuna miradi, kwa mfano Kata yangu ya Ugala katika Jimbo la Nsimbo, kuna mradi wa umwagiliaji mpaka sasa hauna ufanisi. Serikali mpitie upya tuone nini kifanyike ili wananchi waweze kufaidika.

Vilevile kutokana na mazingira; hivi tukichimba visima na ambavyo tuka-reserve maji haiwezekani kutumia katika umwagiliaji? Kama nchi ya Israel wana ile drop irrigation na sisi tuna maji ya visima hakuna uwezekano ili tuondokane na kugombana na Mheshimiwa January Makamba kuhusu uharibifu wa mito? Tuwe na option nyingine ya pili kwa maeneo machache, likiwa kama ni pilot study. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Suala la Financing. Tanzania Agriculture Development Bank ipanue ku-finance na kukopesha watu. Masuala ya vikundi hayana tija; kuna msuguano watu katika kuungana. Sasa waone namna gani ya ku-finance mtu mmoja mmoja na in a long term na katika interest ambayo itakuwa iko ndogo. Maana tukiwezesha tukawa na commercial farming, maana yake tutazalisha kwa tija na tutakuwa na ziada ambayo tutaweza kuuza katika nchi hata Kenya. Kenya wanachukua mahindi Tanzania, wanauza South Sudan, kwa nini sisi tusiuze moja kwa moja?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tukiongeza uzalishaji katika nchi yetu, tutaweza kuongeza na kunyanyua uchumi. Tunaona GDP kwenye Kilimo ina 90 percent kwa data za 2013 lakini kwenye Pato la Taifa tuna 28.7 percent. Kwa hiyo kilimo kwa ardhi tuliyonayo itaenda kuongeza sana. Pia uje utuambie mradi ule wa Mkulazi – Morogoro umefikia wapi? Isiwe kwa suala la uzalishaji wa mazao yanayotokana sukari, yaani miwa, pia mazao mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni suala la...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa. (Makofi)

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza namshukuru Mungu. Pia napenda niwapongeze Wenyeviti wote wa Kamati ya Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, kwa mawasilisho mazuri ambayo yanaenda kusaidia utendaji kazi wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba niipongeze Serikali kwa ujumla nikianza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Watendaji wote kwa namna ambavyo juhudi zao zimeleta mabadiliko katika mashirika haya ya Umma ambayo yako chini ya TR. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba niipongeze Kamati ya PIC, imekuwa na ushirikiano mkubwa sana, wanakamati wana ari na mori wa kufanya kazi na ushauri wao wametoa mzuri sana, wa kujituma katika kufanya kazi ya Kibunge kama ambavyo tumeagizwa na wananchi. Kwa uchache pia, naomba nimpongeze Athumani Mbuttuka na wasaidizi wake wote kwa kazi nzuri na kuchukua maoni ambayo Wabunge tunayatoa na wanayafanyia kazi. Tumeona mwaka jana 2019 wametoa ripoti nzuri sana ambayo itakuwa ni msaada kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na suala la uwekezaji kiujumla. Uwekezaji tunapata mapato ambayo hayatokani na kodi. Nami pia naungana na Waheshimiwa Wabunge kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuchukua hatua na kuweza kuanzisha Kampuni ya Twiga Mineral Company ambayo ni muunganiko wa Barrick na sisi na tunahisa 16% ambazo haziwezi kupunguzwa and diluted. Kwenye economic benefit ni 50 kwa 50. Hii ni hatua nzuri ambapo tutaongeza mapato yasiyotokana na kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wito, tumsaidie Mheshimiwa Rais kwenye almasi kama alivyosema na kwenye Tanzanite. Kwa hiyo, nako tuweze kupata faida zaidi na kuongeza mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kuzungumzia suala la gawio. Ili tuweze kupata gawio zuri na nchi iweze kufaidika na mapato ambayo hayatokani na kodi lazima tufanye vitu viwili; kwanza, tudhibiti matumizi na pili, tuongeze mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lilitunga Sheria ya Fedha Na. 16 ya mwaka 2015 ambapo inatakiwa gharama za uendeshaji zisizidi 60% lakini mashirika mengi yamekuwa yanazidi hii asilimia. Sasa tuombe TR pamoja na Serikali kwa ujumla kuendelea kusimamia ili kuweza kudhibiti mapato na mwisho wa siku itapatikana faida ambayo itakuwa inaongezeka kila mwaka na gawiwo litakuwa zuri kwa Serikali na kuongeza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa pili wa shilingi ni kuhusiana na mapato kiujumla kwenye kufanya biashara. Tutoe wito kwa mashirika yote kuwa wabunifu kwenye kuongeza aina za biashara ambazo zitaenda kuongeza mapato; na hii itapelekea faida pia kuweza kuongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala pia la ukusanyaji wa madeni. Kwenye ripoti na tumekuwa tukijadili kwenye Kamati kwmba taasisi nyingi hazikusanyi madeni ipasavyo. Tunajua kuna taratibu za kifedha ambazo deni likikaa muda mrefu inabidi uliripoti kwenye vitabu na matokeo yake linaenda kupunguza ile faida ambayo inaweza kupatikana. Kwa hiyo, tutoe wito kwa Watendaji wote wa Mashirika kuhakikisha kwamba wanakusanya madeni ili kuondoa hasara ambazo zitatokana na kutokukusanya madeni. (Makofi)

Pia kuna suala la kulipa madai mbalimbali na hasa ya kisheria kikodi. Kwa mfano, watu wamekatwa makato ya mifuko ya jamii kama NSSF lakini hayawasilishwi na ile inapelekea kisheria kuwa na penalty. Kwa hiyo, hili linatakiwa pia lizingatiwe kwa mashirika yetu ili kuondokana na hasara zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sera ya gawiwo, tuombe TR ahakikishe kwamba makampuni yote yanakuwa na sera ya gawiwo kwamba kwenye faida baada ya kodi ni kiasi gani kitaenda kwenye uwekezaji na kiasi gani kitaenda kugawiwa kama faida kwa ajili ya wanahisa wote kuweza kupata mgao wao tumeona baadhi ya mashirika hayana sera ya gawio matokeo yake kiasi gani kigawiwe maamuzi yanakuwa hayafanyiki na yanakuwa hayako consistency.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo Kamati yetu ilifanikiwa mwaka huu kukutana na kampuni ambazo tunahisa asilimia hamsini au chini ya hapo, kwa lugha nyingine tunaita minority. Hii imetia chachu kubwa sana kwa haya makampuni, tumeweza kutoa ushauri kwa sababu na sisi tuna hisa na wameweza kulisikiliza sana hili Bunge. Kwa hiyo tuombe kama kutakuwa na njia zaidi ya kuboresha na namna gani ya Bunge kuendelea kukutana na hizi kampuni ambazo tuna minority ziweze kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna suala la uwekezaji, kuna wakati sasa tunahitajika sisi wenye hisa tuwekeze zaidi kwenye hizi kampuni za minority. Kwa hiyo, mahali ambapo panaonekana kwamba panatija Serikali isisite kufanya vetting ya uhakika na kufanya uwekezaji ambapo mwisho wa siku tutakuwa na faida inayotokana na huo uwekezaji, return on investment. Kwa mfano, tulitembelea Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, tumeona kwamba kikiongezeka uzalishaji utaongezeka, zaidi ya tani milioni moja na laki tano zitakuwa zinazalishwa na faida nyingine wakulima wetu wadogo wadogo wataenda pia na wenyewe kuongeza vipato kutokana na ongezeko. Sasa hivi wanatoa tani kama laki sita na sitini, kwa hiyo, uzalishaji ukiongezeka wataenda kutoa tani zaidi ya milioni moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iangalie na kuharakisha mazoezi yote ya ufuatiliaji, mahali ambapo panahitajika kutoa mtaji, basi wahakiki na watoe mtaji kwa wakati maana mwisho wa siku tunakuwa na gawio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni utekelezaji wa maagizo tuliyotoa mwaka jana, mojawapo ili kurahisisha Ofisi ya TR ni kwenda kwenye TEHAMA ambayo itamrahisishia kwenye kufuatilia mashirika na haya makampuni na tulishauri mwaka jana kwamba waingie kwenye mfumo, lakini kwenye ripoti ya TR, bado wako kwenye mazungumzo. Kwa hiyo tungeomba suala hili liharakishwe ili ufuatiliaji wa haya mashirika zaidi na makampuni zaidi ya 260 uwe unakuwa kwenye finger tips, kwa mfano tumeona makampuni mengi yako duniani lakini wanadhibiti dunia nzima kwa kupitia mifumo hii ya TEHAMA. Kwa hiyo, kwa upande huo itasaidia Ofisi ya TR na pia ikama iweze kuongezwa ili tija iweze kuongezeka kwenye hii Ofisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia pia niombe tuzingatie sana hii Sheria ya Public Corporation Acts ya1993 ambayo ina mazingatio muhimu katika kudhibiti matumizi mbalimbali ndani ya Ofisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa hii nafasi na nashukuru Mungu ametuwezesha tuko salama mpaka muda huu. Kwanza nianze kupongeza watendaji ndani ya hii Wizara wakiongozwa na Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangwala, pamoja na Naibu wake Mheshimiwa Constantine Kanyasu; na nipongeze watendaji wote na taasisi zilizoko chini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni leo tu Mkurugenzi wa TFS ametatua kero ambayo iko kwenye Jimbo langu naomba nimpongeze sana Professor Dos Santos Silayo kwa kuitikia kilio hicho kwa haraka, na kazi ambazo unazifanya ndani ya ndani ya muda huu uko kwenye hii taasisi unaleta mambo mazuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuchangia kuhusiana na Hifadhi ya msitu wa Msaginia wenye ramani JB 215 ulotokana na GN 447 ya tarehe 24 Disemba, 1954, maana yake ni kabla ya Uhuru wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna changamoto katika msitu huu kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza katika mawasilisho ambayo tumewasilisha kwenye ile kamati ambayo iliundwa na Mheshimiwa Rais; na nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kusikiliza kilio cha sisi Wabunge na wananchi kuhusiana na maeneo haya na kuunda kamati hii ambayo inamshauri namna ya utatuzi; kuna vijiji ambavyo vilipimwa ndani ya msitu huu, kijiji cha Igongwe na Matandarani, na ramani namba 48870 ilitoka. Vilevile katika ramani hii ya msitu wa Msaginia kuna vijiji ambavyo kwenye ramani vimekatwa lakini GN hii 447 bado haijabadilishwa, na vijiji hivi kisheria bado vinasoma viko ndani ya hifadhi. Vijiji hivyo ni Msaginya, Mwenge, Songambele, Mtakuja, Kapalala, Magamba, Makongoro, Isanjandugu pamoja na kijiji cha Namba moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika Msitu huu wa Msaginia nikienda sambamba na Hifadhi ya Wanyama ya Katavi, chini ya hifadhi hiyo, inapakana na Kijiji cha Stalike; sasa kuna eneo la Kitongoji cha Stubwike ambapo kuna sehemu Serikali iliwatoa wananchi kwasababu mbalimbali tu za kiusalama dhidi ya wanyama wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maombi Yangu. niombe sasa Serikali tuone namna ya kubadilishana sehemu ya kitongoji cha Stubwike na hifadhi ya msitu ambao uko chini ya TFS. Yaani Stubwike tuwamegee Katavi National Park, lakini kwa ukubwa huo hata mkitoa na bonus mmege sehemu ya msitu wa TFS ili sasa mwingiliano kati ya wananchi na Katavi National Park tuupunguze, na mpaka itakuwa ni barabara ambayo inayoelekea Mpimbwe kwenye Jimbo la Kavuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kwenye Msitu wa North East Mpanda. Msitu wa North East Mpanda tulivyokaribisha wakimbizi kutoka nchi ya Burundi mwaka 1972, tuliweka makazi pale ya wakimbizi, ambayo ni ya Katumba. Niiombe Serikali iendelee kushughulikia eneo hili kwasababu ni ndani ya hifadhi ya msitu uolimegwa. Wananchi wanaishi mule kwa miaka hii mingi zaidi ya miaka 40, na shughuli na ujenzi na sasa TAMISEMI imeingia, tunaboresha miundombinu tunapeleka umeme na tunapeleka maji. Niiombe Serikali, muone namna bora ya kutatua jambo hili kwa haraka. Kama tuwe na mpango wa matumizi bora ya ardhi na kupima mipango mji basi lifanyike kwa haraka ili tuondoe hali ya sintofahamu kwasababu wananchi hawa wamekuwa sasa hawawezi kufanya maendeleo kwasababu bado mamlaka ziko zinasimamia maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo ndani ya makazi hayo hayo kwa ufadhili ya UNHCR ilijengwa shule ya msingi ambapo ina vyumba vya madarasa sita nzuri kabisa matundu ya vyoo na nyumba za walimu ziko mbili. Thamani yake ni si chini ya milioni 150. Sasa niombe Wizara tumesha iachia ile shule baada ya kufanyika ile eviction; lakini hebu tuombe muichukue ndiyo iwe moja ya makambi ya mafunzo ya vijana wenu, kwa aidha mtupe fedha au mtujengee shule kama hiyo hiyo katika maeneo ambayo tunauhitaji wa vyumba vya madarasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika msitu huo wa North East Mpanda tunaomba Serikali tunaomba Serikali ingalie namna gani huenda kwenye msitu North East Mpanda au Msitu wa Msaginia kuna maeneo ambayo yamekuwa na uvamizi wa miaka mingi. Wananchi wanalima pembezoni mwa Msitu huu wa Msaginia na eviction zilifanyika na niseme kwa bahati mbaya ilitokea tarehe 24 Disemba, mwaka jana kuna wananchi watano walijeruhiwa baada ya kuonesha kuwa walitaka kupambana na askari wa Usu na wakafyatua risasi ziliwajeruhi watu watano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili kuondoa adha hii ya wananchi wetu kuumizwa kutokana na uvamizi hebu tuombe sehemu ya Msitu wa Msaginia kwa kipande cha kutoka Sitalike mpaka unakuja Maili Kumi watumegee maeneo ambayo tayari sasa hivi yanalimwa zaidi ya miaka 20, katika mpango huu ambao Rais anauruhusu ili wananchi hawa wapate maeneo ya kulima. Maana kwa upande mwingine kwa mfano Kijiji cha Mtisi katika Kata ya Sitalike ni shughuli za madini ambazo maeneo yale huweze kufanya shughuli za kilimo kutokana na ardhi ilivyo. Kwa hiyo tuombe sana Serikali tuondoe mgogoro huo wa wananchi basi kwa kumega hiyo sehemu wapate sehemu za kulima, itatusaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo katika mpaka wa Kijiji cha Sitalike na hifadhi ya Katavi National Park kuna Mto wa Katuma. Sasa niombe serikali hebu tumege sehemu ya mto hata kama kilometa moja tuwape wananchi kwa ajili ya uvuvi wa samaki aina ya kambare. Hii itakuwa ni moja ya ujirani mwema ambayo inawasaidia sana wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie juu ya suala utalii, tumeona Serikali inafanya juhudi kubwa sana, watalii wanatoka 1.3 milioni mpaka 1.5. Sasa tuiamshe mbuga yetu ya Katavi tuna uwanja mzuri wa ndege wanaleta watalii kutoka nchi mbalimbali basi wapate wadau wa kuboresha, kujenga hoteli na mbuga yetu ni nzuri wanyama very natural na tembo wakubwa katika nchi hii wanatoka Katavi na kuna yule twiga chotara ambaye tupo kwenye Mbunga ya Katavi. Hebu tuletewe watalii ili tukuze uchumi na vijana wetu wapate ajira za kubeba na kuongoza watalii katika Mkoa wetu wa Katavi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho lakini si dogo, niombe sasa kwa Wizara hii pia halmashauri zetu zinahitaji kuongeza mapato ya ndani basi tuone kwa Sheria ya Misitu ya mwaka 2002, watumegee sehemu kwa ajili ya kuweka malisho na tuweke block za malisho sehemu ya msitu kwa ajili ya halmashauri yetu kuongeza mapato ya ndani kwa kuweza kuweka wafugaji na kuweka sehemu za malisho. Kwa hiyo, wakitumegea na sheria inaruhusu, tuombe Waziri awasilishe kwa mujibu wa Sheria ya Misitu, 2002, Na.14, halmashauri yenyewe ipate sehemu ya msitu, hii ikiwa ni sehemu ya kuongeza mapato ya ndani tukizingatia kwamba vyanzo vingi sasa hivi vimeshuka vya kimapato kwenye halmashuri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, niseme tu napongeza Serikali, nampongeza Rais wetu kwa kusikiliza kilio na kuunda ile Kamati, nampongeza Mheshimiwa Dkt. Kigwangala, alifika Stubuiko yote, Makutanio alitembelea na pia Mheshimiwa Kanyasu ameenda amefunga mafunzo, ameona jinsi gani Katavi ilivyo, sasa waende wakainyanyue na iweze kunyanyua mkoa wetu kiiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kupongeza Serikali, nipongeze Wizara na watendaji kiujumla na taasisi zote zilizoko chini ya Wizara hii ya Nishati kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya, na Waziri na Naibu wake wanazunguka sana katika Nchi yetu hii ya Tanzania kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi unaenda vyema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaenda kwenye hoja zangu za jimboni, naomba kidogo kuna masuala niweke sawa. Nianze na alipoishia kaka yangu, Mheshimiwa Simbachawene, kuhusiana na rafiki yangu Mheshimiwa Silinde; katika mchango wake amezungumzia gharama za umeme hususan kwenye gesi pamoja na matumizi ya bomba, linatumika kwa asilimia 6 pamoja na gharama za kutanua Mradi wa Kinyerezi.

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba Bunge litambue kwamba kuna wengine wanajua bomba lililopo ni moja tu ambalo linasafirisha gesi kutoka Mtwara, hapana, yapo mabomba mawili. Kwanza tuna bomba dogo na Serikali iliona kwamba hili bomba ni dogo ndiyo maana tulivyokuja kuongeza bomba lingine ikawa ni kwamba limetengenezwa bomba kubwa ili kuweza kuchukua ujazo mkubwa kutokana na ambavyo uwekezaji utakuwa unafanyika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kutumika kwa asilimia sita tuna-save future investment kama tungekuwa labda tayari tuna bomba lingine ambalo ni dogo. Na pindi kwamba uzalishaji na visima vingine vya gesi vitaongezwa basi tayari tutakuwa na means ambayo ipo inayotosheleza kusafirisha hiyo gesi.

Mheshimiwa Spika, na uwekezaji ambao unafanyika wa kuongeza hapo Kinyerezi hizo bilioni 60 ambazo amezisema ikiwa ni moja wapo ni kuendana na Sera ya Nishati katika kuwa na energy mix kama ambavyo wengine wameweza kuchangia. Na kimsingi, masuala ya ku-quantify investment cost, kwamba unalinganisha mpaka zinafika trilioni sita, ni masuala ya kitaalam na wataalam wamekwishakaa wakaangalia kwamba uwekezaji wa kwenye Rufiji Hydropower wa more than six trillion ni kwamba utakuwa na manufaa kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, na manufaa hayo, kwanza umeme wa maji ndiyo umeme ambao ni wa gharama nafuu sana duniani kote. Uniti moja gharama yake ni shilingi 36 wakati umeme unaotokana na gesi ni shilingi 547. Angalia tofauti ya zaidi ya shilingi 500 kama na 11...

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

MHE. RICHARD P. MBOGO: …sasa kama tuna-save…

SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Mbogo; Mheshimiwa Silinde.

T A A R I F A

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, nataka nimpe taarifa kutokana na kwamba anakwenda kwenye ule mchango ambao nilichangia. Na wakati nachangia nilisema tunachotaka sisi ni kufikiri kibiashara, na mantiki yangu ni nini; nilikuwa nachukua kwamba think beyond the box, kwamba ukichukua 1.4 trillion ukaenda uka-expand Kinyerezi leo hii ndani ya miezi sita utapata megawati 4,440, ndani ya miezi sita. Hii 1.4 trillion haileti ile megawati 2,000 leo wala kesho.

Mheshimiwa Spika, sasa nikasema leo ukipata six trillion ukaingiza ukafanya expansion utapata megawati 18,500 ambazo umeme wake tutazalisha nchi mbalimbali, tukiuza kule nikasema ndiyo tunakwenda kuweza kwenye Stiegler’s Gorge. Sasa hii ni sawa na mtu ana nyumba pagala halafu ana kiwanja amepata milioni 10 anafukuzwa na mwenye nyumba, unaambiwa sasa nenda kamalizie pagala lako…

SPIKA: Ahsante, dakika yako imeisha.

MHE. DAVID E. SILINDE: …haya, ahsante, ameelewa lakini.

SPIKA: Utazipata hizo kwa gesi ipi wakati inayokuja ni 6% only? Endelea Mheshimiwa Mbogo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, ninaomba ulinde muda wangu. Nafikiri akafanye cost benefit analysis tena kuangalia uwekezaji kwenye Hydropower kwa miaka ijayo na lifespan ya gesi ni by 2047 inakuwa haipo.

Mheshimiwa Spika, suala la kutumia umeme wa maji pia ni suala la msingi kwa uchumi wa nchi yetu. Hii Rufiji Hydropower itakuwa na faida mojawapo, itapunguza gharama, kwa hiyo Watanzania zaidi ya milioni 50 watafaidika na unafuu wa gharama kwa sababu watatumia umeme ambao una bei nafuu. Production cost kwenye viwanda zitapungua upande wa utility kwa sababu umeme utakuwa una bei nafuu. Kwa hiyo, ile economic benefit itakuwa kwenye sekta karibu zote, mpaka kwenye kilimo, kwenye sekta zote economic benefit ya umeme wa bei nafuu itakuwepo.

Mheshimiwa Spika, jana wakati inawasilishwa hii taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani, walizungumzia kwamba ujenzi wa hii Rufiji Hydropower, kwamba utaongezeka kwa asilimia 30 na msemaji akasema itafikia bilioni 9 US Dollars, takribani trilioni 22. Lakini ukichukua kimahesabu ongezeko la asilimia 30 toka kwenye bilioni 3.7 unafika bilioni 4.8 – sijui hesabu zake alizifanyaje – na tunajua katika ujenzi siku zote variation huwa zinakuwa ni ndogo sana. Kwa hiyo, nafikiri sentensi zingine za gharama zinakuwa zinapotosha Umma, kwamba huu mradi utakuwa ni wa gharama sana. Ingekuwa ni vyema sasa na Waziri uje uwaeleze vizuri gharama za mradi zitakuaje.

Mheshimiwa Spika, ilizungumziwa kuhusu matumizi ya fedha nje ya ukomo wa bajeti. Naomba niwakumbushe; Sheria ya Bajeti kuna kifungu kinaruhusu kutumia nje ya ukomo ambao tumeidhinisha na taarifa inaletwa Bungeni. Na tena kuna asilimia, ikiwa inafika asilimia 9 ndiyo iko chini ya idhini ya Waziri.

Mheshimiwa Spika, pia katika ile taarifa waliitisha mikataba kwamba iletwe Bungeni, lakini naomba nikumbushe; uliunda Kamati Maalum ya kwako ya kuchunguza Serikali itafaidika vipi na gesi asilia na ilitoa mapendekezo, mojawapo pia ni kupitia mikataba yote. Kwa hiyo, kazi uliifanya kabla hata wao wanaokuja sasa kuiagiza Serikali kwamba ifanye.

Mheshimiwa Spika, niseme tu Sheria ya Uchimbaji Gesi, gharama ya gesi ni kubwa sana na Serikali tumejitoa kwenye ile gharama. Kwa sababu ukichimba na usipopata inakuwa ni hasara kwa aliyechimba, na nakumbuka katika hili Bunge lako Tukufu, Mheshimiwa Zitto Kabwe aliwahi kuisifu sana Serikali kwa kuweka utaratibu huu katika Sheria ya Uchimbaji wa Gesi. Kwa hiyo, niombe tu kwamba Serikali inafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Spika, na kuhusiana na mazingira, kwamba Stiegler’s inakwenda kuharibu mazingira yote; hapana. Angalia, tumejenga miundombinu mingi katika nchi yetu; barabara, reli, tulikata miti. Wangetoa ushauri kwamba hebu tutengeneze uoto maeneo mengine kama hii Dodoma pamoja na Singida.

Mheshimiwa Spika, la mwisho, niombe sasa Serikali kwenye suala la mafuta tuangalie namna gani Kampuni ile ya TIPER jinsi gani ambavyo sasa itakwenda kuhusishwa katika kutunza mafuta ili tu-control kodi inayotokana na mafuta na tuweze ku-control uhitaji wa mafuta katika nchi yetu. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa Mwaka 2016
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata nafasi hii. Kwanza, nimpongeze Waziri na Naibu wake na kwa msaada wa Mwanasheria Mkuu kuweza kuuleta muswada huu tuweze kuujadili.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo lingekuwa ni maoni katika hii miswada ambayo tunapatiwa ni suala zima la tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, wakati mwingine kunatufanya Wabunge kidogo tuweze kuelewa tofauti. Kwa mfano, unakuta Kiingereza kinasema kwamba Mkemia Mkuu anateuliwa na Rais lakini ukienda kwenye Kiswahili imetafsiriwa kwamba Mkemia Mkuu atateuliwa na Waziri. Sasa inakuwa inatupotosha kwenye upande wa Kiswahili na sisi wengine siyo wengi tunaojua lugha hii ya Kiingereza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala zima la huu muswada, muswada uko vizuri, nampongeza Mheshimiwa Waziri na timu yake kwa kuweza kupokea maoni ya Kamati lakini na sisi Wabunge tuna maoni kidogo ambayo tungeomba yaingie na tutaweza kuleta Jedwali la Mabadiliko.
Sehemu ya kwanza ni kifungu cha 5(2)(a) katika dawa zilizotajwa pale upande wa kemikali zimetajwa tu za viwandani lakini kiujumla kwenye huu muswada tuna kemikali za viwandani na za majumbani. Sasa labda Waziri atatuambia ilikuwa ni kosa la kusahaulika au kiutaalamu kwenye kifungu hiki cha 5(2)(a) kwamba kemikali za majumbani hazitakiwi kutajwa. Hiyo tutaileta kwenye schedule of amendment.
Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu kingine ni kwenye sifa za Mkemia Mkuu. Kifungu 10(1) kinasema kwamba Mkemia Mkuu atateuliwa na Mheshimiwa Rais. Sasa kwenye sifa pale kuna uzoefu na masuala ya elimu, lakini kuna kitu kimoja ambacho kimesahaulika. Leo hapa tuna miswada miwili, wa Maabara na Wataalam (Chemist Professional Act). Sifa mojawapo ya Mkemia Mkuu ambaye atateuliwa na Rais awe ni yule ambaye amesajiliwa katika Baraza letu la Wataalam wa Mambo ya Kemia, hilo nalo ni muhimu sana. Kuna watu ndiyo wamesoma, wana elimu nzuri lakini unakuta kwamba hayuko professional, mtu ana miaka 20 na elimu yake. Hata wenye fani zingine za uhasibu kama sisi kama hujasajiliwa na Bodi ya Uhasibu wewe siyo mhasibu, ni karani.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kwenye uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi kimesema sifa awe ni mtu ambaye amefanya kazi kwenye taasisi za Serikali. Kwa mujibu wa michango ambayo imetolewa na Wabunge hapa tunahitaji tupate Mwenyekiti wa Bodi ambaye hatakuwa tu na uzoefu wa mambo ya utumishi lakini pia awe na utaalam wa mambo ya kemia ili awe ni mtu ambaye anasimamia vizuri hiki chombo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 7(2) katika ile Bodi nzima kuna mwakilishi anayetoka Wizara ya Afya. Ukiangalia katika ile Bodi nzima ina wataalam wa fani mbalimbali, kuna mtu anayetoa Hazina, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, kwenye vyuo lakini tungeomba kwa sababu hii taasisi ni nyeti na ni mambo ya kitaalam sana hayahitaji ubabaishaji basi mwakilishi anayetoka Wizara ya Afya awe angalau na uzoefu hata wa miaka mitatu na elimu yake iwe ya mambo ya kemia ili aungane na yule mwingne ambaye anatoka kwenye upande wa vyuo ambaye amesomea mambo ya kemia, pathology na baiolojia na vitu vingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine kwenye huu muswada, kifungu cha 13(1) tumeona kwamba katika teuzi za watu wa maabara Waziri anashauriwa na Mkemia Mkuu lakini ukienda kifungu cha 14 kwenye uteuzi wa wakaguzi Waziri anashauriwa na Bodi. Sasa ukienda kwenye hierarchy maana yake kifungu cha 13 pale Bodi inakuwa imerukwa, Waziri anashauriana moja kwa moja na Mkemia Mkuu kwa hiyo Bodi itakuwa haijui Mkemia Mkuu na Waziri wameshauriana nini. Kwa hiyo, tunahitaji kifungu cha 13(1) Waziri ashauriwe na Bodi. Kwa hiyo, hii nayo tutaileta kwenye schedule of amendment. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 15 cha wajibu wa hawa wakaguzi kwenye kuteketeza zile sampuli, pale inaonesha kwamba huyu mkaguzi aidha yeye au kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinaweza kuteketeza hizi sampuli ambazo zimetumika kwa mujibu wa hii sheria, lakini sasa ukiangalia hapa tunakuwa hatuna ule udhibiti (internal control). Kwa hiyo, tungeomba kwamba ashirikiane na isiwe ni mbadala.
Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu kingine ni cha 39 cha mambo ya mahesabu. Tunahitaji tuangalie kwamba baada ya mwaka wa fedha kuwe na miezi mitatu ya kuandaa ripoti halafu tena miezi mitatu inaongezeka kwa ajili ya ukaguzi, halafu ndiyo inaenda kwa Waziri na kwenye Bunge. Hapa kwenye hii Bill yetu tumeweka miezi mitatu ambapo mahesabu yanakuwa hayajafungwa. Kwa hiyo, lazima iwe miezi sita kwa Waziri kupewa na miezi mitatu wawe wamekamilisha kufunga mahesabu kama ilivyo kwenye Sheria ya Fedha. Pia director‟s report ni muhimu sana iwepo kwenye hii taarifa ili sasa aoneshe mwenendo mzima wa hii taasisi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye upande wa professionals na yenyewe inaendana na hii kwenye mahesabu hapa vipindi viko tofauti. Tutavileta kwenye schedule of amendment ili Bunge liweze kutuunga mkono ili tuendane na sheria zingine za mambo ya fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa yoye hayo, naomba kushukuru na naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, wa Mwaka 2016
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa hii nafasi, nitaenda haraka kidogo kwa sababu muda siyo rafiki sana. Kwanza niipongeze Serikali na Wizara husika kwa kuweza kuwasilisha huu Muswada, kwa sababu sasa hivi Serikali yetu mwelekeo ni kwenye nchi ya viwanda na tukiangalia nchi ya Tanzania imebarikiwa sana. Tuna Bahari, tuna Maziwa katika hii dunia tumebarikiwa mno. Kwa hiyo, hizi sheria kuja kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali inabidi tuziboreshe na ziweze kutumika ipasavyo kwa ajili ya kunyanyua uchumi na kutengeneza ajira katika nchi yetu ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Muswada huu kuna maoni maeneo mbalimbali ambayo nimeweza kuyaona, nikianzia na Muswada huu wa agriculture, kuna comment ilitoka kuhusiana na mambo ya mifugo. Ingekuwa ni bora iunganishwe iwe ni kilimo na mifugo ili na wenyewe tuweze kutengeneza ajira na kunyanyua uchumi, mifugo iweze kuchangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kifungu cha Nane uteuzi wa Mkurugenzi kinaeleza kwamba Rais atamteua baada ya kushauriwa na Waziri. Tumepitisha Miswada takribani minne, lakini ushauri kama huu nakumbuka hapa haukuungwa mkono suala la kushauriwa Rais kupitia Mawaziri wetu katika uteuzi. Kwa hiyo, itabidi tuwe na consistency tuweke kama katika Miswada mingine ambayo tumepitisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni Baraza la Taifa la Ushauri. Naona tuone jinsi gani ya kuhusisha pia na Bodi mbalimbali za Mazao wawe ni moja ya Wajumbe kwenye hili Baraza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 14 ni maeneo ya tafiti, lakini nilivyoangalia humu ndani kuna baadhi ya Mikoa ambayo imesahaulika kuwekewa kuwa ni sehemu pia ya Vituo vya Tafiti. Kwa mfano; mapendekezo ambayo nitayaleta Mkoa wa Njombe tuwe na Kituo cha Utafiti ili kiweze kukidhi Mkoa wa Iringa na Ruvuma; na pia Mkoa wa Katavi tuwe na Kituo cha Utafiti ili tuweze kukidhi Mikoa ya Katavi, Kigoma na Rukwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kifungu cha 16 kwamba tutakuwa tuna-commission baadhi ya kazi, sasa ni wakati gani ambapo tutaweza kuwajengea uwezo vijana ambao wamemaliza kwenye vyuo vyetu, kwa nini tusiwajiri na wafanye hizi kazi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tukienda Kifungu cha 18(2) kwamba Taasisi inaweza ikafanya biashara kwa kuuza, kununua hizi tafiti. Ningeshauri kwamba Waziri ajaribu kuangalia tusije tukauza utafiti ambao ukatoka na Tanzania isiweze kufaidika. Tukienda Kifungu cha 19, kuhusu utangazaji wa matokeo ya utafiti, tumeonesha tu kwamba tuna-review na kupitia kwa mtu ambaye ametutumia mali za Taasisi na kufanya utafiti, ili tuweze kuwa na tafiti zilizo bora, nitashauri Waziri aangalie hata wale ambao wanafanya tafiti kwa gharama zao wenyewe wawe wanakuwa reviewed na hii Taasisi ili tuwe na matokeo mazuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 20 kimenifurahisha kuhusu kufanya utafiti mpaka nje ya mipaka. Tunakumbuka Vietnam miaka ya 1970 walichukua zao la korosho lakini walichukua kwetu wamepeleka nchini kwao na ni moja ya nchi duniani ambazo zinatoa sana zao la korosho. Kifungu cha 20(3) kuna masuala ya watu ambao wameathirika kutokana na huu utafiti, tutaomba Waziri aziweke athari kwenye Kanuni ili ziweze kusaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 23, mtu anayeomba kusajiliwa kama Mtafiti au Taasisi yake anaweza akakataliwa, lakini hapa hakuna nafasi ya jinsi gani mtu anaweza akakata rufaa au akarekebisha makosa aliyoyafanya na kuweza kuomba tena, hilo nalo tutaomba Waziri aliangalie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala ya utafiti kufanywa na mtu wa nje lazima ashirikiane na wa ndani yaani Mtanzania kifungu cha 24, basi kwenye Kanuni ielezwe faida itakayopatikana, Mtanzania atakuwa na asilimia kiasi gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la adhabu, masuala ya adhabu kwa makosa mbalimbali hayana consistency, adhabu zake kidogo zimekuwa ni ndogo na suala ambalo limepigiwa kelele sana mtu anapofanya kwa nia njema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye upande wa research, upande wa Wavuvi, Kifungu cha 6(1)(c) kwamba utafiti na uchunguzi magonjwa ya samaki lakini kwenye maji hatuna samaki tu, tuna viumbe wengine pia wanaishi ndani ya maji sasa wenyewe kuhusu magonjwa yao utafiti hautafanyika? Kuna hadithi zile za nguva, tuna mamba, tuna viboko, tuna vyura na tuna nyoka wengine ambao wanaishi ndani ya maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Wavuvi kuna Kifungu cha 8(4) kidogo kinanitatiza hapa, Waziri anapewa Mamlaka ya kubadilisha kwa namna yoyote ile atakavyoona suala la Jedwali baada ya kuwa ametangaza. Sasa majedwali tunapitisha humu ndani Bungeni na hayo marekebisho Waziri akifanya atarudisha tena Bungeni? Kwa hiyo sioni haja ya kumpa Mamlaka haya Waziri kufanya mabadiliko kwenye majedwali wakati majedwali haya tumepitisha hapa ndani Bungeni maana yake akifanya marekebisho lazima alete tena huku. Kwa hiyo, ni bora tumwachie huru kwenye upande wa Kanuni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine upande wa Wavuvi ni uteuzi wa Naibu Mkurugenzi. Ametajwa lakini kazi zake hazijatajwa. Kwa hiyo, tutakuwa na mtu ambaye functionally atakuwa yupo kusubiri Mkurugenzi hayupo yeye ndiyo akaimu, hivyo sioni haja ya kuwa na Naibu Mkurugenzi katika hii sheria na nitaleta mapendekezo kwamba aondolewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la mtu ambaye hajakamilisha utafiti arudishe gharama, sasa je, akishindwa na hizo adhabu zimetajwa? Kwa hiyo basi, tuweke mazingira ya kwamba mtu awe na dhamana kwa pesa tunayompa ili akishindwa utafiti basi iwe ni moja ya kinga ya kumwezesha kurudisha pesa ambayo tuliweza kumpatia kufanya hiyo kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna suala la kuomba vibali katika kifungu cha 20, napendekeza taasisi yenyewe ndiyo itoe kibali na siyo mtu aende kwenye Tume ya Sayansi na Teknolojia, tutaweka ukiritimba kwenye utoaji wa vibali kwa watu wanaotaka kufanya utafiti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni dhana nzima ya watu ambao wamefanya vizuri, kuna suala la intellectual property inabidi tuliangalie kwa umakini zaidi ili watu wetu ambao Mungu amejaalia na wameweza kufanya utafiti waweze kufaidika na kile ambacho wamejaaliwa. Kifungu cha 31, masuala ya report, kinasema siyo chini ya miezi miwili, hii inatakiwa iwe miezi mitatu na kifungu cha 33 imeandikwa miezi mitatu kwenye report ambayo imekaguliwa iwe angalau miezi sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala mengine ni jedwali; tumetaja bahari, tumetaja vituo lakini tumesahau Ziwa la Rukwa ni moja ya Ziwa kubwa nalo liingie kwenye jedwali la kwanza kama moja ya vituo vya utafiti kwa sababu hata hivyo hivi karibuni tu Serikali ilisema kuna madini yamepatikana kule ambayo ni adimu. Mapendekezo mengine nitayaleta kwenye jedwali la marekebisho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, 2017
MHE. RICHARD P.P MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nimpongeze Mwanasheria Mkuu kwa kuwasilisha mabadiliko haya ya Sheria ya Bajeti pamoja na ya Ofisi yake. Naomba Wabunge kwanza tujiulize hizi taarifa ya utekelezaji ni kwa ajili ya nani, zina manufaa gani katika shughuli zetu za Kibunge. Unapopata taarifa yoyote, performance report unaangalia na aina ya taasisi ambayo inatoa hiyo ripoti.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia kwa upande wa Serikali, Serikali siyo kampuni inayofanya biashara, iko kwenye ushindani kwamba inahitaji ipate daily, weekly, monthly or quarterly reports kwa ajili ya kufanya maamuzi ili kuboresha biashara wasitoke katika ushindani, Serikali haiko hivyo. Serikali shughuli zake zimenyooka, zinaeleweka, vyanzo vya mapato haishindani na watu wengine. Kwa hiyo, kubadilisha hii Sheria kutoka miezi mitatu mpaka miezi sita kwa ajili ya kupata taarifa ya utekelezaji maamuzi waliyofanya ni sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia hizi ripoti zinatusaidia katika kufanya maamuzi ya mbeleni, katika kupanga mipango. Vyote vinatusaidia, pia katika kudhibiti. Hata hivyo, tunayo mikakati na Serikali inafanya kazi kila siku. Tuna Baraza la Mawaziri lina vikao vyake, tuna Baraza la Kazi lina vikao vyake, tuna Watendaji Makatibu Wakuu katika Idara, katika Wizara mbalimbali wana vikao vyao vya ufuatiliaji, kwa hiyo suala la kufuatilia utekelezaji upo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya Wabunge wamezungumzia kuhusu halmashauri kwamba Kamati ya Fedha na Mipango zinakaa kila baada ya miezi mitatu, lakini halmashauri zingine zinakaa kila mwezi zinapitia mapato na matumizi ya kila mwezi na kushauri nini kifanyike. Kwa hiyo, ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za Serikali upo kuanzia ngazi ya Serikali Kuu mpaka kwenye halmashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala limezungumzwa na wenzangu wa Upinzani kwamba kubadilisha hii sheria tunakwenda kupunguza mamlaka ya Bunge, hiyo sio sahihi. Tuko kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 63, tunaisimamia na kuishauri Serikali na tutaendelea hivyo hivyo. Kanuni zetu, kazi za Kamati kwa mujibu wa Katiba tutaendelea nazo kwenye vikao vyetu taasisi mbalimbali zitaendelea kuleta ripoti.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, ukifuata sheria mbalimbali ambazo tumepitisha kwa taasisi zilizopo, zinafunga mahesabu mwezi Juni, wanapewa miezi mitatu kuandaa hizo ripoti, kwa hiyo Septemba 30 wanawasilisha. Baada ya hapo zinakwenda kwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Serikali na yeye atapeleka kwa Waziri husika, Waziri husika ataleta kwenye Bunge kwa kupitia hizo Kamati; hizo sheria zingine hatujazigusa. Kwa hiyo, madaraka ya Bunge bado yapo pale pale tofauti na Kambi ya Upinzani wanavyosema.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kwamba tumeahidi kwenye mikutano fedha nyingi ndiyo maana tunabadilisha, hela tunapeleka kwenye ndege, sio sahihi. Tulichokiahidi ndicho ambacho tunaendelea kutekeleza na mkiangalia wakati kila Wizara ambayo imesoma bajeti yake hapa, ilieleza utekelezaji wa bajeti ya 2016/2017, mfano tu Wizara ya Nishati na Madini walitekeleza kwa asilimia 52 mpaka kufikia mwezi Machi. Sasa nini ambacho kimefanyika ni kwamba utekelezaji bado unaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kupata misaada na mikopo; nchi nyingi kupata misaada na mikopo ni pamoja na masharti ambayo unayatimiza na mkiangalia taarifa ya ripoti ya Wizara ya Fedha wakati bajeti inasomwa, tumepata mikopo mingi mwezi Juni na Mei na mpaka Juni hapo Waziri wa Fedha anasema tumepata mkopo wa dola milioni 500 kutoka india. Kwa hiyo, yote haya ni mambo ambayo yataingia kwenye taarifa ya utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa kubadilisha hii sio kwamba tunaenda kupunguza ufanisi, hatupunguzi, ufanisi utabaki pale pale na Bunge tutaendelea kusimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja imegusiwa kwamba muda ni mrefu. Suala la muda halina tija, suala ni kuangalia. Unaweza ukaletewa ripoti kila mwezi, lakini je mfumo uliopo unadhibiti watu kufanya kwa ufanisi? Kwa hiyo, unaweza ukapewa kila siku ripoti au baada ya miezi mitatu lakini je mfumo uliopo unadhibiti kufanya kazi kwa ufanisi, hilo nalo la kuangalia. Kwa hiyo, tusiangalie tu ripoti lazima tuangalie na mifumo na ndio maana sasa hivi mnasifia uongozi uliopo kwamba unafuatilia, nayo ni mambo ambayo mtaona kwamba yanasaidia kwenye utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia imeonekana hapa kama vile CAG anapunguziwa majukumu. Hakuna sheria
yoyote ambayo imebadilishwa hapa kwamba CAG ataenda kupunguziwa majukumu katika utekelezaji wake wa kazi za kila siku; CAG atabaki pale pale. Atakuwa anatekeleza na anaripoti kwenye Bunge na sehemu zote zinazohusika na wengi kama mchangiaji Hongoli alivyosema, tunapewa vitabu kibao na leo wengi tutaondoka na vitabu hapa…

TAARIFA...

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nasikitika kwamba kaka yangu Zuberi Kuchauka ananifahamu vizuri, sikutegemea atoe taarifa kama hiyo. Ni kwamba Wabunge wote tunafanya kazi kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 63(2) kuisimamia na kuishauri Serikali na majukumu mengine tunafanya kupitia Kamati. Kwa hiyo, taarifa yake sio sahihi, kilicho kizuri kwa Serikali tutapongeza na mahali ambapo wanakosea huwa vile vile tunashauri na tunakosoa na mimi ananielewa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie tu kwa kusema kwamba mabadiliko ya sheria hii sio mabaya kama wanavyodhani na kama wanavyofikiria. Suala kwamba CAG tulimpa bajeti ndogo sio sahihi, bajeti alipewa na Serikali iliahidi kwamba ataongezewa na aliongezewa na bajeti hii kama alivyoileta bilioni 12 za World Bank na zingine zimetoka Serikalini karibuni bilioni 60, kwa hiyo ana bilioni sabini na kitu. Kwa hiyo, bajeti ya CAG iko vizuri, kwa hiyo sio kwamba tume- impair independence yake kwa kufanya kwamba tunampa bajeti ndogo, hilo lazima walielewe kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia tu naomba niseme kwamba sio rahisi kupata taarifa kwa wakati kwa sababu taarifa zingine tunapata kutoka taasisi binafsi ambao hawatoi ushirikiano kwa Serikali. Kwa mfano, suala la takwimu, ukisema leo hii unaandaa pato la Taifa, unaandaa taarifa sio za Serikali tu, mpaka taasisi binafsi lazima upate takwimu zao na mauzo yao ili uweze kujua kwamba pato la Taifa likoje. Sasa watu wetu wa NBS (National Bureau of Statistics) wakifuatilia kwenye taasisi za binafsi wanapata shida kwenye kupata takwimu, watu hawafanyi declaration kwa hiyo ni jambo linalochukua muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, suala la kuomba miezi sita lipo sahihi na bado kimfumo wa kiteknolojia hatujaunganishwa vizuri; tuna EPICAR mfumo wa uhasibu, bado sehemu zingine haujakamilika, kuna Halmashauri mpya bado hazijakamilika. Kwa hiyo kiteknolojia bado, lakini Serikali bado inaendelea na jitihada. Kwa hiyo, lazima waelewe kwamba suala la miezi sita sio kwamba Serikali imekurupuka, imeangalia maeneo mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Ahsante sana kwa nafasi.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2017.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza naomba nimpongeze Waziri na timu yake kwa namna ambavyo wameweza kuleta mabadiliko ya sheria mbalimbali kutokana na maoni ya wadau pamoja na Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo ningependa kulisema ni kuhusu hizi tozo zilivyoshushwa na baadhi ya vyanzo vya mapato kutoka kwenye Halmashauri ambayo yatakusanywa na TRA. Naomba niwakumbushe Wabunge wenzangu kinachofanywa na Serikali siyo kwamba ni kwa nia mbaya, siyo kwamba ni kwa nia ya kisiasa. Halmashauri haziendeshwi kwa asilimia mia moja na mapato ya ndani. Kuna fedha zinazotoka za Mfuko wa Local Government Capital Development Grants, hizi mbona mnapokea halafu hamzilalamikii? Kwa hiyo, naomba mlizingatie.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la msingi ni kwamba, namwomba Mheshimiwa Waziri utoke tu waraka ambao utamwelekeza Katibu Tawala wa Mkoa kuhusiana na halmashauri zilete maombi na jinsi gani zilivyoathirika kutokana na haya mabadiliko.

Mheshimiwa Nabu Spika, mfano mzuri kwenye Halmashauri ya Nsimbo kutokana na mabadiliko ya hii sheria, tozo kutoka asilimia tano kwenda tatu upande wa tumbaku kwenye bajeti hii tulikuwa na milioni 440 kwa kupunguza hii itapungua kwa milioni 176. Wakati huo hiyo milioni 440 tulishaipangia kuongeza zahanati moja, kituo cha afya kimoja, kujenga sekondari na kuboresha miundombinu ya maji, kwa hiyo tunaenda kuathirika.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Waziri wa Fedha nafikiri wa-revise tupandishiwe zile Capital Development Grants ili tuweze kutimiza yale ambayo tulikuwa tumejiwekea kwenye bajeti, nitashukuru sana. Pia mazingira yanatofautiana kuhusu hii tani moja, tutaomba baada ya mwaka mmoja tukupe mrejesho kwamba kutokana na tani moja kushuka chini hakuna tozo, mazingira yanatofautina. Sisi tuna wale petty trader’s ambao mtu anabeba kwenye baiskeli, kwenye punda, kwa hiyo ndiyo wengi ambao walikuwa wanatupa vipato. Kwa hiyo, tutampa mrejesho Mheshimiwa Waziri baada ya mwaka mmoja tumeathirika kiasi gani, halafu wataangalia namna gani ya ku-revise. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwenye upande wa mbegu zinazozalishwa ndani, tunaomba tena waziangalie kwenye mabadiliko ya tozo na sheria mbalimbali za kodi ili na wao waweze kunyanyuka na wananchi ambao ni wakulima wengi waweze kupata mbegu kwa bei ambazo ni nafuu, kama sekta ya elimu ambavyo wameiona kwenye SDL, OSHA na mambo ya fire basi na uzalishaji wa mbegu nao waweze kuwaangalia. Pia kwenye mifugo na kwenye waweze kuangalia mambo ya chanjo na vifaa na dawa waweze kupunguziwa upande wa kodi na tozo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu machinga, rafiki yangu Mheshimiwa Haonga, nimemshangaa kuona anasema kwamba machinga wasilipe kodi. Nimpe tu taarifa akienda Kariakoo sasa hivi watu wa maduka pale ndani hawauzi, wanaouza pale nje ni Machinga ambao wamezagaa. Sasa tunasema na kila mtu anayepata kipato inatakiwa alipe kodi. Ndiyo maana Serikali imesema wanarasimisha watapewa na vitambulisho. Kwa mfano, yeye anakatwa pay as you earn lakini mkulima hana hiyo pay as you earn kwa hiyo atalipa kodi ya aina nyingine, hii yote ni katika kuchangia Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa Machinga ningeomba Waziri kama itakufaa aangalie ile penalty kwa mtu ambaye atakuwa amekiuka ya Sh. 200,000/= mpaka Sh. 1,000,000/= au kifungo cha mwaka na kisizidi miaka miwili. Naomba tuiweke kulingana na mtaji mtu alionao, kuna Machinga wengine wana mtaji wa Sh.200,000/=, wengine mtaji wa Sh.100,000/=. Kwa hiyo, nafikiri hizi penalty tungeziweka kutokana na category ya mtaji ili isimuumize. Utaenda kumchaji mtu penalty ya Sh.1,000,000/= wakati mtaji wake ni Sh.200,000/=, matokeo yake ataenda tu gerezani, hivyo, tutaongeza gharama ya wafungwa huko kwenye magereza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni declaration, mtu anavyofanya wrong declaration kwenye ku-forge hizi invoice hasa kwenye importation, tozo imepandishwa toka dola 10,000 mpaka 20,000. Inawezekana mtu akawa na mzigo mkubwa. Kwa hiyo, ningeomba iwe minimum dola 10, 000 na nyingine iwe kwa percentage...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2017
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. kwanza naomba nishukuru kwa hii nafasi. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutupa uhai mpaka dakika hii.

Naomba nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kufanya kazi na Kamati hii na wameweza kufanya vizuri sana kwanza kwa kuchukua maoni ya Kamati na kuweza kuyafanyia kazi na kwa ushahidi, ukiangalia muswada huu
hatuna schedule of amendment mezani za Wizara, inaonesha jinsi gani walikuwa wasikivu na wameweza kuchukua maoni ya Kamati na wadau mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache tu; la kwanza ambalo naomba nisisitize upande wa Serikali, kwamba baada ya kuunganisha hii mifuko, naomba sana tuangalie suala la kulinda hizi ajira za watumishi waliopo katika hii mifuko. Kama tukiangalia suala la wastaafu wangapi ambao ni wafanyakazi ndani ya hii mifuko, basi tuzilinde ajira kwa watu waliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili limezungumziwa kuhusu suala la kujitoa. Kuna sekta nyingine ambayo hatujaiangalia kwa umakini. Kwa mfano, mtu labda ana miaka 50, anajitoa katika mfuko kwa sababu tu amepata ajira au kwa mfano, mtu amechaguliwa kuwa Mbunge, anaenda kwenye sheria nyingine ya wastaafu kwa upande wa kisiasa, ambapo kuingia kwenye hii mifuko inakuwa ni hiari.

Sasa kwa mtu ambaye ameacha kazi, ameingia kwenye Ubunge, kwa nini mtu kama huyo asifikiriwe kwenye fao la kujitoa aliye tofauti zaidi ya kukaa miezi sita ile na kusubiri na kuingia kwenye ule mfuko ambao ali-serve. Kwa hiyo, tuangalie na maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la michango kwa upande wa asilimia tano kwa 15. Tumeona kwamba kuna hiari, mtu anaweza akaongeza lakini azidi asilimia 50. Sasa ni bora kwa wakati mwingine tunaweza kubadilisha, tuache tu asilimia tano kwa 15; asilimia tano kwa mwajiriwa na asilimia 15 kwa mwajiri, kuliko ile section 18(6) ambayo imeweka uhiari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la section 25, tumezungumzia kuhusu umri wa kustaafu. Umri wa hiari ni miaka 55 na umri wa lazima ni miaka 60. Tukumbuke kwamba ni jana tu tumeipitisha ile sheria kwa zile kada za Madaktari na Wahadhiri, lakini sasa huku kwenye mifuko hakuna haja ya kuongeza kipengele kikatambua ile sheria ambayo tumepitisha jana kuhusu hizo kada za Madokta pamoja na Wahadhiri ambao ni Maprofesa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda section 39(1), inazungumzia endapo mnufaika ambaye ni mstaafu amefariki kwamba warithi watalipwa kiasi alichokuwa analipwa cha mwezi cha huyu mstaafu, watalipwa kwa miezi 36. Sasa endapo mtu amestaafu ana miaka 62, bahati mbaya amefariki, halafu beneficiaries wanalipwa miezi 36: Je, kama mtu kastaafu kwa lazima miaka 60 halafu akaendelea kuishi mpaka miaka 75, angeweza kulipwa shilingi ngapi katika hiyo miaka 15 ya uhai wake?

Mheshimiwa Mwneyekiti, leo hii beneficiaries tunawapa fao la miezi 36 tu. Hatuoni katika probability ambayo tunaiangalia hapa, kwa namna nyingine hatujui sasa siyo Mungu wa kujua kwamba lini mtu atakufa, lakini nashauri tuweke categories tuwe na range kama tatu; kama mtu amefariki ana zaidi ya miaka 70 ndiyo hiyo miezi 36, lakini kama mtu amefariki kati ya miaka 60 na 65, hii miezi ya kuwalipa hawa wanufaika iongezeke ifike hata miezi 72 au 60 ili wanufaika waweze kufaidika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, tunaunganisha hii mifuko, lakini imezungumziwa kwenye hii sheria, bahati nzuri imebeba vizuri suala la kama la makato haya ya lazima hayakuwasilishwa katika hii mifuko, yeye mwajiriwa itakuwa siyo mzigo wake. Kuna mashirika mengine ya Serikali, mengine yaliweka madeni na hasa hizi statutory deductions za nyuma, sasa Serikali inabeba vipi? Kwa mfano, Air Tanzania unakuta ilikuwa inadaiwa na TRA, inadaiwa na mifuko, inadaiwa na SACCOS mbalimbali, kama za wanahewa, sasa madeni kama haya yanabebwaje kuja kwenye hii mifuko?

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Ofisi ya AG kwa kuleta Muswada huu. Ni jambo ambalo limekuwa la miaka mingi maana tangu matamko yatoke na mambo mbalimbali yaliyofanyika, ni miaka ambayo wengine ndio tulikuwa tumezaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala la Muswada huu wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi limejieleza kwa faida zake ambazo ni nyingi lakini kwa uchache tu, kwanza suala la urahisi wa kufika Makao Makuu, tunaona Dodoma ni katikati ya nchi ya Tanzania, hata sisi tunaotoka Katavi tumepunguziwa kilometa karibuni 460 kufika Dar es Salaam. Maana kilometa 700 tu unafika hapa Dodoma na ni muda ambao utakuwa ni economical kwa watu mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la kiuchumi, tunavyotanua na kuhamisha Makao Makuu ya nchi tunaongeza fursa mbalimbali kwa maeneo mengine. Kwa mfano, sasa hivi katika mji huu tutaweza kuongeza ajira kwa wananchi ambao tumehamia hapa, wengi wamenunua viwanja, wamejenga. Kwa hiyo, biashara zimeongeka hapa. Tukiangalia tu barabara ya kwenda Medeli hapa, shoppers anajenga hapo, kwa hiyo, ajira zitaongezeka. Kwa hiyo tunavyotanua Makao Makuu pia tutaboresha mji na hata namna nyingine ya kiutalii tunaweza kuongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna masuala ya maendeleo kiujumla. Wengi mmeona kodi za nyumba zilivyokuwa hapa Dodoma kabla na baada ya kutangazwa kuhamia kwa Makao Makuu na vitu vingi bei zimebadilika. Viwanja bei zimebadilika, kodi za nyumba bei zimebadilika, kwa hiyo, mapato ya wananchi katika hili Jiji la Dodoma yameweza kuongezeka kwa watu ambao wanamiliki mali ambazo hazihamishiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya kiusalama kama nchi kiujumla hayalengi tu kwa usalama wa mtu mmoja mmoja, tunaangalia usalama kiujumla wa nchi. Kwa hiyo, hatuangalii usalama wa mtu mmoja mmoja kama matukio yanafanyika nchi nzima, Dar es Salaam yenyewe ndiyo inaongoza kwa matukio na ni nchi nzima matukio yanafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili la kuhamishia Makao Makuu tunapongeza Serikali za Awamu zote ambazo zimepita kuanzia wazo ambalo lilitolewa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere baada ya kutoa tamko na utekelezaji ulianza. Mwaka 1979 tulikopa fedha tuka nchi ya Brazil na ndiyo tukajenga kiwango cha lami hii barabara ya kuja Dodoma mpaka ikafika hapa. Kwa hiyo, yote haya yalikuwa ni maandalizi ya kuhamia Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona Bunge lilihama kutoka Karimjee – Dar es Salaam na tukaanza na ukumbi wa Msekwa na ukaja huu ukumbi mpya. Yote haya ni maandalizi ya kuhamia Makao Makuu Dodoma. Chuo Kikuu na vyuo vingine vimejengwa. Kwa hiyo, yote hayo yalikuwa ni maandalizi ya kuhamia katika huu Mji Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kupendekeza katika huu Muswada, kuna kipengele ambacho kinampa Mheshimiwa Rais kuweza kubadilisha mipaka ya Mji, basi tuone namna bora kama wachangiaji wengine ambavyo wameweza kuchangia, namna Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ilivyo na Halmashauri ya Jiji inakuwa kama inaizunguka. Kwa hiyo, kama kiutawala tunaweza kutanua eneo vizuri, basi ikipendezwa tuweze kubadilisha maeneo ya mipaka na angalau hata Ikulu yetu ya Chamwino ihamie iwe chini ya Jiji la Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala zima la miundombinu. Tunajua kuna mipango mizuri sana ambayo Serikali imeshaitoa, namna ambavyo magari yatakuwa hayaingii katikati ya mji. Basi ujenzi huo ukikamilika, tuombe sasa iende sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya ndani ambayo ni ya zamani ambayo ilianzishwa na CDA. Kwa mfano, barabara za Area D ambazo ni za lami zina mashimo mengi sana ambapo inapaswa yakarabatiwe maana inakuwa ni nafuu upite kwenye barabara ya vumbi kuliko kupita barabara za area D za lami ambazo zimekuwa na mashimo mengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sasa mamlaka husika, TARURA na nyingine ziweze kukarabati hizo barabara ili angalau mtu apite maeneo ambayo yako safi na salama zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na dhana inaonekana kwamba kuhamia Dodoma hakuna kipaumbele na matokeo yake ni kwamba fedha au gharama hizo zipelekwe kwenye huduma za jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge ambao wanazungumzia kuhusu gharama za kuhamia Dodoma hazifai, tupeleke kwenye Vituo vya Afya; Waheshimiwa Wabunge wote hapa tunaingia kwenye Halmashauri na Halmashauri zetu ziko kwa mujibu wa Katiba. Utengenezaji wa bajeti, Serikali Kuu haiingilii Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kila mtu kwenye Halmashauri yake aangalie kutokana na mapato ya ndani, ni kati ya asilimia 40 mpaka 60 wanatakiwa wapeleke kwenye miradi ya maendeleo. Kwa hiyo, kama una upungufu wa Zahanati, vyumba vya madarasa, Vituo vya Afya, tumia mapato ya ndani ya Halmashauri uweze kukidhi matatizo yaliyoko kwenye Jimbo lako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango kazi ambao Serikali inakuwa unauleta lazima utekelezwe wote at parallel. Huwezi ukasema u-concentrate na kitu kimoja umalize ndiyo uende kwenye kitu kingine. Miradi mingine inakuwa ya kimkakati kwa ajili ya kuzalisha pesa uweze kuingiza kwenye miradi mingine. Kwa hiyo, lazima vyote viende kwa pamoja na iendane na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho tu kwa kumalizia, suala la kupunguza msongamano wa watu kuhamia kwenye miji ya kibiashara la lenyewe litapungua. Tukiangalia sasa hivi watu wengi siyo tu watumishi wa Serikali na Taasisi zake kwamba wamehamia Dodoma, hata baadhi ya wafanyabiashara wengi wamehamia hapa Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili nalo linaongeza tija katika mji huu na kupunguza msongamano kwenye Jiji la kibiashara kama Jiji la Dar es Salaam. Kwa hiyo, tunapoanzisha miji mipya, tunapunguza kwa namna fulani asilimia fulani ya msongamano kwenye miji mingine ambayo iko too concentrated kama Jiji la kibiashara la Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naomba kuunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza naomba niipongeze Serikali kwa kuona umuhimu sana wa kuleta na kurekebisha baadhi ya vifungu katika Sheria hii ya Ubia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi faida zilizoko katika kutekeleza haya marekebisho ni nyingi sana tofauti na vile
ambavyo tunafikiria. Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaona kwamba tumechelewa au tunabadilisha sera mara kwa mara lakini naomba nigusie maeneo machache kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida za kuwa na PPP, kwanza tunakaribisha mitaji na tukikaribisha mitaji tunaiwezesha Serikali kujikita kwenye maeneo mengine ambayo zaidi yanakuwa ni ya huduma za jamii. Kwa hiyo, kwenye miradi ile ya kimkakati ambayo ni ya kibiashara tutaweza kuisaidia Serikali kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kurekebisha maeneo mbalimbali kwa mfano kwenye kuondoa baadhi ya taratibu na kumpa Waziri mwenye dhamana tumepunguza urasimu. Suala la Waziri kutekeleza moja kwa moja baadhi ya masuala, tunapunguza urasimu. Kwa mfano, kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri anasema mlolongo mrefu wa michakato ya uidhinishaji wa miradi ya ubia ambao unaathiri kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa miradi ya PPP, maana yake tunapunguza bureaucracy. Ukishaondoa bureaucracy tutaendana na muda na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vigezo ambavyo tayari vimewekwa vitatusaidia sana. Kwa mfano, mijadala ambayo inaendelea ili kutengeneza eneo hilo la miradi mbalimbali kama Liganga na Mchuchuma na LNG ya Lindi, tukiweka maeneo haya na kwa kufuata hii sheria tutanufaika kama nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, marekebisho haya ya vipengele mbalimbali tutakaribisha zaidi wawekezaji na kwa namna nyingine tutaleta uzoefu ambao umetumika maeneo mengine na pia tutaleta teknolojia. Kwa hiyo, tutakuwa na technology transfer maana wataalam wa kampuni ambayo inaingia ubia na Serikali wataleta teknolojia ambayo vijana wetu na watumishi wetu watajifunza na tutaweza kui-capture kwa urahisi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwepo pia na maboresho haya niombe sasa kuna kipengele cha Waziri kwamba kwa vile viwango vidogo katika hii miradi (Small Scale PPP Project) kwamba Waziri kwa kutumia Maafisa wake Masuuli anaweza akaidhinisha moja kwa moja. Basi tuombe tupate ufafanuzi aidha kama kutakuwa na mwongozo wa kanuni miradi hii midogo ni ya kiwango gani, labda kama katika kiasi cha shilingi au dola ambayo sasa Waziri ataweza kuiidhinisha moja kwa moja bila kupitia kwenye Steering Committee, kwa hiyo hiyo tutaomba tupate ufafanuzi wa Serikali katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabadiliko haya ya PPP yamepelekea kufanya na mabadiliko ya sheria nyingine kwa mfano Sheria ya Mafuta. Kimsingi katika Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, National Oil Company ambayo ndiyo kwa sasa ni TPDC inatakiwa ifanye uwekezaji usiopungua asilimia 25 kwa kupata wabia kama hivi. Kwa hiyo, kwa marekebisho haya sasa itaenda kurahisisha katika utekelezaji wa miradi ya uwekezaji na tumeona TPDC ina nia ya kusambaza gesi asilia katika majumba na wameanza Pilot study upande wa Mikocheni kule Dar es Salaam, hivyo hii itasaidia. Kwahiyo hizi zote consequential amendments za Sheria Mbalimbali tunatumainia sasa itaondoa vikwazo na watu kwenye kufanya maamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna baadhi ya Wajumbe wamechangia kwamba Serikali imekuwa ikiwatenga Sekta Binafsi. Hii tunaona siyo kweli kwa sababu kwenye hotuba ya Waziri ameeleza kwamba utekelezaji wa PPP umekwishaanza na wengi tumepanda yale mabasi ya mwendokasi, tukiona ile DART tayari tunaona ni utekelezaji upande wa TPDC, CBE Serikali imeeleza kwamba maeneo hayo inakwenda kuingia kwenye ubia.

Kimsingi siyo kila eneo au aina ya sekta unaweza ukaachia sekta binafsi ifanye. Kwa mfano, masuala mazima ya kiusalama au ya kiafya huwezi ukaachia sekta binafsi. Kwa hiyo, lazima tuzingatie usalama wa nchi na mali zake pamoja na watu wake, kila jambo huwezi ukaachia sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia lazima tuangalie na mazingira ya kuharakisha maendeleo. Kama vile SGR tumeanza kwa fedha zetu za ndani likiwa ni lengo kubwa la kuharakisha miradi hii ili tuweze kuitekeleza kuliko kukaa kwenye masharti ambayo yanakuwa hayana tija kwa upande wa wananchi na Serikali kiujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungeomba pia tupate ufafanuzi mzuri, tumeona Waziri mwenye dhamana atasimamia sera, sheria na kanuni kwenye masuala ya PPP. Sasa ule ushauri mwingine kama inaweza ikatengenezwa, pia ile Steering Committee inaweza ikampa ushauri Waziri katika masuala ya PPP hiyo collaboration basi kama kuna mahali tume-over look basi tutaomba mhusika Waziri mwenye dhamana aweze kutuelezea namna gani tutakuwa na collaboration kati ya Steering Committee pamoja na Waziri mwenye dhamana ambae anasimamia sera, sheria na kanuni kwenye masuala ya PPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo tumeliona katika namna ya kuingia kwenye hii miradi ili tuweze kupata tija zaidi kama kwenye kanuni tuone aina ya uwekezaji na muda ambao mtu ataweza kupata fidia ya uwekezaji alioupata tunapokuwa na amortisation of investment. Hebu tuwe na muda ambao utakuwa ni win win situation ili kila mtu ambae amewekeza pale nchi ifaidike na yule ambaye anaewekeza nae aweze kufaidika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kitu kikubwa cha kuzingatia tunavyokuwa kwenye PPP tuangalie sana masuala ya thamani ya mradi maana tumekuwa na changamoto, baadhi ya watu wanaleta thamani ya juu zaidi tofauti na uhalisia na bei za soko. Yote hiyo ni katika kulenga kujinufaisha yeye mwenyewe ambae amekuja atachukua kingi kuliko kile ambacho sisi tutakuwa tumekilengea. Kwa hiyo, value for money tunatakiwa tuzingatie zaidi, tumekuwa na cases zaidi, kwa mfano kwenye miradi ya uchimbaji wa madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza, nianze kuipongeza Serikali kwa hatua ambayo wameifanya ya kutambua taaluma hii kwamba inabidi ikae kwenye hali ya professional na tukijua idadi kubwa ya watu ambao wameajiriwa kwenye upande wa ualimu ndio wanaoongoza nchini Tanzania na ndiyo msingi wa maendeleo wa Taifa letu kupata wataalam wa maeneo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda kwenye vifungu kwa haraka haraka nikianza na kifungu cha 5 kuhusiana na Bodi. Kama wengine ambavyo wamechangia kwamba Waziri ndiye ambaye atamteua Mwenyekiti wa Bodi, nafikiri
tutengeneze consistency, other Professional Boardies Rais ndiye anayeteua, halafu pia tuongeze suala la qualification kwamba Mtanzania angalau awe na shahada mbili halafu amekuwa senior for a minimum of ten years. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchanganyiko wa wale members nane, subclause (3), wale wawakilishi kutoka kwenye vyama wawe wawili badala ya mmoja. Halafu ile subclause (4), pale kwenye two members appointed by the Minister awe mmoja. Kwa hiyo, kwenye marekebisho upande wa kifungu cha 5, napendekeza yawe namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukitoka hapo tunaenda kifungu cha 6(2) na (3) jinsi gani Bodi ambavyo itaweza kushirikiana na Wizara hasa katika utunzi wa mitihani ambayo itakuwa zaidi ya ki-professional. Tutahitaji kwenye kanuni zitengenezwe ili ziwe zina-guide vizuri kuliko leo hii kiongozi huyo anakuja na maoni binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoka hapo tunaenda kifungu cha 8 kwamba Bodi inaweza ikateua members wachache kama sub-committee. Sasa napendekeza hapa iongezwe iwe at least three members kwa sababu haijatajwa idadi, kwamba kwa sub-committee wanaweza wakateuliwa watu wangapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naenda kifungu cha 10 kwenye suala la Msajili. Suala la Msajili iongezeke sifa, maana hapa hazijatajwa kwamba Msajili atakuwa na sifa za aina gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu kifungu cha 11 kwa Deputy Registrar napo sifa hazijatajwa. Nashauri pia na yenyewe sifa angalau zitajwe hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 14 kwamba Waziri anaweza akateua wale ma-supervisor katika ngazi ya mkoa na wilaya, sasa tunaona hapa ile chain of command tunai-break. Mtu wa wilaya na mkoa ambaye ni supervisor anateuliwa na Waziri, kwa nini asiteuliwe na Chief Executive Officer ambaye ni Registrar? Inawezekana mtu ambaye ana- hire na ku-fire kwenye management, controlling inakuwa ni rahisi. Kwa hiyo, hapa ibadilishwe, badala ya appointment of supervisory officers kuwa Waziri awe Registrar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 21(1)(b) kwamba ili mtu asajiliwe awe na uzoefu wa mwaka mmoja. Napendekeza hii iondoke kama ambavyo na wengine wamependekeza kwa sababu mtu unaweza ukamsajili bila hata kuwa na uzoefu kwa sababu ndiyo amepata kazi. Sasa tukiweka uzoefu wa mwaka mmoja halafu ndiyo asajiliwe, tutaondoka kwenye sifa za wao kusajiliwa. Kwa hiyo, napendekeza hii ya uzoefu iondoke, hata kwenye Bodi hizi nyingine hawaangalii sana uzoefu, wanakusajili unakuwa kama graduand halafu baadaye unaendelea ku-practice katika hiyo professional. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 21(4) kinazungumzia suala la mitihani ya Bodi. Kutokana na wingi wa walimu ambao wanahitimu, itakuwa ni ngumu sana ku- monitor na kwa sababu kuna collaboration kati Bodi na Wizara, basi tuondoe hii mitihani ya Bodi tuweke tu moja kwa moja kule kwa katika vyuo vyetu ambavyo watakuwa wanahitimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 24 kimezungumzia kuhusu payment of annual registration fees. Kwa sababu walimu kwanza mishahara yao siyo mikubwa na mtu ndiyo anaanza kazi, ananunua kitanda na analipa kodi. Kwa hiyo, tunapendekeza kwamba kwenye regulations zile annual fee ziwe katika kiwango ambacho wataweza kukikidhi au ku-afford waweze kulipa na isiwe kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 28 ambacho kiko sambamba na kifungu cha 34 kinazungumzia temporary registration ya foreigners. Mngejaribu kuangalia kwa mfano mtu anapata working permit ya miaka mitatu au miaka
minne au mitano, iendane angalau na license ambayo anapewa. Kwa hiyo, hilo pia liweze kuangaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 67 kwenye reciprocal recognition, kama mtu anatambulika na Bodi ya nje ya nchi yawezekana kule wana terms labda ya five years au ten years, sasa na hapa napo haikutaja moja kwa moja na sisi huku license zetu ni baada ya miaka miwili mtu ana- renew. Kwa hiyo, tuwe na consistency, tumpe license kulingana na Bodi ya nchi anayotoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 72 kwenye suala la Waziri kutunga kanuni, tuongeze pale katika kutunga kanuni sifa za wale supervisors ngazi ya mkoa na wilaya. Sifa zao zitajwe kule ili atakapoteuliwa tuwe na vigezo ambavyo vitaweza kufuatwa, ambao ndiyo mtiririko mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo, niende kwenye consequentials amendment. Tukiangalia, tuna Sheria ya Teacher’s Service Commission, kazi zake zimetajwa pale, lakini nikiangalia baadhi ya kazi kidogo zina mwingiliano kwa asilimia fulani. Kwa mfano, section 5(g) inasema kwamba, supervise teachers in-service training programmes. Mtu tayari yuko kazini, kwa hiyo, TSC ndiyo wana-supervise hizo in-service training programmes. Kama zile za muda mfupi kwa nini zisiende kwenye Professional Board? Kwa hiyo, nafikiri Mheshimiwa Waziri ni bora akaangalia suala hili. Hii inaenda sambamba na section 5(i). Kwa hiyo, zile training ambazo zinazidi miezi sita, zibaki TSC na za chini ya miezi sita ziwe kwenye upande wa Professional Board. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu ni huo. Nafikiri na masuala mengine tutayaleta kwenye schedule of amendment. Naomba niunge mkono hoja na niipongeze Ofisi ya AG, nimeona kwenye financial reporting safari hii wamezingatia ule muda wa kupeleka ripoti kwa CAG na kwa Waziri tofauti na Bills ambazo zilikuwa zinapita huko nyuma, kwa hiyo, hongereni sana.