Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (23 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Katavi limepokea wafugaji wengi na mifugo yao na sasa maeneo hayatoshi kwa makazi, kilimo na malisho. Naomba eneo la hifadhi ya msitu wa Inyonga lipunguzwe na kuongezwa vijiji vya Mapili, Kamalampaka, Songambele, Imalauduki, Kafulu, Nzega, Kaulolo, Masigo, Nsemkwa na Ipwaga.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kuchangia hoja katika Bunge lako Tukufu, kabla sijafanya hivyo naomba nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia amani nchi yetu na kutuwezesha sote kuwepo hapa kushiriki katika Mkutano huu ambao ni wa kwanza wa bajeti tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)
Aidha napenda kutumia fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zilizopita. Ushindi huo ni ishara ya imani kubwa ya wananchi waliyonayo kwa Rais, Makamu wa Rais na kwa Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza pia Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa, Mbunge kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile napenda kuwapongeza Mheshimiwa Spika na Naibu Spika kwa kuteuliwa kwao kuliongoza Bunge hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Mhandisi Gerson Lwenge, Mbunge, kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji na pia namshukuru kwa ushirikiano mkubwa anaonionesha katika kutekeleza majukumu yanayozikabili sekta za maji na umwagiliaji. Natoa shukurani zangu kwa Mheshimiwa Rais kwa kuniteua kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Wizara inayomgusa kila mwananchi katika kurudisha imani hiyo kubwa ninaahidi kuwatumikia wananchi wa Tanzania kwa uadilifu haki bila upendeleo, nina ahidi kufanya hivyo kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyonijalia na kwa ufupi niseme hapa..Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe shukrani kwa wananchi wa Jimbo la Katavi kwa imani yao waliyonipa kwa kunichagua kuwa Mbunge wao kwa kura nyingi za kishindo.
KUHUSU UTARATIBU...
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe shukurani kwa wananchi wa Jimbo la Katavi kwa imani yao waliyonipa kwa kunichagua kuwa Mbunge wao kwa kura nyingi za kishindo. Nawaahidi nitawatumikia wote, kwa nguvu zangu zote kadiri Mwenyezi Mungu atakavyonijalia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwapongeze Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge letu Tukufu na pia kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kuchaguliwa kwao kwa kuwawakilisha wananchi waliowachagua katika Bunge hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile naomba nichukue fursa hii kuishukuru familia yangu nikianzia na mke wangu kwa ushauri na ushirikiano mkubwa wanaonipa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, sasa naomba nichukue nafasi hii kuchangia hoja mbalimbali ambazo zimeibuliwa na Wabunge kupitia kwenye bajeti ambayo imewasilishwa na Mheshimiwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu muda niliopewa ni dakika 15, itabidi nipite kwenye maeneo machache ya ujumla, maeneo mengine yatahitimishwa na Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na suala la madeni. Waheshimiwa Wabunge wengi wamezungumzia changamoto ya madeni kwamba ni kweli Wakandarasi ambao waliingia mikataba kwa ajili ya miradi ya maji, kumekuwepo na madeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe taarifa ifuatayo:-
Miradi ya Maji Vijijini tuliingia mikataba ya shilingi 887,844,161,282. Hadi leo fedha ambazo zimeshalipwa ni shilingi 553,175,872,452 na kiasi kilichobaki ni shilingi 334,668,288,830. Hata hivyo, certificates tulizonazo mkononi ni za thamani ya shilingi 10,822,464,268. Tunamshukuru Mheshimiwa Waziri wa Fedha anaendelea kutupatia pesa na ameahidi kutupatia fedha hizi na zitakuwa zimelipwa kabla ya mwaka wa fedha huu tulionao.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Miradi ya Maji Mjini, tuliingia mikataba ya shilingi 1,379,471,322,665. Fedha iliyolipwa ni shilingi 1,266,610,684,020. Fedha tunayodaiwa ambayo tuna hati za madai mkononi ni shilingi 50,594,881,957.
Waheshimiwa Wabunge, kwa bahati nzuri kwa sababu hii miradi imekuwa inachangiwa na wafadhili, wadau wanaopenda kuchangia katika maendeleo yetu ya kuleta maji, Benki ya Maendeleo ya Ufaransa tayari wamekubali kwamba deni hili wao watalilipa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tayari wameshaanza kutoa tayari fedha kwa ajili ya kulipa deni hili. Kwa hiyo, mpaka tunamaliza mwaka wa fedha huu tulionao, mwezi Juni tarehe 30, tutakuwa hatudaiwi katika miradi ya maji kwa maana ya hati ambazo zimeshawasilishwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu wakandarasi wanaendelea na kazi, wanaweza wakaleta certificates nyingine na tutaendelea kwamba kila tukipata certificate tunapeleka Hazina ili tuweze kupewa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nitoe maelekezo katika hili. Mamlaka zote kuanzia category A, B, na C; ambapo category C mara nyingi ziko upande wa Halmashauri; pale ambapo Wakandarasi wa miradi ya maji wana mkataba, wakishapata certificate, basi watutumie ili tuweze kuipeleka Hazina, tuweze kupata pesa.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi hatuwezi kupeleka hela mahali ambapo hujaingia mkataba na ambapo hujazalisha. Tumegundua hilo tatizo kwamba watu wengi wanasema kwamba hela haijaja, kumbe unakuwa hujaleta certificate ili tuweze kuipeleka Hazina. Hazina haiwezi kutoa hela kama wewe hujaingia mikataba na kama wakandarasi hawajazalisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nitoe maagizo kwa Wakurugenzi wote ambao wanahusika na Miradi ya Maji, kwamba hatuwezi kuleta pesa mpaka walete hati za madai, kuhakikisha kwamba kazi hiyo imeshatekelezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge pia katika michango walioneshwa kutokuridhishwa wakati mwingine na hali ya utekelezaji wa miradi. Wakati mwingine viwango vya utekelezaji vinakuwa viko chini. Certificates hizo tukizipokea, wakati mwingine tutalazimika kuunda timu katika Wizara na kwenda kukagua hiyo miradi kuangalia kama kweli kazi hiyo imetekelezeka.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, Waheshimiwa Wabunge wamechangia kuhusiana na fidia kwenye maeneo oevu. Mpaka sasa hivi kwa upande wa Mkoa wa Kagera kwa ajili ya mradi wa kujenga mabwawa yale ya kutibu majitaka, tayari tumeshapeleka shilingi 1,800,000,000 kwa ajili ya kulipa fidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika Mkoa wa Singida tayari tumeshapeleka shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kulipa fidia kwa chanzo cha Mwankonko na chanzo cha Irawo tunaendelea kufanya tathmini ili baada ya kukamilisha basi tuweze kupeleka hela kwa ajili ya fidia. Kwa hiyo, nako naagiza, maeneo yote ya vyanzo oevu, tathmini ikishafanyika tunaomba mtuletea hati za fidia ili tuweze kuzipeleka Hazina ili kutupatia pesa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge pia wamechangia kuhusu madeni ya maji ambayo yanatokana na Taasisi za Serikali ambazo hazijalipa bili zao. Mpaka hapa tunapozungumza, tuna deni la shilingi bilioni 31, ukikusanya kwa mamlaka zote nchini. Sasa hivi tunafanya mazungumzo na Hazina na tayari wameonesha mwelekeo kwamba madeni haya watayalipa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja hii ilichangiwa pia na Mbunge wa Viti Maalumu wa Tabora, Mama yangu Mheshimiwa Munde, ambaye alionesha kwamba Mamlaka ya Maji ya Mkoa wa Tabora inashindwa kujipanua kwa sababu inadai taasisi za Serikali. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Munde kwamba sasa hivi Serikali inafanya utaratibu wa kuhakikisha kwamba sasa hivi fedha hizi zinalipwa ili hizi Mamlaka za Maji ziweze kuendelea kupanua mitandao ya maji kwa ajili ya wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge pia walichangia kuhusu tatizo la upungufu wa wataalam wa Mamlaka za Maji. Ni kweli tuna upungufu mkubwa wa wataalam kwa Mamlaka zote za Maji nchini. Kwa upande wa Wahandisi tunahitaji Wahandisi 6,282. Kwa sasa waliopo ni Wahandisi 1,538. Upungufu huu ni mkubwa, ni upungufu wa zaidi ya Wahandisi 4,744. Vilevile tunahitaji Mafundi Sanifu na Mafundi Mchundo 4,005. Waliopo ni 752 na upungufu ni 3,253.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na changamoto hiyo, Wizara tayari imeshachukua hatua zifuatazo; tuliomba kibali cha kuajiri watumishi 475, kwa bahati nzuri kibali hicho kimetolewa kwa hiyo kwa mwaka huu wa fedha tunaomaliza, tayari tumeajiri wataalam 475 na wameshasambazwa kwenye Mamlaka mbalimbali za Halmashauri pamoja na Mikoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna changamoto moja tunaipata tunapopeleka hawa wataalam; nitoe taarifa kwamba kuna baadhi ya Mikoa wamewakataa hawa wataalam, na Mikoa hiyo ni pamoja na RAS Dodoma, RAS Mbeya, RAS Arusha, RAS Dar es Salaam, Halmashauri za Manyara, Songea, Urambo na Geita. Hawana makosa kufanya hivyo kwa sababu na wao pia wanayo mamlaka ya kuajiri. Kwa hiyo, tunaona kwamba kama wamefanya hivyo, hao waliowarudisha tutawapeleka maeneo mengine ambayo wanahitajika. Kwa hiyo, tunaomba nao wachukue hatua ya kuajiri ili tusiwe na upungufu wa wataalam.
Mheshimiwa Naibu Spika, najua muda wangu mdogo, nimeshapigiwa kengele, lakini niliona nisimalize bila kuzungumzia maombi ya Mheshimiwa Mchengerwa, ambaye ameomba tuanze kufikiria, kutengeneza mradi wa kuchukua maji kutoka Mto Rufiji na kuyaleta Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2005 mawazo hayo yalikuwepo na Serikali ilichukua hatua kutafuta vyanzo 26. Vyanzo hivyo vilitembelewa lakini ikaonekana kwa mahitaji ya maji ya Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo, vyanzo vilivyopatikana ambavyo viko karibu vina uwezo wa kulisha maji mpaka mwaka 2032. Kwa changamoto ambazo sasa hivi tunaanza kuzipata, tayari tunaanza kujipanga ili kuhakikisha kwamba tunaanza usanifu wa kutoa maji kutoka Mto Rufiji ili tuweze kukidhi mahitaji ya maji ya Mji wa Dar es Salaam; na hasa baada ya kuwa na kiwanda cha kuchakata gesi kwa ajili ya kutengeneza umeme, ambacho miaka miwili ijayo kitakuwa kinahitaji lita milioni 100 kila siku kwa ajili ya kupooza ile mitambo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mchengerwa kwamba hatujatenga fedha katika mwaka wa fedha unaokuja, lakini wazo hili tunalichukua na taratibu pengine mwaka kesho kutwa wa fedha tutaanza kuweka fedha kidogo, kwa ajili ya kuanza kufanya upembuzi yakinifu.
Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge, nimalizie pia kwa kuzungumiza mradi wa maji wa kutoa Mto Ruvuma kuleta Mjini Mtwara Mikindani. Taratibu za kuongea na wafadhili zinaendelea vizuri na hivi ninavyoongea, wale Wachina, Wafadhili wenyewe wapo hapa Tanzania na mazungumzo yanaendelea vizuri. Kama hali itaendelea kama ilivyo, tunatarajia mpaka mwezi wa saba tunaweza tukawa tumesaini mikataba.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nanyamba ana vijiji kwenye chanzo cha huu mradi. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba vijiji vyako hivyo vitapewa maji pia kutoka katika huu mradi. Kwa bahati nzuri ni kwamba mtambo wa kutibu maji utajengwa kwenye chanzo. Kwa hiyo, wananchi wako watapata maji ambayo ni safi na salama. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nisingependa nipigiwe kengele. Basi kwa haya machache, naomba niishie hapo, nashukuru sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi uliyonipa. Kwanza naomba nimpongeze Waziri na Naibu Waziri wa Wizara hii nyeti kwa manufaa ya Watanzania kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia hotuba hii, kwa kweli inatoa mwelekeo mzuri wa kutufikisha mahali ambapo tutakuwa kwanza tuna chakula cha kutosha, lakini pia tutaendeleza uchumi wa viwanda ambapo sehemu kubwa itategemea kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikiliza Waheshimiwa Wabunge wengi wanavyochangia na wameishauri Serikali kwamba ni vizuri tuwe na mkakati wa kutosha wa kuinua kilimo cha umwagiliaji. Ni kweli nakubaliana nalo na ni kweli kwamba asilimia zaidi 75 ya kilimo chetu tunategemea mvua na kilimo cha mvua kwa kweli siyo endelevu, kama mvua hakuna maana yake hakuna kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa vyovyote vile lazima tuweke mkakati na ndiyo maana tayari tumeanzisha Tume ya Umwagiliaji ambayo ndiyo itakayosimamia eneo hili la umwagiliaji. Tumeona tuwe na Tume ili wawe na nguvu zaidi kuliko kufanya kama idara ya Serikali. Kwa hiyo, Tume tunayo na sasa hivi wanaandaa mpango kabambe wa umwagiliaji katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye bajeti yangu kwamba tuna hekta 29,000,000 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Bahati nzuri tumepata msaada kutoka shirika la JICA ambalo limetufadhili kuandaa mpango ule, sasa hivi tunafanya manunuzi ya kupata Mhandisi Mshauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu katika kuendeleza sekta ya kilimo tumekuwa na miradi midogo midogo ya kusaidia wakulima wadogo wadogo, kila Halmashauri imekuwa na miradi lakini kwa sehemu kubwa miradi hii haijawa endelevu. Kwa hiyo, sasa tunataka tufanye mkakati wa kuhakikisha kwamba miradi hii ya umwagiliaji ambayo iko kwenye Halmashauri zetu inakuwa endelevu kwa kuipa nguvu kupitia hii Tume ya Umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kazi kubwa na ya muhimu kwanza maji kama ambavyo wanavyosema ni muhimu kwa binadamu lakini ni muhimu kwa mifugo yetu na ni muhimu kwa kilimo. Kwa hiyo, tutajenga mabwawa na mabwawa haya haya ndiyo tutakayoyatumia tupate maji
ya umwagiliaji ili tuweze kuinua kilimo chetu na tuwe na uhakika wa chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti,Kwa hiyo, hii ndiyo kazi kubwa ambayo tunakwenda kufanya, hatutaweza kuendeleza kilimo kwa kutegemea mvua. Kwa hali ya tabia ya nchi inavyoonekana sasa mvua imekuwa inapungua kila mwaka kwa hiyo tukitegemea mvua kilimo chetu kitakuwa si endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia amani nchi yetu na kutuwezesha Wabunge wote kuwepo hapa kushiriki katika Mkutano huu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Rais, Champion wa Maji kwa kuendelea kuniamini na kuamini wafanyakazi wa Wizara ya Maji ili tuweze kutatua tatizo la maji kwa wananchi wa Tanzania. Namshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mama yetu Mheshimiwa Samia Suluhu, Mheshimiwa Rais alimteua Mama na suala la maji ni la mama, kwa hiyo anatusimamia vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuendelea kusimamia vizuri shughuli za Bunge na tunaendelea vizuri kwa amani kabisa bila fujo ya aina yoyote. Namshukuru Mheshimiwa Spika, nawe Mheshimiwa Naibu Spika na leo ndio umekalia kiti hicho kwa jinsi mnavyoliongoza Bunge kwa weledi mkubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa ushirikiano wenu, kwa miongozo yenu na kwa jinsi mnavyotuombea, lakini jinsi ambavyo mnaendelea kushirikiana nasi ili azma hii ya kuondoa tatizo la maji katika nchi yetu liweze kufikiwa bila tatizo lolote.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nami niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole za dhati kwa wananchi wote nchini hususan wananchi wa Arusha, kwa msiba mkubwa wa ajali ya gari uliogharimu maisha ya wanafunzi, Walimu, dereva na shule, msiba uliotutokea mwezi huu, msiba mgumu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikitika sana kwa sababu barabara ile nimeisimamia mwenyewe kutoka Makuyuni mpaka Ngorongoro. Tunaomba roho za vijana hawa na hawa watu wazima wote Mungu aziweke mahali pema peponi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nichukue nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Lwenge, amenipa ushirikiano mkubwa sana, ameniongoza ndiyo maana hata nimeweza kufahamu mambo mengi kwa muda mfupi. Namshukuru sana Mheshimiwa Lwenge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Katavi kwa ushirikiano wao mkubwa wanaonipa mimi Mbunge wao, unaosaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika Jimbo letu, naendelea kuwaahidi kwamba nitawatumikia kwa kadiri Mwenyezi Mungu atakavyonijalia na kwa nguvu zangu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile naishukuru familia yangu sana kwa jinsi inavyonishauri na jinsi inavyonipa ushirikiano ikiongozwa na mke wangu ambaye ni Mwalimu Bora Jeremiah Ulaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda kuwa ni mdogo, nianze kuunga mkono hoja au shughuli yetu hii ya leo na niombe Waheshimiwa Wabunge mpitishe ili tukafanye kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepokea michango mingi sana kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge, michango ambayo kwa kweli inatutetea ili tuweze kuhakikisha kwamba tunatimiza kuwapatia wananchi wa Tanzania majisafi na salama lakini pia tuweze kuboresha kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza mchango wangu kwa kilimo cha umwagiliaji. Nchi yetu mwaka 1990 ilifanyika study ambayo ilibaini kwamba tuna hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, lakini ambazo zimeendelezwa ni hekta 461,000. Baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, nashukuru maeneo niliyofanya ziara; nimekwenda kuona jinsi gani hili eneo dogo ambalo limeendelezwa jinsi linavyofanya kazi na nimebaini upungufu uliopo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimetembelea eneo la Mang’ola, nimekwenda kuona kilimo pale Wilaya ya Karatu, wanalima mara tatu. Hekta moja inatoa kuanzia tani tano mpaka tani kumi lakini hekta moja hiyo hiyo inalimwa mara tatu. Ni maeneo machache sana ambayo yameshafikia hatua hiyo ya kilimo kwamba hekta moja inaweza ikalimwa mara tatu. Maeneo mengi yanalimwa mara moja na ni kipindi cha mvua tu; kipindi cha kiangazi hatuwezi kulima kwa sababu hakuna maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana Serikali kwa sasa imeweka Mhandisi Mshauri ambaye anapitia maeneo yote ili kubaini upungufu uliopo ni kwa nini hatuwezi kulima mara tatu ili tuweze kuondokana na tatizo la njaa katika nchi yetu. Upungufu huo ukishapatikana utaainishwa na malengo yetu ya kuhakikisha kwamba tunaandaa hekta nyingine millioni moja katika huu muda wa miaka mitano, nina hakika kwamba yatafikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo letu ni kuhakikisha tunalima mara mbili hadi mara tatu, kwa sababu hata hizo hekta chache ambazo nazo hazitumiwi kwa efficiency inayotakiwa, lakini bado zina uwezo wa kuchangia chakula kwa zaidi ya asilimia 25.

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo cha umwagiliaji ndiyo uti wa mgongo wetu na Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza kwamba nchi yetu inakuwa ya viwanda na viwanda hivyo vitatumia rasilimali ya kutoka mashambani ili tuweze kunyanyua uchumi wa wananchi wetu twende kwenye uchumi wa kati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutahakikisha kawamba kilimo hiki cha umwagiliaji tunakisimamia ipasavyo. Kwa sababu Waheshimiwa Wabunge mlipitisha tume, katika huu muda mfupi ambao nimekaa nao, nimebaini upungufu uliopo. Upungufu uliopo, ni kweli kama mnavyolalamika Waheshimiwa Wabunge miradi mingi ambayo tulipata hela za wafadhili haijajengwa katika ile hali ambayo tulikuwa tunaitarajia. Kila ukiuliza, ukienda kwenye Halmashauri, Halmashauri wanakwambia ni matatizo ya Tume; ukiongea na watu wa Tume, wanakwambia ni matatizo ya Halmashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeongea na Waziri wangu kwamba hiyo miradi iliyokuwa inaendelea iendelee, lakini miradi mipya yote itakayokuja, tunataka tuone mtu mmoja anaitekeleza na sio mwingine, itakuwa ni Tume ya Umwagiliaji, ili kama kuna upungufu katika ile tume, Waheshimiwa Wabunge tuweze kuurekebisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepata michango mingi, Mheshimiwa Mwalongo, Mbunge wa Njombe Mjini ameongea kitu cha msingi sana, kwamba Halmashauri yake ina matatizo ya Wahandisi, ina matatizo ya wataalam wa manunuzi. Ni kweli, lakini nashukuru bajeti ya mwaka 2016, mliagiza Wizara ya Maji na umwagiliaji kwamba mnataka tuunde Wakala wa Maji Vijijini. Mheshimiwa Waziri atalielezea vizuri, niwahakikishie kwamba tumeshaanza. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, hata mimi mwenyewe baada ya kuteuliwa katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji, kwa sababu nimetoka kwenye Wakala wa TANROAD niliona ili tuweze kwenda hakuna namna nyingine, ni lazima tuunde wakala ujitegemee, ufanye kazi kama ambavyo TANROAD imekuwa inafanya, ufanye kazi kama ambavyo REA inafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mwalongo tatizo hilo alilonalo la wataalam wa manunuzi litakwisha baada ya sisi kuwa na Wakala wa Maji Vijijini. TANROAD imefanikiwa kwa sababu wataalam wa manunuzi ndani ya TANROAD ni Wahandisi hao hao wanaojenga barabara, ndiyo maana mambo yanakwenda vizuri; tunaelekea huko Waheshimiwa Wabunge. Sasa hivi inaandaliwa na tutakapoileta hapa, tutawaomba Waheshimiwa muipitie, mtushauri na muipitishe ili tuanze utekelezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Musukuma katika mchango wake, nilikuwa nafikiri nami ataniuliza what is your weakness? Alisema kwamba miradi hii, bajeti hii hatuwezi kuitekeleza kwa mwaka mmoja.

Waheshimiwa Wabunge tumejipa miaka mitano, tumeanza na bajeti hii tumeitendea haki, tumeingia mikataba, tutatekeleza. Hebu tupimeni baada ya miaka mitano mtaona tutafanya nini? Huu mwaka mmoja tumejitahidi, tumeelewa tunatakiwa kufanya nini. Kwa hiyo, tupeni muda tuifanyie kazi. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wako Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia uchimbaji wa visima vya Kimbiji na Mpera. Waheshimiwa Wabunge tayari visima 17 vimeshakamilika na niwaambie tu kwamba visima vitatu bado, lakini vinakamilika mwezi Juni, 2017 maana yake ni mwezi ujao. Visima hivi vikikamilika, visima vya maeneo ya Mpera vitahudumia wakazi wa maeneo ya Gongolamboto, Chanika, Luzando, Pugu, Mpera, Chamazi, Kidunda, Ukonga, Kinyerezi na Uwanja wa Ndege.

Mheshimiwa Naibu Spika, visima vya maeneo ya Kimbiji vitahudumia wakazi wa maeneo ya Temeke, Kisarawe, kibada, Kimbiji, Kigamboni, Tuangoma, Mkuranga, Kongowe, Mbagala, Kurasini, Mtoni, Tandika, Keko na Chang’ombe. Serikali inaendelea kutafuta fedha ili tuweze kuweka miundombinu ya usambazaji.

Waheshimiwa Wabunge, naomba mtuamini, tunaifanya hii kazi ili tuhakikishe wananchi wote wa Dar es Salaam na Pwani wanakuwa na majisafi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Ignas Malocha, Mbunge wa Kwela. Amesema kwamba tumekuwa tukiomba pesa mfululizo kwa miaka mitano, hatujawahi kupewa. Tatizo ni nini? Anaelekeza kwenye miradi ya Maleza, Izia na Mfia. Mheshimiwa tutaweka fedha, tumeanza. Kama nilivyosema, utekelezaji wetu unakwenda miaka mitano, nimhakikishie wananchi wake watayaona sasa matokeo kwamba tunatekeleza maeneo yote haya aliyoyahitaji yakiwemo pamoja na maeneo ya umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Pudenciana Kikwembe amesema mradi wa umwagiliaji wa Mwamapuri kwamba haujatengewa fedha katika bajeti ya mwaka huu; anaomba mradi huo utafutiwe fedha. Skimu ya umwagiliaji ya Mwamapuri ipo Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. Skimu hii ina zaidi ya hekta 13,000 zinazofaa kwa umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie Mheshimiwa Pudenciana Kikwembe, tayari upembuzi yakinifu umeshakamilika na tayari tumeshapata gharama, tunahitaji shilingi billioni 15 ili tuweze kuikamilisha hiyo skimu ikiwa ni pamoja na kujenga Bwawa la Ilalangulu ambalo litatunza maji ili tuhakikishe kwamba skimu hiyo inafanya kazi mwaka mzima isifanye kazi wakati wa mvua tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele ameuliza, katika nyakati hizi mbaya za mabadiliko ya tabianchi, licha ya kwamba sasa maeneo yetu bado ya misitu na miti kiasi, lakini suala la uharibifu wa mazingira litasababisha ukame utakaosababisha uhaba wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Mpina ameeleza vizuri sana nini kinafanyika, sheria tunazo, lakini kikubwa Mheshimiwa Masele sisi ni Madiwani, lazima tukae na wananchi wetu, tuongee nao, tubadilishe tabia sisi wenyewe. Hatuwezi kuishi kwa sheria tu, lazima tuwe na tabia ya kufahamishana tuelewe kwamba misitu ni uhai na uhai ule siyo wa misitu wala siyo wa wanyama tu, ni pamoja na sisi binadamu. Tukielimishana, basi suala hili la mabadiliko ya tabianchi halitakuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, Wabunge wengi wamelalamika, miradi mingi ya maji tumetekeleza, lakini haifanyi kazi. Ukienda kuangalia, pamoja na matatizo yaliyokuwepo kwamba labda imejengwa vibaya, labda usanifu ulikuwa mbaya, lakini maeneo mengi ni kwamba vile vyanzo vilivyokuwa vimetarajiwa vimekauka. Sasa kama vimekauka, maji ya kuingiza kwenye bomba utayapata wapi? Haiwezekani. Tatizo hili sisi wenyewe, ndugu zangu tuhakikishe kwamba tunasimamia, tunaongea na wananchi wetu kuhakikisha kwamba tunadhibiti uharibifu wa misitu kwa sababu misitu ni uhai.

Mheshimiwa Naibu Spika, wapo Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia suala la kwamba mradi kutumia hela nyingi. Ukienda kuuliza, unaambiwa hii design iliharibiwa na Consultant. Mikataba iko wazi! Iko design liability ya Consultant. Kama Consultant ameharibu na ikathibitishwa kwamba ameharibu, lazima anailipia. Hizo fedha za kujenga huo mradi tutazipata kutoka kwenye insurance yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, iko michango mingi sana ya Waheshimiwa Wabunge ambayo hatuwezi kumaliza kuijibu yote, lakini tutahakikisha kwamba kwa muda mfupi michango yote hii tutaiandika na kuhakikisha kwamba tunawapatia Waheshimiwa Wabunge kabla ya kumaliza hili Bunge ili kila mtu awe na nakala na aone mchango wake na majibu ambayo tumeyapata.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Anna Lupembe, Mbunge wa Viti Maalum, maji yasiyotibiwa, malengo yetu na ndiyo Sera yetu kuhakikisha kwamba maji yote ya matumizi ya binadamu yanatibiwa ili mtu aweze kunywa maji yaliyo safi na salama. Concept hii tumeiona, Waheshimiwa Wabunge mmechangia, tukinywa maji yaliyo safi na salama tunapunguza hata kwenda hospitali na gharama za kununua madawa zitapungua. Hilo ndilo lengo letu. Sisi Wizara ya Maji hatupendi tuwe sababu ya kumaliza fedha za nchi hii kwa Serikali kununua madawa mengi kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Mheshimiwa Kapufi amezungumzia maji ya Ikorongo. Tayari tumeshasaini mkataba mmoja na wa pili utasainiwa ili tuhakikishe kwamba tunaongeza kiwango cha maji kufikia lita milioni
10.2 zinazohitajika katika Mkoa wa Katavi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Munde, Mbunge wa Tabora, tunakushukuru sana kwa pongezi. Tumesaini mikataba; mkataba ule ni wa zaidi ya shilingi bilioni 600, tunasimamia utekelezaji. Tumejipanga kuhakikisha kwamba unakamilika katika muda uliotarajiwa ili tuhakikishe tunamaliza yale matatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Mheshimiwa mama yangu Mheshimiwa Sitta amelalamikia kuhusu mradi tunaotoa maji Malagarasi kuleta Tabora kwamba utachukua muda mrefu. Tutahakikisha kwamba katika huo muda tunaosubiri ili tuweze kupata fedha kujenga huo mradi ambao utachukua miaka mingi, tutahakikisha kwamba tunafanya hatua za dharura ili wananchi wa Kaliua, Urambo waweze kupata maji yaliyo safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri hapa nimeshapigiwa kengele tayari, nimalizie kwa kuunga mkono hoja, lakini nawaomba Waheshimiwa Wabunge, kila bajeti inapokamilika, tunawapatia vitabu. Katika mizunguko yangu ambayo nimekwenda huko kwenye Halmashauri, unakutana na Mkurugenzi anasema yeye haelewi kama ana bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Kabisa, kabisa mama yangu. nimeyaona haya na siyo Halmashauri moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana Waheshimiwa Wabunge, baada ya leo, kesho mpigie Mkurugenzi wako, basi msomee hata kama hukumpa kitabu, kwamba Wizara ya Maji na Umwagiliaji una shilingi kadhaa ili waweze kujipanga. Zipo, lakini hawaangalii.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kunipa pumzi. Pili nimshukuru Mheshimiwa Rais, ameniamini miezi 23 katika nafasi ya Naibu Waziri, lakini baadae ameniamini zaidi na kunikabidhi nafasi ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Ninamshukuru sana na ahadi yangu kwake na ahadi kwa wananchi wa Tanzania ni kwamba nitawatumikia kuhakikisha wanapata huduma ya maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeze sana Waziri wa Fedha, ndugu yangu Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, kwa kuleta mpango mzuri huu ambao hauna maneno mengi, lakini ukiuangalia unatupeleka moja kwa moja kwenye uchumi wa kati ili tuhakikishe kwamba, wananchi wetu wanakuwa na maisha bora. Niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na michango hii yote kwetu ni dira, tutaifanyia kazi, tutashirikiana na ninyi na tunaomba muendelee kutu- support ili tuweze kutekeleza majukumu yaliyo mbele yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninayo michango ya kiujumla kwenye Wizara yangu ya Maji na Umwagiliaji na nianze na tatizo ambalo tumekuwanalo nab ado tunalo sasa hivi kuhusiana na utoaji wa huduma ya maji vijijini na mijini, hasa kupitia katika mamlaka. Tunazo mamlaka za aina tatu, tuna mamlaka ya daraja la tatu, mamlaka daraja la pili na mamlaka daraja la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, daraja la kwanza wanajihudumia kwa asilimia 100, ikiwa ni kulipa mishahara, kununua madawa na kulipa gharama za umeme. Madaraja ya pili na daraja la tatu ni kwamba madaraja haya inabidi yasaidiwe hasa katika kulipa bili za umeme. Daraja la pili linasaidiwa kwa asilimia 50, daraja la tatu linasaidiwa kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko changamoto katika mamlaka hizi, zipo mamlaka ambazo zipo chini ya Wizara ya Maji na ambazo zipo chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tulishakaa na Serikali tukayaainisha medeni na tukakubaliana kwamba Serikali sasa hivi inaendelea kutafuta fedha ili iweze kulipa madeni yote ya nyuma. Tumejipanga kuhakikisha kwamba hatuendelei kuzalisha deni jingine na ndio maana tumekuja na mfumo wa mita za LUKU upande wa maji ili tukishaiweka mwananchi unalipia ndio uweze kupata huduma ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu katika hili, Waheshimiwa Wabunge na Serikali kwa ujumla ni kwamba sasa tunajadili mapendekezo ya maendeleo ya mwaka ujao wa fedha pamoja na mwongozo wa bajeti, Serikali tuhakikishe watu wote wanatenga bajeti kwa ajili ya kuzihudumia hizi mamlaka za daraja la tatu na daraja la pili ili mwaka ujao wa fedha tena isitokee kwamba mtu anakatiwa umeme kwa sababu hajalipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua Nzega sasa hivi wamekatiwa na maeneo mengine pia lakini kama alivyosema Mheshimiwa Waziri wa Nishati kwamba tutakaa tuhakikishe kwamba wananchi hawa wanapata huduma ya maji. Changamoto ninayoipata ni kwamba umeme ukikatika, maji yakikosekana hatuangalii kwamba ni umeme linarudi kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe sana hasa Serikali tuhakikishe kila mtu kwenye Taasisi yake mwaka ujao wa fedha atenge bajeti kwa ajili ya kulipia gharama hizo za umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuweza kutekeleza azma ya kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata maji safi na salama, bajeti ya mwaka 2006/2007 tulianzisha programu ya maendeleo ya sekta ya maji. Katika programu hiyo tulipanga kutekeleza miradi 1,810, hadi sasa kupitia progamu hiyo ya awamu ya kwanza ambayo ilikamilika mwezi Juni mwaka 2017, tumefanikiwa kutekeleza miradi 1,423, miradi iliyobaki ni miradi 378 lakini tunaendelea na utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo ya utekelezaji wa miradi hiyo, tumetengeneza vituo 117,000 vya kuchotea maji, kama vituo vyote vingetoa maji, sasa hivi tungekuwa na asilimia 78 ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijiji. Bahati mbaya sana kutokana na changamoto mbalimbali, asilimia 35 ya hivi vituo havitoi maji na matokeo yake sasa huduma ya maji inayopatikana kwa sasa ni asilimia 63.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia bajeti ya mwaka huu wa fedha tulionao 2017/2018 Waheshimiwa Wabunge vile vitabu mlivyopewa kwenye bajeti za Halmashauri tumeweka kifungu cha fedha kwa ajili ya Halmashauri kuhakikisha kwamba wanarejesha huduma kwa kukafuta vyanzo vingine. Tumeweka incentives kwamba ukirejesha huduma ya kituo kutoa maji, unapata sterling pound 50 na ukiweka kituo kipya unapata sterling pound 1,500. Fedha mnazo zimeainishwa kwenye bajeti, kwa hiyo tujitahidi kuhakikisha kwamba tunarejesha hiyo huduma ambayo tumeweka vituo lakini vile vituo havitoi maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ambayo imejitokeza mpaka hivyo vituo vikakosa kutoa maji hadi sasa tumebaini kuna changamoto za aina tatu. Kwanza ni wananchi kushindwa kuendesha miradi hasa miradi ambayo unakuta kwamba mradi umewekwa katika kijiji wakaweka jenereta ambayo inatumia diesel, wananchi wanafikia mahali wanashindwa kumudu gharama ya kununua mafuta na matokeo yake ni kwamba mradi ule upo lakini hautoi maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekutana na mradi wa namna hiyo wakati wa ziara zangu nikiwa Manispaa ya Mji wa Singida nikakuta kuna mradi una vituo vya kuchotea maji zaidi ya 19, maji yapo lakini wamesitisha huduma kwa sababu mashine iliyowekwa ya kusukuma maji inatumia diesel na hawana uwezo wa kununua hiyo diesel, sasa hivi tumeelekeza kwamba miradi yote ambayo inatumia jenereta za diesel tuhakikishe kwamba tunaweka solar na ndio maana tuna bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilishangaa Manispaa hiyo bajeti ya mwaka 2016/2017 walikuwa na shilingi bilioni mbili lakini hawakutumia hata senti tano na bado walishindwa kununua umeme wa kutumia nguvu ya jua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ni mabadiliko ya tabianchi na sisi wananchi kulima kwenye vyanzo vya maji, matokeo yake vyanzo vimekauka na miradi tuliyotekeleza tukiwa tunatarajia kwamba chanzo kitakuwa mahali fulani, maji hakuna na matokeo yake sasa maji hayatoki katika hiyo miradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya tatu ni pamoja na usanifu mbaya, tumekutana na usanifu mbaya. Wataalam wanakwenda kusanifi kipindi cha mvua, kwa hiyo, kwa vyovyote maeneo yote unakuta yana maji, baada ya kiangazi lile eneo ulilobaini linakuwa halina maji. Kwa hiyo, sasa hivi tunasimamia kuhakikisha usanifu unafanyika wakati wa kiangazi ili chanzo kikipatikana kinakuwa na uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tumeanza awamu ya pili ambayo itakamilika mwaka 2020. Katika awamu hiyo, tunatarajia kutumia zaidi ya dola bilioni 3.3 na tunalenga kutengeneza miradi ya maji vijijini 4,015 na hadi sasa tayari tumeshasaini miradi 150 na tunaendelea vizuri kabisa. Hii ni miradi itakayotekelezwa katika vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna miradi zaidi ya 33 ambayo tunatarajia tuitekeleze miradi ambayo ni mikubwa. Miradi hii ni pamoja na mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda, tuna mradi wa maji wa Mtwara Mikindani, tuna mradi wa usambazaji wa maji kutoka visiwa vya Kimbiji na Mpera na tuna miradi ya maji 17 katika miji 17 ambayo itafadhiliwa na mkopo nafuu kutoka Serikali ya India. Fedha hii imeshapatikana, taratibu za kukamilisha kusaini financial agreement ziko mbioni na wakati wowote ikishasainiwa basi tutaendelea na utekelezaji wa miradi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna mradi mkubwa wa maji utakaopeleka Wilaya zote za Simiyu, huu ni mradi mkubwa utakaotumia zaidi ya dola bilioni 300 na tender tumeshatangaza tayari. Kwa hiyo, tunasimamia kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunao mradi tunaendelea na usanifu wa kutoa maji Mto Malagarasi kupeleka Tabora na kama tutaufanikisha mradi huu na maji yakawa mengi, tuna malengo ya kupanua huduma hii ili iweze kusambaa na mikoa mingine kama tulivyofanya maji ya kutoka Ziwa Victoria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mradi wa maji wa uondoaji wa majitaka katika Mji wa Dodoma nao pia tunaendelea nao kutafuta fedha. Pia tuna mradi wa maji kupeleka Mji wa Kisarawe na juzi meagiza ikifika mwezi wa tano mkataba wake uwe umeshasainiwa ili wananchi wa Kisarawe waweze kupata huduma ya majisafi na salama. Pia Kisarawe sasa hivi kuna eneo ambalo viwanda vinaendelea kujengwa na tayari tuna kiwanda cha cement pale kinafanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mradi wa maji kwa ajili ya Mji wa Kilolo. Tuna mradi wa maji wa HTM nao pia taratibu zinaendelea…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa Mwaka 2017
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kupewa nafasi hii, nimeambiwa dakika tatu lakini nilikuwa nina mengi, dakika tatu zinatosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nitoe shukrani kwa kwa Kamati ya Sheria Ndogo, kwa bahati nzuri nimeshiriki. Pamekuwa na michango mizuri sana kuhusu uboreshaji wa hizi sheria ndogo za DAWASA.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nitoe shukurani kwa Kambi ya Upinzani, kuanzia page ya tano mpaka page sita safari hii wameandika vizuri sana. Utakuta hata lugha ya vijembe iliyotumika inakubalika. Nimesoma hapa, kufanya usafi kila Jumamosi ni siasa nyepesi lakini pia kufunga biashara kila Jumamosi kwa ajili ya usafi wanasema ni siasa nyepesi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili linafanyika kwa sababu bahati nzuri mimi nimehudumia sana Jiji la Dar es Salaam. Kuna mifereji ya maji ya mvua mikubwa sana iko kule chini lakini Dar es Salaam population imeongezeka, wakati huo kilikuwa Kijiji, ikaja ikawa Mji, ikawa Jiji. Tusipozuia manailoni, karatasi na takataka zile ngumu zitakwenda kujaa kwenye mifereji ya chini ya ardhi kule, ndiyo maana sasa hivi tumeanzisha utaratibu kwamba tukusanye zile takataka ili zibebwe, zikatupwe, zichomwe mahali maalum, zisiendelee tena kuzuia mifereji iliyo huku chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuhusu Wabunge wamechangia suala la DAWASA na DAWASCO, kubwa ni kwamba Mheshimiwa Mbunge Waitara amesema kwamba wakati tunafanya mabadiliko ya Sheria Ndogo DAWASCO kuna miradi mingi ambayo wameianzisha, hawajaikamilisha. Hatuvunji DAWASCO, DAWASCO, ipo na DAWASA ipo. Kwa hiyo, ule utekelezaji wa miradi iliyokuwa imeanzishwa utaendelea mpaka ikamilike na tunaendelea kuboresha zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika hili suala la maji ya mvua, kwamba mvua ikinyesha barabara zinajaa maji, maeneo ya wananchi yanajaa maji. Ni kweli kabisa kwamba miundombinu ya maji ya mvua ni michache kwa sababu Jiji la Dar es Salaam, population imeongezeka, majengo yameongezeka. Kwa sasa hivi tumeanza kupata fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji taka na tayari Waziri wa Fedha amesaini mkataba, tumepata zaidi ya dola milioni 100 kutoka Korea na utekelezaji utaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Zuberi Mohamedi Kuchauka amezungumzia kwamba tatizo la maji taka si tatizo la DAWASCO wala la DAWASA, nakubaliana na yeye. Wakati ule Miji yetu ilikuwa kama Vijiji, hakukuwa na haja hiyo, ikaja ikawa Miji, haja haikuwa kubwa, ilipofikia kuwa miji ndiyo tukawa na mashirika ya majitaka, sasa hivi limekuwa Jiji. Kwa sasa ndiyo maana tumeanza, tunabadilisha sheria na kuweka hili jukumu liwe na ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo machache, naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kukushukuru wewe mwenyewe kwa jinsi ambavyo umeendesha majadiliano ya Miswada hii miwili vizuri kwa utulivu mkubwa. Niishukuru Kamati yangu ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa jinsi walivyotoa taarifa na niwashukuru kwa sababu tumeshirikiana nao vizuri na ndiyo maeneo mengi ambayo walikuwa wametoa hoja kipindi tunajadili kwenye Kamati, Serikali imekuwa sikilivu na sehemu kubwa zaidi ya asilimia 80 ni kwamba Serikali imeyakubali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maoni ya Kamati ya kudumu ya Bunge walitaja kwamba utoaji wa huduma za hali ya hewa umeanza hata kabla ya uhuru. Jambo hili ni kweli huduma za hali ya hewa zilikuwa zinatolewa na iliyokuwa Directorate ya hali ya hewa kabla ya uhuru ambayo Makao yake Makuu yalikuwa Nairobi. Baada ya uhuru tuliendelea na baada ya kuvunjika ile Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, mwaka 1978 ndiyo tulitoka kwenye Sheria, Sura namba 157 na marejeo ya 2002. Mwaka 1999 Wakala wa Hali ya Hewa ilianzishwa kwa Sura ya 245 na marejeo yake ya mwaka 2002 na tangazo la Serikali namba 405 la mwaka 1999.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo huduma za hali ya hewa zimekuwa zinatolewa hata kabla ya uhuru na tumeendelea nayo kwa sababu ni huduma ambayo ni muhimu sana sana, huwezi kuiacha. Kwa hiyo tumeendelea kuboresha sheria kadri ambavyo tunakutana na changamoto na ndiyo maana hata sasa hivi tumeleta hii Sheria ili tuweze ku-improve zaidi. Lengo kubwa la Sheria hii ni kwamba tangazo la Serikali namba 405 la mwaka 1999 lilianzisha Wakala, wakati Sheria ya Wakala ni Sheria ya Tanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo msukumo wa Muswada huu ilikuwa ni kwamba kwa mujibu wa Katiba kama ambavyo amezungumza AG ilikuwa ni lazima tutoke kwenye Wakala twende kwenye mamlaka ili sasa tuweze ku-comply na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nami niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwamba tumejadili vizuri na kuona kwamba kwa kweli Muswada huu ulikuwa na umuhimu tufanye hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru AG kwa kutoa ufafanuzi mahsusi hasa kuhusiana na hoja ya Mheshimiwa Saada Mkuya. Ni kweli kwa sasa taratibu za kiserikali na siyo sheria kama alivyosema AG, katika kudumisha na kutatua changamoto za Kimuungano, zimebadilika tangu mwezi Novemba, 2018. Wakati taratibu hizo zinabadilika, sheria hii ilishakwenda katika ule utaratibu wa zamani na tumefika hapa tulipofika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa data kidogo tu ni kwamba Muswada huu umeandaliwa kwa utaratibu wa zamani ambapo Muswada ulijadiliwa na IMTC, Mei, 2018 na Baraza la Mawaziri Oktoba, 2018. Niseme tu kwamba umeshirikisha upande wa Zanzibar tangu mwaka 2017. Kwa hiyo, umeshirikisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia utaratibu ule wa zamani lakini siyo huu wa sasa hivi ambao umeanza Novemba, 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe tu mama yangu Mheshimiwa Saada Mkuya kwamba aelewe siyo makusudi. Kikao cha Novemba, 2017 ambapo idadi kubwa ya wadau walishiriki na kutoa maoni yao, mkutano huo wa wadau ulifunguliwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili Zanzibar ambaye anajulikana kwa jina la Ahmed Kassim. Kwa hiyo, ushiriki wa Zanzibar umekuwepo kwa asilimia kubwa mno ila kuanzia Novemba, 2018, sheria zote ambazo zimekuja zitafuata huo utaratibu wa Kiserikali ambao ameutaja AG na ambao wala siyo sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru pia maoni ya Kambi ya Upinzani. Kwa kweli leo na wao wameunga mkono na wametoa hoja nyingi ambazo na sisi tunaziona kabisa kwamba zina mantiki na tutaendelea kuzifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani, hoja ya upande wa Upinzani ya Mamlaka kutoa vibali na wakati huo huo inakuwa ni mdhibiti kunaweza kuwa na mgongano. Suala hili tumeliona lakini jinsi ambavyo limewekwa na sheria hakutakuwa na mgongano wa aina yoyote lakini ni hoja nzuri. Mara nyingi sheria hizi zinavyotungwa tunaanza kuzifanyia kazi na pale ambapo tutaona kwamba pengine kuna kitu kinaleta changamoto katika hivi vitu viwili, baadaye tunarudi, tunazungumza ndani ya Bunge, Serikali inafanyia kazi na tunarudisha Muswada unakuja kurekebishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na mapendekezo ya idadi ya wajumbe ambao wamepangwa na sheria kwamba ndani yake tuwe na gender. Suala hili mtaliona kwenye amendments tumekubaliana kwamba gender tumeizingatia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kulikuwa na mapendekezo tuweke idadi sasa kwamba hawa watakuwa wangapi. Katika hili suala la gender, kwa mfano, kwa sasa hivi hali ilivyo TMA ambaye ni CEO ni jinsia ya kike lakini inaweza ikatokea sasa akaja Mwenyekiti wa Bodi akawa naye ni jinsia ya kike. Sasa tukisema tuweke mmoja wa jinsia ya kike au wawili wa jinsia ya kike, kwa uteuzi tu wa Rais labda na mimi Waziri unaweza ukakuta kwamba tumeshawaweka wote ni akina mama. Sasa tukisema tuweke wawili au watatu, naiona kama tunaweza tukanyima haki kwa sababu hadi sasa hivi jinsia hizo zinachukuliwa tayari zipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ni hoja ambayo inazungumzika kwa maana ya Serikali na sisi tumekubali kwamba hii lazima tuitambue na ndiyo maana kwa maana ya sheria tumesema kwamba gender tumeingiza kwamba lazima itambuliwe lakini ni namna gani uteuzi unafanyika, hii itategemea sasa na hali katika kipindi hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tu Waheshimiwa Wabunge mtukubalie tu kwamba kwenye hili suala la jinsia itategemea na hali katika hicho kipindi. Suala la msingi ni kwamba tayari iko katika sheria kwamba itazingatiwa. Pale ambapo haitazingatiwa mtakuwa na haki ya kutuhoji kwa sababu tayari imeshatambuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sifa ya Mtendaji Mkuu, nimshukuru mwenzangu aliyetangulia ameitaja. Kwanza kabisa ni kwamba kwa sasa Tanzania ndiyo Mwenyekiti wa kuandaa mpango wa kuwa na satellite ya Afrika. Huyu ambaye ni CEO wa sasa wa TMA Tanzania ni mama na ana sifa hii ya doctorate. Kwa jinsi ambavyo dunia ilivyo sasa kwenye hili Shirika Kidunia ni kwamba wengi wana hizo sifa za kuwa na doctorate lakini tunasema hili tunalibeba, tutaliangalia kwenye vikao hivyo vya kidunia kwa sababu wenzetu wote wako hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaweza tukawa wa kwanza kuja kumweka Mtendaji ambaye na degree ya pili tu wakati nchi zote zingine zina wale ambao wana doctorate. Hoja tunaiona kweli ina msingi, tunaweza tukawa tunanyima haki ya mtu hapa lakini kwa ku-comply na wale wenzetu kama alivyozungumza Mheshimiwa Nditiye unaona kuna haja kabisa tuendelee na hivi mpaka hapo baadaye na wenzetu watakapoanza ku-exercise. Inawezekana kuna maana fulani ndiyo maana na wao wameweka hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati zote zimezungumzia kuhusu adhabu lakini nishukuru kwamba adhabu nyingi tumezi-cover kuanzia kwenye maoni ya Kamati, kwenye amendments ninyi wenyewe mtaona yatabaki maeneo yale yaliyo machache. Yapo masuala ya msingi na Waheshimiwa Wabunge, kwa mfano, unapozungumzia radar; ziko radar kwa ajili ya meteorology lakini ziko radar kwa ajili ya kuongoza ndege. Ile radar kwa ajili ya masuala ya meteorology kwa sasa gharama yake ni kati ya shilingi bilioni
4.5 mpaka shilingi bilioni 5. Kwa hiyo, zile adhabu zinazowekwa sehemu kubwa ni za kumfanya mtu asije akafanya kosa kwa sababu kile kifaa kikiharibika kwa kweli hasara yake ni kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ziko adhabu nyingi ambazo zimeainishwa kule ndani, kwa mfano, mtu anatoa taarifa inaleta madhara makubwa, radar ya TMA ndiyo inayoongoza ndege kwa maana ndiyo inayotoa taarifa ya hali ya hewa kule ngani, kwa hiyo, pilot anapoendesha anatumia data za watu wa Hali ya Hewa (Meteorology) na bado pilot anaposafiri, ninyi wenyewe tumepanda ndege kutoka Dar es Salaam au tunavyokwenda Dar es Salaam, akifika karibu na Dodoma anasema nitakapopata taarifa za Dodoma nitawaambia, sasa inaweza ikatokea kwa sababu mitandao sasa hivi iko mingi aka-pick data ambazo siyo zenyewe zikasababisha ajali kwenye ndege. Ile ajali kwa kweli gharama yake ni kubwa mno na ndiyo maana mmeona Serikali imezingatia zile adhabu ili kufanya tuwe na eneo moja tu ambalo linaweza likatoa taarifa na siyo eneo lingine zaidi ya TMA.TMA kila data inapochakatwa katika muda wa dakika 15 lazima i-respond kwenye standard za dunia kwa hiyo inapotolewa inakuwa data ambayo ndiyo yenye ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia suala la maeneo yale ambayo tutaweka au mtu binafsi ataweka vifaa hivi kwa ajili ya kupima hali ya hewa. Katika lile eneo ni mita ngapi mtu haruhusiwi kuingia kwenye kile kifaa. Sasa ile tunasema ni site specific, itategemea na eneo lenyewe limekaaje kwa sababu
unaweza ukaweka standard kwamba ni mita 20 au 30 lakini lile eneo likawa na matatizo ya aina fulani, tunawaomba Waheshimiwa Wabunge kwamba hili tuwaachie wataalam wao wata-determine. Baada ya kuweka kifaa pale mahali fulani wao sasa ndiyo watasema eneo gani mtu haruhusiwi kuingia hapa, upande fulani ni mita kadhaa, upande fulani ni mita kadhaa, kuliko sisi kuliweka katika sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Saada Mkuya alikuwa ameweka mapendekezo kwamba Mkurugenzi Mkuu au CEO akiteuliwa upande wa Tanzania Bara basi upande wa Tanzania Visiwani awepo MKurugenzi Msaidizi. Wazo ni zuri lakini sheria tuliyonayo sasa haija-cover hilo. Kwa mujibu wa Mamlaka nyingi tulizonazo zinakuwa na Mkurugenzi Mkuu mmoja tu. Kwa sababu huo ndiyo utaratibu tulionao, tukisema kwenye sheria hii tubadilishe hivyo itakuwa inaenda tofauti na Mamlaka nyingine ambazo tayari zinakuwa na Mkurugenzi mmoja lakini Wakurugenzi wengine wapo. Kwa hiyo, ningemwomba tu Mheshimiwa Saada Mkuya akubaliane nasi ili sasa hii sheria iweze kupita. Labda baadaye tutakapokwenda huko na kuangalia mahitaji ya hilo basi linaweza likafanyika.

Kuhusu wajumbe katika hiyo Bodi, hata sasa kuna wajumbe kutoka Zanzibar, kwa hiyo, hilo halina wasiwasi. Wajumbe kutoka Zanzibar ni lazima hata sasa tunawaweka wapo kwenye hii Bodi ambayo ipo kwa sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbatia alitoa mchango mkubwa sana kuhusiana na hizi data kwamba ziwe ni data ambazo ni precise na amezungumzia kwamba hata suala la wataalam wale wawe na elimu ya kutosha. Akasema kwamba kuna scope, time, cost, quality lakini suala la efficiency, integration, risk management lakini kitu kikubwa ni human resource. Ndiyo maana sasa hivi hata katika vyuo vikuu tayari course ya meteorology ipo, kwa hiyo, tutahakikisha kwamba data hizi zinatolewa vizuri. Ali-cite example ya mvua iliyonyesha juzi na ikaleta mafuriko. Kwa bahati nzuri Hali ya Hewa walionyesha na lile eneo lilikuwa na red.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunasema maoni haya tumeyapokea na huko tunakokwenda tutayafanyia kazi. Waheshimiwa Wabunge tunaomba tu kwamba Muswada wetu huu muujadili na kuupitisha kwa sababu ni Muswada muhimu na mambo ya hali ya hewa ni ya muhimu kwa ajili ya wakulima na wanannchi wengine. Kwa hiyo, tunaomba sana Waheshimiwa Wabunge waweze kuupitisha Muswada huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisije nikapigiwa kengele mara ya pili, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kukushukuru wewe mwenyewe kwa jinsi ambavyo umeendesha majadiliano ya Miswada hii miwili vizuri kwa utulivu mkubwa. Niishukuru Kamati yangu ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa jinsi walivyotoa taarifa na niwashukuru kwa sababu tumeshirikiana nao vizuri na ndiyo maeneo mengi ambayo walikuwa wametoa hoja kipindi tunajadili kwenye Kamati, Serikali imekuwa sikilivu na sehemu kubwa zaidi ya asilimia 80 ni kwamba Serikali imeyakubali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maoni ya Kamati ya kudumu ya Bunge walitaja kwamba utoaji wa huduma za hali ya hewa umeanza hata kabla ya uhuru. Jambo hili ni kweli huduma za hali ya hewa zilikuwa zinatolewa na iliyokuwa Directorate ya hali ya hewa kabla ya uhuru ambayo Makao yake Makuu yalikuwa Nairobi. Baada ya uhuru tuliendelea na baada ya kuvunjika ile Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, mwaka 1978 ndiyo tulitoka kwenye Sheria, Sura namba 157 na marejeo ya 2002. Mwaka 1999 Wakala wa Hali ya Hewa ilianzishwa kwa Sura ya 245 na marejeo yake ya mwaka 2002 na tangazo la Serikali namba 405 la mwaka 1999.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo huduma za hali ya hewa zimekuwa zinatolewa hata kabla ya uhuru na tumeendelea nayo kwa sababu ni huduma ambayo ni muhimu sana sana, huwezi kuiacha. Kwa hiyo tumeendelea kuboresha sheria kadri ambavyo tunakutana na changamoto na ndiyo maana hata sasa hivi tumeleta hii Sheria ili tuweze ku-improve zaidi. Lengo kubwa la Sheria hii ni kwamba tangazo la Serikali namba 405 la mwaka 1999 lilianzisha Wakala, wakati Sheria ya Wakala ni Sheria ya Tanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo msukumo wa Muswada huu ilikuwa ni kwamba kwa mujibu wa Katiba kama ambavyo amezungumza AG ilikuwa ni lazima tutoke kwenye Wakala twende kwenye mamlaka ili sasa tuweze ku-comply na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nami niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwamba tumejadili vizuri na kuona kwamba kwa kweli Muswada huu ulikuwa na umuhimu tufanye hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru AG kwa kutoa ufafanuzi mahsusi hasa kuhusiana na hoja ya Mheshimiwa Saada Mkuya. Ni kweli kwa sasa taratibu za kiserikali na siyo sheria kama alivyosema AG, katika kudumisha na kutatua changamoto za Kimuungano, zimebadilika tangu mwezi Novemba, 2018. Wakati taratibu hizo zinabadilika, sheria hii ilishakwenda katika ule utaratibu wa zamani na tumefika hapa tulipofika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa data kidogo tu ni kwamba Muswada huu umeandaliwa kwa utaratibu wa zamani ambapo Muswada ulijadiliwa na IMTC, Mei, 2018 na Baraza la Mawaziri Oktoba, 2018. Niseme tu kwamba umeshirikisha upande wa Zanzibar tangu mwaka 2017. Kwa hiyo, umeshirikisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia utaratibu ule wa zamani lakini siyo huu wa sasa hivi ambao umeanza Novemba, 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe tu mama yangu Mheshimiwa Saada Mkuya kwamba aelewe siyo makusudi. Kikao cha Novemba, 2017 ambapo idadi kubwa ya wadau walishiriki na kutoa maoni yao, mkutano huo wa wadau ulifunguliwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili Zanzibar ambaye anajulikana kwa jina la Ahmed Kassim. Kwa hiyo, ushiriki wa Zanzibar umekuwepo kwa asilimia kubwa mno ila kuanzia Novemba, 2018, sheria zote ambazo zimekuja zitafuata huo utaratibu wa Kiserikali ambao ameutaja AG na ambao wala siyo sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru pia maoni ya Kambi ya Upinzani. Kwa kweli leo na wao wameunga mkono na wametoa hoja nyingi ambazo na sisi tunaziona kabisa kwamba zina mantiki na tutaendelea kuzifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani, hoja ya upande wa Upinzani ya Mamlaka kutoa vibali na wakati huo huo inakuwa ni mdhibiti kunaweza kuwa na mgongano. Suala hili tumeliona lakini jinsi ambavyo limewekwa na sheria hakutakuwa na mgongano wa aina yoyote lakini ni hoja nzuri. Mara nyingi sheria hizi zinavyotungwa tunaanza kuzifanyia kazi na pale ambapo tutaona kwamba pengine kuna kitu kinaleta changamoto katika hivi vitu viwili, baadaye tunarudi, tunazungumza ndani ya Bunge, Serikali inafanyia kazi na tunarudisha Muswada unakuja kurekebishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na mapendekezo ya idadi ya wajumbe ambao wamepangwa na sheria kwamba ndani yake tuwe na gender. Suala hili mtaliona kwenye amendments tumekubaliana kwamba gender tumeizingatia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kulikuwa na mapendekezo tuweke idadi sasa kwamba hawa watakuwa wangapi. Katika hili suala la gender, kwa mfano, kwa sasa hivi hali ilivyo TMA ambaye ni CEO ni jinsia ya kike lakini inaweza ikatokea sasa akaja Mwenyekiti wa Bodi akawa naye ni jinsia ya kike. Sasa tukisema tuweke mmoja wa jinsia ya kike au wawili wa jinsia ya kike, kwa uteuzi tu wa Rais labda na mimi Waziri unaweza ukakuta kwamba tumeshawaweka wote ni akina mama. Sasa tukisema tuweke wawili au watatu, naiona kama tunaweza tukanyima haki kwa sababu hadi sasa hivi jinsia hizo zinachukuliwa tayari zipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ni hoja ambayo inazungumzika kwa maana ya Serikali na sisi tumekubali kwamba hii lazima tuitambue na ndiyo maana kwa maana ya sheria tumesema kwamba gender tumeingiza kwamba lazima itambuliwe lakini ni namna gani uteuzi unafanyika, hii itategemea sasa na hali katika kipindi hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tu Waheshimiwa Wabunge mtukubalie tu kwamba kwenye hili suala la jinsia itategemea na hali katika hicho kipindi. Suala la msingi ni kwamba tayari iko katika sheria kwamba itazingatiwa. Pale ambapo haitazingatiwa mtakuwa na haki ya kutuhoji kwa sababu tayari imeshatambuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sifa ya Mtendaji Mkuu, nimshukuru mwenzangu aliyetangulia ameitaja. Kwanza kabisa ni kwamba kwa sasa Tanzania ndiyo Mwenyekiti wa kuandaa mpango wa kuwa na satellite ya Afrika. Huyu ambaye ni CEO wa sasa wa TMA Tanzania ni mama na ana sifa hii ya doctorate. Kwa jinsi ambavyo dunia ilivyo sasa kwenye hili Shirika Kidunia ni kwamba wengi wana hizo sifa za kuwa na doctorate lakini tunasema hili tunalibeba, tutaliangalia kwenye vikao hivyo vya kidunia kwa sababu wenzetu wote wako hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaweza tukawa wa kwanza kuja kumweka Mtendaji ambaye na degree ya pili tu wakati nchi zote zingine zina wale ambao wana doctorate. Hoja tunaiona kweli ina msingi, tunaweza tukawa tunanyima haki ya mtu hapa lakini kwa ku-comply na wale wenzetu kama alivyozungumza Mheshimiwa Nditiye unaona kuna haja kabisa tuendelee na hivi mpaka hapo baadaye na wenzetu watakapoanza ku-exercise. Inawezekana kuna maana fulani ndiyo maana na wao wameweka hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati zote zimezungumzia kuhusu adhabu lakini nishukuru kwamba adhabu nyingi tumezi-cover kuanzia kwenye maoni ya Kamati, kwenye amendments ninyi wenyewe mtaona yatabaki maeneo yale yaliyo machache. Yapo masuala ya msingi na Waheshimiwa Wabunge, kwa mfano, unapozungumzia radar; ziko radar kwa ajili ya meteorology lakini ziko radar kwa ajili ya kuongoza ndege. Ile radar kwa ajili ya masuala ya meteorology kwa sasa gharama yake ni kati ya shilingi bilioni
4.5 mpaka shilingi bilioni 5. Kwa hiyo, zile adhabu zinazowekwa sehemu kubwa ni za kumfanya mtu asije akafanya kosa kwa sababu kile kifaa kikiharibika kwa kweli hasara yake ni kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ziko adhabu nyingi ambazo zimeainishwa kule ndani, kwa mfano, mtu anatoa taarifa inaleta madhara makubwa, radar ya TMA ndiyo inayoongoza ndege kwa maana ndiyo inayotoa taarifa ya hali ya hewa kule ngani, kwa hiyo, pilot anapoendesha anatumia data za watu wa Hali ya Hewa (Meteorology) na bado pilot anaposafiri, ninyi wenyewe tumepanda ndege kutoka Dar es Salaam au tunavyokwenda Dar es Salaam, akifika karibu na Dodoma anasema nitakapopata taarifa za Dodoma nitawaambia, sasa inaweza ikatokea kwa sababu mitandao sasa hivi iko mingi aka-pick data ambazo siyo zenyewe zikasababisha ajali kwenye ndege. Ile ajali kwa kweli gharama yake ni kubwa mno na ndiyo maana mmeona Serikali imezingatia zile adhabu ili kufanya tuwe na eneo moja tu ambalo linaweza likatoa taarifa na siyo eneo lingine zaidi ya TMA.TMA kila data inapochakatwa katika muda wa dakika 15 lazima i-respond kwenye standard za dunia kwa hiyo inapotolewa inakuwa data ambayo ndiyo yenye ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia suala la maeneo yale ambayo tutaweka au mtu binafsi ataweka vifaa hivi kwa ajili ya kupima hali ya hewa. Katika lile eneo ni mita ngapi mtu haruhusiwi kuingia kwenye kile kifaa. Sasa ile tunasema ni site specific, itategemea na eneo lenyewe limekaaje kwa sababu unaweza ukaweka standard kwamba ni mita 20 au 30 lakini lile eneo likawa na matatizo ya aina fulani, tunawaomba Waheshimiwa Wabunge kwamba hili tuwaachie wataalam wao wata-determine. Baada ya kuweka kifaa pale mahali fulani wao sasa ndiyo watasema eneo gani mtu haruhusiwi kuingia hapa, upande fulani ni mita kadhaa, upande fulani ni mita kadhaa, kuliko sisi kuliweka katika sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Saada Mkuya alikuwa ameweka mapendekezo kwamba Mkurugenzi Mkuu au CEO akiteuliwa upande wa Tanzania Bara basi upande wa Tanzania Visiwani awepo MKurugenzi Msaidizi. Wazo ni zuri lakini sheria tuliyonayo sasa haija-cover hilo. Kwa mujibu wa Mamlaka nyingi tulizonazo zinakuwa na Mkurugenzi Mkuu mmoja tu. Kwa sababu huo ndiyo utaratibu tulionao, tukisema kwenye sheria hii tubadilishe hivyo itakuwa inaenda tofauti na Mamlaka nyingine ambazo tayari zinakuwa na Mkurugenzi mmoja lakini Wakurugenzi wengine wapo. Kwa hiyo, ningemwomba tu Mheshimiwa Saada Mkuya akubaliane nasi ili sasa hii sheria iweze kupita. Labda baadaye tutakapokwenda huko na kuangalia mahitaji ya hilo basi linaweza likafanyika.

Kuhusu wajumbe katika hiyo Bodi, hata sasa kuna wajumbe kutoka Zanzibar, kwa hiyo, hilo halina wasiwasi. Wajumbe kutoka Zanzibar ni lazima hata sasa tunawaweka wapo kwenye hii Bodi ambayo ipo kwa sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbatia alitoa mchango mkubwa sana kuhusiana na hizi data kwamba ziwe ni data ambazo ni precise na amezungumzia kwamba hata suala la wataalam wale wawe na elimu ya kutosha. Akasema kwamba kuna scope, time, cost, quality lakini suala la efficiency, integration, risk management lakini kitu kikubwa ni human resource. Ndiyo maana sasa hivi hata katika vyuo vikuu tayari course ya meteorology ipo, kwa hiyo, tutahakikisha kwamba data hizi zinatolewa vizuri. Ali-cite example ya mvua iliyonyesha juzi na ikaleta mafuriko. Kwa bahati nzuri Hali ya Hewa walionyesha na lile eneo lilikuwa na red.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunasema maoni haya tumeyapokea na huko tunakokwenda tutayafanyia kazi. Waheshimiwa Wabunge tunaomba tu kwamba Muswada wetu huu muujadili na kuupitisha kwa sababu ni Muswada muhimu na mambo ya hali ya hewa ni ya muhimu kwa ajili ya wakulima na wanannchi wengine. Kwa hiyo, tunaomba sana Waheshimiwa Wabunge waweze kuupitisha Muswada huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisije nikapigiwa kengele mara ya pili, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuungana na wenzangu kwa masikitiko makubwa sana kwa tukio ambalo limetokea mchana wa leo. Mimi nakaa Area ‘D’, nimesikia bunduki, lakini baadaye nakuja kupata taarifa kwamba ni Mbunge mwenzangu ambaye amejeruhiwa. Kwa kweli inasikitisha sana, kwa siku ya leo inaleta uwoga kidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kutoa shukrani kwa Kamati ya Bunge ambayo inashughulikia miundombinu ya maji kwa michango yao mizuri ambayo wametushauri kuanzia tulipoanzia michango hii kwenye Kamati. Pia nashukuru sana Maoni ya Kambi ya Upinzani ambao wameunga mkono moja kwa moja kwenye jambo hili. Nashukuru kusema kwamba kwenye masuala kama haya, kwa sababu tunajenga nchi kwa pamoja, sisi wote ni Watanzania, kwa hiyo, inabidi tuungane tuache suala la tofauti za itikadi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tunavyoongea, tayari tuna Interim Secretariat na imeshafanya kazi kubwa sana. Hii Interim Secretariat Ofisi yake iko Kyela, nami nimeshatembelea pale. Ndani ya Watumishi; tuna Watumishi wa kutoka Malawi na Watumishi wa kutoka upande wa Tanzania. Makubaliano yaliyopo ni kwamba hata tutakapokuwa tumekamilisha hii Kamisheni, ikisharidhiwa ni kwamba Ofisi zitakuwa Kyela.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari tangu Sekretarieti ilipoanza, Serikali ya Malawi na Serikali ya Tanzania wanachangia hela kuendesha ile Sekretarieti ya mpito; na imefanya kazi kubwa sana. Imeshakamilisha feasibility study, imeshakamilisha detailed design na imefanya semina mbalimbali na mikutano mbalimbali na Wafadhili na kutangaza kuhusu huu Mradi wa Bonde la Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari kuna indication kubwa kwamba Wafadhili wanasubiri tupitishe hili ili sasa mazungumzo ya mwisho yaweze kufanyika, tufanikiwe kutekeleza ule mradi. Kwa hiyo, suala kama hili Waheshimiwa Wabunge kwa kuliunga mkono, sisi kwa kweli kama Watanzania na kama Wabunge na Wizara ya Maji tunafarijika zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia juzi kulikuwa na Mkutano wa SADC, nami Mheshimiwa Waziri alinituma niende kule. Katika miradi miwili ambayo imepita; imepitishwa na SADC, ni pamoja na huu Mradi wa Songwe. Umepitishwa kwa sababu una components tatu ndani yake kama alivyokuwa amezungumza Mheshimiwa Mwakyembe. Tutazalisha umeme pale, tutatengeneza skimu za umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna hekta za mwanzo 6,200; na kati ya hekta hizo, hekta 3,150 ziko upande wa Tanzania na hekta 3,050 ziko upande wa Malawi. Kwa hiyo, wananchi wa maeneo ya Tanzania na huku watafaidika na umeme na bado watafaidika na kilimo cha umwagiliaji, kilimo chenye uhakika.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia maji yatachakatwa majisafi na salama. Kwa hiyo, sehemu ya maji yatakwenda upande wa Tanzania na sehemu ya maji watatumia watu wa Malawi. Kwa hiyo, sioni katika mpangilio kama huo ambao tuna-share umeme, tuna-share huduma ya maji safi na salama na tuna-share kilimo cha umwagiliaji, jamani undugu utazidi hapo. Unatarajia kuwe na ugomvi kweli hapo? Hata matatizo mengine yaliyopo kwenye lile Ziwa Nyasa, tuna imani kabisa kwamba utatuzi wake sasa utakuwa rahisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge katika michango yao wamezungumzia suala la ushirikishaji wa jamii. Tangu mwanzo hii Interim Secretariat ilivyoanza, imeshirikisha wananchi kutoka ngazi za Vitongoji, imekuja kwenye Vijiji, mpaka Kata, mpaka Wilaya. Wameshirikishwa na minutes zipo na taarifa hizi tumezitoa kwenye Kamati. Kwa hiyo, kila mwananchi yuko aware na suala hili na wanalisubiri kwa hamu kabisa kwamba Kamisheni hii ipitishwe na Bunge letu ili ianze kufanya kazi, wao wanasubiri kupata maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, hebu tujaribu kuiangalia mipaka kwa wale ambao wanaishi kwenye mipaka. Kama maendeleo yakiwa upande mmoja kwingine kukawa hakuna maendeleo, maisha yanakuwaje katika hilo eneo? Kwa maana ya hii Kamisheni kwamba maendeleo yatakayopatikana yatakuwa shared upande wa Tanzania na upande wa Malawi. Kwa hiyo, tutazidi kuimarisha undugu wetu na ushirikiano utakuwa mkubwa. Migogoro mingine midogo midogo wakati mwingine unaitatua automatically kwa kuweka huo ushirikiano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, tunawashukuru sana na tunawaomba kwa kupitia kwenye michango ambayo wengi mlipata nafasi ya kuchangia, wengi mnaridhia na hili. Kwa hiyo, mwisho kabisa tunawaomba mridhie ili hatua nyingine ziweze kuendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo, namalizia kwa kushukuru tena, ahsanteni sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia hizi Kamati mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kusema kwamba mwanadamu ameumbwa kufikiria mambo mengi sana kila baada ya dakika moja na fikra hizi anaziwekea mipango matakwa na haraka anaweza akaamua kutekeleza. Sisi Wabunge tena ambao hatuzidi hata 400 tuna kazi ya digest fikra za Watanzania zaidi ya milioni hamsini kuziwekea mipango, bajeti na kusimamia Serikali katika utekelezaji na tunaisimamia Serikali humu Bungeni pia tunaisimamia Serikali tukiwa katika Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Wizara ya Maji baada ya bajeti ni kutoa miongozo ya utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Halmashauri. Moja ya miongozo ambayo imetolewa ni kwamba Serikali haiwezi kupeleka fedha katika Halmashauri lazima kwanza kazi zitekelezwe, kazi ifanyike katika viwango vinavyotakiwa. Kama kazi yetu sisi Wabunge basi ni kusimamia utekelezaji katika Halmashauri, kama kazi yetu tungeitekeleza vizuri kwenye Halmashauri hata hoja za kuisimamia Serikali ndani ya Bunge kwa vyovyote vile zingepungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimelizungumza hili kwa sababu nazunguka katika Halmashauri mbalimbali, nakutana na changamoto nyingi kama ambavyo zimeainishwa na CAG katika taarifa zake. Waheshimiwa Wabunge wametoa michango,

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lubeleje amezungumzia visima vimechimbwa sita tangu mwaka 2002 lakini havijawekewa pampu. Miongozo ipo nimpongeze sana Mheshimiwa Lubeleje ni kweli amekuwa kila wakati nikikutana naye ananiomba niende kwenye Jimbo lake nikaangalie hali hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Mheshimiwa Gerson Lwenge akiwa Waziri aliwahi kwenda kule lakini juzi nimemtuma Naibu Waziri wangu na nimwahidi Mheshimiwa Lubeleje baada ya Bunge nitaenda nae tena kule, nimeshatoa miongozo kwamba kama umechimba kisima na maji yapo tengeneza quotation, lete tukupe fedha ili uweze kununua hiyo pampu ili wananchi wapate maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Bobali nikushukuru umeongea vizuri miradi mingi inakamilika bila kuwa na viwango vya thamani ya fedha inayotakiwa. Kama nilivyosema wasimamiaji ni sisi wenyewe kwenye Halmashauri. Sisi ndiyo tunaosimamia Serikali Bungeni na tunasimamia Serikali kwenye Halmashauri. Sheria tumezitunga wenyewe inabidi tuzisimamie na Serikali yetu kwa sasa wenyewe ni mashahidi mtu akifanya ufisadi ni moja kwa moja hatua zinachukuliwa hapohapo. Hili halina mashaka kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Abdallah Chikota umetoa mfano wa mradi wa Korogwe kwa Mheshimiwa Maji marefu ule mradi ulisanifiwa ukaanza kutekelezwa hadi maeneo ya Mlembule lakini ikaja kuonekana kwamba mradi ule unatoa maji kutoka Vuga, watu wa Vuga hawakupewa yale maji, tulipokuja ku-review ule mradi wataalam wetu waliweka hela nyingi sasa hivi tunarudia tena ili uweze kutekelezwa. Ninachoomba tu Waheshimiwa Wabunge tusaidiane katika maeneo yetu ili mambo yaweze kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia mtiririko wa fedha kama nilivyozungumza, kwanza niwashukuru sana kuweka Mfuko wa Maji. Mfuko wa Maji kila mwezi unatoa fedha hadi Desemba katika bajeti iliyopangwa ya bilioni 158 tayari Hazina imeshatoa bilioni themanini na kila mwezi kila anayezalisha certificate tunamlipa. Kwa hiyo, suala la mtiririko wa fedha ili uwe mzuri ni sisi Waheshimiwa Madiwani maana yake Wabunge lakini tukirudi kwenye Halmashauri tunakuwa Madiwani, tusimamie utekelezaji wa miradi wazalishe walete hati ili tuweze kulipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwalongo ni kweli nilitembelea Njombe. Hii miradi yote aliyoizungumza Utengule na Changalikwa tuliitembelea, tukakuta changamoto utekelezaji haukuwa mzuri, tayari tumeunda Tume iende ikachunguze na kitu chochote kitakachopatikana ambacho ni kibaya, basi sheria itachukua mkondo wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ni dakika tano nimeweka mambo kidogo, nilikuwa na mambo mengi nafikiri haya yanatosheleza. Nakushukuru sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuishukuru Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji. Katika muda wote ambao wamekuwa na Wizara yangu wamesaidia sana kubaini changamoto, kuishauri Wizara katika utendaji, lakini pia wametoa ushauri mzuri sana kwa upande wa Serikali katika hatua ya kuhakikisha kwamba tunatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ili tutakapofika mwaka 2020 tufikishe maji asilimia 85 vijijini na asilimia 90 hadi asilimia 95 mijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imebainisha kuhusu mtiririko wa fedha. Nikiri kwamba, mtiririko wa fedha, hasa upande wa mfuko wa maji ni mzuri sana kwa sababu hadi kufikia Desemba tulikuwa tumeshavuka asilimia 50 na leo hii tena Hazina imetoa bilioni 14 kwa ajili ya kulipia hati za madai za wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji vijijini na mijini. Lakini Kamati ilibainisha pia kuhusu asilimia ya maji iliyopo upande wa vijijini kwamba ni asilimia 56.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Awamu ya Kwanza ya utekelezaji wa Mpango wa Sekta ya Maji nchini tulibainisha kutekeleza miradi 1,810 hadi desemba tulishatekeleza miradi 1,466. Katika miradi hiyo 1,466 vituo vya kuchotea maji tumefikisha 122,635 na iwapo kama vituo vyote hivyo vingetoa maji sasa hivi tungezungumzia asilimia 81.5 kwa hiyo, tulikuwa tunakaribia kwenda asilimia 85.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepata changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya maeneo kukauka maji pamoja na mambo mengine, matokeo yake ni kwamba vituo vinavyotoa maji ni vituo 83,575 ndiyo sawa na asilimia 56. Vituo ambavyo havitoi maji ni vituo 39,060 sawa na asilimia 44. Lakini kwa kutambua hilo katika bajeti ya mwaka huu wa fedha tulionao Serikali imetenga shilingi bilioni 53.6 na fedha hii imepelekwa kwenye Halmashauri zote kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vituo ambavyo havitoi maji basi fedha hiyo inatumika ili kuhakikisha kwamba vituo vinatoa maji. Kwa hiyo, kama Halmashauri zote zitafanyakazi vizuri tuna hakika mpaka tunafika mwezi wa sita tutakuwa tumeshapandisha hadi kwenda zaidi ya asilimia 76, 77 na tutaendelea kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge niwashukuru sana kwa kuendelea kusimamia Wizara hii ya Maji na Umwagiliaji na ndiyo maana sasa hadi tunafika Ijumaa waheshimiwa wabunge inabidi sasa tutoe table ambayo tunasambaza kwa wabunge wote katika mikoa ili waweze kujua katika Halmashauri yako ni vituo vingapi ambavyo havitoi maji. IIi tuweze kusaidiana kuzisukuma Halmashauri kwa sababu fedha zipo watumie fedha ile waweze kurudisha huduma ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pamoja na Waheshimiwa Wabunge wamechangia kuhusu kilimo cha umwagiliaji. Kweli ni kilimo muhimu ili tuweze kuwa na uhakika wa chakula. Mwaka 1970 Serikali ya Japan ilitusaidia kufanya study na ikabainisha kwamba nchi yetu ina zaidi ya hekta milioni 29.4 ambazo zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji na katika hizo tulitengeneza scheme za umwagiliaji hekta 461,326 sawa na asilimia 1.6.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ambayo tumekutana nayo kwamba scheme hizi zilitengenezwa bila kufikiria sasa vyanzo vya maji ambavyo vinaweza vikafanya kwamba kilimo ili kilimwe mara mbili, mara tatu kwa mwaka. Kutokana na changamoto hiyo sasa hivi kuna master plan ambayo pia tumepata msaada kutoka Serikali ya Japan ambayo ilianza mwaka 2016 na tunatarajia tarehe 1 Julai watakuwa wamekamilisha kufanya study ya hiyo Master Plan. Ili sasa kuweza kuainisha scheme za umwagiliaji pamoja na vyanzo vya maji ili tutakapokuwa tumezitengeneza wananchi waweze kulima muda wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia Wakala Maji Vijijini, Bunge lilituagiza tukaunda sekretarieti na tayari Sekretarieti imefanya kazi na kuwasilishwa kwa wadau wa Wizara ya Maji na TAMISEMI na sasa hivi mwezi huu wa pili mwishoni hiyo taarifa itafikishwa kwa Mawaziri wa TAMISEMI na Waziri wa Maji na Umwagiliaji tuweze kuipitia na baadaye tupeleke sasa kwenye hatua nyingine lengo itakapofika tarehe Julai, basi Wakala huu utakuwa umeanza kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo miradi ya kimkakati, miradi ya kimkakati tuna Bwawa la Farkwa, tuna Bwawa la Ndembela Lugoda lakini pia tumeweka Bwawa la Dongo. Bwawa hili litajengwa katika halmashauri ya Kiteto ambayo litasaidia sasa kuvuna maji ya mvua zinazonyesha maeneo ya Manyara kuleta mafuriko Mkoa wa Morogoro, tunaanza kujenga mabwawa ili sasa hayo maji tuweze kuyahifadhi maeneo na yaweze kutumika kwa matumizi ya majumbani ambayo tuna uhakika baada ya bwawa hili maji yatakwenda Gairo, yatakwenda Kibaigwa na vijiji vya Wilaya ya Kiteto pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua iliyofikiwa tayari tumeshatangaza tender na sasa hivi tuko kwenye uchambuzi ili tuweze kumpata muhandisi mshauri atakayefanyakazi kwa haraka sana na malengo yetu ni kwamba bajeti inayokuja tuweke fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia siku zote tatu tangu tarehe 7 hadi leo tarehe 9 Mei, 2018 ametujalia afya njema na kuendelea kujadili bajeti yetu ya maji na umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kulishukuru Bunge lako tukufu kwa kujadili hoja ya hotuba ya Wizara yangu niliyoiwasilisha hapa Bungeni tarehe 7 mwezi Mei, 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja hizi zimechangiwa na Wabunge 145, ninawashukuru sana. Napenda kuliarifu Bunge lako kuwa Wizara yangu imechukua na itafanyia kazi ushauri na mapendekezo ya Waheshimiwa Wabunge pamoja na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ili kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa wananchi wote wa nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo kutokana na muda mfupi nilionao ninaahidi hoja zote tutazijibu kwa wananchi na kuwasilisha kwenu kupitia kwenye Hansard, na ninawaahidi Waheshimiwa Wabunge kwamba kabla hatujamaliza Bunge tarehe 29 Juni, 2018 Mwenyezi Mungu akitujaalia salama, basi majibu ya hoja zote mtakuwa mmeshayapata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Wakati na mimi naanza ubunge, naingia kwenye Bunge lako tukufu nilikutana na hoja ya dola milioni mia tano kutoka Serikali ya India lakini namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba nikiwa sasa kama Waziri wa Maji na Umwagiliaji hoja hii sasa imekamilika. Taarifa ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha kama ulivyoona wewe mwenyewe Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wote watakaoguswa na mradi huu wamefurahi. Kwa maana ya fedha hizi kwenda kugusa kwenye hii miji 17, basi zile fedha ambazo ilikuwa tuzipeleke tumege kwenye fungu hili tulilotenga kwa fedha za ndani kupeleka maeneo yale zitakuwa zimeokolewa na zinaweza zikapelekwa maeneo mengine. (Makofi

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nisome tu maeneo yatakayofaidika na hizi dola milioni 500 ambazo mkataba wetu wa kifedha utasainiwa kesho, ni pamoja na Muheza, Wanging’ombe, Makambako, Kayanga, Songea, Zanzibar, Korogwe, Njombe, Mugumu, Kilwa Masoko, Geita, Chunya, Makonde, Manyoni, Sikonge, Kasulu na Rujewa. Kwa hiyo, utaona fedha hizi itakapokuwa tumeanza kazi zitanufaisha wananchi wengi sana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe taarifa tu kwamba hiyo Kamati iliyoko India, pia ilichukua watumishi watatu wa Wizara yangu ya Maji na Umwagiliaji. Wakitoka huko watakuwa wameshakamilisha na mpango wote wa manunuzi. Kama unavyofahamu Wizara yangu na jinsi ninavyoipeleka, wakishasaini mkataba huo basi mimi mara moja kazi inaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya majibu ya hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji; Serikali kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo, inatekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo ilianza mwaka wa fedha 2006/2007 na itakamilika ifikapo mwaka 2025. Utekelezaji wa programu hii unahusisha programu ndogo tano ambazo ni usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji, huduma ya maji vijijini, huduma ya maji mijini, usafi wa mazingira mijini, kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira na kujenga uwezo wa kitaasisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, awamu ya kwanza ya programu hii ililenga kujenga miradi 1,810 na hadi sasa tumeshatekeleza miradi 1,469 ambayo imekamilika. Miundombinu ya maji iliyojengwa ina vituo vya kuchotea maji 102,586 ambavyo vina uwezo wa kuhudumia jumla ya wananchi 30,972,000 sawa na asilimia 85.2 iwapo kama vituo vyote vilivyojengwa vingekuwa vinatoa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vituo 86,877 tu ndivyo vinatoa maji, vituo vilivyobaki havitoi maji. Hivi ndivyo ambavyo vimeshusha asilimia ambayo tungetarajia kuipata sasa hivi. Tungetarajia kuwa na asilimia 85.2; lakini tuna asilimia 58 hadi 59.76. Sababu mbalimbali zipo ambazo zimefanya hivi vituo ambavyo vimeshajengwa kwa fedha hizi ambazo tulichangiwa na wahisani mbalimbai pamoja na fedha za ndani zimekuwa hazitoi maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa michango yenu Waheshimiwa Wabunge nimewasikiliza kwa umakini sana, ni kweli kwa Mheshimiwa Mbunge ambaye tumeenda kutekeleza mradi kwenye eneo lake na aliwaambia wananchi sasa mmeona nimeleta fedha, halafu leo hii yale maji hayatoki, kuna uwezekano mkubwa lile Jimbo ukaanza kulikimbia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimewasikiliza kwa makini sana Waheshimiwa Wabunge, na hasa kwa kuzingatia na mimi kwa sababu nasafiri kila eneo, sababu zote ambazo mmezitoa, mmetoa sababu nyingi kwamba hela inaliwa, uadilifu hakuna, hela inagawanywa, inapelekwa kule kwenye Halmashauri halafu inarudishwa Wizarani, siwezi kuwakatalia hilo kwa sababu hapa ushahidi upo kwamba tumetekeleza miradi, lakini kuna miradi mingine ambayo haitoi maji. Waheshimiwa Wabunge, niwape taarifa tu kwamba suala hili nilishaanza kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Rais, Rais huyu mimi huwa nawaambia watumishi kwamba ukitaka kutekeleza kazi vizuri tekeleza kwa Rais huyu, kwa sababu Mheshimiwa Rais yeye anapenda kazi, hana majungu, hana maneno na mimi kwa sababu ninamfahamu nilikuwa nimeshajiandaa. Mheshimiwa Naibu Waziri Kakunda amezungumza kwamba utaratibu wa utekelezaji wa miradi ya maji, Wizara yangu kazi yake ni kupanga bajeti, kutoa miongozo na maelekezo lakini utekelezaji unafanyw ana Wizara kutoa miongozo na maelekezo, lakini utekelezaji unafanywa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nimeshaifanyia kazi Ntomoko muda wote, kwa hiyo, pale Mheshimiwa Rais alivyosema Mheshimiwa Waziri najua unanisikia hawa watu wa watomokoe, saa 24 nilikuwa nimeshawatomokoa tayari kwa sababu nilielekezwa na Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu alienda Mara katika ziara yake akaniagiza kwamba fanya uchunguzi miradi yote ya Mkoa wa Mara na hata katika michango hii Waheshimiwa Wabunge wamelalamikia miradi iliyotekelezwa Mara. Natarajia ripoti ile imerudi na Mheshimiwa Waziri Mkuu nitamkabidhi ripoti hii Ijumaa. Waheshimiwa Wabunge lakini niseme tu kwamba yale maeneo yote tuliyotarajiwa kwamba tumepigwa wakandarasi wame-surrender wao wenyewe kwa barua kwamba, miradi hii wanaachana nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana nasema jamani tuna kiongozi mzuri, Mheshimiwa Rais kwa sababu anatenda haki. Hata yule ambaye alizowea tabia fulani sasa anaanza kukimbia mwenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema kwa ufanyakazi wangu a ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji nasema hili ni somo, kama yule ambaye ulikuwa unashirikiananae yeye mwenyewe ameanza kushtuka hivi wewe bado unabaki kuwa na akili hiyo? Itakuwa ni kitu cha ajabu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge tumekwenda mpaka kwenye Mradi wa Mugumu tumeufanyia kazi. Tumegundua matatizo yote yaliyojitokeza, lakini ule hatuwezi kuusimamisha, tunatoa kibali mkandarasi aendelee na kazi ili mradi ule ukamilike.

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo sababu mbalimbali ambazo zimetolewa na Waheshimiwa Wabunge, lakini pia, na Wizara yangu kuna sababu mbalimbali ambazo wameniambia. Hivi vituo vilivyojengwa vikatumia hela nyingi vimeshindwa kutoa maji, moja ya sababu ni kukauka kwa vyanzo vya maji. Hata hivyo kama Wizara tunajiandaa kuhakikisha tunatunza rasilimali zote za maji, tunazuwia kuvamiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana nikushukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri katika hotuba yako umezungumza kwamba, hata pale Songea sasa tunakwenda kulipa fidia. Tumeshajiandaa na tumetenga bajeti, Waheshimiwa Wabunge tunahitaji shilingi bilioni 18 ili tuweze kulipa yale maeneo yote makubwa, maeneo oevu ili yasiweze kuingiliwa na shughuli za kibinadamu. Tunayawekea sheria na tutawekea utaratibu na wale watakaokuwa wanayalinda, ili tuhakikishe kwamba, tunatunza rasilimali za maji, maana vinginevyo kila wakati tutakuwa tunatekeleza miradi halafu miradi ile inakuwa haileti tija inakauka, kwa hiyo itakuwa tumetumia fedha miradi inakuwa haitoi maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, uchaguzi wa teknolojia. Umetekeleza mradi kijijini bila kupima uchumi wa eneo lile, unapeleka generator ya kutumia dizeli, wananchi wanafika mahali hawawezi. Vyombo vya watumiaji maji tunavyoviunda hivi bado hatujaviimarisha, lakini tunaendelea kuwafundisha ili wawe na uwezo wa kusimamia hii miradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niishukuru sana TAMISEMI wanaendelea kuvisajili na kuvifundisha, na mimi kazi yangu ni kutoa fedha ili waendelee kutoa elimu kwa hivi vyombo vya watumiaji maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakiri, kama walivyosema Waheshimiwa Wabunge, miradi mingi haikusanifiwa vizuri na ndio maana imetupeleka huko ilikotupeleka; tumepoteza fedha. Hata hivyo tayari mwaka huu nimeshaunda timu ya wahandisi ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na wanaanza kufanya kazi. Wahandisi hao watapitia usanifu wote wa kwenye halmashauri hata wataalam washauri watakaonunuliwa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maji, wakishakamilisha wataalam hawa waandisi tutahakikisha kwamba, wanapitia zile nyaraka, ili tuweze kuokoa fedha, value for money lazima ipatikane.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kumekuwa na muingiliano ambao unatusumbua kama Serikali. Hapa panasimamiwa na taasisi hii, pengine TAMISEMI, huku wanasimamia Wizara, huku anasimamia Mhandisi Mshauri ambaye ameajiriwa na analipwa pesa, hawa watu wanatuchanganya, tunataka kutengeneza mfumo ambao utasimamiwa na mtu mmoja ili kama tunamlaumu tunamlaumu mtu mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kupata hoja nyingi za ubadhirifu wa fedha kwenye miradi ya maji, katika huu muda wa siku tatu ilikuwa tukitoka hapa tunakwenda kukaa na Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo, namshukuru sana na tarehe saba tulivyomaliza hotuba hapa nilikwenda kukaa na wafadhili, kumbe na wafadhili nao lilikuwa linawauma, wameafiki kwamba kuna haja ya kuunda timu ya wataalam watakaopitia miradi yote iliyotekelezwa, kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge mnapendekeza. Mlipendekeza kwamba iingie Kamati ya Bunge, lakini kabla hamjafika hapo sisi tayari tumeshaunda kamati na kamati hii itasimiwa na Profesa Mbwete wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaendelea kujaza wataalam ili tuhakikishe kwamba miradi yote iliyotekelezwa katika programu hii iliyoanza mwaka 2006/2007 inapitiwa, na Waheshimiwa Wabunge tutatumia sheria, tutatumia nyenzo zote ambazo zimewekwa na Serikali. Mheshimiwa Rais
amesema jamani hela ya maji awamu hii ni sumu, kama kuna mtu alihujumu basi wakati wake umefika.

Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi ndugu zangu na kwa umri nilio nao kwa kweli sina huruma na mtu ambaye ni mwizi na niko hivyo hata huko nilikotoka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni imani yetu kwamba Kamati hii itafanya kazi kwa uadilifu, na nitaisimamia, na tunaendelea kuchagua watu ninawajua, waadilifu ninawajua wako wengi tu ambao tutawaweka pale. Kwa hiyo, ninachowaomba Waheshimiwa Wabunge, naomba sana watakapokuja kwenye Halmashauri zenu, kwenye maeneo yenu muwape support kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia ninawaomba Waheshimiwa Wabunge, sisi ni Madiwani. Baada ya bajeti hii kupita wanapokwenda kutenegeneza mipango kazi kwenye halmashauri na sisi tuwepo, ni muhimu sana hili. Kwa sababu, wakati mwingine napata shida nakwenda kwenye halmashauri nakwenda na Mheshimiwa Mbunge, tunafika kule wakati wanapanga mpango kazi kumbe hata sisi madiwani hatukuwepo, wote tunakuwa wageni, naomba tushirikiane.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nikija kwenye jimbo lako nataka nipate taarifa kutoka kwa wewe Mbunge, kwamba hapa kuna hili, ili niweze kufanyia kazi kwa sababu na mimi ni mtaalam. Naomba sana Waheshimiwa Wabunge ushirikiano wenu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka kwenye bajeti ya mwaka jana niliwaambia Waheshimiwa Wabunge, ndiyo maana tunawapa hivi vitabu vya bajeti. Tukishakamilisha hii bajeti Waheshimiwa Wabunge na ninawaomba sana, muipitishe, ili tutekeleze miradi ya maji baada ya hapo mwambie Mkurugenzi wako wa Halmashauri una shilingi kambi katika mwaka ujao wa fedha ili aanze kujipanga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wengi wameonesha kwamba, fedha hazijatengwa, akiwemo mama yangu Mheshimiwa Magdalena Sakaya, nitakuonesha hela yako iko wapi kwenye kitabu bila wasiwasi wowote. Una fedha ya kutosha imetengwa, hatuwezi kuacha Halmashauri ya Kaliua. Nchi hii Rais ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ndio Rais wa Watanzania. Ni Rais ambaye ametokana na chama tawala, Chama cha Mapinduzi, kwa hiyo, wananchi wote hawana mtu mwingine atakayewahudumia ni Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge katika Bunge la mwaka jana walimuelekeza Waziri wa Maji na Umwagiliaji aangalie uwezekano wa kuunda Wakala wa Maji Vijijini. Ninaomba kutoa taarifa kwamba tumefanya kazi hiyo mliyotuelekeza, tumeshirikiana kati ya Wizara yangu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Ofisi ya Rais, Utumishi na Wizara ya Fedha na Mipango, tayari tuliunda kamati imeanza kuangalia uwezekano wa kuunda taasisi hii muhimu sana ya Wakala wa Maji Vijijini. Tumeshafika hatua ya mbali kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, strategic plan tayari, business plan tayari imeshaandaliwa, framework document tayari imeshaandaliwa, establishment order nayo imeshaandaliwa tayari. Kwa hiyo, taratibu za kisheria zinaendelea, lakini pia sasa tunaingia kupata maoni ya wadau kwa mujibu wa taratibu na tunatumia sheria ya uanzishwaji wa wakala Executive Agency Act, Cap. 245. Tutafika stage ambayo tutaomba ridhaa ya mamlaka husika, ili uweze kuanzisha huu wakala. Kwa hiyo, yale mliyoelekeza Waheshimiwa Wabunge tayari tumeshaanza kuyafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Waheshimiwa Wabunge walipochangia sana hotuba hii, na nishukuru kwa kweli Waheshimiwa Wabunge wamechangia na mimi nimefuatilia sana. Kulikuwa na tofauti kubwa za kitakwimu kati ya kitabu kilichoandikwa na Wizara ya Maji, lakini pia na kitabu kilichotolewa na Hoja za Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna tofauti ya kitakwimu kuhusu fedha za maendeleo zilizopokelewa na Wizara kati ya Taarifa ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa iliyopo katika Hotuba yangu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019. Tofauti hiyo imetokana na muda wa kuwasilisha Taarifa hizo. Nirudie tena, tofauti hiyo imetokana na muda wa kuwasilisha taarifa hizo, hadi tunakutana na Kamati mwezi Machi, fedha zilizopokelewa kwa Fungu 49 zilikuwa sawa na asilimia 22 kama Taarifa ya Kamati ambavyo ilikuwa imeelekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tunakamilisha maandalizi ya hotuba ya bajeti hadi tunakutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mwezi Mei, 2018 Wizara ilishapokea fedha zaidi, hivyo tuliona ni muhimu kutoa taarifa hadi kipindi hicho kwa sababu Hazina tayari walishatuletea fedha nyingine. Taarifa iliyowasilishwa katika Kamati mwezi Machi ilijumuisha fedha za nje zilizopokelewa kutoka hazina kwa njia ya exchequer pekee. Aidha, kuna fedha za wafadhili ambazo hupelekwa moja kwa moja katika miradi ya maendeleo kabla ya kuingizwa kwenye exchequer.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha hizi zinapelekwa kwenye miradi mbalimbali baada ya utekelezaji ambapo badaye baada ya mwaka Hazina huwa wanaziingiza kwenye exchequer. Lakini kwa sababu tulikuwa tunaendelea kukusanya taarifa baada ya kupata taarifa hizo tulilazimika kuingiza hizo fedha na baadae kuwasilisha kwenye Kamati ya Bajeti. Baada ya kuziingiza sasa tukawa tumepata, sasa fedha ambazo tulikuwa tumezipata hadi mwezi Mei ni shilingi bilioni 359.9 ambayo inafanya sasa fedha ambazo zimetolewa na Serikali hadi kufikia mwezi Mei ni asilimia 56. (Makofi)

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge hiyo ndio tofauti ambayo tumeiona kati ya Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na taarifa ambayo tumeitoa mwishoni kwa sababu ilibidi tukiri fedha ambazo tayari tumeshapewa na Waziri wa Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kuishukuru sana Kamati yangu ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Tumefanya ushirikiano kwa muda mfupi, lakini tumefanya mengi. Tangu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iundwe au iteuliwe mwezi Machi, 2018 Wizara yangu imeshakutananayo mara tatu, tarehe na ajenda tulizojadili tulipokutana ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya tarehe 26 na tarehe 27 Machi, tulikutana na Kamati ili kupokea na kujadili na kupitisha bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka 2018/2019; tarehe 7 Aprili tulikutana na Kamati kupokea taarifa kuhusu utendaji wa Tume ya Umwagiliaji, lakini tarehe 20 Aprili, 2018 tulikutana na Kamati kwa ajili ya kupokea Taarifa Kuhusu Utendaji wa DAWASA na DAWASCO na mchakato wa kuunganishwa kwa taasisi hizi mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kikao cha kujadili taarifa ya utendaji wa DAWASA na DAWASCO Wizara iliwasilisha kwa kina taarifa ya uamuzi wa Serikali wa kuunganisha taasisi za DAWASA na DAWASCO na hatua iliyofikiwa katika mchakato huu. Ilielezwa kuwa kuanzia tarehe 01 Julai, mwaka 2018 Shirika la DAWASCO litakoma na kutabaki na Shirika moja la DAWASA lililofanyiwa maboresho ya kimuundo na majukumu. Hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, kuandaliwa kwa kuundo na majukumu mapya ya DAWASA; mbili kuandaliwa kwa muundo na utumishi wa DAWASA; lakini tatu ni kuandaliwa kwa muundo na mishahara ya DAWASA na nne ni kuandaliwa kwa orodha ya kazi, maelezo ya kazi na kanuni za utumishi za DAWASA. Pia namba moja hadi nne tayari zimeshawasilishwa kwa Msajili wa Hazina na Utumishi kwa ajili ya idhini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kufanya tathmini ya madeni na mali za DAWASA na DAWASCO; Kamati maalum iliundwa kufanya kazi hii na imemaliza kazi yake na imewasilisha taarifa yake jana kwa Katibu Mkuu, jana tarehe 8 Mei, 2018. Kwa sababu hizi taasisi mbili zinaungana kwa hiyo, lazima kubainisha madeni ambayo taasisi zinadaiwa na madeni ambayo taasisi zinadai.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kukamilisha mchakato wa kuunganisha DAWASA na DAWASCO ni pamoja na; kuandaa De- Establishment Order ya DAWASCO kwa sababu tarehe 01 DAWASCO itakoma; kuunda Bodi ya DAWASA, kufanya marekebisho ya Sheria ya DAWASA ya mwaka 2001 na ile ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009 kwa sababu hatuwezi kuwa na sheria mbili wakati taasisi hizi zinafanya kazi moja. Hatua zote hizi zinakwenda vizuri kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika mchakato wote huu wafanyakazi wa DAWASA na DAWASCO kupitia vyama vyao vya wafanyakazi pamoja na wafanyakazi wote kwa ujumla wao wameshirikishwa kikamilifu. Hakuna taharuki yoyote inayotokana na mchakato huu katika Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa taasisi hizi mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo taarifa ya Kamati imekiri kwa kuishukuru Wizara katika taarifa yake ukurasa wa 52 kwa ushirikiano mkubwa ambao imekuwa ikiupatia Kamati yangu tangu Kamati ilipoteuliwa mwezi Machi, 2018. Wizara yangu itaendelea kuipa Kamati ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kibunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na changamoto pia ambazo zilikuwa zimeainishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, lakini hoja hizi ambazo ziliibuliwa wakati tunapitia kutafuta majibu tumekuja kukuta kwamba ni hoja ambazo pia zilikuwa zimeibuliwa na CAG. Sasa kwa sababu zimeshaibuliwa na CAG, na kwa mujibu wa taratibu hoja zimeibuliwa na CAG na zikaletwa katika Bunge, ninamuagiza Katibu Mkuu na nifurahi tu kwamba, majibu tayari wameshajibu sasa wanasubiri taratibu za kiserikali kwa ajili ya kuitwa na kupeleka PAC.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimuagize Katibu Mkuu ahakikishe kwamba hoja hizi zipelekwe, ili kwa mujibu wa sheria iliyopo hoja zikishaibuliwa upo utaratibu maalum ambao unatumiwa, ili kuweza kuzifikisha kwenye Kamati ya PAC na baadae sasa ndio zitatolewa majibu kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Maji pia ina tume ya umwagiliaji, Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA imekamilisha kuandaa upya mpango kabambe wa umwagiliaji. Mpango huu umeweka dira, malengo na mikakati ya kuendeleza sekta ya umwagiliaji kati ya mwaka 2018 hadi mwaka 2035. Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia hali ya upatikanaji wa rasilimali maji katika mabonde tisa na umeainisha kwa karibu na malengo ya Programu ya Pili ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo. Tunaamini utekelezaji wa mpango huo utahusisha na kuinua sekta ya umwagiliaji hapa nchini. Tukishakuwa na umwagiliaji maana yake ni kwamba kilimo chetu kitakua, kilimo kitakuwa na uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, utafiti uliofanywa na timu hii ya Wajapan imebainisha mambo mengi sana. Tumekuwa na scheme za umwagiliaji ambazo zinafanya kazi mara moja kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge wamesema ni kweli, zinafanya kazi mara moja kwa sababu zilijengwa bila kujengewa chanzo cha maji. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge nina imani taarifa hii inakabidhiwa mwezi Mei na baada ya hapo sasa tutatoa taarifa rasmi kwa Kamati yetu ili pengine kwa jinsi itakavyoamua Kamati tunaweza kuja kutoa taarifa katika Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia miradi ya maji mijini tunaendelea kutekeleza. Mfano Jiji la Dar es Salaam na nishukuru sana na Mheshimiwa Naibu Waziri wangu amezungumzia. Jiji la Dar es Salaam tumetengeneza miradi mikubwa kwenye vyanzo vya maji vya Ruvu Juu na Ruvu Chini na maji sasa yanapatikana yapo kwa wingi. Kitu kilichobaki ni kuhakikisha kwamba tunaweka miundombinu ya kutosha ili tuweze kuyasambaza maji kwenda kwa wananchi na tayari tumeshaanza. Serikali imefanya utafiti, imefanya utafiti/study na kuona kwamba tunahitaji dola milioni 100 ili tuweze kukamilisha kusambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa kwanza wa dola milioni 32 umeanza na unakaribia kukamilika. Baada ya muda mfupi tumepata tena dola milioni 45 ambayo tunakaribia kutangaza tender ili tuendeleze kusambaza mabomba kwenye maeneo mengine ambayo bado hayajapata huduma ya maji safi na salama katika jiji la Dar es Salaam. Kwa kufanya hivyo Waheshimiwa Wabunge ni kwamba pia tutapunguza na upotevu wa maji na tunaendelea kutafuta teknolojia nzuri na tunafanya trial mbalimbali kama Mji wa Tanga kwa sasa, bomba likivuja ule mtandao wa bomba umeainishwa kwenye simu yako ya mkononi, kwa hiyo itakuwa ni rahisi ku-detect sasa kama maji yanavuja ni rahisi kutuma wataalam waende wakaone hapo kuna nini, kuna wizi na kuziba ili tuendelee kupunguza upotevu wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru tena sana Waheshimiwa Wabunge sipendi tena nipigiwe kengele kwa sababu kengele ya kwanza imeshapiga, lakini niwashukuru sana Wabunge kwa michango yao na niseme nitaendelea kama nilivyo tabia yangu napenda kuongea na Mbunge yeyote aniambie hoja moja kwa moja na nilivyo ukiniambia naifuatilia na lazima nitakuja hata kwenye jimbo lako ili tuizungumze ili niweze kuifikisha katika Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba sana Wabunge, Wizara yangu kwa kweli kama mlivyosema ninyi wenyewe ina mapenzi mazuri kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji safi na salama.

Ninaomba mtupitishie bajeti hii ili tuweze kuendelea kupambana kwa kushirikiana na ninyi na taasisi mlizonazo kwenye majimbo ili tuweze kupata maji safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maneno haya naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye kwa rehema zake nyingi ametujali afya njema na kutuwezesha kukutana katika Bunge hili Tukufu la Bajeti ili kuweza kukamilisha kazi tuliyoianza tarehe 9 Mei 2019 ambapo niliwasilisha hoja hii.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge na Katibu wa Bunge kwa kusimamia kwa ufanisi mkubwa majadiliano yote kwenye Mkutano huu wa Kumi na Tano wa Bunge hili tukufu.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee napenda pia kumpongeza Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake anaoendelea kutuonyesha wasaidizi wake katika majukumu yetu ya kila siku Bungeni.

Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii pia kuwashukuru Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati zote za Bunge kwa kufanya kazi kwa karibu na Wizara yangu. Kipekee nimshukuru Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso, pamoja na Wajumbe wake ambao wameiongoza Wizara vizuri katika utekelezaji wa miradi ambayo imeainishwa kwenye Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Ninaahidi kwamba Wizara ninayoiongoza itafayafanyia kazi masuala yote yaliyoshauriwa na Kamati hizo.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kumshukuru Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa maoni, ushauri na mapendekezo yake kuhusu bajeti ya Wizara yangu.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kuwatambua Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia katika bajeti yangu. Waheshimiwa Wabunge 18 walichangia wakati wa majadiliano ya hoja ya Waziri Mkuu, Waheshimiwa Wabunge 91 wamechangia kwa kuzungumza katika bajeti hii inayoendelea na Waheshimiwa Wabunge 66 wamechangia kwa maandishi wakati wa majadiliano ya hoja ya Wizara yangu. Nawashukuru sana kwa michango yao.

Mheshimiwa Spika, hivi punde Waheshimiwa Naibu Mawaziri wa Wizara yangu wameanza kujibu baadhi ya hoja za Waheshimiwa Wabunge kwa kuzingatia maeneo ya kisekta (sekta ya ujenzi na sekta ya mawasiliano na uchukuzi). Niwashukuru sana kwa jinsi ambavyo wamejibu baadhi ya hoja za Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, naomba nihitimishe kwa kujibu hoja za kisera pamoja na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizojitokeza. Naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba Wizara itajibu hoja zote za Wabunge kwa maandishi na kuwapatia Waheshimiwa Wabunge wote majibu ya hoja hizo kwa njia ya kitabu kitakachoandaliwa kabla ya hitimisho la Mkutano huu wa Bunge la Bajeti.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo wote tunafahamu, mkataba wa miaka mitano kati ya wananchi na Serikali waliyoichagua ni kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 ambayo itahitimishwa mwaka 2020. Baadhi ya ahadi zilizomo kwenye Ilani ya Uchaguzi ni pamoja na ujenzi wa reli ya SGR, ukarabati wa reli ya kati, ukarabati wa bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga, ufufuaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), ukamilishwaji wa barabara zinazounganisha mikoa, uboreshaji wa mawasiliano nchini na ufufuaji wa Kampuni ya Meli. Ahadi hizi zinatokana na kilio cha muda mrefu cha Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili tukufu ambao wamekuwa wakiishauri na kuitaka Serikali kuwa na miradi ya vipaumbele na kuitekeleza ili nchi iweze kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye uchumi wa kati.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hayo, ndiyo maana sehemu kubwa ya bajeti ya maendeleo imeelekezwa kwenye Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na hata leo ameongeza zaidi ya shilingi bilioni 90 kwenye Wizara hii. Hii ni kutokana na majukumu makubwa ambayo Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeyabeba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa inakaribia kukamilisha ahadi ilizozitoa kupitia Ilani yake ya Uchaguzi. Napenda kulihakikishia Bunge lako tukufu kwamba, nikiwa mwakilishi wa Mheshimiwa Rais kwenye eneo la Sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikiana na Naibu Mawaziri pamoja na Wataalam wa Wizara tutaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na ahadi alizozitoa Mheshimiwa Rais zinazohusu Sekta hii ili kufikia mwisho wa mwaka 2020 ziwe zimekamilika.

Mheshimiwa Spika, aidha, tutaendelea kupambana na kuzitatua kero za wananchi zitakazojitokeza wakati tukiendelea na utekelezaji wa Ilani hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusu deni la makandarasi, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2018 madeni ya makandarasi na Wahandisi Washauri yalikuwa shilingi bilioni 833 ambayo yalivuka na kuingia mwaka wa fedha 2018/2019. Katika mwaka wa fedha 2018/2019 makandarasi waliendelea kutekeleza miradi na kuzalisha hati za madai mpya, Serikali imekuwa ikiendelea kulipa madeni ya makandarasi na wahandisi elekezi ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2019 deni lilikuwa shilingi bilioni 962.

Mheshimiwa Spika, naomba kulitaarifu Bunge lako tukufu kwamba Wizara ya Fedha na Mipango hadi mwezi huu Mei itakuwa imelipa shilingi bilioni 609. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa jinsi ambavyo ameitikia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuhakikisha kwamba katika mwaka huu wa fedha, tutakapoingia mwaka mpya wa fedha tena hatutavuka na deni kubwa, na kwa jinsi hiyo basi miradi yote ambayo tumeiainisha kuanza katika mwaka ujao wa fedha tutaanza kuitekeleza bila wasiwasi wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia sana kuhusu deni la TAZARA, lakini pia kwenye Taarifa ya Kambi ya Upinzani walizungumzia deni la TAZARA ambalo linaonekana kufikia shilingi bilioni 434. Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha amejaribu kulifafanua deni hili, lakini moja tu nizungumzie kwamba, Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge deni hili unapolizungumzia ni deni la nchi mbili, ni deni la Tanzania pamoja na Zambia. Katika deni hili ukiliangalia shilingi bilioni 237 ni deni ambalo limetokana na Itifaki ya Serikali ya China, kwa hiyo, itifaki hii inahusisha pia upande wa Zambia, lakini nishukuru kwa madeni ambayo yanatuhusu sisi huku yakiwepo malipo ya wastaafu Mheshimiwa Waziri wa Fedha ameyaelezea vizuri.

Mheshimiwa Spika, katika michango ya Wabunge, wamezungumzia kwa uchungu sana kuhusiana na utaratibu wa majadiliano yanayoendelea kati ya Serikali na Mwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo. Nilichojifunza kwa Waheshimiwa Wabunge ni kwamba Serikali ifanye haraka kuhakikisha kwamba majadiliano hayo yanakamilika.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa kwamba majadiliano yangali yanaendelea, lakini kuna baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walisema kwamba Serikali imekataa, sina taarifa ya hilo. Na baada ya kumaliza Bunge nilijaribu kuwasiliana na Mamlaka kuulizia kama majadiliano yameshafikia ukomo lakini ni kwamba majadiliano yanaendelea. Ila ni kweli kwamba yamechelewa kutokana na masharti ambayo yanaonekana hayana manufaa kwa upande wa Serikai ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba Waheshimiwa Wabunge waridhie kwamba Serikali bado inaendelea na majadiliano na Bunge lako tukufu limekuwa muda mrefu linaishauri Serikali isije ikaingia mikataba ambayo haina maslahi kwa umma. Kwa hiyo, Serikali inaendelea na pale itakapokuwa imefikia ukomo wa yale majadiliano, nikuahidi tu kwamba Serikali itatoa taarifa kwa Waheshimiwa Wabunge ili na wao waweze kutoa mawazo yako. Kwa hiyo, niseme tu kwamba bado tunaendelea na majadiliano kuhusiana na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 15 wa kitabu cha bajeti ulizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara (express way) ya Dar es Salaam – Chalinze. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia TANROADS ilimwajiri Mhandisi Mwelekezi (Transaction Adviser) kutoka Korea. Transaction Adviser huyu aliajiri makampuni mengine 11 yenye uzoefu na utaalam na miradi ya PPP kutoka duniani kote ili kuishauri Serikali namna bora ya kutekeleza mradi wa Dar es Salaam – Chalinze (express way) kwa utaratibu wa Public Private Partnership, alimaliza kazi hiyo mwezi Desemba, 2016.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya PPP Wizara ya Fedha na Mipango ilitoa idhini tuendelee na hatua zingine za utekelezaji tarehe 22 Mei, 2017. Aidha, wakati idhini ya Wizara ya Fedha na Mpango inatolewa tayari Serikali ilishaanza juhudi za kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam, ambazo ni ujenzi wa bandari kavu ya Ruvu, ukarabati wa reli ya meter gauge na ujenzi wa reli ya SGR. Hivyo, busara ya Serikali zilipelekea kuamua kufanya mapitio upya ya taarifa ya upembezi yakinifu ili kupunguza madhara (risk) ambayo yangehamia upande wa Serikali kumlipa mwelekezi ambaye angejitokeza kuwekeza katika mradi huu kwa kuwa magari ya kubeba mizigo yangeanzia Ruvu badala ya kuanzia bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa usanifu wa mradi huu wa express way ilikuwa ni kwamba barabara inakwenda kuanzia bandari ya Dar es Salaam na kwamba ilikuwa inategemea tozo sasa za magari ambayo yatakuwa yanabeba mzigo kuanzia bandari ya Dar es Salaam. Lakini sasa hapa katika kwa sababu study zote zilikuwa zinaendelea, SGR na baada ya kuonekana kwamba bandari ya Dar es Salaam sasa imekuwa na mizigo mingi uwezo wake utapungua ndiyo tukaamua kujenga bandari ya Kwara. Ukiangalia study hiyo sasa inabidi irudiwe kwa sababu kama mwekezaji alikuwa anategemea tozo zake azipate kutoka kwenye magari ni lazima hiyo iweze kurudiwa ili kuona kama bado tunaweza tukachukua mkopo kwa mwekezaji na kwamba mkopo huu utalipwa katika muda unaostahiki.

Mheshimiwa Spika, hilo ndiyo ambalo limefanya kwamba, kwa sababu tunaendelea na ujenzi wa SGR na ambao tunategemea itabeba zaidi ya tani milioni 17 kwa mwaka, wakati huo huo tumejenga dry port ya Kwara na kwamba SGR ikishafika Morogoro tunatarajia kujenga tena dry port nyingine Morogoro kwa hiyo, ikiwa kwamba zile parameters ambazo zilikuwa zimetumika, wakati wa kusanifu huo mradi wa express way ziweze kurejewa tena ili tuweze kupata mradi ambao utakuwa na manufaa. Sambamba na hilo, Serikali imefanya maamuzi inajenge Kilometa 19.2 barabara nane ambao na tayari mradi umeshaanza, kwa hiyo, yote hayo inabidi yarejewe ili kuona kwamba kama mradi huo tutautekeleza utaendelea kuwa na manufaa.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia pia kuhusu ujenzi wa viwanja wa ndege vya Kigoma, Sumbawanga, Tabora na Shinyanga. Mikataba ya ujenzi wa viwanja vya ndege vya Sumbawanga, Tabora, Shinyanga na Kigoma ilisainiwa tarehe 30 Juni, 2017 kati ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na wakandarasi wa ujenzi chini ya ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya. Utekelezaji wa miradi hii umechelewa kuanza kwa kuwa baada ya Serikali kuhamisha miradi ya ujenzi wa viwanja vya ndege kupeleka Wakala wa Barabara, mambo yafuatayo yalijitokeza na ambayo yamechelewesha utekelezaji wa mradi huu.

Mheshimiwa Spika, moja, mfadhili ambaye ni Benki ya Uwekezaji ya Ulaya alitaka kujua taarifa juu ya mtekelezaji mpya wa mradi huu yaani TANROADS. Serikali ilielekeza kuwa TANROADS ni Idara ya Serikali inayoaminika Serikali na imetekeleza miradi mbalimbali ya wafadhili, pia imepata Hati safi za ukaguzi kwa miaka saba mfululizo. TANROADS imekuwa ikifanya manunuzi makubwa ya Taasisi nyingine kama vile TACAIDS na ujenzi wa zahanati zinazofadhiliwa na washirika mbalimbali wa maendeleo. Baada ya maelezo hayo ya Serikali, mfadhili alielewa na kukubali kwamba kazi ile sasa isimamiwe na Wakala wa Barabara.

Mheshimiwa Spika, kinachoendelea sasa hivi imebidi ku-review sasa ile Financing Agreement ili kuondoa TAA na kuweka TANROADS ili sasa no objection iweze kutoka. Sasa hivi kwa mujibu wa taarifa za Hazina ni kwamba shughuli hii ya ku-draft hiyo document ya Financial Agreement kwa kuweka TANROADS na kuondoa TAA iko kwenye hatua za mwisho kwa sababu taratibu hizi za mikopo zina taasisi nyingi za kupitia ndiyo maana uchelewaji umekuwa mkubwa. Niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge hasa kwenye haya maeneo ambayo yamekuwa earmarked Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga kwamba miradi hii Waheshimiwa Wabunge itatekelezwa tuko kwenye hatua ya mwisho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia kwamba katika miaka mitatu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya kimkakati. Wakataka kujua sasa kwanza impact ya utekelezaji huo, nishukuru kwamba jibu hilo amelijibu Mheshimiwa Waziri wa Fedha alipopewa zile dakika zake 10. Ziko faida nyingi siwezi kuzirudia lakini Mheshimiwa Waziri wa Fedha ameshazizungumzia.

Mheshimiwa Spika, nitaomba nizungumzie kidogo kuhusu local content. Katika mradi wa SGR makubaliano kati ya Serikali na mkandarasi kuhusu ujenzi wa mradi huu, ni kwamba asilimia 35 ya malipo yanayolipwa kwa mkandarasi yafanyike kwa fedha za ndani. Lengo ni kuhakikisha kwamba, mkandarasi anatumia siyo chini ya asilimia 35 ya fedha zote za mradi katika matumizi ya rasilimali za ndani.

Mheshimiwa Spika, malighafi kama kokoto, mchanga, nondo na saruji anavyovitumia mkandarasi vyote ni vya ndani ya nchi. Aidha, matengenezo na uzalishaji wa mataruma ya zege unaofanyika hapa nchini katika Kambi za Soga na Kilosa unatumia malighafi za humu nchini. Kiasi cha saruji kinachotarajiwa kutumika katika kipande cha Dar es Salaam hadi Makutopora kwa mujibu wa mkataba ni mifuko ya cement au ya saruji 9,200,000 sawa na tani 460,000 za saruji. Kwa upande wa chuma, kiasi tani 115,000 zitatumika kutoka viwanda vya ndani. Chuma cha reli kinachotoka Japan ni asilimia 5.2 tu ya thamani ya mradi na hii ndiyo fedha ambayo tunaitoa kwenda kupeleka nje kwa hiyo ni asilimia 5.2, kwa hiyo asilimia kubwa inabaki hapa ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, mradi utatumia mataruma 1,204,000 ambayo ni asilimia 5.6 ya thamani ya mradi wote wa malighafi zake zote zinatoka hapa nchini na zinazalishwa hapa nchini maana yake zinatumia nondo za hapa nchini, zinatumia mchanga hapa nchini, cement hapa nchini pamoja na kokoto ni hapa hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati kadhaa za Bunge lako tukufu zimetembelea maeneo haya na kujionea uzalishaji unavyofanyika kwa kutumia malighafi zinazozalishwa ndani ya nchi. Licha ya malighafi karibu zote zinazotumika katika mradi huu kuwa za ndani ya nchi ukitoa reli yenyewe ambayo inaagizwa kutoka Japan kwenye kiwanda pekee kinachotoa reli za viwango vya juu, asilimia 20 ya wataalam wabobezi katika mradi huu ni wazawa, na kwamba asilimia 80 ya wataalam wa kati na nguvu kazi ni Watanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa jumla ya wazawa 14,140 wamepatiwa ajira katika mradi huu ambapo asilimia 90 ni Watanzania. Ukiacha wananchi wengine wanaojihusisha na shughuli zisizo rasmi katika maeneo ya mradi, hii ina maana kwamba malipo ya watumishi hawa kiasi cha shilingi bilioni 5.2 kwa mwezi, sawa na shilingi bilioni 62 kwa mwaka ni fedha zinazotumika ndani ya nchi moja kwa moja kutoka kwa watu ambao wameajiriwa kwenye mradi. Aidha, wakandarasi zaidi ya 500 wadogo wadogo wa ndani wamepewa kazi katika mradi huu, baadhi ya kazi hizo ni pamoja na za ujenzi, ugavi na utoaji wa huduma mbalimbali ambapo wote hawa wanalipwa na fedha za mradi huo.

Mheshimiwa Spika, mbali ya faida zilizoanza kuonekana katika hatua ya ujenzi, manufaa makubwa ya mradi yataanza kupatikana baada ya ujenzi kukamilika. Mradi wa SGR unatarajiwa kuhudumia tani milioni 17 za mizigo kwa mwaka, mizigo hii ni pamoja na ile ya nchi za jirani zisizo na bandari za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa upande wa miradi ya barabara, viwanja vya ndege, majengo na vivuko katika mwaka wa fedha 2015/2016 hadi mwaka 2017/2018 jumla ya miradi 4,816 imetekelezwa na makandarasi wazawa na miradi 116 imetekelezwa na makandarasi wa nje. Aidha, jumla ya ajira 362,854 zilizalishwa katika sekta ya ujenzi katika miaka hiyo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017 jumla ya ajira 109,846, mwaka 2017/2018 jumla ya ajira 116,864 na mwaka 2018/2019 jumla ya ajira 136,144 zimezalishwa katika maeneo mbalimbali ya ujenzi ikiwemo miradi ya barabara, miradi ya viwanja vya ndege, miradi ya vivuko na miradi ya ujenzi wa majengo ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nizungumzie kuhusu Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), mpaka sasa Serikali inatoa huduma kwa kutumia ndege mpya sita (6) zilizonunuliwa na Serikali kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika, ndege tatu aina ya Bombadier Q4100-8 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, ndege mbili (2) aina ya Air Bus A2200-300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja na ndege moja aina ya Boing 787-8 Dream Liner yenye uwezo wa kubeba abiria 262. Aidha, ATCL imekabidhiwa na Mheshimiwa Rais ndege mbili zifuatazo; moja aina ya Foker 50 yenye uwezo wa kubeba abiria 44 na ya pili aina Foker 28 yenye uwezo wa kubeba abiria 70.

Mheshimiwa Spika, pia ATCL inatarajia kupokea ndege aina ya Bombader–8 mwezi Novemba mwaka huu 2019 na Boeing 787 Dream liner ambayo inatarajiwa kupokelewa Januari, 2020. Ili kuendelea kuiongezea uwezo ATCL, Serikali imetenga fedha katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2019/2020 kununua ndege nyingine moja aina ya Bombardier Q4100-8 na ndege mbili aina ya Airbus. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ATCL kwa kutumia ndege sita zinazotoa huduma kutoka Dar es Salaam kwenda katika vituo 10 ndani ya nchi vikiwemo Bukoba, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar na vituo vitano nje ya nchi ambavyo ni Bujumbura, Entebbe, ….Harare na Lusaka. Aidha, ATCL inatarajia kufungua kituo cha Johannesburg mwezi Juni, 2019, Mumbai mwezi Julai, 2019 na Kituo cha Guangzhou kabla ya mwisho wa mwaka wa 2019. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa kuwa na safari zinazounganisha Mji wa Dodoma na sehemu nyingine za nchi, ATCL kufuatia maombi ya Waheshimiwa Wabunge imeamua kuifanya Dodoma kuwa sub-hub. Aidha, ATCL inaangalia sasa uwezekano wa kuanzisha safari za kutoka Dodoma kwenda KIA, kutoka Dodoma kwenda Mbeya, kutoka Dodoma kwenda Mwanza na kutoka Dodoma kwenda Zanzibar. Sambamba na vituo hivyo, ATCL ipo kwenye maandalizi ya mwisho ya safari za kwenda Mkoa wa Katavi Mji wa Mpanda na kuangalia uwezekano wa kuanzisha safari kati ya Dar es Salaam na Tanga kupitia Pemba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamekuwepo na dhana kwamba ununuzi wa ndege na gharama za awali na uwekezaji katika mifumo, mitambo na miundombinu zimehamishiwa kwenye Fungu 20, yaani Ikulu. Suala hili siyo la kweli kwa sababu gharama hizo zimetengewa fedha katika Fungu 62 ambalo ni la Sekta ya Uchukuzi. Aidha, gharama za uendeshaji wa ATCL zinatokana na mapato ya ndani ya kampuni kama inavyooneshwa katika hesabu za ATCL zinazokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, ununuzi wote wa ndege unafanywa na Wizara yangu ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na ni Fungu 62 ambalo linapitishwa na Bunge lako Tukufu; na hata katika bajeti hii tunaomba mpitishe shilingi bilioni 500 ili tuweze kununua ndege nyingine tatu ambapo moja itakuwa ni Bombardier na mbili ni Airbus. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa wataalam marubani, ni kweli kwamba uwiano wa marubani wenye leseni katika nchi yetu kwa sasa ni asilimia 49:51 ambapo wazawa ni asilimia 49 na wageni ni asilimia 51. Hata hivyo, Serikali ina mikakati ya kuongeza marubani wazawa kwa kuwasomesha hapa nchini katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kupitia Mradi wa East African Skills for Transformation and Regional Integration Program. Mradi huu utatekelezwa kwa mkopo wa dola za Marekani milioni 21.5 kutoka Benki ya Dunia na utaanza kutekelezwa rasmi mwezi Juni, 2019. Nitoe tu taarifa kwamba fedha hizi, financial agreement imeshasainiwa, tayari tunazo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kupitia mradi huu, chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kusomesha marubani 10 kwa mwaka. Aidha, Wizara yangu inafanya mawasiliano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu iweze kuwakopesha wanafunzi wa kozi ya Urubani. Kwa sasa ili rubani aweze kuingia katika soko la ajira atatakiwa kusoma na kupata leseni ya biashara kwa gharama ya shilingi milioni 132.6.

Mheshimiwa Spika, Serikali pia ina Mfuko wa Kusomesha Marubani ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA ambao una uwezo wa kusomesha takriban marubani watano hadi 10 kwa mwaka kulingana na makusanyo katika mwaka husika. Mfuko huu mpaka sasa umesomesha wanafunzi watano ambao wameshahitimu na kuajiriwa kwenye sekta. Aidha, wanafunzi 10 wataanza masomo mwezi Oktoba, 2019. Serikali itaendelea kuhakikisha inaongeza idadi ya marubani na wahandisi wazawa katika kipindi kijacho.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia Bandari ya Mtwara na hasa Kamati yangu ya Miundombinu. Serikali ilibuni mradi wa kuboresha Bandari ya Mtwara kwa lengo la kuboresha huduma zake za sasa na wakati ujao na baadaye katika ukanda wa Mtwara. Katika kutekeleza hili, kumekuwepo na hoja ya kujengwa na kuchimbwa kwa urefu wa kina cha mita 13 badala ya 15 na urefu kati ya maji yanapojaa na sakafu ya gati ya mita tano badala ya mita 5.5.

Mheshimiwa Spika, vipimo vilivyozingatiwa wakati wa kujenga na kuchimba Bandari ya Mtwara vilitokana na ushauri wa awali uliotolewa na Mtaalam Mshauri MSURS kutoka Uingereza ambao ni urefu wa kina wa mita 13 na urefu kati ya maji yanapojaa na sakafu ya gati ya mita tano. Aidha, uchambuzi wa kina wa kitaalam unaonesha kuwa vipimo hivyo vinavyotumika ni sahihi kwa meli na shehena tarajiwa katika bandari hiyo.

Mheshimiwa Spika, Bandari ya Mtwara kutoka kwenye kina ambacho ni low tide inajaa mpaka mita nne. Kwa hiyo, ukichimba draft ya mita 13 wakati maji yamejaa, yatafika mpaka mita 17. Kwa hiyo, meli ya aina yoyote ni lazima ita- dock kwenye Bandari ya Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri Nditiye amezungumzia suala la usajili wa laini za simu, lakini naomba nitoe taarifa kwamba takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2018 idadi ya wananchi nchini ilikadiriwa kuwa milioni 54.2 ambapo watu 52.6 wanaishi Tanzania Bara na wananchi milioni 1.6 wanaishi Tanzania Visiwani. Aidha, asilimia 50 ya Watanzania wana umri chini ya miaka 18. Kwa kuwa zoezi la usajili wa laini za simu linamalizika mwezi Desemba, 2019 Serikali itahakikisha wananchi wenye kustahili kusajiliwa na NIDA wanasajiliwa ili kuwezesha wananchi kuendelea kupata huduma za mawasiliano zilizo salama. Kuna Waheshimiwa Wabunge walionesha kwamba pengine kuna baadhi ya vitambulisho ambavyo havitumiki, lakini nashukuru kwamba Mheshimiwa Eng. Nditiye amelizungumzia vizuri.

Mheshimiwa Spika, tunatambua uwepo wa uhitaji wa vitambulisho vingine vyenye biometria vinavyotumika kwa sasa kusajili laini za simu ikiwa ni pamoja na pasi za kusafiria, leseni za udereva, kitambulisho cha Mpiga Kura pamoja na Zan ID. Hivi vyote vinatumika katika kusajili laini za simu. Sasa hivi kuna kamati maalum ambayo inafanyia kazi. Kitu kinachotakiwa ni kwamba laini zote kwa kutumia vitambulisho vyote vinavyosajiliwa lazima visomane na lazima visomane pamoja na kitambulisho cha Taifa na hili litatusaidia kukwepa madhara tunayoyapata ya wananchi kuibiwa.

Mheshimiwa Spika, lengo letu tunataka kila laini ya simu, kila mtumiaji awe anafahamika. Kwa hiyo, kwa sasa ni vitambulisho vyote vinatumika na wataalam wapo wanaendelea na kuhakikisha kwamba wanafanya utafiti ili kwamba vitambulisho vyote hivi viweze kusomana pamoja na kitambulisho cha Taifa.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizochukuliwa na Serikali kuiongezea mtaji TTCL. Naomba pia kutoa kutoa ufafanuzi kuhusu jitihada zilizochukuliwa na Serikali katika kutoa mtaji kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania. Serikali inaendelea kutekeleza mikakati yake madhubuti ya kuboresha mashirika yaliyokuwa yamebinafsishwa lakini yakashindwa kujiendesha kwa ufanisi. Kwa msingi huo, imetunga Sheria Na. 12 ya mwaka 2017 ya kuanzisha Shirika la TTCL likiwa linamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali imeendelea na juhudi za kuhakikisha kwamba TTCL sasa inapewa mtaji. TTCL ilipewa kibali cha kukopa jumla ya shilingi bilioni 96 na ilishakopa shilingi bilioni 66. Sasa hivi iko kwenye process ya kumalizia kukopa shilingi bilioni 30 ili iweze kuwekeza na TTCL iwe ni Taasisi ambayo inaweza ikajitegemea. Nashukuru kwamba kwa muda mchache mwaka 2019 iliweza kutoa gawio na mwaka huu tayari imeshajipanga kutoa gawio.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetengeneza corridor tatu; ya kwanza ni ya kutoka Dar es Salaam kupitia Tanzam highway kwenda mpaka Zambia, corridor ya pili ni ile ambayo inakwenda Central Corridor na ndiyo maana tunajenga SGR, lakini tunayo corridor ya tatu ambayo inatoka Mtwara kwenda mpaka Mbambabay na ninashukuru kwamba Serikali tayari imeshakamilisha barabara ya lami kutoka Mtwara kwenda mpaka Songea na kwenda mpaka Mbinga na sasa hivi tunajenga kilometa 66 zilizobaki.

Mheshimiwa Spika, corridor hii ikishakamilika na kwa sababu sasa hivi tunanunua flow meter ili ziweze kufungwa Bandari ya Mtwara na flow meter zifungwe Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Bandari ya Tanga, tunataka tuwezeshe corridor zote hizi ili ziweze kuhudumia nchi jirani na kujiongezea mapato.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Bandari ya Tanga tayari muda wowote mkataba utasainiwa. Nilitembelea Tanga, Tanga ilikuwa imeshakwenda chini sana, lakini tunahakikisha sasa kwamba Tanga inaamka. Kwa sababu yale magati mawili yaliyojengwa yamejengwa kwenye draft ambayo ni ndogo, maji ya kina cha mita tatu mpaka nne. Mikataba tutakayosaini tunataka tufanye dredging ili kuongeza kina kwa sababu kwa Tanga sasa hivi meli ilikuwa ikifika inakwenda kupaki mita 1,400 halafu mizigo sasa inapakiwa na matishari kuleta kwenye magati huku ambayo yanaweza yakatembea kwenye kina kidogo. Matokeo yake ilikuwa ina-discourage wenye meli kuja kuleta meli zao Tanga.

Mheshimiwa Spika, hilo tunaliondoa na hiyo ndiyo ambayo Waheshimiwa Wabunge mlikuwa mnaizungumzia. Tunapambana na Bandari majirani. Tunataka tufanye dredging na kwa mujibu wa taarifa ambayo ninayo, TPA mmeipongeza, wanatarajia mpaka itakapofika mwezi wa Tatu mwakani dredging itakuwa imekamilika. Ikishafika mwezi wa tisa wataongeza tena magati mawili yenye ukubwa wa mita 300, 300. Hii itawezesha sasa Bandari ya Tanga iweze ku-compete na bandari nyingine za jirani.

Mheshimiwa Spika, tukiwa na Bandari ya Tanga na wakati huo huo tunaendelea kukarabati Bandari ya Dar es Salaam ambayo tunafanya dredging kwenda mita 15 na gati Na.1 limeshakamilika, utaona kwa wale wanaopita Dar es Salaam sasa hivi hata kule meli zinaanza kupungua, lakini kwa ujumla, meli zinaongezeka kwa Bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, malengo yetu ni kwamba tunataka tuboreshe bandari zetu na tunajenga gati lingine la shilingi bilioni 137 kwa upande wa Mtwara. Tunataka tuhakikishe kwamba meli nyingi sasa zinakuja kupaki katika Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Tanga pamoja na Bandari ya Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza kutekeleza kuhakikisha kwamba inafufua usafiri kwenye maziwa. Upande wa Ziwa Nyasa tayari kuna meli tatu na zinafanya kazi. Upande wa Ziwa Victoria tumeshasaini mkataba wa meli moja kubwa itakayobeba abiria 1,200 na tani 400 pamoja na ujenzi wa chelezo, tunakarabati na zile meli za zamani; Mv Victoria na Mv Butiama. Kwa upande wa Kigoma tunatarajia kusaini tena meli moja mpya ambayo itakuwa inabeba abiria pamoja na mizigo na kukarabati meli ya MV Liemba. Taratibu za manunuzi zimekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunachotarajia sasa hivi ni muda wowote tutasaini mkataba kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2019. Malengo yetu ni kuhakikisha kwamba maziwa yote sasa yanatumika kiuchumi. Niseme tu kwamba Mkoa wa Katavi tayari tumeshapata mfanyabiashara mmoja ambaye ananunua tani 1,200 kila mwezi tutakuwa tunampelekea Congo.

Mheshimiwa Spika, pia kuna madini ambayo yamepatikana upande wa Kongo ambayo yatakuwa yanapitisha tani 2,000,000 kwa mwaka. Ndiyo maana tayari tunaendelea na mazungumzo ya pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika ili tuwe na matishari ya kutosha pia katika Bandari ya Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu muda naona unanitupa mkono, nimalizie kwa kutoa taarifa pia kwa Waheshimiwa Wabunge kwamba meter gauge kutoka Dar es Salaam kwenda Isaka inaendelea na ukarabati, inafufuliwa. Meli yetu hii ya meter gauge kwenye usanifu wake ilikuwa imesanifiwa kubeba tani milioni tano kwa mwaka, lakini ilikuwa imeshuka mpaka inabeba tani 300,000. Baada ya ukarabati huo, tutarudisha sasa kwenda kwenye hizo tani zinazotakiwa.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa ushauri ambao umetolewa na Waheshimiwa Wabunge kwamba tuangalie namna ya kuikodisha TRC ili iweze kuhudumia pamoja na reli ya TAZARA. Nimshukuru sana na Mheshimiwa Turky, leo kazungumza kitu ambacho nimewahi kukisikia mara ya mwisho wakati alipotembelea yule Waziri wa Ethiopia aliyejiuzulu. Nao nchi yao waliipeleka vizuri kutokana na hizi bond. Kwa hiyo, ushauri wako Mheshimiwa Turky nimeupokea.

Mheshimiwa Spika, baada ya haya machache, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako lipitishe kifungu kwa kifungu na lipitishe bajeti ya Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, naomba kuta hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kushukuru kwa kupata nafasi hii ili na mimi niweze kujibu baadhi ya hoja ambazo Waheshimiwa Wabunge wamezichangia wakati wa kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niseme kwamba, naunga mkono hoja ya hotuba yote ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu, imeelekeza, imeeleza utekelezaji wa miradi ya maji katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2017/2018. Hotuba imeeleza kwamba kwa upande wa vijijini tayari huduma ya maji safi na salama imefikia asilimia 60 na kwa upande wa mijini huduma ya maji safi na salama imefikia asilimia 78. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tunaendelea na utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo tuliianza mwaka 2006/2007. Programu ya kwanza iliisha mwaka 2017, Juni. Katika awamu hii ya kwanza tulilenga kutekeleza miradi 1,810; lakini hadi leo tayari tumeshatekeleza miradi 1,468. Miradi hiyo tumejenga vituo vya kuchotea maji 123,888 lakini katika vituo hivyo ni asilimia
60 tu ya vituo ndio vinavyotoa maji kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo kwamba miradi mingi tuliweka pump za kutumia dizeli, jenerata za kutumia dizeli ambazo Jumuiya za Watumiaji Maji wameshindwa kuziendesha. Hata hivyo yapo maeneo ambayo hizi jumuiya tulizoziunda kwa ajili ya kuendesha miradi ambayo imekamilika wao wenyewe wameshindwa kuziendesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo yaliyolengwa kwamba maji yatapatikana kutoka maeneo hayo lakini kutokana na mabadiliko ya tabianchi maeneo hayo yamekauka maji. Hivyo, Katiba bajeti inayokuja tunataka tuhakikishe kwamba vile vituo vyote ambavyo tayari vimeshajengwa na havitoi maji tutaweka fedha, tutatenga bajeti ili kuhakikisha kwamba tunapeleka yale maji na tunaondoa changamoto zote ambazo zimejitokeza zinazofanya vituo vyote hivi visitoe maji kwa sababu kama vituo hivi vyote vingetoa maji sasa hivi tungekuwa tunazungumzia upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini tungekuwa tumefikia asilimia 85 kama ilivyoelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa mijini tayari tuko asilimia 78. Miradi mingi imeshatekelezwa katika maeneo ya mijini na maji yapo, kwa mfano katika Jiji la Dar es Salaam. Sasa hivi bajeti inayokuja tutatenga bajeti ili kuendelea kupanua mtandao, ili wananchi wengi waweze kupata maji tuweze kufikia asilimia iliyoelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwamba maeneo ya miji tufike asilimia 95. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lako tukufu katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Waheshimiwa Wabunge waliielekeza Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuunda Wakala wa Maji Vijijini. Naomba kutoa taarifa kwamba Wizara inaendelea na taratibu za uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini wenye majukumu ya kujenga miradi, kusaidia usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji vijijini. Kwa sasa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imekamilisha kazi ya kuandaa nyaraka muhimu ambazo ni strategic plan, business plan na framework document kwa kutumia Sheria ya Uanzishwaji wa Wakala nchini ili kusaidia uanzishwaji wa wakala hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nyaraka hizo zitaenda sambamba na maoni ya wadau na baadae itapelekwa kwenye mamlaka husika kwa idhini ya uanzishaji wa taasisi hiyo. Mategemeo ya Wizara ni kuwa Wakala wa Maji Vijijini, utaanza kufanya kazi kuanzia mwezi Julai kwenye bajeti ya 2018/2019. Kwa hiyo, tupo mahali pazuri katika kuhakikisha kwamba tunaanzisha Wakala wa Maji Vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo Waheshimiwa Wabunge wameligusa sana ni kuhusiana na mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India ambao utatuwezesha kutekeleza miradi 17, kati yake 16 ikiwemo Tanzania Bara na mradi mmoja Tanzania Visiwani. Upatikanaji wa fedha hizi umechelewa kutokana na majadiliano kati ya Serikali ya India na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imechukua muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, majadiliano haya yamechukua muda mrefu kutokana na sababu kwanza Bunge letu tukufu mwezi Septemba lilibadilisha Sheria ya VAT, kwa hiyo, ili kukamilisha taratibu Sheria ya VAT ianze kufanya kazi imechelewesha kuweza kusaini Financial Agreement, lakini kwa sasa tumefikia hatua nzuri na niwahakikishie tu Waheshimiwa Wabunge kwamba, fedha hizi dola milioni mia tano tunatarajia kuzitumia kwenye bajeti ijayo kwa mwaka wa fedha 2018/2019…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kunipa nafasi na mimi niweze kujibu majibu ya Serikali kupitia mawasilisho ya Kamati hizi mbili; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa michango mingi ambayo Wabunge wamechangia lakini nianze kwa kusema kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko makini na imejipanga. Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli inatambua ilipo, inatambua Tanzania iko wapi, inawajua Watanzania wote na mahitaji yao, inatambua inatoka wapi na inakwenda wapi lakini pia inatambua mahusiano ya nchi yetu ya Tanzania na dunia. Hilo huwezi kulijua kama utabaki huko uliko. Nimpongeze sana Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mheshimiwa Chacha Ryoba ni muda mfupi amekuja na ameshatambua tatizo alilokuwa nalo akiwa huko na sasa yuko huku anaelewa maana ya nchi nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Bunge ni kutunga sheria na sheria hizi utekelezaji unafanywa na Serikali. Pia kazi ya Bunge ni kusimamia na kushauri Serikali lakini inatekeleza hayo kupitia kwenye miundo ambayo imewekwa na Bunge lenyewe. Sasa hivi tunajadili Kamati hizi mbili na taarifa tunayoijadili iko ndani ya vitabu hivi vya Kamati, jana tulichambua taarifa za CAG. Sasa wakati mwingine unaona mtu anajadili kitu ambacho hakipo ndani ya hizi taarifa lakini ni kwa sababu tu ungekuwa umeshakuja huku haya usingeyafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu wameshayazungumza kwenye umma, basi nitayajibu. Nianze na ATCL. Wabunge wa Chama cha Mapinduzi nashukuru sana kwamba mmesaidia kulizungumza hili. Kwa sababu Shirika la Ndege usiliangalie kwenye kitu kimoja tu kwamba halijaleta faida, tena faida yenyewe bado haijapitiwa na CAG ili uweze kupewa taarifa kwamba kuna faida au kuna hasara. Shirika letu la Ndege limejipanga lina Business Plan na waendesha ndege (pilot) mpaka sasa hivi tunao 50 na ni ndege zote kuanzia kwenye Dreamliner mpaka Bombardier Airbus. Tutaendelea na ununuzi wa ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niwape tu faida, kila ndege tunayonunua mikataba tunayoingia ni pamoja na ufundishaji wa ma-pilot. Kwa hiyo, tuna mpango ambao ni endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimewaambia kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi imejipanga. Ndiyo maana sasa hivi inakarabati gereji ya KIA ambayo itakuwa gereji kwa ajili ya matengenezo ya ndege. Serikali ya Chama cha Mapinduzi imejipanga ndiyo maana Chuo cha NIT tunajenga ndiyo kiwe Chuo Kikuu cha Aviation ambapo mafundi wa kutengeneza ndege watafundishwa (maintenance engineer) lakini pamoja na ma-pilot.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ester Bulaya ametoa taarifa sijui amezipata wapi…

MBUNGE FULANI: Kwako.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Wewe shemeji yangu Mheshimiwa wewe, hatuchukui mambo ya mitaani, bado hatujaenda kutengeneza hizi ndege ili tuweze kujua tumetumia shilingi ngapi lakini bado CAG hajapitia haya ili tuweze kujua kama kuna faida ya shilingi bilioni 4, umeyapata kutoka kwenye kitabu kipi, hata mimi mwenyewe Waziri sijui. Haya ni mambo ya mitaani na wewe ni Mbunge mzoefu siyo vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na taaarifa nazo naona kama ni za kutoka mitaani, watu wanazungumzia PUMA. PUMA sina taarifa kwamba yeye ndiyo ana monopoly ya biashara ya mafuta duniani. Vivyo hivyo sina taarifa kwamba PUMA ana monopoly ya mafuta Tanzania. Waheshimiwa Wabunge, Bunge limetunga sheria na sheria hizo zinatekelezwa na Serikali kwamba mtu anayepewa mkataba wa ku-supply mafuta ya ndege anapewa muda, kuna siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho na ikifika siku ya mwisho anafanyiwa evaluation kama anaenda vizuri ataendelea, kama haendi vizuri basi sheria ndiyo zinazosema kwamba hawezi kuendelea. Sasa nitashangaa kama Bunge au Mbunge ndiyo anayesimamia kwamba PUMA apewe leseni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Waheshimiwa Wabunge acheni Serikali ifanye kazi yake, na Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, iko makini kama mnavyoona Mawaziri wake hawalali, kila mtu anafanya kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Engineer Kamwelwe, kabla ya…

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, taarifa zote mbili.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kutoa maoni yangu katika mawasilisho ya Kamati za Kudumu za Bunge zote mbili. Nianze kwa kuwashukuru Wenyeviti na Kamati zao kwa kufanya kazi nzuri na hasa Kamati yangu ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kwa jinsi ambavyo imeonesha weledi mkubwa sana kwenye Wizara yangu. Maeneo mengi sasa wanayafahamu vizuri na imekuwa ni bahati tu kwa sababu ajira yangu yote ilikuwa kule ndio maana naweza nikaenda nao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niwashukuru sana kwa michango yao ambayo ni michango ya kujenga. Wamezungumza vizuri sana na kila wakati wananipa maoni na hayo maoni Serikali inayafanyia kazi. Kwa hiyo, nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati yangu ya Kudumu ya Bunge, imeshauri katika maeneo mbalimbali, wameelekeza kwamba fedha za miradi ya maendeleo zitolewe kwa haraka. Nitoe taarifa kwamba nimshukuru sana Waziri wa Fedha hata mwezi wa 12 alitoa shilingi bilioni 200 na tumelipa tayari kwa ajili ya miradi ya barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuhusiana na bandari, kwa sababu bandari ndio lango kuu la uchumi katika nchi yetu. Waheshimiwa Wabunge wamependekeza kwamba asilimia 40 ya makusanyo ya bandari, basi yabakie kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya bandari. Baada ya tamko hilo niliwasiliana na Waziri wa Fedha lakini kwa mujibu wa sheria kwa sasa, hela zote za retention, hiyo Sheria ya Retention imeshafutwa ili ziweze kubakizwa kwenye taasisi za Serikali. Kwa hiyo hela yote inakusanywa na kupelekwa Hazina, lakini sisi tutaomba na kwa sababu bandari, inakarabatiwa sasa hivi kwa kuongeza kina, tunajenga magati nane kutoka sifuri mpaka saba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi ule tayari tumeshakamilisha gati namba moja na ndio lenye kina kirefu lina mita 15 kwenye low tide, kwa hiyo meli kubwa inaweza ikakaa pale na sasa hivi tunaendelea na study kwa ajili ya kuongeza pia kina cha ule mlango wa kuingilia meli kubwa. Kazi inaendelea vizuri na kwa kusimamiwa pia pamoja na hii Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ununuzi wa flow meter ili tuwe na flow meter zenye uhakika na mpango wetu ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na maeneo matatu ya flow meter. Kwa sababu wakati mwingine tunakuwa na meli zaidi ya sita za mafuta, sasa zikichelewa sana zinasababisha gharama kwa watumiaji. Kwa hiyo, tayari Serikali mwaka ujao wa fedha study zimeshafanyika, tutaomba fedha ili tuweze kuongeza flow meter.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Kudumu ya Bunge imezungumzia kuongeza gati namba 13 na namba 14, tayari tumeshafanya mazungumzo na Benki ya Dunia baada ya kukamilisha huu mradi unaoendelea unaojenga magati nane, tutakwenda tena tukaongeze hayo magati namba 13 na namba 14.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika michango ya wabunge wamechangia kuhusiana na hii sheria mpya, Sheria mpya ya Kudhibiti Uzito wa Magari ambayo ni ya East Africa. Chanzo cha sheria hii ni usikivu wa Serikali, lakini pia ni usikivu wa Serikali kutoka kwenye Bunge na Wabunge walikuwa na haki kwa sababu miradi mingi tulikuwa tunatekeleza, lakini baada ya muda mfupi, barabara zinaharibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kupokea maoni ya bunge lako Tukufu, Serikali ilii-engage consultant, ilitoa fedha, wakafanya study, ile study ndio iliyotuelekeza kwamba haya magari ya super single ndio yanayoongoza kuharibu barabara, kwa nini? Kwa sababu wanatumia size ya matairi ambayo ni 385/85 lakini kama size ya matairi itakwenda kwenye 465/67, basi hiyo effect haiwezi kuwepo. Sasa kwa sababu tayari tunayo sharia, niwaombe tu wasafirishaji waendelee kutumia sheria hiyo, lakini kama itabidi, itabidi tena tuite consultant ili tuweze kufanya study nyingine kwa ajili ya kuboresha. Serikali ni wasikivu na bandari haiwezi kufanya kazi bila reli, lakini bandari haiwezi kufanya kazi bila barabara pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wametoa mfano mzigo wa Zambia, ni kweli kabisa Zambia wana mzigo wa tani zaidi ya milioni 10 wanasafirisha kwa mwaka. Hata hivyo, mzigo unaopitia bandari ya Dar es Salaam ni tani milioni 2.2, ni malengo yetu sisi kwamba tuweze kuchukua mzigo mkubwa zaidi. Ndio maana nishukuru Waheshimiwa Wabunge ambao wamezungumzia pia Reli ya TAZARA, reli ile inatakiwa kubeba tani milioni tano kwa mwaka, lakini sasa hivi inabeba chini ya tani laki tatu kwa mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi Serikali ilitoa shilingi bilioni 10 tunakarabati vichwa saba ambavyo vitakamilika kabla ya mwezi wa Saba ili tuendelee kuongeza sasa uwezo wa ile reli kubeba mzigo zaidi. Malengo yetu kama walivyoshauri Waheshimiwa Wabunge kwenye Kamati ya Miundombinu, tutakaa pamoja na wenzetu wa Zambia, kwa sababu reli ile tunaichangia mali kwa asilimia 50 kwa 50. Tutakaa nao ili tuweze kuboresha zile sheria za zamani, tuboreshe ili sasa tuweze kuona ni namna gani kwamba tuta- improve matumizi ya ile reli ili iweze kutumika vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tulikaa tumekodisha kampuni moja ya wa South Africa ambayo inaitwa Calabash. Calabash ni kampuni ya wastaafu waliokuwa wanafanya kazi kwenye reli ya South Africa kule. Baada ya kustaafu wamenunua vichwa na mabehewa kwa hiyo tumewakodisha ndio wanaobeba mzigo kupitia ile reli, tunawalipa kwa kila trip, kila trip moja wanalipa milioni 20 na bado nafasi hiyo ipo hata Watanzania wengine wanaweza wakafanya hivyo na Calabash wameongeza uwezo wa kubeba mzigo, wanabeba tani 150,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mengi ya kuzungumza, lakini nikushukuru kwa kunipa hii nafasi na niwapongeze sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao. Nawashukuru sana. (Makofi)
Azimio la Kuridhia Itifaki ya Kinga na Maslahi ya Kidiplomasia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (The East Africa Community Protocol on Information and Communication Technology)
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kukushukuru wewe mwenyewe na Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, ambayo ndiyo mshauri mkuu katika uendeshaji wa Wizara yangu ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote ambao wamechangia katika itifaki hii pamoja na Kambi ya Upinzani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Kudumu ya Bunge, imeshauri maeneo saba wakati inawasilisha maelezo yake. Nikiri kwamba maeneo hayo nimeyapokea na kwamba yataendelea kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaje maneno machache ambayo Kamati ya Bunge imeshauri, kwamba ziko taasisi nyingine, kama akina Vodacom, akina Halotel ambao nao wameweka mkongo wa Taifa. Uzuri wa hii itifaki ni kwamba sasa inaweka misingi katika kujadiliana kuhusu masuala haya, kwa sababu iko imani kwamba hata nchi nyingine pia inawezekana kuna jambo kama hilo. Sasa baada ya itifaki hii, basi itifaki inaweka msingi, haya masuala yote yatajadiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu udhibiti wa mkongo, kwa bahati nzuri nchi yetu tayari ina taasisi ya TCRA ambayo ndiyo mdhibiti wa masuala ya mawasiliano pamoja na hii miundombinu yote, zipo taasisi za Serikali ambazo zinadhibiti ili kuhakikisha kwamba shughuli yote inafanyika kwa usalama mkubwa na bila kupoteza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imehoji pia kwamba Tanzania sasa inaridhia, kwa hiyo, nchi nyingine zichukue hatua za kuridhia itifaki hii ili tuweze kwenda pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mheshimiwa Nsanzugwako, ametaja nchi tatu ambazo tayari zimesharidhia. Kwa hiyo, nasi tutakuwa wa nne, baada ya muda tutamalizia na hiyo nchi moja ambayo imebaki. Kwa taarifa tulizonazo, kila nchi inashughulikia suala hili kwa sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzani, pia nayo ilitoa maoni mazuri tu, kwanza kuhusiana na gharama za maunganisho kuwa ni kubwa. Itifaki hii inakuja kujibu hilo, ikiwepo pamoja na gharama za roaming. Baada ya kuridhia itifaki, sasa tutakaa pamoja. Ni ukweli usiopingika kwamba taasisi za watoa huduma wa mawasiliano, kila taasisi ina tariffs zake. Kwa hiyo, kulikuwa na ugumu fulani, lakini baada ya itifaki hii, tutakutana nao na kujadiliana nao kwa sababu wanaotoa huduma Tanzania ndio wanaotoa huduma Kenya, ndio wanaotoa huduma Uganda, wawe na tariffs za pamoja ili gharama za roaming ziweze kuwekwa kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia walizungumza suala la kuwa na sarafu ya pamoja. Kama nilivyozungumza kwamba itifaki hii, ndiyo msingi wa kujadiliana haya mambo yote ili kuhakikisha kwamba msingi wa itiofaki ni kwamba wananchi wapate gharama nafuu, basi unafikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana Wabunge wanne waliochangia, kuanzia na Mheshimiwa Ruth Mollel, akaja Mheshimiwa Nsanzugwako, Mheshimiwa Chumi na Mheshimiwa Maige. Kwa ujumla tu ni kwamba wote wamekubaliana na kuunga mkono itifaki hii iweze kuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia, itifaki inayopendekezwa kuridhiwa, inaweka misingi ya awali ya pamoja baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa nchi wanachama wanakubaliana kushirikiana katika masuala ya kujenga, kuendeleza na kutumia miundombinu ya TEHAMA, huo ndiyo msingi kwamba shughuli zote sasa, itakapofikia kwenye kuunganisha kwenye mipaka, tunakuwa tuko pamoja, kwenye masafa tunakuwa pia tuko pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maneno haya, kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayolipa madaraka Bunge la Jamhuri ya Muungano kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa; na kama nilivyowasilisha, mapema leo hoja ya azimio, kwa kuzingatia Kanuni ya 54 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, sasa naliomba Bunge lako Tukufu, kwa kuzingatia Kanuni ya 79 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, kufanya maamuzi kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki hii ya Afrika Mashariki ya Mitandao ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano na kwa lugha ya kigeni, East African Community Protocol on Information and Communication Technology Networks.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mpango huu wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na upendo hasa kwetu sisi Watanzania, kwa kutufanya tuendelee kudumisha amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru uongozi wa Chama cha Mapinduzi katika ngazi zote kwa kuendelea kuliteua jina langu ili niingie kugombea. Pia niwashukuru wananchi wenzangu wa Jimbo la Katavi ambao wamenirejesha kwa mara nyingine ya pili katika Bunge hili.
(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niipongeze sana Wizara ya Fedha kwa Mpango mzuri lakini nitoe ushauri kwa upande wa TRA. Mpango wa Pili wa Maendeleo uliweka makadirio ya kukusanya shilingi trilioni 107 na niipongeze sana TRA wamekusanya zaidi ya asilimia 80. Ni kazi nzuri hongereni sana lakini ni kwa sababu ya usimamizi mzuri wa Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha hiyo katika miaka mitano imefanya kazi kubwa sana lakini ni imani yangu kwamba wangeweza kukusanya Zaidi. Kwa kuzingatia kwamba kwenye Mpango huu wa Tatu unaoanza mwaka 2021 kwenda 2022 matarajio ni kukusanya shilingi trilioni 114 kwa ajili ya kutekeleza mipango ya maendeleo kwa muda wa miaka mitano mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashauri TRA, ni lazima wadumishe uhusiano kati ya TRA kwa maana ya Serikali na wafanyabiashara. Wabunge wenzangu wamechangia kwamba wafanyabiashara watatu wanakwenda kununua bidhaa moja China lakini makadirio ya TRA yanatofautiana katika yale makontena matatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni rahisi na kwa bahati nzuri Serikali yetu imeshaweka mkongo wa Taifa, teknolojia ya kidigitali tunayo, tunaweza tuka-transfer fedha kwa kutumia teknolojia ya kidigitali. Badala ya wafanyabiashara kutembea na dola mfukoni kwenda China kununua bidhaa, kwa nini tusifanye benki transfer? Tukifanya benki transfer na rekodi zikawepo TRA ukadiriaji hauwezi kuchukua muda, tutakwenda haraka na mlundikano wa makontena ndani ya bandari unaweza usiwepo tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi navyoongea kuna watu wanakimbia mizigo yao kwa sababu analeta mzigo lakini makadirio yanakuwa makubwa kuliko ile fedha aliyonunulia na ile mizigo inaendelea kurundikana bandarini. TRA wanayo sheria baada ya siku 14 wanatakiwa kuweka ule mzigo katika mnada lakini hilo halifanyiki. Niwashauri sana TRA, ili muweze kukusanya fedha nyingi tuwe na mahusiano mazuri. Niombe tu, ikiwezekana hata Bunge litunge sheria kwamba sasa manunuzi ya bidhaa kutoka nje lazima fedha ipelekwe kwa benki transfer badala ya kuweka mfukoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hii miaka mitano, Mheshimiwa Dkt. John Magufuli, kutoka ndege moja amenunua ndege sasa zimefika kumi na mbili…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Oooh! Muda umeisha. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. ENG. ISACK A. KWAMWELWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kutoa maneno machache ya kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nianze kwa kuungana na Wabunge wenzangu kutoa pongezi kwa Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Jimbo la Katavi wamenituma pia nitoe pole kwa Mheshimiwa Rais kwa kuondokewa na jembe letu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na ahadi yetu kwake yeye Mheshimiwa Rais, tutamuunga mkono, tutafanya kazi kwa bidii ili kuyaenzi yale yote ambayo yameachwa na Rais wetu Hayati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe pongezi kwa hotuba nzuri iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, hotuba ambayo imegusa vipengele vyote vya dira iliyotolewa mwaka 2015 pamoja na dira iliyotolewa na hotuba ya Rais mwaka 2020. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya uchache wa muda, nitoe shukrani kwa yale yote ambayo yamefanywa katika Jimbo langu, hasa katika miaka mitano hiyo iliyopita kwa kuanza na Wizara ya Ujenzi ambayo imeanza na inaendelea kujenga barabara ya kutoka Tabora kwenda Mpanda, barabara ambayo ni uti wa mgongo wa Mkoa wetu wa Katavi na hasa nipongeze kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la Ugala ambalo lilikuwa linafanya Jimbo langu lisifikiwe na magari kwa muda miezi mitatu kila mwaka, lakini kuanzia mwaka huu pamoja na mvua hii, hatujapata hiyo shida. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba tu kwamba kuna barabara nyingine muhimu sana ambayo sasa hivi imeanza kutumika. Kuna mabasi yanatoka Mbeya yanapita Katavi yanakwenda Mwanza; na siku hiyo hiyo yatoka Mwanza pia yanaelekea kwenda Mbeya na barabara siyo nyingine, ni Inyonga - Maji ya moto kupita Mloo kwenda Kamsamba na inafika mpaka Mbeya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ni potential kwa aina yake kwa sababu Ziwa Rukwa ndiyo Ziwa ambalo lina gesi ambayo ni ya muhimu sana inaitwa Helium. Ni nchi chache sana duniani ambazo zina gesi ya namna hiyo. Sasa ni muhimu sana kukumbuka kuanza kutengeneza miundombinu kwa sasa kabla hatujaanza kuchimba hiyo gesi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naishukuru sana Wizara ya Nishati, juzi wamesaini mikataba yote kwa ajili ya REA III. Wamekamilisha sasa vijiji vilivyokuwa vimebaki katika Jimbo langu; Kijiji cha Ilunde, Kijiji cha Isegenezya, Kijiji cha Mapili ambacho mimi mwenyewe nimezaliwa, Kijiji cha Masigo na Kamalampaka, vyote vimeingizwa. Kwa hiyo, baada ya mradi huu kukamilika, jimbo langu litakuwa na umeme kwa asilimia 100. Nawashukuru sana Wizara ya Nishati; Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naishukuru Wizara ya Kilimo. Jimbo langu kwa asilimia 100 ni wakulima. Tunalima mazao ya chakula pamoja na mazao ya biashara na zao kuu la biashara ni Tumbaku. Kule tuna vyama vitatu vinavyoshughulikia tumbaku. Tuna Chama cha Ukonongo, tuna Chama cha Ilela na tuna Chama cha Utense. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Chama cha Ukonongo ndiyo ambacho kimekaa muda mrefu sana, lakini kilikuwa kimetengeneza deni kwa wakulima na hivi ninavyozungumza wakulima bado wanadai shilingi milioni 400. Namshukuru sana Naibu Waziri wa Kilimo, amefanya kazi kubwa na juzi Morogoro ametoa maelekezo. Kwa sababu audit imeshafanyika, kwa hiyo, nashukuru kwamba wakulima sasa watalipwa ile shilingi milioni 400. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu imefikia uchumi wa kati, lakini imefikia uchumi wa kati kwa sababu ya ushirikiano tulionao sisi Watanzania lakini hasa nin kwa sababu ya hii mihimili mitatu ambayo ilifanya kazi yake vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukianza kwa mhimili wa Bunge, umewajibika kwa kuchambua bajeti na kuzipitisha. Pia wakati wa utekelezaji, tukiwa kwenye Majimbo kule tulikuwa tunaangalia yale yaliyokuwa yamepangwa na Serikali kama hayatekelezwi tunakuja kutoa taarifa katika Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia napongeza mhimili wa Serikali ukiongozwa na Waziri Mkuu, ndio wametekeleza yote yaliyofanyika. Vile vile mhimili wa Sheria wa Mahakama ambao umeleta utulivu kwa wananchi kwa kuondoa uonevu, ndiyo maana kila mtu amewajibika mpaka tumefikia sasa kwenye uchumi wa kati.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, kengele imegonga.

MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia hotuba hii ya Utawala Bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina hazina kubwa sana ya viongozi wetu wastaafu ambao wamepita ngazi za juu, kuanzia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pamoja na Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunao Marais upande wa Jamhuri ya Muungano, lakini na Zanzibar; tunao Mawaziri Wakuu wastaafu, tunao Makamu wa Rais wastaafu, tunao Ma-chief Secretary wastaafu, lakini pia tunao mpaka Maspika na Naibu Maspika wastaafu. Hawa viongozi wetu ni hazina kubwa sana kwa nchi yetu. Ukienda kule Ulaya wenzetu wana Mabunge ya waliochaguliwa, lakini kuna Bunge ambalo wanaita kwa mfano kama Canada wanaita The House of Queen na Uingereza wanasema The House of Lord. Hili Bunge la pili linakuwa na wale viongozi wastaafu ambao walishatumikia zile nchi na kila muswada unapopitishwa na Bunge la waliochaguliwa hauwezi kupita moja kwa moja, lakini lazima uende ukapate ushauri kwanza kwa wale viongozi wastaafu ambao walishatumika katika zile nchi na kwa kufanya hivyo nchi inakwenda vizuri na utawala bora unakwenda vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa namuomba Mheshimiwa Waziri wa Utumishi, Ndugu yangu Mchengerwa jaribu kuliangalia hili na ikiwezekana kutengeneza mfumo rasmi katika nchi yetu ili tuweze kuwatumia hawa viongozi wetu wastaafu kwa sababu wanayohekima, wana busara nyingi na bado wanauzoefu mkubwa wanaweza wakatushauri hata katika ndani ya Bunge, hilo lilikuwa la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nizungumzie Jimbo langu na nimuombe sasa Mheshimiwa Waziri anisikilize pamoja na Naibu Waziri. Jimbo langu wananchi kwa kutumia Mfuko wa Jimbo pamoja na michango yao walijenga zahanati kumi kwenye hii miaka mitano iliyopita katika hizo zahanati kumi ni zahanati mbili mbili tu ndiyo ambazo zimefunguliwa, zahanati nane bado kwa sababu ya kukosa watumishi. Nimuombe sana Mheshimiwa Waziri kwamba hizi zahanati nane, mtakapo fanya ajira utuletee watumishi ili wananchi waendelee kufaidi jasho lao, wamejenga zahanati wenyewe lakini wanakosa huduma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu, nataka nizungumzie Shirika letu la Reli na nimpongeze sana Mheshimiwa Rais jana katika hotuba yake amezungumza jinsi gani ambavyo Serikali imekarabati reli ya kutoka Tanga kwenda Kilimanjaro mpaka Arusha na baada ya kukarabati reli hiyo kumekuwa na manufaa makubwa, ajira zimeongezeka, lakini pia mzigo kutoka Tanga wa cement kupeleka Kilimanjaro na Arusha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu train inavuta mabehewa kumi ya cement bei imepungua tofauti na kubeba na lori. Hoja yangu nini, ukarabati ule umefanywa na Watanzania, vijana wetu na waliofanya ngazi ya darasa la saba na kushuka chini. Vijana hawa ile reli ilikuwa imechoka sana wamefanya kazi nzuri, tulikuwa tuna mapendekezo kwamba hawa vijana wangefikiriwa kuajiriwa kama wanavyoajiriwa watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mfumo wetu wa ajira una sheria unasema kwamba hauwezi kuajirwa mpaka awe amefika form four, ni form four gani ambaye atakuwa pigilia, ni form six gani ambaye atakubali kufanya ya pigilia, akakae kule kwenye magenge. Nimuombe Mheshimiwa Waziri kama inashindikana basi hiyo sheria ifanyiwe amendment kwa kuletwa hapa Bungeni ili angalau tuweke tu hiyo kwamba ni special tuwaajiri hawa vijana, waendelee kutengeneza ile reli. Kwa sababu tukiacha itaharibika tena kama ilivyokuwa imeharibika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho, na mimi nizungumzie kidogo suala la utawala bora, lakini kwa kusema nini maana ya nidhamu, nini maana ya heshima, kwa sababu nikichukulia mfano kwenye Halmashauri kumekuwa na tabia ya kuwahamisha watumishi hovyo hovyo kwa matakwa ya mtu mmoja anayeitwa Mkurugenzi, transparent inakosekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati nipo mtumishi niliwahi kwenda Canada, Montreal, ndiyo nilikokwenda kujifunzia kozi yangu ya leadership, nilichokigundua kule tulipewa semina kama wewe ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda, kiwanda kinazalisha vizuri na marketing officer wanafanya kazi vizuri, yule Meneja wa Uzalishaji usimpandishe madaraka, usimpe cheo kwa kumpandisha madaraka ile skill aliyokua anafanya azalishe zaidi. Lakini...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri Innocent Bashungwa pamoja na Naibu Mawaziri David Silinde na Festo Dugange, Wabunge wenzangu wamesema hawa Mawaziri wanafanya kazi vizuri, wanatusikiliza Wabunge lakini wanasikiliza mpaka wananchi wetu. Tunawapa hongera sana na mnamsaidia vizuri sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipongeze pia Katibu Mkuu Prof. Liziki Shemdoe, wiki iliyopita mimi pamoja na timu yangu ya Halmashauri yangu tulikwenda ofisini kwake kumtembelea tulikuwa na hoja nne baada ya masaa sita hoja moja alikuwa ameshaijibu na hoja hiyo nilikuwa nimeomba Mwalimu wa jinsia ya kike kwenye Sekondari ya Kata ya Ilunde ambayo ipo na kidato cha tatu na ina wasichana wengi lakini haikuwa na mwalimu wa jinsia ya kike. Katika muda wa masaa sita alikuwa ameshampanga tayari mwalimu wa kike na ninaimani kwamba mwisho wa mwezi huu ataripoti kwenye ile sekondari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika masuala yaliyotupeleka yalikuwa manne katika muda wa masaa 24 yote walikuwa wameshayatekeleza. Ndio maana mimi Wizara hii ile timu ya Katibu Mkuu, Naibu Katibu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na Wakurugenzi ushirikiano niliouona jinsi walivyotuhudumia nimewaita kwamba hawa ni 24 hours action, wanafanya kazi vizuri na kwakweli Wizara hii ikienda namna hii kweli inatekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri ambayo ameiandaa vizuri na aliisoma vizuri kwa sauti ya kusikika tena kwa utaratibu, ukurasa wa pili alizungumzia jinsi alivyotumia fedha alizotoa Mama yetu, fedha za UVIKO amechambua ni maeneo gani ambayo fedha ile ameitumia, katika vitu alivyovieleza ni pamoja na ununuzi wa magari ya ofisi, lakini pamoja na ununuzi wa magari ya wagonjwa, sasa Mheshimiwa Waziri nikuombe nina Kata moja ya Ilunde ipo mbali sana na Makao Makuu ya Wilaya, katika hayo magari niombe gari moja lipelekwe kwenye ile Kata gari la Wagonjwa Kata ya Ilunde.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu hauwezi ukapiga simu mtu anaumwa gari litoke kilometa 100 limchukue mgonjwa halafu limrudishe tena kilometa 200 tutakuwa tuna risk maisha ya mgonjwa. Mheshimiwa Waziri nikuomba sana kwamba utakaponunua magari kumbuka gari moja liende kwenye hiyo Kata inaitwa Kata ya Ilunde.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri pia umenijengea hospitali ya Wilaya kwenye Jimbo langu kuna gari moja tu, sasa kitakuwa ni kitu cha ajabu kwamba hospitali ya Wilaya haina gari la wagonjwa inaazima gari kwenye kituo cha afya ambayo ulitupa mwaka jana, niombe sana hili Mheshimiwa Waziri ulikumbuke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishukuru sana Serikali katika bajeti ya Wizara hii, sio hii tunayoiomba sasa hivi ila hii ambayo tunaitekeleza tunaimaliza mwezi Juni, Serikali ilitoa bilioni 22.87 kwa ajili ya kulipa madeni ya wazabuni, nikushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwamba sekondari yangu ya A-Level ya Inyonga umetoa shilingi 72,000,000 kulipa madeni ya wazabuni lakini nikuombe bado kuna wazabuni wanadai shilingi 175,000,000 tena wazabuni hawa ni akinamama lishe sehemu kubwa, na wale ambao wamepewa asilimia 10 na Halmashauri wamepewa zile fedha na bado mkawafanyisha biashara nyinyi wenyewe, sasa ni kitu cha ajabu kwamba mnashindwa kuwalipa na kama ukishindwa kuwalipa maana yake na wao watashindwa kurudisha zile fedha tulizowakopesha zile asilimia 10.

Niombe sana Mheshimiwa Waziri kabla hatujafunga mwaka hii shilingi 175,000,000 tuitoe ili hawa wazabuni hawa ambao tumewakopesha fedha sisi wenyewe tuweze kuwalipa na wao waweze kulipa kwenye Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna watumishi wenzenu Mheshimiwa Waziri, wapo Walimu wanadai malimbikizo ya shilingi 136,000,000, kuna wafanyakazi wengine wasio Walimu wanadai zaidi ya Shilingi 789,000,000 niombe pia kwasababu hawa ni watumishi wenzenu hebu walipeni ili mambo yaweze kwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri hii Wizara kwenye bajeti ya mwaka huu…

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Eng. Isack Aloyce Kamwelwe, muda wako umekwisha.

MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kutoa mchango wangu kwenye Wizara hii ya Utumishi na Utawala Bora. Samahani nina kikohozi kwa hiyo, sauti yangu sio nzuri sana, lakini nitajitahidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuendelea kuijalia amani nchi yetu, lakini ameendelea kutupa pumzi Watanzania na Wabunge ili tuendelee kutekeleza majukumu yetu ya kibunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipongeze sana viongozi wa Wizara hii, nikianza na Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, Naibu wake Mheshimiwa Deo Ndejembi, Makatibu Wakuu wakiongozwa na Ndugu Ndumbaro pamoja na watendaji wote. Wizara hii ni Wizara inachunga watu, Ndugu Ndumbaro ni mtaratibu na ni mtu mwenye hekima na anaishi kwa utaratibu na yuko makini sana. Kumchunga binadamu inabidi uwe na akili ya ziada kwa hiyo, nawapa hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze sana Wizara hii kwa hotuba nzuri, hotuba makini na imechambua vizuri kuhusu masuala ya utumishi. Misingi ya uongozi wa nchi yetu ililetwa na waasisi wa nchi hii akiwemo baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere pamoja na Mzee Karume. Walitoa matamshi yao ya uongozi kwamba, ili nchi hii iweze kuendelea inahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uongozi bora tunauona kwa Rais wetu mpendwa. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Sita, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, katikati ya bajeti ya 2021/2022 alifanya jitihada za kutafuta fedha Shilingi trilioni 1.3. Baada ya kuileta fedha ile akaipeleka Kamati ya Bajeti, Kamati ya Bajeti wakaona hii sio size ya Waziri wa Fedha aliyezoea kupanua vifungu, hii hela ni ya kupanua ukomo wa bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha ililetwa hapa na Wabunge tukapitisha kwa hiyo, sheria hapo ukiangalia utawala bora umetekelezwa. Fedha, bajeti ikaongezeka kutoka trilioni 36 mpaka trilioni 37.94 tunampongeza sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sasa angalia miongozo ambayo imetolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, bajeti yam waka huu wa fedha 2021/2022 makusanyo ya ndani walikuwa wamepanga kukusanya Shilingi trilioni 17. Hadi quarter ya tatu TRA walishakusanya trilioni 16. Na kwa ukusanyaji huu wa trilioni 1.84 kwa mwezi ina maana kwamba malengo yatafikiwa na yatapitwa, haijawahi kutokea ni kwa mara ya kwanza tutaona kwamba bajeti inakusanywa kwa asilimia 100. Nampa hongera sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pamoja na changamoto za kiuchumi wa dunia zinazoendelea bado Mheshimiwa Rais ameendelea kupambana kupanua vyanzo vya mapato. Ni hapa juzi tu mnaona jinsi ambavyo anaongoza suala la kampeni ya masuala ya utalii kupitia Royal Tour. Matokeo yake unaona bajeti tunayoijadili leo ya mwaka ujao wa fedha sasa tutaingia kwenye Shilingi trilioni 41. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha hizi zilizotolewa za Uvico na mimi nishukuru kwamba, jimbo langu lilipata 3,467,110,000 lakini zimefanya nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, zimejenga madarasa ya sekondari pamoja na madarasa ya shule shikizi. Kwa upande wa nchi nzima fedha hizi zimejenga zahanati na kujenga vituo vya afya na hospitali za wilaya. Maana yake ni nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, activities zimepanuka. Activities zikipanuka maana yake zinahitaji watumishi, lakini kutokana na kazi aliyoifanya Mheshimiwa Rais wetu kwamba, ameongeza fedha mpaka za kuajiri. Niipongeze sana hii Wizara kwa kuajiri kwa kuweka mpango. Kwanza wameshatangaza nafasi za kuajiri watu elfu 11, lakini na sasa wataajiri nafasi za watu elfu 32; na Mheshimiwa Waziri ametuonesha maoteo ya mwaka ujao pengine wa fedha, wanaweza wakatangaza tena nafasi elfu 30. Hongera sana, kweli hapa tunaona siasa safi na uongozi bora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wenzangu wamesimama kila mtu akasema kwake kuna upungufu kiasi gani wa wawatumishi. Mimi katika Halmashauri yangu ya Mlele nina upungufu wa watumishi 915. Kati ya hao walimu ni 149, lakini wahudumu wa afya ni 546, watendaji wa vijiji 8, lakini kada nyingine ni wahasibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasahivi tutakwenda kujadili ripoti ya CAG na mimi ni Mjumbe wa Kamati ya PAC. Wakati mwingine hizi hati zenye mashaka na hati chafu zinaletwa kwa sababu ya watu kutokuwa na weledi. Niombe sana na kushauri, kwamba hii kada ya wahasibu na hasa wahasibu wenye CPA, wenye degree pamoja na hizi diploma; na kwa sababu, kwenye bajeti kumewekwa fedha za skill development hawa wakifanyiwa semina nzuri nina hakika kabisa kwamba, hizi hati chafu na hati zenye mashaka zitapungua. Na zinapopungua ndivyo tunavyompa moyo zaidi Mheshimiwa Rais wetu, ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa furaha.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kutokana na hali yangu ya sauti hii, sikupanga kuongea mengi, lakini nimalizie tu kwa kusema kwamba, naunga mkono hoja. Nashukuru sana. (Makofi)
Makadirio na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia kwenye hii Wizara muhimu sana ya Ujenzi na Uchukuzi.

Mheshimiwa Spika, tarehe 18 ya mwezi huu wa Tano, wiki iliyopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alizindua barabara ya Tabora kwenda Mpanda kilometa 343. Wananchi wa Jimbo langu la Katavi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Katavi wamenituma nitoe salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Wanamshukuru sana na wanaishukuru Serikali kwa kutenga jumla ya Shilingi bilioni 473 na kuhakikisha kwamba barabara hii imekamilika kwa lami kutoka Tabora hadi Mpanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sipendi kukumbuka tulipotoka kwa sababu kabla ya kujengwa barabara hii kwa kiwango cha lami, kipindi cha masika tulikuwa miezi mitatu hadi minne hatuwezi kuitumia hiyo barabara na ndiyo barabara fupi inayotuunganisha na Makao Makuu ya nchi Dodoma pamoja na wakati ule nikiwa Dar es Salam.

Mheshimiwa Spika, tulikuwa kipindi cha masika ama upite Nyakanazi hadi Kigoma ndiyo urudi na barabara ya Uvinza kuja Mpanda; au upitie kwako Mbeya uende Tunduma, ndio ukazunguke Sumbawanga ndiyo uende Mpanda. Kwa kweli wananchi walikuwa wanateseka, wanatumia gharama kubwa.

Mheshimiwa Spika, sasa angalia mazingira kama hayo, kama kuna mgonjwa, kweli angepona? Sasa hivi ndiyo maana wananchi wa Mkoa wa Katavi wamenituma nimshukuru Mheshimiwa Rais. Ni kweli kwamba Sera ya ujenzi imeahidi kuunganisha Mikoa yote. Sisi kwanza tunashukuru kwamba Mkoa wa Tabora na Mkoa wa Katavi umeunganishwa. Pili, tunashukuru kwamba Mheshimiwa Waziri tayari ameshasaini mkataba wa kutoka Kibaoni kwenda Stalike. Maana yake ni nini? Barabara ile ikikamilika tutakuwa tumeunganishwa na Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Katavi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia tunazidi kuomba, kazi imeshaanza, tuna kilometa 37.5 za kutoka Mpanda kuelekea Uvinza; namwomba Mheshimiwa Waziri, wakati atakapohitimisha, hebu atuambie amejipangaje kukamilisha hii barabara ya kutoka Katavi, kutoka Mpanda, kwenda Uvinza ili tuweze kuungana na ndugu zetu wa Kigoma? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia wananchi wanamshukuru Mheshimiwa Rais kwamba hii miaka iliyopita mitatu au minne, alitoa Shilingi bilioni 48, ametujengea bandari ya Karema. Niwaambie tu wachumi wetu wa Wizara ya Ujenzi pamoja na Uchukuzi, angalieni wenzetu wa DRC, wiki iliyopita meli ya kwanza imetia nanga Bandari ya Karema pamoja na kwamba imekamilika kwa asilimia 80, na imekuja na mzigo mkubwa wa copper. Wameshaona faida ya barabara ya kutoka Tabora kwenda Mpanda na faida ya kujenga Bandari ya Karema, wameanza kuleta mzigo ili uweze kuja mpaka Bandari ya Dar es Salaam uweze kupekekwa kwenye soko Asia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, usafirishaji wa mizigo kutoka DRC ni ama utapita Bahari ya Atlantic kwa kupita South Africa au upite Bahari ya Hindi. Kusafirisha kupitia Bahari ya Hindi na Asia, ndiyo kwenye soko, ndiyo njia ambayo ni rahisi, ndio maana unaona wenzetu wameharakisha sana kuanza kuitumia hii Bandari ya Karema, kwa sababu lami tayari ipo kutoka Mpanda hadi Tabora, wanaitumia hiyo ili kupeleka mzigo Bandari ya Dar es Salaam, nasi tuweze kuongeza uchumi.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hilo, namwomba Mheshimiwa Waziri, hebu tupe neno, sasa hii barabara ya kutoka Mpanda kwenda Karema takribani kilometa 110 una mpango gani na hiyo barabara? Naomba sana utakapokuwa unahitimisha bajeti yako, sina mpango wa kushika shilingi kwa sababu sisi Wana-Katavi tuna furaha sana kwa hilo. Kwa hiyo, tunaimani kwamba utaendelea kutukumbuka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Mheshimiwa Waziri ana taasisi nyingi. Kuna taasisi ya TANROAD, TPA, Kampuni ya Meli Tanzania, TBA, TEMESA, reli TRC na Mamlaka ya Hali ya Hewa. Ile barabara ya kutoka Mpanda kwenda Karema tunaomba sana pia ijengwe reli. Tuna imani kwamba mzigo wa kutoka DRC utakuwa mkubwa sana. Cha kufanya, kwa sababu tunaendelea kujenga reli ya SGR, naomba kutoka Mpanda kwenda Karema tuweke tuta la SGR lakini reli tuweke ya miter gauge. Baadaye itakapokuwa uchumi umekaa vizuri, tutakuja kung’oa ile reli na kwa sababu tuta litakuwepo, tuweze kuweka sasa yale mataluma ya SGR. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jana kulikuwa na uchangiaji hapa kuhusu Mwanza, Ziwa Victoria, kwamba tunajenga meli Ziwa Victoria. Mimi nilikuwa Waziri wa Wizara hii. Uganda kila mwaka kuna mzigo wa tani milioni saba mpaka nane. Kwa hiyo, kitendo cha kujenga meli Ziwa Victoria kiendelee. Katika ile tani milioni nane, sisi huku kupitia Bandari ya Dar es Salaam, inapita tani haizidi 300,000.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kuna soko ambalo ni zuri kabisa. Naomba wachumi wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na Ujenzi hebu harakisheni, soko la Uganda lipo na hawana sehemu nyingine ya kupitisha.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ENG. ISACK A. KAMWELWE: Mheshimiwa Spika, naona unaniangalia. Nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)