Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Maryprisca Winfred Mahundi (511 total)

MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii niulize maswali mawili ya nyongeza lakini kwanza nipende kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuweka msukumo kwenye mradi huu. Pia niipongeze Serikali kwa maana ya Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa kufanya kazi vizuri na kufuatilia vizuri mradi huu na kuondoa wakandarasi ambao ni wazembe ambao wanachelewesha huduma kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza la nyongeza, kwa kuwa Desemba ni mbali kwa mahitaji ya maji katika Mji Mdogo wa Same kata za Njoro, Kisima, Stesheni pamoja na Same Mjini; na kwa kuwa Serikali hivi sasa inachimba visima viwili virefu, je, visima hivi vitakamilika lini ikiwa ni pamoja na kuweka pump kusudi wananchi hawa waweze kupunguza makali ya ukosefu wa maji kabla ya Desemba kufika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuongozana nami baada ya Bunge hili ili twende tukakague kata kwa kata, kijiji kwa kijiji, kitongoji kwa kitongoji kuhusiana na utekelezaji wa mradi huu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nipenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli tunafahamu kwamba Desemba ni mbali na maisha lazima yaendelee. Sisi Wizara ya Maji tuko imara kabisa kuhakikisha kwamba tatizo sugu la maji tunakwenda kulishughulikia kwa haraka sana. Wizara tumejipanga vyema chini ya Jemedari wetu Mheshimiwa Jumaa Aweso ambapo katika Mji wa Same kisima kipya kimeshachimbwa eneo la Stelingi chenye kina cha mita 200. Kazi hii ilianza Oktoba 2020 na itakamilika mwezi huu Februari 2021. Kama Quick-win program ya kuongeza uzalishaji wa maji katika Mji wa Same utahudumiwa na visima virefu viwili vilivyopo Stelingi na Kambambungu pamoja na chemichemi mbili za Mahuu na Same Beach.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa suala la kuongozana na wewe Mheshimiwa Mbunge usiwe na hofu, hiyo ndiyo shughuli yangu. Mheshimiwa Mbunge nitampa upendeleo mara baada ya Bunge hili tutakwenda, tutahakikisha wananchi wa Same Magharibi wanapata maji ya kutosha na hilo tatizo litabaki kuwa historia. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na napenda kumjulisha tu Mheshimiwa David kwamba timu kubwa ya club kubwa ya pale Msimbazi iko humu ndani basi na kesho tunakukaribisha. (Makofi/Kicheko)
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Mradi huu ulizinduliwa mwaka 2009 na baadaye ulikabidhiwa katika Mamlaka ya Maji Mwanhuzi lakini ulipokabidhiwa usambazaji wa maji haukufanyika kama ulivyokusudiwa. Nataka kujua Serikali ina mkakati gani kuhakikisha vitongoji vya Mwambegwa, Bulianaga, Jileji na Vibiti vinasambaziwa maji ikiwemo kujengewa tanki kupitia Wakala wa Maji Vijijini?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kwamba maji ya Bwawa la Mwanyahina yamefikia kiwango cha mwisho, yakitibiwa hayawezi kutakasika na wananchi tumekuwa tukiwatumainisha kuhusu ujio wa mradi wa wa maji wa Ziwa Victoria. Nataka kujua Serikali katika utekelezaji wake wa hatua za awali umefikia hatua zipi? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Komanya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Ziwa Victoria tayari utekelezaji wa awali unaendelea. Vilevile ili kuendelea kuhakikisha vijiji hivyo alivyovitaja vinaendelea kupata huduma ya maji wakati tukisubiri mradi ule wa muda mrefu tayari wataalam wetu wameweza kufanya usanifu na kuweza kuweka mkakati wa kuchimba visima 10.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa tayari visima vitatu vimechimbwa na viwili angalau vimeonyesha kwamba vina maji ya kutosha. Pale Mwandoya lita 40,000 kwa saa itaweza kupatikana katika moja ya visima ambavyo vimechimbwa.

Vilevile Mwankoli kisima kimeweza kupatikana chenye uwezo wa kutoa maji lita 8,500 kwa saa. Kwa hiyo, Wizara itaendelea kuhakikisha kuona kwamba maeneo yote tunayashughulikia na maji yanapatikana bombani.
MHE. MASACHE N. KASAKA:Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini kwa kuwa mpango huu wa kutumia maji ya Ziwa Nyasa ni wa muda mrefu na Serikali imekuwa inatoa ahadi hii mara kwa mara na hata kwenye ziara yako Mheshimiwa Naibu Waziri ulipofika na ulituahidi mradi huu utaanza.

Je, ni lini mradi huu utaanza ili walau kata za Kajunjumele, Ipinda, Kasumulu pamoja na Kyela Mjini waweze kunufaika?

Swali la pili kwa Wilaya yangu Wilaya ya Chunya kwa mwaka huu wa fedha zilitengwa fedha kwa ajili ya kuhudumia miradi ya maji kwa vijiji vinane lakini mpaka sasa hivi fedha hizo hazijaweza kutoka.

Je, ni lini fedha hizo zinaweza zikatoka ili sasa watu wangu wa vijiji vya Sangambi, Shoga, Kambikatoto, Lualaje, Nkung’ungu, Soweto na Itumbi waweze kunufaika nahii miradi ya maji? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally, Mbunge wa Kyela nipende kusema kwamba upembuzi yakinifu unaendelea na muda wa kufika mwezi Mei utakamilika na tunatarajia mwaka mpya wa fedha 2021/2022 Serikali itakwenda kutekeleza mradi huo.

Kuhusiana na swali lake la nyongeza kwa Wilaya ya Chunya nipende kusema kwamba Serikali imeweka jicho la kipekee kabisa kwa Wilaya ya Chunya na Chunya ni moja ya ile miji 28 ambayo tunaitarajia kuja kuitekeleza kwa fedha ambazo tumezipata za mkopo kutoka Serikali ya India kupitia benki ya Exim. Kwa hiyo kuanzia mwezi huu Machi shughuli ya kazi katika vijiji vya Sangambi na vile vijiji vya jirani pia vinakuja kutekelezwa, ahsante.
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali naomba kuongeza maswali ya nongeza mawili kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru Serikali kupitia Mheshimiwa Dkt. Magufuli, lakini pia na Waziri wa Wizara ya Maji pamoja na Naibu Waziri kwa usimamizi mzuri wa mradi unaoendelea katika Jimbo la Nkenge wa Kyaka Bunazi wa bilioni 15.1 na Mheshimiwa Naibu Waziri nikushukuru sana juzi ulitoka kule kuangalia maendeleo ya mradi.

Mheshimiwa Spika, mradi huo unahudumia vijiji saba katika Kata za Kyaka na Kasambia lakini kata zingine na vijiji ambavyo vimezunguka mradi huo. Je, ni lini Serikali itaongeza thamani ya mradi ya huo ambao una tenki lenye zaidi ya lita milioni mbili kuzunguka Kata za Nsunga, Mutukula, Bugorora, Bushasha ili thamani ya mradi iweze kuongezwa?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili Wilaya ya Misenye ambayo ni ndani ya Jimbo la Nkenge, ina vyanzo vingi vya maji na vyanzo hivi ni pamoja na Mto Kagera, lakini tuna Mto wa Ngono. Je, ni lini Serikali itaona ni vizuri kutumia vyanzo hivyo vya maji kuweza kupeleka maji katika vijiji ambavyo vinazunguka vyanzo hivyo vya Kata za Kakunyu, Kilimile, Mabale pamoja na Miziro? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nipende kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge na niseme kwamba mradi huu mkubwa ambao umeutambua na Mheshimiwa Waziri alifika pale na nikupongeze wewe binafsi kwa namna ambavyo umekuwa ukitoa ushirikiano katika Wizara yetu na nikuhakikishie tu kwamba mradi huu kuongezwa thamani tayari michakato imeanza na wataalam wetu wanafika huko hivi karibuni na kila kitu kitakwenda sawa kama ambavyo uliweza kuongea na Mheshimiwa Waziri alipokuwa ziarani katika jimbo lako.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kutumia vyanzo vingine vya maji ili kukidhi na kuondoa shida ya maji katika vijiji vile vingine Mheshimiwa Mbunge nikuahidi tu kwamba tunatarajia kufikia mwezi Juni, tutakuwa tumekamilisha hatua mbalimbali za kuona namna gani tunaibua vyanzo vipya lakini vyanzo vile vilivyoko tunaviboresha na kuona mtandao wa maji unaendelea kutawanyika katika jimbo lako vijiji vyote ambavyo havina maji kwa sasa viweze kupata maji. Ahsante.
MHE. FREDRICK E. LOWASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yako mazuri. Ni kweli kwamba Wananchi wa Jimbo la Monduli wanamwamini sana Mheshimiwa Rais na wanaimani kubwa sana na ahadi yake, lakini ni kweli pia tunaamini uongozi wa Wizara ya Maji ukiongozwa na ndugu yangu Mheshimiwa Juma Awesso, hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili ya nyongeza; tayari Monduli kuna miradi ambayo ipo ya maji lakini inasuasua, tunaomba kauli ya Serikali kuhusu mradi na mpango ambao mmejipanga nao.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, tunaomba kuhakikishiwa usimamizi mzuri juu ya ahadi hii ya Mheshimiwa Rais. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge Lowassa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miradi ambayo inasuasua mpango wa Wizara ni kuhakikisha kwamba miradi yote inakamilika kufikia wiki ya maji mwaka huu mwezi Machi na tayari wataalam wetu wanaendelea kufanyia kazi kwa maana ya miradi ambayo imetekelezwa kwa kutengeneza miundombinu lakini maji hayako bombani, tunatarajia kufikia mwezi Machi, Wiki ya Maji miradi hiyo itaanza kutoa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu usimamizi wa ahadi ya Mheshimiwa Rais, wote tunafahamu ahadi ni deni na ahadi hii ni ya Mheshimiwa Rais, naomba nimpe amani Mheshimiwa Mbunge kwamba miradi hii tutakwenda kusimamia na nafahamu alikuwa na ahadi na Mheshimiwa Waziri kwenda jimboni kesho lakini ile safari imeahirishwa kwa sababu ya msiba mkubwa uliotokea pale ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa hiyo hali itakapotulia kwenye Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Waziri atakwenda na kuhakikisha usimamizi unafanyika vizuri. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa mradi huu kama alivyosema yeye mwenyewe utachukua miezi 24, miaka miwili na wananchi wa Njombe wakati huo wataendelea kupata tabu na kuteseka hasa wakati wa kiangazi maji yanapopotea kabisa. Je, Serikali itakuwa tayari kutekeleza miradi mingine midogo midogo ambayo baadhi imekwishabuniwa na inafahamika na mingine inaweza kubuniwa, kwa vile Njombe tumezungukwa na mito kila upande?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Serikali ilishatekeleza mradi mdogo katika Mji wa Kibena pale Njombe, kwa kupeleka maji mpaka Hospitali ya Wilaya ya Njombe na kuna tanki kubwa sana wamelijenga pale na tanki hilo lina maji mengi na saa nyingine yanabubujika na kumwagika. Kwa bahati mbaya wananchi wa eneo la Kibena ambao wanaishi maeneo yale bado hawana. Je, Serikali haioni kama itakuwa ni busara na jambo jema badala ya maji yale kuwa yanabubujika na kumwagika sasa wakatoa pesa na kuweka mradi mdogo wa kutawanya maji ili wananchi wa Kibena wapate kuwa na maji ya uhakika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwanyika kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa suala la hofu kwa sababu mradi utaanza mwezi Aprili na yeye anapenda visima ama miradi midogo midogo, nipende tu kumwambia kwamba tayari Wizara inafanya mchakato huo na hili linashughulikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na mradi ambao unapeleka maji kwenye hospitali ya Kibena pale kwa kuhitaji distribution tayari Wizara imetoa maelekezo kwa mameneja walioko pale wanafanyia upembuzi yakinifu ili kuona namna gani kama distribution itawezekana. Naomba kukupa amani Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi huu ambao tunauanza mwezi Aprili, tutaenda kuufanya kwa kasi nzuri na tutaweza kutawanya maji kadri mradi unavyokamilika hatutasubiri mradi ukamilike mpaka mwisho, ukifika hata asilimia 40 wale ambao wanapitiwa na lile eneo ambalo miundombinu imekamilika maji yataweza kutoka. (Makofi)
MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali la nyongeza. Kwanza napenda kupongeza Wizara ya Maji, Mheshimiwa Waziri Aweso na Mheshimiwa Engineer Maryprisca ya kutembelea Mikoa yetu ya Kusini, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na Njombe, kazi nimeiona, mmefanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu moja la nyongeza, pale Mkwajuni Makao Mkuu ya Wilaya pana mradi mkubwa wa maji wa milioni 760 toka mwaka 2018. Mkandarasi ametumia fedha zake binafsi karibuni asilimia 80 anakamilisha mradi, lakini anakwamishwa na malipo ya Serikali baada ya kumaliza zile kazi, certificate anapeleka lakini halipwi. Galula pana mradi wa maji, Kapalala pana mradi wa maji. Hii miradi mitatu kwenye jimbo langu imekuwa ni kero sana kwa wananchi na wale wakandarasi wameshamaliza lakini wanasubiri certificate ili waweze kulipwa. Je, ni lini Serikali itawalipa fedha zao ili miradi ya maji ikamilike?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, malipo yote ambayo wakandarasi wamefanya kazi na kazi zinaonekana malipo yote yanaendelea kushughulikiwa na hivi karibuni Serikali itawalipa.
MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini pia naishukuru Serikali kwa kuweza kutekeleza Mradi wa Maji kwa Mji wa Chunya uliogharimu zaidi ya milioni 900 lakini mradi huu mpaka sasa hivi haujaweza kuwanufaisha wananchi wa Wilaya ya Chunya na hata kiwango cha upatikanaji wa maji bado kiko chini ya asilimia 30. Tatizo kubwa tukiuliza tunaambiwa mara umeme unakuwa ni mdogo, mara maji ni machache. Sasa Serikali itueleze, je, tatizo ni nini mpaka mradi huu uliotumia fedha nyingi za Serikali haujaweza kuwanufaisha watu wa Chunya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwenye mradi mkubwa wa maji wa bwawa la Matwiga design ya mwanzo ilikuwa inasema itanufaisha vijiji 16, lakini kwenye review ilivyokuja utekelezaji wake ni vijiji nane. Je, Serikali haioni haja sasa kuweza kurudisha hii design ya mwanzo kurudisha vijiji 16 ili wananchi wa Tarafa ya Kipendao waweze kunufaika na mradi huu wa maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Masache Kasaka kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nia na lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama na ya kutosheleza. Niseme tu msimamo wa Serikali ni kuona kwamba miradi iliyokamilika na matunda yale ya mwisho maji bombani yanapatikana. Kwa mradi huu wa Chunya Mjini nipende tu kusema kwamba Mheshimiwa Mbunge nilifika Chunya na tulitembea pamoja, mradi ule umekamilika tatizo ni hili la umeme ambalo linaendelea kushughulikiwa ili liweze ku-support ile pump maji yaweze kwenda ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa swali la Bwawa la Matwiga, niseme kwamba, katika miradi ambayo ilichukua muda mrefu kutekelezwa ni pamoja na huu, lakini kwa nia njema ya Serikali hii na mkakati mkubwa wa Wizara chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Waziri mradi ule sasa hivi unatekelezwa vizuri na mimi pamoja na Mheshimiwa Mbunge tulifika pale tukiongozana na Mtendaji Mkuu wa RUWASA kwa maana ya Director General. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, yale maji ambayo tuliyaona pale kwa pamoja kwenye kile chanzo hayatatoa tu kwa vijiji vile nane, tayari kama Wizara tumekubaliana tutakuja kutoa maji katika vijiji vyote 16.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa Mradi wa Maji Chunya unafanana na ule mradi wa 2F2B pale Tegeta A, ujazo wa lita milioni sita. Je, Wizara inaweza ikatuambia ni lini mradi ule utakamilika ili uweze kusaidia wananchi wote wa Goba?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ule mradi wa tanki Mshikamano kwa ajili ya wananchi wa Mpiji Magohe, Makabe yote na Msakuzi.

Je, ni lini pia mradi huo utakamilika ili wananchi wapate maji salama?

SPIKA: Swali sio lako, kwa hiyo unapaswa kuuliza swali moja tu, sasa chagua mojawapo katika hayo ya kwako.

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Niweze kufahamu mradi unaotaka kujengwa mshikamano kwa ajili ya wananchi wa Mbezi, Makabe na Mpiji Magohe utakamilika lini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Mtemvu kutoka Kibamba kama ifuatavyo:-.

Mheshimiwa Spika, Wizara sasa hivi inapitia miradi hii yote ambayo usanifu wake ulikamilika. Kwa hiyo nipende tu kumwambia Mheshimiwa Mbunge huo mradi upo katika miradi ambayo inakwenda kutekelezwa awamu hii kabla mwaka huu wa fedha haujaisha.
MHE. NOAH L. S. MOLLE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri , lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Serikali ina nia njema ya kutoa huduma ya maji, kulikuwa na miradi ya mwaka 2009 miradi ya Likamba, Musa, Nengu, Olotushura na Loskito, je, ni lini sasa Serikali itakamilisha miradi hiyo ya muda mrefu?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa kulikuwa na ahadi ya Mheshimiwa Waziri wa Maji katika kukarabati Mradi wa Ilmuro inayohudumia Kata za Oljoro na Laroy. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Waziri? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Lemburis Saputu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mradi huu ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2009, nipende tu kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge miradi hii tunakuja kuitekeleza na nimeshafika eneo lake. Nimwahidi namna ambavyo tuliongea pale site tutakuja kufanyia kazi haraka iwezekanavyo na pamoja na hii ahadi ya Mheshimiwa Waziri aliyepita, ukarabati wa Mradi huo wa Ilmuro pia unakuja kufanyiwa kazi hivi karibuni. Fedha tayari zipo na mgao unaofuata na mgao unaofuata na Mheshimiwa Mbunge yupo na atakwenda kutekelezewa mradi huo.
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali na niipongeze Serikali kwa namna inavyochukua hatua juu ya mradi ule. Pamoja na hayo mradi ule katika Kijiji cha Mwagulanja umeacha sehemu kubwa sana ya wananchi wa Isuka takriban kilometa nne kufikia point ambapo maji yamewekwa.

SPIKA: Mheshimiwa swali lako ni Nyashimo…

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Spika, ni Kata ya Nyashimo sasa hicho Kijiji nilichokisema. Naomba tu kuuliza Serikali nini mpango sasa wa kufanya extension kutoka kwenye ule mradi kwenda kwenye Kijiji cha Mwagulanje kule Isuka ili wananchi wa kule nao waweze kupata maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Simon Lusengekile, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, huu mradi unaendelea kutekelezwa. Extension ni kazi ambayo hata yule Meneja aliyeko pale anaweza kufanya, kwa hiyo nimwaminishe Mheshimiwa Mbunge kwamba kufika mwezi Machi, tutaanza kuzitekeleza extension, lakini kwa kutumia wataalam wetu ambao wako kule.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kyerwa kuna changamoto kubwa ya maji na hasa Kata za Kibale, Bugomora na Mrongo ila ninavyoongea hapa Kijiji cha Mgorogoro kuna tanki kubwa la maji ambalo tangu limewekwa…

SPIKA: Ni wapi huko unakokuulizia?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, Kata ya Kibale.

SPIKA: Kata hiyo iko kwenye Wilaya gani?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kyerwa, Jimbo la Kyerwa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, tanki limewekwa kama urembo halijawahi kutoa maji. Kila siku wananchi wakiona habari za maji wananitumia message na sasa wamenikumbusha. Ni lini lile tanki katika Kijiji cha Mgorogoro litaanza kutoa maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anatropia kuhusu tenki kubwa lililokamilika lakini halitoi maji. Mkakati wa Wizara ni kuona kwamba miradi hii ambayo miundombinu imekamilika kufikia mwezi wa tatu kwenye Wiki ya Maji tunataka kuona kwamba maji yanatoka.

Mheshimiwa Spika, nimuahidi Mheshimiwa Anatropia kwamba nitafika huko Kyerwa na kuona nini kinasababisha maji hayatoki. Lengo ni kuona kwamba maji yanapatikana bombani. (Makofi)
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza naipongeza Serikali kwa juhudi za kuwapatia wananchi wa Kyerwa maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijauliza maswali, kwenye majibu aliyotujibu, kuna sehemu ambayo haiko sahihi. Vijiji vya Kibale, Nyamiaga na Magoma hakuna kisima ambacho kimechimbwa. Kwa hiyo, hiyo taarifa aliyonipa siyo sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, huu mradi ni muhimu sana kwa ajili ya wananchi wa Jimbo la Kyerwa. Mheshimiwa Waziri ananihakikishia kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022 atatenga fedha kwa ajili ya mradi huu ili uweze kutekelezwa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Ziko Kata ambazo haziko kwenye huu mradi, Kata za Bugomora, Kibale, Murongo pamoja na Businde. Serikali ina mpango gani wa kuzipatia maji Kata hizi ili nao watoke kwenye adha wanayoipata? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Bilakwate, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza kuhusu kutengwa fedha kwa mwaka wa fedha ujao kwa mradi huu mkubwa, azma ya Serikali ni kuhakikisha miradi hii yote tunaitekeleza kwa wakati. Hivyo, katika mwaka wa fedha ujao 2021/2022 mradi huu utapatiwa fedha kwa awamu na utekelezaji wake utaanza mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ambazo amezitaja Mheshimiwa Mbunge, napenda tu kusema kwamba tutahakikisha maeneo yote yenye matatizo ya maji, maji yanapatikana. Kwa mradi huu mkubwa ambapo bomba kubwa litapita, michepuo ya maji pia itazingatiwa; na kwa maeneo ambayo michepuo haitafika kwa urahisi, basi uchimbaji na ujenzi wa visima utazingatiwa katika mwaka wa fedha ujao.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali ila naomba yafanyike masahihisho. Ni Mji wa Mangaka, sio Banyaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, maswali yangu mawili ni kama ifuatavyo; la kwanza; kwa kuwa Mradi huu wa kuvuta maji kutoka Mto Ruvuma kwenda Mji wa Mangaka unaanzia Kata ya Masuguru, unapita Nanyumbu, Chipuputa, Kilimanihewa hadi Sengenya ambapo matenki yatajengwa. Swali, je, vijiji vitakavyopitiwa na bomba hili vitanufaika vipi na mradi huu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; tunatambua kwamba mradi huu utachukua miaka miwili na wananchi wa Jimbo langu wana shida kubwa ya maji. Serikali ina mpango gani wa dharura wa kuwanusuru wananchi hawa wakati wanasubiri mradi kukamilika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Yahya kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ameuliza, kwa sababu Mradi wa Ruvuma utapita kwenye hizi Kata tano alizozitaja, vijiji vitanufaikaje. Kama tunavyofahamu Sera ya Maji hairuhusu Kijiji cha B kianze kupata maji A kikarukwa. Nipende kusema kwamba vijiji vyote ambavyo mradi huu utavipitia, basi watapata maji kwa sababu lile bomba kuu litaruhusu michepuo kwa vijiji vile vinavyopitiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile ameongelea suala la muda mfupi. Mradi huu tunautarajia uchukue miezi 12 na tunatarajia uanze mwezi Mei mwaka huu. Mheshimiwa Mbunge hii kazi itafanyika kwa kasi kwa sababu tayari fedha zipo, hivyo itakuwa ni kazi ya muda mfupi na maji yataweza kuwafikia wananchi wetu kwa wakati. (Makofi)
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jitihada kubwa za Serikali za kumaliza tatizo la maji katika Mji wa Tunduma, bado changamoto kubwa imebaki kuwa kukosekana kwa chanzo cha uhakika katika Mji wa Tunduma. Je, nini mkakati wa Serikali wa kutekeleza ahadi aliyotoa Mheshimiwa Rais wakati wa uchaguzi ya kuvuta maji kutoka chanzo cha uhakika kilichopo katika Mji wa Ileje? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Juliana Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Songwe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, chanzo cha uhakika cha maji kwa Mji wa Tunduma kama alivyoongelea chanzo cha maji kutoka Ileje, feasibility study inaendelea kufanyika na mara itakapokamilika basi mradi ule utatengewa fedha kwa awamu na utekelezaji utaanza mara moja. Vile vile kwa nyongeza pale Tunduma nimeshafika na kuona namna gani bora ya kuweza kupatikana kwa maji kwa sababu miundombinu ya awali tayari ilikamilika Mheshimiwa Mbunge niseme tulishaweza kumpa maelekezo Meneja wa Maji Mkoa, RUWASA na yule Engineer ni Engineer ambaye tunamtegemea katika Wizara na anafanya kazi vizuri sana. Hivyo, nikuhakikishie shida ya maji katika Mji wa Tunduma inakwenda kuwa historia. (Makofi)
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Sisi Namtumbo kule tuna miradi ya maji yenye takriban miaka nane lakini bado haijakamilika na kuna changamoto ya ukamilifu wa miradi hiyo hasa vifaa na mabomba. Je, Mheshimiwa Waziri anaweza kuwa tayari kuongozana nami kabla ya Bunge la Bajeti kwenda kuona miradi hiyo na changamoto yake na kuona ni jinsi gani atatuongezea nguvu ili kukamilisha miradi hiyo? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vita Kawawa unataka kuongozana na Naibu Waziri au Waziri? Ni yupi uliyemwomba kati ya hao? (Makofi/Kicheko)

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri. (Makofi/Kicheko)
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa namna anavyojibu maswali vizuri na nimpongeze na Mheshimiwa Mbunge kaka yangu Kawawa kwa kazi kubwa anayoifanya Namtumbo. Kubwa mimi nipo tayari kuongozana naye. Mkoa wa Ruvuma pia ni moja ya mikoa ambayo tumeainisha hii changamoto ya maji na tumewapatia zaidi ya bilioni nane na katika wilaya yake tumeipa 1.3 billion katika kuhakikisha tunatatua tatizo la maji. Kwa hiyo, tunamtaka Mhandisi wa Maji, Namtumbo aache porojo, afanye kazi kuhakikisha wananchi hawa wanaweza kupata huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Waziri anajua Mradi wa Maji wa Bunda umetumia zaidi ya miaka 13, tayari maji yameshatoka Ziwa Victoria, kata saba za mjini wameanza kueneza mtandao wa maji na takriban milioni 300 zilienda. Ninachotaka kujua kama Mbunge senior wa eneo lile na kipenzi cha Wanabunda, ni lini Kata 14 zitapata maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, Mbunge wa Viti Maalum, kuhusiana na Bunda mradi uliokaa kwa miaka 13 kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Maji lengo letu ni kuona kwamba tunaleta mapinduzi makubwa sana kuona maji sasa yanakwenda kupatikana. Miradi hii ambayo miundombinu imekamilika bado maji hayatoshelezi, wataalam wanaendelea na kazi na tutahakikisha maji yanaenda kupatikana. Napenda kusema kwamba Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo alishafika kwangu mara kadhaa na suala hili tunakwenda kulitekeleza haraka. Ziara yangu baada ya hapa ni kuelekea ukanda huo, basi Bunda napo pia nitafika na maji yatapatikana. (Makofi)
MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii. Kabla ya yote nipongeze sana Wizara ya Maji. Napongeza Wizara ya Maji, Naibu Waziri alikuja kwetu Rungwe Jimboni, ametembelea miradi, ameona matatizo ya maji kwa wananchi wa Rungwe. Naomba sasa niulize swali langu; je, ni lini mradi wa maji wa Mji Mdogo wa Tukuyu utaanza kutekelezwa hasa baada ya Naibu Spika kutembelea na kutuahidi pale. Lakini pia upembuzi yakinifu ulishafanyika…

NAIBU SPIKA: Umeshauliza swali.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantona Mbunge wa Rungwe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji mdogo wa Tukuyu tunafahamu kabisa miundombinu yake ni chakavu na idadi ya watu imeongezeka, tayari maelekezo yapo kwa Meneja wa Maji Mkoa wa Mbeya na ameshaanza manunuzi ya vifaa vya kazi na kufikia mwezi Machi kazi zitaanza kufanyika pale Tukuyu na upatikanaji wa maji unakwenda kuboreshwa. (Makofi)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali imekiri kabisa kwamba wananchi wa Tarime asilimia 20 ndiyo wanaopata maji. Tatizo la maji ni Tanzania nzima. Sasa napenda kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa miradi ya muda mfupi; visima virefu, Mradi wa Bwawa la Nyanduma ambalo tumekuwa tukilitengea fedha lakini haziendi na miradi mingine kama ya Gamasala na kwingineko kwa Tarime Mji, napenda kujua, ni lini Serikali itaenda kuchimba vile visima 23 ambavyo wameahidi kuanzia mwaka 2016 viweze kuwa suluhisho la muda mfupi kwenye Kata ya Kitale, Nyandoto, Kenyamanyoli na Mkende wakati tunasubiria Mradi wa Ziwa Victoria? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, jana wakati wameweka Mpango hapa, Serikali imekiri kabisa kwamba imepeleka maji vijijini kwa asilimia 70.1, wamechimba visima miradi 1,423 ambapo kuna vituo…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther, naomba uulize swali tafadhali.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Miradi hiyo ina vituo 131,000. Kwa Rorya tuna mradi mkubwa kule Kirogo ambao umetumia zaidi ya shilingi bilioni 1.3, ulitakiwa kuwa na vituo 23…

NAIBU SPIKA: Swali Mheshimiwa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: … lakini kuna vituo vitatu tu ambavyo vinatoa maji. Ni lini sasa Serikali itahakikisha maji yanatoka kule Kirogo kwa vituo vyote 23 na siyo vituo vitatu tu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi, salama na ya kutosheleza kwa maeneo yote ya nchi yetu ya Tanzania. Hivi karibuni Mheshimiwa Waziri alikuwa ziarani hapo Tarime na aliweza kuwasiliana na kuambatana na Mbunge wa Tarime Mjini ambaye ni Mheshimiwa Kembaki na Mbunge wa Tarime Vijijini, Mheshimiwa Naibu Waziri Waitara na Mheshimiwa Waziri ametoa ahadi hivyo visima vyote vitachimbwa ndani ya kipindi hiki cha miaka mitano. Kwa kuanza, katika mwaka wa fedha ujao, visima vitachimbwa na maji safi na salama yatapatikana bombani kwa wananchi wote wa Tarime. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kama nilivyojibu kwenye jibu langu la awali ambalo ni jibu langu la msingi. Eneo la Rorya visima hivi vitatu kwa sasa hivi vinapata maji kati ya 27. Vijiji hivi vinakwenda kupatiwa huduma kupitia Mwaka wa Fedha 2021/2022 lakini vile vile tayari Wahandisi wetu wa eneo lile wanaendelea na hii kazi na visima vile ambavyo vilisalia vinakwenda kuchimbwa na kuhakikisha kuona kwamba vinakwenda kutoa maji ya kutosheleza kwa wananchi wote wa Rorya.
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa ziara yake aliyoifanya ndani ya Jimbo langu la Rorya ikiwa ni pamoja na maelekezo ya Mradi wa Kirogo kwamba mkandarasi aliyetekeleza ule mradi kwa kiwango cha chini achukuliwe hatua. Kwa hiyo, nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa maamuzi makubwa na mazuri aliyoyafanya kipindi alipofanya ziara yake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mradi huu wa maji unaotoka Ziwa Victoria kwenda Tarime unaanzia ndani ya Jimbo langu la Rorya, zaidi ya Kata 11 na vijiji zaidi ya 28 vinategemea kufaidika na mradi huu. Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kuanza kutekeleza mradi huu hata kama ni kwa awamu ili kutatua changamoto za mradi huo wa maji ambao kimsingi utashughulika na Jimbo la Rorya, Tarime Vijijini na Tarime Mjini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari Serikali tumeweka mikakati kuhakikisha tunaondoa changamoto ya maji kwenye maeneo yote yenye shida hiyo. Kwa Jimbo la Rorya, napenda kumwambia Mheshimiwa Mbunge, tayari Wizara iko kwenye michanganuo ya kuleta fedha katika maeneo hayo. Vilevile nimwambie tu kwamba baada ya Bunge hili, fedha awamu hii inayofuata, Jimbo lake pia limezingatiwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Rwakajunju ulioko Karagwe, nimeshauliza sana maswali katika Bunge la Kumi na Moja na mara zote huwa najibiwa kwamba mradi huo utatekeleza hivi karibuni lakini hadi sasa bado haujatekelezwa. Nini majibu ya Serikali kuhusu mradi huu ili kuwatua ndoo akina mama wa Karagwe? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi huu utatekelezwa kwa awamu katika mwaka wa fedha wa 2021/2022.
MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Wizara ya Maji. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwenye Mradi wa Maji Tukuyu nimeridhika, lakini kuna mradi mwingine ambao unaendelea katika Mji wa Ushirika, Kata ya Mpuguso. Tenki tayari limeshajengwa, mabomba tayari yameshafika kwenye tenki, usambazaji wa maji bado kwa wananchi kwa muda mrefu. Naomba Wizara ituambie wananchi wa Rungwe lini itaanza kusambaza maji kwa wananchi wa Rungwe?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; tuna Kituo cha Afya cha Ikuti ambacho kina matatizo makubwa sana ya maji. Nilikuwa naomba Wizara iwaambie wananchi wa Ikuti, Jimbo la Rungwe, ni lini maji yatasambazwa hasa baada ya upembuzi yakinifu wa mradi ule kuonekana kwamba, ni milioni 100 tu ambayo itapeleka maji kutoka kwenye chanzo cha maji mpaka kwenye Kituo cha Afya cha Ikuti? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, Anton Albert Mwantona, Mbunge wa Rungwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi unaoendelea pale miundombinu yake imeshakamilika, imebaki tu usambazaji wa maji. Mheshimiwa Mbunge mradi ule unakwenda kukamilika wiki chache zijazo na maji yatafika mabombani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Kituo cha Afya cha Ikuti kupata maji, Mheshimiwa Mbunge Serikali tutalifanyia kazi na namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, ndani ya muda mfupi utekelezaji wake utakuja kufanyika.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwanza nimpongeze Naibu Waziri wa Maji pamoja na Waziri wake kwa kuufuatilia Mradi wa Nyanghwale na hivi karibuni unaenda kukamilika, nawapongeza sana. Swali langu ni kwamba, kwa kuwa mradi huu unaenda kukamilika. Je, bajeti ijayo Serikali imejipanga vipi kwenda kuweka mpango wa kusambaza maji kwenye kata zifuatazo: Kata ya Busolwa, Nyanghwale, Ijundu, Kakola, Shabaka na Mwingilo. Je, Wizara imejipanga vipi kwenda kusambaza maji hayo kwenye bajeti ijayo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hussein Amar, Mbunge wa Nyanghwale, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuweka mipango mahususi kuhakikisha mradi ule ambao tayari upo kwenye utekelezaji kwenye hatua za mwisho unakwenda kukamilika.
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Suala la maji la Tukuyu linalingana kabisa na matatizo ya maji katika Jimbo la Makambako. Mambo ya upembuzi yakinifu yalishafanyika. Je, Serikali ina mpango gani kupeleka maji au kutatua tatizo la maji katika Mji wa Makambako kwa sababu, tumekuwa tukiwaahidi watu kwa muda mrefu, ni lini sasa mradi ambao tumekuwa tukiwaambia wananchi utaanza kutekelezwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deo Sanga, Mbunge wa Makambako, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Makambako ni moja ya miji 28 ambayo inakwenda kunufaika na mradi ule mkubwa ambao tumeshapata fedha kutoka Benki ya Exim. Hivyo, Serikali inakwenda kuanza kutekeleza miradi hii yote ndani ya miji 28 ifikapo mwezi Aprili. Mheshimiwa Deo Sanga mradi wa maji Makambako nao ni sehemu ya miradi ya miji 28 hivyo kufikia mwezi Aprili wataalam wetu pamoja na wakandarasi watafika site kuanza kazi.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Nitoe shukrani kwa Serikali kwa majibu mazuri kabisa ya kuridhisha kwa ajili ya wananchi wa Biharamulo lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Miji ya Nyakanazi, Nyakahura na Nyanza ni miongoni mwa sehemu ambazo zinapanuka kwa kasi katika Wilaya ya Biharamulo lakini bado zina ukosefu wa maji. Naomba kujua au kusikia kauli ya Serikali jinsi gani hawa wananchi wataweza kupatiwa huduma ya maji katika mwaka huu wa fedha au mwaka ujao ili tuweze kuondoa kero hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Kata ya Kaniha na Nyantakala zinabeba shule mbili kubwa za boarding pale Biharamulo na shule zile zina uhaba mkubwa wa maji. Naomba kupata kauli ya Serikali ni lini wataweza hata kuchimbiwa visima viwili virefu katika shule zile ili watoto hao waweze kuondokana na adha ya kupata maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Engineer Ezra John Chiwelesa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua vema tatizo la maji lililopo pale Biharamulo. Hivi karibuni Mheshimiwa Waziri alikuwa katika Kata ya Nyakahura kwenye ziara yake ya kikazi. Kwa sasa maji toka Bwawa la Nyakahura ambapo vijiji vinne vinapata maji, tunatambua utekelezaji wake unakwenda vizuri kwa vijiji vile vinne.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia tunafahamu kuna ushirikiano mzuri kati ya RUWASA pamoja na BWSSA. Tayari Serikali inafahamu chanzo kile bado hakitoshelezi kwa sababu ya ongezeko la watu. Tayari Serikali kupitia EWURA imeshatenga fedha za usanifu wa maji kutoka kwenye Mto Myovozi. Lengo ni kuona kwamba eneo lote la Nyakahura linakwenda kupata maji safi na salama ya kutosheleza hivi karibuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kwenye kwenye Kata ya Nyanza usanifu unaendelea. Pia tutahakikisha maji ya kutosha yanakwenda kupatikana. Tayari kuna chanzo chenye uwezo wa lita 50,000 kwa saa ambapo maji haya yatasaidia sana mpaka kwenye Kata ya Nyanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali inatambua umuhimu wa maji mashuleni. Tayari kwenye Shule ya Mbaba kuna kisima kirefu pale kimechimbwa na maji yanapatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Nyantakara, mradi umetekelezwa. Pale tuna mradi mkubwa tu ambapo fedha zaidi ya shilingi milioni 300 zimeelekezwa na maji yatafika mabombani muda sio mrefu, haitazidi wiki tatu.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, naipongeza Serikali kwa majibu mazuri lakini pia nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hotuba yake aliyoitoa tarehe 30 Mjini Tabora ambayo ilituhakikishia kwamba tutapata maji na baadaye pia kuongezewa zaidi na Mheshimiwa Waziri wa Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, Serikali haioni kwamba changamoto kubwa ya maji sasa inakaribia kupata ufumbuzi baada ya kuhakikishiwa kwamba mradi utafika huko, Mheshimiwa Waziri anaweza kuja Urambo kwa sasa hivi akaangalia hali halisi na huenda akaongezea hata maeneo yatakayonufaika na mradi huo?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia tumuandalie mkutano wa hadhara arudishie maneno hayahaya ili wananchi wa Urambo waendelee kuishi kwa matumaini na kushukuru Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa kwa sababu amekuwa ni mfuatiliaji mzuri sana. Kwa kuwa ahadi ya Mheshimiwa Rais lazima tuitekeleze kwa nguvu zetu zote na Urambo inakwenda kunufaika, niseme niko tayari kuja Urambo na mkutano wa hadhara hapa ndiyo mahala pake. Nitahakikisha naelekeza vema jamii ya Urambo na watamuelewa Mheshimiwa Mbunge kwamba sasa matatizo ya maji yanakwenda kufikia ukingoni.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona. Naomba na mimi niulize swali moja tu, ni lini Serikali ya Chama cha Mapinduzi itakwenda kutekeleza miradi ya visima 10 vilivyochimbwa Jimbo la Singida Magharibi katika vijiji vya Minyuge, Mpetu, Kaugeri, Mduguyu pamoja na Vijiji vya Mnang’ana, Munyu na Irisya ukizingatia Jimbo la Singida Magharibi ni miongoni mwa Majimbo ambayo yana changamoto kubwa sana ya maji? Naomba nipate jibu serious kutoka kwenye Serikali serious. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kingu kutoka Singida Magharibi, kama ifuatavyo:-

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Siyo daktari.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Nimekutunuku au siyo. Wanasema dalili nje huonekana asubuhi, daktari rudi shule ukapate hiyo profession. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya Serikali ni maeneo yote ambayo yalishafanyiwa usanifu tunakuja kuhakikisha kazi zinafanyika ndani ya wakati. Hivyo visima vyote vitachimbwa kadiri ambavyo vipo kwenye bajeti na maji tutahakikisha hayaishii kwenye kisima bali yanatembea kwenye bomba kuu na kuwafikia wananchi kwenye mabomba yao katika makazi lakini vilevile katika vituo vya kuchotea maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, haya yote yanakwenda kutekelezwa kwa kipindi hiki kilichobaki cha mwaka wa fedha na mwaka wa fedha 2021/2022. Isitoshe nitafika kuona eneo husika na kuleta chachu zaidi kwa watendaji wetu, japo tayari tuna watendaji wazuri katika Wizara na wanafanya kazi vizuri sana. (Makofi)
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ninayo maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikipoteza pesa nyingi sana, hasa kwenye miradi na miradi ya maji ikiwapo hasa huu mradi wa Chipingo. Hii imetokea mara nyingi kutokana na watendaji ambao sio waaminifu wakishirikiana na wakandarasi kuhujumu Taifa kwa kutotimiza majukumu ya mikataba yao. Je, Serikali ina tamko gani kuhusiana na suala hili? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, sina shaka na utendaji wa Wizara hii; Mheshimiwa Aweso pamoja na timu yake wanachapa kazi sana lakini wale watendaji wenu kule wanawaangusha. Je, Mheshimiwa Waziri au Naibu Waziri anakubali kuambatana na mimi kwenda kuangalia hali halisi mkajiridhisha kisha mkatatua changamoto hii kwa umakini kabisa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge Issa Mchungahela kutoka Jimbo la Lulindi, kama ifauatvyo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa sasa hivi tumekuwa tukifanya jitihada za kuona kwamba watendaji wanaendana na kasi ya hitaji la Wizara yetu kwa sababu, madeni yote na miradi ambayo imekuwa ya muda mrefu awamu hii tunaelekea kuikamilisha.

Mheshimiwa Spika, hivyo, napenda kumtoa hofu Mheshimiwa Mbunge kwa hawa watendaji ambao wanakiuka maadili yao ya kazi na kuweza kuwa wahujumu katika shughuli zao tayari tunawashughulikia na tayari tuna mkeka mpya wa Wahandisi ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao kadiri ambavyo tunahitaji watuvushe.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusiana na suala la kuambatana, Mheshimiwa Mbunge aondoe hofu. Hiyo ndiyo moja ya majukumu yangu na ninamhakikishia baada ya kukamilisha ziara yangu kwenye maeneo mengine, basi na hata huko Masasi pia nitakuja na nitajitahidi kufika kwenye majimbo yote kuona suala la maji linakwenda kupata muarobaini.
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile mradi huu wa Chankorongo ulioko Ziwa Victoria unaweza tu kupita katika vijiji alivyovitaja; je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba maji kutoka Ziwa Victoria yanaweza kufika kwenye maeneo ya Nyarugusu, Bukoli na Kata ya Nyakamwaga? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Magessa, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa eneo la Nyarugusu, maeneo ya machimbo haya Serikali tayari tuko kwenye mpango wa kupitisha mradi mkubwa pale wa maji kutoka Geita na utapita eneo hilo maji yanayotoka Ziwa Victoria na eneo lile pia, watapata extension kwa maana ya mtandao wa mabomba, maji yatafikia hapo na vilevile nipende kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge namna ambavyo waliweza kuzungumza na Mheshimiwa Waziri alipokuwa ziara katika eneo lake, basi yale mazungumzo yamezingatiwa kama ambavyo umeona tayari Meneja yule aliweza kubadilishwa na sasa hivi yupo Meneja mwingine ambaye yupo tayari kuendana na kasi ya Wizara hivyo, eneo la Nyarugusu pia litapata maji.
MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ya maji ya Busanda inafanana kabisa na changamoto ya maji iliyoko Korogwe Mjini. Nimekuwa nikifuatilia kwa Mheshimiwa Waziri na ameniahidi tatizo la Korogwe litatatuliwa na mradi wa miji 28 ambao Korogwe ni sehemu ya mradi huo.

Je, Serikali inawaahidi vipi wananchi wa Korogwe kwamba lini mradi huu utatekelezwa ili kuweza kutatua changamoto ya maji ambayo inawakabili wananchi wa Korogwe Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Alfred Kimea, Mbunge wa Korogwe Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipende kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa sababu amekuwa ni mfuatiliaji mzuri na nimeshaweza kuongea naye mara kadhaa na kumhakikishia eneo lake kupata maji na uzuri Korogwe Mjini ipo ndani ya ile miji 28 ambayo fedha tayari zipo na muendelezo wa maandalizi unaendelea na hivi karibuni kuanzia mwezi Aprili miji ile 28 shughuli za kupeleka maji zinakwenda kuanza mara moja.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mradi huu wa Busanda unafanana sana na ule mradi uliopo Wilaya ya Ubungo, hasa mradi wa 2f2b, unaoanzia Changanyikeni, Chuo Kikuu mpaka Bagamoyo na hasa ujenzi wa tanki kubwa la lita milioni sita pale Tegeta A, Kata ya Goba. Je, mradi huu utakamilika lini ili wananchi wote wa Kata ya Goba wapate maji safi, salama na yenye kutosheleza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtemvu kutoka Kibamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi yote hii ambayo tayari utekelezaji wake unaendelea Wizara tunasimamia mikataba na namna ambavyo mkataba unamtaka yule mkandarasi kukamilisha mradi ule. Mheshimiwa Mbunge ninakupa uhakika kwamba tutasimamia kwa karibu na mradi ule utakamilika ndani ya muda ambao tumeupanga.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mradi wa maji wa Wilaya ya Muleba ambao unalenga kusaidia kata sita ambao umefanyiwa usanifu tangu mwaka 2018. Je, Wizara itaujenga lini na utakamilika lini kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa Wilaya ya Muleba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daktari, Mbunge kutoka Muleba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu ambao usanifu wake umekamilika nao tayari Wizara tunaendelea na michakato kuona kwamba mradi huu tunakuja kuutekeleza ndani ya wakati.

Waheshimiwa Wabunge pale tunaposema kwamba, maji ni uhai, Wizara tunasimamia kuhakikisha kuona kwamba, wananchi wote wanaenda kupata maji safi na salama ya kutosheleza kwa lengo la kulinda uhai wa wananchi. Hivyo, Mheshimiwa Daktari nikuhakikishie kwamba, namna usanifu umekwenda vizuri na utekelezaji wake nao unakuja vizuri namna hiyo.
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa tatizo la maji katika Mji wa Mpwapwa limekuwa la muda mrefu. Na kwa kuwa, Serikali imekiri kwamba, ni kweli limekuwa la muda mrefu na kwamba, wana mpango wa kuchimba visima viwili katika eneo la Kikombo ili kuongeza upatikanaji wa maji katika mji ule.

Je, ni lini uchimbaji huu wa visima hivi viwili utakamilika ili watu wa Mpwapwa nao wapate unafuu wa shida ya maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; mwezi Januari timu kutoka Wizara ya Maji ilikuja kutembelea katika Jimbo langu, tulikagua miradi miwili ya maji mmoja katika Kijiji cha Vingh’awe na mmoja katika Kijiji cha Manhangu; na mradi ule wa Vingh’awe ulitengenezwa siku nyingi, lakini historia iliyopo ni kwamba ulipochimbwa miundombinu ilijengwa chini ya kiwango; ulifanya kazi siku tatu tu mabomba yalipasuka, lakini tenki ambalo lilijengwa below standard pia nalo lilibuja lote halafu ule mradi ulikufa, lakini mradi wa Manhangu pia una story inayofanana.

Je, Serikali inasemaje kuhusu hili, maana walikuja kukagua na wakaahidi kwamba wataifanyia matengenezo ili ifanye kazi. Je, ni lini watakuja kurekebisha hiyo miradi miwili?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa George Malima, Mbunge wa Mpwapwa kama ifuatavyo:-

Swali lake la kwanza ni lini mradi ule unakwenda pesa zitapelekwa ili mradi uendelee kutekelezwa. Jibu lake kwa sababu mradi uko ndani ya mwaka wa fedha huu 2020/2021 Mheshimiwa Mbunge nakuhakikishia kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha kwa maana ya mwezi Juni hii fedha itakuwa imefika na tutasimamia utekelezaji wake kwa karibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ameongelea kuwa mwezi Januari kuna timu kutoka Wizarani ilikwenda na ni kweli. Miradi hii anayoiongelea ya Vingh’wale pamoja na Manhangu kwa pale Mpwapwa ni kati ya miradi ya ule mpango wa vijiji kumi ambao Wizara imekuwa ikiifanyia kazi na vijiji hivi kwa hakika vilikuwa na changamoto kubwa sana ya maji, lakini kwa awamu hii sisi tumejipanga kuhakikisha kuona kwamba miradi ile kwenye ile programu ya vijiji kumi tunakwenda kuisimamia ambayo ina vijiji takribani 177 vyote tunakwenda kuhakikisha tunarekebisha pale ambapo kidogo palikuwa na mapungufu. Lakini vilevile tutahakikisha wananchi wetu wanakwenda kupata maji safi na salama na ya kutosheleza.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ili nami niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilianza mpango wa kulipa fidia kwa wananchi wa Mtwara Vijijini waliopitiwa na bomba la maji mwaka 2015; nataka kujua mradi huu umekwamia wapi wakati uthamini ulishaanza kufanyika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shamsia kutoka Mtwara Vijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi ambao umeshafanyiwa usanifu Serikali tumejipanga tunakuja kuhakikisha kuona kwamba usanifu ule unakamilika na utekelezaji wake utakamilika. Miradi yote namna ambavyo ipo kwenye mikataba namna ambavyo tumekuwa tukiianza tunakwenda kuhakikisha kwamba maji yanatoka na changamoto zote ambazo zilikuwepo huko nyuma kwa kipindi hiki tunakwenda kuzimaliza.
MHE. ALI J. MAKOA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana; kwa kuwa tatizo la Mji wa Mpwapwa linafanana na Mji wa Kondoa, Halmashauri ya Mji wa Kondoa ina tatizo kubwa la muda mrefu la maji na tatizo ni uchakavu wa miundombinu.

Ni lini Serikali itapeleka fedha kutatua tatizo la miundombinu chakavu ya maji iliyojengwa miaka ya 1970?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ali Makoa kutoka Kondoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi yote ambayo muda wake wa uhai umekwisha kwa maana ya lifespan imesha- expire sasa hivi tayari tumeshaanza mchakato wa kuona namna gani mwaka ujao wa fedha kukarabati labda kwa kubadilisha mabomba kama yamechakaa sana au kuongeza mabomba kwa maana ya mtawanyo wa miundombinu au kuona kwamba kama kipenyo kilikuwa kidogo tutaweka mabomba makubwa kulingana na idadi ya watu namna ilivyoongezeka na uhitaji wa maji safi ulivyoongezeka hivyo nipende kumwambia Mheshimiwa Ali Makoa kuwa Kondoa napo tunakwenda kupaletea mapinduzi makubwa kuondoa changamoto ya maji.
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa ajili ya nafasi hii ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri kwamba, hayaleti matumaini ya moja kwa moja kwa wakazi wa Butiama naomba nijielekeze kwenye maswali kama ifuatavyo; Swali la kwanza; kwa kuwa, miradi hii ambayo Mheshimiwa Waziri ameitaja hapa utekelezaji wake umekuwa ni wa kusuasua sana kwa lugha nyingine umekuwa na mwendo wa kinyonga. Je, nini kauli ya Serikali basi kuhusiana na bili zinazotolewa kwa wakazi wa Butiama bila kupatiwa huduma?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa, kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kumtua mwanamke ndoo kichwani. Swali langu ni kwamba, ni lini basi Serikali itatekeleza kauli mbiu hii kwa matendo kukamilisha miradi yote ya Serikali nchi nzima ambayo imeonekana kusuasua mpaka sasa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na masuala ya bills, maeneo mengi yalikuwa na tatizo hili, lakini tayari Wizara tunashughulikia kwa karibu kuona kwamba, mtu anakwenda kulipa bili kulingana na matumizi yake. Tunaendelea kuweka mbinu mbalimbali kama kumhusisha moja kwa moja mtumiaji maji kwa kushirikiana na msomaji mita wataangalia kwa Pamoja, watasaini kadi na hapo sasa yule mlipaji atakwenda kulipa bili kulingana na matumizi yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na kumtua mwanamke ndoo kichwani; hili suala sasa hivi ni tayari linatekelezeka. Maeneo mengi ya Tanzania sasa hivi akinamama wameshakiri hawabebi tena maji vichwani na tayari Wizara tunaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha maeneo yote ya pembezoni mwa miji kwa maana ya vijijini nao wanakwenda kukamilika katika mpango huu na kazi zinaendelea. Tayari tuna ari kubwa sana kama Wizara na watendaji wetu wametuelewa mwendo wetu ni mwendo wa kasi ya mwanga. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. changamoto za maji ambazo wanakumbana nazo wananchi wa Butiama zinafanana sana na changamoto zinazowakuta wananchi wa Wilaya ya Nkasi. Natambua kwamba, Serikali imekuwa inapeleka fedha katika miradi mbalimbali katika Wilaya ya Nkasi ambayo haijaweza kumaliza changamoto za maji. Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka wa kutumia chanzo cha Ziwa Tanganyika ambacho ni chanzo cha uhakika ili kuweza kumaliza changamoto za maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Nkasi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Maji tayari tuna mikakati kabambe ya kuweza kutumia mito, maziwa na vyanzo vyote vya maji pamoja na Ziwa Tanganyika. Kwa hiyo, kufikia mwaka ujao wa fedha Serikali tunaendelea kuona namna bora ya kuweza kutumia Ziwa Tanganyika kutatua tatizo la maji eneo la Nkasi.
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. pamoja na majibu mazuri na maelezo mazuri ni ukweli usiopingika kwamba, tatizo la maji katika nchi yetu ni tatizo kubwa na kama ambavyo Mheshimiwa Aida amesema kuhusiana na matumizi ya Ziwa Tanganyika. Je, sio wakati sahihi kwa Serikali kuhakikisha kwamba, Mkoa wote wa Rukwa, Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Songwe unaanza kutumia chanzo cha uhakika cha Ziwa Tanganyika, ili kupata maji maeneo yote? Kwani imethibitika kabisa matumizi ya maji kutoka Ziwa Victoria yamekuwa ni ufumbuzi mkubwa katika maeneo mengi, sasa si wakati muafaka kwa hiyo mikoa niliyoitaja kutumia chanzo hicho? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Kandege, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu awali, tayari Wizara tuna mikakati ya kuona maziwa yote ambayo yanapatikana katika nchi yetu tunakwenda kuyatumia kikamilifu katika kutatua tatizo kubwa la maji katika mikoa inayohusika. Hivyo mikoa yote ambayo inapitiwa na ziwa hili tutakwenda kuifanyia kazi na hakuna mkoa utakaorukwa, tutagawa maji kulingana na bomba litakavyopita kadiri mradi utakavyosanifiwa, ahsante.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Naitwa Eng. Samweli Hhayuma, Mbunge wa Jimbo la Hanang.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo la maji lililopo Butiama lipo pia kwenye Mji wa Katesh kwenye Jimbo langu; na kwa kuwa Serikali imeshawekeza shilingi bilioni 2.5 kuleta maji mjini na maji yale sasa yapo tayari kutumika. Je, Wizara iko tayari kuongeza fedha kidogo ili maji yaweze kusambazwa kwa wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuongeza fedha katika miradi ambayo ipo katika hatua za utekelezaji ni jukumu la Wizara. Hivyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge fedha zitakuja kwa awamu kama ambavyo imekuwa kawaida yetu kuhakikisha mradi huu unafikia lengo la kupata maji bombani. Lengo la Wizara siyo tu kujenga hizo structures ambazo zipo tayari, tutaleta fedha kuhakikisha maji sasa yanafika bombani.
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini kwa kuwa Serikali inatambua jambo hili ambalo nimesema nataka kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, ni lini Serikali itamaliza kero ya maji katika ukanda huu wa baridi ambapo kuna vyanzo hivyo na hivyo kufanya tatizo la maji kuwa historia katika maeneo ya Kata za Migohole, Kasanga, Mninga, Mtwango, Idete pamoja na maeneo mengine ya Makungu, Kiyowela na Mtambula?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la nyongeza, kwa kuwa suala la maji ni mtambuka na ni muhimu sana, katika eneo hilo la Mufindi Kusini kulikuwa na mradi ulikuwa unaitwa Imani, ni lini Serikali itakwenda kuufufua kwa kuboresha miundombinu ili wananchi waliokuwa wananufaika waweze kunufaika especially kwenye Kata za Ihoanza, Malangali, Idunda, Mbalamaziwa, Nyololo, Maduma na Itandula?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba majibu.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Mbunge David Kihenzile kwa namna ambavyo amekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa matatizo ya maji katika Jimbo lake. Hii ni kawaida yake kwa sababu pia amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ameuliza tatizo la maji litakoma lini, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kama Ilani ya CCM inavyotutaka Serikali kuhakikisha kufika mwaka 2025 tuweze kukamilisha maji vijijini kwa 95%, kwa maeneo ya Mufindi tutahakikisha mwaka ujao wa fedha tunakuja kuweka nguvu ya kutosha ili libaki kuwa historia.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile suala la kufufua miundombinu, katika maeneo mbalimbali suala hili linaendelea kutekelezwa. Katika eneo la Mufindi, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kabla ya mwaka huu wa fedha haujaisha tutakuwa tumeshafanya kwa sehemu kubwa kuona miundombinu chakavu tunaitoa na tunaweka miundombinu ambayo inaendana na matumizi ya sasa.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Liwale unakua kwa haraka sana na mahitaji ya maji yamekuwa ni makubwa na uhaba wa maji ni mkubwa sana. Bajeti iliyopita tuliletewa fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kutafuta chanzo cha pili cha maji cha Mji wa Liwale lakini mpaka leo tunaambiwa DDCA hawana nafasi ya kuja Liwale. Ni lini Serikali watakuja sasa kutafuta chanzo cha pili cha maji kwa ajili ya Mji wa Liwale?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Liwale. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anafuatilia na amekiri tumewapatia shilingi milioni 100. Nachoweza kumwambia hawa DDCA nitawasimamia na nitahakikisha ndani ya mwezi huu Aprili watakuja ili waweze kuona kwamba shughuli ambayo ilipaswa kufanyika basi sasa inaenda kutekelezwa.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Wilaya ya Kilolo inafanana kabisa na Wilaya ya Mufindi; na kwa kuwa vyanzo vya mito kama Mto Mtitu na Mto Lukosi vinachangia kwa kiwango kikubwa kwenye vyanzo vikubwa vya mabwawa na pia ni vyanzo ambavyo vinasaidia katika nchi yetu. Je, ni lini Wizara itajibu kiu ya wananchi kwa kutatua tatizo la maji kwa kutoa fedha kwenye Mradi wa Mto Mtitu ambapo tayari RUWASA walishatoa na maji hayo yatafika hadi Iringa Mjini lakini pia yatahudumia kata zaidi ya 15 za Wilaya ya Kilolo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kilolo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama yeye mwenyewe Mheshimiwa Mbunge alivyokiri kwamba tayari shughuli zinaendelea pale kupitia Wakala wetu wa Maji Vijijini (RUWASA). Kadiri tunavyopata fedha tunahakikisha tunagawa katika maeneo yote ambayo miradi ipo kwenye utekelezaji.

Kwa hiyo, pamoja na mradi huu ambao upo katika Jimbo lake na ni Jimbo ambalo tumelitendea haki kwa sehemu kubwa sana, tutaendelea kupeleka fedha kadiri tunavyopata ili kuhakikisha mito yote ambayo mmebarikiwa watu wa Kilolo na maeneo mengine yote tunashughulikia kwa wakati. Lengo la Wizara ni kuhakikisha wananchi wanapata maji bombani na si vinginevyo.
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri kwa kufanikisha kufanya upembuzi yakinifu na kutengeneza zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ile kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali imesema inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara hiyo na wananchi walio katika maeneo au waathirika wa barabara hiyo bado wanakiu ya kupata fidia yao kwa ajili ya maeneo hayo. Je, ni lini Serikali itaanza kutoa fidia kwa waathirika wa barabara hiyo kutoka Mtwara Pachani, Lingusenguse, Nallasi mpaka Tunduru mjini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Serikali imetenga shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida kwenye barabara hiyo; na kwa kuwa madaraja manne kwenye barabara hiyo yamezolewa na mvua, Mto Sasawala, Lingusenguse, Mbesa pamoja na Lukumbule. Je, Serikali haioni haja ya haraka kupeleka hizo shilingi bilioni 2.2 ili kukamilisha kurekebisha madaraja hayo yaliyoharibika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mpakate, Mbunge wa Tunduru Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la fidia litaanza pale ambapo barabara itaanza kujengwa. Awamu ya kwanza ilikuwa ni kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ambao kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi umeshakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwa nini fedha ya matengenezo iliyotengwa kwa kuwa madaraja yameshazolewa isipelekwe huko. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Tunduru kwamba mpaka leo asubuhi madaraja yote ya kutokea Tunduru daraja la kwanza la Mbesa, Mchoteka sasa yanaweza yakapitika na hivi leo wameanza daraja kubwa la Mto Sasawala na tunaweka ndani ya muda mfupi daraja hili litaanza kupitika ili kuweza kuunganisha Tunduru na eneo la Mtwara Pachani. Ahsante.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA, Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Kwa majibu yaliyotolewa na Serikali, nilikuwa ninamuomba Mheshimiwa Waziri kwa kushirikiana na mimi pamoja na Madiwani wa Wilaya ya Rungwe aweze kufuatilia uhalali wa majibu waliyompatia, hilo swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Kijiji cha Mpuguso Itula, Lukoba kinapata maji kutoka chanzo cha Kasyeto lakini, Kasyeto yenyewe ambayo inatoa chanzo cha maji wanakijiji wake hawapati maji. Je, ni lini Serikali itahakikisha watu hawa wa Kasyeto pamoja na Mpumbuli wanapata maji, maana wao ndiyo wanaotoa chanzo cha maji nao si wanufaika wa maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa majibu ambayo Serikali imeweza kutoa hapa ni majibu yenye uhakika. Hata hivyo tutatuma timu yetu kwenda kufanya uhakiki wa kuona uhalali wa maelezo ya Mheshimiwa Mbunge. Vilevile kwa vijiji vya Mpuguso na vijiji jirani, na vile vijiji ambavyo chanzo cha maji kinatokea kama ilivyo ada ya Wizara ya Maji vijiji ambavyo vinatoa chanzo cha maji huwa ndio wanufaika namba moja.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hili ninaendelea kutoa maelekezo kwa watendaji wote wa Wizara ya Maji na RUWASA, pamoja na Mamlaka kuhakikisha maeneo yote ambayo yanatoa vyanzo vya maji lazima wawe wanufaika namba moja.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Serikali imeweza kutoa fedha nyingi sana za walipa kodi masikini kwenda kwenye miradi ya maji, lakini uhalisia ni kwamba miradi mingi sana haitoi maji kwa ukamilifu au mingine haitoi maji kabisa. Ningependa kujua, ni lini Serikali itafanya ukaguzi kwenye miradi yote nchi nzima ambayo haitoi maji ili sasa iweze kutubainishia bayana ni miradi ipi kwa fedha kiasi gani zimewekezwa na haitoi maji kwa wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli fedha nyingi zimeelekezwa katika miradi ya maji na ndiyo maana tatizo la maji linaendelea kupungua. Namna ambavyo tatizo lilikuwa huko awali ni tofauti na sasa hivi, na tayari sisi Wizara tunafanya kazi kwa makusudi kabisa usiku na mchana ili kuhakikisha kuona kwamba miradi yote ambayo haitoi maji itatoa maji. Tayari miradi ambayo ilikuwa ya muda mrefu haikuweza kutoa maji. Baadhi tayari inatoa maji na tayari watendaji wetu wanaendelea kufanya kazi. Tutahakikisha miradi yote ambayo maji hayatoki maji yatatoka bombani.
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa swali la msingi la Halmashauri ya Rungwe linafanana sana na tatizo la Halmashauri ya Rorya ambayo kwa 2015/ 2020, Serikali ilitupa zaidi ya bilioni 7.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji zaidi ya miradi 12, lakini mpaka sasa ninavyozungumza hakuna mradi ambao umetekelezwa kwa kiwango cha 100% na wakandarasi wameshalipwa fedha na hawapo site.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri alifanya ziara mwezi wa kumi na mbili na akatoa maelekezo kwamba wakandarasi hao wakamatwe lakini mpaka leo ninavyozungumza hakuna mkandarasi aliyekamatwa badala yake kuna fedha inatoka kuja kukamilisha miradi ambayo kuna wakandarasi wamekula fedha.

Mheshimiwa Spika, swali langu ni, je, lini Serikali sasa itaona umuhimu wa kuleta wakaguzi kwenye Halmashauri ile ili kujiridhisha ile fedha bilioni 7.9 kwa miaka ile mitano imetumika vipi na yule ambaye kweli ametumia hizo fedha pasipo kutimiza wajibu wake achukuliwe hatua zinazo stahiki? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Chege kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali ilitoa fedha nyingi sana kwa Halmashauri ya Rorya, na swali lake anahitaji kujua lini wakaguzi watapelekwa kuona namna gani wale ambao walikula fedha wanashuhulikiwa. Sisi kama Wizara tayari tumeunda timu yetu ambayo itazunguka majimbo yote kuona kwamba miradi ambayo fedha ilitoka na wakandarasi wakafanya janja janja basi wanakwenda kushughulikiwa na kama kuna mtumishi yeyote wa Serikali aliweza kujihusisha pamoja na hawa wakandarasi na yeye sheria itafuata mkondo wake.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nipende kumjibu Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi karibuni watafika Rorya na wote ambao wanastahili kutumikia sheria basi sheria itafuata mkondo wake.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya mimi kuuliza swali la nyongeza kwenye Wizara hii muhimu.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Chemba ni kati ya wilaya ambazo zinachangamoto kubwa sana ya maji. Nilitaka kujua tu Serikali, ni lini itawapatia maji wananchi wa vijiji; Chandama, Changamka, Babayo, Maziwa pamoja na Ovada?

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
NAIBU WAZIRI MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kunti kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa Wilaya ya Chemba pia taasisi yetu ambayo iko pale inaendelea kufanya jitihada kuona vijiji hivi ulivyovitaja vinapata maji mapema iwezekanavyo. Naomba mtupe muda tuweze kufanya kazi, siku si nyingi kabla ya mwaka huu wa fedha tayari tutapunguza idadi ya vijiji ambavyo havina maji kwa Chemba.
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Maswali yangu ya nyongeza ni kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, kule Magunga ukitoka Magunga kwenda Lumuli kuna mradi ambao ulihasisiwa na Marehemu Dkt. William Mgimwa zaidi ya miaka saba iliyopita bahati mbaya haukutekelezwa, lakini sasa tunaishukuru Serikali imepeleka kiasi cha milioni kama 200 hivi kuanza kwa kutengeneza tenki kwa kutumia force account, lakini ninaona kwamba kasi yake ni ndogo.

Je, Wizara ina mpango gani hata kwa kutumia Wakandarasi ili maji yale yafike Kata ya Lumuli ambapo wananchi wake wamesubiria kwa muda mrefu sana.(Makofi)

Swali la pili, kumekuwa na mradi ambao pia ulianzishwa na aliyekuwa Mbunge na Katibu wa Bunge hili George Francis Mlawa wa Nyamlenge. Mradi huu ulikuwa wa maji tiririka ambao ungezifikia Kata kama tano, ukianzia Lyamgugo, Luhota, Mgama, Bagulilwa mpaka Ifunda, lakini sasa mmebadilisha scope mnachimba visima, wasiwasi wangu ni kwamba ikitokea tetemeko la ardhi na kule tupo kwenye bonde la ufa, visima vile mkondo huwa unahama maji yanakosekana.

Je, Serikali sasa ina mpango gani kupeleka pesa za kutosha ili turudi kwenye scope ya zamani na maji yapatikane katika Kata hizo tano ambazo nimezitaja?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kiswaga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru Mheshimiwa Kiswaga kwa kuishukuru Serikali ya Mama Samia, tayari Magunga kazi zinaendela pale tumeanza na hii milioni 200 lakini fedha tutaendelea kuleta kwenye migao inayofuata, lengo ni kuona wananchi wote wa eneo lile wanaendelea kupata maji ya uhakika ya kiwa safi na salama bombani.

Mheshimiwa Spika, kijiji cha Lumuli hapa kipo kwenye mpango wa fedha za mwaka 2021/2022 na mradi huu kadri ambavyo tumeweza kufanya mashirikiano na Mheshimiwa Mbunge tutautekeleza kwa kupitia Mkandarasi lengo iweze kufanyika kwa haraka na wananchi wa Lumuli nao waweze kunufaika na fedha hizi ambazo Mheshimiwa Rais ameendelea kutupatia Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Spika, eneo la Nyamulenge pia lipo kwenye mpango wetu wa muda mrefu. Kwa sasa hivi tumechimba visima virefu ambavyo vinatumia pump za umeme kwa sababu ya kuona kwamba kwa muda huu wananchi waweze kuendelea kupata huduma ya maji. Lakini katika mipango ya muda mrefu kama ambavyo tumeendelea kuwasiliana mara kwa mara na tulishaweza kushauriana kwa muda mrefu katika mpango wa muda mrefu chanzo hiki cha Nyamlenge tutakuja kukitumia kwa mradi wa maji ya uhakika maji ya mserereko ambayo eneo lile litapata maji ya kutosha na vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi huu vitaweza kunifaika.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, ndani ya Mkoa wa Njombe Wilaya ya Wanging’ombe kuna mradi wa maji wa Igando - Kijombe wenye thamani ya bilioni 12. Lakini mpaka sasa hivi tunavyozungumza ni bilioni mbili tu ambazo zimekwenda kwenye mradi ule na mkandarasi yuko site lakini amesimamisha mradi hule hauendelei kwa sababu Serikali haijapeleka pesa.

Je, lini Serikali itapeleka hizo bilioni 10 ili mradi ule uweze kukamilika na Wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe waweze kupata maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la
Mheshimiwa Neema Mgaya, kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Spika, hili suala tumeshalifanyia kazi kama Wizara na kwa ushirikiano mkubwa ambao tumekuwa nae Mheshimiwa Neema pamoja na Mheshimiwa Dkt. Dugange, tumeweza kufatilia na fedha tutaleta mgao ujao tutaendelea kutoa fedha kidogo kidogo, tutaleta bilioni Moja ili kazi ziendelee na mgao unaofuata pia tutaendelea kuleta fedha kadri tunavyopata.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulingana na andiko la huu mradi pamoja na kujenga bwawa, ni kuhakikisha kunakuwa na mtandao wa maji kutoka kwenye bwawa kuelekea Vijiji vya Lipupu, Maratani, Mchangani A na Malema na baadhi ya Vijiji vya Kata ya Mnanje:-

Swali je, ni lini utekelezaji wa uwekaji wa miundombinu ya maji utaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Ahadi hii ya kujenga bwawa katika Kata ya Mikangaula ilitolewa tarehe 28/07/2011 na Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Mrisho Jakaya Kikwete. Swali langu; ni miaka 11 ndiyo mradi huu unatakiwa kutekelezwa:-

Je, Wizara haioni wakati umefika ahadi ya viongozi wa juu hasa Marais wetu ikachukuliwa kama ni agizo na ikatekelezwa haraka iwezekanavyo, badala ya kusubiri miaka 11 ndiyo itekelezwe? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mtandao wa maji tunaelekea sasa kwenda kuutekeleza. Katika kutengeneza mabwawa, tunaanza kuhakikisha uhakika wa chanzo cha maji ambapo sasa bwawa limeshafika asilimia 95 na sasa hivi kazi zitakazofuata ni kuukamilisha. Hii 5% iliyobaki kufikia mwisho wa mwezi wa Tano au kabla ya kumaliza mwaka huu wa fedha ni kuona kwamba tunakwenda kusambaza mitandao ya mabomba kuelekea kwa watumiaji wetu wote wa Nanyumbu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la pili, amesema mradi umeanza tarehe 28/07/2011. Kama wote tunavyokumbuka, miradi hii kwa kipindi hicho ilikuwa chini ya Halmashauri zetu za Wilaya. Kwa hiyo, wale wenzetu kidogo walishindwa kumaliza miradi hii na ndiyo maana RUWASA ikaanzishwa. Sote tunafahamu RUWASA sasa hivi ina mwaka mmoja na miradi korofi yote kama huu imekuwa ikifanikiwa kwa kuweza kukamilishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge napenda tu kukuhakikishia kwamba tunakwenda kutimiza ahadi hii kwa kutumia RUWASA na wote tunafahamu namna RUWASA ambavyo wamekuwa wakikamilisha miradi chechefu, kwa hiyo, na mabwawa haya pia yanakwenda kukamilika. (Makofi)
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza maswali ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, la kwanza; nafikiri mradi ambao Mheshimiwa Naibu Waziri ameujibu ni ule mradi unaotoa maji Mayembechini na kupeleka Manispaa ya Mtwara na Nanyamba itafaidika kwa kutoa maji Nanguruwe kupeleka Nanyamba: Serikali haioni sasa kwa sababu usanifu huu ni wa zamani, wafanye review ya usanifu ili maji yatoke moja kwa moja Mayembechini na kupeleka Nanyamba na hivyo kunufaisha Kata ya Kiromba, Kiyanga na Mbembaleo; na vile vile, itasaidia kupeleka Wilaya za jirani kama Tandahimba na Jimbo la Mtama jirani na Jimbo la Nanyamba? (Makofi)

Swali langu la pili; ili kuboresha upatikanaji wa maji katika Mji wa Nanyamba, pia mradi wa Makonde ambao unanufaisha Halmashauri nne lazima upatiwe fedha za kutosha za ukarabati: Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati mkubwa wa Mradi wa Makonde ili Halmashauri ya Nanyamba, Tandahimba, Newala Mjini na Vijijini wapate maji ya kutosha? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa ukarabati wa mradi tunafahamu kuna baadhi ya maeneo miradi ipo chakavu ikiwepo Nanyamba. Tayari Wizara imeshatoa maelekezo kwa Wahandisi wetu walioko maeneo hayo na ukarabati huu unatarajia kuanza mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Spika, kwa Mradi wa Makonde vile vile, tutaendelea kupeleka fedha kwa awamu kadiri tunavyopata ili kuhakikisha mradi huu wa Makonde kwa ukubwa wake na umuhimu wake, tutaendelea kuukarabati na kuuongezea thamani ili uendelee kutoa huduma kwa wananchi wa Nanyamba.

Mheshimiwa Spika, vile vile, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota kwa namna ambavyo ameendelea kufuatilia upatikanaji wa maji safi na salama ya kutosheleza katika Mji wa Nanyamba na tuseme tu kwamba kwa sisi Wizara tumejipanga kuhakikisha Nanyamba maji yanakwenda kupatikana. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa suala la upatikanaji wa maji safi na salama bado ni tatizo sugu katika Mkoa wa Mtwara na hivyo kupelekea akina mama kutumia maji ya kuokota okota na hivyo kuongeza gharama za matibabu kwa sababu ya matazizo ya homa za matumbo na kadhalika.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba tunamaliza tatizo la kuongeza gharama za matibabu kwa sababu ya upatikanaji wa maji ya kuokota okota ambao unapelekea wananchi kuendelea kupata homa mbalimbali? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hokororo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya umuhimu wa upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Mtwara, Serikali kwa kupitia Wizara ya Maji, tayari tumejipanga kuhakikisha tunakwenda kutumia maji ya Mto Ruvuma. Tutakapoweza kufanya mradi huu, adha ya maji katika Mji wa Mtwara, Nanyamba na maeneo yote ya mwambao ule yanakwenda kukoma kwa sababu itakuwa ni suluhisho la kudumu. Kwa hiyo, tunatarajia mwaka ujao wa fedha kutumia maji ya Mto Ruvuma.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kidogo Wagogo mnapata shida kuita jina Hussein, jina langu ni Hussein Nassor Amar, ni Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale.

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nianze kuishukuru Serikali kwa kuendelea kukamilisha mradi ya maji katika Jimbo la Nyang’hwale. Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja na tukafanya nae ziara. Tukawa na upungufu wa shilingi milioni 250 tu ili tuweze kukamilisha mradi huo. Je, Naibu Waziri, ahadi yake ataikamilisha lini ya kupeleka milioni 250 ili kuweza kukamilisha Mradi huo wa Nyang’hwale? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor wa Jimbo la Nyng’hwale, kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika, hizi fedha tayari tuko kwenye utaratibu wa kuzipeleka, tutazipeleka katika awamu mbili, wiki ijayo tutajitahidi kupunguza awamu ya kwanza na baada ya hapo tutajitahidi kukamilisha kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha.
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali ya nyongeza mawili. Swali la kwanza; kwa kuwa kuna miradi inayoendelea katika Jimbo la Makambako, Mradi wa kwanza mkandarasi yupo Usetule-Mahongole; mkandarasi wa pili yuko Ibatu; na mkandarasi wa tatu yuko Mtulingana, Nyamande na Bugani. Je, ni, lini Serikali itawalipa wakandarasi hawa ili waweze kumalizia miradi hii kwa sababu wanakwenda kwa kususasua ili wananchi waendelee kupata maji yaliyokusudiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa mradi huu wa kutoka fedha Serikali ya India miji 28 ikiwemo na Mji wa Makambako. Miradi hii tangu yupo Waziri Profesa Maghembe inazungumzwa na kwa mara ya mwisho alipokuja Rais ambaye ni Marehemu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, wananchi wa Makambako waliuliza ni lini mradi huu utaanza? Sasa nataka kujua kwa sababu kuna baadhi ya watu wanataka kuwekeza viwanda pale, wanakosa kuweka viwanda, tunakosa wawekezaji wengi ni kwa sababu mradi huu haujaanza. Sasa nataka Serikali iniambie hapa na iwaambie wananchi wa Makambako, ni lini mradi huu utaanza ili wananchi waendelee kuwekeza viwanda kama ambavyo wanahitaji pale Mji wa Makambako? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deo Sanga, Mbunge wa Makambako, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, lini wakandarasi watalipwa? Tayari wakandarasi mbalimbali wameanza kulipwa na Wizara inafanya jitihada kila tunapopata fedha kuendelea kupunguza list ya wakandarasi ambao wanadai Wizara. Kwa hiyo kadri tunavyoendelea kupata fedha, list itakapomfikia mkandarasi huyu na yeye pia atalipwa.

Mheshimiwa Spika, Miji 28 utekelezaji wake kama nilivyojibu kwenye swali lake la msingi, mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu 2021 utekelezaji wa miradi hii utaanza na itatekelezwa kwa miezi 24.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali madogo ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, leo hii ukienda Longido kwenye vijiji vya Noondoto, Matale, Wosiwosi na Ngereani, utalia kwa jinsi wananchi wanavyopata shida ya maji na hususan akina mama; wanalazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 10 kutafuta maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile, akina mama hawa mara nyingine wanalazimika kwenda kulala kwenye vyanzo vya maji kusubiria maji yanayochuruzika. Swali langu kwa Serikali: Je. Waziri yuko tayari kwenda Longido kuona hali halisi ya maeneo haya? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa changamoto ya Wilaya ya Longido linafanana kabisa na changamoto walizonazo akina mama wa Monduli hususan kwenye Kata za Moita, Lekruko na Naalarami: Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia akina mama wa Monduli haki yao ya msingi ya kupata maji safi na salama? Nakushukuru. (Makofi)
MHE. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa kufika Longido ni moja ya majukumu yangu na tayari maeneo yale nilishatembelea nikiwa na Mbunge wa Jimbo na nimeshawasiliana naye kwa kirefu sana. Hata hivyo nitajitahidi kufika tena kuona namna gani tutaendelea kusaidiana na wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, mipango ya Wizara ni kuhakikisha maeneo yote yanafikiwa na maji bombani. Tupo kwenye mkakati kabambe wa kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo yamekuwa na matatizo ya vyanzo rahisi kama chemchemi, basi visima vinaendelea kuchimbwa na tayari Wizara wataalam wake wako huko wanaendelea, hata sasa hivi hapo Chemba tayari visima vinachimbwa na maeneo mbalimbali katika Majimbo yote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namwondoa hofu Mheshimiwa Mbunge, akina mama tuna lengo jema la kuhakikisha tunawatua ndoo kichwani; Wizara tuna lengo jema kuhakikisha tunaokoa ndoa hizi ambazo akina mama wanalala kwenye vyanzo vya maji; tunahitaji akina mama walale nyumbani na familia zao. (Makofi)
MHE. CATHERINE MAGIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza tunaishukuru Serikali kwa mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 520 katika Jiji la Arusha. Mradi huu changamoto yake kubwa unapita katika maeneo ya mjini, lakini maeneo ya pembezoni kwenye Kata kama Olmoti, baadhi ya sehemu za Muriet, Moshono na Olasiti hazifiki. Je. Serikali haioni sasa kuna umuhimu mkubwa wa mradi huu wa maji kuhakikisha unapita katika Kata za pembezoni mwa Jiji la Arusha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mji wa Arusha una bahati kubwa sana, kwa sababu una mradi wenye fedha nyingi sana na ni mradi ambao tunautarajia umalize kero ya maji katika Jiji la Arusha. Katika maeneo haya aliyoyataja, ni jana tu nimekuwa nikiongea na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Arusha, aliyeongozana na timu iliyotoka kule ikiwa pamoja na Mheshimiwa Diwani Miriam, tayari nimeshafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, maeneo ambayo yako pembezoni, wenzetu wa Mamlaka ya Maji ya Arusha, pale tayari na wenyewe wanaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuona namna bora ya kuendelea kutanua mitandao ya mabomba kuwafikia wananchi. Hili nalo tutalisimamia kwa karibu kabisa kuhakikisha maeneo yote ya pembezoni, Mamlaka pamoja na RUWASA wanawajibika ili maji yaweze kuwafikia wananchi. (Makofi)
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona. Nitumie fursa hii kumwomba Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba maji ya Ngaresero hayataweza kufika katika Wilaya ya Longido, kwa hiyo, nafikiri kuna haja ya kurekebisha hapo. Hata hivyo, nashukuru kwa jitihada ambazo Serikali inaenda kufanya katika kutupatia maji kwa gharama yoyote, iwe ni mabwawa au chemichemi ama chanzo chochote cha maji salama katika eneo la Wilaya ya Longido.

Mheshimiwa Spika, naomba tu kutumia fursa hii kuikumbusha Serikali kwamba, kuna ahadi ambayo imerudiwa tena na tena ya kutoa tawi la maji ya Mto Simba ambayo yamekwenda mpaka Mjini Longido na sasa hivi yanaelekea Namanga. Naiomba sana Serikali Kijiji cha Eilarai eneo la Motong’ wapate maji maana ni Kijiji cha kwanza kilichopitiwa na bomba hilo kubwa na wananchi wale wameendelea kunikumbusha kwamba ahadi imetolewa na Mawaziri watatu hadi sasa; Mheshimiwa Waziri Mbarawa, Mheshimiwa Waziri Kamwelwe na huyu aliyeko sasa hivi wakati ule akiwa Naibu Waziri. Kwa hiyo, ni lini Serikali itakwenda kuwapelekea watu wa Imotong’ maji safi na salama ya Mto Simba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kuhusu maji ya Mto Simba, ni mpango mkakati wa Wizara kwenda kutumia mito, maziwa na vyanzo vyote vya maji kuhakikisha maeneo yote tunayafikia. Kwa upande wa Longido, Mheshimiwa Mbunge tuna mpango wa kuendelea kuona chanzo hiki cha maji cha Mto Simba kinakwenda kutumika katika mwaka wa ujao wa fedha.
MHE. NICODEMUS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza sijaridhishwa na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji kwamba kuna visima 26 Mbogwe. Naomba tu tuongozane naye akanionyeshe pale vilipo hivyo visima virefu vinavyotoa maji, maana mimi ni Mbunge wa Mbogwe na ninaishi Mbogwe na kuna taabu kubwa sana katika Sekta ya Maji. Ndiyo maana nikaiomba Serikali sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mbogwe ni Wilaya ambayo ipo karibu na mradi wa maji pale Kahama, ni vyema sasa Wizara ya Maji itupelekee mradi mkubwa wa Ziwa Victoria, maana hivyo visima anavyovisema Mheshimiwa, nakuomba twende na wewe, usifuate mambo ya kwenye makaratasi ukajionee na unionyeshe pale vilipo visima.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi/Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ombi lake namba moja limepita, kwani huo ni moto wa namna ya kutekeleza majukumu yangu; nimekuwa nikiambatana na Wabunge wengi, hata weekend hii tu nilikuwa Mbinga. Kwa hiyo, mimi kutembea huko, kwangu ni moja ya majukumu yangu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Nicodemus mantahofu, tutakwenda na miradi hii tutahakikisha mambo yanakaa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kupitia mradi wa Ziwa Victoria, hili Ziwa litatumika vyema kwa maeneo yote ambayo miradi hii mikubwa itapitia. Mheshimiwa Nicodemus, wewe ni Mbunge katika Wabunge mahiri, umekuwa ukifatilia suala hili, tumeliongea mara nyingi na umeonyesha uchungu mkubwa kwa wana Mbogwe. Nikuhakikishie, Mbogwe maji yatafika na katika mwaka ujao wa fedha mambo yatakwenda vizuri pale Mbogwe. Tuonane baada ya hapa, tuweke mambo sawa, tuone namna gani tunaelekea. (Makofi/Kicheko)
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Matatizo ya Jimbo la Mbogwe yanafanana vile vile na matatizo ya Jimbo la Igalula. Tuna Mradi wa Ziwa Victoria katika Jimbo la Igalula, lakini mradi ule mpaka sasa hivi umesimama:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha mradi wa kupeleka maji katika Kata za Goweko, Igalula, Kigwa na Nsololo ili wananchi waanze kutumia maji ya Ziwa Victoria? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mradi ambao tayari utekelezaji wake umeanza ni lazima ukamilike. Sisi Wizara ya Maji tunapoanza kazi ni lazima zikamilike. Kwa mradi huu ambao umesimama napenda nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tuonane baada ya hapa, lakini vile vile wiki ijayo tutaangalia fungu la kupeleka fedha ili pale kazi iliposimama, utekelezaji uendelee na tutahakikisha mradi huu unaisha ndani ya wakati ili maji yaweze kupatikana Igalula. (Makofi)
MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa hii nami niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa, Mkoa wa Tabora ulifanikiwa kupata maji ya Ziwa Victoria; na kwa kuwa, Mheshimiwa Rais alipokuja kwenye Kampeni alisema kwamba, sasa maji ya Ziwa Victoria yapelekwe Urambo, Kaliua na Ulyankulu:-

Je, Mheshimiwa Naibu Waziri ni lini sasa mnatarajia kuyatoa maji hayo Tabora Mjini na kuyapeleka Urambo, Kaliua, Ulyankulu pamoja na Sikonge? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Maeneo ya Urambo, Kaliua, Ulyankulu na Sikonge, yote haya tumeendelea kuyaweka katika mikakati ya Wizara kuona namna ambavyo tutaendelea kupata fedha ili maeneo haya yote maji yaweze kufika. Tutafanya jitihada za makusudi kuona kwamba tunapeleka fedha mapema na hii itakuja kuingia mwaka ujao wa fedha.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Naipongeza Serikali kwa usambazaji wa maji ya Lake Victoria.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, tatizo lililo katika ukanda huo linafanana kabisa na lile la Rombo na wanawake hawa wamezeeka sasa na kutoka upara kwa ajili ya kubeba maji:-

Ni lini sasa Wizara hii itaona ni wakati muafaka wa kusambaza maji ya Lake Chala kwa wale wananchi wa Rombo katika Mji ule wa Holili, Kata za Mahida, Ngoyoni na tambarare yote ya Rombo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Maeneo ya Rombo Mheshimiwa Shally nimeshafika. Nimeacha maagizo ya kutosha na hata miradi ambayo ilikuwa inasuasua pale niliacha maagizo na utekelezaji unaendelea. Nikutoe hofu kwamba nitarudi tena kuhakikisha ule mradi mkubwa tunakwenda kuutekeleza

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sana mama yangu, amekuwa ni mfuatiliaji mzuri pamoja na Mbunge Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, wote mmekuwa mkifuatilia kwa jitihada kubwa. Hatutawaangusha. Sisi Wizara hatutakuwa kikwazo kwenu kwa sababu tunahitaji Wana-Rombo waweze na wao kupata ladha ya mageuzi makubwa ambayo yako ndani ya Wizara ya Maji. (Makofi)
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza niishukuru Serikali kwa majibu mazuri na ufuatiliaji na usimamizi madhubuti wa mradi huu, lakini nina swali la nyongeza. Mosi, kwa kuwa mradi huu utachukua miezi 24 tangu kuanza kwa utekelezaji wake maana yake ni miaka miwili, lakini pia utakuwa ni mradi wa kutoka katika chanzo cha maji kuelekea katika miji hii miwili niliyoitaja ya Kilwa Masoko na Kilwa Kivinje, lakini viko vijiji ambavyo vitakuwa mbali na mradi huu. Je, Serikali itakuwa tayari kwa upendeleo wa kipekee kutenga bajeti kwa mwaka huu kwa ajili ya vijiji angalau vitatu vya Nainokwe, Limalyao pamoja na Mandawa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally Mohammed Kassinge kutoka Kilwa Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tunapoongelea miezi 24 wakati fulani kwa sababu ya changamoto kubwa ya maji ni muda mrefu, lakini naendelea kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo ameendelea kuwa karibu na sisi na kwa hakika namna ambavyo anafuatilia tutahakikisha tunakamilisha vile vijiji sio vitatu, ila kwa sasa hivi kwa mwaka huu wa fedha tutajitahidi tumchimbie kisima kimoja cha maji, lakini hivi vingine vitaingia kwenye Mpango wa Mwaka ujao wa Fedha. Haya maeneo ya vijiji vyake vitatu ambavyo viko mbali na mtandao wetu wa mabomba tutahakikisha tunakuja kuwahudumia wananchi kwa mtandao wa visima.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Tatizo la maji lililopo Kilwa linafanana kabisa na matatizo ya maji yaliyoko Jimbo la Ndanda hasa zaidi upande wa Magharibi kwenye Kata za Mlingula, Namajani, Msikisi, Namatutwe pamoja na Mpanyani. Swali langu, je, ni nini hasa mpango wa Serikali wa muda mfupi wa kuhakikisha kata hizi nilizozitaja zinapata maji kabla hatujaingia kwenye kiangazi kikuu kinachoanza mwezi Julai na Agosti. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwambe kutoka Ndanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Maji wakati wote tunajitahidi sana kuona tunatatua tatizo la maji kwa kutumia vyanzo mbalimbali kwa sababu tuna michakato ya muda mrefu pamoja na kutumia Mto Ruvuma kwa mwaka ujao wa fedha, lakini katika kuona kwamba wananchi tunakwenda kuwapunguzia makali ya matatizo ya maji kwa mwaka huu wa fedha, Mheshimiwa Mwambe kama ambavyo umekuwa ukifuatilia mara zote, tumeongea mara nyingi. Kwa hiyo, hili nalo tukutane tuone tuanze na kisima upande upi ili tuweze kupunguza haya matatizo. Maji Ndanda ni lazima yatoke, mabomba yamwage maji, tuokoe ndoa za akinamama, tutahakikisha hawaendi kukesha kwenye vyanzo vya maji. (Makofi)
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nafurahi sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika Kata ya Masaka yenye Vijiji vitatu vya Sadani, Wanging’ombe pamoja na Makota havina kabisa maji hata kijiji kimoja. Je, Waziri sasa wakati anaangalia uwezekano wa kupata maji ya kutiririka anaweza hata akatuchimbia visima ili wananchi wa kule waendelee kunufaika na huduma ya maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nipende kujibu swali la Mheshimiwa Jackson Kiswaga, Mbunge wa Kalenga. Mheshimiwa Kiswaga ni Mbunge ambaye kwa kweli nimeshazungumza naye mara nyingi na tayari tuna mradi kule tumekubaliana nakwenda kuuzindua.

Nipende kumhakikishia katika masuala ya visima Waheshimiwa Wabunge, hiki ni kipaumbele kimojawapo cha Wizara, tutafika Kalenga, tutachimba visima viwili, yeye ndiye atakayetueleza wapi zaidi kuna tatizo sugu ambalo mitandao ya mabomba ya maji ya kawaida hayafiki, basi visima Mheshimiwa Kiswaga atavipata.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ambayo kwa kweli yanatia Faraja, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ukurasa wa 150 Ibara ya 100 imeweka bayana kwamba, tunataka tupeleke maji vijijini kwa asilimia 85 lakini mijini kwa asilimia 95. Na kinachoonekana hapa kinakosekana ni elimu kwa wananchi, je. Wizara iko tayari sasa kuja na mpango Madhubuti wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili wawe na utaratibu huu mzuri wa kuvuna maji? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa, maji yanapotiririka yanaharibu miundombinu kwa kiasi kikubwa na mara nyingi ni miundombinu ya barabara, reli lakini pia wakati mwingine na mabwawa na scheme za umwagiliaji. Na kwa mfano, katika eneo la Kongwa mara kadhaa tumeona kwamba, barabara inasombwa na maji lakini pia, kule katika Mto Mkondoa eneo la Kilosa, reli mara kadhaa inasombwa na maji. Sasa kwa nini Serikali isije na mkakati mahsusi wa kuhakikisha kwamba, tunakuwa si tu, na mabwawa machache lakini tutafute mabwawa mengi nchi nzima ambayo yatakuwa yanazuia maji ambapo maji haya yatatumika kwa matumizi ya kunywa lakini pia, kwa ajili ya matumizi ya kilimo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Ilani inatutaka kufika mwaka 2025 vijijini kote maji yawe yamefika kwa asilimia 85 na maeneo ya Miji kwa asilimia 95. Wizara inaendelea kutekeleza Ilani kwa ufasaha sana na maelekezo ya Mheshimiwa Waziri wetu wa Maji ni kwamba, maji haya ya mvua kwetu sisi tunayachukulia kuwa ni fursa na sio laana. Hivyo, nipende kumwambia Mheshimiwa Shangazi kwa umahiri alionao, Wabunge wote humu ndani tunafahamu umahiri wa Mheshimiwa Shangazi vile ni Mwenyekiti wa Simba Sports Club humu Bungeni. Lakini vile vile, ni Katibu wetu sisi Wabunge tunaotokana na Chama Cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninafahamu tutaendelea kushirikiana lakini Wizara tutaendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi namna bora ya uvunaji wa maji katika makazi yetu na kama Wizara ya Maji, tutaendelea kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI, ili tuweze kuunganisha nguvu ya pamoja kuona wananchi tunawapa elimu, namna bora ya kufanya design, namna pale wanapojenga makazi yao. Kwasababu, mvua hizi tukiweza kufanya ni zoezi la shirikishi, maji yatakuwa ni mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, na hata kwenye mashule yetu kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi tutahakikisha na wao tunaendelea kutoa elimu kwa wakuu wa shule, ili kuona hata kwenye mashule yetu, watoto wasiendelee kuteseka. Maji hayana sababu ya kwenda kuharibu miundombinu mingine ambayo tunahitaji katika maisha yetu ya kila siku na maji haya tuweze kwenda kuyatumia vyema. Lakini vile vile, tutaendelea kuona namna bora ya kupata matenki ya bei nafuu kwa maeneo ya vijijini, ili ikiwezekana basi maji haya yaweze yakavuliwa kwa ushiriki wa pamoja na isije ikapelekea tena kuwa ni gharama kwa mwananchi mmoja mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, na katika swali lake la pili, kama Wizara nipende tu kusema nimepokea ushauri huu tutaendelea kuufanyia kazi Mheshimiwa Shangazi tutaonana, ili tuweze kuendelea kushauriana vema na Wizara tutakwenda kutekeleza vema. (Makofi)
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, katika Wilaya ya Ngorongoro, Mkoa wa Arusha kuna mradi mkubwa wa maji wa vijiji (8) maarufu kama Mradi wa Magehe, mradi huu unagharimu bilioni 8, upembuzi yakinifu umeshafanyika kilichobaki ni utekelezaji tu. Nilitaka kufahamu ni lini Serikali itatekeleza mradi huu mkubwa kwa wananchi wa Ngorongoro?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imezingatia mradi huu wa maji wa Magehe kwa umuhimu wake na tunaona kabisa ni mradi mkubwa ambao utakwenda kugharimu Serikali shilingi bilioni 8. Nikutoe hofu Mheshimiwa Catherine namna ambavyo umeweza ukafatilia suala hili muda mrefu na umekuwa ukiliuliza mara kwa mara kwangu pamoja na kwa Mheshimiwa Waziri, tutatekeleza mradi huu kwa awamu katika mwaka wa fedha ujao.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Jimbo la Mbulu Vijijini liko juu ya Bonde la Ufa na vijiji vingi sana havina maji, ni kwasababu ya Bonde la Ufa. Na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alifika wakati wa kampeni na kuahidi vijiji vile vitapata maji kutoka kwenye Ziwa la Madunga, Je. Mheshimiwa Waziri, lini ahadi ya Mheshimiwa Rais itatimizwa kwa wananchi hawa kupata maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge suala hili kama tulivyokubaliana, tunaliingiza kwenye mpango mkakati wetu wa mwaka wa fedha 2021/2022 na mradi huu utaaanza utekelezaji wake mara moja mara baada ya Mwaka wa Fedha mpya kuanza.
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Kwanza kabisa, nimshukuru Waziri na Naibu Waziri wake kwa namna ya kipekee kabisa, kwa namna ambavyo wananipa ushirikiano. Mheshimiwa Rais, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alipokuja kwenye ziara ya kuomba kura, alisema atahakikisha anachagua Waziri ambaye anawaza nje ya box na hakika watu hawa wanafanya hivyo. Sasa swali langu, nawashukuruni pamoja na kunipa mabwawa manne, lakini nataka kujua sasa, ni lini ujenzi huo wa hayo mabwawa utaanza? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, mabwawa haya manne yatajengwa kwa nyakati tofauti kulingana na fedha tutakavyokuwa tunazipata, ninaamini Mheshimiwa Mbunge wewe ni shahidi mzuri pale Chemba tumepatendea haki sana, hivi majuzi tu tumetoka kuchimba visima na hata haya mabwawa tunakuja kujenga mwaka ujao wa fedha lakini tutaanza kwa awamu taratibu mpaka kuhakikisha mabwawa yote yanakamilika. (Makofi)
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa swali niulize swali dogo la nyongeza. Natambua Wizara imetupa mradi mkubwa wa maji kutoka Nkome kwenda Nzela Rwezela lakini nilitaka kuuliza swali dogo. Tunayo Kata ya Rubanga haina kabisa mfumo wa maji na kina mama wanatembea umbali wa kilometa 10 kupata maji katika Kijiji cha Mwamitilwa, Mtakuja, Ludenge, Je. Serikali haioni umuhimu wa kunipatia angalau visima viwili viwili katika vijiji hivyo vitano? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Kata ya Rubanda, Serikali inafahamu umuhimu wa kuleta visima na kama nilivyoongea na wewe Mheshimiwa Musukuma, wewe ni Mbunge ambaye umefatilia suala hili kwa karibu, tayari tumekutengea visima viwili vya kuanzia katika mwaka wetu wa fedha ujao. (Makofi)
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nampongeza Naibu Waziri wa Maji kwa kutoa majibu mazuri, lakini nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Serikali imekuwa ikitenga pesa nyingi sana kwenda katika miradi mbalimbali katika Mkoa wetu wa Katavi na miradi hiyo huonekana kwamba haikidhi kutokana na ongezeko kubwa la watu katika Mkoa wa Katavi hususan Wilaya ya Mpanda. Je, ni lini Serikali itatoa maji kutoka chanzo cha uhakika cha Ziwa Tanganyika ili kukidhi mahitaji ya maji ya watu katika Mkoa wetu wa Katavi hususan Mji wa Mpanda ambao unaongezeko kubwa sana la wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kutokana na Serikali ilitenga fedha nyingi sana kwenda katika Mradi wa Mamba katika Wilaya ya Mlele, Jimbo la Kavu na mradi huo umekamilika, lakini mradi huo umekamilika kwa kuacha baadhi ya vijiji vingi sana kupata maji. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa kuja kufanya ziara katika Mkoa wetu wa Katavi, kujionea jinsi gani Serikali imetenga pesa nyingi, lakini mradi huo umeonekana uko chini ya kiwango kwa baadhi ya vijiji vingi sana kutokupata maji? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Martha Lugangira, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Swali lake la kwanza, lini Serikali itatumia Ziwa Tanganyika kupelekeka maji katika Mji wa Mpanda na Mkoa wa Katavi? Wizara imeshakamilisha usanifu wa miradi yote mikubwa ambayo itatokana na maziwa yetu makuu, ikiwemo Ziwa Tanganyika. Hivyo, kwa mwaka ujao wa fedha tunatarajiwa kuanza kazi hizi endapo kadri namna ambavyo tutakuwa tunapata fedha ndivyo namna ambavyo miradi hii ya Maziwa Makuu itakuwa inatekelezwa. Hivyo, hata kwa Mkoa wa Katavi nao tutauangalia kwa jicho la kipekee kabisa kwa umuhimu wake na niendelee kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge kutoka Mkoa wa Katavi hasa Mheshimiwa Martha akiwa Mbunge wa Viti Maalum ameweza kuwajibika mara nyingi sana kufuatilia suala hili na sisi kama Wizara hatutamwangusha Mheshimiwa Martha pamoja na Wabunge wote wanaotoka ukanda ule.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili anasema mradi umekamilika lakini baadhi ya maeneo maji hayatoki, anatamani mimi niweze kufika huko. Nimwahidi Mheshimiwa Mbunge mara baada ya Bunge hili la Bajeti, tutapanga pamoja ratiba ambayo itakuwa rafiki kwetu sote ili niweze kufika Mpanda nijionee na kabla ya mimi kusubiri hadi Mwezi Julai huko, nitaagiza wahusika pale tuna Managing Director wa Mamlaka ya Maji.

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile tuna RM wa pale, nitawaagiza waanze kufuatilia ili mpaka mimi nitakapokuwa naelekea huko kwa ajili ya ziara ikiwezekana wawe wameshafanya marekebisho na maji yaweze kutoka. (Makofi)
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa vijiji vya Aicho vina vijiji pacha vya Gembak, Kamtananat, Maretadu-Chini, Khaloda, Umburu, je, ni lini vijiji hivi vitachimbiwa visima vya maji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwakuwa Wakala wa Maji alishachimba visima sita Jimbo la Mbulu Vijijini katika Kijiji cha Khababi, Labai, Endagichani, N’ghorati, Gendaa Madadu-Juu, je, lini sasa watamalizia kazi ya usambazaji kwa sababu walishamaliza kazi ya uchimbaji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Zacharia, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, lini vijiji pacha ambavyo amevitaja Mheshimiwa Mbunge vitapata visima vya maji. Wizara tumeendelea kujipanga kwa dhati kabisa kuona kwamba kwa miezi hii miwili iliyobaki katika mwaka huu wa fedha kuna maeneo ambayo visima vitaendelea kuchimbwa na kwa mwaka ujao wa fedha tumetenga visima vingi vya kutosha karibia majimbo yote. Kwa hiyo na vijiji hivi tutaendelea pia kuvipa mgao kadri fedha tutakavyoendelea kuzipata.

Mheshimiwa Spika, kuhusu visima sita vilivyochimbwa usambazaji wa maji utaanza lini, tayari tumeendelea kujipanga, maeneo ya aina hii tunahitaji kuona wananchi wanapata maji kutoka kwenye mabomba. Kwa hiyo, usambazaji utaendelea kuwa wa haraka. Kwa eneo hili la visima sita naagiza watu wa Babati (BAWASA) wajipange vizuri kwa sababu ipo ndani ya uwezo wao waweze kukamilisha kazi hii.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali langu la kwanza: Serikali ilianza mpango wa kulipa fidia kwa wananchi wa Mtwara Vijijini waliopitiwa na bomba la maji kutoka Mto Ruvuma mwaka 2015. Nataka kujua, mradi huu umekwama wapi ikiwa tayari wananchi walishaanza kufanyiwa uthamini ili mradi huo uanze? (Makofi)

Swali la pili: Fedha zilizotengwa ili kutekeleza mradi wa maji wa Mto Ruvuma ambapo wananchi walishaanza kupewa utaratibu wa malipo ya fidia mwaka 2015 zimeenda wapi? Serikali inawaambia nini wananchi wa Mtwara Vijijini kuhusu mradi huo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ni kweli fidia hii ilianza kutekelezwa mwaka 2015. Mradi huu wa Mto Ruvuma ni ile miradi mikubwa ambayo mkakati wake lazima uwe madhubuti ili mradi usiishie njiani. Hivyo fidia namna ambavyo baadhi wameshalipwa, wale ambao bado hawajalipwa nao wanakuja kukamilishiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, kufikia mwaka ujao wa fedha 2021/2022 tumeweka mikakati ya kuona kwamba, tunakuja sasa kukamilisha miradi ya maziwa makuu ikiwepo mradi wa Mto Ruvuma pamoja na miradi mingine. (Makofi)
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona na kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Wilaya ya Kilwa kuna changamoto inayofanana na Wilaya ya Mtwara katika huduma hii ya maji:-

Je, Serikali ni lini itatekeleza mradi wa maji kutoka Mto Rufiji ili kuwaondolea changamoto ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kilwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Serikali ina mipango mikakati ya kuona kwamba Mto Rufiji iwe ni sehemu ya miradi mikubwa ya kutoka maziwa makuu na mito, kuona kwamba maji yale sasa yanakwenda kunufaisha wananchi. Hivyo, kwa watu wa Kilwa pia tunaendelea kuwasihi waendelee kutuvumilia kidogo, huenda mwaka 2021/2022 kadiri tutakavyokuwa tunapata fedha, watu wa Kilwa pia watapata maji kupitia Mto Rufiji. (Makofi)
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi tena niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa Kijiji cha Matandarani hakina kabisa hata kisima kimoja na wananchi wanakunywa maji machafu siku zote; na kwa kuwa, mradi huu mpaka sasa hivi una asilimia 10 tu na mradi huu ni wa muda mrefu ambapo wananchi wanauona, lakini juhudi ambazo zinatakiwa zifanyike hazipo: Je, lini mradi huu utakwisha? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, vijiji vyote ambavyo amevitaja Mheshimiwa Naibu Waziri ni kweli havina maji kabisa: Mtisi hakuna maji kabisa, ukienda Kijiji kinachofuata cha Magula hawana maji kabisa; na huu mradi mmesema unaenda mpaka Ibindi, kata jirani, nako hakuna maji kabisa: Je, Serikali ina mkakati gani kupitia hii miradi na kuhakikisha inakwisha kwa haraka kwa sababu, wananchi wanapata taabu sana? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Awali ya yote napenda kumpongeza Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, amekuwa mfuatiliaji wa karibu sana katika suala hili la tatizo la maji katika maeneo haya ya Vijiji vya Matandarani, Ibindi, Mtisi na Magula.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumwambia tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa kupitia jitihada zake, mimi binafsi kama Naibu Waziri ninakuhakikishia mara baada ya hili Bunge tutakwenda pamoja mpaka kwenye mradi huu. Usanifu wa mradi huu unatuonesha utakamilika mwezi Septemba. Hata hivyo, tutajitahidi kwa hali na mali tufanye kazi hii usiku na mchana na kurejesha muda nyuma ili mradi huu sasa usiishe Septemba, basi tujitahidi hata ikiwezekana uishe kabla ya usanifu muda unavyoonekana. (Makofi)
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanza naomba niishukuru Serikali kwa kuwa mradi huu wa Likuyusekamaganga ambao ulitumia muda mrefu umeanza kuonyesha dalili na sasa vituo vitano vinatoa maji kati ya vituo hamsini na tatu vilivyopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili (a) na (b);

(a) Kwa kuwa mradi wa Njoomlole, Ligunga, Lusewa na Kanjele mabomba yametandazwa ila tunapewa sababu ya kutokuwa na viunganishi katika mradi huo. Je, Serikali viunganishi hivi vinatoka wapi kwa nini wasituletee mara moja ili watu wapate maji? (Makofi)

(b) Swali la pili, kwa upande wa Mji wa Namtumbo, vitongoji vyake na maeneo la Rwinga, Minazini, Lusenti, Libango, Suluti na Luegu wanapata maji mara moja kwa wiki mgao wake ni mkubwa sana na watu wanalalamika sana.

Je, Serikali inaweza ikafanya uboreshaji wa huu wa haraka ili wananchi wapate maji inavyotakiwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, mabomba ni kweli yametandazwa na hivi viunganishi tayari na vyenyewe vimeshafika hapa nchini. Nipende kumuagiza Meneja wa Mkoa wa RUASA – Ruvuma kuhakikisha mradi huu anakwenda kuukamilisha mara moja na maji sasa yaweze kuwafikia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lako la pili, umeongelea kuhusiana na ule mgao mkali wa mara moja kwa wiki, tayari sisi kama wizara tumeendelea kujipanga kuhakikisha mgao wa maji maeneo yote yanakwenda kushughulikiwa na tunapunguza hayo maumivu ya mgao wa maji. Na hili pia ninamuagiza RM – Ruvuma kuhakikisha anaendelea kuona namna bora ya kufanya kupitia vyanzo tulivyonavyo kuhakikisha mgao huu unapungua kutoka mara moja kwa wiki angalau mara nne kwa wiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vile vile nipende kuagiza mameneja wa Mikoa wote hata pale Mwanza kwenye Jimbo la Ilemela maeneo ya Ilalila, Kahama, Nyamadoka, nahitaji kuona kwamba kila mmoja anawajibika vema. Kwa hiyo, mameneja wote wa Mikoa waweze kuhakikisha wanawajibika na maji yanaweza kuwafikia wananchi. (Makofi)
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona, kwa kuwa tatizo la maji lililopo katika Jimbo la Namtumbo linafanana kabisa na tatizo lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika Kata ya Riroda, Duru, Hoshan, Gidas, Hewasi.

Je, ni lini Serikali itakamilisha miradi ya maji yaliyopo katika maeneo hayo ili kumtua mama ndoo kichwani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali lengo jema kutoka Wizara ya Maji ni kuona kwamba miradi yote ambayo inatekelezwa inakamilika kwa wakati. Kwa hiyo, hii miradi ambayo ipo Babati inaendelea na utekelezaji itakamilika kulingana na muda wake wa utekelezaji namna ambavyo usanifu ulionyesha.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwenye hili suala la maji, ninashukuru sana kwamba matatizo haya yanayotokea kwenye Jimbo la Namtumbo yanafanana sawa kabisa na matatizo yaliyopo Jimbo la Ndanda hasa kwenye Kata za Mlingula, Msikisi, Namajani pamoja na vijiji vyake. Ninataka kufahamu sasa mpango mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kabla ya kiangazi kikuu tunapata maji ya kutosha na uhakikisha kwenye maeneo haya. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, mpango mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tatizo la maji linapungua. Na ndiyo maana Wizara ya Maji iliweza kuunda chombo hiki cha kushughulikia maji vijijini pamoja na usafi wa mazingira kwa maana ya RUASA. Hivyo maeneo yote ambayo kwa sasa hivi yamekuwa yakipitia changamoto ya maji tunaendelea kuyashughulikia kwa karibu kabisa kwa nia ya dhati kuona kwamba tatizo la maji tunakwenda kulipunguza kama si kulimaliza.

Mheshimiwa Naibu Spika, basi na maeneo ya Ndanda kama tulivyoongea Mheshimiwa Mbunge nimekuahidi kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha tutakuja angalau tuanze na kisima kimoja, viwili. Lakini mpango wa muda mrefu ni utaanza mwaka ujao wa fedha.
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulizwe swali la nyongeza kwenye Wizara hii ya Maji.

Kwa kuwa Wilaya ya Longido ni moja ya wilaya kame sana nchini na kwa kuwa tuna baadhi ya milima ambayo inavyanzo vya chemchem kwenye misitu ya Serikali kama mlima Gilay, Mlima Kitumbeine, Mlima Longido na chemchem iliyopo matali A na chemchem zinazotoka upande wa West Kilimanjaro Kata za Ormololi na Kamwanga na kuna mabonde ambayo yangeweza kuchimba mabwawa pamoja na visima kirefu... (Makofi)

NAIBU SPIKA: Swali Mheshimiwa.

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Naibu Spika, Je, Serikali ina mpango kusaidia kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa Jimbo la Longido.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Steven Kiruswa, Mbunge wa Longido, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuona kwamba maeneo yote ambayo yana matatizo ya maji tunakwenda kuyashughulikia. Mheshimiwa Dkt. Steven tumekuwa tukiwasiliana kwa karibu na nampongeza sana kwa ufuatiliaji wake wa karibu wa suala hili. Nachoweza kumhakikishia kama tulivyozungumza, Kijiji cha Opkeli, Kata ya Mundarata; Kijiji cha Ogira, Kitongoji cha Ingokin, maeneo haya yote tunakwenda kuyashughulikia. Lengo ni kuona maeneo yale yote maji yanakwenda kutoka bombani iwe kwa chanzo cha maji cha kisima ama chanzo kingine cha maji.
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mloo wenye wakazi zaidi ya 70,000 unakabiliwa na changamoto kubwa sana ya maji. Naomba kufahamu nini mpango wa Serikali katika kuwatua ndoo wanawake wa Mji Mdogo wa Mloo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Juliana Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tayari imeendelea kutoa maelekezo na kutekeleza miradi maeneo ya Mloo mpaka Tunduma. Kote huko tunaendelea kuhakikisha maji yanakwenda kupatikana. Katika maeneo ambayo nimefanya ziara yangu ya awali kabisa ni Mloo pamoja na Tunduma. Tayari tumemsimamisha yule mtumishi ambaye hakuwa tayari kuendana na kasi ya sasa na tukamweka pale Meneja wa Mkoa wa RUWASA kwa sababu ni mtendaji mzuri. Pia tayari mkeka tumeshauandaa tunaenda kuongeza timu maeneo yale ya Mloo na Tunduma ili kuhakikisha maji yanakwenda kutoka.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na nashukuru sana.

Kwa niaba ya wakazi wa Wilaya ya Meatu sasa napenda niulize kwamba ni lini sasa zoezi hili litaanza kwa sababu yapata wiki mbili hivi sasa hatujapata maji katika Wilaya ya Meatu na kuna vijiji ambavyo vinaukame sana kwa mfano Bukale, Mwambegwa na Chambara ni vijiji vingi sana hatuna maji kabisa leo yapata wiki mbili wakazi wa kule tunahangaika, tunapata taabu. Serikali ituambie sasa ni lini itatuletea maji huko kwetu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza Mjika kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama jibu langu la msingi nilivyosema mwezi Agosti, 2021 mradi huu unakwenda kuanzwa na suala hili ni jana tu jopo kamili la wizara liliweza kukaa na hawa wenzetu wa KfW na Mheshimiwa Waziri aliwahitaji watoe commitment yao namna ya kuweza kutekeleza mradi huu kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge nafahamu namna ambavyo unafuatilia suala hili ninakupongeza sana. Nikutoe hofu nitaongozana na wewe tutaenda kuhakikisha kwamba kila namna ambavyo ilikuwa imepangwa inakwenda kutekelezwa kwa wakati.
MHE. ALEXANDER P. MNYETI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Majibu haya anayonipa Naibu Waziri wa Maji ni majibu ambayo yametolewa mwaka 2002 swali lilipoulizwa na Mheshimiwa Dalali Shibiliti, majibu hayo hayo; miaka kumi baadaye akauliza Mheshimiwa Charles Kitwanga akapewa majibu hayo hayo; nami nauliza miaka kumi baadaye napewa majibu haya haya.

Mheshimiwa Spika, nataka kujua, maji Usagara yanakwenda lini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mnyeti Mbunge wa Misungwi. Awali ya yote Mheshimiwa Mnyeti pamoja na wananchi wote wa Misungwi poleni sana kwa adha hii ambayo imewapata kwa muda mrefu. Mheshimiwa Mbunge kama anavyofahamu Awamu hii ya Sita, ni awamu ambayo inakwenda kumaliza kama sio kupunguza kwa sehemu kubwa tatizo la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama tulivyomsikia Mheshimiwa Rais, yeye mwenyewe akiwa hapa ndani kwa kutumia Bunge lako hili Tukufu aliahidi kuweka nguvu kubwa ya kuona kwamba matatizo ya maji yanakwenda kutatuliwa. Hivyo kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, kwenye bajeti yetu ya mwaka 2021/2022, tunakuja Misungwi kuhakikisha tatizo hili sasa linabaki kuwa historia. (Makofi)
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwanza nianze kuishukuru Serikali kwa kukamilisha kwenda kukamilisha mradi huu ambao ni wa kihostoria.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa sababu unaenda kukamilika mradi huu ambao utahudumia zaidi wananchi 51,500,000 mradi huu unaenda kukamilishwa mwezi Juni. Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa yupo tayari kuambatana nami kwa ajili ya kwenda kuukabidhi mradi huo na kufanya sherehe kwa sababu mradi ule ni wa kihistoria kuanzia mwaka 1975? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuendelea kusambaza maji baada ya kukamilisha vijiji hivyo 12 katika kata zifuatazo: Kata ya Nyugwa, Nyijundu, Kaboha, Shabaka, Nyangh’wale na Busolwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza kusambaza maji katika kata hizo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Amar Nassor Hussein, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nipende kupokea pongezi za shukrani kutoka kwako na pia suala la kuambatana na Mheshimiwa Mbunge, mimi na yeye tayari tulishafika pale Nyangh’wale, basi nitatoa nafasi hii kwa majimbo mengine ila nikishakamilisha nitaweza kutafuta nafasi ya kuja sasa kusheherekea.

Mheshimiwa Spika, mpango wa kusambaza maji katika kata alizozitaja Mheshimiwa Mbunge upo tayari kwenye mipango mikakati ya mwaka ujao wa fedha. Hivyo naomba tuendelee kuvuta Subira, tutakwenda mwaka ujao wa fedha kuona maji sasa yanaendelea kuwasogelea wananchi katika makazi yao.
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Naishukuru sana Serikali kwa kutuchimbia visima katika Jimbo la Ikungi Mashariki na Ikungi Magharibi. Hata hivyo, visima hivi havina kabisa mtandao wa maji. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha visima hivi vinakuwa na mtandao wa maji ili kuwawezesha wananchi wa majimbo haya mawili la Ikungi Mashariki na Ikungi Magharibi kuweza kupata maji safi na salama? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali ya nyongeza ya Mheshimiwa Aysharose, Mbunge Viti Maalum kutoka Singida, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kutambua kazi kubwa ambayo Wizara imefanya kuchimba visima vya kutosha na kwa sasa hivi kazi inayofuata ni kuona mtandao unakwenda kuwafikia wananchi. Hivyo Serikali huwa tunaangalia kwanza kupata chanzo na uhakika wa chanzo ukishapatikana tunajenga vituo vya kuchotea maji. Sasa tupo kwenye utaratibu wa kuona kwamba mtandao huu unaendelea kuwasogelea wananchi kadri mahitaji yanavyohitajika. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Wewe ni shahidi Mradi wa Maji Bunda sasa hivi unachukua takribani miaka kumi na tatu, najua kuna awamu ya tanki imekalimilika. Awamu nyingine ilikuwa ni kuhakikisha wanasambaza mabomba na kueneza mtandao wa maji katika kata zote 14. Hivi ninavyozungumza ni kata saba tu tayari ndiyo zimeanza kusambaza mradi wa maji na wana uhakika wa kupata maji angalau kwa asilimia 50. Je, ni lini sasa Wizara itahakikisha kata zote 14 za Bunda Mjini zinapata maji na ukizingatia humu ndani mimi ndiyo nawasemea hakuna anayewasemea. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nipende kupokea pongezi kwa kuona kwamba tanki limekamilika na angalau asilimia hamsini ya usambazaji umeshakuwa katika utekelezaji. Kwa sababu tuna kata 14 na kata saba tayari utekelezaji unaendelea hiyo ndiyo kazi ya Wizara ya Maji.

Vilevile kama ambavyo umemtaja Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo kazi hii imefanyika kwa usimamizi madhubuti. Mbunge wa Jimbo amekuwa akifuatilia mara nyingi na kwa sababu Mbunge wa Jimbo amekuwa akiwasiliana na Wizara mara kwa mara ndiyo maana maji kata saba, kati ya kata 14 yameweza kutolewa. (Makofi)
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Lakini ninalo swali moja tu la nyongeza. Kutokana na uhaba mkubwa wa maji katika Wilaya ya Muleba na jiografia ya Wilaya ya Muleba inapakana na Ziwa Victoria. Serikali inao mpango wowote wa kutumia Ziwa Victoria kuvuta maji kwa ajili ya Wilaya ya Muleba? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mhehsmiwa Naibu Spika, Mradi wa Ziwa Victoria ni mradi wa kimkakati na ni mradi ambao tunautarajia uhudumie maeneo mengi sana kwasababu ni mradi unaopita katika majimbo mengi na mikoa mbalimbali. Hivyo niweze kumwambia Mhehimiwa Mbunge kwamba maeneo yake ambayo bomba hili kubwa litakuwa likipita basi na yeye atanufaika katika vijiji vile ambavyo viko kilometa 12 kutoka kwenye bomba kwa pande zote kulia na kushoto.
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, nilikuwa nataka niiulize Serikali ni lini itamaliza kero ya maji ambayo imekuwa ni sugu katika Kata ya Wazo, Mitaa ya Nyakasangwe, Mitaa ya Salasala na Mivumoni Kata ya Mbezi Mtoni, Sakuveda na Mabwepande Mtaa wa Mbopo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kupitia DAWASA wanafanya kazi nzuri sana maeneo yote ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja. Na tayari mikakati kabambe inaendelea na kufikia mwaka ujao wa fedha maeneo mengi sana ya maeneo hayo yote uliyoyataja Mheshimiwa Mbunge yatakuwa yamefikiwa na maji bombani.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali juu ya upatikanaji wa maji katika maeneo yetu hasa Mji wa Itigi ambapo mimi ndio Mwakilishi wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahadi hii ya kuvuna maji katika Mji wa Itigi, ni swali la pili nauliza katika Bunge hili, Bunge lililopita niliuliza swali kama hili. Majibu yalikuwa tunajiandaa, dalili inaonesha kwamba watafanya.

Je, ni lini sasa uvunaji huu utaenda kufanya katika Mji wa Itigi na maeneo ambayo umeyataja ya Kayui, Muhanga na Kaskazi kujenga mabwawa?

Mheshimiwa Naibu Spika, Lakini swali la pili, nashukuru pia Serikali kwa kukamilisha mradi mkubwa wa maji katika Mji wa Itiga ambao una manufaa makubwa kwa wananchi lakini unawatua akina mama ndoo kichwani. Lakini gharama za kuunganisha maji yale kwenda ndani ni gharama kubwa sana. kwa hiyo, mtu wa kijijini kwa shilingi 200,000 ni hela nyingi. Je, Serikali ipo tayari kupunguza gharama za uunganishaji maji ili wananchi wanufanike na mradi huu mkubwa ambao Mbunge wao amehangaika nao kuupata na wizara imesaidia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, uvunaji huu wa maji tunautarajia kuutekeleza katika mwaka wa fedha ujao kwa maana mwaka 2021/2022. Mheshimiwa Mbunge ahadi hii imekuwa ikitolewa toka huko awali lakini kwa sasa hivi kama tulivyokuwa tumeendelea kuongea RUWASA imekuwa ni mkombozi, RUWASA imekuwa ni chachu ya mageuzi ya utekelezaji wa miradi ndani ya Wizara. Hivyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge ili sasa linaingia kwenye utekelezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusiana na gharama za uunganishaji, hili nalo limekuwa ni tatizo sugu. Hata hivyo, kama tulivyomsikia Mheshimiwa Waziri wakati wa uwasilishaji wa bajeti, ni suala ambalo tayari lipo katika uangalizi mkubwa ambapo tunahitaji kuona wananchi wanaenda kupata nafuu kubwa katika uunganishwaji wa huduma ya maji sio tu katika Mji wa Manyoni bali kwa Tanzania nzima.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kilombero, napenda kushukuru kwa majibu mazuri ya Wizara na tunaombea kweli huu mkopo upatikane na mradi huu ufanyike.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, ni lini Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kutembelea Jimbo la Kilombero ili apite angalau kuzungumza na wananchi wa Zinginai, Magombera, Kanyenja, Mpanga na Muhelule ambao wana shida kubwa ya maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kutokana na hali ya udharura wakati tukisubiri mradi huu wa maji tayari Serikali ilishachimba kisima kikubwa katika Kata ya Lumemo ambapo kinatoa lita 30,000 kwa saa. Changamoto ni tenki la kuhifadhi maji yale kuwasambazia wananchi. Katika hali hii ya udharura, je, Serikali haiwezi kutujengea tenki wakati tunasubiri mradi wa maji wa Kiburubutu - Ifakara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hili la kwenda Kilombero ni moja ya majukumu yangu. Mheshimiwa Mbunge mara baada ya Bunge hili tutaweka utaratibu mzuri ili niweze kufika hapo. Naamini mpaka mwisho wa Bunge hili hata mradi huu utekelezaji utakuwa umeanza, kwa hiyo, nitakuja nikiwa na bashasha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na ujenzi wa tenki kwa kisima kile ambacho tumekichimba, nia na dhamira kabisa ya Wizara ni kuona wananchi wanapata maji kwa umbali mfupi. Tumeshaweza kutoa fedha ya kuchimba kisima ni dhahiri lazima tutoe fedha ya ujenzi wa tenki. Nimuahidi Mheshimiwa Mbunge, kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha, ujenzi wa tenki utaanza kufanyika. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, nimeyasikia majibu ya wizara. Kwa kuwa mpango wa Serikali ulijiwekea malengo kufikia mwaka 2025 upatikanaji wa maji vijijini itakuwa ni asilimia 85. Na leo ni mwaka 2021 na umekiri hapa kupitia majibu yako takwimu ambazo umezisoma kwamba upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Nkansi ni asilimia 48 tu. Kwanza takwimu hizi si halisia. Lakini napenda kuwaambia Serikali kwa kuwa mpaka sasa tuna asilimia 48 hamuoni sasa kuna jitihada za ziada za kutumia chanzo cha Ziwa Tanganyika ili kuweza kufikia asilimia 85 kama malengo tuliyojiwekea? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Swali la Pili, huu mradi wa maji Namanyere wananchi wameanza kuangalia mabomba toka mwaka jana hawapati maji mpaka leo. Ningependa kujua kuna mkakati upi wa ziada wa Serikali wa kuweza kupelekea wananchi wa Namanyere na Kata zote za Jimbo la Nkasi Kaskazini maji ili waendane na kauli mbiu ya Mama Samia ya kumtua mama ndoo kichwani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mpango wa Serikali kufika mwaka 2025 kadri ya ilani ya Chama Tawala inavyotaka vijijini maji yatapatikana kwa asilimia 85 na zaidi ikiwezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo nipende kukutoa hofu Mheshimiwa Mbunge na nikupongeze unafuatilia kwa makini sana masuala haya ya wananchi wako na wewe ni mwanamke ndio maana unaongea kwa uchungu kwasababu unafahamu fika kubeba maji kichwani kwa umbali mrefu namna ambavyo ilivyotabu.

Kwa hiyo tutahakikisha tunawatua kina mama ndoo kichwani. Wewe ni Mbunge mahiri mwanamke na mimi ni Naibu Waziri Mwanamke wote tunafahamu adha ya kubeba maji kichwani tutashughulikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, huko nyuma tunafahamu fika RUWASA haikuwepo na kwa mwaka mmoja tu tumeona namna ambavyo RUWASA imefanya kazi kwa bidii. Na kufufua miradi ambayo ikisuasua na sasa hivi maji yanapatikana mabombani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutumia Ziwa Tanganyika Mheshimiwa Aida, kama ambavyo tumetoka kuongea kwa kirefu hapa majuzi wakati tunapitisha bajeti yetu. Huu ni mpango mkakati wa kutumia vyanzo hivi vya uhakika, kwa hiyo Ziwa Tanganyika nalo lipo kwenye mikakati ya wizara tutahakikisha tunalitumia ili kuona kwamba mabomba yapate kutoa maji na sio kushika kutu. Kwa hiyo, haya yote uliyoyaongea yapo kwenye utekelezaji wa wizara na ifikapo mwaka 2021/2022 mwaka mpya wa fedha Ziwa Tanganyika nalo tayari lipo kwene mpango mkakati wa utekelezaji. (Makofi)
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, Ahsante. Naomba kuiuliza wizara maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Tatizo la maji kwenye Jimbo la Newala Vijijini limekuwa ni sugu, wananchi wa Newala Vijijini wanakunywa maji ya kuokota ambayo wanaokota kipindi cha mvua, maji ambayo huwa yanaoza na yanatoa harufu. Lakini tunacho chanzo kikubwa cha Bonde la Mitema ambalo Serikali ikiwekeza kwa kiasi kikubwa bonde lile litatua kabisa changamoto za maji kwa sababu maji yaliyopo katika bonde lile yana mita za ujazo zipatazo 31,200 lakini mahitaji ya wananchi wa Newala, Tandahimba pamoja na Nanyamba kwa siku ni mita za ujazo 23,441.

Je Serikali imejipangaje kuhakikisha inaweka fedha za kutosha katika bonde la Mitema ili tatizo la maji liweze kukoma na wananchi waweze kupata maji ya kutosha?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika kituo cha Mto Ngwele kulikuwa na tatizo la pump house pamoja na transformer. Lakini bahati nzuri Januari mwaka huu pump house imerekebishwa na TANESCO wameshapelekwa pale transformer iko pale haijafungwa hadi leo hii ikaweza kusukuma maji. Nini kauli ya Serikali kwasababu wananchi wanaendelea kutaabika kupata maji wakati transformer iko pale wanashindwa kuifunga. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge kwanza nakupongeza sana wewe ni Mbunge wa Jimbo, mwana mama Hodari na umekuwa ukifuatilia kwa uchungu sana masuala la maji ili kuokoa kina mama wenzako kuhakikisha wanatuliwa ndoo kichwani kama ambavyo wizara tunakesha, tunafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba kina mama lazima tuwatue ndoo kichwani na maji yapatikane umbali mfupi kutoka kwenye makazi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake namba moja anauliza fedha za kutosha kuwezesha bonde la Mitema. Hii ni moja ya kazi ambazo tumeagiza RUWASA waweze kushughulikia, hii itafanyika ndani ya mwaka wa fedha ujao na kuona kwamba tuanze kuuona usanifu unakamilika na kila kitu kinakwenda vizuri ili maji yaweze kupatikana kwenye chanzo cha uhakika. Wakati tuna hitimisha bajeti yetu nimeongelea suala la Newala hata mimi ni mwana mama nisingependa kuona watu wanaendelea kutumia maji ya kuokota kwa karne hii na tumshukuru Mungu tumempata Rais mwana mama ambaye kiu yake kubwa ni kuona kina mama wanatuliwa ndoo kichwani. Mheshimiwa Mbunge Maimuna hili tutashirikiana kwa pamaja kuona kwamba tunakamilisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kuhusiana na transformer ambayo ipo pale. Sisi kwa upande wa wizara yetu tuliweza kushughulika na pump house na imeshakamilika. Kwa hiyo, tutaendelea kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Nishati kuona kwamba sasa ile transformer inakwenda kufungwa haraka iwezekanavyo ili matumizi ya umeme kwenye kusukuma maji yakaweze kufanyika na watu wakanufaike na mradi ambao umeshakamilika.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri naomba kujibu maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; suala la mradi huu wa Dola za Kimarekani milioni 500 ni mradi ambao umekuwa wa kila siku tunaendelea kusimuliwa, kuandikiwa kwenye vitabu, lakini utekelezaji wake hauleti tija kwa Watanzania. Kama Waziri alivyosema kwamba mradi huu ndio ulitarajiwa kwenda kukidhi maji kwa wananchi wa Wilaya ya Chemba ukiwemo Mji wa Chemba. Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya visima viwili ambavyo vimechimbwa mwaka 2017 lakini mpaka leo visima vile havijafungwa pump wala miundombinu yoyote haijaweza kutekelezwa? Lini Serikali itatoa fedha ili kwenda kukamilisha huo mradi wa visima hivyo viwili ambavyo vimechimbwa mwaka 2017 na mpaka sasa ni miaka minne? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Wilaya ya Chemba tunatarajia kupata maji ya kutosha kutokana na mradi mkubwa wa Bwawa la Farkwa, lakini bwawa hilo si tu kwa Wilaya ya Chemba bali litasaidia pia kupunguza adha ya maji kwenye Jiji la Dodoma, Wilaya ya Bahi na Wilaya ya Chamwino. Natamani kusikia kauli ya Serikali, ni lini mradi huu utakwenda kuanza rasmi kwa sababu hata kwenye bajeti ya maji hakujatengwa fedha za kwenda kuanzisha huu mradi badala yake tunasubiri fedha za wafadhili. Kwa hiyo nataka nijue Serikali ni lini inaenda kuanza Mradi wa Farkwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kunti Majala, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipende kumpongeza Mheshimiwa Kunti, amekuwa ni mfuatiliaji mzuri pamoja na kwamba ni mjumbe katika Kamati yetu ya Maji, amekuwa na mchango mkubwa, lakini vilevile nipende pia kumpongeza kwa sababu ana mahusiano mazuri na Mbunge wa Jimbo, wamekuwa wakifuatilia kwa pamoja masuala haya. Sisi kama Wizara tumesema kwamba Chemba maji lazima yaje. Pamoja na kwamba kuna visima hivi viwili vilichimbwa mwaka 2017, lakini mwezi Machi, 2021 tumeongeza kuchimba visima vinne, ili visima vile vinne vya mwaka huu tunakuja sasa kutengeneza mtandao wa usambazaji maji kuelekea kwenye vituo vya uchotaji maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili anaongelea Bwawa la Farkwa. Hili bwawa ni juzi tu Mheshimiwa Waziri ametoka kuliongelea kama moja ya mikakati ya kuhakikisha maji Chemba yanafika. Pamoja na hilo tuna Mradi mkubwa wa Ziwa Victoria ambao pia Chemba utafika. Kwa hiyo bwawa hili litakwenda sambamba na mradi huu mkakati wa Ziwa Victoria. Tuendelea kuvuta subira, tumetoka mbali tunakokwenda ni karibu, maji Chemba yanakuja bombani.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza niipongeza Wizara ya Maji kwa kazi wanayoifanya, lakini naomba kuuliza swali dogo la nyongeza. Kutokana na ongezeko la watu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Makete, hasa hasa Makete Mjini tuna uhitaji mkubwa wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuuliza ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji wa kutoka Kitulo, Isapulano kwenda Iwawa Makete Mjini ili kuongeza upatikanaji wa maji kutokana na kwamba tayari kama halmashauri tulishawasilisha andiko letu la mradi wa bilioni 3.1 kwenye Wizara? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Festo Sanga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli andiko hili tumeshalipokea pale Wizarani na mipango ya kuona namna gani ya utekelezaji itaweza kufanyika tayari pia tunashughulikia. Pia nipende kumpongeza sana Mheshimiwa Festo Sanga amekuwa ni mfualitiaji mzuri wa miradi hii yote, yeye mwenyewe amefuatilia na sasa hivi tumeshampelekea Mradi wa Maji wa Lupila milioni 100, lakini vile vile tumempelekea Mradi wa Maji wa Bulongwa milioni 100. Yote haya ni matunda ya yeye kuwasemea vyema wananchi wake. Hivyo sisi kama Wizara hatutakuwa kikwazo kwa Mheshimiwa Sanga na kwa wote anaowawakilisha, tutahakikisha na mradi huu wa bilioni 3.0 nao tunakuja katika utekelezaji. (Makofi)
MHE. KENETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, swali langu la msingi ilikuwa ni kwamba Mkoa wa Dodoma unapata mvua kidogo lakini kumekuwa na upotevu mkubwa wa maji kipindi mvua inavyokuwa inanyesha.

Lengo la swali langu ni je, Serikali ina programu gani mahsusi, acha hii ya kudonoa donoa, programu mahsusi ya kuanza kukinga maji ambayo yanapotea kwa kiasi kikubwa kwa miaka nenda rudi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; tunajenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza. Lakini, mradi huu ni mkubwa unapita kwenye mabonde na mito mingi. Je, Serikali kupitia Wizara ya Fedha, Kilimo na Wizara ya Ujenzi haioni kwamba tuongeze sehemu ya mradi ule kwa ajili sasa ya kuweka mabwawa na kutengeneza upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo badala ya fedha nyingi zinajenga kwenye reli lakini mradi ule hauna pact ambayo ingeweza kusaidia kwenye Sekta ya Kilimo. Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, mpango mahsusi wa Serikali kutumia maji ya mvua kama nilivyoelekeza, tuna mpango wa kuchimba mabwawa ambayo yataweza kuvuna yale maji na yatasambazwa kwa wananchi wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ni kuhusiana na ujenzi wa reli ya kisasa. Pamoja na kwamba hii ni nje ya Wizara yangu nipende tu kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge kwamba reli hii ni ya thamani kubwa sana na ni ya manufaa makubwa kwa wananchi hivyo, kila suala lina mkakati wake na umuhimu wake. Masuala ya mabwawa kuongezwa, sisi kama Wizara ya Maji tutashughulikia. Licha ya kwamba mradi huo wa reli manufaa yake yataendelea kuzingatiwa. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Mbali na mkakati wa Serikali katika jibu lake la msingi la kuchimba mabwawa na marambo. Jimbo la Bunda Mjini limekuwa na changamoto sana ya ukarabati wa marambo.

Sasa ni lini Serikali mtatukarabati Rambo la Nyabehu, Kinyambwiga na Gushigwamara ili sasa wananchi wa maeneo hayo wapate huduma ya maji vile vile mifugo iweze kupata huduma ya maji. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ukarabati wa mabwawa na marambo kwa ajili ya mifugo, sisi kama Wizara tunaendelea kukarabati awamu kwa awamu kadri fedha inavyopatikana. Hivyo, pia kwa suala hili la Bunda Mjini, Bwawa la Nyabehu, Kinyambwiga pamoja na hilo lingine yote yapo katika mkakati wa Serikali kuona kwamba yanarudi katika hali bora. Hivyo, nipende kukupongeza Mheshimiwa Esther kwa kufuatilia na uongeze ushirikiano na Mbunge wa Jimbo ili mambo yakae sawa zaidi. (Makofi)
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri na Waziri wake wa maji kwa kututengea kiasi cha shilingi bilioni 2,146,000,000 kwa ajili ya huduma kwa watu wa Kilindi, baada ya shukrani hiyo ningependa tu nimuulize swali moja tu Mheshimiwa Naibu Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na maelezo mazuri ya kwamba wanafanya tafiti na tafiti hiyo itatoa majibu ndani ya mwezi ujao, sasa nataka tu kupata commitment ya Mheshimiwa Naibu Waziri je, wananchi wa Wilaya ya Kilindi wategemee nini kuhusiana na uhakika wa mradi wa huu ambao utahudumia zaidi ya vijiji 12? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua kama ifautavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipende kupokea pongezi zake kwangu pamoja na Mheshimiwa Waziri kwa hakika tunashirikiana vema na wewe pia nikupongeze kwa sababu unatupa ushirikiano mzuri na tutaendelea kufanya kazi bega kwa bega kuhakikisha suala la maji tunakwenda kulitatua kwa pamoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na lini sasa commitment ya serikali kwenye Mradi huu wa Diburuma ni kwamba tayari kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi utafiti unaendelea na hivi punde mwezi ujao tunakwenda kukamilisha usanifu hivyo kutokana na gharama ambayo itapatikana sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha kutumia chanzo hiki tukiamini kabisa kitakuwa ni chanzo endelevu na sehemu kubwa zaidi ya vijiji 10 ninafahamu zitapitiwa kwa hiyo tutaendelea kushirikiana kuona kwamba chanzo hiki tunakwenda kukitumia tutakitafutia fedha ili kuona kwamba tunatimiza azma ya kuleta maji.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Wizara, naomba kuuliza:-

Serikali ina mpango gani wa kutanua mradi wa maji wa Mji Mdogo wa wa Laela ili uweze kupeleka katika Kata ya Mnokola na Miangalua kwa sababu hivyo visima vimeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi katika Kata hizo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali inao Mpango wa kusambaza maji kutokana na vyanzo mbalimbali tulivyonavyo, na tutahakikisha tunafanya hivyo hivyo pamoja na chanzo hiki cha Rahela pia tutaenda kukifanyia kazi mwaka ujao wa fedha.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwanza kabisa naishukuru Serikali imeweza kuingiza kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwenye mradi huu. Mradi huu ulifanya kazi miezi mitatu tu na watu wakaihujumu ile miundombinu kwa kuiba vifaa kama solar, betri na pampu. Sasa swali langu linakuja, ni lini sasa Serikali itarudisha vifaa hivi ili wananchi waweze kuendelea kupata maji? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wezi wapo wanajulikana kabisa kwenye Kata ile, Serikali ina mpango gani sasa wa kuwachukulia hatua kazi za kinidhamu? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake namba moja lini vifaa vile vitarudishiwa pale kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi na kadiri ambavyo tumekuwa tukiongea naye kuhusu suala hili na nimpongeze kwa namna ambavyo amekuwa mfuatiliaji mzuri. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba suala hili hatutazingatia zaidi kwenye vile vifaa vya solar, tutazingatia kuleta umeme kwa kupitia REA ili tuwe na umeme wa uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na wale wezi kuchukuliwa hatua, kwanza niombe ushirikiano Zaidi, tuendelee kuwasiliana, hawa wezi Mbunge akiwa kama mwakilishi wa akinamama wa eneo lile, aende akaripoti polisi, lakini tumekuwa tukimsikia mara nyingi Mheshimiwa Waziri wetu kwamba mwisho wa kuchezea miradi ya maji ni sasa. Kama una mambo ya kutaka kuchezea, kachezee kitambi chako. Kwa hiyo, tutaendelea kuhakikisha kwamba miradi ya maji mwisho kuchezewa. (Makofi)
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina swali moja dogo la nyongeza. Mradi wa Maji wa Litembo una uchakavu mkubwa wa miundombinu hali iliyopelekea Kijiji cha Langandondo kukosa maji kwa miaka minne mvululizo, lini mradi huu unaenda kukarabitiwa na wananchi wale wa Langandondo waweze kupata maji Kata ya Litembo. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Liuka Benaya, Mbunge wa Mbinga Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, uchakavu wa Mradi wa Litembo kama Wizara tunautambua na tayari tumetoa maagizo kwa Meneja wa RUWASA tayari na yeye anaendelea kujipanga ili kuhakikisha kwamba mwaka ujao wa fedha nao tuweze kutupia jicho la utekelezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kumpongeza Mheshimiwa Liuka amekuwa ni mfuatiliaji mzuri, tumeondoka hapa wakati wa weekend tumekwenda Mbinga Vijijini tumefanya kazi nzuri na miradi hii yote ya uchakavu pale anafahamu tulishakubaliana utekelezaji wake utafanyika kwa haraka.
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Serikali tayari imemaliza kushauriana na wenzetu wa KFW na tayari kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022 Serikali imetenga bilioni 19 za ndani kwa ajili ya kuanza mradi huu. Je, ni kiasi gani kimetengwa kwa kutoka kwa hawa marafiki zetu wa KFW kwa ajili ya mradi huu kwa mwaka wa fedha 2021/2022?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa, miradi mingi ya maji imekuwa ikitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu tu na Mkoa wetu wa Simiyu wananchi walio wengi ni wakulima na wafugaji. Je, Waziri anawahakikishiaje wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwamba, mradi huu utaenda kuwasaidia katika zoezi zima la umwagiliaji na matumizi ya mifugo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Simon Lusengekile, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza anahitaji kufahamu ni kiasi gani kimetengwa na hawa wenzetu wa Serikali ya Ujerumani:-

Mheshimiwa Spika, kwa majibu ya rahisi ni kwamba, sisi tumetenga hiyo milioni 19 ambavyo imesomeka kwenye bajeti yetu na kwa Serikali ya Ujerumani wametenga bilioni 55 kwa ajili ya mradi huu. Na huu mradi ni mradi mkubwa ambao utakwenda kugharimu zaidi ya bilioni 444, fedha za ndani zitakazotumika zitakuwa ni bilioni 124 na fedha za KFW 320.

Mheshimiwa Spika, kwa suala la kuzingatia umwagiliaji na ufugaji, sisi kama Wizara tumezingatia na tumeweza kuona kwamba tunaenda kuhakikisha kukabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi katika Mkoa wa Simiyu. Na shughuli kubwa ambazo zitaendelea kufanyika ni ujenzi wa mabwawa ambayo yatatumika katika umwagiliaji, lakini vilevile malambo katika namna ambavyo tutaendelea kupata fedha katika miaka ya fedha ya mwaka 2021/2022 pia malambo kwa ajili ya mifugo yatajengwa.
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, nikushukuru, kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa ahadi ya kuanza upembuzi yakinifu tangu mwaka wa fedha 2019/2020, 2020/2021 na leo mwaka 2021/2022 lakini upembuzi yakinifu huu hauishi na umechukua zaidi ya miaka mitatu kwa mradi huu wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye Miji ya Malya, Sumve na Malampaka.

Je, Serikali haioni sasa umefika wakati wa kuwaambia uhalisia watu wa Sumve ili wajue ni lini wanapata maji haya ya bomba kutoka Ziwa Victoria?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria yameshafika kwenye Mji wa Ngudu na Serikali imejenga pale tenki la maji la lita milioni mbili na Naibu Waziri aliwahi kutembelea tukiwa naye; na katika mradi ule usanifu unaonesha maji yanatakiwa yafike katika Jimbo la Sumve katika Kata za Lyoma, Malya, Mwagi, Nyambiti na Wala.

Je, Serikali inasema nini kuhusu kusambaza maji haya ya bomba kwenye Kata hizo za Jimbo la Sumve?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kasalali Emmanuel kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mradi wa maji wa Ziwa Victoria kufikia Kata ambazo zipo ndani ya Jimbo la Sumve, tayari Wizara inaendelea kuona uwezekano wa kukamilisha hilo na mara fedha itakapopatikana suala hili tunakwenda kulitimiza.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili tenki ambalo limekamilika usambazaji wa maji katika maeneo yale ya wakazi, suala hili tayari linafanyiwa kazi. Wizara tumeshaagiza mamlaka husika pale Mwanza na wataendelea kufanyia kazi kwa haraka sana kwa sababu tayari fedha nyingi ya Serikali imeshatumika, hivyo tunahitaji kuona kwamba wananchi wale wanakwenda kunufaika na kufaidi maji haya ambayo tunatarajia yatoke bombani.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, naomba niulize Serikali ni lini kupitia Wizara ya Maji itapeleka maji kutoka Ziwa Victoria katika Mji wa Bihalamuro kama alivyoahidi Hayati Rais Magufuli mwaka jana akiwa anaomba kura kwa ajili ya kuwatua ndoo wakina mama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver, Mbunge wa Viti Maalum, Kagera kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maji kutoka Ziwa Victoria yanatarajiwa pia kunufaisha wakazi wa Jimbo la Biharamulo na hii binafsi nilishaenda kufanya ziara maeneo ya Biharamulo na mipango mikakati inakwenda ukingoni sasa ili tuweze kuona mwaka ujao wa fedha kadri ambavyo fedha itakuwa ikipatikana, Biharamulo nao wawe wanufaika namba moja.

Mheshimiwa Spika, nipende kumpongeza Mheshimiwa Oliver amekuwa mfuatiliaji mzuri na sisi hatutakuwa kikwazo, tutahakikisha wote ambao mnafuatilia kwa kina hii kazi ya usambazaji maji na kuleta maji kutoka Maziwa yetu Makuu ikiwa ni mpango mkakati wa Wizara kutumia Maziwa Makuu inakwenda kutimia. (Makofi)
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, katika majibu ambayo ameyatoa ametaja mradi wa maji katika Kijiji cha Muhange ambao unapata maji kutoka Mto Mgendezi kwenda Muhange Centre na kwenda Muhange ya Juu. Hata hivyo mradi huu sasa maji yanayotoka hayafai kwa matumizi ya binadamu kwasababu ni machafu. Lakini vilevile mradi huu haukukamilika kama ilivyokusudiwa. Je, nini kauli ya Serikali kuhusiana na mradi huu?

Pili, kutokana na mradi wa maji na changamoto hizi ambazo nimezitaja, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kufuatana nami ili akazione hizo changamoto na hatimaye kutoa suluhu ya miradi hii?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aloyce Kamamba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nipende kusema nimesikitika kuona kwamba Mheshimiwa Mbunge anasema maji ni machafu na mradi haujakamilika vizuri kwa sababu swali lake la pili ni ombi la kuambatana na mimi nipende kukuhakikishia Mheshimiwa Mbunge mara baada ya Bunge hili tutakwenda pamoja na nitakwenda kujihakikishia na wakati tunaendelea kukamilisha session hii ya Bunge ninatoa maagizo kwa Meneja wa eneo lile aweze kuwajibika haya maji yaweze kufanyiwa treatment kadri ya utaalamu wetu wa Wizara ili wananchi waweze kupata maji safi na salama. (Makofi)
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi, majibu haya ni mazuri kuyasikia kwenye masikio na yanafurahisha, lakini siamini kama kuna ukweli wa kutosha kwasababu kwa mfano hili swali (c) kuhusu Mradi wa Maji Karabagaine nimewahi kuliuliza humu ndani majibu yakawa ni haya haya kwamba mradi huu utaanza, lakini mpaka leo haujaanza. Sasa leo nitaaminije kinachosemwa hapa ni kweli?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante nipende kujibu swali la Mheshimiwa Jasson Rweikiza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Wizara tupo katika mageuzi makubwa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na mradi kama huu wa Karabagaine ni mradi wa muda mrefu lakini ni katika ile miradi ambayo tayari tupo katika mpango wa kuona kwamba utekelezaji wake unafikia sasa mwisho.

Mheshimiwa Spika, hivyo nipende kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo ameshafuatilia kwa muda mrefu na jitihada kubwa namna ambavyo tumeweza kushirikiana pamoja nikuhakikishie mradi huu unakwenda kutekelezwa katika mwaka wa fedha huu 2021/ 2022 na itawezekana kwa sababu tumedhamiria kuleta mageuzi makubwa.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa swali dogo la nyongeza; wewe ni shahidi mradi wa Bunda umechukua muda mrefu sana takribani miaka 13; lakini moja katika makubaliano kwenye mkataba wa mradi ule ni kujenga vitu kabla mradi haujafika Bunda Mjini kwenye eneo linalotoka kule Nyabeu.

Sasa nataka kuuliza maeneo yanayopita mradi kama Gushigwamara, Kinyambwiga, Tairo, Guta na Bunda Store kabla hayajafika centre; ni lini mtaweka vituo ili wale wananchi wa maeneo yale wasisikie tu mradi umetoka chanjo cha maji vijiji ambavyo vinapita havijapata maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Bulaya kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, sisi kama Wizara tayari tunaendelea na kuona kwamba maeneo ya miradi ambayo imekaa muda mrefu inakamilika, na sera ya maji inataka pale kwenye chanzo na kadri ambavyo mradi unakwenda tunaendelea kusambaza maji. Yule wa karibu ya chanzo ataendelea kupata maji kwa kwanza kulikoni aliyekuwepo kule mbali. Hivyo nikuhakikishie Mheshimiwa Ester Bulaya kwamba maeneo yote ambayo umeyataja yatazingatiwa katika kuona kwamba miundombinu ya usambazaji maji inawafikia. (Makofi)
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali.

Serikali imekamilisha mradi wa maji katika Mji wa Kateshi mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 lakini mpaka sasa mradi huo haujaanza kufanya kazi.

Je, ni lini Serikali itaanza kusambaza maji ili wananchi wa mji wa Katesh lakini maeneo ya Mogito ambayo chanzo kimeanzia pamoja na maeneo mradi unapopita watanufaika na maji haya katika miji hii na kata hizi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu swali la Mheshimiwa Asia Halamga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mradi wowote ukishakamilika sisi kama Wizara tunapenda kuona maji yanawafikia wananchi kwenye vituo vya kuchotea maji, hivyo mara miundombinu yote itakapokamilika maji mara moja yataanza kutoka katika mradi huu wa Katesh. Tunafahamu tumeshatumia fedha nyingi za Serikali ambazo ni jasho la wananchi, hivyo hatuko tayari kuona fedha imeshatumika halafu kile tunachokitarajia kisipatikane. Pia niendelee kukupongeza Mheshimiwa Asia mwendo wako ni mzuri wewe unawakilisha vizuri vijana na sisi kama Wizara hatutakuwa kikwazo kuona kwamba unafika mbali. (Makofi)
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kuniona kunipa swali la nyongeza.

Kwa kuwa katika miradi 28 ambayo inatakiwa ipelekewe maji na Mji wa Makambako ni miongoni katika miji hiyo 28; ni lini mradi huo utaanza katika mji wa Makambako?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sanga Mbunge wa Makambako kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, miradi yote ya miji 28 mpaka dakika hii taratibu zote zimeshakamilika hivyo wakati wowote ule miradi hii katika miji yote 28 tunakwenda kuanza kufanya kazi mara moja.
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, nikushukuru, kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa ahadi ya kuanza upembuzi yakinifu tangu mwaka wa fedha 2019/2020, 2020/2021 na leo mwaka 2021/2022 lakini upembuzi yakinifu huu hauishi na umechukua zaidi ya miaka mitatu kwa mradi huu wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye Miji ya Malya, Sumve na Malampaka.

Je, Serikali haioni sasa umefika wakati wa kuwaambia uhalisia watu wa Sumve ili wajue ni lini wanapata maji haya ya bomba kutoka Ziwa Victoria?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria yameshafika kwenye Mji wa Ngudu na Serikali imejenga pale tenki la maji la lita milioni mbili na Naibu Waziri aliwahi kutembelea tukiwa naye; na katika mradi ule usanifu unaonesha maji yanatakiwa yafike katika Jimbo la Sumve katika Kata za Lyoma, Malya, Mwagi, Nyambiti na Wala.

Je, Serikali inasema nini kuhusu kusambaza maji haya ya bomba kwenye Kata hizo za Jimbo la Sumve?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kasalali Emmanuel kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mradi wa maji wa Ziwa Victoria kufikia Kata ambazo zipo ndani ya Jimbo la Sumve, tayari Wizara inaendelea kuona uwezekano wa kukamilisha hilo na mara fedha itakapopatikana suala hili tunakwenda kulitimiza.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili tenki ambalo limekamilika usambazaji wa maji katika maeneo yale ya wakazi, suala hili tayari linafanyiwa kazi. Wizara tumeshaagiza mamlaka husika pale Mwanza na wataendelea kufanyia kazi kwa haraka sana kwa sababu tayari fedha nyingi ya Serikali imeshatumika, hivyo tunahitaji kuona kwamba wananchi wale wanakwenda kunufaika na kufaidi maji haya ambayo tunatarajia yatoke bombani.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, naomba niulize Serikali ni lini kupitia Wizara ya Maji itapeleka maji kutoka Ziwa Victoria katika Mji wa Bihalamuro kama alivyoahidi Hayati Rais Magufuli mwaka jana akiwa anaomba kura kwa ajili ya kuwatua ndoo wakina mama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver, Mbunge wa Viti Maalum, Kagera kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maji kutoka Ziwa Victoria yanatarajiwa pia kunufaisha wakazi wa Jimbo la Biharamulo na hii binafsi nilishaenda kufanya ziara maeneo ya Biharamulo na mipango mikakati inakwenda ukingoni sasa ili tuweze kuona mwaka ujao wa fedha kadri ambavyo fedha itakuwa ikipatikana, Biharamulo nao wawe wanufaika namba moja.

Mheshimiwa Spika, nipende kumpongeza Mheshimiwa Oliver amekuwa mfuatiliaji mzuri na sisi hatutakuwa kikwazo, tutahakikisha wote ambao mnafuatilia kwa kina hii kazi ya usambazaji maji na kuleta maji kutoka Maziwa yetu Makuu ikiwa ni mpango mkakati wa Wizara kutumia Maziwa Makuu inakwenda kutimia. (Makofi)
MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Spika, asante. naipongeza Serikali kupitia DAWASA kwa kazi nzuri iliyofanyika kule Mbwawa wananchi sasa wamepata maji kwa mradi kukamilika kwa asilimia 90. Pamoja na hayo nina maswali mawili madogo ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, mradi huu wa matenki mawili ya maji katika Kata ya Pangani, kwa maana ya Mtaa wa Vikawe na Mtaa wa Pangani, unaodhaminiwa na Benki ya Dunia unajengwa kwa kusuasua. Tenki la Vikawe limefikia asilimia 50, lakini tenki la Pangani kwa ajili ya kuhakikisha sasa wananchi wa Kata ya Pangani wote wanapata maji bado halijaanza kujengwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhimiza sasa, ili hili tenki la pili liweze kuanza kujengwa?

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, wananchi wa Kata ya Misugusugu na Visiga na hususan maeneo ya Zogoale, Jonuga pamoja na Saeni, kupitia Zegereni Viwandani, wana shida kubwa ya maji na wanahangaika kutumia maji ya visima na haya ni maeneo muhimu ya uchumi katika Jimbo letu la Kibaha Mjini. Ninafahamu kuna mradi wa takribani bilioni 3.3 unaotakiwa kujengwa.

Je, ni lini Serikali sasa inaanza kujenga mradu huu, ili kuwaondolea wananchi kero na kustawisha uchumi katika Mji wetu wa Kibaha?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Silvestry Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mji wa Kibaha ni moja ya miji ambayo Serikali imeelekeza fedha nyingi kwa kuona kwamba, maji sasa yanakwenda kupatikana. Katika eneo la Pangani ni mradi mkubwa ambao tayari Serikali mpango ni kuelekeza zaidi ya bilioni tano na kazi zinatarajiwa kuanza mapema robo ya kwanza ya mwaka wa fedha ujao, kwa maana ya kuanzia mwezi wa tisa tunatarajia kazi itaenda kuanza katika mradi huu.

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile katika maeneo ya viwandani, kama mwenyewe Mheshimiwa Mbunge alivyoongea, na nipende tu kumshukuru kwa kuweza kutoa pongezi zake kwa Serikali. Ni kweli Wizara bado imelekeza fedha za kutosha zaidi ya bilioni tatu na katika mwaka ujao wa fedha tunatarajia mradi huu uweze kutekelezwa na kasi ya mradi huu itategemea upatikanaji wa fedha katika Wizara, lakini lengo letu kubwa tunaelekea kwenye mageuzi makubwa. Miradi kama hii yote mikubwa tutahakikisha tunaisimamia kwa wakati.
MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, Serikali baada ya kukamilisha miradi ya maji, hasa vile visima virefu, huanzisha kamati za watumiamaji, lakini kamati hizi zimekuwa zikishindwa kujiendesha na hivyo kufikia mahali kushindwa kabisa kutoa huduma au kufa. Na ningependa kushauri pengine Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wale watumishi wanaotakiwa kuajiriwa na watumiamaji, na hizi kamati, waajiriwe moja kwa moja na Wizara badala ya hizi kamati halafu zile fedha kidogo zinazopatikana zielekezwe kwenye ukarabati na ununuzi wa vifaa?

Mheshimiwa Spika, lakini swali lingine la pili. Serikali ilichimba visima virefu katika Kijiji cha Misinko na Kijiji cha Kitongoji cha Gairo katika Kijiji cha Sagara, lakini baada ya kukamilisha kuchimba visima vile maji yale yalionekana yana chumvi nyingi sana na hivyo hayafai kwa matumizi ya binadamu. Serikali iliahidi kuchukua sample ya yale maji na kuyapima ili yaweze kutumiwa na binadamu, jambo ambalo hadi sasa halijafanyika.

SPIKA: Sasa swali Mheshimiwa.

MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kuhakikisha kuja na mkakati mbadala wa kuwapatia maji safi na salama wananchi wa vijiji vile? Na hapa ningeomba Mheshimiwa Naibu Waziri angeambatana na mimi twende tukaonje yale maji yalivyo na chumvi na hayafai kabisa kwa matumizi ya binadamu.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Abeid Ramadhan, Mbunge wa Singida Kaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la Kamati za Watumiamaji, hili Mheshimiwa Waziri ameshakuwa akiongea mara nyingi na ameshawaagiza mameneja wote wa maeneo yote ya Mamlaka za Maji pamoja na RUWASA kuona kwamba, wanaajiri vijana wetu wanaotokana na chuo chetu cha maji pale Dar-Es-Salaam, hasa kwenye eneo la uhasibu. Hii ni kwa sababu, kumekuwa na ubadhirifu mkubwa sana katika hizi jumuiya.

Mheshimiwa Spika, na mfano mzuri uko pale kwenye Jimbo lake Pangani. Palikuwa hakuna mhasibu, waliweza kukusanya labda laki saba tu kwa mwezi, lakini baada ya kumuajiri binti ambaye ni mhasibu, msomi, mwenye profession hiyo sasa hivi wanaweza kukusanya takribani milioni nne na nusu. Hivyo, tunaendelea kutoa wito katika majimbo yote tuweze kushirikiana kuona kwamba, kamati zile tunaruhusu hawa vijana wanaajiriwa.

Mheshimiwa Spika, na kuhusiana na mishahara yao itoke Serikalini; kwa sasa hivi inakuwa ni ngumu, lakini kwa sababu wao wenyewe wanakusanya fedha za kutosha wana uwezo wa kujisimamia na kuweza kulipana hiyo mishahara. Pamoja na hilo, tayari Mheshimiwa Waziri ametupia jicho la ziada kuona nyakati zile za kiangazi namna gani ya kuweza kuzisaidia jumuiya hizi.

Mheshimiwa Spika, lakini katika suala la maji chumvi kuweza kupatikana baada ya kisima kuchimbwa:-

Mheshimiwa Spika, tayari pia wataalamu wetu wameelekezwa kwenda kusimamia na kuona namna bora ya kuona chumvi hii inaweza ikatibika. Na endapo itashindikana basi, chanzo mbadala cha maji kitaweza kufikiriwa na kutumika katika utoaji maji kwenye jamii.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali langu, je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Naibu Waziri ya kuvipatia huduma ya maji Vijiji vya Nkonekoli, Nkure, Njani, ambayo aliitoa wakati alipozuru jimboni kwetu mwezi Disemba kuelekea sikukuu za Christimas? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Pallangyo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ahadi ni deni, kwa sababu tumeahidi lazima tuje tutekeleze. Mara baada ya utaratibu mzima wa upatikanaji wa fedha kwenye eneo lako, lazima wataalamu waje na ni lazima maji yapatikane kwenye Jimbo lako la Arumeru, ahsante.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Namshukuru pia Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali na wananchi wa Jimbo la Geita Vijijini wamekusikia. Hata hivyo, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa majibu haya sasa ni mara ya pili napewa katika katika Bunge lako Tukufu, namuomba Mheshimiwa Waziri yupo tayari sasa baada tu ya Bunge hili kuambatana nami kwenda kuona mazingira halisi ya wananchi wangu wanavyokaa ili aweze kutekeleza mradi huu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mradi huu unaishia katika Kijiji cha Idoselo, Vijiji vya Mkorani, Ibisabageni, Dubanga, Isulobutundwe vijiji ambavyo wananchi wake wanachota maji umbali wa kilometa tisa, 10 mpaka 20. Je, Wizara haioni umuhimu wa kunipatia angalau visima wakati wao wakisubiri mradi huu wa maji uende mpaka kwao?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunilinda suala la kuambatana na Mheshimiwa Musukuma lakini mara baada ya kutoa kibali hicho nitakuwa mtiifu kwako nitakwenda kutimiza majukumu yangu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusiana na visima, nimtoe hofu Mheshimiwa Musukumu tutakuja kuangalia hali halisi, wataalam wetu tutawaagiza wafike pale. Tumetenga visima vingi sana ili maeneo yote ambayo ulazaji wa mabomba unakuwa ni mgumu basi huduma ya visima vya maji iweze kupatikana. (Makofi)
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na ninalo swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, uzoefu unaonyesha maeneo mengine duniani ikiwemo China kwa kutumia vyanzo vya kudumu imeweza kuiunganisha nchi yake kutoka kaskazini kwenda kusini kwa vyanzo vya maji. Tanzania tuna Ziwa Nyasa, Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika; ni lini Serikali itatumia vyanzo hivi muhimu kuiunganisha nchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Maziwa makuu ni moja ya mikakati ya Serikali kuweza kutumika na kuwa suluhisho la tatizo la maji katika nchi yetu. Hivyo, napenda kukuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Ziwa Tanganyika katika eneo lako litatumika kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi.
MHE. SELEMANI M. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Wakati tunasubiri mradi wa kuyatoa maji Ziwa Tanganyika kupeleka Mpanda Mjini, Serikali iliahidi kutupatia shilingi milioni 240 kwa ajili ya kukarabati vyanzo vya maji na kuhakikisha vijiji vile ambavyo vilitakiwa vipate maji, vinapatiwa maji:-

Je, Serikali inatupatia majibu yapi kupeleka hizo fedha shilingi milioni 240?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Wizara tuliahidi hizi fedha ziweze kwenda kusaidia kukarabati miundombinu muhimu ili vile vijiji viweze kupata huduma.

Mheshimiwa Mbunge hizi fedha mapema tunavyoanza mwaka wa fedha 2021/2022 zote zinatumwa katika Wilaya yako, lengo ni kuona kwamba ule mradi unakarabatiwa na wananchi wanapata maji safi na salama.
MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, yanayoleta matumaini kwa wananchi zaidi ya 80,000 katika vijiji 20 vya Jimbo la Bukene ambao sasa wanakwenda kupata majisafi na salama kutoka Ziwa Viktoria: Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari baada ya Bunge hili la bajeti tuongozane kwenda Bukene ili apeleke hizi taarifa njema na kuwaandaa wananchi kupokea mradi huu muhimu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nakushukuru sana kwa kupigilia msumari ruhusa ile ya Spika aliyoiongea jana.

Mheshimiwa Naibu Spika, basi napenda tu kukuhakikishia, kwenda kwenye majimbo yenu Waheshimiwa Wabunge ni moja ya majukumu yangu. Hivyo, baada ya Bunge hili Bukene nitafika, tutafanya kazi vizuri kwa pamoja, lengo ni kuona majisafi na salama yanapatikana bombani kwa wananchi wetu. (Makofi)
MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa fedha za ujenzi wa mradi wa maji ya Ziwa Viktoria kutoka Ziba, Nkinga zipo: Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza mradi huu wa kupeleka maji maeneo hayo?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mradi huu alioutaja wa maji kutoka Ziwa Victoria kuelekea maeneo yote ambayo ameyataja, tunatarajia kuutekeleza mwaka ujao wa fedha 2021/2022.
MHE. ALEXANDER P. MNYETI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Nasikitika sana kwamba majibu haya, ndiyo haya haya ambayo huwa yanatolewa kila mwaka. Unajua kinachouma ni kwamba, vyanzo vya maji vyote vikubwa unavyovijua vinavyopeleka maji Tabora, Nzega, Igunga, Kahama na Shinyanga vinatoka Misungwi, lakini wana-Misungwi hawapati fursa ya kupata miundombinu ya maji. Naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri: Ni lini Chuo cha Ukiriguru na Kituo cha Utafiti kitapata maji? Kwa sababu, majibu haya, ni haya haya ya miaka yote.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kufahamu hilo.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimejibu kwenye jibu langu la msingi, hiki nilichokijibu ndiyo mpango mkakati wa Wizara. Kama mnavyofahamu Wizara ya Maji tuko kwenye mpango mkubwa sana wa mageuzi. Hivyo, tuache kuangalia mambo yaliyopita, tuangalie ya sasa hivi na utekelezaji wetu sisi ambao tuko, nafikiri mnauona. Kwa hiyo, napenda tu kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, suala hili la maji katika hiki chuo mwaka ujao wa fedha kazi zinakuja kutekelezwa kadiri ya mipango ilivyo ndani ya Wizara.
MHE. JUMANNE A. SAGINI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu fasaha ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Lakini kama alivyosema mradi huu wa Mugango, Kiabakari, Butiama ndio kwanza wanaanza utekelezaji. Lakini, kwa kuwa Mji wa Musoma una maji mengi kiasi Wizara imewahi kutamka kwamba, wingi wa maji mpaka mabomba yanapasuka na umbali kutoka Musoma mpaka baadhi ya hizi Kata anazozitaja ni mfupi. Kwa nini Serikali isiamue kutoa maji Musoma Mjini na kuyafikisha vijiji vya Kata za Bukabwa, Nyankanga na Bwiregi, ikiwemo Ryamisanga, Kamugendi, Kitasakwa na Masurura? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, ni lini Serikali itaanza kutumia Mto Mara kama chanzo cha maji na kuyapeleka kwenye vijiji vya Kata za Nyamimange, Buswahili na Sirorisimba? Vikiwemo Wegero, Paranga, Kongoto, Buswahili, Nyambiri, Rwasereta na Kitaramanka. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo ameeleza Mji wa Musoma una maji mengi ni kweli na ni dhahiri wakati wote huduma ya usambazaji maji huwa ni rahisi, ila kupata chanzo cha maji ndio kazi. So, kwa sababu tayari maji Mji wa Musoma ni mengi, nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri tayari watendaji wetu wameweka katika mipango mikakati yao. Kadri tutakavyopata fedha, watahakikisha tunaendelea kutumia hiki chanzo tulichonacho, ili kunusuru yale mabomba yasiendelee kupasuka tutasogeza huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni matumizi ya Mto Mara. Naamini wakati wa usomaji wa bajeti hapa Mheshimiwa Waziri alijidadavua ya kutosha kwamba, maji yote ya mito mikuu huu ndio mpango wa kuona kwamba, Wizara inakwenda kuyatumia kwa vyanzo vya uhakika. Hivyo, Mto Mara pia, ni moja ya Mito ambayo kama Wizara, tunatarajia tuitumie kama chanzo cha uhakika. Hivyo, kulingana na namna tutukavyokuwa tunapata fedha, tutahakikisha mito na maziwa makuu yote tunakwenda kuyatumia kwa ufasaha. (Makofi)
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mradi wa Maji Kintinku - Lusilile, ulianza kutekelezwa toka mwaka 2013 na ulikadiriwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni tisa, na Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba endapo mradi huu ungekamilika ungeweza kuwanufaisha wananchi zaidi ya 55,000 wa vijiji 10 vikiwemo vya Mvumi, Lusilile, Ngwasa na Mwiboo.

Mheshimiwa Naibu Spika, toka nimeingia ndani ya Bunge hili nimekuwa nikiulizia mradi huu na kuupigia kelele; je, Serikali haioni kuna umuhimu wa kutenga fedha za kutosha ili mradi huu ukamilike na uweze kuwanufaisha wananchi wa Jimbo la Manyoni Mashariki?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi za walipa kodi, lakini ipo miradi ambayo imekamilika ya Mtama A na Mtama B; na miradi hii haitowi maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha miradi hii inatoa maji na wananchi wanapata huduma hii ya maji? Nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aysharose kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mradi ulianza mwaka huo alioutaja 2013 lakini jitihada nyingi zimeshafanyika baada ya RUWASA kuanzishwa na amini Mheshimiwa Aysharose kwa namna ya ufuatiliaji wako wa mara kwa mara na hata umeomba kuweza kwenda na mimi kule na nimeshakuahidi tutakwenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nikupe taarifa tu kwamba kwa kipindi hiki toka mwezi Mei mpaka dakika hii ninavyoongea huu mradi umeshakamilika zaidi ya asilimia 95, bado sehemu ndogo tu mradi huu unaenda kukamilika na ni fedha nyingi tayari zimeshaelekezwa huko na sehemu iliyobaki fedha pia itapelekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miradi ambayo imekamilika suala la Wizara ni kuona kwamba maji yanatoka mara baada ya miradi hii kukamilika. Hivyo, kwa miradi yote ambayo imeshakamilika nipende kuendelea kuwaagiza wataalamu wetu maeneo yote, miradi ambayo imekamilika wahakikishe wanaanza kupekeka maji katika vituo vya kuchotea maji ili wananchi waweze kunufaika na fedha ambazo Serikali imepeleka katika maeneo yote, hivyo na wewe katika eneo lako la Singida Mashariki pia maji yataanza kutoka katika maeneo yote miradi ilipikamika.
MHE. SEIF K. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuweka kumbukumbu vizuri naomba kurekebisha kidogo vijiji vya Ulaya, Nkinga na Barazani, kwamba viko Tarafa ya Manonga na si Tarafa ya Simbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza, kwasababu ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Makamu wa Rais na sasa ndiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni lini Serikali itapeleka maji ya Ziwa Victoria katika Tarafa ya Simbo hasa Makao Makuu ya Tarafa ya Simbo na Tarafa ya Manonga, hasa Makao Makuu ya Tarafa pale Choma cha Nkola kwa kuwa maeneo hayo yana idadi kubwa ya wananchi wanahitaji huduma hii ya maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Seif Gulamali kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti Tarafa hizi mbili, ya Simbo na Manonga zote zipo katika mpango mkakati wa kukamilisha utekelezaji wa kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria. Mwaka ujao wa fedha wa 2021/2022 kadiri tutakavyopata fedha tutafikia maeneo hayo yote muhimu. (Makofi)
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Kwanza napenda kuipa shukrani Serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jinsi inavyofanya kazi zake katika Wizara hii ya Maji, inatekeleza kwa hali na mali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sasa hivi ni mkazi wa Dodoma nakaa maeneo ya Mkalama. Eneo lile la Mkalama maji yapo mengi sana lakini mabomba yanakuwa yanapasuka sana maji yanatoka na hovyo. Mimi mwenyewe binafsi nakuwa nahisi huruma. Kwa hiyo nimwambie Mheshimiwa Waziri, kama Serikali imeliona suala hili kule sehemu ya Mkalama basi ifanye kazi zake kwenda kuyaziba yale mabomba ili maji yasitoke hovyo. Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza kutoka kwa Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipende kupokea pongezi kwa namna ambavyo ameridhishwa na utekelezaji wetu. Sasa kuhusiana na tatizo la maji kumwagika baada ya mabomba kupasuka maeneo ya Mkalama nipende kusema kwamba Meneja wa Maji Mkoa wa Dodoma Engineer Aron anafanya kazi usiku na mchana. Lengo ni kuona anakwenda kufanyia kazi mapungufu yote haya yanayoendelea kujitokeza. Siyo tu eneo la Mkalama hata wale wenzetu wanaotoka Ilazo taarifa za matatizo ya maji pale tunazo na tunazifanyia kazi. Tayari tumempa mtu kazi ya kuweza ku-supply mabomba.

Kwa hiyo mabomba haya yakifika, tunatarajia wiki hii yatafika, tunakuja kufanya ukarabati na marekebisho maeneo yote ambayo yana matatizo ya kupasuka na kumwaga maji mitaani.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu namba moja la nyongeza ningependa kufahamu, kwa kuwa katika Mikoa ya Kusini kumekuwa na vyanzo vingi vya maji vinavyotokana na mito mikubwa kama ule wa Rufiji, Ruvuma, Mavuji, Lukuledi, Luhuhu pamoja na Ketewaka kule Njombe. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inamaliza tatizo la maji kwa asilimia 100 kama ilivyofanyika Kanda ya Ziwa kupitia vyanzo hivi vya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Francis Ndulane kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji mzuri. Nipende tu kumjibu swali lake la nyongeza la matumizi ya maji yote yanayopatikana kwenye mito na vyanzo vyote vikubwa vyenye uhakika kwa miradi endelevu. Sisi kama Wizara, mikakati yetu katika mwaka ujao wa fedha na kuendelea, ni kujenga miradi mikubwa inayofanana na mradi huu wa Ziwa Viktoria. Mikakati imekamilika na kwa Kusini pia tumepanga kutumia Mto Ruvuma, Mto Rufiji na Ziwa Tanganyika. Hii yote tutakuja kuitekeleza kadri tutakavyokuwa tukipata fedha. (Makofi)
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Naomba kuuliza swali moja la nyongeza kwamba, katika Jimbo la Newala Vijijini, kuna Mradi wa Maji wa Mnima Miuyu, mradi huu ulikuwa ni wa miezi tisa, ulikuwa ni mwaka 2018 na hadi leo hii haujakamilika. Je, ni lini mradi huu utakamilika ili wananchi wa Jimbo la Newala Vijijini waweze kupata maji ya uhakika? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika ahsante. Naomba kujibu swali la Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi yote ambayo utekelezaji wake umeanza na ipo katika process, yote lazima itakamilika kadri fedha tunavyozipata na kadri ya muda ulivyopangwa. Hivyo nipende kumtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, namna ambavyo amekuwa akizungumza nasi mara kwa mara, tuendelee kuwasiliana kwa karibu na tutakwenda pia kuona kazi imefikia wapi na kazi itakamilika kadiri inavyotakiwa.
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. Lakini kabla ya maswali yangu niweke hii kumbukumbu kwa usahihi kabisa, kwamba kwanza nashukuru Serikali kwa kutupatia jamii ya Longido maji safi na salama kutoka Mto Simba ambayo mpaka sasa yamekuwa toshelevu katika Mji wa Longido ambako ni Makao Makuu ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru pia kwa sababu kazi inaendelea kuelekea Kimokouwa, Eworendeke na Namanga, na ni mradi ambao bado haujakamilika. Nashukuru pia kwa kuwa imefika Engikaret, lakini bado hayajafikiwa Kiserian na baadhi ya maeneo yaliyokusudiwa kama kitongoji cha Wasinyai na Yambaluwa Yambalua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza la nyongeza. Kwa kuwa mradi huu bado una hayo mapungufu ya kufikisha maji katika maeneo hayo;

Je, ni lini Serikali itakwenda kukamilisha huo mradi wa kufikia maji maeneo yote yaliyolengwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa wananchi waliopitiwa na bomba hilo kutoka kule chanzo chake, waliopo kitongoji cha Emotong, ni kitongoji kikubwa sana ile scheme nyingine inayokwenda mpaka Larang’wa na Kamwanga haipitiki huko kabisa;

Je, ni lini watu wa Emotong, Tingatinga, a Engerian ambao nao waliahidiwa kwamba watapata matawi ya haya maji na bado hawajayapata watapata hayo maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Steven Kiruswa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nami nipende kupokea shukrani zake kwa sababu amekiri kazi kubwa ambayo Wizara tumeendelea kufanya katika jimbo lake; na huo tu ni mwanzo wa mageuzi makubwa ambayo wizara inaendelea kuyafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukamilika kwa miradi hii tunatarajia kadri pesa tunavyoendelea kupata, na mwaka ujao wa fedha tutaendelea kuhakikisha hii miradi inakamilika. Hii ni kwa sababu lengo la Wizara ni kuona kwamba miradi inakamilika na wananchi wanapata maji safi na salama ya kutosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitongoji cha Tingatinga na maeneo hayo mengine vilevile wao pia wapo kwenye Mpango Mkakati wa Wizara kuona nao wao pia wanakwenda kunufaka na maji safi na salama. Hivyo nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge kama ulivyoona kazi imeweza kufanyika kwenye maeneo mengine na maeneo haya pia kazi itakuja kufanyika na maji bombani yatapatikana.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru na ninashukuru sana kwa majibu mazuri sana ya Serikali; na nishukuru juzi tu wakati wa Mbio za Mwenge tulizindua miradi ya Wezamtima na kutembelea miradi mingine ya maji kule Nchinila. Pamoja na haya ninashukuru sana kwa majibu haya ambayo wananchi wangu wa Kibaya pale, na nniafurahi kusema watakuwa wamesikia majibu haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Je, ni lini sasa Serikali itajenga Bwawa la Dongo ambalo lipo kwenye mpango wa Mwaka huu wa Fedha 2021/2022. Lakini wakati huo huo pale pale Dongo tuna Mlima Njoge unatiririsha maji; na kwa kuwa tanki ambalo limejengwa ni zamani sana, ni la mwaka 1965, na katika Vijiji vya Dongo na Chang’ombe wananchi wameongeza; ni nini kauli ya Serikali kuhusu kujenga tanki kubwa la maji; pengine la lita laki moja, laki mbili ili wananchi hawa waendelee kunufaika wakati wanasubiria bwawa hili la Dongo ambalo tunasuburia kwa hamu sana? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Edward Olelekaita, Mbunge wa Kiteto kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nipende kukushukuru kwa kukiri kazi kubwa ambayo imefanyika na hata Mwenge wetu wa uhuru umeweza kuzindua miradi ile. Lakini vilevile nipende kukujibu swali lako, kwamba ni lini bwawa la Dongo litafanyikwa kazi. Umeshajibu wewe mwenyewe kwamba mwaka ujao wa fedha tayari mpango mkakati umeuona uko pale hivyo tusubiri muda. Na kadri fedha itakavyokuja ndivyo kasi ya ujenzi wa lile bwawa itakuwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kuhusiana na hili bwawa lililojengwa miaka ya 1965 tunafahamu ongezeko la wananchi ni kubwa. Tayari tuna mikakati ya kuja kukarabati tanki hilo, lakini vile vile kuongeza matanki mengine kadri fedha tutakavyopata, na mwaka ujao wa fedha naamini tutakuja kufanya hizi zote. Lengo ni kuona wananchi wanapata maji safi na salama ya kutosheleza na wananchi wote wapate maji bombani.
MHE: ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili na mimi nipate kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naishukuru Serikali kwa kutupatia fedha kwa ajili ya maji ya Mji wa Liwale. Hata hivyo mpaka leo DDCA wametutia changa la macho, ni mwezi wa sita huu hawajaja; na Mheshimiwa Waziri ameniambia kwamba kuna uwezekano tukachukua watu binafsi wakaanza kuchimba pale. Lakini nimewasiliana na Mhandisi anasema asilimia 30 ya fedha hizo tayari DDCA walishachukua na walishaingia mitini.

Je, ni lini DDCA watakuja kutuchimbia maji Wilaya ya Liwale?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zuberi Kuchauka Mbunge wa Liwale kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Zuberi ni jana tu tumeongea na Mheshimiwa Waziri amekupa hayo maelekezo. Kwa hiyo nipende tu kuongezea pale alipoongea bosi wangu kama alivyokuhakikishia, pale DDCA wanapozidiwa kazi basi watu binafsi tutawapa vibali ili waweze kuja kuchimba hivi visima. Na visima hivi mwaka ujao wa fedha ninaamini vitachimbwa na mambo yatakaa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na fedha iliyochukuliwa na DDCA fedha ikichukuliwa maana yake ni lazima kazi ije ifanyike. Kwa hiyo kwa ile asilimia ambayo wamechukua lazima watakuja kufanya hiyo kazi.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi naomba kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Mji Mdogo wa Matui Wilaya ya Kiteto una wakazi wengi na unaendelea kukua kwa kasi.

Nini kauli ya Serikali juu ya upatikanaji wa uhakika wa maji safi na salama kwa wananchi wa Matui pamoja na viunga vyake?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asia Mbunge wa Viti Maalum vijana kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo haya ya Matui huko Kiteto nayyo ni miongoni mwa maeneo ambayo Wizara imetoa jicho la kipekee kabisa. Tunafahamu kuwa ni maeneo ambayo watu wameongezeka sana, hivyo mwaka ujao wa fedha kila eneo tutalitupia jicho, na kwa eneo hili la Matui pia tutalipa kipaumbele.
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza mradi wa kutoka Ileje Mto Songwe kuja Tunduma ulifanyiwa upembuzi yakinifu kutoka mwaka elfu 2013 na kampuni ya networkers kutoka Marekani. Mradi huu ulikuwa unagharimu kiasi cha Shilingi bilioni tatu. Sasa nataka kujua;

Je, ni lini mradi huu utakamilika ili wananchi wa Tunduma waweze kunufaika na maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwa kuwa wananchi wa Kata ya Mpemba na Kata ya Katete wamekuwa wakitegemea mradi wa maji kutoka katika Wilaya ya Mbozi maeneo ya Ukwile, lakini mradi huu umekuwa ukisumbua sana kutokana na miundombinu kuwa mibovu, miundombinu iliyopo ilitengenezwa kutoka mwaka 1971 sasa nataka kujua;

Je, ni lini Serikali itaweza kuboresha miundombinu hii ili wananchi wa Kata ya Katete na Kata ya Mpemba waweze kupata maji kwa ukamilifu kabisa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Stella Fiyao kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu wa maji kutoka Ileje kwenye Mto Bupigu ni mradi mkubwa. Kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi mwaka ujao wa fedha 2021/2022 mhandisi anatarajiwa kuja kwa ajili ya usanifu wa kina, na tunaratajia mwaka ujao wa fedha usanifu wa kina utakamilika. Kwa hiyo, kadri tutakavyokuwa tukipata fedha mradi huu utatekelezwa kwa haraka sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ni kutokana na maeneo ya Mpemba na Katete kupata maji kwa kusumbua sumbua. Binafsi nimeshafika pale kwenye mradi ule, nilikwenda nikiwa na Mbunge wa Jimbo na tulifanya kazi vizuri sana na niliacha maagizo ya kujitosheleza. Na yule meneja ambaye alikuwa pale ambaye kidogo alisuasua tulimbadilishia kazi, tulimwondoa pale na sasa hivi anakuja meneja mwingine mwenye maagizo kamili ili miradi hii yote iweze kutekelezwa kwa kina.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Licha ya kutengwa bajeti katika maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Kyerwa katika Kata ya Kikukuru haikutengwa hata Shilingi moja; kata hiyo ina vijiji vitatu ambavyo hakuna hata kijiji kimoja chenye maji na wananchi wanatembea umbali wa muda mrefu kutafuta maji.

Sasa nataka kujua ni mpango gani mahususi wa kusaidia hiyo kata ili waweze kujikwamua na wao kupata maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anatropia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata hizi alizozitaja katika Jimbo la Kerwa nazo pia zimepewa jicho la kipekee kabisa. Unaweza ukaona kwenye bajeti yetu huku haikupangiwa, lakini kipekee nipende kumshukuru Mheshimiwa Rais ambaye ameweka mkazo katika kuona miradi yote ya maji nchini itafanyiwa kazi. Kama mlivyomsikia, mama yetu ametuahidi kutuongezea fedha zaidi ili miradi yote iweze kutekelezwa. Hivyo nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge, mradi huu pia tutakuja kuutekeleza.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kunipa nafasi.

Naomba kufahamu, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji wa Ziwa Basutwa ambao utasambaza maji kwa vijiji tisa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hhayuma Mbunge wa Hanan’g kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi yote ambayo inapatikana kupitia maziwa makuu, mito na vyanzo vikubwa vya maji vyote vimepewa kipaumbele na Wizara. Na kama tulivyowahi kumsikia hapa ndani Mheshimiwa Waziri yeye mwenyewe ameshaji-commite kwa Serikali, kwamba lazima tutajitahidi kutatafuta fedha ili tuweze kuona maziwa makuu na vyanzo vikubwa vya maji vyote tunakwenda kuvitumia kadri fedha tutakakuwa tunazipata.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri. Kwa kuwa katika majibu yake ya msingi amesema kwamba mradi wa muda mrefu wa Shelui – Tinde utaweza kukidhi mahitaji ya wananchi wa Shinyanga: Je, ni lini sasa Mradi wa Shelui –Tinde utaanza kwa kuwa mkataba umeshasainiwa toka tarehe 25 mwezi wa Pili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa tunajua Sera ya Maji ni kuhakikisha kwamba inasambaza maji katika vijiji vyote ambavyo vinapitiwa na bomba kuu la Ziwa Victoria.

Je, ni lini Serikali itaanza kusambaza maji katika Kata za Lyabukande, Lyamidati, Nindo, Imesela na Didia?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mradi huu kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi tunatarajia kutoa maji Ziwa Victoria na Shelui – Tinde pia itakuwa ni moja ya wanufaika mwaka ujao wa fedha, kadiri fedha tunavyozipata.

Mheshimiwa Mwenyrkiti, napenda sana kumshukuru Mheshimiwa Rais, tumesikia jana wakati Bajeti ya Serikali Mheshimiwa Waziri akihitimisha pale, Mheshimiwa Rais ametuongezea fedha ambazo zitatusaidia kuongeza maeneo mengi katika nchi hii kuhakikisha maji ya uhakika yanakwenda kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile suala la usambazaji maji katika miradi yetu hii ni lazima ifanyike. Lengo ni kuona kwamba, wananchi wanapelekewa maji karibu na makazi yao na kupunguziwa umbali mrefu wa kutembea. (Makofi)
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali lini itakamilisha mradi wa maji wa visima vya Kimbiji na Mpera kuwasaidia wananchi wa Halmashauri ya Kigamboni waweze kupata maji safi na salama; na pia katika Kata za Tuangoma, Chamazi, Mbande, Mianzini, Kibondemaji na Charambe wote hawa waweze kunufaika na mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Visima hivi vya maji vya maeneo ya Kimbiji, Kigamboni na maeneo haya yote ya ukanda ule vinatarajiwa kuhakikishwa vinakamilika mwaka ujao wa fedha, kadiri fedha ambavyo tutakuwa tukiendelea kuzipokea ndani ya Wizara yetu. Maeneo ya Tuangoma, Majimatitu, kote huko Wizara inatupia jicho la kipekee kabisa. Tunafahamu ongezeko la wakazi ni kubwa, hivyo na sisi tutahakikisha tunafanya kazi usiku na mchana ili maji yaweze kuwafikia wananchi wa maeneo haya.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwenye Wilaya ya Kyerwa, Kata ya Bugomora, Kata ya Mlongo, Kata ya Kimuli na Kata ya Kyerwa Kagenyi, kuna miradi ambayo usanifu wake umekamilika, lakini mpaka sasa hivi Serikali bado haijatoa fedha ili miradi hii ianze. Lini Serikali itatoa fedha miradi hii ianze? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa hiyo compliment. Kwa swali la Mheshimiwa Mbunge kutoka Jimbo la Kyerwa, eneo hili pia Serikali tumeendelea kulipa jicho la kipekee. Wizara kupitia RUWASA na mamlaka pale Mji wa Kyerwa wataendelea kushirikiana kuhakikisha miradi hii yote ambayo haijakamilika iweze kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na Serikali ya Awamu ya Sita.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Changamoto ya maji katika Kata za Murongo, Kibale, Bugomora ambazo ni kata za mpakani mwa Mto Kagera zinaweza kumalizwa kama kukianzishwa mradi mkubwa wa maji kutoka Mto Kagera kuja kuhudumia wakazi. Je, ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha tunapata maji ya kutosha kutoka Mto Kagera kuhudumia hizi kata ambazo ziko pembezoni mwa huo mto? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anatropia, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kumpongeza Mheshimiwa Anatropia, hakika akina mama tunasemeana vema. Tunafahmu mwanamama ndiye anayepata shida ya kubeba maji kichwani na sisi kama Wizara tumesema lazima tumtue mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maji kutoka Mto Kagera sisi kama Wizara ni moja ya vipaumbele vyetu kutumia mito na maziwa makuu kuhakikisha maji yanapatikana. Kama nilivyomjibu Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo, Mheshimiwa Anatropia tutakuja pamoja na Mheshimiwa wa Jimbo tutaweka mambo sawa, Kyerwa maji yatapatikana. (Makofi)
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali nimeyaona lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria ulioanza mwaka 2005 ukamalizika mwaka 2018, ambao ulikuwa unatoa maji Ziwa Victoria kuleta Bunda Mjini, na kwa kuwa mradi huo ulikuwa umejumuisha vijiji 30 ambavyo leo tunaviuliza hapa, na kwa kuwa bajeti ya mwaka 2020/2022 imeonyesha kwamba Jimbo la Bunda Vijijini litapewa maji ya Ziwa Victoria kutokea Bunda Mjini. Swali la msingi hapa ni lini sasa Waziri wa Maji ataenda Jimbo la Bunda Vijijini kutangaza mradi huu ambao ameugusia kwenye bajeti ya 2021/2022? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Serikali imetumia milioni 40 kufanya utafiti wa vijiji sita ambavyo vina uhaba wa maji kwenye maeneo hayo na maeneo hayo ni Mihingo, Tingirima, Rakana, Jaburundu, Salama A, Kambubu. Serikali imetumia milioni 40 kutengeneza tathmini ya mkakati wa kuchimba na makinga maji kama malambo ya maji hayo. Ni lini sasa itaenda kukamilisha mradi huo ambao uko hapo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Getere kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Getere kwa ufuatiliaji wa karibu sana na kwa namna ambavyo tumeendelea kushirikiana naye. Nipende kumuambia tu Mheshimiwa Getere kwamba, suala hili la Bunda kuweza kutumia maji ya Ziwa Victoria ni suala ambalo ni la kimkakati Kiwizara na tunafahamu maji yameshafika pale Bunda Mjini na kwa eneo lake la Bunda Vijijini, Serikali ipo katika mkakati wa kuona kwamba mipango yetu ya muda mrefu inakwenda kufanikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, na baada ya Bunge hili Wizara itatuma wataalamu pale kwenda kuangalia uwezekano wa kutumia yale maji yaliyofika Bunda Mjini na ikishindikana, basi watafanya review mpya kabisa kuona kwamba sasa maji kutoka Ziwa Victoria yanafika Bunda Vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulingana na swali lake la pili la kuhusiana na malambo sita ni kweli, Serikali tulipeleka milioni 40 na malambo yale tutakwenda kuyajenga awamu kwa awamu. Tayari lambo la kwanza lipo kwenye utekelezaji asilimia 40 lakini shughuli za ukamilishaji wa lambo hili, utaendelea baada ya mgao ujao wizara kupeleka fedha na kuhakikisha malambo yote sita kila tunavyopata fedha tutapeleka ili yaweze kukamilika. (Makofi)
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Mradi wa maji Bunda Mjini ulikuwa wa thamani ya shilingi 10,600,000,000 fedha zilizokwisha kutolewa mpaka sasa ni shilingi 2,600,000,000 bado shilingi bilioni nane. Je, ni lini Serikali itamalizia fedha hizi ili mradi ule uweze kukamilika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maboto kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mradi ule umeweza kupelekewa fedha hizi shilingi bilioni 2.6 na bado hizo shilingi bilioni 8 na fedha hizi tayari zipo kwenye mpango wa Wizara kuona kwamba tunaendelea kupeleka fedha. Ili kuweza kukamilisha mradi ule na tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameendelea kuifanikisha Wizara ya Maji, kwa kuongeza fedha tofauti na namna ambavyo tulipitisha kwenye bajeti yetu. Hivyo, mradi kama huu na wenyewe pia tunaupa jicho la kipekee kabisa kuhakikisha kwamba unakwenda kukamilika. (Makofi)
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nina penda kushukuru sana kwa majibu mazuri ya Waziri. Lakini nina maswali mawili tu ya nyongeza. Katika Mkoa wa Simiyu kuna Wilaya tano lakini Wilaya ya Meatu ndio ina ukame sana kuliko Wilaya zote hizo tano. Nilipenda kujua ni lini sasa Serikali itachimba visima virefu vya maji na kusambaza katika vijiji hivyo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Naibu Waziri yuko tayari kuambatana pamoja nami twende naye katika Wilaya ya Meatu aone wakina mama wanavyopata adha ya maji katika Wilaya ya Meatu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Minza Mjika kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nipende kupokea pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge. Lakini vile vile nipende kumpongeza na yeye, kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ushirikiano mkubwa ndani ya Wizara ya Maji. Amekuwa mfuatiliaji mzuri sana akisaidiana na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo kaka yangu Simon wanafanya kazi nzuri kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali katika mwaka huu wa fedha 2021/2022 ni kuchimba visima virefu katika Wilaya ya Meatu. Tunatambua namna gani wakinamama wanapata shida ya maji katika Mji ule. Hivyo, tumshukuru Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, ameliona hili na ameshatupatia fedha tutaenda sasa kifua mbele kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kuambatana kwangu ni kawaida. Hivyo, niseme Mheshimiwa Minza usiwe na wasiwasi baada ya Bunge hili, baada ya kumaliza ratiba ya Mikoa niliyoipanga nitakuja kwako Simiyu hususani Meatu. Lengo ni kuona hali halisi na kuongeza chachu na ufanisi wa miradi yetu ya maji. (Makofi)
MHE. JUMANNE A. SAGINI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri kuhusu maji Busega. Lakini tatizo la maji Busega linakaribia kufanana na tatizo la maji Butiama. Huu ni mwezi wa tano kwenye Kijiji cha Butiama cha Baba wa Taifa hawajapata maji na wataalam wanasema ni tatizo la mashine. Sasa Naibu Waziri atuambie lini wananchi wa Butiama wataweza kupata maji kutoka Ziwa Victoria? Na ambapo tayari kuna bomba lililochakaa lakini tatizo ni mtambo unashindwa kusukuma. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sagini, Mbunge wa Butiama kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara tunatambua eneo lile miradi ni mchakavu lakini tayari tumeshaelekeza wataalamu wetu kuweza kuipitia na ukarabati kufanyika, pamoja na mradi wa muda mrefu mradi wa Ziwa Victoria nao upo katika mipango mkakati ya Wizara.
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, Jimbo la Tabora Kaskazini vijiji 58 vitapata maji ya Ziwa Victoria. Swali, Je, Serikali ina mpango gani kuchimba visima virefu katika maeneo ambayo bomba la Ziwa Victoria halipiti?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maige Mbunge wa Tabora kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu fika mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria umeweza kufika katika Mkoa wa Tabora. Lakini kwa maeneo ambayo mradi huu hauwezi kufika kwa sababu, bomba kuu linapopita ni kilomita 12 kulia na kushoto wanaweza kunufaika moja kwa moja.

Maeneo ambayo yako ndani zaidi mpango wa Serikali ni kuchimba hivi visima virefu na tayari Serikali imeviandaa visima zaidi ya 500 kwa ajili ya nchi nzima. Hivyo niweze kumtoa hofu Mheshimiwa Maige na yeye ataweza kuingia katika mgao wa visima hivi. Lengo ni kuona kwamba wananchi wenye imani kubwa kwa Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wanaweza kuhudumiwa na kutuliwa ndoo kichwani. (Makofi)
MHE. JOHN M. SALLU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini naomba Serikali ituhakikishie kwamba, katika kipindi hicho cha miezi tisa kweli huu mradi unaweza kumalizika maana tuna shida kubwa sana ya maji pale. Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kitandula kwa kuwasilishwa na Mheshimiwa John Sallu kwamba, Serikali tumejipanga ndani ya miezi tisa mradi utakamilika na tunaendelea kuongeza nguvu kuhakikisha ikiwezekana kabla ya miezi (9) kufika iwe imekamilika.
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali. Pamoja na majibu mazuri ya wananchi wa vijiji hivi ambavyo vimetajwa, nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza: Pamoja na Naibu Waziri kutamka hapa kwamba vijiji hivi vitapata maji mwakani na kingine cha Ikelu kina asilimia 98: Tatizo ambalo lipo aniambie hapa, Wakandarasi hawa wamesimama, hawaendelei kwa sababu hawajalipwa fedha; ni lini watalipwa fedha ili waweze kukamilisha miradi hii? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili: nazungumza kwa uchungu, Pamoja na kwamba Wizara ya Maji wanafanya kazi nzuri sana na Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu wa Awamu ya Sita, kazi yake ni nzuri sana. Kuna jambo ambalo nataka nizungumzie hapa unisaidie katika miji 28 ambayo ilikuwa ipate maji kupitia fedha za mkopo nafuu kutoka India, limezungumzwa kwa muda mrefu, mojawapo ni Makambako nayo ipo kwenye miradi hiyo… (Makofi)

SPIKA: Sasa swali Mheshimiwa.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, sasa swali. Katika Mji wa Makambako ambao unategemea mradi huu mkubwa, una Kata tisa. Unapitiwa na Kata tisa. Wananchi hawa tumekuwa tukiwaambia kwa muda mrefu: Ni lini Mkandarasi atakwenda kuanza kutengeneza mradi huu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deo Kasenyenda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, naomba kusema Wakandarasi tayari malipo yanaendelea na malipo tunalipa kwa awamu kadri ambavyo tunapata fedha. Ninaamini hata Wakandarasi wa Makambako nao kwa mgao wa mwezi huu wa Kumi ambao tunaugawa mwezi huu wa Kumi na Moja, nao wataingizwa katika malipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na miji 28, napenda kumshukuru Mheshimiwa Waziri wetu Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso, amefatilia kwa karibu sana suala hili na tayari wakandarasi wapo; na wenzetu kutoka Benki ya Exim kutoka India wamefika Tanzania, hapa Dodoma juzi na jana pia tulikuwa na kikao nao. Hivi ninavyoongea kikao kinaendelea ndiyo maana Mheshimiwa Waziri hapa hayupo. Kwa hiyo, niseme tupo mwishoni kabisa kuona kwamba story za suala hili la miji 28 sasa linafikia ukingoni. Tumshukuru sana Mheshimiwa Rais ameweza kusimamia kwa karibu suala hili mpaka linaelekea ukingoni. Ahsante. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi, nami niulize maswali mawili ya nyongeza. Kabla sijauliza, tunafungwa sana na Sheria ya Takwimu, lakini naomba Bunge lako Tukufu, sheria hii isiwe ni kichaka cha kutoa takwimu za uongo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Naibu Waziri anasema upatikanaji wa maji ni asilimia 52, wakati nafika hapa Meneja ananijibu ni asilimia 27. Sijui nani mkweli kati ya hizo taarifa? Nakosa maneno ya kusema kwa sababu ya Sheria ya Takwimu kwa sababu mtaniambia nimefanya research kupitia nini?

Mheshimiwa Spika, na mimi naomba kusema kwa sababu kwa miradi hiyo…

SPIKA: Hapa Bungeni unaruhusiwa, wewe sema tu, mradi usidanganye tu.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, Wana- Nkasi wanasikia, akisema asilimia 52, wakati Kata zenye uhakika wa kupata maji hazizidi mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa kuna miradi miwili ambayo ni miradi kichefukichefu; Mradi wa Isale na Mradi wa Namanyere ambao una zaidi wa miaka mitatu; na miradi hiyo hata ikikamilika haiwezi kabisa kutatua changamoto ya maji Jimbo la Nkasi Kaskazini: Serikali haioni sasa kuna haja ya kuchukua Maji Ziwa Tanganyika ambayo ni kilometa 64 tu kuweza kumaliza changamoto ya maji? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili: Kwa kuwa Serikali imepata huo mkopo ambao imegawa kwenye Wizara za Kisekta ikiwepo Wizara ya Maji, napenda kujua, Jimbo la Nkasi Kaskazini tunapata kiasi gani ili angalau ikapunguze makali ya changamoto za maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aida Joseph Khenani kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kumpongeza Dada yangu, Mheshimiwa Aida, kwa ufuatiliaji wa suala hili la miradi hii ya maji na nipende kukuhakikishia Mheshimiwa Aida kwamba miradi hii ambayo umeiita kichefuchefu tayari Wizara tumeipa nguvu na tutaisimamia kwa karibu sana kuona kwamba inakamilika. Kwa sababu lengo la Mheshimiwa Rais ni kumtua ndoo Mama kichwani nasi kama Wizara ya Maji ni wanufaika wakubwa wa fedha kutoka Serikali Kuu, hivyo, nikutoe hofu, nikuhakikishie tutasimamia na miradi hii itakamilika kama ambavyo miradi mingine mingi zaidi ya 200 ilivyoweza kukamilika.

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu kuhusu fedha za Covid. Katika Jimbo la Nkasi Kaskazini pia wamekuwa wanufaika wa hizi fedha ambazo Mheshimiwa Rais ameweza kuzipigania. Tumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, kwa sababu wananchi wa Nkasi Kaskazini na wao wametengewa milioni 500 kwa lengo la kufanya mradi wa Mpata.

Mheshimiwa Spika, lengo la hizi fedha ni kufanya mradi utakaokamilika ndani ya miezi sita, miezi tisa, uweze kutoa maji na wananchi wanufaike. Hivyo, tumeweza kuweka mradi mfupi ambao ndani ya shilingi milioni 500 utakamilika na wananchi watanufaika moja kwa moja. Kwa miradi hiyo ya Namanyere tayari ipo ina bajeti, kama Namanyere ina bilioni 1.5. Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge nitaendelea kukupa ushirikiano kama ambavyo tumekuwa tukiwasiliana. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, nashukuru.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani sasa hivi tunavyozungumza ambayo inahudumiwa na mitambo ya Ruvu Chini, nazungumzia Bagamoyo, nakuja Jimbo langu la Kawe pale, nakwenda Kinondoni, Temeke, kuna uhaba mkubwa sana wa maji.

Mheshimiwa Spika, Serikali inasema kwa sababu kuna upungufu wa maji, yaani kina cha maji kimepungua. Sasa ninataka Serikali iniambie, kwa sababu kupungua kwa maji kwa vyovyote vile kuna uhusiano na mabadiliko ya tabianchi, dunia nzima sasa hivi inazungumzia climate change. Leo nimemsikiliza Rais anasema anataka Serikali mtenge fedha za climate change.

Mheshimiwa Spika, nataka nipate majibu sahihi ili tatizo hili lisiwe la kudumu, kuna mkakati gani wa muda mfupi na muda mrefu kuweza kukabiliana na upungufu huu wa maji ili wananchi wa maeneo husika waepukane na kero hii? Hasa kwa kuzingatia miradi husika tumejenga kwa fedha za mikopo za mabilioni ya shilingi ambayo Taifa linalipa sasa hivi. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Halima Mdee kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli mitambo yetu ya Ruvu Chini hapa katikati ilipata hitilafu ya kupata maji kwa upungufu lakini kama Wizara tuna mabonde tisa ambayo yanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa sana kuona kwamba tunadhibiti tatizo hili. Tatizo hili ni kwamba matumizi ya shughuli za kibinadamu kwa sehemu kubwa ndiyo yameathiri.

Mheshimiwa Spika, huwa tunatoa vibali kwa wenzetu kufanya umwagiliaji maeneo karibu na vyanzo vyetu vya maji lakini vina muda. Muda ambao unapaswa kutumika ni muda ule wenye high season, maji yanakuwa mengi na muda huu wa kiangazi vile vibali huwa vina-expire. Sasa wale wamwagiliaji wamekuwa wakiendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo sasa hivi kama Wizara tayari tumeweka task force kuhakikisha hakuna atakayetumia maji yale kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji na shughuIi nyingine yoyote isipokuwa kuelekeza maji katika mitambo yetu kwa ajili ya kuchakata kwenda kwenye matumizi ya kibinadamu.

Mheshimiwa Spika, mkakati mwingine wa Wizara yetu ni kuona tutaendelea kutoa elimu ya kutosha, matumizi sahihi ya maji katika maeneo yote yenye mito tiririka ili vyanzo vyetu vya maji visiweze kuathirika kama ulivyosema. Tayari tumeshatumia fedha nyingi kujenga miundombinu ambayo Serikali inatarajia wananchi waweze kupata maji ya kutosha, safi na salama wakati wote. (Makofi)
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Licha ya majibu mazuri ya Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza: -

Mheshimiwa Spika, naamini kuwa Wizara ya Maji inafanya kazi sana kwa jitihada zao, licha ya jitihada hizo, lakini bado watu wanataka maji. Kata ya Ruaha ambayo iko kwenye Jimbo hilohilo la Mikumi, Wilaya ya Kilosa waliahidiwa na Mheshimiwa Rais Awamu ya Tano kupatiwa maji. Kwa hiyo, nauliza ni lini watapatiwa maji? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Kata ya Lukobe ambayo iko Manispaa ya Morogoro tulitembelea kamati yangu na wananchi wakaahidiwa kuwa watapariwa maji kuanzia mwezi wa nane hilo tanki la mguru wa ndege, lakini mpaka sasa hivi ninavyoongea tanki hilo halijawahi kupata maji na sasa ni mwezi wa 11 na ahadi ilikuwa mwezi wa nane, wananchi wanakunywa maji ya visima ambayo ni maji yasiyo Safi na salama. Na wamenituma wanauliza ni lini watapatiwa hayo maji kupitia kwenye tanki hilo la Mguu wa Ndege? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, kipekee nipende kumshukuru Mheshimiwa Mama yangu Dkt.Christine Ishengoma kwa namna ambavyo anaendelea kufuatilia suala hili la maji katika maeneo ya Mkoa wa Morogoro na nikushukuru sana Mheshimiwa Christine Ishengoma kwa ushirikiano ambao umeendelea kutupa sisi Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Spika, kwa swali la kwanza Kata ya Ruaha; tayari RUWASA wameshafanya taratibu zote na sasa hivi wametangaza ili tuweze kumpata mkandarasi. Na tunaamini kwa kasi ambayo tunaenda nayo watu wa Ruaha nao watakwenda kunufaika muda si mrefu.

Mheshimiwa Spika, kwa eneo hili la mguru wa ndege wakati wa ziara na mimi nilikuwepo. Mheshimiwa Dkt. Christine kama ambavyo tumekuwa tukiwasiliana kwenye suala hili, lile tanki hata ukipita pale barabarani unaliona kubwa, zuri, lenye ubora kabisa limeshakamilika na sasa hivi tunaingia kwenye awamu sasa ya usambazaji na tayari Wizara tunapeleka fedha kwenye mgawo huu unaokuja kwa lengo la kuona sasa maji yanakwenda kuwafikia wananchi wote wa eneo la Lukobe. Ahsante.
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa sera yetu sasa itachukua muda kuihuisha mpaka mwaka 2022; na kwa kuwa mpaka sasa kuna miradi mingi sana ya maji inaendelea na kwa kuwa pamoja na Sera hii kuna uhitaji wa maji wa kila mwananchi anahitaji kiasi gani kwa siku. Je, miradi inayofuata kwa sasa, Serikali imejipangaje kuhakikisha inakuwa endelevu?

Mheshimiwa Spika, la pili, mradi mmojawapo ambao umeathirika sana kwa Wilaya ya Kyela na hii Sera ya Maji ya watu 250 kuchota kwenye kituo kimoja ni Mradi wa Ngana group. Serikali imejipangaje sasa kuhakikisha mradi huu unafufuliwa na unakuwa katika viwango vya sasa ili kukidhi matarajio ya wana Kyela? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Ally Mlaghila, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa miradi ambayo inaendelea sasa hivi ni miradi endelevu na tayari tunajitahidi kuhakikisha kuona kwamba tunapata vifaa vya kufanya uchunguzi kabla ya kuingia kwenye miradi na tumshukuru kabisa kwa kipekee Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan, kwa kupitia fedha ambazo tumepewa tayari tumeagiza mitambo saba kwa ajili ya kuchunguza maeneo ambayo yatatuletea vyanzo endelevu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa Mradi wa Ngana Group tayari umeshafufuliwa, wiki hii fedha zaidi ya shilingi milioni 500 tunaelekeza huko, ili kuona kwamba shughuli za awali zinaanza kutekelezwa. (Makofi)
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, bado Mji wa Namtumbo una uhaba mkubwa wa maji na kwa kuwa kuna fedha hizi za UVIKO zinazohusiana na sekta ya maji, Serikali inaweza ikaelekeza fedha hizo RUWASA wakazielekeza katika ukarabati wa chanzo cha maji kinacholeta maji Namtumbo na kutandaza bomba la maji jipya? Kwa sababu, chanzo hicho ni cha toka mwaka 1980 ili kutatua tatizo la maji ya pale Namtumbo Mjini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa pia tuna miradi ya maji ya Luhimbalilo na Ikesi na maji ya Kumbala, Litola, miradi hii imekuwa kizungumkuti bado hatujui itaisha lini. Je, Serikali mnaweza mkaja mkatusaidia kuona nini kinachokwamisha ucheleweshaji wa miradi hii miwili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani yaliyoulizwa na Mheshimiwa Vita Kawawa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, fedha za UVIKO kutumika kwenye kuboresha chanzo cha maji. Hizi fedha za UVIKO sisi kama Wizara tumeelekeza kwenye miradi ambayo itakwenda kukamilika na kuleta huduma mara moja kwa jamii. Tunataka miradi ambayo inaleta majawabu kwa haraka hivyo, namna ambavyo Mkoa umeelekeza ile fedha ni sahihi. Kuhusiana na kazi hii ya kukifanyia hiki chanzo cha maji kinachotegemewa pale Namtumbo, tutatumia fedha za Mfuko wa Maji kuhakikisha kwamba tunakuja tunahakikisha chanzo kinatumika kikamilifu kwani vyanzo ni vichache. Hivyo, tunapopata vyanzo kama hiki tutakitumia kikamilifu ili kuleta tija kwenye jamii yote ya Namtumbo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Vijiji vya Ikesi pamoja na hivyo vingine, Serikali inatoa jicho la kipekee kabisa kuona kwamba maeneo haya ambayo kwa muda mrefu yamepata shida ya maji, tunakuja kuleta ufumbuzi na maji bombani yatapatikana kwa wananchi. (Makofi)
MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Jimbo la Songwe ni pana ni kubwa na lina vijiji viko very scattered na kutoka kijiji kwenda kijiji baadhi ya vijiji kuna Mito kama Maleza au Rukwa na Some. Sasa, tuko Novemba sasa na tayari watu wa RUWASA wanatuambia tumeshapata fedha kwa ajili ya kupeleka maji kwenye vijiji hivyo. Lakini mpaka sasa hatujaona wakandarasi kuanza kazi sehemu hizo na sehemu nyingi Tanzania nzima watu wa RUWASA wanasema wanafanya manunuzi lakini wanachelewa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali naomba ituambie ni lini hasa Wakandarasi wataanza kumwagika kwenye Wilaya zetu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji? Ukizingatia tunaenda kwenye wakati wa mvua? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza kutoka kwa Mheshimiwa Phillipo Mulugo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Maji na Usambazaji wa Maji Vijijini RUWASA ni kweli palikuwa na changamoto katika eneo la ununuzi lakini tayari Mheshimiwa Waziri amewaagiza na wamejipanga. Kipekee nimpongeze Engineer Kivigalo anafanya kazi nzuri ambaye ni DG wa RUWASA. Usimamizi wa kufanya manunuzi yaende kwa wakati sasa hivi utakuwa umeshaboreshwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lini tunakuja tayari tupo kazini sisi Wizara ya Maji, katika eneo lako huenda ndiyo limechelewa tu kupata wakandarasi lakini maeneo mengi kazi zinaendelea. Hivyo, nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa tuonane tuone tunaweka sawa mambo kazi zikaanze mara moja. (Makofi)
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi na mimi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Jiji la Dodoma takribani sasa ni miezi mitatu mfululizo kumekuwa na mgao wa maji usiokuwa na taarifa. Leo mitaa mbalimbali kwenye Kata ya Ipagala, Kata ya Dodoma Makulu, lakini Kata ya Nzuguni wana siku ya tano hakuna maji.

Nataka kupata kauli ya Serikali ina mkakati gani madhubuti wa dharura wa kuondoa changamoto hii kubwa inayowakumba wakazi wa Dodoma, lakini na wageni mbalimbali wanaoingia kwenye Jiji letu hili kufanya shughuli zao mbalimbali? Kwa sababu, imekuwa ni kero kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kunti, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Jiji la Dodoma tumepitia kidogo changamoto katika mitambo yetu ya Mzakwe na pale Mailimbili. Tatizo kubwa ilikuwa ni umeme na tumewasiliana kwa karibu sana Mheshimiwa Waziri Aweso, pamoja na Mheshimiwa Makamba. Wamefanyia kazi hili suala kwa pamoja kuona kwamba lane ile ya umeme inayofanya uwezeshaji pale kwenye vile vyanzo usiwe disturbed. Kwa sababu, imekuwa disturbed huko mbele kulingana na ugawaji huu wa umeme wa REA, lakini sasa hivi wanaendelea kufanya maboresho ili kuona kwamba umeme usikatike kwenye vyanzo vyetu.

Mheshimiwa Spika, kwa dharura sana pale inapobidi sana Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira hapa Dodoma anajitahidi kuona kwamba maboza yanazunguka huko kutoa huduma pale inapobidi sana, lakini tayari maji yanarejea katika mfumo wake baada ya umeme kidogo kuwa unapatikana.

SPIKA: Labda Mheshimiwa Waziri kwa kuunganisha tu. Kwa kuwa ufumbuzi wa uhakika ni maji haya kutoka Ziwa Victoria, nini kinaendelea hivi sasa kutoka Ziwa Victoria kuja Mji wa Dodoma? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuja hapa Dodoma ni katika miradi yetu mikubwa ambayo tunategemea fedha kutoka nje. Wiki iliyoisha siku ya Ijumaa Wizara (wataalam) waliweza kuketi na World Bank kuendelea kufanya mazungumzo kuona huu mradi sasa unaingia kwenye utekelezaji.
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, kwanza nashukuru sana kwa majibu ya Serikali. Naomba nitumie nafasi hii kuishukuru sana Serikali kwa kutenga shilingi bilioni
1.3 kwa ajili ya mradi huu ambao ni wa muda mrefu. Naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza: -

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa katika awamu ya kwanza inahusu vijiji vitano; na kwa kuwa maji haya yanatoka katika Kijiji cha Lukululu ambao ndio wanalinda hata vyanzo vya maji, lakini hawapo katika awamu ya kwanza; na kwa kuwa maji yanapotoka Kijiji cha Lukululu yanakuja Mlangali yanakwenda Shaji na Mahenje, lakini Kijiji cha Shaji ambacho kiko katikati hakiko katika mpango huu wa kwanza: -

Je, atakuwa tayari kubadilisha huu mpango ili hivi vijiji viwili, cha Lukululu ambako maji yanatoka na kile cha Shaji viwepo katika awamu ya kwanza? Hilo ni swali la kwanza.

Swali la pili: Kwa kuwa Mbewe umeitaja na imeandikwa kwenye maeneo mawili; kwenye mpango awamu ya kwanza na awamu ya pili; sasa kuna kijiji ambacho kimesahaulika kilitakiwa kiingie katika vile vijiji kumi vya awamu ya pili, ambacho ni Ihoa: -

Je, Serikali itakuwa tayari sasa kukiingiza hicho kijiji ili nacho kiwemo katika orodha ya vijiji vitakavyopata maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hasunga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa Vijiji hivi vya Lukululu na Shaji sifa yake tu namna ambavyo ipo inafaa kuingia kwenye awamu ya kwanza, hivyo hatutakariri namna ambavyo tuliweka. Kwanza, Sera ya Maji inatutaka kijiji kile ambacho chanzo kipo kiwe mnufaika namba moja, hivyo tutazingatia hilo kama Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na maji kufika Ihoa, hii nayo nimeipokea. Kwa kuwa nia njema, dhamira safi ya Mheshimiwa Rais ni kuona kwamba maeneo yote yanafikiwa na huduma ya maji safi na salama, tutafikisha maji Ihoa pia. (Makofi)
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa utekelezaji wa miradi ya maji umekuwa ukitumia wakandarasi; na kwa kuwa wakandarasi hawa wanachukua muda mrefu sana kukamilisha miradi hii ya maji; na kwa kuwa yuko mkandarasi alipewa mradi aumalize ndani ya mwaka mmoja na sasa ni mwaka wa sita unakwenda wa saba hajakamilisha mradi huo; na kwa kuwa mimi nia yangu ni kuhakikisha miradi yote ya maji niliyoshiriki kupitisha fedha Bungeni hapa inakamilika ndani ya kipindi cha miaka mitano. Je, Serikali inaweza kuturuhusu kutumia force account kutekeleza Mradi huu wa Maji wa Ngara Mjini na miradi mingine ili miradi hii ikamilike kwa wakati, tena ndani ya kipindi cha miaka mitano? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Ndaisaba Ruhoro, amekuwa ni mfuatiliaji na yeye mwenyewe amekuwa akienda mbele zaidi katika shughuli hizi za miradi ya maji. Hata nilipomtembelea pale jimboni, alionesha jitihada kubwa sana ya kuona kwamba miradi inakamilika.

Mheshimiwa Spika, kutumia force account ni moja ya namna ambavyo tunatekeleza miradi yetu sisi Wizara ya Maji. Hivyo, katika miradi hii ambayo imechukua muda mrefu, tayari miradi zaidi ya 100 tumeweza kuruhusu force account na imekamilika. Hivyo na huu nao tunaupokea, tutahakikisha wenzetu waliopo pale Ngara na wao wanafanya jitihada ya kuona mradi unakamilika. Ahsante.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza nipongeze Wizara ya Maji kwa juhudi zinazoendelea za kuwapatia wananchi wa Jimbo la Kyerwa maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kyerwa tunao Mradi wa Vijiji 57, lakini mradi huu tumekubaliana utajengwa kwa awamu. Hata hivyo, zipo Kata kama Businde, Songa Mbele, Kikukuru, Kitochenkula; kata hizi haziko kwenye awamu hii ya kwanza. Je, Serikali iko tayari angalau hata kuchimba visima ili hawa wananchi ambao wanapata wakati mgumu waweze kupatiwa maji safi na salama wakati wanasubiria mradi mkubwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Innocent Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna mradi mzuri sana pale kwenye Jimbo la Kyerwa na Mheshimiwa Innocent amekuwa bega kwa bega na Wizara. Tumekuwa tukishirikiana naye sana Mheshimiwa Mbunge. Kwa visima kuchimbwa kwa dharura wakati miradi mikubwa ikiendelea na utekelezaji, hii ni moja ya jitihada za Wizara na tumetenga zaidi ya visima 500 kuona kwamba tunavichimba katika maeneo ambayo miradi yake inachukua muda mrefu. Hivyo, kwa kata hizi ambazo ziko pembezoni kwenye Jimbo la Kyerwa nalo tutalifikiria kuona visima vinachimbwa.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Jimbo la Momba lina vijiji 72 na vitongoji 302. Katika vijiji hivyo, vijiji ambavyo vinapata majisafi na salama ambayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu haviwezi kuzidi 20; isipokuwa tunatumia mbadala wa maji ambayo yametuama kwenye madimbwi na kwenye mito midogo midogo ambapo tunakunywa pamoja na ng’ombe, punda, mbuzi na wanyama wote: -

Je, ni lini Serikali itaona katika vijiji vilivyobaki, watusaidie kutuchimbia visima vya dharura wakati tunaendelea kusubiri miradi mikubwa ya maji ili tuendelee kupata maji safi na salama kama ambavyo binadamu wengine wanapata maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Condester, Mbunge wa Jimbo la Momba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Jimbo la Momba bado lina changamoto ya maji na ni moja ya maeneo ambayo yapo kimkakati katika Wizara na tumetupia jicho la kipekee kabisa pale. Visima ni moja ya miradi ambayo tunakuja kuitekeleza ndani ya Jimbo la Momba. Hivyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge awe na Subira, tutakuja kutekeleza wajibu wetu, kwa sababu wananchi wale pia wapo Tanzania. Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan, amesema wanawake wote lazima tuwatue ndoo kichwani. Mantahofu, tunakuja kufanya kazi Momba. (Makofi)
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini bado, changamoto ya maji kwenye Jimbo la Momba ni kubwa sana. Naomba kuiuliza Serikali niongeze maswali mawili kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vijiji ambavyo umevieleza tunavyo vijiji 72 na vitongoji 302 inaonyesha kwamba hata nusu ya vijiji hivyo vitakuwa bado havijapata maji safi na salama. Ombi langu kwa Serikali, viko baadhi ya visima ambavyo vilishawahi kuchimbwa nyuma na wakoloni, vilishawahi kuchimbwa nyuma na wamishionari lakini pia na baadhi ya wakandarasi ambao walikuja kujenga barabara kwenye Jimbo la Momba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza, nini kauli ya Serikali kwenda kuvitembelea visima vile ambavyo vimeshawahi kufanya kazi vizuri huko nyuma kutokana bado kuna changamoto ya maji vinaweza vikatusaidia vikawa kama njia nyingine ya mbadala kutatua changamoto ya maji? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kwa kuwa, baadhi ya vijiji ambavyo vimeonyesha vinao miradi hiyo ya maji lakini zipo Taasisi kama Vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Sekondari havipati utoshelevu wa maji. Watoto wetu especially wa kike wameendelea kuteseka sana kufuata maji wakati mwingine zaidi ya kilomita 10. Mfano, Shule ya Sekondari Chikanamlilo, Shule ya Sekondari Momba, Shule ya Sekondari Uwanda, Shule ya Sekondari Ivuna, Shule ya Sekondari Nzoka na shule zingine 13 ambazo ziko ndani ya Jimbo la Momba pamoja na Zahanati na Vituo vya Afya kama Kamsamba na Kapele. Je, ni nini kauli ya Serikali kutuchimbia visima virefu ili Taasisi hizi ziweze kujipatia maji yake bila kutegemea kwenye vile vituo ambavyo tunang’ang’ania na wananchi na havitoshelezi? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Condester, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kutembelea visima ambavyo ni chakavu hii ni moja ya jukumu letu na tayari, Mheshimiwa Waziri amewaagiza watendaji wote kwenye mikoa yote, kwa maana ya Regional Managers (RMs) na Managing Directors (MDs) wasimamie visima vyote ambavyo ni chakavu. Vile ambavyo uwezekano wa kuvirejesha katika hali njema ya kutoa maji safi na salama vyote viweze kurejeshwa katika hali nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Jimbo la Momba sisi kama Wizara tumeshaleta Shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuchimba visima virefu. Hivyo, visima hivi ambavyo vya kukarabati lakini uchimbaji wa visima virefu kwenye swali lako la pili la nyongeza, navyo tayari vimeshaanza kufanyiwa kazi katika baadhi ya maeneo. Tayari visima vitano vimeshachimbwa kati ya visima 30.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, napenda tu kumtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, kwamba sisi kama Wizara tutakwenda kuhakikisha katika sehemu zote ambako Taasisi za Serikali zipo kama zile Shule alizozitaja pamoja na Vituo vya Afya na Hospitali maji ni lazima yafike na huo ndio Motto wa Wizara. (Makofi)
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwenye Jimbo la Ndanda tuna mradi mkubwa wa maji uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni tano uliokusudiwa kuhudumia Kata ya Mwena, Kata ya Chikundi pamoja na Kata ya Chikukwe. Hata hivyo mradi huu unafanya kazi kwa kiwango cha chini kabisa kwa sababu inaonekana ilikuwa ni poor designing.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu kwa Mheshimiwa Waziri, je, haoni haja ya kuwaagiza wataalam wake wakakague mradi huu na kupeleka mapendekezo bora Serikalini, ili kuweza kuboresha ili wananchi wa Kata hizo wapate maji kwa kipindi chote cha mwaka?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecil Mwambe, Mbunge wa Ndanda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la kupeleka wataalam wakakague mradi huu na ni mradi ambao unakwenda kugharimu Serikali fedha nyingi zaidi ya Shilingi bilioni tano. Hii ni moja ya majukumu yetu Mheshimiwa Mbunge, tayari Mheshimiwa Waziri, amewasisitiza sana watendaji wanatakiwa kufuatilia hii miradi. Hivyo, nami napenda kusisitiza Managing Director na Regional Manager wa Mkoa wa Mtwara wahakikishe wanakwenda kusimamia huu mradi kuona unatekelezwa kadri ambavyo unapaswa kuwa. (Makofi)
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuweza kuuliza swali la nyongeza. Changamoto ya maji iliyopo katika Jimbo la Momba haitofautiani na changamoto iliyopo katika Jiji la Dodoma, kwamba kuna baadhi ya maeneo yamekuwa yakikosa maji hata kwa wiki tatu kwa maelezo kwamba mitambo ya Mzakwe imezimwa kutokana na ukosefu wa umeme.

Napenda kufahamu, je, Serikali inatoa kauli gani kuhusiana na kadhia hii ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa kukosa maji mara kwa mara. Ahsante.(Makofi)
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote kwanza nimpongeze Naibu wangu kwa kazi nzuri na namna gani anavyojibu maswali hapa Bungeni. Hata hivyo, nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge, lakini kwanza nimpongeze Mama yangu Toufiq, kwa kazi kubwa na nzuri anayofanya katika Mkoa huu wa Dodoma. Tukiri kabisa sisi kama Wizara ya Maji hapa Jiji la Dodoma kumekuwa na ongezeko kubwa la watu, uhitaji na uzalishaji wa maji katika Jiji la Dodoma uwezo wa mtambo wetu ni lita milioni 60 na mahitaji yake ni lita milioni 103 kutokana na ongezeko kubwa la watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti kwa hiyo maelekezo mahususi ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa Wizara yetu ya Maji, kwa sababu lazima tumtue mwana mama ndoo kichwani. Tunakwenda kuyatoa maji ya Ziwa Victoria na kuja kuyaleta katika Jiji hili la Dodoma, ili kuhakikisha kwamba tunaondokana na changamoto hii. Kwa mkakati wa muda mfupi tunaendelea kuchimba visima virefu katika maeneo mbalimbali, ili kuongeza uzalishaji kwa muda mfupi na wananchi waendelee kupata huduma ya maji. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Jimbo la Tabora Mjini ni kati ya Majimbo ambayo yamenufaika na Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria, lakini mpaka sasa baadhi ya maeneo ya Jimbo hilo hayana maji kabisa. Je, Serikali imekwama wapi kusambaza maji kwa wananchi wa Tabora Mjini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hawa, kutoka Tabora kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi ule mkubwa kutoka Ziwa Victoria ni mradi ambao ni endelevu na ni mradi wenye manufaa makubwa sana. Maeneo mengi ambayo yamekuwa yanapaswa kupitiwa na mradi ule yataendelea kupata maji kwa wakati wote. Kwa maeneo machache ambayo kama bado hayajapata maji, wataalam wetu wanaendelea kufanya kazi kuhakikisha usambazaji wa maji ni zoezi endelevu. Hivyo waendelee kuvuta subira muda si mrefu na wao watapata maji. (Makofi)
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa swali la nyongeza. Ni wazi Wizara hii imekuwa ikifanya kazi kubwa kuhakikisha huduma ya maji inafika katika maeneo mengi. Katika maeneo ya Majiji, Manispaa na Miji kumekuwa na changamoto ya milipuko ya moto. Ambapo ukiuliza unaambiwa visima vya maji ambavyo vitajaza kwenye magari maji kwa wepesi havipo. Swali langu nilitamani kufahamu ni nini mkakati wa Wizara kuhakikisha katika project, kila mradi unaokuwa unaandaliwa kunakuwa na setting ya visima au matanki ambayo yatajaza maji kwa haraka katika magari ya zimamoto? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema Mwandabila, kutoka Songwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili swali aliloliuliza ni utekelezaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani na hawa wenzetu wa Zimamoto wanaufahamu wajibu wao. Taasisi zote za Serikali ambazo zinahitaji huduma ya maji wanafahamu wanapaswa kufika katika ofisi zetu kwenye mikoa yao. Ili waweze kuongea na wataalam wetu na kuona njia njema ya kutumia ili waweze kupata huduma ya maji katika ofisi zao. Taasisi zote za Umma zinapeleka maji kwa gharama zao na pale inapobidi kupata huduma ya kiupendeleo basi huwa wanafika na kuweza kueleza tatizo husika. Hivyo, wenzetu wa Zimamoto wanafahamu wapi wafike ili waweze kufanya vyema. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa majibu yaliyotolewa, lakini watu wa Kyerwa hawana majikwa asilimia 56 kama Serikali inayoeleza. Changamoto ya upatikanaji wa maji ni kubwa zaidi, naweza kusema ni asilimia kama 25. Kwa hiyo, naomba Serikali ifanye mkakati wa maksudi wa kuwasaidia watu wa Kyerwa wapare maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba, ametaja Mradi wa Runyinya, Chanya, Kimuli, Rwanyango, Nyamiaga na Nyakatera ambapo ukiweza kusainiwa na kuanza utapunguza kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa maji. Nataka kujua ni lini sasa mkataba utasainiwa kwa sababu imekuwa ni kila siku mkataba unakaribia kusainiwa. Nataka nijue ni lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Wananchi wa Kata za Nyakatuntu, Kimuli, Kamuli, Bugara na maeneo mengine wana changamoto kubwa ya maji na wameahidiwa watakuwa kwenye mradi wa vijiji 57 ambapo iwapo utatekelezwa ungepunguza changamoto ya maji. Haujaanza na hatujui unaanza lini. Nataka nijue ni lini huo mradi utaanza na kukamilika ili kuondoa adha kubwa ya maji kwa wananchi wa Jimbo la Kyerwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Anatropia kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, napenda kumpongeza Mheshimiwa Anatropia kwa maswali yake mazuri na ninamwona ana ushirikiano wa karibu sana na Mheshimiwa Bilakwate, Mbunge mwenye Jimbo, ambaye ameendelea kufuatilia miradi hii yote. Mheshimiwa Innocent Bilakwate ni juzi ametoka Ofisini kuhakikisha anaweka sawa miradi hii ambayo inaenda kufanyika katika Jimbo la Kyerwa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tuna mradi wa Kamuli ambao kijiografia upo juu. Tunatarajia mradi huu kwenda kutekelezwa hivi karibuni na utekelezaji wa mradi huu utasaidia kusambaza maji katika vijiji vingi vya Jimbo la Kyerwa. Hivyo, napenda kukutoa hofu Mheshimiwa Mbunge, miradi hii itasainiwa kwa taratibu za Wizara zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, percentage za usambazaji maji katika Jimbo la Kyerwa ni asilimia za kitaalam, siyo za kufikirika kuangalia tu kwa macho na ukasema ni asilimia 20. Ni asilimia zilizotajwa na watalaam, zimefanyiwa kazi na tuna uhakika na kazi tunayoifanya. Nasi Wizara ya Maji siyo wababaishaji, lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunamtua ndoo mama kichwani kama ambavyo Mheshimiwa Rais wetu anatutaka. (Makofi)
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Nianze kwanza kwa kutoa pongeza nyingi sana kwa Serikali kwa namna ilivyoshughulikia matatizo ya wananchi wa Jimbo la Buchosa. Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kwa juhudi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo mradi wa Lumea, Nyakariro, Karebezo hadi Nyehunge wa shilingi bilioni 1.6. Mradi huu ni kichefuchefu, ulijengwa chini ya kiwango, mabomba yanapasuka, maji yanamwagika chini na wananchi hawapati maji: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kumwuliza Mheshimiwa Waziri, ni lini atatembelea mradi huu ili kuweza kuwa na utaratibu wa kufanya maboresho na wananchi waweze kupata maji?

Pili, ni lini Serikali itapeleka watalaam kuchunguza na kugundua watu waliohusika na ubadhirifu kwenye mradi huu ili waweze kuchukuliwa hatua kuepusha kuharibu sifa ya Mheshimiwa Waziri na Serikali kwa ujumla. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Eric Shigongo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la kwenda kutembelea Mheshimiwa Mbunge mantahofu, mara baada ya Mkutano huu tutakwenda kutembelea na kujionea na kuona kwamba kazi zinaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la Watalaam kwenda kuchunguza, Mheshimiwa Waziri ameshatengeneza task force ya kufuatilia miradi yote kichefuchefu na kuona kwamba inafanyiwa kazi na inakamilika na huduma ya maji inapatikana bombani na tunamtua ndoo mwanamke kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, napenda kusema kwamba, ile task force naamini wamesikia na ninasisitiza maagizo ya Mheshimiwa Waziri mara wasikiapo maagizo haya waweze kwenda mara moja ili kuchunguza na miradi ile iweze kukamilika na lengo la kutoa maji na kumtua mama ndoo kichwani liweze kutimilika. (Makofi)
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru sana kupata nafasi ya kuuliza swali, lakini niishukuru sana Wizara ya Maji kupitia kwa Waziri mwenye dhamana wamefanya kazi kubwa sana ya kupeleka huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shida kubwa ya Mkoa wa Katavi tunahitaji kupata chanzo cha uhakika cha maji na chanzo hicho kipo Ziwa Tanganyika ambalo linaweza likatatua tatizo la maji kwa kupeleka huduma kwa Wilaya zote tatu kwa maana ya Wilaya Tanganyika, Wilaya ya Mlele na Wilaya ya Mpanda.

Ni lini Serikali itakuja kutatua tatizo la kupeleka huduma ya maji kuliko kutumia fedha nyingi wanazozitumia kuandaa miradi midogo midogo ambayo haina tija?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakoso kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyoendelea kufuatilia suala la matumizi ya vyanzo vya uhakika kama Ziwa Tanzanyika. Wizara tumejipanga kuona kwamba maziwa yote tunakwenda kuyatumia tukiamini tunakwenda kutatua tatizo hili la maji na tutamtua ndoo mwanamama kichwani kama ambavyo Mheshimiwa Rais anatutaka na tumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kutupa fedha Wizara ya Maji. Hivyo, kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi tuko katika kufanya usanifu ili kuona mwaka 2022/2023 matumizi ya maji makuu kama vyanzo vya maji vya uhakika yaweze kufanyika.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto hii ya maji inayokuba mji wa Mpanda inafanana sana na changamoto ya maji katika jimbo langu Nanyumbu. Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitumia takribani shilingi bilioni moja kujenga bwawa katika kata ya Maratani ili vijiji vya Lipupu, Maratani. Mchangani A na Malema viweze kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu haukufanikiwa na Waziri mwenye dhamana alifika katika jimbo langu na kuahidi kutoa kuchimba visima viwili katika kila kijiji hivi nilivyovitaja.

Je, ni lini ahadi hii ya Mheshimiwa Waziri itatekelezwa ili wananchi katika jimbo hili waweze kunufaika na hii ahadi ya Mheshimiwa Waziri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Yahya Mhata, Mbunge wa Nanyumbu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi ni deni na kwa sababu ameahidi Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana, Mheshimiwa Mbunge ninakuhakikishia mgao ujao visima vitakuja kuanza kuchimbwa fedha italetwa.
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Katika Mji wa Karatu tuna bodi mbili za maji, Bodi ya KARUWASA inauza maji kwa shilingi 1,700 kwa unit, Bodi ya KAFIWASU inauza maji kwa kwa unit 3500. Sasa ni lini Serikali itaweza kuweka bei ya uwiano katika Jimbo la Karatu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Karatu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi gharama za kulipia maji zimekuwa zikifanyiwa marekebisho kila inapobidi kwa kuzingatia uendeshaji wa mradi wa maji wa eneo husika. Hivyo, kwa Jimbo la Karatu nao mchakato unaendelea na tunaamini kabla ya mwaka huu wa fedha kukamilika basi bei hizi zitakuwa rafiki na itakuwa kwa manufaa zaidi ya wananchi.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwanza nianze kumpongeza Waziri wa Wizara ya Maji pamoja na Naibu kwa kuendelea kutukamilishaia mradi wetu ambao ulikuwa unaitwa ni mradi kichefuchefu wa Wilaya ya Nyang’hwale kutoka Nyamtukuza kwenda Bukwimba kwamba sasa hivi maji hayo tayari tumeanza kuyatumia, lakini kuna tatizo moja maji yale si safi na salama, hawajajenga chujio la maji.

Je, Serikali inatuahidi nini kwenda kujenga hilo chujio la maji ili tuweze kupata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Amar kutoka Nyang’hwale kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan huu mradi ulikuwa kichefuchefu lakini kwa sasa hivi kama alivyokiri mwenyewe Mheshimiwa Mbunge kwa jitihada zake za ufuatiliaji pamoja na mashirikiano mazuri sasa hivi maji yanatoka. Kuhusiana na chujio ni hatua inayofuata na yenyewe pia tutakuja kukamilisha. Ahsante.
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutupatia fedha za mradi wa maji katika cha Ibatu.

Swali, kwa kuwa mkandarasi aliyopewa mradi huu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Kijiji cha Ibatu mpaka sasa ameingia mitini, hakuna shughuli zinazoendelea. Nini mpango wa Serikali na kwa nini Serikali isiweke mkandarasi mwingi au ikafanya kazi wizara yenyewe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deo Sanga kuhusiana na mradi wa Ibatu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tumefuatilia huyu mkandarasi Farbank Company na tayari tumewaagiza mameneja ambao wako pale Njombe wanafanyia kazi. Kwa sasa hivi mkandarasi amerejea kazini siku hizi mbili, lakini tumempa muda wa maangalizo kwa wiki mbili na baada ya hapo basi sheria itafuata mkondo wake.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri na wananchi wa Urambo wana imani na Wizara hii inafanya kazi kubwa, lakini kwa leo naiomba Serikali itoe kauli hapa. Lini maji haya yanafika Urambo kutokea Tabora ambapo yameshafika kutoka Lake Victoria?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la ngongeza la Mheshimiwa Margaret Sitta kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema lini mradi utaanza kutekelezwa, kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha, mradi utaanza kutekelezwa. (Makofi)
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ili nami niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Serikali ilianza mpango wa kulipa fidia wananchi wa maeneo yaliyozunguka Mradi wa Mto Ruvuma, sasa nataka kujua kwa nini Serikali inakwama kuendeleza mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shamsia kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli fidia ilishaanza kulipwa na itaendelea kumaliziwa ndani ya mwaka huu wa fedha, lakini mradi huu wa Mto Ruvuma ni katika ile miradi yetu ya kimkakati ndani ya Wizara kuona kwamba vinakuwa nyanzo vya kudumu kwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru; hali ya upatikanaji maji Wilaya ya Mkinga kwa sasa ni mbaya sana. Hivi ninavyozungumza mabwawa takribani matano yamekauka, tumeanza kuona dalili za ugonjwa wa homa ya matumbo. Sasa Wizara ilituma wataalam kufanya usanifu wa mradi mkubwa wa kutoa maji Mto Zigi kwenda mpaka Horohoro ambapo kazi hiyo inakamilika kesho. (Makofi)

Je, Serikali iko tayari kwa udharura huu kuhakikisha inaharakisha mchakato wa kupata wakandarasi, ili mradi ule uanze kushughulikiwa haraka iwezekanavyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kitandula, Mbunge wa Mkinga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, sote tunafahamu maji ni uhai na sisi kama Wizara ya Maji hatupendi kuwa kikwazo na kusababisha milipuko ya magonjwa. Kwa kutambua hilo kama Wizara tunamshukuru Mheshimiwa Rais aliongoza dua na sasa hivi mvua zimeanza kunyesha vizuri, mabwawa yaliyokauka tunayatarajia yarudi katika hali yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika usanifu huu unaoendelea ambao tunautarajia ukamilike kesho, tutaharakisha kuona kwamba lile bwawa ambalo linafanyiwa usanifu na maeneo yale ya Mkinga yote tunakwenda kuyafanyia kazi kwa haraka. Ninawaagiza ile timu iliyotumwa kule na Mheshimiwa Waziri ifanye kadri ya maagizo ya Mheshimiwa Waziri yaliyopo ili kuona tunaharakisha jambo hili. (Makofi)
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Manyoni Mashariki tuna mradi mkubwa wa shilingi bilioni 10 unaojulikana kwa jina la Kintinku-Lusilile. Kwanza naishukuru Serikali mpaka sasa hivi tayari chanzo cha maji kimepatikana. Lakini ningependa kusikia majibu ya Serikali ni lini sasa mkandarasi wa kusambaza maji, katika mradi huo katika Kata za Kintinku, Maweni na Makutupora ataanza kazi? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Pius Chaya; ni kweli mradi huu una vijiji 11 na tayari vijiji vitatu vimeshaanza kufanyiwa kazi na wiki ijayo tunatarajia kusaini mkataba wa kukamilisha vijiji nane vilivyobaki na tayari tumetenga fedha zaidi ya shilingi bilioni 3.3 ili mradi huu uweze kuendelea katika utekelezaji wake. (Makofi)
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa muda wa kuuliza swali la nyongeza.

Mji wa Mpanda ni kati ya miji 28 ambayo inatakiwa kupewa mradi wa maji; ni lini mradi huu utaletwa Mji wa Mpanda? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kapufi kutoka Mpanda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi hii ya miji 28 tutarajie itaanza ndani ya mwezi huu wa pili au wa tatu kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha.
MHE. HUMPHREY H. POLEPOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa za Kitafiti zinasema kila mwaka tani milioni tatu za udongo zinaingia katika Ziwa Victoria na kulipunguzia Ziwa hilo kina cha maji. Serikali ina mpango gani na iko katika hatua ipi ya kutekeleza National Water Grid au mtandao wa maji wa kitaifa kutoka Kusini, Kaskazini, Magharibi ili kuweza kupunguza pressure katika Ziwa Victoria? Nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Polepole kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna hii changamoto ya matope kuingia katika vyanzo vyetu vya maji na sisi kama Wizara tuna ofisi zetu za mabonde zinazoshughulika na kazi hizi na tayari Mheshimiwa Waziri amewaagiza. Hivyo, tayari hili linafanyiwa kazi kuona kwamba tunaendelea kutunza na kuvilinda vyanzo vyetu vya maji. (Makofi)
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Naomba nataka nielewe sisi kule kwetu Mtwara nimechimbiwa visima vitatu katika Jimbo langu, lakini takriban mpaka sasa hivi karibu miezi minne inakimbilia na mvua zinaanza kunyesha na visima vile tayari vimeshaanza kuziba.

Ni lini sasa visima vile vitamaliziwa kwa taratibu zingine za upatikanaji wa maji? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtenga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamshukuru Mwenyezi Mungu; Mheshimiwa Rais alitupatia fedha na visima vimechimbwa, kinachofuata ni mtandao wa usambazaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa agizo kwa Mameneja wa Mtwara wafanye kazi haraka iwezekanavyo ndani ya mwezi mmoja, waweze kuona kwamba utaratibu wa mwendelezo wa visima hivi inaweza kufanyika. (Makofi)
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Nataka kuiuliza Wizara kwamba ni lini sasa Serikali ina mkakati wa kusambaza maji katika Kata ya Mwaluguru, Kata ya Jana, na Kata ya Ikinda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala la usambazaji maji ni suala ambalo litafanyika mara baada ya kukamilika kwa miundombinu yote kwa sababu lengo ni kuona baada ya uchimbaji wa visima, usambazaji uweze kufuata na akinamama waweze kutuliwa ndoo kichwani.
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza naomba nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali. Vile vile naomba niishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi ya Lusaka, Mradi wa Mpepai na mradi wa Lifakara. Mwaka 2020 Serikali ilianza kutekeleza mradi katika Kata ya Myangayanga na Kata ya Ruahita, miradi hiyo miwili hadi sasa bado haijatekelezwa. Kwa hiyo nataka nijue, je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza miradi katika hizo kata mbili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jonas Mbunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hizi kata alizozitaja ziko kwenye mpango wa utekelezaji na kwa Mbinga Mjini tunatarajia hadi kufika 2023 Disemba, labda vitabaki kama vijiji viwili tu ambavyo vitakuwa bado havijapata maji. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwa namna ambavyo tunashirikiana nampongeza sana na nimhakikishie maji Mbinga yanakwenda kupatikana.
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Naomba kumuuliza swali Mheshimiwa Waziri. Je, ni lini Serikali itafikisha huduma ya majisafi na salama katika Wilaya za pembezoni katika Mkoa wa Mtwara?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Agnes Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara imejipanga kutumia Mto Ruvuma kuona maeneo yote ya pembezoni yanaenda kupata maji na Wizara tunaendelea kutafuta fedha, naamini ndani ya mwaka ujao wa fedha maeneo mengi ya pembezoni mwa Mtwara yataenda kupata maji.
MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Changamoto ya maji Wilaya ya Chunya ni kubwa sana. Sasa naomba nimuulize swali Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba Mradi wa Maji wa Kiwira umekuwa unatajwa muda mrefu na mpaka sasa utekelezaji wake haujaanza na mradi huu utafaidisha Wilaya ya Chunya pamoja na Mbeya Mjini. e, ni lini sasa Serikali itatoa fedha mradi huu uanze kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Masache Kasaka, Mbunge kutoka Chunya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba kumpongeza Mbunge Kasaka kwa kazi nzuri aliyoifanya Chunya, miradi ambayo ilikuwa kichefuchefu toka mwaka 2012, Mradi wa Matwiga sasa hivi upo kwenye hatua nzuri na tayari tumeshampata mkandarasi anakuja kule kwa ajili ya usambazaji wa vijiji vinne vya awali na huu Mradi wa Kiwira wiki ijayo tunakwenda kusaini mkataba ili mradi uanze utekelezaji. Hivyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana na kwa kazi nzuri anayoifanya Wanachunya wanakwenda kufaidika. (Makofi)
NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nimekuwa nikiuliza mara kwa mara Mradi wa Maji wa Igando Kijombe ndani ya Wilaya ya Wanging’mbe. Mradi huu sasa hivi ni muda wa miaka mitatu imepita, bajeti yake ya kwanza ni bilioni 12, lakini hadi sasa ni bilioni nne tu ambazo zimekwenda kwenye mradi hule, muda umekuwa mrefu na mradi huu ni muhimu kwa wananchi wa Wilaya Wanging’mbe. Je, ni lini mradi huu utaenda kukamilika ili uweze kuleta tija kwa wananchi wa Wanging’ombe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge amekuwa akitoa ushirikiano sana katika mradi huu, lakini napenda kumwarifu Mheshimiwa Mbunge huu mradi tayari tumeutembelea hivi karibuni na nimpongeze kwa ushirikiano na Mheshimiwa Dkt. Dugange ameweza kufuatilia. Vile vile niseme tu kwamba tayari mkandarasi anaendelea na kazi na kwa sababu mradi huu ulikuwa ni mkubwa tunafikia phase za mwisho, maeneo ambayo tayari yalikamilika wananchi wameanza kupata huduma ya maji. Hivyo napenda kumtoa hofu Mbunge, mradi huu unakwenda kukamilika ndani ya sera ya kumtua ndoo mama kichwani, tumshukuru Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuisimamia vizuri. (Makofi)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na niseme kwa dhati kabisa kwamba nimefurahishwa sana na majibu ya Serikali na wananchi wangu wa Dosidosi, Kijungu na Dongo watakuwa wamesikia haya.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mradi ule wa milioni 400 wa Kaloleni uliotokana na fedha za UVIKO na kwa kweli niishukuru Wizara ya Maji na meneja wa RUWASA aliyeko pale ni mzuri sana, anafanya kazi vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, sasa swali langu dogo tu, je, ni lini Wizara ya Maji watakuwa tayari twende Kiteto, hususan pale Dongo, ili tukatembelee mradi mkubwa wa bwawa hili ambalo limewekwa kwenye mpango wa Serikali?Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Olelekaita kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimepokea pongezi zote na tuendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa sababu anaendelea kutoa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la kufika Kiteto, niko tayari, nitafika Kiteto na tutafanya kazi. Sisi tunasema na kutenda, tutafika Kiteto.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, ahsante nimeridhishwa na majibu mazuri ya Serikali, lakini je, Naibu Waziri yuko tayari kuja Jimboni kwangu ili kuweza kutembelea miradi hiyo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge Zidadu kwa umahiri wake wa ufuatiliaji wa miradi ya maji. Suala la kuja Jimboni manta hofu, nitafika. (Makofi)
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante; kauli ya Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni kumtua ndoo mama kichwani, lakini Tukuyu kuna shida sana ya maji, Serikali ilipanga kutoa fedha shilingi bilioni
4.5 kumaliza tatizo la maji Tukuyu mjini. Lakini mpaka sasa wamepeleka shilingi milioni 500 tu sasa akinamama wa Tukuyu hali ni mbaya sana kutafuta maji.

Sasa je, ni lini Serikali itapeleka hizo fedha kiasi cha shilingi bilioni nne ili kumaliza tatizo la maji Tukuyu mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli na hii si mara ya kwanza Mheshimiwa Suma Fyandomo kufuatilia na amekuwa akifuatilia kwa ushirikiano wa karibu kabisa na Mheshimiwa Mwantona na sisi Wizara ya Maji tumekaa jana, tumeshaweka kwenye mpango tunaongeza shilingi milioni 500 nyingine ili kazi ziweze kuendelea na mgao ujao tutaongeza tena shilingi milioni 500 hadi kuweza kukamilisha mradi huu muhimu kwa sababu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan lengo ni kuona maeneo yote maji yanapatikana bombani na Tukuyu ni moja ya eneo muhimu sana na Mheshimiwa Mbunge tutafanyakazi kwa pamoja, tutaleta maji kuhakikisha wakinamama wa Tukuyu pia tunawatua ndoo kichwani.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Katika Jimbo langu la Kwela Serikali ilileta fedha shilingi bilioni 2.9 kwa ajii ya mradi ndani ya kata ya Ikozi, lakini mpaka sasa mradi huo haujakamilika ni kama umetelekezwa. Nataka nijue commitment ya Serikali ni namna gani ambavyo watawahakikishia ndani ya muda mfupi wananchi wa kata ya Ikozi wanapata maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sangu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miradi yote ambayo tayari utekelezaji unasubiriwa ama umeanza Mheshimiwa Waziri ameshaagiza watendaji wetu mikoani wote kuhakikisha hii miradi inakamilika hivyo Mheshimiwa naomba nikutoe hofu kazi zinakuja kufanyika mradi lazima utekelezwe. Mama Samia anasema kumtua ndoo mama kichwani siyo option, ni lazima. (Makofi)
MHE. MOHAMMED MAULID ALI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nilitaka kumwuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mpango gani wa Serikali katika bajeti ijayo kuhusu suala zima la kutoa maji kwenye maziwa na kupeleka kwa wananchi? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mohamed Maulid Ali kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Wizara, nimesema katika jibu langu la msingi, ni kuona kwamba tunakwenda kutumia vyanzo vya uhakika, ikiwemo maji ya maziwa makuu. Hivyo tuko kwenye mpango huo, lazima tutatekeleza. (Makofi)
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa Mto Kiwira unapita maene mengi sana ya Wilaya ya Kyela ikiwemo Vijiji vya Lema, Mwalisi, mpaka Bujonde. Na kwa kuwa mto huo umelalamikiwa na wananchi wa maeneo hayo kuwa na uchafuzi mkubwa ambapo inafikia hatua mto unanuka na unakuwa na rangi ya damu.

Je, ni lini Serikali itaunda Tume Maalum kufanya utafiti wa nini kinasababisha maji hayo yawe machafu?

Mheshimiwa Spika, mbili, kwa kuwa wananchi wengi wa eneo hilo baada ya kukosa maji ya Ngana wanatumia kwa ajili ya kunywa na kuoga. Je, ni lini Serikali sasa itaanza ujenzi wa mradi wa Ngana?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Ally amekuwa mfuatiliaji mzuri, amekuwa anakwenda zaidi ya uhitaji wa kupata maji yakiwa bombani lakini pia amekuwa akizingatia suala la usalama.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na bonde hili maji haya yanapochafuka, Mto Kiwira ni Mto ambao tunautumia kwa miradi mingi, naomba kutumia Bunge lako Tukufu kuagiza Bonde husika lifanye kazi kadri ambavyo inatakiwa kisheria. Vilevile Wizara tutaendelea kusimamia. Tayari Mheshimiwa Waziri amekuwa akitoa maagizo kadhaa kwa Mabonde yote kuhakikisha shughuli za maji kuwa salama yafanye usimamizi unaotakiwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili la lini ujenzi wa Ngana utaanza, kwa furaha kubwa ninapenda kukuarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi huu tayari tumeshatangaza na hivi karibuni kabla yam waka huu wa fedha kuisha tutapata Mkandarasi na lazima kasi zije zianze kwa kasi kwa sababu tunafahamu umuhimu wake kulingana na jiografia ya eneo hilo. (Makofi)
MHE. MICHAEL M. KEMBAKI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, katika Mji wetu wa Tarime tunategemea chanzo kimoja kikuu cha maji ya Bonde la Ndurumo, lakini kumetokea baadhi ya watu kuanzisha plant za kuchenjua dhahabu kandokando ya chanzo hiki.

Je, Serikali inatuhakikishiaje watu wa Tarime kwamba maji tunayotumia yapo salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, maji yote ambayo yanafika kwa mlaji wa mwisho kwa maana ya mwananchi ni maji salama ambayo tayari Wizara kupitia Idara ya Maabara inakuwa imeshafanya kazi yake, hivyo ninapenda kuwatoa hofu wananchi wote wanaoishi kandokando ya wachimbaji kwamba maji yanafanyiwa kazi katika maabara.
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Mradi wa maji wa Litembo, Mahenge kutokea Mwogelo, mwaka jana niliuliza swali hapa na nikapewa majibu mazuri na Mheshimiwa kwamba tayari fedha imetengwa na mradi unaanza kujengwa. Kwa bahati mbaya mradi huu unatoa maji Litembo tu.

Je, ni lini maji yatatoka Mahenge na Langandondo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachokiongea Mheshimiwa Mbunge lakini Mheshimiwa Mbunge unafahamu kwa namna ambavyo tumekuwa tukiwasiliana tumeweza kufanya kazi sasa Litembo inapata maji. Kwa hiyo, maeneo haya ya Mahenge tayari tunapeleka Mkandarasi ambaye ataanza kazi hivi karibuni na kuona kwamba maeneo yote haya mawili yaliyobaki nayo yanakwenda kunufaika na maji bombani.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana kwa pamoja kama ambavyo umekuwa ukifanya. (Makofi)
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, ninaomba nimshukuru Mheshimiwa Rais na Wizara kwa kuidhinisha na kutekeleza mradi wa dharura katika Mji wa Mwaluzi siku si chache wananchi wataanza kunufaika na Mto semu.

Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto zilizoainishwa katika majibu ya Serikali ninamuomba Mheshimiwa Naibu Waziri afike Jimbo la Meatu katika Bwawa hilo ilia one hizo adhan a kuchukua hatua za haraka ili kunusuru bwawa hilo lililogharimu Shilingi Bilioni 1.8 bila kunufaisha wananchi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mradi huu ulitekelezwa na Wizara, RUASA Wilaya kwa mwaka uliotajwa tayari mipango mingine imewekwa. Je, ukarabati huu utafanywa kwa ngazi ya Mkoa au ngazi ya Wizara? Ninakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninapenda kupokea pongezi na kwa hakika tuna kila sababu ya kuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameitendea haki hii Wizara ya Maji. Tumeendelea kupata fedha na ndiyo maana tunaona kila kona miradi ya maji inaendelea kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, kufika Meatu ni moja ya taratibu zangu za kazi, naomba nikupe taarifa Mheshimiwa Mbunge pamoja na Wabunge wote wanaotoka Mkoa wa Simiyu ratiba yangu ni kuanzia tarehe 25 mwezi huu kuwa Simiyu hivyo tutafika maeneo haya yote korofi ili kuona tunafanya kazi kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na ukarabati tutafanya kwa kushirikiana na watendaji wetu ambao wapo katika Mkoa ule na Wizara hatuna pa kukwepea ni lazima tuwajibike katika hilo. (Makofi)
MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Spika, Jimbo la Shinyanga Mjini katika Kata za pembeni, Kata ya Chibe, Mwalili, Old Shinyanga, Kizumbi na Mwawaza kuna shida kubwa sana ya maji, watu wanakunywa maji ya kwenye madimbwi.

Ni nini mpango wa Serikali kupeleka mtandao wa maji kwenye Kata hizi kwa sababu hata sasa ukiwafuata Mamlaka ya Maji wanasema hawana fedha kwa ajili ya kupeleka maji safi na salama. Nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba wanapeleka fedha na kupeleka maji katika Kata hizo za pembezoni.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Salome Makamba, maeneo ya Shinyanga Mjini ni kweli imekuwa ni moja ya maeneo ambayo yamekuwa changamoto ya maji, lakini Wizara hapa tulipo chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan siyo Wizara ya wananchi kunywa maji kwenye madimbwi.

Mheshimiwa Spika, hili tayari tumeendelea kulifanyia kazi na maeneo haya yote ambayo bado yana changamoto, Wizara tutaleta fedha, tutasimamia kuhakikisha kwamba Majimbo yote, maji yatapatikana ili kuona wananchi wanapata maji safi bombani na ya kutosha. (Makofi)
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ninataka kujua ni lini Serikali itakamilisha mradi mkubwa wa maji wa Mwanga, Same, Korogwe ili kusaidia usambazaji wa maji kwenye vijiji vya Kata ya Mtomazi na Mkumbara katika Wilaya ya Korogwe? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, huu ni mradi mkubwa ambao umeshachukua muda mrefu lakini Wizara tunaendelea kutekeleza tunaamini ndani ya muda wa usanifu tunakwenda kukamilisha wa phase hii ambayo tupo. Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana na hongera kwa kuendelea kufuatilia mradi huu muhimu. (Makofi)
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Swali langu nimeulizia Mji wa Itigi ila imejibiwa vijijini. Basi, sasa je, Serikali ipo tayari sasa kuvuna maji katika Mji wa Itigi ili kujenga bwawa linaoitwa Mkalamani ambalo lipo palepale Mjini Itigi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kujibu swali lake la nyongeza la kuvuna maji katika Mji wa Itigi.

Mheshimiwa Spika, Mji wa Itigi ni moja ya Miji ambayo upatikanaji wake wa maji unaendelea vizuri kwa sasa ni zaidi ya asilimia 70. Kwa hiyo, kwenye masuala ya uvunaji wa maji tunazingatia zaidi maeneo ambayo maji yanapatikana kwa shida zaidi, lakini pale itakapobidi basi tutafanya hivyo.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza tunaishukuru Serikali kwa hatua hizo za awali. Ili mradi uweze kwenda na wakati ni lazima yale maeneo ambayo mabomba yanapita yawe wazi. Na ili yale maeneo ambayo mabomba yanapita yawe wazi, lazima wananchi walipwe fidia.

Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi hao?

Swali langu la pili; je, ni lini mradi wa Igongwe wa Kata Nne za Jimbo la Njombe Mjini utapatiwa pesa ili Mkandarasi aendelee na kazi yake? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Mgaya kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninampongeza Mheshimiwa Neema kwa ufuatiliaji. Suala la fidia tunaelekea kulipa kadri mradi unavyoendelea kujengwa na kila kitu kitakuwa kinakwenda kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, suala la mradi wa Igongwe kwenye Kata Nne, fedha zitaendelea kwenda kadiri tunavyozipata, na fedha ambazo zinafuata msimu ujao, huu mradi pia nao upo katika mpango.
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mradi wa Maji wa Izuga ni mradi wa muda mrefu, na kwa kuwa fedha iliyobaki ili mradi ukamilike ni milioni 76 tu. Kwa kuwa Mkandarasi yuko tayari walau apewe milioni 15 ili mradi ule ukamilike. Sasa, upo tayari baada ya Bunge hili mimi na wewe tuongozane mpaka Wizarani kuhakikisha kwamba Mkandarasi analipwa walau hiyo milioni 15 wananchi wapate maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mkandarasi atalipwa, nami niko tayari kwenda naye site.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Serikali kwa kupata mkandarasi wa maji kwa ajili ya mradi wa Kiwira ambao utalisha wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya. Sasa je, ni lini Serikali itatoa fedha ili mkandarasi aanze kufanya kazi mara moja?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali muhimu la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Mbeya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimpongeze Mheshimiwa Suma kwa ufuatiliaji mzuri wa mradi huu muhimu ambao utakwenda kuleta manufaa kwa Mbeya Jiji na Wilaya jirani. Lini fedha inakwenda kupelekwa, tayari kazi zimeshaanza na Wizara tunafanya ununuzi na kupata Wakandarasi kwa sababu Mhandisi Mshauri ameshakamilisha kazi yake. Hadi kufikia Desemba mwaka huu mradi utaendelea na utekelezaji. Kwa hiyo, kwa kila hatua fedha inatolewa. Fedha ilishaanza kutolewa toka Februari na sasa hivi ipo katika maandalizi ya kumpata Mkandarasi.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili nami niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itakamilisha mradi wa maji uliopo Kata ya Mango Pacha Nne ili kuwatua ndoo kichwani akina mama hawa ambao kwa muda mrefu, tokea tumepata uhuru, hawajawahi kabisa kufurahia huduma hii ya maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shamsia Mtamba, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi utaendelea kuletewa fedha. Ninakupongeza Mheshimiwa Mbunge, ameshafuatilia sana huu mradi, fedha inakuja na mimi na wewe tutakwenda site kuhakikisha kazi inakamilika. Lengo ni kuona mwana mama anatua ndoo kichwani na ni dhamira safi ya Mheshimiwa Rais ambayo anayo kwa muda mrefu.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa Serikali ilitenga pesa kwa ajili ya ujenzi wa chujio la maji Wilayani Nyang’hwale kwenye bajeti ya 2022/2023 shilingi milioni 220.

Je, Serikali itatoa lini pesa hiyo na ujenzi uanze mara moja?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hussein Amar, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Hussein kwa sababu tulishafuatilia awali, mradi sasa umefikia hatua nzuri. Suala la chujio, hizi milioni 200 zitaletwa kwa wakati, mgao ujao pia tutapunguza hii fedha, angalau milioni 100 ili kazi ziendelee kufanyika.
MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, utekelezaji wa agizo la Rais la kupeleka maji katika Kata Nne za Mererani, Endiamtu, Naisinyai, Shambarai na Oljoro Na. 5 umeanza katika Kata Mbili za Mererani na Indiamtu.

Je, ni lini sasa Wizara itatekeleza agizo hilo la Rais katika Kata zilizosalia kupitia Mradi ule Kabambe wa bilioni 400 wa Jiji la Arusha?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Christopher Ole-Sendeka, Mbunge wa Simanjiro, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maagizo ya Mheshimiwa Rais kinachofuata ni utekelezaji, ndiyo maana katika Kata Nne tayari Mbili zimeshaanza kutekelezwa na Kata hizi Mbili pia lazima tuje tuzitekeleze ndani ya muda ambao Mheshimiwa Rais ametuagiza.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ninapenda kufahamu ni lini Serikali itapeleka maji Vijiji vya Kipingu na Kiogo ili kunusuru akina mama wanaoliwa sana na mamba? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kamonga kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali tayari tunao utaratibu wa kwenda kuhakikisha maeneo ya Kiogo na maeneo yote kandokando ya Ziwa yanapata huduma ya maji safi na salama bombani ili kunusuru wananchi ambao wanaliwa na mamba. Tayari nimeshamuagiza Meneja wa Mkoa wa Njombe na ameshaniahidi ndani ya muda mfupi atahakikisha eneo ambalo mradi ulikuwa haujafika unakwenda kukamilika. (Makofi)
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona, maana nimesimama muda mrefu sana.

Mheshimiwa Spika, katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mwaka wa Fedha uliopita tulikuwa na miradi mitatu mikubwa. Mradi wa Machiga, Mradi wa Chandama na Mradi wa Visima 13, lakini mpaka leo wakandarasi wote hawako site; naomba kujua kauli ya Serikali juu ya Wakandarasi hawa. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Monni, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Monni tumekuwa tukifanya kazi kwa pamoja na amefika Wizarani mara nyingi, nampongeza kwenye hilo. Miradi hii mikubwa ninaamini ameshaongea na Mheshimiwa Waziri, ameshaongea na Mheshimiwa Katibu Mkuu, tunakuja kutekeleza na Wakandarasi watafuata namna ambavyo wamesaini mikataba yao.(Makofi)
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kuna mradi mpya unaojengwa wa visima kutoa maji Hai kwenda Arusha, lakini kwenye vile vyanzo ambavyo maji yanapita kama kanuni na sheria zinavyotaka kwamba, maeneo ambayo yanaptikana vyanzo vya maji watu wapate. Sasa nauliza swali langu; je, ni lini Serikali itatengeneza miundombinu maeneo ya Hai kwenye mradi mkubwa unaoenda Arusha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Sera ya Maji inataka maeneo yote ya vyanzo vya maji, wale wanaozunguka makazi yale wananchi wawe wanufaika namba moja. Katika visima hivi anavyoviongelea tayari sisi kama Wizara tuna utaratibu ambao tunaendelea nao, pesa itakapokamilika tutakuja kuendelea kuhakikisha wananchi wote wale wanaokaa kuzunguka vile visima wanaendelea kupatiwa huduma ya maji.
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naipongeza Wizara kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye sekta ya maji na nina swali moja la nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambayo yanachagiza huduma za kijamii kufika viganjani mwa watumiaji. Je, Wizara haioni umuhimu wa kuweka mpango kazi mahususi, yaani ikifika 2025 mita hizi janja ziweze kutumika na watu majumbani?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Judith Kapinga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe taarifa kwamba, tayari Wizara imeshakuwa na huo mpango na tayari umeshaanza kutekelezwa. Baadhi ya sisi hapa ndani pia tutakuwa mashahidi, hata mimi mwenyewe nyumbani kwangu natumia prepaid meter, kwa hiyo, sio kwamba, bado watu hawajaanza kutumia majumbani, tayari tumeanza, lakini kwa kuangalia kama modules za kufanya tu utafiti kuona kwamba, ufanisi wake umekaaje, lakini mpaka kufika hiyo 2025 anayoongelea Mheshimiwa Mbunge, nimtoe hofu jamii kubwa sana itakuwa tayari inatumia prepaid meters.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na ningependa kujua, Serikali ina bei maalum elekezi ya unit moja ya maji kwa sababu, kila halmashauri inajipangia bei na mwisho wa siku mzigo unabaki kwa mwananchi; kwa mfano Bunda, unit moja 1,800/= ukienda maeneo mengine ni 1,000/= mpaka chini ya 1,000/=. Je, hamwoni kuna haja ya kupanga bei maalum ili kuwaondolea mzigo wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari Wizara ilishatangaza kupitia Waziri mwenye dhamana, bei elekezi kwenye maeneo yote ilishatangazwa. Bei hazifanani kulingana na uwekezaji wa miradi. Mradi ambao unatumia source ya kusuma maji kama ni diesel, bei yake haiwezi kufanana na inayosukuma maji kwa kutumia umeme wa TANESCO, tofauti na bei ambapo maji kutoka katika chanzo chake yatakuwa yanasukumwa na umeme wa jua, lakini vilevile ukubwa wa mradi kulingana na jiografia ya eneo ulipo huo mradi. Hivyo, bei haziwezi kufanana, lakini bei elekezi tayari zimetolewa kulingana na mradi namna ambavyo ulitengenezwa.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante:-

Mheshimiwa, Mwenyekiti, hivi karibuni Mheshimiwa Waziri wa Maji alifanya ziara Wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha na kuahidi mradi mkubwa wa maji utakaoanzia katika tanki ya gari popo, utakaonufaisha vijiji 12 vya Kata ya Meserani, Lepurko, Moita na kata nyingine. Je, ni lini hasa mradi huu mkubwa wa maji utaanza rasmi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Catherine Magige, Mbunge Viti Maalum, Arusha, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mradi huu upo kwenye mpango wa Wizara, kama alivyoelekeza Mheshimiwa Waziri na wakati wowote ule mradi unaenda kuanza. Tunasubiri tu mafungu yakae vizuri, mradi unakuja kutekelezwa na tutahakikisha vijiji vyote 12 vinafikiwa na maeneo yote ya karibu ambayo bomba kuu litapita kwenye mradi huu yatakwenda kunufaika.
MHE. MWANTUM M. ZODO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Mkomazi na Kata ya Mkalamo katika Jimbo la Korogwe Vijijini ni Kata ambazo zimepitiwa na Mto Ruvu lakini Kata hizo hazina maji kabisa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha wanapeleka maji kwenye Kata hizo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mradi mkubwa wa maji wa Mwanga, Same, Korogwe ni mradi ambao unasuasua. Je, Serikali ina mpango gani wa kwenda kukamilisha mradi huo wa maji ili kuondoa adha ya maji kwa wananchi wa Wilaya ya Korogwe? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zodo kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Zodo kwa ufuatiliaji mzuri kwani wakinamama lazima tusemeane na tuhakikishe tunawatua ndoo kichwani akinamama wote wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata hizi mbili alizoziongelea za Korogwe Vijijini zipo kwenye mpango, mradi huu ukishakamilika kwa awamu hii ambayo utekelezaji unaendelea awamu inayofuata Kata hizi Mbili pia zitapata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na mradi wa Mwanga, Same, Korogwe nimetoka huko hivi majuzi mradi ni mzuri sana na kazi zinaendelea. Mheshimiwa Mbunge pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote wanaotoka kwenye maeneo ya mradi huu baadhi tuliweza kuongozana mradi ni wa mafanikio makubwa sana na unaendelea kutekelezwa na utakuwa manufaa maeneo yote ambayo unapitia.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nikiri kwamba Wizara ya Maji imetutendea haki Tarime angalau hali ya maji imeboreshwa. Nisipompongeza Mheshimiwa Waziri Aweso na Naibu wake itakuwa sijawatendea haki. Pamoja na kazi nzuri ambayo imefanyika naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza ni kwamba pale Sirari kuna mradi wa maji ambao tathmini ilifanyika ya kwanza ilikuwa shilingi 1,200,000,000, lakini tukarudia tathmini tukapata shilingi 534,000,000, sasa mradi unaendelea vizuri, imebaki shilingi 70,000,000 tu ili mradi ukamilike. Naomba nijue ni lini Serikali itapeleka fedha hizo pale mradi ukamilike Sirari ambapo ina wapigakura zaidi ya 17,000 ambao ndio ushindi wangu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ningependa tu nijue kwamba ni lini sasa huu Mradi wa Ziwa Victoria utaanza kwa sababu hili ni swali muhimu sana kwa Mbunge wa Tarime Vijijini, Sirari, Nyamongo na Nyamwaga lini mwaka wa fedha huu, mwaka wa fedha ujao au upi, ni lini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nipende kupokea shukrani kwa namna ambavyo tunaendelea na kazi mbalimbali kwenye miradi mingi kote nchini lakini hususan kwenye Jimbo la Tarime Vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu ambao bado tu milioni 60 upo kwenye mchakato na mgao ujao kwa maana ya mwezi huu wa tano tutahakikisha tunawaletea hii milioni 60 ili mradi ukamilike, lengo ni kuona maji yanatoka bombani na tunawatua akinamama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, miji 28 tunatarajia kuanza kutekeleza hivi karibuni, tayari kile kipingamizi ambacho kilikaa kwa muda mrefu kimekwisha. Kipekee nipende kumpongeza na kumshukuru sana Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameingilia kati na sasa hivi tunakwenda vizuri, ni mfupa wa muda mrefu, lakini mama Samia ameweza kuutafuna, tunakwenda kuanza kazi katika miji 28.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Wilaya ya Ngara ina vyanzo vikuu vya maji ambavyo ni Mto Ruvugu na Mto Kagera. Pamoja na uwepo wa vyanzo hivi tatizo la maji katika Wilaya ya Ngara limekuwa ni kubwa mno.

Je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kujenga mradi mkubwa unaotosheleza wananchi wa Wilaya Ngara? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum, kutoa Mkoa wa Kagera kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Ngara ni moja ya wilaya ambayo tumeipa jicho la kipekee kabisa kuona kwamba tunaenda kutatua changamoto za maji. Niseme tayari tuna miradi ambayo ipo kwenye utekelezaji, lakini tuna miradi ambayo tutaendelea nayo hivyo tatizo la maji linakwenda kukoma.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Miradi ya Maji ya Wilaya ya Nkasi imekuwa ikusuasua sana pamoja na Mradi wa Namenyere ambao Waziri aliahidi ndani ya Bunge kwamba utakamilika mwezi Desemba mwaka jana, mpaka leo mwezi wa Nne mradi huo haujaweza kuwanufaisha watu wa Wilaya ya Nkasi. Je, ni lini Serikali itaondokana na fikra za kutumia mabwawa badala ya kutumia Ziwa Tanganyika ambapo ni kilomita 64 tu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kadiri tutakavyopata fedha tutakwenda kutumia Ziwa Tanganyika kukamilisha miradi ya maji.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Mkoa wa Katavi una miradi mingi midogomidogo ambayo imeletwa na Serikali na tunaipongeza, lakini mwarobaini wa Mkoa wa Katavi kuepukana na miradi hiyo midogomidogo ni kuleta Mradi wa Maji wa kutoka Ziwa Tanganyika kuleta makao makuu, je, ni lini mradi huu utaanza kufanyiwa kazi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kakoso, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Katavi ni moja ya eneo ambalo litakwenda kunufaika na maji kutoka Ziwa Tanganyika kama nilivyojibu kwa Mbunge wa Nkasi, tutakapopata fedha hii ni miradi yetu ya kimkakati tutakwenda kutekeleza.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii. Ni lini bonde la Maji la Mitema ambalo lipo Jimbo la Newala Vijijini ambalo lina maji ya kutosha litafanyiwa kazi ipasavyo ili wananchi wa Newala, Tandahimba na Nanyamba waweze kupata maji ya uhakika kwa sasa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna, Mbunge wa Jimbo la Newala, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mikoa ya kusini tunakwenda kuinufaisha na miradi yetu mikubwa ya Mto Ruvuma pamoja na maeneo yote ambayo yanatupatia maji ya kutosha. Hivyo bonde la maji la Mto Mitema nalo lipo kwenye mikakati yetu na kuona kwamba maeneo yote ya Newala tunakwenda kuondokana na maji ya kuokota na maji aina zote ambayo hayafai kwa matumizi ya wanadamu. (Makofi)
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa
Naibu Spika, ahsante sana. Mji Mdogo wa Gairo ni mji ambao una matatizo ya maji, sasa naomba kujua Mradi wa Maji wa kutoka kwenye Milima ya Nongwe ni lini utakamilika ili wananchi wa Gairo waweze kupata maji ya kutosha?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Christine Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Morogoro, Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Maji, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hii anayoiongolea uendelevu wake unatokana na mapato ya fedha, kwa hiyo kadri tutakavyoendelea kupata fedha, namna ambavyo tumekuwa tukipeleka fedha nyingi sana kwenye maeneo yote, tutapeleka fedha kwani na Gairo pia tunatamani waondokane na tatizo la maji.
MHE. SHABAN O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Takribani miaka sita sasa imepita katika Kata ya Kwai iliahidiwa na Serikali mradi wa maji lakini mpaka sasa mradi ule hakuna chochote kilichofanyika. Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji katika Kata ya Kwai ili wananchi waondokane na adha hii wanayoendelea kuipata sasa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kata zake nyingi katika jimbo tumeshazishughulikia, hivyo hata kata hii ipo katika mkakati wa kuona kwamba na wao wanaenda kupata maji safi na salama ya kutosha. Tukishindwa kukamilisha ndani ya mwaka huu wa fedha basi mwaka ujao wa fedha tutahakikisha hii kata nayo inakwenda kunufaika na kumtua mama ndoo kichwani.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Swali langu, ni lini sasa kituo cha afya kinachoitwa Malawi kilichopo Yombo Vituka kitapata maji? Tumepata vifaa vizuri sana vya ndani ya hospitali lakini maji tunayotumia ni ya visima, leo na tuko mjini.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kilave, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kutoa huduma ya maji katika maeneo kama ya hospitali, shule ni moja ya vipaumbele vyetu.

Kwa hiyo maeneo haya ambayo bado yanatumia maji ya visima tunatoa kipaumbele na tutahakikisha kwenye kituo cha afya tutapeleka maji safi na salama bombani kwa lengo la kuona kwamba wanaendelea kuishi kwenye karne ya mama Samia kwa sababu Serikali ya Mama Samia imeweza kutoa fedha nyingi kwenye miradi ya maji.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante Mradi wa Maji Matamba - Kinyika wenye thamani ya bilioni mbili ndani ya miaka minne sasa Wilaya ya Makete bado haujakamilika. Naomba kujua, je, ni lini Serikali itasambaza mabomba pamoja na kujenga ofisi ili wananchi wa Wilaya ya Makete waweze kupata maji kwa uhakika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nipende kumpongeza Mheshimiwa Neema kwa ufuatiliaji mzuri wa miradi mbalimbali katika Mkoa wa Njombe. Kwa upande wa Makete nilifika huko na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo tulitembelea miradi hii yote na mradi huu ni kipaumbele cha Wizara kwa sababu unakwenda kuhudumia wananchi wengi na lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona maji yanapatikana katika maeneo yote. Maeneo ambayo muda mrefu hayajapata nayo yanakwenda kupata, hivyo hivi karibuni tutaendelea na utekelezaji wa mradi huu ili kuona kwamba maji yanapatikana.
MHE. INNOCENT. S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza niishukuru Serikali kwa juhudi za kuendelea kuwapatia maji wananchi wa Jimbo la Kyerwa lakini tunao mradi wa Kyelwa, Nyaruzumbura, Nyakatuntu mpaka Kamuli, mradi huu tumeupitisha kwenye bajeti iliyopita lakini mpaka sasa mradi huu haujaanza, je, ni lini utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bilakwate, Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hii yote ambayo mtaji wake ni ukubwa bado tunaendelea kuona kwamba tunapata fedha na kwenda kuitekeleza. Hivyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge Bilakwate tunakwenda kuutekeleza huu mradi na si kwa kuona kwamba tunatekeleza tu wajibu wetu, bali tunazingatia pia uhai kwa sababu maji ni uhai.
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naipongeza Wizara ya Maji kwa miradi inayotekelezwa ndani ya Jimbo la Mkenge Wilaya Misenyi, lakini miradi hiyo ya Igayaza, Byamte, Baishozi, Rutunga na Lwamachi Nakitobo imesimama kwa sababu ya kasi ndogo ya wakandarasi kwa kukosa fedha ambapo wameshaomba certificate Wizara ya Maji. Je, ni lini sasa wakandarasi hawa watalipwa ili miradi iweze kukamilika kwa wakati?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kyombo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari wiki iliyopita tumeanza kulipa wakandarasi, hivyo huenda na mkandarasi huyo akawemo ndani ya ile listi na tunaendelea kulipa. (Makofi)
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, asanye Mradi wa Matamba Kinyika ni mradi ambao ulikuwa unatekelezwa kwa bilioni nne lakini Mheshimiwa Waziri Aweso amepambana hadi umetekelezwa kwa bilioni mbili, lakini mradi huu una miaka minne na hadi sasa haujakamilika. Wananchi wa Kitongoji cha Itani, Mlondwe, Ngonde na Nungu bado wanahangaika na maji kupitia mradi huu. Je, ni lini Serikali itakamilisha mradi huu ili wananchi wao wapate maji ya uhakika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipokee shukrani, salamu za pongezi kwa niaba ya Waziri. Mradi huu kama alivyosema kwa jitihada za Mheshimiwa Waziri ameweza kuona kwamba ameupunguza na sasa hivi tutaendelea kuleta fedha ili kuona kwamba tunaenda kuukamilisha hivi punde, kama si ndani ya mwaka huu wa fedha kufika Juni, kabla ya mwaka 2022 kwisha tutahakikisha kwamba tunakuja kufanya kazi kwa sehemu kubwa.
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante./ Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuishukuru sana Wizara ya Maji wamefanya kazi kubwa, lakini nina swali moja la nyongeza. Kijiji cha Ombiri kilikuwa na bwawa la asili ambalo sababu ya mvua kubwa kingo zake zimekatika. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha wanarudisha bwawa lile kwa ajili ya watu wa kijiji kile? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Monni, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tunafahamu bwawa la Ombiri katika Kijiji cha Ombiri, limepata matatizo, sisi kama Wizara kwa umuhimu wa bwawa namna ambavyo tunaendelea kuyajenga, kwa hiyo, bwawa hili ambalo limepata hitalafu sisi kama Wizara tumelipa kipaumbele, tutakuja kulitekeleza kwa kulikarabati vizuri.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Mradi wa Maji wa Nyantukuza, Jimbo la Nyangh’wale umeenda kukamilika na kwa sababu kuna ukame mkubwa wa maji, je, Serikali ina mpango gani wa kusambaza maji kutoka chanzo hicho kwenye kata zifuatazo: Nyidundu, Nyalubele, Shabaka, Kaboha na Mwingilo, je, Serikali ina mpango gani wa kusambaza maji hayo kwa haraka ili kupunguza adha hii ya ukame wa maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Nyangh’wale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mradi ule ni mradi ambao tunatarajia uondoe matatizo ya maji katika kata hizo hizo ulizozitaja. Naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo sasa Wizara tunapambana kuona tunakabiliana na hili tatizo la ukame, tutafika na kuona uwezekano wa kuweza kusambaza maji katika kata alizozitaja Mbunge. Ahsante.
MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, hata hivyo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ni lini hasa magari mapya ya Wilaya zingine za Mkoa wa Simiyu yatapelekwa ili kuweza kusimamia miradi ya maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Mkoa wa Simiyu una changamoto kubwa ya vyanzo vya maji, je, RUWASA wamejipangaje, kupeleka mitambo ambayo itasaidia katika kunusuru changamoto kubwa ya maji huku tukisubiri Mradi Mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lucy, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa ameuliza lini haswa, mara baada ya magari kufika Mheshimiwa Mbunge magari yatafika sisi ni watu wa kuahidi na kutekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu vyanzo vya maji Mkoa wa Simiyu, naomba nimkumbushe Mheshimiwa Mbunge, kwa Mkoa wa Simiyu tuna mradi mkubwa zaidi ya bilioni nne ambao unatekelezwa kwa mabadiliko ya tabia nchi. Kwa hiyo, Mkoa wa Simiyu tayari umeshatupiwa jicho la kipekee kabisa na tayari miradi hii imeanza kutekelezwa. Vilevile vyanzo vya maji na kwa kutumia magari haya ambayo Mheshimiwa Rais ametupatia fedha nyingi, tayari ni tarehe 11 magari yatazinduliwa na tayari utaratibu wa kufika katika mikoa mbalimbali utaendelea.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Katika kipindi cha bajeti niliuliza swali la msingi kuhusiana na utekelezaji wa maji ya kutoka Mto Rufiji, nikaelezwa kwamba katika mwaka huu wa fedha wa 2022/2023, upembuzi yakinifu ungefanyika, sasa napenda kujua Serikali imefikia hatua gani katika upembuzi yakinifu uliotarajiwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Francis, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mto Rufiji ni moja ya mito muhimu sana kwa vyanzo vya maji ambavyo sisi tunavitumia. Tayari wataalam wetu wameshaanza kazi na tunatarajia watakamilisha upembuzi yakinifu kwa namna ambavyo muda umepangwa.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Napata shida sana mimi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, kwamba mradi wa zaidi karibu bilioni 300 sasa hivi unapewa shilingi 4,000,000,000, any way, ngoja niende kwenye maswali ya nyongeza.

Swali la kwanza; je, ni lini sasa Serikali itakamilisha mradi wa phase II ili kuhakikisha Wilaya ya Mbarali, Rungwe, Kyela na Chunya, Mbeya Mjini na Mbeya Vijijini ili waweze kupata maji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mheshimiwa Rais alivyokuja mwezi Agosti, 2022 alipita pale Wilayani Rungwe, alitoa agizo kwamba kufika mwezi Oktoba mradi wa maji unaoendelea pale Tukuyu uwe umekamilika, lakini sasa hivi Kata zote Bagamoyo, Msasani, Buliaga, Bitigi, Makandana, Kawetele maji ni shida kweli kweli. Sasa je, ni lini Serikali itakamilisha mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumpongeza Suma Fyandomo amekuwa akifuatilia mradi huu muhimu, ni mradi wa kimkakati, phase II ambayo anaiulizia kupitia wilaya nyingine zote, itafanyika baada ya phase one kukamilika.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa hivi tayari kupitia Mhandisi Mshauri ameshamaliza kuandaa nyaraka za zabuni kwa kufikia tarehe 26 Oktoba, kupitia Mamlaka ya Maji na tayari Mamlaka ya Maji imetoa nyaraka za zabuni za kandarasi za ujenzi katika mradi huu na tunategemea kwa namna ambavyo wakandarasi wameshapatiwa tarehe 8 Novemba, kandarasi nne zimeshafanikiwa kufika kwenye eneo la mradi, kuangalia hali ya mradi ili sasa ifikapo tarehe 7 Disemba tunatarajia vitabu vya zabuni viwe vimetoka, kwa hiyo wataenda kuvichukua. Ikifika mwisho wa mwezi Disemba sasa hapo ujengaji wa mradi phase one ndio unaanza. Kwa hiyo kwa maeneo hayo aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge, yatafanyiwa kazi baada ya phase one kukamili.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na agizo la Mheshimiwa Rais, binafsi nilifika Tukuyu, nilikwenda kwenye chanzo, nilihakikisha tarehe ambayo tulimwahidi Mheshimiwa Rais, tuliweza kufikisha maji yale kutoka kwenye kile chanzo na tulishayaingiza kwenye existing line za Tukuyu Mjini na maji tayari yalishaanza kuingia kwenye maeneo yote. Kwa hiyo, kipindi hiki cha ukame, sio tu Tukuyu wala sio tu Mbeya, ni maeneo yote ya Tanzania tunapitia changamoto kwa sababu vyanzo vyetu vya maji kina kimeshuka.

Mheshimiwa Spika, kwa kupitia Bunge lako Tukufu, niombe sisi Wabunge wote tumwombe sana Mwenyezi Mungu mvua zinyeshe, hiyo ndio itakuwa suluhu na maeneo yote tutaendelea kupata maji kwa uzuri.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwenye Mji wa Liwale upo mradi wa kuupatia maji mji ule na tumechimba visima vitatu Kijiji cha Turuki, lakini mradi ule sasa umesimama kwa muda mrefu. Je, lini hatima ya mradi ule ili Mji wa Liwale upate maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zuberi Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tulifika Liwale, mwenyewe nilikwenda Liwale, lakini vile vile Mheshimiwa Waziri amekwenda Liwale na huu mradi uliosimama, naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge nitaufuatilia leo hii na baada ya Bunge hili naomba tuonane.
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi. Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kipindi hiki ina tatizo kubwa sana la maji. Naishukuru Serikali tuko katika Miji 28 lakini tunacho chanzo kizuri cha Ikorongo kwa kipindi hiki cha shida ya maji, Serikali inasema nini kwa kutu-support ukizingatia upembuzi yakinifu umeshafanyika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sebastian Kapufi, Mbunge wa Mpanda Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa crisis ambayo tuko nayo sasa hivi ya ukame, vyanzo vyote ambavyo tunaviona bado vina maji mengi tunakwenda kuvitumia ili kuhakikisha tunakwenda kupunguza shida ya maji katika jamii zetu. Hivyo nitalichukua hili la chanzo cha Ikolongo na nitaagiza mara moja watu wetu ambao wako Mpanda kuhakikisha wanakifikia hiki chanzo na kuona kinatumika ipasavyo. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa suluhisho pekee la kumaliza changamoto ya maji Wilaya na Nkasi, Mkoa wa Rukwa ni maji kutoka Ziwa Tanganyika. Ningependa kufahamu mchakato huo umefikia wapi wa kutoa maji Ziwa Tanganyika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aida Khenani, Mbunge wa Nkasi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, matumizi ya Ziwa Tanganyika yapo kwenye mkakati wa Wizara na tayari baadhi ya maeneo tumeshaanza kuyatumia maji ya Ziwa Tanganyika. Hivyo kwa maeneo ya Nkasi na maeneo yote ambayo yapo karibu na Ziwa Tanganyika, tunaomba waendelee kuvuta subira tutakwenda na tutahakikisha chanzo hiki cha uhakika tunakitumia.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Hali ya upatikanaji wa maji katika Kata ya Makanya, Kwekanga na Kwayi ni mbaya sana na ukizingatia sisi hatuna matatizo ya vyanzo vya maji. Je, ni lini Serikali itapeleka maji kwa haraka iwezekanavyo katika kata hizo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kata hizi alizozitaja pamoja na Makanya zipo kwenye utendaji wa kiwizara. Naomba nitumie Bunge lako Tukufu kumwarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba nitasimamia kuhakikisha ndani ya mwaka huu wa fedha haya maeneo yanapata maji.
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru kwa kunipa nafasi hii. Jimbo la Mtwara Mjini ni jimbo ambalo kidogo lina shida ya maji, lakini niishukuru Serikali kwa kutuletea bilioni 19 kwa ajili ya usambazaji wa maji kwenye Jimbo la Mtwara Mjini. Hata hivyo, tumechimba visima toka mwaka jana na vile visima vitatu mpaka sasa hivi havina mwelekeo wowote. Je, ni lini Serikali itamaliza visima hivi ili wananchi wapate maji kwenye Jimbo la Mtwara Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nnaomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Mtenga, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nipende kupokea pongezi zake kwa Serikali kwa kazi kubwa ambayo imeshafanyika Mtwara. Kupitia visima hivi hata jana tumeongea na Mheshimiwa Mbunge, tayari nimeshawaagiza wale watendaji wetu pale Mtwara wanakwenda kulifanyia kazi na hili ni agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu, maeneo yote ambayo visima vilishachimbwa sasa hivi watendaji ni lazima kuvipa vipaumbele ili kuhakikisha vinasambaza maji kwenye maeneo yote ya wananchi.
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi. Je, ni lini Serikali itamalizia Mradi wa Bwawani katika Mji wa Karatu ili kukidhi uhitaji wa maji katika Mji wa Karatu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daniel Awack, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ameulizia kuhusu kumalizia mradi ambao tayari upo kwenye utekelezaji. Miradi hii tunapoianza inakuwa na ukomo wake, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutasimamia vizuri mradi ule ambao Mheshimiwa Waziri yeye mwenyewe ndio alifika pale na kutatua hii changamoto, hivyo tutasimamia kuhakikisha ndani ya muda wa mkataba mradi unakamilika.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, nina maswali mawili mafupi ya kuongeza: -

Mheshimiwa Spika, kupanda miti na kutunza miti ni mambo mawili tofauti. Hata hivyo, na mimi nilishiriki kupanda hiyo miti Wami-Ruvu. Je, kuna mpango gani ambao umewekwa madhubuti wa kutunza hiyo miti 96,500 iweze kustawi angalau asilimia 70?

Swali la pili; Chuo cha Kilimo SUA mnakishirikishaje katika utunzaji wa vyanzo vya maji na pia katika utunzaji wa uoto wa asili, hasa kwenye milima ya Uluguru ambako ndio kuna vyanzo vya maji ambavyo vimeharibiwa kwa wingi?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Charistine Ishengoma, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma ambaye pia ni Mwenyekiti wetu wa Kamati ambayo inafanya vizuri sana. Mheshimiwa Dkt. Ishengoma kama alivyosema naye alishiriki kupanda miti, hii miti sote tumepeana majukumu kuona kwamba haifi na itapona zaidi ya asilimia hizo 70 ambazo amezitolea mfano.

Mheshimiwa Spika, suala la ushirikishaji wa Chuo cha SUA Wizara tumekuwa tukishirikiana na wataalam mbalimbali katika makongamano na namna ya kuona tunabadilishana uzoefu. Hata hapa juzi tulikuwa na kongamano zuri pale Dar- es-Salaam, yote ni kuona kwamba, tunashirikisha wataalam mbalimbali ili tuweze kuona tunapata elimu nzuri kwa watendaji, vilevile kutoa elimu kwa wananchi kuona vyanzo vya maji inakuwa ni jukumu la wote, tunavitunza na vyanzo hivi vinabaki kuwa ni endelevu kwa sababu tuna miradi mikubwa ambayo inaendelea kutekelezwa kwa kupitia fedha za Wizara. (Makofi)
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na wimbi la uharibifu wa vyanzo vya mito ya maji katika Wilaya ya Namtumbo kutokana na mifugo. Vyanzo hivyo vya maji ndivyo vinatiririsha maji katika Mto wa Luwebu, mto mkuu ambao unakusanyika na kukutana na Mto Kilombero ambao una-form Mto Rufiji na maji yake yanaenda kwenye mradi wa umeme.

Je, Serikali inaweza kusaidia kwenda kudhibiti uharibifu wa mifugo katika vyanzo hivyo vya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maeneo haya yote anayoyataja tayari Bonde la Mto Ziwa Nyasa linafanyiwa kazi na tayari mipaka inaendelea kuwekwa ili kuzuia shughuli za kibinadamu kwa wafugaji na wale wanaofanya ukulima mdogomdogo.
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na mimi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mji wa Sikonge unategemea sana Bwawa la Maji la Utyatya ambalo lilijengwa mwaka 1959, kuna uchafuzi mwingi kwa kipindi kirefu, uchafu mwingi umeingia kwenye hilo bwawa. Mwaka 2017/2018 Serikali ilipanga shilingi milioni 400 kwa ajili ya kulisafisha hilo bwawa, lakini haikuleta fedha kwa sababu kuna maeneo ambayo yalitakiwa Halmashauri iweze kuyalinda vizuri na mpaka sasa hivi yameshalindwa vizuri.

Je, hizo fedha zitakuja lini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph, Mbunge wa Sikonge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, chanzo hicho tutaendelea kuja kukifanyia kazi na Bonde husika tayari limeshapewa maagizo. Nami kwa kupitia Bunge lako tukufu naomba niendelee kusisitiza Wakurugenzi wote wa Mabonde waweze kuwajibika kwa sababu vyanzo hivi ni mkakati wetu kama Wizara kuona kwamba, tunavilinda ili viweze kutuletea uendelevu wa miradi ambayo tunaendelea kuijenga. (Makofi)
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Spika, ahsante: -

Mheshimiwa Spika, kuna korongo la Mto Barai katika Kijiji cha Durgeda ambalo linaleta uharibufu katika chemchemi ya Mto Durgeda. Waziri alitoka mwezi huu wa Tatu katika neo lile alisema kwamba, utekelezaji ungeanza ndani ya mwezi mmoja.

Je, lini utekelezaji wa Mto huu Barai utaanza ili kuokoa chemchemi ya Mto Durgeda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daniel AwaCk, Mbunge wa Karatu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, korongo hili ni moja ya maeneo ambayo Bonde la Mto Pangani wanashughulika nalo. Hivyo, niseme tu kwamba, shughuli zitaendelea na sasa hivi wapo kwenye maandalizi wanakuja kutekeleza majukumu yao.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, mbali ya watu kuharibu mazingira, I mean miti na kadhalika kwenye vyanzo vya maji, kumekuwa na wimbi kubwa la watu kwenda kujenga kwenye vyanzo vya maji kwenye mito na maeneo mengine hatimaye kusababisha maji kushindwa kupita kwenye mikondo yake na wengine ni vigogo tu.

Je, Wizara yako kushirikiana na NEMC mna mkakati gani madhubuti wa kuhakikisha watu hawaendi kujenga kwenye vyanzo vya maji?(Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Bulaya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nampongeza Mheshimiwa Ester kwa kuweza kufuatilia vyanzo vyetu vya maji. Maeneo haya namna yanavyojengwa tunayafanyia kazi siyo tu na NEMC, tuna Wizara ya Kisekta sasa hivi tunapita huko. Moja ya shughuli tunayofanya ni kukataza na kuondoa wale wote ambao wamejenga kandokando ya vyanzo vya maji. (Makofi)
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwa namna ya pekee nitoe pongezi kwa Mheshimiwa Naibu Waziri na Waziri na Wizara nzima ya Maji kwa utekelezaji wa miradi hii aliyoitaja swali lake na majibu ni mazuri sana. Hivi sasa Kata ya Nanganga, Mumburu unatekelezwa mradi wa maji wa shilingi milioni 500, Ndanda shilingi milioni 400, Chiwata mradi unaendelea shilingi milioni 500. Hata hivyo, napenda kufahamu toka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba, wakati wa usanifu wa miradi ya Kata ya Mpanyani alipokuja Katibu Mkuu tulikubaliana kwamba Kijiji cha Mraushi patawekwa tenki. Je, ni lini kazi ya ujenzi wa tenki Kijiji cha Mraushi itaanza kufanyika?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kati ya Mwena na Liloya kuna mradi unaoendelea. Kwa bahati mbaya sana mradi huu unafanya kazi vizuri sana wakati wa mvua na wakati wa kiangazi haufanyi kazi vizuri, unahitaji tena kufanyiwa marekebisho. Je, ni lini Serikali itakwenda kuufanyia marekebisho Mradi wa Liloya-Mwena? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nipokee pongezi, nafahamu anayeshukuru anaomba tena, tutarudi Ndanda tutaendelea kufanya kazi pamoja Mheshimiwa Mbunge na nampongeza Mbunge kwa uwajibikaji wake mzuri.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa tenki tunautarajia ndani ya mwaka wa fedha 2022/2023 uweze kukamilika. Vile vile katika ule mradi ambao tayari unatoa huduma japo maji kidogo yana chumvi na wakati wa kiangazi inaleta shida, Mheshimiwa Mbunge hili tumeshaliongea mara nyingi, amefika ofisini na sisi tayari tumeshalifanyia kazi, tumeshatoa maagizo pale Mtwara. Kwa hiyo, litaendelea kuangaliwa kwa jicho la kipekee kuhakikisha wananchi wanakwenda kupata maji safi, salama na ya kutosha. (Makofi)
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Shule nyingi za sekondari na primary Mkoani Mara hazina miundombinu ya maji. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha miundombinu hiyo inawafikia ili kuepuka magonjwa ya milipuko? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ghati Chomete, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mara, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Ghati amekuwa ni mlezi mzuri sana wa watoto mashuleni na amefuatilia sana hili suala la huduma ya maji mashuleni. Naomba nitumie Bunge lako Tukufu kuwaagiza Viongozi wa Mkoa wa Mara kwa maana ya MD na RM wahakikishe wanapeleka maji mashuleni, hili tulishaagiza, ni ufuatiliaji na utekelezaji tu, hivyo waweze kufanya kuanzia sasa na mwaka ujao wa fedha. (Makofi)
MHE. MICHAEL M. KEMBAKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali langu ni kwamba, katika mji wetu wa Tarime Mjini tunacho chanzo cha Nyandurumo ambacho ndicho kinacholisha maji katika Mji wetu wa Tarime, lakini Nyandurumo hii ipo katika Kata ya Kenyamanyori. Wakazi wa Kenyamanyori hawana maji.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba, wakazi wa Kenyamanyori wanapata maji ili waweze kutunza chanzo hiki ambacho ni muhimu sana katika Mji wetu wa Tarime? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Spika ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Michael, Mbunge wa Tarime, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nampongea Mheshimiwa Michael, alishaniona katika hili. Sera ya Maji inataka vijiji vyote vilivyopo katika eneo la chanzo wawe wanufaika namba moja. Naendelea kutoa maagizo kwa MD na RMs waweze kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao. Tunakwenda kuhakikisha watu wote wanaopitiwa na mtandao wa bomba wananufaika na maji.
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Naomba niulize swali la nyongeza.

Ni lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Kata ya Kazuramimba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nashon, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miradi yote ambayo ipo kwenye utekelezaji, tunaendelea kwa kasi nzuri sana kuhakikisha inaisha ndani ya wakati. Mheshimiwa Mbunge kama tulivyozungumza, tutasimama kwa pamoja kuhakikisha mradi huu unaisha ndani ya wakati. (Makofi)
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Katika Kata ya Mbezi Juu, Mtaa wa Mbezi Mtoni na Sakuveda kuna changamoto kubwa ya maji. Ni lini Serikali itapeleka miundombinu hii ili wananchi waweze kupata huduma hii? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Felista Njau, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, sisi lengo letu ni kuona tunatua akinamama ndoo kichwani na Mheshimiwa Felista amefuatilia hili, ameshaongea nami. Kama tulivyozungumza, mantahofu, haya maeneo yote maji yatapelekwa na tunataka kuhakikisha ukifika mwaka 2025 maeneo yote ya vijijini yatapata maji kwa asilimia 85 na asilimia 95 kwa maeneo ya mijini. (Makofi)
MHE. ALEXANDER P. MNYETI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo langu siyo kubishana na Mheshimiwa Waziri kuhusu asilimia zinazopatikana pale Misasi. Kwa mtizamo wangu kwa sababu naishi huko, kutoka asilimia 40, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Waziri kwamba upatikanaji wa maji Misasi ni chini ya asilimia Nne hakuna maji, watu wanatafuta maji, hakuna maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Mkandarasi aliyetekeleza mradi huu naweza nikasema ni kandarasi ya kitapeli, na Wizara imerithi miradi mingi ya kitapeli ya sampuli hii kwenye Taifa letu. Wakandarasi wanachukua fedha, lakini hawatekelezi miradi iliyokusudiwa kulinga na mkataba. Mradi huu tangu mwaka 2013 leo ni miaka tisa, kupeleka maji kilomita 15 kutoka chanzo cha maji, imekuwa ni stori za hapa, stori za pale, stori za kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, ni lini upo tayari twende Misasi ukawaeleze hizi stori wananchi wa Misasi wewe mwenyewe kwa sababu Wabunge tumeshachoka, tumeshayaeleza mambo haya kila siku, mradi huu umesimama, Mkandarasi haeleweki, fedha ameshachukua, hakuna kinachoendelea site.

MWENYEKITI: Haya ahsante.

MHE. ALEXANDER P. MNYETI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, ni lini mtaanza kuyafuta makandarasi ya namna hii kwenye Taifa letu, kwa sababu tumejaribu kufuatilia, Mkandarasi huyu kote alikotekeleza miradi hii yote ni feki, hakuna anachokifanya anachukua fedha.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Alexander Mnyeti, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameuliza lini kufuatana na mimi mara baada ya Bunge hili tutakwenda kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na Wakandarasi feki, tayari Wizara imeshughulika nao ipasavyo, huyo unayemuongelea tutaendelea kumfuatilia pia tufanye kama tulivyofanya kwa wengine. (Makofi)
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa maji kutoka mto Mavuje, kuelekea katika miji ya Kilwa Masoko na Kilwa Kivinje, ni lini utaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mbunge wa Jimbo la Kilwa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ni mradi muhimu sana kwa Jimbo la Kilwa na tunafahamu namna ambavyo Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifuatilia kwa karibu sana. Mheshimiwa Mbunge mradi huu tunakwenda kuutekeleza mwaka ujao wa fedha.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesimama hapa kwa ajili ya mradi mmoja tu, mradi wa Mwanga, Same, Korogwe. Ukitaja Moshi, katika Mkoa wa Kilimanjaro, Mji mkubwa unaofuata ni Same, lakini takribani ni miaka kadhaa toka tumepata uhuru same haijawahi kupata maji safi na salama na wanaogea maji ya kununua mpaka leo.

Je, ni lini sasa ule mradi ambao tuliambiwa ungekamilika mwaka jana Septemba utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally, Mbunge Viti Maalum kutoka Kilimanjaro kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu wa Same -Mwanga ni mradi ambao ni mkubwa na umetumia fedha nyingi na sisi kama Wizara tumefuatilia kwa karibu na tayari kazi zinaendelea. Hivyo nipende kusema mradi huu utakamilika ndani ya wakati kwa namna ambavyo usanifu unaonesha.
MHE. DKT. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, umenipandisha cheo nafaa kuwa profesa, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Miji 28 ni mradi ambao ulikuwa unaifaidisha sana Geita Mjini na Geita Vijijini, lakini kila tukiuliza hapa tunaambiwa tunakamilisha makaratasi.

Je, Mheshimiwa Waziri, ni lini mradi wa Miji 28 ambao unalifaidisha Jimbo la Geita kwa Kata utaanza? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daktari Musukuma kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya Miji 28 tayari tumefikia hatua nzuri sasa ya manunuzi na mradi huu unaelekea kwenye utekelezaji kabla ya mwezi Juni, 2022.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitoa takwimu za upatikanaji wa maji kwenye maeneo yote takribani nchini ambazo hazina uhalisia. Sasa ni lini Serikali itafanya rejea ili iweze kuja na uhalisia wa upatikanaji wa maji kwenye maeneo yetu nchini kuliko ilivyo sasa hivi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la takwimu, ni suala la pana, pale tunaposoma takwimu 40 percent, maana yake kuna calculation zinazofanyika, zinazojumuisha mtandao wa mabomba, pamoja na namna ambavyo ukubwa wake umefikia katika eneo la usambazaji. Hivyo masuala ya takwimu, katika mifumo ya usambazaji wa maji yanahesabu zake, lakini kikubwa ninachoweza kusema tusiangalie tu hii takwimu, angalieni kazi inayofanywa na Wizara ya Maji, mabadiliko ni makubwa, mageuzi ni makubwa na tutaendelea kuwafikia wananchi wote kutoa huduma safi ya maji safi na salama. (Makofi)
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Nataka kufahamu Je, Serikali ni kwa kiwango gani inatakeleza mkakati wa hifadhi na matumizi endelevu ya maji, kama vile kujenga au kutengeneza miradi ya uvunaji maji ya mvua kama vile ilivyoainishwa kwenye ukurasa 36, 37(a)(3) cha Ilani ya Chama cha Mapinduzi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zainab Katiba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miundombinu ya mabwawa ndani ya Wizara ya Maji, kwa sasa tuna mabwawa Sita ambayo yako kwenye utekelezaji, lakini tuna sanifu mbalimbali ambazo zinaendelea na nyingine zimekamilika na katika utekelezaji huo, tayari tunatarajia kuwa na bwawa kubwa la Kidunda, ambalo wenzetu wa DAWASA chini ya uongozi wa Cyprian tayari wamepata kibali cha kuweza kwenda kumpa kazi Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri na hawa wote wameshaenda kuoneshwa site na tunarajia lile Bwawa la Kidunda liweze kuwa ukombozi mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa hapa Dodoma Bwawala Farkwa na lenyewe pia tunaendelea kulifanyia kazi ili liwe ni jibu sahihi la miradi kuwa endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo yote ya nchi tunatarajia kuchimba mabwawa mengi. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameweza kuruhusu zaidi ya shilingi bilioni 34 tunazitumia kwa ajili ya kuleta mitambo seti Nne kwa ajili ya kuchimba mabwawa, vilevile seti 25 za kuchimba visima na seti za kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi ziko nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya mitambo hii yote kuwasili nchini Waheshimiwa Wabunge, tutafikia Majimbo yote kwa urahisi na suala la kuvuna maji ya mvua litapewa kipaumbele na kuona kwamba linaenda kuleta uendelevu wa miradi.
MHE. PHILIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana niweze kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maji imekuwa ikijipambanua vizuri sana kwamba inafanya vizuri na sisi tumeona lakini wana mapungufu mengine ni makubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi navyosema Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, miradi mingi inachelewa kwa sababu RUWASA hawana tender board. Bodi ya manunuzi haipo kabisa katika Mikoa hiyo na hii inasababisha miradi mingi inachelewa. Hivi navyosema Jimboni Songwe miradi mingi toka mwaka jana imesuasua kwa sababu tenda bodi ya pale Mkoani haipo na wanatumia tenda bodi ya kwa RAS pale.

Je, ni lini Serikali sasa itawezesha Mikoa kuwa na bodi ya manunuzi ili miradi iweze kuharakishwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Philipo Mulugo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, inapendeza wote tukiwa na ufahamu wa pamoja kwamba hizi bodi huwa zina ukomo wa muda wake, bodi nyingi zime-expire muda wake, tayari Mheshimiwa Waziri ameaanza kufanyia kazi na maeneo yote yatapata boards ambazo zitaharakisha utendaji wa kazi zetu.
MHE. DANIEL B. SILLO: Mheshimiwa Spika, ahsante, ninaomba Mheshimiwa Naibu Waziri afanye mawasiliano na wataalam wake wa maji wanaohusika na eneo husika, kwa sababu taarifa anazosema nadhani haziko sahihi na ambazo ninazo. Amesema kazi zinazofanyika labda angesema kazi zitakazofanyika kwa sababu mradi huo kwa sasa umeishia Kata ya Magugu.

Mheshimiwa Spika, la pili; miradi yetu ya maji mingi inachelewa kwa kuwa na utaratibu wa manunuzi ambao huchukua muda mrefu sana.

Sasa Wizara ina mpango gani wa kuboresha kitengo hicho cha manunuzi ili mradi uweze kukamilika kwa wakati? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Daniel Sillo, Mbunge wa Babati Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala la kuwasiliana na watendaji naomba nilipokee na nitalifanyia kazi kwa karibu sana kuhakikisha kazi zote zinafanyika kwa wakati kama ambavyo inapaswa.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusu uboreshwaji wa hatua za manunuzi, Kiwizara tunaendele kuhakikisha tunatumia taratibu ambazo hazitachelewesha miradi na pale itakapobidi basi ushauri tunapokea na tutafanyia kazi. (Makofi)
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru sana kwa majibu ya Serikali; lakini naomba nitoe ombi moja, kwamba niombe waharikishe sana kuweza kupatikana kwa huyo mkandarasi ili kuweza kuwapunguzia adha ya maji wanawake wenzangu wa Mji wa Tunduma, Mji wa Vwawa pamoja na Mji wa Mlowo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitakuwa na swali moja la nyongeza. Hali ya upatikanaji maji katika Wilaya ya Songwe ambayo ina kata 18 ikiwepo Kata ya Mkwajuni, Kata ya Saza pamoja na Galula sio ya kuridhisha, naomba nipate kauli ya Serikali kwamba ina mpango gani wa kuboresha hali ya upatikanaji maji katika Wilaya ya Songwe, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Juliana Shonza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nipende kupokea pongezi zake, nawe nakupongeza kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa masuala ya maji ili kuhakikisha mwanamke anatuliwa ndoo kichwani.

Mheshimiwa Spika, kuharakisha kupata mkandarasi, hii ni moja ya jitihada tunayoifanya Wizara. Nikuombe Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana kuhakikisha tunakwenda sambamba na lengo la kumtoa mama ndoo kichwani linakamilika kwa wakati. Maeneo ya Wilaya ya Songwe, Mkwajuni na Kisasa, tayari Serikali inaendelea na jitihada mbali mbali kuhakikisha matatizo ya maji katika maeneo haya tunakwenda kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, miezi michache iliyopita gari la uchimbaji visima lilikuwa kule Wilayani Songwe na liliweza kufanya kazi ya uchimbaji visima katika maeneo kadhaa. Kazi hii itaendelea, lengo ni kuona visima vile tunavipata, tupate vyanzo vya maji ili tuweze kusambaza maeneo yote ambayo bado yanaathirika na tatizo la maji. (Makofi)
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Wizara inafahamu kwamba baadhi ya maeneo mtandao wa maji haujafika; je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapatia maji wananchi hawa kwa dharaura?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Naibu Waziri yupo tayari kuongozana nami kwenda kuona adha kubwa wananchi wa kata hizi wanazopata katika kukosa maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali yake mawili, Mheshimiwa Abdallah Chaurembo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mkakati wa dharura, mara zote DAWASA imekuwa ikijitahidi kuona inafanya kila linalowezekana wananchi wasikose maji kabisa, lakini nawaomba uvumilivu kwa sababu visima tisa ambavyo tunatarajia kuja kuvichimba katika maeneo yale ya Kimbiji; na tutajenga tenki kubwa maeneo ya Lugwadu la Shilingi milioni 15. Haya matatizo yatakoma kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa hivi jitihada ndogo ndogo zinazoendelea kufanywa na DAWASA, naomba tuendelee kuwavumilia. Kuongozana nawe ni sehemu ya majukumu yangu, hakuna neno, tutakwenda kufanya kazi. (Makofi)
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Jiji la Mwanza hususan Manispaa ya Ilemela inakabiliwa na tatizo la maji. Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua visima virefu vya maji ambavyo havifanyi kazi kwa muda mrefu; mfano, Nsumba Kata ya Kiseke, Mtongo Kata ya Kayenze, Lugeye Kata ya Sangabuye na Kisami Kata ya Bugogwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Furaha Matondo, Mbunge Viti Maalum Mwanza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli maeneo haya aliyoyataja hususani eneo hili la Jimbo la Ilemela kwa Mheshimiwa dada yangu Angelina Mabula tayari tumeanza kazi ya ufufuaji wa visima. Tayari visima viwili vimeweza kufufuliwa na kazi zinaendelea kuhakikisha visima vyote ambavyo bado vina maji ya kutosha tunakwenda kuvifufua.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii, katika mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 520 wa Mkoa wa Arusha kuna baadhi ya kata ya wilaya ambazo mradi huu unapita lakini maji hayajasambazwa katika Wilaya ya Arumeru na Arusha Mjini.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kusambaza maji kwenye maeneo haya?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi huu ni mkubwa na umetumia fedha nyingi na tunatarajia tija iwe ni kubwa maeneo yote ambayo mradi unapita lazima maji yatawafikia. Naomba niwe nimelipokea na kuhakikisha nalifuatilia kwa karibu maji yaweze kuwafikia kwa haraka.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, siko mbali sana na swali alilouliza mtu wa Mbagala kwa sababu kata ulizozitaja ndiyo mtandao huo huo wa Kata ya Buza, Makangarawe, Sandali na Vituka. Tunaomba na sisi maji haya yaweze kusambazwa kule kwetu.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba niseme nimepopkea, maji yatafika.
MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kuniona. Mradi wa maji wa Matwiga phase one ni wa muda mrefu na unakwenda kwa kusuasua. Je, ni lini Serikali sasa itaukamilisha mradi huu ili wananchi wa Kipembawe waweze kunufaika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi huu unafanyiwa kazi kwa jitihada kubwa sana, Mheshimiwa Mbunge naomba uendelee kuwa na subira kidogo, mambo mazuri yanafika pale.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, Wilaya ya Makete mlitupatia shilingi bilioni 1.7 za mradi wa maji kutoka Lumage kwenda Madihani na kutoka Usalimwani kwenda Mfumbi, mkandarasi hajafika hadi leo.

Ni ipi kauli ya Serikali dhidi ya mkandarasi huyu ambaye anaigharimu Serikali hadi sasa kwenye suala la maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Festo Sanga, Mbunge wa Makete kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, sisi kama Wizara tulishatoa tamko kwa wakandarasi wote ambao watataka kuturudisha nyuma watarudi wao. Mheshimiwa Mbunge nafuatilia mkandarasi huyu sababu zilizompelekea kutofika, mimi na wewe naomba tukutane baada ya Bunge hili tuweze kufanyia kazi.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Katika maeneo yenye changamoto kubwa sana ya maji ikiwemo ni Jimbo la Mtwara Vijijini, je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inaondoa kero hii ya maji katika Jimbo la Mtwara Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Shamsia, Mbunge wa Mtwara Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge naamini unafahamu jitihada ambazo zinafanywa na Wizara katika eneo lako na tumeshaongea mara nyingi, Mheshimiwa Mbunge naomba tuendelee kuwasiliana kama unavyofanya tutakuja kuhakikisha maji yanafika maeneo yote ambayo tayari miradi inaendelea.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, kuna utekelezaji wa maji katika miji 28, ningependa kufahamu ni jambo gani linakwamisha uwezeshaji wa utekelezaji wa mradi huu hadi hivi sasa haujaanza katika miji 28?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Yahya Mhata kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi wa miji 28 kimacho unaweza ukaona haujaanza lakini tayari wakandarasi walifika maeneo yote na tayari wanaendelea kufanya kazi ambazo siyo za site lakini kuanzia Februari hii tunatarajia wakandarasi wengi kuja kuanza kuwaona huko kwenye site na kufanya kazi zile zinazoonekana kwa macho moja kwa moja.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Jimbo la Kigoma Kusini vipo vijiji vilivyopakana kabisa na Ziwa Tanganyika lakini vijiji hivyo havijapatiwa maji. Ni mpango upi wa Serikali kuvipatia vijiji hivyo vinavyopakana na Ziwa Tanganyika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maeneo haya anayoyatamka Mheshimiwa Mbunge tayari jitihada zinafanyika na sisi kama Wizara tunatamani kuona tunatumia vyanzo vya uhakika kwa miradi yetu kwa hiyo vijiji hivi ambavyo viko pembezoni mwa Ziwa Tanganyika navyo ni sehemu ya maeneo ambayo tunaendelea kuyawekea mkakati wa kupata maji.
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Spika, Vijiji vya Kata ya Mkundi, Nanyanga pamoja na Mchichira, Wizara ilileta mitambo ya kuchimba maji na maji yakapatikana lakini mpaka leo wananchi wale hawajaanza kuyatumia maji yale. Je, ni upi mpango wa Serikali kuhakikisha inaleta vitu ili wananchi waweze kutumia maji.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Katani Katani kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuchimba kisima ni hatua moja, baada ya hapo tunakuja sasa kwenye usambazaji. Hivi punde tutajitahidi kuhakikisha visima hivi vilivyochimbwa siyo tu kwenye eneo lako hata pale Mtwara mjini tuna visima tulishachimba na sasa tunaelekea sasa kwenye utekelezaji wa usambazaji Mheshimiwa Mbunge.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na jitihada kubwa ambayo Serikali imefanya ya kutupa mkandarasi Palemon kwa ajili ya maji katika Kijiji cha Puulu, Songambele na Ngee. Mkandarasi huyu ana zaidi ya miezi mitano toka alipoonyeshwa mradi hajaonekana kabisa, wananchi wanalalamika, nini kauli ya Serikali kuhusu mkandarasi huyu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Stella Manyanya, Mbunge wa Nyasa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, naomba kutumia Bunge lako Tukufu kusema wakandarasi wote ambao hawajafika kwenye maeneo ya kazi wafike mara moja kadiri ya mikataba yao inavyowataka. Nje ya hapo sisi kama Wizara tutachukua nafasi yetu na wasije wakatulaumu.
MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake, lakini pia nina swali la nyongeza kwamba, wana mkakati gani wa kuwachukulia hatua wale wananchi ambao wanaharibu kwa makusudi miundombinu ya maji tukizingatia mahitaji ni makubwa ya wananchi mjini na vijijini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Tauhida ambalo limeulizwa kwa niaba yake: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipokee pongezi lakini mkakati ambao tunaendelea nao ni kuchukua sheria. Sheria ziko bayana, kwa hiyo yoyote ambaye atakutwa sheria itafuata mkondo wake.
MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha usanifu wa matenki na michoro ya miundombinu katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria inayoenda katika Miji ya Urambo, Sikonge na Kaliua inaisha? Kwani usanifu huu ulitakiwa uishe Desemba, 2022 na ukizingatia Miji hii tayari ipo kwenye exemption ya kodi ili Mkandarasi aweze kwenda site na wananchi wa maeneo haya waweze kupata maji kwa urahisi. Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jacqueline, Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, usanifu ulipaswa kukamilika Desemba na sasa ni Januari, tuko mwishoni kabisa kukamilisha na lengo letu ni kuhakikisha dhumuni la kupeleka maji maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge tunakwenda kukamilisha kwa wakati.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ikiwa wananchi wanapoharibu miundombinu ya maji wanachukuliwa hatua, je, ni ipi kauli ya Serikali pale ambapo miradi au miundombinu inapokuwa imekamilika watu wa mwenge wanapokuja kuzindua mradi, maji yanatoka lakini baada ya wiki mbili, hakuna maji tena, mnachukua hatua gani kwa udanganyifu wa wakandarasi wao ambao wanaidanganya jamii na hakuna maji na limekuwa ni jambo ambalo limezoeleka kwenye miradi mingi ya maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Condester, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, udanganyifu wa aina hii Mheshimiwa Waziri alishaukomesha kwa kutuma vikosi kazi kuhakikisha mradi kama umezinduliwa unabaki kuwa endelevu. Nitafuatilia mradi huo anaouongelea Mheshimiwa Mbunge kujua tatizo ni nini ili kuhakikisha huduma iliyokusudiwa inapatikana.
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza: Sambamba na visima hivi viwili kuchimbwa Mpwapwa Mjini, lakini mwaka wa 2021 kilichimbwa kisima kimoja katika Shule ya Sekondari ya Berege na mpaka sasa hivi akijaanza kufanya kazi: Je, ni lini kisima hiki nacho kitaanza kutoa huduma kwa wanafunzi wale wa Shule ya Sekondari ya Berege?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kwamba, kuna Miradi mitatu ya maji inatekelezwa katika Jimbo la Mpwapwa katika Kata ya Ving’hawe, Lupeta na Kijiji cha Igojiwani Kata ya Mima, lakini kasi ya utekelezaji wake imekuwa hafifu; je, nini tamko la Wizara kuhusu utekelezaji hafifu wa miradi hii? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge George Malima, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kusema, miradi yote ambayo imeanza kutekelezwa Waheshimiwa Wabunge ni lazima ikamilike.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu ambao utekelezaji wake Mheshimiwa Mbunge George ameuona ni hafifu, tutausimamia. Mradi namna mkataba umesainiwa tutajitahidi ukamilishwe ndani ya wakati. Kwa kisima kilichochimbwa shuleni, pia ni moja ya mikakati ya Wizara kuhakikisha maeneo kama haya ya shule au hospitali na vituo vya afya yanapata huduma ya maji safi na salama bombani. Hivyo kisima hiki kilichochimbwa pia tunakuja kukifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa agizo kupitia Bunge lako Tukufu, Watendaji wa Mkoa wa Dodoma wanaofanya kazi maeneo haya, wahakikishe wanatoa hizi sintofahamu haraka iwezekanavyo.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Wananchi wa Kijji cha Kigorogoro Kata ya Kibale kwa muda mrefu walikuwa na changamoto ya maji ya kisima. Kilichimbwa kisima, lakini kilipoanza kutoa maji, yakawa ni maji yenye chumvi kali wananchi wakashindwa kuyatumia. Naomba kuuliza swali: Ni lini wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro watachimbiwa kisima kingine ambacho hakina maji ya chumvi, ukizingatia wapo kwenye ukanda wa Mto Kagera? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo ambalo kisima kimechimbwa na maji yakaonekana siyo rafiki kwa matumizi ya binadamu huwa tunayaacha na kutafuta mbadala wake. Ninaamini maeneo hayo watendaji wahusika wanaendelea kutafuta eneo mbadala na maji safi na salama lazima yaweze kuwafikia wananchi wa Kigorogoro.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kupeleka maji katika Kata ya Kwai, Kwekanga pamoja na Makanya?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Shekilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kata hizi alizozitaja Mheshimiwa Mbunge Shekilindi, nimeongea naye juzijuzi na nimemhakikishia kwamba kazi hii tutaenda kuifanya. Tumeshakubaliana kwamba tunakwenda kuangalia mradi na tutahakikisha unatimizwa kufanyiwa kazi yake kwa wakati.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Napenda kuuliza, katika Wilaya ya Meatu tuna shida sana ya maji. Kwa Mkoa mzima wa Simiyu Wilaya ya Meatu inaongoza: Je, ni lini Serikali italeta maji safi na salama katika Wilaya Meatu ili wananchi wa kule wanufaike? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Simiyu una bahati sana. Una mradi mkubwa ambao unaenda kutekelezwa kwa kutumia kigezo cha mabadiliko ya tabia ya nchi. Mradi ule utafikisha maji maeneo ya Meatu, Maswa na maeneo yote yaliyo karibu kuhakikisha wananchi wanapelekewa maji safi na salama. Nafahamu Mheshimiwa Minza nawe pia umefuatilia sana suala hili, na nilifika Meatu na tunaendelea na kazi. (Makofi)
MHE. NOAH L. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kuna mradi wa vijiji tisa vya Oldonyo Sambu, Lengijave na Oldonyo-Wass ambao wanasumbuliwa na maji ya fluoride na imekuwa ikisuasua utekelezaji wake: Je, ni lini sasa Serikali itatoa fedha za kutosha kwa ajili ya kukamilisha mradi huu ambao wananchi wanateseka na maji ya fluoride? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Noah, Mbunge wa Arumeru, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tulipata tatizo na changamoto hii bado ipo, lakini sisi kama Wizara tayari tuna hatua mbalimbali tumeshazichukua na fedha tunatarajia mgao ujao. Mheshimiwa Mbunge nawe katika mradi ule tutapata. Lengo ni kuona tunatekeleza miradi mikubwa ambayo maeneo yake, maji yake chini hayana fluoride ili tuweze kunusuru watoto wanaoweza kuzaliwa na ulemavu na watu wote ambao wanateseka na maji yenye fluoride. (Makofi)
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona, niulize swali dogo moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya Jimbo la Kibamba maeneo ya King’azi A, B na maeneo ya Manzese Malamba Mawili ni maeneo ambayo wananchi wanaendelea kukosa maji safi na salama kwa kutumia maji ya chumvi ya visima vifupi; na ahadi ya Serikali ni kujenga tenki kubwa la ujazo siyo chini ya lita milioni kumi pale Kilimahewa: Je, ni lini sasa Serikali itaanza kutekeleza mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mtemvu, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tenki lipo kwenye hatua za mwisho kabisa kuja kuanza kutekelezwa, usanifu umekamilika. (Makofi)
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi ya swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna changamoto kubwa sana ya maji kwenye Kata ya Mtambula katika Jimbo la Mufindi Kusini; je, Serikali haioni wakati umefika sasa kuwapelekea maji sasa wananchi wa kata hii?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tayari tumeona umuhimu na tupo katika taratibu za kuhakikisha hayo maeneo uliyoyataja Mheshimiwa Mbunge, tunayaletea maji safi na salama yakiwa bombani.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi hii. Naomba nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake haya, nimkumbushe tu upatikanaji wa maji ni jambo moja, lakini upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wetu ni haki yao ya msingi na wanahitaji maji haya safi na salama muda wote.

Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha mikakati hii ya kusafisha maji katika Wilaya ya Arumeru ili wananchi wetu waweze kupata maji safi na salama? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kwa kuwa madhara ya madini haya ya fluoride ni makubwa sana kwa wananchi wetu yanayopelekea kupata udumavu na ulemavu.

Je, Serikali haioni sasa haja ya kuanzisha program maalum kwa ajili ya kuwatibu wananchi hawa? Ahsante (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nipokee pongezi zake, lakini vilevile naye nimpongeze kwa namna ambavyo ni mfuatiliaji mzuri na kwa sababu ni mama ndiyo maana anaongelea hata masuala ya ulemavu kwa watoto kwa sababu ni kweli watoto wanaathirika na watu wazima pia. Kama Wizara tunaendelea na utaratibu wa kuona namna njema ya kuwa sehemu ya kuwafariji hawa walioathirika na madini ya fluoride.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la lini mradi huu utakamilika. Tayari mradi upo katika utekelezaji, mradi mkubwa ambao utaleta maji katika maeneo yote ambayo yameathirika. Sasa hivi tunatarajia tu mgao ujao wa fedha tuendelee kuleta fedha katika Jimbo la Arumeru.
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante; je, ni lini Serikali itajenga mtambo wa kusafisha na kutibu maji katika Chanzo cha Mgombezi - Ilula?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nyalusi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chanzo cha Mgombezi ni moja ya vyanzo muhimu sana katika eneo la Iringa. Katika mwaka ujao wa fedha tuna mradi mkubwa sana wa USD Million 88.4. Kupitia mradi huu tunatarajia chanzo kile pia kiwe sehemui ya wanufaika kwa kupata eneo la treatment plant, lakini vilevile maeneo ya Kilolo pia yatapata kunufaika na tunatarajia pia kuwa na uboreshaji wa huduma ya maji safi na maji taka katika eneo la Iringa.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa kutibu maji ni gharama sana ili yafikie hatua ya kuwa maji safi na salama na wananchi kuyatumia kwa uhakika, lakini maji hayo hayo yanayogharamiwa sana na Mamlaka za Maji na RUWASA na wote ambao na Wizara pia yanatumika kuonyeshea magari, yanatumika kwenye kuzima moto, yanatumika kwenye kufrashi vyoo.

Je, ni lini sasa Serikali hii ya Tanzania italeta mpango mzuri wa kutumia maji safi na salama kwa ajili ya wananchi na maji hayo mengine kwa ajili ya takataka? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Wizara ni kuhakikisha maji yote ambayo yanatumia gharama kubwa katika kuyatibu yaweze kutumika kwa matumizi sahihi ya majumbani na kwa kazi kama alizozitaja za uoshaji wa magari, tayari Wizara tuna mpango wa kuona kwamba raw water, maji ambayo bado hayajatibika yaweze kutumika.
MHE. MWANTUM M. ZODO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Wananchi wa Wilaya ya Handeni Mjini wanapata maji kutoka kwenye Kisima cha Nderema ambao ni Mradi wa Serikali, tunaishukuru sana Serikali. Hata hivyo, kisima hicho maji yake yana chumvi sana, je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha wanaenda kuchuja maji yale ili yawe maji safi na salama?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zodo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kisima chochote ambacho kimechimbwa na maji yake bado yana tope Serikali kupitia Wizara tumeendelea na mipango madhubuti ya kuhakikisha tunapata treatment plant kwenye maeneo hayo, hivyo Mheshimiwa Mbunge, pamoja na hiki kisima ulichokitaja na chenyewe kipo kwenye Mpango wa kuweza kujengewa treatment plant. (Makofi)
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kama chujio limekamilika kujengwa, kwanini maji yanatoka machafu na wakati mwingine wananchi wanashindwa kuyatumia?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; Mkataba wa uboreshaji wa miiundombinu ya maji katika Manispaa ya Mtwara Mikindani wenye thamani ya Shilingi bilioni 19 ulisainiwa mbele ya Mheshimiwa Waziri. Nataka kujua utekelezaji wake umefikia hatua gani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tunza Malapo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la maji kutoka machafu baada ya ukamilishaji wa chujio ni suala la kiufundi. Ni sehemu chache ambapo mabomba ni chakavu wakati fulani bado yanaleta udongo kwa ndani lakini tayari watendaji wetu wanalifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mkataba kusainiwa mbele ya Mheshimiwa Waziri uko sahihi, tayari Shilingi bilioni 19 zimetengwa, Mkandarasi ameshapatikana, yuko kwenye mobilization, anafanya uandaaji wa site na hivi punde atalipwa advance payment ili kazi zianze.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali kwa majibu mazuri, lakini niongezee nyongeza moja kwamba hadi leo hii lile eneo ambalo tulilizungumza na liliuliziwa swali, Serikali imetekeleza vizuri na limeziba lile eneo, kwa hiyo tunawapongeza sana. Swali moja dogo la nyongeza; kwa kuwa wakulima wa bonde hilo walikuwa wanazuiwa kuendeleza shughuli zao za kilimo katika maeneo hayo kutokana na Mto Ruvu kupungua kasi yake ya maji na sasa eneo lile limeshazibwa.

Je, Serikali inampango gani sasa wa kuwasaidia wakulima wale waendelee na shughuli zao za umwagiliaji mdogo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipende kushukuru kwa kupongeza jitihada kubwa ambayo taasisi ya DAWASA imeweza kufanya na sasa maji hayatapakai tena. Vile vile Serikali ina mipango mbalimbali kuhakikisha suala la maji kuchepuka kutoka kwenye mto tunakwenda kulidhibiti. Hili tutalifanya kwa kutumia Bonde la Maji ya Wami-Ruvu na tayari wameshapata mhandisi mshauri ambaye anafanya usanifu kwa ajili ya kujenga bomba kuu moja ambalo wananchi watapaswa kujiunga katika kikundi kimoja ili waweze kuhudumiwa kwa sehemu moja halafu wao sasa ndio watachepusha kwenye maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuipatia Wizara fedha. Tayari tumeshaingiza mitambo ya kuchimba mabwawa na tunatarajia kama Wizara tuweze kuchimba mabwawa madogo madogo ambayo nyakati za mvua tutaweza kuvuna maji, tutayahifadhi pembezoni mwa mto huko ili wananchi waweze kuja kuyatumia kwa ajili ya umwagiliaji na wasiweze kudhuru mto katika shughuli za kuleta chanzo cha maji kwa shughuli za kibinadamu.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Vijiji vya Changarawe katika Kata ya Masanze na Vijiji vya Malangali, Muungano, Mamoyo, Kibaoni na Maluwi katika Kata za Tindiga na Mabwerebwere mito yake imepoteza mwelekeo, inahatarisha maisha ya watu. Sasa nilikuwa naomba kuuliza Serikali;

Je, ni madhara kiasi gani kwa wananchi wetu yatokee ili Serikali ichukue hatua?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, aaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dennis Londo (Mb) kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba, ni kiasi gani cha madhara ili Wizara iweze kuchukua hatua. Wizara hatusubiri madhara lakini tayari tunachukua hatua kwa kutimiza majukumu yetu kuhakikisha maji hayawi laana, maji ni neema. Maeneo ambayo maji yanachepuka na kusababisha maeneo ya wananchi kuvamiwa tayari tumeyapa kipaumbele. Kwa maeneo aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge, hasa Mto Miombo ambao unasababisha madhara kwenye kata alizozitaja ya Masaza, Masava na nyingine tayari mkandarasi yupo site anafanya utafiti. Lengo ni kuona maeneo yote ambayo yanaathirika na maji yanapochepuka kwenye mto hasa nyakati za masika tunakwenda kuyadhibiti, yanaenda kutumika vizuri kwa shughuli za kibinadamu. Shughuli ambazo zinafanyika na wananchi hawa za mboga mboga, kilimo kidogo kidogo basi yote yatajengewa miundombinu rafiki ili kulinda mto kwa sababu kulinda vyanzo vya maji ni jukumu letu sote.
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nikiri kwamba nimelipenda sana jibu la Serikali, lakini zaidi ya hapo naomba niulize swali moja tu la nyongeza.

Kwa kuwa ni miaka 55 iliyopita tangu mradi huu ambao tunautumia sasa ulipojengwa na kwa kuwa walipoujenga mradi huu, chanzo cha maji kilikuwa kimoja kwa sababu Kata ya Kihurio ilikuwa na vijiji viwili tu na kwa kuwa sasa hivi Kata ya Kihurio ina vijiji vitano na population imekuwa kubwa sana takribani watu zaidi ya 10,000.

Je, Serikali haioni kwamba itakapojenga mradi huu mpya, ijenge vyanzo vya maji ambavyo ni zaidi ya chanzo kimoja?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anne Kilango kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru kwa kuridhika na majibu ya Serikali, lakini vilevile nikupongeze kwa ufuatiliaji wa eneo hili la Kihurio.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Wizara kila ongezeko linapotokea la watumia maji, tunaboresha vyanzo na intake zetu hivyo Mheshimiwa Mbunge hili nimelipokea na tutalizingatia wakati tunatekeleza mradi huu mkubwa.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Kwanza niishukuru Serikali kwa kuchimba maji katika Mradi wa Dambia na yanapatikana kwa wingi.

Je, Mheshimiwa Waziri lini mnajenga Mradi ule wa Dambia ambao unaufahamu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Massay kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tumeshachimba kinachofuata sasa ni hatua za usambazaji. Mradi huo ulioutaja ujenzi wake mara tukipata fedha tunakuja kuanza mara moja.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, ningependa kujua mpango wa Serikali kutumia chanzo cha maji ya Ziwa Nyasa kuhudumia wananchi wa Kata ya Ruhuhu na Manda kwa sababu wananchi hawa wanaliwa sana na mamba hasa Kitongoji cha Panton?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Kamonga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, matumizi ya Ziwa Nyasa kama chanzo endelevu tayari tuna miradi ambayo tumeanza kuitekeleza ukanda wa Nyasa pamoja na Ruhuhu. Tunafahamu eneo ambalo wananchi walikuwa wakiliwa na mamba na tayari tulishaagiza RM Njombe ameanza usanifu na anakuja kutekeleza.
MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kuiuliza Serikali; je, ni lini italeta mradi wa maji kwenye Tarafa ya Ngerengere?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Taletale kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Ngerengere ipo kwenye mpango wa Wizara, Mheshimiwa Waziri alishapita maeneo hayo. Mheshimiwa Mbunge tuko mbioni kuleta mradi huu wa maji tutatumia Mradi wa Chalinze ama Morong’anya kuhakikisha maji yanafika Ngerengere.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, zaidi ya 85% ya wakazi wa Wilaya ya Muleba hawana maji safi na salama; je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Wilaya ya Muleba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oscar, Mbunge wa Muleba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ujenzi ule wa mradi kutoka Ziwa Victoria upo kwenye mpango wa Wizara. Mara tutakapopata fedha tutaendelea kuzileta kwa mafungu ili mradi huu tuanze kuutekeleza.
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi.

Ni lini Serikali itatekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu ya kupeleka maji Kijiji cha Mtunduwalo iliyothibitishwa kwamba maji yale sasa hayawezi kutumika kwa matumizi ya binadamu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kapinga, Mbunge wa Mbinga Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maelekezo ya viongozi wakuu yote tunayatekeleza na suala hili la kupeleka maji Ruanda nalo pia lipo kwenye utaratibu wa kuona kwamba hivi punde tunakuja kuhakikisha maji Ruanda yanaletwa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante; swali langu ni je, ni lini Serikali itafanya tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Kata za Mwika Kaskazini, Mamba Kaskazini, Marangu Mashariki, Mwika Kusini na Kilemu kwa sababu miradi hiyo ina matatizo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Charles Kimei, Mbunge wa Vunjo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge, maeneo hayo yote uliyoyataja tuna miradi ambayo inaendelea na usanifu na miradi ambayo tunaitafutia fedha na katika mgao ujao na hata Jimbo la Vunjo nalo litakuja kupatiwa fedha ili miradi hii ianze kutekelezwa kwa wakati.
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nataka kujua ni lini mradi mkubwa wa maji kutoka Wilaya ya Ileje, Mto Songwe kwenda Jimbo la Tunduma utaanza kutekelezwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stella, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi huu ni mradi mkubwa na tayari umeshaanza utekelezaji kwa hatua za awali na tunatarajia maji Tunduma yatafika kwa sababu ni mradi ambao unajengwa kwa awamu.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi ya maswali madogo ya nyongeza.

Swali langu la kwanza, kwanza niipongeze Serikali kwa nia ya dhati ya kutatua kero kwenye Mji wa Mpui na Laela kwa kutumia chanzo cha Ziwa Tanganyika na Mto Momba.

Je, ni lini mkandarasi anayefnaya Mradi wa Kaoze Group ataripoti kuanza kazi kwenye Kata ya Kaoze, Kilanga One na Kipeta?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa tatizo la maji kwenye Mji Mdogo wa Mpui ni kubwa sana na mmesema mnaenda kuchimba kisima kimoja.

Je, Serikali hamuoni kuna haja ya kuendeleza mpango wenu wa kutumia Mto Kazila kupeleka maji katika Mji Mdogo wa Mpui?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deus Sangu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimepokea pongezi, nikupongeze nawe pia kwa sababu ufuatiliaji wako katika suala hili umekuwa ni mzuri.
Mheshimiwa Spika, lini mkandarasi atakwenda, ni mwezi wa tatu mwanzoni; wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu tunatarajia mkandarasi huyu atafika site na kuanza kazi ya mradi.

Mheshimiwa Spika, matumizi ya Mto Kazila, ni kweli usanifu ulifanyika. Mto huu upo mbali kodogo wa kilometa 21 na ipo kwenye Wilaya tofauti na ambapo mradi upo. Kwa hiyo, tutachimba kisima kwa sababu tuna uhakika tutapata maji ya kutosha kama tulivyochimba maeneo mengine katika jimbo lako Mheshimiwa Mbunge. Itakapobidi kutumia Mto Kazila kwa sababu Wizara tunahitaji kuona tunatumia vyanzo vyote ambavyo vinatuletea miradi endelevu, Mto Kazila pia tutautumia.
MHE. HAMIS M. MWINJUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Tatizo la upatikanaji wa maji katika Mji wa Muheza bado ni kubwa pamoja na juhudi nyingi zinazofanywa na Serikali.

Je, ni lini mradi wa miji 28 ambao tunaamini kwamba ndiyo suluhisho la kudumu la tatizo hili utaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hamis, Mbunge wa Muheza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi wa Miji 28; miradi hii yote imeshaanza kutekelezwa kwa hatua za awali za kukusanya taarifa na kukamilisha taratibu za kuanza ujenzi tayari zimeshaanza ni vile hamzioni wanakusanya taarifa. Mradi huu ni design and build, kwa hiyo mwezi huu wa tatu tunatarajia wakandarasi waanze kuonekana sasa site na kuanza kufanya ujenzi.
MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa wananchi wa Kigoma Mjini wameahidiwa mradi mkubwa wa maji kukamilika tangu mwaka 2020 na sasa tuko mwaka 2023 na mradi haujakamilika.

Je, ni nini kauli ya Serikali kwa wananchi wa Kigoma Mjini kuhusu mradi huo mkubwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sylvia, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi Kigoma Mjini, mimi mwenyewe nimefika mwezi Novemba, mradi upo kwenye hatua za mwisho kabisa na maji yataanza kutoka hivi punde.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona.

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Kilwa, katika Vijiji vya Marendego na Kinjumbi kumekuwa na miradi ya maji ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa zaidi ya miaka mitatu hivi sasa.

Ningependa kumuuliza Mheshimiwa Waziri kwamba ni lini miradi hii itakamilika ili wananchi wa vijiji hivyo waweze kupata huduma ya maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Francis, Mbunge wa Kilwa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, vijiji hivyo ulivyovitaja Mheshimiwa Mbunge ni kweli kazi zimeendelea zikifanyika. Baada ya Bunge hili naomba tuwasiliane ili tuweze kuona tunafika pamoja katika miradi hii.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ningependa kujua mradi mkubwa wa maji tambarare ya Mwanga mpaka Same unakamilika lini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Mathayo, Mbunge wa Same kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi huu ni mradi mkubwa, utekelezaji wake unaendelea, pamoja na changamoto zake, Wizara inaendelea kuona tunafanya kila linalowezekana mradi uweze kukamilika na lengo la matumizi haya kwa wananchi wa Same, Mwanga mpaka Korogwe yaweze kukamilika.
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wananchi wa Arumeru kwanza kabisa tutoe shukrani kwa majibu mazuri ya Serikali, vilevile kwa niaba ya Mheshimiwa Pallangyo anatoa shukrani nyingi sana kwamba aliomba Shilingi Bilioni 2.7 fedha hizo zimefika na tayari zimeanza kufanya kazi, lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mradi wa maji Kijiji cha Litoho, Kata ya Ukata, unaotokea Liwanga unatoa maji muda wote sijui nisema machafu lakini yasiyokuwa pure yana udongo kwa hiyo yanahitaji ujenzi wa chujio. Je, ni lini Serikali itajenga chujio katika mradi huo.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali kwanza nipende kupokea shukrani kutoka kwa Mbunge wa Arumeru, kwa kweli kupeleka fedha ni wajibu wetu na kipekee tumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu anaendelea kutoa fedha kwenye miradi hii mikubwa ili wananchi waweze kuondokana na matatizo ya maji na kubeba ndoo kichwani.

Mheshimiwa Spika, kwenye ujenzi wa chujio naomba nitoe ahadi kwamba ni moja ya majukumu yetu kama Wizara nimelipokea tutalifanyia kazi. (Makofi)
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, tatizo la chanzo cha maji cha Geita ni kubwa na ningependa kufahamu ni lini Wizara itakarabati ili kuongeza kiwango cha maji kinachozalishwa kwa ajili ya Mji wa Geita.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kanyasu Mbunge wa Geita kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara tumeweka mkakati wa kuona kwamba vyanzo vyote vya maji viweze kutoa maji safi salama na ya kutosha, hivyo hata kwenye Mji wa Geita lipo katika mikakati yetu nipende kumuomba Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana kama ambavyo anafany,a lengo ni kuona wananchi wanaenda kupata maji safi na salama.(Makofi)
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwanza niipongeze Serikali kwa kukamilisha mradi wa maji kutoka Nyamtukuza Wilayani Nyang’wale na sasa hivi maji tumeyapata lakini maji haya si safi na salama kwa sababu mradi ule haukutengenezewa chujio la kuyatibu yale maji.

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga chujio la kutibu maji ili wananchi wasije wakaugua na kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya matibabu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hussein Amor Mbunge wa Nyangwale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nipokee shukrani zake kwa sababu mradi huu ni ile moja ya miradi vichefuchefu na hapa tunampongeza Mheshimiwa Waziri ameweza kusimamia mradi sasa unatoa maji, suala la chujio ni suala linalofuata katika mwaka ujao wa fedha tutahakikisha na suala la chujio nalo linapewa nafasi.
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza swali moja la nyongeza.

Nilishawahi kuripoti mradi wa Kalumea - Nyehunge Nyakalilo ni kichefuchefu, Mheshimiwa Waziri aliahidi kutembelea mradi ule ili aweze kutoa fundisho kwa watu wanaochezea fedha za Serikali naomba kuuliza tena.

Je, Mheshimiwa Waziri wako tayari kutembelea mradi wa Lumea ili kwenda kutoa fundisho kwa Wakandarasi wanaotumia vibaya fedha za Serikali?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shingongo Mbunge wa Sengerema, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Sengerema mimi mwenye nilifika na tuliweza kufanya kazi nzuri na maeneo yale tuliyopita yanakwenda vizuri kwenye mradi huu anaouongelea Mheshimiwa Mbunge mara baada ya Bunge hili tutawasiliana kuona namna gani ya kuweza kufika pale kwa pamoja.
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Spika, katika miradi ya maji ambayo iliyoko katika maeneo yetu tunao mradi mkubwa wa maji eneo la Nyasibu, Mbungo, Ngoma ambao na wenyewe umekaa kwa muda mrefu nini majibu ya Serikali ili mradi huo uanze kama ulivyopangwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Tabasamu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi huu wa Nyasibu tayari tumeshawaagiza vijana wetu waweze kuona namna ya kuweza kuuendeleza Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa tuonane tuweke vizuri ili suala kwa sababu huu mradi ni muhimu wote tunafahamu.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mafupi na mazuri. Pia naipongeza sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo inashughulika na changamoto kubwa ya maji na wananchi wa Jimbo la Kishapu kwa ujumla. Tangu mwezi wa pili tarehe 11 mkataba baina ya Emirates Builders wenye thamani ya Shilingi bilioni 6.5 umesainiwa kwa ajili ya usambazaji wa maji ya Ziwa Victoria katika Kata nne; Kata ya Laghana, Mwamashare, Igaga, na Ngofila.

Swali: Je, Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba inatoa ile 20% kama advance payment ili mradi huu uanze kutekelezwa kwa wakati kwa maana Mkandarasi mpaka sasa yuko site?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kuambatana nami kwenda Jimboni kuona changamoto zilizoko katika Jimbo la Kishapu na kuhakikisha kwamba atasukuma kazi hii kwa haraka ili mradi maji yaanze kutoka katika Jimbo la Kishapu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Butondo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, advance payment tayari zimeanza kutolewa kwa Wakandarasi wote, naamini Emirates naye atakuwa katika list. Suala la kuambatana naye ni moja ya majukumu yangu, hakuna shaka. Nitafika kuhakikisha mradi unatekelezwa. (Makofi)
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria unaotoka Mangu kwenda Ilogi ni mradi uliochukuwa muda mrefu sana kutoka 2016. Mwaka 2021 niliuza swali la msingi juu ya mradi huo wa maji. Waziri akaniambia Juni mwaka 2021 mradi ule ungezinduliwa. Sasa ni lini Serikali itazindua mradi wa maji unaotoka Mangu mpaka Ilogi. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Iddi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miradi hii ya Ziwa Victoria tunaendelea kuitekeleza. Ipo katika hatua mbalimbali kwa kila eneo, lakini maji ya Ziwa Victoria yataendelea kutumika vizuri, kuhakikisha huduma ya maji safi na salama itapatikana.

Mheshimiwa Spika, ni hivi karibuni uendelezaji na utekelezaji wa mradi huu unaendelea kufanyiwa kazi.
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Moja ya vijiji vilivyoathirika na machafuko ya Mto Mara ni pamoja na Kijiji cha Kwiguse, Marasibola na Kyamwame na Serikali iliahidi kupeleka maji mbadala kwenye vijiji hivi ambavyo havitumii maji haya kwa sasa. Nataka nijue Serikali imefikia wapi kwenye mpango huu wa kuhakikisha wale wananchi wanapata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nimepokea, tutawasiliana na Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, nilitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kulipatia Jimbo la Mbagala maji safi na salama yenye uhakika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Chaurembo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maeneo hayo ya Mheshimiwa Mbunge tayari kuna miradi inayoendelea, ipo kwenye utekelezaji hatua za mwisho. Hivi punde maji safi na salama yataunganishwa katika existing lines ili wingi wa maji uweze kuongezeka kwa wananchi. (Makofi)
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Katika Jimbo la Kawe Kata ya Wazo, mitaa ya Nyakasangwe, Mivumoni na Salala, miundombinu ya maji kwa maana matenki tayari imeshajengwa. Ni lini sasa Serikali itahakikisha maji yanatoka katika mitaa hiyo ili kuwaletea wananchi wale nafuu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Felista Njau, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maeneo yote ya Kawe miradi iko mwishoni. Hata jana tu nimemwona Mkuu wa Mkoa akiwa na watendaji wetu wa DAWASA wakifuatilia kule, hivyo miradi iko mwishoni. Muda siyo mrefu maji ya kutosha safi na salama yataanza kutoka.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Wilaya ya Muleba iko kando kando mwa ya Ziwa Victoria, na tuna mradi wa kuvuta maji kwa ajili ya Kata sita za Wilaya ya Muleba; usanifu umekamilika.

Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza huo mradi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali Mheshimiwa Mbunge wa Muleba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mara usanifu wa mradi unapokamilika, tunatarajia tuwe na kipindi kifupi cha mwezi mmoja au miwili kuona sasa tunatumia maandiko ya Mhandisi Mshauri ili mradi uanze kutekelezeka. Hivyo, kwa
sababu usanifu umekamilika, tupo katika utaratibu wa kuona sasa tunapata mkandarasi aje kutekeleza huu mradi.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, nawapongeza Wizara ya Maji, wanafanya kazi vizuri sana; na waendelee kufanya hivyo hivyo.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kwa kuwa huu mradi wa maji wa Ziwa Victoria kutoka Bunda Mjini kwenda Bunda Vijijini ni wa muda mrefu sana na una baraka zote za Waziri wa kwanza na Waziri aliyepo sasa hivi Mama Samia Suluhu Hassan, sasa Wizara ipo tayari kuweka mchakato wa single source ili kumpata mkandarasi wa haraka zaidi wa kutekeleza mradi huu?

Mheshimiwa Spika swali la pili; kwa kuwa tuna miradi kichechefu katika vijiji vya Kata ya Nyamswa; vijiji vya Makongoro A, Makongoro B, na Bukama na Vijiji vya Mgeta na Nyang’aranga; sasa ni lini Waziri atafika eneo hilo kusikiliza kero za wananchi kwenye miradi mibovu ya siku nyingi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili Mheshimiwa Gitere kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kupokea pongezi zake. Niseme, tuendelee kushirikiana. Lengo ni kuona tunafikisha maji safi na salama kwa wananchi na kuwatua akina mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Bunda Mjini kuelekea vijijini kutumia single sources; nimepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge kwa sababu lazima tuajiri mhandisi mshauri ili aweze kutufanyia upembuzi yakinifu na kutuandalia maandalio ya kazi. Baada ya kumpata Mheshimiwa Mbunge wazo lako tutalifanyia kazi kwa kulipa kipaumbele.

Mheshimiwa Spika, kuhusu miradi chefuchefu, ni lengo la Wizara kuimaliza miradi chefuchefu yote, hivyo kufika kwenye maeneo ambayo bado maji ni tatizo ni moja ya majukumu yangu nikuombe Mheshimiwa Mbunge, mara baada ya Bunge hili la bajeti, mwezi wa saba tutaona namna njema ya kufika maeneo yote ambayo yanamiradi ambayo haifanyi vizuri.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada kubwa za Serikali kusambaza maji vijijini jitihada hizi zinaweza kuwa bure iwapo gharama ya kuunganishiwa maji kwenye nyumba za wananchi hazitashuka. Je, Serikali haioni sasa ni wakati umefika wa kuangalia hizi gharama za kuunganishiwa maji kwa wananchi, especially wananchi wa vijijini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa George Mwenisongole kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, gharama za uunganishi Wizara tunaendelea kuzipunguza kwa kuzisogeza bomba kuu ambalo litambunguza umbali wa kutoka kwenye main line kwenda kwa watumiaji, na tayari kazi hii imeanza katika maeneo mbalimbali. Hivyo, ninatarajia kuwa hata katika jimbo lake pia huduma hii itamfikia.
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru ni lini Serikali itapeleka maji katika Kata ya Kisesa Bujorwa Bukandwe Bujashi ambazo zina matatizo ya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Boniventura Kiswaga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maeneo yote ambayo bado miradi haijaanza ama miradi imeanza lakini ipo kwenye utekelezaji tutakavyopata fedha, ndani ya mwaka huu wa fedha na mwaka ujao tutakuja kuendelea na kazi ya usambazaji wa maji.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mji wa Tarime ilipaswa upate maji kutoka Ziwa Victoria kwenye mradi wa miji 21 na Waziri wakati wa bajeti iliyopita aliahidi hapa kwamba kufikia Septemba utakuwa huo mradi umeshaanza na kuelekea matumaini ya kumalizika, lakini mpaka sasa hivi bado haujaanza. Sasa, ni lini huu mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda mji wa Tarime utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni miji 28 siyo miji 21. Miji 28 itaanza kutekelezwa hivi punde kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mabwawa ambayo yanajengwa na tumeleta kwenye Wizara yako, Bwawa la Mungahai, Dirimu, Yaeda Chini, Masieda, Endagichani, Basodere, Eshdeshi, Getire na Haribapeti.

Je, ni lini unatujengea mabwawa haya ambayo tumeshayaleta kwenye Wizara yako?

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa Waziri alikuja Haydom na akaahidi kwamba tusubiri wali wa kushiba unaonekana mezani, na akaahidi kisima cha Haydom.

Je, ni lini kinachimbwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Massay kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mabwawa, mabwawa haya yapo katika ngazi mbalimbali za utekelezaji na maeneo mengi ya nchi tunafikiria kuchimba mabwawa kwa lengo la kuhifadhi maji ya mvua kutumika wakati wa kiangazi, hivyo mwaka ujao wa fedha naamini maeneo kadhaa yatapata huduma hii.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusiana na kisima alichokiahidi Mheshimiwa Waziri, ahadi ni deni lazima tutakuja kuchimba hiki kisima, tutaangalia bajeti hii kabla haijakamilika mwaka huu wa fedha na ikibidi basi mwaka ujao wa fedha kisima hiki kitapatikana. (Makofi)
MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Spika, naomba kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, mradi unasuasua hauendi vizuri sana kwa sababu ni mwezi wa Nane sasa hivi hakuna kinachoendelea kule kwenye mradi, ukiuliza kwanini unasuasua wanatuambia kwamba ni kwa sababu unatekelezwa kwa force account na watumishi wapo busy na mambo mengine.

Je, Serikali ipo tayari kutafuta Mkandarasi badala ya kutumia force account ili mradi uweze kwenda haraka na wananchi wapate huduma ya maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza na Mheshimiwa Mwantona kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nipende kukupongeza kwa ufuatiliaji mzuri wa hili suala la maji la Tukuyu Mjini na hata jitihada ambazo zimefikiwa kwa kilometa tatu ni kwa sababu ya ushirikiano, hivyo ninapende kukuondoa hofu.

Mheshimiwa Spika, force account ni moja ya namna ambavyo inasaidia katika Wizara na miradi inakuwa vizuri, lakini suala la kuweka Mkandarasi kwa baadhi ya maeneo naomba tuseme tumeipokea na tutaweza kushauriana namna bora ya kulifanyia kazi. (Makofi)
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Katika Mji wa Kasulu maji yanayotoka kwenye mamomba ni machafu na yana tope, tulileta ombi hili ndani ya Bunge lako na Waziri akaahidi kumaliza tatizo hilo. Je, ni lini sasa tatizo hilo la maji katika Mji wa Kasulu litapatiwa majibu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Kasulu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maji machafu na tope; hii tunaendelea kufanyia kazi kuona tunajenga machujio, lakini vilevile kutumia dawa kutibu maji haya ili yaendelee kuwafikia wananchi yakiwa safi na salama.
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa changamoto iliyopo Rungwe inafanana na Mradi wa Maji katika Jiji la Arusha.

Je, Wizara ina mpango gani kuhangaika na changamoto ya malalamiko ya wananchi ya bill kubwa za maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Gambo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, bill kubwa za maji tunaendelea kulifanyia kazi kwa kutoa ushirikiano wa wasoma mita na mtumia maji, lakini vilevile tuna mfumo ambao tayari baadhi ya mikoa umeanza kutumika kuona kwamba unatumiwa message una hakiki kwamba ndicho ulichokitumia kisha unaletewa bill sasa ya malipo. Hivyo bill kubwa ukomo wake umeshafikia kwa sababu ya unified billing system.
MHE. IDDI KASSIM IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nataka kumuuliza Naibu Waziri; Kata ya Mwanase, Mradi wa Maji wa Izuga umechukua muda mrefu sana. Sasa ni lini Serikali itapeleka fedha ya kuwalipa wakandarasi ili waweze kumaliza mradi huo wa maji wa Izuga?
MHE. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Iddi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kupeleka fedha; tayari wakandarasi wanaendelea kulipwa, hivyo ninaamini hata mkandarasi huyu naye yupo kwenye foleni ya kulipwa. Tayari Katibu Mkuu pamoja na timu nzima inayohusika inaendelea kufanyia kazi suala hili la malipo.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuishukuru sana Serikali, lakini nimshukuru Waziri kwa majibu mazuri na kwa juhudi ambazo wanaendelea kuzifanya kuhakikisha kwamba huu mradi unakamilika.

Mheshimiwa Spika, nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa tayari vijiji vitatu vimeanza kupata maji, ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba zile Jumuiya za Watumia Maji zinakuwa jumuiya endelevu zenye uongozi imara hususani kuweka mafundi katika ngazi ya kata ili waweze kusaidia?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kuna maeneo ambayo Wizara imechimba visima mara tatu wamekosa maji, kwa mfano; Kijiji cha Mpapa, Igwamadete na hata Mazuchii. Nini mpango wa Serikali kuja na njia mbadala kunusuru vijiji hivi? Ahsante sana.
MHE. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Dkt. Pius Chaya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nipende kupokea pongezi zake, lakini ni kwa sababu ya mashirikiano aliyonayo Mheshimiwa Mbunge na tuendelee kushirikiana lengo ni kuona tunapeleka maji kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na jumuiya kuwa na mafundi ngazi ya kata tayari hili ni agizo limeshatolewa na Mheshimiwa Waziri na maeneo mengi yameshafanya. Hivyo nipende kutoa agizo kwa watendaji waliopo katika jimbo lako kama hawajafanya hivyo wanapaswa kufanya hivyo haraka iwezekanavyo kuwa na fundi ngazi ya kata.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na njia mbadala; sisi kama Wizara maeneo yote ambayo yana changamoto ya maji ardhini, tunaendelea kuona chanzo kilicho karibu kiweze kuleta maji safi na salama. Mheshimiwa Mbunge hili tuendelee kushirikiana kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana, lengo hivi vijiji ambavyo maeneo haya maji ardhini ni shida, basi nao tuweze kuwapelekea kupitia njia nyingine.
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina maswali madogo ya nyongeza.

Je, Serikali inawahakikishiaje wananchi wa Tarime, Rorya, Sirari, Nyamwaga, Nyamongo na Serengeti kwamba, mradi huu wa kutoka Ziwa Victoria utaenda kuanza mwaka huu wa fedha 2022/2023?

Swali la pili, wananchi wa Mji wa Tarime kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia chanzo cha maji kutoka Mto Nyanduruma, lakini maji yale ni machafu na yana rangi ya tope.

Je, Serikali ni lini itaweka chujio la maji ili kuwawezesha wananchi wale kupata maji safi na salama? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ghati Chomete kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kumpongeza Mheshimiwa Ghati Chomete kwa maswali mazuri na amekuwa akifuatilia sana hii miradi, kwa sababu ya mashirikiano katika suala la lini maji ya Ziwa Victoria yatatumika, tayari tumeshafikia hatua zote ziko sawa na sasa tunasubiri tu idhini ya kupata nafasi ya Mheshimiwa Rais ili aweze kushiriki katika kusaini ili mradi wa Miji 28 uanze kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la chujio pia tayari ni moja ya mikakati ya Wizara na tunatarajia kufikia mwaka ujao wa fedha nalo pia litapewa kipaumbele.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Katika Mkoa wa Simiyu tuna Wilaya Tano, lakini Wilaya ya Meatu inaongoza kwa ukame wa maji.

Je, ni lini sasa tutapata maji ya kutoka Ziwa Victoria maana juzi tu Naibu Waziri amefika pale tumepata maji lakini maji yenyewe yameshakuwa ni ya mgao mtatusaidiaje katika Wilaya ya Meatu?(Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Meatu ni kama alivyoeleza Mheshimiwa Mbunge, niliweza kufika mimi mwenyewe na ninakushukuru sana Mheshimiwa Minza kwa ushirikiano wako kwa namna ambavyo tumeweza kupunguza ile changamoto ya maji machafu na sasa hivi angalau mnapata maji kwa zamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji ya uhakika kutoka Ziwa Victoria tayari unaendelea kufanyiwa kazi, kama unavyofahamu tayari watu wameshaanza kulipwa fidia zao na ule ni mradi maalum kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi, hivyo tutarajie mwaka huu ujao wa fedha shughuli zote zitakwenda kufanyika vizuri.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Naomba nimuulize swali la nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri, Shule ya Sekondari ya Kijombe ina shida sana ya maji ambayo iko ndani ya Wilaya ya Wanging’ombe. Je, lini Serikali itahakikisha kwamba inapeleka maji katika shule ile kwa sababu ni shule ya bweni ili watoto wetu waweze kupata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema Mgaya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nampongeza Mheshimiwa Mbunge Neema kwa ufuatiliaji wa usalama wa watoto wetu na hili ni agizo ambalo tayari Wizara imelitoa katika mikoa yote. Naomba nitumie Bunge lako Tukufu niendelee kuwaagiza watendaji wetu wa Mkoa wa Njombe wahakikishe Sekondari ya Kijombe inapata maji safi na salama.
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Mkoa wa Kigoma umejaaliwa neema ya kuwa na Ziwa Tanganyika na Mto Malagarasi, lakini ni mkoa ambao bado unakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji. Je, nini mkakati wa Serikali kutumia maji ya Mto Malagarasi na Ziwa Tanganyika ili kumaliza uhaba wa maji katika Mkoa wa Kigoma hususan Jimbo la Muhambwe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Florence, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya vyanzo vya maji vya Maziwa Makuu na mito mikubwa ni moja ya mikakati ya Wizara, hivyo Mto Malagarasi na Ziwa Tanganyika navyo pia viko kwenye mikakati ya Wizara kadiri tutakavyokuwa tunapata fedha za kutosha tutatoa kipaumbele kwenye vyanzo hivi vikubwa ili tuendelee kupata miradi endelevu.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya kutia moyo ya Serikali, shule za msingi 459 za Wilaya za Misenyi, Ngara, Biharamulo, Bukoba Vijijini pamoja na Muleba katika Mkoa wa Kagera hazijaunganishwa na maji safi na salama. Kwa hiyo ningependa kupata commitment ya Serikali ni nini itakwenda kufanya kuhakikisha shule hizi zinaunganishwa na maji safi na salama ili kutoendelea kuweka hatari afya za watoto zaidi ya laki nne wanaosoma kwenye shule hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Mtaa wa Kisindi na Kashenye katika Kata ya Kashai, Bukoba Manispaa ina changamoto kubwa sana ya maji. Je, Wizara hii itakwenda kufanya nini kupata ufumbuzi wa haraka ili kutua ndoo akinamama ambayo ndiyo dhamira ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nampongeza sana Mheshimiwa Neema kwa ufuatiliaji mzuri. Suala la maji mashuleni, kwenye vituo vya afya, kama nilivyoongea kwenye maswali mengine, hili ni agizo ambalo Wizara imetoa kwa watendaji wote mikoani. Hivyo nitarajie mabadiliko makubwa sana katika shule zote za Mkoa wa Kagera zitafikiwa na maji safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la maji katika mitaa aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge dhamira ya Mheshimiwa Rais ni kuona kwamba watu wote wanafikiwa na maji safi na salama na ya kutosha, hivyo mitaa hii pia naamini kabla ya mwaka huu wa fedha haujaisha, wataweza kupatiwa huduma ya maji safi na salama na ikiwezekana basi kufikia mwaka ujao wa fedha pia zoezi litaendelea ili kuona maeneo yote yanapata maji safi na salama.
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza niseme tu ukweli kwamba, Mheshimiwa Naibu Waziri ni miongoni mwa viongozi wakweli sana. Sasa naomba Mheshimiwa Naibu Waziri au Serikali ituambie, kwenye ule Mradi wa Miji 28 bomba kutoka Tabora kwenda Sikonge litaanza kulazwa lini? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nikushukuru kwa pongezi. Kwenye hii mijii 28 hivi karibuni tunamtarajia Mheshimiwa Rais aweze kushiriki katika kusaini ambapo sasa kazi zitaanza na bomba hilo litalazwa mara baada ya mradi huu kuanza kufanyiwa kazi.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Jimbo la Mbulu Vijijini liko ukanda wa juu wa Rift Valley visima vingi vilivyochimbwa na Serikali kwenye Shule na Taasisi nyingi vimekauka. Bahati nzuri tuna Ziwa Basutu tuna ziwa Madunga, je, ni nini mpango wa Serikali wa kupeleka maji kwenye Jimbo hilo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Mbulu Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mbulu Vijijini tayari huduma ya maji inaendelea kupatikana kwa wananchi. Maeneo ambayo maji bado hayajafika tunaendelea na kazi. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge kuvuta subira, maeneo yake yote ya Jimbo yatafikiwa na huduma ya maji safi na salama.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji katika Mji wa Kisesa, Bujora, Bukandwe na Bujashe katika Wilaya ya Magu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Matondo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote na yeye nimpongeze kwa sababu ni mfuatiliaji mzuri katika masuala ya huduma ya maji. Maeneo ya Kisesa, Bujora na kote alikokutaja Mheshimiwa Mbunge tunatarajia kuendelea kupeleka huduma ya maji safi na salama.
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wakati Taasisi zisizo za Kiserikali zinahamasisha hedhi salama na kwamba kutakuwa na maadhimisho ya hedhi salama tarehe 28 ya mwezi huu, je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba katika shule za msingi na sekondari na hasa tunaposema hedhi salama moja ya kikwazo ni ukosefu wa maji. Kwa nini Serikali isiweke kwenye mikakati yake kila mradi wa maji unapoenda mahali popote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ihakikishe maji hayo yanafika kwanza kwenye shule zetu za msingi na sekondari ili kuhakikisha changamoto hiyo ya hedhi salama inaondoka?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hokororo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Maji tayari tunahakikisha shule, vituo vya afya na zahanati zote zinapatiwa huduma ya maji safi na salama. Kwa kuzingatia hili la watoto wa kike tunapomtua mama ndoo kichwani tunahakikisha pia huyu mama ajaye pia anabaki na afya yake kwa kupata maji safi na salama. Hivyo watendaji wetu mikoa yote wanafahamu hili na wataendelea kulifanyia kazi.
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi. Utekelezaji wa ujenzi wa vyoo shuleni kupitia program ya usafi wa mazingira inazingatia uwepo wa maji. Je, ni upi mkazo wa Serikali katika uvunaji wa maji katika majengo ya Serikali zikiwemo shule zetu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Leah Komanya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara itaendelea kuhakikisha shule zote zinapata maji safi na salama pamoja na vituo vya afya. Lengo ni kutimiza kauli ya maji ni uhai na maji yatazingatiwa kufika na Waheshimiwa Wabunge niwatoe hofu, shule zote katika majimbo yetu zitafikiwa na huduma ya maji safi na salama.
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Shule za Jimbo la Kalenga pamoja na Shule ya Kalenga Primary School karibu kabisa na fuvu la Mkwawa haina maji. Je, ni mpango gani wa Serikali wa kuchimba visima sasa badala ya kupeleka maji ya mserereko maana kuchimba visima ni kazi rahisi katika shule zote za Jimbo la Kalenga? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, uchimbaji wa visima katika maeneo ambayo ni rafiki tutaendelea kwa sababu tayari tunafanya zoezi hilo. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge wa Kalenga kama eneo lake linafaa kwa visima mantahofu visima vitakuja kuchimbwa na watoto watapata maji shuleni.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Waziri aliahidi kwamba ataingiza mchakato wa kuingiza LUKU za maji ili kudhibiti gharama zisizo sahihi zinazosomwa na wale wanaosoma. Je, huu mchakato umefikia wapi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kimei, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, LUKU za maji tayari katika baadhi ya mikoa imeshaanza kutumika mita hizo ambazo zinatoa uwezekano wa kulipa kulingana na matumizi yako. Mchakato unaendelea kwa mikoa mingine, lakini tayari tuna pilot Mikoa kama Iringa, Mbeya inafanya vizuri kwa baadhi ya maeneo ambayo tayari imefungwa, hivyo tutasambaza maeneo yote ambayo zitaweza kufikia.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na sheria zote zilizonukuliwa katika Ofisi ya Waziri. Je, Ofisi hiyo inashirikiana vipi na Ofisi ya TAMISEMI, Ardhi, Kilimo na Mifugo katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinahifadhiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa nini Serikali isianzishe tuzo maalum kwa ajili ya vijiji na Kamati za Maji zinazohifadhi vyanzo hivyo kikamilifu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maryam, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tayari Wizara tunashirikiana na hizi wizara ambazo tunaingiliana kimajukumu na hili tumeendelea kulifanya hasa katika ziara ya Wizara za Kisekta tumekuwa tukiendelea kutoa elimu ya pamoja.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusiana na tuzo maalum kama nimemsikia vizuri. Tuzo maalum ni moja ya vitu ambavyo tunavitoa kwenye Jumuiya za Watumia Maji. Tunatoa tuzo kwa maana ya kuwapa motisha ili kuona kwamba wananchi wanashiriki moja kwa moja kwenye utunzaji wa vyanzo vya maji. Vilevile kama ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, kwa niaba ya Waziri, naomba niseme nimepokea, tutaendelea kuongeza nguvu. (Makofi)
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza. Ni kweli, nikiri kwamba mradi huu unaendelea na utakapokamilika, tuweke rekodi sawa, utanufaisha wananchi 4,792 badala ya laki moja na kidogo.

Mheshimiwa Spika, nataka niulize maswali mawili ya nyongeza pamoja na haya, kwamba wananchi wa kata ile wako zaidi ya 12,000, mradi huu ukikamilika unakwenda kuhudumia wananchi 4,700. Nataka nijue mkakati wa Serikali walionao ili kuhakikisha angalau wananchi wote waliosalia kwa zaidi ya elfu kumi na mbili na kidogo wanaweza kupata maji safi na salama?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kuna kituo cha afya ambacho kinajengwa kwenye kata ile, hivi ninavyozungumza wananchi wanatafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya. Nilitaka nijue kama mpango huu wa mradi huu nao pia utahakikisha maji yanafika kwenye eneo la kituo cha afya ambacho kinajengwa kwenye Kata ile ya Rabour?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Chege kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na maji ya bomba yaliyo safi na salama yakiwa ya kutosha. Hivyo niombe Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana, vijiji hivi vyote vitapata maji.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusiana na kituo cha afya, nimekuwa nikiongea hapa mara nyingi, tumeshaelekeza watendaji wetu kwenye mikoa yote na wilaya zote kuhakikisha maeneo yote yanayotoa huduma za afya, kwa maana ya vituo vya afya, zahanati hospitali yote yanakuwa na mitandao ya maji safi na salama ya kutosha. Lakini vilevile eneo lake Mheshimiwa Chege nalo ni moja ya maeneo ambayo tunakwenda kuyafanyia kazi na kituo cha afya nacho ni miongoni mwa vituo vitakavyoenda kunufaika.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itachimba visima vya maji katika Kata ya Mwabazuru, Budekwa na Busiriri Wilaya ya Maswa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nipende kumpongeza sana Mheshimiwa Esther, amekuwa akifuatilia hivi visima.

Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kuhakikisha maeneo haya yanayohitaji huduma ya maji kupitia visima yanafikiwa, hivyo hata Wilaya ya Magu nayo ni miongoni mwa wilaya ambazo tunakwenda kuzifikia. Mwaka ujao wa fedha tuna visima vya kutosha tulivyovitenga katika bajeti yetu, hivyo tutahakikisha kwamba Magu nao wanapata.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza napenda kutoa shukrani za dhati kwa majibu mazuri ya Serikali yanayotia matumaini, lakini hata hivyo namshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanznaia, Mama yetu Mama Samia Suluhu Hassan, tumepata fedha zile za UVIKO, tumejenga chujio na sasa hivi tunapata maji safi ka Mji wetu wa Liwale. Nina swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, vipo Vijiji vya Ngongowele, Makata, Mtatawa, Kihangala, Kipelele, Nguta, Mpengele, Ndapaka, Mlembwe na Nangano. Vijiji hivi bado havijapata maji safi na salama. Naomba kupata comfort kutoka Serikalini, ni lini wananchi wa vijiji hivi wataweza kufikiwa na mradi wa maji ili kutimiza ile azma ya kumtua Mama ndoo kichwani iweze kukamilika? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Kuchauka Zuberi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, napenda kupokea shukrani zake na vile vile tumuombee Mheshimiwa Rais, kwa ababu adhma ya kumtua Mama ndoo kichwani hakika inatekelezwa maeneo yote.
Mheshimiwa Spika, vijiji alivyovitaja Mheshimiwa Mbunge tayari RUWASA Mkoa inafanyiakazi na mwaka ujao wa fedha tutavifikia kwa kila kijiji, kila tunapopata fedha kuhakikisha maeneo yote ya Liwale yanakwenda kupata maji safi na salama.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, kuna mradi wa Kiwira ambao naweza kusema ni mradi mama kwa sababu utawatua ndoo kichwani wanawake wengi wa Mkoa wa Mbeya. Mkandarasi alishasaini mkataba, lakini mpaka sasa hivi hajaanza kazi ya ujenzi wa mradi huo. Sasa je, ni lini mkandarasi huyo ataanza kazi rasmi ya ujenzi huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Tunaishukuru sana Serikali kwamba ilitoa ahadi ya kuleta fedha zaidi ya Shilingi bilioni nane kwenye mradi wa Kyela Kasumulu, mradi huo ambao utawasaidia wananchi wa Kata ya Nkuyu, Ndandalo, Mbugani, Kajunjumele, Bondeni, Serengeti, Kyela Mjini, Ikolosheni, Itungi na Ipyana: Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili mradi huo uanze kujengwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Suma Fyandomo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mradi wa Kiwira, tayari umeanza kushughulikiwa. Kuhusu mkandarasi kutoonekana site, lakini kuna kazi za awali tayari zimeshaanza na suala la kupeleka hela kwenye mradi wa Kyela Kasumulu, huu mradi tumeshaupelekea hela mara nyingi na tutaendelea kuupelekea kadiri tunavyopata fedha.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafsi ya kuuliza swali la nyongeza. Mradi wa Lunyinya – Chanya na Mradi wa Kilela – Rutungu – Lusungiro, miradi hii imesimama kwa muda mrefu kwa sababu mkandarasi hajalipwa. Ni lini mkandarasi atalipwa ili miradi hii iweze kukamilika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji hivi vyote alivyovitaja vina miradi miwili, hii miradi ni kweli tayari imeanza kufanyiwa kazi na malipo yanaendelea kufanyiwa kazi. Tayari fedha zimepatikana wiki iliyopita, baadhi ya wakandarasi tunaanza kuwapunguza, kuwalipa. Hivyo, mkandarasi huyu pia tunatarajia aweze kulipwa fedha yake.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; hivi sasa ipo mitambo ya Serikali kupitia DDCA inayochimba Bwawa la Kwenkambala na kwa Mahizi. Kwa nini Serikali isiibakishe mitambo hii ndani ya Wilaya ya Handeni itakapokamilisha Kwenkambala na kwa Mahizi ili iendelee kuchimba mabwawa hayo mawili ambayo unayazungumzia Mheshimiwa Naibu Waziri?

Mheshimiwa Spika, swali la pili mradi wa HTM mkandarasi tayari amekwishapewa msamaha wa kodi na alikwishakamilisha usanifu. Ni lini mkandarasi huyu atakuwa site kuanza ujenzi mara moja kwa mradi huu mkubwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa Mbunge wa Handeni Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mitambo kubaki Handeni hakuna tatizo tutahakikisha inabaki mpaka imalize kazi. Kuhusu mradi wa HTM lini utaanza tayari, mkandarasi anapaswa kuwa site; kwa hiyo baada ya hapa Mheshimiwa Mbunge tuonane ili tufatilie kwa pamoja kuhakikisha mkandarasi anakuwepo site.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba niulize Maswali mawili madogo tu: -

(i) Je, Serikali inaweza ikatudokeza kidogo kitu gani tutegemee kutokana na huo mwongozo?

(ii) Kwa vile Serikali imeweza kutoa ruzuku kwa maunganisho ya umeme, ni nini kinazuwia kutoa ruzuku kwa maunganisho ya maji ilhali tunajua maji ni uhai?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge.

Swali la kwanza, kwa nini tunashindwa kutumia ruzuku kwenye maunganisho ya maji; hili suala naomba nilichukue tuweze kulifanyia kazi. Vilevile swali lake la kwanza naomba niwe nimelipokea nitalifanyia kazi.
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Njoro II, Rombo, ili kuwatua akinamama wa Rombo ndoo kichwani?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zuena Bushiri, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu tunaendelea na utekelezaji wake; na kadiri tunavyopata fedha, Mheshimiwa Mbunge wewe ni shahidi, tunaendelea kupeleka fedha ili mradi huu ukamilike, kwa sababu lengo la Serikali ni kuona akina mama tunawatua ndoo kichwani.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itakuja na bei elekezi ya kuunganisha maji nchi nzima kama ilivyo kwenye umeme?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, Profesa Ndakidemi kuhusu bei elekezi nchi nzima kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, uunganishaji wa maji tunazingatia umbali kwa sababu ya mabomba na miundombinu ambayo inatumika. Tunaangalia kutokea kwenye main line kuja kwa wewe mtumiaji pale ulipo ndivyo ambavyo gharama inakwenda.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa wananchi wa Kibamba wanayo shukrani ya kukamilisha matenki ya Tegeta A – Goba na Mshikamano – Mbezi na mtaa Msumi hauna maji toka kupata uhuru.

Je, ni lini Serikali mtapeleka miundombinu ya kutosha, ili Mtaa huu wa Msumi, Kata ya Mbezi kupata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtemvu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari Wizara tumeagiza vifaa vya kuhakikisha mradi huu na miradi yote ya eneo lile la jimbo lake tunakwenda kuikamilisha. Tayari tumeshagharamia miundombinu ya matenki makubwa kwa hiyo sasa usambazaji ndio unaofuata.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wananchi wengi wanalalamikia sana bili kubwa za maji pale ambapo hata hawatumii maji nikiwemo mimi, ilhali hatupo hapa Dodoma naletewa bili kubwa. Ni lini sasa Wizara ya maji italepa prepaid meters kwa wengi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, prepaid meters tunaendelea kufunga maeneo mbalimbali. Kwa hiyo naomba niseme tu Mheshimiwa Mbunge, tuendelee kuwasiliana, hata wewe ukihitaji leo unaweza ukafungiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile bili kubwa hizi za maji Waheshimiwa Wabunge pamoja na wananchi wote naomba niseme kwamba, tuangalie miundombinu yetu. Wakati fulani ni wewe mhusika peke yako ndiye unaepata bili kubwa kwa sababu, labda mita yako hapo nje inapitisha hewa au kuna tatizo la uvujaji. Kwa hiyo hizi bili kubwa naomba tutoe taarifa kwa mafundi wetu, ili tuweze kuzidhibiti.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mradi wa Kilela, Lutunguru na Isingiro, mradi huu unajengwa kwa awamu mbili, mkandarasi anakaribia kukamilisha awamu ya kwanza. Ni lini Serikali itatangaza awamu ya pili ili mradi huu uweze kukamililka? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Wataalamu walifika kwenye Kata ya Businde, Bugala, Kibale pamoja na Kikukuru wakapima vijiji vichache ili wananchi waweze kupatiwa maji lakini adha ni kubwa wananchi wanayoipata. Je, Serikali iko tayari kupima vijiji vyote vya kata hizo ili wananchi hawa waweze kupatiwa maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Innocent Bilakwate kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mradi ule wa kwanza alioutaja unaopita kwenye vijiji vya Kilela, Lutunguru ni kweli awamu ya kwanza umeshakamilika na sasa tunaelekea kwenye usambazaji na tunatarajia mwezi Mei kuweza kuutangaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la pili, maeneo ambayo ameyataja Mheshimiwa Mbunge ni kweli vijiji vilishapimwa na tayari tunaendelea na utaratibu wa kuona kwamba maeneo haya yote ambayo miundombinu ya maji kuyapitia iko mbali basi tuweze kuchimba visima na tayari tumshukuru Mheshimiwa Rais ile mashine ambayo ilipaswa kufika Mkoa wa Kagera sasa inatarajiwa kutoka Karagwe na kuelekea Kyerwa lakini vile vile vijiji ambavyo havikupimwa tunavitarajia navyo vipimwe viingie kwenye mpango wa kupata maji safi na salama.
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Jimbo langu la Kalenga limekuwa halina chanzo cha uhakika cha maji ambacho kinaweza kikapeleka maji kwenye kata zaidi ya moja. Mfano Kata ya Masaka haina maji kabisa. Je, ni lini sasa Serikali itatafuta chanzo kimoja kikubwa ili tuweze kupeleka maji zaidi ya kata moja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Kalenga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli maeneo haya anayotaja Mheshimiwa Mbunge ambaye ni Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira. Ni kweli vyanzo vyake vinapata changamoto kama chanzo kile cha Nyamlenge kwa sasa tunashuhudia wote kwamba kinaendelea kujaa mchanga lakini watu wetu wa bonde wanaendelea kufanya kazi nzuri kuhakikisha vyanzo vinabaki salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maeneo yote ya Kalenga tunaendelea kufanya utafiti, tunatarajia kutumia labda Mto Lyandemberwa ambao unaweza ukasaidia eneo la Kalenga kupata maji safi na salama yakiwa bombani.
MHE. ENG. DKT. LEONARD M. CHAMURIHO: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia fursa hii ya kuuliza swali. Kijiji cha Kyabakari kimekosa huduma ya maji kwa muda wa miezi mitatu sasa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba kijiji hicho kinapata maji japo kuwa kuna mradi mkubwa wa maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Leonard Chamuriho kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kijiji ambacho kinaweza kikakosa maji miezi mitatu na tayari kina miundombinu ya maji ni suala la kufuatilia changamoto ilipo. Naomba nilichukue tutahakikisha maji yanarejea kwa wananchi ili kuondokana na kero ambayo wanaipata kwa sasa.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu ya Serikali, Mbunge wa Mufindi Kusini Mheshimiwa David Kihenzile, amekuwa akipigania sana na akiomba ukarabati wa mradi wa Imayi, yaani Kata za Ihoanza, Malangali na Idunda; na ule wa Vijiji tisa wa Kata za Mbalamaziwa na Itandula, lakini mpaka sasa haujaanza: Je, ni lini Serikali itapeleka fedha? Pamoja na kwamba mmesema fedha zimetengwa, lini Serikali itapeleka fedha mradi huo uweze kufanikiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Mradi wa watumia maji wa Magubike, Kata ya Nzihi Jimbo la Kalenga umejengwa na wafadhili wa Marekani wanaoitwa WARIDI, lakini tayari walishajenga intake na tank lipo tayari, changamoto ni namna ya usambazaji wa maji kwenda katika vijiji sita pamoja na vitongoji vyake: Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili kupeleka miundombinu hiyo wananchi waweze kupata maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRTI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Grace Victor Tendega, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Wizara tumejipanga vizuri, mradi huu wa Mbalamaziwa ambao unaenda kuhudumia vijiji tisa, tayari tumeshapata Mkandarasi na tunatarajia bajeti ijayo Mkandarasi huyu aanze kazi kwa sababu kila kitu kimeshakamilika. Mradi wa Malangali ni mradi mkubwa ambao tunatarajia utatumia zaidi ya Shilingi bilioni sita. Dhamira njema ya Mheshimiwa Rais ya kumtua Mama ndoo kichwani inaenda kukamilika kwa sababu bajeti ijayo tutahakikisha tunaleta fedha kwa awamu na kwa wakati ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati, na wananchi waweze kunufaika na maji safi na salama ya kitoka bombani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la intake na tenki kukamilika kwenye Jimbo la Kalenga, tayari tunaendelea na utaratibu kuona kwamba usambazaji wa maji tunakuja kuufanya ndani ya bajeti hii tunayoimalizia, pia kwa bajeti ijayo, tutakuja kuhakikisha maeneo yote ambayo yanapaswa kufikiwa na maji, yanakwenda kufikiwa. (Makofi)
MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Naibu Spika, tokea Tanzania imepata uhuru, kuna vijiji mkoani Mara hawajawahi kuyaona maji toka Setikalini: Je, Serikali ina mpango gani kupeleka maji katika Wilaya ya Serengeti na vijiji vyake na Wilaya nyingine ambazo zinazungukwa na utajiri wa Ziwa Victoria? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Agnes Marwa, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo haya aliyoyataja katika eneo la Serengeti, tayari tuna miradi ambayo tunatarajia wananchi waweze kunufaika na maji safi bombani. Nasi Wizara ya Maji, toka tumeanza kuhakikisha tunaleta mageuzi ndani ya Wizara hii, maeneo ambayo hayajawahi kupata maji, yanapata maji sasa hivi. Hivyo, wananchi wa Serengeti nao wakae mkao wa kupata maji safi na salama bombani.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Naomba kuuliza;
Je, Serikali ina mikakati gani mahususi ya kutatua tatizo la maji lililoko sasa hivi katika Wilaya ya Longido?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Swai, Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miradi ambayo iko Longido yote iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji, na lengo ni kuhakikisha tunakamilisha miradi hii kwa wakati.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, huu ni mwaka wa nane Serikali iliahidi kupeleka maji katika Kata za Makanya, Mlola, Kwai, Kwekanga hadi Kilole.

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake hii ya kupeleka maji katika maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shabani Shekilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwenye kata hizi zote alizozitaja Mheshimiwa Mbunge tuna miradi ambayo tunaielekeza katika mwaka wa fedha ujao. Lakini vilevile maeneo yote ambako miradi tulishaanza kuitekeleza tutakwenda kuikamilisha. Mheshimiwa Mbunge hili tumeshajadiliana muda mrefu na ameshafika ofisini mara nyingi. Naomba nimpe ahadi kwamba baada ya hapa kama tulivyokubaliana tutakwenda na tutahakikisha miradi ile tunaifanya vizuri.
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nina maswali mawili ya nyongeza. Kijiji cha Londokazi, Kalundi na Ntalamila wana changamoto kubwa sana ya maji.

Je, ni lini Serikali itakwenda kuchimba visima ili kuondoa adha hiyo ya maji?

Swali la pili, Jimbo la Nkasi Kusini vipo vijiji karibia 20 mwambao mwa Ziwa Tanganyika ambavyo hakuna barabara na hata hii miradi ya maji na vifaa vinashindwa kufika kule, kwa hiyo wananchi wanaendelea kuteseka wanakunywa maji ya kwenye visima pamoja na mifugo. Je, ni lini na ni mpango gani Serikali kwa kushirikiana na TARURA waweze kuchonga maeneo hayo ili vifaa vya miradi ya maji iweze kufika katika vijiji hivyo ambavyo ni Msamba, Kilambo cha Mkolechi, Izinga, Mbwiza, Lyela, Kasanga, Kasapa, Lupata, Lyapinda, Ninde, Kapumpuli na Kilabu cha Mkolechi? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Vincent Mbogo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, uchimbaji wa visima sasa hivi tayari gari liko kwenye mkoa wako na tutakuja kuchimba visima kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha. Vifaa vyetu kupitika katika barabara ambayo ni mbovu tutafanya mawasiliano na Wizara husika tutahakikisha mitambo ile inafika kwenye vijiji hivi na vijiji hivi vinaweza kuchimbiwa visima ili waweze kupata maji safi na salama na kufaidi ile azma ya Mama kumtua ndoo Mama kichwani. (Makofi)
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona. Mradi wa maji kutoka Kijiji cha Lumea, Kalebezo hadi Nyehunge ulijengwa chini ya kiwango, mabomba yanapasuka na kusababisha maji kukatika. Mheshimiwa Naibu Waziri aliwahi kuahidi kwamba atautembelea mradi huo ili ikiwezekana kuufanyia ukarabati na marekebisho upya.

Je, yuko tayari kutembelea mradi huu ili kujionea yanayoendelea?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Eric Shigongo kuhusiana na mradi huu ambao tayari Mheshimiwa Mbunge tumeongea mara kadhaa alipofika Wizarani, niseme kwamba niko tayari na tutakwenda kuhakikisha maeneo yote ambayo yalipata uharibifu tunayafanyia kazi kwa haraka. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mradi wa Maji Kyerwa Nyaruzumbula mpaka Kamuli utaanza lini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu tayari tuna mkandarasi wakati wowote mradi utaanza kufanyiwa kazi. (Makofi)
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Ni lini mabomba yaliyosambazwa katika Kata mbalimbali ya Jimbo la Mbagala yataanza kutoa maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Chaurembo, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mabomba yaliyosambazwa lazima mwisho wa siku yatoe maji, miradi yetu sisi inapokamilika lazima mwisho wa siku itoe maji. Hivyo nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge maeneo yote ambayo tumeshasambaza unafahamu kazi nzuri ya DAWASA inayoendelea kufanyika, kuna matenki makubwa yameshakamilika na sasa hivi yamebakia kwenye hatua za mwisho kabisa ili yaweze kufikia maeneo yote ambayo tayari yana mtandao.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Upo Mradi wa Mwabusiga katika Kata ya Kishapu wenye thamani ya shilingi milioni 314, mradi wa maji ya Ziwa Victoria. Mradi huu unatekelezwa chini ya mpango wa force account na uko katika Mfuko ule wa Maji na bahati mbaya kabisa fedha sasa hazijaja. Ziko taratibu za ununuzi wa mabomba na vifaa vingine ambavyo vinahitaji fedha. Sasa lini Serikali itakwenda kuleta fedha na ukizingatia mwaka wa fedha sasa tunakwenda kuumalizia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mradi huu suala la fedha kila mwezi tunakuwa na mgao. Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa naomba tuonane ili mgao unaofuata mwanzoni mwa mwezi Juni tuweze kuupatia fedha.
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kuishukuru Serikali kwa kuanza kutekeleza miradi katika Vijiji vya Sepukila na Kitelea pia kuandaa kutekeleza miradi ya maji katika Vijiji vya Tukuzi na Mateka. Vijiji vya Nzokai, Kilimani, Rudisha, Mikolola na Njomlole vina changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji. Nataka nijue sasa ni lini Serikali itaandaa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi kwenye maeneo haya. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipokee shukrani zake kwa Serikali, lakini zote ni jitihada zake za ufuatiliaji wa karibu na ushirikiano wake mzuri ndani ya Wizara yetu ta Maji. Mheshimiwa Mbunge, nawe tunakupongeza katika hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji hivi alivyovitaja Mheshimiwa Mbunge tayari vipo katika hatua mbalimbali za kuona kwamba na vyenyewe tunavifikishia maji safi na salama bombani. Hivyo, katika mwaka ujao wa fedha, vijiji hivi navyo tutavigusa katika namna ya kuona huduma inapelekwa.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba kujua katika bajeti ya mwaka 2022/2023, Serikali iliahidi kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Jimbo la Bunda. Je, ni lini ahadi hii itatimizwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Jimbo la Bunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tayari mradi ambao unatarajiwa kupelekwa Bunda umefikia hatua nzuri, Mhandisi
Mshauri yuko site. Mheshimiwa Mbunge nakupongeza kwa kufuatilia, kama tulivyoongea wiki iliyopita ofisini, tayari Mhandisi Mshauri anakamilisha na wiki hii tunamtarajia arejeshe taarifa ya kuona tathmini ya thamani ya mradi ambao tutakwenda kuujenga.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Ninapenda kufahamu kwenye Vijiji vya Mpanyani Shule ya Sekondari, Huria, Chiroro, Masiku pamoja na Namichi tayari pameshachimbwa visima virefu. Je, ni lini sasa Serikali iko tayari kuweka pampu kwenye maeneo haya ili wananchi waweze kupata maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji hivi alivyovitaja vyote tunatarajia viweze kuendelezwa visima vilivyochimbwa. Tumshukuru Mheshimiwa Rais tumeendelea kupata fedha za P4R, Mikoa yote itapelekwa fedha, kwa hiyo tunatarajia sasa distribution itakwenda kufanyika na wananchi wataanza kunufaika na visima vilivyochimbwa.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niulize swali la nyongeza. Mradi mkubwa wa maji uliogharimu takribani shilingiza bilioni 520 za Kitanzania kule Arusha sasa hivi karibu unamalizika. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga miundombinu ya kusambaza maji katika vijiji ambavyo bomba kuu limepita?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mradi huu tuko mwishoni kabisa na tayari vijiji vingi vimenufaika, tayari maji haya kutoka kwenye mradi yameingizwa kwenye laini ambazo zina-exist. Vilevile maeneo yote ya vijiji hivyo alivyovitaja na vingine vyote ambavyo vimepitiwa na bomba kuu vinakwenda kupata huduma ya maji safi na salama.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naishukuru Serikali kwa majibu mazuri, hasa kwa mradi wa Chagongwe kusikia kuwa utaanza. Licha ya hivyo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata 29 za Manispaa ya Morogoro zinapata maji ya mgao. Je, kuna mkakati gani wa kupata maji safi na salama kila siku kwenye Kata hizo 29 za Manispaa ya Morogoro? (Makofi)

Swali la pili, mradi wa Magadu ambao upo kwenye Manispaa ya Morogoro umechukua muda mrefu na haujakamilika; je, ni lini utakamilika na kuanza kutoa maji kwa wananchi kwenye Kata hizo zinazozunguka? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kwenye maeneo yote ya Mji wa Morogoro tuna mradi mkubwa wa AFD ambao tunatarajia ukaongeze uzalishaji wa maji na tatizo hili la mgao mkali wa maji pale Morogoro tunatarajia litapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile mradi wa Magadu tayari tumeutekeleza kwa asilimia 90, Mheshimiwa Mbunge anafahamu tulishaongea pamoja hili na tumefuatilia kwa pamoja Wakandarasi wanaendelea na kazi na tayari Wizara tumeshapeleka fedha, tunatarajia kufika mwezi Juni huu mradi wa Magadu nao uanze kutoa huduma kwa wananchi. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilio cha maji safi na salama Tanzania ni kama wimbo wa Taifa na wanaoteseka zaidi ni wanawake. Sasa hivi tunavyoongea ni masika na maji yanapotea na hakuna kinachoendelea kutoka Serikalini.

Je, ni lini sasa Serikali itatumia kuvuna maji haya ya mvua kuwaponya wanawake wa Makanya, Hedaru, Hundugai, Ngoyoni na Holili kule Kilimanjaro? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Josepha Raymond, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ni tabia ya maji ya mvua kupotea, lakini sasa hivi Wizara tumejipanga kujenga mabwawa maeneo yote ambayo yamekuwa na mafuriko na maji yanapotea kuelekea baharini. Tutachimba mabwawa Mheshimiwa Mbunge na tayari mitambo tunayo. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha nyingi kutumika kuleta mitambo mikubwa mitano ya kuchimbia mabwawa.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini pia naishukuru Serikali kwamba kuna mradi mkubwa wa Makonde ambao wametupatia fedha unatekelezwa kwenye Wilaya yetu ya Newala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la msingi lilihusu Jimbo la Newala Vijijini. Kumbuka kwamba Newala ina Majimbo mawili ambayo ni Newala Mjini na Newala Vijijini, kwa hiyo swali lilikuwa specific kwa Newala Vijijini. Sasa kwa kujumlisha hivi tutashindwa kupata uhalisia wake wa tatizo hasa ni nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi sasa, pamoja na yote yaliyojitokeza, kwenye Jimbo la Newala Vijijini kuna Mradi wa Maji wa Mnima – Miyuyu ambao umeanza kutekelezwa tangu mwaka 2018, na mradi ule ulikuwa ni wa miezi tisa. Mpaka sasa utekelezaji wake ni asilimia 65 tu. Pia changamoto ambayo inasababisha mradi huu kutokamilika ni kukosekana kwa fedha. Fedha zilizokuwa zimetengwa ni bilioni 1.3, zimelipwa milioni 614 tu. Je, ni lini Serikali itamaliza fedha zilizobakia ili wananchi wa Newala Vijijini waweze kupata maji?

Swali la pili, kwenye Vijiji vya Mkudumba, Mnyengachi, Mnyambe, Mnima, Bahati, Mikumbi, Mkongi, Namangudu, Nangujane, Chilende, Mkoma, ‘two’ pamoja na Lihanga kuna miradi ya maji ambayo inatekelezwa. Lakini miradi ile ina changamoto ya upatikanaji wa fedha.

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili miradi hii ikamilike? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Miyuyu tatizo ni fedha na swali lake la pili tatizo pia ni fedha. Naomba niwe nimepokea masuala haya ya Newala Vijijini na nitafanyia kazi mimi mwenyewe kwa ukaribu kuhakikisha fedha zinakwenda na kazi inakamilika kwa wakati.
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa maeneo mengi katika Mkoa wa Lindi yana maji ya chumvi. Je, ni lini Serikali itawapatia maji safi na salama wananchi wa Kata za Ngunichile, Tarafa ya Kilimarondo na Namapwia kwenye Wilaya ya Nachingwea, Lihimalyao, Kibata na Kandawale kule Wilaya ya Kilwa? ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Tecla kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo yote aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge ni kweli yana shida ya maji ya chumvi, Mheshimiwa Mbunge unafahamu mradi wetu mkubwa ambao tayari tumeongea, hata juzi tulikuwa pamoja na tayari tunautengea fedha ule mradi ili sasa tuweze kupata maji ya uhakika yakiwa safi na salama na kuondokana na visima hivi vinavyotuletea maji ya chumvi.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Katika kupunguza adha ya maji hususan Manispaa ya Ilemela, Serikali iliahidi kufufua visima vyote ambavyo havifanyi kazi. Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kufufua visima hivyo ili kuondokana na changamoto ya maji katika Manispaa ya Ilemela? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Furaha Matondo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu visima kufufuliwa Ilemela, tayari tumeshaagiza na katika mwaka ujao wa fedha tutahakikisha visima hivi vyote ambavyo vimechimbwa na bado vina maji mazuri tutavitumia kuhakikisha vinaongeza huduma ya maji katika maeneo yote ya Ilemela. (Makofi)
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kupeleka fedha, kiasi cha shilingi bilioni 138 kutoa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Rorya na Tarime. Nini kauli ya Serikali juu ya maji hayo kwenda katika Kata ya Komaswa, Manga, Nyamongo, Sirari, Pemba, Mbugi na Nyamwaga? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Marwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Ziwa Victoria wa kupeleka maji Rorya na Tarime, tayari usanifu unaendelea na Mheshimiwa Mbunge tumezungumza hapa juzi na nimekupa Katibu wangu amefanya kazi nzuri na wewe. Tutahakikisha mradi huu tunakuja kuutekeleza kwa wakati. (Makofi)
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, hasa kwenda kwenye chanzo cha uhakika. Pamoja na majibu hayo mazuri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Kata ya Mlangali na Lugarawa ni kata ambazo zina ongezeko na kasi ya idadi ya watu tofauti na uwepo wa huduma za maji. Nini mpango wa Serikali kutenga fedha hizo kwenye bajeti ijayo ili kata hizo mbili ziweze kupata maji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kitongoji cha Lutala la Kisaula, vina idadi kubwa ya wananchi na hadhi ya vijiji, lakini kwa muda mrefu vimekuwa na changamoto ya maji. Mheshimiwa Naibu Waziri, alishaelekeza wataalam wa-extend Mradi wa Iwela kuhudumia maeneo hayo...

SPIKA: Swali lako Mheshimiwa.

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini maelekezo hayo ya Serikali yatatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kamonga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mlangali na Lugarawa Mheshimiwa Mbunge, tulikwenda na tumeshudia kwa pamoja, lakini tayari kama Wizara tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili tuweze kutumia vyanzo vile vya uhakika; ile mito yetu miwili, Mto Salali na Mto Mbiliwili. Tutahakikisha tunatumia mito hii pale ambapo usanifu utakapokamilika na kuonekana na maji ya kutosha, ndiyo mto ambao tutautumia. Hili Mheshimiwa Mbunge amefuatilia kwa muda mrefu na tulikwenda pamoja.

Mheshimiwa Spika, vile vile, masuala ya Kitongoji cha Kisaula na Lutala, wakati Mheshimiwa Waziri anahitimisha hapa hoja za bajeti yetu ya mwaka 2023/2024, tayari imeonesha tumetenga Shilingi milioni 20.7 kwa ajili ya kufanya upimaji, usanifu na kupanua mtandao wa maji kutoka Mradi wa Maji Iwela. Kwa hiyo, hili tayari tumeshalifanyia kazi. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili.

Mheshimiwa Naibu spika, swali la kwanza. Kwa kuwa maji chini ya ardhi ni Pamoja na chemchem zinazofumuka wakati wa masika na kupotea wakati wa kiangazi hasa mkoani Kilimanjaro;

Je, Serikali inazitambua na kuziwekea udhibiti chemchem hizo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa utafiti wa Chuo Kikuu cha SUA kimebaini kuwa maji chini ya ardhi yanapungua sana lakini Serikali haijaweza kudhibiti maji ya mvua ya kila msimu na kila mwaka yanayotiririka na kutuharibia barabara. Serikali ina mpango gani sasa wa kufanya project ambayo itaweza kudhibiti hali hiyo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shally Raymond, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, chemchem zote za Mkoa wa Kilimanjaro ni chemchem ambazo zina manufaa makubwa katika kuongeza maji katika miradi yetu inayoenda kwa wananchi. Hivyo tunailinda na kuidhibiti na tunaitambua vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, kuhusu maji chini ya ardhi hupungua na sasa maji yanapotea. Hapa tumshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan, tuna mitambo mitano ya kuchimba mabwawa na lengo la kuchimba mabwawa haya ni kuhakikisha maji yote ya mvua tuweze kuyatunza kwa ajili ya mhitaji wakati wa kiangazi. Tunataka kuonesha kwamba mvua ambazo Mwenyezi Mungu anatupatia siyo laana bali ni baraka na yanakwenda kutumika vizuri.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kumekuwa kuna utaratibu wa uuzwaji wa maji kupitia ma – bowser ya magari kwa gharama kubwa kwa wananchi na ilihali ya Serikali imeweka mtandao mzuri sasa hivi wa maji Kibamba;

Je, Serikali mko tayari kutoa kauli ya usitishaji wa uuzaji wa maji kupitia magari?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mtemvu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, usitishaji wa kuuza maji kwenye magari, huu sio utaratibu rasmi. Tutalifanyia kazi pamoja na Wizara husika.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza. Napenda kujua kama ratiba ya kukamilisha mradi mkubwa wa maji kutoka Mwanga kwenda Same mpaka Korogwe imebaki pale pale mpaka mwaka kesho mwezi wa Nne wananchi wa Same wanapata maji kutoka Mwanga?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa sasa hivi wananchi wangu wa Same hawana maji: Serikali ina mpango gani wa dharura kuchimba visima virefu katika Kijiji cha Ishire, Kitongoji cha Kavambuhu, Majevu, Kirinjiko, Makanya pamoja na Mabilioni?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza. Wizara tutafanya kila jitihada kuhakikisha mradi huu unakamilika ndani ya wakati kadiri tulivyosaini mkataba na mkandarasi.

Mheshimiwa Spika, kwa suala la dharura, maeneo yote yenye dharura kama Same Mjini na hasa maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Mathayo, tutafanya kila jitihada kuona mashine ambazo Mheshimiwa Rais ametununulia tuweze kuondoa changamoto hii, basi tutakwenda kuchimba hivi visima. Lengo ni wananchi kupata huduma kwa wakati.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Wananchi wa Kiegea, Mkundi pamoja na Kilimanjaro bado hawapati maji ya kutosha; je, ni lini watapata maji ya kutosha kutoka kwenye mradi wa Mguu wa Ndege? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Christine. Huu mradi mimi na yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati tulifika na kuufuatilia kwa karibu sana na anaendelea kuufuatilia. Mpaka sasa tumeshaweza kutekeleza mradi kwa asilimia 86. Maeneo ya Kihonda Kaskazini na Kilimanjaro, hivi navyoongea tayari wameshaanza kupata huduma.

Mheshimiwa Spika, maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Dkt. Christine na yenyewe pia tunaendelea kufanya jitihada kuona kwamba kufikia Desemba, mwaka huu 2023 na yenyewe pia yaweze kupata huduma ya uhakika.
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mji wa Nyeunge una idadi kubwa sana ya watu na unahudumiwa na mradi wa maji wa Rumea, Karebezo hadi Nyeunge ambao ulijengwa chini ya kiwango; je, Serikali iko tayari kuufanyia kazi mradi huu ili uweze kutoa huduma ya uhakika?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Eric Shigongo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala hili la ukarabati wa mradi, Mheshimiwa Mbunge ameshafika ofisini na tumeweza kuongea pamoja na wataalam. Naomba nimhakikishie, tulivyomuahidi mradi huu ni lazima tunakwenda kuutekeleza na tutahakikisha ukarabati uwe na tija na huduma inayotarajiwa ya maji safi na salama bombani iweze kupatikana kwa wakati.
MHE. MICHAEL M. KEMBAKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba kuuliza swali la nyongeza. Ni lini Serikali itapeleka fedha kwenye miradi ya Itununu, Tabweta ili iweze kukamilika na wananchi wa Tarime wapate maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Michael Mwita, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miradi hii aliyoitaja ipo katika mpango wa kulipa fedha katika miezi hii ya Julai na Agosti. Fedha zimechelewa kufika, lakini kuanzia wiki hii wakandarasi wapo kwenye utaratibu wa kuweza kulipwa kwa lengo la kuendelea na utekelezaji wa miradi hii.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Jiji la Dodoma limeendelea kukumbwa na kadhia kubwa ya uhaba wa maji: Je, Serikali ni lini mtakamilisha mradi wa visima vya Nzuguni ili kuondoa kadhia hii inayowakumba wananchi na wakazi wa Jiji la Dodoma? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kunti Majala, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ukamilishaji wa visima vya Nzuguni, kadiri tunavyopata fedha tutaendelea kumwezesha mkandarasi ili viweze kukamilika ndani ya miezi ya mkataba tuliyokubaliana naye. Tunafahamu changamoto kubwa inayokumba Jiji la Dodoma na tunaendelea na jitihada nyingi sana kuona kwamba pamoja na visima hivi na vyanzo vingine, tuweze kuondoa adha ambayo ipo kwenye Jiji la Dodoma.
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, kwanza niruhusu nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa ambayo nimeipata kuja kuuliza swali hapa. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa imani yake kubwa kwa kuniamini, nimefanya kazi na nimetua kijiti kwa Mheshimiwa Silaa na niko tayari kutoa ushirikiano wakati wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nina swali la nyongeza. Kwanza natambua kwamba Serikali imeweka katika bejeti yake kuongeza chanzo kingine cha maji katika Jiji la Mwanza, hususan Manispaa ya Ilemela kutokana na changamoto kubwa ya maji katika mji ule: Je, ni lini utekelezaji wa mradi huo wa chanzo kipya cha maji utaanza kutekelezwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula Mbunge wa Ilemela kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nipende kumpongeza kwa sababu suala hili amesha lileta mara kadhaa katika ofisi zetu na niseme tu jitihada zako zimesababisha Mheshimiwa Waziri Jumaa Hamidu Aweso kukuletea Mkurugenzi wa mamlaka mpya mwanamama, mchapakazi. Jitihada zako zimesababisha kuileta task force ya wataalam kuona kwamba Mwanza sasa inaenda kupata suluhu.

Mheshimiwa Spika, chanzo hiki kipya Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula naomba nikupe amani kwamba kadri wataalam wetu watakapo kamilisha kazi waliyopewa na Mheshimiwa Waziri Jumaa Hamidu Aweso, chanzo hiki mara moja kinakwenda kufanyiwa kazi ndani ya mwaka huu wa fedha.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi hii. Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imechimbiwa visima zaidi ya kumi na tano lakini hadi sasa havijapata pump ya kuendesha visima hivyo. Je, ni lini Serikali itatoa fedha ili visima vyote ambavyo vimechimbwa ndani ya jimbo langu viweze kufanya kazi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Yahya Ally Mhata kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, visima vilivyoko Nanyumbu tunavishughulikia na manunuzi ya pump yako kwenye hatua za mwisho.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali yanayotia moyo, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Mji wa Nachingwea ni mji unaokua haraka sana. Upo Mradi wa Maji pale Nachingwea ambao tayari sasa hivi imeonekana mradi ule hautoshelezi. Je, Serikali iko tayari kutupatia fedha Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ili kupanua Mradi ule wa Maji wa Mji wa Nachingwea?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kama ilivyo kwa Mji wa Nachingwea unakua haraka, Mji wa Liwale nao una mradi sasa una miaka zaidi ya miwili kwa ajili ya maji katika Mji wa Liwale. Je, Serikali ipo tayari kutupatia fedha ili tuondokane na adha ya maji pale Mjini Liwale? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Amandus, kwa niaba yake yameulizwa na Mheshimiwa Kuchauka, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu pesa Nachingwea kwa ajili ya kupanua mradi; nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, hili tunalifanyia kazi. Tayari lipo kwenye mipango kuhakikisha katika Mji wa Nachingwea wanapata huduma ya majisafi na salama na ya kutosheleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pesa Liwale, nimelipokea, tutalifanyia kazi. Pia naomba kumpa taarifa, wale wawekezaji wetu walishafika Liwale, naamini atakuwa amewaona, watakwenda kufanya usambazaji wa visima vilivyochimbwa. Yote hii ni kuona kwamba jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kumtua mama ndoo kichwani Liwale nazo zinaweza kukamilika.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Katika Mji wa Kasulu eneo la Mwilamvya kuna tatizo la upatikanaji wa maji. Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la maji katika Mji wa Kasulu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Genzabuke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya Kasulu tayari pia tuna mipango ya kuona kwamba tunakuja kuongeza huduma ya maji. Mwaka huu wa fedha tutafanya kazi kubwa sana Kasulu kuhakikisha maeneo ambayo maji hayajafika yaweze kupatikana.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini je, sasa Serikali haioni ipo haja ya visima vile ambavyo vilichukuliwa na DAWASA ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam viweze kurudishwa mikononi mwa wananchi, kwa sababu tangu vilipochukuliwa mpaka sasa hakuna marekebsho yoyote na ndiyo maana tunakosa maji mahali pengine kwa sababu visima vilikuwa ni vingi lakini DAWASA hawavifanyii kazi. Hivyo virudishwe kwa wananchi ili maji yaendelee kupatikana kulingana na hizi asilimia 30 mlizosema mpaka sasa yanapatikana?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili je, lini Serikali sasa mtarekebisha au mtaweka mabomba, kwani yaliyopo ni chakavu a ya zamani sana ambapo sasa hivi yanatitirisha maji tu na ni upotevu tu wa maji kwa Serikali lakini sasa tuombe muweze kuyarekebisha na wananchi tuendelee kupata maji safi katika mabomba ya majumbani? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawilii ya nyongeza ya Mheshimiwa Dorothy Kilave, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, visima vilivyochukuliwa kurudishwa kwa wananachi, visima hivi vilichukuliwa kwa sababu za kiufundi. Sasa hivi namna ambavyo kwa mfano Wizara ya Afya inaweza kumiliki hospitali zake, nasi Wizara ya Maji tunahitaji kumiliki vyanzo hivi vya maji vyote ili viwe chini ya uangalizi wa wataalam wetu. Kwa hiyo, cha kufanya hapa hatutavirudisha kwa wananchi bali tutaongeza nguvu kuhakikisha visima hivi vinakwenda kutumika na kuongeza usambazaji wa maji kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kubadili mabomba chakavu tayari hili lipo kwenye mkakati wa mwaka huu wa fedha 2023/2024 utaona Mheshimiwa Mbunge kazi huko namna ambavyo vijana wanachakarika. Nimpongeze sana CEO wa DAWASA ameingia kwa kasi na watendaji wake wote wanafanya kazi kwa kasi. Wiki iliyopita nimefanya ziara pamoja na DAWASA maeneo haya yote ninayozungumzia Mheshimiwa Kilave, nimeweza kuyapitia.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Nataka kujua wananchi wa Kata ya Kamoli hutembea muda mrefu kufata chanzo cha Kitagata ambacho hakijatengenezwa vizuri, hivyo kukanyaga maji na kuchota maji machafu. Nataka nijue mkakati uliopo kuimarisha hicho chanzo cha maji lakini yakivutwa ili kuwa karibu na makazi ya watu badada ya kutembea umbali mrefu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata hii ya Kamoli kuboresha chanzo na kuleta usambazaji. Katika mwaka huu wa fedha Mheshimiwa Mbunge kuna kazi itafanyika kuona kwamba chanzo hiki kinaendelea kuwa toshelevu kinakuwa endelevu na usambazaji wa kuwasogezea huduma wananchi ni moja ya kazi yetu mama Wizara ya Maji, tutafanya hilo Mheshimiwa Mbunge.
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Wakati wa usanifu wa maji kutoka Igunga kwenda Shelui wataalam wa Wizara waliwaaminisha wananchi kwamba yangetengenezwa matoleo kwa ajili ya kusambaza maji kwenye hizi kata ya Nguvumoja, Lugubu na Itumba lakini mradi umekamilika na matoleo ya maji hayajawekwa na wananchi hawajapata maji.

Je, Wizara hamuoni kutokutekeleza kwa kipengele hichi ni kuwachonganisha wananchi na Serikali yao sikivu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwa kuwa Wizara mmekuwa na utaratibu wa kutoa fedha kwa matokeo (P4R) na Mkoa wa Tabora tunafanya vizuri sana.

Je, hamuoni ni wakati sasa mtoe fedha ili kwenda kukamilisha huu mradi ili wananchi waendelee kuwa wanafurahia Serikali yao ya Chama cha Mapinduzi? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Awali ya yote ninapenda kukupongeza Mheshimiwa Ngassa kwa ufuatiliaji, lakini Mheshimiwa Ngassa Wizara hata siku moja haitaweza kuwa chonganishi kati ya Serikali na wananchi, tutaweza kufanya kwa bidii kubwa sana kuhakikisha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama mwenye uchungu wa wanawake wanaobeba ndoo kichwani inatekeleza miradi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutotoa matoleo ni sababu za kiufundi Mheshimiwa Mbunge, wakati fulani wakati usanifu unafanyika tulitarajia ingewezekana lakini population ya watu Tanzania sasa hivi inakua kila leo, kwa hiyo usanifu huu mpya utaleta maji ya kutosha na yatakuwa endelevu kwa eneo zima hili la Igunga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu P4R tuna kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza sana Dkt. Samia, tulikuwa na Mikoa 17 pekee yenye kupata fedha za P4R lakini sasa hivi ni Mikoa yote 25 Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amepambana fedha zimepatikana kwa Mikoa yote, na eneo la Tabora kama ulivyosema linafanya vizuri tayari fedha pia zimeanza kupelekwa na fedha zimeongezeka. Kwa hiyo, ninakutoa hofu, hili mimi na wewe naomba tuonane ili tuweze kuweka sawa. (Makofi)
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mradi wa maji wa Usalimwani - Mvumbi, Kitulo- Ijuni, Kidepwe - Madihani, Mariwa - Ikete ni miradi ambayo imesimama. Ni lini Serikali itatoa fedha ili miradi hii iweze kukamilika kwa ajili ya wananchi wa Wilaya ya Makete?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sanga, Mbunge machachari kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha tayari zimeanza kutoka wiki hii, tutarajie hata Wakandarasi wanaofanya miradi hiyo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge watalipwa.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na namshukuru Waziri kwa majibu mazuri. Changamoto ya kukosa maji katika Kata ya Kwekanga, Kwai, Malibwi, Mbwei, Makanya na Mlola ni changamoto muda mrefu sana. Suala hili nimeliongelea zaidi ya takribani Mikutano Kumi bila mafanikio yoyote na wananchi wangu wakiendelea kupata tabu ya maji.

Je, nini mkakati wa dharura wa Serikali kupeleka gari la kuchimba visima katika kata nilizozitaja?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kuna Mradi wa Magamba eneo la Gelwa Ali unaitwa Mtaa Na. 9 na survey imeshafanyika. Mradi ule ukikamilika unakwenda kuhudumia kata zaidi 13. Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kumpongeza Mheshimiwa Shekilindi, amekuwa mfuatiliaji nilikuahidi nitafika jimboni Mheshimiwa Mbunge, kipindi kilichopita sikuweza, baada ya Bunge hili nitahakikisha tunakwenda kuona maeneo haya na kuweka msisitizo ili kuhakikisha miradi hii inatekelezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa dharura tayari Mheshimiwa Mbunge tumekutengea shilingi milioni 300. Tunataka baada ya ukamilishaji wa hii survey visima hivi vichimbwe na hatutaishia tu kuchimba visima. Tutahakikisha tunasambaza na kujenga vichotea maji kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, fedha za Miradi ya Mbao tayari usanifu umekamilika. Mheshimiwa Mbunge, tayari tutaendelea kukuletea fedha. Sasa hivi tumekutengea milioni 300 na mgao ujao tutahakikisha tunakutengea fedha. Mimi mwenyewe nitakuja jimboni kuleta msukumo hii miradi iweze kutekelezeka.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, muuliza swali alisisitiza ukosefu wa maji katika maeneo ambayo ameyataja ya Mabwepande, Wazo pamoja na Mbezi Juu. Swali la kwanza; je, ni lini Serikali itaongeza speed ya kumaliza hiyo kazi ili wananchi Waheshimiwa Wabunge, pale waweze kupata hayo maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Mradi wa Maji kutoka Masoko katika Wilaya ya Rungwe unafanana kabisa kama ambavyo wanahangaika watu wa Wazo.

Je, ni lini watahakikisha watu wa vya Kasyeto, Mpumbuli pamoja na Segela wanapata maji kwa sababu ilipoanzishwa maji katika Mto Masoko tulitegemea sana watu wa maeneo haya wapate maji safi na salama na kwa wakati sahihi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Halima James Mdee, Mbunge Viti Maluum, yaliyoulizwa kwa niaba yake na Mheshimiwa Sophia Mwakagenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lini Serikali itaongeza kasi? Tayari tumejipanga na na kuanzia sasa tunaongeza kasi na kuhakikisha maeno haya yote tunakwenda kuyafikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na Mradi wa Masoko Rungwe, Mheshimiwa Mbunge ni shahidi mimi na yeye tulishawahi kuongea tukiwa Mbeya na hili tutalifanya pamoja mimi na yeye baada ya Bunge hili na kwa kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo, tutahakikisha hili suala la Mradi wa Masoko sasa linafikia mwisho wake.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya wakazi wa Jiji la Arusha kuletewa bili za maji tofauti na matumizi yao na hivi juzi Mamlaka ya Maji ya Jiji la Arusha imetangaza kuongeza gharama za maji kuanzia kesho. Je nini kauli ya Serikali?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Catherine Magige, Mbunge Viti Maalum kutoka Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipende kumpongeza amekuwa akifuatilia sana suala la hizi bili za maji kwa Jiji la Arusha na maeneo yote. Hata hivyo, kwenye suala la ongezeko la bei ambaho imetangazwa hapo kesho ni utaratibu tu ambao upo kikanuni na tayari EWURA waliweza kufuata taratibu zote na kushirikisha wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara ambayo iliweza kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na manung’uniko haya sisi kama Wizara tumelipokea na kuona namna gani tutalifanya. Lengo ni kuona huduma za maji zinabaki kuwa endelevu na zinaboreshwa kwa kutumia hizi fedha zinazochangiwa na wananchi, lakini vile vile kuhakikisha wananchi wanatumia katika gharama tunaziweza.
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Serikali nina swali moja la nyongeza. Kama katika Mji wa Karatu waliweza kushusha bei kutoka shilingi 3,500 mpaka shilingi 1,300 kwa unit. Je, inashindikana nini katika jimbo hilo hilo katika eneo la RUWASA vijijini majini kuuzwa kwa shilingi 2,500, kwa nini kwenye jimbo moja isishushwe bei ikawa ya uwiano Karatu Mjini na Karatu Vijijini ikawa na bei moja kuliko kuwa na bei mbili katika Mji wa Karatu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai, Mbunge wa Karatu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei za maji hazifanani kwa sababu ya teknolojia zinazotumika kusambaza maji. Teknolojia ambayo inatumika eneo la RUWASA ni tofauti na pale mjini. Kwa hiyo sisi kama Wizara tunachokifanya ni kuhakikisha bei zinakuwa rafiki kwa wananchi wa eneo husika. Kwa hiyo, kwenye maeneo haya ambayo yanahudumiwa na RUWASA bei ziko tofauti kwa namna ambavyo maji yanasukumwa na gharama za uendeshaji.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.

Kwanza kabisa ninamshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Naomba uniruhusu nimshukuru Mheshimiwa Rais wangu ametupatia fedha shilingi bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Ziwa Victoria kuleta Simiyu na Wilaya zake Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu, mkataba tumesaini juzi tarehe 27 mwezi wa Tano. Ahsante sana Mama yangu.

Mheshimiwa Spika, swali dogo, kwa kuwa Mkoa wa Simiyu ni Mkoa wa wafugaji; je, napenda kujua mradi huu utahudumia na upande wa mifugo pia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Esther Midimu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, namshukuru kwa kutambua jitihada za Mheshimiwa Rais na tutaendelea kuunga jitihada zake kwa kuhakikisha tunasimamia vema fedha zote ambazo anazielekeza kwenye miradi hii mikubwa. Kuhusiana na mifugo wakati Mheshimiwa Waziri akisaini mradi huu mkubwa alioshukuru Mheshimiwa Mbunge Esther, tayari tumetenga malambo sita kwa ajili ya mifugo, hivyo mifugo pia itanufaika. (Makofi)
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba mradi wa kutoa maji kutoka Mto Mafumbo kwenda kwenye Mji wa Mlowo na Vwawa unatekelezwa kwa haraka, ili kuondoa adha ya wakazi wa Mlowo na Vwawa wanaokabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa George Mwenisongole, Mbunge wa Mbozi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mto Mafumbo ni moja ya chanzo kilichogunduliwa na Ofisi yetu ya Bonde la Ziwa Tanganyika na tayari Ofisi ya Vwawa - Mlowo wanashughulika na chanzo hiki kuhakikisha kiweze kutumika. Wameshaandika proposal imekuja Wizarani, ninaahidi tutafanyia kazi kwa sababu ya umuhimu wake. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Natambua zaidi ya bilioni 10 zimetumika katika mradi wa maji Bunda kutoka Nyabeu kuleta Mjini. Bado kuna tatizo la usambazaji katika Kata zote 14, tunahitaji shilingi bilioni saba ili kata zote 14 zipate huduma ya maji safi na salama.

Ni lini sasa Serikali mtakamilisha usambazaji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, maeneo haya aliyoyataja Kata Saba tayari kama Wizara tunayafanyia kazi na usanifu unaendelea, tutahakikisha usambazaji hautachukua muda utakamilika ndani ya wakati. (Makofi)
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, Serikali ilifanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Mradi wa Kalole Group utakaohudumia Kijiji cha Skaungu, Kazi, Katonto na Kalole: Je, ni lini Serikali itaanza kujenga mradi huu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Serikali iliahidi kupitia Mradi wa MAU kuchimba visima kwenye mji mdogo wa Laela na Mpui ambapo kuna changamoto kubwa ya maji. Nataka kujua, hivyo visima vya dharura mtaanza kuchimba lini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deus Sangu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mradi wa Kaole sisi kama Wizara tumeshajipanga kwa mwaka ujao wa fedha tutakwenda kuutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, maeneo haya mawili ya Laela na Mpui, Mradi wa MAU unaendelea kufanya kazi kwa maana taratibu zinaendelea kukamilishwa na tayari kwa pale Laela utaratibu umekamilika na mwezi huu wa Juni mwishoni tutaanza kuutekeleza kwa kuchimba kile kisima. Pale Mpui mkandarasi ambaye ataenda kufanya usanifu ameshapatikana na mwezi huu Juni anakwenda kufanya kazi. Mara baada ya kumaliza usanifu, tutachimba visima hivi tulivyoahidi kwa wananchi. (Makofi)
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Tunaishukuru sana Serikali kwa kuanza kutekeleza miradi ya Vijiji vya Mkongokieyendo, Minyinga pamoja na Sakaa, lakini kwa masikitiko makubwa, mpaka sasa miradi ile imesimama na inasemekana mkandarasi hajalipwa fedha: Ni lini sasa Serikali italipa fedha ili mkandarasi amalizie miradi ile ambayo ina faida kubwa kwa wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtaturu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji hivi vyote alivyovitaja Mheshimiwa ni kweli miradi inaendelea na sisi kama Wizara tumeshaanza kulipa wakandarasi. Hapo katikati kidogo fedha hatukuwanayo, lakini tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, ametupatia fedha tayari na tunaanza kulipa wakandarasi. (Makofi)
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuahidi kupeleka mradi mkubwa wa Shilingi bilioni 42 kwa ajili ya wananchi wa Kinazi A na B na maeneo ya Msingo ambao hawana kabisa majisafi na salama. Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza mradi huu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Issa Mtemvu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tumshukuru Mheshimiwa Rais. Shilingi bilioni 42 ni mradi mkubwa. Mheshimiwa Mbunge hongera pia kwa kuendelea kufuatilia miradi hii mikubwa ya kimkakati na mradi huu tunaanza kuutekeleza mwaka ujao wa fedha. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Wananchi wa Kata za Kimuli, Businde na Bugara hupata changamoto sana ya maji hasa tunapoelekea wakati huu wa kiangazi, lakini ni eneo ambalo lina mvua za kutosha: Je, ni nini mkakati wa Serikali wa kujenga matanki makubwa ili wakati wa mvua tuwe tunavuna maji na wakati wa kiangazi kama hiki tunachokiendea wananchi wanaweza kupata maji ili kuondoa adha wanayopitia kuchota maji ambayo ni tope? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anatropia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kata hizi alizozitaja zina changamoto ya maji na sisi kama Wizara tunafahamu. Ushauri wa kujenga matanki makubwa tunauchukua, lakini vile vile tumejipanga kuhakikisha maeneo haya yote tunakwenda kuyapatia majisafi na salama. (Makofi)

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Je, ni lini wananchi wa Kata ya Ng’ang’ange katika Wilaya ya Kilolo watapatiwa fedha ya mradi wa maji au kuchimibwa visima ili waweze kupata majisafi na salama kwa sababu sasa hivi wanatumia maji ya mito? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakupongeza Mheshimiwa Dkt. Ritta, hata juzi nimekuona ukiwa na Mheshimiwa Waziri Aweso kuhakikisha changamoto ya maji inakwenda kutatuliwa ukiongozana na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo. Vile vile katika kata hii uliyoitaja ya Ng’ang’ange sisi kama Wizara tunafahamu na tunakwenda kupeleka utatuzi kwa kuchimba visima na unafahamu gari tumeshaifikisha, umeiona wewe mwenyewe. Kwa hiyo, kisima hiki kitachimbwa ndani ya mwaka ujao wa fedha. (Makofi)

MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Moja; kwa kuwa wananchi wa Mufindi Kusini wameamua kuwa na shughuli mbalimbali mbadala ili wasikate miti na kuharibu vyanzo vya maji. Je, Serikali iko tayari sasa kuwaunga mkono na itaanza lini kuchimba mabwawa ili waweze kufanya shughuli zingine mbadala kama za uvuvi katika eneo la Mufindi Kusini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuzingatia unyeti na uzito na umuhimu mkubwa wa Mto Ruaha kwenye Taifa letu. Je, Serikali iko tayari kufanya elimu kwenye Mamlaka za Serikali Mitaa ili itoe fursa kwa wananchi kujua pengine umuhimu wa kuhifadhi mto huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa David Kihenzile, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na uchimbaji wa mabwawa katika maeneo aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge. Kwanza nimpongeze kwa sababu alishiriki katika hili kuona kwamba tafiti inakamilika na kupita Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji, tafiti ile Mheshimiwa Mbunge imeshakamilika na tunatarajia mwaka ujao wa fedha tuweze kuchimba mabwawa maeneo yale ambayo tunaona yatakuwa ni msaada kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kwa suala la fedha kwa ajili ya kuendeleza semina mbalimbali kutoa elimu kwa jamii; kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, tayari sisi kama Wizara tumeanza kutoa elimu kwa hasa viongozi wa vyombo vya watumia maji, lakini sasa hivi tutakwenda zaidi kwa viongozi na makundi mbalimbali na jukumu hili litatekelezwa na Bonde la Rufiji.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri na yenye tija, naomba niulize maswali mawili madogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Jimbo la Vunjo kuna mabwawa mawili moja linaitwa Urenga katika Kata Kirua Vunjo Mashariki na nyingine ni Koresa Kata ya Kirua Vunjo Kusini yameharibika sana sasa hivi ni kama vile hayapo. Nataka nijue kama Waziri atakubali kutembelea eneo hili na kuyaona haya mabwawa ili aone kama watafanya nini kuyakarabati? (Makofi)

Swali la pili. Je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu ukamilishaji wa miradi iliyoanza mwaka juzi kule Mamba Kaskazini na Kusini, Mwika Kaskazini na Kusini na Marangu Mashariki na Magharibi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Charles Kimei kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kutembelea mabwawa ambayo kwa sasa hayafanyi vizuri. Mheshimiwa Mbunge, naomba nikuhaidi baada ya Bunge hili tutakwenda kuyatembelea na kuona nini kinaweza kufanyika kupitia watalaam wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na kukamilisha miradi Mheshimiwa Mbunge pia hili tutakapokuwa tunatembelea tutaona kwa nini miradi hii haijamilika kwa wakati? Nakuhakikishia tutahakikisha inakamilika ili wananchi waweze kupata huduma. (Makofi)
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, ni dhahiri nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa utekelezaji wa miradi hii iliyotajwa na Serikali, tunawashukuru sana Serikali. Pamoja na changamoto sasa iliyopo tayari miradi ya Tegeta A na Mshikamano tunayo mizuri usambazaji wa mabomba umekuwa ni changamoto sana kwa sababu ya yale maboza, magari yanayouza maji kwa wananchi…

SPIKA: Swali lako Mheshimiwa.

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kwa sababu tayari wanatakiwa wasambaze watoe kauli hapa ya kusitisha uuzaji wa maji kwa magari. Hilo ni swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa kuna mradi huo wa usambazaji maji…

SPIKA: Mheshimiwa Issa Mtemvu, hebu ngoja kwanza, Naibu Waziri kwa sasa hivi hasikilizi mchango, anataka swali ili akujibu kwa sababu hiki ni kipindi cha maswali na majibu. Muulize swali Naibu Waziri akujibu.

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza Serikali mpo tayari kutoa kauli ya usitishaji wa uuzaji wa maji kwa magari Jimbo la Kibamba kwa sababu mlishatekekeleza miradi miwili kule?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa sababu King’azi hakuna maji kabisa wanatumia maji ya chumvi, ni lini mradi wa usambazaji Dar es Salaam Kusini utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mtemvu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na uuzaji wa maji kwenye magari hili suala tulishalipigia marufuku kwa maeneo mengi na hususani eneo la Kibamba, lakini tutaendelea kuhakikisha kwanza tunahakikisha miradi ile imekamilika na uhakika wa maji ya uhakika wa kila siku kwa wananchi, suala hili naamini litatekelezeka.

Mheshimiwa Spika, suala la Dar es Salaam kusini maeneo ya King’azi usambazaji wa mabomba, tunatarajia mapema mwaka wa fedha ujao kuanzia mwezi Julai au Agosti, suala la usambazaji wa mabomba katika maeneo haya yote aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge tunakuja kuyafanyia kazi.
MHE FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Jiji la Dodoma limekuwa lina matatizo sana ya upatikanaji wa maji na hivyo kuwa kero kubwa sana kwa wananchi. Je, ni nini mkakati wa Serikali wa kupunguza tatizo hili ili kusudi wananchi waweze kufaidika na maji safi?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fatma Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Dodoma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali kwa Jiji la Dodoma Waheshimiwa Wabunge naamini ni mashahidi tunaendelea kufanya kazi nyingi sana kuona tunakwenda kukomesha tatizo la maji katika Jiji la Dodoma kwa umuhimu wake kama Makao Makuu ya Nchi tuna miradi mingi mikubwa, ya kati na midogo, tunatarajia mwaka ujao wa fedha miradi mingi itaanza kupeleka huduma ya maji maeneo yote ambayo yanapata changamoto.

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakamilisha miradi ya maji katika Kata ya Duru na Yasanda, Jimbo la Babati Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asia, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, maeneo ya Babati Vijijini, Miradi ambayo ipo kwenye utekelezaji tunaendelea kupambana kuona inakamilika ndani ya wakati na maeneo ambayo usanifu umekamilika pia mwaka ujao wa fedha tutaendelea kuongeza nguvu katika maeneo yote ya Babati Vijijini ili kupata maji safi na salama.

MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kuuliza, je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya maji katika Tarafa ya Ngerengere?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hamisi Taletale, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Tarafa ya Ngerengere tayari tuna miradi ambayo ipo kwenye utekelezaji, lakini tuna mipango thabiti ya kuona kwamba eneo hili nalo linaenda kupata huduma ya maji safi na salama mwaka ujao wa fedha Mheshimiwa Mbunge atashuhudia shughuli nyingi sana zikifanyika katika Tarafa hii.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, ni lini Wizara ya Maji itaanza kujenga au kutekeleza Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya Wilaya ya Muleba?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kikoyo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ziwa Victoria kwa Muleba Mheshimiwa Mbunge alikuja tukaongea na menejimenti, tulishakubaliana mwaka ujao wa fedha tunakwenda kukamilisha usanifu na kuanza kuona uwezekano wa kufanya mradi huu.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itapeleka Mradi wa Maji katika Kata ya Kalulu na Kata ya Jakika? Ahsante.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Kata hizi alizozitaja mwaka ujao wa fedha tunatarajia kupeleka maji safi na salama kwa kupitia visima vilevile maeneo mengine tutatumia vyanzo vile vilivyo vya uhakika.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Nitumie nafasi hii kwanza kutoa pongezi na shukurani kwa Wizara pamoja na Serikali kwa ujumla kwa hatua mbalimbali zinazofanyika kuhakikisha Visiwa vya Ukerewe vinapata maji safi na salama. Swali langu, Serikali sasa iko tayari kutoa maelekezo ili wakati wa usambazaji wa maji wataalam wazingatie mtawanyo kuhakikisha kwamba kila kitongoji kinafikishiwa mtandao huu wa maji? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph Mkundi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza napokea shukrani zako na wewe nakupongeza kwa sababu umekuwa mfuatiliaji na tumekwenda Ukerewe zaidi ya mara mbili mimi na wewe na kazi nzuri unaifanya.

Mheshimiwa Spika, suala la usambazaji maji kwa kila kitongoji, hiyo ni moja ya mipango ya Wizara. Nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo tumeweza kutatua changamoto ambayo ilikutesa kwa muda mrefu, suala la usambazaji maji pia tunakuja kulifanyia kazi na nitoe wito kwa Mameneja wote wa Wilaya ambao wananisikiliza waweze kuhakikisha wanafika katika vitongoji vyote na maji yanasambazwa kadri ya miradi ilivyosanifiwa. (Makofi)
SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipanga kupeleka shilingi bilioni 195 ili kumaliza changamoto ya maji katika Mkoa wa Shinyanga. Nataka kujua Serikali imefikia wapi kutekeleza mpango huu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Salome Makamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuleta shilingi bilioni 195 katika eneo la Shinyanga ni miradi ya kimkakati ambayo Wizara tunaendelea kutafuta fedha. Mara tutakapopata fedha tutaendelea kuzileta kwa awamu ili kuhakikisha mradi huu unatekelezeka. (Makofi)
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kuna changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa maji katika Kata ya Bonyokwa Jimbo la Segerea. Je, ni lini changamoto hii itakwisha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecilia Paresso, Mbunge Viti Maalum kuwa maeneo ya Segerea, Bonyokwa tuna miradi ambayo iko mwishoni kabisa kukamilika, tunatarajia mapema mwaka wa fedha ujao maeneo haya yote yanakwenda kupata huduma ya maji safi na salama.
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, mradi wa maji Kiwira unaanza lini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa umuhimu kabisa naomba kujibu swali hili kwa heshima kubwa.

Mheshimiwa Spika, mradi umeshaanza kutekelezwa kwa maana ya kwamba tayari maeneo kama ya New Forest na Mchangani Mkandarasi ameshaanza kujenga camp ili kuona kwamba anafanya mobilization lakini maeneo ya Intake na maeneo ya Sistila kule juu karibu ya MUST wanaendelea na clearance kwa ajili hiyo ya kujenga camp kuona kwamba kazi zitaanza mara moja lakini suala lililoko mezani kwa sasa hivi, tayari Wizara ya Fedha imetoa exchequer ambayo imeingia kwenye Wizara ya Maji ukiisoma unaiona sasa hivi tunachosubiri tu ni fedha kuingia kwenye account na mamlaka kuweza kuingiziwa hiyo fedha mara moja Mkandarasi alipwe aendelee na mradi. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa hiyo hela zinachelewa wapi kwenu au Wizara ya Fedha?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niombe kufanya marekebisho kidogo kwa sababu Bonde la Wami Ruvu sio Bonde la Mto Ruvu haya ni mabonde mawili tofauti lakini pamoja na marekebisho hayo na majibu mazuri ya Serikali juu ya Bonde la Wami Ruvu naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali haioni sasa ni muda sahihi Wizara ya Maji kushirikiana na Wizara ya Mifugo kwenye Jimbo la Kibaha Vijijini kwenye Kata ya Kwala na Dutumi kujenga mabwawa ili kuzuia mifugo isiende kuharibu kingo za Mto Ruvu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa kuna kazi nzuri imefanywa na Serikali kwenye Bonde la Wami Ruvu la kuunda vikundi na kutambua namna wanavyoweza kutoa huduma kwa wafugaji.

Je, Shughuli hizi ambazo zimefanywa kwenye Bonde la Wami Ruvu Serikali haioni sasa ni muda sahihi kuja kuzifanya kwenye Bonde la Mto Ruvu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Michael Mwakamo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote Mheshimiwa Mbunge nakupongeza kwa uelewa, hili ni Bonde la Wami Ruvu lakini unahitaji zaidi tujikite kwenye Bonde la Ruvu na huku kote Bodi yetu ya Maji ya Wami Ruvu inafanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na ushirikiano na Wizara ya Kilimo nikutoe hofu sisi ni Serikali tunafanya kazi kwa team work kwa hiyo, tutashirikiana na Wizara ya Kilimo kuhakikisha tunaendelea kujenga maeneo ya kunyweshea mifugo maeneo yale kule yenye wafugaji kwa lengo la kuzuia uharibifu kwenye kingo za huu Mto Ruvu na hili tutalifanya kwa umoja wetu kwa kushirikiana kama Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Jumuiya za watumia maji upande wa Ruvu. Tutahakikisha viongozi ambao wanasimamia Bonde la Wami Ruvu namna walivyofanya upnde huu wamesikia watafanya. Lengo ni kuhakikisha ushirikishwaji wa pamoja unafanyika kwa pande zote.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na ninashukuru kwa majibu ya Serikali. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa sasa Serikali imetamka wazi kwamba mradi huu utaanza bajeti ijayo 2023/2024 sasa Serikali inaweza kuwaambia wananchi wa Bunda kwamba ni Bajeti kiasi gani imetengwa kwa mradi huo?

Swali la pili; kwa kuwa Serikali imetumia zaidi ya milioni 52 kufanya usanifu yakinifu kama kuchimba malambo ya Salama A, Lakana, Burundu, Kambugu, Tingirima na Mihingo. Je, ni lini miradi hii itakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Boniphace Getere kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na bajeti kwenye Jimbo la Bunda, Mheshimiwa Mbunge unafahamu na nikupongeze kwanza kwa ushirikiano wako ulifika Wizarani umeweza kukutana na Waziri na Katibu Mkuu. Yote hii ni jitihada ya kuona kwamba hili linafanyika. Kwa eneo lako la Bunda zaidi ya bilioni 1.7 imepangwa na itaenda kutumika kutokana na zile bilioni 750 kwenye ule mradi wa Ziwa Victoria kwako ni zaidi ya bilioni 1.7.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na uchimbaji na ukamilishaji wa haya mabwawa Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Waziri alishakuelekeza vizuri na tumshukuru zaidi Mheshimiwa Rais kwa kutupatia sisi Wizara ya Maji vifaa au vitendea kazi. Tumeshapata mitambo na huu mtambo mmojawapo wa kuchimba mabwawa unaletwa Bunda mahsusi kuhakikisha haya Mabwawa yanakwenda kuchimbwa na yanakamilika na Mheshimiwa Mbunge tutakuharifu tutakwenda pamoja kwa sababu tunashirikiana vizuri.
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa tayari Mkandarasi anayetekeleza mradi wa Nduku Busangi Ntobo na mradi wa Mwarugulu tayari amesha supply vifaa na hajalipwa fedha. Kufanya hivyo, umesababisha mradi kusimama. Ni lini sasa Wizara itaenda kumlipa fedha mkandarasi ili aweze kutekeleza miradi hiyo miwili ya Mwarugulu na mradi wa Busangi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hii yote uliyoitaja ni kweli utekelezaji unaendelea na ulipwaji wa madeni kwa wakandarasi tayari tumeanza kama Wizara. Fedha tunavyozipata tunaendelea kupunguza madeni na kuhakikisha wakandarasi wote walipwe ili waweze kuendelea na miradi hii.
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, haya ndio majibu bora kabisa ya Serikali, natoa pongezi kwa Mama Samia Suluhu Hassan lakini pia Waziri Aweso na Waziri Prisca Mahundi. Niliomba maji haya kwa ajili ya shule hiyo na nimepewa na wanafunzi pale na jamii yote niipongeze Serikali sana sana, naomba nitoe shukrani zangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali moja tu la nyongeza. Shule hii ina wanafunzi 1500 na ni wengi sana kwa hiyo bill ya maji, ankara imekuwa kubwa sana. Je, Serikali inaweza kutoa ruzuku sehemu ya ankara hii ili wote wapate maji, sasa wanafunzi wanachangia maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Awali ya yote nipende kupokea pongezi za Mheshimiwa Mbunge lakini na yeye pia ni kupitia jitihada zake kama mwenyewe anavyosema, alikuja ofsini tuliweza kuongea kwa pamoja na maombi yake tumeyafanyia kazi. Kuhusiana na kuona mradi huu unabaki kuwa endelevu suala la bill shuleni na wanafunzi wote waweze kupata maji kila siku, Mheshimiwa Mbunge nimelipokea tutalifanyia kazi kwa pamoja.
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata nafasi. Mtaa wa Mikwambe Kata ya Twaangoma kuna mgogoro wa kisima cha maji ambacho kimejengwa katika kiwanja ambacho amemilikishwa mtu binafsi. Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua mgogoro huo ili wananchi waendelee kupata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Chaurembo kama ifauatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mgogoro huo upo lakini DAWASA tayari wanaufanyia kazi na kwa niaba ya Wizara DAWASA watahakikisha mgogoro huu unaisha kwasababu maeneo ya aina hii yamekuwa mengi na tumekuwa tukimaliza. Kwa hiyo, hata hili pia sisi kama Wizara tutahakikisha linakamilika ili huu mradi uweze kutoa huduma kwa wananchi.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kumekuwa na changamoto ya wanafunzi kwenye Jimbo la Momba kupoteza maisha kwa ajili ya kwenda kufata maji mtoni. Siku za usoni tulipoteza mwanafunzi wa Momba Secondary na tukapoteza mwanafunzi wa Sekondari ya Kamsamba kwa sababu wanaenda kufata maji mtoni kwa mwendo mrefu. Je, ni ipi kauli ya Wizara ya Maji kwa udharula wake kwenda kutuchimbia visima kwenye hizi Sekondari ili tusiendelee kupoteza maisha ya watoto wetu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Condester kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikupe pole sana kwa wananchi kupata kadhia hizi lakini sisi kama Wizara ni sehemu ya kuona kwamba tunafikisha maji safi na salama maeneo yote yanayotoa huduma, na kwa eneo hili la shule naomba nikuahidi kwamba tutakuja kuwachimbia kisima na kama kuna kisima jirani basi tutafanya extension ili kuhakikisha wanafunzi hawaendi mtoni na kupata madhara.

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nataka nimwombe Mheshimiwa Naibu Waziri, Je, yupo tayari kuongozana na mimi Mbunge wa Jimbo la Mbozi kwenye mji wa Mlowo kuangalia hivyo vyanzo vya maji na kuhakikisha kwamba yote aliyosema yataenda kutekelezwa kwa wakati?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa George Ranwell Mwenisongole Mbunge wa Jimbo. Awali ya yote nipokee pongezi lakini Mheshimiwa Mbunge na wewe nakupongeza na ninakusihi tuendelee kushirikiana. Ufuatiliaji wako wa karibu ndio matunda ya miradi hii kufika hatua hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuongozana Mheshimiwa Mbunge, kama tulivyoongea ulipokuja Wizarani kufuatilia miradi hii, niko tayari na tutakwenda kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa wakati.

MHE. DKT. PIUS STEPHEN CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa hii nafasi kuuliza swali la nyongeza. Katika Jimbo la Manyoni Mashariki kuna mradi wa maji wa Kintiko wa vijiji 11 Mkandarasi alisaini Mkataba mwezi Februari mwaka huu lakini mpaka sasa hivi kazi haijaanza. Nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba Mkandarasi anaanza kazi ya kumalizia huu mradi? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Chaya Mbunge wa Jimbo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo anaongelea Mheshimiwa Mbunge ni kweli lakini nampongeza kwanza Mkandarasi ameanza kufanya kazi zile za awali na kinachosababisha hajaanza anasubiria advance payment lakini ninamsihi pale anapoweza kuendelea kufanya aendelee kwa sababu malipo haya yako mwishoni na yeye pia atalipwa kwa sababu tumeshapokea andiko lake.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Serikali imenunua magari ya kuchimba maji katika kila Mkoa na yako chini ya DDCA. Je, ni lini yatakuwa chini ya Wahandisi wa maji wa Mikoa?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare kuhusiana na magari ya uchimbaji visima kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwa sasa hivi magari haya yako chini ya DDCA tayari taratibu za ndani za kiwizara zinaendelea wakati wowote mambo yote yatakaa sawa kwa RMs wa Mikoa yote.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji. Wilaya ya Mbongwe ina maeneo yaliyo na changamoto ya maji. Je, ni lini Mbogwe mtatupa gari hilo la kuweza kuchimbia visima ili wananchi waweze kupata maji safi na salama kupitia hayo, magari mliyoleta?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maganga Mbunge wa Mbogwe kama ifuatavuyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Maganga anafatilia sana na hili tumeshaongea. Mheshimiwa Maganga naomba uiamini Wizara, mimi mwenyewe na wewe tutakwenda kuhakikisha kazi zinakwenda kuanza kwa wakati na visima vitachimbwa.

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Je, ni lini Serikali itatusaidia changamoto ya maji katika kata ya Kasokola katika Manispa ya Mpanda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Awali ya yote nipende kumpongeza Mheshimiwa Mbunge Kapufi kwa kweli umekuwa ukifuatilia kata hii na nikuhakikishie katika maeneo ambayo tunakwenda kupeleka jitihada ni pamoja na kata hiyo uliyoitaja kuhakikisjha wananchi nao wananufaika na hekima kubwa anayotumia Mheshimiwa Rais wetu kuhakikisha wanawake tunawatua ndoo kichwani.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani kutuongezea visima virefu Mkoa wa Simiyu tukiwa tunasubiri mradi wa Ziwa Victoria?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nampongeza Mheshimiwa Esther Midimu kwa kweli naye pia ni mfatiliaji mzuri lakini nikupongeze kwa sababu ulishiriki katika usainishaji wa mradi ule mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria lakini masuala haya ya uchimbaji wa visima pia yatakwenda sambamba na maji kuvutwa kutoka Ziwa Victoria na visima hivi vyote mwaka ujao wa fedha tutajitahidi maeneo mengi kuyafikia.

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, nilitaka kujua ni lini sasa Serikali itapeleka fedha kwenye mradi uliochukua muda mrefu mradi wa Inkana Isarye ulioko Nkasi Kusini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali la pili, nilitaka kujua ni lini sasa Serikali itakamilisha mradi wa kutoa maji katika Ziwa Tanganyika na kusambaza Mkoa wa Rukwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Awali ya yote nipende kumpongeza Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata Mbunge wa Viti Maalum kwa ufatiliaji wake mzuri na nipende kuhakikishia malipo ya mradi huu ambao umechukua muda mrefu ni mmoja wa vipaumbele vya Wizara kuhakikisha miradi yote inakamilika. Lengo la kupata maji bombani linatimia kwa sababu tunahitaji kuona tunapunguza umbali mrefu wananchi wa kutembea, vilevile kusambaza maji kutoka Ziwa Tanganyika ni moja ya vipaumbele vya Wizara. Mheshimiwa Bupe hili nalo pia Wizara tunalipa uzito na tutahakikisha maeneo yote ya Nkasi Kusini na Kaskazini kote tuweze kuyafikia na miradi iweze kukamilika.
MHE DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Jimbo la Njombe Mjini pamoja na kwamba linaonekana ni jimbo la mjini, uhalisia ni kwamba lina vijiji vingi sana ambavyo bado havina huduma ya maji kama Uliwa, Ihanga, Mikongo, Liwengi na Mtira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawajaingizwa katika mpango mkubwa wa maji wa P4R. Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba na vijiji hivi vinapata huduma hii ya maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deodatus Phillip Mwanyika Mbunge wa Njombe Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo yote haya aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge ni kweli. Mheshimiwa Mbunge nikupongeze hili mimi na wewe tumeshalijadili na tayari tumeanza kulifatilia. Maeneo ambayo hayata nufaika na mradi wa P4R ambao tunautekeleza kwa kutimiza vigezo vya masharti ya namna ambavyo unatekelezeka yatafanyiwa huduma kwa kupitia fedha za mfuko wa maji lakini vile vile fedha nyingine ambazo tunazipata kwenye namna nyingine ya upatikanaji wa fedha ndani ya Wizara.

Mheshimiwa Mbunge, nikuondoe hofu, kwa maeneo ambayo P4R haitafika haimaanishi hatutaweza kutekeleza miradi. Tutatekeleza miradi na wananchi watapata maji safi na salama ya kutosha na wote wataendelea kunufaika na kutuliwa ndoo kichwani.
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwanza niishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi wa Igalula kwa kuanza kujenga bwawa kwa ajili ya kutatua changamoto, lakini tatizo hili pia lipo Igunga kwenye Kata za Itumba, Lugubu na Nguvumoja. Maji yamekuwa yakijaa kwa sababu ule ni ukanda wa Bonde la Mbeya ambalo linakwenda mpaka Igalula.

Je, ni lini Serikali itafanya kwa wananchi wa Jimbo la Igunga katika kutatua changamoto hii? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nipende kupokea shukrani kwa Serikali kutekeleza wajibu wake, na kwa maeneo ya kata ulizozitaja kwenye Jimbo la Igunga Mheshimiwa Mbunge na yenyewe pia tutaendelea kuwaletea wataalam waweze kufanya usanifu na tuweze kuchimba mabwawa maeneo yote ambayo yatasaidia kuondosha na kupunguza mafuriko.
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru, katika Kata za Fukayosi na Makurunge katika Jimbo la Bagamoyo, DAWASA Chalinze wamesambaza miundombinu ya maji mwaka wa pili sasa lakini maji hayatoki.

Je, ni lini sasa maji katika maeneo haya yatatoka?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, naomba niwe nimelipokea, nikalifanyie ufuatiliaji kwa nini maji hayatoki na usambazaji umefanyika.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa tatizo la maji kutiririka hovyo wakati wa mvua ni tatizo kubwa sana kwa maeneo ambayo yako kwenye milima ukiwemo Mkoa wa Kilimanjaro.

Ni lini sasa Serikali italeta muswada hapa Bungeni ili nyumba zote zinazojengwa ziwekewe vikinga maji na kutumia maji yale ya mvua?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuleta muswada niseme nimelipokea, lakini sisi kama Wizara tayari tumejipanga na kuona kwamba mabwawa tutakayoyachimba tutaweka kwenye maeneo yote ambayo ni korofi kwa sasa, na tumshukuru Mheshimiwa Rais ameweza kutupatia vitendea kazi, tumeshanunua seti tano kwa ajili ya uchimbaji wa mabwawa.

Mheshimiwa Spika, lakini hilo aliloliongea Mheshimiwa Mbunge naomba niseme nimelipokea.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, wakati Serikali ikitumia gharama kutafuta vyanzo vya maji, Kyerwa ina vyanzo ambavyo viko tayari; moja ni Mto Kagera lakini na Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza, ni lini Ziwa Victoria na Mto Kagera vitatumika kuwapatia wananchi maji safi na salama ili itimie asilimia 80 kama maeneo mengine?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, wakati Serikali ikiwa na kaulimbiu ya kumtua mama ndoo hata miradi michache iliyopo ya maji wananchi hutembea umbali mrefu kwenda kufuata vyanzo hivyo vya maji.

Swali langu, ni lini au ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha maji hayo yanapatikana kwenye kaya za watu kama ilivyo maeneo ya mjini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Anatropia Theonest kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, lini Serikali itatumia Ziwa Victoria? Kwenye bajeti yetu ya mwaka 2023/2024 Mheshimiwa Waziri alisisitiza hapa kwamba Ziwa Victoria ni moja ya chanzo ambacho kitaendelea kutumika kwa sababu tayari tumeanza kukitumia kwa maeneo ya Kyerwa na Kyerwa ni Jimbo ambalo nimekwenda mara tatu mimi mwenyewe na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo, kwa hiyo, ni jimbo ambalo nimelifanyia kazi sana. Lengo ni kuhakikisha kwamba kwenye hili swali lako la pili kwamba lini kuona kwamba maeneo yote yatafanyiwa kazi kupata maji safi? Ndio kazi inayoendelea na ni maagizo ya Mheshimiwa Makamu wa Rais ambaye nilikwenda naye pale Kyerwa lakini na sisi kama Wizara tunaendelea kuyafanyia kazi Jimbo la Kyerwa.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafsi na mimi niulize swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuishukuru Serikali kwa kutuletea Mradi wa Maji kutoka Lake Victoria ni lini sasa Serikali italeta mabomba ili kazi ianze kwa kasi kutokana na shida ya maji tuliyonayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Margaret Sitta kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni lini mabomba yatafika? Mwezi wa saba tunatarajia mabomba yawe yamefika kutoka India na tayari kazi zimeshaanza, wakandarasi wa miji 28 tayari wapo kazini. Nikupongeze kwa ufuatiliaji na nilishakuahidi kwamba tutakwenda pamoja Urambo na kuhakikisha mabomba yanaanza kufanya kazi. (Makofi)
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa swali la nyongeza. Kwanza niipongeze Wizara tayari imeanza kutumia Mto Kagera kuwapatia wananchi wa Kyerwa maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali, Mradi wa Maji wa Kata ya Kimuli ambao unapeleka kwenye vijiji vitatu tayari umeanza, lakini mkanadarasi haendi vizuri kwa sababu bado hajalipwa pesa ya certificate ya kwanza; je, ni lini Serikali itamlipa mkandarasi huyu ili wananchi wa Kata ya Kimuli waanze kupata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Innocent Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nipokee pongezi kwa sababu kazi inayofanyika ni kwa sababu ya ufuatiliaji wake makini, na kuhusiana na malipo ya mkadarasi Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Wizara tunaendelea na michakato ya kuona wakandarasi wote tunakwenda kuwalipa kwa sababu ni wengi wako kwenye maandalizi ya malipo.
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi, pamoja na majibu mazuri na kazi nzuri inayofanywa na Wizara hii kwa maana ya Naibu Waziri na Mheshimiwa Waziri, ninayo maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Tarafa ya Suba yeye vijiji 20 na sio 17 vijiji vinne kwa maana ya Kijiji cha Ruhu, Muundwe, Kibuyu na Mkengwa ni vijiji ambavyo havina mradi wowote wa maji mpaka sasa. Ninataka nipate kauli ya Serikali juu ya vijiji ni lini sasa vitapata maji safi na salama?

Mheshimiwa Spika, lakini swali langu la pili, pamoja na vijiji 16 kuwa na maji safi na salama lakini vitongoji katika vijiji hivi maji hayajatapakaa kwenye vitongoji. Nayo pia nilitaka nipate kauli ya Serikali, kwamba Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuhakikisha angalau vitongoji kwenye vijiji hivi 16 vinapata maji safi na salama kwa ajili ya huduma ya maji kwa wananchi hao?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Chege kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, awali ya yote niseme nimepokea marekebisho ya idadi ya vijiji vyake lakini vilevile katika maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge nipende kumuelekeza Meneja wa Wilaya aendelee kufanya jitihada za kuona anapata visima ili vijiji hivi vipate maji. Mheshimiwa Mbunge eneo lako ni moja ya maeneo yanayonufaika na mradi ya miji 28. Kwa hiyo, wakati miji 28 utekelezaji unaendelea na ni kwa sababu ni mradi wa muda mrefu, jitihada za miradi ya muda mfupi zitaendelea kufanyika na ushirikiano wako namna ambavyo umekuwa ukiufanya, tutahakikisha tunafanya yale tuliokubalina.

Mheshimiwa Spika, katika vijiji hivi 16, vitongoji ambavyo havina maji tutahakikisha tunasambaza maji, Meneja wa Wilaya tayari tumemuelekeza na ninamsisitiza ili ahakikishe maeneo yote yanapata maji safi na salama. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Mpango wa kutekeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Kata za Magata, Muleba, Buleza, Chikuku na Kagoma utaanza lini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Kagera, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge Oliver, kwanza tulishakaana naye ofisini na tulishamwelekeza. Mheshimiwa Mbunge nakupongeza kwa ufuatiliaji, hizi kata ulizozitaja kama tulivyokubaliana ni lazima mwaka ujao wa fedha tuhakikishe na zenyewe zinakwenda kupata maji safi na salama. (Makofi)
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, mwaka 2018, Serikali ilichimba kisima kwenye Kijiji cha Mayi lakini mpaka leo hakijaweka miundombinu na hivyo hakitumiki, nini kauli ya Serikali?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mwaka wa 2021/2022 Serikali ilitangaza kandarasi ya visima 13, mpaka leo imechimba vitatu tu na hivyo tunawadanganya wananchi. Naomba kujua Waziri anasema nini juu ya visima hivyo ambavyo havijachimbwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Monni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kisima kilichochimbwa mwaka 2018, Mheshimiwa Mbunge tutakisimamia kuhakikisha tunaleta usambazaji kwa wanufaika wote kwenye kile kisima. Kwa visima hivi ambavyo tulivipitisha mwaka wa fedha 2022, Mheshimiwa Mbunge Serikali haiwezi kudanganya kwa sababu suala letu sisi ni kuhakikisha tunapeleka huduma kwa wananchi. Kwa hiyo, vile visima vilivyobaki lazima tuvifanyie kazi tutakuja kuvichimba kadiri tunavyopata fedha katika mwaka wa fedha 2023/2024.

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Je, ni lini visima vilivyochimbwa katika majimbo ya Ndanda, Nanyumbu na Tandahimba wananchi wake wataanza kuyatumia maji hayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Agnes Hokororo, Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Hokororo naye pia ameshafika ofisini na tumeweza kujadiliana masuala ya visima vyote vilivyochimbwa kwenye haya majimbo aliyoyataja. Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa tuonane ili tuweze kupanga mkakati baada ya Bunge hili twende kule site tutaangalia namna gani ya kuona tunatekeleza kwa pamoja.
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Sengerema kuna mitambo imewekwa kwa ajili ya kuchimba visima na visima vilivyochimbwa ni vitano kati ya visima 38. Nini kauli ya Serikali kuhusiana na mitambo hiyo kukaa leo mwezi wa pili iko Sengerema na visima havichimbwi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Tabasam, Mbunge wa Sengerema, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mitambo hii tumeisambaza mikoa yote na Mkoa wa Mwanza ni mnufaika kwa mitambo ambayo iko Sengerema ilikuwa na michakato inafanyika ili kuona tunaendelea kutenda kazi na nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge mara baada ya Bunge hili kazi zitaendelea na mitambo ile itamaliza visima 38 na kuhamia wilaya nyingine.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nimesikia majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa ninazungumzia kata 97 za Mkoa wa Rukwa ambazo hazina maji kutoka Ziwa Tanganyika na hapa wanasema wamejiandaa kwa mwaka wa fedha kumwandaa mtaalam mshauri.

Je, ni lini utaratibu wa kumpata huyo mtaalam mshauri na process kuanza mpaka mradi kukamilika kuanza kutoa maji kwa Mkoa wa Rukwa?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, mwaja jana kata tano za Jimbo la Nkasi Kaskazini, tulinunua maji ndoo moja shilingi 800 mpaka 1,000.

Je, mna mkakati gani wa dharula wa kuweza kupeleka maji kwenye hizo kata wakati tunasubiri mradi mkubwa wa Ziwa Tanganyika ambao ndio suluhisho la jambo hili?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimpongeze Mheshimiwa Aida Khenani, amefuatilia hili suala kwa muda mrefu na sisi kama Wizara tunakupongeza na hatutakuangusha na hatutakuwa kikwazo. Hizi Kata zote tutakuja kuhakikisha zinapata maji safi na salama. Lakini kwenye hizi kata tano za swali lako la pili, mkakati wa Wizara kwenye maeneo ya aina hii ni kutumia vyanzo vya maji rafiki vilivyokaribu, ikibidi kuchimba visima. Na kwa sababu tayari tuna magari basi tutachimba na kuweza kujenga vichotea maji na kuwasambazia wananchi ili kupunguza adha ya maji.
MHE. HAMIS M. MWINJUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na nashukuru kwa majibu mazuri na ya kutia moyo ya Serikali hasa kuhusiana na bomba la kilomita 14.5 na tarehe yake ya kukamilika. Hili ni moja ya matatizo tu nataka kupata commitment ya Serikali kuhusiana na tarehe ya kukamilika kwa mfumo mzima wa usambazaji ukiachilia mbali kilomita 14.5? Hilo ni la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kama muda utaruhusu naomba kuambatana na aidha Waziri au Mheshimiwa Naibu Waziri kwenda Muheza ili jibu atakalonipa kwenye swali langu la nyongeza akawape wananchi wa Muheza pamoja na kujionea mwenyewe jinsi miundombinu ya usambazaji wa maji Wilayani Muheza kwenye Kata hizi za Mbaramo, Genge, Masuguru, Tanganyika, Majengo na Kwemkabala vilivyokuwa hoi, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hamis Mohamed Mwinjuma kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napenda kukupongeza sana Mheshimiwa Mbunge jitihada zako za kuweza kushirikiana na Wizara zinafahamika, commitment ya Wizara ni kuhakikisha muda ambao usanifu unataka mradi kukamilika tutajitahidi kufanya hivyo hizi kilomita 14.5 kuhakikisha zinakamilika na maji yatoke bombani, wananchi waweze kufurahia fedha ambayo Mheshimiwa Rais ametaka iwafikie. Lengo ni kuwatua akina Mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuambatana ni moja ya taratibu zote mara baada ya Vikao vya Bunge aidha mimi ama Waziri ukinihitaji mimi hakuna neno tutakwenda tukafanye kazi. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa, katika Mji wa Ilula uliyoko katika Wilaya ya Kilolo unao mradi ambao umeshakamilika kwa muda mrefu lakini changamoto kubwa ni usambazaji wa maji katika vitongoji vyote.

Je, lini Serikali au katika bajeti hii itatoa pesa ili maji yaweze kusambazwa katika Mji wa Ilula? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kabati kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni shahidi Mheshimiwa Kabati ni mfuatiliaji mzuri sana wa miradi ya maji kukamilika. Suala la mradi ambao tayari umekamilika usambazaji unafuata hiyo ndiyo hasa Wizara inashughulika nayo. Sisi tunapenda kusema mradi umekamilika pale maji yanapotoka bombani mwananchi ananufaika. Hivyo kwa mradi kama huu ambao umekamilika usambazaji ndiyo hatua inayofuata kwa mwaka ujao wa fedha.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza maji ya Ziwa Bassotu kwa siku za karibuni yamekuwa yakisambaa na kuingia kwenye mashamba ya watu na nyumba:-

Je, Wizara ya Maji iko tayari kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira) kuangalia na kufanya tathmini ya tatizo linalofanya hayo maji yasambae na hatimaye kulitatua?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mradi huu karibu miaka mitatu ya fedha imekuwa ikitengewa chini ya Shilingi bilioni moja na tathmini ya awali ni Shilingi bilioni 12:-

Je, Wizara sasa iko tayari kutenga fedha zaidi ili mradi huu ukamilike kwa wakati?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Samweli Hhayuma, Mbunge wa Hanang’ kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Wizara tunafanya kazi kwa ushirikiano na Wizara ambazo tunakuwa tunaingiliana kikazo. Hivyo tupo tayari kushirikiana ili kuondoa hiyo adha kwa wananchi na vilevile kutenga fedha zaidi. Tutaendelea kufanya hivyo na pale tunapoendelea kupata fedha tutaongeza bajeti kwenye eneo hilo ili miradi hii ikamilike.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Umekuwepo mradi wa Kwembe-King’azi wa muda mrefu ambao uliahidiwa kukamilika mwezi wa Kumi na Mbili mwaka 2021 mbele ya Mheshimiwa Waziri na mpaka sasa haujaanza:-

Je, ni lini mradi wa Kwembe-King’azi A utaanza ili wananchi wa pale waweze kupata maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu tunaendelea katika hatua zake za mwisho kabisa na unaelekea kwenye utekelezaji.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kumekuwa na tatizo kubwa la Wakandarasi kushindwa kuchimba visima. Katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Mkandarasi ana miezi sita, ameshindwa kuchimba visima vya Aicho, Boboa na Titimu:-

Je, Serikali imefikisha hatua gani kuleta mitambo ya kila mkoa kuchimba visima vyetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, napenda kuendelea kumshukuru Mheshimiwa Rais, ametupatia fedha ya kutosha, taratibu zote zilishafanywa. Kabla ya mwaka huu wa fedha kwisha tunatarajia mitambo ile yote iwe imeshafika Tanzania na iweze kwenda kufanya kazi inayokusudiwa.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza: Mradi wa Kata ya Katuma ulipata Mkandarasi HEMATEC ambaye aliingia mkataba wa kufanya kazi tarehe 14 Desemba, 2021, mpaka sasa Mkandarasi huyo hajawahi kufika kwenye eneo husika:-

Je, Serikali haioni sasa ni wakati wa kuchukua hatua za dharura ku-terminate huo mkataba ambapo kimsingi mradi huo unatakiwa ukamilike tarehe 20 mwezi wa Sita?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili: Tunapongeza jitihada zinazofanywa na Serikali na kuleta miradi mingi kwenye eneo la kwetu. Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Tanganyika hana gari la kumsaidia kufanya kazi:-

Je, ni lini Serikali italeta fedha au kuleta gari ili liweze kusaidia kutoa huduma kwenye eneo hilo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu, maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Moshi Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini, kama ifutavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, napenda kumpa pole Mheshimiwa Mbunge, amekuwa akifuatilia sana huyu Mkandarasi, lakini sisi kama Wizara hatutafumbia macho Mkandarasi yoyote mzembe, hata kama tumesaini mkataba, lakini ukienda kinyume na mkataba, tutakuweka pembeni kwa sababu hatuko tayari kufanya kazi na mtu anayetuchelewesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo kwa kutumia Bunge lako Tukufu, naomba nitoe wito kwa ma-RM wote ambao Wakandarasi wao wanalalamikiwa kama huyu HEMATEC, RM wa eneo hili. Nitapenda ulete taarifa yako kesho asubuhi ili kujua ukweli wa suala la huyu Mkandarasi na endapo itabainika ni mzembe, tutamchukulia hatua stahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na DM wa Tanganyika kupatiwa gari, utaratibu unaendelea. Tunashukuru sana utendaji mzuri wa Director General wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo, ameendelea kufanya taratibu za kuona ma-DM wote wanapata vyombo vya usafiri. Hivyo katika magari yatakayokuja, naamini DG ataweka pia msisitizo kwa eneo la Tanganyika kwa umuhimu wake.
MHE. ABUBAKAR D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Ukizingatia majibu mazuri ya Serikali ni kwamba tumebakiwa takribani na mwezi mmoja mpaka kufikia mwisho wa mwaka wa Serikali.

Swali la kwanza je, ni lini tutaenda kusaini mkataba huo kwa ajili ya kuanza mradi huo wa miji 28 wa Kiburubutu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili je, Serikali itakuwa tayari kwenda kusainia mikataba ya miradi ya miji 28 site maeneo ya matukio ilikuwathibitishia wananchi wa Jimbo la Kilombero kuwa Serikali ya CCM inaendelea kuupiga mwingi sana?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante; naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abubakari kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, wakati wowote mradi huu utakwenda kusainiwa kwa umuhimu wake na heshima kubwa na kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Rais wa kuhakikisha mradi huu sasa unaenda kwenye utekelezaji wakati wowote Mheshimiwa Rais akipata nafasi naamini tutakwenda kusaini mkataba huu kwa wingi wake.

Mheshimiwa Spika, swali lako namba mbili sasa Wizara tumejipanga tutaelekea kwenye hii miji 28 yote tutatawanyika na kila eneo husika tutasaini mkataba hapo.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante, ningependa kuuliza kutoka katika Wilaya ya Busega. Wilaya ya Busega ina changamoto kubwa sana ya maji hasa katika Kata ya Nyaruhande, Rutubija na Ngasangu. Je, ni lini Serikali itapeleka maji safi na salama katika kata hizo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Busega binafsi nimeshfika pale na kufanya kazi kubwa sana kuhakikisha kata zote zinapata maji na katika kata hizi alizozitaja tayari tuna mpango madhubuti wa kuhakikisha maji yanawafikia wananchi yakiwa safi na salama na ya kutosha.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa ruhusa yako naomba niishukuru Serikali mradi wa maji Namtumbo Mjini bomba jipya na chanzo kipya cha maji unaendelea vizuri. Kumbara, Litola mabomba ya chuma yamefika kwa ajili ya ukamilishaji.

Swali langu kwa kuwa Serikali ilitenga fedha kwa Mradi wa Mgombasi ambao unapita katika Kijiji cha Nangero, Mtumbati Maji na Mgombasi yenyewe mpaka sasa hivi mradi huo haujaanza katika bajeti hii. Je, ni lini mradi huo utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Namtumbo ni moja ya maeneo ambayo yamepewa kipaumbele sana kuhakikisha tatizo la maji sugu linakwenda kuisha na mradi huu ambao ameutaja na wenyewe upo katika hatua za mwisho kabisa kuanza utekelezaji. Hivyo nipende kutoa wito kwa mameneja wetu wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanafuata taratibu na kuhakikisha mradi unaanza mara moja.
MHE. ESTER N. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji wa Bunda unaotoka Nyabehu hivi sasa hivi una takribani miaka 15; na mimi Ester Bulaya huu ni mwaka wa 12 naulizia mradi huu. Ni lini mradi huu utakamilika ili wananchi wa Bunda Mjini wapate maji katika kata zote 14 na usifike mwaka wa 13 nikiwa nauliza hili swali?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Bulaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Bunda tayari tupo kazini na kama miaka 15 kazi haikufanyika basi Mama Samia fupa lililomshinda fisi linakwenda kutafunwa, tumejionea miradi ambayo imekuwa sugu na sasa hivi inatoa maji, hivyo, Bunda pia wakae mkao wa kufungua bomba na kupata maji safi na salama na kata zote 14 tunahakikisha zinakwenda kupata maji safi na salama. (Makofi)
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Serikali ilitenga fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maji kule Arumeru Mashariki mwaka huu wa fedha lakini kuna mradi ambao hatujajua hatma yake.

Je, ni lini mradi wa maji Kata ya Ibaseni, Maji ya Chai na Kikatiti utaanza kutekelezwa kwa maana ya kwamba upo kwenye miradi inayopaswa kutelezwa mwaka huu? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Pallangyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge yeye mwenyewe kazi kubwa tuliyoifanya jimboni kwake, nimekwenda na tumetembelea miradi yote ambayo ilikuwa ni historia maji kufika tayari unafahamu maji yanatoka. Hivyo, katika mradi huu ulioutaja endapo mwaka huu wa fedha utaisha utekelezaji utakuwa haujakamilika mwaka ujao wa fedha ni lazima maeneo haya yote tuje tuendelee kufanyia kazi na kuhakikisha maji yanapatikana. (Makofi)
MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kata ya Kichiwa hasa vijiji vya Kichiwa, Tagamenda, Upami na maeneo mengine kuna ahadi ya muda mrefu ya kupelekea maji kwa wananchi. Je, ni lini ahadi hii ya Serikali itakwenda kutekelezwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, maeneo haya aliyoyataja yapo katika mipango ya Wizara katika kuhakikisha maji yanawafikia wananchi. Kata hizi tutakwenda kuzitekeleza kadri ya jiografia yake, endapo bomba kuu itachukua muda mrefu kuwafikia basi visima virefu vitahusika lengo ni kuhakikisha maji yanapatikana bombani. (Makofi)
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa Wizara ya Maji kupitia DAWASA inaendelea na kazi nzuri ya upanuzi wa miundombinu ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, lakini yapo maeneo jirani na mitambo hiyo hayana maji kwa mfano; Kata ya Mzenga, Vihingo, Kisarawe.

Je, ni lini Serikali itasambaza maji kwenye kata hizo ambapo ni jirani kama kilometa 20 kutoka Mji wa Mlandizi? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Subira Mgalu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nipokee kwanza pongezi na kutambua kazi kubwa inayofanywa na DAWASA; maeneo haya uliyoyataja Mheshimiwa Mbunge yanaelekea kufikiwa baada ya miradi mikubwa sana ambayo inaendelea kufanyika pale DAWASA na maeneo yote ya huko ulikotaja Mzinga, Kisarawe kote yanatarajiwa kupata maji ifikapo mwaka ujao wa fedha. (Makofi)
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, Mradi wa Rangwi ambao ameutaja hapa ambao una vijiji karibia vinne vya Goka, Nhelei, Kalumele na Mamboleo ni mradi ambao sasa umechakaa, lakini pia eneo la usambazaji limekuwa dogo kwa sababu idadi ya watu imeongezeka. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuboresha mradi huo?

Pili, katika kata ya Sunga, Tarafa hiyo hiyo ya Mtae vijiji vyote vinne havijawahi kuwa na mradi wowote wa mfumo wa maji ya bomba. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka na kata hii ya Sunga iweze kupatiwa miundombinu ya maji safi ya bomba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shangazi kama ifuatavyo;-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tunafahamu mradi ule umechakaa na kama Wizara tayari tumeuweka kwenye mpango wa mwaka 2022/2023 ili kuona kwamba tunakwenda kukarabati na kuweza kuwafikishia wananchi wote wa maeneo aliyoyataja maji mengi, safi, salama na ya kutosha.

Swali lake la pili anaulizia kuhusu Kata ya Sunga ambayo ina vijiji vinne ni kweli mtambao wa mabomba kwenye kata hii haukuweza kufikiwa kulingana na jiografia ya eneo lenyewe. Vyanzo ni kweli viko vingi katika eneo lile, lakini vyanzo vingi viko maeneo ya chini na wananchi vijiji viko kwenye miinuko kwa maana kwenye milima hivi kidogo kama tunavyofahamu jiografia ya Lushoto lakini kama Wizara tunaendelea kuona uwezekano wa kupata vyanzo vya kujitosheleza maeneo yale ya juu na hatimaye kabla ya mwaka ujao wa fedha tutahakikisha tunapata na kuweza kuwafikishia maji ya bombani wananchi wote wa Kata ya Sunga yenye vijiji vinne.
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru naomba niulize swali moja dogo la nyongeza.

Mji wa Kasera ambayo ndiyo Makao Makuu ya Wilaya ya Mkinga bwawa lake linalopeleka maji hapo linakaribia kukauka, tumeleta maombi ya dharura takriban shilingi milioni 51. Je, ni lini fedha hizi zitapatikana?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kitandula, Mbunge wa Mkinga, kama ifuatavyo. Tunatarajia wiki ijayo kuwapelekea shilingi milioni 51 kwa ajili ya bwawa hilo. (Makofi)

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Jimbo la Kibiti kata ya Mtawanya kuna vijiji vya Bumba, Msola na Makima vina shida kubwa sana ya maji. Ni nini tamko la Serikali kuhusiana na kuweka maji katika maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Twaha kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kata hii anayoiongelea tumeshazungumza mara kadhaa na Mheshimiwa Mbunge na tayari tunaiweka kwenye utaratibu wa kuona kwamba tunawaletea wananchi maji bombani yakiwa safi na salama.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, ningependa kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri mradi wa miji 24 ni mradi ambao ulikuwa ni mkombozi sana kwenye Mji wa Geita ambapo Jimbo la Geita Vijijini kata tano zilikuwa zinafaidika Senga, Kagu, Nyawilimilwa, Bugurura na Kakubiro. Lakini tumekuwa tukiahidiwa kila siku hatuoni mwelekeo; je, ni lini Serikali itaanza sasa kutekeleza mradi huo wa miji 24?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Musukuma kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa NaibU Spika, kwanza niseme siyo vijiji mini 24 bali ni miji 28, lakini vile vile Geita Mjini kata hizo tatu zinakwenda kunufaika hivi punde subira yavuta heri. Maandalizi yote yamekamilika tunasubiri tu kusaini, tunasubiri na muda na nafasi ya Mheshimiwa Rais.

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itaboresha usambazaji wa mabomba ya maji katika Kata ya Bariadi, Mtaa wa Kidinda, Majengo Viwandani?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, usambazaji wa maji katika mji wa Bariadi kwenye maeneo aliyoyataja ni moja ya maeneo ambayo tumeyapa jicho la kipekee kuhakikisha tunakwenda kuyafikia lengo ni kumtua mwanamama ndoo kichwani na kusambaza maji safi na salama.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimia Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa mradi huo umechukua muda mrefu na sasa wananchi wanakunywa maji ya floride na wanazaliwa watoto wenye vichwa vikubwa, vibiongo na miguu kupinda. Je, Serikali haioni sasa kufanya haraka kwa ajili ya kukamilisha mradi huo?

Swali la pili, je, Naibu Waziri wa Maji baada ya Bunge hili atakuwa tayari kwenda kukagua mradi huo ili kujionea hali halisi ya wale wananchi wanavyoteseka?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Saputu kama ifuatavyo;-

Mheshimiwa Naibu Spika, huu mradi tumeweka nguvu kubwa lakini tumekusikia Mheshimiwa Mbunge tutaongeza nguvu.

Swali la pili kukagua mradi mara baada ya Bunge hili Mheshimiwa Mbunge unafahamu nilishakuja Jimboni kwako hivyo sitasita kufika tena kuhakikisha huduma ya maji inapatikana.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru; Mheshimiwa Waziri Engineer rafiki yangu nadhani wananchi wa Nyatwali nilikukutanisha nao kata yao wana mradi mkubwa umekamilika na wamekuambia huo mradi haujazinduliwa, kigugumizi cha kuzindua huo mradi ni kitu gani?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya kama ifuatavyo:-

Ni kweli Mheshimiwa Ester tulikutana na wale madiwani na wananchi wa ile kata nilikubali nitakuja tusubiri Bunge liishe tutafika na litazinduliwa kwa sababu tunahitaji wananchi wapate maji.
MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, wananchi wa Mkoa wa Katavi hususani Wilaya ya Mpanda Kata za Majengo, Kashaulili, Mpanda Hotel wamekuwa na mgao wa maji hawapati maji kila siku, lakini lipo Bwana la Milala ambalo lilikuwa ni chanzo cha maji sasa hivi bwawa hilo halitumiki kwa sababu limechafuka. Je, Serikali ina mkakati gani wa kusafisha bwawa hilo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Ziwa Tanganyika ndiyo chanzo kikuu cha kutoa matatizo ya maji kwenye Mkoa wa Katavi; Serikali ina mkakati gani wa kuharakisha upembuzi yakinifu ili maji yaweze kutoka Ziwa Tanganyika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Taska Mbogo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, awali yayote napokea pongezi, lakini vilevile napenda kurudi kwenye jibu langu la msingi eneo la Mpanda linakwenda kunufaika hivi punde na ule mradi wetu mzuri ambao tumeusubiri kwa muda mrefu na Mheshimiwa Rais hivi punde anakwenda kufanya yake na maji yanakwenda kuanza kutekelezwa kupitia mradi wa miji 28.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na bwawa kuchafuka, tutaangalia uwezekano wataalamu watakwenda kuangalia uwezekano wa kuona kama bwawa hili litatufaa au litatupotezea fedha, kama litakuwa linahitaji fedha nyingi ambayo haina tija sana kwenye matokeo tutaendelea na mikakati mingine, lakini suala la msingi ni kuhakikisha wananchi wanakwenda kupata maji safi na salama bombani.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la matumizi ya Ziwa Tanganyika ni moja ya mikakati ya wizara nimekuwa jibu hili mara kadhaa tutakwenda kutumia Ziwa Tanganyika kwasababu hakuna asiyefahamu kwamba ni chanzo ambacho kitatuletea tija kubwa sana na miradi itabaki kuwa endelevu kwa vizazi na vizazi.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na kilio kikubwa sana kwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu hususani Wilaya za Busega, Itilima na Meatu; je, ni lini akina mama wa mkoa huo watafaidika na maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Simiyu unakwenda kunufaika na mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria mradi ambao ni mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira na tunatarajia maeneo hayo yote aliyoyataja yanakwenda kunufaika, Meatu ipo katika mpango huo na tayari wananchi wameanza kulipwa fidia. (Makofi)

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwanza niipongeze Serikali na Wizara yake ya Maji kwa kuzidi kutukamilishia mradi wetu wa maji na maji yameshaingia maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Nyang’hwale, lakini wananchi wanalalamika bei ya maji ni kubwa ukilinganisha na mjini. Nyang’hwale tunalipa shilingi 2500 kwa unit moja wakati Mji wa Geita na Mwanza wanalipa 1,350.

Je ni lini Serikali itatoa kauli kwa Wilaya ya Nyang’hwale kupunguza bei ya maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Amar, Mbunge wa Nyang’hwale kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya Nyang’hwale pamoja na maeneo mengine kama Karatu tunafahamu bei bado si rafiki sana kwa wananchi na hii ilisababishwa na utekelezaji wa mradi, lakini kama Wizara tunaendelea kufanya mapitio ili kuona kwamba bei zinakwenda kuwa bei rafiki kwa wananchi. (Makofi)
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru; mradi wa maji wa Nansio Jimboni Ukerewe ulishakamilika na kuanza kutoa huduma, lakini bado maji hayajaweza kuwafikia wananchi wote zinahitajika bomba takribani kilometa kama 67 ili kuweza ku-cover eneo lote na maji yawafikie wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari sasa kusaidia mamlaka hii ya maji bomba hizi ili huduma ya maji iweze kuwafikia wananchi wote kwenye Mji wa Nansio? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Ukerewe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaposema mradi umekamilika tunahitaji kuona maji bombani, hivyo kama tumeshakamilisha mradi wa fedha nyingi hili suala la usambaji wa mabomba kuwafikia wananchi ndiyo jukumu letu kubwa. Hivyo nipende kukutoa hofu Mheshimiwa Mbunge tutafika na tutafanya kwa pamoja na wananchi wanakwenda kunufaika na maji bombani.

MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, kwa kuwa nimekuwa nikifuatilia mradi huu kwa muda mrefu sana na majibu ya Serikali yamebaki kuwa haya haya.

Sasa naomba kupata commitment ya Serikali inawahakikishiaje wanawake wa Mlowo, wanawake wa Vwawa na Tunduma kwamba ni kweli kwa mwaka wa fedha ujao watatuletea mradi huu wa kutoa maji Ileje na kuweza kuyasambaza kwenye maeneo hayo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa kuwa Serikali imekiri kwamba hatuwezi kumaliza tatizo la maji kwa kujenga miradi midogo midogo; sasa naomba kufahamu tunaye mkandarasi ambaye anatatujengea miradi ya maji katika Kata ya Mkwajuni pamoja na Galula kule Songwe, lakini mpaka sasa hivi hajamaliziwa fedha na huo mradi umeanza mwaka 2019.

Je, ni lini sasa Serikali itammalizia fedha mkandarasi huyo ili kuweza kuwapunguzia adha ya maji wanawake wa Wilaya ya Songwe? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shonza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, commitment ya Serikali ni kuhakikisha maji yanapatikana maeneo yote nchini na hili tumeona jitihada za dhati kabisa Mheshimiwa Rais ametoa fedha nyingi zaidi ya asilimia 95 mpaka sasa, mpaka tumalize mwaka huu wa fedha itakuwa zaidi ya hapo. Hivyo, Serikali tutafika maeneo yote na kuhakikisha miradi ambayo haikutekelezeka inakwenda kutekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na mkandarasi kulipwa Mkwajuni – Songwe wakandarasi wanaendelea kulipwa kulingana na walivyofanyakazi walivyo raise certificates na kuna sababu mbalimbali zinazopelekea hawa baadhi ya wakandarasi malipo yao kuchelewa hivyo niwatake wakandarasi wote wafanyekazi kadri ya mikataba nakwa ambaye hajalipwa basi aweze kufuata taratibu ili malipo yake yaweze kufanyika mara moja.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Waziri mwaka jana wakati akijibu swali langu la msingi kwenye swali la nyongeza aliniahidi kunipatia fedha kwa ajili ya kuchimba kisima kimoja cha maji katika Kijiji cha Nainokwe.

Je, lini fedha hizi zitakwenda ili wana Nainokwe wakafarijike kutokana na adha ya maji wanayoipata?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli nilifika tulifanya pamoja ziara na kisima hiki ni lazima kichimbwe. Mheshimiwa Mbunge tafadhali baada ya session hii ya leo tukutane ili tuweze kufuatilia pamoja hii fedha itoke. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru; Tarafa ya Murongo imepatakana na Mto Kagera ambako ni chanzo kikubwa cha maji, lakini hizo kata hazina maji.

Nataka kujua nini mkakati wa Serikali katika kuwatua kina mama ndoo kusaidia upatikanaji Kata ya Kibingo, Bugomora, Murongo, Kibale, Kimuli, Bugara na Businde? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anatropia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tarafa hiyo ya Murongo aliyoitajwa ni moja ya maeneo tunaendelea kuyafanyikazi na kwasababu ipo karibu na chanzo cha uhakika naomba nitoe wito kwa wananchi tuendelee kuvumilia, tunakotoka ni mbali tunakokwenda ni karibu, hizi kata zote zinakwenda kupata huduma ya maji na salama.
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pia naishukuru Serikali kwa majibu, naomba kuuliza swali moja tu la nyongeza. Taarifa nilizonazo ni kwamba, mpaka sasa mkataba wa mradi huu haujasainiwa na kwa muda uliobaki Waziri anatuhakikishia kwamba, tutaweza kusaini mkataba huo na ujenzi wa mradi huu uweze kuanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dunstan Kitandula, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ndio. Wizara tutaweza kusaini mkataba na kazi zitaanza.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa muda mrefu sana Serikali iliahidi kupeleka maji katika Shule ya Nanja, Kijiji cha Mti Mmoja na Lepurko vilivyoko katika Wilaya ya Monduli, Mkoa wa Arusha, lakini hadi leo haijatimiza ahadi yake. Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza ahadi yake katika vijiji hivi, ili wanafunzi hawa na wananchi waepukane na adha hii kubwa ya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuliahidi eneo la shule hii pamoja na hiki kijiji alichokitaja viweze kupatiwa huduma ya maji. Hatujapeleka kwa sababu ya mtawanyiko wa majukumu, lakini ni lazima tutapeleka maji katika shule hii na hiki kijiji na maeneo ya shule nyingine zote katika Jiji la Arusha, lakini vilevile na vijiji vyote.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Licha ya juhudi kubwa za Serikali za kutatua changamoto ya maji Mkoani Tanga, bado Wilaya ya Muheza inapata maji kwa mgawo tena saa 8.00 za usiku. Je, ni lini Serikali itawezesha maji yale kutoka mapema ili wanawake wa Muheza waweze kupumzika usiku?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Tanga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, eneo la Muheza kutoa maji ya mgawo usiku wa manane, huu sio utaratibu mzuri na tunataka kukomesha hili. Naomba wananchi wawe watulivu na subira, tutahakikisha huduma ya maji inapatikana saa zote na kama ni saa chache basi muda rafiki.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakabidhi Mradi ulioko katika Kata ya Vuje, Wilaya ya Same, ambao ulianza tangu 2018 ambao uligharimu takribani Sh.1,300,000,000?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, miradi ikishakamilika ni wajibu wa Wizara kukabidhi kwa wananchi na unaendeshwa na vile vikundi vidogo vidogo ambavyo vinaundwa na wananchi. Kwa hiyo na mradi huu ambao umeshatumia fedha ya Serikali zaidi ya bilioni ni lazima nao uje ukabidhiwe kwa wananchi, ili lengo la kufikisha huduma ya maji kwa wananchi liweze kutimia.
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Je, ni lini mkandarasi wa kujenga Mradi wa Ngana Group atapatikana?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally Mlaghila, Mbunge wa Kyela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ngana Group taratibu ziko mwishoni. Tunatarajia kabla ya mwaka huu wa fedha kwisha, mkandarasi atapatikana na kazi ziweze kuendelea.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni nini dhamira au msukumo wa Serikali wa kufikiria kuanzisha taasisi moja badala ya kuimarisha taasisi zilizopo na hususan hii taasisi ya KAVIWASU kwa sababu imekuwa ikifanya vizuri zaidi kulinganisha na ile taasisi ya Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; utozaji wa bei kati ya taasisi hizi mbili hutofautiana na ni ukweli kwamba hiyo taasisi ya Serikali inapata unafuu na bei yake inakuwa nafuu kwa sababu, inapata ruzuku kutoka Serikalini, ilhali ile taasisi iliyoanzishwa na wananchi haipati unafuu wowote na gharama zinabaki palepale. Serikali kwa mara nyingine mpo tayari kuipa ruzuku taasisi hii ya wananchi ili kuunga mkono jitihada za wananchi katika kupata maji katika Mji Mdogo wa Karatu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Cecilia Paresso, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, lini tutaweka hizi taasisi kuwa moja; mara baada ya taratibu zote za Kiserikali kukamilika tutahakikisha tunafanya hizi taasisi mbili inakuwa moja kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, utozaji wa bei unatofautiana, chombo ambacho kinasimamiwa na Serikali kinapewa ruzuku na kile cha wananchi hakipewi ruzuku; kitakachofanyika ni kitakuwa chombo kimoja kwa hiyo, ruzuku ya Serikali itaingia na lengo la Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama mpendwa anayetaka akinamama tuwatue ndoo kichwani, tuhakikishe huduma zinakuwa chini, tutahakikisha bei zinakuwa rafiki kwa wananchi na ruzuku pale inapobidi itakuwa inafika kwa wakati.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwanza niipongeze Serikali kwa sababu mradi huu unatumia takribani shilingi 3,000,000,000 kwenye utekelezaji wake lakini tayari wameshatoa shilingi 500,000,000. Ni lini Serikali itatoa shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kukamilisha mradi huu kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Iwawa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuna mradi wa Matamba - Kinyika ambao Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 2.8 kuujenga, lakini hadi leo hamjaukamilisha takribani miaka saba.

Ni lini Serikali itakabidhi mradi huu kwa wananchi wa Kijiji cha Nungu, Ng’onde, Mbela na Hitani ili waweze kupata huduma ya maji kwa sababu imebaki tu eneo la distribution kwa maana ya usambasaji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Festo Sanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi ambao tayari tumeshautolea shilingi milioni 500 na utekelezaji wake unakwenda vizuri ni ule mradi ambao umetumia fedha za mapambano dhidi ya UVIKO-19 na fedha iliyobaki tutaendelea kutoa kuanzia mwezi huu wa Juni, tutaendelea kuongeza fedha. Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa tuonane tuliweke sawa hili kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Mradi wa Matamba - Kinyika ni kweli mradi umechukua muda mrefu, lakini ni katika ile miradi ambayo ilikuwa ni chechefu na tayari tunaendelea kuikwamua, hivyo mradi huu pia kwa sasa hivi umeshafikiwa hatua nzuri ni zaidi ya asilimia 80 umeshaweza kutekelezwa, tutakuja kuumalizia hivi punde na watu wa IRUWASA watakabidhi kwa watu wa NKOMBEWASA ili waweze kufanyakazi ndani ya mkoa wao.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mradi wa Maji wa Uhambi Ngeto ambao umetengewa fedha kwa mwaka huu umekuwa ukitafutiwa mkandarasi tangu mwaka umeanza na mpaka sasa mkandarasi hajaanza kazi.

Je, ni lini mkandarasi huyu atapata mkataba ili aweze kufanyakazi kukamilisha mradi ule?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu swali la Mheshimiwa Justin, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli mradi huu bado haujapatiwa mkandarasi lakini taratibu zipo mwishoni kabisa. Mheshimiwa Mbunge naomba tuwasiliane baada ya hapa tuliweke sawa suala hili.
MHE. JERRY W. SILAA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, tunaishukuru sana Serikali kwa mradi mkubwa wa maji wa Kibamba, Kisarawe na Pugu ambao tayari umeaanza kusambazwa kwenye kata mbalimbali za Jimbo la Ukonga. Swali langu je, Serikali sasa ina mpango gani wa usambazaji wa Kata ya Kitunda, Mzinga, Kivule na Kipunguni ambazo hazina usambazaji wa maji haya safi na salama ya DAWASA? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jerry Silaa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyokiri Serikali tumeendelea kufanya kazi nzuri kwa Mkoa wa Dar es Salaam na katika maeneo haya aliyoyataja tayari tunafedha zaidi ya shilingi bilioni 25 kwa ajili ya mradi huu na sasa hivi tayari mkandarasi ameshapatikana tunaratajia kufika mwishoni mwa mwaka 2022 haya maeneo yote usambazaji wa maji utakuwa umewafikia.

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kuniruhusu kuuliza swali la nyongeza.

Tunayo miradi ya World Bank ambayo ilianzishwa katika Jimbo langu la Nanyumbu, miradi ile ni chechefu; je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba miradi ili chechefu inafanyakazi katika Kata ya Mnanje, Kijiji cha Holola, Kata ya Nandete, Chiwilikiti na Ulanga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tuna speed kubwa sana ya kuhakikisha miradi yote iliyokaa muda mrefu inakamilika. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais ameendelea kutupatia fedha na tunaona namna kazi kubwa anayoifanya Mheshimiwa Rais kwa kuijali Wizara ya Maji na kuona kwamba akina mama wanatua ndoo kichwani.

Mheshimiwa Mbunge kwenye maeneo haya uliyoyataja tunakuja kuyafanyia kazi. (Makofi)
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza nitoe shukrani kwa Serikali ambapo jana tuliweza kusaini Mkataba wa kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Kilwa Masoko wenye thamani ya shilingi bilioni 81. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini niulize swali la nyongeza sasa, kumekuwa na hali chechefu katika utekelezaji wa miradi ambayo inahudumiwa na Mfuko wa Maji ikiwemo mradi ambao unatekelezwa katika Kijiji cha Kinjumbi kutokana na mlolongo mrefu wa malipo.

Je, Serikali ina utaratibu gani ambao umeupanga ili kupunguza mlolongo mrefu wa malipo ili miradi hii inayotekelezwa kwa mfuko wa maji iweze kuhudumiwa kwa ufanisi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ndulane, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nipende kupokea shukrani kwa uzinduzi wa miradi ya maji ya miji 28, kwenye hili tumpongeze sana Mheshimiwa Rais na tumshukuru na tumuombee kwa sababu kazi aliyoifanya ni kazi iliyotukuka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusiana na malipo ya Mfuko wa Maji kuwa na mlolongo mrefu, Mheshimiwa Mbunge unaelewa hapo nyuma kulikuwa na matumizi mabovu ya fedha katika hali ya udhibiti ilipaswa Wizara kuweka taratibu zote hizo, lakini tunaendelea kuziboresha kuhakikisha kwamba udhibiti utaendelea lakini pia fedha itatoka ndani ya wakati.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na nakuomba kwa ruhusa ya kiti chako nitangulize shukrani kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa tamko lake la jana kwamba sasa mradi wa Mwanga, Same, Korogwe unakwenda kuanza tumepata usingizi watu wa Kilimanjaro.

Mheshimiwa Spika, baada ya shukrani hizo naomba nimuulize sasa Naibu Waziri; je, ni lini mradi mkubwa wa chanzo cha maji cha Ziwa Chala ambao utawapatia maji wananchi wa Holili, Ngoyoni, Chala na wengine tambarare ya Rombo utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mradi wa Ziwa Chala unatarajiwa sana kuona kwamba unakwenda kutatua tatizo la maji, lakini Ziwa Chala tukitaka kutumia mradi ule maana yake ni mradi wa ku-pump, ni mradi ambao utaleta gharama kubwa na matokeo yake wananchi watalipa huduma kwa gharama kubwa.

Mheshimiwa Spika, lakini tayari kuna miradi mitatu pale ya gravity inayoendelea kujengwa katika Mji wa Rombo na tunatarajia miradi hii ikija kukamilika kwa sababu ni miradi ya miserereko itakuwa ni miradi rafiki kwa wananchi na tatizo la maji linakwenda kukoma.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi, nami niungane na wenzangu kuipongeza Serikali kwa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Makonde ambao mkataba umesainiwa jana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini ningependa kujua sasa kuna mradi mkubwa wa kutoa maji mto Ruvuma, Kijiji cha Mahechini kupeleka Manispaa ya Mtwara mradi ambao utanufaisha Jimbo la Nanyamba Mtwara Vijijini na Manispaa ya Mtwara; je, mradi huu utaanza kutekelezwa lini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdallah Chikota kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hakika nimeelewa anayeshukuru anaomba tena, tayari ni jana tu Mheshimiwa Rais ameweza kufanya jambo zito sana la kuona Mradi wa Makonde unaenda kufanyiwa kazi, lakini mradi huu wa Mto Ruvuma nao ni moja ya mikakati ya Wizara tunakwenda kuhakikisha maji ya Mto Ruvuma yanakwenda kutatua matatizo ya maeneo yote ambayo utayapitia. Mara tutakapopata fedha tutaingia kwenye mradi huu.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawilli ya nyongeza.

Swali la kwanza; Serikali ina mpango gani sasa wa kuwalipa fidia wananchi ambao walikuwa wanaishi katika eneo lile na walikuwa wanalima mashamba yao?

Swali la pili, shida iliyoko Ikozi ni sawa na shida iliyoko Mpui kata ambazo zinakaribiana, Serikali sasa ina mpango gani wa kukamilisha mradi ulioko Mpui pale ambao mradi upo lakini wananchi hawapati maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wa kulipa fidia, tayari Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa maeneo ambayo miradi inapita tumeshaanza malipo na mradi wa eneo hili pia watafikiwa hivi punde. Kata zinazokaribiana hiyo Kata ya Mkuyu na yenyewe pia kuna mradi, mradi huu sasa hivi tunaendelea kuufuatilia kwa karibu sana kuhakikisha dhima ya Serikali kumtua mama ndoo kichwani inakwenda kutekelezeka hata kwa wananchi watokao Mkuyu.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri swali kwamba tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri ambayo ameifanya jana kwa miji 28 kupata mradi wa maji na kwa kweli kwa nchi nzima kuna mabadiliko makubwa sana ya maji hata Tarime kuna mabadiliko makubwa sana.

Sasa nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba nilikuuliza swali hapo ukasema Tarime itapata maji katika miji ile 28, lakini kwenye hii list ya jana Tarime haimo; nini kauli ya Serikali juu ya watu wa Tarime ili waweze kusubiri maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Waitara kama ifuatavyo: -

Tarime imo Rorya, Tarime ipo kwenye mradi wa miji 28; vuta subira wakati wa utekelezaji utakapoanza utashuhudia kwamba Tarime imo. (Makofi)
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mchakato wa uvunjwaji wa Bodi hii haukishirisha wananchi na hapa mmekiri mlienda kwenye Mamlaka ya Serikali, kwa wawakilishi wa wananchi lakini hamkufika kwa wananchi. Je, ni lini mtafika kwa wananchi na kuwapa sababu za kwa nini mlivunja mradi huu? (Makofi)

Swali la pili, mmeeleza kwamba baada ya chombo hiki kuundwa kuna ufanisi wa maji, naomba niwaambie Wizara hakuna ufanisi wowote matokeo yake tumerudi kwenye adha kubwa ya ukosefu wa maji katika Mji wa Karatu. Ni lini na kwa haraka mtarekebisha tatizo hili ili wananchi waweze kupata maji kwa uhakika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Cecilia Paresso, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba nirudie tena Mheshimiwa Waziri yeye mweyewe, Jumaa Hamidu Aweso na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo walishirikiana na Waheshimiwa Madiwani waliweza kushirikisha wananchi. Kama wananchi hawakupata taarifa wote basi kuendelea kutoa elimu ni moja ya jukumu la Wizara, kwa hiyo tutaendelea kutoa elimu kwa sababu dhamira ya Wizara ni njema kabisa, lengo la kuunganisha hivi vyombo ni kupunguza mzigo wa gharama za bei kwa wananchi na kabla ya kuviunganisha mwananchi aliweza kulipia unit ya maji shilingi 2,000 na baada ya kuviunganisha tunamshukuru sana Mheshimiwa Waziri alihakikisha bei zimeshuka na sasa hivi ni shilingi 1,300.

Mheshimiwa Spika, kuonesha ufanisi mkubwa wa mradi wa huduma ya maji, tayari Wizara, Karatu tumeiangalia kwa jicho la kipekee kabisa na tayari kazi zinaendelea, tutahakikisha huduma ya maji Karatu wataendelea kuboreshewa lengo ni kupata maji safi na salama bombani yakiwa ya kutosha.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri ahsante sana kwa majibu yako kwa maswali ya Waheshimiwa Wabunge. Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Mwanakhamis Kassim Said, Mbunge wa Magomeni, sasa aulize swali lake.
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza ninaishukuru Serikali kwa majibu yake mazuri na yenye matumaini makubwa kwa jengo la Mchinga na kwa Manispaa yetu ya Lindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali la nyongeza, sambamba na hili tuna suala zima la ukarabati kwenye Kata yangu ya Milola na chanzo kiko kule Chipwapwa, fedha tulizozipata ni shilingi milioni 50 na jana wamesaini mkataba, lakini mahitaji ni shilingi milioni 490.

Je, fedha zilizobaki zitapatikana lini na hii ikiwa na maana kwamba huu ndiyo mwisho wa bajeti wa 2021/2022?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Salma Rashid Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Mchinga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kata aliyoitaja ni kweli fedha zimekwenda kwa utangulizi, lakini kama ilivyo kawaida kila mgao unapokuwepo tunaendelea kuleta fedha. Kwa wiki hizi mbili zilizobaki za kumaliza mwaka huu wa fedha tutajitahidi kuona uwezekano wa kuongeza fedha kadri ya mahitaji. Ahsante. (Makofi)

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Mradi wa Maji wa Bunda kutoka Nyabeu tayari Serikali imeshafikisha Bunda Mjini, lakini changamoto kubwa iliyokuwepo ni miundombinu ya usambazaji maji, ni ya zamani, ndiyo maana mpaka leo wananchi wameshindwa kupata maji safi na salama. Je, ni lini sasa Serikali watahakikisha wanaweka miundombinu mipya ili kata zote 14 za Bunda Mjini ziweze kupata maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Bulaya, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyokiri maji yameshafika mjini; lengo la Wizara ni kuhakikisha maji yakishafika katika maeneo ya mwanzoni, basi sasa usambaji utafuata na miundombinu ya zamani yote tunakwenda kuendelea na ukarabati kuhakikisha tunaleta mabomba na miundombinu ambayo itaendana na idadi ya watu waliopo kwa sasa. Hivyo, nipende kukwambia tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mwaka ujao wa fedha tutaendelea na ukarabati wa mradi huu. (Makofi)

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwenye Kata ya Nyakatuntu kuna chanzo cha maji Kitoboka, na kwenye Kata ya Songambele kuna chanzo cha maji Kitega ambacho wananchi wanapata adha kuhusu maji safi na salama. Je, ni lini Serikali itaboresha chanzo hiki lakini pia kukamilisha visima ambavyo tumetengewa kwenye bajeti? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bilakwate, kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, visima hivi ambavyo amevitaja Mheshimiwa Mbunge tunaendelea kuvifanyia kazi kuona kwamba pamoja na hivi vyanzo vya maji alivyovitaja vyote tuweze kuvitumia, lengo ni kuona tunapata maji mengi yatakayoweza kuwafikia wananchi wengi. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge avute Subira, kazi ambayo tumeianza kwa pamoja tutakwenda kuikamilisha. (Makofi)
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nina maswali mawili ya nyongeza:-
Swali la kwanza, tunashukuru kwa Shilingi Bilioni 1.1 ambayo Wilaya ya Rungwe ilipata kati ya Shilingi Bilioni Nne ambayo ilikuwa ni bajeti. Sasa Serikali haioni umuhimu wa kuhakikisha angalau tunapata nusu ya bajeti ambayo ilikuwa iliombwa ili kuwasaidia watendaji kufanyakazi yao vizuri?

Swali la pili, kumekuwa na ahadi za viongozi mbalimbali wanaokuja kwenye Wilaya zetu na kuahidi wananchi kupata maji kwa wakati. Sasa Serikali haioni umuhimu wa miradi ile inayoahidiwa na viongozi iweze kufanyika haraka na watu waweze kupata maji kama ambavyo watu walipata ahadi hasa katika hivyo vijiji 155 vya Rungwe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kupokea kwanza shukrani na anayeshukuru anaomba tena ndiyo swali lako la pili linapoelekea. Ni kweli tumefika Wilaya ya Rungwe na tumeahidi na tunakwenda kutekeleza ni suala la muda tu Mheshimiwa Mbunge naomba utupe nafasi tufanye kazi.
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Naomba kufahamu ni lini Serikali itaanza Upembuzi yakinifu katika mradi wa maji katika Kijiji cha Lukululu uliopo katika Jimbo la Vwawa? Ahsante.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Juliana Shonza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, upembezi yakinifu tunatarajia kuanza mwaka ujao wa fedha na kadri fedha itakapopatikana kasi itakuwa ni kubwa, lengo ni kuwafikia wananchi wote ili waweze kupata maji safi na salama bombani.

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kuna vijiji vya Machiga na Chandama kuna mradi wa maji ambao tayari Kandarasi yake ilitangazwa na Mzabuni akapewa lakini mpaka leo hayupo site. Nini kauli ya Serikali kuhusu Mzabuni huyu kuwepo site? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Monni, Mbunge wa Chemba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wakandarasi wote ambao tumesaini nao mikataba wanafahamu sheria na taratibu na tayari Mheshimiwa Waziri ameshaongea mara nyingi, hatutakawa na mzaha na wale Wakandarasi ambao wanachelewa kufika site hivyo Mheshimiwa Mbunge hili nimelipokea na tutalifanyia kazi kwa karibu.
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia majibu ya Serikali, yanaonesha kwamba zoezi hili lilianza mwaka 2019 na mpaka leo ni takribani miaka mitano, wameweza kufungia wananchi 345 ambayo ni sawa na asilimia 0.285 kwa miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizingatia kwamba wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini wamekuwa wanalalamika kwa muda mrefu sana kuhusiana na bili kubwa za maji na kubambikiwa bili; je, nini kauli ya Serikali kuhusiana na changamoto hii? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili ni kwamba, kama kwa miaka mitano tumeweza kufungia wananchi kwa maana ya 345 kati ya wananchi 120,899 ambao wanatakiwa kufungiwa mita za LUKU za namna hiyo; je, Serikali imejipangaje kuweka timeframe kuhakikisha kwamba wananchi wote 120,899 wanafungiwa mita za maji kama za LUKU?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mrisho Gambo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kujipanga kuhusiana na ubambikaji wa bili kwa wananchi, hili tayari tumeshalifanyia kazi kubwa sana. Zoezi hili limeanza taratibu kwa sababu ya kutoa elimu na kuhakiki hizi dira ambazo tumekuwa tukizitoa nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba tumejipangaje sisi kama Wizara, tayari tumetoa fursa kwa vyuo vyetu vya ufundi hapa nchini; Chuo cha Ufundi Arusha, pamoja na Chuo cha Ufundi cha Dar es Salaam, (Dar es Salaam Institute of Technology) ambao sasa tayari wanaendelea kutengeneza mita hizi. Lengo ni kuona tunataka kusambaza mita kwa bei nafuu. Kwa sababu mita za awali tulikuwa tumezitoa nje, bei kidogo ilikuwa juu kwa wananchi, nasi kama Serikali tunaangalia uwezekano wa kumpunguzia gharama za maisha mlaji wa mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba zoezi la ufungaji mita za malipo kabla, zitaendelea vizuri na siyo tu kwa Arusha, bali nchi nzima. (Makofi)
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa, tarehe 7 Agosti, 2022 Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotembelea pale Rungwe Serikali ilitoa ahadi kwamba mradi huu ungekamilika mwezi Oktoba, 2023; na kwa kuwa, tarehe hiyo imepita sasa; je, Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza akawaeleza wananchi wa Tukuyu kwamba ni lini sasa mradi huo utakamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mradi wa Maji uliopo Wilaya ya Mwanga, Kata ya Kileo, sehemu inaitwa Mnoa, ambao unakusudia kuwahudumia wananchi wa Vijiji vya Kileo, Kituri na Kivulini, wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3; je, ni lini sasa mradi huu utakamilika ili wananchi wa vijiji hivi vitatu vya Kileo, Kituri na Kivulini, Kata ya Kileo waweze kupata maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Albert Anton Mwantona, kwa niaba yake limeulizwa na Mheshimiwa Joseph Tadayo, lini mradi huu utakamilika; kipande ambacho tulimwahidi Mheshimiwa Rais kukamilika, kilishakamilika. Ni hizi kilometa tisa kutoka kule kwenye chanzo cha Mto Mbaka mpaka pale kwenye tanki. Ni mimi mwenyewe kabla ya ule mwezi wa Kumi nilikwenda pale Tukuyu na tukahakikisha maji yameweza kuingizwa kwenye existing line.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo ambalo limebaki kama nilivyosema, kufikia mwezi Aprili tunatarajia tanki liwe limekamilika lijazwe na kuongeza uzambazaji kwa existing line na kuongeza line mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kwenye swali la pili la kutoka Mwanga, Mradi wa Moa, huu mradi umekamilika kwa asilimia zaidi ya 95 na tayari maeneo ambayo yanapitiwa na mradi huu yanaendelea kukamilishwa, na mwezi huu Februari tunatarajia maji yaweze kufika kwenye vijiji hivi alivyovitaja vya Kileo na Kivulini. Kwa watu wa Kituri, wenyewe kwa sasa hivi wanapata maji kutoka kwenye Mradi wa Kifaru. Kwa hiyo, wapo kwenye mpango wa kuongezewa extension kutoka kwenye huu Mradi wa Mnoa, baada ya hawa ambao hawana maji kabisa kupata, nao watapelekewa maji vilevile. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana; bei ya maji pale Same sasa hivi ni kati ya shilingi 4,000 mpaka shilingi 5,000 kwa ndoo na adha hii inawakumba sana wanawake wa Same; ni lini sasa Mradi wa Mwanga – Same – Mombo utakamilika ili waweze kupunguza adha hii?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa mama yangu kuhusu Mradi wa Same – Mwanga – Korogwe; mradi huu kwa sasa hivi tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, ameweza kutuwezesha na wakandarasi wote kwenye kila kipengele wapo kazini. Kufikia mwezi Juni, 2024 tunatarajia mradi uwe umekwisha. Mpaka leo hii mradi upo asilimia 86.
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuweza kuuliza swali nyonyeza, nina maswali mawili.

Makao Makuu ya Wilaya ya Nkasi yana changamoto kubwa sana ya maji, ni nini mpango wa kutoa maji Ziwa Tanganyika ambao unaanzia Kata ya Wampembe kupeleka maji Wilayani Nkasi ?

Swali la Pili, Vijiji vya Mwinza, Diela, Katenge, Lupata, Lyapinda, Kasanga Ndogo, Katenge, Msamba, wananchi wanaliwa na Mamba wanapofuata huduma ya maji. Je, ni lini kama Wizara mtakaa na Wizara ya Maliasili ili muainishe maeneno yale ambayo wananchi wanapata huduma ya maji muwawekee wavu ili wananchi wasiliendelee kuliwa na mamba? Kwani ndani ya mwaka mmoja wameliwa watu Kumi. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya Ziwa Tanganyika kupeleka maji Makao Makuu ya Wilaya. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge, umefuatilia sana na tayari Wizara tunaendelea na taratibu za kuona kwamba Ziwa Tanganyika tunaweza kuleta maji pale na maji yawe ya uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la wananchi kuliwa na mamba. Mheshimiwa Mbunge nakupa pole sana kwa wananchi kupata hii kadhia, tutalichukulia kwa umakini mkubwa kuhakikisha kwamba tunakutana na wenzetu wa Maliasili basi tuje tuweke hiyo mipaka ya kuhakikisha wananchi wanachota maji maeneo yenye usalama. (Makofi)
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Skimu ya Nalasi iligharimu zaidi ya milioni 800 na ilifanya kazi kwa mwezi mmoja, na sasa haifanyi kazi kutokana na matatizo ya kiufundi. Katika kampeni tuliahidi kwamba Skimu hiyo itafanyiwa matengenezo, lakini mpaka sasa hii ni mara ya pili nauliza swali hili naambiwa litafanyiwa maboresho;

Je, ni lini Serikali itafanya maboresho makubwa kwenye skimu ile ambayo imegharimu pesa nyingi na haifanyi kazi, ili wananchi wa Vijiji vya Nalasi, Lipepo na Chilundundu vipate huduma ya maji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; mwaka jana mwezi Agosti RUWASA Mkoa waliingia makataba na Kampuni ya Chikwale Company Limited wa uchimbaji visima 18, pamoja na kisima kimoja kirefu katika Kijiji cha Nalasi na Vijiji vingine vya Azimio, Semeni, Angalia na Mwenge ili kuboresha upatikanaji wa maji, lakini mkandarasi yule mpka sasa hajafanya kazi ya aina yoyote;

Je, ni lini Serikali itapeleka Mkandarasi mwingine mwenye uwezo wakuchimba visima vile ili kuwapatia maji wananchi wa Jimbo la Tunduru Kusini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Daimu Mpakate, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali linalosema ni lini tutafanya ukarabati wa Skimu hii ya Nalasi; kama nilivyiojibu kwenye jibu langu la msingi; Mheshimiwa Mbunge naomba uamini kwamba sisi tutakuja kukamilisha ukarabati huu kadiri ya muda huu tulioahidi hapa na nitasimamia. Mheshimiwa Mbunge tutafika pamoja katika mradi huu na kuhakikisha unafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali namba mbili, kwamba ni lini Mkandarasi mwingine apatiwe aweze kuchimba visima hivi; naomba niwe nimelichukua tukalifanyie mchakato kuona kwa nini huyu ameshindwa na kuona namna njema ya kuhakikisha visima hivyo vinachimbwa.
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, naomba kumuuliza Naibu Waziri, kwanza kwa kuwashukuru namna ambavyo wanatatua kero ya maji katika Jiji la Mwanza hususani Wilaya ya Ilemela. Wamekuja na mkakati wa matokeo ya muda mfupi, wameanza kusambaza sim tank katika maeneo yenye changamoto.

SPIKA: Swali Mheshimiwa, mmesimama Wabunge wengi.

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, swali langu ni kwamba walishafanya survey katika maeneo ambyo wanaweza kuchimba visima kwa ajili ya ku-save maji hapo;

Je, ni lini visima vitajengwa katika Kata ya Kayenze Mtaa wa Lutongo ambako tayari feasibility study imeshafanyika na maji yalipatikana?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Angeline Mabula kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tumeshafanya survey na baadhi ya maeneo katika vijiji hivyo alivyovitaja tumepata maji. Katika eneo la kata aliyoitaja tumepata maji kidogo lakini maji hayo tutahakikisha tutayatumia kujenga vichotea maji vichache ili wananchi wale waweze kupata huduma ya maji.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya Mradi wa Maji katika Wilaya ya Monduli ambao utapita katika Vijiji vya Mbuyuni, Makuyuni, Losimingoli na Naiti? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Catherine Magige kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa eneo la Monduli kazi mbalimbali zinaendelea kwenye mradi huu na niseme katika mwaka huu wa sedha, tutahakikisha tunakamilisha wananchi waweze kupata maji safi na salama.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa wananchi wengi Wilaya ya Nyang’wale wamefungiwa mita za maji na kushindwa kuendelea kutumia maji yale kwa ajili ya mita zao kwenda speed sana na kuwa bili kubwa;

Je, Serikali ipo tayari kutuma tume kwenda kuchunguza mita hizo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hussein Amar, Mbunge wa Nyang’wale kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tutatuma wataalam waweze kwenda kuchunguza mita hizo ili wananchi waweze kulipia bili kulingana na matumizi yao.
MHE. DANIEL B. SILLO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa maji wa Ziwa Madunga ulitakiwa usainiwe tangu 15 Oktoba, lakini mpaka leo haujasainiwa;

Je, ni lini mkataba huu utasainiwa ili wananchi wapate maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sillo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mradi huu wa Ziwa Madunga tunatarajia wiki hii Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo tumeweza kuwasiliana ofisini, tutahakikisha mkataba huu unasainiwa.
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba kwanza turekebishe taarifa kidogo. Jimbo la Ngara linaitwa Jimbo la Ngara na siyo Jimbo la Ngara mjini, naomba turekebishe taarifa.

Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa kwenye Taarifa ya Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba wananchi 170,000 wa Ngara Mjini, Kanazi, Kidimba, Nyamiaga na Murukulazo hawana huduma ya maji; na kwa kuwa visima viwili vya milioni 600 vinavyojengwa sasa haviwezi kutekeleza mahitaji ya maji ya wananchi wote hawa.

Je, Serikali ipo tayari kuanza kujenga mradi huu mkubwa wa bilioni 41, kwa kutumia mapato ya ndani yanayotoka Serikali, wakati ikiendelea kutafuta fedha kutoka nje?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; hivi karibuni Mheshimiwa Waziri wa Maji alifika Ngara na kuahidi kumlipa Baraka Makogwe hela yake ya fidia ya shilingi milioni 104, ambye bwana huyu ardhi yake uimechukuliwa na Wizara ya Maji nae neo lake limejengwa tenki kubwa la maji na huyu bwana hajalipwa kwa muda mrefu sana;

Je, ni lini, Serikali italipa fedha ya bwana Baraka Makogwe? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ndaisaba, Mbunge wa Ngara kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu kuweza kutumia mapato ya ndani kuanza mradi wa bilioni 41; Mheshimiwa Mbunge ushauri umepokelewa kwa sababu tumekuwa tukifanya hivi kwenye miradi mingi naamini na hili nalo tutalitupia jicho la ziada.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kulipa fidia, Mheshimiwa Mbunge ahadi ni deni kwa sabbau Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ameweza kuahidi; nikuhakikishie huyu mwananchi atalipwa fidia kadiri ambayo inatakikana.
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali.

Swali la kwanza, ni kweli kwamba visima hivi vimechimbwa, lakini kwa hivi sasa vimesimama na hakuna fedha ya kuendeleza. Je, Serikali italeta lini fedha ili kukamilisha uchimbaji wa visima hivyo?

Swali la pili, mradi wa maji kutoka Kijiji cha Lumeya, Nyakalilo, Kalebezo, Mizolozolo mpaka Nyehunge haufanyi kazi ipasavyo kwa sababu mambomba yake yanapasuka. Je, Serikali iko tayari pia kuukarabati mradi huu ili uweze kufanya kazi kwa ukamilifu wake? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, lini fedha itakwenda kwa ajili ya kuendeleza visima. Tayari Mheshimiwa Waziri ametoa maagizo kwa Mameneja wa Mikoa wote kuhakikisha hivi visima vinaweza kuendelezwa na tija ya uchimbaji visima hivi kunaweza kupatikana kwa maji bombani kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukarabati mradi ambao umekamilika lakini mabomba yanapasuka, hapa kwanza tumshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kutupatia fedha na kuhakikisha miradi inakamilika. Unapoona mabomba yanapasuka maana yake maji yamekuwa ni mengi tofauti na ilivyokuwa nyuma. Kwa hiyo, tuko tayari kukarabati ili kuhakikisha maji mengi yaliyopatikana sasa yanawafikia wananchi. (Makofi)
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu ya Serikali. Sasa nina maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa coverage ya maji katika Wilaya ya Ikungi ni asilimia 53 ambayo iko chini sana, kuna maeneo ambayo yana changamoto kubwa. Sasa nataka tu nijue, ni nini mpango wa Serikali wa muda mfupi kuwapatia maji wananchi wa Wilaya ya Ikungi kwa maana ya Kata za Kikio katika Kijiji cha Nkundi, Lighwa katika Kijiji cha Mwisi na Issuna katika Kijiji cha Issuna A, Kitongoji cha Manjaru?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kuna visima vilivyochimbwa ambavyo bado havijawekewa miundombinu. Nilitaka nijue kwamba, visima hivyo katika vijiji vya Msule, Mkinya, Mang’onyi na Mbwanchiki pamoja na Ujaire.

Ni lini sasa Serikali itatenga fedha ya kujenga miundombinu ili kuondoa adha ya maji katika maeneo haya niliyoyataja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mpango wa muda mfupi kwenye kata na vijiji alivyovitaja Mheshimiwa Mtaturu, ni kwamba tutaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha tunakuja kuchimba visima.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie Bunge lako Tukufu nimwagize RM Singida, ahahakikishe anakwenda kwenye hizi kata, wafanye usanifu ili kuona wapi tunaweza tukapata maji chini ya ardhi ili sasa waweze kupelekewa gari wakachimbe visima na wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, lini tutatenga fedha kwa ajili ya miundombinu kwenye visima tulivyochimba; kwa utaratibu wa Wizara, tukishachimba visima kazi inayofuata ni usambazaji. Kwa hiyo, nina uhakika kama mwaka huu wa fedha kwa maana ya kuanzia leo mpaka Juni, Wizara tukawa tumepata fedha ambazo hazitoshelezi kuwafikia, mwaka ujao wa fedha lazima maeneo haya yote tuje tusambaze maji katika visima ambavyo tumevichimba.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuuliza swali la nyongeza. Mabwawa mawili, Bwawa la Luguru na Bwawa la Mwamapalala, Wilaya ya Itilima, Mkoa wa Simiyu yana hali mbaya, yamejaa tope: Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa mabwawa hayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Midimu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mabwawa haya aliyoyataja niseme tu kwamba, tuko kwenye utaratibu wa kuona kama tutaweza kuendelea kuyatumia tuje tuweze kuyakarabati. Pia kwa Mkoa wa Simiyu tuna mradi mkubwa sana ambao unakwenda kutatua changamoto ya maji katika maeneo haya mengi. Kwa hiyo, huenda tusikarabati, lakini tukautumia mradi ule wa mabadiliko ya tabianchi kuhakikisha maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge tunayapelekea maji safi na salama. (Makofi)
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuwa Mji wa Kisesa na Bujora una hali mbaya sana ya upatikanaji wa maji; na kwa kuwa Serikali imetoa fedha kujenga tank kubwa la cubic meter milioni tano: Je, ni lini usabazaji wa mabomba utaanza katika Mji wa Kisesa na Bujora?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Boniventura Kiswaga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli, maeneo aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge yapo kwenye mchakato wa utekelezaji wa mradi mkubwa ambao huu Mji wa Kisesa tayari mabomba makubwa ya nchi 10 yameshaanza kulazwa kama kilometa tatu hivi, lakini tayari mabomba ya nchi nane pia yako pale site. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge. Nimpongeze kwa kufuatilia, lakini hizi kazi tayari zimeanza, na amekiri tank kubwa linajengwa pale Bujora, na penyewe pia utaratibu unaendelea wa kuongeza mabomba ambayo yatatosheleza mradi huu mzima wa Kisesa na Bujora.
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kutokana na tatizo la maji katika Wilaya hizi za Mkoa huu wa Dodoma, naomba niulize swali kwamba ni lini Bwawa la Farkwa litaanza ujenzi kama ilivyo katika mkakati wa Serikali? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Khadija Taya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, napenda kusema nina furaha kubwa sana kwa sababu, sasa ujenzi wa Bwawa la Farkwa upo tayari kwenye pipe. Ni wiki iliyopita tu wameweza kusaini mkataba wa kazi hii kuanza na tutarajie kazi itakwenda vizuri kwa sababu ni mradi ambao tunautarajia sana katika kupunguza changamoto ya maji kwenye Jiji la Dodoma. (Makofi)
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia majibu ya Serikali, yanaonesha kwamba zoezi hili lilianza mwaka 2019 na mpaka leo ni takribani miaka mitano, wameweza kufungia wananchi 345 ambayo ni sawa na asilimia 0.285 kwa miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizingatia kwamba wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini wamekuwa wanalalamika kwa muda mrefu sana kuhusiana na bili kubwa za maji na kubambikiwa bili; je, nini kauli ya Serikali kuhusiana na changamoto hii? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili ni kwamba, kama kwa miaka mitano tumeweza kufungia wananchi kwa maana ya 345 kati ya wananchi 120,899 ambao wanatakiwa kufungiwa mita za LUKU za namna hiyo; je, Serikali imejipangaje kuweka timeframe kuhakikisha kwamba wananchi wote 120,899 wanafungiwa mita za maji kama za LUKU?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mrisho Gambo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kujipanga kuhusiana na ubambikaji wa bili kwa wananchi, hili tayari tumeshalifanyia kazi kubwa sana. Zoezi hili limeanza taratibu kwa sababu ya kutoa elimu na kuhakiki hizi dira ambazo tumekuwa tukizitoa nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba tumejipangaje sisi kama Wizara, tayari tumetoa fursa kwa vyuo vyetu vya ufundi hapa nchini; Chuo cha Ufundi Arusha, pamoja na Chuo cha Ufundi cha Dar es Salaam, (Dar es Salaam Institute of Technology) ambao sasa tayari wanaendelea kutengeneza mita hizi. Lengo ni kuona tunataka kusambaza mita kwa bei nafuu. Kwa sababu mita za awali tulikuwa tumezitoa nje, bei kidogo ilikuwa juu kwa wananchi, nasi kama Serikali tunaangalia uwezekano wa kumpunguzia gharama za maisha mlaji wa mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba zoezi la ufungaji mita za malipo kabla, zitaendelea vizuri na siyo tu kwa Arusha, bali nchi nzima. (Makofi)
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa, tarehe 7 Agosti, 2022 Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotembelea pale Rungwe Serikali ilitoa ahadi kwamba mradi huu ungekamilika mwezi Oktoba, 2023; na kwa kuwa, tarehe hiyo imepita sasa; je, Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza akawaeleza wananchi wa Tukuyu kwamba ni lini sasa mradi huo utakamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mradi wa Maji uliopo Wilaya ya Mwanga, Kata ya Kileo, sehemu inaitwa Mnoa, ambao unakusudia kuwahudumia wananchi wa Vijiji vya Kileo, Kituri na Kivulini, wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3; je, ni lini sasa mradi huu utakamilika ili wananchi wa vijiji hivi vitatu vya Kileo, Kituri na Kivulini, Kata ya Kileo waweze kupata maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Albert Anton Mwantona, kwa niaba yake limeulizwa na Mheshimiwa Joseph Tadayo, lini mradi huu utakamilika; kipande ambacho tulimwahidi Mheshimiwa Rais kukamilika, kilishakamilika. Ni hizi kilometa tisa kutoka kule kwenye chanzo cha Mto Mbaka mpaka pale kwenye tanki. Ni mimi mwenyewe kabla ya ule mwezi wa Kumi nilikwenda pale Tukuyu na tukahakikisha maji yameweza kuingizwa kwenye existing line.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo ambalo limebaki kama nilivyosema, kufikia mwezi Aprili tunatarajia tanki liwe limekamilika lijazwe na kuongeza uzambazaji kwa existing line na kuongeza line mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kwenye swali la pili la kutoka Mwanga, Mradi wa Moa, huu mradi umekamilika kwa asilimia zaidi ya 95 na tayari maeneo ambayo yanapitiwa na mradi huu yanaendelea kukamilishwa, na mwezi huu Februari tunatarajia maji yaweze kufika kwenye vijiji hivi alivyovitaja vya Kileo na Kivulini. Kwa watu wa Kituri, wenyewe kwa sasa hivi wanapata maji kutoka kwenye Mradi wa Kifaru. Kwa hiyo, wapo kwenye mpango wa kuongezewa extension kutoka kwenye huu Mradi wa Mnoa, baada ya hawa ambao hawana maji kabisa kupata, nao watapelekewa maji vilevile. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana; bei ya maji pale Same sasa hivi ni kati ya shilingi 4,000 mpaka shilingi 5,000 kwa ndoo na adha hii inawakumba sana wanawake wa Same; ni lini sasa Mradi wa Mwanga – Same – Mombo utakamilika ili waweze kupunguza adha hii?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa mama yangu kuhusu Mradi wa Same – Mwanga – Korogwe; mradi huu kwa sasa hivi tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, ameweza kutuwezesha na wakandarasi wote kwenye kila kipengele wapo kazini. Kufikia mwezi Juni, 2024 tunatarajia mradi uwe umekwisha. Mpaka leo hii mradi upo asilimia 86.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri lakini nina maswali mawili ya nyongeza; kwanza nishukuru Serikali kwa kuweka Mji wa Kasulu kati ya miji 28 itakayonufaika na mpango wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza kwa wakati huu ambapo kuna mlipuko wa kipindupindu je, Serikali ina mpango upi wa dharura wa kuweza kuwasaidia wananchi wa Kasulu ili kuondokana na tatizo la maji machafu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili katika Halmashauri ya Kasulu DC zipo kata ambazo tayari zimeshachimba visima lakini maji hayajasambazwa kutokana na ukosefu wa miundombinu ya mabomba. Kata hizo ni Kata ya Kasangezi, Lusesa, Hurugongo na Shunguliba. Ni lini Serikali itamaliza matatizo hayo katika kata hizo nilizozitaja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Genzabuke kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tupokee pongezi zako na tumshukuru Mheshimiwa Rais ambaye ameweza kupigania huu mradi wa miji 28 sasa tayari unatekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na mlipuko wa kipindupindu Mheshimiwa Genzabuke sisi kama Wizara tuko imara sana kuona kwamba kama chujio halipo lakini tunatibu maji kwa kutumia chlorine hatutoi maji bila kuyatibu. Kwa hiyo, huenda maji yakawa na tope kidogo lakini yametibiwa na chlorine. Kwa hiyo, vidudu vinakuwa vinauliwa na tunawasihi wananchi kuhakikisha wanachemsha maji, wanakula vyakula vya moto ili tuweze kupunguza maambukizi ya kipindupindu.

Mheshimiwa Naibu Spika, visima tayari, bado kusambaza, tayari Serikali tumeanza kufikia visima vyote vilivyochimbwa na vina maji ya kutosha kuona tunaleta usambazaji. Vilevile kama kisima kina maji kidogo tunaweka japo vichotea maji viwili, vitatu katika lile eneo ili wananchi waweze kufikiwa. Hivyo nikupongeze dada yangu Mheshimiwa Josephine kwa ufatliaji huo na niseme kwamba tutakuja kuhakikisha visima vyote vilivyochimbwa vinaweza kuleta tija ya wananchi kupata maji safi na salama bombani.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, Mradi wa Maji wa Malampaka Male utaanza lini?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Esther, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Malampaka upo kwenye hatua za mwisho kabisa na kuona kwamba tunaanza kuutekeleza.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwanza nimpongeze Naibu Waziri kwa ziara yake nzuri aliyoifanya katika Wilaya ya Lushoto na sasa maji yanatiririka pale kwenye Kata ya Kwai. Naomba kuuliza ule mradi mkubwa ambao uta-cover kata 13 za Wilaya ya Lushoto ni lini utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ulenge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipende kukushukuru kwa pongezi zako lakini kwa kazi kubwa na wewe unayoshiriki kuifanya katika Jimbo la Lushoto katika majimbo yale matatu ushiriki wako niliweza kuukuta na hongera sana pia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mradi huu wa kata 15 ambao umeutaja tayari Serikali tunaendelea na hatua za mwisho kabisa ili tuweze kuja kuuanza mara moja na utekelezaji utaendelea mwaka ujao wa fedha.
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali ambayo ni mazuri na nashukuru pia kwamba mradi unaenda vizuri kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri. Sasa maswali mawili:-

Swali la kwanza ni nini kauli ya Serikali kuhusu bei ya maji maana hata kule ambako miradi imekamilika kuna mahali ambako bei ya maji ni kubwa sana hadi shilingi 5,000 kwa unit ambazo ni lita 1000, kama kule Kyamurairi na sehemu nyingine ambako maeneo mengine ni shilingi 1000 lakini kule ni shilingi 5,000.

Swali la pili, kuna Kata Sita ambazo nako kuna mradi unaosemwa siku nyingi Kata ya Izimbya, Kaitoke, Mugajwale, Ruhunga, Katoro na Kaibanja, ambako Mheshimiwa Naibu Waziri amewahi kufika tukazungumzia jambo hilo na anazifahamu Kata hizo, mradi huo unaanza lini kutekelezwa? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jasson Rweikiza kama ifuatavyo:-

Awali ya yote ni kweli nilifika na Mheshimiwa Mbunge nakupongeza, tulifanya hii kazi kwa pamoja na tutakuja tena kuona kwamba tunakamilisha miradi hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na bei za maji ninaomba kutoa taarifa ni wiki ya jana tu Mheshimiwa Waziri ametoa bei elekezi kwa miradi yote nchi nzima. Hivyo maeneo ambayo yana bei ambazo kidogo siyo rafiki kwa wananchi kama maeneo yako ya Bukoba Vijijini, hata pale Karatu yote tumeyazingatia na bei elekezi zimetolewa na Mheshimiwa Waziri kwa kuzingatia nguvu inayotumika kusukuma mitambo yetu. Kama ni mafuta, kama ni umeme wa jua kama ni mserereko, kama ni umeme wa TANESCO pamoja na pump za mikono, yote haya Mheshimiwa Waziri ameshatoa maelekezo na sasa hivi bei zitakwenda kuwa rafiki sana, wiki ijayo kwa maana ya mwaka mpya wa fedha zitaanza kutumika.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusiana na Kata Sita alizozitaja Mheshimiwa Mbunge tumeshirikiana kwa pamoja na tayari usanifu nafahamu unaendelea, kadri tutakavyopata fedha tutaleta Mkandarasi mapema sana ili Kata hizi zote ziweze kupata maji na maeneo haya ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakipata matatizo ya maji tunakuja kuyashughulikia.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkoa wa Dar es Salaam miundombinu yake ya maji ni ya muda mrefu sana, kwa sababu tulipata maji muda mrefu kabla ya Mikoa yote. Sasa hivi miundombinu ile ni mibovu na inamwaga maji mengi hasa katika Jimbo letu la Temeke.

Je, Serikali mna mkakati gani wa kuelekeza tena upya miundombinu ya maji katika Mkoa wetu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dorothy Mbunge wa Temeke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna baadhi ya maeneo ya Temeke yana changamoto ya mabomba kupasuka kwa uchakavu na maji sasa yamekuwa mengi kwa sababu ni miradi mikubwa iliyotekelezwa na DAWASA, hivyo nipende kukutoa hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeanza utekelezaji nimeshafuatilia hili maeneo ya Tandika, Tandale maeneo ya Wailess na Temeke penyewe tayari wameanza kubadilisha yale mabomba yaliyochakaa.

Mheshimiwa Spika, maeneo ambayo bado maji yanaendelea kuvuja tunaendelea kufanyia kazi na kadri tutakavyopata fedha tunakuja kukamilisha maeneo yote ambayo maji yanavuja. Hili siyo tu kwa Temeke Waheshimiwa Wabunge niseme Mikoa yote, Majimbo yote tumetoa maelekezo kuhakikisha maeneo ambayo maji sasa yamekuwa ni mengi na mabomba yamechakaa yanashindwa kuhimili presha ya maji haya, tunakuja kufanyia ukarabati.(Makofi)
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Tatizo lililopo Bukoba Vijijini linafanana kabisa na tatizo lililopo Mtwara Vijijini. Kata ya Mango Pacha Nne, kuna mradi wa maji hadi leo haujakamilika. Je, ni lini Serikali itamalizia mradi huu ili kumtua ndoo kichwani mama wa Mango Pacha Nne ambaye kwa muda mrefu wamekuwa na changamoto kubwa ya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shamsia, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge amefuatilia hili sana na nimhakikishie nitafika Mtwara vijijini lakini tayari naendelea kusisitiza maelekezo tuliyoyatoa kwa watendaji wetu waweze kufanya kazi usiku na mchana ili mradi ule uweze kukamilika na akinamama na familia zote za Mtwara Vijijini ziweze kunufaika na kazi nzuri inayofanywa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Tunampongeza Mama Samia tumeshapata fedha asilimia 95 ya bajeti ambayo tunakwenda kuimaliza hivi punde. (Makofi)
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru mradi wa maji wa Isunga Kadashi ni moja ya miradi ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri aliitembelea katika Jimbo la Sumve na tukaahidiwa kwamba mradi ule utaanza kutoa maji ndani ya miezi miwili, lakini hadi sasa ninapozungumza ni zaidi ya mwaka sasa umepita na mradi ule hautoi maji.

Je nini tamko la Serikali kuhusu kitendo hicho ambacho kinapelekea watu wa Kijiji cha Isunga kutokupata maji kwa muda? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tamko la Serikali kwenye mradi ambao mimi na Mheshimiwa Mbunge tuliutembelea ni kufuatilia na kuhakikisha maji yanatoka, Mheshimiwa Mbunge naomba niwe nimelipokea nilifanyie kazi kwa nini maji hayajatoka hadi sasa. (Makofi)
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kijiji cha Mrelu ni eneo kame sana na kimeshachimbwa kisima. Je, ni lini Wizara italeta fedha ili maji yale yaweze kusambazwa?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba arudie swali.

SPIKA: Mheshimiwa Hhayuma hujasikika vizuri.

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kijiji cha Mrelu ni eneo kame sana na sasa hivi kisima kimeshachimbwa na wananchi wanaishukuru sana Serikali. Je, ni lini fedha zitapelekwa ili maji yale yaweze kusambazwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hhayuma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mara tunapopata chanzo cha uhakika, kusambaza ni moja ya wajibu wetu mkubwa na hiyo ndio tija ya dhima ya Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Mbunge mwaka ujao wa fedha mapema kabisa miezi ya mwanzoni tunaenda kusambaza maji katika eneo hili ambalo tumechimba kisima.
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mradi wa Nduku – Ntobo - Busangi ni mradi uliopangwa kiasi cha shilingi 750,000,000 ili uweze kukamilika na tayari hatua za manunuzi, mabomba yote ya plastiki yamenunuliwa, lakini kimekwamisha tu bomba za chuma.

Sasa je, ni lini Serikali itaenda kulipa fedha ili mabomba haya yaweze kununuliwa na mradi uweze kukamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama yeye alivyokiri ni mradi ambao unakwenda kuleta tija katika eneo hili na tayari baadhi ya mabomba yamefika, bomba hizi za chuma tayari zimeshaagizwa. Tumshukuru Mheshimiwa Rais ametoa fedha nyingi, kazi zimekuwa nyingi, hivyo hata wanaozalisha haya mabomba wamezidiwa, kwa hiyo kidogo kumekuwa na ucheleweshwaji. Hata hivyo, tumeshawaongezea nguvu ya kuona kwamba wanaweza kufanikiwa kuleta mabomba haya ndani ya muda. Hivyo, tunaomba Mheshimiwa Mbunge avute Subira, mabomba ya chuma yanakuna na kazi hii lazima ikamilike.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri wa maji pamoja na timu yake yote kwa kazi nzuri wanayoifanywa kwa miradi ya maji, lakini nina maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Mkoa wa Shinyanga una Majimbo sita na Jimbo la Ushetu ni mojawapo lakini Majimbo matano yana miradi mikubwa ya maji ya Ziwa Victoria isipokuwa Jimbo la Ushetu ambalo ni kilometa kama 17 tu ilipo miradi mikubwa wa maji. Leo hii maji hayo yameenda Tabora, yameenda Shelui, Mkoani Singida. Sasa nataka nipate commitment ya Serikali ni lini sasa maji haya ya Ziwa Victoria yataanza kupelekwa kwa wananchi wa Jimbo la Ushetu?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kuongozana na mimi kwenda kushuhudia adha wanayoipata wananchi wa Jimbo la Ushetu hasa katika Kata za Uyogo, Mapamba, Ushetu, Ulowa, Ubagwe na Ulewe ambako sasa wanauziwa ndoo ya maji kwa shilingi 1,500 hadi 2,000? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Emmanuel Cherehani, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napokea shukrani za Mheshimiwa Cherehani. Naamini anafahamu wiki iliyopita tayari watendaji wetu kutoka Makao Makuu ya RUWASA walikuwa jimboni kwake na chanzo cha wale watendaji kufika pale ni kwa sababu tunaenda kuanza mradi huu ambao tutachukua maji ya Ziwa Victoria kuleta kwenye maeneo haya ambako miradi inahitajika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la kuongozana na Mheshimiwa Mbunge nilishamjibu kwamba baada ya watendaji wetu wataalam wakishamaliza eneo lao, nitakwenda kuongeza hamasa ya kuona miradi hii inatekelezwa ndani ya muda uliopangwa. (Makofi)
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Spika, ahsante. Tarehe 29 mwaka 2021 niliuliza swali la msingi juu ya mradi ya Ziwa Victoria wa kwenda Kata za Goweko, Igalula na Nsololo na majibu ya Serikali hadi kufikia Juni, 2022, utakuwa umekamilika, lakini mradi huu upo asilimia 30. Nataka kauli ya Serikali, je, mradi huu utakamilika lini na wananchi wa Kata za Kigwa, Goweko na Nsololo wataweza kupata maji ya Ziwa Victoria?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Venant Protas, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifuatilia sana huu mradi, lakini changamoto za kiufundi ndizo zilizopelekea mradi huu kusuasua na sasa hivi ufumbuzi umeshapatikana. Mheshimiwa Mbunge kama tulivyoongea avute subira tunakwenda kukamilisha mradi huu na lengo ni kuona wananchi wanapata maji safi, salama na ya kutosha tena bombani.
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, ahante sana kwa kunipa nafasi. Chanzo cha maji cha Lojo kilichopo katika Kijiji cha Matongo pale Ikungi ni chanzo kikubwa ambacho kilifanyiwa utafiti mwaka 2010.

Je, ni lini sasa Serikali itaweza kukiendeleza chanzo kile ili kiweze kutosheleza maji katika Mkoa mzima wa Singida? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Miraji Mtaturu, Mbunge wa Ikungi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli chanzo hiki tunakitarajia kuwa ni moja ya vyanzo vitakavyopunguza tatizo maji katika eneo lake. Kukiendeleza chanzo hiki mwaka ujao wa fedha tutarudi kuona namna bora ya kutumia maji haya. Lengo ni kuona kwamba tunapunguza tatizo la maji katika eneo lake lote. (Makofi)
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Muleba na hili swali nimeuliza mara nyingi sana hapa Bungeni. Tunapakana na Ziwa Victoria na Wilaya ya Muleba ina matatizo makubwa sana ya maji pamoja na kwamba tupo kando kando ya Ziwa Victoria. Tuna mradi ambao usanifu na upembuzi yakinifu umekamilika wa kuchota maji kutoka ziwa Victoria na kuyasambaza kwenye Kata sita za Gwanseli, Magata, Kabuganga, Muleba Mjini, Buleza, Kagoma na Kikuku. Je, ni lini utekelezaji wa huo mradi utaanza kwa ajili ya wananchi wa Wilaya ya Muleba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ishengoma Kikoyo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru kwa kukiri kwamba pamoja na changamoto hizo lakini kazi zinaendelea kufanyika ndani ya Jimbo lake na hizo kata zote alizozitaja tunaendelea kuzifanyia kazi. Mimi na Mheshimiwa Mbunge tulitembelea chanzo kile kingine pale Kizuri ambacho kinatoa maji mengi na tunakiboresha. Kutumia maji ya Ziwa Victoria tutayatupia kwenye maeneo haya yote ambayo yapo mbali na vyanzo vingine. Maeneo yale ambayo Mheshimiwa Mbunge tumeshaongea mara nyingi na nimefika pale, ambayo yanapata maji tutaendelea kutumia vyanzo vilivyopo. Kwa maeneo ambayo ni muhimu kutumia maji ya Ziwa Victoria, tunakwenda kufanya kazi nzuri na maeneo haya yote aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge tutahakikisha maji yanapatikana.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Mradi wa Maji wa Patandi unaotekelezwa katika Kata ya Keri umeacha vitongoji vinne katika Kata ya Gwarusambo ambako ndiko vyanzo vya maji vinapatikana.

Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kuambatana nami kwenda site kutatua hizo changamoto? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Pallangyo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, nimeshafika Jimboni kwa Mheshimiwa Dkt. Pallangyo na tumefanya kazi nzuri, maeneo ambayo hayakupata maji kwa miaka mingi sasa hivi yanapata. Hivi vitongoji vinne vilivyobaki navyo vinaenda kwenye mwaka ujao wa fedha na vitapata maji. Suala la mimi kufika Jimboni kwa Mbunge, asijali kama ambavyo nilikwenda nikimaliza maeneo ambayo sijafika, nitarudi tena.
MHE. DANIEL B. SILLO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali napenda kujibu swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, yapita miaka miwili sasa toka Serikali ipeleke mabomba katika Miji Midogo ya Dareda na Galapo kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya maji chakavu.

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukarabati miradi hii chakavu katika Miji hii ya Galapo na Dareda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daniel Sillo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, miundombinu chakavu katika maeneo aliyoyataja tayari Mamlaka ya BAWASA inashughulikia na imeomba fedha milioni 511 ya kufanya kazi hii ambayo imekatishwa watu wa Plasco lakini vilevile kuhakikisha maeneo chakavu yanafanyiwa kazi.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa Kiteto tumekosa vyanzo vya uhakika vya maji, ni lini Serikali itatuletea mradi wa Simanjiro ufike Kiteto?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Olelekaita, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa Simanjiro kuelekea Jimboni kwake taratibu zinaendelea uhakikisha mara tukipata fedha tutaweka mkakati maalum kuhakikisha tunapeleka kule maji ya uhakika.
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na kusema kweli napongeza kwa hatua ambazo zimefikiwa katika mradi huo, tunachosubiri ni utekelezaji hapo mwakani mwanzoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mradi mwingine wa maji pale Kemondo, Mradi wa Maji Kemondo umechukua miaka mitatu, karibia minne bila kukamilika. Kwa nini unachelewa hivyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza na nipokee pongezi zake, ninakushukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kupokea namna ambavyo taratibu tumeendelea kuzifanya na kwa ushirikiano wako Mheshimiwa Mbunge ninakuhakikishia mradi huu utaenda kuanza mara moja kadri tulivyosema.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mradi wa Kemondo umechelewa kwa sababu ya kusubiria pampu ambazo zilikaa muda mrefu pale bandarini kupia michakato mbalimbali ya kiutaratibu, lakini mpaka hivi ninavyoongea tayari zile pampu zimeshachukuliwa, anazo Mkandarasi, kupitia Bunge lako Tukufu naomba nimuagize huyu Mkandarasi mwenye pampu za mradi wa Kemondo mara moja kufika mwisho wa wiki hii lazima pampu hizo ziweze kufika kwenye mradi. (Makofi)
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Naomba kujua mradi mkubwa wa maji kutoka Momba kwenda Tunduma mpaka Mbozi umefikia hatua gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Stella Fiyao, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi mkubwa anaouongelea ni mradi wetu wa kimkakati kama Wizara, tukitambua changamoto kubwa ya maji katika Mji wa Tunduma vilevile Mji wa Momba. Mradi huu tayari utekelezaji unaendelea na tutahakikisha unakwisha kwa wakati.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza. kazi aliyopewa sasa hivi Mkandarasi ambaye anafanya ukarabati mkubwa ni kupeleka maji katika matenki makubwa na hakuna fedha za distribution.

Je, Serikali ina mpango gani wa dharura kutenga fedha nyingi kwa ajili ya usambazaji wa maji kwenye vijiji husika na mradi huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili ni kutaka kujua maendeleo ya mradi wa kutoa maji Mto Ruvuma na kupeleka Mtwara Manispaa ambao utanufaisha Wilaya ya Mtwara na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba.

Je, mradi huu utaanza kutekelezwa lini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Chikota kama ifuatavyio: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, distribution, katika miradi yote ambayo fedha zinaanzisha miradi ya kutengeneza vyanzo, distribution huwa zinafanywa na mamlaka zetu. Hivyo Mheshimiwa Mbunge mpango wa Wizara ni kuhakikisha mara baada ya kukamilika eneo la kwanza la utekelezaji, namna ya kufanya distribution ndiyo kazi ambayo itafuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la pili, maendeleo ya matumizi ya Mto Ruvuma kupeleka maji Mtwara, hiki ni kipaumbele cha Wizara. Mto Ruvuma ni Mto ambao tunautegemea sana kama chanzo cha uhakika hivyo na chenyewe pia kitaendelea kutumika kadri fedha tunavyopata kwenye Wizara, tutahakikisha tunatekeleza Mradi huu wa Maji wa Mto Ruvuma.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa masikitiko makubwa ndani ya Bunge lako Tukufu naomba niseme kwamba Mama yetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ana kauli yake ya kumtua ndoo mwanamke kichwani, lakini Wizara ya Maji ndani ya Jimbo la Momba mmeipinga kauli hii kwa vitendo, imeikataa kabisa hiyo kauli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hapa nimekuja na clip kwenye simu yangu naomba uletewe hapo mbele wewe kama Spika wetu ili angalau wewe uweze kuangalia uone. Kama maji haya ambayo wana-Momba wanatumia, binadamu wa kawaida wanafaa kutumia kutumia haya maji. Mwezi wa sita ulinipa nafasi ya kusimama hapa kuomba mwongozo kwa Wizara ya Maji ili wanichimbie visima vya dharura, mpaka leo hivyo visima pamoja na watoto kuteseka hakuna hata tone la maji.

Mheshimiwa Spika, mradi ambao Wizara ya Maji wanasema huu wa bilioni 9.5 mwaka jana mwezi ya nne waliniondoa hapa Bungeni kwenda kukabidhi mradi kwa mkandarasi na tukaitwa mkutano mkubwa kwa wananchi na wakaahidi kwamba, kufikia mwaka huu mwezi wa sita mradi wa maji utakuwa umekamilika.

Mheshimiwa Spika, leo tunavyoongea wiki moja iliyopita ndiyo wametupatia milioni mia tano kati ya bilioni 9.5 na leo mbele ya Bunge lako tukufu Wizara ya Maji wanasema kwamba mradi huu utakamilika Desemba. Mimi nikienda kwa wananchi ndiyo naonekana tapeli. Sasa kati ya mimi na Wizara ya Maji wakina nani ni waongo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba hii clip uiangalie kwa niaba ya Bunge ili uone hii clip wewe uwe shahidi ikikupendeza ili uoneshwe hapa ili Mheshimiwa Rais aone kama Watanzania tulio mchagua, mimi Mbunge wa kike mtoto wake, wanawake wameniamini wanaweza wakatumia maji haya. Mimi naomba hii clip uone na Mheshimiwa Waziri Mkuu yupo hapa aione hii clip…
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru kwa nafasi hii lakini nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa namna anavyojibu maswali yake vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, kubwa Bunge lililopita tulipata concern ya Mheshimiwa Mbunge, Dada yangu Condester na mimi kama Waziri wa Maji nilifika Jimboni kwake na tukafika maeneo mbalimbali kuona hali ipo miradi ambayo inaendelea lakini kwa udharula nilitoa kiasi cha shilingi bilioni moja kuhakikisha kwamba tuna-support miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niombe sana Waheshimiwa Wabunge wakati mwingine tunaweza tukawakatisha tamaa watendaji wanaofanya kazi kubwa. Lakini kazi inafanyika na sisi kama Wizara ya Maji na ipo miradi ya kimkakati kuhakikisha kwamba tunalisaidia Jimbo la Momba.

Mheshimiwa Spika, nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sisi kama viongozi wa Wizara ya Maji hatutokuwa kikwazo kwa Wananchi wa Momba kupata Huduma ya Maji Safi na Salama katika kuhakikisha kwamba tunamtua mwanamama ndoo kichwani. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nimeletewa hapa hizo clip na nafikiri, hebu msaidizi njoo mfikishie Mheshimiwa Waziri pale ili apate hii picha.

(Hapa Waziri wa Maji alikabidhiwa simu iliyokuwa na clip yenye kuonesha akinamama wa Momba wakichota maji)

SPIKA: Lakini hoja ya Momba Waheshimiwa nadhani mtakumbuka kuna kipindi zilitajwa takwimu hapa ndani kuhusu maji, akasimama Mbunge wa Momba kuelezea kwamba hizi takwimu kwake yeye hazina uhalisia. Akasimama tena kama alivyosema kwenye Bunge nadhani ni Bunge la Bajeti ama lipi? Alisimama tena akaeleza maelezo yakatoka kwamba vikachimbwe visima kwa sababu magari yameishanunuliwa na Mheshimiwa Rais, vikachimbwe visima vya dharura yakatoka majibu hapa.

Mheshimiwa Waziri, anasema alishatoa bilioni moja maana yake hii milioni mia tano ni ya kuongezea kwenye ile bilioni moja ili utekelezaji uendelee. Lakini hali ya hawa wananchi nimekuletea hizo clip hapo siyo hali inayokubalika kwenye hivyo visima wanavyochota maji na kwa hiyo hali iliyoko hapo maana yake kwenye ardhi hiyo yapo maji. Kwa sababu hawa wanawake wametumbukia kwenye hicho kisima maana yake ikienda gari ikachimba hicho kisima hata kama ni kimoja, viwili, vitatu kwa wakati miradi mikubwa ikiendelea wachimbiwe hivyo visima nadhani nimekuletea hiyo clip umeishaipata au umeishaipata clip?

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, sisi haya ni maelekezo na tunayapokea na kama ana ufahamu Mheshimiwa Mbunge, mimi nilifika na tukatembea maeneo mengi na tukaweka mkakati. Kikubwa hayo ni maelezo jukumu letu ni kwenda kuyatekeleza. (Makofi)

SPIKA: Sawa, sasa kwa sababu kipindi hiki ni cha mvua lazima pia tuwe na uhalisia. Mheshimiwa Condester haya maji yanachotwa kipindi hiki au ni kipindi cha kiangazi? Ili na mimi nitoe maelekezo ambayo yanaeleweka hapa mbele, haya ni ya kipindi hiki cha mvua ama kipindi cha kiangazi? Hizi clip ni za sasa hivi au za kipindi cha kiangazi?

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, hizo clip nimechukua mwaka jana Mwezi wa Kumi na Mbili. Kwa hiyo, kipindi cha mvua watu ambao hawana mabati…

SPIKA: Hamuoni sasa hii yaani ni kipindi hiki?

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, ndiyo.

SPIKA: Haya. Mheshimiwa…

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, wakati mvua zimeishaanza.

SPIKA: Sawa. Mheshimiwa Waziri ameishapokea hayo maelekezo kwa sababu magari yapo kila Mkoa, gari lililoenda Songwe ama Mkoa wa jirani liazimwe lipelekwe likawachimbie kisima hawa wamama nadhani umeona hiyo hali iliyoko hapo. Kwa hiyo, nadhani hilo linaweza kufanyika ndani ya muda mfupi. Kwa sababu tayari hapo pana maji yale mambo ya usanifu, yakinifu, upembuzi, sijui nini hapo maji yapo na kwa sababu tayari wanayatumia hayo kawachimbieni hayo hayo wakati mnaendelea na utafiti wenu ili wananchi wa Momba waweze kupata maji. (Makofi)
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na mimi niulize ni lini Vijiji vya Mdundwalo, Maposeni, Malamala na Kimbango Nyasa vitapatiwa hivyo visima vya maji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Ntara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Dkt. Ntara tayari usanifu unafanyika, gari la kuchimba visima liko kule tumeishachimba kisima kikatoka maji machache sana kiasi kwamba hayawezi hata kupanda kwenye kichotea maji hata kimoja. Niwapongeze sana Regional Manager (RM) Ruvuma niliwaagiza, kwa sababu Dkt. Ntara hili swali ameishaniuliza mara nyingi tukiwa kwenye kiti. Tumeishafanyia kazi na wananchi wametoa ushirikiano kuna mto unaitwa Mpulanginga, huu mto umeonekana una maji ya kutosha kwa maeneo ya Mdundwalo na Maposeni. Lakini vilevile maeneo haya mengine ya Nyasa vilevile baada ya gari kumaliza hapa tunarajia liende huko likaweze kuchimba visima ili wananchi wapate maji safi na salama. (Makofi)
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Wilayani Rungwe kuna tatizo kubwa la maji hasa Kata ya Bulyaga, Makandana, Bagamoyo, Kawatere, Msasani na Ibigi. Sasa je, ni lini ujenzi wa tenki ambalo linatakiwa kuhudumu Kata hizo utakamilika? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Suma Ikenda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Suma Fyandomo kwa kufuatilia Mradi wa Maji Tukuyu lakini ushirikiano mkubwa sana wa Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo, Mheshimiwa Mwantona amefuatilia pia kwa karibu Mradi wa Maji Tukuyu Mjini na hili tenki ujenzi unaendelea na fedha milioni mia tano tunarajia kupeleka tena mgao wa mwezi huu. Kwa hiyo, nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge na mradi huu unakwenda kukamilika na wananchi wa Tukuyu wanaenda kupata huduma ya maji safi na salama. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi niulize swali swali la nyongeza. Ningependa kufahamu Serikali mnamkakati gani wa ziada kumaliza changamoto kwenye zile Kata tano za Makao Makuu ya Wilaya ya Nkasi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aida Khenani, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mkakati wa ziadi kuhakikisha zile Kata tano zinapata maji ni kwenda kupeleka miradi ya muda mfupi ya uchimbaji wa visima ili wananchi waendelee kupata maji wakati utaratibu wa kutumia Ziwa Tanganyika unaendelea kufanyiwa kazi.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Je, ni lini sasa Serikali itatatua changamoto ya maji ambayo ipo kwa muda mrefu katika Kata ya Lipwidi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shamsia lini Kata hii aliyoitaja tunapeleka maji? Mheshimiwa Shamsia kwanza nikupongeze kwa sababu umeishafuatilia sana lakini jitihada zinazoendelea pale Jimboni umeziona viongozi wetu wa Mkoa wa Mtwara wanaendelea kufanyia kazi na Kata hii inakwenda kupatiwa huduma ya maji safi na salama muda siyo mrefu.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Halmashauri ya Itigi haijachimbiwa visima katika bajeti mbili zilizopita na gari la Mkoa wa Singida limekuwa likienda huku huku mara Msomera mara wapi? Sasa lini Serikali itakwenda kuchimba visima katika Halmashauri ya Itigi, katika Jimbo langu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Yahaya Massare, Mbunge wa Itigi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hili eneo ambalo linatakiwa likachimbwe visima lipo kwenye mpango na kwa sababu gari lipo pale Mkoani tunarajia likimaliza upande umoja liliopo litakwenda katika maeneo haya na maeneo yote ambayo yanatakiwa kuchimbwa visima, visima vitachimbwa.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Sisi watu wa Mkoa wa Njombe tunatambua kazi kubwa iliyofanywa na Serikali katika Mradi huu wa Maji wa Igongwi. Lakini vilevile tunatambua sababu mojawapo ya kusababisha mradi huu wa Igongwi kutokuendelea ni kutokana na kutopeleka fedha kwenye Mradi wa Maji wa Ruvuyo Wilaya ya Ludewa ambako ndiyo chanzo cha maji kinatokea. Je, lini Serikali itapeleka pesa kwenye Mradi wa Ruvuyo ili kuweza kuruhusu mradi huo wa Igongwi uendelee?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pil; Kuna baadhi ya Vijiji ambavyo viko ndani ya Jimbo la Njombe Mjini kikiwepo Kijiji cha Ihanga havikuwekwa kwenye mradi wa maji vijijini kimakosa. Je, lini Serikali itaweka vijiji hivi ambavyo viko kwenye Jimbo la Njombe Mjini havikuhesabika kama viko vijijini kuwekwa kwenye Mradi wa Maji Vijijini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Mgaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimpongeze kwa ufuatiliaji. Mheshimiwa Neema hili umeishawahi kuniuliza mara kadhaa na nimeishalifanyia kazi kulingana na ufuatiliaji wako. Ili huu mradi upate kuendelea ni kweli fedha hapa katikati zilisimama lakini tumshukuru sana Mheshimiwa Rais tayari fedha Januari hii tumeanza kupokea ndani ya Wizara. Kwa hiyo, ni moja ya maeneo ambayo tutakwenda kupeleka fedha kwa awamu ili kazi ziweze kuendelea.

Mheshimiwa Spika, Eneo la Njombe mjini hivi vijiji ambavyo havikuhesabika katika miradi ya vijijini, ilifanyika hivyo kwa sababu ya jiografia yake. Lakini kwa ushirikiano wako wewe pamoja na Mbunge wa Jimbo wote mmeweza kufikisha suala na Viongozi wa Mkoa wa Njombe wameishapewa maelekezo kuona kwamba vijiji hivi navyo vinapelekewa huduma ya maji safi na salama. (Makofi)
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mradi wa Maji Awamu ya Pili wa Jimbo la Bukoba Mjini unaohudumia Kata tano; Kata ya Buhembe, Nyanga, Kashai, Kahororo na Nshambya umekwama tokea mwaka jana japokuwa mkandarasi yuko site.

Je, Serikali ipo tayari kupeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 253 kwa dharula ili wananchi wa kata hizi tano waweze kupata maji safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Lugangira, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mradi unaendelea kutekelezwa ndiyo maana umeweza kusema yule Mkandarasi yuko pale lakini suala la kupeleka fedha milioni 253 ni jukumu la Wizara nikuhakikishie Mheshimiwa Neema hizi fedha zitapelekwa ili kazi ziweze kuendelea. (Makofi)