Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Mohamed Suleiman Omar (1 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji
MHE. MOHAMED SULEIMAN OMAR: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu kwa azma yake ya kumtua mama ndoo kichwani. Pili nampongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara kwa kujitoa kwao kuhakikisha miradi ya maji inakamilika tena kwa ubora kabisa.

Namuomba sana Waziri kuwachukulia hatua watendaji wasio waaminifu na wakandarasi hovyo hovyo ili kuhakikisha miradi ya maji inakamilika kwa wakati tena kwa ubora unaotakiwa.

Mheshimiwa Spika, napongeza uamuzi wa Wizara kwa kutaka kuanza kutumia mita ya malipo ya awali, hili litaondoa malalamiko kwa wananchi kwa kubambakiziwa bill kubwa.

Mheshimiwa Spika, nashauri vijiji na vitongoji vitakavyopitiwa na mabomba ya miradi ya maji basi navyo vipatiwe maji.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.