Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Mbarouk Juma Khatib (1 total)

MHE. MBAROUK JUMA KHATIBU aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi katika eneo ambalo linajengwa Bandari Kuu ya mizigo Zanzibar?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbarouk Juma Khatibu, Mbunge wa Jimbo la Bumbwini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka ya Bandari ambayo imejenga bandari ya mizigo eneo la Manga Pwani – Zanzibar imetenga eneo na imeandaa michoro kwa ajili ya kujenga ofisi zitakazotumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama kikiwemo kituo cha polisi, ninakushukuru.