Contributions by Hon. Edward Olelekaita Kisau (20 total)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii, lakini kabla ya yote nimshukuru sana Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kunipa afya hii njema hadi leo niko Bungeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili niwashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Kiteto kwa imani kubwa na wamenichagua kwa kura nyingi sana. Nawaahidi kabisa kwamba nitawajengea heshima kubwa hapa Bungeni haijawahi kutokea. Vilevile nikishukuru Chama changu Cha Mapinduzi kwa kuniteua na nikapeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nijielekeze kutoa maoni yangu kwa Mpango huu wa Maendeleo. Mpango wa Maendeleo ni mzuri sana na kwa kweli katika kupitia zipo taarifa kama tatu hivi ambazo ni kubwa kweli. Kwa hiyo, maoni yangu ya kwanza nafikiri kama hatutayatendea haki sana mapendekezo haya kwa siku zilizopangwa kama nne hivi. Document ya kwanza ina kurasa karibu 164; ya pili 51; nyingine 107. Sasa ukichanganya zote na dakika tano hizi utajua kabisa kwamba pengine tungehitaji wiki mbili hivi za namna ya kuzungumza ili tuweze kuishauri Serikali vizuri sana katika mpango huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na muda kuwa mchache, nijielekeze kwenye kilimo. Kilimo hapa tumeambiwa kwamba pato la Taifa ni 27% na kinawaajiri Watanzania zaidi ya 65%. Nimshukuru sana Rais kwamba mapendekezo ya maendeleo mwaka huu ni kuwekeza nguvu kwenye kilimo. Tukiwekeza nguvu kwenye kilimo na hususan mbegu zipatikane kwa wakati na kuwaondoa wakulima kwenye jembe la mkono na ku-mechanize, tutaweza kulikwamua Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mahusiano katika kuendeleza kilimo siyo tu yana tija kwenye uchumi, lakini vilevile na mahusiano makubwa sana ya kupunguza umaskini kwa Watanzania walio wengi. Kwa hivyo kwa kweli naomba Wizara ya Kilimo isilale katika hii miaka mitano, tuwekeze nguvu kubwa sana kwenye kilimo na kwenye mbegu, unajua nchi zile zilizoendelea sasa wana-patent hizi mbegu, kwa hiyo tusiwekeze tu kwenye kufanya utafiti, lakini pia tu-patent mbegu zetu ili tuweze kulinda masoko yetu huko mbele ya safari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiwekeza kwenye kilimo, kwenye mifugo, kwenye uvuvi na tukaweka nguvu zetu zote huko tutakuwa tumeshughulika na vitu wanavyoita watu wengine the really economies kwa sababu ndiyo Watanzania wengi wako huko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni umeme na ningemwomba sana Waziri wa Nishati anisikilize vizuri hapa, Hotuba ya Mheshimiwa Rais ukurasa wa nane na nimeshamwandikia Mheshimiwa Waziri memo nyingi sana kuhusu suala la umeme. Nafurahi sana tumewekeza kwenye umeme na nawapongeza sana na Wizara wakati wanajibu maswali hapa walisema hivi, kwamba wamejiwekea miezi 18 kumaliza tatizo la umeme kwa vijiji vyote vilivyobaki. Hii ni ishara nzuri sana, lakini ni lazima sasa tuangalie umeme tulionao, Mheshimiwa Rais alisema hivi na naomba ninukuu, ukurasa wa nane wa hotuba ya 2015; “Mheshimiwa Spika eneo lingine ni TANESCO, TANESCO pamekuwa ni suala la kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara na kuwepo na umeme wa mgao na hilo limelalamikiwa sana na wananchi wetu.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto kwa miezi mitatu sasa umeme ni kukatikakatika halafu hatupati taarifa yoyote ile. Sasa wakati tunawekeza huko kutengeneza umeme, lazima sasa tuwe na uhakika wa umeme tulionao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda naunga mkono hoja lakini…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante kengele imeshalia
MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Ahsante sana.
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii nichangie mpango huu. Kwanza nimpongeze sana Waziri wa Fedha kwa umahiri wa ku-present mpango huu. Katika kusoma mpango huu ziko baadhi ya taarifa ambazo ndiyo zinaongoza mpango huu. Moja ni Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, nyingine ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, nyingine ni hotuba mbili za Mheshimiwa Rais, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, na Mungu amlaze mahali pema peponi; nyingine ni Dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2020 na nyingine ni Agenda 2063. Lakini muhimu kuliko yote ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025, hii hapa.
Mheshimiwa Spika, kama kuna ilani bora ambayo imewahi kuandikwa kwa utaalam mwingi sana na kwa lugha nyepesi sana ambayo Watanzania wanaifahamu ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2025. Na kama kuna zawadi ametuachia Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Bunge hili mkitaka heshima kwa Watanzania, na legacy ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ni kuleta mpango unaotekeleza ilani ya miaka mitano ijayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wakati tunatafuta kura, nimenunua ilani hizi na nimewapa wananchi wangu, nimewaambia wasome; Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji. Kwasababu miradi ya kimaendeleo ipo. Kama Bunge hili linataka heshima kwa Watanzania tuisaidie Serikali kutekeleza ilani hii kwa asilimia 100. Na sisi tutakuwa tumejenga heshima kubwa sana kwa Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na kwa wale ambao walikuwa Chato, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema hivi; mwanasiasa kwa level ya Urais ukichaguliwa miaka mitano ya kwanza unafanya bidii ile miaka mitano ili uchaguliwe tena, lakini miaka mitano ile mingine ya mwisho unaacha legacy.
Mheshimiwa Spika, ilani hii ina tafsiri zote mbili. Ni legacy ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kama tutakuwa tumetekeleza kwa asilimia 100. Lakini vilevile kwa lugha ya kisheria, ni fast turn ya Rais mama Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kama tutawekeza nguvu kutekeleza ilani hii kwa maana ya fast turn ya Mheshimiwa Rais wetu na legacy ya Dkt. John Pombe Magufuli, maana yake mpango huu tunatakiwa tu-double katika kuleta utekelezaji wa namna ya kutekeleza ilani hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukizungumza mambo ya kilimo, mimi nilikuwa naongea na wataalam wangu wa Wilaya ya Kiteto hapo. Kati ya hekta 1,000 walizowekeza kwa ajili ya umwagiliaji, ni hekta 15 tu ndiyo zinatumika. Na nilizungumza na Mheshimiwa Bashe hapa, excellent, alinishauri tulete andiko la mradi ili tuweze kuongeza hekta zile kwa ajili ya umwagiliaji, na tumeshaandika Mheshimiwa Naibu Waziri, the ball is on you.
Mheshimiwa Spika, sisi tunachotaka baada ya miaka mitano wananchi wale, Watanzania wale waliokuwa wanalia siku ile waweze kufuatilia ilani yao na kila kitu kilichosemwa kiwe kimetekelezwa kwa asilimia 100.
Mheshimiwa Spika, ilani hii inazungumzia barabara mbili kuu nzuri sana; Barabara ya kutoka Kongwa – Kiteto – Simanjiro mpaka Arusha, kilometa 430, ni mikoa karibu minne; Dodoma, Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Unaunganisha mikoa minne, ni uchumi. Najua barabara hii iko kwenye ilani hii, lakini sasa tuweke vipaumbele.
Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Tanga – Kilindi – Kiteto mpaka Singida, karibu mikoa mingine mitatu. Tulete sasa mkakati wa namna ya kutekeleza ilani hii ili wananchi hawa, Watanzania hawa waweze kusema legacy ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli imetekelezwa kwa imani kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, namalizia na kitu kimoja alichosema Mheshimiwa Rais wetu juzi. Kuna concept inaitwa ya Serikali moja, ambayo sasa naomba Mawaziri wasikilize vizuri sana; sisi Halmashauri yetu ya Kiteto kwa mara ya kwanza baada ya mvua za miaka miwili hii tumepata maji mengi sana na tuna Samaki sasa na wafugaji wameanza kula Samaki sasa. Na wilaya yangu imetengeneza kama source ya mapato kwamba ni pato jipya, wameanza kutoa leseni. Anakuja Wizara ya Maliasili na Utalii anasema ninyi mmepewa leseni lakini hamruhusiwi kuvuna; concept ya Serikali moja.
Mheshimiwa Spika, naomba sana Ofisi ya Waziri Mkuu ishughulike na hii concept ya Serikali moja. Kitu ambacho wananchi hawataki kusumbuliwa kabisa ni Wizara moja inakupa leseni moja halafu mwingine anatoka anasema haiwezekani, hiyo confusion tuondoe. Tukiondoa hiyo wananchi wetu watakuwa wamenufaika.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru na ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Kwanza kabisa, nimpongeze Waziri na timu yake kwa hotuba nzuri sana. Niseme tu nilifarijika sana kuwaona Machifu wale kutoka Iringa na nguo zao za asili. Tujue tu nchi yetu ina tamaduni nyingi sana na style ziko nyingi sana za namna ya kutambua tamaduni hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, TAMISEMI ni hati ya kila kitu kinachoendelea nchi hii. Kama nilivyokwishasema siku nyingi tu Mwenyezi Mungu awabariki sana watu walioandika ilani hii. Niwatambue Mheshimiwa Dkt. Bashiru na Mheshimiwa Polepole wako hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wakati tunatafuta kura safari hii hatujatoa ahadi zile nyingi za wanasiasa kwa sababu Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeweka kila kitu. Kwa hiyo, kazi yetu iliyobaki sasa ni kuhakikisha Ilani hii inatekelezwa kwa asilimia 100. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wameongea Wabunge wengi hapa kuhusu TARURA. Nimshukuru, nilikuwa na jirani yangu hapa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hii ameniambia imeongezwa karibu bilioni mia moja na kitu kwa TARURA; kama ni kweli tuwapongeze sana, lakini bado Kamati imeendelea kusisitiza nia ya kuiongezea pesa TARURA. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Wilaya yangu ya Kiteto tunatengewa shilingi bilioni moja, milioni 400 na…
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.
SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Tabasam.
T A A R I F A
MHE. TABASAM H. MWAGAO Mheshimiwa Spika, nampa Taarifa mzungumzaji, anasema TARURA imeongezewa bilioni 100 ni pesa ndogo sana hizo, hazitoshi kabisa. Naomba uendelee. (Makofi)
SPIKA: Unapokea Taarifa hiyo Mheshimiwa Mbunge wa Kiteto?
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakubali na ninapokea Taarifa hiyo, lakini lazima tuseme kwamba wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu anafunga Bunge la mwezi wa pili, alisema hivi, naomba nimnukuu: “Mheshimiwa Spika kumejitokeza mjadala unaohitaji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara za mijini na hasa vijijini. Vyombo vya TARURA na TANROADS vinafanyia kazi na sasa tutakusudia kuongeza uwezo wa vyombo hivi na hivyo Waheshimiwa Wabunge tumepokea ushauri wenu.” Kwa hiyo, waliyofanya tuwashukuru, lakini kama walivyosema Kamati na kama alivyosema Mbunge aliyenipa taarifa, tuendelee kuongeza pesa kwa TARURA. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilikuwa natoa taarifa tu kuhusu Kiteto, mfano, tunapata karibu shilingi bilioni moja na mia nne na hamsini na nne na chenji kidogo, lakini uhalisia ni shilingi bilioni saba. Huo ni mfano tu kwamba tunahitaji pesa nyingi sana kwa TARURA.
Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mbunge wa Same, Mheshimiwa Mama Kilango, ni kweli Wilaya ya Kiteto ni kubwa unachukua Mkoa wa Kilimanjaro unachukua na Jimbo la Kongwa, combine, ndio Wilaya ya Kiteto, kubwa sana. Kwa hiyo, nakubaliana naye kwamba tunapotengeneza vipaumbele hapa tuangalie jiografia ya majimbo haya, ni kubwa sana. Mheshimiwa Spika alikuja kunitafutia kura, tumetembea kata nne tu, nakushukuru sana, lakini kila mkutano tulioufanya kero namba moja ni barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna Kata yangu moja inaitwa Dongo, yaani ni kubwa saba, kwa hivyo ndugu zangu tuangalie sana suala hili. kila mkutano niliofanya na nilikuwa naangalia notice zangu wakati natafuta kura, kila mahali nimekwenda changamoto naandika, barabara. Tukifanya hivyo Watanzania watakuwa wamefarijika sana. Barabara za Kata za Sunya, Asamatwa, Magungu, Dongo, Makame, Katikati, Robosoid, Mserengine, Olpopori, Kiberesa, Nigish, Mbeli na Kiteto ni bread basket, mahindi yote yanayokuja huku yanatoka Kiteto, kwa hivyo, tuongeze juhudi katika kutengeneza barabara hizi ili wananchi hawa waongezee bidii.
Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ambayo hata Kamati imesema, ni hizi asilimia 10 ambazo ziko kwenye Ilani yetu. Kwa hiyo, sisi ni kutembea na Ilani tu, ukurasa wa 30, tuwe wakali kwa halmashauri zile ambazo hazitengi asilimia kumi. Sio kwamba tu wana-violate takwa la kisheria, lakini hawasomi Ilani yetu. Kati ya vitu ambavyo Wabunge tunatakiwa tuwe wakali sana hapa ni tuhakikishe Ilani hii inatekelezwa kwa asilimia 100. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, vituo vya afya. Ndio maana mimi nasema Ilani hii naipenda sana, inasema kila mahali tutajenga vituo vya afya, Wilaya ya Kiteto kati ya kata 23 tuna vituo vya afya viwili tu. Kwa hiyo, nafikiri tukija hapa mtuulize Bwana Olelekaita una kata ngapi ambazo hazina vituo vya afya, halafu tufanye mathematics simple, kila mwaka mnatakiwa mnipa ngapi ili baada ya miaka mitano tutekeleze, hivyo tu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tukisema tunapeleka computer kwenye sekondari kadhaa, mimi ninazo 18, kwa hiyo, ningekuja tu hapa nidai computer zangu 18. Labda kitu cha kufanya pia ni kujaribu ku-cost hii Ilani yetu ili tujue tunahitaji gharama ya shilingi ngapi miaka mitano ijayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wananchi sasa kwa muamko huu ambao umeoneshwa kupitia TAMISEMI wamechanga michango kwa ajili ya vituo vya afya; Dosidosi, Matui, Ndedo, kazi zinaendelea. Kwa hivyo, inatakiwa tu mkono wa Serikali kidogo ili tushirikiane kutekeleza Ilani hii. Kwa hiyo, tuangalie vipaumbele hivi na tutembelee maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, mimi nimekwenda kwenye kata moja katika mkutano wa hadhara, kumbe nikagundua wananchi wala hawataki hata ule mkutano wananiambia tu twende tukuoneshe kituo cha afya. Nilivyofika pale ikabidi niseme na mimi kwa Mfuko wa Jimbo nitaweka mkono hapa na nimeshafanya hivyo, lakini sasa pesa ya Serikali, mtuunge mkono ili wananchi wale wajue kwamba wakihangaika Serikali na yenyewe inaweka mkono. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni hati. Walimu wapo wengi sana wanajitolea, wanaomba ajira hizo tena kwa miaka mingi tu. Mimi nilikuwa naongea na Afisa wangu hapa akaniletea karibu majina 100 tu kwa Kiteto na wako walimu wazuri wenye taaluma tena za Kiswahili, mabingwa. Tumepitisha sheria hapa ya kuruhusu Kiswahili sasa kianze kutumika na tuna wataalamu wamejaa wanasubiri.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Mheshimiwa muda wako umeisha.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na ninaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Kwanza kabisa nampongeze Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu yao wote.
Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru, juzi alituwekea foundation nzuri sana. Tunapozungumza habari ya kilimo au mifugo na uvuvi, kama asilimia 65 au 70 ya Watanzania wako huko; we have no option, lakini Bunge hili umenisaidia, kwamba baada ya miaka mitano Watanzania wanufaike na sekta hizi za mifugo, uvuvi na kilimo. Najua pengine tutakuwa tumechelewa mwaka huu, lakini tunaanza kutema cheche hapa ili sasa mwaka wa fedha ujao Serikali ijue kabisa, kama tunataka kuweka legacy kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, ni lazima tu-commit pesa nyingi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilikuwa nasoma takwimu za Serikali hapa, tunaambiwa kuna mifugo karibu milioni 33.6. Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeainisha vitu vingi sana ambavyo tumeahidi kufanya kwa miaka mitano ijayo. Hekta za mifugo kutoka 2,788,000 hadi hekta 6,000,000. Kwa hiyo, maana yake tumeahidi kutenga hekta 3,211,000. Ili mifugo iweze kustawi ni lazima wawe na maeneo.
Mheshimiwa Spika, mzungumzaji aliyepita alikuwa anasema ng’ombe anazaliwa Kagera anaishia Lindi, there is absolutely nothing wrong. Ng’ombe kuhama ni coping mechanism ya magonjwa, wanatafuta maji na malisho. Wafanye nini sasa kama hifadhi zinachukuwa maeneo yao? Kuhama kubaya ni ile ya kusababisha migogoro na watumiaji wengine wa ardhi. Hiyo hapana, lakini kuhama ni coping strategy.
Mheshimiwa Spika, vile vile ilani inazungumza na nilikuwa nasoma hotuba ya Wizara hapa; inasema mtajenga majosho 129. Ni kidogo sana na hii inatokana na bajeti yenu kuwa ndogo sana. Kwa mfano, Kiteto peke yake majosho tunayohitaji ni 48, kwa sababu ilani inasema lazima katika kila kijiji chenye mifugo kiwe na josho. Sasa kama mnapewa bajeti ya kutengeneza majosho 129, Kiteto peke yake inahitaji 48, haiwezekani. It is a very big joke.
Mheshimiwa Spika, vile vile ilani imesema tutajenga mabwawa kama 400 hivi kwa miaka mitano. Kwa hiyo, in average ni mabwawa karibu 91 kila mwaka, lakini hapa ninyi mmepewa mabwawa manne tu. Kama siyo manne, Matano. It is a very big joke. Kwa Kiteto peke yake, pungufu ya malambo ni 44, halafu tunaweka kwenye bajeti manne.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tumedhamiria kwamba Bunge hili liwanyanyue Watanzania katika sekta hizi muhimu sana, nashauri; kwa sababu nilikuwa naangalia hapa, uvuvi na mifugo; na imetokea trend siku hizi ukichanganya mifugo na kilimo kuna sekta moja itapewa pesa nyingi kuliko nyingine. Ukichanganya maji na mifugo kuna sekta moja itapewa hela kutoka nyingine. Sasa maji tunafanya vizuri, kilimo tunaelekeaelekea hivi kidogo, sasa mmechanganya uvuvi na mifugo. Sasa uvuvi inachukua bajeti mmetenga hapa karibu shilingi bilioni 90 na kitu kwa uvuvi halafu mifugo shilingi bilioni 16.
Mheshimiwa Spika, tukitaka kufanya vizuri zaidi labda huko mbele tutenge kabisa, tuwe na Wizara maalum ya Mifugo, tuwe na Wizara maalum ya Uvuvi, tuwe na Wizara ya Kilimo. Tukitenga hivi tutaweza kuweka nguvu kubwa zaidi.
Mheshimiwa Spika, nami napendekeza tena, lazima tuji-commit, kuweka asilimia 10 ya mapato yetu kwenye uvuvi, kwenye mifugo na kilimo. Tukifanya hivyo tutaweka investment, lazima iwe serious. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mzungumzaji aliyepita alikuwa anatoa mifano ya nchi nyingine kama Ethiopia, Rwanda na Uganda; na Botswana by the way, ndiyo inafanya vizuri zaidi kuliko nchi yoyote Afrika kwa ku-export beef, lakini angalia investments zao, ni kubwa zaidi.
Mheshimiwa Spika, nami nakubaliana nawe. Kuna siku nimetembelea NARCO hapo, kwenda kuangalia ng’ombe pale. Ni kweli, yaani hata majani yaliyoko pale hayawezi kumalizwa na ng’ombe walioko NARCO. Ni afadhali mngewapa wafugaji tu. Kwa hiyo, ni lazima tuangalie tija kwa miradi tunayowekeza kwenye sekta hizi.
Mheshimiwa Spika, tulikuwa tunasoma ilani hapa; tani za kunenepesha mifugo nchi hii ni 900,000 peke yake na tuna ng’ombe milioni 33 na tumejiwekea malengo ya kutengeneza hizo tani milioni nane. Kwa hiyo, huo ni mfano tosha tu kwamba hatuja-invest heavily kwenye mifugo. Kwa hiyo, tusishangae sana.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, pato la Taifa asilimia 7.9 siyo kidogo. Wakati mwingine huwa nafikiri kwamba hatutengenezi mipango sahihi ya ku-capture contribution ya mifugo. Kama kuna wanywa bia hapa, hakuna mnywa bia hata mmoja asiyekula nyama. Nami sitaki kuvuruga Bunge lako, lakini ningesema leo wanyooshe mikono wanaokula nyama hapa, watasimama mpaka wale waandishi wa habari ambao wanapiga kamera hapa. Hiyo ni contribution ya mifugo. Kwa hiyo, I think hamjaweza ku-capture kabisa contribution ya mifugo.
Mheshimiwa Spika, kwa Jimbo la Kiteto peke yake tuna mifugo 500,000, mbuzi 500,000, siyo kidogo hiyo, ni contribution kubwa sana. Ripoti zeni zinasema kuna watu milioni nne wanategemea direct income kutoka kwenye mifugo katika nchi hii. Kwa hiyo, lazima tuwe serious katika ku-invest, tuweke pesa nyingi ili mifugo yetu iweze kuleta tija kwa Taifa.
Mheshimiwa Spika, nilikuwa naangalia ripoti zangu za Kiteto hapa wataalam wanaohitajika, ukiangalia wataalam wanaohitajika kwenye sekta hii ni 106 halafu waliopo ni 35, pungufu 40. Kwa hiyo lazima kweli tu-invest kwenye mifugo na uvuvi kama tunataka kwenda mbele huko. Miaka miwili iliyopita sisi tumepata mvua kubwa sana na Kiteto sasa tuna wafugaji wanakula Samaki sasa.
T A A R I F A
MHE. ESTHER MATIKO: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Esther Matiko nimekuona.
MHE. ESTHER MATIKO: Mheshimiwa Spika, ahsante nataka tu nimpe taarifa ndogo mchangiaji wakati anachangia amesema tukiamua kuazimia nakuchukua walau asilimia kumi ya mapato, tungeweza kufika mbali upande wa mifugo, uvuvi hata kilimo. Nimkumbushe tu kwamba ni Azimio la Malabo ambalo tumelisaini ambalo linatutaka walau tutenge asilimia kumi ya bajeti ya Serikali kwenye eneo la kilimo, mifugo na uvuvi. Kwa hiyo, siyo kwamba tuhiari tu kama mapato ila ni Azimio ambalo tumelisaini. Ahsante. (Makofi)
SPIKA: Taarifa hiyo unaipokea Mheshimiwa Edward.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakubali na napokea, lakini ninataka tu nimuambie kwamba hatuhitaji Malabo actually ili tuamue ku-invest ten percent. Malabo declaration ni kwamba tu wametusaidia, lakini kweli kama tungekuwa tunasubiri Malabo declaration na Malawi na hata hivyo pamoja na declaration hiyo investment inayoenda kwenye kilimo ni less than one percent, less than one percent. Kwa hiyo, kwa kweli lazima, lazima tutoke huku tu-invest every kwenye uvuvi, tu-invest every kwenye mifugo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nasema hivi, siku hizi Kiteto tumepata kama mabwawa mawili ya samaki na tumeanza kujifunza kula samaki na wilaya yangu kwa mara ya kwanza kwa mwaka fedha wamesema tutapata kodi kama milioni nane hivi inatokana na Samaki na wafugaji wameanza kutengeneza leseni kutoka kwenye halmashauri.
Mheshimiwa Spika, halafu anakuja mtu wa maliasili eti anawaambia wale wafugaji wale brand new, watu ambao wanataka kula samaki for the first time, halafu unawaambia tena eti hairuhusiwi, sijui nini, yaani tunawaongezeeni watu wa kula samaki ili tuongeze tija zaidi halafu mtu anatwambia mambo ya leseni yametoka wapi ni confusion na ndio ile Mheshimiwa Rais wetu alikuwa anasema concept of one government. Kwa hiyo, kwa kweli lazima tuwatetee, lakini baada ya kusema haya lazima sasa na ninyi mifugo muwe serious nilikuwa nasoma ripoti zenu hapa.
Mheshimiwa Spika, wanasema eti ng’ombe milioni sita zimekamatwa kwenye mapori tengefu, ng’ombe milioni sita ipo kwenye ripoti hapa, na kwanza nashangaa kwa sababu hawajaandika jimbo langu na kila siku wanakamatwa hapo na pori hili Tengeru linaitwa Mkongoroyo, lazima muwatete wafugaji hawa, ipo kwenye ripoti zenu. Naona Waziri anamuuliza mwenzake hapo. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, ukisoma ukurasa wa 205 nendeni mkasome data za mifugo kukamatwa kwenye mapori haya, ni lazima kama nchi tusimame huu ni uchumi hatutaki ng’ombe hizi zikamatwekamatwe hovyo ni uchumi wa wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi; na niungane na Wabunge wengine kukupongeza kwa unavyouendesha mjadala huu. Kwa kweli kama kuna mjadala ambao umefanyika kwa ufanisi sana. Ni mjadala huu wa ripoti ya CAG; na si kwa bahati mbaya, kwa sababu hii ndiyo imebeba kila kitu cha nchi hii, kwa hiyo nikupongeze sana, I am very proud, as your student, I am very proud. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niwapongeze sana Wajumbe wa Kamati hizi zote tatu, LAAC, PIC na PAC, kwa kweli wamefanya kazi nzuri sana, na ni kazi ngumu kwelikweli. Mimi nadhani mwaka mmoja uliopita halmashauri yangu iliitwa kwa hiyo nilishuhudia mahojiano kati ya Kamati yetu ya LAAC na halmashauri; inafanana kabisa na process zile za cross-examination za mahakama, ni nzuri sana. Kwa hiyo kwa kweli tuwapongeze sana.
Mheshimiwa Spika, nimejaribu kuangalia zile ripoti zota za CAG, takriban repoti 17, kama zote tutazifuatilia, pages 3,632. Hii maana yake nini? Ni kwamba, huko mbele ili tuweze kupata muda mzuri wa kuchangia vizuri, labda pengine tuangalie pia muda ili Wabunge waweze kuchangia. Niwapongeze Wabunge wale wote ambao wamepitia ripoti hizi, kwa kweli kazi nzuri sana wamefanya.
Mheshimiwa Spika, mimi nazipongeza pia halmashauri zilizofanya vizuri. Wale ambao wamefanya vibaya tuweze kuwasema sana. Tusipo shughulika na wale wanaofanya vibaya inaondoa uzalenda wa wale wanaofanya vizuri, kama alivyokuwa anasema Mheshimiwa Shigongo. Lazima wanaofanya vibaya waadhibiwe.
Mheshimiwa Spika, Jaji mstaafu wa Kenya aliwahi kusema hivi, “the greatness of any nation lies in its fidelity to the its constitution and adherence to the rule of law but above all respect to God”.
Mheshimiwa Spika, CAG ameshafanya kazi yake ya kikatiba na ameonesha madudu ambayo yamefanyika kila mahala. Kazi iliyobaki ni ya Bunge. Bunge liko kwenye trial wanasubiri sasa kuona Bunge litachukua maamuzi gani. Kwa hiyo, kwa kweli tufanye maamuzi ambayo yatasaidia nchi hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama walivyosema Wajumbe wengine hapa, Mheshimiwa Rais anafanya kazi nyingi sana, anahangaika kila mahala kutafuta pesa kwaajili ya miradi ya Tanzania. Lakini ukisoma ripoti hizi, na ukaangalia mfano tu wa zile fedha alizotafuta kwaajili ya miradi ya UVIKO, ilivyoleta heshima kila mahala nchi hii, halafu unaambiwa ni TirionI 1.3 tu; lakini ukisoma ripoti hii unaambiwa kuna zaidi ya Tirioni 1.8 zimepotea. Maana yake kwamba, kama hizi fedha tungeweza kupeleka kwenye miradi mingine heshima yetu ingekuwa kubwa zaidi na zaidi.
Mheshimiwa Spika, hakuna kitu kimenisikitisha sana kama unakuta unaambiwa eti kuna halmashauri 47 wamenunua dawa zimeharibika. Fedha zimetumika na maisha ya Watanzania tunayaweka kwenye wakati mgumu wa kuwa na dawa ambazo zimeharibika, this is shame. Kwa hiyo si tu kwamba fedha zao zimepotea lakini wanaweza pia wakapata madhara ya afya kutokana na dawa ambazo zimeharibika.
Mheshimiwa Spika, nilitaka pia kupata clarification kwa ripoti hii ya CAG, ukurasa wa tano. Kwenye ku- summarize zile recommendation, wanazosema 10,824 kwenye jedwali namba mbili wanasema utekelezaji unaendelea kwa recommendation 10,864.Lakini paragraph iliyopo juu hapo, wanasema mapendekezo 1,864 sawa na asilimia 17 hayajatekelezwa, lakini ukiangalia kwenye chati ambayo hayajatekelezwa ni 3,637, nadhani hiyo confussion lazima iwe clarified ili tujue. Kwa sababu hapa ni kama ime swap kidogo.
Mheshimiwa Spika, habari za halmashauri zimezungumzwa hapa na sisi tunakutana hapa kama wawakilishi wa wananchi, na kila mahala tunakokwenda hakuna maji, hakuna barabara, hakuna zahanati hakuna vituo vya afya, madarasa, madawati halafu ukiambiwa kuna fedha zinapotea na watu wapo na Sheria zipo ni hatari kidogo.
Mheshimiwa Spika, ukisoma ripoti hii, Mheshimiwa Attorney General ambaye kwa kweli namheshimu sana, I think is the only man, amekuwa DPP amekwenda judicial na Sasa ni Attorney General na is the most qualified, by the way. Naomba ulisaidie Bunge hili, next ripoti tusipate ripoti inayo tokana na mikataba ambayo inafungwa fungwa kwa ajabu ajabu. Bunge hili lilifanya mapinduzi ya sheria kwa kufanya wanasheria wote kuwa chini yako, hata wale wa halmashauri, nadhani nia ilikuwa ni mfanye quality assurance ili walau basi yale yanayotokana na mikataba mmusaidie CAG ili ripoti ijayo isiwepo.
Mheshimiwa Spika, kuna suala la TAMISEMI, na ripoti imezungumzwa hapa, kwamba hamrejeshi fedha, na sijui kama Waziri wa TAMISEMI yuko hapa. Nakushukuru na nakupongeza sana, ulisema unataka kuweka misingi ili wanao kufuata wakutane na misingi hiyo. Sasa, kuna suala linatusumbua kila wakati, kutorejeshwa kutoka hazina pesa mnazochukua kwa kigezo kwamba mwaka umeisha. Tumeshazungumza hapa, mnapeleka fedha na hamrudishi. Kwa mfano Kiteto imechukuliwa fedha milioni nane ya mfuko wa jimbo ambayo ilitakuwa iwe imejenga darasa Zambia Kata ya Lengateu, hamtaki kuleta milioni 32 za Basket Fund. Mheshimiwa Waziri kama unanisikiliza hizi pesa Monday, Tuesday Wednesday or next week hizi fedha zije tena. Haiwezekani mnatutengenezea hoja, kesho ripoti za CAG zije halafu mnatuambia kwamba miradi imechelewa, kumbe ni ninyi. Tulishasema hapa mzipeleke hizo fedha. Mheshimiwa Waziri hiyo ndiyo test yako ya Kwanza.
Mheshimiwa Spika, yamezungumzwa mambo mengi hapa, wizi takriban kila mahala, eti mpaka kwenye Balozi zetu; that is how desperate we area, mpaka kwenye Balozi. Sasa ukiona madudu yanafanyika mpaka kwenye Ubalozi basi ujue kwamba tuko desperate sana.
Mheshimiwa Spika, ripoti ya CAG inatuambia, kati ya maagizo ya Bunge hili 619 kwa mamlaka 99 eti kuna maagizo 264 ya Bunge lako hili hayajatekelezwa. Sasa ndiyo tutashangaa zile za Waziri wa Elimu na Bodi ya Mikopo, honestly kama maagizo 264 ya Bunge hili hayatekelezwi!
Mheshimiwa Spika, nimesoma ripoti ya Bodi ya Mikopo inasikitisha sana, kwamba wananchi masikini hata wale wanaotokana na familia za TASAF ambao kimsingi walitakiwa kuwa na dirisha maalum, wanakosa mikopo. Watoto wa wakulima, watoto wa single parent eti wanakosa mikopo. Mwalimu Nyerere alishasema hapa, ukitaka kumsaidia mtoto wa masikini, mpe elimu. Elimu haizuii umasikini, lakini ni silaha ya kupambana na umasikini. Sasa tusipoweka fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wetu, watapambanaje na umasikini?
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kweli hili la Bodi ya Mikopo, nashukuru sana kwa maazimio ya Bunge yaliyofanyika juzi. Wanafunzi wanahangaika kila mahali, wanatusumbua sisi Wabunge; “napiga simu hapa niangalie kama nitapata mkopo.” Wanafunzi ambao hali zao wanatoka kwenye familia ambayo ni masikini sana. Inasikitisha sana.
Mheshimiwa Spika, kwa maneno yangu ya mwisho kabisa, kwa sababu ni lazima tutengeneze majawabu. Nilikuwa nasoma kitabu fulani hapa. Institute inaitwa, Wajibu Institute of Public Accountability, wanasema hivi, naomba ninukuu, kwa sababu inaweza ikatusaidia mbele huko.
“Naombeni ushauri, Serikali kuiwezesha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa ndani kuwa na fungu au Vote ili kumjengea uwezo na kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi. Aidha, wajibu wa kumshauri Mkaguzi Mkuu wa ndani awe anapeleka taarifa hizi kwa Katibu Mkuu Ikulu ili taarifa zake zimfikie kwenye Baraza la Mawaziri ambalo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mwenyekiti wake. Ripoti hii ikimfikia Rais kabla ya Septemba, tarehe 30, ambapo itakuwa ni miezi tisa baada ya mwaka wa fedha wa Serikali kumalizika, hii itampa fursa Mheshimiwa Rais kujua hali ya utendaji wa Serikali kabla ya ripoti ya CAG.”
Mheshimiwa Spika, nadhani hili likichuliwa pengine linaweza likasaidia ku-improve ripoti huko mbele. Nakubaliana na maagizo yote na ripoti zote mbili, naomba Bunge hili sasa lionyeshe kazi yake.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii na kwa wale ambao hawafahamu Mheshimiwa Naibu Spika ni Mwalimu wangu, alinifundisha Law School of Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa napenda nimpongeze sana Waziri wa Maji; Waziri wa Maji kati ya wageni wangu niliowatambulisha leo, nilitembelewa na waliogombea na mimi, aliyegombea kupitia ACT Wazalendo Ubunge na aliyegombea kupitia CUF, wa ACT Wazalendo Ndugu Kamota amekubaliana na kasi ya Chama cha Mapinduzi na kazi anazofanya Mbunge hapa na amekubali kuungana na Chama cha Mapinduzi. Namshukuru sana kwa uungwana wake mzuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiteto nilishazungumza hapa ni takribani square kilometa 17,000 ni majimbo mengine kama matano hivi ni jimbo kubwa sana. Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi ambayo naongelea kila wakati kwasababu, ndio social contract ya kwetu na wananchi ukurasa wa saba na naomba ninukuu kabisa “Kuongeza kasi ya usambazaji maji safi na salama kwa asilimia 85 vijijini na 95 mijini”.
Mheshimiwa Waziri, kwanza kabisa naomba bajeti ya Kiteto msiipunguze hata nukta moja, tuanzie hapo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vile vile, kwanza Mkoa wa Manyara overall ni asilimia 58 tunapata maji below national average kwa hiyo, katika kutengeneza vipaumbele hivi tuangalie mikoa ambayo ipo nyuma. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukiacha Manyara sasa, Wilaya ya Kiteto ni asilimia 52 na Mji wa Kibaya ambao ndio mji wetu kwa miaka 20 sasa, ni asilimia 44 maji na miundombinu pale mjini yamechakaa ni ya mwaka 1980. Mheshimiwa Waziri, ukitutengea milioni 100 tutaweza kufumua mifumo ya maji ile na kutengeneza vizuri sana, ili Mji wa Kibaya ambao ndio sura ya wilaya ipate maji ya kutosha. Kata kama za Njoro Mji wa Matui, Kijungu, Lengatei, Dongo hazina maji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Hotuba ya Rais mama Samia Suluhu Hassan, ukurasa wa 29... (Makofi)
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Olelekaita kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani.
T A A R I F A
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni mdau wa Wilaya ya Kiteto nalima mashamba yangu kule, Mheshimiwa Mbunge ametaja kata ambazo zinakosa maji kwenye eneo hilo na nilikuwa namkumbusha tu kwamba asisahau Kata ya Dosidosi ambayo nimewekeza pia. Ahsante sana. (Makofi/Kicheko)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge alikuwa anaendelea kutaja kata zake. Haya unaipokea taarifa hiyo, unakumbushwa kwamba kuna kata inayohitaji.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea sana sana kabisa na nimkumbushe tu kwamba Katibu wa Mbunge anatoka Dosidosi. Na napokea sana na niseme tu kwa kuwa amenikumbusha, nilipata bahati ya kutembelewa na aliyekuwa Makamu wa Rais ambaye ni Rais wetu sasa Mama Samia Suluhu Hassan, kunitafutia kura na kituo cha kwanza kabisa ni Dosidosi. Dosidosi ni Kijiji cha kwanza tu ukitoka Kongwa na kutokana na ukame wa Jimbo la Kiteto, Mheshimiwa Rais aliahidi mabwawa Kiteto. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nakushukuru sana na ni kweli kama alivyosema naendelea kutaja kata zangu ambazo hazina maji; Kata ya Njoro, Kata ya Makame, Kata ya Lolera. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nasema hotuba ya Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan ukurasa wa 29 naomba ninukuu. “Aidha, kwa maeneo yasiyokuwa na vyanzo vya maji tutajielekeza katika ujenzi wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua”. Kutokana na jiografia ya Jimbo la Kiteto mabwawa, na kuna ahadi ya muda mrefu ya Serikali ya bwawa la Dongo, Kata nzima ya Dongo. Bwawa hili likijengwa vijiji sita na kata mbili zitanufaika na mradi huu na wananchi walishatenga eneo kubwa tu. Kwa hiyo, namuahidi Waziri kati ya maeneo ambayo tutakwenda ni Dongo ukaone bwawa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, shida nyingine, kutokana na ukubwa wa Wilaya hii engineer ni mmoja tu na mafundi wako watatu, haiwezekani. Tunaomba engineers wawili tunaomba na mafundi sita, hatutaki wengi sana sisi sio selfish sana hao tu Mheshimiwa Waziri. Tukipata na magari mawili kutokana na jiografia ya jimbo hili utatusaidia sana na maji yatapatikana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la maji wanaoumia sana ni wakina mama kwa hiyo, kama tutaweza kutimiza takwa hili la Chama Cha Mapinduzi tutakuwa tunawasaidia wakinamama wengi sana nchini. Baada ya kusema hayo nakushukuru sana kwa nafasi hii, ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi na kwanza kabisa nimpongeze professor Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri na timu yake na nawapongeza sana kwa sababu kwenye hotuba hii walau Kiteto imetajwa mara mbili tu, ukurasa wa 30 na ukurasa wa 127, lakini nawapongeza tena zaidi kwa sababu walau ninyi mmefuatilia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, na tunaka kila wizara tufuatilie Ilani hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukisoma Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ukurasa wa 42 tulijiwekea malengo ya kutengeneza tani laki 710 za alizeti, lakini kwenye hotuba hii nyinyi mmeweka tani milioni moja excellent tunataka tuwe na mwelekeo huu wa Ilani yetu. Lakini vilevile ukurasa wa 42 tulisema tutajenga maghala 14 kwenye mikoa hii ipo hapa excellent. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, vilevile tumesema kwenye ukurasa wa 43 tutawapatia vijana 400 kutoka mikoa tisa vifaa ipo kwenye hotuba yenu hapa safi sana. Lakini sasa nataka muongeze hivi vijana 400 mikoa tisa, kila mkoa tunataka mgawanye mlete mathematics ni vijana 44, na mkifika kwenye mikoa ile tunataka mtuambie mkoa ina wilaya ngapi na vijana wangapi watoke humo mimi nimeshapiga mahesabu nisipopata vijana sita kutoka Kiteto, Manyara mtakuja kutueleza mmefuata nini sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, suala la umwagiliaji Kiteto ambayo nilikwisha kusema ni bread basket, kilimo cha mvua ni asilimia 99.9 kati ya hekta 1385 ambazo tumetenga kwa ajili ya umwagiliaji ni 0.00 percent ndio inatumika haiwezekani. Ni lazima tuwe wakweli kabisa tunaposema kilimo, kilimo inachangia pato la Taifa asilimia 29, 28 au 26 data zenu zote zinasema hivyo na inawaajiri watanzania asilimia 65 halafu tunapokuja kwenye bajeti tunawatengea bilioni 300, haifiki hata bilioni 300 honestly watafanya nini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Maputo declaration na Malaba declaration inasema nchi zime-commit kuongeza asilimia 10 kwenye agriculture, hii haifiki hata percent moja, hata hii program tunayosema tunafuatilia hii program ya kuendeleza kilimo ya pili ili-commit bilioni 13 kwa ajili ya kilimo we are not even one percent kwa hiyo, lazima tuwe serious tunapozungumzia agriculture. Imeajiriwa watanzania 65 pato la Taifa kubwa namna hiyo halafu tunawekeza sijui kwenye masekta gani huko tuwe serious kwa kweli tunapozungumzia agriculture. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na Ilani yetu imesema vilevile Chama Cha Mapinduzi tunataka kutoa wakulima kwenye jembe la mkono na kwenda kwenye matrekta, yamekuja matrekta hapa ya Urususi hapa wakulima wangu Kiteto wamechukua karibu matrekta 100, halafu mnawapeleka kwa Wizara ya Viwanda is a confusion yanatakiwa matrekta haya yawepo kwenye Wizara ya Kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ili kwa sababu nyinyi mpo karibu na wakulima hawa halafu mnawaambia kwamba yale matrekta yale yalikuwa ya bei nafuu ni uongo mtupu, trekta bilioni 45, trekta milioni 55, sasa kuna unafuu gani hapo halafu mabovu kwanza, hebu tuwapatie wakulima matrekta haya wapate kuzalisha. Namshukuru sana waziri kwenye hotuba yako umewashukuru wakulima kwa sababu ni kweli, kilimo nchi hii ingekuwa wakulima wale hawalimi wala tusingekuwa na chakula. (Makofi)
SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Edward.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika baada ya hayo nashukuru naunga mkono hoja ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwasababu ya muda nitatoa tu hongera ya jumla hivi, mnielewe. Nitawapongeza baadaye. (Kicheko/ Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ukurasa wa 113 unasema hivi, naomba sana wataalam wetu waisome sana: “Kuimarisha mahusiano kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi.” Mahusiano ya wananchi na hifadhi ni mabovu sana. Hilo moja. Ilani inaendelea kusema hivi, ili Sekta hii iwe endelevu, lazima mjali haki na maslahi ya wananchi. Hamwangalii sana maslahi ya wananchi wakati mwingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasoma vitu vingi tu hapa, nilichogundua ni kwamba, kama walivyosema wasemaji wengine, utalii tangu tumepata uhuru mambo yote bado yapo kikoloni zaidi; ni boots and guns, fences, fines, mnaanza kuua watu, mnachukua ng’ombe wa watu; hiyo siyo sustainable. Mwache! Uhifadhi ili uwe endelevu, ni lazima ushirikishe wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeambia kwenye data hapa kwamba sasa tunaongelea asilimia 32 mpaka 40 ya nchi hii, iko kwenye hifadhi, it may not be enough, lakini lazima mfahamu tumeongezeka. Ni dhana ya kikoloni ambayo ni exclusion, expansion, removable, nature, then people later, haiwezi kuwa sustainable. Nchi nyingine zimeshabadilika, wameanzisha model ambazo zina-accommodate watu na uhifadhi. WMA ni classic example, inawezekana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo ya kukaa na kuanza ku-characterize ardhi za watu, eti corridor, eti buffer zone, eti wildlife or pastoral area, I mean! Mheshimiwa Waziri, kuna tangazo laki hapa nililisoma asubuhi hapa. Umewaelekeza watu wako wachaji ng’ombe 100,000 kwa kichwa cha ng’ombe. Miaka miwili iliyopita ilikuja sheria hapa ya kutaka kulishawishi Bunge lilete faini ya shilingi 100,000 kwa kichwa na Bunge lilikataa, hongereni sana. Sasa limeanza kurudi kwa mlango wa nyuma.
Mheshimiwa Waziri, this is illegal, haiendani na sheria zetu, nawe ni Mwanasheria, Wakili tena Dokta kabisa. Nakushauri sana, please rethink kuhusu hili, it is illegal, it is unlawful. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndiyo maana kuna wengine walikuwa wanasema hapa hatufuati sheria. Sheria haijasema hai-punish ng’ombe, inam-punish mwenye ng’ombe, ndiyo logic ya sheria. Sasa ninyi mkianza kuleta; na sheria iko hapa, haisemi hivyo. Fine kwa group minimum imetolewa na sheria na maximum. Kwa hiyo, mna-range pale. Hii idea ya kuleta sheria ya kichwa cha ng’ombe it is illegal, haipo! Kesho nataka nisikie hii inakuwa supported na sheria gani? Kama hamtasema, nitashika shilingi kwa mara ya kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuache. Nchi hii sasa tusipofikiria kuleta model zinazotuchanganya Pamoja, huu uhifadhi utafeli. Suala la mifugo, mimi nina mwananchi wangu Kijiji cha Warkyushi kuna pori linaitwa na Mkungunero. Pori la Mkungunero by GN liko Kondoa, Dodoma; lakini wanatuambia eti beacon ziko Kiteto, how? Kwanza kisheria ukishakuwa na GN ambayo ina-conflict na GPS points maana yake kisheria ni kwamba you can’t enforce, lakini wewe unakamata ng’ombe kila wakati. Mheshimiwa Hayati Rais Magufuli…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante.
MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Leo sauti yangu siyo nzuri sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kama walivyosema Wabunge wengine, kweli bajeti hii ni ya wananchi. Kwa hiyo, pongezi za kwanza ziende kwa Mheshimiwa Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan na za pili ziende kwa Waziri wa Fedha, mzee wa wananchi. Unajua timu ya wananchi lazima pia upende wananchi, si ndiyo bwana! Hongera sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza pia rafiki yangu Naibu Waziri. Hii timu imejipanga vizuri sana. Zaidi nampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge na Makamu Mwenyekiti na timu yote ya bajeti. Hii bajeti tunayoisifia bila shaka imepita kwenye mikono mingi sana kuanzia kwa Kamati ya Bunge, wataalam na timu nzima ya Wizara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu, mimi naichukulia Wizara ya Fedha kama ndiyo financiers, ni kama benki hivi. Kwa hiyo, lazima m-scrutinize miradi yote inayoletwa, halafu mwangalie ile ambayo ina tija. Wakati mwingine nikiangalia watafiti, ningefurahi sana kama Wizara hii ingekuwa na thinktanks wa nchi hii wote wawekwe kwenye Wizara ya Fedha. Kwa sababu kila kitu at the end kinakuja kwenu; ili kuangalia baadhi ya miradi mingine na kujua kwamba baada ya miaka mitano ijayo tutaweza kutekeleza ilani ambayo tumeinadi kwa Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ya pili, pesa hizi za Watendaji Kata, Maafisa Tarafa, zimefurahisha sana wananchi kule majimboni, big up! Hata hivyo wakati niko kwenye shughuli za mwenge, akaninong’oneza Mtendaji wa Kata, akaniambia, waambie watukumbuke na pikipiki pia na sisi kama walivyofanya kwa Maafisa Tarafa. Hii itasaidia sana. Ni ujumbe tunawapa. Vile vile kupunguza faini kwa boda boda imewafurahisha sana wananchi, big up! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja nyingine nataka niweke sawa hapa. Kuna Waheshimiwa Wabunge wamekuwa kila wakisimama hapa, wanasema walipa kodi ni milioni mbili na nusu mpaka milioni tatu kati ya milioni 60, is not true. Shilingi milioni 60 unajua ni pamoja na Watoto! Sasa is a bit unfair kusema walipa kodi ni milioni mbili au milioni tatu eti kwa milioni 60 ya Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, data zetu zinasema, watu asilimia 68 ya population ya nchi hii hawalipi kodi kwa sababu ni below age na wengine ni wastaafu. Kwa hiyo, wakati mnasema wanaolipa kodi, I think is good to be fair; tunaongelea watu kama milioni 20 hivi, lakini ni kweli kama ni watu milioni mbili au milioni tatu wanalipa, tujitahidi.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Olelekaita taarifa.
Mheshimiwa Esther matiko.
T A A R I F A
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpa taarifa mzungumzaji kwamba ni juzi tu tulipewa semina na wataalam na hata akipitia zile power point walisema wanaolipa kodi ni chini ya 5% of the population. Sasa population ina-include na watoto wadogo hata waliozaliwa leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpa tu hiyo taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Olelekaita.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa taarifa nyingine za kuambiwa na wewe unaangalia. Si ndiyo bwana! Kwa sababu na sisi ni wataalam, watoto hawawezi kulipa kodi, wale waliostaafu hawawezi kulipa kodi. Sasa mimi nasema, kwa wale Waheshimiwa Wabunge wanaosema asilimia ya watu wanaolipa kodi ni milioni mbili kati ya milioni 60, this is what I want to correct. Mimi sizungumzii ile 5% waliyosema hawalipi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu tena, hili Bunge tumeshazungumza hapa, tukasema hili Bunge baada ya miaka mitano, tunataka tujulikane kwamba ni Bunge la wakulima, wafugaji na wavuvi, kwa sababu asilimia 65 ya Watanzania wako huko. Mimi ninachoomba, kwa bajeti zijazo tujipange. Asilimia 10 ya mapato yetu tuwekeze kwenye kilimo. Natarajia huko mbele, tufanye hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine Ilani ya Chama cha Mapinduzi tunafurahi sana mmeongeza hela kwenye TARURA, big up! Nasi wengine tumeshafanya hata mikutano na tumeshakubaliana hiyo hela inaenda wapi? Kwa kweli tutasimamia ili hizi pesa zisipotee. Vile vile Ilani ya Chama cha Mapinduzi huko mbele huko tulishakubaliana, tukasema ukurasa wa 71 wa Ilani hii na naomba ninukuu: “kufanya mrejeo wa mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Barabara kati ya TANROAD na TARURA.” Ili tupate pesa nyingi kwa TARURA ni lazima tu-revisit hii formula ambayo tulikubaliana isiwe 30 kwa 70 tena, hapana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukubaliane kwa bajeti nyingine zijazo huko; na kwa kuwa ni commitment iko kwa kwenye ilani, tusema ni asilimia kama ni 50 kwa 50 ama 60 hata iende TARURA na TANROADS kwa sababu tulishakubaliana hivyo. Hii itaongeza chanzo kikubwa kwa barabara zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wamezungumza kuhusu tozo za utalii. Mheshimiwa Waziri, wenzetu jirani hapa baada ya Covid wao wametengeneza kitu kinaitwa Covid- 19 and Tourism in Kenya; Impact, Measures Taken, Recovery and Pathways. Yaani wanaangalia baada ya janga hili, tukakwama, kwa sababu ni kweli hii Covid-19 imepeleka hii sekta ya tourism down to its knees.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, walitakiwa – na ninyi sasa muangalie from that eye – na hiyo document nitakuletea, wataalam wetu waangalie ili na ninyi muweze kutengeneza a stimulus package, recovery package, ili huko mbeleni tuweze kunufaika. Kwa sababu ni kweli imepelekwa chini zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri mwingine; tumezungumza hapa sana kuhusu mambo ya umwagiliaji. Na tunajua ni kweli ardhi tunayo, mvua tunapata; tusipowekeza kwenye umwagiliaji hatutaweza kumkwamua mkulima. Tuwekeze.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu bajeti hizi, nilikuwa naangalia Wizara ya Mifugo kwa mujibu wa ilani wanatakiwa wajenge mabwawa karibu 95, lakini kwa sababu ya uchache wa bajeti yao, wamepewa mabwawa matano tu. Sasa kwa miaka mitano tukiendelea na trend hii, baada ya miaka mitano tutakuwa tumetengeneza mabwawa 20, na tuli-commit kama 400 hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wakati mwingine tunapotengeneza plans hizi tujaribu kuangalia. In fact, nilishasema wakati mwingine, na ninarudia, labda Wizara ya Fedha iangalie ilani hii projects zote zilizoko kwenye ilani, tufanye tathmini tujue in terms of figures, how much projects zote ambazo tumesema tutafanya baada ya miaka mitano tuzungumze in terms of money ili kila mwaka tujue kabisa tukipata bajeti hii ikaenda kwenye barabara tutaweza baada ya miaka mitano kufanya vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano nilikuwa naangalia hapa kilometa za barabara kwa miaka mitano ni karibu 8,000. Sasa tusipotengeneza bajeti ya kujibu hizi 8,000 kila baada ya mwaka mmoja, tutajikuta baada ya miaka mitano tutashindwa kufanya barabara zote ambazo tumekubaliana. Lakini tuki-cost ilani yetu vizuri itatuongoza, itatoa mwongozo mzuri sana huko mbele tunakokwenda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii ni kweli ni ya wananchi. Na hotuba ya mama Samia Suluhu Hassan mimi nawashauri sana Mawaziri muisome vizuri sana ile. Kuna miradi kabisa anataja anasema huu ndio moyo wangu – iko kwenye hotuba yake. Ni vizuri tujielekeze huko ili kiu ya mama yetu kwa Watanzania ikapate kupata suluhu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja nyingine fupi sana nataka nizungumze. Imejitokeza huko mbele kuna mkanganyiko fulani; Wizara ya Ardhi wanawapa kijiji hati, TAMISEMI wanatambua, lakini anakuja bingwa mwingine kule kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii anaanza kuwavuruga wananchi wale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, concept ya Serikali moja anayozungumza mama yetu; msipeleke confusion kule kwa wananchi. Ninyi mkutane humu, mnyongane wenyewe kule maofisini halafu muelewane kabla hamjaenda kwa wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo Zilizowasilishwa katika Mkutano wa Pili wa Bunge
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii na mimi niweze kuchangia kwenye hotuba hii ya Kamati ya Sheria Ndogo na kwanza kabisa niwapongeze Wajumbe wote wa Kamati ya Sheria Ndogo, wakiongozwa na Dkt. Wakili Msomi Mheshimiwa Rweikiza; Makamu Mwenyekiti rafiki yangu Wakili Msomi Ridhiwani Kikwete, Wakili Msomi Ramadhani, Wakili Msomi Edwin na Wajumbe wote wa Kamati hii, kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana na wamefanya kazi kubwa ambayo kama walivyosema kwenye taarifa yao, kazi ya kutunga sheria ni ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, lakini kwa mujibu wa Ibara ya 97(5) ya Katiba imelipa Bunge mamlaka ya kukasimu madaraka haya kwa mamlaka zingine ndogo zinazotunga sheria.
Mheshimiwa Spika, lakini ni vyema tukafahamu kwamba ikitokea dosari kwenye sheria ndogo, anayepata lawama ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo kazi inayofanywa na hii Kamati ya Sheria Ndogo ni kazi kubwa sana wanafanya kwa niaba yetu wote kwa hiyo niwapoongeze sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na nilikuwa nasoma taarifa yao wanasema mpaka Februari, 2021 sheria ndogo zilizofanyiwa kazi na kuletwa ripoti hapa ni karibu sheria ndogo 915. Ni kazi kubwa sana na wamechambua vizuri sana wakaonyesha dosari mbalimbali zilizoko kwenye sheria nyingi ndogo zinazotungwa na mamlaka hizi za chini. Kwa mfano kwenye ukurasa wa 14 wanasema kuna sheria zaidi ya 15 ilikuwa na shida ya uandishi na ni kweli uandishi wa sheria sio kazi ndogo sana legal drafting ni soma kabisa linafundishwa na watu wengine wanachukua degree zao, kwa hiyo, sio kazi ndogo sana.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ndio maana Bunge liendelee kufanya hiyo oversight, kuangalia sheria ndogo hizi, ili zisiwe na dosari ya aina yoyote. Lakini ukisoma pia taarifa yao wanasema kuna sheria zaidi ya 10 utekelezaji wake ni mgumu sana kwa jinsi ilivyotungwa na wakati mwingine zinaleta kero nyingi sana kwa wananchi, lakini nyingine hata kuna sheria ndogo baada ya wao kufanya uchambuzi, yanapingana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo sio zile sheria mama tu, lakini hata zinakwenda mpaka zinakinzana na sheria mama, which is very....
Mheshimiwa Spika, nashukuru na Kamati nimesikia kuna sheria ndogo ya Halmashauri ya Kiteto hapa ambaye inatoza watu shilingi 20,000 kwa kweli ni sheria imepitishwa Disemba hapa kwa mujibu wa GN hiyo, hata mimi Mbunge wa Kiteto bado sihifahamu hii sheria vizuri, lakini nitaangalia hii kwa ukaribu zaidi kwa sababu sasa sijui…
SPIKA: Yaani Mheshimiwa hiyo sheria ni kwamba sasa mmegeuza majando yale kuwa ni chanzo cha mapato ya Halmashauri; yaani ndio mantiki yake. Kwa hiyo sasa matokeo yake watu wanakuja kuweka majando Kongwa. (Kicheko)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika ahsante sana na jirani yangu unajua mimi na wewe vitu vingi tunashirikiana pamoja na wananchi wetu wa pande zote mbili wanafanya shughuli hizi, lakini lazima tuangalie ili isilete kero kwa wananchi kwa sababu inawezekana wale wanafanya shughuli hiyo labda wanatoza hela nyingi zaidi mpaka Halmashauri labda imefikiria labda ni chanzo cha mapato, lakini ni kweli nakubaliana na kamati tutaangalia vizuri sana ili isilete kero kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, lakini zipo sheria nyingi sana hapa mimi wakati nachangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ile kero ile ya kutoza ng’ombe shilingi 100,000 kwa kichwa, nilisema hapa inakinzana na Sheria ya Wanyamapori na nilishamwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwanza hawafahamu kuna ng’ombe unaweza kununua kwa shilingi 100,000. Sasa kama faini inaweza kutozwa kwa shilingi 100,000 sasa si afadhali nikuachie huyo ng’ombe mimi nikanunue mwingine huko sokoni.
Mheshimiwa Spika, lakini kwa kuwa inakinzana na sheria mama tusikubali kabisa madaraka ya Bunge hili na mamlaka hizi za chini zituletee kero za namna hiyo na kutufanya watu waichukie Serikali kumbe mtu mmoja tu ndio ametunga sheria hizo, lakini sheria nyingine ya shoroba au marafiki zangu wa wanyamapori ilitungwa sheria na Bunge wakaambiwa wakatunge regulation kwa ajili ya shoroba hizi.
Mheshimiwa Spika, lakini Bunge likasema muoneshe haki za wananchi kwenye sheria hiyo yaani ndio obligation ya kwanza wao wakaweka masharti kwamba hawaruhusiwi kufanya moja, mbili, tatu wakati interest ya Bunge ilikuwa ni kuona haki gani wananchi wanazo kwenye sheria hizi.
Mheshimiwa Spika, mijadala ya sheria ndogo hizi na naendelea kupongeza Kamati hii na muendelee kutufanyia hii kazi wananchi wengi wanaumia kwa sababu ya sheria hizi ndogo ndogo ambazo zinatungwa na mamlaka za chini bila kuangalia sheria mama ama Katiba ama na sheria nyingine za nchi.
Mheshimiwa Spika, nilikuwa naangalia hotuba hii na kama ulivyosema Sheria ya Tafsiri (The Interpretation Act) kifungu cha 36 kama alivyosema hapa inasema; “Subsidiary legislation shall not be inconsistent with the provisions of the written law under which it is made, or of any Act, and subsidiary legislation shall be void to the extent of any such inconsistency,” inapatikana kwenye sheria hiyo. Kwa hiyo, ni clear kwamba sheria ndogo hairuhusiwi hata kisheria tu infact haitakiwa iwe operational kama itakuwa inconsistency na sheria mama.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na huo ndio mchango wangu kwa leo, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria kwa hotuba yake nzuri sana, ametuwakilisha vizuri Kamati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ni siku ya Katiba na Sheria ndogo; ni Sheria tu leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya vitu ambavyo nachangia leo, naanza na suala la ajira na kazi kwa sababu liko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini ni jambo ambalo limekuwa na Changamoto nyingi sana. Vijana wetu wengi wako hapa wanahangaika wakitafuta ajira. Kila Mbunge hapa kila wakati analetewa majina, CV za vijana wengi wakitafuta kazi. Wakati interview zinafanyika, aidha nafasi ni 30 wanaletwa watu hapa 4000, 5000; si, sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi tumeona wameanza kubadilisha kidogo, sasa wameanza kugawa kwa zone, ili kuwaondolea vijana usumbufu kuhangaika k wenda sehemu moja wako 3000, 4000 halafu nafasi ni 50 tu. Kwa hiyo, ndilo jambo moja tu ambalo nilitaka nishauri Serikali mbadilishe na mje model ambayo itawasaidia kuwaondolea usumbufu vijana hawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila Mbunge hapa, ukisikia ajira zimetoka 10,000 hesabu za haraka haraka ni kwamba unachukua idadi ya majimbo unagawa ili walau kila Mbunge kwake kule aone vijana wake kadhaa wamepata ajira. Hilo ndilo tegemeo la kila Mbunge hapa na tunataka hivyo. Hatutaki tusikie ajira ziko 10,000 lakini ajira zinavyoenda unashangaa humuoni mtoto wa Kiteto ama kutoka jimbo lolote la Mbunge hapa; mnatugombanisha na wananchi. Kwa hiyo, tengenezeni model nzuri sana itakayotusaidia. Kama mnavyogawa poesa za miradi, kwa mfano kama ilivyokuwa UVIKO; mbona imewezekana na miradi imekwenda kila mahala. Tunataka kwenye ajira pia Mlete Model ambayo itatusaidia wote tuone kwamba tumejumuishwa na suala la ajira na Kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala jingine muanzishe, anzisheni mijadala; mnajua hatusemi hili ni la kwenu peke yenu, tuanzishe nijadala ya mara kwa mara ya namna ya kuboresha suala la ajira nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ni ofisi au idara inayoitwa ya Mpigachapa wa Serikali (Government printer); sijui wabunge wangapi wanafahamu hii Government printer; hata sisi Kamati yetu kwa mara ya kwanza tumefahamu jana zaidi baada ya kuja kutuonesha na tukaona; lakini kazi kubwa inayofanywa na idara hii ni kubwa zaidi. Inasimamia Nembo na Bendera ya Taifa inasimamia kuchapisha nyaraka za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mahakama na Bunge. Hata bendera tulizonazo; na mwaka jana hapa tulirumbanarumbana kidogo kujua ipi bendera sahihi ya Bunge; na siku hizi vipeperushi vingi sana vipo mtaani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ofisi hii haijawezeshwa ipasavyo Serikali imekuja na mkakati mzuri sana wa kuboresha ofisi hii ama idara ya Mpiga Chapa wa Serikali; ni Ofisi muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana kwa mfano walikuwa wanatuambia kwamba, kama wangeweza kupata pesa wangeweza kuchapisha nakala milioni sita ambayo ingeweza kupatia Serikali bilioni 20. Lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti sasa hivi wanapata nakala laki sita peke yake. Kwa hiyo ni muhimu wabunge wafahamu kwamba ofisi hii muhimu sana ya Serikali inayohifadhi nyaraka na alama za Taifa letu ni muhimu iwezeshwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) vilevile haipati pesa za kutosha ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Mimi nilipata nafasi ya kumtembelea DPP siku moja, nilishangaa sana, ofisi yake ni ya ajabu sana. Najua sasa hivi wanajenga ofisi yao; lakini ni vyema Serikali ikatenga pesa ili watu hawa wanaofanya kazi kubwa wapate kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni Law School of Tanzania. Law school of Tanzania; na mimi ni mwanafunzi wa Law School of Tanzania, first cohort. Ukisikia mambo yanayoendelea huko wakati mwingine unasoma vijana wale wanenda kufungua kesi; mahakamani ni dhahiri kwamba kuna jambo la kufanywa na Serikali. Kwa mfano ripoti ya Dkt. Mwakyembe muilete bungeni tuangalie, tu-interrogate ili na sisi tuweze kushauri namna bora; na Mheshimiwa wakili msomi, Mavunde tulikuwa cohort moja first cohort; lazima, hata wewe unajua unamawazo mazuri ya namna ya kuboresha hiyo zaidi ili vijana wetu wasisumbuliwe lakini tuwatengeneze Wanasheria wazuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na Kamati imesema hapa labda kuna haja ya kuanzisha ile entry exam. Lakini sheria ile iliyounda law school ni kama ilimlazimisha kila mtu kwenda Law School of Tanzania, ambayo si sawa. Waende wale ambao wanataka kuwa mawakili. Kwa hiyo kama kuna haja ya kufanya hivyo basi ni vizuri tuangalie mifumo ile. Na pengine baadhi ya courses, kwa mfano Mheshimiwa Mavunde wakati tunasoma accounting for lawyers; sawa ni important lakini kwa nini, but why do you examine me on accounting for lawyers inanisaidia nini? Halafu baadaye inanishushia tu grade zangu hainisaidii chochote. Kuna course nyingine ni muhimu lakini ukini-examine accounting for lawyers kweli? Na mengine mengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu lugha ya uandishi wa sheria; Bunge hili lilipitisha sheria hapa ya kusema tutumie Kiswahili, jambo ambalo ni jema sana; Watanzania wengi lazima wafuatilie, waweze kusoma sheria tunazotunga na waweze kuelewa kwa lugha hiyo. Hta hivyo kwa sababu Tanzania si kisiwa peke yake, ni vyema kama walivyoshauri Kamati, tupate sheria hizi zote kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili, Kwa sababu si kwamba sheria zetu tunazotunga zina Mahakamani peke yake bali pia zinatumika kufundisha wanafunzi; na wanafunzi wanatoka kila mahali duniani kuja kwenye Mahakama zetu na kwenye vyuo vyetu. Kwa hiyo ni muhimu sana ili tuondokane na mambo kama hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho nitazungumzia habari za Mahakama. Hii program mliyoanzisha Mahakama ya-integrated justice, ile Mahakama Jumuisho, ni program nzuri sana. Siku hizi mahakama zetu unatembelea mahakama utafikiri ni hoteli kabisa. Hata ukitembelea judiciary square hapa naambiwa ni jingo sijui la sita ama la kumi Southern of Sahara, ni nzuri sana, program ile ni nzuri sana. Lakini sasa tunataka haki zitoke kwenye majengo yale. Sisi hatutaki kwa sababu ni jengo refu tu, no, challenge sasa ni kwamba we want justice kutoka kwenye Mahakama hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imezungumzwa hapa na sheria ndogo; wakati mwingine Bunge linashauri kuhusu jinsi tunavyotafsiri sheria zetu. Hakuna kitu kibaya sana kama Serikali msipofahamu bunge lilimaanisha nini kwenye sheria hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala la mifugo, ina-touch hii Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na vifungu vinavyotumika kila wakati ni Kifungu cha 116 cha Sheria ya Wanyamapori kwenye ku-compound offenses. Kama juna eneo ambalo tunafanya hovyo kuliko yote ni kwenye compounding of offenses. Sheria, na Bunge lilisema hivi, Section 116, na ninaomba kunukuu; “This section shall apply to offenses committed under the Act in relation to protected areas, the director may compound an offense by requiring a person to pay a sum of money provided that such money shall not be less than two hundred thousand shillings and not exceeding ten million shillings”
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ndivyo Bunge lilivyosema; a person. Lakini wanakaa waswahili fulani tu kule wanaanza kuhesabu vichwa vya mifugo halafu wanasema lipa laki moja moja; that is not the intention of the law. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili likinyamazia vitu kama hivi; na si Bunge kabisa, ni mtu mmoja bingwa tu, alivyosema Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo hapa. Haya makosa yaliyogundulika takriban kanuni 31 zenye kasoro za kiuandishi zinakwenda kinyume na Katiba. Haya ni makosa tu yamegundulika kwa kusoma zile sheria, lakini wangekwenda field leo wakajua ni watu wangapi wameumia kwa sababu ya sheria hizo ni mbaya zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Sheria ya TANAPA Section 20A bado inazungumzia kwamba fine kama unataka ku-compound should not exceed one hundred thousand, should not exceed; lakini a person pays. Sasa, wakati Bunge linatunga sheria definition of livestock maana yake ni mbuzi kondoo nguruwe farasi kuku ndama hata mayai. Sasa laki moja leo ng’ombe ni wa laki moja na nusu ama laki moja halafu unataka kutoza fine ya shilingi laki moja utafanya Bunge hili lisiaminike hata kidogo. Lakini kumbe wala sio sisi, ni wale wanaosimamia sheria. Kwa hiyo Waheshimiwa Mawaziri muwe wakali sana. Bunge hili likisema na likishauri kanuni hii haifai ama hii compounded haifai ni vyema mkasimamia kwa nguvu zote ili Bunge liendelee kuheshimika…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante sana kengere ilishalia muda mrefu.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na ninaunga mko hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi, na nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria na Wajumbe wote wa Kamati kwa kazi kubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa sababu ya muda, niwapongeze Mawaziri wote ambao wanakuja kwenye Kamati yetu, wote, kuanzia Ofisi ya Waziri Mkuu, Chief Whip, Attorney General, Waziri wa Sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu mambo ya Ajira, Muungano – wote kwa ujumla wenu, kwa kazi kubwa ambazo kwa kweli mmefanya kwa utekelezaji wa kazi katika Wizara zenu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Katiba na Sheria kwa muda wa mwaka mmoja imeweza kufanikiwa kurekebisha sheria karibu 58, siyo kazi ndogo sana; utungwaji wa sheria siyo kazi ndogo sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwenye sheria hizo, kati ya sheria maarufu sana ambazo tumebadilisha ni kuruhusu Kiswahili kitumike kwenye mahakama zetu na kutafsiri sheria zetu ziende kwa Kiswahili. Kwa kweli kati ya sheria ambazo nazikumbuka na mabadiliko mazuri sana kwa Watanzania ni kuruhusu Kiswahili kianze kutumika ili watu waanze kufuatilia mashtaka kwenye kesi za mahakama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kinachonifurahisha zaidi ni kwamba Ilani ya Chama Cha Mapinduzi baada ya sisi kusema kwamba tubadilishe sasa sheria ziende kwa Kiswahili, Wizara ya Katiba na Sheria walitakiwa kwa mujibu wa ilani yetu wawe wametafsiri sheria 157. Lakini kwa kasi yao wamerekebisha na kutafsiri sheria 208; hongereni sana. kasi hii ikiendelea mtakipa Chama Cha Mapinduzi heshima kubwa sana kule. Kama ilivyo kwenye ilani, ukurasa wa 167. Na ninaomba ninukuu: -
“Kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sheria mbalimbali kwa kutafsiri sheria 157 kutoka Lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili”
Mheshimiwa Mwenyekiti, big up. Ninyi mmevuka lengo. Najua mna kazi kubwa sana, kwa sababu hata mnatakiwa kutafsiri subsidiary legislation na zile nyingine karibu 39,000; mtakuwa na kazi kubwa sana. kwa hiyo, naamini Wabunge watawaelewa wakati wa bajeti, mkileta bajeti hapa mpewe pesa nyingi muendelee kuchapa kazi kubwa zaidi. Kwa hiyo kwa miaka mitano ninyi mmeshaturahisishia kazi. Sheria zile principal zipo karibu 449, ninyi meshavuka kabisa; hongereni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Wizara ya Katiba na Sheria ilitakiwa, kwa mujibu wa Ilani yetu, kuboresha majengo ya mahakama. Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria tulipata nafasi ya kutembelea mikoa mbalimbali kuona miradi ya mahakama; tumeanzia Kongwa, tumekwenda Morogoro, tumekwenda Njombe, tumekwenda Dar es Salaam, tumekwenda Arusha na leo tumekwenda Dodoma kuona jengo kubwa la mahakama, Judiciary Square ambayo inasadikiwa litakuwa jengo bora kuliko Central and Southern Africa, na Waheshimiwa Wabunge tunawakaribisha. Wizara ya Sheria wanatuambia mwaka huu Desemba, watafungua hili jengo. Jengo zuri halijawahi kutokea; hongereni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mabadiliko mengine ambayo ni muhimu sana ni mabadiliko ya kuwaruhusu mawakili kwenda kwenda kwenye mahakama za mwanzo. Hii siyo tu inafungua fursa ya ajira lakini inawafanya wananchi wapate huduma za uwakilishi kwenye vijiji vyao; excellent.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kati ya sheria zilizobadilika ni kuweka break ile nolle prosequi na amicus curiae kwenye mambo ya sheria, itaongeza, na itapunguza mashtaka yale ambayo yanawasumbua wananchi sana. na vilevile kusema upelelezi ukamilike ndiyo tuendelee.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema hivi…
MWENYEKITI: Malizia sentensi ya mwisho Mheshimiwa Olekaita.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sentensi moja. Na kwa kuwa Wizara ya Katiba na Sheria mna kazi maalum ya kufanya, naomba niseme Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 29, alipokuwa akihutubia UN, na mimi nasema he for she; alisema yafuatayo: -
“Aware that being passionate about gender equality is not sufficient, my government is reviewing policy, legal framework in order to come up with actionable, measurable plans to ensure economic empowerment for women but also aspects pertaining to gender equality and gender parity.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, mlete sheria hizi tuzibadilishe. Nakushukuru sana, naunga mkono hoja asilimia 100; ahsante sana. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Kuongeza Mamlaka ya Mahakama ya Afrika Mashariki
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ili niweze kuchangia Itifaki hii ya kuongezea Mahakama ya Afrika ya Mashariki nguvu ya kisheria ya kuanza kusikiliza kesi za biashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Waziri wa Katiba na Sheria na Mheshimiwa Naibu Waziri na timu yao yote kwa kazi ambayo wamefanya. Kazi ambayo Bunge imepewa ifanye sasa ni kwa mujibu wa Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema hivi na naomba ninukuu:
“Kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake ni lazima inahitaji kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, tunafanya kazi ya kikatiba kabisa ya Bunge na niwapongeze Mawakili Wasomi wale ambao wameanza mjadala, Mheshimiwa Mwinyi ambaye kwa kweli hili ndiyo eneo lake la kujidai Afrika Mashariki na Mheshimiwa Zainab Katimba, Mheshimiwa Jerry Silaa na Wakili maarufu sana hapa Bungeni Mheshimiwa Thadayo. Kwa kweli sasa napata wakati mgumu kusema baada ya hao wote kusema. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Afrika Mashariki sisi kama Taifa, kwanza ni faida kubwa kwetu kwa sababu Makao Makuu ya Mahakama hii ya Afrika Mashariki ipo Arusha Tanzania. Kwa hiyo, tayari kwa wenzetu wale Mahakama hii kuwepo kwetu ni faida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama walivyosema wengine hizi Itifaki za Common Markets, Monitoring Union na Customs Union tayari zimeshapitishwa lakini kwa integration ambayo inaenda vizuri sana, mkishaanza kuingia kwenye Itifaki hizi za Common Markets, Customs Union na Monitoring Union ni lazima mtarajie kwamba disputes zitatokea na kwa mujibu Treaty hii ukisoma article 5 and 6 imeeleza kabisa misingi ya Treaty hii kwamba ni lazima tumekubaliana tusuluhishe migogoro yetu kwa namna ya kisheria nzuri na hakuna namna bora zaidi, zaidi ya kwenda Mahakamani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ili Wanachama wa Afrika Mashariki waweze kufurahia protocols hizi za Monitory, Customs Union na Common Market lazima kuwe na Mahakama ambayo likitokea jambo, yeyote kati ya wale anaweza kwenda Mahakamani na akapata haki yake. Kwa hiyo, ni muhimu kabisa na hata nje ya dunia wakitaka kuangalia kama integration yetu ni nzuri sana, wataangalia kama kuna mechanism kwamba jambo likitokea unaweza kwenda Mahakamani na ukapata redress. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii jurisdiction kwa kweli wamefanya kazi nzuri sana. Labda nimtoe wasiwasi dada yangu aliyekuwa anazungumza hapa, nilikuwa naangalia hii protocol yenyewe article 3 kwamba hainyang’anyi haki za Mahakama zetu kusuluhisha migogoro hii. Ukisoma hiyo article 3(2) inasema hivi naomba ninukuu: “The extension of jurisdiction under paragraph 1 shall not preclude the exercise of jurisdiction conferred upon other bodies by the Treaty or the relevant laws of the Partner States”.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hakuna confusion hapo. Hii ni option tu kwamba party anaweza kwenda Mahakama hii ya Afrika Mashariki kama ni jambo linalohusiana na mambo ya customs union, common market ama monitoring union. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ukisoma Treaty yenyewe imeeleza kabisa kwamba, mtu anaweza kwenda kwenye Mahakama zetu na akaomba Mahakama zetu zitoe tafsiri ya Treaty hii ya Afrika Mashariki. Kwa hiyo hakuna confusion. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nagusia alichosema Mheshimiwa Tadayo. Unajua wakati wa Supreme Court of Kenya wakati kesi hizi zinaendelea, kati ya messages nyingi tulizozipata tunaulizwa hivi huku kwetu tuna wanasheria wazuri kama wale ambao tulikuwa tunawaona kwenye TV? Jibu ni ndiyo. Kabisa! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, lakini ni kweli, lazima tujiandae kwa sababu Afrika Mashariki ni competitiveness. Ukishakuwa competitive ni lazima soko sasa litafunguka. Kwa hiyo, niwatoe wasiwasi tu, wako Wanasheria wazuri sana, hapa kwetu tu ni minus TV ndiyo maana hamuwaoni, lakini kesi zikiwa live mtawaona, tena wako wazuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, lakini ni kweli, tuendeshe elimu nzuri sana ili watu wetu wajiandae kabisa namna ya kushirikiana na wenzetu wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nguzo kuu ya Afrika Mashariki ni kitu kinaitwa widening and deepening of integration. Kwa hiyo, hii ni stage moja wapo ya sisi kuendelea ku-widen scope ya Afrika Mashariki na kui-deepen. Kwa hiyo, kila wakati kumbuka to widen and deepen the integration kwa sababu tuliamua. Hii ni uchumi na kwa kweli kwa nchi zote za Afrika Mashariki na sasa nchi nyingine zinaongezeka, ziko Saba sasa, nchi yetu iko strategically positioned kuwa mnufaika mkubwa sana wa integration ya Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Kamati imefanya kazi nzuri sana. Ninaomba tulishawishi Bunge hili likubali kupitisha Itifaki hii bila kuchelewa ili Mheshimiwa Waziri na timu yake wakaendelee kufanya kazi nzuri sana. Na sisi kwa kweli we are Leaders in the region, lazima tuoneshe leading role kwenye vitu kama hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya, nakushukuru. Ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii na kabla ya yote kabisa nimpongeze sana Mama yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa aliyofanya kwa mwaka mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru pia Makamu wa Rais, Dkt. Isdor Mpango na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kuendelea kumsaidia Rais wetu kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nimshukuru sana Waziri wa TAMISEMI na timu yake yote kwa hotuba nzuri sana. Nimshukuru vilevile jirani yangu hapa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Makamu wake na timu yote na Kamati yote ile kwa kuendelea kuwakilisha Bunge vizuri kusimamia TAMISEMI.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiteto peke yake kwa mwaka huu uliopita, tumepata miradi ya zaidi ya shilingi bilioni saba hongereni sana. Wananchi wa Kiteto wamepanga na wameniomba nije niwashukuru sana kwa miradi na heshima kubwa mliyoijengea Kiteto. Madarasa ya shule shikizi peke yake ni shilingi 1,140,000,000 tumejenga madarasa 57; madarasa ya sekondari madarasa 44, shilingi milioni 880; vituo vya afya bilioni moja, vituo viwili vya afya vya tarafa zile na sisi tumepanga, nimeongea Mkurugenzi wangu asubuhi hii. Sisi tutamaliza hiyo kazi tarehe 20 Mei, mwezi mmoja kabla ambao mmetuwekea na nakukaribisha sana Mheshimiwa Waziri ututembelee ili vituo vile vingine vitatu vya tarafa tulivyokubaliana, hapa tulishakubaliana tujenge kwenye tarafa zote, Tarafa ya Makame, Dosidosi na Kibaya. Kwa hiyo, sisi sasa tunawadai tatu tu na kwa kweli kwa speed tunayokwenda nayo na nakualika Mheshimiwa Waziri uje uone ili mtupatie hizo fedha zingine tumalize biashara ya Tarafa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumepata fedha shilingi 1,500,000,000 kwa TARURA tunawashukuru sana. Na namshukuru sana kumuona Engineer Seif hapa, nimualike atembelee Kiteto. Kiteto ni jimbo kubwa sana ni kubwa kuliko Mkoa wa Kilimanjaro na tuna Meneja pale mzuri sana, shida yetu ni gari. Terrain ya Kiteto, jiografia na umbali wake, kwa kweli mtuletee Landcruiser moja nzuri sana ili kazi hii iendelee kufanyika vizuri zaidi. Namualika vilevile Mkurugenzi Mkuu wa TARURA atembelee Kiteto, karibu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tumepata shule za sekondari mbili mpya shilingi 1,200,000,000 na kazi zinaendelea. Bado sasa na kama kata nne hivi hazina sekondari na kwa kuwa tulishapanga tujenge sekondari kwa kata zote; tukiendelea na kasi hii Kata za Makame, Leseri, Lolela na Ndiligish na uzuri Mwenyekiti wangu wa Halmashauri yupo hapa juu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, ninaushauri sana ambao nilishakuutoa siku nyingi kidogo; ipo miradi, miradi ya wananchi ambayo imejengwa na nguvu za wananchi na niitumie nafasi hii kuwapongeza sana wananchi Kiteto. Mheshimiwa Waziri nipo na karatasi hapa miradi zaidi ya 119 ipo kwenye stage mbalimbali ambazo zimejengwa na nguvu za wananchi. Wakati tunapata fedha za UVIKO-19 tulitamani zile fedha zingemalizia miradi ile iliyojengwa na wananchi, lakini kutokana na masharti ya fedha za UVIKO tulimuelewa sana aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI kwamba kwa sababu ya masharti tusingeweza kumalizia majengo yale. Lakini kwa kweli kwa juhudi hii iliyooneshwa na wananchi madarasa tu peke yake kwa mfano tu Kiteto tuna miradi 80 inaendelea kwenye vijiji 50 kati ya vijiji 63 vya Wilaya ya Kiteto. Lakini kwenye miradi ya shule shikizi bado tuna uhitaji wa madarasa 26. Lakini kwa zahanati 13 hizi nguvu za wananchi wa Kiteto kwa kweli zina-deserve Serikali iwaunge mkono, kwani tulishatoa ushauri Mheshimiwa Waziri I am sure kwa kweli m-consider hizi nguvu za wananchi ili wananchi waendelee kupata ari ya kuchangia miradi kwa kweli tutafarijika sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni la watumishi; ripoti ya CAG inaniambia Kiteto tuna upungufu wa watumishi 651. Sasa watumishi wakipungua kwa kweli ufanisi wa kazi utapungua nao zaidi. Kwa hiyo, naomba na ninafurahi sana kuona kwamba Waziri wa Utumishi ametoa ajira zile na ametoa breakdown kwamba walimu nafasi 12,000, afya 10,000, kilimo 814, mifugo 700, uvuvi 204, maji 261, sheria 53; tunachowaomba ajira hizi zinavyotoka mtumia formula mliyotumia wakati mnagawa fedha za Uviko, wote tupate. Heshima mliyowajengea Wabunge kwa fedha kwa hizi za UVIKO-19 mkifuata formula hii wallah nawaambia wale wanaotaka majimbo haya watapata taabu sana huko mbele kwa sababu mtakuwa mmewajengea heshima Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile maslahi ya watumishi, yakiangaliwa yanaongeza ufanisi zaidi. Na wameyazungumza Waheshimiwa Mabunge hapa kuhusu maslahi ya Madiwani kwa kweli Madiwani wetu wanafanya kazi nzuri zaidi. Tuwaangalie namna ya kuboresha maslahi yao. Lakini vilevile Wenyeviti wa Vijiji na Wenyeviti wa Mitaa wanafanya kazi kubwa sana tuwaangalie namna ya kuwasaidia ili kujenga ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini walikwisha kusema wengine hapa, tukiwapa uwezo, tukitengeneza zile semina za kuwajengea uwezo Madiwani na Wenyeviti, itaongeza ufanisi zaidi katika kusimamia miradi. Kwa hiyo, zile semina za kuongeza uwezo zitasaidia sana msiziache. Kwa kweli Madiwani wetu wangekuwa wanapata from time-to-time wapate semina kama hizo itaongeza ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni la TARURA; nawashukuru sana kwa kuongeza fedha kwa TARURA, lakini ni kweli Ilani ya Chama cha Mapinduzi tulishasema hivyo, tunataka tuongeze fedha nyingi zaidi najua mmeongeza fedha karibu bilioni 100 tena nawapongeza sana. Tunataka fedha za TARURA ziendelee kuwa nyingi zaidi ili barabara za vijijini na mijini zikapate kufunguka; barabara zitaongeza kasi ya uzalishaji. Kwa hiyo, kwa kweli endeleeni kuangalia TARURA kila wakati ikipatikana fedha muongeze fedha kwa ajili ya TARURA.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna majengo haya ya Halmashauri; Kiteto tuna jengo la Halmashauri ambalo sasa linaendelea kwa muda mrefu kidogo na kuna fedha karibu milioni kama 400 hivi bado; na mkandarasi anasema kwa kuwa malipo yamechukua muda mrefu kidogo tangu mwaka 2016 anaanza kufikiri kwamba zile fedha ni kidogo. Kwa hiyo, nawaombeni sana, hii miradi mkitoa fedha kwa utaratibu ili zisichelewe mtatuepusha sisi na matatizo ya huko ya kuanza kugombana na wakandarasi. Kwa hiyo, mkitugawia milioni 400 hiyo lile jengo tulimalizie kwa sababu mmeshatumia fedha nyingi sana na tunawashukuru sana. Kwa hiyo, nakukumbusha Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nyingine, kwenye ajira hizi hasa za walimu muangalie sana namna ya kuwajali walimu ambao wamekuwa wakijitolea kwa miaka mingi kidogo; hiyo iwe criteria kabisa namba moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vijana wetu ambao wamemaliza elimu zao na wakaona wasikae bure nyumbani waendelee kutusaidia wanafanya kazi kubwa sana. Mkiweka hiyo kama criteria wale wote ambao wana-volunteer na wanaendelea kutufundishia watoto wetu hiyo iwe criteria namba moja. Mheshimiwa Waziri usikubali kabisa kumuacha mwalimu ambaye ana record ya kuendelea ku-volunteer, mkifanya hivyo mtakuwa mmetenda kazi nzuri sana; na tuangalie wafanyakazi wetu wote wanao-volunteer kwenye sekta fulani fulani kila mtu anaye- volunteer nia yake ikitokea kanafasi basi apewe priority. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli baada ya kusema haya, mimi nakushukuru sana naunga mkono TAMISEMI mtakijengea heshima Chama cha Mapinduzi kwa sababu ukisoma ilani...
NAIBU SPIKA: Ahsante sana kwa mchango mzuri.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nakushukuru sana naunga mkono hoja ahsanteni sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. EDWARD K. OLELEKAITA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii na kama walivyosema wenzangu niwape pole sana Wabunge kwa msiba wa Mbunge mwenzetu Engineer Nditiye, tunamuombea Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa muda ni mdogo sana naomba nichangie hoja hii kwa kusema hivi Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020/2025 imetaja Kiswahili mara 39 namna tunavyotaka kutumia Kiswahili kwa mustakabali wa Taifa letu. Ukurasa wa 17, 130, 167, 168, 184, 185, 186, 244, 246, 247, 268, 286,287 na 288. Ukisoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi utaona Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alivyofafanua namna tunavyotaka kutumia Kiswahili, kwa Muswada huu utatusaidia kama Taifa kuanza kubadilisha sheria zetu kwa lugha ya Kiswahili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na nikinukuu tu kwa ruhusa yako ukurasa wa 167; “Kuongeza uwelewa wa wananchi kuhusu sheria mbalimbali kwa kutafsiri sheria 157 kutoka lugha kiingereza kwenda ya lugha ya Kiswahili.” Kwa hiyo, takwa hili la kubadilisha sheria kwenda Kiswahili ni kwa mujibu ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama walivyokwisha kutangulia wengine Kiswahili kwa Taifa letu inatambulisha Taifa, Kiswahili kimetumika katika ujenzi wa Taifa letu hata wakati tunatafuta uhuru Kiswahili kinaleta utamaduni wa Taifa letu. Kiswahili ni sawa sawa na uzalendo, ukombozi wa Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiswahili ni tunu ya Taifa letu. Kwa hiyo, tumpongeze sana Mheshimiwa Rais ni wakati sasa wa muafaka tuanze kuzungumza Kiswahili kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tafiti nyingi zinaonesha nchi nyingi sana Finland, Ireland, Bangladesh, Malaysia, Hong Kong, Hong Kong ilifika mahala wakaanza kuandamana nchi nzima wanakataa kiingereza kisitumike kwa sababu waliokuwa wengi Hong Kong wanazungumza chinese sasa sisi tumeanza hata hata kabla ya Watanzania hawajaanza kuandamana. Lakini sababu nyingine kimsingi sana ya kisheria ni haki ya mtu kufahamu lugha ya mashitaka kwa kiingereza wanaita due process, huwezi kumshitaki mtu ukaleta hati ya mashitaka kwa lugha ya kigeni, haelewei.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nyingine kuna kitu kinaitwa kwa kisheria uhalali wa lugha inayotumia (legitimacy) Watanzania wengi wanaongea Kiswahili kuendelea kuwa na sheria zilizoandikwa kwa lugha za kigeni ni kukosesha legitimacy sheria zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tukiwa na lugha ya Kiswahili kwenye sheria zetu, kwanza inajenga uelewa, vilevile inaleta watu kuheshimu sheria kwa sababu wanafahamu sheria kwa Kiswahili, wanafahamu lugha tuliyoandikia sheria. Lakini ukileta sheria zilizoandikwa kwa lugha za kigeni tutakuwa tunawasumbua Watanzania wasipo fuata sheria kwa sababu lugha hiyo imeandikwa ni ya kigeni. Kwa hiyo inaleta obedience, inaleta respect kama unaelewa lugha hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada ulio mbele ya Bunge umeandikwa kwa kiingereza na kanuni zetu zinachanganya by the way na hukumu zetu sasa kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati zimeshaanza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili, kwa hiyo mabadiliko ya sheria yatarahisisha sana kazi hii ya tafsiri ya sheria zetu ziende kwa lugha ya Kiswahili.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama walivyokwisha kusema wengine nchi zinazozungumza Kiswahili sasa ni Rwanda, Uganda, Burundi, South Sudan, sehemu ya Mawali, Somali, Zambia, Mzumbiji, DRC na Visiwa vya Comoro. Kwa hivyo Kiswahili tayari kina soko kubwa sana ni zaidi ya watu milioni mia mbili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 2) wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Nishukuru pia kwa kuwa mchangiaji wa kwanza kwa Muswada huu.
Mheshimiwa Spika, lakini kabla ya yote niwashukuru sana Wabunge kupitia ule Mfuko wa Faraja kwa support waliyonipa nilipompoteza mzee wangu. Tuendelee kumuombea alale mahali pema peponi.
Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Katiba na Sheria kwa umahiri mkubwa sana. Sisi ambao tunafanya kazi naye na Wajumbe wenzangu watakubaliana nami kwamba tuna-enjoy leadership yake nzuri sana. Vilevile niwapongeze Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria; nikupongeze, sijui ulitumia nini kuitengeneza timu hii ya Katiba na Sheria, tuna-enjoy sana, it’s a very good team, inaongozwa na Mawakili maarufu sana kama Senior Counsel Tadayo, ana miaka karibu 40 ya practice. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, vilevile niwapongeze wadau waliokuja kwenye Kamati ya Katiba na Sheria. Kwa kweli tulijifunza mambo mengi sana kwa wadau wale. Alikuja kijana mmoja mwanasheria kutoka Tangible Initiative anaitwa Kulwa William Mduhu, very young, very brilliant. Tulijifunza mambo mengi sana kupitia kwake na wadau wengine waliokuja kwenye Kamati yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hii inasisitiza tu kama tulivyosema kwenye ripoti ya Kamati kwamba Serikali ihakikishe kwamba inawashirikisha wadau katika marekebisho ya sheria mbalimbali. Tunajifunza mambo mengi sana kutoka kwa wadau. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna mambo mawili au matatu hivi niweke mkazo kwenye ripoti yetu. Nimpongeze Attorney General, Wizara ya Katiba na Sheria na CPD kwa kweli kwa ushirikiano mkubwa waliotoa wakati wa majadiliano kati ya Kamati na timu ya Serikali. Kama alivyosema Mwenyekiti wetu, kati ya vitu ambavyo tulizungumza ambapo kwa kweli msingi wake tulikuwa tunaufahamu, frustration wanayopata Makatibu Wakuu pale ambapo bodi hazipo na amendment iliyokuwa inaletwa ilikuwa ni kujaribu kuongeza muda ili kazi zisikwame lakini baada ya majadiliano tukasema na ni msingi tu wa kisheria kwamba hatuwezi kuongeza muda kwa sababu itakuwa ina-conflict sasa kazi za bodi zikiendelea kufanywa na mtu mmoja for an unlimited time. Kwa hiyo, baada ya mashauriano wakaamua ku-withdraw; that is excellent. Kwa hiyo, nawapongeza sana kwa kukubaliana na Kamati. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya Sheria ya Mawakili ni fursa nzuri sana kwa Mawakili kwa kuwaruhusu Mawakili kwenda kwenye Mahakama za Mwanzo. Mwaka 2016 Bunge lilileta mapendekezo ya kuongeza pecuniary jurisdiction ya property, kusema sasa kwenye Mahakama za Mwanzo unaongeza thamani ya kesi ambazo zinaweza zikasikilizwa na Mahakama za Mwanzo na fear ya mawakili that time ni kama sasa mnawanyang’anya kazi kwa sababu hela nyingi sasa zinakwenda Primary Court na Mawakili hawaruhusiwi kwenda. Kwa hili, I am sure Mawakili watakuwa excited kwamba sasa wanakwenda kwenye Primary Courts, zile kazi ambazo zilikuwa zimefungwa by restriction of law sasa watakwenda, that is excellent.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba tunaleta huduma karibu na wananchi ili wapate fursa ya kusikilizwa na kupata uwakilishi wa Wakili kwenye Primary Courts, mapendekezo haya vilevile yanazungumzia kutengenezwa kwa Bodi hizi za Mikoa zinazo-discipline advocates ili ku- protect society from advocates lakini vilevile ku-protect advocates kwa kuleta process ya kusikiliza zile kesi na malalamiko ya mawakili.
Mheshimiwa Spika, lakini wakili akiwa na cheti chake tukafikiri decision ya kusema sasa huyu wakili hafai na kwamba cheti anyang’anywe isifanywe na Kamati za Kimkoa kwa sababu kwanza composition ya Kamati zile na ile ya Kitaifa ni tofauti. Quality ya watu walioko kwenye National Committees ni Attorney General, DPP na ukiangalia sasa na composition ya wale wa mikoa ambao ni Registrars tusifanye kwamba ni rahisi sana hivi vyeti vikaondolewa kwa sababu watu wamehangaika na kwa kweli lazima viwe protected ziendelee kufanya kazi nyingine hizi za usuluhishi na mwisho wa siku wananchi wawe protected ile kuondoa cheti ibaki kwenye National Committee. Kwa hiyo, I think it is an excellent provision.
Mheshimiwa Spika, suala la nidhamu ni lazima kwa kweli liwe controlled. Hakuna profession ambayo watu wanaweza wakafanya watakalo. Kwa hiyo, kuwa na hizo Disciplinary Committees zitasaidia sana kuondoa malalamiko kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, baada ya marekebisho haya kuna mambo mengi yatabadilika. Nilikuwa naangalia Cheti cha Wakili kikishatengenezwa huwa kinaandikwa hivi na ninaomba ninukuu, kinasema kwamba: “Is an Advocate of the High Court and before the Court’s subordinate thereto save for Primary Courts”
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tumesema Mawakili watakwenda kwenye Primary Courts, Wizara sasa iweke regulations in place ili vyeti vya mawakili from next year iondokane na hilo sharti ili lisilete mapingamizi ya kisheria baada ya sheria hii kupita kwa sababu atakuja mtu ana certificate of practice lakini imeandikwa is an advocate of the High Court and Court’s subordinate thereto save for primary courts. Kwa hiyo, naomba suala hilo lishughulikiwe ili lisilete mkanganyiko wa kisheria.
Mheshimiwa Spika, Kamati imesisitiza kwamba wakati mwingine sheria inatoa mamlaka kwa mamlaka za chini kutengeneza regulations fulani fulani na sisi tukasisitiza kabisa kwamba wakati mwingine hizi mamlaka za chini zijue kabisa kwamba jukumu la kutunga sheria ni la Bunge, kwa hiyo, ziwe very careful kuangalia sheria mama ili wasilete lawama kwa Bunge.
Mheshimiwa Spika, nilikuwa naangalia pia Amendments ya Sheria ya The Land Disputes Courts ya kuruhusu sasa wale Wenyeviti wawe Public Servant na nilikuwa naongea na Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, kwamba Kiteto haina Mwenyekiti, akaniambia tatizo ni hili. Sasa baada ya amendments hizi, naamini Kiteto sasa na wilaya zingine itakuwa mandatory kuwa na hawa Wenyeviti.
Mheshimiwa Spika, nina kitu kidogo tu, siku hizi ukisoma sheria hiyo na inasema na hii sasa inapelekea sheria zetu, siku hizi kuna mjadala unaitwa making laws work for women and men ama gender sensitive legislation. Ukiangalia kifungu kile kinaendelea kusema Chairman, and so on, sasa isituletee mkanganyiko tukafikiri kwamba wanaostahili kuwa Wenyeviti ni wanaume peke yao. Kwa hiyo, hiyo ili tuangalie isije ikaleta nanii fulani hivi.
Mheshimiwa Spika, mabadiliko haya ya sheria yatawezesha mabadiliko makubwa sana na yataleta haki kwa wananchi na yatafanya wananchi wafurahie haki hizi ambazo zimeletwa na mabadiliko ya sheria.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (Toleo la Kiingereza)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Nimpongeze Waziri wa Fedha na Naibu wake na timu nzima kwa kuleta hotuba nzuri inayohusiana na The Finance Bill.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianzie kwenye Mabadiliko ya Sheria ya Kodi, section 23 ya Finance Bill ambayo watu wengine walikuwa wanazungumzia hii kodi hii ambayo ni two percent withheld kwa mazao yanayotokana na kilimo, mifugo na uvuvi. Nawapongeza Kamati ya Bajeti ambayo wameichambua sana na hata wao wameona. Kama alivyosema Mheshimiwa Waziri kwenye hotuba yake nia sio kumtoza mkulima ama mfugaji au mvuvi lakini sasa sheria haiko clear kum-protect mtu huyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu amendments zime-define a resident cooperation, pale anaponunua vitu kutoka kwa mtu anayeitwa a resident person. Sasa a resident person is not defined. Sasa isipoangaliwa vizuri inawezekana baadaye huyo resident person aka-include mkulima, mfugaji na mvuvi. Kwa hiyo, kwa jinsi mlivyo-define hiyo resident cooperation ni vizuri pia m-define a resident person huyu sasa ambaye anauza kama mlivyo-define vizuri kwamba resident cooperation hai-include SACCOS, AMCOS na vitu vingine. Nahofia tusije tukajikuta kwamba yule ambaye tulitaka kum-protect is not protected. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naangalia hotuba ya Mheshimiwa Waziri hapa, kuna paragraph ambayo is not clear kwenye hizi amendment na nia yake ilikuwa ni nzuri sana. Kuondoa sharti lile linalomlazimisha mlipa kodi ambaye anataka ku-object ile assessment la kulazimishwa kulipa one third kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 13 wa hotuba yake. Sasa ukiangalia sasa Sheria ya Kodi, section 51 ambayo ndio inaleta sharti hilo haipo kwenye amendment.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni vizuri pengine muangalie kama nia ilikuwa ni kuondoa sharti lile kwa sababu nilielezea vizuri sana siku ile, ukasema ni kweli mtu anaweza aka-inflate ile tax. For example, one third of 30 billion is too much. Kwa hiyo, ni kweli kama sharti ilikuwa ni ku-relax hii, basi muangalie section 51 kwa sababu ndiyo inayozungumzia masharti hayo na haiko kwenye amendment. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia pia kwenye Kamati na Schedule of Amendment iliyoletwa na Serikali, kulikuwa na wazo la kumfanya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ku-audit mashirika ambayo Serikali ina more than 50 percent share na inaonekana Kamati na Serikali wamekubaliana. Hata hivyo, ukiangalia ile Finance Act definition iliyokuwa inatolewa kwa public authority imekuwa extended Zaidi, imekuwa more broaden ku-include vitu vingi sio share peke yake, kuna vitu vingi sana vimeongezwa pale ambavyo actually ina-justify sasa kwamba hata anaweza aka-audit yale ambayo hata kama Serikali haina 50 percent share.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kuna haja ya kufanya re-alignment kuangalia exactly intention ilikuwa ni nini. Kwa sababu unavyo-broaden definition ya public authority ku-include vitu vingine beyond ile 50 share, maana yake unakaribisha sasa intention ya ku-audit hata zile nyingine. Kuna Mheshimiwa Mbunge alisema hata pale tunapoweka dhamana kwa miradi hii ambayo tuna ubia na watu wengine regardless ya share it is good iwe-audited na I think hii amendment ilikuwa inajaribu ku-cover more broadly vitu kama hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingine ambayo nilitaka kugusia kidogo ni TARURA. Kuna hili suala la TARURA ambapo tunawasifu sana na hata mlivyoweka kwenye amendment ya kifungu kile ni nzuri sana. My own concern ni moja, unajua tulishasema hivi tunahitaji fedha nyingi sasa ziende TARURA, kwa hiyo, hatulindi ile 100 peke yake mnayoongeza kwenye mafuta, tunataka pia ku-revisit ile formula ya TANROADS na TARURA ambayo imekuwa ni 30 percent na 70 percent ambayo tulisema it is unfair.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mbunge nilikuwa naongea naye akaniambia in fact kwa kuwa tuliwapa mzigo mkubwa sana TANROADS kwa sababu walikuwa na kazi ya kuunganisha mikoa mingi na hiyo kazi imepungua actually, imebaki tu sasa barabara ya Kiteto, Dodoma, Arusha, Tanga, Manyara na Kigoma na sehemu zingine chache sana. Kwa hiyo, it is high time na kwa kuwa Ilani yetu inazungumza kwamba tureje formula ile ya TANROADS na TARURA, hizi amendment tunavyoenda kuzifanya ni vizuri Mawaziri wale wakaja pia na formula sasa, sio tu ku-protect hii one hundred ambayo tunaweka kwenye mafuta lakini kuangalia sasa ile formula ya Mfuko wa TARURA na TANROADS ili Mfuko huu uwe na fedha nyingi zaidi ili barabara za vijijini ziendelee kuwa nyingi zaidi. Kwa hiyo, ni vizuri muangalie kwenye amendment hiyo ili fedha ziweze kupatikana zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho nimekiona kuna amendment ambayo nia I think ilikuwa ni njema, pale mnaposema mnataka ku-defer 12 months kabla ya ku-impose ile restriction ya yale makampuni kuwa na saver. Section 64 mnasema kwamba amendment inayohusiana na primary saver na sub-section (8) na (10) zinakuwa deferred zianze kufanya kazi 12 months later.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, huko mbele tena section 71 mnataka kuleta offence kwa mtu ambaye ata-fail ku-maintain ile primary saver. Sasa kama una-defer hizi sub-sections tatu maana yake ni kwamba hata hii section 71(m) ambayo ina-impose offence kwa yule ambaye ata-fail kuweka ile primary data saver lazima pia iwe deferred. Otherwise mtaleta confusion mna-defer section zinazo-put obligation kwa mtu kuwa na hiyo primary data lakini yule ambaye hatakuwa nayo unataka kum-punish even before 12 months ambayo ulitaka ku-defer. I think it is a drafting issue, ni issue tu ya ku-realign ili ikae vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache sana, nakubaliana na amendments hizi, I think nia ni njema sana na imekubaliana na mawazo mengi sana ya Wabunge. Nakushukuru sana. (Makofi)
THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO. 5) ACT, 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza kabisa nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati na Wajumbe wote. Pia nimshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, CPD na Wizara ya Sheria.
Mheshimiwa Spika, nitachangia mambo machache sana. La kwanza labda ni-clarify hii issue ya Kikatiba.
Mheshimiwa Spika, Ibara hii inayozungumzwa ya 147(4), mimi sijui hata kwa nini watu wanajadili kwa sababu, sisi tunazungumza habari ya majeshi. Ibara hii Waheshimiwa wanazungumza hapa ni definition ya mwanajeshi ambayo ni vitu viwili tofauti. Kwa hiyo, nadhani hii iishie hapa, lakini kwa wanaotaka kujifunza zaidi wasome Ibara ya 151, definition ya neno Askari, wataelewa zaidi likitumika kuhusiana na jeshi. Naomba ninukuu:
“…likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake ni pamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya jeshi hilo ni mtu anayewajibika kinidhamu.”
Mheshimiwa Spika, hizi ni terminologies. Unajua watu wasifikiri kila kitu kilichoko kwenye Katiba unaweza ukasema is unconstitutional na nitakupa tu mfano huko mbele ili Wanasheria waweke hii sawasawa. Huwezi kusema sheria hii is unconstitutional kwa sababu haina rangi ya Katiba, tunafahamu hii rangi ya Katiba, si ndio?
Mheshimiwa Spika, huwezi ukasema sheria hii is unconstitutional kwa sababu haina page numbers pamoja na kwamba, Katiba ina page numbers. Kwa hiyo, hili tumezungumza habari ya jeshi, sasa watuambie kama ile ibara inazungumzia jeshi ama mwanajeshi? Sasa sisi hatuzungumzi habari ya definition ya mwanajeshi, hatuzungumzi. Hilo moja.
Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Mwinyi pale, sasa naogopa kusema Wakili Msomi Mwinyi. Alichosema ni kwamba…
SPIKA: Unaruhusiwa Mheshimiwa.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, sawa, kumbe naruhusiwa, nashukuru.
SPIKA: Kabisa. Nimeshaelimishwa kwamba, ni wasomi. (Kicheko)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Ni kweli, unajua hizi ni lugha za Mawakili, ukim-address wakili mwenzako is a sign of respect, ilikuwa haina haja ya kusema kwamba, sisi tuna nanihii zaidi, ahsante.
Mheshimiwa Spika, kwa hivyo tulichokuwa tunakisema kifungu wanachosema Waheshimiwa Wabunge ni mfano tu kwamba, mwanajeshi atoke kwa makundi haya, kwa mfano tu, lakini kama nilivyosema haizungumzii majeshi inamzungumzia mtu mmoja. Definition ya mtu anayeitwa mwanajeshi.
Mheshimiwa Spika, wakati tunajadiliana kwenye Kamati tuliona suala alilokuwa analizungumzia Mheshimiwa Londo. Hata sisi tunachokisema kwa sababu, sheria hii ni kweli imeongeza hiyo forced marriage na imeongeza kitu kinaitwa forced begging ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili maana yake ni ndoa za lazima kwa maana ya forced marriage na kumlazimisha mtu kuishi kwa ombaomba.
Mheshimiwa Spika, maoni ya Kamati, tuliishauri Serikali ku-define baadaye haya maneno ili yasilete mkanganyiko wa tafsiri na sheria nyingine kwa sababu, tunajua jamii nyingi za Watanzania baadhi ya ndoa hizi bado ni arranged kati ya wazazi na lakini ikitafsiriwa vizuri tu baadaye kwenye kanuni haitaleta mkanganyiko huo. Kwa hiyo, hata sisi tuliona, lakini kwa kuwa hii sheria haiku-define basi maoni ya Kamati tumeomba Serikali baadaye iondoe huo mkanganyiko kwa sababu tunajua Sheria ya Ndoa inazungumzia aina ya ndoa hizo ambazo jamii zetu nyingi sana wakiwemo wa Kiteto kuna hiyo tafsiri ya ndoa.
Mheshimiwa Spika, pia tulikuwa tumeomba, huku kulazimishwa mtu kuwa ombaomba inaweza pia ikawa na tafsiri pana ya kisheria. Kwa hivyo, tuliomba pia, baadaye Serikali iweke kwa namna ambayo kwa sababu, unajua kimsingi mtoto akiwa mtaani leo ana wazazi, akikutwa na hali ile sasa ya ombaomba maana yake ni kwamba, wazazi wameshindwa kutimiza hiyo obligation. Sasa tukasema baadaye pia, Serikali ifafanue kwenye kanuni ili isiwe kila mtoto anayekutwa mtaani ionekane basi wazazi wake wana- fall kwenye hii trafficking, kwa sababu, wakati mwingine familia zetu ni tofauti tofauti, viwango vya hali ya kimaisha ya Watanzania wote haifanani. Kwa hivyo tulisema na Kamati iliona hilo na kuiomba Serikali kulifafanua kwenye regulations ili iondoe utata huo na kwa kuwa hii sheria hai-define haya maneno itawekwa vizuri sana kwenye kanuni.
Mheshimiwa Spika, kitu kingine tulichoona kwenye Kamati, ni kwamba, pengine bado kwenye sheria nyingi nyingi utakutana na hili neno department. Tumeona kwenye amendments zile bado inasema kwamba, pamoja na mabadiliko haya litaendelea kutumika neno hilo, kwa mujibu wa Kifungu kile cha 3 kwamba, nanii itaendelea kutumika kama idara.
Mheshimiwa Spika, inasema:
“The Department established under subsection (1) shall be a Force within the Ministry and in that capacity”.
Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, kwa kuwa sasa intention ni kufanya jeshi liwe independent. Kwa hiyo, kuna haja sasa kuangalia baadaye hizi sheria nyingine ili isitokee confusion ya word department na jeshi kwa sababu, department ni small unit. Bado lugha ile ya kizamani wakati bado ilikuwa ni department ndani ya jeshi ili iwe in order, usitokee tena mkanganyiko.
Mheshimiwa Spika, kwa hivyo tuliliona pia hilo kama Kamati, tukashauri kwamba, kwa kuwa, bado sheria nyingi including sheria hii ambayo inakuwa amended ya Police Force…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naungana na Kamati na naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2021
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Nami niungane na waliokupongeza kwa kura nyingi sana za kishindo. Hiyo ni ishara ya kutosha kabisa kwamba Bunge lina imani nawe, nami nafarijika kwa sababu ni Mwalimu wangu. Nakushukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Muswada wa Marekebisho wa Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2021, (The written Laws Miscellaneous Amendments (No. 7), 2021); kwa kweli kama kuna wakati tunawapokea wadau wanaotoa maoni yao wakishangilia mapendekezo yanayoletwa na sheria ni wakati tunapokea wadau wakitoa maoni kwenye sheria hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Jaji Dkt. Feleshi, ni mtu mwenye experience ya kuwa DPP, amekuwa kwenye bench na sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ni Mbunge, what an experience! Kwa kweli sisi Wajumbe wa Kamati tulinufaika sana. Kwa hiyo, nampongeza sana na tuna imani kubwa sana naye. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri wa Sheria, CPD na Watalaam wote. Kamati yetu ilinufaika sana wakati wa mjadala wa sheria hii. Kati ya mapendekezo yanayoletwa sheria hii, ni Ibara ya 22 inayoongeza Kifungu kinachozungumzia Sheria ya Mashtaka Kifungu Kidogo cha (2) kuleta kitu kinachoitwa amicus curiae.
Mheshimiwa Spika, amicus curiae, friend of the court ni practice nzuri sana. Kwa hiyo, kuletwa kwa mara ya kwanza sasa kwa Mahakama zetu kuanza kutumika kwenye kesi hizi za Jinai, kwa kweli ni progress kubwa sana ya sheria. Amicus curiae imekuwa inatumika wakati wa kesi hizi za Kikatiba zaidi, lakini sasa kuleta pia kwenye kesi za Jinai inaongeza ufanisi mkubwa zaidi. Kwa hiyo, ni innovation kubwa sana, nawapongeza sana.
Mheshimiwa Spika, kama alivyosema mzungumzaji aliyepita, kuna kitu kinaitwa nolle prosequi ambayo kwa kweli imewatesa Watanzania kwa muda mrefu sana. Mtanzania anakaa miaka saba, nane halafu anaachiwa halafu anakamatwa baada ya dakika mbili, halafu kesi inaanza upya, regardless miaka ambayo amekaa Mahakamani. Mapendekezo haya yanayoletwa na kifungu kidogo cha (3) itaweka break kidogo sasa ili madaraka haya yasitumike vibaya. Kwa hiyo, hii ni innovation kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama alivyokuwa anasema Mheshimiwa Rais wetu hapendi sana kesi zilizopo Mahakamani ambazo hazina ushahidi wa kutosha ziendelee kutesa Watanzania. Kwa hiyo, kwa kweli this is excellent! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, najua madaraka ya DPP yanakuwa regulated na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, article 59(b). Sheria msingi wake ilikuwa lazima iwe kwa nia njema ya kutenda haki, lakini nyingine ni kuzia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki, nyingine kubwa zaidi ni maslahi ya Umma. Kwa hiyo, yote yakiwa exercised kifungu hiki kitaleta mapinduzi makubwa sana kwenye criminal justice system. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna kifungu cha 131 (a) cha kukataa kesi zifunguliwe wakati upelelezi haujakamilika. Imekuwa ni wimbo kwa prosecution. Kila wakati wanaleta kesi halafu wanaimba kusema upelelezi bado haujakamilika na Mahakama inafungwa na wale wengine wanafungwa, hawawezi hata ku-control proceedings. Kwa Kifungu hiki sasa, kitalazimisha Ofisi ya Mwendesha Mashtaka na wale wapelelezi kufanya upelelezi, ndipo wafungue kesi Mahakamani. Kwa hiyo, kwa kweli it is brilliant innovation. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni Sheria ya Economic and Organized Crimes Control Act ambapo zamani ama kabla ya sheria ilivyo sasa na Mawakili wengi wanafahamu; mfano, kesi thamani yake ni shilingi milioni kumi au zaidi ya milioni kumi kidogo. Ili huyo mtu apate dhamana, unakwenda Mahakama Kuu kupeleka maombi madogo kwa ajili ya dhamana kwa sababu Mahakama za chini hazina mamlaka.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii ya kuongeza sasa thamani iwe ni shilingi 3,000,000/= kwa Mahakama za chini, itasaidia sana watu wasisumbuke. Kesi zikifunguliwa kwenye Mahakama za chini, chini ya shilingi milioni 300, generally ni 80% ya kesi zinazokwenda kwenye Mahakama zetu hizi. Kwa hiyo, dhamana zitakuwa zinatoka ili kuondokana na msongamano mkubwa wa kesi za Mahakamani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna Kifungu cha 39, Ibara ya 39 na 40 ambayo inapendekeza kuongeza kifungu kidogo cha
(6) na hii ni habari ya michezo, kwa Sheria hii inayoitwa The National Sports Council of Tanzania Act. Tunakumbuka Bunge hili lilipitisha The Finance Act na kusema 5% ya sports betting iende kwenye Mfuko wa Michezo, lakini isingewezekana sasa bila mabadiliko haya. Kwa sababu, mabadiliko haya yanaanzisha huo Mfuko sasa, ili pesa hizo ziende na kwa kweli, tufanye mapinduzi kwenye sekta ya michezo. Hii itawezesha hata tununue zile Video Assistant Referees, itaondoa malalamiko mengi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kesi ya jana tu ya Mbeya Kwanza, yale mabao mawili yale huku linakataliwa, haya yote yatakuwa solved kama tungekuwa na Video Assistant Referee. Itaondoa hizi mbeleko za kubebwabebwa. Kwa hivyo, hii kwa kweli itafanya tasnia ya michezo tuipende sana na tuendelee kushangilia bila pressure; bao mbili za jana zilikuwa zina changamoto kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naomba niwaombe Bunge liunge mkono. Kwa kweli, mapendekezo haya yataleta reform kubwa sana.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa, 2022
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi na mimi nitoe mawazo yangu kwa Muswada huu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 1 wa mwaka 2022.
Mheshimiwa Spika, kwanza, ninampongeza sana Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Katiba na Sheria kwa kuwasilisha vizuri sana mada hii. Vilevile niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria kwa michango mizuri, na walitoa mawazo mazuri sana wakati tunajadili Muswada huu.
Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Serikali vilevile wakati wa mijadala na Kamati, kwa kweli wamechukua mawazo karibu yote ambayo yalikuwa yanasemwa na Kamati, hili ni jambo jema sana. Ninawashukuru pia wale ambao tuliwaalika waje watoe maoni yao na walikuja Tanganyika Law Society na wengine wengi, tulibahatika kama Kamati, tulinufaika sana na michango yao.
Mheshimiwa Spika, kama walivyosema Wabunge wengine, Muswada huu umekuja wakati muafaka kabisa, tayari sheria tuliyokuwa nayo, The Management Act 2015, ilikuwa inaleta mkanganyiko mkubwa wa namna Serikali inavyojiandaa kukabiliana na maafa. Niwapongeze Serikali kwa kujaribu kufanya case studies nyingi. Wameangalia Sheria ya Afrika Kusini, sheria ya India na maeneo mengine kwa ajili ya kuboresha Pamoja na international standards by the way.
Mheshimiwa Spika, concept moja nzuri sana kwenye Muswada huu ni concept inaitwa Afya Moja (One Health Concept). Ni concept ambayo ni jumuishi, kwa kuwa majanga ni mambo ambayo ni complicated kidogo inagusa karibu kila mahali, walivyokuja na approach hii ya One Health Concept (Afya Moja) imesaidia Muswada huu kutengeneza a holistic approach kwenye namna ya kukabiliana na maafa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, taarifa ya Kamati yetu ya January/February 2022 kulikuwa na wazo la Bunge la kuiomba Serikali kwamba wakati wa kuleta Muswada huu wahakikishe kwamba Waheshimiwa Wabunge na wao wanakuwa sehemu ya hizi Kamati za maafa. Nafarijika sana kwamba Serikali imelisikia hili katika Ibara ya 11(2) utakuta uwakilishi. Tena tuliwaambia uwakilishi kwa ngazi za wilaya na mikoa, lakini wao walivyotengeneza ile structure kutoka Taifa wamewaweka Wabunge hata kwenye level ya Kitaifa, big up. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika Ibara ya 11(2), Ibara ya 13, Ibara ya 17 na Ibara ya 22 ya Muswada huu, kwa hiyo utaona kabisa kuanzia ngazi ya Taifa, mkoa, wilaya mpaka na Madiwani wapo. Kwa sababu wakati wa mijadala ilikuwa ni kitu cha ajabu kidogo kwamba, maafa yanatokea halafu kuna watu wanakaa kujadili halafu Mbunge ambaye ni Mwakilishi wa wananchi yuko nje. Akiulizwa na wananchi nini kinaendelea anasema tusubiri Kamati na vikao vitoke. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri, this is a very good initiative, itatufanya na sisi sasa tuanze kushiriki. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tena mmefanya vizuri kwa sababu mnajua kazi ya Bunge ni oversight, kwa hiyo hamjawaweka kwenye zile Kamati zinazofanya kazi, ni zile Kamati elekezi ili waweze kuendeleza lile jukumu lao la oversight. Big up. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna kitu kingine ambacho ni innovation nzuri sana, kuanzisha Mfuko huu wa Usimamizi wa Taifa, lakini kubwa kuliko yote ni kuruhusu sasa sheria iseme kwamba ni lazima Serikali itaweka pesa inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii ni initiative nzuri sana.
Mheshimiwa Spika, ukisoma Sheria ambayo sasa itafutwa baada ya Sheria hii kupita, ilikuwa inazungumza habari ya kutafuta hela za misaada, donations na vitu kama hivyo, lakini sasa ni jukumu la nchi kuweka sehemu ya bajeti yake kwenye Mfuko huu. Hii ni innovation nzuri sana. Unajua hata kabla hujaongea na wengine wanaokuchangia lakini umeshaweka commitment ya kwako ya fedha inayopitishwa na Bunge, nadhani ni initiative nzuri sana. Big up. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kimsingi hata nchi nyingine – tutaangalia baadaye – in fact wamefika mahali wana-dictate kuweka percent fulani ya National Budget. Hiyo ni stage ya juu sana lakini ninyi mmeanza vizuri kwa kuruhusu Bunge hili lipitishe bajeti ya kuweka pesa kwenye Mfuko huu.
Mheshimiwa Spika, Muswada huu vilevile kilichonifurahisha sana ni kwamba imetajwa Red Cross hapa. Red Cross kwa kweli Wabunge wengi hapa ni mashahidi – wamekwenda kila Jimbo. Kiteto, Manyara, kila mahali, kuweza kutambua mchango wa Red Cross nchi hii na kuwajumuisha kwenye Kamati hizi ni innovation nzuri sana. Tunawaomba tu muendelee kuwapa support nzuri wanayoihitaji ili waweze kusaidiana na Serikali katika jukumu hili.
Mheshimiwa Spika, ukisoma Muswada huu vilevile utakutana na volunteers (watu wanaojitolea), kwa sheria kuthamini na kutaja role ya volunteers vilevile ni kitu kizuri sana, ita-encourage watu waendelee kujitolea kwenye masuala haya ya majanga. Tunachoomba tu Serikali, pamoja na kwamba maafa ni jambo ambalo kuna Kamati nyingi na kuna watu wengi wanaohusika, sisi tunachoomba tu ni kuangalia suala la urasimu, isije ikawa ile complication ya watu wengi kuwepo ikaleta urasimu katika kufanya vikao na of course budget wise, isije ika-inflate budgets unnecessarily kwa sababu tunavutana kutafuta pesa kwa ajili ya majanga haya.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, nashukuru na ninaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)