Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge (25 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi hii. Awali ya yote, naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha na mimi kuwa Mbunge katika Bunge hili lako tukufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee kabisa, niwashukuru kwa unyenyekevu mkubwa kina mama wa Tanga kwa kuniamini na kunifanya kuwa mwakilishi wao. Nami nawaahidi sitawaangusha na Mwenyezi Mungu anisaidie.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchukua fursa hii pia kuwapongeza Mawaziri wote ambao wameanza kufanya kazi zao vizuri kabisa. Kipekee niwapongeze Mawaziri ambao wameshafika katika Mkoa wetu wa Tanga ili kuweza kutatua changamoto zetu wakiwemo Waziri wetu Mkuu, Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa na Naibu Waziri wa Maji ambaye amekuja kuwatua akina mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee kabisa, nimpongeze Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa hotuba nzuri ambayo ni mwendelezo na utekelezaji wa maono yake makubwa kwa taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 26 -28, Mheshimiwa Rais wetu amepanga kuimarisha miundombinu ili kukuza uchumi na sekta ya uzalishaji. Labda niseme kwamba Mheshimiwa Rais ana vipaumbele sahihi kwa maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nathibitisha hili kwa usemi ama kauli ya Rais wa 35 wa Marekani, Rais John Kennedy mwaka 1961 aliwahi kusema kwamba: “American economy is good because of its infracture and not infracture of America is good because of its economy”. Natafsiri kwamba uchumi wa Marekani ni mzuri kwa sababu ya miundombinu yake na siyo miundombinu ya Marekani ni mizuri kwa sababu ya uchumi wake. Kwa hiyo, yule aliyekuwa akidanganya wananchi kwamba vitu siyo maendeleo amuulize John Kennedy tangu mwaka 1961 alisema kwamba miundombinu ndiyo mpango mzima na Mheshimiwa Rais amechagua vipaumbele sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika suala la miundombinu, Mheshimiwa Rais amepanga kuendelea na upanuzi wa bandari zetu. Labda niseme kwamba bandari ya Tanga imekaa muda mrefu ikiaminika kwamba kuna mwamba usioweza kuvunjwavunjwa na kina chake kuongezwa. Kwa mapenzi makubwa ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameweza kutenga takribani shilingi bilioni 172 na bandari ya Tanga imeongezwa kina chake tayari imekaribisha meli kubwa zimeweza kutia nanga. Watu wa Tanga tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa hilo na tumempa kura nyingi za kishindo lakini tutaendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili maono yake yatimie katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spia, lakini katika suala la upanuzi wa bandari, naomba kuishauri Serikali. Kupanua bandari ni jambo moja muhimu na zuri kwa kuwa bandari ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu lakini ni lazima tujue kwa nini bandari zetu zinapoteza vina vyake.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hii ya kubanua bandari zetu imeligharimu taifa fedha nyingi sana. Mradi wa Tanga ni shilingi bilioni 172 lakini upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam unaligharimu taifa shilingi bilioni 336, lakini kuongeza kina bandari ya Dar es Salaam takribani shilingi bilioni 200 na zaidi zitatumika.

Kwa hiyo, nashauri Serikali kama kweli inaamini bandari ndiyo uti wa mgongo wa taifa hili, ni lazima tufanye study kujuwa ni kwa nini kina cha bandari zetu kinapungua. Tunayo mataifa wahisani, JICA na KOICA tushirikiane nao ili kuhahikisha tunafanya study ya kina kujua ni kwa nini vina vya bandari zetu vinapungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatekeleza miradi hii mikubwa lakini kiukweli hatuna wataalam wa Port and Coastal Engineering ambao watashirikiana na wahandisi washauri kuweza ku- implement miradi ile accordingly. Niiombe Serikali yetu pia kama kweli bandari ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu tuhakikishe tunawekeza kuhakikisha tunapata wataalam wa Port and Coastal Engineering kwa sababu watu wanaichukulia bahari kama ni kitu cha asili kwamba ni mgodi usiomalizika, this is very wrong concept.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma kidogo port and cost engineering university of Tokya…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili imeshangonga Mheshimiwa.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, kumekuwa na ongezeko la mabubu na viziwi kila mwaka, mwaka wa fedha 2018/2019 kulikuwa na mabubu na viziwi 6,103; mwaka 2019/2020 walikuwa 6967; mwaka 2020/2021 idadi ya mabubu na viziwi walikuwa 7246 na mwaka 2021/2022 walikuwa 8508. Ongezeko hilo kila mwaka lina based implication watoto hao wanapokuwa mashuleni Serikali inatoa ruzuku kwa chakula kwenye shule za vitengo maalum.

Mheshimiwa Spika, tuna shule 213 na vitengo 10 vinavyofundisha mabubu na viziwi. Serikali imetumia bilioni 3.4 kwa shule ya mabubu na viziwi mwaka wa fedha 2018/2019; mwaka 2019/2020 bilioni 3.9; mwaka 2020/2021 bilioni nne na mwaka wa fedha 2021/2022 bilioni 6.3.

Mheshimiwa Spika, gharama ya walimu wanaolipwa kuwafundisha wanafunzi hao, na hata uhitaji wa wataalamu wa kuzungumza kwa alama ni mzigo mkubwa kwa Taifa ambao tunaweza kuuepuka. Hata hivyo ustawi wa rasilimali watu unapungua na well being ya mtu husika inaharibika na familia nyingi zinataabika. Kwa kuwa gharama za matibabu na hata vifaa vya mabubu na viziwi ni gharama kubwa. Serikali imeshapeleka nje watoto wengi kupandikizwa vifaa vya usikivu. Gharama ni kubwa upasuaji na machine ni dola 35000. Serikali imesema katika hotuba ya Waziri kuwa wamepandikiza usikivu kwa watoto 14 hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa mara ya kwanza wakati wa awamu ya kwanza ya Waziri Ummy upasuaji umefanyika hapa nchini na bado Serikali haingalii chanzo cha yote hayo.

Mheshimiwa Spika, ushauri au mapendekezo yangu kwa Serikali; waweke audiometer katika Hospitali za Wilaya, audiometer ni kipimo cha kujua usikivu wa mtoto. Audiometer bei yake ni kati ya shilingi milioni sita had inane, na iwe ni lazima mtoto akizaliwa apimwe usikivu. Pia ABR iko muhimbili peke yake, Serikali iongeze ABR kwenye hospitali za rufaa nchini ili kubaini watoto wakiwa wadogo na kupunguza idadi ya mabubu na viziwi; matibabu hayo yaingizwe kwenye matibabu yanayohudumiwa na Bima ya Afya na pia Serikali iweke bei elekezi ya vifaa tiba kama hakuna sheria ya bei elekezi basi, Serikali ilete muswada, tutengeneze sheria.

Mheshimiwa Spika, Serikali iweke vitengo vya speech therapy kila hospitali ya rufaa na hospitali za Wilaya ili kuwasaidia watoto wa-develop speech, lakini watafute namna ya kuongeza wataalam wa speech therapy kwa sababu hawapo nchini na ni wachache mno. Watu wanapoteza usikivu kwenye migodi lakini vifaa ni ghali sana na hata wanaopata stroke wanahitaji mazoezi ya speech, vitengo vya speech na wataalamu waongezwe nchini.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2023.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote, niendelee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama mahali hapa kwa ajili ya kuchangia Muswada huu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Kamati, imefanya kazi nzuri na kubwa ya kuchambua Muswada huu. Vilevile naipongeza Serikali kwa dhamira yake nzuri na njema ya kuhakikisha manunuzi ya umma yanaleta thamani kwenye jamii na kuhakikisha miradi hiyo inadumu kwa muda unaotakiwa.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na Ibara ya 75 ya Matumizi ya Rasilimali za Ndani. Kama ambavyo Mheshimiwa Waziri ameelezea, kwamba lengo la kupitia upya sheria hii ni ili kuhakikisha changamoto zilizojitokeza zinakwenda kuboreshwa kwa kupitia sheria hiii mpya ya mwaka 2023.

Mheshimiwa Spika, moja ya kitu ambacho ninaona kabisa kitakwenda kukinza utekelezaji wa sheria hii ni pamoja na kutokufanya analysis ya kina kwenye miradi iliyojengwa kwa rasilimali za ndani kwa maana ya force account. Hiii ni changamoto kubwa ambayo inapoteza fedha nyingi za umma na analysis ya kina kabla ya kuja na sheria hii, haijafanyika.

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu gani? Kama kungekuwa kumefanyika tathmini ya kina kuona kiasi gani fedha za umma hazijatumika ipasavyo kwa kutumia force account, tusingeruhusu kwenye sheria hii kikomo cha thamani kuwekwa kwenye kanuni. Ilitakiwa sheria iende moja kwa moja izungumze kiwango cha fedha kitakachotumika kwenye force account.

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu, hata katika sheria iliyopita ilikuwa ni hivyo hivyo, lakini miradi mikubwa mingi imetekelezwa na force account. Naomba nitoe mfano hai. Hospitali ya Uhuru, Chamwino imejengwa kwa force account na mpaka leo hospitali ile mradi unashindwa kufungwa kwa sababu ya changamoto ambazo zimejitokeza. Ukienda kwenye jengo lile, pale reception tu ukifika unaweza ukaiona thamani ya fedha jinsi ilivyofinyangwa katika mradi ule. Yote ni kwa sababu tunaamua kuifinyanga Sheria hii ya Manunuzi ya Umma na kuamua kuweka vipengele vya thamani ya fedha ambavyo vitaweza kutajwa moja kwa moja kumpa mtu fulani mamlaka pekee ya kuweza kuainisha thamani ya fedha. Hii haitaweza kurudisha thamani ya fedha za umma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sipingi kabisa matumizi ya force account katika nchi yetu, lakini ni ukweli usiopingika, ni lazima tukubaliane na sheria ilivyoelekeza. Naomba niisome Ibara ya 75 sehemu ya pili inasema: “Matumizi ya rasilimali za ndani yatakuwa halali endapo kazi za ujenzi ni ndogo, zimetawanyika na zipo katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi kiasi kwamba makandarasi wenye sifa hawawezi kushiriki na kufanya kazi kwa bei nafuu.” Je, Uhuru Hospital, eneo lile halifikiki? Je, mradi ule ni mdogo? Ni wazi tuliamua kuifinyanga sheria.

Mheshimiwa Spika, vilevile imezungumza kwamba, “force account itatumika iwapo Taasisi Nunuzi ina wafanyakazi wenye sifa na vifaa vya kusimamia na kutekeleza kazi za ujenzi zinazohitajika.” Leo ni nani asiyefahamu kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa hakuna idadi ya waandisi wa kutosha? Hakuna mafundi mchundo wa kutosha? Ni nani hajui? Ni miradi mingi inatekelezwa kule kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kutumia force account. Tunaifinyanga sheria.

Mheshimiwa Spika, vile vile, sheria imezungumza wazi kwamba, “matengenezo au ujenzi iwe ni shughuli za kawaida za kila siku za taasisi nunuzi.” Angalia ukubwa wa Tawala za Mikoa, angalia ukubwa wa kazi za Serikali za Mitaa. TAMISEMI ina majukumu mengi makubwa, mazito kwa Taifa hili, lakini mnakwenda kuchanganya majukumu yale ambayo kiukweli yanakwenda kusababisha upotevu wa fedha za Serikali. Wataalamu hawapo, wakati huo huo majukumu ya TAMISEMI ni mengi, lakini bado mnakwenda kutumia nguvu nyingi kwenda kufanya vitu ambavyo vingeweza kufanywa na watu wengine.

Mheshimiwa Spika, vilevile inazungumza kwamba Ibara ya 75(2) kazi za ujenzi zinatakiwa kuelekezwa bila kuvuruga utekelezaji wa shughuli za taasisi zinazoendelea. Sisi ni mashahidi walimu wanaacha kufundisha, madaktari wanaacha kufanya kazi zao za kitaalamu walizoajiriwa nazo wanakwenda kufanya kazi za force account, wanakwenda kusimamia miradi. Hakika tunaifinyanga sheria hii. Ni lazima tutengeneze kwenye sheria hii ukomo wa wazi bila kumpa mamlaka mtu mwingine kwa kuhakikisha sheria hii inaenda kutekelezwa ipaswavyo.

Mheshimiwa Spika, naomba kusema kwamba changamoto kubwa ya force account ni pale ambapo yule local fundi amekabidhi kazi halafu kunatokea upungufu. Zile defects ambazo zinakwenda kurekebishwa, zinakwenda kurekebishwa kwa kwa liability ya nani, wakati wewe taasisi nunuzi ambaye ni Local Government umenunua material mwenyewe, umekwenda kusimamia kazi mwenyewe? Local fundi unambana vipi kwamba upungufu uliotokea unatokana na yeye? Huku ni kuleta contradiction na mambo haya yanapoteza fedha nyingi za umma.

Mheshimiwa Spika, vilevile changamoto nyingine kubwa ya force account ni quality assurance. Hakuna test zinazofanyika katika kudhibiti ubora. Kwa sababu inahitaji adequate supervision ya kutosha kwenye miradi ile. Lakini walimu wana kazi zao za kufundisha, madaktari wana kazi zao nyingine na wahandisi na mafundi mchundo ni wachache. Je, hizo test zinafanyika vipi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jamani naomba niwaambie, tunakokwenda Taifa hili litakosa wataalam makini wa kuweza kufanya kazi za ujenzi nchini. Kwa nini ninasema hivi? Ili mhandisi aweze ku-qualify vizuri ni lazima atoke chuoni, baada ya kupita kwenye practical industrial training, aende akakae na mkandarasi mwenye miradi mizuri kwa muda kadhaa ili awe competent. Ili asajiriwe kama Professional Engineer halafu ndiyo aende akatekeleze miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama miradi mikubwa inapelekwa kwenye force account, hakuna training kule. Hakuna chochote kinachoweza kufanyika kumjenga mhandisi graduate aliyetoka shuleni. Tunalipeleka wapi Taifa hili katika taaluma hii ya uhandisi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuache kufanya mzaha katika mambo ya msingi. Lazima kuna bodi iliyopewa mamlaka. Iliyotengenezwa kwa ajili ya wakandarasi nchini. Bodi ile ina sajiri, inaajiri na inatumia fedha za umma lakini wakati huo mnazuia private sector ku-excel. Kwa sababu ya kutokuwa na imani katika ubora wa kazi nyingine ambazo zinafanyika.

Mheshimiwa Spika, kuna watu wanaamini kwamba, miradi inayofanywa na wakandarasi ina gharama kubwa zaidi kuliko force account. Sasa tafiti zilizofanywa na Baraza la Ujenzi Tanzania (National Construction Council) wakishirikiana na Bodi ya Uhandisi, Bodi ya Quantity Surveyor na Architect na Bodi ya Wakandarasi nchini; inaonyesha kwamba miradi mingi iliyotekelezwa kwa force account imeshindwa kumalizika kwa wakati kwa sababu ya upungufu wa fedha. Makadirio yaliyofanyika hayakukidhi haja ya mradi. Kwa hiyo, miradi mingi imeshindwa kufungika kwa wakati. Hiyo ni kwa mujibu wa tafiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tukubaliane, hii Ibara ya 75 inazungumzia suala zima la size ya mradi. Kwamba mradi ukiwa mdogo, ni wapi imekuwa well defined kwamba mradi mdogo ni wa size ipi? Yaani unaposema huu mradi ni mdogo au mradi huu ni mkubwa, ni kitu gani kinaelezea ukubwa wa mradi au udogo wa mradi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mradi unaweza ukawa mdogo lakini ile complexity nature ya mradi wenyewe, ukasababisha usifanywe under force account. Kwa hiyo, tunaposema size ya mradi ni lazima tu-clarify well, tu-evaluate well size ya mradi huu. Otherwise, tunaendelea kufinyanga fedha za Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, ni muda mrefu ninasikitika, nchi hii tumewahi kupita kwenye kufanya kazi kwa force account lakini baadaye analysis zikafanyika, zikaonekana tutoke huko tufanye under contract basis. Ajabu tumerudi tena kupoteza fedha nyingi za umma kwenye miradi isiyokamilika kwa wakatim kwenye miradi isiyofikia viwango vinanyofanyika hali inaumiza, inasikitisha.. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hakika sheria hii ikatekelezwe ipasavyo na size ya mradi inayotumika kwenye force account iwekwe wazi kwenye sheria hii. Asipewe mtu mamlaka ya kwenda kutengeneza kanuni ili kuhakikisha tunakwenda kutumia fedha za umma kama ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naona unaniangalia. Ninakushukuru. Ninaomba niunge mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Mpango wa Miaka Mitatu wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sote tunafahamu kwamba Serikali yetu imewekeza kwa kiwango kikubwa katika upanuzi wa bandari zetu. Nafikiri ni maono makubwa pia ya Rais wetu kuboresha bandari zetu kwa sababu amepanua barabara ya Morogoro lakini pia amejenga na reli, yote haya ni ili kuleta ufanisi katika biashara ya bandari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba Serikali iweke mpango kuhakikisha ina-enforce law ili basi ile slow moving traffic katika barabara ya Morogoro na fast moving traffic zisiweze kuchanganyika pamoja ili intended use ya zile fly overs ambazo zimetengenezwa ziweze kuleta maana katika Taifa letu. Ndugu zetu wanaotumia maguta, mikokoteni ni muhimu kwa Taifa letu pia lakini haileti mantiki tuweze kutengeneza fly over ili fast moving traffic zikimbie halafu unavuka unashuka chini unakutana na guta na mkokoteni. Naomba sheria na taratibu nzuri ziwekwe ili kuhakikisha kwamba watumiaji hawa wanatafuta namna ya kufikisha mizigo yao sokoni Kariakoo lakini sio kwa kutumia barabara ile iliyopanuliwa na inayotaka mgari yaende haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie pia kwenye suala zima la parking lots. Serikali imekuwa ikikusanya mapato kwa maana ya parking fees katika mitaa yetu wakati zile barabara zimetengenezwa kwa upana ule kwa sababu maalum. Leo sehemu ya barabara inatumika kama parking lots, hii inakwenda kinyume na matumizi halisi ya barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikali iweke mpango na kwa kuwa sasa tunakwenda kuwa na adequate public transport, tunazo DART lakini tutakuwa na treni za mjini, Serikali iweke Mpango wa kutengenza parking kule ambapo DART inaanzia ili mtu anapotoka nyumbani kwake aweze ku-park gari yake sehemu salama na aingie katikati ya Majiji yetu bila ku-congest majiji yetu kuliko kutumia maeneo ya barabara. Hii inakwenda against na mipango halisi ya ku-design barabara zile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba kuchangia maana halisi ya DART (Dar es Salaam Rapid Transit) au DORT (Dodoma Rapid Transit), mana halisi ni kuhakikisha kwamba katika kila kituo chetu cha mwendokasi kunakuwa na schedule ya kupita kwa magari yale. Kwa maana kwamba labda gari ya kwanza itaanza saa 11, nyingine itakuwa saa 11:10 ndiyo maana ya Rapid Transit. Kama hatuwezi kuweka hizo schedule zikafahamika Rapid Transit hazitakuwa na maana, zitakuwa sawasawa na daladala zetu tu, hamna tofauti. Kwa hiyo, niiombe Serikali iweke Mpango wa kuhakikisha kwamba hizi tunazoziita Rapid Transit zinafika kwenye kituo kwa interval ambazo zitakuwa known kwa wananchi ili nao waweze kutoka katika nyumba zao na waweze kutumia usafiri bila kukaa muda mrefu katika vituo vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imepanua bandari zetu na imepanua pia bandari ya Tanga lakini kiukweli TRA wanachangia kuhakikisha bandari ambazo ziko nje ya Dar es Salaam hazipati wateja kwa sababu tax clearance inachelewa. Dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu ni Mbunge wa Tanga Mjini amekuwa aki-hustle kutafuta wateja watumie Bandari ya Tanga baada ya kuwa imeshaongezwa kina chake lakini unfortunately wateja wanakimbilia Bandari ya Dar es Salaam kwa sababu tax clearance inachelewa bandari za mikoani.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Kengele imeshagonga Mheshimiwa, ahsante sana.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi hii ya kuchangia Mpango wa Tatu wa Maendeleo kwa Miaka Mitano wa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, leo nitachangia vitu vikubwa viwili, na kwa kuanzia nitaanza na suala zima la monitoring and evaluation yaani ufuatiliaji na tathmini. Nimejaribu kusoma Mpango wa Tatu wa Maendeleo, umeeleza vizuri sana kwamba Mpango wa Pili wa Maendeleo haukutekelezwa ipasavyo. Na miongoni mwa sababu kuu ni kwa sababu hakukuweko na mpango Madhubuti wa ufuatiliaji na tathmini. Na imeelezwa pia mpango wa pili ulichelewa kuanza, umeanza miaka miwili baadaye.

Mheshimiwa Spika, lakini Mpango wa Tatu pia umeeleza kwamba idara mbalimbali za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zilitengeneza namna zao zenyewe za kufanya tathmini na ufuatiliaji bila kufuata mipango yetu mizuri iende kufanya kazi na kuleta matunda tarajiwa. Ni lazima tujipange vizuri katika ufuatiliaji na tathmini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia nchi zetu za jirani, South Africa ina taasisi maalum ya tathmini na ufuatiliaji ndani ya Ofisi ya Rais. Na ukiangalia Uganda, wana taasisi maalum ya ufuatiliaji ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Ukiangalia Ghana ina Wizara maalum ya ufuatiliaji.

Mheshimiwa Spika, lakini Tanzania tathmini na ufuatiliaji umepewa vi-sub sectors katika Wizara sita tofauti; Wizara ya Fedha imo, Ofisi ya Waziri Mkuu imo, TAMISEMI imo, Utumishi imo, National Audit imo na NBS. Wote wanafanya ufuatiliaji na tathmini bila kuwa na heading entity. Nani ana- lead evaluation and monitoring katika Tanzania yetu; hayupo. Naomba niishauri Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, ilibebe suala zima la ufuatiliaji na tathmini ili tuweze kupata matunda tarajiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kaka yangu, Mheshimiwa Reuben juzi alizungumza suala zima la kuwepo na Sheria ya Ufuatiliaji na Tathmini. Naungana naye mkono asilimia 200. Lakini vilevile ni lazima tuanze na sera nzuri zenye miongozo ya kuhakikisha ufuatiliaji na tathmini inafanyika katika mikakati yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala zima la kuwa na sera na sheria litatusaidia sana kuhakikisha miradi yetu inakwenda kusimamiwa ipasavyo, lakini pia itazuia kukubali mifumo holela ya mataifa yanayotupa udhamini. Kila anayetupa udhamini anakuja na mfumo wake wa tathmini. Sisi kama nchi hatuwezi kukubali kupokea mifumo holela kwasababu tu tunapewa pesa, ni lazima tuwe na taasisi imara ambayo itasimamia ufuatiliaji na tathmini na siyo ku-accept kila mfumo kutoka nchi za nje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba Nchini kwetu Tanzania tunafanya vizuri mno katika suala zima la monitoring, lakini tathmini za kina hazifanyiki. Mara nyingi tunafanya vikao vingi, tunaandika ripoti nyingi lakini tathmini za kina hazipo. Kwa hiyo, ni lazima tukubali kutengeneza taasisi imara ambayo itasimamia na kubuni mifumo sahihi ya ufuatiliaji na tathmini. Bila namna hiyo, bila kufanya hivyo hatuwezi kutoka. Na ndiyo ule utelezi aliousema dada yangu, Mheshimiwa Jesca. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia suala la ushirikishwaji wa wanawake katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa letu. Naomba ku-refer Mheshimiwa Rais wetu, mama Samia Suluhu alipokuwa anazungumza na Naibu Waziri wa Michezo alipomwambia kwamba wanawake nao wakanufaike na vipaji vyao katika Sekta ile ya Michezo. Ilinisababisha kufikiri kwamba kumbe mpaka leo bado katika Taifa letu kuna idara ambazo sera zake sio gender inclusive, maana yake ilikuwa hivyo.

Mheshimiwa Spika, bado katika taifa letu kuna idara ambazo sera zake sio gender inclusive, this is maana yake lilikuwa hivyo, lakini ukikumbuka Mkukuta ulishaweka wazi ikielekeza wizara zote kwamba zikawe na sera ambazo zina- include ushirikishwaji wa wanawake. Sasa kama mpaka leo hazipo maana yake ni nini? Wawawake wanakuwa wakiweka pembeni katika mpango wa …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Aisha, Ahsante sana; Mheshimiwa Tumaini.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika,ahsante, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi hii ya kuchangia katika Wizara hii ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano). Awali ya yote nichukuwe fursa hii kuwapongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati husika. Naomba nichangie kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuna suala zima disaster preparedness. Tumesikia sasa hivi kwenye mitandao wakizungumzia suala nzima la Cyclone ya Jobo, lakini hii inatokana na sawa sawa na yaliyosemwa kwenye ripoti ya Intergovernmental Panel on Climate to Change (IPCC) ambayo inazungumza suala zima la ongezeko la joto pamoja na ambazo zinaleta mvua nyingi, lakini imekuwa ni Mamlaka ya Hali ya Hewa peke yake inayoonekana inashikilia kidedea suala hili.

Mheshimiwa Spika, upande huu wa athari za mazingira zinazotokana na mvua nyingi na kupelekea mafuriko, upande huu wa Wizara hii ya Mazingira haitoi ushirikiano wa bega kwa bega na hali ya hewa kuhakikisha kwamba wananchi wanaandaliwa kwa hali kama hizi za mabadiliko ya hali ya nchi ili kuendelea kuishi salama hasa wananchi wanaoishi pembezoni mwa Bahari za Hindi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo hili ni la muhimu sana kwa sababu imeshatokea, maeneo ya karibu na bahari yanamomonyoka. Kwa mfano, Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere pale Kigamboni, ilitokea ndani ya Dar es Salaam Road mpaka kile chuo kikataka kuezuliwa. Kwa hiyo, suala hili ni muhimu kabisa, kuandaa wananchi waishio pembezoni mwa bahari ili kuweza kujikinga na vimbunga hivyo vinavyoweza kutokea.

Mheshimiwa Spika, naomba pia kuchangia kuhusiana na kumomonyoka kwa Kisiwa cha Toten kilichopo Mkoani Tanga. Tanga tumebarikiwa, tuna kisiwa kizuri na Mamlaka ya Bandari wanakitumia kisiwa kile, wametengeneza mnara unaoongoza meli unaoitwa mnara wa Ulenge juu ya kisiwa kile, lakini kisiwa kile kina erode na hakuna measures zozote ambazo zinachukuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naiomba Sekta ya Mazingira ikashirikiane na Mamlaka ya Bandari itengeneze shoreline protections kwenye bahari zetu ili kuendelea kuvikinga visiwa vyetu pamoja na maeneo yaliyoko kwenye mwambao wa bahari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba pia nichangie kuhusiana na suala nzima la asbestos. NEMC walishaweka hii sheria ya kwamba asbestos ni harmful kwa maisha ya binadamu, lakini mpaka sasa yapo majengo mengi ambayo yameezekwa na asbestos na hata kwenye mabomba, underground utilities zipo ambazo ni za asbestos. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali ifanye survey ya kutosha ili kuweza kubaini majengo yote ambayo mpaka sasa yameezekwa na asbestos na itoe tamko rasmi kwa wanaoyamiliki ili kuweza kuezuliwa na kuangamiza asbestos zote nchini ili tuendelee kuishi tukiwa na afya njema. Ma-technician wetu, wahandisi wetu, wanakwenda kufanya kazi katika mazingira ambayo asbestos bado zipo. Ni hatari sana kwa afya zao. Naomba sana Waziri na Serikali ichukuwe hatua muhimu kwa ajili ya jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, naomba kuishauri sana Wizara ya Mazingira katika suala zima la ukataji miti ovyo. Tutafute njia mbadala ya kutengeneza mkaa. Zipo research nyingi ambazo zinaonyesha tunaweza kutumia sold waste kutengeneza mkaa, kama briquette. Hizi sold waste zitakapoondolewa kwenye miji yetu, maana yake bado Sekta ya Mazingira inanufaika kwa miji yetu kuwa misafi na salama, lakini wakati huo huo tunapata energy mbadala ya kuzalisha moto badala ya kukata miti ovyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia umuhimu wa sisi kutengeneza mkaa kwa kutumia sold waste, itawapelekea wanaweke wetu wa vijijini waendelee kupika hali ya kuwa wako watanashati kwa sababu kuni zinawafanya wawe wachafu kutokana na moto. Kwa hiyo, naomba sana tufike wakati tutengeneze mkaa kutokana na takataka tunazozizalisha katika majumba yetu.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunisimamia na kuniongoza mpaka kufikia hapa nilipo. Naomba kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayofanya katika ujenzi wa miundombinu ya nchi yetu na kipekee kabisa nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa uwasilishaji mzuri wa Makadirio ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha unaokuja wa 2021/ 2022. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia suala nzima la ndege. Serikali imefanya kazi nzuri ambayo siyo ya kubezwa kwa kununua ndege nane nzuri kabisa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu. Katika mwaka wa fedha unaokuja, tumetenga shilingi bilioni 450 kwa ajili ya kununua ndege nyingine tatu, lakini vile vile, kwa ajili ya kuboresha karakana zetu za viwanja vya ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana Serikali iweke msisitizo katika karakana zetu ndege ni karakana hii bilioni 450 iliyotengwa kwa hakika naona haitoshi kwenda kununua ndege tatu, kumalizia deni la Airbus na vilevile, kufanya karakana zetu za ndege. Naona kama ni kizungumkuti. Nafikiri ni muhimu tukaziboresha karakana zetu kwa uhakika zaidi wa kuhakikisha ndege zetu zitadumu kuliko kuongeza ndege nyingine tatu hali ya kuwa karakana zetu zinahitaji maboresho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuishauri Serikali iliangalie jambo hili kwa kina. Ndege ni karakana, tusipofanya hivi shirika letu la ndege litakuja kurudi nyuma kama huko nyuma tulipotoka; na mzimu wa Marehemu utatuandama kama hatutatengeneza karakana za ndege Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia pia na kuhusiana na kiwanda cha ndege cha Tanga. Kule tunafahamu kuna mgogoro na umewekwa katika bajeti. Naomba Serikali ikamalize mgogoro ule ili kuweza kujenga kiwanja cha ndege cha Tanga. Ni tangu Mheshimiwa Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati anazindua mradi wa bomba la mafuta, aliahidi kiwanja cha ndege kule kujengwa lakini mpaka leo tunakwenda kusaini mkataba wa bomba la mafuta, kiwanja cha ndege cha Tanga bado hakijajengwa. Serikali iweke commitment kuhusiana na jambo hili. Ni fedheha kama wataalamu watakaokuja kejenga bomba la mafuta watatokea Kenya wakati Tanga tuna kiwanja cha ndege. Tunahitaji kiwanja cha ndege hicho kiingizwe katika commitment ya Serikali na kijengwe haraka iwezekanavyo. Ni miaka minne sasa imepita. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia kuhusiana na bandari. Niliwahi kusema jamani, tunafanya miradi mikubwa sana ya upanuzi wa bandari zetu, lakini tunahitaji tafiti na wataalam wa kujua kwa nini kina cha bandari zetu zinapungua? Bila tafiti tutaendelea kutumia mabilioni ya pesa kuongeza kina cha bandari zetu, lakini mwisho wa siku tunapiga mark time; leo tutafanya capital dragging, baadaye tutafanya maintenance dragging lakini hatujui sababu kwa nini kina cha bahari kina pungua? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Western California Beach ya Marekani iliwahi ku-sediment, yaani kina kupungua; na sababu kuu ilikuwa ni ujenzi wa mabwawa ya maji ya umeme. Sasa tuangalie mahusiano ya mito yetu na bahari zetu ambapo tunajenga au tunapanua hizi bandari zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, inasemwa kwa mujibu wa port and coastal engineering, mto hata ukiwa na kilomita 150 unaweza kuleta madhara katika bandari iliyoko huku. Kwa hiyo, bila tafiti pia hatuwezi kusema kwamba huu utaratibu wa kuongeza kina kwa maana hii ya dragging ni wa faida kiasi gani kwa Taifa letu? Kwa sababu siyo njia pekee ya ku-control sedimentation, zipo njia nyingine. Je, tunafanyaje cost comparison analysis kama hatuna tafiti za kujua vyanzo vingine vinavyosababisha sedimentation na njia ya ku-control? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie suala nzima la Bandari ya Tanga kuhusu ufanisi wake…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)


MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, samahani naomba nimalizie…

NAIBU SPIKA: Kengele imeshagongwa Mheshimiwa. (Makofi)

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kidogo aah.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, muda wangu umebana sana. Kwa hiyo,…

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niunge mkono hoja, nashukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu na niwapongeze sana Mawaziri na Naibu wake kwa utekelezaji mzuri wa majukumbu yao. Vilevile nimshukuru na kumpongeza sana Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati kwa wasilisho zuri ambalo limetupa guidance ya kutosha kuweza kuchangia hotuba hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni hivi karibuni tunaona nchi zetu mbili na Marais wetu; Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Uganda wakitia saini ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima mpaka Chongoleani Jijini Tanga. Kwa mujibu wa maelezo ya mradi huu unatajwa kwamba takriban ajira 6,000 – 10,000 zinaweza kutokea na kuna fursa nyingi sana za kibiashara zinaweza kutokea kwa watu ambao mradi huo utapita. Naomba kuishauri sana Wizara i-manage expectations za wananchi wetu katika maeneo ambayo mradi huu unapita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maana yangu ni nini? Tusije tukawaahidi wananchi wetu kwamba kutakuwa na fursa nyingi sana za kibiashara mwisho wa siku ikawa kinyume chake. Tunaiomba Serikali na kuishauri ituletee tathmini walioyofanya katika ujenzi wa TANZAM wakati wanajenga bomba ya mafuta kutoka Tanzania mpaka Zambia fursa gani zilipatikana na za aina gani na wananchi waweze kujiandaa. Vilevile tulipojenga bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam watuletee tathmini ya ajira na fursa za kibiashara ambazo wananchi waliweza kufaidika ili watu wetu waweze ku-manage matarajio yao ili mradi ule ukafanyike vizuri bila kusabbisha chaos wakati wa utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile naomba sana kuishauri Serikali i-coordinate na Wizara nyingine ambazo zitarahisisha utekelezaji wa mradi huu. Tunafahamu kwamba wakati wa ujenzi huu kutakuwa na huduma za consultation kati ya wataalam wa mradi na ninyi wataalam wa Serikali, ina maana kwamba kutakuwa na safari nyingi sana kati ya Tanga na Dodoma, kati ya Tanga na Uganda kwa ajili ya consultation za utekelezaji wa mradi huu. Hata hivyo, inashangaza ninyi Wizara ya Nishati mmekaa kimya, Kiwanja cha Ndege cha Tanga hakijajengwa mpaka sasa, mna mpango gani na wataalam wa mradi huu hamuoni kama mtawasababishia difficulties katika utekelezaji wa kazi zao? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mnafikiri Hayati wetu alipotoa ahadi ya kutekeleza ujenzi wa kiwanja kile pale Chongoleani wakati anazindua mradi huu maana yake ilikuwa ni nini? Maana yake ni kutaka ku-facilitate utekelezaji wa mradi huu kwa haraka. Kwa hiyo, niiombe Serikali kwa maana ya Wizara ya Nishati ya Madini ika-coordinate vyema na Wizara ya Ujenzi ili Kiwanja cha Ndege cha Tanga kijengwe haraka iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile katika mradi huu tunafahamu kwamba gesi itachimbiwa ardhini kwa maana ya lile bomba lakini tunafahamu kwamba lazima kuwe na facilities kama za zima moto katika maeneo yote ambayo bomba hili litapita. Wizara hii inapaswa ku-coordinate na Wizara ya Maji kuhakikisha maeneo yote yale ambayo mradi huu unakwenda kupita kunakuwa na maji ya kutosha incase kama bomba linakwenda kuvujisha lazima tuwe na tahadhari za kutosha kuhakikisha wananchi wetu wanaendelea kuishi salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunashukuru kwa upande wa Chongoleani kaka yetu Mheshimiwa Aweso maji yamekwenda lakini maji yale hayatoshi. Ni lazima tujenge water high drinks za kutosha katika maeneo yale ili wananchi wetu waweze kuishi salama.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote niwashukuru Mawaziri na niwapongeze sana kwa collabo nzuri ya kupiga kazi, hakika inatupendeza sana. Tunaona kabisa kwamba mafanikio makubwa yanakwenda kupatikana kwa kuunganika kwenu na kufanya kazi pamoja kwa bidi. Ni mfano mzuri tuwaige Mawaziri hawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia kwenye Wizara hii ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa kwenye GDP ya Taifa letu. Mkoa wa Tanga nasi tumebarikiwa kuwa na Hifadhi ya Saadan kwa kilomita zaidi ya 1,062. Hii Hifadhi ya Saadan ni hifadhi ya kipekee kabisa Afrika Mashariki kwa kuingiliana na Bahari ya Hindi. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa uoto huu wa asili, lakini lazima tukiri kuna changamoto ambazo zinatukabili ku-enjoy zawadi hii ya Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kule Wilayani Pangani kuna vijiji ambavyo vinataabika mno kwa kutokuweza kuwa-control wanyama waliopo ndani ya Hifadhi ya Saadan. Kwa mfano, Kijiji cha Buyuni kiko ndani ya Hifadhi ya Saadan, pia Kijiji cha Mikocheni, Sange, Mkalamo, Bulizaga hivi vyote vinaathirika mno kwa tembo wengi sana ndani ya hifadhi ile. Vijiji hivi vimekuwa vinasua sua katika kilimo kwa sababu ya kuwepo kwa tembo wengi sana, lakini hata miundombinu ya barabara ambazo barabara zetu ni za gravel zinapata shida mno kwa sababu ya uwepo wa tembo wengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Afisa Mhifadhi Mkuu anakiri wazi kwamba tembo hawa ni wengi wananishinda nguvu. Nahofia kumwambia kaka yangu wa Songea tuongozane wote, lakini natamani kabisa Mawaziri hawa watoke pamoja tuone namna gani tunakwenda Pangani tushirikiane na watendaji wa Pangani kuweza ku-control hali ile. Tembo wanaingia kwenye mashamba kuanzia saa 12.00 jioni na wanatoka saa 1.00 asubuhi na ni hatari kwa watoto wetu wakati ambapo wanakwenda mashuleni. Tunaomba sana sana tuunganike kwa pamoja tukatatue changamoto zilizopo Wilayani Pangani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia pia kule Handeni, vijiji viwili na wananchi wawili walishawahi kuuawa kwa ajili ya tembo. Tuone namna nzuri ya kupambana kwa pamoja kwenda kuziondoa changamoto hizi, ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali kupitia Wizara hii ya Maliasili na Utalii iliwahi kutoa zuio kwa kusafirisha viumbe hai kwenda nchi za nje. Miongoni mwa viumbe hai vilivyozuiliwa ni pamoja na vipepeo wanaozalishwa na watu binafsi katika Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga. Kwa kuwa basi, katika hotuba ya Mheshimiwa Rais, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, alitoa wito kwa Watanzania tufuge wanyama mbalimbali na viumbe hai kwa ajili ya kujiongeza kiuchumi. Je, Wizara hawaoni kuendelea kuliweka zuio linaendelea kuwadumaza wananchi waliokuwa wakifuga vipepeo hao kiuchumi? Ionekane haja sasa kwenda kuliondoa zuio hili ili wananchi waweze ku-enjoy kufanya biashara ile ya kusafirisha viumbe hai kuvipeleka nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuongeza basi mapato ya Wizara hii ya Maliasili na Utalii, nasi tujaribu kujikita kuzifanya hizi routes zetu za ndege zinapopita nazo zi-move zifanye maneuvering around a Mlima Kilinjaro. Naziona juhudi za Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kuutangaza Mlima Kilimanjaro kwamba upo Nchini Tanzania, lakini wenzetu hiyo ndiyo technic wanayoituma. Niliwahi kumpa mtu zawadi ya kahawa ya Kilimanjaro, nikamwambia kawaha hii inatoka Tanzania ananikalia inatoka ananiambia inatoka Kenya. Nikamwambia tu-google hapa, tulivyo google ndio akakubali kwamba kama Kilimanjaro ipo Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, aliniambia, nilipoingia Nairobi, nilipitishwa maeneo yale nikauona Mlima wa Kilimanjaro kwa mbali kwa hiyo sisi tunashindwaje ku-coordinate na ATCL kuhakikisha kwamba ndege zetu nazo zinafanya maneuvering around area ya Mlima Kilimanjaro ili tuweze kuwavuta watalii zaidi nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tuone haja basi ya kutengeneza festivals ambazo kila mwaka zitakuwa zinafanyika au kwa season maalum na zitangazwe all over the world kuhakikisha watalii zaidi wanakuja nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi ya kuchangia, awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi hii ya uhai, kipekee kabisa niwashukuru sana Mawaziri wetu wa Wizara hii ya Mipango na Fedha kwa uwasilishaji mzuri wa bajeti yetu, lakini pia kwa kujibu kwa umakini na uweledi mkubwa Hoja za Wabunge, Mwenyezi Mungu aendelee kuwasimamia katika majukumu yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na vilevile nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati Mzee wangu Sillo kwa kazi nzuri aliyofanya ya kuitengeneza bajeti hii mpaka hapo ilipofikia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kipekee kabisa na kwa dhati ya nafsi yangu nimpongeze Mwanamama jasiri, Mwanamama hodari Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa usikivu mkubwa alionao kuhakikisha kwamba anakwenda kuondoa shida na taabu kwa Watanzania. Kama jina lake linavyoitwa Samia kwamba ni msikivu, Mama yetu ameitendea haki Watanzania kwa kusikiliza vizuri kabisa hoja za Wabunge na kuzifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niliwahi kuchangia suala zima la kupunguza urasimu katika kodi za viwanja na mapango hili linakwenda kutekelezwa kwa kuhakikisha kwamba kodi za mapango yatalipwa kwa kupitia LUKU, niipongeze sana Wizara kwa usikivu huo nami nimeipokea kwa mikono miwili sana. Tahadhali moja ambayo naomba kuitoa wizara tafadhalini tujaribu kuangalia kwa wale ndugu zetu wanaofanya kazi ya biashara ya real estate isije kulipiwa kodi katika yale majengo ambayo kuna LUKU zaidi ya moja ndani lakini akaenda kulipa kodi moja kwa moja tutakuwa tumewabana wafanyabiashara wale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile niipongeze sana kwa suala zima la kuhakikisha tunakwenda kuziboresha barabara za TARURA, hili ni jambo kubwa sana kwa uchumi wa Tanzania na kuhakikisha kwamba sekta ya ujenzi inakwenda kuongeza na kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye Pato la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hoja hii ya kuongeza fedha katika mafuta ili tuweze kujenga barabara za TARURA, mimi naomba nichukue nafasi hii pia kuwatoa Watanzania wasiwasi. Watanzania wanafahamu kwamba unapoongeza fedha katika mafuta basi tunakwenda kuongeza mfumuko wa bei, kwa mujibu wa data za National Bureau of Statistics. Lakini Watanzania nawaomba tuwahakikishie kwamba, mama yetu mweledi mwenye upeo wa mbali ameangalia vizuri sana, kwa sababu factor muhimu katika kuhakikisha mfumuko wa bei ni suala zima la gharama za usafirishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapotoa nyanya zetu kutoka Iringa zinapokuja Dar es Salaam, msimu wa mvua barabara hazipitiki, hakika mfumuko wa bei utakuwa juu. Lakini tunapokwenda kuiangalia GDP ya taifa letu tunakwenda kuangalia uzalishwaji wote wa makampuni na watu binafsi. Kwa kilichofanyika hapa, in a long run tutaongeza per capital income ya Mtanzania na nchi yetu inakwenda kukua katika uchumi wa mbele wa taifa hili. Hongera sana mama yetu Samia Suluhu Hassan, hongera sana Mawaziri mliofanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya Watanzania wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine naomba nichangie kuhusu suala la uchukuzi. Sisi Watanzania tuko kwenye umoja wa East Africa na tuko kwenye umoja wa SADC lakini hatuko kwenye umoja wa COMESA. Sasa, kwa kuangalia Overload Control Act ya East Africa na Overload Control Act ya SADC tunapata confusion kidogo hapa. Wafanyabiashara wetu wanapolipa transit charge kwa kila kilomita 100 ndani ya Tanzania analipa dola 16,000. Lakini huyu huyu Mtanzania anapokwenda Kenya kwa mujibu wa East Africa anatakiwa alipe dola 10, lakini wanaotoka SADC na wanaotoka Uganda ndani ya ukanda ule wa East Africa wanalipa dola 10.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana Serikali iende ikaliangalie hili ili kuhakikisha wafanyabiashara wetu nao wanakwenda kufanya biashara katika harmonizing way ili wanaokuja Tanzania nao waweze kufanya biashara kwa kutumia transit charge ya dola 10 badala ya 16. Kwa sababu wenzetu ambao wapo kwenye COMESA wana-take advantage ile ya kutukandamiza sisi. Wale wa SADC wanapokwenda Kenya wanalipa 10 lakini wanapokuja Tanzania wanalipa 16. It is obvious wata-run away from Tanzania na wataenda kukimbilia Kenya na Uganda. Kwa hiyo naomba hili uliangalie.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine naomba sana kuishauri Serikali. Tumepata mwarobaini wa barabara za vijijini kwa kutumia TARURA; lakini naomba niishauri Serikali kwa unyenyekevu mkubwa. Ni kwamba, barabara zetu kuu (trunk roads) na barabara zetu za regional roads pamoja na district roads thamani yake ni trilioni 21 za Tanzania. Thamani hii tusipoilea ipasavyo tutakuja kurudi nyuma na tutaanza kuzijenga barabara hizi upya. Naomba tuangalie namna nzuri ya kuhakikisha kwamba barabara hizi, trunk roads, regional roads na district roads zinafanyiwa periodic maintenance ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwasababu gani, ukiangalia corridor ya TANZAM ambayo ni muhimu sana kwa sababu ndiyo inatuvutia wateja kutoka Malawi, Zambia pamoja na Lubumbashi – DRC. Corridor hii ni chakavu na imechoka sana, tunataka kuwaambia nini wafanyabiashara wanaopita katika njia hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, tuchukulieni mfano tu, kile kipande cha Chalinze – Mlandizi it is almost collapsed, lakini tukiangalia kutoka Dodoma mpaka Iyozi it is almost collapsed, ukiangalia Tunduma mpaka Igawa it is almost collapse. Sasa hii TANZAM corridor, ambayo ndiyo inatuletea wateja kwenda bandari ya Dar es Salaam, tunaiambiaje? Kwa hiyo, niishauri sana Serikali, kwa heshima na taadhima, despite ya njia nzuri tuliyoifanya upande wa TARURA, tuangalie namna ya kulea trillion 21 ya mtandao wa barabara za mikoa na barabara kuu pamoja na barabara za wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa data zilizopo, kwa mwaka wa fedha uliopita, barabara kuu na barabara za mikoa na barabara za wilaya zimefanyiwa periodic maintenance kwa asilimia 42 tu. Na ukienda barabara za wilaya ambazo zipo chini ya TARURA, zimefanyiwa maintenance kwa asilimia 28 tu, na asilimia 52 hazijafanyiwa periodic maintenance, kilichofanyika ni just sports improvements na wala hakuna over laying. Nini tunakwenda kufanya? Maana yake tutakuja kuanza afresh kama tusipoamua kutenga fedha kwa ajili ya maintenance ya barabara kuu, barabara za mikoa na barabara za wilaya. Ukiangalia hata barabara ya Kibiti-Lindi-Mtwara ambapo kuna mfanyakazi mkubwa kule Dangote; Dangote anatoa mizigo yake kuleta huku mjini, anakwendaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tuone namna ya kuhakikisha wafanyabiashara wetu wanapokuja Tanzania wanakuwa in a good way ya kufanya biashara na kuwa- attract zaidi ili waje kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba kuunga mkono hoja asilimia 100, nashukuru sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika mjadala huu unaoendelea. Awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu Mwenye Enzi na Utukufu kwa kunisimamisha mahali hapa muda na wakati kama huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nichukue nafasi hii kuchangia katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali katika kipengele cha 9.2 cha Usimamizi wa Manunuzi na Mikataba. Kwa mujibu wa CAG amesema kwamba Taasisi 16 zilinunua bidhaa na huduma zenye thamani ya shilingi bilioni 77.62 bila kutumia mfumo wa TANePS

Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni ya 342 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2013 kama ilivyorekebishwa mwaka 2016 imezitaka taasisi za Serikali zinazofanya manunuzi ya Umma kutumia mfumo huo wa TANePS. Pia Waraka Na. 4 wa Wizara ya Fedha umezitaka taasisi hizo kuanza haraka kufanya manunuzi ya Umma kuanzia tarehe 01 Januari, 2020. Kwa maana mpaka leo ni miaka miwili na ushei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uhakika wa taarifa zilizopo ni kwamba mfumo wenyewe wa TANePS ni shida tupu. Ukiangalia maelezo ya CAG aliyoyatoa ukurasa wa 141 akielezea umuhimu wa mfumo wa TANePS amesema kwamba kushindwa kutumia mfumo wa TANePS katika manunuzi kunakwamisha jitihada za Serikali katika kuongeza ufanisi, kupunguza muda wa manunuzi na kuboresha uwazi katika manunuzi ya Umma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba mfumo huu bado una changamoto kubwa na kwa kiasi kikubwa hauleti uwazi uliokusudiwa, wala ufanisi uliotarajiwa. Nasema hivi kwa sababu gani? Katika mfumo huo wa TANePS kwanza mfumo wenyewe jinsi ambavyo umenunuliwa kutoka huko uliponunuliwa ni changamoto kubwa, ni aibu tupu kusema kwamba unanunua mfumo ambao haukupi full access ya kuutumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefanya evaluation report, nimefanya tathmini ya tender na mfumo huu lengo lake ilikuwa ni kufanya tathmini ya zabuni na kufanya usimamizi wa mradi, maana yake contract administration inafanyika ndani ya mfumo. Malipo yote unayowalipa Wazabuni uyanafanya ndani ya mfumo. Kadri unapolipa certificate namba moja, hivyo hivyo inapungua mpaka mradi wote unakamilika. Cha ajabu, mfumo huu bu hauipi PPRA wala taasisi inayofanya manunuzi ya Umma full access ya mfumo huu. Maana yake mfumo huu so far ni kimeo na kama umenunuliwa, tumenunuliwa na tumepigwa. Haiwezekani ununue mfumo ambao haukupi full access (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Taarifa.

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kumpa taarifa mzungumzaji Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ulenge kwamba mfumo huo ambao anauzungumza, TANePS ni kweli ulikuwa na changamoto lakini Serikali imeamua kujenga mfumo mpya unaoitwa NEST na upo Iringa na unajengwa na wazalendo kutokana na changamoto hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mfumo tulionao sasa utapunguza gharama na utakuwa ni wa uwazi na utakuwa unakamilisha zabuni zote kwa uhakika na kwa muda maalum.

Mheshimiwa Mwenyeki, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ulenge, unapokea taarifa?

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa taarifa hiyo, lakini naomba kama Serikali tusirudie makosa hayo kila kukicha. Kwa nini tununue mfumo kwa fedha nyingi halafu baadaye tuje tutafute mfumo mwingine kwa ndani, zile pesa value for money yake tunaisemaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ni vizuri umetoa taarifa hiyo kaka yangu Mheshimiwa Naibu Waziri Chande, nimeipokea vizuri kabisa, lakini je, tumefanya tathmini ya kina ya kuangalia ni hasara kiasi gani tumeingia? Mfumo unaokuja mtuhakikishe kwamba utakwenda kutatua changamoto zifuatazo: Mfumo huu wa TANePS kwanza kabisa ukimaliza evaluation report ulikuwa hautoi full detailed evaluation report; ulikuwa unatoa taarifa ambayo inatoka kama mtindo wa excel. Wakati tulipokuwa tukifanya manunuzi na zile zabuni, tulikuwa tunapata taarifa kamili (full detail) ya mchakato mzima wa zabuni, lakini mfumo huu wa TANePS umekuwa haufanyi hivyo. Hata baada ya hapo, unapoingia tena ukitaka kufanya mwendelezo wa mradi kwa maana ya usimamizi, haukupi access kwa maana ya mpaka ulipe tena fedha. Kwa nini tumeingia kwenye mifumo ya aina hii? Ina maana kweli hatuna weledi wa kutosha wa kujua mifumo inakuaje? Kwa nini tupewe mifumo ambayo haitupi full access? Kwa nini huwezi ku-edit report baada ya kuingiza katika TANePS? Hii siyo sawa, tunafanya makosa yanayojirudia kila siku. Ina maana ndiyo Tanzania kweli ni kichwa cha wenda wazimu? Kwa nini tuje na mifumo ya aina hii? Tumesema lengo ni kupata ufanisi na uwazi lakini TANePS hautoi ufanisi na uwazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali kwa hatua ambazo mmezichukua. Tunawapongeza sana na hili, lakini ukweli lazima tuuseme kwamba kuna hasara tumeingia ili jambo hili tulichukulie very serious, manunuzi ya Umma ni suala kubwa kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba nichangie sura ya tisa kwa maana ya ukurasa wa 139 unaozungumzia hasara ya Shilingi bilioni 68.73 zimepatikana kwa Serikali kulipa riba kwa wakandarasi. Naomba nisirudie sana, kaka yangu Mheshimiwa Ndulane amezungumza vizuri, amekuwa kwenye utendaji huko TANROADS, ameelezea vizuri kabisa jinsi malipo yanavyofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba CAG ameonesha kidole kwa mtu ambaye siyo stahiki. Kama kweli tunatafuta solution, kama kweli tunataka kuondoa changamoto hizi, CAG anyooshe kidole kwa mtu anayestahili. Kumtaja TANROADS kama ndiyo chanzo cha riba hizi au upotevu huu, nafikiri kuna shida, sielewi labda utendaji wa CAG ukoje? Kwa sababu namwini CAG katika uzoefu wake wa usimamiaji wa miradi, lakini anaponyoosha kidole kwa mtu asiyestahili sifikiri kama ni sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ndulane amezungumza vizuri sana, kule Wizara ya Fedha na Mipango unapeleka certificate ya malipo, watu 10 wote wale ni wa nini? Halafu hawaendi site, wanakaa nazo tu ofisini. Certificate inakutaka uende site ukafanyea measurement ya kazi iliyofanyika. Mnakaazo kule siku 10 nzima Wizara ya Fedha na Mipango, zinafanya nini? (Makofi)

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa wapi? Mheshimiwa Mtemvu.

T A A R I F A

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nilitaka nimpe taarifa mzungumzaji, Mheshimiwa Engineer Mwanaisha ya kwamba CAG, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali anachokifanya, akienda kwa implementer wa mradi anamhoji juu ya kutokamilika kwa mradi husika bila kuangalia alitakiwa kupokea hiyo hela kwa nani? Pia ana jukumu la kwenda kwenye Wizara ya Fedha chini ya fedha ambazo zinatokea kwenye GoT - Government of Tanzania; na kule pia mtoaji fedha anahojiwa vilevile, mbona wewe una jukumu la kutoa fedha kwenye taasisi kadhaa na hujazitoa kwa wakati? Kwa hiyo, nilitaka kumwambia, hiyo ndiyo kazi ya CAG, ameifanya sahihi kwa yule anaye- implement mradi na pia kwa mtoaji wa fedha. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ulenge, unapokea taarifa?

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa elimu, lakini nimkumbushe kaka yangu Mheshimiwa Issa Mtemvu, kwamba yeye ni mhasibu kweli, lakini hapa hasimami kwa CAG. Hapa tunatafuta solution, kwa nini miradi inaleta riba nyingi? Kwa hiyo, sisi kama tunataka kutoa maazimio na kuishauri Serikali, inabidi kuangalia mambo in wide perspective, hatusimami upande wa CAG. Kama Wizara ya Fedha haijapeleka pesa kwa wakati, miradi yote ya DEVO ni kimeo nchini humu. Mkandarasi yeyote akipata mradi wa DEVO, siku zote sisi tunajua atapata shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni miradi ya mantainance pekee ambayo inatokana na fedha za fuel levy ndiyo yenye uhakika wa malipo. Miradi ya development hailipwi kwa wakati yote. Chanzo cha fedha cha miradi ya DEVO ni Serikali, fedha zinatoka Hazina.kwa hiyo, ni lazima tuyaseme haya ili tuije na mapendekezo sahihi na maelekezo sahihi kwa Serikali. Sasa hapa Mheshimiwa Mtemvu, uzoefu wako kwenye auditing na uhasibu lakini wewe sio CAG hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi Shilingi bilioni 68.73 kwa uhakika ni kwamba ni riba peke yake, lakini hasara ni kubwa zaidi ya hii. Kwa maana gani? Hapa bado hatujaingiza fedha. Kama una Mwandisi Mshauri kwa mfano, anasimamia mradi huu, unapochelewa kumlipa mkandarasi, maana yake unaongeza na muda wa usimamizi wa mradi. Kwa hiyo, na mwandishi mshauri naye anaongeza malipo yake. Kwa hiyo, cost and time over run nazo ni thamani kubwa katika mradi. Achia wafanyakazi ambao ni client ambao wana supervised miradi kila siku na kufuatilia kila siku kule site.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni fedha nyingi sana kiukweli za Watanzania walalahoi zinapotea. Tangu nimekaa kwenye Serikali zaidi ya miaka kumi kabla ya kuja huku, miradi yote ya DEVO pesa haziji kwa wakati, haziji at all, shida ni nini?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia.

Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mwenye enzi na Utukufu kwa kunijaalia kusimama mahali hapa muda na wakati kama huu. Lakini kipekee kabisa nimpongeze mtekelezaji mkuu wa malengo ya nchi yetu mama yetu Samia Hassan Suluhu kwa ubunifu mkubwa anaoufanya katika kuongoza Taifa letu. Kipekee kabisa nimpongeza kwa hizi shilingi trilioni 1.3 ambazo kwa hakika miradi yote imekwenda kuwalenga wananchi wa chini moja kwa moja. Anastahili pongezi na tumuombee kwa Mwenyezi Mungu aendelee kufanya kazi zake kwa umahiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo naomba kuishauri Serikali katika biashara ya bandari. Ametangulia kuzungumza mwenyekiti wangu wa kamati lakini naomba na niseme yafuatayo. Serikali imeboresha miundombinu ya bandari zetu kubwa lakini kiukweli Serikali haijajipanga kukamata soko la land locked countries. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Mashariki ya Kongo kuna shehena nyingi sana ambazo zinatupita Serikali sasa ianze kufanya makubaliano ya kufanya joint operation katika bandari ya Kalemi eneo la Kalemi au bandari ya Kalemi kuna reli ambayo inatuunganisha moja kwa moja mpaka Zambia. Kwa hiyo, tukifanya joint operation katika bandari ya Kalemi maana yake tunaweza kuzipata shehena zinazoingia na kutoka katika bandari ya Kongo Mashariki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala zima la kufanya joint operation katika bandari za wenzetu siyo suala la ajabu tulishawahi kufanya joint operation katika Port Bell Bandari ya Uganda, na sasa hivi ninavyozungumza tayari Durban imeshafanya makubaliano na DRC na Zambia na Malawi ili kuweza kupata soko lile la Mashariki ya Kongo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini disadvantage ambayo Durban wanayo hawana direct contact ya maji moja kwa moja na DRC. Lakini sisi Mwenyezi Mungu ametujaalia tunayo direct contact na DRC lakini hatujaamua kuitumia fursa ile ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niishauri Serikali au niishauri Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari waanze sasa mazungumzo na nchi ya DRC ili tuweze kupeleka mitambo yetu katika bandari ya Kalemi na tuweze kuli-win soko lile katika Mashariki ya Kati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda kwa taarifa zilizopo tayari wenzetu wa nchi Jirani wanalimendea soko lile la Kongo Mashariki tayari meli yao ya SGR inaelekezwa kule ili ku-win mizigo ile inayoingia na kutoka Kongo Mashariki sasa ni wakati wetu sahihi wa kuamua kufanya mazungumzo ili tuweze kuli-win soko lile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanya matengenezo bandari ya Tanga lakini sasa ili bandari ya Tanga iweze kuleta faida na tija inayotarajiwa ni lazima mambo yafuatayo yafanyike. Kwanza reli ya Tanga mpaka Arusha ambayo imeshakarabatiwa iweze kufanya kazi. Serikali imetengeneza kilometa 470 Tanga mpaka Arusha lakini reli ile mpaka sasa haifanyi kazi sasa ili bandari ya Tanga wapate wateja wa Kilimanjaro na Arusha ambao wanakimbilia Mombasa reli ile ni lazima ifanyekazi. Serikali ijipange sasa katika mwaka unaokuja wa fedha bandari ile ya Tanga iweze kuunganishwa na soko la Arusha na la Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vile vile reli ile ya Tanga mpaka Arusha ikiweze kusogezwa mpaka Musoma ambapo kuna bandari kule pia tutaweza kuli-win soko la Uganda kupitia kule Victoria. Lakini vile vile reli ile ikiweza kufika Arusha na tayari barabara ya Tanga, Handeni Kibirashi mpaka Singida imeanza kujengwa maana yake tutalivuta soko la Rwanda kwenda Tanga ni karibu zaidi kuliko kukimbilia kwenda … mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapofanya investment kubwa vile vile Serikali ifanye simultaneous mambo mengine bila kuchelewesha delay ya return of that investment. Lakini umuhimu wa barabara ya Handeni Kibirashi mpaka Singida sasa hivi pia umuhimu wake ni rahisi mno kusafirisha mitambo pamoja na vifaa vingine vya ujenzi vinavyokwenda kujenga bomba la mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niiombe Serikali kilometa 20 ambazo zimetengwa kufanywa wakati huu ziongezwe barabara ile iweze kuisha kwa haraka kwa maslahi mapana ya Taifa hili. Naomba kuzungumzia suala zima la utekelezaji wa miradi yetu kupitia force account na nalisema hili kwa mapenzi makubwa kwa nchi yangu. Kuna usemi unasema kwamba if you think education is expensive then try ignorance na mimi nasema if you think…

MWENYEKITI: Hapo Mheshimiwa inabidi u-declare interest umo haumo?

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, haya na-declare the interest kwamba na mimi ni mkandarasi mdogo mdogo lakini vile vile nazungumzia professional liability ambayo kwenye force account haipo. Lakini vile vile ninacho kiangalia ni ubora wa vinavyozaliwa kwenye force account.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba halmashauri zetu ambazo sasa force account ndiyo imekuwa inatekelezwa kwa kiwango kikubwa hazina wahandisi na tunapokwenda kununua material ya ujenzi kwa kutumia zile Kamati za Manunuzi zilizoundwa hawafanyi test za material nondo hata kama unakwenda kuinunua kwenye hilo duka nondo lazima ui-test kabla ya kuipeleka site. Kuna test ambazo zinatakiwa kufanywa kwa nongo kama bending test, tensile strength test zinabebwa na kupelekwa site bila hizi test kwa sababu hakuna wahandisi halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vile vile tunaponunua hata kokoto kuna test zake ambazo zinatakiwa zifanywe kabla ya kusema kokote hii itaenda kutumika mahala fulani sisi tunabeba tunapeleka site ni liability kubwa sisi tunaamini tuna-save lakini naomba sana tufanye tathmini ya kina katika majengo yote ambayo yamejengwa na force account ili tuone kweli kuna saving? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakwambia hakuna saving kwa sababu gani Mheshimiwa CAG amesema kuna baadhi ya halmashauri nyingi zimeshindwa kufanya retirement baada ya kununua manunuzi hii maana yake ni nini? Serikali imeweka mwongozo wa kufanya kazi kupitia force account. PPRA wametengeneza guidelines lakini guidelines ile haitumiki ndiyo maana wameweza kununua moja kwa moja bila ya kutengeneza framework contract ili uweze kushindanisha bei kati ya supplier mmoja na mwingine lakini wewe unakwenda direct kwenye duka kwenye kiwanda unanunua wakati hakuna framework contract otherwise kusingekuwa hakuna retirement ya materials.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikwambie kitu kimoja kule Dar es Salaam kuna jengo lilidondoka pale Chang’ombe tunaliita Chang’ombe village Mhandisi aliyesimamia lile jengo alifungwa lakini katikati ya Jijji kuna jengo lilidondoka Mhandisi aliyesimamia lile jengo alifungwa lakini katika force account hakuna professional liability…

MWENYEKITI: Nimeambiwa kumbe ya pili tayari.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru naomba kutoa hayo kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi hii ya kuchangia, leo nitachangia Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama mahali hapa muda na wakati kama huu. Lakini pia kipekee kabisa niwapongeze Kamati hii ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa kwa mapendekezo yao mazuri kabisa waliyoyatoa hasa kwa asilimia 10 ya fedha zile za Serikali za Mitaa. Kiukweli kabisa ni wakati sahihi sasa kuhakikisha tunakuwa na mfumo madhubuti ambao uta-enhance transparence, ita-enhance accountability ili fedha hizi ziweze kuleta tija kwa makundi yale yaliyolengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Ripoti ya Hali ya Uchumi iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya mwaka 2020 imesema kwamba ili Taifa letu libaki katika uchumi wa kati wa chini au ili tusonge mbele kitu kimojawapo ni kuhakikisha tunatengeneza uchumi shirikishi na kuondoa umasikini, na mimi ninaamini kabisa kabisa kupitia asilimia 10 tunakwenda kufanya uchumi shirikishi na kupunguza umasikini kwa wanawake wa Taifa hili na makundi maalum. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha zinazotoka kwa ajili ya asilimia 10 kwa Tanzania yetu hii ni fedha nyingi, ni fedha ambazo zinapangwa kupangiwa utaratibu mzuri na maalum ili zilete tija na athari chanya kwa makundi yaliyolengwa. Ukiangalia takwimu mwaka 2019/2020 Serikali yetu imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 717, inamaana asilimia 10 ni bilioni 71 point, lakini mwaka 2021 Serikali yetu imekusanya kwa Tanzania nzima shilingi bilioni 757, asilimia 10 ni zaidi shilingi bilioni 76; lakini mwaka 2021/2022 Serikali yetu imepanga kukusanya shilingi bilioni 863 inamaana asilimia 10 ni itakuwa shilingi bilioni 86 za Kitanzania, ni fedha nyingi sana ambazo ni lazima tutengeneze utaratibu mzuri kuhakikisha unaleta tija kwa makundi yaliyopagwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kanuni zetu ambazo zimetolewa kwa ajili ya asilimia 10 zina madhaifu, pamoja na mwongozo ambao ulitolewa Machi, 2020 nao unahitaji maboresho. Kwa mfano katika mwongozo pamoja na kanuni kifungu cha 21(d), imeitaka TAMISEMI iwaelekeze Wakurugenzi wa Halmashauri kufungua akaunti moja tu ya kuhifadhi zile fedha pamoja na marejesho. Sasa fedha za marejesho zile ni fedha nyingi tukichanganya kwenye akaunti moja maana yake tunakwenda kupunguza uwajibikaji na accountability. Nashauri kanuni ielekeze kuwepo na akaunti ya marejesho pamoja na akaunti ya mikopo ile ya makusanyo ili ya asilimia 10. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ukiangalia kanuni ya 21 kifungu cha 37(a), kinasema kwamba Halmashauri zote zitoe mafunzo kwa wale wanaopata mikopo. Lakini mafunzo yake yanalenga ujasiriamali, yanalenga uongozi, hayazungumzi namna ambavyo wapewa mikopo watazijua hizi kanuni na taratibu ambazo zimewekwa. Kwa maafisa maendeleo ya jamii wengi na maafisa ustawi wa jamii wengi wana take advantage kwa sababu hawaelekezwi yale makundi maalum namna ambavyo kanuni hizi zinaelekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kumekuwa na malalamiko mengi, wanawake wanasema tunaomba mikopo kila mara lakini hatujulishwi kwamba nimepata au nimekosa ninaahangaika nakwenda na kurudi kila mara. Lakini kanuni inaelekeza ndani ya siku saba mpe taarifa mwanamke yule kwamba umepata mkopo au hujapata, inamaana siku saba zikipita mwanamke yule ata assume amepata mkopo. Kwa hiyo, tunaomba sana kanuni hizi zielekezwe kwa akinamama na makundi yaliyolengwa, ili waweze kutumia fursa hii ipasavyo.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Engineer Mwanaisha.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, oooh! Kumbe muda umeisha nakushukuru sana ahsante. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mwenye enzi na utukufu. Nami nitachangia kwenye Kamati hii ya Miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kazi kubwa anayofanya kuhakikisha miradi yote aliyoikuta inakamilika. Ni juzi tu tumeshuhudia Waziri wa Fedha akiingia mkataba wa mkopo nafuu kwa ajili ya barabara za miradi inayokwenda kasi, karibia Euro milioni 178, ni mkataba ambao umeingiwa kwa ajili ya kujenga barabara zile; nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa jitihada kubwa anazofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba nichangie pia kuhusiana na bandari. Nazungumzia Bandari ya Mwambani. Kuanzia mwaka 1975 Bandari ya Mwambani Jijini Tanga ilishawekwa msingi ikitajwa kwamba ni miongoni mwa bandari zenye kina kirefu cha asili Nchini Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na eneo lenye hekta 174.2 lilishatengwa, na bilioni 2.59 zilishalipwa kwa wananchi kupisha eneo lile la ujenzi wa bandari, na tayari Mamlaka ya Bandari ilipeleka Serikalini andiko kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ile ya Mwambani kwa ajili ya kumpata mwekezaji na kujenga under PPP (Public Private Partnership).

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni miaka mitano sasa imepita Serikali iko kimya kuhusiana na Bandari ile ya Mwambani. Ninaiomba sasa Serikali iweke wazi mipango yake kuhusiana na Bandari ya Mwambani Jijini Tanga. Je, zile bilioni 2.59 zilizotolewa Jijini Tanga maana yake kwamba zingewekezwa sehemu nyingine Mkoani Tanga zingeweza kuleta tija vilevile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Serikali iko kimya mpaka sasa kuhusiana na ujenzi wa Bandari ya Mwambani? Mwekezaji kweli amekosekana kujengwa under PPP? Lakini, je, Serikali imeshatenga kiasi gani kwa upande wake wa public tujue mwekezaji ameshindikana vipi kupatikana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana kuishauri Serikali iipe kipaumbele Bandari ya Mwambani kwa sababu tunashindana na Bandari ya Mombasa na Bandari ya Mwambani eneo lile ni potential, tangu mwaka 1975.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kuhusiana na mradi wa barabara ya mwendokasi. Tumejenga miradi ile na inakwenda vizuri, lakini mpaka sasa mfumo wake wa tiketi hauruhusu wananchi kuweza kulipa as per distance travelled. Anayetoka Kimara kwenda Kariakoo na anayetoka Kimara kwenda Ubungo wote wanalipa bei moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaiomba Serikali iboreshe mfumo ule wa tiketi za kielektroniki kuweza ku- accommodate uwezo wa mwananchi kulipa as per distance travelled. Ndivyo tunavyoona kwenye nchi za wenzetu; mtu anakwenda ana-punch kila anaposhuka ili kulipa as per distance aliyotembea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hii yote inatokana na nini; kwenye ujenzi wetu mwanzoni hatuku-accommodate dart ambazo zinaruhusu mifumo mingine ya umeme kuingia chini. Tumejenga vituo, tumejenga barabara, lakini zile conduit darts ambazo zinakubali mifumo ya umeme na fiber kuingia kwenye vituo vyetu haikuwekwa. Na ndiyo sababu baadhi ya vituo vyetu usiku vina giza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaomba tukiwa tunaelekea kwenye phases nyingine za miradi hii, likumbukwe hili, kwamba we need to provide darts katika primary structuring za miradi ile kuhakikisha kwamba tunaweza ku- accommodate mifumo mingine kuruhusu efficiency katika mradi mzima ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee kuchangia kuhusiana na mfumo mzima wa single window system kuziwezesha bandari zetu kuweza kufanya kazi kwa ubora zaidi. Serikali yetu naomba iharakishe kumaliza mfumo huu ambao umefika hatua za mwisho ili bandari zetu ziweze kutoa mizigo kwa haraka. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mwenye kunemesha neema kubwa na mwenye kuneemesha neema ndogondogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukuwe fursa hii sasa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi kubwa anayofanya kufuatilia shughuli za kila siku za Serikali, hakika anaitendea haki nafasi yake hii. Pia nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kazi kubwa anayofanya ya kuhakikisha anatuletea maendeleo Watanzania na hakika Mheshimiwa Rais wetu amedhihirisha upendo wake kwa Watanzania wote kwa kuanzisha Wizara maalum ya wanawake jinsia na makundi maalum.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii inaonekana kabisa adhma ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha anakwenda sambamba na malengo 17 maendeleo endelevu ya dunia ya kuhakikisha kwamba hakuna anayeachwa nyuma katika maendeleo endelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, natambua kwamba Serikali ilianzisha na kuunda Tume ya Sekretarieti ya Ajira kwa mujibu wa kifungu cha 29(1), Sura 298, iliipa mamlaka ya Sekretarieti ya Ajira iajiri kwa niaba ya Serikali. Sasa hili Wizara hii mpya ambayo imeundwa iweze kufanya kazi na kuleta tija kwa makundi yale yaliyolengwa wakiwemo waajiri wangu wanawake wa Mkoa wa Tanga. Naiomba na kuishauri itoe kibali cha muda kwa Wizara hii ili iweze kuajiri Maafisa Maendeleo Jamii Kata na Afisa Maendeleo Jamii ya Vijiji kwa sababu ni wachache mno.

Mheshimiwa Naibu Spika, peke yake kuna upungufu wa 2,322 Maafisa Maendeleo Jamii Kata, kwenye ngazi ya kata, lakini Maafisa Maendeleo Jamii wa Mkoa kuna upungufu wa 2,284 na Maafisa Maendeleo Jamii wa Wilaya kuna upungufu wa Afisa Maendeleo Jamii 41. Niiombe sasa Serikali itoe kibali kwa mamlaka ya ajira za wilaya na za mkoa na hata ngazi ya wizara hii ili iweze kuajiri kwa muda ili wizara hii mpya ikaweze kuleta tija kwa makundi yaliyolengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia kuchangia ukurasa wa 10 mpaka wa 13 wa hotuba ya Mheshimiwa Rais ambao umeeleza mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza mpango na bajeti ya mwaka 2021/2022. Miongoni mwa mafanikio yaliyotajwa ni pamoja na kukamilika kwa kulipa fidia maeneo ya kipaumbele katika mradi wa bomba la mafuta linalotoka Hoima mpaka Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa taarifa zilizopo miongoni mwa maeneo ya kipaumbele ni pamoja na eneo la Mkuza ambapo ndiyo bomba linalazwa mita 30, kwa maana ya 15 kutoka kila upande lakini Mkoani Tanga takribani wananchi 100 hawajalipwa mpaka sasa kutoka mwaka 2018 Juni. Sasa mkisema kwamba mnawalipa maeneo ya kipaumbele vipi wananchi hawa waliopisha eneo la Mkuza mpaka leo hawajalipwa? Tunaishauri Serikali iwalipe wanachi hawa tangu Juni, mwaka 2018 ni miaka minne sasa wameyatoa maeneo yao na mpaka leo bado hawajalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna makampuni ambayo yalikuja tangu Julai mwaka 2019 kuchukua maeneo katika upande ule ambapo mradi utaelekea. Alikuja TPA, alikuja Mihan Gas, amekuja Ngorongoro, amekuja Simba lakini wengi wao pia hawajalipa. Kwa mfano, Black Oil wamechukua hekta 200 hawajalipa mpaka sasa na tathimini ilikwishafanyika vilevile Ngorongoro hekta 100 hawajalipa mpaka sasa na sasa hivi ni takribani miaka minne inakwenda mnawaambia nini wananchi wale wa Tanga waendelee kukaa Idle mpaka lini sasa?

Niiombe na kuishauri Serikali iwahimize makampuni haya yaliyochukua maeneo kule Mkoani Tanga kwa ajili ya bomba la mafuta, wafanye hima na haraka kuhakikisha wananchi wale wanalipwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani tumeshafanya tathmini na kila kitu leo unakuja kumwambia mnazi wake ulikuwa asilimia 50 sasa hivi mnazi umefika asilimia 100 umlipe kwa thamani ile ya asilimia 50 haiwezekani! lazima wa- consider time value of money kwa sababu ni muda mrefu sasa umepita. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nizungumze suala la elimu nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kuwapa mabinti second chance ya kurudi mashuleni baada ya kujifungua na inaonekana kuna baadhi ya watu ni kama wanaona kitu kile hakiwezekani, binafsi yangu nampongeza sana sana Mheshimiwa Rais kwa azma yake hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tujiulize katika Taifa letu hili sisi wanawake tulioolewa tumetoa second chance mara ngapi kwa waume zetu labda wanapotutenda au akina Baba mmetoa second chance mara ngapi kwa wake zenu wanapowatenda, inakuwaje binti aliyepata ujauzito asipewe second chance ya kurudi shuleni? Mimi ninampongeza sana Mheshimiwa Rais amejipanga vizuri, kuhakikisha kwamba no one is left behind katika maendeleo endelevu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshauri sana Mheshimiwa Rais wetu pamoja na Serikali yetu kwamba ili sasa Binti yule ayafikie malengo ambayo Mheshimiwa Rais wetu anayatamani na ninafikiri hii itakuwa legacy kubwa kwa Mheshimiwa Rais ni kuhakikisha anajenga mabweni nchi nzima kuwapunguzia watoto wanaotembea mwendo mrefu na hapo katikati ndiyo wanapopata vishawishi na kuharibiwa, pia kuwatengenezea mazingira wezeshi ya kuweza kusoma kwa bidii. Naiomba sana Serikali iweke legacy hii wakati huu wa Mheshimiwa Rais wetu mwanamama kabisa, kuhakikisha wajukuu zake na watoto wa kike wanapata mazingira mazuri wezeshi ya kusoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuongezea hapo, naomba niikumbushe sasa Serikali ikamalizie bweni katika shule ya Sekondari ya Mfundia kwenye Kata ya Kerenge kule Korogwe Vijijini. Bweni limeshajengwa lakini limekaa muda mrefu halijakamilika, binafsi yangu nimekwenda kujitolea kupeleka milango katika bweni lile ili watoto wa kike waweze kusoma, lakini mazingira bado hayajakaa vizuri namuomba sana Mheshimiwa Waziri husika ahakikishe bweni lile kwenye shule ile ya Mfundia Korogwe Vijijini linakamilika na mabinti wetu waweze kusoma. Mtu ukitembea ukifika shule ya Mfundia hakika mazingira is very conducive kwa kupiga book lakini mabinti wanahangaika mazingira siyo wezeshi. Niiombe sana Serikali ikamilishe jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia niseme kwamba wakati tukimtazama Mheshimiwa Rais wetu jinsi ambavyo anapambana kwenda sambamba na dunia kama mwenyewe alivyosema ukitaka kwenda mbali nenda pamoja lakini ukitaka kwenda peke yako ina maana utakwenda haraka. Anaonyesha dhamira yake ya dhati kwenda na ulimwengu lakini cha ajabu sera zetu za nchi hii baadhi bado zipo nyuma. Wakati tunafikiria au dunia inazungumza maendeleo endelevu 17 kuna sera bado zipo kwenye maendeleo ya millennia! inasikitisha kwa kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaziomba zile Wizara ambazo bado zina sera zilizopitwa na wakati zirekebishe sera zao yaani kuna Wizara kila uki-google inakuletea sera ya mwaka 2002 wakati tumeshatoka huko sasa hivi tupo mwaka 2020. Tunaomba sana sera hizi ziboreshwe ili kwenda sambamba na mipango ya maendeleo endelevu kama ambavyo Mheshimiwa Rais anayatendea haki. (Makofi)

Mheshimiwa Rais amefanya vizuri kwenye lengo Namba Tano la Maendeleo Endelevu, lengo Namba 10 la Maendeleo Endelevu na hata alipokaa juzi na kutafuta maridhiano ametekeleza lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Dunia inakuaje sasa sera za ndani ya nchi mpaka leo nyingine zipo rasimu unakuwa na rasimu ya sera miaka mitano, miaka saba kwa nini zisikamilike ili kwenda sambamba na maono ya kidunia na maono ya Mheshimiwa Rais wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niishie hapa nashukuru sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi hii ya kuchangia. Pia nimshukuru Mwenyezi Mungu nwingi wa rehema mwenye enzi na utukufu. Nami naomba kuchangia kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka miwili iliyopita kwa mara ya kwanza nilipochangia hapa Bungeni nilinukuu usemi wa Rais wa 35 wa Marekani John Kennedy, aliposema kwamba “uchumi wa Marekani ni mzuri kwa sababu ya miundombinu yake na wala si miundombinu ya marekani ni mizuri kwa sababu ya uchumi wake”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu inaamini hivyo pia kwa sababu imetengeneza miradi mingi ikaipa majina ya miradi inayochochea uchumi shirikishi na uchumi shindanishi na imetengeneza miradi ya vielelezo. Kwa hiyo Serikali yetu pia inaamini katika hilo. Hata hivyo tatizo kubwa nililoliona ni kwamba utekelezaji wa miradi ni lazima uhakikishe pia hauongezi Deni la Taifa iwe ni Deni la ndani au Deni la nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu gani? Jambo hili linawezekana kutekeleza miradi bila kuongeza Deni la Taifa, hili linawezekana. Ila, pale tu ambapo hatuna budi ya Kwenda kukopa basi tukope mikopo ambayo ina masharti nafuu. Ambapo kama tunaipata IMF na World bank mikopo yote ile ina masharti nafuu na ndiyo tunaitumia kukopa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo nililoliona ni kwamba, tunahama sasa kutekeleza miradi yetu kwa kutokuongeza Deni la Taifa kwa kiwango kikubwa, tunakwenda kutaka kutekeleza miradi huku tukiliongeza Deni la Taifa kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano; umetanganzwa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kibaha – Mlandizi – Chalinze - Morogoro kwamba utajengwa under EPC+ Finance; kwa maana ya kwamba Mkandarasi anafanya usanifu, anafanya ujenzi na analeta mleta fedha ambaye ndiye huyo Financia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Waheshimiwa Wabunge wameonesha kweli tunahitaji kujenga miundombinu yetu bila kuongeza Deni kubwa la Taifa letu. Mheshimiwa Shabiby jana alisema ni vizuri tukijenga miradi yetu kwa kutumia PPP. Kamati imeeleza vizuri kwamba PPP ina changamoto ya sheria yake kwamba masharti ni magumu na mtaji uliowekwa ni kiwango kikubwa. Nafikiri sasa ni wakati sahihi Serikali ikafanya haraka kuirekebisha Sheria ya PPP ili tuweze kutekeleza miradi bila kuongeza Deni la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye PPP Mbia anajenga halafu ana-operate kwa faida baadaye anaturudishia Serikalini wakati huo huo hakuna interest ambayo sisi tumeichukua kutoka kwake. Kwa hiyo PPP ni njia sahihi n ani nzuri kwa ajili ya kutekeleza miradi yetu bila kuongeza Deni la Taifa na EPC+Finance tunahitaji tui-study vizuri sana kabla ya kuingia kwenye njia hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, njia nyingine ambayo kama Taifa itatusaidia sana kufanya miradi yetu bila kuongeza Deni la Taifa ni kwa kutumia infrastructure bond; na tumekuwa tukilisema hili mara kadhaa. Kwenye infrastructure bond tunachochea uchumi shirikishi. Wananchi wenyewe wa Tanzania wanashiriki katika kutekeleza miradi yao ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenye uzoefu na treasury bills wanaweza kusema hapa. Watanzania wapo wengi wenye fedha ambao wanaweza wakatoa milioni kadhaa wakaweka kwa muda wa miaka mitano,kumi au kumi na tano; na sisi kupitia fuel levy ambayo tunapata bilioni 900 kila mwaka, tunaweza kutenga bilioni 300 kila mwaka kwa ajili ya kurudisha hizi bonds za watu. Kwa nini tusitumie njia hii ambayo itatusaidia Watanzania wenyewe kuweza kujiletea maendeleo wakati huo huo deni la taifa halikui? Hata hivyo tumeitangaza barabara ile kwamba tutaijenga under EPC+Finance; je, kiuhalisia tunakopesheka sasa hivi? Mimi ninavyoona, ni kama tumeshamaliza quarter yetu yote. Sasa huyu financier anayekuja, tunaendaje kuchukua pesa kutoka kwake wakati tumemaliza quarter yetu yote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile huyu financier siyo yale mashirika makubwa ya dunia kama vile African Development Bank, IMF na World Bank, tuna uhakika gani na riba yake kama haitakuwa kubwa kuliko ya World Bank na IMF? Kwa sababu tumekuwa tukitekeleza miradi ya design and build kwa kutumia mtindo wa kwamba tuna design tuna-build halafu tunaomba mkopo World Bank au IMF au African Development Bank, halafu tunaulipa kwa riba ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunarudi kwenye EPC plus finance ambako vile vile Mkandarasi anabuni na kujenga, lakini anakuja na financier. Je, huyu financier riba yake itakuwa ndogo kama ya World Bank? Itakuwa ndogo kama ya African Development Bank? Itakuwa ndogo kama ya IMF? Kwa hiyo, mimi na-discourage EPC plus finance, we better tukaamua kukaa chini na kuiangalia vizuri infrastructure bond. Wenzetu wameweza kufanya haya, kwa nini sisi Tanzania tunaogopa kuingia kwenye infastracture bond?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ghana wanatekeleza miradi yao kwa kutumia infrastructure bond, Kenya imetengeneza sheria ya kufanya hivyo kwa kutumia infrastructure bond, sisi tunaogopa nini? Tunahitaji uchumi shirikishi na infrastructure bond inamwezesha Mtanzania kuweza kujenga barabara zake na yeye kuchangia maendeleo yake. Inakuwaje tuna- hesitate kuingia katika njia hii? Shida iko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria yetu ilivyo sasa hivi, mwenye mamlaka ya kukopa ni Wizara ya Fedha peke yake. Wenzetu South Africa wanatekeleza EPC+Finance lakini wameipa Road Authority mamlaka ya kukopa. Maana yake ni kwamba inapotokea hali kama hii ya sasa kwamba quarter yetu tumeimaliza, Road Authority ana mamlaka ya kukopa; lakini sisi sasa hivi hatuwezi kutekeleza under EPC+Finance. Kwa nini tusitumie infrastructure bond kutengeneza uchumi shirikishi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa katika nchi zote za SADC, ni Tanzania peke yake ndiyo haina toll road so far. Ni dhana tu ambayo imejengeka kwamba toll road ni mpaka zijengwe na hela za mbia labda IPP ndiyo tutengeneze toll roads, siyo kweli. Nchi kama Zambia hata madaraja yao ikiwa na span zaidi ya 100 tu inakuwa ni toll, watu wanalipia. Unaona! Kwa hiyo, pale pale tunakuwa tuna-generate mapato ya ndani kuweza kuendeleza miundombinu yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi huko nyuma miaka ya 1990, nimejaribu kutafuta na kupitia, tuliwahi kuwa na toll gates Ubungo, Chalinze, Makambako na Segera. Magari yalikuwa yanasimama na yanalipia, lakini sasa hivi tumetengeneza mentality ya kwamba mpaka tujenge under PPP ndiyo tunaweza tukaweka toll roads, siyo kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiingia Zambia, ukisoma Road Authority yake kwenye annual report inaonesha wazi kwamba wana-operate na both. Wanafanya toll roads na vilevile wanatumia fuel levy. Kwa nini sisi tushindwe kwenda kama nchi za wenzetu za jirani? Nimemaliza hapo na-insist tujenge kwa kutumia infrastructure bond ili tuweze kuwa na uchumi shirikishi na vilevile tuweze kupunguza deni la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kuhusiana na TAA. Kwa mujibu wa malengo yaliyowekwa kwa kuanzisha TAA, imepewa jukumu la kuendeleza miundombinu na vilevile kwa maelezo ya ICAO (International Civil Aviation Organization) inataka kila Mamlaka ya Viwanja vya Ndege iwe na chanzo cha mapato; na sisi tumeweka Passenger Service Charge ambayo tunapata Shilingi bilioni 65 kila mwaka ili iweze kuendeleza viwanja vya ndege, lakini hii Shilingi bilioni 65 yote inachukuliwa na TRA na mamlaka iliyozalisha haipati hata Shilingi moja; je, tutaendelezaje viwanja hivyo vya ndege?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanya kazi nzuri, Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana kupitia Royal Tour, lakini so far viwanja vya ndege vina hali duni. Tuwarudishie TAA pesa yao ili waweze kuboresha viwanja vya ndege kwa mujibu wa vikao.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahasante sana kwa nafasi ya kuchangia ikiwa leo ni mara ya kwanza katika mwaka huu wa 2023; na sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye Enzi na Utukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata fursa hii ya kuchangia kwenye Kamati hizi mbili, na nitajikita kwenye Kamati ya Bajeti ambayo ina watu mahiri, makini na Bingwa kabisa. Napenda nitumie fursa hii kuwapongeza kwa kazi kubwa ambayo wanafanya na wanasikiliza kwa umakini maoni ya wataalamu waliopo ndani ya Bunge hili na kuweza kuyafanyia kazi. Nawapongeza sana Kamati ya Bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nakwenda kuchangia kipengele cha 2.11 inayohusu Pato la Taifa. Kamati imeishauri Serikali kuweka mikakati ya kuchochea uzalishaji katika sekta za uzalishaji kama vile utalii, kilimo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba niishauri kamati kuongezea yafuatayo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kuongeza Pato la Taifa tunafahamu mchango wa utalii katika Pato la Taifa. Na pato letu la Taifa walau lirudi pale kwenye asilimia saba kama ambavyo kama imesema. Tunafahamu Mheshimiwa Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ameshafanya kazi kubwa ya kulitangaza Taifa hili kwenye sekta nzima ya utalii. Lakini tusipokuwa makini kazi kubwa iliyofanywa na Mheshimiwa Rais inaweza isilete matunda tarajiwa kama tusipoamua kuboresha viwanja vya ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru Wizara ya Mawasiliano imekwenda juu ya Mlima Kilimanjaro ikaweka mtandao kule. Tusifikiri tu wanaweza kupeleka yaliyo mazuri kwa wenzao kwamba bwana nipo juu ya Mlima Kilimanjaro njooni Tanzania kuna hivi lakini pia wanaweza wakapeleka yaliyo mabaya kama tusipoamua kuboresha viwanja vya ndege nchini Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa International Civil Aviation Organization (ICAO) inazitaka kila mamlaka za viwanja vya ndege kuwa na vyanzo vya mapato. Sisi Tanzania tumeweka passenger service charge ambayo n idola 40 kwa kila anayesafiri kwenda nje na shilingi 10,000 kwa kila ambaye anasafiri ndani ya nchi. Hela ambayo katika low season tunapata bilioni 40 na katika high season tunafika bilioni 55. Fedha hizi zinachukuliwa na TRA na mamlaka ya viwanja vya ndege haiwezi kufanya lolote katika kuboresha viwanja vya ndege kwa sababu haina fedha ya kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni kwa nini mamlaka inayosimamia viwanja vya ndege (TCAA) iweze kuwa na mapato lakini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege isiwe na mapato?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni kwa nini Mamlaka inayosimamia Viwanja vya Ndege TCAA iweze kuwa na mapato lakini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege isiwe na mapato? Kwa hiyo ili kuifanya kazi ya Mheshimwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kulitangaza Taifa hili kupitia Royal Tour kuwa endelevu, ni lazima tuiache Mamlaka ya Viwanja vya Ndege iboreshe Viwanja vya Ndege kwa kuachiwa ile hela inayokusanywa kwa passenger service charge itumike na mamlaka ile na isiwe inang’ang’aniwa na TRA, wenyewe hawapati hata shilingi moja. Kwa mtindo huo hatuwezi kuifanya kazi nzuri ya royal tour kuwa kazi endelevu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa taarifa iliyopo ni kwamba Kenya wanafuata Sheria hii ya ICAO, wanakusanya Viwanja vya Ndege wenyewe, Rwanda wanafanya hivyo, Malaysia wanafanya hivyo. Kwa hiyo nchi nyingi za jirani zenye viwanja vya ndege ambavyo ni bora wameweza kukusanya hizi fedha wenyewe na kuboresha miundombinu yao. Sasa Tanzania tuamue sasa kufanya juhudi za Mheshimiwa Rais za Royal Tour kuwa sustainable na kuleta tija inayotarajiwa kwa kuhakikisha tuna viwanja vya ndege vilivyo bora kwa kuiachia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege fedha ile ya passenger service charge ili waweze kufanya kazi yao ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumekuwa tukishauri hapa kwamba Mamlaka ile iachiwe Wahandisi wa kuweza kufanya kazi zile za Kihandisi na suala hili limekuwa linapotoshwa kidogo hapa kidogo Bungeni kwamba, Wahandisi waliopo TANROADS hawawezi kufanya kazi katika Viwanja Vya Ndege. Issue siyo suala la Uhandisi hapa, issue ni Mamlaka ambayo TAA imepewa. Mhandisi aliyekuwepo TANROADS yuleyule anaweza kufanya kazi Viwanja vya Ndege kulekule, issue ni impact of the road ndiyo ambayo inaangaliwa katika design tu pale, ndege inaposhuka impact yake ni nini na gari inapopita barabarani impact yake ni nini. Kwa taarifa tu iliyopo Wahandisi waliosimamia Viwanja vya Ndege ndiyo walewale walihamishwa wakapelekwa TANROADS. Kwa hiyo suala siyo knowledge, suala ni mamlaka iliyopewa TAA, warudishiwe Wahandisi wao ili waweze kufanya kazi ipasavyo kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kuchangia kuhusiana na maoni mahususi ya Kamati ya Bajeti kipengele cha 7.1. Kamati imeishauri Serikali iandae mpango wa uhitaji wa rasilimali wa Taifa ili taaluma zinazozalishwa ziwe sawa na mahitaji ya maendeleo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza sana Kamati katika kipengele hiki, lakini naomba kusema kwamba suala la taaluma yetu nchini haliwezi kuanza katika level ya juu wakati mwanafunzi anakwenda Chuo Kikuu, suala la taaluma, suala la rasilimali watu linapaswa kuanzia tangu mtoto akiwa tumboni kwa mama yake. Sasa Mheshimiwa Rais amefanya mpango mzuri wa lishe lakini tuhakikishe kunakuwa na afua endelevu. Kukosekana kwa afua endelevu kumesababisha akinamama wajawazito wanakosa damu ya kutosha na vilevile kuzaa uzao ambao hauna afya njema. Ndiyo hapo tunasema Taifa linakuwa na udumavu, udumavu umeshuka sasa hivi kwa asilimia 34, lakini hakika tunapaswa kushuka zaidi ili tuweze kuzalisha Taifa lenye watu wenye uwezo wa kubuni, uwezo wa kufikiri na uwezo wa kufundishika. Kwa hiyo kama Taifa tunapozungumzia suala la rasilimali watu ni lazima tuwekeze nguvu huku chini mtoto anapokuwa tumboni na mtoto atakapozaliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa iliyopo nikwamba Tanzania tunazalisha mabubu kila kukicha, kadri siku zinavyoendelea idadi ya mabubu inaongezeka. Mwaka 2018/2019 tulikuwa na mabubu 6,103 nchini, lakini ninavyozungumza sasa hivi mwaka 2023 tuna mabubu 8,503 nchini. Serikali inatoa fedha nyingi katika shule za mabubu hapa nchini kwa ajili ya kuwezesha chakula chao, kuwalipa Walimu wao, lakini jambo hili kama lingeangaliwa tangu mtoto anapozaliwa idadi hii ya mabubu isingekuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoteza fedha nyingi unnecessarily, Serikali sasa iamue, kila mtoto anapozaliwa apimwe usikivu. Haya mambo yanawezekana, kila Hospitali ya Wilaya kuwe na kifaa cha kupimia usikivu kwa mtoto anapozaliwa na kifaa kile huwezi amini hakihitaji mabillion ya fedha, kina-range kwenye shilingi milioni nani mpaka milioni 10 kipimo cha kupima usikivu, lakini kwenye hospitali zetu zote za wilaya vifaa vile havipo, ni nini tunatengeneza na ni rasilimali gani tunaitaka nchini? Kwa hiyo Serikali iamue ku- save hizi fedha zote ambazo zinapotea bure, iongeze nguvu katika vifaa vinavyoweza kupima usikivu mara mtoto anapozaliwa. Nchi za wenzetu zinafanya hivyo, lakini sisi tunaangalia tu macho yake ya njano, amelia kwa wakati, amegeuzwa miguu chini, anaonekana mtoto yuko salama, lazima tufanye extra kwa ajili ya kupata afya bora ya mtoto aliyezaliwa ili Taifa lipate rasilimali zilizo bora zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nashukuru sana kwa fursa hii.(Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi mwenye Enzi na Utukufu kwa nafasi hii ya kusimama mahala hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nami nichukue nafasi hii pia kuwapongeza sana Mawaziri wa Wizara hii ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mawaziri wengine waliopita katika Wizara hii kwa hatua mbalimbali ambazo wanazichukua katika kuhakikisha kwamba taifa letu linakwenda kwenye elimu ambayo ina-respond to the middle of the time and society.

Mheshimiwa Naibu Spika ukisikiliza michango ya Wabunge wote ambao wamechangia tangu jana, hakika tunahitaji kama taifa kuwa na elimu ambayo ina-respond to the need of the time and society. Mheshimiwa Kishimba amekuwa akitoa mifano ambayo inaonekana kama mifano ya utani utani, lakini kiuhalisia ni kwamba tunahitaji elimu ambayo ina- respond to the need of the time and society. Maana ya kusema hivi ni nini, ni kwamba ni wakati sahihi kama taifa sasa tuendelee ku-enhance katika practical science.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa na vyuo vyetu ambavyo vinatoa elimu mbalimba za kiufundi. Kwa mfano labda tumekuwa tunasoma labda mechanical engineering, lakini kwenye mechanical engineering utakuta unafundishwa zaidi namna ya ku-resolve forces katika mifumo ile ambayo inaendesha mitambo ule badala ya kufundishwa pia na production. Kwa hiyo mimi nishauri, nishauri sana, badala ya kuwa Department ya Mechanical Engineering kama kweli tunataka kwenda kwenye Industry na elimu ambayo ina meet the need of time and society, tulipaswa kuwa na Mechanical Engineering and Production ili tuweze kutengeneza mind set ya production katika mifumo ya uzalishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzangu wametangulia kusema hapa kwamba lengo namba nne la Maendeleo Endelevu la Dunia ni Elimu. Lakini naomba niseme kwamba lengo lile linazungumzia quality education, lakini uhalisia nchini kwetu tuna inequality in acquiring education. Hakuna usawa nchini katika kupata elimu. Kwa nini nasema hivi; sote sisi ni mashahidi kwamba elimu tuliyonayo wala si ya kwetu tumefanya kuletewa na wakoloni. Mkoloni A aliingia Mkoa A, Mkoloni B aliingia Mkoa B na Mkoloni C aliingia Mikoa C. Tumeona hapa Curriculum au Mtaala wa Kwanza ulikuwa wa Ujerumani na Mtaala wa Pili wa Elimu ulikuwa wa Mwiingereza, lakini hatujawahi kusikia Mtaala wa Tatu wa Elimu ulikuwa ni wa Mwarabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nikizungumza hivi nazungumza kulenga kwamba hakuna usawa katika upatikanaji wa Elimu nchini Tanzania kwa sababu kuna mikoa bado ipo nyuma kielimu. Mikoa hii iko nyuma kielimu si kwa kutaka kwao. Kama ambavyo vilevile naweza nikasema Adolf Mkenda hakutaka kuzaliwa Kilimanjaro kama ambavyo Chikota hakuta kuzaliwa Mtwara; imetoka tu by chance. Vivyo hivyo Adolf Mkenda hakutaka Mjerumani aende Kilimanjaro bali ilitokea tu by chance. Kwa hiyo mimi nataka kusema kama nchi wakati tunafikiria kwenda kwenye quality education vilevile tufikirie kwenda kwenye equality in acquiring education. Kwa mujibu wa sustainable development goals tunasema kwamba no one should be left behind in stantiable development. Kwa hiyo kama hakuna equality kwenye education inamaana kuna watu bado wataendelea kubaki nyuma katika maendeleo endelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tafiti zinaonesha kwamba, mzazi ambaye hakufika au hakupata elimu ni ngumu mtoto wake kufika elimu ya juu. Tafiti pia zinaonesha kwamba, ili tuweze ku-brake poverty circle elimu ni factor muhimu sana. Nini nataka kusema, inamaana katika taifa hili bado kuna Mikoa itaendelea kuwa kwenye absolute poverty na wengine wataendelea kuwa hivyo kwa mujibu tu wa ukoloni ambao umetuletea elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimi ninaomba kama taifa, wakati tunakwenda kutengeneza au tunakwenda kufanya mapitio ya Sera ya Elimu vilevile tufanye tafiti ya kujua ni kwa nini baadhi ya mikoa nchini Tanzania iko nyuma kielimu. Na tuje na recommendations ambazo zitaweza kusaidia mikoa ile kuinuka kielimu bila kuathiri ambao wameshaendelea kielimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, na maana yangu ya kusema hivi ni nini, inawezekana tunapeleka resources mahala ambako hakuhitajiki resources hizo. Namaanisha kwamba inawezekana kuna mahala tunahitajika kuongeza nguvu za mind set and transformation change lakini tunapeleka mavitu ambayo mengine hayahitajiki. Kwa hiyo kama Taifa ninaomba sana tufanye tafiti kuja kujua ni kwa nini baadhi ya maeneo yako nyuma kielimu nchini Tanzania na maeneo mengine yako mbele kielimu na tuje na recommendations ambazo zitakazotuwezesha kutengeneza mtaala utakao-meet u-meet the need of the time and society.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile, kama taifa letu tunapaswa pia Elimu i-align na mipango mingine ya taifa hili. Nimejaribu kupitia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ile item 2114 ya Usimamizi wa Elimu Maalum; na kuna utekelezaji kadhaa pale ambao umefanyika. Hata hivyo kiuhalisia bado inaonekana kwenye elimu maalum tuko nyuma ya wakati. Tumeshindwa ku-align na mipango mingine ya taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye elimu maalum kuna haja ya kuzalisha walimu wa speech therapy ili kwenda sawa na mipango ya Wizara nyingine za taifa letu. Serikali imeshatumia billions of money wamepeleka watoto India kwenda kupandikiza usikivu, lakini wanaporudi nchini watoto wale hakuna mahala ambako wanawekwa ili ku-develop speech. Hakuna madarasa ambayo yameingizwa katika elimu maalum ili watoto wale waweze ku-develop speech na walimu...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante, kengele ya pili. Ahsante kwa mchango mzuri.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: …kama Taifa tuone namna ya ku-align mipango yetu na mipango ya elimu pamoja na mipango mingine ili watoto wetu waweze kupata kile ambacho kinahitajika kupatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote nimpwekeshe Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa neema kubwa ya Rais wetu tuliyenaye Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na watendaji wake mahiri, wazalendo, wenye kupambana kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake kwa jitihada kubwa na mahangaiko makubwa mnayoyafanya kuhakikisha
rasilimali maji inakuwa chanzo kikuu cha maendeleo ya Taifa letu. Lazima tuwe wakweli kwamba Mheshimiwa Aweso pamoja na Naibu Waziri wake wamekuwa wanahangaika sana kipindi kirefu kwa sababu, ni miaka mingi miundombinu ya maji haikuwa inafanyiwa matengenezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu ya maji ni chakavu Tanzania hii, na ndiyo sababu imesababisha katikakatika ya maji kila kukicha. Kwa hiyo, Serikali hii ya Mama Samia Suluhu Hassan inafanya jitihada kubwa kuanza kuboresha miundombinu ya zamani ya maji pamoja na miradi ile chechefu ambayo imeshafanyika, pia kutengeneza miundombinu mipya ya maji. Naipongeza sana sana Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan. Hakika imedhamiria kabisa kuleta huduma bora kwa wananchi wa Tanzania. Bila shaka, haihitaji tochi. Kazi kubwa ya Mama Samia Suluhu Hassan inafanyika, na watendaji wake wako mahiri kabisa kuhakikisha wanafanya kazi vizuri kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania amesema Waziri leo wakati anazungumza kwenye hotuba yake na Mheshimiwa Kapufi naye amezungumza, ni kwamba, sisi Tanzania ndiyo wa kwanza Afrika kuwa na maziwa makubwa Afrika nzima. Pia Tanzania ndiyo wa pili Afrika ukiacha DRC Kongo kwa water bodies. Vile vile, kiukweli so far so good, rasilimali maji hii tunavyoiangalia, ni kwa jicho la huduma tu zaidi, hatujaangalia potential kubwa ya maji tuliyonayo Tanzania katika upande pia wa kuongeza mapato ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababu gani? Naomba niseme wazi, kaka yangu, Mheshimiwa Aweso, nakupenda sana, unajua; na umewasifia sana watendaji wako, ni vizuri kuwa na imani kubwa na watendaji wako, ni jambo jema, lakini mimi nasema hapa, Wahandisi wa rasilimali maji wa Bodi za Mabonde ya Maji, bado hawajafanya assignment yao sawasawa kukusaidia kufanya kazi yako vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivi? Mpaka leo, juu ya potential kubwa tuliyonayo ya maji, hatuna Integrated Water Master Plan Tanzania, hatuna. Kamati imezungumza hapa kwamba tunahitaji National Water Master Plan. Master Plan tulizokuwanazo mpaka sasa ni za mikoa mikoa; ya Mkoa wa Tanga ni ya mwaka 1976; ya Mkoa wa Ruvuma, Kigoma na Iringa ni ya mwaka 1982. Ukisoma Water Master Plan zile za mikoa, utagundua kwamba inaonesha tu maeneo ambayo unaweza kupata maji, lakini hakuna details za undani zaidi, kwa maana maji yale yako kwa kiwango gani? Maji yale yana ubora gani? Naamini wahandisi wa rasilimali maji, kama watafanya tafiti ipasavyo, hivi vitu vinaweza kujulikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, madhara yake ni nini? Madhara ya kutokujulikana kiwango cha maji kilichopo. Leo umetutajia uhitaji wa maji kwamba ni Shilingi bilioni 60 meter cubic, lakini hizo nina uhakika umeangalia consumption per person, ukazidisha na idadi ya Watanzania. Kwa hiyo, watu wa bodi za maji wanapaswa kufanya tafiti kujua underground water scope ikoje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa na kasumba kubwa ya kuchimba visima. Tunachimba sana visima na Wabunge hapa tunaonekana tunahitaji sana kuchimba visima, lakini bodi za maji ndiyo zinapaswa kututengenezea mechanism ya kuhakikisha visima vile vitaendelea kuwa na maji. Hiyo inawezekanaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima wa-establish coordinates katika visima vilivyopo sasa na waweze kuonesha underground water channel, relationship yake na kisima kipya kinachojengwa. Kwa sababu mkondo wa maji una tabia wa kunyang’anyana maji. Visima vingi vikichimbwa sehemu moja, bila kujua capacity yake kule chini, ina maana kwamba kisima kimoja kitanyang’anya maji upande mwingine, at the end of the day ni kwamba visima vinakauka na hakuna sustainability. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimshauri sana kaka yangu kipenzi, watu wa bonde za maji wafanye tafiti ya kutosha, watuambie scope ya underground water. Kwa sababu huwezi kufanya management yoyote ya maji kama hujui capacity uliyonayo underground. Leo miji inatanuka, watu wanaongezeka, tunachimba visima kiholela, mwisho wa siku inaonekana miradi siyo sustainable, kwamba maji hayatoshi, maji yanakatika, ni kwa sababu bodi za maji; Wahandisi wa Rasilimali Maji hamjafanya tafiti za kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana mumsaidie ndugu yangu yule. Mheshimiwa Aweso ni mzalendo, anapambana, na ana maono mapana kwa ajili ya Wizara hii ya Maji. Msaidieni vya kutosha. Anaweza kufanya makubwa zaidi mkimpa mawazo. Ninyi ni wataalam, mko pale, fanyeni assignment yenu sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naomba kuzungumzia, katika nchi ya Uholanzi, wenzetu sasa hivi, ile distribution ya water supply, anakaa ofisini, anai-monitor through GSI Technic (Geographical Information System Technic), inamwezesha ku-monitor distribution ya water supply. Hii ndiyo imesaidia ku-manage upotevu wa maji. Tuna maji mengi yanapotea lakini hatuna proper management ya upotevu wa maji. Sisi tuna wadau, tuna wahisani, tunashirikiana na nchi mbalimbali na wadau wako tayari, tunashirikiananao, watuwezeshe upande huu ili tuweze kudhibiti upotevu wa maji kwa kiwango kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiweza kufanya tafiti za kutosha, ina maana tutaweza hata kuvuna maji, tutaweza hata kuondoa chumvi kwenye maji, lakini watu wa mabonde ya maji bado hamjafanya assignment yenu sawasawa, na potential kubwa ya maji tuliyonayo Tanzania, bado hamjaiangalia kwenye jicho la kiuchumi. Miundombuni imekuwa chakavu muda mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Tanga uwekezaji mkubwa ulifanyika kuanzia miaka 1990 na 1995. Wakati huo miundombinu yote imeshakuwa mibovu, maji yanakatika kila siku. Ina maana hakuna proper strategic maintenance program ya miradi ya maji. Kwa nini leo imeji-accumulate miradi mingi kwa wakati mmoja? Ni kwa sababu hiyo. Huko nyuma mmeshindwa kufanya ipasavyo. Sasa msimwangushe Mheshimiwa Aweso.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Aweso amekiri wazi kwamba, ule usemi wako unasemaje? Ukinizingua, tutazinguana. Yuko very serious na anachokifanya, msimzingue. Tunatamani Wahandisi mfanye kazi zenu vizuri, kwa ueledi na maarifa. Fanyeni tafiti za kutosha. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Eng. Mwanaisha.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Nilikuwa…

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia mbili na tano. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Nishati
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi ya kuchangia.

Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mwenye enzi na utukufu kwa kuniwezesha kusimama mahali hapa muda na wakati kama huu. Nichukue fursa hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuboresha hali ya maisha ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika kazi kubwa amefanya katika Wizara mbalimbali, katika Wizara hii ya leo mahsusi kabisa hakika Mama amefanya mengi ambayo tunapaswa kuyasemea vizuri bila woga kabisa. Mama amefanya ubunifu katika suala zima la kumalizia mradi mkubwa huu wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pia ameongeza ubunifu mkubwa katika usambazaji, usafirishaji wa umeme nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika nimeisikiliza vizuri hotuba ya Mheshimiwa Waziri, hotuba hii imesheheni mikakati mizuri na mikubwa ambayo Serikali wameipanga kuhakikisha kwamba tunakwenda kupata umeme wa uhakika. Niwaombe ndugu zangu Wabunge mapungufu madogo madogo yaliyokuwepo kwa mikakati hii iliyotajwa leo, ninahakika inakwenda kuisha kabla ya kufika 2025. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema hivi kwa sababu gani? Sasa hivi shirika la umeme nchini linauwezo wa kufua megawatt 1822 mpaka kufikia Mei, 2023 mahitaji halisi ni 1431. Maana yake TANESCO kwa uboreshaji wa mitambo iliyokuwa chakavu sasa inakwenda kuzidi kiwango kinachotarajiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, nimepita kwenye banda pale nimeona kwenye real time display majira ya saa nane mchana, umeme ulikuwa unazalishwa megawatt 1,426 na vituo vyote kuanzia Mtera, Pangani, Kihansi, Hale mitambo yote ilikuwa on time inafanya kazi zake sawa sawa. Vilevile, hata mashine sita za Songas zote zinafanya kazi vizuri sasa hivi. Ni mashine moja tu pale Songas ndiyo inafanyiwa matengenezo na pale kwetu Hale mashine moja tu ndiyo ambayo ilikuwa haifanyi kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niiombe Serikali ifanye hima na kumalizia matengenezo katika kituo cha Hale, vilevile na ile mashine moja ya pale Songas iweze kuzalisha umeme ipasavyo. Naiona dhamira kubwa na njema ya Serikali yetu kuhakikisha tunapata umeme wa uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisemee kidogo mradi unaoendelea wa Bwawa la Mwalimu Nyerere. Hakika juzi nimepita kwenye Boots zile za nishati na nimeweza kushuhudia mradi ule kupitia Visual video ya mradi ule mzima. Hakika binfasi nime–fall in love with that project. Hakika natamani nipate kama siku tatu au nne niende nikatembelee mradi ule. Ni mradi mtamu sana kwa mafundisho makubwa ya Taifa letu na ni mradi wa kihistoria kabisa. Ninaiomba sana Serikali na hii naamini ni shemu ya contract administration, tuhakikishe kwamba material yote yaliyotumika katika mradi ule yanahifadhiwa mahali maalum, iwe kama ni museum ya mradi ule kwa ajili ya vizazi vijavyo kuendelea kujifunza kwenye bwawa lile, nina hakika hata kwa ajili ya future maintenance program, material zile zilizotumika sasa zikihifadhiwa vizuri itajulikana kwa urahisi zaidi kwa ajili ya matengenezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona wenzetu wa hitches on bridge wameweza kufanya museum ambayo kila anayekwenda anaona material yote ya mradi ule ulivyotengenezwa lakini kama ninyi ambavyo mmeonesha ubunifu wa cameras zile ambazo tumefanya visual observation ya mradi ule vilevile, na wao wameweka darubini ambayo mtu anaweza akaingiza hela pale na akawa anaona hitches on bridge jinsi ambavyo ina-operate. Kwa hiyo, kwa namna hiyo tunaweza tukapata hela ndogo ndogo kwa ajili ya kufanya utalii wa ndani kupitia mradi ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeona Aswan Dam ya Egypty, tumeona Akasombo Dam ya Ghana, wenzetu wanatumia Dam zile kiutalii pia. Niombe sana Kaka yangu naamini ubunifu wako, umeonesha makubwa ndani ya kipindi chako na hili mkashirikiane na Wizara ya Maliasili na Utalii tuweze kupata utalii wa ndani kwa maana ya kupata boat tuweze ku–sell around the dam na tuweze ku–enjoy neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inapendeza zaidi kwa sababu tayari kuna mbuga ya Mwalimu Nyerere katika eneo lile, ni nafasi nzuri kabisa ya kutengeneza kind of resorts ndani ya maeneo yale ili kuweza kuvutia zaidi watalii na liingizwe bwawa lile katika utalii wa Afrika. Kwa sababu ni bwawa ambalo naamini kwa ukubwa litakuwa ndilo la pili ukitoa la Ethiopia. Wenzetu wa Egypt ambao wanatujengea nao tumekwishawapiga chini, wapo na 2110 sisi tuna 2115. Kwa hiyo, ni mradi wa heshima ni mradi wa kihistoria kwa Taifa leu. Ninawapongeza sana Serikali kwa juhudi kubwa mnazozifanya kuhakikisha mradi huu unakamilika vizuri na hakuna longo longo pigeni kazi, msiogope maneno ya wanaosema, kazi yenu inaonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kaka yangu January nikutie nguvu na nikutie moyo kwamba katika Quran sura ya 41 katika ayatul hashir inasema hivi “Tahsabuhum Jami’an wa qulubuhum Syattaa” utawaona watu wameunganisha nguvu kama vile ni wamoja lakini nyoyo zao zina uadui. Wanaunganisha tu nguvu ili wa defeat the strong, you know you can’t strengthen the weak by weakening the strong. Kwa hiyo, Kaka yangu nikwambie piga kazi, kazi yako ni kubwa na mimi nimeielewa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii pia kuipongeza Serikali kwa kutuletea transformer ya megawatt 55 pale katika kituo cha Majani mapana. Kazi hii tunaishukuru sana Serikali kwa sababu wale wawekezaji na wenye viwanda waliokuwa wakilalamika kwa sababu ya low voltage tatizo hilo Tanga linakwenda kuisha kabisa. Naomba kutumia fursa hii kuwambia wawekezaji popote walipo karibuni Tanga, tuna uwezo mkubwa wa umeme wa kuhudumia viwanda vyote vya Tanga vilivyopo sasa hivi na hata viwanda vingine vijavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru sana kwa transformer ile ambayo sasa hivi imekwishafika site na inafungwa bado tu Commissioning. Tunashukuru sana Serikali, Watendaji wa TANESCO, Ndugu yangu Maharage kazi yako ni njema, mmejipanga vizuri na sisi tunaona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika nakumbuka kuunganishiwa umeme ilikuwa inachukua mpaka miezi mitatu, chini ya uongozi wa Maharage sasa hivi baada ya kulipia umeme unakufikia nyumbani ndani ya siku nne. Ni mapinduzi makubwa ambayo Watanzania tunapaswa kuwapa nguvu na moyo ndugu zetu hawa ambao wana nia njema ya kuliendeleza Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niwapongeze Serikali nimeona mmetenga fedha kwa ajili ya gridi imara, ni jambo kubwa ambalo litaimarisha umeme wa maeneo yetu. Kule Simiyu, Ruvuma, Kilindi kote tunakwenda kunufaika na mradi huu wa gridi imara. Hakika ninayaona mapinduzi makubwa katika sekta hii ya nishati kwa uboreshaji huu wa gridi imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ahsante sana. (Makofi)
Azimio la Bunge Kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba Baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa Lengo la Kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuchangia katika jambo hili tukufu kabisa lenye mustakabali mpana wa maendeleo ya Taifa letu. I(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na mimi kupata fursa ya kuchangia katika makubaliano ya kukubaliana na nchi ya Dubai katika kuendesha baadhi ya maeneo katika bandari zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwamba naomba ni–declare interest, niliyesimama mbele yenu niliwahi kuwa Manager wa Usimamizi wa Mradi katika Bandari ya Dar es Salaam upanuzi kutoka gati…

SPIKA: Mheshimiwa Mwanaisha Ulenge, ngoja tuliweke vizuri hili.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Ndiyo.

SPIKA: Tunapojadili mkataba wa namna hii, ukasema unataka kuweka maslahi yako wazi na ni mkataba unaohusu uwekezaji, maana yake una maslahi ya kifedha kwenye hawa wawekezaji moja wapo.

Sasa kama ni hoja ya kusema umeshawahi kufanya kazi mahali, ama unamfahamu fulani nenda moja kwa moja, ondoa hayo maneno yako unataka kuonesha maslahi yako kuwa wazi kwenye jambo hili. (Makofi)

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Dhamira yangu ni kutaka kusema kwamba ni nina uzoefu na bandari na yale upanuzi uliofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam na katika kitu ambacho ninakikumbuka mpaka leo ni kwamba Bandari ya Dar es Salaam imepanuliwa kutoka gati zero mpaka gati namba 7 na bado tunakwenda kupanua gati namba 8 mpaka gati namba 11. Haya yanayokwenda kufanyika sasa hivi ya kutafuta mbia kuendesha Bandari ya Dar es Salaam katika baadhi ya maeneo ninasema Mama Samia anaendelea kuwa mtekelezaji wa yale aliyokwishatangulia akiwa kama Makamu wa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama Mama Samia amefanya mengi katika SGR na katika mengine yote ambayo ameshirikiana na mtangulizi wake yeye akiwa Makamu wa Rais, naomba niwaambie Watanzania popote mlipo na hili la uwekezaji wa kumpata mbia katika Bandari ya Dar es Salaam ni sehemu ya muendelezo ule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu gani? Makubaliano na liyetupa fedha ambaye ilikuwa ni Benki ya Dunia mwaka 2017 alipotupa mkopo wa dola za milioni 305 katika Bandari ya Dar es Salaam kutengeneza ile jumla ya milioni 421 ambayo ndiyo trilioni moja ya Tanzania ambayo imetumika kuwekeza katika Bandari ya Dar es Salaam miongoni mwa loan agreement iliyoingiwa na ile Benki ya Dunia ni kuhakikisha kwamba tunaweza kurudisha fedha ile tuliyowekeza pale kwa haraka na Benki ya Dunia katika makubaliano yale imezungumza na sisi tukayakubali kwamba bandari ile itaendeshwa kwa ubia, imesema wazi kwenye loan agreement mwaka 2017. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa niseme kwamba Serikali haikukurupuka wala Mama Samia hakukurupuka kama ambavyo wengi walidhani wamefikiri. Mama Samia anafanyakazi kwa mujibu wa maandiko ambayo ameyakuta muda mrefu katika Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwamba uwekezaji wote mkubwa unaofanyika katika Taifa letu na katika nchi zozote duniani hauwezi kufanyika kwa kukurupuka tu, ni lazima tafiti, ni lazima stadi zifanyike, ni lazima tutafute traffic forecasting, haiwezekani tufikirie mwekezaji leo kama hatujaangalia Bandari ya Dar es Salaam mwaka 2045 itakuwa na mzigo gani? Haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niwaambie Watanzania, Port Master Plan ya mwaka 2008 ambayo imefanyiwa mapitio mwaka 2018 na Mhandisi mshauri anayeitwa Anova Consult ambaye wala si Mtanzania, katika taarifa yake ya mwisho yote yanayofanyika sasa hivi katika Taifa letu kuanzia upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Tanga, Bandari ya Mtwara, SGR yote yako katika maandiko yaliyofanyiwa tafiti. Serikali haikurupuki, Serikali inafanya mambo kwa maandiko, Watanzania tujifunze kusoma, Watanzania tujifunze kutafuta taarifa, Watanzania tusiishi kwa hofu, tujifunze zaidi hii ni summary report hii ni taarifa fupi ya Port Master Plan ya mwaka 2008 inazungumza yote hayo na page ya 31 mpaka 34 inazungumza suala zima la mzigo utakaokuja Bandari ya Dar es Salaam mpaka mwaka 2045. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile limezungumzwa kwenye page ya 32 suala zima la upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam na vilevile katika page ya 34 imezungumza suala zima la Bandari ya Dar es Salaam kuendeshwa under PPP. (Makofi)

Sasa niwaambie ndugu zangu, Serikali yetu haiongozwi na watu wasiokuwa na akili timamu, Serikali yetu inaongozwa na watu wenye akili madhubuti. Watanzania sisi tusiyumbishwe na kupelekwa pelekwa haya mambo yako kwenye maandishi, tujifunzeni kusoma Watanzania. Inavyoonekana ni kama vile Mheshimiwa Rais amekwenda Dubai, akatekwa tu, akasaini tu yaliyosaniwa, siyo kweli. Ni kumkosea heshima Mheshimiwa Rais wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mama yule ni mama makini, mama yule ni mama mwenye kuipenda Tanznaia kwa mapenzi makubwa sana. Ni fedheha huku kuendelea kusema kama sisi tunaweza kununuliwa bahasha hii ninunuliwe mimi Mwanaisha Ulenge? Bahasha hii nyepesi namna hii ininunue mimi? I see, Watanzania naomba muwe na imani kubwa na Serikali yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali hii ina masikio na Serikali hii ina macho, Serikali hii ina wataalam, Serikali hii inafanya tafiti. Kwa hiyo, naomba niwaambie Mama Samia ndiyo kidedea wa kutekeleza hata yaliyokuwa yamefichamana. Haya anayoyatekeleza mama Samia yalikuwa kwenye maandishi tangu mwaka 2008, Mama Samia leo anakuja kutekeleza. Mama huyu ni kichwa mwanamama wa Kizimkazi, Mungu anedelee kumsimamia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumekuwa na tabia Watanzania ya kujilinganisha na Singapore kwamba mwaka 1960 Singapore ilikuwa masikini kama sisi. Tumekuwa na tabia ya kujilinganisha na South Korea kwamba mwaka 1960 ilikuwa kama sisi, lakini tumekuwa na tabia ya kujilinganisha na Malaysia kwamba walikuwa kama sisi.

Sasa katika kitabu hiki nilichokishika mkononi hapa ambacho kimeandikwa na Mtanzania mwenzetu aliyefanya tafiti za Afrika nzima...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Malizia kwa sekunde 30.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: ...ambacho kinaitwa Poverty within, not in the skin kinaeleza kwamba Malaysia, Singapore and South Korea walitoka katika umaskini ule kufikia walipofikia sasa kwa sababu waliamua kuingia katika advancement in technology.

SPIKA: Haya ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote, nimshukuru Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile, nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya kuboresha uchumi na maisha bora kwa Watanzania. Kwa hakika naomba nifanye nukuu kutoka kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri na nimekuwa nikilisemea hili kwamba Mama Samia anapiga kote kote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huo anafanya miradi mikubwa na midogo, wakati huo huo wastaafu wanapata stahiki zao, wafanyakazi wamepandishwa madaraja na wamelipwa mishahara. Hakika Mama anastahili maua kama alivyosema Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba. Vile vile, tunasema Mama yuko kazini na kazi inaendelea. Pia, wale ambao waliofikiri Mama Samia hawezi, hakika wameona anakwenda anafukunyua, anaibua ili kuhakikisha kwamba anafanya kazi yake sawasawa. Kwa hiyo, niwaombe Watanzania waelewe kwamba hakuna wakati wa kumpangia. Kuna wakati watasema ana–copy na ku–paste kwa sababu wanawake hawawezi, Hapana, wanawake tunaweza, tuna–initiate, tunabuni na tunasogeza. Mama yuko kazini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie bajeti hii ya 2023/2024. Niipongeze Serikali kwenye suala zima la kuongeza mapato. Nitachangia vipengele viwili vya ukurasa wa 27 na ukurasa wa nane kwenye Mapato na Uchumi wa Kidigitali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikali, Desemba, 2022 waliweza kufanikiwa kukusanya zaidi kwa kupata trilioni 2.53 ambazo hazijawahi kutokea kukusanywa, zimekusanywa kipindi hiki cha Mama Samia Suluhu Hassan. Vile vile, Serikali imekiri kwamba mafanikio yale yalitokana na kuboresha mifumo. Hata hivyo, bado naamini na Serikali inaamini hivyo kwamba tunaweza kukusanya zaidi mapato yetu ya ndani. Pia, wengi wamezungumza hapa kuhusu suala zima la kuongeza mapato ya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nishauri kwenye suala zima la uchumi wa kidigitali. Sasa hivi Serikali imebuni lakini tunategemea EFD machine pekee katika kuhakikisha kwamba tunakusanya kodi. Hata hivyo, kwenye EFD tunajua kulingana na baadhi ya Watanzania ambavyo walivyo, hawataki kulipa kodi utakuta mtu amenunua kitu cha 100,000 anapewa risiti ya 10,000 au wakati mwingine hapewi risiti kabisa. Sasa, nini kifanyike kuhakikisha kwamba automatic by default mfanyabiashara atahakikisha analipa kodi? Nafikiri ni increase visibility ya cash flow ya mfanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Taifa tunaweza kujua kila simu ya Mtanzania inayoingia imepigwa kwa dakika ngapi na shilingi ngapi, nina hakika kabisa kwa kutumia uchumi wa kidigitali, tunaweza kujua cash flow ya kila mfanyabiashara nchini. Pia, iwapo cash flow yake itakuwa visible, there is no way huyu mtu atakwepa kulipa kodi, atalipa kodi accordingly.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kutumia uchumi wa kidigitali, naomba sana tu–encourage kulipa malipo kwa Lipa namba, tu–encourage kuhakikisha VISA Card zinatumika, tuhakikishe kwmba tuna–discourage malipo ya cash (cash money isitumike katika kuhakikisha tunafanya manunuzi). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakapokuwa tunalipa cashless kwa kutumia card, tuna increase visibility ya cash flow ya biashara yoyote ile nchini. Pia, itakuwa ni rahisi ya kuhakikisha kwamba mfanyabiashara analipa kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niishauri Serikali kuhakikisha kwamba inaweka utaratibu na mikakati ya kuhakikisha kwamba Watanzania hatulipi fedha taslimu (tunalipa kwa kutumia lipa namba na tunalipa kwa kutumia VISA Card). Of course, mwanzoni tutahitaji elimu, lakini hata mbuyu ulianza kama mchicha. Naamini Tanzania imeweza kubuni mambo mengi na ndio sababu tumeweza kusogea. Hivyo, hili pia linawezekana, tu–increase visibility ya cash flow ya mfanyabiashara yeyote yule, ni solution pekee ya kuhakikisha kwamba kodi inalipwa. Vile vile, through EFD only bado kodi inakwepwa. Hilo ni la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 43 umezungumzia uwezeshaji, viwanda na biashara. Sasa, wakati Serikali inasema imeendelea kuboresha mazingira ya kibiashara, nimekuwa najiuliza, kwa nini viwanda ambavyo vimekwishaanzishwa vinakufa? Serikali imefanya tathmini gani katika viwanda ambavyo vinakufa ili kuhakikisha havifi na vinasaidia kusimama? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kule kwetu Tanga, mimi roho inaniuma sana. Kiwanda cha Kutengeneza Mazulia ambacho kipo Tanga Mjini kimekufa wakati sisi ndio tunazalisha mkonge. Kwa nini Serikali haikuona haja ya kuweka juhudi kuhakikisha kiwanda kile hakifi? Kwa nini kule Lushoto Kiwanda cha Usambara Factory ambacho kinatengeneza tomato na nyanya zinazalishwa Lushoto, kwa nini kiwanda kile kimekufa? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali watakapokuja ku–windup watupe kwa nini viwanda hivi vimekufa na Serikali wamefanya juhudi gani kuhakikisha viwanda hivi havifi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi hii ya kuchangia. Awali ya yote namshukuru Mungu na nichukue fursa hii pia kuwapongeza sana Mawaziri wanaofanya kazi kwenye Wizara hii ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha Taifa letu linakua kwenye uchumi wa kidijitali, na pia kuhakikisha Taifa letu linakwenda kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia hapa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri mikakati mbalimbali ambayo wanayo kuhakikisha wanakwenda kuifanya kazi yao kikamilifu. Naomba nichangie kwenye suala zima la usalama mitandaoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ameeleza vizuri mikakati yake hapa, lakini kitu ambacho sijakisikia ni intrusion detection system. Mara nyingi matukio yanatokea halafu ndiyo watu wanaanza kuhangaika wakati tunaweza kutengeneza tools ambazo zitagundua mapema kabla mtu hajaweza kuiba. Wakati anataka kuingia kufanya uhalifu wake, tools zile zinaweza ku-detect.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana Wizara hii ikafanye kazi zaidi. Naamini weledi mkubwa wa wataalam waliopo kwenye Wizara hii. Tumempata Dkt. Mwesiga, ni mwalimu wangu, naamini uwezo wake katika mambo haya, pia tuna Dkt. Pido, watu wote hawa ni wataalam wazuri, waje na mifumo ambayo itagundua mapema wizi unaotaka kufanyika kabla tukio halijafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshangaa kuona baadhi ya Ofisi za Serikali watu wanaiba mitandaoni wakati tunaweza kutengeneza intrusion detection system zikagundua mapema mambo haya. Kwa hiyo, naomba sana katika mikakati yenu, mbebe na hili tuone tunakuja na mifumo ya kugundua mapema kabla jambo halijatokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba kusema kwamba, mwaka 2021 mwishoni tumeona kule Iringa, mfanyakazi wa Selcom ameweza kuhamisha Shilingi bilioni mbili na zaidi. Maana yake ni nini? Ni kwamba bado kuna shida ile ile katika wizi wa mitandaoni. Wakati kama Taifa tunakwenda kusema tunataka uchumi wa kidijitali, kuna mwananchi mmoja mmoja anazoroteshwa uchumi wake kidijitali. Suala la wizi wa mitandaoni ni tishio kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumewaaminisha wananchi kwamba tunaweza tukahifadhi fedha zetu mitandaoni, lakini bado kuna hali ngumu kwa sababu wizi huo ni mkubwa mno. Kwa hiyo, naomba niishauri sana Serikali ihakikishe haraka inakuja na ile sera. Sera hii imechelewa sana. Katika nchi 54 za Afrika, ni nchi 28 tu ambazo zimekuwa na sera hii na tunataka Tanzania tuwe miongoni mwao, tusisubiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona nchi za Ulaya wana ile General Data Protection Regulation, tunataka na sisi kama Taifa twende kwa mwendo huo. Tunahitaji huduma hizi kwa haraka. Wala tusiridhike na yaliyoletwa na ITU (International Telecommunication Union) kusema kwamba sisi tumekuwa wa pili kwa usalama mitandaoni. Jinsi ambavyo wamechukua survey ya data zile, is wrong. Huwezi kuchukua kwa kutumia mfumo wa questionnaire. Walitakiwa kutafuta uhakika zaidi. Tatizo hili la usalama mitandaoni ni kubwa. Naomba sana kama Taifa tulibebe kwa uzito wake na juhudi hizo ziongezwe kupata mifumo ambayo itagundua tatizo hilo mapema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba, sisi kule kwetu Kilindi tuna shida kubwa mno ya kukosa mawasilioano. Kwanza naipongeza Vodacom kwa initiative yake ya mfumo ule wa mama; ile program ya mama, ya kuhakikisha inatatua tatizo la dharura mama anapokuwa mjamzito. Ndiyo maana halisi ya Wizara hii, kurahisisha huduma fulani za kijamii. Nawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara hii i-support initiative ile ya Vodacom kuhakikisha inapeleka minara katika maeneo yale. Kwekivu, Kimbe, kule Kilindi hakuna kabisa mawasiliano. Yule mama mjamzito hata akipiga simu kwa yule dereva, dereva usiku hapatikani saa 8.00 ya usiku, tunatatua vipi tatizo lile? Inakuwaje katika kutatua tatizo la dharura? Tunaomba tupeleke minara ili wale akina mama waweze kutatua tatizo la kukimbia kwenye vituo vya afya kwa haraka zaidi na mapema zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

Mweshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania wa Mwaka 2022
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika Muswada huu wa Sheria ya Ulinzi Binafsi. Kipekee kabisa niipongeze Serikali hii ya Mama Samia Suluhu Hassan ambayo kwa hakika imeonesha uwezo mpana wa kufanya maoteo ya kesho kwa Taifa letu. Uwepo wa Muswada huu wa Sheria ya Taarifa Binafsi hakika ni matokeo ya kuwa na Serikali yenye maono mapana na kuiangalia kesho kwa upana wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia Muswada huu wa Sheria ya Taarifa Binafsi hakika ni Muswada sahihi kwa wakati sahihi ambao unakidhi haja ya sasa ya matakwa ya maendeleo ya kiteknolojia.

Mheshimiwa Spika, Sheria hii ya Taarifa Binafsi ukiangalia malengo yake na ukiangalia misingi yake kwa hakika imelenga kuleta maadili katika matumizi ya teknolojia ya Habari.

Mheshimiwa Spika, wanasayansi wanasema kwamba; the next world war will become between the human kind technology na wengine wanadiriki kusema kwamba the next pandemic itakuwa ni ya technology. Kwa hiyo niipongeze Serikali kwa maono mapana ya kuhakikisha Taifa hili tunakwenda kujikinga ipasavyo kwa ukuaji wa teknolojia hii.

Mheshimiwa Spika, katika Ibara ya 5 ya Muswada huu wa Sheria imezungumza suala zima la usafirishaji wa taarifa binafsi. Kipengele hiki kimenifurahisha kwa sababu moja kuu ifuatavyo; kama Taifa tumeweza kuiangalia maana halisi na muktadha pana wa teknolojia ya habari. Suala zima la kusafirisha taarifa binasfi linaweza kufanywa na mtu mwenyewe binafsi kwa kuji-subject katika mitandao ya kijamii, kwa maana ya kwamba unapoingiza taarifa zako huna uhakika wa asilimia mia moja kwamba facebook hatoweza kuzitumia vinginevyo. Vilevile tunajua kwamba makampuni yaliyopo ndani yanatumia software ambazo server zake hazipo humu nchini kwetu. Server zipo mbali huko katika Mataifa yaliyoendelea zaidi ya kiteknolojia, kwa maana data zinakuwa zinahamishwa whether tunataka au hatutaki, Sheria hii imembana mkusanyaji kuhakikisha kwamba anatengeneza sera kamilifu zitakazolinda usalama wa taarifa binafsi. Akienda kununua server huko aliponunua taifa hili atuhakikishie kwamba data zitakazokuwa served externally au internally zinaendelea kulindwa kwa usalama wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimefurahishwa mno na kipengele hiki Ibara ya 5 pamoja na Ibara ya 65 ambayo imemtaka mkusanyaji kutengeneza sera kwa ajili ya kulinda usalama wa taarifa binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwamba Sheria hii ni muhimu sana kwa Taifa letu, kama ambavyo wenzangu wengine wametangulia kuzungumza, katika kuuendea uchumi wa kidigitali sheria hii ina umuhimu wa aina yake. Vilevile sheria imeweka vizuri mazingira ya utekelezwaji kwa maana imeunda Tume na tume ikawekewa executive board itakayokuwa inadhibiti utekelezaji wa shughuli zake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile naomba niseme kwamba, katika Ibara ya 51muktadha mpana wa ukusanyaji wa mapato umeelezwa kwa maana ya vyanzo vya mapato, lakini bado naiona Serikali ina kazi ya kufanya katika eneo hili, tunahitaji kupata outline ya uwazi kuona ni kiasi gani ile muktadha halisi wa uchumi wa kidigitali unafafanuliwa katika vyanzo vya mapato ili tusiweze kuendesha tume hile ambayo itakuwa ina ajiri kwa kuendelea kutoka kwenye vyanzo vingine vya mapato wakati huu muktadha wa uchumi wa kidigitali unaweza kujizalishia ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nashauri kabisa Wabunge wenzangu tuipitishe Sheria hii. Lakini Serikali ikakae chini ije na outline nzuri ya vyanzo vya mapato wa kuendesha ile Tume pamoja na Bodi ambayo itaanzishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sheria hii naona kabisa kuna haja baadae ya ku-harmonize Sheria nyingine ambazo zipo ili kuweza kukidhi haja na utekelezaji wenye ufanisi wa Sheria hii. Nasema hivi kwa sababu gani? Kwenye Sheria hii kuna haki ya kusahaulika kwa maana ya kwamba, kwa maana ya kwamba data zangu zimekuwa zinatumika kwenye kampuni Fulani, labda ninapofariki inatakiwa nipate haki ya kusahaulika ndani ya muda fulani, lakini ukiangalia Money Laundering Act inazungumzia miaka 10 ya haki ya kusahaulika. Ukiangalia Tax Act inazungumzia miaka Saba ya haki ya kusahaulika, ukiangalia Sheria ya TCRA inazungumzia miaka Mitano ya haki ya kusahaulika.

Mheshimiwa Spika, Vodacom unapokuwa na lane yao ndani ya miezi mitatu haujaitumia unasahaulika ndani ya miezi mitatu, kwa hiyo sheria hii i- harmonize na iweke usawa kwamba kama ninapotumia lane fulani ya Vodacom, ninasahulika ndani ya miaka mitatu na mimi vilevile ninahaki ya kusahaulika haraka iwezekanavyo baada ya kuonekana nimefariki au vingine vyovyote vile. Tunasema sheria ni msumeno inakata huku na huku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile naomba niseme kwamba, kutokana Muswada huu wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi, tunafahamu kwamba kunakuwa na hackers, kunakuwa na crackers na kuwakuwa na a lot of watumiaji ambao kwa mujibu wa upeo wao mkubwa wa Sheria hii wanaweza kufanya lolote kwenye sheria hii. Mimi ninaungana kabisa na mwenzangu aliyetangulia kwamba sheria hii inapaswa kuitwa Sheria ya Ulinzi Binafsi na Faragha. Maana halisi ya kuanzishwa au kutafuta kulinda sheria binafsi ni baada ya kwamba teknolojia imetuacha wazi. The technology threats ndiyo ambayo inapelekea kuundwa kwa taarifa binafsi.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo basi neno la maana na la msingi ni faragha ili kuweza kulinda taarifa binafsi ili kumfichia mtu faragha zake. Ukweli ni kwamba hata Taifa letu linahitaji faragha, kiukweli kabisa tunahitaji faragha na ni muhimu sana kipengele hiki kuingia katika jina la Muswada huu, kwa maana ya kwamba….

SPIKA: Ahsanteni sana Mheshimiwa.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naunga mkono hoja (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika Muswada huu wa Sheria ya Ulinzi Binafsi. Kipekee kabisa niipongeze Serikali hii ya Mama Samia Suluhu Hassan ambayo kwa hakika imeonesha uwezo mpana wa kufanya maoteo ya kesho kwa Taifa letu. Uwepo wa Muswada huu wa Sheria ya Taarifa Binafsi hakika ni matokeo ya kuwa na Serikali yenye maono mapana na kuiangalia kesho kwa upana wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia Muswada huu wa Sheria ya Taarifa Binafsi hakika ni Muswada sahihi kwa wakati sahihi ambao unakidhi haja ya sasa ya matakwa ya maendeleo ya kiteknolojia.

Mheshimiwa Spika, Sheria hii ya Taarifa Binafsi ukiangalia malengo yake na ukiangalia misingi yake kwa hakika imelenga kuleta maadili katika matumizi ya teknolojia ya Habari.

Mheshimiwa Spika, wanasayansi wanasema kwamba; the next world war will become between the human kind technology na wengine wanadiriki kusema kwamba the next pandemic itakuwa ni ya technology. Kwa hiyo niipongeze Serikali kwa maono mapana ya kuhakikisha Taifa hili tunakwenda kujikinga ipasavyo kwa ukuaji wa teknolojia hii.

Mheshimiwa Spika, katika Ibara ya 5 ya Muswada huu wa Sheria imezungumza suala zima la usafirishaji wa taarifa binafsi. Kipengele hiki kimenifurahisha kwa sababu moja kuu ifuatavyo; kama Taifa tumeweza kuiangalia maana halisi na muktadha pana wa teknolojia ya habari. Suala zima la kusafirisha taarifa binasfi linaweza kufanywa na mtu mwenyewe binafsi kwa kuji-subject katika mitandao ya kijamii, kwa maana ya kwamba unapoingiza taarifa zako huna uhakika wa asilimia mia moja kwamba facebook hatoweza kuzitumia vinginevyo. Vilevile tunajua kwamba makampuni yaliyopo ndani yanatumia software ambazo server zake hazipo humu nchini kwetu. Server zipo mbali huko katika Mataifa yaliyoendelea zaidi ya kiteknolojia, kwa maana data zinakuwa zinahamishwa whether tunataka au hatutaki, Sheria hii imembana mkusanyaji kuhakikisha kwamba anatengeneza sera kamilifu zitakazolinda usalama wa taarifa binafsi. Akienda kununua server huko aliponunua taifa hili atuhakikishie kwamba data zitakazokuwa served externally au internally zinaendelea kulindwa kwa usalama wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimefurahishwa mno na kipengele hiki Ibara ya 5 pamoja na Ibara ya 65 ambayo imemtaka mkusanyaji kutengeneza sera kwa ajili ya kulinda usalama wa taarifa binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwamba Sheria hii ni muhimu sana kwa Taifa letu, kama ambavyo wenzangu wengine wametangulia kuzungumza, katika kuuendea uchumi wa kidigitali sheria hii ina umuhimu wa aina yake. Vilevile sheria imeweka vizuri mazingira ya utekelezwaji kwa maana imeunda Tume na tume ikawekewa executive board itakayokuwa inadhibiti utekelezaji wa shughuli zake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile naomba niseme kwamba, katika Ibara ya 51muktadha mpana wa ukusanyaji wa mapato umeelezwa kwa maana ya vyanzo vya mapato, lakini bado naiona Serikali ina kazi ya kufanya katika eneo hili, tunahitaji kupata outline ya uwazi kuona ni kiasi gani ile muktadha halisi wa uchumi wa kidigitali unafafanuliwa katika vyanzo vya mapato ili tusiweze kuendesha tume hile ambayo itakuwa ina ajiri kwa kuendelea kutoka kwenye vyanzo vingine vya mapato wakati huu muktadha wa uchumi wa kidigitali unaweza kujizalishia ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nashauri kabisa Wabunge wenzangu tuipitishe Sheria hii. Lakini Serikali ikakae chini ije na outline nzuri ya vyanzo vya mapato wa kuendesha ile Tume pamoja na Bodi ambayo itaanzishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sheria hii naona kabisa kuna haja baadae ya ku-harmonize Sheria nyingine ambazo zipo ili kuweza kukidhi haja na utekelezaji wenye ufanisi wa Sheria hii. Nasema hivi kwa sababu gani? Kwenye Sheria hii kuna haki ya kusahaulika kwa maana ya kwamba, kwa maana ya kwamba data zangu zimekuwa zinatumika kwenye kampuni Fulani, labda ninapofariki inatakiwa nipate haki ya kusahaulika ndani ya muda fulani, lakini ukiangalia Money Laundering Act inazungumzia miaka 10 ya haki ya kusahaulika. Ukiangalia Tax Act inazungumzia miaka Saba ya haki ya kusahaulika, ukiangalia Sheria ya TCRA inazungumzia miaka Mitano ya haki ya kusahaulika.

Mheshimiwa Spika, Vodacom unapokuwa na lane yao ndani ya miezi mitatu haujaitumia unasahaulika ndani ya miezi mitatu, kwa hiyo sheria hii i- harmonize na iweke usawa kwamba kama ninapotumia lane fulani ya Vodacom, ninasahulika ndani ya miaka mitatu na mimi vilevile ninahaki ya kusahaulika haraka iwezekanavyo baada ya kuonekana nimefariki au vingine vyovyote vile. Tunasema sheria ni msumeno inakata huku na huku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile naomba niseme kwamba, kutokana Muswada huu wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi, tunafahamu kwamba kunakuwa na hackers, kunakuwa na crackers na kunakuwa na a lot of watumiaji ambao kwa mujibu wa upeo wao mkubwa wa Sheria hii wanaweza kufanya lolote kwenye sheria hii. Mimi ninaungana kabisa na mwenzangu aliyetangulia kwamba sheria hii inapaswa kuitwa Sheria ya Ulinzi Binafsi na Faragha. Maana halisi ya kuanzishwa au kutafuta kulinda sheria binafsi ni baada ya kwamba teknolojia imetuacha wazi. The technology threats ndiyo ambayo inapelekea kuundwa kwa taarifa binafsi.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo basi neno la maana na la msingi ni faragha ili kuweza kulinda taarifa binafsi ili kumfichia mtu faragha zake. Ukweli ni kwamba hata Taifa letu linahitaji faragha, kiukweli kabisa tunahitaji faragha na ni muhimu sana kipengele hiki kuingia katika jina la Muswada huu, kwa maana ya kwamba...

SPIKA: Ahsanteni sana Mheshimiwa.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)