Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Mahmoud Hassan Mgimwa (33 total)

Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya. Naomba nimpongeze Dkt. Mpango kwa uwasilishaji wake mzuri.
Naomba kuishauri Serikali katika mambo yafuatayo:-
Ni vyema kuweka wazi mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika Mpango wa Kwanza 2011 – 2016 ili tujue tatizo ni nini? Serikali imeamua maamuzi yapi kwa yale mambo ambayo bado hayajakamilika.
Mpango huo ulilenga kutanzua vikwazo vya kiuchumi na kupunguza umaskini na kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukuuaji wa pato la Taifa 6.7% - 7% unalingana na upatikanaji wa huduma za jamii kama afya, maji na elimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukuaji wa uchumi uende sambamba na kupunguza umaskini.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri alipaswa kuweka wazi vigezo vilivyotumika kujua uchumi wa Taifa unakua, income per capita peke yake hatoshi kwa sababu upatikanaji wa income per capita unajumuisha matajiri sana na maskini sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, mfumuko wa bei unasababishwa mara nyingi na cost push inflation na demand pull inflation. Naipongeza sana Serikali kwenye eneo la demand pull inflation ni muda mrefu sasa tumeweza kuhimili mahitaji ya chakula ndani ya nchi lakini kwenye cost push inflation.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ametaja eneo la mafuta, ni vyema Serikali ikajipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana na wa bei nafuu. Serikali ihakikishe umeme wa makaa ya mawe, maji na upepo unapatikana ili kupunguza adha ya umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali ihakikishe barabara za uhakika maeneo yote yenye kilimo cha uhakika kwa lengo la kupunguza gharama pia reli ianze kufanya kazi kwenye maeneo yote muhimu.
Mheshimwa Spika, eneo lingine ni kuhusu thamani ya shilingi ambayo inashuka na haiko stable.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema sasa Serikali ikaweka mkakati wa kuondoa matumizi ya dollarization ambayo nchi nyingi duniani zimedhibiti eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunauza kidogo nje ya nchi kuliko tunavyonunua. Ni vyema sasa tujidhatiti kuongeza kuuza nje ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo; asilimia sabini na tisa ya Watanzania inategemea kilimo, ni vyema tukajipanga katika eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye amenijalia kusimama leo hii mbele ya Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Dkt. John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri ya kusimamia uwajibikaji na uadilifu katika Serikali yetu. Pamoja na kazi nzuri bado anaendelea kutumbua majipu ndiyo maana leo hii wenzetu wa upinzani wameamua kuweka mpira kwapani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, waswahili wanasema mwenye wivu ajinyonge, tutaendelea kumpongeza Dkt. John Pombe Magufuli na tutaendelea kumuunga mkono kwa kazi anayoifanya katika nchi hii. Kwa namna ya kipekee naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri na kwa kazi nzuri anayoifanya kuisimamia Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kunirudisha tena katika Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nitaanza kwa kujielekeza katika ukuaji wa uchumi. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema mwaka 2015 uchumi ulikua kwa asilimia 7.1, mwaka 2014 uchumi ulikua kwa asilimia 7. Ni kweli uchumi unakua, lakini ninaomba Serikali inapozungumzia suala la ukuaji uchumi lazima waangalie na hali halisi ya maisha ya Mtanzania. Ukuaji wa uchumi unatakiwa uende sambamba na huduma za jamii kama afya, elimu pamoja na maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vipaumbele ambavyo amevizungumzia Mheshimiwa Waziri Mkuu vya ukuaji wa uchumi amezungumzia suala la kilimo. Jana katika hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti alisema asilimia 79 ya Watanzania wameajiriwa katika eneo la kilimo, lakini ukuaji katika eneo hili unakua kwa asilimia 3.4 ambao ni ukuaji mdogo sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Waziri Mkuu amesema wakulima ni asilimia 66.3 ya Watanzania wote ambao wako kwenye eneo hili. Serikali ni kweli imeona kwamba, zaidi ya asilimia 79 ya Watanzania wameajiriwa katika sekta hii ya kilimo, lakini bado Serikali haijaamua kuwekeza kwenye eneo hili, katika eneo hili hakuna Mbunge ambaye haguswi. Tunaiomba Serikali iangalie kwa macho yote katika eneo hili haswa katika mfuko wa pembejeo, ule mfuko wa pembejeo umewekewa hela ndogo sana kulinganisha na pesa ambazo zinatakiwa ziwepo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutawekeza vizuri katika eneo hili la kilimo nina hakika kabisa hata eneo ambalo tumekusudia kwenda kwenye Mpango wa Pili wa viwanda tutakwenda vizuri, kwa sababu Mheshimiwa Mwigulu pamoja na Waziri wa Viwanda ni watoto pacha, kama tutafanya vizuri kwenye kilimo automatically tutafanya vizuri kwenye viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaomba sana, kwenye eneo la pembejeo Serikali iongeze mfuko wa pembejeo ikilinganishwa na ilivyo sasa, kwa sababu unawagusa Watanzania karibu wote, aidha inagusa wananchi wa Chama cha Upinzani na wa Chama Tawala, kwa hiyo tunaiomba Serikali iwekeze sana kwenye eneo hili. Lakini la msingi zaidi tunatakiwa tuhakikishe zile pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati, zikiendelea kuchelewa zitaendelea kuwapa matatizo wakulima wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, eneo la kilimo ni eneo very sensitive, Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Kilimo, benki hii ya kilimo ilianza miaka mitatu iliyopita, na tulikubaliana kwamba, benki hii ianze kwa mtaji wa shilingi bilioni 100, lakini jambo la kusikitisha mpaka leo benki hii ya kilimo imepewa shilingi bilioni 60 wanashindwa kumudu na wanashindwa kuwasaidia wakulima.
Hivyo, tunaomba benki hii iongezewe mtaji na kama tulivyokubaliana kila mwaka benki hii ya kilimo iendelee kupata mtaji.
Mheshimwia Mwenyekiti, kwa kifupi bilioni 60 hazitoshi! Tunaomba benki hii isiwepo Dar es Salam tu, iende hadi kwenye site ambako wakulima wapo. Itakuwa bora kama benki hii ya kilimo itakuwepo kwenye mikoa haswa ya kilimo na iwafikie wananchi, utaratibu wa kupata mikopo uwekwe uwe wazi na wananchi wajue ni haki yao kupata mikopo ya riba nafuu. Tukifanya vizuri kwenye eneo hili kama nilivyosema awamu ya pili ya mpango tutakwenda tukiwa kifua mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ninalotaka kuchangia kidogo ni kuhusu mfumuko wa bei. Mheshimiwa Waziri Mkuu amezungumzia sana mfumuko wa bei na jana Waziri wa fedha alizungumzia mfumuko wa bei. Lakini Waziri wa Fedha jana alizungumza jambo moja kwamba, tukidhibiti eneo la mafuta tutakuwa kwenye hali nzuri ya kuzui mfumuko wa bei.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kabisa mfumuko wa bei unasababishwa na mambo makubwa mawili, la kwanza Cost Push Inflation na la pili Demand Pull Inflation. Tunapozungumzia Cost Push Inflation ni kweli kwenye eneo la mafuta tunaweza tukawa kwenye eneo hili, lakini hatuwezi kuzungumzia eneo la mafuta peke yake bila kuzungumzia umeme, kama tuta- control bei ya umeme itakuwa iko chini na umeme utapatikana kwa wakati, automatically utapunguza cost of production.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuishii kwenye jambo hilo tu, vilevile nilitaka tuzungumzie suala la infrastructure kwa maana miundombinu kama tuna uhakika na miundombinu mizuri automatically tutakuwa tumefanya vizuri. Kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kuipongeza sana Serikali kwenye suala la Demand Pull Inflation Serikali iko vizuri na Watanzania tumekuwa tuna chakula kingi na hatuagizi nje ya nchi. Kwa hiyo katika jambo hili tuko vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo huwa tunalipigia sana kelele hapa suala la dollarization lakini Serikali imekuwa siyo sikivu haisikii kwenye jambo hili. Tunaomba hawa watu ambao wanaendeleza utaratibu wa dollarization kwa njia moja au nyingine ina-affect uchumi wa nchi hii, thamani ya shilingi automatically inapoteza mwelekeo kutokana na dollarization.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekisoma kitabu cha Waziri Mkuu, nimeona haikuzungumzia kabisa suala la uvuvi. Tunatakiwa tuwekeze kwenye eneo la uvuvi, eneo la uvuvi ni eneo muhimu ambalo tunawekeza mara moja na baada ya kuwekeza nina hakika tutakuwa tume-create ajira za kutosha, vijana wengi wanaweza kujiajiri katika eneo hili na tukapata mtaji mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatakiwa tuwe waangalifu na tunatakiwa tuwe waangalifu na tuwekeze hasa kwenye bahari kuu ili kusudi tuweze kupata mitaji mikubwa. Kuna baadhi ya nchi hapa duniani kama Sychelles zinaishi kwa uvuvi na sisi hatuna sababu ya kutokupata mapato makubwa kwenye eneo la uvuvi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu nyingine ninayotaka kuzungumzia ni kuhusu suala la maji. Maji ni muhimu sana kwa maisha ya Mtanzania na kwa masikitiko makubwa katika Jimbo langu ambalo lina Kata 11 maji ni tatizo, sina hata Kata moja ninayoweza kuzungumzia suala la maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wetu ile senti 50 ambayo imeingizwa kwenye tozo ya mafuta ingeongezwa ikawa shilingi 100 badala ya shilingi 50 kusudi tuweze kupata maji katika Majimbo mengi na katika maeneo mengi. Tunaiomba Serikali inapoleta bajeti kwenye eneo la maji tuongeze hatuna sababu ya kutochangia kwenye eneo la mafuta badala ya shilingi 50 tuweke shilingi 100 ili mfuko wa maji uendelee kukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni suala la miundombinu. Ili tuone uchumi unakua vizuri ni vema tukahakikisha miundombinu yetu ni ya uhakika. Katika eneo langu lina matatizo katika barabara ya Mapanda, Usokami, Ihalimba na Kinyanambo, barabara ya Mtili, Ifwagi, Mdabulo na Ihanu. Tumewaandikia wenzetu wa TAMISEMI kwa vile hivi sasa barabara zile hazipitiki, tumewaandikia kwenye mfuko wa emergency watusaidie katika eneo hili. Wakitusaidia nina uhakika kabisa tunafanya vizuri katika maeneo haya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo la nishati. Tunazungumzia sana sasa hivi nishati ya gesi, tumesahau habari ya makaa ya mawe. Makaa ya mawe ni muhimu sana, ukiangalia wenzetu wa South Africa asilimia 57 ya umeme unatokana na makaa ya mawe. Sisi hatuna sababu ya kutokuwekeza kwenye makaa ya mawe, tulitakiwa tujenge transmission line kutoka Makambako kwenda Songea mpaka Mbinga ambayo gharama yake ilikuwa shilingi bilioni 60 na wenzetu wa SIDA walishakubali kutusaidia kwenye eneo hili. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba Serikali inasuasua kwenye eneo hili! Kuna uwezekano wa ku-produce megawati 120 kwenye kilowati 210.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tusipofanya hivyo kwenye eneo hili tutakuwa tunawaonea watu wanaotoka kwenye maeneo hayo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. MAHAMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara hii nyeti katika uchumi wa wa nchi yetu. Hongereni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu utajielekeza katika maeneo yafuatayo:-
Kwanza barabara ya Kinyanambo A – Isalavanu – Sadani – Madibira - mpaka Rujewa yenye urefu wa kilometa 141 ambayo imekuwa inawekwa katika Ilani ya Uchaguzi za mwaka 2000, 2005, 2010, 2015. Cha kusikitisha, hata kilometa moja haijawahi kujengwa kwa kiwango cha lami. Naomba sana Mheshimiwa Waziri anapokuja kuhitimisha bajeti hii, atupe maelezo ya kina, sababu zinazofanya barabara hii isianze kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, barabara ya kutoka Mtili – Ifwagi – Mdabalo – Ihanu – Isipii mpaka Mpanga TAZARA – Mlimba; barabara hii inaunganisha Wilaya ya Mufindi na Kilombero Mkoa wa Iringa na Morogoro. Vikao vyote muhimu katika kupandisha hadhi barabara hii vimefanyika mwaka 2013 na Mheshimiwa Rais ambaye alikuwa Waziri wakati huo anajua. Cha kusikitisha, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameandika barua mara nyingi Wizarani lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Ni vyema Mheshimiwa Waziri atuambie kwa nini hajatuma wataalam wake mpaka leo? Barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu hasa wakazi wa Tarafa ya Ifwagi ambako kuna misitu mikubwa na viwanda vya chai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya kutoka John Corner mpaka Mgololo ni barabara muhimu sana na fedha inayotumika kufanya matengenezo ni kubwa sana. Ni vema Serikali sasa ikaanza kutengeneza hata kilometa mbili mbili tu kila mwaka kuliko kuendelea kutenga fedha za kila mwaka kwenye matengenezo ya changarawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa Serikali kukubali kurudisha Kituo cha Reli cha Mpanga TAZARA, lakini naomba sana, kituo hiki pamoja na kile cha Kimbwa kifanyiwe ukarabati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Mheshimiwa Waziri atusaidie pamoja na minara iliyojengwa Ikweha na Igunzi, lakini wananchi hawapati mawasiliano katika Jimbo hili. Pili, minara iliyojengwa Mapanda na Isipii haisaidii wananchi waliopo kwenye maeneo husika kupata huduma hii muhimu ya mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema sasa Serikali ikanza Ujenzi wa Airport ya Nduli pamoja na barabara ya Ruaha National Park ambayo ni muhimu sana kwa utalii katika nyanda za juu kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyenipa afya nipate nafasi ya kuchangia kwenye ajenda hii muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Mpango pamoja na Naibu Waziri na wasaidizi wao kwa ujumla kwa kazi kubwa wanayoifanya katika Wizara yao. Lakini namshukuru tena Mheshimiwa Dkt. Mpango, amesema kwenye maandiko yake kwamba atatuzingatia na kuufanyia kazi ushauri wetu. Nakuomba Mheshimiwa Dkt. Mpango, haya tunayozungumza kama Wabunge wenzako uyachukue na kuyafanyia kazi kama ulivyoahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu unaanza kujielekeza kwenye hali ya kiuchumi. Mheshimiwa Dkt. Mpango amesema uchumi wa Tanzania unakua, ni kweli kwa maelezo yake uchumi wa Tanzania unakua. Lakini unapotaka kuangalia vigezo vya kukua kwa uchumi, lazima tuangalie na hali halisi ya Mtanzania, je, iko sawa, inaenda sambamba na ukuaji wa uchumi anaouzungumza Mheshimiwa Dkt. Mpango? Ukiangalia utaona mambo yako tofauti, tunazungumza uchumi unakua, lakini hali za Watanzania zinaendelea kuwa mbaya siku baada ya siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Dkt. Mpango, kwa hiyo inawezekana vigezo ulivyovitumia kusema uchumi wa Tanzania unakuwa ni tofauti na vile ambavyo tunavifikiria sisi. Kwa mfano, kupata hela ni tatizo, lakini leo hii ukipata pesa unaweza ukashindwa hata kujua umetumia kununua nini, purchasing power inazidi kushuka siku baada ya siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka Mheshimiwa Dkt. Mpango atuambie, tuko kwenye inflation period au deflation period. Kwenye deflation period kama upatikanaji wa pesa unakuwa mgumu, automatically unawasaidia wale waliokuwa na pesa kidogo kuweza kununua vitu vingi katika circulation, lakini mtu anakuwa na hela ndogo aliyoipata, uki-change shilingi 10,000 hata hujui imefanya nini. Kwa hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mipango mimi nakuomba uliangalie jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tujiangalie, tupo kwenye depression au tuko kwenye recession period. Hayo mambo yote mawili tunatakiwa tuyaangalie kwa wakati mmoja...

MWENYEKITI: Anaitwa Dkt. Mpango, siyo Dkt. Mipango.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Dkt. Mpango, tupo kwenye depression au tuko kwenye recession period, mimi naona kama tunakwenda kwenye depression, tunatoka kwenye recession kwenda kwenye depression. Kwa hiyo ninamuomba sana Mheshimiwa Dkt. Mpango aliangalie jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejitahidi kwenye suala la bureau de change, lakini bado tuna tatizo kwenye dollarization, bado matumizi ya dollarization yanaendelea kutawala katika nchi hii na shilingi ya Tanzania inaendelea kushuka siku baada ya siku. Sasa unatuambia uchumi unapanda, shilingi inashuka, uki-compare unaona hapa kuna tatizo. Kwa hiyo, vigezo ambavyo Mheshimiwa Dkt. Mpango amevizungumza tunaona haviendani na hali halisi ambayo iko mtaani. Kwa hiyo namuomba sana Mheshimiwa Dkt. Mpango aangalie na haya mambo ambayo yanawahusu Watanzania wa kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika document yake hii ya Mpango mzima hawajazungumzia hali halisi ya wakulima ambao nchi hii asilimia 67 mpaka 72 ni ya wakulima. Kwa hiyo, unakuta mpango mzima wa maendeleo wa nchi hii umewaweka kando wakulima na hawa wakulima ndiyo wanaotuweka hapa madarakani. Kwa hiyo, ninaona hapa kwenye eneo la kilimo kwa ujumla kuna tatizo. Kwa hiyo namuomba sana Mheshimiwa Dkt. Mpango aliangalie na hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tuliahidi kwamba tutatengeneza Kiwanda cha Mbolea hapa nchini kule Mtwara lakini mpaka leo kiwanda hicho hakijatengenezwa. Kingeweza kutengenezwa kiwanda kile cha mbolea kule Mtwara nina uhakika mbolea ingekuwa chini kuliko ilivyo sasa hivi. Tulikuwa tumekwenda kwenye mpango wa bulk procurement, bei imeshuka kidogo, lakini tungekuwa tumetengeneza kiwanda chetu hapa nchini bei ingekuwa chini zaidi na nina uhakika kwamba haya ambayo wakulima na Wabunge wengi tunalalamikia yasingekuwa kama ilivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano tunajiuliza, kwa nini wenzetu wa Zambia wanauza gunia la mahindi shilingi 20,000 kwa nini sisi tunauza shilingi 35,000? Kwa hiyo tuna maana kwamba mbolea kule iko cheap zaidi kuliko kwetu, lakini sisi tuna access ya kutengeneza mbolea hapa ndani ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hata ule uchumi wa viwanda ambao ndugu yangu, Mheshimiwa Jafo, anauzungumzia sana, tunaomba uliangalie eneo hili sensitive la wakulima kwamba kile kiwanda cha mbolea tulichokizungumzia ambayo raw material tunayo ya kutosha kule Mtwara kingeanza as soon as possible tuwasaidie wakulima walio wengi katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi namuomba sana Waziri wa Fedha atakapokuja atuambie kile kiwanda ambacho tumekivumilia miaka mingi kwa nini mpaka leo hakijaanzishwa na sababu zipi zinazopelekea kutokuanzishwa kwake. Sasa matokeo yake ni kwamba kila siku tunakuja na miradi mipya ambayo haina tija. Unaanza mradi wa zamani to a level fulani unafika unauacha unakuja kwenye mradi mpya. Kwa hiyo hapa ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wengi wamezungumzia suala la mahindi, na mimi nataka ni- declare interest, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimo. Kwenye kilimo tumelizungumzia na bahati nzuri leo Mheshimiwa Waziri amelizungumza na baadhi ya Wabunge wanaotoka kwenye maeneo hayo. Kamati yetu tulikaa na Mheshimiwa Waziri siku tatu kuzungumzia tatizo la mahindi, tumbaku na mbaazi na tukatoa directive kwamba Mheshimiwa Waziri aje hapa kwenye Bunge lako Tukufu aeleze mkakati wa Serikali kuhusu mahindi yatauzwaje, mbaazi itauzwaje na tumbaku itauzwaje, lakini amekaa kimya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na sisi Wajumbe wa Kamati tulikuwa tunategemea yale ambayo yanaulizwa na Waheshimiwa Wabunge yangekuwa yameshazungumzwa hapa Bungeni kabla na Wabunge wakatoa maazimio ya pamoja. Kwa hiyo, wakulima wetu wanakwenda mwezi wa 11 wanaanza kupanda mahindi, hawajui nini wafanye hata kama tumekubaliana leo kwamba tunataka kufungua masoko, bado ni tatizo. Aje hapa kwenye Bunge lako Tukufu atoe tamko la Serikali kwamba kuanzia leo watu wauze mahindi yao popote wanapotaka ili waweze kupata haki zao za msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme, kama nilivyosema hapo awali, kila siku Serikali ina mawazo mapya. Tulikuwa tunategemea tutatengeneza umeme kwa kutumia makaa ya mawe, wenzetu wa Mchuchuma, Ngaka, Kiwira. Lakini mpango huu upo zaidi ya miaka 30, sasa tukijiuliza kwa nini tunaenda kwenye mipango mingine wakati mpango huu ambao ulikuwa umeshaanza tumeuacha. Kwa hiyo unakuta hata baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wakisema kuna baadhi ya miradi imekuwa biased, watu wanaamua kwenda kwenye miradi mingine wanaacha miradi mingine, hili litatuletea matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri atuambie kwa nini wameamua kuacha mradi wa umeme. Sweden kuputia Kampuni yao SIDA Grand walikubali kutoa hela, dola milioni 60, kwa ajili ya kusaidia kutengeneza transmission line ya kutoka Makambako mpaka Ngaka, lakini Serikali imekaa kimya. Na tatizo la pale ni transmission line tu na umeme ule ni cheaper kuliko umeme mwingine wowote. Kwa hiyo, tunataka kwenda kwenye vyanzo vingine vya umeme wakati tulikuwa tunaweza kupata umeme wa rahisi ambao Serikali ilikuwa haiingizi hela yoyote kama alivyosema Mheshimiwa Nape pale, kwa nini twende kuingiza hela kwenye miradi ambayo haina tija katika nchi hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi naomba tuangalie na mje na majibu kwa nini mradi wa umeme wa Ngaka mpaka sasa hivi haujaanza kazi. Kwa nini mradi wa uchimbaji wa chuma mpaka sasa hivi haujaanza kazi kule Liganga. Hii inakatisha tamaa sana, tunaona kwamba kuna baadhi ya maeneo wanapewa priority ya hali ya juu na kuna baadhi ya maeneo hawapewi kitu chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukija kwenye maeneo ya barabara, tunatakiwa tuendelee kufungua barabara. Kuna barabara ya kutoka Kinyanambo A kwenda Isalavanu, Madibira mpaka Rujewa, ni barabara imezungumzwa karibu katika awamu tano. Toka mwaka 2000 ile barabara inazungumzwa, na ni barabara muhimu sana kiuchumi. Kwa watu wanaotoka Mbeya wakiamua kukatisha kwenye barabara ile wanapunguza zaidi ya kilometa 75 kuliko wakipita barabara ile ya kupitia Makambako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye uchumi hili ni jambo zuri sana. Lakini kila siku wanasema tutaanza kesho au kesho kutwa, lakini ukianglia katika mpango wake na ile barabara is very sensitive, inapitia kwenye mbuga za wanyama, inapitia kwenye maeneo ya kilimo kikubwa cha mpunga, inapitia kwenye kilimo kikubwa cha mahindi, inapitia kwenye maeneo ya madini, wameiacha haijaanza kushughulikiwa. Kwa hiyo kuna walakini hapa.

La pili, unakuta barabara ya kutoka Mafinga kwenda Mtiri mpaka Mgololo. Barabara ile ina zaidi ya viwanda vikubwa kumi ambavyo vinatoa kodi zaidi ya shilingi bilioni 50 lakini Serikali haitaki kuijenga kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, hili ni tatizo; watu ambao wanachangia hela nyingi kwenye nchi hii wanasahaulika. Kwa hiyo, mimi namuomba sana Mheshimiwa Waziri mipango yake awe anaangalia na watu wana-contribute nini katika Taifa hili, sio ajielekeze kwenye maeneo tu ambayo anayaona yeye. Watu wanachangia hela nyingi kwenye Mpango wa Taifa lakini matokeo yake ni kwamba hatupeleki kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanikiwa kwenye eneo la umeme lakini bado kwenye eneo la maji. Mheshimiwa Waziri amezungumzia eneo la maji Dar es Salaam tu, ina maana watu wa Tanzania wengi wanakaa Dar es Salaam. Katika Mpango wake mzima ameonesha kwamba maji yanatakiwa yaende kwa wingi katika Mkoa wa Dar es Salaam, kwa nini kwenye Mikoa, Wilaya, Vijiji na Majimbo mengine yasiende? Kwa hiyo kama tulivyofanya kwenye maazimio ya Bunge lililopita kwamba tuli-ringfence kwa ajili ya kupata umeme wa uhakika, sasa hivi nguvu zetu zielekezwa kwenye eneo la maji ili maji yapatikane katika maeneo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kwenye Kamati yetu tumependekeza hata Bunge lililopita tuongeze shilingi 50 kwenye kila lita ya mafuta ili maji yaende kwenye maeneo yaliyokuwa mengi, lakini tukikwambia utasema kwamba tutaongeza inflation rate, hatuwezi kuongeza inflation rate kwa utaratibu huo. Kwa sababu sisi kama Wabunge tumekubali na tutakuwa tayari kwenda kutetea hoja zetu, kwamba tuna sababu za msingi za kuongeza shilingi 50 kwenye maji ili maji yaende kwenye maeneo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyenipa nafasi niweze kuchangia kwenye Bunge lako Tukufu. Kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kukushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri na kazi nzuri anayoifanya katika kusimamia. Kwa namna ya kipekee nimpongeze sana dada yangu, Waziri, Mheshimiwa Jenista Mhagama pamoja na ndugu yangu, Naibu Waziri, Mheshimiwa Antony Mavunde, kwa kazi nzuri sana wanayoifanya katika maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu utajielekeza kwenye maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ni kwenye eneo la kilimo. Kwa maelezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, amesema kwamba Watanzania walioajiriwa katika Sekta ya Kilimo ni kati ya asilimia 65 mpaka 75. Pamoja na ajira ya Watanzania wengi katika eneo hili, lakini bajeti inayopelekwa kwenye eneo hili ni ndogo sana ikilinganishwa na mahitaji halisi ya kwenye bajeti hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tulikuwepo kwenye Makubaliano ya Maputo na Maraba ambapo katika makubaliano haya tulikubaliana kwamba asilimia 10 ya bajeti itengwe kwa ajili ya Sekta ya Kilimo. Katika hali ya kusikitisha kabisa, katika eneo ambalo linaajiri watu wengi, hata asilimia tano ya bajeti iliyotengwa kwenye eneo la kilimo haitokani na Bajeti Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nichukue fursa hii kumshauri sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama tunataka tuwasaidie wale wakulima na kama kweli tuna target ya kweli kwenda kwenye uchumi wa viwanda, ambapo katika uchumi huo raw material ya kutosha inapatikana kwenye eneo hili la kilimo zaidi ya asilimia 85, tutakuwa tunajidanganya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama we are serious enough tu-invest kwenye eneo hili ili tuwe tuna uhakika kwamba tunaweza kuwasaidia wakulima na ile dhana ya kwenda kwenye uchumi wa viwanda itapatikana kama wakulima wengi watapata fursa za kulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mfano tu, mwaka 2017 kumekuwa kuna mgogoro mkubwa sana. Wakulima wamejitoa, wamelima sana lakini matokeo yake wamepata hasara, tumeshindwa kununua yale mazao kwa sababu tulikuwa hatuna masoko ya uhakika. Naishukuru Serikali kwa kuruhusu kwamba sasa hivi mahindi tunaweza tukauza nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, NFRA wameomba kwenye bajeti yao shilingi bilioni 86, lakini cha kusikitisha inaonekana Serikali haitaweza kuwapa hata robo ya ile hela waliyoomba. Sasa tutakwenda kweli tunakokusudia? Kwa hiyo, uchumi ule wa viwanda hauwezi kupatikana kama hatutakuwa serious kwenye kuwekeza kwenye eneo hili la kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kusikitisha sana, haya ni masikitiko ambayo tunayo wawakilishi wananchi; mara ya mwisho Mheshimiwa Waziri Mkuu alikaa na Mawakala wa Pembejeo lakini mpaka leo halijatoka tamko lolote la Serikali kwamba ni lini watawalipa wale Mawakala wa Pembejeo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitegemea Waziri Mkuu alipokuja kwenye kusoma hotuba yake hapa, angesema mpaka sasa hivi tumeona Mawakala kadhaa ndio ambao wako supposed kulipwa kwenye hili eneo. Sasa Mawakala wanakufa, mali zao zinataifishwa na mabenki kule, hali inazidi kuwa mbaya. Kwa hiyo, nataka Waziri Mkuu atakapokuja kuhitimisha namwomba sana azungumzie hili kwani mawakala wanataka kumsikiliza kule nje, atoe kauli ili waweze kujua kwamba Serikali yao imeamua kuwasaidia kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekubali kwamba tunataka tuwekeze kwenye eneo la kilimo, lakini tunawekezaje kwenye eneo hili? Nataka nizungumzie kidogo suala la pareto. Pareto inalimwa nchini hapa, lakini cha kusikitisha kabisa, ile hatua ya mwisho ya kuitengeneza ile pareto ili tupate bidhaa, haifanyiki hapa nchini. Yale material yanachukuliwa yanapelekwa Marekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nimesema tuwekeza sana kwenye eneo hili. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, tuwahamasishe wakulima katika maeneo mbalimbali, walime pareto kwa wingi ili ile final product ipatikane hapa ndani ya nchi. Ikipatikana itatusaidia kama Tanzania kupata hela nyingi katika maeneo haya. Refining ifanyike hapa hapa Tanzania. Tukifanya hivyo kwenye eneo hili, tutakuwa tuna uhakika wa kutengeneza ajira ya kutosha ambayo wananchi wetu watapata kutoka kwenye maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka niseme tu kwamba ili twende kwenye uchumi wa viwanda, lazima tuhakikishe Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda inafanya kazi simultaneously. Wasipofanya kazi kwa pamoja, uchumi wa viwanda utakuwa hadithi katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo napenda kuchangia ni eneo la maji. Maji ni uhai. Ukizungumza hapa, hakuna Mbunge ambaye hana tatizo la maji. Sasa sisi kama Wabunge tumekuja na hoja mbalimbali kuhusu kesi ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwanza, sisi kama Wabunge tuliomba Serikali iongeze Sh.50/= kwenye kila lita ya petrol. Kwa masikitiko makubwa, katika hotuba ya Kamati ya Kilimo ya mwaka 2015/2016, Bunge lako hili liliazimia kwamba Sh.50/= iongezwe pale, lakini maazimio ya Bunge yanashindwa kutekelezwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, atakapokuja Mheshimiwa Waziri Mkuu atuambie, kwa nini wanashindwa kutekeleza maazimio ambayo Bunge lako Tukufu limepitisha hapa? Maji ni uhai, lakini kwa masikitiko makubwa sana tuna tatizo. Serikali ilikuwa inatakiwa ipate shilingi bilioni 500 kutoka kwenye Serikali ya India kwa ajili ya kupeleka maji katika miji 17. Serikali inapata kigugumizi gani cha kutokusaini ule mkataba? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maji yangeenda kwenye ile miji 17, nina uhakika kabisa tungepunguza gap kubwa la matatizo ya maji katika maeneo haya. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali, kwa sababu Head Prefect wa Serikali ndio Waziri Mkuu; aje atuambie Serikali iko tayari sasa hivi kusaini mkataba wa shilingi bilioni 500 ili miji 17 iweze kupata maji ya uhakika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na Waheshimiwa Wabunge wengi waliochangia, kwamba imefika wakati sasa uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini uwepo, kwa sababu maji yana tija. Kwa mfano, bajeti ya mwaka 2017 nyingi ambayo tumefanikiwa katika maeneo imetokana na Mfuko wa Maji. Mfuko wa Maji ulitengewa shilingi bilioni 158 na mpaka sasa hivi zimeshatumika shilingi bilioni 130 ambazo zinatokana na Mfuko wa Maji. Asilimia 66 ya bajeti ambayo imetoka kwenye maji inatokana na Mfuko wa Maji. Kwa hiyo, kuna haja ya kuongeza hela kwenye Mfuko huu ili watu walio wengi waweze kupata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiongeza hii shilingi 50, nina uhakika kabisa tutapata shilingi bilioni 316. Tukiamua kila shilingi bilioni kumi tukaipeleka kwenye kila mkoa, baada ya miaka mitatu kutakuwa hakuna kabisa tatizo la maji. Kwa hiyo, tunaiomba sana Serikali, sisi ndio wenye wananchi; ukiongeza hiyo Sh.50/= sisi ndio tutakwenda kuwaambia wananchi kwa nini tunataka Sh.50/= iongezwe kwenye maeneo haya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme tu, sisi kama CCM, Serikali ya CCM, naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu tuichukue ajenda ya maji kama ndiyo ajenda ya kufa na kuzikana kusudi tuweze kuwatua akinamama ndoo kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka kuchangia ni eneo la…

T A A R I F A . . .

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeipokea taarifa. (Kicheko/Makofi))

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeipokea taarifa kwa sababu Mbunge mwenzangu anataka Mheshimiwa Waziri Mkuu asikilize zile hoja, sisi Wabunge tunasema nini? Waziri Mkuu ndio Head Prefect wa Mawaziri wote, atusikilize. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maazimio very sensitive ya Bunge ambayo Bunge lako Tukufu limepitisha, hasa la kuongeza Sh.50/= kwenye tozo ya maji. Wabunge wote kilio chao cha msingi ni maji. Nimesema tu kwa niaba ya Waheshimiwa Wabunge wenzangu, tunataka tuichukue agenda ya maji kama ndiyo ajenda kuu katika Serikali yetu hii ya Awamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka kulizungumzia ni eneo la mifugo na uvuvi. Kuna baadhi ya Wizara kazi yake ni ku-consume tu. Wizara ya Miundombinu yenyewe inapewa hela na kutumia tu, lakini kuna baadhi ya Wizara zikiwezeshwa zitakuwa zinapewa hela na zenyewe zinatoa hela. Kwa hiyo, ufike wakati tuziangalie Wizara kama ya Mifugo na Kilimo, kwamba kama ikiwezeshwa vizuri to some extent tunategemea kupata hela (returns) kutoka kwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umekuwa ni utaratibu wa kila mwaka kwa hizi Wizara hatowezeshwa fedha za kutosha. Kwa hiyo, ufike wakati tuzisaidie hizi Wizara. Eneo hili ndilo ambalo linatengeneza ajira kwa urahisi kuliko maeneo mengine yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo la mwisho ambalo nataka nilizungumze kuhusu maziwa. Hili eneo la maziwa ni very sensitive. Kama tunaweza ku-protect maziwa yanayotoka nje ya nchi, tutakuwa tumeisaidia nchi yetu kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kuvilinda viwanda vya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ajili ya kuvilinda viwanda vya ndani ni lazima tu-protect viwanda vyetu kwa kuongeza kodi kwa bidhaa za nje. Kwa masikitiko makubwa asilimia 80 ya maziwa yanayokuwa imported kutoka nje ya nchi, yanaliwa na viongozi na taasisi za Serikali. Kwa hiyo, badala ya kusaidia kuvilinda viwanda vyetu vya hapa nchini, sisi tumekuwa ndio tunachangia kuvi-promote viwanda vya nchi za nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, litoke tamko kama lililotoka kwenye furniture kwamba sasa umefika mwisho wa kutumia maziwa kutoka nchi ya nje, hasa kwenye ofisi zetu za Serikali.
Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukutu tena kwa kunipa nafasi ya kuhitimisha Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji. Naomba nichukue fursa hii kuwapongeza Maziri wa Kilimo Mheshimiwa Japhet Hasunga pamoja na Manaibu Mawaziri wake; Mheshimiwa Mgumba na Mheshimiwa Bashe.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nimpongeze Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Luhaga Mpina na Naibu wake, Mheshimiwa Abdallah Ulega. Naomba nichukue fursa hii tena kumpongeza Mheshimiwa Profesa Mbarawa Makame, pamoja na Naibu wake Jumaa Aweso kwa ushirikiano wanaotupatia kama Kamati na kazi nzuri wanazofanya katika kutekeleza majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana Serikali kwa kutekeleza baadhi ya maazimio ya Bunge lililopita. Naomba nichukue fursa hii tena kuiomba Serikali iendelee kutekeleza maazimio ya Bunge lililopita yale ambayo bado hawajayafanyia kazi. Nawapongeza wote waliochangia katika ripoti yetu. Katika wachangiaji 21, 20 wamechangia katika hii Kamati yetu ya Kilimo, Mifugo na Maji, nawapongezeni sana.

Mheshimiwa Spika, katika Sekta ya Kilimo hoja ambayo imechangiwa na Wabunge wengi ni suala la bajeti ndogo. Kila Mbunge alipokuwa anasimama hapa, ukiyasikiliza maelezo yake kwa kina alikuwa anazungumzia udogo wa bajeti; na siyo udogo wa bajeti tu; na kiwango cha pesa kinachokwenda katika utekelezaji wa hiyo bajeti.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Kamati tuliliona hili, ndiyo maana katika miongoni mwa maombi yetu tumekuomba Wizara hii ya Kilimo iingie kwenye Wizara za vipaumbele kwa sababu ndiyo Wizara ambayo inaajiri Watanzania walio wengo na ndiyo Wizara inayotoa malighafi ya kutosha. Asilimia 80 ya malighafi hapa nchini yanapatikana katika Wizara hii ya Kilimo. Kwa hiyo, tunkuomba sana hii Wizara ya Kilimo iingie kwenye Wizara za vipaumbele.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Tanzania tuliingia kwenye Azimio Malabo au Maputo Declaration. Azimio hili linasema Serikali inatakiwa itenge asilimia 10 ya bajeti kuu kwa ajili ya Sekta ya Kilimo. Tunaiomba tena Serikali iliangalie jambo hili kwa sababu hata 4% katika bajeti kuu ambayo inakwenda kwenye maeneo ya kilimo haiendi. Eneo hili ni very sensitive na tunahitaji kuona viwanda vyetu vinafanya kazi nzuri. Kwa hiyo, kama tunataka twende kwenye uchumi wa viwanda, hatuna sababu yakutokuboresha katika sekta hii ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo lilichangia na baadhi ya Wajumbe wengi ni suala la horticulture; kilimo cha mboga mboga pamoja na kilimo cha matunda. Kilimo cha mboga mboga na matunda kitatusaidia kupata fedha nyingi za kigeni, lakini kuna tatizo katika eneo hili. Kuna takribani kodi zaidi ya 45 ambazo zinawakwaza kwa njia moja wakulima katika eneo hili.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ifike wakati Serikali ilitambue jambo hili kusudi tuendelee kupata mapato ya kutosha tuangalie mchakato huu ambao uko kwenye blueprint, ifanyike mapema iwezekanavyo kusudi tuweze kuondokana na hii adha wanayoipata wakulima wetu. Mheshimiwa Waziri wa Kilimo amejitahidi kuzungumzia suala la mbegu, lakini katika suala la mbegu tatizo kubwa lipo, bado kuna tatizo la bajeti.

Mheshimiwa Spika, ili tupate mbegu bora na za uhakika, lazima tujielekeze katika kuwekeza kwenye eneo la utafiti. Hata hivyo, tuna shida kwenye eneo hili la utafiti. Mara nyingi tunazungumza kwamba Serikali imetenga asilimia moja kwenye bajeti kuu kwa ajili ya eneo hili la utafiti, lakini ni shilingi ngapi linakwenda kwenda kwenye eneo hili la utafiti? Kwa hiyo, ifike wakati Serikali ijiekeleze kwenye eneo hili kuongeza kwenye bajeti eneo la utafiki kusudi tuweze kupata mbegu za uhakika na nyingi katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Kamati tuliiomba Wizara ya Kilimo ifanye marekebisho ya Sera na Sheria ya Kilimo na iletwe Bungeni mapema ili kuondoa ukakasi uliopo. Mabadiliko haya yatawasaidia wakulima. Kwa mfano, mkulima wa mahindi wa Mufindi anapoanza kulima mahindi yake hakuna sehemu yoyote Serikali ina-interfere. Anaingia shambani, analima, anapanda, anaweka mbolea, anavuna. Anapoanza kuvuna tu, akitaka kuanza kuuza Serikali inaingia kati, inaanza kusema kwamba sasa hivi mahindi yasiuzwe. Kwa hiyo, ifike wakati tuwekewe Sera na Sheria iliyokuwa bora ambao itaondoa ukakasi uliokuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo wamechangia wachangiaji wengi ni eneo la mifugo. Hili ni eneo muhimu na kama tulivyozungumza kwenye ripoti yetu kwamba Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na mifugo mingi katika bara la Afrika, lakini je, kuwa wa pili katika Bara ya Afrika na kuwa na mifugo mingi inaleta tija? Hilo ndilo suala la kujiuliza.

Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya vizuri kupitia Wizara yetu ya mifugo kwa kupitisha chanjo nyingi kwa mifugo yetu. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri amelitekeleza zoezi hili vizuri, lakini bado kuna shida kwenye eneo hili. Kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanatakiwa yaangaliwe kwa kina kusudi tupate ng‟ombe walio bora wenye quality bora kusudi tuweze kupata soko zuri katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi sisi kama Watanzania tuna soko la uhakika Dubai na Oman, lakini hatuna soko la uhakika nchi za SADC na Ulaya. Kwa nini hatuna soko la uhakika? Ni kwa sababu quality ya ng‟ombe wetu haijafikia hadhi ya nyama ambayo inaweza kuuzwa kwenye Soko la Dunia. Sisi kama Kamati tunaendelea kuishauri Serikali iangalie kwa kina kwenye eneo hili kusudi tupate ng‟ombe waliokuwa bora na tuweze kupata soko la uhakika katika nchi za Ulaya na SADC.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Uvuvi ni muhimu sana kwa mustakabali wa uchumi wa nchi yetu. Kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wavuvi wetu, lakini namshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa uvuvi tena, alianza mchakato wa kuhakikisha tunafanya mabadiliko ya Sheria ya Uvuvi. Mchakato huu umechukua muda mrefu. Tunaomba mchakato huu uje Bungeni kwa sababu tunaamini kabisa mchakato huu ndiyo mwarobaini ya malalamiko ya wavuvi katika nchi yetu. Kwahiyo, miongoni mwa maazimio yetu, tunaomba Serikali iharakishe kuleta mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni eneo la maji. Katika wachangiaji wetu akiwemo Mheshimiwa Jitu Soni, amezungumzia kodi ya mitambo ya kuchimba visima iangaliwe. Ni kweli kuna haja ya kuangalia kwa sabbau Watanzania wana matatizo mengi ya maji. Kwa hiyo, Serikali iangalie zile kodi ambazo siyo za lazima kwenye eneo hili zipunguzwe kusudi watu wengi waweze kupata maji.

Mheshimiwa Spika, kuna shida nyingine, kuna watu wengi katika nchi hii wamejitolea kuisaidia nchi yetu katika Sekta ya Maji, lakini kuna tatizo. Wanapoanza kufanya kazi za kusaidia katika Sekta ya Maji kuna shida, wanapoagiza vifaa kutoka nje, Serikali inaendelea kuwatoza kodi nyingi ikiwemo VAT. Ifike wakati wale wote ambao wanasaidia nchi yetu kupata maji, Serikali isamehe kodi za VAT pamoja na kodi mbalimbali kusudi wale wafadhili wetu waweze kujielekeza zaidi katika maeneo makubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine la mwisho ambalo nataka kuchangia hapa ni eneo la force account. Wizara ya Maji imeamua kabisa kujielekeza katika kuhakikisha miradi yake inatatuliwa kwa utaratibu wa force account. Force account inapunguza gharama, inaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi na inapunguza ubadhirifu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na faida hizi tatu tulizoiona hapo juu, lazima tuweke angalizo. Tunaweza kuwa tuna faida hizi za msingi hapa tatu, lakini je, ubora wa miradi uko sawa? Kwa hiyo, tujiangalie, tunapokwenda kwenye force account tuhakikishe na miradi yetu inakuwa bora.

Mheshimiwa Spika, la pili, tunawaondolea ajira Watanzania wengi wenye makampuni ya maji. Kwa hiyo, kwenye eneo hili lazima tuhakikishe Serikali inafanya kazi yake kuhakikisha na watu wengi ambao wamesajili makampuni ya kutekeleza miradi ya maji wanapata fursa ya kufanya hiyo. Kwa sababu kwa kuziondoa hizi kampuni za maji kunakosesha kodi kwenye Serikali na kunaondolea ajira vijana wetu hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, la mwisho wataalam wa kutosha kwa kutekeleza hiyo miradi ya force account hatuna. Wengi wamesimama kulizungumzia suala la force account, lakini kwa nini Wizara ya Maji imeamua kujielekeza kwenye force account kuna shida sehemu.

Mheshimiwa Spika, BOQ za miradi ya maji zinaandaliwa na wataalam wa Wizara ya Maji. Ifike sehemu Serikali iangalie wataalam wake wanavyoandaa hizo BOQ wanaandaa kwa uhalisia? Kama hawaandai kwa uhalisia Serikali iwachukulie hatua waandaji wote BOQ ambao wanafanya ulaghai katika maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya, sasa naomba Bunge lako Tukufu lipitishe Maazimio tuliyoleta pamoja na marekebisho ya takwimu yaliyoletwa na Serikali kupitia Wizara ya Uvuvi na Mifugo.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. JUMANNE K. KISHIMBA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. MOHAMED H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nichukue fursa hii kumpongeza ndugu yangu, Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, Waziri wa Maliasili pamoja na mdogo wangu Mheshimiwa Kanyasu kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara yao, waendelee kuchapa kazi, sisi tuko nyuma yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu utajielekeza kwenye ushauri zaidi. TANAPA - Hifadhi ya Taifa tulikuwa tuna hifadhi 16 na katika hifadhi 16 hifadhi tano tu ndizo zilizokuwa zimeweza ku-break even point; Hifadhi ya Arusha National Park, Kilimanjaro National Park, Serengeti, Manyara na Tarangire, lakini hifadhi nyingine 11 zilizokuwa hapo awali zilikuwa hazijaweza ku-break even point na sasa hivi tumeiongezea TANAPA hifadhi nyingine tano kwa hiyo, wana hifadhi 11, kwa hiyo, mzigo uliokuwa unaendeshwa katika hifadhi hizi nyingine 11 umeongezewa nyingine tano zimekuwa 16, kwa hiyo, kwenye eneo hili tuna hifadhi 16 ambazo hazi--break even point, kwa hiyo, TANAPA tumewaongezea mzigo mkubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili tunatakiwa tuliangalie kwa makini. Lengo letu ni kuhakikisha hizi hifadhi zinatuletea mapato ya kutosha, lakini kama hatutakuwa tuna mkakati mzuri wa kuhakikisha tunazisaidia hizi hifadhi zikapata mapato ya kutosha hilo ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna hifadhi kama Saadani. Saadani ina utalii wa aina yake, hapa tunaweza tukapata hadi maeneo ya fukwe. Sasa naiomba sana Wizara ije na mikakati mizuri ambayo itatusaidia kwenye hifadhi hizi 16 ambazo tumeziorodhesha sasa ziweze ku--break even point, otherwise tutakuwa hatuna sababu ya kuongeza kwa sababu kwenye taarifa yake ambayo Waziri ameizungumza amesema bado kuna hifadhi mbili kwa maana ya Moyowosi na Rubando Rumanyika, wanataka kuziingiza kwenye Hifadhi za Taifa kwa hiyo, tutakuwa tunazidi kuwaongezea hawa wenzetu wa Nationa Park mzigo mzito. Tunajua Dkt. Kijazi anafanya kazi nzuri, lakini watakuwa wanambebesha mzigo ambao atakuwa anashindwa kuufanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ushauri wangu kwenye eneo hili, gawio ambalo linapelekwa kwenye Serikali Kuu hawa wenzetu wangeli-retain kusudi waweze kuzihudumia hizo hifadhi zilizobaki kwenye maeneo haya. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliangalie hili. Tunataka hizi hifadhi ziendelee kutupatia pesa, kwa hiyo, hilo gawio tuli-retain kwenye hizi hifadhi kusudi hawa wenzetu wa National Park waweze kufanya kazi yao vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, lazima wenzetu watuambie wana mikakati gani ambayo wameitengeneza kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha utalii hapa nchini? Sisi kama Watanzania tumekuwa mara nyingi tunategemea utalii wa nje; je, tuna mikakati gani ya kuhakikisha tunakuza utalii wa ndani?

Mheshimiwa Naibu Spika, utalii wa ndani unaweza kuboreshwa tu kama tutatengeneza infrastructures za uhakika ambazo zitawasaidia watu wa kawaida waende kutalii ndani. Gharama za utalii zikiwa ziko rahisi zaidi Watanzania wengi watapata nafasi ya kwenda kupumzika. Kwa mfano Saadani, Mbuga ya Saadani iko karibu na mikoa mashuhuri kama Mkoa wa Dar-es-Salaam, Morogoro na kadhalika, kama tutaitengezea utaratibu wa infrastructure kwa maana ya maboma mle ndani yakawa bei rahisi, itakuwa rahisi kwa watu siku za weekend, Jumamosi na Jumapili kwenda pale Saadani na kupumzika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo nataka kuchangia ni suala la Ruaha National Park. Ruaha National Park ni mbuga ya pili kwa ukubwa katika Bara la Afrika baada ya Mbuga ya Kruger ile ya South Africa, lakini pamoja na ukubwa uliokuwepo hii mbuga inaonekana iko idle na hakuna mkakati wowote ambao unaonesha unataka kuikuza hii Mbuga ya Ruaha National Park. Kwa Sababu tuna interest ya kuhakikisha utalii ulioko pale katikati ya Tanzania uwe unalingana na ule wa Kusini mwa Tanzania, kwa hiyo, tutengeneze mkakati tuhakikishe na mbuga kama ya Ruaha Nationa Park inapewa kipaumbele na inaboreshwa kusudi iwe miongoni mwa mbuga muhimu katika nchi yetu. Ruaha National Park ni mbuga ambayo ina tembo wakubwa ambao huwezi kuwalinganisha na tembo wanaopatikana katika maeneo mengine yoyote hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo nilipenda kuchangia ni eneo la msitu na eneo hili nataka tena kutoa ushauri. Mheshimiwa Waziri naomba atusaidie sana tuangalie bei na tozo mbalimbali kwenye eneo hili la mazao ya misitu. Biashara ya msitu katika Mikoa ya Njombe na Iringa ni moja ya biashara nzuri sana katika mkoa wetu, lakini cha kusikitisha kwa sababu ya tozo hizi zilizopo biashara hii imeshakuwa ngumu. Uchumi wa Mufindi ulikuwa unategemea sana biashara ya msitu, lakini kwa sasa hivi kutokana na tozo zilizopo nyingi kwenye hili eneo imekuwa ngumu hizi biashara kufanyika kwa hiyo, watu wameshaanza kuhama. Mbao zimekuwa bei ghali kwa hiyo, kumetokea mbadala, watu badala ya kuezeka kwa kutumia mbao, sasa hivi wanaezeka kwa kutumia vyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri aliangalie hili jambo. Tumewekeza hela nyingi kwenye eneo la msitu, lakini tukiendelea kuliacha hili zao likaendelea kukaa kwa utaratibu huu litapotea kabisa na msitu utakuwa hauna thamani tena. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri zile tozo zilizopo kwenye eneo hili ziangaliwe upya na thamani na gharama za kuuza mbao kwenye eneo hili tuziangalie upya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri ni mahusiano, Mheshimiwa Waziri angetusikiliza ingekuwa bora zaidi kuliko anachokifanya sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mahusiano yaliyopo kati ya maliasili pamoja na maeneo yetu katika Majimbo ya Mufindi Kaskazini; katika Jimbo la Mufindi Kaskazini ni eneo ambalo tumewekeza sana katika Mradi wa Sao Hill kwa maana tumepanda miti mingi, lakini infrastructure nyingi zinaharibiwa sana wakati wa uvunaji wa misitu, lakini maliasili hawachangii chochote katika utengenezaji wa ile miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunamwomba Mheshimiwa Waziri jambo hili aliangalie kwa kina. Sisi watu wa Mufindi Kaskazini hili jambo linatusikitisha sana. Tukiwaomba hata siku nyingine wenzetu watupe makatapila na mimi kama Mbunge wao nitoe hela kidogo katika Mfuko wa Jimbo nichangie, hawako tayari kwenye jambo hili. Kwa hiyo, itafika kipindi sisi watu wa Jimbo la Mufindi Kaskazini tutakataa wenzetu wasiende tena kwenye msitu, watumie barabara za kwao, wasitumie barabara zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha atwambie tunajengaje mahusiano ya kuhakikisha wenzetu walioko kule Sao Hill wanatusaidia katika kutengeneza infrastructure za barabara zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la mwisho ambalo nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri, kule katika Jimbo la Mufindi Kaskazini kuna maeneo mawili ambayo ni mazuri sana kwa ajili ya utalii. La kwanza lipo Mpangatazara. Kule Mpangatazara kuna kisiwa ambacho kinahama, asubuhi utakuta kisiwa kiko kushoto baadae utakuta kiko Kaskazini. Kwa hiyo, Mheshimiwa Naibu Waziri namwomba sana Waziri awatume wataalam wake waje kwenye maeneo yale na waangalie, pale pana utalii mkubwa kwenye hilo eneo la Mpangatazara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine katika eneo hilo kuna waterfalls za Mpangatazara ambazo huwezi kuzipata sehemu yoyote hapa nchini. Kwa hiyo, utalii uko kwenye maeneo mengi, lakini kitu kingine, tulikuwa tuna vyura va Kihansi ambao walivuma sana miaka ya nyuma, lakini leo hatusikii chochote kuhusu vyura wa Kihansi, vyura hawa wanazaa, hakuna vyura wowote hapa duniani ambao wanazaa. Kwa hiyo, namuomba sana Mheshimiwa Waziri, wenzetu wazungu walikuja wakawachukua wale vyura wakawapeleka Ulaya, lakini sisi Watanzania tumenyamaza kimya hatutaki kuendelea kuukuza utalii katika eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namuomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja atwambie sisi kama Watanzania tuna mkakati gani kuhakikisha tunaendelea kuenzi eneo hili la utalii wa vyura ambao wanazaa ambao huwezi kuwapata sehemu yoyote hapa duniani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. Nawataka vijana waendelee kuchapa kazi. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia kwenye hoja hii muhimu, lakini kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kukupongeza sana kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuongoza Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumpongeza Waziri na Naibu wake wa Fedha kwa bajeti yao iliyokuwa nzuri. Lakini kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuanza kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kutenga asilimia 40 ya bajeti ya mradi wa maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa kuipongeza sana Serikali kwa kuanza kutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais, za kupeleka shilingi milioni 50 kwenye kila kijiji na kwenye Serikali za Mitaa. Naiomba Serikali ihakikishe inatengeneza utaratibu unaoeleweka kusudi zile hela shilingi milioni 50 ziweze kuwafikia walengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumshauri sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwamba moja ya majukumu ya Bunge ni kuishauri Serikali, lakini leo hii tumeona Waheshimiwa Wabunge wengi wamezungumzia sana tatizo la maji. Nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri, sisi Wabunge tumetumwa maji kwenye maeneo yetu, kwa hiyo tunataka tuone maji yanatoka. Katika eneo hili Wabunge wametoa hadi utaratibu ambao unaweza kutusaidia tukapata hela kwenye maeneo hayo. Kwa hiyo, sioni sababu ya Mheshimiwa Waziri kuanza kusita tumesema tuongeze shilingi 50 kwenye tozo la mafuta kwa maana ya dizeli na petroli. Sisi wenyewe Wabunge ndiyo tutakuwa tuko tayari kwenda kuwasemea wka wananchi kusudi wajue kwa nini tumeongeza pesa hizo, sasa sioni sababu ya Serikali kusita kwenye eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, adha ya maji inaeleweka na wanaopata tabu katika eneo hili ni wakina mama na ndoa nyingi zimekuwa zinamashaka kwa sababu ya tatizo la maji katika mjini pamoja na vijijini. Kwa hiyo, namuomba sana kaka yangu Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake waliangalie hili jambo kwamba moja ya miongoni mwa sera za Chama cha Mapinduzi ni kuhakikisha watu wanapata maji katika maeneo yao. Na hapa sisi kama Wabunge tumetoa commitment kwa kusema tuko tayari kuruhusu tutoe shilingi 50 kwenye mafuta ya dizeli na petroli kusudi tuhakikishe wananchi wetu wanapata maji katika maeneo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunamuomba sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri waliangalie hili jambo watakapokuja kuhitimisha hapa waone asilimia karibu 95 au 96 ya Wabunge wote wanataka kuhakikisha maji yanapatikana katika maeneo yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ya Bajeti wakati inajadiliana na Wizara ilitoa mapendekezo na ilikubaliana na hoja kwamba ile tozo ya shilingi 50 sehemu ya tozo ya shilingi 50 ipelekwe kwenye afya kwa maana ya kuboresha vituo vya afya na zahanati. Kwa hiyo, hatuna sababu ya kutokukwepa kwenye eneo hili. Ni lazima tukubaliane na hii hoja kusudi wananchi walio wengi wapate huduma kwenye afya pamoja na zahanati.
Mheshimiwa Naibu Spika, sababu alizokuwa anazitoa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwenye eneo hili, wanasema kwamba kuongeza tozo kwenye eneo hili tutakuwa tumeongeza mfumko wa bei. Siyo kweli, mwaka 2015 bajeti iliyopita tuliongeza tozo ya shilingi 50 kwenye maeneo haya, wakati uli mafuta yalikuwa yana rank kutoka shilingi 2100 mpaka 2500 na sasa hivi mafuta yana rank toka 1600 mpaka 1900 na mfumko wa bei uliendelea kubaki vilevile. Kwa hiyo, ninataka kumwambia Mheshimiwa Waziri asiingie woga kwenye eneo hili, watu wanataka maji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuomba hela hizi za maji naiomba Wizara ihakikishe hizo hela zinaenda kwa wakati kumekuwa kuna tatizo la kuzichelewesha hizi hela ziende kwa wakati kwenye maeneo haya. Matokeo yake ni kusababisha miradi ya maji kuendelea kuwa ya gharama zaidi, kwa sababu mradi unapochelewa kufanyiwa kazi automatical gharama za maji zinapanda.
Leo hii sisi Wabunge wa CCM ndio tupo ndani tunajadili, kwa hiyo tunamwomba sana Waziri wa Fedha akubaliane na hoja hizi kwa sababu ndizo zinazowagusa wananchi waliokuwa wengi. Tutaonekana Wabunge wa CCM tumetoa maamuzi mazuri kwa maslahi ya Taifa hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka kulizungumzia ni suala la kilimo. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, alisema asilimia 67 mpaka 72 ya Watanzania wanategemea kilimo, na yeye mwenyewe, wakati anazungumzia suala la mpango alizungumzia asilimia 67 ya Watanzania wanategemea suala la kilimo. Kulikuwa hakuna sababu ya kutokuongeza ruzuku ya pembejeo katika eneo hili. Kwa hiyo, tunamuomba Waziri aliangalie hili jambo.
Mheshimiwa Naibu Spika, yeye mwenyewe Mheshimiwa Waziri amekuja hapa ametuambia tuna kwenda kwenye mpango wa Viwanda, tunaendaje kwenye mpango wa viwanda kama malighafi hatuwezi kupata kutoka kwenye kilimo? Tunamwomba Waziri kusudi tuweze kupata malighafi ya kutosha, lazima tuhakikishe wakulima wanapata pembejeo kwa bei rahisi na wamesaidiwa katika eneo hili. Kwa hiyo, nataka nimuombe ndugu yangu aliangalie na hili jambo la kuongeza mfuko wa pembejeo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la Benki ya Kilimo, hili ni suala very sensitive na ni nyeti sana, kwa hiyo tunaomba kwenye benki hii waongezewe mtaji, na ifunguliwe matawi yote katika nchi hii ya Tanzania kusudi wale amabo tumewakusudia waweze kusaidiwa katika maeneo husika. Tuna kwenda kwenye uchumi wa viwanda, lengo kubwa ni kuhakikisha tunapata mapato ya kueleweka na tunapata ajira. Serikali inajitahidi kuwashauri wawekezaji wa ndani na nje kwenye eneo hili waje kuwekeza. Na wawekezaji wanawekeza kwa nguvu kubwa sana, itakuwa ni kosa kuendelea kuzitoza malighafi katika eneo hili. Kwa hiyo, nilikuwa namuomba Waziri anapokuja atuambie kwa nini ameamua kutoa tozo ya crude oil kutoka sifuri kwenda asilimia kumi. Tayari watu wameshawekeza hela zao pale na tayari kuna ajira ya uhakika katika eneo hili. Ni vyema aangalie ni utaratibu gani utakaotusaidia kupata kodi, kwenye eneo la wafanyakazi Pay As You Earn na kwenye kodi za kawaida. (Makofi)
Eneo lingine ambalo nataka kulizungumzia ni eneo la utalii. Katika bajeti iliyopita utalii ulichangia asilimia 17 kwenye Pato la Taifa na ilikuwa utalii inaongoza kwenye kuchangia katika Pato la Taifa lakini leo hii tunaweka...
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Awali ya yote napenda kuwapongeza Wenyeviti wote waliowasilisha leo mada zao hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa majukumu makubwa ya Bunge letu Tukufu ni kuishauri na kuisimamia Serikali, lakini kumekuwa kuna tatizo hapa. Tutazungumza, tutasema, lakini hayo tutakayokuwa tumeyazungumza na kuyasema na kuwashauri wenzetu wa Serikali watakuwa hawayafanyii kazi kama siku za nyuma. Kwa mfano, katika bajeti iliyopita sisi Waheshimiwa Wabunge wote kwa kauli moja tulishauri tuongeze tozo ya maji kutoka sh. 50 kwenda kwenye sh.100 na Wabunge wanajua matatizo yaliyopo kwenye majimbo yao. Cha kusikitisha kabisa Serikali ilikataa hili jambo na hela ambayo inafanya kazi sasa hivi ni hela ya Mfuko wa Maji, hela iliyokuwa kwenye bajeti kuu haipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawashawishi Waheshimiwa Wabunge wenzangu ili hoja ambayo tulikuja nayo kwenye bajeti tuendelee nayo na yawe ndiyo maazimio ya Bunge ili hiyo sh. 50 iongezwe ili kwenye bajeti ya safari hii tusiume maneno; kwamba tozo ya maji imetoka kwenye sh.50 kwenda kwenye sh.100 ili tuendelee kupata maji katika maeneo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninalopenda kushauri katika Wizara hii ya Maji ni suala la mita; tuwe na mfumo wa prepaid kama ilivyokuwa umeme, kwa sababu miongoni mwa watu wanashindwa kulipa maji kwa wakati matokeo yake Sekta hii ya Maji inashindwa kujiendesha. Kwa masikitiko makubwa taasisi nyingi za Serikali zimeshindwa kulipa na ndizo zilizoweka mzigo mkubwa sana kwenye taasisi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sekta hii kutengeneza hifadhi, kuchimba mabwawa ya kutosha ili maji yawe ya uhakika kwa muda mrefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la kilimo. Asilimia 67 mpaka 72 ya Watanzania ni wakulima na Serikali imesema kwamba inataka kwenda kwenye uchumi wa viwanda, tutaendaje kwenye uchumi wa viwanda kama hatujawekeza vya kutosha kwenye eneo la kilimo? Tuna matatizo kwenye eneo la pembejeo, naiomba Serikali katika eneo la pembejeo tuangalie kwa nafasi kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya nyuma tulikuwa tuna eneo kubwa la kutoa ruzuku katika eneo hili, lakini cha kusikitisha ruzuku inayotoka safari hii ni ndogo kuliko iliyokuwa siku za nyuma, mfuko wa ruzuku katika eneo hili umepungua. Kwa hiyo, waongeze mfuko wa ruzuku tofauti na uliokuwepo miaka iliyopita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa, Serikali imekuwa hailipi pesa za mawakala, kwa hiyo wametengeneza gap kubwa kati ya mawakala na wakulima wetu waliokuwa kijijini. Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 64, huu mwaka wa tatu na baadhi ya mawakala wameuziwa nyumba zao na baadhi ya mawakala wamekufa kutokana na shock walizokuwa nazo katika maeneo. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali ijiangalie na iwalipe hawa mawakala kusudi waweze kufanya kazi zao mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye eneo la ukame. Hapa kwenye eneo la ukame kuna tatizo. Naishauri Serikali ipeleke mbegu ambazo zinahimili ukame katika maeneo husika, lakini vilevile katika yale maeneo ambayo kwenye ripoti yetu tumeyasoma leo, zile halmashauri 55 ambazo zina matatizo ya chakula tunaiomba Serikali ipeleke chakula haraka iwezekanavyo. Kwa sababu tunaweza tukashindwa kupeleka chakula kwa wakati tukasababisha inflation, chakula kitakuwa kiko juu kwa sababu ya demand pullinflation katika maeneo yale,kwa hiyo hata ule mfumuko wa bei tunaouzungumzia kwamba tunaweza tukau-control, tatizo la chakula likiendelea kuwepo katika maeneo husika automatically inflation itaongezeka katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa tunaiomba Serikali iondoe kodi kwenye mbegu zinazozalishwa hapa nchini. Unakuta mbegu zinazotoka nje ya nchi hazina kodi lakini mbegu zinazozalishwa na Watanzania zina kodi. Haya ni masikitiko makubwa sana, waziondoe hizo kodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunaomba Serikali iongeze mtaji kwenye Benki ya Kilimo, mtaji uliopo sasa hivi hautoshi. Kwa hiyo, wakulima wetu hata kama wanataka kufanya kazi kwa ajili ya kuisaidia hiyo sekta ya viwanda ambayo inataka kuja hatuwezi kupata kwa sababu benki katika sekta hii haipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie kidogo kuhusu ranchi. Tuna tatizo, kuna baadhi ya ranchi zilichukuliwa na watu binafsi na zinaendelea kumilikiwa na watu binafsi. Hatuna sababu ya zile ranchi kuendelea kumilikiwa na watu binafsi ikiwa hawazitumii kwa yale makusudi tuliyoyakusudia; matokeo yake mifugo mingi inazurura kwenye hifadhi za Taifa na kuleta kero ambazo hazina sababu. Kwa hiyo wale watu ambao wanatumia ranchi zile ambazo hazina sababu ya kutumiwa wanyang’anywe zirudishwe Serikalini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ninalotaka kuzungumzia kidogo ni suala la maliasili. Nataka kuzungumzia suala la VAT kwenye maliasili. VAT inapokuwepo automatically unaongeza gharama za utalii, kwa hiyo Serikali yetu badala ya kupata mapato tunayostahili kupata, hatuwezi kupata mapato yale kwa wakati, kwa hiyo Serikali iliangalie upya suala la VAT. Wenzetu wa Kenya tulikwenda nao kwa kauli moja, lakini ilipofika wakati wa utekelezaji Wakenya wakaji-withdraw kwenye hili jambo wakatuacha tukakaa peke yetu, kwa hiyo utalii wa hapa nchini ukawa gharama zaidi kuliko wa kwao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la miundombinu. Miundobinu ya utalii katika nchi yetu ni dhaifu, kwa hiyo tunatakiwa tujiangalie kwenye hili eneo, tuboreshe miundombinu katika maeneo ya utalii na tujenge nyumba za bei rahisi kwenye hifadhi zetu ili watu wa kawaida waweze kwenda kutalii. Kwa hiyo kuna haja ya kutunza utalii wa ndani katika nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ardhi. Maafisa wengi wa ardhi, hasa maafisa wa mipango miji wamekuwa wana matatizo makubwa sana katika maeneo yao, hawafanyi kazi zao ipasavyo matokeo yake watu wanaendelea katika ujenzi holela.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo machache, naunga mkono hoja. Naomba yale maazimio yote ambayo yametolewa na Kamati zilizohusika tuyapigie kura na yaweze kutekelezwa na Serikali.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa naunga mkono hoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Pombe Magufuli, lakini kwa namna ya kipekee, naomba nimshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake. Pia niwapongeze ndugu yangu Waziri, Mheshimiwa Jenista Mhagama na Naibu wake kwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nitauelekeza katika maeneo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza kuwawezesha wananchi kiuchumi. Katika kampeni yetu ya uchaguzi ya mwaka 2015, Ilani ya Chama cha Mapinduzi tuliahidi kupeleka shilingi milioni 50 kwenye kila kijiji na kwenye kila Serikali ya Mtaa. Huu ni mwaka wa pili sasa toka tulipotoa ahadi ile. Ni vyema tukatekeleza ile ahadi. Tumebakia na mwaka mmoja tu wa kufanya kazi, mwaka 2018, 2019 tutaenda kwenye uchaguzi, tusipotimiza ahadi ambazo tumeziahidi wenyewe itakuwa vigumu sana mwaka 2019 kuomba kura hasa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu nakuomba, kupitia kwenye Serikali yetu ya Chama chetu cha Mapinduzi tutekeleze ahadi hii muhimu kwa sababu wananchi waliokuwa wengi kule vijijini na kule kwenye Serikali zetu za mtaa walikuwa wanategemea wapate shilingi milioni 50 hizi kusudi ziweze kuwatoa kwenye stage moja kwenda kwenye stage nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ambalo nataka kuchangia ni suala la kilimo. Watanzania kati ya 67% mpaka 70% wameajiriwa katika eneo hili. Tumekusudia kwenda kwenye uchumi wa viwanda, lakini hawa wananchi ambao wameajiriwa kwenye eneo hili hatuwapi facilities za kutosha. Ukiangalia pembejeo sasa hivi ni ghali sana kuliko siku za nyuma. Kwa hiyo, ule uchumi wa viwanda ambao tumekusudia kwenda utakuwa mgumu sana kwa sababu malighafi ambazo tumekusudia kuzipata hatutazipata kwa sababu wakulima hawa watakuwa hawana uwezo wa kulima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namuomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu aliangalie sana hili eneo la pembejeo hasa mbolea kwa wakulima wetu zisiendelee kupanda bei. Mheshimiwa Waziri Mwigulu kipindi kilichopita alituahidi kwamba mbolea itauzwa bei rahisi, itauzwa kama
soda, lakini haya yaliyokuwa tumeahidiwa hayafanyiki na hatuyaoni. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iliangalie sana eneo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo hili hili la kilimo Mheshimiwa Waziri Mkuu kuna hawa wenzetu mawakala wa pembejeo ambao wanaidai Serikali takribani shilingi bilioni 68. Huu ni mwaka wa nne wanadai hela zao na hawajalipwa mpaka leo. Kuna baadhi ya watu wameshaanza kuuziwa nyumba zao na wengine wanakufa. Kwa hiyo, tunamuomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu atengeneze utaratibu wa kuhakikisha hawa watu wanaodaiwa hela zao katika maeneo haya wanalipwa baada ya kuwa wamehakikiwa vizuri. Kuendelea kuwaacha na madeni, watakufa na hali zao zitaendelea kuwa mbaya. Serikali yetu ni sikivu, nina uhakika hawa watu watalipwa hela zao haraka iwezekanavyo baada ya uhakiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka kuchangia ni suala la maji. Maji ni tatizo kubwa na kule kwenye jimbo langu kuna tatizo kubwa sana la maji. Cha kusikitisha ni kwamba tatizo hili limekuwa kubwa na linaendelea kuwa kubwa siku baada ya siku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi kubwa ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali. Mwaka jana katika mambo mengi ambayo sisi Wabunge tuliishauri Serikali kwenye bajeti iliyopita hayakutekelezwa likiwepo la kuongeza tozo ya kutoka shilingi 50 kwenda shilingi 100. Tulikuwa na uhakika kama tungeweza kuongeza tozo kwenye eneo hili Mfuko wa Maji ungeendelea kuwa mkubwa na hatimaye watu wengi wangepata huduma ya maji katika maeneo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana kupitia Waziri Mkuu, muwe mnatusikiliza na sisi Wabunge. Hakuna Mbunge ambaye anataka kero ya maji iwepo katika maeneo yake. Kwa hiyo, tunaomba sana Waziri Mkuu kwenye jambo hili atusikilize na sisi Wabunge. Sisi Wabunge wenyewe tumekubali kwamba ile shilingi 50 iende kwenye shilingi 100 na tutatolea majibu kwa wananchi kwa nini tumeamua kuongeza tozo katika eneo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilitaka kuchangia katika sehemu ya maji ni kwamba katika Jimbo langu la Mufindi Kaskazini kuna vyanzo vikubwa viwili vya maji. Katika Tarafa ya Sadani kuna vyanzo vya maji vya Mto Kihata. Hili eneo linahitaji shilingi bilioni mbili tu ili eneo hili liweze kusaidia kutoa maji katika vijiji 19. Tumeshaleta maombi mara kwa mara katika Wizara ya Maji lakini mpaka leo halijashughulikiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini eneo lingine la pili ni Tarafa ya Ifwagi. Tuna taasisi ya RDO ya watu binafsi imetusaidia kutoa maji kwa kata takribani tano na wanalisha vijiji takribani 30. Serikali haijatia mkono wake wowote katika eneo hili. Ni wakati umefika sasa kwa Serikali yetu kutia mkono. Kwa masikitiko makubwa kwenye eneo hili inafika wakati hawa wanatozwa VAT, kwa hiyo, badala ya kuwapa moyo wanakosa moyo wa kushughulikia eneo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka kulizungumzia ni barabara. Tuna barabara kubwa mbili katika Jimbo langu la Mufindi Kaskazini ambazo nataka mziangalie
kwa macho mawili. Barabara moja ni kutoka Kinambo A – Isalavanu – Saadani - Madibila - Lujewa. Mwaka 2010 na 2015 barabara hii iliingia kwenye Ilani ya uchaguzi, kwa maana ya vipindi vyote vitano imeingia kwenye Ilani ya Uchaguzi lakini hata kilometa moja haijawahi kutengenezwa. Kwa hiyo, tunakosa majibu ya kuwajibu wananchi kwenye maeneo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamuomba sana Waziri Mkuu kwenye jambo hili aliangalie. Nakuomba Waziri Mkuu ufanye ziara katika Wilaya ya Mufindi kwa sababu hakuna kiongozi yeyote wa kitaifa ambaye amekuja katika Wilaya ya Mufindi kujionea hali halisi. Nataka nikuambie miongoni mwa maeneo ambayo tunapata kura nyingi CCM ni Wilaya ya Mufindi. Wananchi wa Wilaya ya Mufindi wasije wakakata tamaa kwa sababu yale mambo ambayo tumeyaahidi hayafanyiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine tulilokuwa tunaomba mtusaidie ni barabara ya kutoka Johns Corner - Mgololo na barabara ya kutoka Mchili – Ifwagi – Mdabulo – Ihanu - Tazara - Mlimba. Barabara hii inaunganisha Wilaya mbili na mikoa miwili. Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi haina uwezo wa kuitengeneza barabara hii. Kwa hiyo, tunaomba sana ipandishwe hadhi na tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kupeleka barua kupitia kwenye Road Board ya Mkoa, lakini kwa bahati mbaya mpaka leo Waziri mhusika hajawahi kutujibu kwenye eneo
hili.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mheshimiwa Makamu wa Rais na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa utendaji huu mzuri uliotukuka, naomba tuwapongeze sana. Naomba nichukue fursa hii
kumpongeza sana kaka yangu Profesa Mbarawa pamoja na Naibu wake Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara hii, pamoja na watendaji wote wa Wizara yao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijielekeze sasa katika mchango wangu, nitaanza na barabara ya kutoka Kinyarambo A - Salavanu – Saadani - Madibila – Rujewa. Barabara hii inaunganisha Wilaya mbili, barabara hii inaunganisha mikoa miwili na inaunganisha Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Rujewa, Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Mbeya.
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii kama tulivyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2000, kwamba itajengwa kiwango cha lami, 2005 itajengwa kwa kiwango cha lami, 2010 itajengwa kwa kiwango cha lami, na 2015 itajengwa kwa kiwango cha lami; lakini hizo ahadi zimekuwa hewa mpaka leo hakuna hata kilometa moja iliyojengwa kwa kiwango cha lami, katika barabara hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ikijengwa itasaidia kwa kiwango kikubwa sana kukuza uchumi katika eneo hili na barabara hii ni shortcut ya barabara ya kutoka Mbeya itapunguza zaidi ya kilometa 60, hii ni manufaa makubwa sana katika uchumi huu. Kwa hiyo, namuomba sana Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha hoja yake atueleze sababu zipi zimepelekea barabara hii inaonekana kwenye Ilani ya Uchaguzi kwa vipindi vitano, lakini mpaka leo haijajengwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, inakuwa vigumu sana kurudi kwa wananchi wetu kuwaambia kwamba mpaka leo hii hatuna hoja za msingi kama watu wa CCM, watu wa Serikali, kwa nini vipindi vitano mfululizo mpaka leo haijajengwa? Naamini kabisa kaka yangu Profesa Mbarawa atakuja kuniambia maneno haya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kesi ya pili ninayotaka kuzungumzia ni barabara ya kutoka Mtili – Ifwagi – Mdaburo
– Ihanu – Isipii – Tazara – Mlimba. Barabara hii inaunganisha Wilaya mbili, inaunganisha Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Kilombero, ina urefu wa kilometa 116, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi haina uwezo wa kujenga barabara hii.
Mheshimia Naibu Spika, katika vikao vyetu vya mwaka 2013, 2014 na 2015 tulipitisha katika Wakala wa Barabara wa Mkoa wa Iringa na Mheshimiwa Rais ambaye alikuwa Waziri wakati uliopita alikubali kupeleka wataalam kwa ajili ya kufanya utafiti kuona kama ina hadhi ya kupandishwa kuwa barabara ya TANROADS, lakini mpaka leo hii Mheshimiwa Waziri hawajaleta wataalam wa aina yoyote katika hili eneo. Namuomba sana kaka yangu atakapo kuja atuambie ni lini atatuletea hao wataalam kwa ajili ya kuja kufanya upembuzi yakinifu na barabara hiyo iweze kupandishwa kiwango.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo nataka kulizungumzia ni suala la barabara kutoka Jets corner - Kibao mpaka Mgololo, barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa Wilaya ya Mufindi na uchumi wa Mkoa wa Iringa kwa ujumla. Eneo hili lina viwanda vingi vya mbao pamoja na chai, lakini ni muda mrefu hakuna hata kilomita moja ya barabara ya lami iliyojengwa katika eneo hili, ukichukulia kuna makampuni ambayo yanalipa mabilioni ya pesa kwenye kodi ya Serikali katika nchi hii. Kwa hiyo, tunaiomba sana Serikali itupie macho mawili eneo hili kusudi tuweze kupata barabara ya lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni suala la uwanja wa ndege wa Mkoa wa Iringa wa Nduli. Huu uwanja ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Iringa ukichukulia Iringa ni sehemu ambayo ina- base kubwa sana ya utalii. Kwenye eneo hili naomba niunganishe na barabara ya Ruaha National Park. Ruaha National Park ni mbuga ya pili kwa ukubwa katika Bara la Afrika, baada ya mbuga ya Kruger ya South Africa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kuna haja ya kuukuza uchumi wa nchi hii katika eneo la Ruaha National Park kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami. Kuna watalii wengi sana wanapenda kutembelea katika maeneo haya, lakini tatizo kubwa linakuwa hatuna barabara ya lami na hakuna uhakika wa kufikika kwenye hili eneo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama barabara hii itapata kiwango cha lami nina uhakika kabisa ile mbuga ya Kruger haina sifa ambazo Ruaha National Park inazo. Automatically Ruaha National Park inaweza kuwa mbuga ya namba one kwa ukubwa katika Bara la Afrika.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana kaka yangu Profesa Mbarawa kwa kufungua kituo cha reli pale Mpanga Tazara ambacho kilikuwa kimefungwa, sasa hivi kinafanya kazi. Ninachomuomba ndugu yangu wakifanyie ukarabati kile kituo cha reli pamoja na kukifanyia ukarabati kituo kidogo cha pale Kimbwe kusudi wananchi katika eneo hili waendelee kupata huduma.
Mheshimiwa Naibu Spika, namuomba sana Mheshimiwa Profesa Mbarawa Sheria za Barabara zifanye kazi, kwa sababu uharibifu mwingi unatokana kwa sababu zile sheria watu hawaziangalii, watu wanaharibikiwa magari yao, wanaacha magogo matokeo yake barabara zinaendelea kuharibika; hata ile dhana bora ya kutaka tupate barabara nzuri katika nchi hii inakuwa haina maana.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kwenye masuala ya mawasiliano, kuna maeneo matatu ni muhimu sana katika Jimbo langu ya Mufindi Kaskazini. Eneo la kwanza ni eneo la Ikwera, tayari mnara umeishajengwa, lakini kwa masikitiko makubwa huu mwezi wa sita sasa hivi ule mnara haufanyi kazi. Eneo la Mapanda mnara umeishajengwa lakini kwa masikitiko makubwa mpaka sasa hivi mnara haufanyi kazi. Eneo la Isipii mnara umeishajengwa lakini kwa masikitiko makubwa mpaka sasa hivi minara haifanyi kazi.
Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri naomba utakapokuja kuhitimisha bajeti yako, utuambie kwa nini mpaka leo minara hii haifanyi kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache naomba niunge mkono hoja.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kuwapongeza sana kwa kazi nzuri Mheshimiwa Waziri pamoja Naibu Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu utajieleza kama ifuatavyo:-

Kuhusu uzinduzi wa zahanati, wananchi wamefanyakazi nzuri za kujenga zahanati, tatizo kubwa lililopo ni uzinduzi wa zahanati hizo kwa sababu ya kukosa wataalam, vifaa pamoja na allocation ya dawa. Naomba sana Mheshimiwa Waziri au Naibu Waziri wa Afya aje kwenye Majimbo yetu ili uzinduzi wa hizo zahanati ufanyike haraka iwezakanavyo ili kutovunja nguvu za wananchi waliojitolea katika ujenzi huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ni vituo vya afya, katika ilani ya chama chetu, tuliahidi kujenga kituo cha afya katika kila kata, naomba sana Serikali ituunge mkono kwenye maeneo haya ya kujenga vituo vya afya hii itakuwa suluhisho la kudumu na kwa namna ya kipekee niipongeze Serikali kwa kujenga vituo vya afya vya mfano kila Jimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni eneo la dawa katika zahanati zetu. Vituo vya afya pamoja na hospitali zetu naomba sana muongeze migao ili wananchi wasiendelee kusumbuka.

Kuhusu tiba kwa wazee ni vema sasa Serikali ikaweka mkakati wa kuhakikisha huduma zote muhimu zinapitika kwa wakati katika kitengo hicho cha wazee na kuwa wanapata dawa kwa wakati na madaktari wawepo wakati wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, chapeni kazi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nichukue fursa hii kuunga mkono hoja zote za Kamati ya Kilimo, Mifugo pamoja na Maji kwa sababu mimi ni Mjumbe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais pamoja na Serikali yake kwa ujumla kwa jinsi wanavyofanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukumu makubwa ya Bunge ni kuishauri Serikali. Kamati yetu mwaka jana tuliishauri Serikali, tukaomba tuongeze tozo kutoka shilingi 50 kuwa shilingi100; lakini kwa bahati mbaya Serikali haikukubaliana na ushauri wa Kamati na mwaka huu Kamati yetu tena imeishauri Serikali, tuongeze tozo kutoka shilingi 50 mpaka shilingi 100. Haya yanajieleza wazi, tunaona kuna gape hapa, kama hii tozo ingekuwa imetozwa toka mwaka jana hili gape linalozungumzwa sasa hivi lisingekuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana Serikali iwe inasikiliza ushauri wa waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa naomba anieleze kwa nini Serikali ina kigugumizi cha kusaini mkabata wa Tanzania na Australia ambao ulikuwa unaweza kutoa maji katika majimbo matatu ya Wilaya ya Mufindi pamoja na Wilaya ya Kilolo, kwa nini Serikali inapata kigugumizi? Hela ziko wazi, tulichotakiwa ni kusaini tu ule mkataba; kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa naomba atupe majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo langu la Mufindi Kaskazini lina kata 11, lakini cha kusikitisha hakuna hata kata moja yanye maji. Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni zetu moja ya vipaumbele muhimu tulisema tupate maji, lakini ukienda kwenye kata za Ikwea, Sadani, Igombavanu, Ihalimba kote hakuna maji. Ifike wakati hawa Waheshimiwa wenzetu Mawaziri waje watusaidie kujibu hoja huko kwenye maeneo yetu, lini maji yatapatikana katika maeneo haya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Mufindi miongoni mwa Wilaya kubwa hapa nchini, ina majimbo matatu, lakini cha kusikitisha tumepata bilioni 1.5 kwenye Jimbo la Mufindi Kusini, Mufindi Kaskazini pamoja na Mafinga Mjini. Kwa nini tunapata hela? Uwiano wa kugawa hii hela unapatikana vipi? Kuna baadhi ya maeneo zimekwenda shilingi bilioni 200, why? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tufike sehemu kuwe kuna uwiano ambao unaridhisha. Unakuta kuna maeneo mengine yanaonekana yako bora zaidi kuliko maeneo mengine. Waziri aje atwambie wanatumia vigezo gani kupeleka shilingi bilioni 200 kwenye maeneo mengine na kwenye eneo lingine hakuna hata senti tano? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna baadhi ya taasisi kama RDO zinafanya kazi kubwa sana za maendeleo katika maeneo yetu. Hii taasisi ya RDO inasaidia kuleta support ya maji katika kata ya Ndabulo, lakini kwa masikitiko makubwa sana Serikali hatuwaungi mkono. Inafika sehemu hata vifaa ambavyo vinasaidia kuleta maji katika maeneo yale vinachajiwa (be charged) VAT. Watu wanatoa maji bure kwa wananchi, leo tunaendelea kuwa-charge VAT. Badala ya kuwasaidia hawa watu tunawa-demoralise.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna miradi ya World Bank kama miradi ya Ukami, Mapanda pamoja na Igomaa, mpaka leo mwaka wa saba miradi hii haijatekelezwa na hela zilishalipwa. Atakapokuja Waziri hapa atueleze kwa nini miradi hii haijakamilika na Serikali inatakiwa ichukue hatua gani kusudi hii miradi ikamilike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mzee Pinda aliahidi kutoa shilingi milioni 295 kwa ajili ya kuendeleza bwawa la kilimo pale Nundwa, lakini mpaka leo hela hizi hazijatolewa. Kwa hiyo, mimi namuomba sana Mheshimiwa Waziri, baada ya bajeti hii aje atembelee kwenye maeneo yetu aone hali halisi katika maeneo yetu ili kusudi aweze kutusaidia watu wa Jimbo la Mufindi Kaskazini na Wilaya ya Mufindi kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Naomba kuchukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara yake. Mimi ni mjumbe wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, kwa hiyo naungana moja kwa moja na mapendekezo ya Kamati yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania walio wengi takribani asilimia 67 mpaka 70 wameajiriwa kwenye sekta hii ya kilimo. Kwa hiyo, kama Serikali imedhamiria kweli kutupeleka kwenye Uchumi wa Viwanda tunatakiwa kuongeza bajeti kwenye sekta hii ya kilimo. Badala ya bajeti hi kukua bajeti hii inaendelea kupungua kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sikubaliana na kuendelea kuipunguza hii bajeti, naomba Serikali iliangalie kwa jicho la huruma, kwamba eneo hili ndio eneo pekee ambalo linatoa ajira ambayo haina shaka katika nchi hii. Kwa hiyo ni vyema tukaongeza bajeti kwenye eneo hili kusudi watu walioajiriwa kwenye eneo hili waendelee kupata facilities kwa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana kabisa na pendekezo la Serikali la ununuzi wa pembejeo kwa pamoja (bulk procurement). Tumeona kwenye mafuta tumefanikiwa sana na naamini kwenye pembejeo vile vile tutafanikiwa sana kwa ajili ya hii bulk procurement. Hii itatusaidia pembejeo itanunuliwa kwa wingi na naamini zitafika kwa wakati kwenye site.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kule kwetu Mufindi, ukipeleka pembejeo baada ya mwezi wa Tisa, wakulima hawawezi kulima. Kwa hiyo, tunamwomba sana Mheshimiwa Waziri ambaye amelileta pendekezo hili kwenye Kamati yetu na sisi tumelikubali na Waheshimiwa Wabunge
naamini tutalikubali kwamba hizi pembejeo zinunuliwe kwa wakati na zifike kwenye site kwa wakati. Pia tunaamini kwamba Serikali itakapopata kazi ya kununua hii, hakuna matatizo tena ya bei kwenye hizi pembejeo. Kwa sababu kuna watu walikuwa wanajipatia faida bila sababu. Kwa hiyo, nina hakika kabisa watu wetu wa Mufindi watalima wakiwa hawana shaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo napenda kuchangia ni Benki ya Kilimo. Tuna benki ya kilimo na takribani ina miaka minne lakini benki hii haikui. Kwa hiyo, kusudi tuwasaidie wakulima walio wengi katika site kule ni vyema Serikali ikaongeza mtaji kwenye hii benki. Mtaji huu utawasaidia wakulima wadogo wadogo kukopa kwenye eneo ambalo halitakuwa lina interest kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile, tunaiomba sana Serikali ifungue matawi kwenye site. Unakuta benki ya kilimo matawi yapo Dar es Salam, Arusha, yako wapi, kule site kwenye wakulima wadogo wadogo wa viazi, wakulima wadogo wadogo wa miwa, hatujafungua benki za kilimo. Wakulima wadogo wadogo wa nyanya kama vile ukienda kwenye majimbo ya wenzetu kama ya Kilolo, Ilula, Mufindi na Mdabulo. Tunaomba sana Serikali ifungue matawi kwenye maeneo haya na ihakikishe mikopo inaendelea kuwa kwa riba nafuu kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema hapo nyuma, azma ya Serikali ni kutupeleka kwenye uchumi wa viwanda. Ukitaka kuangalia kwa haraka haraka, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni watoto pacha ambao wanakwenda simultaneous. Kwa hiyo, bado naendelea kusisitiza tu kwamba hatutapata mafanikio ya kutosha kama hatutawekeza kwa kiasi kikubwa kwenye eneo hili la kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo napenda kuchangia ni eneo la SAGCOT, hawa wenzetu wa SAGCOT ambao wanawasaidia wakulima wadogo wadogo wamejielekeza kwenye maeneo machache, tunaomba wafike kwenye maeneo mengine hata maeneo ya kule Mufindi. Wakifika kwenye maeneo haya, watasaidia sana kuhakikisha watu wanaboresha miundombinu na wanapata masoko ya uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule kwetu katika Wilaya yetu ya Mufindi Jimbo la Kusini na Kaskazini ni wakulima wakubwa sana wa chai. Kwa masikitiko makubwa, chai imekuwa inaharibika, inapotea, kwa sababu hatuna miundombinu ya uhakika. Wananchi wameshaanza kukata tamaa kwenye maeneo haya, kwa sababu wamelima chai na chai ni kilimo cha muda mrefu hawajui wafanye nini. Kuna baadhi ya watu wameshaamua kwamba wakate ile miti ya chai wapande mazao mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo namwomba sana Mheshimiwa Waziri; last time alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkubwa wa chai lakini hakufika. Namwomba Mheshimiwa Waziri afike kwenye site aone adha wanayoipata wakulima wa chai katika maeneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo tuliyokuwa nayo ya chai katika Wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Njombe na Mkoa wa Iringa kwa ujumla, kwa maana ya Kilolo ni makubwa sana na kama yatahudumiwa vizuri tutalima chai nyingi kuliko wanavyolima wenzetu wa Kenya. Kwa hiyo, utaalam unatakiwa uongezwe katika maeneo haya. Ni aibu kuona chai ya Mufindi, Kilolo na Njombe soko lake linaenda kufanyiwa Mombasa kwenye Taasisi inaitwa KATEPA, wakati TATEPA hapa Tanzania haifanyi juhudi za kutosha. Hatuna sababu ya kuendelea kutumia masoko ya wenzetu, wakati sisi wenyewe tunatakiwa tujiangalie na tuimarishe masoko yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kulizungumzia ni suala ambalo limekuwa tatizo la muda mrefu, madai ya mawakala. Mawakala wanadai hela zao muda mrefu sana na kuna baadhi ya mawakala wengine wameshaanza kupata matatizo, wengine wameshaanza kufa na wengine wameshaanza kuuziwa assets zao ambazo walizitumia kupata mikopo. Kwa hiyo, atakapokuja Mheshimiwa Waziri aje na majibu hapa. Last time waliambiwa wamwone Mheshimiwa Waziri Mkuu, lakini mpaka leo hii mawakala wapo hapa Dodoma wanataka wasadiwe kwenye hili eneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni eneo la kilimo cha umwagiliaji pamoja na kilimo cha vinyungu. Wilaya ya Mufindi hekta 350,000 zimechukuliwa na Maliasili; kwa hiyo watu wengi katika Wilaya ya Mufindi wanalima katika vinyungu, hawana ardhi. Ukiwaambia wasilime kwenye vinyungu hawana sehemu yoyote ya kulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunamwomba sana Mheshimiwa Waziri alione jambo hili. Hata siku zile wakati tunaomba kura tulikuwa na lengo, kwamba tuwasaidie na wapiga kura wengi ambao walitupa kura ni kutoka katika eneo hili la vinyungu. Sasa leo hii unawaambia watu kwenye vinyungu wasilime, wakalime wapi hawa watu? Leo unawaambia wasilime kwenye vinyungu wakalime wapi? Mbadala wake ni nini? Labda kuna lengo hapa hamtaki Kigola, Chumi na Mgimwa warudi kwenye majimbo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo hili naiomba Serikali, Mheshimiwa Waziri atakapokuja, kama kweli Serikali wameamua sisi tusilime kwenye vinyungu, watuambie mbadala wake tuujue hapa leo hii. Kwenye jambo hili tutashika shilingi. Kwenye jambo hili Mheshimiwa Tizeba ni rafiki yetu lakini hatutamwangalia kwa sababu tukiendelea kumbembeleza kwenye jambo hili sisi ndio tutakuwa si Wabunge tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo hili, ndiko tunategemea kupata viazi vya uhakika, kwenye eneo hili tunategemea kupata mpunga wa uhakika na kwa eneo hili tunategemea kupata miwa. Sasa badala ya kuongeza ajira kwa watu, tunataka watu wengi wawe majambazi. Hoja ya kuwaambia leo hii watu waondoke kwenye vinyungu sisi hatukubaliani nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kuna jambo sasa hivi linaendelea, naomba Mheshimiwa Waziri kwa mamlaka aliyonayo alizuie. Kule kwetu sasa hivi wameshaanza kufyeka mahindi kwenye vinyungu. Kwa hiyo tunamwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha aseme na watu wanahitaji elimu. Namwomba sana Mheshimiwa Tizeba atuangalie sana…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti,nameomba sana Mheshimiwa Tizeba, atakapokuja kuhitimisha hotuba yake hapa atuambie mbadala wa vinyungu ni nini.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi kwa Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara hii. Naungana na Kamati yangu ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu kuongeza tozo kwenye mafuta ili kuboresha Mfuko wa Maji. Ni vyema Serikali ikakubaliana na hoja za Waheshimiwa Wabunge kuhusu kuongeza tozo kwenye Wizara hii ili kuongeza pesa ambazo zitapelekwa kwenye Majimbo mbalimbali kutatua kero kubwa ya maji ambayo inawaumiza akinamama wengi waliopo vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo langu kuna mradi mkubwa wa Kihata ambao tumeuombea mara nyingi hapo Wizara ya Maji. Kwa masikitiko makubwa, mpaka leo hatujajibiwa. Ni vyema Serikali ikawa inatoa support kwenye taasisi zinazojitolea kuwekeza katika Sekta ya Maji. Katika Jimbo la Mufindi Kaskazini kuna NGO inaitwa RDO, imewekeza kwa kiasi kikubwa katika Sekta hii ya Maji, lakini Serikali imekuwa haitoi support ya aina yoyote. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri tukutane na NGO hii ili Serikali iweze kuwekeza pia. Ni vyema sasa Serikali ikasimamia na kujua kwa nini misaada ya World Bank haijakamilika mpaka leo; na pesa zinapotea bure? Ni vyema Mheshimiwa Waziri anapohitimisha atuambie ni hatua zipi zitachukuliwa na Serikali kwenye hii miradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, bwawa la mto Liandimbela mpaka leo imekuwa hadithi. Mwaka 2014 Mheshimiwa Pinda Waziri Mkuu Mstaafu aliahidi shilingi milioni 295 kwa ajili ya kuendeleza bwawa la umwagiliaji wa Nundwe. Mpaka leo maji ni tatizo, lakini hakuna uwiano wa kupeleka fedha za maendeleo katika Majimbo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Kaka yangu Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake. Lakini kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Jemedari wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nijielekeze kwenye vipaumbele viwili. Kwanza Mchuchuma na Liganga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Mchuchuma na Liganga ulisainiwa mwaka 2012, sasa hivi ni takribani miaka mitano hakuna jambo lolote linaloendelea katika lile eneo. Kwa hiyo, nataka Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa atueleze sababu zipi ambazo zimesababisha mpaka leo mradi ule haujaanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili katika eneo hilo, nataka Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa atuambie kwa nini Serikali mpaka leo haijaanza kujenga transmission line ya kutoka Makambako - Songea mpaka Ngaka? Hakuna umeme rahisi baada ya umeme wa maji kama umeme wa makaa ya mawe na nchi nyingi duniani ikiwemo Marekani, South Africa wanategemea umeme wa makaa ya mawe. Sasa ni jambo la kushangaza sana sisi kwenye eneo ambalo tuna makaa ya mawe ya kutosha tunashindwa kutumia facility iliyopo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wa Sweden kupitia SIDA Grants walikuwa tayari kuisaidia Serikali hii dola za Kimarekani milioni 64 kwa ajili ya kujenga transmission line ambayo ingeweza ku-produce megawati 120 yenye kilowati 220 ambayo ingekuwa source kubwa ya kuwasaidia watu wa Kusini pamoja na maeneo mengine. Umeme huu ungekuwa ni rahisi kuliko umeme mwingine automatically ungeenda kupunguza cost of production na ungefanya bidhaa ambazo tuna-produce ndani ya nchi hii ziwe cheaper zaidi. Kwa hiyo, namuomba sana Mheshimiwa Waziri, atakapokuja hapa atuambie kwa nini mradi huu haujaanza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo jingine ambalo napenda kuchangia ni suala la Kurasini Hub. Mwaka 2012 tulienda Beijing tukasaini ule mkataba wa Kurasini Hubs na sisi kama Serikali ya Tanzania tulipewa majukumu, miongoni mwa majukumu tuliyopewa ilikuwa ni kukubali kulipa fidia watu wa Kurasini wote na hilo jambo tumelifanya, lakini toka mwaka huo mpaka sasa hivi hatujaanza. Kama Kurasini Hub ingekuwa ime-take place tungeweza kuteka biashara za nchi zote za East and Central Africa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa njia moja au nyingine tunashindwa kufanya shughuli za msingi ambazo zingelisaidia Taifa hili kupata mapato. Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa atuambie nikwa nini mpaka leo Kurasini Logisitic Hub haijaanza kufanya kazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba Mheshimiwa Waziri aangalie sana vijana wake wa TRA kuhusu tarrifs na export, hizi kwa njia moja au nyingine zinasababisha sisi tupoteze biashara. Kulikuwa kuna Wakongo, Wamalawi na Burundi wengi waliokuwa wanakuja kununua bidhaa hapa nchini, lakini cha kusikitisha unaweza kukuta colgate ya gramu 1,000 na colgate ya gramu 250 zinatajwa katika tarrif moja. Matokeo yake inasababisha gharama za ushuru kwa wafanyabiashara wa hapa nchini zinakuwa kubwa, matokeo yake wanashindwa kuziuza kwa watu wa nchi za nje na wale wanahama kwenda kule. Ule ushuru ungekuwa cheap automatically tungeweza kuuza sana na tungepata kodi nyingine kupitia VAT.

Kwa hiyo, tufanye utaratibu tuhakikishe tunaangalia kwenye hili eneo kusudi tuweze kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kuunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naunga mkono hoja taarifa ya kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maliasili na Utalii ilikuwa ndio inayochangia kwa kiasi kikubwa sana katika pato la Taifa, lakini sasa imeanza kushuka. Ni vyema tukaanza kuimarisha miundombinu ili kuboresha utalii na vile vile ni vyema tukatengeneza utaratibu wa kuimarisha utalii wa ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TANAPA kuna hifadhi 16 ni tatu tu zinazo-break ever point, Wizara itengeneze utaratibu wa kuhakikisha kila hifadhi inajiendesha hakuna sababu za msingi ambazo zipo kwa hifadhi ambazo hazijiendeshi. Nchi ya Seychelles inajiendesha kwa utaliii tu why not Tanzania?
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naunga mkono taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji. Naomba kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ni vyema Serikali (Wizara ikawa inatoa fedha zote zinazoidhinishwa na Bunge, kuliko ilivyo sasa, fedha kidogo inayotolewa na Serikali katika hizi Wizara ambazo zinatoa ajira kubwa kwa Watanzania. Pia nashauri Serikali iongeze bajeti katika Wizara hizi tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imekuwa kawaida ya Serikali kutotekeleza ushauri na maagizo yanayotolewa na Bunge lako Tukufu kila mwaka, kwani mapendekezo yamekuwa yanajirudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni mbolea kutofika kwa wakati. Vile vile kutokuanza kwa uzalishaji wa mbolea katika viwanda vyetu viwili vya Kilwa na Mtwara pamoja na malighafi tuliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuongezewa mtaji na kufungua matawi kwenye maeneo ya kilimo kuliko hivi sasa kwamba matawi mengi yako Mjini. Pia Mheshimiwa Waziri wa Kilimo apewe nafasi kubwa katika kuendesha benki hii kuliko ilivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuongeza tozo kwenye Mfuko wa Maji hadi Sh.100/= kwa lita ya petroli na dizeli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kuwe na mahusiano kati ya Wizara ndani ya Serikali ili kutekeleza dhana ya mapinduzi ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni uvuvi. Hapa pana ajira kubwa, Serikali inatakiwa kuacha tabia ya kuharibu zana za wananchi wanyonge badala yake ishughulike na viwanda.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Profesa Mbarawa pamoja na Naibu Mawaziri wote wawili. Mchango wangu unajielekeza kwenye mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kuhusu barabara, hili ni eneo muhimu sana kwa uchumi katika jimbo langu la Mufindi Kaskazini na Wilaya Mufindi. Barabara ya kutoka Mtiri – Ifwagi – Mdaburo – Ihamu – Isipii – Mpanga TAZARA mpaka Mlimba inaunganisha mikoa miwili ya Iringa na Morogoro (Wilaya za Mufindi na Kilombero) lakini shida yake imekuwa kubwa sana kwani haipitiki kabisa na TARURA haina uwezo wa kuunga barabara hii. Ikumbukwe Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kuipandisha hadhi kuwa ya TANROADS. Mheshimiwa Waziri nimeshakuja kwako mara kadhaa lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuinusuru barabara hii yenye uchumi mkubwa wa chai, kahawa, pareto, msitu wa mbao, maharage, mahindi na utalii ambao ungeongeza pato la Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema sasa Mheshimiwa Waziri atupe mkakati wa kukabiliana na barabara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya kutoka Kinyanambo A – Isalavani – Sadani – Madibira – Rujewa ambayo ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi toka mwaka 2000 – 2005 - 2010 – 2015 – 2020, lakini hata kilometa moja tu haijajengwa. Ni vyema Mheshimiwa Waziri atuambie lini Serikali itaanza kutekeleza ujenzi wa barabara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya kutoka J Corner – Mtiri – Sawala – Mgololo kutokufungwa kwa kiwango cha lami, ni vyema sasa Serikali ikafunga barabara hii kwa kiwango cha lami ambako kuna uchumi mkubwa wa viwanda kikiwemo kiwanda kikubwa kuliko vyote vya karatasi Afrika na Viwanda vya Chai zaidi ya vitano.

Mheshimiwa Naibu Spika, mawasiliano, nimeongea mara nyingi na Mheshimiwa Waziri kuhusu maeneo ambayo hayana mawasiliano ikiwamo maeneo ambayo minara imefungwa lakini haifanyi kazi kama mnara wa Mapanda, Kata ya Mapanda, mnara wa Vodacom haufanyi kazi na mnara wa Ikwiha, Kata ya Ikwiha haufanyi kazi, kwa hiyo, hakuna mawasiliano. Katika Vijiji vya Uhafiwa, Mapanda, Ukami, Ihimbo na Chogo pia Ikurha, Uginza, Ilangamoto, Ihamu, Isipii na Mpanga Tazara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa uchukuzi, naomba sana Mheshimiwa Waziri waweke kituo cha abiria kwenye Kata ya Mpanga TAZARA, Kijiji cha Mpanga TAZARA, reli ya TAZARA.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, naomba nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri, dada yangu Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya. Naendelea kumpongeza sana kwa sababu mwaka 2011/2012 na 2012/2013 Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda. Kwa hiyo, yupo kwenye nafasi sahihi kabisa. Miongoni mwa hoja nyingi ambazo zimezungumziwa hapa, Engineer anazifahamu. Kwa hiyo, atakuwa kwenye nafasi nzuri sana kumwelekeza Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwanza ni Mchuchuma na Liganga. Mwaka 2012 pale Mlimani City, Dkt. Cyril Chami akiwa Waziri, Tanzania kupitia NDC tulisaini mkataba wa Liganga na Mchuchuma, mimi nikiwepo na Naibu Waziri alikuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ninapozungumza ni takriban miaka sita. Mambo yote ya msingi kwenye mkataba ule tulikubaliana na naamini kwa kiasi kikubwa yametekelezwa. Inasikitisha sana miaka sita imeshapita toka sasa hakuna kitu chochote kilichofanyika kwenye Mchuchuma na Liganga. Kama kweli tunataka kwenda kwenye uchumi wa viwanda, miongoni mwa maeneo ambayo tutatakiwa tuyaenzi kwa nguvu zetu kubwa ni eneo la Mchuchuma na Liganga ambapo malighafi za uhakika za umeme na chuma zinapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, makaa ya mawe ya Mchuchuma na makaa ya mawe ya Ngaka yanaweza kuzalisha umeme wa megawatt 120. Tulikuwa tuna tatizo kubwa la transmission line, lakini kwa bahati nzuri tumepata hela kwa wafadhili na transmission line ile inajengwa. Kwa
hiyo, umeme umeshapatikana, sasa kigugumizi kinatoka wapi cha kutoanzisha mradi wa Mchuchuma? Naamini kabisa Mheshimiwa Waziri akija hapa atatuambia ni sababu zipi zinapelekea leo mpaka miaka sita imefika hatujafanya chochote kwenye mradi mkubwa huu wa Liganga? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Awamu ya Tano, tumejielekeza kwenye uchumi wa viwanda. Tunapotaka kuzungumzia habari ya viwanda kuna baadhi ya mambo tunatakiwa tuyaangalie kwa karibu zaidi. Malighafi kubwa ambayo inatakiwa ipatikane kwenye eneo hili inatakiwa itoke kwenye kilimo. Tumejipanga vipi ku-invest kwenye kilimo kusudi tuwe na uhakika wa kupata raw materials za kutosha? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa viwanda unakwenda simultaneously na uchumi wa kilimo. Tunaweza tukajenga viwanda vikubwa hapa nchini lakini kama malighafi hakuna, tutakuwa tuna hadithi, tutakuwa na viwanda ambavyo haviwezi kufanya uzalishaji. Kwa hiyo, tujiangalie, tunapotaka kujenga viwanda, tujiulize, hiyo malighafi inatoka wapi? Kwa hiyo, nashauri, tunapojiangalia kwenye uchumi wa viwanda, tujiangalie na namna ya kuandaa malighafi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilitaka kulichangia na kumwomba Mheshimiwa Waziri aje kuniambia ni suala la Kurasini Logistic Center. Tumelipa fidia zaidi ya shilingi bilioni 90 kwenye Kurasini Logistic Center na tulisaini mkataba wa mwaka 2013 na Wachina kwa ajili ya kujenga logistic ile lakini leo ni miaka mitano hatujafanya chochote na shilingi bilioni 90 imeshakwenda pale. Kwa hiyo, tusije kuwa tuna matumizi ambayo siyo sahihi. Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anakuja, aje atueleze kwa nini mpaka leo logistic center haijaanza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Viwanda kwa kazi na juhudi kubwa anayoifanya katika eneo lake, lakini pamoja na kazi kubwa anayoifanya, tunatakiwa sisi kama Tanzania tujipange namna ya kuvi-protect viwanda vyetu vya ndani. Kwa mfano, tuna viwanda vikubwa tu vya maziwa hapa nchini na maziwa mengi tunayotumia hapa nchini yanakuwa-imported kutoka nje, matokeo yake tunashindwa kuvisaidia viwanda vya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye taasisi nyingi za Serikali utakuta maziwa yanayotumika ni ya nchi za nje. Ukiuliza sababu zipi zimesababisha kutumia hizo Lactogen na maziwa mengine kutoka nchi za nje, hupati majibu. Kwa hiyo, kama tulivyofanya kuzuia importation ya furniture za nje, ifike wakati na Serikali izuie importation ya maziwa kutoka nchi za nje. Sisi kama Watanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na ng’ombe wengi katika Afrika. Kwa hiyo, tutumie utamaduni huo na rasilimali tuliyonayo kuhakikisha tunafanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pamba huwa linaajiri watu wengi sana. Ukienda Cambodia pamoja na kwamba hawalimi pamba lakini watu wengi wameajiriwa katika industry ya textile. Kwa hiyo, ifike wakati sasa tuanzishe viwanda vingi hapa nchini vya nguo, naamini vitaajiri watu wengi kuliko kujielekeza kwenye kuuza rasilimali yetu ya pamba tutakuwa hatuitendei haki. Tuko tayari kumuunga mkono Mheshimiwa Waziri kwa kuhakikisha raw material zinazopatikana kwenye maeneo ya pamba, nyingi zinatumika ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo wenzetu wa viwanda wamefanya vizuri sana. Kwa mfano, eneo la BRELA (Msajili wa Makampuni), siku za nyuma palikuwa na shida sana, lakini sasa hivi wamefanya vizuri sana. Usajili unafanyikia online na unafanyika kwa kipindi kifupi. Kwa namna ya kipekee, tumpongeze Mheshimiwa Waziri na Mtendaji Mkuu wa BRELA kwa kazi nzuri anayoifanya katika maeneo yake. Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni, kama anafanya vizuri, naomba tumpongeze sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo machache, naomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Kilimo
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba pamoja na dada yangu Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Juzi kwenye hotuba yetu ya maji tulizungumza sana tatizo la Maafisa Ugani kwenye eneo la maji, siku ya pili akalitolea maagizo kwamba Maafisa Ugani sasa hivi wawajibike direct kwenye Wizara ya Maji pamoja na Ardhi. Tunamuomba tena Mheshimiwa Rais Maafisa Ugani hawa kwenye eneo la kilimo tunaomba wawajibike direct kwa Katibu Mkuu ili kusudi wawe na control moja kwa moja kutoka Wizarani otherwise tatizo litaendelea kuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima wamejiajiri katika sekta hii. Kwa masikitiko makubwa sana bado hatuitendei haki hii asilimia 75. Ukiangalia kwenye bajeti yetu na ukiangalia kwenye makubaliano yetu na nchi za Afrika Mashariki na zile za Kusini Mashariki za SADC na sisi Watanzania tulisaini Maputo na Malabo Agreement kwamba asilimia 10 ya bajeti kuu itengwe kwenye sekta ya kilimo, lakini ukliangalia kwenye analysis mpaka sasa Tanzania ndiyo nchi ya mwisho tuna asilimia 3.1, hii ni aibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo ambalo tunaajiri Watanzania wengi hakika tunatakiwa tupeleke bajeti ya kutosha. Kwenye eneo hili tunategemea kutengeneza ajira ya kutosha na ndiko itakakopatikana raw material ya kutosha kwa ajili ya viwanda vyetu. Tumekusudia kwenda kwenye uchumi wa viwanda, tunaendaje kwenye uchumi wa viwanda kama hatuna uhakika wa kupata raw material ya kutosha? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu tunaiomba Serikali iangalie upya kwenye eneo hili. Hata kama hatuwezi kufika asilimia 10 ya bajeti kuu tufike hata 6 au 7 tulingane na wenzetu wa Uganda na Kenya, lakini kuendelea kuwa kwenye mstari wa mwisho kwa asilimia 3.1 haifurahishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilitaka kulizungumzia ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo. Tulipokuwa tunatamka kwamba tunataka tuanzishe Benki ya Maendeleo ya Kilimo tulikuwa tunaamini kabisa benki hii itakuja kwa ajili ya manufaa ya wakulima, lakini ukiangalia structuring yake utakuta kwanza yenyewe haipo kwenye site ya wakulima, makao makuu yako Dar-es-Salaam, haya tujiulize Dar-es-Salaam kuna mashamba makubwa kiasi gani? Taratibu za kumsaidia mtu apate mkopo kama ana shida ya kupata mkopo aende Dar-es-Salaam akatafute mkopo mtu kutoka Mufindi au Njombe? Kwa hiyo, Serikali iangalie upya itengeneze matawi nchi nzima na ilenge wakulima kwenye site, tunataka tupate matawi ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika analysis mpaka sasa hivi mtaji walionao Benki ya Kilimo ni shilingi bilioni 67 na mahitaji ya Watanzania ni shilingi bilioni 800, tofauti ni kubwa sana. Kwa hiyo, naomba sana Serikali tuongeze mtaji kwenye benki hii ili kusudi tupate uhakika wa kuajiri Watanzania walio wengi kwenye eneo hili na ambako inapatikana raw material ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa lazima niliseme jambo hili tena. NFRA ambao ndiyo wanahakikisha usalama wa mazao yetu na chakula chetu hapa nchini waliomba shilingi bilioni 86, lakini kwenye bajeti tumewatengea shilingi bilioni 15. Mgogoro mkubwa wa wakulima wa mahindi unaanzia hapa na kwenye eneo hili kama Mheshimiwa Waziri hatakuja kuonesha kwamba ataongeza hela nitakuwa mtu wa kwanza kushika shilingi hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tumepata tatizo kubwa sana kwenye eneo la mahindi. Kwa mfano, sasa hivi kwetu Mufindi debe la mahindi ni Sh.3,000 ambalo lina kilo 20, kilo moja ya sukari ni Sh.3,000 wapi na wapi? Kwa hiyo, mtu akitaka sukari kilo moja ni lazima auze debe moja la mahindi, itafika sehemu tutakata tamaa kulima mahindi. Serikali isipotamka kupagusa hapa kwenye NFRA nitawashawishi Wabunge wenzangu tunaotoka Mufindi na maeneo mengine kwamba tunapigwa. Hatuna jambo la kujivunia katika Mikoa ya Iringa, Njombe na Mikoa yote ya Kusini kama mahindi yetu tuliyokuwa nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaipongeza Serikali imeamua kujenga maghala na vihenge ya kisasa kabisa katika Kanda Nane, sasa kwa shilingi bilioni 15 tutaweka nini humu? Tumejenga majengo ambayo yanagharimu fedha nyingi lakini hela za kuweka hayo mahindi kwenye maeneo haya, hazipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tusiendelee kuwaonea watu wa Mufindi na wa maeneo mengine kwenye eneo hili, mimi sipo tayari. Waziri ni rafiki yangu tumekua wote na mimi ndiye Mwenyekiti wake wa Kamati lakini leo nasema najivua Uenyekiti wa Kamati, nabaki kama Mbunge wa Mufindi Kaskazini. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikali, kulikuwa kuna jambo la madeni ya mawakala Serikali ikasema lazima ihakiki. Haya Serikali mmehakiki baada ya kuhakiki what next? Kwa nini tusiseme mawakala hawa wanadai, hawa hawadai, kusudi Serikali iwalipe ambao wanadai? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie. Hawa mawakala wengine wanakufa, wanauziwa majumba yao, wana hali mbaya kwenye maeneo mbalimbali. Ifike wakati Serikali itoe tamko mawakala wanaodai ni hawa na hawa hawadai. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Maofisa wa Serikali ambao wameshiriki kwenye utapeli, kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria? Tunaenda kushughulika tu na mawakala? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nataka niseme tu kwamba naunga mkono hoja lakini nasema hivi Mheshimiwa Waziri asipokuja na majibu kuhusu kuongeza hela NFRA nitashika shilingi yake.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Naomba nichukue fursa hii kuwapongeza sana Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa kazi nzito walioifanya katika Wizara hii ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia tu kwa haraka haraka huwezi kujua kazi wanayoifanya Waheshimiwa hawa wawili. Leo hii kwa mfano nchi nzima kuwe hakuna nyama nchi nzima, hakuna maziwa, hakuna samaki utaona umuhimu wa Wizara hii. Wizara hii ni nyeti sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi Wizara hii pia inachangia kwenye Pato la Taifa kwa kiasi kikubwa kuliko Wizara nyingine nyingi. Kwa masikitiko makubwa, wanapelekewa bajeti ndogo. Ukiona kwenye maelezo ya Mheshimiwa Waziri, wamekusanya sana kwenye maduhuli. Sasa yale makusanyo waliyokuwa wanakusanya kwenye maduhuli, mengine yangekuwa yanarudi kwenye bajeti zao ili ziwasaidie kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi Wizara hii imetoka kwenye utaratibu wa kufanya identification ya ng’ombe walioko hapa nchini kwa kuwapiga chapa. Tuna ng’ombe takriban milioni 29 na kila mchangiaji alikuwa anatoa shilingi 500/=. Kwa hesabu ya haraka haraka tu, wamekusanya karibu shilingi bilioni 14. Tujiulize ni kiasi gani cha pesa kinarudi kwa ajili ya kusaidia kwenye sekta hiyo ya mifugo?

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni jambo la msingi sana. Kwa hiyo, collection inayopatikana katika maeneo yao, tungetengeneza utaratibu wa kuhakikisha fedha zinarudi kwa ajili ya kuwasaida wakulima pamoja na wavuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo pekee ambalo linatoa ajira kwa urahisi ni eneo la uvuvi. Una-invest mara moja lakini una uhakika wa kufanya miaka yote katika eneo hili. Wizara inatakiwa itambue hilo; na kuwa karibu sana na kuwashirikisha sana katika kazi zao sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibi Spika, miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na Wabunge wengi ni mahusiano kati ya Wizara, pamoja na sekta binafsi. Kwa hiyo, namshauri Mheshimiwa Waziri alione hili gap alipunguze. Kuna watu wanataka wakae, wazungumze pamoja kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni eneo la tasnia ya maziwa. Tuna viwanda vikubwa vitano katika nchi hii. Tuna takwimu ya ng’ombe milioni 29 ambao nimezungumza. Kwa masikitiko sana, asilimia 85 ya maziwa yanayotumika hapa nchini yanatoka nje ya nchi. Sasa tujiulize, huu wingi wa ng’ombe unasaidia nini katika tasnia ya maziwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wanaogopa ku- invest katika eneo hii kwa sababu ya tozo mbalimbali zilizopo ambazo hazina tija kwa watu wetu. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri, zile tozo ambazo hazina tija, tuziondoe kusudi watu waweze kujiunga katika maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo letu ni ku-protect viwanda vya ndani. Wewe ni shahidi maofisi yote ya Serikali yanatumia maziwa kutoka nje. Ukienda kwenye ofisi yoyote hapa au majumbani utakuta Nido au Lactogen kutoka nchi za nje. Kwa nini tusitumie maziwa ya ndani? Kwa utaratibu huu, tunaendelea kuvidhoofisha viwanda vya ndani badala ya kuvisaidia. Kwa hiyo, ifike wakati tuweke ban kama tulivyoweka ban kwenye furniture kwamba sasa ni marufuku kuagiza maziwa nje, tutumie maziwa yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba nichukue fursa hii kuwapongeza sana Waheshimiwa Mawaziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo na Mzee wangu Mkuchika pia bila kuwasahau Naibu Mawaziri Mheshimiwa Kakunda, Kandege pamoja na Watendaji wote kwa kazi nzuri zinazofanyika katika Wizara zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu unajitokeza katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, afya; katika eneo hili kwanza naomba sana hospitali ya Mafinga Mjini iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga, ipandishwe hadhi na iwe hospitali ya rufaa kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Wilaya nzima ya Mufindi pamoja na wakazi wengine wanaopata huduma kutoka wilaya nyingine na mkoa mwingine kama wakazi wa Madibila, Mapogoro kutoka Wilaya ya Rujewa, Mkoa wa Mbeya pia kumekua na ajali nyingi sana zinazotokea katika maeneo haya na zinakuwa zinahudumiwa na hospitali hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Mufindi Kaskazini lina Tarafa nne (4) lakini tuna vituo viwili tu vya afya na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi haina hospitali. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI aliangalie jambo hili kwa macho mawili, kwa kuanzia tu hata tukiwa na kituo kimoja kwenye kila tarafa tutakuwa tumeanza nyema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ina watumishi asilimia 28 za watumishi. Kwenye Idara ya afya kuna upungufu wa asilimia 72. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri alione jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi tuna zahanati nne ambazo zimekamilika, zahanati hizo ni Mwitikila, Mufindi Kaskazini; Kiponda Nyigo na Igoda, Mufindi Kusini; lakini bado hazijafunguliwa sababu wataalam na vifaa, lini zahanati hizo zitafunguliwa ili kutokuvunja au kudhoofisha nguvu ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali iunge mkono juhudi za wananchi wanaojenga Zahanati kama vile Igomtwa na Wambi Mbelwa na Makongomi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara; kuna haja ya kuongeza pesa kwenye Taasisi ya TARURA ili iweze kufanya kazi zao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna barabara muhimu sana katika Jimbo la Mufindi Kaskazini lakini wakati wa mvua haipitiki kabisa. Barabara hii ni kutoka Mtili – Ifwagi – Idaburo – Ihanu – Isipii – Mpangatazara - Mrimba. Barabara hii inaunganisha Mikoa miwili, Iringa na Morogoro, Wilaya ya Mufindi na Kilombero ina ukubwa wa zaidi ya kilomita 106.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Jafo anajua tatizo la barabara hii, naomba sana tupewe pesa ya kutosha kwa ajili ya matengenezo ya barabara hii yenye uchumi mkubwa kwani kuna kilimo cha chai, pareto, maharage, misitu mikubwa ya mbao pamoja na eneo la utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naunga mkono hoja ya bajeti zote mbili ya TAMISEMI pamoja na Utumishi na Utawala Bora.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kwa kumpongeza ndugu yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango pamoja na dada yangu Mheshimiwa Dkt. Ashatu. Kwa namna ya kipekee, nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri na ya kizalendo anayoifanya katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwambie Ndugu yangu Mheshimiwa Silinde namheshimu na najua wakati mwingine anachangia vizuri, lakini kuna watu katika nchi zingine wanampongeza Mheshimiwa Dkt. Magufuli anafanya vizuri. Profesa Patrick Lumumba mpaka amembandika jina na kumuita Magufulification kutokana na performance yake. Kuna watu wanataka kujifunza the way Mheshimiwa Dkt. Magufuli anavyofanya kazi nzuri katika nchi ya Tanzania. Kwa hiyo, mnyonge mnyongeni lakini kuna maeneo tunafanya vizuri. Katika nchi za Afrika Mashariki na Kati hata wenzetu wa Kenya wanatamani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli awe Rais wao. Ameweza kusimamia matumizi ya pesa kwa nidhamu na kuna baadhi ya mambo makubwa ambayo tumeweza kuyafanya kwa hela yetu hiyo ya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni rasimu ya bajeti na siyo bajeti. Sisi Wabunge ni wajibu wetu kuikosoa na kuielekeza Serikali kwenye maeneo ambayo tunaona kuna upungufu. Kwa hiyo, tukikataa kabisa kwamba hakuna jambo la maana lililofanywa kwenye hii rasimu ya bajeti tutakuwa tunakosea. Yapo mambo mazuri Mheshimiwa Dkt. Mpango amekuja nayo nasi lazima tuyaunge mkono.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi ni viongozi wa wananchi, tumetoka kwenye Majimbo yetu, pamoja na uzuri wa rasimu hii ya bajeti lakini kuna maeneo Mheshimiwa Dkt. Mpango alitakwa ayaangalie kwa ukaribu sana kwa sababu yanawagusa watu direct. Kwa mfano, eneo la kilimo linaajiri Watanzania wasiopungua asilimia 66.6 na yeye anajua, lakini ukiangalia bajeti iliyokwenda kwenye eneo hili hairidhishi kabisa. Tunaomba aliangalie maana tulitakiwa tuweke bajeti ya kutosha kwa sababu kwenye eneo hili kuna ajira, kuna usalama wa chakula, kuna malighafi ya viwanda ambapo tunataka twende kwenye uchumi wa viwanda. Sasa tusipowekeza vizuri kwenye eneo la kilimo tunategemea nini, tutaendaje kwenye uchumi wa viwanda? Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Dkt. Mpango tuliangalie mara mbili eneo hili la kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia wenzentu ambao tumesoma bajeti pamoja nchi za Afrika Mashariki na Kati, asilimia 10 ya bajeti nzima ndiyo wametenga kwenye bajeti ya kilimo, lakini bajeti yetu haifiki hata asilimia 3. Sasa tujiangalietutafika huko. Shilingi bilioni 170 against shilingi triolioni 32 wapi na wapi? Tutakwenda kwenye uchumi wa viwanda kweli? Kwa hiyo, Mheshimia Dkt. Mpango naomba sana eneo hilo tuliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambayo anaiongoza mwenyewe. Wale watu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo hawapeleki hela kwa wakulima. Walianza na mtaji wa shilingi bilioni 60, ukakua ukafika shilingi bilioni 67, wakakopa mpaka wakafika shilingi bilioni 287, lakini tujiulize kwenye shilingi bilioni 287 ni kiasi gani wamewakopesha wakulima? Utakuta hela zile wanazokopa na wenyewe wanaenda kuweka dhamana kwenye mabenki mengine, ndiyo madhumuni ya kufungwa hiyo benki? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mpango kwenye jambo hili nataka awaambie tumeanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima siyo kwa ajili kufanya biashara. Wafanye yale ambayo tumekubaliana katika uanzishaji wa Benki hii ya Kilimo, kwenye jambo hili hatuko sawa. Mahitaji ya Watanzania kwenye eneo hili ni shilingi bilioni 800 lakini hata shilingi bilioni 287 zingekuwa zinakwenda direct kwa wakulima sasa hivi wakulima wangekuwa wamebadilika kwenye eneo hili. Kwa hiyo, naomba eneo hili tuliangalie sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo amelizungumzia ni suala la Bodi ya Mazao Mchanganyiko, amesema wanataka kuunganisha Bodi. Mheshimiwa Dkt. Mpango, hawa wananchi ndiyo wanatengeneza hela zao pale, mnataka mfanye nini pale, interest yenu ni ipi? Kama kuna watu wana ubadhirifu wa hela si wapelekwe Mahakamani. Wamelalamika kwenye maeneo ya korosho lakini hakuna hata mtu mmoja mpaka leo amepelekwa mahakamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sikubaliani na hoja ya kutaka kuunganisha Bodi, kwenye eneo hili siwezi kukubaliana hata kidogo. Mkitaka kwenda vizuri kwenye eneo hili angalieni Bodi za Udhibiti (Regulatory Board) zina tozo mbalimbali ambazo hazina tija na tozo hizo zinawagandamiza sana wakulima na kuwaongezea gharama. Kwa hiyo, naomba tuangalie sana kwenye maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wana shida ya maji na Wabunge wote tulikuwa tunasema hapa tunataka maji na mpaka tukasema tuko tayari kuwashawishi watu wetu kuongeza tozo la shilingi hamsini, lakini hakuna respond yoyote tuliyopata. Mwaka jana collection ya ndani iliyokuwa inatakiwa iende kwenye maji ilikuwa shilingi bilioni 250 lakini mpaka tunakuja kwenye bajeti ni shilingi bilioni 26 tu ambayo ni asilima 11 ya collection ya ndani ambayo ilikwenda kwenye maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bajeti ambayo ilikuwa inatokana na Mfuko wa Maji ya shilingi bilioni 158 hela zote karibu zimekwenda kwenye miradi ya maji. Kwa hiyo, tukiongeza kwenye eneo hili tutafika mbali. Sasa Waziri hajakubaliana na shilingi hamsini angesema basi niwafikirie hawa Wabunge hata niwape shilingi thelathini au shilingi ishirini, akituacha hivi anatuacha solemba. Kazi ya Wabunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali, lakini inawezekana ikawa kila siku tunashauri hakuna hata siku moja mmewahi kuchukua mawazo ya Wabunge mkaamua kuyafanyia kazi. Kwa hiyo, tunaomba eneo hili mliangalie.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine Mheshimiwa Dkt. Mpango amezungumza vizuri sana kuhusu kusamehe kodi kwenye chakula cha mifugo, yuko sahihi. Kama unasamehe kodi kwenye chakula cha mifugo halafu unatoza kodi kwenye mashudu umesamehe wapi sasa hapo? Unasamehe kushoto kulia unachukua hela ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sikubaliani na hiyo hoja, hujasamehe hapo. Umetuvisha blanketi hapo, kwamba nimesamehe kodi kwenye chakula cha mifugo halafu unasema mashudu yatozwe VAT, haiwezekani. Kama tumeamua kusamehe kodi, iwe ni kwenye maeneo yote ili kusudi tupate tija kwenye eneo la kilimo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo napenda kuchangia ni suala la viwanda vya maziwa na nyama. Mheshimiwa Waziri yuko sahihi, ameamua kuvilinda viwanda vya ndani kwa kuongeza kodi ya mazao ya mifugo kwa maana ya mazao ya nyama na maziwa yanayotoka nje ya nchi, lakini tunavisaidiaje viwanda vya ndani hapa. Namwomba ili kusudi twende kwenye ushindani halali, maana sasa hivi maziwa yetu ukilinganisha na maziwa ya Kenya na yanayotoka Uganda maziwa ya Tanzania gharama zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii tena kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuhitimisha hoja yangu ya taarifa ya mwaka ya Kamati ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji. Pia naomba nichukue fursa hii kuwashukuru sana Wajumbe wa Kamati yangu ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa kuandaa taarifa nzuri ambayo imeungwa mkono na wachangiaji walio wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote kwa jinsi walivyokuwa wanafuatilia mijadala iliyokuwa inaendelea hapa Bungeni. Wabunge waliochangia walikuwa 19; 6 wamechangia kwa maandishi na 13 wamechangia kwa kusema.

Mheshimiwa Spika, katika michango ya Waheshimiwa Wabunge, wote wameonekana kuunga mkono mapendekezo na Maazimio ya Kamati. Kwa hiyo, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwamba kwenye mambo yote tuliyowasilisha wametuunga mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee, niwashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri; Mheshimiwa Hasunga, Mheshimiwa Prof. Mbarawa na Mheshimiwa Mpina, wote walipokuja kutoa maelezo yao hapa walionyesha hawana tofauti na Kamati na wamekubaliana na hoja zilizowasilishwa na Kamati. Wametuahidi mbele ya Bunge lako Tukufu watakuwa tayari kuzifanyia kazi hoja zote zilizowasilishwa na Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nijielekeze katika maeneo machache kabla sijahitimisha hoja ya mjadala huu. Eneo la kwanza, Kamati yangu inakuomba wewe kupitia Bunge lako Tukufu uandae Kamati Maalum itakayokuwa inashughulikia Maazimio yanayotokana na taarifa za Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kwa nini sisi kama Kamati tumeliona jambo hili? Hii ni kwa sababu kila mwaka tumekuwa na tabia ya kurudia hoja za Kamati, kwa hiyo, tunashindwa kuelewa ni hoja zipi ambazo zimeazimiwa na Bunge lako Tukufu zimetekelezwa na kama tungekuwa tunapata taarifa ya utekelezaji wa hoja hizo tungekuwa kwenye position ya kutozirudia tena. Kwa hiyo, sisi kama Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji tunakuomba sana uunde Kamati Maalum itakayokuwa inashughulikia hoja mahsusi kama ambavyo tunawasilisha wakati huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo la pili ambalo napenda kulitolea maelezo kidogo ni kuhusu Bodi ya Mazao Mchanganyiko. Tunaomba Bodi hii ipewe pesa ya kutosha kwa sababu ni eneo pekee ambalo Serikali imejiingiza kufanya biashara kisheria. Malalamiko yaliyokuwepo kwenye maeneo mengi ya wakulima wa mahindi, mbaazi na nafaka mbalimbali kama Bodi ya Mazao Mchanganyiko itapewa pesa za kutosha matatizo ya wakulima kwenye hayo maeneo hayatakuwepo.

Mheshimiwa Spika, pia pesa hizi wapewe kwa wakati. Unakuta safari hii Bodi ya Mazao Mchanganyiko imepewa pesa mwezi Desemba wakati mazao yanavunwa mwezi wa Juni, kwa hiyo, tunaweka wakulima katika kipindi kigumu. Kwa hiyo, hata kama sasa hivi wanapata nafasi ya kwenda kununua mazao kwenye maeneo hayo, wakulima watakuwa na shida ya kuanza kulima upya katika msimu wa kilimo. Kwa hiyo, tunaomba Bodi ya Mazao Mchanganyiko ipewe pesa ya kutosha au itengenezewe utaratibu wa kupata mikopo kwa njia rahisi kusudi kuweza kununua mazao kutoka kwa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili kwenye eneo la Bodi ya Mazao Mchanganyiko wawe na wafanyakazi wa kutosha. Sasa hivi asilimia 95 ya wafanyakazi wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko wapo Mtwara, kwa hiyo, maeneo mengine hawawezi kupata zile huduma za Bodi ya Mazao Mchanganyiko. Hata utaratibu wa kununua nafaka kwenye maeneo mengine sasa hivi haupo, wamefanya concentration kwenye eneo moja tu la korosho, hakuna wafanyakazi wowote ambao wamewaweka kwa ajili ya kununua nafaka kwenye maeneo mengine. Naomba hili tuliangalie na waongezewe vifaa kwa maana ya magari. Mara ya mwisho wamepewa magari nane (8) lakini hayakidhi kutokana na hali halisi kwa sababu ni eneo pekee ambalo litamsaidia mkulima aweze kufanya kazi zake ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Benki ya Maendeleo ya Kilimo ilianzishwa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima, kwa hiyo, ifanye kazi specific kwa sheria iliyoanzisha benki hii. Pale katikati Benki ya Kilimo nayo ilikuwa inaanza kutengeneza utaratibu wa kukopesha hela kwa watu wengine, ifungue matawi kwa ajili ya wakulima, wavuvi pamoja na wafugaji waweze kupata hela kwa riba nafuu ingeweza kuwasaidia sana watu kwenye maeneo yetu. Kusudi twende kwenye viwanda lazima tuhakikishe tunawawezesha sana watu wetu kwenye maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mpina na Naibu wake Mheshimiwa Ulega, kwanza wamekuwa wasikivu sana. Kutokana na changamoto zilizojitokeza katika Operesheni Sangara wameamua kuanzisha mchakato wa marekebisho ya Sheria Na.22 ya mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za 2009. Kama tutaendelea kuwa na malalamiko bila kurekebisha sheria tutaendelea kuwalaumu Mawaziri hawa lakini nawashukuru wamekubali, wamesikiliza hoja za Wabunge na leo hii Waziri ametamka wazi kwamba watahakikisha huo mchakato wa kubadilisha Sheria Na. 22 ya mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake unafanyika kabla ya mwezi Julai, 2019. Kama sheria zile zitarekebishwa mapema, malalamiko yote ambayo yapo kwa wavuvi hayatakuwepo kwa sababu wavuvi nao watakuwa wana haki ya kusema zile changamoto ambazo zinawakuta kwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo napenda niwapongeze wenzetu hawa sekta ya mifugo na uvuvi ni kuanzisha Dawati la Sekta Binafsi. Hapa wananchi wanapata nafasi ya ku-chip in. Taasisi nyingi zimejihusisha kwenye sekta hii, kwa hiyo matatizo yote ya wafugaji na wavuvi yanaweza kutatuliwa kwenye Dawati hili na tumeliona hili jambo, ndiyo maana wamekuwa tayari hadi kuanzisha mchakato wa marekebisho ya sheria.

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii tena kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Maji kwa kuleta Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2018. Sheria hii itakaposainiwa na Mheshimiwa Rais itaboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi na majitaka ambalo lilikuwa tatizo kubwa katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni imani yangu kuwa safari hii Serikali itakubaliana na mapendekezo ya Wabunge ya kuongeza shilingi 50 kwenye kila lita ya mafuta kwa maana ya petroli pamoja na dizeli. Tukiongeza shilingi 50 kwenye huu Mfuko wa Maji wa Taifa tutaweza kutunisha fedha zake ambapo utasaidia watu wengi katika vijiji waweze kupata maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii tena kuipongeza Serikali chini ya Rais wetu mzalendo Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua madhubuti alizochukua katika kuimarisha tasnia ya korosho. Ni matumaini yangu kuwa Wizara yenye dhamana itaendelea kushughulikia changamoto zilizobainika pamoja na ushauri wa Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hakuna jambo lolote muhimu katika nchi linaloweza kuendelea bila research. Ni wakati muafaka sasa hivi wa Serikali kutenga asilimia 1 ya DGP kwa ajili ya research. Kwenye eneo hili tunaiomba sana Serikali iondoe kigugumizi kwa sababu kumekuwa na malumbano katika research. Hakuna mtu anayekataza research, wafanye research na watuasaidie kuweka wazi kusudi tuweze kuwasaidia wakulima wetu katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba Bunge lako Tukufu liazimie hoja na Maazimio ya Kamati kama yalivyowasilishwa na Kamati.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi nzuri ya kizalendo anayoifanya katika nchi yetu. Mchango wangu utajikita katika maeneo matatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni afya. Jimbo la Mufindi Kaskazini lina Tarafa nne, lakini kwa masikitiko makubwa tuna kituo kimoja kinachofanya kazi cha Ifwagi. Nakupongeza wewe binafsi pamoja na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutupatia shilingi milioni 400 kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Ifwagi na sasa kiko katika hatua za mwisho, lakini Tarafa tatu zilizobaki hazina Kituo cha Afya. Naomba nichukue nafasi hii kuiomba Serikali itusaidie kupata Kituo cha Afya kimoja kwa kila Tarafa nasi wananchi tuko tayari kusaidia katika shughuli za maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni miundombinu ya barabara. Kumekuwa na tatizo kubwa la miundombinu katika Jimbo la Mufindi Kaskazini. Barabara hazipitiki kabisa; Barabara ya Mtili – Ifwagi – Mdeburo – Ihenu – Mpanga – Tazara – Mrimba. Barabara ya Tambaranyimbo – Uyele – Ikwaha - Kwa Twanga haipitiki kabisa na TARURA ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba sana kupitia Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI aingilie kati barabara ya Kinyanambo A – Isalavenu –Igombavanu, Sadani – Madibira - Rugisa ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM toka mwaka 2000/2005, 2005/2010, 2010/2015, 2015/2020 lakini haijajengwa hata kilometa moja ya lami. Ni vyema sasa Serikali ikasema ili tuweze kuwaambia wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu ni kuhusu miundombinu ya maji. Ni vyema sasa Serikali ikakubaliana na Wabunge kwa kuingiza tozo ya shilingi 50 ambayo sisi tuna uhakika ikiongezwa itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri ya kizalendo anayoifanya katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jafo na Mheshimiwa Mkuchika, kwa kazi nzuri wanazozifanya, bila kuwasahau Naibu Mawaziri; mjomba wangu Mheshimiwa Kandege na ndugu yangu Mheshimiwa Mwita Waitara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu utajielekeza katika maeneo makubwa manne. La kwanza ni barabara. Sisi Wabunge tunaotoka vijijini ndio tuna mtandao mkubwa sana wa barabara kuliko wanaotoka mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inayopelekwa TARURA ni ndogo sana kuliko bajeti inayopelekwa kwenye miundombinu. Ifike wakati sasa hizi bajeti ziwe 50 kwa 50. TARURA wapate asilimia 50 pamoja na miundombinu wapate asilimia 50.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna sababu za msingi kusema hayo. Kwenye vijiji ndiyo kwenye wakulima na ndiyo kwenye wananchi waliokuwa wengi. Kwa hiyo, malighafi na chakula vinatoka vijijini. Kwa hiyo, tusipoboresha barabara za vijijini ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Jafo ni shahidi, nimekwenda Wizarani kwake nikiwa na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi kumlalamikia miundombinu ya barabara iliyoko katika vijiji vyetu. Barabara ya kutoka Mtili – Ifwagi – Mdabulo – Ihanu – Isipii mpaka Tazara mpaka Mlimba ni barabara mbaya sana. Toka TARURA wameingia madarakani hawajawahi kutengeneza zaidi ya kilometa 30.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii inaunganisha mikoa miwili, Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Iringa. Tumemwomba Waziri aje kwenye barabara hii, lakini hajafika, lakini najua leo atakapokuwa ana-wind up atatuambia lini atafika Mafinga, atafika Mufindi kukagua barabara hii, kusudi aweze kuwasaidia wananchi wa maeneo yale wapate usafiri wa uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo hili watu wanakufa kwa sababu miundombinu imekatika. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri alione hili jambo. Kwenye eneo hili tuna vijiji zaidi ya 30, tuna kata zaidi ya tisa, miundombinu haipitiki, kwa hiyo namwomba sana Mheshimiwa Jafo afike kwenye eneo hili. Bahati nzuri alipata nafasi ya kufika Mdabulo Sekondari, akaona hali halisi ya hiyo barabara, yeye ni shahidi. Kwa hiyo, tunamwomba afike kwenye eneo hili na watu wa Mufindi wanataka kusikia kauli yake kuhusu barabara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine la barabara ni la Tambalang’ombe, Uyole, Ugwenza, Ikweha na Kwatwanga, nalo ni tatizo. Ukienda kwenye Jimbo la Mufindi Kaskazini, haya maeneo hayapitiki kwa sababu yanasimamiwa na TARURA na TARURA hawana fedha hatuwezi kuwalaumu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri afike kwenye maeneo haya aone hali halisi na aone malighafi za wananchi zinavyoharibika kwenye maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matumaini yangu Waziri atatembelea kwenye maeneo haya na atajionea hali halisi. Hata hivyo, tunamwomba sana Waziri atuletee upya tuiangalie Sheria ya TARURA, kwa sababu sisi kama Wabunge hatuna control ya TARURA, Madiwani hawana control ya TARURA, TARURA hawawajibiki kwa Madiwani, hawawajibiki kwa Wabunge, kwa hiyo, TARURA wenyewe ndiyo wanaamua barabara gani itengenezwe. Sisi tuna matatizo ya barabara kama wangekuwa wanahusika kwa Wabunge au kwa Madiwani, tungewaambia anzeni na barabara hii, hii acheni. Kwa hiyo, kwa utaratibu huu, wanatengeneza barabara wanazozitaka wao, siyo tunazozitaka sisi wawakilishi wa wananchi. Kwa hiyo, Sheria ya TARURA, ibadilishwe, tuiangalie upya, kwamba wawe wanawajibika kwenye Kamati za Fedha za Halmashauri, kusudi tuweze kuwashauri tuanze na barabara gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo naomba kuchangia ni eneo la afya. Jimbo la Mufindi Kaskazini lina tarafa nne (4), lakini tuna kituo kimoja tu cha afya na mwaka jana tuliahidiwa kupelekewa milioni 300 kwenye kituo kimoja cha afya, lakini mpaka leo hazijafika. Kwa hiyo, pamoja na kazi nzuri aliyoifanya Mheshimiwa Jafo ya kutupelekea milioni 400 kwenye kituo cha afya cha Ifwagi, tunaomba kwenye kile kituo kiwepo, tupelekewe milioni 300 na hii ilikuwa ni ahadi ya kipindi kilichopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tusiishie hapa, kwa sababu tuna tarafa nne, at least kwenye kila tarafa tupate kituo kimoja cha afya, tutakuwa tumefikia jinsi gani ya kuwasaidia wananchi. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Jafo kwenye kila tarafa moja, tupate kituo kimoja cha afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka kuchangia...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Kangi Lugola pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri Engineer Yussuf Masauni kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi nzuri wanayoifanya, naomba nipewe majibu sababu zipi zinasababisha askari wote wenye cheo cha nyota moja kushuka chini wamewekewa ukomo wa kustaafu miaka 55. Hii sheria au kanuni haiwatendei haki askari hao; kwa nini Serikali isiangalie upya utaratibu huu na kuwaweka katika utaratibu wa miaka 60 kama ulivyo kwenye maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nachukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Prof. Ndalichako pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri, Olenasha kwa kazi nzuri wanayoifanya katika sekta ya elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi zangu, naomba sana Mheshimiwa Waziri aendelee kupigania elimu bora katika nchi hii. Mwaka juzi kuna baadhi ya shule za Serikali na shule binafsi zilipata kashfa ya udanganyifu wa mitihani, hili ni jambo baya wala halikubaliki. Pamoja na adhabu mlizochukua ikiwa ni kufutia mitihani na kuzifungia shule hizo, naomba sana adhabu hizi zisiweze double standard kwa kuziadhibu shule binafsi na kuziacha shule za Serikali wakati kosa ni lile lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule za binafsi zimenyimwa nafasi ya wanafunzi wao kufanyia mitihani katika shule zao, wamebadilishiwa centre za mitihani pamoja na kuendelea kuwafundisha wanafunzi katika shule zao na mbaya zaidi hata matokeo yakitoka yanalenga katika shule walizofanyia mitihani. Ombi langu adhabu iwe common kwa yeyote atakayefanya kosa, kubagua ni dhambi. Naomba kuchukua fursa hii kuwaombea msamaha wenye shule za binafsi kwa muda wote huu watakuwa wamejifunza kosa lao na hawatakuwa tayari kulirudia tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naunga mkono hoja, Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri endeleeni kuchapa kazi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushurkuru sana kwa kunipa nafasi. Pia naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Waziri, Mheshimiwa Kamwelwe; Naibu Waziri, Mheshimiwa Nditiye pamoja na mtani wangu kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara hii ya miundombinu. Vile vile naomba nichukue fursa hii kusema kwamba naungana na taarifa ya Kamati, taarifa ya Kamati imekuwa nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, miongoni mwa maoni ya Kamati, imeelekeza kwa Serikali na Wizara kwamba umefika wakati kuwe kunatengwa bajeti ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami kwa barabara zinazounganisha mkoa na mkoa. Katika Jimbo la Mufindi Kaskazini nina barabara kubwa tatu; barabara ya kwanza inaanzia Kinyanambo C, Itimbo mpaka Kihansi.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa Wilaya ya Mufindi, ndiyo kwenye bwawa la Kihansi ambalo linatoa umeme megawatt 180, lakini cha kusikitisha barabara hii haina hata kilometa moja ya lami. Pia barabara hii inaunganisha Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Morogoro kwa maana ya Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Kilombero, sasa ufike wakati Serikali ione kuna haja ya kupeleka barabara ya lami kwenye eneo hili ambako kuna umeme wa uhakika na siyo umeme tu, hata eneo mkubwa wa msitu wa Sao Hill liko katika Tarafa ya Kibengu. Kwa hiyo, uchumi mkubwa katika Jimbo la Mufindi Kaskazini unalala katika barabara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ni eneo la barabara kutoka Kinyanambo A, Isalavanu, Igombavanu, Sadani mpaka Ludewa, barabara hii ina kilomita za mraba 151. Katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005, sisi CCM tulisema barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami, tukarudia 2010 na tukarudia 2015 -2020, lakini cha kusikitisha hakuna hata kilomita moja ya lami iliyojengwa katika eneo hili. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha aje hapa atueleze sababu zipi zinapeleka barabara hii isijengwe kwa kiwango cha lami. Mwaka 2009 ilifanyika tathmini ya kuangalia zile nyumba zote ambazo ziko kando kando ya barabara ambazo mpaka leo wananchi wamekaa mkao wa kula lakini miaka kumi imepita, hakuna hata mwananchi moja aliyelipwa fidia. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha atatuambia wale watu waendelee kusubiri au kuna utaratibu mwingine ambao Serikali imejipanga kuhakikisha watu wanalipwa fidia? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingine ambayo ni barabara muhimu inaunganisha tena Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Morogoro, ni barabara inayoanzia Kijiji cha Mtili, Ifwagi, Mdabulo, Ihanu, Isipii mpaka TAZARA mpaka Mlimba. Barabara hii ina kilometa za mraba 136, lakini barabara hii haipitiki kabisa, ni tatizo katika Jimbo la Mufindi Kaskazini. Kwenye barabara hii nako kuna uchumi mkubwa, kuna bwawa ambalo linatoa umeme megawatt saba, barabara hii kuna uchumi wa chai, uchumi wa msitu na uchumi wa pareto, lakini barabara haipitiki kabisa. Sasa ni vyema Serikali ikaona kwamba kuna haja barabara hii kuihamisha kutoka TARURA kuipeleka TANROADS.

Mheshimiwa Naibu Spika, TARURA hawana uwezo hata wa kutengeneza kilomita 20 kwenye barabara hii. Kwa hiyo hali imekuwa mbaya, hivyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri alione hili. Mheshimiwa Rais alipokuwa Waziri wa Miundombinu alikuwa ameshaanza mkakati wa kutaka kuihamisha barabara hii kuipeleka TANROADS, lakini hilo zoezi limekufa ghafla na sielewi tatizo liko wapi. Vilevile Mheshimiwa Rais alipokuwa amekuja pale Mufindi aliahidi kwamba atahakikisha yale maeneo yenye utata kama barabara hii inachukuliwa na kuwa ya TANROADS. Kwa hiyo namwomba sana Mheshimiwa Waziri atakapokuwaa anahitimisha atuambie anatusaidiaje watu wa Mufindi ili tuendelee kuwa na uchumi uliokuwa imara.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ambalo nataka kulizungumzia ni eneo la mawasiliano. Katika Jimbo la Mufindi Kaskazini kuna matatizo ya mawasiliano katika Kata tatu au nne hivi; ya kwanza Kata ya Ikweha hakuna mawasiliano kabisa; pili Kata ya Mapanda hakuna mawasiliano kabisa; tatu Kata ya Ihanu; na nne Kata ya Mpangatazara. Tumekuwa tunauliza maswali mara kwa mara hapa na Waheshimiwa Manaibu Waziri wameniahidi mara nyingi kwamba watakuja kutembelea na kuja kuangalia matatizo ya mawasiliano katika hayo maeneo, lakini mpaka leo hawajafika. Sasa nataka wanapohitimisha hapa wanihakikishie mbele ya Bunge lako Tukufu, ni lini watakuja kwenye maeneo haya kusudi waweze kujua matatizo ya mawasiliano katika maeneo haya...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu kwanza nitajielekeza kwa mtindo wa maswali. La kwanza nilitaka kumwuliza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, nini role la NDC hapa nchini?

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu wa NDC tumewapa majukumu mengi sana, lakini ukiangalia hakuna hata jukumu moja katika yale tuliyowapa mpaka leo lililotekelezwa. Tukianzia na suala la Mchuchuma na Liganga, Mchuchuma na Liganga iko chini ya NDC. Mwaka 2012 tulisaini mkataba na Wachina hapa kuendeleza maeneo ya Liganga na Mchuchuma, lakini mpaka leo hakuna jambo lolote lililofanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili yanapatikana material ya uhakika kwa ajili ya viwanda vyetu kwa maana ya chuma pamoja na makaa ya mawe. Kwenye makaa ya mawe tulikuwa tunaweza kupata umeme wa uhakika ambao tungeweza kupata umeme wa Megawati 50, lakini mpaka leo hakuna jambo lolote linalofanyika. Sasa nataka Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anakuja hapa aje kutuambia sababu zipi zilizosababisha mpaka leo hii mradi ule haujaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa namwomba ndugu yangu Mheshimiwa Mheshimiwa Rashid angetoka pale amwache Mheshimiwa Waziri atusikilize tunachokisema, kwa sababu atakuwa anamchanganya.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ambalo nilitaka kuchangia ni suala la umeme, kwa maana ya umeme wa upepo. NDC walituhakikishia kwamba tungepata umeme wa upepo maeneo ya Makambako na Singida, lakini mpaka leo hatujaona juhudi zozote zilizofanyika katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la tatu ni suala la Arusha General Tyre. Hiki kimekuwa kilio cha miaka mingi, lakini mpaka leo hakuna chochote tunachoambiwa kuhusu suala la General Tyre. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa tunataka atupe majibu ya maeneo haya manne, kwa nini hayafanyiki? Kama hakuna majibu ya kutosha, hatuna sababu ya kuendelea kuwa na NDC kwa sababu, tutakuwa tuna watu ambao tunawalipa mishahara, lakini kazi zao hatuzioni.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ambalo nilitaka kulichangia ni suala la Kurasini Logistic Centre/Kurasini Logistic Hub. Eneo hili ni sentitive. Serikali ya Tanzania tumelipa shilingi bilioni 90 kwa ajili watu waondoke kwenye maeneo yale, lakini huu ni mwaka wa saba hakuna jambo lolote la maana lililofanyika pale. Ule ni mradi mkubwa ambao ulikuwa unagombewa na nchi zaidi ya kumi, lakini kwa namna ya kipekee Wachina walitufanyia upendeleo kutupa ule mradi, lakini hakuna jambo lolote la maana linalofanyika katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, cha kusikitisha kwenye kitabu cha Mheshimiwa Waziri, hakuna hata sehemu moja ambayo amezungumzia Kurasini Logistic Centre. Kwa hiyo, nataka atuambie kwamba zile shilingi bilioni 90 zimepotea au zimekwenda wapi? Kama ingekuwa hatuzihitaji kuzitumia kwenye maeneo haya, bora tungezipeleka kwenye maeneo mengine. Mheshimiwa Waziri kanyamaza kimya, kitabu kizima hakuna hata sehemu imezungumzia habari ya Kurasini Logistic Centre. Kwa hiyo, shilingi bilioni 90 zinapotea bila utaratibu wowote.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine nataka kuzungumzia ni utekelezaji wa Mradi wa Bagamoyo SEZ. Pale napo tumelipa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuwalipa watu fidia. Sasa kwa utaratibu ambao siyo wa kawaida, hela zitakuwa zinapotea kwa utaratibu huu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri atuambie, sababu zipo zinasababisha hii miradi mikubwa ambayo ingeweza kuinua uchumi mkubwa wa nchi hii inapotea bila utaratibu?

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la mwisho nililotaka kuchangia ni suala la viwanda vinavyobinafsishwa. Ifike wakati sasa, Dar es Salaam Stock Exchange ivisajili viwanda vyote vinavyobinafsishwa. Hii itasaidia ku-control tax evasion. Kwa hiyo, huyu regulator (CMSE) ni vyema akaleta sheria hapa Bungeni kwamba viwanda vyote vilivyobinafsishwa visajiliwe kusudi tuweze kuvi-control kwenye soko.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Waziri Dkt. Kalemani na Mheshimiwa Naibu Waziri Subira Mgalu kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata umeme.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu utajikita katika maeneo mawili. Kwanza maeneo ambayo hayana umeme. Katika Jimbo la Mufindi Kaskazini Kata ya Mpangatazara yenye Vijiji vya Mpangatazara na Kimbwe hakuna umeme kabisa. Pia katika Kata ya Ikwila hakuna umeme Kijiji cha Ikwila, Ilangamoto, Ugunza Kata ya Igombavanu, Vijiji vya Uhembila na Matikitu Kata ya Sadani Vijiji vya Ufosi na Mbugi, Kata ya Kobanga Kijiji cha Kipanga Kata ya Mdabulo Kijiji cha Ilasa, Kata ya Mapanda kijiji cha Chozo, Uhafiwa Ihimbo.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili ni kuhusu mahusiano yetu ya wananchi wa Tarafa ya Kibengu na TANESCO. Mara ya mwisho mimi pamoja na Mheshimiwa Diwani wa Mapanda pamoja na Wenyeviti wa Vijiji wa Kata ya Mapanda pamoja na TANESCO tulifanya kikao kwenye ofisi ya Mheshimiwa Waziri Dkt. Kalemani na TANESCO waliahidi kuboresha miundombinu kwenye Barabara ya Uhemi, Uhafiwa mpaka Ihimbo; na barua waliniandikia mimi Mbunge kama mwakilishi wa wananchi. Hata hivyo, kwa masikitiko makubwa tunaenda mwaka wa pili hata kilometa moja hawajatengeneza.

Mheshimiwa Spika, namuomba sana Mheshimiwa Waziri aingilie kati. Juzi nilikutana na DG wa TANESCO naye aliahidi kama mwanzo.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ni gharama kubwa ya kuingiza umeme wa bwawa la Mwenga lililopo Wilaya ya Mufindi. Gharama zimekuwa kubwa sana kuliko zilizoelekezwa na Serikali, pia wana tabia ya kuwatishia watu. Naomba sana Mheshimiwa Waziri aje katika jimbo langu kama alivyoahidi ili aone hali halisi na matatizo wanayoyapata wananchi kutokana na ukiritimba na wawekezaji wa Mwenga Hydroelectric power.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Dkt. Mpango, pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Ashatu kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mchango wangu nilioutoa kwa kuzungumza, naomba niongezee kidogo katika Sekta mbili za Mifugo na Uvuvi pamoja na Utalii. Naomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha atakapokuja kuhitimisha hotuba yake anipatie majibu ya maswali kadhaa ambayo naona yana ukakasi kwangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini tunaagiza maziwa ya unga kutoka nje ya Tanzania ilhali Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya kuwa na ng’ombe wengi Barani Afrika baada ya nchi ya Ethiopia? Mheshimiwa Waziri atueleze tunapoteza kiasi gani cha mapato kwa kuruhusu uagizaji wa maziwa haya ya unga; kwa kilo moja ya unga ina uwezo wa kuzalisha boksi nne za lita nne nne.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanini Serikali imeruhusu matumizi ya imported milk kwenye ofisi za Serikali badala ya kuelekeza matumizi ya maziwa ya ndani kama tulivyofanya katika eneo la furniture? Moja ya malengo ya kutoza kodi (import tax) ni ku-protect home industries, lakini tumepunguza sana kodi kwenye eneo hili; tunalindaje viwanda vya ndani ambavyo vinatoa ajira kubwa kuanzia kwenye ufugaji, soko mpaka viwandani?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini Serikali isishushe export levy ya ngozi ghafi kuliko kuendelea kuacha ngozi ghafi nyingi kuendelea kuoza ilhali viwanda vya ndani havina uwezo wa kutumia ngozi ghafi yote tuliyonayo?

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ni eneo la maliasili na utalii. Ni vyema Serikali ikawekeza sana kwenye eneo hili. Kwa mfano kwenye Hifadhi zetu za Taifa (TANAPA) tulikuwa na hifadhi 16 na ni tano tu ndizo zilizokuwa zina- break even point. Tumeongeza hifadhi nyingine tano, jumla sasa tunazo 21, na bado zinazo-break even ni tano (5) tu. Kwa hiyo tumeiongezea mzigo mkubwa TANAPA. Ombi; gawio linalopelekwa Hazina lisitishwe au lipunguzwe. Tuongeze mkakati kuhakikisha tunaongeza hifadhi zingine zinazo-break even kwa kukuza utalii wa ndani kwa kurekebisha na kuboresha miundombinu ya barabara na maeneo ya kuishi (makambi).

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni Msitu wa Sao Hill. Eneo hili linaingiza pesa nyingi kwenye Pato la Taifa lakini kuna tatizo kubwa sana kwenye eneo la miundombinu; barabara hazipitiki kabisa na ndiko kwenye eneo kubwa la uvunaji wa misitu. Ni vyema sasa Mheshimiwa Waziri wa Fedha akapeleka pesa kwa ajili ya kuboresha barabara za Mtili, Ifwagi, Mdafuro, Ihemu, Isipii – Mpangatuzwa mpaka Mrimba – ambako kuna pareto, chai pamoja na msitu mkubwa bila kusahau eneo la umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naunga mkono hoja.