Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon Haji Makame Mlenge (6 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nikiwa mmoja wa mchangiaji katika Wizara hii ya Mambo ya Ndani. Kwanza, nianze na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika hapa tukiwa katika hali ya afya na uzima. Namwomba Mwenyezi Mungu kwa wale ambao wana afya mgogoro, basi awaponyeshe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende katika mchango wangu katika Wizara hii. Nianze tu na Polisi. Niseme tu kwamba, Polisi ndio ambao wanatufanya tuendelee na vikao vyetu tukiwa huru na salama kutokana na kazi zao. Nawashukuru kwa hilo kwa sababu tumeondoka mitaani kwetu lakini bado hatujapata migogoro kutokana na kazi zao nzuri, hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niseme kutokana na umuhimu wao wa kazi, japokuwa na wenzangu wamesema sana suala la ajira, lakini naomba, ili waweze kufanya kazi vizuri, basi suala la ajira lisiachwe nyuma, liangaliwe kwa umakini na umahiri mkubwa. Kwa sababu ndilo ambalo litasababisha kuweza kufanya kazi zao vizuri. Sitakaa sana hapa kwa sababu watu wengi wamezungumza.

Mheshimiwa Spika, nije kwenye suala la usafiri. Suala la usafiri ni changamoto kubwa katika Jeshi la Polisi, pia tukizingatia kwamba hawa ndio ambao wanatufanya tuweze kukaa kufanya kazi kwa amani na usalama, lakini wanaposhindwa kupata usafiri wa kutosheleza, maana yake huenda tukaja tukawalaumu siku moja lakini watakuwa hawana tatizo la kulaumiwa.

Mheshimiwa Spika, nitoe mfano, ndani ya Jimbo langu nina vituo viwili vya Polisi; nina Kituo cha Chwaka lakini pia nina Kituo cha Jozani. Vituo hivi viwili vyote vinafanya kazi, lakini vikiwa havina usafiri wa aina yoyote. Sijui wanapangaje kazi zao mpaka waweze kufanya kazi vizuri. Kituo cha Chwaka, eneo lake hili lina mahoteli yasiyopungua 18 kwa wale wa Shirika la Umeme, wanaita mahoteli makubwa ambapo wameweka katika ngazi ya kushughulikia maalum, lakini hawana usafiri. Sasa sijui, kazi hizo zinaweza zikafanywa vipi iwapo wataendelea kukosa usafiri? Ikiwa Serikali wanaelekeza sana nguvu zao na tunapiga kampeni kila siku kuona utalii unaongezeka, lakini hatuwapatii usafiri katika maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, la kushangaza zaidi; na nimsemee ndugu yangu Naibu Waziri, kwa sababu hana nafasi nzuri ya kusema maana yeye ni mtetezi wa Serikali ndani ya Jimbo lake. Kile kituo hakina usafiri na kinapokea kesi nyingi sana. Kwa hiyo, suala la usafiri ni jambo muhimu sana ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Mheshimiwa Spika, niongelee kidogo suala la maslahi. Suala la maslahi nalo lina changamoto. Niiguse suala la maslahi ya wastaafu, kwa sababu wenzangu wamesema, sitaki niende sana hapa ili muda wangu usije ukamalizika, lakini nazungumza zaidi kuhusiana na utaratibu mzuri wa Askari Polisi pale ambapo linatokezea tatizo la kufiwa na mfanyakazi, wanakuwa na utaratibu mzuri sana. Pengine unapotaka kuchukua maiti unaweza kuwajulisha wakakwambia hata, usimguse maiti, tunakuja wenyewe kumchukua na kumpeleka katika sehemu husika.

Mheshimiwa Spika, hiyo ilinitokea mimi mwenyewe, pale marehemu ndugu yangu alipofariki. Wakati nawajulisha na nilikuwa nimeshatafuta usafiri, nikaambiwa kwamba wanakuja kumchukua wenyewe na ikabidi usafiri ule niutumie kwa mambo mengine na nisiutumie kwa kumpeleka marehemu. La kushangaza ni kwamba, anapofariki mtu, basi wanachukulia kwa umuhimu, wanamshughulikia, lakini kwanini wasishughulikie maslahi yao?

Mheshimiwa Spika, naomba sana kwa jeshi la Polisi waone kwamba huyu Askari wanapokuwa naye ni mtamu na anapokufa wana hamu sana ya kwenda kumzika. Pia, wawe na hamu ya kuona mafao yao yanapatikana kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nafikiri katika tarehe 19 nilikuwa na swali la msingi la kuhoji kutokana na Askari ambaye amefariki toka mwaka 2003 hadi leo warithi hawajapata mafao; mpaka na wao wafe! Kwa hiyo, siyo jambo zuri. Kama uliweza kwenda kumchukuwa wakati amefariki na ulikuwa unamtumia, basi ni vizuri na kuona maslahi yao yanapatikana kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali yangu hapa, tuone kwamba watu wote siyo sawa, kwa hiyo Askari Polisi wawe wanachukua jukumu la kuwashauri wale wafiwa. Wengine hawana uwezo wa kufika. Sisi tulipata maslahi yetu kwa kupitia wakubwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, siyo utaratibu mzuri.

Mheshimiwa Spika, ahsante. Naunga mkono hoja.
(Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuweza kupata fursa nikawa miongoni mwa wachangiaji wa Wizara hii ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kuniwezesha kufika hapa nikiwa katika hali ya uzima na pili niweze kuishukuru Serikali kwa kuweza kufanya kazi zake vizuri na baadaye kuweza kupata tija. Wizara hii inakazi kubwa ambayo inaifanya nchi hii iweze kutimiza yale malengo yake, ambayo yamejiwekea kwenye Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya nchi. Niseme kwamba nchi hii kwanza niwape shukurani kwa kuwezesha kuyatimiza yale ambayo wameahidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku moja hapa Waziri wa Nishati alizungumzia kuhusu vinasaba kusema suala hili analihamisha kwa mwekezaji mmoja tu na baadaye kulipeleka kwa Serikali kwamba hili suala limeweza kutimia. Lakini pia kusema kwamba yale ambayo tulikuwa tunafanya uchunguzi wa magari (inspection) ambayo tulikuwa tunafanya nje leo tunaifanya hapa.

Mimi kwangu niseme hilo ni jambo jema kwa sababu Watanzania wengi wataweza kupata ajira. Ushauri wangu tu hapa niseme kwamba Wizara iweze kusimamia Watanzania wale wasije wakapata hasara kwa sababu ya kuweza kuleta kufanya uchunguzi katika nchi yao. Iwe ni tija lakini pia waweze kusomeshwa, kutolewe elimu watu waweze kupata elimu na wajue nini kinaweza kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niondoke hapo nije kwenye mfumo wa ukusanyaji kodi kwa njia ya electronic - ETS ambayo mwenzangu ameshaizungumza kwa hiyo, sitakaa sana kulizungumzia suala hili. Lakini tu niseme kwamba Wizara iweze kukaa na kujadili upya kuliangalia suala hili kwa kina kwa sababu wenye Viwanda ni suala ambalo wanalilalamikia na kama kitu kinalalamikiwa ni vizuri kikaangaiiwa tija inapatikana vipi? Hasa kwa sababu fedha zake ni za kigeni lakini pia fedha zile hazizunguki ndani ya Tanzania. Kwa hiyo, ningeomba Wizara wakaweza kuliangalia suala hili kwa umakini mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende tu pale ambapo hasa nimekusudia kusema maneno yangu leo hii. Niseme kwamba twende kuboresha huduma kwa sababu naamini huduma ni njia moja ya kuweza kufanikisha yale malengo yetu ambayo tumejiwekea. Huduma itakapokuwa haifikii pale ambapo tunapataka kwa hivyo, hii mipango yetu tunaweza tusifikie katika malengo ambayo tumejiwekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema kwamba tuweze kwenda kuboresha huduma; kwa sababu Wizara hii ya Viwanda na Biashara ndio ambayo inaweza kuangalia namna nzuri ya kuweza kuendeleza viwanda, lakini wakishaangalia namna hiyo nzuri ya kuweza kuendeleza viwanda wanaoshughulikia ni wengi. Kwa hiyo, ningemshauri Mheshimiwa Waziri kwamba wakae wadau wote ambao wataweza kuifanya biashara iende vizuri. Kwa mfano, hapo nyuma nilikuwa nikikaa kwenye tv namuona tu pengine Waziri kutoka Mazingira anaenda kufunga kiwanda, hii hapa tutakuwa hatuna huduma bora, ni vizuri tukafanya pale tukakaa pamoja na Wizara zote zinazohusika katika kuendeleza masuala ya kibiashara, ili tuweze kufika katika yale malengo ambayo tumekusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme kwa mfano TRA katika safari zetu ambazo tumepita, mimi ni mmoja ya Wajumbe kwenye Kamati ya Viwanda na Biashara. Katika safari zetu tulikopita, kila mahali ukikutana na wafanyabiashara, ukikutana na wenye viwanda wanailalamikia TRA. Mwenzangu amesema hawa TRA ni nani, lakini katika sehemu moja tu ndipo ambapo tumefika pale watu wakaizungumza vizuri TRA. Lakini ukija ukimuangalia yule ambaye amezungumza vizuri TRA, amezungumza kwamba ameanza kwa Katibu Mkuu, akaja kwa Kamishna baadaye watendaji wakapewa maelekezo mahsusi, lakini wenyewe hawawezi kufanya kazi ile kuonesha namna ya huduma bora. Na tukikosa huduma bora hatuwezi kufanya biashara ile ambayo tumeilenga katika Mpango wetu wa Tatu wa Maendeleo. Kwa hiyo, niseme twende kuboresha huduma ili huduma yetu iwe bora zaidi, sasa hivi iko bora lakini iwe bora zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la VAT; nalo limekuwa ni kikwazo kwa wafanyabiashara na wenye viwanda kwa sababu tunawacheleweshea kurejesha fedha zao ambazo fedha hizi ziko kisheria. Lakini kuchelewa kurejesha fedha zao maana yake unaenda kuwakwamisha na unapowakwamisha wafanyabiashara, unapowakwamisha wenye viwanda maana yake unawakwamisha Watanzania. Kwa hiyo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri tukaliangalia vizuri…

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Mwenyekit, naomba dakika moja kuweza kuhitimisha suala langu.

MWENYEKITI: Malizia tu sentensi yako.

MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante niondoke hapo, niseme tu ushauri wangu…

MWENYEKITI: Usiondoke, yaani wewe malizia sentensi yako.

MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Ushauri wangu kwenye hili, ushauri wangu wale wenye viwanda pamoja na Serikali kufanya kiurafiki zaidi kwa sababu inaonekana kwamba mfanyabiashara anavutia kwake, Serikali inavutia kwake, maana yake hapa hatuwezi tukaenda tukatengeneza nchi ya viwanda. Ili tutengeneze nchi ya viwanda wafanyabiashara waone kama kulipa kodi ni haki yao ya kimsingi, lakini Serikali kukaa na wafanyabiashara na wakaona kwamba wafanyabiashara tunafikisha pale malengo ambayo Serikali inaitaka hili ni jambo zuri. Kwa hivyo, ningeliomba Serikali yangu ikaifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi kuweza kupata fursa hii ya kuweza kuchangia jioni hii. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa nikiwa katika hali ya uzima. Pili, ninakishukuru Chama changu Cha Mapinduzi kwa kuweza kusimamia mpaka ikafika hapa kuletwa bajeti ambayo kila mtu anaiangalia kwa mtazamo chanya. Nakishukuru sana chama changu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi ninaipongeza sana bajeti hii hasa kwa sababu imeweza kutaja maeneo mengi ambayo yanaenda kuwagusa wananchi wa nchi hii. Mfano wa maeneo hayo ni kama vile elimu, barabara, maji michezo, wafanyakazi, bodaboda, nakadhalika. Haya yote inaonekana kwamba Serikali imekusudia kufanya na kuleta maendeleo makubwa katika kipindi hiki cha awamu ya sita. Kwa hiyo na mimi nitatoa mchango wangu mdogo ili tuweze kuona namna gani tunaenda kuboresha zaidi ili kuweza kufikia yale malengo ambayo tumeyakusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa mwanzo nitaanza kugusa kupitia mifugo. Najua kwamba Serikali imeshajidhatiti hasa kupitia Waziri anayehusika na sekta hii. Wakati bajeti yake ilipopitishwa alijidhatiti na kuona kwamba anaenda kuleta mabadiliko makubwa ili kuweza kutimiza zile haja za wananchi na Bunge hili ambalo michango yao wameitoa. Lakini niweze kusema kuna maeneo ambayo yanaweza yakagusa wananchi hasa wale wa chini, kama vile ambavyo tumesema katika mpango wetu, kwamba tunaenda kuangalia maendeleo ya watu. Niseme kwamba Serikali ikasimame zile benki zetu ili ziweze kurejesha riba za mikopo, kama ambavyo mama ameshauri, kwamba mikopo ipunguzwe riba.

Kwa hiyo ikipunguzwa riba kuna makundi ya vijana kina mama, walemavu tunaweza tukawapa elimu na wakaweza kusomeshwa ili kuweza kutimiza haja zao kwa kupitia mifugo kama vile kuku. Inaonekana kwamba soko la mifugo hii ya kuku bado lipo kwa sababu soko hili bado linakuja kutoka nje, kuna import kupitia kuku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama tutaweza kufanya vizuri maana yake sisi tunaenda kujiwekeza zaidi ili tufanye export badala ku-import. Watu wana import kutoka mfano Brazil na maeneo mengine kuleta kuku nchini ilhali sisi tuna uwezo mkubwa wa kufanya ufugaji huu na baadaye sisi tukaweza ku-export. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije katika dhana nyingine ambayo katika kichwa changu inaniambia kwamba tukiweza kuifanya basi ile adhma yetu ya bajeti nzuri tunaweza tukaifikia. Watu wengi wanazungumzia miundombinu, lakini nataka kuzungumza kuhusu jambo kubwa la huduma ambalo linaweza likasababisha kuona yale matakwa yetu yanaweza kufikia kwa urahisi. Kwa sababu inaonekana tukishindwa kulitilia mkazo suala la huduma basi tunaweza kutapanga mambo mazuri lakini yakashindwa kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano niseme tu, bajeti hii kila mtu anayekuja hapa anaisifu; lakini si hapa tu hata kwenye mitandao watu wote wanaisifu bajeti hii kutokana na uzuri wake. Sasa tukishindwa kutoa huduma iliyokuwa sahihi maana yake hii bajeti haitakuja na majibu; na kama itakuja bila majibu basi tutabakia na vitabu vyetu kuwa vizuri, lakini hatutapata kile ambacho tulikikusudia kukipata katika jambo hili. Kwa hivyo niseme kwamba tuboreshe huduma hili yale ambayo tumeyakusudia yaweze kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano TRA tumesema kwamba tunaenda kujenga viwanda vingi, lakini baada ya kujengwa kuna watu ambao tumewapa kazi kwa kila mwezi kuweza kuvipitia na kupata huduma katika maeneo haya. Kama huduma hizi hazitakuwa stahiki maana yake tunaweza tukapelekea wawekezaji kutokuridhika na kuweza kuondoka, yapo maeneo ambayo tulipita tukaona kwamba wawekezaji waliondoka kutokana na huduma tu kuwa si nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo jambo hili la kuweza kutoa huduma bora tulitilie mkazo mkubwa sana; na nipendekeze kwamba katika eneo hili tuwape elimu, hasa TRA ambao wanaenda kukutana na wafanyabiashara katika muda wote ambao wanakutana na wanazungumza na wanapanga ili wafanyabiashara waweze kulipa kodi. Kodi hii bila kulipa katika hali ya kirafiki maana yake tutaendelea kuhesabu kusema kwamba tuna watu milioni zaidi ya hamsini lakini wanaolipa kodi ni watu milioni 5. Lakini iwapo kama dhana hii ya kutoa huduma itakuwa ni rafiki maana yake tunaenda kuongeza walipa kodi, kwa sababu kila mtu atakuwa ana nia ya kwenda kuwekeza lakini pia kulipa kodi kwa sababu huduma anayoipata ni rafiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme jambo lingine; mfano wa bandarini. Tukiiona bandari yetu maana yake ina hudumia nchi nyingi lakini bado hatujafikia viwango. Watu wanalalamika kwa kuona kwamba watu wanaondoka kutoka bandari yetu wanaenda katika sehemu nyingine lakini ukizingatia mbali ya miundombinu je, huduma yetu tunayoitoa watu wanairidhia? Na kama hwawataridhika maana yake wataondoka. Kwa hivyo lazima tuboreshe suala la huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini sana Serikali kwa namna ambavyo imejidhazititi na suala hili litapewa kipaumbele kikubwa hili kuweza kufikia malengo ambayo tunayataka. Sasa nije katika suala ambalo mimi mwenyewe linanipata mtihani mkubwa, suala la ubinafsishwaji wa benki ya FBME. Kwanza hapa ni-declare interest. Miongoni mwa waathirika na mimi ni mmoja wao. Kwa kweli jambo hili tukishindwa kuliangalia vizuri, Serikali na kwa sababu Serikali ndiye mdhibiti wa benki hizi za biashara ambazo zinakuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo wanastahiki kuangalia zile dhima ambazo Serikali wamebeba kwa ajili ya kuwafanyia Watanzania ambao wameathirika. Mimi mwenyewe tarehe 8 Mei 2017 wakati naondoka zangu naenda benki nikiwa sina pesa mfukoni, naenda benki mlangoni nakutana na polisi. Lakini kwa sababu sikuwa jambazi wala sikwenda pale kwa jambo baya sikujishughulisha nao. Nataka kuingia ndani benki wakaniambia soma hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikakuta kwamba benki imezuiwa huduma. Pale bado kidogo nichanganyikiwe kwa sababu mfukoni nilishamaliza na pesa zangu zote zilikuwa ziko benki. Kwa kweli nimeondoka pale nimejikaza, lakini niko barabarani akili nilikuwa sina. Kwa hiyo jambo hili ni kubwa sana, na hapa limezungumzwa mara nyingi lakini ufumbuzi wake unakuwa mgumu. Mimi mwenyewe nimeenda BOT mara mbili kusikiliza jambo hili. Cha kusikitisha sana ninapoenda BOT nakutana na wananibembeleza na kuniambia usiwe na shaka. Pesa benki hii inayoza kutosha mtalipwa nyote na pesa nyingine zitabakia lakini mpaka leo hatujalipwa. Kwa hiyo hata wakibeleza inakuwa ni bure tu lakini kama mimi niliumia nikiwa mfanyakazi wa Serikali baada ya mwezi mmoja nikalipwa pesa zangu angalau nikapata kujizuiwa je, wale wengine ambao walikuwa si wafanyakazi wakoje

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hapa kuna watu wamepoteza maisha yao kutokana tu na kuathirika na kukosa haki yao na benki hii kama tumeambiwa ina fedha za kutosha kwa nini atulipwi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Fedha ndiye msimamizi mkuu kupitia BOT. Wale wadau kama kule Zanzibar walikaa pamoja kutafuta njia na kuona namna gani tufanye na wakajikusanya wakachagua viongozi na wakaona namna gani tufanye. Wakaandika barua ya kuweza kuonana na Wakuu wa BOT. Barua hii hapa, Waziri naomba hii barua nimkabidhi aone namna gani, lakini majibu yake mpaka leo hayajapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndiyo tunayozungumza ili huduma, kwamba kama hatutatoa huduma inayostahiki, basi watu wengine wanaweza wakapata taabu kwa sababu ni jambo dogo tu hili la kuwajibu na kukaa nao, kuzungumza nao wakawabembeleza kama ambavyo nimebembelezwa mimi, lakini lilikosekana. Kwa hiyo naomba mhudumu aje uichukue barua hii umpe Waziri ilia one namna njema…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia fursa hii ya kuwa miongoni mwa wachangiaji katika Ofisi hii ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Niseme tu kwamba Muungano huu una tija sana na ndiyo maana leo na sisi tuko hapa tunajilabu na kusema ambayo tunayazungumza kupitia suala hili la Muungano. Katika mchango wangu nitaonyesha faida ambazo nimezipata ndani ya Jimbo langu kupitia suala hili la Muungano, lakini hasa mchango wangu utaenda kuzungumzia suala la mazingira katika upande wa hifadhi hai ya mazingira.

Mheshimiwa Spika, Tanzania tumepata bahati ya kuwa na hifadhi hai zisizopungua sita. Katika hifadhi hai hizi sita ambazo zimetambuliwa na UNESCO kuwa hizi tayari zimeshafikia katika kiwango cha hifadhi hai. Kutokana na ziara ya mama ya uzinduzi wa Royal Tour, hifadhi hizi nina wasiwasi kwamba zinaweza zikazidiwa na wageni. Kwa hiyo niseme tu kabisa kwamba hifadhi hizi tuweze kuziangalia kwa kiwango kikubwa, kwa sababu hizi hifadhi hai tusiweze kupoteza asili ambayo ipo ndani ya hifadhi hizo kwa sababu tutakapopoteza asili ya hifadhi hai, tunaweza kupoteza ile huduma ambayo tunaweza kuitoa kwa wale wageni ambao tunawatarajia watakuja katika kutembelea hifadhi hai hizi.

Mheshimiwa Spika, matarajio yetu makubwa ni kwamba, wageni watakapokuja waweze kupendezwa na hifadhi hai hizi ili wawe na ndoto za kuweza kurudi, lakini pia wakazisimulie vizuri ili kuweza kuongeza tija ya kupata wageni. Hifadhi hai hizi ambazo zipo katika nchi yetu ya Tanzania ikiwemo Ngorongoro, Lake Manyara, Serengeti, East Msambara, Gombe na Jozani Chwaka. Kwa bahati nzuri Hifadhi ya Jozani iko katika eneo la Jimbo la kwangu na imepata bahati ya kusajiliwa toka mwaka 2016, lakini kwa bahati mbaya sana hifadhi hii haijakamilisha utaratibu ambao unaotakiwa na UNESCO ikiwemo uzinduzi wa hifadhi hai.

Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, tarehe 24 na tarehe 25 baada ya kuzungumza, walikuja Zanzibar wakafanya kikao pamoja na Idara ya Mazingira pamoja na Idara ya Misitu na kwa bahati nzuri walinialika nikashiriki katika kikao hicho cha kuweza kuona namna gani tunaondoka katika hatua ile ambayo tulikuwa nayo mwanzo ya kutokufanya uzinduzi, lakini hivi sasa mazungumzo yanaenda ili kuweza kufikia hatua ya uzinduzi.

Mheshimiwa Spika, tarehe 25 tulitembelea katika eneo lile la Jozani ambalo linategemewa kuwa hifadhi hai pale ambapo tutakamilisha utaratibu kama ambavyo umeelezewa. Hata hivyo, namwomba tu kaka yangu Waziri Jafo, najua watu wake wamekuja kumpa habari na wamefanya kazi nzuri, Wizara yake inafanya kazi nzuri, lakini ningefurahi sana hata yeye mwenyewe akawa miongoni mwa watembeaji katika eneo hilo ili tuweze kuona namna gani tunaenda kuitengeneza Jozani ili ifikie katika kiwango kizuri.

Mheshimiwa Spika, wakati niko mdogo nilikuwa kijijini kwangu tunazungumza kwamba msitu hautaweza kumalizika hata siku moja, kwa sababu kweli kulikuwa na msitu ambao ulikuwa wewe mwenyewe unaogopa kutembea, lakini leo hii misitu hii hakuna, misitu ile imebakia katika eneo chache hili la Jozani.

Mheshimiwa Spika, zamani wakati tunatembea, ilikuwa ukienda kazini msituni maana yake unakutana na wanyama tofauti tofauti wakiwemo chui leo chui haonekani, lakini ukirudi mnakaa mnasimuliana, unakuta leo mwenzako anakwambia tumekutana na chui, huyu anakwambia tumekutana na nani, lakini leo hakuna, uoto huu tunautegemea sana katika eneo la Jozani. Naomba tuliangalie sana na Mheshimiwa Waziri basi, naomba siku moja tufuatane twende Jozani.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, muda wako umekwisha.

MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania wa Mwaka 2022
MHE. HAJI MAKAME. MLENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa kuwa miongoni mwa wachangiaji wa Muswada wa Uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kabla ya kuchangia Muswada huu wa Uwekezaji, yale maoni yote yanayotokana na Kamati ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara naunga mkono kwa sababu nami ni miongoni mwa wanakamati ya Uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, niende moja kwenye Muswada huu kuhusu jina la Muswada. Jina la Muswada limeandikwa jina la uwekezaji. Muswada wa mwaka 2022, jina hili ndilo ambalo linatokana na Sheria ile ambayo tunaenda kuifuta ya mwaka 1997. Hatuna tatizo na jina la Muswada lakini ingependeza zaidi kwa sababu Sheria hii ni ya Uwekezaji na uwekezaji ni sehemu muhimu sana katika Taifa, Taifa linategemea sana wawekezaji na ndiyo maana Sheria hii tumeenda kuibadilisha na kuleta Sheria mpya ivutie wawekezaji waje kufanya uwekezaji ndani ya nchi ili nchi iweze kupata mapato na kupata ajira ya watu wetu lakini kuweka uwekezaji na kupata fedha nyingi katika uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Kamati katika sehemu hii tulipendekeza Sheria hii iitwe kuwa ni Sheria ya Kuvitia na Kulinda Uwekezaji Tanzania ya mwaka 2022. Aidha, wakati tulipokuwa tunazungumza na kujadiliana na Serikali walikubaliana na sisi na walikuja na kipengele kimoja tu ambacho pengine hawakukubaliana nasi, nao tulikuwa hatukai pamoja, hatuwezi kujadili ili kuweza kuona tunafikia katika hatua moja. Kwa bahati mbaya sana schedule of amendment tumeipta hapa asubuhi leo wakati karibu Muswada unasomwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nakubaliana na Kamati yangu kwamba Muswada huu uwe na jina la kuvutia na kulinda uwekezaji Tanzania. Jina hili ni sehemu ya uwekezaji, tumeangalia nchi mbalimbali wamebadilisha jina la sheria yao na wameweka majina ambayo yanaweza yakavutia uwekezaji, hii ni sehemu ya kuvutia, jina maana yake mwwekezaji anapofungua tu sheria anakutana mwanzo na hili jina. Hili jina ikiwa sehemu ya kivutio maana yake litamshawishi kuona kwamba yeye anakuja kuwekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile niende katika Sehemu ya Pili. Tuliona kwamba hiki kituo kubadilisha jina na kuitwa kituo, tuna majina mengi ya vituo ikiwemo jina la kituo cha Polisi na vituo vingine, kwa sababu hawa wanaenda kufanya kazi kubwa. Tumewapa mamlaka makubwa, tumewafanya watu hawa waweze kuwashawishi wawekezaji waje Tanzania waweze kuwekeza, maana yake tumewapa majukumu makubwa, kwa nini tunaogopa kuwapa mamlaka? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mjadala ulikuwa mkubwa ndani ya Kamati yetu juu ya suala hili, Kamati yetu tunasema kwamba tunapenda na tunashauri Serikali kituo hiki kisiwe kituo na iwe Mamlaka kwa sababu hii itawapa nguvu ya kufanya kazi zile ambazo zimekusudiwa, kuita kituo maana yake bado tuna hofu ya kwamba hawa wanaweza kufanya kitu gani? Lakini tukiwapa Mamlaka maana yake tumewawezesha yale ambayo tunayatarajia wao waende wakayafanye. Kwa hivyo inatakiwa tuje na jina hili kwenye ushauri wetu nami naunga mkono ushauri huu wa kituo hiki kubadilisha jina na kuitwa Mamlaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mchango wangu wa mwisho ni kwamba tuliishauri Serikali kuongezwe Kifungu cha 38, hivi Vifungu vipo 37 lakini kiongezwe Kifungu cha 38 ambacho maalum kitawangalia wazawa. Kwa nini tunataka kuwaangalia wazawa? Kwa sababu wao ndio ambao wanatakiwa washike uchumi wa nchi hii. Wazawa tunapowaacha nyuma maana yake tunaweza tukakosa watu ambao wanaweza kuhimili uchumi wa nchi hii, tukikosa watu wanaoweza kuhimili uchumi wa nchi hii ni hatari, kwa hiyvo tuwaangalie Watanzania namna nzuri ambayo wanaweza kuwa mabillionea kama marehemu alivyosema katika hotuba yake wakati amekuja Bungeni hapa. Kwa hiyo, nasi tumeona kwamba ipo haja Kifungu hiki kiwepo na wazawa wasaidiwe. Kwa nini tumesema hivyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati mwingine linatokea tatizo wazawa wanakosa nguvu ya uwekezaji hasa pale ambapo inatokea wanakuja wageni wanakopa pesa mabenki ya nje, wanapokopa mabenki ya nje riba inakuwa ndogo sana lakini mabenki yetu bado riba ipo juu wanashindwa kushindana. Kwa hiyo, Kifungu hiki ni vizuri kikaongezwa na kuangaliwa maalum kwa Watanzania na kuona kituo au mamlaka ya uwekezaji ina uwaangalia Watanzania namna njema ambavyo anaweza kuwakuza kuwekeza ili waweze kuboresha uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema awali kwamba naungana na maoni yote ambayo yametolewa na Kamati yangu, lakini leo nimekusudia kuboresha katika maeneo haya ambayo nimeyazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

Kwa sababu hawa wanaenda kufanya kazi kubwa tumewapa mamlaka makubwa, tumewafanya watu hawa waweze kuwashawishi wawekezaji waje Tanzania waweze kuwekeza. Maana yake tumewapa majukumu makubwa, kwa nini tunaogopa kuwapa mamlaka?

Mheshimiwa Spika, mjadala ulikuwa mkubwa ndani ya Kamati yetu juu ya suala hili na Kamati yetu imegonga na kusema kwamba tunapenda na tunaishauri Serikali kituo hiki kisiwe kituo na iwe mamlaka kwa sababu hii itawapa nguvu ya kufanya kazi zile ambazo zimekusudiwa. Kutokuita kituo maana yake bado tuna hofu ya kwamba hawa wanaweza kufanya kitu gani, lakini tukiwapa mamlaka maana yake tumewawezesha yale ambayo tumeyatarajia wao waende wakafanye. Kwa hiyo, tuje na jina hili, ni ushauri wetu na mimi naunga mkono ushauri huu wa kituo hiki kubadilisha jina na kuitwa mamlaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini niende katika mchango wangu wa mwisho kwamba tuliishauri Serikali kwamba kiongezwe kifungu cha 38. Hivi vifungu viko 37, lakini kiongezwe kifungu cha 38 maalum ambacho kitawaangalia wazawa. Kwa nini tunataka kuwaangalia wazawa? Ni kwa sababu wao ndio ambao wanatakiwa washike uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, wazawa tunapowaacha nyuma maana yake sisi tunaweza tukakosa watu ambao wanaweza kuhimili uchumi wa wa nchi hii. Tunapokosa watu ambao wanaweza kuhimili uchumi wa nchi hii, hii ni hatari kwa hivyo, tuwaangalie Watanzania namna nzuri ambayo wanaweza kuwa mabilionea kama marehemu alivyosema katika hotuba yake wakati anakuja Bungeni hapa. Kwa hiyo na sisi tumeona kwamba ipo haja kuona kwamba kifungu hiki kiwepo na wazawa wasaidiwe, kwa nini tumesema hivyo?

Mheshimiwa Spika, wakati mwingine linatokea tatizo wazawa wanakosa nguvu ya uwekezaji, hasa pale ambapo inatokea wanakuja wageni wanakopa pesa nje, yaani benki za nje. Wanapokopa benki za nje riba inakuwa ndogo sana, lakini benki zetu bado riba iko juu, wanashindwa kushindana. Kwa hiyo, kifungu hiki ni vizuri kikaongezwa na kuangaliwa maalum Watanzania na kuona Kituo au Mamlaka ya Uwekezaji inawaangalia Watanzania namna njema ambavyo wanaweza kuwakuza kuwekeza ili waweze kuboresha uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema awali kwamba naungana na maoni yote ambayo yametolewa na Kamati yangu, lakini leo nimekusudia kuboresha katika maeneo haya ambayo nimeyazungumza. Ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022