Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Adelardus Lubango Kilangi (30 total)

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuongea lakini kwa sababu ndiyo nafungua mdomo wangu kwa mara ya kwanza katika Bunge hili Tukufu, basi nianze kwanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai. Nimshukuru pia Mheshimiwa Rais kwa kuniteua kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwashukuru na kuwapongeza Mheshimiwa Spika, Naibu Spika Mwenyekiti na Wenyeviti wote. Naomba kuwashukuru na kuwapongeza Wabunge wote na hata Watanzania wote ambao wako nyuma yetu (Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kuchangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yalizuka masuala kama mawili hivi matatu ya kisheria yaliyohitaji ufafanuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Swali la kwanza lilitoka kwa Mheshimiwa Abdallah Mtolea aliyependa kufahamu uhalali wa Mheshimiwa Rais kumpatia msamaha Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utoaji wa msamaha kwa wafungwa upo kwa namna mbili kisheria; namna ya kwanza ni msamaha wa Rais ambao unatolewa chini ya Ibara ya 45 ya Katiba. Hata hivyo, nieleze hii inaitwa prerogative of mercy ni kama Kiswahili chake nimeshindwa kukipata kwa haraka, lakini ni kama mamlaka ya kutoa msamaha au huruma. Sasa mamlaka haya yanaongozwa na sheria itwayo Presidential Affairs Act na kifungu husika ni kifungu cha tatu (3) (Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, namna ya pili ya utoaji wa msamaha ni kupitia Bodi ya Parole huu unaitwa msamaha wa Parole. Aina hii inaongozwa na sheria itwayo The Parole Boards Act na kifungu husika ni kifungu cha nne (4) cha sheria hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msamaha uliotolewa na Mheshimiwa Rais kwa Nguza Viking pamoja na Jonson ni ule wa aina ya kwanza na ambao unaongozwa na hiyo sheria niliyoitaja ya Presidential Affairs Act.

Mheshimiwa Mwenyekiti, palikuwa pia na maswali kutoka kwa Mheshimiwa Suzan Lyimo ni maswali mawili. La kwanza, aliuliza kama ni halali na inakubaliwa kisheria kwa Serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi kuhusiana na Sheria ya Ndoa baada ya miaka miwili kupita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni kwamba kwa Serikali kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya kesi hiyo je, inakubaliana na ndoa za utotoni. Kesi aliyokuwa anaizungumzia ni miscellaneous civil cause No. 5 ya 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza kama ni halali kukata rufaa baada ya miaka miwili kupita ni suala la procedure na kwa vyovyote vile swali hili linaweza likajitokeza rufaa itakapokuwa inasikilizwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ndiyo hilo kwamba kwa Serikali kukata rufaa dhidi ya kesi hiyo inakubaliana na ndoa za utotoni. Ni wazi Serikali ilivyokata rufaa imetoa sababu na sababu hizi zitakuwa ni sehemu ya vitu vinavyobishaniwa ile rufaa itakapoanza kusikilizwa. Kanuni ya 64(1)(c) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inakataza kuzungumzia jambo lolote linalosubiri uamuzi wa Mahakama na kwa hiyo hatuwezi kulizungumzia hapa. Ahsante sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo Zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Nne na Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nami naomba kuchangia hii hoja iliyopo Mezani ambayo ni Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge kuhusu Sheria Ndogo. Nianze kwa kuwapongeza sana Kamati kwa kazi nzuri ambayo wameifanya ya kutuchambulia hizi sheria ndogo na kuona kama ziko sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajielekeza katika mapendekezo mawili niliyoyasikia kutoka kwenye michango ya Waheshimiwa Wabunge. Na la kwanza ni kwamba waandika sheria katika Wizara na taasisi mbalimbali wanaoandika hizi sheria ndogo wafanye kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili kwa namna fulani limeanza kufanyika kwa sababu wanasheria wote wa Serikali katika Wizara na taasisi mbalimbali sasa wamefanywa kuwa ni mawakili wa Serikali na kimsingi wanafanya kazi zao chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia tumeshatengeneza mfumo wa uratibu kwa kuwaratibu hao wanasheria. Kwa hiyo, nafikiri pendekezo hili halitakuwa na changamoto kubwa ya kulitekeleza kwa sababu kimfumo na kimuundo sasa limekwisha fanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo la pili ni lile la kuboresha viwango vya waandishi wa sheria. Kama ambavyo umeona waandishi wa sheria wanahitajika siyo tu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lakini hata katika Wizara na taasisi mbalimbali za Serikali kwa sababu zinajihusisha kwa namna moja au nyingine katika kuandika sheria ndogo. Suala hili la kuboresha na kupandisha viwango tumeshaliona na ninapenda nilitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba tumeshaandaa mpango wa mafunzo na kwa kwelli sehemu fulani ya mafunzo hayo na yatakayokuwa yanahusu uandishi wa sheria yataanza katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa hatutafanya mafunzo haya kwa wanasheria waliopo kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali peke yake, lakini kama nilivyosema, tutawahusisha wanasheria walio katika Wizara na taasisi nyingine za Serikali lakini pia tutawahusisha wanasheria wanaofanya kazi Bungeni, tutawahusisha pia wanasheria walio katika Muhimili wa Mahamaka kwa sababu hao wote kwa namna moja au nyingine wanahusika na uandishi wa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie tu dakika moja kwa kusema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshaandaa mpango na inaanza kuutekeleza ndani ya miezi mitatu ijayo ya kuanzisha chuo au taasisi ya mafunzo kwa ajili ya wanasheria wa Serikali. Tumegundua kwamba wanasheria wa Serikali pengine walikuwa wamesahaulika lakini wanahitaji taasisi yao maalum kwa ajili ya kuwafundisha haya mambo mbalimbali wanayoyahitaji ikiwemo masuala ya uandishi wa sheria. Ninatumaini mwaka kesho tutakapokutana tena hapa nadhani observations za hii Kamati zitakuwa zimebadilika. Ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika kuhitimisha hoja iliyopo mezani ambayo inahusu Sheria ya PPP. Mchango wangu nitauelekeza kwenye mambo mawili. Swali la kwanza litakuwa la utatuzi wa migogoro ambalo liliibuliwa katika michango ya Mheshimiwa Halima Mdee na pia Mheshimiwa Khatib Haji naye amejielekeza katika suala hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, palikuwa na maoni kwamba utatuzi wa migogolo usifanyike kwenye mahakama za ndani, ufanyike kwenye neutral ground na Mheshimiwa Halima alitoa mifano ya ICSID, MIGA na kadhalika. Pia alisema kwamba tatizo kubwa ni mikataba na kwa kweli siyo mfumo wa utatuzi wa migogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo nitapenda kuligusia ni suala la mfumo wa sheria ambalo hili liligusiwa kwenye mchango wa Mheshimiwa Msigwa. Yeye alizungumza kama mambo matatu hivi kwamba tuna shida pengine katika sheria zetu, masuala ya sanctity of contracts, masuala la clarity of regulatory framework, masuala ya utatuzi wa migogoro na pia akarejea masuala ya MIGA kwamba tumesaini mikataba ya MIGA na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi sheria ya PPP ni sheria ya masuala la mambo ya uwekezaji, ni mojawapo ya sheria zinazosimamia masuala ya uwekezaji. Unapozungumzia sheria zinazosimamia masuala ya uwekezaji, yapo matatizo makubwa mawili yanayojitokeza na pengine ndiyo yaliyopelekea baadhi ya Wabunge waliochangia hoja hiyo kutoa hoja walizotoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la historia ya sheria hii, sheria hii imepita hatua zipi na hatua zipi mpaka kufikia tulipo sasa hivi? Hapa nazungumza katika sheria hii iko katika ngazi ya kimataifa, ngazi ya kikanda, inakuja kwenye ngazi ya kitaifa na inakuja kwenye ngazi ya mahusiano kati ya wawekezaji pamoja na Serikali. Hilo ni jambo la kwanza ambalo naliona ni tatizo kwamba hatuangalii historia, haturudi katika historia, hatujipi nafasi ya kujifunza kutoka katika historia.

Jambo la pili ambalo naona ni tatizo, ni kwamba hatuangalii mambo yanayoendelea sehemu mbalimbali duniani na hasa yanayoendelea katika nchi zinazoendelea, katika nchi za Afrika na mwisho Tanzania. Kwa hiyo, tunajenga fikra kwamba haya tunayoyafanya Tanzania ni sisi wenyewe tunayafanya peke yetu, hali siyo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kurudi kidogo katika historia, jambo ambalo ni muhimu sana. Ukizungumzia sheria zinazosimamia masuala ya uwekezaji, pamekuwa na mabishano ya muda mrefu, hayajaanza leo kati ya nchi zinazoendelea, kati ya nchi zinazopokea uwekezaji, dhidi ya nchi zilizoendelea na dhidi ya nchi zinazotoa mitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabishano haya yamekuwa katika maeneo makuu manne; sheria zipi zinapaswa kusimamia ile tunaita admission of investments, sheria zipi au misingi ipi inatakiwa kutumika katika ku-control host states, zile nchi zinazopokea investments; sheria zipi zinatakiwa kutumika katika kudhibiti (control) makampuni ambayo yanafanya uwekezaji na pia mwisho suala la nne masuala ya utatuzi ya migogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sheria imekuwaje? Katika ngazi ya kimataifa imeanza kwa kutengenezwa kwa kitu kinaitwa principles of customary international law (sheria za mapokeo). Katika Sheria za Mapokeo ipo misingi mingi sana huko ndani yake, lakini itoshe tu kusema kwamba nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea zilibishana sana kuhusu ni zipi hasa au ni ipi hasa misingi ya customary international law ambayo tunaikubali wote.

Mojawapo ya mambo yaliyobishaniwa sana tukiongozwa na nchi za South America na nchi nyingine za Asia kama Iran na kadhalika kwamba utatuzi wa migogoro unatakiwa ufanywe wapi? Ndiyo maana tukapata kile kitu kinaitwa Calvo Doctrine. Nchi za South America miaka ile ya 1960 mwanzoni inasema: “utatuzi wa migogoro ya uwekezaji ifanyike kwenye nchi uwekezaji unapofanyika” nchi zilizoendelea zikakataa. Kwa hiyo, huo ubishani umekuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa baada ya kutokukubaliana sana katika sheria za customary international law, ndiyo tuka-move katika hatua nyingine. Nchi zilizoendelea zikaja na wazo la kutengeneza mikataba ya kimataifa, multilateral investment treaties na ziko nyingi. Katika eneo hilo pia hatukukubaliana nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea kwa sababu moja kuu, mikataba mingi na ambayo ilikuwa inatungwa kwa wakati huo ilikuwa ina lengo la kumpendelea mwekezaji na kuikandamiza nchi ambayo inapokea ule uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu nitoe mifano michache hapa ya mikataba ambayo haikuweza kufanikiwa kwa sababu ilipingwa na nchi zinazoendelea. Mwaka 1967 nchi zinazoendelea zilitoa kitu kinaitwa Convection on Protection of Foreign Property, ilikataliwa na nchi zinazoendelea. Mwaka 1975 iliteuliwa Code of Contract on Transnational Corporations ilikataliwa; mwaka 1976 iliteuliwa Declaration on International Investment and Multinational Enterprises ilikataliwa; na mwaka 1992 kiliteuliwa kitu kinaitwa Multilateral Agreement on Investment ilikataliwa. Zote hizi zimekataliwa kwa sababu nchi zinazoendelea zinafikiri kwamba mfumo huo unatengenezwa kibabe na nchi zilizoendelea kuzigandamiza nchi zinazoendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kushindwa katika Multilateral Treaties ukaja sasa mfumo mpya, Bilateral Investment Treaties, hizi nazo zimepingwa sana na nchi zinazoendelea na kwa sababu pia zina masharti ambayo yanatupa shida. Baada ya kuona sasa Bilateral Investment Treaties nazo zinapata shida, ndiyo tumekuja kwenye kitu kinaitwa makubaliano kati ya mwekezaji na nchi husika (State Investor Agreement). Hizi nazo zimepingwa na nchi zinazoendelea, kwa nini? Kwa sababu ile agreement nayo inatengeneza sheria yake peke yake na kwa namna moja au nyingine imezichukua zile principles za customary International Laws zilizokataliwa na kuziweka kinyemela kwenye hiyo mikataba. Kwa hiyo, nchi nyingi sasa hivi zinasema tusiweke mikataba, mwekezaji atumie sheria ya nchi ile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuje kwenye suala la nini kinachoendelea duniani? Nimesema kwamba tunapokuwa tunazungumza hapa tusijitazame wenyewe, tuangalie nini kinachoendelea sehemu nyingine zote duniani? Katika nchi zote zinazoendelea na katika majukwaa mbalimbali, kuna mijadala inayohusiana na mfumo wa sheria zinazoshughulikia masuala ya uwekezaji na nchi zote zinazoendelea zina msimamo mmoja, haziridhiki na mfumo uliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata katika Bara za Afrika ndiyo mijadala iliyopo. Kwa unyenyekevu mkubwa sana nitaeleza, mimi nimekuwa Mwenyekiti wa ile Tume ya Sheria za Kimataifa za Umoja wa Afrika kwa miaka sita na haya ndiyo yalikuwa mazungumzo siku zote. Nchi za Afrika haziridhiki na mfumo uliopo. Sasa tulichofanya Tanzania ni hatua za kishujaa kweli kweli, ni nchi chache duniani zilithubutu kuchukua hatua hizo kama Iran miaka ya 1950, ilichukua hatua hizo dhidi ya uwekezaji wa Marekani. Walipewa msukosuko mkubwa, walihangaishwa, lakini waliweka misingi tunayoitumia mpaka leo kwenye mambo ya OPEC. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa labda nimalizie kwa ku- address ile hoja kwamba twende kwenye neutral forum. Tusitumie Mahakama zetu twende kwenye neutral forum. Na mimi nauliza swali, hizo neutral forum ni zipi? Kuna mtu yeyote anaweza kunitajia hiyo neutral forum? Mheshimiwa Mdee alitaja kuna ICSID, kuna MIGA na kadhalika. Nani ameitengeneza ICSID? Nani ameitengeneza MIGA? Ni World Bank. World Bank ndiyo financier mkubwa kwa investors wengi. Nani mchangiaji mkubwa kwenye World Bank? Swali rahisi tu. Kwa hiyo, huyo huyo ambaye ndio financier mkubwa ndiye ametengeneza mifumo ya utoaji haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hiyo mifumo ina matatizo gani? Ina matatizo makubwa sana. Hili liko wazi, limeandikwa na wasomi, wataalam na watu mbalimbali, siyo kutoka nchi zinazoendelea tu, hata nchi zilizoendelea zenyewe hawaridhiki pia. Mfumo huo unadhibitiwa na watu wachache sana. Hii International Arbitration inadhibitiwa na watu wasiozidi 50. Hawa ndio Arbitrators kwenye kesi zote. Kwa hiyo, wamejipanga na wanajuana, na wewe ukiwa na kesi watakwambia, choose an arbitrator from the list of arbitrators approved by the tribunal. Hakuna namna! Huwezi ukapeleka mtu wako hapa akaenda kuwa arbitrator. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hao unaowaambia wachague, wamepatikana wapi? Mfumo wenyewe haupo predictable, tumezoea kwamba katika mahakama nyingine za kawaida uamuzi unapofikiwa, sheria iko wazi, taratibu ziko wazi. Katika hizi international tribunals sheria wakati mwingine haziko wazi, taratibu haziko wazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna shida ya arbitrators, hawa kuegemea upande wa investors, hilo liko wazi, hatusemi Tanzania peke yetu, hapana. Watu wengi walio-observe mambo yanavyofanyika katika international arbitration wameeleza wazi kwamba arbitrators wazo biased. Nawe kaangalie record ya nchi zilizokwenda kwenye arbitration kwa mfano International Center for the Settlement of the Investment Disputes (ICSID).

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zinazoendelea zimeshindwa kwa percentage kiasi gani? Karibu 90 percent, siyo Tanzania peke yake. Kwa hiyo, huo mfumo unaoitwa neutral, siyo neutral, wala hautufai. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu, Mahakama zetu ni nzuri sasa hivi. Zimefanya maboresho makubwa mpaka tuna Commercial Court ambayo inasimamia masuala tu ya biashara na uwekezaji, Mahakama zetu zinaweza zikafanya kazi vizuri kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia muda kuwa mchangiaji wa pili kwenye sheria hii tunayoijadili.

Mheshimiwa Spika, nitagusia mambo mawili, matatu katika mchango wangu. Kwanza, itakuwa inahusu Mfuko wa Korosho, halafu nitazungumzia kidogo Tume ya Mipango, nitazungumzia Suala la Akaunti ya TSA na kama muda utaniruhusu, nitazungumza kidogo kulikuwa na suala linalohusu kutozwa kwa VAT kwa umeme unaouzwa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, nikianza na suala la Mfuko wa Korosho, kulikuwa na tuhuma hapa kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amelipotosha Bunge katika suala hili na katika masuala kadhaa. Ninalopenda kusema mbele yako, wazi kabisa kwamba position aliyoitoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiyo sahihi kabisa kisheria. Jambo la kwanza lililozungumzwa katika eneo hilo la korosho ni kwamba, tozo ya export levy, ilianzishwa na wakulima.

Mheshimiwa Spika, hiyo siyo sahihi, tozo ya export levy au levy kwa ujumla haikuanzishwa na wakulima. Levy hiyo ilianzishwa na Sheria ya Cashewnuts Board of Tanzania ya mwaka 1984 na ni kifungu cha saba (7). Nisome tu kwa rejea kwa sababu mambo haya wakati mwingine inabidi msomeane ili watu waamini. Kifungu kinasema:

“7(1) The Minister may, after consultation with the Minister for the time being responsible for Finance and with the Board, and by order published in the gazette, impose a levy on cashewnuts or any category, cashewnuts produced or processed in the United Republic.

(2) Levy imposed under sub-section (1) shall be computed and collected at such rate and in such manner as
may be prescribed by regulations made under this Act and shall form part of the financial resources of the Board.”

Mheshimiwa Spika, hizo regulations za mwaka 1996 zinasemaje, hizo regulations ambazo zinaitwa cashewnuts marketing regulations za mwaka 1996, Kifungu cha 21 kinasema;:

There will be payment of export levy and quality standard to be observed.

Kifungu kidogo katika hicho kifungu cha 21, kinasema:

The exporter shall prior to making shipment of each export consignment observe quality standards are specified in relevant sales contract and pay export levy applicable.

Mheshimiwa Spika, export levy haikuanzishwa na wakulima, ilianzishwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, nini hasa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa. Je, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ulikuwa na athari ya kusema export levy ni fedha za wakulima au ni fedha za Serikali. Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu Ole Nasha, alitoa maelezo kidogo, wakati hoja hiyo ikitolewa.

Mheshimiwa Spika, itoshe kusema, Bodi ilikuwa inakusanya export levy na ile percentage inayokwenda kwenye Mfuko wa Korosho ilikuwa inatolewa na Bodi ilianzia mwaka 1996. Mwaka 1998 baada ya kutokea ubadhirifu, Serikali ilitoa maelekezo Bodi ya Korosho isipeleke zile fedha kwenye Mfuko wa Korosho.

Mheshimiwa Spika, baada ya uamuzi huo, Mfuko wa Korosho ukafungua kesi Mahakama Kuu, kama nilivyoeleza katika maelezo yangu ya awali, Mahakama Kuu kimsingi ilisema mambo matatu, Bodi ilikuwa inakusanya zile fedha
za kwa niaba ya Serikali, zile fedha ni za Serikali na Serikali ndiyo ina mamlaka ya kupanga matumizi ya fedha hizo. Mfuko wa Korosho haukuridhika ukakata rufaa Mahakama ya Rufaa. Mahakama ya Rufaa ilisema nini? Mwisho kabisa, sentensi ya mwisho, “the appeal is lacking in merit, we accordingly dismiss the appeal with costs.”

Mheshimiwa Spika, unapokuwa na kesi, Mahakama fulani ikaweka msimamo na Mahakama Kuu, niliweke hili wazi, kisheria Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa zinajulikana kama Court of Record. Ni Mahakama zinazoweza kuweka msimamo wa kisheria. Sasa Mahakama Kuu imetoa maamuzi wamekata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa, Mahakama ya Rufaa imetupitia mbali rufaa, maana yake nini? Uamuzi wa Mahakama Kuu unabaki.

Mheshimiwa Spika, katika hukumu hii ni kweli Mheshimiwa Cecil Mwambe nafikiri alikuwa anafanya reference, Mahakama ya Rufaa ilizungumza, zungumza mambo mengi, lakini kama alivyoeleza vizuri kabisa Mheshimiwa Ole Nasha, katika hukumu yeyote na hii tunaitoa katika misingi ya uangalizi wa sheria, tunapokuwa tunaiangalia hukumu tunaifanyia analysis ya namna gani.

Mheshimiwa Spika, kuna kitu kinaitwa dictum uamuzi wa mwisho, kuna kitu kinaitwa orbiter dictum ni maoni ya Jaji, wanayoyazungumza yote hayo yalikuwa ni maoni ya Jaji, lakini uamuzi wa mwisho ambao ni dictum, ni hii appeal is lacking in merit, we accordingly dismiss it, tena na gharama juu. Msimamo wa Mahakama Kuu ndiyo msimamo unaobaki mpaka hapo.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, kulikuwa na madai kwamba, wakulima wa korosho, waliingia mkataba na TRA, uliopelekea yale mabadiliko katika Finance Act, 2010 na ikaweka ile formula ya asilimia 65 kwa 35, huu ni upotoshaji. Hakuna mtu yeyote binafsi anaweza kwenda kukubaliana na TRA, namna ya kutoza kodi na mahali pa kuzipeleka. Kwa hiyo, tukomee hapo ni upotoshaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho kuna mapendekezo, tuiache Finance Act 2010 katika suala la korosho iendelee kubaki ilivyo. Finance Act ya 2010 ilifanya ammendments kwenye ile sheria Cashewnuts Industry ya 2009. Kama nilivyoeleza katika mchango wa awali hii Sheria ya Finance Act ya 2010 iliyorekebisha Sheria ya Cashewnuts Industry 2009, ilikuwa na matatizo ya kimsingi ya kisheria haifai kuiacha ilivyo.

Mheshimiwa Spika, tatizo la kwanza nilieleza ilitambua Mfuko ambao haujaanzishwa kwa mujibu wa sheria kama ilivyoelezwa katika Katiba Ibara ya 135(2), pia kama ilivyolezwa katika sheria mbalimbali. Kwa hiyo haiwezekani kuendelea na sheria inayoutambua Mfuko ambao haupo kisheria, lakini pia haujaanzishwa na amri ya Waziri kwa kadri au na minajili ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Fedha za Umma, 2001 (The Public Finance Act, 2001). Kwa hiyo, hilo lilikuwa tatizo la kwanza kisheria.

Mheshimiwa Spika, tatizo la pili, lipo humo, kwa sababu hii Finance Act, 2010 sasa inamtaja TRA ndiye mkusanyaji wa hizi export levy, lakini ukienda Kifungu cha 24(1) cha Sheria ya TRA, kinasema TRA akishakusanya hizi fedha anapeleka kwenye Mfuko Mkuu (Consolidated Fund), hawezi kupeleka sehemu nyingine, lakini hata hii Katiba, Ibara ya 135(2) iko wazi, makusanyo yote yanayofanywa na Serikali yanakwenda Mfuko Mkuu. Kwa hiyo, Sheria hii ilivunja Katiba, sheria hii ilivunja Sheria ya TRA, ilivunja Sheria ya Finance Act. Haiwezi ikaachwa.

Mheshimiwa Spika, Sasa nihame kutoka kwenye Korosho niende kwenye Tume ya Mipango.

Mheshimiwa Spika, basi kwa haraka haraka kabisa, kufuta Sheria hii ya Tume ya Mipango hakuna shida, kwa sababu cha msingi ni majukumu, majukumu yake yataahamishiwa katika Wizara ya Fedha na kutunga sheria nyingine mpya kama itahitajika siyo jambo zito wala kubwa, hili linaweza likafanyika kwa muda mfupi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la TSA kuvunja Katiba, hasa kile kifungu cha 143(2)(a) kwamba fedha zinazokusudiwa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali, basi lazima ziwe zimeidhinishwa na Bunge na kwamba katika TSA kutaingia aina fulani ya fedha zinazoitwa unspent funds. Fedha hizo zilishaidhinishwa kwenye bajeti iliyotangulia ila imefika mwisho wa mwaka wa fedha, mwaka wa fedha una limit yake, haziwezi kutumika baada ya hapo, zinaingizwa zinahesabiwa kuwa ni unspent funds lakini zilikuwa zimeshaidhinishiwa matumizi yake.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kuna utaratibu ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, anatoa kibali cha kuzitumia zile fedha kwa makusudi yaliyokuwa yameidhinishwa na Bunge na anatoa kipindi maalum ambapo fedha hizo ziwe zimetumika.

Mheshimiwa Spika, nizungumze kidogo kwa ufupi kuhusu suala lililoibuka la kutoza VAT Umeme unaopelekwa Zanzibar. Mapendekezo yalikuwa ni kwamba tulete mabadiliko katika hii Finance Bill, ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilikuwa ni kwamba, ingefaa mabadiliko haya yafanyike kupitia Miscellaneous Amendments kwa sababu moja kubwa, Miscellaneous Ammendments huwa zinapita kwenye Baraza la Mawaziri, zitapita kwenye Kamati ya Bunge, Kamati ya Baraza la Mawaziri kuhusu masuala ya Miswada na hapo tutaweza kuwa na Waziri wa Fedha, Waziri wa Nishati kwa sababu ni suala la Nishati hilo, lakini pia Waziri anayehusika na masuala ya Muungano kwa sababu pengine yako masuala ya mahusiano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Kwa hiyo, ushauri


wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali isiingie katika Finance Bill hii, ishughulikiwe katika Miscellaneous Amendments, Mheshimiwa Spika, ahsante.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.8) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala huu unaohusu Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 8 ya mwaka 2019. Tumepata jumla ya michango 11 kwa mdomo lakini pia kwa maandishi kuna Waheshimiwa Wabunge watano waliochangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza na mchango wa hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani ambayo nitajielekeza hasa kwenye hoja inayohusu sheria ya Mawakili ndiyo imejitokeza kwa nguvu zaidi lakini pia wachangiaji wengine wameigusia na kuna hili suala la mikutano ya mawakili na Kambi Rasmi ya Upinzani na baadhi ya wachangiaji wanapendekeza turudie utaratibu wa zamani, lakini na baadhi ya wachangiaji wameeleza vizuri. Uzoefu unaonesha kwamba utaratibu huo wa zamani wa kukutana mawakili wote sio tu kwamba hauna tija, lakini umekuwa haufanyi kazi na matokeo yake maamuzi yamekuwa yanaishiwa kufanywa na kikundi cha watu wachache na tunaona mazingira kama haya yakitokea kwenye vyama vingine vya namna hiyo njia bora ni kwenda kwenye uwakilishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia palikuwa na aina fulani ya tuhuma kwamba Serikali inaingilia Chama cha Mawakili. Labda nianze kwa kueleza kwamba Chama hiki cha Mawakili sio chama cha kibinafsi kwa asilimia 100, si kweli! Kwa sababu chama chenyewe kimeanzishwa kwa Sheria ya Bunge, hakikuanzishwa kwa labda memorandum of understanding, constitution au namna yoyote. Imeanzishwa kwa Sheria ya Bunge maana yake ni kwamba Bunge lilikaa likapitisha sheria ya kuanzisha chama hiki. Kwa hiyo, isifike mahali wanachama wa chama hiki wakaisahau historia na wakaanza kudai kwamba ni chama binafsi kwa asilimia 100, si kweli!

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia zipo sababu kwa nini Serikali ni lazma iangalie hiki chama kinafanya nini, kwa sababu Mawakili hawa ni Maafisa wa Mahakama (Officers of the Court), lakini pia ni notaries public, ni watu wanaoshuhudia viapo na ni commissioners for oath yaani wanashuhudia viapo na nyaraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti haya kimsingi yanajulikana ni majukumu ya Serikali, lakini Serikali imeyakaimisha majukumu hayo kwa mawakili binafsi na ndiyo maana miongoni mwa mawakili hawa binafsi kuweza kuteuliwa hata Majaji na tunafahamu wako wengi wameteuliwa kutoka miongoni mwa mawakili hawa. Kwa hiyo, ni lazima Serikali iangalie chama hiki kinajiendesha namna gani na kama zikionekana dosari na kasoro ni lazima Serikali izifanyie kazi kwa sababu kama huko ndiyo unaweza ukatoa Majaji, hawa ndiyo wanashuhudia viapo, wana majukumu mengi sana makubwa huwezi ukawaacha wakaenda wanavyofikiri wanaweza kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mchango ulitoka kwa Mheshimiwa Ally Saleh alizungumzia hivyo hivyo Chama cha Mawakili, lakini maelezo ndiyo hayo niliyokwisha yatoa.

Aidha, Mheshimiwa Lubeleje alizungumzia mabadiliko kwamba una suala la madai, lakini baadae linageuka kuwa jinai, nilitaka kueleza tu kwamba inategemea na matukio yanayotokea mle.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano watu wanaweza kuwa wanashtakiana kwa masuala ya ardhi, lakini mmojawapo ameingia tena inaitwa kabisa ameingia kwenye ardhi ile kwa jinai kwa hiyo kutakuwa na kesi hapo ya kudaiana nani mmiliki hasa wa ardhi, lakini pia inaweza ikaibuka jinai kwa sababu mmojawapo wa wale watu aliingia kwa jinai kwenye ardhi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabadiliko ya Sheria ya Mtoto ameyazungumzia pia Mheshimiwa Lubeleje, lakini akasema ni vyema kufanya mabadiliko ya Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipende tu kurudia kwenye sheria hizi kile ambacho Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria ameshazungumzia. Unapogusa Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi zina changamoto kubwa sana. Sheria hizi zinagusa imani za dini, mila na desturi na kwa hiyo, huwezi kufanya haraka yoyote katika kuzibadilisha. Kuzibadilisha kwake kunahitaji mashauriano mapana katika jamii na ni lazima muwe na muafaka ambao utazingatia hizo hisia za kidini au misimamo ya kidini, mila na desturi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mkundi amezungumzia suala la sheria ya uvuvi na lile suala la kuiondolea Halmashauri mamlaka ya kusimamia sekta na pia kiwango cha faini. Kwenye kiwango cha faini Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amelieleza, lakini kwenye hili suala la kuiondolea Halmashauri mamlaka ya kusimamia sekta ya uvuvi, napenda kusema kwamba baada ya mashauriano ndani ya Serikali kwa haraka tumeona ni vyema tufanye mabadiliko kidogo. Kwa hiyo, tuna further schedule of amendments ambayo italetwa na Serikali kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwakasaka amezungumzia juu ya Tanganyika Law Society kwa ujumla. Mheshimiwa Dkt. Tizeba amerudi kwenye suala la uvuvi na faini na nimekwishaeleza, Mheshimiwa Mhagama amezungumzia maabara ya maziwa na kutoa pongezi na pia suala la Chama cha Mawakili Tanganyika. Namshukuru sana kwa kueleza kwamba uhalisia ndiyo huu kwamba chama hiki sasa kinakuwa na kitakuwa na wanachama wengi zaidi, haitawezekana kuwa na mikutano yenye tija wanapokutana mawakili wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Peneza amezungumzia suala la Chama cha Mawakili Tanganyika na anasema nafikiri Serikali inakiangalia chama hiki kwa jicho hasi, si kweli hata kidogo, nimeshaeleza kwa kirefu. Ni lazima Serikali iangalie chama hiki kinakaa katika misingi ya professionalism na si vinginevyo na inapoona viashiria vyovyote vya kuipora ajenda ya chama hiki na kukipeleka kwenye uelekeo ambao si sahihi ni lazima ichukue hatua. Kama ilivyoelezwa sheria ilipotungwa kulikuwa na mawakili 14 sasa hivi ni 9,000. Mazingira yamebadilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Sixtus Mapunda naye amezungumza na ninamshukuru sana kulieleza vizuri suala la uwakilishi. Mheshimiwa Msigwa amezungumza suala la kuishtaki Halmashauri sasa ni siku 90.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nieleze kidogo hapa, tatizo tulilokuwa nalo limekuwa ni tafsiri ya neno Serikali kwa sababu utaratibu wa kisheria wa kutoa notice wa siku 90 unapoishtaki Serikali umekuwepo siku zote kwenye Government Proceedings Act na unajulikana, lakini shida ilikuwa ninii tafsiri ya neno Serikali. Sasa tukirudi kwenye Ibara ya 6 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi, Serikali ni pamoja na Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.

Kwa hiyo, tulichofanya ni kurekebisha tu hiyo dosari ambayo imekuwepo na siku 90 bado ni muhimu sana kwa sababu siku hizi pia Serikali inapenda pia kufanya uchunguzi juu ya madai yanayoletwa dhidi yake kuona kama ni sahihi kwa sababu pia yamekuwepo madai mengi fake dhidi ya Serikali, lakini pia kama kuna madai sahihi Serikali pia inapenda siku hizi kufanya majadiliano. Kwa hiyo, ndani ya hizo siku 90 Serikali inaweza ikaamua kwamba nadhani hapa inafaa kufanya majadiliano badala ya kwenda kwenye mlolongo mrefu wa Kimahakama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mwisho Mheshimiwa Kakunda ametoa pongezi kuhusu suala la usuluhishi, lakini akatoa tahadhari kwamba zinapotungwa kanuni basi msuluhishi asiwe Jaji au Hakimu. Hapa nieleze kidogo tu kwamba tofauti na mifumo iliyopo kwa sababu ipo tayari mifumo ya usuluhishi na inatambulika kisheria. Kuna usuluhishi ambao unahusisha na Mahakama (Court Amnesty Mediation), kuna usuluhishi kwenye mambo ya ndoa, upo utaratibu wake wa kisheria, kuna usuluhishi kwenye mambo ya kazi, kuna usuluhishi wa mambo ya ardhi.

Sasa sheria au mabadiliko haya yanagusa ule usuluhishi mwingine ambao hauguswi au hauingii katika maeneo hayo niliyoyataja ambayo yana sheria zake. Sasa kwenye usuluhishi huu unaotengenezewa haya mabadiliko ya sheria hapa wale wahusika wenyewe katika mgogoro ndiyo wataamua wanauendeshaje usuluhishi wao na mwisho watakapokubaliana wakielewana, wakipenda wataweza ku-register yale makubaliano yao. Kwa hiyo, kwenye hili hawatapangiwa awe Jaji au Hakimu, watapanga wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri na tumeipokea na tutaendelea kupokea ushauri huu mzuri unaotoka kwa Waheshimiwa Wabunge na kuufanyia kazi ndiyo maana baada ya mashauriano na Kamati ya Katiba na Sheria iliyopitia Muswada huu, Serikali imeleta Jedwali la Marekebisho (schedule of amendments) hata muda mfupi uliopita tena tumeongeza further schedule of amendments na hii inaonesha kwamba Serikali ina usikivu na kupokea ushauri wa Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninaomba kutoa tena hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.3 wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2021 (The Written Laws Miscellaneous Amendments (No. 3) Act, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote ambao wametoa michango yao mbalimbali na kwa kweli kwa kiasi kikubwa imeonesha kwamba wanaunga mkono na wanaelewa umuhimu wa marekebisho ambayo Serikali imeyaleta na kuyapendekeza. Pia wametoa maoni mbalimbali kadhaa ya kuboresha hapa na pale na nitaomba kwa haraka haraka kabisa nipitie maoni mbalimbali yaliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge na panapohitaji kutoa maeleza au ufafanuzi kidogo, basi nitumie fursa hii kufanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumemsikia Mheshimiwa Tadayo amezungumza juu ya umuhimu wa kuwepo kwa timu ya wataalam ya kusimamia mikataba kama hii. Mheshimiwa Waziri wa Nishati ameeleza vizuri lakini niongezee tu kwa kusema kwamba zitakuwepo timu mbili ambazo zitakuwa zinafanya kazi na Wizara ya Nishati.

Mheshimiwa Naibu Spika, ya kwanza itakuwa ni timu ya wataalam ambayo kazi yake itakuwa ni kuangalia masharti mbalimbali ya Mkataba huu siku hadi siku na kuona kama kuna wajibu wowote kwa upande wa Serikali au nchi yetu ambao tunatakiwa kuutekeleza na utekelezwe ipasavyo na kwa wakati. Hiyo ni timu ya kwanza; na ya pili itakuwepo timu ya washauri na litakuwa ni jopo la watu kadhaa ambao watampatia ushauri Mheshimiwa Waziri wa Nishati pale ambapo ataona anahitaji ushauri katika utekelezaji wa mradi huo. Kwa hiyo, jambo hilo limeshafanyiwa kazi tayari.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja kutoka kwa Mheshimiwa Ramadhan Suleiman Ramadhan, ameeleza vizuri kwamba marekebisho haya yanahusu mikataba ambayo Baraza la Mawaziri limeidhinisha. Kwa hiyo, Serikali imeidhinisha na kwamba marekebisho haya yatagusa miradi yote ya kimkakati na siyo tu suala la huu mradi wa bomba la mafuta, lakini pia akaeleza vizuri kabisa kwamba nia kuu hapa ni kuweza kuoanisha sheria zetu na wajibu zilizoko katika mikataba mbalimbali ambayo pia kwa namna moja au nyingine tumeisaini au tumeiridhia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Ng’wasi Kamani amezungumzia pia suala lile lile la lengo la Muswada la kuoanisha sheria na wajibu katika mikataba mbalimbali. Kuhusu masuala ya fursa Mheshimiwa Waziri wa Nishati amelieleza vizuri kabisa na nisingependa kuongezea zaidi hapo kwa sababu maelezo yake yanajitosheleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mhagama ameeleza naye pia kwamba Muswada huu kwa kadri anavyoelewa hauhusu bomba la mafuta peke yake, bali inagusa na miradi mingine kama hiyo na huo ndiyo ukweli na ametoa mifano kadhaa hapo katika kujenga hoja yake na tunamshukuru sana kwa kutusaidia kuongeza ufafanuzi katika Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Nusrat Shaaban Hanje, kiujumla anaunga mkono marekebisho haya kwa sababu anafikiri yanaangalia maslahi mapana ya nchi. Hata hivyo ameonesha wasiwasi wake katika eneo la uwajibikaji kisheria na amekuwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba marekebisho hayo pengine yataishia kulipa Baraza la Mawaziri mamlaka makubwa sana na kulinyima Bunge mamlaka yake kadri ya mujibu wa Katiba pamoja na Sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika jambo hili, itanibidi kueleza kidogo kwa sababu wasiwasi huu ni mkubwa siyo mdogo. Nilitaka kuanza kueleza kwa kurejea Katiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Katiba imelipatia Bunge mamlaka yake kuhusiana na mikataba kama hii. Ukisoma Ibara ya 63(3)(e) inaeleza waziwazi mamlaka ya Bunge na inasema, nitaisoma: “Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake, Bunge laweza (a) Kujaddili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.”

Mheshimiwa Naibu Spika, pengine ni vema tukasoma pia nakala ya Kiingereza tuone nayo inatuelezaje kama hapo tutakuwa hatujaelewa vizuri. Nakala ya Kiingereza inasema: “for the purposes of performing its functions the National Assembly may (e) deliberate upon and ratify all treaties and agreements to which the United Republic is a party and the provisions of which require ratification.”

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani ibara hii ya Katiba iko wazi kabisa na inajieleza, hii inahusu mikataba ya Kimataifa na katika nakala ya Kiingereza imezungumzia ku-ratify yaani kuridhia, lakini hili litatumika tu pale ambapo pia masharti ya mikataba ile yanataka uridhiwe na uubadilishe mkataba ule uwe sheria kwa kiingereza inasema: “incorporation of the provisions of the treaty into our laws” yaani kuubadilisha ule mkataba kuwa sheria zetu, ndiyo mara nyingi inafanyika hivyo, japokuwa Bunge linaweza tu likaridhia tu mkataba bila kuwa na haja ya kuibadilisha kuwa sheria yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilichotaka kusema ni kwamba mamlaka ya Bunge katika sehemu hiyo yapo na yanabaki kama yalivyoelezwa katika Katiba. Kwa taarifa tu, ule mkataba kati ya Tanzania na Uganda kuhusiana na bomba hili la mafuta, inter-governmental agreement ililetwa katika Bunge lako Tukufu na Bunge likaweza kufahamishwa juu ya uwepo wa mkataba huo. Kwa sababu masharti yake hayakuwa yanahitaji kuridhia kwa maana ya neno la ratification, basi ratification haikufanyika kwa sababu haikuhitajika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, nieleze pia kwamba katika sheria yetu ya The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act, kifungu cha 12 kimeeleza na nitakisoma kwa sababu kinagusa mamlaka ya Bunge:

“All arrangements or agreements entailing extraction, exploitation or acquisition and use of natural wealth and resources may be reviewed by the National Assembly.”

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirudie: “All arrangements or agreements entailing extraction, exploitation or acquisition and use of natural wealth and resources may be reviewed by the National Assembly.”

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mipango yote makubaliano yanayohusu kuchimba, kutumia hizi mali asilia yanaweza kurejelewa na Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo ni vema tukaeleza hapa na hili ni mojawapo ya mambo ambayo tumeyaleta kwenye mabadiliko. Sheria yetu hii ilikuwa haitofautishi kati ya maliasili zetu zinazochimbwa au zinazotokea Tanzania na zile ambazo zinatokea katika nchi nyingine na hapa kwetu zinapitishwa peke yake. Kwa hiyo nilichotaka kusema hapa ni kwamba japokuwa kifungu hiki cha sheria kipo lakini hakiwezi kikatumika sasa kwenye huu mradi tunaouzungumzia, kwa sababu mradi huu unahusu rasilimali ambazo zinatokea kwenye nchi nyingine, siyo za kwetu na hatuwezi tukatengenezea sheria kuzisimamia rasilimali za nchi nyingine. Sisi hapa kama alivyoeleza vizuri Mheshimiwa Kamani tunatoa tu njia ya kuzipitisha rasilimali hizo, lakini kwa ujumla mamlaka ya Bunge hayajaguswa, ndiyo hoja ya msingi niliyotaka kuizungumza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Stella Manyanya pia ametoa mchango na kuunga mapendekezo ya Serikali, namshukuru sana. Namshukuru sana pia Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, amefafanua kwa kina zaidi kwamba sheria hii au mabadiliko haya yana lengo la kutoa tafsiri na kuwezesha yale masharti ya kimkataba ambayo tumeshaingia. Mapendekezo haya ni kwa ajili ya nia ya kuondoa changamoto ya utekelezaji wa mikataba hiyo.

Pia namshukuru sana kwa ufafanuzi wake mahiri alioutoa kwenye eneo la ukamataji wa mali za Serikali kwamba, itahusu tu zile mali ambazo zinahusiana moja kwa moja na mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, basi naomba nihitimishe kwa kuwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri, kama nilivyoeleza hapo awali tumepokea maoni mazuri ambayo yanalenga kuboresha Muswada na kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge, basi ni ushahidi kwamba Waheshimiwa Wabunge na Bunge lako kwa ujumla linaunga mkono jitihada za Serikali za kuwezesha miradi yenye maslahi mapana kama ule Mradi wa Bomba la Mafuta kwa ajili ya kuweza kutekelezwa na nchi bila vikwazo vyovyote vya kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO. 5) ACT, 2021
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuhitimisha hoja kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 5 Mwaka 2021. Nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge waliotoa maoni yao katika michango yao mbalimbali tumepokea maoni kutoka kwa Mheshimiwa Agnesta Lambert, Mheshimiwa Abdallah Mwinyi, Mheshimiwa Denis Longe, Mheshimiwa Edward Kisau, Mheshimiwa Joseph Anania Tadayo, Mheshimiwa Dkt Pindi Chana, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Simbachawene ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mheshimiwa Spika, katika michango hiyo mambo makuu yaliyojitokeza ni kama matatu hivi na nitachukua nafasi hii kuyatolea ufafanuzi. Jambo la kwanza ni suala la kuitambua Idara ya Uhamiaji kuwa Jeshi ambayo imeibuliwa katika mchango wa Mheshimiwa Agnesta lakini Waheshimiwa Wabunge wengine wamechangia na katika mchango wake alijikita katika Ibara ya 147(4) ambayo inagusa neno mwanajeshi.

Mheshimiwa Spika, hii imeshaelezwa na Wabunge wengine waliochangia wakisema kwamba ibara hiyo inagusa au inazungumzia neno mwanajeshi na siyo jeshi na kwamba kama tunahitaji kupata ibara mahususi inayohusiana na jeshi au kuanzisha jeshi ni Ibara ya 147(2) lakini pia Ibara 151 ya katiba. Sitazirudia kuzisoma kwa sababu zimesomwa mara kadhaa ibara hizo.

Mheshimiwa Spika, lakini nilitaka nisema neno moja kwamba kunapoibuliwa hoja au wasiwasi kwamba katiba imevunjwa au inaelekea kuvunjwa ni vema yakatolewa maelezo ya kina ili wasiwasi huo usiwepo na ufafanuzi huo uingie katika kumbukumbu za Bunge.

Mheshimiwa Spika, kwa kuanzia Ibara 147(4) ni lazima isomwe pamoja na Ibara ya 147(3) naomba niisome hiyo fasili ya (3) itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa isipokuwa tu atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika Ibara ya 5 ya katiba hii. Kwa hiyo hiyo ndiyo inatangulia sasa ibara ndogo ya (4) inasema kwa madhumuni ya ibara hii mwanajeshi maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, maana yake ni nini hapa neno mwanajeshi lililotumika katika Ibara ya 147(4) linaendana na kilichotamkwa katika fasili ya tatu kwamba itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa. Kwa hiyo, neno mwanajeshi hapa limetumika katika muktadha ule wa kuzuia kujiunga na chama chochote cha siasa na kwa hiyo ndiyo maana inatumika tu kwenye ibara hii.

Mheshimiwa Spika, lakini niseme zaidi kuhusu hapo hadi mwaka 1992 ibara ndogo ya (3) na ibara ndogo ya (4) hazikuwepo kwenye katiba hizi zimeingizwa wakati wa kujadili sheria ya marekebisho ya katiba iliyofanyika mwaka 1992 na yale marekebisho yalikuwa na sababu mahsusi lakini ili kuthibitisha hilo nadhani ni vema tukarudi katika majadiliano ndani ya Bunge tarehe 30 na tarehe zilizofuata za mwezi Aprili mwaka 1992.

Mheshimiwa Spika, mtoa hoja alikuwa ni Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais na alikuwa anaeleza au anawasilisha Muswada wa Sheria ya mabadiliko ya nane katika katiba ya nchi ya mwaka 1992 katika ukurasa wa 118 wa Hansard unaoakisi majadiliano ya tarehe 30 Aprili, 1992 mtoa hoja alisema lengo la kufanya mabadiliko katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuuondoa mfumo wa chama kimoja cha siasa na kuanza mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Mheshimiwa Spika, ukienda katika ukurasa wa 121 katika majadiliano ya tarehe 30 hiyo hiyo Aprili 1992 kipengele cha (vii) anasema pendekezo hii ni baadhi ya masuala ambayo yatafanyiwa marekebisho katika katiba na yanayopendekezwa na sheria hiyo ni pendekezo kuhusu wanajeshi, vyombo vya ulinzi na usalama na watumishi wengine wa ngazi za juu wa umma kujiunga na vyama vya siasa. kwa hiyo huo ndiyo muktadha wa hayo mabadiliko tunayokuja kuyaona yaliyotokea.

Mheshimiwa Spika, akihitimisha hoja yake ambayo ilichukua siku kadhaa hii ilikuwa ni tarehe 7 Mei 1992 ambayo iko katika ukurasa wa 659 wa Hansard mtoa hoja anasema Wabunge wengine ambao kwa kweli walikuwa wengi zaidi walipendekeza kwamba wanajeshi wasihusishwe kabisa na masuala ya siasa.

Mheshimiwa Spika, lakini ningependa kuwaarifu ndugu Waheshimiwa Wabunge kwamba katika Muswada huu wakati wa kusoma mara ya pili Serikali itapendekeza badiliko la ziada kwenye Ibara ya 147 katika hiyo ibara ya 147 kama mtakavyoona mimi kwangu iko kwenye ukurasa wa 73 huo ni wa mtoa hoja tutaongeza kifungu kingine kidogo baada ya kifungu cha pili cha katiba ambacho kitasema kuwa wanajeshi wasiingie katika vyama vyovyote vya siasa.

Mheshimiwa Spika, yalipokuja hayo marekebisho kwenye sheria yenyewe ukienda Ibara ya 36 ya Muswada wa sheria ya mabadiliko ya (8) ya Katiba ya nchi ambayo ilikuja kuwa Sheria namba (4) ya mwaka 1992 ibara ya 36 ndiyo inabeba hivyo vifungu viwili vilivyoongezwa katika Katiba. Ibara ya 36 ilivyosomeka wakati huo ilisema Ibara ya 147 ya katiba inafanyiwa mabadiliko kwa kuongeza baada ya ibara ndogo ya pili, ibara ndogo zifuatazo: Kwanza ni ibara ndogo ya (3) na inasema hivi itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa isipokuwa tu kwamba atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya (5) ya Katiba hii.

Mheshimiwa Spika, kifungu kingine ndiyo hicho kidogo cha (4) kinachosema kwa madhumuni ya ibara hii mwanajeshi maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa. Kwa hiyo, ninarudia kusema kwamba Ibara ya 147(4) inahusika tu na kile kilichosemwa katika ibara ya 147 (3) na haihusiani hata kidogo na suala la kuanzisha Jeshi au Majeshi ibara sahihi ni 147(2) na 151. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mchangiaji pia alieleza kwamba ili kuanzisha Jeshi unahitaji hati ya Rais ya kuanzisha Jeshi na akawa anarejea natumaini anataka kurejea Ibara ya 33 ya Katiba ambayo anasema Mheshimiwa Rais ni Amiri Jeshi Mkuu na ni kweli 33(2) inasema Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu lakini hiyo haisemi kwamba anapokuwa na sifa hizo tatu kunapotakiwa kuanzishwa Jeshi ni lazima atoe hati haijaandikwa mahali popote pale. Kwa sababu tunayo tayari ibara ya 147(2) imejitosheleza katika jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, naomba niende katika hoja nyingine ambayo ilikuwa inahusu suala la kwamba baadhi ya mihadarati inayozuiwa Tanzania inaruhusiwa katika nchi nyingine ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na pengine nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na hoja hii imetolewa na Mheshimiwa Mwinyi. Sasa nadhani hatuwezi tukatunga sheria kwa ajili ya nchi nyingine lakini litabaki ni suala la mashirikiano na mashauriano katika nyanja za Kimataifa na kuona kama linaweza kuwa ni mojawapo ya masuala ambayo nchi hizi zinaweza zikalichukulia msimamo wa pamoja. Lakini kwa ujumla Serikali imelichukua jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, hoja ya tatu ambayo nafikiri ni vema kuitolea ufafanuzi inahusu tafsiri ya neno exploitation kwenye ile sheria ya anti-trafficking in persons unajua Waheshimiwa Wabunge mbalimbali wameeleza wasiwasi wao katika baadhi ya maneno yaliyotafsiriwa hapo na hasa kama tulivyosema neno exploitation ambalo chini yake ziko tafsiri au mazingira mbalimbali ambayo yanaweza kuhesabiwa kama ni exploitation. Lakini yaliyozungumzwa zaidi ni hili la servitude kwamba linaweza likaendana likapingana pengine na mazingira tuliyonayo. Lakini nilitaka kumtoa wasiwasi Mheshimiwa Mbunge aliyetoa hoja hiyo kwamba ili servitude ihesabike kuwa ni exploitation lazima iwe involuntary na tafsiri hiyo ipo katika sheria ya sasa.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kulikuwa na wasiwasi juu ya forced labor na hasa katika mazingira hayo hayo pia ya kwetu ya kiafrika lakini basi nimuondoe wasiwasi kwa sababu maelezo yametolewa kwamba hii haitajumuisha mazingira ambapo yanahusisha watoto wanaoishi na ndugu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na mwisho kabisa kuna neno forced marriage hili nalo Waheshimiwa Wabunge wameonesha wasiwasi lakini ninapenda kuwatoa wasiwasi huo kwa sababu unapolizungumzia neno forced marriage linapaswa kusomwa kwa muktadha wa kifungu cha 4(1)(b) pamoja na (c) cha sheria kama ilivyosasa lakini nafikiri ni vema nikasoma sasa hivyo vifungu nilivyovitaja ili nieleze ni muktadha gani unaozungumziwa hapa unapozungumzia juu ya forced marriage ambayo ni mojawapo ya makosa ya trafficking in persons.

Mheshimiwa Spika, sasa kifungu hiki kinasema a person commits an offence of trafficking in persons if that person… tunakuja (b) Introduces or matches the persons to a foreign nation for marriage for the purpose of acquiring, buying, offering, selling or trading the person in order that person be engaged in prostitution phonography, sexual exploitation, forced labor, slavery, involuntary servitude or date bondage.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, neno forced marriage muktadha wa kwanza ndiyo huo ambao nimeusema hii itaitwa forced marriage if a person introduces or matches a person to a foreign nation for marriage and or those other things ambazo nimevieleza.

Mheshimiwa Spika, lakini (c) inasema offers or contracts marriage real or simulated for the purpose of acquiring, buying, offering, selling or trading a person in order that person be engaged in prostitution, phonography sexual exploitation forced labor or slavery involuntary servitude or date bondage.

Kwa hiyo mazingira mengine ambapo kutakuwa na forced marriage ndiyo hayo ambayo yameelezwa katika kifungu kidogo hicho. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wasiwe na wasiwasi neno forced marriage litatafsirika kwamba muktadha wa hivyo vifungu nilivyovisoma.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru tena kwa mara nyingine kwa kunipa nafasi ya kuhitimisha hoja hii lakini pia kutoa ufafanuzi katika maeneo mbalimbali ambapo Waheshimiwa Wabunge wameonesha wasiwasi na baada ya majumuisho haya naomba tena kutoa hoja.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Katiba na Sheria
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia hoja iliyoko mezani. Nitaanza kwa kuchangia kwa maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambayo ilizungumza mambo mawili yanayohusu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, Kamati imeshauri na kupendekeza kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inahitaji kuimarisha Mfumo wa Uandishi wa Sheria pamoja na usimamizi wa mikataba kwa namna ambayo itaweza kusaidia kulinda maliasili zetu za Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema kwamba ushauri huo wa Kamati umepokelewa na kwamba hatua tayari zimeanza kuchukuliwa. Katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali sasa tunaanza kujenga uwezo mahsusi kuiwezesha ofisi hiyo iweze kushughulika na hii mikataba, kwa sababu hii mikataba ina mambo ambayo yako a bit complex, yanahitaji utaalam wa juu. Kuna sheria za mikataba huko ndani, kuna sheria za uwekezaji, kuna sheria za Kimataifa, kuna sheria za aina mbalimbali ambazo zinahusika humo. Tumeligundua hilo na tunalifanyia kazi tuweze kuwa na wanasheria waliobobea katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unavyofahamu, hata Mheshimiwa Rais amechukua hatua kadhaa za kuweza kuiboresha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kiasi kwamba sasa inaweza ikakabiliana na changamoto na technicalities zote zilizomo katika masuala ya mikataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia imetoa ushauri kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iongezewe rasilimali ili iweze kufanya kazi zake vizuri. Naomba tu nikuhakikishie kwamba ombi hili limeshapokelewa tayari na Serikali, kwa maana ya kwamba bajeti ya mwaka huu nafikiri kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaongezeka kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna michango kadhaa ya Waheshimiwa Wabunge na baadhi imeelekezwa kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, labda nitaomba niizungumzie kidogo. Mheshimiwa Zuberi - Mbunge wa Liwale ambaye mchango wake pia umeongezewa nguvu na Mheshimiwa Richard Ndassa ambaye amezungumzia uwezo wa Wanasheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa kuingia mikataba kwamba pengine imeonekana mikataba hiyo haikuwa na tija na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza katika maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, hatua zinachukuliwa. Mheshimiwa Rais ameanza kutusaidia kwa kuchukua hatua kuirekebisha na kuibadilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sisi huko ndani tumejipangia mikakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ndassa alisema ni vyema sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikawa na specializations kule ndani. Tunakubaliana naye kwa asilimia mia moja. Yanapokuja masuala ya ujenzi, ni vema ukawa na mtaalam wa sheria za ujenzi; yakija mambo ya kodi, uwe na mtaalam wa sheria za kodi; yakija mambo ya mipaka, migogoro ya mipaka na kadhalika uwe na mtaalam wa sheria hizo na ndiyo ofisi nyingine za Wanasheria Wakuu duniani zinavyofanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu nimhakikishie Mheshimiwa Ndassa kwamba tumeona hatuhitaji tu kuwa na wanasheria ambao wako specialized, lakini kuna baadhi ya maeneo tunahitaji tulete ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hata wataalam wasio wanasheria. Kwa mfano, una mambo ya construction ya ujenzi wa barabara, kwa kweli inafaa sana mkawa na engineer wa mambo ya barabara. Kuna mambo labda ya afya, ni vema mkawa na mtaalam wa mambo ya afya ambaye sio mwanasheria, atatusaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa pia na michango mingine nitapenda nijielekeze kwa mchango wa Mheshimiwa Lema, amezungumza kwa kweli kwa hisia juu ya mwenendo wa kesi mbalimbali na ametaja kesi ya Mwale, Ringo Tenga, Kitillya na Sioi; ninafikiri kwa ujumla sekta ya sheria ina lengo moja la kuboresha utoaji wa haki. Hilo ndiyo lengo la sekta ya sheria. Nikisema sekta ya sheria ninachukua kwa ujumla wake Mahakama, Wizara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ni vema nikalisema hili kwa sababu mchango huo unazungumzia kwa kweli kusimamia utawala wa sheria na alikuwa akipata mashaka kidogo tunapozungumza kwamba kama kesi iko Mahakamani tusizungumzie hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukitaka kuweka msisitizo katika kusimamia utawala wa sheria, ukitoa hoja ambayo inapingana na essence ya utawala wa sheria, inaleta matatizo kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana nyingine ni kwamba Mheshimiwa Mbunge nadhani alipenda kusema kwamba tusifungwe sana na taratibu zetu zinazosema tusilizungumzie suala linapokuwa liko Mahakamani. Hili liko katika Kanuni zetu za Kudumu za Bunge, kanuni ambazo Bunge lenyewe limetunga, Kanuni ya 64(1)(c) ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016 inasema kwamba tusijadili jambo ambalo Mahakama haijalitolea uamuzi; ni kanuni zetu. Hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi wazi kwamba Mahakama itafanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa wala kutiwa shinikizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatari ya kujadili mambo ambayo yako Mahakamani ni namna moja ya kuipa Mahakama shinikizo. Kwa hiyo, labda niseme tu kwamba wale wote tulioko katika sekta ya sheria, tunafanya kazi ya kuhakikisha kwamba mfumo wa sheria unakuwa bora zaidi. Mifumo yote duniani, hata ukienda Marekani, utakuta kuna matatizo yake. Watasema mfumo huu una shida na mfumo huu una shida. Siku zote kinachofanyika, ni kufanya juhudi ya kuuboresha. Basi tusipendekeze kuboresha mfumo wetu wa sheria kwa kuvunja sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vinginevyo, huo ndio mchango wangu na ninaunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia katika hoja iliyoko mezani. Mimi nitajielekeza zaidi katika masuala ya kisheria kwa sababu katika michango mbalimbali iliyotolewa kwa maandishi na kwa mdomo umeonyeshwa wasiwasi tofauti tofauti kuhusu hasa hizi sheria mpya tulizotunga mwaka jana za Permanent Sovereignty na ile ya Review ya Mikataba. Kwa hiyo, kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali nafikiri ninao wajibu wa kutoa maelezo kidogo hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niruhusu katika maelezo yangu haya niirejee kidogo historia. Kuna wakati fulani hapa Waziri wa Katiba na Sheria aliwahi kuzungumza umuhimu wa historia ya sheria na mara nyingi mambo mengi tunakuwa hatuyaelewi kwa sababu historia ya kitu husika tunakuwa hatukifahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria yetu ya Madini imeanza wakati wa Mjerumani. Mwaka 1895 Mjerumani alitunga sheria iliyokuwa inagusa masuala ya ardhi na akasema kwamba kwa sehemu kubwa ya ardhi ya iliyokuwa German East Africa, Tanganyika baadaye, iliwekwa chini ya Mfalme wa Ujerumani, lakini hiyo ikiwa ni pamoja na madini yote yaliyokuwa katika ardhi ile. Pia akatoa leseni za uchimbaji wa madini, palikuwa na uchimbaji tayari maeneo mbalimbali ikiwemo Geita na akayapa makampuni ya Ujerumani.

Mheshimiwa Naibu Spika, alivyochukua utawala Muingereza akatunga sheria na kati ya sheria za kwanza kabisa kutunga ilikuwa ni sheria inayogusa masuala ya madini. Kwa ufupi katika sheria hizo aliyaweka madini yote yanayopatikana Tanganyika wakati ule na kwa sasa Tanzania chini ya Mfalme wa Uingereza wakati huo. Pia aliweka taratibu ambazo zilihakikisha kwamba ni makampuni kwa kweli kwa sehemu kubwa ya Uingereza au ambayo yalikuwa na connection ya Uingereza ndiyo yangeweza kuchimba madini katika nchi hii. Kwa hiyo, kwa ufupi huo ndiyo ukawa msimamo wake wa kwanza katika sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1929 sheria ikabadilishwa na alikuwa bado Mkoloni ni huyo huyo Muingereza lakini ilibakiza misingi ile ile; kwamba madini yote ni mali ya Mfalme wa Uingereza na kampuni za kuchimba madini yale sehemu kubwa yanatoka Uingereza na huo ndio ukawa msimamo. Pia ulikuwa msimamo kwa ujumla katika sheria zinazosimamia uwekezaji kwa maana ya kwamba sehemu kubwa ya wale waliopewa nafasi ya kuwekeza katika nchi, hii ikiwa ni pamoja na kuchimba madini, walitoka Uingereza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1959 miaka miwili kabla ya Uhuru, World Bank wakijua kwamba Tanzania wakati ule Tanganyika itapata uhuru walifanya ziara ya kuja kumuona Mwalimu, wakamwambia Mwalimu tunafikiri ni vema nchi yako ikabadilisha sheria zinazohusu uwekezaji na ambayo ingegusa pia uwekezaji katika madini. Akawauliza mnataka nifanye nini? Wakasema inabidi uzirekebishe sheria hizi ili ziweze kuruhusu na kutoa uwazi kwa makampuni mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali waweze kuja kuwekeza hapa. Mwalimu akawauliza akasema mbona hizi sheria zimekuwepo toka Muingereza na Mjerumani alipokuwepo na zina shida gani sasa, kama ni hivyo basi tutaziacha hizo hizo sheria ziendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya uhuru nchi ilichukua hatua na kupitia katika Katiba ya TANU ya mwaka 1965 ilianza kuweka vipengele vinavyosema sasa hizi maliasili zilizoko Tanzania yakiwemo madini ni mali za watu wote, ni mali za Watanzania. Mwaka 1967 kama tunavyofahamu kulikuwa na Azimio la Arusha na katika lile Azimio baadhi ya athari zake ilikuwa ni kwamba uwekezaji mkubwa ni lazima urudi mikononi mwa wananchi, mikononi mwa Taifa na msimamo huo ukaathiri pia sekta ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1977 tulipopata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 walau vipengele vinavyohusu rasilimali vikaingia katika Katiba hasa katika Ibara ya 9 na Ibara ya 27. Mwaka 1979 tukafanya mabadiliko mengine makubwa ya Sheria ya Madini na haya ni baada ya uhuru. Katika mabadiliko hayo, maana shinikizo lilikuwa limeshaanza wakati ule basi tukaruhusu kampuni kuanza tena kurudi kuwekeza katika masuala ya rasilimali na hasa madini; maana mwaka 1967 msimamo wa sera ulikuwa kama unayaondoa yale makampuni lakini pia tukaruhusu wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, miaka ya 80 na 90 mwanzoni kukatokea kitu kinaitwa Washington Consensus. Kwenye Washington Consensus ambayo ilisimamiwa na World Bank, IMF na Marekani pamoja na mataifa mengine makubwa uliwekwa mkakati wa makusudi wa kurudi Afrika na kuyadhibiti tena madini ya Afrika. Kwa sababu nchi nyingi za Afrika miaka ya 60 zilikuwa zimechukua misimamo ambayo ilikuwa inayanyima makampuni kutoka nje nafasi ya kuyaendeleza au kuya-exploit madini hayo. Hiyo ndiyo ilitupelekea kwenye Sheria yetu ya Madini ya mwaka 1998 ambayo kwa kweli kwa kiasi kikubwa ilikuwa na influence ya mtazamo wa World Bank. Baada ya hapo palikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kwa ujumla, ndiyo ikapelekea mabadiliko fulani ya msingi yaliyofanyika miaka ya 2010 hususani katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nieleze kwa ufupi, hizi sheria mbili tulizotunga mwaka jana chimbuko lake ni nini, pamekuwa na maswali, sasa tumetunga sheria, tumebadilisha sheria, tumewa-discourage investors, tumewa- disappoint investors, hizo sheria zimetokea wapi? Sheria hizi kimsingi zilikuwepo kupitia maamuzi ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Hayo Matamko ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1952, mwaka 1958, 1962, 1966, 1974 na kuendelea na baadaye yaliingia katika mikataba ya kimataifa ikiwemo zile International Covenant on Civil and Political Rights, International Covenant on Economic and Social Right ya mwaka 1966. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu cha msingi cha kuzungumza hapa na ambacho tunakipata sasa katika hizi sheria mbili za mwaka jana ni zile haki nne (4) kuu muhimu ambazo unazikuta katika haya Matamko ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pamoja na ile Mikataba ya Kimataifa iliyotungwa katika uelekeo huo. Ya kwanza, haki ya nchi kutambuliwa kwamba inamiliki maliasili. Nimeeleza Muingereza na Mjerumani walivyochukua nchi jambo la kwanza walisema rasilimali zote za madini ni mali ya Mfalme au yako chini ya Mfalme.

Mheshimiwa Naibu Spika, haki ya pili ni haki ya kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa rasilimali hizi. Hii ni ya msingi sana kwa sababu kuna haki ya kutunga sheria, kuna haki ya kuangalia uendelezaji, kuna haki ya kuangalia processing, kuna haki ya kuangalia masoko, uuzaji na kila kitu. Hizi haki zote ziko humu ndani. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, haki ya tatu, ni haki ya nchi na watu wake kushiriki katika uendelezaji. Naweza nikasema kwa uhakika kabisa kwamba sheria na mfumo uliokuwa umewekwa wakati wa Muingereza na kwa mtazamo wa Washington Consensus ulikuwa umewekwa kwa namna ambayo hauipi nchi na watu wake nafasi ya kushiriki katika kuendeleza hizo rasilimali. Haki ya nne ni haki ya nchi kufaidika na rasilimali hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya mambo manne utayakuta vizuri sana katika hizi sheria mbili tulizozitunga mwaka jana. Kwa hiyo, kimsingi sheria zilikuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niongezee dakika moja na nusu kwa sababu nazungumzia masuala mazito ya kisheria, sheria hizi ni sheria msingi kwa maana kwamba zinakuwa na effect kwenye sheria nyinginezo za nchi hii ambazo zinagusa rasilimali na ndiyo maana zikawekwa chini ya usimamizi na uangalizi wa Waziri wa Katiba na Sheria. Baadhi ya misingi ile iko kwenye Katiba na baadhi ya misingi ile inatakiwa ifanye kazi katika sheria mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie tu kwa kusema kwamba pana wasiwasi mwingi, tutashtakiwa, tutafilisiwa, sijui tutapata shida gani kwa sababu ya kutunga sheria hizi, tumezitunga kwa kuzingatia haki yetu iliyoko katika Sheria za Kimataifa. Kwa upande mwingine kama nchi hatupaswi sasa kuogopa. Bara la Afrika kwa ujumla limekuwa linatishwa sana, lakini kama nchi tumejipanga, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali sasa iko vizuri kabisa, tuna Ofisi sasa ya Wakili Mkuu wa Serikali na kama kunajitokeza jambo lolote nchi kama nchi hatupaswi kuwa na wasiwasi wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Katiba na Sheria
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia katika kuhitimisha hoja iliyopo mezani. Nami nitajitahidi kupitia masuala kadhaa na hasa nitajikita kwa yale yaliyoibuliwa katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, imezungumzwa juu ya sheria zinazodaiwa zinakiuka katiba, mifano imetolewa; Cybercrimes Act, Media Services Act, Accesses to Information Act na nyinginezo na kwamba hizi zinaingilia uhuru wa kujieleza na uhuru wa kupata habari na haki nyinginezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kusema tu ni kwamba masuala ya haki na uhuru yana mipaka na hii imeelezwa vizuri sana katika Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 30. Hata tukienda katika zile sheria za Kimataifa, kama ile International Covenants on Civil and Political Rights, tunaona Ibara ya 19 inazungumzia juu ya uwepo wa mipaka katika haki mbalimbali zilizoelezwa katika sheria hiyo. Kwa hiyo, ninachotaka kusema hapa tu ni kwamba, sheria hizi zinakuwepo, haki na uhuru vipo katika katiba lakini haki na uhuru huo una mipaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, linamhusu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwamba anayo mamlaka ya kutoa maelekezo ya kufanya upelelezi anapoona jambo fulani limetokea na kwamba analaumiwa hapa kwamba hajachukua hatua yoyote kwenye matukio kadhaa yaliyotokea, kwamba hakutoa maelekezo kwamba upelelezi ufanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kusema ni kwamba Mkurugenzi huyu wa Mashtaka, huwa anatoa maelekezo pafanyike upelelezi kama anaona upelelezi huo haujafanywa na chombo chochote kinachopaswa kufanya uchunguzi. Kama kuna vyombo kadhaa; kimoja au viwili au vitatu vinavyofanya uchunguzi katika jambo hilo, hana haja ya kutoa maelekezo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu lilikuwa linahusu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika majukumu yake ya kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu masuala ya mikataba na kwamba pengine ofisi hii haijafanya vema katika jukumu hilo. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kweli imekuwa na changamoto za hapa na pale, lakini kwa sasa hivi maboresho makubwa yamefanyika katika ofisi ile hasa katika eneo hili la uchunguzi wa mikataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulilizungumza hili hata mwaka jana kwamba tumeweka hata masuala ya ubobezi katika uangalizi wa mikataba. Kwa hiyo, sasa hivi wanasheria wetu wako specialized. Kama ni mikataba ya mambo ya ujenzi, kama ni mikataba ya rasilimali, kama ni mikataba ya financing, kama ni mikataba ya manunuzi na kadhalika sasa tumeweka specializations katika ofisi ile na nafikiri ofisi inafanyakazi vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia imeanzishwa idara maalum ambayo inahusika na kutoa ushauri pia. Kwa hiyo, kama kuna upungufu wa capacity kule kwenye idara inayohusika na mikataba hii idara nyingine inayohusika na ushauri kwa ujumla inasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne lililoelezwa katika taarifa hiyo ni kushindwa kutoa ushauri sahihi kwenye kesi mbalimbali na hasa zilizofunguliwa nje ya nchi na hadi kupelekea Serikali kupata hasara kubwa na mifano hapa imetolewa Kesi ya Konoike, kesi ya Sterling iliyokuwa inahusiana na zile ndege zetu, kesi iliyofunguliwa na ACACIAs, kesi iliyofunguliwa na Symbion, Eco energy pengine na nyinginezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda tu kutoa taarifa kwa zile kesi mbili za kwanza, kesi ya Konoike na kesi ya Sterling, actually mashauri haya yameshamalizika, kwa sababu pia palikuwa na mazungumzo kati ya hawa wadai pamoja na Serikali. Niseme tu hapa kwamba hata fedha zilizolipwa katika mashauri haya ni ndogo sana sana sana kuliko zile ambazo zinaelezwa au zilioneshwa katika zile hukumu mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, katika kesi ya Konoike inasemwa ilikuwa ni shilingi bilioni 80, lakini iliyolipwa ni kidogo kabisa. Kwenye kesi ya Sterling nayo ilisemwa ni zaidi ya shilingi bilioni 80 lakini iliyolipwa ni chini ya hata ya theluthi moja ya kiasi hicho kinachotajwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kesi zile nyingine za ACACIAs, Symbion, EKOenergy zinaendelea, kwa hiyo, hatuwezi kuzizungumzia sana. Hata hivyo, hawa wahusika waliotushitaki katika kesi hizo, wao wenyewe ndio wamekuwa wa kwanza kuomba pawe na mazungumzo kati yao na Serikali. Serikali imepokea wito huo na kwa hiyo, mazungumzo yanaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine lilikuwa ni kuhusu mkataba wa Afrika kuhusu mambo ya demokrasia, chaguzi na utawala, yaani African Charter on Democracy Elections and Governance na kwamba Tanzania haijatia saini mkataba huo; na kwamba Mataifa 35 yameshatia saini mkataba huo na kufanya sheria ya nchi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza hapa kwenye hii idadi siyo sahihi. Mataifa ambayo yametia saini na kuufanya huo mkataba kuwa sehemu ya sheria za nchi zao, yaani ratification hayajazidi 11 hadi sasa hivi. Napenda tu kusema kwa haraka haraka kwamba kuna mambo kadhaa ambayo bado yanajadiliwa na yanaonekana bado ni kikwazo kwa nchi nyingi kuweza kutia saini mkataba huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawili makubwa, kuna suala la unconstitutional change of government halijatafsiriwa vizuri na kuelezwa vizuri; na masuala yanayohusu uangalizi wa uchaguzi (election monitoring). Sasa nchi nyingi bado zina mashaka, nini hasa majukumu ya waangalizi wa uchaguzi na kadhalika. Kwa hiyo, siyo Tanzania peke yake na kila mara tunashauriwa kwamba nchi ichukue tahadhari ya kutosha kabla ya kuingia tu kwenye mkataba wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine lililoibuliwa katika taarifa hiyo ni suala la Katiba na linaingiza masuala ya Muungano. Taarifa hii kwa namna moja au nyingine inaijadili au inaizungumza Katiba ya Zanzibar na inahoji katika maeneo fulani fulani kwamba kwa nini katiba ya Zanzibar kwa mfano inamsimamo huu, haimtambui Rais kuwa ndiyo Mkuu wa nchi yote kwa Jamhuri ya Muungano, pamoja na Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hili niliweke vizuri kabisa. Bunge hili lina mamlaka na uwezo wa kuzungumzia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba ya Zanzibar ni ya Zanzibar na hata anayeweza kuizungumzia kwa kweli kwa mamlaka kama ninavyoweza kuizungumzia hapa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ndio anayeweza kuizungumzia authoritatively Katiba ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana hata likitokea shauri lolote linalogusa Katiba ya Zanzibar, shauri hilo haliwezi likafika katika Mahakama ya Rufaa ambayo ni Mahakama ya Muungano, shauri hilo litakomea katika Mahakama Kuu ya Zanzibar na huo ndio utaratibu na misingi ya Kikatiba tuliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mambo ya Muungano, tunazungumza kwamba tuna changamoto. haya yote yaliyoelezwa katika ile taarifa ni changamoto za Muungano. Mpaka sasa hakuna jambo la kikatiba ambalo limebishaniwa rasmi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ipo Ibara katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni vema tuwe tunaisoma kila wakati, inayosema: “kama kutakuwa na jambo linalobishaniwa kati ya Serikali hizi mbili, itaundwa Mahakama Maalum ya Katiba.” Kwa kumbukumbu zilizopo Mahakama hii haijawahi kuundwa kwa sababu hakujatokea jambo linalobishaniwa; na kwa hiyo, yaliyopo haya yote ni changamoto za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumezungumzwa pia juu ya mashauri mbalimbali yaliyoko nje ya nchi, nadhani huu ni mchango wa Mheshimiwa Zitto, akazungumza juu ya kuangalia publiic intrest katika mashauri hayo na akatolea mfano wa kesi ya Standard Charterd Hong Kong; na akaeleza kuna kitu kinaitwa indemnity ambayo iliwekwa na wahahusika wa ile kampuni ya IPTL na kwamba kwa nini wasitolewe mahabusu kwa sababu waliweka ile indemnity? Sasa hapa nahitaji kueleza kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumezungumzwa pia juu ya mashauri mbalimbali yaliyoko nje ya nchi, nadhani huu ni mchango wa Mheshimiwa Zitto. Amezungumza juu ya kuangalia public intrest katika mashauri hayo na akatolea mfano wa kesi ya Standard Charterd Hong Kong na akaeleza kuna kitu kinaitwa indemnity ambayo iliwekwa na wahusika wa ile kampuni ya IPTL na kwamba kwa nini wasitolewe mahabusu kwa sababu waliweka ile indemnity.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hapa nahitaji kueleza kidogo. Ni kweli kabisa kwamba wale watu waliopo mahabusu kuhusiana na Escrow Account katika ile kampuni ya IPTL waliweka indemnity. Hata hivyo, indemnity ile ilikuwa ni kuipa kinga Serikali iwapo litatokea shauri lolote na kutakuwa na hasara fulani au malipo fulani yanayotakiwa kufanyika, indemnity hiyo ita-cover ama hasara hiyo au malipo hayo au mahitaji yoyote yale. Kwa hiyo kimsingi indemnity inagusa masuala ya madai, ni mashauri ya madai, inagusa kwenye madai, kwamba unanipa kinga ikija kutokea shauri lolote linaibuka hapa wewe utanilipa gharama pengine za kesi, wewe utanilipa gharama pengine za kesi, wewe utalipa gharama fulani, wewe utalipa chochote nitakachotakiwa nilipe, ikiwa ni pamoja na yale ambayo mahakama mbalimbali za kimataifa zimeamuru Standard Chartered Hong Kong walipwe kimsingi wanatakiwa kulipwa kutoka kwenye indemnity hii lakini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Muda wetu...

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika moja;

MWENYEKITI: Haya, endelea.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, dakika moja tu nimalizie hapo, kwa sababu ni suala la muhimu kidogo. Indemnity hii haigusi masuala ya jinai, sasa wahusika hawa aliowataja Mheshimiwa Zitto wana kesi, wapo ndani au mahabusu kwa sababu ya kesi za jinai. Nadhani kuna mashtaka kadhaa yanayowahusu kwenye jinai hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa wasaa wa kuanza kuwa mchangiaji wa kwanza upande wa Serikali. Nitajielekeza moja kwa moja kwa hoja iliyoibuliwa na Mheshimiwa Nsanzugwanko (Mbunge), lakini pia alikuwa ananukuu Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika ukurasa wa 16 na 17 ambayo inahusu zoezi la kuhuisha vibali vya uwindaji ambapo Mheshimiwa alizungumza na iko hivyo katika taarifa kwamba Mheshimiwa Waziri alihuisha vibali hivyo mwezi Januari, 2017 lakini mwezi Oktoba akatoa tangazo la kuvifuta. Mwezi Disemba akatoa tena tangazo au maelekezo ya kuongeza kipindi cha miaka miwili kwa vibali hivyo. Kwa hiyo, maoni ya Kamati pamoja na Mheshimiwa Mbunge ni kwamba Mheshimiwa Waziri alivunja sheria, na kwa hiyo, akaomba mahsusi Mwanasheria Mkuu wa Serikali atoe position.

Mheshimiwa Spika, position ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika suala hili ni kwamba Mheshimiwa Waziri hakuvunja sheria. Mheshimiwa Waziri alipochukua hatua hizi na imeelezwa vizuri katika ile barua ya kwanza ya kuongeza muda ya mwezi Januari lakini pia na kwenye hayo mawasiliano mengine ya mwezi Oktoba na mwezi Disemba kwamba alikuwa anachukua hatua hizo kwa ajili ya kuweka mfumo mzuri zaidi wa uendeshaji wa vitalu kwa namna ambayo Taifa litaweza kufaidika zaidi kuliko hali ilivyo sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nilikuwa napenda kukuthibitishia na kukuhakikishia na kumhakikishia Mheshimiwa Mjumbe pamoja na Kamati kwamba Mheshimiwa Waziri alipofanya hivyo alikuwa pia anatekeleza sheria.

Mheshimiwa Spika, swali litakuja ni sheria gani hii ambayo Mheshimiwa Waziri alikuwa anaitekeleza. Sasa nitaomba nilikumbushe Bunge lako tukufu kwamba mnamo mwaka jana mwezi wa saba Bunge hili lilitunga sheria na hii sheria inaitwa The Natural Wealth and Resources Permanent Sovereignty Act. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lengo kubwa la hiyo sheria ilipotungwa mwaka jana na Wabunge wote ni mashahidi nafikiri mijadala ilikuwa mikali na kadhalika, lakini ilikuwa zaidi kuhuisha Ibara za 9 na 27 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sehemu hii ya Katiba katika sheria tunasema inahitaji enabling law uweze kuitekeleza. Sasa nadhani ni vema nikarejea kwa ufupi na kwa haraka kabisa Ibara za 9 na 27 za Katiba zinasemaje. Nitakwenda Ibara ndogo (c) na Ibara ndogo (i) lakini nitakwenda zaidi (c) inatosha; kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kumzuia mtu mwingine kumnyonya mtu mwingine. Hiyo ni Ibara ya 9. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 27 inasema; watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja na kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadae ya Taifa lao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishasema palikuwa na matatizo katika suala zima la hivi vibali vya uwindaji na kwa hiyo Mheshimiwa Waziri akachukua hatua hizo kulingana na hii sheria mpya. Nafikiri niende pia kwenye hiyo sheria mpya ya The Natural Wealth and Resources Permanent Sovereignty inatuambia nini. Naomba niende kifungu cha 6(1) na ninaomba niirejee hapa kinasema; “It shall be unlawfully to make any arrangement or agreement for the extraction, exploitation or acquisition and use of natural wealth and resources except where the interest of the people of the United Republic are fully secured.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aliongozwa na kifungu hicho, lakini kipo kifungu chenye nguvu zaidi ambacho actually kinampa maelekezo Waziri na hana jinsi nyingine. Kifungu cha 6(3) na chenyewe naomba nikisome; “It shall be the duty and responsibility of the Government. all organs and persons or authorities exercising executive, legislative or judicial functions to take cognizance of, observe and apply the provisions of this Act.”

Mheshimiwa Spika, kifungu hicho kinamfunga Waziri kwamba ni lazima ajue kwamba sheria hiyo ipo na kwa hiyo ni lazima chochote anachofanya kuanzia sheria ilipotungwa aongozwe na sheria hiyo.

Mheshimiwa Spika, sasa ninaelewa baada ya kusema hayo swali linaibuka je, kuna mgongano wa sheria. Position ya Mwanasheria Mkuu tena hapa katika swali hili ni kwamba hakuna mgongano wa sheria kwa sababu hii ni sheria msingi na umsingi wake unapatikana kwenye kifungu hicho nilichosema cha 6(3) kwa hiyo ina nguvu kuliko sheria nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, muda umekwisha nakushukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 4) wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) wa mwaka 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika uchangiaji, Mheshimiwa Mbunge mmoja amechangia kwa maandishi na Mbunge mmoja amechangia kwa maneno. Liko jambo moja ambalo nitapenda kulizungumzia na ambalo liko kwenye hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na jambo hilo ni wasiwasi uliooneshwa katika hotuba hiyo katika kufuta maneno, tourist agent na badala yake kuweka maneno tourism operator ambayo yanapatikana katika Ibara ya 30 ya muswada. Kwa kadri ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani maneno tourism operator yanapunguza wigo na amefanya rejea kwenye Government Notice, GN No. 269 ya tarehe 17 Julai, 2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni vyema kufahamu kuwa hiyo GN No. 269 inayo misamiati miwili ambayo ni tour operator na tourism agent na GN hiyo imetengenezwa chini ya Sheria ya Tourism Act, lakini katika Muswada huu, tunazungumzia juu ya tourism operator, kwa hiyo hatuzungumzii tour operator wala hatuzungumzii tourism agent tunazungumzia tourism operator. Pia, huu sio msamiati mpya, ni msamiati ambao uko kwenye Sheria ya sasa ya Utalii yaani Tourism Act, Cap 65, kwa hiyo msamiati huu umechukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye hiyo Tourism Act, Cap 65 na ni kwa sababu kuu mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ya kwanza, ni kutumia msamiati wa aina moja kwenye hizi sheria mbili zinazogusa mambo ya utalii nayo ni hiyo Sheria ya Tourism Act na hii Sheria ya Bodi ya Utalii yaani Tanzania Tourist Board Act. Sababu ya pili ambayo iko wazi zaidi, ni kwamba, msamiati wa Tourism operator kwa kweli una wigo mpana kuliko Tourist agent ukiitazama kama ulivyotafsiriwa kwenye sheria hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vinginevyo nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri, tumepokea maoni mazuri ambayo yamelenga kuboresha si Muswada tu bali hata masharti mengine ya Sheria mama kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni ushahidi kwamba suala la Marekebisho ya Sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo linamuhusu kila mmoja wetu katika Bunge hili na ni jambo endelevu, ndio maana kila mwaka Serikali inakuja na Muswada wa aina hii ili kuboresha masharti ya sheria zetu na kuzifanya ziendane na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kufanya majumuisho haya ya mjadala wa Muswada huu wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) wa mwaka 2018, yaani (The Written Law, (Miscellaneous Amendments) (No. 4) Bill of 2018], naomba tena kutoa shukrani zangu nyingi na naomba kutoa hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Kumi na Moja wa Bunge
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi, kwanza nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Chenge Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kwa mawasilisho yake na kwa hoja alizotoa na wote tunamfahamu nakumkiri Mheshimiwa Chenge katika umahiri wake wa sheria. Kwa mimi binafsi nimtangulizi wangu, ni kaka yangu amekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa hiyo, huwa napata pia mawazo na ushauri mwingi kutoka kwake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika masuala la sheria siku zote kuna mambo mawili makuu ambayo hata Mheshimiwa Chenge anayafahamu vizuri sana. Kuna masuala ya misingi yaani principles na kuna masuala ya utaratibu yaani procedure au enabling procedures. Tunapokuja suala la udhibiti wa Bunge katika suala la utungaji wa Sheria Ndogo na tukaja kwenye principles hakuna ubishani, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ile Ibara ya 97(5) imeeleza vizuri. Hata hii Interpretation of Laws Act nadhani ni kifungu cha nne haina ubishi. Lakini pia misingi hii kwa wanasheria wanajua iko kwenye principles za Administrative Law, sijui kwa Kiswahili tunaweza kusema Sheria ya Utawala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika principles hakuna shida na tunakubaliana Serikali na Kamati na kila mtu. Kuna changamoto kunapokuja kwenye utaratibu na ndiyo maana Mheshimiwa Chenge mwenyewe katika taarifa hii na ameirudia wakati anahitimisha kwamba waliona na ninapenda tena kurudia kusoma hii sehemu ukurasa wa nne wa ripoti hii kwamba; hata hivyo udhibiti huo yaani udhibiti wa Bunge katika utungaji wa sheria ndogo siyo wa moja kwa moja kwa sababu Bunge halina mamlaka ya kuingilia mchakato wa kutungwa kwa sheria ndogo yoyote mpaka sheria ndogo inapotangazwa katika Gazeti la Serikali na kuwasilishwa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ametueleza vizuri sana Mheshimiwa Chenge vizuri ametuelimisha taratibu zinazotumika katika Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Lakini kwa nini sentensi hii iliwekwa ni kwa sababu ya ile concept hii ni delegated legislation. Kwa hiyo, Bunge kimsingi haiwezi tena likaja na kuanza kujadili zile sheria ndogo kwa sababu litakuwa limefuta ile concept ya delegated legislation na ndio hiyo changamoto pekee iliyopo na ndiyo maana akaeleza juu ya taratibu hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na nilitaka niseme, hata ukienda kwenye kanuni zetu za Bunge Toleo sasa la Januari 2016 ukiangalia ile Kanuni 80 mpaka ya 93 zinahusu utungaji wa sheria unaofanywa na Bunge, hakuna kanuni inayozungumzia Bunge litakavyofanya kazi dhidi ya sheria ndogo ambazo zimeshatungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu tungekuwa tunatumia huu mfumo wa kwanza aliutaja wa affirmative resolution procedure tungekuwa na kanuni hizo kwenye Bunge letu zitatuongoza tunapotunga sheria tunazoziita kubwa huu ni utaratibu, tukija tunaposhughulika na sheria ndogo huo ni utaratibu hatuna huo utaratibu ni kwa sababu tunatumia ile aina ya pili aliyoizungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme na nikumbushe na Mheshimiwa Chenge ni mahiri sana katika hili; katika mfumo sasa wa Common Law siyo wa Commonwealth Parliament, wa Common Law sheria ndogo ndogo kama zina matatizo nini utaratibu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu siku zote umekuwa kupitia kitu kinaitwa judicial review na hiyo inafanyika judicial review moja wapo ya misingi ya judicial review ni kama ile sheria iko ultra vires yaani inapingana au imejipa ukuu zaidi ya ile sheria mama ambacho Mwenyekiti alikuwa anakieleza hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, upo utaratibu katika mfumo wa sheria wa Common Law. Sasa nilitaka tu ku-share hilo na kuonyesha shida kidogo. Naomba dadika moja kuna kitu cha muhimu nimalizie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa yamezungumzwa mapungufu katika uandishi wa sheria. Tunayakiri haya kwamba yametokea mapungufu mara kadhaa katika uandishi wa sheria ni mojawapo ya changamoto ambazo Afisa Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekuwa nazo na ndiyo maana mwaka huu Mheshimiwa Rais akaamua kutoa maelekezo ya kuunda.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, na kuusuka upya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa hiyo zile changamoto zilizozunguzwa za uandishi za upungufu wa watu na kadhalika, hizo zitashughulikiwa na zinaendelea kushughulikiwa tunavyoongea, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia kwenye hoja iliyoko mezani. Mchango wangu nitajielekeza zaidi hasa katika kutoa ufafanuzi kwenye mojawapo ya masuala yaliyoibuka wakati wa mjadala. Nielezee zaidi position ya kisheria iko namna gani na hili ni suala la fidia kwa walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira uliotokea katika mgodi wa North Mara Gold Mine unaoendeshwa na Kampuni ya Acacia kule Nyamongo.

Mheshimiwa Spika, pendekezo lililotolewa ilikuwa ni kwamba fine ile ambayo imetozwa kampuni hii basi ingefaa fine hiyo igawanywe kwa wale waathirika wa uchafuzi wa mazingira, lakini basi kama hili haliwezekani, labda itafutwe namna yoyote ya kuwafidia hao walioathirika na uchafuzi wa mazingira uliosababishwa na huo Mgodi wa North Mara unaoendeshwa na Kampuni ya ACACIA.

Mheshimiwa Spika, katika hilo nataka kusema kwamba kuigawa ile fine iliyotozwa kwa waathirika wa mazingira kuna ugumu kidogo kwa sababu hakuna Sheria inayoweza kuruhusu kufanyika jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo lile suala la kuichukua ile fine iliyotozwa na NEMC halafu kuigawa kwa wale wananchi walioathirika hilo jambo lina ugumu kwa sababu hakuna Sheria inayoruhusu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu fidia kwa walioathrika na uchafuzi wa mazingira sheria ipo. Ni hii Sheria inayohusiana na ulinzi wa mazingira (Environmental Management Act) na napenda hapa nisome tu kwa haraka hiki kifungu kwa sababu ni kifungu cha 110(1)(3). Kifungu cha 110 cha hii Sheria ya Environmental Management Act tukianza na kifungu cha kwanza kinasema:

“No person shall discharge any hazardous substance, chemical oil or mixture containing oil in any waters or any segment of the environment”

Hicho ndiyo kinachoanza kuweka zuio na katazo la uchafuzi na kifungu cha 110(3) kinasema:

“Apart from the general punishment provided for under this Act, the person convicted of an offence under this section may be ordered by the court”

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakwenda kifungu kidogo cha 110(3)(b) kinasema:

“To pay the cost of third parties in the form of reparation, restoration, restitution or the compensation as may be determined by the court”.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika msimamo wa kisheria kuna uwezekano wa hawa watu walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira kulipwa ama reparation au compensation au kwa namna yoyote itakayowezekana, lakini ni lazima tuangalie kitu kimoja hapo kwamba hii amri inatolewa na Mahakama na kwa sababu hiyo ni lazima pawe pamefunguliwa kesi ya jinai na Mahakama baada ya kupata ile kesi na uthibitisho ukatolewa inaweza kutoa maelekezo ya kulipa fidia.

Mheshimiwa Spika, katika mazingira tuliyonayo tuna changamoto kidogo, kwa sababu ukienda kifungu cha 194(2) cha Sheria hii hii kinasema, mahali ambapo kosa limekuwa compounded kwa ajili ya yule aliyetenda kosa kutoa fine, basi kesi ya jinai au kesi nyingine yoyote ya kimahakama haiwezi kuendelea kwa sababu itakuwa ni kama umetoa adhabu mara mbili.

Mheshimiwa Spika, sasa lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba suala la fidia kwa watu walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira ni la muhimu kuangaliwa. Kwa hiyo pengine labda baada ya hatua hii ya kulipa fine labda inaweza ikaangaliwa pia hiyo hatua nyingine hapo baadaye ya kulipeleka shauri hilo Mahakamani ili Mahakama itumie mamlaka yake kutoa maelekezo ya kuwalipa fidia walioathrika.

Mheshimiwa Spika, naomba kuhitimisha na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MWENASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa muda na mimi niweze kuchangia hitimisho la hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati.

Mheshimia Spika, katika mchango wangu nitajielekeza moja kwa moja kwa hoja aliyoitoa Mheshimiwa Hawa Ghasia katika mchango wake ambapo alizungumza kwamba katika mazingira ya sasa hivi inaonekana kama hakuna leseni mpya ambazo Mheshimiwa Waziri amezitoa katika sekta hii ya gesi. Pengine sababu mojawapo ya kutokuwa na leseni mpya zinatolewa ni kwa sababu hii mikataba iliyopo ya utafutaji na uchimbaji wa gesi iko kwa AG; na akaniomba kama ninaweza kwa sababu nipo, nizungumzie suala hili ili kuweza kumuepusha Mheshimiwa Waziri na kuondolewa shilingi yake; nami napenda nilizungumzie hili kwa kifupi.

Mheshimiwa Spika, kama unafahamu uliunda Kamati ya kuangalia sekta ndogo ya gesi pamoja na uvuvi. Kamati ile ilikuja na taarifa yake na ilikuja pia na mapendekezo yaliyokuwa katika taarifa ile. Mojawapo ya mapendekezo kama mnavyofahamu vizuri kabisa ilikuwa kwamba iko haja ya kurejea hii mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa gesi (production sharing agreements), na kazi hiyo ikapewa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kwa hiyo ni kweli kabisa kwamba mikataba hiyo anaishughulikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nichukue nafasi hii kueleza tu tumefika wapi katika zoezi hilo. Tulianza kazi na zoezi la kuipitia hiyo mikataba yote, tuliunda timu ilipata wataalam kutoka Wizara mbalimbali na sekta mbalimbali za Serikali; na tukaanza hiyo kazi. Ilitulazimu tuanze kwanza kwa kuwajengea uwazo hii timu ili iweze kufahamu ni kitu gani inakifanyia review. Hilo zoezi lilikamilika, baada ya zoezi hilo lilifuata sasa zoezi la kuipitia mikataba yenyewe; na timu hii imekaa kwa karibu kipindi cha miezi miwili na imefanya kazi ya kupitia ile mikata yote kumi na moja ambayo inahusika na utafiti na uchimbaji wa gesi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya zoezi hilo tuligundua kwamba kuna kitu ambacho ni muhimu sana kukiangalia, kwa kiingereza wanaita economic and financial modeling. Kwa sababu hapo ndipo siri nzima ilipolala, kama mnapoteza au kama mnafaidika au kama mnapata iko kwenye economic and financial modeling. Kwa hiyo tukaweka tena awamu nyingine ili timu hii ikae na ikafanya kazi hiyo kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja. Ninavyozungumza timu hiyo imemaliza hiyo kazi ya kuangalia economic and financial modeling. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, walichokifanya katika zoezi hili ilikuwa ni kuangalia financial na economic modeling gani ilitumika katika hizi PSAs.

Kwa hiyo, baada ya hiyo kazi wakagundua kwamba ni lazima turudi tena tuangalie sisi kama nchi tunapendekeza economic na financial modeling ipi. Sasa katika hilo zoezi la tatu ambalo nimelitaja, timu hii inakutana tena kuanzia tarehe 6 Juni, na itamaliza kazi yake tarehe 25 Juni.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwa ufupi kwa sababu mambo mengi bado yapo kwenye taarifa hii, zoezi hili limetufanya tuelewe matatizo mengi yaliyo kwenye mikataba hii na mapungufu ambayo tunahitaji tuyafanyie kazi. Pia, kikubwa kabisa tutakachokipata kwenye zoezi hili litatufahamisha yaani lita-inform tunapoanza majadiliano ya LNG, kwa sababu hii mikataba mingi ilisukwa kwa namna ambayo baadae ingekuja ku-influence chochote ambacho tungekubaliana kwenye LNG.

Mheshimiwa Spika, ni hayo tu niliyokuwa napenda kushirikisha na kwa ujumla ninaunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo Zilizowasilishwa katika Mkutano wa Pili wa Bunge
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia kidogo katika taarifa ya Kamati ya Sheria Ndogo.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla kama ambavyo imekuwa ikitokea kila mwaka tunazipokea changamoto mbalimbali ambazo zimeainishwa na Kamati na kwa kweli tunawashukuru na kuwapongeza sana. Kama ambavyo wengi wa Waheshimiwa Wabunge wamezungumza hapa ndani, wanafanya kazi kubwa sana ya kufanya uchambuzi na hasa kwenda kwenye maudhui. Kwa sababu, sisi wakati mwingine tunaangalia tu yale masuala ya kiufundi ya kisheria, lakini masuala ya maudhui kwa kweli, Waheshimiwa Wabunge na Kamati wanaweza wakatusaidia sana katika eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kila wakati tunapokea mapendekezo hayo na maono hayo tunayachukua na tunayafanyia kazi kila mwaka. Lakini pengine wengi watakubaliana nasi kwamba kadri tunavyokwenda hizi changamoto zinazidi kupungua, ndio kusema kwamba, tunazifanyia kazi changamoto ambazo zinakuwa zimekwishaelezwa kila wakati uchambuzi unapofanyika.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa ufupi tu zimeelezwa bado zile zile changamoto za sheria ndogo kupingana na sheria mama, kuna masuala ya kuweka tozo katika Kanuni au katika sheria ndogo, kuna masuala ya kutoshirikishwa wadau wakati wa utengenezaji wa sheria ndogo na pengine katika mazingira baadhi ya sheria hizi zinaonekana zinabeba labda maslahi binafsi.

Mheshimiwa Spika, sisi kama walivyosema Wabunge wengine tunaendelea kusisitiza kwamba misingi ya utengenezaji wa sheria ndogo ipo wazi na imeelezwa vizuri sana na tumeendelea kuieleza. Tunaomba kwamba misingi hiyo iendelee kufuatwa wakati wa utengenezaji wa hizi sheria ndogo na wakati wowote misingi hii isiachwe.

Mheshimiwa Spika, lakini kuna jambo nilipenda niliseme hapa, sheria nyingi zinazolalamikiwa ni sheria ndogo zilizotungwa na Halmashauri zetu. Sasa katika Halmashauri zetu Waheshimiwa Madiwani ndio wanahusika, lakini pia Waheshimiwa Wabunge pia ni Wajumbe katika Mabaraza hayo. Nilikuwa napenda kutoa wito kwamba ningewaomba sana Waheshimiwa Wabunge, wachukue muda wa kutosha waangalie hizo sheria zinazopendekezwa katika Halmashauri hizo na kuona kama baadhi ya changamoto hizi ambazo zinalalamikiwa zipo na basi zifanyiwe kazi katika ngazi hiyo. Tukifanya hivyo na Wabunge wote wakitimiza wajibu wao tutakuwa tumepunguza sana changamoto nyingi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu changamoto za kiuandishi tumekuwa tunaendelea kuzungumza kwamba tuna zoezi na ambalo ni endelevu la kuwapatia uwezo wanasheria wetu waliopo maeneo mbalimbali kwenye Halmashauri, kwenye Taasisi, kwenye Wizara, uwezo wa kuweza kufanya hiyo kazi ya uandishi wa sheria katika weledi unaotakiwa. Hata hivyo, kama ambavyo tumekiri na imeelezwa na watu wengi taaluma ya uandishi wa sheria sio jambo rahisi. Kwa hiyo, pengine hutegemei sana kwamba, kwa semina ya wiki moja utaweza kuwafanya watu wawe na umahiri kama alionao Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Mheshimiwa Spika, lakini vinginevyo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ipo tayari wakati wote na tunatoa msaada wakati wowote tunapotakiwa kuweza kuboresha hizi sheria ndogo.

Mheshimiwa Spika, kwa mchango huo, naomba kuwasilisha na nakushukuru sana kwa nafasi. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi kwa ajili ya
kuanza kuhitimisha hoja iliyoko mbele yetu kuhusu Muswada Namba Mbili wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaelekeza hoja zangu kwa hoja zilizotolewa na wachangiaji kadhaa hapa nikianza na maoni ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani na hasa wasiwasi aliouonesha kuhusiana na suala la mamlaka ya Rais ya kutunga sheria na kwamba angependa kuona kwamba kila sheria itungwe na Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipenda kusema kwamba masuala ya sheria kama wanavyofahamu wanasheria mbalimbali yanaongozwa pia na kitu kinaitwa nadharia ya sheria (legal theory). Legal theory unaweza ukaisema ni kama manual unayohitaji unapohitaji kutumia kitu kama gari au mashine au kitu chochote. Legal theory,inakuongoza. Katika masuala ya utungaji washeria, nadharia ya sheria au legal theory inatuambia ziko namna nne zinazosababisha kutengeneza sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namna ya kwanza ni kwa kutumia Bunge na hii ndiyo wengi tunaifahamu na tumeizoea, lakini pia iko namna ya pili utengenezaji wa sheria kwa codification, kwa bahati mbaya sina neno kwa haraka la Kiswahili linaloweza kutafsiri hapa kwa haraka. Nikueleze tu watu wengi hawafahamu kwamba katika sheria zetu tuna sheria zinaitwa codes hazikutungwa na Bunge kuanzia mwanzo ingawa baadae Bunge lilifanya kazi ya kufanya marekebisho au kuweka nyongeza. Mojawapo ikiwa ni Penal Code, wengi hatujui kwamba haikutokana na Sheria ya Bunge,Civil Procedure Code, haikutokana na sheria ya Bunge, hizi zilitengenezwa kwa mfumo wa codification.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aina ya tatu ni sheria zinazotokana na maamuzi ya Mahakama (court decisions) wanasheria wanafahamu by way of precedence. Aina ya nne ni kutengeneza sheria inaitwa Legislation by Rex yaani mtawala mwenye mamlaka anakuwa anapewa nafasi pia ya kutengeneza sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sheria zetu ukienda katika Katiba, Ibara ile ya 36(1) inagusia mamlaka ya Rais ya kutengeneza sheria, lakini pia tuna sheria inayoitwa Presidential Affairs Act ambayo pia inampa nguvu Mheshimiwa Rais kuweza kutengeneza sheria na anaweza akatoa decrees, orders na proclamations. Hizi sheria zinazozungumzwa ambazo Waheshimiwa Wabunge walikuwa wakichangia zilitengenezwa kwa mtindo wa orders. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nilitaka nikuhakikishie kwamba hapa hakuna Katiba iliyovunjwa, hakuna utaratibu uliovunjwa, Mheshimiwa Rais ana mamlaka haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nijielekeze kwa ufupi kwenye hoja zilizotolewa na Mheshimiwa Salome. Kuna hoja tatu ambazo zinahitaji kuzieleza kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwanza ni suala la viongozi wa TLS wasiwe wanasiasa. Wachangiaji hawaelezi kwamba katika zile qualifications kuna qualifications zaidi ya wanasiasa, wasiwe watumishi na kadhalika na nyingine hazikuzungumziwa, imezungumziwa tu ya wasiwe wanasiasa, lakini hii ni sheria ya aina gani? hii ni sheria inayozuia conflict of interest na tuna sheria nyingi sana katika nchi hii zinazozuia conflict of interest na ni sheria za kawaida. Sasa hata ukienda kwenye kanuni ambazo Mheshimiwa Jaji Mkuu alizozitoa kwa ajili ya Mawakili zinaitwa Professional Ethics and Etiquette Regulations amezungumzia pia kuzuia conflict of interest. Wakili asiingie katika jambo ambalo ana conflict of interest, lakini ziko sehemu nyingi sana na Waheshimiwa Wabunge wanafahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja kwamba Administrator General asiteuliwe na Rais na ni vyema ateuliwe na Waziri. Ni maoni lakini nataka kurudia tu kwamba Mawaziri wote kama alivyozungumza Mheshimiwa Jenista Mhagama wanateuliwa na Rais na wanatekeleza madaraka yao kwa niaba ya Rais. Sasa Rais anawateua Mawaziri na Waziri ndiyo alikuwa anamteua Administrator General, hapa sasa inataka kusemwa Rais mwenyewe amteue Administrator General. Hata akiteuliwa na Waziri bado indirectly ameteuliwa na Rais kwa sababu Waziri anatekeleza madaraka ya Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kuna suala la mali inayohusishwa na jinai. Katika muswada huu imeeleza waziwazi kwamba suala la uuzaji wa mali hizi linahusisha mali ambazo ama zinaweza kutoroshwa au zinaweza kuharibika. Kwa hiyo, hizo ndizo zitahusika na uuzaji huo. Lakini pia katika muswada huu huu kumewekwa safe guard kwamba baada ya uuzaji huo fedha zitawekwa katika akaunti maalum na kwamba kitakachotokea baadae kitategemea na maelekezo ya Mahakama au itakavyokuwa vinginevyo.

Kwa hiyo, ile mali kimsingi haipotei kwa sababu fedha zitawekwa kwenye akaunti maalum lakini ndiyo utaratibu pia hata kwenye Mahakama zetu kuna mambo mengi tu yanahusisha fedha na fedha zile inaamriwa ziwekwe kwenye akaunti maalum ya Mahakama na bada ya hapo kitakachotokea itaamriwa ama arudishiwe mlalamikiwa au zitataifishwa moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba nichukue fursa hii kukushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuhitimisha hoja kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.3 wa mwaka 2018. Aidha, nakupongeza kwa namna ambavyo umeweza kuongoza mjadala wa Muswada huu vizuri. Hoja hii imechangiwa na jumla ya Waheshimiwa Wabunge nane ambao wamechangia kwa kuzungumza ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri. Kwa hakika tumepokea maoni mazuri ambayo yamelenga kuboresha siyo Muswada tu, bali hata masharti mengine ya sheria mama na namna bora ya kutekeleza sheria husika.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wa kuchangia Muswada huu ni ushahidi kwamba Bunge hili linatambua umuhimu wa marekebisho ya sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo na kwa hakika jambo hilo ni endelevu. Serikali itaendelea kuleta Bungeni marekebisho ya aina hii kila inapoonekana kuna umuhimu huo kwa lengo la kuboresha masharti ya sheria zetu na kuzifanya ziendane na wakati.

Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Omary Mchengerwa, Mbunge ambaye alisoma Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa kutoa maelezo mazuri ya ufafanuzi juu ya maudhui ya Muswada pamoja na mapendekezo ya marekebisho kwenye Muswada. Naamini maelezo yake ambayo yaliainisha maoni ya wadau waliofika kwenye Kamati hiyo, yamewasaidia Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwa ujumla kuelewa vyema maudhui ya Muswada huu. Maoni na ushauri wa Kamati vimezingatiwa kwa kiasi kikubwa na vimeuboresha Muswada huu kama inavyoonekana kwenye Jedwali la Marekebisho ambalo Waheshimiwa Wabunge waligawiwa ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, namshukuru pia, Mheshimiwa Ally Saleh, ambaye alitoa maoni kwa niaba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria kwa hotuba na maoni yake kuhusu Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwashukuru pia Mawaziri na Manaibu Waziri ambao pia wamechangia katika Muswada huu. Mheshimiwa Profesa Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria; Mheshimiwa Dkt. Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango; Mheshimiwa Angeline Mabula, Naibu Waziri wa Ardhi; na Mheshimiwa Dkt. Ashatu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, naomba sasa nijibu hoja kadhaa au kutoa ufafanuzi kwa hoja zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge. Kama nilivyosema, Wabunge nane walichangia.

Mheshimiwa Spika, kabla ya hayo, nami niseme kidogo juu ya sintofahamu iliyotokea kwenye Ibara ya 11, 12 na 13 za Muswada. Kama nilivyoeleza katika hotuba yangu hapo mwanzoni, Serikali iliondoa Ibara hizo tatu. Ibara hizo zinahusu zile mobile courts, special courts na small claims na tulifuata maelekezo ya Kanuni ya 88(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwa tumefuata utaratibu huo, hatukutegemea kwamba suala hili lingeingia tena kwenye hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na hata kwenye hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani. Basi, tutaendelea na haya mengine yaliyobaki.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na mchango kutoka kwa Mheshimiwa Gekul aliyesema kwamba marekebisho katika Ibara ya 31 ya Muswada huu yanalenga kuleta vikwazo na ni vyema kuwa na nafasi ya kukosoa takwimu za Serikali. Nataka tu kumfahamisha Mheshimiwa Gekul kwamba, nadhani alikuwa hajaangalia yale marekebisho katika Jedwali la Marekebisho yaliyoletwa na Serikali, Ibara (g) kwa sababu imefanya marekebisho katika sehemu hiyo.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa pia na maoni kutoka kwa Mheshimiwa Mtolea, aliyezungumza kwamba katika haya masuala ya Mabaraza ya Ardhi yanahitajika mabadiliko makubwa katika sheria kuliko haya ambayo yanaonekana ni madogo madogo na kwamba ziko changamoto nyingi tungezifanyia kazi zote kwa pamoja. Nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba changamoto ni nyingi katika eneo hili la utatuzi wa migogoro inayohusu ardhi, lakini zinafanyiwa kazi. Hatua hizo ziko za muda mfupi na za muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya mambo Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria wakati fulani alipata nafasi ya kuyazungumza, huwezi ukayatatua kwa haraka haraka kwa sababu kuna masuala huko ya imani, ya kimila, ya mapokeo na kadhalika ambayo yanahitaji mjadala mrefu na mpana wa Kitaifa. Huwezi ukasema usubiri mpaka hayo yote uwe umeyajadili na kufikia muafaka. Unaweza ukachukua hatua kwa yale ambayo unaweza kuyachukulia hatua wakati huo. Kwa hiyo, mabadiliko haya ni kati ya mambo ambayo yameonekana kwamba yanaweza yakafanyiwa kazi kwa muda huu na hayo mengine yataendelea kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Halima alitoa maoni yake kwamba anafikiri lengo la mabadiliko ya Sheria ya Takwimu ni moja tu, ni kudhibiti. Napenda kusema kwamba, kwa kweli karibu nchi zote na hasa zilizoendelea zina sheria na ni sheria madhubuti za kusimamia takwimu. Kwa kweli, kwa nchi zilizoendelea nafikiri sheria zao pengine ni kali zaidi kuliko hata sheria tulizonazo kwa sababu, wanajua takwimu ni kila kitu. Takwimu ni uchumi, ni siasa, ni mendeleo, ni amani, ni maridhiano na mshikamano. Kwa hiyo, hawafanyi mchezo na takwimu. Ndiyo maana hata katika baadhi ya vyuo vikuu wale wanaoandika zile tasnifu za uzamivu (Ph.D) kama ina takwimu za aina fulani Serikali inaweza ikaamua kwamba zisitolewe kwa sababu ya maslahi mapana ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni kweli kwa upande mmoja kwamba lengo la sheria hii ni kuweka udhibiti lakini ni udhibiti chanya ili kuhakikisha kwamba wote tunakwenda pamoja na hakuna mtu anayetumia nafasi ya takwimu kupotosha, kueleza kitu kisicho cha ukweli, kueleza kitu au kutoa kitu ambacho hakijafanywa kwa njia za kisayansi, kwa njia zinazokubalika kitaalamu na kitaaluma na kwa hiyo, anatupotosha. Tumeshaambiwa, sehemu nyingi sana katika nchi mbalimbali zimepata matatizo kwa sababu ya takwimu. Hata yale mauaji ya kimbari ya Rwanda kulikuwa na masuala ya takwimu humo yaliyohusika na yalichangia.

Mheshimiwa Spika, hitimisho. Baada ya maelezo haya, naomba kukushukuru tena kwa kunipatia fursa hii ya kutoa maelezo ya kuhitimisha hoja iliyo mbele ya Bunge lako Tukufu. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge wote waunge mkono marekebisho kama yalivyopendekezwa katika Muswada na Jedwali la Marekebisho.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuanza kuhitimisha hoja iliyoko mezani. Katika uchangiaji mbalimbali uliofanyika yameibuka masuala na hofu kwamba Muswada huu na hasa katika vifungu vyake fulani unaweza kuwa unakinzana na Katiba. Nafikiri ingefaa nikajielekeza tu zaidi katika yale maeneo ambayo kuna wasi wasi kwamba kuna ukinzani na Katiba.

Mheshimiwa Spika, na nitazungumza mambo mawili jambo la kwanza ni hili takwa linalowekwa katika sheria kwa anayetaka kusajili chama cha siasa kwamba wazazi wake wote wawili wawe raia wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, na katika jambo hilo kumeibuka hisia kwamba kunaweza kuwa na ubaguzi katika hilo, kuna suala la kuwaganya raia katika matabaka ambayo ni muendelezo wa ubaguzi, kwamba kifungu hicho kinaweza kuwa kinavunja Ibara ya 39 ibara ndogo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ibara ya 47, na kwamba kwa nini kifungu hiki kinaweka viwango vya juu zaidi kwa nafasi ya yule anayetaka kuandikisha chama ukilinganisha na nafasi ya mtu anayekuwa Rais.

Mheshimiwa Spika, nitajielekeza katika msuala hayo manne, tukianza na la kwanza suala la ubaguzi, limeelezwa vizuri sana katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tunapokuwa tunazungumza niombe niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge kila wakati tukizungumza juu ya ubaguzi tuende Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo suala hilo limeelezwa vizuri sana. Lakini la msingi katika ibara hiyo ni maana ya neno ubaguzi na jambo gani linaingia katika wigo wa ubaguzi na jambo gani haliingii katika wigo wa ubaguzi hilo ni muhimu sana.

Mheshimiwa Spika, sasa ukisoma ibara ndogo ya (5) katika ile Ibara ya 13 imeeleza vizuri sana suala la ubaguzi na imeeleza ni kitu gani hakitengenezi ubaguzi. Ukiisoma hiyo ibara ndogo ya (5) mambo ambayo hayatengenezi ubaguzi ni pale ambapo kumewekwa masharti au sifa za lazima za jambo fulani. Kwa mfano ukisema kwamba mwenye haki ya kupiga kura ni mtu mwenye miaka 18 hizo ni sifa za lazima, mtu anayeweza kupewa labda leseni ya kuendesha gari au awe na miaka 18 hizo ni sifa za lazima panapowekwa sifa au masharti ya lazima kwa kitu fulani huo sio ubaguzi hiyo ibara ndogo imeeleza vizuri kabisa.

Mheshimiwa Spika, au panapochukuliwa hatua za makusudi ili kurekebisha matatizo mahususi katika jamiii hizo hatua zikichukuliwa siyo ubaguzi, vingenevyo kama tukisema hivyo ukieda katika ibara nyingi tu za Katiba utaona ubaguzi Ibara ya 39(1) inayozungumzia sifa za kuwa Rais imeeleza mambo mengi awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa maana yake inabagua ambao siyo raia wa Tanzania wa kuzaliwa na imeeleza mambo mengi sana, awe na umri wa miaka 40 maana yake ambaye hajafikisha miaka 40 ha- qualify awe aliyependekezwa na chama cha siasa anazo sifa za kumuwezesha kuwa Mbunge. Na ukienda kwenye sifa za kuwa Mbunge na kwenyewe zipo sifa nyingi hajawahi kutiwa hatiani yote hiyo ni masharti yanayoweka sifa na hizi ni sifa za lazima na hii imeelezwa kwenye hiyo Ibara ya 13 ibara ndogo ya tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, na hata ukienda kwenye ile bill of white kuanzia Ibara ya 12 mpaka ya 29 utaona baadhi ya ibara zinasema kila mtu ana haki, lakini baadhi ya ibara zinasema kila raia. Kwa hiyo, sasa hapo tena inabagua hazingumzii kila mtu inazungumzia pia raia na hizo ziko wazi Ibara ya 17, Ibara ya 22, Ibara ya 28, Ibara ya 29 hayo ni masharti ya lazima kwa ajili ya jambo fulani na hayo masharti yanapowekwa inakuwa siyo ubaguzi. Kwa hiyo, kinachokuja kuwekwa sasa kwa huyu atakayekuja kuandikisha chama cha siasa ni masharti ya lazima na inapokuwa ni masharti ya lazima siyo ubaguzi. (Makofi)

Mheshimiwa spika, otherwise kumezungumzwa jambo la matabaka ya raia sheria hii haiweki matabaka ya raia kwa sababu sheria yenyewe ya uraia imezungumza aina tatu za uraia, kuna uraia wa kuzaliwa, kuna uraia wa kurithi, kuna uraia wa kuandikishwa. Sasa yako mambo ambayo ni lazima tutaje kwamba katika jambo hili tunataka aina fulani ya raia, kwa mfano kwenye nafasi ya uraisi tumesema tunataka aina ya raia wa kuzaliwa, lakini kwenye nafasi ya Mbunge tumesema tu raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuwa katika zile aina tatu za uraia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, halafu kuna mapendekezo kwamba au kulikuwa na maoni kwamba unaposema wazazi wote wawe raia yanakinzana na ibara ya 39(1) ibara ya 47(4) si kweli hizi ibara zimeweka masharti ya lazima au qualification za lazima kwa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais na tukisoma hiyo sehemu ya Katiba iko wazi inahusu nafasi ya Rais, inahusu nafasi ya Makamu wa Rais. Kwa hiyo, ukisema kwamba kwa yule atakayekuja kuandikisha chama cha siasa tunapoweka masharti hayo yanakinzanana haya siyo sahihi kwa sababu haya masharti yanahusu tu nafasi ya Rais na hayahusu jambo jingine lolote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda nizungumzie hili suala la pili ambalo pia kumekuwa na wasiwasi kwamba msajili anapewa mamlaka yaku-suspend shughuli za chama nadhani ni kusitisha hivi au kusimamisha shuguhuli za chama na kwamba kufanya hivyo ni kuvunja Katiba. Naomba nikuthibitishie kwamba jambo hili halivunji Katiba hata kidogo. Kulitolewa hoja hapa nilisikia kwamba masharti mojawapo yaliwekwa ili chama kiweze kuwa suspended hayamo kwenye Ibara ya 20(2) ambayo imeorodheshwa kwamba mambo haya yakifanyika chama kinaweza kuwa suspended au kuwa deregistered.

Mheshimiwa Spika, tusisahau kwamba Katiba lazima isomwe kwa ujumla wake iko Ibara ya 26(1) inayozungumzia ulazima wa kila mtu na sasa hapa mtu anaweza kusema ni mtu ukisoma ile version ya kiingereza inasema every person na katika kiingereza a person could be a legal person or natural person kwa hiyo, kila mtu inamaanisha ama taasisi au mtu binafsi na kwamba ama taasisi au mtu binafsi anawajibu wa ku-observe sheria zote za nchi. Ana wajibu wa kuangalia kwamba sheria zote za nchi zinasimamiwa na kutelezwa ipasavyo na ninamshukuru sana Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria amelieleza vizuri sana hilo kwamba baadhi ya mambo pengine hayamo kwenye Katiba baadhi ya mambo ambayo yanakatazwa hayamo kwenye Katiba lakini yako kwenye sheria nyingine ikiwemo sheria ya kanuni ya makosa ya jinai na kwa hiyo ni sahihi kuiweka katika sheria hii.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza).
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2019. Katika mjadala huu jumla ya Waheshimiwa Wabunge 10 wamechangia kwa kuzungumza na hatukupata michango wka maandishi.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri. Tumepokea maoni mazuri ambayo yamelenga kuboresha si tu Muswada, bali hata masharti mengine ya Sheria mama husika na kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni ushahidi kwamba suala la marekebisho ya sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo linamhusu kila mmoja wetu. Katika Bunge hili, hili ni jambo endelevu na ndiyo maana mara kwa mara Serikali inakuja na Miswada ya aina hii kwa ajili ya kuboresha sheria zetu hasa tunapoona kwamba utekelezaji umetupatia changamoto kidogo.

Mheshimiwa Spika, kuna hoja mbalimbali zilizotolewa, nawashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri wote ambao wamechangia katika kuhitimisha hoja hii na wamezijibu baadhi ya hoja hizo na nafikiri sitakuwa na haja tena ya kurudia hizo hoja ambazo wamesaidia kueleza kwa ufasaha kabisa.

Mheshimiwa Spika, nafikiri liko jambo moja ambalo pengine ingekuwa ni vizuri nikalitolea ufafanuzi na hili ni suala la import permit kwa wale wanaotaka kuingiza madini kutoka nje ya Tanzania na tumeyasikia maoni ya Waheshimiwa Wabunge, nafikiri hata wakati wa mijadala kwenye Kamati jambo hili liliibuka sana na hofu nyingi zilioneshwa kwamba kwa mfano, majirani zetu hawana masharti kama haya tubadilishe masharti isiwe kwamba mtu anapewa permit labda anapokuwa anaingia au kabla ya kuingia, lakini turahisishe utaratibu na tuitoe permit hii kwenye maeneo watakapokuwa wanauzia yaani kwenye masoko.

Mheshimiwa Spika, sasa napenda kueleza haya machache yafuatayo: Kwanza hili suala la import permit kwa madini siyo jipya, zipo import permit ambazo tayari zinatolewa na Wizara ya Madini hasa kwa madini yanayotoka nje kupitia bandarini yanayohitajika kwa ajili ya viwanda vyetu. Hawa wote wanaoingiza madini haya wanapata import permit inayowawezesha kuingiza madini haya. Kwa hiyo kwa kweli Kisheria na kiutaratibu siyo jambo jipya, tunachotaka kufanya sasa, tuliingize kwenye Sheria Mama.

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini tuwe na import permit? Import permit ni kama jicho linalosaidia kuangalia madini yote yanayoingia na tukiiondoa hii import permit kwanza tutaingiza mgongano na Sheria iliyopo kwa sasa hivi kwa sababu tuna kifungu cha tano cha Sheria ya Madini (Mining Act) kinachozungumza kwamba madini yote katika nchi hii popote yalipo ardhini, juu ya ardhi na kadhalika ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huu huwa ni msingi unaowekwa katika Sheria zote za Madini za nchi mbalimbali. Ukienda kusoma Sheria yoyote ya nchi yoyote itasema, madini yale yote ni mali ya Serikali ile au ni mali ya nchi ile na sasa wanaruhusu mtu mmoja mmoja aweze kuyamiliki hayo kupitia utaratibu wa kisheria kupitia leseni. Kwa hiyo tukiodoa import permit tutaanza kuwa na mgogoro na kifungu hicho.

Mheshimiwa Spika, pia kuna kifungu kinachosema kwamba, mtu hataruhusiwa kuchimba au kufanya jambo lolote kuhusiana na madini, hiki ni kifungu cha sita bila kuwa na leseni au kitu chochote kinachomruhusu kufanya namna hiyo.

Mheshimiwa Spika, zaidi liko tatizo kwenye kifungu cha 18 ambacho kinafanya ni kosa kwa mtu kukutwa na madini ya namna hii vinginevyo awe ama ana leseni ya uchimbaji ile primary mining license au mining license au special mining license au Broker’s license au Dealer’s license na sisi tukasema huyu anayeyaleta haya madini nchini yeye tunam-cover namna gani? Ndiyo tukasema afadhali tuwe na import permit kwa sababu ile import permit itampa ruhusa ya kuwa na haya madini na popote pale atakapokutwa nayo atakuwa ana haki ya kuwa nayo kwa mujibu wa hiyo import permit.

Mheshimiwa Spika, pia tukiiondoa kabisa tutapata shida na baadhi ya madini. Tunayo madini kama almasi ambayo yana masharti na masharti hatukuyatengeneza wenyewe, yako katika ngazi ya Kimataifa, yanatokana na mambo ya Kimberly process. Kwa mfano, kuna mambo ya blood diamond na kwa hiyo kuna masharti ambayo yamewekwa, mtu akiingiza almasi lazima tujiridhishe kwamba almasi ile haijatoka tunasema kwenye conflict places na imepitia ule utaratibu uliowekwa Kimataifa. Vile vile kuna madini sijui yanaitwaje kwa Kiswahili (Radioactive minerals) ambayo pia ni lazima tuyawekee udhibiti wa namna fulani. Sasa tusipokuwa na hii import permit madini kama haya yanayosema almasi, radioactive minerals pengine na madini mengine ya aina mbalimbali tutakuwa tumeyapa nafasi ya kuingia kwa kweli bila kujiridhisha kwamba yamefuata utaratibu. Kama nilivyosema kwa sehemu kubwa lengo la import permit ni kumlinda huyu anaye-import haya madini, kwa sababu hataweza kusema kwamba amevunja sharia, atakuwa yuko-covered vizuri sana na Sheria.

Mheshimiwa Spika, katika majadiliano kwa mfano, wakati wa Kamati kuna baadhi ya Wabunge walisema, sasa mtu huyu akija na haya madini akayauza akapata fedha zake labda Dola 200,000 anaondoka nazo namna gani? Ni wazi ilielezwa na Waziri wa Fedha kwamba iko Sheria inayomtaka tu afanye declaration anapofika mpakani kwamba ana fedha hizi ametoka nazo. Hata hivyo, anaweza kuulizwa zaidi kwamba ulipoingia hukuwa na hizi fedha umezipata wapi? Hivyo, import permit itamsaidia, atasema nilikuja na madini na hii ni import permit niliyoingia nayo, atakapouza pale atapata receipt atakapolipa zile royalties na zile charges zingine, atakuwa na receipt na hii itamsaidia zaidi, itamfanya mazingira yake yawe rahisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, kikubwa hapa ni kuhusu utaratibu na napenda kusema kwamba katika majadiliano haya tumezungumza sana kuhusu utaratibu na naomba nikuhakikishie tena na Wabunge wote na naomba waliamini hili, kwamba tumeurekebisha na kuufanya rahisi sana. Katika jedwali letu la marekebisho ukienda kile kifungu cha 86A(2) katika ile Ibara ya 26(b) ya jedwali la marekebisho tumesema:

“(2) A person importing minerals shall make a declaration in a prescribed form indicating the type and quantity of minerals intended to be imported and the purpose of importation.”

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo atatuambia, anajaza tu form halafu anatuambia ni madini gani, ni kiasi gani na ameleta kwa kusudi gani; kuyauza, ku-process au ni transit, au lengo lingine lolote. Halafu kinachofuata kinasema:

“(3) Upon making a declaration under subsectin (2), the Commission shall” hatusemi “the commission may” tumesema “the Commission shall, without prejudice subsection (5) and section 86B and 86C issue to the declarant a Minerals Import Permit prior to importation or at the entry point.”

Mheshimiwa Spika, hii maana yake ni kwamba, anaweza kujaza hii form kabla kabisa hajayaleta madini au anaweza kujaza hii form wakati anaingia kwenye nchi. Kwa hiyo hii ndiyo requirement peke yake ya msingi, declaration peke yake, akishaweka declaration, anapewa permit.

Mheshimiwa Spika, basi naomba ninapohitimisha hoja yangu hii niwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri, nawashukuru Kamati na wote waliohudhuria Kamati. Nawashukuru pia wadau kwa maoni mbalimbali waliyoyatoa ambayo tumeyazingatia yametusaidia katika kuboresha Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba tena kutoa hoja.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nizungumzie suala moja tu, nalo ni suala la ushiriki wa Zanzibar katika Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kama lilivyoelezwa na Mheshimiwa Saada Mkuya. Ili kulizungumzia hili ni vema kila mara kurudi kwenye Katiba na kuona inatuambia nini na baada ya hapo tulizungumze suala lenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(d) lina mamlaka ya kutunga Sheria kwa mambo yote yayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo maana yake inahusu Tanzania Bara na inahusu pia Tanzania Zanzibar. Kama tunavyofahamu pia kwamba Bunge hili linaweza likatunga Sheria kwa mambo mengine yote yanayohusu Tanzania Bara peke yake kwa mujibu wa Ibara ya (64)(1).

Mheshimiwa Mwenyekiti, yanapokuja masuala ya kutunga Sheria ambayo pia itatumika Zanzibar, Katiba imeweka masharti hayo na wameeleza vizuri katika Katiba, jambo la kwanza ni lazima jambo ambalo linatungiwa Sheria liwe linahusu mambo ya Muungano ukiangalia Ibara ya (64)(4)(c) na pili Sheria itamke yaani Sheria hiyo inayotungwa itamke kwamba itatumika pia kwa upande wa Zanzibar. Hii imeelezwa waziwazi kabisa katika Ibara ya 64(4)(b).

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa linapokuja suala la uhitaji na ulazima wa mashauriano kati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, utaratibu ukoje. Utaratibu wa mashauriano kati ya Serikali hizi mbili haujawekwa kwenye Katiba au Sheria yoyote, lakini uko kwenye utamaduni wa kiutendaji wa hizi Serikali mbili. Kwa hiyo utaratibu wa namna ya kushauriana hauko kwenye Katiba hauko kwenye Sheria, lakini umejengwa katika utamaduni wa utendaji wa hizi Serikali mbili. Sasa katika hili ni vema kueleza kwamba kumekuwa na tamaduni tofauti, kumekuwa na utamaduni uliotumika kabla ya Novemba, 2018 yaani mwaka jana na utaratibu ambao umeanza kutumika kuanzia mwezi Novemba, 2018 yaani mwaka jana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya Novemba utaratibu uliotumika ilikuwa ni katika hatua za awali za matayarisho wataalam wa kutoka upande wa Zanzibar waliitwa na walishirikishwa katika hatua mbalimbali za kuutengeneza Muswada wa Sheria na ushiriki wao ulihesabiwa kuwa wamewakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Novemba, 2018, Serikali hizi mbili zimekubaliana, lakini bado kama nilivyosema haijaandikwa katika Sheria yoyote, ila zimekubaliana kwamba sasa itakuwa ni lazima Katibu Mkuu Kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amwandikie Katibu Mkuu Kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili apate maelezo yake kwamba Muswada huo au jambo hilo limejadiliwa na limepitia katika ngazi mbalimbali zinazohitajika kujadili au kuhusishwa katika jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Muswada huo tunaozungumza uliandaliwa wakati tunatumia bado mfumo wa zamani kwa sababu ilikuwa ni around mwezi Mei, 2018. Kwa hiyo katika utaratibu huo wataalam mbalimbali kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walishirikishwa katika hatua mbalimbali za kuandaa Muswada huu. Hivyo basi, umekuja kwa sababu ulifuata huo utaratibu wa zamani, lakini utaratibu aliokuwa anauzungumzia Mheshimiwa Saada huo umeanza kutumika mwezi Novemba, 2018, lakini bado nieleze kwamba hizi ni taratibu tu za kiutendaji ambazo zimekubalika kati ya hizi Serikali mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nizungumzie suala moja tu, nalo ni suala la ushiriki wa Zanzibar katika Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kama lilivyoelezwa na Mheshimiwa Saada Mkuya. Ili kulizungumzia hili ni vema kila mara kurudi kwenye Katiba na kuona inatuambia nini na baada ya hapo tulizungumze suala lenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(d) lina mamlaka ya kutunga Sheria kwa mambo yote yayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo maana yake inahusu Tanzania Bara na inahusu pia Tanzania Zanzibar. Kama tunavyofahamu pia kwamba Bunge hili linaweza likatunga Sheria kwa mambo mengine yote yanayohusu Tanzania Bara peke yake kwa mujibu wa Ibara ya (64)(1).

Mheshimiwa Mwenyekiti, yanapokuja masuala ya kutunga Sheria ambayo pia itatumika Zanzibar, Katiba imeweka masharti hayo na wameeleza vizuri katika Katiba, jambo la kwanza ni lazima jambo ambalo linatungiwa Sheria liwe linahusu mambo ya Muungano ukiangalia Ibara ya (64)(4)(c) na pili Sheria itamke yaani Sheria hiyo inayotungwa itamke kwamba itatumika pia kwa upande wa Zanzibar. Hii imeelezwa waziwazi kabisa katika Ibara ya 64(4)(b).

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa linapokuja suala la uhitaji na ulazima wa mashauriano kati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, utaratibu ukoje. Utaratibu wa mashauriano kati ya Serikali hizi mbili haujawekwa kwenye Katiba au Sheria yoyote, lakini uko kwenye utamaduni wa kiutendaji wa hizi Serikali mbili. Kwa hiyo utaratibu wa namna ya kushauriana hauko kwenye Katiba hauko kwenye Sheria, lakini umejengwa katika utamaduni wa utendaji wa hizi Serikali mbili. Sasa katika hili ni vema kueleza kwamba kumekuwa na tamaduni tofauti, kumekuwa na utamaduni uliotumika kabla ya Novemba, 2018 yaani mwaka jana na utaratibu ambao umeanza kutumika kuanzia mwezi Novemba, 2018 yaani mwaka jana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya Novemba utaratibu uliotumika ilikuwa ni katika hatua za awali za matayarisho wataalam wa kutoka upande wa Zanzibar waliitwa na walishirikishwa katika hatua mbalimbali za kuutengeneza Muswada wa Sheria na ushiriki wao ulihesabiwa kuwa wamewakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Novemba, 2018, Serikali hizi mbili zimekubaliana, lakini bado kama nilivyosema haijaandikwa katika Sheria yoyote, ila zimekubaliana kwamba sasa itakuwa ni lazima Katibu Mkuu Kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amwandikie Katibu Mkuu Kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili apate maelezo yake kwamba Muswada huo au jambo hilo limejadiliwa na limepitia katika ngazi mbalimbali zinazohitajika kujadili au kuhusishwa katika jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Muswada huo tunaozungumza uliandaliwa wakati tunatumia bado mfumo wa zamani kwa sababu ilikuwa ni around mwezi Mei, 2018. Kwa hiyo katika utaratibu huo wataalam mbalimbali kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walishirikishwa katika hatua mbalimbali za kuandaa Muswada huu. Hivyo basi, umekuja kwa sababu ulifuata huo utaratibu wa zamani, lakini utaratibu aliokuwa anauzungumzia Mheshimiwa Saada huo umeanza kutumika mwezi Novemba, 2018, lakini bado nieleze kwamba hizi ni taratibu tu za kiutendaji ambazo zimekubalika kati ya hizi Serikali mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie fursa hii kukushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala huu kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2019. Jumla ya Waheshimiwa Wabunge saba wamechangia muswada huu kwa kuzungumza nao ni Mheshimiwa Najma, Mheshimiwa Ally Saleh, Mheshimiwa Lathifah, Mheshimiwa Daniel Mtuka, Mheshimiwa Asha Abdallah, Mheshimiwa Prof. Jumanne Maghembe na Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hoja mbalimbali zilizotolewa za Waheshimiwa Wabunge kuna masuala ya jumla lakini pia kuna masuala yanayogusa sheria mojamoja. Kwa ajili tu ya rekodi nitapenda kujibu kidogo hoja aliyoiibua Mheshimiwa Lathifah kwamba Muswada huu umeletwa kwa hati ya dharura kwa ajili tu ya kuweka rekodi vizuri, si sahihi kwamba Muswada huu uliletwa kwa hati ya dharura.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kulikuwa na maoni juu ya DPP kushirikiana na ngazi nyingine na wadau wengine wa Serikali anapotekeleza majukumu yake. Hili tumelipokea lakini Waheshimiwa Wabunge wakijielekeza kwenye aya h hasa kipengele (b) na (c) cha jedwali la kwanza la marekebisho la Serikali hili limefanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda kwenye sheria mojamoja, tuanze na Sheria ya Mawakili; hapa nisingependa kuharibu tena maneno na maelezo mazuri sana ambayo ameyatoa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria. Kwa hiyo, kwa kweli nisiharibu maelezo hayo mazuri lakini niseme tu pendekezo la posho Serikali imelichukua na kwa sababu ni suala la kiutawala litafanyiwa kazi kiutawala. Pendekezo la mafunzo limepokelewa nalo ni la kiutawala linafanyiwa kazi kiutawala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia palikuwa na hoja ya Mheshimiwa Lathifah na yenyewe kwa lengo la kuweka pia rekodi vizuri iliyokuwa inaonesha wasiwasi kwamba mabadiliko haya ya sheria yanavunja Ibara ya 13(2) ya Katiba. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa na wengine wote wenye wasiwasi huo kwamba hakuna uvunjaji wowote wa Katiba kwa sababu hapa linazungumziwa suala la ubaguzi lakini mara nyingi tunapokuwa tunarejea Ibara ya 13(2) kuhusu mambo ya ubaguzi huwa tunasahau kurejea pia Ibara ya 13(5) inayoeleza ubaguzi ni nini. Ukisoma Ibara hiyo utaona kwamba katika jambo hili hakuna ubaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sheria ya Vizazi na Vifo, tumepokea maoni kuhusu kutoa mafunzo kwa wale watakao kaimu majukumu ya Msajili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na hasa hapa inagusa makosa yaliyoachwa kwenye orodha ya makosa ambapo plea bargaining inaweza kutumika. Majibu yetu ni kwamba nadhani hii tayari ni hatua tumepiga na tuone sheria itaendaje na sheria inaishi, pakionekana tena kuna haja ya kurekebisha maeneo hayo tutaleta marekebisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya Kurejesha Wahalifu (Extradition Act) hapakuwa na hoja kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya Mashauri yanayohusu Serikali (Government Proceedings Act) hapakuwa na hoja kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Mahakama za Mahakimu (Magistrates Courts Act) pia hapakuwa na hoja kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya Taifa ya Mashitaka ambayo inaendana na ile Sheria ya Taasisi ya Kupamba na Kuzuia Rushwa palikuwa na changamoto kidogo kuhusiana na mamlaka ya DPP. Na hapa tena nisingependa kuharibu maelezo mazuri kabisa ambayo Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria, Mheshimiwa Mchengerwa ameyatoa kuyaeleza hapa. Kwa hiyo, ningeomba labda niache hivyohivyo. Lakini tukiangalia katika jedwali la Serikali aya ya h eneo hili limeboreshwa vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sheria ya Mapato ya Uhalifu (Proceeds of Crime) kumetokea hoja nzito inayogusa suala la mali inayohusishwa na uhalifu na hasa lile suala la kurudi nyuma kwa miaka 5. Ninapenda kutoa taarifa kwamba Serikali imelitafakari hili kwa kina na kwa sababu ya usikivu wake imeamua kufuta kabisa hicho kipengele c kilichokuwa kinafanya rejea ya miaka 5 na hii tumeileta kwenye jedwali la pili la marekebisho ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hoja zake na majibu yake ni kama ile Sheria ya Mawakili na kama nilivyosema Mheshimiwa Mchengerwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria amelieleza vizuri sana, isingefaa tena kuharibu maelezo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sheria ya Chama cha Msalaba Mwekundu (Tanganyika Red Cross Society) kulikuwa na wasiwasi kwamba imepelekwa kwenye Wizara isiyo ya Muungano. Na hapa nimeona ni vema nieleze kidogo, katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kimsingi tuna masuala ya Muungano na yasiyo ya Muungano na kwa hiyo na Wizara nazo zinafuata mpangilio huo na kwa kweli Kikatiba si sahihi sana kusema kuna Wizara ya Muungano na Wizara isiyo ya Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini basi kama alivyoeleza Mheshimiwa Ally Saleh ambaye ndiye aliibua hoja hii, jambo hili la masuala haya ya Red Cross Society na Red Crescent Society imetokana na Mikataba ya Kimataifa. Na Mikataba ya Kimataifa ni masuala yanayohusu mambo ya nje na haya mambo ya nje ni masuala ya Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuhitimisha, ninawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri, tumepokea maoni mazuri ambayo yamelenga kuboresha si Muswada tu bali hata masharti mengine ya sheria mama na kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni ushahidi kwamba suala la marekebisho ya sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo linamuhusu kila mmoja wetu na ni jambo endelevu ndiyo maana kila mwaka Serikali inakuja na Muswada wa aina hii ili kuboresha masharti ya sheria zetu na kuzifanya ziendane na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoa shukrani hizo, naomba tena kutoa hoja.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii ya kuweza kutoa hitimisho la hoja iliyopo mezani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niaze kwa kusema naishukuru sana Kamati ya Katiba na Sheria kwa kuuchambua Muswada huu kama tulivyosema na kutoa maoni mengi. Kama Kamati yenyewe ilivyokiri katika taarifa yake iliyowasilishwa hapa Bungeni, mambo mengi ambayo waliyapendekeza na kuishauri Serikali yamechukuliwa na yamefanyiwa kazi na yako katika Jedwali la Marekebisho lililoletwa na Serikali. Kwa hiyo, hata kwa hoja nyingi zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge hapa, kwa kweli wakiangalia Jedwali la Marekebisho la Serikali limeshazichukua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendelea kuwashukuru wachangiaji, baadhi ya michango yao imejielekeza katika kupendekeza mambo ambayo yataboresha zaidi hizi sheria mbalimbali zilizopo kwenye Muswada huu zitakapoanza kutumika. Kama tunavyofahamu, sheria ni kitu kinachoishi na kwa hiyo, tutaanza kuzitumia sheria hizi na kadri tutakavyokuwa tunazitumia tutakuwa tunaona kama yako mahitaji mengine ya kufanya marekebisho au maboresho na siku zote tutakuwa tunazileta hapa Bungeni kwa ajili ya kuziboresha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepata wachangiaji kadhaa waliochangia kwa mdomo lakini pia wapo waliochangia kwa maandishi. Kama nilivyosema hoja nyingi kwa kweli zimeshajibiwa tayari kwenye lile Jedwali la Marekebisho lakini ziko hoja chache ambazo napenda kuzipitia kwa harakaharaka na kuzitolea maelezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Electronic and Postal Communications Act, kumetolewa michango kadhaa, Mheshimiwa Profesa Maghembe amezungumzia juu ya mtu kuingilia namba ya simu ya mtu mwingine na kujifanya ni huyo mtu mwingine. Napenda kutoa majibu hapa kwamba ziko adhabu kadhaa ambazo zimetolewa kwenye sheria hiyo na zitadhibiti suala hili. Kama ikionekana bado kuna mianya inayoweza kutumiwa na hawa wahalifu, kama nilivyosema, tutaileta tena Bungeni sheria hii kwa ajili ya kuziba mianya hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa pia na suala la miamala kwenye mitandao, wakati mwingine miamala haiendi inavyotakiwa kuwa, muda wa maongezi na kadhalika. Nataka kusema tu kwamba, iko mitambo ya kudhibiti masuala hayo lakini hata Mamlaka za Serikali kama TRA zinafuatilia kwa mfano masuala ya miamala kwa sababu ziko kodi pia za kulipwa huko. Kama ikionekana bado kwa sheria ilivyo kuna changamoto, kama tulivyosema, Serikali iko tayari kuileta tena Bungeni hapa na kufanya marekebisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine lililojitokeza ambalo ni kubwa kidogo, kumtoza faini mtu anayetumia line ambayo haijasajiliwa na kwa nini faini isitozwe kampuni. Sheria inaweka wajibu kwa mtumiaji na kwa kampuni. Kwa hiyo, kila mmoja ana wajibu wake, mtumiaji ana wajibu wake na kampuni ina wajibu wake na hata adhabu zimepangwa hivyo hivyo. Lengo ni kwamba pasipatikane mtu akatafuta excuse na kusema mimi nilikuwa sijui kwa sababu kama anatumia line inategemewa atumie line yake kuwasiliana. Kama anatumia line ya mtu mwingine, ajiridhishe kwamba ile line imesajiliwa. Kwa hiyo, tumeweka hivyo ili kusudi tusipate mwanya wa watu kukwepa wajibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mapendekezo mengi ya kuboresha sheria, kama nilivyosema, tutayachukua kwenye marekebisho ya baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya Firearms and Ammunition Control, sikusikia hoja kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya National Arts Council, hili ni Baraza la Sanaa, kulikuwa na pendekezo kwamba sheria hii inapaswa ifutwe tu na kuandikwa upya. Napenda tu kumjibu Mheshimiwa Profesa Maghembe kwamba kama tunavyosema, sheria inaishi na kwa hiyo, hata hizi hatua tulizochukua kwa sasa hivi nadhani ni za kupongezwa. Kama bado kutaonekana kwamba kuna mahitaji mengine hakuna jambo litakalotuzuia kuja kuifanyia tena marekebisho sheria hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya National Examination Council of Tanzania, kulikuwa na michango ya maandishi kutoka kwa Mheshimiwa Anatropia na Mheshimiwa Lucia. Wamezungumzia kuingiza wasiohusika na taaluma, nadhani ya mambo hayo ya elimu au mitihani kwenye Kamati, kwa mfano, RAS, DAS, RPC au OCD.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika masuala haya ya mitihani, si masuala tu ya taaluma yanayohusika lakini pia kuna masuala ya utawala, kutoa zile logistics za kusafirisha mitihani na kuna masuala ya usalama kuhakikisha kwamba mitihani haiibiwi wala haivuji. Kwa hiyo, hawa wanaoingia wanaingia kwa sababu ya hayo majukumu mengine, majukumu ya kiutawala na kiusalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lucia alikuwa na maswali kadhaa yanayohitaji ufafanuzi, ni maswali mengi kidogo sitaweza kuyasoma yote hapa, lakini naomba tu nimweleze kwamba, hii ni sheria, baada ya sheria kuna kanuni, taratibu na miongozo inatungwa. Miongozo, taratibu au miongozo ndiyo mara nyingi huwa inatoa ufafanuzi kwenye utekelezaji wa sheria hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya National Security Council, Mheshimiwa Ally Saleh aliibua hoja na hii ni hoja ya kikatiba. Ni kweli Katiba ya Zanzibar inatambua uwepo wa Makamu wa Pili wa Rais lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa Ibara ya 105, inamtamka Waziri Kiongozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliwahi kutoa ufafanuzi kidogo kwenye suala hili, nikasema kimsingi ni lazima tusome pia Ibara ya 102(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatambua uwepo wa Katiba ya Zanzibar na nikasema huu ndiyo msingi wa hoja. Kama yako mabadiliko kwenye Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaitambua Katiba ya Zanzibar, kimsingi hapo hakuna mgongano. Hata kama kuna mgongano wa kitafsiri, tulisema, tunatumia ule msingi mkubwa kabisa wa kutatua mgongano wa tafsiri ya Katiba (harmonization).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hapa hatuwezi tukasema tusubiri tena mpaka hii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibadilishwe, kwa sababu ni mchakato mrefu, Katiba haibadilishwi kama sheria inayotungwa na Bunge, kinachofanyika ikitokea hali kama hiyo, ni harmonization. Kwa hiyo, hapa kitakachofanyika ni hicho, harmonization na kwa hiyo, hakuna mgongano wowote. Kimsingi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaitambua Katiba ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye sharia ya Weights and Measures, hapakuwa na hoja nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Sheria ya Wildlife Conservation, tumepokea michango na mawazo mbalimbali lakini kama nilivyosema, sehemu kubwa ya masuala haya tulikuwa tayari tumeshayafanyia kazi kwenye Jedwali la Mabadiliko lililoletwa na Serikali. Hata hivyo, kama yako mambo mengine ya kuboresha kama nilivyosema, nafasi bado zipo, tutaangalia tunaitekelezaje sheria hii, tunapata matokeo gani na basi mwisho wa siku kama liko jambo ambalo linahitaji kufanyiwa marekebisho, hatutasita kulileta tena Bungeni kwa ajili ya kufanya marekebisho. Kwa sasa hivi, tujaribu kuona haya marekebisho yatatupeleka na kutufikisha wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuhitimisha kwa kusema kuwa nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri. Tumepokea maoni mazuri ambayo yamelenga kuboresha Muswada huu lakini pamoja na masharti mengine ya sheria mama. Kwa kuwa sheria ni kitu kinachoishi, yatakapohitajika mahitaji ya kufanya marekebisho tena, hatutasita kuyaleta Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maelezo hayo, naomba tena kutoa hoja.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 7 wa mwaka 2019. Nianze kwa kuishukuru tena Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa kupitia Muswada huu na kutushauri vema, na ushauri pamoja na maoni yao tumeyachukua vema kama ambavyo inaonekana kwenye Jedwali la Marekebisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge mbalimbali waliochangia Muswada huu na kutoa maoni yao. Tumepata Waheshimiwa Wabunge 7 waliochangia kwa mdomo, Mheshimiwa Susan Lyimo, Mheshimiwa Sixtus, Mheshimiwa Ally Saleh, Mheshimiwa Mariam Kisangi, Mheshimiwa Mwakasaka, Mheshimiwa Amina Mollel na Mheshimiwa Salome Makamba. Pia, tumepata michango miwili kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu pia kwa kutoa maelezo kwa ufasaha na kwa kina kwenye baadhi ya hoja zilizoibuliwa na Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo, mimi nitagusia maeneo machache tu ambayo yaligusiwa katika michango ya baadhi ya Waheshimiwa Wabunge. Nitaanza na mchango wa Mheshimiwa Suzan Lyimo aliyechangia mojawapo katika mchango wake kuhusu Sheria ya Animal Welfare na akagusia yale makosa kwa wanyama. Nilipenda kumueleza kwamba, kuna maneno ambayo tulikuwa tumeyasahau wakati tunamalizia huu Muswada na sasa tumeyaleta katika Schedule of Amendments. Tume-qualify yale makosa kwamba kama haya makosa yatafanyika kwa makusudi na kwa nia mbaya jedwali linaonesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mchango wa Mheshimiwa Sixtus Mapunda ambaye aligusia pamoja na mambo mengine Sheria ya Ugaidi. Basi alipenda kufahamu ni matendo ya kigaidi yaorodheshwe katika sheria hiyo. Napenda tu labda kumueleza Mheshimiwa Sixtus kwamba maoni yake tumeyapokea, tutaendelea kuyatafakari vizuri zaidi na kwa kuwa Bunge litakuwepo basi tutakuwa na nafasi pengine ya kutumia nafasi nyingine kuweza kuyaingiza hayo katika Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wa Mheshimiwa Ally Saleh aliyegusia kuhusu Sheria ya Ugaidi, na katika mchango wake basi alipenda kwamba sheria hiyo itaje, linapokuja suala la utengenezaji wa kanuni na Mheshimiwa Waziri mhusika kwamba hizo kanuni ni lazima ziwasilishwe Bungeni. Basi, ningependa tu pia kumuondoa hofu Mheshimiwa Ally Saleh kama anavyofahamu, utaratibu huu wa kuleta hizo Sheria Ndogo kwa sababu Kanuni ni sehemu ya Sheria Ndogo, kuzileta Bungeni upo tayari kisheria. Kwa hiyo, pengine hakuna haja sana ya kuandika kwenye sheria yenyewe husika kwamba hizo Kanuni zitakazotengenezwa na Mheshimiwa Waziri mhusika, basi ziletwe Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena niwashukuru kwa mara nyingine Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri, kama nilivyosema tumepokea maoni mengi mazuri ambayo yamelenga kuboresha si Muswada tu bali hata masharti mengine. Na kwamba mengine yameweza kufanyiwa kazi kwa sasa hivi lakini mengine bado yana nafasi ya kufanyiwa kazi siku za usoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni ushahidi kwamba suala la marekebisho ya sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo ni jambo muhimu siku zote na ni jambo endelevu na ndio maana kila mwaka Serikali huwa inaleta Miswada ya aina hii kwa ajili ya kuboresha sheria zetu na kuzifanya ziendane na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba tena kutoa hoja.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia katika kuhitimisha hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria kuhusiana na sheria hii ya usuluhishi wa migogoro au arbitration. Nianze kwa kusema jambo moja na la msingi sana kwamba Muswada wa sheria hii ulikabidhiwa Kamati ya Sheria Ndogo inayoongozwa na Mheshimiwa Chenge. Kamati hiyo imefanya kazi kubwa na nzuri sana. Ninaipongeza sana. Imetoa mapendekezo mengi na imefanya majadiliano ya kina tena katika mazingira mazuri kabisa ya maelewano na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na hata upande wa Serikali umechukua nafasi ya kutoa ufafanuzi na maelezo na kuweza ku-clarify maeneo mengi ambayo pengine yalikuwa hayaeleweki. Na ushuhuda wa hayo yote ninayoyazungumza ni kwenye ukubwa wa jendwali la marekebisho ambalo limeletwa na Serikali. Maana yake ni kwamba hii inaonesha ni kwa kiasi gani upande wa Serikali umeyabeba yale maoni mbalimbali ya Kamati na katika maeneo machache pengine ambapo mabadiliko hayo hayakuingizwa kwenye jedwali basi upande wa Serikali ulitoa ufafanuzi wa kina kuelezea maeneo hayo na Kamati ikaridhika.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo nijielejkeze katika hoja chache ambazo pengine ni za msingi na ya kwanza iko katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani inayosema sheria hii haitumiki Zanzibar na kwa sababu hiyo inaendeleza au inaweka ubaguzi. Si kweli kwa sababu tunaelewa vizuri hili ni suala la utungaji wa sheria na suala la utungaji wa sheria linaongozwa na Katiba. kwa hiyo, Katiba yetu imetueleza kwa sababu tuna Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuna Baraza la Wawakilishi, hivi vyombo vinafanyaje kazi katika utungaji wa sheria na kwa hiyo, nilikuwa napenda kwa ajili ya kuweka mambo vizuri nirejee kwa haraka katika Katiba na Katiba yetu inatuambia nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuelekee katika Ibara ya 64(4)(a) inasema; sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lolote haitatumika Tanzania Zanzibar ila kwa mujibu wa masharti yafuatayo (A) sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania Zanzibar, Sheria hii haikutaja hivyo. Lakini ni sababu gani sheria hii haikutaja hivyo? Ni kwa sababu Zanzibar inayo sheria yake ya usuluhishi wa migogoro, arbitration Act na kwa hiyo, Bunge hapa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haliwezi likaingia tu na kutunga sheria ambayo itatumika Zanzibar kwenye mazingira ambayo Zanzibar ina sheria yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ni vyema ikafahamika unapozungumza sheria ya usuluhishi wa migogoro inagusa pia mifumo ya Mahakama na tunafahamu Mahakama sio jambo la Muungano isipokuwa kwenye Mahakama ya Rufaa. Lakini ngazi nyingine za Mahakama sio suala la Muungano na kwa sababu si suala la Muungano Ibara nyingine za Katiba zinahusika, 64(2) inasema; Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika Tanzania Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la wawakilishi na hata tukienda kwenye Ibara ya 106(3) inaeleza muktadha huo huo yaani madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na hii ndiyo tafsiri sahihi ya Katiba na sio ile tafsiri ambayo hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani ilieleza haikuangalia vifungu hivi vya Katiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo ningependa kuligusia ni hili suala lililoelezwa kwamba sheria hii inajumuisha mabadiliko ya sheria za kawaida nne kwenye sheria hii ya arbitration kwa kutumia consequential amendments na kwamba njia sahihi ilitakiwa kuwa miscellaneous amendments. Ni vyema ikafahamika consequential amendments au miscellaneous amendments zote ni njia zinazotumika kurekebisha sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, Consequential Amendments inatumika wapi? Inatumika pale unapokuwa una sheria fulani lakini kuitunga kwake ni lazima kutaathiri sheria nyingine, unalazimika kufanya Consequential Amendments kwenye hizo sheria nyingine ili ui-harmonize na hii sheria unayotunga.

Mheshimiwa Naibu Spika, Miscellaneous Amendments ni marekebisho ya kawaida, unafanya marekebisho mbalimbali ya vifungu vya sheria. Kwa hiyo, hapa cha msingi ni yale marekebisho yaliyokusudiwa kwa sababu mwisho wa siku utumie Consequential Amendments au Miscellaneous Amendments utafika kwenye point ile ile, utakuwa umefanya marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, hizo sheria zote ambazo zinarekebishwa kwa Consequential Amendments maana yake zinaguswa na Sheria ya Arbitration na hatuwezi tukaziacha huko hivyo mpaka tutakapokuwa na Miscellaneous Amendments.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu ni tafsiri pengine isiyo sahihi kuhusu Sheria ya Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act na kifungu cha 11 kimegusiwa. Nilitaka tu niseme, kwanza siku zote tunapima matumizi ya sheria au changamoto zilizopo katika sheria baada ya kuanza kuzitumia na baadhi ya wachangiaji wameeleza vizuri kabisa hapa. Siyo Bunge hili tu, ni Mabunge yote wakati wote yanaleta Miscellaneous Amendments au amendments za aina nyingine, kwa sababu baada ya kuanza kuitumia sheria, basi imeonekana kwamba kuna changamoto unazotakiwa kuziondoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitoa ufafanuzi kwenye Kamati kwamba tunapokwenda kwenye kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act kimsingi hakikuwa kimefunga kabisa kuweza kutumia mifumo mingine. Nilieleza na labda nisome tena hapa nirudie, inasema: “pursuant to Article 27(1) of the Constitution, permanent sovereignty over natural wealth and resources shall not be a subject of proceedings in any foreign court or tribunal.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilieleza kwenye Kamati na ninajua Wajumbe wa Kamati walinielewa vizuri. Tunapotumia neno “foreign court or tribunal” tunazungumzia Mahakama au Baraza lililopo katika domestic setting ya nchi ile. Yaani tunazungumzia Mahakama au Baraza katika nchi nyingine. Ndiyo maana hata msemo unapotumika wa kisheria, foreign law haujumuishi sheria au mifumo ya Kimataifa. Foreign law inahusiana na sheria za nchi tu fulani husika. Kwa hiyo, nikasema kimsingi ilipotungwa hii sheria palikuwa na hiyo space, lakini sasa subsection (2) na (3) haiku-reflect vizuri hiyo space iliyokuwa imetokea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, siyo kweli kwamba marekebisho haya sasa yanataka kutambua mifumo ya Kimataifa, siyo kweli hata kidogo. Mifumo hii ya Kimataifa kwa namna moja au nyingine ilikuwa imeshatambuliwa ndani ya sheria hii, lakini sasa hivi marekebisho haya yanataka tu kuliweka hilo vizuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nilisikia sentensi moja kwamba Afrika inazalisha migogoro lakini watalaam wa kutatua migogoro wapo Ulaya. Siyo kweli. Bara la Afrika limeshaamua na hata ile Principle yenyewe ya Permanent Sovereignty of Natural Resources, migogoro tunaitatua wenyewe hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.6 wa Mwaka 2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii pia kwa mara nyingine kuishukuru Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo ambayo ilifanya kazi kubwa sana ya kuuchambua Muswada huu na kwa ushauri wao na mashauriano tuliyofanya na Serikali ambayo kwa kweli kwa kiasi kikubwa yamefanya kazi imekuwa ndogo. Kwa sababu mambo mengi tumeweza kukubaliana na tumeyaingiza katika Jedwali la Marekebisho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwashukuru wadau mbalimbali waliotoa maoni yao mbalimbali ambayo mengi tumeyapokea na tumeyafanyia kazi. Niwashukuru Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja hii na jumla ya Wabunge nane wamechangia kwa kuzungumza lakini pia Wabunge wawili wamechangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimshukuru pia Mheshimiwa Mheshimiwa Dkt. Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango kwa kufanya majumuisho na kuchangia katika kutoa ufafanuzi kwenye baadhi ya hoja zilizotolewa na hasa masuala yanayohusu ile Sheria ya VAT. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni mengi sana yametolewa, kwa ujumla kama Serikali tunasema tunayapokea na kila mara tunasema na kusisitiza sheria ni kitu kinachoishi. Kwa hiyo, kama kutahitajika tena mahitaji mengine hapo baadaye, basi hatutasita kuyaleta hapa Bungeni kwa ajili ya kuyafanyia marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya utangulizi huo, sasa niruhusu nipitie katika Muswada wenyewe. Nitaanza na hii Sheria ya Energy and Water Utilities Regulatory Authority ambapo tumepata maoni mengi na mengi tumeshayafanyia kazi kwenye Jedwali la Marekebisho. Hapa nitagusia kwa ufupi hoja iliyoibuliwa na Mheshimiwa Sabreena ambaye alikuwa anazungumzia juu ya hili suala la kufifilishwa kwa makosa (compounding of offences), Bodi ya EWURA ihusishwe katika mchakato huo. Sisi kwa upande wa Serikali tunafikiri kwamba tukisema tuihusishe Bodi katika kufifilisha makosa, mlolongo utakuwa mrefu zaidi na kutakuwa na ucheleweshwaji na hatutaweza kufikia ile azma tuliyokusudia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya Ferries (Sheria ya Vivuko), kwanza katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani lakini pia kutoka kwa Mheshimiwa Sabreena, kulikuwa na pendekezo la kutaja zile shughuli mahsusi zinazokatazwa katika kifungu cha 12(2) cha sheria hiyo. Katika majadiliano yetu na Kamati tulisema wazi kwamba shughuli ambazo zinaweza kukatazwa na nyingi na ukisema uziorodheshe iko hatari ya kuziacha nyingine. Hata hivyo, kuna kigezo muhimu sana ambacho kinatumika nacho ni kwamba ni shughuli yoyote ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa kivuko (chombo) pamoja na lile eneo kwa ujumla, kwa hiyo, shughuli hizo ndiyo zinakatazwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye sheria hiyo hiyo pia kulikuwa kuna maoni kutoka kwa Mheshimiwa Salome Makamba ambaye pia alipendekeza kuwekwe orodha ya makosa yanayozuiliwa kufanyika katika ule umbali ulioelezwa ambapo kivuko kinafanya kazi. Jibu langu kama jibu nililotoa hapo juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Salome pia alipendekeza adhabu itoke kiwango cha juu kutoka shilingi milioni kumi iliyopendekezwa na Serikali hadi shilingi milioni tano na pengine kwa sababu labda hiyo shilingi milioni kumi iliyopendekezwa na Serikali haina kigezo. Napenda kusema kwamba pendekezo hili la kupandisha adhabu actually lilitokana na Kamati yenyewe ambayo Mheshimiwa Salome pia ni mjumbe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia alikuwa na wasiwasi kwamba Mahakimu wanaweza kupata shida kujua watoe adhabu gani kwa aina gani ya makosa. Napenda tu kumuondoa wasiwasi huo kwa sababu Mahakimu wamepata mafunzo ya namna ya kutoa adhabu. Kwa hiyo, wao watapima kosa lililofanyika na wataangalia kwa mujibu wa sheria ni adhabu kiasi gani itolewe kwa kosa hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa pia na pendekezo la Mheshimiwa Mariam kwamba kuna boti au wapiga mbizi au waogeleaji ambao wanafanya shughuli zao karibu na vivuko na kwamba wanaweza kushiriki kwenye masuala ya uokoaji ikitokea ajali. Anashauri uwekwe utaratibu ili watakaposhiriki kwenye kazi hizo isisemekane kwamba wamevunja sheria. Mapendekezo hayo yanachukuliwa na masuala mengine kama haya yanaweza kuelezwa vizuri katika Kanuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya Gaming, kutoka katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kulikuwa na pendekezo kwamba pawepo na mfumo wa kielektroniki wa kudhibiti michezo ya kubahatisha. Napenda kusema kwamba actually Serikali imeshaanza kutengeneza mfumo huo. Katika Bunge hili tulipitisha Sheria ya e-Government ambayo inatoa mamlaka kwa chombo hiki kuweza kusimamia masuala yote ya TEHAMA ndani ya Serikali. Kwa hiyo, hii ni mojawapo ya michakato inayosimamiwa katika utaratibu huo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kutoka kwenye hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani tena, palikuwa na wasiwasi kwamba Bodi imepewa mamlaka makubwa sana na pengine inaweza kuingilia vyombo vingine vya Serikali hasa vinavyohusika na uchunguzi. Majibu yetu ni kwamba Bodi hapa imepewa mamlaka na majukumu ya kushughulika na masuala ya gaming tu (michezo ya kubahatisha) na haitashughulika na masuala mengine. Pia, tunafahamu kwamba viko vyombo vingine vya Serikali, vyombo vya dola, ambavyo vina majukumu ya kijumla kwa mfano, polisi, hawa hawatazuiwa kuingilia kati katika masuala fulani fulani ambapo pengine kuna jinai imetendeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya Tafsiri ya Sheria (Interpretation of Laws Act), kutoka Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, palikuwa na mapendekezo kwamba mamlaka ya Makatibu Wakuu kutekeleza majukumu ya Bodi yapunguzwe kutoka miezi kumi na mbili hadi miezi mitatu. Maelezo ya Serikali ni kwamba mapendekezo ya Serikali yanaangalia uhalisia wa hali halisi, wakati mwingine michakato hii ya kuwapata Wajumbe wa Bodi na Wenyeviti ambayo inahusisha michujo na upekuzi inaweza ikachukua muda wa zaidi ya miezi mitatu ndiyo maana tulisema miezi kumi na mbili. Siyo lengo la Serikali kwamba michakato hii itakuwa inachukua miezi kumi na mbili, itakuwa inafanyika kwa haraka inavyowezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya Penal Code (Kanuni ya Adhabu), kutoka kwenye mchango wa

Mheshimiwa Taska alieleza kwamba suala la upigaji picha, kunaweza kutokea mazingira ya kuhitaji kupiga picha ya yale matukio tuliyosema ya maiti au matukio ambayo yanaweza kuleta mshtuko. Panaweza kuwa na mahitaji ya kupiga picha kwa ajili ya kuhabarisha umma kwa nia njema, lakini pia kwa ajili ya kutunza ushahidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kusema kumba katika Jedwali la Marekebisho tumeweka mazingira ambayo mtu anaweza kupita picha hizo na tumesema kuna utaratibu ambao utapaswa kufuatwa. Pia bado Waziri mwenye dhamana anaweza kutengeneza Kanuni ambazo zitaweka pia maelezo na utaratibu mzuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vinginevyo kwenye sheria nyingine pamekuwa na maoni mengi na mapendekezo kama nilivyosema, ni maoni na mapendekezo mazuri ambayo mengine tutayachukua na tutayaangalia na kuona ni namna gani hizi sheria zitakuwa zinatekelezeka na kama nilivyosema, ikionekana haja ya kufanya mabadiliko tena hatutasita kuyaleta hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nihitimishe kwa kusema kwamba nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri. Tumepokea maoni mengi mazuri ambayo yanalenga kuboresha Muswada huu na hata masharti ya sheria mama na sheria mbalimbali. Kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni ushahidi kwamba suala la marekebisho ya sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo ni jambo muhimu linamhusu kila mmoja wetu na ni jambo endelevu. Ndiyo maana kila mara na kila mwaka Serikali inakuja na Miswada ya aina hii ya kurekebisha sheria mbalimbali ili kuboresha masharti yaliyomo katika sheria hizo kuzifanya ziendane na wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2019
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.3 wa mwaka 2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaendelea na majumuisho kwa kifupi kabisa naomba nilisemee suala aliloliibua Mheshimiwa Amina Mollel linalohusu kesi ya mtoto kubakwa kwa sababu kadri ya maelezo yake barua ile imeelekezwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, natumaini tutaipata. Kama ulivyoelekeza na kufafanua mwenyewe, kwa kuwa hii kesi ilikuwa Mahakamani na mshtaki alikuwa ni Jamhuri akisimamiwa na Ofisi ya DPP - Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali na Mahakama imetoa uamuzi huo, hatua inayofuata kama ulivyoeleza ni kukata rufaa.

Mheshimiwa Naibu Spika,pia nilipenda niongeze zaidi hapo, iwapo pengine itagundulika Hakimu aliyehusika katika kutoa hukumu hiyo pengine hakufuata maadili ya kazi yake, zipo taratibu za kisheria za kushughulika na Mahakimu katika masuala na mazingira kama hayo. Zipo Kamati za Maadili chini ya Mahakama, lakini pia kuna vyombo vingine vinavyoshughulika na masuala hayo. Pia kuhusu wale Wanasheria waliohusika iwe ni Wanasheria wa Serikali katika Ofisi ya DPP au wale Wanasheria binafsi wa utetezi, kama itaonekana pia kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa maadili, ipo Kamati ya Nidhamu ya Mawakili na ikigundulika hivyo watafikishwa huko, lakini pia vipo vyombo vingine. Kwahiyo tutalifuatilia suala hili.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika,baada ya kutoa maelezo hayo, niwashukuru Waheshimiwa Wabunge waliotoa michango yao mbalimbali. Jumla ya Wabunge 10 wametoa michango kwa kuongea na sikupata mchango wowote uliokuja kwa maandishi. Pia niwashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri waliochangia katika kuhitimisha hoja hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hivyo, naomba sasa nijielekeze katika kujibu hoja mbalimbali zilizotolewa na nitaanza kuzungumza kwa mambo ya ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nitaanza kujielekeza katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na ninachopenda kusema tu ni kwamba asilimia kubwa ya mambo yaliyozungumzwa au kugusiwa katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani tayari yamefanyiwa kazi katika jedwali la marekebisho (Schedule of Amendment) iliyoletwa na Serikali na nafikiri basi wahusika wakilitazama lile jedwali wataona namna hayo mambo mbalimbali tumeyafanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vinginevyo palikuwa na hoja kwamba sheria hizi zimekuja kwa haraka na kadhalika, lakini nafikiri zimetolewa maelezo, kwamba sheria inaweza kubadilishwa muda wowote kulingana na mazingira. Pia kulikuwa na wasiwasi kwamba kulikuwa na nia ovu, naomba nieleze Bunge lako Tukufu kwamba hakuna nia ovu yoyote hapa na lengo ni kujiwekea utaratibu mzuri kwasababu hakuna nchi ambayo inaendeshwa bila utaratibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ulitokea upotoshaji mkubwa na kutia hofu hasa katika mitandao na sehemu mbalimbali, lakini nafikiri upotoshaji huo ulitokana na ukweli kwamba wengi walisoma tu haya marekebisho yaliyopendekezwa na Serikali lakini hawakuwa wamesoma zile sheria mama ambazo zilikusudiwa kurekebishwa, wangesoma zile sheria mama wangepata ufafanuzi moja kwa moja katika zile sheria na wangeliona tatizo ambalo Serikali ilipenda kulishughulikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nijielekeze katika hizi sheria mbalimbali zinazorekebishwa nikianza na Companies Act, namshukuru sana Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe ameeleza kidogo, kuna historia ndefu katika jambo hili. Nimesikia kuna kuja hoja tuangalie best practice na kadhalika. Napenda kusema hata sisi tunaweza tukaweka best practice na wengine wakajifunza. Tusiwe kila wakati tukizungumzia best practice tuwe tunasema tunajifunza kwa wengine hata sisi tunaweza kuweka best practice. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tafsiri ya neno kampuni imezungumzwa, kipindi cha kuhama nacho kimezungumzwa, tumeweka utaratibu ambapo kama mtu hataweza kuhama kwa muda uliopangwa kuna utaratibu wa kulishughulikia jambo hilo. Pia suala la kampuni inapofutwa tumeweka utaratibu wa vizuri zaidi ambapo huyu anayeathirika anaweza ku-challenge kuanzia ile level ya notice au kampuni inapokuwa imefutwa kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya Copyright na Neighbouring Rights Act, kimsingi tumepata michango ya Waheshimiwa Wabunge na nadhani wengi wanakubaliana nasi kwamba lengo la sheria hii ni kulinda haki miliki ikiwemo za wasanii wetu. Huo ndiyo msimamo wa Serikali na actually ndiyo msimamo wa wadau pia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya Films and Stage Plays, sheria ina lengo la kudhibiti uoneshaji wa filamu katika mazingira ambayo yanazingatia maadili ya taifa letu. Pia kuna yale masuala ya kuja kupiga picha hapa nchini na sisi tusipate faida yoyote, basi sheria pia inataka kuliangalia jambo hili. Hapa tumezingatia pia zile sheria mbili tulizotunga mwaka 2017 na hasa ile moja ya The Natural Wealth and Resources (Permanent and Sovereignty Act).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya NGOs, tumeisikia michango iliyotolewa lakini hoja kubwa na ambayo imezungumzwa na wachangiaji wengi ni ku-regulate, kuweka mazingira mazuri ambapo NGOs zitafanya kazi kwanza kwa kutekeleza malengo yaliyokusudiwa lakini pia kuhakikisha kwamba hazitoki nje ya mstari kwa kufanya yale ambayo hayakutarajiwa. Kama nilivyosema hapo awali, kila nchi lazima iwe na utaratibu na sijapata kuona nchi ambayo haiongozwi kwa utaratibu wowote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Society Act kulikuwa na maoni fulani kwamba pengine taasisi za kidini zinaondolewa kwenye sheria hii. Napenda kusema kwamba palikuwa na kosa dogo la kiuandishi hapo, mashirika na taasisi za kidini zinaweza kujiandikisha kama societies, tumerekebisha changamoto hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria ya Statistics, ni kweli tumeirudisha tena Bungeni na hii ni kwa sababu sheria yoyote inapotungwa unaanza kuangalia utekelezaji wake na changamoto zinazojitokeza kwenye utekelezaji huo na siku zote haizuiliwa kuileta tena kwa ajili ya kurekebisha dosari ambazo zimeonekana. Jambo hili ni la kawaida na Bunge hili limekuwa linafanya hivyo toka lilipoanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Sheria Shipping Agencies, Mheshimiwa Mmasi alipenda kupata maelekezo kidogo kuhusu kuacha kumpa leseni ya kuwa agent au kufanya kazi kama agent mtu ambaye ni mmliki wa meli au operator na kadhalika. Lengo kubwa hapa ni kutenganisha suala la umiliki wa meli au operator na kadhalika na suala kuwa agent. Kwa sababu kilichojitokeza kwa uzoefu ni kwamba walewale wamikili wa meli ndiyo haohao walitoka wakatengeneza uwakala huko.

Mheshimiwa Naibu Spika, naona kengele ya pili imelia lakini nachopenda kusema kwa kuhitimisha, maoni haya tumeyapokea na kwa kweli kama nilivyosema awali tayari yalishaingizwa katika Jedwali la Marekebisho la Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme kwamba nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri, tumepokea maoni mazuri ambayo yanalenga kuboresha si Muswada tu bali hata masharti mengine ya sheria mama. Kwa ujumla, maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni ushaidi kwamba suala la marekebisho ya sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo linamhusu kila mmoja wetu katika Bunge hili na jambo endelevu. Ndiyo maana kila mwaka Serikali inakuja na Muswada wa aina hii ili kuboresha masharti ya sheria zetu na kuzifanya ziendane na wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 2) wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala wa Muswada huu wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, Namba 2 wa Mwaka 2021 (The Written Laws Miscellaneous Amendments No. 2 ACT, 2021).

Mheshimiwa Spika, tumepata nafasi ya kupokea maoni mengi mbalimbali na ambayo yamesaidia sana katika kuboresha Muswada huu ambao uko mbele yetu; na maoni mengi yametoka kwa uchangiaji wa mdomo; lakini pia yapo maoni ambayo tumeyapata kwa maandishi. Sasa kwa sababu sheria ni kitu ambacho kinaishi kila wakati maoni hayo tunayachukua na tutayatumia kwa kuendelea kuboresha.

Mheshimiwa Spika, lakini basi niende kwenye michango binafsi ya Waheshimiwa Wabunge ambako ningependa kusema mawili-matatu. nikianzia na Mheshimiwa Edward Kisau, ambaye amezungumzia juu ya mabadiliko ya Sheria ya Mawakili na kwamba ni fursa kwa hawa mawakili.

Mheshimiwa Spika, nilitaka kusema tu kwamba hili limetokana na usikivu wa Serikali, kwa sababu hilo lilikuwa ni ombi la mawakili wenyewe kuwawezesha kuweza kufika hata kwenye Mahakama za Mwanzo; na kuhusu suala la vyeti vyao kubadilishwa ili kusudi ionekane kwamba wanaweza kufika mpaka Mahakama ya Mwanzo; hilo litafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, tulipata pia maoni kutoka kwa Mheshimiwa Salome Makamba, ambaye naye ametoa maoni mbalimbali; lakini nitagusia zaidi hili la Sheria ya Vizazi na Vifo, ambapo amependekeza vitolewe vyeti vya kifo kulingana na idadi ya wake waliokuwepo:-

Mheshimiwa Spika, nilipenda tu kumuelewesha Mheshimiwa Makamba kwamba, unapozungumzia juu ya ndoa kuna uwezekano wa kuwa na ndoa mbili au tatu au nne, kulingana na Imani; na hizo zote ni ndoa na kila moja inaweza kupewa cheti cha ndoa. Lakini unapozungumzia kifo kama ni yule mwanaume aliyefariki, yule mume wa hao, kifo ni kimoja. Huwezi ukatoa vyeti vinne kwa kifo kimoja. Hata hivyo maoni yake na mapendekezo yake yametiliwa maanani. Pengine unaweza kufanyika tu utaratibu wa kiutendaji wa namna ya kulifanyia kazi hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia, alizungumzia juu ya on line registration ya kampuni. Nilipenda tu kumuondoa wasiwasi, kwamba utaratibu huu hauondoi au hauondoi kule kutambulika kwai le manual registration. Kwa hiyo, si kwamba, utakapofanyika usajili kwa online basi utaondoa kutambulika kule kwa manual registration, lakini ni hatua tu ya kuendana na nyakati na teknolojia.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Khadija Shaaban ametoa mapendekezo mengi katika mchango wake na ninaona kwamba takriban yote yameshafanyiwa kazi tayari na Serikali kwenye Jedwali la Marekebisho.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Abdullah Ali Mwinyi ameweka tu msisitizo na kujenga hoja zaidi kwenye maoni yaliyotolewa na Kamati, lakini kwa ujumla maoni yake kama ilivyokuwa maoni ya Kamati yameshafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana ametoa mapendekezo kwamba, neno ethics katika lile jina la ile kamati ya mkoa libaki. Kwenye schedule of amendments tuliliondoa hilo neno ethics kufuatia ushauri wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria. Na akasema pia kwamba, neno hilohilo sasa liongezwe kwenye ile Kamati ya Kitaifa, kwa hiyo, iitwe Advocates Ethics Committee.

Mheshimiwa Spika, Serikali ilikubali ushauri wa Kamati wa kuliondoa neno hili ethics kwa sababu mbili, lakini kubwa kabisa ni kwamba, neno hilohilo ethics linatumika kwenye kamati iliyoko chini ya Chama cha Mawakili wa Tanganyika. Kuna Advocates Ethics Committee ambayo hii yenyewe iko chini ya Chama cha Mawakili wa Tanganyika, kwa hiyo ikaonekana kwamba ukiliweka na huku tunaweza kuleta mkanganyiko.

Mheshimiwa Spika, lakini sababu ya pili ni kwamba, Kamati hii haishughulikii mambo ya maadili pekee, kuna mambo mengi zaidi ambayo inayashughulikia. Kwa hiyo pengine ikaonekana kwamba tuchukue ushauri wa Kamati tuliondoe neno ethics; lakini maoni mengine ya Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana tayari yameshafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kunambi ametoa ushauri mbalimbali kuhusu mabaraza ya ardhi. Nimshukuru sana Mheshimiwa Lukuvi, Waziri wa Ardhi, ametoa ufafanuzi wa ziada katika maeneo hayo. Hata hivyo mapendekezo yake pia, na mengine, tutayatilia maanani katika fursa zijazo za mabadiliko ya sheria.

Mheshimiwa Spika, Asha Juma naye amezungumzia kuhusu hiyo Sheria ya Vizazi na Vifo na suala la utoaji wa cheti cha kifo, lakini amesisitiza umuhimu wa kutunza vizuri kumbukumbu, ili kusudi pasiwe na changamoto inapokuja suala la kuchukua cheti hicho cha kifo. Hili ni la kiutendaji zaidi na Serikali imelichukua.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Agnesta ametoa ushauri juu ya mchakato wa kutunga sheria na akapenda sana kwamba, mapendekezo, na ninashukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria amelieleza vizuri, kwamba yanayokuja ni mapendekezo, lakini angetamani sana kwamba mapendekezo hayo yangekuja so perfect kiasi kwamba Kamati isiwe na kazi yoyote.

Mheshimiwa Spika, nadhani hii si sahihi sana, kwa sababu huu ni mchakato na ni utaratibu wa kawaida wa utungaji sheria uliopo katika nchi za Jumuiya ya Madola. Kunaletwa mapendekezo na mapendekezo hayo yanasimamia msimamo fulani. Sasa siku zote huwa kuna misimamo tofauti, pengine Serikali inaweza kuwa na msimamo wake lakini na wawakilishi wa wananchi wanaweza kuwa na mtazamo wao.

Mheshimiwa Spika, na katika hiyo hatuwezi kusema msimamo upi au mtazamo upi ni sahihi kuliko mwingine. Cha
muhimu ni kwamba kunakuwa na mashauriano, ili hatimaye tunakuwa na msimamo unaotokana na mashauriano na makubaliano ya pande mbili, ndilo jambo la msingi hapa; na huwezi ukasema kwamba mtazamo au msimamo fulani huu ni sahihi au si sahihi, n.k. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nadhani kama tulivyosema, kwamba Serikali itakuwa inatoa mapendekezo siku zote; na ndiyo maana tunakuwa na Kamati hii. Kamati hii inatarajiwa kuchunguza na kuyapima mapendekezo hayo halafu tunafanya mashauriano kwa misingi ya hoja. Na basi, upande wa Serikali utakapoona kwamba kweli katika jambo hili lililoletwa kuna changamoto kadha wa kadha basi katika usikivu wake inaweza ikapokea mapendekezo ya Kamati.

Mheshimiwa Spika, na kama ulivyosema, kwamba kukubali mapendekezo haya ya Kamati si dalili ya udhaifu, infact ni dalili ya strength.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Joseph Thadayo naye ametoa mapendekezo na maoni kadhaa. Ameizungumzia Sheria ya Makampuni, na kwamba inagusa sekta binafsi na anayakaribisha sana marekebisho mbalimbali yaliyopendekezwa. Niseme tu pia kwamba hii imetokana na mapendekezo haya ambayo pia yametokana na kilio kutoka sekta binafsi. Kwamba kuna mambo kadhaa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho. Na mapendekezo mbalimbali aliyoyazungumzia yameshafanyiwa kazi na Serikali.

Mheshimiwa Spika, basi naomba nirudie tena kuwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri waliyoitoa; na tumepokea maoni mbalimbali yaliyotolewa ambayo tunafahamu yana lengo si tu la kuboresha muswada lakini pia hata masharti mengine ya sheria kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, na basi maoni haya yanayotolewa ni ushahidi kwamba suala la marekebisho ya sheria ni suala endelevu na kila wakati ni lazima tuwe tunazirejea sheria zetu na kuona zinafanyaje kazi. Ndiyo maana kila mara Serikali inakuja na mapendekezo ya maboresho ya sheria.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ninaomba kutoa hoja.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, Naafiki.
THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO. 4) ACT, 2021
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue tena fursa hii kukushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu huu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, Na. 4 wa Mwaka 2021 ambapo jumla ya Waheshimiwa Wabunge 10 wamechangia kwa mdomo na hatukupata uchangiaji wa maandishi.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla Waheshimiwa Wabunge wengi wameibua hoja ambazo pia tulikutananazo kwenye Kamati ya Katiba na Sheria na hoja nyingi zimefanyiwa kazi tayari na upande wa Serikali, kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge wenyewe wameshuhudia. Nirejee hoja chache ambazo zimetolewa kwa sababu, ama zinahitaji ufafanuzi kidogo au labda Serikali tumechukua hatua tena katika hoja hizo.

Mheshimiwa Spika, hoja ya kwanza inahusu Ibara ya 23 ambapo palikuwa na swali iwapo tafsiri ya neno “gross value” au maneno “gross value” yanahusisha pia makaa ya mawe na chuma? Ningetaka tu kutoa ufafanuzi kwamba, tafsiri kama ilivyo katika Kifungu cha 4 cha Sheria ya Madini, ambapo neno “minerals” linajumuisha makaa ya mawe pamoja na chuma. Kwa hiyo, nilipenda kumfafanulia Mheshimiwa Mbunge aliyechangia hilo kwamba, tafsiri ya neno “gross value” inahusisha makaa ya mawe na chuma.

Mheshimiwa Spika, katika Ibara ya 34 ya Muswada ambayo inagusia pamoja na mengine, marekebisho ya Kifungu cha 23(b) cha sheria inayorekebishwa. Hapa changamoto au ombi lilikuwa ni kwamba, katika marekebisho hayo kiwango cha chini cha faini pamoja na kifungo havijawekwa. Tumeona pungufu hilo, kwa sababu tumeshakubaliana kwamba, tunapotunga sheria inayozungumzia faini au kifungo inapotaja kiwango cha juu au kiwango cha chini basi kile kiwango kingine kiwepo. Kwa hiyo, kama ikitaja kiwango cha chini basi kiwango cha juu kiwepo na ikitaja kiwango cha juu peke yake lazima kiwango cha chini kiwepo.

Mheshimiwa Spika, tumelipokea hili na Serikali imeleta sasa hivi marekebisho ya ziada (Further Schedule of Amendments) kwa ajili ya ku-accommodate kuweka kiwango cha chini cha faini pamoja na kiwango cha chini cha kifungo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine ni Ibara ya 49, Sehemu B ya Muswada ambapo lilijitokeza swali, kwa nini malipo ya mafao ya Maspika na Naibu Spika wastaafu isitajwe kuwa yapitie kwenye Ofisi ya Clerk of the National Assembly, yaani Katibu wa Bunge, badala ya Office of the National Assembly, yaani Ofisi ya Bunge. Kuweka mahsusi kwamba ni nani pale atakayehusika? Kama ilivyo kwa upande wa Majaji ambapo mapendekezo yanasema kwamba mafao hayo yatapitia kwa Chief Court Administrator.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba, katika kifungu hiki mapendekezo yetu ya awali yalikuwa ni kupitia Office of the Clerk of the National Assembly, lakini baada ya mashauriano ikaonekana kwamba labda tutumie Office of the National Assembly, baada ya mchango huu uliotolewa na Mheshimiwa Mbunge nasi baada ya kutafakari kwa haraka tumeona kwamba, nadhani hakutakuwa na changamoto yoyote tukipokea mapendekezo hayo, kwa hiyo, tayari tumeshayaingiza kwenye further schedule of amendments ambayo imeletwa sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, hayo ndio yalikuwa maeneo ambayo tumeona tuyatolee ufafanuzi na kwa sababu, pengine kuna hatua ambazo tumechukua. Vinginevyo, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri kwani tumepokea maoni mengi mazuri ambayo yanalenga, sio tu kuboresha muswada huu uliopo mbele yetu, lakini pengine hata sheria nyingine mbalimbali ambazo fursa ikipatikana siku za usoni basi tutafanya marekebisho hayo.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni muendelezo wa ushahidi kwamba, suala la marekebisho ya sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji madhubuti wa sheria zilizopo basi kwanza linamhusu kila mmoja wetu lakini pia ni jambo endelevu, ndio maana kila wakati Serikali huwa inaleta miswada kwa ajili ya kuboresha masharti ya sheria zetu ili ziweze kutekelezeka vizuri na ziendane na wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo ninaomba kutoa hoja.

WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, Naafiki.