Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Philip Isdor Mpango (43 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza na mimi napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu kwa heshima na dhamana kubwa ambayo amenipatia ya kuwatumikia Watanzania katika nafasi ya Waziri wa Fedha na Mipango. Napenda kumuahidi na kupitia Bunge hili kuwaahidi Watanzania wote kwamba nitaitumikia nchi yangu kwa uwezo wangu wote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Rais, nimeisoma na naomba kwanza niseme mambo matano kwa faida ya Watanzania ambao hawajaisoma hii hotuba na wengine pengine hawakuisikiliza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, kwamba Tanzania mpya itajengwa na sisi Watanzania wenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kila Mtanzania ni lazima afanye kazi kwa bidii na kujituma (selflessness) na hili ndilo linatuwezesha kugeuza maisha ya dhiki kuwa kama Mbinguni, yaani change of hell into paradise, lakini ni lazima tujitume, tutoke jasho ili kukuza uchumi wa Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu, rushwa, ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya mali na rasilimali zote za umma ni lazima tuvipige vita kwa nguvu zetu zote bila kuoneana haya. Kwa nafasi ambayo Mheshimiwa Rais amenitunukia, ni lazima mapato ya ndani ya kodi na yasiyo ya kodi, ni lazima yakusanywe kikamilifu kwa mujibu wa sheria. Hatutawachekea wakwepa kodi wala watumishi wa Mamlaka ya Ukusanyaji Mapato (TRA), wala Wizara na Idara za Serikali zinazokusanya maduhuli.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwetu sisi kama Wizara ya Fedha na Mipango, hawa ni nyoka, ni sawa na kucheza na cobra. Hatutakubali, tunawathamini sana wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo, lakini watii Sheria za Kodi na sheria nyingine za nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la nne, ni lazima kuwa na hofu ya Mungu katika kuwatumikia wananchi. Ni lazima tuwe na uchungu na maisha duni ya Watanzania walio wengi vijijini na mijini. Hawa hawana uhakika wa chakula, wanakula mchunga ndiyo mboga yao bila fursa ya kuchagua; wanakunywa maji yasiyo salama, watoto wao wanakaa chini shuleni na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la tano, amani na mshikamano katika nchi yetu, hii ni nguzo kuu ya maendeleo na ni lazima ilindwe kwa nguvu zote. Hivyo ni lazima kuzuia na kuzima ninachoita chaos of democracy kama tukio la jana na leo asubuhi hapa Bungeni. This is true costly to our country and we cannot afford it. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nisemee hoja mbili, tatu, nyingine nitazieleza kwa ufasaha zaidi wakati tunajadili Mpango kuanzia kesho. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ujenzi wa reli mpya ya kati kwa kiwango cha standard gauge, natambua Watanzania wana kiu kubwa sana ya kuwa na reli ya kisasa, lakini ni ukweli pia kwamba haitawezekana kujenga reli hiyo kwa Bajeti ya Serikali. Inakadiriwa ujenzi wa reli hiyo utagharimu kati ya dola za Kimarekani bilioni sita mpaka saba ambayo ni sawa na shilingi za Kitanzania trilioni 13.15 mpaka trilioni 15. Ni fedha nyingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Ununuzi wa Umma, niwataarifu kwamba Wizara iko katika hatua ya mwisho wa kuandaa marekebisho ya sheria hiyo na tutaileta for first reading nafasi ikipatikana ndani ya Mkutano huu wa Bunge. (Makofi)
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, nawaomba Watanzania wote wamuunge mkono kwa vitendo vya dhati Mheshimiwa Rais wetu na viongozi wasaidizi wake waandamizi kujenga Tanzania mpya. Tunaiunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Rais kwa asilimia 200 na tunawaahidi Watanzania usimamizi mahiri kwa bajeti ya Serikali na maendeleo ya uchumi wa Taifa letu kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniruhusu kusimama hapa ili kuweza kuhitimisha mjadala wa Bunge lako Tukufu kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia 2016/2017 mpaka mwaka 2020/2021.
Pili, nikushukuru wewe binafsi, pia Mheshimiwa Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha vizuri majadiliano kuhusu Mpango huu ambao niliuwasilisha tarehe 20 Aprili, 2016.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutambua michango iliyotolewa kwanza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini, lakini pia Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, ambaye ni Naibu Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote, waliochangia ama kwa kuzungumza au kwa maandishi. Ukiacha Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, jumla ya Wabunge 44 wamechangia hoja yangu ambapo Waheshimiwa Wabunge 34 wamechangia kwa kuzungumza na 10 wamechangia kwa maandishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi binafsi na kwa niaba ya watumishi wenzangu wa Wizara ya Fedha na Mipango, tumefurahishwa sana na mjadala juu ya Mpango huu ulivyoendeshwa. Kwa ujumla sisi tunaona kwamba mjadala umechukua mwelekeo wa Tanzania kwanza ambapo hoja nyingi zilizotolewa zilitanguliza zaidi maslahi ya Taifa. Ni matarajio yangu kwamba mwelekeo huu utaendelezwa katika majadiliano yote ya Mkutano huu wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sehemu kubwa michango ilikuwa yenye tija ikilenga kuboresha Mpango wenyewe, lakini pia kulikuwa na michango ya kukosoa ili kujenga (constructive criticism) na mingine ilikuwa ni ya kuomba ufafanuzi ili kuongeza uelewa. Nafikiri huu ndiyo utaratibu ambao Watanzania wangependa kuona ndani ya Bunge lao na nawapongeza kwa dhati na kuwashukuru sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, wapo wachache ambao walichukua mkondo tofauti na baadhi walichangia kwa jazba. Ninaomba wajiangalie tena na wabadilike na hasa huku tunakoendelea na Bunge hili la Bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile naomba niwashukuru kwa dhati Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa ufafanuzi mzuri wa hoja ambazo zinagusa sekta wanazoziongoza. Nafikiri hii inathibitisha kuwa Serikali yenye dhana ya Hapa Kazi tu inazingatia siyo tu uwajibikaji lakini pia teamwork. Ninawashukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nirejee kwa kifupi masuala kadhaa ambayo yalisisitizwa na Waheshimiwa Wabunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, tumesikia msisitizo mkubwa sana juu ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani na ni kweli hiki ni kipaumbele kikuu cha Serikali ya Awamu ya Tano. Tumesikia mmesisitiza umuhimu wa kupanua wigo wa mapato, kwamba Serikali ibuni vyanzo vipya na kujumuisha sekta isiyo rasmi katika mfumo wa kodi na tuangalie sekta zinazoibukia. Tumesikia kwamba ipo haja ya kuchukua hatua madhubuti kuziba mianya ya kukwepa kodi na tozo mbalimbali na hasa kwenye sekta ambazo zinakua haraka kama mawasiliano (telecommunications), madini na sekta ya ujenzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumesikia umuhimu wa kuimarisha matumizi ya vyanzo mbadala vya mapato kama vile hati fungani za miundombinu (local government bonds). Pia ushirikiano wa taasisi za fedha katika kukopesha (loan syndications). Mkazo umewekwa kwenye maeneo ambayo bado tunaweza tukakusanya vizuri zaidi na hasa mapato yanayotokana na rasilimali za nchi yetu, ikiwa ni pamoja na rasilimali za bahari, ardhi, misitu na utalii.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumesikiliza ushauri kwamba ni lazima sasa zoezi la kutathimini uwezo wa kukopa (credit rating) ili kupanua wigo wa sekta binafsi na Serikali kukopa, hili tumelisikia. Ipo pia haja ya kuboresha baadhi ya sheria ikiwemo ile ya mikopo, dhamana na misaada, namba 30 ya mwaka 1974.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumesikia msisitizo kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji na Waheshimiwa Wabunge wamesisitiza sana tuhakikishe upatikanaji wa malighafi; kuendelea kujenga na kuimarisha miundombinu yetu kwa ajili ya viwanda vilivyopo na tunavyotarajia vianzishwe, wamesisitiza upatikanaji wa ardhi kwa maendeleo ya viwanda katika mikoa yote na miji yote na kushughulikia changamoto ambazo zilijitokeza katika kutekeleza Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Waheshimiwa Wabunge, wamesisitiza umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa sekta ya kilimo, kama msingi wa maendeleo ya viwanda, kilimo cha umwagiliaji, umuhimu wa kuimarisha masoko ya mazao na upatikanaji wa bei nzuri kwa wakulima wetu. Tumeendelea kupokea ushauri kuhusu umuhimu wa kuongeza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo na pia Benki ya Wanawake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, umetolewa ushauri mbalimbali kwamba iko haja ya kuimarisha Mpango huu upande wa mikakati ya kuendeleza viwanda ikiwa ni pamoja na kulinda viwanda vya ndani, kuhakikisha tunaongeza thamani ya bidhaa tunazozalisha viwandani, pia kukamilisha tathimini ya viwanda vilivyobinafsishwa ili kuweza kuviendeleza na kufufua vile ambavyo vimekufa kabisa.
Mheshimiwa Naibu Spika, wamesisitiza uboreshaji wa rasilimaliwatu na hususani tuhakikishe kwamba rasilimaliwatu inaendana na mahitaji ya viwanda. Kwa kuboresha mitaala ya elimu na kadhalika. Pia kufanya jitiahada ya kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja na mitaji kutoka nje. Kwa kweli nawashukuru sana kwa michango hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nitoe ufafanuzi wa hoja chache, nikitambua kwamba siyo rahisi kufafanua hoja zote ambazo zilisemwa au kuandikwa. Kama ulivyosema nitatoa ufafanuzi wa baadhi tu ya hoja kuongezea pale ambapo Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri walipoishia.
Moja, kulikuwa na hoja kwamba namna gani Mpango umejikita katika kupunguza utegemezi?
Mheshimiwa Naibu Spika, utegemezi una madhara mengi sana ikiwa ni pamoja na kukosa uhuru. Naomba uniruhusu nitoe mfano wa kule nilikozaliwa. Akinamama kutoka Mkoa wa Kigoma wanafahamu vizuri kwamba ukiazima kitenge cha rafiki yako, ukaenda harusini na umefuatana naye, basi pale unapojimwaga mara nyingi anakukumbusha kwa kusema; “ucheze vizuri usije ukachana kitenge changu.” (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli utegemezi unaendana na masharti na wao wenyewe wanasema there is no free lunch. Baadhi ya wafadhili wanaingilia hata maamuzi ya mambo yetu ya maendeleo. Upatikanaji wa hizi fedha za misaada hauna hakika na hivyo ni lazima kuchukua hatua kupunguza utegemezi kwa kuongeza kiwango cha fedha za ndani kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa tunafanya hivi. Mwaka 2011/2012 tulitenga shilingi trilioni 1.87 kwa ajili ya maendeleo, lakini kufikia mwaka huu wa fedha tunaomalizia tulikuwa tumetenga shilingi trilioni 4.2 na nia yetu kwa kweli ni ya dhati kabisa. Ni lazima tuendelee kuongeza fedha yetu ya ndani ambayo tunaitumia kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana wakati nikiwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti nilisema wazi na ninarudia, tumeamua kutenga shilingi trilioni 8.7 kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha ambayo ni asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini si hivyo tu, bado tumeendelea kuwa na dhamira ya dhati ya kuongeza kiwango cha makusanyo ya mapato ya ndani ya kodi na yasiyo ya kodi. Kwa hiyo, mwaka 2014/2015 wastani wa makusanyo ya kodi katika Pato la Taifa ilikuwa ni asilimia 12.01 mwaka 2020/2021 ambao ndiyo mwisho wa Mpango niliouwasilisha dhamira yetu ni kwamba sasa ifike asilimia 18 ya Pato la Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia tumeendelea kupunguza matumizi ya Serikali yasiyo ya lazima na kuelekeza hizo fedha kwenye maendeleo, lakini hasa kwenye ujenzi wa viwanda ambapo maana yake tunajenga uwezo wa nchi yetu kujitegemea zaidi na hatimaye tuweze kuondokana kabisa na utegemezi. Tumesisitiza umuhimu wa kujenga mazingira ya uendeshaji biashara na uwekezaji nchini na hiyo yote ni dhamira kwamba, hatimaye tutakapokuwa tumekuza uwekezaji nchini tutakuwa tumejinasua kwenye utegemezi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie hoja hii tu kwa kusema na kuwahakikishia Watanzania kuwa dhamira ya Serikali yetu ya kuondokana na utegemezi, ni thabiti kabisa na wale wenzetu wanaotaka tuendelee kubebwa hadi uzeeni mimi nawasihi wajitambue maana dunia imebadilika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa tunataka uhusiano wa kibiashara na washirika wa maendeleo, tunataka uhusiano wa uwekezaji zaidi na huu ndiyo uhusiano endelevu, huu ndiyo utatuhakikishia uhuru wa kiuchumi na ndiyo uhusiano ambao unaheshimika yaani wenye dignity kama nchi na ndio utakaotuhakikishia sovereignty ya nchi yetu inabakia kuwa salama. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ilikuwepo hoja, kwa nini Serikali inaleta Mpango mpya wakati Mpango uliopita umetekelezwa kwa asilimia 26 tu? Kitaalam tathmini ya utekelezaji wa Mpango wowote unatumia vigezo vingi, upatikanaji wa rasilimali fedha ni moja tu ya vigezo. Viko vigezo vingi kama muda wa utekelezaji, thamani halisi ya hicho tulichopata, lazima tuangalie malengo, outcomes and impact (matokeo). Lazima pia tutathimini madhara yaliyotokana na utekelezaji na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo siyo sahihi hata kidogo kutumia kigezo kimoja tu kuhukumu Mpango kwamba haukufanikiwa. Tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano ipo na Waheshimiwa Wabunge, tuliwagawieni kitabu ambacho kimeeleza kwa kina tulivyotathimini utekelezaji. Kwa kweli tulibaini kwamba ukizingatia viashiria vingi itakapofika mwezi Juni, 2016 utekelezaji utakuwa ni takribani asilimia 60 na tuliweka wazi sababu ambazo zilipelekea Mpango huu usifike asilimia 80 au 90. Isitoshe ulimwenguni kote hakuna Mpango unatekelezwa asilimia 100. Hata Mpango wako binafsi haufiki asiliamia 100. Ndiyo ukweli wenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tulibainisha sababu kubwa zilikuwa ni upungufu wa rasilimali fedha, ushiriki mdogo wa sekta binafsi na udhaifu katika usimamizi. Serikali ya „Hapa Kazi tu‟ ni Serikali inayosema ukweli kwa maana ya kutaka kujirekebisha, ndiyo maana hatufichi sababu ambazo zilipelekea utekelezaji usifike kule ambako tungetaka na ndiyo maana katika Mpango huu tumesisitiza maeneo ambayo tumeona yalikuwa na udhaifu. Hivyo Mpango niliouwasilisha utaendelea kutekeleza miradi muhimu kama miundombinu, nishati, usafirishaji na maendeleo ya rasilimali watu ambayo ni lazima tuendelee kutekeleza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kuwa Serikali ina mikakati gani kupata fedha kwa ajili ya ugharamiaji wa Mpango. Nafikiri nimeshalieleza. Kuna aya mahsusi katika kitabu cha Mpango ambayo inaeleza vyanzo mbalimbali kwa ajili ya ugharamiaji wa Mpango, lakini kikubwa ni lazima tuelekeze nguvu ku-tap resources zilizoko kwenye sekta binafsi (PPP).
Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za Serikali nilisema zinatumika kama chambo, Kiingereza kizuri ni leveraging private capital. Hiyo ndiyo itakayotupeleka mbele. Miradi mikubwa kama ujenzi wa reli ya kati, kuijenga kwa Bajeti ya Serikali nilieleza katika Bunge lililopita ni kazi ngumu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, palikuwa na hoja kwamba kuna ukwepaji mkubwa wa kodi unaofanywa na Makampuni ya Simu. Ni hoja nzuri ambayo tunaendelea kuifanyia kazi. Lakini naomba niseme kuwa hizi hisia zipo kwamba makampuni haya hayatupatii takwimu sahihi juu ya muda wa maongezi (airtime) unaotumiwa na wateja na hivyo wanavujisha mapato ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muda wateja walikuwa wanatumia kadi (scratch cards) na hapo ilikuwa ni rahisi kuweza kufuatilia mapato ya kampuni za simu na kuhakiki au kulinganisha idadi ya kadi ambazo zilikuwa zimenunuliwa hapa nchini na zile walizokuwa wameagiza, zilizotumika na zilizobaki.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa teknolojia imebadilika; siku hizi unaweza ukanunua airtime kwa njia ya kielektroniki. Sasa hapa changamoto inakuwa ni kwamba, unajuaje mauzo halisi ya muda wa maongezi kwa Makampuni ya Simu kwa siku, kwa mwezi na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, simu za mkononi sasa zinatumika kwa ajili ya kusafirisha fedha na ni kwa kiwango kikubwa na haya makampuni yanapata mapato kutokana na hizo transfers. Serikali imefanya juhudi kupitia TCRA ili kuwezesha mapato haya kwa maana ya commission charges hasa kwa upande wa foreign traffic na hili limewezekana kwa kufunga mtambo ambao unaitwa TTMS (Telecommunication Traffic Monitoring System).
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo tulilonalo ni kwamba mfumo huu umetusaidia sana kujua hayo mapato kwa zile simu za international. Kazi ambayo inafanyika hivi sasa ni kuhakikisha kwamba muda wa maongezi kwa simu za ndani yaani local traffic nazo ziwe zinaweza kutambuliwa katika mfumo huu. Kwa hiyo, tunahitaji kuunganisha hii TTMS na mfumo mwingine unaoitwa Airtime Revenue Monitoring Solution (ARMS). Na kazi hii itakapokamilika hapo ndipo tutaweza kuwabana na kuwa na uhakika huo wa muda ambao kwa sasa hatuwezi kuu-capture vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, Jumamosi hii nimeitisha Mkutano kati yetu Wizara, Wizara ya Uchukuzi, TCRA yenyewe na Mamlaka ya Mapato Tanzania ili tuharakishe kazi hii ya kuhakikisha kwamba huu mfumo wa ARMS unakuwa integrated na huu wa TTMS. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, labda niseme mambo mengine mawili. Moja, kuna Mheshimiwa Mbunge anasema wanawake wamesahaulika. La hasha, naomba nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba kwetu sisi tukisema viwanda, kwetu sisi tukisema umeme vijijini, tukisema maji, focus yetu ni akinamama. Kwa kweli Mheshimiwa Rais alinipa Naibu Waziri mwenye uwezo mwanamama. Sasa kama na yeye amejisahau nitashangaa kweli kweli! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna hakika kabisa wala hatubabaishi akinamama ndiyo wamebeba uchumi wa nchi hii. Mpangaji yeyote wa mipango katika nchi kama ya kwetu ambaye hatambui mchango mkubwa wa akinamama katika uchumi wa Taifa, basi huyo hafai kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, reli ya kati. Naomba niseme kwamba umuhimu wa kujenga reli mpya ya kati na matawi yake yote hapa nchini hauna mjadala hata kidogo. Ni dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga reli mpya kwa kiwango cha standard gauge haraka inavyowezekana. Ndiyo maana pamoja na hali ngumu tuliyonayo, tumeamua kwamba tutatenga shilingi trilioni moja mwaka unaokuja kwa kuanzia tuone uwezekano wa kujenga angalau kilometa 50 mpaka 100 za reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge. Kwa sababu reli hii ni fursa itakayotuwezesha kutumia fursa pekee ya Tanzania tuliyonayo kijografia yaani ni unravel opportunity ambayo Taifa hili inayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, reli ya kati ndiyo itatuwezesha kuhakikisha kwamba biashara ya mazao yetu ya kilimo, ya chakula na ya biashara, uendelezaji wa madini lakini pia utalii. Vile vile kuhakikisha kwamba utangamano katika Afrika Mashariki na nchi zinazotuzunguka unaimarika na ni ukweli ulio bayana, Tanzania tunafaidi kutokana na utangamano wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumewekeza katika baadhi ya miundombinu na reli hii ndiyo itatusaidia kuhakikisha kwamba tunafaidi. Naomba nisisitize tu kwamba tatizo letu kubwa hapa nilieleza kikao kilichopita reli hii inakadiriwa ili kuijenga itatumia kati ya dola za Kimarekani bilioni 7.5 mpaka bilioni 9.0. Hizi ni fedha nyingi, siyo fedha kidogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, challenge kubwa inayotukabili kama Taifa ni kutafuta financing kwa ajili ya kujenga reli ya kati. Mjadala siyo kuijenga, hapana. Kazi kubwa tuliyonayo ni kupata fedha. Trilioni moja hii tuliyotenga ni kuonesha resolve tuliyonayo kama Serikali kwamba lazima tujenge hii reli na kwa hiyo nayo tunaitumia kama chambo kuvutia wawekezaji ili waone seriousness tuliyonayo ya kujenga reli yetu ya kati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe tu, kilicho muhimu Waheshimiwa Wabunge, ni kuwa na mkakati ambao ni credible wa kujenga hii reli. Kwa ushauri wangu tusijidanganye kusema kwamba sisi “lets do it alone” tujitazame tu ndani. Tukijenga matawi ya ndani peke yake haitatosha. Hatuna mzingo wa kutosha nchini kufanya ujenzi wa reli yetu ya ndani uwe sustainable. Kwa hiyo, ni muhimu na niwaombe Waheshimiwa Wabunge, maana wale wanaosema tusifikirie kujenga na extension ya kwenda Rwanda, jamani mbona hawasemi tufunge ile barabara ya kwenda Rwanda ambayo mizigo inapita hapa. Transit-trade peke yake inatuingizia mapato in foreign currency na sasa ni sekta ya pili kwa ukubwa kutuingizia mapato ya kigeni hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo niwaombe tu, tutafute strategy ambazo ni credible na sidhani kabisa kwamba strategy ya kujenga reli inayosema haya matawi ambayo yanatupeleka nchi jirani tusijenge, hapana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimeliahidi Bunge lako Tukufu kwamba nitaleta ufafanuzi wa hoja zote tulizozipokea kwa maandishi na Waheshimiwa Wabunge watapata nafasi ya kuzisoma taratibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba uniruhusu nihitimishe kwa kusema yafuatayo:-
Kwanza, kulihakikishia tena Bunge lako Tukufu kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuzingatia maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge ili kuboresha utekelezaji wa Mipango yetu ya Maendeleo ili kufikia malengo ambayo tumekusudia. (Makofi)
Pia tuna dhamana ya kuleta mabadiliko makubwa kuanzia upangaji wa mipango na utekelezaji wake ili kuiwezesha nchi yetu iondoke kwenye lindi la umaskini na hasa kwa wananchi wengi ambao wanaishi vijijini, lakini hata sehemu nyingine za miji yetu. Kama nilivyosema jana asubuhi wakati nikiwasilisha hoja yangu, kila Mtanzania ni lazima atambue wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii, kwa uadilifu, kwa nidhamu na uzalendo wa hali ya juu ili kujenga Tanzania mpya kwa faida yetu sisi, lakini pia na vizazi vijavyo na watoto wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie tena kuzitaka Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wajielekeza kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mpango huu ili tuweze kufikia azma yetu ya kujenga uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu. Nilisema jana na narudia tena, atakayeshindwa kusimamia utekelezaji wa miradi hii tuliyoibainisha aachie ngazi. Kama hataki kuachia, tutalala naye mbele. Wananchi wetu maskini wamechoka na huu umaskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia niwahakikishie sekta binafsi ya Tanzania kwamba tumedhamiria kuboresha mazingira yao ya kuwekeza, lakini pia kuhakikisha kwamba wawekezaji wa Kimataifa nao wanafanya biashara ambayo wao wanapata na sisi tunapata. Kwa hiyo, falsafa ya Hapa Kazi Tu itahamia vilevile kwenye kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Tunawaomba wawekezaji wote wa ndani na wa nje waweke nguvu zaidi katika sekta zote, lakini hasa katika maeneo ya kipaumbele ambayo tumeyabainisha katika Mpango. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe Watanzania wote watambue kwamba ni lazima tujinyime, lazima tujitume na kuvuja jasho ili kupata maendeleo tarajiwa. Wajibu wa kwanza wa kuiendeleza nchi yetu ni wa sisi wenyewe Watanzania. Akili za kutosha tunazo, Mungu alitujalia rasilimali nyingi na fursa tele. Hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kuwa semi-industrialize country inapofika mwaka 2025, inawezekana kabisa hata kabla ya hapo. Tutekeleze falsafa ya Hapa Kazi Tu kwa vitendo na Tanzania mpya tutaiona. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, naomba kutoa hoja.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa fursa. Nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hoja nzuri sana ambayo ametuletea; lakini pia Mheshimiwa Jenista Mhagama na Mawaziri wenzangu ambao wanasimamia sheria ambazo zimeletwa Mezani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, nichangie tu hoja chache; moja kubwa ni ile rai kwamba tukwamue miradi ambayo imeshaanza kutekelezwa na ambayo kwa masharti ya mkataba inataka msamaha wa VAT utolewe. Niseme tu kwamba ushauri huu ulishatolewa wakati wa majadiliano juu ya Sheria ya Fedha ya mwaka huu na niseme tena kwamba Serikali inaendelea kuufanyia kazi ili tupate suluhisho la kudumu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachofanya sasa hivi tunafanya uchambuzi wa kina kwa miradi yote ambayo imekwama, mikataba ambayo inahusika, kiasi cha VAT ambacho kinapaswa kusamehewa na basi mapendekezo yatapelekwa kwenye ngazi za maamuzi Serikalini na pale itakapobidi kurekebisha Sheria ya VAT hatutasita kuiwasilisha hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani ni vizuri niseme kwamba Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali kukwamua miradi hii, na moja wapo Serikali imekuwa inalipia kodi baadhi ya miradi husika lakini pia tumekuwa tunarekebisha vipengele vinavyohusika vya kimkataba.

Mheshimiwa Naibu Spika, asubuhi leo lilisemwa suala la kusamehe VAT kwenye taulo za kike, na ninaomba niseme tena kwamba tunaendelea kama Serikali kulifanyia kazi kubaini namna bora zaidi ambayo tutawawezesha watoto wetu wa kike na hasa walioko shuleni waweze kupata bidhaa hizo. Hii ni pamoja na uwezekano wa kuzigawa hizo taulo bure shuleni na gharama na bajeti zake, litakapokuwa limeiva tutalileta hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nisisitize pia kwamba ni kweli tutazingatia Serikali; maana yake ni Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa. Vilevile kuhusu utekelezaji wa kupunguza zile tozo za taasisi za udhibiti, tulianza wakati wa bajeti iliyopita na tunaendelea kufanya hivyo, yale yanayohusu marekebisho ya sheria tutafanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda niseme tu la mwisho, ni kweli kabisa ilielezwa hapa michezo hii ya kubahatisha inaongeza mapato ya Serikali kama ilivyoelezwa lakini kuna madhara pia. Tunachofanya, madhumuni kabisa ya kuleta marekebisho haya ni kuhakikisha kwamba tunadhibiti haya madhara na tunayo mikakati thabiti ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba tunakuwa na udhibiti imara lakini pia kuhakikisha kwamba elimu kwa Umma inatolewa ili tudhibiti hizi addiction na hii michezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru tena kwa nafasi hii na ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
uchumi wa Taifa, pia imepita kwenye maeneo ya Viwanda vya Chai, Karatasi, Mgololo na Mbao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme; naomba Serikali ipeleke umeme Kata ya Mtambula, Idunda, Itandula, Kiyowela, Idete, Makungu na katika maeneo ya vituo vya afya na maeneo ya shule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maji; naomba kutengenezewa miundombinu ya maji. Kuna matanki ya maji 12 hayafanyi kazi sababu miundombinu ya maji imeharibika, ilijengwa 1970, naomba Serikali iitengeneze miundombinu hii ili kuondoa adha kwa wananchi wa Kata ya Igowole, Nyololo, Idunda, Itanduka na Kibao ambao wanapata shida kubwa ya kukosa maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Vituo vya Afya; naomba Serikali imalizie kujenga vituo vya afya katika Kata ya Mtwango, Mninga na Makungu. Wananchi wamejenga kuta bado kumalizia tu.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Naomba Mheshimiwa Mbowe…
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa!..
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge naomba ukae chini. Jamani Waheshimiwa Wabunge, wakati wa wind-up hakuna taarifa. Naomba tuendelee na Waheshimiwa Mawaziri. (Makofi)
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Jambo la kwanza niweke bayana kwamba wale wanaochangia, wasome kwanza mafungu maana yake nini. Mheshimiwa Mbowe alichanganya kati ya Fungu 62 na Fungu Na. 98. Fungu 62 ni Uchukuzi ambalo ni fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Bunge hili liliidhinisha shilingi bilioni 143.5 na hadi tarehe 31Machi, fedha ambazo zilikuwa zimetolewa ni shilingi bilioni 56.69. Fungu Na. 98 ni Ujenzi. Fedha za ndani ambazo Bunge hili liliidhinisha ni shilingi bilioni 798.26 na kati ya hizo, shilingi bilioni 606.64 zilikuwa ni kwa ajili ya Mfuko wa Barabara. Shilingi bilioni 191.62 ni kwa ajili ya miradi ya ujenzi, miradi mbalimbali, vivuko, madaraja na nyumba za Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hadi kufikia tarehe 31 mwezi Machi, fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi, zilikuwa shilingi bilioni 931.3. Kati ya hizo, shilingi bilioni 323.95 zilikuwa ni za Mfuko wa Barabara. Shilingi bilioni 607.35 zilikuwa ndiyo za ujenzi wa nyumba, vivuko na kulipia madeni ya Wakandarasi. Sasa ukichukua fedha zilizoidhinishwa ukatoa zile ambazo zimekwisha tolewa mpaka sasa, zilizozidi ni shilingi bilioni 133.04 ambazo ni sawa na 0.6% ya bajeti yote ya mwaka ambayo ni shilingi trilioni 22.5.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria inasema hivi, kwanza kwenye kanuni za sheria za bajeti kanuni ya 28(1) inasema, nanukuu: “All reallocations between Votes shall require the approval of the Minister.” Kwa hiyo, sheria imenipa mamlaka.
La pili, 28(2) inasema hivi, “reallocations between Votes shall not exceed 5% of the total Government Budget.”
Nimeshawapigieni hesabu hapa, zilizozidi ni 0.6%. Hakuna mahali popote ambapo sheria ya nchi au sheria ya bajeti imevunjwa. Ndiyo maana nasema huo ni uongo ulio dhahiri na kwa kiongozi kama yeye kutoa takwimu ambazo hazina ukweli ni upotoshaji wa Bunge, ni upotoshaji wa wananchi wa Tanzania. Serikali ya Awamu ya Tano ni makini, inasoma kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya nchi na sheria zote zinazoongoza utekelezaji wa bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisemee hoja nyingine moja ambayo ilitolewa, ambapo ilishauriwa kwamba fedha zote za Mifuko ambayo iliundwa na Sheria za Bunge zipelekwe kama zilivyopitishwa na Bunge na ziende kwa wakati. Tunakubaliana kabisa na hiyo hoja na Serikali imeanza kuchukua hatua. Tumefungua account maalum kwa kila Mfuko ambao umeanzishwa ili kuhakikisha kwamba fedha hizi za Mifuko hiyo zinalindwa. Kwa hiyo, tahadhari tu hapa ni kwamba utoaji wa fedha hizi utategemea hali ya mapato katika kipindi husika, lakini Serikali imechukua hatua hii, tunaupokea ushauri, tutaendelea kuzingatia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kulisemea ni ushauri ambao tulipokea kwamba tozo kwenye mafuta ziwekwe kwenye Mfuko wa Maji na iongezwe kutoka Sh. 50/= hadi Sh. 100/= kwa lita ili kuondoa tatizo la maji. Hii ni hoja ya msingi na kwa upande wa Serikali tunasema, kwa sasa hivi, tunafanya uchambuzi wa mapendekezo ya wadau mbalimbali ili tuweze kurekebisha Sheria za Kodi na tozo ikiwa ni pamoja na haya mapendekezo ambayo Waheshimiwa waliyatoa. Kwa hiyo, napenda kuwahakikishia tu kwamba tutakapokuja mwezi wa Sita kuleta bajeti, ushauri mbalimbali ambao tumepokea, unafanyiwa uchambuzi na mapendekezo yanayotakiwa tutayaleta mbele ya Bunge lako Tukufu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali kadhalika, kulikuwa na hoja inafanana na hiyo ambayo ilielekezwa. Kulikuwa na hoja ya Mheshimiwa Jitu ambayo alishauri kama hivyo kwamba tuweke tozo kwenye mafuta na fedha hizo tupeleke kwenye Mfuko wa Mazingira.
Ushauri kama nilivyosema, umepokelewa. Mheshimiwa Jitu Soni ndiye alitoa ushauri huu. Kama nilivyosema, tumeshafungua Akaunti Maalum na tutahakikisha kwamba hizo fedha tunazi-ring fence, lakini ushauri tumeupokea, tunaendelea kuufanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nisemee hoja ya mwisho. Tulipokea ushauri kwamba ukuaji wa uchumi unatakiwa uende sambamba na kuongezeka kwa huduma za maji, umeme na miundombinu. Utekelezaji wa mipango na sera mbalimbali za Serikali, lengo lake ni kuhakikisha kwanza uchumi wa nchi unakua. Kama keki haikui, maana yake hicho tunachogawana ni kidogo mno. Kwa hiyo, ushauri wake ni mzuri kabisa kwamba tukuze kwanza ile keki na hapo ndiyo itatuwezesha kugawana vizuri na kupeleka huduma bora zaidi za jamii za umeme maji na miundombinu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja na ushauri mzuri kwamba Serikali iangalie namna ya kuongeza bajeti ya Mfuko wa Pembejeo ili kuboresha Sekta ya Kilimo. Serikali inapokea ushauri huo na tunaendelea kuufanyia kazi kwa sababu nchi hii bila kilimo, nchi ya viwanda haitawezekana. Kwa hiyo, ni hoja ya msingi, tunaipokea na tutaifanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya mchango huo, naomba kwa mara nyingine tena kuunga mkono hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa asilimia mia mbili. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia hoja iliyoko mbele yetu. Niseme moja kwa moja kwamba naiunga mkono hoja iliyotolewa kwa 200%. Kwa kuwa hoja ni nyingi, tunaahidi kuleta majibu ya hoja zote kwa maandishi lakini nizungumzie chache.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, kulikuwa na maswali hapa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji zimetengwa wapi. Katika mwaka wa fedha ujao kiasi cha shilingi bilioni 59.5 kimetengwa kwenye Fungu 21 - Hazina, sub-vote 2001, mradi namba 4,903, uwezeshaji wa vijiji. Hiyo imefanywa kwa makusudi kuruhusu taasisi zote zinazohusika ziweze kuandaa utaratibu mzuri wa matumizi ya hizi fedha na fedha hizi zitaratibiwa na Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ambalo napenda kulisema ni hoja ya Mheshimiwa Mchungaji Msigwa kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imeikuta Hazina tupu. Kama ilivyo kwa Serikali zote duniani, Serikali ya Awamu ya Tano imerithi mambo mengi mazuri kutoka Serikali ya Awamu ya Nne. Macroeconomic stability ni dhahiri, umeme vijijini uko wazi, Serikali ya Awamu ya Nne imejenga barabara nyingi na madaraja na Serikali ya Awamu ya Nne imepeleka maji vijijini. Vilevile tunakiri kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imerithi pia changamoto na hili ni kawaida kuna changamoto za kibajeti kama ukusanyaji hafifu wa mapato na kadhalika lakini si kweli hata kidogo kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ilikuta Hazina iko tupu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo inadhihirishwa na yafuatayo, Serikali imeendelea kugharamia kazi za msingi za ulinzi na usalama wa nchi yetu. Hakuna hata wakati mmoja kuanzia tulipochukua madaraka tumelegalega. Siyo hivyo tu, Serikali imegharamia shughuli za mihimili mingine yote ya dola ikiwemo Bunge. Pia Serikali imeendelea kulipa madai mbalimbali ya wakandarasi, watoa huduma na kadhalika. Si hivi tu chini ya mpango wa Policy Support Instrument na IMF ambao wanakuwa wanafanya tathmini huru ya utekekelezaji wa bajeti ya Serikali na mwenendo wa uchumi kwa ujumla, mara ya mwisho walikuwa nchini Disemba, hakuna mahali popote katika taarifa yao wanaonesha kwamba Hazina ya Tanzania ilikuwa tupu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia vigezo vya kimataifa viko bayana. Deni la Taifa ni himilivu nchi yetu inakopesheka. Tumeendelea kulipa mishahara ya watumishi bila kutetereka. Kwa hiyo, kwa kweli namshangaa sana Mheshimiwa Msigwa kwa madai yake hayo ambayo kwa kweli siyo sahihi. Kama ana ushahidi kinyume cha hayo niliyoyasema au hivyo vigezo nilivyoeleza alete uthibitisho Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, madai ya walimu waliyosimamia mitihani kidato cha nne mwezi Oktoba. Mwaka 2015/2016 tulitenga shilingi bilioni 17.7 kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa mitihani ya kidato cha nne. Hii inahusisha usimamizi, usafirishaji wa mitihani na ulinzi. Oktoba mwaka jana tulitoa fedha zote shilingi 17,762,472,220 kwa ajili ya kugharamia hiyo mitihani na hizi zote zilipelekwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi wa pili TAMISEMI ikaleta madai ya nyongeza ya shilingi 6,846,552,000. Hizi bado tunazifanyia mchanganuo kwa maana ya gharama ya malipo haya yaliyopungua na kuangalia matumizi ya fedha ambazo tulitoa awali. Uchambuzi huu utakapokamilika Serikali italipa fedha kwa wanaostahili haraka inavyowezekana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja ya wastaafu ambao hawalipwi pensheni zao Hazina ambao hawalipwi kwa kiwango cha shilingi laki moja. Serikali imesikia kilio cha wastaafu hao kupitia kwa wawakilishi wao na tutalifanyia kazi haraka na tutalijulisha Bunge lako hatua ambazo zitachukuliwa. Kwa nafasi hii, wenzangu wa Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali wako hapa, ninawaagiza walifanyie kazi suala hili mara moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, madeni ya walimu. Kuna hoja kwamba Serikali hailipi madeni ya walimu, Serikali ilipe stahili za walimu. Serikali imekuwa inalipa madeni na stahili za walimu miaka yote. Nitatoa tu mfano, mwaka 2014/2015 tulipokea madai ya shilingi 19,631,843,225. Tulipofanya uhakiki tulilipa shilingi 5,665,772,117.93 ambazo tulilipa mwezi Julai, 2015. Mwaka huu wa fedha wa 2015/2016 tulipokea madai ya shilingi 29,800,000,000 na baada ya kuhakiki Oktoba, 2015 tumelipa shilingi 20,125,578,770.05.
Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya sababu ya kukataa baadhi ya madai, kuna madai ambayo yaliwasilishwa zaidi ya mara moja na yako madai ambayo yaliwasilishwa kwa kiwango cha juu kuliko uhalisia. Mtu anawasilisha madai ya shilingi 600,000,000; badala ya shilingi 600,000 na yako madai ambayo yalishalipwa yakawasilishwa tena na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninachosema, ni lazima Serikali ipate nafasi ya kufanya uthamini kabla ya kuweza kulipa madai haya. Tuna thamini sana mchango wa walimu, tunajua sisi wote tusingekuwa hapa bila mchango wa walimu. Kwa hiyo, tutaendelea kulipa madai halali ya walimu na watumishi wengine wa umma kadiri yanavyowasilishwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie jambo moja la fedha za vijana na wanawake ziko wapi kwenye bajeti? Bajeti inavyoainishwa kimataifa (International Budget Classification) huwa haiendi kwenye makundi ya jinsia, wazee, vijana na kadhalika. Ni wazi vilevile bajeti ya maji inagusa moja kwa moja akina mama, bajeti ya umeme vijijini kadhalika na barabara za vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuelekeza bajeti ya Serikali kwenye maeneo hayo ambayo yanagusa akina mama moja kwa moja, bajeti imetoa kipaumbele kwenye sekta na maeneo ambayo yanagusa wanawake moja kwa moja. Kwa mfano, kwa mwaka ujao wa fedha asilimia tano ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri yametengwa kwa ajili ya vijana. Asilimia tano ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri yametengwa kwa ajili ya wanawake. Shilingi bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya vijana kwenye Fungu 65, Ofisi ya Waziri Mkuu, shilingi bilioni 15 zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ujuzi kwa vijana ambao hawana ajira na hizi nazo ziko kwenye Fungu 65. shilingi 1,955,000,000 zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha wanawake kiuchumi na ziko Fungu 55.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba Serikali inatambua umuhimu wa wanawake katika maendeleo ya Taifa letu na kamwe hatutasita kuchukua hatua za kibajeti ambazo zinawawezesha wanawake kutekeleza majukumu yao katika Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa kuna suala la mizigo kupungua katika Bandari za Dar es Salaam kutokana na wafanyabiashara kulalamikia VAT pamoja na Single Customs Territory kwa mizigo ya Congo. Ni kweli katika siku za karibuni tumeangalia mizigo inayopita katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya mwezi Disemba mwaka jana na mpaka Machi mwaka huu kuna upungufu ukilinganisha na kipindi kama hicho katika mwaka uliopita. Kwa mfano, makontena ya kwenda Congo yamepungua kutoka 5,529 mpaka 4,092 ambapo ni upungufu wa 26%. Pia yale yanayokwenda Malawi nayo yamepungua kutoka 337 mpaka 265 na yale yanayokwenda Zambia nayo yalipungua kutoka 6,859 hadi 4,448. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa ushuru wa forodha kwa miezi hiyo hiyo, ukusanyaji umeendelea kuwa juu ya malengo. Ukiangalia takwimu hizi tunazosema ni kwamba idadi ya makontena katika kipindi hichohicho imepungua hata kwa nchi ambazo hazimo kwenye mfumo wa Single Customs Territory. Kwa hiyo, nachosema ni kwamba hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya upungufu wa mizigo inayokwenda nchi jirani ikiwemo Kongo na huu mfumo wa Single Customs Territory. Nasema hivi kwa sababu, kwanza kwa upande wa kodi ya VAT hatutozi kodi kwenye transit cargo pamoja na kuwa Sheria ya VAT inatozwa kwa huduma ndogondogo peke yake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili bado Serikali inalifanyia kazi kwa sababu taarifa za kiuchumi za hivi karibuni…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, sekunde tano, muda umeisha.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ikiwa ni pamoja na World Economic Outlook ya 2016, ukuaji wa uchumi wa China umeporomoka kwa miaka ya karibuni na umegusa biashara katika nchi nyingi ulimwenguni ikiwemo Tanzania. Kwa hiyo, sasa hivi tumeshawaagiza TPA na TRA kufanya uchambuzi wa kina kuona mwenendo huu wa mizigo katika bandari ya nchi jirani ikiwemo pia Dar es Salaam ili tuweze kuona ni nini kinaendelea. Taarifa ya jana…
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa.
WAZIRI WA FEDHA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 – Wizara ya Fedha na Mipango
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kuniruhusu kusimama hapa ili kuhitimisha mjadala wa Bunge lako Tukufu kuhusu Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2016/2017 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 niliyoyawasilisha tarehe 8 Juni, 2016.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee nakupongeza sana kwa umahiri na weledi wa hali ya juu ulioonesha katika kusimamia Kanuni za Bunge wakati wote wa kikao hiki cha Bunge la Bajeti. Hakika viwango vyako ni vya kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, japokuwa Mheshimiwa Kakunda, mwanafunzi wangu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alichomekea sehemu fulani akidai kwamba mimi ni bahiri. Nadhani alimaanisha kwamba ni bahari wa kutoa maksi za upendeleo. Nataka niliambie Bunge lako Tukufu kwamba viwango vyako Mheshimiwa Naibu Spika ambavyo umevionyesha humu ndani hakika ningekuwa bado niko kule chuoni ningekupatia maksi za haki, asilimia 100 kama walivyofanya Maprofesa wako wa Sheria pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini pia University of Cape town, hongera sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutambua michango iliyotolewa na Kamati ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini. Japokuwa ameingia mitini, napenda pia kutambua mchango wa Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango lakini pia michango ya Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza au kwa maandishi hapa Bungeni, nawashukuru wote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya Wabunge 171 wamechangia hoja niliyowasilisha. Kati ya hao, 146 wamechangia kwa kuzungumza na 25 kwa maandishi. Napenda kuwashukuru wote. Pia niwashukuru Waheshimiwa Mawaziri tisa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliochangia asubuhi hii. Kipekee namshukuru sana Mheshimiwa Dokta Ashatu Kachwamba Kijaji kwa kunisaidia kujibu hoja kwa umahiri mkubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hatua ambazo zilipongezwa na Wabunge wengi wakati wa mjadala huu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/2017. Moja ambalo Waheshimiwa Wabunge mlilisema na kulipongeza ni Serikali kuthubutu kuweka lengo la bajeti ya shilingi trilioni 29.5 ikilinganishwa na shilingi trilioni 22.5 mwaka huu fedha tunaomalizia na kati ya hizo kutenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Miradi hii ya maendeleo ni pamoja na uthubutu wa kuanza kujenga reli mpya ya kati kwa kiwango cha standard gauge, barabara, umeme, ununuzi wa meli mpya na ndege tatu za abiria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia Waheshimiwa Wabunge walipongeza sana uamuzi wa Serikali kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi na hadi sasa tumefikia wastani wa shilingi trilioni 1.2 kwa mwezi kwa kuziba mianya ya uvujaji wa mapato na kuimarisha matumizi ya vifaa vya kieletroniki (EFDs). Pia Waheshimiwa Wabunge walipongeza uamuzi wa Serikali wa kusimamia nidhamu ya matumizi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo. Pamoja na mambo mengine Waheshimiwa Wabunge wamepongeza azma ya kufanya kazi na kurejesha nidhamu ya watumishi kazini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, yako mambo mengine mengi ambayo Waheshimiwa Wabunge walipongeza. Napenda nimalizie tu na moja la mwisho ambalo ni azma ya Serikali kujielekeza kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015, ahadi za Viongozi Wakuu na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2020-2025 ili kutatua kero za wananchi hasa masikini.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Waheshimiwa Wabunge walitoa ushauri katika maeneo mbalimbali, nitazungumzia machache. Moja, Waheshimiwa Wabunge wameshauri kuongeza tozo ya mafuta ili mapato hayo yatumike kupanua huduma za maji na kukamilisha vituo vya afya na zahanati vijiji. Pia walishauri kwamba mfumo wa kodi uboreshwe ikiwa ni pamoja na kufuta kodi zaidi, ushuru na tozo za kero kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanyabiashara hasa wadogo. Pia kutoa ahueni ya kodi kwenye taulo za akina mama na vifaa vya watu wenye ulemavu, vifaa vya michezo, zana za uvuvi na kulinda viwanda vya ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge walishauri kwamba ni muhimu kuimarisha elimu na kuhakikisha inaendana na mahitaji na wataalam wa Tanzania ya leo na kesho. Walishauri Serikali ichukue hatua za ziada kuimarisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na hususan kuongeza kilimo cha umwagiliaji, pembejeo, ugani, utafiti, mnyororo wa thamani, masoko, ruzuku, mikopo na bajeti ya kilimo. Waheshimiwa Wabunge waliishauri Serikali ipanue wigo wa kodi hasa katika sekta ambazo zina mapato makubwa kama mawasiliano, madini, maliasili na ardhi na sekta zenye fursa kama uvuvi na biashara kwenda nchi jirani lakini pia e-commerce, gawio kutoka kwenye mashirika ya umma na kuhakikisha kila mwananachi analipa kodi stahiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri uliotolewa ni mwingi sana na mzuri na Serikali itauzingatia katika bajeti hii na bajeti zinazokuja.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nianze kufafanua baadhi ya hoja na kama nilivyosema michango ilikuwa mingi haitakuwa rahisi kujibu hoja zote pamoja na zile zilizojibiwa na Waheshimiwa Mawaziri, nitajibu chache tu. Najua hoja hizi nyingine zilielezwa kwa hisia kali na wengine walinikaribisha Bungeni wakisema Waziri wa Fedha na Mipango amewa-beep Waheshimiwa Wabunge na wengine walisema Waziri wa Fedha hana jimbo ndiyo maana haoni machungu. Mimi nadhani walikuwa wananikaribisha tu Bungeni, kazi ya Waziri wa Fedha ina changamoto nyingi, inanilazimu niwe mtu ambaye hana maneno matamu tu lakini matupu, inanilazimu niwe mkweli na kuwaeleza kile ambacho kinawezekana na kile kisichowezekana ili kujenga nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja moja ambayo ilisemwa sana ni pendekezo la kuongeza tozo ya Sh.50 kwenye mafuta kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Maji na kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya na zahanati vijijini. Niseme tu kwamba hili ni pendekezo ambalo lina lengo zuri na Serikali inalipokea. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, ni vyema kutambua kwamba kufuatia kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia gharama ya mafuta yote ambayo tumeagiza kama taifa kutoka nje imepungua kwa takribani asilimia 20 na imechangia kushuka kwa mfumuko wa bei na sasa mfumuko wa bei uko asilimia 5.2 na mwenendo huu umeleta ahueni kwa maisha ya wananchi wetu walio wengi. Hata hivyo, Serikali imeamua kwamba kwa wakati huu hatutaongeza tozo kwenye mafuta ili wananchi waendelee kunufaika na huo unafuu wa bei ya mafuta. Ni wazi kwamba ongezeko la tozo katika mafuta ya petroli na dizeli litasababisha kupanda kwa bei ya mafuta jambo ambalo litaongeza gharama ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa chakula na bidhaa ikiwa ni pamoja na vifaa vya ujenzi na huduma nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niwaambie Waheshimiwa Wabunge pia kwamba wataalam wa uchumi wanashauri kwamba katika kipindi ambacho kuna uwepo wa bei ndogo ya mafuta, ni wakati mzuri kwa nchi kuwekeza hususan katika miundombinu, viwanda ambavyo ni energy intensive na kuendeleza ujuzi na teknolojia. Kwa hiyo, ndiyo sababu Serikali inaona kwamba ni busara zaidi badala ya kuongeza tozo kwenye mafuta tujielekeze kuongeza bajeti ya kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ya usafirishaji, nishati na elimu sambamba na kutumia pesa zilizopangwa kwa ufanisi zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu mkubwa wa huduma ya maji nchini ambayo pia ni Ilani ya CCM, tuliongeza bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Maji kutoka shilingi bilioni 373 hadi shilingi bilioni 690.16 kwa mwaka ujao wa fedha. Kwa hiyo, kama Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI alivyoeleza, Serikali inapenda itumie mwaka huu kujipanga na kujua majengo ya afya ambayo yamekwama kwa mwaka huu ili utekelezaji uanze ukiwa umepangwa vizuri mwaka 2017/2018. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ilikuwa ni pendekezo la kuondoa msamaha wa kodi ya mapato kwenye kiinua mgongo cha Waheshimiwa Wabunge. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, kodi ya mapato inatozwa kwenye vyanzo vyote vya mapato na kiinua mgongo ni chanzo kimojawapo cha mapato kinachotambuliwa na sheria na hutozwa kodi. Kupitia Jedwali la Pili la Sheria ya Kodi ya Mapato kiinua mgongo kinacholipwa kwa Wabunge wakati wanapomaliza muhula wa miaka mitano kimesamehewa kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, msamaha huu hauzingatii usawa wa utozwaji kodi kwani watu wengine wote wanaopata malipo ya kiinua mgongo, iwe ni sekta binafsi au utumishi wa umma wanatozwa kodi katika mapato hayo. Kwa hiyo, hatua niliyoitangaza tarehe 8 Juni, 2016 imechukuliwa ili kujenga msingi wa usawa na haki katika ulipaji wa kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la kufanya marekebisho hayo hivi sasa ni kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaotumika kukokotoa stahili za Mbunge endapo ukomo wa Mbunge yeyote utatokea katika kipindi cha kuanzia sasa (Julai 2016) na kuendelea. Pia mabadiliko haya yanafanyika sasa ili kuzingatia msingi wa utozaji kodi ambao unataka kodi iwe inatabirika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niliarifu Bunge lako Tukufu na wananchi wa Tanzania kwamba siku nilipowasilisha pendekezo hili la kufuta msamaha wa kodi kwenye kiinua mgongo cha Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanza alinishangaa akasema yeye ni Mtanzania na ni lazima Watanzania wote walipe kodi ili kuijenga nchi yetu. Kwa kuwa kiongozi lazima aongoze kwa mfano, Mheshimiwa Rais alielekeza kuwa yeye ni Mbunge wa Tanzania yote na anapenda awe wa kwanza kukatwa kodi stahiki kwenye mafao yake ya kustaafu. Naomba nirudie, alielekeza kuwa yeye ni Mbunge wa Tanzania nzima na anapenda awe wa kwanza kukatwa kodi yake stahiki kwenye mafao yake ya kustaafu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napenda kufafanua kwamba marekebisho niliyowasilisha tarehe 8, Juni, 2016 maana yake ni kuwa kiinua mgongo cha viongozi wote wa kisiasa ambao wametajwa kusamehewa kodi chini ya Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa sasa kitakatwa kodi. Maana yake ni kwamba Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, kiinua mgongo chake kitakatwa kodi. Mheshimiwa Waziri Mkuu, yeye ni Mbunge wa Ruangwa, kiinua mgongo chake kitakatwa kodi. Mheshimiwa Naibu Spika na wewe kiinua mgongo chako kitakatwa kodi. Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, sisi wote ni Wabunge, lazima tuongoze kwa mfano, kiinua mgongo chetu kitakatwa kodi. Vivyo hivyo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kiinua mgongo chao kitakatwa kodi. Waheshimiwa Wabunge, hii ndiyo dhamana ya uongozi, we have to lead by example. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, palikuwepo hoja ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwamba imetengewa fedha kidogo na haitaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Wengine walizungumza kwa lugha kali kidogo kwamba Waziri wa Fedha na Mipango ana dhamira gani na CAG, je, CAG ni adui wa Serikali, la hasha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukomo wa bajeti ya OC ilitengwa kwa mafungu mbalimbali kwa kuzingatia maamuzi ya Serikali na mkakati wa kupunguza matumizi ya kawaida ili tuelekeze fedha nyingi zaidi kwenye miradi ya maendeleo. Katika kufikia ukomo wa matumizi mengine kwa Serikali nzima, uchambuzi wa kina ulifanyika ili kubaini mahitaji ya fedha ambayo siyo ya lazima kwa wakati huu na hayawezi kuathiri utendaji. Kwa hiyo, tulitazama yote hayo na fedha ambayo tumeweza kutenga kwa sasa ndiyo hiyo na tuna hakika kabisa kwamba Ofisi ya CAG itaendelea kufanya kazi yake ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua umuhimu wa majukumu ya msingi ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kama ilivyo kwa taasisi nyingine nyeti ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama, mihimili mingine ya dola na uwezo wa kukabiliana na dharura, kama patajitokeza mahitaji ya lazima, napenda tena kusisitiza mbele ya Bunge lako Tukufu kwamba tutahakikisha kwamba ofisi hiyo haikwami. Mahitaji hayo ya ziada yatazingatiwa wakati wa mapitio ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, uhuru wa CAG katika kufanya kazi zake ni wa kikatiba na hautaingiliwa. Waziri wa Fedha na Mipango atakuwa mtu wa mwisho kukwamisha kazi za ofisi hiyo ambayo inamsaidia kufichua mchwa wa fedha za umma kwenye Wizara na halmashauri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja ya tathmini ya hali ya umaskini kimkoa. Naomba tu niseme kwamba viashiria vya kupima umaskini nchini huwa vinapatikana kwa kutumia utafiti wa mapato na matumizi ya kaya ambao unafanyika katika nchi yetu kila baada ya miaka mitano. Utafiti huo kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2011/2012. Utafiti huo ukichanganya na taarifa zinazotokana na sensa iliyofanyika mwaka 2012 ndiyo unatuwezesha kuweza kuchambua hali ya umaskini wa kila mkoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba sababu ambazo zinaeleza kwa nini kiwango cha umaskini katika Mikoa kama Mwanza, Kigoma, Singida, Geita na Kagera ni kikubwa ukilinganisha na Mikoa kama Lindi na Mtwara ni nyingi. Kwanza kwa ujumla umaskini wa kipato ni mkubwa zaidi pale ambapo kuna wananchi wengi zaidi wanaishi vijijini ukilinganisha na mijini. Kwa mfano ukiangalia Mkoa wa Mwanza, mwaka 2000/2001 wakati bado Geita iko humo kiwango cha umaskini kilikuwa ni asilimia 48. Umaskini wa kipato wa Geita kabla ya kugawanywa ulikuwa ni asilimia 62.3 lakini baada ya kutenganishwa kiwango cha umaskini wa kipato katika Mkoa wa Mwanza unateremka lakini kiwango cha umaskini katika Mkoa wa Geita kinaendelea kubakia juu na sababu kubwa ni kwamba wananchi wengi zaidi wa Geita wanaishi vijijini ambapo shughuli zao za uzalishaji mali hazikidhi kupunguza kiwango cha umaskini kwa kasi inayotarajiwa. Ukiangalia wilaya ambazo ziko karibu na miji, kiwango cha umaskini ni kidogo zaidi kuliko kiwango cha umaskini katika maeneo ya vijijini.
Mheshimiwa Naibu Spika, umaskini pia ni lazima uende na hali ya kimaeneo. Kwa mfano, Mkoa wa Kigoma kwa kiasi kikubwa umaskini wa kipato katika mkoa huu unachangiwa na miundombinu hafifu ya usafirishaji ambayo inapunguza fursa ya kufikia masoko. Kigoma pia inabeba mzigo mkubwa sana wa wakimbizi na kusababisha ziada ambayo inazalishwa kutumika kulisha wakimbizi na kupunguza ustawi wa kaya katika mkoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama ni mkakati, cha kwanza ni kutambua kwamba kuna hilo tatizo na sababu zake lakini pia kujielekeza sasa kufungua fursa katika mikoa na wilaya husika. Pia kuja na interventions kama zile za TASAF ambazo zinalenga kusaidia kaya maskini kabisa lakini pia miradi ya afya na maji na pia specific interventions ambazo zinakwenda kushughulikia matatizo katika maeneo mahsusi kama vile tatizo la mnyauko wa migomba kule Kagera na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema tutawasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kwa hoja zote ambazo Waheshimiwa Wabunge walizitoa. Naomba nieleze moja kabla ya kuhitimisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ililetwa hoja hapa kwamba dollarization imekuwa ni kero kubwa na inasababisha thamani ya shilingi kuteremka. Naomba tu niseme dollarization ni matumizi ya sarafu ya kigeni katika nchi husika sambamba na sarafu ya nchi hiyo. Dollarization kitaalam inachochewa na vitu kadhaa hususan mfumuko wa bei kama ni mkubwa lakini pia kama thamani ya sarafu ya nchi husika nayo inateremka lakini katika nchi ambazo hakuna usalama.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Tanzania sababu kubwa ni kwamba tumekuwa na mapato kidogo ya fedha za kigeni lakini pia dola imeongezeka sana nguvu kutokana na kuongezeka kwa uchumi wa Marekani na kuchelewa kupata misaada ya general budget support. Kwa kawaida wananchi wanatumia hiyo sarafu ya kigeni ili kujikinga na athari za mfumuko wa bei yaani they hedge against the inflation risk. Mazingira mengine ambayo yanachochea dollarization kama nilivyosema ni kukosekana utulivu wa kisiasa ambayo sisi bahati nzuri hatuna.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuondoa hili tatizo linahitaji muda na ukichukua hatua za kiamri, za kiutawala kusema tu sasa kuanzia leo watu wasitumie dola, uzoefu wa nchi mbalimbali ulimwenguni unaonesha kwamba hizo sera hazifanyi kazi. Utatia woga katika uchumi na watu wataanza kukimbiza fedha za kigeni na kuleta matokeo yasiyotarajiwa. Kwa hiyo, mkakati siyo kulazimisha au kudhibiti matumizi ya hizo dola, inatakiwa iende sambamba na sera za kisoko za kudhibiti tatizo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa watu ambao wanapenda kusoma wanaweza wakatafuta jarida linapatikana kwenye internet „Dollarization in Sub-Saharan Africa: Experience and Lessons 2015‟, inawaonesha experience ya nchi nyingine na hatua ambazo walichukua hazikufanikiwa. Kwa hiyo, tunachukua kila tahadhari kuhakikisha tunaendelea kubakia na uchumi wetu tulivu.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niwasihi Waheshimiwa Wabunge, kwamba bajeti niliyowasilisha inajielekeza kuanza kazi ngumu ya kuitoa Tanzania kutoka nchi inayotegemea kilimo duni kuwa nchi ya uchumi wa viwanda, nchi ambayo wananchi wake wameondoka kwenye lindi la umaskini ili twende mbele. Kwa hiyo, yote tunayopanga, katika mipango na bajeti ya Serikali, ni muhimu sana kutanguliza maslahi ya Taifa letu lakini pia maslahi ya Watanzania maskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Bunge lako Tukufu kuikubali bajeti hii, utekelezaji wake utahitaji kujitoa. Mheshimiwa Makamba amesema tutahitaji sacrifice, tutahitaji selfless service to our country. Tunahitaji kuvuja jasho ili tuweze kuwainua maskini.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna mambo mawili tunaweza kufanya, tunaweza tukaamua kuendelea na mazoea yaani business as usual ambayo siyo option kwetu lakini njia sahihi ni kuachana na mazoea. Ili kuachana na mazoea lazima tuanze sisi viongozi. Itatubidi tuachane na maslahi binafsi hata kama mara kadhaa inaonekana tunayavisha koti au kilemba cha maslahi ya wengi.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Nilikuwa nasema tuna dhamana kubwa ya kuleta mabadiliko makubwa katika kuendesha shughuli zote za umma na matumizi ya rasilimali za Taifa ili tuweze kupiga hatua kubwa za kuitoa nchi yetu katika umaskini. Ni lazima kila mwananchi atambue wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika nyanja zote na uzalendo kwa Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie tena kuzielekeza Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuzingatia hatua za kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kusimamia matumizi ya Serikali na hatua za kupunguza gharama na kulipa na kuzuia ongezeko la madeni ya Serikali. Serikali ina dhamira ya dhati ya kuchukua hatua hizo na naomba Watanzania watambue kwamba ni lazima kujinyima, kujituma na kuvuja jasho ili kupata maendeleo na kupunguza utegemezi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie tena, wajibu wa kwanza wa kuiendeleza nchi yetu ni ya sisi Watanzania wenyewe, tunazo akili za kutosha na rasilimali nyingi na fursa tele kuweza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na ya uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Nawaomba tena Waheshimiwa Wabunge kuunga mkono hatua zinazoongozwa na Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa tunaimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, mapato ya kodi na yasiyo ya kodi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo yenye tija na hususani ujenzi wa viwanda kwa manufaa ya Watanzania wote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nikushukuru sana kwa kuliongoza vizuri sana Bunge toka asubuhi na mchana huu. Niungane na waliotangulia kusema kwamba haya wanayofanya upande mwingine yasikukatishe tamaa. Chapa kazi, fanya kazi ambayo Bunge hili lilikuchagua kufanya na hakika Watanzania wanajua umahiri wako na matunda ya kazi yako njema. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango mizuri sana na ushauri wao na naahidi kabisa kwamba ushauri ambao mmetupatia tutaufanyia kazi na tutauzingatia katika kutekeleza bajeti ijayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya Waheshimiwa Wabunge 36 wamechangia hotuba yangu; waliochangia kwa kuzungumza ni 24 na waliochangia kwa maandishi ni 12. Kwa kuwa baadhi ya michango ni ushauri lakini hata hoja hizi si haba, kwa muda ambao ninao sitaweza kujibu zote, lakini naomba kuliahidi Bunge lako Tukufu kwamba tutawasilisha majibu ya hoja zote kwa maandishi ili Bunge liwe na rejea na kumbukumbu.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo machache ya utangulizi, basi naomba nitoe maelezo kwa baadhi ya hoja ambazo zimejitokeza wakati Waheshimiwa Wabunge wakijadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango na taasisi zake.
Mheshimiwa Naibu Spika, labda nianze na hoja ambayo ilijielekeza kusema kwamba ni vizuri kama Serikali tuangalie tutakavyoweza kuzuia athari zinazoweza kujitokeza katika kukopa na kutumia instrument mbalimbali za masoko ya fedha kama vile hedging na swaps.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hili labda tu niseme kwamba, Wizara ya Fedha na Mipango katika ukopaji tunazingatia Mkakati wa Kati wa Usimamizi wa Madeni, kwa Kiingereza inaitwa Medium Term Debt Strategy, lakini pia Sheria ya Madeni. Mkakati huu unaelekeza tukope wapi, sarafu zipi, riba gani, kama ni fixed rates au variable rates, lakini kubwa ni kwamba tuhakikishe Serikali inakopa kwa gharama nafuu na zenye athari ndogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika ukopaji wa deni la nje kuna athari nyingi ambazo zinaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya riba (Interest Rate Risk) lakini pia mabadiliko ya viwango vya kubadilisha fedha (Exchange Rate Risk). Tunaweza tukatumia vyombo mbalimbali ikiwa ni pamoja na instruments ambazo aliyetoa swali alipendekeza, ikiwa ni pamoja na hedging na Interest Rate Swaps. Hivi ni vyombo ambavyo hata hivyo vina gharama kuvitumia na pia vinahitaji utaalam wa hali ya juu katika kuotea viwango vya riba katika masoko ya fedha ya Kimataifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niseme tu kwamba, kimsingi hizi instruments kwa sasa zinatumika zaidi kwa nchi ambazo ziko kwenye mikopo ya kibiashara na ambazo zina viwango vya riba vinavyobadilika mara kwa mara, lakini mahali pia ambapo madeni yako katika sarafu moja. Kwa hiyo, tunavyoendelea huko mbele tutaangalia tukiongozwa na, kama nilivyosema, Medium Term Debt Strategy ili kuona polepole na sisi tunavyoweza kutumia hizi instruments zikatusaidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nisemee kidogo suala la deni la Taifa na nimshukuru sana Mheshimiwa Mtemi Andrew Chenge kwa ufafanuzi wake mzuri alipolielezea kwa nini linaongezeka. Naomba tu nisisitize kwamba kwa kweli kwa Taifa kama letu ambalo lina mahitaji makubwa sana ya maendeleo, ni lazima tuendelee kukopa na ukikopa maana yake unaingia kwenye deni. Tuna mahitaji makubwa sana ya miundombinu, kwa hiyo lazima tukope. Kwa sasa hatuna vyanzo vya fedha vya kutosha kuweza kukidhi hayo mahitaji yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kikubwa Mheshimiwa Chenge amekieleza, ni kwamba tunakopa kwa masharti gani? Hili ni jambo la kuangalia. Kwa hiyo riba kiasi gani, tutalipa kwa muda gani, grace period na masharti mengine, haya lazima kuyachambua kwa umakini. La muhimu zaidi, tunakopa hizi fedha kufanyia nini?
Mheshimiwa Naibu Spika, kila mara huwa nasisitiza nchi inavyokopa haina tofauti na mtu binafsi. Kama unakopa ukaenda kustarehe ukalewea pombe na kadhalika basi unajua kabisa huo mkopo hauna faida kwako wewe na familia yako na Taifa ni hivyo hivyo. Kama unakopa na unazitumia kuongeza uwezo wako wa kuzalisha, unaongeza uwezo wako wa miundombinu bora ambayo inawasaidia wawekezaji na wananchi kuweza ku-move goods and services, hilo ndilo jambo jema.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kinachotakiwa ni umakini, kwamba mikopo hiyo tunaifanyia jambo gani. Kwa nchi yetu, kikubwa tumeelekeza mikopo hiyo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. Ni wazi kabisa miundombinu kama umeme Kinyerezi, barabara nyingi ambazo zimejengwa nchini, madaraja na kadhalika, yote haya kwa fedha za ndani peke yake tusingeweza, kwa hiyo ilitulazimu kwenda kukopa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa upande wa tathmini ya deni la Taifa, kwa kweli hapa tunafanya tathmini mara nyingi. Kila mwaka tunafanya tathmini chini ya ushirikiano wetu na Shirika la Fedha la Kimataifa na wao wanashiriki, hatufanyi peke yetu. Kwa hiyo hizi estimates, tunapoangalia uhimilivu wa deni la Taifa kulinganisha na vigezo vya Kimataifa, kwa kweli hakuna uchakachuaji. Kwa hiyo, moja tunatazama uwiano kati ya deni na pato la Taifa (debt to GDP ratio) na Kimataifa ni kwamba debt to GDP ratio inatakiwa isizidi asilimia 50, ndiyo viwango vya Kimataifa na kwa Tanzania hivi sasa tuko asilimia 19.9.
Mheshimiwa Naibu Spika, kigezo kingine ni deni la nje kwa uwiano wake na uwezo wetu wa kuuza bidhaa nje (export) na hapa ulimwenguni ukomo wastani ni asilimia 200, Tanzania sasa hivi tuko asilimia 97.7. Pia tunaangalia uwiano kati ya deni la nje na mapato yetu ya ndani na ukomo wa Kimataifa ni asilimia 300, sisi bado tuko asilimia 145.3 kwa hiyo tunaangalia vigezo kama hivi na zaidi ya hapa na kimsingi vigezo vyote vinatuonesha kwamba deni letu ni himilivu.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kidogo kuhusu Serikali kutoa non-cash bond. Naomba niliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Serikali ilishaamua kutoa cash bond na tumechelewa kidogo kwa sababu tumekuja kupata taarifa kwamba baadhi ya madai ya Mifuko yana maswali mengi. Kwa hiyo, kwa maana kwamba sasa tunatoa cash bond kwa kuzingatia madai yapi ilikuwa ni tete na ilikuwa ni muhimu sana kufanya uhakiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu ilashamuagiza Internal Auditor General kufanya uhakiki na bahati nzuri hivi ninavyozungumza amekamilisha uhakiki, anamalizia tu ku-polish ile ripoti yake ili tuweze kufanya uamuzi na kuendelea kutekeleza uamuzi wa Serikali wa kutoa cash bond.
Mheshimiwa Naibu Spika, tulishauriwa na nafikiri alikuwa Mheshimiwa Prosper Mbena, kwamba tuangalie upya mwenendo wa benki kwa sababu kwa kweli hali ya interest rates si nzuri na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, nithibitishe tu kwamba Serikali tumeanza kufanya hivyo. Mtakumbuka kwamba katika kikao kilichopita cha Bunge lako nililieleza Bunge lako uamuzi wa Serikali, kwa mfano kuagiza kwamba fedha ambazo zinashikiliwa na Benki za Biashara, fedha za Serikali za taasisi ambazo zinashikiliwa kwenye benki za biashara zifunguliwe akaunti Benki Kuu ili tuweze kuona fedha hizo ni kiasi gani na zinatumika kufanya nini badala ya benki za biashara kuzitumia kufanya biashara, ikiwa ni pamoja na kufanya biashara za hati fungani za Serikali hiyo hiyo. Kwa hiyo hatua kama hii ni moja ya hatua ambayo inazilazimisha sasa hizi benki ziondoe too focus kwenye makampuni makubwa na kwenye miji ili sasa ziangalie na kwenda kutafuta wateja hata vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunaangalia pia sababu nyingine ambazo zinasababisha interest rate katika benki kuwa kubwa na hii ni pamoja na kutoa elimu ili wananchi wa Tanzania wawe na hakika kabisa kwamba unapokwenda kukopa lazima urudishe na lazima utaratibu huu uendelee kujengwa siyo unakwenda kukopa halafu unaingia mitini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, lazima kuchukua hatua za makusudi kabisa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba Mtanzania anajulikana alipo anafanya shughuli gani, mali zake ni zipi ambazo amekopea na kadhalika. Hizi zote ndizo zinazochangia kwenye gharama za mikopo, kwa hiyo, lazima hizi tushughulike nazo ili riba hatimaye ziweze kuteremka.
Mheshimiwa Naibu Spika, ilikuwepo hoja ya pia kwamba wafadhili kupunguza ahadi zao ni kweli haikubaliki na kwamba ni vizuri Serikali ijulishe dunia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme tu kwamba kwenye hotuba yangu nimeeleza baadhi ya hatua ambazo tumechukua ili kukabiliana na tatizo hili. Moja kubwa ni kuendelea na mazungumzo na wadau wetu wa maendeleo. Kama nilivyoeleza asubuhi tumekwishafikia uamuzi kwamba tunatafuta, tumepata mtaalam elekezi ambaye ni third part na yeye ataangalia pande zote mbili ili kuona changamoto ambazo zinajitokeza (concerns) kwa pande zote ili tuweze sasa kuandaa utaratibu mzuri zaidi wa hii misaada ya wafadhili na kuhakikisha kwamba ahadi zao zinatekelezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ilitolewa observation kwamba pana upotevu mkubwa sana wa mapato bandarini ikiwa ni pamoja na bandari bubu. Hili halina ubishi na Serikali na Wizara inafanya jitihada za makusudi kabisa kuimarisha ulinzi na kuhakikisha kwamba tuna patrol team ambayo inakagua baadhi ya hizi bandari zikiwemo bubu na kufuatilia pale ambapo tunakuwa tumepata taarifa za kiintelijensia juu ya watu ambao kwa makusudi wanatumia bandari zetu kuikosesha Serikali mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli pia kwamba nchi yetu ni kubwa na mipaka yetu ni mirefu, kwa hiyo, njia za panya bado ni nyingi. Wito wangu kwa Watanzania ni kuendelea kutupatia taarifa kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu ili tuweze kwa kadri inavyowezekana kudhibiti mipaka yetu na bandari zetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tulishauriwa hapa kwamba Tume ya pamoja ya fedha ifanye kazi yake. Mheshimiwa Waziri anayesimamia masuala ya Muungano alilieleza vizuri kwamba kwa kweli waraka ulishaandaliwa ambao ni pamoja na kuhakikisha kwamba, kwa mfano mgawanyo wa mapato baina ya Serikali zetu mbili, unafanyika vizuri na kwa makubaliano ya pande zote na tume ya pamoja ya fedha kwa kweli ni interest ya kila mtu kwamba ifanye kazi yake vizuri ili Muungano wetu uendelee kuimarika.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa kulisemea ni hili la malipo ya wazabuni kwamba watalipwa lini? Niseme tu kwamba Wizara ya Fedha na Serikali kwa ujumla imedhamiria kuongeza kasi ya kumaliza malimbikizo halali, nirudie tena malimbikizo halali ya madai ya wazabuni. Bahati nzuri kwa kuwa sasa makusanyo ya Serikali yanaimarika kwa kweli ni dhamira ya dhati kabisa ya Serikali kwamba tuyamalize haya mapema inavyowezekana.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia nitumie nafasi hii kusisitiza kwa wazabuni, wote ni muhimu sana wanapowasilisha madai yao yakawa ni ya kweli. Pawepo uaminifu katika madai ambayo yanawasilishwa kwa sababu kila mara Ofisi ya Internal Audit General inapofanya kaguzi zake, inapofanya uhakiki tumegundua kuna madai mengi hewa. Kwa hiyo, nao watusaidie, ni sehemu ya kufanya machelewesho kwa sababu ni lazima tuhakikishe kwamba tunalipa madai halali na siyo kutumia fedha za umma isivyo sawasawa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tulipokea maoni kwamba utumbuaji wa majipu mamlaka ya mapato umezaa mapato zaidi. Ni kweli na napenda nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba kwa hili tutaendelea tutawatumbua Watumishi wasio waadilifu, tutawashughulikia kikamilifu. Wakati huo huo niwapongeze sana watumishi wema wa Mamlaka ya Mapato ambao wameendeelea kufanya kazi yao nzuri sana na kwa sasa tuna zaidi ya trilioni moja kama mapato ya Serikali ya kodi kila mwaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Shirika la Bima la Taifa, kama mpango wa kulifufua na kuliongezea uwezo uko wapi? Hata bodi kwamba iko na walio wengi kwenye management wanakaimu. Napenda niseme tu kwamba, Wizara yangu imefikia hatua nzuri kuteua Wajumbe wa Bodi na ninavyozungumza Wajumbe wanaopendekezwa wanafanyiwa upekuzi na mara baada ya bodi kuundwa basi bodi hiyo nayo tutaielekeza mara moja ishughulikie suala la Maafisa Waandamizi ambao bado wanakaimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia ndani ya Serikali tumekwishatoa maelekezo kwamba kwa kadri inavyowezekana Taasisi za Umma na Mashirika yake zitumie National Insurance Corporation ili tuweze kuhakikisha kwamba tunaliongezea mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja juu ya Mfuko wa Mahakama lakini pia ukweli kwamba kuna upungufu wa Mahakimu lakini hata hali yenyewe ya Mahakama zetu, Mahakama za Mwanzo hairidhishi na inahitaji kuboreshwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni jambo la msingi kabisa na Serikali inatambua hili, ndiyo maana mapema mwaka huu Mheshimiwa Rais, aliagiza Mfuko wa Mahakama uongezewe fedha na tulifanya hivyo, tuliwaongezea fedha za maendeleo Shilingi bilioni 12.6 na moja ya kazi ya fedha hizi ni kwa ajili ya kuhakikisha miundombinu ya Mahakama inajengwa na Serikali itaendelea kufanya hivyo kwa kuwa tunatambua umuhimu wa Mhimili wa Mahakama katika kutoa haki.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nilisemee suala la tuhuma ambazo zimetolewa kuhusu Benki Kuu kufungua makampuni na watumishi wanachukua tenda za Benki Kuu ambazo zinajumuisha kazi za siri. Naomba tu nikiri hapa kwamba taarifa hii nimeisikia hapa mbele ya Bunge lako Tukufu na namwomba Mheshimiwa aliyetoa hoja hii atupatie taarifa kamili niko radhi kabisa tuzungumze tupate hizo taarifa na tutazifanyia kazi tuhuma hizi mara moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nilisemee hili la kwamba Serikali haijasaidia kukuza sekta binafsi na hususani baadhi ya kodi na sheria ambazo zinakuwa ni kero kwa Waajiri na pengine na baadhi yao hazina tija.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba niseme kwamba namwombaMheshimiwa Mbunge aliyetoa hoja hii asubiri na asikilize hotuba yangu ya bajeti ya Serikali Kuu Jumatano ijayo kwa hamu baadhi ya mambo haya tutayashughulikia. Hata hivyo, niseme tu kwamba ni kweli baadhi ya vipengele vya sheria yetu ya kazi vimekuwa vinalalamikiwa na wawekezaji na kwamba pengine haitoi fursa kwa waajiri kuchukua hatua ingawa pia kuna upande mwingine kwamba baadhi ya waajiri nao wanawanyanyasa wafanyakazi wao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba Serikali ni sikivu, imesikia na inaendelea kusikia na ndiyo maana Mheshimiwa Rais, kati ya makundi ya kwanza aliyokutana nayo mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wawakilishi wa wafanyabiashara na kusikiliza kero zao ili kuweza kuhakikisha kwamba mazingira ya kuwekeza na kufanya biashara ikiwa ni pamoja na marekebisho yanayotakiwa kwenye hizi sheria yanafanyiwa kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nilifuata hatua za Mheshimiwa Rais wetu na nimeshafanya mikutano na wafanyabiashara Dar es Salaam na Arusha lakini lengo ilikuwa ni hilo hilo, kwamba tuzielewe vizuri changamoto ambazo wanakabiliana nazo ili tuweze kuzifanyia kazi na kupata suluhisho mara moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, nisisitize kwamba wakati nawasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano hapa nilisema wazi kabisa kwamba Serikali ya Awamu ya Tano moja ya msisitizo mkubwa ni kuhakikisha kwamba mazingira ya biashara na uwekezaji haya tutayawekea mkazo zaidi katika awamu hii maana hatutaweza kujenga viwanda katika nchi yetu kama mazingira ya wawekezaji na waajiri hayako sawasawa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja pia kwamba kwa nini Serikali isiingie katika uwekezaji mkubwa na hususan wa miundombinu kupitia PPP. Niseme tu kwamba kwa kweli hii ndiyo njia nzuri na njia mbadala ya kuhakikisha kwamba nchi changa kama yetu basi itakuwa na uwezo wa kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo na hasa ile ambayo inagharimu fedha nyingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba niseme mawili. Bahati mbaya ni kwamba experience ya nchi yetu katika PPP haikuwa nzuri sana. Mtakumbuka kwa mfano tulipopeleka utaratibu wa PPP kwenye sekta ya maji na kwenye sekta ya umeme matokeo yake yalikuwa si mazuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukweli pia ni kwamba PPP bado ni mfumo mgeni na unahitaji ujuzi ikiwa ni pamoja na negotiation katika kuingia ubia. Kwa hiyo tumeanza sasa, ndiyo maana tunacho kitengo pale ndani ya Wizara ya Fedha kwa ajili hii, ambacho bado kinajengwa. Tumeanza na miradi michache, ni matumaini yangu kwamba tutapiga hatua nzuri na kwa haraka kutumia mfumo huu kwa haraka zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, labda nimalizie kwa kusema juu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina. Ofisi ya Msajili wa Hazina ni chombo muhimu sana maana hili ndio hasa jicho la Serikali kwa ajili ya kumiliki mali ambazo tumewekeza kwenye taasisi mbalimbali za umma.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba Ofisi hii imefanyiwa maboresho makubwa ikiwa ni pamoja na marekebisho ya sheria inayoongoza chombo hiki, lakini pia tumebadilisha uongozi ikiwa ni pamoja na kupata Treasury Registrar mpya ambaye ana uzoefu kutoka sekta binafsi lakini pia tunaendelea na jitihada za kuiongezea taasisi hii watumishi wenye weledi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo niseme tu kwamba uzuri katika kipindi kifupi ambacho mabadiliko haya yamefanyika tumeanza kuona matunda kwa maana ya kuongezeka kwa mapato, lakini dividend kutoka kwenye Mashirika haya. Kwa hiyo, nafikiri ni hatua nzuri, Waheshimiwa Wabunge naomba tuendelee kuiunga mkono ofisi hii ili ifanye kazi yake vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uwezo wa Mashirika kama TTCL kwa nini nashindwa kuingia kwenye ushindani naomba niseme tu kwamba tumekuwa na changamoto toka tulipo anza kuingia kwenye ubinafsishaji na management ya TTCL kwa kweli bado ni mpya inaendelea kujipanga. Naamini ndani ya muda mfupi tutaona mabadiliko.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini haya Mashirika kwa kweli hatuwezi kusema tu kwamba kwa sababu kwa sasa hivi yanaonekana ni mzigo basi tuyatupe. Ni muhimu ni sisitize kwamba baadhi ya haya mashirika ikiwa ni pamoja na TTCL ni mashirika ambayo ni ya kimkakati, very strategic kwa ajili ya usalama wa nchi lakini pia kwa maana ya contribution yake kwenye uchumi wa Taifa. Kwa hiyo, hatuwezi kuyatupa tu, ni lazima tuyafanyie kazi ili tuweze kuyafufua.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa kumalizia nichukue nafasi hii kuwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri na ushauri wao. Kama nilivyosema naahidi kuwa ushauri mliotupatia tutaufanyia kazi na tutauzingatia vizuri kwa umakini katika utekelezaji wa bajeti hii na bajeti zijazo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tutakapoingia kwenye hatua zinazofuata Waheshimiwa Wabunge waunge mkono hoja yangu ili tuweze kuendelea kutekeleza haya ambayo tumewaelezeni toka asubuhi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kuniruhusu kusimama hapa ili kuhitimisha mjadala wa Bunge lako Tukufu kuhusu Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2016/2017 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 niliyoyawasilisha tarehe 8 Juni, 2016.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee nakupongeza sana kwa umahiri na weledi wa hali ya juu ulioonesha katika kusimamia Kanuni za Bunge wakati wote wa kikao hiki cha Bunge la Bajeti. Hakika viwango vyako ni vya kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, japokuwa Mheshimiwa Kakunda, mwanafunzi wangu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alichomekea sehemu fulani akidai kwamba mimi ni bahiri. Nadhani alimaanisha kwamba ni bahari wa kutoa maksi za upendeleo. Nataka niliambie Bunge lako Tukufu kwamba viwango vyako Mheshimiwa Naibu Spika ambavyo umevionyesha humu ndani hakika ningekuwa bado niko kule chuoni ningekupatia maksi za haki, asilimia 100 kama walivyofanya Maprofesa wako wa Sheria pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini pia University of Cape town, hongera sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutambua michango iliyotolewa na Kamati ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini. Japokuwa ameingia mitini, napenda pia kutambua mchango wa Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango lakini pia michango ya Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza au kwa maandishi hapa Bungeni, nawashukuru wote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya Wabunge 171 wamechangia hoja niliyowasilisha. Kati ya hao, 146 wamechangia kwa kuzungumza na 25 kwa maandishi. Napenda kuwashukuru wote. Pia niwashukuru Waheshimiwa Mawaziri tisa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliochangia asubuhi hii. Kipekee namshukuru sana Mheshimiwa Dokta Ashatu Kachwamba Kijaji kwa kunisaidia kujibu hoja kwa umahiri mkubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hatua ambazo zilipongezwa na Wabunge wengi wakati wa mjadala huu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/2017. Moja ambalo Waheshimiwa Wabunge mlilisema na kulipongeza ni Serikali kuthubutu kuweka lengo la bajeti ya shilingi trilioni 29.5 ikilinganishwa na shilingi trilioni 22.5 mwaka huu fedha tunaomalizia na kati ya hizo kutenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Miradi hii ya maendeleo ni pamoja na uthubutu wa kuanza kujenga reli mpya ya kati kwa kiwango cha standard gauge, barabara, umeme, ununuzi wa meli mpya na ndege tatu za abiria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia Waheshimiwa Wabunge walipongeza sana uamuzi wa Serikali kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi na hadi sasa tumefikia wastani wa shilingi trilioni 1.2 kwa mwezi kwa kuziba mianya ya uvujaji wa mapato na kuimarisha matumizi ya vifaa vya kieletroniki (EFDs). Pia Waheshimiwa Wabunge walipongeza uamuzi wa Serikali wa kusimamia nidhamu ya matumizi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo. Pamoja na mambo mengine Waheshimiwa Wabunge wamepongeza azma ya kufanya kazi na kurejesha nidhamu ya watumishi kazini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, yako mambo mengine mengi ambayo Waheshimiwa Wabunge walipongeza. Napenda nimalizie tu na moja la mwisho ambalo ni azma ya Serikali kujielekeza kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015, ahadi za Viongozi Wakuu na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2020-2025 ili kutatua kero za wananchi hasa masikini.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Waheshimiwa Wabunge walitoa ushauri katika maeneo mbalimbali, nitazungumzia machache. Moja, Waheshimiwa Wabunge wameshauri kuongeza tozo ya mafuta ili mapato hayo yatumike kupanua huduma za maji na kukamilisha vituo vya afya na zahanati vijiji. Pia walishauri kwamba mfumo wa kodi uboreshwe ikiwa ni pamoja na kufuta kodi zaidi, ushuru na tozo za kero kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanyabiashara hasa wadogo. Pia kutoa ahueni ya kodi kwenye taulo za akina mama na vifaa vya watu wenye ulemavu, vifaa vya michezo, zana za uvuvi na kulinda viwanda vya ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge walishauri kwamba ni muhimu kuimarisha elimu na kuhakikisha inaendana na mahitaji na wataalam wa Tanzania ya leo na kesho. Walishauri Serikali ichukue hatua za ziada kuimarisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na hususan kuongeza kilimo cha umwagiliaji, pembejeo, ugani, utafiti, mnyororo wa thamani, masoko, ruzuku, mikopo na bajeti ya kilimo. Waheshimiwa Wabunge waliishauri Serikali ipanue wigo wa kodi hasa katika sekta ambazo zina mapato makubwa kama mawasiliano, madini, maliasili na ardhi na sekta zenye fursa kama uvuvi na biashara kwenda nchi jirani lakini pia e-commerce, gawio kutoka kwenye mashirika ya umma na kuhakikisha kila mwananachi analipa kodi stahiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri uliotolewa ni mwingi sana na mzuri na Serikali itauzingatia katika bajeti hii na bajeti zinazokuja.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nianze kufafanua baadhi ya hoja na kama nilivyosema michango ilikuwa mingi haitakuwa rahisi kujibu hoja zote pamoja na zile zilizojibiwa na Waheshimiwa Mawaziri, nitajibu chache tu. Najua hoja hizi nyingine zilielezwa kwa hisia kali na wengine walinikaribisha Bungeni wakisema Waziri wa Fedha na Mipango amewa-beep Waheshimiwa Wabunge na wengine walisema Waziri wa Fedha hana jimbo ndiyo maana haoni machungu. Mimi nadhani walikuwa wananikaribisha tu Bungeni, kazi ya Waziri wa Fedha ina changamoto nyingi, inanilazimu niwe mtu ambaye hana maneno matamu tu lakini matupu, inanilazimu niwe mkweli na kuwaeleza kile ambacho kinawezekana na kile kisichowezekana ili kujenga nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja moja ambayo ilisemwa sana ni pendekezo la kuongeza tozo ya Sh.50 kwenye mafuta kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Maji na kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya na zahanati vijijini. Niseme tu kwamba hili ni pendekezo ambalo lina lengo zuri na Serikali inalipokea. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, ni vyema kutambua kwamba kufuatia kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia gharama ya mafuta yote ambayo tumeagiza kama taifa kutoka nje imepungua kwa takribani asilimia 20 na imechangia kushuka kwa mfumuko wa bei na sasa mfumuko wa bei uko asilimia 5.2 na mwenendo huu umeleta ahueni kwa maisha ya wananchi wetu walio wengi. Hata hivyo, Serikali imeamua kwamba kwa wakati huu hatutaongeza tozo kwenye mafuta ili wananchi waendelee kunufaika na huo unafuu wa bei ya mafuta. Ni wazi kwamba ongezeko la tozo katika mafuta ya petroli na dizeli litasababisha kupanda kwa bei ya mafuta jambo ambalo litaongeza gharama ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa chakula na bidhaa ikiwa ni pamoja na vifaa vya ujenzi na huduma nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niwaambie Waheshimiwa Wabunge pia kwamba wataalam wa uchumi wanashauri kwamba katika kipindi ambacho kuna uwepo wa bei ndogo ya mafuta, ni wakati mzuri kwa nchi kuwekeza hususan katika miundombinu, viwanda ambavyo ni energy intensive na kuendeleza ujuzi na teknolojia. Kwa hiyo, ndiyo sababu Serikali inaona kwamba ni busara zaidi badala ya kuongeza tozo kwenye mafuta tujielekeze kuongeza bajeti ya kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ya usafirishaji, nishati na elimu sambamba na kutumia pesa zilizopangwa kwa ufanisi zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu mkubwa wa huduma ya maji nchini ambayo pia ni Ilani ya CCM, tuliongeza bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Maji kutoka shilingi bilioni 373 hadi shilingi bilioni 690.16 kwa mwaka ujao wa fedha. Kwa hiyo, kama Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI alivyoeleza, Serikali inapenda itumie mwaka huu kujipanga na kujua majengo ya afya ambayo yamekwama kwa mwaka huu ili utekelezaji uanze ukiwa umepangwa vizuri mwaka 2017/2018. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ilikuwa ni pendekezo la kuondoa msamaha wa kodi ya mapato kwenye kiinua mgongo cha Waheshimiwa Wabunge. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, kodi ya mapato inatozwa kwenye vyanzo vyote vya mapato na kiinua mgongo ni chanzo kimojawapo cha mapato kinachotambuliwa na sheria na hutozwa kodi. Kupitia Jedwali la Pili la Sheria ya Kodi ya Mapato kiinua mgongo kinacholipwa kwa Wabunge wakati wanapomaliza muhula wa miaka mitano kimesamehewa kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, msamaha huu hauzingatii usawa wa utozwaji kodi kwani watu wengine wote wanaopata malipo ya kiinua mgongo, iwe ni sekta binafsi au utumishi wa umma wanatozwa kodi katika mapato hayo. Kwa hiyo, hatua niliyoitangaza tarehe 8 Juni, 2016 imechukuliwa ili kujenga msingi wa usawa na haki katika ulipaji wa kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la kufanya marekebisho hayo hivi sasa ni kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaotumika kukokotoa stahili za Mbunge endapo ukomo wa Mbunge yeyote utatokea katika kipindi cha kuanzia sasa (Julai 2016) na kuendelea. Pia mabadiliko haya yanafanyika sasa ili kuzingatia msingi wa utozaji kodi ambao unataka kodi iwe inatabirika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niliarifu Bunge lako Tukufu na wananchi wa Tanzania kwamba siku nilipowasilisha pendekezo hili la kufuta msamaha wa kodi kwenye kiinua mgongo cha Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanza alinishangaa akasema yeye ni Mtanzania na ni lazima Watanzania wote walipe kodi ili kuijenga nchi yetu. Kwa kuwa kiongozi lazima aongoze kwa mfano, Mheshimiwa Rais alielekeza kuwa yeye ni Mbunge wa Tanzania yote na anapenda awe wa kwanza kukatwa kodi stahiki kwenye mafao yake ya kustaafu. Naomba nirudie, alielekeza kuwa yeye ni Mbunge wa Tanzania nzima na anapenda awe wa kwanza kukatwa kodi yake stahiki kwenye mafao yake ya kustaafu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napenda kufafanua kwamba marekebisho niliyowasilisha tarehe 8, Juni, 2016 maana yake ni kuwa kiinua mgongo cha viongozi wote wa kisiasa ambao wametajwa kusamehewa kodi chini ya Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa sasa kitakatwa kodi. Maana yake ni kwamba Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, kiinua mgongo chake kitakatwa kodi. Mheshimiwa Waziri Mkuu, yeye ni Mbunge wa Ruangwa, kiinua mgongo chake kitakatwa kodi. Mheshimiwa Naibu Spika na wewe kiinua mgongo chako kitakatwa kodi. Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, sisi wote ni Wabunge, lazima tuongoze kwa mfano, kiinua mgongo chetu kitakatwa kodi. Vivyo hivyo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kiinua mgongo chao kitakatwa kodi. Waheshimiwa Wabunge, hii ndiyo dhamana ya uongozi, we have to lead by example. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, palikuwepo hoja ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwamba imetengewa fedha kidogo na haitaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Wengine walizungumza kwa lugha kali kidogo kwamba Waziri wa Fedha na Mipango ana dhamira gani na CAG, je, CAG ni adui wa Serikali, la hasha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukomo wa bajeti ya OC ilitengwa kwa mafungu mbalimbali kwa kuzingatia maamuzi ya Serikali na mkakati wa kupunguza matumizi ya kawaida ili tuelekeze fedha nyingi zaidi kwenye miradi ya maendeleo. Katika kufikia ukomo wa matumizi mengine kwa Serikali nzima, uchambuzi wa kina ulifanyika ili kubaini mahitaji ya fedha ambayo siyo ya lazima kwa wakati huu na hayawezi kuathiri utendaji. Kwa hiyo, tulitazama yote hayo na fedha ambayo tumeweza kutenga kwa sasa ndiyo hiyo na tuna hakika kabisa kwamba Ofisi ya CAG itaendelea kufanya kazi yake ipasavyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua umuhimu wa majukumu ya msingi ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kama ilivyo kwa taasisi nyingine nyeti ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama, mihimili mingine ya dola na uwezo wa kukabiliana na dharura, kama patajitokeza mahitaji ya lazima, napenda tena kusisitiza mbele ya Bunge lako Tukufu kwamba tutahakikisha kwamba ofisi hiyo haikwami. Mahitaji hayo ya ziada yatazingatiwa wakati wa mapitio ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, uhuru wa CAG katika kufanya kazi zake ni wa kikatiba na hautaingiliwa. Waziri wa Fedha na Mipango atakuwa mtu wa mwisho kukwamisha kazi za ofisi hiyo ambayo inamsaidia kufichua mchwa wa fedha za umma kwenye Wizara na halmashauri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja ya tathmini ya hali ya umaskini kimkoa. Naomba tu niseme kwamba viashiria vya kupima umaskini nchini huwa vinapatikana kwa kutumia utafiti wa mapato na matumizi ya kaya ambao unafanyika katika nchi yetu kila baada ya miaka mitano. Utafiti huo kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2011/2012. Utafiti huo ukichanganya na taarifa zinazotokana na sensa iliyofanyika mwaka 2012 ndiyo unatuwezesha kuweza kuchambua hali ya umaskini wa kila mkoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba sababu ambazo zinaeleza kwa nini kiwango cha umaskini katika Mikoa kama Mwanza, Kigoma, Singida, Geita na Kagera ni kikubwa ukilinganisha na Mikoa kama Lindi na Mtwara ni nyingi. Kwanza kwa ujumla umaskini wa kipato ni mkubwa zaidi pale ambapo kuna wananchi wengi zaidi wanaishi vijijini ukilinganisha na mijini. Kwa mfano ukiangalia Mkoa wa Mwanza, mwaka 2000/2001 wakati bado Geita iko humo kiwango cha umaskini kilikuwa ni asilimia 48. Umaskini wa kipato wa Geita kabla ya kugawanywa ulikuwa ni asilimia 62.3 lakini baada ya kutenganishwa kiwango cha umaskini wa kipato katika Mkoa wa Mwanza unateremka lakini kiwango cha umaskini katika Mkoa wa Geita kinaendelea kubakia juu na sababu kubwa ni kwamba wananchi wengi zaidi wa Geita wanaishi vijijini ambapo shughuli zao za uzalishaji mali hazikidhi kupunguza kiwango cha umaskini kwa kasi inayotarajiwa. Ukiangalia wilaya ambazo ziko karibu na miji, kiwango cha umaskini ni kidogo zaidi kuliko kiwango cha umaskini katika maeneo ya vijijini.
Mheshimiwa Naibu Spika, umaskini pia ni lazima uende na hali ya kimaeneo. Kwa mfano, Mkoa wa Kigoma kwa kiasi kikubwa umaskini wa kipato katika mkoa huu unachangiwa na miundombinu hafifu ya usafirishaji ambayo inapunguza fursa ya kufikia masoko. Kigoma pia inabeba mzigo mkubwa sana wa wakimbizi na kusababisha ziada ambayo inazalishwa kutumika kulisha wakimbizi na kupunguza ustawi wa kaya katika mkoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama ni mkakati, cha kwanza ni kutambua kwamba kuna hilo tatizo na sababu zake lakini pia kujielekeza sasa kufungua fursa katika mikoa na wilaya husika. Pia kuja na interventions kama zile za TASAF ambazo zinalenga kusaidia kaya maskini kabisa lakini pia miradi ya afya na maji na pia specific interventions ambazo zinakwenda kushughulikia matatizo katika maeneo mahsusi kama vile tatizo la mnyauko wa migomba kule Kagera na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema tutawasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kwa hoja zote ambazo Waheshimiwa Wabunge walizitoa. Naomba nieleze moja kabla ya kuhitimisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ililetwa hoja hapa kwamba dollarization imekuwa ni kero kubwa na inasababisha thamani ya shilingi kuteremka. Naomba tu niseme dollarization ni matumizi ya sarafu ya kigeni katika nchi husika sambamba na sarafu ya nchi hiyo. Dollarization kitaalam inachochewa na vitu kadhaa hususan mfumuko wa bei kama ni mkubwa lakini pia kama thamani ya sarafu ya nchi husika nayo inateremka lakini katika nchi ambazo hakuna usalama.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Tanzania sababu kubwa ni kwamba tumekuwa na mapato kidogo ya fedha za kigeni lakini pia dola imeongezeka sana nguvu kutokana na kuongezeka kwa uchumi wa Marekani na kuchelewa kupata misaada ya general budget support. Kwa kawaida wananchi wanatumia hiyo sarafu ya kigeni ili kujikinga na athari za mfumuko wa bei yaani they hedge against the inflation risk. Mazingira mengine ambayo yanachochea dollarization kama nilivyosema ni kukosekana utulivu wa kisiasa ambayo sisi bahati nzuri hatuna.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuondoa hili tatizo linahitaji muda na ukichukua hatua za kiamri, za kiutawala kusema tu sasa kuanzia leo watu wasitumie dola, uzoefu wa nchi mbalimbali ulimwenguni unaonesha kwamba hizo sera hazifanyi kazi. Utatia woga katika uchumi na watu wataanza kukimbiza fedha za kigeni na kuleta matokeo yasiyotarajiwa. Kwa hiyo, mkakati siyo kulazimisha au kudhibiti matumizi ya hizo dola, inatakiwa iende sambamba na sera za kisoko za kudhibiti tatizo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa watu ambao wanapenda kusoma wanaweza wakatafuta jarida linapatikana kwenye internet „Dollarization in Sub-Saharan Africa: Experience and Lessons 2015‟, inawaonesha experience ya nchi nyingine na hatua ambazo walichukua hazikufanikiwa. Kwa hiyo, tunachukua kila tahadhari kuhakikisha tunaendelea kubakia na uchumi wetu tulivu.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niwasihi Waheshimiwa Wabunge, kwamba bajeti niliyowasilisha inajielekeza kuanza kazi ngumu ya kuitoa Tanzania kutoka nchi inayotegemea kilimo duni kuwa nchi ya uchumi wa viwanda, nchi ambayo wananchi wake wameondoka kwenye lindi la umaskini ili twende mbele. Kwa hiyo, yote tunayopanga, katika mipango na bajeti ya Serikali, ni muhimu sana kutanguliza maslahi ya Taifa letu lakini pia maslahi ya Watanzania maskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Bunge lako Tukufu kuikubali bajeti hii, utekelezaji wake utahitaji kujitoa. Mheshimiwa Makamba amesema tutahitaji sacrifice, tutahitaji selfless service to our country. Tunahitaji kuvuja jasho ili tuweze kuwainua maskini.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna mambo mawili tunaweza kufanya, tunaweza tukaamua kuendelea na mazoea yaani business as usual ambayo siyo option kwetu lakini njia sahihi ni kuachana na mazoea. Ili kuachana na mazoea lazima tuanze sisi viongozi. Itatubidi tuachane na maslahi binafsi hata kama mara kadhaa inaonekana tunayavisha koti au kilemba cha maslahi ya wengi.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Nilikuwa nasema tuna dhamana kubwa ya kuleta mabadiliko makubwa katika kuendesha shughuli zote za umma na matumizi ya rasilimali za Taifa ili tuweze kupiga hatua kubwa za kuitoa nchi yetu katika umaskini. Ni lazima kila mwananchi atambue wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika nyanja zote na uzalendo kwa Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie tena kuzielekeza Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuzingatia hatua za kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kusimamia matumizi ya Serikali na hatua za kupunguza gharama na kulipa na kuzuia ongezeko la madeni ya Serikali. Serikali ina dhamira ya dhati ya kuchukua hatua hizo na naomba Watanzania watambue kwamba ni lazima kujinyima, kujituma na kuvuja jasho ili kupata maendeleo na kupunguza utegemezi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie tena, wajibu wa kwanza wa kuiendeleza nchi yetu ni ya sisi Watanzania wenyewe, tunazo akili za kutosha na rasilimali nyingi na fursa tele kuweza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na ya uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Nawaomba tena Waheshimiwa Wabunge kuunga mkono hatua zinazoongozwa na Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa tunaimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, mapato ya kodi na yasiyo ya kodi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo yenye tija na hususani ujenzi wa viwanda kwa manufaa ya Watanzania wote.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya kuongoza Wizara hii nyeti sana na vilevile kwa hotuba yao nzuri sana ambayo kwa kweli ni ya kina. Na niseme moja kwa moja kwamba naunga mkono hoja iliyotolewa na nawaomba Waheshimiwa Wabunge wakubali kuidhinisha bajeti hii kama ilivyowasilishwa, maana hii ndio msingi wa uchumi wa viwanda ambao tunajaribu kujenga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia nzima kinachotofautisha nchi maskini na nchi ambazo zimeendelea ni ubora wa miundombinu yake. Sasa tatizo ni kwamba, ujenzi wa miundombinu bora tunaihitaji wote, lakini ina gharama kubwa sana na hivyo ni lazima tuijenge kwa awamu, lakini twende kimkakati tukianza na maeneo ambayo yatatusukuma kwa haraka kama Taifa. Kwa hiyo, sequencing ni lazima na hakuna nchi yoyote ulimwenguni ambayo ina uwezo wa kujenga miundombinu yote wanayoihitaji kwa wakati mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizichangie hoja chache ambazo zilizungumzwa humu ndani na moja wapo imejirudia ni ile inayohusu uhamisho wa fedha. Nisisitize tu kwamba, uhamisho wa fedha ambao unafanywa na Serikali baina ya mafungu na ndani ya mafungu unaongozwa na sharia; kuna vitu viwili vikubwa ambavyo vinazingatiwa katika kufanya uhamisho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni kutekeleza maamuzi ambayo yana maslahi kwa Taifa na sheria inasema hivyo, lakini la pili, unaweza ukafanya uhamisho; Waziri wa Fedha anaruhusiwa kufanya uhamisho pale ambapo kuna mahitaji ya dharura. Ukisoma Sheria ya Matumizi (Appropriation Act), inasema vizuri katika kifungu kile cha 6(1), inaeleza ni mazingira gani ambayo Waziri wa Fedha anaruhusiwa kufanya uhamisho, sijui kama ni lazima nisome, lakini Waheshimiwa Wabunge nawasihi tena kwenda kuziangalia zile sheria vizuri. Hatuwezi kufanya uhamisho kinyume cha sheria, ziko bayana, lakini vilevile Sheria ya Bajeti, Kanuni ya 28(1), inasema wazi kwamba reallocations zote kati ya mafungu ni lazima zipate idhini ya Waziri wa Fedha kwa hiyo, huwezi tu ukafanya hivi hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sio hivyo tu, kifungu cha 41 kinasema vilevile kwamba kinaweka masharti ya kufanya uhamisho kati ya mafungu na kinasema; all reallocations between votes shall not exceed 5% of total government budget na haya yote tumekuwa tunayazingatia. Sasa nilikwisha liarifu Bunge lako tukufu kwamba katika mwaka huu wa fedha tulionao, Fungu 98 - Ujenzi; Bunge hili liliidhinisha shilingi bilioni 798.26 kwa ajili ya fedha za maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia mwezi Machi tulishatoa shilingi bilioni 931 kwa ajli ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Na nilishaeleza hili kwamba ukichukua tarakimu hizi ni kweli kabisa tumeshatoa fungu zaidi ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwenye hicho kifungu, lakini narudia kwa kuzingatia maelekezo ya sheria. Fedha zilizotolewa na Serikali zilitoka Fungu 21 ambalo ni Mradi Namba 6294 ambapo Bunge, kwenye kifungu kile lilikuwa limeidhinisha shilingi bilioni 628.5 kwa ajili ya kulipia madeni mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulihamisha fedha kutoka fungu hili kwenda fungu 98 kulipia madeni ya miundombinu kwa hiyo, nilishalieleza na fedha zilizozidi ni shilingi bilioni 133.04 ambazo ni sawa na asilimia 0.6 tu ya bajeti yote ya Serikali ya shilingi trilioni 22.5. Kwa hiyo, narudia tena katika kufanya uhamisho wa fedha tunazingatia kikamilifu Sheria ya Bajeti, hakuna mahali ambapo tunakiuka utaratibu huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kulisemea kulikuwa na ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwamba tutenge fedha zaidi kwa ajili ya mindombinu na angalau ifike asilimia 20 ya bajeti yote ya Serikali. Ninawaelewa vizuri kabisa, kama nilivyotangulia kusema miundombinu ndio kikwazo kikubwa ambacho kinachelewesha maendeleo ya nchi yetu, kwa hiyo, ni ombi halali kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka ujao wa fedha 2016/2017 tumetenga zaidi ya shilingi trilioni saba kwa jaili ya miundombinu kwa maana ya uchukuzi, barabara, maji, mawasiliano, nishati na umwagiliaji. Na hii peke yake ni asilimia 24 ya bajeti yote ya Serikali, kwa hiyo, tunapiga hatua kuelekea kwenye ushauri huu ambao tuliupokea kutoka kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nisemee moja lingine ambalo linahusu Himaya ya Forodha, kwa pamoja ni Single Customs Territory, hili nilikwishalielezea, lakini linajirudia tena. Kwa hiyo, niseme mfumo huu unawezesha ushuru wa forodha wa mizigo inayoingia kwenye nchi kama ya kwetu ulipiwe moja kwa moja katika nchi ambayo mizigo ile inafikia badala ya kwenda kulipiwa kwenye destination country. Sasa huu ni mfumo mpya ambao unatumika kwa Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwa Congo pia tumekubaliana kwamba tutumie mfumo huu. Sasa wale ambao walizoea utaratibu wa zamani na wakawa wanakwepa kodi chini ya utaratibu wa zamani wanaukimbia huu ili wasilipe kodi ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nilishalitaarifu Bunge lako kwamba pamoja na kuona hitilafu hiyo, nilikwishatoa maagizo kwa TRA na Mamlaka ya Bandari kulichunguza jambo hili kuona jinsi ambavyo kweli, linaathiri kiasi cha mizigo inayopita katika Bandari yetu ya Dar es Salaam. Na nilisema hivyo kwa sababu ukiangalia trend katika bandari nyingine ulimwenguni kwa miezi ya karibuni na hususani kuanzia mwezi Januari, tunaona pia bandari nyingine ambazo haziko katika mfumo huu nazo mizigo yake imeathirika. Na nilieleza kwamba hisia mojawapo inaweza kuwa ni madhara ya kuporomoka kwa uchumi wa China ambao ume-affect biashara katika nchi ambazo inafanya nazo biashara, lakini hili linahitaji kufanyiwa uchambuzi wa kina ili kujua ukweli ni nini na kuweza kuchukua hatua ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme pia kuhusu mgongano ambao unasema kuna mgongano wa tozo ya hifadhi za mizigo. Moja inalipwa kama customs… (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe binafsi, Mheshimiwa Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha majadiliano kwa ufanisi kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nitambue michango mizuri iliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini na Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninatambua pia mchango wa Waziri Kivuli na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango Mheshimiwa Halima James Mdee, Mbunge wa Kawe. Aidha, ninawashukuru kwa dhati Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia mjadala huu ambapo kwa kuzungumza walichangia Wabunge 70 na kwa maandishi wamechangia Wabunge 48 wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri na Waheshimiwa Naibu Mawaziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla mjadala ulikuwa mzuri na baadhi ya maoni yalitolewa kwa hisia kali na mimi ninaamini kwamba, kwa kuzingatia umuhimu wa uchumi katika nchi yetu ni jambo jema tukawa tunachambua, tukabishana na hatimaye turidhiane juu ya vipaumbele, mikakati na hatua stahiki za kukuza uchumi wa Taifa kwa namna ambayo ni endelevu zitakazo wezesha nchi yetu kufikia malengo ya dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia kuwa tumepokea michango na hoja nyingi tena sana kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge naomba niahidi hapa kuwa nitawasilisha Bungeni taarifa ya maandishi inayofafanua hoja zote zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema yako maoni na ushauri mwingi uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge, ninaomba nisiseme kwa kifupi yale yaliyosemwa ni mengi sana, nilitamani walau niseme hata kumi tu kwa msisitizo ili mjue kwamba tunasikia, lakini kwa ajili ya muda naomba nijielekeze zaidi kufafanua hoja chache hasa zile ambazo nadhani ni muhimu tukaelewana vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni hoja kubwa ambayo toka mwanzo mpaka mwisho imesemwa kwamba uchumi unahali mbaya, uchumi umedorora na kwamba kuna manung’uniko ya wananchi mtaani.
Mheshimiwa Naibu Spika, uchumi wa Taifa unapimwa kwa vigezo vingi, haupimwi kwa kigezo kimoja wala viwili, nitasema baadhi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, viko vigezo vya ujumla, ukuaji wa Pato la Taifa. Uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Januari mpaka Juni, 2016 kwa wastani umekuwa kwa asilimia 6.7 ukilinganisha na asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Asilimia 6.7 ni kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi. Ngoja niwapeni mfano, wastani wa ukuaji wa uchumi kwa Sub-Saharan Africa kwa mwaka 2016 ni asilimia 1.4 tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya wanakuwa kwa asilimia 6, Uganda asilimia 4.7, Mozambique asilimia 6.5, Tanzania quarter hii iliyokwisha asilimia 7.2 jamani tujitendee haki. Sekta zilizokuwa zaidi hapa kwetu ni uchukuzi na uhifadhi wa mizigo, uchimbaji wa madini, mawasiliano, sekta ya fedha na bima, na hizi zimekuwa kati ya asilimia 17.4 mpaka asilimia 15. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mfumuko wa bei. Januari, 2016 tulikuwa asilimia 6.5, Juni, 2016 asilimia 5.5, Septemba, 2016 asilimia 4.5, hicho ni kigezo kimojawapo.
Mheshimiwa Naibu Spika, akiba ya fedha za kigeni, Ni dola za Kimarekani bilioni 4.1 mwezi Septemba, 2016 ambayo inatuwezesha kununua bidhaa na huduma kwa kipindi cha miezi minne. Urari wa biashara (current accaount deficit), imepungua kutoka dola milioni 1,207 katika quarter ya Julai mpaka Septemba, 2015, imerudi dola milioni 601.8 Julai mpaka Septemba, 2016. Jamani vigezo vyote hivi vinatuonesha tuko vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwenendo wa sekta ya kibenki. Sekta hii imeendelea kukua na ina mitaji na ukwasi wa kutosha. Mitaji ukilinganisha na mali iliyowekezwa, nilisema wakati natoa hoja hapa, total risk waited assets na off balance sheet exposures ni asilimia 19.08 ukilinganisha na kiwango cha chini ambacho ni asilimia 12 tu. Mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu ikilinganishwa na kiwango cha amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to demand liabilities) asilimia 34.18 wakati kiwango cha chini kinachohitajika ni asilimia 20.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli shida kubwa tunayoona pamekuwepo na mikopo chechefu. Septemba, 2015 ilikuwa ni asilimia 6.7 sasa imeongezeka kufikia asilimia 9.1, na ndiyo sababu tumeona mabenki ambayo yamepata hasara; CRDB kati ya Julai na Septemba wamepata hasara, TIB Development Bank wamepata hasara, na sababu ni hiyo ya mikopo chechefu. Twiga Bancorp nayo tumeiweka chini ya uangalizi wa Benki Kuu, lakini siyo kitu cha ajabu. Crane Bank Limited ya Uganda nayo imewekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu yao mwezi uliopita. Imperial Bank ya Kenya nayo iliwekwa chini ya uangalizi Oktoba, 2015 na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya kibenki kwa ujumla ilipata faida, pato kwa rasilimali (retain on assets 2.53) na kadhalika, naweza nikaendelea kueleza lakini sisi tunavyotazama vigezo vingi vya uchumi vinatuonesha tuko sawa sawa. Nitakuja huko kwingine kwanini tunasikia maneno mengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, viwango vya ubadilishanaji fedha (exchange rate) hatuko pabaya. Ule upungufu, wastani umekua shilingi 2,172 kwa dola moja mwezi Januari, 2016, Julai zikawa shilingi 2,180 na bado mapaka Septemba bado tuko 2,188, kwa hiyo, stability ya exchange rates siyo mbaya kama watu wanavyosema maneno.
Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa mwenendo wa bajeti, na hizi namba nitakazo sema ni preliminary. Mapato ya ndani kwa quarter iliyopita, mapato ya ndani ukijumlisha na fedha kutoka own sources za Halmashauri tulikuwa na shilingi bilioni 3,948.4 Mapato ya ndani ukitoa yale ya Halmashauri inakuwa ni shilingi bilioni 3,814.4, tulipata GBS grant kutoka EU shilingi bilioni 36.1 na kwa upande wa matumizi Waheshimiwa Wabunge tumekwenda vizuri. Matumizi ya kwaida katika quarter ya kwanza, fedha zilizotolewa kwa robo ya kwanza ni asilimia 26.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumetoa shilingi trilioni 4.5 wakati bajeti ya matumizi ya kwaida kwa mwaka huu mzima ni trilioni 17.7 lakini pia kwa upande wa matumizi ya maendeleo hapa tuna changamoto, tunazikiri lakini mwaka ndiyo umeanza quarter ya kwanza ina changamoto mwezi wa kwanza mapato yanakuwa kidogo, mwezi wa 9 ndipo mapato kidogo yana-pick up.
Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya maendeleo. Tumesha kutoa shilingi bilioni 915 ambayo ni asilimia nane ya lengo ambalo tulikuwa tumekusudia. Kwa upande wa matumizi kutokana na fedha za nje, na hapa ndipo challenge ilipo, ni asilimia moja tu ambazo tumeweza kutoa, tulikuwa tumepata shilingi bilioni 45.9
Mheshimiwa Naibu Spika, ulipaji wa madeni ya ndani. Katika kipindi cha Julai mpaka Oktoba, 2016 tumelipa madeni mbalimbali ambayo yamehakikiwa na Mkaguzi wa Mkuu Ndani wa Serikali, tumelipa jumla ya shilingi bilioni 187.5 na haya yanajumuisha madeni ya wakandarasi wa barabara, maji, umeme, wazabuni mbalimbali na madeni ya watumishi wa umma na tunaendelea kulipa kupitia mafungu yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, ulipaji wa deni la nje. Kuanzia Novemba, 2015 hadi Oktoba mwaka huu, Serikali imetumia jumla ya shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya kulipia madeni ya nje. Malipo ya mtaji ni shilingi bilioni 709, malipo ya riba shilingi bilioni 487.2.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme hivi; Serikali itaendelea kulipa kwa wakati mikopo yote iliyoiva kwa mujibu wa mikataba; kwa kuwa kama hatufanyi hivyo tutahatarisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi zetu na wahisani na taasisi za fedha za kimataifa na mabenki ya nje. Aidha, nchi isipolipa kwa wakati inaweza kushitakiwa kwenye Mahakama za Kimataifa na kusababishia nchi yetu kupata hasara na pengine hata tukakosa kabisa mikopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutolipa kwa wakati kutaisababishia nchi yetu kulipa gharama kubwa za ziada (penalty) kulingana na makubaliano kwa hiyo ni lazima tulipe. Serikali imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha kwamba Deni la Taifa linadhibitiwa na linaendelea kuwa himilivu na linalipwa kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, ruzuku ya pembejeo. Mwaka huu wa fedha jumla ya shilingi bilioni 25 zilitengwa kwa ajili ya kununua Pembejeo. Hadi kufikia Oktoba tumekwisha kulipa shilingi bilioni 10.
Mheshimiwa Naibu Spika, ununuzi wa chakula cha hifadhi. Mwaka huu wa fedha tulitenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kununua chakula cha hifadhi ya Taifa. Mpaka kufikia Oktoba mwaka huu tumekwishakutoa shilingi bilioni 9.
Mheshimiwa Naibu Spika, utoaji wa fedha za Mfuko wa Jimbo. Serikali ilitenga shilingi bilioni 10.4 kwa ajili ya mfuko wa kuchochea maendeleo jimboni. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni tisa ni kwa ajili ya Tanzania Bara na shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Serikali inatarajia kutoa fedha hizo mwezi huu wa Novemba. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, yamekuwepo kama nilivyosema manung’uniko mitaani lakini sisi tunavyoyatafsiri ni kwamba yametokana na jitihada na hatua zilizochukuliwa na Serikali kurudisha nchi kwenye utaratibu na nidhamu ya kazi katika utumishi wa umma, kurejesha nidhamu ya matumizi, kuondoa matumizi ya Serikali yasiyo ya lazima, kupambana na wizi na ubadhirifu wa fedha na mali ya umma, kuhimiza ulipaji kodi na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, Serikali inaamini kuwa hatua hizi ni kwa maslahi mapana ya Taifa letu, na maumivu ni ya kipindi cha mpito wakati tunaweka mambo sawa ili tuweze kurudisha mifumo kwenye utaratibu unaokubalika na ambao ni endelevu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu, naomba nitumie usemi tena wa kiingereza; there is no gain without pain. Maendeleo hayatakuja hivi hivi, we have to sacrifice ndugu zangu. Lazima tu- sacrifice kama kweli tunataka vizazi vijavyo viweze ku-enjoy maisha in the future, lakini kama tunakula tu leo haiwezekani tutaendelea kubaki maskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, upo utaratibu wa Serikali yenyewe, taasisi binafsi na mashirika ya kimataifa kufanya tathmini huru ya uchumi wa nchi na kutoa maoni juu yake kadri wanavyoona. IMF walikuwa hapa wiki moja iliyopita na wamekamilisha tathmini ya mwenendo wa uchumi wetu. Taarifa iko kwenye mtandao, someni. Wamesema wenyewe si maneno yangu wamesema kabisa wameridhika na hali ya uchumi wa Taifa letu lakini hii haina maana kwamba hatuna changamoto, haitawezekana.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kidogo kuhusu misingi ya mpango. Niliambiwa hapa kwamba tulivyoiweka hapa inajenga mazingira ya kushindwa tayari. Mimi nafikiri hapa tatizo lilikuwa dogo tu, neno misingi ambalo tulilitumia katika kitabu cha mapendekezo ya mpango kililenga kumaanisha assumptions. Hakika Serikali ya Awamu ya Tano tunafahamu vizuri hali halisi ya mazingira wezeshi kwa uwekezaji nchini kama ambavyo imetathminiwa na Benki ya Dunia katika Doing Business Report. Tunafahamu utabiri wa hali ya hewa na maoteo ya upungufu wa chakula katika nchi yetu, we are not naïve Waheshimiwa Wabunge, we are not naïve at all.
Mheshimiwa Naibu Spika, assumptions huwa tunazifanya na si lazima ziwe halisi, huwa tunazifanya ili kurahisisha uwekaji wa malengo kwa mwaka ujao wa fedha. Wachumi wanafahamu na ni utaratibu wa kwaida kabisa. Kwa mfano; unapotaka kuchambua biashara baina ya nchi mbalimbali ulimwenguni huwa unafanya assumtions unasema assume there only two trading nations, lakini kila mtu anajua nchi mbili duniani hazi-trade peke yake, kwa hiyo, nadhani hili lilikuwa ni suala la lugha tu, tafsiri yetu pengine assumptions haikuwa sahihi, lakini maana yetu ilikuwa ni assumptions na siyo hicho ambacho kilielezwa humu ndani.
Mheshimiwa Naibu Spika, fedha kutopelekwa kwenye Halmashauri. Naomba niseme tu kwamba katika kipindi cha Julai mpaka Oktoba fedha zilizotolewa zinajumuisha mishahara shilingi trilioni 1.18 sawa na asilimia 33. Matumizi mengineyo shilingi bilioni 192.8 ambayo ni sawa na asilimia 32.2 na fedha za maendeleo shilingi bilioni 173.3 sawa na asilimia 14.3. Lakini mbali na fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu na makusanyo ya ndani ya halmashauri, kiasi cha shilingi bilioni 271 zilizotumika kutekeleza miradi ya maji vijijini ni shilingi bilioni 51.1, umeme vijijini shilingi bilioni 132.4, mfuko wa barabara shilingi bilioni 78.1 na utoaji wa pembejeo kwa wakulima shilingi bilioni 10 katika Halmashauri mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa taasisi za umma kuweka fedha zao kwenye revenue account Benki Kuu tulishauriwa hapa kwamba sasa zirejeshwe. Nafikiri limeelezwa vizuri, naomba niseme tu hivi; uamuzi wa Serikali wa kuzitaka taasisi za umma kufungua account za mapato Benki Kuu utaendelea kubaki kama ulivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge tumepigwa sana, kwanini tuendelee kupigwa? Utaratibu ambao ulikuwa umejengeka ulizinufaisha benki chache na haukuwa na maslahi mapana kwa Taifa. Benki hizo zimekuwa zikipata faida kwa kutumia mgongo wa maskini na sasa basi. Naibu Waziri amesema hapa waende na vijijini wakafanye kazi huko ili turejeshe ushindani katika sekta ya benki.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwamba TRA wanatumia vitisho, mabavu na mifumo kandamizi katika kukusanya kodi. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea na jitihada za kuhakikisha kila anayestahili kulipa kodi analipa kodi stahili na kwa wakati. TRA inatekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi kulingana na taratibu katika sheria na kanuni za kodi. Mlipa kodi anakadiriwa kulipa na kupewa muda wa kuilipa kodi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama kodi hiyo itakuwa haijalipwa kwa muda uliyooneshwa kwenye taarifa ya madai, TRA huchukua jukumu la kumkumbusha mhusika anapewa reminder notice na kumtahadharisha hatua zitakazochukuliwa endapo kodi hiyo itaendelea kutolipwa mpaka tarehe iliyoonyeshwa kwenye reminder notice.
Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zinazochukuliwa kwa mlipa kodi anaekaidi ndizo hizo za kukamata mali na kuziuza kwa njia ya mnada na kuiagiza benki ya mlipa kodi kuhamisha fedha kutoka kwenye account yake kwenda TRA kulipia hilo deni. Hatua hizi zipo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. Hatua hizi si vitisho wala mabavu, wala mifumo kandamizi kwa wafanyabiashara. Ninawasihi sana ni vizuri walipa kodi wakazingatia sheria za kulipa kodi kwa hiari na kuepuka usumbufu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja hapa kwamba Serikali imeokoa fedha kuondoa watumishi hewa lakini wakati huo huo tarifa za Benki Kuu zinaonesha malipo ya mishahara yaliongezeka. Naomba niseme hivi Waheshimiwa Wabunge, Serikali imeendelea kuajiri watumishi kwa mahitaji muhimu. Kati ya mwezi Machi na Septemba, 2016 wameajiriwa watumishi 8,908 wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama, walimu wa vyuo vikuu, watumishi wa kada za afya kwa ajili ya hospitali mpya ya Mloganzila na watumishi wa kada nyingine ambao mishahara yao imeongeza wage bill kwa kiasi cha shilingi bilioni 5.08.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jitihada hizi Serikali imeendelea kulipa malimbikizo ya madeni ya watumishi. Kati ya mwezi Machi na Julai, 2016 shilingi bilioni 11.9 zililipwa kwa watumishi 13,544. Lakini pia Serikali iliamua kujumuisha mishahara yote iliyokuwa inalipwa nje ya pay roll kupitia bajeti ya matumizi (OC) kwenye wage bill ya kila mwezi na hivyo kupelekea ongezeko la shilingi bilioni 33.1 kwa mwezi kwenye wage bill kuanzia mwezi Februari. Kwa hiyo, kwa kweli hizi takwimu hizi zinahitaji tu maelezo lakini kila kitu kipo. Nimesikia kengele imeshalia na kama ambavyo nimekwisha kuahidi ziko hoja nyingi ambazo ningependa kuzitolea maelezo lakini inatosha tu niseme na nimalizie na mambo mawili.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja, vipaumbele vingi. Nimemsikia Mheshimiwa Silinde. Nafikiri tutakapoanza hilo zoezi la kupunguza vipaumbele tutaanza kupunguza na kuondoa miradi katika jimbo la Momba ili ibaki mitatu. Waheshimiwa Wabunge, kazi ya kupunguza vipaumbele katika Taifa letu ni ngumu sana kwa sababu moja; lengo ni kuielekeza sekta binafsi kwenye maeneo ya priority, kwahiyo si kwamba hizi priorities zote ni Serikali iende ikafanye. Lengo letu ni kuielekeza private sector iende kwente priority areas.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile vipaumbele lazima viwe vingi kwasababu fursa katika Taifa letu zinatofautiana sana, kwahiyo ni lazima miradi iwepo ambayo inazingatia fursa za maeneo husika ndiyo maana ni baadhi tu ya sababu kwanini vipengele ni vingi sana. Lakini kimsingi na umaskini wetu jamani niambieni niache nini, niache reli ya kati, niache miradi ya maji, niache Mchuchuma na Liganga, niache zahanati, niache umeme vijijini au niache barabara? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nihitimishe na napenda kuwashukuru Wabunge wote waliochangia na kutupatia ushauri kuhusu vipaumbele na mambo muhimu ambayo sasa tunakwenda kuzingatia katika kazi inayofuata ya kuandaa mpango ujao wa maendeleo kwa mwaka 2017/2018. Napenda niliahidi Bunge lako Tukufu kwamba Serikali itazingatia ushauri tulipokea kwa kadri inavyowezekana.
Mheshimiwa Naibu Spika, hakika haitawezekana kuzingatia kila kitu kinachosemwa hapa. Baadhi yataendelea kuzingatiwa katika mipango ya maendeleo itakayofuata. Na ili Bunge lione wazi kwamba Serikali inasikia na inathamini ushauri mzuri walioutoa ninakusudia kuweka bayana katika kitabu cha mpango wa maendeleo ujao utakapokamilika muhtasari wa ushauri uliozingatiwa na ule ambao tunaona unafaa uzingatiwe katika mipango inayofuata na mambo ambayo bado yanahitaji kuchambuliwa kwa kina kabla ya kuzingatiwa kwenye mipango. Kwa hiyo, ninawaahidi ili msiseme tunapuuza, tunazingatia sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga Tanzania mpya ili kuwaondoa Watanzania kwenye lindi la umaskini kwa haraka. Uamuzi huu unahitaji kuachana na mazoea, unahitaji sacrifice, unahitaji tufanye kazi kwa bidii, unahitaji nidhamu na uadilifu. Tunataka uchumi ambao Wananchi wengi wananufaika nao. Nirudie tena, Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli inawajali wafanyabiashara, lakini hatuna budi wafanyabiashara wetu wazingatie sheria za nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kushukuru sana kwa kuongoza kikao hiki vizuri, lakini pia kwa kunipatia nafasi niweze kuchangia. Vile vile niruhusu niipongeze sana Kamati ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia na Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa Kalambo kwa kazi nzuri sana wanayofanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema kutoka moyoni kabisa, Kamati hii ni very pragmatic, very resourceful na wamekuwa wanatusaidia sana. Serikali nipende kuahidi kwamba itazingatia maoni na mapendekezo ambayo wametupatia katika uandaaji wa bajeti inayokuja na tutaendelea kuzifanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nizungumzie mambo tu machache. Kwanza kulikuwa na hoja ya washirika wa maendeleo kutotoa fedha na kwamba sababu zake hazifahamiki. Sababu za washirika wetu wa maendeleo kutotoa fedha ni nyingi sana. Mojawapo kwa kweli ni yale masharti yenyewe ya kutoa fedha. Yako masharti ambayo hatukubaliani nayo na tunaendelea kuzungumza na wenzetu ili watuelewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja nitoe tu mfano; kwa mfano tulikuwa tunaomba fedha kwa ajili ya kuboresha bandari yetu ya Dar es Salaam, lakini moja ya sharti tulilopewa ni kwamba ni lazima sasa TPA wajiondoe kwenye kuendesha Bandari badala yake aje mtu binafsi kuendesha bandari yetu. Hatukubali hilo Waheshimiwa Wabunge na sisi tunafanya kwa maslahi ya Taifa letu. Tumeshakuwa na uzoefu wa kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mengine ambayo pia wanatusukuma huko ambayo sio sawasawa, ni kinyume cha mila na desturi za Kitanzania na hatuwezi kuzikubali. Kwa hiyo, hiyo ni mojawapo. Pia kuna ukweli kwamba kuna mabadiliko katika mtazamo wa Serikali nyingi ambazo zimeingia madarakani hususan katika nchi za Ulaya. Tumekuwa na majadiliano sisi bado tunadhani kwamba general budget support ndiyo njia nzuri ya wabia wetu kutusaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wao wamebadili msimamo, wanasema wapeleke fedha moja kwa moja kwenye miradi. Tulishakuwa huko, tunajua changamoto za wao kupeleka fedha kwenye miradi wanayochagua kwenye mikoa wanayochagua badala ya kutupa sisi kama Watanzania nafasi ya kusema tumepungukiwa zaidi huku sisi tupeleke kule. Hata hivyo, tunayajadili na tumeunda Kamati maalum ya wataalam kutoka nje na ndani ambao wanaangalia jinsi dialogue yetu inavyokwenda. Naamini kwamba mwezi huu tutakuwa na kikao cha pili, naamini tutafika mahali ambapo tutaelewana vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la msingi Waheshimiwa Wabunge, naomba tena kusisitiza, khanga ya kuazima ni tatizo. Lazima tuielekeze nchi yetu kujitegemea kama Baba wa Taifa alivyotufundisha. Hili ni jambo la msingi sana, mnaona tunapata wakimbizi tunahangaika miaka yote lakini wao wakipata wakimbizi kidogo wanakimbiza fedha zao kwa wakimbizi wa upande mwingine. Kwa hiyo, kwa kweli tujielekeze kujitegemea na ndiyo maana tukazanie zaidi kujenga mapato yetu ya ndani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme mengine haraka haraka. Kwa upande wa takwimu za mfumuko wa bei, wale ambao wana mazoea kuzitazama umegawanyika sehemu mbalimbali. Kuna mfumuko wa bei wa jumla lakini kuna mfumuko wa bei wa chakula lakini pia kuna non food inflation na ukizitazama hizi ziko bayana kabisa kwamba mfumuko wa bei ya chakula daima umekuwa ni mkubwa kuliko mfumuko wa bei wa jumla na sababu kubwa ni kwamba mfumuko wa bei wa Taifa letu unasukumwa zaidi na upatikanaji wa hali ya chakula lakini pia bei za mafuta. Kwa hiyo, hiyo iko wazi tu na nadhani ni mazoea kuziangalia zile takwimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa upande wa kuhusu makampuni ya mawasiliano kujisajili katika soko letu la hisa. Kwenye taarifa ambayo niliisoma humu Bungeni, muda haukuniruhusu lakini mkiisoma ile taarifa kuna kipengele nafikiri ni ukurasa wa 15 kinaeleza vizuri juu ya hatua iliyofikiwa kuyataka makampuni yetu ya mawasiliano kujisajili katika soko la hisa kwa mujibu wa sheria. Nitaomba wasome.
Mheshimiwa Mwenyekiti, limesemwa sana kuhusu Sekta yetu ya Kilimo. Ni kweli growth ya Sekta yetu ya Kilimo imekuwa hairidhishi na nimelisema hili mara kadhaa ndani ya Bunge, lakini ni muhimu tuwe clear. Ningependa kama ingewezekana kama ulivyosema wewe, suala hili la uchumi pengine tukapata muda kweli wa kulijadili labda hata kwenye semina au hivi na Wabunge wakaja wakashiriki kwelikweli kwa maslahi ya Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano; kilimo, tukisema bajeti pekee ya kilimo iongezwe tutabadilisha kilimo sio sawasawa. Najua Maputo Declaration inataka tupeleke 10% ya bajeti iende kwenye kilimo lakini kilimo kinachosemwa ni nini? Wataalam wanasema ili kilimo kiweze kufanya vizuri unahitaji pia sekta nyingine ambazo sio za kilimo nazo zifanye vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa mfano; tunapozungumzia mbolea, mbolea inazalishwa viwandani, unapozungumzia performance ya kilimo lazima uzungumzie upitikaji wa mazao kutoka shambani maana yake ni barabara. Unapozungumzia wataalam wa kilimo maana yake lazima uzungumzie Sekta ya Elimu. Kwa hiyo, ni lazima tuwe waangalifu, sio bajeti pekee ya kilimo. Kuna mambo mengi ambayo ndiyo yanakwenda kuamua performance ya kilimo iweje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa yako mengine ambayo ni ya msingi. Bajeti yetu ya umwagiliaji ikoje, bajeti yetu ya utaalam ikoje? Incentives, hata za kikodi kule kwenye kilimo zikoje? Lazima tuliangalie kwa upana wake ili kweli tuweze kuja na mkakati mzuri kwa ajili ya kuboresha Sekta ya Kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yalisemwa hapa najua Naibu Waziri amelisema kwamba ukuaji wa deni la Taifa, tumekazania zaidi kukopa ndani, kwa hiyo tuna–crowd out private sector. Nisisitize tu, Serikali haina maagizo maalum kwamba tulipe wadeni wetu wa nje peke yake. Nililieleza wakati natoa taarifa Bungeni, ni lazima tuwe makini sana na kuhakikisha kwamba hatuachi kulipa halafu madhara kwenye uchumi yakawa makubwa zaidi. Kwa hiyo, there is a delicate balance that we need to do na ndicho tunachojaribu kufanya. Madeni haya ndugu zangu, mengine tumewapa taarifa, madeni haya mengine tunayolipa yamekopwa toka uhuru, kwa hiyo, hilo ongezeko linaloonekana ni cumulative sio kwamba ni kwa sababu tu imeongezeka katika Awamu hii ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yalisemwa pia kuhusu kwamba tuangalie nchi ili iendelee inahitaji Sound Fiscal and Monetary Policies, Revenue Policies na Good Governance. Nafikiri niseme tena, inabidi tuwe waangalifu, country context na specificity ni muhimu sana. Tanzania yetu ya leo sio Malaysia, wala sio Botswana, wala Korea. Kwa hiyo, ni muhimu sana na wale ambao mnasoma hivi vitabu ni ukweli pia kwa mfano Dkt. Mahathir Mohammed was a dictator! Ndiyo ukweli wenyewe, angalieni South Korea, Park Chu Hi ambaye ndiye aliibadilisha Korea alikuwa dictator, kwa hiyo msiseme tu kwamba good governance and stability ndiyo msingi pekee wa ukuaji wa uchumi katika Taifa. Kwa hiyo, ni muhimu sana tuwe waangaifu na hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lilisemwa pia hapa kwamba pato la Mtanzania linapungua.
Pato la Mtanzania linapungua, si kweli! Pato la wastani la Mtanzania mliangalie vizuri, tumetoka kwenye dola 350 sasa tumefika dola 980, lakini ni vizuri kuzingatia volatility ya exchange rate, kama unatazama tu lile pato la Taifa kwa shilingi, halafu unagawa kwa exchange rate kuna miaka ambayo kwa wastani, exchange rate yetu imeporomoka na hivyo wastani unaonekana kushuka, lakini trend ya pato la Taifa inaongezeka kwa hakika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mapitio ya mfumo wa kodi, naomba nitumie nafasi hii, kuwaomba sana Waheshimiwa Wabunge kwamba kuanzia mwezi huu sasa tutaanza kujadili pale Wizarani mapendekezo ya wadau wote wa kodi nchini, ambayo wamependekeza wengine wameleta. Hamjachelewa yeyote aliye na mapendekezo namna ya kuboresha mfumo wa kodi awasilishe mwezi huu tutaanza kufanya kikao cha kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vipaumbele, nilijaribu kulieleza kwenye moja ya vikao vilivyopita, naomba nisisitize sana kwamba kusema juu ya kuwa na vipaumbele vichache ni rahisi sana, lakini kuvitekeleza katika mazingira ya nchi maskini kama Tanzania ni jambo gumu kweli. Nakumbuka nilimtania Mheshimiwa Silinde hapa, nikasema nitaanza kupunguza vipaumbele vinavyogusa jimbo lake lakini ni ukweli tuna mahitaji makubwa kwenye maji, elimu, kila mahali. Kwa hiyo, kuweza kusema kwamba tujikite kwenye eneo moja tu la reli katika mazingira ya Tanzania haitawezekana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Naibu Waziri alieleza juu ya ukusanyaji wa kodi ya majengo, naomba tu niseme kama alivyoeleza kwamba tumeanza kukusanya. TRA imeanza kukusanya mwezi wa Kumi baada ya kukamilisha maandalizi na kuanzia mwezi wa Kumi mpaka Desemba mpaka sasa zimekusanywa sh. 4,762,369,261. Hata baadhi ya miji ambayo inasemekana hamna chochote si kweli, kwa mfano Kinondoni peke yake kwa hii miezi michache imeshakusanya sh. 1,229,821,142, niseme Arusha Sh. 462, 527, 906, Ilala Sh. 999,193, 088 na takwimu tayari zipo kwa kipindi hiki, kwa hiyo kazi imeanza. Ilikuwa ni muhimu sana kufanya maandalizi stahiki ambayo yanagusa vitu vingi ili tuhakikishe kwamba tunakwenda sawasawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MWENYEKITI: Malizia tu Waziri.
WAZIRI WA MIPANGO NA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, okay, labda niseme tu moja la mwisho kwamba, kwenye tathmini ya deni la Taifa, tazameni kidogo kwa uangalifu taarifa ambayo niliwaletea. Tuna vile viashiria vya uhimilivu wa deni, ni pamoja na deni la nje, uwiano wake na uuzaji wa bidhaa za nje kwa maana ya foreign exchange earnings lakini pia tunaangalia deni la nje uwiano wake na mapato ya ndani. Kwa hiyo, siyo kwamba tunaangalia tu uwiano relative to GDP. Ahsante.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, na mimi naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama tena mbele ya Bunge lako Tukufu kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2017/2018. Utakumbuka tarehe 08, Juni, 2017 niliwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2016, Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2017/2018 na Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba zote mbili nilieleza shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na Serikali katika kipindi cha mwaka 2016/2017 pamoja na mafanikio na changamoto zilizojitokeza. Aidha, nilieleza malengo na miradi ya kipaumbele ambayo Serikali inakusudia kutekeleza katika mwaka 2017/2018 na mapendekezo ya bajeti. Waheshimiwa Wabunge walipata nafasi ya kuzipitia hotuba hizo pamoja na viambatisho vyake na kutoa maoni na mapendekezo juu ya namna bora zaidi ya kufanikisha ajenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaletea Watanzania maendeleo.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha vizuri mjadala huu ambao unatarajiwa kuhitimishwa hivi leo.

Mheshimiwa Spika, napenda kutambua michango iliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini pamoja na maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni yaliyowasilishwa na Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba kwa niaba ya Msemaji wa Kambi hiyo kwa Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, ninathamini sana maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge wote. Wabunge 193 walichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali, kati ya hao wa kuzungumza walikuwa ni 165 na 28 kwa maandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi na Wizara yangu tunawashukuru kwa dhati kabisa kwa pongezi ambazo mlitupatia, nikianza na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alinipigia simu kutoa pongezi zake, lakini pia ninyi Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wengi ambao wametupongeza kutoka ndani na nje ya nchi yetu, kwa kweli mmetupatia nguvu ya kufanya vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati wa mjadala wa hotuba nilizoziwasilisha, Serikali imepokea michango mingi sana na ushauri. Yapo maeneo yaliyoungwa mkono na mengine ambayo yalilenga kuboresha Bajeti ya Serikali au kuikosoa. Napenda kulihakikishia Bunge kwamba tumepokea michango yote yenye afya kwa maendeleo ya Taifa letu. Baadhi tutayazingatia katika bajeti hii na bajeti zitakazofuata; na leo nitadhihirisha tena kwamba bajeti hii haijawahi kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baadhi ya hatua ambazo ziliungwa mkono na Waheshimiwa Wabunge wengi ni pamoja na zifuatazo:-

Kwanza, ni kufuta ada ya mwaka ya leseni ya magari, kutoa msamaha wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote ya ada ya leseni ya magari yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma, kuanzisha maeneo maalum (clearing houses) ya kukagua na kuthibitisha thamani ya madini kabla ya kusafirishwa, kuondoa VAT kwenye bidhaa za mtaji, kusamehe VAT kwenye vyakula vya mifugo, kutoa msamaha wa VAT na ushuru wa forodha kwenye vifaa maalum vya kutengeneza vifaa vya watu wenye ulemavu; pia miradi ya kielelezo itakayopewa msukumo maalum katika mwaka wa 2017/2018 ikiwemo miradi ya maji, zahanati, vituo vya afya, uendelezaji wa elimu katika ngazi zote, ununuzi wa vifaa tiba, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge, uimarishaji wa Shirika la Ndege la Tanzania, miradi ya umeme, miradi ya makaa ya mawe na chuma, uendelezaji wa maeneo maalum ya uwekezaji, ujenzi wa barabara za kuunganisha mikoa na ule wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Uganda hadi Bandari ya Tanga, lakini pia kuendeleza utulivu wa uchumi wa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba nami niungane pia na Waheshimiwa Wabunge wengi waliopongeza juhudi zilizochukuliwa na Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kulinda rasilimali za Taifa letu ili kuhakikisha kwamba Watanzania tunanufaika na rasilimali za nchi na hususan madini.

Mheshimiwa Spika, tunampongeza sana Jemadari wetu Mkuu kwa kuthubutu kufichua na kuweka hadharani udhalimu ambao tumekuwa tunafanyiwa kwa miaka mingi kupitia utoroshaji wa madini na upotevu wa mapato ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunamhakikishia Mheshimiwa Rais wetu kuwa tunamuunga mkono na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu amlinde, ampe afya njema na amtie nguvu katika kazi yake ngumu ya kuongoza mapambano dhidi ya uporaji wa rasilimali za nchi yetu. Ushindi ni lazima na hakuna kurudi nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa niseme kidogo juu ya ushauri uliotolewa na Wabunge wengi. Kama nilivyosema mwanzo, yapo maoni yaliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge wengi katika maeneo mbalimbali ili Serikali iangalie namna ya kuyazingatia katika bajeti hii na zijazo. Naomba kurejea ushauri muhimu sana uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge kama ifuatavyo:-

(i) Kuongeza kasi ya kutekeleza miradi ya maji nchini na hasa vijijini kwa kuongeza bajeti ya maji;

(ii) Kuboresha mfumo wa utozaji kodi ya majengo;

(iii) Kukamilisha haraka utaratibu mzuri na endelevu na kuanza kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji haraka iwezekanavyo;

(iv) Kuongeza kasi ya kulipa madeni ya ndani ya wakandarasi, watoa huduma na watumishi;

(v) Kudhibiti kasi ya ukuaji wa Deni la Taifa;

(vi) Kuendeleza utulivu wa uchumi ikiwa ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei;

(vii) Kuimarisha thamani ya shilingi na kuongeza wigo wa huduma za kibenki hadi vijijini; na

(viii) Kujenga mazingira rafiki kwa uwekezaji na kufanya biashara nchini kwa kudumisha mashauriano na ushirikiano wa dhati na sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nianze kufafanua baadhi ya hoja.

Hoja ya kwanza, Serikali ilishauriwa iongeze tozo ya shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli kwa ajili ya Mfuko wa Maji ili kuwe na chanzo kinachotabirika (ring fence).

Mheshimiwa Spika, hii ilikuwa ni hoja mama ambayo ilitawala mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Baada ya Serikali kutafakari kuleta pendekezo la kufuta ada ya Motor Vehicle License ili kuondoa kero ya muda mrefu ya kutoza ada hiyo hata kama magari hayatembei na kufidia mapato hayo kwa kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa kwa shilingi 40 kwa lita; Waheshimiwa Wabunge walishauri mapato yatakayotokana na hatua hiyo, ndiyo yaelekezwe kwenye Mfuko wa Maji kwa kutambua kwamba kuongeza zaidi ushuru wa bidhaa kwenye mafuta, kutaathiri wananchi wengi kwa kuwa kutasababisha bei za bidhaa karibu zote, chakula, usafiri, usafirishaji, gharama za uzalishaji na gharama za maisha kwa ujumla kupanda sana kutokana na kupandisha bei ya nishati hiyo muhimu tena katika kipindi ambacho bei za mafuta katika Soko la Dunia inatarajiwa kuongezeka kwa wastani wa dola 50 kwa pipa hadi dola 60 mpaka 65 katika mwaka 2018.

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kuelekeza chanzo cha mapato mahususi kwenye matumizi maalum (revenue earmarking) unasaidia kuongeza fedha kwenye eneo linalolengwa na pia kuhakikisha upatikanaji wa fedha (funding stability). Ni kweli pia utaratibu huu umeleta matokeo chanya kwenye programu ya kusambaza umeme vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini. (Makofi)

Aidha, ahadi iliyopo katika katika ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 hadi 2020, ni deni na Serikali ina nia thabiti ya kumtua mama ndoo kichwani katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jitihada za Serikali katika kipindi kifupi cha miezi 18 zinathibitishwa na kukamilika kwa miradi mikubwa ya maji ikiwemo Ruvu Chini ambayo inatoa lita milioni 270 kwa siku; Ruvu Juu lita milioni 196 kwa siku; Visima vya Mpera na Kimbiji lita milioni 260 kwa siku na Sumbawanga lita milioni 13 kwa siku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miradi mingine ya maji iliyokamilika ni Nansio, Ukerewe lita milioni 8.6 kwa siku, Bukoba Mjini lita milioni 18 kwa siku, Musoma Mjini lita milioni 30 kwa siku, Sengerema lita milioni 15 kwa siku, lakini pia mradi ule wa Msanga Mkuu kule Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo, Serikali inapenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge hili kwa ajili ya miradi ya maji kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambazo ni shilingi bilioni 249.5 na Mfuko wa Maji shilingi bilioni 158.5 zitatolewa kuendana na mpango kazi na kupitia Kamati ya Bajeti, Bunge litapewa taarifa rasmi ya utekelezaji wa hadi hii ya Serikali kila nusu mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, hatua nyingine zitakazochukuliwa na Serikali ni pamoja na zifuatazo:-

Kwanza, ni kuharakisha mchakato wa mikopo kwa ajili ya miradi ya maji kutoka taasisi mbalimbali na nchi rafiki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba leo terehe 20 Juni, 2017 nimesaini mkopo wa dola za Kimarekani milioni 400 kutoka Benki ya Credit Swiss ili kugharamia miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna miradi mikubwa sita:- Kwanza kuna mradi wa upanuzi wa huduma za maji Mijini ambao utagusa Mikoa ya Kagera, Rukwa, Dodoma, Morogoro, Pwani, Simiyu, Iringa, Mara na Mwanza. (Makofi)

Mradi wa pili ni mradi wa uchimbaji wa visima na ujenzi wa Mabwawa katika Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Shinyanga na Simiyu. (Makofi)

Mradi wa tatu ni mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya maji Mijini, itagusa Mikoa ya Rukwa, Dodoma, Morogoro, Kigoma, Kagera, Lindi, Manyara, Mtwara, Tabora, Ruvuma na Kilimanjaro. (Makofi)

Mradi wa nne, ni mradi wa upanuzi wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira Dar es Salaam na hii itagusa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. (Makofi)

Mradi wa tano ni kuendeleza na kusimamia rasilimali za maji. Itagusa Mikoa ya Pwani, Rukwa, Ruvuma, Tanga, Kigoma, Dodoma, Manyara, Njombe, Singida, Shinyanga, Tabora, Songwe, Mwanza, Kagera, Geita, Mara na Morogoro(Makofi)

Mradi wa sita ni mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Kahama na Shinyanga na mikoa itakayohusika ni Shinyanga na Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha taratibu za mkopo kutoka Exim Bank of India dola milioni 500 ambazo ni takriban shilingi trilioni 1.3 kwa ajili ya miradi ya maji katika miji 17 nchini. Hivi sasa mkopo huo umeshakufanyiwa uchambuzi na Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Madeni na Waziri wa Fedha na Mipango amesharidhia kwa niaba ya Serikali, fedha hizi zikopwe. Taratibu zinazobaki sasa ni kukamilisha usanifu wa miradi hii na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hatimaye kusaini mkataba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Serikali inafuatilia upatikanaji wa fedha Euro milioni 102 kutoka Green Climate Change Fund kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji ya Simiyu. Pia nchi rafiki ikiwemo Morocco na Misri zimeonyesha utayari wa kugharamia utekelezaji wa miradi ya maji hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa ni kwamba Serikali inatoza Kodi ya Leseni ya Magari kwa mwaka (Annual Motor Vehicle License Fee) kwa Watanzania maskini ambao hawamiliki gari kwa kutoza kodi hiyo katika mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ikiwemo mafuta ya taa unalenga kuwalinda Watanzania dhidi ya madhara ya uchakachuaji wa mafuta (fuel adulteration).

Kwa sasa tofauti ya kodi zinazotozwa kwenye mafuta ya taa na Dizeli ni shilingi 53 kwa lita. Endapo ushuru huu wa shilingi 40 hautaongezwa kwenye mafuta ya taa, tofauti ya kodi itakuwa shilingi 93 kwa lita ambayo itachochea uchakachuaji wa mafuta utakaosababisha uharibifu wa magari na mitambo na kupoteza mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ongezeko la tozo kwenye petroli, dizeli na mafuta ya taa limefikiwa ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wamiliki wa magari kudaiwa ada ya Motor Vehicle License hata kama gari halitembei, lakini pia tumefanya hivyo kwa namna ambayo haitachochea uchakachuaji wa mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatua hiyo pia itaiwezesha Serikali kupata mapato ambayo yatatumika kugharamia huduma muhimu za jamii kama barabara, afya, dawa na vifaa tiba ambavyo Watanzania masikini pia watafaidika nazo.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, palikuwepo na hoja kwamba msamaha (Tax Amnesty) ambayo nilitangaza ile tarehe 8 Juni, 2017 ambayo ulitolewa kwenye Ada ya Mwaka ya Leseni uhusishe na ada ya ukaguzi wa vifaa vya kuzima moto (Fire Inspection Fee).

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, hatua ya Serikali ya kutoa msahama (Tax Amnesty) kwa ada ya leseni ya magari itahusisha pia ada, riba na adhabu ya madeni yote ye fire inspection fee yaliyolimbikizwa miaka ya nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitarudia tena.

Mheshimiwa Spika, hatua ya Serikali ya kutoa msahama (Tax Amnesty) kwa ada ya leseni ya magari itahusisha pia ada, riba na adhabu ya madeni yote ye fire inspection fee yaliyolimbikizwa miaka ya nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba tozo ya shilingi 10,000 kwenye nyumba ambazo hazijathaminiwa hususan za vijijini ni kuwaongezea mzigo wananchi wa kijijini, lakini pia ile tozo ya shilingi 50,000 kwa ghorofa ambazo wanaishi wastaafu iondolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kodi ya majengo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Miji (The Urban Authorities Rating) Sura ya 289. Kifungu cha pili cha Sheria ya Mamlaka ya Miji (The Urban Authorities Act) inabainisha kuwa kodi ya majengo inatozwa kwenye majengo yaliyojengwa kwenye Mamlaka za Majiji, Miji na Miji Midogo. Vijiji havitahusika katika kodi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kodi ya majengo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Miji (The Urban Authorities Rating) Sura ya 289 na kifungu cha pili cha Sheria ya Mamlaka ya Miji (The Urban Authorities Act) inabainisha kuwa kodi ya majengo inatozwa kwenye majengo yaliyojengwa kwenye Mamlaka za Majiji, Miji na Miji Midogo. Vijiji havihusiki katika kodi hii. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Spika, aidha, kwa mujibu wa sheria, wananchi wenye umri zaidi ya miaka 60 hawapaswi kulipa kodi ya majengo wanayoyatumia kama makazi yao wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninasema, aidha kwa mujibu wa sheria, wananchi wenye umri zaidi ya miaka 60 hawapaswi kulipa kodi ya majengo wanayoyatumia kama makazi yao wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja kwamba Serikali isitoze kodi ya majengo kwenye nyumba za tope na tembe.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha (3); “Kodi ya majengo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Miji, Sura ya 289 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Fedha ya mwaka 2015.” Kwa mujibu wa kifungu cha pili cha Sheria za Mamlaka za Miji (The Urban Authorities Act) kinabainisha kuwa kodi ya majengo inayotozwa kwenye majengo yaliyojengwa kwenye Mamlaka za Majiji, Manispaa, Miji Midogo na Halmashauri za Wilaya.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha tatu cha Sheria hii kimetafsiri nyumba zinazotakiwa kutozwa kodi ya majengo kuwa ni nyumba zote zilizoko ndani ya Mamlaka ya Majiji, Manispaa, Miji Midogo na Halmashauri za Wilaya ambazo zimeshajengwa na kuanza kutumika kwa makazi. Kwa maelezo hayo, kodi ya majengo inatozwa kwa nyumba zote zilizoko kwenye Mamlaka ya Majiji, Miji na Miji Midogo ambazo zimeshaanza kutumika kwa makazi kama ilivyobainishwa kwenye hotuba yangu ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018. Hata hivyo, tozo hizo hazitahusisha nyumba za tope na tembe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nilieleze Bunge lako na wananchi kwa ujumla kuwa kodi ya majengo kama nilivyosema itatozwa katika Miji, Majiji na Miji Midogo kwa mujibu wa Sheria za Kodi ya Majengo ya Mamlaka ya Miji Sura ya 289. Kodi hiyo itatozwa katika majengo ya kudumu yaani yale yaliyojengwa kwa tofali za saruji, tofali za kuchoma na kuezekwa kwa bati na siyo za udongo wala zilizoezekwa kwa nyasi au zile za tembe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu uwasilishaji wa mapato ya kodi ya majengo kwa Halmashauri. Mapato ya kodi ya majengo na mabango yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuhifadhiwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, Serikali itaweka utaratibu wa kurejesha mapato hayo kwenye Halmashauri ambapo watatakiwa kuwasilisha mahitaji yao halisi. Aidha, Serikali itapitia mahitaji yao ili kujiridhisha kabla ya kuwarejeshea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya kutokutoza kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye magari ya kubeba wagonjwa. Kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya kwa wananchi wetu na hasa katika maeneo ya vijijini, Serikali imeamua kufanya marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye magari yanayotumika katika kubeba wagonjwa (ambulance). (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kufanya marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa magari yanayotumika katika kubeba wagonjwa (ambulance). Hatua hii itahusisha magari yanayoingizwa nchini yakiwa yametengenezwa mahsusi kwa ajili ya kubeba wagonjwa na kwamba yanaingizwa nchini kwa matumizi ya hospitali au vituo vya kutoa huduma za afya vilivyosajiliwa kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali itatumia utaratibu wa Hati ya Malipo ya Hazina (Treasury Voucher System) katika kusimamia misamaha hii ambapo kodi inayosamehewa italipiwa na Serikali kupitia Hazina kama inavyofanyika kwa taasisi za dini na kadhalika ili kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye ada na vibali vya uwindaji vitolewavyo na Serikali. Serikali inaondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye ada, leseni na vibali vya uwindaji. Hatua hii ina lengo la kuhamasisha ukuaji wa shughuli za uwindaji na sekta ya utalii kwa ujumla. (Makofi)

Kulikuwa na hoja kuhusu ada ya tathmini ya mazingira. kutokana na kilio cha wawekezaji wengi na hasa katika Sekta ya Viwanda, napendekeza kufuta Ada ya Kufanya Tathmini ya Mazingira (Environmental Impact Assessment) kwa wawekezaji wote wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, narudia.

Napendekeza kufuta Ada ya Kufanya Tathmini ya Mazingira (Environmental Impact Assessment) kwa wawekezaji wote wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba Serikali ifanye marekebisho kwenye Sheria ya EPOCA, Serikali imelisikia hili na baada ya kutafakari kwa kina, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya EPOCA ili:-

Moja, hisa za asilimia 25 zitakazouzwa na kampuni ya mawasiliano kwenye Soko la Hisa ziuzwe kwa umma ili kujumuisha Watanzania au Kampuni yoyote ya Kitanzania; Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kampuni zinazomilikiwa kwa pamoja baina ya Watanzania na raia wa nje; raia na kampuni au taasisi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; au raia wa kampuni kutoka nchi nyingine yoyote.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa sharti lililopo kwa mujibu wa sheria ni kwa hisa husika kuuzwa kwa raia wa Tanzania pekee.

Mheshimiwa Spika, ya pili ni kuziondoa kampuni ndogo za mawasiliano ambazo zina leseni ya application service kwenye sharti la kuuza hisa kwenye Soko la Hisa ili kubaki na kampuni kubwa za mawasiliano zenye leseni ya network facility au network service. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatu, Kampuni ya simu itakayoshindwa kufikia mauzo ya asilimia 25 kutokana na kutofaulu kwa toleo kwa umma (Unsuccessful Public Offer),Waziri mwenye dhamana atatoa maelekezo yaani directives ya namna kampuni husika itakavyoweza kutoa hisa kufikia asilimia 25 kwa kadri hali ya soko itakavyoruhusu, baada ya kupokea maombi ya kampuni ya simu iliyotolewa chini ya Sheria ya EPOCA na baada ya kupokea mapendekezo ya Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu watoa huduma na wauza bidhaa katika maeneo yasiyo rasmi kusajiliwa; ili kuhamasisha wafanyabiashara ndogo ndogo, kurasimisha shughuli zao na Serikali iweze kukusanya kodi, utaratibu nilioutangaza kupitia Bajeti Kuu ya Serikali kuhusu kuwatambua wafanyabiashara wa aina hii na kuwapa vitambulisho, itahusisha pia watoa huduma za chakula (caterers), washereheshaji (masters of ceremony) katika shughuli mbalimbali na wafanyabiasha wadogo wasio rasmi wanaofanya biashara katika maeneo rasmi.

Mheshimiwa Spika, naomba nirudie. Ili kuhamasisha wafanyabiashara wadogo kurasimisha shughuli zao na Serikali iweze kukusanya kodi, utaratibu nilioutangaza kupitia Bajeti Kuu ya Serikali kuwatambua wafanyabiashara wa aina hii na kuwapa vitambulisho; itahusisha pia watoa huduma za chakula (caterers), washereheshaji (masters of ceremony) katika shughuli mbalimbali na wafanyabiasha wadogo wasio rasmi wanaofanya biashara katika maeneo rasmi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu utozaji wa tozo kwa kutumia fedha za kigeni kwenye vyombo vya uvuvi vilivyosajiliwa nchini; Serikali imesikia maoni ya Waheshimiwa Wabunge kuhusiana na kero wanayopata wavuvi nchini ya kutozwa tozo mbalimbali kwa fedha za kigeni kwenye vyombo vya uvuvi vilivyosajiliwa nchini.

Mheshimiwa Spika, kuanzia sasa Serikali inaagiza taasisi zote zinazohusika na utozaji wa tozo hizo ziache utaratibu huo mara moja na zianze kutoza kwa kutumia shilingi ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kukusanya kodi inayotokana na mapato kutoka kwenye sekta ya michezo ya kubahatisha.

Kwa kuzingatia ushauri wa Waheshimiwa Wabunge, Serikali imeona kuna uwezekano wa kupata mapato mengi kutoka kwenye sekta ya michezo ya kubahatisha. Hivyo, kuanzia tarehe 1 Julai, 2017 mapato yote yatakayotokana na michezo ya kubahatisha yatakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mheshimiwa Spika, mapato hayo yatawasilishwa Mfuko Mkuu wa Serikali, Serikali itaweka utaratibu wa kuzirejesha fedha hizo kwenye Bodi ya Michezo ya kubahatisha baada ya kuhakiki mahitaji na matumizi ya Bodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba uchumi wa taifa siyo shirikishi, na bajeti iko kinyume na mahitaji ya ukuwaji shirikishi wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, niruhusu nitoe darasa kidogo.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, dhana ya uchumi shirikishi ni pana sana. Kwa lugha nyepesi ukuaji wa uchumi unakuwa shirikishi kama jamii inashiriki na kunufaika katika shughuli kuu zinazokuza uchumi wa nchi. Ndiyo kusema lazima uchumi kwa upana wake uwe unakua na kunemeesha wananchi walio wengi kwa namna ambayo ni endelevu (broad based growth that generate sustain progress in living standards).

Mheshimiwa Spika, ukuaji wa uchumi shirikishi unapimwa kwa viashiria vingi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa fursa za ajira (job creation), kupungua kwa umasikini, kuongezeka kwa tabaka la kati katika nchi (growth of the middle class), kupungua kwa tofauti za kipato (declined in income inequality), kupanuka kwa wigo wa fursa na huduma za kiuchumi na hususan masoko na huduma za kifedha (financial services) na usalama (security).

Mheshimiwa Spika, aidha, ukuaji wa uchumi shirikishi, unajengwa juu ya nguzo (pillars) takriban saba ambazo ni:-

(1) Elimu na ujuzi; (Makofi)

(2) Huduma za kijamii na miundombinu; (Makofi)

(3) Mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi; (Makofi)

(4) Huduma za kifedha na uwekezaji;

(5) Ujasiliamali na ukuzaji wa rasilimalia (accumulation of assets);

(6) Ajira na mafao ya wafanyakazi; na

(7) Uhawalishaji wa rasilimali fedha (fiscal transfers).

Mheshimiwa Spika, kwa Waheshimiwa Wabunge wanaopenda kupata elimu ya kina juu ya somo hili, kuna vitabu na machapisho mengi na wanaweza kujisomea ikiwa pamoja na taarifa ya hivi karibuni ya World Economic Forum ambayo inaitwa The Inclusive Growth and Development Report, 2017. Hivyo, siyo sahihi hata kidogo kuangalia kigezo kimoja tu na kutoa hukumu kwamba ukuaji wa uchumi siyo shirikishi au kwamba bajeti iko kinyume na mahitaji ya ukuaji shirikishi wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa 2016 ambacho kiligawiwa kwa Waheshimiwa Wabunge, tarehe 8 Juni, kinaonesha wazi kuwa Tanzania imepiga hatua nzuri katika viashiria vingi na ujenzi wa misingi ya uchumi shirikishi chini ya dhana ya kujenga uchumi wa viwanda. Bajeti ya mwaka 2017/2018 imejielekeza katika maeneo yote ya msingi kwa ujenzi wa uchumi shirikishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa kila kitu siyo waridi na haiwezekani kuwa na ukuaji wa uchumi shirikishi katika kipindi kifupi, maana maendeleo ni mchakato.

Mheshimiwa Spika, yapo maeneo ambayo bado yanahitaji msukumo zaidi ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo ambayo katika nchi yetu inaajiri takribani theluthi mbili ya Watanzania lakini imekuwa ikikua kwa kasi ndogo na ndiyo maana Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza tija kwenye kilimo kwa kutilia mkazo kilimo cha umwagiliaji kuhakikisha upatikanaji wa mikopo, pembejeo na masoko ya uhakika, kuhamasisha kilimo cha kibishara na kujenga mnyororo wa thamani.

Mheshimiwa Spika, aidha, Tanzania ni mfano bora duniani kwa upande wa huduma za kifedha jumuishi (financial inclusion), ambapo zaidi ya watu milioni 17 wanafanya miamala ya malipo kupitia simu za mkononi.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya kodi na tozo nyingi, tozo 16 ambazo zinatoza wamiliki wa shule binafsi. Serikali imesikia maoni ya Waheshimiwa Wabunge kuhusu kuondoa baadhi ya kodi na tozo kwenye shule binafsi. Serikali imezingatia maoni hayo na imeamua kuondoa tozo zifuatazo:-

Kwanza, ni tozo ya kuendeleza Mafunzo ya Ufundi (SDL); na pili, ni ada ya Zimamoto. Lengo la hatua hizi ni kupunguza gharama kwa wazazi na walezi katika kuwapatia watoto wetu elimu na kuziwezesha shule kutoa elimu kwa gharama nafuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni matumaini ya Serikali kuwa wamiliki wa shule wataipokea dhamira hii njema ya Serikali; na hivyo kupitia viwango na ada wanazozitoza ili kuzipunguza na hivyo kutoa fursa zaidi kwa watoto na vijana kutoka katika familia maskini ili ziweze kumudu ada za shule hizo binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya utegemezi wa kibajeti, kwamba pamoja na ukweli kuwa washirika wa maendeleo kutoka nje wanaendelea kupunguza kasi yao ya kutoa mikopo na misaada, bado bajeti ya Serikali imeendelea kuongeza kiasi cha utegemezi wa mikopo na misaada.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuongeza kasi ya makusanyo ya mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi kutoka kwa washirika wa maendeleo. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2011/2012 kiwango cha utegemezi kimeendelea kupungua kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 3.9 sawa na asilimia 29 ya bajeti; mwaka uliofuta 2012/2013, fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 3.1 sawa na asilimia 21 ya bajeti; mwaka wa 2013/2014 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 3.8 sawa na asilimia 21 ya bajeti; mwaka 2014/2015 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 2.9 sawa na asilimia 15 ya bajeti; mwaka 2015/2016 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 2.3 sawa na asilimia 10 ya bajeti; na mwaka huu wa fedha 2016/2017 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 3.6 sawa na asilimia 12 ya bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwenendo huu unaendana kabisa na fundisho la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere linalosema self-reliance is the means by which people develop. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba Serikali ichukue hatua ya kuyaelekeza mabenki ya kibiashara kupitia Benki Kuu ya Tanzania, kupunguza riba kama ambavyo wao wamepunguziwa ili wananchi waweze kukopa.

Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kutumia Mfumo wa Riba wa Soko Huru, ulichukuliwa na Serikali takribani miongo miwili iliyopita, baada ya mfumo ulikuwepo wa kudhibiti riba, kusababisha benki zetu kuwa na mikopo mikubwa chechefu na kupata hasara.

Mheshimiwa Spika, tangu mfumo wa soko huria umeanza kutumika, mikopo iliyokwenda kwenye sekta binafsi imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, uwiano kati ya mikopo kwa sekta binafsi na Pato la Taifa ilipanda kutoka 4% mwaka 2000 hadi 16% mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika, mfumo wa soko huria pia umesaidia kuelekeza mikopo kwenye shughuli za kiuchumi zenye tija zaidi na hivyo kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi. Kama wengi manavyojua, tumeshuhudia uchumi kukua kwa wastani wa 6.7% kila mwaka katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliopita. Hivyo, haitakuwa busara kurudi katika utaratibu wa kudhibiti riba ambapo hapo awali ulituletea shida. (Makofi)

Aidha, Benki Kuu, ikiwa msimamizi wa benki za biashara, ikitoa maagizo ya kupunguza riba itakinzana na jukumu lake la kuzisimamia benki ipasavyo, maana endapo benki zitapata hasara, itakuwa vigumu kuzichukulia hatua, kwani Benki Kuu itakuwa imehusika katika kuzipangia riba.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu ili kuongeza ukwasi hivi karibuni yaani kupunguza discount rate na sehemu ya amana zinazowekwa Benki Kuu zinaonesha matokeo ya kushusha riba katika soko la jumla, ambapo riba ya mikopo ya siku moja baina ya benki za biashara imeshuka kutoka wastani wa 13% mwezi Disemba, 2016 hadi wastani wa 5% katika wiki mbili za kwanza za mwezi Juni, 2017.

Mheshimiwa Spika, wakati huo huo wastani wa riba ya dhamana za Serikali imeshuka kutoka 15.12% hadi asilimia 7.95. Matokeo haya yanaashiria kwamba riba za kukopesha nazo zitashuka kutokana na nguvu za soko.

Mheshimiwa Spika, tatizo lililopo kwa sasa ni kuongezeka kwa mikopo chechefu ambayo inafanya benki zifanye tahadhari kubwa katika kutoa mikopo pamoja na kuendelea kutoza riba kubwa. Benki Kuu imezielekeza benki zenye uwiano mkubwa wa mikopo chochefu ziweke mikakati ya kurudisha uwiano huo kwenye kiwango kinachotakiwa cha 5% na kuzihimiza kutumia taarifa za Credit Reference Bureaus ili kupunguza mikopo chechefu na riba.

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja ya malimbikizo ya VAT, na madai mbalimbali kwamba ni nini mkakati wa Serikali kulipa malimbikizo hayo?

Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kufungua akaunti ya Escrow kwa ajili ya kufanya marejesho ya madai yanayotokana na ununuzi wa sukari inayotumika viwandani na hivyo kuondoa changamoto zilizokuwepo kama nilivyotangaza siku niliposoma hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kuhusu madai mbalimbali (arrears), Serikali inaendelea kuyahakiki na kulipa. Kama nilivyoeleza katika hotuba ya bajeti, hadi mwezi Juni, 2016 madai yaliyokuwa yamewasilishwa na taasisi mbalimbali yalikuwa ya jumla ya shilingi bilioni 2934.4 ambapo jumla ya shilingi bilioni 1997.9 sawa na asilimia 68.1 zilithibitika kuwa madai halali baada ya uhakiki.

Mheshimiwa Spika, kati ya madai yaliyohakikiwa, Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 796.5 hadi ilipofikia mwezi Machi, 2017 na hivyo kubakia na madai ya shilingi bilioni 1201.4 ambayo yataendelea kulipwa kulingana na upatikanaji wa fedha. Madai yaliyolipwa; wakandarasi wamelipwa jumla ya shilingi bilioni 632.1, wazabuni shilingi bilioni 78.8, watumishi shilingi bilioni 67.5 na watoa huduma shilingi bilioni 17.8.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga shilingi bilioni 1,000 kwa ajili ya kuendelea kulipa madai hayo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu marejesho ya VAT Serikali imeboresha utaratibu wa uhakiki ili kudhibiti changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba fedha za maendeleo zinaonekana kuwa nyingi kwa kuwa zimechanganywa pamoja na fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Mheshimiwa Spika, nitasema tu kwa kifupi kwamba uwekezaji katika elimu ndiyo uwekezaji bora (is the best investment), hivyo kuwezesha vijana wa Kitanzania kusoma elimu ya juu kwa kuwapatia mikopo, ni uwekezaji wa kimaendeleo kwa hakika na ndiyo maana ni lazima ziwekwe kwenye fedha za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba bajeti ya mwaka ujao wa fedha haina chochote kuhusu Benki ya Wakulima iliyoanzishwa mwaka 2015 kwa kusudio la mtaji wa shilingi trilioni moja na kukopesha wakulima 200,000 kwa mwaka, lakini sasa imeishia kukopesha wakulima 3,700 na mtaji wa shilingi bilioni 60 tu kwa miaka mitano. Mbali na shilingi bilioni 60 za awali, Serikali imeshaipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) fedha zaidi za kuongeza mtaji ambazo ni shilingi bilioni 209.5, baada ya Serikali na TADB kutia saini mkataba wa fedha hizo mnamo tarehe 5 Juni, 2017. Fedha hizo zinatokana na mkopo wa Serikali kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na ni sehemu ya utekelezaji kwa awamu azma ya Serikali ya kuipatia benki hiyo mtaji wa angalau shilingi bilioni 800. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kinachoendelea sasa ni taratibu za kibenki za kuhakikisha miamala stahiki inafanyika kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika na TADB, hii ikijumlisha pia Benki Kuu ya Tanzania kupokea fedha hizo kwa dola za Kimarekani ambazo ni milioni 93.5 na kuzibadilisha na kuziingiza kwenye akaunti ya TADB kwa shilingi za Kitanzania zilizotajwa.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi zinategemewa kuongeza kiasi cha mikopo itakayotolewa kwa wakulima na wafugaji na pia kuiwezesha benki kutekeleza mapango wake mpya wa kuwafikia wakulima nchi nzima kwa utaratibu maalum (clustery).

Aidha, Benki ya Maendeleo ya Kilimo tayari imefanya mawasiliano rasmi na Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchi na Wizara ya Kilimo, Utalii, Mifugo na Uvuvi na ile ya Viwanda na Biashara ya Zanzibar na kuwaomba waainishe na kuwasilisha katika benki hiyo miradi ya kilimo ya kipaumbele ambayo mikoa yao inapendekeza izingatiwe zaidi katika kupatiwa mikopo na benki.

Mheshimiwa Spika, kuiongezea mtaji benki yetu ya kilimo, ni sehemu ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano wenye lengo la kufungamanisha maboresho ya sekta ya kilimo na mpango mpana wa nchi kuelekea uchumi wa viwanda na hususan viwanda vile vinavyotegemea kiasi kikubwa malighafi zinazotokana na mazao ya kilimo ya ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa hii Benki ya Kilimo na benki nyingine za maendeleo zinawezeshwa ili kuchangia maendeleo ya kilimo na viwanda kama ilivyodhamiliwa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuhitimisha kuwa kama nilivyoeleza katika hotuba zangu, hatua zilizopendekezwa kwenye bajeti hii, zinalenga kujenga msingi madhubuti wa uchumi wa viwanda na kupanua fursa za ajira na biashara.

Mheshimiwa Spika, dhamira yetu sote ni kufikia kiwango cha uchumi wa kipato cha kati itakapofika mwaka 2025. Ili kushiriki katika mafanikio hayo, ni lazima kila mmoja wetu atakayeshiriki katika shughuli halali ya uzalishaji au kutoa huduma na afanye hivyo kwa juhudi na maarifa ili kuleta tija.

Mheshimiwa Spika, kufanikiwa kwa bajeti hii kunahitaji nidhamu ya hali ya juu katika usimamizi wa mapato na matumizi. Ili kufikia azma hii, juhudi ya pamoja kati ya Serikali na wadau wote zinahitajika ikiwa ni pamoja na kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi kwa kuwekeza zaidi katika maeneo ya kipaumbele.

Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa kila Mtanzania kutimiza wajibu wake hususan kulipa kodi stahiki ili bajeti hii iweze kutekelezwa kama ilivyopangwa na kama Waheshimiwa Wabunge mlivyosisitiza.

Mheshimiwa Spika, napenda nirudie maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwamba kila mwananchi akinunua kitu au huduma, adai risiti na yule anayeuza kitu au huduma na yeye atoe risiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kuwashukuru sana watumishi wenzangu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zake zote kuanzia wahudumu wetu ambao walikesha na sisi usiku kucha ili kuandaa bajeti nzuri kwa Watanzania. Niseme kwa lugha ya kigeni I am proud of you and keep it up in service of our mother land. Maintain professionalism and integrity. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi/ Vigelegele)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, na mimi naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama tena mbele ya Bunge lako Tukufu kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2017/2018. Utakumbuka tarehe 08, Juni, 2017 niliwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2016, Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2017/2018 na Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba zote mbili nilieleza shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na Serikali katika kipindi cha mwaka 2016/2017 pamoja na mafanikio na changamoto zilizojitokeza. Aidha, nilieleza malengo na miradi ya kipaumbele ambayo Serikali inakusudia kutekeleza katika mwaka 2017/2018 na mapendekezo ya bajeti. Waheshimiwa Wabunge walipata nafasi ya kuzipitia hotuba hizo pamoja na viambatisho vyake na kutoa maoni na mapendekezo juu ya namna bora zaidi ya kufanikisha ajenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaletea Watanzania maendeleo.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha vizuri mjadala huu ambao unatarajiwa kuhitimishwa hivi leo.

Mheshimiwa Spika, napenda kutambua michango iliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini pamoja na maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni yaliyowasilishwa na Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba kwa niaba ya Msemaji wa Kambi hiyo kwa Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, ninathamini sana maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge wote. Wabunge 193 walichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali, kati ya hao wa kuzungumza walikuwa ni 165 na 28 kwa maandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi na Wizara yangu tunawashukuru kwa dhati kabisa kwa pongezi ambazo mlitupatia, nikianza na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alinipigia simu kutoa pongezi zake, lakini pia ninyi Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wengi ambao wametupongeza kutoka ndani na nje ya nchi yetu, kwa kweli mmetupatia nguvu ya kufanya vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati wa mjadala wa hotuba nilizoziwasilisha, Serikali imepokea michango mingi sana na ushauri. Yapo maeneo yaliyoungwa mkono na mengine ambayo yalilenga kuboresha Bajeti ya Serikali au kuikosoa. Napenda kulihakikishia Bunge kwamba tumepokea michango yote yenye afya kwa maendeleo ya Taifa letu. Baadhi tutayazingatia katika bajeti hii na bajeti zitakazofuata; na leo nitadhihirisha tena kwamba bajeti hii haijawahi kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baadhi ya hatua ambazo ziliungwa mkono na Waheshimiwa Wabunge wengi ni pamoja na zifuatazo:-

Kwanza, ni kufuta ada ya mwaka ya leseni ya magari, kutoa msamaha wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote ya ada ya leseni ya magari yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma, kuanzisha maeneo maalum (clearing houses) ya kukagua na kuthibitisha thamani ya madini kabla ya kusafirishwa, kuondoa VAT kwenye bidhaa za mtaji, kusamehe VAT kwenye vyakula vya mifugo, kutoa msamaha wa VAT na ushuru wa forodha kwenye vifaa maalum vya kutengeneza vifaa vya watu wenye ulemavu; pia miradi ya kielelezo itakayopewa msukumo maalum katika mwaka wa 2017/2018 ikiwemo miradi ya maji, zahanati, vituo vya afya, uendelezaji wa elimu katika ngazi zote, ununuzi wa vifaa tiba, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge, uimarishaji wa Shirika la Ndege la Tanzania, miradi ya umeme, miradi ya makaa ya mawe na chuma, uendelezaji wa maeneo maalum ya uwekezaji, ujenzi wa barabara za kuunganisha mikoa na ule wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Uganda hadi Bandari ya Tanga, lakini pia kuendeleza utulivu wa uchumi wa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba nami niungane pia na Waheshimiwa Wabunge wengi waliopongeza juhudi zilizochukuliwa na Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kulinda rasilimali za Taifa letu ili kuhakikisha kwamba Watanzania tunanufaika na rasilimali za nchi na hususan madini.

Mheshimiwa Spika, tunampongeza sana Jemadari wetu Mkuu kwa kuthubutu kufichua na kuweka hadharani udhalimu ambao tumekuwa tunafanyiwa kwa miaka mingi kupitia utoroshaji wa madini na upotevu wa mapato ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunamhakikishia Mheshimiwa Rais wetu kuwa tunamuunga mkono na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu amlinde, ampe afya njema na amtie nguvu katika kazi yake ngumu ya kuongoza mapambano dhidi ya uporaji wa rasilimali za nchi yetu. Ushindi ni lazima na hakuna kurudi nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa niseme kidogo juu ya ushauri uliotolewa na Wabunge wengi. Kama nilivyosema mwanzo, yapo maoni yaliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge wengi katika maeneo mbalimbali ili Serikali iangalie namna ya kuyazingatia katika bajeti hii na zijazo. Naomba kurejea ushauri muhimu sana uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge kama ifuatavyo:-

(i) Kuongeza kasi ya kutekeleza miradi ya maji nchini na hasa vijijini kwa kuongeza bajeti ya maji;

(ii) Kuboresha mfumo wa utozaji kodi ya majengo;

(iii) Kukamilisha haraka utaratibu mzuri na endelevu na kuanza kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji haraka iwezekanavyo;

(iv) Kuongeza kasi ya kulipa madeni ya ndani ya wakandarasi, watoa huduma na watumishi;

(v) Kudhibiti kasi ya ukuaji wa Deni la Taifa;

(vi) Kuendeleza utulivu wa uchumi ikiwa ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei;

(vii) Kuimarisha thamani ya shilingi na kuongeza wigo wa huduma za kibenki hadi vijijini; na

(viii) Kujenga mazingira rafiki kwa uwekezaji na kufanya biashara nchini kwa kudumisha mashauriano na ushirikiano wa dhati na sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nianze kufafanua baadhi ya hoja.

Hoja ya kwanza, Serikali ilishauriwa iongeze tozo ya shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli kwa ajili ya Mfuko wa Maji ili kuwe na chanzo kinachotabirika (ring fence).

Mheshimiwa Spika, hii ilikuwa ni hoja mama ambayo ilitawala mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Baada ya Serikali kutafakari kuleta pendekezo la kufuta ada ya Motor Vehicle License ili kuondoa kero ya muda mrefu ya kutoza ada hiyo hata kama magari hayatembei na kufidia mapato hayo kwa kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa kwa shilingi 40 kwa lita; Waheshimiwa Wabunge walishauri mapato yatakayotokana na hatua hiyo, ndiyo yaelekezwe kwenye Mfuko wa Maji kwa kutambua kwamba kuongeza zaidi ushuru wa bidhaa kwenye mafuta, kutaathiri wananchi wengi kwa kuwa kutasababisha bei za bidhaa karibu zote, chakula, usafiri, usafirishaji, gharama za uzalishaji na gharama za maisha kwa ujumla kupanda sana kutokana na kupandisha bei ya nishati hiyo muhimu tena katika kipindi ambacho bei za mafuta katika Soko la Dunia inatarajiwa kuongezeka kwa wastani wa dola 50 kwa pipa hadi dola 60 mpaka 65 katika mwaka 2018.

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kuelekeza chanzo cha mapato mahususi kwenye matumizi maalum (revenue earmarking) unasaidia kuongeza fedha kwenye eneo linalolengwa na pia kuhakikisha upatikanaji wa fedha (funding stability). Ni kweli pia utaratibu huu umeleta matokeo chanya kwenye programu ya kusambaza umeme vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini. (Makofi)

Aidha, ahadi iliyopo katika katika ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 hadi 2020, ni deni na Serikali ina nia thabiti ya kumtua mama ndoo kichwani katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jitihada za Serikali katika kipindi kifupi cha miezi 18 zinathibitishwa na kukamilika kwa miradi mikubwa ya maji ikiwemo Ruvu Chini ambayo inatoa lita milioni 270 kwa siku; Ruvu Juu lita milioni 196 kwa siku; Visima vya Mpera na Kimbiji lita milioni 260 kwa siku na Sumbawanga lita milioni 13 kwa siku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miradi mingine ya maji iliyokamilika ni Nansio, Ukerewe lita milioni 8.6 kwa siku, Bukoba Mjini lita milioni 18 kwa siku, Musoma Mjini lita milioni 30 kwa siku, Sengerema lita milioni 15 kwa siku, lakini pia mradi ule wa Msanga Mkuu kule Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo, Serikali inapenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge hili kwa ajili ya miradi ya maji kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambazo ni shilingi bilioni 249.5 na Mfuko wa Maji shilingi bilioni 158.5 zitatolewa kuendana na mpango kazi na kupitia Kamati ya Bajeti, Bunge litapewa taarifa rasmi ya utekelezaji wa hadi hii ya Serikali kila nusu mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, hatua nyingine zitakazochukuliwa na Serikali ni pamoja na zifuatazo:-

Kwanza, ni kuharakisha mchakato wa mikopo kwa ajili ya miradi ya maji kutoka taasisi mbalimbali na nchi rafiki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba leo terehe 20 Juni, 2017 nimesaini mkopo wa dola za Kimarekani milioni 400 kutoka Benki ya Credit Swiss ili kugharamia miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna miradi mikubwa sita:- Kwanza kuna mradi wa upanuzi wa huduma za maji
Mijini ambao utagusa Mikoa ya Kagera, Rukwa, Dodoma,
Morogoro, Pwani, Simiyu, Iringa, Mara na Mwanza. (Makofi)

Mradi wa pili ni mradi wa uchimbaji wa visima na ujenzi wa Mabwawa katika Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Shinyanga na Simiyu. (Makofi)

Mradi wa tatu ni mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya maji Mijini, itagusa Mikoa ya Rukwa, Dodoma, Morogoro, Kigoma, Kagera, Lindi, Manyara, Mtwara, Tabora, Ruvuma na Kilimanjaro. (Makofi)

Mradi wa nne, ni mradi wa upanuzi wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira Dar es Salaam na hii itagusa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. (Makofi)

Mradi wa tano ni kuendeleza na kusimamia rasilimali za maji. Itagusa Mikoa ya Pwani, Rukwa, Ruvuma, Tanga, Kigoma, Dodoma, Manyara, Njombe, Singida, Shinyanga, Tabora, Songwe, Mwanza, Kagera, Geita, Mara na Morogoro(Makofi)

Mradi wa sita ni mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Kahama na Shinyanga na mikoa itakayohusika ni Shinyanga na Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha taratibu za mkopo kutoka Exim Bank of India dola milioni 500 ambazo ni takriban shilingi trilioni 1.3 kwa ajili ya miradi ya maji katika miji 17 nchini. Hivi sasa mkopo huo umeshakufanyiwa uchambuzi na Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Madeni na Waziri wa Fedha na Mipango amesharidhia kwa niaba ya Serikali, fedha hizi zikopwe. Taratibu zinazobaki sasa ni kukamilisha usanifu wa miradi hii na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hatimaye kusaini mkataba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Serikali inafuatilia upatikanaji wa fedha Euro milioni 102 kutoka Green Climate Change Fund kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji ya Simiyu. Pia nchi rafiki ikiwemo Morocco na Misri zimeonyesha utayari wa kugharamia utekelezaji wa miradi ya maji hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa ni kwamba Serikali inatoza Kodi ya Leseni ya Magari kwa mwaka (Annual Motor Vehicle License Fee) kwa Watanzania maskini ambao hawamiliki gari kwa kutoza kodi hiyo katika mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ikiwemo mafuta ya taa unalenga kuwalinda Watanzania dhidi ya madhara ya uchakachuaji wa mafuta (fuel adulteration).

Kwa sasa tofauti ya kodi zinazotozwa kwenye mafuta ya taa na Dizeli ni shilingi 53 kwa lita. Endapo ushuru huu wa shilingi 40 hautaongezwa kwenye mafuta ya taa, tofauti ya kodi itakuwa shilingi 93 kwa lita ambayo itachochea uchakachuaji wa mafuta utakaosababisha uharibifu wa magari na mitambo na kupoteza mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ongezeko la tozo kwenye petroli, dizeli na mafuta ya taa limefikiwa ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wamiliki wa magari kudaiwa ada ya Motor Vehicle License hata kama gari halitembei, lakini pia tumefanya hivyo kwa namna ambayo haitachochea uchakachuaji wa mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatua hiyo pia itaiwezesha Serikali kupata mapato ambayo yatatumika kugharamia huduma muhimu za jamii kama barabara, afya, dawa na vifaa tiba ambavyo Watanzania masikini pia watafaidika nazo.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, palikuwepo na hoja kwamba msamaha (Tax Amnesty) ambayo nilitangaza ile tarehe 8 Juni, 2017 ambayo ulitolewa kwenye Ada ya Mwaka ya Leseni uhusishe na ada ya ukaguzi wa vifaa vya kuzima moto (Fire Inspection Fee).

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, hatua ya Serikali ya kutoa msahama (Tax Amnesty) kwa ada ya leseni ya magari itahusisha pia ada, riba na adhabu ya madeni yote ye fire inspection fee yaliyolimbikizwa miaka ya nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitarudia tena.

Mheshimiwa Spika, hatua ya Serikali ya kutoa msahama (Tax Amnesty) kwa ada ya leseni ya magari itahusisha pia ada, riba na adhabu ya madeni yote ye fire inspection fee yaliyolimbikizwa miaka ya nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba tozo ya shilingi 10,000 kwenye nyumba ambazo hazijathaminiwa hususan za vijijini ni kuwaongezea mzigo wananchi wa kijijini, lakini pia ile tozo ya shilingi 50,000 kwa ghorofa ambazo wanaishi wastaafu iondolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kodi ya majengo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Miji (The Urban Authorities Rating) Sura ya 289. Kifungu cha pili cha Sheria ya Mamlaka ya Miji (The Urban Authorities Act) inabainisha kuwa kodi ya majengo inatozwa kwenye majengo yaliyojengwa kwenye Mamlaka za Majiji, Miji na Miji Midogo. Vijiji havitahusika katika kodi hii.

Mheshimiwa Spika, kodi ya majengo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Miji (The Urban Authorities Rating) Sura ya 289 na kifungu cha pili cha Sheria ya Mamlaka ya Miji (The Urban Authorities Act) inabainisha kuwa kodi ya majengo inatozwa kwenye majengo yaliyojengwa kwenye Mamlaka za Majiji, Miji na Miji Midogo. Vijiji havihusiki katika kodi hii.

Mheshimiwa Spika, ninasema, aidha kwa mujibu wa sheria, wananchi wenye umri zaidi ya miaka 60 hawapaswi kulipa kodi ya majengo wanayoyatumia kama makazi yao wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja kwamba Serikali isitoze kodi ya majengo kwenye nyumba za tope na tembe.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha (3); “Kodi ya majengo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Miji, Sura ya 289 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Fedha ya mwaka 2015.” Kwa mujibu wa kifungu cha pili cha Sheria za Mamlaka za Miji (The Urban Authorities Act) kinabainisha kuwa kodi ya majengo inayotozwa kwenye majengo yaliyojengwa kwenye Mamlaka za Majiji, Manispaa, Miji Midogo na Halmashauri za Wilaya.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha tatu cha Sheria hii kimetafsiri nyumba zinazotakiwa kutozwa kodi ya majengo kuwa ni nyumba zote zilizoko ndani ya Mamlaka ya Majiji, Manispaa, Miji Midogo na Halmashauri za Wilaya ambazo zimeshajengwa na kuanza kutumika kwa makazi. Kwa maelezo hayo, kodi ya majengo inatozwa kwa nyumba zote zilizoko kwenye Mamlaka ya Majiji, Miji na Miji Midogo ambazo zimeshaanza kutumika kwa makazi kama ilivyobainishwa kwenye hotuba yangu ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018. Hata hivyo, tozo hizo hazitahusisha nyumba za tope na tembe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nilieleze Bunge lako na wananchi kwa ujumla kuwa kodi ya majengo kama nilivyosema itatozwa katika Miji, Majiji na Miji Midogo kwa mujibu wa Sheria za Kodi ya Majengo ya Mamlaka ya Miji Sura ya 289. Kodi hiyo itatozwa katika majengo ya kudumu yaani yale yaliyojengwa kwa tofali za saruji, tofali za kuchoma na kuezekwa kwa bati na siyo za udongo wala zilizoezekwa kwa nyasi au zile za tembe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu uwasilishaji wa mapato ya kodi ya majengo kwa Halmashauri. Mapato ya kodi ya majengo na mabango yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuhifadhiwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, Serikali itaweka utaratibu wa kurejesha mapato hayo kwenye Halmashauri ambapo watatakiwa kuwasilisha mahitaji yao halisi. Aidha, Serikali itapitia mahitaji yao ili kujiridhisha kabla ya kuwarejeshea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya kutokutoza kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye magari ya kubeba wagonjwa. Kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya kwa wananchi wetu na hasa katika maeneo ya vijijini, Serikali imeamua kufanya marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye magari yanayotumika katika kubeba wagonjwa (ambulance).

Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kufanya marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa magari yanayotumika katika kubeba wagonjwa (ambulance). Hatua hii itahusisha magari yanayoingizwa nchini yakiwa yametengenezwa mahsusi kwa ajili ya kubeba wagonjwa na kwamba yanaingizwa nchini kwa matumizi ya hospitali au vituo vya kutoa huduma za afya vilivyosajiliwa kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali itatumia utaratibu wa Hati ya Malipo ya Hazina (Treasury Voucher System) katika kusimamia misamaha hii ambapo kodi inayosamehewa italipiwa na Serikali kupitia Hazina kama inavyofanyika kwa taasisi za dini na kadhalika ili kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye ada na vibali vya uwindaji vitolewavyo na Serikali. Serikali inaondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye ada, leseni na vibali vya uwindaji. Hatua hii ina lengo la kuhamasisha ukuaji wa shughuli za uwindaji na sekta ya utalii kwa ujumla. (Makofi)

Kulikuwa na hoja kuhusu ada ya tathmini ya mazingira. kutokana na kilio cha wawekezaji wengi na hasa katika Sekta ya Viwanda, napendekeza kufuta Ada ya Kufanya Tathmini ya Mazingira (Environmental Impact Assessment) kwa wawekezaji wote wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, narudia.

Napendekeza kufuta Ada ya Kufanya Tathmini ya Mazingira (Environmental Impact Assessment) kwa wawekezaji wote wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba Serikali ifanye marekebisho kwenye Sheria ya EPOCA, Serikali imelisikia hili na baada ya kutafakari kwa kina, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya EPOCA ili:-

Moja, hisa za asilimia 25 zitakazouzwa na kampuni ya mawasiliano kwenye Soko la Hisa ziuzwe kwa umma ili kujumuisha Watanzania au Kampuni yoyote ya Kitanzania; Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kampuni zinazomilikiwa kwa pamoja baina ya Watanzania na raia wa nje; raia na kampuni au taasisi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; au raia wa kampuni kutoka nchi nyingine yoyote.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa sharti lililopo kwa mujibu wa sheria ni kwa hisa husika kuuzwa kwa raia wa Tanzania pekee.

Mheshimiwa Spika, ya pili ni kuziondoa kampuni ndogo za mawasiliano ambazo zina leseni ya application service kwenye sharti la kuuza hisa kwenye Soko la Hisa ili kubaki na kampuni kubwa za mawasiliano zenye leseni ya network facility au network service. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatu, Kampuni ya simu itakayoshindwa kufikia mauzo ya asilimia 25 kutokana na kutofaulu kwa toleo kwa umma (Unsuccessful Public Offer),Waziri mwenye dhamana atatoa maelekezo yaani directives ya namna kampuni husika itakavyoweza kutoa hisa kufikia asilimia 25 kwa kadri hali ya soko itakavyoruhusu, baada ya kupokea maombi ya kampuni ya simu iliyotolewa chini ya Sheria ya EPOCA na baada ya kupokea mapendekezo ya Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu watoa huduma na wauza bidhaa katika maeneo yasiyo rasmi kusajiliwa; ili kuhamasisha wafanyabiashara ndogo ndogo, kurasimisha shughuli zao na Serikali iweze kukusanya kodi, utaratibu nilioutangaza kupitia Bajeti Kuu ya Serikali kuhusu kuwatambua wafanyabiashara wa aina hii na kuwapa vitambulisho, itahusisha pia watoa huduma za chakula (caterers), washereheshaji (masters of ceremony) katika shughuli mbalimbali na wafanyabiasha wadogo wasio rasmi wanaofanya biashara katika maeneo rasmi.

Mheshimiwa Spika, naomba nirudie. Ili kuhamasisha wafanyabiashara wadogo kurasimisha shughuli zao na Serikali iweze kukusanya kodi, utaratibu nilioutangaza kupitia Bajeti Kuu ya Serikali kuwatambua wafanyabiashara wa aina hii na kuwapa vitambulisho; itahusisha pia watoa huduma za chakula (caterers), washereheshaji (masters of ceremony) katika shughuli mbalimbali na wafanyabiasha wadogo wasio rasmi wanaofanya biashara katika maeneo rasmi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu utozaji wa tozo kwa kutumia fedha za kigeni kwenye vyombo vya uvuvi vilivyosajiliwa nchini; Serikali imesikia maoni ya Waheshimiwa Wabunge kuhusiana na kero wanayopata wavuvi nchini ya kutozwa tozo mbalimbali kwa fedha za kigeni kwenye vyombo vya uvuvi vilivyosajiliwa nchini.

Mheshimiwa Spika, kuanzia sasa Serikali inaagiza taasisi zote zinazohusika na utozaji wa tozo hizo ziache utaratibu huo mara moja na zianze kutoza kwa kutumia shilingi ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kukusanya kodi inayotokana na mapato kutoka kwenye sekta ya michezo ya kubahatisha.

Kwa kuzingatia ushauri wa Waheshimiwa Wabunge, Serikali imeona kuna uwezekano wa kupata mapato mengi kutoka kwenye sekta ya michezo ya kubahatisha. Hivyo, kuanzia tarehe 1 Julai, 2017 mapato yote yatakayotokana na michezo ya kubahatisha yatakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mheshimiwa Spika, mapato hayo yatawasilishwa Mfuko Mkuu wa Serikali, Serikali itaweka utaratibu wa kuzirejesha fedha hizo kwenye Bodi ya Michezo ya kubahatisha baada ya kuhakiki mahitaji na matumizi ya Bodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba uchumi wa taifa siyo shirikishi, na bajeti iko kinyume na mahitaji ya ukuwaji shirikishi wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, niruhusu nitoe darasa kidogo.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, dhana ya uchumi shirikishi ni pana sana. Kwa lugha nyepesi ukuaji wa uchumi unakuwa shirikishi kama jamii inashiriki na kunufaika katika shughuli kuu zinazokuza uchumi wa nchi. Ndiyo kusema lazima uchumi kwa upana wake uwe unakua na kunemeesha wananchi walio wengi kwa namna ambayo ni endelevu (broad based growth that generate sustain progress in living standards).

Mheshimiwa Spika, ukuaji wa uchumi shirikishi unapimwa kwa viashiria vingi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa fursa za ajira (job creation), kupungua kwa umasikini, kuongezeka kwa tabaka la kati katika nchi (growth of the middle class), kupungua kwa tofauti za kipato (declined in income inequality), kupanuka kwa wigo wa fursa na huduma za kiuchumi na hususan masoko na huduma za kifedha (financial services) na usalama (security).

Mheshimiwa Spika, aidha, ukuaji wa uchumi shirikishi, unajengwa juu ya nguzo (pillars) takriban saba ambazo ni:-

(1) Elimu na ujuzi; (Makofi)

(2) Huduma za kijamii na miundombinu; (Makofi)

(3) Mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi; (Makofi)

(4) Huduma za kifedha na uwekezaji;

(5) Ujasiliamali na ukuzaji wa rasilimalia (accumulation of assets);

(6) Ajira na mafao ya wafanyakazi; na

(7) Uhawalishaji wa rasilimali fedha (fiscal transfers).

Mheshimiwa Spika, kwa Waheshimiwa Wabunge wanaopenda kupata elimu ya kina juu ya somo hili, kuna vitabu na machapisho mengi na wanaweza kujisomea ikiwa pamoja na taarifa ya hivi karibuni ya World Economic Forum ambayo inaitwa The Inclusive Growth and Development Report, 2017. Hivyo, siyo sahihi hata kidogo kuangalia kigezo kimoja tu na kutoa hukumu kwamba ukuaji wa uchumi siyo shirikishi au kwamba bajeti iko kinyume na mahitaji ya ukuaji shirikishi wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa 2016 ambacho kiligawiwa kwa Waheshimiwa Wabunge, tarehe 8 Juni, kinaonesha wazi kuwa Tanzania imepiga hatua nzuri katika viashiria vingi na ujenzi wa misingi ya uchumi shirikishi chini ya dhana ya kujenga uchumi wa viwanda. Bajeti ya mwaka 2017/2018 imejielekeza katika maeneo yote ya msingi kwa ujenzi wa uchumi shirikishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa kila kitu siyo waridi na haiwezekani kuwa na ukuaji wa uchumi shirikishi katika kipindi kifupi, maana maendeleo ni mchakato.

Mheshimiwa Spika, yapo maeneo ambayo bado yanahitaji msukumo zaidi ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo ambayo katika nchi yetu inaajiri takribani theluthi mbili ya Watanzania lakini imekuwa ikikua kwa kasi ndogo na ndiyo maana Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza tija kwenye kilimo kwa kutilia mkazo kilimo cha umwagiliaji kuhakikisha upatikanaji wa mikopo, pembejeo na masoko ya uhakika, kuhamasisha kilimo cha kibishara na kujenga mnyororo wa thamani.

Mheshimiwa Spika, aidha, Tanzania ni mfano bora duniani kwa upande wa huduma za kifedha jumuishi (financial inclusion), ambapo zaidi ya watu milioni 17 wanafanya miamala ya malipo kupitia simu za mkononi.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya kodi na tozo nyingi, tozo 16 ambazo zinatoza wamiliki wa shule binafsi. Serikali imesikia maoni ya Waheshimiwa Wabunge kuhusu kuondoa baadhi ya kodi na tozo kwenye shule binafsi. Serikali imezingatia maoni hayo na imeamua kuondoa tozo zifuatazo:-

Kwanza, ni tozo ya kuendeleza Mafunzo ya Ufundi (SDL); na pili, ni ada ya Zimamoto. Lengo la hatua hizi ni kupunguza gharama kwa wazazi na walezi katika kuwapatia watoto wetu elimu na kuziwezesha shule kutoa elimu kwa gharama nafuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni matumaini ya Serikali kuwa wamiliki wa shule wataipokea dhamira hii njema ya Serikali; na hivyo kupitia viwango na ada wanazozitoza ili kuzipunguza na hivyo kutoa fursa zaidi kwa watoto na vijana kutoka katika familia maskini ili ziweze kumudu ada za shule hizo binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya utegemezi wa kibajeti, kwamba pamoja na ukweli kuwa washirika wa maendeleo kutoka nje wanaendelea kupunguza kasi yao ya kutoa mikopo na misaada, bado bajeti ya Serikali imeendelea kuongeza kiasi cha utegemezi wa mikopo na misaada.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuongeza kasi ya makusanyo ya mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi kutoka kwa washirika wa maendeleo. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2011/2012 kiwango cha utegemezi kimeendelea kupungua kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 3.9 sawa na asilimia 29 ya bajeti; mwaka uliofuta 2012/2013, fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni
3.1 sawa na asilimia 21 ya bajeti; mwaka wa 2013/2014 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 3.8 sawa na asilimia 21 ya bajeti; mwaka 2014/2015 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 2.9 sawa na asilimia 15 ya bajeti; mwaka 2015/2016 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 2.3 sawa na asilimia 10 ya bajeti; na mwaka huu wa fedha 2016/2017 fedha za nje zilikuwa shilingi trilioni 3.6 sawa na asilimia 12 ya bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwenendo huu unaendana kabisa na fundisho la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere linalosema self-reliance is the means by which people develop. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba Serikali ichukue hatua ya kuyaelekeza mabenki ya kibiashara kupitia Benki Kuu ya Tanzania, kupunguza riba kama ambavyo wao wamepunguziwa ili wananchi waweze kukopa.

Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kutumia Mfumo wa Riba wa Soko Huru, ulichukuliwa na Serikali takribani miongo miwili iliyopita, baada ya mfumo ulikuwepo wa kudhibiti riba, kusababisha benki zetu kuwa na mikopo mikubwa chechefu na kupata hasara.

Mheshimiwa Spika, tangu mfumo wa soko huria umeanza kutumika, mikopo iliyokwenda kwenye sekta binafsi imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, uwiano kati ya mikopo kwa sekta binafsi na Pato la Taifa ilipanda kutoka 4% mwaka 2000 hadi 16% mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika, mfumo wa soko huria pia umesaidia kuelekeza mikopo kwenye shughuli za kiuchumi zenye tija zaidi na hivyo kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi. Kama wengi manavyojua, tumeshuhudia uchumi kukua kwa wastani wa 6.7% kila mwaka katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliopita. Hivyo, haitakuwa busara kurudi katika utaratibu wa kudhibiti riba ambapo hapo awali ulituletea shida. (Makofi)

Aidha, Benki Kuu, ikiwa msimamizi wa benki za biashara, ikitoa maagizo ya kupunguza riba itakinzana na jukumu lake la kuzisimamia benki ipasavyo, maana endapo benki zitapata hasara, itakuwa vigumu kuzichukulia hatua, kwani Benki Kuu itakuwa imehusika katika kuzipangia riba.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu ili kuongeza ukwasi hivi karibuni yaani kupunguza discount rate na sehemu ya amana zinazowekwa Benki Kuu zinaonesha matokeo ya kushusha riba katika soko la jumla, ambapo riba ya mikopo ya siku moja baina ya benki za biashara imeshuka kutoka wastani wa 13% mwezi Disemba, 2016 hadi wastani wa 5% katika wiki mbili za kwanza za mwezi Juni, 2017.

Mheshimiwa Spika, wakati huo huo wastani wa riba ya dhamana za Serikali imeshuka kutoka 15.12% hadi asilimia
7.95. Matokeo haya yanaashiria kwamba riba za kukopesha nazo zitashuka kutokana na nguvu za soko.

Mheshimiwa Spika, tatizo lililopo kwa sasa ni kuongezeka kwa mikopo chechefu ambayo inafanya benki zifanye tahadhari kubwa katika kutoa mikopo pamoja na kuendelea kutoza riba kubwa. Benki Kuu imezielekeza benki zenye uwiano mkubwa wa mikopo chochefu ziweke mikakati ya kurudisha uwiano huo kwenye kiwango kinachotakiwa cha 5% na kuzihimiza kutumia taarifa za Credit Reference Bureaus ili kupunguza mikopo chechefu na riba.

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja ya malimbikizo ya VAT, na madai mbalimbali kwamba ni nini mkakati wa Serikali kulipa malimbikizo hayo?

Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kufungua akaunti ya Escrow kwa ajili ya kufanya marejesho ya madai yanayotokana na ununuzi wa sukari inayotumika viwandani na hivyo kuondoa changamoto zilizokuwepo kama nilivyotangaza siku niliposoma hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kuhusu madai mbalimbali (arrears), Serikali inaendelea kuyahakiki na kulipa. Kama nilivyoeleza katika hotuba ya bajeti, hadi mwezi Juni, 2016 madai yaliyokuwa yamewasilishwa na taasisi mbalimbali yalikuwa ya jumla ya shilingi bilioni 2934.4 ambapo jumla ya shilingi bilioni 1997.9 sawa na asilimia 68.1 zilithibitika kuwa madai halali baada ya uhakiki.

Mheshimiwa Spika, kati ya madai yaliyohakikiwa, Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 796.5 hadi ilipofikia mwezi Machi, 2017 na hivyo kubakia na madai ya shilingi bilioni 1201.4 ambayo yataendelea kulipwa kulingana na upatikanaji wa fedha. Madai yaliyolipwa; wakandarasi wamelipwa jumla ya shilingi bilioni 632.1, wazabuni shilingi bilioni 78.8, watumishi shilingi bilioni 67.5 na watoa huduma shilingi bilioni 17.8.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga shilingi bilioni 1,000 kwa ajili ya kuendelea kulipa madai hayo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu marejesho ya VAT Serikali imeboresha utaratibu wa uhakiki ili kudhibiti changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba fedha za maendeleo zinaonekana kuwa nyingi kwa kuwa zimechanganywa pamoja na fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Mheshimiwa Spika, nitasema tu kwa kifupi kwamba uwekezaji katika elimu ndiyo uwekezaji bora (is the best investment), hivyo kuwezesha vijana wa Kitanzania kusoma elimu ya juu kwa kuwapatia mikopo, ni uwekezaji wa kimaendeleo kwa hakika na ndiyo maana ni lazima ziwekwe kwenye fedha za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba bajeti ya mwaka ujao wa fedha haina chochote kuhusu Benki ya Wakulima iliyoanzishwa mwaka 2015 kwa kusudio la mtaji wa shilingi trilioni moja na kukopesha wakulima 200,000 kwa mwaka, lakini sasa imeishia kukopesha wakulima 3,700 na mtaji wa shilingi bilioni 60 tu kwa miaka mitano. Mbali na shilingi bilioni 60 za awali, Serikali imeshaipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) fedha zaidi za kuongeza mtaji ambazo ni shilingi bilioni 209.5, baada ya Serikali na TADB kutia saini mkataba wa fedha hizo mnamo tarehe 5 Juni, 2017. Fedha hizo zinatokana na mkopo wa Serikali kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na ni sehemu ya utekelezaji kwa awamu azma ya Serikali ya kuipatia benki hiyo mtaji wa angalau shilingi bilioni 800. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kinachoendelea sasa ni taratibu za kibenki za kuhakikisha miamala stahiki inafanyika kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika na TADB, hii ikijumlisha pia Benki Kuu ya Tanzania kupokea fedha hizo kwa dola za Kimarekani ambazo ni milioni 93.5 na kuzibadilisha na kuziingiza kwenye akaunti ya TADB kwa shilingi za Kitanzania zilizotajwa.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi zinategemewa kuongeza kiasi cha mikopo itakayotolewa kwa wakulima na wafugaji na pia kuiwezesha benki kutekeleza mapango wake mpya wa kuwafikia wakulima nchi nzima kwa utaratibu maalum (clustery).

Aidha, Benki ya Maendeleo ya Kilimo tayari imefanya mawasiliano rasmi na Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchi na Wizara ya Kilimo, Utalii, Mifugo na Uvuvi na ile ya Viwanda na Biashara ya Zanzibar na kuwaomba waainishe na kuwasilisha katika benki hiyo miradi ya kilimo ya kipaumbele ambayo mikoa yao inapendekeza izingatiwe zaidi katika kupatiwa mikopo na benki.

Mheshimiwa Spika, kuiongezea mtaji benki yetu ya kilimo, ni sehemu ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano wenye lengo la kufungamanisha maboresho ya sekta ya kilimo na mpango mpana wa nchi kuelekea uchumi wa viwanda na hususan viwanda vile vinavyotegemea kiasi kikubwa malighafi zinazotokana na mazao ya kilimo ya ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa hii Benki ya Kilimo na benki nyingine za maendeleo zinawezeshwa ili kuchangia maendeleo ya kilimo na viwanda kama ilivyodhamiliwa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuhitimisha kuwa kama nilivyoeleza katika hotuba zangu, hatua zilizopendekezwa kwenye bajeti hii, zinalenga kujenga msingi madhubuti wa uchumi wa viwanda na kupanua fursa za ajira na biashara.

Mheshimiwa Spika, dhamira yetu sote ni kufikia kiwango cha uchumi wa kipato cha kati itakapofika mwaka 2025. Ili kushiriki katika mafanikio hayo, ni lazima kila mmoja wetu atakayeshiriki katika shughuli halali ya uzalishaji au kutoa huduma na afanye hivyo kwa juhudi na maarifa ili kuleta tija.

Mheshimiwa Spika, kufanikiwa kwa bajeti hii kunahitaji nidhamu ya hali ya juu katika usimamizi wa mapato na matumizi. Ili kufikia azma hii, juhudi ya pamoja kati ya Serikali na wadau wote zinahitajika ikiwa ni pamoja na kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi kwa kuwekeza zaidi katika maeneo ya kipaumbele.

Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa kila Mtanzania kutimiza wajibu wake hususan kulipa kodi stahiki ili bajeti hii iweze kutekelezwa kama ilivyopangwa na kama Waheshimiwa Wabunge mlivyosisitiza.

Mheshimiwa Spika, napenda nirudie maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwamba kila mwananchi akinunua kitu au huduma, adai risiti na yule anayeuza kitu au huduma na yeye atoe risiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kuwashukuru sana watumishi wenzangu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zake zote kuanzia wahudumu wetu ambao walikesha na sisi usiku kucha ili kuandaa bajeti nzuri kwa Watanzania. Niseme kwa lugha ya kigeni I am proud of you and keep it up in service of our mother land. Maintain professionalism and integrity. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nami niwapongeze Wenyeviti na Wajumbe wote wa Kamati zote mbili kwa kazi nzuri, kwa kweli kazi yao ni kwa ajili ya kuimarisha uwajibikaji na matumizi adili ya rasilimali za umma na hili halina budi kuungwa mkono.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kuchelewa kwa upelekaji wa fedha, niseme tu kwamba nafikiri hili ni tatizo la kimfumo kwa sababu kwa sasa kwa kweli chanzo kimoja tu cha fedha (upande wa kodi) ndicho kinachofanya vizuri wakati vyanzo vingine havifanyi vizuri na kama havifanyi vizuri tunapo-disburse kwa kutegemea kilichokusanywa huwezi ukazipeleka kama inavyotakiwa kama vyanzo vingine havifanyi vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utoaji wa fedha kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa hasa zile za maendeleo; niruhusu tu niseme kwamba, Serikali kuanzia mwezi Julai mpaka Oktoba tuliweza kutoa Shilingi bilioni 177.3 ambayo ni asilimia 14.3 ya bajeti iliyoidhinishwa. Naomba niliambie tu Bunge lako Tukufu kwamba kuanzia mwezi huu wa Novemba Waheshimiwa Wabunge wategemee mtiririko ambao ni mzuri zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kulipa deni la PSPF na madeni mengine ya ndani; naomba niseme tu kwamba Serikali inaendelea na uhakiki wa madeni haya. Tulishakamilisha uhakiki wa deni la PSPF na sasa tunaendelea kuweka utaratibu wa kukamilisha uhakiki wa Mifuko mingine yote ili tuweze sasa kutoa ile hati fungani ya Serikali na kuweza kuyalipa na mtakumbuka kwamba tumetenga bilioni 150 katika bajeti hii kwa ajili ya kulipa madeni hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa madeni ya ndani, niseme tu kwamba tumeanza kulipa na nilishaeleza Bunge lako Tukufu kwamba hadi sasa katika quarter hii tumeshalipa shilingi bilioni 187.5 kwa ajili ya madeni ya wakandarasi mbalimbali, wazabuni na madeni ya watumishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ukusanyaji wa property tax; naomba niliambie Bunge lako Tukufu kwamba hadi sasa TRA haijaanza kukusanya property tax kwa sababu ilikuwa ni lazima kufanya maandalizi ya msingi ya kisheria. Kwa hiyo, kwa mfano kutoa tangazo la Serikali, kazi hiyo imekamilika tarehe 30 Septemba, kuna kuandaa kanuni ambazo zinakamilishwa hivi sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kulikuwa na kuoanisha mifumo mbalimbali ya Serikali – Local Government Revenue Collection Information System na Property Rate Management System na kazi hii imekamilika mwezi Oktoba na sasa TRA imeanza kutoa zile ankara kwa ajili ya kudai property tax kwa kipindi ambacho hakijalipwa. Kwa zile halmashauri ambazo hazitaanza kwenye mfumo huu zilishaelekezwa kuendelea kukusanya property tax kwa utaratibu wa kawaida mpaka hapo zitakapofikiwa na utaratibu wa kukusanywa na Mamlaka ya Mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kushughulikia kesi mbalimbali, TRA imefanya hivyo na hadi sasa Ofisi ya DPP imeshawateua Wanasheria 24 wa TRA kwa ajili ya kuendesha kesi hizo. Pia kufikia Aprili mwaka huu, kulikuwa na kesi 117 ambazo zilikuwa na kodi kubwa tu – bilioni 116 na hizi zimeshughulikiwa. Kati ya Aprili na Septemba kesi 63 zilitolewa uamuzi na kati ya kesi 66 tuliweza kushinda kesi 50.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu TIB; niruhusu tu niseme kwamba, hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu TIB ilikwishatoa notice kwa wateja wake 26 ambao wana mikopo ya karibu bilioni 66, ila kati ya hao wateja watatu ambao wana mikopo ya bilioni 24.7 wamekimbilia mahakamani.
Mheshimiwa Naibu Spika, yalikuwepo pia madai hapa kwamba TIB walikataa kutoa taarifa za wateja. Nafikiri sio kwamba viongozi wa TIB ni kiburi, lakini sheria inawazuia kufanya hivyo. Kifungu cha Banking and Financial Institutions Act ya Mwaka 2006, section ya 48 under the fidelity and secrecy section, inamzuia mtu yeyote kutoa siri za wateja na kufanya hivyo ni kosa, ukifanya hivyo unatakiwa ulipe faini ya si zaidi ya Shilingi milioni 20 au kufungwa kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote. Kwa hiyo, nadhani hiyo ndiyo sababu ya msingi na si kwamba ni ukaidi wameinyima Kamati hiyo taarifa za wateja.
Mheshimiwa Naibu Spika, ilisemwa pia kuhusu mfumo wa IPSAS Accrual Basis; niseme tu kwamba, Serikali inaendelea kujitahidi kutekeleza mpango kazi ambao una-cover miaka mitano ili kuweza kuhakikisha kwamba Mfuko huu unatumika ipasavyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kuimarisha usimamizi wa misamaha ya kodi; ni ushauri mzuri na TRA imekwishaanza kuchukua hatua na niseme tu kwamba udhibiti wa misamaha ya kodi umeongezeka na Mameneja wa Mikoa wa TRA wamepewa maelekezo mahususi kuweka kipaumbele katika kudhibiti misamaha hii. Zile kampuni ambazo zilitumia misamaha vibaya, kampuni hizo zilizotajwa kwenye taarifa ya CAG zimeanza kushughulikiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalize kwa kusema kuhusu zile bilioni takribani 99 ambazo zinasemwa zilirudishwa Benki Kuu; hizo zilikuwa ni exchequer issues na sio fedha taslimu ambazo zilirudishwa Benki Kuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri nimeeleweka, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi, Mheshimiwa Spika, Naibu Spika, Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuendesha vizuri mjadala huu wa bajeti kwa Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutambua michango iliyotolewa na Kamati ya bajeti chini ya Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Hawa Abdurahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini; na Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Kandege, Mbunge wa Kalambo, lakini pia mchango uliotolewa na Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba na Kaimu msemaji Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango; lakini pia Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza au kwa maandishi hapa Bungeni. Ninawashukuru wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya Wabunge ambao wamechangia hoja niliyowasilisha, jumla yao 79 na kati ya hao 41 wamechangia kwa kuzungumza, waliobaki wamechangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema awali, ninafarijika sana kwa michango mizuri iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge wote. Nitapenda nieleze kwa muhtasari majibu ya hoja mbalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge na ninamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji Naibu Waziri wa Fedha na Mipango kwa kunisaidia kujibu baadhi ya hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kabisa sitaweza kujibu hoja zote na wala kujibu kila kitu ambacho kimesemwa kwa sababu ya muda, lakini naomba niwahakikishie kwamba majibu ya hoja ambazo zimechangiwa na Waheshimiwa Wabunge tutazileta kwa maandishi kabla ya kuahirishwa kwa mkutano huu wa Bunge. Baadhi ya hoja nyingine kwa hakika zilikuwa na mwelekeo wa Bajeti Kuu ya Serikali, basi nazo tutajitahidi kuzitolea ufafanuzi kadiri inavyowezekana wakati wa mjadala wenyewe wa Bajeti Kuu ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo hoja ambazo zimetolewa na Kamati ya bajeti; zipo zilizotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na zimerudiwa na Waheshimiwa Wabunge wengi ambao baadhi ya hoja hizo nitapenda nizitolee ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwanza kubwa sana ambayo nitapenda nitumie muda kuieleza ni hoja ya upelekaji hafifu wa fedha na hasa fedha za maendeleo kwamba zimeathiri utekelezaji wa bajeti, lakini hasa miradi ya maendeleo. Bajeti ni maoteo; na maoteo maana yake ni kwamba siyo halisi. Ni maoteo ya mapato na matumizi ya Serikali katika mwaka mmoja. Sasa pamoja na jitihada ambazo zinafanyika kuhakikisha kwamba maoteo yanakaribiana na hali halisi, ulimwenguni kote ni nadra sana mapato yakalingana na matumizi. Really, they seldom balance, ndiyo maana Serikali zote duniani zinakopa. Zinakopa ndani na nje na ndiyo maana kuna kubana matumizi na kupunguza matumizi na ndiyo maana tunaweka vipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utoaji wa fedha kwa mafungu yote, unategemea hali halisi ya upatikanaji wa mapato. Hili limesisitizwa katika kifungu namba 45(b) cha Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015. Najua Waheshimiwa Wabunge wengi wanao weledi wa kuelewa mambo haya upatikanaji wa mapato unategemea mambo mengi. Niseme mawili tu la kwanza, ni ukubwa wa uchumi lakini pia muundo (structure) ya uchumi. Kwa hiyo, kwa mfano, uchumi ambao unategemea kilimo cha kujikimu au uchumi ambao unakuwa na sekta kubwa isiyo rasmi ulimwenguni kote, maana yake ni kwamba wigo wa kukusanya mapato unakuwa ni mdogo. Ukilinganisha nchi ambayo ina industrial base kubwa, nchi ambayo ina viwanda vingi, wao wanakuwa na wigo mkubwa zaidi wa kukusanya mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, viko vingi; nchi ambayo ina Serikali dhaifu na Baba wa Taifa alitukumbusha kama mna-weak governance, kama mna rushwa iliyokithiri, daima hamtakusanya mapato. Ni vizuri pia Waheshimiwa Wabunge tukakumbuka na hili nafurahi sana limesemwa na baadhi ya wachangiaji, tunalo tatizo kwamba hata fedha hizi ambazo zinatolewa, zinatumika vibaya. Kwa hiyo, haitoshi tu kusema tumepeleka fedha, ni lazima kuangalia ile quality of expenditure. Pale Hazina tuna Kitengo cha Expenditure Tracking, kwa kweli ukiangalia taarifa zao ni madudu matupu kwenye Serikali Kuu na pia kwenye Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo taarifa mpaka unasikitika. Mtu anasema amenunua ubao wa mninga, lakini kanunua mpodo, bei tofauti. Ningeweza hata kutaja Halmashauri ambazo wanasema wametumia fedha kwenye mradi; mradi haupo, ni mradi hewa. Uko udanganyifu vilevile, fedha hizi hizi ambazo tunapeleka, kumbe iko haja ya kuangalia mambo mengi, iko haja pia hata ya kuangalia Serikali yetu ukubwa wake, imepanuka haraka sana japo kwa nia njema kabisa ya kufikisha huduma kwa wananchi wake. Ni lazima tujitathimini tuangalie kama inaendana na uwezo wa Taifa letu kumudu ukubwa wa Serikali ambayo imefikia hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia mtakumbuka Waheshimiwa Wabunge, mwaka 1996/1997 tulifanya maamuzi kutokana na nidhamu ndogo ya bajeti. Kabisa kulikuwa hakuna fiscal discipline tukafanya uamuzi kwamba tutatumia fedha kadiri tunavyokusanya, tukaanza utaratibu wa cash budget. Kwa hiyo, ni lazima pia kutumia vizuri kile kidogo ambacho tunakusanya kulingana na uchumi wetu. Kwa hiyo, ndiyo sababu kubwa kwa kweli kwa nini fedha ambazo zimekusanywa mpaka hivi sasa, kigezo kikubwa ni uwezo wetu wenyewe wa uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge, napenda nitumie podium hii kuwataka Maafisa Masuuli wote, tena wa mihimili yote, Serikali, Bunge na Mahakama kutumia vizuri fedha hizi ambazo tunazikusanya kwa wananchi wetu masikini. Kila Wizara, kila Taasisi, Halmashauri, Mashirika, Mihimili yote ni lazima kujifunza kubana matumizi, kutumia fedha hizi ambazo tunakusanya kutoka kwa wananchi vizuri. Tusiangalie tu asilimia ya kiasi cha bajeti iliyokwenda, tuangalie hizo fedha zimefanya nini? Tuangalie uwezo wa taasisi mbalimbali kutumia hata hizi fedha ambazo ziko.

Waheshimiwa Wabunge, ziko taasisi ambazo hata hizo fedha ambazo zimebaki, wanazo kwenye akaunti mpaka leo hii. Kwa hiyo, ni muhimu sana viongozi wote tuhangaike kuhakikisha kuwa kila raia wa Tanzania anatimiza wajibu wake wa msingi wa kulipa kodi ili mapato yaongezeke, lakini ni lazima tuhakikishe kwamba na wale ambao wanakiuka huo wajibu wa msingi kwa kukwepa au kuvujisha mapato, lakini wanaendelea kufurahia huduma za Serikali, hao ni lazima tuwabane, hatuwezi kuwaacha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ambayo ilikuwa kubwa sana ni imani ya wafanyabiashara kwa maana ya private sector confidence. Hoja ilikuwa kwamba baadhi ya matamshi ya viongozi yanakimbiza watu, lakini pia biashara zinafungwa na kadhalika. Nisisitize kwamba private sector confidence ni jambo muhimu sana na ni lazima lilelewe, it must be nurtured. Sekta binafsi tulishakubaliana ndiyo injini ya uchumi wetu, lakini katika maeneo tofauti huwa nasema, Serikali na sekta binafsi zinafanana na mapacha walioungana. Kama mapacha walioungana wasipofanya mambo yao kwa pamoja na kwa maelewano, basi hayo maisha hayawezekani na kadhalika hivyo hivyo kwa upande wa Serikali na sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kadhalika hivyo hivyo kwa upande wa Serikali na sekta binafsi na maana yake ni kwamba lazima pawepo majadiliano (dialogue) kuhusu malengo ya Taifa letu, kuhusu vipaumbele, sera na mikakati. Hii ndiyo sababu kati ya mikutano ya kwanza ambayo Mheshimiwa Rais amefanya mara baada ya kuchukua kijiti cha uongozi wa Taifa letu, mikutano yake ya mwanzo kabisa amekutana na wafanyabiashara chini ya utaratibu wa TNBS na hivi karibuni amefanya nao tena mikutano na katika mkutano ule waliokuwepo ni mashuhuda siyo tu ameelekeza kwamba viongozi wa Serikali ambao watakwamisha juhudi za sekta binafsi katika Taifa letu, hao wawajibishwe mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ameacha wigo wazi na kusema kwamba hata wafanyabiashara ambao wako tayari kuja kuweka viwanda yuko tayari kuwapa tax holiday. Sasa nafikiri ni vizuri kidogo tuwe tunayapima haya ambayo yanasemwa. Mbali na TNBC katika ngazi ya kitaalam kuna majadiliano yanayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi chini ya TPSF (Tanzania Private Sector Foundation), lakini katika ngazi za Mawizara tumeendelea pia kuzungumza. Siyo zamani sana, mimi na mwenzangu Mheshimiwa Waziri wa Viwanda tuliitisha mkutano hapa Dodoma, tukakaa na wafanyabiashara tukawasikiliza na tumekubaliana tataendelea kukutana kila baada ya miezi minne Wizara ya Viwanda na Biashara imekuwa inakutana na wenzetu kutoka Sekta binafsi kwa kuendana na sekta.

Kwa hiyo, tunazungumza na mlango uko wazi kabisa maana Taifa ni letu wote. Tanzania isipoendelea, hakuna cha kusema huyu ni wa Sekta binafsi na huyu ni wa Serikalini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu sana sheria za mchezo zikawa wazi pande zote. Ni lazima sheria za mchezo zisibadilike badilike, siyo upande wa kodi peke yake, lakini pia na mambo mengine nitaeleza kidogo. Ni lazima gharama ya kufanya biashara kwa wafanyabiashara wetu, ziwe ndogo kadri inavyowezekana na ndiyo maana Serikali inahangaika kuwekeza kwenye umeme, kuboresha usafirishaji, kupambana kidete na rushwa, lakini pia kupambana na ukiritimba kama Mheshimiwa Rais wetu anavyoongoza njia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo katika mchezo wowote, mchezo lazima uwe na pande mbili, Serikali inao wajibu, lakini Sekta binafsi nayo inayo wajibu. Kwa mfano, ni muhimu sana sekta binafsi nayo izingatie business ethics. Ukwepaji kodi, madai ya marejesho ya kodi yasiyo na uhalisia lakini pia hata haya yaliyofichuka hivi karibuni kuhusu makasha ya mchanga ambayo yalikuwa yanapelekwa nje, ni kielelezo wazi kwamba hakuna uwazi na Watanzania tumekuwa tunaibiwa. Jamani hili liko wazi, hata watu ambao hawakwenda shule wanajua mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba viongozi wetu wana dhamana ya kulinda rasilimali za Watanzania kwa niaba yao. Kwa hiyo, pale ambapo kuna mushikeli wa wazi, ni lazima waseme na ukweli utabaki kuwa ukweli. Koleo haliwezi kuwa kijiko hata siku moja! Kama Mheshimiwa Rais mwenyewe anavyosema, msema kweli daima atabaki kuwa mpenzi wa Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongezee hapo kuhusu kufungua au kufunga biashara. Kufungua au kufunga biashara ni jambo ambalo limekuwepo tangu binadamu alipoanza kufanya biashara. Jambo la muhimu ambalo tunatakiwa kila mara kuzingatia ni kujua ni kwa nini biashara zimefungwa na kwa nini zimefunguliwa? Aina gani za biashara zimefungwa? Zipi zimefunguliwa? Sababu zake ni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwape tu mfano Waheshimiwa Wabunge. Katika miaka ya 1980 ukiitazama China ilivyokuwa baadhi ya mambo haya tunayoyaona ya biashara kufungwa, siyo jambo geni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina kitabu hapa kimechapishwa mwaka huu ambacho kinaeleza juu ya uongozi ndani ya Kampuni ya HUAWEI, mila ambazo wanazifuata na jinsi ambavyo walikuwa wanaungana na wenzao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kitabu hiki unaona kabisa kwamba phenomena tunayoiona sasa hivi hapa nchini, inafanana kabisa na wenzetu ambacho walikuwa wana-experience China wakati wanafanya mageuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja ninukuu kidogo sehemu ya kitabu hiki. Inasema hivi, nanukuu kwa Kiingereza kama kilivyoandikwa. Inasema: “Over the decades of reform and opening up there have been many countless stories of rise, decline and heart-wrenching downfall of private companies, their many caucuses lining the street of transformation.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, humu ndani anaeleza mengi tu kuhusu biashara zilivyokuwa zinafungwa na zile ambazo zilikuwa zinahangaika na mpaka zikaendelea katika mazingira yao. Kwa hiyo ni kweli kabisa zipo biashara zimefungwa lakini zipo nyingi zaidi zilizofunguliwa. Niseme tu kwamba biashara ambazo zimefunguliwa ni zaidi ya zile zilizofungwa, lakini pia ni muujiza kutarajia kwamba hizi ambazo ni nyingi zilizofunguliwa jana, basi leo leo zitakapofunguliwa zitazaa kodi kuliko hizo ambazo zimekuwepo na zimefungwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tunafanya mabadiliko makubwa ya kimfumo. Kwa kweli hatuwezi kuendelea na uchumi ambao ulijengwa juu ya misingi ya utapeli na ujanja ujanja. Utaratibu uliokuwepo siyo endelevu na ulikuwa unawanufaisha watu wachache. Ni lazima tupige hii hatua na makampuni ambayo yanafuata taratibu hakuna mtu anayasumbua. Mfanyabiashara anayefanya biashara yake halali, anazingatia sheria huyo ni rafiki wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ni kusema tutoe amnesty kwa wale ambao huko nyuma walizoea hivyo na tunawadai kodi; jamani mtakumbuka wakati baadhi ya makampuni yaliondoa makontena bandarini bila kulipa kodi, Mheshimiwa Rais aliwapatia wiki mbili za kulipa kodi. Sasa mnataka amnesty ipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niseme kidogo juu ya Tume ya Mipango na hasa kwa sababu nina historia nayo; toka uhuru ukifuatilia historia ya Tume ya Mipango imekuwa inahama. Leo iko Wizara ya Fedha, kesho ni Wizara tofauti, kesho inakuwa Tume, kesho inakuwa kitu kingine. Nchi nyingine utaratibu huo unaonekana wazi na huu ni mjadala ambao haujawahi kukamilika popote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo faida za Tume ya Mipango kukaa peke yake. Mimi nikiwa Tume ya Mipango, hoja ilikuwa kwamba nakosa hela za kutosha kuendeshea Tume kwa sababu Wizara ya Fedha iko mbali nami. sasa Tume ya Mipango imeunganishwa na Wizara ya Fedha, imekuja kinyume chake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge, pia naomba mkumbuke kwamba mwenye Mamlaka ya kutengeneza Muundo wa Serikali ni mwenye Serikali. Kwa hiyo, tumwachie maamuzi yake. Yeye anaona ni busara zaidi vyombo hivi viwili vikifanya kazi kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumejitahidi katika Wizara ya Fedha kama ambavyo tunafanya kwa Taasisi nyingine yoyote. Tumeipatia Tume ya Mipango fedha kulingana na upatikanaji wa mapato. Hadi kufikia mwezi Machi, 2017 Tume ya Mipango ilikuwa imepokea shilingi bilioni 2.84 ambayo ni sawa na asilimia 70.38 ya bajeti yake ya matumizi ya kawaida. Kwa hiyo, haiwezi kushindwa ku-operate kwa sababu hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tuliambiwa pia kwamba tutoe fedha shilingi bilioni 1.9 zilizobaki kwa Tume ya Mipango ndani ya mwaka huu wa fedha. Kwa kweli hata kama fedha hizi zingekuwepo, Tume haiwezi kutumia fedha zote hizi kwa tija ndani ya mwezi mmoja uliobaki kabla ya mwisho wa mwaka. Let us just be realistic. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ilikuwepo hoja hapa kwamba na ushauri kwamba Serikali ihakikishe Wizara, Idara na Taasisi zake zinatumia mashine za kieletroniki katika kukusanya maduhuli. Huu ni ushauri mzuri tunaupokea kwa moyo mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niliarifu Bunge hili kwamba nimeshatoa maelekezo na tulianza na Wizara zile ambazo zinakusanya maduhuli makubwa kwamba wahakikishe wanatumia mashine za EFD katika kukusanya maduhuli ya Serikali. Niliahidi Bunge lako, tunapomaliza Bunge hili nitakwenda kuhakiki nikianza na Wizara Kuu ambazo zinakusanya maduhuli ya Serikali. Maafisa Masuuli wanisikie waliyeko hapa; wale ambao watakuwa hawatumii EFD hao basi wajiandae kwa shughuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumeendelea na jitihada nyingine ikiwa ni pamoja na kutengeza revenue get way system ambayo itakuwa inatumiwa na Wizara na Idara mbalimbali katika kukusanya Maduhuli ili tuongeze tuboreshe usimamizi wa mapato. Kama nilivyoeleza kwenye hotuba yangu, tumeanza kufanya majaribio ya mfumo huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ilikuwepo pia hoja kwamba katika mwaka 2015/2016 kuna Wakala 11 zililipa takriban shilingi bilioni 2.97 kwa Wazabuni bila kudai risiti za kieletroniki na hii ilisababisha walipa kodi kukosa kodi na kuisababishia Serikali mapato. Naomba tena kusisitiza kwa Wizara, Idara na Taasisi zote za Serikali, kutumia Wazabuni waliosajiliwa na wanaotumia mashine za kieletroniki ili kuhakikisha kwamba mapato ya Serikali hayapotei, asiyefanya hivyo nimeshamwagiza Mlipaji Mkuu wa Serikali awadhibiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikumbushwa hapa kwamba ni muhimu Serikali iendelee kuchukua hatua zaidi kupunguza misamaha ya kodi na hususan kwenye mafuta, lakini pia kwenye makampuni ya uchimbaji madini ili tuweze kufikia lengo la misamaha yote kuwa chini ya 1% ya pato la Taifa. tunakubaliana kabisa na ushauri huu na ndicho tumekuwa tunafanya. Shida kubwa iko kwenye vivutio ambavyo ni vya kimkataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge, zimesikika sauti mara nyingi kwamba ni muhimu sana pia Taifa letu likawa linatoa vivutio ili kuvutia uwekezaji mwingi zaidi. Bado tunabishana, mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kodi sio kivutio peke yake. Kwa hiyo, tutaendelea kuichambua hii mikataba lakini pia hata kuhakiki yale maombi ya misamaha ili kuhakikisha kwamba hautumiki kama upenyo wa uvujaji wa mapato. Lengo letu bado ni lile lile; na tulikuwa tunakwenda vizuri mpaka mwaka 2015/2016 misamaha yote ilibakia kuwa 1.1% ya GDP. Kwa hiyo, tulikuwa tumekaribia lengo kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja kwamba Ofisi ya Msajili wa Hazina inafanya kazi kubwa sana kama msimamizi wa mali za Serikali. Tunakubaliana na tulichofanya mpaka sasa Wizara imeandaa Waraka wa Balaza la Mawaziri ambao una lengo la kurekebisha sheria iliyopo ili kuimarisha usimamizi unaofanywa na Msajili wa Hazina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waraka huo sasa uko kwenye ngazi za maamuzi na kwa kweli Serikali tunaona huo umuhimu wa kuimarisha Ofisi hii, na tutaendelea kuijengea uwezo na hususan iweze sasa kuhakikisha kwamba vile viwanda vyote vilivyobinafsishwa, basi waliokiuka mikataba kama nilivyoeleza kwenye hotuba yangu, tunavirejesha viwanda hivyo Serikalini kama hawawezi kuchukua hatua za dharura kuhakikisha kwamba vinafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja kwa nini Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa ndege, wakati Kampuni yetu ya ndege ina upungufu mkubwa? Kwanza naomba tu niwakumbushe kwamba suala la kununua ndege mahususi kwa ajili ya kuimarisha Sekta yetu ya Utalii, ni kipaumbele ambacho kiko katika mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano ambao ulipitishwa na Bunge hili mwezi wa sita mwaka 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani pia shirika hili ndiyo national pride na ndiyo maana Mheshimiwa Rais na Serikali yake, inahangaikia kupata ndege hizi. Nina hakika wamo Waheshimiwa Wabunge humu ambao wamenyanyasika sana na delays na cancellations za ndege za wenzetu kuja Dar es Salaam. Tutaendelea mpaka lini? Ziko hata nchi ndogo ambazo zina airline zake zinafanya kazi. Kwa nini watalii wapite nchi nyingine badala ya kupita hapa kwetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie kwamba tunatambua upungufu huu na ndiyo maana Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekamilisha ukaguzi wa Shirika letu la Ndege ili kuweze kusafisha mizania ya hii kampuni, lakini pia tumeamua kwamba tutachukua madeni yote ya ATCL ili kuweza kusafisha hiyo mizania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais ameteua Bodi mpya ya Wakurugenzi ambayo ina weledi katika masuala ya usafirishaji wa anga na usimamizi wa fedha. Menejimenti mpya, lakini pia kuhakikisha kwamba shirika linakuwa na mpango wa biashara wa muda wa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mpaka Juni, 2017. Pia wameandaa mpango wa biashara na hatua zote hizi zinalenga kuwa na Shirika la Ndege ambalo litachochea ukuaji wa Sekta ya Utalii, lakini pia kubakiza pride ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja juu ya Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali kwamba kwa yeye kuomba fedha Wizara ya Fedha, basi anakuwa ombaomba, anapoteza uhuru. Kwanza naomba niseme tu kwamba ni good practice kwamba taasisi yoyote ya umma lazima iwe na mahali pa kuomba fedha. Hata mwenye mamlaka anapangiwa hata mshahara. Bajeti ya Ikulu, inajadiliwa humu ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni muhimu pia Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ikawa na mahali ambapo fedha zake zinapitia ili kuomba idhini ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili limeitendea haki bajeti ya CAG. Limekuwa linahoji pale ambapo tunakuwa kwa upungufu wa mapato tumeshindwa kumpatia fedha za kutosha, lakini kwa mwaka ujao wa fedha kama mtaipitisha bajeti ya Wizara yangu, tulikubaliana kwenye Kamati ya Bajeti kwamba Ofisi ya CAG kwa mwaka ujao basi ipewe fedha kama ilivyoomba na tutahakikisha kwamba fedha zinatoka kadri ukusanyaji wa mapato utakavyoruhusu. Uhuru wake uko pale pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna ofisi ambayo ina msaada kwa Wizara ya Fedha kama Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, huyu ndiye anayenifuchulia mchwa. Mheshimiwa Rais alinipa kazi ya kutafuta mapato na kuyagawa kwa mafungu mbalimbali ya Serikali, Ofisi hii ya CAG ndiyo inanionesha nani anatumia vibaya. Kwa hiyo, kwa kweli Wizara ya Fedha itakuwa ni taasisi ya mwisho kabisa kuibana Ofisi ya CAG kwa ya maana kumpatia fedha za yeye kufanya kazi yake ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja kuhusu Mfuko wa Pamoja. Akaunti ya Pamoja ya Fedha kati ya Serikali mbili, hoja ilikuwa kwamba haijafunguliwa na hatua zilizochukuliwa kuhusu suala hilo ni nini? Kufunguliwa kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha kwa kifupi, kutafanyika baada ya uamuzi kuhusu mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha kufikiwa na pande mbili za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyelkiti, hata hivyo kila upande wa Muungano umeendelea kunufaika na mapato ya Muungano yatokanayo na kodi ya mapato, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi yanayopatikana katika kila upande.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme moja tu nimalizie hili kwamba kwa mwenendo wa sasa wa mgawanyo wa mapato ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapaswa kupokea 21%, ndiyo ilikuwa hoja kwamba ilitakiwa ipate 21% na SMT 79% ya mapato. Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Waziri anayesimamia masuala ya Muungano, mgao wa SMZ wa 21% na SMT 79% ni kuhusu ajira, siyo mapato. Ni kuhusu ajira katika Taasisi za Muungano na siyo mgawanyo wa mapato. Kuhusu mgawanyo wa mapato ya Muungano, mapendekezo yake bado yanafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, hoja ni nyingi na tutazijibu kwa maandishi. Naomba kwa heshima na taadhima niishie hapa nikiendelea kuomba kwamba Bunge lako Tukufu likubali maombi ambayo tumeweka mezani ili twende tukatekeleze kazi zilizoko mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba na mimi nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniruhusu kusimama leo tena hapa jioni kuhitimisha hoja ambayo niliiwasilisha tarehe 7 Novemba, 2017 kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019.

Aidha, napenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwako wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kusimamia vyema mjadala wa hoja. Vilevile niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote 124 waliochangia katika mjadala huu ambapo Wabunge 103 wamechangia kwa kuzungumza ikijumuisha Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao kwa kweli mmenipa raha, lakini pia wapo Waheshimiwa Wabunge 12 ambao wamechangia kwa maandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyobainisha katika hoja yangu kuwa lengo lilikuwa ni kuomba maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge wakiwa ndiyo sauti za mawazo na matakwa ya wananchi wetu kuhusu maendeleo ya nchi yao, lakini pia mgawanyo wa rasilimali fedha ili yazingatiwe katika hatua ambayo itafuata baada ya kikao hiki cha Bunge ambayo itakuwa ni kazi ya kuandaa Rasimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na kiwango na ukomo wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha ambavyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge hili zitawasilishwa kwa Wabunge tarehe 11 Machi, 2018 na kufanyiwa uchambuzi na Kamati ya Bajeti kuwezesha ukamilishwaji wa Mpango na Bajeti ambavyo vitawasilishwa wakati wa Bunge la bajeti. Kwa niaba ya Serikali nakiri kuwa lengo hilo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa na narudia kusema ahsanteni sana. (Makofi)

Mhesimiwa Spika, niruhusu kipekee nitambue mchango wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini. Kamati ilitupatia ushauri wa msingi ambao niliuelezea kwa kifupi wakati natoa hoja, lakini vilevile tulipokea mchango uliotolewa na Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba kwa niaba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, nawashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara mbalimbali waliotoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa zinazogusa sekta zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, natoa shukrani kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji kwa kunisaidia kusikiliza kwa makini maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge kwa siku zote tano na kutolea ufafanuzi kwa umahiri hoja zilizotolewa hapa ndani muda mfupi uliopita. Nitumie pia fursa hii kuwashukuru kwa dhati watendaji wote wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Katibu Mkuu, Bwana Dotto Mgosha James kwa kuchambua na kutafuta takwimu na taarifa ambazo zilihitajika kwa ajili ya kutolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali. (Makofi)

Katika majadiliano ya hoja niliyowasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, Serikali imepokea maoni mengi sana. Naomba nitaje baadhi tu kwa kifupi maoni ambayo yalitolewa na Wabunge wengi na hii ni kuthibitisha tu kwamba Serikali inasikia. Maoni hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Mmetushauri kwamba tuweke msukumo pekee kwenye sekta ya kilimo. (Makofi)

(ii) Mmetushauri tujumuishe mkakati mahsusi wa kumaliza kilio kikubwa cha upatikanaji wa huduma za maji nchini kote. (Makofi)

(iii) Mmetuambia kwamba fursa ya uwepo wa rasilimali kubwa ya gesi asilia nchini ni lazima sasa itumike vizuri zaidi. (Makofi)

(iv) Mmetuelekeza tutekeleze kwa dhati utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yaani PPP. (Makofi)

(v) Mmetuelekeza na kutushauri tuongeze kasi ya kutekeleza miradi ya miundombinu ya kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na ile ya Umeme Vijijini REA III lakini pia barabara muhimu za kuchochea uchumi katika mikoa mbalimbali. (Makofi)

(vi) Mmetushauri tuongeze kasi ya kulipa madeni yaliyohakikiwa.

(vii) Mmetushauri tuhakikishe kuwa Deni la Taifa linaendelea kubakia kuwa himilivu na kuanza kupunguza kasi ya kuongezeka kwa Deni la Taifa.

(viii) Mmetushauri tukabiliane na tatizo la ukosefu wa ajira nchini. (Makofi)

(ix) Mmetushauri kuwekeza na kutumia kikamilifu rasilimali za bahari na maziwa (the blue economy).

(x) Mmetushauri kubainisha mkakati wa kuongeza idadi ya watalii na mchango wa sekta ya utalii katika uchumi. (Makofi)

(xi) Mmetushauri kuhusu kuimarisha uhifadhi wa ardhi, kupima na kupanga matumizi yake.

(xii) Mmetushauri kuchukua hatua za kupunguza kasi ya ongezeko la idadi ya watu.

Mheshimiwa Spika, hayo ni baadhi tu, ni masuala kumi na mbili muhimu ambayo tumesikia ushauri wenu lakini yako mengi sana tutayafanyia kazi. Kwa niaba ya Serikali naahidi kuwa wakati wa kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 tutazingatia ipasavyo maoni na ushauri uliotolewa na Bunge lako Tukufu lilipokaa kama Kamati ya Mipango. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kazi yangu, kazi ya Naibu Waziri na wataalam wetu wa Wizara kwa siku hizi tano ilikuwa ni kupokea maoni na ushauri ambao tunakwenda kutafakari na kufanyia kazi, nitapenda nitoe ufafanuzi kwa baadhi tu ya hoja ambazo Waheshimiwa Wabunge mlizitoa. Kwa kweli hoja ni nyingi kama nilivyosema na kwa muda ambao nimepewa si rahisi kujibu zote na naomba niwahakikishie kwamba tutawasilisha majibu na maelezo ya hoja zote kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, lakini kabla sijafanya hivyo, naomba nisisitize tena mambo matatu kwa sababu yanajirudiarudia kila mwaka, ni vizuri tukawa tunaelewana kwa faida ya Taifa letu.

Kwanza, nilichowasilisha Bungeni ile tarehe 7 Novemba, 2017 siyo Mpango ni mapendekezo ya mambo ya msingi na vipaumbele vinavyotakiwa kuzingatiwa katika kuandaa Mpango wenyewe na bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, Mapendekezo ya Mpango na Mwongozo wa kuandaa bajeti yalipitia katika hatua zote ambazo ni kupata maoni ya wadau wa ndani na nje ya Serikali, Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, Kikao cha Makatibu Wakuu (IMTC) na kupata ridhaa ya Baraza la Mawaziri kabla ya kujadiliwa na Kamati ya Bajeti na hatimaye Bunge. Hivyo, mapendekezo ya Mpango siyo mpango wa Dkt. Mpango bali ni Mapendekezo ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo la tatu, Mapendekezo haya ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/2017 - 2020/2021 kwa mwaka wa tatu. Kwa hiyo, wale wanaodai ni copy and paste kutoka Mpango wa mwaka jana ni vema wakazingatia hili.

Mheshimiwa Spika, sasa baada ya maelezo haya, naomba nijielekeze kujibu baadhi ya hoja na nitaomba nianze na ile hoja ambayo naiona ni muhimu sana kwamba Serikali iache kupeleka fedha kugharamia miradi mikubwa ya kielelezo kama Standard Gauge Railway, ununuzi wa ndege mpya, uzalishaji wa umeme Stigler’s Gorge, miradi ambayo inaweza kutekelezwa kibiashara na sekta binafsi. Ilisemwa hapa kuwa utaratibu huo unapunguza fedha kwa ajili ya kugharamia huduma za msingi kwa jamii kama maji na afya na utapelekea kuongezeka kwa mzigo wa Deni la Taifa.

Mheshimiwa Spika, hoja hii ni vema tukaitafakari vizuri. Serikali inathamini sana mchango wa sekta binafsi na tunafahamu kuwa huko ndiko kwenye pesa na mitaji mikubwa na hasa ukizingatia size ndogo ya uchumi wa Taifa letu kwa hivi sasa lakini pia mahitaji makubwa ya wananchi wetu. Hata hivyo, ni muhimu mawazo hayo yapimwe kiuhalisia na bila kusahau historia na uzoefu wa nchi nyingine. Wote mtakumbuka kwa tulikuwa na RITES of India hapa, hivi naomba niulize walijenga kilomita ngapi za reli? Tumesahau kwamba treni karibu zote zilisimama, mizigo ikawa inasafirishwa kwa malori mpaka Serikali ilipofanya uamuzi wa kuondokana na RITES of India. Hivi sasa kweli hata tukikaa hapa si nalisikia linapita hapo, hatuoni treni za abiria na mizigo zinatimua vumbi. Tena nasikia zinaimba kadogosa kadogosa kadogosa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri wangu ameeleza vizuri wazo la kuzalisha umeme eneo la Stigler’s Gorge lilikuwepo kwenye makaratasi kwa miaka mingi. Hivi sekta binafsi si ilikuwepo na ilikuwa inasikia kilio cha kutokuwepo kwa umeme wa uhakika na wa gharama nafuu hapa nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulikuwa na Kampuni hapa ya City Water kwenye sekta ya maji mbona kilio cha maji Dar es Salaam hakijaisha? Yaliyotokea ATCL na TTCL vivyo hivyo, mbona tunasahau haraka hivi? Hata hivyo, sasa tumefanya mabadiliko na tumeanza kufaidi huduma za Bombardier kuja Dodoma, Songea, Kigoma na kwingineko. Aidha, hivi sasa nasubiri gawio mwaka huu shilingi bilioni moja kutoka TTCL kwa mara ya kwanza. Najiuliza hivi umeme huu utakaozalishwa Stigler’s Gorge hautaimarisha upatikanaji wa huduma za afya, elimu na maji kwa gharama nafuu zaidi? Nawasihi ndugu zangu hebu tutafakari vizuri, tusisahau historia, we have the experience. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwasihi sana Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwa ujumla kuwa ni kweli kabisa sekta binafsi ndiyo injini ya uchumi lakini zipo changamoto kiuhalisia. Mzee Kikwete alituambia akili za kuambiwa lazima tuchanganye na za kwetu kabla hatujafika hatua ya kuwa na sekta binafsi yenye nguvu. Kweli natamani sana wawekezaji wa ndani na nje watatupunguzia huu mzigo. Waheshimiwa Wabunge nilieleza mwaka 2016/2017 kujenga Standard Gauge Railway kwa bajeti ya Serikali ni mzigo mkubwa mno, lakini sekta binafsi tuliyonayo bado inahitaji kulelewa ili iweze kubebea jukumu hili na sekta binafsi kutoka nje hawaji wakati tunapowahitaji na hata wakija wana masharti ambayo baadhi ni magumu kwelikweli na mengine hayana maslahi kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miezi michache ilyopita Mheshimiwa Waziri Mkuu aliita makampuni ili watujengee mtambo wa kuchenjua makinikia na alikuwepo mfanyabiashara mmoja kutoka Dubai, kitu cha kwanza alichoanza nacho anasema pesa ninayo lakini sharti la kwanza sovereign guarantee, aah, magumu haya jamani.

Kwa hiyo, katika mazingira haya hivi kweli tutakaa miaka na miaka indefinitely tukisubiri wawekezaji washuke ndiyo tuijenge upya reli ya kati ambayo ina zaidi ya miaka 100. Uamuzi wa Serikali ni kwamba tuanze kujenga kwa vipande yaani lots wakati tunaendelea na jitihada za kuwashawishi wawekezaji na taasisi za fedha ambazo zinaweza kutukopesha kwa masharti ambayo ni ahueni, hatuja-rule out private sector, hapana, lakini hatuwezi kuendelea kusubiri miaka mingine 50 ndiyo tupige hatua ya kujenga reli yetu ya kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba ninong’one na Bunge lako Tukufu, Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadala alinipigia simu na aliniambia hivi, Waziri mwambie ndugu yako Mheshimiwa Nape na Mheshimiwa Bashe kuwa nawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway, wawalete hata kesho, niko tayari kuwapa reli ya Kaliua - Mpanda au Isaka - Mwanza au reli ya Mtwara
- Mchuchuma - Liganga wajenge. Hayo ni maneno ya Mheshimiwa Rais. Natumaini Waheshimia husika will raise up to this challenge from His Excellence the President. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikwa na hoja ya Deni la Taifa linakua kwa kasi kubwa wakati uchumi unakua kwa kasi ndogo na kwamba hali hii itafanya ulipaji wa Deni la Taifa kuwa mgumu sana. Deni la Taifa liliongezeka kutoka dola za Marekani milioni 22,320.76 mwaka 2016 na kufikia dola za Marekani milioni 26,115.2 mwezi Juni, 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 17% na deni hilo ni sawa asilimia 31.2 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na ukomo wa uhimilivu wa asilimia 56. Uhimilivu wa Deni la Taifa hupimwa kwa kuzingatia uwezo wa nchi kulipa deni husika katika muda mfupi, wa kati na muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kulinganisha Deni la Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki ni kama ifuatavyo; Uganda ni asilimia 35.4, Rwanda asilimia 36.6, Burundi asilimia 43.4 na Kenya asilimia 50.4. Hali hii ya nchi za Afrika Mashariki bado ni nzuri ikilinganishwa na baadhi ya nchi nyingine kama Zambia ambayo ni asilimia 57.2, United Arab Emirates asilimia 60.3, Marekani asilimia 73.8, Morocco asilimia 77, Uingereza asilimia 92.2, Misri asilimia 92.6, Msumbiji asilimia 100.3, Italia asilimia 132.5 na Ugiriki asilimia 181.6. Kwa takwimu hizi sisi bado tuna nafasi kubwa ya kuendelea kukopa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, tutaendelea kukopa kwa sababu kuu moja tu, ni kukuza uwezo wetu wa baadaye wa kumudu uendeshaji wa nchi yetu na kulinda uhuru na heshima ya nchi yetu. Napenda nisisitize hakuna dhambi ya nchi kukopa ili mradi nchi husika itumie fedha hizo za mkopo kukuza uwezo wa uchumi, kuzalisha na kurejesha hiyo mikopo, ni lazima iwe prudential borrowing. Kama Mheshimiwa Rais alivyosema alipokuwa ziarani kule Kagera kwa kweli tutaendelea kukopa mpaka kieleweke ili mradi Deni la Taifa tuhakikishe linaendelea kuwa himilivu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda nitoe angalizo kuwa ukokotoaji wa uhimilivu wa Deni la Taifa japokuwa siyo rocket science unahitaji utaalam. Kujua hesabu za kikwetu haitoshi kufahamu namna ya kukokotoa deni in present value terms maana masharti ya mikopo na muda wa kuiva wa madeni haya yanatofautiana sana. Siyo suala la kujumlisha mkopo fulani in nominal terms na kuamua kuwa deni halitakuwa himilivu. Namuomba Mheshimiwa Kishoa na wengine kama wanataka lecture bure kuhusu debt sustainability analysis waje pale Hazina tuko tayari kuwafundisha bila malipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuliombwa hapa tutoe ufafanuzi kwa nini takwimu za Deni la Taifa katika vitabu vya Mpango vya mwaka 2016/2017, 2017/2018 na 2018/2019 zinatofautiana. Katika kitabu cha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2017/2018 takwimu zinaonyesha kuwa Deni la Taifa hadi kufikia Juni, 2016 ni dola za Marekani milioni 18,614.93 wakati katika Mwongozo wa Maandalizi wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019 takwimu zinaonyesha Deni la Taifa hadi Juni, 2016 ni dola za Marekani milioni 22,320.76. Deni la Taifa linajumuisha deni la Serikali la ndani na nje pamoja na deni la nje kwa sekta binafsi. Deni la Serikali la nje linajumuisha mikopo kutoka nchi wahisani, mashirika ya fedha ya Kimataifa pamoja na mabenki ya kibiashara ya kimataifa. Wakati deni la ndani la Serikali linajumuisha dhamana za Serikali za muda mfupi na hati fungani za Serikali pamoja na madeni mengineyo.

Mheshimiwa Spika, takwimu zilizopo katika kitabu cha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/ 2018 za dola za Marekani 18,614.93 ni deni la Serikali na siyo Deni la Taifa kwa kuwa halikujumuisha deni la sekta binafsi. Aidha, mtoa hoja angepitia kifungu hicho hadi mwisho angeona Deni la Taifa hadi Juni, 2016 ni dola za Marekani milioni 23,093.3 na kiasi hiki ni tofauti na kile kilichoripotiwa katika Mwongozo wa Maandalizi na Mpango wa Bajeti wa mwaka 2018/2019 ambapo Deni la Taifa kwa kipindi hicho ni dola za Marekani 22,320.76. Tofauti hii ya dola za Marekani 772 inatokana na kubadilika kwa deni la sekta binafsi na kupungua kwa deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kufuatia kukamilika kwa uhakiki wa madeni hayo.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya taarifa za benki za biashara nchini zinaonyesha kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa mikopo binafsi, mikopo ya biashara na mikopo kwa sekta za uzalishaji. Hali ya kupungua kwa kasi ya ukuaji wa mikopo imetokea katika nchi kadhaa ikiwemo Tanzania kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja na nusu sasa. Katika miezi kumi na mbili iliyoishia Septemba, 2017 wastani wa ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi nchini Kenya ilikuwa asilimia 3.8, Tanzania asilimia 5.0, Uganda asilimia 5.2 na Rwanda asilimia 10.3. Katika nchi zote hizi ukuaji wa mikopo katika kipindi kilichotajwa ulikuwa chini ya nusu ya ukuaji katika kipindi kama hicho kilichotangulia.

Mheshimiwa Spika, kushuka huku kuna sababu mbalimbali ikiwemo kupungua kwa utashi duniani yaani kwa kiingereza general decline and global demand ambako kunajidhihirisha kwa bei za bidhaa duniani kuwa chini kiujumla. Hii inaathiri mapato ya sekta binafsi yaani cash flows na kufanya zisichikue mikopo kwa kasi ile ile.

Pili, mabenki kuongeza tahadhari katika shughuli zao kutokana na hali ya wasiwasi duniani yaani global uncertainty. Matokeo ya kuongezeka kwa hali ya wasiwasi ni pamoja na benki kadhaa kupoteza mahusiano na benki za kimataifa yaani correspondent banks katika kile kinachoitwa de-risking.

Tatu, ni kupungua kwa fedha za bajeti za Serikali kutoka nje ya nchi ambako kumepunguza ukwasi uliokuwa ukisababishwa na matumizi ya fedha hizo na hivyo kuathiri utashi ndani ya nchi kiujumla yaani domestic demand. Mfano, fedha za bajeti kutoka nje zilizotumika zilipungua kutoka shilingi bilioni 2,711 mwaka 2013/2014 hadi kufikia shilingi bilioni 1,774 mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua hatua za kuongeza ukwasi na zinafahamika, Benki Kuu imeshusha riba yake yaani discount rate kutoka asilimia 16 Machi, 2017 hadi asilimia 9 Agosti, 2017. Pia kupunguza kiwango cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara (Statutory Minimum Reserve Requirement - SMRR) kutoa asilimia 10 mpaka 8 Aprili, 2017. Benki Kuu pia imeendelea kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara pamoja na kununua fedha za kigeni kutoka kwenye soko la jumla la mabenki.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hatua hizi, hali ya ukwasi katika mabenki imekuwa ni ya kuridhisha kuanzia kipindi cha nusu ya pili ya mwaka 2016/2017 na hii inadhihirika katika kupungua kwa riba ya mabenki yaani interbank market rate kutoka wastani wa asilimia 13.49 Disemba, 2016 hadi asilimia 3.72 Oktoba, 2017. Kupungua huku kwa riba katika soko la mabenki kumedhihirika pia katika soko la dhamana za Serikali ambako wastani wa riba umeshuka kutoka asilimia 15.12 - Disemba, 2016 hadi asilimia 9.45 - Oktoba, 2017. Matumaini ya Serikali ni kuwa hatimaye matokeo ya hatua hizi yatajionesha katika ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwa nini Benki Kuu imeacha kutoa takwimu za uuzaji na uingizaji wa bidhaa nje (import and export data). Ripoti za uchumi za Benki Kuu za kila mwezi (Monthly Economic Reviews) za Julai, Agosti na Septemba ni kweli hazikuonesha takwimu za biashara ya bidhaa nje ya nchi (trade statistics) na sababu yake ni changamoto za data (harmonization) ambazo zilijitokeza katika kukamilisha takwimu hizo baada ya kuanza kutekelezwa mpango wa Himaya Moja ya Forodha ya Afrika Mashariki yaani EAC-Single Customs Territory. Changamoto hizi zinashughulikiwa na mara zitakapokuwa zimetatuliwa takwimu hizi zitaendelea kutolewa, Serikali haina sababu ya kuficha chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja kwamba mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa hayakugusa Zanzibar. Niseme tu kwamba tumesikia hoja hii na tutajadiliana na wenzetu upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar namna bora ya kulishughulikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Mheshimiwa aliyetoa hoja anafahamu kuwa ilivyo sasa Zanzibar ina Tume ya Mipango Huru lakini pia ina Ofisi ya Takwimu ambavyo sio vya Muungano. Aidha, Zanzibar ina Dira yake ya Maendeleo 2020 na ina Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKUZA) na Maandalizi ya Mipango ya Maendeleo ya Zanzibar inaongozwa na nyaraka hizo na taasisi nilizozitaja, of course, pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtakumbuka kuwa yalikuwepo mawazo katika Katiba Pendekezwa kwamba Taifa lifikirie kuwa na Tume moja tu ya Taifa ya Mipango lakini mchakato haukufika mwisho. Aidha, kuna vikao vya pamoja vya Kiwizara na Kitaifa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kujadili changamoto mbalimbali za Muungano wetu zikiwemo zile zinazohusu masuala ya kodi ambazo Waheshimiwa Wabunge walizisema, biashara na kadhalika na Wizara ninayoiongoza tunashiriki kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, kikao kijacho kimepangwa kufanywa tarehe 17 na 18 Novemba, 2017 Dar es Salaam na nishauri tu kwamba baadhi ya mambo na hoja ambazo zilisemwa ziwasilishwe kwenye jukwaa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Muungano kwenda Zanzibar napenda sana na nimekwishakwenda mara mbili na napanga kwenda huko mara baada ya kikao hiki cha Bunge. Namuomba sana Mheshimiwa Saada aniandalie urojo tu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, aidha, tumefanya vikao na wenzetu wa Zanzibar si chini ya mara nne ndani ya miaka miwili hii ikiwa ni pamoja kikao ambacho aliongoza Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, nyumbani kwake Oysterbay mwezi uliopita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja muhimu ambayo mimi nasema ni ya msingi sana kwamba sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi vipewe kipaumbele katika Mpango na Bajeti kwa kuwa mchango wake ni muhimu sana katika kuwezesha harakati za kufikia uchumi wa viwanda na kupunguza umaskini. Serikali inakubaliana kabisa na hoja hii na tutaizingatia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba toka mwanzo na pia katika wasilisho langu wakati natoa hoja, sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda. Kwa msingi huo, eneo hili litafafanuliwa katika Mpango wa mwaka ujao na litahusisha maeneo yote ambayo Waheshimiwa Wabunge waliyasisitiza ikiwemo upatikanaji wa uhakika wa chakula, malighafi za viwanda, miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa pembejeo, utafiti wa kilimo na mbegu bora na pia kuboresha huduma za ugani, usindikaji wa mazao, miundombinu, hifadhi ya masoko pia kuboresha miundombinu ya uzalishaji wa mifugo na kuongeza bidhaa za mifugo na uvuvi.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, hoja ni nyingi na ningependa tungepata muda zaidi wa kuzifafanua lakini tutazifafanua kwa maandishi.

Kabla ya kuhitimisha hoja yangu, napenda kwa mara nyingine tena kutoa shukrani za dhati kwa Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia hoja hii ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/2019 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019. Nasema hivi kwa dhati ya moyo wangu. Aidha, naomba sana Mbunge yeyote asisite kunikosoa katika utendaji wangu wa kazi kwa maslahi ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, narudia tena, naomba sana Mbunge yeyote asisite kunikosoa katika utendaji wangu wa kazi kwa maslahi ya Taifa letu. Hata hivyo, nawasihi mnikosoe au kunipongeza kwa haki na hofu ya Mungu. Namuomba sana Mungu, napata kigugumizi kusema maneno haya lakini nitasema tu. Namuomba Mungu anipe moyo wa kuyapokea yale yote yaliyonenwa juu yangu pasipo kweli, japokuwa kama binadamu yalinisononesha, napenda nilihakikishie Bunge hili na Watanzania kwa ujumla kwamba mwenendo wa mjadala wa hoja hii umeniimarisha zaidi kuendelea kutimiza wajibu wangu kwa Taifa na naamini Mungu atanisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naendelea kumsihi Mungu awabariki Waheshimiwa Wabunge wote bila kuwabagua wale walionivika joho la ujeuri yaani arrogance na uziwi. Hii imenifanya nikumbuke kuwa watoza ushuru walichukiwa hata kabla ya wakati wa Yesu na hivyo mimi nikiwa msimamizi wa watoza kodi inabidi tu niyapokee. Bahati nzuri ni kuwa wananchi wenu ambao fedha hizi za kodi tunazielekeza kwenye maendeleo yao ikiwemo kununua dawa na vifaatiba, elimu msingi bure, umeme vijijini, kuboresha huduma za maji na kadhalika wamewasikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema hapo awali, Serikali itazingatia maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge katika kukamilisha maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019. Kuthibitisha hili, napenda nirudie kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa Mpango ujao utazingatia kwa kadri inavyowezekana ushauri uliotolewa na Kamati ya Bajeti na Bunge zima likikaa kama Kamati ya Mipango. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siwezi kuhitimisha hoja hii bila kumshukuru kwa dhati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake wa karne, ni chuma kweli kweli. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliposema hayo hakukosea kabisa. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kunitia moyo niendelee kutekeleza majukumu yangu ya msingi ya kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kudhibiti matumizi ya fedha za umma bila uoga kwa faida ya wananchi wanyonge hata pale wachache wanaponidhihaki binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kadhalika namshukuru sana Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Mbunge wa Ruangwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimejifunza katika miaka hii miwili kwamba kweli Waziri Mkuu wetu ni kocha na kapteni mahiri wa utendaji Serikalini kama alivyo kwenye medani za mpira wa miguu. Ahsante sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuendelea kunipa confidence katika utumishi huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wito wangu ni kwa Waheshimiwa Wabunge wote kuendelea kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli katika dhamira yake ya kujenga Tanzania mpya ambapo wananchi wote watanufaika na rasilimali za Taifa ili kuwaondoa kwenye lindi la umaskini. Pamoja na mambo mengine, nawaomba Waheshimiwa Wabunge, kuendelea kuwahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao na Taifa kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, rai yangu kwa Watanzania wote ni kuwa tuungane kwa pamoja na kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu mkubwa kwa nchi yetu. Mageuzi makubwa anayoyaongoza Rais wetu ni magumu tena magumu sana lakini ndiyo njia sahihi kuelekea Tanzania mpya. Kwa mfano, uamuzi wa kuhakikisha fedha za Serikali zinarejeshwa Serikalini ili zitumike kuwahudumia wananchi haukupokelewa vizuri na wahusika lakini ukweli utasimama. Haiwezekani, labda wasubiri nitakapoondolewa kwenye Uwaziri huu, akaunti za Serikali, mfano fedha za polisi zikaendelea kushikiliwa na kampuni binafsi inaitwa Max Malipo kwa ambao hawaijui. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaahidi kuwa yale yote yaliyo chini ya mamlaka niliyopewa nitayasimamia bila kutetereka ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa tunapiga hatua kubwa zaidi katika ukusanyaji wa kodi na mapato yote ya Serikali, kudhibiti mianya ya uvujaji wa mapato na kupanua wigo wa kodi sambamba na kusimamia matumizi ya fedha za umma kama Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 inavyotuongoza.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nianze kwanza kumshukuru Mungu kwa kuniruhusu kusimama tena, lakini pia niwashukuru Wenyeviti wote watatu kwa taarifa nzuri za kujenga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye taarifa yetu ya Hali ya Uchumi na Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali tulilitaarifu Bunge lako kwamba tumekamilisha majadiliano na taasisi mbalimbali za kifedha ili tuweze kukopa takribani Dola 1,460,000,000 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa reli ya kati na hususani kile kipande cha kutoka Morogoro hadi Makutopora. Naona mdogo wangu alipandisha BP hapa ingawa amenikimbia, anasema sijapata ruhusa ya kwenda kukopa kiasi hicho cha pesa nimeipata wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa ya Bunge ni kwamba tunatafuta fedha hizi kutoka kwenye vyanzo viwili vikubwa, kimoja ni Export Credit Agency (ECA) ambapo tunatarajia tutapata Dola za Kimarekani 990,000,000 lakini zilizobaki takribani Dola 470,000,000 tutakwenda kukopa kwenye vyanzo vya kibiashara na hususani Standard Chartered ambayo imepewa jukumu la kuratibu upatikanaji wa hizo fedha baada ya kukubaliana masharti ya mkopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wa mkopo wa Export Credit Agency ni miaka 18 wakati kwa mikopo ya kibiashara ni miaka 10 na disbursement ni miaka minne na urejeshaji wake ni kwa miaka 14 kwa upande wa ECA na miaka sita kwa ile mikopo ya kibiashara. Riba unganishi tunaita all cost margin ni asilimia 2.77. Mikopo hii itapatikana ndani ya miaka minne ambayo ni takribani Dola 365 kwa kila mwaka. Kwa hiyo, ule ukomo wa Dola za Marekani milioni 700 ambazo ziko kwenye bajeti hazitavukwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vitu ambavyo nazingatia sana ni Sheria ile ya Mikopo ndiyo inaniongoza kukopa na sheria zake, hakuna kuvuka. Isitoshe kwa mwaka huu fedha Bunge hili liliridhia bilioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili ambayo ni karibu shilingi milioni 800 bila VAT na gharama nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa pia na maneno kwamba kuna trilioni mbili ambazo hazikujumuishwa kwenye Deni la Taifa. Hazikuwekwa huko kwenye kanzidata ya madeni kwa sababu wakati ule tulikuwa bado tunahakiki yale madeni ya mifuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kulielezea na hili niliseme na hususani kwa Kamati ile ya Viwanda na Biashara, la Benki Kuu kwamba ile structure yake imepitwa na wakati na sasa tufike mahali ambapo Gavana hawi pia Mwenyekiti wa Bodi. Hili nawasihi sana Waheshimiwa Wabunge tuwe waangalifu sana. Tumeangalia nchi nyingine ulimwenguni takribani asilimia 90 ya nchi ambazo zina structure na majukumu ya Benki Kuu kama ilivyo kwetu hapa wana utaratibu kama huu wa kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ya msingi kama mnafahamu, Bodi ya Benki Kuu kazi yake ni sera na supervision, kwa hiyo, wao wanapitisha (approve) broad strategies wakati Gavana anasimamia shughuli za kila siku za Benki Kuu na kama mnavyojua sekta ya kibenki ni hypersensitive. Kwa hiyo, ni muhimu sana tukahakikisha kwamba tunaunganisha hizi shughuli za Gavana ili kuhakikisha kwamba Benki inabakia kuwa strong lakini pia Gavana hawezi ku-provide central leadership na independence ya Benki ya Dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua unapocheza na exchange rate na interest rate, foreign reserves, money supply, nchi nyingine Gavana akiugua, akipata mafua unaona kule interest rate zinavyoitika. Kwa hiyo, ni muhimu sana tuwe waangalifu tusikimbilie kusema tu-separate hizi nafasi mbili itatugharimu sana, ndiyo uzoefu wa ulimwengu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala la utegemezi wa ruzuku ambao umekithiri katika Mashirika ya Umma. Tulipoanzisha haya mashirika shida yetu kubwa ilikuwa ni kutoa huduma kwa jamii kwa urahisi na hususani shughuli zile ambazo hazifanywi na sekta binafsi au kama wanafanya sekta binafsi wanazifanya kwa bei kubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili tuweze kuhakikisha hizo huduma na hususani upande wa afya, elimu na utafiti zinawafika Watanzania walio wengi, Serikali inatoa ruzuku kwa haya mashirika. Kwa sasa hivi, mashirika ambayo yanapata ruzuku yako takribani 175 ukilinganisha na idadi ya taasisi zote ambazo zipo takribani 269. Kwa hiyo, logic ni ile tu kwamba mashirika haya yanafanya shughuli ambazo private sector haiko kule na kama ipo basi wanafanya kwa gharama kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo napenda kulisemea ni juu ya fees ambazo zinakua charged na Regulatory Authorities. Hili nadhani wote tunakubaliana na mnaona juhudi za Serikali ambazo tumefanya katika hotuba ya bajeti ili tuanze kuzi-rationalize na hii ni continuous process tutaendelea kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ni bajeti ya viwanda, limesemwasemwa sana hapa, nataka tu kuomba, taarifa tulizotoa ndizo taarifa rasmi za Serikali. Sasa nimwombe sana Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara na Viwanda kama ana taarifa tofauti na takwimu ambazo sisi tumetoa kwenye taarifa rasmi tuliyowasilisha Bungeni, aziwasilishe kwangu kupitia Meza yako Mheshimiwa ili tuweze kuona shida ipo wapi kwenye hizi takwimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme tu la mwisho, yako mengi muda kidogo, hili la conduct ya Sera za Fedha na Sera za Kibajeti, conduct ya monetary na fiscal policy. Ningefurahi sana ningepata muda wa kulieleza vizuri ili tuelewane hususani Mheshimiwa Bashe. Sisi tunavyoliona haziko contradictory kama zinavyowekwa hata kidogo. Tofauti ya kwanza mimi ninayoona ni kwamba ni muhimu kujua hatua ambazo zinachukuliwa hivi sasa baadhi zina matokeo ya mara moja lakini nyingi zinachukua muda ndiyo uweze kuona tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa hivi sasa, tulichokuwa tunafanya tunaita ni Expansionary Monitory Policy. Kwa lugha nyepesi Expansionary Policy ni pale ambapo tunatumia fedha za kibajeti kuongeza zaidi, kuchachua uchumi kwa kuwekeza kwenye miundombinu, tunalipa madai ambayo yamehakikiwa lakini pia kushusha viwango vya kodi kwenye maeneo ambayo tunataka ku-promote kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sambamba na hiyo unakuwa pia na Expansionary Monitory Policy (Sera za Fedha) ambazo Serikali kama ilivyofanya kupunguza statutory minimum reserve requirement lakini saa nyingine inatumia soko lenyewe la fedha (open market operations) lakini pia kujaribu kucheza na riba za aina mbalimbali. Tunavyoziona sisi zipo complimentary tofauti ni muda ambao tunatarajia kwamba tutaona hizo effects tarajiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la muhimu sana, the captains of industry, kama mnasoma magazeti CEO wa NMB ameliweka wazi, CEO wa CRDB ameliweka wazi, nimefanya mazungumzo na zaidi ya benki 12 zote wameweka wazi kwamba wanavyoona wao sekta ya kibenki sasa imeanza kuimarika the worst is over. Sasa tumuamini nani kuliko the captains of industry wenyewe? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la VAT kwenye bidhaa za maziwa na mafuta ghafi, naomba tu niweke tu on record, haya ni mambo ambayo tayari yamepokelewa na yanapelekwa kwenye Kamati za Kitaalam (Think Tank) kwa ajili ya kuchambuliwa. Namwalika Mheshimiwa Mbunge yeyote ambaye atapenda tutatangaza siku ambazo tutakuwa na ile mikutano akitaka aje ashiriki pia yale majadiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme tena juu ya upitishaji wa shehena kule bandarini. Nafikiri ni vizuri tupanuke kidogo mawazo, mwenendo wa shehena kwenye bandari zetu hautegemei tu hizi fiscal policies hata kidogo. Ni muhimu kuangalia trends za biashara ulimwenguni zinakwendaje, kwa sababu na bandari zingine ukizitazama the volumes of trade, imports and exports zimekwenda chini siyo kwa Tanzania peke yake. Sasa ukiangalia Tanzania peke yake umefumba macho mno, hebu panua wigo kidogo. Kuna vitu vingi ambavyo inabidi kuviangalia, lazima kuangalia uwezo wa bandari yetu kwa maana ya equipments, lazima pia kuangalia in terms of efficiency hata the way we are organize, kwa maana ya watendaji wa mabenki...

(Hapa Kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019; na Mapendekezo ya Serikali Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Rehema zake na kuniwezesha kusimama tena mbele ya Bunge lako Tukufu kuhitimisha mjadala wa Hotuba ya Bajeti Kuu ya Mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, siku ya Alhamisi tarehe 14 Juni, 2018 niliwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2018/2019 na pia Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba hizo nilieleza mambo mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha mwaka 2017/2018. Matokeo ya utekelezaji, changamoto zilizojitokeza, mambo ya msingi ambayo Serikali inakusudia kutekeleza katika mwaka 2018/2019 na mapendekezo ya bajeti.

Mheshimiwa Spika, baada ya mawasilisho hayo, Waheshimiwa Wabunge walipata nafasi kwa siku saba; tarehe 18 – 22 na tarehe 25 na leo tarehe 26 Juni, 2018 ya kujadili Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mujibu wa Kanuni ya 106(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016. Hivyo napenda kutumia fursa hii kukushukuru kwa dhati kabisa wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha mjadala huu vizuri ambao unatarajiwa kuhitimishwa leo jioni kwa kura.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea zaidi, napenda kutambua michango mizuri iliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini. Pia Makamu Mwenyekiti, Jitu Soni, Mbunge wa Babati Vijijini.

Mheshimiwa Spika, nakiri kuwa Kamati hii ilihoji mambo mengi na pia kutoa ushauri kuhusu hatua mbadala au maboresho. Mimi na wenzangu katika Wizara ya Fedha na Mipango, tunaahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Kamati maana tunaamini kwamba Wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti wataendelea kuongozwa na maslahi ya Watanzania walio wengi, hasa wanyonge katika kuishauri Serikali. Ahsanteni sana Kamati ya Bajeti.

Mheshimiwa Spika, aidha, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza na kwa maandishi. Jumla ya Wabunge 208 wamechangia hoja niliyowasilisha. Kati ya hao, 180 wamechangia kwa kuzungumza na 28 kwa maandishi. Naomba niseme kwa niaba ya Serikali, ahsanteni sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu mliyoitoa kwenye bajeti hii kwa niaba ya wananchi mnaowawakilisha.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru pia wananchi wote waliotoa maoni na ushauri juu ya Hotuba ya Bajeti ya Serikali kupitia majukwaa mbalimbali na vyombo vya habari. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inathamini sana michango hiyo, nami na wataalam wa Wizara ya Fedha na Mipango na taasisi zilizo chini yake tumeyapokea na tumejipanga kuyafanyika kazi mambo yote waliyotushauri kwa maslahi ya Tanzania. Baadhi tutayazingatia katika bajeti hii na mengine katika bajeti zijazo.

Mheshimiwa Spika, naomba niweke wazi kabisa, tumeyapokea pia mawazo ya Wabunge kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Hata hivyo, napenda nisisitize kuwa tumepokea yale tu yanayoendana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 (The Tanzania Development Version 2025), Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliopitishwa na Bunge lako Tukufu na Ilani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ambayo imebeba ahadi za Chama Tawala kilichochaguliwa na wananchi na kukipa ridhaa ya kuongoza nchi.

Mheshimiwa Spika, nyaraka nilizozitaja ndiyo chimbuko la ajenda za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wetu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Kamwe hatutasita kumsifia Rais wetu kwa kazi nzuri iliyotukuka anayowafanyia Watanzania wote. Hatuko tayari kuyumbishwa na agenda za kuandikwa. Sisi tunaandika wenyewe na tunatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Tanzania wanayo macho na hawalazimiki kuambiwa tazama. Wale wa Bukoba Mjini wanaona Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyojengwa upya baada ya kuharibiwa na tetemeko la ardhi. Wananchi wa Mwanza wanafurahia daraja la waenda kwa miguu la Furahisha na kivuko kipya katika Ziwa Victoria. Wakazi wa Jiji la Arusha wanaona barabara mpya kutoka Arusha mpaka Tengeru ilivyopendezesha Jiji lao. Wananchi wenzangu wa Kigoma wanaona barabara ya Kidahwe hadi Kasulu imeanza kuwekwa lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Dar es Salaam wanaona barabara za juu katika makutano ya TAZARA ikielekea kukamilika na bandari ikipanuliwa na kuongezewa kina. Wanaifakara sasa wanavuka mto Kilombero kupitia Daraja la Magufuli kwa usalama. Wananchi wa Mtwara wanaona uwekezaji mkubwa wa upanuzi wa Bandari ya Mtwara.

Mheshimiwa Spika, vilevile, wananchi wa Masasi sasa wataondokana na adha ya ukosefu wa maji, kufuatia ukarabati wa miundombinu ya kusambaza maji na ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji Chiwambo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakazi wa Jiji la Dodoma wameikaribisha Serikali na sasa tuko hapa. Wananchi wa Tanga wanashuhudia kuanza kazi ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga. Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeongezeka nchi nzima. Watoto wetu kote nchini wanafaidi elimu bila ada na kadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa yote hayo na mengine mengi, kwa nini tusiisifie Serikali ya CCM na Jemedari wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nirejee kwa muhtasari mapendekezo yaliyoungwa Mkondo na wachangiaji wengi. Kwanza, kufuta kodi ongezeko la dhamani kwa taulo za kike; pili, kupunguza kiwango cha kodi ya Mapato ya makampuni kutoka asilimia 30 hadi asilimia 20 kwa wawekezaji wapya wa viwanda vya madawa ya binadamu na viwanda vinavyotengeneza bidhaa za ngozi; na kulinda wawekezaji wa ndani kwa kuongeza ushuru kwenye bidhaa zinazotoka nje ya nchi ambazo zinaweza kuzalishwa na viwanda vya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nne, ni kusamehe VAT kwenye vifungasho vya madawa ya binadamu vinavyotengenezwa mahususi kwa ajili ya viwanda vinavyozalisha dawa hapa nchini; na tano, kusamehe VAT kwenye virutubisho vinavyotumika kutengeneza vyakula vya mifugo kwa lengo la kupunguza gharama kwa wafugaji na kuhamasisha ufugaji bora.

Mheshimiwa Spika, sita, ni kuanzisha utaratibu maalum wa kusamehe kodi ambao unalenga kusamehe malimbikizo ya nyuma ya riba na adhabu kwa kiwango cha asilimia 100 na pia kuweka msisitizo katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli kwa kiwango cha standard gauge, mradi wa kufua umeme Rufiji, mradi wa makaa ya mawe na chuma, Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Spika, pia mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika kule Lindi. Pia kuna shamba la miwa na shamba la sukari Mkulazi na uendelezaji wa maeneo maalum ya uwekezaji. Hatua zote hizi zililenga kuhamasisha ujenzi wa viwanda hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba pia niseme kwa kifupi hoja na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza tulishauriwa kuongeza tozo ya Sh.50/= kwa lita ya dizeli na petrol lakini pia zilitolewa hoja kuhusu pendekezo la Serikali la kuanzisha mfumo wa stamp za kodi za kielektroniki kwamba itekelezwe kwa uangalifu. Pia tulishauriwa kwamba Serikali itoe mara moja bakaa ya fedha za ushuru wa korosho zinazosafirishwa nje ya nchi kwa Bodi ya Korosho; nne, kwamba kwenye kuanzishwa kwa akaunti jumuishi ya Hazina tuelezwa kwamba hatua hii ni kinyume cha Katiba ya nchi na vilitajwa vifungu; tano, kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii.

Mheshimiwa Spika, pia kulikuwa na hoja kuhusu uhalisia wa bajeti ya Serikali, umuhimu wa kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara nchini. Vile vile ilitolewa hoja kwamba kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi siyo halisia.

Mheshimiwa Spika, ilielezwa kwamba ni muhimu kuboresha mifumo ya ulipaji kodi na kuheshimu sheria zinazosimamia masuala ya ukusanyaji wa kodi, lakini pia ilielezwa kwamba mwenendo wa Sekta ya Fedha hauridhishi; lakini pia kwamba vyanzo vikuu vya mapato ya Halmashauri vinachukuliwa na Serikali Kuu bila kuvirejesha. Lingine ni kwamba Serikali sasa ichukue hatua za madhubuti zaidi kulipa madai mbalimbali na kwamba deni pia la Taifa linakua kwa kasi mno na hivyo lidhibitiwe.

Mheshimiwa Spika, mawazo mengine ni pendekezo la kufuta sheria iliyoanzisha Tume ya Mipango kwamba siyo jambo jema kwa maendeleo ya nchi. Pia kulikuwa na masuala mbalimbali yanayohusu mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali na Muungano wa Tanzania; na vile vile tulishauria kwamba Serikali iangalie tena baadhi ya hatua mpya za mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, kama ulivyosema mwenyewe, ni wazi kabisa kuwa hoja na michango mbalimbali iliyotolewa kwa siku saba na Waheshimiwa Wabunge haiwezi kufafanuliwa kwa muda wa hizi dakika 40. Hivyo kama ilivyo ada, napenda kuliahidi Bunge lako Tukufu kuwa Wizara yangu itatoa ufafanuzi wa kina wa hoja zote na kuziwasilisha kwa maandishi kupitia kwa Katibu wa Bunge kwa ajili ya rejea ya Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hii kuwashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kufafanua vizuri baadhi ya hoja zinazohusu sekta wanazozisimamia.

Mheshimiwa Spika, wakati wote wa mjadala humu Bungeni kuhusu mapendekezo ya Serikali ya Makadirio na Mapato ya Matumizi kwa mwaka ujao wa fedha, Serikali ilisikiliza kwa makini maoni na ushauri kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Serikali sikivu ya CCM ilipokea na kufanyia kazi ushauri wa kizalendo kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge na wadau mbalimbali na sasa napenda kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu mapendekezo ya kufanya marekebisho ya baadhi ya kodi na tozo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni Sheria ya Michezo ya Kubahatisha Sura ya 41. Napendekeza kuwianisha viwango na msingi wa ukokotoaji wa kodi ya Michezo ya Kubahatisha hasa inayoshabihiana. Kwanza, kubashiri matokeo (Sport Betting for land based and on line). Pili, ni sehemu ya mashine 40 (forty machine sites); ya tatu ni Bahati Nasibu ya SMS Lottery na Casino za mtandao (internet casino).

Mheshimiwa Spika, kiwango cha kodi kinachopendekezwa katika michezo hii inayoshabihiana ni asilimia 25 ya mauzo halisi (Gross Gaming Revenue - GGRA) badala ya viwango na wigo uliopo sasa. Pili, kwa michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa (National Lottery) napendekeza kutoza kodi kwa kiwango cha asilimia 20 kwa mauzo halisi (GGR) badala ya asilimia 10 ya mauzo ghafi (Gross Sales) inatozwa sasa.

Tatu, ni kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi (Gaming Tax on Wining) kutoka asilimia 18 hadi asilimia 20 kwenye Bahati Nasibu ya SMS Lottery. Michezo ya kubashiri matokeo Sports Betting, Slot Machine Operations, Bahati Nasibu ya Taifa, sehemu ya mashine 40 na casino ya mtandaoni (internet/online casino). Nne, kupunguza kiwango cha kodi, kwenye zawadi ya ushindi yaani Tax on Winnings kwa michezo ya Casino ya ardhini (Land Based Casino) kutoka asilimi 18 hadi asilimia 12 au chini.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo hayo ya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Michezo ya Kubahatisha, yanatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 29.7.

Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura 148 ili kwanza kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mashudu yanayotumika kutengeneza chakula cha mifugo kama ifuatavyo:-

(a) Mashudu ya Soya HS Code 2304.00.00;

(b) Mashudu ya Pamba HS Code 2306.10.00; na

(c) Mashudu ya Alizeti HS Code 2306.30.00.

Mheshimiwa Spika, lengo la marekebisho haya ni kwa kuwawezesha wafugaji kupata chakula cha mifugo kwa bei nafuu zaidi na hivyo kuhamasisha ufugaji bora na kuongeza mchango wa Sekta ya Ufugaji katika pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, lakini pili, ni vifaa vya kukusanyia kodi taxi instruments ambazo ni stamp za kodi za kielektroniki HS Code 4907.00.90 na pili, ni mashine za kielektroniki za kutolea risiti (Electronic Fiscal Devices) HS Code 8470.50.00.

Mheshimiwa Spika, lengo la mapendekezo haya ni kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani, kwenye stamp za kodi za kieletroniki na mashine za kielektroniki za kutolea risiti ili kuwapatia unafuu wazalishaji wa bidhaa zinazobandikwa stamp za kodi za kielektroniki pamoja na kutoa hamasa juu ya matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti. Hatua hizi pia zinatarajiwa pia kuimarisha usimamizi na udhibiti wa mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo haya ya Sheria za Kodi za Ongezeko la Thamani yatapunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 1.6.

Mheshimiwa Spika, marekebisho ya Sheria ya Michezo ya Kubahatisha pamoja na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla wake yataongeza mapato ya Serikali kwa shilingi bilioni 639.0 hadi shilingi bilioni 646 sawa na ongezeko la shilingi bilioni saba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wengi walichangia hoja kuhusu marekebisho katika Sheria ya Tozo ya Huduma ya Bandari, Sura 264 kwa kurekebisha kifungu cha (3) kinachohusu kuongeza tozo za huduma za bandari kutoka Sh.500/= hadi Sh1,000/= kwa wasafiri ambao ni wakazi nchini na kutoka Dola za Marekani tano (5) hadi 10 kwa wasafiri ambao ni wageni nchini na kuomba kuwa msamaha uendelee kutolewa. Serikali imewasikia na msamaha huo utaendelea kutolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge walizungumzia pia marekebisho katika Sheria ya VAT aya ya 22, sehemu ya kwanza ya jedwali, kwa kufuta msahama wa kodi ya ongezeko la thamani kwa ndege ndogo za kukodisha na kuiomba Serikali iendelee kutoa msamaha huo. Nichukue fursa hii kulieleza Bunge lako Tukufu kwamba Serikali ya CCM imefanyia kazi hili na sasa msamaha huo utaendelea kutolewa kama kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 75 wa hotuba yangu nilipendekeza kufuta leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria ya Afya na Usalama. Napenda kufanya marekebisho eneo hilo lisomeke, “kufuta ada ya leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria ya Afya na Usalama.”

Mheshimiwa Spika, nirudie tena kusema, Chama cha Mapinduzi kimeielekeza Serikali yake kuwa sikivu na maboresho niliyoyaeleza yanathibitisha hilo. Aidha, tutaendelea kufanyia kazi mapendekezo yote na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge na wananchi wengine kwa maslahi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa niende kwenye baadhi ya hoja na ushauri uliotolewa na Wabunge wengi. Kwanza kulikuwa na hoja kwamba Serikali iongeze tozo ya Sh.50 kwa lita ya mafuta ya petrol na desel kwa ajili ya Mfuko wa Maji ili kuwe na chanzo kinachotabirika (ring fence).

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uwepo wa changamoto ya upatikanaji wa maji katika sehemu mbalimbali nchini, mijini na vijijini. Katika kutatua changamoto hii Serikali imekuwa ikitenga fedha kwenye bajeti kwa ajili ya miradi ya maji. Aidha, baadhi ya miradi iligharamiwa moja kwa moja na wadau wa maendeleo wa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi hizi za Serikali na wadau wa maendeleo, bado maeneo mengi mijini na vijijini yanakabiliwa na uhaba wa maji. Kutokana na hali hii, Waheshimiwa Wabunge walipendekeza kuongeza tozo ya Sh.50/= kwa kila lita moja ya mafuta ya petrol na diesel kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Spika, Serikali imechambua kwa kina pendekezo hili. Pendekezo hili ni zuri lakini wakati huu sio muafaka kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, tumetazama mwenendo wa matarajio bei ya mafuta kwenye Soko la Dunia na tunaona wazi kabisa kwamba kwa takwimu tulizonazo mwenendo wa bei ya mafuta ulimwenguni inakwenda juu, kwa hiyo, huu siyo wakati muafaka. Tutatoa takwimu kupitia kwenye Ofisi ya Katibu wa Bunge, kuonesha uchambuzi ambao tumefanya.

Mheshimiwa Spika, kutokana na Ripoti ya Hali ya Uchumi wa Dunia (World Economic Outlook ya IMF) iliyotolewa mwezi Aprili, bei ya mafuta ghafi inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia kati ya wastani wa Dola 60 hadi 70 kwa pipa, ikilinganishwa na matarajio ya awali ya Dola za Marekani 50 mpaka 60 kwa pipa kwa mwaka 2018.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019, bei ya mafuta ghafi inatarajiwa kufikia wastani wa Dola 65.5 kwa pipa na ongezeko hilo linachangiwa na makubaliano ya kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa wanachama wa OPEC na baadhi ya wazalishaji wasio wanachama wa OPEC na hali hii inaweza kusababisha ongezeko la kasi ya mfumuko wa bei, nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kodi na tozo zilizopo kwenye mafuta kwa sasa ni nyingi sana; na bidhaa za mafuta ya petrol na diesel zina kodi nyingi. Pendekezo lililotolewa na Waheshimiwa Wabunge kama lingekubaliwa, ingekuwa ni mzigo mkubwa sana. Kwanza kuna tozo na kodi kwa ajili ya mamlaka mbalimbali za umma, hizo ziko 11; ziko kodi za Serikali Kuu tatu, ziko kodi na tozo za mauzo ya jumla ya mafuta, ziko mbili; kuna tozo na kodi kwa mauzo ya rejareja ya mafuta, ziko tatu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kodi na tozo hizi, ni wazi kabisa kwamba bidhaa za mafuta ya petrol na diesel zimebebeshwa mzigo mkubwa sana katika kuchangia maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, baada ya kufanya tathmini, tumeona kwamba tozo hii ingeongeza bei ya mafuta nchini na kusababisha kupanda kwa pump prices ya mafuta ya diesel na petrol. Tunayo mifano ambayo tumechambua kwa Dar es Salaam, kiasi gani ambacho bei ya mafuta ingeongezeka. Vile vile ingeleta athari kwenye utulivu wa uchumi kwa ujumla (macroeconomic stability) na kusababisha bei za bidhaa na huduma ambazo zinazalishwa hapa nchini kuongezeka (second round effect).

Mheshimiwa Spika, wakati wa Hotuba ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, zilielezwa njia mbadala za Serikali katika kugharamia Miradi ya Maji Nchini. Kwa hiyo, nisingependa kuzirejea, itoshe tu kusema kwamba tumetenga shilingi bilioni
673.2 kwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha kugharamia miradi ya maji mijini ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, ahadi ya Serikali ni kwamba tuna dhamira ya dhati ya kupeleka fedha kwenye utekelezaji wa miradi ya maji kama ilivyopitishwa na Bunge lako Tukufu kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile tumepokea fedha katika mwaka uliokwisha. Tumeshasaini mkataba na Benki ya Exim ya India, Mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekekelezaji wa miradi ya maji katika Miji 21, Tanzania Bara na Zanzibar. Pia tumeshakamilisha majadiliano na Benki ya Dunia ambapo Dola za Marekani milioni 350 zinatarajiwa kupatikana na kati ya kiasi hicho Dola za Marekani 60 sawa na asilimia 17 kitatolewa mwezi Julai, 2018.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja juu ya pendekezo la Serikali la kuanzisha mfumo wa stamp za kodi za kielektroniki. Serikali ilishauriwa itengeneze yenyewe mfumo wa ETS ili kiasi cha fedha ambacho kitalipwa kampuni ya CIPA iwe ni sehemu ya mapato ya Serikali, badala ya mapato yatokanayo na stamp ya kuchukuliwa na Kampuni Binafsi.

Mheshimiwa Spika, tumelichambua sana hili, niseme tu kwamba teknolojia ya kutengeneza mfumo huu ni mpya hapa nchini na hivyo hapakuwa na kampuni au taasisi ya Serikali iliyokuwa na uwezo wa kutengeneza mfumo huo. Kutokana na hilo, ililazimu Serikali itangaze Zabuni ya Kimataifa kwa uwazi na ndipo tulipompata Mzabuni mwenye uwezo na uzoefu wa kutengeneza mfumo huu kati ya Makampuni tisa yaliyojitokeza na hapakuwepo Kampuni ya ndani iliyojitokeza.

Mheshimiwa Spika, pia uwekezaji wa mradi huu ni zaidi ya mwaka mmoja na hivyo gharama za mradi zimezingatia muda huo ili kufidia gharama ya uwekezaji. Mapato yatokanayo na stamp za kodi kwa muda wa mwaka mmoja hayawezi kulingana na gharama za uwekezaji wa mradi huo katika mwaka wa kwanza.

Mheshimiwa Spika, vilevile mfumo huo utakapokamilika kujengwa, utaanza kuunganishwa kwenye viwanda vya uzalishaji kwa awamu kulingana na uhatarishi wa upotevu wa mapato katika bidhaa husika.

Mheshimiwa Spika, napenda niseme tu kwamba mfumo huu una faida nyingi sana ambazo zinazidi hizo gharama ambazo ilikuwa ni wasiwasi wa Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, niseme kuhusu ushuru wa korosho zinazosafirishwa nje ya nchi na matumizi yake. Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Kilimo walifafanua jambo hili kwa ufasaha jana na nisingependa kurudia. Ni vyema niseme na Watanzania wasikie na ikae kwenye Kumbukumbu Rasmi za Bunge lako Tukufu. Mimi Phillip Mpango siwezi kamwe kuwahujumu wananchi, wakulima wa korosho wa Mikoa ya Mtwara na Lindi au mkoa mwingine wo wote ule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwahikikishie Watanzania kuwa Mtwara na Lindi nitakwenda, iwe katika kutelekeza majukumu yangu ya kikazi au kuwatembelea ndugu na marafiki. Hakuna anayeweza kunizuia, ni haki yangu na uhuru wangu kama Mtanzania ambayo haiwezi kupokonywa kwa vitisho. Hata ikibidi kufa katika kutumikia Taifa na iwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika nafasi mbalimbali nilizotumikia Serikali ya CCM na Taifa hili kwa ujumla, nimetumia uwezo wangu wote kuwatumikia Watanzania wa mikoa yote, nimefundisha wanafunzi wakiwa ni pamoja na wanaotoka Mikoa ya Kusini, nilipokuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Dar es Salaam bila upendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, kati ya mambo niliyofanya nikiwa Mshauri wa Rais, Uchumi katika Serikali ya Awamu ya Nne na nilipokuwa Mkuu wa Tume ya Mipango, nilikuwa mstari wa mbele kuishawishi Serikali kuifanya Mtwara iwe kitovu cha ukuaji wa uchumi hapa nchini (Mtwara Growth Pole) na kuingiza miradi mikubwa ya maendeleo, kwa mfano upanuzi wa Bandari ya Mtwara, LNG Plant Lindi, Barabara za uchumi na kadhalika katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.

Mheshiomiwa Spika, mimi na wenzangu tuliishauri Serikali kutenga nafasi za upendeleo kwa vijana kutoka Mikoa ya Kusini kusoma masomo ya sayansi ili baadaye waweze kufanya kazi katika viwanda vinavyohusiana na Sekta ya Gesi Asilia; niliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotaka pamoja na mambo mengine kuhakikisha maendeleo ya Uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa uangalifu na kwa pamoja ambayo iko kwenye Ibara ya 9 (d). Iweje leo niwahujumu wananchi wa Mtwara na Lindi?

Mheshimiwa Spika, kama yupo mtu ana chuki binafsi na Phillip Mpango, pasipo chembe ya ukweli, mimi namwombea msamaha kwa Mungu. Nasema tena, sitayumba katika kusimamia matumizi bora ya fedha za umma kwa mujibu wa sheria. Nawakumbusha wabadhirifu wa fedha za umma, wajue wanakula sumu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, najua muda siyo rafiki, nilitarajia ningesema sana leo, lakini naomba niseme jambo moja kabla sijaenda kwenye kuhitimisha. Kulikuwa na hoja kuhusu mapendekezo ya Serikali ya kufuta sheria iliyoanzisha Tume ya Mipango.

Mheshimiwa Spika, nilieleza katika hotuba niliyowasilisha tarehe 14 Juni, kwamba mapendekezo hayo ni mabadiliko ya kimuundo na siyo kufuta kazi muhimu za kupanga mipango ya maendeleo ya Taifa letu kwa kipindi cha muda wa kati na muda mrefu. Ukifuatilia historia ya muundo ya Taasisi ya Tume ya Mipango, iko wazi kuwa imekuwa inahama, kwa nyakati tofauti toka tulipopata Uhuru, Taasisi hiyo kuna kipindi ilikuwa peke yake kama Wizara kamili au Tume na wakati mwingine ikawa sehemu ya Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Spika, tena jambo hili siyo kwa Tanzania pekee, hata katika nchi jirani za Uganda na Rwanda hivi sasa, fedha na mipango vinaunda Wizara moja (Ministry of Finance and Economical Planning). Lengo kuu ni kuwianisha Mipango ya Maendeleo ya Taifa na ugawaji wa rasilimali fedha, jambo ambalo ni gumu pale ambapo Taasisi hizi zinapokuwa zimetenganishwa.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza, kazi ya kuandaa na kusimamia mipango ya maendeleo ya Taifa ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango, itaongozwa na Kamishna atakayekuwa na fungu lake kuwezesha utekelezaji wa kazi za idara hiyo. Kazi hizo zimeendelea kufanyika vizuri baada ya kuhamisha wataalam wa iliyokuwa Tume ya Mipango ndani ya Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Spika, naomba kuhitimisha. Kama nilivyoeleza katika hotuba yangu, hatua zilizopendekezwa kwenye Bajeti hii zinalenga kujenga msingi madhubuti wa uchumi wa viwanda na kupanua fursa za ajira na biashara. Dhamira yetu sote ni kufikia kiwango cha uchumi wa kipato cha kati itakapofika mwaka 2025. Ili kushiriki katika mafanikio hayo, ni lazima kila mmoja wetu ashiriki katika shughuli halali za kuzalisha na afanye hivyo kwa juhudi na maarifa ili kuleta tija.

Mheshimiwa Spika, kufanikiwa kwa Bajeti hii kunahitaji nidhamu ya hali ya juu katika usimamizi wa mapato na matumizi. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alituusia, nitasema kwa Kiingereza; mwanzo wa kunukuu: “our watch word must be frugality, this must run through the whole expenditure.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, hii inatoka kitabu cha Freedom and Socialism. Ili kufikia azma hii, juhudi za pamoja kati ya Serikali na wadau wote zinahitajika ikiwa ni pamoja na kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi kwa kuwekeza zaidi katika maeneo ya kipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, najua Watanzania tuna kiu kubwa ya kuendelea, tena haraka, lakini tukumbuke kuwa kila safari inaanza na hatua moja ikifuatiwa na nyingine. Vile vile njia ya maendeleo ina vikwazo vingi na haiwezekani kutatua changamoto zote za nchi hii kwa mara moja.

Mheshimiwa Spika, hata nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza na kadhalika bado wanazo changamoto, bado nao wanajenga barabara, reli, hospitali na kadhalika. Hivyo ni muhimu Watanzania tuendelee kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kudumisha amani na umoja wa Taifa letu. Changamoto zitaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote, mjadala wetu wa siku saba umeyatendea haki mapendekezo ya Bajeti niliyowasilisha tarehe 14 Juni, 2017. Kukosoa kwa haki ili kujenga (constructive criticism) na kujikosoa ni sehemu muhimu sana katika harakati za maendeleo ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa jambo kubwa la Kitaifa kama hili la Bajeti ya Serikali, ningestaajabu sana kama kila Mbunge angesimama na kusifia tu mapendekezo niliyowasilisha. Ndiyo maana mwanzo kabisa mwa Hotuba ya Bajeti Kuu nilibainisha kwa makusudi changamoto kubwa zinazotukabili kama Taifa na kwa ukweli, ili tujielekeze kwa pamoja katika kuzitatua.

Mheshimiwa Spika, imani yangu ni kuwa lazima tuwe wa kweli sisi wenyewe na kwa Taifa letu, lakini ni muhimu pia tuishi katika dunia, tusiishi katika dunia ya kufikirika. Kwa Kiingereza, we have to be honest ourselves, honest to our country and be as pragmatic as possible. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatukuandaa bajeti hii kujifurahisha. Tumekuwa wakweli katika kutathmini utekelezaji wa Bajeti 2017/2018, tuliyoifanya. Katika mapendekezo tuliyoleta hapa Bungeni juu ya hatua ambazo tunaamini kwa dhati zitatupeleka mbele kama Taifa. Ukweli ni kwamba ni rahisi sana kusema, rahisi sana kwa rafiki zangu wa upande wa pili kukosoa, lakini nao wanajua kuwa ni vigumu kutenda, ndiyo maana hata walichokisema ni Bajeti Mbadala waliandikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalize kwa kumshukuru tena Mwenyezi Mungu kwa rehema zake. Namshukuru sana Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, wewe mama ni mahiri kweli kweli, umekuwa ni msaada mkubwa sana. Namshukuru sana Katibu Mkuu na Wataalam wote wa Wizara ya Fedha kwa kuendelea kufanya kazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, nawaomba sana Waheshimiwa Wabunge wote kuunga mkono Bajeti hii ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 ikiwa ni hatua nyingine thabiti ya Kujenga Uchumi wa Viwanda Nchini Tanzania na kuboresha maisha ya wananchi wetu. Natanguliza ahsante kwa kura yenu ya ‘Ndiyooo!’

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda nitumie fursa hii kukushukuru sana wewe kwa kuendesha vizuri mjadala huu wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2018/2019 ni dhahiri kabisa ule usemi wa wazee wetu kwamba zipo kazi hatumwi mtoto, naona tangu jana na kwa sehemu kubwa leo Kiti amekalia mwenye kiti. Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutambua michango iliyotolewa na Kamati ya bajeti chini ya mwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini na Makamu wake Mheshimiwa Jitu Soni (Mbunge), pia Wabunge wote kabisa waliochangia kwa kuzungumza na kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, jumla ya Wabunge 56 wamechangia hoja niliyoiwasilisha na kati ya hao 35 wamechangia kwa kuzungumza na Wabunge 21 wamechangia njia ya maandishi. Namshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji (Mbunge), huyu ni Mama mahiri kweli, namshukuru kwa kunisaidia kufafanua hoja nyingi ambazo zimetolewa toka jana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, michango iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni mizuri sana, hata ile ambayo ilikuwa inaegemea zaidi kwenye mitandao isiyo na uhakika bado nayo ni michango tu tunaipokea. Nitapenda nitoe ufafanuzi na majibu ya baadhi ya hoja zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge wote. Kwa wingi wa hoja na pia ukweli kwamba hoja nyingi ni za kutusaidia kuboresha kazi zetu kwa mwaka ujao wa fedha Bunge lako tukufu litakapotupitishia bajeti tuliyoomba, basi nitaomba nitoe ufafanuzi wa hoja chache kwa sababu pia ya muda. Naomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge na wewe Mheshimiwa Spika kwamba majibu ya hoja zote ambazo zimetolewa hapa na Waheshimiwa Wabunge tutaziwasilisha kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo naomba nianze na hoja moja moja. Nilipenda nianze na hoja iliyotolewa mwanzo kabisa wa mjadala kuhusu mashine za EFD kutofanya kazi na kwamba Serikali inapoteza mapato. Kwa umuhimu wake naomba nianze nayo hii.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba kuanzia tarehe 11 Mei, 2018 mashine za kielektroniki za kukusanya mapato hazikuwa zinafanya kazi kutokana na hitilafu ya mfumo ambayo ilitokana na kuharibika kwa kifaa ambacho kinatunza na kuchakata taarifa za wafanyabiashara. Hitilafu hiyo ilisababisha wafanyabiashara wakashindwa kutuma taarifa za mauzo yao ya mwisho wa siku tunaziita “z-report” kwenda TRA. Labda tu kwa taarifa ni kwamba hizi mashine za EFD zimetengenezwa kwa namna ambayo kama usipotuma taarifa hizo kwa siku nne mfululizo basi mashine zinagoma kutoa risiti.

Mheshimiwa Spika, baada ya kutokea tatizo hili wataalam wetu wa Kitengo cha IT cha TRA kimefanyia kazi changamoto hiyo, kwa kweli wamefanya kazi usiku na mchana na hadi sasa bado tunaendelea kulifuatilia jambo hili kwa karibu na mpaka ilipofikia tarehe 1 Juni, 2018 mfumo huu vijana wetu waliweza kuurejesha kwenye hali yake ya kawaida na mfumo ukatengemaa kabisa na kuanza kufanya kazi kama ilivyokuwa awali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatizo lilokuja kuibuka ni kwamba aidha kwa kujua au kwa maksudi baadhi ya wafanyabiashara walizima kabisa mashine zao hata baada ya mfumo kuwa umetengemaa, hivyo mashine zikashindwa kupokea majibu ya taarifa kutoka kwenye mfumo wetu pale kwenye saver kuu na mamlaka ya mapato.

Mheshimiwa Spika, wito wangu kwa wafanya biashara ni kwamba warejee kutumia mishine za EFD kikamilifu na kutoa taarifa kwa mawakala wa EFD au TRA pale ambapo mashine zao zinakuwa hazifanyi kazi.

Mheshimiwa Spika, toka jana nimetoa maagizo kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ahakikishe kwamba maafisa wetu wote wa Mamlaka ya Mapato nchi nzima wanaondoka ofisini na kuwatembelea wafanyabiashara wote wanaopaswa kutumia mashine za kielektroniki ili kuhakikika kwamba zinatumika ipasavyo. Vilevile nimetoa maelekezo kwamba barua zote ambazo zilikuwa zimetolewa na Mamlaka ya Mapato kabla ya leo tarehe 4 Juni, 2018 ambazo ziliwaruhusi wafanyabiashara waendelee kufanya mauzo bila kutumia mashine za EFD kwa kisingizio kwamba hizi mashine hazifanyi kazi, mpaka wengine kataratasi wamezifanyia lamination kama vile tatizo hili nimekuwa ni la kudumu, basi nawaambia rasmi kwamba hizo karatasi hazina uhalali kuanzia sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hitilafu yoyote ya kiufundi itolewe upya, Mamlaka ya Mapato na kwa hawa vendors wa hizi machines kwa ajili ya utatuzi wa haraka.

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile nawasihi sana wafanyabiashara tunawapenda sana, tunawaomba waingize kumbukumbu za mauzo ambazo walizitunza nje ya mfumo wakati hitilafu ilipotokea, sasa waziingize na niwakumbushe tu kwamba hairuhusiwi kwa mfanyabiashara yoyote kutoa risiti zenye thamani tofauti na kiasi halisi ambacho kimelipwa na mteja. Zipo petrol station unakwenda unanunua mafuta, unakuta wamekata hela uliyotoa, nawakumbusha tena kwamba ni kinyume cha sheria na adhabu kali itatolewa kwa mfanyabiashara yeyote atakayekiuka maelekezo haya.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilihusu Tume ya Mipango na hapa tulishauriwa kwamba irejeshwe, Fungu 66 pia lirejeshwe, na kazi zilizokuwa zinafanywa Tume ya Mipango ziendelee kufanywa chini ya ofisi ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Hati ya Majukumu ya Mawaziri (The Ministers’ Assignment of Ministerial Functions Notice, 2016) iliyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mojawapo ya majukumu yaliyokasimiwa kwa Waziri wa Fedha na Mipango ni majukumu ya iliyokuwa Tume ya Mipango, Mheshimiwa Rais amepewa mamlaka haya kwa mujibu wa The Ministers’ Discharge of Ministerial Functions Act Cap. 299 ambayo ilipitishwa na Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika, napenda kulihakikishia Bunge lako tukufu kwamba baada ya majukumu kuhamishiwa Wizara ya Fedha na Mipango, tumeendelea kusimamia na kutekeleza majukumu yote ya yaliyokuwa yakitekelezwa na Tume ya Mipango, ndiyo maana tutawasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka ujao wa Fedha, na shughuli nyingine zote zimendelea kama kawaida. Aidha, ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi, watumishi zaidi ya 50 waliokuwa Tume ya Mipango wamehamishiwa Wizara ya Fedha na Mipango ili kuiwezesha Wizara kuwa na watumishi ambao wana weledi na uzoefu kwenye shughuli ambazo zilikuwa zinatekelezwa na Tume na kulinda institutional memory.

Mheshimiwa Spika, vilevile kama nilivyoeleza kwenye aya ya 3.1.2 ya bajeti ya Wizara ambayo niliwasilisha jana, muundo wa Wizara uko katika hatua ya mwisho ya kuidhinishwa na mamlaka husika na tumefanya mapitio ili kuunda, Division ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa ambayo itaongozwa na Kamishna na itakuwa na kifungu chake kwa ajili ya shughuli za kibajeti.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nilieleze Bunge lako tukufu maana kulikuwa na hoja kwamba sasa hata kazi za mipango hivi hazionekani na Wizara inajielekeza kwenye mambo ya fedha peke yake na kutafuta mapato, hili siyo kweli. Naomba nisisize tena kwamba katika kuandaa bajeti na mipango ya maendeleo bado tunaongozwa na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao nimeshika hapa, 2016/2017 mpaka mwaka 2020/2021. Miradi hii inayosemwa kwamba haikuwepo kwenye mipango siyo sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye mpango huu, ukianza na ukurasa ule wa 80 miradi hii yote hii imo. Kwanza niseme kuna kuimarisha upatikanaji na uhakika wa nishati ya umeme vijijini na mijini, pia kuna kipengele cha ununuzi wa ndege mpya na kufufua usafiri wa anga. Hali kadhalika ukienda ukurasa unaofuata kitabu hiki kinabainisha wazi kabisa, kwamba lengo letu upande wa nishati ni kuongeza uzalishaji wa umeme, kutoka megawati 2,899.3 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo maji, gesi na kadhalika. Kwa hiyo, hii miradi haikuokotwa, iko kwenye kitabu chetu cha mpango.

Mheshimiwa Spika, hali kadhalika kitabu hiki kinabainisha kwamba, moja ya miradi tutakayofanya ni ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha standard gauge. Kwa hiyo, huu ndiyo mwongozo wetu unaotuelekeza kuandaa Bajeti ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja pia kwamba Maafisa wetu wa Mamlaka ya Mapato wanafanya tathmini kwa wafanyabiashara, lakini wanapofanya hivyo wanaweka viwango vya juu kuliko uwezo au faida za biashara husika na kusababisha biashara kufungwa au wafanyabiashara kukwepa kodi. TRA inakokotoa kodi kwa wafanyabiashara kwa kuzingatia taratibu na kanuni ambazo zimebainishwa katika sheria mbalimbali. Kuna Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, Sura ya 332 na Sheria ya Usimamizi na Utawala wa Kodi ya mwaka 2015, Sura ya 438.

Mheshimiwa Spika, pia sheria hizi zimeweka utaratibu wa uwasilishaji wa pingamizi za kodi, kwa wafanyabiashara ambao wanakuwa hawakuridhika na makadirio ya kodi ambayo wanapewa, kwa mujibu wa sheria hizo, pingamizi zinawasilishwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa makadirio ya kodi inayohusika. Sasa utaratibu huu unatoa nafasi kwa Mamlaka ya Mapato kutoa makadirio sahihi kulingana na mapingizi na hoja ambazo zimewasilishwa. Napenda Bunge lako lifahamu kwamba pingamizi za kodi zinashughulikiwa na watumishi wengine tofauti na wale waliohusika na makadirio hayo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo hayo, Serikali inatambua uwepo wa watumishi wake wachache ndani ya Mamlaka ya Mapato ambao wamekuwa wakitoa makadirio ya kodi kinyume cha taratibu zilizowekwa, hawa tumeendelea kuwachukulia hatua mbalimbali za kinidhamu na za kiutawala. Pia tumeendelea kutoa elimu kwa watumishi wetu kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, maadili na sheria, kanuni na taratibu.

Mheshimiwa Spika, tunayo pia tax payer service charter; hii nayo inatakiwa iwaongoze watumishi wetu wa Mamlaka ya Mapato kuzingatia weledi na kanuni zilizowekwa katika ukadiriaji wa kodi. Ni marufuku kwa watumishi wetu wa Mamlaka ya Mapato kukiuka maelekezo hayo, kama kazi ikikushinda huwezi kufuata taratibu haya tupishe wako Watanzania wengi ambao wanaweza kufanya hizi kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Mamlaka ya Mapato inawaelimisha wafanyabiashara juu ya mfumo wa kodi, tunawaelewesha pia juu ya taratibu ambazo zinatumika katika ukokotoaji wa kodi na namna ya kuwasilisha haya mapingamizi. Hatua zote hizi tunalenga kuwahakikishia wafanyabiashara kwamba kwa kweli wanastahili wafanye kazi kwa amani, wanafanya kazi nzuri, wanalipia kodi stahiki kwa mujibu wa sheria na siyo vinginevyo, kodi hizo zinatakiwa zichangie mapato ya Serikali kulingana na ukubwa biashara zao.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kuhusu miradi ya PPP kwamba utekelezaji wake unasuasua. Hili kwa kiasi kikubwa bado ni geni sana katika Taifa letu. Tuna shida kubwa ya utaalamu katika eneo hili na hususan katika nyanja za sheria pia katika nyanja za fedha. Kwanza katika kuandaa credible PPPs, kuzi-package na namna ya kuzi-negotiate. Kwa sababu hiyo Serikali inapokea ushauri na tutaendelea kulifanyia kazi eneo hili sababu ni njia bora mbadala badala ya kutegemea mapato madogo ya Serikali peke yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda niseme kwamba mpaka sasa hivi hatuna Mshauri Elekezi ambaye aliingia mkataba na Serikali kuandaa upembuzi yakinifu kwa utaratibu wa PPP ambaye amesheleweshewa malipo. Kwa hiyo, tutaendelea kuihimiza Serikali nzima na taasisi zake kwamba kabla ya kutangaza zabuni, basi wapatikane wataalam elekezi wa kuandaa miradi ya PPP na kuhakikisha kwamba bajeti inatengwa ya kuweza kugharamia malipo ya wataalam elekezi wa kuandaa maandiko ya miradi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika eneo hili pia kulikuwa na hoja kwamba kuna mradi wa Mchuchuma na Liganga, reli ya Mtwara, Tanga, Moshi, Arusha ambapo Shirika la Reli yetu liliingia mikataba na wakandarasi kwa ajili ya kuandaa upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa miradi hii, kwa utaratibu wa PPP. Napenda nieleze kwamba miradi hii utaratibu uliofuatwa ni ununuzi wa kawaida (traditional procurement) na siyo utaratibu wa PPP, kazi hii ilikamilika mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kuhusu Ofisi ya Msajili wa Hazina. Ni kweli kabisa ofisi hii ina jukumu kubwa la kusimamia Mashirika ya Umma na hoja kubwa ilikuwa kwamba imepokea asilimia ndogo sana ya bajeti kati ya fedha ambazo ziliidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa mwaka huu wa fedha ilitengewa shilingi bilioni 102.23 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, kati ya kiasi hicho shilingi bilioni 95 kilikuwa ni kwa ajili ya kugharamia madai mbalimbali ya Mashirika ya Umma na shilingi bilioni 7.23 kwa ajili ya gharama za uendeshaji wa ofisi.

Mheshimiwa Spika, mpaka kufikia Aprili, fedha zilizotolewa kwa ajili ya OC ni shilingi bilioni 18.62, ambapo shilingi bilioni 5.35 kilikuwa ni kwa ajili ya madai ya Mashirika mbalimbali na shilingi bilioni 13 kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi ikiwa ni pamoja na kulipa madai ya watumishi, wazabuni na watoa huduma.

Mheshimiwa Spika, ninachojaribu kusema hapa ni kwamba ni kweli fedha zilizotolewa kwa ofisi ya Msajili wa Hazina zinaonekana ni kidogo, lakini ni vizuri Waheshimiwa Wabunge, wakazingatia pia kuwa ulipaji wa madai ya Mashirika ya Umma yanategemea kukamilika kwa uhakiki au mashauriano ya kimahakama. Kwa hiyo, hatuwezi tu kutoa fedha mpaka haya mawili yawe yamekamilika.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kuhusu Deni la Taifa kuongezeka kutoka dola za Kimarekani milioni 1,054.6 na kuongezeka kutoka dola za Kimarekani 1,957 na hivyo kupelekea Serikali kulipa riba kubwa. Hoja hapa ilikuwa kwamba Serikali ina mikakati gani ambayo imepanga kwa ajili ya kupunguza Deni la Taifa.

Mheshimiwa Spika, nisisitize kuwa kwamba ni kweli deni limekuwa linaongezeka mwaka hadi mwaka, nirudie tena kusema deni letu jamani ni himilivu kwa vigezo vyote, tutaendeleaje bila kukopa? Lazima tukope hadi Machi, 2018 deni la Serikali lilifikia bilioni 48,889 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 16.3. Kati ya kiasi hicho deni la ndani lilikuwa bilioni 14,158.6 na deni la nje bilioni 35,729.9. Ongezeko hili lilitokana na mikopo mipya yenye masharti nafuu na ile yenye masharti ya kibiashara. Lakini kikubwa tulitumia fedha hizi kugharamia fedha za maendeleo.

Mheshimiwa Spika, tumeendelea kuhakikisha kwamba Deni la Taifa linadhibitiwa na linaendelea kuwa himilivu, mikakati yetu kwanza tunahakikisha kwamba mikopo ambayo inapewa kipaumbele ni ile yenye masharti nafuu. Mikopo ya kibiashara tunaikopa kwa uangalifu sana, ikiwemo kuhakikisha kwamba hii mikopo ni ile ambayo inakwenda kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa letu, ndiyo maana tunapeleka mikopo hii kwa ajili ya kujenga mradi wa umeme unakuwaje na uchumi wa viwanda bila umeme?

Mheshimiwa Spika, tunahitaji kujenga standard gauge railway ili tuweze kunufaika na biashara kwenda nchi jirani, ndiyo umeme utakavyokuwa, mkakati mwingine ni kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ikienda sambamba na kupunguza matumizi yanayoweza kuepukika. Kwa hiyo, niendelee tu kusisitiza kwamba tunao mkakati madhubuti na kila mara tunafanya mapitio ya uhimilivu wa deni kwa kila miezi mitatu na kila mwisho wa mwaka ndiyo tunafanya uchambuzi ambao unahusu eneo lote kwa upana wake, tunafanya pamoja na wenzetu hatufanyi peke yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya ndugu yangu Mheshimiwa Nsanzugwanko, kuhusu kujenga ofisi ya Mamlaka ya Mapato Buhigwe, Kasulu na Kakonko, nilitaka nimwambie tu kwamba Serikali imepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, nia yetu kama Serikali ni kuwapa wananchi wetu huduma kwa urahisi na TRA itajenga ofisi hizo kwa awamu kadri tunavyoendelea kupata mapato na tutatoa kipaumbele kwa maeneo ambayo tayari viwanja vilishapatikana kama ilivyokuwa kwa Kasulu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa nimesikia kengele, kama nilivyokwisha kutoa maelezo ni kwamba tutajibu hoja zote hizi kwa maandishi, naomba nisemee moja tu kwamba kwa nini tunaenda kwenye commercial loans badala ya kwenda kwenye concessional loans ambayo itakuwa ni mzigo kwa wananchi. Napenda tu nisisitize kwamba Serikali ilianza kwenda kukopa kwenye masharti ya kibiashara essentially kutokana na kupungua kwa mikopo yenye masharti nafuu na misaada pamoja na nia ya Serikali ya kuongeza ujenzi wa miundombinu.

Mheshimiwa Spika, hii ni muhimu sana ndugu zangu tuangalie mwenendo wa ulimwengu unavyokwenda, enzi zile ambapo Serikali huko Ulaya zilikuwa zinapenda sana general budget support hakuna tena, tutakaa na reli hii ya kizamani mpaka lini? Tutakaa na umeme wa kubangaiza
mpaka lini ambao una capacity charges za ajabu? Kwa hiyo ni mahitaji yetu haya ya kujenga miundombinu ya msingi kwa ukuaji wa uchumi wetu, ndiyo unaotusukuma tutafute vyanzo mbadala vya mapato.

Mheshimiwa Spika, bado tumeendelea kupata mikopo yenye masharti nafuu kama ile ya Benki ya Dunia, African Development Bank na yote kama nilivyoeleza tunaielekeza kwenye miradi ya maendeleo hatukopi kwa ajili ya kula.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusisitiza tu kwamba ni vizuri Watanzania tukaamka. Maendeleo yana gharama, hakuna maendeleo ya lelemama ya kupata bure. Baadhi ya miradi hii Waheshimiwa Wabunge tunakopa kwa ajili ya vizazi vijavyo, tutatumia reli hii kwa zaidi ya miaka 200 ijayo, lazima tuweze kutoa hiyo sacrifice. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na naomba kutoa hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakushukuru sana, kwa kunipa hii fursa niweze kuchangia kwenye hoja zilizotolewa, lakini nitangulize pongezi zangu za dhati kabisa kwa Kamati ya Bajeti na Mwenyekiti wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia PAC na Mwenyekiti wake, kwa kweli taarifa ni nzuri zina afya, na naamini kabisa zitatusaidia kuendelea na juhudi za kuboresha uchumi wa Taifa, lakini pia zitatuwezesha, kuimarisha utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha mwaka kilichobaki. Na naamini pia kwa upande wa PAC ushauri wao utatusaidia kusimamia utendaji wa Mashirika yetu na yale ambayo yametolewa kama ushauri na Waheshimiwa Wabunge waliochangia niwaahidi kwamba tutayafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa baada ya maneno hayo ya utangulizi, niseme kidogo, nikianza na lile ambalo alilieleza Mheshimiwa Balozi Kamala. Ni kweli kabisa kabisa, naungana naye, uchumi wetu umekuwa unakuwa kwa kasi na dunia yote inajua hivyo, sio tu kwamba ni jambo jema, lakini ni lazima tuhakikishe kwamba uchumi wa Taifa unaendelea kukuwa kwa kasi kubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naungana naye pia kusema ni muhimu tuelekeze pia nguvu kukuza sasa size ya keki yenyewe, ametoa takwimu nzuri. Lakini ni vyema tukumbushane tunakotoka nchi yetu tunatoka kwenye kauchumi kadogo sana, kwa mfano mwaka 2000 GDP ya Tanzania ilikuwa ni dola bilioni 10.1 tu, sasa ndani ya miaka 15 kufikia 2017 uchumi wa Taifa umefikia dola bilioni 52. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo unakuwa haitoshi kwa hakika, ukilinganisha na takwimu na zile alizokuwa anasema kwa nchi kadogo kama Ubelgiji ni kweli, lakini msingi wake ni lazima tubadilishe sasa structure ya uchumi wetu, ili twende zaidi kwenye viwanda, twende zaidi kupanua pia huduma ambazo kama Taifa tuna fursa kubwa au comparative and competitive advantages. Kwa hiyo, nilitaka tu niungane na Mheshimiwa Dkt. Kamala na njia aliyosema ni sahihi, sio tu tuwekeze kama tunavyofanya kwenye Standard Gauge Railway tuwekeze kwenye umeme mkubwa ambao ndio msingi wa kujenga viwanda, tuwekeze kwenye skills za Taifa letu, lakini pia twende kwenye maeneo kama tourism ambayo itatupatia nguvu zaidi ya kuendelea mbele kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ambalo ningependa kulisemea kidogo ni baadhi ya maeneo ambayo aliyasema Mheshimiwa Silinde, nilidhani ametoka sasa namuona, kwanza tu nisisitize wazee wetu walitufundisha mtegemea cha nduguye anakufa fukara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni muhimu sana kama Taifa, na hapa huwa siendi kwenye siasa za vyama, very seriously kama Taifa tusipofika mahali tukasimama, tukajitegemea, tukaendelea kutegemea hawa wajomba wa enzi zile, hatutakwenda, hatutakwenda kabisa. Kwa hiyo, kwa hili ningeomba sana Waheshimiwa Wabunge, tuungane kuhakikisha kwamba hatua zote ambazo Serikali inachukua hivi sasa, ili tujitegemee, kweli tunashikamana ili twende mbele kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijui nisemeje, mimi ambaye nakwenda kuomba kwa niaba ya Taifa ninadhalilika mno, ninadhalilika mno, tumekaa na mradi wa Stiegler’s ili tupate umeme wa kutosha kwa muda mrefu mno. Lakini hivi sasa, wao ndio wanataka watufundishe darasa kwamba sisi ndio hatujui maana ya mradi ule, haiwezekani, haiwezekani hata kidogo, wala hatutakubali na wala hatutakubali,. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Silinde kupitia meza yako nataka tu nimkumbushe kwamba uandaaji wa takwimu za Pato la Taifa na ukuaji wake, unaenda kwa ngazi na inanishangaza kidogo kwa sababu Mtakwimu Mkuu wa Serikali alitoa mada kwa Kamati ya Bajeti namna ya kukokotoa takwimu za Pato la Taifa na mimi nilidhani si tulikuwa tumejitahidi kumuelewesha namna ambavyo tunafanya. Zipo zile za robo mwaka lakini, takwimu za robo mwaka zinakuwa zile ambazo baadhi ya vitu, havijapatikana sawasawa. Kwa hiyo, kwenye robo ya pili inayofuata unakuwa una takwimu nzuri zaidi, za robo iliyotangulia. Kwa hiyo, inawezekana kabisa kwamba takwimu ambazo tumetoa robo iiyotangulia tunapokuja robo ya pili, tukawa tumepata taarifa nzuri na kuzipitia zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sio kitu cha ajabu kabisa ukokotoaji wa pato Taifa, na kama utapenda tena turudie tuko tayari kurudie tukupeleke polepole polepole ili uweze kuelewa pato la Taifa linavyokokotolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ila alinishangaza kidogo kama mwanafunzi wangu wa uchumi aliposema kwamba kama mfumuko wa bei, unateremka kwa nini bei hazipandi, ilinishangaza kidogo, sijui labda nikirudia kwa lugha nyepesi, mfumuko wa bei, ni kama gari linalotembea unaweza ukaamua kutembea kwa speed 100, unaweza ukaamua kutembea kwa speed 40 kwa hiyo tunaposema mfumuko wa bei, umeteremka, hatusemi kwamba bei nazo zimeshuka, tunachosema ni kwamba kasi ya ongezeko la bei limepungua, ndio maana yake, sasa sijui nitalieleza kwa lugha ipi zaidi ili lieleweke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kidogo juu ya mchango wa Mheshimiwa Bashe, nafikiri saa nyingine anakuwa anatumia macho ambayo ni-bit pessimistic. Kwa sababu ni kweli, ukiziangalia zile takwimu, kwa nusu mwaka ambao tulikuwa tumetazama, export nyingi hasa zile za tradition zimepungua. Lakini sababu moja kubwa kwa mwaka huu ni kwa sababu ya tatizo la korosho tulilokuwa nalo na mimi naamini kabisa kwamba tutapata matokeo chanya baada ya muda si mrefu, kutokana na hatua ambazo zinaenda kuchukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini namshangaa pia kwamba baadhi ya mauzo yetu nje kuna component zinaongezeka upande wa bidhaa za viwandani ni wazi kabisa zimeongezeka. Lakini pia baadhi ya bidhaa ambazo sizo za mauzo yetu ya asili nazo zimeongezeka, lakini la msingi ambalo nilitaka kusisitiza hapa, tumefanya mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa biashara nchini ili kuirejesha nchi kwenye misingi halali na ya haki ya kufanya biashara. Sasa ni lazim utarajie kwa sababu biashara ni cyclical biashara sio kwamba kila saa, basi wewe utakwenda tu biashara mauzo yanaongezeka hayapungui hata kidogo, haiwezekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo pamoja na kuwa tunaendelea kulitazama, niliiambia Kamati ya Bajeti kwamba tayari tumeunda timu pale Wizarani ili tuangalie mwenendo wa mauzo yetu nje kwa kipindi kirefu zaidi ili pale ambapo kama kuna structural problems tuweze kuzishughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulitolewa ushauri kwamba Kariakoo ilikuwa ndicho kituo kikubwa cha biashara na hususan tumeshauriwa tutazame sana soko la Congo na Zambia. Ni kweli kabisa na pengine labda hoja iwe kwamba tuongeze kasi katika kulitazama. Lakini kwa mfano dhamira ya Serikali ya kujenga Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Songwe maana yake ilikuwa ni hiyo, kwamba tuweze kupata wasafiri kutoka Congo, Zambia, Malawi na nchi nyingine zinazozunguka mpaka Zimbabwe, kwa hiyo sio kwamba tumefumbia macho soko hili hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jitihada ambazo zinafanyika kujenga Bandari ya Karema zinaelekea huko huko, lakini pia hata hatua ambazo tumefanya kujaribu kuimarisha management ya TAZARA, lakini pia TRA na bandari wamekuwa wanafanya ziara Congo na Zambia ili kuweza kuhakikisha kwamba tunashughulikia zile changamoto ambazo wafanyabiashara kutoka nchi hizo wanakumbana nazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Bashe pia nadhani nilimsikia akisema ni muhimu kwamba hatua zetu za kibajeti zijielekeze pia kwenye uzalishaji. Nakubaliana naye na nafikiri ndiyo sababu tumekuwa tunaelekeza zaidi fedha kwenye miundombinu ambayo itatuwezesha kuchangamsha uchumi wa Taifa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Lakini hata kwa upande wa mabadiliko ya Sheria za Kodi ni wazi kabisa kwamba kupitia bajeti iliyopita, ndiko tulipojielekeza huko kuhakikisha kwa mfano kwamba tunapunguza kodi ya mapato (income tax) kwa ajili ya viwanda vipya mfano upande wa ngozi, lakini pia kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye baadhi ya viwanda ambavyo vinazalisha kwa kutumia raw materials za hapa ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nizungumzie suala la fedha kidogo ambazo zimepelekwa kwa ajili ya maendeleo ya viwanda. Nisisitize tu kwamba utoaji wa fedha unategemea sana upatikanaji wa mapato. Kwa kifupi revenue effort yetu kwakweli bado haitoshi kubeba mzigo mkubwa wa mahitaji yetu kitaifa. Tumefanya vizuri, nilieleza upande wa domestic revenue lakini tumepata changamoto upande wa misaada na mikopo katika nusu ya kwanza lakini tunaendelea kulifanyia kazi na prospects, matumaini yetu ni makubwa katika nusu ya pili ya mwaka iliyobaki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili nisisitize kuwa fedha hizi zilizotolewa si kwa ajili ya kujenga viwanda. Fedha hizi ni kuiwezesha Wizara kufanya facilitation, ni kuiwezesha Wizara kuweza kuielekeza sekta binafsi wapi wawekeze. Kwa hiyo, hizi sio fedha kwa ajili hiyo, msimtegemee kwa kweli Waziri kujenga viwanda na Mheshimiwa Ridhiwani amelieleza vizuri lakini pia Mheshimiwa Mary Nagu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa kweli miezi saba ni kipindi kifupi sana kuweza kufanya evaluation kwamba Serikali imepiga hatua kujenga viwanda. Utaratibu wa kujenga viwanda hii ni long term na tujielekeze zaidi kwamba sekta binafsi katika kipindi hiki imejenga viwanda gani na Serikali ime-facilitate kiasi gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba kwa kweli Serikali imejitahidi kufanya vitu ambavyo ni msingi wa viwanda, kwa hiyo, mnapo evaluate kwamba Serikali imefanya nini kujenga viwanda muangalie effort ya Serikali upande wa umeme, upande wa miundombinu mingine ya maji na usafirishaji, lakini pia jitihada mbalimbali ambazo zimefanyika katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani ya nchi. Ningeweza kulieleza kwa kirefu lakini niishie hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu madeni ya mifuko. Niseme tu kwamba ilikuwa muhimu kwanza Serikali ifanye uhakiki wa yale madai ya kwanza yaliyowasilishwa; na kwa kweli hali ilikuwa si nzuri hata kidogo. Yale madai yaliyowasilishwa tuligundua kwamba kulikuwa na sehemu kubwa ambayo si madai halali na hasa kwa upande wa miradi ya ujenzi ambayo ilitumia fedha hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaangalia sasa upya ule mkakati wetu wa kulipa yale madeni, ikiwa ni pamoja na issuance ya ile special cash bond ya shilingi bilioni 290 na tunatarajia kwamba hizi taratibu zitakamilika hivi karibuni ikiwa ni pamoja na jitihada za kupata fedha pia mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kutusaidia kulipa madeni hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kukosekana Bodi ya Wakurugenzi wa Mashirika na hasa ilisemwa TANAPA, naomba niliambie Bunge lako Tukufu kwamba Serikali tumefanya jitihada na tumeshakamilisha uteuzi wa bodi za taasisi mbalimbali ikiwemo hii ya TANAPA na Bodi hii ya TANAPA inaongozwa na Bwana George Waitara. Kwa hiyo, tumefanya jitihada mbalimbali katika kukamilisha shughuli hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme lingine pia ni kuhusu bajeti ndogo ya ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, ni kweli fedha hizi ni kidogo, na niseme tu kwamba si ofisi peke yake ambayo haijapatiwa fedha, tatizo kama nilivyosema ni sungura mdogo. Sasa hivi tunakamilisha mapitio ya utekelezaji ya nusu mwaka na kwa hakika tutalitazama hili kwa kuzingatia unyeti wa sekta ya mazingira na athari ambazo zinaonekana wazi. Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba kwa kweli mahitaji yetu ni makubwa, tunahitaji sana kujiwekea vipaumbele vya dhati ndani ya sekta na kwa Taifa letu kwa ujumla ili kuweza kuelekeza…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Vizuri sana Mheshimiwa Waziri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu na timu yake kwa hotuba nzuri sana na niseme toka mwanzo kabisa kwamba naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zimetolewa hoja nyingi ambazo ningependa na mimi nichangie baadhi yake. Moja, ilitolewa hoja kwamba kuna mkanganyiko wa takwimu ambapo kwenye hotuba ya bajeti ya mwaka jana ilionesha mapato na matumizi shilingi trilioni 29.5, lakini vitabu vya mapato na matumizi vinaonesha namba nyingine. Niwashauri tu Waheshimiwa Wabunge ni vizuri wakaelewa takwimu hizi maana yake nini.
Mapato yaliyopo kwenye Volume (I) ni mapato ya kodi, yasiyo ya kodi, misaada na mikopo nafuu. Sasa ukichukua matumizi ukatoa mapato kama yalivyo katika Volume (I), ile tofauti ni nakisi ya bajeti. Kwa hiyo, nadhani ni uelewa tu wa kusoma na kuelewa tafsiri ya hizi namba ni nini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine lililosemwa ilikuwa ni kuhusiana na uwiano kati ya ukuaji wa uchumi na madai kwamba hali halisi ya wananchi hailingani na ukuaji wa uchumi. Niseme tu kwamba, kwanza, uchumi wa Tanzania hakuna ubishi kwamba unakua, namba hazidanganyi.
Ukiangalia World Economic Data Base, takwimu za IMF, takwimu za National Bureau of Statistics zote ziko wazi. Katika Afrika, Tanzania ni moja ya nchi, the top five ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana tu Benki ya Dunia wametoa taarifa yao pale Dar es Salaam na inaeleza wazi kabisa katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo namba moja na hata katika Nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu ambazo uchumi wake unakua kwa kasi. Kwa hiyo, hili halina ubishi, tuachane kabisa kubishana na hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu uwiano na hali halisi ni kweli bado ile quality of growth haijafikia pale ambapo wote tunatamani na sababu ziko wazi. Sababu ya msingi ni performance ya sekta ya kilimo ambayo ndiyo inaajiri watu wetu wengi imekua kwa asilimia ndogo sana na wote tunajua, sababu yake kilimo chetu bado kinategemea mvua lakini pia uwekezaji katika sekta ya kilimo ni mdogo sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunajua pia kwamba hali ya maisha ya Watanzania haiwezi kuja mara moja. Ni wazi kabisa kuwa tumeanza kuona mabadiliko katika maisha ya Watanzania. Sababu yake moja ni kwamba baadhi ya sekta ambazo nazo zinaajiri watu wengi nazo zimeanza kukua kwa kasi. Kwa mfano, uzalishaji viwandani sasa unakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 6.3 kwa mwaka lakini biashara pia asilimia 6.5 kwa mwaka, usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 17 na hizi sekta zinaajiri wananchi wetu wengi, ndiko wanakopatia kipato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mkazo wa Serikali uko wazi. Katika mpango wa miaka mitano, tumesema tunataka kujenga uchumi wa viwanda ambao unatumia malighafi ambazo zinazalishwa hapa hapa nchini. Tukiweka jitihada kwenye agro-processing na agri-business, tukaweka jitihada kwenye elimu na ujuzi kama ilivyo katika mipango yetu, haya ndiyo yatakayofanya ukuaji wa uchumi sasa uweze kuleta matokeo yale ambayo tunatarajia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni ukweli pia, vigezo vingine vya hali ya maisha ya wananchi vinaonekana wazi kabisa vimeboreka. Hali ya nyumba imekuwa bora zaidi, hali ya afya, upatikanaji wa umeme, tumepeleka umeme vijijini, yote haya siyo vitu vya kubishia na vinaongeza ubora wa maisha vijijini. Namshangaa sana Mheshimiwa Mbowe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hivi kweli haya hata kule Hai hayaoni? Mimi naona kama yako wazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kulikuwa na hoja kwamba Serikali haina mkakati wa kuinua uchumi vijijini, hii siyo kweli hata kidogo. Someni Mpango wa Miaka Mitano Waheshimiwa Wabunge uko wazi. Tumesema tutaimarisha kilimo cha umwagiliaji, tutaongeza thamani ya mazao na
mifugo, tutainua kilimo cha kisasa, tunapeleka umeme vijijni kama nilivyosema, tunaelekeza fedha kwenye utafiti na mafunzo, tunajenga barabara ili mazao ya wakulima na mifugo yaweze kufika kwenye masoko, hii yote ni mikakati ya kuinua uchumi wa vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na tahadhari kwamba IMF mwezi Januari walisema uchumi unaweza kuporomoka kutokana na kubana matumizi kupitiliza.
Kwanza niseme tu kwamba, matumizi ambayo Serikali inabana ni yale ambayo siyo ya lazima siyo kila matumizi. Serikali imekuwa inajitahidi kuhakikisha kwamba uchumi unaendelea kukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza hii ripoti ya Januari ni kweli ilitoa hiyo caution lakini Mheshimiwa Mbowe pia namshangaa maana ripoti hiyo hiyo ya Januari iliweka wazi kabisa, iliipongeza Tanzania kwa kuchukua hatua kusimamia sekta ya fedha vizuri, kudhibiti mfumuko
wa bei na kusimamia matumizi. Haya yenyewe hayaoni ila caution yenyewe ndiyo anaiona peke yake, kitu cha kushangaza kidogo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunatambua changamoto za kupungua ukwasi katika uchumi wa Taifa letu na tumeanza kuchukua hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza tuliyochukua ni kuendelea kulipa madeni baada ya kuyahakiki. Tumelipa shilingi bilioni 631 mpaka mwezi Machi
kwa ajili ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri, tumelipa shilingi bilioni 67.5 kwa ajili ya watumishi, shilingi bilioni 78.8 kwa ajili ya wazabuni, shilingi bilioni 17.8 kwa ajili ya watoa huduma. Hii yote ni njia mojawapo ya kuongeza tena ukwasi katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni, Benki Kuu imechukua hatua mbili muhimu. Kwanza, imepunguza discount rate kutoka asilimia 16 mpaka asilimia 12, lakini imepunguza pia statutory minimum reserve requirement kutoka asilimia 10 mpaka asilimia nane. Mheshimiwa Dkt.
Chegeni alijaribu kulieleza jana au juzi nafikiri na hatua hizi zinalenga kuongeza uwezo wa commercial banks kukopesha sekta binafsi na hivyo kuongeza ukwasi katika uchumi. Pia tunajitahidi kuongeza nguvu sasa kupata fedha za wahisani na mikopo ya kibiashara kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na hizi zote ni kwa ajili ya kuinua ukwasi katika Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, zimekuwepo hoja kuhusu milioni 50 za kila kijiji. Serikali imefanya tathmini na tumeandaa utaratibu wa kupeleka fedha hizo vijijini. Tumefanya hivi ili tuhakikishe kwamba haturudii makosa yale yale yaliyoambatana na Mfuko wa JK. Imeonekana kulikuwa na
matatizo mengi, kuna vikundi ambavyo vililengwa lakini havikusajiliwa, fedha hazifiki kwa walengwa, hakuna elimu ya ujasiriamali, hakuna hata sheria yenyewe ya microfinance na kanuni zake lakini hata mfumo wenyewe wa ufuatiliaji ni dhaifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, inabidi kwanza kurekebisha haya isije ikaonekana ni kama vilevile kwamba hizi fedha zinatolewa ni kama zawadi. Kwa hiyo, muhimu sana hili lifanyike na hatua tuliyofika sasa umeandaliwa Waraka wa Baraza la Mawaziri ili Serikali iweze kufanya
maamuzi rasmi kabla ya kuzipeleka hizo fedha vijijini. Kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha, tumetenga shilingi bilioni 60, ziko Fungu la 21, Subvote 2001 ni mradi namba 4903 unaitwa village empowerment.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba nitumie fursa hiii kukushukuru kwa kunipa nafasi, lakini pia nawapongeza sana Wenyeviti wawili wote wa Kamati kwa hoja nzuri sana ambazo wamezifanyia kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba nichangie baadhi ya hoja ambazo zimejitokeza humu ndani. Kwanza, kulikuwa na suala la Bajeti ya Fungu Na. 7 - Msajili wa Hazina kwamba ni kidogo, wamepata asilimia 16, hivyo wawezeshwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka huu peke yake ambao tunaendelea kutekeleza, mpaka mwezi Desemba kwa upande wa kuwawezesha Ofisi ya Msajili wa Hazina ili waweze kufanya kazi yao ya kufuatilia hizi Taasisi za Umma, walishapewa asilimi 92 ya OC. Nafikiri tatizo linalojitokeza ni kwa sababu kuna baadhi ya vipengele na hususan fedha kwa ajili ya mitaji ya Mashirika ya Umma, lakini pia fedha kwa ajili ya kulipia madeni ya mashirika, hizi kwa kawaida huwa tunaziweka kwenye kasma ya dharura na haionekani kule kwenye Fungu Na. 7 moja kwa moja. Ni pale tu ambapo zinahitajika ndiyo tunazitoa na zinalipwa kutoka kwenye Fungu lile la dharura.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri ni kwamba tunaenda sasa kuanza mchakato wa bajeti, nafikiri kama ni macho ya ziada kwa ajili ya changamoto zile nyingine ambazo zilisemwa juu ya Ofisi hii muhimu sana, ni kipindi chake cha kuangaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusu kampuni za simu kujiorodhesha kwenye soko letu la hisa la Dar es Salaam. Ilitolewa hoja kwamba mpaka sasa ni Vodacom peke yake ambayo imeorodheshwa wakati tulishakubaliana na sheria inataka mashirika yote ya simu yajiorodheshe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda tu niliarifu Bunge lako kwamba tuko katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa sheria. Kwa mfano, tunatarajia kwamba tigo watawasilisha documents zile zinazohitajika kwa ajili ya kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa itakapofika mwezi ujao Februari, 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Halotel kama mnavyofahamu Waheshimiwa ni kwamba hii kule kwao ni kampuni ya jeshi. Kwa hiyo, panahitajika uamuzi wa wamiliki ili kuihamisha sasa ile kampuni kuwa public company ndiyo iweze kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam. Kwa hiyo, hilo linafanyika hivi sasa, tunatarajia kwamba hatua itafikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Airtel, imechelewa kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa kwa sababu kama mnavyokumbuka tulikuwa na ule mzozo wa umiliki wa hisa na sasa baada ya kutatuliwa lile, ndiyo tutaanza sasa mchakato wa kwenda sokoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kuiwezesha TTCL kifedha, ni kweli kabisa shirika letu hili ni muhimu, tunahitaji kuboresha miundombinu yake. Utaratibu wa kwenda kununua nguzo za mitumba, hili hapana, haliruhusiwi na sheria ambayo ilitungwa na hili Bunge. Kwa aina ya teknolojia, aina ya kazi ambayo inafanywa na shirika letu hili ni muhimu sana tukahakikisha kwamba ile infrastructure inakuwa ni ya kisasa kabisa kutupeleka kwenye uchumi wa kidigitali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tumeanza kuchukua hatua, mwezi Desemba Serikali ilitoa ridhaa kwa TTCL ambapo tuliwaruhusu waweze kukopa dola milioni 15 ambazo ni kama shilingi bilioni 34.2 hivi waweze kukopa kutoka kwenye benki za ndani kwa ajili ya kuweza kupanua miundombinu ya taasisi hii na kadri mahitaji yatakavyojitokeza, basi Serikali itayatazama kwa jicho hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala la marekebisho ya VAT tena kwamba yaje kwa hati ya dharura, particularly ili Serikali isidai kodi ya ongezeko la thamani kwenye miradi kama ile ya Halmashauri inayogharamiwa na fedha za Benki ya Dunia. Niseme tu tunalifanyia kazi, kwa hiyo Bunge litaarifiwa hapo baadaye, maamuzi ya Serikali kuhusu jambo hili ni nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa pia na mapendekezo ambayo yalishawahi kutolewa. Bunge hili huko nyuma liliwahi kueleza kwamba ni muhimu tunapofanya mabadiliko ya sheria zile zinazohusu ushirikiano kule Afrika Mashariki yapite kwenye Kamati ya Bajeti. Nafikiri nilishawahi kuliambia hili Bunge Tukufu kwamba sioni tatizo la kimsingi kutekeleza hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto moja iliyopo ni ya muda. Kwa mfano, mwaka uliopita mchakato wa kuchakata yale mapendekezo ambayo tulikuwa tumeyapata kutoka kwa wadau, yalipopita kwenye task force on tax reforms na baadaye kwenye think tank, siku ile ya mwisho tunafanya kikao ndiyo siku pia Kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilikuwa kinaanza. Kwa hiyo, inakuwa ni timing disconnect kwamba tunafanyaje ili huu mchakato uwe umekamilika ili tuweze kuupitisha kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna changamoto ya pili kwamba Serikali kwa ujumla wake hata Waheshimiwa Mawaziri wenzangu wanakuwa hawajaona hayo mapendekezo. Kwa hiyo, inakuwa ni vigumu kuyaleta kwenye Kamati kabla Serikali haijaji-pronounce.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilitaarifu tena Bunge lako Tukufu kwamba tunapoleta yale mapendekezo kupitia Finance Bill, bado Bunge linayo nafasi ya kushauri juu ya yale ambayo tulikubaliana kule Afrika Mashariki. Kama Bunge au Mamlaka nyingine za Serikali haziridhiki na kile ambacho tulikubaliana kule, sisi tunachofanya ni kwamba huwa tunaandika barua kwa Sekretarieti ya Afrika Mashariki, tunasitisha utekelezaji wa hicho ambacho kilipeleka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia niseme kulikuwa na hoja kwamba uchumi wetu uko vizuri lakini siyo kwa mtu mmoja mmoja. Nirudie tena kusisitiza kwamba mwenendo wa vigezo kuhusu viashiria vya uchumi jumla, tunakwenda vizuri sana. Yaani katika Afrika ni ukweli kabisa tunazidiwa na ncjhi chache sana, lakini ukuaji wa uchumi wa asilimia 6.9 ni ukuaji wa kasi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hili la mmoja mmoja naomba tu nisisitize tu vitu vitatu hivi. Kwanza, ongezeko la ukuaji wa uchumi huwa linaongezeka kwanza kwenye mchango wa kila Sekta kwenye Pato la Taifa na unaona kabisa kwamba baadhi ya Sekta mchango wake kila mwaka unaongezeka, unakua kwa kasi. La muhimu kuzingatia ni kwamba wanaonufaika na ule ukuaji ni wale wanaoshiriki kwenye zile sekta ambazo zinakua haraka. Ndiyo maana msisitizo umekuwa ni kwamba ni lazima Watanzania tufanye kazi. Hilo ni la msingi sana kwa sababu vinginevyo huwezi kufaidika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, wananchi wanafaidika na ukuaji wa uchumi kupitia kwenye huduma za jamii zinazotolewa na Serikali. Kwa hiyo, ndiyo maana tunapoboresha elimu, afya, barabara na kadhalika, ndiyo njia ya pili ya kuwafaidisha wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi. Mwananchi mmoja mmoja, lakini pia Taifa kwa ujumla. Kwa hiyo, ni muhimu sana kufanya uchambuzi vizuri kwamba hiki kinachosema mtu mmoja mmoja haonekani kufaidika ni nini hasa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kuwezesha Sekta ya Kilimo kama tulivyofanya kwenye Sekta ya Madini, nafikiri hoja inaweza kuwa ni ya kutafakari vizuri. Kwa sababu kilicho kikubwa kwa Serikali, kwanza kwa upande wa kilimo ni lazima tuhakikishe kwamba Sera zetu za Kilimo ni nzuri na hususan kwa sababu kilimo ni private sector activity. Kwa hiyo, lazima tuhakikishe kwamba sera zile ni nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la muhimu tujielekeze sasa kwenye miundombinu ambayo inawezesha kilimo na ndiyo hilo ambalo Serikali imekuwa inafanya tena kwa kasi. Miundombinu ya usafirishaji, maghala, umeme na irrigation, hapo ndiyo tutaweza kunyanyua kilimo. Lazima pia tujielekeze kuboresha huduma za fedha kwa wakulima, lazima tujielekeze kwenye huduma za ugani na utafiti kwenye kilimo. Huo ndiyo mwelekeo wa Serikali. Ukisoma ASDP II, huko hasa ndiyo tunapolenga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia lazima tujielekeze kwenye inputs muhimu; mbolea, dawa na mbegu bora. Huo ndiyo mwelekeo na msukumo wa Serikali katika kuboresha na kukiwezesha kilimo. Nafikiri hiyo ndiyo njia sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja nyingine, nafikiri ni tahadhari muhimu juu ya mwenendo wa mfumuko wa bei. Ni kweli mwenendo wa mfumuko wa bei kwa nchi yetu hivi sasa ni mzuri kabisa, isipokuwa tunaziona hizi changamoto zinazooneshwa kwa upande wa chakula na vile vile upande wa nishati. Hili nalo ni muhimu na hasa ukizingatia wakubwa hao ambao wanatunishiana misuli, kwa hiyo, inaelekea kuleta shida kwenye bei ya mafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunachukua tahadhari kama Serikali kwa maana ya kusisitiza nishati mbadala, lakini pia kuhakikisha kwamba tuna akiba ya kutosha ya chakula. Hilo ni muhimu sana ili tuhakikishe kwamba mfumuko wa bei unaendelea kubakia kwenye kiwango ambacho hakiharibu mwenendo wa uchumi wetu kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ilitolewa pia hoja kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inahangaika na maafa haikuwekewa fedha yoyote kwenye bajeti. Naomba tu nikitaarifu kikao chako kwamba kwa kawaida constitution ya nchi yetu inataka asilimia moja ya bajeti yote ya Serikali itengwe kama contingency. Kwa hiyo, endapo itatokea dharura, hatutasita kutumia contingency fund kwa ajili ya kukabiliana na maafa kama yatajitokeza, lakini Mwenyezi Mungu anatupenda, naamini atatuepusha na madhara japo yameanza kutokea kwa wananchi kwa mfano kule Lindi na unaona Serikali ya Mkoa tayari imeingia kazini na pia Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri naomba umalizie maana nimekupa mrefu.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa kumalizia jambo la mwisho tu, kwa upande wa kodi ya majengo, tunapokea ushauri, tutaufanyia kazi kwamba kodi ya majengo pengine ilipiwe kupitia ankara za umeme na maji. Kuna tahadhari pia, kwa sababu siyo ankara zote za umeme ni za matumizi ya nyumba, hilo lazima lifahamike. Vile vile, hata ankara za maji, nyumba nyingi hazina ankara za maji. Kwa hiyo, tuna changamoto kubwa. Ni jambo la kuchakata vizuri tuone kama linaweza likatupa mileage. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nami naomba nianze kwa kweli kwa kuwapongeza Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati hizi sababu wamegusa maeneo muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu na hususani wote kwa pamoja ni lazima tupambane na ubadhirifu dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Serikali Kuu pia katika Serikali za Mitaa. Wamefanya kazi nzuri sana wanastahili pongezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maeneo ambayo ningependa nitoe ufafanuzi kidogo

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na suala la Benki ya Azania, ni kweli Benki ya Azania pale tuna tatizo na tatizo lenyewe ni la kisheria. Benki hii ilisajiliwa kwa Sheria ya Makampuni Sura 212. Kwa hiyo, kwa usajili huo inakuwa ni kampuni binafsi na CAG hawezi kui-audit hata kama inamilikiwa kwa takribani asilimia 92 ya hisa zinashikiwa na mifuko yetu. Kwa hiyo, huo ndiyo utata ulipo ingawa benki hii imekuwa inakaguliwa pia na makampuni ambayo CAG kwa nyakati tofauti anayatumia pia kukagua taasisi mbalimbali kwa niaba yake na wanawasilisha taarifa kwake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamewahi kukaguliwa KPMG, PWC na hivi sasa wanakaguliwa na Ernst and Young. Kwa hiyo, jambo kubwa hapa ninachofikiri ni kwamba CAG wakati utata huu wa kisheria unafanyiwa kazi ni vema angeanza kuzitazama hizi audit report ambazo zinakaguliwa na Ernst and Young.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Pride sijui naweza nikalisema kiasi gani, kwa kifupi ni kwamba hili shauri limepelekwa Mahakamani, liko Mahakama ya biashara na limepangiwa kusikilizwa mwezi Machi tarehe za mwanzoni. Mengine yanayosemwa pengine ni magumu hayapendezi sana labda niyaache kwa sababu ni shauri ambalo liko Mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kulisemea ni kuhusu fedha za maendeleo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Fedha hizi tumejitahidi kutoa kulingana na makusanyo ambayo yamepatikana katika kipindi cha miezi sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa fedha za ndani mpaka kufikia mwezi Desemba tulikuwa tumetoa shilingi bilioni 165.96 ikilinganishwa na lengo la miezi sita la kutoa bilioni 264.8. Maana yake kwa nchi nzima tayari tumekwisha kutoa takribani asilimia 63 ya lengo la nusu mwaka.

Kwa upande wa fedha za nje tulitoa bilioni 205.93 ukilinganisha na lengo la bilioni 174.5, hiyo ni asilimia 118 ya lengo. Nadhani ni vizuri hizi takwimu zikafahamika Mzee wangu Mheshimiwa Lubeleje nikitoa mfano wa Mpwapwa fedha za ndani, Mpwapwa DC walipatiwa shilingi milioni 884.1 wakati lengo ilikuwa ni bilioni 1.48 hii ni asilimia 60. Fedha za nje walipatiwa milioni 606.2 wakati lengo lilikuwa ni milioni 469 hii ni asilimia 129, naweza nikaendelea kutoa mifano mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano OC ya Babati tumetoa milioni 394 kati ya lengo la milioni 465.9 hii ni asilimia 85 kwa Babati TC. Kwa upande wa DC tumetoa mlioni 808 wakati lengo lilikuwa ni milioni 901.9, na hii ni asilimia 90 kwa ajili ya Babati DC kwa OC. Kwa hiyo siyo kweli kwamba hatujatoa fedha, tumetoa fedha. Fedha zinakwenda lakini kwa quarter ya kwanza nakiri kuna tatizo la upatikanaji wa fedha na hapo ndiyo kuna slow down lakini sasa zimeanza kufika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja imesema kwamba CAG hapewi fedha; nadhani ni vizuri tuwe tunajiridhisha na takwimu. Kwa upande wa OC Vote 45 kwa miezi sita tumempatia bilioni 17.8 kati ya lengo la bilioni 22.2, kwa hiyo kwa miezi sita amepatiwa asilimia 80 ya lengo. Upande wa development ni kweli tumechelewa lakini fedha za nje tayari amepatiwa asilimia 41 ya lengo la development katika kipindi hicho. Kwa hiyo ni vizuri nadhani tuwe tunaziangalia hizi namba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Heche alini- challenge na mimi ngoja nim-challenge kidogo. Kwa miezi sita upande wa property tax tumekusanya shilingi bilioni 16.6. Sasa makusanyo ya TRA peke yake kwa mwezi mmoja ni wastani wa trilioni 1.2 kwa hiyo hesabu iko wazi kabisa siyo kwamba hiki chanzo ndicho the major source ya mapato ya Serikali hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kodi ya majengo, sisi tunaongozwa na kifungu cha 65(b) cha Sheria ya Fedha ambayo Bunge hili lilitunga mwaka jana na kinaelekeza kwamba fedha hizi zikusanywe na TRA moja na kuhifadhiwa kwenye Mfuko Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili ni kwamba mgawanyo wa utoaji wa fedha uendane na bajeti ya Halmashauri husika. Na takwimu nilizoanza kuzitoa kwa maana ya fedha ambazo tumepeleka kwenye Halmashauri zinafuata utaratibu huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme pia kuhusu utendaji wa Benki ya Kilimo Tanzania. Ni kweli hili lina matatizo na Serikali imeliona na imeanza kulifanyia kazi. Tayari tumekwisha kutafuta management mpya kwa utaratibu wa search na tayari wamefanyiwa interview na kwa hiyo, baada ya muda mfupi kwanza tunabadilisha management. Na kwa upande wa mtaji ni kweli mwaka 2014 ndipo Serikali ilitoa shilingi bilioni 60 kama mtaji, lakini baada ya hapo tulitoa shilingi bilioni 206 ambazo ulikuwa ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika. Kwa hiyo, suala la mtaji kwa ajili ya Benki yetu hiyo ambayo ni muhimu…

T A A R I F A . . .

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hayo mengine asubiri kesho, Serikali inatoa fedha kuendana na bajeti. Kama Bunge hili lilipitisha kiasi fulani kwa ajili ya Ofisi ya CAG ndizo hizo tunafanyakazi tukishakusanya tutampa hizo na siyo zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naeleza juu ya TADB (Benki ya Kilimo) kwa hiyo mbali ya zile bilioni 60 ambazo tulitoa mwaka 2014, tulitoa pia bilioni mia mbili na sita ambazo tulipata mkopo nafuu kutoka African Development Bank. Baada ya kuimarisha utendaji katika Benki hii hapo ndiyo tutaendela kushughulikia suala hili la mtaji maana hatutaki pia tuendelee kupeleka mtaji ukazame kama kwenye shimo na kupoteza fedha za umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nitapenda kulisema ni fedha ambazo TRA inakusanya kwa ajili ya taasisi mbalimbali. Tunakusanya fedha kwa mfano, wharfage kwa ajili ya TPA lakini pia ziko fedha kwa ajili ya REA, Road Fund, maji; hizi kwa ujumla hazina matatizo. Hazina matatizo kwa sababu marejesho yake yako kwenye bajeti ya matumizi (Appropriation Bill), na hizi zinatolewa kuendana na utaratibu wetu wa mgao wa kila mwezi. Shida inapoonekana sanasana ni kwenye maeneo mawili; kuna bed night levy kwenye utalii na cashewnut levy kwa upande wa korosho asilimia 35. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa fedha zote hizi zinaingizwa kwenye mfuko mkuu wa hazina. Sisi tunachosisitiza ni kwamba ni muhimu sana tujiridhishe na matumizi ya fedha hizi. Fedha hizi mnajua, mifano ni mingi boards zilizokuwa zinakaa nje ya nchi mnafahamu, Kamati ya PAC imetoa mfano wa fedha za ALAT ambazo zimekuwa misused.

Kwa hiyo, ni muhimu sana kwamba fedha hizi zionekane kwenye bajeti ya matumizi na kwahiyo ziombewe na kugawiwa kama utaratibu mwingine unavyofanya. Kwa hiyo hili nadhani shida iko hapa lakini tumelimaliza kwa uoande wa korosho tayari Serikali imeshawapatia shilingi bilioni 10 na kwahioyo pale watakapoleta matumizi mengine yakachambuliwa watapewa fedha wka utaratibu wa kawaida maana wameshaingizwa kwenye mfumo rasmi wa matumizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Na mimi nianze kwa kuwapongeza Mheshimiwa Waziri wa Maji, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu yote ya wataalam kwa kazi nzuri wanayoendelea kulifanyia Taifa hili. Nianze kwa kusema naunga mkono hoja. Napenda kuchangia kwa kujibu hoja chache, moja ikiwa ni ile ambayo ilikuwa ina sema ziko wapi fedha za India, ule opo nafuu wa dola milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika miji 17.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha hizi zilichelewa kupatikana kwa kuwa Serikali ya India iliendelea kusisitiza kwamba matumizi ya fedha hizi lazima zisamehewe kodi zote, za aina zote wala tozo zinazohusika. Na sisi kwa upande wetu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania tulisisitiza kwamba kodi stahiki zilipwe kwa mujibu wa sheria na hususan Kodi ya Mapato. Mtakumbuka mwezi Septemba, 2017 Bunge hili lilifanya marekebisho ya Sheria ya VAT ambapo lilimpa mamlaka Waziri wa Fedha kusamehe VAT kwa miradi ambayo inagharamiwa kwa mikopo nafuu na ile ambayo inagharamiwa na wafadhiri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hili tukalimaliza, nilishauriwa ipasavyo na nikasamehe VAT, lakini zikabaki kodi za mapato, kwa mujibu ya Sheria ya Mapato iliyofanyiwa marekebisho mwaka jana ninaweza tu kusamehe pale tu ambapo nitakuwa nimepata ridhaa ya Baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tumefanya hivi na tarehe 15 Aprili Serikali iliridhia kusamehe kodi za mapato. Kwa kifupi kuna withholding tax on interest kwa Exim Bank kwa kiwango cha asilimia 10 ambazo ni takribani shilingi bilioni 24.9. Pia kulikuwa na kodi ya mapato kwa makampuni na wafanyakazi. Kodi ya Mapato peke yake ni takribani dola milioni 30 na kwa wafanyakazi dola milioni 15. Lakini pia kulikuwa na withholding tax on commitment fees kwa Exim Bank ambazo imebidi tusamehe, takriban dola 375,000 na tano elfu. Pia zipo kodi zingine SDL na ushuru wa forodha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema tarehe 15 Aprili Serikali iliridhia kusamehe pia hizi kodi za mapato, na naomba kulialifu Bunge lako tukufu saa 11 na dakika 27 nimeletewa taarifa na naomba niisome inasema hivi; “Kindly Lebam formed that we have successfully concluded the negations with Exim Bank of India, we will sign the agreement tomorrow morning In Shaa Allah.” (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni taarifa ambayo nimeletewa na kiongozi wa Government Negations Team ambayo iko India kwa ajili ya kumaliza zoezi hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa kulisemea kidogo ni lile ambalo limesemwa kwa hisia sana na lilishatolewa azimio na Bunge lako tukufu kwamba Serikali iongeze tozo ya mafuta kutoka shilingi 50 mpaka shilingi 100 kwa lita na hizo zilizokusanywa zipelekwe kutunisha mfuko wa maji na hususani miradi ya maji vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu niseme kwamba Serikali kupitia kikosi kazi cha maboresho ya kodi, inakamilisha uchambuzi wa faida na hasara ya utekelezaji wa agizo hili na tutalitolea taarifa kwa umma na kwa Bunge hili kupitia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali na uchambuzi ambao tunafanya unahusu mambo mengi.

Kwanza ni pamoja na faida za hatua inayopendekezwa. Lakini pia tunatazama risks zake na ukubwa wake kwa uchumi wa taifa na hili ni muhimu lakini pia kungalia madhara yake na hasa kwa Watu wanyonge wa nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo linafanyika katika uchambuzi huu ni kuangalia vyanzo vingine vya ku-finance maji. Kwa hiyo, ukiaccha huu mkopo wa india ambao nimeshausema, lakini tunaangalia pia mikopo mingine nafuu, na hususani mkopo wa dola milioni 300 ambao tunautaraji kutoka Benki ya Dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Na mimi nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Naibu wake, Mheshimiwa Engineer Manyanya; timu nzima ya uongozi wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisisitize kwamba viwanda ndiyo njia pekee ambayo ilifanya nchi zote ambazo tunaziita zimeendelea kuendelea. Kwa hiyo, hii ni njia sahihi, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na timu nzima kazaneni, mkaze buti, hii ndiyo njia sahihi ya kwenda kadri ya uongozi wa Serikali yetu inavyotaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia niseme mapema kabisa kwamba naunga mkono hoja na nitachangia kwa kutoa ufafanuzi wa mambo machache na mengine tutaendelea kuyafafanua kadri mjadala wa bajeti unavyoendelea mpaka huko mwishoni mwa mwezi Juni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ambalo napenda kulitolea maelezo, pamekuwepo hoja hapa kwamba watu wanateseka sana kwa fedha zao ambazo zimekwama kwenye iliyokuwa benki ya FBME ambayo tuliiweka chini ya ufilisi. Naomba tu niseme kwamba Serikali inawajali watu wake na imekuwa inalishughulikia jambo hili inavyopaswa na kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfilisi ambaye ni Deposit Insurance Board (DIB) imeendelea kulipa amana za wateja na tulianza hiyo kazi toka tarehe 1 Novemba, 2017. Mpaka kufikia tarehe 8 Mei zimeshalipwa shilingi bilioni 2.31 kwa kiwango kile cha juu ya shilingi milioni moja na nusu ambayo imefikia sasa takriban asilimia 53 kati ya shilingi bilioni 4.3 ambazo zilitarajiwa kuwa zimelipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, waliolipwa ni wenye amana takribani 3,203 ambayo ni asilimia 48.1 ya wateja wa iliyokuwa hiyo benki. Malipo yalibaki tutaendelea kuyalipa, hususani yale ambayo yanahusu amana yatafanyika baada ya kuwa tumefanya uhakiki wa mikopo mbalimbali ya wadaiwa na madeni ya hiyo benki. Kwa hiyo, hilo naomba niliachie hapa kwa sasa, nikisisitiza tu kwamba Serikali inawajali wananchi wake na itahakikisha kwamba haki yao inapatikana baada ya taratibu kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala la export levy ya ngozi. Sasa hili, ngozi ghafi ni muhimu sana. Ule uamuzi wa kuweka export levy ulikuwa ni wa makusudi. Ni lazima tulinde ajira, tuuze nje kile ambacho kimeongezewa thamani ndiyo wananchi wetu wataweza kufaidika. Tusipofanya hivyo, maana yake tunawapatia ajira huko ngozi zitakapokwenda. Kwa nini tufanye hivyo wakati tunalia na ajira ya vijana wetu?

Pia kulikuwa na hoja juu ya rai kwamba wafanyabiashara wetu wanapo-declare zile fedha kwenye mipaka, hali inakuwa ngumu kweli! It is very risk na wengine hata wanauawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali ilivyoshauriwa, tutaendelea kuliangalia hili jambo la namna ambavyo watu wetu wana-declare fedha walizonazo pale mpakani. Napenda kutumia nafasi hii kuvitaka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuimarisha usalama katika maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitumie fursa hii kuikumbusha Mamlaka ya Mapato/watumishi wetu wa Mamlaka ya Mapato ni marufuku kutoa siri za wananchi/ wateja wetu wanapo-declare fedha zile. Nitumie nafasi hii kumwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
kuandaa viapo vya watumishi wetu waliopo pale mipakani kuhakikisha kwamba atakayekiuka vile viapo, basi anapata habari yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nadhani ni muhimu niseme kwamba hatua hii ni muhimu kwa ajili ya kuzuia utakatishaji fedha, lakini hata ufadhili wa ugaidi. Kwa hiyo, hili jambo ni international practice na lazima na sisi tuendelee kufanya ili Taifa letu liendelee kuwa salama. Pia wananchi wenyewe husika ni muhimu wakachukua tahadhari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja ya Mamlaka ya Mapato kupuuza invoices za wateja na kuzikadiria upya. Kiini cha shida hii kwa kweli ni udanganyifu. Watu wanatoa value ya hizi invoices zisizo sahihi na ni kwa makusudi kwa sababu kama ingekuwa ni human error

unategemea kwamba basi invoice zilizozidishwa au zile zilizopunguzwa ziwiane, lakini daima sivyo, under invoicing ndiyo kubwa. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwamba wananchi nao wanaohusika, wote tunawataka watoe invoices ambazo ni sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja watumishi wetu wa TRA kudai rushwa. Hili napenda nitumie nafasi hii kulikemea kwa nguvu zote. Hili ni kosa kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano imejitabanaisha kwa kupambana na rushwa. Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge na wananchi ambao wanatusikiliza, watupatie taarifa pale ambapo pana mtumishi yeyote wa TRA ambaye anadai rushwa, nasi tutamtumbua, wala hatutanii. Tupatieni taarifa tutawafanyia kazi ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala pia kuhusu research and development. Ni kweli tunapokwenda kujenga uchumi wa viwanda, research and development ni jambo la msingi sana. Rai yangu ni kwamba Watanzania tushikamane, tuendelee kukusanya mapato zaidi na zaidi kadri inavyowezekana na kupanua wigo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Fedha na Mipango
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, napenda kwanza nitumie fursa hii kukushukuru sana wewe mwenyewe umeongoza kikao hiki toka asubuhi na umerudi mchana tunakushukuru sana, sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini, naomba pia nitambue michango ambayo imetolewa na Kamati ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake - Mheshimiwa George Boniface Simbachawene, Makamu Mwenyekiti - Mheshimiwa Mashimba Ndaki, Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza na kwa maandishi na bado tunaendelea kupokea hata maoni mengine nikiwa hapa mezani nimepokea maoni ya maandishi kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge wawili.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo jumla ya Wabunge 22 niliyo nao mpaka sasa wamechangia hii hoja na kati yao, waliochangia kwa maandishi sasa ni 11 na waliochangia pia kwa kuzungumza ni 11. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli nafurahi kwamba michango ni mizuri ambayo imetolewa na Waheshimiwa Wabunge wote na nitaeleza kwa muhtasari majibu ya hoja mbalimbali ambazo zimetolewa, ingawa sijui kama nitaweza kujibu hoja zote zilizosemwa kwa sababu ya muda, lakini naomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba majibu ya hoja zote zilizochangiwa tutaziwasilisha kwa maandishi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano huu wa Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na baadhi ya hoja ambazo zimechangiwa na Kamati ya Bajeti, moja lilikuwa ni lile la ukiukwaji wa taratibu katika kuanzisha tozo, ada na ushuru kwa baadhi ya Wizara na Mamlaka ya Serikali za Mitaa na ambazo zimeendelea kuleta kero kwa baadhi ya wananchi, lakini pia wafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, pana ukweli kiasi fulani na Wizara ya Fedha na ikijumuisha hivi karibuni tumeziandikia Wizara zote na mamlaka nyingine wahakikishe kwamba wanazingatia utaratibu uliobainishwa katika Sheria ya Bajeti. Pia kwa kawaida mwezi Desemba tunawaandikia wadau ndani na nje ya Serikali kuwasilisha mapendekezo ya tozo, ada na ushuru kabla hazijaanzishwa ili ziweze kuchambuliwa na tuweze pia kuziwianisha ili kuondoa migongano. Wizara inaitisha pia maoni ya wadau mbalimbali kuhusu hizo kodi ambazo zinapendekezwa kuanzishwa au kuzifuta ili kuondoa kero kwa wananchi. Kubwa hapa ni kwamba ndugu zangu wote Serikalini wazingatie huu utaratibu ambao ni wa kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilibaini baadhi ya taasisi ambazo zinapokea mishahara kutoka Serikali Kuu, lakini bado zinatumia utaratibu wa retention. Ushauri wa Kamati umepokelewa na kwa mujibu wa sheria zilizoanzisha hizi taasisi, Bodi za taasisi hizo zimepewa mamlaka ya kuidhinisha bajeti husika katika ngazi ya awali. Vilevile Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 na hususan kifungu kile cha 17 na kifungu cha 22 vimetoa mamlaka kwa Msajili wa Hazina na Katibu Mkuu Hazina kupitia na kuidhinisha bajeti za taasisi na mashirika hayo ambayo tumeyaona. Tutalitazama tunavyokwenda mbele tuone namna ya kuondoa upungufu huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilitupongeza tunawashukuru sana kwa jitihada ambazo tunaendelea kuhakiki na kulipa madeni ya wafanyakazi, wazabuni, watoa huduma na wakandarasi na ni kweli suala hili limekuwa ni la muda mrefu. Pamoja na kupokea ushauri wa Kamati, niseme tu kwamba Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipa madeni ambayo yamehakikiwa kila mwaka. Baada ya uhakiki kukamilika taarifa ya matokeo ya uhakiki huwa inawasilishwa kwa Maafisa Masuuli ambayo inaonesha wadai ambao madeni yao yamekubaliwa na wale madai yao yamekataliwa na sababu za kukataliwa kwake.

Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kuwataka Maafisa Masuuli kuwajulisha wahusika ambao walikuwa na madai lakini madai yao yalikataliwa, maana wao ndiyo wanaowafahamu. Uhakiki wa madeni ya mwaka 2017/2018 na 2018/2019 umeanza na tunatarajia kwamba itakapofika mwezi wa nane, Serikali itakuwa imemaliza na tutaanza utaratibu wa kuyahakiki kwa kila robo mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilishauri Serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu ili kiweze kufanya majukumu yake kikamilifu. Ni kweli kabisa tunatambua umuhimu wa kitengo hiki na kwenye mwaka ujao wa fedha Fungu 13 ambayo ndiyo kitengo cha udhibiti wa fedha haramu, kimetengewa jumla ya shilingi bilioni 2.01 kwa ajili ya OC na shilingi milioni
200.29 kwa ajili ya maendeleo. Tunatenga fedha hizi kwa kuzingatia kiwango cha makadirio ya mapato kwa mwaka ujao wa fedha, lakini pia vipaumbele vya kimkataba ambavyo tunavyo ikiwa ni pamoja na Deni la Taifa lakini pia mishahara ya watumishi wa umma. Kwa hiyo, kwa kuzingatia umuhimu wa kitengo hiki, tutaendelea kukitengea fedha, lakini tunafungwa tu na mapato ambayo yanaweza yakapatikana katika mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilihoji juu ya Sheria ile ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 ambayo inataja kiwango cha juu cha fedha ambazo mtu anaweza kukibeba kama fedha taslimu kuwa ni shilingi milioni 10 tu na kwamba kwa biashara na hususan biashara ya dhahabu kwamba hiki kiasi ni kidogo sana.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Kusimamia Usafirishaji wa Fedha Taslimu ambazo zinavuka mipaka ya nchi (The Anti-Money Laundering (Cross Border Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments Regulations) ya mwaka 2016 wasafiri wakiwa na fedha taslimu, sawa na dola za Marekani 10,000 au zaidi wanatakiwa kutoa taarifa kwa Maafisa Forodha.

Naomba ifahamike kuwa kanuni hizi hazimzuii mtu kubeba fedha taslimu zaidi ya kiwango kilichotajwa, lakini tunachosema ni kwamba ni lazima a-declare, lazima atoe tamko kwa Maafisa Forodha ili tuweze kudhibiti usafirishaji wa fedha haramu kupitia mipakani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilionesha kwamba pamoja na kuwa Tume ya Pamoja ya Fedha imeanzishwa tangu mwaka 2003 mpaka sasa Akaunti ya Pamoja bado haijafunguliwa, japokuwa jambo hili linafanya kazi ni muhimu tuliharakishe. Naomba tu niseme kwamba tarehe 9 Februari, 2019 Mheshimiwa Makamu wa Rais aliongoza kikao hapa Mjini Dodoma na moja ya ajenda iliyojadiliwa katika kushughulikia changamoto za Muungano lilikuwa ni hili. Maelekezo ambayo sisi tulipatiwa ni kwamba tuandae Waraka mpya wa Baraza la Mawaziri kuhusu mapendekezo ya kufungua akaunti ya pamoja. Naomba kulijulisha Bunge lako tukufu kwamba utekelezaji wa maagizo hayo unafanyiwa kazi hivi sasa, kwa hiyo muda si mrefu Serikali itaweza kutoa maamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilibaini kwamba kumekuwa na mifumo mingi sana ambayo inasimamiwa na Wizara yangu ikiwemo IFMS, GPG, GSSP, GAMIS na kadhalika; mifumo yote inasimamiwa na Wizara yangu, uendeshaji wake una gharama kubwa na kwamba ni muhimu sana sasa tuone namna ya kuiwianisha na kuiunganisha na hasa ile ambayo inafanya kazi moja. Pia Kamati ilitusisitiza tuharakishe mchakato wa kujenga mifumo yake na kuondokana na mifumo mingine kutoka makampuni au watu binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekuwa ikitengeneza mifumo kulingana na mahitaji mbalimbali ambayo hayaingiliani katika business process. Hata hivyo kupitia mradi wa PFMRP tayari Wizara imeanza kuunganisha mifumo mbalimbali ya ndani na taasisi nyingine za kifedha ili kubadilishana taarifa na kupunguza gharama za uendeshaji wa mifumo. Pia Serikali imeanza kutengeneza mifumo yake na nashukuru Kamati ya Bajeti imeliona hili, ili tuweze kupunguza gharama kubwa mno ambazo tumekuwa tukilipa wakandarasi mbalimbali. Kwa hiyo, tumetumia wataalam wetu ndani ya Serikali kutengeneza mifumo ya GPG, GSPP na GAMIS, lakini pia mfumo wa kiuhasibu. Pia kwa kutumia wataalam wetu wa ndani tunaendelea kutengeneza mifumo mingine ya nje iliyobaki ili kuondokana na utegemezi wa malipo ya leseni (subscription fee) pamoja na utegemezi wa utalaam kutoka makampuni binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia iliona kwamba pamekuwepo na mwingiliano wa majukumu baina ya baadhi ya taasisi za Serikali na hususan GPSA ambao ni Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini, lakini PPRA - Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi Umma, lakini pia Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Tanzania na Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma. Walitushauri kwamba ni vizuri majukumu ya taasisi hizi kuwa wazi na tuhakikishe zinatekeleza majukumu yake kama ambavyo zimebainishwa kwenye sheria zilizozianzisha. Kamati pia iliona zipo changamoto za wataalam wa ununuzi waliosajiliwa na Bodi ya PSPTB kwenye taasisi na mashirika ya Serikali na hivyo inakwenda kinyume na sheria na suala hilo lazima Serikali ilifanyie kazi haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme tu kwamba tunapokea ushauri wa Kamati na Wizara yangu kwa kushirikiana na hizo taasisi tutapitia na kuchambua majukumu ya kila mmoja ili kubaini maeneo yenye muingiliano kwa lengo la kurekebisha ili taasisi hizo ziweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria iliyozianzisha. Bodi kuendelea kutoa elimu kwa waajiri na waajiriwa juu ya matakwa ya Sheria ya PSPTB inayowataka kuwaajiri au kuajiriwa wataalam wa ununuzi na ugavi waliosajiliwa na hii Bodi. Lakini bodi itawachukulia hatua waajiri wanaoajiri Maafisa Ununuzi na Ugavi ambao hawajasajiliwa kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya PSPTB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nianze kutolea ufafanuzi baadhi ya hoja ambazo zilitolewa; kwanza Mheshimiwa Obama Ntabaliba tunazipokea pongezi zake kwa Serikali na hususan Mheshimiwa Rais, viongozi wa Wizara lakini pia Mamlaka ya Mapato na Benki Kuu ya Tanzania. (Makofi)

Suala la Ofisi ya Msajili a Hazina, Mheshimiwa Naibu Waziri ameshalitolea maamuzi. Naomba niseme kuhusu hotuba yangu niliyoitoa asubuhi imejaa hatua za udhibiti (controls) na hakuna hatua ambazo zinaleta faraja kwa wafanya biashara, naomba Mheshimiwa Obama na Bunge lako wasubiri kidogo, wavute subira hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali itasomwa alasiri ya tarehe 13 Juni, 2019 na baadhi ya haya mambo atapata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala la wale walikuwa wanaendesha maduka ya kubadilisha fedha za kigeni na wapo wachache ambao walikuta wanaendesha hiyo biashara kwa mujibu wa sheria na taratibu za lesini zao, hoja ilikuwa kwamba hawa waruhusiwe kuendelea na biashara yao. (Makofi)

Naomba nilifahamishe Bunge lako tukufu kwamba baada ya Benki Kuu kukamilisha lile zoezi kwa baadhi ya maeneo, wote waliokutwa wanafanya biashara hiyo kwa mujibu wa leseni, masharti ya leseni zao waliruhusiwa kuendelea na biashara zao. Ni wale tu ambao walikutwa wanafanya kinyume cha taratibu hizo ndiyo walifungiwa kuendelea na biashara zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Obama pia alituambia kwamba malipo ya wastaafu yanachelewa sana na pengine tuangalie kwa macho makali kile kitengo kinahusika. Naomba kulitaarifu Bunge lako tukufu kwamba hivi sasa tunaweka mfumo wa kielektroniki ambao utapunguza sana ucheleweshaji, lakini hususan shida kubwa iko kwenye kumbukumbu (records). Kwa hiyo, sisi tunaamini kwamba njia hiyo itaturahisishia na muda si mrefu suala la kuchelewesha malipo ya wastaafu litakuwa ni historia, lakini pia tunapokea ushauri, tutakitazama pia kitengo hiki kwa karibu, kwa maana ya mahitaji ya watumishi lakini pia vitendea kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Balozi Dkt. Kamala alisema vizuri sana kuhusu ukuaji wa uchumi na zile sekta ambazo zinakuwa kwa kasi. Ni kweli kabisa sekta ambayo inaongozwa na Mheshimiwa Mwakyembe ndiyo inayokuwa kwa kasi zaidi kuliko nyingine kwa hivi sasa. Kwa upande wa kilimo naomba kwa kweli niwapongeze sana wakulima wa nchi hii, siyo tu wanatupatia chakula, lakini wanatupatia fedha nyingi za kigeni kupitia mazao ambayo tunauza nje. Kwa mwaka 2016 kilimo kimeendelea kutoa takribani asilimia 27.4 ya pato la Taifa, mwaka 2017 kilichangia asilimia 28.8 na mwaka 2018 kimechangia asilimia 28.2. Hata ukiangalia kwenye mauzo yetu nje kwa wastani kwa hiyo miaka mitatu kwa kila mwaka mazao ya kahawa, pamba, katani, chai, tumbaku, korosho na cloves, kwa ujumla kila mwaka zinaliletea taifa letu mapato ya takribani dola milioni 4197. Hii unaondoa fedha ambazo tunapata kutoka kwenye mauzo ya samaki na yanayotokana na samaki, lakini pia mazao ya mboga mboga na hata mazao ambayo yameongezewa thamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa ukuaji wa sekta ya kilimo kwa kutumia takwimu mpya za pato la Taifa kwa kweli tumeona, hapo zamani kilimo kilikuwa kinakuwa kwa karibu asilimia 3/3.2. Kwa takwimu mpya kilimo kimekuwa kwa asilimia 4.8 mwaka 2016, asilimia 9.2 mwaka 2017 na asilimia 5.3 mwaka 2018. Kwa hiyo kwa kweli wamefanya vizuri sana wakulima wetu wanastahili pongezi. Ukienda kwenye mchanganuo kilimo cha mazao ndiyo kinaongoza kwa kasi kubwa ambacho kimekuwa kwa wastani wa asilimia 5.0 mwaka 2018 na kinafuatiwa na mifugo ambayo nayo sekta ndogo ya mifugo nayo ilikuwa kwa asilimia 4.9, uvuvi imekuwa kwa kasi zaidi ya asilimia 9.2 mwaka 2018. Tunawapongeza sana wavuvi wetu ambao wameleta mafanikio hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mfumuko wa bei katika nchi hii unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mfumuko mdogo wa bei za chakula. Kwa hiyo Mheshimiwa Balozi Kamala alikuwa anasema ni vema nieleze mikakati ya Serikali kusaidia wakulima ambao ndiyo wanachangia kushusha mfumuko wa bei katika nchi yetu. (Makofi)

Naomba niseme tu kwa kifupi kwamba, maelezo yalitolewa wakati wa hatuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo lakini siyo vibaya nikarudia kwamba sisi kama Serikali tunajielekeza kuhakikisha kwamba pembejeo muhimu zinawekewa fedha kwenye bajeti ya Serikali kupitia bajeti ya Wizara husika, hizi zote zinazohusika na mazao, mifugo na uvuvi, lakini pia kwa upande wa misitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia, mkakati mwingine ni kuondoa kodi na tozo za kero. Kodi na tozo za kero kwa wakulima wetu tumekuwa tunazifuta kwa miaka yote mitatu na mimi kabisa ninaamini kwamba tutaendelea na jitihada hizi katika mwaka ujao wa fedha. Lingine ni kuwatafutia mikopo nafuu, na hii tumekuwa tunafanya kwa kuzungumza na taasisi mbalimbali ikiwemo African Development Bank lakini pia Kuwait Fund ambao tumekuwa na majadiliano nao ili watupatie fedha kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji, lakini pia ADB kwa ajili mradi ambao utaweka kongani za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, lakini pia jitihada za kuongeza na kutafuta masoko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba kidogo nijielekeze kwenye Deni la Taifa ambalo limesemwa na watu wengi na naomba nimshukuru sana Mheshimiwa George Boniface Simbachawene kwa darasa zuri sana ambalo amelitoa kuhusu Deni la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Sika, labda nianze na hili ambalo alilisema Mheshimiwa Kamala maana yeye hakuwa na shida sana na sisi kukopa, lakini suala alikuwa na wasiwasi kwamba viashiria vya uhimilivu wa deni vimeanza kuwaka na hivyo Serikali ipunguze kasi ya kukopa. Pia alihoji kwamba tuna mkakati gani wa kuhakikisha kwamba Deni la Serikali haliendelei kukua sana kwa kuwa tunajua tutaendelea kukopa kugharamia miradi yetu mikubwa ya maendeleo, SGR, umeme Mto Rufiji na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa maana ya mkakati, napenda kusisitiza kwamba mikopo ambayo inapewa kipaumbele katika kukopa ni ile yenye masharti nafuu. Ile ya kibiashara kwa kweli tunakuwa waangalifu sana, we are very very cautious na tunapokopa mikopo ya kibiashara tunaielekeza kwenye maeneo mahsusi ya kuchochea uchumi. Kwa hiyo, hatukopi tu mikopo ya kibiashara tukaipeleka popote, hapana.

Mheshimiwa Spika, la pili tumejielekeza sana kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani na lengo letu ni kuwa sehemu kubwa ya bajeti iwe inagharamiwa na fedha za ndani na wakati huo huo tukifanya jitihada kupunguza matumizi ambayo yanaepukika. Lakini mkakati wa tatu ni kufanya marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura ile ya 134 ili dhamana ya Serikali ambayo inatolewa itolewe tu kwa taasisi za Serikali ambazo zinajiendesha na ambazo tuna uhakika zinaweza zikarudisha deni.

Mheshimiwa Spika, mkakati mwingine ni kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Deni la Taifa ndiyo sababu kila mwaka ni lazima tufanye uchambuzi wa uhimilivu wa deni (debt sustainability assessment) kila mwaka ndiyo maana nilitoa taarifa kwamba Desemba, 2018 tumefanya assessment hiyo na bado tunaona kwamba kwa vigezo vyote vya Kimataifa bado tuko vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mkakati mwingine tunaendelea majadiliano na majadiliano nan chi ambazo sio wanachama wa Paris Club na lengo letu hapa ni kuona kama tunaweza tukafikia makubaliano ili nao waweze kutusamehe madeni yao kama ilivyokuwa wakati ule wa HIPC kwa nchi ambazo ni za Club ya Paris.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikopo ya ndani, tunazingatia uwezo wa soko na pia tunazingatia liquidity katika uchumi, lakini pia tunafanya hivyo, tunapokopa tunahakikisha kwamba hatupunguzi uwezo wa taasisi m balimbali kuikopesha sekta binafsi ya ndani. Kama mnavyofahamu, tumeruhusu pia nchi za Afrika Mashariki kushiriki kwenye ununuzi wa dhamana kwenye soko letu hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema vigezo vyote vya uhimilivu tuko vizuri kabisa na niseme tu kwamba kumtoa wasiwasi Mheshimiwa Dkt. Kamala na wengine ni kwamba tunapofanya ule uchambuzi wa uhimilivu wa deni tunafanya kitu tunaita debt stress test na hizi maana yake ni kwamba tunaweka zile namba zote ambazo tunakuwa tumezikusanya kwamba deni letu liko hapa hivi sasa. Je, kama ikitokea tatizo kubwa labda tumepata tatizo kubwa moja ya mazao yetu yanayotuingizia fedha za kigeni imeporomoka, kwa hiyo mwenendo wa upataji fedha za kigeni unakuwaje na mwenendo wa deni letu la Taifa utakuwaje. Kwa hiyo, tunatumia vigezo mbalimbali kujiridhisha kwamba bado tutabakia sawasawa na kwa hiyo, tunapotoa taarifa kwamba deni letu ni himilivu tunakuwa pia tumezingatia debt stress test ambazo tumekuwa tumefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nirudie kusisitiza kukopa sio dhambi ilimradi mikopo hiyo ielekezwe kuongeza uwezo wa kuzalisha mali nchini na pia izingatie uwezo wa nchi yetu kulipa. Nadhani hicho ndicho kitu cha msingi na bahati nzuri ni kwamba Serikali imeendelea kulipa kulingana na mikataba ya madeni hayo kila yanapoiva. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda naomba nilisemee hili tena kwa Mheshimiwa mdogo wangu Zitto Kabwe ambaye alituambia usimamizi wa Deni la Taifa ni tatizo na kwamba kuna upotoshaji kwa mujibu wa Taarifa ya CAG ambayo alikuwa anainukuu. Naomba niseme, tena yupo, afadhali!

Naomba niseme allegation aliyoitoa ni very serious. Mheshimiwa Zitto Kabwe allegation aliyoisema ni very serious, haiwezekani Taifa kama letu tukatunza takwimu za Deni la Serikali kwenye counter book. Hii si kweli na ni udhalilishaji wa Serikali. Kwa kweli Mheshimiwa Zitto Kabwe ulitakiwa ufute kabisa yale maneno, hayafai, sio sahihi na ninajua unafahamu kwamba hatuweki takwimu za Deni la Taifa kwenye counter book. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kutunza kumbukumbu za Deni la Taifa, Wizara ya Fedha inatumia mfumo wa kielektroniki wa kutunza kumbukumbu za Deni la Serikali ambao unajulikana kama Commonwealth Secretariat Debt Recording and Management System (CSDRMS) na mfumo huu unatumiwa na nchi za Jumuiya ya Madola na unahuishwa mara kwa mara kulingana na mahitaji. Aidha, mfumo huu kwa Tanzania ulianza kutumika toka mwaka 1996 mpaka 1997. Kwa hiyo, Mheshimiwa Zitto Kabwe hilo sio sahihi, usipotoshe umma hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, takwimu za deni letu ni sahihi, lakini pia niseme CAG hazuiliwi kufanya ukaguzi wa Deni la Taifa na wala sio mara ya kwanza amefanya, kwa hiyo, kwa mujibu wa taratibu zake alizojipangia akitaka kuhakiki Deni la Taifa atafanya hivyo. Sasa labda niseme tu inawezekana pengine pakawa na tofauti, alikuwa anasema inawezekana kabisa kwamba wale waliotukopesha wana namba tofauti na sisi hili ni jambo la kawaida, tofauti zinaweza kuja kwa sababu ya matumizi ya exchange rate, lakini inawezekana pia hata just human error katika uandishi wa zile takwimu, lakini kikubwa ni kuhakikisha kwamba ile marginal of error inakuwa ni kidogo na kwetu sisi marginal of error ndogo na inakubalika. Hata kukiwa na error baadae reconciliation inafanyika. Kwa hiyo hili sio tatizo hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba pia nitoe maelezo ya nyongeza pale alipoishia Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu ukusanyaji wa mapato ya kodi. Mheshimiwa Zitto Kabwe mimi nakumbuka wakati ule, nadhani siasa inakuchanganya kidogo siku hizi. Wakati ule ukiwa darasani kwangu nadhani ungeweza kuona kwa urahisi kabisa. Uwiano wa mapato ya kodi kwa Pato la Taifa kwa nchi yetu ni kweli umepungua kama Mheshimiwa Naibu Waziri alivyosema, lakini ni rahisi tu, tax effort tunachukua makusanyo ya kodi unagawanya kwa Pato la Taifa. Sasa kilichofanyika baada ya kufanya rebasing ni kwamba GDP imeongezeka kwa kasi kuliko kasi ya ongezeko la kodi na kwa hiyo ndiyo maana utaona kwamba tax effort imepungua, lakini ni kwa sababu ya mabadiliko ambayo tumefanya kwenye Pato la Taifa kwa sababu ni muhimu pia. Ni muhimu kwamba Pato la Taifa liweze kuendana na hali halisi ya uchumi. Wakati ule tulikuwa tunatumia Pato la Taifa kwa kizio cha mwaka 2007 sasa toka mwaka 2007 mpaka mwaka 2019 pametokea tofauti kubwa sana katika structure ya uchumi wetu na ndiyo maana unaona kwamba sekta anayoongoza Mheshimiwa Mwakyembe sasa imekuwa ni sekta ambayo inakua kwa kasi kuliko zote wakati hapo nyuma tu haikuwa hivbyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ni rahisi tu kama denominator inaongezeka kwa kasi zaidi kuliko numerator ni hesabu za kawaida tu Mheshimiwa Zitto Kabwe unatakiwa ukumbuke tu hiyo. Lakini pia ni muhimu kuzingatia kwamba baadhi ya nchi za Afrika Mashariki bado hazijakamilisha rebasing na katika makubaliano tuliyonayo tumekubaliana kwamba tutafanya rebasing ya nchi zote za Afrika Mashariki kwa pamoja na hapo ndiyo unaweza ukafanya ulinganifu mzuri wa hiyo tax effort kwa maana ya uwiano wa mapato ya kodi na GDP.

Mheshimiwa Spika, labda niseme pia kuhusu rai ya Mheshimiwa Peter Serukamba, tunaisaidiaje Benki ya Maendeleo iweze kufanya vizuri zaidi, lakini pia benki zingine kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya uchumi katika Taifa letu. Labda tu niseme kwamba pamekuwepo changamoto za mtaji na hususan kwa benki zetu mbili zile za TIB Corporate na ile ya Maendeleo. Lakini tumekuwa tunashirikiana na benki hizi kama Wizara ili kushughulikia suala la mtaji na ukwasi ili kuweza kuleta tofauti na mafanikio yameanza kuonekana. Mikopo ya mashirika ya umma iliyokuwa hailipwi kwa ushrikiano wa karibu na Ofisi ya Msajili wa Hazina sasa mikopo hii imeanza kurejeshwa. Pia benki imefanikiwa kupata vibali stahiki kutoka kwa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa aili ya kutoa hati fungani ya kiasi cha shilingi bilioni 135 na mpango huu unatazamiwa kukamilika ndani ya mwezi Juni ambao tumeanza, 2019.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nataka tu kusema kwamba zipo jitihada za makusudi kabisa ambazo Serikali inafanya ili kuweza kuhuisha utendaji wa benki hizi.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nisemee juu ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani. Kama utakumbuka palikuwepo na udanganyifu ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya wafanyabiashara wanapodai kurejeshewa kodi ambazo hawastahili na ndiyo sababu tuliamua kwamba ni lazima tufanye uhakiki wa marejesho hayo kwa kiwango cha asilimia 100 na kwa hiyo, tunahakiki nyaraka zote ambazo zinawasilishwa na mwombaji, lakini nyaraka zote pia ya yule aliyemuuzia bidhaa au huduma muombaji wa marejesho na uhakiki wa nyaraka zilizowasilishwa kwa kiwnago cha asilimia umefanyika na hatua inayoendelea sasa ni uhakiki wa nyaraka za muuzaji wa bidhaa iliyonunuliwa yaani third part verification. Tunachukua hatua hii kwa waombaji wote wa marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani ili tujiridhishe kwamba hakuna uwezekano wa kurejesha fedha zaidi ya kiwango sahihi kinachostahili. Ili kukabiliana na changamoto ya ucheleweshaji, Serikali kupitia TRA imefanya maboresho ya mifumo yake ya usimamizi wa kodi ikiwemo EFDMS ili kuweza kutoa risiti moja moja kwa kila muamala badala ya mfumo wa zamani wa kutoa risiti kwa makundi mwisho wa siku. Mfumo huu utaweza kusomana na mifumo mingine kama i- tax ambao unatumika kuwasilisha return za VAT na hivyo kufanya uhakiki kuwa rahisi.

Mheshimiwa Spika, kiasi cha madai yaliyopokelewa ni maombi 1,854 ambayo yana thamani ya shilingi bilioni 697.2 na kati ya hayo, madai yaliyohakikiwa ni 451 ambayo yana thamani ya shilingi bilioni 22.6 na madai ambayo hayajahakikiwa ni 1292 ambayo thamani yake ni shilingi bilioni 713.2. madai yaliyolipwa mpaka sasa ni 152 ambayo yana thamani ya shilingi bilioni 10.6 na madai haya ni takwimu hadi kufikia mwezi wa Aprili, 2019.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa malipo ya ile asilimia 15 kwa waingizaji wa sukari, napenda niseme tu kwamba Serikali imelifanyia kazi na hivi karibuni Serikali itatangaza kwa umma juu ya hatua stahiki ambazo zitachukuliwa kuhusiana na eneo hili.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nitolee ufafanuzi kidogo juu ya suala la vitambulisho vya wajasiriamali. Niseme tu kwa sababu kulikuwa na allegation hapa kwamba ile tozo/ gharama ya kitambulisho kwamba haipo kisheria, sio sahihi kabisa kabisa. Suala hili ni kwa mujibu wa sheria na linaratibiwa na kutekelezwa kwa asilimia 100 na Wizara yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, labda niseme tu kwamba Sheria ya Usimamizi wa Kodi Sura 438 pamoja na marekebisho yake ambayo yalifanywa na Bunge hili tukufu mwaka 2017 katika kifungu cha 22(a) kilimpa mamlaka Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wadogo na watoa huduma ambao ni washereheshaji, machinga, mama lishe, baba lishe na wengineo ambao mauzo ghafi hayazidi shilingi milioni nne.

Kwa hiyo, hili jambo liko kisheria kabisa. Wafanyabiashara wadogo na watoa huduma wanaoangukia kwenye Sekta isiyo rasmi hivyo huweka mazingira ya ushirikiano na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na TRA katika mchakato wa ugawaji wa vitambulisho, ni utaratibu wa makusanyo ya malipo ya gharama ya vitambulisho na ushirikiano huo umegawanyika katika sehemu mbili; kwanza ni kutumia mtandao mpana wa kiutawala ambao uko kule TAMISEMI katika kuwatambua wajasiriamali wadogo pamoja na kugawa hivyo vitambulisho kwenye huo mtandao. Ndiyo uliotumika kugawa hivyo vitambulisho.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa pili ni ule sasa ambao unahusu ukusanyaji wa fedha na gharama za vitambulisho na Wizara ya Fedha kupitia TRA ndiyo inafanya kazi hiyo na fedha zinazokusanywa zote zinapelekwa moja kwa moja kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nirudie tena kwamba jambo hili liko kisheria na sheria ilipita hapa Bungeni, kwa hiyo, ni suala tu la mgawanyo wa majukumu na kama Serikali ni lazima tutumie mtandao mpana wa Serikali kule kwa wale ambao wanaweza kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.

Mhesimiwa Spika, Mheshimiwa Nsanzugwanko nilishatolea maelezo juu ya suala la tax refunds.Hili la kutumia wataalam kunishauri tutalitafakari, lakini pia nikuhakikishie kabisa kwamba Serikali inafanya jitihada kuhakikisha kwamba yale mashirika ambayo Serikali inahisa kama Naibu Waziri alivyozieleza tunajitahidi ku-maximize mapato yanayotokana na taasisi hizo kwa kuzingatia uwekezaji wa Serikali na pia kwa kuzingatia kama ulivyosema umuhimu wa kulinda ajira lakini pia michango ya hayo mashirika. Tunafanya jitihada kubwa na wewe mwenyewe umeona mabadiliko makubwa katika kipindi kifupi kwamba hata sasa hata taasisi ambazo kwa miaka mingi zilikuwa hazileti chochote Serikali sasa zimeanza kuleta gawio.

Mheshimiwa Spika, rai ya kwamba TRA iwe rafiki kwa wafanyabiashara, ahsante kwa kutupongeza kwamba walau mnaona tunaanza kusikiliza, lakini ni rai yangu kwamba tutaendelea kulitilia mkazo ili TRA kweli iwe rafiki wa wafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa Ofisi ya TRA Kasulu na kule Kongwa kwa Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba, nitalitazama kwa jicho la karibu tunavyokwenda mbele katika mwaka ujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja mbalimbali kutoka kwa Mheshimiwa Katani, labda tu niseme kwamba tulipochagua ule mradi wa kimkakati kule Mkuranga nadhani ilikuwa timing problem, lakini tutaliangalia kuhusu mradi wa kimkakati wa kujenga ghala kule Tandahimba kwa kuwa tunatambua kweli Tandahimba ni moja ya Wilaya ambazo zinazalisha korosho kwa wingi. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri ahsante, sasa.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo nakushukuru tena kwa nafasi, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba radhi sauti yangu ina shida kidogo lakini nitajitahidi ili Waheshimiwa Wabunge waweze kusikia majumuisho.

Mheshimiwa Spika, naomba kwanza nimshukuru Mungu kwa Baraka ya upendeleo kwa siku nyingine ya leo ambayo nimepewa kwa ajili ya kutumikia.

Mheshimiwa Spika, tarehe 13 Juni, 2019 niliwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Taarifa ya Hali ya Uchumi ya Mwaka 2018, Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2019/2020 na Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2019/2020; na kwa muda wa siku saba za kazi tangu tarehe 17 hadi leo tarehe 25 Waheshimiwa Wabunge wamepata nafasi ya kuzipitia hotuba hizo pamoja na viambatisho vyake na kutoa maoni na ushauri juu ya namna bora ya kujenga uchumi unaogusa wananchi wengi na kufanikisha utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi lakini pia Mheshimiwa Naibu Spika kwa kuendesha mjadala huu vizuri na kwa kweli unatarajiwa kuhitimishwa leo hii kwa kura ya wazi ya kila Mbunge kama ulivyosema.

Mheshimiwa Spika, jumla ya Wabunge 236 wamechangia hoja niliyowasilisha, na kati ya hao 189 wamechangia kwa kuzunguza, 41 kwa maandishi. Aidha, Waheshimiwa Mawaziri wanne, Naibu Mawaziri wawili akiwemo Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango wamechangia kwa kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zinazogusa sekta wanazosimamia, ninawashukuru sana. Vile vile nina washukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yenu, hakika mmetekeleza wajibu wenu wa Kibunge vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, na kipekee napenda kutambua na kupongeza uchambuzi na ushauri wa Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mheshimiwa George Boniface Simbachawene, Mbunge wa Kibakwe.

Mheshimiwa Spika, lakini pia namshukuru Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba kwa maoni na ushauri aliousoma kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Spika, wakati wa mjadala wa hituba nilizowasilisha, Waheshimiwa Wabunge wengi walimpongeza Mhehsimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi makini na kwa kusikiliza kero za makundi mbalimbali ya jamii na kuelekeza ufumbuzi wa kero hizo. Aidha, walipongeza na kuunga mkono bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha kwa maelezo kwamba bajeti ikaakisi matarajio ya Watanzania na inazingatia maslahi ya taifa na wadau wengi. Kwa niaba ya Serikali nimepokea kwa unyenyekevu shukurani na pongezi zote zilizotolewa kutoka ndani na nje ya Bunge juu ya bajeti hii. napenda niahidi kwamba baada ya bajeti hii kupitishwa rasmi na Bunge, Serikali itafanya kila linalowezekana kuitekeleza kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, yako aadhi ya maeneo mapya ambayo yaliungwa mkono na Waheshimiwa Wabunge wengi nitasema machache tu:-

i. Kwanza ni hatua ya Serikali kufuta au kupunguza ada na tozo 54;

ii. Serikali kukutana na wafanya biashra na kuanza utekelezaji wa blueprint;

iii. Kuanza na kuendeleza ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati

iv. Kutopandisha ushuru wa bidhaa kwa mazoea na hususani sigara na bia;

v. Kuielekeza TRA kubadilika ili kuwa na urafiki na walipa kodi na kupunguza utegemezi wa kibajeti na pia hatua za kikodi kulinda viwanda vya ndani.

Mheshimiwa Spika, yapo maeneo mengi ambayo Waheshimiwa Wabunge wengi wameishauri Serikali iyawekee msukumo wa kipekee katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha na bajeti zinazofuata. Naomba napo nitaje machache tu:-

i) Ni kuweka mkazo zaidi kwenye kilimo hususani utafiti, mbegu bora, huduma za ugani, pembejeo, kuongeza thamani, kutafuta masoko na kilimo cha umwagiliaji

ii) Kuwezesha upatikanaji wa taulo za kike kwa gharama nafuu

iii) Kukwamua upatikanaji wa mikopo ya kugharamia miradi muhimu ya maendeleo Zanzibar; na

iv) Uanzishwaji wa wa mfuko wa pamoja wa fedha za Muungano.

Mhehsimiwa Spika, haya tu ni baadhi lakini yako mengi sana; na kwa kuwa tutaleta majibu kwa maandishi ili kila Mheshimiwa Mbunge asome tutayaorodhesha yote ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuona mamambo makubwa ambayo tuliyachukua.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa kuanza kutolewa ufafanuzi hoja na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge. Kama nilivyotangulia kusema mjadala wa siku saba ni vigumu kuutolea ufafanuzi kwa dakika 50; kwahiyo tutaleta ufafanuzi wa hoja zote na kila Mheshimiwa Mbunge atapata ufafanuzi.

Mheshimiwa Spika, hoja ya kwanza, naomba nianze na hiiambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameieleza kwa kirefu, kwamba msamaha wa kodi wa ongezeko la thamani uliokuwa unatolewa kwenye taulo za kike zinazotambulika kwa HS code 9619.00.10 kwamba urejeshwe na Serikali ichukua hatua za maksudi kuhakikisha wafanya biashara wa bidhaa hiyo wanashusha bei au wanawekewa bei elekezi.

Mheshimiwa Spika, Serikali imetafakari sana juu ya mapendekezo ya Waheshimiwa Wabunge kuhusu hitaji hili muhimu kwa mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla. Kwa kuzingatia maoni na ushauri uliotolewa, napendekeza mambo matatu yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kama vile ambavyo nilieleza kwenye Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali tarehe 13 Juni, 2019; kwamba ni kupunguza kiwango cha kodi ya mapato ya makampuni (Corporate Income Tax) kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 25 kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka ujao wa fedha hadi mwaka 2020/2021 kwa wawekezaji wapya wa viwanda vya kuzalisha taulo za kike. Lengo la hatua hii ni kuvutia uwekezaji katika uzalishaji wa hii bidhaa muhimu sana pamoja na kuongeza ajira na mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hatua ya uwekezaji inaweza kuchukua muda kiasi, na ni nia ya Serikali kuhakikisha kuwa hatua hii inaleta manufaa kwa haraka, Serikali pia imeamua kupunguza kiwango cha kodi ya mapato ya makampuni (Corporate Income Tax) kutoka asilimia 30 hadi asilimia 25 kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka ujao wa fedha hadi mwaka 2020/2021 kwa viwanda vilivyopo vinavyozalisha bidhaa hiyo hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, narudia tena. Serikali pia imeamua kupunguza kiwango cha kodi ya mapato ya makampuni (Corporate Income Tax) kutoka asilimia 30 hadi asilimia 25 kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka ujao wa fedha hadi mwaka 2020/2021 kwa viwanda vilivyopo hivi sasa hapa nchini ambavyo vinavyozalisha bidhaa hii. Aidha, ni matumaini ya Serikali kuwa hatua hii itasaidia viwanda hivyo kuongeza uzalishaji wa taulo za kike na kupunguza bei ya taulo hizo. Kwa upande mwingine itaongeza matumizi ya pamba inayozalishwa hapa nchini, na pia itaongeza ajira, na hii ni pamoja na hatua nyingine ambazo Mheshimiwa Naibu Waziri amezieleza; kwa maana ya ujenzi wa viwanda kimoja na MSD na kingine kule Simiyu kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hii muhimu kwa ajili ya watoto wetu wa kike na wakina Mama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatua ya tatu inabaki ileile kwamba tunafuta msamaha wa VAT uliokuwa unatolewa kwenye taulo za kike kwa kushindwa kuwezesha upatikanaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa bei nafuu kwa walengwa badala yake kuwanufaisha wafanyabiashara. Kwa kweli lengo la Serikali ni kumnufaisha mtoto wa kike na sio wafanyabiashara kujilimbilikizia faida kubwa.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia nafasi hii kusisitiza kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba bidhaa hiyo muhimu inapatikana kwa bei nafuu na hivyo kuwawezesha watoto wa kike na wanawake kuinunua. Kwa msingi huo tutaingia mkataba wa makubaliano yaani performance agreement na kila mwekezaji atakayenufaika na punguzo hili la kodi ya mapato ambao utaainisha wajibu wa kila upande, lakini sasa Serikali itafuatilia pia mwenendo wa bei za hizo taulo za kike. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa kwamba Serikali iboreshe maslahi ya Watumishi wa Umma. Serikali inathamini sana mchango wa watumishi wa umma katika maendeleo ya nchi yetu na si kweli kwamba Serikali imewasahau watumishi kama ilivvyozungumza na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge. Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa maslahi ya Watumishi wa Umma yanaboreshwa. Katika mwaka 2016/2017 Serikali ilipunguza kodi kwenye mishahara yaani payee kutoka digit mbili mpaka digit moja. Aidha, mpaka kufikia bei mwaka 2018/2019, Serikali imelipa madai mbalimbali ya watumishi jumla ya shilingi bilioni 64.97 na pia ilipandisha madaraja watumishi wote waliokuwa wanastahili, ambapo jumla ya shilingi bilioni 14.55 zilitumika kufika Mei, 2019.

Mheshimiwa Spika, naomba nilitaarifu Bunge lako kuwa ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi iko pale pale kama alivyoahidi wakati wa kuadhimisha Sherehe za Mei mosi mwaka huu 2019 kule Jijini Mbeya.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa kupunguza kodi kwenye mishahara ya watumishi, naomba nilitaarifu niwaatarifu Waheshimiwa Wabunge kuwa Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikifanya maboresho ya mifumo ya kodi, tozo na ada mbalimbali ili kuongeza mapato; kuboresha mazingira ya kufanya biashara lakini pia mahitaji ya makundi mbalimbali katika jamii yanayoguswa na mfumo huo. Hata hivyo muundo wa uchumi (economic structure) umebadilika sana tangu miaka ya 90. Aidha, mahitaji ya fedha za kugharamia matumizi ya kawaida ya Serikali na ya miradi ya maendeleo kwa ustawi wa jamii yetu umeongezeka, lakini pia gharama za maisha kwa wananchi na hususani wafanyakazi.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hiyo napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu na Watanzania kwa ujumla kwamba, Serikali inakusudia kuunda timu maalum ya kufanya uchambuzi wa kina utakaohusu kupitia mfumo wa viwango vya kodi, tozo, ada na matumizi ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma kwa lengo la kuviwianisha au kuvibadili ili viendane na wakati. Kazi hiyo pia itapendekeza marekebisho ya sheria na miundo ya taasisi husika. Kazi kama hiyo ilifanyika mara ya mwisho mwaka 1991, miaka 28 iliyopita. Aidha, kwa kuwa kazi hiyo itahusisha kupitia mfumo mzima wa kodi na namna inavyogusa wafanyakazi na makundi mbalimbali ya jamii, wawakilishi wa Vyama vya Wafanyakazi watashirikishwa kikamilifu katika zoezi hilo. Mapendekezo mengine ambayo yanaweza kutekelezwa kwa taratibu za kiutawala yatatekelezwa kupitia nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa kwamba deni la Serikali limeendelea kuwa kubwa mwaka hadi mwaka na hivyo kuathiri uchumi wetu na maisha ya wananchi kwa ujumla. Katika kipindi cha mwaka ulioishia Aprili, 2019, deni la Serikali liliongezeka kutoka trilioni 49.86 na kufikia shilingi trilioni 51.03 Aprili, 2019, ambayo ni ongezeko la asilimia 2.35. Pia ikumbukwe kuna utaratibu madhubuti wa kuhakikisha kuwa mikopo inayochukuliwa inazingatia vigezo vyote vya uhimilivu, makadirio ya fedha zitakazotokana na chanzo hiki yanaidhinishwa na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, ongezeko la deni limetokana na mikopo mipya kama nilivyosema kwenye Bajeti Kuu ya Serikali na imetumika kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo bomba la gesi, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli na mitambo ya kufua umeme na kadhalika. Hata hivyo, mwenendo wa deni katika nchi zenye mazingira karibu sawa na Tanzania nao unaonesha kuwa nako madeni yanaendelea kuongezeka hususan kutokana na mahitaji makubwa ya kujenga miundombinu na huduma muhimu za jamii. Ukiangalia takwimu za Ghana, Ethiopia, Uganda, Kenya na Rwanda unaona, mwenendo ni kama huu wa kwetu.

Mheshimiwa Spika, ilitolewa hoja kwamba Serikali kukopa ndani kinawaathiri sana wananchi hasa wajasiriamali na kushindwa kupata mikopo kwenye mabenki na taasisi za fedha na ilidaiwa kwamba ni kutoka kwenye taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Naomba kutoa maelezo kwamba Serikali inakopa katika soko la fedha la ndani kwa utaratibu wa kutoa hatifungani na dhamana za Serikali kwa muda mfupi kupitia minada. Amana hizo zinanunuliwa na watu binafsi, mabenki, mifuko ya hifadhi ya jamii, mashirika ya bima pamoja na taasisi mbalimbali. Kiwango cha kukopa katika soko la ndani kinazingatia uwezo wa soko, kiwango cha ukwasi katika uchumi pamoja na kuhakikisha kuwa haipunguzi uwezo wa taasisi hizo kukopesha sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, sekta ya benki imeendelea kuwa imara na benki zina ukwasi wa kutosha ambao unakadiriwa kuwa takribani asilimia 30% ya mahitaji ya malipo mbalimbali ikilinganishwa na ukomo wa chini wa asilimia 20%. Kiwango hiki kinatosha kutoa mikopo kwa wateja na kuwekeza katika maeneo mengine ya uzalishaji, lakini pia Benki Kuu imeshusha kiasi cha amana ambacho mabenki yanatakiwa kuweka Benki Kuu (statutory minimum reserve) kutoka asilimia 10% mpaka asilimia 7.5% na hiyo imeongeza ukwasi katika mabenki kwa ajili ya kukopesha na kuwekeza katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, ilikuwepo hoja kwamba Serikali kupitia Wizara ya Fedha imekuwa ikifanya mabadiliko kwenye bajeti iliyopitishwa na Bunge kimya kimya bila kuomba ridhaa ya Bunge, this is very serious allegation. Mpaka kufika Machi 2019 Serikali ilitoa mgawanyo wa matumizi ya kawaida kwa Wizara na Idara Zinazojitegemea, Mikoa na Halmashauri kiasi cha shilingi bilioni 355.815 zaidi ya bajeti iliyokuwa imepitishwa na Bunge ya shilingi trilioni 20.468 na kufanya jumla ya fedha iliyotolewa kuwa shilingi trilioni 20.824 na kwamba hii inakiuka sheria ya bajeti kwa kubadili matumizi ya fedha tofauti na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa maelezo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, baada ya Bajeti ya Serikali kuidhinishwa na Bunge ikiwa ni pamoja na kuidhinisha sheria ya matumizi ya mwaka (Appropriation Act) hatua inayofuata ni utekelezaji wa bajeti ambapo Waziri mwenye dhamana ya fedha amepewa mamlaka ya kusimamia na kudhibiti utekelezaji, ufuatiliji na tathmini kwa mujibu wa kifungu cha 10(2)(b) cha Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015. Kifungu hiki kinasomeka kwamba nanukuu:

“The Minister shall be responsible for controlling and supervising the preparation, execution and monitoring of the budget including adjustment to the budget”.

Mheshimiwa Spika, vilevile Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015 imetoa Mamlaka kwa Waziri wa Fedha na Maafisa Masuuli kufanya marekebisho ya bajeti iliyopitishwa na Bunge wakati wa utekelezaji wabajeti. Marekebisho haya hufanywa ili kuwezesha Mafungu kutekeleza baadhi ya shughuli ambazo makadirio hayatoshelezi kwenye vifungu vilivyotengwa wakati wa maandalizi ya bajeti. Kwa upande wa Maafisa Masuuli ni kifungu cha 27(1) cha Kanuni za Sheria ya Bajeti ambacho kinawapa Mamlaka ya kufanya uhamisho wa ndani ya mafungu yao kwa kiwango kisichozidi asilimia 7% ya bajeti iliyoidhinishwa.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 28(2) cha Kanuni za Sheria ya Bajeti kinampa Waziri wa Fedha Mamlaka ya kufanya uhamisho wa bajeti kati ya Mafungu kwa kiwango kisichozidi asilimia 9% ya bajeti yote ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, mpaka kufikia mwezi Aprili uhamisho wa fedha ndani ya mafungu umefikia shilingi bilioni
964.6 ambayo ni sawa na asilimia 2.7 ya bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka huu wa fedha. Aidha, uhamisho wa Fedha kati ya mafungu ni shilingi bilioni 660.78 sawa na asilimia 2.03 ya bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka 2018/2019, hivyo marekebisho ya bajeti yaliyofanywa kwa mwaka huu wa fedha yako ndani ya wigo unaoruhusiwa kisheria.

Mheshimiwa Spika, Bunge huwa linapewa taarifa ya uhamisho wa fedha kwa mafungu namba moja na namba mbili kwa mujibu wa kifungu cha 41(8) cha Sheria ya Bajeti. Katika mwaka 2018/2019, taarifa hizo za uhamisho wa nusu mwaka yaani Julai mpaka Disemba, ziliwasilishwa kwenye kikao cha Bunge cha mwezi Januari 2019 na nimebeba hapa nakala ya statement of reallocation between vote, reallocation namba moja ya mwaka 2018/2019 ambayo ilishagawiwa kwa Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba tuanze sasa kutumia mfumo wa uchumi wa soko jamii hapa nchini na kwamba mfumo huu umefanikiwa kuziimarisha na kuendeleza nchi mbalimbali duniani na wakati huo kuwaondoa wananchi wa nchi hizo kwenye umaskini na kuwapatia fursa za ajira zenye uhakika. Nafikiri hapa Waheshimiwa Wabunge naomba waniazime masikio kidogo kwa sababu nataka kutoa darasa kidogo. Mfumo wa uchumi wa soko jamii yaani social market economy ni mfumo wa uchumi ambao unaendeshwa kwa kuchanganya misingi ya uchumi wa soko pamoja na dola kutoa huduma za jamii bure kwa wazee, wagonjwa, wasiojiweza, maskini na wasio na kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfumo huu uliasisiwa Ujerumani na Australia ukijulikana kwa jina la Kijerumani, sasa bahati mbaya sijui Kijerumani. Baadhi ya nchi za Ulaya na zilifanyika hivyo kushughulikia hifadhi ya jamii, huduma za afya kwa makundi ya jamii kama hao niliowataja. Sasa msingi wa uchumi wa soko jamii ni soko huria lakini pia utoaji wa social safety net na ili mfumo wa uchumi jamii uweze kufanya kazi ipasavyo, yapo walau masharti matatu ambayo ni lazima yatekelezwe.

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kwamba Serikali iwe na uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha kuendesha Serikali, kugharamia miradi, shughuli za maendeleo na matumizi ya umma na hususan miundombinu ya msingi ya usafirishaji, nishati, afya na kadhalika, lakini mapato ya ziada kuweza kugharamia progam za jamii yaani welfare programmes, hilo ndio sharti la kwanza. Sharti la pili ni lazima nchi iwe na usimamizi madhubuti wa fedha za umma na sharti la tatu lazima pawepo utaratibu wa wazi na wa haki katika kugawa rasilimali na mapato ya nchi kwa makundi ya nchi husika.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maelezo hayo kuhusu huo mfumo wa uchumi wa soko jamii ni wazi kuwa mazingira ya mfumo huo ili ufanye kazi ipasavyo, bado yanahitajika kujengwa hapa nchini na Serikali ya Awamu ya Tano imeweka nguvu kubwa katika kujenga misingi hiyo. Serikali ya Awamu ya Tano imeelekeza nguvu kupanua wigo wa mapato kupitia ajenda ya kujenga uchumi wa viwanda na kuongeza ukusanyaji wa mapato sambamba na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato. Pia Serikali imeweka mkazo katika kusimamia matumizi ya fedha za umma. Serikali pia imechukua hatua kuhimiza kila mtu afanye kazi na kulinda rasilimali za nchi ili ziwanufaishe Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo nawasihi wenzetu upande wa pili wasikimbilie kuiga yaani copy and paste bila kujenga misingi ya mfumo huo kuweza kufanya kazi katika mazingira na tamaduni za Mtanzania. Ni vyema pia kutambua kwamba mfumo huo una upungufu na athari zake, kwa mfano watu wanaoishi kwa kutegemea social protection huko kwingine, wanadharauliwa na kuonekana ni wavivu, wenye akili ndogo na wanaishi kwa jasho la wengine. Pia mfumo huo unaweza kuuwa kabisa utaratibu wetu mzuri wa jamii au familia kusaidiana (social capital) kwa mfano katika kusomesha watoto wa kaka au wa wadogo zetu. Kwa hiyo ni muhimu kidogo tuwe waangalifu, tusiende tu kubeba kilichofanikiwa Ujerumani tukakileta hapa kwetu sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nihamie kwenye hoja moja nzito ambayo ilisemwa sana na ndugu zetu kutoka Zanzibar na hususan ikihusu kuchelewa kusainiwa kwa mkataba wa mkopo wa Saudi na BADEA kuhusu ujenzi wa barabara ya Wete Chakechake, kuchelewa kusainiwa kwa mkataba wa mkopo kati ya Serikali ya Muungano na Exim Bank of China utakaogharamia mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, Terminal Two, lakini pia kuchelewa kusainiwa kwa mkataba wa mkopo kati ya Serikali ya Muungano na Exim Bank ya China kugharamia ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duru.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na mkataba wa mkopo wa Saudi na BADEA kuhusu ujenzi wa barabara ya Wete Chakechake. Kwanza mradi huu unajumuisha ukarabati wa barabara ya Wete hadi Chakechake ambayo ina urefu wa kilomita 22.1. Mradi huu unategemea kufadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka BADEA dola za Marekani milioni 10, Saudi Fund dola za Marekani milioni 11.4, Serkali ya Mapinduzi Zanzibar dola za Marekani milioni 3,000,000 na hivyo kufanya jumla ya dola kuwa milioni 24.4. Licha ya Serikali kusaini mkatana na BADEA, mkataba wa Saudi fund umekwamishwa na kifungu katika mkataba kinachoitaka Serikali kuweka mali zake kama dhamana ya mkopo, mali zilizotajwa katika kifungu hicho ni pamoja na mali za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, mali za Benki Kuu ya Tanzania, Malikale (cultural heritage), mali za kihistoria (historical objects) na mali za Ubalozi, lakini pia mali nyingine zilizoainishwa katika sheria ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri sharti hili ni kinyume cha sheria za nchi na nasema kweli siwezi kusaini mkataba kwa niaba ya Watanzania kwa sharti hili. Wanaosema nina roho mbaya sana, sawa ni maoni yao, lakini mimi Philip Mpango kamwe sahihi yangu haitatumika kuuza nchi. Pia miradi ya Bara inayosemekana imesainiwa kwa sharti hilo kwa hakika haikukopewa kwa sahihi yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na miradi ya Bara inayosemekana imesainiwa kwa sharti hilo kwa hakika haikukopewa kwa saini yangu.

Mheshimiwa Spika, katika kutatua mkwamo huu Serikali inaendelea na mazungumzo ya kidiplomasia na Serikali ya Saudi Arabia kama ilivyoshauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili waweze kuondoa sharti hili. Napenda niwakumbushe pia kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana, Waziri wa Fedha na Mipango anashauriwa na kamati mbili; Kamati ya Kitaalam (TDMC) na Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Madeni (National Debt Management Committee) ambazo zote zina wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hakuna mradi hata mmoja wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao kamati hizi zilinishauri nikope kwa niaba ya Serikali nikakataa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, Mkataba wa Mkopo Kati ya Serikali ya Muungano na Exhim Bank of China kugharamia ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Amani Abeid Karume, Terminal Two. Serikali imekuwa ikifanya majadiliano na Benki ya Exhim ya China ili kupata mkopo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Abeid Amani Karume, (Terminal Two) kwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 60. Majadiliano ya kwanza na benki hiyo yalifanyika Disemba, 2018. Exhim iliialika Tanzania kwa majadiliano ya pili ili yafanyike China mwezi Aprili, 2019.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, majadiliano hayo hayajafanyika kwa vile Serikali bado inafanyia kazi masharti hasi kwenye rasimu ya mkataba. Na tunachotaka sisi ni kurekebisha kifungu cha mkataba ambacho kama ilivyo kwenye mradi niliotangulia kuuelezea nacho kinaitaka Serikali kuweka dhamana baadhi ya mali zake zikiwemo mali za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, mali za Benki Kuu ya Tanzania, mali kale, mali za kihistoria, mali za ubalozi na mali nyingine ambazo zimeainishwa katika sheria za nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, lakini pia tumewataka waondoe sharti la kuhusisha mkopo huu na deni la kiwanda cha urafiki. Kwa hiyo, Serikali inaendelea na majadiliano ya kidiplomasia, ili kitatua mkwamo huo.

Mheshimiwa Spika, mradi wa tatu ni Mkataba wa Mkopo kati ya Serikali ya Muungano na Exhim Bank of China kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri. Mradi huu unatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 200 ambazo zitakuwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Exhim ya China; na Serikali ya Muungano iliomba ipatiwe nakala ya upembuzi yakinifu ya mradi huu ili ufanyike uchambuzi na vyombo husika.

Mheshimiwa Spika, hatua ya Serikali kufanya uhakiki imekuwa ikifanyika kwa miradi mbalimbali inayofadhiliwa kwa mikopo nafuu ili tujiridhishe kabla ya kusaini mikataba husika; na hii tunafanya kwa miradi yote. Lengo letu ni kuepuka kuingia gharama kubwa zisizoendana na thamani ya mradi ili tuhakikishe kuwa Serikali inanufaika vyema na mkopo wa masharti nafuu.

Mheshimiwa Spika, taarifa zote hizi nilizozieleza tulizitoa kwenye kikao cha kujadili changamoto za muungano kilichoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mkamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutolewa maelekezo kuwa kila linalowezekana lifanyiwe kazi ili tufikie mwisho haraka iwezekanavyo. Taarifa za kikao hicho zipo tena kwa maandishi, kwa hiyo inashangaza kweli kwa nini wenzetu hawakupewa hiyo taarifa yake na badala yake ninavikwa roho mbaya sana, naomba tu Mwenyezi Mungu awabariki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja pia kwamba Sera za Uchumi na Fedha za Tanzania Bara zina athari za moja kwa moja kwenye uchumi wa Zanzibar bila Zanzibar kuwa na intervation yoyote, lakini pia kwamba hadi sasa Serikali haijaunda Kamati ya Pamoja ya Fedha ya Muungano na hivyo kuvunja Katiba na pia kwamba mapato ya Zanzibar ni asilimia mbili na mapato ya Bara ni asilimia 98, asilimia 68 mapato yote yanatumika Tanzania Bara wakati asilimia 32 yanatumika kwenye taasisi za muungano; na kwa hiyo Zanzibar inatakiwa ilipwe trilioni 4.6 kutoka kwenye mapato ya muungano kwa kutumia formula ya mgawo wa asilimia 4.5.

Mheshimiwa Spika, naomba nitoe maelezo kwamba, Sera za Uchumi na Fedha za Jamhuri ya Muungano ni jumuishi na zinazingatia mahitaji ya Zanzibar na Tanzania Bara. Sera hizo zinahusisha hali halisi ya uchumi ya pande zote mbili za muungano. Sera ya Uchumi na Bajeti inapitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo linajumuisha Wabunge wa pande zote za muungano. Aidha, Sera ya Fedha hupitishwa na Kamati ya Sera ya Fedha (Monetory Policy Committee) ambayo ina uwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, kuhusu akaunti ya pamoja; ni kweli Ibara ya 133 ya Katiba inazungumzia uwepo wa akaunti hiyo ya pamoja ambapo zitawekwa fedha zote zitakazochwngwa na Serikali mbili kwa kiasi kitakachoamuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri ya Mungano kwa mambo ya muungano.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa pamoja hivi sasa zinaandaa Waraka wa Baraza la Mawaziri na hili ni agizo kutokana na kile kikao tulichofanya mwezi Februari chini ya Mheshimiwa Makamu wa Rais; kuhusu utaratibu wa kuchangia gharama za muungano na kugawana mapato ya muungano ili kuwezesha kuwepo utaratibu wa kudumu wa kuchangia gharama za muungano na kugawana mapato ya muungano.

Mheshimiwa Spika, uamuzi huo wa pamoja utakapofikiwa utawezesha kufunguliwa kwa akaunti ya fedha ya pamoja na kwa kuwa, mapendekezo ya uanzishwaji wa akaunti ya pamoja yapo katika ngazi ya uamuzi makubaliano yaliyopo ni kwamba mapato yanayotokana na utekelezaji wa mambo ya muungano yanayokusanywa Zanzibar yatumike Zanzibar kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo kule visiwani.

Mheshimiwa Spika, aidha, mapato ya muungano yanayokusanywa Tanzania Bara yatumike kugharamia mambo ya muungano na yasiyo ya muungano Tanzania Bara. Kutokana na makubaliano hayo pande mbili za muungano zimeendelea kunufaika na mapato ya muungano yatokanayo na kodi yanayokusanywa na TRA. Mapato hayo ni kodi ya mapato, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi. Pia kila upande wa muungano umeendelea kunufaika na mapato yanayotokana na misaada na mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo pamoja na gawio la Benki Kuu. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa inarejesha mapato ya kodi yanayotokanayo na mishahara ya watumishi (pay as you earn) wa muungano wanaofanya kazi upande wa Zanzibar. Maeleozo yote haya yapo kwenye kumbukumbu za mikutano ambayo tunafanya kwenye vikao rasmi kabisa baina ya Serikali zote mbili kuhakikisha kwamba muungano wetu unadumu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa nchi (Mazingira) ameeleza vizuri; maana palikuwa na hoja kwamba bajeti hii ya Serikali haijaeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo upande wa Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, nirudie tena kusisitiza miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa nchini inatokana na hatua za utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao ni sehemu ya Mpango Elekezi wa Miaka 15 wa kutekeleza Dira ya Taifa. Kwa upande wa Zanzibar kuna dira ya maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2020 ambayo inatekelezwa na SMZ kupitia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini (MKUZA), na sasa ni MKUZA III. Hivyo, utekelezaji wa miradi ya maendeleo upande wa Zanzibar unaainishwa na kutekelezwa kupitia MKUZA III na Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Miradi ya maendeleo kwa upande wa Zanzibar inatekekelezwa baada ya kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kwamba hoja ni nyingi sana, nitazileta kwa maandishi. Naomba uniruhusu niweze kuhitimisha.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyotuambia mara kwa mara, kwamba, maendeleo hayana chama. Tena ameendelea kusisitiza kwamba Tanzania ni nchi yetu wote. Hivyo naomba nihitimishe kwa kusema kuwa bajeti ni nyenzo muhimu ya kufikia matarajio ya wananchi wetu. Na ninawaomba kila mmoja wetu, Waheshimiwa Wabunge, aipigie bajeti hii ya nne ya Serikali ya Awamu ya Tano kura ya ndiyo ili tukaitekeleze kwa manufaa ya Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hii kukushukuru tena na pia kuwashukuru viongozi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango, bila kumsahau Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Care Taker Minister, Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, Wakurugenzi, Wataalam, Watumishi wenzangu wote kwa kujitoa kunisaidia katika kulitumikia taifa letu na wananchi wake usiku na mchana hadi kufikia hatua hii; ninamuomba Mungu awabariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, asante sana kwa fursa hii ya kuhitimisha mjadala huu na asante sana kwa Mungu kwa baraka na nguvu na uwezo alionikirimia kufanya kazi yake mpaka dakika hii.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, naafiki.
The Finance Bill, 2016
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kutoa shukurani sana kwako kwa kuendesha vizuri majadiliano kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha, kwa mwaka 2016/2017 na pia nimpongeze sana Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, kwa jinsi alivyoendesha vikao vya Kamati ya Bajeti kujadili Muswada huu kwa umahiri.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bajeti kwa maoni na ushauri ambao waliutoa. Napenda pia nitambue michango ambayo imetolewa na Waheshimiwa Wabunge, baadhi wamechangia kwa kuzungumza na wengine kwa maandishi. Naahidi kwamba Serikali itafanyia kazi ushauri na mawazo mazuri ambayo tumepata.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumepata hoja nyingi ambazo zilitolewa na Kamati ya Bajeti na Waheshimiwa Wabunge ambazo ningependa kuzitolea ufafanuzi. Hoja moja ilikuwa ni ile ya mapendekezo ya Serikali kuyalazimisha Makampuni ya Simu kujisajili na kuuza hisa zao kwa Watanzania na kuweka adhabu ya kufutiwa leseni kwa kampuni ambazo zitakiuka utaratibu huu. Ilidaiwa kwamba hii ni sawa tu na kutaifisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kulitaarifu Bunge lako kwamba sharti kwa kampuni za simu kuuza hisa kwa wananchi kupitia soko la hisa, kwa kweli siyo jambo jipya na mwaka 2010 Bunge lako lilitunga sharia ya Electronic and Postal Communication Act, ambayo kupitia kanuni zake iliweka sharti kwa kampuni husika kuuza hisa zao kwa wananchi kupitia soko la hisa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Hata hivyo, haikuweza kutekelezeka kutokana na mapungufu ya hiyo sheria. Kwa hiyo, mapendekezo ninayowasilisha hivi sasa kupitia huu Muswada wa Sheria yana lengo la kufanya marekebisho kwenye kifungu cha 26 ili kuondoa upungufu huo na kuiwezesha Serikali kutimiza azma iliyokusudiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia ile hoja iliyojitokeza kwamba adhabu ya kufutiwa leseni kwa makampuni zitakiuka utaratibu huu, kwamba ni sawa na utaifishaji. Sisi tunadhani kwamba siyo sahihi kwa kuwa kisheria utaifishaji unahusisha Serikali kuchukua mali ya watu au kampuni na kuifanya iwe mali yake. Adhabu ambayo inapendekezwa chini ya sheria hii ni kuifutia leseni kampuni kwa kutotimiza mashari ya leseni na hii itahusisha kuchukuliwa kwa mali za kampuni inayohusika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaamini kwamba kama kampuni zitakuwa ni aminifu, zitaweza kutekeleza suala hili ndani ya kipindi cha miezi sita, kama tunavyoliomba Bunge lako na tunaomba Waheshimiwa Wabunge, waiunge mkono Serikali kwenye pendekezo hili. Tunaamini ni njia ambayo itaisaidia Serikali kujua mapato halisi ya haya makampuni na kuwezesha na wao wachangie mapato ya Serikali kwa kutozwa kodi stahiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja nyingine kwamba kuna kampuni nyingine za mawasiliano kama Vodacom na Airtel ambazo tayari zinamilikiwa na Watanzania, na hiyvyo ukiweka masharti kwamba kampuni hizo ziuze hisa zao kwa wananchi ni sawa na kuzilazimisha kuuza hisa mara mbili kwa Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, hizi hisa zinazosemekana ziliuzwa kwa wananchi na kampuni hizi, ziliuzwa kwa watu binafsi, ikijumuishwa watu wa nje ya Tanzania na siyo kwa wananchi. Hii ni kinyume kabisa na masharti ya sheria ya Electronic and Postal Communication Act pamoja na Sheria ya Capital Market and Securities Act ambazo zinaweka utaratibu wa namna ya kuuza hisa kupitia soko la hisa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo napenda niwatoe wasiwasi Wabunge wanaodhani kwamba soko la hisa halitakuwa na uwezo wa kuhimili hisa za kampuni hizi endapo zitauzwa sokoni, napenda nilihakikishie Bunge lako kwamba Dar es Salaam Stock Exchange ina uwezo mkubwa wa kuhimili kuuzwa kwa hisa za kiwango chochote, ambapo ni mfano mzuri na wameweza kuhimili uuzaji wa hisa wa kampuni kubwa kama TBL na TCC.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ambayo ningependa kuisema ni mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Leseni za Biashara yaondolewe kwenye Muswada kwa kuwa hayakuwepo kwenye Muswada wa awali. Serikali imetafakari ushauri huu na kupitia jedwali la marekebisho, tumeondoa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Leseni za Biashara, Sura 208 ndani ya Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016. Aidha, Sheria ya Utawala wa Kodi imefanyiwa marekebisho ili kuhuisha dhana iliyokusudiwa kwenye marekebisho yaliyokuwa yamebainishwa kwenye Sheria ya Leseni ya Biashara, Sura 208.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja Serikali isiongeze ada ya usajili wa pikipiki na usajili wa namba binafsi. Serikali imefanya mabadiliko ya kiwango cha kodi ya usajili wa pikipiki kutoka sh. 45,000/= mpaka 95,000/=. Kiwango hiki kinalipwa mara moja tu wakati mtu anaandikisha pikipiki yake kwa mara ya kwanza. Ada hizi ni njia moja ya kuhakikisha waendesha pikipiki nao wanachangia kuiendesha Serikali yao, tunatambua umuhimu wa pikipiki ndiyo maana zimesamehewa kulipa ada ya leseni ya kila mwaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Uandikishaji na Uhamasishaji wa Magari, Sura 124; usajili magari unafanyika kwa kutumia namba T ikifuatiwa na tarakimu tatu na herufi tatu za alfabeti. Namba hii ni ya kipekee kwa Tanzania na ni kitambulisho cha kutosha kwa nchi ambako gari limesajiliwa na usajili huu unafanyika mara moja tu kwa kipindi cha uhai wote wa gari. Hata hivyo sheria hii imetoa nafasi kwa watu wenye mahitaji binafsi, ambapo inapendekezwa kulipia shilingi milioni 10, kutoka shilingi milioni tano za sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, mfumo huu unaweza kutumia jina la mhusika au kitambulisho kingine. Kwa kuwa mfumo huu ni maalum, mtu anayejisajili kwa utaratibu huu hulipia tofauti na usajili wa kawaida na usajili wao huwa ni wa miaka mitatu tu. Kwa hiyo, usajili wa magari siyo kwa ajili ya mapato tu, lakini pia udhibiti na usalama na kiwango kinachotumika kwa ajili ya usajili maalum kinapaswa kiwe kikubwa cha kutosha ili pasiwe na uwezekano wowote wa utaratibu huu kuchukua nafasi ya mfumo mkuu, kwani kiusalama namba maalum ni dhaifu kidogo kudhibiti. Kwa hiyo, wale wanaotaka kutumia mfumo huo wanapaswa kulipia gharama zinazoendana na manufaa, yaani satisfaction wanayoipata kwa kuutumia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba, Serikali ibadili madaraja yanayotumika katika kupanga kodi ya mapato tax bands. Serikali inapokea pendekezo hili na italifanyia kazi ili kuangalia namna bora zaidi ya kulishughulikia bila kuathiri utekelezaji wa hii bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja nyingine kwamba Serikali itoze asilimia sifuri huduma zinazotolewa kwenye mizigo inayopita nchini. Marekebisho katika kifungu cha 100 cha Muswada wa Fedha kwa huduma zinazotolewa kwenye mizigo inayopita nchini kwetu, unatolewa na kutumiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo kutoza kodi ya VAT ya asilimia 18 ni sahihi na sheria ya VAT ya mwaka 2014, inatoza VAT ya asilimia sifuri kwa bidhaa na huduma zinazouzwa nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinapotolewa na mawakala waliosajiliwa kwenye mfumo wa VAT.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja ya utekelezaji wa ukusanyaji wa kodi ya majengo, utakwenda kinyume cha sera ya ugatuaji wa madaraka, D by D. Sera tajwa haijavunjwa kwa sababu mapendekezo yanalenga kuboresha ukusanyaji, vyanzo halisi vya mapato vya Serikali za Mitaa bado vinabaki kuwa kama vilivyo, kwa ajili ya manufaa ya Serikali za Mitaa. Kinachofanyika katika mapendekezo niliyowasilisha, ni kuongeza tija ili maendeleo ya Halmashauri zetu yafanyike kwa uwazi zaidi na mapato yake kuongezeka ili kuleta ufanisi kwa kutumia njia za kisasa za ukusanyaji wa mapato. Tunaishukuru Kamati kwa kuunga mkono jitihada hizi za Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja pia ya kuondoa kodi ya VAT katika mafuta ya alizeti yanayozalishwa ndani ili kuchochea uzalishaji na kuwezesha mafuta yanayozalishwa ndani kuwa na bei ya kiushindani dhidi ya mafuta ya mawese ambayo bei yake inaendelea kushuka katika soko la dunia.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na nia njema ya Serikali kulinda viwanda vya ndani, uamuzi wa kusamehe VAT kwenye viwanda vya kutengeneza mafuta ya alizeti na kutoza mafuta ya kula yanayoingia nchini; utakinzana na misingi ya kutoza kodi hiyo. Maana VAT siyo kodi ya wazalishaji, bali ni kodi ya mlaji, kwa hiyo VAT haipaswi kubagua bidhaa ya aina moja kwa kuwa mlaji ni yule yule na pia italeta ugumu katika usimamizi. Aidha, hatua imechukuliwa ya kutoza mafuta ghafi ushuru wa asilimia 10 badala ya sifuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja ya kupunguza msamaha wa ushuru wa forodha kwenye Sukari ya Viwandani hatua kwa hatua ambapo mwaka 2016; kiwango kitakuwa asilimia 85; 2017/2018 asilimia 80 na 2018/2019 asilimia 75.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeamua kusitisha utekelezaji wa hatua hii hadi mwaka wa fedha 2017/2018; kwa kuwa ingekuwa ni nchi pekee ambayo ingetekeleza maamuzi haya na hivyo itatoza asilimia 10 kama ilivyo sasa. Hata hivyo, Serikali itaendelea kuwataka watumiaji wa sukari hii kuendelea kulipia kodi asilimia 25 kwanza na kurejeshewa asilimia 15 baada ya kukagua na kuthibitisha uhalali wa matumizi hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kuhusu kupunguza kodi ya zuio ambayo inatozwa kwenye huduma zinazotolewa na makampuni ya hapa nchini. Sheria ya Kodi ya Mapato imeweka kodi ya zuio ya asilimia 15 kwenye malipo yanayolipwa kwa makampuni ya nje kwa ajili ya huduma zinazotolewa hapa nchini. Kwa taratibu ya kodi ya mapato, kodi ya zuio ni kodi ya awali yaani advance corporate tax ambayo inatakiwa kupunguzwa kwenye kodi ya mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, mtoa huduma wa nje ya nchi anayekatwa kodi hii wanapunguza kiasi cha kodi kinachokatwa kwenye malipo yatokanayo na huduma; kwenye kodi ya makampuni husika anapokadiria kodi nchini mwake na kiasi cha kodi kinachowekwa kinalinda wigo wetu wa kodi na kuhamasisha matumizi ya huduma zinazotolewa kwa huduma za ndani.
Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na hoja ya kupunguza adhabu inayopendekezwa kumtoza mtu anayeshindwa kudai risiti au kutunza risiti ya EFD. Adhabu inayopendekezwa ni kuanzia shilingi 30,000/= hadi shilingi 150,000/= au kifungo kisichozidi miezi sita. Hatua hii inalenga kuweka wajibu wa mnunuzi kudai risiti ili kuweka mkazo katika mfumo mzima wa kuweka kumbukumbu za biashara. Kifungu hiki kinaipa mamlaka Mahakama kutoza faini kati ya sh. 30,000/= hadi sh. 150,000/= kwa kuzingatia kiasi cha manunuzi. Kwa kutoa wigo huo wa adhabu Mahakama itatoa adhabu kwa kuzingatia kiasi cha manunuzi.
levy na kutoa unafuu wa ushuru wa bidhaa kwenye shayiri ioteshwayo na inayolimwa hapa nchini. Serikali itayafanyia kazi mapendekezo haya tunavyokwenda mbele, kwa sababu yatakuwa yana impact kwenye mapendekezo ya mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na mapendekezo kwamba, kwenye Ibara ya 71(b)(1) kusamehe kodi ya majengo yanayotumika kwenye shughuli za kilimo. Sheria tayari inasamehe kodi ya majengo yanayotumika kwa ajili ya nyumba za ibada na kulelea watoto.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwasilishe majibu ya hoja zote ambazo tulizipokea kwa maandishi. Naomba tu nihitimishe kwa kusema Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2016 ni sehemu ya Bajeti ya Serikali niliyoiwasilisha mbele ya Bunge lako tarehe 8 Juni na umuhimu wake ni kuwa Muswada huu ndiyo utatuwezesha utekelezaji wa kisheria wa bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge 20 Juni. Ili Serikali iweze kutekeleza ahadi zake katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM, tunaomba Bunge lipitishe Muswada huu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile ili Serikali iweze kutatua kero zinazowakabili wananchi wetu hasa huduma za maji, elimu, afya na barabara tutahitaji fedha; na Muswada huu ndio unaidhinisha kisheria kodi na tozo na hatua mbalimbali za kiutawala za kukusanya mapato ya shilingi trilioni 29.5. Pia itatuwezesha kusimamia utekelezaji wa kauli mbiu ya kuongeza uzalishaji viwandani na kupanua fursa za ajira, lazima tukusanye mapato na nyenzo ya kufanya hivyo ni Waheshimiwa Wabunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016.
Mheshimiwa Naibu Spika, uamuzi wa kujenga Tanzania mpya, unahitaji hatua za kijasiri katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na Muswada huu umetafsiri hatua hizo kisheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, nawaomba Waheshimiwa Wabunge, mridhie Muswada huu ili upite na kuiwezesha Serikali iingie kazini kukusanya mapato kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania na kutekeleza bajeti hii ya kihistoria katika Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, naomba kutoa hoja.
Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2016
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kutoa shukrani za dhati kwako binafsi kwakuendesha vizuri majadiliano kuhusu muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma (The Public Procurement Amendment Act, 2016).
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini kwa kuendesha vyema vikao vya Kamati ya Bajeti wakati ikijadili Muswada huu. Aidha, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Wajumbe wote wa Kamati ya Bunge ya Bajeti kwa maoni na ushauri mzuri ambao umesaidia sana kuboresha Muswada huu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda kutambua michango iliyotolewa hapa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge, Serikali inakiri kwamba michango hiyo ilikuwa na afya. Aidha, hali hii ni kielelezo jinsi ambavyo Waheshimiwa Wabunge kama wawakilishi wa wananchi mmedhaminiwa kuhakikisha ununuzi wa umma ambao unatumia zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali unafanyika kwa ufanisi ili kupata ubora wa thamani iliyokusudiwa. Serikali imepokea ushauri huo na ninaahidi kwamba Serikali itafanyia kazi mawazo hayo mazuri yaliyotolewa. Ninawashukuru pia kwa pongezi za dhati zilizotolewa kwa Serikali kwa jitihada zilizofanyika kuandaa Muswada huu kwa kuzingatia maoni na ushauri wa wadau mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa sasa nitoe ufafanuzi wa baadhi ya hoja za Kamati ya Bajeti pamoja na Waheshimiwa Wabunge kama ifuatavyo:-
Hoja ya kwanza ambayo imesikika sana na imeendelea kusikika hata leo asubuhi ni ile ya kuwaondoa Madiwani katika mchakato wa ununuzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mapema tulipowasilisha muswada huu kupitia kifungu cha 11 Serikali ilikusudia kufuta kifungu cha 31(4) cha sheria ili kuondoa jukumu la usimamizi yaani oversight la Kamati ya Fedha na Mipango ya Halmashauri katika masuala ya ununuzi wa Halmashauri. Hata hivyo baada ya kutafakari maoni ya kamati kupitia aya “D” ya jedwali la marekebisho Serikali imerejesha jukumu la Kamati kama ilivyokuwa awali. (Makofi)
Aidha, kupitia kifungu cha 20 cha Muswada Serikali imefuta kifungu cha 60(4) ili kuondoa sharti la Kamati ya Fedha na Mipango ya Halmashauri kutekeleza majukumu ya kiutendaji ya kufanya uchambuzi yaani scrutiny wa mikataba kabla ya tuzo kutolewa kwa mzabuni na Afisa Masuhuli. Hivyo basi, kifungu hiki kimefutwa ili Kamati ya Fedha na Mipango ya Halmashauri iendelee na jukumu lake la usimamizi yaani oversight na kuchukua hatua stahiki kwa watendaji pale ambapo watendaji wameshindwa kutekeleza majukumu yao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya pili ilikuwa ni kuweka tafsiri ya maneno specialized goods and equipment ili kuondoa utata katika utekelezaji wa sheria. Serikali inakubaliana na pendekezo la Kamati kwamba matumizi ya maneno specialized goods and equipment yanaweza kuleta utata katika utekelezaji wa sheria. Hata hivyo, badala ya kuweka tafsiri ya maneno specialized goods and equipment Serikali kupitia aya A ya jedwali la pili la marekebisho imeondoa neno specialize ili kuleta maana iliyokusudiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya tatu, manunuzi ya Serikali yalingane na thamani ya fedha na kwamba gharama za ununuzi na matumizi ya magari zipunguzwe kupitia ununuzi wa jumla yaani bulk procurement.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Ibara ya 3 ya muswada imeweka sharti kwa ununuzi wa bidhaa na huduma za Serikali kuzingatia thamani halisi ya fedha. Aidha, Serikali hivi sasa kupitia GPSA imekuwa ikifanya ununuzi wa jumla wa magari ambayo kwa kiasi kikubwa umeokoa fedha nyingi za Serikali ikilinganisha na utaratibu uliokuwa ukitumika awali kwa kuwa kwa kila Taasisi au Wizara kufanyaununuzi binafsi wa magari. Serikali itaendelea na utaratibu huu kupitia Ibara ya 23 ya Muswada ambayo inaweka utaratibu wa kuruhusu ununuzi wa bidhaa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile napenda kutoa taarifa kwamba Serikali imepokea na inafanyia kazi ushauri wa Kamati kuhusu umuhimu na uharaka wa kupunguza gharama za ununuzi na matumizi ya magari, ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo ya magari kwa watumishi wanaostahili badala ya kuwapa magari ya ofisi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ilikuwa ni uanzishwaji wa Mfuko wa Uwekezaji wa Wakandarasi ili kuweza kutoa dhamana wakati wa kuomba zabuni. Serikali imepokea ushauri wa kamati na itaufanyia kazi; hata hivyo ni vyema zaidi wakandarasi nao kupitia umoja wao watafakari namna ambavyo wanaweza kuweka nguvu pamoja kuanzisha mfuko unaopendekezwa. Serikali kwa upande wake itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania hususani katika sekta binafsi ikiwemo sekta ya ujenzi ili kuongeza ushiriki wa sekta hii katika uchumi kwa kuboresha huduma za upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kuimarisha soko la mitaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ilikuwa kwamba Serikali itunge kanuni itakayobainisha vigezo vya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi za Zabuni za Halmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 31(3) cha sheria ya ununuzi wa Umma uundwaji wa bodi za zabuni katika Halmashauri hufanyika kwa mujibu wa kanuni zulizotayarishwa chini ya Sheria ya Fedha ya Serikali za mitaa sura ya 290. Kanuni ya 7 ya Kanuni za Uundwaji wa Bodi za Zabuni za Serikali zaMitaa imeweka bayana vigezo vinavyopaswa kuzingatiwa na Afisa Masuhuli wakati wa uteuzi wa wajumbe wa Bodi za Zabuni. Aidha, kanuni hizi imeweka sharti kwamba baada ya Afisa Masuhuli kuteuwa wajumbe wa bodi atapaswa kuwasilisha majina ya wajumbe pamoja na sifa zao kwenye Kamati ya Fedha na Mipango za Halmashauri kwa ajili ya kuidhinishwa na kuthibitishwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha Bodi za Zabuni za Halmashauri zinahusisha wajumbe wenye weledi wa kutosha ninatoa rai kwa Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe katika Kamati za Fedha na Mipango za Halmashauri kutumia vizuri mamlaka yao ya kuidhinisha wajumbe wa Bodi za Zabuni za Halmashauri ili kupata watu wenye sifa stahiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa kupitia Muswada wa Sheria ya Ununuzi yataanza kutumika lini. Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya tafsiri ya sheria mbalimbali Sura ya Kwanza, muswada huu utakapopitishwa na Bunge kuwa sheria utaanza kutumika tarehe ambayo utatangazwa na kuchapishwa katika gazeti la Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ili kuwezesha utekelezaji wa mapendekezo ya muswada huu hivi sasa Wizara ya Fedha na Mipango ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha kanuni zitakazowezesha utekelezaji wake kuanza haraka iwezekanavyo. Kinachochelewesha kidogo ni kwamba ni ukamilishaji wa kanuni.
Mheshimiwa Naibu Spika, ilikuwepo hoja kwamba kanuni ziandaliwe ili kutoa fursa ya ushirikiano baina ya Halmashauri na wahisani katika utekelezaji wa miradi ya PPP.
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi kwamba Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 inasimamia masuala ya ununuzi yanayohusu fedha za Serikali pekee. Ununuzi katika miradi ya PPP baina ya Halmashauri na wahisani unapaswa kutumia taratibu za ununuzi ambazo zinasimamiwa chini ya kifungu cha 76 cha Sheria ya Public Private Partnership ambapo miradi ya PPP isiyozidi dola za kimarekani milioni 70 na umri wa miaka 15 inaidhinishwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo kutokana na umuhimu wa miradi ya aina hii kwa wananchi Serikali tunapokea ushauri wa Kamati na tutaufanyia kazi kupitia kanuni hizo ambazo ziliandaliwa chini ya sheria ya Public Private Partnership.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Umma zinatoa huduma kwa bei ya juu kuliko bei ya soko.
Mheshimiwa Naibu Spika, yamekuwepo malalamiko mengi kuhusu Taasisi na Mashirika ya Umma yanayofanya biashara kutoa huduma kwa gharama za juu kuliko bei ya soko. Serikali katika kukabiliana na tatizo hili imechukua hatua, kwa mfano Ibara ya 24 imeweka utaratibu utakaoziwezesha Taasisi zinazojiendesha kibiashara kama TEMESA, TBA na National Housing Corporation kufanya manunuzi yake moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kupata bidhaa kwa bei ya chini na hivyo kuziwezesha kuwa na unafuu wa bei pindi zitakapotoa huduma. Lakini vilevile Serikali kupitia Ibara ya 38 ya Muswada huu imeweka utaratibu utakaowezesha kuandaliwa kwa kanuni zitakazoweka utaratibu mahususi wa ununuzi utakaofuatwa na taasisi hizi na kuziwezesha kupata bidhaa na huduma kwa bei nafuu na hivyo kuwawezesha kuuza huduma au bidhaa wanazozalisha kwa bei ya soko.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nisisitize tu kwamba baada ya Serikali kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato na ninazidi kuwaomba Watanzania wote na Waheshimiwa Wabunge kulipa kodi ipasavyo ili kuipa uwezo Serikali kulipa watoa huduma kwa wakati. Kwa upande wetu Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba watoa huduma wanalipwa kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba majibu kuhusu hoja zilizowasilishwa na Kamati kupitia jedwali la marekebisho yaani amendment schedule. Pamoja na hayo maoni ya jumla ambayo nimekwisha kuyasemea Kamati ya Bajeti imetoa mapendekezo mengine katika hilo jedwali la marekebisho ambalo limewasilishwa hapa Bungeni. Ningependa kutoa majibu kama ifuatavyo:-
Moja ilikuwa ni kufuta Ibara ya 2(a) ya Muswada ili kuondoa tafsiri ya maneno budget approving authority. Serikali tayari imeridhia pendekezo hili lilipowasilishwa kwenye Kamati wakati wa mjadala wa muswada huu ambapo kupitia aya ya “A” ya jedwali la marekebisho la Serikali Ibara ya 2(a) imefutwa ili kuondoa tafsiri hiyo kama ilivyopendekezwa na Kamati.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali inakubaliana na mapendekezo ya kiuandishi yaliyobainishwa katika aya ya “A”, “B” ya jedwali la marekebisho la Kamati ya Bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, pendekezo lingine lilikuwa ni kuweka tafsiri ya maneneo local firms ili ihusishe kampuni zinazomilikiwa na watanzania kwa asilimia 100 pekee.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakubaliana na pendekezo la tafsiri ya maneno haya kama yalivyobainishwa katika aya ya “A”, “C” ya jedwali la marekebisho ya Kamati ya Bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, kuweka tafsiri ya maneno life saving commodities na kurekebisha kifungu cha 67 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma ili kuweka utaratibu wa ununuzi wa lifesaving commodities. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mapendekezo yaliyobainishwa katika aya ya A, “D”, “C”, “B”, “D” ya jedwali la marekebisho ya Kamati ya Bajeti yana malengo yafuatayo:-
Kwanza ni kuweka utaratibu wa ununuzi wa life saving commodities ndani ya sheria na pili ununuzi wa life saving commodities ufanyike kwa utaratibu wa dharura emergence procurement.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe ufafanuzi kwamba ununuzi wa dawa na vifaa tiba ikiwemo life saving commodities tayari umebainishwa chini ya kanuni ya 139 hadi 147 ya Kanuni za Sheria ya Ununuzi wa Umma. Aidha, kupitia Ibara ya 24 ya Muswada SerikaLI imeweka utaratibu utakaowezesha ununuzi wa bidhaa ikiwemo dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ununuzi wa life saving commodities kufanyika kwa utaratibu wa dharura, Ibara ya 65 ya Sheria ya Ununuzi wa Umma tayari imeweka utaratibu wa ununuzi wa dharura na mazingira yake. Chini ya utaratibu huu, ununuzi wa dharura unahusisha bidhaa au huduma ya aina yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia Kamati ina marekebisho katika Ibara ya 24 ya Muswada kwenye Ibara ya 65B(1). Serikali inakubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Bajeti ya aya ya C(a)(i),(ii) na (iii) yaliyobainishwa kwenye Jedwali la Marekebisho la Kamati ambayo yana lengo la kufanya marekebisho ya kiuandishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kidogo juu ya hoja za Waheshimiwa Wabunge wengine. Hoja moja ilikuwa ni kuweka masharti kwa taasisi nunuzi kununua bidhaa zinazopatikana hapa nchini. Serikali imetekeleza ushauri huu ambapo kupitia Ibara ya 18 ya Muswada imebainisha utaratibu wa kutoa upendeleo maalum kwa kampuni zitazotumia bidhaa au malighafi zinazozalishwa Tanzania. Kampuni za aina hii zitapewa upendeleo maalum pindi zitakaposhiriki katika zabuni za Serikali tofauti na kampuni ambazo zitatumia bidhaa au malighafi zinazozalishwa nje ya nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ilikuwa ni bei ya bidhaa na huduma zinazopangwa na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kwamba ni kubwa na haziendani na bei za soko. Serikali kupitia Ibara ya 17 ya Muswada imefanya marekebisho katika Ibara ya 50 ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ili kwanza kuondoa sharti la kuwepo kwa mikataba baina ya Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) na wazabuni iliyofungamanishwa na bei ili kuondoa utaratibu wa kupanga bei elekezi na badala yake taasisi nunuzi zitafanya utaratibu wa ununuzi kwa kuzingatia bei ya soko kwa wakati husika. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama ya ununuzi kupitia taasisi hii ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa kipindi kirefu. Pili, ni kufafanua tafsiri ya open framework agreement ili kubainisha mikataba baina ya GPSA na wazabuni haitahusisha bei. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ilikuwa kwamba National Board of Materials Management hawakushirikishwa kwenye mchakato wa marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma. Napenda kutoa taarifa kwamba iliyokuwa Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (NBMM) ilifutwa na Serikali kupitia Sheria ya Bodi ya Wataalam na Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board Act) na kuundwa chombo kingine ambacho kinaitwa Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board (PSPTB). Bodi hii ndiyo yenye dhamana ya kusimamia wataalam wa masuala ya ugavi. Aidha, katika hatua zote za maandalizi ya Muswada huu PSPTB imehusishwa kwa kiasi kikubwa. Hata navyozungumza, wataalam wake ni sehemu ya timu ya wataalam wa Wizara ya Fedha na Mipango iliyoshiriki katika majadiliano ya Muswada huu kwenye Kamati ya Bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ni kwamba sifa za Mtendaji Mkuu wa PPRA ziwe zinatambulika na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi. Kwa mujibu wa Ibara ya 23(3) ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Mtendaji Mkuu anaweza kuwa mtu mwenye sifa zozote za elimu kama ilivyobainishwa kwenye Muswada na ambaye ana ujuzi katika masuala ya ununuzi. Hivyo, kutokana na sharti hili mtu ambaye hana ujuzi katika masuala ya ununuzi hawezi kuteuliwa katika nafasi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba Kanuni za Ununuzi za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu zifanane ili kupunguza uvunjifu wa taratibu za ununuzi wa umma. Serikali imepokea mapendekezo haya na tutayafanyia kazi pasipo kuathiri dhana ya ugatuaji madaraka (D by D). (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, palikuwa na hoja pia kwamba ununuzi wa dawa na vifaa tiba uwekewe utaratibu tofauti. Kama nilivyokwishaeleza wakati nikijibu hoja za Kamati ya Bajeti, tayari utaratibu maalum wa ununuzi wa madawa na vifaa tiba umebainishwa chini ya Kanuni ya 139 - 147 ya Kanuni za Sheria ya Ununuzi wa Umma zikisomwa pamoja na Ibara ya 24 ya Muswada.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba, je, GPSA itaedelea kuchagua wazabuni na itaendelea kutoza asilimia mbili ya thamani ya zabuni? GPSA itaandaa orodha ya wazabuni kwa ajili ya kupunguza muda na gharama kwa niaba ya taasisi za Serikali. Hata hivyo, utaratibu huu hautahusisha kupanga bei ya bidhaa au huduma. Aidha, kupitia marekebisho yatakayofanywa kwenye Kanuni, Serikali itafanya mapitio ili kupunguza kiwango cha asilimia 2 kinachotozwa na GPSA kwenye kila thamani ya zabuni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba sheria iweke wazi kiasi kitakachotengwa kwa ajili ya makundi maalum. Kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya Muswada, kanuni zitakazoandaliwa baada ya kupitishwa kwa Muswada huu zitabainisha viwango mahsusi vya thamani za zabuni za taasisi nunuzi zitakazotengwa kwa ajili ya makundi ya vijana, walemavu na akina mama. Lengo la kubainisha viwango hivyo kupitia kanuni, ni kuweka urahisi wa kufanya mabadiliko wakati wowote endapo viwango husika vitaonekana ni vidogo pasipo kusubiri kuwasilisha tena hapa Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba viongozi wa mikoa waache kuingilia Bodi za Zabuni za Halmashauri. Sheria ya Ununuzi wa Umma inasisitiza uhuru wa Bodi za Zabuni katika kutekeleza majukumu yake. Kuingilia shughuli za bodi ni uvunjaji wa sheria na kanuni zinazosimamia ununuzi katika halmashauri. Hivyo, napenda kutoa rai kwa viongozi wa mikoa kuzingatia utaratibu uliowekwa kisheria. Kanuni ya 33 ya Kanuni za Kusimamia Ununuzi wa Umma inaelekeza ni wakati gani viongozi wa mikoa wanaweza na wafuate utaratibu gani kisheria pale ambapo inaonekana pana haja ya kuingilia michakato hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu pika, naomba nimalize kwa kusema yafuatayo:-
(i) Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2016 ni ahadi ya Serikali kupitia bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 ambapo nilibainisha kwamba Serikali itawasilisha Muswada huu katika Mkutano huu wa Bunge unaoendelea.
(ii) Pamoja na mambo mengine, umuhimu wa Muswada huu kwanza ni kutekeleza azma ya Serikali katika bajeti ya kuwa na matumizi bora ya fedha za Serikali kwa kuwa na sheria madhubuti ya ununuzi wa umma na kuziba mianya ya upotevu wa fedha katika ununuzi wa umma na kuhakikisha ununuzi unawiana na thamani ya fedha itakayotumika.
(iii) Kutekeleza ahadi ya Serikali katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya kuwezesha kiuchumi makundi maalum na hususani vijana, wanawake na walemavu kwa kuweka upendeleo maalum kwa makundi haya ili kuyawezesha kushiriki katika zabuni za Serikali ili kuongeza ajira na kipato. (Makofi)
(iv) Kuiwezesha Serikali kusimamia utekelezaji wa kaulimbiu ya ujenzi wa viwanda, kuongeza uzalishaji viwandani na kupanua fursa za ajira kwa Watanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya soko kwa bidhaa na malighafi zinazozalishwa hapa nchini kwa kuhimiza matumizi ya bidhaa na huduma hizo kama kigezo cha upendeleo katika kupata zabuni za Serikali.
(v) Kujenga uwezo wa wataalam wa Watanzania pamoja na kampuni zinazomilikiwa na Watanzania kwa kuwapa fursa zaidi kushiriki katika miradi ya Serikali kwa kupitia kampuni hizo moja kwa moja au kwa kushirikiana na kampuni za nje. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, nawaomba Waheshimiwa Wabunge mridhie na kuupitisha Muswada huu ili kuiwezesha Serikali kutimiza azma yake ya kulinda matumizi ya fedha za Serikali, kukuza uchumi wa nchi na kuweka mazingira ya kuwawezesha kiuchumi wananchi wake kwa ujumla.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo haya, naomba kutoa hoja.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima naomba nichukue fursa hii kukushukuru wewe binafsi na Bunge lako tukufu kwa kunipatia nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala huu kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (The Public Private Partnership (Amendment Act) Bill, (No. 5) 2018). Nakushukuru kwa kuongoza mjadala wa muswada huu kwa umahiri na kwa msingi huo maoni na michango iliyotolewa imeiwezesha Serikali kuboresha maudhui ya muswada huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee naomba kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa George Boniface Simbachawene, kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia wakati wa kuujadili muswada, maoni na ushauri waliotupatia Kamati baada ya kusikiliza maoni ya wadau, yametusaidia kuboresha maudhui ya muswada huu kama majedwali ya marekebisho yanavyosomeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru pia Mheshimiwa Halima James Mdee kwa hotuba aliyoitoa kwa niaba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwenye Wizara ya Katiba na Sheria. Kwa namna ya pekee napenda kumshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusimamia shughuli za Serikali vizuri kwa kutupatia ushauri na maelekezo kila siku ambayo yametuimarisha na kuboresha utendaji wetu wa kazi. Nawashukuru sana Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu kwa ushirikiano ambao walituonesha mimi pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa maandalizi na majadiliano ya muswada huu katika hatua zote. Pia nawashukuru watendaji wa Wizara walioshiriki kwenye hatua za maandalizi na majadiliano ya muswada huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mjadala wa muswada huu jumla ya Waheshimiwa Wabunge 37 wamechangia muswada huu, kwa hiyo kwa namna ya pekee ninawashukuru Wabunge wote waliochangia 31 kwa kuongea na sita kwa maandishi. Kipekee nimshukuru sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi kwa ufafanuzi mahiri wa maeneo ya kisheria yaliyogusa muswada huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yao mizuri waliyoitoa wakati wa majadiliano kwenye Kamati na hapa ndani ya Bunge, bila kuwasahau Wabunge walioleta majedwali ya marekebisho. Tumepokea maoni mazuri ambayo yamelenga kuboresha muswada huu na kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wakichangia muswada huu kwa kweli ni ushahidi kwamba Bunge hili linatambua umuhimu wa mapendekezo ya kurekebisha hii sheria na katika michango yao Wabunge wametoa hoja mbalimbali ambazo na mimi ningependa nizitolee ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Bunge ya Bajeti ilitoa hoja kwamba Serikali iweke sharti kwa Wizara, Idara, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa kumjulisha Waziri husika kuhusiana na orodha ya miradi ya ubia inayopendekezwa kabla ya kuwasilishwa kwenye kituo cha ubia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri huu wa Kamati wa kurekebisha kifungu cha 4(6) ili kuweka sharti ya kuzitaka Wizara, Idara, Wakala na Mamlaka za Serikali kumjulisha Waziri husika kwenye Kituo cha Ubia (PPP Center) tumelizingatia na tumeongeza jedwali la nyongeza la marekebisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Kamati ya Bunge ya Bajeti iliishauri Serikali itumie mwongozo wa kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa na tija, lakini pia kuwa Serikali iwezeshe Mfuko wa Uwezeshaji wa Miradi ya Ubia ili uweze kukidhi mahitaji ya msingi ya miradi. Serikali iweke mazingira wezeshi ili kuongeza Benki za Uwekezaji nchini kuongeza miradi ya ubia lakini pia Kituo cha Ubia kiwe na mpango mkakati wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma kwamba Serikali ifanye mabadiliko kwenye sera na sheria ya uwekezaji ili izingatie uwezeshaji kwenye miradi ya ubia na kwamba Serikali iimarishe soko la mitaji na hisa kwa kuangalia taratibu nyingine zitakazosaidia upatikanaji wa mitaji kupitia masoko ya kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwa kifupi kwamba Serikali imepokea ushauri huu mzuri wa Kamati na itauzingatia katika utekelezaji wa programu na mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa PPP nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani alishauri kwamba utendaji wa Serikali unaonesha kwamba tunarudi kwenye sera za ujamaa ambapo sekta binafsi hairuhusiwi kujenga uchumi. Lakini pia alihoji ni nani msimamizi wa PPP pia akataka tafsiri ya neno Wizara, Waziri kwamba haijaeleweka bayana ni nani msimamizi wa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa inaweka misingi ya uchumi imara kwa kuushirikisha sekta binafsi kuendesha uchumi nchini ambapo mipango ya maendeleo imekuwa inaweka bayana dhamira hii ya Serikali na ni dhahiri kuwa ukuaji wa uchumi wetu unachangiwa na sekta binafsi kama engine ya ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla. Hili linadhihirishwa kwa kutunga sheria, sera pia taasisi zinazoruhusu ushirikishwaji huu wa sekta binafsi. Mfano wa dhahiri kabisa ni nii sheria ya uwekezaji Tanzania, lakini pia sheria ambayo tunaifanyia marekebisho sasa kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. Kwa hiyo, kwa kuzingatia ukweli huu Serikali imewasilisha mapendekezo ya marekebisho ili kushirikisha sekta binafsi na kutoa fursa kwa sekta hiyo kutekeleza miradi ambayo inahusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, kwa mujibu wa kanuni na mgawanyo wa utekelezaji wa majukumu ya Mawaziri kama nilivyosema wakati ninawasilisha hoja, kanuni namba 144 ya mwaka 2016, imeweka bayana kwamba masuala ya PPP yanasimamiwa na Waziri wa Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa tafsiri ya neno Waziri na Wizara, muswada unapendekeza tafsiri ya neno Minister na Ministry au Waziri na Wizara inayosimamia masuala ya PPP na kama Mwenyekiti aliyekuwa anaongoza kikao alivyolieleza vizuri, tunataka kuondoa hitaji la kufanya marekebisho ya mara kwa mara hasa pale ambapo usimamizi wa PPP unakuwa umehamishiwa Wizara nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulikuwepo mchango wa Mheshimiwa Ally Saleh Ally, Mheshimiwa Lucia Mlowe, Mheshimiwa Omari Kigua na Dkt. Immaculate Sware Semesi. Kimsingi kulikuwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kwamba siku za kuidhinisha miradi chini ya kifungu cha 7(a) ni nyingi na wao walipendekeza zipunguzwe kutoka siku 21 hadi 10, lakini pia kwamba benki itakayotumika katika mradi wa PPP itegemee makubaliano kati ya Serikali na wabia badala ya kufungua akaunti hiyo Benki Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wa siku 21 umewekwa kwa kuzingatia ukubwa wa uchambuzi ambao unatakiwa kufanyika kwenye mradi husika ili tuepuke hasara zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo. Miradi hii tunategemea mingine iwe mikubwa na ya thamani kubwa sana, kwa hiyo hatutaki kuifanya kwa haraka haraka, tunataka tujiridhishe na tunaamini kwamba kwa kuangalia pia uzoefu wa nchi nyingine tunaona kwamba siku 21 zitatuwezesha kufanya hiyo kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa benki itakayotumika, kifungu cha 9 cha muswada hakibainishi sharti la kufungua akaunti ya mradi Benki Kuu, mapendekezo ya marekebisho yanakusudia kuondoa sharti la kufungua akaunti Benki Kuu na hivyo kufungua katika benki yoyote badala ya Benki Mahiri ya Uwekezaji. Pia akaunti inayozungumziwa hapa ni kwa ajili ya mfuko wa uwezeshaji yaani PPP Facilitation Fund na siyo akaunti kwa ajili ya wabia kuweka fedha zao za kutekeleza mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kulikuwa na hoja kwamba miradi ambayo ni unsolicited isiwekewe masharti yoyote. Masharti ambayo tumependekeza lengo lake ni kuwa na miradi yenye tija kwa Taifa na hivyo kuepuka kuwa na miradi mibovu kwa kusingizia kuwa kiuhalisia na uzoefu tuliopata tunataka kukwepa wawekezaji ambao siyo makini, ambao wamekuwa wanawasilisha miradi Serikalini ambayo hawakuwa wamepanga kuitekeleza na pia miradi mingine kutokuwa na tija kwa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe tu mfano, kama hatutaweka masharti haya upo uwezekano kabisa wa kupata unsolicited proposal ambayo inaleta mradi ambao unashindana na mradi mwingine ambao Serikali imepanga kufanya. Pia upo uwezekano wa kupata miradi ambayo haina tija kwa Taifa letu, kwa hiyo, ni muhimu sana haya masharti yakawepo kwa unsolicited proposal.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja pia kwamba muda uliopendekezwa katika kifungu cha 12 cha miezi sita badala ya kila robo mwaka ni mrefu sana. Huu muda wa miezi sita (nusu mwaka) ni muafaka kwa kuwa Serikali huwa inawasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti yake kila nusu mwaka.

Waheshimiwa Wabunge, mnakumbuka kwamba tulifanya marekebisho kwenye Sheria ya Bajeti ili tuwe na muda wa uhalisia ambapo Baraza la Mawaziri linafanya marejeo ya utekelezaji wa bajeti na hivyo utekelezaji wa miradi ya PPP pia itafuata utaratibu huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na mawazo kwamba PPP Center iwe Idara ndani ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kupunguza gharama kwa Serikali. Miradi ya ubia ambayo inatekelezwa chini ya sheria hii ni tofauti na ile ambayo inatekelezwa chini ya Sheria ya Uwekezaji na Sura ya 38 ambayo ndiyo miradi ya kibiashara kwa asilimia 100, kabla ya mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2014 kitengo cha uratibu wa PPP kilikuwa chini ya TIC ambapo utekelezaji wa uratibu wa miradi ya PPP ulionekana kuwa na changamoto na hivyo kusababisha Serikali kufanya marekebisho ya sheria hii mwaka 2014, kwa hiyo bado tunapenda kulishauri Bunge lako tukufu kwamba hiki kituo kisiwe ndani ya TIC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ruth Mollel alishauri kwamba utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ishirikishe sekta binafsi kupitia PPP. Sina ugomvi na hili lakini nilitaka tu niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge, si zamani sana tarehe 2 Mei tulikuwa na ugeni wa watu maarufu Profesa Joseph Stiglitz ambaye mnajua ni mshindi wa Nobel ya uchumi lakini pia amewahi kuwa Chief Economist wa Benki ya Dunia. Tulikuwa pia na Profesa Kaushik Basu naye amewahi kuwa Chief Economist wa Benki ya Dunia lakini pia tulikuwa na Profesa maarufu sana kutoka Uingereza, Mama mahiri Profesa Sabina Alkire na siku ile tulikuwa tunajadiliana kuhusu equitable growth and human development in a resource based economy kwa hapa Tanzania. Moja ya vitu ambavyo vilitushtua akili zetu, wabobezi hawa ambao miaka yote wamekuwa wanasisitiza kwamba tuende kwenye soko, walisisitiza sana siku ile umuhimu wa kuwa makini na kutumia The State Strategically katika kuharakisha maendeleo ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya azimio la mkutano ule, naomba uniruhusu niseme kwa kiingereza inasema; “The State has a key role to play in the economy, by addressing market failures directly, directly providing goods and services in some circumstance.” Katika mazingira ya Tanzania mtakumbuka kipindi fulani hapa tulitoa challenge hapa kwamba jamani katika mazingira ya nchi yetu hawa ambao tunasema wawekezaji wapo, wako wapi? Tulitoa fursa hapa ambaye analeta mwekezaji aje awekeze kujenga reli ya kutoka Mtwara kwenda Mbambabay na matawi yake kwenda Mchuchuma na Liganga, aje! Mpaka leo hiyo offer imeshindikana. Kwa hiyo, tusijidanganye kabisa. Miradi ambayo inaweza kuwa commercial lakini ni of national strategic importance msiweke Serikali pembeni. Hivi tutakaa tungoje, tukae na hii reli iliyojengwa mwaka 1905 mpaka Yesu Kristo ateremke? Haiwezekani! Kwa hiyo, ninawasihi sana hivi vitu vingine, akili za kuambiwa tuchanganye na za kwetu kwa manufaa ya Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na wazo kwamba asilimia tatu ya kiasi cha fedha ya miradi ya PPP ambayo inapendekezwa kama commitment fee swali lilikuwa ni kwamba hiyo deposit itawekwa wapi. Kiutaratibu fedha za aina hii zinahifadhiwa na Accounting Officer, Afisa Masuuli katika Akaunti za Amana (Deposit Account). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja hii, Serikali imeboresha kifungu cha 10(3)(a) katika jedwali la marekebisho kwa kumpa Waziri mamlaka ya kutunga kanuni zitakazobainisha utaratibu wa utunzaji na urejeshaji wa hizo fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ilisemwa kwamba commitment ile ya asilimia tatu iondolewe katika miradi ya unsolicited. Dhamana ya kiwango kisichozidi asilimia tatu lengo letu ni kuhakikisha uwepo na uthibitisho na uhakika na nia ya mwekezaji katika kuwekeza kwenye miradi aliyoibuni. Utaratibu huu unatuwezesha kuepuka uwekezaji usiokuwa makini. Kwa hiyo, tunaamini kabisa kwamba hii asilimia tatu ibaki isiondolewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepokea mawazo mazuri sana yaliyotolewa na Mheshimiwa Balozi Adadi Rajab, Mheshimiwa Yussuf Salim Hussein na Mheshimiwa Oran Njeza, hususan kuhusu kuwajengea uwezo wataalam wa sheria katika kufanya majadiliano ya mikataba na uandishi wa mikataba. Kwa kweli, huu ni ushauri mzuri na tutauzingatia. Kifungu cha 4(6) cha Sheria ya PPP kimebainisha maeneo ya fursa ambayo mwekezaji anaweza kuomba uwekezaji wa PPP, lakini baada ya uchambuzi wa miradi kufanyika na kupata idhini ya Kamati ya Kuidhinisha Miradi (Steering Committee), miradi iliyoidhinishwa itatangazwa katika Gazeti la Serikali na magazeti mengine. Kwa hiyo, kabla ya hatua hizo ni vigumu kubainisha ni miradi ipi itatekelezwa kwa PPP ili itangazwe kwa umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mashimba Ndaki namshukuru sana kwa darasa lake zuri sana kuhusu PPP. Kwa kweli alitoa elimu nzuri na tunapokea ushauri kama Serikali na tutauzingatia wakati wa kuingia mikataba na kutoa hakikisho kulingana na mahitaji ambayo yanahusika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishauriwa na Mheshimiwa Yussuf Salim Hussein kwamba Serikali itenge bajeti ya miradi ya PPP. Tunapokea ushauri na tutauzingatia. Kupitia muswada huu imependekezwa kufanyia marekebisho ya Sheria ya Bajeti ili kuwezesha miradi ya PPP kutengewa bajeti. Mheshimiwa Mbaraka Dau alishauri kuwa na mawasiliano ndani ya Serikali kuhusu miradi ya Serikali inayotarajiwa kutekelezwa kwa PPP ili kuwa na kauli moja ndani ya Serikali. Huu ni ushauri mzuri na kwa kweli, inatakiwa iwe hivyo wakati wote. Kwa hiyo, tutaufanyia kazi ili kuboresha mawasiliano ya kiutendaji ndani ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Martha Umbula alishauri Serikali itekeleze andiko la kimkakati (blueprint) ili kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo miradi ya PPP. Ushauri ni mzuri na tutaufanyia kazi ipasavyo. Kama ambavyo tumekuwa tunaeleza Baraza la Mawaziri lilishaujadili na lilishatoa maelekezo ili kuanza kuendelea kuutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Balozi Dkt. Kamala alishauri kwamba Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe Mjumbe kwenye Kamati ya Uidhinishwaji wa Miradi ya PPP ili kuondoa ulazima wa mikataba ya miradi ya PPP kupelekwa kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya vetting.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilifahamishe Bunge lako tukufu kwamba Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mjumbe wa Kamati ya Maamuzi ya PPP yaani ile Steering Committee, lakini hata hivyo utaratibu wa kuwasilisha mkataba Ofisi ya Attorney General kwa ajili ya uhakiki, hili ni hitaji la kisheria chini ya Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (The Attorney Generals’ Discharge of Duties Functions Act, 2015). Kwa hiyo, maana yake tu ni hiyo, bado miradi hii itabidi iende kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali for vetting.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilishalisemea lile ushauri wa Mheshimiwa Njeza kwamba vijana wanaomaliza Vyuo Vikuu wapewe mafunzo kuhusu PPP, tunaupokea kabisa ushauri huu ni ushauri mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Chiza pia alitushauri kuhusu kutoa elimu juu ya uelewa wa PPP kwa watendaji ndani ya Serikali na sekta binafsi na juu ya miradi ya unsolicited proposals, ushauri tunaupokea na tutauzingatia. Na tumeweka vigezo kwa upande wa hiyo miradi ambayo ni unsolicited.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya naomba niahidi kwamba maelezo ya kina ya kufafanua hoja zote tulizozipokea tutayawasilisha kwenye meza yako kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo naomba kutoa hoja.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwako binafsi kwa kuendesha vizuri majadiliano kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2018. Napenda kutambua michango ambayo imetolewa na Kamati ya Bajeti hususani Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza au kwa maandishi hapa Bungeni. Nawashukuru wote kwa michango yenu.

Mheshimiwa Spika, jumla ya Waheshimiwa Wabunge 21 wamechangia katika kuboresha Muswada huu, ambapo Waheshimiwa Wabunge 15 wamechangia kwa kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge sita wamechangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nifafanue baadhi ya hoja ambazo zimetolewa na Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti pamoja na Waheshimiwa Wabunge ambazo ningependa nizitolee ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti ilitoa hoja ya kuongeza aya nyingine ambayo itaruhusu ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji vikali yaani spirits vinavyotengenezwa hapa nchini kwa mchuzi wa zabibu unaotengenezwa hapa nchini kwa kiwango kisichopungua asilimia 75 kinachotoza kodi ya kiwango cha Sh.450 kwa lita.

Mheshimiwa Spika, najua na wewe unalima zabibu nami najifunza naomba nitoe maelezo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, huko nyuma Serikali iliwahi kutoa msamaha wa ushuru wa bidhaa kwa kiwanda cha kutengeneza valour ambacho ni kiwanda tanzu cha TBL. Lengo la kusamehe kodi hiyo ni kutoa unafuu kwa ajili ya kiwanda hicho ili kiweze kununua mvinyo yaani mchuzi unaozalishwa na kampuni ya CETAWICO na hivyo kuwezesha wakulima wa zabibu kupata soko la uhakika wa zabibu.

Mheshimiwa Spika, msamaha huo ulitolewa kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa Bidhaa kwa kipindi cha miaka mitano, mwaka 2002 mpaka mwaka 2007 kwa masharti maalum na ili kuweza kudhibiti matumizi ya msamaha huo kwa kuanzia hati ya msamaha (GN) ilitolewa kwa miaka miwili kwa sharti la kuongeza muda iwapo watakuwa wametekeleza makubaliano yaliyowekwa, yaani masharti ya msamaha huo. Palikuwepo na performance indicators ambazo zilikubaliwa.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maoni ya Wabunge juu ya kuweka mfumo wa kodi ya ushuru wa bidhaa ili kusaidia kiwanda cha CETAWICO na wakulima wa zabibu, Serikali inaangalia uwezekano wa kuweka utaratibu kama huo ambapo itaingia mkataba na viwanda vinavyotumia mchuzi huo na kutoa msamaha huo wa ushuru wa bidhaa kwa kipindi maalum. Serikali itaweka vigezo maalum ili kuhakikisha kuwa msamaha huo unasaidia viwanda vinavyotengeneza mchuzi na kuendelea kuhamasisha kilimo cha zabibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, iwapo Serikali itapunguza ushuru wa bidhaa wa pombe kali inayotokana na mazao ya zabibu ambayo inaitwa valour, HS code 22.08 ambayo inazalishwa hapa nchini, Serikali itapoteza mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 18 kwa mwaka, kwa kipindi hiki bado inatuwia vigumu kupata mahali pa kupata hizi mbadala shilingi bilioni 18. Kwa hiyo naomba utaratibu huu tukiuzingatia tutakuwa tumeweza kutekeleza kile ambacho wakulima wa zabibu wanahitaji.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti pia ilishauri kwamba tuongeze ushuru wa bidhaa kwa Sh.50 katika juisi ambayo inaagizwa kutoka nje, HS code 20.09.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 124(2) cha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura ya 147 kinaelekeza kuongeza viwango wa ushuru wa bidhaa kwa kiasi cha mfumuko wa bei au viashiria vingine vya uchumi jumla, hivyo ongezeko lililofanywa kwenye juisi ni kwa kuzingatia utaratibu huo.

Mheshimiwa Spika, tulishauriwa pia kwamba tuongeze ushuru wa bidhaa kwa Sh.500 kwa bidhaa zenye HS code 2204.10.00, HS code 2204.21.00 na HS code 2204.29.00.
Kifungu cha 124(2) cha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura hiyo ya 147 kinaelekeza kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaa kama nilivyokwishasema kwa kiwango cha mfumuko wa bei au viashiria vingine na hivyo ongezeko ambalo limefanywa kwenye bidhaa tajwa kutoka nchi za nje ni kwa kuzingatia utaratibu huo.

Mheshimiwa Spika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amezungumzia kwa kifupi kuhusu kufuta Sheria iliyoanzisha Tume ya Mipango nami naomba niongezee maelezo, hasa kwa kuzingatia kwamba nilikuwa Mkuu wa Tume ya Mipango takribani kwa miaka sita. Nilieleza hili wakati wa kuhitimisha bajeti tarehe 26, kwamba kwa kweli mapendekezo haya ni mabadiliko ya kimuundo na siyo kufuta kazi muhimu za kupanga mipango ya Maendeleo ya Taifa kwa muda wa kati na mrefu.

Mheshimiwa Spika, pia nilieleza kwamba ukiangalia historia ya muundo wa Tume ya Mipango iko wazi kabisa tumekuwa tunahama. Kuna nyakati Mipango ilikuwa ni Tume, kuna wakati Mipango ikawa ni Wizara inayojitegemea, kuna wakati hata huko nyuma Mipango ilikuwa ni sehemu ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, nilieleza kwamba hata ukiangalia nchi jirani ya Uganda, nchi jirani ya Rwanda wao nao kazi ya kupanga, taasisi inayopanga iko ndani ya Wizara na inaitwa Ministry of Finance and Economic Planning. Lengo hili la kuunganisha taasisi hizi mbili nilieleza kwamba, ugawaji wa rasilimali inakuwa ni gumu kweli wakati hizi taasisi mbili zimetenganishwa, kwa hiyo ni sababu moja ya msingi sana. Sababu ya pili Serikali hii ilishaamua kwamba tujitahidi kadri inavyowezekana kupunguza gharama za Serikali. Hivyo, hiyo ni kati ya mambo yaliyozingatiwa.

Mheshimiwa Spika, kubwa kazi zote ambazo zinafanywa na Tume ya Mipango zimeendelea kufanyika. Watumishi wale baada ya kuwahamishia ndani ya Wizara ya Fedha bado wameendelea kuandaa Mpango wa Maendeleo wa mwaka, kwa kuzingatia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Dira yetu ya Maendeleo ya Taifa 2025. Pia wameendelea kufanya monitoring and evaluation kwa kukagua miradi mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, pia Wataalam hawa tayari wameshaandika mkakati wa kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo ya miaka mitano. Kwa hiyo, hili ndilo jambo la msingi kazi zake zimeendelea kama kawaida kabisa na zinapokuwa chini ya Wizara ya Fedha sasa inakuwa ni rahisi zaidi kuhakikisha kwamba mahitaji yake yanazingatiwa.

Mheshimiwa Spika, yapo maeneo ambayo pia bahati nzuri tulikubaliana na Kamati ya Bajeti labda haya niyaache kwanza kama muda utaruhusu nitayarejea. Kamati ya Bajeti inapendekeza kupandisha tozo ya petrol na diesel kutoka Sh.313 kwa lita hadi Sh.363 kwa lita ambayo ni ongezeko la Sh.50 kwa lita na kiasi hiki cha fedha kinapendekezwa ili kiweze kupelekwa kwenye Mfuko wa Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kupandisha tozo ya mafuta ya petrol na diesel kutafanya bidhaa hiyo kupanda bei na hatimaye kupandisha bidhaa nyingine nchi nzima. Serikali imelitafakari sana jambo hili, tumefanya uchambuzi wa kina, tumetazama mwenendo wa bei ya mafuta katika soko la dunia, ni dhahiri kabisa kwamba bei ya mafuta inapanda. Hata ukiangalia projection za mwaka ujao wa fedha bei ya mafuta inaendelea kupanda, hii itaathiri sana mfumuko wa bei katika Taifa letu na hivyo kuathiri gharama za maisha nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, siyo hivyo tu tulipofanya uchambuzi nilieleza hapa kwamba tulikuta kwamba bidhaa hizi za mafuta zina tozo nyingi sana na kuweka ongezeko hili maana yake ni kwamba tunaendelea kubebesha chanzo hiki kimoja mzigo mkubwa zaidi. Pia kazi kubwa ambayo Waheshimiwa Wabunge walishauri ni kwamba tupate chanzo cha uhakika cha kugharimia miradi ya maji.

Mheshimiwa Spika, hili tumelizingatia kwa maana kwamba kuanzia mwaka ujao wa fedha nimekwishatoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, bajeti ya miradi ya maji ambayo wamepitisha itakuwa kati ya fedha ambazo zinapewa kipaumbele na kuangaliwa kwa karibu kuhakikisha kwamba fedha walizozipitisha zinatolewa kwa kadri inavyowezekana.

Mheshimiwa Spika, naamini kabisa kwamba pamoja na hatua hizi za mapato wakitupitishia maana yake ni kwamba fedha iliyotengwa kwanza kwenye bajeti itatoka, vilevile Serikali imeendelea kufanya jitihada kuongeza vyanzo vingine. Nilieleza kwamba tayari tumeshapata mkopo wa dola milioni 350 kutoka Benki ya Dunia, kati ya hizo dola milioni 60 tayari zimepatikana na zitaanza kupatikana mwezi ujaowa Julai, hata hizo nyingine nazo zinaweza kupatikana kwa haraka itategemea tu kiasi ambacho utayari wa miradi yenyewe lakini fedha ziko tayari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi, tulishalitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba zile dola milioni 500 kwa ajili ya Miji 21 Tanzania Bara na Zanzibar hizi tayari tulishasaini makubaliano, nazo zitapatikana katika mwaka ujao wa fedha bila wasiwasi wowote. Vilevile tumefanya mazungumzo na Shirika la Maendeleo la Ufaransa hawa nao wako tayari kutupatia pesa kwa ajili ya miradi ya maji kuanzia mwaka ujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo muhimu ambalo ningependa kusisitiza, Waheshimiwa Wabunge wanafahamu tumekuwa na matatizo makubwa sana kwa maana ya matumizi ya fedha hizi za miradi ya maji. Kwa hiyo, siyo vizuri tuendelee kupeleka hela bila kupitia upya na kujiridhisha kwamba utekelezaji wa miradi ya maji na fedha zile zitatumika ipasavyo, ndiyo maana Wakala wa kutekeleza Miradi ya Maji Vijijini unakwenda kuanzishwa, pia Wizara ya Maji inafanya marekebisho ili kuhakikisha kwamba fedha hizi zinatumika vizuri. Tukishaweka mfumo mzuri wa kuhakikisha kwamba fedha hizi zinasimamiwa vizuri kwa hakika kabisa Serikali haitasita kuongeza fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulishauriwa pia kwamba tupunguze kodi ya mapato kwa makampuni yanayotengeneza bidhaa zifuatazo: Taulo za akina mama, vifaa vya kilimo, vifaa vya kuhifadhi mazao ya samaki na yenye mkataba na Serikali kutoka asilimia 30 hadi 20 kwa miaka mitano ya mwanzo.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kutoa vivutio vya kikodi kwenye kampuni mpya zitakazoanzisha utengenezaji wa madawa ya binadamu na bidhaa za ngozi na lengo letu ni kuvutia wawekezaji wapya. Aidha, hatua inaakisi
malengo ya Serikali ya kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vya madawa ili tupunguze mzigo wa kununua madawa ya binadamu nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kivutio cha unafuu wa kodi kwa watengenezaji wa bidhaa za ngozi unalenga kuhamasisha uchakataji wa ngozi zinazozalishwa ndani ya nchi. Watengenezaji wa taulo za akinamama waliomba msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwenye sanitary pads ili kufanya bidhaa hiyo iwe bei nafuu. Ni kipaumbele cha Serikali kuvutia wawekezaji katika eneo hili kwa kuwapunguzia kodi ya mapato.

Mheshimiwa Spika, hivyo, katika tasnia vifaa vya kilimo na vifaa vya kuhifadhia mazao ya samaki vifaa vingi katika kundi hili hasa zile za kilimo zina msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani na lengo la Serikali ni kuvutia wawekezaji wapya, lakini Serikali haikusudii kupunguza kodi ya mapato katika tasnia hii ili kulinda mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti ilishauri tufute Sehemu ya Nane ya Muswada na Serikali kupitia jedwali la marekebisho imefuta Sehemu ya Nane ya Muswada. Vilevile ilishauri tufute Ibara ya 30 ya Muswada na kupitia jedwali la marekebisho tumefanya hivyo. Tulishauriwa pia na Kamati ya Bajeti tufute Ibara ya 35 ya Muswada na tumefanya hivyo. Siyo hivyo tu, tulishauriwa kufuta sehemu ya Kumi na Moja ya Muswada na kupitia jedwali la marekebisho tumefanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na suala hapa limesemwa kwamba Tresuary Single Account itamfanya mtu mmoja tu kuchukua fedha zote. Hili siyo sahihi, fedha zinagawiwa kwa kila Fungu husika kupitia exchequer na siyo kwenye akaunti, hivyo haiwezekani kabisa kwamba mtu mmoja anaweza akachukua fedha zote kwa sababu tu zimepita kwenye Treasury Single Account. Fedha hizi zinapita kwa mwenye Fungu mwenyewe na huyo ndiye atakayekuwa analipa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kuhusu kodi ya majengo na vizuri nikalitolea ufafanuzi, kwenye upande wa kodi ya majengo kifungu ambacho kimeondolewa kilikuwa kinarekebisha baadhi ya maeneo katika sheria ili iweze kutekelezwa vizuri, lakini ni vizuri ifahamike kwamba kipengele hicho kilichoondolewa hakiondoi ukusanyaji wa kodi ya majengo kutoka Mamlaka ya Mapato. Ukusanyaji wa kodi ya majengo utaendelea kukusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na siyo Halmashauri kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na ushauri kwamba slot machines zitozwe shilingi elfu 60 badala ya laki moja na kwamba winning tax itozwe asilimia 18 badala ya asilimia 20. Mapendekezo mapya katika Muswada wa Fedha wa 2018 niliouwasilisha Bungeni yalizingatia maoni ya wadau na Waheshimiwa Wabunge ambayo yamelenga kuweka usawa na haki katika michezo inayoshabihiana katika sekta ndogo ya michezo ya kubahatisha. Hivyo, Serikali inapendekeza kuendelea na marekebisho mapya ya Muswada wa Sheria ya Fedha 2018 katika kipengele hiki cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura ya 41 kama nilivyowasilisha Bungeni.

Mheshimiwa Spika, naomba tena nisisitize kwamba Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018 ni sehemu ya bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha niliyoiwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu. Ni muhimu kwa sababu Muswada huu ndiyo unawezesha utekelezaji wa kisheria wa bajeti iliyopitishwa na Bunge tarehe 26 Juni, 2018.

Mheshimiwa Spika, ili Serikali iweze kutekeleza ahadi zake kwa wananchi ikiwemo kutatua matatizo na kero zinazowakabili wananchi ni vema Bunge lipitishe Muswada huu na Muswada huu ndiyo unaidhinisha kisheria kodi, tozo na hatua mbalimbali za kiutawala za kukusanya mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya nawaomba sana Waheshimiwa Wabunge waridhie Muswada huu ili upite na kuiwezesha Serikali iingie kazini kukusanya mapato kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania na kutekeleza bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii na nianze kwa kuunga mkono hoja. Naomba pia nitumie nafasi hii kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Viongozi wa Wizara nikianza na Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu na Wasaidizi wake wote pia Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wote kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kabisa Wizara hii na vyombo vyake vinafanya kazi nzuri sana, wote tunajua nchi yetu iko salama na huu ndiyo msingi wa uchumi katika Taifa lolote, kama Taifa haliko salama basi hata jitihada zote za kujenga uchumi wa Taifa inakuwa ni matataizo. Tunajua pia jinsi ambavyo vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vimekuwa vikitusaidia kama Taifa pale tunapopata dharura na majanga mbalimbali, ku-rehabilitate miundombinu mbalimbali. Pia Jeshi letu limekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma za afya na elimu, kwa hiyo kwa kweli tunawapongeza kwa dhati kwa kazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kuwapa pole Jeshi letu kwa kupoteza Askari ambao walikuwa wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi na usalama ndani ya Taifa letu, lakini pia hata huko nje ya nchi. Serikali na Wizara tunayoiongoza, Serikali itaendelea kuenzi mchango mkubwa wa Jeshi letu na Wizara hii katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya naomba nitolee ufafanuzi mambo machache. Kwanza kama nilivyosema Serikali itaendelea kuwezesha Jeshi kwa kuwapatia rasilimali kadri ya mapato ya Taifa letu yanavyoruhusu. Mathalani Fungu 38 - Ngome kwa mwaka huu wa fedha mpaka mwezi Aprili, upande wa matumizi ya kawaida tuliwapatia shilingi bilioni 307.9 ambayo ni asilimia 132 ya bajeti kwa kipindi hicho, kadhalika upande wa maendeleo Ngome walipata bilioni 13.4 ambayo ni takribani asilimia 202 ya bajeti ya kipindi hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu Namba 39 - JKT kwa upande wa matumizi ya kawaida tuliwapatia bilioni 194.1 ambayo ni sawa na asilimia 201 ya bajeti ya kipindi hicho. Kwa upande wa maendeleo hapa ndiyo tulikuwa na changamoto ambapo tuliwapatia shilingi bilioni moja JKT ambayo ni asilimia 20, kwa kipindi kinachoishia Aprili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu Namba 57 ambayo ni Wizara yenyewe, mpaka mwezi Aprili tuliwapatia shilingi bilioni 4.1 ambayo ni sawa na asilimi 81 ya bajeti ambayo ilipangwa kwa kipindi hicho na kwa upande wa maendeleo tuliwapatia bilioni 169.7 ambayo ni asilimia 99 ya bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kweli kwa upande wa Serikali tunajitahidi sana kuhakikisha kwamba Wizara hii na vyombo vyake vyote vinapewa priority katika utoaji wa fedha kadri makusanyo yanavyoruhusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme ni kweli kabisa chombo hiki ni muhimu sana lakini ushauri kwamba Jeshi letu lisiwekewe ukomo wa bajeti ili kwa kweli naomba niwe mkweli siyo rahisi. Naowaomba Ndugu zangu Waheshimiwa tuelewane tusiwaambie Watanzania visivyo, kwa sababu rasilimali fedha hazitoshelezi mahitaji yetu mengi, lakini pili, yako mahitaji mengi, mengine ambayo nayo ni muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge walisema kwa nguvu kabisa juu ya mahitaji yetu ya maji katika Taifa, wamesema kwa nguvu juu ya mahitaji ya dawa na vifaatiba katika hospitali zetu, wamesema kwa nguvu sana juu ya umuhimu wa Serikali kuwezesha kilimo kukua, haya yote kama unachukua kwenye mtungi mmoja nayo lazima yapate kidogo. Haiwezekani ukasema Wizara yetu hii basi yenyewe isiwekewe ukomo, hili nitakuwa nadanganya na mimi ni msema ukweli daima ni vizuri nikasema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kulikuwa na suala la utoaji wa posho ya chakula kwa ajili ya askari wetu. Naomba niseme tena kwamba tunajitahidi sana kadiri bajeti inavyoruhusu. Mpaka mwezi Aprili, Ngome peke yake tumewapatia zaidi ya shilingi bilioni 155.5 lakini upande wa JKT posho ilifikia shilingi bilioni 64.7. Kwa hiyo, kwa kweli tunajitahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kulikuwa na suala la madeni. Serikali inalipa madeni baada ya kuyahakiki na ni muhimu tufanye hivyo ili tujiridhishe kwamba kuna value for money kwa haya madeni ambayo vyombo vyetu hivi vimeingia. Mpaka kufikia Aprili kwa mwaka huu wa fedha peke yake, upande wa Ngome tumelipa shilingi bilioni 46.2, upande wa JKT tumelipa madeni ya shilingi bilioni 41.1. Kwa hiyo, unaona kabisa vyombo hivi viwili peke yake ni shilingi bilioni 87.5. Kwa hiyo, tunajitahidi kadri tunavyoweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, palikuwepo pia hoja kwamba tulifuta misamaha ya kodi kwenye maduka ambayo yalikuwa yanawasaidia sana askari wetu. Waheshimiwa Wabunge, hatua hii ilichukuliwa na Serikali kuhakikisha kwamba ule motisha ambao ulikuwa unatolewa unawanufaisha walengwa na siyo baadhi tu ya askari na badala yake tuliweka utaratibu wa kuyapatia majeshi yetu posho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kwa upande wa Ngome mpaka kufikia Machi, posho ya fidia kwa misamaha ya kodi tumelipa shilingi bilioni 63.39 na upande wa JKT tumelipa shilingi bilioni 5.7. Kwa hiyo, siyo kwamba hatuwapi motisha askari wetu, hapana, hata kidogo, tunawathamini sana. (Makofi)

Mheshimwia Mwenyekiti, vilevile kwa upande wa madeni, nayo tunajitahidi kulipa baada ya kuyafanyia uhakiki. Mpaka mwezi Aprili, upande wa Ngome tumelipa madeni yaliyohakikiwa ya shilingi bilioni 46.2 na JKT tumelipa madeni ya shilingi bilioni 41.1

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala kwamba Serikali itoe shilingi bilioni mbili ambazo hazijatolewa kwa ajili ya kukarabati miundombinu na ujenzi wa makambi mapya ya JKT. Hadi mwezi Aprili, tumetoa shilingi bilioni moja wa ajili ya ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa makambi mapya ya JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kadhalika ilishauriwa hapa kwamba tutoe fedha kwa ajili ya ukarabati wa Kituo chetu cha Nyumbu na Mzinga. Napenda niliarifu Bunge lako kwamba shilingi bilioni mbili zimetolewa kwa Mashirika ya Nyumbu na Mzinga kwa ajili ya shughuli za utafiti na uzalishaji wa bidhaa ambayo ni sawa na takribani asilimia 40 ya bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala la kulipa stahili za Majenerali Wastaafu. Viongozi hawa wamefanya kazi nzuri sana walipokuwa kazini, tunathamini sana kazi yao na kamwe Wizara yangu na Serikali kwa ujumla hatuwezi kuwaacha. Hadi Aprili, Fungu 57 lilipelekewa shilingi bilioni 2.5 ambayo ni sawa na asilimia 63 ya bajeti ambayo iliidhinishwa na Bunge hili kwa ajili ya stahili za Majenerali Wastaafu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme la mwisho, kulikuwa na ushauri hapa kwamba kwa kweli fidia katika maeneo yaliyotwaliwa kwa ajili ya matumizi ya majeshi yetu ilipwe haraka iwezekanavyo. Ni kweli kabisa madai ya fidia haya ni makubwa lakini napenda nitoe commitment ya Serikali kwamba tutatoa kipaumbele kuyalipa yale ambayo yamehakikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo machache, nirudie tena kuipongeza Wizara na vyombo vyake kwa kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nikushukuru sana kwa kunipa fursa hii nami nichangie hoja hizi zilizoko mbele yetu na hasa kwa kuzingatia kwamba mimi ni mdau wa kila Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, na ninawapongeza Wajumbe na Wenyeviti wa Kamati zote mbili kwa uchambuzi wao mzuri sana, naamini kabisa utatusaidia Serikalini. Labda nianze na moja, lile linalohusu Shirika letu la Posta na hususan fedha zile ambazo walizitumia kulipa pensheni kwa wafanyakazi ambao walikuwa wameajiriwa East African Post and Telecommunications.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufikia Septemba tarehe 30, 2016, tulikuwa tumepokea maombi ya kurejesha takribani shilingi bilioni 5.1 ambazo zilitumika kuwalipa pensheni wastaafu. Kati ya fedha hizo, ilipofika Februari 28, 2017 tulikuwa tumerejesha shilingi bilioni 2.7. Kwa hiyo, napenda tu kusema kama Serikali, tutaendelea kupunguza hilo deni kadiri mapato yanavyoruhusu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu deni lile la shilingi bilioni 26 ambalo linadaiwa na TRA, naomba nilifahamishe Bunge lako Tukufu kwamba kupitia ule utaratibu wa Tax Amnesty, kiasi cha shilingi bilioni 12 ambacho kilitokana na riba kimesamehewa kupitia Mamlaka ya Mapato. Hivi
karibuni Shirika letu la Posta limeleta maombi ya kufutiwa kiasi cha shilingi bilioni 14.8. Naomba niseme tu hili tunaendelea kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la mwisho upande wa Shirika la Posta, ni ushauri kwamba sasa tuliondoe kwenye orodha ya mashirika ambayo yanasubiri kurekebishwa. Hili suala tunaendelea kulifanyia kazi; na kama ambavyo tumefanya hivi karibuni kwa Shirika la Bima la Taifa NIC, tunakamilisha utaratibu pia wa kuliondoa Shirika la Posta kwenye orodha ya mashirika ambayo yanatakiwa kurekebishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia kwamba tayari nimetekeleza agizo lako na natumaini utaendelea kuruhusu tuendelee na mawasiliano na Mheshimiwa Hawa. Tayari tumezungumza na nimemwonyesha hapa, Government Notice ambayo tulishaitoa kwa ajili ya kutoa hati ya msamaha kwa bidhaa ambazo zinatumika kwa ajili ya kujenga Terminal Three ambapo items takribani 277 zimepata msamaha kuanzia Januari tarehe 3. Kwa hiyo, nafikiri hilo limekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda lingine liseme kidogo alilisema Mheshimiwa Kishimba, kodi kwenye madini na hasa dhahabu, nimwombe tu, nakumbuka alichangia vizuri sana kwenye Mkutano wa Mheshimiwa Rais na Wachimbaji Wadogo wa Madini, kile kikao tulichofanya kwa siku mbili, tarehe 22 mpaka 23 Januari, 2019. Kama Serikali, tulipata mapendekezo mengi na namwomba tu avute subira kidogo tu, atapata majibu muda siyo mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo limesemwa sana ni marejesho ya ile asilimia 15 ya import duty kwa importation ya sukari ya viwandani. Niseme tu kwamba Serikali imeanza kulipa; na mpaka kufikia Desemba, Serikali imerejesha shilingi bilioni 11.84 kwa Makampuni, SBC tumepeleka shilingi bilioni 3.5, BONITE shilingi bilioni 1.7, Nyanza Bottling shilingi bilioni 1.5, Coca Cola Kwanza shilingi bilioni 1.9, Bakhresa shilingi bilioni 2.3 na Jambo Food Products nusu bilioni. Kwa hiyo tumeanza kulipa na tunaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme pia kuhusu GN ambayo nimeshaieleza lakini niliseme tu kwa ujumla. GN, Sheria zile za Kodi pale ambapo sheria zinaniruhusu kusamehe kodi, zinanitaka kama Waziri wa Fedha, nijiridhishe kwanza na bidhaa ambazo zinahusika, kama zinakidhi, lazima nijiridhishe kwamba bidhaa hizo, au msamaha huo unazingatia maslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa ni kwamba, tunajitahidi ili misamaha hiyo, isitumike vibaya. Kwa hiyo, kwa miradi mingi, kwa siku za karibuni tunatoa tunaita Global GN ambayo inarahisisha, lakini tumewabana Mawaziri wasimamizi wa Sekta husika, waji-committ kwa maandishi na kuhakikisha kwamba bidhaa zile zinazoombewa msamaha basi zinakidhi matakwa ya Sheria ya Kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maduka ya fedha za kigeni, niseme kwamba zoezi tulilofanya hivi karibuni kupitia Benki Kuu, lilituonyesha mambo mengi ambayo siyo mazuri; kwanza maduka haya yalikuwa ni mengi mno bila sababu, mengine yalikuwa hayakidhi vigezo na mengine yalijihusisha katika utakatishaji wa fedha haramu na mbaya zaidi, ni kwamba Benki Kuu iliona kuna hatari ya kuhatarisha Financial Stability katika Taifa letu. Hili hatutalikubali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaendelea kufuatilia kwa karibu, nasi tunaamini kabisa kwamba mabenki yaliyopo yanatosha kabisa kutoa huduma ya kuuza fedha za kigeni. Kwa hiyo, tunaendelea kufuata kwa karibu lakini la msingi sana ni kuhakikisha Financial Sector Stability katika Taifa letu inalindwa. Lingine lilisemwa hapa kwamba, hawaoni reforms kubwa ambazo tumefanya katika Taifa letu na hili linanishangaza kidogo. Kwa kipindi kifupi katika miaka mitatu, tumeongeza makusanyo ya mapato katika nchi yetu kutoka shilingi bilioni 850 kwa mwezi kwenda karibu trilioni 1.4. Jitihada za Mheshimiwa Rais, za kupiga vita Rushwa ni reforms za wazi kabisa ambazo ni transformative. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanya uwezaji mkubwa sana kwenye miundombinu na kwenye umeme. Zote hizo kama hazionekani ni transformative, basi kweli nashangaa. Tumeshughulikia sana suala la efficiency kwenye public service. Jamani vitu vingine tuwe honesty kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu deni la ndani, in bottom line ni kwamba linaliopika, tumefanya uchambuzi, lakini ni muhimu kwamba tunahakikisha deni hili linakwenda kugharamia miradi ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, as long as tunaendelea kuhakikisha kwamba ni himilivu kwa vigezo vya ndani, halina tatizo, kaa na amani kabisa. Ukitumia BoT Monthly Economic Review ni muda mfupi sana. Nadhani na Mheshimiwa huyu alikuwa mmoja wa watu waliokuwa darasani kwangu miaka ile, ni vizuri akakumbuka kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kulihakikishia …

MWENYEKITI: Mheshimiwa nakuongezea dakika tano. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Napenda tu kulihakikishia Bunge lako Tukufu, vipo vigezo sasa; tumemaliza Household Budget Survey ya mwaka 2017, tumehakiki kwa kushirikiana na baadhi ya wadau wetu na tutaleta taarifa rasmi katika Bunge ili kulieleza Taifa Household Budget Survey imeonyesha nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi tu, kwa mfano, basic need poverty imepungua kutoka asilimia 28.2 sasa imefikia asilimia 26.4. Vile vile umiliki wa rasilimali walizonazo wananchi wetu imeongezeka, lakini vilevile ajira katika sekta ambazo zinakua haraka, nayo imeongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa vigezo tu hivi vichache, ujue kwamba hii ni uhalisi, siyo namba tu. Nilisema suala juu ya vikwazo na usumbufu wakati wa kuingiza mizigo. Serikali inapokea ushauri, tutakaa na Wizara ya Viwanda na Biashara kama ilivyoshauriwa, tutazungumza na waagizaji wa bidhaa nchini; na ipo fursa na hasa baada ya Bunge hili, tutakutana nao ili tuweze kuona shida iliyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tunafanya hivi kama Serikali, lakini kwa sababu ya wingi wa makundi na mgawanyiko ndani ya sekta binafsi, tumekuwa tunakutana na Apex organizations. Kwa kikao kile cha Sekta ya Madini tuligundua kwamba unapata zaidi kwa kuzungumza na makundi maalum badala ya kuzungumza na haya makundi Wakilishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutakutana nao ili tuweze kuona namna nzuri zaidi ya kushughulikia upungufu. Kwa hiyo, ni jambo jema halina tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi, naomba niaze kwa pongezi mahususi kwa Mwalimu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na timu yake mahiri ya Walimu waliobobea ambao amewapa kazi ya kusimamia sekta hii ya elimu hususan dada yangu Profesa Ndalichako. Shemeji yangu Dkt. Ole-Nasha na timu nzima ya Maprofesa ambao wamekaa kule nyuma ya kioo kwa kazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kabisa kwa kusema naunga mkono hoja. Kulikuwa na hoja kwamba fedha zilizotengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, zitolewe zote kabla ya tarehe 30 Juni, 2019. Naomba nilitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba Fungu hili lilitengewa shilingi trilioni 1.4 na mpaka kufikia tarehe 29 Aprili, Fungu hili lilikuwa limepewa shilingi bilioni 890.58, ambayo ni asilimia 63 ya bajeti kwa Fungu hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kutambua umuhimu wa kipekee wa elimu kwa maendeleo ya nchi yetu, Serikali inapenda kuwahakikishia Watanzania kwamba katika kipindi kilichobaki, Serikali itatoa fedha kwa Vote 46 kama Sheria ya Bajeti na hususan kifungu cha 45 (b) kinavyoelekeza. Naomba nikisome ili tuelewane vizuri;Funds disbursements to Vote shall be based on performance approved budgets and funds availability.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja ya bajeti ya elimu inashuka na kuwa bajeti ya maendeleo imekuwa na mserereko wa kupungua, ni kweli, ukiangalia takwimu zinaonesha bajeti ya elimu inapungua katika asilimia kutoka asilimia 17 ya bajeti yote 2015/2016, asilimia 16 mwaka 2016/ 2017, asilimia 15 mwaka 2017/2018, asilimia 14 mwaka huu na asilimia 14 mwaka ujao wa fedha. Hata hivyo, si kweli kuwa bajeti ya maendeleo imekuwa na mserereko wa kupungua, uki-decompose hizi namba, unaona kwamba kilichopungua ni bajeti ya matumizi ya kawaida na imepungua kwa miaka miwili iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwaka 2015/2016, bajeti ilikuwa bilioni 3.2 na hii ni recurrent, ikaongezeka kwenda bilioni 3.7 mwaka 2016/2017, mwaka 2017/2018, ndiyo ikashuka kidogo kuwa bilioni 3.5 na bilioni 3.4 mwaka huu wa fedha na kwa mwaka kesho inashuka kidogo kuwa bilioni 3.1. Kwa hiyo, hiyo ni recurrent na hii inatokana na hatua ambazo Serikali ilichukua ikiwemo kuwaondoa watumishi hewa kutoka katika sekta ya elimu, lakini restructuring ambayo imefanyika katika taasisi mbalimbali ambayo imeondoa baadhi ya watumishi kutoka kwenye taasisi mbalimbali katika Fungu hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia upande wa fedha za bajeti ya maendeleo, hizi zimeongezeka kutoka bilioni 0.6 mwaka 2015/2016 kwenda bilioni moja mwaka 2016/2017, bilioni 1.1 mwaka 2017/2018, bilioni 1.2 mwaka 2018/2019 na bilioni 1.3 kwa mwaka ujao wa fedha. Kwa hiyo, ni vizuri kufanya decomposition ili uweze kusema kweli bajeti inateremka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni muhimu vilevile, Waheshimiwa Wabunge wakatambua mchango mkubwa wa wadau wengine katika elimu nchini na hususan wamiliki wa shule binafsi lakini pia taasisi za kidini, lakini pia ni muhimu kuzingatia kwamba sekta nyingine nazo ni muhimu kwa maendeleo ya elimu yenyewe. Kwa hiyo, ni lazima nazo zipewe fedha, kwa mfano, bajeti ya ulinzi na usalama, vyuo, vijana wetu walioko vyuoni, walioko shule za msingi na sekondari, wanaweza wakasoma pale tu ambapo tunawahakikishia ulinzi na usalama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, afya, maji, kilimo, miundombinu ya umeme na ICT nayo ni muhimu ili kuweza kuboresha elimu. Kwa hiyo, ni muhimu tuangalie mambo yote hayo ili tuweze kuona mwenendo mzuri unaofaa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa zaidi, ni ukubwa wa keki yetu, kwa hiyo, kazi yetu ambayo tunatakiwa tufanye, kwa kweli tujielekeze tupate mapato zaidi, lakini tuweke vipaumbele vizuri vya kisekta na vya kitaifa ambavyo tukivitekeleza vizuri tutakwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja kwamba fedha za udhibiti wa ubora wa shule zitolewe zote kabla ya mwaka huu wa fedha kumalizika. Serikali haina pingamizi kabisa na ushauri huu na kama nilivyoeleza awali, fedha zitatolewa kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, kazi zilizokwishafanyika hadi sasa na mpangokazi kwa kipindi cha miezi miwili iliyobaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Bodi ya Mikopo kwamba ipewe Fungu lake linalojitegemea, tunawashauri Bodi ya Mikopo kuandaa andiko la maombi ya kuwa na Fungu lake linalojitegemea baada ya kushauriana na Wizara mama. Utaratibu wa kuanzisha Fungu unazingatia majukumu na muundo ambao umepitishwa na Ofisi ya Rais (Utumishi) ili kuweza kubainisha ule mnyororo wa mamlaka za utendaji, ili tujiridhishe kwamba fedha ya umma itasimamiwa vizuri na kwa mwongozo zaidi wanaweza wakaonana na Ofisi ya Rais (TAMISEMI).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bajeti ya COSTECH; umuhimu wa COSTECH, kwa kweli unafahamika na ndiyo maana inatengewa bilioni 9.18 kwa mwaka ujao wa fedha na hili tumezingatia tu wigo wa mapato na mahitaji mengine ambayo ni lazima yagharimiwe na Serikali. Hata hivyo, ni vizuri pia kutilia maanani kwamba utafiti ni suala mtambuka na linatekelezwa kwenye taasisi nyingine, ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu, lakini pia taasisi kama TILDO, NYUMBU, TAWIR, TAFOR, CARMATEC, SIDO, VETA, ambazo nazo kwa kiasi cha kikubwa zinategemea fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya kufanya utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuliambiwa Serikali iheshimu makubaliano ya kimataifa, ikiwemo lile Azimio lile la SADC, kwamba Serikali itenge asilimia 20 ya bajeti yote kwa ajili ya elimu. Ni kweli, lakini yapo maazimio mengine ambayo Tanzania iliyakubali, ikiwemo Azimio la Maputo ambalo linatutaka tutenge asilimia 10 ya bajeti yote kwa ajili ya kilimo, afya asilimia 15 ya bajeti yote, utafiti asIlimia moja ya pato la Taifa, asilimia 0.05 ya bajeti kwa ajili ya takwimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tuliambiwa Serikali iheshimu makubaliano ya kimataifa, ikiwemo lile Azimio la SADC kwamba Serikali itenge asilimia 20 ya bajeti yote kwa ajili ya elimu. Ni kweli, lakini yapo Maazimio mengine ambayo Tanzania iliyakubali ikiwemo Azimio la Maputo ambalo linatutaka tutenge asilimia 10 ya bajeti yote kwa ajili ya kilimo; afya asilimia 15 ya bajeti yote; utafiti asilimia 1 ya pato la Taifa; na asilimia 0.05 ya bajeti kwa ajili ya takwimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama Maazimio yote haya yatatekelezwa sekta tatu tu peke yake zitachukua asilimia 45 ya bajeti yote. Sijui kipi hicho kitasalia kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu yetu, ulinzi na usalama, maji, ikiwemo na bajeti ya Mhimili wa Bunge, tutafanyaje? Kwa hiyo, ni muhimu sana huko mbele pengine tukifika lazima tuweze kuyapanga vizuri badala ya kwenda tu kusema tutatekeleza Maazimio haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme moja la mwisho, niliulizwa hapa kwamba upo Waraka wa Serikali unaonesha kwamba Waziri wa Fedha alifuta baadhi ya kodi kwa wamiliki wa shule binafsi na kwamba huo Waraka uko wapi. Serikali haijawahi kutoa Waraka unaofuta kodi kwa wamiliki wa shule binafsi. Mabadiliko mbalimbali ya kodi huwa tunayafanya kupitia Sheria ya Fedha au Gazeti la Serikali kwa mwaka husika na hilo halijawahi kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwanza nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia kwenye mjadala huu wa bajeti ya Wizara hii muhimu sana ambayo inachukua sehemu kubwa ya keki ya bajeti ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea, naomba muungane nami kumpa pole Secretary wangu ambaye alfajiri hii amepotea mume wake, Mama Dionisia Mkoma, ndiyo maana sijakaa vizuri hata mimi mwenyewe.

MBUNGE FULANI: Pole sana.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Ahsante.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nitoe pongezi mahsusi kwa Mheshimiwa Rais ambaye ameendelea kutoa kipaumbele cha juu kwenye ukarabati na ujenzi wa miundombinu msingi, yaani basic infrastructure na hii amefanya kwa umahiri mkubwa tangu alipokuwa Waziri wa Ujenzi; na kwa kweli alitambua mapema sana kwamba miundombinu ni kichocheo na mhimili mkuu wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, pia nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana Mhandisi Kamwelwe na Naibu Mawaziri Mhandisi Elias Kwandikwa, Mhandisi Atashasta Nditiye. Kwa kweli wanatekeleza majukumu yao vizuri pamoja na watendaji wao ambao wamekaa kule nyuma ya kioo wakiongozwa na Makatibu Wakuu husika. Niseme mapema kabisa kwamba naunga mkono hoja ambayo iko mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kusema, ninaunga mkono kwa sababu kwa kweli uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa inachochea uchumi na maendeleo ya nchi na watu wake kwa namna nyingi ambazo Waheshimiwa Wabunge wanazifahamu. Ujenzi wa miundombinu unatengeneza fursa nyingi sana za ajira, lakini pia kipato kwa wananchi wetu. Ujenzi na ukarabati wa miundombinu unatumia nguvu kazi yenye ujuzi na ndiyo maana bench pale tunaona ni Wahandisi watupu au waliowatangulia ni wanasayansi na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, pia miundombinu bora inapunguza sana gharama za uwekezaji na uzalishaji na inaongeza uwezo wa kusafirisha watu, malighafi, bidhaa na kadhalika na kufanya biashara iende kwa haraka zaidi. Kwa kweli moja ya tofauti kubwa ya nchi zetu masikini na nchi zilizoendelea ni ubora wa miundombinu. Kila unaposafiri ukaenda nchi yoyote iliyoendelea, kitu cha kwanza unachoona ni tofauti ya miundombinu. Ndiyo maana katika mwaka ujao wa fedha kwa makusudi kabisa Serikali imeitengea Wizara hii shilingi bilioni 606 zaidi ya bajeti ya mwaka huu wa fedha tuliyonayo ambayo ni takribani asilimia 12.8 ya ongezeko.

Mheshimiwa Spika, mgawanyiko wa fedha kwenye Wizara hii, umezingatia maoni ya wadau mbalimbali na Waheshimiwa Wabunge na hasa kwamba tujielekeze kama Serikali kwenye ujenzi wa reli mpya ya kisasa ili barabara zetu nazo ziweze kudumu lakini pia ili tuweze kupata manufaa makubwa ya kuwa na hiyo miundombinu ya kisasa.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naomba nichangie baadhi ya hoja ambazo zilijitokeza. Kwanza tulishauriwa kwamba Serikali katika ujenzi wa reli ya kati iufanye kwa kuzingatia faida za kiuchumi. Napenda nilihakikishie Bunge lako Mheshimiwa Spika na Watanzania kwa ujumla kwamba kazi hii ya kujenga reli imezingatia fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii ambazo zinapatikana katika ukanda mzima wa reli, fursa za kilimo, madini, mifugo na uvuvi pamoja na biashara miongoni mwa mikoa yetu, lakini pia katika nchi jirani.

Mheshimiwa Spika, lilisemwa sana lile la kipande cha Tabora – Kigoma ambacho inajulikana, nami ni mmoja wa wadau wakubwa, nisisitize tu kwamba hili ni muhimu, halina mjadala, lakini kikubwa ni kwamba tunajenga reli hii awamu kwa awamu na changamoto kubwa tuliyonayo ni upatikanaji wa fedha na tunaangalia options zote ikiwemo na kiasi ambacho kinaweza kugharamiwa na Serikali peke yake au kwa kushirikiana na wabia wengine na pia upande wa mikopo. Punde tutakapomaliza upande huu wa financing hakuna mashaka kabisa. Napenda tujenge hata vipande vyote kwa mara moja. Kwa hiyo, hili tunalifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, tuliambiwa pia tuangalie uwezekano wa kupata mkopo wenye gharama nafuu kuharakisha ujenzi wa reli nchini. Niseme tu kama nilivyotangulia kusema kwamba hili tunalifanya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Shirika letu la Reli, wameanza upembuzi yakinifu kwa miradi ya reli ambayo itatekelezwa kwa utaratibu wa PPP na hususan ile ya Mtwara, Mbamba Bay kupitia Mchuchuma na Liganga na pia ile reli yetu ya Tanga - Arusha – Musoma.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa reli ya kati, naomba niliarifu Bunge lako kwamba Serikali iko katika mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika ili watusaidie ku-leverage private sector investment na PPP na nilipokuwa Abidjan nilikuwa na mazungumzo na Dkt. Adesina kwa ajili ya hii na siyo kwa kipande tu cha kuelekea Kigali, lakini kwa vipande vingine vyote ambavyo bado tunatafuta fedha.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na swali kuhusu deni la TAZARA ambalo uhakiki wake umekamilika na kwamba Serikali ilipe hilo deni lililopo upande wa nchi yetu. Tulipokea madai ya TAZARA bilioni 59.6 kwa ajili ya kulipa madeni ya mishahara na michango kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Kama inavyojulikana madeni hayana yanatokana na changamoto mbalimbali ambazo zilikabili TAZARA kuanzia miaka ya 1990 ikiwemo na kushindwa kabisa kujendesha, lakini pia malimbikizo ya wastaafu. Sasa tumefanya nini kama Serikali, kuanzia 2015 tulianza kusaidia ulipaji wa mishahara ya watumishi wa TAZARA na tunalipa takribani shilingi bilioni
1.25 kwa mwezi na tumefanya hivyo hadi Aprili, 2019 na tumekwishalipa jumla ya bilioni 67.44.

Mheshimiwa Spika, lakini mwaka uliopita 2017/2018, tuliongeza pia mtaji wa TAZARA tukalipa bilioni 10 kwa ajili ya kukarabati vichwa na engine za treni za TAZARA. Kuhusu madai ya TAZARA ambayo yamepokelewa karibuni, tunayafanyia uchambuzi wa kina ili tuweze kupata namna bora ya kuyalipa na kuwezesha shirika kujiendesha kwa lengo kudhibiti uzalishaji wa madeni mapya.

Mheshimiwa Spika, tuliambiwa pia hapa kwamba Serikali iharakishe kulipa madeni ya pension kwa wafanyakazi waliokuwa Posta chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kulipunguzia mzigo shirika. Serikali ilikwishafanya malipo kwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na zoezi maalum la kuwalipa wastaafu lilishafungwa na tulishawaandika hivyo toka Disemba, 2016.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, tunashughulikia hoja zinazowasilishwa na wastaafu kwa kulingana na maombi au malalamiko yanayohusika na malalamiko hayo huwa yanawasilishwa kupitia taasisi ambazo walizifanyia kazi hao wastaafu.

Mheshimiwa Spika, kwa wafanyakazi wa Posta wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, maombi ya madai yenye jumla ya shilingi bilioni sita yalikwishapokelewa na tumekwishalipa bilioni 2.7 kufikia Februari, 2017 na kiasi kilichosalia ambapo nyaraka zilikuwa zina utata kiliwasilishwa kwenye Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwezi Februari, 2019 kwa ajili ya uhakiki malipo yaweze kufanyika.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba mradi wa kuboresha Bandari ya Dar es Salaam...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana bahati mbaya muda umekwisha.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na Maduhuli ya Madeni ya Nyuma ya Ada na Leseni za Magari, Riba na Adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nikushukuru wewe binafsi kwa kuendesha mjadala huu vizuri, lakini pia niwashukuru Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC. Lakini pia Mheshimwa Ernest Silinde aliyetoa Maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, lakini vilevile Mheshimiwa Allan Kiula, Mheshimiwa Godbless Lema, Mheshimiwa Richard Ndassa, Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka kwa mara nyingine na Mheshimiwa Stanslaus Mabula. Lakini pia wale ambao wametoa miongozo mbalimbali kama sehemu ya mjadala.

Mheshimiwa Naibu Spika, basi na mimi baada ya shukrani hizo naomba nihitimishe kwanza kwa kutoa ufafanuzi kidogo. Ilihojiwa hapa kwamba mapato yasiyokusanywa basi nayo yahesabike kama hasara, hili sio sahihi. Kwa mujibu wa Kanuni namba 17 ya Kanuni za Fedha za Umma ya mwaka 2001 upotevu au hasara upo wa aina kama nne. Kwanza kuna hasara ya fedha taslimu yaani cash losses, lakini kuna hasara ya vifaa (store losses), kuna hasara kutokana na misamaha yaani waivers and or abandonment. Lakini pia kuna hasara kutokana na matumizi yasiyo na faida au tija kiingereza inaitwa nugatory payments.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kanuni hii kodi au mapato yasiyokusanywa sio sehemu ya hasara inayotambuliwa kisheria, lakini labda nilieleze kwa lugha nyepesi kidogo. Kwa mfano kama mwezi uliopita nilipanga niuze ngo’mbe wangu wawili ili nifyatue matofali 1000; nikaenda na wale ng’ombe wawili mnadani nikafanikiwa kuuza mmoja tu nikapata fedha za kutosha kufyatua matofali 500 badala ya matofali 1000 niliyolenga, sasa huwezi kuhesabu hiyo kwamba yule ni hasara kwa kuwa nilipoenda sokoni nilitamani niuze wawili nikauza mmoja. Kwa hiyo kwa kweli sio hasara by definition kwa mujibu wakanuni tulizojiwekea, lakini hata katika logic ya kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, ilitolewa hoja hapa kwamba matumizi ya Serikali yanafanyika kinyume na zile ambazo zilipitishwa na Bunge. Hili sio sawa mapato ya Serikali yanakusanywa kwa mujibu wa sheria, sheria zilizotungwa na Bunge, Kodi ya Mapato, VAT, Local Government Finances Act na kadhalika. Lakini pia kila mwaka tunaleta hapa Sheria ya Fedha, huo ndio msingi wa kukusanya mapato ya Serikali na matumizi ya Serikali Waheshimiwa Wabunge yanafanyika kwa mujibu wa Appropriation Act ambayo nayo inakuja hapa Bungeni na sio tofauti na hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, labda nieleze tu kwamba ambacho Serikali inaweza kufanya ni reallocation (kufanya uhamisho) na huu umeelekezwa kwenye Sheria ya Bajeti Cap. 439 na inasema wazi katika kifungu cha 41(1) imeeleza Afisa Masuhuli akipata ridhaa ya Waziri muhusika anaweza kuhamisha fedha. Lakini pia kifungu cha 41(2) kinaweka mazingira matano ambapo Accounting Officer hawezi kufanya uhamisho wa fedha. Kifungu cha 41(3) kinaweka pia mzingira ambayo Accounting Officer kuhamisha fedha baina ya program au kati ya ndani ya vifungu katika mwaka unaohusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 44(4) kinanipa Waziri mamlaka ya kuruhusu uhamisho wa fedha kupitia kanuni na kifungu cha 41(5) kinaweka mazingira ambayo mamlaka ya Waziri kufanya uhamisho wa fedha yamezuiliwa/yamekatazwa lakini siyo hiyotunaleta pia reallocation warrants hapa mbele ya Bunge lako tukufu kila mwaka hapa Bungeni. Kwa hiyo, madai kwamba Serikali inafanya matumizi nje ya fedha zilizoridhiwa na Bunge sio sahihi hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, labda nieleze tena, Mheshimiwa Lema alikuwa na wasiwasi kwamba fedha hizi ni nyingi labda zinakwenda kwenye uchaguzi, sio kweli, fedha hizi kweli ni nyingi lakini kwamba zinakwenda kwenye uchaguzi hapana.

Mheshimwia Mwenyekiti wa Kamati ya PAC ameeleza kabisa vizuri dhana kwa nini ni lazima Serikali ije kuomba msamaha huu kwamba Bunge liridhie kufuta hiki ambacho tumekuja kukiomba leo. Lakini niseme hivi taarifa ambayo CAG alikagua ina kurasa 8,503; lakini magari pia yanayohusika ni magari ambayo ni ya kipindi kirefu kwa kipindi ambacho sheria inatumika mpaka pale tulipokuja kama Serikali kulieleza Bunge lako tukufu kwamba tunayafuta ambayo ni with effect from tarehe 1 Julai, 2017. Kwa hiyo ndio sababu kwamba kwa nini imechukua muda mrefu, lakini pia ni utaratibu wa kawaida kabisa. Kwa hiyo, ni shutuma za uongo kabisa hatupeleki fedha hizi kwenye uchaguzi hata kidogo na kama ambavyo imeelezwa jamani jipangeni, CCM imejipanga katika kugharamia uchaguzi wake. Sasa na ninyi jipangeni, haya madeni ni cumulative ya kipindi kirefu sana. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Rudia hatujasikia.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, aaah, nimesema hivi CCM imejipanga kikamilifu kwa ajili ya uchaguzi wa mwezi Oktoba, na hawa rafiki zetu wajipange.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC alieleza vizuri, tunafuata utaratibu huu ili kuondoa hoja za ukaguzi ambazo zimekaa muda mrefu, lakini vilevile kurekebisha vitabu, lakini ni nafasi pia ya kupokea ushauri wa Bunge imeelezwa vizuri sio suala la kuja kugharamia uchaguzi hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Mabula ametukumbusha kwamba hatua hii imeletwa kwa sababu ilikuwa ni kero kubwa kwa wananchi wetu na lilishangiliwa sana, lakini pia tunataka kusafisha vitabu kama alivyoeleza kwa ajili ya hizi hoja. Sasa hoja za muda mrefu kwenye Halmashauri ni ahidi Bunge lako tukufu kwamba tunaendelea kuzifanyia kazi tukishakamilisha basi zitakuja kwa ajili ya kuomba ridhaa ya Bunge kwa kupitia utaratibu wa kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nianze kwa kuunga mkono hoja iliyosomwa hapa Bungeni na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa umahiri mkubwa kabisa lakini niwapongeze pia mawaziri wote na watendaji katika ofisi yake.

Mheshimiwa Spika, nitajikita kwenye hoja tu moja kubwa ambayo ilisemwa karibu na wachangiaji wote na ni hoja ya corona.

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba niseme ni kweli mlipuko wa virusi vya corona licha ya adhari kubwa za kiafya umekuwa ni tishio kubwa kwa mafanikio ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika bara la Afrika lakini pia na dunia nzima. United Nations economic commission for Africa wamekadiria kwamba ukuwaji wa uchumi wa bara letu la Afrika unaweza kuanguka kwa kati ya asilimia 2 mpaka 3 katika mwaka huu 2020.

Mheshimiwa Spika, lakini Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) tayari wameshatangaza kwamba uchumi wa dunia unaingia kwenye mdororo katika mwaka 2020, economic research. Sasa sisi kama nchi kama zilivyo nchi nyingine tumeanza kupata madhara katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na Waheshimiwa Wabunge wengi waliochangia wamezisema sehemu mbalimbali hususani upande wa utalii kuna shida kubwa na mnyororo mzima wa sekta ya utalii, lakini mapato yanayotokana na biashara mbalimbali ndani na nje ya nchi tunaona tatizo, lakini pia usafiri wa anga biashara za maua tunaona shida uzalishaji viwandani nk.

Mheshimiwa Spika, lakini kubwa kutokana na hali hiyo Serikali imeunda kikosi kazi cha wataalam ambacho kinaendelea kufanya uchambuzi wa kina wa athari hizi zinazojitokeza na niseme tu kwamba hii kazi ni muhimu ikafanyika kwa umakini na ndiyo iweze kuwa msingi wa kuandaa programme ya kiuchumi ya kukabiliana na janga hili vinginevyo tunaweza kuishia alarmist lakini bila fact kutoka kwenye sekta mbalimbali ili tuweze kuhakikisha tunaanda mikakati ambayo kweli ni hakika na timu hii inajumuisha wenzetu kutoka Zanzibar wako kwenye kamati ya kitaalam lakini pia kwenye kamati ya kitaifa ambayo inaongozwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vile vile, katika Wizara yangu tumeelekeza pia na Wizara zote za kisekta ikiwemo benki kuu kukutana na wadau mbalimbali kwa majadiliano ili tupokee mapendekezo yao na baadhi tumeshapokea Tanzania Association of two operators, tumepokea kutoka Umoja wa Mabenki Tanzania Hurting operatos, Shirikisho la Vyama vya Utalii, Tanzania Private sector foundation, kuna ma casino kadhaa lakini Tanzania horticulture Association na wadau wengine na tunawashukuru sana kwa michango yao milango iko wazi tunaomba na wengine watuletee mapendekezo yao katika Sekta mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, nitakacho fanya sasa, naomba nitoe tu vidokezo vya mikakati ambavyo inaandaliwa hivi sasa na viko katika sehemu tu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni ugharamiaji wa mahitaji ya msingi ya vifaa ya kujikinga na corona lakini pia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kutokea huduma za afya ili ni jambo la msingi sana ili tuweze kuokoa maisha ya watu wetu kwa hiyo maana yake ni kwamba ni pamoja na vituo mahususi vya kutolea huduma, tiba za dharura lakini pia lengo kubwa likiwa ni kuzuia maambukizi ya corona kwa hiyo, lazima tufikirie gharama za vifaa kinga person protective equipment masuala ya barakoa, ventilators, gaunt za wahudumu wa afya na madaktari na n.k.

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni pamoja pia na gharama za kutafuta namna ya kuongeza madaktari na watumishi wengine wa afya kwa hiyo, hii ni block ya kwanza na vyanzo vya kugharamia eneo hili ambavyo tunafikiria ni pamoja na bajeti kuu ya Serikali hususani kasima ile ya dharura, mapato ya halmashauri michango ya hiari ya wananchi, makampuni binafsi na umma, misaada ya fedha na vifaa na mikopo nafuu kutoka kwa taasisi za fedha za kimataifa.

Mheshimiwa Spika, pia nchi rafiki na ninapenda nitumie nafasi hii kama mfano tu kutambua mchango wa Twiga Minerals Cooperation Limited ambayo tayari wameahidi kutoa mchango wa dolla za kimarekani 1.8 milioni ambazo zitatumika kusaidia Isolatin Untis Mlonganzila na vituo vingine vya karantini, mabibo hostel. Lakini pia kusaidia Isolation centre Musoma, Shinyanga na Geita, pia ziko fedha kwa ajili ya kusaidia shughuli za kupambana na janga hili katika ngazi za local Government na tunawashukuru sana kwa dhati na tunaomba na wengine waige mfano huu mzuri makampuni mengine, mabenki, taasisi na wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali pia inaendelea kushauriana na IMF na benki ya dunia kuhusu namna nchi yetu inaweza kunufaika na programme za dharura za Taasisi hizo ili kukabiliana na hili janga. Kwa upande wa World Bank na IFS wana programme inaitwa Fast track COVID – 19 facility na IMF wana rapid crediting facility for low income country’s tunaendelea na majadiliano tuone namna ambavyo Tanzania inaweza ikanufaika na sehemu hizi.

Mheshimiwa Spika, nguzo ya pili, ni kupunguza makali ya mdodoro wa uchumi hasa katika sekta ambazo zimeadhirika na nimeshayaeleza, sekta ambazo tayari kuna dalili za kuumia kwa hiyo, hatua ambazo tunafikiria ni pamoja na kuhakikisha hifadhi ya chakula ya kutosha nchini, kuchukua hatua za kibajeti ikiwa ni pamoja ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi katika baadhi ya maeneo na kuzielekeza kuongeza nguvu kukabiliana na corona, lakini kukarabati miundombinu ya usafirishaji ili tuweze kuwafikia wananchi wetu hasa walioko vijijini lakini tutaongeza kasi ya kulipa madeni na malimbikizo ya madai mbalimba lakini pia kuchukuwa hatua za kikodi na za kiutawala zinazolenga kutoa huweni kwa sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, nguzo ya tatu ya mpango ambao unaandaliwa, ni hatua ya kuilinda sekta ya fedha na lengo ni kuhakikisha mabenki yetu yanaendelea kuwa na ukwasi wa kutosha tuna akiba ya fedha ya fedha ya kigeni ya kutosha lakini sarafu pia iendelee kuwa imara na itakuwa ni muhimu tudhibiti ongezeko kubwa la mikopo chechefu lakini hususani kwa kuwapa nafuu mabenki…

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Malizia.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mhehsimiwa Spika, tutatoa unafuu kwa mabenki ili yaweze kufanya loan rescheduling kwa maelezo hayo machache, nilitaka tu niliakikishie tu Bunge lako tukufu kwamba Serikali ipo kazini kuandaa mpango wa kupambana na madhara ya corona ya kiuchumi na muwe na uhakika tutakapo kamilisha tutawasilisha kwa maamuzi ndani ya Serikali na Bunge litapata taarifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2016
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza naomba niwapongeze sana Kamati ya Katiba na Sheria kwa kazi nzuri sana ambayo wameifanya kuchambua mapendekezo ya Serikali ya kurekebisha Sheria ya Mikopo na Dhamana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitoe ufafanuzi kidogo katika masuala mawili, matatu. Kwanza kwa lile la kufaulisha mkopo kwenda Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, naomba niseme tu kwamba baadhi ya wanaotukopesha fedha hizi mathalani Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Saudi Fund na kadhalika wao kama sehemu ya primary loan agreement wanaweka sharti kwamba kabla SMT haijahamisha fedha za mkopo kwenda SMZ, yaani kwenda kwa mnufaikaji, wanahitaji kuona kwamba pana utaratibu wa kuhakikisha kwamba mnufaikaji atawajibika kurejesha zile fedha za mkopo. Kwa hiyo, ni muhimu tuelewane tuna nia njema kabisa, baadhi ya haya wala hata siyo masharti ya SMT, ni masharti ya wale wanaotukopesha. Kwa hiyo, mkiyakataa yale maana yake ni kwamba tumejifungia kupata chanzo hicho cha mkopo wa fedha nafuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hilo ni moja ambalo nadhani nilitaka niliweke vizuri. Lengo ni jema tu, ni kuhakikisha kwamba unawekwa sasa utaratibu wa kisheria ambao haupo kwenye sheria ya sasa ilivyo kuhakisha kwamba fedha ambazo zinakopwa na SMT kwa ajili ya miradi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinawasilishwa kama ilivyokusudiwa.
Pia lengo la pili ni kuhakikisha kwamba mkopo ule unalipwa. Tatu, ndiyo hiyo niliyoanza kueleza kwamba ni kuhakikisha kwamba yale masharti au kwa kiingereza, condition precedent ambayo yanatolewa na baadhi ya wakopeshaji yanatekelezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ningependa kuchangia, napenda tu nisisitize kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikipelekewa asilimia 4.5 ya mgao wa General Budget Support. Nadhani tofauti ni fedha za mkopo ambazo zinaelekezwa kwenye sekta maalum kulingana na mkataba kati ya mkopeshaji na washirika wa maendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napenda tena nirejee kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeendelea na itaendelea kupokea mgawo wake wa asilimia 4.5 ya fedha zote za GBS ambazo zimepokelewa kutoka kwa washirika wa maendeleo kwa mujibu wa mkataba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa miradi tumeangalia namba hizi na kwa leo mchana huu nimejaribu kuangalia deni la nje; deni la nje linaonesha kwamba kuanzia mwaka 1993 mpaka mwaka jana 2016, fedha ambazo zimekopwa na SMT kwa ajili ya Zanzibar zilifikia takribani dola milioni 772.396 ambayo ni takribani sawa na asilimia 2.59 ya deni lote la nje kwa Taifa letu. Kwa hiyo, bado tumeendelea na utaratibu mzuri wa kuhakikisha kwamba, tunafanya on landing kwa Zanzibar. Tunachoweka ni masharti sasa ya kisheria kuhakikisha kwamba, mikopo hii inalipwa kama ambavyo tunakubaliana na wanaotukopesha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nieleze pia jambo lingine la tatu kuhusu utaratibu wa Serikali ku-on lend to Zanzibar, kwamba itakuwaje kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itashindwa kulipa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria imeweka sharti, ukitazama kifungu cha 12(3) kwenye schedule of amendment, tumeweka masharti kwamba kabla ya kuwasilisha mkopo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itabidi idhihirishe, i-demonstrate prudent projections za mapato yake hasa kwa kutazama balance sheet.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kutuwezesha kujua kwamba inaweza kweli ikafikia primary loan obligations. Kwa hiyo, upo utaratibu ambao umewekwa, vilevile kuhusu sharti la kuishirikisha National Debt Management Committee ambayo itafanya uchambuzi wa lile deni kabla ya Serikali ya Muungano kufaulisha mkopo kwenda SMZ. Masharti haya yatatumika pia kwa Halmashauri na Mashirika, ni lazima kupitia ukiangalia kifungu cha 12(4)(i) cha hii sheria kinasema wazi kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumeweka utaratibu mzuri kwa nia njema ili tuhakikishe kwamba kweli mikopo hii inalipwa na nchi yetu inaendelea kunufaika na mikopo nafuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nieleze tena kuhusu madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imenyang‘anywa mamlaka ya kupokea misaada kutoka nje. Ukitazama kifungu cha 15 cha sheria hii kimetoa mamlaka kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupokea misaada pasipo ridhaa ya Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, siyo kweli kabisa kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imenyang‘anywa hayo mamlaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho tulipokea mapendekezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya kuhuisha ushiriki wa Zanzibar katika National Debt Management Committee na hili limezingatiwa katika mapendekezo ambayo tumeweka mbele ya Bunge lako Tukufu ambapo Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa SMZ, lakini pia Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wote hawa sasa tunapendekeza kwamba waingie kwenye National Debt Management Committee. Tunadhani ni jambo jema la kuhuisha utaratibu uliokuwepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kabisa ni pendekezo la Mheshimiwa Chenge, kuhusu kuondoa neno debt stock, neno stock. Sisi tunakubali upande wa Serikali kama ilivyoshauriwa kwamba neno hili linaweza kuendelea kubaki, tunadhani kwamba halina madhara yoyote katika kutekeleza sheria hii. Baada ya maelezo hayo, naomba kuunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2017.
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako binafsi kwa kuendesha vizuri majadiliano kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2017/2018. Aidha, nampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia kwa umahiri wake wakati wa uendeshaji wa Vikao vya Kamati ya Bajeti wakati ikiwa inajadili Muswada huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Bunge ya Bajeti kwa maoni na ushauri wao walioutoa wakati wa majadiliano ya Muswada, ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kuboresha Muswada huu uliowasilishwa mbele ya Bunge zima.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kutambua michango iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza au kwa maandishi. Naahidi kwamba Serikali itafanyia kazi ushauri na mawazo mazuri ambayo yametolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja zimetolewa na Kamati ya Bajeti, kuna hoja za Kambi ya Upinzani pamoja na Waheshimiwa Wabunge ambazo ningependa nizitolee ufafanuzi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba adhabu za makosa ya barabarani zimekuwa kama ni chanzo cha mapato. Napenda kuliambia Bunge lako Tukufu kwamba si kweli kuwa fedha ambazo zinakusanywa na Jeshi
la Polisi ni chanzo cha mapato. Adhabu inayotolewa kwa madereva ni kuhakikisha kwamba madereva wanafuata na kutekeleza bila shuruti Sheria za Usalama wa Barabarani kwa mujibu wa Sheria. Kwa hiyo si kweli hata kidogo kwamba, hiki kimehesabika ni chanzo cha mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kulikuwa na hoja kwamba Serikali kuhamishia fedha za taasisi na mashirika ya umma Benki Kuu inakiuka sheria. Serikali kabisa kabisa haijakiuka na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu, Kifungu cha 32(1) ambacho kinataka Taasisi na Mashirika ya Umma kuhifadhi fedha zao Benki Kuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba kupandisha ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nchini pengine hatuwezeshi zaidi competitiveness ya bidhaa zetu za ndani. Excise Duty tulizoleta mbele ya Bunge lako Tukufu tulirekebisha ushuru wa bidhaa kulingana na mfumuko wa bei na hali ya uchumi. Hatuwezi kurekebisha tu bila kuwa na misingi. Kwa hiyo, ni muhimu Waheshimiwa Wabunge kuzingatia hili, hatuwezi tu kwenda arbitrarily.

Mheshimiwa Naibu Spika, ilikuwepo pia hoja kwamba, ukiongeza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya taa tunawaonea wananchi maskini waishio vijijini. Nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge ambao katika michango yao wamelifafanua hili; nami tu niongeze kwamba kwa kweli hatua ya kuongeza ushuru kwenye mafuta ya taa ililenga kuwalinda Watanzania wote dhidi ya madhara ya uchakachuaji wa mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama zile sh.40/= kwa lita tungefanya kwenye dizeli na petroli peke yake tukaacha mafuta ya taa, huu uchakachuaji wa mafuta ambao tuna uzoefu nao kama Taifa (fuel adulteration), basi ingekuwa ni shida kubwa kwa maana ya vifaa hivi vya moto ambavyo watu wote hata maskini nao wanatumia, ambayo ina madhara makubwa sana kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, fedha ambazo zitapatikana kutokana na chanzo hiki, sehemu ya mapato yanaenda kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo maji, afya na elimu ambayo inakwenda kumgusa mwananchi wa kawaida kabisa, hawa wanaoitwa maskini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba, Serikali ina poka vyanzo vya halmashauri na hivyo kuua dhana nzima ya Decentralisation by Devolution. Hili si kweli hata kidogo. Serikali imeamua kuboresha ukusanyaji wa majengo na tozo za mabango kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania. Serikali itaendelea kusimamia na kuzipatia ruzuku halmashauri zake, ili tuhakikishe kwamba, zinaendelea kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua hii ni utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016 ambayo ilipitishwa na Bunge lako Tukufu. Kwa hiyo, lengo letu si kudhoofisha halmashauri hata kidogo na ndiyo maana tunasema tukishakusanya zile fedha sisi tunaamini kwamba ufanisi utakuwa mkubwa, tutapata fedha nyingi zaidi na ndio maana tutazirejesha kwa kuzingatia Bajeti za Halmashauri lakini vilevile ni lazima tujiridhishe kwamba, matumizi hao yako sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ilikuwepo pia hoja kuhusu kuwatambua na kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wasio rasmi. Naomba niliambie Bunge lako Tukufu, kwanza ni lazima kama Taifa tujenge utaratibu wa kila mtu kulipa kodi, ni lazima na lazima tupate mahali pa kuanzia. Tusidanganyane, kama tunatafuta fedha ya maji, tunatafuta fedha ya dawa hospitali, tunatafuta fedha za kujenga barabara, nimesema na narudia tena, nimeshachoka kuomba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wanao uwezo wa kuchangia maendeleo kulingana na kipato chao. Hata hivy, kwa mwaka huu tunachofanya kwanza ni kuwatambua na nilisema wakati wa Hotuba ya Bajeti Kuu; tunawatambua ili tuweze kuwapatia sehemu muafaka za kufanyia biashara zao, hilo ndilo jambo la msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja ya kurekebisha Sheria ya EPOCA kwa kuondoa Local Share Holder na kuweka Public ili kuondoa dhana nzima ya kuwawezesha Watanzania kumiliki kampuni za simu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme tu kwamba, Marekebisho ya Sheria ambayo yametajwa kwenye hoja hayaondoi dhana na madhumuni ya awali ya Sheria ya EPOCA. Ifahamike kwamba, Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana ina wajibu kisheria wa kusimamia Sheria, Kanuni na Kudhibiti mwenendo wa biashara katika Masoko ya Mitaji nchini na jukumu hili ni pamoja na kuhakikisha ulinzi wa maslahi ya wawekezaji wa Kitanzania katika Masoko ya Mitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mauzo ya hisa katika soko la awali yatafanyika kwa umma nchini Tanzania na baada ya mauzo ya hisa kufanyika mgawanyo wa hisa (Allotment) kwa wawekezaji walioomba kununua hisa utatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa umma wa Watanzania kwanza kabla ya uwekezaji wa nje kupata mgawo wa hisa zilizouzwa na kampuni husika kwa mujibu wa Sera ya Mgawanyo wa Hisa (Allotment Policy). (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na CMSA imekuwa ikitekeleza sera hiyo hata kwenye mauzo ya awali (IPO) ya hisa yaliyofanyika hapo nyuma. Kwa hiyo basi, marekebisho ya Sheria yaliyotajwa kwenye hoja hayaondoi dhana na madhumuni ya awali ya Sheria ya EPOCA.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na hoja kwamba Serikali ilete Muswada Kurekebisha Sheria ya Usimamizi wa Madini ili kuongeza mapato kutoka sekta ya madini kwani clearing fee ile ya asilimia moja si suluhisho. Clearing fee inayopendekezwa ni kwa ajili ya kutambua madini yote yanayochimbwa na kuuzwa hapa nchini na yale yanayosafirishwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, muda ni mfupi, tutawasilisha maelezo kwa maandishi kwa hoja ambazo tumezipokea. Muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2017 ni sehemu ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa Fedha niliyoiwasilisha mbele ya Bunge tarehe 8 Juni, 2017. Muswada huu ndio unaowezesha utekelezaji wa Kisheria wa Bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge tarehe 20 Juni.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili Serikali iweze kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, ikiwemo kutatua matatizo na kero zinazowakabili wananchi ikiwemo huduma za maji, afya, elimu, barabara na kadhalika, ni vyema Bunge lipitishe Muswada huu na Muswada huu ndio unaidhinisha Kisheria hizi kodi na tozo na hatua mbalimbali za kiutawala za kukusanya mapato ya shilingi trilioni 31.7 na uamuzi wa kujenga Tanzania ya Viwanda chini ya uongozi wa Rais wetu unahitaji hatua za kijasiri katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na Muswada huu umetafsiri hatua hizo kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo haya, nawaomba Waheshimiwa Wabunge mridhie Muswada huu, ili upite na kuiwezesha Serikali iingie kazini kukusanya mapato kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania na kutekeleza bajeti hii ya kihistoria katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo haya, naomba kutoa hoja.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2018
WAZIRI FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii ili nami nichangie hoja iliyoko mbele yetu. Nianze kwa kuunga mkono hoja na niwapongeze sana Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria na timu yake yote na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu Mkuu wa Serikali kwa kazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nami naomba niseme mambo machache. La kwanza kulikuwa na hoja ile ambayo ilitokana na malalamiko yalitokea katika Bunge la Bajeti ya kutoza VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) kwenye umeme ambao unauzwa na TANESCO kwa ZECO. Suala lilikuwa kwamba kwa nini marekebisho haya hayakuletwa kwenye Muswada wa Sheria mbalimbali wa mwaka 2018 ili kuweza kumaliza.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nilikuwa nasema, hoja ilikuwa ni kwa nini hatujaleta marekebisho kwenye Muswada wa Sheria Mbalimbali ili kujibu malalamiko ambayo Mheshimiwa Saada Mkuya aliyaeleza Bunge lililopita.

Mheshimiwa Spika, labda niseme tu kwanza Sheria yenyewe ya VAT tunajua ilianza kutumika mwaka 1998. Kwa mujibu wa sheria ile, bidhaa zinatozwa VAT ikiwa ni pamoja na umeme. Sheria ile ikafanyiwa marekebisho tukapata Sheria mpya ya VAT ya mwaka 2014 na kwa bahati nzuri wakati ule Mheshimiwa Saada ndiye alikuwa Waziri wa Fedha.

Mheshimiwa Spika, katika utaratibu ule, ZECO ilikuwa inalipa VAT wanaponunua umeme, halafu Mamlaka ya Mapato ikawa inarejesha VAT kwa Waziri wa Fedha wa Zanzibar. Utaratibu huo ukazusha malalamiko mengi tu ikiwa ni pamoja na matatizo ya marejesho ya VAT, masuala ya uhakiki na kadhalika. Pia wauzaji wa re-exports nao wakawa wanalalamika ikapelekea turekebishe ile sheria Juni, 2016 kupitia Muswada wa Fedha wa mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika, tulichofanya ni nini? Tulichofanya ni kwamba umeme utozwe VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye bidhaa ambazo zinatengenezwa Bara na kuuza Zanzibar. Kwa hiyo, bidhaa zote ambazo zinazalishwa Bara, zitozwe VAT lakini kwa kiwango cha asilimia sifuri, kadhalika upande wa pili nao. Ndiyo marekebisho ya msingi tuliyofanya mwaka 2016. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, shida ikaja kwamba ZECO wakatafsiri kwamba umeme ni bidhaa lakini sheria inasema bidhaa, ZECO wakatafsiri kwamba umeme ni bidhaa na kwa hiyo, unatakiwa uwe zero-rated. Sasa ubishani umekuwa hapa, umeme ni bidhaa au siyo, ni huduma. Kwa hiyo, haya ndiyo tumekuwa nayo. Hiyo ni changamoto ya kwanza.

Mheshimiwa Spika, changamoto ya pili, siku za nyuma kidogo mwaka 2008, EWURA ilipandisha bei ya umeme kwa asilimia kama 21.7 na ikafanya hivyo kwa makundi yote ya watumiaji wa umeme; wale wanaonunua jumla na wale wa umeme wa majumbani. Sasa lilipofanyika hilo, ZECO wakalipinga, wakakataa kabisa kulipa umeme kwa hivyo viwango vipya. Matokeo yake ikawa malimbikizo yanayotokana na hiyo tofauti ya bei, tofauti ya VAT yamekuwa yanaendelea hivi, lakini pia hata ile tozo ya EWURA yenyewe. Kwa hiyo, deni limekua mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Juni, lile deni ukijumlisha vyote limefikia takribani shilingi bilioni 138.7. Kati ya hizo, za kodi peke yake ni kama shilingi bilioni 20.4.

Mheshimiwa Spika, nachojaribu kueleza ni nini? Ni kwamba jambo hili ni pana. Ni kweli kabisa dhamira yetu ilikuwa tungeweza kuleta marekebisho katika Bunge hili, lakini jambo hili ni pana. Kama nilivyosema, kwanza kuna mgogoro kati ya ZECO na TANESCO juu ya ulipaji wa hiyo VAT baada ya yale marekebisho tuliyofanya katika Sheria ya Fedha ya mwaka 2016. La pili, ZECO wakalalamikia viwango vya bei ya umeme ambavyo vilikuwa vimewekwa na EWURA.

Mheshimiwa Spika, siyo hivyo tu, bado tuna changamoto. Sisi tunasheria ya VAT kama ilivyorekebishwa mwaka 2014, lakini Zanzibar nao wana sheria yao ya VAT. Sasa hapa kuna changamoto kidogo. Kwa mfano, sisi Sheria ya VAT ya mwaka 2014 inatoza VAT kwenye huduma za simu (interconnection charges) na tunafanya hivyo kwa kiwango cha asilimia sifuri, lakini Sheria ya VAT Zanzibar ya mwaka 1998 inaelekeza kuwa huduma zote kutoka Bara hazistahili kuwa zero-rated na hili linalalamikiwa sana na wadau upande huu wa Muungano. Siyo tu hivyo, ukiangalia ile Sheria ya VAT ya mwaka 2004, hainipi mamlaka kama Waziri wa Fedha kuweza kusamehe VAT kwenye huduma ikiwa ni pamoja na kwenye umeme.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nachosema ni nini? Nachosema ni hivi, jambo hili ni pana, mawanda yake ni mapana, tusingeweza kufanya marekebisho yale ambayo tulikuwa tumeahidi kufanya kwenye Bunge lililopita.

Mheshimiwa Spika, sasa tumefanya nini? Tumefanya mambo kadhaa, moja, kama Serikali yamekuwepo majadiliano kati ya TANESCO na ZECO juu ya vile viwango ili waweze kupata kiwango muafaka cha bei ya umeme. Haya ni ya muda mrefu toka 2013 wanazungumza. La pili, Wizara ya Nishati na EWURA wametafuta Mtaalam Mwelekezi ambaye anafanya study inaitwa Cost of Service Study ili sasa kuweza kujua gharama ya kutoa huduma ya umeme kwa wateja mbalimbali, hawa wa jumla na wa majumbani, hivi ni nini hasa? Haya ndiyo yatatuwezesha kufanya maamuzi sahihi.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wetu kama Wizara ye Fedha, tumeandaa Waraka tayari, ninayo rasimu ya Waraka na rasimu hii imefikia ngazi ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wameshapelekewa rasimu ya Waraka na ninayo rasimu hapa ili tuweze sasa kupata uamuzi rasmi wa Serikali juu ya jambo hili. Hii ndiyo itatuwezesha tuseme turekebishe Sheria ya VAT ile Sura ya 148 na kwa hiyo, ni muhimu Serikali iweze kuji-pronounce kwa maana ya kwanza kuondoa hizi kero ambazo zimekuwepo muda mrefu lakini pia kuweza kuona madhara yake ya kufanya hivyo ni nini? Kwa mfano, upande wa mapato iko wazi kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilichotaka kueleza ni kwamba Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya mwaka 2018 hatukuweza kufanya hivi ili tuweze ku-accommodate haya mawanda mapana ambayo ninajaribu kuyaeleza.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi na naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza).
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii. Nianze pia kwa pongezi kwa mtoa hoja Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini pia Kamati ambayo ilichambua vizuri sana Muswada huu. Vile vile niwapongeze Mawaziri wenzangu, Mheshimiwa Waziri wa Madini, Mheshimiwa Waziri anayesimamia TAMISEMI, lakini na wachimbaji wadogo ambao kwa kweli pindi Muswada huu utakapopitishwa na Bunge lako utakwenda kuwanufaisha.

Mheshimiwa Spika, nianze na maoni ya Kamati kwa haraka; niseme tu kwamba kwa kweli tutajitahidi kuhakikisha kwamba kanuni zinabakia na nia na dhamira ambayo imeoneshwa na Mheshimiwa Rais kupitia Muswada huu, kwa hiyo msiwe na wasiwasi. Pili, kuhusu kodi kwenye mashine za ukataji wa madini pia VAT kwenye mashine za kusindika mvinyo, naomba niseme tu kwamba tutayangalia haya katika uchambuzi wa mapendekezo ya marekebisho ya kodi kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Spika, nikikimbia kwa haraka kwenye maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani, Muswada huu kwa hakika utaandikwa pia kwa lugha ya Kiswahili, utatafsiriwa, kwa hiyo wananchi wetu wataweza kusoma bila wasiwasi. Kwa upande wa kama mabadiliko haya yameongeza mapato au yamepunguza niwahakikishie tu kwamba uchambuzi ulifanyika na kwa mfano nitatoa tu mfano kwa upande wa ushuru wa bidhaa mapato yatapungua kwa takribani bilioni 5.7, upande wa exemption ya VAT yatapungua kwa milioni 741, lakini withholding tax nayo itapungua kwa milioni 104. Jambo kubwa sana ni kwamba kwanza kwa upande wa mrabaha huu utaongezeka kwa miezi iliyobaki kufikia bilioni 10, pia tunajua kwamba kodi zinatokana na ajira, voluntary compliance ya watu wetu na shughuli za madini ambazo zitaongezeka kutokana na hatu hizi zitatuongezea mapato.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa kodi ya majengo napenda tu niwahakikishie kwamba, TRA inaendelea kukusanya vizuri kwa kipindi cha Julai mpaka Disemba kama ambavyo tulitolea ufafanuzi kwenye Kamati, TRA ilishakusanya bilioni takribani tisa ambazo ni kama asilimia 62 ya lengo, lakini pia tunafanya jitihada nyingine kuhakikisha kwamba TRA inakusanya zaidi. Mwaka jana tuliajiri wafanyakazi 400, tunakwenda kuongeza wafanyakazi wengine 167 tunawaongezea vitendea kazi hususan magari kwa mwaka huu tutawaongezea magari 74, lakini jambo la msingi zaidi tunakwenda kuongeza ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato na Halmashauri za Wilaya na wanashirikiana katika kutambua maeneo na nyumba.Pia kama nilivyosema, kuna taratibu nyingine za kiutawala za kuziwesha Mamlaka za Halmashauri kuweza kuisaidia Mamlaka ya Mapato kukusanya.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa majengo kuuzwa kwa kudaiwa kodi ya nyumba, napenda tu nisisitize kwamba, tumechukua hatua za kupunguza kodi ya majengo na kuifanya iwe ya mfuto. Kwa hiyo inakuwa flat rate ambayo ni ndogo ya asilimia 10 kwa lengo hilo la kuondoa adha hiyo. Pia niwakumbushe wote, sisi wote ambao tuna properties zinazodaiwa kodi kwamba kodi hii inalipwa mara moja tu kwa mwaka na kwa hiyo kila mtu ana wajibu wa kujiandaa kulipa hizo Sh.10,000. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile sisahau kwamba katika mapendekezo tunayoleta hapa, tunaondoa nyumba zile ambazo kwa kweli wanaishi wananchi wetu maskini, tumesema wazi nyumba za tope, za majani zote tunaziondoa kwenye wigo wa kutozwa hii kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda lingine nimeambiwa hapa kwamba wakati wa bajeti tuwe tunasikiliza ushauri wa Waheshimiwa Wabunge, naomba tu niseme kwamba, kuleta mabadiliko sio udhaifu, kuleta mabadiliko ni pamoja na Serikali kuwa flexible, lakini pia ni muhimu sana kukumbuka kwamba wajibu wangu mwingine ni kulinda mapato ya Serikali. Pia msisahau kwenye ushuru wa bidhaa kwenye mvinyo kwa mfano, kwenye zabibu ambazo zinazalishwa hapa nchini kwa kiwango cha asilimia 75 tulipunguza ushuru wa bidhaa, kwa hiyo tunaendelea kluyashughulikia mambo haya kila tunaposikia malalamiko ambayo tunaona ni genuine kutoka kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ilisemwa hapa kwamba pengine utaratibu huu wa Mamlaka ya Mapato kukusanya kodi ya majengo na huu wa D by D, naomba tu nisisitize kwamba Serikali inaendelea kupeleka fedha kwenye Halmashauri kupitia kwenye bajeti zao, lakini vilevile kwa miradi mingine ambayo inapata fedha kutoka kwa wafadhili kama P4R bado tunaendelea kupeleka pia fedha kwenye halmashauri.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hofu ile ya nyumba za vijijini kutozwa kodi, kwenye marekebisho tumebadilisha kifungu cha 10 na tumebadilisha na kukiweka sasa kifungu cha 6(1) ambako tunaeleza kwamba tozo hii sasa itahusu Makao Makuu ya Wilaya ndani ya mipaka ya Makao Makuu ya Wilaya na townships na kwa hiyo hicho kifungu kinachofanya kimsingi ni kuondoa vijiji katika maeneo ambayo yanatozwa hii kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niwashukuru sana wale wote waliochangia kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuja na hatua hii ya kusikiliza wananchi wake na kutuagiza sisi wasaidizi wake ili tuweze kuleta mabadiliko haya.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, najua wewe ni mdau mkubwa sana wa mchuzi wa zabibu, tulikusikia kwa niaba ya wakulima wote wa zabibu na mimi nikiwa mmoja wao, ahsante kwa mwongozo wako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. (Makofi)