Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Saada Salum Mkuya (23 total)

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. SAADA M. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Bajeti ya Serikali. Kwanza kabisa nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango pamoja na Watendaji wote wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kazi nzuri ambayo wameendelea kuifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, truly speaking ni kwamba this time hii bajeti ni very innovative kwa sababu ya measures zake za kodi na naamini kwamba kwa vitendo kabisa tunakwenda kutekeleza ile azma ya East African Community Budget ya Industrilization for job creation na shared prosperity.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maeneo machache ambayo nataka kuchangia. Kwanza ni kuhusiana na madeni ya VAT na Excise ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaidai Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bahati nzuri leo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesoma Bajeti yake ya Serikali na inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 1.315. Kwa hiyo, kati ya mapato hayo ni pamoja na mapato ya VAT na Excise ambayo yanakusanywa na TRA kupitia TRA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania upande huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, bado kuna deni na Mheshimiwa Waziri nadhani analitambua. Kwa hiyo, tusaidiwe ili kule na kwenyewe maendeleo yaweze kutekelezwa. Kuna shida za maji, barabara; na tunaraji sana wakati tunaingia katika bajeti mpya, bado hizi fedha hazijapelekwa, tunamwomba sana Mheshimiwa Waziri hili alifanyie uharaka kwa ajili ya kwenda kukamilisha bajeti kwa SMZ. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusiana na tozo la VAT kwa upande wa ununuzi wa umeme. Tumezungumza sana na Mheshimiwa Waziri wa Nishati na hili safari hii tumelizungumza lakini limekuwa linakwenda mwaka kwenda mwaka kurudi, limezungumzwa sana na watendaji. Wakati ZECO inanunua umeme kama ni essential supply, kwamba inatozwa na VAT na ZECO anakwenda kuuza Zanzibar mwananchi wa Zanzibar ananunua umeme ukiwa na VAT. Kwa maana hiyo, isingekuwa ZECO kwa sababu tu sasa hivi imesema inasubiri hailipi, hailipi Zanzibar, hailipi Tanzania kwa sababu ya huu mkanganyiko. Hata hivyo ZECO siyo mtumiaji wa mwisho. Kwa hiyo, kutokana na principle ya utozaji wa VAT, mlaji wa mwisho ndio anakwenda kutozwa VAT. Kwa maana hii ni mwananchi wa Zanzibar ambaye anatumia umeme ndiye ambaye analipa VAT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwananchi wa Zanzibar ndiye ambaye analipa VAT. Sasa inakuwa haiwezekani VAT yenyewe pia ZECO ambaye ananunua umeme kwa ajili ya kwenda ku-supply kule na yenyewe itozwe VAT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Nishati, nimependa siku ambayo anakamilisha bajeti yake, alisema vizuri sana kwamba nishati ama umeme ni siasa; umeme ni uchumi na umeme ni usalama. Amezungumza vizuri sana Mheshimiwa Waziri, lakini sasa hii isi-apply upande mmoja. Tunaomba nishati hii ama huduma hii muhimu iende vile vile isimamiwe kule na wananchi wa kule waweze nao kuendelea na uchumi wao kuweza kusimamia siasa pamoja na usalama uliopo kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana kupitia Finance Bill Mheshimiwa Waziri wa Fedha lirekebishwe, ZECO asinunue umeme TANESCO ikiwa ni pamoja na VAT. Hili ni jambo ambalo linaweza likarekebishwa, maana yake imekuwa tabu miaka nenda, miaka rudi, lakini ni jambo ambalo tunaweza kulirekebisha kupitia Finance Bill. Kwa maana hiyo sasa, badala ya kupunguza hizi kero za Muungano, tunaongeza kero za Muungano kwa sababu tu ya masuala ya administration. Tunaomba na hili lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kuna baadhi ya taasisi ambazo ni za Muungano ambazo zina-operate Zanzibar, hazilipi umeme ZECO, zinalipa umeme TANESCO. Wanachukua umeme wa ZECO, lakini malipo yanalipwa TANESCO. Nadhani hii haiko sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba hili na lenyewe, lile deni ambalo lipo kutokana na huduma hii lilipwe, lakini usimamizi uwe mzuri zaidi. Taasisi za Muungano ambazo zina- operate Zanzibar zilipe umeme Zanzibar, umeme ndiko ambako unakotolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa haraka haraka nimefurahi sana kuona sasa DCF imekamilika na tutakwenda kutekeleza. Nimefurahi kwa sababu Zanzibar wameshiriki kikamilifu katika development mpaka development ya Action Plan ya DCF. Hili napata experience nzuri kwa sababu mimi mwenyewe wakati niko Wizara ya Fedha Zanzibar, nilishiriki katika development ya Joint Assistance Strategy for Tanzania. Utekelezaji wake ulikuwa ulikuwa ni shida kubwa. Shida kubwa ilikuwa inapatikana pale ambapo tupolikuwa tukizungumza hii mikakati miwili, wakati huo kulikuwa kuna MKUKUTA na MKUZA, tuweze ku- harmonize ili twende kwa pamoja tukatafute misaada ya Kibajeti. Haikuwezekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sasa hivi hii DCF, tumei-develop vizuri, tume-develop sote, tunashukuru sana kwa ushirikiano uliokuwepo lakini implementation yake iwe ni ya kuweza kuhakikisha kwamba hizi strategies zetu zinakuwa harmonized na kwa maana hiyo tunapokwenda kutafuta misaada iwe tunakwenda pamoja, yaani pamoja na inclusion ya Zanzibar, isiwe tunakwenda separate. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, athari ya kwenda separate maana yake nini? Maana yake Mheshimiwa Dkt. Mpango tumeweka safari hii GBS kwamba tuna kiasi cha fedha shilingi bilioni 545. Leo Zanzibar wanasoma bajeti yao, wamesema wao hawawezi kuingiza hii GBS kwa sababu hii ni fedha ambayo kwanza haina uhakika. Sasa Mheshimiwa Dkt. Mpango, naomba atakapokuja kujibu hoja aliweke suala la jinsi gani Zanzibar itaweza kushiriki katika ku-mobilize external resources kupitia General Budget Support na DCF ili na yenyewe ipate uhakika wa mapato yake ya kibajeti. Hoja zipo nyingi, lakini tunaomba kwa umuhimu wa pekee hili alipe nafasi aweze kulijibu katika hoja zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni la kiutawala zaidi, Zanzibar leo wakati inasoma bajeti; nadhani sisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumesoma tokea Alhamisi, lakini ilivyo Zanzibar, yaani ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tungeweza kusoma bajeti kama vile tulivyokubaliana katika East Africa. Kwa nini hatusomi? Sababu zinaweza zikawa nyingi, lakini ninaloliona ni kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa vyanzo vya mapato kutokana na tax measures ambazo ziko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili linawezekana. Tax Force ya Tax Reforms tunaomba iwe ina-include Maafisa wa Kodi na wa Wizara ya Fedha ya Zanzibar. Sasa hivi kilichopo, Zanzibar inaalikwa ile siku moja kama ambavyo wanaalikwa wadau wengine wa nje. SMZ ni part ya SMT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba wakati Maafisa wetu wanapoanza kubuni vyanzo vya mapato, wanapoanza ku-develop tax measures za mwaka wa fedha unaokuja from day one, Maafisa wa Kodi wa Zanzibar pamoja na Maafisa wa Sera za kikodi wa Wizara ya Fedha na Mipango ya Zanzibar wawepo katika tax measures. Hii itasaidia sana kuwa na uhakika wa bajeti hata kule upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili halihitaji mabadiliko ya sheria wala mabadiliko ya kisera linahitaji uamuzi wa Mheshimiwa Waziri wa Fedha ili hawa watu washiriki tuweze kuondoa huu mgongano wa kikodi na vilevile tutapunguza hizi changamoto za Muungano zinazojitokeza. Pia tutaweza kufanya masuala mbalimbali; kwa mfano, Mheshimiwa Dkt. Mpango safari hii, tumeangalia vizuri, angalau corporate tax imepunguzwa. Maana yake nini? Zanzibar haijapunguza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake nini? Maana yake ni kwamba kama kutakuwa na viwanda vipya vitakuwa attracted sana upande huu ambapo hii corporate tax imepunguzwa kuliko kule. Tungekuwa tumekaa pamoja mwanzo, tukashauriana, tukakubaliana, nadhani hizi tax measures zingekwenda vizuri. Kwa maana hiyo, industraliazation for job creation and shared prosperity ingeweza hata ku-apply kwa upande ule mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tulipo sasa hivi tunapokwenda ndipo tunapoleta mkanganyiko na kwa maana hiyo, baadhi ya kodi haziwezi kutekelezeka, kwa sababu upande mmoja haujawa tayari simpy kwa sababu haujapata muda mrefu wa kuweza ku-mainstream na ku- think about hizi tax measures. Kwa hiyo, hilo ni suala la administration zaidi na naamini kabisa Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa uelewa wake, weledi wake, nia yake njema na nzuri kabisa, hili atalifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi na la umuhimu kabla sijamaliza, tunaomba sana fedha ambayo ilikuwa iende Zanzibar, ipelekwe ifanyie maarifa haraka iende ikasaidie shughuli za kiuchumi Zanzibar. Vile vile masuala ya VAT, tusisubiri consultant kwa sababu ni jambo ambalo linawezekana likarekebishwa kupitia Finance Bill hii ambayo ya mwaka 2018/2019. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, sina zaidi, lakini naendelea kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Mheshimiwa Naibu wake na Menejimenti nzima ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya jambo hili la leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri ambayo ameanza na anaendelea kuifanya. Vile vile pongezi kwa Waziri Mkuu na Mawaziri wake kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza majukumu yake. Naomba kutoa mchango wangu kwenye hotuba hii kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Utalii; nimefurahishwa na kupata moyo kwa hatua ambazo Serikali itachukua kuimarisha utalli. Utalii ni sekta ambayo ina potential kubwa sana kwa uingizaji wa fedha za kigeni. Kwa upande wa Zanzibar, Sekta hii ni leading sector kwa mchango kwenye pato la Taifa. However, watalii wamekuwa wakilipia katika nchi zao na hivyo kukosesha pato kwa upande wa nchi. Uelewa mdogo wa changamoto hii kwa upande wa Kampuni za Kitalii kwa hapa nyumbani, umesababisha tabia hii kuendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati ambao utaandaliwa uhakikishe kwa kiwango kikubwa unashirikisha Makampuni ya Kitalii ya hapa nyumbani kuzungumzia changamoto hii na utatuzi wake. Vile vile kwa kuwa Zanzibar inategemea sana utalii, mkakati ushirikishe wadau wa Zanzibar kwa kiwango kikubwa cha majadiliano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, UKIMWI; wakati tukiwa kwenye Kamati, imeonekana bajeti nyingi zimeweka eneo la mkakati wa kudhibiti UKIMWI, kama ni eneo ambalo linasubiri fedha kutoka kwa wafadhili. Hii ni hatari, afya za wananchi na matibabu yake, hayawezi kuwekwa katika mikono ya wafadhili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba, kwenye activities zetu ambazo tunazifadhili kwa fedha yetu ya ndani, issues za HIV/AIDS, Women, Climate change and environment, ziwe mainstreamed humo. Tusisubiri hadi fedha za wafadhili zifike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ukusanyaji wa Mapato; eneo hili ni gumu na lina changamoto nyingi, hata hivyo pongezi kwa Serikali kwa kulipa mtazamo maalum suala la ukusanyaji wa mapato. Matumizi ya mashine ya electronics (EFDs) ziambatane na mafunzo ya watu wetu katika matumizi hayo, hususan kwenye Halmashauri zetu. Eneo hili la ukusanyaji wa mapato ni eneo gumu sana, lakini ni muhimu kuliko yote. Maendeleo yetu bila ya mapato yatokanayo na vyanzo vyetu vya ndani yatakuwa ni magumu mno.
Mheshimiwa Mwenyekiti, approach ya utoaji wa elimu ibadilike now, ijielekeze sana kwa wananchi ili waelewe umuhimu wa ulipaji kodi kwa Serikali kwa kudai risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali. Changamoto hii ikitatuliwa tunaweza kufika mbali zaidi. Vyombo vya habari vya Serikali na binafsi vione umuhimu wa jambo hili. Aidha, katika bidhaa za mafuta tuangalie jinsi gani tunaweza kupata fedha kwa kuongeza angalau shilingi mia ili tupate fedha ziingie katika Mifuko ya Maji na REA kama ilivyopangwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti,Viwanda; dhamira hii ni nzuri katika ujenzi wa Taifa na kiuchumi. Hata hivyo, viwanda vitakavyojengwa vitumie rasilimali zinazopatikana kwa wingi nchini ikiwemo rasilimali watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti,karafuu ya Zanzibar ingepata viwanda vinavyohitaji, tuna hakika Zanzibar ingepata tija kubwa kuliko inavyopata hivi sasa. Liangaliwe hili kwa mapana yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuchangia hoja ambazo ziko mbele yetu. Awali ya yote, nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhana Wataala na kumtakia Rehema Mtume Muhammad (S.A.W).
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo sasa najikita katika hoja ambazo ziko mbele yetu. Kwanza tunaanza na suala la ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri. Tunaipongeza sana Serikali kwa kuwa ni jambo ambalo wamelitilia mkazo mara hii na tunaamini kwamba mifumo ya electronic ambayo imefungwa katika Halmashauri nyingi zaidi ya asilimia 70 kama ilivyoelezwa itakuwa inakwenda kufanya kazi ile ambayo tumeitarajia.
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, Mheshimiwa Waziri tunaomba Public Financial Management Reform Programme iende ikajenge uwezo wa watu wetu kuweza kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki. Njia za elektroniki siyo kwa kutumia tu M-PESA na Tigo Pesa lakini ni uwezo wa watu wetu kuweza ku-intergrate hizi systems katika systems zetu za kufanyia kazi. Maana yake ni kwamba tunataka hata watu ambao wanakwenda kulipa kodi walipe kwa urahisi zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tunatumia benki kwenda kulipa kwa mfano kodi ya ardhi lakini ukishapewa risiti ya benki inabidi mtu aende tena ofisini kupata risiti nyingine, kidogo utaratibu huu unaweza kuleta usumbufu. Kwa hivyo, ni lazima tuone ni jinsi gani tunaweza tukarahishisha mifumo hii ya kielektroniki kuweza vilevile kuwafanya watu waweze kulipa kodi hizi kwa hiari kwa kuhakikisha kwamba hawapati tabu wala vikwazo vyovyote vile wakienda kulipa kodi hizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ni kuhusiana na masuala ya HIV/AIDS, tumeona katika Halmashauri nyingi zimeweka hizi component za ku-address hizi issue za HIV/AIDS, problem iliyokuwepo ni kwamba wengi wanategemea donors yaani miradi mingi ya ku-address issue hizi za UKIMWI zinategemea sana fedha za donors, nadhani huu utaratibu unaweza ukatu-cost baadaye. Sasa hivi kuna indication kwamba maambukizi ya UKIMWI yanaweza yakawa yamepungua katika maeneo fulani lakini inaweza ikatuathiri baadaye kwa sababu financing ya ugonjwa huu tunawaachia donors.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri katika kila component yetu ya maendeleo ni lazima issue hizi za HIV/AIDS ziwe addressed mle kwa kutumia fedha zetu za ndani. Kama jitihada hiyo hatutaifanya kwa kutegemea development partners waje watusaidie kwenye masuala haya ya UKIMWI hapo baadaye inaweza ikatuathiri.
Mheshimiwa Naibu Spika, niende katika suala la Tume ya Maadili, tuna-note kazi nzuri sana inayofanywa na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma. Jambo langu katika Tume hii, isiishie tu kwenye masuala ya mali, madeni lakini vilevile iende ikaangalie behaviors za wafanyakazi. Jambo la msingi ambalo nataka kuli-note hapa hususani kwa watendaji wetu wa afya, sasa hivi tunatumia mitandao lakini utaona kwa mfano inawezekana mwanamke ameathiriwa labda na mumewe au amepata jambo ambalo si zuri anapigwa picha na tunajua kwamba hii picha imepigwa hospitali na imepigwa na mtaalam, anapigwa picha mwanamke yuko utupu kabisa, tunaambiwa huyu mwanamke mume wake amempiga kipigo wakati ni mjamzito yaani maelezo kama hayo, hili jambo siyo zuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, tungependa tusikie issues kama hizo kwa ajili ya kuchukua hatua lakini vitu kama hivyo visichukuliwe kama ni starehe ama visichukuliwe kwamba watu ndiyo wanapashana habari. Jambo hili linakwaza hususan sisi wanawake kwa sababu vitu vingi ambavyo vinatumwa katika mitandao ya kijamii ni vile ambavyo vimemkuta mwanamke na vina udhalilishaji wa hali ya juu. Mitandao mingi utaona picha zingine mtoto amezaliwa labda moyo wake uko nje inatumwa kwenye WhatsApp, ni vitu vya hatari.
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma iende mpaka ikaangalie behaviors za wafanyakazi wetu wanafanya nini hasa. Tunataka watu wahudumiwe na siyo kutumia zile athari ambazo wamezipata kupashana habari ulimwenguni, kuona kwamba hili ni jambo ambalo labda tunaweza tukaliona hivi hivi, iende katika hatua hiyo pia.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuhusiana na Tume ya Ajira. Kwenye Kamati tulikwenda na tukaongea na Tume ya Ajira, wanafanya kazi nzuri sana. System zao ziko vizuri sana na ni system ambazo zimetengenezwa na Watanzania, tunawapongeza sana kwa kazi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini changamoto iliyopo hapa Wazanzibari kwenye Tume ya Ajira wanapata tabu sana kufuatilia ajira ambazo wame-apply hususan katika Taasisi za Muungano. Siku za kufanya interview utawaona Wazanzibari wengi katika vyombo vya usafiri wanakuja Dar es Salaam. Jambo hili tumekuwa tukilisisitiza kuhusiana na facilitation ya Tume hii kule Zanzibar. Lazima kule Zanzibar kuwe na Ofisi za Tume ya Ajira ili iweze kuwafikia Wazanzibari bila kikwazo chochote.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili jambo linasemwa mwaka hadi mwaka kwamba tutafungua Ofisi lakini hazijafunguliwa, kwa kweli vijana wetu wanapata tabu na wanahangaika sana. Kule kuna vijana wazuri tu, wasomi, wamemaliza degrees, they are very good lakini kwa kufuatilia hizi inawakwaza sana kwa sababu ni gharama. Vijana hawa hawajaajiriwa lakini inabidi watafute fedha za kwenda Dar es Salaam kufuatilia maombi ya ajira zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakusudia kabisa kushika mshahara wa Mheshimiwa Waziri kama hatanipa commitment ambayo itatekelezeka kuona kwamba Tume ya Ajira aidha inafunguliwa Zanzibar au kunakuwa na Ofisi kwa ajili ya watu wa Zanzibar kufuatilia masuala ya kazi katika hizi Taasisi za Muungano.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu hii asilimia 10 ya wanawake na vijana. Katika Halmashauri nyingi wanaona kwamba hili jambo ni hisani, hili jambo linaweza likafanyika katika leisure time, hii siyo sawa na hatutarajii iwe hivyo. Tunamwomba Mheshimiwa Waziri achukue hatua kwa wale Wakurugenzi wa Halmashauri ambao hawajatenga hii asilimia 10 na hawana maelezo yoyote. Maana wakati mwingine unaweza ukakuta tuna-review bajeti mtu hajatenga hii asilima 10 na hakuna maelezo ambayo tunaweza tukaridhika nayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hili siyo jambo la kufanywa kwa wakati wanaoutaka wao au kwa mapendekezo yao ndio waweze kutenga, wengine watatenga asilimia tano wengine asilimia mbili, hapana ni asilimia 10 kwa ajili ya kwenda kuwasaidia akinamama na vijana kujiinua kiuchumi. Wengi wanaona kwamba sehemu pekee ya kupata ajira ni Serikalini, Serikalini hakuna ajira, lakini tukiweza kuwapa mtaji pamoja na mafunzo ya ujasiriamali vijana wengi wanaweza wakatoka katika dimbwi la umaskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni madeni. Kweli hili jambo ni kubwa kidogo, ukiangalia suppliers wengi hususan wale locals wamekuwa hawapati malipo yao kwa muda muafaka. Hii inaweza ikasababisha waka-perish katika mzunguko huu wa kiuchumi kwa sababu capital yao imeliwa. Hata hivyo, naipongeza sana Serikali imeona umuhimu wa kulipa madeni hususan ya wazabuni pamoja na watumishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hili suala la wazabuni naomba priority kubwa wapewe kwanza wazabuni wale wadogo wadogo ambao wametoa huduma kwa Serikali lakini zoezi hili liende sambamba na uhakiki wa madeni hayo. Si kila mtu anayeidai Serikali anaidai kiukweli au si kila mtu pesa anayoidai Serikali imepitia katika mifumo sahihi ya manunuzi. Naomba utaratibu uwekwe ili wale watakaolipwa walipwe kwa viwango sahihi na lazima wawe na documentation zote ambazo zinawafanya walipwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni hili ambalo tumekuwa tukilizungumza la viwanda. Tunaipongeza sana Serikali chini ya Rais, Dkt. John Magufuli kwa kuona kwamba sasa ni muhimu Tanzania iende katika uchumi wa viwanda. Viwanda vingi viko katika maeneo yetu…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa umemaliza muda wako.
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.
MHE. SAADA MKUYA SALIM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kupata fursa hii na mimi nichangie katika mjadala uliopo mbele yetu. Na mimi naunga mkono hoja hii ya Serikali kwamba tusisaini mkataba huu kama ulivyo.
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuendelea mbele naomba ku-quote maneno ya Rais Mstaafu ambayo yalikuwa posted kwenye gazeti la East African, Mheshimiwa Mkapa alisema kwamba EPA is bad news for entire region. It is just bad news for entire region wala siyo for Tanzania, but for entire region.
Mheshimiwa Spika, mkataba kama huu kama ungekuwa una terms nzuri, basi nadhani ingekuwa faida kwa region, lakini faida vilevile kwa Tanzania. Terms zake hazifanani na haziendani. Mheshimiwa Rais Mkapa alisema vilevile kwamba the EPA for Tanzania and the EAC never made sense, the maths just never added up yaani zile hesabu zake haziendi kutokana na hali yetu ya kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, pengine ingekuwa sisi kama East Africa tunahitaji zaidi EU wana soko la watu karibu milioni 700, East Africa tuna watu karibu milioni 300 plus, tungekuwa tunawahitaji zaidi kama angalau kungekuwa kuna ule uchumi unaoendana, lakini hatufanani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, isipokuwa tumeuleta huu mkataba hapa na tutaukataa kabisa, lakini tuchukue hii kama ni nafasi ya Tanzania kuweza kujijenga zaidi.
Kwanza, kwenye viwanda, lakini pili pengine Mheshimiwa Waziri ulichukue hili iwe ni changamoto, ingekuwa vyema kwamba huu mkataba tunaukataa, lakini wataalam wetu watuletee alternative, yaani zile terms zinakuja, hizi haziwezekani, what do we want? Tunakoelekea regional integration ndiyo itakuwa inapata nafasi zaidi kuliko bilateral cooperation.
Mheshimiwa Spika, leo hatuuhitaji mkataba kama huu lakini ninaamini sera yetu ya kujenga viwanda itakapokuwa imefanikiwa, tutakuwa tunahitaji mikataba ya aina hii. Kwa maana hiyo, tutakapokuwa tunakwenda, tuone ni jinsi gani tunaweza kujenga uwezo wa watu wetu, kwanza, kuangalia critically mikataba ya aina hii, lakini secondly iendane na policy zetu ambazo pengine tungeweza ku-compete zaidi na mikataba mingine au na masoko ambayo yanaambatana na mikataba kama hii.
Mheshimiwa Spika, mkataba kama EPA unamaanisha nini? Tunakokwenda development cooperation inapungua na badala yake inakuja trade cooperation. Kwa maana hiyo, kama leo tutakuwa tunategemea zaidi development cooperation, kwa maana ya nchi matajiri kusaidia masikini, lakini kesho na nchi matajiri na wao zitataka ku-benefit kutoka kwa nchi masikini kama ilivyo sasa hivi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii ni changamoto kwetu sisi. Tutakuwa tumeshinda leo, lakini ninaamini kwamba ni nafasi nzuri ya kujiweka vizuri zaidi kuona kwamba tutakapokuwa tunakwenda mbele, watakuja wengine na mikataba kama hii, tutaweza ku-face vipi? Hatuwezi kukataa kila siku, lakini ninaamini kwamba tunaweza kuchukua fursa hii kama changamoto na tukajiweka vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kupitia kwako namuomba Mheshimiwa Waziri, ninaamini kwamba mkataba huu utakwenda kuathiri development cooperation na EU. Nadhani tumekuja mwaka 2013, Mheshimiwa Waziri wa Fedha by then, tulikuja tukataka ridhaa ya Bunge kwa ajili ya kuridhiria Cotonou Agreement ambapo ndani yake tunapata misaada mbalimbali. Sasa kama sasa hivi tunakataa huu mkataba ambao ni trade related, sina uhakika wala hatuombi, lakini inawezekana tukaathiri aid cooperation na EU, wanatusaidia!
Mheshimiwa Spika, sasa namuomba Mheshimiwa Waziri, mkataba huu ambao tutaukataa hapa Bungeni leo, ninaamini afanye namna atakavyofanya aende akawaelimishe wananchi wa Zanzibar kupitia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Kwa sababu ninaamini nao watafurahia jambo hili ambalo limekuwa decided na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanapaswa kufahamu jambo ambalo linaendelea ambalo lina maslahi ya Kitaifa.
Mheshimiwa Spika, namuomba Mheshimiwa Waziri, Baraza la Wawakilishi linaketi mwisho wa mwezi huu, aende akawape semina Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili na wananchi wa Zanzibar na wao waweze kuona kabisa kwamba Serikali pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya jambo la maana kabisa kutoku-rectify mkataba kama huu.
Mheshimiwa Spika, la pili, hii inakwenda zaidi kwenye regional integration. Na sisi tunahitaji zaidi tu haya mahusiano. Sasa kwenye hili, pamoja na mambo mengine kama nchi tufanye jitihada zetu kuweza sana kuhimiza South South Cooperation, yale mahusiano yetu na nchi ambazo tunafanana nazo kiuchumi, kimazingira na kiitikadi ili tuone kwamba hatuendi tu mbele tukawa tuna mahusiano na European Union watu ambao tupo tofauti kiuchumi hata kiitikadi, lakini vilevile tuwe tuna sera madhubuti ya kuweza kuimarisha uhusiano wetu na nchi ambazo Kusini Kusini, yaani tunaita South South Cooperation. Mheshimiwa Waziri hilo nakuomba sana ulichukue.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mheshimiwa Waziri la tatu; kwa vile tunategemea athari kubwa itatokana na kutoku-rectify hapa, bajeti yetu itakayokuja tuhakikishe kwamba ile miradi ambayo ilikuwa inafadhiliwa na EU, tuiwekee mikakati ili Serikali yetu iweze kuibeba iende ikafadhiliwe na Serikali yenyewe, ama angalau tutafute alternative. Zanzibar tumefaidika sana na Cotonou Agreement; tumejengewa bandari, vilevile kuna miradi mingi ya maji ambayo EU imesaidia, lakini vilevile kuna miradi mingi ya utawala bora kupitia NGOs imesaidiwa. Tunaomba sana Serikali ijipange ili tuweze kutafuta mbadala wa nani na vipi itasaidia kuweza kuendeleza miradi kama hii.
Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, naunga mkono hoja. Yangu yalikuwa machache sana, kwamba Serikali isisaini, lakini tuchukue hii kama changamoto kuweza kusimama zaidi, kujiimarisha zaidi na watu wetu.
Mheshimiwa Spika, ningependa zaidi kwamba kama unakuja mkataba huu tunaukataa, lakini angalau kungekuwa na mapendekezo mbadala, yaani tuseme kifungu hiki hatukiwezi, hatukitaki, basi tuwe na kifungu kama hiki ili tuendane nacho. Kwa maana na sisi kama block tunawahitaji wenzetu. Leo huu ni mkataba, siyo mzuri, lakini ninaamini wakati ambapo sera zetu zitakaposimama sawasawa na kufanikiwa, tutawahitaji wao na wengine.
Kwa hiyo, naomba zaidi tuwe tunafanya kazi ya ziada. Technical Committees zinapokaa ziwe zinafanya kazi ya ziada na siyo kukataa, lakini vilevile walete mapendekezo kwamba ingekuwa bora jambo kama hili lingekuwa limekaa namna kama hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Namwomba Mheshimiwa Waziri, tunasubiri semina kule Zanzibar ili hili liweze kujadiliwa, lifahamike na wananchi nao wapate kufaidika kutokana na maelezo haya. Nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa hatua madhubuti anazozichukua kuhakikisha kuwa kasi yetu ya uchumi inaendelea kukua kwa kusimamia mapato na kuyaelekezea katika sekta za kiuchumi na uzalishaji. Ni hatua za kupongezwa sana. Aidha nampongeza sana Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wa Wizara na taasisi zake. Naomba maelezo ya kina kuhusu yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ujenzi wa flyovers Dar es Salaam. Hii ni hatua ya kupongezwa sana kwa kuwa ujenzi wa flyovers ni jambo ambalo Serikali za awamu zote imetamani ilifanye. Ni hatua ambayo itawezesha harakati za kiuchumi katika mikoa ya jirani na Der es Salaam. Hata hivyo, wananchi wangependa kufahamu juu ya ujenzi huu sasa na tafsiri yake kiuchumi ukilinganisha na maamuzi ya Serikali kuhamia Dodoma. Ukiangalia kwa sasa foleni ya Dar es Salaam imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwepo wa mabasi ya mwendo kasi. Aidha, uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni pale Dar es Salaam. Swali linakuja, je, hizi flyovers zitaleta economic returns ukizingatia sababu za uwepo wa foleni pale Dar es Salaam zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa? Je, isingewezakana fedha za ujenzi wa flyovers zikatumika kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hapa Dodoma? Naomba maelezo ya kina ili wananchi wapate kuelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, uuzwaji wa hisa za Vodacom. Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kutokana na zoezi la uuzwaji wa hisa za kampuni za simu kuanza kutekelezwa. Mheshimiwa Waziri amesimamia jambo hili tokea marekebisho ya kanuni zake ingawa limechukua muda mrefu. Hata hivyo, mauzo ya hisa za Vodacom bado hayajatangazwa sana kwa wananchi kupata uelewa wake. Vilevile kuna hisia kwamba hisa za Vodacom ziko over priced ukilinganisha na thamani halisi ya kampuni. Tunaomba Wizara ikishirikiana na TCRA na Wizara ya Fedha na Mipango, waliangalie jambo hili kwa umakini ili kuondoa hisia hizi zilizopo.

Mheshimiwa Spika, tatu, Shirika la Simu Tanzania (TTCL). Napongeza hatua kubwa ya mabadiliko katika Shirika la Simu Tanzania. Mabadiliko haya yanapelekea Watanzania kunufaika na kujivunia kuwa na shirika lao wenyewe la simu. Hata hivyo, tunaomba, baada ya hatua hii TTCL iwezeshwe kimtaji iweze kuweka miundombinu sahihi kwenye simu iweze kushindana katika soko la mawasiliano. Changamoto kubwa tunayopata sisi Watanzania ni kutokana na huduma zisizoridhisha za TTCL. Kwa upande wa ISP, TTCL bado hawako vizuri despite ya kutumia miundombinu ya umma (fibre optic).

Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Pemba. Ingawa kwa muda mrefu jambo hili limekuwa likizungumzwa bado hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hadi leo. Uwanja wa Ndege wa Pemba ambao umewekwa katika program ya ujenzi kupitia EAC, Waziri hajazungumza lolote kwenye hotuba yake. Naomba atupatie maelezo kama Waziri mwenye dhamana hii ya mawasiliano na ujenzi kuhusu uwanja huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizari ya Maji na Umwagiliaji
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Na mimi nachukua fursa hii kwanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri na menejimenti yote ya Wizara, kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya. Maana tukisema kwamba hawafanyi kazi vitu vingine vinakuwa siyo katika disposal yao kwa hivyo nadhani hapa tulipo wamejitahidi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye sekta ya maji changamoto zipo nyingi, kuna kurasa ambazo Mheshimiwa Waziri amendika, kurasa 128, 129 na 130 anapongeza zile taasisi za kimataifa na mashirika pamoja na NGO’s ambazo zinasaidia sekta ya maji, ni nyingi kweli. Mimi nadhani tukiangalia kwenye assessment, sekta ambayo inapata support kutoka mashirika ya nje na ya ndani ni sekta ya maji, tuna karibu mashirika 62.

Hata hivyo, tukiangalia fedha ambazo zimepatikana katika kipindi cha bajeti ambayo tunakamilisha mpaka Machi ni fedha ndogo sana shilingi bilioni 181 ambayo ni sawa na asilimia 19 lakini wachangiaji wako wengi kweli. Hapa sasa lazima tujikite katika kuhakikisha kwamba tunaweka mikakati ya kuona kwamba fedha zetu sisi wenyewe za ndani ndizo zitakazokwenda ku-finance sekta ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, issue hapa wala siyo kuongeza bajeti, maana ukisema unakwenda kuongeza bajeti you just increase the numbers and then what? Hakuna hela, it is not about Hazina atoe hela, Hazina hana hela ni lazima aende akazitafute. Kwa hiyo, lazima tutafute chanzo ambacho kitakuwa sustainable ili kuweza kuona kwamba maji yanapatikana. Shilingi 50 kwa mimi ninavyoona tumepata shilingi bilioni 95 ambayo imekwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa, tuongeze shilingi50 nyingine kwenye lita hizo za mafuta. Hata hivyo, tunaweza tukaenda further tukaangalia vyanzo vingine, zile products ambazo zinatokana na maji zinaweza zikatozwa kwa asilimia fulani hata shilingi mbili kwa kila lita ili kusaidia kwenye Mfuko wa Maji, mimi nadhani hatua hiyo inaweza ikatusogeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya maji ina changamoto kubwa na ni sekta ambayo inategemewa karibu na kila sekta nyingine kwa mfano afya, elimu, ujenzi, kilimo na utalii. Sekta hii yenyewe ni lazima iweze kupeleka huduma katika sekta nyingine, hizi sekta nyingine zenyewe haziwezi kusaidia katika sekta ya maji. Kwa hiyo, tunaona kwamba hii ni changamoto na hapa tunaweza tukamsema Waziri, wewe Waziri sijui kizee, sijui nini, no, it is not about that, hii ni changamoto ya Taifa. Kila mtu anasimama labda anamshambulia Waziri, hii siyo katika disposal yake. Kwa hiyo, wakati tunachangia ni lazima tuone tunaisaidia vipi Serikali kupata chanzo cha fedha ambacho ni endelevu, kiko reliable kuweza kusaidia sekta ya maji. Shilingi bilioni 95 zilizopatikana kutokana na shilingi 50 ni asilimia 53 ya fedha ambazo imetolewa, ni hatua kubwa. Kwa hiyo, tukiongeza na nyingine nadhani Mheshimiwa Waziri tutakapokuja hapa mwaka kesho tukifanya tathmini ya sekta ya maji nadhani tutakuwa tumepata mafanikio. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kubwa zaidi lakini siyo kwa umuhimu kwamba nalisema mwisho kwa sababu ya muda, Mheshimiwa Waziri utakapokuja lazima utueleze fedha zinazotoka Exim Bank ya India ambazo mwaka jana ulizisema kwa mbwembwe zote na sisi Wabunge tunaotoka Zanzibar tulishangilia kweli, tukafanya kikao kuzipangia matumizi. Leo hatujaona kitu chochote, 31 million dollors, ni fedha nyingi sana na zinaweza zikabadilisha hali ya maji kule Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimboni kwangu tulitegemea sana fedha hizi mwaka huu ziende zikarekebishe miundombinu ambayo imechakaa mno na tuna dhiki kubwa ya maji, lakini safari hii naona hatujakusikia. Nadhani umesoma a line one or two lakini hatujajua process hii imefikia wapi, tunataka utupe maelezo ya kina. Tunajua kwamba masuala ya mobilization siyo yako, lakini kwa sababu umelizungumza Mheshimiwa Waziri ni lazima ulitolee majibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mimi pia nachukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa ambayo anaifanya. Nadhani hatuna budi vile ile kulipongeza Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania, hususan kwa upande wetu wa Zanzibar nadhani limejitahidi sana kurejesha discipline ambayo ilikuwa imeanza kutetereka, kwa hivyo tunalipongeza sana Jeshi letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja atueleze, kuna hospitali abazo zinaendeshwa na Jeshi. Ni Hospitali za Kijeshi ambazo wananchi wamekuwa na confidence nazo kwa kiasi kikubwa. Mwananchi ukimwambia aende katika hospitali ya kawaida na Hospitali ya Jeshi anakwenda katika Hospitali ya Jeshi kutokana na confidence kubwa aliyokuwanayo juu ya utendaji wa wanajeshi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hospitali hizi ziko katika hali mbaya sana, dawa hakuna, hakuna vifaa, lakini hata wale madaktari ambao si wanajeshi ambao wanapangiwa katika vituo vile wanakuwa hawakai kutokana na mazingira duni ambayo yapo katika vituo vile. Sasa tunaomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha atuambie ni mkakati gani hasa umewekwa kuhakikisha kwamba hivi vituo ambavyo vinatoa huduma kwa wananchi vinaimarishwa ili viwe na ufanisi zaidi kwa watendaji lakini vilevile kwa vifaa na dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inafika hadi kwa mwezi vituo kama vile vinapata OC ya shilingi 100,000, haviwezi kuendesheka kwa namna kama ile. Jimboni kwangu kipo kituo cha namna hiyo, inafika hadi hata panadol ya kuwapa wale wananchi wanaowatibu hawana. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nadhani hili lichukuliwe special consideration na utuambie mkakati ambao unatarajia kufanya katika bajeti hii ya mwaka 2017/2018. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia kuhusiana na wanajeshi wastaafu. Wanajeshi wetu wastaafu Mheshimiwa Waziri wanahangaika sana kufuata mafao yao. Once wanapostaafu tu ile connection baina yao na yule aliyekuwa mwajiri wao inakatika. Kwa hiyo, anapostaafu huyu
mwanajeshi, na hii ni kwa sababu ya experience ninayo, anakuwa hana msaada wowote zaidi ya kuanza kuhangaika kwenda kurudi, kwenda Hazina kudai mafao yao. Pengine wale ambao walikuwa wakihangaika katika kudai mafao yao kwa muda mrefu huenda taarifa zao zimepotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kule jimboni kwangu kuna mwanajeshi amestaafu muda mrefu, ni mtu mzima, amenipa namba yake ya file nimekwenda Hazina, namba ya file ndio, lakini jina silo kabisa. Hii inaashiria kwamba, wale wanajeshi wetu wakistaafu inakuwa ile connection hata zile taarifa zao zinakuwa hazipo, zinapotea, hakuna mtu wa kuwafuatilia. Kwa hiyo, tunaomba sana Mheshimiwa Waziri hawa wanajeshi wetu kuwe kuna mkakati maalum wa kutunza taarifa zao wakati ambapo wapo kwenye ajira, lakini wanapostaafu lazima kuwe kuna usaidizi kutoka katika taasisi zao walizokuwa ili wasiende kule kupata taabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa ni watu ambao wamefanya kazi nzuri kwa Taifa hili, ni watu ambao wameweza kulinda mali pamoja na roho za raia kwa kipindi kirefu na katika wakati mgumu. Haiwi vyema na haiwi busara kuona kwamba wakistaafu ndiyo sasa waanze wao wenyewe kuhangaika, waende Hazina, wapande ngazi warudi; na mara nyingine, hususan familia zile zinazoathirika. Wakati mwingine mwanajeshi anakuwa amefariki na familia ile kuanza kufuatilia mafao ya marehemu inakuwa ni kazi kubwa sana, wanakuwa hawapati usaidizi wowote kutoka katika jeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, kama walivyosema wengi kwamba sasa hivi kumekuwa kuna mchanganyiko baina ya makazi ya raia na Kambi zetu za Jeshi. Tunapata taabu sana sisi ambao tuna majimbo na tukiwa tunataka kukarabati miundombinu ambayo raia wao wenyewe pia wanatumia, lakini zimepita katika maeneo ya Jeshi, tunapata tabu sana. Sasa Mheshimiwa Waziri tunaomba hili nalo liangaliwe vizuri, jinsi gani sasa kama tukitaka kukarabati miundombinu katika sehemu ambazo Kambi za Jeshi zinapita lakini na raia wanatumia, tunafanya nini? Kwa sababu hii imekuwa ni changamoto kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la mwisho ni kuhusiana na mafunzo haya ya JKT. Upande wetu kule Zanzibar hizi nafasi zinakuja…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na mimi nashukuru kupata nafasi hii kuchangia bajeti yetu ya Serikali mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, kwanza nami nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara ya Fedha. Naamini kufikia hapa kwa uzoefu haikuwa kazi rahisi, tumefanya kazi kubwa na tumeleta bajeti ambayo inatafsiri dhana nzima ya Tanzania ya Viwanda. Mengi sana yamo na yanatafsiri hilo, kwa hivyo, ni lazima tukupongezeni kwa kazi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda niende katika maeneo specific, kwanza kuhusiana na ongezeko la Sh.40/= katika mafuta kwa ajili ya ku-compensate ile Road License fee


ambayo imefutwa iliyokuwa ikilipwa kila mwaka. Kiutawala nadhani hili limekaa vizuri zaidi na naamini kwamba Serikali itapata fedha nyingi zaidi kwa ajili ya kutekeleza bajeti yake.

Mheshimiwa Spika, binafsi naomba badala ya kuwa Sh.40/= tungeongeza Sh.10/= ziwe Sh.50/= kwa sababu tutapata ongezeko la Sh.6,950,000,000/=, hizi Sh.10/= specific zikaingie katika Mfuko wa Maji kama vile ambavyo tulikuwa tumeshauri kabla. Kwa sababu hizi Sh.40/= zinakwenda kutekeleza bajeti kwa ujumla wake, naomba tuongeze Sh.10/= tu ili ziwe Sh.50/= ziende zikaingie katika Mfuko wa Maji kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji hususan katika maeneo ya vijijini ambapo ndipo kuna shida kubwa sana ya maji ukilinganisha na mijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pengine wenzangu wanaweza wakauliza sasa tunaenda kuwapa shida sana wananchi ambapo hawatumii magari, lakini maendeleo ya nchi hayahitaji mtu yupo wapi, maendeleo ya nchi hii yanamhitaji mtu aliyeko kijijini na yule ambaye yuko mjini. Huko vijijini ambapo tunasema hawa watu tumewabebesha mzigo kutokana na kuongeza Sh.40/= ya mafuta ya taa lakini wao wana shida kubwa ya maji, wanahitaji sana barabara na umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, hili ongezeko ambalo nashauri Mheshimiwa Waziri lifikirie liende specific kwa ajili ya kuondosha shida ya maji katika maeneo hasa ya vijijini. Nadhani siku ya bajeti ya maji karibu asilimia 60 ya Wabunge wote walisimama na wakapata nafasi ya kuongea kwa sababu ya dhiki ya maji ambayo ipo katika maeneo yao. Kwa hiyo, naomba hili tulifikirie ili twende tukatekeleze bajeti kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile na mimi nisiwe mkosefu wa fadhila sana, niungane na Wabunge wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa hatua za kiutendaji anazozichukua kuona kwamba resources za nchi zinafaidisha wananchi wenyewe. Ni kweli fedha nyingi zimepotea lakini it is high time now kuweza kusimamia zaidi hizi sekta za kiuchumi. Inawezekana sana kama tungekuwa tumesimamia vizuri basi tusingekuwa hapa tunadonoa Sh.10/=, Sh.20/= kwenda kupeleka katika Mifuko ya Maji.

Mheshimiwa Spika, naamini kama tungekuwa tunasimamia vizuri, kwa utajiri ambao Tanzania upo tungeweza kutekeleza bajeti yetu kwa kutegemea kiasi kidogo sana cha misaada ama mikopo ya kibishara kutoka nje. Basi ndiyo hivyo imetokea, tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa sababu amejitoa kuhakikisha kwamba tunasimamia vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili bajeti iwe bajeti ambayo inaleta ufanisi, ni lazima bajeti hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweze vilevile kuona ina-support vipi bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwenye hili Mheshimiwa Waziri nina mambo mengi kidogo. Kwanza ni general budget support (misaada ya kibajeti). Nimeona katika taarifa ya Mheshimiwa Waziri kwamba misaada ya kibajeti tunaotea kupata around bilioni 311. Vilevile kuna maoteo ambayo tunatarajia katika bajeti ya mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, wakati huo huo bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesomwa jana ambayo inaelekeza mwelekeo wa kimaendeleo katika mwaka 2017/2018 lakini bajeti hii ambayo inakamilika ina kasoro ya fedha za general budget support ambazo zimeandikwa kwamba tutazipata. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri, hizi fedha kwanza angalau tujue ni kiasi gani mpaka sasa hivi zimepatikana ili kuona kiasi gani kinakwenda Zanzibar kutekeleza miradi ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haitakuwa busara sana kama bajeti yetu kwa upande wa Jamhuri ya Muungano inatekelezeka lakini kuna upungufu mkubwa katika kutekeleza bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tunaomba tujue ni kiasi gani zimepatikana na hicho kilichopatikana ifanyike haraka, kipelekwe Zanzibar kiweze kutekeleza miradi ya maendeleo. Hii vilevile ni pamoja na hizo fedha za mwaka 2017/2018. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile, mwaka jana tulibadilisha Sheria yetu ya VAT, kuna bidhaa ambazo zilikuwa zimezalishwa hapa na zimekwenda kutumika Zanzibar. Kuna fedha za refunds zinakaribia shilingi bilioni 21, bado hazijapelekwa Zanzibar na hili ni tatizo kubwa sana. Refunds za VAT pamoja Excise Duty zinachelewa kupelekwa Zanzibar, sasa kule tunachelewesha kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri pamoja na usimamizi mzuri wa kibajeti tunaomba asimamie fedha za VAT na Excise Duty ambazo ni refund zipelekwe Zanzibar kwa wakati ili tuweze kutekeleza bajeti vilevile kwa upande ule ambao ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile nataka kuchukua fursa hii kupongeza Shirika letu la Bima la Taifa, kwa mara ya kwanza limetoa gawio kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania shilingi bilioni 1.7. Ni kwa mara ya kwanza limetengeneza faida na limetoa gawio. Hata hivyo, Mheshimiwa Waziri katika eneo hili vilevile tulishauri kwamba taasisi za Serikali pamoja na vyombo vyake viwe vinaweka bima kupitia Shirika letu, hii itaongeza faida katika operation za Shirika letu la Taifa na kwa maana hiyo sasa hilo gawio litazidi zaidi. Kwa hiyo, tunaomba hilo lizingatiwe taasisi zetu za Serikali ziwe zinaweka Bima kupitia Shirika letu la Taifa ili tuweze kupata fedha zaidi kutekeleza bajeti yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili katika hilo hilo kuna ombi la kuanzisha Bima hii ya Kiislamu (Takaful) limekaa kwa Mheshimiwa Waziri muda mrefu sana bila ya kupatiwa majibu. Hizi ni products ambazo zinaendana na wakati tu. Kama tumeruhusu Benki zi- operate kwa principle za Kiislamu, kwa nini tunazuia bima zisi-operate katika principle za Kiislamu? Hili linawezekana lakini limekaa sana muda mrefu kwake bila kupatiwa majibu.

Mheshimiwa Spika, tunaomba sasa litekelezwe ili tuone kwamba wale ambao wana imani za Kiislamu na wao wanapata products ambazo zinaendana na imani zao. Ni biashara na ni products ambazo zinakuwa kutokana na mahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusiana na Benki yetu ya FBME, Mheshimiwa Waziri amezungumza vizuri kwamba hii benki sasa hivi imeshanyang’anywa leseni hai- operate tena. Kuna mambo ya kadha wa kadha yametokea lakini wananchi wameweka fedha zao FBME na katika matoleo ya mwanzo tumeambiwa kwamba hii benki itafanyiwa auditing two weeks za mwanzo na baadaye wananchi wataambiwa benki gani watakwenda kuchukua fedha zao. Hivi tunavyokwenda nadhani tunaingia mwezi wa pili, hakuna taarifa yoyote kuhusiana na fedha au zile amana za wananchi ambazo wanataka wao wenyewe kuzitumia.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wetu wa Zanzibar Tawi la FBME linafanya vizuri zaidi kuliko matawi mingine ya FBME Tanzania. Wananchi wengi wa Zanzibar wameweka fedha zao kwa ajili ya kwenda kutekeleza Ibada ya Hijja baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kama leo hatujui wapi fedha zetu tutazipata mnakwaza watu ambao wanataka kwenda kutekeleza hiyo ibada.

Mheshimiwa Spika, tunaomba tufanyiwe utaratibu kujua kwamba fedha hizi zinapatikana wapi, wananchi waende kuchukua fedha zao ili waweze kufanya pamoja na mambo mengine utekelezaji wa ibada hii muhimu ya Kiislamu baada ya kumaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Namuamini sana Mheshimiwa Dkt. Mpango, najua hili utalisimamia.

Mheshimiwa Spika, vilevile naomba nipate majibu…

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naomba kupata majibu ya masuala hayo niliyozungumzia. Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi namshukuru Mwenyezi Mungu katika Ijumaa hii ya leo kupata nafasi hii adhimu ya kuchangia Mpango huu wa Maendeleo ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wasaidizi wake wote kutokana na kasi ya utendaji na utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza kuchangia Mpango, Mheshimiwa Turky aligusia kidogo tittle ya kitabu hiki ni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili. Cha kusikitisha na cha fadhaa kabisa ni kuona hakuna hata eneo moja lililopangiwa mpango angalau tu ikaelekezwa katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano na hili nataka niliseme wazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia kwako, Mheshimiwa Waziri wa Fedha wakati tunajadili bajeti mwezi Juni, 2017 baadhi ya wenzangu tunaotoka katika upande wa pili wa Jamhuri tulichangia maeneo fulani fulani, lakini kwa masikitiko makubwa hakuna hata eneo moja lililoguswa likajibiwa hoja angalau kule upande wa pili wakasikia. Mimi nilichukua hatua ya kwenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri wa Fedha mbona hujajibu angalau basi hoja mbili ili wananchi wa upande mwingine wa Muungano waone kwamba na wao they are part and parcel ya Jamhuri ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliniambia muda mchache na majibu yalikuwa mengi. Nilijisikia vibaya kwa sababu kama una responsibility ya pande mbili za Jamhuri maana yake angalau ungechukua hoja mbili ukazijibu. Sasa aliniambia kabisa kwamba muda mchache, hoja zilikuwa nyingi kwa hivyo mimi nitakupa document usome, this is exactly jambo ambalo ameniambia nimesikitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunachangia hapa na nimeona tendency ya Wabunge ambao wanatoka upande mwingine wanachangia. Tuombeni Mungu angalau hoja mbili, tatu zijibiwe muda uwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda katika Mpango kuna jambo lingine kabisa la kusikitisha, kwenye eneo la utalii, biashara na masoko, hivi kwa namna gani au kwa namna yoyote unapotaka ku-promote utalii unaiachaje Zanzibar? Yaani hakuna na haielezeki! Utakuwaje na mpango wa ku- promote utalii Tanzania bila kuiingiza Zanzibar, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu yanaweza yakawa very simple ukisema habari ya Zanzibar majibu yanakuwa very simple kwamba hilo siyo jambo la Muungano. Hivi jamani kama kutakuwa kuna Wizara tatu za Muungano kwa nini sisi Wabunge tusiwe watatu tu humu ndani kutoka Zanzibar? Kwa nini tuko 53? Kuna masuala mengine hayahitaji lazima iwe ni Wizara inayoshughulika na Muungano. Kuna issues nyingine zinahitaji coordination za pande mbili. Kama hii issue ya utalii, hivi kweli kutakuwa na programu au project yoyote bila kui-include Zanzibar? Is not possible, haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwenye elimu ya juu, hii imo kwenye jambo la Muungano, there is nothing, Waheshimiwa hakuna jambo lolote ambalo limeguswa. Sasa sijui huu Mpango wa Taifa lipi hatujui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo lingine kwenye masuala ya habari, utamaduni, sanaa, ustaarabu, burudani na michezo. Sasa hivi tumeona Tanzania inaingia katika ramani ya michezo, lakini hakuna specific plan ambayo itaweza ku-accommodate angalau kujenga uwezo wa wachezaji wa michezo mbalimbali katika kuitangaza Tanzania, hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hii sanaa ya uigizaji, hawa waigizaji wameachwa kabisa. Toka juzi tunasikia wao wenyewe wamekwenda Kariakoo, sijui wanapambana na wale piracy na kadhalika, lakini sisi kama Serikali hakuna mpango wowote wa kuwasaidia wasanii wa Tanzania. Leo GDP ya Nigeria imekuwa rebased kutokana na contribution ya sanaa katika uchumi wao. Sisi tumefanya rebase kwa ajili ya kuingiza sectors mpya ikiwemo hii ya sanaa lakini hakuna mpango wa kuendeleza sanaa hii. Kwa hiyo, katika Mpango wetu wa Maendeleo naona hilo limeachwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala ya ushirikiano wa kimataifa, inasikitisha na inashangaza kuona katika eneo muhimu la diaspora limeachwa. Diaspora Ethiopia wameungana pamoja wanajenga hospitali kubwa kabisa ambayo ownership ni karibu asilimia 90 ya Waethiopia wanaoishi nchi za nje, sisi kwetu hakuna jambo lolote ambalo angalau tumeweka consideration ya kuangalia mobilization ya resources kutokana na diaspora, hakuna! Vile vyanzo vyetu vya mapato ni vilevile tokea Taifa hili lilipozaliwa.

Mheshimiwa Dkt. Mpango wewe ni mweledi tumeshakuwepo sana katika semina na vikao vya resource mobilization lazima tuangalie njia mpya ya kuweza ku-tap resources zilizopo ili kuelekeza katika Mpango wetu wa Maendeleo. Kuna role ya diaspora iko wapi, wenzetu wanai- issue diaspora bond na katika article moja ya World Bank, Tanzania imo kabisa katika nchi ambazo zina potential kubwa ya kuweza ku-mobilize diaspora bond. Hebu liangalie hili tutapata pesa nyingi. Watanzania wenzetu wapo kule lakini hawaoni kama Serikali ina nia ya kuweza kuwasogeza karibu ili na wao wakasaidia kuchangia maendeleo pamoja na uchumi wa nchi yao kama ambavyo wanafanya wenzetu wa Nigeria, Ethiopia na Uganda. Naomba eneo hili tuliangalie kwa mapana yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda, sera ambazo zinakuwa employed na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina effect hata kule Zanzibar. Tumeona na tunasifu kazi nzuri sana ya Serikali kwenye list ya viwanda ambavyo vinaendelea kujengwa na ambavyo vimeshajengwa. Waheshimiwa, the list is long lakini hakuna hata sehemu moja tukasema angalau tutashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ku-tap investors ambao wataweza kujenga kiwanda kitakachotumia malighafi ya karafuu, hiyo consideration hakuna, inasikitisha! Sasa Mpango huu wa Taifa, Taifa lipi bila ya Zanzibar, inasikitisha! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini juu ya hivyo, nimesahau jambo moja, nimepata kuulizia hivi jamani Mheshimiwa Waziri wa Fedha anashughulika na pande mbili za Muungano, at any point of time tokea ameteuliwa kuwepo pale ofisini alipata kwenda Zanzibar katika kikao cha kazi, siyo kikao cha kero za Muungano, kikao cha kazi? Nikaambiwa hajafika. Nadhani ni jambo ambalo linasikitisha. Nimeambiwa umekwenda katika vikao vya kero za Muungano, tunashukuru sana kwa sababu ku-participate ni katika hatua ya kutatua kero za Muungano, lakini kikao tu cha kuona kwamba kuna mashirikiano baina hizi Wizara mbili, ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar nimeambiwa hatujamuona Mheshimiwa Waziri. Tunakuomba Mheshimiwa Waziri katika sehemu zako za kazi ni pamoja na Zanzibar uwe unafika angalau usikie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo moja ambalo tulipata faraja kusikia around two weeks ago kwamba Makamu wa Rais amezindua Sera ya Microfinance, lakini kwenye Mpango na katika maeneo ya vipaumbele kwa mwaka 2018/2019 hakuna sehemu ambapo kuna mkakati maalum wa kuweza kusaidia hizi microfinance institutions zikiwemo SACCOs pamoja na VICOBA. Hizi institutions zinasaidia sana hususani akina mama ambao wako vijijini lakini lazima wawe katika aidha policy framework au legal framework ili na wao waweze ku-access mikopo kutoka katika banks. Sasa haijawekewa kitu chochote katika Mpango huu wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu Mheshimiwa Waziri kama nafasi itakuruhusu utakapokuwa unajibu hoja, naomba ujibu pamoja na hili ili wananchi wakusikie hususani wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine kwenye promotion za utalii kule Zanzibar kuna vivutio, tunajaribu kuweka mambo mbalimbali pamoja na wakati wa low season watalii hawaendi lakini sisi tunajaribu kuweka matukio ili tupate ku-tap. Tuna Zanzibar International Film Festival (ZIFF) pamoja na Sauti za Busara, ni vitu ambavyo angalau basi vingekuwa taped katika haya masuala ya mipango ili kuona kwamba utalii umo katika Mpango wa Taifa kusaidia Zanzibar pamoja na Tanzania lakini imekuwa ni competition. Sasa hivi nimesikia kumeanzishwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kupata hii nafasi. Kwanza lazima tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kukupa afya njema na tumekuwa pamoja leo hapa, kwa kweli kama haupo huwa tuna-miss kule kutokukuwepo kwako, kwa hivyo lazima tunamshukuru Mwenyezi Mungu Alhamdulillah rabbil- aalamina, Mwenyezi Mungu aendelee kukupa afya njema.

Mheshimiwa Spika, la pili vile vile nachukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, lakini vile vile pamoja Mawaziri Dada yangu Mheshimiwa Jenista Mhagama kwa kazi nzuri ambayo anaifanya na Manaibu wake wanafanya kazi nzuri sana sana na wanahitaji pongezi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sina hoja nyingi, ni chache. Kwanza nashukuru kwamba hotuba yetu hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu imelizingatia vile vile suala la Muungano, lakini kwa uchache wake imeeleza sana ni kwa jinsi gani hizi activity za kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za Muungano wetu. Tunashukuru kwa ku-note hiyo, lakini nadhani itakuwa busara zaidi tukiendelea mbele ku-note vile vile achievement ambazo zimepatikana katika Muungano wetu huu ambao kesho kutwa tu tunatimiza miaka 54. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati wazee wetu walipokuwa wanaunga, Mzee wetu Karume pamoja na Mwalimu Nyerere waliungana wakijua wanaungana na kila mmoja alikuwa anajua wanaungana katika context ipi. Wakati tunaungana Zanzibar ilikuwa ndogo hata leo wakazi wake nadhani kwa takwimu labda tunaweza kuwa tumefika kama milioni moja na laki tano ni kidogo ukilinganisha na wakati huo ilipokuwa Tanganyika hata leo Tanzania zaidi ya watu milioni hamsini, lakini ilikubalika kwa spirit ya kuwa Muungano wetu utakuwa na mutual benefit katika maeneo ambayo tumekubaliana.

Mheshimiwa Spika, sasa pamoja na mambo mengi ambayo yalikuwa yamezungumzwa hapa na nakuomba sana Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ikiwa Zanzibar haimo hili haliwezi kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Neno la Jamhuri ama jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatokana na uwepo wa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, wiki iliyopita kulitoka mijadala mingi sana hapa na mjadala ambao unazungumzwa na anayezungumza ni mwana CCM anavyoi-portray Zanzibar as if Zanzibar hakuna mamlaka. Sasa naomba leo kupitia Bunge lako Tukufu tunaomba hizi statements za kuidogosha statements za kuidhalilisha Zanzibar ziishe. Lazima tu- recognize Zanzibar ina Serikali inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein, Zanzibar kuna chombo cha kutunga sheria ambacho ni Baraza la Wawakilishi, lakini Zanzibar kuna Mahakama.

Mheshimiwa Spika, unapozungumza kwamba Zanzibar ama Kiwanda cha Mahonda ambacho kinazalisha sukari isiingie kwa sababu si sukari inayozalishwa Mahonda nadhani kuna mis-conception kubwa sana hapa. Nitaomba sana Waheshimiwa Wabunge tunaposimama ni lazima tuwe tuna takwimu sahihi.

Mheshimiwa Spika, tunakubaliana theory zote katika dunia hii za uchumi, theory zote zinasisitiza kuhusu masuala ya production, kwa sababu ndiyo yanayojenga long term growth. Sasa vile vile kwa upande wa Zanzibar ilipokuja sera ama ilipokuja hoja ya viwanda; uchumi wa viwanda ni uchumi wa viwanda kwa Tanzania nzima; na Zanzibar nayo ikajitutumua ikasema na sisi tuna kiwanda.

Mheshimiwa Spika, sasa kupitia Bunge lako vile vile naomba Waheshimiwa Mawaziri namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu tunamshukuru kwa ziara yake aliyoifanya, lakini nadhani itakuwa busara zaidi akifanya special visit kwa ajili ya ku-visit kile Kiwanda cha Sukari Mahonda. Hatukatai walanguzi wapo na walanguzi si peke yao wanatoka Zanzibar hao wanaokwepa kodi wako kila sehemu na Alhamdulillah Serikali zote mbili zinajitahidi katika kupambana nao.

Mheshimiwa Spika, nami naungana na Waheshimiwa wenzangu kwamba hawa watu wasiachiwe, lakini ukianza kuitengeneza Zanzibar as if wale ambao wanakwepa kodi, wale ambao wanakuja na majahazi, wale wanaotembea ni kwamba ndio Zanzibar na ndiyo character ya Wazanzibari, nadhani hili siyo sahihi hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi biashara zipo tunafanya, mimi nadhani katika Muungano wetu hakukuwa na kikwazo hiki cha Inter-trade tunafanya biashara. Kule Zanzibar kuna viwanda vya maji, lakini vile vile vina-compete na viwanda utakuta Kilimanjaro ipo Zanzibar imejaa. Kwa hiyo sisi hatuku- withdraw ipo.

Mheshimiwa Spika, utakuta maji mengi ambayo yanazalishwa Dasani yote yapo na biashara inakwenda, why this so special to sukari? Bidhaa zipo mbalimbali na nadhani statement zinapotoka namna kama hizi, hawa ni watu ambao hawautakii mema huu Muungano wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huu Muungano wetu tunauhitaji sote, wazee wetu walipoungana wameungana kwa spirit ya umoja, lazima sisi tuwe wamoja. Leo unaposimama ukaizungumza Zanzibar huwezi kusimama ukaizungumza Kenya au Burundi namna kama ile. Unapomzungumza ndugu yako kwa maneno ambayo si ya kweli huwezi hata kumwambia mtu mwingine yuko mbali; hili siyo sahihi wenzangu.

Mheshimiwa Spika, ubaya wa mambo tunaozungumza wengine wengi ni wana CCM ambao hata Zanzibar chama kinachoongoza ni Chama cha Mapinduzi.

Tuna Serikali ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi. Sasa unapoongea, sasa hivi nimemsikia kuna Mheshimiwa anasema wafanyabiashara kwa sababu ya sheria kali wamehamia Zanzibar, do you know Zanzibar?

Mheshimiwa Spika, tukizungumza Zanzibar maana yake ni kwamba sisi Waheshimiwa tumekwenda asubuhi jioni tumerudi. Kuna sheria zake, sheria zipo na Serikali inajitahidi, changamoto hazikosi na ziko kila sehemu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Bunge lililopita tumeambiwa, kuna Mheshimiwa alisimama hapa anasema Zanzibar haijawahi kukamata hata kilo moja ya Cocaine, lilizungumzwa ndani ya Bunge hili. Ukiniambia hivyo unadharau mamlaka, unadharau Serikali, unadharau jitihada ambazo zinafanyika. Hawa watu kila siku wanakamatwa na hizi juhudi zinafanyika katika pande mbili zote.

Mheshimiwa Spika, tumeambiwa Mawaziri wanakutana, Mawaziri hawa wanazungumza na wanakuwa wana jitihada zao wenyewe wanazungumza. Sawa changamoto zinatokea tunakubali, lakini si katika context hii ambayo inazungumzwa, lazima tuheshimu.

Mheshimiwa Spika, trust me, Zanzibar ikiwa inazungumzwa kiasi kama hiki sisi Wabunge ambao tunatoka Zanzibar tunajiona humu ndani kama second class MP’s which is not fair. Sisi ni Wabunge kama Wabunge wengine, unapoizungumza Zanzibar na sisi tunapata uchungu kwa sababu kinachozungumzwa si sahihi.

Mheshimiwa Spika, tunawaomba haya mambo ya kukaa ukaanza kudharau mamlaka nyingine ambayo zimo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaomba sana, tunapata tabu sana kule nyumbani, wanatushangaa sana wenzetu, what are you doing there? Kwa sababu kinachozungumzwa kinakuwa hakina fact.

Mheshimiwa Spika, tunaomba jamani tuheshimiane, tuwe vizuri kwa sababu tuna spirit moja katika chombo cha dola ambacho tunakutana na tuna-converge hasa kwenye context ya Muungano ni Bunge lako la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunakuwa wamoja sote tunasimama kwa pamoja tofauti zetu za kiitikadi zipo, lakini when it comes to United Republic of Tanzania hiki ndicho chombo ambacho kina-portrait.

Mheshimiwa Spika, sasa…

T A A R I F A . . .

MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, namheshimu sana ndugu yangu, nilichokizungumza hapa kilichokuwa kimezungumzwa Bunge lililopita Zanzibar hakujawahi kukamatwa hata kilo moja ya unga. Kwa hivyo ninapozungumza vilevile awe ananisikiliza vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, context hii ya ujenzi wa viwanda inasaidia sana katika ujenzi …

T A A R I F A . . .

HE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, naipokea.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa pamoja na hayo hizi ni katika changamoto za maendeleo ya nchi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kupata fursa hii ya kuchangia mpango wetu wa maendeleo. Kidhati kabisa nichukue fursa hii kumshukuru Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake na watendaji ambao wamewezesha kutuletea kitabu hiki kwa sababu natambua kwamba, siyo kazi rahisi, lakini imewezekana na imekuja tumeanza kujadili toka juzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maeneo machache ya kuzungumza. Nianze kwa kutambua achievement moja ambayo imepatikana katika Serikali ya Awamu iliyopita na Awamu hii, hususan katika utekelezaji wa mipango yetu kwa upande wa establishment na implementation kwa Tanzania Agricultural Development Bank ambayo imekuwepo kwa lengo la kusaidia ukuaji wa kilimo kupitia katika sekta mbalimbali lakini vilevile kupitia kwa individual. Mheshimiwa Mbene alizungumza despite kwamba TADB ipo na inaendelea na utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kifedha lakini bado tabu ipo palepale. Kwa maana kwamba individual ambaye amejishirikisha na kilimo akitaka kupata mkopo gharama inakuwa kubwa kwa sababu kwanza TADB requirement yao lazima upitie PASS (Private Agricultural Sector Support) ili wakuandikie plan ambayo mara nyingine inakuwa very expensive kwa mtu ambaye anataka production kwenye kilimo. Tumeweka hiyo TADB lakini masharti yake yamekuwa sawasawa na benki nyinginezo, kwa hiyo, utaona kwamba kumekuwa na ugumu uleule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ingekuwa vizuri kama tumeweka TADB kwa ajili ya kusaidia kilimo isiwe TADB inafanana na commercial banks nyingine. Lazima kuwe kuna utaratibu ambao umewekwa specifically kwa ajili ya kuwapatia mikopo. Inawezekana kabisa rate ni ndogo TADB ukilinganisha na banks nyingine lakini ile gharama ya acquisition ya mkopo yenyewe inakuwa ni kubwa kwa sababu anakumbana na vikwazo vingi. Kwa hivyo, tunaomba TADB utaratibu wa kuwakopesha wakulima pamoja na kampuni zinazojishughulisha na kilimo uangaliwe upya ili tuweze kuona kwamba tunafikia malengo tunayokusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilikuwa nataka kuzungumzia ni katika ukurasa wa 42, udhibiti wa katika matumizi ya fedha za umma, imetokana vilevile na ukurasa wa 41, mahitaji ya rasilimali fedha. Ni jambo zuri katika mambo yote yaliyotajwa kwamba kuhakikisha kuwa kampuni zote ambazo Serikali ina hisa zinaendeshwa kwa ufanisi na hivyo kutoa gawio stahiki kwa Serikali. Ni jambo zuri sana na mimi napata moyo sana kwenye hili kwa sababu kuna sehemu nyingine ambapo Serikali tumekuwa na hisa lakini kweli hatupati gawio kama inavyokusudiwa. Tunaweza kuwa tunapata gawio lakini sio kama inavyostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba nimkumbushe Mheshimiwa Dkt. Mpango, kuna mashirika mengine ya Serikali ambayo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanatoa gawio, Zanzibar haijawahi kupata stahiki yake katika magawio ambayo yapo katika mashirika ya Muungano. Tunaomba katika usimamizi wa utaratibu huu kwa mpango huu Zanzibar iwe inapata gawio stahiki kutokana na mashirika ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo Zanzibar ni sehemu yake nayo inaingia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini si hilo tu, vilevile katika usimamizi wa taasisi na mashirika ya umma, tuhakikishe mashirika ya umma yanajiendesha kibiashara, yanaandaa mwongozo wa gawio utakaotoa utaratibu wa malipo ya gawio kwa Serikali. Hili limeanza kufanyika, nadhani tumeshuhudia sio mbali Mheshimiwa Rais akipokea gawio kutoka katika mashirika yetu ya umma. Kuna mashirika baadhi ya mashirika ni ya Muungano lakini Zanzibar kabisa haijapata senti katika gawio ambalo limetolewa na ni gawio stahiki kabisa kwa hivyo, tunaomba hilo liangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa taasisi ya umma ambayo inatoa gawio ni Benki Kuu ya Tanzania, hakuna gawio lingine linalotoka katika taasisi nyingine. Tunaomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha kuanzia mwaka huu wa fedha Zanzibar iwe inapata stahiki yake kama ilivyo kwa mujibu wa Katiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo huu umetambua sana umuhimu wa miundombinu kwa ajili ya ukuaji wa uchumi. Katika aspect hiyo, imeongelea kabisa ujenzi wa bandari, ujenzi wa barabara pamoja na viwanja vyetu vya ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana wakati nachangia mpango na niliuliza kwa nini mpango huu hauja- integrate Zanzibar, nilipata majibu ambayo kwa wakati ule pengine yalikuwa valid kwamba katika Katiba iliyopendekezwa tunakusudia kuweka Tume moja ambayo itashughulikia mipango. Sasa hivi hatuna matumaini ya Katiba Mpya, Mheshimiwa Dkt. Mpango tunafanya nini, as a follow back position? Kwa sababu huu mpango Zanzibar haimo ni sawa, lakini utekelezaji wake kwa namna yoyote uta-integrate masuala ya Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye masuala ya bandari, kuna barua imeandikwa sijui toka lini kwa ajili ya acquisition ya mkopo kutoka Exim Bank ya China kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri Zanzibar. Document inakwenda inarudi, kwa Mwanasheria imerudi, kwa maoni ya Kamati imerudi, kwa NDMC imerudi, miaka nenda miaka rudi. Kwa taarifa nilizozi-dig out hii Bandari ya Mpiga Duri imeanza kuzungumzwa miaka 25 iliyopita, hakuna kinachoendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu bandari ni kichocheo kikubwa sana cha uchumi hususani uchumi wa visiwa, tunaomba vile unavyo-feel kwamba huu mpango aspect yake kubwa ni pamoja na miundombinu, feel kwa Zanzibar aspect ya ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri. Aspect ya ujenzi wa Terminal III iko katika ngazi zenu, tunaomba mliangalie hili ili sasa na uchumi wa Zanzibar ambao hauja- integrate humu kwenye mpango na wenyewe uweze kuendelea kutokana na mipango ile ambayo itatekelezwa. Tunaweza kule kutengeneza mpango lakini unahusika na wewe moja kwa moja, tunaomba sana hili lizingatiwe tena lizingatiwe kweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitabu cha Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nadhani na wao wanafanya research na wanakuja na alternative. Kuna taarifa hapa imenishtua kidogo hususani ukurasa wa kwanza wanasema kwamba kiwango cha umaskini Tanzania kimefikia asilimia 47, hii ni taarifa ya kutisha na haiwezekani kabisa. Wakati tunafanya research zetu ni lazima tuangalie vyanzo sahihi vya information kwa sababu document hii wanaweza wakaja wengine wakasema kama ni reference document. Unaandika taarifa ambayo tumem-quote William Atwell, mimi nimekuwa very much interested nimekwenda kumtafuta huyu William Attwell ni nani? Yeye mwenyewe katika taarifa ambayo iko kwenye website ya Frontteers Strategy Group amekuwa quoted huyu hiyo asilimia 47 ameipata yeye kutokana na recent visit yake kwa East African countries. How could you just to have a recent visit ukaweza kupata estimate ya 47% ya population. Nadhani this is very wrong. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jumba lina dhamana kubwa katika nchi hii. Sina uhakika kwenye Kanuni zetu lakini just kutoa taarifa kwenye blogs halafu tunakuja tunazileta hapa ndiyo zisaidie maendeleo ya Taifa hili, it’s just very wrong. Tunatarajia takwimu sahihi katika vyanzo vya kuaminika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haraka haraka nimekwenda kwenye website ya World Bank, taarifa ambayo imetolewa mwaka 2017 inasema Tanzania basic poverty line ni 28% lakini food poverty line ni 10%. Sasa tunasema hii 47% imepatikana wapi? Tunaomba sana pamoja na mambo mengine Kanuni zetu ziwe zinazingatia takwimu sahihi kwa sababu wananchi wanaotuamini wanaweza waka-quote hii kama ni takwimu sahihi, hususani kwenye hizi blogs inakuwa ni mawazo ya mtu mwenyewe binafsi rather than kuwa takwimu sahihi.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. SAADA M. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii na naunga mkono hoja za Kamati zetu mbili ambazo zimewasilishwa hapa na tunaendelea kujadili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mchango wangu leo kwanza nataka nitumie forum hii ya Bunge kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na Baraza lake la Mawaziri kuona umuhimu mkubwa uliopo wa kuondosha tozo ya Ongezeko la Thamani kwa umeme ambao ZECO wananunua kutoka TANESCO. Tunashukuru sana sana na kutokana na jambo hili tunaona spirit kubwa iliyopo katika Serikali ya Awamu ya Tano kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo katika Muungano wetu. Kwa hivyo, tunamshukuru sana na naamini Wazanzibari wamefurahi sana kwenye hili na wanaishukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na shukurani hizo, vilevile naomba kuzishukuru Kamati zetu za Bajeti na Kamati yetu ya Nishati na Madini kwa sababu kwa pamoja walitoa uzito mkubwa kuona kwamba Serikali inalitatua tatizo hili kwa haraka zaidi. Tunazishukuru sana Kamati hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee, naomba nitoe shukurani hizi kwa Mheshimiwa Spika kwa sababu alipobaini jambo hili hakusita kulipa uzito unaostahiki na hatimaye limekwenda kutatuliwa. Tunawashukuru sana pia Wabunge wote ambao walikuwa wamelichangia jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na VAT, kiukweli VAT ni jambo moja dogo katika mambo mengi ambayo yanaikabili Shirika letu la Umeme la Zanzibar (ZECO) wakati linaponunua umeme kwa TANESCO. Lazima nikiri, Waziri wa Nishati na Naibu wake wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana na kwa nia hasa ya dhati inaonekana. Nikiongea na Mheshimiwa Waziri ananipa commitment ambayo inatoka kabisa moyoni kwake kwamba wanajitahidi kuhakikisha hata zile gharama nyinginezo ambazo zimeonekana ni mzigo mkubwa sana kwa ZECO ambazo zinakwenda kwa wananchi wanaotumia umeme kule Zanzibar, amekuwa akinipa comfort na commitment ya hali ya juu. Tunataraji sana, sana, sana hili jambo litafanyika kwa uharaka zaidi ili kuona kwamba tunakwenda kupunguza ule mzigo wa gharama ya umeme ambao unanunuliwa na ZECO kutokea TANESCO. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo hili nadhani tunapata mafunzo ya mambo mawili; kwanza ni kuhakikisha ama ni kuona kwamba hata katika zile sekta ambazo hatuzioni ni za Muungano lakini tunajua katika utekelezaji wa activity zetu zina athari katika pande mbili za Muungano. Kwa mfano, kama utaangalia tozo hizi ambazo zinatozwa utaona kwamba Zanzibar wanaweza tu wakanunua lakini kuna athari kubwa katika upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano ambapo vilevile kuna wananchi wa Tanzania nao wanatumia. Kwa hivyo, hilo ni funzo moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini funzo la pili, ni kuona ushirikishwaji wa taasisi zetu hata kama siyo za Muungano. Kwa vile tuko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna umuhimu mkubwa hata katika sekta zile ambazo siyo za Muungano kufanya kazi kwa pamoja ili kuona kwamba hali hii ambayo inaweza tu ikatokea ikaleta mgogoro somewhere inaondoka. Kwa hivyo, hata tunapokwenda katika bajeti tunaomba consideration ya taasisi ambazo zinafanya kazi zinazofanana zifanye kazi kwa pamoja ili kuona kwamba manufaa yanayopatikana yanakuwa ni ya pande mbili za Muungano. Tunaipongeza sana Serikali, tunampongeza sana Mheshimiwa Waziri, tunampongeza sana Naibu Waziri kwa sababu tunaona kwamba ile commitment ni ya dhati kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati imeoimba sana Serikali kuona ule mchakato ama yule consultant ambaye anafanya kazi ya kuangalia gharama nyinginezo aweze kuharakisha. Vilevile tunapokwenda huyo consultant, of course, amepewa terms of reference lakini nadhani hajui kwa dhati jinsi gani hasa hasa hizi sekta mbili zinavyofanya kazi yaani sekta moja lakini katika pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, pengine ingewezekana sisi kama wananchi ama watu wetu wa ndani hata kama ni consultant awe ni mtu wa ndani ambaye anajua kiundani operations za Serikali zetu mbili. Kama tunatafuta mtu mwingine ambaye hata hajui operation yenyewe inavyofanya kazi hataweza kujua kiundani tatizo lililopo na yeye ataangalia katika business level. Hiyo inaweza kabisa kuleta utata katika mapendekezo ambayo atayatoa na pengine sana azimio ambalo tumeazimia lisiweze kufikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna doubt kwamba umeme ni nyenzo kubwa sana katika uchumi wa Taifa hili. Kwa upande wangu unajua sometimes unaweza ukawa unashangaa mtu anapinga mradi wa umeme kwa mfano wa Stigler’s Gorge. Sasa hivi Tanzania tuna uhaba wa umeme na Serikali inafanya initiatives kwa ajili ya kutafuta umeme. Wenzetu pengine walioko nje ambao kwa namna moja ama nyingine wanahisi kutakuwa kuna maslahi wao wanaangalia katika aspect ya mazingira lakini tunaojua hitaji hasa la changamoto hii ni sisi Watanzania. Kwa hiyo, kwenye suala kama hili la kitaifa tukiacha tofauti zetu za kisiasa na kimtazamo, nadhani kuna umuhimu mkubwa wa kui-support Serikali yetu kwenda kuangalia jinsi gani tunaweza kupata umeme wa uhakika na wa kutosha ili kuona kwamba uchumi wetu unapaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tukiangalia tuko katika tuko hiyo development stage tukiwa tunaangalia uchumi kukua, tunakua katika kiwango ambacho bado hatujakua vizuri lakini kinaweka miundombinu ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa uchumi wetu uweze kubeba development za watu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo tunaomba wenzangu hata katika maeneo kama haya ya kitaifa ni lazima tuwepo pamoja na ni lazima tuungane pamoja tuone kwamba tunai- support Serikali kwa nguvu zote kuona kwamba inakwenda kutekeleza jambo hili. Mtu mwingine atakuwa anaangalia kwa mawazo yake mengine, of course tunajua kwamba kuna choice baina ya ukuaji wa uchumi na mazingira, lakini sisi kwa sababu ni Taifa ambalo linaloendelea tunahitaji development, tunahitaji uchumi wetu ukue, lazima choice tuangalie lile ambayo utaleta impact kwa wananchi wengi walio maskini rather than kuangalia hasara kidogo ya upande mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naipongeze sana Serikali na tunatarajia kwamba hizi process ambazo zinaendelea zinakamilika kwa haraka zaidi ili kuona kwamba stiegler’s gorge project ile inafanikiwa na tunataka kuzalisha umeme ili umeme ufaidishe wananchi mmoja mmoja. Naamini the more umeme utakapokuwa unapatikana Tanzania Bara pengine inawezekana hata ile multply effect ikaenda mpaka Zanzibar. Kwa hiyo, kwenye suala la maendeleo hakuna budi lazima tuungane kwa pamoja, tuone kwamba hili jambo linapatiwa ufumbuzi wa haraka na tunaweza kufaidi matunda ya uhuru wetu kama vile ambavyo tumekusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Serikali vilevile kuona kuna umuhimu wa kuanzisha Balozi kule Cuba. Hili suala nadhani tumelisema sana humu ndani na limejadiliwa kwa mapana, lakini kwa sababu Serikali yetu ni Serikali sikivu imeona kuna umuhimu sana wa kufungua ofisi kule Cuba na tunatarajia sana mafanikio yale ambayo tunayo sasa yataendelea kuleta athari chanya zaidi katika uchumi wetu kutokana na kazi ambazo Balozi atakuwa anazifanya kule Cuba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipatia nafasi hii na naunga mkono hoja na nazipongeza Serikali zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuona kuna nia ya dhati kabisa ya kutatua changamoto za Muungano. Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri tunawapongeza pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni dakika tano, itabidi niende haraka haraka. Katika kitabu cha Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 14 ameelezea kuhusiana changamoto ya ongezeko na gharama za umeme ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imehakikisha kwamba changamoto hii inaondoka na tunaipongeza sana kwa hilo. Hata hivyo, changamoto hii ya VAT si kwamba inakwenda moja kwa moja kuondoa gharama za umeme kwa mwananchi wa kawaida wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba Mheshimiwa ukiwa mwenye dhamana ya kuratibu masuala ya Muungano, Wizara ya Nishati ihakikishe kwamba yule Consultant ambaye amepewa kazi ya kuangalia gharama za umeme anamaliza kazi hii mapema zaidi ili wananchi sasa waweze kunufaika kutokana na kupungua kwa gharama hizo. Hii VAT imeondoka lakini haijaondoa hizo gharama kama vile ambavyo tulitarajia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, Mheshimiwa Waziri amejikita zaidi sasa kuendelea kutoa elimu. Mchangiaji aliyemaliza kuongea Mheshimiwa Genzabuke amesisitiza jinsi gani Wizara iangalie hii elimu inapelekwa katika shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu. Naamini Mheshimiwa Waziri wakati hilo linaendelea mimi nadhani elimu kuhusu Muungano ianzie humu ndani katika Bunge letu Tukufu kwa sababu bado tunaona hata baadhi ya Wabunge ile concept ya Muungano haijatuingia sawasawa. Ndiyo maana hata baadhi tu ya kauli zinaweza zikawa zinatoka ambazo unahisi kwamba huyu mtu bado hajafahamu hasa nini maana ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo hata katika ngazi ya watendaji linatokea. Changamoto zinazoonekana ni kwa sababu ya issue za Muungano hazijawa mainstreamed. Kama tumeweza ku-mainstream issue za HIV, gender na mazingira, Muungano ni issue ambayo inatakiwa kuwa mainstreamed, wether iko kwenye eneo ambalo taasisi zetu zinafanya kazi kwenye Muungano au katika taasisi ambazo siyo za Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaloliona sasa hivi Mheshimiwa Waziri anayeshughulika na Muungano yeye ndiye anakuwa responsible kuangalia masuala ya Muungano lakini Wizara ambazo tunaziona tu kikawaida kwamba siyo Wizara za Muungano lakini moja kwa moja lolote linalofanyika katika Wizara zile linaathiri upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, Muungano huu siyo Muungano ambao anausimamia Mheshimiwa January Makamba ni Muungano ambao sote tunakiwa tusimamie katika maeneo yetu tunayofanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa na utaratibu Mawaziri ambao wanachaguliwa katika Taasisi za Muungano mara moja wanakwenda Zanzibar, wanamwona Mheshimiwa Rais na viongozi wengine lakini I do hope hilo haliishii kwenye kwenda kumuona Mheshimiwa Rais, linatakiwa liwe katika kazi zetu za kila siku. Bahati mbaya wale ambao wameji-term kwamba Wizara zao siyo za Muungano hatuwaoni kwenda Zanzibar labda siku ya Sherehe za Mapinduzi, tunaomba sana hii nchi yetu ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 16 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri ameeleza mambo mengi yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na gawio la Benki Kuu. Tunashukuru sana Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutoa gawio. Hii ni taasisi ya Muungano na inasimamia fedha za Serikali lakini bado Mheshimiwa Waziri kuna taasisi za Muungano na gawio halitolewi. Kuna taasisi ambazo zina operate katika Muungano lakini hatuoni gawio kwenda Zanzibar. Kwa mfano, Mashirika yetu kama TCRA, AICC, NIC, TTCL, bado gawio haliendi Zanzibar. Hizi ni taasisi za Muungano na inatakiwa gawio linatolewa kwa Serikali ya Jamhuri na Zanzibar ipate.

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia hoja ambayo iko mbele yetu. Naunga mkono hoja na nitakwenda kwenye maeneo mawili matatu specifically.

Mheshimiwa Spika, kwanza naanza na Shirika letu la Ndege, Air Tanzania. Naipongeza sana Serikali kwa uamuzi huu ambao umekuja kuwa implemented katika awamu hii, lakini tumeanza mazungumzo muda mrefu na tumeanza mipango ya kufufua hili shirika katika awamu zilizopita. Mkurugenzi Mkuu wa shirika anafanya kazi nzuri, lakini tunaomba aangalie utaratibu mzuri zaidi wa kupunguza unnecessary delays, hususan katika safari ambayo tunafanya kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma.

Mheshimiwa Spika, ukipanda ndege mara saba, nadhani mara tano tunapata delays; na tunaambiwa mara nyingi kwamba kunakuwa kuna operational problems, lakini kunakuwa kuna delays. Kwa hiyo, hiyo kidogo inapunguza ufanisi wa shirika letu la ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kiukweli ni kwamba shirika hili ni la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini toka kuanzishwa shirika hili hatujawahi kuwa na Mjumbe wa Bodi anayetoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maana ya Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nataka Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa, asije akaniambia napandikiza, namwambia kwamba hakujawahi kuwa na Mjumbe wa Bodi na hili ni shirika letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nataka tu anijibu kwa nini hakujawahi kuwa na huyo Mjumbe wa Bodi na kuna matatizo gani hasa? Kwa nini asikuwepo? Lini atakuwepo Mjumbe huyu wa Bodi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, tunaipongeza sana Mamlaka ya TCRA kwa kuendesha zoezi hili la usajili wa line za simu. Hoja yangu kubwa hapa ni kwamba hili ni zoezi zuri na litatusaidia kama Taifa, hususan kupunguza uhalifu kwa njia ya mitandao, lakini wakati zoezi hili linaendelea, kitambulisho kikanachotakiwa ni kitambulisho cha NIDA. Kule Zanzibar wengi tuna vitambulisho vya Mzanzibari (Zan ID), hivi kwa nini TCRA haikubali mtu asajili line yake kwa kutumia Zan ID ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetumia pesa nyingi sana kuwekeza? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kule Zanzibar sisi huwezi kuishi, maisha yako hayatakwenda kama huna Zan ID. Sasa tukija kwenye TCRA ambayo tunajua ni Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nini haitambui Zan ID kwa mtu ambaye hana kitambulisho cha NIDA? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba atakapokuja Mheshimiwa Waziri atuambie ni kwa sababu gani TCRA haikubali mtu asajili line yake kwa kutumia kitambulisho chake cha Mzanzibari ambacho kwetu katika miamala yote, katika matukio yote, katika kila unalofanya Zan ID lazima iwepo? Kwa hiyo, naomba hilo lizingatiwe na tuje kupata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, tunapongeza Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuendelea kabisa kuona kwamba inatekeleza kazi zake kwa ufanisi. Kuna maeneo kadhaa ambayo katika mwaka 2019/2020 itaendelea kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuendelea kutekeleza mradi wa kuanzisha vituo 10 vya TEHAMA.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri atakapokuja atuambie hivi huu mradi wa vituo 10 vya TEHAMA, wapi na wapi utatekelezwa na tuone kwamba kwa upande wa Zanzibar vituo hivyo vitajengwa wapi au vitatekelezwa wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ambalo nataka kuzungumzia ni kuhusiana na ndege zetu hizi ndogo. Mara nyingi sisi wa visiwani tunatumia sana ndege hizi ndogo, lakini tunachokiona mara nyingi ni kwamba, badala ya kuwepo marubani wawili kunakuwa kuna rubani mmoja.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2018 au mwaka 2017 wakati lilitokea tatizo kupitia ndege hii ya Coast Airline, nakumbuka Serikali ilitoa tamko kwamba, ni lazima tuhakikishe kwamba ndege zetu hizi ziwe na marubani wawili, lakini umekuwa utaratibu wa kawaida, hata kama tunapanda hizo ndege, tunatoka Dar es Salaam tunakuja Dodoma, rubani anakuwa mmoja.

Mheshimiwa Spika, sasa tunaomba Serikali i-literate yale mazungumzo yake ama tamko lake, tuone kwamba hizi ndege ndogo zinapunguza sana matokeo ambayo hatutarajii, lakini sababu isiwe kwamba kunakuwa kuna rubani mmoja. Hili jambo lipo na limezungumzwa, lakini sasa hivi naona linatoweka na halipewi msisitizo ambao unahitajika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, otherwise nashukuru sana kwa kupata nafasi hii. Naomba sana Bodi ya Shirika la Air Tanzania tuone Zanzibar na yenyewe inakuwepo. Nashukuru. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Mpango wetu wa Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoliendesha gurudumu hili la maendeleo hapa Tanzania. Ameonesha weledi mkubwa hususan katika kuweka usimamizi mzuri kabisa wa rasilimali zetu lakini kurejesha nidhamu ya kazi hususan kwa watumishi wa umma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Naibu Waziri pamoja na timu yote. Kwa kweli mpango hadi kufikia hapa tunaletewa sisi na tunasomewa na kuona kwamba kila kitu kimepangika basi siyo kazi nyepesi, ni kazi ngumu lakini tumeweza ku-manage na kufika leo kwa mujibu wa ratiba ilivyopangwa. Pongezi zenu sana na katika kipindi hiki kwanza nampa pole sana Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango kwa baridi lakini naamini ata-manage kuchukua maoni yetu haya, haitamuathiri of course. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wangu kwanza naomba nitoe maoni ya ujumla. Mpango wetu ni mzuri umepangika na unaeleweka vizuri lakini kidogo naomba katika yale maeneo ya usimamizi ama maeneo ya tathmini ni lazima sasa tuweke wajibu wa kila mdau katika mpango ule. Ukisoma sasa hivi utaona ni wadau wachache wamewekwa pale lakini naamini kwamba kila mmoja wetu kwa nafasi yake ana nafasi kwa ajili ya kutekeleza Mpango wetu wa Maendeleo lakini vilevile ana nafasi kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wenyewe wa Mpango wa Maendeleo. Kwa hiyo, naomba utakapokuja Mheshimiwa Waziri au hiyo version nyingine itakayokuja ambayo ndiyo itaweka frame ya bajeti yetu, wadau wanaohusika katika utekelezaji na tathmini waelezwe kwa kina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mfano, kwa mfano, Waheshimiwa Wabunge hatukutajwa katika Mpango kama as if sisi wajibu wetu tu ni kutoa recommendations hapa lakini actually sisi tuna wajibu wa kusimamia na kuchukua maelekezo haya na kuwapelekea wananchi tunaowawakilisha. Katika changamoto moja iliyoainishwa humu ni kwamba wananchi hawaelewi kwa kina kuhusiana na Mpango huu, sisi kama Wabunge, mbali ya kutoa recommendations hapa lakini tuna wajibu wa kuchukua haya maoni na kila kitu na kuwapelekea wananchi ambao ndiyo tunaowawakilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wananchi wenyewe wana wajibu wa kutekeleza Mpango huu. Kwa hiyo, nashauri wadau wanaohusika waelimishwe vizuri kuhusiana na mpango na sisi kama Wabunge tuna kazi hiyo lakini tuna kazi vilevile ya kupitisha bajeti hapa kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango. Kwa hiyo, hili ni suala technical ambalo nadhani litakwenda kufanyiwa kazi wala halina shida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine ni dogo tu, hizi projects zilizoainishwa humu kuna ujenzi wa campus ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa upande wa Zanzibar. Nadhani ili hili likae vizuri, campus ile ya Zanzibar sasa hivi inaitwa Kampasi ya Karume. Kwa hiyo, naomba tukiiandika tuwe tumeiandika vizuri kwamba sasa hii campus ya Zanzibar siyo campus ya Zanzibar ni ya Karume na imeekwa hivyo kwa umuhimu wake. Kwa hiyo, lazima tu-take note on that. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niende katika maeneo specific. Pengine katika miaka miwili, mitatu iliyopita wakati tunachangia Mpango wengi wetu hususan sisi Wabunge ambao tunatoka Zanzibar tuli-take note kwamba Mpango haukuainisha kitu chochote ambacho kinahusiana na Zanzibar. Inawezekana majibu yalikuwa ni kwamba Zanzibar wana Mpango wao, that’s good lakini Mpango huu wa Maendeleo una areas of support kwa Zanzibar na nadhani ni muhimu tukazieleza ili sasa katika improvement ya Mpango iwe imeainishwa vizuri. Kuna maeneo ambayo hakuna namna lazima yaingie kwa sababu ndiyo wajibu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye masuala ya uwekezaji (investment); inawekana kabisa siyo jambo la Muungano, lakini international cooperation ambayo ndiyo msingi wa kupatikana EFDI’s, ni suala la Muungano. Sasa ikiwa tutaangalia ku-enhance International Cooperation kwa maana ya mashirikiano ya kimataifa bila ya kuangalia upande mwingine katika context ya uwekezaji, hatuwezi kufanikiwa. Huu Mpango wa Taifa una wajibu vilevile wa kuangalia maeneo ambayo yanavuka yanakwenda Zanzibar. Hayo maeneo tunapenda angalau yawe yameainishwa katika Mpango huu, siyo lazima katika utekelezaji wa moja kwa moja, lakini katika mipango yetu ni lazima yaoneshwe kwenye uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingine tunaona kuna makongamano ya wawekezaji yanafanyika, lakini tukiuliza pengine labda ushiriki wa Zanzibar uko wapi, utaambiwa hili siyo jambo la Muungano, lakini international cooperation pale ni jambo la Muungano na ni jambo ambalo linabebwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo hatuwezi kukwepa kwa namna nyingine yoyote, ni lazima tushirikiane kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kuhusiana na biashara, ni vizuri Mpango wetu huu wa mwaka 2020/2021, unaangalia hasa kuimarisha biashara kimataifa pamoja na biashara kikanda. Biashara (Inter Trade) kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar bado imekabiliwa na changamoto kubwa sana hususan pale ambapo biashara ama pale ambapo bidhaa zinazozalishwa Zanzibar zikitaka kuja sasa Tanzania Bara angalau ku-access soko, zinakabiliwa na changamoto kubwa. Biashara ya kikanda, biashara ya kimataifa haitaweza kuimarika kama biashara ndani ya nchi, ndani ya pande mbili itakuwa inakabiliwa na changamoto. Hili lipo katika wajibu wa outline ya Mpango huu ambao tunauelezea na hili ni lazima liangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi Mheshimiwa nadhani Jaku aliuliza swali kuhusiana na changamoto hizi za biashara lakini majibu mepesi, majibu ya moja kwa moja yanayotelewa ni kwamba haya mambo tunayapeleka katika Kamati ya SMT na SMZ. Unajua vitu vingine viko katika capacity yetu, ile Kamati inakutana siyo mara nyingi na kwa wakati mmoja hatuwezi kuainisha changamoto zote zinazoukabili Muungano wetu. Pengine mambo mengine sisi kama watendaji tunafaa sana tusaidie hawa viongozi wetu, siyo lazima twende katika Kamati ile, lakini sisi katika capacity yetu tumeteuliwa kwa sababu ya kuwa na capacity ya kusimamia maeneo yetu. Tunaweza kabisa kuyachanganua bila ya kupita katika kamati, katika cooperation zetu, katika Wizara zetu na taasisi zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, hii inawezekana si moja kwa moja kwenye Mpango, lakini Mpango una wajibu wa kuhakikisha kwamba hata ule Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar na wenyewe unaendelea na unafikiwa ili kuleta matumaini mazuri ya maendeleo kwa Watanzania wote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni utalii, tunashukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa bold vision hii ya kununua ndege zetu. Ndege pamoja na benefits nyingine, ndege hizi zinatumika katika kutangaza utalii, lakini hakuna ndege hata ambayo at least ina nembo ya utalii kwa upande wa Zanzibar. Hakuna! Shirika la Ndege la Tanzania ni Shirika la Muungano. Kwa hiyo ni wajibu hata basi tu kuwe na connotation labda Stone Town au karafuu. Yaani angalau tuwe tumebeba dhana ya utalii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hilo halipo. Kwa hiyo tunaomba utalii siyo jambo la Muungano lakini tools za utalii zinabeba Muungano wetu. Tunaomba basi angalau consideration hiyo iwepo na iwe inatekelezwa. Presence ya Zanzibar katika Shirika letu tuwe tunajua kwamba this is ours, tuwe tuna ile sense of ownership. Tunapongeza sana hizi hatua lakini tunajua kwamba obligation hii ipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye masuala ya umeme tulipiga sana kelele kuhusiana na VAT. Nashangaa mambo madogo kama haya tunachukua muda mrefu sana kulumbana katika nyumba hii, lakini hatimaye hilo limekuwa tunaishukuru sana Serikali. Gharama za umeme bado na Mheshimiwa Waziri amekuwa akisema mara nyingi kwamba hilo jambo linafanyiwa kazi. Linaendelea kufanyiwa kazi, linaendelea kufanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka mitatu, lakini wananchi wa upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaumia na maisha. Mpango huu wa maendeleo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hautakuwa mpango successful kama kwenye sehemu nyingine katika Jamhuri…..

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante sana.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii kuchangia hoja ambayo iko mbele yetu. Kwanza naunga mkono hoja, lakini nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais a Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha kuweka mikakati madhubuti kwa ajili ya kuendeleza sekta ambazo ziko katika Wizara hii. Nampongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri pamoja na viongozi wote katika Wizara hii kwa kufanya kazi zao kwa weledi na ufanisi mkubwa, hongera sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda mimi nitajikita katika eneo moja tu, nalo ni uvuvi wa bahari kuu. Specifically nitajikita katika kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority).

Mheshimiwa Mwenyekiti, taasisi hii ni taasisi ambayo kwa kweli ikiweza kufanya kazi vizuri inaweza ikachangia kwa kiasi kikubwa mapato ambayo Serikali zote mbili zinapata. Vilevile mazingira mazuri yatasababisha wavuvi, wananchi ambao wanajishughulisha na shughuli za uvuvi katika bahari kuu nao kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa wengi walizungumza kuhusiana na suala la some percentage ya hao wanaojishughulisha na uvuvi, lakini ukiangalia Zanzibar, kwa maana ya Unguja na Pemba asilimia 100 kwa sababu ni visiwa ambavyo, kama definition ya visiwa, vimezungukwa na bahari, sasa uone kwamba, taasisi hii kwa kiasi gani ni muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini taasisi hii imekuwa ikikusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali zikiwemo leseni na mambo mengine; lakini katika mwaka 2017 hii royalty au mrabaha wa senti 40 za dola zimesababisha kwa kiasi kikubwa taasisi hii kupungua kwa mapato yake ya kujiendesha kama mamlaka, lakini hata mchango wao kwenda katika Serikali Kuu umetoweka, hususan kwa mwaka 2019 hakuna leseni ambayo imekatwa kutokana na tozo hii. Na cha ajabu, maana si kama tumeweka tozo hii kwamba ndiyo tunaimarisha mapato ya ndani, mapato yameondoka na hawa wawekezaji katika sekta hii wanakwenda nchi nyingine ambazo hazina tozo hii. Kwa maana hiyo mapato ambayo sisi tulikuwa tunatarajia kuyapata tunayapeleka katika nchi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nadhani umepata concern za Wabunge lakini vilevile na za wadau mbalimbali kuhusiana na tozo hii. Hii tozo si kwamba uifute moja kwa moja lakini unaweza ukatoa space ili tuweze kufanya review kuona kwamba je, tunaweza tukaangalia maeneo mengine tupate mapato?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu kwa kinachoonekana sasahivi inaonekana ni kwamba labda utendaji mzuri wa Wizara yetu hii ni kutokana na mapato, lakini utendaji mzuri, yaani mafanikio ya Wizara yetu ni kuona productivity katika maeneo mbalimbali imeimarika na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye Pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Deep Sea Fishing Authority mapato yake kwanza inatakiwa asilimia 50 ijiendeshe yenyewe, kama tunavyojua ni mamlaka, lakini asilimia 30 inaingia katika Mfuko wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na asilimia 20 inaingia katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anafahamu, asilimia 20 kwa namna yoyote, kwa mapato ya aina yoyote ni significant contribution kwa ajili ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ikiwa Mheshimiwa Waziri bado una-resist ku-review hii kanuni, maana siyo sharia, ni kanuni, kwa ajili ya kuondoa tozo hii maana yake unaumiza Serikali hizi. Unaumiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaumiza na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Sisi Mheshimiwa Tizeba nakwambia Zanzibar tunalia, tunalia kwelikweli, tunalia kwelikweli na tumeshazungumza muda mrefu. Mheshimiwa Waziri hii tozo iondoshe kwa muda ili uwape nafasi mamlaka wafanye review waweze kuangalia maeneo mengine. Sisi tunakosa wenzetu wanapata, na si kwamba tunakosa kwa wananchi tu bali unakosesha mapato kwa Serikali zote mbili; Mheshimiwa Waziri liangalie hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sana Mheshimiwa Waziri aje na majibu ambayo yataleta matumaini. Otherwise tutashika shilingi tuone kwamba kwa ujumla wetu sisi kama Wabunge tunalichangia hili maana yake pesa zinaondoka, mapato yanakosekana na hata hao wavuvi, wawekezaji ambao tunatarajia wawepo wanaondoka wanakwenda sehemu nyingine ambapo wenzetu hawana tozo ya aina hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, otherwise naunga mkono hoja na ninaomba sana Mheshimiwa Waziri utakapokuja utueleze kwa kina ni kwa sababu gani tozo hii inaendelea kuwepo na impact yake kuendelea kuwepo kwake. Ahsante. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kutuwezesha leo kuwepo hapa asubuhi, kwa ajili ya kukamilisha majadiliano yetu. Nachukua fursa hii vilevile kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara hii kwa kukamilisha mchakato huu na kuleta Muswada huu hapa Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kalamu ni kitu ambacho muhimu sana. kama tutakitumia vizuri, tunaweza tukajenga nchi yetu na watu wake vizuri. Mwenyezi Mungu katika Sura ya 96, katika Quran kwenye aya ya nne anazungumza kwamba amemfundisha mwanadamu kuandika kwa kalamu, kwa kuonesha umuhimu na hii ni sura ya kwanza wakati inateremshwa Quran. Kwa hivyo kalamu ni jambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu ya kila siku. Kwa maana hiyo, katika content hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kuwa na gut ya kusogeza Muswada huu hapa ambapo tunaujadili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuongelea sana suala zima la uanzishwaji wa Mfuko wa Mafunzo wa Waandishi. Tumezoea sana zikija sheria hapa, pamoja na mambo mengine, kwamba zinakuja na uanzishwaji wa Mfuko. Lakini sheria zinatekelezwa au zimeendelea kutekelezwa isipokuwa utekelezaji wa Mfuko unachelewa sana sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Wabunge wenzangu despite ya kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, tunamwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja mwakani na bajeti Mungu akituweka hai na uzima, tuungane sote kwa pamoja tuhakikishe kwamba Mheshimiwa Waziri ametuambia source of fund ya Mfuko huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu tukiwa tunazungumza tu kwamba, fedha zinazotokana na Mfuko huu ni fedha ambazo zitakazokuwa appropriate hapa na Bunge hii, nadhani haitakuwa sahihi. Maana yake, tunajua fedha ina mambo mengi na kama Mfuko haujawekewa source of fund specific kwa ajili ya implementation ya Mfuko huo, hatuendi mahali popote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri mbali ya mambo mengine tunampongeza, lakini Wabunge wenzangu tuhakikishe kwamba yale maslahi ambayo tunataka waandishi wa habari wayapate, mambo mazuri ambayo tumekuja nayo pamoja na sheria hii ili yatekelezeke, tumwambie lazima tumsimamie Waziri tuone kwamba, ametuletea source maalum ya fund kwa ajili ya utekelezaji wa Mfuko huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hizi sifa zote zinaweza zikapotea kama hili jambo litakuwa halijatekelezwa. Tunakuomba sana, najua utafanya hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili vilevile naunga mkono hoja hii ya kuweko accreditation bodi. Mwandishi wa habari amechukuliwa kama kibarua tu wa kawaida every now and then, sote tumeshuhudia maskini waandishi wa habari ukitoka nje ukiandikwa usitoe pesa uwagawie, yaani wewe mwenyewe unawaonea huruma kutokana na hali ilivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza hii accreditation bodi itampandisha value hata yeye mwenyewe yule mwandishi. Itampandisha value kwamba yeye ni mwandishi ambaye tayari amekuwa accredited yaani ni mwandishi ambaye amepata ithibati. Kwa maana hiyo, mategemeo yetu, maslahi yake kwanza yatakuwa mazuri. Vilevile hata taarifa na habari ambazo ataziandika zitakuwa ni habari ambazo zimetokana na mwandishi ambaye amekuwa accredited. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana hili ni jambo la msingi tukiachia tofauti zetu za kisiasa, lakini hili ni jambo la msingi sana. Kwanza kabla ya yote tunataka Mheshimiwa Waziri, mara tu Rais akishasaini hii, kanuni zisije zikachelewa. Tunaomba tupate na kanuni kwa haraka sana ili tuweze kutekeleza sheria hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo linatia mashaka kidogo Mheshimiwa Waziri na naomba sana tupate advice yako, ni kuhusiana na kazi ambazo zitakuwa zinatekelezwa na bodi. Hususan zile ambazo bodi itakuwa ina-advice the Government on training ya media, kuna media ama kuna journalist ambao watakuwa katika public sector, lakini wengine watakuweko private. Huu Mfuko ama hii bodi itaweza ku-advice vipi waandishi wa habari ambao watakuwa private na wao wakawa facilitated kwenye training ile. Sina uhakika hii itakuwa covered vipi kwa sababu the way it has been written in the Bill ni kwamba ime-accommodate.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua Serikali ama Mfuko utakaoanzishwa sina uhakika how far utakwenda katika kuwasaidia waandishi wa habari, aidha, ambao ni freelancer au ambao wanaandikia vyombo binafsi. Kwa hivyo, hilo tunaliomba pia lifanikiwe. Naamini sana, kwa Muswada huu wa sheria tunaweza tukatengeneza Salim Kikeke wengi kutoka Tanzania kuliko ambaye yuko BBC. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Muswada huu tukiutekeleza vizuri, Mheshimiwa Waziri tutatengeneza akina Christiane Amanpour ambao ni waandishi wa habari weledi tu katika dunia na ambao tunawaamini. Kwa hiyo, tunataka huo utekelezaji uanze mara moja, lakini with specifically kwenye fund kwamba ianze kutekelezwa na Mheshimiwa Waziri atuambie hasa source of fund hii inatokea wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri ni mwanamke, hujatuambia kwenye sheria wala mimi napata ukakasi sana kama hii itakwenda kwenye regulation hajatuambia kwenye sheria hii bodi content ya wanawake iko wapi? Eeh! hajatuambia tunaweza kusema at least two lakini hata wanaweza wakawa watatu mpaka wanne, hii haijasema katika sheria na sijaona kwenye marekebisho yake, kama hili amelirekebisha (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana, waandishi wa habari hususan wanawake, kwanza ni watu ambao wanafanya kazi vizuri sana, vilevile mazingira tu yale yenyewe ya kufanyia kazi, ina-pro mwanaume kuliko mwanamke. Kwa hivyo, tunaona kwamba kuna umuhimu hasa katika bodi hii vilevile wawepo wanawake ambao wataweza kusimamia maslahi ya waandishi wa habari wanawake katika sheria hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine na la mwisho, kalamu hii, nimesema mwanzo, kalamu ni jambo ambalo lina-shape Tanzania yetu. Unaweza ukaandikwa vizuri kwenye gazeti na siku hiyo chart yako ikapanda. Lakini tumeona of recent Mwenyekiti wa Kamati hii alivyopata kiki sana maana yake kila kwenye gazeti anachambuliwa yeye, kutokana tu na Muswada huu.
Naamini kwa sababu na aidha wahariri au waandishi wenyewe hawakusoma na wakaona hasa kitu kilichopo na ndiyo maana kilikuwa kinaandikwa shell will.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa basi kwa maana hiyo, uandishi ni jambo ambalo litasimamia sana mwelekeo wa nchi yetu. Tumeona mwenzangu hapa Mheshimiwa Amina alitaja kilichotokea baada ya gazeti lile la…
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana naunga mkono hoja na natumaini Mheshimiwa Waziri atayatekeleza.
Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kupata fursa hii ya kuchangia hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Mawasiliano. Kwanza kabisa, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai pamoja na afya na kuweza kufika hapa kuendelea na majukumu yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja hii, hasa kwa sababu Serikali inaji-tune katika mabadiliko haya ya kiutendaji kazi. Maana yake tulipokuwa Bungeni kipindi kilichopita mara nyingi tulikuwa tunapata maelezo ni jinsi gani Serikali inataka kujitoa katika ule ubia pamoja na Bharti Airtel na kuwa shirika hili liwe owned a hundred percent by the Government na maoni mengine hatayalitoka upande wa pili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nadhani sasa Serikali imekuja na majibu na naipongeza sana kazi iliyokuwa imefanywa na Serikali ya Awamu ya Nne kuhakikisha kwamba tunatoka kwenye ule ubia na sasa shirika letu linakuwa owned by the Government a hundred percent. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunampongeza vilevile CEO wa TTCL, ndugu Waziri Kindamba ambaye anafanya kazi nzuri as occurence na nadhani huwa anakuja na ideas nyingi sana katika mazingira haya ya kidijitali pamoja na kimawasiliano. Tunampongeza na tunamwomba sana aendelee na jitihada zake za kutaka kubadilisha utendaji mzima wa TTCL. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitazungumzia hasa upande waoperations kwa sababu tumeulizia, kwa sasa hivi hatuwezi tena kuleta amendments, kwa hiyo namwomba sana Mheshimiwa Waziri ayachukue haya ambayo nitayasema ili ayafanyie kazi katika operations zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza hili ni shirika la Muungano, application yake ni Tanzania Mainland as well as to Tanzania Zanzibar, kwa hiyo, tunaomba katika sura ya uongozi, shirika hili liwe katika sura ya Muungano. Tunaomba sana shirika hili upande wa Zanzibar kuwa na may be Resident Director au mtu mkubwa ambaye atakuwa ana-coordinate upande wa Zanzibar na awe ni Mzanzibari kwa ajili ya ku- create ownership lakini vilevile kwa ajili ya kupata support kubwa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu TTCL kwa upande wa Zanzibar ina-serve taasisi za Serikali lakini vilevile kuna Balozi ambazo zinafanya kazi zake Zanzibar na Mashirika ya Kimataifa na asilimia kubwa inategemea sana TTCL. Kwa hiyo, tunaomba sura ile ya kiuongozi iwe ni sura ya Muungano kwa vitendo siyo kwa maneno. Tunaomba kuwe na Mtendaji Mkuu ambaye atakuwa Zanzibar, awe ni Mzanzibari lakini vilevile labda tunaweza tukagawa kwa zone baina ya Unguja na Pemba. Hiyo ita-create ownership lakini vilevile ita-create utendaji mzuri wa TTCL kwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili hata suala la ajira, kuna vijana wengi Zanzibar ambao wanamaliza technical colleges na ni weledi lakini when it comes to ajira hata ukitaka ku-apply TTCL lazima waje headquarters. Tunaomba sana kwa upande wa Zanzibar shirika hili lipewe mandate ya kuweza kuajiri vijana ili waweze kufanya kazi katika shirika lao ambalo lipo upande ule wa pili wa Jamhuri. Hatuwezi kuyaingiza hapa haya lakini katika masuala yote ya kiutendaji Mheshimiwa Waziri tunaomba sana alisimamie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Zanzibar, watendaji ni wazuri mno, mimi nyumbani natumia TTCL, once ikiwa kuna any fault ukiwapigia simu tu kwamba kuna tatizo, wale watendaji wanaharakia kuja kuangalia tatizo liko wapi lakini wanatumia vifaa duni mno. Katika barabara za ndani za Zanzibar ukiona TTCL wanakuja na ile, what they call it, bajaji, ngazi, wakati sasa hivi tuna revamp operation za TTCL, tunaomba kwa upande wa Zanzibar tufikirie vilevile na vifaa.

Wana vifaa duni vya kufanyia kazi wao wenyewe ni weledi, ni mahodari, wanajituma kwa nguvu zote lakini when it comes to vifaa bado vifaa vya kufanyia kazi ni duni, tunaomba hili Mheshimiwa Waziri aliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, TTCL operation zake mara nyingi sisi ambao tuna-rely on TTCL with data na vilevile voice kuna-breakdown ya mara kwa mara na ya muda mrefu. Unaweza ukakaa siku nne au tano usipate data na wala huwezi kupata hata voice. Sasa unaulizia unaambiwa labda mtambo uliharibika, sasa saa nyingine wanakuwa hawana uwezo nalo kwa sababu siyo jambo ambalo limeharibika local, mara nyingi inakuwa ni network nzima. Kwa hiyo, tunaomba sana katika marekebisho haya ya kiutendaji lazima tuangalie hili suala la breakdown ya mara kwa mara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye service delivery, kama nilivyosema, tunaomba TTCL Zanzibar iwe treated kwa major areas kama inavyokuwa Dar es Salaam na Dodoma kwa sababu Zanzibar ile TTCL ina-serve taasisi za Serikali lakini vilevile Mashirika ya Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri kuna jambo moja amelisahau, hii ni Bill ambayo ita-apply kote lakini tumesahau ku-define government. Application ya government hapa ni muhimu kwa sababu kuna infrastructure ownership kama ambavyo imetafsiriwa kwenye ukurasa wa sita ile ya support core network yaani ni ownership ya infrastructure yenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukumbuke kwa upande wa Zanzibar kuna fiber optic which is not part of this. Kwa hiyo, naona kama inaweza ikaleta mkanganyiko. Kwa hivyo, hebu atakapokuja kujibu hizi hoja tunaomba a-define, fiber optic ya Zanzibar is not part of this infrastructure ieleweke hivyo na kwamba hii sheria isije ikakanganya.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuhusiana na Board composition, kuna mtu amezungumza kwamba hili ni Shirika la Muungano lakini nadhani kuna hii tendency ya kufikiria kwamba Shirika la Muungano kwenye Board of Directors una-qualify at least one member representative from Zanzibar. Hivi huwa najiuliza, why at least one member? Hili ni Shirika la Muungano why should not be two? Kwa nini wasiwe wawili? Yaani mtu mmoja ndiyo atakuwa ana- represent Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani huu mwelekeo tuuangalie zaidi inaleta sura ambayo siyo nzuri sana katika mustakabali mzima wa Muungano. Mheshimiwa Waziri aliangalie hili, siwezi kuleta marekebisho lakini naamini hii at least one member should be at least two members, why one? Tunaomba suala hili liangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile limesahauliwa jambo moja muhimu, the way ilivyokuwa qualified hakuna gender consideration. Tunaomba kwenye mambo ya teknolojia kama haya, wanawake sisi ndiyo tuko mbele kweli kweli. Lazima liangaliwe kwenye masuala ya management, teknolojia tuko mbele, tunaweza kweli kweli. Tunaomba sana gender equality iwe-considered katika hii Board composition. Suala la Zanzibar, suala la gender tuangalie kwa makini kweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo limeonekana vilevile kuhusiana na hizo directions ambazo Minister may give to the Board naona tuache Board iwe inafanya kazi yake rather than to accept directions from the Minister. Kama tukiiacha Board ikawa inajiendesha itaweza ku-compete katika mazingira haya magumu, very complex ya kiteknolojia, lakini mara kwa mara Mheshimiwa Waziri akiwa anaingilia na anaweka directions to the Board how to operate hii cooperation nadhani halitakuwa ni jambo la buasara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi maneno yangu yalikuwa ni machache lakini naomba sana Mheshimiwa Waziri ayazingatie katika positive outlook kwa sababu tunaweza sana tukajichanganya kwenye operation zetu. Tunaomba sana, TTCL kwa upande wa Zanzibar inafanya kazi nzuri lakini ipo katika mazingira magumu kiutendaji. Ajira zifikiriwe, TTCL Zanzibar iajiri wenyewe Wazanzibari ambao wana sifa kuingia kwenye TTCL kwa sababu ita-create ownership na vilevile itaweza kufanya kazi nzuri kwa sababu itakuwa ina-serve Serikali lakini ina-serve mashirika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tunaona sana jitihada za TTCL kwenda kwenye underserved areas. Sehemu ambapo kampuni binafsi hazipo ni lazima Serikali iingine huko through TTCL. Kuna sehemu nyingi Tanzania ambazo hazina mawasiliano ya simu, ni challenge lakini kwa TTCL ichukue kama ni opportunity ya kwenda kuwekeza huko kwa sababu ya kibiashara lakini vilevile kwa sababu hii ni social service, wananchi wanapenda kuona Serikali inafanya kazi. TTCL nadhani ina composition kubwa ya fixed landline na hii ni advantage, tunaomba sana tutafute new subscribers wa landlines kwa sababu TTCL is almost monopoly kwenye suala hili la landline. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vile vile kwa sababu ya growing demand, tunataka tubadilishe huu mwelekeo wa TTCL. Katika business plan yetu ambayo tutaitengeneza ama imeshatengenezwa tunaomba tufikirie suala la sisi viongozi kui-support TTCL. Kwa mfano, kama tunataka TTCL i-grow kama ni kampuni ya nchi ni lazima na sisi tuwe tuna-stake maana yake inawezeka katika business plan tukaangalia tu unakuta watu wana simu mbili, tatu, nne pengine hakuna hata moja ya TTCL. Tungefikiria at least simu moja katika simu tano ambazo unazo mojawapo iwe ya TTCL ili kuweza kuliweka shirika letu katika hali nzuri kimapato na liweze kuwa competent katika mazingira haya ya kiteknolojia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii na naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nilichokuwa nimependekeza, kwa sababu sasa hivi tunaona haya mashirika ya Muungano hata yule aliyekuwepo Zanzibar mara nyingi anakuwa hatoki Zanzibar most of the time. I have a very good example wa TCRA yupo na anafanya kazi lakini kwa sababu ya ku-create ownership katika competition kama ya Zanzibar tunaomba awe Mzanzibari ili aweze kufanya kazi katika mazingira yale pale rather than mtu mwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimemshauri Mheshimiwa Waziri hata wakati wa ku-create ajira, ziwe zinafanyika Zanzibar kwa sababu mara nyingi wanapokuja upande mwingine wale ambao hawana uwezo wa kusafiri lakini wana-qualifications hawawezi kupata nafasi hii. Vyovyote atakavyofanya Mheshimiwa Waziri lakini hilo na lenyewe alizingatie siyo lazima iwe 100% lakini at least kuwe kuna component ya Wazanzibari katika suala zima la corporate structure kwa upande wa Zanzibar.
Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018
MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kupata fursa hii ya kuchangia Muswada huu ulioko mbele yetu na nachukua fursa hii kuipongeza sana Serikali kwa kuleta Muswada huu hapa Bungeni na mimi nikiwa mmoja wa Wajumbe wa Kamati hii. Huu ni Muswada ambao comprehensively tumeu-discuss na kutoa maoni yetu na tuko proud kwamba maoni yetu mengi yemechukuliwa na Serikali na yamepelekea kutengenezwa ama kuchapishwa upya kwa Muswada huu wa Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo mawili makubwa, kwanza kuhusiana na wadau ambao wametakiwa kutoa maoni yao katika Muswada huu wa sheria. Nadhani muda ufike sasa tuone umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau wengine mbali ya Serikali ambao wanatoka katika upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mfano katika Muswada huu wa sheria umejadiliwa kwa kina vilevile na wadau ambao sio Serikali kwa mfano TAMWA, Tanganyika Law Society na wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa upande mwingine kwa Zanzibar na hao wadau vilevile wana exist tuna Zanzibar Law Society na wengine ambao pengine wangeweza na wao kutoa maoni yao ili kuona Muswada huu unaboreshwa zaidi. Kwa hiyo, hili ni jambo ambalo lazima sasa tufike tuone kuna umuhimu wake wa kushirikishwa wadau wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, Muswada huu kwa sababu ni Muswada ama sheria hii sasa ni sheria ambayo inakwenda vile vile kutengenezwa muunganiko wa kazi mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakuna namna nyingine isipokuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au kazi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vilevile mara nyingi ziwe wana-coordinate na Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii iende sambamba na uboreshwaji wa miundombinu iliyopo hususani usafiri, kwa upande wa Zanzibar kuja Dodoma ukitaka kumtuma Afisa kwa mfano aje Dodoma labda ku-attend kikao cha masaa mawili au matatu ni lazima apate per diem ya siku tano, kwa sababu anapoondoka Zanzibar anaondoka leo, yaani tukitaka kufanya kikao leo ina maana Mjumbe kutoka Zanzibar aondoke Zanzibar kama juzi ili alale Dar es Salaam halafu achukue basi aje Dodoma, kesho yake ndio ashiriki kikao halafu alale pengine Dodoma na baadaye aende Dar es Salaam, akiwahi boti sawa, hakuwahi inabidi alale Dar es Salaam kabla ya kwenda Zanzibar. Kwa hiyo, kwa upande mwingine inaweza ika- increase cost ya operation kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa utangazwaji huu wa Jiji la Dodoma uende sambamba na uratibu wa shughuli nyingine kama za usafiri kuona kwamba tunapata ile effectiveness hasa ya utekelezaji wa mipango mizuri sana ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tunaomba Shirika letu sio tunaomba nadhani hili lazima liwe linafuatana na hii sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika letu la ndege la Air Tanzania liwe na connection kutoka Zanzibar mpaka Dodoma inawezekana kabisa ikawa kwa wiki mara tatu, lazima iwe hivyo ili tuweze sasa kupata yaani ile ladha ya Muungano ndio ionekane kwa sababu tutakuwa sasa zile kazi zinakuwa zinakwenda kila siku, lakini vilevile kutakuwa kuna facilitation za kuhakikisha kwamba ushiriki wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kazi mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinafanyika effectively bila ya kuongeza gharama kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hili ningeomba sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile inawezekana huu usafiri ni usafiri wa ndege, tunaweza vilevile kuhuisha hata usafiri wa boti ikawa badala ya boti kuondoka saa tisa nusu kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar tukaongeza muda wa kuondoka kwa ajili ya ku-catch up wale wasafiri ambao wanatoka Dodoma wanakwenda Zanzibar. Kwa sasa hivi usafiri huo umekuwa ni shida sana, inabidi lazima kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ku- incur extra cost kwa ajili ya kuweza ku-fit in katika process za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa hivi zipo Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yangu yalikuwa hayo machache na nataraji sana Serikali itayachukua na itayazingatia ili kuona kwamba tunapata sana sasa ile ladha ya utekelezaji wa Muungano wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii kama kutaangaliwa vizuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza Dodoma kuwa Jiji basically siku ya tarehe 26 Aprili kwa ku- indicate ni siku ambayo tunasherehekea Muungano wetu, kwa hivyo tuone umuhimu utangazwaji wa Jiji hili, umuhimu wa siku iliyotangazwa Jiji hili lakini umuhimu wa utekelezaji wa kazi za Serikali zote mbili katika kuhuisha na kuudumisha Muungano wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2018
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii ingawa sijategemea kama nitakuwa mtu wa mwanzo. Hata hivyo kwa sababu leo ndiyo tunakamilisha marekebisho ya sheria mbalimbali kama ilivyo taratibu.

Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue fursa hii kuipongeza sana Serikali, kumpongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Waziri kwa uwasilisho wao lakini vilevile kutokana na uchambuzi mzuri ambao umepelekea sasa kurekebishwa sheria hizi mbalimbali ambazo leo zimeletwa. Katika marekebisho haya kuna sheria kama saba ambazo zinataka kurekebishwa lakini marekebisho haya nilitegemea sana yangefuata ahadi ya Serikali ya kuleta ama marekebsiho ya sheria au taarifa kuhusiana na jambo ambalo tulilizungumza tarehe 28, Juni, 2018.

Mheshimiwa Spika, nimepata faraja kwamba leo uko wewe mwenyewe. Nina Hansard hapa ambayo iliendana na majadiliano ya Sheria ya VAT ya Mwaka 2014 na katika Hansard hiyo tuliongea wengi lakini jambo zuri ambalo nimeliona katika Hansard hiyo, naomba kwa ruhusa yako nisome. Tulipokuwa tukichangia na katika uchangiaji huo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu alizungumza haya:-

“Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo naendelea huko lakini limegusa pia mioyo ya Wabunge kutoka Bara kwa maana halisi uliyoisema ya huo uwiano wa utozaji kodi.” Akaendelea; “Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukitazama mfumo mzuri wa kufikia maafikiano ambayo yanaweza kuwa ni maafikiano ya amani na yenye mwelekeo sahihi na hasa linapotokea jambo la namna hii na wakati mwingine ikiwa na mtazamo wa upande wa pili wa Muungano kama vile unanyimwa haki kwa namna moja ama nyingine ni suala ambalo kwa heshima sana sana Kikao chako cha leo Serikali tunaomba utupe nafasi haraka sana tukakutane na wenzetu wa upande wa pili.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na akaendelea; “…kwa sababu kwa upande mwingine…” Alinyamazishwa, lakini baadaye akaendelea; “Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine inabidi twende tukashughulikie hata kama masuala ya kodi si masuala ambayo yanahitaji kuingizwa na tafsiri ya Kimuungano lakini zipo sheria ambazo zitatakiwa zikafanywie kazi ili kuliweka hili jambo kuwa na harmony”

Mheshimiwa Spika, lakini aliendelea na akazungumza kwamba; “Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Serikali tutoe hapa, na tunatoa commitment tutakapokutana kwenye Mkutano unaokuja jambo hili liwe tumelimaliza kabisa na liwe limepata sura nzuri na tuwe tumeondoa hilo wingu ambalo linaonekana kabisa kwa upande wa pili wa wenzetu unanyanyasika ama kuonewa.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimesoma hii Hansard kwa sababu niliitegemea sana. Siku ya Ijumaa tumefanya marekebisho ya sheria mbalimbali; leo Jumatatu tunamalizia hiki kiporo cha marekebisho mbalimbali, humu ndani hakuna marekebisho ya sheria ama taarifa ambayo ingesabaisha sasa kuona kwamba ile commitment ya Serikali inatekelezwa katika kipindi hiki kama ambavyo iliahidiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili halimo katika haya marekebisho, lakini sisi Wabunge tunapaswa kabisa kuona jambo hili linavyokuwa linaendelea. Hapa ninapozungumza kila mwezi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inabidi i-allocate 700 million shillings kwa ajili ya malipo ya VAT. Hata hivyo, hilo tu siyo jambo lenyewe, tulitoa commitment sheria italetwa lakini hata hiyo sheria ya marekebisho ya sheria nimeangalia kwa undani kabisa hata hiyo Sheria ya VAT ya Mwaka 2014, the way ilivyoandikwa haigusi kabisa kwamba Zanzibar iwe inatozwa VAT kwenye umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa ama kuletwe sheria turekebishe tuondoe huu mkanganyiko au kuletwe taarifa. Leo ndiyo tuko mwezi wa Septemba na tunakamilisha Miscellaneous, we don’t see anything. Serikali iliahidi na tulichukua hiyo ahadi, tuliondoka hapa kwa matumaini kabisa. Mimi nimerudi Zanzibar kila mtu anasema yaani hii relief tutaipata mwezi wa Septemba na niliwaambia kwamba kwa sababu Serikali imetoa commitment, tutapata relief mwezi wa Septemba. We are finishing this thing off today, twende wapi, tuseme wapi? Hakuna hata taarifa ya kusema kwamba haya mambo yanaendelea.

Mheshimiwa Spika, sikuwa na hoja per se naungana na Serikali na Miswada au Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ilizoleta lakini nimekuwa disappointed kuona Sheria ya VAT au angalau maelezo yake hayamo kama vile ambavyo tumeahidiwa. At this point what are we going to do? Tunafanya nini? Jambo dogo ambalo linakwaza na linasababisha maendeleo yazorote kwa upande mwingine wa Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, we are doing a very good job kwa upande wa The Government of the United Republic of Tanzania, lakini kuna vikwazo kama hivi ambavyo they are just unnecessary blocks. Mimi naweza nikasema they are unnecessary blocks ambazo zinasababisha tukwame. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati wa Kamati, kipindi cha Kamati nilipata bahati ya kuhudhuria kwenye Kamati ya Nishati lakini kwa sababu ya agenda hii, wakati tayari kulikuwa kuna ratiba ya hii agenda upande wa Zanzibar aliitwa Meneja wa Shirika la Umeme, alikuja yeye na wenzake wawili, meneja at that level, lakini upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliokuwa wakihudhuria kile kikao; Waziri wa Nishati, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, wa TANESCO na wengine. Tulijadili jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, bahati mbaya kikao kimefanyika at the Ministerial level lakini kulikuwa kuna kikao kingine ambacho bahati mbaya nyingine kulikuwa kunazungumzwa kuhusiana na deni la Zanzibar lakini watendaji ambao wametoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hawakupata nafasi ya kuingia katika maeneo ya Bunge lako kwa sababu za kiutaratibu, sijaelewa, lakini wakawa -blocked, hawakuweza kuingia. Anyway, my point is, tumepata commitment tarehe 28, Juni, mbona mpaka leo hizi sheria zinakamilika hakuna kitu kwenye sheria hizi za marekebisho ya sheria mbalimbali? Hakuna taarifa, hakuna marekebisho kama ndiyo ambayo yalikuwa yakikusudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yangu yalikuwa hayo. I’m sorry to say this lakini kidogo nimepata ukakasi. Nakubaliana na hoja ya Serikali 100 kwa 100 lakini nimekuwa disappointed kuona kwamba ile commitment ambayo ilizungumzwa tarehe 28, Juni, leo haipo; Ijumaa haikuwepo na leo Jumatatu tunakamilisha Miscellaneous Amendments hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante sana nashukuru kwa nafasi hii, nachukua fursa hii,
kuipongeza Wizara kwa ajili ya Miswada hii miwili ya Sheria. Lakini vilevile particularly nitajikita katika Muswada huu wa Tanzania Meteorological Authority Act.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo kawaida Muswada kama huu, ni Muswada wa pande mbili za muungano yaani matumizi yake yatakuwa kwa Tanzania Bara na vilevile kwa upande wa Zanzibar. Lakini lazima nionYeshe masikitiko makubwa sana, kwamba Muswada huu ambao vilevile utakwenda, unakwenda ku-apply sehemu nyingine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haujapita katika Mamlaka za Zanzibar, haujapita katika Mamlaka za Zanzibar. Baadhi ya watendaji wameshiriki katika ku-develop Muswada huo lakini baada ya development haujaenda Zanzibar kwa ajili ya kuona kwa pamoja, ownership lazima kuwe na ownership Muswada huu wa Sheria ambao sisi Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tutaupitisha leo, lakini kwenye Mamlaka za Zanzibar haujapita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nioneshe sana masikitiko yangu katika jambo hili ambalo tumekuwa tukilizungumza muda mrefu, tumekuwa tukitoa our views and comments every now and then katika hisia kali kabisa lakini Muswada huu ambao unakuja 2019 bado una tabu ile ile, ndio ambao unapelekewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru kwamba hao watendaji wameshirikishwa baadhi yao lakini kwa ajili ya kwenda kuwa-approved kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Muswada huu haupo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye board, content ya board imeonekana vizuri, na tumeona kwamba Chairman na Vice Chairman watachaguliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri. Na kwamba mmoja akitoka upande mmoja, na mwingine atatoka upande mwingine. Lakini katika list ya wale wajumbe hakuna Mjumbe ambaye ataiwakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hili litakuwa haliwezekani, hata kama kutakuwa kuna aidha, Chairman or Vice Chairman atatoka Zanzibar si lazima awe anawakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hivyo hili ni kosa kubwa ambalo tunalifanya katika Muswada huu wa Sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine ni jambo ambalo lazima tuliangalie kwamba kwa nini, Director General wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ndio awe Secretary of the Board hii si katika Principle ya Cooperate Governance, kikawaida mara nyingi Mwanasheria wa Mamlaka ndiyo anakuwa Secretary of the Board. Na DG mwenyewe anakuwa ex-official kwa sababu yeye ni DG, lazima awe anaingia kule kwa ajili ya kuripoti day to day works za Mamlaka, yeye asiwe Secretary of the Board badala yake Mwanasheria wa Mamlaka ndiye awe Secretary of the Board. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine na mimi lazima ni- show concern kwamba Director General kwa nini awe na Ph.D? Yaani sio, sio jambo, sio lazima iwe ndiyo minimum requirement asiwe, hata anaweza akawa na Masters ya Meteorological sio lazima Ph.D. Kwa hiyo, nadhani hili tunatengeneza kutokana na criteria iliyopo sasa hivi, DG ana PHD kwa hivyo sio lazima tunatengeneza Sheria ambayo ina kama inaweka qualification za mtu aliyepo haiwezekani, anaweza akawa ana Masters tu ya Meteorogical.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jingine kwa sababu hii ni Sheria ina-apply pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuna-propose vilevile kuwe kuna Deputy Director General ambaye atafanya kazi zake Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ile ni nchi kwa hivyo kama huu ni Muswada wa Sheria ambayo utakwenda kuwa-apply na is very sensitive Sheria ili angalau wa Zanzibar awe Deputy Director General. Kwa bahati nzuri nilihudhuria semina ambayo ilikuwa inatolewa na Mamlaka hii, ambayo itakuwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pale, yule Afisa wa Zanzibar, hivi tunamuita nani, hata sijui, sijajua nani anaitwa lakini yeye yupo ni kama Afisa katika Management which is not the case tunataka yule wa Zanzibar angalau awe Deputy Director General katika Mamlaka hii ambayo tunakwenda kuitunga.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ni katika Kifungu hichi first schedule actually Kifungu cha tatu kinaelezea kuhusiana na re-appointment tenure of appointment kutokana na hiyo marginal note wajumbe wale wameelezwa kwamba Mwenyekiti pamoja na Makamu Mwenyekiti watakuwa na miaka minne halafu watakuwa Wajumbe wengine watakuwa na miaka mitano. Lakini kwenye re-appointment anaonekana members tu na Chairman watakuwa eligible for re-appointment hatuoni nafasi ya Deputy Chairman katika re-appointment yenyewe, sasa yeye anaweza kuwa re-appointed au la.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu wajumbe wamekuwa watakuwa re-appointed na Mwenyekiti mwenyewe atakuwa re-appointed. Lakini Deputy Chairman hatuoni kama yeye atakuwa re-appointed inawezekana kwamba likawa limewekwa makusudi pengine labda tutapata ufafanuzi lakini au inawezekana ikawa ni commission.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo Mheshimiwa Dkt. Kamala amelizungumza ni kwamba katika Sheria hii kuna hizo offence and penalties lakini zimejikita zaidi katika dissemination ya data na tunajua kwamba hapa tumetunga Sheria ya takwimu lakini nafasi ya Sheria ya takwimu katika Sheria hii ikoje au nafasi ya NBS ikoje katika Sheria hii, haijaelezwa na haijafafanuliwa vizuri. Kwa hiyo, na tunaomba hiyo ielezwe na ifafanuliwe vizuri mambo yalikuwa ni mambo hayo tu lakini concern yangu kubwa Sheria hii haijawa-approved na Mamlaka za Zanzibar, asante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018
MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante sana nashukuru kwa nafasi hii, nachukua fursa hii,
kuipongeza Wizara kwa ajili ya Miswada hii miwili ya Sheria. Lakini vilevile particularly nitajikita katika Muswada huu wa Tanzania Meteorological Authority Act.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo kawaida Muswada kama huu, ni Muswada wa pande mbili za muungano yaani matumizi yake yatakuwa kwa Tanzania Bara na vilevile kwa upande wa Zanzibar. Lakini lazima nionYeshe masikitiko makubwa sana, kwamba Muswada huu ambao vilevile utakwenda, unakwenda ku-apply sehemu nyingine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haujapita katika Mamlaka za Zanzibar, haujapita katika Mamlaka za Zanzibar.
Baadhi ya watendaji wameshiriki katika ku-develop Muswada huo lakini baada ya development haujaenda Zanzibar kwa ajili ya kuona kwa pamoja, ownership lazima kuwe na ownership Muswada huu wa Sheria ambao sisi Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tutaupitisha leo, lakini kwenye Mamlaka za Zanzibar haujapita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nioneshe sana masikitiko yangu katika jambo hili ambalo tumekuwa tukilizungumza muda mrefu, tumekuwa tukitoa our views and comments every now and then katika hisia kali kabisa lakini Muswada huu ambao unakuja 2019 bado una tabu ile ile, ndio ambao unapelekewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru kwamba hao watendaji wameshirikishwa baadhi yao lakini kwa ajili ya kwenda kuwa-approved kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Muswada huu haupo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye board, content ya board imeonekana vizuri, na tumeona kwamba Chairman na Vice Chairman watachaguliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri. Na kwamba mmoja akitoka upande mmoja, na mwingine atatoka upande mwingine. Lakini katika list ya wale wajumbe hakuna Mjumbe ambaye ataiwakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hili litakuwa haliwezekani, hata kama kutakuwa kuna aidha, Chairman or Vice Chairman atatoka Zanzibar si lazima awe anawakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hivyo hili ni kosa kubwa ambalo tunalifanya katika Muswada huu wa Sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine ni jambo ambalo lazima tuliangalie kwamba kwa nini, Director General wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ndio awe Secretary of the Board hii si katika Principle ya Cooperate Governance, kikawaida mara nyingi Mwanasheria wa Mamlaka ndiyo anakuwa Secretary of the Board. Na DG mwenyewe anakuwa ex-official kwa sababu yeye ni DG, lazima awe anaingia kule kwa ajili ya kuripoti day to day works za Mamlaka, yeye asiwe Secretary of the Board badala yake Mwanasheria wa Mamlaka ndiye awe Secretary of the Board. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine na mimi lazima ni- show concern kwamba Director General kwa nini awe na Ph.D? Yaani sio, sio jambo, sio lazima iwe ndiyo minimum requirement asiwe, hata anaweza akawa na Masters ya Meteorological sio lazima Ph.D. Kwa hiyo, nadhani hili tunatengeneza kutokana na criteria iliyopo sasa hivi, DG ana PHD kwa hivyo sio lazima tunatengeneza Sheria ambayo ina kama inaweka qualification za mtu aliyepo haiwezekani, anaweza akawa ana Masters tu ya Meteorogical.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jingine kwa sababu hii ni Sheria ina-apply pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuna-propose vilevile kuwe kuna Deputy Director General ambaye atafanya kazi zake Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ile ni nchi kwa hivyo kama huu ni Muswada wa Sheria ambayo utakwenda kuwa-apply na is very sensitive Sheria ili angalau wa Zanzibar awe Deputy Director General. Kwa bahati nzuri nilihudhuria semina ambayo ilikuwa inatolewa na Mamlaka hii, ambayo itakuwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pale, yule Afisa wa Zanzibar, hivi tunamuita nani, hata sijui, sijajua nani anaitwa lakini yeye yupo ni kama Afisa katika Management which is not the case tunataka yule wa Zanzibar angalau awe Deputy Director General katika Mamlaka hii ambayo tunakwenda kuitunga.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ni katika Kifungu hichi first schedule actually Kifungu cha tatu kinaelezea kuhusiana na re-appointment tenure of appointment kutokana na hiyo marginal note wajumbe wale wameelezwa kwamba Mwenyekiti pamoja na Makamu Mwenyekiti watakuwa na miaka minne halafu watakuwa Wajumbe wengine watakuwa na miaka mitano. Lakini kwenye re-appointment anaonekana members tu na Chairman watakuwa eligible for re-appointment hatuoni nafasi ya Deputy Chairman katika re-appointment yenyewe, sasa yeye anaweza kuwa re-appointed au la.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu wajumbe wamekuwa watakuwa re-appointed na Mwenyekiti mwenyewe atakuwa re-appointed. Lakini Deputy Chairman hatuoni kama yeye atakuwa re-appointed inawezekana kwamba likawa limewekwa makusudi pengine labda tutapata ufafanuzi lakini au inawezekana ikawa ni commission.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo Mheshimiwa Dkt. Kamala amelizungumza ni kwamba katika Sheria hii kuna hizo offence and penalties lakini zimejikita zaidi katika dissemination ya data na tunajua kwamba hapa tumetunga Sheria ya takwimu lakini nafasi ya Sheria ya takwimu katika Sheria hii ikoje au nafasi ya NBS ikoje katika Sheria hii, haijaelezwa na haijafafanuliwa vizuri. Kwa hiyo, na tunaomba hiyo ielezwe na ifafanuliwe vizuri mambo yalikuwa ni mambo hayo tu lakini concern yangu kubwa Sheria hii haijawa-approved na Mamlaka za Zanzibar, asante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Serikali Mtandao wa Mwaka 2019
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Aidha, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya na uzima wa kuweza kushiriki katika shughuli zetu za leo hapa Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, shukrani zangu za dhati pamoja na pongezi ziende kwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta Muswada wa sheria hii ambayo itasababisha kuanzishwa kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao ambayo jukumu lake kubwa na mambo mengine itakuwa ni usimamizi na utekelezaji wa huduma za e- government na vilevile usimamizi wa data za kielektroniki pamoja na masuala yanayohusiana na hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa na nikiri kwamba tumepata fursa pana kabisa ya kusoma na ku-articulate Muswada huu na tumepata ushirikiano mkubwa kabisa kwa Wakala pamoja na Wizara ambayo inasimamia Wakala wa Serikali Mtandao kwa sasa. Tumepata maelezo ya kina kabisa na ninaamini kwamba kwa niaba ya wenzangu naweza kuthibitisha hili kwamba tume-articulate vizuri Muswada huu. La kufurahisha zaidi ni kwamba Serikali karibu iliyachukua maoni yetu mengi tuliyokuwa tumeyatoa na imeyaingiza katika Muswada huu. Tunaipongeza sana Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa umahiri mkubwa nachukua fursa hii kwa niaba ya wenzangu, Wajumbe wa Kamati kupongeza umahiri wa kazi za Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Bakari Jabiri. Anafanya kazi nzuri sana na hatimaye kuthibitisha kwamba sasa wakala ili tuweze kudhibiti na kusimamia Serikali Mtandao lazima uende kuwa mamlaka. Tunapongeza sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jitihada hizi zinazoendelea, vilevile Bunge letu Tukufu limeonesha mfano na wakati tunataka kupitisha kuundwa kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao, leo hii tumethibitsha kwamba hata Bunge letu linaelekea katika matumizi ya mtandao kwa maana kwamba Order Paper yetu ilikuwa katika simu zetu, baadhi tumekuja kufundishana humu humu ndani lakini ultimately ni kwamba tumepata Order Paper Kwenye Electronic Devices. Nakupongeza sana Mheshimiwa Naibu Spika.

Mheshimiwa Naibu Spika, dhana ya Serikali mtandao pamoja na mambo mengine, vilevile inaendana kabisa na siyo tu kuweka mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya kutoa service kwa wananchi, lakini vilevile ili tuone kwamba dhana hii ya Serikali mtandao iwe beneficial ni kwamba service delivery kwa wananchi iwe enhanced au iwe imeimarika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili tumeanza kwa sababu sasa hivi tunakuja tu kuweka sheria kwa ajili ya mamlaka, lakini Serikali yetu imeingia katika initiatives hizi za kutoa services kwa wananchi kwa kupitia njia ya mitandao kwa muda mrefu sana. Tukianza pengine kwa upande wa Hazina kuna hizi electronic fiscal devices kwa ajili ya kukusanya mapato. Hili pamoja na changamoto zake, lakini tumeendelea kufanikiwa kwenye hili sasa hivi Serikali mapato yake yanaongezeka kutokana na enhanced devices au services ambazo zinatumia electronic.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile uanzishwaji wa e- government gateway ume-enhance kwa kiasi kikubwa sana na malipo mengi yanafanyika katika mtandao. Katika utaratibu huu nalipongeza sana Shirika letu la Nyumba (NHC), sasa hivi linakwenda vizuri na katika hilo yaani kumekuwa hakuna matatizo so far wanajitahidi sana. Vilevile pamoja na Wizara ya Fedha, mabenki yetu yameendelea kutumia hii e-government initiative. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa upande mwingine, e-government siyo tu kutumia IT lakini e- government lazima iendane na dhana ya reliability ya services zenyewe, iendane vilevile na credibility ya vifaa ambavyo vinatumia e-government. Kwa mfano, sasa hivi tumeona kwamba kutakuwa kuna counters kwa sababu siyo kila mtu anapenda kuona maendeleo kama haya. Kuna baadhi ambao hawapendi maendeleo, hawapendi sana kuiona nchi ina-prosper, wanakuwa wanakwamisha hizi juhudi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiona sasa hivi tumeanza kukamata vifaa vya ki-electronic ambavyo ni fake, EFDs ambazi ni fake; dhana ni nzuri lakini kuna watu wataingia humo na kuweka vitu ambavyo haviendani na dhana nzima. Kwa hiyo, tutakuwa tuna kazi kubwa ambayo itakuwa inatukabili mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, security na trust ya e- government ni jambo kubwa na ni jambo la msingi. Kwa hiyo, mamlaka yetu ambayo tunakwenda kuipa kazi hii ihakikishe kwamba kunakuwa kuna security na trust. Security kwa maana ya vifaa pamoja na mifumo, lakini trust ambayo wananchi wataipa Serikali kwa ajili ya kutumia mifumo hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mamlaka yetu ihakikishe kwamba taasisi zote ambazo zinakwenda kuweka mifumo, yaani e-government systems, ziwe zina-focus kwenye maeneo mapana zaidi; accessibility, integrity, accountability pamoja na transparency, lakini vilevile kuwe kuna usiri (confidentiality) kwenye mifumo yenyewe. Mifumo hii ni zaidi ya kutoa service delivery lakini vilevile inakwenda pamoja na security.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ambazo zitatukabili ni lazima ziangaliwe. Kwanza tuna hakika kwamba kwa sababu sasa hivi tumekwenda kuweka sheria na ni lazima kwa taasisi zetu ziingie katika mifumo hii, kutakuwa kuna leadership failures. Siyo kila mtu kwenye taasisi zetu ambazo zitatakiwa zitoe substances kwa kutumia electronic ways atakuwa na knowledge ya kuweza ku-install na ku-develop systems ambazo zitatoa hizi services. Kwa hiyo, bila shaka mtendaji mkuu yeyote ambaye atakuwepo katika mamlaka hii ahakikishe kwamba hizi taasisi ambazo atazisimamia ziwe na viongozi ambao watakuwa na maono ya kutumia hii mifumo ya kielektroniki.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapokwenda katika mifumo hii tuhakikishe kwamba tunaondoa digital divides, maana yake siyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kutumia hizi electronic systems. Kwa maana hiyo despite kwamba tunaondoka hapa na sasa tunakwenda officially katika kutekeleza hii e-government, ni lazima Serikali iangalie mbadala wa watu ambao watakuwa hawamo katika hiyo digital community. Yaani wao sasa huduma wanazitaka lakini watafanya nini wakati wao hawako included katika hii electronic age ama digital divides?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni lazima Serikali iangalie namna gani itaweza ku-address issues hizi. Maeneo ni tofauti lakini kuna mahitaji tofauti. Kuna watu ambao watakuwa na ulemavu wa uoni, hawaoni, hawawezi kutumia vifaa kama hivi, wao wanakuwa taken care vipi kwenye maeneo yao?

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna maeneo ambayo kutakuwa hakuna mitandao, je, watu kama hao au wananchi kama hao ambao wanataka huduma lakini hawana system ya kufikiwa na huduma, wanafanyiwa nini kwenye maeneo kama hayo? Ni lazima mamlaka yetu iangalie namna bora zaidi ya kuweza ku-articulate issues kama hizo ambazo definitely zipo na zinaendelea. Pia kuna umuhimu mkubwa wa kufanya data protection, yaani kuzilinda taarifa za watumiaji. Kwa mfano, tunaweza tukapata wapi risiti na vitu vingine kama hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ni lazima kuwe kuna coordination ya maeneo ambayo huduma hizi zinatolewa na maeneo ambapo wananchi wanafikia. Kuwe kuna at national level, lakini kuwe katika regional level na kuwe katika district level; kote huko lazima kuwe kuna uratibu mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna sehemu moja nilikwenda kupata huduma lakini system ikawa imefeli, yule mtu ananiambia sasa niende makao makuu, yeye mwenyewe hajaweza ku-address jambo kama lile. Kwa hiyo, mamlaka yetu ihakikishe kwamba kunakuwa kuna technical skills na vilevile kuwe kuna coordination katika kutoa huduma hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile Inflexibility ya workplaces zetu, kuna watu wata-resist tu hizi changes, vipi hao tuna wa-articulate na vipi tunaweza tuka-address hii issue?

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa, siyo kwa umuhimu, lakini naomba nili-address; hii sheria yetu ni sheria ambayo itakuwa inatumika kwa taasisi ambazo zitakuwa ziko kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar kuna e-government as well lakini hatujaoneshwa ama pengine labda Waziri atakapokuja atuambie ni namna gani sasa wataweza ku-converge pamoja na mamlaka ambazo zinatoa e-services kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar? Kwa sababu e-government is all about also security.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tujue kwamba mifumo yetu yote inakuwa katika level nzuri zaidi za kiusalama. Hapa patahitaji mwelekeo wa sera. Sasa je, ni sehemu gani ambazo Serikali zetu mbili hizi zitaweza kukutana na kuweza kueleza mikakati ya kisera kwa ajili ya kutoa usalama wa mifumo yetu ambayo itatumika katika Serikali kwa ajili ya kutoa huduma pamoja na mambo mengineyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, otherwise, nakushukuru na ninaunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)