Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Elibariki Emmanuel Kingu (18 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza kabisa na mimi niungane na baadhi ya Wabunge wenzangu kuwapa pongezi Waziri wa Maji, Mzee wangu Mheshimiwa Engineer Kamwelwe pamoja na kaka yangu Mheshimiwa Aweso. Kwa kweli, wanasema mnyonge mnyongeni, watu hawa wanajitahidi kujituma regardless ya changamoto za kifedha ambazo zipo katika Wizara yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nimpongeze Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Mkumbo. Profesa Kitila, kaka yangu huyu kwa kweli, hongera sana brother, tunaona kuna mabadiliko yanaonekana na unatuwakilisha vizuri watu wa Singida pia kwenye Wizara hii, ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na Wabunge wenzangu kuishauri Serikali na hapa naomba tuelewane. Najua Mheshimiwa Waziri wa Fedha yuko hapa, sisi tunapozungumza kama Wabunge tunazungumza kwa niaba ya wananchi walipa kodi wa hii Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge tumesema tunahitaji shilingi 50 ziingizwe kwenye petroli na dizeli kwa ajili ya kuwasaidia wapiga kura wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuishii kuagiza fedha hizi ziingizwe, tunatoa rai fedha hizi zikiingizwa, Wizara ya Fedha tunawataka sisi kama Wabunge, fedha hizi ziende Wizarani zikatatue kero na changamoto ya maji kwa wananchi wetu. Itakuwa ni jambo la aibu kama tutawapa wananchi wa Tanzania burden hii, fedha hizi ziingie zikatumike katika mipango ambayo Bunge hili halikuwa limependekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi najua Mheshimiwa Waziri wa Maji, najua unyenyekevu wako mzee wangu na Waziri wa Fedha, mama yangu Mheshimiwa Kijaji, wewe ulikuwa mwalimu wangu, huyu mzee mkimpa fedha mimi nina imani kwa jinsi ninavyomjua huyu mzee tatizo na changamoto za maji, mnyonge mnyongeni…

MWENYEKITI: Mu-address kama Mheshimiwa Waziri au Mbunge.

MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa hiyo, Wizara ya Fedha tunachowaomba hizi shilingi 50 tunaomba ziende Wizara ya Maji wakafanye kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuna watu wengine wanakuja wanachangia kuhusiana na mradi wa Stigler’s. Mimi nataka niwaambie, Ilani ya TANU kipindi cha nyuma, kwa watu mnaosoma historia, acha sisi watu wa Chama cha Mapinduzi, Mradi wa Stiggler’s umekuwepo kwenye Ilani ya TANU enzi za Mwalimu Nyerere, la kwanza. La pili, ndugu zangu tuache kushikiwa akili na Wazungu. Miradi yote ambayo Taifa linajua italeta tija Wazungu wanakuja wanasema environmental problem, achacheni na haya mambo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunachotaka Bwawa la Kidunda lijengwe, mradi huu wa Stiggler’s Gorge ukatekelezwe. Kinachotakiwa Serikali chukueni maamuzi magumu kafanyeni serious land conservation. Kuna mambo yataumiza watu, lakini fanyeni kwa maslahi ya vizazi vinavyokuja na kwa maslahi ya hili Taifa. Haiwezekani leo tuogope kutekeleza mradi kwa sababu tu kuna watu wanapiga kelele kwa maslahi ya Wazungu, tuwaache Wazungu wawili/watatu wakavae bukta wapige picha tuache kutengeneza mradi wa nchi kwa maslahi ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, megawati 2,400 zitaweza ku-curb problem ya umeme ambayo nchi tumekuwa nayo toka uhuru. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri na Serikali, kama Rais wetu alivyosimamia sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi tunawakilisha watu wengi humu ndani, nendeni mkatekeleze mradi wa Stiggler’s Gorge kwa maslahi ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ukiangalia hata ma-researchers wanavyosema, angalia gharama za uzalishaji umeme kwa kutumia mambo ya thermo technology, angalia mambo ya gesi, angalia mambo ya wave za bahari, angalia mambo ya nuclear, gharama ya uzalishaji umeme kwa njia ya maji ni ndogo, Wazungu wanajua. Hapa tunazungumzia tunajenga treni ya umeme itakwenda kuendeshwa na umeme upi? Kwa hiyo, tuwe wajanja hasa ninyi watu wa Serikali, simamemi imara kuhakikisha kwamba kile mnachoki- dream sisi tunawaunga mkono, tekelezeni kwa maslahi ya wapiga kura wa Jamhuri hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ambalo nataka nilizungumze, Mheshimiwa Waziri nakuomba mzee wangu, kuna Wabunge wamechangia na mimi naunga mkono. Profesa Kitila Mkumbo kaka yangu, unda Tume ukachunguze kuna miradi hapa ya maji imefanyika, mfano mmoja ni kwangu, kuna miradi ya maji imetumia billions of shillings za walipa kodi haifanyi kazi. Nenda pale kwangu kuna Kijiji kinaitwa Nkwairee zaidi ya shilingi milioni 200 zimekwenda, jana nimetoka kufanya mkutano jimboni kwa wapiga kura mradi haufanyi kazi, watu wamepiga pesa, haya mambo hayawezekani. Hatuwezi kuruhusu Taifa letu fedha za walipa kodi zinatumika watu wanakwenda wanafanya miradi ambayo haina tija at the end of the day mradi unakwisha maji hayatoki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga pale kuna mradi ulitekelezwa kutoka Igunga kwenda mpaka kule Isakamaliwa. Nimeondoka nikiwa kama DC pale, DP zote hakuna centre hata moja inatoa maji. Watu wame-relax Wizarani as if nothing has happened, pesa za walipa kodi zimekwenda. Haya mambo kama kweli tunataka kumsaidia Rais na kuwasaidia wapiga kura na kwa maslahi ya chama chetu tuendelee kutawala na kushika dola lazima tutende haki na kuhakikisha kwamba tunawapelekea watu wetu maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne, Mheshimiwa Waziri ulikuja jimboni kwangu, nakushukuru sana mzee wangu ukazindua mradi wa maji pale Sepuka na ulituahidi na najua kwa sababu Profesa Kitila Mkumbo uko hapa, Mheshimiwa Waziri alituahidi kutuchimbia visima vingine tisa katika maeneo yafuatayo; Mayaha, Misake, Iseke, Mpetu, Kaugeri, Ufana, Puma na Mpugizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba kwa heshima na taadhima na unajua sasa Profesa Kitila Mkumbo hapa na wewe ni home boy, hebu basi bwana fanya mambo yako huko kwa maslahi ya wananchi na wapiga kura wa Jimbo la Singida Magharibi. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri nakuomba utakapokuwa unamaliza majumuisho ya Wizara yako uje na kauli ya kuwahakikishia watu wa Jimbo la Singida Magharibi kwamba kero za maji, kwa mfano, kuna maeneo mzee wangu niliyasema kuna watu wanabeba ndoo za maji kutoka Kata ya Kijiji cha Mlandala…

T A A R I F A . . .

MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, aah, basi bwana kwa heshima kwa sababu huyu Mbunge pia ninamheshimu basi, lakini kwani hujui kwamba Profesa Kitila Mkumbo ni mwenyeji wa Singida? Nimeipokea taarifa yake kaka yangu huyu, naomba niendelee kumalizia mchango wangu. Natambua kama huyu bwana ni Katibu Mkuu wa nchi nzima lakini wewe kubali tu bwana huyu ni wa kwetu pia Singida kule bwana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumalizia kwa kusema Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Dokta John Joseph Pombe Magufuli, mimi nataka nikupongeze sana Mheshimiwa Waziri, toka nimekua kwenye kijiji nilichozaliwa mpaka nimefikisha umri wa kuwa Mbunge sijawahi kuona miradi mikubwa ya maji ikitekelezeka kama kipindi hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa napozungumza Waziri umeleta fedha shilingi milioni 300 tumechimba maji Mtunduru, shilingi milioni 300 tumechimba maji Irisya, shilingi milioni 81 tumechimba maji Mwaru, shilingi milioni 210 tumesambaza maji Sepuka, shilingi milioni 81 tumesambaza maji Nkwairee japokuwa mradi huu nimesema una matatizo, lakini kwa juhudi kabisa Mheshimiwa Waziri nataka nikupongeze wewe na Naibu wako, ahsanteni sana. Njooni tena tuendelee kutatua changamoto za maji kwenye jimbo langu, Mungu awabariki, endeleeni kuisimamia na kuitekeleza Ilani ya chama changu ili CCM tuendelee kushika dola na tuendelee kuwatumikia wananchi wa hii Jamhuri na walipa kodi wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naunga mkono hoja asilimia mia kwa mia.
Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa heshima na taadhima napenda kumshukuru Mungu wa mbinguni, aliyeziumba mbingu na ardhi kwa kunipa fursa hii mchana wa leo kuweza kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa miezi michache iliyopita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nitakwenda moja kwa moja kujikita katika hotuba ya Mheshimiwa Rais katika sekta ya kilimo. Wilaya ya Ikungi ni miongoni mwa Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Singida. Nikiri kwamba Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa michache inayochangia katika Pato la Taifa hasa katika sekta mafuta ya kupikia. Kilimo cha alizeti ni zao kubwa la kiuchumi na kibiashara kwa wakazi wa Mkoa wa Singida, Wilaya yangu ikiwa ni miongoni mwao. Nikiri kwamba so far Serikali yetu bado haijafanya juhudi za makusudi na za kutosha kuhakikisha kwamba inawatafutia wakulima wetu masoko ya kuuza mafuta na kuhakikisha mazao mbalimbali yanayotoka katika Mkoa wa Singida yanapata masoko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mfano katika Wilaya ninayotoka na Jimbo la Singida Magharibi. Wilaya na Jimbo ninalotoka tunakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa masoko ya mafuta yanayozalishwa katika viwanda vidogo vidogo ambavyo kimsingi vinawasaidia wananchi wetu kupata kipato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nilizungumza hili pia na Waziri wa Kilimo tulipopata muda wa kuteta kidogo, tuna changamoto kubwa ya uharibifu wa ndege kwa lugha ya nyumbani wanawaita selengo. Mazao ya wananchi yamekuwa yakiliwa kwa kiwango kikubwa sana lakini kwa kipindi chote cha karibia miaka kumi Serikali haijaja na majibu ya kuweza kuwasaidia wananchi mazao yao yaache kuliwa na hawa ndege. Nilizungumza na kaka yangu Mwigulu Nchemba, ni rai yangu tena kwa Serikali yangu hii ya Awamu ya Tano, watu hawa wanatumia nguvu zao kuzalisha lakini kilio chao kimekuwa hakisikiki sawasawa Serikalini na hawapati majibu juu ya kutatua tatizo lao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mungu wamemchagua Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ni Waziri msikivu, Waziri mwenye moyo wa kuwasikiliza Wabunge, muda wote ukimpigia simu anakusikiliza.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwigulu Nchemba nakuomba kaka yangu spirit uliyonayo endelea nayo, Wabunge wengi wanakupenda kwa sababu huna kiburi, unajishusha chini ya miguu ya watu.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Nakuomba na natoa rai, panga ziara twende Jimboni kwangu ukaone uharibifu mkubwa unaofanywa na ndege wanaitwa selengo kwa mazao ya wanyonge hawa. Nakuahidi ukienda kutatua kero hii Mungu wa mbinguni atakukumbuka na thawabu zake zitakuwa juu yako. (Makofi)
Mhesheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze pia katika sekta ya elimu, nitumie fursa hii kwa dhati ya moyo wangu kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Simbachawene kwa agizo alilolitoa kwa Halmashauri zetu zote kuhakikisha kwamba watoto wa Kitanzania, is a shame kwa nchi, watoto wa Kitanzania kukaa chini ya mbao fifty years of independence. Tunaweza tusielewane hapa tukaona kwamba tunaishambulia Serikali lakini ni aibu kwa nchi watoto wa Kitanzania kukaa chini ya mbao miaka 50 ya uhuru. Haya mambo tusipoyasema sisi Wabunge wa CCM tutawapa nguvu watu wa Upinzani watayasema watabomoa Serikali yetu. (Makofi)
Kwa hiyo, mimi nasema, wito uliotolewa na Waziri Simbachawene na kaka yangu Simbachawene nikutie moyo, toa circular ipeleke kwa Wakurugenzi wako wote nchini, wape deadline na mikakati. Mimi kwa mfano kwenye Jimbo langu nimepeleka proposal Halmashauri, nimewaambia tuko tayari sisi kutoa nguvu kwa kutumia fedha zetu na kutafuta fedha za wafadhili, tuna mapori mengi tunayalinda wakati watoto wa Kitanzania wanakaa chini. Watu waruhusiwe wapate vibali, tukakate mbao, tuchonge madawati, nakuhakikishia suala la watoto wa Kitanzania kukaa chini itakuwa na history katika Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya afya, niiombe Serikali na nimuombe Mheshimiwa Waziri wa Afya, Mheshimiwa Rais alipokuwa akifanya kampeni miongoni mwa ahadi alizozitoa alisema kwamba tutahakikisha tunakwenda kujenga zahanati katika kila kijiji cha Taifa hili. Nimuombe dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu, nina imani naye, ana uwezo wa kufanya kazi, Jimboni kwangu tumeshamuanzishia, tumeanza ujenzi wa zahanati katika vijiji 19. Namuomba Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Serikali pale ambapo Wabunge tunakuwa na initiatives zetu wenyewe na ku-solicit kutafuta fund kwa maarifa yetu, Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi isichelewe kutuunga mkono Wabunge kuhakikisha kwamba tuna-fulfil ndoto na njozi za Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongeze jambo lingine, ndugu yangu amezungumza hapa kuhusiana na Madiwani lakini pia niwatetee Wenyeviti wa Serikali za Vijiji. Kama inawezekana, najua vijiji ni vingi lakini kama Serikali inaweza ikajipanga at least katika kipindi chao cha uongozi cha miaka mitano wakaangaliwa. Watu hawa wanaisaidia Serikali na kufanya mambo makubwa, naomba Serikali pia iweze kuwakumbuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala mwisho ni reli ya kati na reli ya Singida. Ikumbukwe kwamba kipindi cha utawala wa Mheshimiwa Benjamini William Mkapa, Serikali ilitumia mamilioni ya shilingi kufanya uwekezaji wa kujenga reli iliyotoka Dodoma kuja mpaka Singida. Leo ninapozungumza reli hii ya Singida imeachwa haifanyi kazi. Ushauri wangu kwa Serikali ya chama changu, najua tupo watu baadhi tuna interest katika sekta ya transport, tujenge reserve ya kutosha ya mafuta pale Singida, reli ifanye kazi ya kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam mpaka Singida. Magari yanayotoka Mwanza, Bukoba, Kagera, Shinyanga, Tabora wachukulie mafuta pale Singida, hii reli tuliijenga kwa faida gani?
Ndugu zangu kwa nini tunawekeza vitu halafu hatuzingatii suala zima la value for money? Hii reli haina kazi! Najua watu wanaweza wakani-attack maana najua kuna watu wana interest kwenye mambo ya malori na transport, I don’t care, lakini suala la msingi reli ya Singida iliyojengwa inawezaje kutumika hata kusaidia sekta ya barabara ambazo zinaharibika kwa sababu ya malori. Pelekeni mafuta Singida pale tutawapa maeneo ya kuwekeza kama mko tayari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima nirudie tena kwa mara ya mwisho kwa dhati ya moyo wangu na bila chembe ya unafiki na kwa unyenyekevu mkubwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha, naongeza kumuunga mkono kaka yangu Kitwanga, suala la NIDA mlilolifanya jana, nakupongeza Kitwanga simama, we are behind you, tunakuunga mkono.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mimi nataka nikuhakikishie, nimefanya kazi Serikalini, nilikuwa nikifanya kazi Fair Competition Commission mwaka 2010 kabla sijateuliwa na Rais, nimepigwa picha ya kutengenezewa kitambulisho cha Taifa mpaka leo sijapata. Kitwanga kanyaga, tunakuunga mkono na watu wa Mungu tutafunga na kuomba kwa ajili yako. We will pray for you brother.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, kwa heshima na taadhima, naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia, ahsanteni sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia katika mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa mwaka 2017/2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajikita moja kwa moja katika ushauri kwa Serikali. Jambo la kwanza ambalo ninafikiri nitumie nafasi yangu ya uwakilishi kuishauri Serikali ni katika ongezeko la mahitaji ya matumizi katika fedha tunazozipata kutokana na deni la ndani na nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, itakumbukwa kwamba katika kipindi cha mwaka ulioisha 2015/2016 matumizi makubwa ya deni la nje na ndani la Taifa yalielekezwa katika sekta za nishati, barabara, madaraja na viwanja vya ndege. Nataka nimshauri kwa dhati kabisa Waziri wa Fedha, tunakopa fedha kutoka nje na ndani kwa lengo la kwenda kuwekeza kwenye sekta ambazo kimsingi hazina uhusiano wa moja kwa moja katika ku-stimulate ukuaji wa uchumi, kuna tatizo. Ninatoa mfano, tunakopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha za ndani na za nje ya nchi, tunajua sote kwa pamoja asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima. Hivi ndugu zangu katika fikra tu za kawaida, nimeshawahi kuwa Mkuu wa Wilaya pale Igunga, katika vitu ambavyo lazima Waziri wa Kilimo na Waziri wa Fedha mfanye kazi kwa coordination. Ndugu zangu ukiangalia miradi tuliyonayo kama nchi, miradi mikubwa ya schemes of irrigation ni miradi ambayo ilijengwa na muasisi wa hili Taifa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema kwamba nchi tunataka tuwasaidie wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, hivi tunaachaje kwenda kukopa fedha na kwenda kuwekeza kwenye miradi ya kuwasaidia wakulima kufunga irrigation schemes? Nina mfano mmoja na Mheshimiwa Dalaly Kafumu utaniunga mkono.
Nilipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, tuna mto unaitwa Mto wa Mbutu kipindi cha mvua mto huu kuna maji ambayo ukienda kuyaangalia yanayotiririka na kupotea na chini ya Igunga kuna eneo la karibu mpakani mwa Singida na Igunga eneo ambalo ni fertile kwa ajili ya shughuli za kilimo. Tumepiga kelele tukiwa pale kwamba utengenezwe mkakati ifunguliwe irrigation scheme kubwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji wa kilimo cha mpunga Igunga mpaka leo imekuwa hadithi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nataka nitoe ushauri, tunapokopa fedha kutoka katika Taasisi za ndani na nje, pelekeni fedha hizi kwenye miradi ambayo itakwenda ku-stimulate ukuaji wa uchumi na kumgusa mwananchi moja kwa moja kilimo kikiwa cha kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya pili, tunazungumzia habari ya ku-industrialise nchi, how do we industrialise nchi wakati vocational education hakuna mipango yoyote ya kusaidia kwenye vocational education hapa? Nilitarajia Waziri wa Elimu kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha kuwepo na coordination ya kuhakikisha ya kwamba tunapojiandaa nchi kui-industrialise lazima tuwaandae watoto wa Kitanzania kuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi kwenye viwanda tunavyotaka kuvijenga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano, ninawapongeza watu wa NSSF nimeona wameifungua National Milling, ninaona wanaelekea kujenga Kiwanda cha Sukari ambacho wanasema kinakwenda kuajiri watu zaidi ya laki moja, nani tumeshaanza kuwaandaa watoto wa Kitanzania ndani ya miaka tatu kitakwenda kusimama, tumefanya mikakati gani kuwandaa watoto wa Kitanzania kuwa na vocational skills ya kwenda kifanya kazi kwenye viwanda hivi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu niwashauri Mawaziri kwa nia njema Mawaziri wa Serikali yangu, Mawaziri wa Serikali inayotokana na chama changu, niwashauri. Ninawaomba ndugu zangu, mambo mengine hebu tuwe na creative sisi wenyewe tuwe na creativity, kwa mfano, hata suala hili la kumaliza tatizo la madawati tulisubiri mpaka Rais atoe tamko, lakini hivi leo tunaposema nchi tunataka iwe nchi ya viwanda hivi tunajua kwamba tuna walimu wetu mpaka leo hawana nyumba za kuishi? Hivi kwa nini asitokee Waziri mmoja aseme ninaweka mikakati ndani ya kipindi cha miaka mitatu hakuna mwalimu atalala nje, hakuna mwalimu atakwenda kukaa kwenye nyumba ya kupanga linashindikana hilo? Mambo haya tukiweza kuyafanya ndugu zangu tutajenga base ya kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa itakuwa ni elimu itakayoendana na zama hizi tunazozungumza, zama za viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wa pili, kudorora kwa uchumi. Ninaishauri Serikali yangu kwa nia njema, hakuna shaka kwamba kuna viashiria na dalili kwamba uchumi wa nchi yetu to some extent kuna mdororo. Ninatoa ushauri kwa kaka yangu Mheshimiwa Mpango, Mheshimiwa Mpango ninakujua nimefanyakazi na wewe nikiwa Serikalini, ninakujua uzalendo wako haya mambo ya kuteleza hapa na pale tutasaidiana kwa lengo la kulijenga Taifa letu.
Ninakupa ushauri, Mheshimiwa Waziri wa fedha fanyeni kila mnaloweza punguzeni base ya kodi kwa wananchi, kodi zimekuwa nyingi sana. Tume-tax kila maeneo na unapoongeza tax kila eneo definitely lazima utapunguza circulation ya fedha kwenye uchumi. Na ukishapunguza circulation ya fedha kwenye uchumi utakwenda kuathiri masuala mazima ya huduma na uzalishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri ninaotoa kwa Serikali yangu, kuna fedha mlizichukua za mashirika na taasisi mkazipeleka kuziweka kwenye deposit ya Benki Kuu. Watu wa mashirika ya umma, NSSF na mashirika mengine walikuwa wakipata riba kutoka kwenye mabenki kwa hizo deposit. Ninawashauri Waziri wangu rudisheni fedha hizi kwenye mabenki, yaiteni mabenki myape maelekezo yapunguze riba ya mikopo kutoka asilimia 18 mpaka 13 mtakuwa mmeongeza wigo wa Watanzania kukopa na mtakuwa mmesaidia middle class katika business hapo tutakuwa tunajenga uchumi wa nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna theory inasema kwamba kiuchumi, mahali popote unapotaka ku-stimulate uchumi wa nchi kwa lengo la kukuza wafanyabiashara wa kati, ukifanya kitu kinaitwa kupunguza pesa kutoa pesa kwenye mzunguko katika uchumi maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba watu wanapokuwa hawana fedha kwenye uchumi inakwenda kuathiri hata shughuli za uzalishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninatoa ushauri tusi-ignore suala la kusema kwamba pesa hakuna mtaani tukaishia kusema kwamba watu wanapiga dili, hapana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuende extra miles na tutumie wachumi wa Taifa hili tulionao wafanye tafiti, watuambie Tanzania kwa uchumi tulionao ni fedha kiasi gani zinahitajika ziwepo kwenye circulation na watupe majibu ni fedha kiasi gani sasa hivi kwenye circulation hazipo, ziko wapi ili kusudi tuweze kuwa na remedy katika hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nizungumzie suala zima la sera za kifedha (monetary and fiscal policy). Ukiamua kujenga uchumi ambao utaleta ushirikishwaji wa wananchi lazima tuhakikishe ya kwamba uwepo wa fedha nyingi kwenye mzunguko. Inawezekana labda Waziri wa Fedha waliamua kubana fedha kwenye mzunguko kwa lengo la ku-control inflation kwenye nchi kwa maana ya kwamba bei zinakuwa juu na fedha inakisa thamani. Lakini nataka nikwambie kitu kimoja, bado tunaweza kulifanya hili kwa kuziagiza commercial banks zikaweka riba kubwa kwa watu wanaweka deposit. Watu watapeleka fedha kwenye mabenki lakini pia tukaziambia benki zikashusha riba ya mikopo kwa wafanyabisahara wa kati na wakubwa tuta-encourage private sector kuchukua mikopo na ku-invest. Tunaposema tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda tukiacha hali iendelee namna hii kuna hatari kubwa ya Serikali kukwama na kuna hatari kubwa ya nchi kukwama kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia jambo lingine ninalotaka kushauri kwa nia njema kabisa kuna mambo tumekuwa tukiyazungumza hapa kwa muda mrefu. Ninawashauri Mawaziri wangu wanaotokana na chama changu kilichoko madarakani kwa nia njema tunaomba sana Mawaziri wasiwe wanasubiri mpaka matukio ndiyo waweze kuchukua hatua kwa mfano, mwaka jana kipindi tunafungua Bunge la mwezi wa 11, nilikuja na kilio juu ya usumbufu wa ndege wanaokula mazao ya wakulima maskini watu wasio na kipato. Tunazungumza hapa Mheshimiwa Waziri, leo ninapozungumza Singida ndiyo Mkoa tuna-lead katika production ya sunflower lakini leo ninavyozungumza asilimia 70 ya sunflower iliyolimwa kwenye jimbo langu ililiwa na ndege wanaitwa silingwa na mpaka sasa hivi tunavyozungumza nina imani hata Waziri usikute wanasubiri msimu ufike tuanze kupiga kelele tena Bungeni hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba mtimize majukumu yenu kwa lengo la kumsaidia Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Sina mashaka na uzalendo wa Dkt. Magufuli, sina mashaka na uzalendo wa huyu Rais katika kutetea na kupigania maslahi ya Taifa hili lakini inawezekana kabisa kuna baadhi ya wasaidizi kwa makusudi yao wameamua kumkwamisha Rais wetu whether kwa kuogopa kumshauri vizuri. (Makofi/vigelele)
Kwa hiyo, ninatoa ushauri tusisubiri mpaka mambo yaharibike ndiyo tuje kwa ajili ya kuanza kupiga kelele. Wakulima wetu wanahitaji kuiona Serikali yetu iko proactive na kushughulikia matatizo na changamoto zao kabla athari hazijaonekana. (Makofi/vigelele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya elimu, ni wazi kwamba Mheshimiwa Rais Dkt. John pombe Magufuli alipokuja na sera ya elimu bure, niitumie fursa hii kuipongeza sana Wizara ya elimu na kumpongeza Rais japokuwa changamoto ni nyingi lakini ninauona moyo wa kizalendo wa Rais wetu katika kulitetea suala zima la sekta ya elimu. Changamoto tuliyonayo na alizungumza kaka yangu Mheshimiwa Heche, alizungumza leo asubuhi, tumeongeza idadi ya enrolment. Mimi kwenye jimbo langu peke yake asilimia ya wanafunzi walioongezeka kwenye udahili ni asilimia 17.8 kwenye jimbo langu lakini ndugu zangu tunauhaba wa vyumba vya madarasa, hivi ndugu zangu hili nalo tunasubiri mpaka Rais atoke atoe declaration kwamba muanze vyumba vya madarasa? Kwa nini tusiweke mipango mikakati tuseme ndani ya kipindi cha miaka miwili tatizo la changamoto la uhaba wa vyumba vya madarasa litakuwa limetatuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa changamoto kwa Mawaziri, ninatoa changamoto kwa Baraza langu la Mawaziri, nendeni mkakae mjifungie pelekeni proposal Dkt. Magufuli ni Rais msikivu suala la madawati nililizungumza mimi hapa Bunge la kwanza ndiyo nilikuwa Mbunge wa kwanza kulizungumza na alipokuja Singida sisi tulionyesha mfano na chama…(Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa heshima na taadhima nakushuru kwa kunipa nafasi. Waheshimiwa Wabunge na ndugu zangu Watanzania ambao tutapata fursa ya kulisikiliza Bunge letu, nina mambo ya msingi mawili ya kuyazungumza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ieleweke kwamba tunaposema kitu kinachoitwa Serikali lazima tujue ya kwamba wajibu na kazi ya Serikali ni kuhakikisha inasimamia masuala mazima ya ulinzi na usalama ukiachilia mbali masuala ya kiuchumi. Nimeshawahi kubahatika kuwa Kiongozi wa Dola katika mbili ya Wilaya katika Taifa hili. Nataka niwaambie tunaweza tukazungumza mambo hapa kwa sababu ya kishabiki na mihemko ya kisiasa, bila kuangalia masuala mazima ya hatma ya nchi. Ninachotaka kukisema, duniani kote ili watu waweze kukaa kwa amani na utulivu, ni lazima Serikali ijulikane kwamba ipo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala zima la Serikali katika kuwekeza kwa Jeshi la Polisi. Yamezungumzwa maneno mengi, lakini nataka nikwambie sisi wenyewe Wabunge wa CCM haturidhishwi na hali ya Askari wetu wanavyoishi. Tunaiomba Serikali yetu ifanye hatua za makusudi, kwanza kuwapatia posho katika mazingira magumu ya kazi wanayofanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, utakumbuka, kuna wakati mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Iringa, nimeletewa taarifa mabasi yametekwa pale Igunga.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumza na Askari, OCD hana mafuta ya kupeleka Askari. Haya lazima tuyaseme kwa sababu tusipoyasema tutakuwa hatulitendei haki Taifa letu. Natoa wito kwa Serikali yangu, natoa wito kwa Jeshi la Polisi, tengenezeni unit maalum itakayokuwa ina-deal na suala la kuhakikisha supply ya mafuta kwa Ma-OCD nchi nzima. Mafuta haya yasipite kwa Ma-RPC yaende kwa Ma-OCD kule kwa sababu wakati mwingine OCD anaweza akashindwa kumwambia bosi wake, tunao uzoefu huo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Sekta ya Madawa ya Kulevya. Wiki tatu zilizopita kabla Bunge halijaanza, Kamati yetu tumefanikiwa kwenda kuangalia depot inayohifadhi madawa ya kulevya. Tumekwenda pale, mazingira wanayofanya kazi Askari wetu, Mheshimiwa IGP uko hapa, najua utanisikiliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Jeshi la Polisi angalieni namna ya kuwasaidia Askari wanaopambana na watu wanao-deal na drugs muwa-treat kwa special treatment. Tumekwenda kumkuta binti mmoja anafanya kazi kwenye lile ghala ndani hana gloves, hana chochote, amevaa malapa ndani ya ghala la kuhifadhi madawa; ukiangalia ukuta umechakaa mpaka umeweka rangi ya njano. Sasa je, kwa binti wa Kitanzania anayefanya kazi; naliomba Jeshi la Polisi liweze kuwasaidia katika hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, tumekuwa tukizungumza suala zima la kupambana na madawa ya kulevya, lakini leo tunazungumza kwamba Jeshi letu la Polisi hawana hata boti za doria baharini. Linapotokea suala la kufanya surveillance kwenye bahari, hawana boti. Wanawezaje wakafanya kazi watu hawa? Natoa wito kwa Jeshi letu la Polisi na Serikali, naiomba Serikali ifanye kila inaloweza, wapatieni Polisi boti za kisasa, angalau tatu wakafanye doria baharini kupambana na masula mazima ya dawa za kulevya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho. Kuna mengi yamezungumzwa hapa, mambo ambayo kimsingi nimeshangaa sana! Namheshimu sana dada yangu Mheshimiwa Esther Matiko, ni rafiki yangu, nampenda, lakini kusema kwamba hotuba ya upinzani imezuiliwa, nimeshangaa kidogo. Kama mmezuia hotuba ya upinzani, hili naomba mlitolee ufafanuzi, kama kuna hotuba imezuiwa kusomwa hapa. Kwa sababu sijaona kama kuna hotuba imezuiwa kusomwa hapa Bungeni, unless otherwise kama kutakuwa kuna jambo lingine.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nimtie moyo kaka yangu Mheshimiwa Kitwanga, tumekwenda kwenye unit inayo-deal na kuangalia sample za madawa, ndani ya kipindi cha miezi mitatu, Mheshimiwa Kitwanga amesimamia, tumeona sample 256 za madawa ya kulevya ndani ya miezi mitatu. Leo tunavyozungumza mipaka yote hakuna madawa yanaingia kwenye nchi yetu. Mheshimiwa Kitwanga fanya kazi, tunakuunga mkono na sisi tunajua mnachokifanya kwa maslahi ya Taifa hili. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi hii adhimu ya kuchangia katika hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kukupongeza kwa uongozi wako na pia kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kazi kubwa anayofanya kwa kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa juhudi kubwa anazofanya yeye binafsi katika kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafika na hatimaye kuleta matumaini mapya ya kiuchumi kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu. Ukurasa wa 34 wa Hotuba ya Waziri Mkuu imeelezea hali ya kutatua migogoro ya mipaka kati ya vijiji na hifadhi. Lazima kama Taifa tujue idadi ya watu inaongezeka kila siku ilhali eneo la kiuchumi, yaani ardhi haiongezeki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamekuwepo na hali ya wanachi hasa Jimbo langu la Singida Magharibi ambapo wamekuwa wakipoteza mali zao ikiwemo mifugo, fedha, mazao na mambo mengine yanayoathiri maisha yao kwa ujumla. Katika Jimbo langu pekee wafugaji wamepoteza zaidi ya shilingi milioni 140 kwa kulipishwa faini kwa wanyama wao kukutwa katika maeneo yanayosemekana ni ya hifadhi. Hifadhi hii ambayo inafika maeneo ya Muhintiri, Ihanja, Ighombwe, Mwaru, Mtunduru, Minyashe na Makilawa haijawahi kutangazwa kisheria mahali popote kama hifadhi ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wetu wanaongezeka, wakulima na wafugaji wanakosa mahali pa kulima na kuchungia mifugo yao kwa sababu ya mipaka ya hifadhi. Ni wakati muafaka sasa kutokana na ongezeko hili la watu, tunaiomba Wizara ya Maliasili na Utalii sasa kushirikiana na TAMISEMI kuongeza maeneo ya wananchi na kupunguza ukubwa wa hifadhi ili kuondoa migogoro ya muda mrefu isiyokwisha ambayo inagharimu wakati mwingine maisha ya wakulima na wafugaji pamoja na mali zao. Naomba sana wananchi wetu wa kata nilizozitaja watengewe maeneo maalum ya kuchungia mifugo yao badala ya kila eneo lenye malisho kuonekana ni eneo la hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mapendekezo haya, naunga mkono hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya mimi kuweza kuwa na mchango wangu kama Mbunge katika kuishauri Serikali yangu, Serikali ya Chama cha Mapindinzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nianze kwa unyenyekevu mkubwa kabisa kutambua kazi kubwa na commitment kubwa inayofanya na uongozi wetu katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ikiongozwa na jemedari wetu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, its an disputed kabisa kwamba amesema dada yangu Mheshimiwa Munde, legacy ambayo inakwenda kuandikwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ya Awamu ya Tano is an questionable na inakwenda kuonesha vitu ambavyo Taifa litakumbuka vizazi na vizazi.

Mimi nitumie fursa hii kwa dhati ya moyo wangu kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye kwa muda mwingi tumekuwa naye humu Bungeni, tumekuwa tukisema na kupongeza watu wengine lakini tumemsahau kiongozi huyu mkubwa kabisa wa shughuli za Kiserikali Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuhangaika mikoani na kwenye majimbo kupambana na mambo ya kahawa, kupambana na mambo ya korosho, kupambana na mambo ya maji, Mheshimiwa Waziri Mkuu leo mimi kijana wako nataka nitambue kazi yako kubwa unayoifanya katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nitumie fursa hii kumpongeza sana kaka yangu Dkt. Mpango, the good thing kwa Dkt. Mpango ninachokiona mimi miongoni mwa viongozi wenye msimamo hasa katika sekta na Wizara nyeti kama hii, Dkt. Mpango ninakupongeza. Mimi nimebahatika kufanya kazi na Dkt. Mpango nikiwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, kuna kipindi nilifanya coordination ya kuwa-organize vijana wa vyuo vikuu katika sekta ya kilimo, Dkt. Mpango akiwa anafanya kazi Tume ya Mipango alifunga safari kuja kutembelea miradi ya vijana kwa muda wa siku tatu Igunga na kutoa ushauri. Kwa hiyo Dkt. Mpango mimi ninakupongeza wewe ni mzalendo na kubwa zaidi ni kiongozi usiyeyumba katika masuala ya kodi, hiyo ni sifa kubwa sana kwa kiongozi. (Makofi)

Naomba nijikite katika mchango wangu kwa Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi, kwanza, Rais wetu amekuja na vision akitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya ku-industrialize nchi, hili nimelisema toka nilipoingia hapa katika Bunge hili kikao cha kwanza kabisa, tunapozungumzia habari ya kutaka ku-industrialize nchi hatuwezi kuacha kuweka connectivity kati ya mambo ya industrialization na masuala mazima ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niishauri Serikali ya Chama cha Mapinduzi, katika sekta ya kilimo mwanzo tulivyoanza nilianza kuona kwamba tunakwenda vizuri, lakini katikati naona kuna mahali tuna-stuck, tulianza kuzungumzia mazao ya kimkakati, Bunge la kwanza nilizungumzia na kaka yangu Dkt. Mpango uko hapa nilizungumzia habari ya wakulima wa pamba wa lake zone, nilizungumzia habari ya wakulima wa mazao ya alizeti katika mikoa ya kanda ya kati na baadhi ya mikoa ya mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema Tanzania (Taifa letu) tunapoteza fedha nyingi sana katika kuingiza mafuta kutoka nje ya nchi mafuta ya kula nikasema potential tuliyonayo katika kilimo cha alizeti tukiamua kufanya intensive investment Taifa letu litaondokana na habari ya importation ya mafuta tuta-save foreign currency na tutaweza kuinua uchumi wa nchi. Ninachokisema ni kwamba sijaona connection iliyopo kati ya Viwanda na sekta ya kilimo hasa katika kilimo cha alizeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Serikali, ni wakati muafaka sasa kuhakikisha ya kwamba Serikali inatoa incentive package kwa wakulima wa mazao ya alizeti, kaka yangu Dkt. Mpango lichukue hili na mwakani kwenye bajeti

lilete toeni incentive katika mbegu za alizeti, toeni incentive katika masuala mazima ya pembejeo tuweze ku-boost productivity na kuongeza tija ili Viwanda viweze kupata raw material. Mimi hapa ninapozungumza Jimbo langu linapakana na Jimbo la Iramba, kuna kijana mmoja mjasiriamali amefungua Kiwanda cha Alizeti hapa ninapozungumza amepata market Rwanda, anauza Congo, anauza Zambia…

MHE. MARTHA M. MLATA: Anaitwa Yaza.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Anaitwa Yaza, ahsante Mheshimiwa Mama Martha Mlata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo haya tukiweza kufanya Mheshimiwa Waziri tutaweza kulisaidia Taifa hili na tutaweza kutengeneza wajasiriamali wa kati watakaoweza kufanya investment kwa sababu hawa ndio wazawa wenye uchungu na hili Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ushauri wangu ninaoutoa kwa Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi, tunazungumzia suala la viwanda, Rais John Joseph Pombe Magufuli amekuja na ideology ya kutoa elimu bila malipo shule ya msingi, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango uko hapa na mama yangu Mheshimiwa Profesa Ndalichako najua uko hapa ninajua wewe ni mama bingwa ni Waziri uliyeimudu Wizara yako ya Elimu, mimi ninakupongeza sana mama yangu ushauri wangu ninaoutoa, mwakani njooni na mpango wa kuhakikisha vocational education inakwenda kuwa bure kuanzia mwakani, tukifanikiwa kuweka vocational education kuwa bure tutaweza kutengeneza class ya technocrats ambao watakwenda kutumika katika viwanda ambavyo tunampango wa kuhakikisha kwamba Taifa letu linakwenda kuwa Taifa la viwanda. Kama tumeweza kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi Mama Ndalichako ukiwasiliana na Mheshimiwa Dkt. Mpango mkafanya coordination ya kuangalia tuna vyuo vingapi vya ufundi Tanzania, skills zinazohitajika kwa ajili ya kwenda ku-feed watu kwenye viwanda, tukawekeza kwa vijana wetu wa vocational education mimi nataka niwaambie in next ten years viwanda vinavyojengwa hatutategemea technocrats kutoka nje ya nchi tutawatumia wazawa kutoka katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango huu ndio ushauri wa Kibunge mimi nataka muuchukue achaneni na watu wanaopiga blaa blaa! Watu wanaotaka kutukatisha tamaa, kazi ya Wabunge ni kuja kuishauri Serikali na kutoa mawazo mbadala kwa maslahi ya kuhakikisha Taifa letu linasonga mbele, habari ya kuja hapa kuja kuanza kumtukana Dkt. Mpango sijui mpango umefanyaje. Mimi nataka niwaambie jimbo ninalotoka la Singida Magharibi nimezaliwa kijijini mimi baba yangu alikuwa ni mwalimu for almost 30 years chini ya kipindi hichi nimeshuhudia kwa macho yangu najengewa vituo karibu vinne vya afya on the spot mambo haya hayakuwepo kwani hizi fedha zamani hazikuwepo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumza habari ya kuja uchumi wa nchi ni pamoja na ku-improve social service ku-improve social welfare za watu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Dkt. Mpango ushauri wangu mwingine ninaoutoa tuiangalie sasa sekta binafsi kwa kuwaangalia entrepreneurs wa Kitanzania tuwaangalia entrepreneurs wa Kitanzania na kuwalinda. Ndugu zangu nataka niwape mfano mdogo kwa nini tunasema kwamba Kenya is one of the largest ten investers kwenye nchi yetu, Kenya ni miongoni mwa mataifa kumi yaliyowekeza Tanzania sana kwa sababu gani wamekuwa wajanja sana wanachukua private sector yenye teknolojia kutoka nje, wanakuja wanazisajili kwao kazi zote zinatoka East Africa wanatokea Kenya wanakuja Tanzania wanachukua kwa sababu wameangalia fursa kwa jicho la pili. Niwashauri Mheshimiwa Dkt. Mpango na timu yako tusi-dicourage private sector kwa maana ya kuwalinda Wazawa wanapokuwa wamebuni na kuanzisha vitu ninaiomba Serikali yangu ya CCM iangalie hili kwa jicho la ukaribu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti tutakapoweza kutengeneza middle class na entrepreneurs ya kwetu hawa ndio watakaokwenda kuwekeza kwenye Viwanda vya korosho tunavyovitaka hawa wahindi wanaokuja Wafanyabiashara tunawapenda hawawezi kuwa na uchungu kwenda kuwekeza kwenye viwanda vya kubangua korosho tukiwezesha middle class ya kwetu, entrepreneurs wa Kitanzania hawa Mheshimiwa Dkt. Mpango wanatakuwa na uchungu viwanda ambavyo Rais Magufuli anavipigia kelele vitafunguliwa ninawashauri kwa dhati ya moyo wangu kila mahali alipo entrepreneur wa Kitanzania tusimvunje moyo, ninawashukuru sana ninajua hili linaeleweka na ninajua mna- take note na ninajua kaka yangu Dkt. Mpango unaelewa mdogo wako ninachokisema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja kidumu Chama cha Mapinduzi.
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kunipa nafasi ya kuchangia. Kwanza kabisa nikiri kwamba mwaka 1999 na kuelekea mwaka wa 2000, Taifa letu la Tanzania lilipata msiba wa kuondokewa na Hayati Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere. Taifa lilishuka sana na Watanzania waliingiwa na majonzi na wengi wakajiuliza nini itakuwa hatma ya Taifa letu. Hata hivyo, kutokana na uongozi madhubuti na uimara wa chama kilichopo madarakani Chama Cha Mapinduzi, Taifa la Tanzania liliendelea kuwa stable na nchi iliendelea kuwa moja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliendelea kuonekana katika nchi Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, pia mwaka huu pia Taifa la Tanzania lilimpoteza Rais wake ambaye alikuwa kipenzi cha Watanzania, Rais ambaye alikuwa mzalendo, shujaa, jasiri, mwenye kuongoza njia, Rais aliyeaminiwa na umma ambaye na kuleta imani kubwa duniani, kifo chake na maombolezo yake yamedhihirisha namna gani Watanzania na dunia kwa ujumla ilikuwa na imani kubwa na rais huyu, lakini Watanzania wengi waliingiwa na hofu wakaona sasa Tanzania itakwenda wapi. Kuonesha umahiri wa chama kilichopo madarakani kwamba ni chama kinachoweza kuwaandaa viongozi, leo tunapozungumza kila nchi, Raisi aliyepo madarakani Mama Samia Suluhu Hassan, kila mmoja anatoa makofi na pongezi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninachoweza kusema ni kwamba Chama Cha Mapinduzi ni ngalawa imara inayoweza kuwaandaa viongozi wa kuliongoza Taifa wakati wowote wa shida na raha. CCM ni tanuru la kuandaa viongozi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika,, naomba niende kwenye hotuba yangu. Sasa nakwenda kuzungumzia maeneo makubwa mawili hasa katika sekta ya kilimo. Nashukuru namwona kaka yangu Bashe huwa ni Naibu Waziri msikivu sana, mara nyingi Wabunge wanapozungumza huwa ana-take note kwa manufaa ya Taifa. Naomba nitoe takwimu zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, Nchi ya Misri, ambayo kwa asilimia karibu sabini kama sio themanini ni jangwa; nchi ya Israel ni jangwa. Naomba Bunge lako Tukufu lisikilize takwimu zifuatazo: Taifa la Misri katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji licha ya nchi kuwa imezungukwa na mto mkubwa ambao kimsingi chanzo kikubwa cha mto huo kinatoka Tanzania, ukiangalia takwimu zinaonesha Taifa la Egypt moja ya vyanzo vikubwa vinavyofanya nguvu za kiuchumi za Nchi ya Egypt ni kilimo cha umwagiliaji. Kama haitoshi takwimu zinaonesha Taifa la Misri limewekeza zaidi ya hekta milioni 3.4 kwenye Sekta ya irrigation peke yake.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia takwimu suitability ya land ya Misri na Tanzania ni tofauti kama mbingu na ardhi. Availability za resources kama maji, manpower na mengine, ni sawa na mbingu na ardhi, kwa maana ya kwamba Tanzania hiko katika competitive advantage ya ku-invest kwenye kilimo cha umwagiliaji, lakini angalia takwimu kwa nchi yetu. Namwomba kaka yangu Mheshimiwa Bashe na Mheshimwa Waziri wameaminiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Mchango wangu wa kwanza nilipoingia kwenye Bunge hili nilizungumzia habari ya sekta ya Irrigation, that was my first mchango kwenye Bunge la Tanzania. Nilitoa mifano na nikatoa ushauri, namna gani Serikali ya Chama Cha Mapinduzi tunaweza tukalipindua Taifa hili likawa Taifa la ku- export mazao duniani kote na watu wote tukainua uchumi wa Taifa, kwa Tanzania sasa tunapozungumza eneo ambalo tumelitumia peke yake kwa umwagiliaji ni hekta elfu 19 wakati Egypt they have 3.4 million na hawana suitable land kwa ajili ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, natoa takwimu hizi huku nikiwa natambua kabisa, Serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi, kama kweli wataamua kudhamiria kusaidia kilimo cha nchi hii katika sekta ya umwagiliaji, nakwenda kutoa mfano, nimekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga kwa miaka takribani minne. Irrigation scheme kubwa katikja Mkoa wa Tabora iko Wilaya ya Igunga inaitwa Mwanzugi. Production inayofanyika kwa lile shamba dogo, nataka nikuhakikishie, ndio irrigation inayolisha mchele wote wa Rwanda, Uganda pamoja na nchi za Burundi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa takwimu hizo, nilitoa mchango wangu nikashauri, suitable land tunayo ambayo inafaa kwa irrigation, kwa Tanzania tuna potential ya 2.1 million hekta za irrigation katika nchi zetu. Nilitoa mfano tukiamua kuwekeza, Mheshimiwa Bashe kaka yangu na Wizara na wataalam wakaenda pale Igunga peke yake wakaamua kuyatenga yale maji ya Mto Manonga, wakatengeneza mabwawa, irrigation peke yake Mkoa wa Tabora tuna uwezo wa kulisha nchi zaidi ya nne kwa chakula na mazao mengine ya kibiashara tunaweza kuyafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali yangu ya Chama Cha Mapinduzi, hili Bunge ndio mahali peke yake ambapo tunaweza kutoa mawazo ya kuisaidia Serikali, inapotengeneza mipango, Taifa hili likapiga hatua. Kama Rais Hayati Magufuli alivyokuwa anasema, Taifa hili sio maskini, nchi hii tunakosa kuwa na mipango mikakati na mambo ya vipaumbele ambavyo vinaweza vika-turn upside down maendeleo ya nchi hii. Niiombe sana Wizara ya Kilimo, kama kuna eneo Bashe na watu wako na Wizara wanatakiwa kufanya waende wakawekeze katika kilimo cha umwagiliaji, hicho peke yake kitaleta suluhu ya kuongeza export nje ya nchi na kufanya Taifa letu liweze kuendelea.

Mheshimiwa Spika, nimetoa mifano Egypt peke yake ukingalia statistic za dunia, fedha wanazoingiza Egypt kutokana na kuuza matunda, ulitupa fursa mwaka juzi, tulikwenda Egypt na timu ya Taifa, tulikwenda kutembelea miradi. Ile ilikuwa ni fursa ya kimichezo, lakini tulijifunza kitu, tulienda kutembelea Irrigation za zabibu, tukatembelea irrigation mbalimbali, Egypt is complete desert. Hata hivyo, kinachozaliwa nilipoona yale mashamba nikaangalia baraka za nchi yangu Mungu aliyonipa hii Tanzania, I was so much embarrassed. Tuna uwezo Tanzania tunakwama wapi? Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwenye mipango yetu waandike, walete fedha, wasaidie kilimo cha umwagiliaji kwenye Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, ulikuja kunizindulia kampeni kwenye jimbo langu, mahali pekee yake ulipokuja kuzindua kampeni pale Mgungila, pale tuna maji ambayo yanapotea na nakwambia leo tunavyozungumza Mkoa wa Singida, mchele wote karibia asilimia 75 unatoka Mgungila, lakini wale wakulima they are just doing agriculture on their own skills, hakuna mipango ya Serikali, bonde kubwa lina…

Mheshimiwa Spika, haya mambo jamani, napata shida sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Kingu, watu wa kilimo kila wakileta bajeti ni ya kununua laptop, kunuua pikipiki, zinatakiwa zielekee huko.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimwa Spika, kabisa kabisa, yaani hili Taifa nawaambia, tukidhamiria kufanya mambo na hakika kwa hii style ambayo Serikali yetu ilikuwa inakwenda, nakwambia nchi hii in next ten years to come hili Taifa halitasogelewa na nchi yote kwa Afrika kwa sababu kila kitu tunacho. (Makofi)

Mheshimwa Spika, jambo la pili, kwa mfano tumechukulia hata ukiangalia katika kilimo amechangia kaka yangu pale, amezungumza habari ya pesa tunazotumia, sasa hivi potential iliyopo ya ku-import mafuta ya kupika, inakwenda karibia dola billion 275, that is the potential. Sasa tukiamua kufanya PPP aliyokuwa anaisema kaka yangu, tukashirikiana na Serikali, wakafungua block farming ambazo huwa tunazungumza na Mheshimiwa Bashe ya alizeti, nasema, fedha tunazozitumia kuagiza mafuta peke yake kwenye kilimo, block farming zikiwepo za mfano, sisi Singida tumemwambia Mheshimiwa Bashe, tuko tayari kumpa maeneo ya kutosha ya alizeti kufungua block farming ambazo zitakuwa mfano ili Taifa liweze kuzalisha mafuta.

Mheshimiwa Spika, hii nchi tunaweza kufanya mambo makubwa na mazito endapo Serikali itapokea ushauri wa Wabunge na kuacha kuona Wabunge tunaoshauri kama maadui. Maana kuna Mawaziri wengine ukiwashauri, we have to be honest, anakuona adui, yaani unaona kabisa Waziri anakuona huyu mtu adui. Kuna Waziri mmoja nilishauri kwa nia njema, Waziri mwenyewe ni Mheshimiwa Mwambe, nikasema angalieni kuna shida ya masoko ya Watanzania. Mheshimiwa aknijibu in very arrogant way, mimi ni Mbunge mwakilishi wa watu, Mawawiri tunapotoa michango tuheshimiane, we are doing this for interest ya nchi. Jibu alilonipa; wewe bwana kama nyama yako imekosa soko…, mimi siuzi nyama. Nikizungumza hapa kwa niaba ya wafanyabaishara, nisichukuliwe nimetumwa, wale ni Watanzania na sisi ni sauti yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, I am very sorry kama nitakuwa nimem-offend, lakini I was so embarrassed, hilo siyo jibu la Waziri anayetokana na Chama Cha Mapinduzi kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho, naomba nizungumzie upande wa marketing. Upande wa marketing natoa mfano mdogo, Taifa la Ethiopia lilifungiwa kupata market ya kuuza nyama kwa nchi za kiarabu, in within three days, Mawaziri zaidi ya sita walifunga safari kwenda kufungua masoko ya watu wao. Sisi hapa kwetu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima na taadhima, naomba nikishukuru kiti chako kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangu mfupi katika bajeti hii ya Wizara ya Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, namshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Mwijage na pia naishukuru Serikali ya Chama changu; Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika na ndugu zangu, Waheshimiwa Wabunge, nimesoma kitabu hiki cha hotuba ya Kambi ya Upinzani from page one mpaka page ya mwisho. Ukurasa wa tatu, hotuba ya Kambi ya Upinzani wamesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi imechoka kiakili na uwezo wa kufikisha ndoto za Tanzania ya Viwanda, it is impossible.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Kilichojaa kwenye hotuba ya Kambi ya Upinzani ni malalamiko, hakuna alternative ya nini kifanyike kwa mustakabali wa nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma kitabu cha Mheshimiwa Mwijage, kuanzia mwanzo mpaka mwisho amejikita kwenye program, planning, strategy na namna ya ku-industrialize nchi. Kwa hiyo, kama ni watu waliochoka akili, it is the Opposition Camp ambao kimsingi this is nothing! Absolutely nothing! Malalamiko mwanzo mpaka mwisho.

T A A R I F A . . .

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei, kwa sababu nilichokisema from page one to the last page, hotuba imejaa malalamiko, hakuna alternative za ki-strategy, mikakati na source za kupata resources za ku- industrialize nchi. Naomba niendelee.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, wengi wanapuuza mikakati ya Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi katika ku-industrialize; lakini nataka nikuhakikishie, ndani ya miaka michache ijayo Rais John Joseph Pombe Magufuli anakwenda kuli-surprise Taifa kwa kuhakikisha kwamba Tanzania ya viwanda inakwenda kujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kulithibitisha hilo, Serikali ya Chama cha Mapinduzi ya Awamu ya Tano, tayari imeshaanza mikakati ya ku-modernize infrastructure za nchi. Wenzetu Kenya wamejenga standard gauge rail ambayo inatoka Mombasa kwenda Nairobi. Gharama walizozitumia ni Dola bilioni 3.8. Kwa Tanzania, Rais John Joseph Pombe Magufuli anajenga standard gauge kwa ukubwa huo huo kwa gharama ya takriban bilioni mbili US Dollars.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni kuonesha kwamba Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika ku-industrialize nchi amezingatia three E’s za economy; Efficiency, Effectiveness and Economy. Huyo ndiye Magufuli wa CCM na watu wanaotega masikio wakifikiri tutafeli, imekula kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikuhakikishie, mimi binafsi nimesafiri, nimekwenda kutembelea programu mpya; dada yangu Mheshimiwa Jenista nakupa big up sana, wewe na Ofisi ya Waziri Mkuu. Nimekwenda Ngerengere; jana hapa tulikuwa tunawatetea wanajeshi, nimejionea barabara zinazochongwa kwa kiwanda kipya cha five thousand TCD tons; tani 200,000 kwa mwaka. Nimekwenda Kibigiri, nimejionea programu mpya ya 15 TCD kiwanda kinachojengwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa Dodoma tunapozungumza, ndani ya miezi mitatu National Milling inakwenda kufufuka. Kiwanda cha National Milling kinakwenda kuwaka. Tani 60 za unga zinakwenda kuzalishwa na tani 20 za mafuta. Yote ni kazi ya Chama cha Mapinduzi. Taarifa nilizonazo, viwanda vya Mwanza vinakwenda kuwaka na viwanda vyote; the former National Milling vinakwenda kuwaka. Wanaosubiri mkono wa mtu uanguke kama fisi, hii imekula kwao. Sisi Chama cha Mapinduzi tunakwenda kujenga viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu wa pili; naishauri Serikali yangu ya chama changu, Chama cha Mapinduzi…

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walisimama kutaka kumpa mzungumzaji Taarifa)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo ninaloishauri Serikali yangu ni kwamba wajomba zangu wa Kanda ya Ziwa wameteseka kwa miaka mingi katika kilimo cha pamba. Natoa ushauri Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda wafanye coordination. Tunahitaji tuanzishe large irrigation scheme za kikanda ambazo zitawa- accommodate wakulima wetu wa pamba waweze kuwa na sustainable agriculture ambayo itaweza ku-provide raw material kwenye viwanda tunavyotaka kuvijenga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi wa kwanza nilifanya private tour kwa nchi za Ujerumani, Turkey na Russia; textile industry tukiamua kuwa serious kaka yangu Mheshimiwa Mwijage, we have trust and confidence in you; tukiamua kufanya fully utilization ya resources tulizonazo, mito na ardhi, nataka niwahakikishie, ajira ya vijana wanaomaliza Chuo Kikuu tunakwenda kui-curb over just within three years. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa ushauri kwa Serikali ya chama changu, tuanzishe large irrigation scheme; mito Simiyu tukaitege, mito ya Manonga na Igunga tukaitege, tuvune maji tuwe na large scale agriculture. Hii peke yake ndiyo itakwenda kulikomboa Taifa kutokana na adha tuliyonayo ya ukosefu wa ajira kwa vijana katika masuala mazima yanayohusiana na viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tu-engage protectionism approach kulinda viwanda vya ndani. Tunalindaje viwanda vya ndani? Hili nalizungumza, nina uhakika huenda hata vyombo vya usalama humu ndani; kuna watu wanataka ku-temper na uchumi wa nchi yetu, lazima tuwe very serious na lazima tuwe wakali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, hivi karibuni kuna watafiti fulani kutoka Marekani na nataka niwaambie haya maneno kwa sababu tabia ya Mataifa ya ki-capitalist wanapoona nchi changa zinataka kukomaa kiuchumi, wanaanza kupandikiza mambo ya hovyo ili kutuvuruga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangu mdogo kwa ajili ya bajeti hii ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa dhati ya moyo wangu nianze kwa kuipongeza Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa inayofanywa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hasa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na waswahili wanasema ukiona vinaelea ujue vimeundwa, nidhamu kubwa inayooneshwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni kielelezo cha utekelezaji bora wa sera za Chama cha Mapinduzi katika kipindi chote toka Taifa limepata uhuru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, si siri, Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni miongoni mwa majeshi duniani yenye nidhamu ya hali ya juu. Taifa letu la Tanzania tumepata sifa kitaifa na kimataifa, tumeshiriki operesheni mbalimbali duniani na Jeshi letu; ninataka nijivunie hata makamanda mliopo humu kwenye ukumbi; tunasema ya kwamba Chama cha Mapinduzi kinatakiwa kipongezwe kwa kuwa katika kipindi cha takribani miaka 50 ya Uhuru Jeshi letu limekuwa na nidhamu na dunia yote imetutambua kwa kazi kubwa inayofanywa na wapiganaji wetu.

T A A R I F A . . .

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli wa Chama cha Mapinduzi chini ya nidhamu ya Jeshi la Wananchi Tanzania huwezi ku-exclude kwa sababu utendaji na utekelezaji wa sera zote toka tumepata uhuru nchi hii imekuwa ikitawaliwa na Chama cha Mapinduzi, unawezaje ukakitenga Chama cha Mapinduzi, unawezaje ukaitenga CCM na mafanikio makubwa yanayopatikana kutokana na nidhamu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwaambie Waheshimiwa Wabunge, nidhamu ya Jeshi letu na ndiyo maana hata leo mchana wakati kuna hoja zimetolewa juu ya vijana wa Jeshi la Polisi wamepigapiga risasi pale juu kidogo jana kwa sababu ya tukio lilikuwa limetokea kwa Mheshimiwa Malima. (Makofi)Mheshimiwa Mwenyekiti, let me tell you one thing, tunapozungumzia nidhamu ya vyombo vya dola, unajua kuna mataifa mimi nimejaribu kutembeatembea kidogo duniani, kuna mahali haya mambo tunayoyaona Tanzania sisi tunayapuuza lakini nataka niwaambieni hawa wapiganaji wa Tanzania kama ni Bunge tukiamua leo tukasema kwamba kwa nidhamu wanayoionesha mimi natoa rai kabisa Waheshimiwa Wabunge kwa bajeti zinazokuja naomba Jeshi la Wananchi wa Tanzania tulipe kipaumbele cha kwanza kwa sababu wapiganaji hawa wameonesha nidhamu ya hali ya juu na Taifa letu limepata sifa kitaifa na kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende katika sekta nzima ya suala la JKT.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa
Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hizo interruption uzipuuze ili niweze kuendelea na mchango wangu kwa sababu nina muda mfupi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, JKT kama moja ya sehemu ya kuzalisha ajira, ninaomba nitoe ushauri kwa Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi. JKT, ninatoa ushauri, kwa sababu JKT ina-recruit vijana wengi wanakwenda kupata mafunzo, naiomba Serikali tutenge fedha za kutosha, vijana wanapokwenda JKT wakafanya training ya kijeshi, wakamaliza kwa kipindi cha miezi sita wapelekwe na watafutiwe mashamba makubwa wafanye uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii italisaidia Taifa kupata chakula lakini pia vijana hawa kwa kipindi hicho watakuwa wanapata ajira in phase, wamemaliza walichozalisha kinakuwa mali yao wanaondoka wanaingia wengine, hivi ndivyo wanavyofanya mataifa makubwa kama China na mataifa mengine duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ninatoa ushauri, wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania sasa hivi kuna chama chao kinaitwa MUWAWATA, huu ni umoja wa wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kwa maslahi ya usalama wa nchi si sahihi sana umoja huu kuwa nje ya mfumo wa usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hatari hii inaweza ikajitokeza wakaingiliwa na kuanza kulishwa sumu na kusababisha uasi kwenye nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi, MUWAWATA waendelee kuwa na uratibu chini ya Serikali kupitia Jeshi la Wananchi kwa sababu hawa ni wapiganaji wa akiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina takwimu, miaka michache ya nyuma MUWAWATA ulikopeshwa bajaji na wakalipishwa hela nyingi na vikundi vya wafanyabiashara, this is very dangerous kwa security ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa ushauri, kaka yangu Kamanda Mabeyo najua uko hapa, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwinyi, najua uko hapa kipenzi cha Watanzania, ninaomba upeleke hii proposal mkahakikishe kwamba MUWAWATA inakuwa chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Kumi na Moja wa Bunge
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Kwanza kabisa ni wazi inajulikana kabisa ya kwamba jukumu la kutunga sheria ni jukumu la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba. Kinachofanyika kitendo cha ku-delegate mamlaka ya utunzi wa sheria kwenda kwenye mhimili wa executive ni kutokana na ukweli kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haliwezi kukaa kila siku na kutunga hizi regulations ambazo zinatumika kwenye mamlaka za Serikali na Serikali Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi tukiri ya kwamba mimi nikiwa kama moja ya wajumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo tumeshuhudia kwa kiwango kikubwa ukosefu wa umakini mkubwa sana sana sana kwa upande wa executive katika utunzi wa sheria na hasa regulation ambazo kimsingi ndizo zinagusa maisha ya wananchi ya kila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umakini huu umesababisha sisi kutilia mashaka ni kwa kiwango cha namna gani wananchi wetu wanaweza wakawa vulnerable kuathirika kutokana na matumizi ya regulation ambazo tunaweza tukazipitisha na wakati mwingine kwa kiwango kikubwa zinaletwa hapa zikiwa tayari zimeshakuwa gazetted na ziko kwenye operation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia kanuni nyingi zinatungwa, kanuni inasema hivi lakini ukienda kwenye sheria unakuta ni kitu tofauti hakiendani na kitu hata kimoja kuhusiana na sheria husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mdogo, ukienda kuangalia GN. 80 ambayo inaongelea habari za Urban Planning Building Regulation ya mwaka 2018; ukienda kusoma kanuni ya tatu inatoa tafsiri ya neno vehicle ambayo kimsingi ukiangalia tafsiri hiyo iko kabisa kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani kifungu cha 168.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizingatia hilo, ukiachilia mbali kanuni hiyo kutoa tafsiri ya neno vehicle tofauti, lakini bado regulation yenyewe inaongelea habari za Urban Planning Building Regulation, sasa mambo ya vehicle kwenye mambo ya urban yanaingiliana wapi? Hii inaonesha kwa kweli kuna ukosefu wa umakini mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niiombe Serikali, regulations hizi ndizo zinazotumika ku-govern maisha ya kila siku ya wapiga kura na wananchi wetu. Kama mhimili wa Serikali hautachukulia suala la utungaji wa regulation ni kuwa ni suala serious kama alivyosema dada yangu Mheshimiwa Katimba, kuhakikisha kwamba mnapata manpower na skilled labour ambayo itaweza kusaidia Ofisi ya Mwanasheria na watu wa TAMISEMI katika kuhakikisha kwamba regulation zinazokuja ziweze ku-reflect misingi ya uandishi wa sheria katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hilo halitoshi, bado ukienda katika masuala ya uandishi wa majedwali, katika taratibu za uandishi wa sheria majedwali ni sehemu ya sheria, lakini unaweza ukakuta jambo limezungumzwa ukienda kwenye jedwali halipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo kwa namna moja ama nyingine yasipoangaliwa kwa umakini na kwa trend tuliyonayo ya ku-gazette regulation na kuzifanya zitumike na zinakuja baadae kwa sababu ya wingi italeta madhara makubwa sana kwa wananchi wetu. Nina imani ninayasema haya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ananisikiliza ili kusudi yaweze kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia pamekuwa na makosa makubwa ambayo yamekuwa yakifanyika. Misingi ya uandishi wa sheria imekuwa ikikiukwa sana, nikiwa na maana ya drafting principles katika uandishi wa regulations. Mfano mdogo unaweza ukaenda kwenye GN. 90, ukienda katika GN. No. 90 utakuta kwenye ile sheria nyuma ya sheria kuna maelezo ambayo ndani ukiangalia hayana explanation yoyote. Ili maelezo yoyote katika sheria yaweze kupata nguvu ya kisheria, lazima yawe na kifungu kinachotoa support ambacho kinayapa maelezo hayo nguvu ya kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukienda katika hiyo sheria niliyoisema katika GN. 90 ambayo kimsingi inaongelea The Urban Planning (Urban Farming) Regulations, 2018 ambayo inayotoka na sheria mama The Urban Planning Act Sura ya 355, ameizungumzia Mheshimiwa Katimba, lakini nyuma ya sheria nenda kasome utakuta kuna maelezo, hakuna kifungu chochote kinachoyapa maelezo hayo nguvu ya kisheria, huu ni udhaifu mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nitoe ushauri kwa Serikali. Kwa sababu sisi katika Kamati tume-observe makosa ya kimsingi ambayo kimsingi unaona kabisa ya kwamba kuna ukosefu wa umakini wa hali ya juu katika suala zima la utunzi wa regulation. Niiombe Serikali, kupitia Ofisi ya TAMISEMI, kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, toeni semina kwa maafisa ili watu wanapofanya kazi zinazoletwa kwenye Bunge tuweze kuona kwamba Mhimili wa Serikali uko serious katika kuandaa regulation ambazo zinatumika kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, niiombe Serikali kwa umakini mkubwa kabisa, ni muda muafaka sasa regulation zetu kabla hazijakuwa gazette, kwa sababu nyingi sisi kama Wabunge ambao tunasimama kwa niaba ya wananchi zinaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi, tuiombe Serikali kabla hawaja- gazetted regulation na kanuni zozote wazilete kwenye Bunge tuweze kuziridhia ndipo ziende zikawe gazetted kwa ajili ya maslahi ya wapiga kura wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninaunga mkono hoja nina imani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamesikia na nina imani Ofisi ya TAMISEMI pia wamesikia.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa kwa heshima kabisa nianze kwa kuzishukuru Wizara zetu hizi mbili, TAMISEMI na Wizara hii inayoshughulikia mambo ya Utumishi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kumshukuru sana kaka yangu na mzee wangu Mheshimiwa Mkuchika. Mzee Mkuchika nampongeza kwa sababu miongoni mwa Mawaziri wasikivu yeye ni miongoni mwa Mawaziri wasikivu sana. Nakumbuka lilipotokea tatizo la watumishi kuondolewa kazini mimi binafsi nilikwenda ofisini kwake na alipopata taarifa kupitia kwa aliyekuwa anakaimu kama Katibu Mkuu pale Wizarani ambaye pia alinihudumia niliona public service pale, Mheshimiwa Mkuchika nataka nimpongeze sana na watumishi wake wa Wizarani hakika ni watu ambao wana commitment ya kazi. Naomba hilo nilitambue. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nataka nimpongeze Mheshimiwa Jafo. Mheshimiwa Jafo nampongeza sana kwa sababu kwa muda mfupi katika Wizara ambayo Mheshimiwa Rais amemweka kuweza kulitumikia Taifa letu amekuja Jimboni kwangu na Wilaya yangu ya Ikungi zaidi ya mara mbili, Mungu ambariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu ni kwa Mheshimiwa Jafo naelekeza ushauri wangu kwa taasisi ambayo Rais amemweka kuiongoza. Taifa letu linakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa nyumba za Walimu wa shule za msingi na sekondari. Nataka nimshauri kaka yangu Mheshimiwa Jafo, kama tulivyofanya mikakati ya kulisaidia Taifa kuondokana na uhaba wa madawati nchi nzima, natoa rai ni wakati muafaka kwa Serikali yetu kuamua kwa makusudi kukomesha tatizo la ukosefu wa nyumba za Walimu nchi nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka Jimbo la Singida Magharibi. Kuna maeneo unakwenda Walimu wanatembea zaidi ya kilometa saba mpaka nane hawana mahali pa kukaa. Changamoto hii inapelekea utulivu wa Walimu ku-concentrate katika kuwafundisha watoto wetu kuwa mdogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tuliweza kutatua changamoto za madawati kwa kipindi kifupi namwomba Mheshimiwa Jafo, kaka yangu, nina imani na yeye bado ni kijana mwenzetu namwomba akae na Wizara yake, akae na watendaji, wafanye tathmini ya upungufu wa nyumba za Walimu nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kwa sababu ya uzalendo wetu na kulipenda Taifa letu tutakuja kumuunga mkono atakapoleta mapendekezo ya kujenga nyumba za Walimu nchi nzima hapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niongelee suala zima la afya. Ilani ya Chama cha Mapinduzi ilielekeza kujengwa kwa zahanati katika vijiji vyote na vituo vya afya katika kata zote katika Taifa letu. Mimi katika Jimbo langu nimeshaanza kujenga zahanati vijiji vyote kwa nguvu za wananchi na kwa kushiriki mimi Mbunge binafsi na kwa kutumia fedha za Jimbo. Mpaka sasa hivi tunavyoongea, kuna changamoto ya kumalizia pale ambapo wananchi wamefanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa Mheshimiwa Jafo, Jimbo la Singida Magharibi sasa hebu alitumie jimbo hili kama mfano wa majimbo katika Taifa hili kwa sababu sisi hapa tunapozungumza vijiji vyote vya jimbo tumeanza kujenga zahanati. Mimi juzi nimegawa zaidi ya vitanda 85 na nimevipeleka hata pale ambapo zahanati bado hazijakwisha lengo ni kuipa Serikali changamoto ili waone ya kwamba tuna kila sababu ya kuhakikisha wananchi hawa wanafikiwa na huduma za afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tuna maeneo ambapo wananchi wamemaliza kujenga maboma kwa zaidi ya miaka mitatu. Tuna kijiji cha Mnang’ana pale Sepuka wamejenga boma mpaka leo Serikali bado haijapeleka nguvu kwenda kumalizia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuri na changamoto ambazo Mheshimiwa Jafo anakabiliana nazo katika sekta hii lakini bado kuna kila sababu ya kuhakikisha kwamba zahanati ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi, mimi mpaka sasa hivi tuna maboma zaidi ya 17 ambayo tumeanza kuyajenga kipindi mimi nimeingia hapa kama Mbunge lakini bado msukumo wa halmashauri kwenda kumaliza ni mdogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Mheshimiwa Waziri kaka yangu Mheshimiwa Jafo akitoka hapa leo, akifanya mawasiliano na Mkurugenzi wangu atamwambia ni maboma mangapi tumeyasimamisha. Mheshimiwa Naibu Spika anapiga makofi kwa sababu alikuja jimboni kwangu akajionea. Kwa hiyo namwomba kaka yangu Mheshimiwa Jafo maboma ambayo tumeshayasimamisha watuletee fedha tuweze kuyamaliza ili tuweze kuwaunga mkono na kuwatia moyo wananchi hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu, nakwenda kuzungumza habari ya vyumba vya madarasa. Nimpongeze sana kaka yangu Mheshimiwa Jafo. Amefanya kazi kubwa ya kutuunga mkono pale ambapo wanafunzi wetu walikuwa wanatembea umbali mrefu, sisi tumeanzisha programu ya kuanzisha shule za msingi ikiwezekana hata shule tatu katika kijiji. Kwa mfano, Kata yangu ya Minyuge tumeanzisha shule mpya za msingi katika maeneo ya Mayaha, Minyughe na Misake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto kubwa ni kwamba kuna baadhi ya maeneo watoto wanatembea kilometa 14 kwenda kutafuta shule katika makao makuu ya kijiji. Sasa maeneo ambayo tayari sisi kama Wabunge kwa kushirikiana na wananchi wetu tumeanzisha ujenzi wa shule mpya, tunaomba Serikali isichelewe kwenda kuweka nguvu kuhakikisha kwamba madarasa haya yanapauliwa na kumalizwa. Hilo ni la msingi sana katika kuwasaidia watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kuna Kata moja inaitwa Mwaru, kuna eneo linaitwa Mtakuja, watoto wanatembea umbali wa kilometa 16 kipindi cha mvua mito inakuwepo, watoto hawawezi kwenda shule, lakini sisi tumejenga shule pale Mtakuja tumeshamaliza. Kwa kushirikiana na wananchi tumeshamaliza kuipaua. Namwomba Mheshimiwa Jafo anapofanya location ya Walimu Jimbo la Singida Magharibi aliangalie kwa jicho la karibu sana kwa sababu tumeweka commitment na tumeweza kuwasaidia watu wetu katika eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne, nizungumze kuhusiana na barabara. Ombi langu kwa Mheshimiwa Jafo na Serikali yangu kwa ujumla, Serikali yangu sikivu, Serikali ya Chama cha Mapinduzi, naomba Mfuko wa TARURA ikiwezekana asilimia waliyoiweka waiongeze kwa sababu idadi kubwa ya barabara ambazo zinahudumiwa na halmashauri changamoto ya barabara bado ni kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, nina barabara yangu ambayo haijafanyiwa ukarabati wa kutosha kwa takriban miaka miwili inayotoka Puma - Ihanja - Muintiri - Igeransoni. Halmashauri yangu ya Ikungi sehemu kubwa ya mapato inategemea kutoka katika hizi kata ambazo ziko mpakani wa Tabora ikiwemo Igaransoni. Kwa hiyo, naomba kaka yangu Mheshimiwa Jafo chonde chonde…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima nitumie fursa hii kukushukuru wewe binafsi na Bunge lako tukufu kwa kunipa nafasi ya mimi kutoa mchango katika ofisi ya Rais TAMISEMI na Utumishi na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa mimi binafsi naomba ku-declare kwamba Mheshimiwa Freeman Mbowe namuheshimu sana kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa sababu ni mtu makini nina imani. Hata hivyo, kuna vitu ambavyo kaka yangu Mheshimiwa Mbowe amevizungumza naomba nivitolee ufafanuzi kidogo sana hasa katika suala zima la ulinzi wa Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ulinzi wa Rais, naomba nieleweke, kwa namna ambavyo Rais wetu amechukua maamuzi katika masuala mazima ya uchumi wa nchi, usalama wa Rais wetu lazima utakuwa kwenye mashaka makubwa kwa sababu ya maamuzi Rais wetu aliyoyachukua. Wewe ni shahidi, Bunge lililopita Mheshimiwa Zitto Kabwe na timu yake walileta hoja hapa kuna watu walipiga fedha katika masuala ya ESCROW, Mheshimiwa Rais Magufuli ameingia madarakani, watuhumiwa wote waliokuwa wamefanya ubadhirifu kwenye mambo ya ESCROW, amewakamata, sasa wako magerezani. Kwa kiwango cha fedha zilizokuwa zimeliwa, Rais amekamata watu hawa mnataka kuniambia hawa ma-Taikun hawana watu wanaoweza wakaleta insecurity kwa usalama wa Rais? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema Serikali inatekeleza miradi ambayo Wazungu wanaipiga vita, Stiegler’s George, tunakwenda kuzalisha MW2400 za umeme, Wazungu wanapiga vita, Rais kwa ujasiri anatekeleza hilo. Hizi ni ahadi zilifanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jasiri na jemedari Rais wa Awamu ya Tano anayetokana na Chama cha Mapinduzi ameingia madarakani, hajaangalia Wazungu ameangalia maslahi ya nchi, Stiegler’s George inajengwa, mnafikiri Wazungu wanafurahi? Mnafikiri usalama wa Rais utakuwa sawasawa? Leo tunavyozungumza Rais anajenga Standard Gauge, mnafikiri mataifa ya Ulaya wanapenda? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe taarifa, ulinzi wa Rais tena uongezwe mara dufu kwa sababu usalama wa Rais wetu kwa mambo anayoyafanya kwa maslahi ya Taifa hili hatuwezi kuacha usalama wa Rais ukawa katika stake kwa sababu tunaogopa kupiga makofi, Wazungu walikuwa wanataka wavae vichupi wakapige picha kwenye Stiegler’s George kule Ruvu, haiwezekani. Tunaomba Wabunge wa Chama cha Mapinduzi na sisi ndiyo majority, ndiyo sauti ya nchi humu Bungeni, ulinzi wa Rais wetu ikiwezekana uongezwe hata mara kumi zaidi kwa sababu usalama wake hauko sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nalotaka kulizungumza ni suala la utawala bora. Mwaka mmoja baada ya kuingia hapa Bungeni tuliona Taifa letu lilivyojaribiwa na hapa mimi nazungumza kwa sababu toka nimemaliza kusoma chuo kikuu sijawahi kufanya kazi mahali popote zaidi ya kuitumikia Serikali hii. Tumeingia Bungeni hapa kuna mambo mengine Serikali haiwezi kuya-disclose kwa sababu ya siri za nchi, Mataifa ya Ulaya kwa kushirikiana na watu ndani ya nchi mmeona kilichokuwa kinatokea kule Rufiji, watu wameuawa Kibiti, ili Taifa kudhihirisha kwamba lina utawala bora, dola ya Tanzania imekwenda kudhibiti upumbavu uliokuwa unafanyika pale Kibiti na nchi imetulia. Nataka niseme katika suala la utawala bora hakuna mahali ambapo tunaweza tukapigia kelele utawala bora, tunafanya vurugu, tuache Taifa letu liwe torn apart, never shall we allow this. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudi kwenye michango, moja ya vitu pia ambavyo tunaweza tukavizungumza katika utawala bora ni equal distribution of national cake. Nampongeza sana Mkurugenzi wa TARURA na timu yake na Mheshimiwa Jafo na timu yake na Mzee wetu Mheshimiwa Mkuchika, toka nimeingia madarakani fedha zilizoletwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuwasaidia wapigakura wanyonge, walipa kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeletewa fedha shilingi bilioni 1.3 na tumejenga madaraja; tumeletewa fedha za vituo vya afya Sepuka, Ihanja na sasa hivi tuna kituo cha afya kule Iyumbu, yote haya ni mambo ya utawala bora. Zaidi ya hapo, hata kwa Jimbo jirani la kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu ambaye amepata matatizo, hapa napozungumza Serikali ya CCM bila kujali hayupo na anaumwa, zimepelekwa fedha vijiji 19 watu wake wanachimbiwa maji. Leo mnataka kusema nini hapa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu Mheshimiwa Esther Matiko anazungumza hapa, Serikali ya CCM hapa napozungumza imemjengea Kituo cha Afya cha Mkende kwa shilingi milioni 400. Hapa tunapozungumza Serikali imemtengea shilingi bilioni 8 kumjengea soko la kisasa pale kwake Tarime. Hapa tunapozungumza boma lake la Halmashauri amepelekewa shilingi bilioni 2 na shilingi milioni 500 zimeshakwenda. Msije hapa kuwadanganya Watanzania, msije hapa kuudanganya umma, sisi tunachokisema Serikali ya Chama cha Mapinduzi, chini ya Dkt. John Joseph Magufuli inafanya kazi. Nataka niwaambie, mimi kwenye Jimbo langu Rais alipata asilimia 73 ya kura ya uchaguzi uliopita lakini kwa kazi hizi 2020, Rais anakwenda kuchukua zaidi ya asilimia 95 ya kura. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba nitoe rai kwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi…

KUHUSU UTARATIBU

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba unilindie muda wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa nasema sina maana kazi yangu hapa ni kuja kusifu tu lakini upotoshwaji unaofanywa juu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, nikiwa kama Mbunge nayetokana na chama hiki lazima tuje hapa Bungeni tuweze kufafanua ili dunia na Watanzania waweze kujua ni kweli chama chetu na Serikali yetu inatekeleza au haitekelezi. Ndiyo maana nimetoa mfano, Jimboni kwa kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu aliyepata matatizo, hayupo hapa Bungeni lakini Serikali ya Chama cha Mapinduzi imepeleka miradi ya maji katika vijiji 21 na hapa tunapozungumza miradi ya maji inaendelea kutekelezwa. Nimesema miongoni mwa mambo ambayo yanaweza yakaingia katika components za good governance ni pamoja equal distribution of resources na national cake na ndivyo Serikali ya Chama cha Mapindizi inavyofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka nimalize kwa kusema…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana, muda wako umekwisha.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, kidumu Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa dakika hizo tano, lakini mimi pia ninaona tu kwamba ninamshukuru Mungu kwa sababu ili la Bagamoyo miongoni mwa nondo ambazo pia ambazo nilikuwa nimeziandaa nilikuwa nimejiandaa sana kuja kuchangia katika hii project ya Bagamoyo kwanza nikushukuru wewe binafsi kwa uzalendo mkubwa ambao umeuonyesha kulizungumzia hilo, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, mimi nakumbuka mwaka 2012 alipokuja Rais wa China kabla ya hapo Serikali hii ya Chama cha chetu cha Mapinduzi mwaka 2008 ili hire consultant ambaye alifanya kazi ya kufanya feasibility study wakaja na recommendation za ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, lakini kama alivyosema mama yangu Nagu kipindi hicho mimi nilikuwa chini ya Wizara ya Viwanda nilikuwa nikifanya fair competition, Mama Nagu alikuwa bosi wangu, nataka nikuambie kitu kimoja not only kwamba hii Bandari ya Bagamoyo tunaizungumza hapa kwamba ilikuwa ina muhimu, lakini ilikuwa inakwenda kuwa the biggest port in Africa.

Mheshimiwa Spika, namba mbili Bandari hii ya Bagamoyo ilikuwa inakwenda kufanya circulation ya kuingiza makontena zaidi ya milioni 22 kwa mwaka ukilinganisha na Bandari ya Dar es Salaam, kwa wachumi waliokuwa wamefanya feasibility study pamoja na consultant, bandari hii ilikuwa inakwenda kuwa hub ya kuzifungua nchi ambazo ni land locked na mradi huu, nataka nikwambie ulikuwa unakwenda kuongezwa, wawekezaji hawa walikuwa wanakwenda kujenga Standard Railway Gauge ambayo ilikuwa inakwenda ku-connect kutoka Bagamoyo mpaka kwenye Reli ya TAZARA.

Mheshimiwa Spika, mimi nataka nikwambie ndugu zangu wa Serikali mimi ninawaomba hapa sisi kama Wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwa maslahi ya hili Taifa, hatuwezi tukaja hapa Bungeni tukazungumza kwa lengo la kuikwamisha Serikali, nimesoma kitabu hichi, kinachozungumzwa ni kwamba inaonekana kwamba mkandarasi sijui kuna mambo hayako kwa maslahi ya nchi, hatuwezi tukaishia hapo tu, tuangalie vipengele ambavyo vinakwamisha tuviondoe, mradi huu ukatekelezwe kwa maslahi ya hili Taifa.

Mheshimiwa Spika, leo Rais tayari Serikali yetu imeanza kujenga Standard Gauge Railway kutoka Morogoro - Dar es Salam kuja Dodoma, kama tutafanikisha mradi huu tayari hii Reli ya Standard Gauge itaweza kupata access ya kuwa fade na mizigo ambayo tutaichukuwa kutoka Bandari ya Bagamoyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi kwa unyenyekevu mkubwa ninaungana na Wabunge wengine kuisisitiza Serikali this is the grand project kama Spika ulivyosema, tunaishauri Serikali ikakae iangalie wapi tumekwama mradi huu uweze kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, la pili naomba niende jimboni. Katika jimbo langu la Singida Magharibi na Mheshimiwa Waziri nimeshakuona zaidi ya mara tatu mwaka jana watu wangu wa Kata ya Iyumbu walivamiwa na majambazi saa tisa mchana, maduka yakaporwa kila kitu, watu wakakosa access ya kufanya mawasiliano hata polisi kuja kuwasaidia, hakuna minara ya mawasiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka jana tumeletewa kitabu hapa na hili lazima tuliseme, Serikali Watanzania pia wanaona, msiwe manakuja hapa jamani wakati mwingine mnatupiga longolongo tunapata shida huko, tuliletewa vitabu hapa vinavyoonesha takwimu za minara itakayokwenda kujengwa na makampuni ikiwemo TTCL, mpaka leo tunapozungumza, wale wananchi wangu mimi kutoka makao makuu ya Wilaya mpaka ufike Kiyumbu ni zaidi ya kilometa 190 hawana minara ya mawasiliano, makampuni ya private mmeyazuia, sasa tunataka TTCL ikuwe lakini it must be competitive ili tuweze kuwasaidia watu wetu.

Mheshimiwa Spika, la pili kwenye kitabu nimeangalia barabara inayojengwa kutoka Sepuka - Mlandala kwenda Mgugila, ninaomba nimalizie hili kwa uchache sana, barabara hii nimeanza kuiona toka nikiwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga mwaka 2012/2013; imejengwa madaraja yasiyopungua 40, ni mwaka wa kumi hii barabara Serikali wameshindwa kuipandisha/kuijengea tuta la moramu, leo naangalia kwenye kitabu imeombewa milioni 90.

Mheshimiwa Spika, mimi naiomba Serikali wananchi hawa wa Iyumbu, Mheshimiwa Waziri nimeshakufuata zaidi ya mara mbili.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ikungi asilimia 90 ya revenue inapata revenue kutokana na wakulima wanaotoka kwenye Jimbo langu Singida Magharibi kwa sababu tunazalisha mpunga na mchele kwa kiwango kikubwa, lakini wananchi hawa tumeshindwa kuwakamilishia ujenzi wa hii barabara for ten years madaraja yamejengwa. Mimi nasema safari hii sitaingua mkono bajeti ya Wizara hii kama sita pata majibu ya ujenzi wa barabara ya watu wangu kwa sababu watu hawa wamekuwa wakipata shida, nimekwenda personal kulizungumza nimefanya njuhudi na sijapata majibu yoyote nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii muhimu ya kuchangia kwa maandishi Hotuba ya Wizara ya Nishati. Nianze kwa kuipongeza Wizara na hasa Waziri Kalemani na Naibu wake kwa namna ambayo wamekuwa wasikivu na wachukuaji wa hatua wa haraka katika suala zima la kusambaza umeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi walikuwa nje ya REA Phase II; sasa Mheshimiwa Waziri na timu yako nikuombe REA Phase III isitupite tena. Watu wetu wamekuwa wavumilivu na kusubiri ahadi ya utekelezaji wa REA III ambavyo nina imani Vijiji kama, Kitumtu, Minyushe, Igelansoni, Mtunduru, Mwami, Kintandaa, Masweya, Germany, Msosa, Ishombwe, Iyumbu, Magunguruka, Kipunda, Mlandala na Vijiji vyote.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikimsumbua sana Mheshimiwa Waziri kuhusu REA II, baada ya mkandarasi kushindwa kumaliza vijiji vya REA II; ambapo aliondolewa na kupewa mkandarasi mpya ambapo makubaliano yalikuwa nikumnunulia vifaa lakini mpaka leo REA wameshindwa kununua vifaa na kumkwamisha mkandarasi katika kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, naomba sana katika suala la Tipper Serikali ianzishe one stop center ya kuhifadhi mafuta badala ya utaratibu wa sasa wa kila muagizaji kupakua mafuta kutoka nchini na kuyapeleka kwenye matanki yao. Hili linapelekea kuwepo kwa wizi mkubwa ambao Serikali haiwezi ku-control kiwango cha mafuta yanayopakuliwa kutoka kwenye meli kwenda kwenye matanki ya kuhifadhi.

Mheshimiwa Spika, faida ya mafuta yote kuhifadhiwa Tipper ni kwanza tutaweza ku-control na kuwa na uhakika wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini na kuuza nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo ninaunga mkono hoja.
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi na kimsingi naomba ninukuu maneno yafuatayo yaliyosemwa na Mheshimiwa Rais wakati analihutubia Bunge lako Tukufu. Alisema: “Nakwenda kuchangia kwenye maeneo mawili kwa kifupi sana. Nitumie fursa hii kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza kwenye viwanda vya kutengeneza bidhaa za mifugo, nyama, ngozi, maziwa, kwato na kadhalika. Katika hilo tunaahidi kutoa vivutio maalum kwa watakaowekeza katika viwanda hivyo ambavyo vitasaidia kuinua vipato vya wafugaji wetu na pia kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. Hapa nataka niweke bayana kuwa watendaji watakaokwamisha ujenzi wa viwanda tutawashughulikia”. Haya ni maneno ya Mheshimiwa Rais aliyatoa hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, nataka nilipe taarifa Bunge lako Tukufu, global practice na najua hii ni theory kwa international trade mahali popote duniani, Tanzania, Uganda, Kenya, Ethiopia, Somalia na ukisoma katika statistics za dunia Tanzania tumetajwa kuwa nchi namba mbili kwa wingi wa mifugo barani Afrika. Katika hili namuomba sana Waziri wa Viwanda atulie anisikilize lakini pia namuomba Waziri wa Uwekezaji atulie na kunisikiliza.

Mheshimiwa Spika, nataka nilipe Bunge lako Tukufu hotuba ya Rais iliyokuwa imejikita katika kulisaidia Taifa kupiga hatua katika masuala mazima ya viwanda, nimeamua kuchagua eneo dogo na kulifanyia utafiti eneo la mifugo. Angalia hiki kinachofanyika katika nchi yetu ya Tanzania ili kama sisi Bunge tuweze kutoa mchango wa kulisaidia Taifa na kuwasaidia wakulima na wafugaji wetu.

Mheshimiwa Spika, nakupa taarifa wewe na Bunge lako Tukufu gharama za uwekezaji na export ya nyama ambayo imeshasindikwa katika Taifa la Tanzania kwa kiwanda ambacho mtu amewekeza na ameajiri watu, kwa mfano, kiwanda cha Kenya, kilichowekeza na kuwa na uwezo wa kuzalisha kwa mfano nimechukulia mifugo, ng’ombe 1,000 kwa siku, Ethiopia nako ng’ombe 1,000 kwa siku Kenya na Uganda, angalia gharama hizi uone namna gani we are the witch of our own development. Nataka nikuambie wewe na Bunge lako Tukufu mipango ya Serikali na nia ya Rais najua asilimia mia moja ni nia thabiti ya kuhakikisha Taifa linapiga hatua lakini bado hatujafanya harmonization ya sheria, regulation zinakwamisha kupiga hatua kwa sekta nzima ya viwanda katika Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, nakupa mfano, kiwanda kinachochinja ng’ombe 1,000 kwa siku Tanzania kikafanya uzalishaji wa ng’ombe 1,000 kwa kipindi cha mwaka mzima Kenya ili uweze kuzalisha ng’ombe 1,000 kwa mwaka mzima, gharama unazozilipa zile za kawaida tu achana na mambo ya tax, kuna kuja kulipa cooperate tax, PAYE na mambo mengine kwa Kenya inagharimu 1,900,000 kiwanda kinapata kama tozo tozo kutoka Serikalini. Ethiopia kiwanda kinachozalisha nyama ya ng’ombe 1,000 kwa siku, kwa mwezi, kwa mwaka wanalipa 1,008,000.24. Uganda wanalipa 1,900,000. Njoo kwa Tanzania na hii nataka nikuambie na Waziri wetu Mkuu yupo hapa state intervention katika kulinda viwanda vinavyowekezwa na Watanzania au investors wanaotoka nje imekuwa changamoto kubwa kwa Taifa letu. Ndiyo maana tunajenga viwanda vinakaa mwaka mmoja vimekufa, state intervention.

Mheshimiwa Spika, kwa Tanzania kuna bodi na matitiri mengi naomba niyasome uone picha na ninyi Mawaziri mliopo hapa mkasaidie kufikisha vision ya Mheshimiwa Rais katika sekta ya viwanda. Kwa Tanzania kuna kitu kinaitwa livestock and fisheries, ukizalisha nyama kila kilo wanaku- charge shilingi 150 wanasema gharama zao.

Mheshimiwa Spika, cha pili, kuna kitu kinaitwa Bodi ya Nyama, Mawaziri nyie mpo hapa kama nasema uwongo prove me wrong, nimefanya utafiti. Kuna kitu kinaitwa Bodi ya Nyama they take one percent ya FoB kwenye production ambayo imezalishwa na kiwanda. Kuna kitu kinaitwa Chamber of Commerce wanachukua shilingi 55,000 kila certificate per consignment ambayo inakuwa exported. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukifanya calculation mwekezaji atakayekwenda kuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha nyama kwa mwaka mmoja kwa Tanzania nje ya cooperate tax na mambo mengine analipa fedha zisizopungua 860,000,000 wakati Kenya mtu analipa 1,000,000 peke yake. We cannot survival, hatuwezi ku-survival Mawaziri wangu na ndiyo maana viwanda vingi vinafunguliwa tunapiga makofi tunafungua viwanda haviwezi kukabiliana na ushindani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wenzetu wanafanya state intervention na maana ya state intervention ni kwamba wawekezaji wanapoingia na Rais hapa nimeisema vision ya Rais wa Nchi, vision ya Rais wa nchi anasema tutatoa some sort of incentive katika viwanda, lakini wito wangu ninaotoa kwa Serikali yangu sikivu, ndiyo maana mnalalamika hapa, amesema kaka yangu pale, mbuzi wanakwenda kuuzwa Kenya, kiwanda wanawezaje ku-compete na Wakenya, Mkenya mimi juzi nilikuwa Dubai niliamua tu kufanya survey,nimekwenda nyama zote Dubai zinaandikwa imported from Kenya wakati Kenya hawana mbuzi. Afrika nchi zenye mbuzi hata Ethiopia tunawasifu, lakini hawana mbuzi, Ethiopia wanakondoo, mbuzi wanatoka Tanzania na kiasi kidogo Somalia.

Mheshimiwa Spika, ninachokwambia nenda kwenye masoko ya nje,kama utakuta kuna nyama imeandikwa imetengenezwa kutoka Tanzania, hakuna nahii nawaambia Mawaziri wa Mifugo, wasisubiri Rais Magufuli aje atoe matamko wachukue hatua. Yaani if I was the Minister, today ingetoa declaration ya kuhakikisha tozo zote ya ovyo zinazokwamisha viwanda vya nchi hii na kufanya Watanzania wanakosa ajira, ni bora utumbuliwe umefanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa. Wafanye kazi Mawaziri wangu, wasiogope Rais yupo nyumayao. Mheshimiwa Mwambe you are Minister kaka yangu tunakuamini, bado kijana mdogo tunajua uwezo wako, shirikiana na Wizara ya Mifugo saidieni Taifa hili kwa mustakabali wa Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, la pili, Rais jana alizungumza, nilisikiliza hotuba yake na hiyo pia iko katika packageya hotuba aliyotoa hapa Bungeni, suala la uwekezaji tuna changamoto kubwa sana, naomba nikwambie, kazi inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu hakika tunaweza tusiitambue kwa sababu kuna mambo mengine tunaweza tusiyaone Waziri Mkuu na Ofisi yake wanafanya kazi nzito sana katika kusaidia uwekezaji kwenye Taifa hili.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nilipe Bunge lako Tukufu taarifa, Rais jana alipokuwa anatoa takwimu watu wanakwenda kwenye benki wanakopa hela kubwa sana za kuwekeza, wanakimbilia mahakamani. Natoa mfano mdogo sanasana, nenda kachukue takwimu za iliyokuwa Bank M take statisticsangalia list ya watu waliokwenda kuchota bilioni za shilingi za Watanzania mle halafu uwekezaji fedha zimetoroshwa sijui Canada, sijui Kenya na mpaka leo ninavyokwambia its true Ofisi ya Waziri Mkuu imefanya kazi kubwa sana angalau kuna bilioni 200 zimeokolewa kupitia Bank ya Azania.

Mheshimiwa Spika, hili nalisema kwa uchungu kwa sababu hapa Bungeni tunayo Kamati inayoshughulikia Uwekezaji na Mitaji, sina maana waanze kufukua makaburi kujua nani kakopa, lakini ukiangalia kwenye list ya waliokopa, mbaya zaidi hukuti mtu wa ngozi ya namna yangu,I am very sorry to say this, tunaweza tukapigiana kelele na Wabunge hapa vimikopo tunachukua vidogo vidogo kwenye taasisi za fedha, nataka niseme with confidence na with evidence,Taifa hili bado linapigwa sana. Wizi wa rasilimali za nchi bado haujakoma kwenye nchi hii, lazima kama Bunge tudhamirie kwa dhati kusaidia vision ya nchi, Rais atiwe moyo na Bunge sisi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba kutumia wasaa huu kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hotuba ya Waziri Mkuu kwa Bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naomba nitumie nafasi hii kumpongeza sana Waziri wetu Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwa juhudi zake chanya katika mchakato mzima wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka mitano. Waziri wetu Mkuu huyu amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa ufanisi na unyenyekevu mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu utajikita katika sehemu mbili; bandari kwa masaa ya mchakato wa uagizaji mafuta na usambazaji wake na suala zima la biashara ya magari, hasa bonded warehouse.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2012 kilianzishwa chombo kilichokuwa kinaitwa Petroleum Importer Coordinator (PIC) ambapo chombo hiki baadaye kilivunjwa na kuanzishwa PBPA Wizarani ikiwa na majukumu ya kusimamia uagizaji wa mafuta na ku-discharge mafuta kwa wasambazaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo shida katika Taifa letu, shida hii lazima kama Taifa Bunge letu litimize wajibu wake kuishauri Serikali kwa maslahi ya nchi. Serikali yetu ina umiliki wa asilimia 50 katika Kampuni ya Tipper lakini vita inayoikumba kampuni hii utashangaa. Inawezekanaje tunaagiza mafuta nje ya nchi, yakifika Dar es Salaam kila importer anapelekewa mafuta moja kwa moja kwenye deposit yake wakati tunayo Tipper, chombo ambacho kina capacity kuhifadhi mafuta yote ya nchi hii na yaliyopo kwenye transit? Tipper wanapigwa vita eti wanaiba mafuta, sisi tumerogwa na nani? Serikali tuna hisa fifty percent Tipper ina maana Serikali tunaiba mafuta?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaiba mafuta against nani? Tunawaamini zaidi importers wakiwemo Engen, Oryx, Oilcom, Lake Oil kuliko chombo hiki cha umma ambacho tukiweza kuwa na one au single terminal receiving matanki ya Tipper yana uwezo wa kuhifadhi mafuta lita milioni 220, sawa na capacity ya kupakua meli tatu kwa wakati mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tipper ambayo ni sehemu ya Serikali ikipewa jukumu la kusambaza mafuta yote ya Oil Marketing Companies (OMC) wanaweza kusambaza mafuta ndani ya siku tatu baada ya ku-deliver na jambo hili linaweza kufanyika ndani ya siku sita tu kwenye depots. Ni muda muafaka sasa Tanzania kuepuka ujanja na wizi unaofanywa na wafanyabiashara wa mafuta kwa kupiga vita single terminal receiving.

Mheshimiwa Mwenyekiti, single terminal receiving ya mafuta ndiyo mfumo pekee unaotumika duniani kote. Hata mafuta ya transit wanunuzi wa nje ya nchi watachukulia mafuta kutoka Tipper na hivyo kuliingizia Taifa mapato na pia kuisaidia TRA kukusanya mapato yake kutoka eneo moja tofauti na practice ya sasa ya kufuatilia mapato kutoka kwa OMC moja moja kutoka depots zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, damage charges tunazoingia kwa meli kuwa katika foleni, OMC wanalipia wastani wa dola 25,000. Dola 25,000 USD kwa siku, sasa unajiuliza kama hakuna ujanja kwa nini tunafifisha efficiency kwa chombo ambacho Serikali tunaweza ku-monitor uingiaji wa mafuta na usambazaji na kuliingizia Taifa ajira.

Mheshimiwa Waziri Mkuu najua yeye ni mzalendo na mtu wa haki, weka historia katika nchi hii kwa kuhakikisha kuanzia leo mafuta yote yanayoagizwa nchini yanamezwa na Tipper na waagizaji wote wapeleke kwenye deposits zao toka Tipper.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida za kuwa na single receiving terminal ni hizi; moja, hapatakuwa na damage sababu meli zitaweza kumwaga mafuta kwa wakati. Mbili, ili kuepuka wizi au diversion ya mafuta mabomba ya mafuta kati ya SBM na Tipper itenganishwe; na tatu, tutaongeza wigo wa Transit Cargo Consignment.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wetu Mkuu na Serikali wajue kwamba wafanyabiashara wanapoteza wastani wa shilingi milioni 330 kwa gharama za demurrage kwa wastani wa siku @25,000 USD kila meli inapokuja kupakua mafuta, wastani wa call za vessel za mafuta ni 24 kwa mwaka, hivyo wastani huu unapelekea kupoteza pesa karibu 19,776,970,608 kila mwaka zinapotea sawa na wastani wa milioni 824,040,422 kwa kila shipment.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili ni kazi yake kuishauri Serikali, ni wakati muafaka katika majumuisho ya hotuba ya Waziri Mkuu Serikali sasa wakubali kufanya mabadiliko ya haraka kwa maslahi mapana ya nchi yetu kwa kuifanya Tipper iwe mpokeaji na msambazaji wa mafuta yote ya nchi kutoka kwa petroleum traders.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa sasa kwa upakuaji wa mafuta bandarini una kasoro kubwa na unatia walakini wa ukweli wa idadi halisi ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa mfano kwa idadi ya terminal 18 – saa kati ya 36- 54 zinapotea kutokana na kuhamisha umwagaji kutoka terminal moja kwenda nyingine. Taifa letu tuna shida moja tunalalamika sana, tunatengeneza vitu vizuri lakini hatutaki kutekeleza wakati mwingine kwa viongozi wetu kupotoshwa kwa makusudi au kwa kutokujua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tipper ni chombo ambacho Serikali yetu ina umiliki, ukifanya analysis ya kimapato nje ya gawio, Serikali imepata revenue karibu asilimia 68 kutoka Tipper moja kwa moja, Serikali tunapata revenue ya almost 70% kutoka Tipper na oryxy mbili anachukua asilimia 30% tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya ushauri huu, naiomba Serikali yangu sikivu ya CCM kuanza mara moja matumizi ya single terminal receiving. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima kubwa naomba kuleta mchango wangu kwa maandishi katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kwanza pongezi zangu kwa Waziri na Naibu kwa kazi kubwa mnazofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikali yetu ya CCM, lazima tujikite katika kuandaa mitaala ambayo itawapa fursa wanafunzi wanaohitimu waweze kuwa na skills ambazo zitawafanya waweze kujiajiri au kumudu kuendesha maisha yao binafsi katika mazingira ya sasa ya ushindani. Wanafunzi wengi wanaomaliza vyuo na elimu za kawaida za sekondari, wamekuwa wakitegemea sana kupata ajira rasmi kutoka katika taasisi za Serikali na binafsi. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wimbi kubwa la nguvu kazi mtaani ambayo haitumiki kwa maana ya kwamba hawana ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ufike wakati muafaka sasa Serikali yetu iandae mitaala ya namna ya kuwapa elimu ya kujitegemea wahitimu wetu ili wapate technical skill ambazo zitawasaidia kujiajiri au kujitegemea. Hapa tunaweza kupata wahitimu wakaandaliwa katika vikundi mbalimbali tukawapa mikopo ya mitaji hawa ambao tumewaandaa vema ili waweze kuanzisha miradi ya kujiajiri na kujitegemea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tulimaliza shule za msingi na kulikuwa na mafunzo ya elimu ya kujitegemea kama vile uselemara, umeme, ufundi wa magari na kadhalika. Naishauri Serikali yangu kuhakikisha watoto wetu wanaohitimu wanapata skills ambazo zitawasaidia kujiajiri na nchi pia kupata wataalamu ambao tutaweza kuwatumia katika viwanda ambavyo tunavihamasisha vijengwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, naishauri Serikali kupitia mfumo wa kuhakiki vyeti vya wanafunzi wanaoomba mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ambapo kwa sasa utaratibu umetolewa kwa waombaji wanaoomba kupitia online kulazimika kuhakiki vyeti jambo ambalo naona ni kuwapotezea muda na gharama watoto wa Kitanzania. Nashauri Serikali irudishe jukumu la kuhakiki vyeti lifanywe na Bodi ya Mikopo yenyewe na liwe well-coordinated. Wanafunzi wanapoomba mikopo wanaambatanisha na vyeti vyao vya kuzaliwa moja kwa moja, Bodi ichambue na kupeleka majina na nakala za vyeti viweze kuhakikiwa na hivyo kuwasaidia watoto wetu kupunguza gharama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya ya Ikungi, sisi ni wazalishaji wakubwa sana wa alizeti hivyo uhitaji wa ujenzi wa vyuo vya ufundi hauepukiki ili kupata vijana wenye technical skills watakaojiajiri katika usindikaji wa mazao ya kilimo yanayopatikana katika Wilaya yetu. Naomba sasa ujenzi wa VETA utekelezwe katika Kata ya Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mahali ambapo tayari tumeandaa eneo la ujenzi wa chuo hiki ambacho kitakuwa chachu ya maendeleo katika kuwasaidia vijana wa Kitanzania watakaokuwa na uwezo wa kujiajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, natoa rai kwa Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuja na mkakati madhubuti wa namna ya kuandaa mkakati wa ujenzi wa nyumba za walimu nchini. Walimu wetu wanateseka sana katika kupata makazi ya kuishi hivyo kuathiri taaluma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi katika kuchangia mchango wangu na ushauri kwa Serikali katika Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM Serikali iliahidi kutekeleza ujenzi kwa kiwango cha lami katika barabara ya Singida – Sepuka – Ndago – Kizaga yenye urefu wa takriban kilometa 92. Barabara hii imekuwa barabara muhimu sana kwa sababu ya uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara kama vile alizeti, mahindi na kadhalika. Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 Mheshimiwa Rais alipita barabara hii na kuwaahidi wananchi kuwa barabara hii itajengwa kama ambavyo Ilani ya Uchaguzi wa CCM ilielekeza, lakini mpaka hapa tunapoongea utekelezaji wa Ilani katika ujenzi wa barabara hii bado unasuasua na hivyo kuwafanya wananchi kuendelea kupata adha katika kusafirisha mazao na hata mafuta yanayozalishwa katika viwanda ambavyo vimejengwa maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, Serikali yetu imekuwa ikitumia sana fedha nyingi katika matengenezo ya muda mfupi na mrefu ya barabara hii, jambo ambalo kama Serikali itaweka dhamira ya dhati katika kujenga barabara hii kwa Mwaka wa fedha 2018/19 Serikali ilitenga fedha za upembuzi yakinifu wa barabara hii lakini mpaka leo hatua za utekelzahi haueleweki.

Mheshimiwa Spika, katika Sekta hii hii ya barabara, Serikali tangu mwaka 2010 imejenga madaraja katika barabara ya Sepuka – Mkandala – Mgungira tangu madaraja yakamilike leo miaka 9 ujenzi wa tuta la barabara umeshindikana, hivi tumetumiaje pesa za umma kwa mamilioni na kushindwa kukamilisha ujenzi wa tuta tu? Barabara hii ni muhimu sana katika kusafirisha mazao ya chakula na biashara kama vile mchele, alizeti na barabara hii ambayo inaungana na barabara ya Magereza –Mtuduru – Iyumbu imekuwa ya muda mrefu sana mvua zimenyesha watu hawa wanakosa mawasiliano. Ni muda muafaka sasa kwa Serikali kutekeleza ujenzi wa barabara hii muhimu kwa wapiga kura wa Jimbo la Singida Magharibi.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, mawasiliano ya minara ya simu; jiografia ya Jimbo la Singida Magharibi iko very complicated. Toka nimekuja Bungeni tumekuwa tukipewa vitabu vinavyoonesha distribution ya minara ya simu, lakini hakuna utekelezaji wa mnara hata mmoja ambao uliahidiwa na Serikali ambao umejengwa.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2018 wananchi wa Kata ya Iyumbu walivamiwa na majambazi mchana na maduka yote kuporwa pesa, watu wetu hawakuweza kupata msaada sababu ya ubovu wa barabara na ukosefu wa minara ya simu, hakuna mawasiliano ya barabara wala ya simu na kata hizo ndizo zinaendesha halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo asilimia 90 ya mapato yanatoka kule kutokana na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mchele ambao unauzwa Uganda, Rwanda na Burundi na kuliletea Taifa mapato ya ndani.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana vilitolewa vitabu hapa ambavyo TTCL wamepewa market share ili kufungwa minara katika maeneo hayo, lakini hakuna lolote lililofanyika katika kuwasaidia Watanzania hawa.

Mheshimiwa Spika, haya mambo yanatuweka mahali pagumu sana. Naomba minara ya mawasiliano ikafungwe Ikungi, Igholwe na maeneo yote ambayo wananchi wanapata matatizo katika Jimbo la Singida Magharibi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.