Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Raphael Masunga Chegeni (25 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MH. DKT. RAFAEL M. CHENGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kunipa nafasi hii, na mimi niungane na wenzangu wote ambao tumeingia kwenye uchaguzi huu baada ya kuwa tumeshashinda kwenye maeneo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais, Tanzania ya leo imempata Rais ambaye Watanzania wote wanamuhitaji na lazima tuwe na mahali pa kuendelea. Serikali si kwamba inakatika ni mwendelezo. Mheshimiwa Kikwete alifanya kazi kubwa sana kwa Watanzania na Mheshimiwa Magufuli amekuja kuendeleza pale Kikwete alipoishia na kuongeza zaidi kasi. Ni rahisi kuwa msemaji mzuri wa kupinga kila kitu, lakini naomba Waheshimiwa Wabunge sisi ni watu wazima tufike mahali tuwe more objective katika mazungumzo yetu. Watanzania wanatuangalia kutupima kwa jinsi tunavyoongea na uwakilishi wetu humu ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunazungumzia Mpango, tunazungumzia Mpango wetu wa Taifa. Bunge hili ningefurahi sana tukijikita kuzungumza tutoke hapa twende wapi, hivi vijembe na hadithi hazisaidii kwa sasa hivi, bali Watanzania tusema sasa tunataka tu-achieve kitu gani, yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina machache ya kuongea, jambo la kwanza naomba ni-acknowledge kwamba tumeanza Awamu ya Tano ikiwa na deni la shilingi trilioni 1.8, ukiangalia siyo hela ndogo ni hela kubwa sana. Watanzania lazima tufunge mikanda na ndiyo maana Mheshimiwa Rais amekuja na kauli mbiu ya kwamba hapa ni kazi tu. Maana yake ni nini? Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake.
Mheshimiwa Waziri Mpango kama ilivyo jina lake Mpango ameleta mpango mzuri sana, ninaomba Watanzania tuu-support. Mpango huu utakuwa mzuri tu ikiwa tutakubaliana sisi kama Bunge twende na Mpango huu kipamoja na siyo tumegawanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia makusanyo ya kodi tumeona kwa kipindi kifupi baada ya kudhibiti mianya ya kodi yamepanda sana. Sasa hivi the tax and revenue effect ni asilimia 12 ya GDP. Kitu ambacho bado ni chini inapaswa iongezeke. Itaongezeka tu kama tutaweza kuweka miundombinu ya kuongeza uchumi wetu.
Hapa naomba niungane na wasemaji wote, huwezi ukazungumzia uchumi bila kuwa na miundombinu ya uchumi. Lazima swala la miundombinu ya barabara na reli iwekewe kipaumbele kikubwa sana. Reli ya Kati, reli ya TAZARA lazima iwekewe kipaumbele kikubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunaposema viwanda, kweli tunataka nchi ya viwanda lazima tuweke miundombinu ambayo itawezesha viwanda hivi viweze kweli kufanya kazi yake kikamilifu. Ukiangalia leo hii hata kwenye viwanda vya nguo malighafi inayotoka nje au inakuwa rahisi zaidi kuliko mali inayozalishwa hapa nchini.
Kwa hiyo, lazima upande wa nishati tuboreshe nishati ipatikane kwa bei ya ambayo itawezesha uzalishaji wetu uweze kupambana na bidhaa za kutoka nje. Mheshimiwa Muhongo amethibitisha, ni Waziri ambaye amejitoa mhanga, kazi yake ni sahihi na naomba tumuunge mkono jitihada zake hizi (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kwenda mbali na suala zima alilosema Mheshimiwa Mdee suala la kilimo, lazima kilimo vilevile tukipe kipaumbele, hapa siyo kusema ushabiki kwa sababu asilimia kubwa ya Watanzania wanashughulika na kilimo, kilimo hiki kiweze kuwapatia Watanzania ajira na kuongeza pato la Taifa. Bila kufanya hivyo hatutasonga mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia juzi hapa kwamba Msajili wa Hazina ameamua fedha yote kwenye taasisi za Serikali wafungue akaunti Benki Kuu. Ni uamuzi sahihi na nauunga mkono, kwa sababu leo hii kama Serikali iweze kujua kwamba hizi public enterprises zote zinazalisha kiasi gani na mwenye mali ambayo ni sisi Watanzania tujue kinachozalishwa na kinatumikaje. Bila kujua vile inakuwa ni tatizo na ofisi ya Msajili kwa sasa naomba Waheshimiwa Wabunge wenzangu tumuunge mkono sana Msajili aliyepo sasa hivi Ndugu Mafuru, kwa sababu huko nyuma ofisi ya Msajili haikuwa inafanya kazi inavyotakiwa hata haikujua haya Mashirika yanafanya nini yanazalisha nini wanaleta kiasi gani Serikalini, lakini kwa muundo huu mpya itasaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kuna benki hapa zitalalamika lakini Mheshimiwa Mwenyekiti niseme hivi, hela ya serilkali ambayo ipo kwenye mabenki ni trilioni 1.1, katika hela hiyo bilioni 335 iko kwenye current account, haizai faida yoyote ile hawa jamaa wanatumia kuzalisha wenyewe, matokeo yake hata riba zinakuwa ziko juu. Sasa tuweke uwiano sawa ili benki zi-compete vizuri kwamba hakuna pesa ya bure. (Makofi)
Serikali hii ina hela hela zake kwenye current account na inakopa tena kwa riba kubwa zaidi, sielewi ni uchumi wa aina gani huu na sijui wanapokuwa wanafanya wanafikiria kitu gani. wewe hela za kwako uende kukopa tena kwa riba ya juu unafanyaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba katika hili niunge mkono kabisa kwamba Serikali kupitia Msajili wa Hazina waandae utaratibu ambao hautaleta matatizo ili pesa inayozalishwa ichangie kwenye bajeti ya Serikali, ichangie kwenye mapato ya Serikali na kuondoa ufujivu wa fedha ya Serikali. Kuna mashirika hapa walikuwa wanajigawia fedha wanavyotaka wenyewe, Bodi ikiamua imeamua. Tuachane na utaratibu huo, sasa hapa ni kazi tu. Dada yangu Halima Mdee hapa ni kazi tu, lazima pesa ipatikane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Wabunge tunalalamika pengine baadhi ya vitu vyetu havijakaa sawa, ndiyo Serikali haina pesa itatoa wapi na sisi tuhangaike kutoa mchango utaokasaidia Serikali iweze kukusanya mapato ya kutosha na iweze kutoa huduma kwa Watanzania wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuna benki hapa Tanzania 54, lakini mabenki tisa tu ndiyo yamekuwa yakichezea hela ya Serikali mengine hapana! Sidhani kama kutakuwa na ulalamishi wowote ule kwa nini walalamike, isipokuwa tuongeze mapato ya Serikali
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia; huko Busega, asubuhi nilisema hapa, kuna tatizo kubwa na hili siyo la Busega peke yake, ni maeneo yote ambayo yanapakana na hifadhi za Taifa. Naiomba Serikali kupitia Wizara husika na kuwashirikisha Mawaziri wanaohusika na wadau wote, tuwe na mkakati wa pamoja. Tunahitaji tulinde hifadhi zetu za Taifa, tu-promote utalii, lakini wakati huo huo tujali maisha ya wananchi na mifugo yao ili kuweza kujenga usalama na mahusiano ya karibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa agizo la Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii alilolitoa hapa, limefanya kazi. Mifugo ile nimeambiwa bado kuna hapa na hapa lakini baadhi ya mingine imeanza kuachiwa. Naomba Mheshimiwa Waziri ufuatilie tena ili vijana wako wa Game Reserves waheshimu wakulima na wafugaji walio kandokando ya hifadhi hizi. Kwa maana hiyo, tusiwe na uhasama ambao hauna tija yoyote ile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimpongeze Waziri Mkuu. Waziri Mkuu ameanza kazi vizuri, endelea kuchapa kazi, Serikali yako na wanachama wote, Watanzania wote, pamoja na Rais watawaunga mkono, ahsanteni sana.
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nami napenda niungane na wachangiaji wenzangu, kwanza kuwapongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu wake, Waziri wa Fedha na Mipango kwa kuwasilisha Mpango mzuri, Mpango ambao unaonekana una mwelekeo, Mpango ambao unatia bashasha Watanzania kutoka hapa tulipo kufikia malengo ambayo Mheshimiwa Rais ameyaweka Mheshimiwa Spika, ni vigumu sana kuzungumzia Mpango huu kwanza bila kutambua na kufahamu kwamba Mheshimiwa Rais ana nia ya dhati ya kuwapenda Watanzania ya kuwatoa Watanzania kwenye hali waliyonayo waende kwenye hali nzuri zaidi. Itakuwa ni kitu cha ajabu sana kuzungumzia mshahara wa Rais. What is mshahara wa Rais? Ni mtu ameajiriwa na Watanzania, anapata mshahara na ni Rais wa kwanza katika historia hapa nchini aliyetangaza mshahara wake hadharani. Napenda tumpongeze Mheshimiwa Rais kwa hilo kwanza! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, napenda nilipongeze Bunge lako pamoja na Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, kwa sababu suala la kuonekana kwenye TV, Watanzania lengo lao siyo kuona kwenye TV, wanataka kuona nini Wabunge tunafanya ili kuwatumikia wao. Hii inaonekana kwa vitendo, haionekani kwa maneno ya kuja hapa na kupiga porojo. Naomba Watanzania wote watuelewe kwa hilo na wameshaanza kuelewa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa hivi nikwambie, hapa Bungeni hata vijembe vimepungua kwa sababu hakuna anayewaona kule. Mbwembwe zote sasa hivi hakuna anayewaona kule! Ndiyo maana wamekuwa wapole. Nami nasema hivi, watulie tuwanyoe taratibu. Maana ukitaka kunyolewa, tega kichwa chako unyolewe taratibu. Tujengane hapa kwa hoja, tupingane kwa hoja na siyo kwa mbwembwe ambazo haziwasaidii Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, watu wanaona majipu yanatumbuliwa! Mimi nasema hivi na bado, yazidi kutumbuliwa zaidi. Kwa sababu, Watanzania wanasema hivi, moja ya sekta ambayo imekuwa ikisumbua ni Sekta ya Utumishi wa Umma. Kuna baadhi ya watu walishajigeuza kuwa miungu watu, hawaguswi! Sasa majipu yameanza kutumbuliwa, wengine wanasema aah, msitumbue watu, msifanye hivi, mnakiuka haki, haki gani? Haki ya kuwanyima Watanzania haki yao? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nasema acha watumbuliwe majipu na vipele na matambazi na wao kama wanataka, waendelee kutumbuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika Mpango huu, napenda nimsifu Mheshimiwa Rais. Mpango wa Kwanza uliokwisha, ulikuwa wa Shilingi trilioni 44.5. Huu ni wa Shilingi trilioni 107. Uone jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais na Serikali yake amejipanga kuwatumikia Watanzania. Hivi mnataka nini zaidi hapa jamani? Mnataka tutoke hapa twende wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ni mtu ambaye atakuwa na matatizo au upungufu wa akili kidogo, kama ataona Mpango huu unakuwa na kichefuchefu kwake.
MHE. MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, Taarifa! Kanuni ya 68(8).
SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Chegeni, kuna taarifa....
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, wala siipokei kwa sababu ameeleza tu, amezungumza hapa, lakini tutaendelea kuyatumbua yawe yako wapi, yako kwenye shavu, yako wapi yatatumbuliwa tu. Hata wanaosema hawa na wenyewe wengine ni sehemu ya majipu!
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, nao ni sehemu ya majipu! Kwa hiyo, wasione haya! (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba sasa nijielekeze kwenye mpango wa miaka mitano huu ujao kwa sababu haya ni mambo ya msingi. Nchi hii ili tuweze kutoka hapa tulipo, ni lazima kwanza tuangalie mfumo mzima wa kukusanya kodi yetu ili kila Mtanzania alipe kodi na ashiriki kwenye uchumi wa nchi hii. Huwezi kujenga uchumi wa nchi bila kuwa na mfumo mzuri wa kukusanya kodi yake. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napenda nimpongeze Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana hii; kwa kweli, ukiangalia sasa hivi licha ya Wahisani na baadhi ya watu mbalimbali wameshindwa kuanza kutupa pesa zao, lakini mapato yetu yameweza kupanda kutoka Shilingi bilioni 850 kwa mwezi mpaka Shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi; hii ni achievement moja kubwa sana kwa nchi, lakini imepatikana siyo kwa sababu ya mambo ya rojorojo, ni kwa sababu moja tu ya kutumbua majipu. Haya majipu nayo yalikuwa ni tatizo! Ndiyo maana ukusanyaji wa kodi umeweza kuongezeka. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, uchumi huu wetu, naomba Mheshimiwa Waziri alielewe hili; tunahitaji tukusanye kodi kutoka vyanzo vingine mbadala. Tusiwe na msingi wa kudhani kwamba ni kupandisha tu kodi kwenye vitu vilevile, hapana! Tubuni vyanzo vingine mbadala vingi vya kuweza kutupatia kodi. Kwa mfano, haya wa Makampuni ya Simu. Makampuni ya Simu, watu wa TCRA walishawaonesha watu wa TRA kwamba kodi yenu kwa mwezi ni kiasi fulani, sasa kwa sababu mpaka Finance Bill ije, ndiyo kodi iweze kubadilishwa; naomba tuanze kutafuta namna ya kufanya adjustments! Haiwezekani hawa watu wanafanya biashara hawalipi kodi stahiki na hili ni pato moja kubwa sana kwa nchi hii na hawa watu wanakwepa sana kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana kupitia Bunge lako hili, mfumo mzima wa ukusanyaji wa kodi kwa Makampuni ya Simu ni lazima sasa ubadilike, lakini hauishii pale. Hawa watu wamejenga minara kila kona nchi hii. Kuna Halmashauri hazipati Service Levy kutoka kwenye minara hii! Unakuta minara imetapakaa, lakini Halmashauri haipati chochote! Hivi hii inakwenda wapi? Ni lazima Halmashauri zetu ziweze kupata kodi kutokana na hii shughuli ya biashara ya minara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nchi hii ili tuweze kupanua uchumi wetu, ni lazima tuweke miundombinu iliyo sahihi. Huwezi ukazungumzia uchumi wa nchi hii bila kuzungumzia reli. Lazima reli ifufuliwe na kutengenezwa kwa kiwango kinachostahili cha standard gauge ili sasa mizigo iweze kusafirishwa kutoka bandari zetu, kutoka mikoa yetu, ukianzia Mtwara kwenda Mchuchuma, ukitoka Dar es Salam kwenda Kigoma, ukitoka Dar es Salaam kwenda Tanga, Mwanza na yote ile inaleta connectivity ya mawasiliano katika nchi na ili tuweze kupunguza gharama katika utengenezaji wa barabara zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, repair ya barabara ni gharama kubwa sana. Leo hii barabara ya Chalinze imekuwa kama chapati, kwa sababu magari mengi yanapita pale pale. Kila kukicha unakuta barabara inaharibika! Vile vile na magari ya mizigo mikubwa yanapita pale. Kwa hiyo, naomba sana hili suala la miundombinu na hasa reli tuweze kuipa kipaumbele katika mkakati wetu wa kufufua uchumi wetu.
Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya maeneo, kwa mfano Kanda ya Ziwa. Wenzetu wa Mbeya wana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe. Historia yake ukiingalia, ilikuwa ni hela za kujenga uwanja wa Mwanza, ikaonekana hazitoshi zikahamishwa kupelekwa uwanja wa Songwe Mbeya. Mwanza ile ni hub, Uwanja wa Ndege wa Mwanza naomba upewe kipaumbele.
Mheshimiwa Spika, kutoka Mwanza kwenda Serengeti ni kilometa 140, umefika kwenye geti la Serengeti ambapo hata ndugu yangu Mheshimiwa Heche pale na watu wanaokwenda huko akina Mheshimiwa Esther Matiko, ndiyo barabara yao wanapokwenda kule. Unakuta unatumia kilometa 380 kufika kwenye geti la Serengeti kutokea Kilimanjaro, wakati Mwanza ni karibu. Kwa hiyo, naomba sana Mwanza Airport iweze kukamilika ili iweze kufufua uchumi wa nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, naamini kwa kuwa na uwanja wa ndege wa Mwanza itasaidia sana kuleta biashara, itasaidia sana kusukuma uchumi wa Kanda ya Ziwa. Leo hii kwenda Nairobi inabidi pengine upitie Dar es Salaam ndiyo uende Nairobi kwa sababu, ndege hakuna. Kwenda Kampala, inabidi uje Dar es Salaam ndiyo uende Kampala na kadha wa kadha. Naomba sana, uwanja wa ndege wa Mwanza uweze kuimarishwa.
Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya vipaumbele ambavyo tunavyo, lakini suala la kilimo; unaposema tufufue uchumi wa viwanda, ni lazima iwe based na agromechanics na agroeconomy. Sasa hii yote itasaidia sana kufanya wakulima ambao ni wengi zaidi wa Tanzania waweze kuzalisha mazao yatakayochakatwa na kuongezewa thamani, itaondoa na tatizo la ajira kwa vijana, itaondoa na tatizo la kupata kipato kwa watu. Naomba sana suala hili lizingatiwe.
Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la uvuvi na mifugo. Mimi najiuliza, tunachoma nyavu moto, lakini nani analeta nyavu hizo na zinapitia wapi? Kwa sababu huyu mvuvi yeye hana kosa! Amekwenda dukani, amekuta nyavu zinauzwa, ananunua. Sipendi kusema kwamba, tuwaambie watu wafanye uvuvi haramu, lakini hizi nyavu zinaingia hapa nchini na mnajua zinaingiaje. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nasema hivi, wanaoingiza nyavu ambazo hazistahili, basi zipigwe marufuku ili kuondokana na tatizo la kuanza kuwatia hasara wavuvi. Mtu amewekeza kwa shilingi kadhaa kwenye mtaji wake pale, halafu mnakuja mnashika nyavu mnachoma! Hii siyo sahihi.
Mheshimiwa Spika, naomba sana Serikali yetu tuliangalie hilo na hasa nikizingatia kwamba Mheshimiwa Rais amekuja na nia thabiti sana kuwatumikia Watanzania na naomba Waheshimiwa Wabunge wote tumuunge mkono. Kwa kupitia bajeti hii naomba kwa kweli, tujipambanue nayo kwamba ni bajeti ya kumsaidia kila Mtanzania. Kipindi hiki ni kipindi ambacho siyo kizuri sana kwetu, lakini lazima tukubali kwamba mabadiliko yoyote yanahitaji kidogo watu kuumia. Tuumie, lakini kwa nia njema ya kujenga nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, baadhi ya watu wanaweza wakawa wanasema kwa kubeza eti kwamba Mheshimiwa Magufuli ni nguvu ya soda, nawashangaa sana! Mheshimiwa Magufuli ana nia ya dhati! Rais wetu tumemchagua kwa kura nyingi sana, Watanzania wamemwamini na niwahakikishie kwamba amekuwa siku zote anaonesha dhamira yake ya kuwatumikia Watanzania. Kama kuna watu wana mkakati wa kutaka kubadilisha au ku-undermine anachokifanya, tunasema washindwe na walegee! Mshindwe na mlegee kabisa! Mlegee kabisaa! Mjilegeze, mlegee, iwe sawasawa!
Mheshimiwa Spika, nasema hivi, lazima tumuunge mkono! Hataweza kupigana vita hii akiwa peke yake. Waheshimiwa Mawaziri mmeanza vizuri, endeleeni! Sitaweza kuwataja mmoja mmoja, lakini nikianzia kwa Mheshimiwa Lukuvi, kwa Mheshimiwa Jenista Mhagama, kwa Mheshimiwa Mwijage mnamwona kila siku anaweka mambo yake hapa, mnaona! Ukija kwa mzee wa TAMISEMI, ukija kwa Mheshimiwa Mwigulu na wengine wote mnawaona hapa. Timu hii ni nzuri! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ila kuna tatizo moja la kimuundo. Tatizo hili Waheshimiwa Wabunge mlielewe. Leo hii Waziri wa Elimu kwa mfano, anazungumzia mambo ya Sera katika Wizara yake, shughuli zote ziko TAMISEMI. Msingi na Sekondari ziko TAMISEMI, yeye ni wa Elimu ya Juu na Sera. Ukija kwa Waziri wa Afya, yeye anazungumzia Sera. Ukienda kwenye Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali ya Wilaya mpaka ya Mkoa ziko chini ya TAMISEMI! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kuna haja kupitia Mpango huu. Unajua siku zote mnapoona kuna tatizo, mnatafuta namna ya kuweza kulitatua tatizo hilo. Mimi naona kama kuna tatizo hapa! Kwa hiyo, kuna haja ya kujaribu kuoanisha vizuri na kuhuisha vizuri mfumo wa utendaji kazi ndani ya Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naomba wale wote waliokuwa na nia mbaya, walegee na washindwe. Ahsante sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia katika hotuba hii ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2017/2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwanza kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri, amefanya kazi yake na mpango huu ni mpango mzima wa Serikali. Ni matarajio yangu kwamba tunapozungumza mpango huu hatuzungumzii peke yake Waziri wa Fedha, tunazungumza co-ordination yote ya Serikali ndani ya mpango huu. Kwa maana hiyo Waziri Mpango naomba uwe msikivu, lazima uwe msikivu na ujaribu kuyachukua mawazo yote ambayo Waheshimiwa Wabunge tunayatoa hapa kwa mustakabali wa nchi hii.
Mheshimiwa Mpango nikupe tu siri moja, ni mtaalam mzuri, msomi mzuri, lakini una professional arrogance, una kakiburi, na mtu anayekwambia ukweli anakusaidia. Tunasema hivi ili baadae tutoke hapa tulipo tusonge mbele zaidi. Wenzangu wamesema tunaheshimu kila Mbunge aliyepo hapa ndani kwa sababu ameingia kwa nafasi yake, na wewe uko hapa kwa heshima zote, lakini chukua mawazo ya Waheshimiwa Wabunge yafanyie kazi, usipofanya hivi inatupa ugumu sisi na ukakasi wa kusema na wewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikirudi nyuma Mheshimiwa Mpango kwenye bajeti ya Serikali iliyopitishwa mwaka jana, vitu vingi tulipendekeza hapa vilikuwa na mambo mazuri sana, lakini nadhani kwa kufikiria kwako au kwa kuona kwako mambo mengi hayakufanyika kama tulivyokuwa tumependekeza. Hii sisi ilitupa nafasi ngumu sana ya kuelewa sasa tunakwendaje kama Bunge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili mpango huu unapaswa kuwa tenganifu, we should harmonise, mambo yote ambayo yanahusika katika kuwezesha uweze kutekelezeka. Haiwezekani tunapanga mipango, unakuja na kitabu hiki, hutuelezi vizuri kwamba hapa ya mwaka jana tumefanyaje, wapi tumekwama, nini tufanye kwa safari hii! Kwa sababu unapozungumza katika suala la mpango, lazima tu-reflect tumetoka wapi, nini tumefanya, nini tumeshindwa kufanya na nini tukifanye zaidi kipindi kinachokuja. Sasa Mheshimiwa Mpango naomba utusikilize sana, tunapotoa ushauri ni kwa nia njema, lakini vilevile tuki-echo kazi nzuri anayofanya Mheshimiwa Rais. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais amekuwa na nia njema sana, lakini naanza kupata wasiwasi kwamba inawezekana mlio karibu nae hamtoi ushauri stahiki kwake, hii inasababisha baadhi ya mambo mengine yasifanyike kama ambavyo watu wanategemea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tunaomba ifanye kazi kama timu moja. Haiwezekani Serikali hiyohiyo Waziri huyu anasema hiki, huyu anasema hiki, hakuna co-ordination! Na hili ndiyo tatizo ambalo linafanya hata Bunge hili lishindwe kuwashauri vizuri zaidi. Kwa hiyo, naomba sana kupitia mpango huu Mheshimiwa Mpango ongoza wenzako katika kutekeleza mpango huu, lakini uwe msikivu, usikivu wako utakusaidia ili tuweze kufanya kazi vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia sasa hivi tunasema uchumi unakua. Ni kweli, ukienda by figures and facts they never lie, lakini hali halisi lazima iwe translated kwa wananchi wenyewe, waweze kuona kwamba uchumi sasa kweli unakua. Kama hakuna translation, hakuna trickle down effect, hata tungesema namna gani hii itakuwa ni ngonjera ambayo haina mwimbaji.
Nakuomba sana suala zima kwa mfano la kodi, tulisema hivi suala la kuweka VAT on auxiliary services and transit goods italeta matatizo. Tukiweka VAT kwenye tourism sector italeta tatizo! Tumeona yote haya kwa mfano sekta sasa hivi ya utalii imedorora, lakini mnasema eti imekua! Sasa nashangaa inakuaje wakati tunaona kabisa the actual situation hali ni mbaya, wewe unasema inakua!
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumneona suala la bandari, ndiyo kulikuwa kuna ukwepaji kodi, suala la kimfumo na utaratibu TRA wangeweza kufanya kudhibiti, lakini tunategemea kwamba tupate floor nyingi ya mizingo inayokuja tuweze kupata mapato makubwa zaidi, Mheshimiwa Mpango naomba haya mambo ujaribu kuyasikiliza vizuri zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kibaya zaidi tuka-introduce VAT on financial services. Tunaona sasa hivi mabenki yanavyo-suffer. Tunaona jinsi ambavyo hali ya kibenki na hali ya kiuchumi inavyozidi kuyumba. Tunaomba sasa kufanya kosa siyo kosa, kurudia kosa ni makosa. Tujisahihishe, kama kuna mahali tulikosea tujaribu kurekebisha mapema, tusiwe tunajaribu ku-copy mambo fulani na kuja kuya-paste hapa, tuyafanyie kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba suala zima la perception management lifanyiwe kazi. Kuna watu wana perception za kwao kwamba sasa hivi uchumi wa Tanzania unakua, wengine wanasema uchumi wa Tanzania haukui, lakini ninaamini kwamba kwa sababu numbers na figures never lie uchumi unakua, lakini tunachoomba ni translation ya uchumi huo kwa wananchi waweze kuona kwamba uchumi unakua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Halmashauri nyingi hazina fedha, Serikali haina pesa, wananchi hawana hela! Sasa unapozungumza production, kukua kwa uchumi ni pamoja na production, sasa kama production haiongezeki uchumi hauwezi kukua. Wananchi watazidi ku-suffer na ku-suffer, mimi ninaamini kwamba Serikali hii ni sikivu na inajaribu kuyafanyia kazi mambo ambayo yamekuwa yana matatizo yaweze kurekebishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali imebana sana spending yake, lakini fedha iko wapi? TRA makusanyo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 850 mpaka 1.3 trillion, lakini ukiangalia outflow ya pesa tumekuwa na madeni, Deni la Taifa linazidi kupanda utadhani as if Waziri wa Fedha hutumii nafasi yako kuya-manage haya kwa sababu you need to do a financial management, is just a simple financial management.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani pesa zinazidi kutumika zaidi licha ya makusanyo kuongezeka, lakini bado spending yake inakuwa challengeable! Nikuombe sana Mheshimiwa Waziri kupitia mpango huu ninaamini kwamba Watanzania tuna imani na wewe na Bunge hili litumie kama ni chachu ya kukusaidia wewe ufanye kazi yako vizuri zaidi, lakini timiza wajibu wako.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasema hata kwenye maandiko mtu mnyenyekevu hata Mungu anampa baraka, nyenyekea Mheshimiwa Mpango, unapewa ushauri na watu sikiliza. Watu wa Business Community wamekuita mara nyingi ukutane nao unakataa! And then you came to the budget! Kamati ya Bajeti hapa, walikuwa wanasema Waziri tunamuita haji kwenye vikao. Sasa najiuliza kwamba sasa ni Waziri anafanya kazi gani hizi? Ni aibu, ni aibu. Dhamana ambayo unayo ni kubwa, hebu jaribu kuwa msikivu.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni sekta ya kilimo, sekta ya uvuvi ambayo inaajiri watu wengi sana inatakiwa sasa iwekewe kipaumbele, ili wananchi sasa na hasa wakulima, wavuvi na uzalishaji wa viwanda, tunasema kwamba ni Serikali ya viwanda, sera yetu ni ya kujenga viwanda, lakini huwezi ukajenga viwanda ukafanikiwa kama unakuta Waziri wa Viwanda tena wanamuita mzee wa sound! Eti mzee wa sound, Waziri wa Viwanda ni mzee wa sound! Haiwezekani! Tunachotaka sisi ni Waziri azungumze vitu ambavyo vinatekelezeka siyo porojo za kila wakati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tufike mahali tukubali changamoto hizi, tupunguze maneno lakini tuwajibike zaidi na tutekeleze zaidi. Leo hii wananchi wanachotaka ni kuona kwamba matokeo yanapatikana. Mheshimiwa Rais anafanya kazi kubwa sana, anafanya kila njia kuona Watanzania wananufaika na uchumi wao, Watanzania wananufaika na rasilimali zao na ninyi msaidieni sasa kwa nafasi zenu acheni maneno. Acheni kusigana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia wenzetu wa Kenya walianzisha kitu kinachoitwa interest rate capping. Riba kwenye mabenki zinazidi kupanda na zinapopanda ina maana wananchi sasa hivi wanashindwa kukopa fedha, wanashindwa kufanya production, kuna haja sasa Mheshimiwa Mpango suala zima la riba kwenye benki liangaliwe upya. Serikali ifanye serious intervention ili kusudi mabenki haya yawasaidie wananchi kama wanakopa fedha basi ziweze kutumika vizuri katika kukuza uchumi wa nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kusema kwamba lazima baadhi ya gharama nyingine za uzalishaji hapa Tanzania zipungue gharama. Huwezi ukasema unaweka viwanda wakati gharama ya umeme ni ghali, maji ni ghali, halafu kuna series kubwa sana ya kodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kodi zaidi ya 100 ambazo mtu anapaswa kuzilipa, haiwezekani! Ninaomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha kupitia mpango huu hebu jaribu kuja na kitu ambacho kitasaidia ku-harmonise yote haya. Vinginevyo mpango wako ni mzuri na mimi sijawahi kukukosoa, mpango huu ni mzuri, lakini hakikisha kwamba unakuwa msikivu na yale mambo ya msingi yafanyie kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia niwaombe tu Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwamba yawezekana tuna itikadi tofauti, lakini maslahi yetu ni ya Watanzania wote. Hakuna mtu ambaye ana maslahi nje ya Watanzania na lolote unalolifanya ndani ya Bunge hili litusaidie kumsaidia Mtanzania ambaye ndiye ametuweka sisi hapa ndani. Ninaomba sana Waheshimiwa Wabunge kupitia Bunge hili na haki za Wabunge ziweze sasa kuzingatiwa kwa sababu vilevile Mbunge aweze kufanya kazi zake anahitaji kuwa na uwezo wa kufanya kazi zake.
Mheshimiwa Mpango pamoja na yote kapu lote umelikamata wewe na usidhani kwamba watu wanavyokuona namna hii wewe ni Waziri zaidi ya Waziri kwa maana umeshika sekta nyeti, lakini hakikisha kwamba unamshauri Rais vizuri, sikiliza wadau na mtekeleze yale ambayo Watanzania wanahitaji kuyaona. Tungependa kuona kwamba ndoto ya Mheshimiwa Rais Magufuli inatimizwa na Watanzania baada ya miaka mitano tuseme kwamba sasa uongozi wa Awamu ya Tano wa Serikali ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli umeweza kufanya moja, mbili, tatu na tujivunie kwa hilo, lakini naomba katika mpango huu vilevile sekta zote na Wizara zote zinakuwa harmonized hii itatusaidia sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mawaziri wote, Mheshimiwa Chief Whip, mpango huu Mawaziri wanapaswa kuwa humu ndani wasikilize, ni wajibu wao kuona kwamba kila Waziri katika sekta yake anashiriki kikamilifu katika mpango huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Elimu. Kazi yake ni nzuri, tufike mahali Watanzania tuanze sasa kukubaliana. Hii Wizara ya Elimu ina mambo mengi sana, lakini kimuundo wake jinsi ilivyo, mambo mengi tunayozungumza Waheshimiwa Wabunge ni ya TAMISEMI. Ukizungumzia Shule za Msingi, Shule za Sekondari, vyote viko chini ya TAMISEMI na hata ukiangalia suala zima la bajeti yake, sehemu kubwa inagharamia wa Loan Board na taasisi nyingine za juu. Yeye amebaki na function role ya kutunga sera na kusimamia sera. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuna haja ya kuangalia vizuri mfumo mzima na muundo wa Wizara hii ili kweli ifanye kazi na tunaposema elimu hapa, basi moja kwa moja iweze ku-tricle-down kutoka kwa Wizara ya Elimu kuja mpaka elimu ya chini. Sasa hapa kuna gap na hata ukiangalia mazungumzo mengi ya Waheshimiwa Wabunge humu ndani, tunajaribu kuzungumza lakini kimsingi functionally, Waziri wa Elimu ana jukumu dogo sana hapa ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli kuna haja ya kuangalia muundo mzima wa Wizara hii ili sasa unapozungumzia Wizara ya Elimu, iwe na mantiki yenye kwenda mpaka kwa mwananfunzi wa chekechea. Leo hii unakuta Walimu wanadai stahiki zao, wana matatizo yao, wana mambo chungu nzima, hawana motisha, lakini bado kama Wizara ya Elimu, haina majibu ya haya. Haya peke yake yatajibiwa na Wizara ya TAMISEMI zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna debate inaendelea humu ndani, suala la shule binafsi na shule za Serikali. Waheshimiwa Wabunge, naomba nijielekeze kwamba bado suala la ada elekezi ni muhimu zaidi kwa Watanzania wote kwa sababu ukiangalia elimu siku hizi ni biashara. Mheshimiwa Mama Tibaijuka hapa ana shule zake as a business na wengine kadha wa kadha is a business. Sasa kwenye biashara zamani ilikuwa elimu ni huduma, lakini leo wanakopa kwenye mabenki wanawekeza kwenye elimu. Ni kama miradi mingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa usipokuwa na regulation policy hawa watoto wa mkulima watoto wa Mtanzania ambaye hana uwezo wa kuweza kulipa ada, inakuaje? Kwa hiyo, lazima ifike mahali Serikali i-play role yake ya kuwasaidia Watanzania wote. Naheshimu kwamba shule za binafsi wacha mwenye kipato cha juu ampeleke mtoto wake kwenye shule ya binafsi alipie hiyo ada, ana uwezo wake; lakini yule ambaye hana uwezo, tunamsaidiaje? Sasa ni wajibu wa Serikali kuweza kuboresha. Lazima Serikali iboreshe. Inaboreshaje? Waheshimiwa Wabunge hapa tuje na mkakati tuseme iboreshe namna gani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoanza kusema Wizara ya Elimu iboreshe, hataboresha huyu! Serikali kupitia TAMISEMI kwa Mheshimiwa Simbachawene, ndiyo tuipe jukumu kubwa la kuboresha Shule za Sekondari na Shule za Msingi ambao ndiyo msingi wa chimbuko la mwanafunzi wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunasema kwamba lazima kuwe na ada elekezi, Serikali lazima iweke policy hiyo. Hawa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo, watasomaje hizi shule? Hawa watoto ambao Serikali hii imejitolea kuchangia kupitia kodi za Watanzania, kwa sababu leo hii Watanzania katika kuboresha zile kodi za Watanzania, zimesaidia sasa kwenye kuboresha shule hizi. Kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge, katika hili naomba tukubaliane tu. (Makofi)
Mheshimiwa mwenyekiti, katika hali ya kawaida, mitaala yetu ya elimu bado ina mapungufu makubwa sana. Leo watoto wanapohitimu, hatuwatengenezi katika akili ya kujiajiri au kujitegemea. Tunawatengeneza katika akili ya kuajiriwa kitu ambacho ni tatizo. Kwa hiyo, kuna haja ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, naomba mje na mtaala ambao utasaidia wahitimu wanapohitimu iwasaidie kuweza kujitegemeza katika kujenga maisha yao. Bila kufanya hivyo, suala la ajira ni tatizo na bado Watanzania tunazidi kulia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii katika Labour Market Watanzania tunapoenda ku-compete watu wengi hatuwezi kufaulu. Niwape tu mfano. Leo hii Makao Makuu ya Kiswahili yako Zanzibar lakini anaye-head ile timu ni Mkenya kwa sababu Mtanzania hakuna aliyefaulu kujua kusema Kiswahili vizuri kuliko Mkenya.
Kwa hiyo, Watanzania tunakwenda kwenye job Market, hatuna uwezo wa kutaka kuchukua kazi hizi? Anayefuatia pale ni Mganda. Leo Watanzania pamoja na kwamba Kiswahili kilizaliwa Tanzania, kikakua Tanzania, kikaanza kukulia nchi jirani kikafia kwingine na kikazikwa kwingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bado Watanzania tunaenda kwenye soko la ajira tuna tatizo kubwa sana, lakini ni kwa sababu ya muundo na mfumo wa elimu yetu. Naomba sana Mheshimiwa Waziri, wewe una nafasi ya pekee, umekuwa ni mtu ambaye ni mahiri toka ukiwa NECTA. Umefanya kazi nzuri. Tumia sasa utalaamu wako huo kuweza kui-shape Wizara ya Elimu ili Watanzania wapate wanachokitaka. Leo hii ukiangalia, Tanzania ina wasomi wengi sana lakini wakipelekwa kwenye soko la ajira ni wachache wanaweza ku-compete na kupata kazi za Kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana hili tuweze kuliangalia. Vile vile kuna suala la mazingira ya elimu na hasa watoto wa kike. Kuna baadhi ya maeneo watoto wa kike wanashindwa kwenda shule kwa sababu hakuna vyoo. Wanashindwa kujisaidia vizuri kwa sababu ni watoto wa kike; wanashindwa kusoma kwa sababu ni watoto wa kike. Naomba tuweke mkazo, Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Mheshimiwa Simbachawene Waziri wa TAMISEMI, naomba muwe na link nzuri na Wizara ya Elimu. Mfanye kazi kwa maelewano mazuri ili kusudi tuwasaidie watoto wa Mtanzania waweze kuhitimu vizuri na wapate elimu inayotakiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilisoma katika shule za mission Form One mpaka Form Six, ni mdau. Natambua ubora wa shule binafsi, lakini naiomba Serikali hii itusaidie, bado Shule za Serikali zinatakiwa ziboreshwe zaidi ili ziweze ku-compete na shule za binafsi. Tusipofanya hivyo tutakuwa tunacheza mchezo ambao ni wa kuigiza. Mzazi anahitaji asomeshe mtoto wake, lakini tunahitaji quality of education.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima ubora wa elimu tuuzingatie. Tusiwe na wingi tu wa kusema tunaingiza watoto, wanasoma. Tumeanzisha Shule za Kata, zimesaidia sana kuwaelimisha Watanzania, zimesaidia sana mpaka Waheshimiwa Wabunge humu wamesoma Shule za Kata, wako humu ndani. Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Aweso huyu ni zao la Shule ya Kata, leo ni Mheshimiwa Mbunge hapa ndani na wengine, lakini watu walidharau wakasema ni yebo yebo, hakuna cha yebo yebo! Hizi shule zimesaidia, naomba tuziboreshe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni madai ya Walimu. Hivi huyu Mwalimu atakuwaje na moyo wa kufundisha? Atakuwaje na moyo wa kumwelimisha mtoto wa Mtanzania…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nianze kutoa pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba hii nzuri ya Bajeti. Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kweli ameonesha dira nzuri sana na imeonesha kwamba ni kwa kiwango gani uchapaji wake kazi umekuwa ukiongezeka. Kwa maana hiyo hata Mheshimiwa Rais nadhani anamsoma vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu hotuba yake hii amelenga maeneo yote husika na jinsi ambavyo uchumi wa nchi hii na mustakabali wa nchi hii katika ustawi wake unavyokwenda. Kwa kweli nimefarijika na napenda tu nichangie hotuba hii kwa kukupongeza la kwanza na ninaiunga mkono moja kwa moja hotuba hii ya kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Awamu ya Tano Mheshimiwa Waziri Mkuu imekuwa na changamoto nyingi sana. Kila mmoja anaweza kuiona kwa sura yake na kwa muono wake lakini naomba nikiri kwamba kazi wanayochapa Serikali ya Awamu ya Tano haina mfano. Wamefanya uwekezaji ambao ni world class record. Haijawahi kutokea katika kipindi chote cha miaka yote Tanzania toka kuumbwa kwake kuwa na uwekezaji mkubwa kwa kipindi kifupi. Hii ni dalili njema kwamba tunaumia kwa kipindi kifupi tutanufaika kwa kipindi kirefu kijacho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba hii imejilenga katika mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwekezaji mpaka sasa hivi katika public sector ni zaidi ya trilioni 48.5 lakini deni la Taifa ni trilioni 46. Nasema kwamba umewekeza mtaji mkubwa kuliko deni la Taifa. Bado tuko vizuri na hata katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu amezungumza kwamba sisi bado tunakopesheka. Naomba tukope kwa kuwekeza hata ile miradi ambayo ina tija kwa Watanzania, tusikope kwa miradi ambayo hatuna tija nayo. Naona kwa hili mmejielekeza vizuri sana nakupongeza sana wewe pamoja na Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na yote haya ningependa kuzungumzia suala moja ambalo ni tatizo sasa linaanza kujitokeza. Kuna suala la mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Simiyu wilaya mbalimbali za Mkoa wa Simiyu. Mheshimiwa Rais mwaka jana mwezi wa kwanza alikuja na akatoa maelekezo kwamba mradi ule uanze mara moja kwa sababu mahitaji ya maji ni ya msingi sana kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na mwekezaji kwenye mlima wa Ngasamo, Mheshimiwa Rais akasema kwamba yule mwekezaji kwa vile haendelei na uwekezaji basi leseni yake ifutwe. Mheshimiwa Waziri Mkuu ni mwaka mzima sasa umepita toka Rais atoe maelekezo lakini hakuna kinachoendelea. Tumeongea na Waziri wa Maji anasema kuna mambo ya madini, Wizara ya Madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja kubwa hapa ni kwamba hakujakuwa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, kwa hiyo, tulikuwa tunaomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu hebu tuone mamlaka inayohusika ateuliwe huyu Mwenyekiti wa Tume ya Madini ili kusudi leseni iweze kufutwa na mradi uweze kutekelezeka. Bila kufanya vile hatutaweza kusonga mbele, kwa sababu pesa hii inatoka kwa wahisani na moja kati ya sharti lao ni kwamba lazima kuwe hakuna encumbrance yoyote kwenye uwekezaji huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu alibebe hili aongee na Mheshimiwa Rais kama inawezekana huyu Mwenyekiti wa Madini basi ateuliwe mara moja ili kazi ifanyike kwa sababu kazi haziendi kama ambavyo tulikuwa tunatarajia na wananchi wa Mkoa wa Simiyu wanasubiri kwa hamu sana mradi huu ambao ni wa kihistoria. Naomba tuendelee kuiunga mkono miradi kama hii, najua kuna maeneo mengi wana miradi kama hii inaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la wilaya mpya bado ni changamoto. Wilaya ya Busega ni moja ya wilaya mpya ambazo hazijakomaa. Mheshimiwa Waziri Mkuu mwaka juzi alikuja yeye mwenyewe akatembelea Wilaya ya Busega, akaona jinsi tulivyo hatuna jengo. Tunajenga jengo la halmashauri halijakamilika huu ni mwaka wa tatu, hatuna hospitali ya wilaya na miundombinu, hata Mkuu wa Wilaya hana ofisi anatumia Ofisi ya Mbunge kama ofisi yake. Sasa vitu kama hivi ningeomba tuweke kipaumbele kwa sababu palikuwa na miradi mingi mingi midogo midogo bila kukamilisha ambayo imeshaanza tayari. Ningeomba kupitia bajeti hii wilaya ambazo bado zinahitaji kuimarishwa basi zikamilishwe ili tuweze kusonga mbele tumalize moja twende na lingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa suala la wilaya hizi mpya hususani Busega na Itilima kwa Mkoa wa Simiyu na wilaya zingine katika nchi hii ziangaliwe kwa kuwekewa miundombinu ambayo ni muhimu sana stahiki ili ziweze kufanya kazi na kutoa huduma kwa Watanzania kama inavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na haya bado kuna suala la uwekezaji katika viwanja vya ndege. Kiwanja cha Ndege cha Songwe kimeshajengwa lakini kimebaki kukamilika kidogo tu lakini pale hakuna taa za kuongozea ndege kutua pale. Ni uwekezaji mdogo kama bilioni nne hivi. Tunaomba sana Serikali miradi kama hii iweze kukamilishwa kwa sababu leo hii kwa Tanzania tuna viwanja vinne vikubwa. Kiwanja cha Dar es Salaam Julius Nyerere International Airport, kiwanja cha Mwanza, Kiwanja cha Songwe na kiwanja cha Kilimanjaro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda hata Mwanza, tunalilia kwamba uwanja wa Mwanza uweze kujengwa jengo la kushukia abiria. Mpaka leo ni miaka nenda rudi bado hatujatekeleza. Ningeomba tuangalie priority ya kiuchumi, ukiweza kuimarisha Songwe ikaweza kufanya kazi vizuri, ukaimarisha Mwanza ikafanya kazi vizuri, ukaenda na Mtwara ukaimarisha tayari tutakuwa na viwanja ambavyo vitaongeza mapato makubwa kwa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana kama Serikali mjaribu kuangalia vipaumbele ni vipi ambavyo tuweze kuvifanya vitakavyoongeza tija zaidi halafu tu-service viwanja vingine vidogo vidogo kadri ya fedha inavyopatikana, tusisubiri sana fedha ya wahisani ikiwezekana pesa zetu za ndani zitumike kuweza kukamilisha miundombinu ya namna hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo tunalo na ni tatizo kubwa kidogo na hasa sisi wenyeji wa kanda ya ziwa. Mwananchi wa kanda ya ziwa anategemea uchumi wake kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji. Leo hii suala la wavuvi haramu hakuna anayeunga mkono suala la uvuvi haramu lakini bado kitendo kinachofanyika kuhusu kuwanyang’anya vifaa vyao tunaamini wavuvi wao wananunua nyavu kutoka kwenye viwanda na maduka husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, haya maduka ilikuwa ndio chanzo cha kuweza kuyawajibisha zaidi kuliko mnazuia haramu. Maana yake mvuvi yeye anavua apate riziki yake apate kipato chake lakini anatozwa faini ambazo ziko nje ya utaratibu, ananyanyaswa, jamani nadhani kama CCM sisi tunasema kwamba hatutii watu umaskini tumekuwa tunatia watu utajiri. Ningeomba sana sana Mheshimiwa Waziri Mkuu suala hili tuliangalie kwa umakini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mazao kwa mfano pamba mwaka huu kuna uzalishaji mkubwa sana wa pamba katika mikoa inayolima pamba. Tunaomba kuwe na utaratibu mzuri ili zao hili sasa mkulima anufaike nalo, bila kuwa na utaratibu mzuri tutazidi kuwakatisha tamaa wananchi ambao siku zote wamekuwa wakijitoa muhanga kulima pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la wafugaji, migogoro ya wafugaji na hifadhi za Taifa bado ni tatizo kubwa sana. Hata jana hapa kulikuwa na mjadala kuhusu tembo, suala sio dogo Mheshimiwa Waziri Mkuu. Wananchi wanalia kwa sababu wanyama waharibifu kama tembo, viboko wanavamia makazi ya wananchi na kuharibu mazao ya wananchi, lakini wananchi wamekuwa ni waaminifu kulinda rasilimali hizi. Tunaomba na Serikali iweze kuwasaidia angalau kuweza kuona kwamba wanalindwa na wao. Tembo wanaua watu, tembo wanaharibu mali ya watu lakini bado Serikali haiwajibiki kikamilifu, haiwezi kuwasaidia wananchi kwa uharaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata tembo anapotokea kuvamia maeneo ya wananchi, unapoomba msaada wa vikosi vya kuweza kuzuia, inachukua muda mrefu sana. Niombe Wizara husika wajaribu kuongea na watu hawa wahusika wote na tuweze kuwa na mustakabali mzuri wa utumiaji na ulindaji wa rasilimali za Taifa. Wakulima na wananchi wanapenda tulinde rasilimali zetu hizi lakini naomba na Serikali iwajibike kwa kiwango kikubwa sana kuona thamani ya mwanadamu katika suala hili lote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la barabara, wilaya mpya zinapoanzishwa zinakuwa hazina miundombinu ya barabara. Tunaomba ile kilomita tano kwa kila halmashauri mpya itekelezwe na tungeenda angalau kwa kwenda kwa mpangilio kwamba mwaka huu labda halmashauri kama ni kumi, kumi na tano zikamilike, mwaka ujao hizi zikamilike, lakini naona unakuta muda mrefu unakwenda hakuna ambacho kinachofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba sana na Mheshimiwa Waziri Mkuu yuko hapa na bahati nzuri anaijua vizuri sana Busega kwa sababu alikuja Busega na wananchi wa Busega wakamkarimu vizuri na wakampa jina la Chifu Masanja, maana yake Masanja ni mtu ambaye anayekusanya watu, ni mtu wa watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukarimu wa watu wa Busega, naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, basi awafikirie kidogo ili mambo yao yawanyookee. Alipokuwa pale mzee alitoa kauli nzito nzito, yeye sio mtu wa kubabaisha, ni mtu wa kauli nzito na vitendo kama alivyo Rais wake. Hebu aende kwa vitendo ili wananchi wa Busega wapate kumbukumbu nzuri ya maneno yake na uchapakazi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija suala zima la UKIMWI, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukimwi, Mheshimiwa Mukasa ameniomba nizungumze kidogo. Kwa vile suala hili liko katika Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, hawa watu ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI naomba wapewe msaada mkubwa, Serikali iwasaidie. Najua kuna baadhi ya halmashauri zimeshaainisha namna ya kuweza kuwasaidia na kushughulika nao, lakini naomba kama jitihada za kiserikali ziongezwe zaidi. Hawa watu wanahitaji msaada mkubwa zaidi na naomba Serikali iweze kuliangalia kwa nafasi ya pekee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa viwanda ni wa kuondoa umaskini kwa Mtanzania. Ni watu wachache ambao wanaweza kufikiri vinginevyo, lakini naamini kabisa kwamba tukiweza kuunga mkono jitihada ya Serikali ya Awamu ya Tano haya yanayotokea mengine ni mihemko tu na sidhani kama mtu anatoka Zanzibar anasema kwamba sukari haiwezi kuja Bara wakati anazalisha tani elfu nane peke yake na mahitaji ni zaidi ya tani elfu kumi na saba mpaka tani elfu ishirini. Sasa mambo mengine haya tunayaibua bila kuwa na sababu yoyote ya msingi na wanasema kama huna takwimu usiseme kitu, unaibua kitu ambacho hakina maana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini sisi Watanzania wote kwa umoja wetu, mali iliyoko Bara ni kama iliyoko Zanzibar, iliyoko Zanzibar ni kama iliyoko Bara na ndiyo Muungano wetu uliposimama katika misingi hiyo. Tunapoanza kusema unajua mali ya Zanzibar haiwezi kuja huku wakati takwimu yako siyo sahihi, naomba Waheshimiwa Wabunge tujaribu kuliangalia hili na tujaribu kuwa makini zaidi, tusichanganye wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia katika hotuba hii ya bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mheshimiwa Mwijage na Naibu wake wanafanya kazi nzuri sana. Naomba tukiri hilo kwamba wanafanya kazi nzuri isipokuwa tu ni kwamba uwezeshwaji wa kufanya kazi ndiyo kuna matatizo. Hii nadhani sisi kama Bunge tufikie mahali tutafute namna ya kuweza kuwasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni mtambuka, ina mambo mengi sana. Bila kusaidiwa na kuwezeshwa kufanya kazi, itakuwa ni hadithi. Ndiyo maana anajiita ni Mzee wa Sound, ni kweli anapiga sound tu, anazunguka huku na huku, anapiga sound. Nadhani tafsiri halisi ya Mheshimiwa Mwijage mimi ninavyofikiri ilikuwa ni kwamba kauli ya Watanzania katika uchumi wa viwanda iweze kushamiri. Mheshimiwa Mwijage, umefanya kazi nzuri, lakini bado kuna wingu kubwa sana la tafsiri ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tufike mahali kama nchi tuweze kuwa na tafsiri pana na iliyo sahihi. Unaposema viwanda, cherehani tano ni kiwanda, kwa baadhi ya watu tunashindwa kukuelewa vizuri zaidi, kuna vitu vinaitwa factory na industry, sasa ni lazima kuwe na utofauti wa namna hiyo. Tukitofautisha hivyo, tukisema kwamba tumekuwa na viwanda 3,000 na kitu Watanzania wataelewa ni kitu gani. Nadhani tamaa kubwa ya Watanzania ni kuona kwamba mnapozungumzia viwanda ni vya kati na vile vikubwa zaidi ili viweze kuchochea zaidi katika kuleta uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii pamoja na yote inayofanya, kuna vitu ambavyo ni lazima mvisimamie kwa uhakika zaidi. Ni namna gani ya kumsaidia mwananchi huyu na hasa mkulima maana zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima kuongeza thamani ya mazao yao, tukishafaulu pale hiyo ndiyo Tanzania ya viwanda tunayoitaka. Bila hivyo, itakuwa tunaongea kama ngonjera tu. Haiwezekani leo hii tunazidi ku-import vitu kutoka nje ambavyo tunaweza kuzalisha hapa nchini na tukapunguza kutumia fedha zetu za kigeni kununua bidhaa kutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusu mkulima wa pamba. Mkulima wa Pamba ana mateso makubwa sana. Mwaka 2017 alilima pamba na akapata bei nzuri ya Sh.1,200 ikamhamasisha kulima zaidi mwaka huu, lakini utaratibu uliopo mwaka huu unamvunja moyo mkulima wa pamba. Ni vema kuangalia namna ya kuweza kumsaidia, vivyo hivyo hata kwa wakulima wa mazao mengine, tuangalie namna ya kuweza kufufua vinu vya kuchambua pamba ambavyo vitaongeza thamani ya mazao ya mkulima. Namna ya kuanza kuwa na viwanda vya kuweza ku-process bidhaa ya mkulima kama ni pamba, tuweze kupata nguo hapa nchini. Bila ya kufanya hivyo, haiwezekani na lazima tuwe na sera ya kulinda viwanda vyetu. Bila kulinda viwanda haitawezekana. Haiwezekani tunaacha soko letu, tunaingiza tu bidhaa kutoka nje bila kuangalia viwanda vya ndani. Bila ya kuwa na hiyo sera, hatutafanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba sana Mheshimiwa Mwijage pamoja na Wizara yako, hili jambo mliangalie kwa makini, linamgusa Waziri wa Fedha. Lazima tuwe na sera za fedha na za kodi za makusudi kabisa za kulinda viwanda vya ndani. Kama ni kodi, basi tutoze kodi kubwa kwa bidhaa kutoka nje na tufanye zero rating kwa bidhaa za ndani. Tukifanya hivyo itasaidia kuchochea mkulima huyu aweze kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii mkulima wa korosho amepata bei nzuri, wamehamasika zaidi na korosho inaendelea vizuri lakini mazao mengine yanaanguka. Mazao kama chai, kahawa, mbaazi na kadhalika, sina haja ya kuyarudia sana, lakini leo hii Tanzania miaka 57 ya uhuru bado tuna-import mafuta ya kula kutoka nje, hii ni aibu. Tufike mahali tuangalie namna gani nzuri zaidi ya kuwezesha kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini ambazo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kupata uzalishaji wa kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, Wizara hii, Mheshimiwa Waziri acha tu kutembea mikoani, toka nje kaone, fanya economic diplomacy. Zunguka, tembea, unganisha nchi hii na mataifa mengine ili biashara ziweze kwenda. Haiwezekani kuna maonyesho mbalimbali ya kidunia, sijaona Waziri wa Viwanda na Biashara au Naibu wake nao wanafunga safari kwenda kuiunganisha Tanzania na dunia nyingine. Bila kufanya hivyo hatutakwenda tunapotaka. Mheshimiwa Waziri, wewe sio Waziri wa kwenda kijijini kwangu, kwenye kata, wewe Wizara yako ni muhimu sana. Tumwache Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI azunguke na kata na vijiji lakini wewe zunguka nje, tafutia Tanzania masoko na namna ya kuiunganisha kibiashara. Kama huwezi kushona suti, tukusaidie kutafuta suti nzuri uweze kuzunguka. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namheshimu sana Mheshimiwa Mwijage kwa sababu anafahamu na upeo wake ni mkubwa sana na toka amekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, tunaona anavyohangaika, sasa hiyo sound ipige mpaka nje, isiishie hapa peke yake. Msaidie Mheshimiwa Rais, kila siku anazungumza, ninyi wasaidizi wake msipomsaidia itakuwa ni mbio ya mtu mmoja. Hawezi kupiga ngoma mwenyewe akacheza mwenyewe, lazima Mawaziri mumsaidie Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani ifike mahali Watanzania sasa tumsaidie Mheshimiwa Rais zaidi. Kila wakati unaona anavyolia, anavyohangaika, ninyi mnasema kama mlivyoagizwa, sasa mjiongeze zaidi ya hapo. Nami naomba sana kupitia hotuba hii ya bajeti, kwa kweli ningependa sana fungu la bajeti ya Wizara hii tuliongeze. Tufanye kila namna na Mheshimiwa Mpango najua wewe ndiyo unajaribu kumgawa huyu sungura mdogo, lakini tuwe na priority sectors na ministries kwamba tukiweka hela hapa itazaa na kusaidia Watanzania zaidi. Tufike mahali tufikirie zaidi, let’s think big, tusifikirie kidogo kidogo, tufikirie zaidi kwa mustakabali wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Wizara ya Fedha, najua kuna changamoto kubwa sana za kimapato, lakini tujaribu kugawa resources kulingana na mahitaji halisi ya kila Wizara. Wizara hii inatakiwa ipate fedha za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli ya Cotton to Cloth lazima ndiyo iwe wimbo wa Mheshimiwa Mwijage wa siku zote. Naomba katika sounds zake tutamuelewa tu kama kweli atatimiza azma hii. Hii inakuwa record yake kama Waziri ambaye ameanzisha mbio za Cotton to Cloth. Naomba sana viwanda vyetu hapa ndani tuzidi kuvilinda na wanaowekeza hapa ndani tuwasaidie, tuondoe urasimu wa uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TIC iwasaidie. Siku hizi hakuna tax holiday, kuna tax incentives, lakini kuna conflicts. Mtu anakuwa na cheti cha TIC lakini watu wa TRA baadhi ya vitu hawavikubali, tufike mahali tu-harmonize. Haiwezekani mwekezaji anakuja hapa anazungushwa. Tunapata wawekezaji wanakuja hapa Tanzania kupata kibali tu hapa cha kujenga kiwanda au kufanya shughuli hapa, anazungushwa, wengine wanahama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona kuna watu walikuja hapa tukawazungusha wakaenda nchi jirani, wameanzisha viwanda vikubwa vya magari na vingine. Naomba tuache urasimu. Kama tunataka tuisaidie nchi hii Mheshimiwa Mwijage, Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango na wadau wengine wanaohusika tuondoe urasimu kwa watu wanaokuja kuwekeza hapa Tanzania. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumeisaidia nchi yetu kuweza kukuza uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, Mikoa ya Kanda ya Ziwa inategemea sana kilimo, uvuvi na mifugo. Sasa wakulima wanalia, wavuvi wanalia na wafugaji wanalia. Sasa naomba tutoke kule, mtusaidie namna ya kufanya coordination na hasa viwanda hivi viweze kufanikiwa zaidi. Tukifufua viwanda itasaidia kuweka ajira hata kwa vijana. Vijana wengi wako mtaani hawana kazi, tuwasaidie kupitia viwanda. Naomba kuwe na sera mahsusi ya kuwawezesha Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu South Africa walikuwa wana sera inayosema ‘Black Economic Empowerment’ na sisi Watanzania tuwe na Tanzania Economic Empowerment, tuwawezeshe Watanzania. Leo hii Mtanzania ukienda hata kukopa hela unaonekana kama nyanya chungu au pilipili hoho, unaonekana kama mtu wa ajabu tu. Naomba Watanzania wapewe nafasi. Kama mtu anawekeza, apewe nafasi kadri anavyoweza kuwekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Watanzania tuachane na mawazo ambayo ni ya kizamani, tuangalie dunia inavyokwenda sasa hivi. Wawekezaji wanabembelezwa, akishaondoka kuja kumpata inakuwa ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema kwamba Mheshimiwa Mwijage kaza buti. Punguza maneno kidogo tuone kazi zaidi na vitendo. Maana yake tukikutana mtaani hapo, unauliza unataka kiwanda? Kama unacho mfukoni, Mheshimiwa Mwijage acha style za namna hiyo, hebu kuwa serious kidogo. Maneno yako yaakisi kile unakifanya, nina imani una wasaidizi wazuri kwenye Wizara yako, fanyeni kazi kama Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, nami napenda nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia katika Hotuba hii ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Awali ya yote, napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Hasna Mwilima baada ya kupata ushindi usiokuwa na shaka na Mahakama imetenda haki. Hii imeonesha jinsi ambavyo kwa kweli, kesi nyingi zinafunguliwa hazina mashiko yoyote ndiyo maana Sheria inaposimama CCM inachanua.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, najua hujasikia na wala hukuona kwa sababu, Wagogo mna sifa ya kutokuona na kusikia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba nijielekeze kwa michango ya wenzangu, wamesema mambo mazuri, wakati mwingine ushauri kama huu lazima Serikali iusikilize. Ushauri ambao unakuwa na tija, ushauri ambao unakuwa na mwelekeo wa kujenga Serikali yetu na nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, niwatoe hofu ndugu zangu wanaposema yatumbuliwe majibu sijui wapi! MV Dar-es-Salaam na kadhalika. Jamani, msubiri! Mbona mnakuwa na haraka! Mheshimiwa Rais ana dhamira ya dhati ya kuweza kusafisha Serikali yake na kuunda nchi hii ili iweze kuwatumikia Watanzania wote, kwa hiyo, msiwe na haraka, kila kitu kitakwenda hatua kwa hatua. Haiwezekani leo hii ukaanza kutembea na ukaanza kukimbia! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini katika Hotuba hii naona Mheshimiwa Waziri hajazungumzia suala la mikoa mipya na wilaya mpya, kwa sababu, wilaya hizi na mikoa mipya ina miundombinu ambayo kwa kweli, ni kama haipo. Sijaona kwenye bajeti mkakati mahususi kwamba, ni kwa vipi barabara hizi zitaimarishwa ili kuifanya mikoa hii na wilaya hizi ziweze kufanya kazi vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Simiyu hata kwenye Hotuba haujaunganishwa na barabara ya kwenda Singida wala Arusha! Ningeomba katika Hotuba hii Mheshimiwa Waziri, hebu tuainishie kwamba, hata usanifu au upembuzi yakinifu ni lini utafanyika kuiunganisha Simiyu na Singida? Leo hii kuna barabara, lakini haijatajwa Mheshimiwa Waziri, ningeomba sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika barabara ya kutoka Maswa kwenda Bariadi, kilometa 50, hata hazijatajwa Mheshimiwa Waziri hapa, lakini barabara kutoka Maswa kwenda Mwigumbi inawekewa lami na Mkandarasi yupo! Sasa ni kitu cha kushangaza, unaanza kujenga unaacha kipara katikati! Tunafanyaje kazi namna hii? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba sana Mheshimiwa Waziri katika kuhitimisha hotuba yake, ningependa kusikia mkakati kwamba, zile kilometa 50 za kutoka Maswa kwenda Bariadi, Makao Makuu ya Mkoa. Sisi watu wa Simiyu tuliamua wenyewe kwamba, Makao Makuu yawe Bariadi tena kwenye RCC na Mikutano yote ya hadhara, wananchi wakaunga mkono na hatuna ubishi na hilo. Kwa hiyo, ningeomba sana hili liweze kuzungumzwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kingine tunataka kuimarisha uchumi wetu. Hivi unaimarisha vipi uchumi kama Dar-es-Salaam Bandari yenyewe imefungamana? Hata namna ya kusafiri kutoka nje ya Dar-es-Salaam haiwezekani! Magari, mlundikano na hata namna ya kupenyeza mizigo inakuwa ni tatizo! Tumepata wawekezaji wako tayari kuwekeza zaidi ya Dola milioni 200 kujenga Bandari Kavu pale katika Kijiji cha Soga, Kibaha.
Mheshimiwa Spika, leo ni miaka miwili na nusu, wanakwenda, wanarudi, Serikali imeshindwa kutoa maamuzi. Hivi kwa nini Mheshimiwa Waziri akiwa mwenye dhamana hii asione kwamba leo Mheshimiwa Rais anatafuta wawekezaji, wawekeze katika nchi hii na Dar es Salaam aweze kuifungua, haya malori ya mizigo hayapaswi kuingia Dar es Salaam, yakwamie huku bandari kavu.
Mheshimiwa Spika, hata barabara Waheshimiwa wamezungumza kwamba barabara ya Chalinze kuelekea Dar es salaam imekuwa kama chapati, ni kwa sababu gani? Kwa sababu mizigo mikubwa inatokea sehemu moja inapita sehemu moja. Lazima tuziokoe barabara zetu, ningeomba sana Mheshimiwa Waziri anapohitimisha mjadala huu anipe maelezo ni kwa nini tunachelea kupata wawekezaji ambao wako tayari. Kama ni suala la kuzungumza mnaweka terms and condition, mnakubaliana ili tuweze kuifungua Dar es Salaam, mizigo isianzie Bandari ya Dar es Salaam, mizigo ianzie mahali ambapo kuna dry port na tuweze kuokoa uchakavu wa barabara zetu. Katika hili ningeomba sana Mheshimiwa Waziri atupatie majibu.
Mheshimiwa Spika, kingine, unapokuwa na TRL halafu mwenye assets ni RAHCO, hivi inawezekana namna gani? TRL ha-own any asset zaidi ya zile TRL commutive peke yake. Sasa anakuwa na uwezo gani hata wa kukopa? Hawezi kukopesheka huyu, lakini huyu mwenye RAHCO yeye ndiye mwenye mtandao wote, lakini hana uwezo wa kufanya kazi.
Mheshimiwa Spika, ningeomba Mheshimiwa Waziri, suala la Reli na RAHCO aunganishe, aache reli asimamie assets zote zile aweze ku-transact vizuri, aweze kukopesheka na tuweze kuona reli. Naomba sana hii ndiyo njia pekee inayoweza kufufua uchumi wetu, tunaimba uchumi hatuwezi kufufua uchumi wetu kama hatuwezi kuwa na fikra za namna hii na naomba majibu ya subiri, tuachane nayo. Mheshimiwa Rais anasema kwamba, hapa ni Kazi tu, naomba na nyie Waheshimiwa Mawaziri sasa muwe hapa kazi tu, mambo ya kuchelewa kufanya maamuzi tuachane na biashara hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakuja katika suala la uwanja wa ndege wa Mwanza, uwanja wa ndege wa Mwanza una kila sababu za kiuchumi, kimaendeleo na hata za Kikanda. Ukisimamia uwanja wa ndege wa Mwanza zaidi ya mikoa 10 umeihusisha na nchi jirani. Naomba upewe kipaumbele, uwanja huu uweze kukamilika, uwe uwanja wenye hadhi ya Kimataifa ili tuweze kuifungua Kanda ya Ziwa na Mikoa pamoja na nchi jirani kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, hii tunazungumzia kuongeza Pato la Taifa. Ukifungua uwanja wa ndege wa Mwanza ukawa wa Kimataifa, ukawa Serengeti International Airport, tayari ile Serengeti corridor yote umeifungua, tayari umeweza kuvutia wawekezaji, watalii na ndiyo maana uchumi ambao tunauhitaji leo kutoka Mwanza kwenda Entebbe ni dakika 30, Kigali dakika 45, Kinshansa masaa matatu, lakini ukitokea Arusha, Dar es Salaam ni mbali zaidi. Kwa sababu hakuna ndege inayotoka Mwanza kwenda huko kwenye nchi nilizozitaja hizi, naomba sana Waziri anapohitimisha mjadala huu atuambie ni lini uwanja wa ndege wa Mwanza sasa utakamilishwa kwa kiwango cha Kimataifa.
Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Busega, Mheshimiwa Rais alitoa ahadi, barabara ya Dutwa-Ngasamo-Nyashimo ni kilometa 46, alisema itajengwa kwa kiwango cha lami. Naomba nimkumbushe Mheshimiwa Waziri, kwamba barabara hii sasa iwekwe kwenye ahadi za Mheshimiwa Rais, aliahidi kwamba itajengwa kiwango cha lami na kwa sababu gani?
Mheshimiwa Spika, barabara ile ilikuwa barabara ya mkoa lakini ina-link barabara mbili za TANROAD. Kwa hiyo, ina maana kwamba inaelemewa na uzito wa mizigo ya magari yanayopita pale, kwa hiyo, automatically lazima ipandishwe hadhi iwekwe kwenye kiwango cha TANROADS, barabara kuu.
Mheshimiwa Spika, vilevile kuna kipande cha Mkula, pale Mkula ndiyo mzungumzaji anapotoka. Mheshimiwa Rais alitoa zawadi akasema kwamba kwa sababu barabara imepita pembeni na ule Mji wa Mkula ambapo anatoka mzungumzaji na wenyewe uwekwe lami, kilometa 1.45, alitoa ahadi hiyo. Naomba Mheshimiwa Waziri anapohitimisha aniambie kama ahadi hii ameshairekodi vilevile.
Mheshimiwa Spika, cha mwisho, ni namna ya kuboresha usafiri majini. Kweli wenzetu wa Mkoa wa Kagera, naomba nizungumze, ahadi ya meli imekuwepo kwa muda mrefu, lazima tufike mahali Serikali i-respond.
Haiwezekani tukarudia matukio kama mwaka1996 kwa sababu ya uchakavu wa meli. Leo hii MV Victoria imeshachakaa hakuna usafiri reliable kati ya Mwanza na mikoa jirani kama Mkoa wa Kagera. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nina imani wenzangu wa Kanda ya Mwanza…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Maliasili na Utalii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kusema kwamba naunga mkono hotuba hii ya bajeti. Mheshimiwa Profesa Maghembe anahitaji apate fedha akafanye kazi. Pamoja na yote hayo, kuna changamoto nyingi sana ambazo ningeomba leo Mheshimiwa Waziri anisikilize. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lililopo sasa hivi ni tatizo la wafugaji na hifadhi za akiba au mapori ya akiba yanayomilikiwa na TANAPA. Tunapoangalia sasa hivi tunaona kwa udogo wake lakini naona kuna mfukuto mkubwa sana unaweza kujitokeza na ukaleta matatizo ya kijamii katika nchi yetu. Leo hii mfugaji hathaminiwi.
Mheshimiwa Naibu Spika, inasikitisha sana wafugaji wanapoingiza mifugo kwenye pori, ni kinyume cha sheria tunafahamu, lakini kwa sababu mazingira jinsi yalivyo hatujaweza kujenga utaratibu mzuri na mahusiano mazuri kati ya wafugaji, wakulima na hifadhi zetu za Taifa. Tunajua kwamba sheria inakataza na Mheshimiwa anasimamia kwenye sheria, lakini bado kuna tatizo kubwa kwamba ni namna gani tuweke matumizi bora ya ardhi ili mfugaji huyu naye aone kwamba anathaminiwa na anapewa nafasi katika nchi yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna mahali katika nchi hii unaweza ukapuuza wafugaji, haiwezekani! Lazima wapewe nafasi yao na lazima waoneshwe ufugaji bora na wa kisasa au ufugaji ambao ni endelevu. Leo hii ardhi haiongezeki lakini watu wanaongezeka na mifugo inaongezeka. Mara nyingi tusipokuwa wabunifu na naomba Mheshimiwa Waziri anapokuwa anahitimisha hotuba yake hii hebu atuambie katika Wizara yake amejipanga vipi kuweka mkakati kuona kwamba, hawa wafugaji wanapewa stahiki yao, wanaelimishwa, wanasaidiwa namna ya kufuga vizuri lakini pia waboreshe mazao ya mifugo yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii haiwezi kutokea hivi hivi kama Serikali haiweki mkakati madhubuti. Kwenye bajeti hii Mheshimiwa Waziri amesema lakini hajagusia namna gani anaweza kumsaidia mfugaji. Ameangalia zaidi sheria za kulinda hifadhi za Taifa, tunapenda ziwepo lakini bado kuna umuhimu wa kumsaidia mfugaji ili naye aweze kuona ubora na faida ya kufuga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hili lipo katika maeneo ya Kijeleshi. Mheshimiwa Waziri Mkuu alivyokuja katika ziara ya Mkoa wa Simiyu alikuta matatizo katika Wilaya za Busega, Bariadi, Itilima na Meatu. Ina maana ukanda mzima wote wa Simiyu una mgogoro mkubwa sana na tusipotafuta ufumbuzi wa haraka ni tatizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, cha ajabu baadhi ya askari wa wanyamapori si waadilifu na si waaminifu kwani wanawatesa wafugaji hawa, wanatesa mifugo hii. Mheshimiwa Waziri alitoa tamko wakati nauliza swali hapa Bungeni alisaidia mifugo 6,000 iliyokuwa imefungiwa porini kwa siku tatu na wanaomba rushwa, wanaomba hela na wakipewa hela hazifiki zinapotakiwa kwenda, hazikatiwi risiti yoyote ile. Namwomba Mheshimiwa Waziri pamoja na watu wake hili suala likemee kwa nguvu zote na naomba tupate ufumbuzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hiyo haitoshi suala hili ni mtambuka, lazima Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Ardhi, Waziri wa Kilimo, Chakula na Mifugo na Waziri wa Maliasili washiriki kikamilifu. Tusipopata solution itatupa shida sana huko tunapoelekea. Leo wafugaji wanagombana na wakulima, wanagombana na hifadhi, tutafika wapi? Namwomba sana Mheshimiwa Waziri tusaidie katika hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu suala zima la kudorora kwa sekta ya utalii. Tunajua uchumi wa dunia umebadilika sana, lakini napenda kuona Mheshimiwa Waziri anakuja na mkakati. Biashara ya utalii inazidi kudorora lakini ukiangalia biashara ya utalii imekuwa ikiingiza mapato makubwa sana katika nchi hii. Leo hii mahoteli hayana watu, hayana biashara, migahawa haina biashara, watalii hawaji na bado hizi gharama zingine za kuendesha utalii ni kubwa mno.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachomwomba Mheshimiwa Waziri hebu ajaribu kutusaidia kuja na package namna gani ya kuweza kufufua suala zima la utalii katika nchi yetu. Tusione kwamba watalii wanakuja tunafurahia, lakini tuone wanakuja na kutuma fedha ili ibaki hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo napenda kuzungumzia ni suala zima la geti ya Ndabaga ambayo ndiyo kielelezo na kioo cha Western Corridor upande wa Serengeti, lakini ukifika pale lile geti hali-reflect kwamba unaingia kwenye hifadhi kubwa ya Serengeti, limechakaa, liko hovyo hovyo, halina ukarabati wowote ule. Naomba haya mapokezi yaweze kuboreshwa ili kusudi hata mtalii anapokuja aone kwamba nimeingia kwenye kioo cha hifadhi kubwa hapa duniani, naomba Waziri alizingatie hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliwahi kumgusia Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, nikamwambia tujitahidi kuboresha kwa sababu wanasema reception counts before somebody enters into the house, kwa maana kwamba mapokezi ya nyumba, unapofika pale mbele ya uso wa nyumba ndiyo kielelezo kwamba nyumba yako iko vipi kwa ndani. Naomba sana hilo tuweze kulifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine ni suala zima la Hifadhi ya Sayaka, ni pori la akiba la zamani. Mheshimiwa Kiswaga aliwahi kuuliza hapa swali, ile hifadhi haipo, hakuna miti, hakuna nini, huwezi kusema ni hifadhi, wananchi wanalima, mazao yanakatwa eti ni hifadhi. Naomba jamani unyanyasaji wa namna hii tuachane nao. Namwomba Mheshimiwa Waziri atume watu wake waende kwenye hifadhi ya Sayaka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Hifadhi ya Sayaka iko katika Wilaya tatu za Magu, Bariadi na Busega. Kwa upande wa Busega kuna Kata za Nyaruhande na Badugu na upande wa Magu Kata ya Sayaka. Naomba tuangalie kwa ukaribu kama tunadhani ile ardhi haina maana tena ni bora tukajaribu kuacha sehemu za vyanzo vya maji ili wakulima waweze kufanya kilimo cha kujikimu, watu wapate chakula. Leo watu wanalia wana njaa na mnasema kuna hifadhi ambayo imezuiwa wakati haipo. Kwa hiyo, naomba sana hili suala liweze kuangaliwa vizuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine ni suala la tembo waharibifu. Sisi watu wa Busega na sasa hivi nimepata message nyingi wanalia kwamba tembo wanavamia, wanakula mazao yao na kuharibu mashamba yao na hakuna fidia yoyote ile. Naomba Mheshimiwa Waziri tutafute mkakati mbadala wa kujaribu kuzuia wanyama hawa ambao wanakuja kushambulia binadamu pamoja na mazao yao, matokeo yake wananchi wanalima sana lakini siku ya siku wanakosa faida, hawawezi kuvuna. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la hii Operesheni Tokomeza. Kuna watu walinyanga‟anywa silaha zao wakati wa zoezi hili, silaha zao za jadi na silaha zingine ambazo walikuwa wamezisajili hazijarudishwa mpaka leo. Hivi Mheshimiwa Waziri nini dhana nzima ya kuwasaidia wananchi hawa?
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda Waziri anapohitimisha hotuba yake atuambie ni nini hatma ya watu hawa ambao silaha zao zilichukuliwa wakati wa zoezi hili la Operesheni Tokomeza. Kwanza tujue silaha hizi ziko wapi na zinafanya nini na je, watarudishiwa? Ni vema haya yote Mheshimiwa Waziri akayaweka vizuri na nilishazungumza naye anayafahamu, ili kusudi hawa wananchi waweze kupatiwa haki yao bila kuwa na matatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine utalii lazima tuendelee kuu-embrace vizuri. Leo hii Watanzania unafika airport…
MWENYEKITI: Ahsante.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana nami napenda kuunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu jinsi ambavyo ameweza kuiwasilisha nikiangalia inakidhi kwa kiwango kikubwa mahitaji ya Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni rahisi sana kukosoa lakini naomba niwarejeshe Watanzania na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwamba ukiangalia Serikali ya Awamu ya Tano, kwa muda mfupi imefanya mambo mengi na makubwa kwa Watanzania. Tukikumbuka kwamba Serikali
ya Awamu ya tano imeingia ikirithi madeni ya awamu iliyopita kitu ambacho ukikiangalia na hata katika maelezo ya mpango wa Waziri wa fedha, sasa hivi tunalipia karibu trilioni moja, deni la Taifa kwa kila mwezi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukiangalia kwamba Mheshimiwa Rais pamoja na ubinadamu wake hebu tumpe sifa kwa kile anachokifanya kwa ajili ya Watanzania na tumuunge mkono kama Watanzania na kama Waheshimiwa Wabunge ndani ya Bunge hili. Nchi hii tunaiongoza sisi sote, sitegemei kwamba kwa vile uko upande mmoja wewe ni kusema mabaya siku zote. Hebu tuwajenge Watanzania wajue kwamba chombo hiki kinafanya kazi kama mhimili mmojawapo wa utawala hapa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa ku-register kidogo kwamba kwa kipindi ambacho tumeanza kipindi cha bajeti kuna dosari zimejitokeza lazima tuzikubali. Mhimili huu una heshima yake na heshima yake hii lazima ilindwe na Mhimili wenyewe. Vile vile kwa mujibu wa kanuni za Mabunge ya Jumuiya ya Madola, mimi kama Mwenyekiti wa CPA kwa tawi la Tanzania ningeomba sana Mheshimiwa Spika na kiti chake walinde maslahi ya Bunge hili na mustakabali wa Bunge hili kwa sababu haiwezekani tukawa kila siku tunatupa lawama kwa Serikali, tujiulize sisi Kama mhimili tumefanya nini? Haiwezekani kila siku tunasema Serikali, Serikali, Serikali. Bajeti ya Bunge inawezesha Bunge hili lifanye kazi zake kuisimamia Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi za Mbunge ni tatu; ya kwanza ni kutunga Sheria, ya pili ni kuwawakilisha watu waliomchagua kwenye chombo hiki na tatu ni kusimamia na kuishauri Serikali, haya ndiyo majukumu ya msingi ya Mbunge ndani ya Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kumejitokeza maneno yanazungumza hayatii afya kwa Bunge hili. Tunahitaji kauli za Serikali zitoke zikieleza bayana kama kuna tatizo liainishwe. Sitarajii kwamba yamezungumzwa hapa na Waheshimiwa Wabunge wa pande zote mbili lakini kuna Mawaziri wenye dhamana wamekaa kimya. Huku ni kutokuwajibika ndani ya chombo hiki lazima watoe kauli wawaondolee hofu Watanzania ili wajue kwamba Serikali yao wanachofanya ndicho hicho Watanzania wanachokitaka lakini tunapokaa kimya tunaleta a lot of speculations, watu wanakuwa hawaelewi sisi kama Wabunge tunafanya nini. Wananchi wanalalamika, Wabunge wanalalamika, Serikali inalalamika tunakwenda wapi? Kwa hiyo ningeomba sana hii sintofahamu hii, niiombe Serikali, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama Kiongozi wa Shughuli za Serikali ndani ya Bunge ni vyema ukatusaidia kuondoa sintofahamu hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo nikiangalia kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo mazuri sana na lazima tujenge msingi wa uchumi ili tuweze kuendelea. Huku nyuma ukiangalia watu wanalalamika uchumi umebadilika, mdororo wa uchumi siyo kwa Tanzania peke yake, dunia nzima sasa iko kwenye mdororo wa kiuchumi. Tusipofikiria nje ya box nadhani sisi Watanzania ni kama kisiwa ndani ya dunia haiwezekani lakini yanayofanyika tuyapongeze na tuyape jitihada kubwa zaidi ya kuya-support, angalia miundombinu inayofanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi, ndani ya muda mfupi tumeona uanzishwaji wa ujenzi wa reli ya kati kwa standard gauge, historia, miradi ya maji inayoendelea ni historia. Upande wa elimu nawasikitikia ambao wanabeza kwamba eti hakuna elimu bure, jamani nawasikitikia sana,
labda hawajui wanachosema. Haijatokea katika historia ya nchi hii kwamba kila mwezi zaidi ya bilioni 18.7 zinatengwa kwa ajili ya elimu bure kwa mtoto wa Kitanzania. Haya tunapaswa kuyapongeza na Mheshimiwa Rais ukiangalia anachokifanya na naomba Watanzania tujue kwamba dhamira yake ni nyeupe, dhamira yake ni kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania, tumpeni support hii tusimdiscourage.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sijaona kiongozi, mimi ni mgeni ndani ya Bunge lakini ni mwenyeji kidogo. Kazi inayofanyika sasa hivi ni kazi nzuri sana lakini kuna vitu vya kushauriana. Mfano; katika suala zima la kiuchumi, kweli fedha ndani ya uchumi imepungua, ni suala la Waziri wa
Fedha. Hii ni issue ya Micro-economics, mambo ya Monetary Policy na mambo ya Fiscal Policy atusaidie namna gani ya kurudisha fedha katika mzunguko na leo nimesikia kwamba Benki Kuu wameamua kushusha riba ile ya kuwekeza unajua kuna Central Mineral Reserves ambayo ni asilimia 10 ya Mabenki kuwekeza na Benki Kuu wameshusha mpaka asilimia nane. Hii italeta msukumo wa fedha ndani ya mzunguko wa uchumi, nakushukuru Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa kuchukua Monetary Policy ya namna hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukumbuke kwamba jamani tunasafiri kwenye ngalawa moja. Sisi Wabunge bila kujali vyama vyetu nchi hii ni ya kwetu sote, uchumi huu ni wa kwetu wote tufanye kazi kwa pamoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia, naipongeza Serikali. Huko Busega mimi nasema kwamba nina mradi wa maji mkubwa umeshaanza kutekelezwa, sasa niseme nini zaidi ya hili jamani. Umeme wa REA keshokutwa tunaenda kuzindua, mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa nini niikosoe kwa kitu ambacho naona kuna faida kwa Watanzania? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama haitoshi leo hii watoto wameongezeka katika kusajiliwa darasa la kwanza ni historia katika nchi hii. Hivi wewe unayelalamika kwamba Serikali haijafanya kitu unataka ikufanyie nini? Ikuletee Kitanda nyumbani kwako?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, napenda niungane na wenzangu wote kwanza kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Naibu Waziri wa Fedha, pamoja na timu yote ambayo wameandaa Mpango huu vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yawezekana hapa tuna ongea lugha ambayo haieleweki tu, lakini Watanzania sasa wanaelewa, hata Mheshimiwa ambaye amemaliza kuzungumza sasa hivi anasema kwamba eti kwamba tunaua demokrasia, demokrasia ni historia katika nchi yoyote ile, Watanzania sasa hivi naomba niwapeleke kwa statistics.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia mwaka 2015/2016 Uwekezaji kwa wananchi ilikuwa ni zaidi ya trilioni 29.5 .

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016/2017 ukafika trilioni 48.5, 2017/2018 trilioni 55.17, na sasa hivi hadi Juni 2019 ni trilioni 59. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii maana yake nini, translation yake Mheshimiwa ambaye alikuwa anazungumza hapa ni kwamba Watanzania sasa wameanza kuelewa demokrasia ni maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Watanzania wameelewa kwamba kupitia maendeleo haya sasa walichagua Serikali halali ya chama cha halali na ndiyo maana sasa hivi hata wagombea wengi hawajajitokeza kwa sababu hiyo. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Eehhe!

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua tuseme kitu ambacho Watanzania wanataka, hatutaki maneno na porojo, tunataka translation ya uchumi katika maisha ya Mtanzania, na sasa hivi nchi inavyokwenda chini Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ndani ya miaka minne, tumeona mambo mengi yamefanyika na ndiyo watu walikuwa wanahitaji hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo, mnaposema kwamba hakuna demokrasia, jamani, hivi demokrasia maana yake nini? Demokrasia ni kwa ajili ya watu, ni kwa ajili ya watu na kwa mahitaji ya watu, sasa leo Watanzania wameridhika na maendeleo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini, tumesema ujenzi wa misingi ya uchumi. (Makofi)

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MBUNGE FULANI: Taarifa ya nini wewe….

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Chegeni kuna taarifa. Mheshimiwa Frank Mwakajoka.

T A A R I F A

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpa taarifa mzungumzaji anasema wananchi wameridhika na ndiyo maana hawajajitokeza, lakini tunataka tumkumbushe tu kwamba sisi tumesimamisha vitongoji vyote, Mitaa yote na Vijiji vyote nchi nzima, lakini pia hatutaki demokrasia anayosema kama ile ambayo walikuwa wananyang’anyana matokea na Mheshimiwa Kamani. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji demokrasia ya haki ambayo Mtanzania anataka kwenda kupiga kura, ahsante. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Chegeni unaipokea taarifa hiyo?

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naona siipokei. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu nazungumzia hapa ni maendeleo ya Watanzania. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba leo hii, kama umewekeza kwa kiwango hicho, maana yake ni kwamba Watanzania walichokitamani wanakipata, leo ukizungumzia suala la maendeleo, tunazungumzia katika Mpango huu kwamba lazima tujenge misingi ya uchumi wa viwanda, maana yake nini, maana yake kwamba tujielekeze Watanzania sasa kumboresha Mtanzania na aweze kufikia kiwango cha kujenga uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tupunguze porojo na maneno, Watanzania tumeongea sana, miaka nenda rudi, lakini ndani ya minne, tumefanya mambo makubwa sana, ambayo kila mmoja ana historia nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ninyi Wabunge wote, pamoja na mimi tukienda Majimboni kwetu tunaona miundombinu iliyopo, hii ya Afya, Elimu, Maji, Barabara na vyote vile, ni kwa sababu gani kumekuwa na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mipango ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wananchi wanachagua nini, wanachagua maendeleo, hawachagui maneno, Watanzania wanachagua maendeleo, sasa mnapoanza kulalamika kwamba hakuna demokrasia, nawashangaa wakati mwingine, hebu muanzie nyumbani kwenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mna demokrasia gani? Kwa sababu katika baadhi ya vyama hapa hakuna demokrasia ndani ya vyama vyenu, lakini hamlalamiki, sasa niseme kwamba hebu tuji-focus kwenye Mpango wa maendeleo ambao una tija zaidi kwa Watanzania.

MBUNGE FULANI: Una demokrasia!

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango huu ukiangalia mwaka huu peke yake wa fedha tumetenga asilimia 37 ya Bajeti yote kwa shughuli za maendeleo, hao ni Watanzania wanataka hayo, leo umepanga trilioni 12.2 kwa ajili ya Miradi ya maendeleo, na hii ni kwa Watanzania wote bila kujali wa chama gani, na maendeleo hayana chama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu-translate ndoto ya Mheshimiwa Rais na hii naomba Watendaji na Wasaidizi wote, ndoto ya Mheshimiwa Rais kutokana na Watanzania sasa wanapata maisha bora, wanapata maendeleo ya kiuchumi, wanasonga mbele, haya yote utayafanya ikiwa sisi sote tutaenda katika mwendo ule ambao Mheshimiwa Rais anautazama, na mimi niseme kwamba lazima tufike Watanzania tujifunze tufanye namna hiyo, lakini vilevile Miradi ya Mikakati ambayo leo Watanzania tunaifanya, tumeona Miradi mbalimbali haijafanyika, lakini tumeanzisha Miradi mikubwa ambayo hatukuwa nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na Mashirika mengi ya Umma, tuliweza, na mengine yalikufa, mengine hayakufanya vizuri, leo hii kupitia Wizara ya fedha, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na Kamati ya Uwekezaji tumeweka vigezo, KPI ili kusudi uweze kupima mwenendo wa kila Shirika na Taasisi ya Serikali aidha inatoa huduma au inafanya biashara, na lengo lake ni kwamba tuongeze mapato katika mapato yasiyotokana na Kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kabisa kwamba Watanzania tukiimba wimbo mmoja tutafika safari yetu tunayoitaka, lakini tukienda kwa safari hii ambayo kila mmoja anataka aimbe anavyotaka mwenyewe tutashindwa kufika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tuangalie, naomba tuangalie kwamba tunapaswa tujenge kesho, kesho iliyo bora kwa Watanzania, unaijengaje kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kuijenga kupitia Miradi ambayo lazima Watanzania tuisimamie, lakini katika Mpango huu naomba tu Mheshimiwa Waziri wa Fedha naomba tujipange kidogo, hasa kwa Wakulima, Mkulima analima zao lake akijua kwamba akishavuna aweze kuuza, na ndiyo maana ya kuweka mnyororo wa thamani, lakini vilevile kumfanya Mkulima apate tija na Kilimo chake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mkulima anapolima na ningeomba sana liingie hili katika Mpango unaokuja, Mkulima anapolima awe na hakika ya kupata bei ya mazao yake ili hii Mkulima imtie moyo wa kuweza kuzalisha zaidi na tuongeze tija katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mkulima wa pamba ameuza pamba toka mwezi wa tano mpaka leo hii hajalipwa pesa yake, halafu unataka mwaka aanze kufanya Kilimo tena kwa ajili ya mwaka kesho, hii si dalili njema, ninaomba sana wasimamizi ndani ya Serikali lisimamieni hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kuna suala la soko huria lakini kama Serikali lazima itoe guarantee kwa Mkulima huyu au mazao yote, iwe ni Pamba, Korosho, Katani, Chai na mazao mengine yote ili Mkulima apate tija kile ambacho anataka kukizalisha, lakini pili Viwanda hivi vitajiendeleza namna gani. Lazima na guarantee ya mazao yanayotokana na Kilimo chetu, lazima tufungamanishe sasa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo lazima tulifanye kwa nguvu zote kwamba sasa hivi Mtanzania yule yule afungamanishwe na maendeleo ili aweze kupata maisha ambayo tunayohitaji, leo hii mkulima tumemsaidia sana kumwekea miundombinu ya barabara, umeme, maji, upande wa afya, sekta ya afya, upande wa elimu, Serikali inatoa fedha nyingi kila mwaka, lakini yote haya sasa lazima yasimamiwe vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, mwanzoni nilikuwa sikuelewi elewi, lakini nimeanza kwamba sasa kumbe wewe ni msimamizi mzuri sana wa raslimali za Watanzania na ni mzalendo, na hata Katibu Mkuu wako wa Fedha na Naibu wa Waziri wako kweli mnafanya ya kizalendo. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mwambie shikamoo…

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, na ninaambiwa hapa niseme shikamoo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha, nakwambia hapa niseme shikamoo Mheshimiwa Waziri wa Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia Ofisi ya Msajili wa Hazina, endelea kuimarisha, inachangia pato lisilotokana na kodi zaidi ya shilingi trilioni moja sasa hivi kwa mwaka. Ninaomba iwe ni ofisi ambayo inapewa kila aina ya support kusudi itekeleze majukumu yake inavyotakiwa.

Mheshmiwa Mwenyekiti, vilevile Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma, yafuate misingi ambayo imewekwa na kufanya hivyo nina imani tutaweza kufufua uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema kwamba Watanzania tunaanza kumwelewa Mheshimiwa Rais, tuendelee kumwelewa. Makandokando mengine haya, naomba Watanzania tupate fursa ya kuyazunguza, lakini kama ni Mpango, tuuzungumzie Mpango kwa malengo na maslahi mapana ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja hii. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI NA MITAJI YA UMMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii niweze kukamilisha hoja ambayo iko hapa Mezani. Kwanza napenda niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge ambao wamechangia kwa maandishi na kwa kuzungumza hapa Bungeni. Nikianza na Mheshimiwa Augustine Vuma, Mheshimiwa Sonia Magogo, Mheshimiwa Halima Mdee, Mheshimiwa Jitu Soni, Mheshimiwa Richard Mbogo, Mheshimiwa Ester Mmasi, Mheshimiwa Esther Matiko, Mheshimiwa Shally Raymond, Waheshimiwa Mawaziri ambao kwa kweli wamechangia na kutoa ufafanuzi mkubwa sana; Mheshimiwa William Lukuvi (Waziri wa Ardhi), Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe (Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mheshimiwa Stanslaus Nyongo (Naibu Waziri wa Madini), Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (Waziri wa Fedha na Mipango) na Mheshimiwa Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda, sitapenda sana kusema kila mmoja alivyosema, nita-wrap up kwa pamoja. Kwanza napenda niseme kwamba Waheshimiwa Wabunge naomba tuelewe tafsiri ya gawio. Ukisema gawio hatuzungumzii ile dividend per se. Tumesema neno gawio kwa maana tumejumuisha vitu vitano humo ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mashirika ambayo yanafanya biashara (commercial entities) wanalipa gawio na hii inakokotolewa baada ya kuwa umeshapata faida na baada ya faida sasa ndiyo unapata gawio lake. Vilevile kuna mchango wa asilimia 15 wa growth turnover ya kila taasisi ambayo inatoa huduma pamoja na wakala. Vilevile tuna fedha asilimia 70 ya redemption excess capital, rejesho la mtaji uliozidi kwa hizi taasisi za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapata asilimia 28 kutokana na mapato ya TTMS, mfumo wa mawasiliano ya simu na vilevile Serikali inapata mapato kutokana na riba ambayo inakopesha kwenye hizi taasisi. Kwa hiyo, kwa ujumla wake ndiyo gawio. Hata Waheshimiwa waliokuwa wanazungumza hapa ni kwa sababu wanajua dividend; wanasema kwa nini tunapata hasara? Wanatoa dividend, hapana. Hoja ni kwamba kila taasisi ya Serikali ambapo Serikali ina hisa pale ndani, imewekeza, kama siyo gawio, itoe mchango kwa Serikali. Ndiyo maana yake hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema maneno hayo, naomba sasa niwashukuru wale wote waliochangia kwa kuzungumza na kwa maandishi. Pia hoja za Taasisi za Umma kutoa gawio kwa Serikali zimezungumzwa na Wabunge wengi humu ndani. Naendelea kusisitiza kwamba Serikali ihakikishe taasisi zote zinazotakiwa kutoa gawio zinafanya hivyo na mashirika yanayotakiwa kuchangia katika Mfuko Mkuu wa Serikali yanatimiza takwa hilo. Kamati inaamini kuwa bajeti ya Serikali inaweza kuendeshwa kwa kutumia mapato yatokanayo na kodi na mapato yasiyotokana na kodi ambayo ndiyo Kamati yangu imekuwa ikisimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la marekebisho ya sheria na kuhusu suala zima la kufanya kazi kwa taasisi ambazo zinakiuka matakwa ya Sheria ya Fedha Na. 16 ya mwaka 2015, viongozi wake waweze kuchukuliwa hatua. Wakikiuka matakwa ya sheria hii, lazima Serikali iwachukulie hatua kikamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ni kuhusu watumishi kukaimu nafasi. Hili limezungumzwa na Waheshimiwa Wabunge wengi. Kwa kweli tungependa kuona kwamba nafasi ambazo zinakaimiwa, Serikali inachukua hatua za makusudi ili kuweza kupata watendaji ambao ni substantive.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la michango, kwa mfano suala la miradi ambayo haijakamilishwa ya National Housing, Mheshimiwa Lukuvi ameelezea vizuri sana, sina haja ya kurudia tena. Nafikiri hata Mheshimiwa Mdee amemwelewa vizuri, kwamba Serikali imeangalia baadhi ya mikataba ambayo ilikuwa na matatizo, ndiyo maana inafanyia utafiti mzuri ili kupata solution ya kudumu ili mashirika yetu yaweze ku-perform inavyotakiwa. Nakushukuru sana Mheshimiwa Lukuvi kwa kutoa ufafanuzi ambao kwa kweli ni wa kina na ninajua kila mmoja ameweza kuelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala la TTCL na hili Mheshimiwa Dkt. Mpango amelizungumzia vizuri; na suala la STAMICO Mheshimiwa Nyongo amelizungumzia vizuri, sina haja ya kurudia tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la sheria kupitwa na wakati, ni kweli sheria nyingi za taasisi hizi toka kuanzishwa kwake zimepitwa na wakati. Kwa hiyo, kuna haja kubwa ya kuanza kupitia mchakato wa sheria hizi ili kuwezesha mazingira yaliyopo yaendane na hitaji la kisheria la sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la madeni, inasikitisha kuona kwamba baadhi ya taasisi za Serikali zinashindwa kulipa madeni yake, na hata ku-collect madeni ambayo inadai. Kwa hiyo, tunatoa msisitizo kwa Serikali ihakikishe kwamba tatizo hili linaondolewa haraka iwezekanavyo ili taasisi zinazotoa huduma ziweze kuendelea na majukumu yake na kuwa na ukwasi wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwepo wa Sera ya Gawio, limezungumzwa hapa na Serikali imeshasikia, tumeshatoa maelekezo kwamba lazima kila taasisi inayofanya biashara lazima iwe na Sera za Gawio. Hiyo imeshakuwa concluded. Hatuna shaka kwamba Serikali itafuatailia na TR ana maelekezo mahususi ya Kamati yangu kwamba lazima kila shirika na taasisi ya Serikali inayopaswa kutoa gawio iwe na Sera ya Gawio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwekezaji katika taasisi ambazo Serikali ina hisa chache; Serikali inatakiwa kufanya tathmini ya kina na kuona namna bora ya kuwekeza katika taasisi ambazo ina umiliki wa hisa chache kwa kuwa uwekezaji huo utaongeza faida kwa Serikali na njia ya gawio na pia njia ya mafanikio mbalimbali wanayopata wananchi wa Tanzania walio katika maeneo ya uzalishaji wa taasisi hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ni kuhusu suala la Ofisi ya TR. Mheshimiwa Dkt. Mpango amefafanua vizuri zaidi, sina haja ya kuirudia, kwamba iwezeshwe kwa maana ya rasilimali fedha na rasilimali watu iweze kufanya kazi yake vizuri pamoja na kuboresha suala zima la TEHAMA katika ofisi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la Star Media Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe amelieleza vizuri sana. Ilikuwa inasikitisha, baada ya Kamati kushindwa kupata taarifa na kuzungumza na hawa watu, lakini baada ya Serikali kuingilia kati, tumeona mafanikio, mpaka wametoa na gawio la shilingi milioni 500, hiyo ni hatua moja wapo. Naamini kabisa kwamba Serikali itaendelea kulifanyia kazi kwa umakini zaidi na kuhakikisha kwamba suala la Star Media na TBC linapatiwa ufumbuzi unaotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ambayo tunaomba Serikali iichukue kwa nguvu zote ni kurejesha fedha za madai ya VAT. Makampuni na taasisi nyingi zinalalamika, Serikali hamrejeshi. Tunaomba sana hili kama Serikali, tuweke mkazo ili tusizidi kuyaumiza mashirika na kampuni ambazo yame-tie up capital katika suala zima la VAT refund.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, kwa nafasi ya pekee, nafikiri hata Waheshimiwa Wabunge wote kwa ujumla mtaungana nami kabisa. Licha ya Mheshimiwa Jenista Mhagama kuzungumza kwamba NSSF imefanya kazi vizuri zaidi; na kwa kweli kama alivyosema shirika limebadilika, mfuko umebadilika sana. Kwa hiyo, nampongeza Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama kwa jitihada ambazo amezifanya katika Mfuko huu wa Hifadhi ya Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia, yote haya ni tisa, kumi tumpongeze sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli. Toka ameingia madarakani umeona kwamba gawio kwa taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma zilikuwa haziji. Leo hii tumeweza kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 1.05, ni historia. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza kama inawezekana tuwe na Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa hatua hiyo. Fedha hizi ni kwa Watanzania, ndiyo maana miradi inaendelea, inafanyika kwa sababu tuna fedha ambayo ilikuwa haipatikani lakini sasa inapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoa maelezo hayo, naomba kutoa hoja ya Kamati. (Makofi)

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia katika hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Awali ya yote napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu…

SPIKA: Sasa Mheshimiwa Mwakajoka amehamia mbele; tunakushukuru Mheshimiwa. (Makofi/ Kicheko)

Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Chegeni endelea.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na nafurahi kumuona rafiki yangu Mheshimiwa Mwakajoka amesogea mbele kwa wito wa Mheshimiwa Mtulia.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kweli mimi nampongeza sana yeye na timu yake na Mawaziri wa Nchi wawili ambao ni Mheshimiwa Jenista Mhagama na Mheshimiwa Angellah Kairuki na Naibu Mawaziri wawili; Mheshimiwa Mavunde na Mheshimiwa Ikupa.

Mheshimiwa Spika, hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu imeangalia mambo mengi kwa upana mzuri sana, na kwa kweli ukiangalia jinsi ambavyo ameweza kuiainisha kwa kuangalia misingi ya bajeti yake, lakini mambo ambayo yamefanyika kama nchi, unaona kabisa kwamba hotuba hii imejikita katika kuelezea Watanzania nini azma ambayo Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli, anayo kwa Watanznaia. Napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Rais pamoja na wasaidizi wake wakiwemo Makamu wa Rais pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu na wale wote wanaomsaidia.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi kuna janga la Corona. Corona hii imekuja kama magonjwa ya mlipuko, lakini magonjwa ya mlipuko yanakuwa na madhara yake kwa upande wa ugonjwa na upande wa uchumi. Napongeza sana jitihada ambazo Mheshimiwa Spika wewe binafsi pamoja na wasaidizi wako katika Bunge hili na Kamati ya Uongozi kwa kufikia katika maamuzi ambayo sasa Bunge tunaendelea na shughuli zetu kama mihimili mingine lakini kwa kuangalia tahadhari zote na kuelimisha Waheshimiwa Wabunge na wananchi namna sahihi ya kujiepusha na maambukizi ya Ugonjwa huu wa Corona.

Mheshimiwa Spika, huo ni upande mmoja, lakini pili najaribu kuangalia kwamba kama Serikali inafurahisha kuona kwamba mkakati wa Serikali daima, na hasa kufuata tamko la Mheshimiwa Rais kuwaambia Watanzania kwamba sasa tuko kwenye vita ya ugonjwa wa Corona, kila mmoja achukue tahadhari. Aliwasihi Watanzania, lakini pili akasema kwamba Watanzania lazima tukubali kwamba, tuko kwenye mapambano hatuwezi kufunga nchi yetu lazima tusonge mbele, uchumi wetu unahitaji kuwa-supported na Watanzania, lakini tuchukue tahadhari.

Mheshimiwa Spika, hili ni jambo ambalo kwa kweli baadhi walibeza na hali inavyokwenda tunaimani kwamba, pamoja na kwamba ni suala la kisayansi lakini kama kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake ni sehemu kubwa sana ya kupata ushidni wa ugonjwa huu wa Corona kwa Tanzania kwa sababu mpaka leo kwa takwimu ambazo tumezipata bado tuko vizuri.

Naomba Mwenyezi Mungu naye atie mkono wake kwa Watanzania wote, tuheshimu maagizo ya Serikali, kila mmoja wetu tutii uamuzi na tuzingatie masharti ambayo yatatufanya sisi tujiepushe na ugonjwa huu.

Mheshimiwa Spika, huo ni upande wa kwanza. Upande wa pili ni wa kiuchumi. Sasa hivi ni lazima tukubali duniani kote mambo ya uchumi yamepangaranyika, kila mahali mambo yamedorora na sisi hatuwezi kuwa exceptional, we are part and parcel.

Mheshimiwa Spika,mimi niombe kupitia Waziri wa Fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu, tuone namna gani nzuri ya kutafuta a rescue package itakayowasaidia Watanzania tuendelee kupambana na janga hili lakini vilevile tukubali namna sahihi ya kuweza kuimarisha uchumi wetu. Tunahitaji kuishi pamoja na kwamba kuna tatizo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii biashara nyingi zimedorora wala siyo siri lakini ni kwa sababu hali yenyewe duniani ime- shut down. Sisi tunaendelea kadiri tunavyoweza, tunaomba sasa kupata support ya Serikali ili sekta ambazo zitakuwa zimeathirika zaidi kuwe na rescue package ya kuweza kusaidia.

Mheshimiwa Spika, leo hii kuna watu ambao wana marejesho yao kila mwezi. Sasa hivi hali ilivyo mbaya watashindwa kurejesha. Nimeona jitihada za Serikali ambazo zinaendelea kufanyika lakini kuna haja ya kuona ni namna gani kuja na mkakati mzuri wa kuwawezesha Watanzania hawa waweze kupata nafasi nzuri ya kuweza kuondokana na tatizi hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali yetu ni tulivu, ni sikivu na yote haya inayafanyia kazi vizuri. Nakumbuka jana nilikutana na Mheshimiwa Mpango akasema Mheshimiwa Mbunge subiri, wala msipige kelele subiri. Akasema, nakuja na mkakati mzuri kwa namna gani kama Serikali tutajaribu kuhimili na kufufua uchumi wetu na kulinda mdororo huu wa uchumi kwa Watanzania wote. Napongeza sana mawazo ya Mheshimiwa Mpango na mawazo ya Serikali ambayo yatakuja hapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala ambalo nilitaka nilizungumzie, tunapambana na Corona lakini kuna magonjwa mengine nyemelezi na magonjwa mengine ambayo yanaendana na tatizo hilo lazima tuyape kipaumbele, tusiyasahau. Kwa sababu Wizara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inasimamia mambo kama haya, ugonjwa wa HIV – UKIMWI, kuna TB na magonjwa mengine lazima yaendelee kupewa kipaumbele kwa sababu na yenyewe ni sehemu mojawapo ya tatizo hili la Corona.

Mheshimiwa Spika, nikimaliza hapo nakuja kwenye suala la uwekezaji. Kwa vile Wizara ya uwekezaji iko chini ya Waziri Mkuu bado kuna tatizo na sintofahamu kubwa sana, namna gani ya kufanya coordination ya Wizara ya Uwekezaji na Wizara nyingine ili iweze kuleta matokeo chanya kwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, leo hii bado kuna kukinzana kati ya TIC - Kituo cha Uwekezaji na TRA. Mwekezaji anapokuja hapa nchini anapata tax incentives kupitia TIC, akienda TRA wanamwambia hapana kuna kodi lazima ulipe. Kwa hiyo, kuna haja ya ku-harmonise mambo kama haya na kupunguza unnecessary delays katika kufanya maamuzi kwa sababu haya yanatusababisha tunapoteza wawekezaji kwa sababu ya ukiritimba ambao hauna sababu wala tija. Kwa hiyo, naomba sana Mheshimiwa Waziri wa Uwekezaji kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu atusaidie ku-harmonise TRA na TIC ili ziweze ku-facilitate uwekezaji katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais kila siku anazungumza lazima tuvutie uwekezaji wa ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, leo hii ukitaka kutengeneza working permit ya mfanyakazi tozo la labor ni dola 1,100 ukipitia TIC; ukienda Immigration ni dola 2,050, kwa hiyo, utatumia dola 3,150 kupata permit ya mfanyakazi hapa nchini, it is too expensive. Mimi nashauri Serikali ijaribu ku-review hizi fees kusudi tuweze kupata wawekezaji wengi na wafanyakazi wengine ambao wana sifa za kufanya kazi hapa nchini ili iweze kuchangia katika uchumi wetu. Uchumi lazima uendeshwe na watu wote, tuchanganye expertise ya ndani na nje.

Mheshimiwa Spika, kingine ninachokiona ni kuhusu maamuzi, tatizo la maauzi bado ni ugonjwa. Mchuchuma na Liganga leo tuna miaka nenda rudi lakini hadithi na ngonjera zilezile, maamuzi hayafanyiki. Naomba kama Serikali tujitahidi sana kufanya maamuzi tusije tuka-frustrate uwekezaji ambao tunauhitaji hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kingine kuna issue ya BRELA. Leo hii ukienda BRELA ukitaka kusajili kampuni wanakambia lazima uwe na NIDA, ukienda NIDA hawatoi vitambulisho. Sasa unashindwa ku-register makampuni na kufungua biashara nyingine nyingi kwa sababu ya NIDA. Nashukuru kwamba Serikali imeweza kuweka utaratibu mzuri sasa kwamba angalau NIDA wataweza kutoa vitambulisho kwa uharaka zaidi. Hii ni hatua moja muhimu ya Serikali kupongezwa; imetambua hilo na ni vema ilisimamie lifanyike kwa uharaka zaidi.

Mheshimiwa Spika, pia vitambulisho vyetu ni vingi mno, tujaribu ku-synchronize vitambulisho. Leo una kitambulisho cha NIDA, Driving License, una sijui cha wapi ni vingi mno. Tujaribu kuwa na kitambulisho ambacho mtu akiwa nacho kimoja kina-cover kumpa information mtu yeyote na mahali popote pale, itasaidia sana.

Mheshimiwa Spika, lakini kingine nachokiona ni suala la returns za BRELA. Sasa hivi ukienda BRELA kama una kampuni ina miaka mingi haijafanya return siku za nyuma unaambiwa ulipe returns za miaka 10 iliyopita…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ni kengele ya pili Mheshimiwa malizia.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, namalizia. La kumalizia ni suala la wakulima wa pamba. Mimi kwangu katika Wilaya ya Busega wakulima wa pamba mpaka leo hii wanadai shilingi milioni 450 hawajalipwa. Hawa watu wameuza pamba toka mwezi Mei na Juni, 2019 mpaka leo hawajalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu amefanya kazi kubwa sana ya kuwaunganisha wanunuzi wa pamba na hawa wakulima na kadhalika lakini bado Mheshimiwa Waziri Mkuu nikuombe chondechonde hawa wakulima wa pamba walipwe ni muhimu sana. Hawa wakulima toka mwezi Juni, 2019 pesa hajalipwa, hata tukisema wazalishe tena mwaka huu afanye vizuri, haiwezekani tunamnyonya mkulima. Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu hili alisimamie. Najua anafanya kazi kubwa sana, aendelee kufanya kazi hiyo vizuri sana.

Mheshimiwa Spika,baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja hii. (Makofi)
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hotuba ya bajeti ya Wizara hii na napongeza sana jitihada ambazo Waziri na timu yake wanafanya katika kutekeleza majukumu yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, Busega ni Wilaya changa sana haina Hospitali ya Wilaya na watendaji wa kada ya afya wenye sifa na kwa mujibu wa mahitaji. Naomba Wizara isaidie kupatikana fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Wilaya zikiwemo wodi, maabara, theatre na miundombinu stahiki ili wananchi waweze kupata huduma ya tiba. Pia tupewe kipaumbele katika suala la upatikanaji wa watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwa kuwa baadhi ya watumishi yaani kada ya Clinical Officers (AMOs et cetera) wana wajibu wa kuwa wasimamizi wakuu wa vituo na zahanati, lakini unakuta kuna Wauguzi kwa ngazi ya shahada (degree) wanafanya kazi chini yao na pia mshahara hulipwa chini ya hao COs. Je, Wizara ina mpango gani wa ku- rationalize hizi kada kuondoa mkanganyiko wa maslahi kwa watumishi hawa? Naomba Wizara ichanganue kada hizi na maslahi stahiki yatolewe kwa watumishi hao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, kwa kuwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na hasa Busega unaweza kuchukua muda mrefu kukamilika; na kwa kuwa uwepo wa DDH husaidia sana kutoa huduma kwa wananchi ndani ya mkataba, Busega tulishaomba Mkula Hospital iwe DDH na Mheshimiwa Waziri alitembelea na kuahidi kutekeleza kauli hiyo ndani ya miezi mitatu ambayo ilishapita muda mrefu. Hivi sasa imesababisha wananchi walioahidiwa na Mheshimiwa Waziri kwenye mkutano wa hadhara kuona ahadi ya Waziri ilikuwa ni uongo. Je, Serikali kwa nini isiharakishe au kusaidia mchakato wa kukamilisha suala hili? Naomba Wizara kupitia kwa Waziri itimize ahadi ambayo imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi hata kama kuna upungufu basi Wizara isaidie mchakato huo ili kuwezesha wananchi wa Busega na wa jirani wapate huduma hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, kwa kuwa Mhula Hospital kuna Chuo cha Nursing, je, Serikali haioni umuhimu wa kukisaidia ili kiweze kupanuliwa na kutoa mafunzo kwa kada hii muhimu na hasa Mkoa wa Simiyu? Naomba Serikali isaidie upatikanaji wa fedha na watumishi watakaoweza kusaidia chuo hiki muhimu na pia Wizara isaidie namna ya kuboresha badala ya kubeza na kutokutoa ushirikiano unaotakiwa. Ikiwa hoja hizi hazipati majibu stahiki nitashawishika kuomba maelezo zaidi yatakayopelekea nikalale na mshahara wa Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, kwa nafasi ya pekee namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuwa karibu na wananchi wa Busega na hasa katika ziara yake wakati wa uzinduzi wa nyumba za watumishi zilizojengwa kwa hisani na Taasisi ya Mheshimiwa Benjamini Mkapa Foundation. Ahadi yake ya kufanya ziara rasmi bado tunaisubiri kwa hamu. Nawapongeza Naibu Waziri, Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara. Tunashukuru pia kwa msaada wa ambulance.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Elimu pamoja na timu yake kwa kuwasilisha hotuba nzuri na yenye kukidhi mahitaji na matakwa halisi ya Watanzania. Naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inayoisha kwa mwaka huu kwa kiwango kikubwa sana imejitahidi kutekelezwa kulingana na uwepo na upatikanaji wa fedha. Pamoja na yote, naomba niongelee elimu bure. Mpango huu umeleta faraja na matokeo chanya kwa mtoto na mzazi wa Tanzania kwani umesaidia kuwepo na ongezeko la watoto wengi kuanza masomo kwa idadi kubwa. Mpango huu uendelee kuboreshwa sambamba na miundombinu yake, vifaa vya kufundishia, motisha na maslahi stahiki kwa walimu na wadau wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa madarasa ya shule za msingi, napongeza sana Serikali kupitia Wizara hii kwa kusaidia ujenzi wa vyumba vya madara ya shule ya msingi Nyamajashi – Lamadi na shule ya msingi Fogo Fogo - Kabita katika Wilaya ya Busega. Msaada huu umefanikisha kupatikana vyumba na vyoo stahiki kwa wanafunzi ambao kwa muda mrefu ilikuwa ni kero na hasa kwa kukosekana kwa miundombinu hii. Naiomba Wizara iendelee kuweka mikakati na kuboresha shule nyingi katika Wilaya ya Busega ambayo ina idadi kubwa sana ya wanafunzi na uhaba wa miundombinu. Nampongeza Mheshimiwa Waziri na namwomba msaada zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uanzishaji high school. Wilaya ya Busega haina high school. Napongeza sana msaada wa Wizara kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuanzisha shule ya A-Level Busega ambayo ni Mkula sekondari. Hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri na niombe tu Wizara ihakikishe masomo kwa wanafunzi watakaochaguliwa yanaanza. Sambamba na shule ya sekondari Mkula, naomba mwaka ujao wa fedha pawepo na mpango wa kuanzisha shule mbili zaidi za A-level kwani idadi kubwa sana ya wanafunzi hawapati fursa ya kuendelea na masomo kwa michepuo mbalimbali. Nashauri pawepo pia na shule maalum ya A-level kwa ajili ya watoto wa kike (wasichana) ambao wamekuwa wakiathiriwa na mila potofu na kunyimwa fursa ya kusoma.

Mheshimiwa Waziri, kuhusu Chuo cha VETA, tumetenga eneo kwa iliyokuwa kambi ya ujenzi wa barabara ya Nyanguge - Musoma ya Sogesca kwa ajili ya uanzishaji wa Chuo cha Mafunzo Stadi kwa Vijana (VETA). Tunaiomba Serikali kukubali kuanzisha chuo hiki kwa kuwa baadhi ya miundombinu ikiwemo karakana, mabweni na madarasa vipo tayari likiwemo na bwalo la chakula. Hii ni bahati nzuri na mpango nafuu licha ya faida pia eneo hili liko kandokando ya Ziwa Victoria, hivyo suala la maji na umeme tayari vipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhitimisha, naamini Mheshimiwa Waziri atanikubalia maombi yangu na kuonyesha utayari wa kuyatekeleza ikiwemo ya yeye mwenyewe kuja na kutembelea Busega.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami napenda nikushukuru sana kunipa nafasi hii ili kuweza kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niungane na msemaji wa kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri pamoja na wataalam wao kwa kuweza kuandaa bajeti hii ambayo wote tumeisikiliza hapa kwa makini sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maliasili na Utalii ni nyeti sana. Nadhani kama Waheshimiwa Wabunge tunatakiwa tuiangalie kama moja ya Wizara ambazo zinaingiza mapato makubwa sana katika uchumi wa nchi yetu. Wizara hii jinsi ilivyo na inavyofanya kazi ina changamoto nyingi sana na hasa ukizingatia suala la utalii kwa mfano ndiyo sura ya nchi ndani na nje ya nchi yetu lakini kuna vitu ambavyo havijakaa sawa. Kwa maana gani? Kwa maana kwamba kunapaswa kuwa na uwiainishaji kati ya wageni wanaoingia nchini na watu walioko hapa nchini, watu wanaokuja kufanya shughuli hapa nchini na sisi Watanzania tulioko hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya yakiunganishwa vizuri na yakifanyika vizuri yatachochea nchi yetu kupata watalii wa kutoka na kuongeza kipato kwa ajili ya matumizi ya Watanzania. Bajeti yetu hii kwa mfano Mheshimiwa Waziri kasema hapa kwamba kwa mwaka 2015/2016, Wizara hii iliweza kuchangia zaidi ya bilioni 1.9 dola za Kimarekani na mwaka huu unaokwisha wa 2016/2017 imechangia zaidi ya dola bilioni mbili, ni hela nyingi sana hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kuna ukiritimba mkubwa sana mtu anapokuja hapa Tanzania anakutana nao. Mtalii anapoingia hata pale airport, watu wa Idara ya Uhamiaji wanavyowapokea wale wageni, lugha wanayoitumia si lugha ambayo inapaswa kutumika kwa kukaribisha wageni. Kuna haja sana Mheshimiwa Waziri wa Utalii, ajaribu kuongea na hizi Idara ikiwezekana washirikiane kwa karibu zaidi na wawape fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali ili wajue thamani ya kumpokea mgeni pale airport na kumpa treatment inayostahili kwa sababu ni mgeni anayekuja kwa ajili ya kujenga nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta hii ina changamoto nyingi, ina tozo kibao, tozo zaidi ya 36. Hizi kodi na tozo hazina afya au tija kwa ajili ya kujenga sekta hii. Kuna haja ya kuangalia namna ya kupunguza hizi tozo na kodi ili kusudi tuweze kupata mapato mengi zaidi kutokana na watu wanaokuja hapa nchini kwa ajili ya shughuli za kitalii au shughuli nyingine mbalimbali. Haya tunayoyasema hatujaanza leo hata mwaka jana tulishauri. Ningeomba sana Wizara ya Fedha na Wizara ya Maliasili na Utalii wajaribu kukaa na kuona kodi na tozo zipi ziweze kuangaliwa upya. Hii itaongeza ufanisi wa kupata mapato makubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ina changamoto moja nyingine kubwa sana. Wizara hii imepelekea wafugaji katika nchi yao sasa kuonekana ni yatima kitu ambacho ni tatizo kubwa sana. Ukiangalia hivi mfugaji anapokwenda akaingiza mifugo ndani ya hifadhi au kwenye msitu na mtu anayekata misitu kwa ajili ya kuchoma mkaa na kadhalika ni nani mharibifu zaidi ya hapa? Kila siku tunaona magunia ya mkaa zaidi ya milioni 50 yanaingia Dar es Salaam ambayo yanatokana na kukata miti ambao ni uharibifu wa mazingira lakini mfugaji anaonekana ndiyo haramu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba wakati Mheshimiwa Waziri anakuja ku-windup hotuba yake tunataka tuone ni namna mfugaji katika nchi hii naye anapewa nafasi na kuthaminiwa. Kwa mfano kule Muleba, Mkuu wa Wilaya anasema kwamba amewapa notice wafugaji wahame, waende wapi hawa ni Watanzania. Pili, ukisema wahame ina maana kwamba waanze kutafutana wewe umetokea wapi, kila mmoja amfukuze mwenzake. Tutajenga situation ambayo siyo nzuri kwa ajili ya nchi yetu na tutaanza kuleta ubaguzi ambao hauna tija yoyote kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana hili suala la mifugo na hifadhi, ndiyo tunahitaji tuwe na hifadhi lakini naomba tuziangalie sheria. Kuna baadhi ya mashamba mengine yalikuwa ya mifugo sasa hayafanyi kazi, kwa nini tusiyakate yale mashamba yakatumika kwa ajili ya wafugaji kufugia mifugo yao na kutoka kwenye hifadhi? Hata hivyo, tujue kwamba idadi ya wananchi inaongezeka kila kukicha lakini ardhi haiongezeki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na hali hiyo ni lazima kuwe na mustakabali sasa wa kitaifa wa kuangalia kwamba tunahitaji kuhifadhi misitu na hifadhi zetu wakati huohuo wananchi nao wanahitaji kutumia mazao ya mifugo, kufuga mifugo na kufanya kilimo chao, vinginevyo tutachochea vurugu ambayo haina tija kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kuwepo na doria dhidi ya ujangili na biashara haramu ya nyara za Serikali. Hii maana yake ni kuwe na vikosi maalum visaidie kulinda hifadhi zetu hizi au maliasili yetu hii. Wenzetu siku hizi wana teknolojia mpaka kutumia zile ndege ambazo haziendeshwi na rubani (drones) na wana mpaka wale mbwa maalum wa kunusa, naomba tuongeze hiyo jitihada ili kusudi tuhifadhi na kulinda maliasili yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tuitangaze Tanzania. Mimi nimefurahi juzi nilipanda ndege ya Bombadier wameweka kwenye ndege air flying magazine wameonesha baadhi ya picha na mahali vilipo na kuutangaza utalii wa nchi yetu, ni kitu kizuri sana. Tunapaswa tutoke pale tulipo, sasa tumepata ndege zetu lakini vilevile suala la kutangaza utalii nje ya nchi ubadilike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Bodi ya Utalii (TTB) ipewe mamlaka na ipewe fedha kwa ajili ya kuendesha utalii nje ya nchi. Haiwezekani Ngorongoro wanaenda kutangaza kivyao, TANAPA kivyao, sijui nani kivyao, haiwezekani wote wanatoka Tanzania hawa. Hii Bodi ingewezeshwa, tena bahati nzuri imepata Mwenyekiti mzuri sana, Advocate Mihayo, ni wakili mzuri anajua vizuri sana haya mambo. Nina imani kabisa kwamba akiwezeshwa na Bodi ikiwezeshwa tutafanya kazi nzuri sana ya kuitangaza nchi yetu nje ya mipaka yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala lingine ambalo lipo na naomba kwenye kitabu chako ukurasa wa 19 umekosea sana, unasema wananchi walindwe na mali zao dhidi ya wanyama waharibifu, tuna tatizo la tembo wanaharibu mazao na mali za binadamu, lakini bado watu hawapati fidia inavyotakiwa. Tunaomba Wizara yako iunde kikosi maalum ambacho kitasaidia kwa ajili ya kuhifadhi na kuwalinda wananchi pamoja na mali zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitabu chako una-refer kwamba Magu wanapata hicho kifuta jasho na kifuta machozi. Magu hawapakani na Hifadhi ya Serengeti isipokuwa ni Wilaya ya Busega, zamani ilikuwa ni sehemu ya Magu. Naomba rekodi za Mheshimiwa Waziri azibadilishe isomeke Busega badala ya Magu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna kuboresha miundombinu inayopakana na hifadhi, nimeshamwomba Mheshimiwa Waziri barabara ya Kijereshi naomba anisaidie waitengeneze kwani inasaidia sana kuongeza idadi ya watalii wanaoingia Serengeti na iko Busega. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri hili uweze kulifanyia kazi ili kusudi sasa tuweze kuimba wimbo mzuri wa kuongeza watalii na kuongeza mapato katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sana Mheshimiwa Waziri kuzingatia sana suala la Ushirikishaji wa Jamii katika Uhifadhi (WMAs)…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hotuba hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nashukuru sana kupata nafasi hii ili niweze kuchangia Hotuba ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Nampongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na timu yake wameandaa hotuba nzuri sana ambayo nadhani imetupa changamoto ya kuijadili hapa ndani. Vilevile ningependa nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, yeye ana jina lake ambalo kule mtaani katika vile viunga vya viwanda tunamuita mzee wa sound, halafu anasema kwamba yeye mke wake anamwita ni handsome boy. Kazi yake ni nzuri sana Mheshimiwa handsome boy, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ningependa kuzungumzia masuala makuu matatu. La kwanza, kuna haja kubwa sana sasa ya kujaribu kuoanisha vizuri sana kazi anayofanya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na kazi ambayo Mheshimiwa Waziri wa Fedha anaifanya, kwa sababu pale ndipo tunapoanzia kutofautiana. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda anafanya kazi kubwa sana ya kupiga debe na kuhakikisha hii philosophy ya uchumi wa viwanda inaanza kwa kasi sana hapa nchini, lakini bado kuna hiccup kubwa sana upande wa Wizara ya Fedha; kwa sababu huyu ataweza tu kuwa na philosophy ya uchumi wa viwanda kama na mambo yote yanayohusu mambo ya kodi na vivutio kwa wawekezaji yanakwenda samabamba. Vinginevyo itakuwa ni wimbo ambao utaendelea kuimbwa na hatutapata majibu ya haraka haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda nimuombe Mheshimiwa Waziri atoe tafsiri zaidi anaposema viwanda, kwa sababu tumekuwa tukichangia hapa tunasema mimi kwangu hakuna kiwanda, viwanda vimesimama sijui magunia na kadhalika. Tafsiri ya kiwanda kutoka kwa industrial economist ni kitu chochote ambacho kinaweza ku- transform bidhaa moja kwenda kuwa bidhaa nyingine inayoweza kutumika. Kama ni mbao kuwa kitu au meza na kadhalika, kama ni kuchanganya dawa basi iweze kutumika kama dawa na kadhalika, from chemicals to drugs.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo katika hali ya kawaida bado tunapata ukakasi kwamba ni namna gani tunazungumzia dhima nzima ya uchumi wa viwanda. Ukiangalia Serikali inajaribu kuweka miundombinu na mazingira ya kumfanya mfanyabiashara au biashara iweze kufanyika hapa nchini.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu kwa miaka mitano iliyopita, Tanzania tumeweza ku-export nje, India bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 1.12, Kenya dola milioni 793, South Africa dola milioni 698, China dola milioni 620, Japan dola milioni 370. Lakini tumeweza ku-import, Saudi Arabia peke yake ni bidhaa za zaidi ya shilingi bilioni 5.6, China shilingi bilioni 2.23, India shilingi bilioni 1.24, Uarabuni shilingi milioni 789 na South Africa shilingi milioni 567. Kwa hiyo, ukiangalia Tanzania tumeweza ku-export lakini tumeingiza zaidi na hii ndiyo changamoto ambayo inaanzia pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia katika sura nzima, maeneo ya msingi lazima tuangalie namna ya kuweza kuongeza uwekezaji utakaoondoa ukiritimba wote na kuongeza ajira na tija kwa Watanzania, bila kufanya hivyo tutaimba wimbo huu hatutafanikiwa kuufikia. Hii nasema kwa sababu kumekuwa na tatizo kubwa sana sasa hivi hasa la wawekezaji. Wenzangu wamesema, nisingependa kurudia kwamba nchi yetu lazima tuweke utaratibu utakaoweza kuwa rafiki kwa wawekezaji kuwekeza hapa nchini. Mtu hawezi kuwekeza hapa nchini kama kuna uncertainties na unpredictable tax regimes, haiwezekani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimi ninachoomba sana katika hili tumsaidie Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, si la kwake peke yake; na Bunge hili tuna jukumu la kuishauri Serikali yetu, kwamba ni namna gani masuala haya yanaweza kuoanishwa na kuhuishwa kwa ajili ya kuchochea uwekezaji hapa nchini. Sisi si kisiwa, Tanzania tuna vivutio vingi sana, tuna maeneo mengi sana ya kuwekeza lakini sisi na wenzetu tuna-compete hivyo lazima tuweke mazingira ambayo yatajenga assurance kwa mwekezaji anapokuja hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tutambue uwepo na ushiriki kamilifu wa sekta binafsi, hili ni suala la msingi sana. Najua tumekuwa na kasumba kwanza kutokutaka kuipenda private sector, lakini Waheshimiwa Wabunge, bila kuipenda private sector na kuipa nafasi ya ushiriki vizuri hatutaweza kutoka hapa tulipo. Acha Serikali iwekeze pale ambapo panatakiwa huduma itolewe na pengine pasipo faida, lakini maeneo ambayo yanahitaji kupata faida tuwekeze zaidi kwa hawa wawekezaji binafsi na tuingie utaratibu wa PPP, huu utasaidia kuipunguzia Serikali mzigo wa kutumia fedha zake katika kuwekeza na matokeo yake tuisaidie private sector iweze kuwekeza zaidi, Serikali inachotakiwa pale ni kuvuna kodi. Mimi naomba sana hili tuweze kuliangalia.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tuangalie mustakabali mzima kwamba Watanzania tunatoka hapa tulipo namna gani, uwekezaji huu unakuwa na tija gani kwa Mtanzania, lazima tupate tija ya uwekezaji huu katika huduma za afya, elimu na kadhalika. Hata hivyo tatizo lililopo sasa hivi ni mitaji, liquidity sasa hivi kwenye economy imekuwa so tight, lending rates zimekuwa kubwa, watu wanashindwa kukopa fedha na kuwekeza. Njia pekee ni ku-attract mitaji kutoka nje ili kusaidia kuwekeza hapa nchini lakini tutafanya vile kama wawekezaji hawa tutawawekea mazingira mazuri ya wao kuwekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa na hadithi ya Mchuchuma na Liganga miaka nenda-rudi. Mheshimiwa Waziri, hebu tusaidie, pale ambapo unadhani kabisa kwamba inakushinda naomba Bunge hili likusaidie ili utusaidie tutoke hapa tulipo tuache kuimba nyimbo na ngonjera za kila wakati. Ukiangalia ufanyaji biashara hapa Tanzania kila kukicha unakuwa ghali zaidi. Kwenye sekta ya utalii peke yake kuna kodi zaidi ya 36, hivi kweli mtu atawekeza kwa kodi hizi 36? Haiwezekani! Mimi sitaki kuzisoma, ni nyingi sana. Kitu ambacho ninaomba sana Serikali yetu ijaribu kuwa sikivu, na hasa Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lililopita niliwahi kusema Mheshimiwa Waziri wa Fedha atusaidie na kusaidia maana yake ni kwamba ajaribu kuwa kiungo na si mtenganishi wa masuala ya uchumi katika nchi. Nina imani kabisa kwamba Watanzania kama tutafuata msingi mzuri wa uwekezaji, tutasonga mbele. Dhima na dhana aliyonayo Mheshimiwa Waziri wa Viwanda ni nzuri, tunamsikia kila mahali anazunguka, hata ukikutana naye ukamwambia Mheshimiwa nataka kiwanda, anakwambia ntakupa kiwanda, anakupa hata matumaini hata kama hana, hiyo inatosha Mheshimiwa Waziri, unatupa matumaini. Hata hivyo ninaomba utuambie hapa vizuri zaidi tafsiri ya viwanda ili tuweze kuelewa kwa sababu unapotuambia viwanda tunawaza viwanda vikubwa tu. Kuna viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, lakini kunakuwa na linkage ambayo inakuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tunasifika kwa kuwa na uchumi unaokuwa pamoja na sera nzuri au tulivu za uchumi. Hizi lazima ziwe translated katika mahitaji ya Watanzania. Level ya umaskini Tanzania bado ipo katika kiwango cha juu na ndiyo maana hata Mheshimiwa Rais anasema sitaki kuona wananchi masikini wanateseka, he is for the poors, lakini sisi tunafanya nini kusaidia kauli mbiu hii.

Mheshimiwa Rais amejitahidi sana na kwa muda mfupi tunaweza kuona kwamba nchi sasa inaanza kusonga mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeanzisha na miradi ambayo ni mikubwa yenye kusimika uchumi wa nchi, kwa sababu bila kuwa na logistics and division systems huwezi ukapanua nchi yako. Lakini sisi kama Tanzania, leo ujenzi wa reli ni mardi mkubwa sana, unahitaji gharama kubwa sana lakini pindi utakapokwisha utakuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuunga mkono hotuba hii, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza hotuba ya bajeti ya Wizara hii na naunga mkono. Sote tunajua upatikanaji wa fedha na kazi nzuri iliyofanyika kwa kipindi hiki kinachoisha cha mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha, Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara hii wamejitahidi kutimiza wajibu wao kikamilifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya Wizara hii iongezwe ili kutoa nafasi shughuli nyingi za upatikanaji na usambazaji wa maji safi na salama ziweze kufanyika. Hivyo, nashauri kuwepo na tozo ya Sh.50 kwa bidhaa ya mafuta ili kuchangia kutunisha Mfuko wa Maji. Wizara na Kamati husika wawasilishe ombi kupitia Kamati ya Bajeti ili hoja ya kutoza kiasi hicho iingizwe kwenye hotuba ya Waziri wa Fedha kama tozo/kodi mpya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri kuwepo mkakati wa kutunza vyanzo vya maji ambalo ndiyo suala la msingi zaidi ili maji kwa matumizi ya wananchi yapatikane. Wizara kupitia bajeti hii iwe na mikakati itakayopelekea suala la uhifadhi wa vyanzo vya maji kutekelezwa nchi nzima na kila Halmashauri iweze kutenga fedha za kutekeleza mkakati huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lambo la maji Lutubiga – Busega. Mheshimiwa Naibu Waziri alitembelea Wilaya ya Busega na kujionea bwawa la maji ambalo liligharimu fedha nyingi ambalo lilichimbwa na Serikali kupitia Wizara hii lakini halina wala halijawahi kutoa maji kwa matumizi ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, bwawa hili limekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Kijiji cha Lutubiga, Kata ya Lutubiga, Wilaya ya Busega ambao wana uhitaji mkubwa sana wa maji na kwamba hawajapata maji licha ya bwawa hilo kuchimbwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia bajeti hii, naiomba Wizara kwanza itume wataalam ili kutathmini hali hiyo na urekebishaji wa bwawa hili uweze kufanyika mara moja. Hii itasaidia kuwapatia wananchi ambao wamekuwa wakiteseka kwa kukosa maji ilhali tayari Serikali imekwishalipa fedha nyingi ambazo makosa tu kidogo ya kitaalam yamepelekea kukosekana kwa maji, hivyo basi, Wizara ichukue hatua stahiki mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

Kwanza, napongeza taarifa zote mbili za Kamati, lakini nina concern mbili za msingi sana; ya kwanza, upande wa migogoro ya wafugaji, wakulima na hifadhi zetu. Naomba Serikali hili iliangalie kwa mtazamo wa hali ya juu sana. Migogoro hii inasababisha maafa, inasababisha matatizo makubwa sana na kila malalamiko ya Wabunge, hapa tunalalamika kila wakati, sasa naomba Serikali itusikilize. Wananchi kule wana matatizo, lakini cha msingi ni kwamba tunaomba kuwe na ushirikishwaji wa wananchi katika kuainisha mipaka hii na wananchi wapewe nafasi ya kuweza kushiriki katika maamuzi haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, suala la mifugo kukamatwa hovyo hovyo, tunaomba Serikali iliangalie sana.

Tunawatia umasikini wananchi wetu. Tunaomba kama ni sheria, basi iweze kuangaliwa upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la uvuvi haramu. Hakuna ambaye anashabikia uvuvi haramu, lakini mtindo unaotumika siyo mzuri, unaumiza wananchi wetu. Leo tuna wananchi wanakuwa maskini; asubuhi tajiri, jioni maskini. Serikali ya CCM haisemi namna hiyo, wala Mheshimiwa Rais hasemi namna hiyo. Tunaomba Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana hii, hebu waonee huruma wananchi hawa, hawa ni Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, alianzisha utaratibu mzuri sana wa BMU. Leo hii wananchi wanalia, wanaililia Serikali yao, Mheshimiwa Waziri upo, tusaidie! Tena unatoka sehemu ya Kanda ya Ziwa, kitu ambacho ni aibu. Sasa wananchi tusemeje? Wabunge tumesema, tunakueleza Mheshimiwa Waziri, hutusikii. Tunaomba utusikie kwa hili kupitia Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuweke azimio, ni namna gani iliyo sahihi zaidi ya kuweza ku-moderate suala zima la uvuvi haramu? Hatupendi, samaki hawana mpaka. Sisi bila kushirikisha nchi ya Kenya na Uganda, tunafanya kazi bure. Zoezi hili lazima liwe shirikishi la wadau wote wa Ziwa Victoria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tena ukienda Mwibara kwa Mheshimiwa Kangi wanalia, ukienda Musoma wanalia, Busega wanalia, Magu wanalia, Geita wanalia, kila mahali wanalia, Kagera wanalia na sisi tulie humu Bungeni? (Makofi)

Mheshimiwa Waziri naomba uwe msikivu, acha kiburi, kuwa msikivu. Sikiliza maneno ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ni nzuri, nina issues za kuzungumza.

Kwanza napenda nipongeze sana miradi ya kimikakati ambayo inafanywa na Wizara hii; kwa mfano barabara, ujenzi wa reli, vivuko pamoja na ndege, ni miradi ya kimkakati na ni ya kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu dakika ni chache naomba niingie moja kwa moja kwenye hoja zifuatazo; kwanza tunahitaji kuwa na viwanja vya ndege ambavyo vya kimkakati vilevile. Uwanja wa Ndege wa Mwanza naomba sana Mheshimiwa Waziri utakapokuwa unajibu hapo utuambie lini jengo la abilia linajengwa Mwanza. Imekuwa ni hadithi ya muda mrefu, lakini bado uwanja wa Mwanza ni uwanja wa mkakati hata kiuchumi. Nakuomba sana tupate majibu kwa sababu hatuwezi tukawa tunaenda tunarudi, tufike mahali tuwe na uamuzi ambao ni sahihi. Kama ni fedha tenga fedha za ndani zianze kujenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Vivyo hivyo uwekaji wa taa za kurukia ndege kwa Uwanja wa Songwe wa Mbeya nao ukamilike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba vilevile kuhusiana na suala la barabara ya Nyanguge - Busega - Mara Border;ukitoka Mwanza mpaka Nyanguge barabara ni nzuri, ukifika border pale ya Mara na Simiyu kwenda mpaka Musoma barabara ni mzuri, kipande cha Nyanguge mpaka Mara Border ni kibovu sana na kila mwaka ukarabati unafanyiake fedha nyingi inatumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachopenda kujua ni kwamba ni lini sasa barabara hii itarekebishwa kwa kiwango ambacho haitakuwa na usumbufu? Kwamba kila mwaka unaona wakandarasi wako barabarani? Inasababisha ajali na ni kipande ambacho ni muhimu sana; kwa hiyo ningepenga sana kujua hilo, pamoja na daraja la pale Simiyu, ukiwa pale Magu lile la chuma, ni barabara ya miaka nenda rudi mpaka leo hii ni single lane, yaani huwezi ukapishana pale na bado ni chakavu naomba lilekebishwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja suala la barabara ya Nyashimo - Ngasamo mpaka Dutwa kwa Mheshimiwa Mwenyekiti Chenge. Barabara hii Mheshimiwa Rais alihaidi kwamba ijengwe kwa kiwango cha lami, mpaka leo sijaona mkakati wowote wa kujenga kiwango cha lami. Nataka kujua Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-wind up ni lini barabara hii ya Nyashimo-Ngasamo-Dutwa itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami? Ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, aliwaahidi wananchi wa Wilaya ya Busega na Wilaya ya Bariadi, tena wakamshangilia sana na kura zikawa nyingi sana. Naomba hili suala tusimwagushe Mheshimiwa Rais. Kauli ya Mheshimiwa Rais ni maelekezo tosha kabisa. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri utakapokuja hapa nataka kujua ni lini ujenzi wa barabara hii utaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la TTCL. Tunazungumza kuhusu kuboresha mashirika yetu, lakini taasisi za Serikali hazitaki kujiunga na mfumo wa kanzidata wa TTCL; Mheshimiwa Waziri umesema ni makampuni 52 tu, kwa nini ni makampuni 52 peke yake? Naomba kampuni zote na taasisi ya Serikali zitimize maelekezo ya Serikali na walipe madeni. Hizi taasisi au mashirika yasipolipa madeni ya Serikai inakuwa tunakwamisha shughuli za uendelezaji wa mashirika haya. Kwa hiyo, nilikuwa naomba sana mashirika haya ya weze kulipa pesa zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia la mwisho kabisa nakupongeza wewe, lakini naomba hivi barabara ya Nyasimo - Ngasamo - Dutwa nipate majibu, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, naomba kumpongeza sana Mheshimiwa Engineer Kamwelwe, Waziri na Naibu Mawaziri kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao. Serikali kupitia ahadi ya Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutengenezwa kwa Barabara ya Nyashumo – Ngasamo – Dutwa, kilomita 45 kwa kiwango cha lami. Huu ni mwaka wa nne, ningependa kujua ni lini ujenzi wa kiwango cha lami utaanza ili kuwezesha usafirishaji wa bidhaa za kilimo pamoja na usafiri wa wananchi uweze kutekelezwa? Aidha, kumekuwepo na uimarishaji wa madaraja na baadhi ya sehemu korofi kwa kiwango si cha kuridhisha. Hivyo naomba kupata majibu ni lini sasa ujenzi huu wa barabara utaanza.

Mheshimiwa Spika, ahsante.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi niweze kuchangia katika hoja hii. Kwanza napenda niunge mkono hoja hii na nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na timu yake kwa kuandaa bajeti ambayo ni nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kupanga ni kuchagua Watanzania tumefika mahali tukipanga hiki tunalalamika tunasema kibaya, tukianza hiki tunasema hiki ni kibaya, lakini yote Watanzania tufike mahali tunapopanga tuchague wenyewe. Siamini leo hii kwa Tanzania hii tuweze kulalamika sana. Ukichukua mfano kama Tanzania uki-compre na Kenya Uganda nchi zinazotuzunguka hapa hivi. Ni nchi gani ambayo ina rasilimali nyingi na kila neema kama Tanzania. Lakini tuko nyuma kwa sababu tukipanga kitu tunaanza kupinga tena tunakataa. Unataka uchumi wa viwanda unasema hutaki stiegler’s Gorge, tunataka umeme sijui wa aina gani na kadhalika. Tunakwenda wapi? Tunatoka wapi? Kama nchi lazima tuwe national agenda ya pamoja lakini tunakuja hapa tunaanza kuchukua mawazo ambayo hayatusaidii kama nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimesikiliza mijadala yote hapa lakini nasema Watanzania lazima tubadilike kama tunapenda nchi hii lazima tukubali na kwenye mabadiliko lazima wengine waumie. Huwezi kuwa na mabadiliko katika nchi yoyote ile watu wasiumie haiwezekani. Nchi zote ambazo zimeendela watu waliumia sana, sana. Naomba Watanzania na hasa Wabunge sisi Wabunge humu ndani tusiwe ndumila kuwili. Kama tumekubali ajenda ya uchumi wa viwanda twende nayo tutoke nayo. Mnataka baada ya miaka mitano au kumi tufeli tuanze na ajenda gani nyingine tena. Let be serious. (Makofi)

T A A R I F A . . .

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika, amelenga penyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niendelee, kama tunataka utalii katika nchi hii lazima Bodi ya Utalii tuiwezeshe. Haiwezekani tukawa tunaongea ngonjera, utalii, utalii bila kuwezesha Bodi ya Utalii haiwezekani. Lazima kuwe na synergy ya mambo ambayo yanafanyika kama Taifa. Ningeomba sana kwa sababu ya muda sijui nitaongeaje sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo tunataka utalii huu uchochee uchumi wa nchi hii, lakini pamoja na haya lazima tuangalie kuna vitu ambavyo naomba sana Mheshimiwa Waziri uangalie sana hili. Nchi yoyote katika uchumi uweze kuwa vibrant lazima kuwe na biashara zinazofanyika. Watalii waingie hapa kwa gharama ndogo lakini wanakuja ku-spend zaidi hapa wanaingiza uchumi wetu hapa hivi.

Leo hii ukienda Dar es Salaam kwa mfano mahoteli yako tupu, ukienda Mwanza mahoteli yako tupu, ukienda Arusha mahoteli yako tupu. Sasa unasema watalii wanaongezeka, tunajiuliza swali kubwa sana kwamba tunafanyaje. Tuwe na mkakati wa Taifa tuondoe gharama ambazo zinakwaza watalii wasiingie hapa, tuchocheze ili watalii waweze kuingia na tuitangaze nchi yetu kwa urahisi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia gharama za mtu kuingia hapa nchini na kufanya kazi ni kubwa mno, dola 3050 ni hela nyingi sana za Kimarekani kama milioni saba za Tanzania. Hivi kweli biashara gani zinaweza ku-support mambo kama haya. Naomba mambo kama haya Waziri wa Fedha na wadau wengine wote tuongee kama nchi. Tusiongee kama mtu au kama Wizara kwa Wizara in isolation tufanye kazi kwa mtiririko ambao unaunganisha mambo. Lengo la nchi hii bila kuwa na uchumi hatuwezi kusonga mbele, bila kuwa na mapato ya kutosha hatuwezi kusonga mbele na bila utalii ambao ndiyo moja ya kigezo cha kutengeneza mapato katika nchi hii kuongezeka hatuwezi kupata mapato ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi napenda sana niwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa michango mizuri ambayo kwa kweli imetupa afya njema sisi Wanakamati wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na hoja mbalimbali, na taarifa yetu ya kamati imechangiwa na Waheshimiwa Wabunge 21. Sina haja ya kuwataja wote lakini niwashukuru wale wote ambao wamepata nafasi ya kuzungumza na hata mlitoa kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kamati hii ukiangalia msingi wake mkubwa ni kuangalia mapato ambayo hayatokani na kodi (no-ntax revenue) na ndio kigezo kikubwa sana cha uhai wa ufanisi wa Kamati hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hii imejikita kuelezea ni mambo gani ya msingi ili Serikali iweze kuyazingatia. Kama itafanya vile maana yake tutapunguza ile nakisi ya bajeti kupitia mapato ambayo hayatokani na kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachangiaji wengi wamezungumza lakini ningependa nianze na jambo moja kidogo hapa la kufanya clarification.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa ambazo Kamati inazo, Serikali ina taasisi 11 ambazo ina ubia wa kuanzia asilimia 50 na chini ya asilimia 50. Moja ya taasisi hizo zimechangia sana kupata mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 35.9. Katika taasisi zile tatu zinazoongoza kuna Benki ya NMB iliyotoa shilingi bilioni 10 kama gawio, PUMA Energy ambayo Serikali ina asilimia 50 na ninaomba nirudie kwamba Serikali tuna ubia wa asilimia 50 kwenye Shirika la PUMA Energy. Sasa nasikitika sana kama kuna watu ndani ya Bunge au ndani ya Serikali hawa-acknowledge hiyo, huyu ni mtoto wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna asilimia 31.8 kwenye Benki ya NMB, huyu ni mtoto wetu, tuna asilimia 30 kwenye Benki ya NBC, huyu ni mtoto wetu. Tuna asilimia 25 kwenye Tanzania Planting Company Ltd., huyu ni mtoto wetu na ametoa gawio kubwa kuliko wote la shilingi bilioni 13.4. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri sana na naamini kwamba kama una mtoto msaidie na kama ana mapungufu mrekebishe lakini ningeona kwamba ni fahari tuone kwamba taasisi hizi tuzibebe vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inawekeza kwenye Shirika la Ndege - ATCL na Mheshimiwa Rais alikuwa very clear na akasema kwamba Serikali imewekeza pesa nyingi, tunawakabidhi ATCL muendeshe shirika hili, mkishindwa nawanyang’anya nawapa hata Precision. Maana yake ni kwamba tunataka uwekezaji huu uwe na tija kwa Watanzania na tunadhani ni fahari kwa wewe Mtanzania kutumia mali ya kwako, brand ya kwako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa sana kwamba Watanzania tujawe na uzalendo; na hata wenzangu waliochangia akiwemo dada yangu Mheshimiwa Ester Bulaya, amezunguma vizuri, lakini hoja ni kwamba uwekezaji kwenye ndege huwezi ukapata faida leo au kesho. Mashirika yote ya ndege hapa duniani hayapati faida peke yake, isipokuwa yanachochea kukuza uchumi kwenye sekta zote za uchumi wa nchi hiyo. Kwa hiyo, uwekezaji huu tusiuangalie kwa kuangalia faida, tuangalie una multiply effect gani kwenye uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na haya kuna suala la kujua kwamba TRA wanakusanya kodi, Msajili wa Hazina (Treasury Registrar) yeye anakusanya mapato yasiyotokana na kodi. Mapato yapo ya aina tatu makubwa; kuna gawio, redemption of excess capital au mtaji uliozidi na kuna asilimia 15 ya mapato ghafi, haya ndiyo makusanyo yanayopitia katika Ofisi ya TR. Ninachoomba Serikali huyu mtu awezeshwe, kwa maana ya staffing, technology lakini vilevile na namna ya kupata wataalam wenye weledi kuendesha Ofisi ya Msajili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiyafanya haya na kwa bahati nzuri nimeshafanya consultation na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mawaziri husika wameona umuhimu huu kwamba Ofisi ya TR lazima tuiwezeshe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine cha msingi katika hili ni suala la Seikali kutokulipa madeni…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwenyekiti naomba utoe hoja muda umeisha.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA
UMMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika kumi tayari?

MWENYEKITI: Ndiyo, naomba utoe hoja.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya naomba basi niwashukuru wale wote waliochangia ukiwepo wewe mwenyewe kwa kuweza kutupa fursa hii; na basi naomba nitoe hoja kwamba lipokee maoni na mapendekezo ya kamati yetu, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niungane na wenzangu wote ambao wameweza kutoa pongezi na hasa katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa bajeti hii vizuri na naomba tumpongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nina sababu kuu mbili za kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu; katika Mawaziri Wakuu ambao wameshapita katika nchi hii, huyu namwona Waziri Mkuu wa kipekee kwa sababu kwanza anazunguka, kuifahamu nchi na kuwatumikia Watanzania vizuri zaidi, lakini pia anafuatilia vizuri sana utekelezaji wa miradi ya Serikali na shughuli za Serikali kwa ujumla. Tunatakiwa tumpongeze kwa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa huyu ndio kiongozi wa shughuli za Serikali hapa Bungeni, niunge mkono vilevile, kwamba hotuba yake hii ya bajeti ya bilioni mia moja na arobaini na nane tumpatie bila hata kupunguza hata shilingi moja, kwa sababu anahitaji hizi fedha ili kwatumikia Watanzania. Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua kwa mambo mengi sana, wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu, hivi ni wapi ambapo leo hii katika nchi hii hutaona shughuli zinaendelea? Iwe za miundombinu, za maji, za elimu, za afya na kadha wa kadha. Hii imesaidia sasa kuwafungua Watanzania na ndiyo maana kuna siku hapa Mheshimiwa Mbunge Profesa Tibaijuka alisema kwamba, unapopanua huduma ndiyo watu wanahitaji zaidi. Kwa hiyo, Watanzania sasa tunahitaji zaidi maendeleo, kwa sababu tumeanza kuona maendeleo yanakuja. Awamu zote zilifanya kazi vizuri sana, lakini Awamu ya Tano kwa muda wa miaka mine, nadhani kila mmoja anaona na kama anaona, basi kuna kila sababu ya kupongeza shughuli za zinazofanywa na Serikali yetu ya Awamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiangalia katika miradi mingi kwa mfano ya miundombinu, tumeona barabara nyingi zinajengwa, miradi ya umeme tumeona, mradi wa REA sasa hivi katika nchi hii, tunalalamika kwamba baadhi ya vijiji havijafikiwa, lakini karibu kila kijiji miradi hii imeshaanza kutekelezwa. Hii ni hatua moja muhimu sana na naomba tupongeze sana kwamba Serikali inafanya kazi yake vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika yote haya nataka niseme kwamba tunahitaji kuifungua nchi vizuri tuwe na priorities za kimkakati ili tuweze kuendelea tunahitaji kufungua nchi vizuri zaidi, maeneo ambayo ni ya kimkakati tuyaendeleze zaidi. Mheshimiwa Rais alikuwa kule Mtwara, amezungumza vizuri sana namna ya kufungua korido ya Kusini; kuna korido ya Mbeya, uwanja wa ndege wa Songwe, naomba sana sana hicho ni kitega uchumi cha muhimu sana katika nchi yetu hii. Kwa hiyo, lazima ukamilishwe kwa wakati na uweze kutoa huduma, uwanja wa ndege wa Mwanza ukamilishwe vizuri ili uweze kutoa huduma vizuri zaidi, kwa sababu umechukua sehemu kubwa ya mahitaji na watu ambao wanahitaji kuutumia na kwa kiuchumi uko kimkakati zaidi. Pia uwanja wa ndege wa Mtwara na viwanja vingine ambavyo vimetajwa ikiwepo Simiyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii itasaidia sana kufungua nchi yetu, lakini tukiangalia Serikali hii ya Awamu ya Tano tumeweza kuwapata wawekezaji wa umma na wa sekta binafsi, uwekezaji wa umma hadi sasa hivi Serikali imewekeza zaidi ya trilioni 54.8 na mwaka jana kwa mara ya kwanza tumepata gawio la shilingi bilioni 830. Tunapaswa tupongeze sana Serikali hii kwa sababu kuna baadhi ya makampuni na mashirika yalikuwa hayawezi kutoa gawio kwa Serikali, lakini yameweza kutambua umuhimu huu, sasa yanachangia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Hii ni jitihada muhimu sana kwa Serikali yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto ambazo zipo na Waheshimiwa Wabunge nadhani wamezungumza na wengine pia tuzungumze, kuhusu ukamilishaji wa miradi, najua kuna vipaumbele vingi lakini vile vile tunapoanzisha miradi tuikamilishe. Kwa mfano, majengo ya halmashauri hizi mpya za wilaya, kwa mfano Wilaya yangu ya Busega tumejenga jengo huu ni mwaka wa nne halijakamilika. Ukiangalia gharama zinaongezeka. Kwa hiyo ningeomba kwamba Serikali iweke utaratibu majengo ambayo kwa wilaya ambazo hazijawahi kujengewa majengo mapya basi zijengewe majengo hayo yakamilike ndani ya muda ili kusudi tuepuke kuongezeka kwa gharama za ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maboma ya Zahanati, Waheshimiwa Wabunge wamezungumza hapa na madarasa, wananchi wamechangia nguvu ningeomba sana Serikali kupitia bajeti hii tuelekeze nguvu zetu kuhakikisha maboma haya ya zahanati pamoja na maboma ya madarasa yanakamilishwa ili kusudi tupange kingine zaidi. Mnapoanza kitu msipokamilisha mnaanza kingine, inakuwa ni tatizo kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya maji; mimi na wewe nadhani tupongeze sana Serikali hii kwa sababu tuna mradi mkubwa sana wa maji kutoka Ziwa Victoria. Chanzo cha maji kinaanzia pale Busega, mradi huu ni wa kitaifa na utahudumia vijiji vingi na mikoa mbalimbali. Naomba miradi huu utekelezwe kwa wakati, kwa sababu mradi huu fedha zake zinatoka kwenye Climate Fund, basi ukamilishwe kwa wakati. Naomba taratibu zote za ujenzi zifanyike na uweze kukamilika

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miradi ambayo bado najiuliza sana ni TARURA. TARURA Waheshimiwa Wabunge nadhani mtaniunga mkono, wanahitaji kusimamiwa vizuri. TARURA tumewapa majukumu lakini hata na Halmashauri hawako pamoja, hawaingii kwenye vikao inavyotakiwa. Pili, wanafanya miradi hata Madiwani hawajui miradi inavyotekelezwa. Naomba sana kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, suala la TARURA liangaliwe vizuri zaidi ili kusudi liweze kuwa na tija katika kutekeleza miradi yetu ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunahitaji maisha bora, tunayapataje, ni lazima tuwekeze na sekta binafsi lazima iangaliwe. Nashukuru sana Mheshimiwa Rais ameunda Wizara ya Uwekezaji na wamepata Waziri mahiri, naamini Waziri huyu akipewa ushirikiano atafanya kazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi tumeona wawekezaji wengi wanakuja hapa Tanzania halafu wanaondoka bila kuwekeza kwa sababu ya ukiritimba. Pia bado kuna vitu ambavyo vinakinzana kati ya vitu ambavyo vinampa mwekezaji incentives au vivutio vya uwekezaji ambavyo ukienda TRA kwa Mamlaka ya Kodi vinakuwa vinakinzana, matokeo yake mwekezaji anasumbuliwa. Bado kuna vitu vingine ambavyo vinafanya mwekezaji ili aweze kuwekeza vizuri anapata shida sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la vibali vya ufanyaji kazi. Mheshimiwa Jenista Mhagama analifahamu hili, tunaomba sana kuwe na coordination nzuri. Kwa sababu huyu Waziri wa Uwekezaji kama Waziri ameshaomba vibali vya wawekezaji lazima mshirikiane, msomane vizuri zaidi kwa sababu tuta-frustrate wawekezaji ambao ni genuine kwa sababu ya vibali, kumbe masikini hamjapata taarifa sahihi tu. Huyu atajitahidi kutafuta wawekezaji wanakuja hapa nchini, anaongea nao vizuri zaidi, ana wa-assure kwamba Serikali itawapa kila aina ya msaada inapokuja suala la vibali, kunatokea sintofahamu ya hapa na pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kama nchi tusafiri pamoja, kama Serikali msafiri pamoja ili kusudi tusi-frustrate wawekezaji. Ukishampoteza mmoja umepoteza karibu 100. Hii kwetu sisi inatu-cost sasa hivi, unakwenda kwenye nchi ambayo haina chochote wala lolote wanasema eti uwekezaji ni mzuri zaidi kuliko kwetu sisi. Naomba tuondokane na dhana hii na naomba sana Mheshimiwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii ili niweze kuchangia katika hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Hotuba hii ukiisoma ni nzuri na nampongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake kwa kuandaa bajeti hii na hotuba hii ambayo kwa kweli inaakisi kile ambacho wanadhani wanaweza kukifanya mwaka ujao wa fedha. Naomba nianze kwanza kwa masikitiko yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania na hasa na sisi Waheshimiwa Wabunge, tusipokubaliana kwanza kubadilisha mawazo yetu kwa kuthamini kwamba biashara au public sector ndiyo kiini na kitovu cha ajira za Watanzania. Ndicho ambacho kinaweza kukuza uchumi wa nchi hii, short of that hatuwezi kutoka hapa tulipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezoea kuitana majina; fisadi, mwizi, ukimuona mtu anafanya hivi huyu ni mwizi. Hebu jiulize; kama ameweza kuiba na akawekeza hapa nchini, wizi wake uko wapi? Kwa sababu tunavunjana moyo Watanzania, sisi tukiona mtu ametajirika anaitwa fisadi, anakuwa mwizi, haya maneno hayatusaidii kutujenga Watanzania na naomba sana tufanye a total mindset transformation, tusipofanya hivyo Watanzania itabaki ni hadithi tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais ameingia na kuali mbiu sahihi kabisa, hajaianza leo, ameakisi watangulizi wake. Tunataka Tanzania ya viwanda, unapataje viwanda? Lazima kuwe na backward and forward linkages. Hayo unayapata kama Watanzana wameshirikishwa vizuri, lakini leo hii Private Sector ina matatizo chungu nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii kuanzisha biashara Tanzania ni kama mzigo, utatozwa kodi kwenye mtaji ambao unataka uwekeze. Sasa how can you invest on your capital? Tuangalie tu, hiyo capital unakwenda kukopa benki, kabla hujaitumia unatandikwa kodi karibu 42, sasa unakwenda wapi. Sasa ni mambo ambayo sisi kama Watanzania lazima tubadilike. Tusipobadilika itakuwa ni hadithi na ngonjera, tunabaki kila siku tunasema sisi tumelogwa, hakuna aliyetuloga, ni mawazo yetu yamelogana yenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia vibali vya kufanya kazi, unajua uchumi wowote wa nchi ni mixture, unaweza uka-borrow technology, uka-borrow capital kutoka kwa watu mbalmbali uka-invest. Kama huna technology hiyo unai-borrow from outside, lakini sisi hapa tunaona hata wageni ni tatizo, sasa unajengaje uchumi wa kwako peke yako? Tunaomba sana katika hili tubadilike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo ambayo ukiyaangalia, Mheshmiwa Waziri amezungumza kwenye hotuba yake, non-tariff barriers, wamepunguza kutoka 62 mpaka 47, this is very good, lakini leo hii hata kusafirisha mzigo tu ukienda kilometa kadhaa mizani unaambiwa faulisha, mara fanya kitu gani, una waste a lot of time barabarani kabla ya kufikisha mzigo unakokwenda; hivi ndivyo vinavyoleta uchachu katika kufanya biashara hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu vilevile kuna taasisi ambazo zinapaswa kuwa harmonized. Namshkukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuanzisha Wizara ya Uwekezaji, nampongeza sana, angalau sasa, tena kaiweka chini ya Waziri Mkuu, kwamba angalau Waziri Mkuu moja kwa moja anawajibika katika suala la uwekezaji kupitia Waziri ambaye amepewa mamlaka hayo. Hii itasadia kutufanya Watanzania tuthamini namna ya uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi Mheshimiwa Waziri Mkuu amepokea watalii kule Arusha, it’s a business, utalii is a business. Sasa sisi hapa unaangalia kwamba tuna vituo vingi sana, lakini tunalia kwamba hatuna wawekezaji, watakujaje hatujaweka mazingira mazuri hapa kwetu? Naomba Bunge hili litumike kuhakikisha kwamba tunaweka utaratibu mzuri wa ufanyaji biashara, bila hivyo itabaki ni ngonjera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona na naomba nim- quote Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha, alisema kwamba biashara nyingi zinafungwa, lakini nyingi zinafunguliwa, sio kweli. Biashara nyingi zinafungwa sasa hivi na watu wana- scale down, tunapaswa kama Serikali, kama nchi, tujitathmini upya, why, bila kufanya vile unapataje hiyo kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Watanzania tusiseme kwa sababu watu pengine wanapiga makofi huku, hoja ni kwamba lazima tutoke hapa tulipo, tufike mahali pazuri. Kwa hiyo kwa sababu unajua wakati mwingine tusipoambizana ukweli hatuwezi kusonga mbele. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Rais amempa nafasi hii, hebu atumie nafasi hii sasa kuweza kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi ili Tanzania tusonge mbele, hatuwezi kila wakati kuwa tunalia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ukienda by statistics makusanyo ya kodi ya TRA yanazidi kushuka, wakatae wasikatae ukweli ndiyo huo, lakini yanashuka kwa sababu gani? Lazima tuchochee tupate biashara nyingi, unapata kodi hii kutoka kwenye biashara, uta-tax wapi kama hakuna biashara, niombe sana. Marehemu Dkt. Mengi ni mmoja wa Watanzania ambaye alijitahidi sana kufanya biashara mbalimbali, nikiuliza leo hii hapa Tanzania baada ya Dkt. Mengi kufariki, wangapi akina Mengi saa hizi, wangapi? Tukikaa hapa, ukiona hivi unasema wengine hapa Tanzania wapo, lakini unakuta wana passports zaidi ya moja au mbili, unakuta yeye peke yake akifanya biashara asilimia 75 anapeleka nje, lakini ukiwa kama mimi namna hii au wewe au ndugu yangu hapa Mr. White, akipata hela yake hapa ataoa mwanamke hapa, atawekeza hapahapa, hela inazunguka hapa hapa. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona niseme haya kwa sababu naumia kuona kwamba this is my country, lakini kila siku tunalalamika, tunamlalamikia nani? Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, tusaidie. Hata hivyo, lazima wasomane na wenzake, hawezi akafanya kazi in isolation, wasiposomana haiwezkani, naomba apate support kwa Mawaziri wenzake ili tuwe na direction moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais anafanya kazi nzuri sana nimemwona akizunguka, anahamasisha biashara na anasema mfanyabiashara akiwa na shida aniambie mimi moja kwa moja. Hivi kweli wote tutamfikia Mheshimiwa Rais kumwambia matatizo yetu wakati Mawaziri wapo? Wamsaidie Mheshimiwa Rais kufanya kazi hizi, wamsaidie kabisa. Haiwezekani Mheshimiwa Rais kila wakati anazunguka anapiga kelele mpaka anasema watendaji mnaonekana hamnielewi, kama hawamwelewi basi waachie ngazi, ndiyo, it’s true. Tunataka sisi Tanzania ambayo inasonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kusema kwamba leo hii kuna miradi ya kimkakati, Mchuchuma na Liganga kila siku ni hadithi na ngonjera. Mheshimiwa Waziri atapokuwa ana-wind up hapa naomba nipate taarifa sahihi kwamba suala la Mchuchuma na Liganga tunatokaje hapa tulipo? Kila siku sisi tunasema, tunajadili, mwaka huu tunajadili, mwaka unaofuata tunajadili; tunafika wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kingine, Mheshimiwa Dkt. Kingwangala yuko hapa hivi, watu wanapoingia hapa nchini it’s part of the business. The first impression anayoipata hapa anapoingia pale airport, anakuta wafanyakazi wa airport wamenuna kama wamekula pilipili. Wewe unamkaribisha mgeni nyumbani kwako umenuna, unaweza kum-harass mtu, why? Katika nchi nyingine unapokwenda unapewa a very good treatment, lakini hapa akija mgeni ni kama amekuja kwenye madaladala. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba unilindie muda wangu nadhani Mheshimiwa Waziri hakunielewa.

WABUNGE FULANI: Kweli kabisa.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuelewa concept yangu mimi, siyo suala la kutabasamu na kuvaa uniform nzuri ni culture ya kupokea wageni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe kama Waziri mwenye zamana hii hiyo unapaswa uonyeshe kwamba, unajua sikiliza unapompokea mgeni, its all inclusive package, hata tabasamu ni sahihi, hata ku-facilitate kupata mizigo au permit vyote ni muhimu zaidi na kadhalika, wewe kama Waziri wa Utalii unapaswa kuibeba hiyo.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira wa Mwaka 2018
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kuwa mchangiaji katika Muswada huu muhimu sana wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo naomba nikiri kwamba Wizara hii ambayo inaongozwa na Maprofesa akiwemo Profesa Waziri na Katibu Mkuu wake wamefanya kazi nzuri sana. Kwa kweli huu Muswada umejikita sana kuona kwamba Watanzania kile kilio cha maji miaka nenda rudi sasa tunakipatia majibu yanayoeleweka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia wazo la kuwa na sheria moja ambayo itasimamia utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira ni kitu cha muhimu sana. Leo hii miradi mingi sana ya maji inaanzishwa lakini sehemu nyingi miradi hii inakosa coordination. Kwa kuwa na sheria moja itasaidia sana kuleta usimamizi ulio mbashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kilio cha wananchi pamoja na sheria ni kupata huduma ya maji. Leo hii tuna Ziwa ViKtoria kwa mfano, Tanzania tunamiliki zaidi ya 52%, Uganda 32%, Kenya kama 12% au 14% lakini matumizi yetu ya maji ya ziwa hili yapo chini ya 1% wakati Uganda na Kenya wanatumia zaidi. Naomba kupitia Muswada huu na ikiwa sheria tuhakikishe kwamba wananchi wa Tanzania na hasa kina mama tunawatua ndoo kisawasawa, waweze kupata maji kwa urahisi zaidi. Hakuna hitaji la muhimu na la msingi kwa mahitaji ya binadamu kama maji. Kutokana na kuainisha majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti ya Maji na Nishati (EWURA) katika Muswada huu nimefurahi sana kwa sababu inaonyesha namna gani sheria hii itakavyoweza kusimamiwa kikamilifu kwa maslahi ambayo wananchi wote watanufaika nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni umuhimu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Siku zote tumekuwa tukipiga kelele kwamba lazima wananchi ambapo zaidi ya 80% wanakaa vijiji lakini tatizo kubwa ni maji. Serikali ya Awamu ya Tano imejaribu kusikia kilio hiki na hata kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2015- 2020 miradi mingi sana ya maji sasa imeanzishwa lakini tunahitaji iendelee kusimamiwa na kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ninaloliona hapa ni pamoja na fedha kutokutoka kwa wakati. Inakuwa haina maana wala tija kama miradi inaazishwa lakini haikamiliki kwa wakati na hii inaongeza gharama kubwa sana hata kwenye miradi yenyewe. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Katibu Mkuu wake na watendaji wote ndani ya Wizara wahakikishe kwamba miradi hii ambayo imeanzishwa inatekelezwa na inakamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matarajio yangu ni kuongezeka kwa ufanisi na ufuatiliaji katika utoaji wa huduma kwani sasa wataalamu wote wa Wizara wa Maji wako kwenye Wizara ya Maji na wamewekwa kule makusudi ili kuongeza ufanisi. Wataalam hawa walikuwa chini ya Halmashauri sasa watakuwa chini ya Wizara. Mimi naunga mkono lakini natoa angalizo kwamba ni namna gani sasa hawa watendaji watavyoweza kuwajibika moja kwa moja kwenye Halmashauri zao. Tunaanza kuingia kwenye mchezo kama ule watumishi wa TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hii Muswada huu uainishe vizuri kati link ya watumishi ndani ya Wizara ya Maji na Halmashauri wanazozifanyia kazi kwa sababu ndiyo kwenye wananchi kule na ndiyo miradi inatokea kule, ndiyo wenye maji lakini halmashauri hizi hazipewi nafasi ya kusimamia miradi hii. Naomba sana kupitia Muswada huu tuone namna gani hawa watendaji ndani ya Wizara ya Maji wanashiriki kikamilifu katika halmashauri wanazokaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la RUWASA, wakala huyu ni muhimu sana na tumetaka hata kuwa na National Water Fund (Mfuko Maji wa Taifa) ili usaidie kutafuta fedha. Nashauri fedha kubwa iende ika-solve matatizo ya wananchi vijijini kwani maeneo mengi watu wanahitaji maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kuna miradi mingi katika Wilaya ya Busenga, Mradi wa Maji Lamadi zaidi shilingi bilioni 12.6 lakini hakuna Bodi ya Mamlaka ya Maji. Sasa unategemea nini mradi kama huo ambao tumeweka a lot of investment lakini hakuna usimamizi sahihi, hakuna Mamlaka ya Maji. Kwa hiyo, naomba sana Waziri u-take note hili na kwamba kuna haya ya maeneo kama hayo yanayofanana na Busega basi yaweze kuanzishiwa mamlaka hizi kusimamia miradi hii. Uendelevu wa miradi ya maji vijijini utokane na kuboresha miundombinu pamoja na usimamizi wa vyombo na watumiaji wa maji. Bila kufanya hili vilevile haitatusaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeangalia katika Muswada huu nimeona kwamba pamoja na yote haya, Waziri katika suala la faini ni zuri lakini naomba liangaliwe vizuri. Faini zingine hapa mmezitaja ni kubwa mno lakini kwa matumizi ambayo hayaendani. Naomba faini ambazo mmezitaja ziendane na matakwa au ukiukwaji wa sheria ambazo zitakuwa zimevunjwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo kuna matatizo ambayo yanajitokeza ambalo ni kodi kwenye miradi ya maji. Naomba sana hili suala liwekwe clear, hizi kodi zisiwepo watu wasisumbuliwe. Nachoshauri ni kwamba pasiwe na kodi kwenye miradi hii ya maji na itasaidia sana utekelezaji wa miradi hii na hata fedha zile kufanya kazi kwa utimilifu mkubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala ambalo Wizara hii na naomba pengine waweze kuiga kidogo utendaji wa DAWASA. DAWASA baada ya kuwa imeundwa upya na hata katika kufuatilia utendaji kazi wa DAWASA tunaona kabisa kwamba ni moja ya mamlaka ambayo inajipambanua kutatua tatizo la maji kwa wananchi wa Dar es Salaam. Napenda mamlaka zingine ikiwezekana ziige mfano wa DAWASA. Upotevu wa maji wa DAWASA pamoja na Mamlaka ya Maji ya Mwanza (MWAUWASA) na Mamlaka ya Maji ya Arusha (AUWSA), hivi ni vielelezo vizuri sana. Mheshimiwa Waziri hakikisha mamlaka zako zote hizi ikiwezekana wawe na benchmark ziwasaidie kujua namna gani ya kuweza kwanza kupunguza upotevu wa maji ambao ni gharama kubwa sana lakini pili na kupunguza gharama ya watumiaji maji kwa kufanya vile itasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ufungaji wa mita kama za Luku upande wa maji itasaidia sana na hasa kwa taasisi sugu za Serikali hazilipi madeni ya maji, hili ni tatizo. Haiwezekani taasisi hizi zinatoa huduma lakini hazilipwi. Naomba sana Mheshimiwa Waziri wa Maji, Mheshimiwa Rais alishawahi kusema kwamba anayepata huduma asiyelipa maneno ni mawili KATA. Naomba tuiendeleze kauli hii vinginevyo mamlaka hizi hazita-survive, lazima watu watumie maji na walipie huduma hizo. Hasa taasisi za Serikali, naomba Waziri uwe mkali kidogo na madeni yaweze kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana na naunga mkono hoja hii. (Makofi)