Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Eng. Ramo Matala Makani (25 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Waziri wa Kilimo. Pongezi pia kwa Naibu Waziri, hakika nawatakia kila lililo la kheri na Mungu awape ziada ya nguvu, hekima, busara na utashi katika kumsaidia Mheshimiwa Rais.
Mheshimiwa Naibu Spika, shukrani nyingi kwa Serikali kuwakumbuka wakulima wa korosho kwa kuwapunguzia mzigo wa msumari wa kodi/makato mbalimbali katika zao la korosho. Tunaomba Serikali iendelee kuziangalia changamoto zingine zilizopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nia njema ya Serikali kuweka ushuru wa zao la korosho ghafi ziuzwapo nje ya nchi ambayo ilikuwa ni kuendeleza zao la korosho kwa pembejeo, utaalam na kadhalika, imekuwa ikihujumiwa sana. Export Levy inayoratibiwa na Mfuko wa CDTF (WAKFU) inatumiwa vibaya na hovyo. Fedha hizo ni vema zikaenda moja kwa moja kwenye Halmashauri zinazolima korosho ili wajanja wasiturudishe nyuma.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ukarabati jengo la Ofisi ya Madini Tunduru. Tunapongeza na kuishukuru Serikali kwa ukarabati huu. Tunaomba jengo hili liwe chanzo cha uwepo wa wataalam na vifaa stahiki kwa uboreshaji wa sekta ya madini hasa wachimbaji wadogo katika Kata za Ngapa, Muhuwesi na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, uboreshaji huduma ya upatikanaji wa umeme Wilaya ya Tunduru. REA phase II, vijiji 33 vinaendelea kwa usambazaji. Tunaomba kasi ya mkandarasi iongezeke, yuko taratibu sana. REA phase III vijiji 52 nilivyowasilishwa Ofisi ya REA na TANESCO Mkoa wa Ruvuma, naomba vijiji hivi viwe miongoni mwa vijiji kipaumbele vipate umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujua transformer iliyopata matatizo ya kiufundi matengenezo yake yamefikia wapi? Naomba changamoto zilizojitokeza kuhusiana na transformer hiyo iliyopatikana kutoka TANESCO zitatuliwe ili miradi iliyopangwa kutumia transformer hiyo ikamilishwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, Tunduma iko kati ya Songea na Mtwara. Umeme wa njia kuu (national grid) kutokea mradi wa SIDA kupitia Makambako, Songea unaishia Namtumbo pia umeme wa gesi na kadhakika. Kwa njia kuu kutokea Mtwara bado hatujaona wazi mpango wa umeme huu kwenda Tunduru.Naomba Tunduru iingizwe katika mipango ya usambazaji wa umeme kupitia national grid. Wakati tunasubiri mpango wa national grid Tunduru ipatiwe/iongezewe generators (DGs) zenye uwezo na ufanisi. Pia kutengeneza zilizopo na/au kuongeza nyingine kutoka maeneo mengine au mpya.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tunaendelea na mipango yote, tufikiriwe pia kutumia/kupatiwa umeme wa nishati mbadala kwa kadiri itakavyofaa kitaalam. Zikitumika njia za biogas au ile ya kutokana na mabaki ya mazao (biofuel), basi njia hizo zinufaishe vikundi vya wananchi hasa akinamama kwani Tunduru ni mashuhuri kwa uzalishaji mazao ya kilimo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesimama mbele ya Bunge lako Tukufu kwa madhumuni ya kuchangia hoja, wakati nikifanya hivyo niweze pia kama Naibu Waziri kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wakishiriki katika majadiliano ya hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema wake na kwa fadhili zake kutujalia afya njema ya kuwa hapa kwenye Bunge lako Tukufu kutekeleza wajibu wetu kwa Taifa. Aidha, nachukua fursa hii muhimu kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Nampongeza pia Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Mbunge, kwa kuteuliwa na kuthibitishwa na Bunge lako Tukufu kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongeza Mheshimiwa Spika na Naibu Spika kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge letu la Kumi na Moja katika Awamu ya Tano ya uongozi wa nchi yetu, nawapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kuchaguliwa au kuteuliwa kubeba dhamana ya kuwakilisha wananchi na kutenda kazi katika Bunge hili kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Nawapongeza pia Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuchaguliwa na kuendelea kulisaidia Bunge kupitia Kamati zao, Bunge kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba na ya Kikanuni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee naomba kuipongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhandisi Atashasta Justice Nditie, Makamu wake Mheshimiwa Kemilembe Julius Lwota na Waheshimiwa Wajumbe wote kwa namna ambavyo wameendelea kuishauri Wizara yetu ili kuifanya sekta ya maliasili na utalii ifikie malengo yake ya kuchangia zaidi katika ukuaji wa uchumi, kuwaongezea wananchi kipato, kuongeza fursa za ajira na kuboresha huduma za kijamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kumshukuru kwa namna ya pekee Mheshimiwa Rais kwa kuniamini na kuniteua kubeba dhamana hii kubwa ya kumsaidia Waziri wangu kuisimamia sekta hii ya maliasili na utalii nchini. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa nitamsaidia Waziri wangu kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika eneo la sekta ya maliasili na utalii ili kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali itakayokuwa inatolewa mara kwa mara kuyafikia malengo yake. (Makofi)
Mwisho lakini siyo kwa umuhimu nawashukuru wapiga kura na wananchi kwa ujumla wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kwa kunichagua kuwa Mbunge wao na kwamba nipo njiani, mara tu baada ya kukamilisha jukumu hili la Kitaifa tutaungana pamoja katika kuendeleza utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa Jimbo na kwa Wilaya nzima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nijielekeze katika ufafanuzi wa hoja. Napenda nianze kwanza kabisa kwa kusema kwamba michango yote iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge ilikuwa ni yenye afya na ni michango yenye malengo mazuri ukiacha kasoro za hapa na pale, lakini kwa ujumla wake ni michango ambayo kweli tunaipokea na mingi tutaifanyia kazi ili iweze kuongeza tija katika mafanikio ya Wizara. Jukumu letu kama Wizara au jukumu letu kama Serikali katika sekta hii ni kupokea na kuyafanyia kazi maoni hayo na ushauri wote tulioupokea kwa sababu huko ndiko kukubali kushauriwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Katiba hiyo ndio kazi ya Bunge.
Maliasili na utalii ajenda yake kubwa ni uhifadhi. Napenda nirudie katika Wizara hii ya Maliasili na Utalii ajenda kubwa ni uhifadhi. Tunapaswa kuhifadhi tulichonacho, tunapaswa kukilinda tulichonacho kinachotutofautisha sisi na nchi zingine au na maeneo mengine ambayo ni nje ya Tanzania na hilo ndilo linalotufanya sasa hata tuzungumzie utalii kwa sababu wanaokuja hapa wanakuja kuona vitu ambavyo kwao havipo na vinaweza vikaendelea kuwepo na kuboreshwa ili tuweze sasa kuweza kufikia malengo ya kukidhi haja ya watalii.
Sasa wakati tukiwa tunajipanga upya kwenye maeneo ambayo yana kasoro na mapungufu ya hapa na pale, kwa sababu haiwezekani kuwa hakuna maeneo ambayo yanahitaji kufanywa vizuri zaidi. Mimi nina msemo wangu siku zote huwa naurudia mara kwa mara, huwa nasema hakuna mwisho wa kufanya vizuri, kila wakati utakapodhani umefanya vizuri bado kuna namna bora zaidi ya kufanya vizuri zaidi. Sasa kwa sababu hiyo, tunataka tubaki pale pale kwenye lengo la kwamba kwa sababu sekta hii ina husisha makundi mbalimbali kama ambavyo yamekuwa yakijadiliwa tangu pale mwanzoni. Ustawi wa sekta hii unahitaji wafugaji, ustawi wa sekta hii unahitaji pia wakulima wa mazao, ustawi wa sekta hii unahitaji pia wavuvi na watu wengine wote ambao wataweza kuorodheshwa kulingana na shughuli zao mbalimbali wanazofanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wakati tukiwa tunazingatia maslahi ya kila kundi, lakini maslahi ya Taifa ndiyo yatayotakiwa kupewa nafasi kubwa zaidi. Kwa hiyo, tunajipanga katika kuzingatia zaidi maslahi ya Taifa kwa sababu maslahi ya Taifa yanazidi au yanavuka ukomo wa umuhimu kwa mahitaji ya makundi moja moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, unayafikiaje maslahi ya Taifa? Sisi kama nchi tunayo vision, tuna dira; dira yetu ni dira ya 2025. Ukisoma dira utakutana na masuala yote yanayohusiana na uhifadhi, utakutana na masuala yote yanayohusiana na tabianchi kwenye dira ile, tuna kawaida ya kusoma kwa kwenda kwenye search engines na kusoma mambo ya mataifa mengine lakini natoa wito tusome pia na nyaraka ambazo ni za kwetu tulizoziandaa wenyewe na nyingine tumeziandaa humu Bungeni au kuziidhinisha, tusome vision lakini pia tuangalie namna ambavyo tunaweza tukasoma mipango tuliyojiwekea kwa mfano, tuna mipango ya miaka mitano mitano, tuna mipango ya kila mwaka, lakini pia tunayo Katiba yetu, tunazo sheria, tunazo kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuwa tumeshakubaliana juu ya yote hayo na hasa tunapokubaliana juu ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo, basi wajibu wetu baada ya pale hatuna uchaguzi isipokuwa ni kufuata na kutii. Pale ambapo tunaona kwamba kuna sababu yoyote ile ya msingi ya kuweza kubadilisha au kufanya marekebisho kulingana na wakati au kwa sababu nyingine yoyote tutakayoona inafaa, basi tunapaswa kufuata utaratibu ule ule na kuweza kufanya marekebisho ya sheria au hata kufuta kabisa sheria kwa sababu taratibu zipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja kubwa ambayo imebeba mjadala au imefanya mjadala wa Bunge jana na leo uweze kuwa mzito zaidi, watu wamechangia kwa hisia mbalimbali, watu wamechangia wengine baadhi yao kwa jazba tunawasemehe, lakini nataka nisisitize tu kwamba suala la migogoro ya ardhi, migogoro ya mipaka limebeba uzito mkubwa. Napenda niseme kwamba Wizara kwa kuzingatia pia andiko ambalo limeandikwa na Wizara ya Ardhi na ambapo nimekwenda kuchukua takwimu kama ifuatavyo tunaweza kutoa jibu moja tu hapa ambalo ni la mwelekeo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba kwanza tuna jumla ya migogoro 281 kwa kadri ambavyo takwimu zimekusanywa na Wizara ya Ardhi, lakini miongoni mwa migogoro hiyo; migogoro ambayo inahusu hifadhi ni migogoro 35 tu ambayo hii ni asilimia 12.5. Mikoa inayoongoza kwa migogoro ambayo inahusiana na hifadhi na Mikoa yote inayoongoza kwa migogoro yote kwa ujumla ni Kagera, Mara, Tanga na Tabora ambayo inabeba karibu asilimia 50 ya migogoro yote. Mkoa wa Tabora ambao wenyewe ni wa nne kwa idadi ya migogoro kwa ujumla yenyewe migogoro yake asilimia 40 ni migogoro ya hifadhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nirudie hapa sasa baada ya takwimu hizi hoja ya Mheshimiwa Profesa Muhongo kwamba tatizo siyo eneo, tatizo siyo ukubwa wa ardhi na mimi tayari nilikwishaliona hilo kupitia takwimu hizi zilizokusanywa na Wizara ya Ardhi kwamba Mkoa wa Tabora ambao ni miongoni mwa mikoa minne yenye maeneo makubwa lakini ambao una asilimia 40 ya migogoro inayohusiana na hifadhi ndiyo unaoongoza kwa kuwa na eneo kubwa nchini. Tabora wana kilometa za mraba 760,151.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema mwanzoni tutakachofanya sasa hivi ni kuhakikisha kwamba migogoro yote hii sasa Wizara zote zinazohusika zinakwenda kukaa kwa sababu tayari tuna agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhusiana na kushughulikia migogoro hii. Wizara zote sita ambazo naweza kuzitaja hapa haraka haraka ni Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii, TAMISEMI, Wizara ya Maji, Wizara ya Nishati na Madini lakini pia Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wote tunakwenda kukaa pamoja kwa ajili ya kwenda kushugulikia migogoro yote kwa ujumla. (Makofi)
Kuhusu migogoro ya ardhi nimekwishamaliza kwa namna hiyo. Lakini nizungumzie ujangili kidogo kwa sababu muda umeshakimbia sana. Masuala yote yaliyotajwa kuhusu ujangili kwanza tumeunda chombo kipya kinachoitwa TAWA (Tanzania Wildlife Authorty), Mamlaka ambayo inakwenda kuchukua maeneo ambayo yanahusiana na uhifadhi wa mbuga za wanyama zile ambazo zipo nje ya zile zilizopo chini ya TANAPA na Ngorongoro. TAWA inakwenda kuboresha zile mbuga ambazo zilikuwa hazina uongozi wa pamoja kama ilivyokuwa TANAPA na Ngorongoro.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ujumla wake sasa sekta ndogo ya wanyamapori inakwenda kuwa bora zaidi, inakwenda kuboreshwa zaidi baada hasa kuhusiana na masuala ya uhifadhi mambo yanayohusiana na askari wa hifadhi, tunaanzisha chombo kinaitwa Jeshi Usu ambalo ni Paramilitary kwa namna ile sasa tunakwenda kukusanya kwa namna bora zaidi ya kuweza kuboresha mapato ili tuweze kushughulikia zaidi maadili ya askari hawa, mmetaja mambo mengi yanayohusiana na matendo ambayo yasiyofaa ya ukosefu wa maadili, kuyataja moja moja muda hautoshi kama mnavyoona, lakini kwa kuanzisha Jeshi Usu tunakwenda kuimarisha zaidi maadili, nidhamu lakini pia tunakwenda kushughulikia zaidi pia maslahi ya hawa askari, incentives zao, lakini pia tunakwenda kuwafanya waweze kuwa manageable zaidi kuliko ilivyo sasa. Kwa hiyo, kwa njia hii tunaweza kuondoa changamoto nyingi zaidi zinazohusiana na ujangili kwa maana ya eneo hili. Yapo mengine mengi lakini kwa sababu muda hautoshi labda pengine naweza kuishia hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utalii, kila mmoja amezungumza hapa juu ya mapungufu kwenye sekta ya utalii na kwamba kunahitajika uboreshaji. Wanazungumzia vivutio vipya, kwanza kuboresha vivutio vilivyopo pia kwa kubuni vivutio vipya, lakini pia kutangaza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe taarifa kwenye Bunge lako Tukufu kwamba katika ziara zangu nilizofanya kwenye baadhi ya Wilaya nimetoa maelekezo na huu ndiyo msimamo wa Wizara kwamba vivutio vyote vinavyoweza kuorodheshwa kwenye vivutio vya utalii nchini, Wilaya zote tunakwenda kuziagiza ziweze kuorodhesha kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge wanasema hapa, waende wakashirikiane na Halmashauri zinazohusika waorodheshe kwa sababu tunakwenda kuandaa directory ya vivutio vyote vinavyoweza kuwa na sifa ya utalii nchini na ambavyo sasa tutaweza kuvi-market kwa maana ya kuvifanyia utangazaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia miundombinu mbalimbali kwenye maeneo ya utalii. Ni kweli lipo suala la miundombinu ndani ya hifadhi zenyewe kwa maana jinsi ya kuweza kutembelea hifadhi, masuala ya hotels mle ndani lakini pia kuna suala la miundombinu ambayo inakufikisha kwenye hifadhi yenyewe kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Sasa huku upande ambako tunazungumzia miundombinu ambayo inakufikisha kwenye hifadhi, kama barabara, Wizara hii haifanyi kazi peke yake, tunakwenda kushirikiana na Wizara inayohusika, inayoshughulika na mambo ya ujenzi pamoja na mawasilIano na mambo yanayohusiana na hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo suala la Southern Circuit, (Utalii wa Kusini). Tuna mradi mkubwa sana unaitwa REGROW (Mradi wa Kuboresha Utalii Kusini) wa makusudi kabisa chini ya Benki ya Dunia wenye dola za Kimarekani zaidi ya milioni 210. Tunakwenda kufanya vitu vingi sana. Kwanza kuboresha vivutio vyenyewe, lakini pia kwenda kuzitambua mbuga, hifadhi na vivutio vingine vyote vilivyo katika ukanda wa kusini ili kuwe na maana ya circuit kweli kweli, kwa sababu mtalii akifika sehemu moja aweze kupata value for money, kwa sababu anaweza kutembelea zaidi ya kivutio kimoja kwa wakati mmoja kwa sababu ya ukaribu na vitu kama hivyo. Ndani kuna viwanja vya ndege vya ndani ya hifadhi na mambo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema muda hautoshi, nakwenda mbio lakini nataka kusema kwamba wote ambao wameguswa na suala la kuimarisha utalii ukanda wa kusini, nataka kuwaambia kwamba Serikali tayari ina mpango mahsusi kwa ajili ya hilo.
Pia hata kuhusiana na vivutio, tumekuwa na vivutio vya aina iliyozoeleka, wanyama; na Waheshimiwa Wabunge wengi wamesema hapa. Ukweli ni kwamba tunakwenda sasa kuimarisha utalii wa kihistoria, utalii wa kiutamaduni, utalii wa starehe labda (leissure tourism), zote hizi ni aina tofauti za utalii ambazo tunakwenda kuziboresha kwa kutekeleza miradi mbalimbali, lakini kwa mipango mbalimbali ambayo kulingana na wakati na kulingana na jinsi fedha zitakavyopatikana tunaweza kwenda kuufanya utalii ukawa bora zaidi kuliko hivi sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa fursa hii na kwa sababu muda ni wa dakika hizo ulizozitaja ambazo kwa hakika ni muda mfupi sana nichangie tu haya yafuatayo ambayo na amini yatatosha kwa muda huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza tunajadili mapendekezo ya Mpango wa mwaka 2017/2018. Mpango wenyewe bado haujaja lakini majadiliano haya ndiyo yanatarajiwa sasa yaboreshe mpango huo kabla hata haujaletwa hapa mbele yetu na ambao bado pia tutakuja kuuboresha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni Mpango wa Pili, wa mwaka moja moja kati ya ile mitano; na katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano tumejikita kwenye suala la kuelekea uchumi wa viwanda, na kila mmoja anakumbuka kwamba viwanda tunavyovizungumzia hapa zaidi ni vile ambavyo moja kwa moja vinahusiano na kilimo, kwa maana ya malighafi lakini pia kwa maana ya kuongeza thamani mazao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuzungumzia kilimo ambayo maana yake ni kwamba huwezi kuzungumzia viwanda kwa mwelekeo tunaouzungumzia bila kuzungumzia hali ya hewa. Hapa nataka kuipongeza Serikali baada ya kuleta mapendekezo haya ambapo kwenye kitabu tulichonacho hapa ni ukurasa wa nane kwenye misingi ya mpango na bajeti kati ya misingi ile saba inayotajwa pale moja wapo ni hali ya hewa. Hapa naipongeza sana serikali kwa kuzingatia hali ya hewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya hewa kwa upana wake, maana yake ni pamoja na uoto wa asili ambayo ni misitu, lakini pia ni pamoja na suala zima la tabia nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nataka tu niwakumbeshe Waheshimiwa Wabunge, kwa sababu wengi walizungumza pale awali wakitaja changamoto mbalimbali kwenye sekta hii ya mali asili. Mimi nataka niwakumbushe tu kwamba kwa hali hii ilivyo sasa ni mbaya, na hiyo inatokana na ukweli kwamba tumeharibu sana uoto wa asili, kwa maana ya kwamba misitu imeharibika sana. Tumeshatoa takwimu tukisema jumla tuna hekta milioni 48.1 za uoto wa asili, lakini hizo zinapungua kidogo….
Mheshimiwa Mwenyekiti, sentensi ya mwisho ni kwamba tutakapokuwa tunajadili mpango pale utakapokuja kule mbele ya safari, kama ambavyo mapendekezo haya yalivyopendekeza, tuzingatie hali ya hewa, na kwahiyo tuzingatie sana suala la kuhakikisha tunazilinda mali ya asili na kuzingatia masharti ya maliasili.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napenda kumrudishia sifa na utukufu Mwenyenzi Mungu kwa kila jambo. Ninamshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake kwa kutujaalia afya njema na uhai sisi Wabunge, viongozi na watumishi wote wa Bunge wa Bunge lako Tukufu na kwa kutuwezesha kumudu majukumu yetu ya kuwatumikia wananchi tukiongozwa na viongozi wetu wa wakuu wa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru wewe binafsi kwa kunipatia fursa hii adhimu ili niweze kuchangia mjadala ulioko mbele ya Bunge lako tukufu kwa kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wa mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaanza kufafanua baadhi ya hoja za Waheshimiwa Wabunge kwa kadri muda utakavyoniruhusu ninapenda kuwapongeza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiongozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Mhandisi Atashasta Justus Nditiye na Makamu wake Mheshimiwa Kemirembe Julius Lwota kwa kuendelea kuishauri na kuisimamia Wizara yetu katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru wananchi wa jimbo langu la Tunduru Kaskazini kwa kuendelea kuniamini lakini pia nashukuru familia yangu. Pia nawapongeza Waheshimiwa Wabunge wote waliopata fursa ya kuchangia kwa maandishi na kwa kuzungumza na sasa nianze kufafanua baadhi ya hoja zilizotolewa kupitia Taarifa ya Kamati ya Kudumu, Taarifa ya Kambi ya Upinzani na Waheshimiwa Wabunge mmoja mmoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Taarifa ya Kamati kutokana na muda niseme tu kwa ujumla kwamba maoni yaliyotolea kwenye Taarifa ya Kamati mengi ni maoni ambayo hakuna jambo tunaloweza kufanya isipokuwa ni kuyachukua na kwenda kuyafanyia kazi. Tunapokea maoni hayo na ushauri wote ulitolewa toka kwa Kamati kama yalivyoainishwa katika sehemu ya tatu sura ya sita ukurasa wa 22 mpaka 34 wa taarifa hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitapenda kuzungumzia tu mambo mawili kwa muda huu ulionipa. Kwanza nitazungumzia suala la WMAs ambazo kwenye Taarifa ya Upinzani limezungumzwa kwa kirefu hasa ukurasa wa 13 kuna hoja zimetajwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, imezungumzwa hoja ya mgawanyo wa mapato katika WMAs kuwa haufuatwi ipasavyo kwa mujibu wa sheria au kanuni, iko hoja ya kwamba Serikali inachukua kiasi kikubwa cha fedha kinachotokana na mapato ya utalii kwenye hizo WMAs, iko hoja inasema Serikali inachukua asilimia 55 na kuacha kiasi cha asilimia 45 peke yake kwa WMAs.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipengele hiki napenda kusema kwamba Kambi ya Upinzani iende ikaangalie upya kule ambako wameweza kuchukua taarifa hizo na hasa takwimu ili waweze kuja na takwimu ambazo ni sahihi, kwa sababu kwa mujibu wa kanuni zilizosainiwa mwaka 2012 mgawanyo wa mapato yanayotokana na utalii kwenye WMAs hauoneshi kwamba WMAs zinapata mapato kama ilivyoainishwa kwenye taarifa hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato kwenye utalii wa uwindaji yapo ya aina nyingi kama sita hivi, mimi nitaje haraka haraka tu, ipo block fees ambayo WMAs inapata asilimia 75, game fees WMAs inapata hiyo asilimia 45 na nyinginezo. Kutokana na muda kiufupi niseme tu kwamba mapato yanayotokana na shughuli za uwindaji wa kitalii WMAs zinapata mgao ambao si mdogo kulinganisha na ule ambao unakwenda kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia yapo mapato yanayotokana na utalii wa picha. Kwenye upande wa utalii wa picha kanuni zinasema kwamba WMAs zinapata asilimia 70 na wala si asilimia 45 kama ilivyoainishwa. Ninazo hizo takwimu hapa kwa mujibu wa hizo kanuni, Waziri Kivuli akizihitaji nitaweza kumpatia kwa rejea yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia lipo suala la WMA ya Burunge kwamba kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kwamba WMA ya Burunge imepata mapato yafikiayo takribani shilingi bilioni sita na kwamba WMA hiyo inaambulia shilingi milioni 800 pekee. Ukweli ni kwamba kwa sababu mgawanyo wa mapato unakwenda kwa mujibu wa sheria, ni vema tukazingatia kwamba takwimu ambazo zipo sahihi ndizo peke yake zinazoweza kutoa mwelekeo juu ya mgawanyo wa mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kama nilivyosema pale awali kwamba takwimu zilizotolewa na Kambi ya Upinzani zinatakiwa zifanyiwe marejeo kwa maana ya kwamba tunawaalika waje wazitizame kwa sababu kosa kama hili haionekani kama lingeweza kutokea kwa sababu ni kosa kubwa sana. Hii ni kwa sababu jumuiya ya hifadhi ya wanyama pori moja haiwezi kupata pato la shilingi bilioni sita ingawa hakutaja ni kipindi gani. Kwa sababu kwa mujibu wa kumbukumbu tulizonazo kama Serikali pato la shilingi bilioni sita ni pato la WMAs zote nchini, tena si kwa mwaka mmoja, ni kwa miaka mitatu yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa mapato yote ya WMAs kwa muda wa miaka mitatu, 2014/2015, 2015/2016 na 2016/2017 ni shilingi bilioni 5.515. Kwa hiyo, kwa upande huo wa takwimu niseme tu kwamba tunamkaribisha aje aweze kuchukua takwimu sahihi ili aweze kujenga hoja zake sawasawa kwa mujibu wa kumbukumbu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini iko hoja moja iliyozungumzia kuhusu ucheleweshaji wa fedha kwenda kwenye zile WMAs. Kwenye hoja hii tunauona ukweli, kwamba ni kweli kutokana na utaratibu uliopo kwa mujibu wa kanuni muda unaotumika unaweza kufanyiwa kazi na tukaweza kuupunguza ili WMAs zikaweza kupata ule mgao wao kwa wakati ambao ni pungufu ya ule wanaoupata hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninaloweza kulizungumzia kwa sasa ni suala hili la mahusiano au mwingiliano baina ya wanyamapori na shughuli za kibinadamu, hasa mashamba lakini pia makazi ya wananchi, mahali ambapo wakati mwingine hutokea wanyama huharibu mazao mashambani lakini wakati mwingine hudhuru hata wananchi; na baadhi yao hujeruhiwa na pengine wengine hupoteza maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa ninachoweza kusema ni kwamba kwanza napokea pongezi kutoka kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Nsanzugwanko akiwa mmojawapo ambaye ameipongeza Serikali kupitia Wizara kwa kudhibiti ujangili ambao matokeo yake ni kuongezeka kwa idadi ya wanyamapori hasa tembo. Tuna idadi kubwa ya tembo sasa hivi ambao wanavinjari kwenye maeneo mbalimbali, wengine walikuja mpaka UDOM juzi. Hiyo ni mafanikio kwa upande mmoja, lakini kwa upande mwingine wa pili kuna changamoto zinazotokana na ongezeko hilo la wanyamapori hao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kumekuwa kukizungumzwa jambo linalohusiana na vifuta jasho na vifuta machozi. Hapa napo pia kama Serikali kupitia Wizara tumefanya kazi kubwa kwa kulipa sehemu kubwa ya madeni yaliyodumu kwa muda mrefu ambayo kwa muda wa miaka mingi yalikuwa hayajalipwa bado. Hata hivyo, mpaka ninavyozungumza hivi sasa jumla ya fedha takribani shilingi bilioni 2.08 ambazo ni mkusanyiko wa madeni ya mpaka Disemba, 2016 yamelipwa kwa maana ya vifuta jasho na vifuta machozi. Hadi kufikia sasa deni la jumla tulilobaki nalo la vifuta jasho na vifuta machozi ni shilingi milioni 500 peke yake fedha ambazo kwa mujibu wa mpango tuliojiwekea na malengo tuliyojiwekea ndani ya mwaka wa fedha huu tulionao tunatarajia kumaliza kuzilipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema changamoto niliyonayo ni ya muda, lakini kwa ufupi nilitaka nizungumze hoja hizo mbili. Hata hivyo niseme ya mwisho inayohusiana na WMAs kwamba Taarifa ya Kambi ya Upinzani imezungumza kwa kina juu ya changamoto zilizopo kwenye WMAs. Kwa kweli baadhi ya hoja zilizotolewa lazima niseme ukweli kwamba ni hoja ambazo ni za msingi na zinapaswa kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini imekuwa bahati nzuri kwamba na sisi Serikali kwa upande wetu tarehe 9 Mei, 2017 tumekabidhi taarifa iliyofanya uchambuzi baada ya kufanya uchunguzi wa WMAs zote nchini kuangalia changamoto zao na changamoto kwa ujumla kwa mujibu wa sheria tuliyonayo na kanuni zake zinazoendesha WMAs na kwa hiyo tumeorodhesha baadhi ya hatua ambazo Serikali ni lazima ichukue ili kuweza kuboresha utendaji wa WMAs zote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, WMAs zote nchini ambazo kwa ujumla wake zipo 38, kwa sababu ya madhumuni ya msingi ya kuanzisha WMAs ambayo kimsingi ni kuboresha usimamizi, ushirikishaji wa wananchi katika kusimamia uhifadhi nchini, Serikali itahakikisha kwamba tunaongeza mikakati zaidi, mbinu zaidi lakini pia kuwekeza zaidi ili kuweza kuhakikisha kwamba madhumuni hayo ambayo tumeyaainisha kwa mujibu wa sheria yanaweza kutekelezwa kwa manufaa ya uhifadhi nchini lakini kwa lengo la juu kabisa ni pamoja na kupata yale manufaa yanayotokana na shughuli za utalii nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu yale ambayo niliona nikikadiria kwa muda niliopewa yanaweza yakatosha kwa muda huu nimekwisha yakamilisha napenda kuishia hapa na ninaunga mkono hoja, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii. Nianze kwanza kwa kusema kwamba mimi ni mmojawapo kati ya wale wanaoipongeza Serikali kwa kuja na Muswada huu wakati huu na nitakapokuwa natoa maoni yangu nitatoa sababu kwa nini naipongeza Serikali kwa namna ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme mapema kwamba mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu iliyochambua Muswada huu. Kwa hiyo, ninayo sababu pia ya kuipongeza Serikali baada ya kupitia Jedwali la Marekebisho kwa kuzingatia maoni ya Kamati kwa asilimia karibu yote. Kwa hiyo, Muswada wenyewe pamoja na maoni ya Kamati kama tulivyoyatoa kwenye Taarifa ya Kamati pamoja na Jedwali la Marekebisho, vyote naviunga mkono kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda hautoshi, hatuwezi kwenda tukarudia tena yale ambayo ni ya msingi na kila mmoja anayafahamu. Kwa mfano, suala la umuhimu wa hali ya hewa kwa Taifa, kila mmoja anajua umuhimu wa hali ya hewa, lakini nisisitize tu kwa kusema kwamba utekelezaji wa Mipango ya Serikali ya Maendeleo, iwe ni Mipango ile ya Miaka Mitano, Mpango wa Mwaka Mmoja Mmoja na hata Utekelezaji wa Dira ya Taifa kwa ujumla, bila mipango madhubuti ya masuala ya hali ya hewa ni vigumu sana kutekeleza masuala hayo ya Mipango ya Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, historia ya masuala ya usimamizi wa hali ya hewa ni ya muda mrefu tangu kabla ya ukoloni, tunaambiwa ni tangu mwaka 1929. Sheria hii ambayo sasa hivi tunaendelea kujadili na baadaye naamini tutaipitisha, yenyewe ipo kwa muda wa miaka 20 na hii ni sheria iliyounda wakala; Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997. Sasa miaka 20 ni muda mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiona sababu ya kwanza kabisa hapo haraka ya umuhimu wa Sheria hii au Muswada huu inakuwa iko wazi pale, kwamba kutoka Wakala sasa tunataka kuwa na Mamlaka kwa sababu tunataka kukabidhi majukumu ambayo yatakuwa yana uwezo wa kuwa na usimamizi zaidi wa masuala ya hali ya hewa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili limesisitizwa sana wakati tunazungumzia juu ya suala la lengo la Muswada wa sheria hii, kwamba kwenye lengo, masuala ya kuwa na taasisi moja yenye mamlaka kamili kisheria ya kuratibu, kusimamia na kudhibiti huduma za hali ya hewa nchini. Suala hili pia limesisitizwa katika hotuba ya Kamati, lakini hata katika maoni ya Kambi ya Upinzani, imeona umuhimu huo na kusema kwamba malengo yako sawa sawa na kwamba tunakusudia kuwa na sheria ambayo inaweka masharti bora zaidi ya usimamizi, utaratibu na udhibiti wa huduma za hali ya hewa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumepigia mstari kabisa kwamba masuala ya hali ya hewa hayawezi yakashughulikiwa na nchi peke yake in isolation, kwamba Tanzania hatuwezi kushughulikia masuala ya hali ya hewa peke yetu, hili ni suala la Kimataifa. Kwa hiyo, unaiona haja na sisi kuwa kwenye viwango vya Kimataifa au viwango vitakavyokubalika Kimataifa ili kuweza kusimamia masuala ya hali ya hewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo, kwa sababu muda hautoshi nitataja tu vifungu; kifungu cha 26, kifungu cha 27 na kifungu cha 28 na vinginevyo vinazungumza zaidi na kusisitiza juu ya uwepo wa umuhimu wa kuwa na vigezo vya kuwa na taasisi ambayo itakuwa na wataalam wanaokubalika Kimataifa, itakuwa na vifaa vitakavyokubalika Kimataifa na itakuwa na vigezo vyote vinavyoonesha Kimataifa kwamba vinao uwezo wa kushirikiana na taasisi za Kimataifa ikiwepo The World Meteorological Organisation, kwamba kazi zetu zitakubalika katika viwango vya Kimataifa kama tutakuwa tumefikia standards hizo zinazotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni la msingi na kwa hiyo, twende na ushauri uliotolewa kwenye Muswada ili tuweze kuwa na uhakika wa kwamba sasa tuko kwenye viwango hivyo vya Kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imetolewa hoja hapa kuhusiana na suala la uwepo wa taasisi nyingine ambazo na zenyewe zinakuwa na taarifa za masuala ya hali ya hewa. Imetajwa Tanzania Bureau of Standards, imetajwa National Bureau of Statistics, lakini nasema kwa viwango vya Kimataifa tukiwa na taasisi nyingi zinazoshughulikia suala hilo hilo la hali ya hewa, tutapoteza hiyo credibility ya kukubalika na hivyo vyombo vya Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kimataifa inatakiwa kuwe na source moja tu ambayo itakuwa inashughulikia masuala ya hali ya hewa ili yenyewe sasa ndiyo iweze kushirikiana kwa karibu zaidi na vyombo vya Kimataifa katika kushughulikia masuala ya hali ya hewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii kwenye sheria ipo na imewekwa wazi kabisa kwenye kifungu cha nne, kwa ruhusa yako, haraka haraka tu noisome: “The Authority shall, for the purpose of collaboration and cooperation with international organisations relating to meteorological issues being… yakatajwa hayo ambayo yanatakiwa yafanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama kweli tunataka kuwa na taasisi itakayokuwa inaaminika Kimataifa ya kuweza kufanya shughuli za meteorology, lazima tuwe na taasisi iliyoko kwenye viwango bora kwa sura pana. Nimezungumzia vifaa, wataalam na utekelezaji wa majukumu yenyewe Kimataifa ili iweze kukubalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini hata TBS, hata National Bureau of Statistics, wao wakiwa wanataka au wanahitaji takwimu hizi kwa ajili ya custodianship na kwa ajili ya kuzi-distribute, basi itakuwa labda baada ya kibali cha kutoka kwa Mamlaka hii tunayokusudia kuiunda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeanza kuzungumzia suala la Muswada wa Hali ya Hewa, lakini sasa haraka haraka tu, niende nizungumzie Muswada wa Barabara (The Land Transport Regulatory Authority Act, 2018).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa zimetolewa hoja nami nataka nizichangie. Kwanza ni kuhusiana na suala la ajali. Ajali nyingi za barabarani zinatokana zaidi na makosa ya watumiaji barabara ambayo ni makosa ya kibinadamu. Tafiti zimefanyika na imedhihirika wazi kwamba barabara kama barabara au vyombo vya usafiri kama magari na vinginevyo, mchango wake kwenye ajali ni mdogo sana. Sehemu kubwa, asilimia zaidi ya 70, inatokana na watumiaji wa hizo barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa sababu hiyo, ni vyema tukaangalia umuhimu wa kuzingatia namna ya kuweza kudhibiti matumizi ya barabara na matumizi ya vyombo vya moto au vyombo vyote vinavyotumia barabara ili tuweze kupunguza ajali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lilikuwepo suala linalohusiana na wataalam watakaokuwa wanafanya kazi kwenye eneo hili linalosimamiwa na LATRA kwa ujumla wake. Niliona tunazungumzia juu ya suala la ubora wa miradi inayotekelezwa, hasa ya ujenzi wa barabara kwamba lazima ziwe zimefikia vigezo vya gharama, muda na ubora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kwamba katika miaka ya hivi karibuni tumekwenda zaidi ya hapo, tumesema kwamba mahitaji ya wadau (stakeholders’ interests) yameongezeka kuwa ni jambo moja la muhimu na la msingi la kuweza kulizingatia. Tumeongeza lingine, tumesema kudumu kwa masuala hayo (sustainability) ili iweze kuendana na mipango ya maendeleo endelevu duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, limekuepo suala juu ya wataalam kwamba wasiingiliwe kwenye utekelezaji wa majukumu yao. Nami kama mmojawapo wa wataalam, mmojawapo wa wahandisi; naunga mkono, wataalam wasiingiliwe, waachwe watekeleze majukumu yao kitaalam.

Pia tuzingatie ukweli kwamba mtaalam huyo ambaye hapaswi kuingiliwa ni yule tu ambaye anazingatia masharti ya maadili ya taaluma. Kama hazingatii masharti ya maadili ya taaluma, basi utaalam wake unaweza ukawa intervened na watu ambao watakuwa wanaona wazi kwamba hazingatii masharti hayo ya taaluma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kila mtu anajua barabara nzuri kwa macho na kama mtumiaji, anajua tu barabara ni nzuri. Sasa huwezi kuwa na barabara ambayo umeijenga umemaliza leo, baada ya miezi mitatu ikaharibika, halafu ukiulizwa useme usinihoji kwa sababu mimi ni mtaalam. Mtu akiangalia ukuta umepinda, akionyesha kwa macho akikwambia mimi nimenyoosha halafu wewe unasema umetumia kifaa kunyoosha wakati kila mtu anaona kwamba ukuta umepinda, haitakuwa sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, pamoja na kutetea wataalam, mimi mwenyewe kwenye uhandisi huko nimebobea kiasi cha kutosha, ni registered fellow, lakini tunaambiana na kukumbushana kila siku, kwamba ni lazima tuzingatie masharti ya maadili ya kitaalam ili tuweze kukwepa huko kunakoitwa kuingiliwa ili tuweze kui-convince jamii kwamba tunaweza tukafanya kazi zetu sawa sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo machache, nimalizie tu kwa kusema kwamba uchambuzi wa kifungu baada ya kifungu, naamini wakati utakapofika, wakati wa Kamati, tutaweza kupata nafasi ya kuweza kuchangia vizuri zaidi maana kuna vifungu vimekosolewa, kuna vifungu vimechangiwa nami nimeona baadhi ya maeneo ziko hoja za kuweza kujadili zinahitaji input ya kutoka kwa Wajumbe wa Kamati na washiriki wengine wa ndani na Waheshimiwa Wabunge wengine. Kwa hiyo, wakati utakapofika huo wa kujadili vifungu, mimi nitakuwa miongoni mwa wale ambao watakuwa tayari kutoa michango yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema naipongeza Serikali, kwa sababu kwa mfano kwenye Muswada huu wa Hali ya Hewa, vifungu 13 kati ya 59 tulivyonavyo, Serikali imekubaliana na maoni ya Kamati. Kwa hiyo, kwa muktadha huo, sina mashaka kwamba Sheria hii au Muswada huu tunapokwenda kuujadili sasa katika ngazi ya Kamati, kwa maana ya kifungu baada ya kifungu, maeneo mengi sana tunayo majibu kama Kamati na ambayo sikuweza kuyatoa sasa hivi kwa sababu muda hautoshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii. Nianze kwanza kwa kusema kwamba mimi ni mmojawapo kati ya wale wanaoipongeza Serikali kwa kuja na Muswada huu wakati huu na nitakapokuwa natoa maoni yangu nitatoa sababu kwa nini naipongeza Serikali kwa namna ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme mapema kwamba mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu iliyochambua Muswada huu. Kwa hiyo, ninayo sababu pia ya kuipongeza Serikali baada ya kupitia Jedwali la Marekebisho kwa kuzingatia maoni ya Kamati kwa asilimia karibu yote. Kwa hiyo, Muswada wenyewe pamoja na maoni ya Kamati kama tulivyoyatoa kwenye Taarifa ya Kamati pamoja na Jedwali la Marekebisho, vyote naviunga mkono kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda hautoshi, hatuwezi kwenda tukarudia tena yale ambayo ni ya msingi na kila mmoja anayafahamu. Kwa mfano, suala la umuhimu wa hali ya hewa kwa Taifa, kila mmoja anajua umuhimu wa hali ya hewa, lakini nisisitize tu kwa kusema kwamba utekelezaji wa Mipango ya Serikali ya Maendeleo, iwe ni Mipango ile ya Miaka Mitano, Mpango wa Mwaka Mmoja Mmoja na hata Utekelezaji wa Dira ya Taifa kwa ujumla, bila mipango madhubuti ya masuala ya hali ya hewa ni vigumu sana kutekeleza masuala hayo ya Mipango ya Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, historia ya masuala ya usimamizi wa hali ya hewa ni ya muda mrefu tangu kabla ya ukoloni, tunaambiwa ni tangu mwaka 1929. Sheria hii ambayo sasa hivi tunaendelea kujadili na baadaye naamini tutaipitisha, yenyewe ipo kwa muda wa miaka 20 na hii ni sheria iliyounda wakala; Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997. Sasa miaka 20 ni muda mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiona sababu ya kwanza kabisa hapo haraka ya umuhimu wa Sheria hii au Muswada huu inakuwa iko wazi pale, kwamba kutoka Wakala sasa tunataka kuwa na Mamlaka kwa sababu tunataka kukabidhi majukumu ambayo yatakuwa yana uwezo wa kuwa na usimamizi zaidi wa masuala ya hali ya hewa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili limesisitizwa sana wakati tunazungumzia juu ya suala la lengo la Muswada wa sheria hii, kwamba kwenye lengo, masuala ya kuwa na taasisi moja yenye mamlaka kamili kisheria ya kuratibu, kusimamia na kudhibiti huduma za hali ya hewa nchini. Suala hili pia limesisitizwa katika hotuba ya Kamati, lakini hata katika maoni ya Kambi ya Upinzani, imeona umuhimu huo na kusema kwamba malengo yako sawa sawa na kwamba tunakusudia kuwa na sheria ambayo inaweka masharti bora zaidi ya usimamizi, utaratibu na udhibiti wa huduma za hali ya hewa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumepigia mstari kabisa kwamba masuala ya hali ya hewa hayawezi yakashughulikiwa na nchi peke yake in isolation, kwamba Tanzania hatuwezi kushughulikia masuala ya hali ya hewa peke yetu, hili ni suala la Kimataifa. Kwa hiyo, unaiona haja na sisi kuwa kwenye viwango vya Kimataifa au viwango vitakavyokubalika Kimataifa ili kuweza kusimamia masuala ya hali ya hewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo, kwa sababu muda hautoshi nitataja tu vifungu; kifungu cha 26, kifungu cha 27 na kifungu cha 28 na vinginevyo vinazungumza zaidi na kusisitiza juu ya uwepo wa umuhimu wa kuwa na vigezo vya kuwa na taasisi ambayo itakuwa na wataalam wanaokubalika Kimataifa, itakuwa na vifaa vitakavyokubalika Kimataifa na itakuwa na vigezo vyote vinavyoonesha Kimataifa kwamba vinao uwezo wa kushirikiana na taasisi za Kimataifa ikiwepo The World Meteorological Organisation, kwamba kazi zetu zitakubalika katika viwango vya Kimataifa kama tutakuwa tumefikia standards hizo zinazotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni la msingi na kwa hiyo, twende na ushauri uliotolewa kwenye Muswada ili tuweze kuwa na uhakika wa kwamba sasa tuko kwenye viwango hivyo vya Kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imetolewa hoja hapa kuhusiana na suala la uwepo wa taasisi nyingine ambazo na zenyewe zinakuwa na taarifa za masuala ya hali ya hewa. Imetajwa Tanzania Bureau of Standards, imetajwa National Bureau of Statistics, lakini nasema kwa viwango vya Kimataifa tukiwa na taasisi nyingi zinazoshughulikia suala hilo hilo la hali ya hewa, tutapoteza hiyo credibility ya kukubalika na hivyo vyombo vya Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kimataifa inatakiwa kuwe na source moja tu ambayo itakuwa inashughulikia masuala ya hali ya hewa ili yenyewe sasa ndiyo iweze kushirikiana kwa karibu zaidi na vyombo vya Kimataifa katika kushughulikia masuala ya hali ya hewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii kwenye sheria ipo na imewekwa wazi kabisa kwenye kifungu cha nne, kwa ruhusa yako, haraka haraka tu noisome: “The Authority shall, for the purpose of collaboration and cooperation with international organisations relating to meteorological issues being… yakatajwa hayo ambayo yanatakiwa yafanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama kweli tunataka kuwa na taasisi itakayokuwa inaaminika Kimataifa ya kuweza kufanya shughuli za meteorology, lazima tuwe na taasisi iliyoko kwenye viwango bora kwa sura pana. Nimezungumzia vifaa, wataalam na utekelezaji wa majukumu yenyewe Kimataifa ili iweze kukubalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini hata TBS, hata National Bureau of Statistics, wao wakiwa wanataka au wanahitaji takwimu hizi kwa ajili ya custodianship na kwa ajili ya kuzi-distribute, basi itakuwa labda baada ya kibali cha kutoka kwa Mamlaka hii tunayokusudia kuiunda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeanza kuzungumzia suala la Muswada wa Hali ya Hewa, lakini sasa haraka haraka tu, niende nizungumzie Muswada wa Barabara (The Land Transport Regulatory Authority Act, 2018).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa zimetolewa hoja nami nataka nizichangie. Kwanza ni kuhusiana na suala la ajali. Ajali nyingi za barabarani zinatokana zaidi na makosa ya watumiaji barabara ambayo ni makosa ya kibinadamu. Tafiti zimefanyika na imedhihirika wazi kwamba barabara kama barabara au vyombo vya usafiri kama magari na vinginevyo, mchango wake kwenye ajali ni mdogo sana. Sehemu kubwa, asilimia zaidi ya 70, inatokana na watumiaji wa hizo barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa sababu hiyo, ni vyema tukaangalia umuhimu wa kuzingatia namna ya kuweza kudhibiti matumizi ya barabara na matumizi ya vyombo vya moto au vyombo vyote vinavyotumia barabara ili tuweze kupunguza ajali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lilikuwepo suala linalohusiana na wataalam watakaokuwa wanafanya kazi kwenye eneo hili linalosimamiwa na LATRA kwa ujumla wake. Niliona tunazungumzia juu ya suala la ubora wa miradi inayotekelezwa, hasa ya ujenzi wa barabara kwamba lazima ziwe zimefikia vigezo vya gharama, muda na ubora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kwamba katika miaka ya hivi karibuni tumekwenda zaidi ya hapo, tumesema kwamba mahitaji ya wadau (stakeholders’ interests) yameongezeka kuwa ni jambo moja la muhimu na la msingi la kuweza kulizingatia. Tumeongeza lingine, tumesema kudumu kwa masuala hayo (sustainability) ili iweze kuendana na mipango ya maendeleo endelevu duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, limekuepo suala juu ya wataalam kwamba wasiingiliwe kwenye utekelezaji wa majukumu yao. Nami kama mmojawapo wa wataalam, mmojawapo wa wahandisi; naunga mkono, wataalam wasiingiliwe, waachwe watekeleze majukumu yao kitaalam. Pia tuzingatie ukweli kwamba mtaalam huyo ambaye hapaswi kuingiliwa ni yule tu ambaye anazingatia masharti ya maadili ya taaluma. Kama hazingatii masharti ya maadili ya taaluma, basi utaalam wake unaweza ukawa intervened na watu ambao watakuwa wanaona wazi kwamba hazingatii masharti hayo ya taaluma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kila mtu anajua barabara nzuri kwa macho na kama mtumiaji, anajua tu barabara ni nzuri. Sasa huwezi kuwa na barabara ambayo umeijenga umemaliza leo, baada ya miezi mitatu ikaharibika, halafu ukiulizwa useme usinihoji kwa sababu mimi ni mtaalam. Mtu akiangalia ukuta umepinda, akionyesha kwa macho akikwambia mimi nimenyoosha halafu wewe unasema umetumia kifaa kunyoosha wakati kila mtu anaona kwamba ukuta umepinda, haitakuwa sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, pamoja na kutetea wataalam, mimi mwenyewe kwenye uhandisi huko nimebobea kiasi cha kutosha, ni registered fellow, lakini tunaambiana na kukumbushana kila siku, kwamba ni lazima tuzingatie masharti ya maadili ya kitaalam ili tuweze kukwepa huko kunakoitwa kuingiliwa ili tuweze kui-convince jamii kwamba tunaweza tukafanya kazi zetu sawa sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo machache, nimalizie tu kwa kusema kwamba uchambuzi wa kifungu baada ya kifungu, naamini wakati utakapofika, wakati wa Kamati, tutaweza kupata nafasi ya kuweza kuchangia vizuri zaidi maana kuna vifungu vimekosolewa, kuna vifungu vimechangiwa nami nimeona baadhi ya maeneo ziko hoja za kuweza kujadili zinahitaji input ya kutoka kwa Wajumbe wa Kamati na washiriki wengine wa ndani na Waheshimiwa Wabunge wengine. Kwa hiyo, wakati utakapofika huo wa kujadili vifungu, mimi nitakuwa miongoni mwa wale ambao watakuwa tayari kutoa michango yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema naipongeza Serikali, kwa sababu kwa mfano kwenye Muswada huu wa Hali ya Hewa, vifungu 13 kati ya 59 tulivyonavyo, Serikali imekubaliana na maoni ya Kamati. Kwa hiyo, kwa muktadha huo, sina mashaka kwamba Sheria hii au Muswada huu tunapokwenda kuujadili sasa katika ngazi ya Kamati, kwa maana ya kifungu baada ya kifungu, maeneo mengi sana tunayo majibu kama Kamati na ambayo sikuweza kuyatoa sasa hivi kwa sababu muda hautoshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa fursa hii lakini nianze kwa kuipongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa namna ambavyo tumekuwa tukishirikiana kufanya kazi na kutekeleza majukumu yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti,pia nichukue nafasi hii kusema kabisa mapema kwamba naunga mkono maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati, nasema mapema kwa sababu pengine muda hautatosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ziko hoja ambazo nitazipitia haraka haraka katika muda huu mfupi uliopo. Hoja ya kwanza, naona wazi kabisa kwamba Wabunge wote wanakubaliana juu ya umuhimu wa utalii nchini hata michango yao na hoja zote walizozitoa zimejielekeza hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kukumbushana tu ni kwamba kwa sasa hivi Pato la Taifa linachangiwa na utalii kwa 17.2% wengine wanasema 17.5% lakini tuna kazi ya kuendelea kuboresha kwa sababu mwaka 2020 tunatakiwa tuwe tumefikia 18.3% na mwaka 2025 tunatakiwa tuwe tumefikia 19.5%. Yapo mambo ambayo tumekumbushwa na Kamati kwamba tuyafanye vizuri na Wizara imeyachukua kwa ajili ya kwenda kuyafanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa mambo hayo kuboresha miundombinu, lakini nataka nikumbushe tu kwamba upande wa miundombinu sio kila miundombinu ya utalii inatekelezwa na Serikali. Ipo inayotekelezwa na Serikali ambayo ni ile ya kuelekea kwenye vivutio na ile ya ndani ya vivutio tutaelekeza nguvu katika maeneo hayo kwa kushirikiana na Wizara nyingine kama Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu lakini iko miundombinu kama ya hoteli ambayo haitekelezwi na Serikali. Kwa hiyo, kule tutashirikisha tu wadau na sekta binafsi ili waweze kuboresha miundombinu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la kuboresha utalii wa ndani, tayari tumekwishaanza jitihada na jitihada zenyewe ziko katika kutangaza lakini pia katika kuweka mazingira ambayo yatawawezesha watalii wa ndani waweze kupata huduma ya usafiri kwenda haraka. Upande mwingine wa ku-facilitate utalii wa ndani ni upande wa malazi. Wapo Wabunge wametoa hoja hapa kwamba gharama za malazi ni ghali sana kule pengine Serikali ifanye utaratibu wa kupunguza gharama. Katika hifadhi karibu nane au tisa hivi tunazo tayari hostels ambazo zina gharama nafuu lakini pia tunazo nyumba za bei rahisi kwa ajili ya watalii wa ndani, lakini tutaendeleza jitihada hizi ili katika kila eneo ambapo kuna vivutio tuweze kuweka mazingira ambayo watalii wanaweza wakaenda wakiwemo watalii wa ndani na waweze kufanya utalii kwa gharama nafuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo suala la kuboresha upande wa Ukanda wa Kusini. Upande wa Ukanda wa Kusini tayari tuna mradi unaitwa REGROW ambao unajielekeza katika kujenga circuit ya Kusini ya utalii na huku tunajielekeza katika hifadhi kama vile ya Kitulo lakini pia zile nyingine za Katavi lakini pia ukanda mzima ule. Hapa niishukuru Serikali kwa kufungua upande wa Kusini mwa nchi, baada ya kuwekwa barabara ya lami sasa unaweza ukatoka Makambako ukafika mpaka Mtwara kwa barabara ya lami. Barabara ile inaweza sasa ikatumiwa vizuri sana na watalii wanaotoka Kusini mwa Afrika wakitokea upande wa mpaka wetu wa Kusini mwa nchi wanaweza wakatumia barabara ile sasa na kuunganisha Kusini na Mashariki mwa nchi kwa ajili ya kuboresha utalii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuboresha bidhaa za utalii kwamba tuna utalii wa aina moja, nataka niseme tu kwamba tayari tumeshapitia fukwe mbalimbali za bahari na maziwa lakini kwa upande wa fukwe za bahari tumeshapitia fukwe karibu 74 lakini hizi fukwe zina ownership mbalimbali. Wenye hizo fukwe ni watu binafsi, mahali pengine ni Serikali, sasa bado tuko kwenye utaratibu wa kuhakikisha kwamba tunaboresha mazingira ambayo yatawezesha uwekezaji katika maeneo hayo ili tuweze kujielekeza kwenye maeneo mengine ya utalii ukiwemo utalii wa kiutamaduni na utalii wa kihistoria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumzia utalii ingawaje ni kwa kifupi tu nizungumzie kuhusu uhifadhi. Hakuna utalii bila uhifadhi. Suala la uhifadhi limejadiliwa hapa kwa hisia mbalimbali, Waheshimiwa Wabunge wengi sana wamezungumzia kuhusu changamoto mbalimbali za uhifadhi. Kwa sababu ya muda, mimi niseme tu kwa kifupi, niseme maoni yote yaliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge, interest zote za wadau mbalimbali nchi nzima, maslahi ya mtu mmoja mmoja, maslahi ya vikundi mbalimbali yote yatazingatiwa lakini mwisho wa siku tutazingatia maslahi ya Taifa. Ni vigumu sana kukidhi haja ya maslahi ya mtu mmoja au kikundi wakati maslahi ya Taifa yanaangamia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kifupi nikisema hivyo nikienda kujielekeza sasa kwenye zile changamoto za uhifadhi niseme tu kwamba maeneo yote na hii nachukua kutoka kwenye hoja na maoni ya Kamati kwamba hakuna utata kuhusu suala la mifugo yote kuondoka ndani ya Hifadhi za Taifa. Tulisema kwamba yako maeneo ambayo mipaka ya baadhi ya vijiji inaingia ndani ya hifadhi na yako maeneo ambapo baadhi ya vijiji viko ndani kabisa ya hifadhi. Sasa huko kuna changamoto ambazo ni za kisheria zimo ndani ya Serikali, tunazifanyia kazi, tutaweza kuja kupambanua kujua kwamba sasa vijiji vile ambavyo vina utata wa namna hiyo tupitie sheria kwa namna gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, viko vivutio vikubwa muhimu sana kama Ngorongoro kwa mfano kutaja vichache. Ngorongoro umuhimu umeelezwa, lakini mimi niongezee tu kwamba hapo mwanzoni tulikuwa na umuhimu wa Ngorongoro kwa sababu ya Crater zile tatu, Ngorongoro Crater yenyewe, Empakai Crater na Olmoti Crater. Hata hivyo, hivi karibuni utalii wa historia umejumuisha eneo la Olduvai Gorge pamoja na zile nyayo za Laetoli. Haya mawili yamefanya kupandisha hadhi ya Hifadhi ya Ngorongoro kuwa kubwa zaidi na kwa hiyo dunia nzima sasa hivi inakwenda kuona umuhimu wa Ngorongoro zaidi ya vile ambavyo tulikuwa tunaona hapo mwanzoni. Sasa zile changamoto za mifugo kuingia ndani, watu kujenga ndani majengo pamoja na watu kufanya huduma zingine za kijamii zote hizo sasa hivi ni changamoto ambazo tunatakiwa kwenda…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususan miradi ya ujenzi. Nashauri:-

(i) Kandarasi zitolewe kwa ushindani lakini kwa kuzingatia fursa maalum kwa makampuni ya wazalendo na wataalam wazalendo – Wakandarasi, Wahandisi Washauri, Wabunifu na Wakadiriaji Wajenzi na kadhalika. Hii itaboresha zaidi.

(ii) Kujenga uwezo wa ndani ya nchi kwa ajili ya matengenezo (maintanance) ya miradi hiyo na miradi mipya.

(iii) Kuiwezesha sekta kuchangia zaidi uchumi wa nchi na kadhalika.

(iv) Miradi mikubwa yote itumike kama madarasa (vituo vya mafunzo) kwa vitendo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu , vyuo vya kati lakini pia kwa wahitimu wa shahada na stashahada kupitia bodi ili kuhamishia ujuzi na utaalam kwa vitendo nchini. Mifano, bomba la mafuta - Hoima, Stiegler’s Gorge - umeme, madaraja makubwa, viwanja vya ndege vikubwa, reli – Standard Gauge(SGR), majengo makubwa na yenye mahitaji mahsusi na kadhalika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na pongezi kwa Wizara inafanya mageuzi makubwa katika sekta na hivyo kuboresha huduma za afya kwa upana wake. Hongera kwa timu nzima ya Wizara ikiongozwa na Waziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu na wataalam wote na wasaidizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Tunduru na Jimbo la Tunduru Kaskazini, katika Hospitali ya Wilaya chumba cha upasuaji tunaomba replacement na improvement ya vifaa hususan operation beds/tables ikiwa ni pamoja na ukarabati wa chumba chenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uhaba wa wataalam, nafahamu changamoto hii iko karibu katika maeneo yote nchini, naomba Wilaya ya Tunduru itazamwe kama eneo la pembezoni na lililosahaulika kwa miaka mingi (disadvantaged). Tunaomba apatikane DMO kwani aliyepo anakaimu nafasi hiyo. Pia kuna uhaba mkubwa katika vituo vya afya na zahanati hususan Kituo cha Afya cha Matemanga na Nakapanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Matemanga kilitengewa fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa madhumuni ya ukarabati na uboreshaji wa vifaa. Fedha hizo hatujaletewa hadi leo na taarifa za awali nilizonazo, fedha hizo zimepelekwa eneo lingine. Sio muhimu sana kupata/kujua sababu ya kuwa diverted fedha hizo, lakini ninaomba tupatiwe fedha kama ilivyopangwa awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna mahitaji ya gari la wagonjwa; nimesikiliza hotuba iliyosomwa na Mheshimiwa Waziri wa Afya, hongera kwa kutenga fedha kwa ajili ya magari ya wagonjwa (ambulance) 17. Ombi langu ni kupewa angalau gari moja kwa Tunduru Kaskazini ambako Hospitali ya Wilaya iko. Izingatiwe pia kwamba (location) mahali Hospitali ya Wilaya ilipo inasababisha baadhi ya wanaohitaji huduma za rufaa kutoka katika zahanati wanatoka umbali wa kufikia hadi kilometa takribani 100.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Kituo cha Afya Nakapanya, tumekamilisha ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hiki. Ombi ni kupatiwa vifaa vya upasuaji na vingine vinavyoendana na hivyo. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, hongera kwa timu nzima ya Wizara kwa kuendelea kuchapa kazi kwa ufanisi. Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi, wataalam na supporting staff wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu barabara na madaraja, nashukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuitengea fedha miradi ifuatayo katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, Daraja la Fundimbanga, barabara ya Mkoa – Mjimwema – Ngapa – Tunduru - Nachingwea Border.Ninaomba utekelezaji wa miradi ifuatayo ambayo kimsingi ni ukamilishaji wa miradi ya barabara ya Nakapanga – Tunduru itengewe fedha ili ikamilike.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya mchepuo (bypass) ya Mkapunda – Masonya, mzunguko wa barabara (roundabout) – crossroad location. Barabara hii ya Mjimwema –Ngapa – Tunduru/Nachingwea Border ni barabara ya mkoa na ni ya kiwango cha udongo (earth road), ni vema kuweka katika mpango kutenga fedha na kuijengea barabara hii kwa kuwa inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Lindi. Pia kuna daraja la Mto Lumesule katika barabara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uwanja wa ndege wa Tunduru, nafahamu kuwa vipaumbele kwa sasa vimewekwa katika viwanja vikubwa, viwanja vya Mikoa na vya kimkakati. Lakini ni ushauri wangu kwamba vigezo/ vipaumbele vijumuishe maeneo ya mpakani, maeneo yaliyoko mbali sana na viwanja vya ndege vinapotumika; kwa Tunduru kilometa 410 na kilometa 262 kutoka pande zote mbili, viwanja vya ndege vilivyokuwepo vikafungwa maeneo mapya yaliyofunguka na yenye potentials za kuchangia uchumi wa Taifa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba uwanja wa Tunduru upewe kipaumbele.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi kwa Wizara. Hongera sana kwa timu nzima kwa kazi nzuri, Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, wataalam na wasaidizi wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maeneo ya Kihistoria, Utamaduni, Mila na Desturi. Eneo la Masonya Wilayani Tunduru ni tajiri sana kwa mahitaji haya. Ni ombi langu eneo hili liboreshewe miundombinu yake, kutangazwa na kuendelezwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya malikale na utalii ni muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema kushirikisha machifu katika Wilaya ya Tunduru. Chiefdoms bado zina wazee wenye taarifa kubwa na muhimu, licha ya taarifa kutoka halmashauri ya wilaya; Chief Mataka, Chief Ntalika, Chief Kanduru, Chief Mbalamula, Chief Nakoko, kwa kuanzia. Ni vizuri hatimaye huko siku zijazo tukawa na orodha, directory ya maeneo haya muhimu yote na ikazinduliwa kwa matumizi ya kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Ukombozi wa Kusini mwa Afrika hauwezi kuzungumziwa ukakamilika bila kutaja Wilaya ya Tunduru. Kituo cha Masonya ni maarufu kama kambi ya kimkakati kwa harakati za ukombozi wa Msumbiji. Yapo makazi na maficho ya Samora Machel, Mwalimu Nyerere na wengineo. Nashauri Mheshimiwa Waziri atembelee kambi hii tukiongozana nami, ili aone umuhimu wa eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Usikivu wa Redio (TBC). Kukatikakatika na kupotea kwa matangazo, pia usikivu hafifu katika baadhi ya nyakati ni mambo yanayowakera wananchi wa Tunduru. Tunaomba ufuatiliaji na ufumbuzi wa tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maadili, utamaduni, mila, desturi katika Wilaya ya Tunduru huenda hili likawa ni tatizo la Taifa zima. Vinaathiriwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia, hususan, simu za viganjani, TV na kadhalika, kiasi ambacho hata vijijini ngoma za asili zinapotea maadili ya Mtanzania na makabila unapotea. Nini mkakati wa Serikali?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi kwa Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu, wataalam na wasaidizi. Hongereni sana kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni skills development levy; kwa kuwa Wizara ya Elimu ndiyo yenye dhamana, ni vyema ikashauri vyema zaidi juu ya madhumuni ya msingi ya uanzishwaji wa tozo hii. Ni skills zipi zilikusudiwa? Je, kuna mabadiliko ya aina ya skills? Je, ukusanyaji wa tozo hii wa matumizi yake unahitaji kufanyiwa marejesho? Kwa kifupi, jambo hili linatakiwa kutazamwa upya kwa makini zaidi na kwa kushirikisha wadau (wachangiaji) ili na wao wapate huduma zaidi ya kuendelea kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu Vyuo vya Ufundi Stadi. Wilaya ya Tunduru jiografia yake ikiweka mbali sana na Vyuo va Ufundi. Hivyo kuwafanya wahitimu wa elimu ya msingi na hata wa sekondari kukosa fursa hiyo ambayo ingeweza kuwakwamisha kiuchumi na wakachangia uchumi wa Taifa. Pia tunamwomba kuwa considered.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, inawezekana kupandisha hadhi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Nandembo na kuwa Chuo cha VETA na elimu zote zikatolewa hapo hapo? Tunaomba kuwa miongoni mwa wanufaika katika miradi ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kama ilivyoidhinishwa katika kitabu cha bajeti ukurasa wa 124 (item iv).
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi kwa Wizara, Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Wakuu wa Taasisi chini ya Wizara, wataalam, Wenyeviti wa Bodi na kikosi kizima cha Wizara. Majukumu ya Wizara hii ni mengi, makubwa na magumu, tunafahamu, lakini jitihada zenu zinaonekana. Hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Shukrani. Nimrona miradi michache ambayo jimbo langu limebahatika kutengewa fedha, baadhi ni ile inaendelea, hususan ule wa huduma ya maji, Tunduru Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Mradi wa Maji Tunduru Mjini, tunaomba kasi ya utekelezaji iongezeke ili mradi huu ukamilike haraka iwezekanavyo. Tunaomba ukamilifu wa mradi kwa viwango vya kitaalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Miradi ya Maji Vijijini, hali sio nzuri kwa upatikanaji wa huduma za maji vijijini katika Jimbo langu la Tunduru Kaskazini. Kwa kuanzia, naomba vijiji vifuatavyo vipewe kipaumbele; Nakapanya, Muhunesi, Majmaji, Sisi Kwa Sisi, Cheleweni, Huria, Namwinyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, wahandisi, mafundi sanifu na mafundi sadifu; kuna uhaba mkubwa sana wa wataalam katika Wilaya ya Tunduru. Katika hali hii ni vigumu kupata ushauri sahihi kusimamia miradi kwa uhakika na kutekeleza majukumu ya kitaalam. Ushauri huu ni kwa Taifa zima.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushirikiano kati ya wataalam wa Halmashauri ya Wilaya na wale wa Mamlaka ya Mkoa au Mhandisi wa Maji wa Mkoa ni vema kanuni na taratibu zilizopo zikaangaliwa upya. Iwapo kuna kasoro za kisera, kisheria, kanuni na taratibu zirekebishwe na iwapo tatizo ni utekelezaji tu basi wahusika wapewe miongozo kwa msisitizo na wale wanaokaidi bila kujali ni mara ngapi wameshauriwa wachukuliwe hatua stahiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana timu nzima ya Wizara ikiongozwa na Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu kwa kazi nzuri mnayoendelea kuitekeleza Wizarani ili sekta ya kilimo iendelee kuwa miongoni mwa sekta kiongozi katika kuchangia uchumi wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa zinaonesha kuwa kuna uhaba wa Maafisa Ugani kwa viwango vikubwa. Ni vema kwanza Serikali ikaandaa kanzidata (database) ili kujua idadi na ujuzi walionao wale wachache waliopo kwa madhumuni ya kuandaa mkakati kutatua tatizo, skills maalum kwa maeneo maalum, idadi kulingana na mahitaji ya kila eneo, kipaumbele kwa maeneo yenye umuhimu kimkakati; kwa mfano katika uzalishaji wa mahindi the big four regions, na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifano ya uhaba mkubwa wa Maafisa Ugani (Sera ya Afisa mmoja kila kijiji), katika hotuba ya bajeti ukurasa 47 Mkoa mzima wa Kagera, licha ya kuwa mkoa wenye shughuli kubwa na nyingi za kilimo, inao Maafisa Ugani 548 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Tunduru yenye mahitaji ya Maafisa Ugani 227 inao 72 tu, sawa na asilimia 32. Hali hii inasababisha changamoto nyingi kama wakulima kutojua viuatilifu sahihi, viwango na matumizi sahihi. Pia aina za udongo katika maeneo na mazao yanayofaa kustawishwa na kadhalika. Wananchi wengi wanapata mavuno wanayodhani ni mengi katika eneo la ukubwa ambao wangezalisha zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda, Wilaya ya Tunduru imefikia uzalishaji wa tani 20,000 za korosho mwaka 2017/2018. Wilaya ina kiwanda kimoja tu cha kubangua korosho chenye uwezo wa kubangua tani 3400 tu sawa na asilimia 17 tu. Ili kuendana na mkakati wa Kitaifa wa uchumi wa viwanda na ili kuongeza thamani na kuongeza pato kwa mkulima, Halmashauri na Taifa kwa ujumla, lengo (ndoto) ni kubangua korosho zote. Ili tufikie katika lengo la ubanguaji kwa asilimia 100 au karibu na hiyo, tunahitaji viwanda vingi zaidi kama ilivyo kwa nchi kama ya India wanaofanya vizuri. Viwanda hivi ni vidogo na vya kati vyenye wamiliki wa uwezo mdogo hadi wa kati. Viwanda hivyo vinahitaji malighafi, lakini ununuzi wa korosho ghafi unasimamiwa na Sheria ya Tasnia ya Korosho. Kanuni zake na Mwongozo Na. 1 wa mwaka 2017/2018 wa mauzo ya korosho. Sheria, Kanuni na Mwongozo huo siyo rafiki kwa utekelezaji wa hitaji hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itathmini kwa kina jambo hili.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA), ni muhimu kukawa na mtawanyiko mzuri zaidi nchi nzima ili kuwapatia wahitimu husika Form IV, STD VII, hata Form VI wasiopata fursa nyinginezo “Alternative Route” kuelekea maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla. Wilaya ya Tunduma iko mpakani, ni ya siku nyingi (1905) na iko mbali na Vyuo vya aina hiyo, (ukiacha chuo kimoja tu binafsi ambacho access ya wananchi wengi ni limited kutokana na gharma kuwa juu. Tunaomba Wilaya hii ipewe kupaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali inaendelea kukamilisha taratibu za kuwaajiri Walimu waliohitimu katika vyuo na ngazi mbalimbali na wakati kuna uhaba mkubwa wa walimu katika shule zetu, napendekeza Serikali iweke utaratibu wa kuwapa mikataba ya muda mfupi mfupi walimu hao kwa “kujitolea.” Ni wazi kutajitokeza mahitaji ya Resources kidogo. Hata hivyo, wapo baadhi watajitokeza kufanya hivyo. Wanachohitaji ni kutambuliwa na kuwafanya wawe active katika taaluma. Inawezekana pia “motisha” ikawa ni kupata kipaumbele ajira zinapojitokeza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi kwa Serikali kwa ujumla na kwa Wizara kwa namna ya pekee kwa kazi nzuri. Changamoto za Wizara hii (Sekta ya Afya) ni nyingi na za muda mrefu na za aina mbalimbali, hivyo, hata utatuzi wake unahitaji muda, rasilimali fedha na kadhalika, lakini taratibu zitapungua sana kutokana na kasi hii. Nawatakikakila la kheri.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto Kitaifa, ziko nyingi bado, lakini hotuba ya Waziri Ukarasa 155 wa kitabu cha hotuba umeainisha vipaumbele vya Wizara na Bajeti kwa mwaka huu. Wakipata fedha kila mwaka, kama wanavyoomba watafanikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika vipaumbele 11, nimechagua kipaumbele cha (iii) na cha (v) ambavyo vinagusa pia moja kwa moja Jimbo la Tunduru Kaskazini na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Wataalam; uhaba wa Wataalam Kitaifa ni 50% na Tunduru ni 35%. Serikali iendelee kuzalisha Wataalam kupitia Vyuo vyetu vilivyopo, Mabaraza ya Wanataaluma na Bodi za Ushauri yafanye kazi zao vema, ikiwa ni pamoja na kusimamia Professional Ethics, Kanuni za Kusimamia Taaluma ikiwemo mafunzo ya utarajali zikamilike na zitumike, pia (CPD - Continuing Professional Development) iwekewe msisitizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua za kushughulikia nidhamu ya Wataalam zitokane na Vyombo vya Taaluma, isipokuwa kwa makosa yasiyokuwa na kitaalam, watumishi waboreshewe maslahi yao, Vyuo viongoze udahili, uwiano (Ratio) kati ya Madaktari na Wataalamu wa Kada nyingine za juu na Wataalam wa Kada za Kati kwa mujibu wa ILO uzingatiwe. Hatua hii itatoa nafasi ya utoaji wa huduma bora, concentration na kupumzika vikiwa ni vichocheo vinavyotegemeana.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na Jimbo la Tunduru Kaskazini; Hospitali ya Wilaya ni ya siku nyingi, imechakaa (miundombinu), tunaomba ifanyiwe ukarabati. Chumba cha upasuaji mkubwa (major theatre), chumba cha upasuaji mdogo, (minor theatre) OPD, X –Ray, RCH, Maabara, Wards miundombinu yote hii ni chakavu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Vifaa tiba; Vituo vya Afya na Zahanati; Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Jimbo la Tunduru Kaskazini lina Kata 24, lakini kuna Vituo vya Afya viwili na kimoja ambacho kinajengwa. Tunaomba Ambulance ziweze kusaidia kutoa huduma kwa Vituo vya Afya viwili ambavyo viko kilomita 64 pande tofauti (1800).

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Kituo cha Afya cha Nakapanya kipatiwe fedha kwa ajili ya ukarabati kama tulivyobahatika kwa Kituo cha Matemanga. Hii inachagizwa na ukweli huu wa idadi ndogo ya Vituo vya Afya, vitatu tu katika Kata 24. Zahanati pia ni chache, lakini kwa sasa tukiboreshewa Vituo vya Afya tulivyonavyo kwa Wataalam, miundombinu na Vifaa tiba na kupatiwa Ambulances itatusaidia sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa fursa hii ili niweze kutoa mchango wangu kwa ajili ya hoja ya Serikali iliyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, tunajadili Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/2019, lakini pia tunajadili Mapendekezo ya Serikali Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, nitaanza kujadili Makadirio ya Mapato na Matumizi. Kwanza niipongeze Serikali kwa kutenga asilimia 37 ya bajeti yote kwa shughuli za maendeleo. Kufanya hivi ni kuendana na mpango wetu wa miaka mitano ambao tulishaupitisha hapo awali wa kwamba tutakuwa katika kila bajeti ya kila mwaka tunatenga fedha kwa ajili ya maendeleo kati ya asilimia 30 na asilimia 40. Kwa hiyo, bajeti hii imeweza kukidhi matakwa hayo ya mpango wa miaka 5 tulionao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda pia kupongeza kwa sababu Serikali imefanya jambo kubwa lifuatalo, pengine wenzangu hawajaliona au wameliona; ni kwamba fedha za ndani ambazo Serikali imeweza kuchangia, kwa mwaka uliopita, mwaka 2017/2018 ambayo ilikuwa ni asilimia 38, kwa fedha za ndani zilikuwa asilimia 75 na fedha za nje zilikuwa asilimia 25. Mwaka huu Serikali imeamua kuongeza mchango wa fedha za ndani na kupunguza mchango wa fedha za nje, kwamba kwa mwaka huu wa fedha mchango wa fedha za ndani ni asilimia 82 wakati mchango wa fedha za nje ni asilimia 18. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii itaweza kwenda kutusaidia kuondoa tatizo kubwa sana ambalo limekuwa likisababisha budget performance kuwa siyo nzuri kwa sababu ya kulegalega kwa utoaji wa fedha za nje. kwa mfano, katika mwaka ulioisha wakati utekelezaji kwa upande wa fedha za ndani ulikuwa asilimia 85, fedha za nje zilikuwa asilimia 15 tu peke yake; lakini kwa mwendo huu tunaoenda nao pengine tutafika mahali.

Mheshimiwa Spika, nataka kuishauri Serikali twende hivi, ikiwezekana tufike mahali ambapo fedha zote za maendeleo zitatokana na fedha za ndani na fedha za nje ziwe ni fedha za ziada, tutaweza kwenda kwa kasi na kuweza kutekeleza vizuri zaidi malengo yetu katika miradi ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya muda labda ningesema jambo moja tu kwamba ingekuwa wadau wa fedha za nje (wachangiaji kutoka nje) nao wangechangia asilimia 85 kama tulivyochangia sisi kwa fedha za ndani, budget performance kwa kufikia mwezi Aprili mwaka huu ingekuwa ni asilimia 73. Mahali ambapo hata sisi wenyewe kama tungechangia asilimia 100 na wafadhili wangechangia asilimia 100 kwa mwezi Aprili tungekuwa tumefikisha asilimia 85.4 na kwa hiyo kuwa na mwelekeo wa kuweza kupata matokeo mazuri zaidi ya kibajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu hali ya uchumi na mpango wa maendeleo wa Taifa tumefanya vizuri sana, kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na Serikali. tuna mafanikio ya kiuchumi kwa upande wa uchumi wa Taifa kwa vigezo vya uchumi wa Taifa kwa jumla, lakini pia kwa ongezeko la Pato la Taifa na udhibiti wa mfumuko wa bei. Si tu kwa ndani lakini pia hata katika eneo la Afrika na Kusini mwa Sahara, miongoni mwa nchi za SADC na nchi za Afrika Mashariki, takwimu zinajieleza, kwa sababu ya muda siwezi kusoma takwimu hizo, lakini tumefanya vizuri sana kiwango cha kuweza kujipigia Makofi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kufanya vizuri huko kumeelezwa kwenye taarifa hiyo hiyo kwamba kumetokana na jitihada za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu, lakini pia kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya madini na pia kuimarika kwa sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, napenda hapa niwapongeze wachapa kazi wote wa Tanzania, walipa kodi wote, wizara kwa niaba ya Serikali nzima pamoja na uongozi wa juu wa Serikali wakiongozwa na Jemedari Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri wa Tanzania akisaidiwa na wasaidizi wake wa karibu kabisa Makamu wa Rais mama yetu Mama Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pengine tungeweza kuona namna ambavyo tunaweza kufanya vizuri hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ili tuweze kufanya vizuri zaidi kipo kitu kimoja ambacho ni nyenzo hatujakitumia sawasawa na hiki siyo fedha, mali wala mtaji mwingine wowote ule isipokuwa tu lugha ya Kiswahili. Pengine wengine wakinisikia nikisema Kiswahili wanaweza wasielewe, lakini watafiti duniani kupitia The World Economic Forum wamesema hivi, kwanza wamesema speaking more than one language can boost economic growth. Pia wamesema multi lingualism can fuel exports increase salaries and help innovation. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki tuna shida kidogo kwenye mkataba wenyewe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kiswahili hakipewi umuhimu. Kwenye kifungu cha 137 cha Mkataba wa Afrika Mashariki imeandikwa hivi Article 137, official language.

137._ (1) The official language of the community shall be English,

(2) Kiswahili shall be developed as a lingua franca of the community.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu moja kwa moja hapa kupitia Serikali tushauri ili katika uwanja ule wa Afrika Mashariki na Kiswahili kitumika kama official language. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sababu ya msingi ya kusema hivyo ni kwamba nyaraka muhimu ambazo zinatoa mwelekeo wa kimaendeleo na kuweza kuzungumzia mipango mbalimbali ya Afrika Mashariki kama mkataba wenyewe, lakini vision ya East Africa ya mwaka 2050, pia mipango kama development strategy, protocols zote pamoja na facts and figures na mambo ya ripoti za kila mwaka zote zipo kwa Kiingereza.

Mheshimiwa Spika, tunaweza kushindwa kuwafanya Watanzania walio wengi kushiriki katika ushindani huo kwa sababu ya kikwazo cha lugha. Hii inawezekana kwa sababu duniani huko ziko taasisi nyingine zinazounganisha au zinazojumuisha nchi nyingine nyingi zaidi SADC, European Union, COMESA CARICOM, ikiwemo na nyingine nyingi. Hata Umoja wa Mataifa wenyewe una lugha sita rasmi, UN ina six official languages ikiwemo Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Ki-Russia na Ki-Spanish. Hii inawezesha kwanza ushiriki wa watu wote wanaohusika katika muunganiko huo na kuwawezesha kuweza kuelewa mipango mbalimbali na kuweza kulinganisha mipango ya nchi zao na ile ya nchi hizo za mijumuiko katika hizo forums.

Mheshimiwa Spika, nirudi tena upande wa Tanzania, tunao mpango wetu wa muda mrefu unaitwa The Long Term Perceptive Plan (LTTP) wa mwaka 2011/2012 mpaka mwaka 2025/2026. Kwenye kipengele cha institutional framework Serikali ilipangiwa jukumu la kutawanya nyaraka zote za maendeleo kwenda mpaka kwa wananchi. Vision yenyewe huo mpango wenyewe wa muda mrefu lakini mipango ya miaka mitano yote huu wa kwanza na huu wa pili na wa tatu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Namalizia kwa kusema kwamba mipango yote hii Serikali iweze kutekeleza kwanza kwa kuitafsiri nayo iwe ya Kiswahili, halafu iweze kuitawanya na kuipeleka kule kwa wananchi ambao ndio watekelezaji wa hii mipango, tutaweza kuona namna ambavyo tunaweza kuongeza kasi ya utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na wataalam wote kwa mwelekeo wa mabadiliko makubwa katika Sekta ya Madini nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Mwaka 2017 ambayo sasa yanatarajiwa, yakitekelezwa vyema, yataboresha tija katika sekta ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, uimarishaji wa usimamizi wa sekta ya madini kwa mujibu wa Sheria ya 2017 (mabadiliko). Nashauri Serikali iweze kusogeza huduma za ushauri wa kitaalam, usimamizi na kadhalika na uwepo wa wataalam wa kutosha na wenye weledi stahiki kama ilivyosisitizwa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa 2011/2012 - 2015/2016 na 2016/2017 - 2020/2021.
Kwa Tunduru tuanze kwa kupatiwa Mthamini wa Madini haraka. Tunaomba Serikali iongeze/iboreshe bajeti kwa Wizara hii muhimu kwa uchumi wa nchi, iwe ni mbegu tayari kwa mavuno zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ielekeze nguvu zaidi katika madini ya vito (gemstones). Madini makuu yaliyozoeleka ni muhimu kama yale ya vito. Hata hivyo, bado kama Taifa tunahitaji kuelekeza nguvu katika uchimbaji na shughuli zote husika za madini ya vito ikiwemo uongezaji thamani. Katika kutekeleza haya, Serikali ielekeze nguvu katika maeneo yenye potential au yaliyogundulika kuwa na aina na viwango (types and quantities) za madini ya vito.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Serikali iandae/ iboreshe kanzidata ya maeneo yenye madini ya vito (aina na viwango) katika maeneo yote nchini. Tunduru inayo madini ya vito ya alexandrite ambayo kwa Tanzania, kwa mujibu wa Taarifa ya GST ya mwaka 2011, yanapatikana Tunduru, Mbulu na Nachingwea. Madini haya ni miongoni mwa yale adimu duniani ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye madini haya, nchi yetu ikiwa ni miongoni mwa nchi 10 bora zenye viwango vya madini hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, madini hayo ya alexandrite ni yenye thamani kubwa yakiwa ni ya sita duniani ikitanguliwa na red diamond, taaffeite, grandidierite, serendibite na diamond. Alexandrite ina thamani ya Dola za Kimarekani 12,000 kwa karati moja. Ni muhimu sasa kwa Serikali kuweka nguvu kubwa vya kutosha kwa shughuli za madini ya alexandrite. Tafsiri nyepesi ni kwamba maeneo yenye madini haya yapewe umuhimu katika uboreshaji wa shughuli za madini hususan madini ya vito.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tunduru, zaidi ya alexandrite inayo madini ya vito mengine ya dhahabu, dismuth na Sapphire kwa mujibu wa GST (2011). Taarifa kwenye mitandao zinaonesha uwepo wa madini ya vito zaidi Tunduru kama ifuatavyo: Chrysoberyl, chrysoberyl var; alexandrite, corundum, corundum var, ruby, corundum var, sapphire, diamond, garnet group, magnesio taaffeite – 2N’ 2S, Magnesio Taaffeite – 6N 3S, spinel, tourmaline na zircon.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu ni kwamba Serikali kupitia GST ifanye utafiti wa kina vizuri zaidi ili kuthibitisha taarifa hizi. Ikithibitika, eneo la Tunduru liorodheshwe kuwa eneo lenye uwezo wa kuchangia Pato la Taifa, lakini pia Halmashauri iboreshe bajeti yake, hivyo nguvu zaidi iwekwe huko Tunduru.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla hali hii maana yake ni utafiti zaidi, vifaa zaidi, wataalam zaidi na kadhalika ambapo kwa ufupi ni bajeti zaidi. Serikali iboreshe bajeti ya Wizara ya Madini.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, pongezi kwa Serikali kwa upana wake na Wizara kwa namna ya pekee kwa kazi kubwa na ya mfano wanayoifanya, hongera sana.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Tunduru Kaskazini na bajeti ya mwaka 2019/2020; nashukuru kwa miradi ifuatayo ambayo imetengewa fedha. Ukurasa wa 348, daraja F/ Mbanga – shilingi milioni 20 (ukamilishaji). Nina mashaka na utoshelevu wa fedha hizi kukamilisha kazi iliyobaki kwani bado kazi ni kubwa.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 348 - matengenezo ya barabara Mjimwema – Ngapa - Tunduru/Nachingwea Boarder – shilingi milioni 60. Barabara hii ni muhimu saba kuunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Lindi. Tunaomba ijengwe kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 348 - ujenzi wa Daraja la Ngapa katika barabara ya Mindu – Ngapa - Nachingwea/ Tunduru Boarder – shilingi milioni 60. Jumla ya fedha zote ni shilingi milioni 140. Kwa kulinganisha na mahitaji katika Jimbo langu, pamoja na kushukuru kwa tulichopata tunaomba yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, mahitaji ya miradi muhimu sana. Barabara ya Mkoa – Mjimwema - Nachingwea Boarder. Tunaomba ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami, likiwemo Daraja la mto Lumesule.

Mheshimiwa Spika, barabara ya mchepuo (Tunduru- By-Pass), ni bahati mbaya haikupata umuhimu katika bajeti, tunaomba izingatiwe.

Mheshimiwa Spika, Tunduru Round about; hapa kuna barabara inayokwenda Songea, Mtwara na Msumbiji. Makutano ya barabara katika eneo hili, wakati wa ujenzi wa barabara za Tunduru – Matenanga – Namtumbo – NA – Tunduru – Nakapanya – Mangaka - Taaluma na umuhimu, ikiwemo usalama. Tunaomba yafanyike marekebisho ya kitaalam.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mironde – Kalulu - Selous Game Reserve, ni barabara ya kimkakati; katika ziara yake Waziri Mkuu akiwa Kalulu alielezea umuhimu wake na kusisitiza kwamba Serikali itaijenga.

Mheshimia Spika, nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nakushukuru kwa fursa hii. Kwa muda wa dakika tano nachoweza kusema ni haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, pongezi kwa ujumla kwa Serikali lakini mahsusi kabisa kwa Wizara ambayo hoja yake iko mezani, Mheshimiwa Profesa Mbarawa na timu yake nzima, Mheshimiwa Jumaa Aweso, Profesa Kitila Mkumbo - Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu – Eng. Kalobelo, Wakurugenzi wote pamoja na wataalam kwa ujumla pamoja na wafanyakazi wengine wa kada saidizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nashukuru Serikali kwa sababu katika Jimbo la Tunduru na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa ujumla tulipata fedha kwenye bajeti hii jumla ya shilingi bilioni1.27; shilingi milioni 300 mjini na milioni 974 vijijini. Siwezi kutumia muda mrefu sana kurudia kusema kwamba fedha hizi hazitoshi lakini ieleweke tu kama ujumbe kwa Wizara kwamba hasa kwa mradi wa mjini ambao unahitaji fedha karibu shilingi bilioni 16, bajeti ya shilingi milioni 300 kwa mwaka maana yake mradi huu utachukua karibu miaka zaidi ya 50. Kwa hiyo, tutafutiwe fedha kwa kutoka vyanzo vingine na kwa style nyingine tuweze kukamilisha mradi wa Tunduru Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Tunduru uko mahali pa kimkakati hata kitaifa. Ni mji ambao uko katikati ya umbali wa kutoka Bandari ya Mtwara mpaka Bandari ya Mbambabay. Pia kule tuna zoezi maalum la kimkakati Kitaifa la Mtwara Corridor, maendeleo ya kitaifa yatakavyoweza kuchangiwa na maendeleo ya Kusini kupitia Miradi ya Ukanda wa Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya Mheshimiwa Waziri yenyewe ilishamaliza mjadala hapa Bungeni na hasa pale ilipokuwa inazungumzia changamoto. Imetaja changamoto tano lakini kila changamoto Wizara imetoa mapendekezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya kwanza upungufu wa fedha kwa ujumla katika kutekeleza miradi ya maji nchini. Wao wamesema Serikali inaendelea kutafuta fedha na mimi narudia Serikali iendelee kujipanga kutafuta fedha za kutosha kwa ajili ya kutekeleza miradi yote muhimu kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma hii ya maji ambayo ni muhimu na kila Mbunge akisimama anaeleza namna gani mahitaji ya maji ni muhimu kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ya pili muhimu kabisa kupita hata hiyo ya kutafuta fedha, wamesema hivi na hii nitaisoma kabisa, 5.2, ukurasa wa 108, anasema: “Uwezo mdogo katika utekelezaji, usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji”. Kitaalam hii wanaita low absorption capacity, uwezo mdogo wa kutumia fedha ulizonazo kwa tija na kutumia fedha kwa tija maana yake utekeleze mradi ufanikiwe. Mafanikio ya mradi yanatafsiriwa kitaalam kwamba ujenge mradi kwa wakati, uwe na ubora, kwa gharama zile ambazo zimekadiriwa na uwe endelevu (sustainability) utakaozingatia mazingira lakini pia uhakikishe wale walengwa (stakeholders) wanapata yale matarajio yao, ndiyo maana ya mradi uliofanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya maji ukisikiliza michango ya Wabunge wote haikidhi haya niliyoyaeleza, mambo karibu matano. Sababu kubwa ni nini? Sababu kubwa ipo muda hautoshi ningeweza kuieleza iko kwenye utaalam.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Engineer Makani.

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi; hongera sana kwa Wizara, Mheshimiwa Waziri na wasaidizi wake wote Wizarani. Pia hongera kwa Jeshi letu kwa upana wake ikijumuisha uongozi wa ngazi zote. Hongera sana kwa kazi iliyotukuka, sio tu kwa kuendelea kulinda mipaka yetu, bali pia kwa kuendelea kuingilia kati katika kazi na majukumu mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kama vile ujenzi/urudishaji wa huduma za dharura kufuatia maafa, kuharakisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali Kuu, zoezi la ukusanyaji korosho na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, teknolojia zilizopitwa na wakati; nimesoma changamoto hii katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri (hotuba ya bajeti) katika vifaa, mitambo, vitendea kazi na kadhalika, ni jambo la kuendelea kuishauri Serikali kuendelea kuboresha bajeti ya Wizara ya Ulinzi, lakini kwa upande mwingine nashauri Wizara iboreshe mpango wa elimu endelevu kwa wataalam waliopo (Continuing Professional Development (CPD) na kuzalisha wataalam kulingana na mahitaji. Hii itasaidia uendelevu (sustainability).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mipaka; katika mpaka wa Kusini wenye jumla ya kilometa 1,536 Wilaya ya Tunduru ni sehemu yake (eneo la kandokando ya Mto Ruvuma), kutokana na ishara za kukua kwa changamoto za kiulinzi katika mpaka nashauri Kambi ya Jeshi iliyokuwepo katika eneo la Kitanda, nje kidogo ya Mji wa Tunduru irejeshwe na kuboresha kwa kuondoa changamoto zilizosababisha kambi hiyo kufungwa siku za nyuma.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, pongezi; hongera sana kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Wakurugenzi, Wataalam wote, Wakuu wa Taasisi hususan REA na Watumishi wote wa Wizara.

Mheshimiwa Spika, kazi ya kutekeleza malengo kama yalivyoanishwa katika Ibara ya 43(c), 43(f) na 43(g) kwa mfano, Ilani ya CCM imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa kiwango kikubwa. Hongera kwa Wizara, Serikali kwa upana wake chini ya Mheshimiwa Dkt. Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano, hongera sana kwa CCM. Tukiendelea hivi na pengine kuongeza kidogo kasi na ufanisi, sekta ya nishati inakwenda kupaisha nchi.

Mheshimiwa Spika, hali ya usambazaji umeme chini ya REA; Jimbo la Tunduru Kaskazini; Mheshimiwa Waziri kwanza nashukuru kwa kazi kubwa iliyofanyika Tunduru Kaskazini, hata hivyo nimeambatisha hapa orodha ya vijiji ambavyo bado vinahitaji kuwekewa msukumo ili navyo vinufaike na maelekezo ya Ilani ya CCM.

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa umeme Tunduru; Mheshimiwa Waziri kwa miaka mingi tangu tupate uhuru hali ya upatikanaji umeme Tunduru ilikuwa duni sana. Tunashukuru kwa kutuunganisha katika gridi ya Taifa kupitia Mahumbika- Lindi-Mtwara circuit. Pamoja na mafanikio haya tunaomba umeme wa gridi ya Taifa kutokea Route ya Makambako. Songea-Namtumbo usiishie Namtumbo bali uendelezwe hadi kufikia Tunduru ili upatikanaji wa umeme Tunduru uwe wa kutosha na kuaminika zaidi.

Mheshimiwa Spika, ifuatayo ni orodha ya vijiji visivyokuwa na umeme Tunduru-Kaskazini katika Hamashauri ya Wilaya ya Tunduru.
N a . K A T A V IJI JI V IT O NG O J I V IK U B W A
1 . J a kika K in d a m b a Ja r ib u n i
2 . K id o d o m a L e g e z a m w e n d o M a c h e m b a
M a ji y a S w e la
3. L ig un g a T w e n d e m b e le M b a r ik iw a
4 . N a k a p a n y a T u lie n i M c h o lo l o
5. N a m iu n g o N a m m a n g a Na n g o lo m b e
M n e n je
Pa c h a n n e
M ta n d ik a
6. M a jim a ji M g et a
So n g a m b e le
7. N a m w in yu C h a n g a r w a w e B
8 . S is i k w a S is i L e lo le lo Se v u y a n k e Na k a te te
9 . M a so n y a N a m b a r a p i
M k a le k a w a n a
10 . M L. M a g ha r ib i M k o n d a M a lo m b e
M s in jili
11 . N g ap a N g a p a
M n a z im m o ja C h a w is i N g a p a M t o n i Jiu n g e n i
12 . M u h u w e s i T e m e k e
M w a n g a z a
13 . M in d u L iw a n g ula
1 4 . N a m a k a m b a le R w a n d a
15 . M a te m a n g a Fu n d i m b a n g a
1 6 . M c h a n g a n i M c h a n g a n i Ng a lin je
K id u g a lo
1 7 . N a n d e m b o T u m a in i Am k a
Na n g u n g u lu
1 8 . K a lu lu R a h a le o
M b u n g u la ji
Ju m la 3 0 (2 7 ) 1 4

Mheshimiwa Spika, vijiji vya Kata tano za Tinginya, Nakayaya, Mlingoto Mashariki, Nanjoka na Majengo vina umeme na kimoja kilichobaki kwa Kata ya Nampungu kiko kwenye mpango wa phase III, round I.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitongoji vilivyoorodheshwa ni vikubwa na vinajitegemea na vina shughuli nyingi na watu wengi.

Mheshimiwa Spika, Vijiji vya Nangungulu na Amka viko jirani na Nandembo lakini vinajitegemea, pia Kijiji cha Mchangani ni kikubwa sana na kina eneo muhimu lisilokuwa na umeme.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu sanaa na burudani. Inaongoza kwa kasi ya kukua – 13.7%, lakini inachangia kidogo sana 0.3%. Tuongeze uwekezaji katika Sekta hii. Ikijumuishwa na utamaduni tuboreshe mchango katika utalii especially katika eneo la program ya urithi wa ukombozi wa Afrika elimu ya UNESCO yaani – The African Liberation Heritage Programme.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa miradi mikubwa (kielelezo na kimkakati). Tuboreshe manufaa ya kukamilika kwa miradi, improve project completion benefits e.g technology transfer kwa wanafunzi na wataalam wachanga, nafasi za ajira, local materials, maintenance - for rest of the project life.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wa diaspora, haujajitokeza vyema katika mpango na bajeti 2019/2020.

Mheshimiwa Naibu Spika, mapato ya kodi kupungua; mojawapo ya sababu ni biashara ya magendo katika ufukwe. Ufukwe una urefu wa kilometa 900 kutoka Tanga hadi Mtwara. Eneo la ufukwe litumike kama fursa kwa utalii wa fukwe. Mipango ipo hasa katika FYDP’s lakini ni vyema tukatafsiri kwa vitendo, iwekwe miongoni mwa vipaumbele kukamilika, Sekta Binafsi ni njia bora na rafiki zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, zao la korosho; mchango wa kilimo 28.3% ndiyo unaongoza katika Pato la Taifa. Mchango wa kilimo cha mazao ndiyo unaongoza miongoni mwa nyinginezo ndani ya kilimo. Korosho inaongoza mazao yote, hivyo kuboresha uzalishaji, masoko na uongezaji thamani ni muhimu. Suala la malipo ya mkulima wa korosho lishughulikiwe kama darura, hiyo itasaidia.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kukushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuwa miongoni mwa wachangiaji jioni ya leo. Nimshukuru kwa namna ya pekee kabisa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya afya na uzima alionipatia na kuweza kusimama hapa leo. Mchango wangu mimi ni kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza bajeti ya mwaka 2019/2020 tunayoijadili inakwenda kutekeleza mpango wa mwaka mmoja wa mwaka 2019/2020 huo huo. Huo mpango wa mwaka mmoja tunaoujadili ni sehemu ya mpango wa miaka mitano unaoendelea ambao unaisha mwaka 2020/ 2021 ambao na wenyewe pia ni sehemu ya Dira ya Taifa tuliyojiwekea tangu mwaka 2000.

Mheshimiwa Naibu Spika, Dira ya Taifa ambayo inaendelea kudumu kwa muda wa miaka 25, mipango yetu ya miaka mitano na mpango mwaka mmoja mmoja kwa miaka mitano yote tulipitisha wote kidemokrasia. Kwa kuwa tulipanga wote basi hata kutekeleza tutekeleze wote kila mmoja akiwa amesimama kwenye nafasi yake. Ikiwa katika utekelezaji tunakutana na mafanikio basi tutajipongeza na pale ambapo tutakuwa hatuwezi kufikia malengo basi tutafute sababu kwa nini hatujafikia malengo na tutatue tatizo hili. Kukaa pembeni na kulalamika haitasaidia mtu mmoja mmoja wala haiwezi kusaidia Taifa, tuweze kuangalia namna bora zaidi ya kuweza kutekeleza mipango tuliyojiwekea wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Dira, nataka niishauri Serikali ijaribu kuangalia kipindi ambacho Dira inadumu kwa sababu nimeangalia ya Kenya nimeona wao Dira yao iliyoko sasa inaishia mwaka 2030, Uganda inaishia mwaka 2040, Rwanda ya kwanza inaisha mwaka 2020 lakini ya kwao ina miaka 20 wakati ya kwetu ni ya miaka 25, Kenya ni miaka 22, Uganda miaka 32. Halafu hao wa Rwanda wanayo tayari kwenye mpangilio dira mpya, wanazo mbili tayari; itakayoishia mwaka 35 na itakayoishia kwama 2050, hizi ni za vipindi vifupi vifupi vya miaka 15. Je, ni vizuri kupanga Dira ya muda mrefu sana au muda mfupi au muda wa kati.

Mheshimiwa Naibu Spika, natazama pia hata malengo ya kidunia, nimeziangalia MDG’s zinadumua miaka 15, hata the Sustainable Development Goals na zenyewe pia ni miaka 15, sasa sisi Dira yetu ilikuwa ni miaka 25, hebu tujaribu kuona hapo nini kinaweza kufanyika pengine kuna namna bora zaidi ya kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ni suala la ufuatiliaji na tathmini, naipongeza Serikali sana kwa sababu kwenye kitabu cha hotuba ya bajeti safari hii ukurasa wa 33 Serikali imezingatia sana suala hili na imeliweka vizuri kwa sababu, taarifa za huko nyuma za kina za kupitia utekelezaji wa mipango iliyotangulia zilizungumza suala hili kwamba, lilikuwa ni suala ambalo lilikuwa ni gape. Kama muda ungetosha ningeweza kusoma hiki kipengele kimoja kwenye Comprehensive Review Report for Tanzania Five Years Development Plan ile ya kwanza ya 2011/2012 mpaka 2015/ 2016.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa kuwa, muda hautoshi siwezi kwenda kusoma kunukuu, lakini kifupi ilikuwa inaonesha kabisa kwamba, kukosa kufanya ufuatiliaji na tathmini ni mojawapo ya changamoto kubwa ambazo zilikuwa zikiturudisha nyuma katika kutekeleza mipango yetu. Kwa hiyo, naipongeza Serikali hatua ambayo imeichukua sasa hivi ya kuweza kuhakikisha kwamba, sasa haturidii au tumerekebisha makosa yale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili kwenye uchangiaji, hili ninataka tu kurejea mchango ambao ulitolewa humu ndani na mmojawapo wa wachangiaji akiwa anazungumzia mradi mmojawapo kati ya miradi ya kimkakati, mradi wa reli ya kati ambayo inaboreshwa kwenye kiwango cha Standard Gauge. Alisema mchangiaji mmoja kwamba, hakuna jipya, mbona hii nchi ina Standard Gauge Railway tangu mwaka 75/76 na ambayo ilijengwa na Nyerere na kaunda. Kwa kifupi alionesha kabisa kutothamini, ni kama kuudharau mradi huu wa Standard Gauge Railway.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu niwafahamishe wale ambao hawafahamu kwamba, kukamilika kwa mradi wa SGR huu tunaokwenda kuujenga sasa hivi kunakwenda kuifanya Tanzania kuingia kwenye kundi la nchi ya pili kuwa na speed train katika Afrika. Tuna treni moja tu ambayo inakwenda kwa kilometa 320 kwa saa, iko Morocco, lakini baada ya hiyo zinazofuata zote ni 160 kilometres per hour ambayo ndio sisi tunakwenda kuifikia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mradi huu ni mradi mzuri, ni bora na ni muhimu. Na kifupi tu ni kwamba, uchukue tu mfano kwamba, maana yke, tafsiri yake ni nini ya haraka ni kwamba, watu wanaweza kutoka Dar-es-Salaam na kufika hapa Dodoma ndani ya saa pungufu ya tatu au wakichelewa sana saa tatu. Ni sawasawa na mtu atakayekuwa anasafiri kutoka mojawapo ya vitongoji vya Dar-es-Salaam kwenda katikati ya mji kwenda kufanya kazi kwa siku. Maana yake utaokoa muda kwa hiyo, utaongeza tija katika uzalishaji kwa sababu watu watakuwa wanakwenda kwa haraka. Kwa hiyo, naishauri Serikali iendelee kuongeza kasi ya kutekeleza mradi huu kwa haraka kwa sababu ni mradi wa manufaa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jabo langu la pili la kuchangia ni nafasi ya lugha ya Kiswahili katika kutekeleza miradi ya maendeleo au katika kuharakisha maendeleo ya nchi. Historia ya nchi hii inatuambia wazi kabisa kwamba, hata tulipokuwa tunatafuta uhuru mojawapo ya silaha ambayo inatamkwa waziwazi kabisa kwamba, ilitumika na ikasababisha tukapata uhuru kirahisi na pengine mapema sana ni lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo, maana yake ni kwamba, ni vema kwenda na Kiswahili pia, hata katika hatua ya kutafuta maendeleo, umefanya vita ya kutafuta uhuru, sasa fanya vita ya kutafuta maendeleo kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu gani, Kiswahili kinaelimisha, Kiswahili kitarahisisha kutoa taarifa kwa watu, kitaunganisha watu pamoja na pengine niweze kunukuu tu msemo mmoja wa Kingereza unasema, if you want to go fast go alone but if you want to go far go together, maana yake wengi kwa pamoja ndio mnaweza mkafanya jambo la kudumu, sustainability. Sasa kama unataka kufanya jambo la kudumu lazima ushirikishe watu wengi. Watu wengi mnawezaje kuweza kuwasiliana vizuri, ni kwa kutumia lugha ambayo kila mmoja ataielewa.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)