Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi (33 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kutoa mchango wangu kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na hoja yangu itakuwa upande wa Mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kwa kutoa masikitiko yangu kuwa sekta hii ya mazingira imepewa kipaumbele cha chini sana, ukizingatia muda kwanza uliotengwa kujadili na hata sekta ya mazingira ilivyowekwa na Kamati ya Bunge imechanganywa na Viwanda na Biashara. Nataka tu nisisitizie umuhimu wa sekta hii ukiangalia hali ya nchi yetu ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania bado ni nchi maskini na tunategemea rasilimali tulizonazo ambazo ni mazingira katika sekta mbalimbali. Uvuvi huko kwenye maji, ukulima mashambani, ufugaji, yote haya ni mazingira. Ukiangalia Serikali kwa sasa mazingira imeipa priority ndogo sana, mfano tu mdogo, sasa hivi kuna harakati tukiongelea mazingira tunachokiona kwenye Vyombo vya Habari au harakati zinazoendelea ni kutoa warning kwenye viwanda au kufunga viwanda kwamba vinachafua mazingira ama tunasema kwamba tufanye usafi kwa kufagia au kupiga deki maeneo fulani. Kwa hiyo, hii concept nzima ya mazingira inakuwa sivyo inavyotakiwa iwe.
Mfano wa pili, kwenye mazingira ambavyo tumeipa priority ndogo sana na inashangaza, asilimia kubwa yetu, takribani asilimia 65 ya wananchi wa Tanzania ni wakulima. Ukulima uko wa aina gani? Ukulima huu uko katika kuvuna rasilimali au kupanda mazao kwenye haya maeneo, je, haya maeneo yanayolimwa yanafanya kazi vile inavyotakiwa kwenye kutunza mazingira ili huu ukulima wetu uwe endelevu?
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia sekta ya mazingira pia katika shughuli za uvuvi, je hizi rasilimali tunazozichukua katika nchi yetu tunavuna vile inavyotakiwa? Sasa hivi kuna kesi kubwa sana mifano ya uvuvi haramu ambayo inaharibu hayo mazingira ya samaki. Hiyo ni mifano tu michache.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu inaongelea kwamba, tunataka uchumi wa viwanda, lakini uchumi huu wa viwanda rasilimali zinatoka wapi? Ni kwenye haya haya mazingira. Hii ni sekta ambayo imeibeba nchi, lakini cha kushangaza ni sekta ambayo imepewa priority ndogo sana. Rasilimali zetu tunazitoa katika mazingira kwa nini hatuipi mazingira priority inayotakiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri ni katika hata hii Taasisi inayoshughulikia mazingira, National Environment Management Council (NEMC), imepewa bajeti kiasi gani ili kutekeleza majukumu ya kusimamia sera ya mazingira nchini, sifuri si ndiyo kwa mwaka huu wa bajeti? Je tutapitisha? Hilo ni suala la kuzingatia. Hapo nilikuwa naonesha tu umuhimu wa mazingira na jinsi ambavyo bahati mbaya hatujaipa sekta umuhimu katika nchi yetu vile inavyotakiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza tu mifano michache kwa Wajumbe wengi ambao tupo humu ndani, tumepita njia ya Morogoro kufika hapa Dodoma. Katikati ya Morogoro na Dodoma nafikiri Wajumbe wengi wameona athari za mafuriko zilizotokea. Mfano mzuri ni Mto Mkondoa unao-flow kutoka Singida mpaka huko chini Morogoro, hapo katikati tunaona maeneo ya Kibaigwa wakazi wamepata madhara. Kuna reli ya kati eneo la Godegode, kila mwaka reli hii ya kati inatumia mamilioni ya pesa kurekebisaha na madhara ni nini? Ni kutokana na yale mafuriko yanayotokea katika Mto Mkondoa ambayo uharibu rasilimali hii muhimu ya nchi. Kwa hiyo, hela nyingi inatumika kugharamia hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mwingine mzuri ni wale wananchi wanaoishi maeneo hayo, wanapata madhara makubwa. Wanapoteza mashamba yao, rasilimali zao nyingine zinaharibika, livelihoods zinakwisha, vyanzo vyao vya mapato pia vinaathirika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaanza lini kuchukulia umakini kwamba haya mafuriko tunayoyaona ni consequence ya kutokutunza mazingira kwa hali ya juu kwenye shughuli za kilimo au shughuli za mining, michanga inaingia kwenye mito, mito inakosa zile channel zake za asili, yanatapakaa maji all over the place. Mifano iko mingi hata kule Dar es Salaam, barabara ya Bagamoyo, maeneo ya Mbezi ni mafuriko maeneo ya Massana kila siku, kwa sababu ya miundombinu mibovu na mipango au mikakati ya kutunza hii mito haiko sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano wa tatu ni Uvuvi. Uvuvi ni sekta muhimu sana ambayo bahati mbaya haitiliwi mkazo. Unapofanya uvuvi haramu, mfano wa kutumia mabomu, unaharibu rasilimali ya ile bahari, mazalia ya samaki. Hata hivyo, tukumbuke kwanza kule baharini, bahari siyo tu kwa ajili ya shughuli za uvuvi, bahari yenyewe ndiyo kiini ambacho kina-influence hali ya hewa. Sasa hivi tunaimba climate change, climate change. Climate change vyanzo ni vingi, mojawapo pia ni uharibifu wa sehemu kama za bahari. Namba mbili, hii climate change tunayolia na mafuriko tunayoyaona impact yake inazidishwa na kutotunza hayo mazingira. Mfano halisi ni hizi floods tunazoziona na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikibaki hapo kwenye mabadiliko ya tabianchi, mazingira yanagusa karibu sekta nyingi, kwenye mifugo, kwenye kilimo, kwenye uvuvi, kwenye mining na kadhalika, ukiangalia hata work plans za Wizara mbalimbali au Bajeti hamna kipengele kinachoonyesha kwamba hizi sekta mabalimbali zitakabiliana vipi na mabadiliko ya tabianchi, hamna bajeti, hatuna sera ya climate change, tuna strategy tu. Kwa mfano, ukiangalia huu Mkutano uliokwisha wa Climate Change Forum wa Paris, walichokubaliana, mbona hatujakiwekeza sisi katika nchi yetu?
Kwa hiyo, nafikiri ni muhimu sana kuangalia issue za mazingira kwa upana wake na umuhimu wake katika nchi yetu na katika uchumi wa nchi yetu. Tusiangalie tu kwa narrow set kwamba ni usafi, mazingira si usafi bali mazingira yamebeba kila kitu katika kila sekta ya nchi hii. Tunasema viwanda, rasilimali mnazozitumia viwandani zinatoka kwenye hayo mazingira au hata ukiangalia afya ya jamii inayohusika ambayo watafanya kazi kwenye hivyo viwanda au shughuli mbalimbali za uchumi, wasipokuwa na afya ya mwili na akili ambayo inakuwa influenced na mazingira, huwezi kuwa na Taifa imara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, issues za mazingira zinagusa kila Mtanzania, zinagusa issue za economy, zinagusa issue za afya, zinagusa issue za elimu, zinagusa sekta mbalimbali na hata nchi imeiona hii, lakini katika karatasi. Policies au sera katika environment zipo tu kwenye paper work lakini hatuoni katika utekelezaji. Naishauri Serikali iangalie tena kwa upya, iende ikaji-analyse kwa sababu tunatakiwa tu-report back kwa nchi nyingine ambazo zimekubaliana nazo nini tunakifanya kwenye kutunza mazingira na pia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu kwa sasa. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nataka kuanza kutoa inputs zangu katika Wizara hii kwa kujiuliza: Je, ni mafaniko yapi tunayo katika Sekta ya Elimu, ukiangalia… okay, samahani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni inputs gani tunaziona katika Sekta ya Elimu? Matokeo gani tunayaona katika Sekta ya Elimu kwa kuangalia shughuli za kiuchumi au shughuli za huduma za maendeleo ya jamii? Je, uchumi wetu una-reflect elimu tuliyonayo? Au huduma za kijamii kama ni afya, Madaktari wanatuhudumia vile tunavyotakiwa kupata? Sekta nyingine kama za Utalii, Service Provisions, zikoje? Je, zina-reflect kiwango cha elimu tulichonacho?
Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko ambayo yametolewa na Wajumbe ni mengi hata kwa Wizara nyingine zilizopita na hii yote ina-reflect level yetu ya elimu ikoje. Kwa hiyo, sitajikita sana katika kusema changamoto ni zipi za miundombinu, lakini changamoto ni zipi ukiziangalia katika outcome na jinsi ambavyo ina-affect elimu yetu kwa ujumla na uchumi wetu kwa ujumla? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika Sera ya Elimu yenyewe, katika kipengele cha muda wanafunzi wanaoanza shule, hii pia inaweza ikawa na outcome au ikaleta impact ambayo siyo sahihi. Watoto wadogo, miaka minne, mitano, mitatu, wanaamshwa saa 10.00 au 11.00 alfajiri, wamepumzika saa ngapi? Akili zikoje? Ukiangalia hata watoto wadogo wa Shule za Msingi Dar es Salaam, miundombinu hairuhusu wale watoto. Wanafika shuleni wamedumaa au hawana hizo akili, hawako creative. Kwa hiyo, chochote unachomfundisha yule mtoto hakiwezi kukaa, hiyo tayari ina impact katika siku za usoni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mitaala au curriculum zetu, ni masomo gani yanafundishwa? Kwa elimu ya sasa hivi, je, curriculum ipo sawa? Watoto wadogo wa primary school au nursery, content wanayofundishwa ni sawa? Watoto wanafundishwa mambo makubwa ambayo ni repetitive, ya kazi gani? Hii inaleta udumaivu au udumavu. Samahani sijui Kiswahili, hakiko vizuri sana, nayo ni reflection ya elimu yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia issue za mitihani ya primary au „O‟ Level, mwanafunzi au mtoto huyu anapewa one time chance, ambayo si sawa. Mtihani unafanya kwa siku moja mtoto wa Darasa la Saba, miaka yote saba inakuwa judged na siku moja. Hii lazima iwe reflected, haiko sawa. Au mtoto wa Form Four au Form Six, miaka yote hiyo minne au miwili aliyosoma inakuwa judged one time na chochote kinaweza kikatokea. Kwa hiyo, tunamnyima huyu mtoto nafasi au fursa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niguse kwenye issue ya Vyuo Vikuu na specialization. Tuna vyuo vya Serikali, naona hapa list inaonyesha vyuo 31. Ni chuo gani au vyuo hivi vikuu vime-specialize kwenye nini? Chuo Kikuu hakiwezi kuwa na faculties saba au nane. Hao wanaofundisha, wanaotoa huduma, hao Walimu wana qualities zinazotakiwa?
Kwa hiyo, lazima na hiyo nayo namshauri Mheshimiwa Waziri mhusika mwangalie specialization katika vyuo lazima iwe reflected inavyotakiwa na wataalamu wanaotakiwa wawepo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, issue nyingine ni miundombinu lakini kwenye njia ya ku-deliver elimu au kutoa mafunzo. Ni mbinu gani zinatumika kufundishia? Style tuliyonayo sasa hivi shuleni, hasa Shule za Serikali na hasa vijijini ni Mwalimu anaandika notes ubaoni na wanafunzi wanafanya kazi ya ku-copy. Kinachofuata ni ku-cram kile Mwalimu alichofundisha.
Sasa mtoto huyu anayefaulu, asilimia kubwa ni yule mwenye uwezo wa ku-cram halafu anakuja kutema baadaye kwenye exam. Hii nayo inakuwa reflected kwenye Vyuo Vikuu. Wanafunzi wanaokuja hawako creative, lakini tunaendelea kuwa na system za kukremisha. Sasa kama umejaliwa kukremisha ndiyo you have a better chance ya kufaulu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni vizuri kujiuliza au kujitathmini, tutaendelea hivi mpaka lini? Tutaendelea kusema madarasa hayatoshi, Walimu hawatoshi, miundombinu hafifu lakini tunataka nini? Serikali kama Serikali tuna strategy gani ya kusema kwamba elimu yetu i-focus kwenye nini ili izae kitu gani? Kwa hiyo, ni lazima tujiulize: Je, ni vipaumbele vipi tulivyonavyo, kama hivyo vipaumbele vipo na tunajiwekea nini katika elimu? Au imekaaje kimkakati ku-reflect uchumi wetu na nini tunataka kukijenga katika nchi yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi katika muktadha huo, naomba tujikite na tu-concentrate kuangalia kwamba elimu yetu ipo katika standard gani na tunataka ku-achieve nini na matokeo hayo ya elimu tunataka yaweje? Tu-focus kwenye impact au outcome ya mfumo mzima wa elimu tunataka uwaje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu kwa sasa. Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Naibu Spika, malengo makuu (objectives) ni matatu badala ya manne. Lengo la nne lililotajwa kama ufuatiliaji si sawa, hii ni 4001 ya kufuatilia utendaji kazi ili kufuatilia malengo tajwa, page one.
Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2017/2018 kunakosekana the main priorities, page 18-22 ya hotuba ya Waziri. Maeneo tajwa ni 39, ni mengi mno kuweza kufanikisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, the concept (dhima) ni kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu. Hali halisi ya kiuchumi, je, tumefanikisha kwa kiasi gani dhana ya kilimo ni uti wa mgongo? Focus ya uchumi wa viwanda ni ipi? Ni rasilimali gani zinalengwa kwa aina gani ya viwanda? Kuna rasilimali watu inayolengwa maalum kwa aina gani za viwanda? Je, ni masoko gani yanayolengwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, mpango unatakiwa kuainisha main strategies zitakazowezesha kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi. Mfano, ni maeneo gani makuu matatu Serikali inatakiwa ku-focus into ili kusukuma maendeleo katika sekta nyingine?
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru nitatoa maoni yangu na mapendekezo katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Kabla ya kutoa mapendekezo yangu nataka turejee katika Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara 63(2) kujikumbushia tu Waheshimiwa Wabunge. Sehemu hii inasema kwamba:- “Bunge litakuwa chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii”. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nimeamua kusema haya au kujikumbushia nini kinatuongoza katika nchi yetu kama Wabunge? Nina muda wa mwaka mmoja na zaidi hapa Bungeni, nikizingatia haya tuliyoambiwa, lakini ukiangalia mwenendo wetu nimeona kuna upungufu kwa jinsi ambavyo tunaishauri na kuifuatilia Serikali. Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasimama hapa Mbunge mmoja mmoja tunatoa mapendekezo yetu kwa Wizara husika, tunatoa mapendekezo yetu kama Kamati husika lakini sisi tunaotoa hayo mapendekezo hatufuatilii utendaji, hakuna accountability upande wa pili. Waziri atakuja kujibu atasema sawa nimepokea au sawa hili sikubaliani nalo au hili nitalifanyia kazi lakini ukija mwaka unaofuata au Bunge linalofuata hatujui nini kimetekeleza au kama kweli kimetekelezeka. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano dhahiri, mwaka 2013 au 2014, kuliundwa Kamati Maalum ambayo ilikuwa inachunguza na kuleta mapendekezo juu ya hii migongano baina ya wakulima, wafugaji, wawekezaji na mambo ya ardhi. Kamati ile ilitoa mapendekezo mazuri sana kwa Serikali lakini huu ni mwaka 2016 bado tunaongelea lugha hiyo hiyo. Kamati zinatoa mapendekezo hayo hayo hatuoni accountability kutoka upande wa pili. Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mwingine pia sisi ambao tulikuwa mtaani by then tulikuwa tunasikia kuhusu ESCROW, RICHMOND, Kamati zilitoa mapendekezo yake lakini sisi tuliotoka mtaani na sasa tumeingia Bungeni hatujui haya mapendekezo yaliishia wapi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachotaka kushauri, Kamati kama itaona inafaa waongeze katika mapendekezo yao kwamba Bunge linatakiwa liwe na special monitary and evaluation plan, mikakati ya kutathmini tunachokipendekeza kwa Serikali au tunachokishauri kwa Serikali je kinatekelezeka na kinatekelezeka kwa wakati gani. Hii itatusaidia kama Serikali yetu kuzipambanua hizi changamoto na ku-move forward.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliuliza hapa na pale nikaambiwa wakati uliopita Bunge lilikuwa na kitengo cha kufuatilia ahadi za Serikali Bungeni, the government assurance unit. Sasa nataka kujua hiki kitengo kilikufa au kwa nini hakifanyi kazi kikatuambia ili tusiwe tunajirudiarudia kama Kamati au kwa Mbunge mmoja mmoja kushauri au kupendekeza mambo yale yale kila wakati. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa pili napenda kugusia kwenye mambo ya maadili kwa Kamati hii husika. Nimesoma booklet nikaona muundo wa Kamati, ina wajumbe 10 kutoka Chama Tawala na wajumbe sita (6) kutoka upande wa Upinzani. Sasa maadam hii Kamati ni special siyo kama Kamati nyingine inayoshughulikia maadili ya Wabunge, napendekeza ingekuwa ina 50-50 chance ili kuwe na uwazi au kusiwe na upendeleo wa aina yoyote hata na hao wajumbe wahusika wawe na mawazo mbadala. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nilichokiona kwa Wabunge wenzetu waliopewa adhabu mbalimbali, evidence gani zilitumika? Hata vyombo vya habari, waandishi wetu wa habari wako hapa ndani, kukitokea tafrani humu ndani utaona upande wa Upinzani ndiyo unaoshutiwa kwamba wamefanya fujo. Hata hivyo, in every action there is a reaction yaani kwenye kila tukio lazima kuna sababu nyuma yake, lazima kuna mmoja…
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Nitatoa mchango wangu katika sekta ya mazingira katika Wizara hii, ningependa tu tukumbushane na kusisitiza kwamba mazingira ni suala mtambuka, mazingira ni uhai, mazingira ni kila kitu. Mazingira haya ni ardhi, ni hewa, ni maji, ni kila kitu ambacho kinatufanya sisi kama Watanzania tuishi au kama binadamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha kwamba mazingira ukiangalia kwenye mfumo mzima wa Wizara zote hizi tulizonazo hata ukiangalia katika bajeti kipaumbele chake kipo kidogo sana. Hii iko dhahiri kabisa hata kwenye masuala ya maendeleo bajeti ya maendeleo ilivyo finyu au mfuko wetu wa maendeleo ulivyofinywa, hii inachanganya kidogo. Sasa hatuwezi kukuza sekta za kiuchumi au za kijamii tukiweka mazingira kando.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia suala la ardhi, ardhi tunaitumiaje katika masuala ya madini, ukulima, ufugaji, kila kitu kinatoka ardhini lakini ardhi yetu ukiangalia kwa Tanzania karibu asilimia 61 ya ardhi yote ina mmomonyoko wa udongo, hali ya ardhi ni duni. Sasa kama una ardhi duni ina maana hata misitu haifanyi vizuri, mazao hayafanyi vizuri, na hii hali inaendelea namna hii na hatuna mipango mikakati au madhubuti ambayo iko-reflected kwenye bajeti ya kutunza ardhi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kwenye masuala ya bahari na mambo ya mwambao, bahari yetu ina matumbai karibu ukubwa wa hekari 3,580 za mraba, tuna misitu katika mwambao wetu yenye karibu hekari 70,000 inakatwa hovyo, matumbai yanapigwa mabomu kwenye uvuvi wa haramu tunaharibu mazingira. Effect yake tunakuja kuiona pale tunapoharibu mazingira baharini na misitu ya mwambao, hii yote inakuja kuleta madhara kwenye hali ya hewa. Tunaongelea mafuriko, tunaongelea mabadiliko ya tabianchi, hii inatokana na sisi kuharibu mazingira yetu ya baharini na hata kwenye ardhi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nigusie suala la misitu nchini kwetu. Kuna uvunaji holela na ukataji wa holela na uuzaji holela wa misitu. Misitu ndiyo hii inayofanya tupate maji kiasi gani au hali ya hewa iendeleeje, kwa hiyo kunahitajika kuonesha reflection kwamba kuna haja ya kutunza mazingira ukiangalia hasa katika sekta ya misitu. Mfano Tanzania tunapoteza karibu hekari laki tatu na sabini kwa ukataji holela wa misitu, je, tunai-replace vipi? Mikakati madhubuti hatuioni ikiwa reflected kwenye sekta hii ya mazingira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili nataka niligusie kwa urefu kidogo na hili ni kuhusu usimamizi wa taka, taka ngumu, taka kwenye maji na taka za kielektroniki. Kwa mfano, Mji wetu wa Dar es Salaam una-potential ya kuwa mji popular duniani ni mzuri na wenye kuvutia, lakini takwimu na information za mwaka 2010 inaonyesha Mji wa Dar es Salaam umeshika namba nane dunia nzima kwa uchafu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuangalii tu mandhari ya uchafu lakini zile impact na effects zinazoletwa na uchafu. Kwanza ni magonjwa, karibu asilimia 80 hapa nchini kwetu hatuna mfumo mzuri wa ukusanyaji wa taka na kuzitenga zile taka. Taka ngumu, taka ambazo haziwi degraded biologically, zote zinachanganywa na ukiangalia kwa Mji mkubwa kama Dar es Salaam ambao unaongoza kwa idadi ya watu tuna sehemu moja tu ya dumping site- Pugu ambayo ina eneo karibu la hekta 75.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zile takataka zinazotupwa kule Pugu jinsi ambavyo zinakuwa treated haziendani sawasawa na utunzaji wa mazingira. Zinatupwa, hamna mechanism maalum ya kuzuia uchafu ule wenye sumu usisambae katika mifumo ya maji, hakuna njia ya kuzuia kwamba unapochoma moto ule moshi una madhara gani kwenye hali ya hewa na hata kwenye afya za binadamu. Kwa hiyo, kunahitajika kuwe na mfumo madhubuti wa kuchanganua taka na jinsi ya kuzi-treat hizo taka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tuna vifaa vya simu, tuna computer, fridge, television, lakini hakuna mfumo madhubuti wa kuhakikisha kwamba taka za aina hii ya elektroniki zinatunzwaje au zinatolewaje katika mazingira ili zisilete madhara yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitagusia pia kwenye Mfuko wa Mazingira. Tumejiwekea mkakati, tumeweka mfumo mzuri lakini kwa bahati mbaya hatujawa serious au makini na mfuko huu. Ni kwa sababu pia hatuja-reflect umuhimu wa kutunza mazingira na kusimamia mazingira. Sasa hivi Serikali yetu tunataka kuwa na mfumo wa viwanda lakini huoni ile link ya hii system mpya kwamba tuwe na mfumo wa viwanda au uchumi wa viwanda ina-link vipi na mazingira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hatujajua au hatujachanganua kwamba hivi viwanda vinatumia rasilimali gani na rasilimali hizi tunazozivuna na zinazoenda kuwa treated huko kwenye viwanda zitakuwa zina effect gani kwenye mazingira. Mfuko huu hauna fedha, kwa mfano kwenye kitabu hiki cha maendeleo ya bajeti, zimetengwa milioni mia tatu tu na chenji, utafanya nini na milioni mia tatu kwenye suala la mazingira ambalo ni mtambuka? Je, mta- address nini? Issues za hewa, za maji, za ardhi au issues zinazotokana na uharibifu wa mazingira kutokana na viwanda. Je, mikakati ni ipi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfuko huu unaweza ukawa na sources nyingi za kujipatia fedha, mfano TRA wanavyoweka extra charges kwenye magari chakavu au yaliyozeeka na kadhalika hela hizi zinatumikaje? Kwa hiyo, kuna umuhimu wa Serikali kuweka kipaumbele kwenye mfuko huu kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na usimamizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna National Environment Action Plan yetu ya 2013-2018. Hii imekaa kimaandishi tu lakini action plan yetu hii haina budget line na haina indicators au indicators zilizopo ni chache. Hii inaonesha dhahiri kwamba hatujawa waangalifu au hatuoni uthamani wa mazingira, mazingira ambayo yanayotufanya tuwe tumesimama hapa tukiwa tuna afya. Kwa hiyo, naomba hili liangaliwe upya. (Makofi)
Mheshimwa Mwenyekiti, kuna msemo ambao unasema kwamba kama huna information au data then huna right ya kuongea. Sasa ukiangalia research ambayo inasimamiwa na taasisi yetu ya NEMC haina hela ya kufanya tafiti. Sasa tunapokaa tunasema kwamba kuna mafuriko, kuna mabadiliko ya tabianchi, hali ya hewa haieleweki, mvua za masika hazieleweki, hatuwezi kusema kwa confidence, tunakuwa tu tunahisi au tunafikiria itakuwa hivyo lakini hatuna data ambazo zina back up kwamba hali ya hewa inakuwaje, ardhi yetu tuitumiaje, sasa tutafanyaje hizi kazi kama NEMC haipewi hela ya research? Yote yanakuwa batili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishie hapo kwa kusisitiza kwamba, mazingira ndiyo yanayoshika rasilimali zetu tunazotumia, natural resources, tusiidharau, tutazidi kulalamika kwamba hakuna maendeleo endelevu kwa sababu kutwa tunaharibu mazingira yetu na mazingira yetu hatuyatunzi wala hatuyapi kipaumbele katika kuyafanyia research, katika ku-disseminate hiyo information, awareness raising haipo wala usimamizi wake ambayo iko reflected kwenye bajeti haupo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo, nashukuru.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Nashukuru Mheshimiwa Spika, kwanza naunga mkono maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika bajeti hii na nitajikita kwenye masuala makuu mawili ambayo ni kilimo na mambo ya mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini nimeamua kugusia kilimo kwa sababu nchi yetu bado ipo kwenye category ya kimaskini na karibu asilimia 70 ya Watanzania wanategemea kilimo na katika hao asilimia 70, asilimia 80 ni wanawake. Sasa kwa nini nimeamua kuchagua kilimo kwa sababu naona kwenye kitabu cha mpango cha Mheshimiwa Waziri 2016/2017 malengo hayakugusa kilimo wala hayakugusa mazingira. Katika kilimo aligusia tu shamba la miwa na kiwanda cha sukari ambacho kitaanzishwa huko Mkulazi, kitabu hicho hicho baadaye 2017/2018 hajagusia tena kilimo, lakini amegusia tena shamba hili hili la Mkulazi, mazingira pia haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, inashangaza kwamba hatuwezi kutoka kwenye huu umaskini katika nchi yetu, wenzetu mfano nchi ya Mexico ilikuwa maskini tena hata kuliko sisi nafikiri. Hata hivyo, mwaka 1940 waliamua kujikita kwenye kilimo na walichagua zao moja tu la ngano, sasa hivi Mexico ni nchi ya 13 duniani kwa utajiri na ni nchi ya 11 duniani yenye uwezo ya kununua bidhaa. Sasa sisi tunaimba tu tunagusa mambo mengi, mipango mingi ambayo haina focus na focus yenyewe ambayo tunayo tumesema sisi kilimo ndio uti wa mgongo lakini hatukipi priority.

Mheshimiwa Spika, sasa ni lini Mheshimiwa Waziri ataamua sasa tutoke hapa tulipo akaacha legacy katika nchi hii kwa kipindi hiki alichonacho, akajikita katika kilimo kukitengeneza kilimo? Kilimo sio tu kimekuwa hakitukomboi Watanzania, bali pia kimekuwa kikishuka. Kilimo kimeshuka kutoka asilimia 2.3 mwaka 2015 mpaka asilimia 0.3 mwaka 2016. Sekta ya Kilimo ambayo tegemeo kwetu na ambayo inaweza kututoa kwenye hali tuliyonayo, sekta ya kilimo ilitengewa bilioni 101 hadi sasa zilipelekwa bilioni 3.3 tu sawasawa na asilimia 3.31.

Mheshimiwa Spika, mifugo na Uvuvi vilitengewa bilioni 15.8 hadi sasa zilitolewa bilioni 1.2 tu sawa na asilimia nane, sasa tunavukaje hapa? Fedha za maendeleo katika sekta hii ya kilimo ambayo ni kilimo, mifugo na uvuvi na shughuli zote zinazohusiana na uvunaji na kilimo, zilitolewa chini ya asilimia 97 katika Wizara hii. Sasa tutaongea sana, tutapanga sana lakini hatuwezi kutoka hapa tulipo kwa kutokuwekea kilimo kipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka 2015 nchi yetu ilianzisha Benki ya Kilimo ambayo ilitarajiwa kupewa trilioni moja, lakini Benki hii mpaka sasa imepewa bilioni 60 tu. Benki hii ili-target kuwapa mikopo wakulima 200,000 kila mwaka, lakini mpaka sasa ni wakulima 3,700 tu wameweza kupata mkopo. Kwa hali hii hatuwezi kuvuka hapa tulipo, umaskini bado utaendelea kuwa pamoja nasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa nane wa kitabu cha Mpango kimesema kwamba baadhi ya shughuli za kiuchumi zilishindwa kufikia maoteo ya viwango vya ukuaji ikiwemo sekta ya kilimo ambayo ni dhahiri sasa tunajua kwa sababu gani ambayo iliweza kukua kwa asilimia 2.1 tu. Shirika la Chakula Duniani (FAO) 2014 ilisisitiza tena kwa nchi maskini za Afrika tujikite katika kilimo, kilimo ndio kinachoweza kutuletea maendeleo.

Mheshimiwa Spika, jopo hili la wataalam limesema kwamba tuendelee kushikilia Maputo Declaration ambayo tuli-commit Watanzania kutenga ten percent ya bajeti yetu kwenye shughuli za kilimo na kuhakikisha pia kwamba kilimo hiki angalau kinakuwa kwa six percent kwa mwaka, sisi tupo chini ya hapo, tunaongelea two point, one point, hatuwezi kuvuka. Naomba bajeti iangaliwe upya iweze kujikita katika hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mifano iko mingi ya nchi ambazo ziliweza kuendelea, hata Wakoloni wetu Waingereza miaka ya 1800 walikuwa na agricultural revolution ndio wakafika hapo sasa hivi, sasa kwa nini sisi hatuamki wakati tuna mifano na tukijua kwamba population yetu asilimia kubwa ni hawa wakulima? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali pia katika ukurasa wa saba wa kitabu cha Mpango namba 12 imekiri kuwa mfumko wa bei ulikuwa pia umechangiwa na ukame au kuchelewa kwa msimu wa mvua. Wabunge wengi ni Wabunge wa maeneo ya vijijini ambao wanashughulika na kilimo na Wabunge wengi tumeona njaa mwaka huu na bado wananchi wetu wanalia kwa njaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasisitiza kwamba Serikali sasa inabidi iwekeze pia kwenye sekta ya maji, kwenye irrigation hatuwezi kuvuka kwenye kilimo cha sasa hivi cha kutumia jembe na kutegemea mvua tukasema kwamba tutaweza kupata maendeleo.

Mheshimiwa Spika, nilipatwa na kigugumizi, nimepatwa na bumbuwazi kuona kwamba issue ya road license malipo yake yamepelekwa kwenye lita ya mafuta. Wiki kadhaa zilizopita humu Wabunge karibu asilimia kubwa waliosimama kwenye sekta ya maji, walikuwa wanapendekeza Sh.50/= kwenye kila lita ya mafuta kwa ajili ya Mfuko wa Maji, sasa road license mnajaribu kumbeba nani katika hili, inamsaidia nani? Ile tozo ya shilingi 40 kwa kila lita inakwenda kujenga barabara, barabara inamsaidiaje Mtanzania ambaye anakufa na njaa?

Mheshimiwa Spika, kwa nini hiyo hela wasitafute means nyingine za kuwasaidia hao wenye kudaiwa hiyo road license au malimbikizo yao, badala ya kuwapongeza kwa kuweka kwenye lita ya mafuta. Mheshimiwa Shabiby yeye anakuja na concept yake kwamba inakuwa ina unafuu lakini haina unafuu, inakwenda kuwakandamiza wakulima, inaenda kutukandamizi sisi, maji ni uhai tutaendeleaje hivi?

Mheshimiwa Spika, hii naomba iangaliwe upya iwe reviewed ile Sh.50/= ambayo ilikuwa inakwenda kwenye Mfuko wa Maji iendelee kuwepo kwenye Mfuko wa Maji kwa sababu hii ndiyo itakayotukomboa sisi, bila maji maendeleo yanapatikana wapi? Bila maji kilimo hakipo, hatuwezi kuwa tunategemea kilimo cha mvua wakati kuna mabadiliko ya nchi ambayo hata sisi tumeshindwa ku–accommodate. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, dhima ya bajeti ya mwaka wa 2017/2018 imejikita katika kujenga uchumi wa viwanda utakaochochea ajira na ustawi endelevu wa jamii. Naomba tu niwaachie hili swali, kivipi? Hapo tu, naomba mkajitafakari kwa hapo, najua mna timu yenu ya wataalam, Mawaziri najua mpo vizuri, naomba mtujibu, kivipi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 19 na 20 wa kitabu cha Mpango kimegusia suala very briefly mabadiliko ya maisha ya watu. Hotuba ilipogusia hili naona ilijizungusha bila kutuambia haijajielekeza umaskini utashuka au utashushwa kwa kiwango gani? katika nchi yetu na nafikiri walishindwa kujieleza utashuka kwa kiasi gani kwa sababu wameshindwa kushika zile sehemu muhimu ambazo zitatutoa wananchi kuondoa umaskini; kilimo na maji, elimu na vinginevyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bajeti iliyopita ilitekelezwa kwa chini ya asilimia 30 na miradi ya maendeleo haijawahi kuzidi asilimia 40. Nafikiri hapo ndio maana Mheshimiwa Waziri alipata kigugumizi cha kuweza kutueleza kwa umakini, umaskini unaweza ukaondoshwaje...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Nina mambo saba ambayo nataka nigusie na nitajielekeza katika taarifa iliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi pamoja na Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nigusie kwanza suala la NFRA. Kumekuwa na sintofahamu mwaka wa fedha 2016/2017 kuhusu njaa, kukatokea statements mikanganyiko kuhusu kuna njaa au hakuna njaa nchini. Hii ilijitokeza kwa sababu baadhi ya mikoa ilizalisha vizuri na mikoa mingi zaidi nchini kwetu ilikuwa kwenye hali ya ukame na kutokuwa na chakula. Nchini kwetu tumejiwekea tu mfumo mzuri wa kuwa na NFRA ambayo basically inatakiwa i-regulate mifumuko ya bei ya vyakula kwa kuhifadhi na kutoa vyakula hivi masokoni ili ku-balance bei ya chakula na kuhakikisha kwamba kuna chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kusikitisha ni kwamba budget allocation ambayo inatakiwa iende specifically kwa ajili ya NFRA ina utata, fedha hazitolewi kwa wakati na ni kidogo kwa hiyo mazao yanayonunuliwa ni machache na hayaendani sawasawa na msimu. Kwa hiyo, pesa zinapatikana nje ya msimu na kuathri mzungunguko mzima wa stock na mazao kwa ujumla wake. Naona tunaelekea kwenye dalili hizohizo kwa 2017/2018, kwa hiyo naomba Wizara iangalie tena hili kwa upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo nataka niligusie ni kuhusu taasisi zetu za tafiti ambazo ziko chini ya Wizara ya Kilimo ambazo pia zipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Huwezi kufanya mabadiliko yoyote au decision yoyote bila kuwa na scientific back up ya information au kuwa na data mahsusi. Cha kushangaza tunapopitisha bajeti humu ndani, hizi taasisi mahsusi za kufanya utafiti kwa ajili ya fertilizers au mbegu kadhaa au kwa ajili viuadudu kadhaa, haipangiwi hata senti tano. Inashangaza tunasema kwamba Tanzania inategemea kilimo, majority ya wananchi wetu ni wakulima, huu uti wa mgongo mbona hatuuwezeshi kwa kuziwezesha hizi taasisi zetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano tu, tuna shida, nafikiri juzi tumeona Waheshimiwa Wabunge Ulanga imeingiliwa na panya, wanavamia mipunga, Serikali iliwahamasisha wakulima wa pamba wakalima sana wakaingiliwa na wadudu (viwavijeshi) na kadhalika. Kwanza hatuna hata bajeti ya kuweza ku-handle, mfano kwenye issue ya pamba Serikali imetoa bilioni tatu tu ili kuweza ku-save mazao hayo kati ya bilioni 39. Kuna Mfuko wa Waziri Mkuu hapa kuhusu maafa hakuna kitu, Wizara iliombwa iweze ku-shuffle kidogo bajeti yake, Hazina haijatoa hata senti tano kwa ajili ya ku- deal na hao wadudu wanaovamia mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, NFRA ina hela tata, TPRI kwa mfano au taasisi nyingine za shughuli za tafiti hakuna hela, yametokea majanga hakuna hela. Sasa tunaongelea matumbo yetu kuhusu chakula na pia tunaongelea mazao ya biashara, hii nchi inasimamaje na wakati uti wa mgongo hatuuwezeshi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu ambalo nataka niligusie kwa juu juuu pia ni bei elekezi na soko la bidhaa za mazao yetu. Tumeweza kulima mazao ya chakula, tumeweza kulima kidogo kwa kuchechemea mazao ya biashara. Serikali inaji-commit wakulima walime mazao fulani, mfano dhahiri ni mwaka jana na mwaka huu bado tuna-suffer na wakulima wetu wa mbaazi, soko halieleweki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tulihangaika huku kuhusu mazao ya mahindi, tukatokea na sintofahamu Kambi ya Upinzani ilishauri ruhusuni hata kutoa mazao hayo, NFRA inunue na kutoa mazao bei iwe elekezi ambayo ni nzuri kwa wahitaji, tuuze mazao yetu, mahindi yetu nje ya nchi. Decision imekuja kuongelewa hapa tukabezwa upande wa Upinzani lakini baadaye mlikuja kusema go ahead, lakini it is too late. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya mifumo ya masoko yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nigusie kuhusu uvuvi haramu na njia zinazotumiwa na Wizara husika kuudhibiti. Kwa mfano, mwezi huu uliopita, Wizara yangu hii ya Mifugo na Uvuvi ilijikita Mwanza ilikuwa Ukerewe, ikisema inadhibiti uvuvi haramu. Sasa unajiuliza ni kudhibiti au ni kumkandamiza huyu mvuvi? Ni ipi njia sahihi ya kumdhibiti huyu anayeitwa mvuvi haramu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwenye taarifa ya habari kwamba Katibu Mkuu wetu wa Uvuvi ameteketeza nyavu haramu za shilingi bilioni 2.6 Mwanza kwa ujumla wake. Unajiuliza hizi nyavu za gharama hii zimeingiaje nchini? Miaka nenda rudi tunasema tunachoma moto tonnes and tonnes za hizi nyavu lakini unajiuliza kwamba unadhibiti vya kwenye maji, vya kwenye ardhi je? Kwa sababu ukiangalia hata hiyo mode mnayoteketeza mnaharibu pia mazingira. Kwa hiyo, kwanza mnaharibu mifuko ya wale walionunua hizo nyavu, mnaharibu uchumi wa wale wavuvi wahusika kwa sababu hamwendi tu kuharibu nyavu bali hata zile sehemu zao za kuvulia, camps zao mnachoma moto, vifaa vyao vya kuvulia kama maboti mnachoma moto, kulikoni? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, badala ya ku-solve issue permanently mnakuwa mnagusiagusia na kuweka gharama kubwa na kutia watu hasara na kuharibu mazingira mengine kwa kuchoma yale manailoni in open space. Kuna vikundi vya BMU, je, mmevihamasisha, mmeviwezesha kuweza kujikidhi kwa sababu vipo specifically kwa ajili ya ku-regulate uvuvi haramu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tano ambalo naomba nigusie ni kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilomo (TADB). Benki hii ilianzishwa nafikiri 2015 na ikapewa mtaji wa 60 billion na mpaka tunaongea sasa hivi benki hii haijawezeshwa, imeokoteza hapa na pale sasa hivi ina only 66 billion kama mtaji kati ya bilioni 800 ambayo inatakiwa iwe nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea maendeleo ya kilimo, yanatoka wapi? Hii benki iliwekwa mahususi kwa ajili ya kuendeleza kilimo… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mungano na Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi ili nitoe maoni yangu katika Wizara hii husika na nitajikita katika eneo la mazingira. Katika eneo hili nitagusia maeneo matatu ambayo ni Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira; hali ya misitu nchini na athari za mazingira yaani environmental impact assessment ambayo inaratibiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Miradi kupitia NEMC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kuzungumzia kuhusu Mfuko wa Mazingira na naomba ni- quote hotuba ya Waziri akisisitiza kwamba sekta zote za uzalishaji mali zinategemea mazingira na hivyo rasilimali zinazotokana na mazingira zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi na hivyo shughuli zisizo endelevu za uzalishaji mali zimechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Nilikuwa nataka tujikumbushie pia siyo tu kwenye mali au kwenye uchumi lakini sekta zote za kimazingira ndiyo uhai wetu, ndiyo tunachokitegemea. Ni hewa tunayoivuta, maji tunayoyanywa, ni vyakula tunavyovipata kutoka kwenye ardhi au wanyama au mimea yoyote. Cha kushangaza hiki tunachokitegemea ili tuwe hai, wenye afya na wenye uchumi mzuri wa binafsi na wa nchi hatuupi kipaumbele na kipaumbele hiki jinsi kilivyo chini kimekuwa reflected kwenye bajeti inayotengewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfuko huu wa mazingira ambao unasimamia dhamana ya uhifadhi wa mazingira nchini mwaka unaoenda kuisha 2017/2018 ilikuwa umetengewa shilingi milioni 300 tu na hawakupata hata senti. Mwaka huu wa fedha unaokuja 2018/2019 imetengewa shilingi milioni 500 tu. Sasa sijui kati ya hizo shilingi milioni 500 zinaenda kufanya nini na probability ya kuzipata haipo wakati hili ni eneo nyeti ambalo ndiyo linalotuweka hapa duniani na linatufanya tuishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu cha Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, ukurasa wa 16 walionesha chanzo ambacho tunaweza tukapata fedha kidogo kwa ajili ya Mfuko huu wa Hifadhi wa Mazingira nchini. Pale kwenye bullet ya pili wamesema kwamba tozo zinazotokana na shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira ni nyingi lakini zinakusanywa na taasisi au idara nyingine za Serikali. Kamati inashauri tozo hizo walau kwa asilimia tano ziingie katika Mfuko wa Mazingira mfano tozo za magari chakavu, mkaa, mafuta na magogo.

Mimi nilikuwa na-propose siyo asilimia tano tu bali twende hata asilimia 90 kingine kidogo ndiyo kibaki kwenye sekta nyingine ili ku-make sense. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo langu la pili nililokuwa nataka niliongelee ni tathmini athari za mazingira ambapo wanasimamiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Hii ni nyenzo ya pili ya kusimamia hali ya mazingira yetu nchini, lakini hawa NEMC ambao ndiyo kitendea kazi chetu na wasimamizi nao wamekatwa mikono. Bajeti hii iliyopita wamepata tu asilimia 36 ya kile walichokiomba ili wafanye kidogo wanachoweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hizi hela zinazotengwa na nyingine za maendeleo hawapati kabisa, tunafanya hivi makusudi kujiharibia wenyewe au hatuna wataalam wa kusisitiza umuhimu wa mazingira nchini na katika uchumi na hali ya wananchi wetu. Tatizo ni nini? Ni Serikali haina macho na masikio, hatujifahamu au tunajifahamu lakini tunafanya makusudi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mifano michache, sasa hivi ni nyakati za mvua za masika, Dar es Salaam tunalia mafuriko, Arusha tunalia mafuriko na Morogoro tunalia mafuriko. Ukiangalia kwa upana wake mafuriko ya Dar es Salaam literally hayakutakiwa kuwepo. Mafuriko ya Dar es Salaam yamechangiwa na mito mikuu miwili mmojawapo ni Mto Msimbazi. Kwa mfano tu kwenye Bonde la Mto Msimbazi eneo la Jangwani kuna mradi pale wa Serikali (UDART), sasa unajiuliza NEMC walikuwa wapi, environmental impact assessment (tathmini ya uharibifu wa mazingira) iko wapi kwa sababu hii mito ina overflow kwa sababu mto una njia yake ya asili. Sasa tunapoanza kuingilia njia za asili za mito aidha kwa ujenzi au kutupa taka mle ndani tunaifanya iteme (overflow) kwa sababu tumeingilia lile bonde. Sasa unajiuliza, mkono wa NEMC ulikuwa wapi kwenye mradi wa UDART kwa sababu tayari wananchi wa kawaida waliondolewa. Sasa tunalalamika mafuriko na kuwaletea wananchi hasara na vifo juu yake kwa sababu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nataka nijiulize nikawa nasema okay, NEMC hawana hela, lakini nawafahamu NEMC wana wataalam, ni colleagues wangu, kwa hiyo shida siyo utaalam. Hapa sasa kuna la ziada zaidi ya hela. Tukumbuke kwamba NEMC ni mkono wa Serikali, NEMC huyu ndiye mtathmini wa shughuli za Serikali kwenye masuala ya mazingira, NEMC ana-evaluate vipi mradi wa Serikali ambapo naye ni mpango wa Serikali? Kwa hiyo, decisions tunazifanya politically badala ya kufanya kitaaluma. Kwa hiyo, nafikiri hii NEMC iangaliwe kwa jicho la ziada iwe an independent entity ya kusimamia madhara haya tunayoyaona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nigusie haraka haraka, kuna proposal naona inaanza kuzaa matunda ya uzalishaji wa umeme Stieglers Gorge. Mradi huu proposal ya kwanza ilianza 1960 lakini umeenda ukisuasua siyo kwa bahati mbaya lakini ni kwa sababu ya athari za mazingira. Stieglers Gorge iko ndani ya Selous Game Reserve, the largest game reserve, si ndiyo? Ina wanyama na ikolojia ambazo ni unique, ni world heritage site. Mradi huu ambao unaenda kuanzishwa unaenda ku-affect Mto Rufiji na vyote vinavyohusiana na Mto Rufiji. Kwenye mdomo wa Mto Rufiji kuna mangroves/mikoko, ni msitu mkubwa kuliko yote kwa East Africa. Mto Rufiji ndiyo unaoifanya Mafia yako iwepo Mheshimiwa Dau, naomba uniunge mkono kwenye hili. Mradi huu unaenda ku-affect Ramsar Site ya Mafia, Kilwa na Rufiji. Sasa tunaenda kuangalia siyo uhai tu shughuli za uvuvi bali na wananchi wote wanaotegemea pale, maeneo yote ya Kilwa, Rufiji, Mtwara wote mnaenda kupata changamoto za kimazingira na za kusihi. Sasa tunavyoongelea haya mambo ya environmental impact assessment ndugu zangu tusiende politically (kisiasa).

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Katika Wizara hii maoni yangu yatajikita katika elimu ya msingi na sekondari. Nimeamua ku-concentrate hapa kwa leo kwa sababu hawa ndiyo foundation. Tunasema elimu ni ufunguo wa maisha na hawa ndio foundation yetu, ni msingi wa kile tunachokizalisha katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa mwaka huu uliopita ni asilimia 60 ya wanafunzi wetu wa elimu ya msingi na sekondari wamefeli. Nita-specify katika kidato cha pili na cha nne kwa mwaka 2017, wanafunzi hawa wamepata division four na division zero. Ni janga wala siyo dogo, lakini Serikali inatakiwa iliangalie sana na kati ya hawa waliobaki asilimia 40 ya waliofaulu 90% wametoka katika shule binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto kadhaa za wamiliki wa hizi shule binafsi wanakuwa wanakandamizwa na Serikali. Mifano miwili kutoka kwa wanafunzi wale wanafunzi wanaosoma katika hizi shule binafsi hawana ruhusa au hawawezi kwenda kusoma shule za government kama kukatokea tatizo lolote. Pia hawa wanafunzi wanaosoma shule binafsi hawapati mikopo kwa ajili ya kupata access ya elimu ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika shule binafsi ambazo sasa zinatuokoa katika elimu zetu za msingi na sekondari, wana maeneo ambayo yanawakandamiza. Moja kati ya hayo wanasema kwamba wanalipishwa service levy na Halmashauri husika. Wanalipishwaje service levy wakati hawa tayari wanatoa service ya elimu? Naomba muwaangalie kwa jicho la kitofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo shule binafsi wanakandamizwa sana ni kwenye malipo ya property tax, wanalipa viwango sawa kama vile ni kumbi au ni hoteli wakati hawa ni watoa huduma wa elimu. Kwa hiyo, kama kuna umuhimu wa kulipia property tax basi wawe kwenye certain criteria/category ya kuangalia hawa ni watoa huduma lakini siyo wafanyabiashara wa moja kwa moja kulipisha madarasa au kumbi za shule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawazo mengi mbadala yametolewa na Kamati husika imetoa maoni mazuri sana naomba yazingatiwe. Moja kati ya hayo ni kujifunza kwa nini shule binafsi zinafanya vizuri ukilinganisha na shule hizi za Serikali. Majibu yapo pale, walimu na wanafunzi wanakuwa treated vipi na miundombinu inakuwa treated vipi. Huitaji rocket science kusema kwamba kwa nini tunafeli kwa sababu mazingira ni hafifu katika shule zetu za Serikali. Naomba tujifunze kutoka private sector na tusiwa-treat kama competitors bali tuwa-treat kama ni partners, ni wadau ambao wanaliokoa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoongelea maendeleo pia yanakuwa reflected kwenye bajeti ambazo tunazi-set aside kwa ajili ya maendeleo. Umuhimu wa elimu wala hauhitaji mjadala, kwa mfano ukienda kwenye subvote 2001, kwenye Basic Education Office, item ya 4321, Primary Education Development Programme LANES, mwaka 2016/2017 mliwatengea shilingi bilioni 65, mwaka 2017/2018 mliwatengea shilingi bilioni 39 na 2018/2019 mmewatengea shilingi bilioni nne tu. Sasa tujiulize lengo hapa la Serikali ni nini? Tayari tunafanya vibaya sana, hamuoni kama hii ni alert inabidi tujibadilishe. Tayari kuna tatizo, lakini hatuweki nguvu ambayo inakuwa reflected kwenye bajeti husika ili kuinua kiwango cha elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ambayo imeimbwa sana ni issue ya walimu, kwenye elimu ya hawa wanaoelimisha ambao ni walimu pamoja na idadi yao. Ratio yetu ya sasa hivi mnasema ni uwiano wa 1:50 wakati inayotakiwa ki-standard ni uwiano wa 1:25. Hapo hapo tunasema kwamba baadhi ya walimu wa sekondari wanaenda kufundisha sasa primary school, inakuwaje wakati tayari kuna upungufu wa walimu na bado mnataka tena kuwatoa kwenye level nyingine kuwapeleka kwenye level nyingine ambapo hawa walimu hawajasomea kwa sababu ule ualimu ni taaluma ambayo ina level mbalimbali, aidha, ni wa sekondari, chuo kikuu au nursery. Naomba tuliangalie kwa uangalifu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo linguine ambalo nataka niligusie ni kuhusu continuous assessment. Tunajikita kuwa grade hawa wanafunzi wetu kwa mitihani mikuu labda ni darasa la nne, form two, form four au form six lakini kati ya hawa wanafunzi ambao tunawa-grade ambao tunawapa siku moja au mbili kuwa-assess na kubadilisha maisha yao, tunakuwa hatuwatendei haki na baadhi ya hawa wanafunzi katika…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Katika Wizara hii maoni yangu yatajikita katika elimu ya msingi na sekondari. Nimeamua ku-concentrate hapa kwa leo kwa sababu hawa ndiyo foundation. Tunasema elimu ni ufunguo wa maisha na hawa ndio foundation yetu, ni msingi wa kile tunachokizalisha katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa mwaka huu uliopita ni asilimia 60 ya wanafunzi wetu wa elimu ya msingi na sekondari wamefeli. Nita-specify katika kidato cha pili na cha nne kwa mwaka 2017, wanafunzi hawa wamepata division four na division zero. Ni janga wala siyo dogo, lakini Serikali inatakiwa iliangalie sana na kati ya hawa waliobaki asilimia 40 ya waliofaulu 90% wametoka katika shule binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto kadhaa za wamiliki wa hizi shule binafsi wanakuwa wanakandamizwa na Serikali. Mifano miwili kutoka kwa wanafunzi wale wanafunzi wanaosoma katika hizi shule binafsi hawana ruhusa au hawawezi kwenda kusoma shule za government kama kukatokea tatizo lolote. Pia hawa wanafunzi wanaosoma shule binafsi hawapati mikopo kwa ajili ya kupata access ya elimu ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika shule binafsi ambazo sasa zinatuokoa katika elimu zetu za msingi na sekondari, wana maeneo ambayo yanawakandamiza. Moja kati ya hayo wanasema kwamba wanalipishwa service levy na Halmashauri husika. Wanalipishwaje service levy wakati hawa tayari wanatoa service ya elimu? Naomba muwaangalie kwa jicho la kitofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo shule binafsi wanakandamizwa sana ni kwenye malipo ya property tax, wanalipa viwango sawa kama vile ni kumbi au ni hoteli wakati hawa ni watoa huduma wa elimu. Kwa hiyo, kama kuna umuhimu wa kulipia property tax basi wawe kwenye certain criteria/category ya kuangalia hawa ni watoa huduma lakini siyo wafanyabiashara wa moja kwa moja kulipisha madarasa au kumbi za shule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawazo mengi mbadala yametolewa na Kamati husika imetoa maoni mazuri sana naomba yazingatiwe. Moja kati ya hayo ni kujifunza kwa nini shule binafsi zinafanya vizuri ukilinganisha na shule hizi za Serikali. Majibu yapo pale, walimu na wanafunzi wanakuwa treated vipi na miundombinu inakuwa treated vipi. Huitaji rocket science kusema kwamba kwa nini tunafeli kwa sababu mazingira ni hafifu katika shule zetu za Serikali. Naomba tujifunze kutoka private sector na tusiwa-treat kama competitors bali tuwa-treat kama ni partners, ni wadau ambao wanaliokoa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoongelea maendeleo pia yanakuwa reflected kwenye bajeti ambazo tunazi-set aside kwa ajili ya maendeleo. Umuhimu wa elimu wala hauhitaji mjadala, kwa mfano ukienda kwenye subvote 2001, kwenye Basic Education Office, item ya 4321, Primary Education Development Programme LANES, mwaka 2016/2017 mliwatengea shilingi bilioni 65, mwaka 2017/2018 mliwatengea shilingi bilioni 39 na 2018/2019 mmewatengea shilingi bilioni nne tu. Sasa tujiulize lengo hapa la Serikali ni nini? Tayari tunafanya vibaya sana, hamuoni kama hii ni alert inabidi tujibadilishe. Tayari kuna tatizo, lakini hatuweki nguvu ambayo inakuwa reflected kwenye bajeti husika ili kuinua kiwango cha elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ambayo imeimbwa sana ni issue ya walimu, kwenye elimu ya hawa wanaoelimisha ambao ni walimu pamoja na idadi yao. Ratio yetu ya sasa hivi mnasema ni uwiano wa 1:50 wakati inayotakiwa ki-standard ni uwiano wa 1:25. Hapo hapo tunasema kwamba baadhi ya walimu wa sekondari wanaenda kufundisha sasa primary school, inakuwaje wakati tayari kuna upungufu wa walimu na bado mnataka tena kuwatoa kwenye level nyingine kuwapeleka kwenye level nyingine ambapo hawa walimu hawajasomea kwa sababu ule ualimu ni taaluma ambayo ina level mbalimbali, aidha, ni wa sekondari, chuo kikuu au nursery. Naomba tuliangalie kwa uangalifu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo linguine ambalo nataka niligusie ni kuhusu continuous assessment. Tunajikita kuwa grade hawa wanafunzi wetu kwa mitihani mikuu labda ni darasa la nne, form two, form four au form six lakini kati ya hawa wanafunzi ambao tunawa-grade ambao tunawapa siku moja au mbili kuwa-assess na kubadilisha maisha yao, tunakuwa hatuwatendei haki na baadhi ya hawa wanafunzi katika…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kupata nafasi, na mimi niweze kutoa maoni yangu katika hoja iliyopo mezani.

Mheshimiwa Spika, nitaanza kwa sekta ya uvuvi. Naanza na sekta ya uvuvi kwa masikitiko makubwa sana kwa sababu ni sekta ambayo inaweza ikalitoa Taifa hili katika hali ya uchumi uliodorora tulionao sasa hivi. Sekta hii Mwenyezi Mungu ametujalia rasilimali ambazo tunaweza tukazitumia, tuna maziwa makubwa matatu hapa nchini yenye kilometa za mraba zaidi ya 54,000; Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Mheshimiwa Spika, tuna maziwa size ya kati na madogo zaidi ya 45; tuna mito mikubwa mingi, mizuri zaidi ya 20 na kitu; tuna Ukanda wa Pwani wa Bahari wa kilometa 1,420 na ukanda huu ndani ya maji ambayo wavuvi wetu wanavua zina kilometa za mraba 64,000 na ukanda wa uchumi EEZ wa zaidi ya kilometa za mraba laki mbili na kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, rasilimali zipo, viumbe ambavyo tunaweza tukavivuna au kuvifuga vipo, wavuvi na wanaofanya shughuli za uvuvi wako zaidi ya milioni nne, wavuvi wenyewe wako 200,000 na zaidi. Sasa ukiangalia rasilimali watu tulionayo na rasilimali zenyewe za uvuvi tulizonazo haziendani na tunachokipata. Maduhuli ya mwaka 2017 yaliyokusanywa na Wizara kwenye sekta ya uvuvi ni shilingi bilioni 21 tu. Nina uhakika pia kwamba shilingi bilioni hii 21 imeongezeka kwa sababu ya shilingi bilioni sita tuliyoipata kwenye operation sangara.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii bajeti yake kubwa yote ni shilingi bilioni 14 tu, lakini iliyoenda hii bajeti inayoishia mwaka 2017/2018 ni asilimia 52 tu. Bajeti ya maendeleo iliyotengwa katika sekta hii ilikuwa ni shilingi bilioni mbili, lakini kwa miaka mitatu yote iliyopita inasomeka sifuri kwenye vyanzo vya ndani. Sekta ya uvuvi sasa hivi wakisema wanafanya chochote cha maendeleo, basi ni katika mikopo ya Benki ya Dunia kwenye Mradi wa Sio Fish, lakini kama Taifa hatujawekeza katika sekta hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia mifugo na uvuvi kwa ujumla wake tunachangia katika pato la Taifa asilimia saba na kitu. Asilimia 5.6 inatoka kwenye sekta ya mifugo na asilimia 1.9 inatoka kwenye uvuvi, lakini ukiangalia hata hiyo mifugo yenyewe haijapewa kipaumbele japokuwa ina- contribute more hata kuliko kwenye sekta ya madini ambayo ina-contribute 4.5 nafikiri katika pato la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia uwekezaji jinsi ulivyo mdogo, tunasema kwamba kuna changamoto katika uvuvi, tunaenda kwenye ufugaji (aquaculture) lakini kitengo hiki kilitengewa shilingi milioni 800 tu katika kuhakiksha Aquaculture inakua nchini na imepata sifuri na haikuweza hata kukusanya maduhuli yoyote, inasomeka sifuri.

Mheshimiwa Spika, tangu miaka ya 1990 au 1980 tulikuwa tuna viwanda takribani 18 vya uchakataji wa mazao ya samaki. Tunapoongea sasa hivi, tuna viwanda nane tu, vingine vyote vimefungwa. By then katika viwanda 18 walikuwa wameajiri wafanyakazi 4,000 na zaidi na walikuwa wana-produce tani 1,000 na kitu za samaki. Sasa hivi viwanda vya samaki vimeajiri watu chini ya 1,000 na wana-produce tani chini ya 200, nafikiri ni tani 170 za samaki.

Mheshimiwa Spika, niende moja kwa moja kusema kwamba kumekuwepo na kilio kikubwa sana katika usimamizi wa rasilimali hizi za uvuvi ambazo tayari hatuzipi vipaumbele. Serikali ilianzisha mchakato mzuri kabisa kupitia sera yake ya 1997 ya uvuvi ya kutengeneza hivi vikundi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi yaani BMUs. Sasa hivi nchini nafikiri tuna BMUs 700 na kitu. Vikundi hivi katika upande wa Pwani pamoja na Ziwa Victoria, vimeterekezwa na Serikali. Kazi mahususi ya vikundi hivi ilikuwa ni kujisimamia wenyewe na kusimamia kazi za kulinda rasilimali hizi za uvuvi.

Mheshimiwa Spika, tumeshindwa kugatua madaraka kwamba Wizara husika iachie TAMISEMI isimamie BMUs kama ilivyo kwenye sheria tuliyojiwekea wenyewe namba 22 ya mwaka 2003 ya Uvuvi. Badala yake kumekuwa na mkanganyiko wa nani asimamie rasilimali za uvuvi wakati Halmashauri husika through TAMISEMI ndiyo walitakiwa wasimamie hao wavuvi wadogo wadogo wakiongozwa na BMUs?

Mheshimiwa Spika, sasa tumeona kumekuwa na matukio ya kutokujipanga vizuri kwa Serikali na kuanzisha hizi operation za papo kwa hapo ambazo zinaleta gharama kubwa sana katika utekelezaji wake na kuwaumiza wale wananchi, wakati tungekuwa na zile BMUs tungeziwezesha na kutoa elimu, basi hawa BMUs wangeweza kuzilinda hizo rasilimali na kuleta tija katika sekta hii ya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri tu ni katika Halmashauri ya Pangani, walikuwa wanatumia mawakala kukusanya mapato ya uvuvi. Walikuwa wanakusanya takribani milioni 25,000, lakini Halmashauri hii ya Pangani ilihusisha BMUs na wakawatumia hao BMUs kama mawakala na sasa hivi wameweza kukusanya mapato ya shilingi bilioni 140 na kitu, yaani ime-triple the amount.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tukiwawezesha, siyo tu wanaweza kuingiza fedha za Halmashauri husika na kujiwezesha na wenyewe pia kujifanyia shughuli zao, lakini pia wanalinda zile rasilimali za uvuvi. Sasa kwa nini hatuwi na hii mikakati ambayo tumejiwekea ambayo ni endelevu na iko tangible? Badala yake tunakurupuka na operesheni ambazo zinaleta vilio. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini nimesema tunakurupuka? Mbele yangu hapa, hii barua nafikiri nakala imekufikia, ni kutoka kwenye Chama cha Wavuvi wakiomba Bunge liingilie kati kwenye Operation Sangara na nina-quote machache waliyoyaandika. Wanasema ili kupata uhalisia wa mambo tunaomba kukutana na Kamati husika tuzungumze nayo, lengo likiwa ni pamoja na kuundwa Tume ya kutembelea na kuzungumza na wavuvi kwenye maeneo husika, hivyo kubaini hali halisi ya matokeo ya operation hizi.

Mheshimiwa Spika, ni kama ilivyokuwa kwenye Operation Tokomeza, yaani ya majangili, miaka ya nyuma Bunge na Umma walipata kujua uhalisia wa matokeo ya operesheni hiyo na matukio mengine baada ya Bunge kuunda Tume na kurejesha ripoti zake Bungeni.

Mheshimiwa Spika, sidhani kama wavuvi wamejitungia, ndiyo maana wamekuwa na uwezo wa kuja hapa Bungeni kutoa kilio chao kwamba hiyo operation ilivyoendeshwa imeleta madhara makubwa sana, kwa sababu baadhi ya maeneo wametumia nguvu za ziada, risasi za moto, mapanga na mabomu. Wameleta madhara makubwa sana.

Mheshimiwa Spika, hatukatai, mimi kama mwana mazingira sikatai kuhusu kutunza mazingira au kuleta operation special kwenye maeneo ambayo ni sugu ya uharibifu wa mazingira. Ila ni njia na mikakati gani tunayoitumia ili zilete uharibifu?

Mheshimiwa Spika, mfano tu mzuri ili tuweze kwenda sawa, traffic akikamata gari au basi lenye abiria akamkuta dereva hana leseni au amebeba mzigo siyo au amezidisha idadi ya abiria, nini kinafanyika? Anampa faini au anaenda mahakamani.

Mheshimiwa Spika, sasa kwenye uvuvi, mvuvi anapokamatwa kama ametenda kosa, labla hana leseni au amevua samaki kwa kutumia nyavu sizo, basi huyu mvuvi atatozwa faini, watataifisha zile mali na wanachoma moto mtumbwi au boti. Traffic ana uwezo wa kuchoma gari moja kwa sababu umevunja sheria? Traffic anataifisha gari kama umevunja sheria? Basi haya ndiyo yaliyotokea katika Operation Sangara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nia na lengo la Wizara inaweza ikawa nzuri lakini utekelezaji wake umeleta maafa makubwa zaidi kwa wavuvi hawa. (Makofi)

Kwa hiyo, naliomba Bunge lako liunde Tume kama walivyoomba hawa wavuvi, waangaliwe kwa jicho cha ziada ni nini kimetokea ili tupate kujifunza kwa operesheni zijazo, kwa sababu najua wanaenda operation namba mbili sijui au ni namba tatu, liangaliwe hivyo hivyo katika operesheni nyingine zitakazokuja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kumeletwa mbele yangu kilio kutoka kwa wavuvi, Chama cha Wavuvi vilevile wakihusisha operation hii na upatikanaji wa nyenzo za kuvulia. Sasa hivi nyenzo hizi kama vile nyavu na maboya yamekuwa ya bei juu sana kwa sababu ya kutokuingizwa au na baadhi ya hizi nyenzo zimezuiwa kuingizwa katika border ya Sirali. Kwa hiyo, wanaomba nyavu hizi ziwe available na ziweze kupatikana na kwa bei ile ambayo inaleta tija katika Taifa.

Mheshimiwa Spika, niliongelee jambo lingine lililoletwa mbele yangu ambalo ni Sheria ya Uvuvi. Wadau wakuu wa Sheria ya Uvuvi ambao ni wavuvi wenyewe, wanalalamika kwamba hawajahusishwa katika kuirekebisha sheria hii mpya ambayo inakuja soon mezani kwako, wapate kuzingatiwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, nashukuru na mengine nitaandika kwa maandishi.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kupata nafasi hii ili kutoa mchango wangu katika hoja iliyo mezani kwetu. Kwenye kitabu cha Mpango Hotuba ukurasa wa 15, mpaka 16, Mheshimiwa Waziri ameonesha changamoto tulizonazo ambazo zinatuletea mkwamo katika maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, changamoto hizo zilizotajwa, zipo tano, na tatu kati ya hizo, ameonesha kwamba ni ukosefu wa fursa za ajira, changamoto katika sekta ya kilimo, akisema kuna uwekezaji mdogo, tija ndogo, kutegemea mvua, sambamba na mchango mdogo wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa. Pia kuwepo kwa wigo mdogo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambao uwiano wa mapato ya ndani na Pato la Taifa ni takribani asilimia kumi na tano tu, ikilinganishwa na wastani asilimia kumi na saba.

Mheshimiwa Spika, niliposoma hivi, hizi kurasa za kwanza, nilitegemea kwamba huko mbeleni kurasa zinazofuata basi ni kuzigeuza hizi changamoto, kuwa opportunities (fursa). Sasa tukienda ukurasa zinazofuatia wanasema fursa, zipo, anakiri kwamba kuna nguvu kazi kubwa katika Taifa; halafu vikaishia hapo akaenda kuanza kuelezea mafanikio.

Mheshimiwa Spika, nilisikitika baada ya kuona hivi, kwamba ahaa kumbe tunajua shida yetu ni nini, kwa hiyo kwa nini hizi changamoto zisiwe reflected kwenye mipango yetu tunayojiwekea? Kwa nini changamoto hizi zisiwe reflected kwenye bajeti ambayo tutaitenga? Ukiangalia mipango tuliyonayo linganifu na bajeti tunayoitenga haviendani. Mpango wetu wa Miaka Mitano wa Taifa na mpango wa mwaka mmoja mmoja kwa kila mwaka wa fedha na bajeti tunazozitenga katika huo mwaka husika ni vitu vitatu tofauti. Hotuba ya mpango, hotuba ya bajeti, kitabu cha mpango, mapendekezo ya mpango havina uhusiano, ni kama vile vimeandikwa na taasisi tatu tofauti.

Mheshimiwa Spika, pia kuna mkinzano mkubwa sana kati ya sera na vipaumbele vyetu. Tunasema tuna Sera ya Serikali yetu ya Tanzania ni ya Viwanda. Viwanda hivyo haviwi reflected kwenye mipango strategy ni viwanda vya aina gani, sources za raw materials za hivyo viwanda ni vipi? Mheshimiwa usitingishe kichwa, kila kitu kimeandikwa kwenye vitabu, sijavitoa hewani. Ukiangalia pia na kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa letu, vivyo hivyo haiwi reflected japo inaonesha kwamba Kilimo kina contribute zaidi, nikisema kilimo, ni kilimo chenyewe, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu; tunasema ina- contribute asilimia thelathini, kinachofuata ni asilimia kumi na tano kutoka sekta ya ujenzi.

Mheshimiwa Spika, Sasa tunatokaje hapa kwa sababu tuna maandishi ya tofauti tofauti? Nikawa nawaza shida ni watendaji, shida ni matamko ya kisiasa au kuna kitu cha ziada? Mfano tu wa haraka haraka labda kuna sintofahamu ya wafanyakazi katika Wizara husika inayohusiana na mambo yetu ya bajeti na mipango. Aidha, wafanyakazi hatuna motivation au kuna hidden agenda ambayo siielewi, kwa sababu kila kitu kiko wazi na Waziri mwenyewe amesema changamoto ni zipi zinazotukwamisha tusiende lakini hakuna solution, tunaruka hapa na pale.

Mheshimiwa Spika, katika kitabu chetu cha Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano ilisemwa kwamba tutahitaji takriban trilioni mia moja na saba kwenye shughuli za maendeleo ili tuvuke, ikimaanisha kwamba Serikali yenyewe itakuwa inatoa trilioni 11.8 takribani na sekta binafsi zitachangia trilioni 9.6, jumla trilioni 21 kwa ajili ya shughuli za maendeleo ili tuweze kuvuka.

Mheshimiwa Spika, lakini bajeti hii inayoishia na bajeti inayokuja tumetenga tuu trilioni 11 na kwa ajili ya shughuli za maendeleo na ni contribution ndogo sana kutoka katika Sekta binafsi. Mwaka huu unaoishia kati ya trilioni kumi na moja tuliweza kutoa trilioni 5.12 tu. Kati ya fedha hizo za maendeleo, kilichotolewa katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ni asilimia 34. Tunaenda kujenga reli, kununua ndege na kadhalika, trilioni 1.7 zilitoka. Hizo zilizobaki sasa trilioni 2.43 ndizo zilienda kwenye sekta nyingine zilizobaki katika wizara nyingine. Cha kushangaza, katika hizo trilioni mbili zilizobaki, mifugo na uvuvi, hawakupata hata senti tano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia sasa hiyo sekta ambayo ndio wananchi wengi tunasema wapo humo, according to statistics za nchi inasema inaajiri asilimia 66 lakini ninahisi ni zaidi ya hiyo asilimia 66.3 ya kaya zote nchini, ambao wanajishughulisha na shughuli za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu.

Mheshimiwa Spika, tunasema kwamba kilimo huchangia kwa ujumla wake, asilimia 20 ya mauzo ya nje na kinakua kwa pace ndogo sana, haishangazi kwa ni nini kwa sababu hatujawekeza katika hii sekta. Mifano tu dhahiri ya nchi za wenzetu, mfano nchi ya Brazili, wenyewe wametoka, ni nchi ya nane kwa uchumi mzuri duniani. Hata hivyo walitokaje? Wali-invest kwenye kilimo hususan kilimo cha kahawa. Wali-invest kwenye kilimo cha kahawa na waka- invest kwenye viwanda ambavyo vinashughulika na shughuli za kahawa, ikainua sekta nyingine baada ya kufanikisha kilimo.

Mheshimiwa Spika, sasa leo hii Tanzania labda tuna shida ya kuwa na rasilimali nyingi mno ambazo zinatakiwa zijenge uchumi, kwa hiyo hatujui Tanzania inasimamia wapi. Tanzania uchumi wake unaendeshwa na nini, tukimwuliiza leo Waziri wa Fedha, Tanzania inaendeshwa na nini? Is it kilimo, kilimo chenyewe ambacho hatuja-invest? Ni utalii, madini au ni kitu gani? Leo hii ukiwafundisha watoto wa shule Tanzania inajivunia kwenye nini katika kuendeleza uchumi wake hatuwezi kusema.

Mheshimiwa Spika, kama sekta hiyo sasa, ambayo tunasema ndiyo inayoajiri watu wengi zaidi, yaani wananchi ndiyo wanayotegemea hii sekta imenyamaziwa kimya, mifugo na uvuvi imenyamaziwa kimya. Sana sana sasa hivi tuna sintofahamu ya jinsi ya kutoka kwa kudhibiti uvuvi haramu tena kwa kutumia njia ambazo si sahihi, za kuzidi ku-frastrate hawa wananchi wachache.

Mheshimiwa Spika, mfano tu, sawa tumewanyima fedha za kufanya shughuli za maendeleo, lakini sekta hizi; si kilimo, si uvuvi, si kwenye sekta ya mifugo, kuna upungufu wa zile asilimia 50 ya wale maofisa wanaotakiwa wawaguse wananchi na kuwashika mkono kuinuka hapo walipo. Kwa mfano, Maafisa Ugani ambao ni muhimu sana waliopo ni elfu saba na kati ya vijiji elfu kumi na tano na, wakati kila kijiji kilitakiwa kiwe na Afisa Ugani mmoja.

Mheshimiwa Spika, sasa hapa tunatokaje tokaje? Hatuwezi kutoka tutakuwa kila siku uchumi uko mdogo, kila siku tunaletewa makablasha na maandishi ambayo hayaendi kufanya kazi. Sasa unajiuliza ni kwa nini, wakati kila kitu kiko obvious na tunaweza tukatoka hapa? Nia ya Serikali ni nini?

Mheshimiwa Spika, katika kutuchanganya pia sasa Serikali kwa hiyo hela kidogo iliyonayo na hatuoni mkakati dhahiri wa kulea hizi sekta ambazo zinaweza zikatutoa, sasa wanakuja na proposal ya kuweka fedha zote za Taifa hili katika Mfuko mmoja ilhali kuna mifano mingi ambayo inawakwaza Wananchi. TRA wanasema wanakusanya mapato lakini literally wanakuwa wanashikia wa sekta binafsi fedha zao. TRA inadaiwa bilioni thelathini na sita kutoka katika sekta ya sukari, hii sukari ya viwandani, ile asilimia 15, wamegoma kurejesha. TRA hawa hawa wanadaiwa na Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) bilioni 14.8. TRA hao hao wanadaiwa na REA.

Mheshimiwa Spika, apart from hayo madai wanayodaiwa ambayo hela sio zao nao wanazi-claim kama mapato na kudanganya Bunge lako kwamba in totality uchumi unakua, uchumi haukui, hizi ni hela za watu, Bodi ya Korosho wanadai bilioni themanini na moja, lakini in totality mwaka wa Fedha uliopita na huu wanawadai milioni mia mbili na, lakini wanaziweka kwenye Mfuko Mkuu na kusema kwamba mapato yameongezeka, lakini si mapato hizi ni hela walizokopa kwa watu wa Sekta tofauti tofauti.

Mheshimiwa Spika, kuna issue pia ya ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma, kama ni wakandarasi, na kadhalika. Mfano, TANROADS na TBA nchini wamekuwa wana-delays za kulipa wakandarasi na watoa huduma mbalimbali. Kwa mwaka huu wa fedha unaoisha TANROADS na TRA wanadaiwa jumla bilioni mia tano themanini na saba…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, sasa kwa mwenendo huu, kuna mchezo sasa hivi wa Serikali kupora mapato ya wengine kwa kusema kwamba tunawawekezea lakini hawayarejeshi, kuna mtindo wa kuchelewesha au kutokupeleka kabisa kwa wale wanaowadai Serikali. Sasa inasikitisha kwamba na changamoto zote hizi Serikali bado sasa inataka kurudi kwenye Centralization System na kuacha Decentralization ili tu kuficha ile aibu kwamba tuna shida ya fedha katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii haiwezi kututoa hapa kama hatuwezi kuleta mikakati mahsusi ya kututoa hapa zaidi ya wao Serikali, kung’ang’ania mapato ambayo si yao ili kuficha tuu aibu kwamba tuna shida katika uchumi wetu. Naomba kama Serikali kama inataka kurudi kwenye Centralization System waache D by D, walete sheria hapa Bungeni ili tuweze kuja na mkakati wa kusema kwamba tumeshindwa huku tunataka kurudi huku kuliko kutuchanganya wananchi na Bunge lako kujua kwamba direction ya Serikali hii inaendajeendaje.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii na mimi niweze kutoa maoni yangu katika mpango ulio mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipata fursa kwenye Kamati yetu ya Bajeti kuongea na Serikali kuhusu Mpango huu na ninaomba nirejee tena kwa issues nilizozi-raise. Nilikuwa nasema ni ngumu kujua nchi yetu inasimamia uchumi gani na ina mipango gani kwa ujumla wake. Mfano, muhula wa Mheshimiwa Rais Mwinyi alisimamia soko huria na ni kipindi hiki ambacho mashirika mengi na viwanda vyetu vya Serikali vilifungwa. Alipokuja Mheshimiwa Mkapa alisimamia ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma na aliimarisha TRA pamoja na kuzingatia zaidi katika ulipaji wa madeni ya nchi. Kipindi cha Mheshimiwa Kikwete yeye alikuwa na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania na alijikita zaidi katika ujenzi wa miundombinu. Muhula huu tulionao sasa Mheshimiwa Magufuli amesimamia uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu nilikuwa najiuliza, core business ya nchi hii ni nini? Mwanafunzi labda anapojifunza uchumi au jiografia ya nchi fulani uchumi wao ni wa nini? Tunatoa mawazo mbalimbali, Wajumbe wengi hapa wanaongelea kuhusu sekta nzima ya kilimo kwamba wananchi wengi wa nchi hii tumesimamia katika ufugaji, uvuvi na kilimo chenyewe au bidhaa za misitu, ndio majority ya wananchi wetu. Katika nchi yetu kila kipindi cha miaka kumi tuna lengo fulani, lakini taswira kubwa ya nchi ni nini? Umaskini upo pale pale na mikakati na mipango hii tunayojiwekea kila wakati huenda ikibadilika na mara nyingi haifikii hata nusu ya malengo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti,tukiangalia katika kitabu chetu cha Mpango kwa ajili ya mwaka huu wa fedha unaotaka kuja, vipaumbele vimewekwa katika maeneo nane. Kati ya hayo, saba ni kwenye sekta ya miundombinu na moja imeongelea kuhusu kusomesha kwa wingi wataalam kwenye fani ya ujuzi adimu, mfano uhandisi, urubani, udaktari bingwa na ufundi. Tunarudi kwenye swali nchi yetu inaenda kwa kutegemea nini? Tunarudi pale pale kwenye sekta ya kilimo. Sasa uko wapi huu mfungamanisho wa kile tunachokifanya na hii sera ya viwanda tuliyona sasa hivi? Uko wapi mfungamanisho wa hii sera ya viwanda na shughuli za elimu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ungetegemea kwamba kwa miaka hii mitano ya muhula huu mpya wa Mheshimiwa Rais Magufuli tunasema kuhusu viwanda, tungeona iko reflected kwenye sekta ya elimu, VETA zinafanya nini, vyuo vikuu vinafanya nini kwa ajili ya viwanda gani? Tungeona mfungamanisho wa sekta ya viwanda na shughuli za kilimo kwa ujumla wake. Pembejeo zikoje, tuna shida ya masoko, vifaa vya ukulima na vifaa ya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mabunge yaliyopita kulikuwa na Kamati kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu na tulionyesha ni rasilimali ambayo iko tu hatujaifanyia investment yoyote. Tangu niingie Bunge hili nilikuwa naona kuna mipango inaongelea kuhusu bandari ya uvuvi ili kuijenga sekta ya uvuvi hususan katika bahari kuu, lakini haipo humu ndani, iko silent.(Makofi)

Mheshimiwa Menyekiti, sasa unajiuliza Serikali yetu inataka kusimamia nini? Kwa hiyo, inakuwa ni rahisi sisi kama Wajumbe wako kuweza kuchangia katika Mpango, lakini inakuwa ni kama Q&A, tunatoa mapendekezo majority ya hayo mapendekezo yanakita kwenye sekta ya kilimo, lakini majibu yanayokuja tutarudia pale pale kwenye miundombinu. Miundombinu kwa ajili ya nani na kwa ajili ya nini? Ni wakati gani unatakiwa u-invest katika miuondombinu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea SGR inaenda kihatua hatua kwa fedha za ndani, inaishia Morogoro, itaishia hapa Dodoma and then what? Tunataka lane sita ya kutoka Dar es Salaam, mradi wa Chalinze - Dar es Salaam, ulikuwepo ni mzuri lakini umeishia katikati, tunataka nini? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Hoja yangu itajikita katika ukurasa wa 25 wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo imeelezea kuhusu kusimamia miradi ya Shirika la Taifa (NHC).

Mheshimiwa Spika, kwa kifupi naungana na maoni ya Kamati kwamba National Housing Corporation imesitisha miradi yake ya ujenzi kwa maendeleo ilhali kwamba iko katika mikopo. Sasa mikopo hii inazidi kukusanya riba inakuwa ni hasara katika uchumi wa nchi. Kwa hiyo, naomba Serikali ijitathmini kwa upya ili kuwezesha shirika hili likaendeleza kazi yake.

Mheshimiwa Spika, suala la pili katika maoni ya Kamati, ukurasa wa 23 inaongelea tishio la kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu. Sasa naomba nijikite zaidi katika kulichanganua hili.

Mheshimiwa Spika, mto huu wa Ruaha Mkuu, ni moja ya mito ambayo ni muhimu sana katika nchi yetu. Kwanza, inasaidia katika Sekta nzima ya Utalii ambayo ina-link na sekta nyingine za kiuchumi kwa ujumla wake. Katika hali ya sasa, Sekta ya Utalii ina-contribute 17% ya tunachokipata kama forest contribution takribani sawasawa na Dola bilioni 2.1 kwa mwaka. Kwa hiyo, ni sekta ambayo ikilelewa au ikiangaliwa kwa jicho la ziada inaweza ikatutoa katika hii hali ya umasikini na kwenda kwenye uchumi wa kati.

Mheshimiwa Spika, ni kwa sababu gani inaweza ikatutoa hapa tulipo? Sekta ya Utalii inagusa sekta nyingine mbalimbali. Ni mambo ya hoteli, mambo ya usafirishaji, mambo ya vyakula, mambo ya exchange rate, ina-influence hapo. Kwa hiyo, tuiangalie kwa jicho la ziada kwa sababu
mto huu Ruaha ndio unaobeba, kama Kamati walivyoeleza vizuri, ni roho ya Ruaha National Park. Sasa hii National Park ndiyo kubwa zaidi hapa nchini na inaongoza kwa idadi kubwa ya tembo na simba.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tusiiache tu juu juu jinsi ambavyo inaweza ikatutoa hapa tulipo ilhali sasa hivi huu Mto Ruaha unakaribia kufa. Kwa sababu Mto huu resource yake ni maji, maji haya sasa hivi yamepungua, sasa hivi kunakuwa kuna misimu mirefu ya kuwa hakuna maji. Karibu asilimia 77 ya chanzo cha Mto Ruaha kwenye Bonde la Ihefu na Usangu yameharibiwa. Kwa hiyo mto ule unaenda kufa.

Ya pili, inaenda kuua vyanzo vyetu vya umeme. Tanzania sasa hivi tunategemea takribani asilimia 70 ya umeme kutoka kwenye vyanzo vya maji, ikiwepo Kidatu, Mtera na sasa hivi tuna-propose mradi mpya wa Stiegler’s Gorge. Sasa nini kina-feed katika mabwawa makubwa ni huu Mto Ruaha Mkuu. Mtera karibia asilimia 56, Kidatu karibia asilimia 25 na kwenda Stiegler’s Gorge kinacho-contribute yale maji ni asilimia 25 ya huu mto ambao tayari unakufa.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nataka pia tutafakari jinsi huu mto ambavyo unaenda kuharibu. Tumejikita kwenye Sekta ya Umeme tunategemea maji. Hivi karibuni tumepitisha mradi wa Stiegler’s Gorge ambao ulikuwa unaleta sintofahamu na nilisimama kwenye Bunge lililopita.

Mheshimiwa Spika, wenzetu wa Kenya jirani, asilimia 65 ya chanzo cha umeme wao ni kutoka kwenye jotoardhi (Geothermal) na sisi Tanzania tuna hiyo potential ya ku-top umeme wetu ambao tuna uhakika nao kutoka kwenye Geothermal. Nafikiri Mkoa wa Songwe au Mbeya wana uwezo huo. Tuna Rift Valley ambayo ni source ya hiyo Geothermal.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, investment ambayo tunaweza tukaiweka katika kutafuta umeme katika nchi hii ambao unaweza uka-boost sekta zote including utalii ni umeme wa uhakika. Kwa hali ilivyo sasa mtakumbuka kwa wale wahenga wenzangu, mwaka 2006 Mtera ilikauka. Tulikosa umeme kwa muda gani? Kwa hiyo, mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa mazingira, mito yetu iko katika hali mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Makamba atani-support kwenye hilo, yaani hapa naomba tusifanye ubishani wala tusifanye siasa. Nchi yetu ina hali mbaya katika Mito yetu, mmojawapo ni Mto Ruaha, Mto Ruaha ndiyo huo umebeba utalii, ndiyo umebeba sekta ambayo inaenda kukuza huo utalii including umeme.

Kwa hiyo, naomba tutafakari kwa upya. Hata kama sasa tumeamua kuendelea hivyo hivyo na tumelazimishia kufanya Stiegler’s Gorge, basi Wizara sekta husika iangalie jinsi ya kufufua hii mito iweze kutiririsha maji. Kama ikiwa too late, basi turudi nyuma tena tujitathmini. Kama kweli tunahitaji kutumia Stiegler’s Gorge kama chanzo chetu cha maji wakati kinaenda kuharibu utalii Ruaha, kinaenda kuharibu utalii Selous Game Reserve. Yaani kunakuwa na sintofahamu iliyopitiliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kwa hali ya pekee bila kuleta ushabiki, naomba tujitafakari kwa upya kama kweli tunataka kukuza sekta yetu ya utalii ambayo tuna uhakika katika kuimarisha uchumi wetu. Sisi wenyewe pia tujitafakari kama kweli ile engine ya kuleta maendelea ambayo ni umeme, basi tuangalie vyanzo vingine vya umeme tusitegemee Hydroelectric Power.

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Basi kama hatutaki kutoka hapo, tuangalie means mbalimbali za kuweza kuimarisha upatikanaji wa maji katika mito yetu.

TAARIFA

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, sielewi anani-support point yangu au alikuwa anakinzana na point yangu, sijaweza kupata conclusion. Naomba niichukulie positive kwamba tusitegemee chanzo kimoja cha umeme maji ambacho kina sintofahamu kubwa kwa sababu ya uharibifu wa mazingira, kwa sababu ya shughuli za kiuchumi. Nimetoa mfano kwamba chanzo cha maji cha huu Mto Ruaha ni katika Bonde la Ihefa, si ndiyo!

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, bonde hili limeharibiwa kwa asilimia 77 kwa sababu ya shughuli za kiuchumi, kilimo cha rice farming, kwa hiyo lazima tu-balance kwani ukiwa na diversity kubwa ya vyanzo vya umeme una uhakika na upatikanaji wa umeme, lakini tusitegemee 70 percent ya umeme wetu iwe chanzo chake ni maji, ambacho kina sintofahamu.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa niende kwenye Kamati ya Kilimo, Mifugo, Maji na Uvuvi, naomba nijikite katika ukurasa wa 64, nakubaliana na maoni ya Kamati ambayo tunasema lazima tufufue Shirika letu la Uvuvi Tanzania na nataka nisisitize kwamba sio tu kulifufua Shirika hili, bali tutengeneze na miundombinu rafiki ya kufanya hili shirika liweze kufanya kazi. Tununue meli za uvuvi, tujenge bandari ya uvuvi na iweze pia kuziwezesha zile taasisi ambazo zitakuwa zinategemeana na Shirika hili ikiwa ni pamoja na Tanzania Fisheries Research Institute. Tunaita ni Taasisi ya kufanya Research lakini Taasisi hii, haijawezeshwa kufanya kazi kwa kukosa rasilimali fedha, Wataalam tunao lakini hatuna rasilimali fedha katika taasisi hii ili kuweza kukuza sekta ya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa ….

SPIKA: Ahsante. Muda wako umekamilika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Nitaanza kwa kutafakari kwa pamoja. Ni dhahiri kwamba Taifa letu bado halijatambua thamani ya mazingira na afya ya mazingira na hili lipo linajionesha dhahiri ndani ya Serikali baina yetu sisi hapa Wabunge hata na jamii inayotuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema haya kwa sababu ukiangalia tu kwa Wizara zilizopita humu ndani Waheshimiwa Wabunge tulikuwa tunagombania nafasi za kuchangia kama ni TAMISEMI au ni Utawala Bora au ni Ofisi ya Waziri Mkuu na vitengo vyake lakini sasa kama tulikuwa tunakimbilia kutetea shule, barabara, vyakula, afya na kadhalika tulitakiw atujue kwamba kiini kinachotubeba sisi kama Taifa na afya na uchumi wa Taifa, ni mazingira. Mazingira ndiyo kiini cha maendeleo. Tungelitambua hilo tukaisimamia Serikali ipasavyo tungetoka kwenye huu umaskini, kwa sababu hali ya umaskini inajengwa na vitu vikuu vitatu, uchumi duni, utawala bora na uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Tanzania mazingira ndiyo yanayotubeba, kwa sababu hata hao wananchi wetu huku vijijini asilimia 96 wanategemea maliasili, zaidi ya asilimia 90 wanategemea nishati kutoka kwenye maliasili. Kama tunaongelea viwanda, maji safi na salama inategemea na hali ya mazingira iliyopo. Kama mazingira yanachechemea hatutakaa tukote katika dimbwi la umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitunga Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1997 kama Mheshimiwa Waziri husika alivyosema na iliainisha mambo sita makuu ya uharibifu wa mazingira. Tuliainisha changamoto za uharibifu za vyanzo vya maji, hii tunaangalia mito, mabwawa, bahari na kadhalika; tuliainisha uharibifu mkubwa wa maji safi ambayo yanaenda kujenga uchumi kwa sababu kusipokuwa na wananchi wanaopata maji safi inaenda kuharibu afya yao binafsi, mifugo au na chochote kinachotegemea maji safi; tuliainisha uharibifu wa ardhi, ardhi ndiyo iliyobeba miundombinu ambayo tunaitegemea sisi aidha sekta za kilimo na vinavyobebwa na kilimo au ni shughuli za madini na kadhalika; na tuliainisha kwamba kuna upotevu mkubwa wa makazi ya viumbepori na bioanuwai. Hivi vyote kwa ujumla wake ni nguzo hizo sita ambazo zinabeba shughuli za kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka 22 iliyopita Mheshimiwa Waziri umesema haya na sasa hivi tunachanganua hii sera kwa upya wake, ardhi inasemaje, uharibufu wa ardhi upo katika percent ngapi na una-reflect vipi hali ya uchumi? Kwa sababu unapoharibu ardhi ina maana unaharibu na uzalishaji ambao unategemeana na ile ardhi. Kama unaharibu vyanzo vya maji hupati maji safi au maji yanayotakiwa unaenda kuwa reflected kwenye shughuli za kiuchumi. Tunalia kila siku kuhusu bajeti ya maji haitoshi, sasa tungeweza ku-link kuhusu upatikanaji wa maji, budget wise na upatikanaji maji kwenye kutunza vyanzo vya maji na njia za maji basi tungeweza kwenda sambamba na kukuza uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera yetu imeainisha mambo sita makubwa ambayo bado hayana ufumbuzi kwa sababu bado tunaharibu mazingira, sasa nayo yanakuwa reflected kwenye uchumi wetu. Uchumi wa mtu mmoja mmoja unategemea na hayo mazingira kwa sababu kila mtu anayategemea mazingira hayo. Mfano tu mfupi, usipokuwa na maji safi kwanza ukinywa maji machafu au maji hayako salama jamii hiyo husika inapata maradhi, kwa hiyo, inaenda ku-reflect bajeti ya afya, bdo tunazidi kuididiza. Kama hupati maji kwa ajili ya kilimo chako cha umwagiliaji unategemea mvua na sasa hivi kuna mabadiliko ya tabianchi ina maana uzalishaji wako utakuwa wa wasiwasi hutakaa utoke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiweza kuipa nguvu Sheria yetu ya Mazingira ambayo imeainisha mambo makuu manne, kuna utafiti, uelimishaji na kadhalika, hii sekta inaweza ikatutoa hapa kwenye dimbwi la umaskini.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri. (Makofi)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuwape bajeti inayotakiwa, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi ili name niweze kutoa mawazo yangu katika Wizara hii iliyo mbele yetu. Ni dhahiri kwamba uchumi wa nchi, maendeleo ya jamii na ya mtu mmoja mmoja kwa kiwango kikubwa hutegemea masuala ya elimu kwa upana wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hizi dakika chache nitagusia Sera yetu ya Elimu kwa ujumla na hali ya elimu katika vyuo vyetu vya elimu ya juu pamoja na dhana nzima ya sayansi na teknolojia. Sera yetu jinsi ambavyo tunazidi kuirekebisha nafikiri ilikuwa inakidhi wakati nchi yetu ilikuwa inasimamia sera ya ujamaa na kujitegemea lakini kwa nyakati hizi sasa za soko huru na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, Tanzania Sera yetu ya Elimu na mitaala ya elimu yetu inawafanya vijana tunaowazalisha wanakuwa siyo competitive kwenye soko ndani ya nchi, East Africa Community na duniani kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwa nini Sera yetu hii inatuweka katika dhama za zamani na siyo za kisasa. Mfano mdogo tu kwenye mitaala, mitaala yetu tunayoitunga ni mepesi na rahisi kufuatilia lakini realistically haituvushi pale tunapotaka kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano tu mzuri tuna somo la Development Arts and Sports kwa wanafunzi wa grade one. Hili ni somo la vitendo lakini unawafundisha watoto ukuti ukuti, jumping rope theoretical na unawapa mtihani tunataka kukidhi nini wakati hili ni somo la mchezo. Kwa hiyo, tuangalie tunataka ku-achieve nini kuanzia elimu ya msingi, sekondari mpaka vyuo au technical school.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la muda wa kuanza shule na usafiri kwa wanafunzi vijijini na mijini. Kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 nilitoa proposal hebu tuangalie kwa upya muda watoto wanaotakiwa waanze shule hususani wa shule za msingi. Unapoanza safari yako yoyote saa kumi na moja au saa kumi na mbili alfajiri unakutana na wanafunzi vitoto vya miaka sita, saba wamelala saa ngapi, wanaamka saa ngapi, efficient inatoka wapi? Unawaambia saa kumi na mbili na nusu wafike shule, saa moja masomo yanaanza na kadhalika, wanafunzi wa vijijini wanatembea kwa umbali mrefu saa ambazo si sawa na wanafunzi wa mijini usafiri nao ni wa shida na wanapata shida, kwa hiyo, by the time mtoto anafika shuleni amechoka mentally na physically hawezi kupokea kile anachofundishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo kwa walimu wanaowafundisha hawa wanafunzi wanakuwa kwenye level za stress. Ndiyo maana unakuta adhabu zinazotolewa zinaweza zikawa za kupitiliza kwa sababu kwanza mwalimu huyu hana mshahara unaomkidhi, ana malimbikizo ya mishahara na marupurupu mbalimbali kitu ambacho hakimpi motivation vya kufundisha plus anavyoenda shule tayari ana stress. Kwa hiyo, level ya elimu haiwezi kupanda au kuwa improved kwa mazingira tunayoishi sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti suala lingine kwenye sera ambalo nataka liangaliwe ni mitihani ya kuhitimu especially ya darasa la saba. Wanafunzi hawa hatuwatendei haki kwa sababu ni siku moja ya kukutathimini wewe uende kutoka level moja kwenda nyingine. Nafikiri tuangalie jinsi ya kuwafanyia tathmini wanapotoka daraja moja kwenda lingine, wale ambao labda unasema hawakufaulu kwa sababu pia kuna malalamiko mengi ya kuvuja kwa mitihani na usahihishaji mbovu, kwa hiyo, unampa one time chance ambayo siyo fair. Basi yule ambaye hajafaulu apewe nafasi ya ku-reseat au assessment nyingine zitafutwe au hawa wanafunzi ambao kwa asilimia kubwa vijana, zaidi ya vijana milioni tano au sita tunawaacha hawaendi sekondari kwa sababu hakufauli hii elimu ya msingi tuwape alternative labda za kwenda shule za vocational training au ku-reseat ile mitihani ya primary kama wana nia ya kwenda sekondari waweze kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala linguine…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba dakika moja tu.

MWENYEKITI: Haya, chukua dakika moja.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine adhabu kali zifuatiliwe upya kwa sababu zinaenda kinyume na haki binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nigusie suala la elimu ya juu na sayansi na teknolojia. Kama Wizara inavyosomeka ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lakini hii sanyansi na teknolojia haiwi reflected hata kwenye bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ilitengewa shilingi bilioni moja ikasomeka sifuri hawakupata chochote safari hii, nasoma hapa kwenye randama wametengewa shilingi bilioni 3.5 tena kwa fedha za nje…

MWENYEKITI: Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi name niweze kutoa mawazo yangu katika mapendekezo ya mpango ulio mbele yetu. Nilifikiria kwanza nina dakika 10 au 15 sina uhakika na dakika tano. Basi nitajitadi basi nilikuwa na mambo matano kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza nilikuwa nataka niligusie ni kuhusu ufuatiliaji na tathmini (monitoring and evaluation) ya mpango wetu ulio mbele yetu. Mpango huu ni proposal ya kumalizia mpango wa miaka mitano 2016/2017, 2020/2021, lakini kwa bahati mbaya kilichoandikwa humu ndani kwenye ule mpango wa miaka mitano ni kwamba tungeweza kufanya tathmini ya mpango huu wa pili wa maendeleo wa taifa wa miaka hii ambayo tunaenda kuimalizia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni ngumu kufuatilia mapendekezo ya mpango wa kwenda kumalizia kama huku nyuma hatujajitathmini. Mpango wa kwanza umeisha na huu unaenda kuisha ukingoni bila kujitathmini tumewezaje kufanyakazi. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kufanya tathmini kwa kuwa tathmini ndiyo inakupa dira ya nini tunafanya maelekeo yetu yakoje, kuna mabadiliko ambayo tunatakiwa tuyachukue ili tuweze kuboresha na kuweza kufanikisha malengo yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mpango wa miaka mitano umeandika vizuri sana, hauna hata kasoro, kwa kweli umekaa technically correct. Sasa shida inakuja kwenye utekelezaji; kwa mfano ukurasa 128 (7.4.4) unaongelea mahususi kuhusu tathmini ya mpango wa pili huu wa maendeleo ambao tunaenda kuhitimisha, na kipengele cha pili pale kinasema kuwa kutakuwa namapitio ya muda wa kati wa utekelezaji;na tumeji-commit katika mpango huu kwamba tutaanzisha Mkutano wa Rais wa Mpango wa Pili wa Maendeleo katika muda wa kati wa utekelezaji ili kuangalia namna bora ya kubadili ama itaonekana ulazima wa kufanyia review. Sasa inakuwa ni ngumu kuendelea kutoa mapendekezo ilhali yale mapendekezo hatuyaoni yanafanyikaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo ninataka niligusie ambalo linahusiana na tathmini ni kwamba kumekuwa na changamoto nyingi sana ya upatikanaji wa fedha za maendeleo, maendeleo ndio huo utekelezaji wa mpango. Katika wizara na taasisi nyingi tumeshindwa kufika malengo, tuko below 50. Sasa tuna mpango ambao unaendana na nini tumekiamua na bajeti kiasi gani kiweze kutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona tuna changamoto ya kibajeti katika kutekeleza shughuli za maendeleo. Nilikuwa nategemea kwamba tungekuwa tumefanya tathmini ili tujiangalie ukusanyaji wetu wa mapato na mapungufu yake ni yapi ili tuweze kuboresha. Kwahiyo tunaenda kumalizia huu mpango wa pili lakini hatujui bado tunachangamoto za kimapato. Sasa ingekuwa ni vizuri basi; najua wataalamu wapo na uwezo huo tunao; tukapata huo mchanganuo kwamba setbacks zilikuwa ni nini ili kwamba huu mpango wa miaka mitano tunakwenda kuumalizaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti,katika hili, kama tungekuwa tumefanya tathmini tungeweza kujionesha kwamba tumeutekeleza kwa asilimia ngapi katika sekta mbalimbali. Sasa hivi ni vigumu kusema kwamba sekta ya kilimo ina perform kiasi gani. Moja ya mfano, katika sekta ya kilimo ambayo ndiyo uti wa mgongo wa nchi yetu tunaoimba kila siku, ambao unaweza sasa kuubeba huo mpango wetu wa kusema uchumi wa viwanda. Tulijiwekea target kwamba tunapomaliza miaka hii mitano ya mpango kilimo chetu kingekuwa kimefikia kukua kwa asilimia 7.6 japokuwa huku pia huku pia napo inasomeka asilimia kumi naa! Hata hivyo ukiangalia kwa miaka hii mitatu iliyopita ile asilimia imeshuka, na huu mwaka ulioishia kilimo kimekua kwa asilimia 5.3. Sasa tulikuwa tunategemea kwamba tunapokaa hapa kama kamati tunatokaje ili kupandisha viwango hivyoambao tulijiwekea katika hii miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu na ambalo naomba niligusie ni kuhusu masuala ya ardhi. Imeandikwa pia vizuri sana katika kitabu chetu cha mpango ambapo sekta ya ardhi tumeona kwamba ni key katika maendeleo ya kiuchumi kwasababu ni rasilimali ambayo tunaiishi na tunaweza kuzalisha katika hiyo ardhi. Hata hivyo kumekuwa na migongano mingi ya jinsi ambavyo tunaweza tukaitumia ardhi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unaweza ukarejea, ukurasa wa 110 kumekuja na njia mbalimbali na maboresho mbalimbali katika usimamizi wa matumizi bora ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika IV, V, VI, Serikali iliji- commit kuimarisha mfuko wa fidia wa ardhi ili kuondoa ucheleweshwaji wa malipo ya fidia baada ya kufanyiwa tathmini. Namba tano tuliji-commit kwamba kuna haja ya kufanya mapitio ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.4 na Sheria ya Ardhi Na. 5; na commitment ya sita tuliweka kwamba kuhakikisha mipango sahihi ya matumizi bora ya usimamizi wa ardhi. Sasa tusipo-invest kwenye matumizi bora na usimamizi bora wa ardhi; tumeongea katikakamati yetu hata hotuba yetu ya Kambi ya Upinzani Bungeni imeongelea hiyo component;inabidi sasa tuwekeze. Tunasema tu tunaenda kufanya mambo ya viwanda, shughuli yoyote ya rasilimali yoyote lakini kama ile ardhi ina shida hatuwezi kuvuka; kama tunavyokwenda kuboresha miundombinu. Tumeona kuna tensions nyingi katika kutengeneza miundombinu ili kukuza uchumi lakini unaleta shida ya fidia kwa wananchi. Tumeona migogoro mbalimbali ya rasilimali kama ni kilimo au wafugaji kwenye masuala ya ardhi. Tumeona jinsi matumizi mabaya ya ardhi yanavyoleta matokeo ya mafuriko na kadhalika, yanaenda kuturudisha nyuma badala ya kusonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilikuwa naomba Serikali iangalie hili kwa upya. Kwamba kuna umuhimu sasa wa kuwekeza katika matumizi bora ya ardhi, tuwe tuna properplanning ya ardhi ili kuweza kutuvusha hapo na isiwe kikwazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala langu la nne nafikiri, au ni la tano, linauhusiano moja kwa moja pia na ardhi. Mimi niko kwenye Chama cha Wabunge ambacho kinapigania masuala ya kutokomeza Malaria (TAPAMA). Moja ya issue ambayo tunaizungumzia, imekuja sasa wiki hii katika majadiliano yetu, ni jinsi mambo ya sekta ya afya yanavyo link moja kwa moja na sekta ya ardhi. Mfano bora ni kwenye masuala ya malaria. Serikali inatumia gharama kiasi gani katika kudhibiti malaria au katika kuleta tiba ya malaria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukiangalia, kinachosababisha Serikali inawekeza sana katika tiba katika afya ni kwasababu tunakosa matumizi bora ya ardhi; na wengiambao wanaguswa na kutokuwa na matumizi bora ya ardhi ni watu wa kima cha chini, na hawa watu wa kima cha chini ndio watu walio more prone kwenye magonjwa kama ni ya mlipuko au ni malaria. Sasa tukiwa tunamaboresho ya matumizi bora ya ardhi plus kuboresha makazi ya hawa wananchi basi tunaweza tukatokokeza haya magonjwa ambayo yanaturudisha nyuma kama wananchi kwasababu magonjwa haya yanaenda kutu- affectakili katika utendaji kazi na kutumia rasilimali kubwa ya nchi. Kwahiyo naomba Serikali iangalie jinsi yaku–link up matumizi bora ya ardhi na shughuli za kiuchumi na shughuli za kiafya na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti,…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Dkt. Sware

MHE. DKT. IMMACULATE S. SWARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Nitajikita katika maeneo manne na nitachangia ripoti kutoka Kamati ya Bajeti ambayo mimi pia ni Mjumbe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kwanza nataka niligusie ni juu ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura ya 148 (Value Added Tax). Naishauri Serikali iliangalie suala hili kwa sababu, kwa hali tuliyonayo sasa Serikali inapopata mikopo mfano kutoka World Bank ile mikopo inakuwa taxed. Sasa mkopo unautozaje kodi, hususan vile vifaa ambavyo vinatumika kama capital inayoenda kutekeleza ile miradi, kwa hiyo, unachukua mkopo, mkopo tena unaukata kodi. Naomba Serikali iangalie hili jambo upya, japokuwa kuna baadhi ya maeneo tumeyafanyia marekebisho kwenye sheria iliyopita. Kwenye sheria iliyopita tulifanyia kwenye baadhi ya maeneo, lakini kwa ujumla wake naomba sheria hii iangaliwe upya Value Added Tax especially katika mikopo tunayoichukua kutoka World Bank ili kutekeleza miradi mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ninalotaka nigusie ni suala la ambalo lina ukakasi kidogo nalo ni katika uchumi wetu, ukuaji wa uchumi. Kumekuwa na sintofahamu kwamba, ukiangalia uchumi wa watu au purchasing power kwenye field tunasema uchumi hauko vizuri, lakini tukija kwenye paper work na taarifa za Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tunahakikishiwa kwamba, tupo vizuri. Kuna baadhi kweli ya sekta zinafanya vizuri kiuchumi nazo zimetubeba, mfano ni sekta ya madini na ujenzi na sekta hizi zimeweza kufanya vizuri kwa kuwa Serikali imewekeza, ime-feed in funds kwenye hizi Wizara husika na imefanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sasa kwa nini Serikali isiangalie kwamba, kumbe ukiiwezesha sekta inaweza ikatutoa kama ilivyofanya kwenye madini na ujenzi, basi hivyohivyo ifanye kwenye sekta ambayo ni very sensitive katika uchumi wetu kwa sababu majority ya Watanzania tuko kwenye sekta ya kilimo. Kilimo chenyewe uvuvi au ufugaji au kwenye forestry, basi Serikali iangalie hivyo, ili kututoa kwenye huu mkwamo wa kiuchumi katika level ya watu mmoja-mmoja na purchasing power kwa sababu huku chini hatuko vizuri, lakini ukiliangalia hilo katika micro economy level tunaona kwa ujumla wake iko vizuri, lakini majority ya Watanzania tunalia njaa ndio hali ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu naomba niligusie ni kuhusu Shirika la Taifa la Mawasiliano (TTCL). Suala hili tumeweza kulijadili kwa kina katika Kamati yetu ya Bajeti na hali tumeiona kwamba, shirika hili lina uwezo wa kufanya vizuri na kutukwamua katika hali ya uchumi tulionao kutuwezesha kama shirika la mawasiliano namba moja litawezeshwa. Hili pia, sio suala tu la kukuza uchumi bali pia ni hali ya security ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hali liliyonayo sasa hivi shirika hili linamiliki minara 207 tu kati ya minara 14,000 ambayo inamilikiwa na sekta nyingine binafsi. Kwa hiyo, shirika hili likiwezeshwa kama wataenda kwenye teknolojia advanced zaidi kama tuta-invest zaidi labda ni satelite level au kununuliwa telephone towers au watawekeza kwenye mambo ya mawasiliano kwa ujumlka wake au internet basi shirika hili linaweza kutoka, lakini kwa hali iliyopo sasa hivi shirika hili linasuasua na ni vigumu kwake ku-compete na mashirika mengine kwenye masuala ya mawasiliano na pia tuna-risk nchi yetu kwenye masuala ya security, kwa sababu huyo anayemiliki mawasiliano kwa ujumla wake ni muwekezaji kutoka nje, akiamua kuzima mitambo tunaweza tukapata hali ambayo si shwari katika nchi. Kwa hiyo, naomba Shirika la Mawasiliano liangaliwe kwa jicho la ziada kwenye masuala sio tu kukuza uchumi potential yake ila pia katika security ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho ambalo naomba niligusie kutoka katika taarifa yetu ya Kamati na naomba nisisitizie kwa Serikali walichukulie jambo hili kwa unyeti wake nalo ni hali ya mfumuko wa bei. Japokuwa hali ya mfumuko wa bei imekuwa ikishuka mfano ukilinganisha mfumuko wa bei umeshuka kutoka 5.5% mwaka 2017 mpaka 3.5% mwaka 2018, lakini hali hii ya mfumuko wa bei inaweza ikabadilika kwa hali tunayoi-experience sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasena hivi? Namba moja, hali ya chakula iko hatarishi kwa sababu ya hali ya hewa tunayoiona. Ni mikoa mingi sana sasa hivi ina-experience hali ya mafuriko sio tu ambayo inaondosha uchumi wa wananchi katika mashamba au makazi yao, hii pia wale ambao wamefanikiwa kulima mazao tayari sasa hivi yana hali mbaya kwa sababu ya mvua zinazoendelea kunyesha na majira ambayo hayatabiriki; hilo ni katika Mikoa ya Kigoma, Tanga, Dar-es-Salaam, Iringa, Lindi na kadhalika, kwa hiyo, kuna hali mbaya ya viashiria vya kutokuwa na chakula nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia pia kwa sababu, tuna taasisi yetu ya NFRA na Bodi ya Nafaka ya Mazao Mchanganyiko hatukuwapandishia bajeti, hatukuwawezesha kibajeti. NFRA last time 2019/2020, hatukuwaongezea bajeti na kazi yao hawa vyombo hivi vya NFRA ni kuhakikisha usalama wa chakula nchini, usalama wa chakula nchini ndio usalama wa nchi wenyewe. Tumetoka kuuza mazao yetu nje na sasa tunawa-task tena NFRA kufanya biashara ilhali chombo hiki kazi yake mahususi ni kuhakikisha usalama wa chakula nchini kwa kununua chakula. Kwa hiyo, naiomba Serikali kupitia maoni yetu ya Kamati ya Bajeti ilichukulie suala hili kwa ukubwa wake na unyeti wake, NFRA, Bodi ya Mazao ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko yaangaliwe kwa jicho la kipekee, ilhali tuhakikishe security ya nchi yetu kwa kupitia chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho ni kitu ambacho tunakiona na tuna- experience ni hali ya haya majanga yanayotokea aidha ni kwa sababu ya haya mabadiliko ya hali ya tabia-nchi au pia ni miundombinu yetu wenyewe tumeiharibu basi, mvua zinazonyesha zinakuwa zinaharibu miundombinu na kuharibu kile ambacho ni sources za income sisi kama wananchi. Kwa bahati mbaya bajeti iliyopita tuliyoipitisha hatukumpatia Mheshimiwa Waziri Mkuu fedha yoyote katika Mfuko wa Maafa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijui tutafanyaje Mheshimiwa Waziri husika wa Fedha na Mipango tuna dalili mbalimbali za viashiria vya milipuko ya magonjwa, tuna viashiria mbalimbali vya hali ya wadudu wanaoenda kuharibu mazao, sasa tuko kwenye in between tutatokajetokaje. Tunajisifia mfumuko wa bei ndio uko vizuri na unashuka, lakini viashiria vyote vinaonesha kwamba, tunakoenda tutakuwa tuna hali mbaya sana. Kwa hiyo, naomba sana kwenye haya mambo manne Wizara husika naomba ichukulie kwa umakini wake kwa sababu, ni maeneo ambayo ni nyeti sana kama Taifa letu na kuweza kutukwamua katika hali ya uchumi tuliyonayo. Nashukuru sana kwa nafasi. (Makofi)
Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba Kigosi Kuwa Hifadhi ya Taifa Kigosi pamoja na Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba la Igalla Kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury)
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi, na mimi ninaridhia Azimio hili la Mkataba wa Minamata kuhusu zebaki, namba moja kwa sababu ya madhara yaliyo makubwa sana kimazingira na kiafya katika jamii kutokana na matumizi haya ya zebaki na namba mbili ni kwa sababu matumizi haya ya zebaki nchini yako makubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, article namba 3 ya mkataba huu unaongelea masuala ya ni nchi kutambua ni kiasi gani cha zebaki ilichonacho na nimepitia leo asubuhi ripoti ya mazingira kwa mwaka huu inaonesha kwamba Tanzania kwa sasa tumeweza kutengeneza au kusambaza zebaki katika mazingira tani 33.5 ambayo kwenye Mkataba wamesema kwamba nchi inaweza inatakiwa isi-exceed tani 10 katika ku-generate zebaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, article namba 7 ya mkataba huu pia inaongelea kuhusu uchimbaji mdogo wa dhahabu ambao unatumia zebaki na hapa nchini kuna wachimbaji wadogo takribani milioni 1.5 na wengi wao wakiwa katika Ukanda wa Ziwa Victoria, kwa hiyo idadi ni kubwa wanaofanya shughuli za kiuchumi, lakini pia wanajiweka katika risk ya contamination wao wenyewe kujiharibia afya na walio wazunguka na mazingira pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuna umuhimu sana wa kuwafatilia nini ambacho Mkataba huu unaelekeza ili kuwasaidia wananchi kiuchumi na kuwapa alternative sources katika shughuli zao za uchimbaji wa dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo hapo article saba inasema kwamba nchi lazima itengeneze na kupitisha mpango kazi, au mpango mikakati, ni jinsi ya ku-deal na zebaki hususani katika wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, article namba 12 katika mkataba huu, unaelezea kuhusu mkakati kwamba nchi iwe na mkakati mahsusi wa kurekebisha madhara ambayo yametokea kutokana na zebaki katika mazingira, sasa nilikuwa nataka nisisitizie kuwa nimesema asilimia kubwa ya wanaotumia zebaki ambayo inaathiri mazingira ni katika Ukanda wa Ziwa na tunajua kwamba karibu asilimia 90 ya uchimbaji wa dhahabu uko katika Ukanda wa Ziwa na asilimia kubwa ya wachimbaji hao ni wale wadogo wadogo ambao wanatumia zebaki katika kuchenjua hiyo dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiria na lazima sasa tufate mwongozo wa huu mkataba kuangalia jinsi tunai-save vipi Lake Victoria yetu na wale ambao wanafanya shughuli za uchumi kuzunguka eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nisisitizie hapa article namba 13 inamuhusu Waziri husika ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wangu wa Bajeti kuhusu sasa hapo Mfuko wa Mazingira una kazi maalum na mahsusi, kwa hiyo, naomba Wizara ya Fedha wangekuwepo hapa waone kuwa tunaenda kuridhia mkataba huu sisi kama nchi, lakini mfuko wetu wa mazingira unasoma sifuri wakati tuna mambo mahsusi ya kimazingira ambayo yanatakiwa yafanyiwe kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo article 13 katika mkataba huu unaongelea kuhusu rasilimali fedha na utaratibu wa jinsi ya kutumia hizo fedha katika kurekebisha madhara au kutoa elimu kuhusu zebaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa naomba niguse kwenye article 16 ya mkataba huu unaongelea masuala ya afya. Shida ya hii zebaki katika afya zetu zinaweza zisionekane papo kwa hapo na madhara yake ni makubwa sana kwa sababu yanaenda kubadili DNA yako (vinasaba vyako) na pia yanakaa kwenye mazingira kwa miaka elfu na maelfu, haviondoki hivi hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna tayari ambayo wameshapata madhara ya kiafya kutoka kwenye zebaki basi naomba kuwe na mkakati mahsusi wa Kiserikali wa kuwa na vituo vya afya mahsusi na wanaotoa huduma mahsusi kwa wale ambao tayari wamepata madhara ya zebaki...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Ahsante kwa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana niweze kuchangia katika Wizara hii muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitajikita katika sekta ya misitu kwa sababu sekta hii ni muhimu sana kwa uhai wetu na kwa uhai wa Nchi yetu kwa masuala ya kijamii pamoja na kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali yetu kuhusu suala la misitu iko bado tete sana kwa sababu zaidi ya asilimia 90 ya nchini kwetu tunategemea bidhaa zinazotokana na misitu hususani kwa shughuli za Nishati aidha kwa kutumia kuni au shughuli za mikaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tuna suala zima la Sheria ambazo zinaangalia sekta hii kwa ujumla ambazo zinajikanganya inavyoshughulikia misitu yetu. Tuna Sheria mbalimbali mfano, The Local Government Finance Act na Mining act nafikiri mwaka jana tulifanya marekebisho katika Mining Act na Finance Act kwenye masuala ya uvunaji wa chumvi katika maeneo hususani ya mwambao.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kule maeneo ya mwambao tuna misitu mahususi sana, misitu ya mikoko. Sasa baada ya kufuta taratibu ambazo zinashughulikiana na mazingira, watumiaji au mining katika maemeo haya imekuwa kubwa sana na mikoko hii imekuwa ikikatwa kwa kasi sana na misitu hii ni muhimu sana katika utunzaji wa mazingira na inasaidia kutu-shield na zile dhoruba za baharini. Sasa tunapozidi kuikata hii miti tunazidi kujiweka katika mazingira hatarishi pale tunapopata dhoruba kama wenzetu wa Mozambique hiki kimbunga kilichopita kwa bahari nzuri hakikutupata ilihali ingetupata basi madhara yake yangekuwa makubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Sheria yetu ya Mipango Miji ya mwaka 1982 inakataza shughuli za kilimo na upandaji wa miti kwa ujumla wake katika maeneo ya miji. Sasa nafikiri Sheria hii iangaliwe upya kwasababu unapokuwa na miti au misitu tunasema maeneo ya Miji tunasema ni mapori lazima yaondolewe. Lazima tuliangalie hili kwa ukubwa wake na mapana yake na effect ambazo zinaweza zikajitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nigusie suala la biashara la soko la mbao Nchini; biashara hii inaweza ikatuinua kiuchumi, tunaongelea mabilioni ya Dola za Kimarekani katika biashara hii lakini biashara hii kwa sasa hivi imekuwa kama biashara haramu ambapo tunavuna sana kuliko kuangalia uvunaji endelevu na jinsi soko hili linavyotakiwa kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba suala la biashara la soko la mbao Nchini liangaliwe na pia tuweze kuviendeleza viwanda vyetu vya ndani vya kutumia mbao viweze kutumia mbao yenyewe kama mbao hata zile by product nazo ziweze kuzalisha na kuleta manufaa kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nigusie suala la TFS; TFS sasa hivi ni kama agency. Naomba kulia mkazo kwamba sasa igeuke kuwa regulatory authority najua mchakato unaendelea basi naomba ufanywe kwa haraka ili TFS iweze kusimamia masuala yote ya mazingira na miti maeneo ya mijini, vijijini, halmashauri wawe na authority ya kuweza ku- regulate na siyo kuingilia Sheria na Sera mbalimbali ambazo zinawakwaza wao sasa hivi kutekelza majukumu yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuangalia umuhimu wa misitu Nchini na Nchi zinazotuzunguka, Tanzania imeingia maridhiano na makubaliano mbalimbali ya Kimataifa basi naomba Tanzana sasa ijikite na iwe reflected kwenye bajeti na watupe update. Kwa mfano, hapa hapa Nchini tumeingia mkataba wa Zanzibar declaration status iko wapi hususani katika soko la biashara ya mbao, African forest scape restoration borne challenge na UN-CCD sasa Tazania imesimama vipi ili kuweza kuboresha hali ya miwitu yetu Nchini? Tunaomba Mheshimiwa Waziri anapohitimisha basi atupe status yetu ikoje au kuna vikwazo gani ili Bunge hili liweze kusaidia kuweka mambo vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba nigusie status ya Community base forest management; najua kuna policy mahali sijui imeishia wapi sasa uharibifu mkubwa wa mazingira haya ya misitu yanatokea katika vijiji vyetu. Vijiji tumevipa mamlaka, naomba Serikali husika, Wizara husika iangalie masuala ya Vijiji vinasimamiaje misitu ili viwe endelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii, nami niweze kusema machache kuhusu hoja iliyo mbele yetu. Nina masuala matano tu ya kugusia kwa ufupi yanayohusu mwenendo wa bajeti yetu na itakavyoenda kutekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kwanza naomba Wizara husika au Serikali ichukue ni juu ya umuhimu wa kuwa na soko katika kukuza uchumi wetu. Tunazalisha malighafi mbalimbali, kwa bahati mbaya malighafi hizi kama ni kutoka kwenye Sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi au Misitu, tuna shida katika value chain yetu, haiko vizuri, usindikaji wa mazao haya hauko vizuri ambao ni competitive Kimataifa au pia katika kuvutia soko la ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna umuhimu sana wa kuangalia masoko katika Sekta mbalimbali zinazogusa Wizara au Taasisi husika na Wizara yenyewe au Wizara ya Viwanda na Biashara kutafuta masoko ya ndani, kuboresha soko la ndani, kuji-advertise nchi yetu kwa masoko ya nje ili tuwe na uhakika pale tunapozalisha, basi kile tunachozalisha kiweze kutuletea tija na kukuza uchumi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona mifano mbalimbali katika Sekta ya Mifugo, tuna shida katika ngozi, tumeona katika Sekta ya Mifugo, hivyo hivyo kuna shida katika uzalishaji wa maziwa. Tuna-import zaidi kuliko ku- export. Kwa hiyo, nafikiri ni wakati muafaka wa kujitathmini kwa upya na kuweka msisitizo mkubwa katika kuangalia soko linafanyaje kazi nchini ili kukuza uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili nataka niligusie ni kufungamanisha viwanda na sekta nyingine na malighafi ambazo zina-feed in kwenye hivyo viwanda na masuala mazima ya elimu. Tunataka nchi yetu iendeshwe na Sera ya Viwanda lakini viwanda hivi vina changamoto nyingi. Kwa hiyo, naomba kuishauri Serikali, Wizara husika, Viwanda na Biashara, uwekezaji, Wizara ya Fedha na Mipango hebu iangalie ina-connect vipi na Wizara nyingine husika ambazo zina feed in kwenye viwanda? Naomba sera iangaliwe kwa upya ili tuweze kuviimarisha viwanda vyetu siyo kinadharia, bali sasa tuanze kufanya hivi kivitendo.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la tatu nataka niligusie ni umuhimu wa mazingira na jinsi mazingira yanavyoweza yaka-shape maendeleo ya nchi kiuchumi na katika jamii yake kiafya. Nilikuwa nimepitia kitabu hiki cha Hali ya Uchumi wa Taifa katika Mwaka 2018 ukurasa wa 112 kwenda 113 sura ya nane inaongelea kuhusu mazingira na hali ya mazingira nchini ilivyo. Ninaomba tu ninukuu baadhi ya aya kutoka aya ya 161 na 162, inasema kwamba, “mwaka 2018 Serikali iliendelea kusimamia mazingira kwa lengo la kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kwa binadamu ikiwa ni pamoja na kudhibiti athari za matumizi ya Zebaki (Mercury) katika uchimbaji mdogo mdogo.”

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ni mbaya sana kwa sababu asilimia kubwa ya Zebaki inatumika katika wachimbaji wadogo na asilimia kubwa ya hawa wachimbaji inayozidi asilimia 30 wameshaathirika. Hapa hatuangalii tu athari ya hawa wachimbaji wadogo wanavyotumia madini haya ya Zebaki.

Mheshimiwa Naibu Spika, madini haya yana athari kubwa sana. Huu ni mfano tu mmoja wa uhalibifu wa mazingira katika mazingira yenyewe na katika afya ya wahusika, kwa kuwa ikishaingia katika mfumo wa mazingira, madini haya siyo rahisi kutoka na yanaendelewa kurithiwa kizazi kwa kizazi kwa wanyamapori, samaki, mifumo ya maji na binadamu wenyewe; inaenda kuharibu kizazi na afya ya yule ambaye ameathirika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mantiki hii, mazingira ndiyo uchumi, mazingira ndiyo maendeleo, lakini kwa bahati mbaya hatuiangalii kwa jicho hilo kama Serikali ili kutuvusha hapa tulipo. Hii ipo reflected hata kwenye bajeti yenyewe ya mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa naibu Spika, tumetengeneza Mfuko wa Mazingira hapa nchini, lakini mfuko huu badi haujawezeshwa kufanya kazi ile inayotakiwa, umenyimwa fedha tangu uanze. Kwa hiyo, kuna umuhimu sana wa kuangalia mazingira na tuanze sasa ku-link mazingira na shughuli za uchumi wetu. Unapoharibu mazingira, unaharibu vyanzo vya maji, unapoharibu maliasili ina maana utaenda kugharamia zaidi katika kuboresha yale mazingira yawe katika hali ya uzalishaji. Kwa hiyo, naomba tuiangalie kwa mantiki hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nipo hapo kwa mazingira kwa umuhimu wake aya ya 162 inasema, “mwaka 2018 Serikali iliendelea kudhibiti uharibifu wa ardhi ikiwa ni pamoja na kukamilisha tathmini ya hali ya uharibidu wa ardhi nchini, Tathmini hiyo inaonesha kuwa takribani asilimia 75% ya ardhi yetu hapa Tanzania inakabiliwa na upungufu wa rutuba na uharibifu wa ardhi.”

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mantiki hiyo, uzalishaji wowote wa kiuchumi katika ardhi unaenda kuharibiwa unakuwa wa chini. Utalima lakini utatumia nguvu nyingi kupata mavuno yanayotakiwa kwa sababu tayari ile ardhi haina rutuba na haina hali ya kukuwezesha wewe kuzalisha kile unachokitaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuangalie kwa jicho la ziada kuwezesha mazingira nchini kutunzwa, kwa hiyo, iwe reflected katika bajeti kuwekea hela katika kudhibiti ili mazingira haya yaweze kutulea sisi. Kwa hali iliyopo sasa hivi ni tete sana na tutatumia gharama kubwa katika kuirejesha ardhi hii au mazingira yetu ili yaweze kutuzalishia bidhaa mbalimbali na kukuza uchumi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la nne ambalo nataka niligusie kwa ufupi ni umuhimu wa utafiti na data. Any informed decision lazima iwe na backup na tafiti na data fulani. Kwa hiyo, naona jambo hili bado halijapewa kipaumbele katika Serikali yetu ili kuweza kuboresha bajeti yetu iweze kujiendesha yenyewe. Tunaweza tukafanya decision fulani fulani lakini haina backup ya data nzuri, yaani lazima kuwe na takwimu nzuri ili iweze kukuelekeza kwamba mikakati yako uipangaje au priorities zako ziendaje?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwenendo huo basi, ninaiomba National Bureau of Statistics iwezeshwe kwa rasilimali watu na kiuchumi iweze ku- coordinate kama ndiyo Bureau yetu ya Statistics na taasisi mbalimbali kama COSTECH ziwezeshwe ku-collect data na kuzihifadhi ili tuweze ku-make sound decisions.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho naomba niligusie, tuweze kujiuliza wote kwamba hii bajeti iliyoletwa mbele yetu is it gender sensitive? Je ime-accommodate matabaka mbalimbali katika kukuza uchumi wetu? Naomba nisemee hilo kwa kutoa tu mfano kwa suala zima la taulo za kike wa Hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 38 na 39 unaozungumzia kuhusu Sheria ya Kodi ya Mapato, inasema kwamba inaenda kupunguza kiwango cha kodi ya mapato kwenye makampuni ambayo yanaenda kuzalisha taulo za kike.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali la kujiuliza je, hii movie ya Serikali inaweza kwenda kuwasaidia watoto wa kike kuwa na uwezo wa kupata hizi taulo za kike ambayo ni muhimu sana katika afya yao na katika kujenga uchumi wa nchi?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, najua maongezi hayo, majadiliano tunafanya pamoja na Kamati ya Bajeti, lakini ningependa tu kuweka msisitizo ijitafakari kwa upya ni nini Serikali ifanye ili taulo hizi za kike ambayo ni muhimu sana kwa afya, ni muhimu sana katika ukuaji wa uchumi kwa tabaka hili wa jinsia ya ‘Ke’ waweze kuangaliwa; kwa wale ambao hawako mashuleni wanaipataje kwa bei ambayo ni rafiki na ni rahisi kupata? Wale walio mashuleni, watoto wa kike wanawezaje kupata hizi taulo za kike?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kusema hayo, ahsante sana kwa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto nyingi sana katika mfumo wa elimu hivyo ni vyema Wizara ikajiwekea malengo mahususi (prioritise list ya issues) ambayo yanatakiwa kuwa addressed mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna ubora hafifu wa ufundishaji, hakuna mfumo maalum (pedagogical skills) ambao unatumika katika kufundisha mashuleni, jambo hili linatakiwa kupewa kipaumbele cha juu kabisa kwani lina impact kubwa sana katika kuelimisha.

Katika mfumo wa sasa tunakosa walimu bora ukilinganisha na miaka ya zamani (mpaka 1990) ambapo walimu wengi walikuwa wana dedication kubwa sana katika kufundisha na kuelimisha. Walimu walikuwa na uelewa mpana wa masomo wanayoyafundisha, walikuwa na more ethics na walikuwa creative katika kuhakikisha somo lake husika linaeleweka na kupendwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna umuhimu mkubwa wa kufumua upya utaratibu wa upatikanaji wa walimu (mchujo na mafunzo), kuboresha malipo kwa walimu na mazingira rafiki ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mazingira duni ya kusomea wanafunzi, kuna haja kubwa ya kufanya assessment katika kila Wilaya na kwamba kila Wilaya itoe list ya shule ilizonazo katika kila Kata, hali ya shule husika na kadhalika ili kuweza kupanga mipango na utekelezaji wa mikakati husika na kuweza ku-address challenges kama matundu ya vyoo, madarasa, maabara, vitendea kazi (mazingira duni ya kujifunzia).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto ya usawa (wa kike na wasiojiweza); still ipo dhahiri hasa kwa watoto/vijana wa kike, wasiojiweza/walemevu. Mazingira ya sasa katika shule nyingi kuanzia za awali mpaka vyuoni nyingi hazina mazingira rafiki ya kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kuweza kuhudhuria masomo au hata shughuli za practicals ama shughuli za michezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukosa falsafa ya elimu yetu, hii ipo dhahiri katika utahini, shuleni, udhibiti wa ubora wa elimu katika uandaaji wa elimu. Je, nchi yetu inasimamia katika nini? Dira ni nini? Kuna link yoyote katika mlengo wa uchumi wa kati na uchumi wa viwanda? Hii ipo reflected vipi katika education system yetu? Haya ni masuala muhimu ya kuzingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwajibikaji mdogo kwenye elimu, hakuna policy yoyote itakayoweza kutekelezwa bila kuwa translated kwenye bajeti. Ni muhimu kuweka bayana Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuonesha (ku- tally) zimepanga kujenga madarasa mangapi. Zimeletwa shilingi ngapi kwa mwaka 2017/2018? Wizara ya Elimu ina mpango mkakati gani wa kumaliza tatizo la madarasa?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii muhimu ina changamoto nyingi sana ikilinganishwa na mikakati inayoendana na utatuaji wake. Hii ipo dhahiri kabisa ukiangalia umuhimu wake unaopewa na Serikali Kuu kupitia budget allocation na upatikanaji fedha husika kwa shughuli mbalimbali inayohusu sekta hii. Changamoto hizi zinajulikana ila hazipewi attention inayotakiwa kama:-

(i) Vitendea kazi/vifaa/teknolojia za kilimo, uvuvi na ufugaji asilimia kubwa ya wananchi hutumia vifaa kale kama majembe na mashoka katika century hii;

(ii) Tegemezi ya kilimo cha mvua;

(iii) Mfumo wa masoko ulio una upungufu mwingi na uliopitwa na wakati. Mfano, hatuna ama hakuna reliable, efficient market data na information;

(iv) Maeneo mengi hakuna kabisa/ipo katika hali hafifu ya adequate production and post-harvest technologies;

(v) Pembejeo za kilimo; utengenezaji, upatikanaji na usambazaji wa mbolea, mbegu ni hafifu na hauzingatii microclimate ya maeneo husika, ucheleweshwaji, low quality;

(vi) Extension officers; kuna upungufu mkubwa. Hawa ni kiungo muhimu katika kusaidia wakulima, wavuvi na wafugaji kwa ajili ya kuelimisha na consultation kuipa umuhimu kupitia budget, research, Maafisa Ugani kutahakikisha kupatikana kwa chakula (food security) katika nchi yetu;

(vii) Kuimarisha Taasisi za Utafiti mfano, TAFIRI na TAWIRI. Bila kuwa na takwimu siyo rahisi kufanya maamuzi. Taasisi hizi inabidi kupewa kipaumbele kwa kuhakikisha zinatengewa bajeti mahsusi kwa ajili ya tafiti, kukusanya data na kuajiri watafiti;

(viii) Sekta ya uvuvi; Serikali iangalie sekta hii kwa jicho la pekee ni eneo lenye potential kubwa sana katika kuimarisha uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla wake. Sekta inahitaji kuimarisha research and data collection, kuwa na bandari ya uvuvi, kudhibiti uvuvi haramu, kuimarisha Deep Sea Fishing Authority (monitoring, licensing e.t.c);

(ix) Wizara inahitaji kuwa strengthened kupitia budget allocation/ release of funds ili iweze kusimamia sera yake. Kiwango cha bajeti inayokuwa allocated inaenda kinyume na maazimio ya Malabo. Kwa kipindi cha takribani miaka 10 Serikali imekuwa ikitenga chini ya asilimia mbili ya bajeti ya Taifa. Hata fedha hizi zinazotengwa kwa asilimia kubwa zimekuwa zikitolewa chini ya asilimia 50.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muktadha huu ni dhahiri Tanzania haitakaa ibadilike katika kukuza uchumi wake. Wizara inatakiwa kuja na mipango mikakati katika kuhakikisha sekta hizi muhimu (kilimo, mifugo na uvuvi) zinatuvusha kutoka katika umasikini.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha za maendeleo zinazotolewa na Hazina zimekuwa zikipungua kila mwaka na kusabaisha madhara kwa Watanzania 70% wanaotegemea rasilimali ardhi kwa shughuli za kilimo. Ushauri; Wizara ijipange ili kuhakikisha inatengewa fedha za kutosheleza ili kufanikisha malengo yake. Wizara iunde strategic team ili kufanya tathmini na kuja na mikakati mahususi ya kuiwezesha kutengewa na kupatiwa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo haijaweka mikakati ya wazi ya kufungamanisha sekta ya kilimo na sekta ya viwanda, wakati ni dhahiri malighafi (raw materials) nyingi za viwanda husika zinategemea products za kilimo. Ushauri; Wizara ya Kilimo iweke wazi uhusiano wake na sekta ya viwanda, hii pia italeta chachu ya kutengewa bajeti halisia, itasaidia ku-justfy umuhimu wa sekta ya kilimo katika kukuza na kuimarisha viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu pembejeo; kuna changamoto nyingi sana katika eneo hili, maeneo mengi nchini yamekuwa na kilio cha kukosa mbolea ama kutopata kabisa ama kuja kwa kuchelewa sana. Mbolea zimekuwa za ubora hafifu maeneo mengi, hususan ya vijijini kwa sababu za miundombinu mibaya ya barabara mbolea imekuwa ya bei ya juu sana. Sekta hii imekosa mfumo thabiti wa kuuzia pembejeo zisizo na ubora kwenye soko. Mfumo wa sasa wa bulk procurement kwenye mbolea umeongeza changamoto kwenye biashara ya mbolea. Ushauri, Wizara ijitathmini kwa upya na kuja na solution ya kudumu katika kuwezesha/ kuboresha mfumo mzima wa upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna upungufu mkubwa wa rasilimali watu katika sekta ya kilimo (wataalam na maafisa ugani) ambao wameajiriwa na wachache waliopo wanafanya kazi katika mazingira magumu (ukosefu wa vitendea kazi). Ushauri, Wizara ije na document inayoonesha ni wataalam wangapi wanaohitajika na katika maeneo gani na kufikisha suala hili katika taasisi/Wizara husika ili lipatiwe ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mapungufu makubwa sana ya udhibiti wa mazao baada ya kuvuna (post harvest losses), hali hii husababishwa na idadi ndogo sana ya maghala nchini, kwa sasa kuna takribani maghala 1,200 wakati kuna vijiji 13,000. Hali na hadhi/teknolojia zinazotumiwa wakati wa kuvuna na kusindika mazao ni duni sana. Hali hii husababisha upotevu mkubwa wa mavuno, takribani 20% ya mazao hupotea baada ya mavuno. Ushauri; Wizara ijipange kimkakati na hata kushirikisha private sector kuhakikisha angalau kila kijiji/kata kinakuwa na ghala la kisasa linaloendana na mazao husika yanayolimwa katika eneo husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kilimo sio kipaumbele kwa Serikali (rejea kitabu cha mpango cha sasa). Basi ni bora Wizara ikajitathmini kwa ujumla wake ili Wizara hii muhimu na nyeti ikawa more visible.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 100 wa hotuba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kipengele (c) kimeongelea juu ya ukaguzi wa ufanisi wa kazi katika Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU). Mheshimiwa Waziri anaelezea hatua za kuvunja Bodi ya Wadhamini na kumsimamisha kazi Meneja wa Kitengo cha Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu kwa vigezo vya matokeo ya ukaguzi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Performance Audit/CAG).

Je, imekuwaje Waziri akimbilie kufanya maamuzi kama haya? Mbona Mawaziri wengine katika sekta zao hawakufanya maamuzi haya? Performance Audit zimefanyika kwa taasisi mbalimbali za Serikali na malengo yake yalikuwa ni kuboresha. Je, Mheshimiwa Waziri aliwapa nafasi ya kujibu yaliyojitokeza? Ripoti ya CAG haioneshi maeneo ya ukaguzi wala vigezo vilivyotumika katika kufanya hiyo performance audit. Pia ripoti hiyo haielezi chochote kuhusiana na udhaifu uliotajwa.

Mheshimiwa Spika, katika miaka miwili mfululizo MPRU haikutengewa kiasi chochote cha fedha kutoka Serikalini. Iweje Wizara itegemee MPRU kufanya utofauti chanya?

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 113 na 114 wa kitabu cha hotuba imeonesha utekelezaji wa majukumu ya hifadhi za bahari na maeneo tengefu chini ya MPRU. Hotuba imebainisha utekelezaji wa kazi zake (MPRU) pamoja na malengo yake ya kuendeleza mipango kazi yake kwa mwaka 2018/2019; je, ni kwa nini Wizara haikubainisha kushindikana kwa MPRU kutekeleza majukumu yake kwa ulinganifu wake na matokeo ya ukaguzi wa CAG?

Mheshimiwa Spika, natambua kuwa MPRU hukusanya maduhuli ya takribani slingi bilioni moja kwa mwaka na kwa mwaka wa fedha 2017/2018 mwezi Machi, 2018 yalifikia shilingi bilioni 1.1. Je, uamuzi huu wa Mheshimiwa Waziri wa kuvunja bodi na kumwondoa Mkurugenzi kunatuhakikishiaje maboresho ya mapato?

Je, maamuzi yaliyofanywa na Mheshimiwa Waziri ni sehemu ya mapendekezo ya CAG? Kama siyo, yanasaidiaje katika utekelezaji wa mapendekezo ya CAG na maslahi mapana ya Kitengo?
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, takribani asilimia 90 ya Watanzania hutumia nishati ya kuni na mkaa kwa matumizi ya nyumbani, hali hii huleta uharibifu mkubwa wa misitu nchini. Inasemekana kwa wastani hekta 400,000 hupotea kila mwaka. Ni kwa nini Wizara hii isishirikiane na Wizara ya Nishati ili kuja na mikakati mahsusi ya kutumia nishati mbadala nje ya mazao ya misitu?

Mheshimiwa Spika, TFS imekuwa ikitoa leseni za kuvuna bidhaa za misitu ya kwenye ardhi ya kijiji bila kushauriana na mamlaka husika ya kijiji. TFS imekuwa ikikusanya tozo (collecting revenues) kwenye bidhaa za misitu zilizovunwa kinyume cha sheria, ikiwa ni pamoja na mkaa na mbao na kujiongezea mapato. Pia kuna malalamiko kuwa TFS haina ushirikiano mzuri na jamii zinazojishughulisha na hifadhi za misitu (community foresty management) na kuwachukulia kama washindani, hali hii pia hujitokeza kwa kukwamisha harakati za CSOs na NGOs.

Mheshimiwa Spika, ripoti ya NARFOMA inaonesha kuna jumla ya hekta milioni 48 za misitu wakati idadi ya watu ni trakribani milioni 50. Kwa hiyo bila usimamizi sahihi wa misitu tutaangamia. Kuna haja ya kuwa na mipango sahihi ya kuangalia, kwa mfano matumizi ya biomass energy, mikaa bado ni changamoto. Mashaka haya yanabidi kushughulikiwa ikiambatana na marekebisho ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji katika misitu inapaswa kukuzwa kwa kuzingatia vigezo vya utunzaji/uvunaji endelevu (sustainable harvesting) ili ku-address economic, environmental and social issues.

Mheshimiwa Spika, kuna alternatives nyingi nchini za vyanzo vya umeme ambavyo havina madhara makubwa sana katika ekolojia ya maeneo husika pamoja na jamii inayoitegemea, sasa basi, ni kwa nini Serikali inang’ang’ania kutumia Stieglers Gauge ilhali itasababisha madhara makubwa kwa rasilimali maji, maliasili na shughuli za kiuchumi? Rufiji Basin Hydropower Master Plan imeainisha maeneo mengine yenye uwezo wa kutoa umeme kama Kihansi, Ruhudji, Mnyera na Kilombero.

Mheshimiwa Spika, ukataji wa miti zaidi ya 1,430 km2 ni janga kubwa kwa Taifa, hasa kwa maeneo ya Kusini (Selous), Rufiji Delta na kadhalika katika maandalizi ya mradi huu wa Stieglers.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, hatuwezi kuondoa umaskini bila kuigusa sekta inayoajiri Watanzania wengi, hivyo basi, napendekeza kuondoa kodi kwenye Uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kuboresha na kukuza uchumi kupitia sekta hii.

Mheshimiwa Spika, wananchi walio wengi wanaojishughulisha na kilimo wameachwa na Serikali kujitegemea wenyewe. Serikali ingewekeza angalau asilimia 40 katika sekta hii, itasaidia katika kuboresha na kuimarisha/ kukuza mnyororo wa thamani (Agricultural value chain), na kwa jinsi hii itaweza kutengeneza ajira nyingi katika ngazi mbalimbali (vitongoji – wilaya – mikoa) na itakuwa na major impact katika nchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali haijaweka wazi mikakati ya wazi ya kufungamanisha sekta ya kilimo, na sekta ya viwanda. Ni wakati sasa suala hili likaangaliwa katika upana wake.

Mheshimiwa Spika, Suala la Pembejeo Katika Ujumla Wake. Kuna uhaba na ucheleweshwaji wa kusambaziwa kwa Wakulima, ubora hafifu, kutokufika kwa wakati (msimu), bei kuwa juu kwa baadhi ya maeneo na kukosekana mfumo thabiti kuzuia pembejeo zisizo na ubora kwenye soko kwa kuzingatia haya. Wizara ifanye tathmini na kutengeneza mikakati mahsusi ya kuboresha haya.

Mheshimiwa Spika, Raslimali Watu Katika Sekta ya Kilimo. Kuna upungufu mkubwa wa wataalamu na maafisa ugani katika sekta hii. Hata kwa wafanyakazi waliopo (especially maafisa ugani) wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa ukosefu wa vitendea kazi. Wizara ilifanyie kazi suala hili.

Mheshimiwa Spika, Udhibiti wa Mazao Baada ya Kuvunwa (Post-Harvest Losses); hii husababishwa na:-

(i) Wakulima kuwa na elimu ndogo na miundombinu hafifu ya kutunza/ku-store mazao yao (na hata wakati mwingine kusababisha kutokea kwa aflatoxins) na (kuhatarisha afya za binadamu na mifugo);

(ii) Idadi ndogo sana za maghala za kuhifadhi (kati ya vijiji 13,000, kuna maghala mangapi?);

(iii) Teknolojia zinazotumiwa wakati wa kuvuna na kusindika ni duni sana, hii husababisha upotevu mkubwa wa mavuno (n20% ya mazao hupotea baada ya mavuno).

Mheshimiwa Spika, Kuimarisha na Kuboresha Mfumo wa Masoko (Ndani ya Nje ya Nchi). Changamoto ni nyingi na kusababisha hasara na ugumu wa maisha (hususan kwa wakulima wadogo). Wizara/ Serikali ijifanyie tathmini ili kuboresha suala hili.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Naibu Spika, sababu kuu zinazosababisha uharibifu katika misitu/ uvunaji wa kupitiliza na usio endelevuni;

Mheshimiwa Naibu Spika, uzalishaji usio endelevu wa mkaa; Shughuli za kilimo; Biashara haramu ya mbao (illegal timber trading) na mkanganyiko katika sheria zinazosababisha degradation ya misitu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema Serikali ikajipanga na kuja na mikakati mahususi na kuja na time plan itakayotumika kuboresha na kurekebisha changamoto hizi ili kuleta tija katika nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Maridhiano/Mikataba ya Kimataifa. Tanzania imeingia mikataba ya kimataifa kama, UN-CCD, Bonn Challenge, African Forest Landscape restoration, na Zanzibar Declaration kwa lengo mahususi la kuboresha soko la mazao ya misitu nje na ndani ya nchi, na kuhakilisha hali ya misitu nchini inaboreshwa. Ni nini status katika kutekeleza matakwa ya mikataba hii hapa nchini?

Mheshimiwa Naibu Spika, TFS Kuwa Regulatory Authority Kutoka Kuwa Agency. Kutekeleza hili kwa wakati itasaidia TFS na hivyo kujenga ufanisi katika kusimamia misitu yote nchini bila kuleta changamoto za mgongano wa kimamlaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, Soko la Mbao Nje na Ndani ya Nchi. Tuna potential kubwa nchini katika sekta hii ila bado tupo nyuma sana kwani tunaendeleza biashara hii traditionally. Viwanda vingi nchini havi maximize recovery ya mbao na pia tupo nyuma katika grading ya mbao na kukosa fursa ya kujipatia fedha za kigeni. Kuna umuhimu wa kuviendeleza/kuvifufua viwanda vya mbao; kwa mfano viwanda vya Fiber Board-Arusha, Tembo Clipboard-Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kuhusu Soko la Mbao. Serikali ijikite katika kuongeza aina za mbao kutoka traditional types za mbao mfano, Mvule, Mkongo na Mninga na badala yake ku-diversity resources nyinginezo za aina za miti/miti mbadala.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna haja kwa Serikali kujitathmini katika suala la soko la mbao nje ya nchi kwani tunapoteza kama nchi mabilioni ya fedha za kigeni kutoka illegal traded timber Soko kuu la magendo limekithiri kwa malighafi nchi za Asia na hususan China. Ni nini status ya nchi baada ya kusaini The Zanzibar Declaration on Illegal Trade in Timber and Forest Products?

Mheshimiwa Naibu Spika, what is the status of community based forestry management and the commitment of the Government to uphold what it sets out in the forest policy of 1998? We are told there is draft revised policy, what is the current status and how rights of those depending on community forestry are being upheld?
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, 2017
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi ili niweze kutoa mawazo yangu na mchango wangu katika marekebisho ya Sheria ya Bajeti hasa kwenye vifungu ambavyo vinaenda kuleta marekebisho kwenye reporting kutoka quarter kwenda kila baada ya miezi sita kama taarifa za matumizi, utekelezaji na taarifa za mapato na matumizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitajikita kwenye kuchangia hoja yangu kwa kuunga mkono hoja/maoni yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Nitaanza kwanza na ushauri ili tujue tunaendaje endaje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tumeona tuna changamoto tunashindwa ku-deliver quarterly, hatuna haja ya kubadili sheria, tuongeze muda bali inabidi tuangalie kwenye system zetu tufanyeje kazi ili tuweze ku-improve performance. Kama ni mambo ya software ama mfumo wa reporting una kasoro basi huo ufanyiwe marekebisho na sio sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba Tanzania ni wajumbe wa Commonwealth, sasa ni Mabunge yapi katika Commonwealth countries zinaenda ku-report kwa kutumia kila baada ya miezi sita na sio quarterly. Kwa nini sisi tunataka kuwa wa tofauti na ni sababu gani nzito zinazotaka kufanya sisi tubadilishe mfumo wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Bungeni hapa tunakutana mara nne kwa mwaka kwenye Kamati zile tendaji ili tuweze kuisimamia Serikali na kushauri otherwise pale tunapotakiwa kushauri. Sasa tunapokutana kwenye Kamati tunaletewa taasisi ama Wizara mbalimbali za Serikali zinaelezea utekelezaji wao, tunazichunguza utekelezaji wao; sasa ule utekelezaji tunaupimaje bila kuangalia matumizi yalikuwaje na sources za mapato zilikuwaje. How are you going to analyze bila ripoti ya mapato na matumizi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni hivi; mfumo wa quarterly reporting haujashuka tu, kuna benefits zake; ndio kuna changamoto zake lakini benefits naona zipo nyingi kuliko upungufu wa kuripoti quarterly. Tunavyopanga mipango yetu, tunataka kupitisha bajeti ya mwaka, ile budgeting imekuwa shaped na tulichokipanga kwa mwaka

huo. Sasa Waheshimiwa Wabunge wenzangu tunapimaje miezi sita half a through, mwezi wa Saba, Nane, Tisa, Kumi, Kumi na Moja na Kumi na Mbili ndio uangalie kuna shida gani? Hapo tayari tumebakiza miezi sita tu inayobaki, sio rahisi kufanya rectification zozote kama kuna upungufu mahali fulani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hatuwezi kuboresha utendaji wa progamu au malengo au shughuli za kiutendaji kwa kusubiri mwisho wa mwaka au karibuni nusu mwaka. Kipimo kizuri cha utendaji na ndio tunachokifanya, si tunalipana mishahara kila mwisho wa mwezi, Ofisi si zinatakiwa zilipe bills kila mwisho wa mwezi, kwa hiyo kuna accounting system ambayo kila mwisho wa mwezi inafanya checks and balances. Sasa shida iko wapi ku-compile kila mwezi ukaripoti miezi mitatu mitatu. Kwa nini usubiri miezi sita? Hapo hatuoni kama tunaweka loophole ya kufanya yasiyotakiwa kwenye utendaji wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, system ya quarterly pia inasaidia kuboresha uwazi na kuongeza umahiri; yule kama ni Accounting Officer au Program Officer unampa muda, miezi sita; wa Kwanza, wa Pili, wa Tatu, wa Nne, wa Tano na wa Sita na zile ripoti anazo kila mwezi anatakiwa afanyie kazi; hapo tunaipa nafasi ya kulega lega na kutokuweka udhibiti thabiti wa kusimamia mapato na matumizi. Ni bora ujue tatizo liko wapi mwanzoni kuliko kusubiri miezi kadhaa baadaye. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kuna umuhimu wa kuboresha udhibiti juu ya taarifa za fedha ambao at least quarterly ulikuwa unatupa mwangaza na sisi Waheshimiwa Wabunge tunapokutana kila Kamati, hii ilikuwa inatupa uwezo wa kufanya kazi zetu vizuri.
Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania wa Mwaka 2017
MHE. DKT. IMMACULATE S. SWARE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi kutoa maoni yangu katika kujenga au kurekebisha Muswada wa Sheria mpya ya Wakala wa Meli Tanzania. Nina mambo matano tu ya kuongelea lakini la kwanza ningependa kujua ni kwa nini NASACO ilifutwa na sasa tuna propose NASAC.

Mheshimiwa Spika, uanzishwaji huu wa NASAC umeleta mgongano wa sheria katika usimamizi wake. Ukiangalia kifungu cha 41 katika sheri hii mpya inayokuwa proposed, kinaleta mkanganyiko katika usimamizi na udhibiti wa shughuli nzima za uendesahaji wa shughuli za usafiri baharini.

Mheshimiwa Spika, nashukuru; tuna Sheria ya Wakala wa Meli Na. 11ya mwaka 2002, tuna Sheria ya SUMATRA Na. 9 ya 2001, tuna Merchant Shipping Act na sasa tuna-propose NASAC ambayo inaenda kuwa wakala, inaenda kusimamia na kudhibiti. Sasa hizi sheria nyingine zina kuwa redundant au hazijitoshelezi ndo maana NASAC inakuja kubeba kila kitu na tunasema kwamba sheria hizi tunazozi-propose zinaenda kuwa juu ya sheria hizi nyingine.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 7(1) na 7(2)(a) vinaleta utatanishi katika kuleta limitation ya kuzuia wafanyabiashara or the private sector kushughulika na shughuli za usafirishaji. Kifungu cha 7(1) kinasema: “The Corporation shall represent all principals in shipping business and may delegate the mandate to a shipping agent licenced in accordance with this Act. Hata hivyo, ikaja ika- limit asilimia mia moja kwamba hawa private sector hawatoweza kusafirisha nyara za Serikali au madini katika hii. Sasa inaleta mkanganyiko kwamba huyu NASAC ndiyo anakuwa anajisafirishia mwenyewe, anaji- regulate mwenyewe na anadhibiti mwenyewe. Kwa hiyo kunakuwa na conflict of interest na haya mashirika mengine au hizi taasisi zingine zitakuwa zitafanya kazi gani.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 11(b) kinaipa mamlaka NASAC ya ku-regulate mashirika mengine ya nje, inataka iwe na mamlaka ya kusimamia meli ambazo zimepewa leseni zetu zenye majina yetu. Kwa hiyo, naomba tukiangalie kifungu hiki kwa umakini ili pia tuweze kuzingatia mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania imeingia na hizo sheria za Kimataifa za usimamizi wa mambo haya katika kusafiri baharini, bahari kuu. Kwa hiyo naomba tusije tukajikanganya au tukawa tunakanyaga sheria.

Mheshimiwa Spika, sheria imempa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hili sijui niseme nyenzo kubwa sana yaani inampa yeye binafsi aweze kusema kwamba nafuta leseni, inafutwa kwa muda gani na kwa sababu hizo hii haijakaa sawa. Mamlaka husika haiwezi kusimamia na kufuta leseni kwa kumtegemea Mkurugenzi kwa utashi wake binafsi. Kwa hiyo lazima kuwe kuna chombo mahususi au kuwe kuna time limitation kwamba leseni inapofutwa basi inafutwa kwa kipindi gani.

Mheshimiwa Spika, hapohapo katika eneo hili sheria hii haimpi mtu uwezo wa kuwepo Kamati Maalum ya kufanya uchunguzi; lazima kuwe kuna Bodi au Committee ya kusema kwamba inachunguza nini ili iweze kuweka mwelekeo wa hiyo leseni inafutwa au inasimamishwa na kwa kipindi maalum. Hata huyu aliyefutiwa leseni hamna kipengele kinachomwonesha kwamba atachukua hatua gani kama amefungiwa leseni yake yaani anaenda kulalamikia wapi na atasimamia miongozo ipi.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho, ni kwamba Mu swada huu haujatoa maelekezo au hatua mtu anaweza kuzifuatilia kama hajatendewa haki, kwa hiyo lazima vipengele vyote viwe mahususi vya kuonesha kwamba umiliki unasimamiwaje na unasimamiwa na nani, huwezi kumwachia NASAC peke yake au huwezi kumwachia Mkurugenzi mhusika peke yake akawa anatumia utashi wake binafsi katika kusimamia mwenendo huu.

Mheshimiwa Spika, nilipokuwa nasoma Muswada huu ulikuwa umeanza na kusema kwamba Muswada huu utakuwa unasimamia the shipping services kwenye sea ports na inland waterways; lakini unapoendelea kuusoma huu Muswada umeng’ang’ania tu maritime, je activities ambazo zinafanywa kwenye inland waters kama ni Lake Tanganyika au Lake Victoria zinasimamiwa na nani au bado tena tutakuwa tuna-concentrate na usafiri wa baharini huku inland water zitaacha hizi sheria zingine zi-take charge.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa ujumla wake Muswada nauona una kasoro nyingi, Muswada umempa mamlaka NASAC ya kuwa mtendaji, msimamizi, wakala na ndiyo kila kitu, kitu ambacho si sawa.

Mheshimiwa Spika, ni hayo tu kwa uchache. Ahsante.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi. Natambua kwamba Serikali imeyachukua maoni karibu yote ya Kamati yetu ya Bajeti lakini nataka kuongeza mambo machache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, katika Muswada wetu ukurasa wa 6, kuna amendment katika section 10A,
Ibara ya 9 ambayo inasema kwamba fedha hizi za PPP zitaingizwa katika a bank account. Sasa ingependeza hii bank account ikaelezewa iko wapi? Itolewe tafsiri kama iko kwenye BoT, iko kwenye commercial banks, kwa sababu pale walikuwa wameshaji-commit kwamba itakuwa kwenye reputable investment bank, lakini sasa wameiacha iko very vague. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni katika Ibara ya 10, ukurasa huo huo wa 6, amendment of section 15. Ibara ya 10 iko specifically ikiongelea sifa zilizoainishwa za miradi ya kipekee ya uwekezaji kwa njia ya ubia (unsolicited projects). Ukiangalia katika hiyo Ibara ndogo ya (a) inasema:-

“The project shall be a priority to the Government at the particular time and broadly consistent with the government’s strategic objectives”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sifa hii iliyowekwa hapa kwa nini unam-limit huyu mbia ambaye anataka kuingia ubia na Serikali kwamba huo mradi wake lazima uwe sambamba na priorities za government at a particular time kwa muda specific na strategic objectives? Nikakaa nawaza, tuna dira au sera yetu ya kusema kwamba ni uchumi wa viwanda, lakini uchumi huu wa viwanda unaendeshwa na nini? Masuala ya elimu yapo, kilimo kwa upana wake kipo, mifugo, uvuvi na vinginevyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sekta nyingi ambazo zinakwenda ku-feed in kwenye sekta ya viwanda. Sasa huyu mbia kama yuko kwenye wilaya au mkoa fulani, kila wilaya na kila sehemu ina specific needs zake na ina progress fulani katika sekta fulani, kama ni ya viwanda at that particular time tunayoiongelea sasa hivi. Kwa nini sasa unambana huyu mbia unasema, kuwa kwenye priorities za hiyo government? What priorities? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijawahi kuona katika Bunge hili tunasema priority ya mwaka huu ni maji, yaani bajeti
inabeba tu masuala ya maji au bajeti hii mwaka huu tunataka kuona masuala ya kilimo tunavuka yaani iko too broad. Kwa hiyo, kwangu naona haina mantiki na haiko sawa, labda wai-shape vinginevyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ndogo ya (b) pia inasema:-

“The private proponent does not require Government guarantee or any form of financial support from the Government.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakiri, tuko wote kwenye Kamati hii ya Bajeti; tulikuwa na discussion ndefu sana hapa, lakini bado naona kipengele hiki kipo kama kilivyo, hata kwenye amendment sioni chochote. Tunasema tunaingia ubia (partnership), partnership maana yake nini? Yaani wewe hutaki commitment ya aina yoyote, hutaki guarantee ya aina yoyote, partnership maana yake nini? Kwa nini Government inajitoa asilimia 100 na hapa tunasema ni Public Private Partnership? Kuna sisi wananchi, kuna private sector, lakini huyu Government anasema hapana, mimi siji-commit kwa lolote lile. Where is the partnership in here? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado nasisitiza hiki kifungu hakijakaa sawa na inaonesha kwamba tunaendelea kuweka mazingira magumu kwa mwekezaji. Yaani wewe hutaki kumsaidia huyu mwekezaji kwenye issues tu labda za land, utaalamu na vitu vinginevyo, au finances za aina yoyote; yaani unajitoa asilimia 100. Kwa hiyo, bado haina mantiki yoyote kuwepo hapa kwa sababu haiendani na hiki kilicho mezani kuhusu issue ya partnership. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya (3) ukurasa huo huo wa 6, Serikali imefanya amendment na kifungu hiki kilikuwa kinaongelea kwamba yule mwekezaji aoneshe commitment na commitment hiyo aoneshe kifedha ili kwamba usilete usumbufu wa aina yoyote, kuonesha seriousness, basi deposit. Tulitoka kuanzia asilimia 15, tukaenda 5%, sasa hivi naona inasomeka 3% ya kile anachokikadiria ku-commit katika ule mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele cha (3A) sasa kinasisitiza kwamba, the Minister may make regulations prescribing procedure for refund ya ile commitment. Huyu private sector anayeingia ubia, hizi projects ni za mabilioni ya fedha na fedha hii ya huyu private sector haitoki mfukoni, wengi wao ni mikopo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, narejea kipengele nilichokiongelea unasema kwamba hutaki commitment ya aina yoyote lakini unataka guarantee from huyu mbia; unataka hela, kwamba mpeni 3% unachokikadiria ambacho utakitumia, sijui ni shilingi trilioni 2, shilingi trilioni 3 au shilingi trilioni 20, unataka 3%. Tukabanana kwenye Kamati kwenye suala hili kwamba siwezi tu nikakupa, for what purpose? Inaingia kwenye mfuko gani? Una role gani pale mpaka uichukue hela yangu ambayo mimi nakwenda ku-invest na hela hizi zina riba kubwa kwa sababu ni za mikopo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unatuambia kwamba the Minister may make regulations. Sasa kwa layman kama mimi kwenye sheria au kwenye hii lugha ya kusema ‘may,’ kwa hiyo, ina maana it is not mandatory. Unaweza ukajisikia usitengeneze hizo regulations ukabaki na 3% ya hela ya mdau, unafanyia nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ni hivyo basi, mimi nina-propose kipengele hiki kisomeke the Minister shall make regulations na on top of that kwa wataalam wanisaidie kwenye lugha hii ya kisheria, siyo tu waseme shall make regulations na aseme ni muda gani hizi hela zitakuwa refunded ili kusilete ile lugha ya ‘kiendacho kwa mganga hakirudi’. Kwa sababu tumeona Serikali yetu ina hako kamchezo ka kuchukua hela za wadau na kutozirejesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nataka niligusie ni katika utaratibu mpya wa uidhinishaji wa miradi ya PPP. Ukiangalia hii, iko kwenye taarifa yetu ya Kamati ya Bajeti, ukurasa ule wa 2 kutoka mwisho, kuna chart pale, inaonesha kwamba utaratibu wa kwanza unaanza kwa Wizara, Idara, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa ndiyo wanaoanza initiation ya kuandaa maandiko ya miradi na kufanya pembuzi yakinifu. Inateremka mpaka kule chini inasema sasa Waziri wa Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji watafanya uidhinishaji wa miradi pamoja na mikataba wakishirikiana kutengeneza ile mikataba pamoja na AG.

Mheshimiwa Mwenyekiti, issue yangu ya kwanza kwenye hili, hapa wadau wa kwanza inategemeana na huo ubia unaanzia katika level ya Wizara au Idara sijui ni ndani ya Wizara au ni Idara katika mamlaka husika au through TAMISEMI. Nikawa najiuliza, ametoka kuchangia Mheshimiwa Ruth Mollel akagusia kuhusu hizi Local Government Authorities, tunataka tuingie ubia na mwekezaji kwenye Local Authority fulani, je, mamlaka hizi kwanza tunajua zina shida ya kifedha, ana uwezo huo wa kufanya kazi na huyu private sector? Serikali za Mitaa zina wataalam wanaoweza kufanya hizi pembuzi yakinifu? Kwa hiyo, kuna issue hapa ya resources za kifedha na resources za wataalam, wako sawa kuweza kufanya haya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukishuka sasa chini kwenye kutengeneza contracts kati ya huyu private sector na Serikali, pale inasema sasa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji. Mkanganyiko wa kwanza wakati tunauchambua huu Muswada kwenye Kamati tulikuwa tuna shida ya definitions za Minister na Ministry, tulikuwa tuna shida ya mkanganyiko wa Minister responsible for finance, Minister responsible for investment na Minister responsible for PPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Muswada huu definition ya kwanza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi. Mchango wangu utajikita katika Muswada wa Hali ya Hewa. Kwanza kabisa ninaunga mkono kuletwa kwa muswada huu ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo tu machache ambayo tunahitaji kuyapatia ufafanuzi ili twende vizuri. Nikiangalia Muswada huu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kazi wanazozifanya naona zinajikita zaidi chini ya Wizara ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira; kwa sababu wizara hii chini ya Makamu wa Rais inahusika katika Kusimamia Kanuni ya Mazingira 2004 na moja ya masuala yanayozingatiwa zaidi ya mazingira ni masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, sera ndio wenyewe wanaisimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikiangalia hapa katika ukurasa wanane wa muswada wetu clausefive majukumu (functions) za hii mamlaka tunayoenda kuianzisha inaenda kufanya kazi naona zinashabihiana na katika Wizara ya Muungano na Mazingira. Sasa sijui hapo structure zinakuwaje au utekelezaji utakuwaje. Vivyo hivyo concern yangu, nikijikita katika angle hiyo clause ya 7 ya muswada huu inaonesha mfumo wa bodi, na katika kuangalia wale board members sioni representative yeyote akitoka katika wizara hii ya Muungano na mazingira ambayo wenyewe ndio wameibeba Sera ya Mabadiliko ya Tabianchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni katika ujumla wake lakini naomba niende sasa katika kipengele kimoja kimoja. Katika kipengele (clause) cha 11 inaongelea kuhusu kumpata director generalwa mamlaka hii. Sasa vigezo vilivyowekwa pale katika kifungu kidogo cha 2 (a) na (b) vinaongelea kwamba mkurugenzi huyu lazima awe na PhD na lazima awe na experience ya miaka 10 japo naona amendment mmeweka miaka nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi vigezo bado ni vikubwa sana na haviko kiuhalisia. Kwa nini PhD?PhD haiendani naefficiency ni vigezo vipo vingi. kwa hiyo, tusinyime sawa hata kama ni PhD ya metrology haimaanishi kwamba mtu mwenye masters ambaye ana experience na ana skills za uongozi; kwa sababu huyu 100 percent sio a technical person but ni manager/supervisor of so at least awe na idea ya nini kinaendelea. Experience ya eight yearsni nani huyu? Mimi nilikuwa bado na-propose hata kwenye amendment yangu kigezo cha PhD kiondoke na awe na experience of at least five years. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaenda kwenye clause ya 12(d), majukumu ya huyu director, katika (d) inasema kwamba moja ya kazi zake nito identify areas in which metrological instruments maybe installed. Sasa mimi nasema huyu si mtendaji per se, huyu ni msimamizi wa watendaji/ mamlaka; basi kazi yake iwe ni ku-ensure kwamba installation ya hizo instruments zipo katika targeted areas. Yeye haendi field akaanza ku-install hizo instruments.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa pia naomba nichangie katika clause ya 19. Nilikuwa nimeitafakari sanaclause hii labda watufafanulie watakapokuja kutupa mrejesho. Clause 19 vifungu vyote vya 1 na 2 vidogo anasema a person shall not engage in metrological observation, weather forecasting activities or weather modification activities. Kwa hiyo, leo hii mimi Sware Semesi siwezi kumwambia fulani kwamba leo kuna dalili ya mvua itanyesha mvua, mtanifunga;kwa sababu hapa unaniambia nitakuwa nimevunja sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huku maeneo tunayoishi kuna wataalam do forth wanaweza wakakwambia mvua zinaweza zikaanza lini watu wanaanza kulima lini. Sasa so far hatuna miundombinu ya ku-alert,kwamba masika hii itaanza wiki hii au hali ya hewa itakuwaje lakini kama tungekuwa tunayo tayari hiyo structure ya ku-alert wananchi wafanye shughuli zao kama ni za kilimo au mambo ya usafirishaji au shughuli za uvuviunaweza ukaana kwa sababu tayari mna efficiency kwenye hiyo area.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii clause ilivyokaa kama ilivyokaa huwezi kuni-limit mimi kusema kwamba kesho inaweza kunyesha mvua au isinyeshe. Yaani huwezi kuni- limitmimiin person kutabiri as long as sijaenda kwenye media na kutangazia taifa kwamba kesho kutatokea mafuriko kwa sababu sina hiyo authority lakini hiki kifungu kilivyokaa kama kilivyo kina utata mkubwa na mtaleta sintofahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, clause ya 28 inaongelea udhibiti au kusimamia maeneo ambayo utafunga zile instruments za kurekodi weather conditions.Katika kifungu kidogo cha 3(c) wanasema kwamba hauna ruhusu ya ku- conduct any activities kwenye maeneo ambayo hizo instruments zimefungwa lakini hamsemi ni muda gani authority itampa mtu ambaye anataka kufanya activity za ku-collect data. Kwa hiyo, nafikiri kile kifungu cha 28(3) (c) inabidi m-specify time badala ya kuicha tu inavyosema until such time.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naenda kwenye kifungu cha 29. Kifungu hiki cha 29 kinaongelea liability ya board and employees. Sasa hapo kuna utata kwa sababu mmesema kama mtu ata-interfere kama ni instrument au ata-interfere kwenye eneo la instruments zilivyofungwa au atatumia data visivyo, wote kuna liability. Kwa yule mtoa taarifa, mamlaka inasema kwamba ikitoa taarifa ambayo kwa njia moja au nyingine ikaniletea madhara, siwezi kuwashtaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nipendekeze kwamba kipindi hiki, yaani hii Bodi lazima na yenyewe iwe liable. Usiseme it shall not be liable as a result ya hizo information nilizozitoa as a result of reliance on meteorological information provided by the Authority. Kwa sababu kama mnatoa information inaweza ikaleta panic au la na hiyo panic isitokee labda, lazima muwe na liability. Hamwezi kujitoa, ninyi mamlaka hamwezi kushtakiwa. Lazima mshtakiwe kama mmetoa information ambayo inaweza ikasababisha sintofahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijikite katika clause ya 30 inayoongelea kuhusu hakimiliki. Kidogo hapa inaleta utata ukiangalia Kifungu kidogo cha 30(2) kuelekea 31. Kifungu hiki kinaelekeza kwamba unatumiaje taarifa inayotolewa na mamlaka husika. Wana-limit kwamba hiyo taarifa inayotolewa, kwa mfano inatoka kwenye media, basi third party hawezi kuitumia hiyo information.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda unaweza ukawa umetoa information kwenye chombo cha habari au kwenye gazeti limeandika, mimi kama Sware Semesi siwezi kwenda ku-share hiyo information? Tayari ameshaku-acknowledge kwamba hiyo information inakwenda kwa media. Kwa hiyo, naomba kifungu hiki pia kiangaliwe kwa upya wake au kinahitaji rewriting pale mnapo-limit nani atumie information zenu mnazozitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 32, clause 32 pia, 32(1) nayo nimeona haijakaa sawa. Hiki kifungu kinaelezea matumizi ya ardhi kwa ajili ya vyombo au hivyo vifaa vya uchukuaji wa hali ya hewa. 32(1) inasema kwamba, “The Authority may, for the performance of its function, after giving reasonable notice…” Sasa naomba hapa ikae sawa kwa sababu hii ni sheria, haiwezi ikawa vague; what is reasonable notice?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kawaida nafikiri standard anakwambia kwamba unatoa notice miezi mitatu kabla ya kutekeleza jambo fulani. Kwa hiyo, nafikiri sheria hii pia ijikite kusema reasonable notice pale unapotaka kutumia ardhi ya mtu fulani ili ufunge vifaa vyako, basi mpe notice yule mhusika ionyeshe ni ya muda gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naomba niligusie ni katika kifungu cha 42. Kifungu hiki kinahusiana na makosa ya uharibifu wa vyombo au vifaa vya kukusanyia takwimu za hali ya hewa. Sasa Kifungu hiki cha 42(1)(b) kinasema kwamba a person who approves the occupation of land within the limit of the protected area, yaani kile kifaa kinavyofungwa kwenye eneo fulani, je, mimi ninaweza nisisogelee lile eneo kwa distance kiasi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima useme ni radius kiasi gani? Perimeters ni zipi? Ukisema protected area, mimi siwezi kujua. Kwa hiyo, hapa mnaweza mkamtia mtu hatiani ukasema amesogelea kifaa cha ku-collect hizo data zenu lakini hamjanipa distance kiasi gani. Kwa hiyo, badala ya kusema tu within the limitations za protected area, nafikiri lazima m-specify ili kuwa fair. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala langu la mwisho ambalo nataka niligusie ni katika kifungu cha 52.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Endelea.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kifungu cha 52 kinaongelea kuhusu kukata rufaa. Kwa hiyo, kama umeona hujatendewa haki na mamlaka, rufaa yako ya mwisho inakwenda kwa Waziri. Nafikiri kwamba it is fair kwamba rufaa ya mwisho basi mweze kwenda Mahakamani na siyo kwenda kuleta complains zangu kupitia Bodi, kama sijaridhika na Bodi basi nakwenda kwa Waziri; basi niwe na uwezo wa kwenda Mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi. Mchango wangu utajikita katika Muswada wa Hali ya Hewa. Kwanza kabisa ninaunga mkono kuletwa kwa muswada huu ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo tu machache ambayo tunahitaji kuyapatia ufafanuzi ili twende vizuri. Nikiangalia Muswada huu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kazi wanazozifanya naona zinajikita zaidi chini ya Wizara ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira; kwa sababu wizara hii chini ya Makamu wa Rais inahusika katika Kusimamia Kanuni ya Mazingira 2004 na moja ya masuala yanayozingatiwa zaidi ya mazingira ni masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, sera ndio wenyewe wanaisimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikiangalia hapa katika ukurasa wanane wa muswada wetu clausefive majukumu (functions) za hii mamlaka tunayoenda kuianzisha inaenda kufanya kazi naona zinashabihiana na katika Wizara ya Muungano na Mazingira. Sasa sijui hapo structure zinakuwaje au utekelezaji utakuwaje. Vivyo hivyo concern yangu, nikijikita katika angle hiyo clause ya 7 ya muswada huu inaonesha mfumo wa bodi, na katika kuangalia wale board members sioni representative yeyote akitoka katika wizara hii ya Muungano na mazingira ambayo wenyewe ndio wameibeba Sera ya Mabadiliko ya Tabianchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni katika ujumla wake lakini naomba niende sasa katika kipengele kimoja kimoja. Katika kipengele (clause) cha 11 inaongelea kuhusu kumpata director generalwa mamlaka hii. Sasa vigezo vilivyowekwa pale katika kifungu kidogo cha 2 (a) na (b) vinaongelea kwamba mkurugenzi huyu lazima awe na PhD na lazima awe na experience ya miaka 10 japo naona amendment mmeweka miaka nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi vigezo bado ni vikubwa sana na haviko kiuhalisia. Kwa nini PhD?PhD haiendani naefficiency ni vigezo vipo vingi. kwa hiyo, tusinyime sawa hata kama ni PhD ya metrology haimaanishi kwamba mtu mwenye masters ambaye ana experience na ana skills za uongozi; kwa sababu huyu 100 percent sio a technical person but ni manager/supervisor of so at least awe na idea ya nini kinaendelea. Experience ya eight yearsni nani huyu? Mimi nilikuwa bado na-propose hata kwenye amendment yangu kigezo cha PhD kiondoke na awe na experience of at least five years. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaenda kwenye clause ya 12(d), majukumu ya huyu director, katika (d) inasema kwamba moja ya kazi zake nito identify areas in which metrological instruments maybe installed. Sasa mimi nasema huyu si mtendaji per se, huyu ni msimamizi wa watendaji/ mamlaka; basi kazi yake iwe ni ku-ensure kwamba installation ya hizo instruments zipo katika targeted areas. Yeye haendi field akaanza ku-install hizo instruments.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa pia naomba nichangie katika clause ya 19. Nilikuwa nimeitafakari sanaclause hii labda watufafanulie watakapokuja kutupa mrejesho. Clause 19 vifungu vyote vya 1 na 2 vidogo anasema a person shall not engage in metrological observation, weather forecasting activities or weather modification activities. Kwa hiyo, leo hii mimi Sware Semesi siwezi kumwambia fulani kwamba leo kuna dalili ya mvua itanyesha mvua, mtanifunga;kwa sababu hapa unaniambia nitakuwa nimevunja sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huku maeneo tunayoishi kuna wataalam do forth wanaweza wakakwambia mvua zinaweza zikaanza lini watu wanaanza kulima lini. Sasa so far hatuna miundombinu ya ku-alert,kwamba masika hii itaanza wiki hii au hali ya hewa itakuwaje lakini kama tungekuwa tunayo tayari hiyo structure ya ku-alert wananchi wafanye shughuli zao kama ni za kilimo au mambo ya usafirishaji au shughuli za uvuviunaweza ukaana kwa sababu tayari mna efficiency kwenye hiyo area.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii clause ilivyokaa kama ilivyokaa huwezi kuni-limit mimi kusema kwamba kesho inaweza kunyesha mvua au isinyeshe. Yaani huwezi kuni- limitmimiin person kutabiri as long as sijaenda kwenye media na kutangazia taifa kwamba kesho kutatokea mafuriko kwa sababu sina hiyo authority lakini hiki kifungu kilivyokaa kama kilivyo kina utata mkubwa na mtaleta sintofahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, clause ya 28 inaongelea udhibiti au kusimamia maeneo ambayo utafunga zile instruments za kurekodi weather conditions.Katika kifungu kidogo cha 3(c) wanasema kwamba hauna ruhusu ya ku- conduct any activities kwenye maeneo ambayo hizo instruments zimefungwa lakini hamsemi ni muda gani authority itampa mtu ambaye anataka kufanya activity za ku-collect data. Kwa hiyo, nafikiri kile kifungu cha 28(3) (c) inabidi m-specify time badala ya kuicha tu inavyosema until such time.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naenda kwenye kifungu cha 29. Kifungu hiki cha 29 kinaongelea liability ya board and employees. Sasa hapo kuna utata kwa sababu mmesema kama mtu ata-interfere kama ni instrument au ata-interfere kwenye eneo la instruments zilivyofungwa au atatumia data visivyo, wote kuna liability. Kwa yule mtoa taarifa, mamlaka inasema kwamba ikitoa taarifa ambayo kwa njia moja au nyingine ikaniletea madhara, siwezi kuwashtaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nipendekeze kwamba kipindi hiki, yaani hii Bodi lazima na yenyewe iwe liable. Usiseme it shall not be liable as a result ya hizo information nilizozitoa as a result of reliance on meteorological information provided by the Authority. Kwa sababu kama mnatoa information inaweza ikaleta panic au la na hiyo panic isitokee labda, lazima muwe na liability. Hamwezi kujitoa, ninyi mamlaka hamwezi kushtakiwa. Lazima mshtakiwe kama mmetoa information ambayo inaweza ikasababisha sintofahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijikite katika clause ya 30 inayoongelea kuhusu hakimiliki. Kidogo hapa inaleta utata ukiangalia Kifungu kidogo cha 30(2) kuelekea 31. Kifungu hiki kinaelekeza kwamba unatumiaje taarifa inayotolewa na mamlaka husika. Wana-limit kwamba hiyo taarifa inayotolewa, kwa mfano inatoka kwenye media, basi third party hawezi kuitumia hiyo information.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda unaweza ukawa umetoa information kwenye chombo cha habari au kwenye gazeti limeandika, mimi kama Sware Semesi siwezi kwenda ku-share hiyo information? Tayari ameshaku-acknowledge kwamba hiyo information inakwenda kwa media. Kwa hiyo, naomba kifungu hiki pia kiangaliwe kwa upya wake au kinahitaji rewriting pale mnapo-limit nani atumie information zenu mnazozitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 32, clause 32 pia, 32(1) nayo nimeona haijakaa sawa. Hiki kifungu kinaelezea matumizi ya ardhi kwa ajili ya vyombo au hivyo vifaa vya uchukuaji wa hali ya hewa. 32(1) inasema kwamba, “The Authority may, for the performance of its function, after giving reasonable notice…” Sasa naomba hapa ikae sawa kwa sababu hii ni sheria, haiwezi ikawa vague; what is reasonable notice?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kawaida nafikiri standard anakwambia kwamba unatoa notice miezi mitatu kabla ya kutekeleza jambo fulani. Kwa hiyo, nafikiri sheria hii pia ijikite kusema reasonable notice pale unapotaka kutumia ardhi ya mtu fulani ili ufunge vifaa vyako, basi mpe notice yule mhusika ionyeshe ni ya muda gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naomba niligusie ni katika kifungu cha 42. Kifungu hiki kinahusiana na makosa ya uharibifu wa vyombo au vifaa vya kukusanyia takwimu za hali ya hewa. Sasa Kifungu hiki cha 42(1)(b) kinasema kwamba a person who approves the occupation of land within the limit of the protected area, yaani kile kifaa kinavyofungwa kwenye eneo fulani, je, mimi ninaweza nisisogelee lile eneo kwa distance kiasi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima useme ni radius kiasi gani? Perimeters ni zipi? Ukisema protected area, mimi siwezi kujua. Kwa hiyo, hapa mnaweza mkamtia mtu hatiani ukasema amesogelea kifaa cha ku-collect hizo data zenu lakini hamjanipa distance kiasi gani. Kwa hiyo, badala ya kusema tu within the limitations za protected area, nafikiri lazima m-specify ili kuwa fair. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala langu la mwisho ambalo nataka niligusie ni katika kifungu cha 52.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Endelea.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kifungu cha 52 kinaongelea kuhusu kukata rufaa. Kwa hiyo, kama umeona hujatendewa haki na mamlaka, rufaa yako ya mwisho inakwenda kwa Waziri. Nafikiri kwamba it is fair kwamba rufaa ya mwisho basi mweze kwenda Mahakamani na siyo kwenda kuleta complains zangu kupitia Bodi, kama sijaridhika na Bodi basi nakwenda kwa Waziri; basi niwe na uwezo wa kwenda Mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi.