Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Ester Michael Mmasi (34 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. ESTHER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii, awali ya yote ninamshukuru Mwenyenzi Mungu kwa nafasi hii aliyonipatia na pia wananchi wangu kutoka Kilimanjaro akina mama wale kwa upendo wao ninawashukuru sana, niombi langu kwa Mwenyenzi Mungu aweze kuniongoza kwa hekima za Kimungu niweze kuutumikia utumishi wangu huu kwa moyo wa uadilifu, kwa moyo wa kujitoa na kujituma, nitamsihi sana Mwenyenzi Mungu anisimamie katika utumishi wangu huu mpya.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada yakusema hayo, nimesimama mbele yako kumpongeza Mheshimiwa wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, kwa hotuba yake nzuri. Hotuba yake ilivaa kiatu cha Mtanzania mwenye kipato cha hali ya chini, kiatu chake kilivaa kila aina ya mtu ambaye alikuwa na uhitaji na imani yake katika Serikali yetu hii ya Awamu ya Tano.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuanza tu kuchangia moja kwa moja katika hotuba hii mimi nitapenda kujikita kwenye mambo mawili kama siyo matatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikaanza na kwenye suala la ajira, ni kweli kwenye ukurasa ule wa 15, Mheshimiwa Rais alianza kuonyesha kwamba na alikiri pale kwamba ni kweli Tanzania suala la ajira bado ni changamoto kubwa na ukiangalia takwimu zinasema ingawa uchumi umekuwa kwa asilimia 7.1 lakini asilimia 28 ya Watanzania bado ni maskini. Lakini katika kutatua changamoto hii Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alielekeza hisia zake na alielekeza weledi wake kwa kusema kwamba njia mojawapo ya kujitoa kwenye umaskini ni pamoja na kuwa na viwanda na akasema pale tukiwa na uchumi unaotegemea viwanda pengine tutazalisha ajira za asilimia kama 40 hivi. Sasa katika hili mimi nitapenda kuchangia changamoto ambazo tuko nazo na ndiyo imekuwa kama ajenda ya dunia lakini pia imekuwa ni ajenda ya Watanzania walio wengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuanza na suala la ajira. Katika suala hili la viwanda Mheshimiwa Dkt. Joseph Pombe Magufuli, alianza kwa kuonyesha kwamba ni vema sana uchumi wa Tanzania ukalenga ule ubepari wa Kitaifa na tukatoka kwenye ubepari mamboleo. Ubepari mamboleo ni uchumi ule unaokuzwa au unaojengwa kwa uchuuzi, yaani hautumii malighafi ya ndani wewe unaagiza malighafi kutoka nje unalisha viwanda vya ndani, na kwa kufanya hivi kutoka kwenye ubepari mamboleo kwenda kwenye ubepari wa Kitaifa ndiyo njia pekee ya kujenga uchumi wa Tanzania na uchumi wa viwanda ulioimarika na kasema kwamba pamoja na viwanda hivi aliweka umuhimu wa kukuza sekta ya uvuvi, kilimo na ufugaji na katika hotuba yake pia alipokuwa anaongea na wafanyabiashara alionyeshwa kusikitika kwake na akasema inasikitisha sana kuona Tanzania ndiyo nchi pekee yenye mifugo mingi ikianza na Ethiopia Tanzania ikiwa ya pili lakini hatuna viwanda vya samli, hatuna viwanda vya ngozi, leo hii hatuna viwanda vya uvuvi alionyeshwa kusikitishwa.
Sasa katika mchango wangu katika sekta hizi tatu ni upi? Mimi nitapenda kusema kwamba ukianza na suala zima la kilimo ni kwamba ifike sasa Serikali yetu iweze kutambua changamoto kubwa ambazo tuko nazo.
Moja, ikiwa ni vikwazo vya kisheria, ukiangalia hasa sheria hii ya Vyama vya Ushirika, mathalani mimi ninayetoka Kilimanjaro, leo siwezi kulima kahawa na nikawa na direct control na ile kahawa. Watu wengi walikuwa discourage waka-prone zile kahawa ambalo ni zao kuu la uchumi na tunajua kabisa mchango wa zao kuu kama hili. Kwa hiyo, hii inakatisha tamaa, ifike sasa tutoke kwenye sheria kandamizi, sheria za kikoloni ambazo haziwezi kumsaidia Mtanzania wa leo. (Makofi)
Lakini pia katika suala zima la ajira, mimi ninafikiri ifike sasa Tanzania ichukue hatua madhubuti, mimi niliangalia juzi bajeti ya Kenya ya mwaka 2014/2015 ni bajeti ya juzi tu, niliona pale wenzetu walivyojidhatiti katika suala la ajira, kuna mfuko pale wa vijana, lakini mfuko huu kwa Tanzania yetu ya leo mfuko huu umefichwa katika Baraza la Taifa la Uwekezaji. Mimi ninashauri, kwa ombi ninaomba sana Wizara husika iweze kutoa mfuko ule pale ulipo, uwe ni mfuko wa kujitegemea vijana wetu waweze kupata ajira kupitia mfuko ule. Kwa nchi ya Kenya waliweza kutenga shilingi trilioni 8.1 sawa na pesa za Kitanzania shilingi bilioni 32.4, kwa pesa za Kitanzania hizi ni hatua madhubuti katika kumsaidia Mtanzania.
Lakini pili, nikija haswa kwenye suala la hili la ajira nafikiri sasa ifike muda ofisi husika au Wizara husika iweze kutumia tafiti zinazofanyika Tanzania. Mathalani, katika taasisi za umma kuna convocation office kule wanafanya tracer studies nyingi na kuonyesha na kubaini kijana huyu anayemaliza leo kesho atakuwa wapi na anafanya nini.
Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu kwa Wizara husika ni kwamba tafiti ziingizwe kwenye matumizi, donors wengi wanatoa pesa nyingi ziende kwenye tafiti lakini haziingizwi kwenye matumizi.
Mathalani tunaenda kwenye uchumi wa viwanda tusipojikita kwa kuangalia suala la research and development siamini kama tutafika. Juzi watu wengi walikuwa wanajiuliza hapa tutalindaje viwanda vyetu, jibu ni kwamba tutahitaji kutupa jicho letu kwenye upande wa pili, suala la research and development tulipe uzito wa hali ya juu. Walimu wanakesha maofisini wanafanya tafiti, lakini tafiti zile zimebaki kuwa kwenye makabati. Ninaomba ofisi husika iweze kutoa uzito wa pekee kwenye suala research and development, tukifanya hivi tutalinda uchumi wetu wa Tanzania, tutalinda viwanda vyetu vya ndani.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye suala la elimu, ninashukuru Mheshimiwa Rais alionyesha umuhimu kwamba elimu iwe bure, lakini changamoto nikianza pale mimi nilipopita mathalani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nimefanya research nimetembea na data nitakazozitoa ni data ambazo nimezitoa field, ninaongea kwa masikitiko makubwa, ninaongea nikiumia na nimeguswa sana. Mathalani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chuo kikubwa kama kile hakina hostel kwa wanafunzi, wanafunzi wanauwawa, wanafunzi wanapigwa risasi, mwaka jana tarehe 15 Desemba kijana mwaka wa nne wa CoET alipigwa risasi akiwa anasoma Yombo five, lakini pia mwaka 2013, ninakumbuka ilikuwa tarehe 23 Aprili, kijana Henry Chuo cha Uhasibu Arusha alipigwa risasi akiwa anasoma, akiwa anatoka bwenini…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Michael muda wako umekwisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii adhimu nami niweze kuchangia kwenye Bunge lako Tukufu. Kabla sijajikita kwenye hoja kwanza kabisa ningependa kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kutupatia Profesa Joyce Ndalichako. Profesa Ndalichako namfahamu, mama huyu si Mwanasiasa, kama ni siasa tumfundishe sisi humu ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Profesa Mama Joyce Ndalichako huyu ni mama ambaye ni result oriented character, hivyo ndivyo ninavyoweza kum-define. Kwa hiyo, Profesa Ndalichako nakupa moyo sana, kazi yako inaonekana na kwa hili tunamrudishia sifa na heshima Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niende kwenye hoja za msingi. Sasa hivi pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais ameonesha nia dhahiri ya kuweza kuongeza fursa za mkopo kwa vijana wetu wa vyuo vya elimu ya juu, kwa maana ya kwamba kuongeza fursa za rasilimali fedha ili vijana wetu waweze kupata mikopo na kuweza kujimudu kule mashuleni, lakini pia tumekuwa na changamoto kubwa na Mheshimiwa Waziri hapa amekiri, ya masuala mazima ya urejeshaji wa fedha hizi za mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jana tu nimepata taarifa kwamba katika target za Wizara hii au Taasisi hii ya Loans Board ilikuwa ipate bilioni 37 hadi ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha huu yaani tarehe 30 Juni, lakini mpaka mwezi jana ninapoongelea tarehe 30 Aprili kumekuwa kuna marejesho ya shilingi bilioni 22 tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa nimsaidie Mheshimiwa Waziri, nimesikia hapa akisema pengine ni namba ya defaulters, defaulters wamekuwa ni wengi. Mheshimiwa Waziri naomba nikiri hapana, yawezekana ndiyo kuna namba ya defaulters lakini tatizo si hivyo tunavyoliona leo. Tuna tatizo kubwa ambalo nafikiri bado halina commitment ya Serikali, tatizo hili ni masuala mazima ya ajira kwa kijana mhitimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tumeshuhudia Mawaziri wetu wengi hapa wamekuja wamefanya mawasilisho ya bajeti. Hata hivyo, nilikuwa makini, of course nilitoka kidogo, niliporudi nikasikiliza vyema, mikakati ya kumtoa kijana aliyehitimu kuingia kwenye soko la ajira. Nikasikia mipango mingi, nimesikia pale kuna masuala ya skills mismatch program ambayo hii ni mkakati wa kuwajengea uwezo vijana wahitimu kwenda kuingia kwenye ajira. Hapa nimejiuliza kijana yupi kwa ajira ipi tuliyoiandaa hapa? Tunahitaji commitment Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumesikia plan ambayo imetoka Wizara ya Ardhi kwamba, kutakuwa na land tenant support system ambayo ina mpango wa kurasimisha kwa kuwapa wakulima wadogowadogo hati za kimila ili waweze kukopesheka katika mabenki ambayo ni mabenki ya TIB, ambayo kuna Mabenki ya Kilimo. Hata hivyo, nikajiuliza hili kijana mhitimu leo anafaidikaje kwenye dirisha hili la TIB, kijana huyu anafaidikaje kwenye mkopo huu ambao tunaambiwa wa Benki ya Kilimo kwa zile rasilimali fedha zilizowekwa pale bilioni 60? hii inakatisha tamaa, tunahitaji commitment ya Serikali kuweza kuwanasua vijana wetu kwenye suala zima la changamoto ya ajira. Tusikae tukijikita kwenye masuala ya defaulters, hakuna kitu kama hicho kuna zaidi ya hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumesikia maelekezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akitoa maagizo pale TAMISEMI kwamba, isitokee Ofisi ya TAMISEMI inapitisha mpango wa ardhi na matumizi unless kutaonesha ni kiasi gani cha ardhi kitatengwa katika kusaidia wakulima au vijana hawa kuingia kwenye suala zima la kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kutenga ardhi tu mbona haitoshi pembejeo ziko wapi? Inasikitisha sana. Mimi nimetoka Kilimanjaro, vijana wangu pale wameshuka mabega, vijana wamepata vilema vya mabega, wamekuwa potters katika kubebea wazungu mizigo yao. Jana tumesikia hapa Kilimanjaro ilivyobarikiwa na suala zima la maliasili, lakini vijana wale wamekata tamaa, mabega yamewashuka, wameishia kuvuta bangi, ni nini hiki? Tunahitaji commitment ya Serikali kwenye suala zima la ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona pale na nitamfuata kaka yangu Japhary anisaidie, Kilimanjaro nimeona pale kuna White Elephant moja imejengwa na NSSF, kama kweli kulikuwa na visibility study katika jengo lile, Jengo lile limejengwa kwa bilioni 67 lakini mpaka leo ninavyoongea, mwaka wa tatu huu, kama kurudisha lile jengo siyo zaidi ya bilioni moja. Inasikitisha sana mipango na sera hai-reflect changamoto tulizonazo katika suala zima la ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, amesimama Waziri hapa leo akatueleza changamoto ambayo imetokana na, niseme tu mipango haiko makini katika taasisi zetu hizi. Tumesikia suala la Saint Joseph ambalo naamini kila mtu atakayesimama hapa ataliongela kwa uchungu wa aina yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, TCU naifahamu vizuri, nimefanya kazi Kurugenzi ya Elimu ya Juu na nilifanya pale niki-head ile section baada ya Mama Sawasawa kuondoka. Mheshimiwa Mama Ndalichako mume wake amenifundisha kazi, Profesa wangu alikuwa pale juu asubuhi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi ni mdau na nasema haya kwa sababu nimeyafanyia kazi ofisi kwangu. Hii TCU imegeuka kibanda cha kuchangisha upatu kwa wananchi wasio na uwezo. Pale TCU leo unaenda kusoma nje ya nchi ukirudi ukiwa una degree yako moja unatakiwa utoe shilingi 50,000, kwa masters degree 150,000, kwa PHD unatakiwa utoe karibu 200,000. Unaambiwa hii kupata accreditation letter, accreditation letter ipi na wakati kuna list ya accredited institution unapata kwenye mtandao wa TCU kupata not even authentication letter hii ni accreditation letter ambayo tayari pale kuna list unapata. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inaumiza sana TCU hawa wanaenda leo kuwakagua Saint Joseph tumeona, badala ya TCU wao kwenda kuwakagua wanawa-charge mpaka fees, inasikitisha sana, audit fee Saint Joseph wanalipa na wamelipa kwa miaka yote, leo hii wanawarudisha wanafunzi 489 majumbani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wetu wanapata psychological torture na mimi kama kijana mwenzao ambaye nimesoma kwa uchungu, sitakaa kimya kwenye Bunge lako hili Tukufu, nasema kwa uchungu, naomba vijana sasa waangaliwe, hatutakubali na hatutakuwa wa kupiga makofi kama vijana hawatatengewa hazina yao, kama vijana hawatapewa stahiki yao katika hii nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoongelea TCU kuna masuala yanayonisikitisha sana, tumeambiwa hiki ni kitengo katika kuangalia ubora wa shule, tunasema quality assurance, nimejiuliza wana-insure nini? Mimi nimefanya ofisi ya postgraduate, nilikuwa napokea dissertations zote, wote mliopita hapa, nimekaa nimesoma dissertation ya kila mmoja wenu.
Mheshimiwa Mwenyekiti inasikitisha sana, unakuta dissertation moja inakuwa submitted pale OUT chuo kishiriki, the same dissertation inakuwa submitted in university of Dar es Salaam, tunasema tuna Board inayo-insure quality for good sake, no haiwezekani. Tumeona vitu vya kutisha kwenye Board hii, wamekaa wanacheza mchezo wa kibati halafu wanakuja kusema wana-insure quality, for good sake, hili tutalisema bila kumumunya maneno. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wamesimamishwa hawa, tumeambiwa pale Bodi imesimamishwa lakini haitoshi. Kuna psychological torture ya vijana 489 wako mtaani. Inaumiza sana sisi tumezaa matumbo yetu yamezaa tuwasemee hawa watoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vipo vitu vinavyosikitisha, leo anatoka kijana amepata discontinuation kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; lakini mwanafunzi huyo huyo anakwenda kuwa admitted kile Chuo cha pale, kinaitwa not CBE, wanaenda kuwa admitted kwenye vyuo vingine na hali wameshafeli na wanapewa mkopo, hii inasikitisha sana. Una-transfer credit za mwanafunzi ambaye ameshafeli na Bodi inamwongezea mkopo, hii tunasema hapana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunao vijana waliokuwa misplaced kwenye hil,i inabidi tulisemee. Leo kuna vijana waliomaliza kidato cha nne wanakwenda kusoma degree ya ualimu, kwenye fani ya sayansi, unampeleka pale Chuo Kikuu cha Dodoma; for good sake tunawafahamu, baadhi wako funded na World Bank, lakini wapo wengine wamekuwa misplaced baada ya mkorogano wa Chuo cha Saint Joseph, wamepelekwa pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, unataka kutengeneza Mwalimu, ethics za ualimu anazipata wapi pale kwenye mihadhara ya Chuo Kikuu? Hatuwezi kujenga Taifa lililoelimika, hatuwezi kujenga uchumi wa nchi wakati tunapuuza suala zima la ujuzi na maarifa kwa vijana wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji kupata maelezo ya kina, juzi Mama Sitta alisimama hapa akashika shilingi kwenye Bunge lililopita, tulidai tuwe na Teachers Professional Board, hili nitalidai pia, kwa udi na uvumba katika Bunge hili. Tunahitaji kuwa na chombo ambacho kita-insure quality ya elimu ya juu kwa vijana wetu hawa, inasikitisha sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimetoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, napenda ku-declare interest. Kuna suala zima tunaita institution charter, kile ni kivuli cha kuficha maovu ndani ya vyuo vikuu. Nilimwomba Mheshimiwa Waziri tushuke twende naye tukaone maovu yanayofanyika kule, viko vitu vya kutisha. Unakuta kiongozi wa Chuo ana magari matatu, ana gari la kubebea mbwa chakula, la kumpeleka mama kwenye kitchen party na la baba. Hatuwezi kukubali, wafanyakazi wetu wanateseka…
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Mmasi muda wako umekwisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTHER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mchango wangu kwa kuzungumza ndani ya Bunge bado nimeona ni vyema niweze kuwasilisha mchango wangu wa maandishi kwa maslahi mapana katika kuboresha elimu ya Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliposema kuna haja ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu kushuka vyuoni kote nchini Tanzania ili kujionea changamoto za walimu pamoja wanafunzi hapa nilimaanisha yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo michango ya wakuu wa vyuo vikuu kutumia madaraka yao vibaya ilhali universities charter ikiwa inatoa kinga ya wakuu hawa kutoingiliwa katika utendaji wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo wakuu wa vyuo wamekuwa wakimiliki magari mawili hata matatu wakitengea mafuta lita 500 mpaka 1200 kwa mwezi kwa ajili ya shughuli za kiutendaji na shughuli za familia zao. Hii ni kukosa utii ku-abuse nafasi yao na usaliti wa misimamo ya Mheshimiwa Rais katika dhana nzima ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo wakuu wa vyuo vikuu wanaolindwa na security, mathalani auxiliary police 12 hadi 18 kwa siku moja tu na wakati huo wanafunzi wamekuwa na matukio ya kuumizwa na wezi na vibaka kwa kukosa ulinzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoangalia suala la misuse of public resources kwa upande wa wakuu wa vyuo vikuu ninapata feelings kwamba at sometimes we need to break the rules for example university charter inatumika kama sehemu ya kuiibia Serikali kwani pamoja na kutumia nafasi zao kwa maslahi yao binafsi lakini pia tumeona Serikali inavyoibiwa kwa miradi inayoendeshwa na baadhi ya vyuo ambapo Wizara husika inafika hata kukosa taarifa rasmi za kiasi gani chuo husika kinazalisha kwa mwezi kupitia miradi ya ndani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo masuala ambayo yana maslahi mapana kwa taifa hili hususan katika dhana nzima ya utumishi uliotukuka. Katika masuala ya TCU ambayo mengi yametugusa mimi binafsi napenda nikiri kuwa nimeridhia kabisa kwa suala la kutodahili wanafunzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi 489 wameonekana wamekosa sifa na vigezo katika kudahiliwa kwenye vyuo vikuu, lakini hii haimaanishi tunaitoa TCU katika kujibu hoja zetu za msingi.
Mathalani kwa kuwa TCU ndiyo inayosimamia ubora wa elimu (Higher learning institutions) na ndiyo inayoweka vigezo vya udahili, ndiyo inayokagua na kupitisha mitaala na ndiyo inayokagua ubora endelevu wa taasisi za umma nchini Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani Chuo Kikuu cha St. Joseph, ni nini sasa hatma ya vijana hawa 489 ambao wameonekana kukosa sifa na vigezo? Je, watawapeleka shambani wakalime ili ndoto ya ajira kwa vijana hawa ikapate kutimia?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninahoja maswali haya kwani kimsingi Serikali imepoteza kiasi cha fedha kupitia udhamini wa mikopo iliyowahi kutoka huko nyuma, lakini pia kibinadamu vijana hawa wameathirika kisaikolojia. Ni vyema Wizara ikawa na mkakati maalum katika kumaliza changamoto za namna hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na adhabu ya Mheshimiwa Waziri katika kusimamisha Bodi ya TCU lakini itoshe kusema adhabu hii haitoshi kwani katika kusimamisha bodi hii na watendaji wakuu bado mishahara wataendelea kuchukua, hivyo ni vyema Tume ya Uchunguzi ilichukulie hatua stahiki mapema iwezekanavyo ili Mheshimiwa Waziri aweze kupata timu sahihi ya watendaji itakayoweza kwenda sambamba na kiu ya Mheshimiwa Waziri katika kuleta ubora wa elimu ya juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hitimisho langu ningependa niombe mwongozo wa Mheshimiwa Waziri kuna sababu gani ya msingi iliyoilazimu Wizara ya Elimu katika kutenganisha mamlaka ya Bodi ya Mikopo na TCU kwani kimsingi TCU ina kurugenzi zote muhimu zinazoweza kusimamia mikopo ya elimu ya juu tofauti na leo tunapoona loans board inatengwa na TCU.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya TCU kuna kurugenzi ya udahili admission, accreditation, quality, assurance pamoja na finance. Nia nini haswa kilichopelekea kutenganisha mamlaka ya loans board na TCU? Ahsante, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi napenda nichangie kwa njia ya maandishi bajeti ya Wizara ya Maliasili kwa mwaka 2016/2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi wake kwa Profesa Jumanne Maghembe, Waziri mwenye dhamana Wizara ya Maliasili na Utalii. Mimi binafsi naamini shule na weledi wa Profesa Maghembe katika Wizara ya Maliasili na Utalii ni silaha nzuri katika ujenzi wa makuzi ya sekta ya maliasili na utalii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na pongezi hizi pia ningependa nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi wake wa Engineer Ramo Makani katika ujenzi wa sekta ya utalii. Mimi napenda kusoma vitabu vya Peter Senge ambaye ameandika masuala mengi ya management, ambapo moja ya michango yake aliweza kuonesha mahusiano ya kada za Injinia na best management practice.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nichangie kwa kujikita zaidi kwenye suala zima la mahusiano ya michezo na utalii. Moja kwa moja kwa uhusika wangu kwenye mbio za marathon zilizofanyika mapema mwezi Feburuari, 2016. Katika mbio hizo lipo jambo moja kuu la utangazaji wa maliasili kupitia michezo ambalo nilifikiri ni vyema tusilipuuzie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika marathon iliyofanyika mkoani Kilimanjaro ambapo Mheshimiwa Waziri wa Habari na Michezo alikuwa mgeni rasmi tuliona kwa pamoja namna ambavyo maliasili ya uoto wa Mlima Kilimanjaro unavyotumika na makampuni binafsi katika kujipatia vipato vya mtu mmoja mmoja. Katika marathon hii, napenda Bunge lako Tukufu limtambue Ndugu John Harrison mzaliwa wa South Africa ambaye ndiye aliyeandaa mbio hizi za marathon.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuonyesha masikitiko yangu makubwa katika maandalizi na uendeshaji wa mbio hizi za marathon. Mbio hizi zilizoshirikisha Mataifa ya nje, zaidi ya watu 30,000 na wazawa 70,000 hapakuwa na ushiriki wowote wa TANAPA, wala Tanzania Tourist Board. Tulichokiona pale ni Gapco, Tigo, TBL, Serengeti Breweries na kadhalika. Napenda pia Bunge lako Tukufu litambue theme iliyobeba mbio za marathon katika ku-promote Mlima Kilimanjaro ilikuwa; “Mbio zetu, Bia zetu.” Hapa ninahoji hivi kwa nini isingelitokea walau tunakuwa na theme inayosema “Mbio zetu, Utalii wetu”? Hizi ndizo t-shirt tulizovaa katika kongamano hili zenye ujumbe wa “Mbio zetu, Bia yetu.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwangu lilikuwa ni jambo la fedheha kuona Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana katika Wizara ya Habari anavalishwa t-shirt inayo promote Bia ya Kilimanjaro na siyo Mlima Kilimanjaro. Hii ni aibu kwa Wizara, aibu kwa Taifa na aibu kwa Mataifa yote yaliyoshiriki katika mbio hizi ambao walifika takribani 30, 000 katika mbio zile. Tulikuwa na watoto wadogo waliokimbia takribani 7,000, swali langu ni ujumbe gani tulioutoa kwa vijana hasa wadogo? Ni lini watafahamu umuhimu wa uwepo wa outo wa kivutio hiki muhimu katika Mkoa wa Kilimanjaro?
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa hoja yangu ni moja, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipangaje kutangaza vivutio vya nchi yetu kupitia olympic games itakayofanyika mwezi Agosti, 2016 nchini Brazil? Nchi yetu na hususan Wizara ya Maliasili na Utalii itueleze imejipangaje kutumia fursa za michezo katika kutangaza maliasili yetu katika olympic ya mwezi Agosti, 2016? Tanzania ni sehemu ya delegates watakaohudhuria olympic games, ambapo katika event hii tunatarajia tutakuwa na zaidi ya viewers three billion. Kwangu hii ni sehemu muhimu katika kutangaza maliasili yetu. Ningependa kupitia majibu ya karatasi kutoka kwa Waziri, nini mpango wa Serikali katika kutangaza maliasili ya Tanzania?
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa Bungeni tuna half marathon ambapo Mheshimiwa Waziri Mkuu aliwahi ku-host event ya namna hii, Wabunge tumewahi kuwa sehemu ya ushiriki. Hapa nina hoja, je, Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana, hatuoni umuhimu wa kutumia hata hizi platform za Ofisi ya Bunge katika ku-promote maliasili yetu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hili nami napenda nimuombe Mheshimiwa Waziri kupitia ofisi yake aone na atambue umuhimu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wafugaji, wakulima, na wadau wote katika sekta ya maliasili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, personally napenda niseme kuwa suala ka ecological system lina two key players; uoto wa maliasili, binadamu na shughuli zake hapa namaanisha shughuli za kilimo na ufugaji lakini katika wahusika hawa wawili binadamu katika utashi wake ndiye amepewa uwezo wa kuleta balance kati ya uoto wa maliasili pamoja na wanyama na suala zima za kilimo sasa hapa nilitaka niseme nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi maingiliano ya uoto wa maliasili na wanyama pamoja na wakulima ni binadamu pekee mwenye uwezo wa kuhifadhi maliasili ya Tanzania kwa ujumla wake. Kilimanjaro leo vivutio vya maporomoko ya maji yaani water falls yametoweka, mito imekauka; Mto Karanga Kikafu pamoja na Bwawa la Nyumba ya Mungu yote yameonesha dalili za nje, nje za kutoweka katika uso wa Tanzania kama wakazi wa Kilimanjaro bado wataendelea kuchoma misitu na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, ni ushauri wangu kwa Wizara husika kutoa elimu ya kutosha ili uoto wa asili uendelee kuwepo kwa vizazi na vizazi. Nchi ya Rwanda imekuwa ni role model kwa Tanzania na East Africa katika suala zima la uhifadhi wa mazingira, hapa tujiulize nini wastani wa wanyama kwa mfugaji mmoja mmoja? Nafikiri katika jibu tutakalolipata tutaweza kupiga hatua kutokea hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hitimisho langu pia ningependa niiombe Serikali yangu iweze kukumbuka royalties kwa wananchi wangu wa Mkoa wa Kilimanjaro kutokana na natural endowment tuliyonayo kwa Mkoa wa Kilimanjaro. Nasisitiza kwamba vijana wa Kilimanjaro wamebaki kuwa watazamaji, wahitimu wa vyuo vikuu wamebaki kuwa wabeba mizigo ya wazungu wanaokuja kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kilimanjaro kama mikoa mingine nayo imekuwa ni sehemu ya wahanga katika suala zima la huduma za jamaii ilhali Mlima Kilimanjaro wenyewe na vivutio vyake vinachangia pato la sekta ya utalii kwa zaidi ya asilimia 34. Shule za Mkoa wa Kilimanjaro zina uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo, katika shule za msingi na sekondari, hakuna madawati; zipo baadhi ya shule za msingi watoto wanakaa chini, vijana wengi wameingia kwenye mkumbo wa kuvuta bangi na dawa za kulevya. Hii yote ni kutokana na hali ya kukata tamaa baada ya kukosa ajira na kubaki na ajira ya vibarua vya wazungu/watalii katika nchi yetu. Naomba kuwasilisha.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikirejea maneno ya Wanasheria wanasema kwamba, mara nyingi haki yako inapoishia ndipo haki ya mwenzio inapoanzia. Tunapoangalia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18(a) inatuambia kwamba, kila Mbunge ana haki ya kutoa mawazo yake hapa Bungeni, lakini pia, haki hii inaenda sambamba na wajibu. Ukiangalia Kanuni ya 74(4) na (6) ya Sheria ya Haki na Kinga na Maadili ya Bunge utaona pale kwamba, kila Mbunge basi anapaswa kuheshimu Kiti cha Spika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo ninasikitika sana nimekuja hapa ninauliza kulikoni. Inakuwaje leo naambiwa kuna Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lakini demokrasia hiyo basi Majimbo haya yote yanawekwa mfukoni kwa mtu mmoja na leo tunahubiri habari ya demokrasia. Hili suala tumesema hapana. Leo tumefika mahali ambapo mhimili wa Bunge unakosa heshima. Ifike mahali tuseme mwisho na hatutaki kuona haya. Kiti cha Spika hakihitaji mwanasiasa, Kiti cha Spika kinahitaji weledi, mwanazuoni anayejitambua. Kiti cha Spika kinahitaji guru wa sheria; kwa hiyo, ninaomba hawa wenzangu ambao leo wako mitaani ambapo wametoka nyumbani kwa ridhaa za waume zao na wengine wametoka nyumbani kwa ridhaa za wake zao wafike mahali waone hili siyo mahali pake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijielekeze sasa moja kwa moja kwenye hoja yangu ya msingi. Leo ninapenda pia kumpongeza Waziri mwenye dhamana, Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango kwa kazi yake nzuri, pamoja na yote tumeona kabisa suala zima la maendeleo tumetenga asilimia 40, leo ninapoongea hapa ninapata mashaka kwenye hili, tunapopeleka fungu hili lote kubwa kwenye masuala mazima ya maendeleo wakati sera na mipango ya nchi haziko nkwa ajili ya kumlinda mzawa hii ni hatari sana kwa Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo nimesoma ukiangalia kwenye hotuba ya Waziri Mkuu page ya 24 utaona pale inatueleza kwamba kupitia Sheria ya Ajira na Wageni Namba 1 ya mwaka 2005 ambapo utekelezaji wake ulianza Septemba, 2015 Serikali waliweza kujipatia mapato ya takribani shilingi bilioni 21.01 lakini mbona mimi nafika kuona kwamba, hapa hapana. Hatuwezi kujivunia vyanzo hivi ambavyo vinakiuka taratibu na misingi ya ajira.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninasema haya kwa sababu katika mchakato huu au katika Wizara hii tumeona Serikali pale imetuambia kwamba mnamo miezi sita kuanzia mwezi Septemba mpaka mwezi Machi mwaka huu Serikali iliweza kuridhia vibali vya wageni 779 ambao walikuwa hawana vibali vya kuishi nchini wala vibali vya kufanya kazi nchini Tanzania. Wizara iliridhia na watu hawa wakaingizwa kwenye ajira rasmi, wakapokonywa vijana wetu ajira na wakaingia mitaani. Leo tunaona Wachina wamekuwa mamalishe kule, Wachina wanauza mitumba, ajira ya kijana Mtanzania hailindwi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninafikiri vyanzo viko vingi, wenzangu wameongelea kuhusu utalii na maliasili; ninapenda kusemea suala la Wizara ya Maliasili. Ukiangalia bajeti ya Kenya mwaka jana ilitenga shilingi bilioni 84, wakati huo bajeti ya maliasili ya nchi ya Tanzania kwa mwaka jana ilitenga shilingi bilioni 6.2 kwa ajili ya ku-promote maliasili yetu Tanzania, katika kutengewa kule tuliona kwamba ni shilingi bilioni mbili tu ndio ilienda kwenye matumizi! Nikiwa Westminster University nasoma nilipata kualikwa kwenye moja ya kongamano ambapo hawa Bodi ya Utalii walikuja nchini Uingereza kutangaza maliasili.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilisikitika sana, nilienda pale nikakuta kwamba wenzangu Watanzania, wakati Wakenya wameleta pale chui, wameleta simba, Watanzania wamebaki kugawa business card. Watanzania wamebaki kugawa kalenda, ni vitu vya kusikitisha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niliambatana juzi na Mheshimiwa Nape Nnauye, Waziri mwenye dhamana ya Habari na Michezo tulienda pale Kilimanjaro. Inasikitisha sana, kile kivutio cha Mlima wa Kilimanjaro tulienda pale kukimbia Mbio za Marathon za ku-promote maliasili ya Tanzania, lakini cha kusikitisha tumeenda tumevalishwa t-shirt inasema; Mbio Zetu Bia Yetu yaani bia ya Kilimanjaro! Hiki ni nini?(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani, tunahitaji maliasili Tanzania…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ester, muda wako umekwisha!
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru na mimi kunipa nafasi hii niweze kuchangia kwenye Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wajumbe walionitangulia utaona wengi wameonesha kusikitishwa ama kuwa na mkanganyiko fulani kwenye masuala haya ya D by D yaani ugatuzi wa madaraka. Leo hii Wizara ya Elimu tunaambiwa kwamba wao ni wabeba sera lakini utekelezaji wa azma hii ya kutoa elimu bora kwa Watanzania wameachiwa TAMISEMI.
Mheshimia Mwenyekiti, ifike mahali hebu tuone hili suala linahitaji umakini mkubwa sana kwa upande wa Serikali, kwa nini ninasema hivyo? Ukiangalia hapa michango yetu mingi kwenye elimu tunaongelea vyuo vikuu lakini tunapwaya sana au tunakuwa na machache sana ya kusema ama tunakuwa na insight finyu sana kwenye masuala mazima ya elimu kwa upande wa shule za misingi lakini hata sekondari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wenzangu watakubaliana na mimi, yako mambo mengi ambayo bado yanahitaji michango yetu, michango mikubwa ambayo tunaweza kusema na ifike mahali Serikali iweze kutuelewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala zima ya uendeshaji wa shule za msingi na sekondari zipo changamoto nyingi lakini solution zinazokuja hapa tunashangazwa kusikia kwamba Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa wanachukua madaraka kwa kuwafukuza walimu kuona kwamba walimu hawa ndiyo wanaosababisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, najiuliza hivi viongozi hawa waliwahi kukaa chini na kufanya tathmini kujiuliza hata hii standard ambayo imekubalika kwenye mpango wa BEST taarifa ya mwaka 2012/2015 ile student ratio yaani mwalimu mmoja kwa wanafunzi 44 haya wanayasemea wapi?
Tunachosikia ni walimu kufukuzwa mashuleni hili hatutakubaliana nalo. Lakini wamejiuliza kuhusu miundombinu? Lakini wamesahau walimu wanadai satahiki zao miaka na miaka. Ifike mahali tuone kwamba tunahitaji kauli ya mwisho kabisa ya Serikali juu ya hatma ya walimu wetu, stahili za walimu, haki za walimu wetu zinalipika na tunahama kwenye hii ajenda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni shahidi na mimi pia ni shahidi na Wabunge wenzangu ni mashahidi. Mwaka jana kwenye uwasilishaji wa bajeti ya Serikali nilipata taarifa kwa Dada yangu ninayempenda sana, Kiongozi wangu mahiri, Mheshimiwa Angellah Kairuki ambaye ni Mheshimiwa mwenye dhamana Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma akisema kwamba kuna Bodi ya Mishahara na wamejipanga comes this February kwamba madai ya walimu yatakuwa yamefika sehemu ambapo Serikali itakuwa na kauli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafikiri tutakapofika kwenye majumuisho tunahitaji kauli ya Serikali ni lini masuala haya yatakwisha? Tumechoka kuimba nyimbo hii miaka kenda mia, tumechoka, inasikitisha na inaumiza sana. Ukiangalia wengi hapa tumefika kwa sababu ya uwezo wa walimu wetu. Hatukufika hapa kwa sababu ya ngonjera, midomo mizuri ya kuimba ngonjera hizi, tulikaa darasani, tukaelimishwa, tukaelemika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa lililoelimika ni Taifa ambalo litafika kuthamini nguvu kazi ya Serikali na kufanya tafsiri yenye maana kwenye masuala mazima ya maendeleo. Kwa nini nasema hivi? Tumeongea masuala ya mikopo na Wabunge wengi wamechangia kwenye upande huu.
Mimi nimeenda pale chuo cha NIT majuzi hapa nikakuta pale kuna vijana wa mwaka wa pili na mwaka wa tatu, wananfunzi 38. Wanafunzi hawa hawajalipiwa ada ambao kwa ujumla wao wanafunzi hawa wanasoma programu ya uinjinia wa vyombo vya angani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana hawa wanaosoma Engineering Maintenance in Aircraft wamefika mahali wako stucked hawana pa kwenda. Mimi najiuliza kweli tunafika mahali tunashindwa kutafsiri hatua ya Serikali katika masuala mazima ya maendeleo? Leo tumeagiza ndege mbili, tuna mpango wa kuongeza ndege, lakini tumerudi nyuma kutafsiri rasilimali yetu ambayo itakwenda kuwezesha hatua hizi za Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli! Leo hatujajipanga pengine tunafikiria kwenye ku-poach lakini ni gharama sana. Sisi tunaweza kuajiri mtu wa Emirates? Hatuwezi. Tunapoanza hapa tumemchukua Mkurugenzi wa ATCL Senegal lakini pia Technical Manager wa ATCL tumemchukua Rwanda. Hawa watu tutashindwa kufika mahali kuona ufanisi wao kwa sababu tumefika mahali ambapo tunashindwa kutafsiri investment inayofanywa na Serikali kwenye masuala mazima ya maendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ifike mahali tuone kwamba hawa vijana wetu wa NIT wanaosomea uinjinia na urubani pale wafike mahali Serikali iwalipie ada yao. Ada yao ni shilingi 10,500,000/=, shilingi 400,000,000 Serikali inapata ugumu gani kulipa hawa watoto wakasoma? Tutawaacha yatima mpaka lini? Lakini hatuoni unyeti, hatuoni nguvu ya Serikali tunayo invest pale na hata kuweza kuwakomboa vijana wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni gharama sana kumsomesha mwanafunzi ambaye anasoma course hii hapa NIT ukimpeleka Rwanda ni shilingi milioni 80, lakini kweli tunafika hapa kudharau na kuona kwamba comes rain, comes sun mambo yatakuwa sawa? Siyo sawa, ifike mahali tuone kwamba sisi kama Wabunge, sisi kama viongozi wenye dhamana tuna kila sababu ya kuisemea Serikali yetu na kuonesha njia pale inapobidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala haya ya mikopo ni masuala ambayo inabidi kwa kweli tuweze pia kuoanisha. Leo wanamaliza wanafunzi 250,000 mathalani, lakini tunajiuliza baada ya hapa ni vipi? Tunasema hii fund iweze kuzunguka na kuweza kufikia watoto maskini zaidi na zaidi lakini mbona hakuna uwiano hapa? Wanaomaliza ajira zao ziko wapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, last year hapa tumekaa, tumeongea masuala mengi, kutakuwa na Benki ya Wakulima, leo hii katika zile shilingi bilioni 55 nakumbuka, zimetoka only three percent tukasema kutakuwa na dirisha la vijana, mimi nikauliza hapa, dirisha la vijana likiwepo wanakopeshekaje hawa watu? Wakiwa na Hati za Kimila watakopesheka, God forgive! Mashamba haya nani kawapa watoto?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ifike mahali tupunguze ngonjera tuende kwenye vitendo. Tuna mengi ya kujibu tutakapokwenda kuomba kura majimboni. Ninarudia kusema kwamba Taifa lililoelimika ni Taifa ambalo litafika kukaa chini na kufanya tathmini ambayo inalenga maendeleo chanya katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni pesa nyingi sana zinapotea pale Bodi ya Mikopo. Mimi nimesikiliza, ninyi ni mashahidi, tulipitisha hapa sheria mbili juzi tu hapa, kulikuwa na ile Valuation and Valuer Registration Act ya mwaka 2016, lakini pia tulipitisha ile Procurement Act. Procurement Act ilikuwa inatambua asilimia 30 ya vijana waweze kutambulika Serikalini, waweze kufanyakazi na Serikali kwa maana kwamba kutoa service, kufanya consultancy na vitu kama hivyo. Uwezo mmewajengea wapi? Mikopo wakatoe wapi hawa vijana? Wavunje ofisi zetu? Tupunguze maneno tuende kwenye vitendo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani, tutakuwa hatutendei haki Taifa hili kama ujana wangu huu nakuja Bungeni kupaka lipstick na kupaka wanja na kurudi nyumbani, haiwezekan! Mimi sitakuwa tayari kupaka lipstick hapa ndani na wakati vijana hawana kazi, tutakuwa hatutendei haki Taifa hili. Sisi ni vijana akina Mheshimiwa Bulembo mnisikilize, tusimame hapa na tuisemee Serikali yetu kwa nia njema kabisa, lazima vijana watambuliwe, lazima vijana wapewe status yao katika hii nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mengi ya kusema nafikiri nikiendelea naweza nikatoa machozi, naomba niishie hapo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Katiba na Sheria
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nikushukuru kwa kunipa fursa hii adimu nami niweze kuchangia kwenye Bunge lako hili Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kabla sijaenda mbali, napenda sana kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutupa si tu Waziri lakini pia ametupa encyclopedia ya sheria katika Bunge hili. Si encyclopedia ametupa guru wa masuala ya sheria katika muktadha huu. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais, kwa kweli ametutendea haki sisi Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nichangie masuala ya ajira kwa vijana kwa mlengo wa sheria. Kwa kuanza naomba nichangie Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ni kwa namna gani inasigina fursa ya ajira kwa vijana wetu lakini si hivyo tu ni kwa namna gani sheria hii imetumika katika kupora rasilimali ya Tanzania na kusafirisha na hata wazawa tumebaki kuwa watazamaji katika muktadha huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukianza na Sheria hii ya Madini ya mwaka 2010, ukiangalia Kanuni ya 16(1) inaruhusu mgeni kusafirisha madini nje ya nchi. Tukienda kifungu cha 16 tunaona kabisa hata kwenye maonyesho ya kibiashara, mgeni anaruhusiwa kununua madini na kusafirisha nje ya nchi. Si hivyo tu, tunaambiwa kwamba mgeni ambaye amekuja kwa visa siku tatu nchini Tanzania anaruhusiwa kusafirisha madini kwa kadri awezavyo lakini tu kama ata- comply kwenye requirement na miongozo ya kisheria. Namba moja atalipa mrahaba unaotakiwa kwa kusafirisha madini hayo lakini pia Kamishna wa Madini atakapokuwa ametoa kibali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini si hilo tu, inasikitisha sana kuona kwamba mchimbaji mdogo ambaye ni brokers licensed holders ananyimwa kibali cha kusafirisha madini nje ya nchi. Hii hatutokubali hata siku moja, sisi ambao tunaamini vijana wetu vitovu vyao vilivyozikwa katika ardhi ya Tanzania, kijana ambaye anajua kuongea lugha ya Kiingereza ananyimwa fursa ya kufanya biashara nje ya nchi kwa kigezo ambacho hatukielewi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye Sheria ya Madini kifungu cha 18 unaona adhabu iliyotolewa, unaambiwa kwamba mtu atakapokuwa amefanya biashara akakiuka haya yote katika muktadha wa sheria, adhabu ni miaka mitatu jela au shilingi milioni 10 tu, hii tunakataa. Tunakataa kwa sababu hata kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi tumeagizwa tutetee haya. Nitasoma ni kwa namna gani Ilani ya Chama cha Mapinduzi imesimama kuona kwamba imefika mwisho tuzuie biashara ya utoroshaji wa madini. Hili tulili-swear kwa wananchi wetu, naomba nirejee. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ukurasa wa 34, kipengele ‘K’ kinasema:-
“Katika kipindi cha 2015 hadi 2020, Chama cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali yake kutekeleza mambo yafuatayo: Kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi itakayowezesha kupunguza au kukomesha kabisa vitendo vya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi na biashara haramu ya madini nchini”. Hii ni Ilani ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema kwamba imefika mwisho, tunachotaka kuona ni kwamba viwanda vya uchenjuaji wa madini vinajengwa nchini Tanzania. Kwenye sheria hii kwenye kifungu cha 52 wameweka obligations za mwekezaji lakini hatujaona kipengele kinachomlazimisha mwekezaji kuweka plants katika nchi ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili nalitetea kwa nguvu zote kwa sababu naamini kiwanda cha uchenjuaji wa madini kitakapojengwa Tanzania, kwanza tutatengeneza ajira kwa vijana wetu lakini pili tutaongeza thamani ya madini na tatu mimi kama mwana Kilimanjaro, ninyi ni mashahidi tulipoenda juzi kwenye msiba Kilimanjaro, mliona Kilimanjaro hatuna ardhi. Mkoa wa Kilimanjaro ardhi iliyobaki ni kwa ajili ya makaburi ya bibi na babu zetu, hatuna pa kulima. Mimi ninapotetea viwanda hivi vya uchenjuaji vijengwe ni kwa sababu vijana wangu watapata ajira kwenye migodi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona nchi ya Botswana ilivyopiga hatua. Miaka 40 wananchi wa pale wamebaki kuwa watazamaji kwenye masuala haya ya uwekezaji wa madini lakini baada ya kubadilisha sheria na kusema kwamba viwanda vya uchenjuaji vijengwe katika nchi ya Botswana ndipo ambapo nchi hiyo imeweza kuchangia asilimia 50 ya pato la ndani katika bajeti yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi vijana wa Chama cha Mapinduzi, sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, tunasema kwamba tuna kila sababu viwanda hivi vijengwe. Tofauti na Mheshimiwa Kaka yangu wa Siha pale, Mheshimiwa Dkt. Mollel, nilishangaa sana tarehe 20 mwezi huu hapa Bungeni aliona hakuna mantiki lakini amesahau vijana hawa wa Kilimanjaro hawana pa kulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitasema hata kama Mwanri hayupo, nitatetea vijana wa Kilimanjaro, nitatetea Siha, Hai, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Same na Mwanga, nitasema bila kuogopa, msiogope vijana wangu mimi nipo. Nitasema nitapaza sauti kwa ajili yenu Kilimanjaro. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya lakini pia tukumbuke dada yangu Mheshimiwa Angellah Kairuki hata tungepitisha vifungu vyake mamia na maelfu, hana obsorption capacity ya kutengeneza ajira hizi ni sisi tumsaidie. Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria mimi na wewe ni mashahidi tulienda kufungua mabweni ya Chuo Kikuu pale lakini uliona juhudi za Mheshimiwa Rais, alitoka nje ya mikataba, alitoka nje ya utaratibu akaona kwamba tutengeneze ajira kwa kufanya TBA waweze kufanya kazi, vijana na akinamama waajiriwe ili tuweze kusonga mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumwambia Mheshimiwa Waziri tunadaiwa, Ilani hii tuliahidi watu, nasema kwamba ifike mahali tujenge viwanda. Nitasoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi maana imeniagiza niseme, ukurasa wa 34 kwenye kipengele cha 10 tumeambiwa pamoja na majukumu haya Chama cha Mapinduzi kitafanya yafuatayo:-
“Kitasimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamani madini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa”.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasadiki hili na nitalisema siyo leo tu, kesho na kesho kutwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika musuala haya ya ajira ukienda ukasoma Public Procurement Act ya Kenya utaona ni kwa namna gani kijana anathaminika katika nchi ile. Katika sheria ile ya Kenya inasema asilimia 30 ya public procurement activities zinafanywa na vijana na kunakuwa na dawati maalum katika Ofisi ya Rais. Mheshimiwa Waziri naomba utusaidie, ulipokuwa Kitengo cha Sheria kama Dean wafanyakazi wako walikuwa na imani sana na wewe, ulikuwa mkali lakini ulikuwa tayari kutetea maslahi ya Tanzania. Nakuomba Mheshimiwa Waziri usiishie kufundisha pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tunadaiwa ajira, Ilani hii imetuagiza tutengeneze ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu gani? Hata Bertha Soka, Mkurugenzi wa PPRA alikuwa hapa Dodoma, kuna siku…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi napenda nichukue fursa hii niweze kuchangia mawazo yangu katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Kabla sijakwenda moja kwa moja kwenye mada zangu naomba kwa heshima na dhati ya moyo wangu nimpongeze Mheshimiwa Ummy Mwalimu kwa juhudi zake mahsusi katika usimamizi na uendeshaji wa masuala ya afya ya Mtanzania, afya ya akina mama na watoto pamoja na afya ya ustawi wa jamii yetu hususani kwa rika la vijana na wazee pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu afya ya mzazi, Mheshimiwa Waziri pamoja na juhudi zako za dhati katika kunusuru akina mama wanaojifungua lakini pia na watoto wachanga bado tunayo changamoto kubwa sana kwenye vifo vya akina mama wanapojifungua. Takwimu zinaonesha kwenye kila vizazi hai 100,000 tuna vifo 556 vya kina mama wanopoteza maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali yangu, sambamba na changamoto hii ya vifo vya akina mama wanaopoteza maisha pindi wanapojifungua lakini tunayo changamoto kubwa ya vifaa tiba na miundombinu ya kitabibu kwa upande wa tiba za watoto wachanga. Ni kweli tuna vifo vingi vya kina mama pindi wanapojifungua lakini pia tuna vifo vingi vya watoto wadogo/wachanga kutokana na changamoto ya uwepo wa PRE NATAL ICU (PI) kwa watoto under five years.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kitendo kinachokatisha tamaa na morale ya matabibu walio wengi nchini Tanzania hususan katika Hospitali ya Muhimbili ambayo kimsingi wamekuwa na historia ya kazi nzuri ya kitabibu ya kuokoa maisha ya vichanga especially pale inapotokea emergence ya upasuaji kwa watoto wachanga. Wengi wa madaktari wamewahi kusema tumekuwa na kazi nzuri theatres lakini kazi zetu nyingi zinaharibikia kwenye vyumba tunapowalaza watoto wagonjwa ambao wamewahikufanyiwa upasuaji kwa kuwa vyumba vya ICU kama PRE NATAL ICU zimekuwa na msongamano mkubwa wa watoto kwa kuwa katika Hospitali za Mikoa, Wilaya na Halmashauri hatuna huduma za vyumba vya watoto za PRE NATAL ICU.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ushauri wangu kwa Serikali yangu kuwa Wizara hii iweze kuongezewa fungu la uboreshaji wa miundombinu ili hospitali zetu ngazi za Mikoa na Wilaya ziweze kupata wodi za PRE NATAL ICU ili kunusuru vifo vya watoto wachanga. Sambamba na hili pia niombe Serikali yangu iangalie kwa jicho la kipekee kabisa vifo vya kina mama wanaopoteza maisha pindi wanapojifungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo changamoto kubwa ya afya ya akina mama especially case ya cancer ya shingo ya kizazi. Ni rai yangu kwa Serikali kupitia taasisi za tafiti za afya ya binadamu tuweze kufanya utafiti wa kina ili kubaini nini changamoto tulizonazo kwenye mfumo mzima wa afya ya mama na msichana ambayo inasabisha ongezeko la ugonjwa wa cancer ya shingo ya kizazi. Sanitary towels zote zinazosambazwa kwa umma wa Watanzania zifanyiwe utafiti wa kina, jamii zenye mila za kutotahiri wanaume nazo zifanyiwe tafiti za kina ili kubaini kwa nini ongezeko kubwa la cancer ya kizazi. Ikiwa HPV Vaccine ndiyo jawabu la kinga ya maambukizi basi Serikali yangu ije na majibu kwa umma wa Watanzania ili tupate suluhisho la kudumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasichana waliopo kwenye umri mdogo wanapoteza maisha kwa kasi isiyokubalika, tuiombe Wizara itusaidie kuja na suluhisho la kudumu kwenye suala zima la ongezeko la cervical cancer.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu HIV & AIDS, ni kweli tunayo changamoto kubwa ya tiba na vifaa tiba pamoja na mifumo ya uendeshaji tiba kwa watu wenye maambukizi ya VVU. Kupitia data ya USAID Novemba, 2016 Serikali ya Tanzania imekuwa ikichangia kwenye tiba ya HIV & AIDS kwa asilimia tatu tu ikilinganishwa na michango ya nchi wahisani kama mathalani USA ambayo imekuwa ikichangia takribani asilimia 71.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo changamoto ya utegemezi mkubwa kwenye dawa za ARV kutokana na kwamba mifumo ya TEHAMA ambapo asilimia 100 ya mifumo ya kitabibu imetengenezwa na kufadhiliwa na Wamarekani. Naona shida kuona hata masuala ya mifumo ya uendeshaji wa tiba ya wagonjwa walioathirika CTC2 (Care & Treatment Clinic) ambayo mfumo huu unatumika katika kuhifadhi kumbukumbu za wagonjwa wote walio na maambukizi ya VVU, DI+IS 2. Mfumo huu nao unatumika kuhifadhi kumbukumbu za wagonjwa; kwa kitaalam mfumo huu unatambulika kama District Health Information System ambao nao unafadhiliwa na Wamarekani kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi napata taabu sana kuona tunashindwa kuendana na principle ethics za namna ya kuhifadhi ama kutunza usiri wa wagonjwa hawa ikiwa mifumo hii itaachiwa mashirika ya nje waitengeneze na kuifadhili. Je, nini nafasi yetu kama nchi katika kulinda privacy za wananchi wetu wenye maambukizi ya VVU? Ni dhahiri kabisa kwa utendaji huu hatuna assurance ya sustainability ya mifumo hii na hata tiba za dawa ikiwa Tanzania itakubali kusimama kama mtizamaji. Three percent of contribution as a country is too peanut for us to stay safe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Serikali ni kwamba ione sababu za msingi katika kutumia rasilimali ya Tanzania kwa ajili ya kuunda mifumo ya kitabibu. Ndani ya DIT (Dar es Salaam Institute of Technology) tunao vijana wazuri wenye umahiri mkubwa katika kuunda software kama software developers na vijana hawa wana utaalam na uzoefu wa kutosha kwenye masuala ya programming, tuwape nafasi vijana wetu wa Kitanzania kwenye ushiriki mzima wa masuala ya TEHAMA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga hoja mkono juhudi za Serikali kupitia wasilisho la hotuba hii muhimu kwa ustawi mzima na afya ya kina mama na watoto. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa kunipa muda nami niweze kuchangia katika Wizara hii muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda tu nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanaoifanya. Mama yangu Mheshimiwa Ndalichako, Profesa wangu mwema, kwangu katika mchango wangu hata siku moja katika Bunge hili, tofauti na ilivyochangiwa na Waheshimiwa Wabunge wengine, mimi sitamwomba aache legacy, legacy ameiacha tayari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri atakumbuka katika Baraza la Mawaziri wote, mtu wa kwanza aliyekuwa na uthubu ni yeye. Alikubali kukana nafsi yake, akajitwisha msalaba wake, akafuta GPA bila kungoja makelele ya Waheshimiwa Wabunge, kwenye hili alisimama mwenyewe. Nampongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, alisimama akaona kero ya wanafunzi wanaohangaika mitaani kutafuta hifadhi, alisimamia hili ndani ya miezi minane alituonesha kwa mfano, mimi pamoja na Mheshimiwa Mwenyekiti tulikuwa mashahidi. Tulikuja kwenye ufunguzi wa hostels za Chuo Kikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu. Mimi ni Mbunge wa kwanza katika Bunge hili jipya kulia kwamba naomba miundombinu iliyowekwa pale UDOM ijae, tunapoteza pesa nyingi lakini Mheshimiwa Waziri hukunipa nafasi nije kulalamika mara ya pili. Jana nimeona umetoa waraka kwamba Central System Admission ifute ile process kwamba vyuo visidahili ila TCU iweze kudahili wanafunzi kwa maana ya kwamba kwa kufanya vile vyuo vingi vilikuwa vinabaki empty, tunaweka resources nyingi lakini pia hatuna matumizi nayo. Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niende kwenye mchango moja kwa moja katika Wizara hii muhimu. Nianze tu kumwambia Mama Ndalichako, tunafahamu na Tanzania inafahamu na sisi wadau tunafahamu kwamba changamoto kubwa katika Wizara yake imekuwa ni urejeshaji wa masuala mazima ya mikopo Elimu ya Juu. Mheshimiwa Mwenyekiti tunakiri hilo.

Mheshimiwa Mwenyikiti, pia kama utaangalia, juzi tukiwa Mei Mosi tulipata taarifa kwamba katika mwaka huu wa fedha tunaomaliza, deni ambalo limekuwa halijalipika mpaka leo ni seven trillion, deni tulilotakiwa kulirejeshwa Bodi ya Mkopo ni seven trillion lakini mpaka leo ni shilingi bilioni 400 tu zimerejeshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mama yangu Mheshimiwa Ndalichako, legacy ameiacha tunataka tuilinde. Naomba asikilize yafuatayo, kwamba sisi Tanzania mwaka 1999 tulituma delegation yetu kwenda nchi ya Kenya kujifunza wenzetu wanafanya nini, lakini kule tulichokiona, asilimia 40 na ni practice ambayo mpaka leo ndivyo ilivyo. Asilimia 40 ya tengeo la fedha ya Bodi ya Mkopo ndiyo Serikali ina-meet lakini asilimia 60 ni other key players, kwa maana ya kwamba ni financial sectors ndiyo ina-dish-out pesa katika kusomesha wanafuzi. Mimi siombi tufike huko, lakini angalizo lipo moja; tusipoangalia, tunaweza tukashindwa kufikisha tumaini letu kwa wananchi wetu walio wengi wanaotutegemea sisi kuweza kusaidia vijana wao waweze kwenda shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia leo tatizo kubwa ni ajira. Tulikaa hapa kwenye Miscellaneous Amendment tukasema kwamba tukate asilimia 15 ili fedha hii iweze kurejeshwa, lakini Mheshimiwa Mwenyekiti tunasahau kwamba tulisema tukate asilimia 15, wakati tunaangalia entry qualification, eligibility qualifications ya mtu ambaye anaweza kupata mkopo, cha kwanza tuliangalia uhitaji. Kama ni uhitaji, ni obvious kwamba wanafunzi hawa wametoka kwenye familia maskini. Sasa kama wametoka kwenye familia masikini na ajira hakuna, tunategemea hii asilimia 15 tunam-task mwanafunzi au mzazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tupate muda tutafakari upya. Asilimia 15 ni rahisi sana kuwekwa kwenye majarida yetu, ni rahisi sana kuja kuijengea hoja Bungeni, lakini watakaoteseka ni wananchi wetu wa vijijini wasiokuwa na uwezo. Kama hivi ndivyo tupate muda tutafakari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa nakuomba, unao wenzako hapo, kila siku wanawasilisha ripoti zao na kusema ni kwa namna gani wanaenzi masuala mazima ya Sera ya Ajira, lakini vitu havikutani. Hatuoni direct linkages. Wewe ni shahidi, tulikaa hapa juzi, mama huyu Mheshimiwa Mama Kairuki, Waziri wa Utumishi, alituambia kwamba ameahidi kutoa ajira 58,000 nchini Tanzania lakini absorption capacity bado haikidhi tija. Wanafunzi wanaomaliza ni 250,000 lakini unaona absorption capacity, ajira ni 58,000 kwa mwaka. Hatuwezi kufika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia Wizara Ardhi, inastawi, inashamiri, ni vema tumempata kiongozi mahiri, ni sawa; lakini pia ukiangalia vijana wanaomaliza Chuo cha Ardhi wanakosa kazi kupitia hata sheria tunazoleta Bungeni. Tulileta hapa Valuation and Valuer Registration Act ambayo ni sheria ya masuala mazima ya wapima na wathamini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi tuliyopewa na Mheshimiwa Waziri ni kwamba Wizara yake itasajili makampuni 57 ambayo yataingia kwenye suala zima la kupima ardhi. Tukamwuliza hapa, akasema pia vijana kupitia zile three categories ambapo kuna full valuer na temporary registration valuer walisema kwamba hata vijana graduate wanaruhusiwa kuingia na kuweza kufanya kazi za uthamini katika muktadha wa masuala mazima ya ardhi. Katika makampuni 57 yaliyoingia na kusajiliwa hakuna hata kampuni moja ya graduate wa nchi hii, mzawa wa nchi hii aliyeweza kuingia na kuweza kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, masuala ya ajira bado yamekuwa ni changamoto. Ninyi ni mashahidi kwamba vijana hawa wanahangaika, vijana hawa wanatulilia, tutawapeleka wapi? Mwaka 2020 unafika, tutajibu nini? Ilani imeeleza, Sera ya Ajira inaeleza, lakini vijana wamelia kwa kila sauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri, akae na Wizara nyingine wamsaidie tuweze ku-link na kuweza kuzalisha ajira. Leo tunavyoongea, ukuaji wa Sekta ya TEHAMA ni mkubwa, lakini wanafunzi wa DIT wanatumika wapi? Hawatumiki! Angalieni mifumo inayotumika katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye financial sector, 40 percent ya kazi za ICT inafanyika nchi ya India na Kenya. Watanzania hawashiriki katika muktadha mzima na masuala ya ajira. Legacy tutailinda pale ambapo tutaweza kufanikiwa kwenye mtihani huu wa urejeshaji wa mkopo wa Bodi. Sisi kutunga sheria ngumu bado siyo jibu kwa sababu bado tunampelekea mzigo mkulima, fukara na masikini kule kijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo masuala mazima ambayo sisi kwetu bado tunahuzunika sana. Sisi kama akinamama, wewe ni shahidi, tumekuwa na kesi nyingi sana kwenye masuala mazima ya ngono katika Vyuo Vikuu vya Tanzania yetu. Leo ngono inatumika kama kipimo na kigezo cha ufaulu katika shule zetu ama vyuo vyetu nchini Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mama Ndalichako ni shahidi, tumekuwa na kesi nyingi. Atakumbuka juzi hapa, Mhadhiri wa Chuo cha NIT, huyu anaitwa Bwana Samsom Mahimbo, alidiriki kumshawishi mwanafunzi na TAKUKURU walimkamata kwamba ili afaulu mtihani wake wa supplementary ni lazima atoe rushwa ya ngono.

Mheshimiwa mwenyekiti, sisi ni wazazi, matumbo yetu yanatuuma. Hatuwezi kuangalia dhambi hii! Hatuwezi kuangalia udhalilishaji wa wanafunzi wetu. Imesemwa hapa na waliowasilisha kwenye ripoti zao hapo mbele, imesemwa kabisa, ukimsomesha mwanamke umesomesha Taifa. Tumechoka kuona kudhalilishwa kwa watoto wetu mashuleni. Walimu hawa wanachukuliwa hatua gan? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri akija aniambie Bw. Samson Mahimbo alichukuliwa hatua gani? Asisahau, aniambie Bw. Kelvin Njunwa, ni Institute of Accounts, Dar es Salaam alichukuliwa hatua gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu yangu, kaka yangu mpendwa Mheshimiwa Simbachawene alienda hapa Hombolo kwenye kesi kama tatu alienda na ku-rule out za masuala ya ngono. Hawa watu wanachukuliwa hatua gani? Hatuwezi kusema tunatengeneza rasilimali ya nchi hii kwa kutumia vigezo ambavyo havina ushindani. Hatuwezi kutengeneza rasilimali ya nchi kwa kuwa na watu ambao hatujielewi wala hatujithamini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaenda kwenye uchumi wa kati, tunaandaaje rasilimali watu ya nchi yetu ya Tanzania? Tunaenda kwenye uchumi wa viwanda, tumejiandaaje kuingia kwenye uchumi wa viwanda endapo utafaulu mtoto mwanafunzi wa Chuo Kikuu unapimwa kwa utoaji wa ngono? Tutaenda wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ni mama, amezaa, Wizara yake inasimamiwa na akinamama, Semakafu ni activist mzuri, ananijua na ananisikia. Semakafu Kamishna wake ni activist mzuri; namwomba alipo atusaidie. Tutaangalia haya mpaka lini? Tumechoka, macho yetu yanaumia, nafsi zetu zinauma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hilo tu. Nilikuja kwenye Bunge lako hili Tukufu, niliongelea sasa wanafunzi wa Chuo cha NIT, nikaomba unisaidie kwamba tumejipanga kwenda kwenye uchumi wa kati, tumejipanga ku-promote Tourism Sector yetu kwa kufufua usafiri wa anga, well and good. Tume- invest a lot kununua ndege, well and good, lakini tumejipangaje kuandaa rasilimali watu katika muktadha mzima huu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa sababu hata maandiko ya dini wanasema atakayeshindwa kushukuru, huyo ni mnyang’anyi. Namshukuru sana, nilikwenda nikamwomba kwamba watoto hawa wa NIT waruhusiwe kufanya mitihani. Milioni kumi… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii, nami niweze kuchangia kwenye Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaenda mbele kwenye mada zangu, kwanza kabisa kwa unyenyekevu mkubwa na kwa nia njema kabisa, naomba niwapongeze viongozi wetu, Mheshimiwa Waziri na Naibu wake namwona anatabasamu kwa sababu anafahamu ninafahamu jitihada
zake, ninafahamu kiu yako kuona vijana wa nchi hii wanashiriki rasmi kwenye sekta ya kilimo. Nawapongeza sana, vijana wanawapongeza sana. Pia wanasema kwamba, asiyejua kushukuru huyo ni mnyang’anyi. Mimi siwezi kuwa mnyang’anyi kwenye Bunge hili Tukufu.

Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri, ninanukumbuka nilikuja hapa Dodoma nikawafuata pale Wizarani, ninyi mlinipa kibali cha kuweza ku-organize vijana wote nchini Tanzania, wakaja tukapanga mipango. Siyo hivyo tu, mlinisimamia na mimi nikafanikisha azma yangu ya kuanzisha vikundi vya ushirika katika nchi ya Tanzania. Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, mnafahamu nimeanzisha Ushirika wa Vijana Wahitimu, nimeanzisha kule Buchosa, Geita, Bukombe, siyo hivyo tu, nimeanzisha Kigoma ambapo huko pia nimetafuta shamba ekari 1,000, Mto Malagarasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, wamenisaidia nimeanzisha ushirika Songea, Dodoma, nimeanzisha ushirika wa vijana graduates Mkoa wa Dar es Salaam, lakini Mheshimiwa Waziri naomba tu kukwambia kwamba, vijana wale bado wanakusikiliza, wamekupa macho yao yote na matumaini yao kwako. Ninaomba kwa moyo wa unyenyekevu kabisa, usiwaache vijana wale. Uliwapa matumaini makubwa, uliwasimamia na ukasema utawaongoza. Ninakuomba usimame mstari wa mbele uongoze Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi katika mawasilisho ya Wizara ya Viwanda tuliona kabisa mpango wa Serikali katika kufufua viwanda. Najiuliza kule Mkulazi ambapo mnasema tutazalisha tani 200,000 za sukari, hatuoni kwamba huu mradi utahitaji outgrowers kwa maana kwamba utahitaji malighafi kutoka nje ya Mkulazi project! Tunawaandaaje vijana hawa?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, shamba la Mbigiri, mmesema mtazalisha miwa tani 30,000 kwa mwaka, mmewaandaaje vijana hawa? Ukiangalia kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 31(v) umesema moja ya mikakati katika Wizara ni kuona kwamba vijana wanashiriki kwenye sekta ya kilimo kikamilifu.

Mheshimiwa Waziri najiuliza leo, tukiwa katika mawasalisho ya bajeti zenu huu mwaka wa fedha unaoisha Juni, 30 tuliona mipango mingi, nikauliza hawa vijana watashirikije? Mkasema kwamba atapewa hati za kimila ili waweze kukopesheka katika mabenki. Najiuliza tukiangalia fungu la maendeleo, tumetenga shilingi bilioni 101, lakini zimeenda asilimia tatu tu. Fedha za kawaida tulitenga shilingi bilioni 109, tunaona zimeenda shilingi bilioni 62 sawa na asilimia 54. Ninajiuliza, kwa nini vote three matumizi ya kawaida yanakuwa ni makubwa, lakini fungu la maendeleo linakuwa hamna kitu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, najiuliza leo, katika hii shilingi bilioni 150 mliyoitenga this year, mtatupa shilingi ngapi vijana hawa waweze kupatiwa hati za kimila na waweze kukopesheka kwenye mabenki? Mheshimiwa Waziri unafahamu na umekuwa ukituhutubia hapa kwamba NMB wametenga shilingi bilioni 500 katika kusaidia vijana, lakini wewe ni shahidi, nimezunguka NMB wananijua, kama wapo waniangalie, CRDB wananijua, nimezunguka na vijana wa Taifa hili hakuna wanakokopesheka. Hiki ni nini?

Mheshimiwa Waziri, ona huruma kwa vijana wako. Unafahamu vijana wanavyokulilia, umepokea simu za mchana na usiku, tibu kilio cha Watanzania, tibu kiu ya vijana hawa waweze kushiriki kwenye sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Waziri unaelewa, wamekuja vijana, mara ngapi wanakupigia simu? Vijana wako tayari wanataka kulima. Siyo hivyo tu, CRDB, Agribusiness Loans Unit, nimekwenda pale wananijua. Nime-mark time several times; nimefanya vikao na Makatibu Wakuu, wananijua, wako hapa waulize. Nimeongea nao usiku na mchana, vijana hawasaidiki katika nchi hii.

Mheshimiwa Waziri unafahamu Benki ya Kilimo, tulitenga shilingi bilioni 60 lakini ombi la Dar es Salaam tu lilikuwepo bilioni 55. Ni nini hiki? Tukiwa wadogo tulisoma hadithi za Abunuasi, leo mimi na utu uzima wangu ukiniambia nisome kitabu cha Abunuasi siwezi kusoma. Mheshimiwa Waziri ninakuomba uangalie, Taifa linakutegemea.

Mheshimiwa Waziri, siyo hivyo tu, TIB, Women’s Bank tumeona, Women’s Bank sasa hivi ina-run the second with high growth rate in NPL; you know it! Mheshimwia Waziri unafahamu. Benki hii tuliambiwa kutakuwa na dirisha la akina mama waweze kukopesheka na waingie kwenye kilimo. Hamna kitu! TIB the same, it is running the third with higher NPL growth rate ambayo ina asilimia 52 Women’s Bank na hii TIB ina asilimia 32.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulifungwa vinywa hapa na Mheshimiwa Waziri wa Afya akatuambia kwamba CAG atafanya kazi atuletee ripoti. Waheshimiwa Wabunge wenzangu na akina mama wa Bunge hili, ninaombeni tusikae kimya, tuisemee Benki ya Wanawake. Wanawake wanatutegemea sisi tuwasemee. Tunajiuliza leo kama Benki ya Kilimo ilikuwa ina-operate under Central Bank guidelines, ilitakiwa iwe na Bodi. Benki hii inakuwa Head wa Risk Manager, kuna board members, watu hawa wamewajibishwa lini? Benki za Taifa hili zinakufa, wamama waende wapi? Vijana waende wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu. Tumeona mambo makubwa ambayo yametukatisha tama. Vijana hawa wanahangaika. Mmeongea kwenye Sera ya Ajira, lakini hakuna tumaini tena. Ninaowasemea hapa ni watoto wa maskini, pengine hatuwajui. Watoto wa maskini ni wale ambao tunapoenda kule kula nyama kwenye minada, ni wale watoto ambao wanakinga makombo yetu kwenye beseni, wanaenda nyumbani wanapika. Siamini kama kuna mtoto wa maskini ambaye anachungwa na mbwa kwenye nyumba yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto wa maskini ni wale ambao tunapopeleka watoto wetu China, wanabeba mabegi, wanaenda airport wanawapungia watoto wa matajiri mikono. Hawa ndio watoto wa masikini ninaowasemea katika Bunge hili. Mheshimiwa Waziri tuna imani nawe, ukiamua inawezekana. Wizara yako ikiamua vijana wetu watashiriki rasmi kwenye Sekta ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anafahamu asilimia 75 ya wananchi wa Taifa hili ni wakulima, usiwaache; lakini asilimia 65 za ajira za uhakika zinapatikana kwenye Sekta ya Kilimo. Vijana wamenituma niwasemee. Vijana wamenituma nipaze sauti zao kwa niaba yao. Nakuomba kabisa utakapokuja kuhitimisha hapa, utuambie una mpango gani kwa vijana hawa waweze kushiriki kwenye project ya Mbigiri - Morogoro, utuambie vijana hawa watashiriki vipi kwenye National Milling ambayo umesema inafufuliwa hapa Dodoma. Malighafi hizi, vijana wana nguvu za kutoa malighafi kwenda kwenye viwanda hivi. Nakuomba uwashirikishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliongea habari ya AGOA, kuondolewa vikwazo vya kimasoko kwa nchi ya Marekani kupitia mlango wa SADC. Najiuliza, ni nani aliyeweza kufaidika kwenye mlango huu wa AGOA? Wanatoka Wahindi nchi ya India wanakuja Tanzania wananunua cashew nut yetu, wanapitia kwenye mradi huu wa AGOA, Watanzania tumebaki watazamaji!

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa linasikitika, linahuzunika, tusaidie Mheshimiwa Tizeba una uwezo. Mheshimiwa Olenasha mna uwezo na mna nguvu; na ninajua mna passion ya kweli katika Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha popote alipo na mama Ashatu Kijaji, tunawaomba kabisa kwa moyo wa dhati na unyenyekevu, Taifa linawaangalia. Toeni hela wasaidieni akina Mheshimiwa Olenasha wafanye kazi. Toeni hela Mheshimiwa Tizeba aweze kufanya kazi, Taifa linawaangalia. Ninaomba kwa moyo wa dhati na unyenyekevu, Bunge hili lisikie sauti ya vijana wa Tanzania hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani nisiendelee sana, pengine ninaweza nikafika sehemu nyingine. Naomba niishie hapo, naunga mkono hoja asilimia mia. Ahsante sana.
Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, nina heshima ya pekee kusimama kwenye Bunge lako Tukufu nami kuweza kuchangia kwa kifupi sana kuhusiana na documents hizi tatu ambazo tumeletewa, tuweze kuzipitia kwa minajili ya kuweza kulinda na kuhifadhi maliasili ya Tanzania, kuweza kulinda amani na usalama wa nchi yetu na kuinua uchumi wa Tanzania kupitia mradi wa Hoima - Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitajielekeza tu kwenye Azimio hili moja la mkataba kuanzisha Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe, kwa sababu kimsingi sikuweza kupitia documents zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza kabisa na kurasa ya saba Article No. 7, uundwaji wa hii Council, tukisoma pale Section (1) tunasema kwamba Board Members watakaoiunda hii Council, tume-mention kwamba hatutakuwa na zaidi ya watu sita.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika watu sita, tuka- mention relevant Ministries ambazo tunafikiri zitatengeneza hii Board Composition kwenye kusimamia hii Council. Pia tuka-mention Wizara ya Maji, Ardhi, Energy, Irrigation, Agriculture and Local Government. Katika hawa watu sita, ukiangalia hizi Wizara hapa, tunapata watu watano, lakini hii nafasi moja tumeacha kwenye discretion power ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri pengine ni vizuri Wizara ikajaribu kuangalia au ku-consider technical personell ambaye ana specified background ya finance au accounting management.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu ukiangalia kwenye majukumu haya ya hii Bodi, utaona pale kwenye page eight Section (c), tunasema kwamba pamoja na majukumu mengine hii Council itakuwa na majukumu ya: “to establish guidelines for financial and technical assistance and development of projects and programs.” Pia ukienda
(d) tunasema kwamba, pamoja na majukumu mengine, hii Council itakuwa na majukumu ya ku-approve the budget of the Commission by the joint Steering Committee and such blah blah blahs.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, concern yangu, nafikiri ni vyema kwa kuwa tume- consider Deputy Ministers ndio ambao watatengeneza hii Council, kwenye nafasi za watu sita tume consider Deputy Minister’s watano. Ni concern yangu kwamba pengine either tu-consider na Deputy Minister from the Ministry of Finance ama tuwe specified tuseme kabisa tutahitaji kuwa na technical personnel mwenye specified background in financing or accounting. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hivyo, nikija page nine, kwenye the Committee; uundwaji wa hiyo committee, ukisoma pale Section One inasema kwamba hiyo Committee itaundwa na Wajumbe watano, lakini hatujaona background of the relevant Ministries ambao wataunda hii Committee kama ambavyo ilikuwa kwenye Council.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni ushauri wangu pia tuseme hawa members wana background gani; au watatoka kwenye Bodi gani; au ni Ministries gani? Tusiache tu hivyo ina-hang. Kismsingi naona kama vile tunahitaji kuongeza kitu hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukija pale the Chairmanship of the Committee, tumesema kwamba huyu Chairman atakuwa anaishi kwenye nafasi yake kwa muda wa mwaka mmoja na itakuwa ina-rotate, lakini pia nikawa nahoji ni vyema basi tungeona the life span au project duration kwa maana kwamba mimi ningeweza kusema mbona one year haitoshi? Sasa napata shida kwa sababu hata sijui life span ya hii project, yaani the Shared Watercourse Projects. Kwa hiyo, ni vyema basi tukaona kabisa hii project ni ya muda gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kimsingi naona hivyo, kwa sababu naweza nikasema kwamba mwaka mmoja hautoshi au nikashindwa kupata relevance ya mwaka mmoja kwa sababu kimsingi sijui hata life span ya hii project. Kwa hiyo, concern yangu kwenye section hiyo ilikuwa ni hiyo niliyoi-mention.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nikienda section 12 kwenye Sekretariet, tunasema pamoja na Bodi itakayoteuliwa; appointing authority of cource imekuwa mentioned, lakini pia tukasema itakuwa headed na Executive Secretary pia itakuwa assisted na Deputy Executive Secretary lakini who are the body? Hatujaona bado hii bodi ni akina nani? Wako wangapi? Wanatoka wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukiangalia functions, it means zinatakiwa ziwe performed na a certain number of people, lakini siyo tu Executive Secretary au Deputy Secretary. Kwa hiyo, kimsingi naona tuna haja kabisa ya kusema idadi ya Board Members, ikibidi pia na background zao, lakini siyo tu kusema kwamba itakuwa headed na nani kwa sababu tayari tuna duties and responsibilities to be performed by a certain number of people.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimejaribu kwenda kwa haraka haraka page number 15, kuhusu dispute resolution. Ukiangalia kwenye hii dispute resolution, the way imekuwa drawn, hutaona who is the specified body to deal with the disputes or misunderstandings. Nadhani ingekuwa ni muhimu kabisa na itakuwa na tija kama tutaweka the governing board ya kuweza ku-overseas disputes au misunderstandings.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka mpaka Ziwa Malawi, ile misunderstanding ambayo tuliyokuwa nayo, nafikiri ni fundisho tosha. Kwa hiyo, kimsingi napenda kabla ya ku-question kwa nini SADC Tribunal iwe ndiyo Appellate Board lakini pia ni muhimu tukaona kwamba kunakuwa na governing board ya ku-overseas any dispute that may arise during the execution of this project.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukisoma hii document inakwambia host country ni Tanzania na Makao Makuu yatakuwa Mbeya kule Songwe. Sasa kama host country ni Tanzania, kwa nini Appellate Board inabaki kuwa SADC Tribunal? Kimsingi niki-refer hata kuna Mjumbe mmoja ameongea humu ndani, lakini siangalii kwake, naangalia kama nilivyoelewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipitisha hapa juzi Miswada ya kuweza ku-govern our natural resources, ile Permanent Sovereignty Act ambayo tulijikita na tukasema kabisa kwamba any dispute or misunderstands zitakuwa dealt within the country. Kimsingi ukiangalia hii document na ukiangalia vitu ambavyo tumepitisha Miswada na Sheria ambazo tumepitisha nadhani hapa kunaleta ukakasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba naunga mkono hoja asilimia mia, mawasilisho yaliyoletwa na Wizara husika katika muktadha mzima wa kuijenga Tanzania yenye uchumi wa kati, lakini pia ni subject to minor corrections where necessary. Ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kufidia muda wangu ambao nilipoteza kwa siku ya Ijumaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda leo niongee na wanawake wenzangu wa Bunge lako. Sisi Wabunge bila kujali itikadi zetu za vyama tunakutana kwenye jukwaa moja la Kibunge la Wanawake. Jukwaa hili linaitwa TWPG yaani Tanzania Women Parliamentary Group. Pia katika jukwaa hili tunakutana kwenye agenda moja kwa kawaida katika kila mwaka tunakuwa na ajenda kama wanawake. Nitawakumbusha wanawake wenzangu ambao mmefika hapa pengine naona wengi wetu sasa tunakata network, tumejitoa kwenye agenda hatujui hata tunachokifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2015 tulikuwa na ajenda kama wanawake wa Tanzania iliyokuwa inasema Orange the World nadhani Mheshimiwa Susan unasikiliza. Siyo hivyo tu, tukasema kwamba agenda hii haijagusa a real context ya Tanzania, tukasema kwamba tubadilishe ajenda. This year ninapoongea kwamba mwaka huu unaoishia tarehe 30 Juni, sisi kama wanawake tumebeba ajenda moja inayosema rudisha rasilimali ya mwananchi kwa wananchi. Uhuru wa uchumi uwasaidie wanawake na wanaume walioko pembezoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, anachokifanya leo Mheshimiwa Rais ninajiuliza ni nani aliyetutoa kwenye ajenda ya kurudisha rasilimali ya nchi hii kwa wananchi kama siyo sisi wenyewe tumefika mahali hatujielewi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamekuja hapa ndugu zangu, wameshindwa kukaa na kuangalia, katika nchi ya Tanzania tunazo changamoto nyingi, lakini leo tunakuja hapa tunatoa mustakabali mzima, tunachangia hotuba yetu hii ya Wizara ya Fedha, wenzetu hawa wanakuja na ngonjera mia, 1000 ambazo zinatutoa kwenye ulingo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwaambie hawa ndugu zangu, hivi mnatambua kwamba, mpaka Machi 2017 tuna changamoto kubwa ya bajeti ndogo ya Fungu la Maendeleo kwenye Wizara ya Maji? Mnafahamu tuna asilimia
19.8 tu zilizokwenda? Mnafika hapa mnakuja kutuambia Mheshimiwa Rais ameita wezi Ikulu! Ngoja niwaulize ninyi wanawake, hivi najiuliza na mimi ndio na mimi nipo, najiuliza na mimi ni mwanamke ndio, kwa sababu wamesimama hapa watu wanakuja kusema kwamba Mheshimiwa Rais ameita wezi Ikulu! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi Canadian Embassy kama Mheshimiwa Rais ataanza kualika watu Ikulu, Canadian Embassy watafanya kazi gani? Basi tufute hii Embassy ya Canada tuifute, lakini sio hivyo tu, ninaongea na sisi wanawake na mimi nipo katika hilo ninaloliongelea hapa, lakini kama sio hivyo mkaja mkatuambia kwamba tukaombe msamaha! Jamani ngoja niwaambieni, msamaha wa kweli ni msamaha ambao utaambatana na vitendo katika kupeleka tumaini la kweli kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Rais anachokifanya ni kupeleka tumaini la kweli kwa wananchi na kama msamaha ungekuwa ni jibu, leo mimi ninakaa pale Dar es Salaam niko Tegeta, ninatarajia ningemuona Mheshimiwa Halima yuko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alikuja hapa akatoa kauli nisameheeni, baada ya kuambiwa mpaka na maaskofu, kuambiwa na mapadri kaombe msamaha, akaja akaomba msamaha. Yuko wapi kama kauli ya msamaha ndio jibu? Sio jibu, ni dhamira ya dhati katika kupeleka tumaini la kweli kwa wananchi. Mheshimiwa Rais ana dhamira ya dhati katika kupeleka tumaini la kweli kwa wananchi. Tumpe nafasi, hii nafasi ni ya Chama cha Mapinduzi, hii Serikali ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi, tunaongozwa na manifesto, tupeni nafasi tufanye kazi katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na haya ninayoyaongea ninapenda tu niwaambie wanawake wenzangu, hebu tusimame katika nafasi zetu. Hebu tuache ngonjera nyingi humu ndani, hazina mantiki, hazitusaidii, tuna mengi. Ukienda kule Jimboni ukamwambie mwanamke nilienda kutafuta gold ni nani aliipiga au nilienda kutafuta, nilienda nikatetea ajenda hii ilikuwa ya UKAWA au ajenda hii ilikuwa ya CCM! Hivi kwa nini tuna haja gani sisi kutoka kwenye ajenda yetu kama wanawake? Tuna kauli moja tu, rudisha uchumi wa Tanzania ukamsaidie mwanamke aliyeko pembezoni, hii ndio ajenda yetu, hiki ndicho tulichotumwa tuje kufanya katika Bunge lako hili Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa kuchangia hotuba hii ya Mheshimiwa Mpango. Naomba niguse suala la kilimo. Ni kweli ninapenda sana niipongeze sana Wizara yako, Mheshimiwa Waziri kwamba kwa mara ya kwanza Serikali hii imejitahidi katika kumtua mkulima mizigo mizito aliyonayo. Nimeona kwamba kuna produce cess ambazo mmetoa VAT kwenye masuala ya kilimo cha biashara, lakini pia kilimo cha chakula. Sio hivyo tu, nimeona mmetoa msamaha wa kodi hata kwenye capital goods ili kuweza kuhamasisha na kuboresha viwanda vyetu nchini vinavyozalisha ngozi, mafuta na dawa za binadamu, hii ni hatua nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio hivyo tu, mlitoa kodi 108 katika Bunge hili, kodi 108 kwa mwaka mmoja. Lakini sio kodi 108 za mazao, pia mliweza kutoa kodi kwenye tani moja ya vyakula zinazotozwa na Halmashauri za Wilaya. Siyo hivyo tu mmeleta bulk procurement system katika kupeleka pembejeo kwa wakulima wetu, hizi ni hatua nzuri sana. Lakini Mheshimiwa Waziri bado tuna changamoto kubwa, nimetafuta sana miundombinu ya maji ya umwagiliaji mmeiweka wapi? Nimeenda kwenye Wizara ya Maji sikuona, nimeenda kwenye Wizara ya Kilimo sikuona, fungu hili liko wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri tunayo changamoto wewe ni shahidi, kwenye hali ya uchumi wa Tanzania mwaka 2015/2016 umeandika wewe mwenyewe kwa maandishi kwamba, bajeti ya Kilimo, Fungu la Maendeleo Vote 43 ilienda asilimia tatu tu, hii ni changamoto kwetu. Mheshimiwa Waziri siyo hivyo tu, kilimo kimechangia asilimia moja kwenye Pato la Taifa, hii ni changamoto ambayo hatuna majibu. Mheshimiwa Waziri ni lazima tuweze kufahamu ili tuweze kupata malighafi za kulisha viwanda vyetu ni lazima Tume ya Mipango ya Taifa isimame katika nafasi yake na iweze kutoa ushauri maridhawa katika kuongoza Taifa lako hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na masuala ya kilimo mimi ninafikiri nasi wanawake wenzetu tufahamu kwamba, ipo haja ya kusemea kwa sababu, mwanamke wa Taifa hili anazalisha kiwango cha …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
HE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuwa mchangiaji wa mwisho kwenye Kikao hiki cha Bunge. Ninapenda sana kumpongeza Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana pamoja na Naibu Waziri, hakika mmetutoa kimasomaso, hakika mmejibu kiu ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya yanayotendeka, kwa sakata zima la makinikia, Mkoa wa Kilimanjaro umeniagiza kwenye Bunge lako hili Tukufu kwamba, wao wamesimama na Mheshimiwa Rais kwa sababu nao ni wahanga hata kupitia machimbo ya Tanzanite. Kwa hiyo, wamenituma niseme kwenye Bunge lako hili Tukufu, ikitokea leo Mheshimiwa Rais anaomba kwenda Mkoa wa Kilimanjaro watahitaji miezi sita waweze kupanua ule uwanja uliompokea juzi kwenye Mei Mosi ili waweze kukaanae na kumpa hongera hizi. Kwa kweli Mheshimiwa Rais popote ulipo pokea pongezi za dhati kutoka kwa Mkoa wangu wa Kilimanjaro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasita leo kujiuliza maswali mengi, nimemuangalia kaka yangu Mheshimiwa Januari Makamba simuoni! Nilitaka nimuulize neno moja, hivi huu sio ule utabiri wa Mzee Makamba tulipokuwa pale kwenye ule Mkutano Mkuu ambapo walisema alisema huyu ajaye atatubatiza kwa moto, hivi huu sio moto? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu, imefika tunaongea hata tusiyoyajua. Network zimekata, connection hakuna, links hakuna chochote kinachoendelea katika Bunge hili. Wamekuja watu hapa wanatuambia kwamba makinikia ni suala la mtaani, limeletwa hapa kuja kutufunga midomo, kuja kuchafua Bunge, wapi na wapi?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu pale, namheshimu sana Mheshimiwa Ally Saleh, tuko kikao kimoja kule SADC, michango yako naiheshimu sana, lakini kwa kweli leo umenifanya pengine hata nitakosa usingizi juu ya mchango wako juu ya leo. Mbona ilipaswa mpaka tunapokuja kuchangia tuwe tumesoma ripoti ya Profesa Mruma, lakini pia na ripoti ya Profesa Osoro, kwani hatufahamu…

TAARIFA ....

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sioni tofauti ya kutugawa na migongano ya kifikra na kimaslahi. Ripoti imeeleza bayana tunapoteza shilingi trilioni tisa kwa mwaka mmoja kwa miaka 17, tumepoteza shilingi trilioni 108. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaotambua uchungu wa wavuja jasho wa Taifa hili lazima tulisemee hapa. Kuna direct link, tunaona mahusiano ya moja kwa moja kwenye upotevu huu wa pesa pamoja na michango yetu katika Bunge lako hili Tukufu hususan kwa kupitia Wizara hii, Wizara hii na bajeti ya fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sio hivyo tu, kama sio huu ubatizo wa moto, ninashangaa wengine wanasema hapa sisi tumekuja kuimba nyimbo za mashetani! Ngoja nikuulize rafiki yangu kijana wewe unayejiita kijana wa Dodoma hii, sikiliza, sisi hatuimbi nyimbo za mashetani, ndugu yangu tunaimba za kucheza Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Ninyi mlikaa kwenye Ilani yenu, mlihubiri kufufua wafu, akina Balali mlituambia mnataka kumfufua Balali, ni nani anayeimba nyimbo za mashetani humu ndani? Ni nani anayeongea lugha za kufufua mashetani humu ndani kama sio wao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio hivyo tu, wamejitahidi sana kutuvunja mioyo humu ndani. Walikuja wakatwambia kwamba, tutaenda kushtakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kuchangia mchango wangu mdogo kulingana na uwasilishwaji wa Taarifa ya Kamati ya Sheria Ndogo, lakini pia na uwasilishwaji wa Kamati ya Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaenda mbali napenda kuipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya uongozi wa Mheshimiwa Jenista Mhagama pamoja na Mheshimiwa Mavunde kwa kazi yao nzuri ya kuweza kufanya majukumu yao yakawa na tija hata kwa sisi Wanakamati wa Sheria Ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wajumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo tulikuwa na malalamiko mengi ya muda mrefu. Na malalamiko yetu yalikuwa ni Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina furaha ya pekee kusimama katika Bunge lako hili Tukufu kutoa pongezi za dhati kwa Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kweli wameutendea haki mhimili huu wa sheria. Ninaomba jambo moja lifanyike. Ni dhahiri kwamba tumempata Mpiga Chapa wa Serikali ambaye anakaimu kwa nafasi yake, Bwana Kaswalala. Bwana Kaswalala amefanya mambo mengi, ameleta reforms nyingi, ametengeneza retantion strategies, lakini ameleta mabadiliko kwa muda mfupi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bwana Kaswalala mpaka leo anakaimu. Hata hivyo pamoja na suala hili la kukaimu ambalo tumeona kimantiki halileti tija kwa mtu ambaye tunamuona ana uwezo katika nafasi hii tukashindwa kum- confirm. Kwa hiyo, ni ombi langu kwa Wizara hii, ni ombi langu kwa Ofisi hii tuweze kum-confirm Bwana Kaswalala kwa sababu ukiangalia Sheria za Utumishi wa Umma provision ni three months tofauti na hapo mtu ame-qualify tunampa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala zima la mitambo mibovu kwa Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali. Tukipata mitambo imara ndio namna pekee ya kuweza kutunza siri na kuhifadi nyaraka za Serikali. Tunaiomba ofisi husika iweze kumsaidia Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ili aweze kujikimu kupitia mitambo ya kisasa na aweze kufanya kazi ambayo sisi tunamuagiza kama Bunge Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo masuala ambayo mimi ninapenda niyaongelee. Kuna suala la ucheleweshwaji wa utungaji wa sheria ndogo. Juzi Mheshimiwa Kemilembe wakati ana-wind up report yake, lakini pia hata leo nafikiri nimemsikia Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mazingira, ali-cite Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi linanisikitisha sana. Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009 mpaka leo hatuna kanuni ndogo zinazoongelea ushoroba. Ninapoongelea kutokuwepo kwa kanuni ndogo tayari ni mzigo mkubwa kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitoe takwimu zifuatazo, kutokuwepo kwa utungaji wa Sheria hii Ndogo ya Masuala ya Ushoroba imeleta madhara yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka wa jana mwezi wa kwanza mpaka mwaka huu tumekuwa na vifo vya Watanzania 484 kwa nchi ya Tanzania, lakini pia tumekuwa na hasara hekta 42,000 kwa nchi ya Tanzania ambayo inaitaka Wizara ilipe fidia ya shilingi bilioni moja kwa madhaifu haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi sote ni Wabunge, tukiwa Bungeni hapa tulisikia tembo wamekatisha, anapita anaenda UDOM. Ninajiuliza tunahitaji nini? Je, tembo hawa waingie hapa ndani ndipo tujue madhara yanayotokana na sheria hii? Inasikitisha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoongelea ucheleweshaji wa utungaji wa sheria hii, mamlaka inayohusika na masuala mazima mipango miji imeshindwa kuzingatia taratibu na hatimaye hizi corridor za wanyama zimekuwa zikitumika na kubalishwa matumizi, na hata leo hii tunakuwa na majengo makubwa.

Mimi ninaomba serikali tujifunze kwenye ujenzi wa Jengo la TANESCO. Tumejenga kwa billions of money, pesa za Watanzania baada ya siku mbili tunashusha ghorofa.Tujifunze kwenye hili ni lazima tuweze kutunga sheria hizi ili tuweze kuondokana na mizigo isiyo ya lazima kwa serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitapenda niongelee suala zima la ushiriki wa wanakamati kwenye masuala ya kuisimamia serikali yetu. Ukisoma Ibara ya 63(2) inasema; “Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kusimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaombe kwa masikitiko makubwa, Kamati yangu ikiwa tulipata safari ndefu tukasafiri kwa muda mrefu nafikiri ilikuwa safari haikuzidi dakika kumi kwa sababu tulikoka jengo la Bunge hapa tukaenda pale Sabasaba nakumbuka…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimia Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa na ninaomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, na mimi niweze kuchangia kwenye Bunge lako hili tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kuwapongeza Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana pamoja na Naibu wake, Mheshimiwa William Tate Olenasha, kimsingi mnafanya kazi nzuri. Niwape moyo, hakuna kazi ambayo mtaifanya mithili ya malaika, sisi ni binadamu kazi yetu ni kukosoa, lakini msife moyo kazi mnaifanya na sisi tunaiona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, alichangia ndugu yangu Mheshimiwa Catherine Ruge, nadhani hayupo, nilipenda angekuwepo naye anisikilize. Alikuita Madam Professor sioni statistics usiogope! Mheshimiwa Waziri unakumbuka niliposimama hapa nililia na wewe nikakuomba hostels za wanafunzi umetupa. Tulikulilia kuhusu Mloganzila umetupa, Mheshimiwa Oscar amekiri pale alikuomba nyumba za Walimu wake umempa. Mheshimiwa Waziri tunataka vitu tangible chini ya Wizara yako, vitu ambavyo tutaviona, hatutadai statistics, tutakudai Ilani ya Chama cha Mapinduzi ilielekeza nini na wewe unafanya nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ninakupa hongera, isitoshe ninakushukuru sana kwa kuwa tayari katika kui-support Uni Life Campus Program na kwa hakika tumeona utayari wako katika kutengeneza Taifa linalojiheshimu na taifa ambalo lina uwezo wa kushindana kwenye soko la ajira. Mheshimiwa Waziri pokea pongezi zangu za dhati kutoka kwa wanafunzi wote Vyuo Vikuu nchi nzima. Uni Life Campus Program inazunguka nchi nzima na hii ni feedback ya wanafunzi wao, ni feedback ya walimu, ninakupa pongezi, endeleeni. (Makofi)

Mheshimwa Mwenyekiti, ninasimama kuchangia kuhusu Mfuko wa Bodi ya Mikopo. Nina machache sana ya kuongea katika hili na nitaongea hapo tu sitataka kwenda mahali pengine. Mheshimiwa Waziri, pamoja na pongezi ambazo hata ndugu yangu Mheshimiwa Oscar amezitoa, ni kweli, tumeona mafanikio mazuri sana. Tunapoongelea Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, tumeona kumekuwa na ongezeko kubwa la wafaidikaji wa Bodi ya Mkopo. Utakumbuka miaka kumi, ninapoongelea hivi ninamaanisha mwaka 2005 mpaka mwaka 2015, tumekuwa na wafaidika 390,922 lakini kwa miaka miwili tu 2015 mpaka 2017, tumekuwa na wafaidika wapya 113,922.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hii ni pongezi ambayo haipaswi kubezwa, sisi tuliokuwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi, tuliokuwa na party manifesto mikononi mwetu tunasema hii ndiyo kazi ambayo tulipewa dhamana na wananchi wetu na sisi tukaitekeleza bila hofu. Makelele haya yasiwatishe, tuna mengi ya kujibu tunapofika mwaka 2020. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, tumeona masuala mazima ya urejeshwaji wa mikopo Bodi ya Mikopo, tumeona kuna hatua kubwa imepigwa. Tunapoongelea katika miaka kumi iliyopita, urejeshwaji wa Bodi ya Mikopo tofauti na alivyokuja Badru, tuliweza kukusanya shilingi bilioni 101 katika miaka kumi, lakini katika miaka miwili tu 2015 hadi 2017, chini ya uongozi wa Ndugu Badru, tumeweza kukusanya shilingi bilioni 285. Kwa kweli Mheshimiwa Waziri hizi ni pongezi zetu kwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kwa sababu sisi ndiyo wenye Ilani na tunajua kwenye ilani kuna nini.

Endelea na kazi hii kwa sababu huu ni utume wa kanisa na sisi tuna imani na wewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na haya, tunasema kabisa ukiangalia kwenye ripoti ya CAG na ripoti ya Bodi ya Mikopo tunapoongelea katika mwaka 2005 toka uanzishwaji wa Bodi ya Mikopo mpaka muda huu tuliosimama hapa pesa ambayo ilipaswa kuiva na kurejeshwa ilikuwa shilingi bilioni 585 lakini katika pesa hizi, shilingi bilioni 235 bado hazijaweza kurejeshwa. Pamoja na ukusanyaji mzuri lakini zipo pesa ambazo imeshindikana kurejeshwa lakini explanation tofauti na explanation ya CAG Bodi ya ya Mikopo inasema hawa ni pamoja na wanafunzi ambao wako kwenye grace period ya miezi 24.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnakumbuka hata Wabunge tulipitisha Miscellaneous Amendment ya kutaka asilimia 15 kutoka kwenye asilimia nane, hapa kuna kitu ambacho inabidi tukiangalie, something is alarming. Kwa sababu mwisho wa siku lazima tuone mfuko huu unaweza kujiendesha na ukisoma ripoti ya CAG ziko pesa nyingi hazijaweza kurejeshwa. Sasa tunatoa wapi, vyanzo ni vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nasema something is alarming kwa sababu sioni nguvu ya Serikali ilipojikita katika kuona kwamba vijana hawa wanaajirika kwa wakati. Mheshimiwa Waziri mwaka jana 2017 ukiangalia ikama ya Serikali tulisema tutaajiri vijana 52,000 lakini sad enough tumeweza kuajiri vijana 16,800 sawa na asilimia 32, Mheshimiwa Waziri tunakwenda wapi? Je, tulitengeza ile Paralegals Act katika kuja kutoa hukumu isiyo kuwa na hatia kwa vijana wetu. Mwisho wa siku hawa watapaswa kurejesha pesa hizi, watazitoa wapi endapo Serikali yetu inashindwa kujipanga katika kuandaa ajira kwa vijana wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ninapoongea suala hili hapa katika Wizara hii ya Elimu utakubaliana na mimi tuna graduates zaidi ya laki sita kwa mwaka, lakini it is less than ten percent wanaingia kwenye ajira rasmi za Serikali. Mheshimiwa Waziri inabidi tukaze buti kuona kwamba vijana wetu tunawaandalia mazingira makini ya wao kuweza kuajirika na kuweza kuona kwamba bodi hii inajiendesha kwa fedha hii kuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ukiangalia page ya 15 ripoti ya Waziri Mkuu alisema kwamba ametoa shilingi milioni 783 kwa vijana 840 sawa na asilimia 0.105. Mheshimiwa Waziri sioni mwelekeo kidogo ninapata giza hapa ukiangalia vijana wanaomaliza, wanao graduate na vijana wanaoingia kwenye soko la ajira hata kwa kujiajiri bado hai-reflect nguvu yetu, hai-reflect majibu ambayo tunapaswa kutoa kama wabeba ajenda na kama wabeba Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoongea suala la VETA ambalo hata dada yangu Mheshimiwa Janet Mbene ameliongelea, VETA is almost dying, Mheshimiwa Waziri ni vema ukaangalia. Ripoti ya CAG page 138 inaonesha kabisa kuna matatizo pale, VETA haijulikani ni regulator, haijulikani ni key player! Anatuambia kabisa ukisoma page ya 138 kwenye chuo kimoja ambacho kilikuwa sampled hapa Dodoma unaambiwa uwiano wa wanafunzi ni moja kwa kwa113, mwalimu mmoja wanafunzi 113! Mheshimiwa Waziri ubora wa elimu unatoka wapi hapa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajiandaa kuingia kwenye Tanzania ya viwanda tunaongea nini katika takwimu hizi. Licha ya hivyo utaangalia kwenye moja ya mipango ya Ofisi ya Waziri Mkuu tumesema tuna programu ya uanagenzi kwa nini programu hii ya uanagenzi katika mwaka huu wa fedha 2018 tumesema wafaidika watakwenda kuwa 10,500. Kwa nini programu hii nguvu kazi ya Taifa inayoelekezwa katika programu hizi tena kwa kupeleka vijana wetu kwenye vyuo holela vya mtaani, mathalani Don Bosco siwezi kuita holela sijui! Hatujui mitaala yake mnapeleka vijana kule kwenda kujifunza kuandaa na Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Waziri atakapokuja kuhitimisha mada yake atuambie amejiandaaje kutumia fursa hizi katika kuona kwamba Bodi ya Mikopo inajiendesha, vijana wanaingia kazini akija hapa atuambie nini mipango yake kama Wizara, nini mipango yake kama Waziri mwenye dhamana katika kuona kwamba bodi hii inaweza kujikimu kutokana na fedha ambazo zinatoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko mipango mingi ukiangalia Ofisi ya Waziri Mkuu pia kuna hela nyingi zimewekwa bilioni 15 katika kusaidia vijana waingine kwenye kilimo, umejiandaaje Mama Ndalichako, umejiandaaje Bodi ya Mikopo ili vijana hawa waweze kurudisha pesa? Hizi ni fursa umejipangaje. Ukienda kwenye private sector ambazo tunategemea vijana wengi wanaweza kuajiriwa tazama TBL ni almost imefungwa, wamebaki gate keepers wamebaki, wamebaki watu wachache sana pale, vijana wetu wamekosa ajira TBL, angalia payroll ya TBL inafanyikia Mauritius, kule wana enjoy tax…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Kumi na Moja wa Bunge
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia kwenye Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kwamba wengi wetu sisi Wabunge hapa ndani tuna mikataba na wananchi waliotutuma tuje tuwawakilishe katika Bunge lako tukufu. Ipo mikataba tuliyoingia kuna psychological contracts watu wana matarajio na sisi lakini haya yote yatatimilika pale ambapo siyo tu kwa kupitisha bajeti ya Serikali, lakini ni pamoja na kuangalia masharti hasi yanayotokana na sheria mbovu katika nchi hii ambayo yanaruhusu mianya mikubwa ya upotevu mkubwa wa fedha katika Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye muktadha wa wasilisho la Sheria Ndogo hasa nikijikita kwenye dhana nzima ya local content policy. Ninaomba nichangie kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikichukulia mfano wa Kampuni ya PUMA ambapo Serikali ina hisa asilimia 50 na wawekezaji wana hisa asilimia 50. PUMA kwa muktadha wa sheria hasi na sheria zenye vigezo vigumu visivyotekelezeka ni dhahiri kwamba PUMA anaenda kupoteza kiasi kikubwa cha mapato yake. Kwa sheria iliyopo ambayo ni sheria hasi, PUMA anapoteza lita 2,500,000 kwa mwezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu tukiangalia nafasi ya PUMA au umuhimu wa PUMA katika ujenzi wa uchumi wa taifa hili; juzi tu hapa nikiwa pamoja na Kamati ya PIC tunaona PUMA alitoa shilingi bilioni tisa gawio la Serikali. Ni dhahiri kwamba hatutasimama katika kuona kwamba sheria hizi zinafanyiwa marekebisho ya haraka ni dhahiri hata hili gawio pengine tunaweza tukalipoteza kwa siku zijazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muktadha wa sheria hii ninaomba nieleze Bunge lako hili tukufu kwamba Shirika la TIPER ambalo Serikali ina asilimia 50. Tukija SINOTASHIP ambao ni Wakala wa Meli Tanzania kupitia ushirika wa Uchina na Tanzania itapoteza kazi kubwa nchini Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu, ninapoongelea Benki ya NBC ambayo Serikali ina hisa asilimia 30; lakini ukija NMB ambapo Serikali ina hisa asilimia 31 ni dhahiri Serikali ama nchi kwa ujumla wake tutashindwa ku-realise faida ya kuwa na uwekezaji wa aina hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hitaji la local content policy inaongea pale siyo tu kwamba kampuni ya kizawa iwe na asilimia 51 ya uwekezaji, lakini pia kuna takwa la kisheria kuhusu rasilimali watu kwamba katika mfumo huu wa local content policy, asilimia 80 ya top management ni lazima wawe wazawa wa Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na Dkt. Mpango ni shahidi juzi nilimuona, lakini siyo hivyo katika mazungumzo yangu na Dkt. Mpango nikimuelezea dira na mwelekeo wa makao makuu ya nchi hapa Dodoma niliweza kumtahadharisha nikamwambia kwamba Mheshimiwa Dkt. Mpango hapa tunapoongea wapo baadhi ya Mabalozi ambao hawajajua hata ofisi wataijenga wapi Dodoma hapa, lakini tayari wameanza ku-grab ardhi na kupita kwenye Halmashauri zetu kutafuta resources za kuweza ku-grab.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hatutakuwa na mpango madhubuti wa kuweza kulinda wazawa wetu katika Taifa hili ili waweze kushiriki kupitia mpango huu wa local content policy kwenye lile takwa la kisheria la asilimia 80 ni dhahiri tutaenda bado kutokuwa na majibu sahihi hasa tunapoongelea ukuaji mkubwa wa ukosefu wa ajira nchini Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuongea na Mheshimiwa Mpango, lakini pia niliongea na Mstahiki Meya na yeye pia alikiri kwamba ni muhimu sana tukawa na sheria nzuri zenye tija ambazo zitaweza kumlinda mzawa wa Taifa hili ili na yeye aweze kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzangu wote wameongea na kimsingi wote tunaona umuhimu wa Serikali kufanya mapitio ya haraka ya sheria hii. Kama tuliweza kuleta masuala mengi kwa hati ya dharura na hili hata ikibidi liende nje ya utaratibu lije kwa haraka. Hii ni kwa sababu Ofisi ya TR ina malalamiko makubwa, ina mzigo wa mashirika mengi ya Serikali yasiyokuwa na tija katika Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na unyenyekevu ninaomba sasa nimalizie kwa kuomba kwamba Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Wizara husika iweze kutendea haki suala hili ambalo Wabunge wengi wamechangia na kuguswa kwa aina yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Pia naungana na wenzangu wote ambao wamepongeza Kamati zote hizi tatu kwa kazi zao nzuri lakini pia na kwa ripoti ambazo ziko well informed.

Mheshimiwa Spika, nitapenda kujielekeza kwenye Kamati ya Huduma za Jamii na nitajikita kama kawaida kwenye masuala mazima ya uboreshaji wa elimu ama mfumo wa elimu ambao tunao. Ni dhahiri kwamba kumekuwa na jitihada mbalimbali katika kuinua fursa za elimu kwa watoto wetu. Jitihada hizi zinaonekana pale ambapo tunaona migomo mingi imepungua au imefutika katika elimu za juu lakini pia kero nyingi ambazo walikuwa nazo wazazi mathalani masuala ya ulipaji ada kwa elimu ya awali yameondoka. Watu wengi tumetoa pongezi hizi kwa Mheshimiwa Rais hasa tukitambua mchango wa Serikali unaoongozwa na Mawaziri wake na Naibu Waziri tunawapongezeni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika nchi mbalimbali duniani kote lakini pia katika ulimwengu wa kwanza elimu inatumika kama nyenzo kuu katika kukuza uchumi na kupelekea maendeleo ya dhati kwa Taifa husika. Misingi hii ya ujenzi wa uchumi ni dhahiri kwamba katika nchi mbalimbali haifanani.

Mheshimiwa Spika, kwa nchi ya Tanzania uchumi wa sasa tunavyouangalia, tunajitahidi kuwekeza hata katika miundombinu ya elimu, tunajikita hasa kwenye ku-promote uchumi wa viwanda (Industry Economy), lakini pia katika Mataifa yaliyoendelea, wamehama katika mfumo huu wa kusukuma uchumi kupitia Industry Economy kwenda kwenye knowledge economy. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Safi sana.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, tunapoongelea knowledge economy tunaangalia nchi ya Tanzania inavyowekeza nguvu nyingi katika kuinua uchumi mathalan ujenzi wa Stiegler’s Gorge, uwekezaji wa anga na uwekezaji kwenye Bahari Kuu, uwekezaji wa utalii na masuala mengineyo, bado tunaona kuna kila sababu kwa nchi ya Tanzania kuona umuhimu wa promote au ku- embrace knowledge economy kwa maana ya kwamba elimu au mfumo wa elimu uinue zaidi masuala ya ujuzi na maarifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu bila kuoanisha muktadha huu vizuri ni dhahiri kwamba hata nguvu zinazowekezwa na Serikali zitakosa mapokeo chanya kwa vijana ambao wanaandaliwa kwa mifumo ya elimu ambayo tuko nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, inasikitisha sana kwamba kupitia ilani bado tuna maswali mengi ya kujibu kwenye masuala ya ajira. Ninapoongelea knowledge economy ni dhahiri kwamba vijana wetu watashiriki rasmi kwenye kuandaa ajira zao wenyewe, watatoka kwenye kusimama kwenye nafasi ya utazamaji na badala yake wataingia na kuwa key players katika kuandaa ajira zao wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoongelea uchumi unaojengwa na maarifa pamoja na ujuzi, ni kwamba vijana wetu kama nilivyosema wanaweza wakajiandalia ajira zao. Ukiangalia sasa na niliwahi kusoma kitabu cha Henry Mintzberg ambaye aliandika kitabu kimoja kizuri sana MBA’s But Not Managers inaeleza vizuri masuala haya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nimetoka Kilimanjaro na dada yangu Mheshimiwa Stella Ikupa ni shahidi, tulikwenda Kilimanjaro na maelekezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu tukitaka kuwatengenezea ajira vijana wetu; na kwa Mkoa wa Kilimanjaro tulipata fursa za kuwatengenezea ajira vijana 800 kila Wilaya. Tulikuwa tumepanga kuboresha ajira za vijana kupitia kilimo kwa watoto mia moja moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dada Stella ni shahidi, lakini pia tunaye Eng. Kahabi ambaye ndio alikabidhiwa jukumu hili. Nilipita kila Wilaya, nilisikitika, hakuna graduate hata mmoja aliyeweza ku-respond kwenye mradi huo wa Serikali ambao wameweka fedha, wameweka wataalam katika kuwafundisha vijana katika kuingia rasmi kwenye Sekta ya Kilimo. Kilimanjaro tuna fursa nzuri sana ya kimasoko, tumepakana na Kenya, lakini wanafunzi hawajaandaliwa kwenda kuingia kwenye ushindani wa kibiashara, wanafunzi hawajaandaliwa kwenda kuandaa ajira zao au kushiriki kwenye ajira zisizo rasmi.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuongelea changamoto ambazo pia nimezisikia zimeongelewa hapa asubuhi. Tunafahamu kwamba Serikali ilifuta Vyuo 19, nia na makusudi ni kuleta tija katika mfumo wa elimu. Tunaipongeza sana Serikali na tuko pamoja na Serikali katika maamuzi haya. Katika muktadha huu wa kufuta vyuo, lakini bado kuna dosari chache ambazo zimeonekena na ninafikiri ni vizuri Serikali ikaingilia kati na kuona.

Mheshimiwa Spika, imeelezwa kwamba wanafunzi wengi baada ya kuhamishwa kwenye vyuo hivi, unaenda mtu ana-inquire loan status anaambiwa loan not registered. Siyo hivyo tu, wapo wanafunzi kwa Mkoa wangu wa Kilimanjaro ambao walitoka St. Stephano Memorial University ambao walipelekwa Chuo cha Mweka, lakini wengine walipelekwa Masoka na wengine walipelekwa Ushirika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtu anasoma let’s say BBA, lakini anapopelekwa Masoka anaenda kuingizwa kusoma HR akiwa tayari ana background ya miaka miwili amesoma Accounts au amesoma BBA. Akienda Masoka, baada ya miaka miwili kukaa kwenye Chuo kile alichofutwa, anaenda kule anaingizwa kwenye mfumo wa kusoma HR anaitwa ni graduate.

Mheshimiwa Spika, Taifa kwa lililoendelea hatuwezi kujikita kuandaa bomu kwa Taifa hili kwa maana ya kwamba tunaona kuna uwekezaji mkubwa unaofanywa na elimu ya juu kupitia Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote wa Loans Board. Kwa hiyo, nafikiri ni jambo ambalo inabidi liangaliwe vizuri sana.

SPIKA: Mheshimiwa Ester unaweza ukarudia kidogo hicho kitu? Kimefanyika cha namna hiyo?

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, ndiyo. Ninao ushahidi, kuna wanafunzi ambao walitoka St. Stephano Memorial University ambao walipelekwa Mwika na Ushirika. Walikotoka walikuwa wamesajiliwa masomo mengine, walipofika kwenye vile vyuo walivyokuwa dispatched wameenda kulazimika kusoma masomo mengine ambayo walikuwa hawana foundation nayo. Nasema hapa nikiwa na ushahidi wa mwanafunzi ambaye alikuwa anasoma BBA akaenda Mwika akalazimika kusoma HR. Ni Mwika kama sikosei, Ushirika, akalazimika kusoma HR. Nafikiri hapa inabidi pengine Wizara itusaidie.

SPIKA: Subiri kidogo Mheshimiwa Ester, Profesa amesimama.

T A A R I F A

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi nimpatie taarifa Mheshimiwa Ester Mmasi.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa tu nataka kumpa taarifa kwamba, utaratibu ni kwamba mwanafunzi anapohama, anahama na kozi kama alivyo. Kwa hiyo, utaratibu wa mwanafunzi kwenda kubadilisha, hicho ni kitu ambacho, kama anao ushahidi naomba anipatie ili niweze kuufanyia kazi. (Makofi)

SPIKA: Ndiyo maana na mimi nilistuka kidogo, nikamwambia hebu rudia hilo, maana yake ni jipya. Endelea Mheshimiwa Ester.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, nitafuatilia, nitampatia document Mheshimiwa Waziri ili kwa pamoja tuone ni kwa namna gani tunaweza kuboresha haya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siyo hivyo tu, lakini kuna changamoto ya masuala ya Bima ya Afya. Tunaona wanafunzi wanaosoma Vyuo; Private University vis-à-vis public Universities, yaani hivi vyuo vinafsi na vyuo vya Serikali, unakuta ulipaji wa bima hizi unatofautiana. Utakuta kwa mfano mwanafunzi anayesoma kwenye Chuo cha Serikali analipa Sh.50,400/=, lakini wale wanaosoma vyuo binafsi wanalipa shilingi 100,000/=.

Mheshimiwa Spika, napenda Wizara yako ifahamu, masuala haya yanaleta sintofahamu kubwa kwa sababu siyo wote wanaoenda kwenye Private University wako vizuri au wazazi wao wana uwezo wa kuwapeleka na kuhimili maelekezo yote ambayo yanaondoa masuala mazima ya uniformity kwenye muktadha huu.

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri husika au Wizara husika itusaidie kuona hapo tunafanyaje? Kwa sababu kimsingi wanafunzi hawa wanaotoka kwenye background za wazazi wa wakulima, wafugaji na vitu kama hivyo. Kwa hiyo, kuwa kwenye Private University, haimaanishi kwamba mtoto huyo au mzazi huyo alipenda kwenda pale. Wengine tunalazimika kwa kuchangiana kwenye ukoo, kukopa, kuweka rehani vitu mtoto aende kwenye hicho chuo asibaki nyuma. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri na hilo pia atusaidie kuangalia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ipo concern ya uporaji wa mali kupitia taasisi zetu hizi za elimu. Inafahamika na nilishawahi kumwona Mheshimiwa Waziri wa Elimu, lakini pia suala hili limewahi kuletwa na Mheshimiwa Mizengo Pinda, mwaka 2006, vile vile hapa Bungeni liliwasilishwa mwaka 2016 kwamba kuna shule ambayo inaitwa Shule ya Kolila ambayo inatokana na Kijiji cha Old Moshi ambacho kinaitwa Sudan.

Mheshimiwa Mweneyekiti, Shule ya Kolila ni shule ya wazawa na ni shule ya kijiji ambapo Kijiji hicho cha Old Moshi kilikuwa na ekari zake 40. Kijiji kilijitahidi kikajenga madarasa 10, lakini cha kusikitisha katika shule hii, Shule ya Kolila imeingia kwenye mgogoro mkubwa na mvutano mkubwa na dhehebu la Kikristo ambalo sitapenda kulitaja nisije nikaleta migongano huko ya kiimani.

Mheshimiwa Spika, Shule Kolila ni Shule ya Wanakijiji, shule ile ikaja baada ya wanakijiji kukosa nguvu ya kuiendeleza ikakodishwa kwa shirika hilo la taasisi ya kidini. Kinachosikitisha, leo hii shule ile haikuwahi kuendelezwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Ester, muda hauko upande wako.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, nitaomba pia nikabidhi taarifa hizi TAMISEMI na kwa Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia kwa dakika hizi chache ambazo umenipatia. Nina heshima ya pekee kabisa na ninasimama kwa unyenyekevu mkubwa nikiwapongeza Waziri na Naibu Waziri wa Wizara hii husika, lakini pia na kwa taarifa yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitapenda kukita mchango wangu kwenye vipengele viwili. Kama ambavyo imewasilishwa, kuongelewa na kujadiliwa na Wabunge wengi hapa ndani suala la Liganga na Mchuchuma, nami nitapenda nijielekeze huko kwa maslahi mapana ya ajira kwa vijana wetu wa Kitanzania. Pia nataka kuongelea ushiriki wa vijana mathalan graduates wa nchi hii katika muktadha mzima wa masuala ya biashara na ujenzi wa viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa nimesimama nimeshika kitabu kilichoandikwa na Wizara ambayo wamewasilisha hapo mbele. Nitapenda nirejee ukurasa wa 15. Ninaongea haya kwa masikitiko makubwa na sijui; ninaongea kwa sababu kaka yangu Mheshimiwa Kakunda wewe ni Mheshimiwa Waziri ambaye ni mmoja wa wajumbe ambao nimekuwa nikizunguka na ninyi kwenye programu zangu za vijana. Kwa hiyo, unafahamu fika maneno waliyokuwa wanakwambia vijana wale. Nimezunguka na wewe mikoa mingi tu na umeniahidi tutazunguka mikoa mingi ukasikilize changamoto za wanafunzi wa Vyuo Vikuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana mama yangu, Mheshimiwa Ndalichako ambaye ni mlezi wa wazo langu hili pamoja na kaka yangu Mheshimiwa Olenasha, nawashukuruni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ninaongea ikiwa hii ni sauti ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Nikiangalia ukurasa wa 15 pale Section No. 29, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa ninaomba Mheshimiwa Waziri ikibidi ondoa huu utata hapa. Naongea hivi nikiwaomba hata wasaidizi wenu wanisikilize na waamini kwamba Wabunge tunasoma. Waamini hata taarifa zilizotolewa na Mheshimiwa Spika kwamba, hili ni moja ya Bunge mahiri ambalo vijana na Wabunge wote tunajituma katika kusoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitapenda urejee hapa, nawe ni Mwanasheria, utanisaidia na utaniongoza pamoja na Kiti chako hapo mbele. Hapa tunaambiwa moja ya changamoto iliyosababisha mkwamo wa project hii ya Liganga na Mchuchuma ni pamoja na pale ambapo mwekezaji yule alitokea kudai additional incentives, yaani vivutio vya ziada. Hii ilisababisha kukwama kwa mradi huu kwa maana ya kwamba, baada ya kupitishwa na Bunge lako hili Tukufu sheria zile mbili za kulinda na kuhifadhi maliasili ya nchi hii (Natural Wealth Resources Permanent Sovereign Act na Natural Wealth Resources Renegotiation of Unconscionable Terms 2017) ndiyo ilisababisha kukwama kwa mradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninasikitika kusema huu ni uwongo mkubwa na sijui kwa nini tunaandikiana vitu kama hivi, kwa sababu moja. Hapa wanasema, kwenye section 29 kwamba, wakati majadiliano yanaendelea kuhusu vivutio hivyo vya ziada, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupitisha sheria hizi mbili na ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 27 ya Azimio la Umoja wa Mataifa ya sheria hizi mbili, mikataba yote ya nyuma ya aina hiyo, yaani ya Liganga na Mchuchuma pamoja na Liganga, yaani zile sheria mbili za kulinda na kuhifadhi maliasili ya nchi hii zilisababisha kuwa ni sharti la kimkataba kwamba Mradi wa Liganga na Mchuchuma ukapitiwe vipengele vile.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikumbukwe masharti ya sheria zote hizi mbili ni pale ambapo tunaona mikataba hii ilikuwa na masharti hasi. Haikuwahi kuandikwa mahali popote kwamba baada ya kupitisha sheria zile, basi Liganga na Mchuchuma ilitakiwa iende ikapitiwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutapitia Liganga na Mchuchuma kama pale ambapo tumeona kulikuwa na masharti hasi. Pengine upande wa Wizara unafahamu masharti hayo hasi yako wapi, lakini hii sidhani kama ni kweli. Nasema hivi kwa sababu, wanasema pia ati mchakato wa kupitia upya mkataba huo unaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimrudishe Mheshimiwa Waziri na nirejee haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika sheria zile ikumbukwe tunaambiwa katika Part Two, Ibara ya 4(1) inasema, “For effective performance of the oversight and advisory functions stipulated under article 63(2) of the Constitution, The National Assembly may review any arrangement or agreement made by the Government relating to natural resources.”

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye Article 5, ukienda kwenye section 5 ya Sheria ile ya Renegotiation for Unconscionable Terms inasema, “Where the National Assembly consider that certain terms of arrangements and/ or agreement of the natural wealth and resources of the entirely arrangement or agreement of natural resources made before the coming into force of this Act and for the interest of the people of The United Rupublic of Tanzania, the reason of Unconscionable terms it may by resolution advise the Government to initiate renegotiation.”

Mheshimiwa Naibu Spika, yaani inamaanisha hivi, pale ambapo itabainika kuna masharti hasi, ni Bunge hili litapeleka, litapitisha azimio (resolution). Likishapitisha azimio Wizara husika ndani ya siku 30 itaenda kwa mwekezaji na kumpa matakwa ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema huu ni uwongo kwa sababu hakuna azimio lolote lililowahi kupitishwa na Bunge lako hili Tukufu kupitia Mkataba wa Liganga na Mchuchuma, hakuna mahali popote. Tunachukia sana, nami binafsi sipendi kuandikiwa taarifa ambayo nikiisoma ninaona huu ni upotoshaji. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninadiriki kusema kwamba ninafikiri Wizara ijipange kutuambia pale kuna kufidia. Kuna fidio lile ambalo mlifanya tathmini mwaka 2017, pengine hizi ndiyo tuziite masharti hasi. Siamini kwamba eti sheria hizi mbili zimesababisha kwamba Liganga na Mchuchuma isimame kwa sababu tu sheria hii ina matakwa hayo ya kisheria. Bunge hili halijawahi kupitisha azimio mahali popote. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Kwanza kabisa napenda kuwapongeza Ofisi ya TR kwa kazi nzuri wanaoifanya pamoja na Kamati ya PIC lakini pia Ofisi ya Mheshimiwa Spika kwa sababu wamekuwa bega bega na sisi kuona kwamba tunapeleka ufanisi kwenye Mashirika yote ya Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi zipo nyingi lakini kwa kwenda haraka ningependa kwenda moja kwa moja kwenye mada na nitapenda nichangie mashirika mawili, nitapenda nichangie shirika la TAWA ambalo linahusika na uhifadhi wa Wanyamapori lakini pia nitapenda nichangie Kampuni ya Kilombero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAWA ilianzishwa kupitia Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Na.5 ya mwaka 2009, lakini pia katika kifungu cha 8 ilimpa mamlaka Mheshimiwa Waziri kuweza kuunda chombo chenye mamlaka kamili katika kusimamia na kuhifadhi wanyamapori. Hata hivyo, mpaka leo hapa ninapoongea takwa hili la kisheria halijatimilika na Kamati yetu inasema kwamba kuna umuhimu kabisa wa kuona TAWA wanapatiwa sheria yake kwa maana ya kwamba tunaamini kabisa tutakapopata sheria yake TAWA itaenda kujiendesha kwa mapato tofauti na ilivyo sasa. Tunasema kwamba ni wakati mahususi TAWA iweze kujipatia sheria yake kwa sababu tumeona kazi kubwa TAWA inayofanya. Hapa ninapoongea ardhi tengefu zote zaidi ya asilimia sitini katika nchi yetu zinasimamiwa na TAWA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo haitoshi, ninapoongea hapa kwa mfano mapori tengefu yote yanasimamiwa na TAWA, lakini pia mapori ya akiba, wetland, open areas zinasimamiwa na TAWA, Ramsar sites zinasimamiwa na TAWA lakini pia utalii wa baharini unafanyika na TAWA na vitu kadha wa kadha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema sasa ni muda mahususi TAWA iweze kupatiwa sheria yake kwa sababu kwa muda mfupi toka ianze kufanya kazi mwaka 2016, TAWA ilipata mtaji kutoka Ngorongoro wa shilingi milioni mia tatu hamsini, lakini ninapoongea hapa leo TAWA imeweza kutengeneza faida ya shilingi ya bilioni 48 kwa mwaka. Kwa hiyo, hii ni positive move na tuna-recommend kwamba tunaomba sasa Serikali ione umuhimu wa kukipatia chombo hiki sheria yake mahsusi ili kiweze kujiendesha chenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majukumu haya na record nzima walizoliweka TAWA pia kwa namna ambavyo walivyojianzisha wenyewe walikuwa na magari machache sana na Mkurugenzi kwa kipindi hicho alikuwa anatumia gari ya TANAPA kufanya operations za taasisi. Hadi sasa ninapoongea, TAWA ina magari 77 brand new zero kilometer, kwa hiyo haya ni mafanikio makubwa kwa muda mfupi wa miaka mitatu. Kwa hiyo, tunasema kwamba ni muhimu sasa Serikali ikaamua kugatua madaraka pamoja na operations zote ziende TAWA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na haya tunaposema TAWA ipewe majukumu yake, tunafahamu kabisa, kwa mfano Sheria Na.5 kifungu cha 8 ambacho kinamtaka Waziri atoe mamlaka kamili ya chombo hiki ni kwamba kwa sasa katika sheria hii ilivyo, Mheshimiwa Waziri ndiye mwenye mamlaka ya kutoa vitalu vya kitalii vya uwindaji. Haya ni makosa, tutakapopata sheria hii mamlaka haya yataenda kwenye Board of Directors, lakini pia Kamishna wa TAWA atakuwa na mkono wa moja kwa moja kusimamia haya kwa sababu atakaposimamia na kuweza kutoa mwenyewe vitalu, tunaamini kabisa ataenda kuhifadhi sustainable management kwa taasisi hii ya TAWA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoongea hapa hata utalii wa picha Mheshimiwa Kamishna wa TAWA anakuwa hana mamlaka kamili, ingawaje jukumu hilo liko katika taasisi yake lakini hasimamii yeye, suala hili linasimamiwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba kabisa Wizara husika pamoja na Serikali ione kuna ulazima kabisa wa kuipa TAWA sheria yake ili iweze kushindana kama tunavyoona TANAPA inavyofanya vizuri, Ngorongoro inavyofanya vizuri, tukiipatia TAWA sheria yake na Meja Jenerali Semfuko alivyokuwa imara, tunaamini kabisa TAWA itaenda kufanya wonders katika hii dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia nichangie suala la Kilombero. Ni dhahiri kama walivyosema wajumbe wenzangu, kwa sasa tuna umuhimu kabisa wa ku-support suala hili na tunaomba Serikali iwe makini na isimame na sisi katika kuona kwamba kibali kili walichoomba hawa watu toka miaka miwili iliyopita, basi kitolewe kwa sababu domestic demand ya sasa ya sukari ni tani 550, lakini kwa sasa tuna tani laki tatu na elfu hamsini katika viwanda vyetu vya ndani. Kwa hiyo, tunajua kabisa tuna gap, hivyo, ni vizuri sasa tukakubali kiwanda hiki kipanuliwe kwa sababu kitakapopanuliwa, sasa hivi Kilombero Sugar inachangia shilingi bilioni 350 katika uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika plan hii ya expansion itaenda kuchangia bilioni 700, lakini pia wafanyakazi wataenda kuongezeka kutoka elfu nane mpaka elfu kumi na saba. Uchakataji wa malighafi katika taasisi ile unasema kwamba asilimia sitini ya raw materials ambayo ni miwa itazalishwa na out growers ambao ni mama zetu, dada zetu, vijana waliokuwa disparate walikosa ajira, wamezagaa kule Morogoro, ardhi ni nzuri, maji yapo, kwa hiyo, tunaomba kabisa Serikali itilie mkazo jambo hili kwa sababu sisi wabeba ilani tunayo ya kujibu, suala la ajira bado ni kizungumkuti, lakini ardhi tunayo, maporomoko ya maji tunayo na kiwanda kipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo nyuma mpaka Waziri alilazimika kwenda kiwandani pale kwa sababu kulikuwa na migomo mingi sana, wakulima wadogowadogo kila wakipeleka miwa wanaambiwa mara sucrose haipo, mara hivi, watapewa terminologies zote zile ili mradi tu kuonesha kwamba hawahitaji miwa mingi kwa kiasi hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaamini tutakapokwenda kupanua kiwanda kile malighafi tunayoambiwa asilimia 60 ya malighafi itatoka kwa wakulima wadogo wadogo, kiwanda kitachukua yote kwa sababu sasa hivi wakienda wanapewa terminology ngumu, lakini hii ni kuonesha kwamba kiwanda walichonacho kwa sasa hakiwezi ku-accommodate mazao yote ambayo yanapatikana katika muktadha huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo mengi ya kuzungumza katika hili, lakini nafikiri kwamba ni vizuri sana Serikali ikaona umuhimu wa kupanua kiwanda hiki, kwa sababu hata kama tunataka tuipe Mkulazi ambayo ni taasisi ya Serikali pengine, na-assume hivyo, labda tukiisaidia Kilombero sisi tutakosa stock yetu. Hapana, leo ukienda Mkulazi tumewapa ardhi, tumetoa wafungwa magereza wamekwenda wamelima, wamesafisha, tumefanya kila kitu, lakini Mkulazi haina uwezo, leo miwa ya Mkulazi inaachwa kule porini, imetelekezwa kwa sababu hata kiwanda hakijanunuliwa, kinu hakipo, tuwape wawekezaji ambao wako tayari. Hakuna nchi ambayo inakataa au hakuna nchi ambayo haikubali uwekezaji wa watu binafsi na sisi pia naamini hatupo huko na kwa kuwa hatupo huko, naomba sasa Serikali ione umuhimu wa ku- accommodate hawa wenzetu, tuwape kibali ambacho wamekisotea kwa miaka miwili leo ili waweze kuanza kufanya upanuzi huo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya machache narudia tena, napenda kuipongeza Kamati yangu kwa kazi nzuri iliyofanya. Natambua kabisa katika mashirika tuliyoyahoji, kipaumbele chetu cha kwanza kilikuwa ni kuona kwamba Bodi za Wakurugenzi zinakuwepo, baadhi ya taasisi nyingi, asilimia 70 tulizokutana nazo ambazo zilikuwa hazina bodi sasa hivi zina bodi. Pia nafasi za kukaimu; asilimia 72 ya nafasi zote zilizokuwa zinakaimishwa, sasa hivi wameenda kupata substantive post, lakini, siyo hivyo tu, Kamati yetu pia ilisimama kikamilifu kuona kwamba na wanawake wanapewa nafasi katika mashirika haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo awali wakati tunaanza shughuli zetu za uendeshaji wa shughuli yetu tulikuja kubaini wanawake wengi wanaachwa kwenye ngazi za maamuzi, kwa hiyo kupitia Mheshimiwa Chegeni alikuwa imara sana kuweza kuona kwamba shirika linakuwa na namba nzuri ya wanawake wanaosimama katika ngazi za maamuzi. Kwa kweli katika hili naipongeza sana Kamati yangu, kwenye suala la gender tulisimama vizuri, Mheshimiwa Chegeni nampongeza mno pamoja na nafasi yake aliyonayo alisimama kikamilifu kuwatetea akinamama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya machache nakushukuru sana na naomba kuunga mkono hoja taarifa zote za Kamati kama zilivyosomwa na kuwakilishwa. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia katika Bunge lako Tukufu. Kabla sijaenda mbali napenda kumpongeza sana Waziri mwenye dhamba Dkt. Kalemani pamoja na dada yetu mpendwa dada Subira, kazi zenu zinaonekana. Mimi nimekuwa nikitembea mikoa mbalimbali kuongea na vijana wa vyuo vikuu, wengine wamediriki kuniambia kwamba wazee wao wamefika hata kuwasahau watoto wa majirani lakini majina yenu nyuso zenu wanazijua fika. Mmetembea Tanzania mmezunguka mikoa yote vijiji kwa vitokoji. Tunawapa pongezi za dhati kwenye hili la kusimami sekta ya nishati msiyumbe kwa kweli mpo vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nitajikita kwenye taasisi moja tu ya TPDC. Sambamba na pongezi zangu kwa Wizara na viongozi wa Wizara lakini pia ninapenda kwa namna ya pekee nimpongeze Engeneer Msomba pamoja na timu yake, mwenyekiti wa bodi Bakukula lakini pia wadada watatu ambao wameonekana kujituma sana katika taasisi ya TPDC nanyi pia mpokee pongezi za za dhati. Ninamfahamu Venosa lakini pia ninamfahamu Dorah, ninamfahamu Maria. Kwa kweli sisi kama wanawake vijana tunawapongezini sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, TPDC kwa miaka ya nyuma ulikuwa ukiitaja hapa Bungeni, nafikiri hata kama michango ukiipata ni michango dhaifu, kwa sababu kila mtu alikuwa ame-tend ku-withdraw, hakuna mtu mwenye hamu ya kutaka kuisikiliza TPDC ni nini, lakini, kwa heshima na taadhima napenda kuipongeza Taasisi hii ilienda ikajitafakari ikaja na turnaround strategy na leo ninathubutu kutaja mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye Taasisi hii ya TPDC. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kupitia Gesi ya Kinyerezi I na II, TPDC imeweza kufanya mambo makubwa katika nchi hii, umeme viwandani, kwa sasa Dangote analipa shilingi bilioni tano za Kitanzania kila mwenzi, lakini siyo hivyo Goodwill Ceramic analipa 2.2 bilioni kwenye uchumi wa Tanzania kutokana na Kinyerezi I na II. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Cocacola juzi amepewa umeme wa gesi, analipa shilingi milioni 150 kwa mwezi, ninapoongea hapa Lodhia Steel, lakini pia NAF Industries leo hii wanaenda kulipa shilingi milioni 512 kwa mwezi kwa sababu ya gesi ya Kinyerezi I na II. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambasamba na haya, TANESCO kwa mara ya kwanza kabisa na nitaomba ikikupendeza wenzetu hawa waweze kutafakari ni nini walichokiandika katika ukurasa wa sita kwa sababu wametuambia bado kwamba TANESCO inalipa capacity charge, huu ni uongo na ni upotoshaji mkubwa, nitaomba niweke rekodi hizi vizuri katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapoongea hapa kwa mara ya kwanza tumeondokana na capacity charge za Aggreko, tumeondokana na capacity charges za Artumas, tumeondokana na capacity charges ambazo tulikuwanazo kwenye Richmond saga katika Bunge lako hili Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Hizi ni pongezi za hali ya juu, sisi ni waumini katika...

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

MBUNGE FULANI: Hebu endelea.

MBUNGE FULANI: Endelea.

MBUNGE FULANI: Endelea.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mmasi kuna taarifa. Mheshimiwa Mwakajoka.

T A A R I F A

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kumpa taarifa mchangiaji, anasema tumeondokana na TANESCO, wameondokana na capacity charge wanazotoa kwenye makampuni yanayowauzia umeme, si kweli, anazungumzia capacity charge zinazoondolewa kwa wateja wadogowadogo, lakini TANESCO bado wanalipa capacity charge wanakonunua umeme kwenye makampuni mbalimbali, kwa hiyo anachoongea ni uongo kabisa huyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa pamoja na kwamba unachotoa ni taarifa Kanuni uliyotumia siyo, kama unaona anasema uongo, ungetumia Kanuni ya 63 ama 64. Mheshimiwa Ester Michael Mmasi.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, utamaduni na utaratibu wa Bunge lako tukufu ikiwa Mbunge anapotosha, ni sharti alete kithibitisho, niko radhi kuleta uthibitisho kwenye Bunge lako tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, capacity charge aliyokuwa analipwa na Serikali, shilingi bilioni 6.9 imeondoka kwenye mahesabu ya TANESCO na huo ni uthibitisho tosha, data ninazo lakini haitoshi, mimi niko pamoja na wengine huko kwenye Kambi yenu, tunahudumu Kamati moja, haya masuala tunaongea kwenye Kamati, kwa nini nidanganye leo hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, asinipotezee muda, naikataa taarifa yake, Sambamba na matokeo chanya haya, lakini leo hii kwa mara ya kwanza mwaka wa tatu leo, TANESCO imeondokana na ruzuku ya bilioni 143 iliyokuwa inalipa kwa mwaka. Haya ni mafanikio makubwa, hakuna wa kubeza katika hili, sisi ni waumini wa maendeleo ya Taifa hili, sisi ndiyo wabeba Ilani wa Taifa hili tupeni nafasi tufanye kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana TPDC, naupongeza uongozi, ampongeza Waziri na Naibu Waziri, kazi inaonekana, leo TPDC ina rekodi faida ya shilingi bilioni 9.57 na mpango wa miaka ijayo tunaenda kurekodi bilioni 59 na huu ni mpango wa miaka mitatu ijayo ni nani wa kubeza katika hili. Uthibitisho ninao, nitaleta mkinitaka nilete katika Bunge hili, TPDC kwa turnaround strategy imeenda kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya nishati ya gesi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu nitapenda niongelee Sheria ya Mafuta na Gesi, ya mwaka 2015, Sheria namba 21. Katika Sheria hii niseme tu kwamba nafikiri Wizara ipate muda iweze kufanya rejea na kuondokana na yale masharti hasi, ambayo yako katika ile sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii TPDC sharti la kwanza katika ile sheria inaitaka TPDC ifanye kazi kibiashara, ijiendeshe kibiashara, irekodi faida, lakini sharti lililowekwa katika sheria ile wanasema kwamba raslimali ya gesi na mafuta irudi Serikalini. Leo TPDC akitaka kununua mitambo, either katika kufanya utafiti wa upper stream or downstream ama katika kununua mitambo ya kusafirisha gesi itapaswa kupita kwenye utaratibu wa Kiserikali kuandika minute sheet, kuandika folios iende kwenye Cabinet Ministers ndiyo waweze kupata approval. Kwa sharti la kisheria kwamba hii TPDC iweze kujiendesha Kibiashara, nafikiri ni muhimu sana, Wizara ikaona umuhimu wa kuondokana na hizi red tapes hazitatusaidia. (Makofi)

Mheshishimiwa Naibu Spika, sambasamba na takwa hili la kisheria...

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ester Mmasi kuna taarifa. Mheshimiwa Salome Makamba.

T A A R I F A

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mimi napenda kumpa taarifa ndugu yangu Mheshimiwa Ester Mmasi kwamba taarifa zinazotolewa kwenye ripoti ya Kambi zinatokana na sources ambayo mojawapo ni ripoti ya CAG. Sasa tunaomba utufahamishe, hicho unachokisema unakitoa wapi? Usije ukawa unatulisha matango pori humu.

MBUNGE FULANI: CAG na wewe nani mwongo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Salome Makamba unauliza swali huku unatoa taarifa, taarifa ni kwamba mtu kile anachokisema unakuwa unamwongezea kama hakijakamilika ama kimekaa namna fulani, sasa wewe unamuuliza swali ili aanze kujibizana na wewe jambo ambalo haliruhusiwi.

Mheshimiwa Ester Michael Mmasi malizia mchango wako.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, hapa kuna homa ambayo haijapata tiba, dengue leo inatiba, lakini homa ya kwetu humu ndani, haijapata tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, iko hivi TANESCO leo anaambiwa anarekodi hasara, si kila hasara ni hasara, mtu anapodaiwa si kosa la jinai na kudaiwa si hasara, nini kigumu katika hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niikatae taarifa ya rafiki yangu mpenzi, comrade wangu Salome, naomba niendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye masharti ya Sheria hii ya mwaka 2015 ya Petroleum Act inatuambia kwamba ni sharti kwamba Taasisi hii iweze kuwa Mfuko wa Rasilimali ya Gesi na Mafuta, ni sharti zuri sana, haina mjadala, lakini katika masharti ya Mfuko huu, leo hii TPDC mwaka huu wa fedha peke yake imepeleka bilioni 66, lakini Mfuko huu una jumla ya bilioni 102, lakini toka TPDC imeanza kupeleka kule hakuna a single coin iliyoweza kutoka na kwenda kufanya re- investment kwenye masuala ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo Waziri amesimama pale anasema kwamba anaenda kwenye mpango wa nyumba 200, baada ya hapo nyumba 1000, leo tunatakiwa tuongelee nyumba 10,000 au 20,000 leo tunatakiwa tusikie maendeleo ya kuleta nishati ya gesi Dodoma, lakini tuko Dar es Salaam pale tunahitaji Mfuko huu ufanye kazi Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mfuko wa REA unafanya kazi, tuondoe sharti la kisheria la asilimia tatu, halitatusaidia Mheshimiwa Waziri. Tunaomba sharti la asilimia tatu kama kifungo cha Waziri iondoke kwenye ile sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hili, upo mkopo wa EXIM Bank of China ambayo ni shilingi 1.225 bilioni US Dollars. Kwa kuwa moja ya jukumu la Serikali katika kuandaa mazingira wezeshi ya investors ni pamoja na kuweka miundombinu. Leo hii Serikali imeenda imekopa pesa China inakuja inamwekea TPDC ina m-charge zile pesa. Leo hii TPDC ameandikiwa rekodi ya bilioni ya 340 kama rejesho lake, yaani huyu amepewa hesabu kama ni mdaiwa wa mkopo huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni jukumu la Serikali kuandaa miundombinu ili TPDC aweze hata kukopesheka akienda leo sokoni hawezi kukopesheka, kwa sababu anaonekana ana taarifa chafu. Naomba Mheshimiwa Waziri aje atuambie ni kwa nini asione umuhimu wa kuondokana na mkopo huu kwa Taasisi ya TPDC ili iweze kufanya kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili imeshagongwa Mheshimiwa, ahsante sana. (Makofi)

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu juu ya kukithiri wa masuala ya ngono katika vyuo vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyochangia kwenye mchango wangu wa maneno kuwa ni kweli tulipofika leo masuala ya ngono yameonekana yanahusika moja kwa moja katika kupandisha alama ya ufaulu na imefanya wanafunzi wenye uwezo mdogo kuonekana kuwa vinara kwenye ngazi ya ufaulu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri kwa Serikali kutokana na mchango wangu juu ya ukithiri wa ngono vyuo vikuu. Ombi langu kwa Serikali ni kwamba kama ilivyofanya kwenye wasilisho la Miscellaneous Amendement na adhabu zake kwa yeyote atakayempa mimba mwanafunzi aliyekuwepo masomoni ama kumuoa mwanafunzi basi adhabu yake iwe ni miaka 30 jela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe kwa unyenyekevu mkubwa Wizara ya Elimu ituletee muswada wa sheria kwa walimu wote vyuo vikuu watakaobainika kuwa na mahusiano na wanafunzi basi adhabu ya kwanza iwe ni kusitisha ajira na kufungiwa miaka kadhaa bila kuajirika mahali kokote sambamba na adhabu ya kichapo cha hadharani ili kukomesha kabisa tatizo hili. Ni ushauri wangu adhabu pia itoe option ya kifungo jela.

Pamoja na adhabu niliyopendekeza pia ni rai yangu kwa Bunge lako Tukufu, Ofisi ya Spika iridhie ombi langu la uwepo wa special register book itakayobainisha usajili wa makosa ya ubakaji, ulawiti, ndoa za utotoni/wanafunzi na hata watuhumiwa wote vyuo vikuu waliobainika kuwa na mahusiano na wanafunzi vyuo vikuu ili iwe rahisi kwa sisi Wabunge kufanya follow up ya makaosa haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango juu ya uandaaji wa rasilimali watu kwa ajili ya usafiri wa anga ili kuweza kupata tija kamili kulingana na uamuzi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuoanisha na kuendeleza Shirika la ATCL; pamoja na mchango huu pia napenda nimshukuru sana Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako pamoja Mheshimiwa Mbarawa kwani baada ya juhudi zangu za kuonana na uongozi wa wanafunzi NIT sambamba na kikao cha tarehe 30/01/2017 na Mkurugenzi Mtendaji Shirika la ATCL nilibaini changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wa NIT hususani vijana wanaochukua mchepuo wa Aircraft Maintenance Engineering.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi tajwa wana changamoto ya ada kubwa isiyohimilika kwa wazazi walio wengi ambao wengi wao wameonekana kuwa na uchumi mdogo usiohimili ukubwa na uzito wa ada iliyopendekezwa na NIT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi ya Rwanda katika ku- promote expertiseya masuala ya usafiri wa anga walianza kwa kuandaa rasilimali watu kutoka katika nchi yao. Ada kwa masomo ya Engineering ni kiasi cha shilingi 40,000,000 na masomo ya urubaini ada (direct fee) ni kiasi cha shilingi 80,000,000 na katika kukabiliwa na changamoto ya uandaaji wa rasilimali watu kwa ajili ya usafiri wa anga, nchi ya Rwanda iligharamia masomo ya wanafunzi wa fani ya usafiri wa anga kwa asilimia 100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu, kwa nini nchi yetu tunapata vigugumizi katika kukabiliana na kiasi cha ada ya shilingi milioni kumi kwa masomo yanayopatikana ndani ya nchi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi hawa wanahitajika kuanza practical training this June lakini hata ndege ya mafunzo hakuna. Katika mazungumzo yangu na Mheshimiwa Profesa Mbarawa hivi majuzi nilielezwa Chuo cha NIT pamoja na Shirika la ATCL wamejipanga kukodi ndege za mashirika binafsi ili wanafunzi waweze kufanya practical training.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumenunua ndege mbili, focus yetu ni kuwa na ndege sita, sasa kwa nini mafunzo haya ya practical training NIT yasipewe kipaumbele? Kwani kufika kukodi ndege kwa ajili ya practical training na ilihali tunayo ndege ya Shirika la ATCL ipo Mwanza, ambayo inahitaji matengenezo kidogo na badala yake tukodi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoteza matumaini kwani wakati Mheshimiwa Rais anapambana ili kutujengea utamaduni wa kuondokana na matumizi yasiyo na umuhimu na kubana rasilimali fedha ya Taifa, lakini baadhi ya Taasisi bado tunaona Serikali ina fedha ya kupoteza kwa kufika kukodi ndege za mashirika binafsi kwa makusudi ya kufanikisha practical training (PT) yaani mafunzo kwa vitengo kwa wanafunzi wetu wa NIT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe kwamba huwezi kuandaa engineer wa masuala ya ndege bila kumpa mwanafunzi elimu ya vitendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali ni kama ifuatavyo:-

(i) Ndege ya Shirika la ATCL iliyoegeshwa (park) Mwanza ipatiwe fedha na Wizara ya Fedha chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na chini ya usimamizi wa karibu wa Wizara ya Elimu ili kwa pamoja tumsaidie Mheshimiwa Rais katika kuimarisha usafiri wa anga ili kwa pamoja tuweze kuimarisha uchumi wa nchi yetu.

(ii) Ni ushauri wangu Serikali kupitia Wizara ya Elimu iweze ku-revive Civil Aviation Training Fund ili kwa pamoja tuweze kuifikisha elimu stahiki kwa walengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa furaha na imani kubwa naomba kuunga mkono hoja wasilisho la Bajeti Wizara ya Elimu kwa asilima mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba niunge mkono hoja ya wasilisho la bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kwa moja niende kwenye hoja ya msingi juu ya masuala ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Ni ukweli usiopingika kuwa bado tuna changamoto kubwa juu ya kukabiliana na majanga ya ujambazi kutokana na vifaa duni katika Jeshi la Kujenga Taifa na hata kwa askari wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 hususani kwenye bajeti ya Jeshi la Askari tuliomba Serikali iidhinishe bajeti ya manunuzi ya magari mawili ya bullet proof ili kuweza kupambana na uhalifu nchini Tanzania, lakini cha kusikitisha hadi tunaelekea mwisho wa mwaka wa fedha 30 Juni hakuna hata gari moja lililonunuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ninapoandika mchango wangu huu ni kweli kuwa Taifa limepoteza nguvu kazi ya Jeshi la Askari hadi sasa tuna jumla ya askari 13 -15 waliopoteza maisha kwenye uharamia wa Rufiji, lakini pia tuna takribani jumla ya wananchi 20 - 30 waliopoteza maisha kwenye sakata la ujambazi Rufiji siyo hivyo tu uharamia wa Benki Mbagala na Dar es Salaam City Centre, wapo wananchi wengi waliopoteza maisha pamoja na Jeshi la Wananchi na hata askari kwa ajili ya kukosa magari ya bullet proof.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kikosi cha Jeshi la Wananchi nchini Kenya pamoja na Jeshi la Askari ni ukweli kwa nchi ya Kenya ina hazina ya magari ya bullet proof zaidi ya mia mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mauaji yanayoendelea ni dhahiri kwamba kama Wizara kupitia Jeshi la Wananchi na JKT kama vile Ngome na JKT hatutajipanga vizuri ni ukweli usiopingika kwa changamoto hizi hazitafika kwenye ukomo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji Jeshi la Wananchi lipewe fedha ya kutosha ili waweze kununua vifaa vya kisasa katika kukabiliana na uhalifu nchini kwetu. Wizara ya Jeshi la Kujenga Taifa haijatengewa fedha katika kununua magari ya bullet proof na silaha muhimu za kijeshi katika kukabiliana na uhalifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika wasilisho la ripoti ya Kamati pia tumesikia kuwa Wizara ya Jeshi la Kujenga Taifa pia liko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa National Defense Policy. Pamoja na ukweli kuwa tumeona juhudi nzuri na utendaji kazi mzuri wa Mheshimiwa Waziri kwenye Wizara yake, lakini kwa kutokuwepo kwa sera hii muhimu ni ukweli usiopingika kuwa pengine kuna uzembe mkubwa katika kitengo cha sheria katika Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni maombi yangu kuwa Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha hoja ya Wizara yake atuambie ni kwa nini hadi leo Sheria ya Ulinzi ya mwaka 1966 imepitwa na wakati. Je, nini tamko la Waziri mhusika kwenye changamoto hii? Naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina heshima ya pekee naomba kuwasilisha mchango wangu wa maandishi ili nami niweze kuwasilisha ushauri wangu juu ya ufanisi wa shughuli za Serikali chini ya Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu nitapenda niguse masuala makuu matatu nayo ni kilimo, ufugaji pamoja na miradi mikubwa ya uwekezaji kwenye sekta ya miundombinu hususan miradi ya ujenzi wa barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ugomvi wa wakulima na wafugaji na hata migogoro kati ya wafugaji na Serikali yamekuwa yanakithiri siku hadi siku na moja kati ya vyanzo vingi vinavyopelekea migogoro hii ni pamoja na conflict of interest. Kwa upande wa wafugaji, wakati Serikali inaweka juhudi za makusudi katika kuhifadhi eco -system kwa kusisitiza wafugaji wafuge kwa idadi ndogo ambayo ni manageable, wafugaji nao wamekuwa kwa muda mrefu wakiongeza idadi ya mifugo ili kuweza ku-maximize profit bila ya kuwa na mchango wowote kwa Serikali kupitia Halmashauri husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hali ya kawaida huko vijijini unaweza kukuta mfugaji mmoja anamiliki ng’ombe 2000, mbuzi 500 na hata kondoo 300 lakini mfugaji huyu unakuta hachangii chochote kwenye miundombinu ya uhitaji wa wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kosa kubwa tena nafikiri lisilopaswa kufumbiwa macho kwa mfugaji mwenye umiliki wa idadi tajwa ya wanyama wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni moja kufikia kudai Halmashauri imjengee bwawa la kunyweshea wanyama maji ama majosho ya kuogeshea wanyama. Ni Mawazo yangu na ushauri wangu kwa Serikali kuwa majosho, mabwawa, nyumba za Madaktari wa wanyama na gharama ndogo ndogo zinazofanana na hizi basi zisitoke tena Serikali Kuu kupitia Halmashauri na badala yake wafugaji washiriki kikamilifu kabisa kwenye ujenzi wa miundombinu tajwa kwani kwa kufanya hivi nao watakuwa responsible kwa miundombinu hiyo in case kutakuwa na uharibifu ama kuzuia uharibifu. Vile vile kwa wafugaji hawa wenye idadi kubwa ya wanyama itafika mahali watakubali kwa wepesi kauli na miongozo ya Serikali juu ya kufuga kwa tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niunge mkono hoja na maelekezo ya Serikali na kwa kupitia speech za Mheshimiwa Rais juu ya utayari wa Serikali, katika kutoa vyakula vya msaada naamini kabisa hakuna sababu yoyote ya Serikali kutoa chakula cha msaada na badala yake Serikali ihimize wananchi wawajibike katika kutafuta chakula, kuhifadhi na kutumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali yangu iweze kusaidia wananchi wake katika kushiriki kikamilifu kwenye kilimo, tumtoe Mkulima wa Taifa hili kwenye kilimo cha msimu mmoja kwenda kwenye kilimo cha misimu miwili kwa kufikisha pembejeo kwa wakati pamoja na kuvuna maji ya mvua ama kwa kuchimba visima au mabwawa ili kuwezesha kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Elimu Bure bado ni sera ya msingi na ina umuhimu mahsusi katika ustawi wa Taifa hili, lakini si jambo baya Serikali ikafikiria kuja kupongeza baadhi ya items kwenye package nzima ya elimu bure. Ikiwa tutafaulu kumnyanyua mkulima na tukatengeneza ajira nafikiri elimu bure inaweza kufanyiwa tathmini kikamilifu ili kuona kama kuna sababu za msingi katika kuendelea na sera za elimu bure ama laa. Siyo mbaya Serikali ikaenda na sera ya elimu bure kwa miaka 10 ikiwa uchumi na pato la mmoja mmoja utaimarika basi nafikiri elimu bure yawezekana ikaja kuwa ni mzigo mkubwa kwa Serikali yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la shilingi milioni 50 kwa kila kijiji nalo linahitaji kuwa redefined, tunahitaji kuwa na tafsiri mpya juu ya umuhimu na impact tarajiwa kupitia gawio la milioni 50 kwa kila kijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, binafsi naona kuna sababu za msingi kabisa kuchelewa kuitoa hiyo milioni 50 kama hatutakuwa na tathmini kamilifu juu ya umuhimu na matarajio ya Serikali juu ya gawio la shilingi milioni 50 kwa kila kijiji. Ni ushauri wangu kwa Serikali yangu kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi iweze kueleza kwa ukamilifu hiyo shilingi milioni 50 ni kwa ajili ya nini, sera iseme matarajio ama mlengo wa Serikali juu ya gawio la shilingi milioni 50 kwa ukamilifu wake. Leo kuna watu wanafikiri hii fedha ni zawadi ya Serikali ama ujira wa uchaguzi kwa wananchi waliotuchagua, wengine wanafikiri hii fedha ni VICOBA na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miradi ya ujenzi wa barabara, utamaduni tulionao kwa muda mrefu katika miradi hii ya barabara ni kwamba Serikali kupitia vyanzo vyake mbalimbali, imekuwa ndio ikifanikisha miradi ya ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara kupitia makandarasi nje na ndani ya nchi. Nikiwa sipingani kabisa na utaratibu huu wa Serikali, lakini nafikiri ingekuwa jambo jema kabisa kama Serikali ingefanya tathmini (cost and benefit analysis) na kuona kama tuna sababu mahsusi kwa miradi kama hii itegemee fedha za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli kuwa mifumo ya udhibiti juu ya ubadhirifu wa mali ya Serikali bado haijaimarika na ndiyo maana Mheshimiwa Rais bado amekuwa akikabiliana na zoezi la kuwawajibisha Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali kila iitwapo leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawazo yangu ni kuwa Serikali iangalie upya juu ya umuhimu wa Serikali kushiriki moja kwa moja kwenye miradi ya reli, bandari, barabara, viwanja vya ndege, madaraja, meli na umeme, ni mtazamo wangu kuwa miradi hii mikubwa mikubwa iachiwe taasisi binafsi (private sector), Serikali ibaki kukusanya kodi na mapato mengineyo. Fedha ya Serikali ibaki kwenye mahitaji muhimu mfano elimu, afya, ajira na hata ulinzi wa wananchi na mali zao. Kwa kufanya hivi Serikali itabaki na majukumu machache ya kisera na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja ya Serikali. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Serikali yetu ya Awamu ya Tano, Mungu Mbariki Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni mwendelezo wa mchango wangu wa maongezi. Tofauti na juhudi ndogo inayowekezwa na Serikali katika kumuandaa kijana kuweza kujiajiri nje ya mfumo wa ikama ya Serikali, pia Serikali imeshindwa kusimamia sekta binafsi hususani financial institutions ili kuweza kutoa ajira za kutosha kwa vijana wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TBL leo ime-downsize waajiriwa wake kinyume kabisa na matakwa ya sera ya ajira. TBL amehamishia payroll Mauritius kwa kuwa kwa kuhamishia payroll nchi ya Mauritius definitely mwekezaji anaingia tax heaven na kwa kufanya hivyo kumenyima vijana wetu ajira.

TBL imebaki na gate keepers na Idara ya Uzalishaji. Tanzania imebaki kuwa na idadi kubwa ya walevi ikiashiria pengine ndiyo sehemu ya faida ambayo nchi imejipanga kupokea kupitia uwekezaji wa TBL. Swali langu ikiwa hivi ndivyo, nini hatma ya Mfuko wa Bodi ya Elimu ya Juu? Vijana hawaingii kwenye soko jipya la ajira na walioko kwenye soko la ajira wanatolewa nje pasipo kauli yoyote ya Serikali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia taasisi za fedha (banking industry) it almost kama haipo. Benki za Standard, NBC, Stanbic pamoja na Barclays kazi ya IT yote inafanyika Kenya, ukija sehemu ya malipo kazi hizi zinafanyika nchi ya Chennai - India na servers za IT zikiwa hosted nchi ya South Africa. Personally nimewahi kumfuata Waziri wa Mipango kwenye kikao cha Bunge la Bajeti mwaka 2017/2018 na alichonieleza ilikuwa hii ni common practice kwa nchi za Afrika na hata Ulaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Elimu inazalisha vijana wa kutosha fani ya IT - DIT na UDSM- Engineering Department na kwenye baadhi ya taasisi za elimu ya juu, lakini kwa utamaduni huu hatuwezi kufikia malengo ya urejeshwaji makini kwa Bodi ya Mikopo. Aidha, wakati Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mpango akinijibu hoja hii ambayo nilimfikishia mezani kwake na akanijibu kuwa hii ni common practice amesahau nchi za Uganda na Mozambique wanafanya vizuri kabisa kazi za IT katika sekta za mabenki ziko hubbed nchini mwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu kwa Serikali ni vema Wizara ya Elimu ikafanyia kazi hoja za CAG juu ya wasiwasi wake na uhimili wa Mfuko wa Bodi ya Mikopo. Ikiwa Mashirika ya uwekezaji yataachiwa yajiendeshe holela kwa kufuta ajira za vijana wetu hii itapelekea:-

(i) Kuchochea kasi ya ukosefu wa ajira kwa nchi yetu;

(ii) Ku-drain skills, capability and knowledge za vijana wetu wa fani ya IT kwa kuendelea ku-outsource kazi nyingi nje ya nchi kwani mwisho wa siku hata Serikali ni vigumu sana ku-realize dividend na kupoteza fedha nyingi na hata kuondosha ari ya kuzalisha ajira kwa vijana wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho Serikali ione namna bora ya ku-motivate walimu elimu ya juu. Madai ya walimu elimu ya juu hayafanyiwi kazi, walimu wamesimamishwa promotions kinyume kabisa na matakwa ya miundo ya utumishi wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, I submit, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, nasimama kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, kwanza kabisa kuipongeza Wizara husika kwa juhudi zao katika kuinua Tanzania ya viwanda na hata kueneza falsafa ya Tanzania ya Viwanda. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naona ni vyema kupongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujikita kwenye maeneo mawili. Mosi, utekelezaji wa mradi wa makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma, pamoja na ushiriki wa vijana kwenye uchumi wa viwanda na biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapofanya mapitio ya report ya Wizara, page ya 15 sura ya 28, 29 na 30, nadiriki kusema Wizara ya Viwanda na Biashara pengine iridhie kuendesha sehemu ya sentensi inayosomeka kwenye sura namba 29 ambayo kwangu naona ni upotoshaji mkubwa kwa Taifa, hasa tunapofanya marejeo ya Ilani ya Chama Tawala sambamba na utungwaji wa sheria mbili za ulinzi wa maliasili za nchi (Natural wealth Resources Permanent Sovereignty Act, 2017) pamoja na Sheria ya Natural Wealth and Resources Contract Review Renegotiation of Unconscionable Terms 2017).

Mheshimiwa Naibu Spika, ninasema ama naishauri Wizara kufuta kipengele hiki chote kwa sababu moja; sababu za mkandarasi kuomba vivutio vya ziada hauna nafasi kwenye sheria zote mbili, kwa sababu sheria hizi mbili au hususan Sheria inayohusu mapitio ya mikataba yenye masharti hasi, hakuna mahali popote inapo-deal na maombi ambayo yako nje ya mkataba. Ikumbukwe na kama ilivyoandikwa na Wizara ukurasa wa 15, ombi la mwekezaji la kuomba vivutio vya ziada havikuwepo kwenye terms za mkataba, kwani hii ni addition incentives na siyo sehemu ya mkataba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inapotosha kwa kueleza Umma na Watanzania kwamba mkataba wa Liganga na Mchuchuma umekwama kwa sababu moja ya matakwa ya sheria zote hizi mbili; ni pamoja na kufanya mapitio ya mkataba kati ya NDC na Sichuan Hangda Group na kwamba baada ya Mkandarasi kutaka vivutio vya ziada hii imesababisha Wizara kufanya mapitio ya mkataba. Huu ni uwongo kwa sababu tunapofanya Part III inayoeleza procedure on how to deal with the Review Renegotiation of Unconscionable Terms, imeweka bayana utaratibu wa kisheria utakaotumika kufanya mapitio haya ya mikataba yote iliyoonekana kuwa na masharti hasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, najiuliza, inakuwaje leo Wizara inatuambia kutokana na masharti hasi ya mkataba wa Liganga na Mchuchuma, basi mchakato wa kufanya mapitio unaendelea na angali jukumu hilo ni la Bunge? Naishauri Wizara irejee sheria ya masharti hasi Ibara ya 4(1) – (5), inasema bayana kwamba jukumu la kufanya mapitio ya mikataba hasi ni la Bunge. Rejea pia Katiba ya Nchi Ibara 63(2), hii ni kwa kuwa mradi wa Liganga na Mchuchuma hauna unyeti wowote (sensitivity) kama ambayo ingekuwa ni mradi wa chini ya Taasisi ya Idara za Usalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Wizara husika imetuambia kuwa mchakato wa mapitio ya mkataba wa Liganga na Mchuchuma unaendelea: Je, ni lini Bunge lako Tukufu liliwahi kutoa azimio la mapitio ya mkataba wa Liganga na Mchuchuma? Kwani ukirejea mkataba wa masharti hasi, ni lazima Bunge lako litoe azimio la kufanya mapitio ya Liganga na Mchuchuma, kitu ambacho hakikuwahi kutokea. Sasa ni kwa nini tunaambiwa mchakato unaendelea? Rejea Part II 5(3) of this Act.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaongelea umuhimu wa kuendelezwa kwa mradi wa Liganga na Mchuchuma kwa sababu vijana wetu hawana ajira na pia ukiangalia pamoja na chuma kinachozalishwa nchini, Tanzania ni asilimia 80 na asilimia 20 tu ndiyo inayoagizwa nje ya nchi, lakini bado ajira hailindwi. Kati ya ajira 23,150,000, ajira 20,000,000 zote ni ajira za muda ambapo ajira za muda mrefu ni 3,150 tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye mchango wangu wa ushiriki wa vijana kwenye Sekta ya Biashara na Viwanda, ikumbukwe Bunge lako hili Tukufu lilipitisha kusudio la kushirikisha vijana kwenye zabuni (tenders) ambapo vijana walionekana wenye kuwapa nafasi/dirisha maalum ili waweze kushiriki rasmi kwenye michakato ya zabuni, lakini swali langu kwa Wizara: Je, ni kwa nini kwenye kitabu cha Mheshimiwa Waziri hakuna taarifa yoyote inayohusu ushiriki wa vijana kwenye Sekta ya Viwanda na Biashara?

Mheshimiwa Naibu Spika, nchini Kenya upo mfuko maalum Youth Enterprises Development Fund ambapo vijana wenye umri kati ya miaka 18 - 35 walihusishwa kikamilifu. Haitoshi, pia nchi ya Kenya imekuwa ikitenga kiasi cha fedha kwenye kila Bajeti yao ya mwaka wa fedha ambapo five years back mfuko huu ulikuwa na USD 940,000. Malengo ya mfuko huu ni pamoja na kutoa startup capital, create Mark space and incubators for young graduates and dropout students.

Mheshimiwa Naibu Spika, halikadhalika nchi yetu ya Tanzania chini ya Wizara hii imekuwa na Mfuko wa Maendeleo ya Wajasiliamali Wachanga (NEDF) ambapo last financial year ilitengwa shilingi bilioni 15 ambayo haikuwahi kutoka hata senti moja. Ushauri wangu kwa Serikali, iweze kutoa fedha angalau asilimia 50 ya fedha ya maendeleo. Last financial years kati ya shilingi bilioni 100 ilitoka shilingi bilioni 12, fedha za maendeleo. Serikali ikiweza kutoa at least asilimia 50 ya fedha za maendeleo, basi Mfuko wa NEDF uongezewe fedha hata kufika shilingi bilion 50 - 100 ili vijana wengi zaidi waweze kupata start up capital na hata suala la uhaba wa ajira uondoke.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. ESTHER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa napenda kutoa pongezi zangu kwa Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Hasunga pamoja na Manaibu wake kwa wote wawili Mheshimiwa Bashungwa pamoja na Mheshimiwa Omary Mgumba kwa juhudi zao katika kuinua wakulima wa Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, nitapenda kujielekeza mchango wangu juu ya ushiriki wa vijana kwenye kilimo cha biashara kama ajira mbadala na hatima ya ustawi wa kipato cha mtu mmoja mmoja.

Mheshimiwa Spika, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 sambamba na rasimu ya mwaka 2017 ya Sera ya Taifa ya Ajira ikisomwa pamoja na mkakati wa Kitaifa wa kuwezesha vijana kwenye sekta ya kilimo (2016 – 2021) instruments zote hizi zimetia mkazo wa kutosha juu ya umuhimu wa kuwezesha vijana kujihusisha na shughuli za kiuchumi ikiwemo shughuli za kilimo cha kisasa.

Mheshimiwa Spika, sambamba na miongozo tajwa ya kisera na kisheria ikumbukwe kuwa kwa sasa nchi yetu ya Tanzania inazalisha graduates zaidi ya 700,000 kwa mwaka na kwa bahati mbaya graduates si zaidi ya 40,000 sawa na asilimia (6 – 10) ndio wanaoingia kwenye soko la ajira rasmi, lakini haitoshi Serikali imekuwa iki-spend takribani shilingi bilioni 427 kugharamia elimu ya vijana vyuo na vyuo vikuu kupitia HESLB.

Sambamba na hili pia, Serikali imekuwa iki-spend takribani kati ya Shilingi bilioni 20 mpaka 23 kwa mwezi kwenye utekelezaji wa sera ya elimu bure. Nguvu zote hizi ni vyema zikaakisiwa kwenye ukuaji wa uchumi hasa tunapoangalia ushiriki wa vijana katika muktadha mzima wa ajira kwani kwa kufanya hivi ndivyo tunavyoweza kushabihisha uwekezaji mkubwa wa Serikali kwenye elimu na ujuzi wa vijana wetu na uchumi endelevu wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishaandika hapo juu, juu ya sera ya mikakati ya kushirikisha vijana kwenye sekta ya kilimo ni dhahiri kwamba, bado tuna changamoto kubwa sana katika kutengeneza ajira za kilimo cha biashara kwa kundi kubwa la vijana. Changamoto tulizonazo kwa mantiki hii ni pamoja na yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kukosekana kwa mitaala ya somo la kilimo kwenye elimu ya awali, sekondari na hata kwenye baadhi ya vyuo vikuu visivyokuwa na mchepuo wa kilimo.

Mheshimiwa Spika, pili, kukosekana kwa usimamizi mzuri juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana chini ya Halmashauri zetu. Fedha zinazotoka (41%) kwa baadhi ya Halmashauri zetu zimekuwa zikitoka kama sehemu ya utamaduni na hakuna mechanism nzuri ya kuona fedha hizi zinakwenda kwenye kusudio la kuondosha tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu. Mafungu haya yangeelekezwa kwenye kilimo cha biashara na hata usimamizi ukawekwa vizuri, naamini vijana wengi wangeondokana na adha ya ukosekanaji wa mitaji na hata wangeweza kushiriki kwenye shughuli za kilimo cha biashara.

Mheshimiwa Spika, tatu, kwenye Bajeti ya Wizara ya Ardhi ya 2016/207 Wizara ya Ardhi chini ya Mheshimiwa Waziri Lukuvi alielekeza Wakurugenzi wote wa Mipango Miji kutenga maeneo maalum na mahususi kwa ajili ya vijana wetu ili waweze kushiriki kwenye kilimo. Pamoja na maelekezo na mikakati ya Wizara ya Ardhi katika kuona vijana wanapata maeneo ya kilimo, lakini bado hakuna kilichotekelezeka mpaka sasa. Vijana wamekosa hatima ya ajira zisizo rasmi pamoja na maneno mazuri ya baadhi ya waajiri.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2018/2019, Wizara ya Viwanda na Biashara ilitenga fedha kupitia Mfuko wa NEDF kiasi cha shilingi bilioni 17, ili kusaidia wajasiriamali wadogowadogo kama startup capital, lakini hakuna kilichotoka hata tunapokwenda mwisho wa mwaka wa fedha 2018/2019. Vijana wamekosa fedha za kushiriki kwenye sekta ya kilimo cha biashara kupitia Mfuko huu. Hata hivyo, vijana wamekosa kutumia fursa mbalimbali za kilimo biashara, mfano mwaka 2016/2017, Wizara ya Viwanda na Biashara ilitangaza kufungwa dirisha maalum kwa kundi la akinamama na vijana kushiriki kwenye zabuni za Serikali.

Mheshimiwa Spika, zipo taasisi mbalimbali za Serikali zinazonunua biashara za mazao mfano FNRA na hata Taasisi za Ulinzi na Usalama, Jeshi na Magereza ambazo zimekuwa zikitangaza tenda mbalimbali kwa kuwa vijana wetu hawajaandaliwa inakuwa ni vigumu vijana wetu kuweza kutumia fursa mbalimbali. Fursa za AGOA pia bado hazijatumiwa kutokana na kukosekana na mipango madhubuti ya Wizara ya Kilimo katika kushirikisha vijana kwenye masuala ya kilimo cha biashara.

Mheshimiwa Spika, ifuatayo ni sehemu ya ushauri wangu kwa Serikali:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, mradi wa kuwainua vijana kupitia mradi wa kilimo cha vizimba (greenhouse) chini ya Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ipitiwe upya na badala yake mradi huu ulenge zaidi katika kilimo shirikishi cha biashara. Pia mradi utoe dira na mwelekeo sahihi juu ya masoko ya bidhaa inayolengwa kufundishwa kupitia mradi huu.

Mheshimiwa Spika, mradi ulenge kutoa elimu ya mnyororo wa thamani ya mazao ya kilimo biashara, mradi ulenge kutoa ajira za kudumu kwa kuelekeza vyanzo vya fedha ambazo ni tengeo la vijana kwenye Wizara mbalimbali, mfano, Mfuko wa Vijana wa Taifa, fedha za vijana kupitia halmashauri zetu (4%). Serikali kupitia halmashauri zetu ielekeze kila halmashauri itoe sheria ndogo itakayotaka halmashauri zetu kutenga sehemu maalum ya ardhi ili vijana wapate mahali pa kuendesha shughuli za kilimo.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Elimu iandae mtaala maalum wa kilimo na vijana wetu wafundishwe nadharia ya kilimo cha biashara kutokea ngazi ya chini ya elimu.

Mheshimiwa Spika, pia Wizara iharakishe katika kutoa mkakati wa kitaifa wa kuhusisha vijana kwenye Sekta ya Kilimo. Mkakati huu bado unasomeka kama rasimu na siyo mkakati rasmi wa kitaifa.

Mheshimiwa Spika, kwa haya machache naomba kuunga mkono hoja ya bajeti Wizara ya Kilimo. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali, napendekeza Wizara ione umuhimu wa kuleta Sheria ya Mafuta Namba 21 ya Mwaka 2015 Bungeni ili Bunge liweze kufanya marekebisho ya sheria hii. Ni rai yangu Serikali iweze kurejesha mamlaka ya Waziri katika kutoa leseni za vitalu, lakini pia, vibali vya uchimbaji wa gas & oil. Ni ushauri wangu Serikali iweze kuondoa sharti la sheria la asilimia 3 kwenye Mfuko wa Rasilimali ya Gesi na Mafuta ili kuruhusu matumizi ya Mfuko wa Rasilimali ya Gesi na Mafuta kwenye miradi ya maendeleo. Mathalani shughuli za usambazaji wa gesi majumbani.

Mheshimiwa Spika, ni ushauri wangu kwa Wizara ya Fedha kuona umuhimu wa kutoa fedha yote kama ilivyoombwa na Taasisi ya TPDC juu ya uanzishwaji wa Kituo cha CNG (ie, Compressed Natural Gas) Mlalakuwa, Ubungo. Taasisi hiyo kupitia Wizara ya Nishati imeomba kiasi cha takribani TShs. bilioni 16; hapa ninapochangia mabasi ya UDART, yaani mabasi ya mwendokasi 300 yatakayoingia Tanzania Mwaka wa Fedha 2019/2020 yote yatatumia CNG. Mbali na hapo, tayari TPDC imeshapokea maombi ya wateja wakubwa wanne, wawili Kigamboni, wawili Kibaha, Pwani. Ninaona tuna sababu ya msingi ya kuhakikisha PST kupitia Wizara ya Fedha inatoa fedha zote kama ilivyoombwa na Taasisi ya TPDC.

Mheshimiwa Spika, pia ninashauri Serikali i-support pendekezo pamoja na kiasi cha fedha kilichoombwa na Wizara katika ukarabati wa Tank Number 8 la kuhifadhi oil & gas, yaani Strategic Oil & Gas Reserve Tanks, kwani kwa kufanya hivi Wizara itaondokana na adha ya ukodishaji wa maghala ya kuhifadhi mafuta na gesi. Tanzania leo hii ina reserve ya gesi kiasi cha futi za ujazo trilioni 57.54, lakini pia, Tanzania ina lita za petroli milioni 125.22, dizeli lita milioni 94.78 pamoja na mafuta ya taa na ya ndege lita milioni 18.34. Hivyo ninaona umuhimu mkubwa wa Wizara ya Fedha kuona umuhimu wa kutoa fedha zote za ujenzi na ukarabati wa Tank Number Eight kama ilivyoombwa na TPDC.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe nchi ya Japan ambayo haina gesi ardhini ina reserve kubwa ya gas & oil, na hata Trinidad; zote hizi zina reserve kubwa ya gesi kwa sababu walikubali kwanza kuwekeza kwenye miundombinu ya kuhifadhi oil & gas.

Mheshimiwa Spika, na mwisho, NAT Oil ambayo ni Taasisi ya Serikali kwenye biashara ya gesi na mafuta; ninashauri kwa moyo dhati Sheria ya Petroli iletwe Bungeni, ili TPDC iweze kushindana na kampuni za kigeni, kwa mfano Trafigura Oil & Gas Company from Singapore, Kampuni ya Addax, kampuni ya Uswizi iliyowekeza kwenye tasnia ya gesi na mafuta ambayo pia ndiyo kampuni ya Oryx. Vilevile hata Kampuni ya TOTSA from France yenye umiliki wa Total pamoja na Sahara from Nigeria.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. Ahsante.
The Written Laws (Miscellaneous Amendment) (No.2) Bill, 2016
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, nami nina furaha ya pekee kuweza kupata nafasi hii ya kuweza kuchangia katika Bunge lako hili Tukufu. Naomba nichangia Sheria ya Elimu Sura Namba 353 (The Education Acts Cap.353.)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee napenda kuipongeza Serikali kwa kuja na adhabu hii kali ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza ikamkomboa mtoto wa Kitanzania ili aweze kupata stahiki yake katika hii nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo mtoto wa kike amevalishwa taswira ya chombo cha starehe; leo mtoto wa kike amevalishwa taswira ya chombo cha uzalishaji; leo mtoto wa kike ametolewa darasani kwa sababu tu ya wale watu wenye uchu ya mahitaji ambayo kimsingi hayana tija katika maendeleo mazima ya nchi ya Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, labda nianze kuelezea tatizo hili la ndoa za utotoni. Ukiangalia ripoti ya WHO ya mwaka 2015 mwezi Juni, inatuambia kwamba Tanzania ni nchi ya pili ambayo inaongoza kwa ndoa za utotoni ikianziwa na nchi ya Nigeria. Ukija kwenye taarifa ya Amnesty International ya mwaka 2015, Novemba inakwambia Tanzania ni nchi pekee katika Bara la Afrika inayozalisha ndoa za utotoni 16 kwa siku moja; yaani kila siku moja tuna ndoa za utotoni 16.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda sana kuipongeza Serikali yangu kwa kuja na mustakabali mzima wa kuweza kukomesha tabisa hii mbaya ambayo imemtoa mtoto wa Kitanzania darasani na kumweka sehemu isiyokuwa na majibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, labda kwa kuanza kuchangia, niseme tu kwamba, hii adhabu ni nzuri na ni adhabu ambayo wote tuna imani nayo, lakini hii adhabu ya miaka 30 jela naomba nitoe maoni yangu; kimsingi ni adhabu ambayo nafikiri inabidi ifanyiwe marekebisho ili kuondokane na kuwa na sheria ambazo ziko makabatini zinakosa kwenda kutumika.
Ninasema hivi kwanini? Ukiangalia ripoti ya Amnesty International inayokwambia kwamba tunazalisha ndoa za utoto 16 kwa siku, hivi leo Tanzania tutahitaji kujenga Magereza mangapi kwa ajili ya kuweza kuwaadhibu hawa wanaoenda kinyume na sheria hii?
Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri kama hatutakuwa makini, tunaweza tukafika tukatoka kwenye priority yetu kama nchi, tukaenda sasa kujikita na vitu ambavyo pengine tutahitaji kuwa na suppliment budget kwenda huko. Kwa hiyo, nashauri, nafikiri ni vyema sasa Serikali ione umuhimu wa kuja na sheria ambayo itakidhi na itatoa jibu sahihi na dira sahihi katika kumkomboa mtoto wa Kitanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukiniambia unampeleka jela mtu ambaye anahusika kwenye kosa hili, kule tutapeleka wanafunzi. Pia ukiangalia mlengo wa nchi, tunataka kwenda kwenye uchumi wa kati: Je, tutajenga lockup ngapi? Hatuoni kwamba nguvu kazi ya vijana wa Kitanzania zitaishia lockup?
Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri Sheria ya Ndoa iangaliwe, ndiyo imebeba haya yote! Mkanganyiko wote unatoka kwenye Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kwa sababu Sheria ya Ndoa inaruhusu mtoto kuolewa akiwa na miaka 15 kwa idhini ya mzazi. Hiki kitu inabidi tukiangalie kwa umakini.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukija kwenye Sheria ya Vilevi ya mwaka 2008 inaruhusu mtoto wa Kitanzania miaka 16 kutumia pombe. Inabidi pia sambamba na hili, tuweze kuona umuhimu wa kuondokana na sheria kandamizi, sheria zisizo na tija katika malezi na makuzi ya kijana wa Kitanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nasema haya kwa sababu nchi ya Tanzania leo hii tumeridhia mikataba mingi. Tumekuwa na mikataba kwa mfano International Convensions and Eliminations of all Forms of Violence Against Women, yaani CEDAW ya mwaka 1999 lakini pia tumekuwa na Maputo Declaration, tumekuwa na The Law of the Child ya mwaka 2009, lakini pia tumekuwa na African Charter of the Right of the Welfare of the Child and Harmful Practices Against Women and Forced Early Marriages.
Mheshimiwa Naibu Spika, nasikitika kusema kwamba, kama hatutakuwa makini, tutaishia kwenye hizi sheria za Kimataifa ambazo leo tumezisaini, lakini bado ziko makabatini.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme mchango wangu kama ufuatao: nafikiri kwamba, pamoja na kupitia Sheria ya Ndoa na Sheria ya Vilevi, tukumbuke kwamba Tanzania tuna wiki tatu tu tumetoka kuridhia sheria inayoitwa The Modern Law in Eradicating Child Marriage ambayo tumeiridhia pale Swaziland. Tanzania kama nchi washiriki, tume-sign Mkataba huu wa Kimataifa kuondokana na ndoa za utotoni.
Kwa hiyo, ni vyema sasa Serikali iweze kuona umuhimu wa kupitia Sheria ya Ndoa, lakini pili, ifike mahali tuone umuhimu wa kuwa na hizi program, yaani program za malezi na makuzi, mfano Sexual Health Reproduction Training kwa mitaala ya Shule za Msingi na hata Sekondari.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Serikali ione ina wajibu sawasawa na sahihi kabisa katika kuona kwamba tunaondokana na tatizo hili. Pia nafikiri sasa Tanzania ije na mkakati maalum wa kuweza kuondokana na tatizo kubwa la ongezeko la kuzaliana, yaani ongezeko la idadi ya watu.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tuna watu milioni 45 kwa nchi ya Tanzania, lakini kama hatutakuja na mpango kabambe wa kuondokana na tatizo kubwa la ongezeko la watu, yaani ongezeko la kuzaliana, hata huko tunakotaka kwenda, nafikiri tunaweza tukakwama kama hatutakuwa makini. Pia mtoto wa kike ataona naye ana wajibu katika kuona kwamba naye anachangia ile growth ya 2.5 per annum kwenye suala zima la ongezeko la watu kwa nchi ya Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, nami naomba pia nichangie ile Labour Institutions Act Cap. 300. Nakubaliana kabisa na wazo la Serikali la kuweza kupitia sheria hii na pia nakubaliana kwamba kufanya mapitio katika sheria hii, ndiyo pale ambapo tunaweza tukapata mapato kwa ajili ya suala zima na dhana nzima ya Tanzania ya viwanda. Kwa sababu makusanyo yatakayotokana na hifadhi ya jamii ni dhahiri kwamba yanaweza kutumika vizuri kabisa katika kuondokana na suala la ajira kupitia Tanzania ya viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nafikiri katika kipengele hiki ni vyema sasa Serikali ikaja kama alivyosema pale Mheshimiwa Hawa Mchafu kwamba hii adhabu inayotolewa, shilingi laki moja bado ni ndogo sana kwa taasisi za Umma ambazo wengi wao wamekuwa wanakwepa suala zima la ukasanyaji na kuwasilisha michango hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini liko suala la Loans Board. Juzi Mheshimiwa Waziri pale katika taarifa zake, Profesa Ndalichako alieleza kwa kusikitika kwamba Tanzania leo suala zima la urejeshaji wa mikopo imekuwa ni kizungumkuti. Leo ninavyoongea, mwezi jana, Bodi ya Mkopo ilikuwa na changamoto kubwa sana kwenye suala la urejeshaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri pia, kama walivyofanya nchi ya Kenya kuingiza suala zima la penalty kwenye Katiba yao ya nchi, Serikali kupitia sheria hii ya Labour Institutions Act Cap. 300, ione na i-insist pale kwamba watu wote including waajiri watakaokiuka kupeleka marejesho yanayotokana na kusomesha wanafunzi, basi nao wapate adhabu kali kupitia huu Muswada.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo Bodi ya mkopo ilikuwa marejesho tunapaswa tupeleke…
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naunga mkono hoja kwa maana ya kwamba Sheria hii ya Ndoa za Utotoni na adhabu hii ipewe misingi yenye tija ili sheria hii iweze kutumika. Ninamaanisha kwamba badala ya miaka 30 kuwe na ile mizania ya adhabu ninachoongea hapa, badala ya…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, nilidhani unaunga mkono hoja unakaa, naona unaendelea kuongea.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, niwie radhi, sikuelewa kengele hizi zilivyogonga. Uniwie radhi sana, naunga mkono hoja kama nilivyowasilisha, ahsante.
Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, wa Mwaka 2016
MHE. ESTHER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii ili nami niweze kuchangia kwenye Bunge lako hili Tukufu, zaidi nitajikita kwenye Muswada huu wa Sheria ya Uvuvi kama ulivyowasilishwa kwenye kikao chako kwa siku ya leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kuipongeza Wizara ya Kilimo na Uvuvi, binafsi naona dhamira ya dhati kwa viongozi hawa wawili. Mimi mwenyewe nikiwa na Mheshimiwa Charles Tizeba pamoja na Naibu wake tumefanya vikao na Taasisi za Elimu ya Juu kwa maana ya graduates kwa mikoa sita na hii ni phase ya kwanza. Kwa utaratibu wa Wizara ambao wameuweka, naona dhamira ya dhati katika kuona kwamba vijana wetu wanaingia mashambani wanalima, pia watakapoingia kwenye mabwawa yao ya samaki wavune samaki. Pongezi zangu za dhati kwa Viongozi wangu Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri, Kaka yangu Mheshimiwa Ole-Nasha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nianze kabisa moja kwa moja kuchangia Muswada huu mzuri ambao umeletwa kwetu ili kwa pamoja tuweze kuona uchumi wa nchi yetu unaimarika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza kabisa kwenye Clause 6(1), nitapenda pale kwenye section (a) tuweze kuongeza baadhi ya maneno. Hii nasema ili tuwe na continuity nzuri. Ukisoma section (b) na (c) utaona kila kwenye function ya hii institute kunakuwa na maana; yaani kazi, jukumu la taasisi pamoja na maana halisi ya jukumu hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitapenda kwenye section (a) ambayo inasema kwamba, “the function of the institute shall be to carry out and promote the carrying out of the enquiries, experiments and research in fisheries and aquaculture and generally.” Kwa hiyo, naomba hapa tuongeze maneno yafuatayo, kwamba, moja ya jukumu la hii taasisi ni pamoja na
“carry out and promote the carrying out of the experiment and research so as to provide scientific data and information to enhance sustainable exploitation management and conservation of Tanzanian fisheries resources and promote aquatic environment of Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, nikienda kwenye ile Clause 6(3), hapa tunaongelea ushirikishwaji wa taasisi nyeti katika utafiti wa viumbe vya baharini. Ameliongelea pale Mheshimiwa mwenzangu aliyenitangulia, dada yangu Mheshimiwa Sakaya kwamba tuone sasa Serikali kupitia Muswada huu, taasisi za elimu ya juu zishirikishwe na zitumike kikamilifu katika nyanja hizi za utafiti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu kwanza, mimi ni mdau kwenye taasisi ya Elimu ya Juu, lakini pia uwakilishi wangu, nawakilisha Elimu ya Juu. Nimefanya kazi kwenye Taasisi ya Elimu ya Juu. Pale nimeona ambavyo Walimu wangu wameishia kukata tamaa, wanafanya research nzuri sana za kuweza kusaidia hii nchi, lakini research hizi zinabaki kufungiwa kwenye makabati. Taasisi za Elimu ya Juu zimekuwa ni centre of excellence, lakini hazitumiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara husika iweze kufanya na kupokea haya marekebisho na kuweza kuingiza ushiriki wa taasisi za utafiti, elimu ya juu, kupitia Taasisi ya Tume ya Vyuo Vikuu Nchini Tanzania kuona nao wanakuwa ni sehemu ya wadau katika kutoa ushauri katika Taasisi hii ya TAFIRI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja, asije akaniingiza kwenye kipengele (g) kuniambia kwamba, kuna kipengele (g) ambacho kinasema “and any other person or body of persons established by under any written laws which are performing the same functions as to those specified in sub-section (1).” Naomba asinipeleke huko.
Taasisi ya Elimu ya Juu ni taasisi nzito na ni taasisi yenye unyeti wa pekee katika masuala mazima ya tafiti katika Muswada huu ninavyouangalia. Kwa hiyo, naomba yenyewe itokee pale kwa uzito wake na kwa upekee kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija Part III, Clause (8); pale tunaongelea Composition and Proceedings of Board. Kitu ambacho nakiona hapa, “composition” ni neno limewekwa pale, lakini ukiangalia kwenye huu mtiririko, sioni composition ya Board of Directors. Wameanza pale kwa kueleza kwamba, there shall be a Board of Directors of the Institute, which shall be responsible for the exercise of the functions and the management of the Institute.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini unaposema “there shall be a Board,” hiyo bodi nani kaiweka? Inawekwa na nani? Number of Board of Directors, hatuoni; appointing authority by the Board of Directors, hatuoni; Appointing authority by the Chairperson of that Board, haipo; members composition, hatuioni. Hiyo Bodi inaletwa na nani na inahalalishwa na nani kuwepo pale? Kwa hiyo, tunahitaji maelezo kamili. Katika hili, naomba, Taasisi ya Elimu ya Juu ipewe nafasi yake katika hili suala zima la Board Composition. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikienda hapa Clause 12, utaona pale kwenye maneno “Director General and other staff of the Institute,” hapa tunaongelea appointment, functions and power of the DG. Tunaambiwa kwamba Mheshimiwa Rais ndiye atakuwa na mamlaka ya kumteua DG katika taasisi hii na wakatoa pale academic qualifications. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunaambiwa kwamba, General Director anatakiwa awe na Doctorate Degree in Fisheries au Aquaculture. Hii naomba niseme, inabidi tui-recast na badala yake tuseme kwamba, primary iwe ni First Degree and Second Degree in Fisheries or Aquaculture. Unaposema Doctorate Degree; huwezi kupata discipline ndani ya Doctorate Degree. Doctorate Degree is all about methodology and tools that has been attained by that particular person.
Kwa hiyo, kusema kwamba, a primary iwe Doctorate Degree kwenye field hii mimi nakataa. Naomba kwamba primary iwe ni first Degree and second Degree kwenye this particular field; na badala yake tuseme pia kwamba, awe na first Degree katika hizo subjects plus Doctorate Degree in related subject.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivyo? Ni kwamba katika Ph.D level unaweza ukawa na candidate ambaye amefanya Ph.D katika GIS in Marine Ecosystem, lakini unaweza ukawa na Ph.D Candidate ambaye amefanya GIS kwenye Climate Change and Marine Ecosystem, lakini unaweza ukawa na Ph.D Candidate ambaye amefanya Ph.D kwenye Development Studies na Fisheries.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kwenye suala la Doctorate Degree isiwe primary factor na badala yake First Degree na Masters Degree ndiyo iwe primary kwa sababu, hapo the only place tunaweza ku-capture discipline. Huwezi ku-capture discipline kwenye Doctorate Degree, huwezi! Hapo uta-capture methodology na tools ambayo haimsaidii mtu katika ku-head sections kama hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuongelea masuala ya Clause 19(1), conduct of research by local researchers. Hapa tumeona kwamba, local researcher anapoenda kwenye field ni lazima aandike proposal, aombe request kwenye taasisi husika; lakini nafikiri ili kuweza ku-safeguard our marine by diversity ni vyema kwanza tukaanza na ku-seek permission.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababu gani? Mtu anaweza aka-develop proposal akatumia gharama nyingi na muda, lakini atakapofika ku-submit kuomba permission akaambiwa haifai na ikawa redundant. Kwa maana nyingine, ni vyema kwanza mtu akaanza ku-seek permission ndipo aje ku-develop proposal.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, kwenye foreign researchers tunaambiwa kwamba, foreign researcher anatakiwa a-submit final report upon the completion of that particular research. Sidhani kama ni sahihi sana kwamba foreign researcher anapaswa ku-submit final lakini progressive report hazipo. Nasema hivi kwa sababu, sisi ni mashahidi, tumeona upotevu mkubwa na uharamia mkubwa kwenye Hifadhi za Taifa, ni kwa sababu, tunakosa controls.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukikosa controls kwenye ecosystem, tunataka nini tena? Tumeshanyang‟anywa maliasili kule kwenye mbuga zetu za Taifa; tena na kwenye viumbe vya bahari tunyang‟anywe kwa sababu tu ya kutokuwa na macho ya kuona vitu kama hivi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji control zilizoimarika. Kwa hiyo, ninaposema kwamba, mtu yeyote atapaswa kuomba permission, lakini pia, ku-submit progressive report, hii ni sehemu ya controls kuona kwamba, tunalinda na kuhifadhi maliasili ya Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, nina suala hapa ambalo Mheshimiwa ndugu yangu pale Halima Mdee jana aliliongelea, lakini sijui ilikwendaje, niseme tu tusione shida, hata kama mkipitisha kwangu, tusione shida, ipitishwe tu. Jana ndugu yangu pale, Mheshimiwa Halima Mdee alihoji, nami hapa nahoji…
MWENYEKITI: Ahsante.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia kwenye Bunge lako hili Tukufu. Kwanza kabisa naomba niseme kwamba naunga mkono hoja iliyoletwa mezani na kama tulivyoagizwa jana kwamba itakapofika pale haitalala itasainiwa hebu tuitendee kazi fursa hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nipende tu kuanza kueleza wenzangu kwamba Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi kwanza haijafilisika. Kwa nini nasema hivyo? Mkononi kwangu nimeshika Ilani ya Chama cha Mapinduzi na Mheshimiwa Waziri kaka yangu Mheshimiwa Nape Nnauye naye alikuwa ni mmoja mshiriki katika kutengeneza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikisoma ukurasa wa 216, aya ya 157, nitawasomea taratibu ili tuendelee ku-cement msimamo wetu kwa nini tunaona kwamba Muswada huu una tija kwa Watanzania walionyimwa fursa katika tasnia ya habari. Aya ya 157 inasema, ili kuendeleza tasnia ya habari na uhuru wa vyombo vya habari katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii 2015-2020 chama kitaielekeza Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uhuru wa vyombo vya habari na kufanya yafuatayo:-
Kipengele cha kwanza kinasema, kuharakisha mchakato wa kupitisha na kuanza kutekeleza Sheria ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Tunayo sheria hii na tutaitendea kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia imeendelea kusema hivi, kuimarisha uwezo wa Idara ya Habari Maelezo kama Msemaji Mkuu wa Serikali. Tunayo Idara ya Maelezo, naomba mrejee Part III, kipengele cha 4 na cha 5. Tunaye Mkurugenzi wa Habari Maelezo na hiyo ndiyo tunamaanisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 216, aya ya 157, kipengele (e) kinasema, kuanzisha Mfuko na kuwaendeleza wanahabari kitaaluma. Hii tunapata Part III, aya ya 21 pale utasoma Media Training Fund, haya yote yanapatikana huko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele (f) kinasema, kuhakikisha kwamba kunakuwepo na uhuru wa vyombo vya habari ili vitekeleze wajibu wake inavyopaswa kwa mujibu wa sheria. Napenda warejee Part IV, section ya 24 - 25 ambayo imeongelea Independent Media Council.
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda tu niwaweke wenzangu vizuri, unajua bahati mbaya sana wakati Chama cha Mapinduzi kinakaa kutengeneza Ilani na miongozo ya nchi hii ili kuleta heshima katika mifumo yote ya Serikali wenzetu walikaa na kutengeneza Ilani yao kufikiri ama kujielekeza kwenye kufufua wafu, lakini Chama cha Mapinduzi hakikujielekeza huko, tulikaa katika kutunga miongozo ambayo tunaiweka ndani ya mifumo ili nchi yetu iweze kupata heshima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasiasa wenzangu tumekuwa hodari sana na mahiri sana ku-point fingers kwa nchi zilizoendelea mathalani Kenya, ona Wakenya wamefanya hivi lakini bila kufunga mikanda, bila kupita kwenye transition kama hizi, bila kuweka mifumo hivi tunafikaje huko wenzetu walikofika? Hivi tunahitaji nini katika hili? Tunahitaji binoculars kuona haya, mbona tunahitaji macho ya kwenye miili yetu kuona haya. Inasikitisha sana na hili ni jambo la aibu. Pia sishangai kaka yangu Mheshimiwa Sugu ulikuwa na haki ya kuja na maneno kama yale na ngonjera kama zile, angekuwa ndugu yangu Mheshimiwa Semesi Sware tungekana urafiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba Muswada huu ni mzuri, tumeongea pale kwamba tunahitaji kutengeneza ajira ambayo italeta heshima kwa Mtanzania. Pia tunahitaji kulinda ajira hizi na ndiyo maana tukasema tunahitaji ku-secure ajira za mwanahabari tuwe na mikataba. Pia tukaenda mbali tukasema hata hisa Mtanzania aweze kumiliki hisa kiwango cha 57%. Sasa wewe unakuja unamtetea Mzungu ambaye huja-share naye utaifa, ambaye huja-share naye dini, ambaye hata ukipata upungufu wa damu hawezi kukupa damu yake, tunahitaji nini ndugu zangu hebu tumwogope Mwenyezi Mungu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishika vitabu paletukaapa tukumbuke viapo vyetu tulisema tunakuja kutumikia nchi yetu ya Tanzania. Mnataka kupotosha umma kwa kuwa tu tumepita kwenye siasa zenye ngonjera nyingi zisizokuwa na vitendo. Kipindi kimefika siasa ni lazima ziende kwa vitendo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kwenda haraka haraka kwa sababu muda haupo. Nikienda section 7 na hiki kipengele tumepigiwa sana makelele, kwenye obligation of the media houses na ilikuwa inajikita kuongelea obligation especially kwenye upande wa private media house. Kifungu cha 7(1)(b)(iv) kinasema:-
“To broadcast or publish news or issues of national importance as the Government may direct”.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba Mheshimiwa Nape Nnauye hiki kipengele kinatutendea haki na usibabaike wala isitokee unasitisha msimamo huu wala isitokee unafanya amendment katika mlango huu. Mlango huu ni mlango ambao utatunza amani ya nchi yetu, lakini pia ni mlango ambao utafunga kila aina ya pesa chafu zilizokuwa zinapitia katika mlango huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwape mfano, mimi pamoja na wenzangu kwenye Bunge hili hili tulipata ridhaa ya kusafiri na kwenda nchi ya South Afrika na Mheshimiwa Ally Saleh pale akirudi atakuwa shahidi itaingia kwenye Hansard aje ani-prove mimi kwamba naongea uongo hapa. Nahitaji Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana aliweke hili katika regulations na atoe maelekezo sahihi kabisa bila kupindisha ni mambo yapi ambayo yatapaswa kutangazwa ama kuwa published kwenye private media house na ni mambo gani ambayo hayapaswi kutangazwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipokwenda South Africa ndugu zangu baadhi watakumbuka haya akiwepo kaka yangu Mheshimiwa Zedi pale, tulilipiwa business class. Tumeenda kule kama Wabunge wenye dhamana ya kuongoza wananchi tunaenda kuambiwa tuje ku-promote lesbianism and gayism, bisexual transgender na tulisafiri na mwandishi wa habari ambaye ametoka kwenye private media house. Vitu hivi ni vya kusikitisha, vya kudhalilisha, tunapewa mizigo kuja kuleta nchini mwetu na mwandishi wa habari amelipiwa business class kuja kuhubiri habari za lesbianism and gayism. Leo hii mnasema kwamba tuache milango hii wazi Mheshimiwa Nape kaka yangu haiwezekani. Haiwezekani tukaacha milango hii wazi, haiwezekani kabisa, mwenye macho aone haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende kwenye Bodi ya Ithibati. Dada yangu Mheshimiwa Jenista Mhagama anayesimamia ajira za vijana…
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja asilimia mia na ndugu zangu tunaoendelea kuunga mkono tuunge kwa ujasiri wa hali ya juu.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2016
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia kwenye Bunge lako hili Tukufu. Kwanza napenda pia kumpongeza Mheshimiwa Rais, pia nimpongeze Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana pamoja na Naibu wake kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kumtendea haki kijana wa Kitanzania ili naye aweze kupata fursa ya kuweza kwenda elimu ya juu, kwa maana kwamba fursa ile ya mkopo ya elimu ya juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinasema kwamba, kwenye bajeti ya mwaka 2015/2016, Bodi ya Mikopo ama Wizara ya Elimu iliweza kutenga shilingi bilioni 340 na wanufaikaji katika Mfuko huo walikuwa ni wanafunzi 90,000. Hata hivyo, baada ya Mheshimiwa Rais kuingia madarakani na kupitia ilani na ahadi yake kwa wananchi alitambua dhamana yake aliyopewa na wananchi na hata kuongeza fursa ile ya mkopo kutoka bilioni 340 mpaka bilioni 473 kwa kipindi cha miezi mitatu; hili tunabidi tutoe pongezi za dhati kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanza kuchangia kwenye Muswada huu au Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria hii ya Bodi ya Mikopo, naomba nianze kujikita kwenye kifungu kile cha 17 ambacho kinaongelea board composition ya Bodi hii ya Mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yameletwa mapendekezo kwako kwamba na NACTE pengine na wao wapate nafasi. Mimi nimeenda mbali nikaona kwamba, suala la affirmative action ni suala muhimu sana kwetu sisi akinamama, nafikiri tunahitaji representative from women collision platform ambaye atakuwepo pale katika kutetea maslahi mazima ya masuala ya gender.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema hivyo kwa sababu, suala la gender au suala la usawa wa kijinsia ni suala nyeti sana. Hii ni agenda ya kidunia, ni agenda ya Watanzania, lakini pia ni agenda yetu sisi wanawake wa Bunge hili, yaani Women Parliamentary Conquers. Tunaomba nafasi ya mwakilishi kutoka platform ya wanaharakati wa masuala ya gender.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikienda pia kifungu cha 18 utaona pale tunaongelea liability and obligation of loan beneficiary. Ukisoma pale 19 section (1) inaongelea kwamba ni wajibu wa loan beneficiary kuweza kurudisha mkopo ndani ya mwaka mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda section 19(5)(a) inaongelea kwamba, beneficiary who engage in self-employment, any trade or occupation of professional shall, yaani hapa Serikali inajaribu kumtambua kijana ambaye ame-struggle aliko struggle, akafika sehemu akajipatia kipato ili aweze kulipa mkopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunafika hapa kuona kwamba suala la ajira ni suala la kijana aweze ku-struggle mwenyewe na kuweza kutoka. Ni dhahiri kwamba Serikali, pengine inajivua jukumu hili, sisi Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye bajeti iliyopita, tulisimama hapa tukasomewa mipangilio ya Serikali yetu hii katika kumkwamua kijana wa Kitanzania. Kwa sababu, bila ajira hakuna kulipa hayo madeni na kinachotukalisha hapa ni ajira kwa Mtanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulisema kwamba Mfuko wa Vijana wa Taifa, utengewe bilioni moja. Kaka yangu Mavunde pale, amekuwa na jitihada kubwa sana za kutaka kusaidia vijana wenzake, lakini atakwama kama Mheshimiwa Mpango hataweza ku-release zile pesa ziende pale kujenga ajira ya Mtanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tofauti na mpangilio wa ajira, ni kwamba tunao utaratibu mbovu sana kwenye Bodi hii ya Mikopo. Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana, kwenye hili nitaomba tusikilizane. Iko hivi, nasema utaratibu mbovu pamoja na changamoto tulizonazo, kwamba pesa hizi hazirudi, lakini pia kuna utaratibu mbovu ndani ya board hii. Mheshimiwa Waziri ni shahidi. Ukienda pale Chuo cha Kampala International University (KIU), Bodi ya Mikopo ina-release pesa nyingi kuwasomesha vijana wa Kitanzania kwenye fani ya Ufamasia, lakini ukienda kwenye Baraza la Mafamasia Tanzania, vijana wale hawaajiriki popote. Huu ni utaratibu mbovu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namsihi Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana aliangalie hili suala kwa macho yenye upana, kwa sababu inawezekana tukatambua nguvu zake na jitihada zake, lakini bado akakwamishwa na watendaji ambao bado hawajielewa kwenye nafasi zao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nauliza hivi inashindanika nini kwa Bodi ya Mikopo ku-release pesa za kutosha kuongeza enrolment kwa chuo hiki cha Dodoma ambapo tayari…
Mheshimiwa Mwenyekiti, na ninasema kwamba tusikilizane, nilichosema kwenye bajeti ya mwaka 2014/2015, bajeti iliyokuwa imetengwa ni shilingi bilioni 340. Bajeti ya mwaka 2015/2016 ilitengwa shilingi bilioni 473. Kwa hiyo, nilichoongelea hapo ni mafaniko ambayo tunayapata ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba unilindie muda wangu naomba kuendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo nilichokuwa nimejenga hoja yangu ni kwamba, hebu tuone umuhimu wa kuweza kudahili wanafunzi wa kutosha kwa chuo chetu cha UDOM kwa sababu pale kuna College of Health ambayo nafikiri tukijengea uwezo tukamaliza hii miundombinu ambayo iko pale, ambayo pengine tunafikiri bado inaweza isi-accommodate vijana kwa kiwango kile tunachokitaka. Tukimalizia infrastructure ambayo iko pale UDOM ni dhahiri kwamba tutapeleka pale vijana, watakopesheka na ni dhahiri wataingia kwenye mfumo wa kuajirika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na nasema hivi kwa sababu, ukiangalia takwimu, hizi ni takwimu za juzi tu, nimezipata siku ya Ijumaa. Tunasema kwamba, kwenye enrolment of this academic year, ninavyoongelea Ijumaa iliyopita. Takwimu zinasema hivi, tulikuwa na wanafunzi 7311, ambao walikuwa wanatakiwa kudahiliwa Chuo Kikuu cha UDOM, lakini mpaka siku ya Friday kulikuwa na wanafunzi 3906 sawa na asilimia 50.3 ambayo tayari walikuwa wamepata mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tukijaribu kufunga Mfuko ambao unavuja, kule KIU tukauleta pale UDOM ni dhahiri wanafunzi hawa wataingia kwenye mfumo wa ajira. Kwa hiyo, huu utaratibu uangaliwe upya, sio utaratibu wenye afya na sio utaratibu ambao utaweza sisi kutufikisha kwenye azma ya kumsaidia mtoto wa Kitanzania na kwenye azma ya kuona kwamba, Mfuko huu unashindwa kukidhi malengo ya Tanzania tunayoitaka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo suala hapa ukisoma section 19. Pale naanzia (a) ambayo inaongelea hiyo hiyo liability and obligation of loan beneficiary. Utaona kwamba ni jukumu la mfanyakazi au la mtumishi aliyeajiriwa kuhakikisha kwamba pesa zinakatwa. Lakini pesa hizo, ahakikishe yeye pamoja na majukumu ya mwajiri, huyo huyo ahakikishe pesa inaingia Loans Board.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nifike kusema kwamba yawezekana labda Loans Board imepungukiwa uwezo wa kuleta ufanisi katika board ile. Basi ninachoshauri ni kwamba, kwa kuwa tunaona majukumu ya Board tumpe na mtumishi ambaye ameajiriwa, kwenye utumishi wa umma, kwamba iwe ni jukumu lake kuhakikisha pesa zinakatwa na mwajiri, pesa zinaenda Loans Board. Pengine tuone umuhimu wa kuweza kushirikiana na financial institutions na kutoa hili jukumu la Loans Board, kulipeleka kwenye financial institution na sisi tukalipa management fee ili tuweze kuondokana na mizigo ambayo tunafikiri kwamba haitatufikisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu, bajeti nzima ya kuendesha haya masuala ya uratibu wa Mfuko huu, inafika karibu bilioni 30. Kama tutapeleka kwenye financial institution ni dhahiri kwamba hizi pesa bilioni 30, tutaokoa billions of money tukapeleka kwenye Mfuko huu na vijana wetu wakazidi kufaidika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kwenda kwenye section ya 20 ambayo inaongelea obligation ya employer. Tunaona pale kwenye section ya 21(1) inaongelea kwamba kutakuwa na adhabu, pale ambapo mwajiri atakuwa amekata makato ya mwajiriwa ambaye ni loan beneficiary wa Loans Board na akashindwa kuwasilisha pesa ile Loans Board.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba nina mashaka ipo changamoto kwamba mifumo ya board haisemezani yenyewe kwa yenyewe. Central system admission haisemezani na Loans Board, Loans Board haisemezani…
MWENYEKITI: Ahsante, kengele ya pili.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia kwenye Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimpongeze Waziri mwenye dhamana kwa hiki alichotuletea mezani. Sheria hizi mbili kimsingi zimelenga kuleta ukombozi wa kiuchumi nchini Tanzania. Sheria hizi mbili zimejaribu kuleta uhalali wa umiliki wa maliasili ya Tanzania pia zimejaribu kuweka umuhimu wa Bunge kuwa kama chombo pekee cha kuweza kupitia mikataba yote yenye masharti hasi na mikataba yote isiyo na masharti hasi ili kuendana na Azimio ambalo Tanzania kama nchi tumeridhia, Azimio Namba 1803 lililoazimiwa na United Nation General Assembly 1962. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hivyo tu sheria hizi mbili zimelipa Bunge dhamana kubwa ya kupitia mikataba hii ili kuweza kulinda maslahi mapana ya Taifa. Sheria hizi pia zinaendana na Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo pia inasema kwamba Bunge litakuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyote ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu. Kupitia wasilisho la Miswada hii miwili ya sheria ni kwamba sasa Bunge linapewa hati na mamlaka kamili ya kuweza kupitia mikataba ambayo itakuwa inaletwa Bungeni kwa maslahi mapana ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zimekuja opinions, tunafikiri kwamba Bunge pamoja na kupitia pia waweze ku-ratify, nadhani hii ni double standard. Ukiangalia Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumepewa nafasi ya kuweza kuisimamia na kuishauri Serikali. Tunapoenda kusema tunataka tu-ratify, sisi Wabunge tuna dhamana ya ku-ratify International Conventions tu kwa nafasi zetu katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Kwa hiyo, mimi bado napinga na ninasema kwamba hapana tuna kila sababu ya kuona kwamba Muswada huu ni mzuri na una maslahi mapana ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, opinion nyingine ilikuwa suala la muda. Niseme tu tofauti na watu wote waliosimama kupinga Miswada hii kutokana na suala la muda kwa kufuta kumbukumbu zao juu ya Muswada wa Sheria ya Habari ambao ndiyo hawa walitusumbua lakini ukapita. Pamoja na hao waliochangia, watu wengine walioweza kuchangia wakifanana na sura zao au mitizamo yao ilikuwa ni Chama cha Bodaboda Dodoma, wauza mitumba nafikiri Dakadaka Group na Lamkachema Group. Ukisoma ripoti ya Kamati, ukurasa wa 10 utaona mawazo yao hayo yote yanafanana na hiki ambacho wamekisema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wamekuja wadau na wadau ambao sisi tuliweza kuwaelewa kwa ukaribu na pengine mimi kwa hofu yangu, nilifikiri wangeweza wakatukana kwenye hili. TLS ambao wao ndio wamemtoa Rais nafikiri wa Dunia au ni Rais wa Tanzania wa upande huo wa sheria walikuja wakai-support Serikali. Mimi niko tayari kupokea adhabu yoyote kutoka kwenye Kiti chako, TLS walianza kusema wamepata muda wa kutosha, wanashukuru Serikali imewapa muda wa kutosha katika kufanya uchambuzi wa sheria hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia sheria hizi, hii Permanent Sovereignity ina vifungu nane tu lakini ni A3 iliyotumika hapa, kuna page mbili ukitoa preamble, two pages! Hebu tuwe wa kweli na tuache wizi, huu ni wizi. Unakaa hapa unalipwa posho kusoma kurasa mbili za A3, unaniambia kwamba unahitaji some ages?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli inanisikitisha, muda tuliotoa unatosha. Mheshimiwa Mnyika atakumbuka tumeanza ku-discuss Ijumaa, tulikuwa na Kamati ya Mheshimiwa Mchengerwa, tulikuwa na Kamati ya Mheshimiwa Doto Biteko lakini hata yeye tunafahamu alikuwa na Kamati yake ambapo aliendesha mpaka usiku wa manane jana. Sasa huu muda tunaolalamika hautoshi ni muda upi tena? (Makofi)212

Mheshimiwa Naibu Spika, tusisahau, Mheshimiwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia kwenye Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimpongeze Waziri mwenye dhamana kwa hiki alichotuletea mezani. Sheria hizi mbili kimsingi zimelenga kuleta ukombozi wa kiuchumi nchini Tanzania. Sheria hizi mbili zimejaribu kuleta uhalali wa umiliki wa maliasili ya Tanzania pia zimejaribu kuweka umuhimu wa Bunge kuwa kama chombo pekee cha kuweza kupitia mikataba yote yenye masharti hasi na mikataba yote isiyo na masharti hasi ili kuendana na Azimio ambalo Tanzania kama nchi tumeridhia, Azimio Namba 1803 lililoazimiwa na United Nation General Assembly 1962. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hivyo tu sheria hizi mbili zimelipa Bunge dhamana kubwa ya kupitia mikataba hii ili kuweza kulinda maslahi mapana ya Taifa. Sheria hizi pia zinaendana na Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo pia inasema kwamba Bunge litakuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyote ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu. Kupitia wasilisho la Miswada hii miwili ya sheria ni kwamba sasa Bunge linapewa hati na mamlaka kamili ya kuweza kupitia mikataba ambayo itakuwa inaletwa Bungeni kwa maslahi mapana ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zimekuja opinions, tunafikiri kwamba Bunge pamoja na kupitia pia waweze ku-ratify, nadhani hii ni double standard. Ukiangalia Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumepewa nafasi ya kuweza kuisimamia na kuishauri Serikali. Tunapoenda kusema tunataka tu-ratify, sisi Wabunge tuna dhamana ya ku-ratify International Conventions tu kwa nafasi zetu katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Kwa hiyo, mimi bado napinga na ninasema kwamba hapana tuna kila sababu ya kuona kwamba Muswada huu ni mzuri na una maslahi mapana ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, opinion nyingine ilikuwa suala la muda. Niseme tu tofauti na watu wote waliosimama kupinga Miswada hii kutokana na suala la muda kwa kufuta kumbukumbu zao juu ya Muswada wa Sheria ya Habari ambao ndiyo hawa walitusumbua lakini ukapita. Pamoja na hao waliochangia, watu wengine walioweza kuchangia wakifanana na sura zao au mitizamo yao ilikuwa ni Chama cha Bodaboda Dodoma, wauza mitumba nafikiri Dakadaka Group na Lamkachema Group. Ukisoma ripoti ya Kamati, ukurasa wa 10 utaona mawazo yao hayo yote yanafanana na hiki ambacho wamekisema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wamekuja wadau na wadau ambao sisi tuliweza kuwaelewa kwa ukaribu na pengine mimi kwa hofu yangu, nilifikiri wangeweza wakatukana kwenye hili. TLS ambao wao ndio wamemtoa Rais nafikiri wa Dunia au ni Rais wa Tanzania wa upande huo wa sheria walikuja wakai-support Serikali. Mimi niko tayari kupokea adhabu yoyote kutoka kwenye Kiti chako, TLS walianza kusema wamepata muda wa kutosha, wanashukuru Serikali imewapa muda wa kutosha katika kufanya uchambuzi wa sheria hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia sheria hizi, hii Permanent Sovereignity ina vifungu nane tu lakini ni A3 iliyotumika hapa, kuna page mbili ukitoa preamble, two pages! Hebu tuwe wa kweli na tuache wizi, huu ni wizi. Unakaa hapa unalipwa posho kusoma kurasa mbili za A3, unaniambia kwamba unahitaji some ages?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli inanisikitisha, muda tuliotoa unatosha. Mheshimiwa Mnyika atakumbuka tumeanza ku-discuss Ijumaa, tulikuwa na Kamati ya Mheshimiwa Mchengerwa, tulikuwa na Kamati ya Mheshimiwa Doto Biteko lakini hata yeye tunafahamu alikuwa na Kamati yake ambapo aliendesha mpaka usiku wa manane jana. Sasa huu muda tunaolalamika hautoshi ni muda upi tena? (Makofi)212

Mheshimiwa Naibu Spika, tusisahau, Mheshimiwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania wa Mwaka 2017
MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi hii, naomba nijikite moja kwa moja kwenye Muswada.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuchukua fursa hii kuwapongeza Mawaziri kwa kazi yao nzuri. Kimsingi, nikianza na Section 7(1) napata picha na hisia kwamba tumefika mahali ambapo tunajaribu kutengeneza mwendelezo wa sheria.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoanza kusema, nasema naungana kabisa na Serikali kwa wazo lao na kwa wasilisho lao la kuweza kuleta Muswada huu, lakini pia nikiwa nasoma Muswada huu nimefika kupata feelings na mawazo kwamba huu ni wakati pia wa kufanya mwendelezo na finishing kwa hizi sheria mbili au tatu tulizozipitisha kipindi ambapo tunafanya mapitio ya Sheria ya Madini.

Mheshimiwa Spika, ukisoma Section 7(1) naona kabisa pale gist ya Serikali ni pamoja na kuona kwamba ile Natural Wealth and Resources Permanent Sovereignty Act, tunapata mwendelezo wake kwenye end to end controls. Kwa hiyo naungana na Serikali kwenye wazo kwamba kutakuwa na majukumu sole mandates of corporation ambayo hayataingiliwa na mtu awaye yeyote na ikiwemo masuala ya madini na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Spika, lakini pamoja na kuungana na Serikali katika wazo hili, napata maswali ambayo pengine nafikiri ni vizuri kama Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-wind up ajaribu kutupitisha ili kwa pamoja tuweze ku-own hii sheria kama wasimamizi wa shughuli za Serikali.

Mheshimiwa Spika, najaribu hapa kujiuliza, ni sawa Serikali itafanya majukumu haya, hakuna mjadala na ili tuweze kulinda sheria zetu ambazo sisi pia tunazipitsha hapa Bungeni, lakini nafika pia kujiuliza kwamba kama ambavyo Wabunge wengine wamesema, pengine ni sawa Serikali itakuwa key player, lakini wakati huohuo itakuwa ni mdhibiti wa shughuli hizi za wakala wa shughuli za baharini, lakini sasa najiuliza, nani atakayekuwa nafanya oversight, who is the oversight body kwenye masuala haya mazima.

Mheshimiwa Spika, lakini pia ninapojaribu kuangalia mtiririko huu wa Section 7(1), najaribu pia kukumbuka kwa harakaharaka tulipokuwa tunafanya mapitio ya Sheria ya Madini, tulijaribu pia kuona baadhi ya mashirika ambayo hayafanyi vizuri tuka-mention STAMICO. Sasa mimi sipingani na Serikali na naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja, lakini nitashukuru kupata mwelekeo wa Serikali, ni nani atakayekuwa anafanya oversight functions kwenye muktadha mzima kulingana na section hii.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia muktadha mzima wa section hii pia, tunaona kwamba Serikali itakuwa ni key player kwenye hii business, lakini wakati huohuo atakuwa regulator na najaribu kuangalia kama mimi ndiye nitakayefanya na mimi ndiye nitakaye-regulate, sasa nani atakaye-perform oversight function. Sina tatizo, ni suala la uelewa. Kwa hiyo, nafikiri ni vyema kama Serikali ikija na majibu ya kutuelewesha, kwa sababu umekuwa ni mtazamo wa watu wengi humu ndani.

Mheshimiwa Spika, nakuja Section 7(3); inasema kwamba hakutakuwa na mwingiliano, hakutakuwa na any organization au institution au kampuni ambayo itaingilia majukumu haya ya hizi sole assignments za Serikali, yaani kwa maana ya kwamba hakutakuwa na mwingiliano wa hizi biashara ambazo zitafanywa na Serikali.

Mheshimiwa Spika sasa ukija Section 7(3) inatoa adhabu ikiwa mtu ataingilia majukumu haya yaliyotamkwa ambayo yatakuwa ya Serikali tu, adhabu yake itakuwa ni miaka isiyopungua miwili, lakini ukienda Section 42(2) utaona
kwamba disclosure of information mtu anapewa adhabu ya mpaka kifungo cha miaka mitano.

Mheshimiwa Spika, sasa nikija kwenye major offence kama hii unaona kwamba kuna penalty ambayo kimsingi haijibu tija ya section kama hii napata hofu. Naomba atakapokuja Waziri ajaribu kuona kwamba, mimi nashauri kwamba at least isiwe chini ya miaka mitatu badala ya ilivyowekwa hapa miaka miwili. Kama kweli tunataka kuweka controls katika muktadha mzima wa sheria hii.

Mheshimiwa Spika, nikija Section (9) inaongelea power to suspend and revoke licence. Sina tatizo kwenye kipengele hiki lakini ni suala tu nafikiri la uelewa. Ukiona hapa Section 9(1) inasema kwamba Director General anaweza ku- issue revocation of the licence kwenye mazingira ambayo yatatolewa na yeye, yaani kwa maana nyingine hakuna legal instrument inayotoa mazingira ya ku-nullify hiyo licence au kuifuta leseni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nafikiri kwamba ni vyema tukajaribu pia ku-envy kauli za Mheshimiwa Rais ambapo mara nyingi akikaa na wawekezaji anajaribu kuona kuna umuhimu kabisa wa ku-create fair environment for private sector participations, especially kwenye biashara kubwa kama hizi. Kwa hiyo maana na kiu yangu ni kuona tunatengeneza mazingira rafiki kwa ushiriki wa private sector kwenye masuala haya muhimu.

Mheshimiwa Spika, utaona hapo kwamba hata aki- suspend leseni, muda wa ku-suspend leseni pia utakuwa determined na yeye. Naomba kutoa experience ndogo sana ambayo nimekuwa nikifundishwa ninapokuwa nashiriki masuala ya Kamati yangu chini ya Mheshimiwa Mtemi Chenge. Tulikuwa tunaona kipindi fulani Petroleum Act ambayo ilikuwa na ukakasi sehemu fulani ambapo tulijaribu kuishauri Serikali na ikafika mahali ikatukubali. Najaribu kutengeneza loophole ya kitu kama hiki kama hakitaangaliwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, kwenye Sheria ile Petroleum Act walisema kwamba kutakuwa na mazingira fulani ambayo Mheshimiwa Waziri amepewa mamlaka ya ku-localise on transit petroleum goods ambayo yalikuwa pengine yanasafirishwa kwenda nje ya nchi, yeye anaweza ku- declare a state of emergency. Yaani unampa Waziri nafasi ya ku-declare state of emergency, lakini kinadharia yapo mambo ambayo sisi Waheshimiwa Wabunge tunayafahamu, tuliona watu walio-abuse nafasi zao. Yupo mtu ambaye nafikiri aliwahi hata kutumia nafasi hii vibaya aka-localise on transit petroleum goods mwaka 2015 na akaiingiza Serikali kwenye hali ya hatari kabisa na ikawa na sura kama ni sehemu ya uhujumu uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo loophole kama hii kumwachia Waziri aweze ku-determine; kwanza tunaweza kujikuta tunafuta mazingira mazuri au rafiki kwa wawekezaji wa nje kuweza kuwekeza katika sekta hii; nikitambua kwamba Serikali yako majukumu ambayo watafanya wao kabisa hayataingiliwa, lakini yapo majukumu au shughuli za biashara ambazo zitafanywa na mawakala.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo rai ni kwamba, naomba ingekuwa vizuri kama tunge-specify huo muda ambao utafuta leseni na mtu ambapo anaweza akaomba upya. Pia tuweze kuona mazingira ambayo yanapelekea mtu kufutiwa leseni; au kuwe na Advisory Board ambapo Mheshimiwa Waziri akiona kitu kimeenda contrary basi anaweza aka-seek opinion ya Advisory Board kuweza kumshauri ili hata yeye aweze ku-endorse penalty kama hii.

Mheshimiwa Spika, haya yote ni katika ku-create transparency lakini pia ni katika ku-enforce mazingira rafiki kwa private sector participation kwenye masuala haya. Naongelea section 11, section 11 pale kuna marekebisho mengi lakini kwa harakaharaka nimechukua amendment ya Serikali, nimeiona iko well accommodated kwa hiyo sitaigusa; utaona kuna repetition nyingi nadhani hizo minor acha niziache niende harakaharaka;

Mheshimiwa Spika, nikienda section 13, hapa kuna vitu ni minor lakini nafikiri mradi document inatoka kwa Mheshimiwa Profesa Mbarawa ni vizuri tukaangalia. Ukisoma section (i) inasema approve nilikuwa na-recommend kwa sababu atakumbuka hapa Mheshimiwa Angela Kairuki juzi tulileta miscellaneous amendment na wakasema masuala yote remuneration or salary or matter related to salaries lazima yawe approved na President Office, Permanent Secretary establishment. Kwa hiyo, nashauri Bodi; kama Bodi haina mamlaka ya ku-approve mafao, mishahara, wala kitu chochote, badala yake ita-recommend kwenye relevant authority, haina mamlaka ya kufanya hivi kama kweli tu kwa kuwa naamini tuko hapa katika kusimamia sheria tunazozitunga lakini si kufanya double standard.

Mheshimiwa Spika, section hiyo hiyo, utaona hapa wanaongelea ku-approve Organization structure and scheme of service; lakini anaongea tena vitu vingine including assessment of need establishment branches; these are two different things; nafikiri hapa tu- decompose na badala yake including assessment iwe ni new paragraph na ianze carring out the appraisal of the Organization strategic plan. Kwa hiyo hapa hii haina mahusiano organogram haina mahusiano na hiyo appraisal of the strategic plan; kwa hiyo I think hapa tume-condense two things at per.

Mheshimiwa Spika, ukija tena (k) to approve changes salaries; nafikiri ni vyema tuka-amend; lakini pia ukija; (m) approve code of conduct ipo kwenye Labour Law, approve, supervise financial regulation hizi zote nafiki ni better kama tungesema ku-recommend Governance documents ambapo Governance documents kuna scheme of service, kuna staff regulation, financial regulation na vitu kama hivyo. Kwa hiyo hii inakuwa kama ni repetition na ina-create unnecessary noise.

Mheshimiwa Spika, nakwenda section 15, hii inaongelea renew of the contract ya Director General; kama ulivyoona unyeti wa taasisi hii ambayo inakwenda kuanzishwa na Serikali na wasiwasi wa wajumbe wengi tukiona kwamba pengine Serikali inashindwa kuleta ufanisi wenye tija katika sekta hii. Nashauri kwenye ku-renew contract mtazamo wetu uwe kwenye performance base pay; lakini pia renew of the contract should be upon the satisfactory performance of an individual persons; yaani isiwe tu kwamba mimi ku-renew mkataba wako ni automatic iwe upon satisfactory performance. Lakini hapa ipo upon terms of reference ambazo ziko kwenye mkataba wa barua; kwa hiyo naomba hiki kitu kwa kuwa unyeti wa taasisi hii tunayokwenda kuifanya isiwe ni automatic. Tujaribu kuweka utofauti na kweli tuoneshe tunataka tupite kwenye njia iliyo sahihi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa baraka zako nitaendelea kuzilinda.

Mheshimiwa Spika, ukija section 25 tunasema kwamba pale marginal note inasema offices and other staff of the corporation, of course nitajikita kwenye item (2), anakwambia “The Corporation may appoint consultants and experts of the Corporation in various disciplines on such terms and conditions as the Corporation be determine, its quite fine; sina tatizo lakini nafikiria kwa sababu sisi nasi ni waumini wa local content policy, nafikiri kwamba Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-wind up aweze kutuonesha mazingira haya ya hizi ku-sub contract za taasisi na kwenye masuala ya experts na consultants, ushiriki wa Watanzania katika muktadha mzima wa biashara hii ya uwakala wa shughuli za baharini basi tuweze kuona hapo unatuambia nini ili nasi kama wawakilishi wa wananchi tuweze kwenda kujenga hoja huko tunakotoka.

Mheshimiwa Spika, naenda pia section 40, section 40 inaongelea engagement of contract or sub-contractor and supplies. Section 40(1) utaona pale kwamba wanasema shirika litafanya kazi yake kulingana na utaratibu wa kisheria, mojawapo ni katika ku-comply na sheria na taratibu za PPRA hapa alipokuwa anamaanisha nafikiri hivyo. Hata hivyo, tunaposema kwamba its function unless the contractor, subcontractor or supplier is licensed or registered by a proper authority or institution.

Mheshimiwa Spika, to me nimejiuliza what is proper authority, kwa sababu the proper thing to me might not be a proper thing to you; to me I suggest this should be replaced by relevant authority and a not proper kwa sababu relevant it command effectiveness, it command efficient and all that, kwa hiyo nashauri kwamba hii proper iondoke na badala yake ije relevant ambayo ndiyo inakuwa tuna-reflect PPRA.

Mheshimiwa Spika, ukisoma pale item (2) of the same section 40 tumeona kwamba kuna penalties ambazo zimekuwa established pale; lakini utaona kwamba mtu akienda kinyume, aki-breach matakwa ya kisheria na hata ku-engage watu ambao hawako recognized na PPRA, inasema kwamba mtu atapigwa faini not less than 20 million; lakini unaona kabisa kwenye disclosure of the information ukiangalia item 44(2) disclosure of an information of an individual person faini inaenda mpaka milioni 50. Kwa hiyo nafikiri hapa pengine tuongeze adhabu kwa sababu nia hapa ni kuweka controls; badala ya hii 20 milioni iende mpaka 50 milioni nafikiri hivyo na wengine watakapochangia wataangalia kwa upande wao. Hapa nafikiri adhabu bado ni ndogo ikiwa kweli nia yetu ni ku-establish controls katika muktadha mzima wa sheria hii.

Mheshimiwa Spika, naomba mengine atakuja kwenye schedule of amendment ambayo nimejaribu pia ku- highlight, naomba niwaachie na wengine.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa muda wako.