Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Ester Alexander Mahawe (27 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante. Ninaomba tu niende haraka haraka kwa sababu, muda nao ni mfupi sana, lakini pia nashukuru kwa nafasi niliyoipata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua suala la barabara ya Karatu - Mbulu limezungumzwa sana. Barabara hii ilimng‟oa Mheshimiwa Marmo baada ya miaka 25 kuwa Mbunge kwenye Bunge hili, kumbe ni kwa sababu tu mambo mengi kwa kweli hayapelekwi vile inavyokuwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa siyo hivyo tu, ilifika mahali wananchi wa Mbulu walikasirika wakaamua kuchagua debe la gunzi badala ya debe la mahindi mwaka 2010, lakini wamerudisha imani baada ya Mheshimiwa Mama Samia Suluhu, Makamu wa Rais, kupita wakati ule wa kampeni na yeye binafsi kupita katika barabara ile ya Magara akaona jinsi ambavyo anapita juu ya maji, alipofika daraja la Magara, akaahidi wananchi ya kwamba daraja hilo lazima litatengenezwa katika kipindi hiki. Tunamshukuru sana pia Rais, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, kupitia kwa Waziri wake wa Ujenzi nina hakika ya kwamba, hili litakuwa limemgusa kwa namna ya pekee maana tumelisema sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa pili wa daraja la Magara kuna huduma muhimu kama shule na kituo cha afya, ambako wakati wa masika watu wa upande mwingine wa kutoka Mbulu hawapati huduma stahiki, wanafunzi wanashindwa kwenda shule wakati wa masika mpaka masika itakapokwisha. Tunaomba, haidhuru tujengewe daraja lile kama hatutaweza kupata barabara kwa kiwango cha lami ili kwamba wananchi hao waweze kuunganishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama hiyo haitoshi; daraja hili upembuzi yakinifu ulikwisha kukamilika na kwa namna hiyo kwa ajili ya ahadi ya Serikali ya tangu mwaka 2011 wakati wa Rais Mstaafu Kikwete, wadau mbalimbali kama TANAPA waliweza kusogeza huduma zao karibu. TANAPA wamefungua geti na REA tayari wamepeleka umeme pale wakijua kwamba daraja hili linatengenezwa karibuni ili wananchi wa pale wapate kuhudumiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme tena habari ya barabara ya Mbulu - Haydom. Haydom kama tulivyosema ni Hospitali ya Rufaa, ni hospitali kubwa inategemewa na mikoa kama minne, tunaomba tusaidiwe ili kwamba, wannchi wetu waweze kupata huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ninaomba nizungumzie suala la FastJet. FastJet kwa kweli ni karaha, tunaambiwa kwamba hapa ni suala la soko, haiwezekani. Msafiri gani anasafiri bila begi?
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona. Kwanza kabisa naomba nitoe shukrani za dhati kabisa kwa Mungu wa mbinguni kwa ajili yangu na wengine wote tuliojaliwa kuingia mwaka 2016 na kuletwa humu na wananchi wetu. Zaidi sana nielekeze pia shukrani zangu za dhati kwa Chama cha Mapinduzi ambacho kimenipatia fursa hii ya kuwawakilisha wanawake wa Manyara. Vilevile niwapongeze wanawake wa Manyara kwa kunipatia nafasi hii ili nije niwawakilishe katika Bunge hili Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo, naomba nielekeze michango yangu moja kwa moja nikianza na elimu. Naomba ku-declare interest ya kwamba mimi ni mwekezaji wa ndani katika masuala ya elimu, kwa maana ya shule za binafsi. Nipende kuanza kumpongeza sana Mheshimiwa Profesa Ndalichako ambaye ameweza kusikiliza kilio cha Watanzania cha kuondoa GPA na kurudisha mfumo wa division. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichokuwa kinafanyika ni sawa na kuvalisha mtu mchafu gauni la gold. Kwa hiyo, niseme tu Mheshimiwa Profesa Ndalichako na timu yako hongereni sana maana mmedhamiria kuboresha elimu ya nchi yetu Mungu awabariki sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile hakuna nchi ambayo imewahi kuendelea duniani pasipo kuwekeza kwenye elimu, hata maneno matakatifu yanasema; “Mkamate sana elimu usimwache akaenda zake maana yeye ndio uzima wako.” (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niseme tu, kulingana na Mpango uliopo mbele yetu wa kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli imeazimia kuwekeza sana kwenye elimu kwa kuanza kutoa elimu bure, basi nafikiri ni wakati muafaka kuangalia changamoto zinazokabili tasnia ya elimu nchini. Kwa hiyo kwanza kabisa, nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona ya kwamba, potelea mbali vyovyote inavyoitwa ya kwamba ni kupunguza makali kwenye elimu ama ni elimu bure, lakini iwavyo vyovyote ili mradi mtoto wa Kitanzania sasa anakwenda kupata elimu bila vikwazo vya aina yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niwaambie tu ndugu zangu Wapinzani, msibeze kila kitu kinachofanywa na Serikali hii, Serikali inajitahidi sana ninyi si Mungu ama malaika ambapo mngepata nafasi hii kwamba mngeweza kuchange dunia in a day. Kila kitu kinakwenda taratibu, hatua kwa hatua, changamoto zilizopo kwenye elimu bure zinafanyiwa kazi na zinakwenda kwisha. Kwa hiyo, tambueni juhudi za Serikali kwenye hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kwenye mchango wangu wa elimu. Naomba sasa pia Serikali ijitahidi sana kufanya kazi na sekta binafsi maana kuna wadau wengi sana wamewekeza kwenye elimu na ifike mahali watu hawa waonekane kama siyo competitors isipokuwa ni partners wanaoweza kusaidia kusomesha watoto wa Kitanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu wawekezaji wa ndani katika suala la elimu wanakabiliwa na kodi zisizopungua 13, ndiyo maana inaonekana watu hawa wanatoa elimu kwa gharama ya juu sana mpaka mambo ya ada elekezi yanaingia humu. Shule za binafsi zinalipa property tax, income tax, service development levy, city levy, land rent, mabango ya shule yale yaliyo kwenye TANROADS tunalipa kwa dola. Sasa sijui mambo ya dola yanakujaje tena na halafu inaitwa TANROADS halafu tunalipa kwa dola, sasa si tuite tu USROADS. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna kodi ya corporate tax, working permits kwa walimu ambao siyo Watanzania. Mwalimu mmoja mpaka uweze kumpata anatumia sio chini ya shilingi milioni saba ndipo aweze kupata working permits na residence permit. Wakati huo huo tuna upungufu wa walimu wasiopungua laki tisa, tulionao ni laki mbili thelathini na nane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna upungufu wa Walimu wa sayansi na hisabati wasiopungua elfu ishirini, Wizara ama nchi ina uwezo wa kutengeneza Walimu wasiozidi elfu mbili kwa mwaka. Kwa hiyo, tunachukua note less than ten years kutengeneza Walimu tunaowahitaji wa sayansi. Hii imekuwa pia changamoto kubwa kwa ajili ya maabara ambazo tumezijenga majuzi kati, tuna maabara kila mahali sasa, lakini changamoto kubwa imebaki kwa Walimu wa masomo ya sayansi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ifike mahali sasa kama inawezekana Serikali ione umuhimu wa kupunguza gharama za kuwapata Walimu kutoka nchi jirani kwa gharama ndogo residence permit na working permit ili waweze kusaidia katika shule zetu.
MHE. WAITARA M. MWIKABWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kidogo suala la afya. Naomba katika suala la afya kwa sababu Serikali pia imeamua kuwekeza sasa kwenye afya ya wananchi wake. Nizungumzie kidogo hospitali ya Hydom, hospitali ya Hydom ipo katika Mkoa wa Manyara lakini ina-save Mikoa ya Singida na Mikoa ya Arusha kwa maana ya wenyeji wa Karatu na maeneo mengine hata ya Meatu. Kwa hiyo, ifike mahali sasa Serikali isaidiane kabisa kama ilivyoahidi kwenye mfumo huu wa PPP kusaidia hospitali ya Hydom kuendelea kutoa huduma njema na toshelevu kwa wananchi wake wa karibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie tena kidogo suala la utalii, utalii wetu umekuwa na changamoto nyingi za kuandamwa na kodi nyingi, mfano wa TALA Licence ni dola 2000 kwa mwaka bila kujali anayelipa ni mzawa ama mageni. Nashauri Serikali ifike mahali wazawa wapewe first priority na kwa gharama rahisi kidogo ili wanapowekeza kwenye suala la utalii, basi vijana wengi wakapate ajira kupitia utalii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, magari mengi yamekuwa grounded, utalii umekuwa threatend na masuala haya ya Al-Shabab na hata Ebola. Wazungu kule nje hawajui umbali wa mahali Ebola ilipo na Al-Shabab ulipo, kwa hiyo, utalii umeshuka. Mimi naishi Arusha, kwa hiyo, niseme tu utalii umeshuka na imefika mahali hayo magari ya watalii sasa yamekaa tu yanafanya kazi za kubeba abiria wa kawaida.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna changamoto, nimesafiri mwenyewe Disemba mwaka uliopita, nimepita geti la Naabi pale wageni wanapoteza masaa yasiyopungua mawili mpaka matatu wakati wa kujiandikisha kuingia hifadhini. Sioni kwa nini hili liendelee wakati tupo kwenye dunia sasa ya sayansi na teknolojia. Muda mwingi mno unapotea foleni na jam inakuwa kubwa pale getini. Namwomba sana Mheshimiwa Jumanne Maghembe aweze kuangalia hilo ni kiikwazo. Mtu anayekwenda day trip kuingia pale chini crater na kurudi anapoteza masaa yasiyopungua matatu. Kwa hiyo, naomba hili nalo…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza naomba tu ni-declare interest mapema kwamba mimi ni mdau wa elimu pia, ni mwalimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa sera ya elimu bure ama elimu bila malipo, lakini inayogharamiwa na Serikali. Ninajua kila kitu kina mwanzo mgumu, mtoto hazaliwi leo akakimbia, hata nani angekuja na Sera hii na yeye angeweza kuyumbayumba hapa katikati. Hata ndege inapotaka kuruka huwa kuna tatizo mara nyingi na mwisho wa siku ikifika kwenye cruising point inasimama sawasawa na inakwenda. Mimi niseme tu niwatie moyo sana Mheshimiwa Waziri Mama Ndalichako pamoja na Mheshimiwa Engineer Mama Stella Manyanya, tunawaamini sana akinamama tuko nyuma yenu, pigeni mzigo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba kama inavyoeleweka elimu ni ufunguo wa maisha. Na hata neno la Mungu linasema, mkamate sana elimu asiendezake, mshike sana maana huyo ndio uzima wako. Ninaomba tu niiombe Serikali yetu sasa, hebu iwekeze sana kwenye elimu. Taifa lolote ambalo elimu yake haijakaa sawasawa linazalisha watumwa ambao watakwenda kutumia matajiri.
Kwa hiyo, mimi naomba tu Serikali yetu iendelee sasa, hii ingekuwa ni Wizara ambayo ilipaswa ipate bajeti kubwa kuliko Wizara nyingine zozote kwa umuhimu wake. Itoshe sasa walimu na ualimu kutokupewa kipaumbele katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu waliopata division four karibu na zero ndio wanaokwenda kusoma ualimu, unategemea nini na hawa watu ndio wanaotuanzishia msingi wa elimu nchi hii. Msingi wowote, hata kama ni nyumba unajenga huwezi ukaanza na msingi mbovu huko juu ukaweka zege, hiyo nyumba ni lazima itadondoka at the end of the day. Wale aliofaulu wakapata first class ndio wanaosubiri kuwapokea hawa watoto watakapofika Chuo Kikuu wakati hawa watoto wana mwanzo mbaya. Ifike mahali walimu nao wapewe nafasi ya ku-up grade, waweze kuboresha elimu zao na wapewe nafasi ya kwenda kujiendeleza. Na ikiwezekana hata watu wanaotokea division one na two waende wakasomee ualimu kwani kuna dhambi gani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo litazamwe sana, imekuwa hivyo kwa miaka mingi, tutaendelea kumtafuta mchawi, mchawi ni sisi wenyewe ambao tunaweka sera mbovu kwenye elimu, mwisho tunabakia kulalamika kila iitwapo leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa naomba tu nizungumzie pia, suala la mitaala. Mitaala hii imekuwa ikibadilishwa kila wakati, ifike mahali kuwe na Standing Orders kwenye Wizara ya Elimu, sio kila Waziri anayeingia anaingia na lake, tunachanganywa. Wakati tukiwa tunasoma wengi wetu tulioko hapa, nakumbuka kuna kitabu kimoja cha Kiswahili, kitabu chenye lile shairi linalosema karudi baba mmoja toka safari ya mbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka nilikuwa naimba lile shairi nikiwa darasa la kwanza japo haikuwa level yangu kwa sababu, lilikuwa linaimbwa na ndugu zangu walionitangulia, kulikuwa kuna system nzuri. Nani ametuloga tukaondoa hiyo system? Tuangalie tulikoangukia ili tuweze kuboresha elimu yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyowahi ku-declare interest, nimesema mimi ni mdau katika shule binafsi. Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 inaeleza kwamba shule sio biashara, shule ni huduma. Mwalimu Nyerere alisema watu wa asasi za kidini na wenye mapenzi mema waweze kuisaidia Serikali katika kutoa elimu, lakini leo tunashindwa kuelewa tumekuwa maadui? Kwa nini isifike mahali Serikali ikaona sisi ni partners badala ya competitors wakati tunawasomesha Watanzania hao hao? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni nchi peke yake ambayo shule zisizo za Serikali zinalipa kodi. Tumetembea nchi mbalimbali humu duniani, wanapata capitation grant kutoka kwenye Serikali zao, wanalipiwa walimu wao mishahara. Sisi tunafanya kila kitu wenyewe, tunakopa mikopo 24% interest kwenye mabenki, unanunua ardhi, unajenga shule, unalipa mishahara, unalisha watoto, unafanya kila kitu, leo tunaambiwa ada elekezi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hii ni sawa na kwamba mtoto wako mimba umebeba mwenyewe, mtoto umemlea mwenyewe, shule umempeleka mwenyewe, anayekuja kuoa anakupangia mahari. Sasa namna hii tutafika? Ikiwa tu bado tuna ukakasi na tuna mahitaji makubwa kwenye shule zetu za Serikali, tutakapoanza tena kuzitibua hizi zisizo za Serikali ambazo hata kwa kunukuu tu niseme, shule 50 bora mwaka jana katika kidato cha nne zilikuwa zimetoka kwa shule binafsi, yaani tunavuruga huku wakati hata huku bado hatujaweka sawasawa! Kwa kweli, hatutendewi haki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mlolongo wa kodi. Ada elekezi si tatizo, lakini mimi nilikuwa ninaishauri Serikali ituondolee huu msururu wa kodi ili kwamba tuwasaidie hata watoto watokao kwenye mazingira magumu. Niseme tu ukweli, mimi shuleni kwangu nina watoto 67 yatima ninaowa-sponsor mwenyewe. Watoto hawa wametelekezwa, ni shule ipi ya Serikali ambayo inaangalia hawa watoto wa namna hii? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wamiliki wa shule binafsi wanajitahidi sana kuchukua watoto hawa. Serikali iondoe hizi kodi ili tuweze kuwasaidia watoto wengi wa namna hii, tupunguze wingi wa watoto wa mitaani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunalipa kodi zifuatazo, inawezekana Wabunge hawafahamu ama wananchi huko nje hawajui; na hizi kodi unapozi-impose kwetu hakuna mwingine atakayezilipa ni mlaji ambaye ni mzazi. Iko hivi, tunalipa Land Rent, Property Tax, Business License, Sign Boards Levy, City Service Levy, Corporation Tax, SDL, Workers Compensation Fund, Work Residence Permit Fee, Fire, OSHA, taja yote tunalipa. Tunafanya biashara gani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaisadia Serikali kusomesha Watanzania, kabla ya hapo watu walikuwa wanasomesha watoto Kenya na Uganda. Tumejitoa muhanga, wengine wamekufa kwa pressure kwa ajili ya kudaiwa na mabenki, wengine mna ushahidi hapa wameshindwa kulipa madeni ya benki mtu anakufa na pressure na wamiliki wengi wa shule wana-suffer na masuala ya pressure na sukari kwa sababu ya ugumu wa kuendesha hizi shule. Leo ni nani mwenye shule ambaye ana biashara nyingine pembeni ya uendeshaji wa shule? Kama ulikuwa unaendesha nursery school uta-up grade utafungua primary, bado ni elimu ileile! Utatoka primary utaanzisha secondary, utatoka secondary utaenda colleges! Yet tunawasomesha Watanzania hawa hawa, kwa nini Serikali isitupatie dawati pale Wizara ya Elimu, ili kwamba, na sisi tuweze kutoa maoni yetu pale? Ili kusaidia mitaala hii inayotungwa watu wakiwa wamejifungia vyumbani bila kupokea maoni ya wadau wengine?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ilifanyika semina ya walimu wa darasa la kwanza na la pili hapa Dodoma, hatukuelezwa watu wa shule binafsi kwamba, kuna semina ya namna hiyo na wakati kwenye shule zetu kuna wanafunzi wa namna hiyo. Tunatengwa, sisi tumebaki yatima, Serikali ituangalie sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia tukaambiwa tupake magari rangi ya njano, tunaongezewa gharama, gari moja ni shilingi milioni tatu mpaka tano, mwingine ana magari 50 ni shilingi ngapi hizo? Nani atazilipa kama sio mzazi wa Kitanzania? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi tukubali, kama ni hiyo ada elekezi basi ije tujue kwamba ada elekezi imekuja, lakini hatulipishwi kodi za namna hii zinaumiza sana. Tuna madeni kwenye mabenki kwa ajili ya kujenga madarasa wanakosoma watoto wa Kitanzania, hata mtu akifa leo anaacha shule inaendelea kusomesha Watanzania, lakini wewe umekufa na pressure kwa ajili ya uendeshaji wa shule za namna hii. Tutaendelea hivi mpaka lini? Itafika mahali hawa wadau watafunga hizi shule zao basi turudishe watoto Kenya na Uganda kama ndicho tunachokitafuta. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano wa shule yenye watoto 350 ambao ada yake labda makusanyo kwa mwaka ni kama shilingi milioni 216, lakini shule kama hii inalipa kodi shilingi milioni 85, kwa faida ipi anayotengeneza mwenye shule? Weka tu chakula cha mtoto shilingi 10,000 hata kwa siku 90 anazokaa mtoto shuleni ni shilingi ngapi? Tunaumizwa. Ifike mahali sasa kilio chetu kisikilizwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nilikuwa nafikiri there is no fair play here. Wizara ya Elimu ama TAMISEMI ina shule zake, watu binafsi wana shule zao, lakini anayetu-monitor ni Wizara ya Elimu. Ni sawa na mchezaji wa simba awe referee wakati yanga na Simba wanacheza, hivi kweli hatapendelea timu yake? (Makofi)
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninaomba dakika zangu kumi, kila nikichangia ninapewa dakika mbili, dakika tano wakati wengine wametumia dakika kumi; naomba unitendee haki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimpe tu pole Mbunge wangu Mheshimiwab Issaay, inatia hasira wakati mwingine lakini pole sana kaka yangu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze tu kwa kusema, ni kweli kwamba sekta ya utalii inatoa mchango wa asilimia 25 ya pato la fedha za nje katika nchi yetu, lakini ni kweli wakati mwingine inakuwa inaumiza baada ya kuona kwamba uharibifu mkubwa unafanywa na wanyama... Wabunge naomba tusikilizane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uharibifu mkubwa unafanywa na wanyama, lakini badala yake fidia ama kifuta jasho kinachotolewa ni kweli kwamba ni kidogo sana. Hii ndiyo inayopelekea kwa kweli watu kupata shida wakati wa kampeni za uchaguzi baada ya kuona kwamba hawatendewi haki. Inafika mahali labda wanyama wanaonekana wa thamani kuliko mwanadamu. Ni kweli kwamba hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niseme kwa upande wa Wilaya ya Babati Vijijini, wanyama walifanya uharibifu na Mheshimiwa Jitu Soni kwa zaidi ya miaka mitano amekuwa akifuatilia kifuta jasho cha wananchi husika, lakini katika pesa ambazo zinafikia zaidi ya shilingi milioni 100 ameambulia kupata shilingi milioni 12, tunaomba Wizara hii sasa iweze kuangalia namna gani hawa wananchi walioathirika wanaweza kupata fidia hiyo japo kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nitoe shukrani za dhati kwa TANAPA kwa kuweza kufungua geti la Sangaiwe pamoja na geti la Mamire ili kuweza kuruhusu wananchi kufanya biashara zao ndogo ndogo. Niombe Wizara iweze kutusaidi kukusanya hiyo 0.3 levy ili kwamba mapato haya yaweze kuwa ya msaada kuliko inavyofanyika sasa, maana hoteli zinazozunguka hifadhi hizo zimekataa kata kata kulipa tozo hizo za 0.3 percent.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huo naomba pia niseme miaka michache iliyopoita wakati wa Operation Tokomeza mama mmoja kule katika Kata ya Galapo, Mkoani Manyara aliauwa, ikaundwa Tume ya Kijaji mpaka sasa hatujapata jibu lolote kuhusu mauaji yale. Tunaomba Wizara itusaidie kujua nini kiliendelea kuhusu mauaji yale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na zaidi sana naomba ni-declare interest kwamba mimi pia ni mdau wa utalii. Kuna utitiri mkubwa wa kodi zisizopungua 15 katika uwekezaji huu wa utalii. Haiwezekani wananchi wetu wakalifikia goli la kuondokana na umaskini wakati kodi ni nyingi kupita kiasi. Mheshimiwa Mchengelwa ametoka kuzungumza habari ya night bed levy.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sijui ni nini maana ya mtalii. Inawezekana mtu akitoka Arusha kwenda Dar es Salaam kwenda kumuuguza mgonjwa wake Muhimbili na akawa analala kwenye hoteli pale Dar es Salaam anaweza akawa anaitwa mtalii. Tatizo ni kwamba kodi hii haiko-fair. Kama ni Mount Meru Hotel inalipa one point…
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kodi hii ya night bed levy kwa kweli imekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wadogo. Unakuta mtu hoteli yake anauza vyumba kwa shilingi 30,000 au 50,000 analipa the same amount na mtu ambaye ana hoteli ya kitalii, au let us say hoteli ya Mount Meru ama hoteli nyingine kubwa za nyota nne au nyota tano. Sasa usawa uko wapi? Hili litazamwe na Wizara hii, Mheshimiwa Maghembe tunaomba ulitupie jicho, night bed levy imekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wadogo kama wale wenye guest houses wanatozwa kodi kwa nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wakati huo huo niseme pia TALA license imekuwa ni kilio cha muda mrefu. Hapo Kenya wanatoza dola 300 kwa TALA license, lakini pia wanatoza kwa gari hawatozi kwa kampuni. Huku kwetu una gari moja, tano, mbili, mia tano unatozwa dola 2,000 kwa nini? Hili kimekuwa kilio kikubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kulipia TALA license unalipa land rent, unalipa tax zote 15, huyu mtu anapataje faida? Anawezaje kutusaidia kuongeza ajira kwa vijana wetu? Nilisema tena watu wengi wameweka magari yao nyumbani, wameshindwa kufanya biashara ya utalii kwa ajili ya utitiri wa kodi. Ifanyike review kwenye kodi hizi ili utalii wetu uweze kuleta tija katika nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niseme tu, inawezekana sana kuhakikisha kwamba pia na misitu yetu inatusaidia. Ukienda nchi za watu watoto wanagombana na wazazi wao kubadilisha ipad, laptop mpya, smart phones, sisi tunajadili habari ya dawati wakati misitu iko hapo. TFS wanakusanya zaidi ya shilingi bilioni 50, ni ukataji wa miti tu unaendelea, hakuna miti inayorudishwa kupandwa. Tutakwenda hivi mpaka lini? Mtoto kukaa kwenye dawati Tanzania inakuwa ni privilege, kweli? Tutaondoka lini huko?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa nafikiri kwamba tunaweza kurekebisha hali hii, kama tuna sera mbovu basi tuziangalie tena, tuzirekebishe ili kwamba yote yanayoendelea katika nchi hii yawe ni kwa maslahi ya Mtanzania maskini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme haraka haraka juu ya Mlima Hanang. Mlima ule ni wa tatu kwa urefu hapa Tanzania, lakini kuna uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea katika Mlima Hanang. Tunaomba ikiwezekana mlima huu ukabidhiwe kwa TANAPA ili waweze kuulinda maana uharibifu unaofanyika pale ni mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nisiendelee sana, niwaachie na wenzangu wengine dakika chache zilizobaki.
Mheshimiwa Mwenyekiiti, nakushukuru sana na ninaunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kwanza niwapongeze tu walioandaa bajeti hii, lakini pia nielekeze zaidi mchango wangu kwenye suala zima la afya. Afya ni jambo la msingi sana kuzingatiwa katika uwekezaji wowote ule unaotakikana kama tulivyosema kwamba tunataka kutengeneza Tanzania ya viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii Tanzania ya viwanda ambayo tunataka kuitengeneza bila kujali ama kuweka kipaumbele kwenye afya za watu wake ambao wengi ndio wazalishaji, wengi ndio wanaofanya kilimo cha mkono, ama ni wakulima wadogo wadogo ambao wako vijijini; hawa watu tusipowapelekea zahanati za kutosha, tusipopeleka Vituo vya Afya vya kutosha, tusipowapelekea watumishi wa kutosha wa kada za afya, hawa watu wanawezaje kusaidia uzalishaji na hatimaye viwanda vyetu vikafanya kazi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona upungufu kidogo katika bajeti yetu hii kwamba ingawa Serikali imeweka kipaumbele kwenye Sekta ya Kilimo na kuainisha kwamba mazao ya kilimo yatakuwa moja ya malighafi kwenye viwanda hivyo, bado vipaumbele vinaenda kwenye kujenga reli, barabara, Viwanja vya Ndege na kadhalika; lakini kwenye vyanzo vya kilimo ambavyo ndivyo vitakuwa malighafi, kusababisha uzalishaji ukue hakujawekewa mkazo huku; na asilimia 80 ya wanawake walioko kijijini ndio wakulima, lakini bajeti hii haioneshi ni jinsi gani afya ya mwanamke huyu imezingatiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikirudi upande wa Mkoa wa Manyara na Wilaya zake zote, hatuna watumishi wa kutosha katika kada ya afya na hatuna vituo vya kutosha. Kwa mfano, katika Kata ya Eshikesh, mama mjamzito anatembea kilometa 40 kwenda kwenye Zahanati ya Yaeda Chini.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya hii ya Mbulu Vijijini haina Hospitali ya Wilaya wala gari la wagonjwa. Akinamama hawa wanapata shida kusema ule ukweli; siyo Mbulu tu, tuna maeneo kama Simanjiro, mahali ambapo gari la wagonjwa ni moja, hawana Hospitali ya Wilaya, wanatumia Hospitali ya KKKT. Mama akishindwa kujifungua, anatakiwa apatiwe operation lakini anatakiwa alipe shilingi 400,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi yule mama wa Kimasai anayetembea na punda, anayepoteza muda wote kwenye maji, ni saa ngapi ametafuta shilingi 400,000 za kuweza kumsaidia yeye kwenda kujifungua? Nafikiri tungehakikisha kwamba kipaumbele kinawekwa kwanza kwenye afya, watu wetu wakiwa na afya njema watazalisha kwa tija. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile, nizungumzie hili suala la asilimia tano ya akinamama na vijana. Tulijinadi sana kwenye kampeni zetu kupitia asilimia tano kwa akinamama na vijana. Sasa inaonekana sehemu kubwa ya own source inakusanywa na Serikali Kuu. Changamoto ipo kubwa; mara nyingi, hata leo Mheshimiwa Umbulla ameuliza hapa, akinamama ama Wabunge wa Viti Maalum hawaingii kwenye Kamati ya Mipango na Fedha ya Halmashauri zetu, ndiyo maana hizi fedha zimekuwa misused wakati mwingi. Hakuna mtu wa kuzisimamia; tunaziona tu kwenye makaratasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuliwahakikishia akinamama ambao ndio wamekipa Chama chetu kura nyingi ya kwamba tunakwenda kudai asilimia hizi. Je, tunarudije kwao? Tunaomba hizi fedha ambazo zinatengwa kwa ajili ya akinamama, kwa mwaka huu haidhuru, basi kwa mara ya kwanza zifike katika ukamilifu wake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna shilingi milioni 50 kila Mtaa na kila Shehia na kila Kijiji. Nako tulijinadi kwa sababu ni ahadi ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri tu kwamba pamoja na Mikoa 10 inayotaka kutengwa hapa ya pilot run, nashauri ili wananchi wetu mioyo yao isikunje ngumi, kwa nini isitumike mikoa yote, halafu haidhuru vichukuliwe vijiji hata kama ni vitano kwa kila mkoa? Maana changamoto na mazingira hayafanani. Haidhuru na sisi tupate cha kusema tukirudi kwa wananchi wetu. Hawa kumi tu, tuseme Mkoa wa Manyara, haufanani na Dar es Salaam; Mkoa wa Manyara haufanani na Kilimanjaro; changamoto zinatofautiana. (Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sijajua kwamba labda hawa walioweka hivyo kwamba wanachukua mikoa kumi wamezingatia nini. Ila nashauri tu, kama inawezekana, mikoa yote ichukuliwe na vijiji haidhuru vitano vitano kila Mkoa ili tuone kwamba tunawezaje kuokoa maisha ya wananchi wetu kupitia mikopo hii ya shilingi milioni 50 kupitia SACCOS.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna mgongano wa maslahi. Pale mwongozo unapoelekeza kuwa mapato yote ya mamlaka ya Serikali za Mitaa yawasilishwe Serikali kuu, changamoto kwenye mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kwamba fedha hizi huwa zinachelewa sana kuteremka chini huko kwenye Halmashauri zetu. Sasa itakuwaje ikiwa fedha hizi zinakusanywa na Serikali Kuu?
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nasoma kiambatanisho cha masuala ya afya; elimu ya watoto wetu wa kike ni tatizo. Imeelezwa sana, kwamba tunaomba kodi ziondolewe kwenye vifaa vyote vinavyosaidia akinamama pamoja na mabinti mashuleni. Kwenye towel zao kodi iondolewe. Binti anakosa shule siku saba katika mwezi. Mwisho wa siku inaonekana watoto wa kike ni vilaza; kumbe ni kwa sababu hawa-attend shule inavyotakiwa kama wanavya-attend watoto wa kiume.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hili litazamwe upya, tuwasaidie watoto wetu wa kike. Utakuta miundombinu kwenye shule, watoto 400 vyoo viwili au watoto 600 vyoo vitatu, watoto wa kike wanapataje kujisitiri? Je, bajeti hii inamwangaliaje mtoto wa kike? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ili tuweze kushea hii keki sawasawa, naomba tuwekeze zaidi kwa akinamama ambao ni waaminifu hata wanavyochukua mikopo kwenye mabenki, wamekuwa wakirejesha kwa uaminifu mkubwa. Kwa hiyo, naomba sana akinamama watazamwe kwa jicho la pekee ili waweze kusaidia pato hili la Taifa hasa kupitia kilimo na ujasiriamali. Hakuna asiyejua kwamba akinamama ndiyo wanaokimbia kimbia asubuhi mpaka jioni kutafuta riziki za familia zao, kupitia biashara ndogo ndogo. Akinamama hao watazamwe kwa jicho la pili ili waweze kusaidia katika kukua kwa uchumi wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kuna upungufu mkubwa wa urari baina ya matumizi ya kawaida na yale ya maendeleo. Matumizi ya kawaida ni karibu mara tatu ya yale ya maendeleo. Kwa hiyo, nashauri tu kwamba, bajeti hii iangalie ni jinsi gani inaweza ikawekeza zaidi kwenye bajeti ya maendeleo, japo imepandishwa mpaka asilimia 40, lakini kama inawezekana, iendelee kusogea hata ifike mahali iwe asilimia 50 kwa 50.
Mheshimiwa Naibu Spika, basi naomba nisisuburi kengele inayofuata, niseme tu kwamba yangu ni hayo. Zaidi sana, nawalilia akinamama waweze kusaidiwa na bajeti hii pamoja na watoto wa kike ili waweze kupata elimu sawasawa pamoja na watoto wa kiume.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naunga hoja mkono.
Azimio la Bunge Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Udhibiti wa Matumizi ya Dawa na Mbinu za Kuongeza Nguvu Michezoni
MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza kabisa naomba niunge mkono hoja. Tunafahamu kabisa michezo ni furaha, michezo ni elimu na michezo ni afya, niseme tu kama nchi ni kweli kwamba tumechelewa kukubaliana na Azimio hili. Kwa hiyo, kwa kuwa imeletwa sasa basi niwaombe na Wabunge wenzangu kwa pamoja tupitishe Azimio hili ili nchi yetu iweze kufaidika kama faida zilivyoorodheshwa katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia niseme inafahamika kabisa kwamba madhara ya kutumia dawa hii ni makubwa kama yalivyoelezwa. Kama nchi sidhani kama tuna sababu ya kutokupitisha Azimio hili kwa sababu hatuna woga, tuna Watanzania wachezaji wazuri sana ambao wameiletea nchi hii heshima kwenye football, kwenye riadha na kadhalika. Kwa uchache tu nitambue heshima waliyoileta wanariadha hawa wafuatao:-
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna watu kama akina Simon Robert, John Stephen, John Bura, Nada Saktai, Focus Wilbroad Aweso, Francis Nada na Zebedayo Bayo, hawa watu wamefanya kazi kubwa katika nchi hii. Niseme tu tusiogope; tuwekeze kwenye michezo, tunao watu ambao bado wanaweza wakailetea nchi hii heshima.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia michezo inahitaji uwekezaji, tuendelee kuwekeza kama ilivyokuwa zamani kwenye UMISHUMTA na UMISETA tuendelee kutengeneza vijana wenye vipaji kuanzia katika utoto wao ili waweze kuiletea nchi yetu heshima na wakipata kuwekewa misingi na miundombinu mizuri nina hakika wala hatuhitaji kutumia madawa ya kuongeza nguvu maana vijana hawa watakuwa wameandaliwa vizuri na hatimaye wataweza kufanya vizuri katika michezo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana kwamba hawa watu waliowahi kuiletea nchi yetu heshima hatukuona namna yoyote tukiwaenzi, namna yoyote ya kuona kwamba walileta mchango mkubwa wa fedha, wa heshima katika nchi yetu; hii inawakatisha tamaa wale wengine wadogo ambao wanaibuka katika tasnia hii ya michezo kama riadha, football na michezo mingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nafikiri kwamba juhudi za hawa watu zitambulike, kuwe na namna maalum ya kuhakikisha kwamba hawa watu wanakumbukwa. Sasa hivi hawa karibu wote niliowataja hapa ukiacha Filbert Bayi ambaye atleast yeye amejiingiza kwenye masuala ya elimu, wengine wote wanapata shida, wanakufa katika umaskini uliotopea kule vijijini, wengine wamejiingiza kwenye ulevi na maisha duni yanawaandama kama watu ambao hawakuwahi kuifanyia nchi hii kitu.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia niseme tu kwamba hakuna asiyefahamu kwamba Manyara kwa ujumla, mimi of course nimetoka Manyara, kwa ujumla Manyara imeiletea sana heshima Tanzania katika suala zima la riadha. Kwa hiyo naendelea kuiomba Serikali iendelee kuwekeza katika Mkoa wa Manyara tupate Sports Academy kule Manyara ambayo inaweza ikasaidia kuendelea kuibua vipaji. Bado tuna watoto hawa wa kifugaji wengi tu ambao kwa mazingira ya Manyara hayana tofauti na mazingira kama ya Ethiopia, wanaweza wakaibeba nchi hii na bado heshima ya nchi ikarudi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nashukuru tu kwa mchango huu na naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, nianze kuunga mkono hoja kwa kuipongeza Serikali ya CCM chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, kwa kazi kubwa wanayofanya ya kurejesha nidhamu na uwajibikaji katika nchi yetu. Japokuwa hali hii kwa kuwa ni ngeni kwa wengine na kinyume cha matazamio yao wameitafsiri katika namna hasi. Ombi langu, tuendelee hivi hivi huku tukibaki katika lengo letu la kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye lindi la umaskini, ujinga na maradhi na kuwapeleka kwenye nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2030.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa nijikite kwenye hoja yangu. Bila kusahau naomba ku-declare interest kwamba mimi ni mdau wa elimu wa shule binafsi. Naomba nielekeze mchango wangu kwenye ushirikiano kati ya Umma na Binafsi (PPP) katika uwekezaji kwenye sekta zote muhimu nchini ikiwemo elimu, afya, viwanda, miundombinu na kadhalika. Nafahamu kuwa Serikali yetu sikivu ya CCM ina nia njema sana katika hili hivyo naomba nitoe ushauri ufuatao:-
(i) Kubainisha wazi na bayana majukumu ya kila upande katika utekelezaji wa sera ya PPP katika sekta ya elimu (utungaji wa sera, sheria, miongozo, uchangiaji wa gharama za elimu, usimamizi wa taasisi za elimu, upimaji na udhibiti ubora);
(ii) Kuwa na mifumo imara na endelevu ya mawasiliano (dialogue structure) baina ya pande zote mbili ili kupeana taarifa za mara kwa mara na uzoefu mbalimbali wenye tija kwa maendeleo ya nchi; na
(iii) Kuwe na mifumo imara yenye kujengeana uwezo baina ya pande zote mbili kwa vile kila upande unacho cha kujifunza kutoka kwa mwenzake.
Mheshimiwa Naibu Spika, pale Serikali itakapofungua milango katika PPP ni hakika tutaona mafanikio na mabadiliko makubwa ya kiuchumi ndani ya muda mfupi sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, niishauri pia Serikali kuweka vipaumbele vinavyotekelezeka. Mpango huu ni mzuri lakini umekuja na vipaumbele vingi sana. Tukiendelea hivi tutabaki kupapasa tu na hatutafika tuendako.
Mheshimiwa Naibu Spika, mifumo yetu ya kodi si rafiki hali inayopelekea kutishia kuongezeka hali ya rushwa hasa katika chombo chetu cha kodi (TRA). Kuwe na mazingira rafiki na dialogue structure baina ya TRA na mlipa kodi badala ya vitisho na kuuza kwa mnada mali za wafanyabiashara kwani kwa kufanya hivyo Serikali inakosa pesa na wale wafanyabiashara wanakuwa wamefilisika na mwisho tunaishia kuumia kama nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ina mpango wa kutupelekea kwenye Tanzania ya viwanda, basi niishauri Serikali iweke nguvu kubwa kwenye kilimo cha umwagiliaji ili viwanda vyetu viweze kufanya kazi kwa kipindi chote cha mwaka. Endapo hatutawekeza kwenye kilimo cha kisasa ambapo asilimia 80 ya Watanzania ndiyo wahusika wakuu katika hili, ni bayana hatutaweza kumwondoa huyu Mtanzania maskini kwenye lindi la umaskini.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nitoe ushauri wangu kwa Wizara ya Afya. Ni dhahiri kwamba ni pale tu watu wetu watakapokuwa na afya njema ndipo tutakapoweza kufanikiwa katika mambo yote. Mtu mgonjwa asiyeweza kutibiwa kwa wakati hawezi kamwe kufanya uzalishaji wa aina yoyote ile.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nigusie suala la ukosefu wa dawa MSD. Suala hili linaipeleka Serikali yetu pabaya sana. Naomba hili suala la dawa lifanyiwe kazi kwa gharama yoyote ile ili kulinusuru Taifa na vifo vya watoto na kizazi kijacho kwa kukosa chanjo za muhimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, mapendekezo haya ya Mpango bado hayajaweka bayana ni jinsi gani huduma ya maji zitafika vijijini ili kumtua ndoo mama wa Kitanzania. Asilimia zaidi ya 80 ya muda wa wanawake hawa wazalishaji inapotea kwenye kusaka maji usiku na mchana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nipende tena kupongeza juhudi za Serikali kwa jinsi pia inavyoshughulikia suala zima la mikopo ya elimu ya juu inayotishia amani ya wapiga kura wetu. Busara ya hali ya juu itumike ili kumaliza tatizo hili na kila mhusika abaki akiwa ameridhika.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, niunge mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika ahsante sana. Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutupa afya sisi wote tulioko ndani ya Jengo hili Tukufu la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza kabisa nielekeze pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi yake nzuri sana anayoifanya kupitia kwa Mawaziri hawa wawili wa TAMISEMI, Mheshimiwa Simbachawene na Mheshimiwa Jafo, kwa kweli kazi inafanyika. Niseme tu kwa upande wa Mkoa wa Manyara tunashukuru sana Serikali, tayari tumeanza kuona kwamba kwa kweli kazi inapigwa. Tunategemea kuboreshewa zahanati zetu katika Wilaya nne za Mkoa wa Manyara; Wilaya ya Mbulu Mjini na Jimbo la Mbulu Vijijini, Babati Mjini, Babati Vijijini na Wilaya ya Simanjiro, zahanati ile ya Urban Orkesumet inakwenda kuboreshwa sasa kwenda kwenye hadhi ya kituo cha afya; shughuli hii siyo ndogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba nipongeze juhudi za Serikali. Tumekuwa na kilio cha maji muda mrefu katika Wilaya ya Simanjiro sasa mradi mkubwa wa maji kutoka Mto Ruvu unaelekea katika eneo la Orkesumet Makao Makuu ya Wilaya ya Simanjiro, ni mradi ambao utaondoa tatizo la maji kwa kiwango kikubwa sana, kwa kweli naipongeza Serikali. Wale wanaosema hakuna kinachofanyika na bajeti iliyoletwa hapa mwaka jana ni hewa siyo kweli.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia niseme kwamba tayari tender ya Daraja la Magara ambalo tumekuwa tukilipigia kelele sana watu wa Babati na watu wa Mbulu, imetangazwa. Niiombe Serikali iwahishe kupeleka fedha daraja lile lianze kutengenezwa ili wananchi wetu waanze kupona.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijielekeze kwenye TASAF. Mfuko huu wa TASAF kwa kweli binafsi katika kutembea kwetu tulipokuwa kwenye Kamati katika Mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe ulionesha mafanikio makubwa sana katika kuondoa umaskini wa wananchi wetu. Wananchi hawa wenyewe wametoa ushuhuda jinsi gani Mfuko huu umekuwa wa msaada sana kwao. Watoto wanakwenda shule, watoto
wanapelekwa clinic kwa idadi kubwa, watu wanapata bima ya afya; huu siyo Mfuko wa kubezwa hata kidogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, niiombe Serikali na yenyewe iweze kuchangia sehemu inayotakiwa kuchangia ili Mfuko huu uendelee kudumu na kuendelea kusaidia kwa sababu wananchi wengi wameshatoka katika hali ya umaskini. Wale walio-graduate unaona kabisa tayari wana nyumba bora, maisha yao yamebadilika. Ni Mfuko ambao kwa kweli unahitaji kuongezewa nguvu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hapo hapo pia niseme kwamba kuna changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza kwenye zile kaya ambazo zilionekana ziliingizwa kinyume na utaratibu. Ninachoshauri tu ni kwamba, haki itendeke kwa watu wale ikiwa huenda wengine waliondolewa bila kuona kwamba wanastahili ama la maana pia walipaswa kurejesha fedha zile walizokwishapewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri kwamba wale waratibu waliohusika kuingiza watu ambao hawakuhusika wao wawajibike zaidi kuliko mwananchi ambaye hali yake ni duni na alishapewa fedha zile za kujisaidia na bado anapaswa kurudisha. Kama alipewa kwa sababu ni maskini anazitoa wapi leo? Kwa hiyo, nashauri hili lifanyike kwa umakini mkubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna huu MKURABITA. MKURABITA katika maeneo ya Njombe tumeona watu wametoa ushuhuda. Wale ambao ardhi zao zimerasimishwa na tayari wanatumia zile hati zao kuchukua mikopo mikubwa katika Mabenki tofauti. Tulishangaa kuona kwamba mtu ana uwezo wa kukopeshwa kuanzia milioni 100 mpaka 400 kwa kutumia hati hizi za Kimila, kwa kweli ni hatua kubwa mno Serikali imepiga katika hili. Niendelee kuitia moyo Serikali yangu ya kwamba sasa iendelee kupanua wigo wa kusaidia hati hizi za kimila zipatikane katika maeneo mengine ambayo hayajafanyiwa kazi namna hiyo. MKURABITA ushirikiane na Halmashauri zetu mbalimbali nchini ili wananchi
wetu waweze kufaidika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia wakati mwingine kuna changamoto katika upelekwaji wa fedha. Tunafahamu mambo yaliyofanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kwenye Serikali yetu kupitia Mheshimiwa Rais ni mambo makubwa na mambo mengi ambayo kiukweli hayapaswi
kudhihakiwa, bali tumtie Rais wetu moyo kazi inapigwa sana. Hata hivyo, niombe, bajeti hii tunayoijadili sasa iweze kupelekwa kwa wakati katika Halmashauri zetu. Kuwe na ushirikiano mkubwa na wa kutosha kati ya Serikali Kuu na Halmashauri zetu ili kwamba kazi ziweze kufanyika kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, ilijitokeza pia changamoto kuhusu zile asilimia tano za wanawake na tano za vijana. Kwa sababu ya kucheleweshwa kwa fedha hizi za OC kufika kwa wakati katika Halmashauri, imeonekana ile asilimia 10 kuelekezwa katika mambo mengine katika Halmashauri kwa, mfano; suala la madawati, maabara na vitu vya namna hiyo, hatulaumu zote ni kazi, lakini kwa sababu fungu hili lipo kisheria basi Serikali iangalie namna bora zaidi ya kufikisha zile fedha kwa wakati ili akinamama na vijana waweze kujikwamua katika lindi hili la umaskini kupitia kukopeshwa fedha zile za asilimia tano za vijana na tano za wanawake.
Mheshimiwa Naibu Spika, najua tayari tulimaliza changamoto za madawati, sasa hivi maeneo mengi tuna changamoto kubwa ya upungufu wa madarasa, mashimo ya vyoo pamoja na nyumba za Walimu. Ni kweli kwamba elimu bora inahitaji uwekezaji, hakuna muujiza; Walimu hawa watakapokuwa pia wamepata maeneo mazuri kwa maana ya madarasa toshelevu watafundisha watoto wetu vizuri na wanafunzi hawa wataelewa. Pia matundu ya vyoo yaendane sawa sawa na idadi ya wanafunzi walioko kwenye shule husika. Nafahamu Serikali yetu sikivu imejipanga kwa hili kwa mwaka huu wa 2017/2018 ili kuhakikisha tunaondokana na changamoto hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili la upungufu nalo linaendelea kwenye maeneo mengine kama zahanati ambapo tuna upungufu mkubwa wa vyumba ama nyumba za wafanyakazi wa kada ya afya. Waganga wetu hawana mahali pa kuishi, wanaishi mbali na maeneo ambayo
yanapaswa kutolewa huduma za afya. Tunaomba pia Serikali itazame hilo katika kipindi hiki cha bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa dakika chache zilizobaki niweze kusema machache kuhusu habari ya utumishi na utawala bora. Nasikitika sana kwa bahati mbaya sana niliyoiona kwenye hotuba ya dada yangu Mheshimiwa Ruth; sikuona, hotuba yao haikugusa suala zima la rushwa ambalo Serikali yetu imepambana nalo na sasa inaanza kuwa hadithi. Si hivyo tu, utawala bora ni pamoja na uhakiki mkubwa na mrefu uliofanywa na Serikali ili kuondoa mianya yote iliyokuwa inatumika kupoteza fedha za nchi hii. Kazi hiyo imefanyika kwa umakini mkubwa na fedha nyingi zimeokolewa, lakini hili hatukuliona pia likizungumzwa. Kwa hiyo, niseme tu, najua kwamba kazi yao siyo kuisifu Serikali yetu, lakini sisi kama Waheshimiwa Wabunge wa Chama Tawala, kwa kweli tunapongeza sana juhudi hizi ambazo zimefanywa katika awamu hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini niombe tu kwamba juhudi hizi ziendelee kufanywa na Serikali. Nampongeza sana Mheshimiwa Angella Kairuki….
T A A R I F A....
MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika siipokei kwa sababu unapojua kusema mabaya tu ujifunze kusema na mema pia.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala zima la uwajibikaji (accountability) lilikuwa halipo mahali pale, leo kuna accountability ukifika hata kwenye ofisi zetu za Serikali unasikilizwa hakuna tena njoo kesho, njoo kesho kutwa, ni sehemu ya utawala bora. Unafika hospitali unatibiwa hakuna
rushwa ni sehemu ya utawala bora. Hii kazi inafanywa na Serikali hii ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia ubadhirifu haupo tena, tayari Serikali ipo kazini inapambana na suala zima la ubadhirifu wa mali ya umma; hayo yote tumeyaona, mbona hatukuyaona kwenye hii hotuba? Wamesema hii ni Serikali ya kuhakiki, yes, we are after accountability, lazima kuwe na uhakiki ili kila mmoja awajibike kwa zamu yake. Wakati Serikali haihakiki wanasema Serikali gani hii, leo inahakiki wanasema Serikali ya kuhakiki; wanadamu hawana jema, Mawaziri wetu chapeni kazi tuko nyuma yenu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nizungumzie suala la performance based payments. Kuna zile on call allowances, labda kwa Madaktari na Manesi au kwa Walimu wetu. Wakati mwingine baadhi ya Walimu wametuhumiwa labda wanafanya biashara ya bodaboda wakati wa vipindi, kwa hiyo labda madarasa hayafundishwi inavyotakiwa. Ifike mahali ile performance based payment ifanye sehemu yake ili kuboresha huduma katika taasisi mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja. Ahsante sana.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii na mimi niweze kutoa mawazo yangu katika Bunge lako Tukufu. Kwanza kabisa naomba nitoe shukrani zangu za dhati na pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Ummy pamoja na Mheshimiwa Kigwangalla. Amezungumza mwenzangu Mheshimiwa Mama Martha Umbulla muda si mrefu ya kwamba juzi tu tuna kama siku mbili, tatu alitoka katika Mkoa wetu wa Manyara kwa sababu ya Hospitali ya Haydom, kwa kweli tunamshukuru sana Mheshimiwa Ummy lakini kubwa zaidi nimshukuru pia na Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye alisema atamtuma Waziri wake kwenda kuangalia jinsi gani Hospitali ya Haydom inaweza ikawa Hospitali ya Rufaa ya Kikanda kwa sababu hospitali hii inahudumia watu wengi sana, inahudumia Mikoa siyo chini ya mitano, ina Wabunge wanaoweza kuisema humu ndani siyo chini ya 20, kwa hiyo hili siyo jambo dogo. (Makofi)

Nimuombe sana sada yangu Mheshimiwa Ummy kwamba ikiwezekana kwa vile ile hospitali iko kijijini, kuna umbali wa zaidi ya kilometa 900 kutoka Haydom mpaka Muhimbili, kuna umbali wa zaidi ya kilometa 400 kutoka Haydom mpaka KCMC, kuna umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka Haydom mpaka Hospitali ya Mkoa wa Manyara, tunakuomba sana Mheshimiwa Ummy kwa hili acha legacy. Watu wa Haydom, watu wa Mkoa wa Manyara, Arusha kupitia Wilaya yake ya Karatu, Meatu, Simiyu upande mkubwa sana wa Simiyu hawatakusahau, Singida ndiyo usiseme hata Dodoma.

Tunakuomba sana Mheshimiwa Waziri Ummy hospitali hii iweze sasa kufikiriwa kuwa Hospitali ya Kikanda ili kwa ukanda huu tuwe tumepata hospitali ya rufaa ya kuweza kumaliza matatizo ya wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Baada ya pongezi hiso naomba sasa nijielekeze katika pongezi hizo, nisisahau kumshukuru Rais wangu ametoa vitanda kwa kila Halmashauri. Kwa kweli Mheshimiwa Rais Mungu ambariki sana jamani kazi inafanyika, tunaona kwa macho ya nyama, Mungu ambariki sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya yetu ya Babati tuna changamoto mbalimbali, ninaomba tu niongelee kwa uchache hospitali yetu ya Mkoa wa Babati haina theatre inayoeleweka, haina x-ray inayoeleweka, haina haya ultra- sound inayoeleweka, haina wataalam wa radiology, tunaomba sana Mheshimiwa Ummy, tunajua kazi inafanyika, tunajua mnajitahidi sana, lakini penye changamoto lazima tuseme, tunaomba muikumbuke hospitali hii ya Mkoa wa Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna Hospitali ya Mrara ambayo inatoa huduma kama Hospitali ya Wilaya pale, tunakuomba sana Mheshimiwa Ummy changamoto nilizozitaja zilizoko katika Hospitali ya Mkoa zipo na kwenye hospitali ya Mrara, tunaomba uikumbuke hospitali hii. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri, pia nisisahau kuishukuru Wizara yako Mheshimiwa Ummy umepeleka vifaa vya kutosha na wataalam wa kutosha katika Kituo cha Afya cha Magugu hili lazima tukupongeze sana. Kwa kweli, tunakushukuru sana, tumeona juhudi zenu na pale kwa kweli sasa neno upungufu hakuna, ahsanteni sana kwa hili mlilolifanya pale Magugu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ninaishukuru Serikali kwa sababu sasa inafanya sana kazi nzuri kupitia PPP, tayari imepeleka ruzuku katika Hospitali ya Dareda, hii ni Hospitali ya Mission ambayo inahudumia wananchi wengi sana wa Wilaya ya Babati Mji na Babati Vijijini Halmashauri zote hizi zinasaidiwa sana na hospitali hii ya Dareda, kwa kweli naishukuru Serikali imepeleka ruzuku pale ya kutosha lakini pia inasaidia kulipa watumishi wa kada hii ya afya wa hospitali ile. Kwa kweli kwa ujumla wake, niiombe Serikali iendelee kutoa ushirikiano kwa hospitali hizi za makanisa ambazo kwa kweli ni hospitali teule katika maeneo yetu, zinafanya kazi nzuri sana kutoa huduma kwa wananchi. Hivyo, niipongeze Serikali kwa kukubali kufanya kazi kupitia PPP na hizi hospitali za makanisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika Wilaya yetu ya Babati tuna mapungufu, tuna vituo saba na mahitaji yetu ni vituo 25, tuna zahanati 32 mahitaji ni zahanati 102; tunaomba sana haya mapungufu yatazamwe kwa jicho la kipekee sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashauri kwamba badala ya kuhangaika kuja kuweka labda Hospitali ya Wilaya pale Babati, ningeshauri zile fedha ambazo zilipaswa kuelekezwa kwenye ujenzi wa hospitali, vituo hivi vikiboreshwa vinaweza vikachukua nafasi kubwa sana ya kumaliza tatizo kiasi kwamba hata umuhimu wa kuwa na hospitali ya Wilaya pale unaweza usiwe wa lazima sana. Hivyo, naomba Kituo cha Bashnet, Hospitali ya Dareda pamoja na Kituo cha Mrara hozpitali hizi zikiboreshwa ukweli ni kwamba taabu itakuwa imekwisha maana wananchi hawa watakapokuwa wanahitaji huduma yoyote ya rufaa wataelekea Haydom ambako siyo mbali. Naomba tuboreshe kwanza huku chini ili tuweze kusaidia wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa pia la hospitali zetu katika Mkoa mzima wa Manyara hatuna ambulance. Kwa mfano, Wilaya ya Simanjiro imesemwa tayari kwamba tuna ambulance moja ambayo ni mbovu kila wakati ipo garage. Tunaomba jiografia ya Mkoa wa Manyara imekaa kidogo ni tatizo. Kwa mfano, Wilaya ya Simanjiro kutoka kata moja kwenda kata nyingine unakuta siyo chini ya kilometa 50 mpaka 80, kwa hiyo tunapokuwa na ambulance ambayo kwa kweli haipo vizuri tunapata shida.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisisahau pia kuishukuru Serikali, tayari pale Simanjiro tunapanua wodi sasa, huduma ya mama na mtoto inakwenda kupatikana vizuri sana pale Orkesment, ninaishukuru sana Serikali kwa kuliona hili. Pia nisisahau kuishukuru hospitali ya Orkesment ya KKKT, hospitali teule iliyoko pale Simanjiro inaendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi wetu. Niiombe tu Serikali kama nilivyosema kwa sababu gharama kwa kiwango fulani ni kubwa katika hospitali hizi ambazo zina muundo wa hospitali binafsi, ninaomba ile Urban Orkesment itakapokuwa imeboreshwa vizuri na kuwekwa vifaa vyote vinavyotakikana, kwa kweli wananchi wetu watapata huduma bora ya afya pasipokuwa na tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nizungumze suala sasa la afya ya mama na mtoto - uzazi salama. Uzazi salama ni kitu muhimu sana, kama takwimu zinavyoonesha kwamba akina mama wasiopungua 30 wanakufa kila iitwapo leo. Hii idadi siyo ndogo, tunaomba katika vituo hivi vya afya huduma hii iboreshwe, katika zahanati zetu huduma hizi ziboreshwe. Kwa mfano, katika Wilaya ya Simanjiro, kata ya Ngorika pana umbali wa kilometa 60 kutoka Ngorika mpaka Orkesment. Nilikuwa naomba ikiwezekana ile zahanati iliyoko pale iweze kupandishwa hadhi kidogo, iweze kukaa vizuri ili wale wananchi wa Ngorika waweze kupata huduma pale Ngorika maana kutoka Ngorika mpaka Orkesment mtu anatembea kilometa 60 kwa kweli huu umbali ni mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyosema jiografia ya Simanjiro ni zaidi ya square kilometer 17,000 hiyo Wilaya ni kubwa sana na sehemu kubwa ni pori, kwa hiyo tunaomba msaada wenu sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba nizungumzie suala la ndoa za utotoni; vifo vingi vimekuwa vikitokea kupitia ndoa hizi za utotoni. Ninaomba sana ikiwezekana Mheshimiwa Waziri sasa alete marekebisho ya sheria hii huku ndani. Ninawaomba wakina baba mlioko humu ndani, ninawaomba sana akina mama watoto wetu wanateketea. Hii biashara ya kusema kwamba kigezo cha mtoto wa kike kuolewa ni baada ya kuvunja ungo hii siyo sahihi. Siku hizi watoto kwa ajili ya hizi chips, corie na kadhalika wanavunja ungo wana miaka 10, wana miaka 11, wana miaka tisa, hivi kweli mtoto huyo ame-qualify kuwa mke wa mtu?

Jamani akina baba tunaomba mtusaide, hawa ni watoto wenu kama siyo wa kwako ni wa mjomba wako, kama siyo wa mjomba wako ni wa kaka yako, kama siyo wa kaka yako ni wa shangazi yako. Ninaomba katika hili tuungane jamani, tuweke itikadi zetu pambeni, tunafahamu mambo mengine ya kidini yapo humu na imani za watu tunaziheshimu, lakini ili kuokoa nafsi hizi za watoto wa kike tunaomba basi tushirikiane kwa pamoja ili kwamba watoto wetu waweze kupona. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba niunge hoja kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa nimshukuru sana Mungu kwa ajili ya kutujalia afya sisi wote tuliomo humu ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na pole kwa wanafunzi waliopoteza maisha kule Arusha na nimpe pole mmiliki wa shule ya Lucky Vincent. Pia niwashukuru sana wale Wamarekani waliokuja kuchukua wale majeruhi watatu na kuwapeleka Marekani kwa ajili ya matibabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa ku- declare interest, mimi ni mdau wa shule binafsi. Nimwombe sana Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, hivi navyozungumza magari mengi ya shule katika kila mkoa yanakamatwa na kuwekwa yard. Gari asubuhi limetoka na wanafunzi nyumbani, linapeleka wanafunzi shule, wakienda kushusha watoto magari yale yanachukuliwa yanapelekwa yard kwamba gari hili bovu, tumepata pressure kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule zitafungwa ndani ya wiki mbili kuanzia sasa. Tunaomba wamiliki hawa wa shule binafsi wapewe nafasi ili wakati ule wa mwezi wa saba kipindi shule zikiwa likizo hayo mapungufu yaliyoko kwenye hayo magari yakafanyiwe kazi lakini wawaache watoto sasa hivi waendelee na shule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inaumiza kuona kwamba tunafanya vitu kwa kukurupuka. Hawa ma-traffic walikuwepo barabarani miaka yote wakati hawa watoto wanaenda shuleni na hayo magari. Leo imetokea ile ajali imekuwa mateso kwa wamiliki wengine. Mheshimiwa Mwigulu tusaidie kwenye hili, wasitishe hilo zoezi. Shule zitakapofungwa mwezi huu wa Saba magari yatarekebishwa halafu ndiyo michakato mengine iendelee. Hilo ni ombi kwa Mheshimiwa Mwigulu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie suala la hivi vitabu. Mimi nina maswali kama matano na Mheshimiwa Profesa Ndalichako atakapokuja hapa tunaomba atusaidie. Je, ni nakala ngapi za vitabu vya darasa la kwanza, la pili na la tatu vilivyokwishasambazwa. Pili, vitabu vimetayarishwa kwa gharama za walipa kodi Watanzania ambavyo ni vibovu, nani anawajibika kwenye hili? Fedha kiasi gani zimetumika kuandika, kuchapisha na kusambaza vitabu hivi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitabu hivi vilitumia muda wa miaka mitatu kuviandaa, tunasema vitabu hivi sasa havifai viondoke sokoni, je, ni muda gani zaidi utatumika mpaka tupate vitabu mbadala wa hivi? Sisi wamiliki wa shule binafsi, mfano mimi nimenunua vitabu vya shilingi milioni 18, najiuliza nalipwa na nani gharama zile? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naongea na Mheshimiwa Mulugo amenunua vitabu zaidi ya shilingi milioni 30, nani analipa gharama hizo? Wakati hawa watu wa TET wanaandaa huu mtaala, tuliomba kwamba wawashirikishe watu wengine mbalimbali kwa maana hata kutoka kwenye sekta binafsi ili waweze kupata inputs, wakajifungia vyumbani, wakakataa ushauri, leo wamekuja na vitu vibovu, nani anawajibika? Kwenye vitabu nimemaliza, ninavyo hapa ni upuuzi mtupu unaendelea hapa. Hata Kiingereza cha mtoto wa English Medium wa darasa la tatu hawezi kutunga vitabu vya namna hii. Sijui ni wataalam gani walitumika kutunga hivi vitabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya vitabu naomba nielekee kwenye suala zima la kodi kwenye shule binafsi. Waheshimiwa Wabunge wenzangu, naomba leo mnielewe, wakati mmiliki wa shule binafsi anaposimama na kuzungumza habari ya kodi 15 tunazizungumza, niliwahi kuzisoma hapa Bungeni mkashika vichwa, hatujitetei sisi maana kodi hizi mnazilipa ninyi ambao watoto wenu wanasoma kwenye hizo shule, tunawatetea akinamama ntilie na wananchi wa Tanzania kwa ujumla wao. Maana kama kwenye shule ada ingekuwa Sh.200,000 inakuwa Sh.400,000 kwa ajii ya hizi kodi na anayezilipa ni wewe mwananchi sio mimi mwenye shule, mimi ni wakala tu wa kuzikusanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaposimama hapa, ile negative attitude kupitia kwa wamiliki wa shule tuliopo humu Bungeni iondoke kwamba hawa watu wamekuja kutetea maslahi yao binafsi. After all kipele kinachokuwasha wewe mgongoni mwako unakijua wewe mwenyewe na maumivu yake, sasa nisiposema mimi atasema nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imagine majengo ya shule yalivyo makubwa unatakiwa ulipie property tax. Sheria ya Elimu ya mwaka 1977 iliomba watu binafsi waweze kuisaidia Serikali kutoa elimu kwa nchi hii. Sheria ya Elimu ya mwaka 1977 inatutambua sisi kama watoa huduma, Wizara ya Fedha inatutambua sisi kama wafanyabiashara, tushike lipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya nchi yetu inasimamiwa na Wizara zaidi ya moja, Wizara ya Elimu, TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi yaani nazungumzia SUMATRA huko kwenye mabasi na kadhalika, kwa hiyo, kila mtu anakupiga kivyake. Kusema ule ukweli it is like a crime for you owning a school in this country, wakati Uganda na Kenya mtu anayetaka kuanzisha shule anasaidiwa na Serikali almost 60%. Leo sisi watu wamejitoa, halafu haya mambo yangekuwa yamewekwa bayana wakati unatafuta usajili wa shule kwamba kuna kodi hizi na hizi, these are the criteria hakuna mtu angeanzisha shule kwenye hii nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna dirisha la wawekezaji kusamehewa kodi wanaokuja kuchukua Tanzanite zetu, ardhi zetu, malighafi mbalimbali lakini mwekezaji Mtanzania ambaye yeye ndiye ana uchungu na Watanzania wenzake, anayewekeza kwenye elimu ya nchi hii hana msamaha wa kodi hata kwenye vitu tu kama cement, bati na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya wenye shule 100 ukiwapima wote wana pressure na sukari labda wasiokuwa na maradhi haya ni wawili. Ni tabu tupu. Kama Serikali tu yenyewe inashindwa kutengeneza miundombinu mizuri na kutoa elimu bora kwa watu wake sembuse mtu mmoja? Ifike mahali Serikali itambue juhudi zinazowekwa kwenye hizi shule na watu binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, nimwombe Mheshimiwa Profesa Ndalichako, ilikuja barua kutoka kwa Kamishna wa Elimu kwamba hakuna mwanafunzi kukaririshwa darasa. Naomba nisome effect ya hilo suala la kutokumkaririsha mtoto darasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, matokeo ya mwaka jana na mwaka juzi ya kidato cha nne, wanafunzi waliopata division one mpaka division three ni 53,000. Mwaka 2015 wanafunzi waliopata division four na zero 354,000. Wanafunzi waliopata division one mpaka three mwaka 2016 ni 54,000 na wanafunzi 347,000 waliopata division four na zero. Yet mnatuambia hakuna kukaririshwa darasa, hivi tunawaandaa watoto wamalize darasa la saba na form four au tunawaandaa ili elimu wanayoisoma iwasaidie? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, huko kwetu kwenye shule za binafsi ni mapatano ya mzazi na mwenye shule, kila shule ina joining instruction kwamba mtoto wako asipofikia hii marks kwa kweli hawezi kwenda mbele na mzazi ana sign na tunakubaliana. Imetokea tu mzazi mmoja amekwenda kulalamika huko Wizarani ndiyo inakuja kuandikwa waraka wa namna hii, this is not fair!

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tunashangaa ufaulu ambao ni mbovu kiasi hiki, watoto wanaofaulu division one mpaka three ni 54,000 kwenye malaki ya wanafunzi unatoa waraka kama huu. Naomba Wizara ya Elimu itazame hivi vitu. Wakati mwingine wanapotoa maamuzi ya namna hii watushirikishe. Ninayezungumza ni Mwenyekiti wa wadau wa shule binafsi Tanzania niko humu humu ndani. Tunaomba tushirikishane hivi vitu vingine maana tunaumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna wanafunzi zaidi ya laki saba kwenye shule za binafsi Tanzania. Tumeajiri zaidi ya watu 45,000 Walimu na wasio walimu, kuna matrons, madereva, wapishi na kuna kila kitu. Tunachangia uchumi wa nchi hii kwa kununua vyakula na mahitaji mengine, sisi sio watu wadogo, tunaomba tutambulike kwenye hii nchi kwamba tunasomesha Watanzania wenzetu. Hakuna Mchina atakayekuja kujenga shule hapa, hakuna Mwingereza atakayekuja kujenga shule Tanzania ili Watanzania wasome. Wakiwasaidia kwenye elimu watawatawala namna gani? Sisi ndiyo wenye uchungu na Tanzania na ndiyo maana tumewekeza kwenye elimu. Kwa hiyo, tunaomba juhudi zetu zitambulike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tunacheza na referee mchezaji. Watoa elimu nchi hii ni TAMISEMI na watu wa shule binafsi lakini sisi tumekuwa watu wa kupokea maelekezo kutoka TAMISEMI, kutoka Wizara ya Elimu, tunaletewa tu hatushirikishwi. Kuwe na chombo maalum ambacho kita-regulate elimu ya nchi hii ili kuwe na fair play kati ya watoa elimu. Tuanzishe chombo kinaitwa Tanzania Education and Training Regulatory Authority ili kama kuna shule ya msingi ya Serikali haina choo ifungwe kama inavyofungwa shule ya mtu binafsi ambayo haina choo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa namshukuru sana na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kuthubutu kuthubutu kuanza kushughulika na masuala haya ya mchanga wa dhahabu, makinikia kwa lugha nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huko nyuma tulikuwa tunalalamika sana kwamba kuna mikataba mibovu tumeingia, tunapata hasara, hatulindi rasilimali za nchi. Leo Mheshimiwa Rais amethubutu kufanya hiki, ninashangaa kuna watu wanabeza hiki kinachoendelea. Ni ajabu sana.
(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni hatua kubwa sana ambayo Rais ameifikia, sisi kama wananchi wa Tanzania bila kujali itikadi zetu za vyama, ni lazima tumpongeze Mheshimiwa Rais kwa hatua hii. Hata kama kungekuwa na concequences zozote ambazo nchi inakwenda kuzipata kwa hili ambalo Rais amelifanya, ni lazima tukubaliane kama nchi kwamba hili ni letu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, wale wanaoanza kutoa lawama bado mapema, tayari Wizara ya Nishati na Madini inakuja, tusubiri, tuache nafasi ya Wizara nyingine kuendelea kuchangia kuhusu hili suala zima la mchanga wa dhahabu. Kwa hiyo, naomba tuwe na kumbukumbu kwamba tuliilaumu sana Serikali kwamba haichukui hatua, sasa Mheshimiwa Rais amechukua hatua. Napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa sababu hatua hizi zikiendelea kuchukuliwa, uchumi wetu unakwenda kutengemaa na hatimaye maisha mazuri yaliyoahidiwa yanakuwa ya uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia bajeti hii iliyoko mbele yetu. Ni ukweli usiopingika kwamba haiwezekani mtu mwenye nia ya dhati na mzalendo kwenye Bunge hili ukasimama bila kuanza kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nilipokuwa natazama kitabu cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, niliona jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais hakukurupuka kwenda kuzuia madini yetu kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Ilikua ni sehemu ya vipaumbele ambavyo Mheshimiwa Rais alivizungumza alipokuwa hapa Bungeni akihutubia tarehe 20 Novemba, 2015 na habari ya madini ilikuwa kipaumbele chake Namba nne (4).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya. Hawa wanaosema jana amemkaribisha mwizi Ikulu, yaani tunasema hiyo ni danganya toto, maana Mheshimiwa Rais alisema anakaribisha wahusika kwenye meza ya majadiliano, wala hakuandika invitation letter ya kumleta yule Mwenyekiti hapa. Watu walijipima wenyewe, wakaona jinsi gani tumetiwa hasara na Makampuni yao hayo, wakaona wabebe mzigo huo wa kuja ku-negotiate mambo yaliyofanyika ya kutia nchi hii hasara na Rais wetu na mambo haya yamefanyika hadharani. Kwa hiyo, hawa ndugu zetu wakikosa la kusema, ni bora wakati mwingine wakanyamaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niseme, watu hawa mara nyingi wanawasumbua hawa Waheshimiwa Mawaziri kwa maswali na vitu vingine vya namna hiyo na michango Bungeni humu wakihitaji Serikali kupeleka mahitaji kwenye Majimbo yao; wanahitaji elimu, maji na afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa, kama siyo Mheshimiwa Rais ameamua kuchukua jukumu hili zito la kujitoa muhanga akaamua kutetea rasilimali kwa ajili ya wananchi wa nchi hii, hivi hawa watu hayo mahitaji muhimu ya watu wao watayatoa wapi? Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais na tunaendelea kumwombea Mungu aendelee kumpa maisha marefu, maana ana mpango wa kututoa mahali tulipo kwenda mahali pengine. Ni sawa na Musa alivyowatoa wana wa Israel kwenye nchi ya utumwa ya Misri na kuwapeleka Kanaani. Ndicho anachokifanya Mheshimiwa Rais kwa sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwa bajeti nzuri sana ambayo imekuja mbele yetu. Tunafahamu kwamba kazi kubwa inafanyika. Naipongeza na timu nzima ambayo iko chini ya Wizara hii ya Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumza habari hii ya bajeti, naomba nianze na suala la makusanyo ya mapato. Naipongeza pia Serikali kwa sababu sasa imechukua hatua ya kuweza kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ili kudhibiti upotevu wa fedha hasa katika Halmashauri na maeneo mengine mbalimbali nchini. Ninachokiomba na kuishauri Serikali yangu ni kwamba, katika mgawanyo huu sasa wa ile Keki ya Taifa baada ya makusanyo haya kufanyika, basi mgawanyo wa Keki ya Taifa uweze kwenda sawia kwa nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nikizungumza hili, naomba nizunguzie suala zima la elimu. Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kukubali kupeleka katika shule zetu shilingi bilioni 18 kila mwezi kwa ajili ya elimu bila malipo. Ni kweli na ni dhahiri kwamba watoto sasa wanasoma mashuleni na changamoto zilizokuwepo huko nyuma hazipo tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nazungumza hivi, karatasi niliyoibeba mkononi mwangu inaeleza orodha ya shule ambazo zitakarabatiwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa ile bajeti ya 2016/2017. Nitoe masikitiko yangu kwamba Mkoa wa Manyara shule inayokwenda kukarabatiwa ni moja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetazama Mikoa mingi; Dar es salaam na Mikoa mingine, kila mtu aliiona hii karatasi. Kuna mikoa imepata bahati ya kukarabatiwa shule saba, sita, nane au nne lakini Mkoa wa Manyara tunakarabatiwa shule moja tu ya Nangwa iliyoko Wilayani Hanang. Naona kidogo hapa haijakaa sawa sawa. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri Ndalichako katika hili nalo atuangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna shule kongwe, tuna shule inaitwa Endagikoti ambayo iko Wilayani Mbulu, ilianzishwa mwaka 1929, tuna shule iko Mbulu inaitwa Dawi, imeanzishwa mwaka 1917; hizi shule ni kongwe. Masikitiko mengine ni kwamba, hatuna high schools kwenye Mkoa wa Manyara. Tuna high schools chache mno, mfano Wilaya ya Simanjiro haina high school hata moja; Hanang haina high school hata moja; Wilaya ya Mbulu ina high school mbili. Kwa hiyo, naomba, kwa sababu kipaumbele cha kwanza cha Mtanzania ni elimu na tukimkamata huyu elimu tukaacha kumwacha aende zake, watoto wetu watakombolewa. Naomba sana kwa hili tukumbukwe katika Mkoa wa Manyara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru na kuipongeza bajeti hii kwa kuwa inatambua akinamama; Mama Lishe, akinamama wanaofanya biashara zao ndogo ndogo na vijana hawa Wamachinga, hili ni jambo kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu kutambua hili. Wakati haya ya kurasimisha biashara zao yanafanyika, naiomba Serikali iangalie namna gani itakusanya kodi kwenye Makampuni makubwa ambayo hayakusanyi kodi inavyotakiwa ili ikiwezekana hawa watu wapewe baada ya kutambuliwa na kupewa maeneo ya kufanyia biashara zao, waweze kupatiwa muda wa kutosha ili kwamba sasa ifikie mahali nao waweze kuchangia kodi. Siyo kwamba wanapewa maeneo na wakati huo huo basi wanaanza tena kutozwa kodi wakati wanakuwa hawajajijenga vile inavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nasema bado tuna vyanzo vingi vya kodi vinavyoendelea kupotea; kuna Makampuni makubwa ambayo yanakwepa kodi. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais, juzi hapa alizindua data center kwa ajili ya collection ya mapato yote yanayotakiwa kukusanywa katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya Makampuni makubwa kama ya simu, Makampuni ya uchimbaji ambayo yamehodhi vitalu vikubwa kwa ajili ya uchimbaji lakini hawachimbi, vitalu hivyo vimekaa tu. Naomba Serikali ifanye tathmini ya kutosha waone kwamba Serikali inakwenda kufaidika na nini. Najua Mheshimiwa Rais ameshaanza hili na nina hakika tunakwenda kufanikiwa siku zijazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusisahau pia kwamba tatizo kubwa la maji bado lipo pale pale. Hatukuona ile Sh.50/= ambayo Waheshimiwa Wabunge wengi wameipigia kelele humu ndani ya kuongezwa kwenye mafuta ili kwamba tuweze kumtua mama wa Kitanzania ndoo kichwani. Bado naendelea kuililia na kuiomba Serikali yangu itazame hili kwa jicho la tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, akinamama wengi ambao ni wazalishaji na wachangiaji wa uchumi wa mapato ya nchi hii, wanapoteza muda mwingi kwenye kutafuta maji. Tunaomba ile Sh.50/= iongezwe kwenye mafuta ili kwamba tuweze kumtua mama ndoo kichwani. Wakati huo huo, Mkoa wa Manyara ni Mkoa wa wafugaji; tuna Kata kama za Ndedo kule Kiteto; kata nyingi tu za pale Kiteto, Simanjiro, Kata za Dongo, Kijungu, Lolera, Olboloti; Kata hizi hazina maji kabisa ya bomba wala mabwawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba ikiwezekana watu hawa wapate kuchimbiwa mabwawa. Juzi tulikuwa na mafuriko ya kutosha hapa nchini. Naiomba Serikali yangu kupitia hizi Halmashauri zetu, wahakikishe hawa watu wanachimbiwa mabwawa wakati ambapo mvua imesimama kama hivi, ili nyakati za mvua tuweze ku-track yale maji yaende kwenye hayo mabwawa kupunguza hii changamoto ya maji. Mbona ni rahisi! Kwa hiyo, naomba hasa maeneo ya Kiteto na Simanjiro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika Wilaya ya Hanang’ tunahitaji mabwawa pia, maana nako katika zile Kata tuna wafugaji wengi tu. Tukiweza kuwawekea wafugaji hawa maji kupitia mabwawa, wataacha kuhamahama, watakaa kwenye maeneo yao, maana rasilimali za kutosha zitakuwepo pale, maji pamoja na mambo mengine wanayoyahitaji. Naomba sana Mkoa wa Manyara ukumbukwe katika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna matatizo ya mawasiliano baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kiteto, tuna shida katika Kata za Ndedo pamoja na Makame. Bado watu hawa wanaishi ile karne ya kupanda juu ya miti ili uweze kuzungumza na ndugu yako aliyeko upande mwingine. Kwa hiyo, namwomba sana Waziri husika ama Mheshimiwa Waziri katika bajeti hii aikumbuke Wilaya ya Kiteto na maeneo mengine mengi tu ya Mkoa wa Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze pia masuala mazima ya mazingira ya ulipaji kodi. Naishauri sana TRA; naishauri Wizara ya Fedha waweze…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili nami niweze kuchangia hoja iliyopo mbele yetu ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kabla sijaanza naomba nitoe shukrani zangu za dhati kabisa na pongezi za kutosha kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa Awamu ya Tano kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya hususan katika Mkoa wetu wa Manyara. Napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Rais, alikuja mwaka jana mwezi Julai kuzindua barabara ya lami ambapo kwa mara ya kwanza ndiyo tunaiona lami Mkoa wa Manyara, hususani eneo la Simanjiro Mererani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale kutokana na swali langu nililoliuliza hapa Bungeni tarehe 31, Januari kwamba ni lini Mkoa wa Manyara hususan Kituo cha Afya cha Mererani kitapatiwa ambulance na nikajibiwa hapa na Mheshimiwa Jafo ya kwamba atalifanyia jambo hilo kazi.

Kwa kuwa Rais ni Waziri wa TAMISEMI pia, alichukua hoja hiyo na juzi alipokuja kufungua ukuta pale Mererani alikuja na ambulance hiyo, kwa hiyo namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kile alichowatendea watu wa Manyara, hususani eneo la Mererani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimekuwa nikiuliza mara kadhaa hapa Bungeni jinsi gani yale madini ya Tanzanite yanayochimbwa pale Mererani yanaweza kuwafaidisha wakazi wa Manyara maana yanachimbwa pale na yanauzwa Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, namshukuru Mungu kwamba tayari sasa tunaelekea kwenda kufaidika na madini haya ya Tanzanite kutokana na kwamba tayari ukuta umejengwa wa kuzuia upoteaji wa madini haya ambayo mara nyingi yamekuwa yakifaidisha mataifa ya nje zaidi kuliko wakazi wa Tanzania na hususani watu wa Simanjiro na Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwa ajili ya wananchi wa Tanzania ya kuweza kuzuia upotevu wa madini haya ya tanzanite na madini mengine ya dhahabu na kadhalika. Kila mtu ni shahidi hapa ni nini ambacho Rais amekifanya karibuni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba yale yote yanayofanyika katika nchi yetu ni kwa manufaa ya wananchi wenyewe.

TAARIFA . . .

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikatae taarifa hiyo. Unajua mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mtoto hazaliwi akakimbia siku hiyohiyo. Kazi inayoendelea kufanyika na imekwishafanyika ya jinsi gani ya kuhakikisha madini haya yananufaisha Watanzania hakuna ambaye hajui. Kwa hiyo, wenzetu wanashindwa tu ku- appreciate juhudi zinazofanywa na Rais pamoja na Serikali kwa ujumla. Naomba niendelee na mchango wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inajulikana kabisa kwenye ule ukuta unakwenda kuwekwa CCTV cameras, unakwenda kuwekwa electrical fence juu yake, kwa hiyo kwa namna moja ama nyingine haya madini hayataendelea kupotea, sambamba na kuhakikisha kwamba mikataba hiyo inaendelea kutazamwa kwa ajili ya kuhakikisha madini haya yanaendelea kutunufaisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kupitia pia kwa Waziri, Mheshimiwa Jafo pamoja na timu yake ya Naibu Mawaziri kwa yale ambayo wametufanyia watu wa Mkoa wa Manyara. Tayari Mkoa wa Manyara tumepokea fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikienda pale Mbulu tumepokea fedha kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Daudi, Kituo cha Afya cha Dahwi na Dongobesh pia. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kupitia Ofisi ya TAMISEMI kwa kuona changamoto hii na kuifanyia kazi. Natoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Mbulu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo ukisogea pale Babati tayari tumepata fedha kwa ajili ya Kituo cha Nkaiti nacho tayari kimejengwa lakini pia tumepata ambulance kwa ajili ya kituo hicho. Hizi juhudi sio za kubezwa, Serikali inafanya kazi na tunaona kwa macho ya nyama na tunaendelea kushuhudia. Hanang tumepata kwa ajili ya Kituo cha Simbai pamoja na ambulance, kwa hiyo, niseme tu naishukuru sana Serikali hii kwa ajili ya kile ambacho inaendelea kutenda kwa ajili ya watu wetu wa Manyara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikisogea kwenye suala zima la elimu, tumepata pia fedha, milioni 215 kwa ajili ya ukarabati wa shule mbalimbali, Shule ya pale Kiteto, tumepata fedha Mbulu, tumepata fedha Hanang, tumepata fedha maeneo mbalimbali kwenye Mkoa wetu wa Manyara kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule ikiwemo hostels, yakiwemo madarasa na ofisi za Walimu na matundu ya vyoo; kwa hiyo, niishukuru sana Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisemee kidogo mfuko wa asilimia tano za akinamama na asilimia tano za vijana. Nimesoma kwenye hotuba ya Waziri wa TAMISEMI jinsi gani ofisi yake ina mkakati wa kuhakikisha fedha hizi zinatengenezewa mwongozo mzuri wa namna gani ziwafikie walengwa hawa ili kuendelea kupunguza na kuondoa umaskini kwa vijana na akinamama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia Mheshimiwa Jafo, amesema wana mpango wa kuondoa riba katika mikopo wanayopewa akinamama na vijana, hili jambo ni jema sana na naitakia kila la heri ofisi ya Waziri, Mheshimiwa Jafo hili jambo likapate kufanikiwa ili watu wengi wakapate kukopeshwa fedha hizi na hatimaye tuendelee kuondoa umaskini kwa ajili ya watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru pia kwa ajili ya suala zima la miundombinu ya maji katika Mkoa wa Manyara, inaenda ikiimarika. Hata hivyo, nina ombi moja, kuna mradi wa maji mkubwa unaoendelea katika Wilaya ya Mwanga karibu na Bwawa la Nyumba ya Mungu, mradi huo unapakana sana na Vijiji vya Ngorika katika Wilaya ya Simanjiro na wale watu wa Ngorika hawana maji kabisa na mradi huo unaondoka kutoka kwenye eneo hilo la Ngorika ama karibu na Bwawa la Nyumba ya Mungu kuelekea Mwanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi lao ni moja tu kupitia Wizara hii ya TAMISEMI, kwamba ikiwezekana na wao waweze kupata connection ya maji hayo kwa sababu wako jirani sana, ili kwamba na wenyewe waendelee kufaidi matunda ya Serikali hii ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mafanikio yote niliyoyasema changamoto hazikosekani, naomba tu niseme bado tuna changamoto ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Manyara hususani maeneo ya Kiteto. Kipindi hiki Kiteto wamekuwa kama kisiwa, hawafikiki kwa sababu ya barabara kuvunjika sana kipindi hiki cha mvua. Niombe tu TARURA, najua wanafanya kazi kubwa na wanafanya kazi nzuri, kila mtu ameona hapa ya kwamba TARURA wanafanya kazi kubwa na barabara zao ni nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ikiwezekana wapate hata asilimia 50 kwa 50, TANROADS 50, TARURA 50, ili kwamba barabara nyingi zinazotumiwa na wananchi wengi maskini ziweze kutengenezwa na ziweze kupitika, waweze kuuza mazao yao, waweze kufanya biashara zao na hatimaye waondokane na umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kila mtu ni shahidi, mvua zimekuwa zikiendelea kunyesha kipindi hiki, barabara nyingi zimevunjika katika maeneo mbalimbali ya nchi hii, kwa hiyo, naomba ile dharura waliyoiomba TARURA wapatiwe ili waweze kuboresha baadhi ya maeneo korofi sana na wananchi waweze kuendelea na shughuli zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisichukue muda mrefu sana lakini niseme tu kwamba, tunaendelea kuona upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo katika shule zetu na hali hi imekuwa ikileta shida kwa wanafunzi wetu especially watoto wa kike. Naomba Ofisi ya Rais,TAMISEMI atakapokuja hapa Mheshimiwa Jafo hapa atuambie ni mkakati na mpango gani Ofisi hii imeandaa wa haraka sana yaani kama crash program ya kuhakikisha mwaka kesho hatuji hapa kuzungumzia suala la upungufu wa matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa tuna zaidi ya upungufu wa matundu ya vyoo 270,000. Ni aibu kuendelea kuzungumza suala la upungufu wa vyoo katika karne hii naomba, Mheshimiwa Jafo atakapokuja nina hakika yeye ni mchapakazi pamoja na Naibu Mawaziri na watu wa kwenye Ofisi yake watuambie ni mkakati gani mahsusi ulioandaliwa kuondoa tatizo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nisisahau suala zima la watoto wakike ambao wanabebeshwa mimba wangali bado wako shuleni. Hili suala si suala la kuchukulia mzaha mzaha, hawa watoto wanakatishwa masomo yao bila ridhaa yao, lakini ninaona bado hata ule mfumo uliyowekwa si rasmi wa wao kurudi hatuwatendei haki...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa mzungumzaji)

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili nami niweze kuchangia hoja iliyopo mbele yetu ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kabla sijaanza naomba nitoe shukrani zangu za dhati kabisa na pongezi za kutosha kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa Awamu ya Tano kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya hususan katika Mkoa wetu wa Manyara. Napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Rais, alikuja mwaka jana mwezi Julai kuzindua barabara ya lami ambapo kwa mara ya kwanza ndiyo tunaiona lami Mkoa wa Manyara, hususani eneo la Simanjiro Mererani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale kutokana na swali langu nililoliuliza hapa Bungeni tarehe 31, Januari kwamba ni lini Mkoa wa Manyara hususan Kituo cha Afya cha Mererani kitapatiwa ambulance na nikajibiwa hapa na Mheshimiwa Jafo ya kwamba atalifanyia jambo hilo kazi.

Kwa kuwa Rais ni Waziri wa TAMISEMI pia, alichukua hoja hiyo na juzi alipokuja kufungua ukuta pale Mererani alikuja na ambulance hiyo, kwa hiyo namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kile alichowatendea watu wa Manyara, hususani eneo la Mererani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimekuwa nikiuliza mara kadhaa hapa Bungeni jinsi gani yale madini ya Tanzanite yanayochimbwa pale Mererani yanaweza kuwafaidisha wakazi wa Manyara maana yanachimbwa pale na yanauzwa Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, namshukuru Mungu kwamba tayari sasa tunaelekea kwenda kufaidika na madini haya ya Tanzanite kutokana na kwamba tayari ukuta umejengwa wa kuzuia upoteaji wa madini haya ambayo mara nyingi yamekuwa yakifaidisha mataifa ya nje zaidi kuliko wakazi wa Tanzania na hususani watu wa Simanjiro na Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwa ajili ya wananchi wa Tanzania ya kuweza kuzuia upotevu wa madini haya ya tanzanite na madini mengine ya dhahabu na kadhalika. Kila mtu ni shahidi hapa ni nini ambacho Rais amekifanya karibuni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba yale yote yanayofanyika katika nchi yetu ni kwa manufaa ya wananchi wenyewe.

TAARIFA . . .

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikatae taarifa hiyo. Unajua mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mtoto hazaliwi akakimbia siku hiyohiyo. Kazi inayoendelea kufanyika na imekwishafanyika ya jinsi gani ya kuhakikisha madini haya yananufaisha Watanzania hakuna ambaye hajui. Kwa hiyo, wenzetu wanashindwa tu ku- appreciate juhudi zinazofanywa na Rais pamoja na Serikali kwa ujumla. Naomba niendelee na mchango wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inajulikana kabisa kwenye ule ukuta unakwenda kuwekwa CCTV cameras, unakwenda kuwekwa electrical fence juu yake, kwa hiyo kwa namna moja ama nyingine haya madini hayataendelea kupotea, sambamba na kuhakikisha kwamba mikataba hiyo inaendelea kutazamwa kwa ajili ya kuhakikisha madini haya yanaendelea kutunufaisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kupitia pia kwa Waziri, Mheshimiwa Jafo pamoja na timu yake ya Naibu Mawaziri kwa yale ambayo wametufanyia watu wa Mkoa wa Manyara. Tayari Mkoa wa Manyara tumepokea fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikienda pale Mbulu tumepokea fedha kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Daudi, Kituo cha Afya cha Dahwi na Dongobesh pia. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kupitia Ofisi ya TAMISEMI kwa kuona changamoto hii na kuifanyia kazi. Natoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Mbulu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo ukisogea pale Babati tayari tumepata fedha kwa ajili ya Kituo cha Nkaiti nacho tayari kimejengwa lakini pia tumepata ambulance kwa ajili ya kituo hicho. Hizi juhudi sio za kubezwa, Serikali inafanya kazi na tunaona kwa macho ya nyama na tunaendelea kushuhudia. Hanang tumepata kwa ajili ya Kituo cha Simbai pamoja na ambulance, kwa hiyo, niseme tu naishukuru sana Serikali hii kwa ajili ya kile ambacho inaendelea kutenda kwa ajili ya watu wetu wa Manyara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikisogea kwenye suala zima la elimu, tumepata pia fedha, milioni 215 kwa ajili ya ukarabati wa shule mbalimbali, Shule ya pale Kiteto, tumepata fedha Mbulu, tumepata fedha Hanang, tumepata fedha maeneo mbalimbali kwenye Mkoa wetu wa Manyara kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule ikiwemo hostels, yakiwemo madarasa na ofisi za Walimu na matundu ya vyoo; kwa hiyo, niishukuru sana Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisemee kidogo mfuko wa asilimia tano za akinamama na asilimia tano za vijana. Nimesoma kwenye hotuba ya Waziri wa TAMISEMI jinsi gani ofisi yake ina mkakati wa kuhakikisha fedha hizi zinatengenezewa mwongozo mzuri wa namna gani ziwafikie walengwa hawa ili kuendelea kupunguza na kuondoa umaskini kwa vijana na akinamama.


Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia Mheshimiwa Jafo, amesema wana mpango wa kuondoa riba katika mikopo wanayopewa akinamama na vijana, hili jambo ni jema sana na naitakia kila la heri ofisi ya Waziri, Mheshimiwa Jafo hili jambo likapate kufanikiwa ili watu wengi wakapate kukopeshwa fedha hizi na hatimaye tuendelee kuondoa umaskini kwa ajili ya watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru pia kwa ajili ya suala zima la miundombinu ya maji katika Mkoa wa Manyara, inaenda ikiimarika. Hata hivyo, nina ombi moja, kuna mradi wa maji mkubwa unaoendelea katika Wilaya ya Mwanga karibu na Bwawa la Nyumba ya Mungu, mradi huo unapakana sana na Vijiji vya Ngorika katika Wilaya ya Simanjiro na wale watu wa Ngorika hawana maji kabisa na mradi huo unaondoka kutoka kwenye eneo hilo la Ngorika ama karibu na Bwawa la Nyumba ya Mungu kuelekea Mwanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi lao ni moja tu kupitia Wizara hii ya TAMISEMI, kwamba ikiwezekana na wao waweze kupata connection ya maji hayo kwa sababu wako jirani sana, ili kwamba na wenyewe waendelee kufaidi matunda ya Serikali hii ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mafanikio yote niliyoyasema changamoto hazikosekani, naomba tu niseme bado tuna changamoto ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Manyara hususani maeneo ya Kiteto. Kipindi hiki Kiteto wamekuwa kama kisiwa, hawafikiki kwa sababu ya barabara kuvunjika sana kipindi hiki cha mvua. Niombe tu TARURA, najua wanafanya kazi kubwa na wanafanya kazi nzuri, kila mtu ameona hapa ya kwamba TARURA wanafanya kazi kubwa na barabara zao ni nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ikiwezekana wapate hata asilimia 50 kwa 50, TANROADS 50, TARURA 50, ili kwamba barabara nyingi zinazotumiwa na wananchi wengi maskini ziweze kutengenezwa na ziweze kupitika, waweze kuuza mazao yao, waweze kufanya biashara zao na hatimaye waondokane na umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kila mtu ni shahidi, mvua zimekuwa zikiendelea kunyesha kipindi hiki, barabara nyingi zimevunjika katika maeneo mbalimbali ya nchi hii, kwa hiyo, naomba ile dharura waliyoiomba TARURA wapatiwe ili waweze kuboresha baadhi ya maeneo korofi sana na wananchi waweze kuendelea na shughuli zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisichukue muda mrefu sana lakini niseme tu kwamba, tunaendelea kuona upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo katika shule zetu na hali hi imekuwa ikileta shida kwa wanafunzi wetu especially watoto wa kike. Naomba Ofisi ya Rais,TAMISEMI atakapokuja hapa Mheshimiwa Jafo hapa atuambie ni mkakati na mpango gani Ofisi hii imeandaa wa haraka sana yaani kama crash program ya kuhakikisha mwaka kesho hatuji hapa kuzungumzia suala la upungufu wa matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa tuna zaidi ya upungufu wa matundu ya vyoo 270,000. Ni aibu kuendelea kuzungumza suala la upungufu wa vyoo katika karne hii naomba, Mheshimiwa Jafo atakapokuja nina hakika yeye ni mchapakazi pamoja na Naibu Mawaziri na watu wa kwenye Ofisi yake watuambie ni mkakati gani mahsusi ulioandaliwa kuondoa tatizo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nisisahau suala zima la watoto wakike ambao wanabebeshwa mimba wangali bado wako shuleni. Hili suala si suala la kuchukulia mzaha mzaha, hawa watoto wanakatishwa masomo yao bila ridhaa yao, lakini ninaona bado hata ule mfumo uliyowekwa si rasmi wa wao kurudi hatuwatendei haki...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza nianze kwa kuunga mkono hoja hii ya Wizara ya Elimu iliyoko mbele yetu, pia naomba ni-declare interest kwamba mimi ni mdau wa elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianzie alipoishia dada yangu Mheshimiwa Bura kwa suala zima la TEHAMA katika shule zetu hasa za Serikali, siyo tu kwamba mtoto anaiona computer akiwa labda secondary, I mean O-Level pia hatuna mtaala wa TEHAMA katika kidato cha tano na cha sita, kwa hiyo kuna connection inakosekana hapo katikati kutoka kidato cha nne mpaka Chuo Kikuu, ninaiomba Wizara ya Elimu ione namna gani wataandaa mtaala wa TEHAMA wa kidato cha tano na cha sita ili watoto hawa waweze kupata muendelezo mzuri wa masomo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze sana Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nimpongeze pia Waziri wa Elimu, Naibu Waziri na watendaji wote kwa kazi nzuri wanayoifanya tunafahamu kwamba changamoto ni kubwa, Tanzania ni kubwa na mahitaji ni makubwa hilo tunalitambua, tuseme tu kwa yale ambayo tayari yamekwishakufanyika kwa kweli binafsi kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu niendelee kuwapongeza, pongezi kubwa sana zimuendee Profesa Ndalichako najua anajitahidi sana na timu yake lakini yale ambayo bado hamjaweza kuyafanya ndiyo haya ambayo tutayasema na tunaendelea kuwaombea Mungu awasaidie ili muweze kuyafanikisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie suala zima la ufaulu wa wanafunzi kuanzia kwenye level ya primary kwenda sekondari. Ni kweli kwamba wanaomaliza shule ni wengi, lakini wanaofaulu kwa ufaulu unaotakiwa ni wachache, elimu ni uwekezaji tuwekeze sana kwenye elimu ili kwamba nchi yetu iweze kupona. Elimu ni uhai, elimu ni maisha nilikuwa nafikiri kwamba hata bajeti ya mwaka huu itakapoletwa kusomwa hapa badala ya kuwa na priority lukuki hebu tuanze na priority namba moja mwaka huu iwe elimu halafu tuone kama hatutaoka hapa tulipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila elimu bora nchi hii haiwezei kukombolewa, naomba niseme machache kupitia Wizara hii hasa Mkoa wa Manyara, wanafunzi wa shule wanaosoma katika shule za Wilaya ya Simanjiro na Wilaya ya Kiteto wanasoma umbali mrefu sana hizo ni Wilaya ambazo ni za kifugaji, watoto wanatembea mwendo mrefu kwa mfano pale Orkesment ile shule ndiyo inayotegemewa na Kata nyingi Kata za Kitwahi na vijiji vyake mtoto anatembea kilometa 20 mpaka 30 kwa siku, mtoto huyu akifika shuleni ni lazima atakuwa amechoka na hawezi kumsikiliza mwalimu vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ninaomba ile shule ina hosteli waongezewe miundombinu ya hosteli ili wale watoto wa kifugaji waweze kupata mahali pa kuweza kutulia na kusoma. Vivyo hivyo katika Kata za Ndedo na Kata zingine za Wilaya ya Kiteto. Wilaya hizi zimekuwa za mwisho muda mrefu katika Mkoa wa Manyara kwa sababu ya miundombinu yake ya umbali wa kutoka watu wanakoishi na shule ziliko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nizungumzie ufaulu wa Kidato cha Nne kwa miaka mitatu minne mfululizo, wanafunzi ambao wamekuwa wakifaulu kwa division one mpaka three ni wachache mno. Kwa miaka mitatu 2015 – 2016 - 2017 ni wanafunzi 95,000 tu kati ya wanafunzi zaidi ya laki moja wanaomaliza kidato hicho, ifike mahali tukae kama nchi tujadili mustakabali wa elimu nchi hii, vinginevyo kila siku tutakuja na huu wimbo na bahati mbaya sana ni hii tunatumia Sheria ya Elimu ya mwaka 1978, Sera ni ya mwaka 2014 hivi vitu havi-match ndiyo maana mambo mengi yanashindwa kwenda. Sheria iletwe, ibadilishwe, iendane na wakati tulionao sasa vinginevyo huu wimbo bora elimu na siyo elimu bora hautokaa uishe kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba sana Profesa Ndalichako atakapokuja hapa aseme ni namna gani sasa tutaondoa hizi zero nyingi na four nyingi kwenye matokeo haya ya kidato cha nne niliwahi kuzungumza hapa kwamba hivi tunachokifanya ni kuhakikisha mwanafunzi amemaliza
shule ama ameelimika? Kwa hiyo, niwaombe sana watu wa Wizara ya Elimu mtakapokuja hapa hebu mje na mkakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kwa vile sasa hatuna ajira za kutosha niliwahi kushauri hata kwenye Kamati nilikokuwepo mwanzo ya TAMISEMI kwamba na niliwahi kuomba Wizara ya elimu pia tuweke mtaala wa ujasiriamali (entrepreneurship) kwenye elimu kwa sababu ni kweli hatuna ajira za kutosha ili wanafunzi wetu watoke wakiwa na skills, wale watakaokuwa wameshindwa kuendelea na masomo waweze kujiajiri ili kupunguza changamoto ya ajira. Siyo hivyo tu, ninajua kwamba Mheshimiwa Rais na Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikipambana sana na suala zima la rushwa, Biblia inasema: “Mfundishe mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeomba mara nyingi ikiwezekena hata suala la rushwa na ubaya wake liwekwe kwenye mtaala ili watoto wafundishwe kuanzia kindergarten ubaya wa rushwa watakapokuja kuwa watu wazima kama sisi wanafahamu madhara ya rushwa, sasa hivi tunaongea na samaki mkavu ambaye ameshakuwa mkubwa unamkunja anavunjika, kwa hiyo, haisaidii, vile vitu ambavyo vinahitaji moral discipline viwekwe kwenye mitaala yetu ili kuweza kusaidia kuwajenga Watanzania ambao watakuwa wazalendo na nchi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie Chuo cha Ualimu Mamira kilichopo Mkoani Manyara. Chuo kile ni chuo cha Grade A, wameomba kuanzisha diploma pale kwa maana ya waweze kuwekeza kwenye Walimu wa wa sayansi tu, ombi lao nina hakika lipo kwenye meza ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, wameomba walimu kama watano wa sayansi ili waweze kuwafundishwa walimu wa diploma wa sayansi ili kuweza uondokana na upungufu wa walimu wa sayansi tulionao, ninaomba ombi hilo kama inawezekana lishughulikiwe haraka ili mwaka huu waweze kusajili walimu wa level ya diploma na tuweze kuendelea kupunguza huo upungufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, walimu wa sayansi ni kilio nchi nzima; naomba kushauri kwamba badala ya ku-split hizi effort ndogo ambazo zinafanywa na Serikali, kwa vile shule ziko nyingi hususani shule za kata za Serikali kama inawezekana shule chache ziwe identified kama ni ni kila Wilaya tuwe na shule mbili sinazo-deal na sayansi, maabara zake ziboreshwe na walimu wa sayansi wapelekwe kwenye shule hizo badala ya kuhakikisha kila shule inafundisha sayansi wakati walimu wa sayansi hatuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna upungufu wa zaidi ya walimu 26,000 wa sayansi, walimu hawa wanastaafu, wanabadilisha taaluma, wengine wanafariki, kwa hiyo itatuchukua zaidi ya miaka 15 mpaka kuhakikisha tunapata walimu, juhudi za makusudi zinahitajika kuhakikisha kwamba kupanga ni kuchagua, kwa hiyo, tuchague kwamba shule kadhaa zifundishe sayansi na shule zingine ziendelee na masomo mengine ili kuweza ku-utilize walimu tulionao badala ya kuzalisha zero za sayansi kila mwaka, ifike mahali sasa tufikiri nje ya boksi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisemee kwa haraka shule ya watoto walemavu ya Katesh A iliyopo Wilayani Hanang’, shule ile ina watoto walemavu wapatao zaidi ya 150 na ni shule ya mchanganyiko kuna watoto wasio walemavu pia. Shule ile ni kama imesahaulika sana, pale kuna watoto wenye albinism wanapata shida, hawapati yale mafuta kwa ajili ya ngozi zao, miundombinu ya ile shule ni kama imesahaulika kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe sana Mheshimiwa Waziri aweze kuangalia namna gani wale wanafunzi wa ulemavu tofauti kwenye shule ya Katesh A pale Hanang’ waweze kupatiwa msaada ili na wao waweze ku- enjoy masomo yao kama watoto wengine wasio na ulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme suala la ukaguzi. Ni kweli kwenye kudhibiti ubora tunaona wapo Wadhibiti Ubora wengi lakini zaidi wamekuwa wakidhibiti ubora kwenye private schools wanasahau kudhibiti ubora kwenye shule za Serikali. Ukiona shule hizo wanazosema ni za private zinafanya vizuri ni kwa sababu wao wamejikita zaidi kwenye kudhibiti upande wa pili badala ya shule ya Serikali ambazo pia ndiyo nyingi. Automatically mtu mwenye shule binafsi yeye mwenyewe ni mdhibiti namba moja, maana hakuna anayetaka ku-invest kwa hasara.

Kwa hiyo, wao wange-focus zaidi hata kwenye shule za Serikali maana watoto wetu wengi wako kule na mengi hayafanyiki kule. Ninawaomba sana watu wa ukaguzi wapatiwe vifaa kama walivyosema wenzangu kama ni bodaboda hizi ama pikipiki kwa ajili ya ukaguzi ili waweze kuzifikia hizo shule, shule ni nyingi na miundombinu ni…

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi ninapenda kukushukuru kwa ajili ya kupata nafasi hii ya kuchangia hotuba ya bajeti. Pia napenda kupongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais, Mheshimiwa Dkt. Magufuli pamoja na Wizara hii ya Fedha Mheshimiwa Dkt. Mpango na Naibu Waziri wake wanafanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua tumesikia sana humu ndani watu wakisema bajeti hii ni hewa ama bajeti ya tangu mwaka 2016 ni hewa. Sasa nashangaa sijui hawa ndugu zetu wanaishi nchi gani ambako hawaoni maendeleo makubwa anayoendelea kufanyika ndani ya nchi hii. Wenzangu wamesema tumeona mengi bajeti ya Wizara ya Afya imekwenda juu sasa hivi mpaka madawa yana-expire hayana watumiaji kule kwenye hospitali zetu, lakini bado watu wanasema bajeti ni hewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuchukua nafasi hii kupongeza sana Wizara ya Fedha kwa kuweza kuondoa tozo ya VAT katika taulo za watoto wetu wa kike. Kimekuwa ni kilio cha Wabunge wanawake na Wabunge wanaume ndani ya Bunge hili kwa ajili ya watoto wetu ambao mara nyingi wamekuwa wakikosa shule kwa takribani siku 70 ndani siku zile zote za kusoma. Hili siyo jambo dogo, tunaishukuru sana Wizara hii na Serikali kwa ujumla, Mungu awabariki sana kwa jambo hili jema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitoka kwa mtoto wa kike naomba nielekee kwa akinamama ambao muda mwingi wamekuwa wakitafuta maji na muda wao mwingi ukiwa

umepotelea kwenye suala zima la kusaka maji vijijini. Wabunge wenzangu wamezungumza suala la tozo ya Sh.50 kwenye mafuta, nami naomba niungane nao ya kwamba tuweze kutoza hiyo Sh.50 na kuweza kuongeza kwenye bajeti ya maji ili kuweza kumtua mwanamke ndoo kama ambavyo Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi ya 2015/2020 inasema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kwamba jambo lingine lolote katika maisha kwa mfano hata umeme unaweza ukawa ni option, lakini maji hayana mbadala. Kwa hiyo niiombe sana Wizara hii ya Maji iweze kupatiwa fedha na zaidi sana ipate hii Sh.50 ili kwamba akinamama waweze kuondokana na adha kubwa ya utafutaji wa maji na huku muda wao mwingi ukipotelea huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nizungumze suala la kutokupelekwa kwa fedha kwenye Halmashauri zetu mbalimbali nchini kwa wakati, pia fedha hizo zimekuwa hazipelekwi tu kwamba kwa wakati. Hii imekuwa ikiathiri hata ile asilimia 10 ya wanawake na vijana kwa kiwango kikubwa kwa sababu yale makusanyo ya ndani ambayo ndiyo yanapaswa kutoa asilimia 10 yamekuwa hayafanikiwi kwa kiwango kikubwa kwa sababu Wakurugenzi wetu wanaishia kutumia hizo fedha kwa ajili ya kukidhi matakwa na mahitaji mbalimbali katika Halmashauri zao kwa sababu ya kukosa fedha zile ambazo zinatakiwa kutoka Serikali Kuu kurudi kwenye Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niiombe sana Serikali itazame hili kwa jicho pana kidogo ili kwamba fedha hizo kama ambavyo tulizungumza huku nyuma kwamba siyo ni za kihuruma huruma bali zipo kisheria ziweze kuwafikia wanawake na vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma hapa tumekuwa tukipendekeza katika Bunge hili kwamba kuna kundi maalum la walemavu. Hili kundi limesahaulika. Bado imeonekana asilimia tano vijana, asilimia tano akinamama, lakini bado naendelewa kushauri kama ambavyo iliwahi kushauriwa

hapa tutenge asilimia mbili katika hizo 10 ziende kwa walemavu. Hili ni kundi maalum. Mtu anaweza akawa na ulemavu wa kiungo kimojawapo lakini akawezeshwa na bado akaweza kufanya biashara ama kazi ambayo inaweza ikamfanya yeye na familia yake wakapata maisha. Kwa hiyo, nilikuwa naomba kundi hili lizingatiwe la walemavu katika zile asilimia tano za vijana itolewe hapo asilimia moja na kwa akinamama itolewe asilimia moja zipelekwe kwa kundi hili rasmi la walemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu cha hotuba ya Waziri tumeona jinsi ambavyo amekuja na miradi ya kielelezo kama Stiegler’s Gorge mradi ambao kwa sehemu kubwa pia umekuwa ukibezwa. Niseme kama tulivyosema tunaelekea kwenye Serikali ya viwanda ama uchumi wa viwanda hatuwezi kuwa na uchumi wa viwanda pasipokuwa na umeme toshelevu. Kwa hiyo, naunga mkono hoja suala zima la huu umeme wa Stiegler’s ili kwamba tuweze kupata viwanda vya kutosha na hatimaye tuondoke katika umaskini na kuingia katika uchumi wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimpongeze Waziri amekuja na Tax Amnesty kwa maana ya kwamba zimeondolewa riba katika madeni ya wafanyabiashara wengi wanaodaiwa, lakini muda uliotolewa nina wasiwasi kwamba hautoshi. Huu muda wa miezi sita kwa vile hawa watu wako hapa hapa nchini na hawaendi mahali popote na hawatoroki na Wazungu wanasema the payment delayed is interest saved, kwa nini basi Waziri asitazame namna gani wanaweza haidhuru hata miezi 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa wamepewa muda mfupi wa miezi sita hii inaweza ikasababisha hawa wafanyabishara wakakimbia tena benki kwenda kukopa kwa riba ya juu ili kuweza kulipa haya madeni waliyopewa muda wa miezi sita. Hii inaweza ikaathiri working capital yao. Kwa hiyo, nilikuwa namuomba Waziri atazame namna gani anaweza akaangalia tena kwa mara nyingine, namna gani anaweza akaongeza huu muda kwani madeni haya yatakapolipwa bado uchumi wetu utaendelea kukaa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa kuliko yote niwaombe tena wafanyakazi wa TRA wanapodai kodi waweze kuwa friendly na wale watu wanaowadai kodi. Tunajua kodi ni jukumu la kila Mtanzania na bila kodi nchi yetu haiwezi kwenda lakini haidhuru waweze kuwa na lugha rafiki na nina hakika Watanzania ni watu waungwana na waelewa watalipa tu hizo kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kumekuwa pia na changamoto kubwa kwenye suala zima la kilimo. Tumeona bajeti ya kilimo ya mwaka 2017/2018, ilikuwa imetengewa takribani bilioni 150, lakini sana kwa mwaka huu tumeona imeshushwa kwa asilimia 34.7 nini kimetokea. Huku tunazungumza uchumi wa viwanda. Viwanda vyetu vinategemea raw material kutoka sehemu kubwa ya wakulima kwa maana ya kwamba nchi hii ina wakulima asilimia zaidi ya 65 ama asilimia 66. Sasa kama bajeti hii imeshuka kwa kiwango hiki kama hatutaweka nguvu kubwa kwenye suala zima la kilimo tunatoa wapi malighafi ya kupeleka katika viwanda vyetu? Kwa hiyo, naomba sana Wizara itazame namna gani itaondoa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii nami niweze kutoa mawazo yangu katika bajeti hii ya Wizara ya Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba huwezi kuanza kuzungumza habari ya madini na rasilimali za nchi hii pasipo kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais. Nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa nia yake ya dhati ya kulinda maliasili ya Taifa hili yakiwemo madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nia yake ya dhati imepelekea kujengwa kwa ukuta katika Mji wa Mererani Mkoani Manyara ambako ndiko nakotokea mimi. Nia hii ya dhati imepelekea Jeshi letu la Ulinzi kulinda ukuta ule, nimeona watu wanabeza ulinzi wa Jeshi letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukizungumza suala zima la uzalendo, uzalendo huo unapatikana jeshini kwa asilimia 100. Isingewezekana tuweke ukuta wa gharama kiasi kile halafu tuweke walinzi wa Jadi. Kwa hiyo, mimi nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa ujenzi wa ukuta ule na hatimaye kuweka Jeshi letu kulinda maliasili zilizoko pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajua kwamba bado tunahitaji CCTV Camera kwa ajili ya kudhibiti upotevu ama utoroshwaji wa madini kwa namna nyingine, maana eneo lenyewe ni kubwa ni kilometa zaidi ya 24. Kwa hiyo, niombe tu Serikali iendelee na nia yake ya dhati kabisa ya kudhibiti upotevu wa madini, siyo tu madini ya tanzanite yaliyoko Mererani lakini maeneo mengine yote ambako madini ya namna mbalimbali kama dhahabu na madini mengine yanakopatikana ili madini haya yaweze kusaidia uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nitoe pongezi za dhati kwa Mawaziri wa Wizara hii nikianza na Mheshimiwa Angellah Kairuki, Mheshimiwa Doto Biteko na Mheshimiwa Stanslaus Nyongo. Hawa watu wanafanya kazi, tunawaona muda mwingi wapo field na kazi yao inaonekana kusema ule ukweli. Kazi yao imepelekea sasa kuongezeka kwa mapato haya kupitia mauzo ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukirudi katika eneo la Mererani ongezeko la pesa ambayo ilikuwepo kabla ya 2017/ 2018 tumeiona, ongezeko limekuwa kubwa madini haya sasa yanawafaidisha wananchi wa Manyara pamoja na Tanzania kwa ujumla. Niseme hongera kwa Rais, hongera kwa Serikali kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue pia nafasi hii kupongeza Bunge lako Tukufu ambalo lilifanyia marekebisho Sheria ya Madini ya mwaka 2017 na Kanuni zake saba zilizoundwa kwa ajili ya kuhakikisha malengo ya kulinda na kudhibiti rasilimali hii ya madini yanatimia. Mwaka jana tulipitisha hapa Sheria mbili za The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) na The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms), kisa ni kwamba lazima tuhakikishe madini haya yanawanufaisha Watanzania ambao ni wazawa na ndiyo wenye uchungu na madini haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la EPZA pale Mererani. Naomba Serikali itusaidie kuhakikisha kwamba EPZA wanawavutia wawekezaji ili lile eneo pale liweze kutumika. Tuna eneo kubwa tu ambalo lina almost hekari 1,311 ambalo ni kwa ajili ya uwekezaji. Tunaomba Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Madini pamoja na EPZA waweze kujenga eneo lile ili kuweza kuwavutia wawekezaji ili madini yale yachakatwe, yauzwe mahali pale na ajira na mapato yaweze kuongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie ajira katika sekta ya madini. Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa mwaka 2012 tulikuwa na ajira kati 500,000 mpaka 1,500,000. Nataka tu kufahamu ni takribani miaka sita sasa tangu tafiti hizo zimefanyika, maana kwenye kitabu hiki sijaona ajira hizo zimeongezeka ama zimepungua kwa kiwango gani kwa mwaka huu 2017/2018. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukiangalia dira na dhima ya Wizara hii ya Madini ni kuhakikisha pia wanabuni na kusimamia sera, mikakati na mipango ya kuendeleza sekta ya madini; kusimamia migodi na kuhamasisha shughuli za uchimbaji pamoja na utafutaji wa madini; kuratibu na kusimamia uongezaji wa thamani ya madini kwenye biashara ya madini; kukuza ushiriki wa wazawa yaani local content kwenye shughuli za utafutaji; kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo ya wachimbaji wadogo; na kusimamia taasisi na mamlaka zilizoko chini ya Wizara hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa dhima ya Wizara hii inajieleza, tuna wachimba wadogowadogo nchi hii. Eneo la Mererani tuna wachimbaji wadogowadogo wanaitwa Apolo, niombe Serikali iweze kusaidia kuwapa elimu ya kijiolojia kwamba madini haya yanapatikana wapi zaidi, ukiacha eneo tu la Mererani lakini pia wapatiwe elimu ya namna ya uchimbaji na ruzuku ili waweze kusaidia familia zao na kuongeza mapato kwa ajili ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, siku za nyuma kulikuwa kuna pesa wanapewa wachimbaji wadogowadogo kama ruzuku. Nishauri kwa kuwa zile fedha wakati mwingine utakuta walikuwa wanagawana nusu kwa nusu na hawa waliokuwa wanawapatia hizo fedha zikawa haziwanufaishi kihivyo, wapewe vifaa vya uchimbaji. Hivyo vifaa vya uchimbaji vinaweza vikawasaidia wachimbaji hawa wadogowadogo na kuwainua na hatimaye kuwa wachimbaji wa kati na wakubwa ambao wataongeza thamani ya kazi wanayoifanya na hatimaye kuongeza mapato. Kwa hiyo, niombe sana watu hawa wapatiwe mafunzo ya kutosha ya kiteknolojia ili na wao waweze kuchimba kisasa zaidi kuliko kuchimba kwa njia ambazo ni za kizamani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo ya smelter yamesemwa na Wabunge wenzangu na mimi nichangie hilo. Ni muhimu kupata smelter sasa kwa sababu katika uchimbaji kwa mfano wa dhahabu ama tanzanite kuna madini mengi madogomadogo ambayo yangeweza kuongeza thamani ya madini yetu yanapotea kwa sababu smelter hii ilikuwa inatumika nje ya nchi. Niweze kuiomba Serikali na kuiombea Serikali yangu iweze kufanikisha suala la uwekaji wa smelter hapa nchini ili tuweze kufaidika na madini yale mengine yanayopatikana baada ya kuchenjuliwa kwa yale madini makubwa kama dhahabu na tanzanite. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wachimbaji wadogowadogo ambao ni wanawake, ni nini mkakati wa Serikali katika kuhamasisha na kusaidia kuwapatia wanawake wachimbaji elimu ya kutosha ili na wao waweze kuongezeka kimapato na hata uwezo. Maeneo mengi yanayozunguka madini haya, wanawake kazi yao imekuwa ni kupika ama kufanya biashara ya mama ntilie. Ifike sasa mwanamke pia ainuliwe katika suala zima la uchimbaji wa madini. Wapo wanawake kadhaa tunawafahamu ambao kwa kweli wameweza kufanya hizi kazi, wamesomesha watoto wao, wamejenga nyumba zao na kusaidia ongezeko la mapato katika Serikali yetu. Kwa hiyo, naomba Wizara iangalie kwa macho mawili suala zima la kumuongezea mwanamke uwezo wa uchimbaji wa madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bado madini haya hayajatangazwa vilivyo duniani ya kwamba yanatokea Tanzania na katika kijiji kidogo hicho ama maeneo madogo haya ya Simanjiro. Niliwahi kusafiri kwenda Marekani mwaka 2011 nikatembelea Taasisi moja inaitwa Tanzanite Liquidation Channel iko Austin pale Texas pale Marekani. Taasisi ile nilipofika pale ilikuwa imeajiri Wamarekani 400 wanaofaidi kupitia tanzanite inayotoka Mererani lakini karibu kabisa na maeneo ambako tanzanite hiyo inatoka, ukifika ukizungukia zile shule zilizoko maeneo yale, mfano shule moja inaitwa Imishie hawana...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nami nimshukuru Mungu kwa kupata nafasi ya kuchangia hoja zilizopo mbele yetu za Wizara zote mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue nafasi hii pale alipoishia kaka yangu Papian na mimi nichukue nafasi hii kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano ambaye ndiye aliyependwa na Watanzania kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 - 2020. Huwezi kusimama katika Bunge hili ukashindwa kusema habari za Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, vinginevyo wewe hautakuwa mzalendo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengi yamefanyika katika nchi hii. Kabla sijaenda mbali, nielekeze pia pongezi hizo kwa Waziri wa TAMISEMI, kaka yangu Mheshimiwa Jafo na Naibu wako, nielekeze pongezi hizi kwa ndugu yetu Mheshimiwa Mkuchika na Naibu Waziri Mheshimiwa Dkt. Mwanjelwa, Mungu awabariki sana kwa utendaji wenu uliotukuka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na nukuu hii inasema: “A good leader is not measured by how long he/she stayed in a particular position, it is measured by how many positive changes you brought over there.” Tangu Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mambo makubwa yamefanyika katika nchi hii na ni kazi yetu sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kuzitafsiri kazi hizo kwa wananchi wetu kupitia Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye suala zima la afya, niipongeze Wizara ya Afya pamoja na hii Wizara ya TAMISEMI kwa upande wa miundombinu. Tangu mwaka 1961 mpaka leo tulikuwa na vituo vya afya visivyozidi 695 lakini ndani ya miaka mitatu kutokana na utendaji uliotukuka wa Serikali ya Awamu ya Tano tumejengewa vituo vya afya zaidi ya 300. Unaanzaje kubeza juhudi kama hizi? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, wanasema mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais na Wizara ya TAMISEMI, hongereni sana, kazi yenu ni nzuri sana, mnaokoa vifo vya akina mama na huduma za afya zinapatikana. Ni kweli changamoto ndogo ndogo bado zipo, wanasema hata Roma haikujengwa siku moja, hatuwezi kumaliza changamoto kwa siku moja. Hii nchi ni kubwa, wananchi wake ni wengi na mambo yanayotakiwa kufanyika ni mengi lakini lazima tu-recognize juhudi zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano tangu 2015 to date. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie na suala la elimu. Ni kweli kwamba kuna changamoto lakini lazima tuseme yale mazuri makubwa yaliyofanyika. Changamoto ya ukosefu wa miundombinu ni kwa sababu ya elimu bure ambayo imetolewa katika kipindi hiki cha Awamu ya Tano. Usajili umekuwa ni mkubwa sana katika shule zetu ambao umepelekea kupungua kwa matundu ya vyoo, madarasa na kadhalika lakini bado kazi kubwa imefanywa na maboma mengi yamejengwa. Sisi tu Mkoa wa Manyara tumeletewa fedha za EPforR zaidi ya shilingi bilioni saba kwa ajili ya kumalizia maboma katika Mkoa wa Manyara, naishukuru sana Serikali hii ya CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yamejengwa matundu mengi ya vyoo lakini bado kuna changamoto. Niendelee kuiomba Wizara ya TAMISEMI waweze kuzingatia hitaji hili kwa sababu kwa asilimia kubwa lina-affect watoto wa kike wanapokuwa kwenye mizunguko yao ile ya mwezi wanashindwa kuhudhuria shule kwa sababu ya mazingira mazuri ya maeneo hayo ya kujisitiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masula mazima ya upungufu wa walimu wa sayansi ni kilio kikubwa. Tumejenga maabara za kutosha na tunatengeneza nchi ya viwanda, ni lazima tuwekeze kwenye elimu na walimu wa sayansi. Upungufu wa walimu wa sayansi ni mkubwa, upungufu huu ni janga la kitaifa. Tuwa-motivate watoto wetu kuanzia kwenye level za primary school kupenda sayansi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli walimu wa sayansi huwa ni wakali na wakati mwingine watoto wasipoelewa ukali unapozidi basi unakuta wanatoa adhabu mbalimbali na watoto hao wanajikuta wamechukia masomo hayo ya sayansi na hisabati. Niwaombe walimu wenzangu twende taratibu, tunahitaji kuwajenga wanasayansi ili nchi yetu iweze kupata wataalam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kwa uchache suala zima…

T A A R I F A

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa, Mheshimiwa Ester subiri.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba uwasihi Wabunge wamsikilize kwa makini Mbunge ajaye wa Jimbo wa Babati Mjini. Ahsante. (Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ester Mahawe, naomba uendelee.

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa ruhusa hii ya kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la elimu, mimi natokea Mkoa wa Manyara ambako wenyeji wetu wengi ni wafugaji na shule zetu nyingi za sekondari hazina mabweni na hosteli za kutosha. Nishukuru tumepata hosteli kadhaa, siyo chini ya 10 katika Mkoa wetu wa Manyara lakini hazitoshi hasa Wilaya ya Kiteto na Simanjiro, wale watoto wanatembea umbali mrefu mno. Kama unavyofahamu sisi wafugaji watoto wa kike wanaolewa haraka sana, naomba ili ku-rescue watoto hawa, shule hizi ziweze kupata hostels ili watoto wale waweze kumaliza masomo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende kwenye suala la afya. Nishukuru sana kwa ajili ya mambo mengi yanayoendelea kufanywa na Serikali hii lakini nina ombi la dhati kabisa kwa ajili ya magari ya wagonjwa katika maeneo mbalimbali katika Mkoa wa Manyara. Hospitali ya Mbulu haina gari la wagonjwa, lililopo ni chakavu na Kituo cha Afya cha Ngusero hakina gari la wagonjwa, tunaomba sana kusaidiwa. Niliwahi kuomba gari la wagonjwa kwa ajili ya Kituo cha Afya Orkesmet mbele ya Makamu wa Rais, nina hakika ombi hili linaendelea kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mkoa wa Manyara, jiografia za Kiteto na Simanjiro zimekaa vibaya kuliko mahali pengine popote nchi hii. Akina mama wakati mwingine wanapata tabu wanapopelekwa hospitali kujifungua. Naomba tena gari kwa ajili ya Orkesmet na Kituo cha Afya cha Ngusero, Kiteto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba gari kwa ajili ya Hospitali ya Mrara, Babati Mjini, gari ni moja na ni chakavu. Kama hiyo haitoshi, Hospitali ya Wilaya ya Babati Mjini ilianza kama zahanati miaka ya 1956, imeongezwa jengo moja moja baadaye ikawa kituo cha afya, leo imekuwa Hospitali ya Wilaya, majengo yapo scattered hayana mpangilio, wodi ya wazazi ipo mita 100 kutoka theatre. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe unafahamu ukiingia kwenye kile chumba ama miguu itangulie kaburini au wewe mwenyewe mzima mzima. Sasa imagine theatre ipo 100 metres kutoka kwenye labor ward. Hili jambo nakuomba sana Mheshimiwa Jafo ulitazame kwa macho ya huruma. Naomba sana suala la Hospitali ya Mrara litazwamwe vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna upungufu wa watumishi wa kada ya afya katika Mkoa mzima. Tunajua juzi TAMISEMI wamejitahidi sana, wameachilia ajira lakini bado tuna upungufu kadhaa. Kada ya afya ni muhimu sana, ndiyo inayo-save maisha ya wananchi wetu. Ikitokea tu bajeti kidogo ya kuweza kuruhusu kuongeza watumishi wa kada ya afya tunaomba Manyara tukumbukwe kwa namna ya tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijamaliza nilikuwa naomba nizungumzie suala la lishe. Ni kweli kwamba tuna tatizo la lishe…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ester malizia, muda wako umeisha.

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba niseme tu udumavu ulipo Mkoa wa Manyara ni asilimia 36 na hili linachagizwa na ukosefu mkubwa wa maji; akina mama wengi wanatoka asubuhi wanarudi usiku hawana hata muda wa kuwaandalia watoto wao chakula kizuri hata kama kipo. Naiomba sana Serikali yangu, Ofisi hii ya TAMISEMI itusaidie kutazama namna ambavyo tutamalizana na changamoto ya miundombinu ya maji ili hatimaye tuweze kupata vijana wazuri watakaolilea taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja, Mungu akubariki sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia fursa hii, ya mimi nami kuweza kutoa mchango wangu, katika Wizara hii ya Elimu, naomba ku-declare interest ni mdau wa shule binafsi na mwalimu kwa taaluma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuweka tu rekodi vizuri, kwa mchango wa Kaka yangu Kigola, ninaomba ndugu zangu Watanzania, tutofautishe English Medium Schools na International Schools hivi ni vitu viwili tofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, English Medium Schools ni hizi ambazo hakuna English Medium School Tanzania ninayoifahamu ambayo ina-charge zaidi ya 4.5 milion, hakuna hata moja, hata moja, zingine zote zinazo-charge above that ni International Schools. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mjadala tulishaufunga ni uchaguzi huria, kama ilivyo hoteli kama ilivyo huduma nyingine yoyote, nadhani ifike mwisho mambo ya kujadili ada elekezi na vitu vya namna hiyo kwa sababu mtu halazimishwi.

MBUNGE FULANI: Tuongelee humu ndani.

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, amlete shuleni kwangu ada ya day ni laki nane na nusu kwa mwaka, milioni mbili kwa mwaka kwa bweni, mwambie aje kwangu, hiyo nayo itamshinda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuweka hiyo rekodi sawa, ninaomba sasa nimpongeze sana Mheshimiwa Prof. Ndalichako, kwa kazi nzuri inayofanyika ya kuinua Elimu katika nchi hii. Naibu wako Mheshimiwa Ole Nasha, Dkt. Akwilapo, Katibu Mkuu, Mama Ave Maria Naibu Katibu kwa kweli watu hawa wanaipeleka elimu yetu mahali pazuri pamoja na kwamba changamoto ndogo ndogo zipo nina hakika nia ya dhati na njema ipo ya kuhakikisha tunamaliza changamoto hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizo ninaomba kwa vile mengi yatasemwa na wenzangu, nijikite kwa yale ambayo sisi tulioko kwenye field ndiyo tunayapitia na hakuna mwingine wa kuyasema isipokuwa sisi tulioko huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba hili lisichukuliwe kwamba tumekuja humu ndani kwa sababu ya maslahi binafsi, ninaweza kufa kesho na kesho kutwa, lakini Watanzania wapo, vizazi vyetu vitabaki, tunachotaka ni kuboresha elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Elimu, ni uwekezaji, tunazungumzia Uwekezaji wa vitu vingi, Rais amekuwa akipigania kuhakikisha wawekezaji wanakuja kuwekeza Tanzania ili kuweza kupata fedha za Kigeni, na hatimaye Watanzania wapate ajira na vitu vya namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba nimuombe Rais, aangalie suala zima la Uwekezaji kwenye Elimu. Tunaweza tukawekeza kwenye Viwanda, ikiwa hatujawa- train watu wetu vizuri, inavyotakiwa bado uwekezaji wetu katika maeneo mengine unaweza usiwe wa tija sana. Nikizungumza hili ninajua Mheshimiwa Dada yangu Angellah Kairuki, sasa umepewa nafasi ya uwekezaji, kusimamia uwekezaji katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba sana tuwekee dirisha la wawekezaji wa Elimu Tanzania, maana hawa ndiyo wanaowajenga wataalamu wetu watakao iendesha nchi hii kesho na kesho kutwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikisema hivi ni kwa sababu ya gharama kubwa ya uendeshaji wa shule hizi, ujenzi wake na vitu vya namna hiyo. Niliwahi kusema Uganda, ukifahamika tu wewe unataka kujenga shule, wanakuondolea VAT kwenye constructions material zote, zote unaondolewa, kwa sababu wanajua unakwenda kuwekeza kwa ajili ya jamii ya kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo na sisi tuangalie, namna ambavyo tutaweza kupunguza gharama zingine kwa wamiliki na waendeshaji wa hizi shule, tunapitia wakati mgumu sana. Niliwahi kusema ukiwapima waendeshaji wa shule, wengi wana pressure na sukari kwa sababu ya changamoto ya uendeshaji wa hizi shule. Nikisema hivi changamoto, mojawapo kwa mfano, vitabu, suala la vitabu, mwaka juzi tulizungumza hapa na vile vitabu vikaondolewa kwenye system.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jukumu la vitabu kutunga, kuvihakiki, kuvisambaza na kazi zingine zote imepewa TET au TAI lakini kwa bahati mbaya tu naomba Bunge lako Tukufu lifahamu ya kwamba TET hawajawahi kututungia vitabu watu wa English Medium schools mpaka leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa pata picha hawa watoto wanafundishwaje na ni watanzania na wako kwa mujibu wa Sheria? Ninapozungumza hivi ni pamoja na kutokuwa na mtaala wa lugha ya kiingereza, pamoja na kutokuwa na vitabu, hii inaleta mno changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia jambo lingine ni TET hawa hawa wamepewa I mean, mandate ya kuhakikisha wanatoa ithibati kwa waandishi wa vitabu vya ziada, jambo ambalo mpaka sasa, kuanzia 2015 hakuna mwandishi wa vitabu vya ziada aliyepewa ithibati na TET na watu wa English Medium wamekuwa wakitumia vitabu hivyo hivyo vya waandishi vya ziada visivyo na ithibati ndivyo vinavyotumika kufundishia, pamoja na kwamba bado hizo shule zinajitahidi kujikongoja kufanya vizuri katika mitihani hii ya mwisho ya kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe sana Mheshimiwa Prof. Ndalichako, naomba ufatilie suala TET, TET wanakuangusha, wao ndi wenye mujibu wa kutoa hivyo vitabu na mihutsari na mitaala. Tunaomba basi waangalie na hawa watu wa English Medium kwa jicho la huruma. Kama vile haitoshi, walimu wa shule za Serikali wamepatiwa mafunzo ya jinsi ya kutumia huo mtaala mpya wa Kiswahili uliotoka, lakini kwa bahati mbaya sana, walimu wanaofundisha private schools hawajapewa mafunzo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na juzi, wametoa barua TET ya kwamba ukitaka ku-train mwalimu kupata elimu ya huu mtaala mpya kila mwalimu anatakiwa alipiwe shilingi laki tatu. Hawa walimu wanawafundisha wa-Nigeria au ni watanzania? Kuna vitu vingine sijui kama hata Rais anavifahamu ama Wizara inavijua kwa style hiyo. Hebu pata picha tuna walimu zaidi ya 40,000 wa private schools, 40,000 mara 300,000 ni over 12 Bilioni wanazifanyia nini? Hizi pesa? Wakati TET iko pale, kwa ajili ya kutoa na kusimamia Elimu mitaala na miongozo, hii haiko sahihi tunaomba watuangalie na sisi ni watanzania, tunafundisha watoto wa Kitanzania, ndiyo wako humu wengine wamesoma wakina Mlinga hawa wamesoma English Medium leo ni Wabunge wazuri kama mnavyo waona wasingesoma huko, wasingekuwa hivyo kwa hiyo TET tunaomba watuangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine kwa haraka mwaka juzi Waziri alifuta kodi ya zimamoto humu ndani, nilipongeze hilo Jeshi letu, linafanya kazi vizuri, wamekuja hapa juzi wametupa Elimu ya namna ya kuzima moto sisi Waheshimiwa Wabunge. Lakini cha kusikitisha kodi hiyo imerudishwa kwa mlango wa nyuma, ukaguzi wa masuala ya zima moto unalipia Certificate shule, laki 500,000 lakini ile elimu ya kuja kupambana na habari ya kuzima moto, kila mwanafunzi anachajiwa shilingi 20,000 ina maana shule ikiwa na wanafunzi 500 unalipa shule yako milioni 10, kwa nini inaonekana kama vile kwenye private schools ndiyo mahali pekee pa kuchukulia pesa? Kwa nini, kwa nini?

Mheshishimiwa Mwenyekiti, juzi sisi Wabunge tumefundishwa hapa, ni ile ya kuweka tu petroli pale na kuzima ule moto, wanafunzi wa private wanatakiwa walipe 20,000 kila kichwa, tunakoelekea ni wapi? Yaani private schools zimekuwa ni vyanzo vya kutafutia pesa kweli? This is not fair? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna swali liliulizwa juu ya watoto yatima hapa na watoto wa mitaani, na vitu vya namna hiyo, naomba nitoe mapendekezo kwa Serikali yangu, tunafundisha watoto, nimemsikia hata mwenzangu, Mheshimiwa Shangazi akizungumza hizi shule za Makanisa, ndiyo zinasaidia yatima, on board shuleni kwangu nenda leo wako 50 over 200 wamemaliza shule watoto yatima waliokuwa mtaani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, on board wako 50, lakini bado pesa kama hizi unatakiwa uzitoe kweli, mngetuacha tuwasomeshee watoto hawa mtaani, kupunguza haya majanga? Na watu wa private pia wameomba ikiwezekana hata wapangiwe idadi kadhaa ya wale watoto kila mkoa, kulingana na shule zilizoko, wachukue wale watoto yatima na watoto mtaani, wawasomeshe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, waachwe kufatwa fatwa na hivi vitu vingine kama mara kodi fire, mara rent, sijui land rent na vitu vingine visivyo na tija. Kwa hiyo, nilifikiri private schools ni mahali peke yake ambako watoto hawa wa mtaani wanaweza kuwa absorb na wakasaidiwa na tukamaliza janga la watoto wa mtaani katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tunapata dialogue nzuri sasa hivi, nimpongeze sana Mheshimiwa Prof Ndalichako, pamoja na Katibu Mkuu at least wanatushirikisha kwenye baadhi ya mambo mengi sasa kuhakikisha kwamba kunakuwa na fair play katika uendeshaji wa hizi shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema mambo haya ya msingi kabisa, hasa suala la vitabu tunaomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja atuambie ni lini TET watatoa vitabu kwa ajili ya hizi shule za kiingereza na lini hasa tutapata mitaala na lini hasa na ni kwa nini wanachaji shilingi 300,000 kwa kila mwalimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukipeleka huyo mwalimu kwenye hiyo kozi kumbuka unamlipia gharama za usafiri, chakula, malazi, ina maana mwalimu mmoja ana-cost shule zaidi ya shilingi milioni moja, haya kuna shule zina walimu mpaka 400, 450 huyo mwenye shule anazipata wapi hizo pesa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutamkamua huyo mzazi anayesomesha watoto wake kwenye hizi shule mpaka lini? Naomba kuunga hoja mkono lakini mama Ndalichako, ukija hapa tunaoamba utuletee majibu ya haya. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. ESTHER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nianze na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya na siha njema sisi sote katika Bunge lako Tukufu. Pili, nipende kumpongeza sana Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Serikali na watendaji wote hasa wa Wizara hii muhimu ya Maji na Umwagiliaji kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujitahidi kumtua mwanamke ndoo kichwani kama ilivyo ahadi ya chama chetu cha CCM kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri shahiri hakuna asiyejua umuhimu wa maji katika muktadha mzima wa afya bora, uhai na maendeleo endelevu ya kila familia. Hii ni kutokana na kwamba hata mwili wa binadamu tu una asilimia 75 ya maji, hivyo maji ni uhai.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua Serikali inafanya kila iwezalo ili kumaliza kero ya maji katika maeneo mengi nchini. Binafsi ningeshauri tozo ya mafuta ifikie sh.100/= kwa kila lita moja ya diesel/petrol; iongezwe kwenye Mfuko wa Maji ili wanawake waweze kuondokana na kero ya kutafuta maji kwa masaa mengi, hali inayosababisha ndoa zao kuvunjwa, kukosa muda wa kufanya shughuli nyingine za ujasiriamali ili waweze kujikimu kimaisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nisikitike tu kuwa pamoja na bajeti ya maji iliyotengwa katika bajeti ya 2016/2017 kufikia zaidi ya bilioni mia tisa, bado fedha zilizopelekwa hadi Aprili mwaka huu kuwa asilimia 20 tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wote wanaomba kuongezwa fedha hizo zilizopungua hadi bilioni mia sita katika bajeti hii ya mwaka 2017/2018. Naomba nitofautiane nao kimtazamo kwani hata hizo bilioni mia tisa zilizotengwa hazikupelekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niishauri Serikali yangu Tukufu kwamba, kwa kuwa kuna Halmashauri takriban 185 nchini, basi haidhuru kila Halmashauri ingetengewa shilingi bilioni moja ili kupunguza makali ya kero ya maji katika kila Halmashauri, halafu bajeti tengwa ya zaidi ya bilioni mia nne zielekezwe kwenye miradi maalum (mikubwa). Hii itaondoa malalamiko mengi kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nizungumzie hali ya maji katika Mkoa wangu wa Manyara. Naomba kwa moyo wa dhati kabisa niishukuru Serikali yangu kupitia kwa Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara hii ya Maji na Umwagiliaji kwa kuupatia fedha Mradi wa Maji wa Mto Ruvu katika Wilaya ya Simanjiro ambapo wakandarasi wapo site na kazi inaendelea vizuri sana. Ombi langu kwa Mheshimiwa Waziri ni kwamba ahakikishe fedha zinaendelea kupelekwa na pia kuhakikisha mkandarasi anafanya mradi huu kwa umakini mkubwa na (value for money) thamani halisi ya fedha inayolingana na mradi wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua wananchi wa Simanjiro kwa aina ya jiografia ya wilaya, pamoja na mkoa wetu kuwa ni mkoa wa wafugaji bado tuna mahitaji makubwa ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na wanyama pia. Wakati Waheshimiwa Wabunge wakiomba Wizara hii kuongezewa fedha, ndipo na mvua kubwa inaendelea kunyesha kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa wananchi pamoja na miundombinu hapa nchini. Binafsi najiuliza ni kwa nini Wizara isijiongeze na kuchimba mabwawa wakati wa kiangazi?

Mheshimiwa Naibu Spika, mabwawa hayo yangeweza kutega maji hayo yanayopotea bure kipindi hiki cha masika. Haiwezekani tunalia ukame majira yote ya mwaka wakati tungeweza kuepuka baadhi ya kero isiyo ya lazima kwa kukusanya maji ya mvua kwenye mabwawa na majosho.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningeshauri pia Halmashauri zetu zitengeneze Sheria Ndogo (bylaws) zitakazowezesha kila nyumba, kaya yenye paa la bati kuwa na mfumo wa kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya kupunguza makali ya kutafuta maji mbali kipindi cha kiangazi. Naomba niendelee kushauri kuwa katika sh.100/= hii, asilimia 70 iende vijijini na asilimia 30 iende mijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna asiyejua adha kubwa wanayoipata akinamama wa vijijini ambao wanatumia asilimia 80 ya muda katika kutafuta maji ya ndoo moja au mbili kwa kutwa nzima. Ni imani yangu fedha hizi zikielekezwa kwa kiasi kikubwa vijijini tutakuwa tumewaokoa akinamama hawa na majanga mengi wanayoyapata wanapokuwa kwenye harakati za kutafuta maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uchache niseme tu Wilaya ya Kiteto katika Mkoa wetu wa Manyara asilimia zaidi ya 65 ni eneo kame sana ambapo hata wakichimba visima virefu bado wanakosa maji. Naiomba Wizara ya Maji na Umwagiliaji iangalie ni mbinu gani mbadala itakayotumika katika kuwasaidia akinamama hawa wa Kiteto waondokane na adha ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba niishauri Serikali yangu sikivu kuanzisha Mfuko wa Maji Vijijini ili kusaidia katika suala zima la monitoring. Mfuko huu pia utasaidia kwa kiwango kikubwa kutambua maeneo yenye kero iliyopitiliza na kuweza kuyatatua kwa haraka zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, adha ya maji safi na salama ni chanzo kikubwa sana cha maradhi yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama (waterborne diseases) kama kipindupindu, kuhara, kutapika na kadhalika. Serikali yetu inapoteza zaidi ya fedha za kimarekani dola milioni 72 kila mwaka ili kutibu magonjwa hayo. Je, si vyema tukakinga kuliko kuponya kwa kuthubutu kupeleka fedha nyingi kwenye bajeti hii ili kuepukana na matumizi makubwa ya kugharamikia matibabu ya wagonjwa hao na hata vifo vinavyosababishwa na magonjwa hayo (Waterborne diseases)?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake kwetu sisi sote. Pili, naomba kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri na Naibu wake wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingika kwamba Mawaziri hawa wanafanya kazi kubwa na nzuri sana ya kuhakikisha wanaondoa kero zote zisizo za lazima, hasa migogoro baina ya wakulima na wafugaji. Miaka michache iliyopita tulishuhudia mapigano na uvunjifu wa amani baina ya wananchi mbalimbali kwa sababu ya ama kuingiliana kimipaka ama wasio na uwezo wengi kunyang’anywa ardhi zao na matajiri wachache. Hata hivyo, tangu Mheshimiwa Lukuvi pamoja na Naibu wake Mheshimiwa Angelina Mabula waingie kwenye Wizara hii, kero hiyo imepungua kwa asilimia kubwa sana. Hivyo, naomba tena kutumia fursa hii kuwapongeza sana kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku zote penye mafanikio hapakosi changamoto. Niendelee kuiomba Wizara hii kuendelea kupanga miji yetu na kutoa elimu juu ya matumizi mazuri ya ardhi. Kwani ardhi haiongezeki bali watu ndiyo wanaongezeka sasa ni wakati muafaka wa Serikali yetu kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya ardhi ili kuliondosha Taifa letu lisiingie kwenye migogoro isiyo ya lazima huko tuendako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tunayo Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi na kwa mujibu wa sheria No.6 ya mwaka 2007 inayoipa Tume hii mamlaka ya kupanga Ardhi kwa matumizi endelevu ili kuondoa umaskini wa wananchi wetu. Basi niliombe Bunge lako Tukufu litenge bajeti ya kutosha ili kuwezesha Tume hii kuweza kutekeleza majukumu yake kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi sote tunafahamu kuwa wanaochangia uchumi wa nchi hii kupitia kilimo ni wanawake, lakini kwa bahati mbaya sana sheria za kimila zinamnyima mwanamke haki ya kumiliki. Katiba ya nchi pamoja na Sheria ya Ardhi zote zinatambua mwanamke kumiliki ardhi lakini sheria za kimila zinamfanya mwanamke ku-access ardhi na siyo ku-own ardhi. Hii inafanyika kupitia mumewe au wazazi wake. Pale owner ambaye ni mume au mzazi anapofariki mwanamke huyu hunyang’anywa ardhi hiyo kwa kuonekana ardhi ni mali ya mwanaume.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika hili ni kwamba, tunaomba sheria hizi za kimila ziletwe Bungeni, zitazamwe upya ili ziweze kumpa haki mwanamke kumiliki ardhi. Naomba pia nizungumzie kwa ufupi migogoro baina ya wakulima na wafugaji. Tatizo hili bado ni kubwa sana katika maeneo mengi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, ningeshauri Serikali iweke mpango mkakati ili kuweza kutenganisha maeneo ya kilimo na ufugaji. Pia, wafugaji wetu wapatiwe elimu ya kutosha ili waweze kuacha kufuga kizamani bali waweze kufuga kisasa na kibiashara zaidi. Hii itasaidia sana kupunguza migogoro isiyo ya lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, niipongeze Ofisi ya Rais kupitia MKURABITA. MKURABITA wamesaidia sana kushirikiana na Halmashauri mbalimbali nchini kurahisisha ardhi na kuwapatia wananchi hati za kimila. Hati hizi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro ya kimipaka baina ya wananchi. Vile vile, wananchi wameweza kutumia hati hizo kukopa fedha katika benki mbalimbali na kuwasaidia kufufua wajasiriamali. Hali hii imepunguza sana kwa kiasi kikubwa umaskini kwa wananchi wetu. Hivyo basi, naomba sana Wizara hii ya Ardhi iweze kushirikiana na MKURABITA ili wananchi wengi hasa wasio na uwezo waweze kumiliki ardhi.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa niipongeze taarifa ya Kamati na kuunga hoja mkono kwa kazi nzuri iliyofanywa. Pili, niipongeze Serikali ya Awamu ya Tano ya Chama cha Mapinduzi chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupambana na kuziba mianya yote ya upotevu wa fedha na hatimaye kuboresha huduma za afya na elimu nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli usiopingika kwa MSD inafanya kazi nzuri sana ya usambazaji wa madawa katika hospitali mbalimbali nchini kwa wakati. Niombe Serikali yangu sikivu iweze kuongeza fedha katika bajeti ili taasisi hii iweze kutekeleza majukumu yake vilivyo. Naomba niipongeze tena Serikali kwa kazi nzuri iliyofanya ya kuhakikisha inapiga vita uingizwaji wa dawa za kulevya nchini. Hali hiyo imesaidia sana nguvu kazi ya Taifa isiendelee kupotea na pia kwa mkakati mzuri wa uanzishwaji wa sober houses ili kuwasaidia vijana wote walioathirika na matumizi ya madawa haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingika kuwa mtoto wa kike hasa wa kijijini wanakosa siku tano mpaka saba kuhudhuria shule pindi anapokuwa kwenye siku zake. Ndiyo maana mimi na Wabunge wanawake wote waweze kupaza sauti ili pale Serikali yetu itakapopata uwezo uweze kutazama jambo hili kwa jicho la tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu sasa Wizara ya Elimu imekuwa Wizara ya matamko na nyaraka hali inayopelekea kushuka kwa elimu. Takwimu zinaonesha mpaka sasa ufaulu unazidi kushuka hasa katika elimu ya sekondari. Ni asilimia 28 tu ndiyo wanaopata daraja la kwanza hadi la tatu na asilimia 72 wanapata daraja la nne na sifuri. Iko haja ya kutazama mifumo ya utolewaji elimu ndani ya Wizara hii kwani bila hivyo tutakuwa tikizalisha nguvu kazi duni na hafifu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa ninapenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara ya Maji chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo, kazi wanayofanya ni kubwa sana, hongereni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizo naomba nieleze changamoto kadhaa wanazopitia wakazi wa Mkoa wa Manyara hasa wanawake kwa kuwa wao ndiyo wanaopata adha kubwa ya utafutaji wa maji kwa ajili ya familia zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua juhudi kubwa zilizofanywa na Wizara ya Madini ya kujenga ukuta katika eneo la Simanjiro Kata ya Mererani kwa nia njema ya kuhifadhi madini yetu. Wananchi wa kata nne zinazozunguka ukuta huo ambazo ni Marerani, Naisanyai, Endiamtu na kadhalika walikuwa wanapata maji kutoka Tanzanite One lakini hivi sasa hayo maji yapo ndani ya ukuta ambako movement za kuingia ndani ya ukuta ziko monitored sana, hivyo ningeomba Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Halmashauri ili mabomba yatolewe nje ya ukuta na wananchi waweze kuendelea kupata maji kama ilivyokuwa mwanzo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikizungumzia suala hili hali ni tete zaidi kwa vijiji vya Emishiye na maeneo ya jirani na vijiji hivyo kwani ukuta wa Mererani una kilometa za mraba 24.5 ili akinamama wa Emishiye wapate maji hayo yaliyoko ndani ya ukuta wanatembelea kilometa zaidi ya 30. Akinamama ndiyo gumzo ya uchumi wa familia yoyote, sasa kama mama anatumia saa 12 kutafuta maji? Maji yenyewe haya ninayozungumzia si kwamba ni maji mazuri kwa kiwango hicho, maji haya yana floride, mifugo na wanyama wanaotumia maji haya wamepinda miguu na kung’oka meno kabla ya umri wao.

Naiomba Serikali yangu sikivu iwaonee huruma wakazi hawa wa Simanjiro ili waweze kupatiwa maji kutoka West Kilimanjaro ili wapate ahueni ya maradhi yanayosababishwa na madini haya ya floride. Kwa sasa wakazi hawa wananunua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi 500 gharama hii ni kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ya ukosefu wa maji ni kubwa Mkoani Manyara, Wilaya ya Kiteto ni moja ya Wilaya zinazoongoza kwa ukame zifanyike juhudi za makusudi ili kutega maji haya ya mvua yanayopotea ili kupata mabwawa yatakayosaidia watu na mifugo wakati wa kiangazi. Wilaya ya Babati, Kata ya Singu tuna shida kubwa ya maji tunaomba msaada wa Wizara yako kama tunaweza kupata maji kutoka BAWASA.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na naomba kuunga hoja mkono.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kumshukuru Mungu kwa ulinzi, nguvu na afya aliyonijalia mimi na Wabunge wenzengu wote humu ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia zaidi ya 65 ya wananchi wa Tanzania ni wakulima. Ni kweli kwamba kaulimbiu yetu ni kufikisha nchi yetu kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na ili kufika huko tunakotaka kwenda ni lazima tufufue viwanda vyetu. Mazao ya kilimo ndiyo malighafi ya kufanya viwanda vyetu vizalishe, vitoe ajira, vituletee fedha za kigeni na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu sasa Wizara ya Kilimo ilikuwa haipewi kipaumbele kabisa, pamoja na kuwa ndiyo Wizara pekee ambayo ina uwezo mkubwa wa kuondoa umaskini wa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua kwa dhati ya moyo wangu juhudi kubwa ya Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, ninatambua nia ya dhati ya Mawaziri wa Kilimo ya kuleta mapinduzi ya kilimo, lakini ifike mahali watalaam wa Wizara hii wafikiri njia bora na sahihi ya kumkomboa mkulima huyu maskini anayevunja shamba kwa mikono yake, anayepanda, kupalilia na kuvuna mazao yake kwa gharama na jasho jingi, ni kwa namna gani kazi yake hiyo itamlipa? Kwani wakati akilima hakusaidiwa na mtu wala Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa wafanyakazi wa nchi hii wanapopokea mishahara yao baada ya kufanya kazi kwa mwezi mzima, ni kwa nini mkulima huyu abebe gharama zake mwenyewe halafu baadae apangiwe wapi akauze?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa kilimo cha mahindi kimeshamiri sana hapa nchini, mbali na kuwa zao la chakula, lakini sasa hivi zao hili limekuwa la kibiashara, pia na wananchi wengi wanalima kama zao la biashara. Mwaka 2017 Serikali ilipofunga mipaka ili mahindi yasiuzwe nje, wakulima wengi wamepata hasara kubwa sana. Mahindi mengi yameoza na yaliyobaki yanauzwa kwa debe moja shilingi 5,000, gunia ni shilingi 25,000. Kumbuka mbegu ya mahindi kilogramu mbili ni shilingi 12,000, weka gharama za kilimo, palizi na kuvuna. Kwa heka moja mkulima anapoteza zaidi ya shilingi 600,000, lakini leo anauza mahindi kwa debe shilingi 5,000 kuna tija gani hapo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mkulima huyu aliyelima mbaazi na bado mbaazi inakosa soko huko India, mkulima huyu amelemewa.

Naomba Serikali ione ni kwa namna gani sasa mkulima huyu atasaidika. Suala la pamba kuuzwa kwenye ushirika nalo ni janga lingine. Ninaomba sana Serikali yangu iangalie kwa upya jambo hili na ikiwezekana ijipe muda kidogo wa kufanya utafiti ili kujiridhisha vilivyo ili hatimaye tusije kutukamuumiza tena mkulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema ukweli bajeti iliyotengwa mwaka 2017/2018 yenyewe ilikuwa ndogo lakini kinachouma zaidi ni kiasi kidogo sana kilichopelekwa. Kama kweli tunataka kutoka hapa tulipo kiuchumi, ni lazima tuwekeze vya kutosha katika kilimo chenye kuleta tija hasa kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zote zilizoendelea katika uchumi wa kilimo, wamewekeza zaidi katika kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni na mpaka sasa bado mvua kubwa zinaendelea kuleta mafuriko makubwa na maafa, lakini inashangaza sana kuona kuwa hatuwekezi kwenye utengenezaji wa mabwawa ili maji hayo yaweze kutumika katika kilimo cha umwagiliaji. Pamoja na kwamba hii siyo njia pekee, tunahitaji kuchimba visima virefu ili kutekeleza azma hiyo. Naishauri Serikali, Wizara ya Maji ifanye kazi sambamba na Wizara ya Kilimo ili uwekezaji huo wa kilimo cha umwagiliaji, kiweze kufanikiwa ili tupate malighafi ya kutosha ya viwanda vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wengi waliomaliza vyuo va kazi na Vyuo Vikuu hawana ajira. Nashauri Serikali itenge maeneo yanayofaa kwa kilimo, vijana hawa wakopeshwe zana kama matrekta na kadhalika ili waweze kujiajiri kwenye kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kusema nashukuru sana. Naunga mkono hoja.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kutoa maoni yangu kwa Wizara hii ya Maliasili na Utalii. Utalii unachangia pato la Taifa kwa asilimia 17.5 lakini changamoto za Wizara hii kutokuuza pato hilo kama zilivyo nchi jirani kazi zinazotuzunguka ni nyingi mno, kati ya hizo naomba nitaje zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, bado hatujatenga bajeti inayotosheleza Wizara hii kufanya (marketing) matangazo ya kutosha kwa ajili ya ufinyu wa bajeti. Tanzania ni nchi pekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki yenye vivutio vingi na visivyopatikana maeneo mengine lakini nchi hizo kama Kenya, Uganda, Rwanda na na kadhalika kutenga bajeti kubwa ya matangazo ya hifadhi na maliasili zao na hivyo kupata fedha nyingi zinazochangia chumi zao.

Mheshimiwa Spika, naomba kuishauri Serikali yangu iweze kuongeza bajeti ya Wizara hii ili tuweze kupata watalii wengi na tupate kuongeza fedha za kigeni.

Mheshimiwa Spika, nitoe masikitiko yangu kuhusu suala la single entry katika hifadhi hasa Ngorongoro na Serengeti. Huko nyuma wageni waliingia katika hifadhi na kutoka kwenda kwenye vijiji vya jirani kwa ajili ya kula, kunywa na pengine kuleta hali iliyofanya vijiji vya jirani kupata mapato ikiwa pamoja na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja. Leo hii wakazi wengi wamebakia kuwa maskini na wengine wamekuwa vibaka. Kwa kukosa ajira walizokuwa wakizipata kupitia watalii hao.

Mheshimiwa Spika, ni ajabu sana na utashangaa kuacha system ya zamani na kuanzisha single entry eti ni kwa sababu tu mgeni anaweza kutoka na permit yake ikatumika na mtu mwingine, sababu hii inasikitisha kama nchi ina wataalam na wanaishi katika dunia yenye teknolijia kubwa kiasi hiki wanashindwa kujua yupi kaingia na yupi katoka, ndiyo mtalii yule yule? Ni ajabu sana.

Mheshimiwa Spika, kuna tozo na kodi lukuki ambazo zinazokatisha tamaa watalii wengine kutokuja Tanzania. Kodi hizi pia zimekuwa kero kwa wafanyabiashara wa utalii hasa tour operators na watu wa mahoteli. Naomba nishauri Serikali ikae na wadau wa utalii na ione ni kwa jinsi gani wanaweza kuondokana na kero ambazo si za lazima zinazokatisha tamaa wawekezaji hawa.

Mheshimiwa Spika, kwa nini tusiige kutoka kwa nchi kama Dubai na nyinginezo ambazo unakuta wanachaji viza ya dola za Marekani 150 tu ili kuvutia watalii wengi kuja huku kwetu? Watalii hawa wakija wanalala, wanakula, wanatembelea mbuga na kadhalika na kwa vyovyote vile lazima watuachie fedha nyingi za kigeni, kwani tunawakatisha tamaa kwa kuwawekea tozo nyingi zisizo na maana.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara hii ikae na wataalam na ione mbinu mbadala kwa kuongeza idadi ya watalii kutoka idadi ya watalii milioni 1.3 haidhuru mpaka milioni tatu. Mimi najua tunaweza na ninawaombee Mawaziri wetu, wataalam na watendaji wa Wizara hii kwa Mwenyenzi Mungu ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga hoja mkono.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi wake kwetu sote. Ninaomba sasa na mimi nitoe mawazo yangu katika Wizara hii mumhimu ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa. Pamoja na umuhimu mkubwa uliopo ndani ya Wizara hii iliyobeba asilimia zaidi ya 65 ya wananchi wa Tanzania. Bila Wizara hii uhai wetu unakuwa mashakani kwani hii ndiyo Wizara ya chakula. Hivi karibuni imethibitika kuwa hata mazao tuliyokuwa tunayatambua huko nyuma kama mazao ya chakula kama maharage, mahindi na mpunga sasa yamekuwa sehemu ya mazao ya biashara. Kama ndivyo basi naomba nishauri Wizara yafuatayo;

Mheshimiwa Spika, kuongeza idadi ya Maafisa Ugani ili waweze kuwasaidia wananchi kulima mazao haya muhimu kwa tija. Kutoa elimu juu ya kilimo cha kisasa ya mazao haya muhimu. Kujenga maghala ya kutosha ya kuhifadhia mazao haya. Njia pekee ya kujihakikishia usalama wa chakula nchini ni kufanya kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana huko ndiko ambako Serikali haipeleki fedha za kutosha ambazo zingeweza kutekeleza azma hiyo. Kama hili halitoshi wakulima wamekuwa wakicheleweshewa pembejeo, jambo linalowasababishia hasara kubwa wakulima wetu.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa sisi wote tunahubiri suala la Serikali ya Viwanda. Zaidi ya asilimia 60 ya malighafi ya viwanda hivi tunategemea kutoka mashambani. Ni vyema sasa tuone umuhimu wa kuanzisha vituo vya ushauri na kuondoa changamoto zote zinazowakwaza wakulima wetu ili tuweze kufanikiwa kama taifa kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025. Kwa kuwa Wizara hii ndiyo Wizara pekee ya kututoa mahali tulipo ili kufikia malengo ya Serikali ya Viwanda tuliyojiwekea ni dhahiri kuwa bajeti ambayo imekuwa ikitengwa imekuwa ndogo sana kiasi cha kutotosheleza mahitaji makubwa yaliyopo.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii pia ina changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi, jambo ambalo limekuwa kikwazo katika utekelezaji wa kazi nyingi katika Wizara hii. Ni rai yangu sasa Serikali ione ni kwa njia gani tunawekeza katika Wizara hii ya Kilimo ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea ya kuondokana na uhaba wa chakula pamoja na kupata malighafi toshelevu kwa ajili ya viwanda vyetu.

Mheshimiwa Spika, nipende kuishauri Serikali yangu kuwekeza katika kilimo cha mazao mkakati kama kahawa, Pareto, tumbaku na kadhalika ili tuendelee kujenga uchumi wetu lakini pia kujipatia fedha za kigeni.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nitoe pongezi za dhati kwa Wizara ya Nishati, nikianza na Mheshimiwa Waziri Kalemani, Naibu Waziri Subira Mgalu pamoja na Watendaji wote wa Wizara wakiongozwa na Katibu Mkuu. Kazi kubwa imefanyika katika awamu hii ya tano chini ya Serikali makini inayoongozwa na Jemedari wetu Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kuhakikisha vijiji, vitongoji na kaya zote zinapata umeme ifikapo mwaka 2025.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa mradi wa REA III tayari umepeleka umeme katika maeneo yote ya liyopitiwa na msongo wa umeme wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 670. Kero ilikuwa kubwa, hata hivyo ni imani yangu kwa sasa wananchi hawa watajenga imani kubwa kwa Serikali yao makini. Pamoja na kazi nzuri inayofanywa ya kuzima vibatari vyote katika kaya zote ifikapo 2025, bado kuna vijiji vingi sana havijapatiwa umeme katika Mkoa wa Manyara. Niiombe Wizara kupitia kwa Mheshimiwa Waziri kuuangalia mkoa huu kwa jicho la huruma kwani mpaka sasa vijiji vilivypata umeme ni vichache kuliko ambavyo bado havijapata umeme.

Mheshimiwa Spika, changamoto hiyo ya mkoa wetu hasa vijiji vyake ni kwamba kutokuwekeza umeme kunaziathiri zaidi taasisi mbalimbali za kijamii kama vile shule za sekondari, zahanati pamoja na vituo vya afya. Jambo hili linalorudisha nyuma maendeleo ya wananchi wetu na hata wengine kutopata huduma stahiki hasa ya kitabibu.

Mheshimiwa Spika, kwa ufupi sana naomba nigusie suala la deni kubwa la TANESCO. Deni hili limekuwa kubwa sana kwa kuwa linachagizwa na gharama ya upelekaji wa miundombinu ya gesi kutoka Mtwara. TANESCO ndiyo wanaoligharimia bomba hilo la gesi, jambo ambalo linafanya gesi hiyo kuwa ghali na umeme kuuzwa kwa bei kubwa sana. Umeme wa TANESCO utauzwa kwa bei nafuu pale tu ambapo Serikali itaipunguzia TANESCO gharama ya miundombinu ya gesi bomba.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naomba kuwasilisha.