Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Joseph Leonard Haule (29 total)

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Naomba niongeze maswali mawili ya ziada. Serikali iliagiza Wakurugenzi wa Halmashauri waorodheshe mashamba ambayo yametelekezwa na wameshafanya hivyo. Je, ni lini Serikali itakwenda kutupa majibu ya moja kwa moja?
Swali la pili, kwa kuwa kuna wawekezaji wana mashamba makubwa mfano mashamba ya Miombo Estate, Kilosa Estate, SUMAGRO, Isanga Estate ambao wamebadilisha matumizi na kuvunja sheria na utaratibu, Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kuyarudisha mashamba hayo kwa wananchi wa Jimbo la Mikumi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli maelekezo yalikwishatolewa kwa Wakurugenzi wote na hasa kupitia katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa ili kuweza kuainisha migogoro yote iliyopo katika maeneo hayo ili Wizara iweze kuchukua hatua mpaka sasa mashamba ambayo tayari yamekwishaainishwa na kuletwa pale Wizarani ni jumla ya mashamba 75, lakini pia tunavyo viwanja 694. Haya yameainishwa ni katika mashamba yale kuanzia mwaka 2002 mpaka 2015 na utoaji wake sasa tayari uko katika process za kawaida.
Mheshimiwa Spika, vile vile kwa wale ambao wameshindwa kabisa kuendeleza na tayari mapendekezo yameshaanza kushughulikiwa kwa ajili ya kubatilishwa kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha Sheria ya Ardhi, Sura ya 113 tunatarajia pia kuwa kazi hiyo itafanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni, kwa sababu haya yako katika utaratibu na maelekezo yamekwishatolewa.
Waheshimiwa Wabunge, ninachowaomba kwa sababu pia kila Mbunge alipata maelekezo hayo ambayo tunawaomba mfanye kazi hiyo kwa kusaidiana na Halmashauri zenu muweze kuleta na kuainisha migogoro yote na siyo migogoro yote inapaswa kuletwa Wizarani kuna mingine ambayo pia inaweza ikamalizwa na ofisi zetu za Kanda kwa sababu tuna ofisi karibu katika Kanda nane nchi nzima. Kwa hiyo, kuna mengine yanaweza yakatatuliwa katika maeneo hayo ilimradi tu taratibu nilizozitaja katika jibu la msingi basi ziweze kufuatwa na Wizara itakuwa tayari kuyashungulikia.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Suala la Arumeru Magharibi linafanana sana na tatizo ambalo lipo Mikumi, je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa kero ya maji katika Kata ya Mikumi, Ruaha, Uleling’ombe na maeneo ya Tindiga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Waziri katika majibu yake ametoa taarifa kwamba tunaingia katika progamu ya pili kupitia sera ya mwaka 2002 ya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya Watanzania wote watakuwa wanapata maji katika vijiji na asilimia 95 katika miji.
Mheshimiwa Mbunge, kwa upande wa Jimbo lako la Mikumi na Kata zake, tutahakikisha kwamba tunazipa kipaumbele kuhakikisha zinapata maji katika hii progamu ya pili. Na ninakuomba sana baada ya Bunge hili tuwasiliane ili tuweze kupata taarifa iliyo nzuri zaidi tuanze utekelezaji.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Suala hili la Mbeya Vijijini linafanana sana na tatizo sugu la umeme katika Jimbo letu la Mikumi.
Swali langu ni kwamba, je, ni lini Serikali itapeleka umeme huu wa REA kwenye Kata za Tindiga, Mabwerebwere, Ulaya, Zombo, Muhenda, Uleling’ombe na Vidunda?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa hapa tulipofika REA Awamu ya Pili tunatarajia ikamilike mwezi Juni mwaka huu. Vijiji vyote ambavyo vitakuwa vimesalia bila ya kuwa na umeme pamoja na vijiji alivyovitaja Mheshimiwa Mbunge vya kwenye Wilaya pamoja na Jimbo la Mikumi, vyote tunatarajia tuvifikishie umeme kwenye REA Awamu ya Tatu. Kwahiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba vijiji vyake vyote vitapata umeme wa REA Awamu ya Tatu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwapongeze sana Waheshimiwa Wabunge, kama tutakavyoleta bajeti yetu, tuna matumaini makubwa kwamba bajeti yetu ya kupeleka umeme vijijini itapitishwa na Waheshimiwa Wabunge na ikishapitishwa, kama tunavyosema siku zote, kwa sababu suala la umeme ni la kufa na kupona, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupeleka umeme kwenye vijiji vyote.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka kwenye Awamu ya Tano ifikapo 2025 vijiji ambavyo vitakuwa havina umeme vitakuwa ni vya kutafuta. Kwahiyo, vijiji vyote vitapata umeme wa REA Awamu ya Tatu. Ahsante.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili la Nachingwea linafanana sana na tatizo la Mikumi. Ningependa nipate majibu ya Serikali ni lini itatengeneza barabara ya lami ya kutoka Kilosa kwenda Mikumi yenye urefu wa kilometa 78, ambayo ni kichocheo kikubwa sana cha uchumi wa Kata za Mikumi, Muhenda, Ulaya, Zombo, Masanze pamoja na Magomeni?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, natambua juhudi za Mheshimiwa Haule na umekuja ofisini, tumeongelea kuhusu hii barabara na ninawashukuru mlipitisha bajeti yetu, katika bajeti ile unafahamu kwamba kuna bajeti ya kujenga hiyo barabara. Mimi nakuhakikishia, tutahakikisha tunasimamia vile fedha ambazo mmetutengea tutatekeleza ikiwa ni pamoja na kujenga eneo hili la barabara ya kutoka Kilosa hadi Mikumi.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza naishukuru sana Serikali kwa kutenga bajeti ya daraja hili la Ruhembe kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017. Hata hivyo, kutokana na kilio na mateso makali pamoja na vifo vya watu wa Ruhembe ambao wamekuwa wakilia kwa muda mrefu, Serikali ipo tayari kuleta pesa hizi kule Mikumi katika robo ya kwanza ya mwaka 2016/2017?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nimesema hapa tumetenga shilingi milioni 700 na hii milioni 700 Mheshimiwa Joseph Haule anachosema ni kweli, katika lile daraja tumepoteza watu wengi sana, takribani watu wanane hivi kwa mujibu wa takwimu nilizozipata na mtu mmoja ambaye tumempoteza pale ni mtumishi wa Serikali katika Ofisi yetu ya TAMISEMI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba, jambo hili sisi wengine tunalifuatilia na tunalijua vizuri sana. Ndiyo maana tumeona katika suala zima la bajeti, mwaka jana waliomba shilingi milioni 600, lakini kilichopitishwa Hazina ilikuwa ni shilingi milioni 300 na ilikuja milioni 100 peke yake. Katika msisitizo mwaka huu tukaona ile milioni 700 lazima irudi katika bajeti kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linatugusa sana kwa sababu, wananchi pale wakitaka kuvuka kufika ng‟ambo ya pili ni mpaka watembee au wazunguke karibu kilometa 20. Tatizo ni kubwa, ndiyo maana ofisi yetu sasa imefanya harakati za kutosha kuhakikisha tunawasiliana na wenzetu wa TANROAD na hivi sasa nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunapewa daraja la mudam lile la chuma kupitia ofisi ya TANROAD, si muda mrefu sana angalau liweze kufungwa wakati tukisubiri mpango mrefu kuhakikisha daraja lile linajengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kufanya hivyo sasa angalau tutapunguza kilio cha watu wa eneo lile na imani yangu kubwa ni kwamba, watu wa TANROAD kuanzia wiki hii sasa muda wowote watakwenda kulifunga ili kuondoa tatizo kwa wananchi wa eneo lile.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Spika, kwanza ninasikitika sana kwa majibu ya Naibu Waziri anaposema kwamba wafugaji hawapati maji kwa sababu wakulima wamekuwa wakikinga hayo maji, nadhani wana upungufu wa research. Inaonesha kwamba mto Mkondoa na mto Miyombo inafika mpaka sehemu ambazo wafugaji wapo na tatizo lao kubwa siyo maji, tatizo lao kubwa ni malisho. Ndiyo maana wameonekana sehemu za Malangali wakilisha katika sehemu za mashamba ya watu na sehemu ambazo watu wamehifadhi mazao yao.
Mheshimiwa Spika, lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Tindiga pamekuwa siyo mahali salama kwa watu kuishi na kwa kilimo kwa sababu wafugaji wameonekana ku-take over maeneo yale na hapa nnavyozungumza na wewe pamekuwa na mauaji kila mwezi; tarehe 8 Juni ameuawa kijana anaitwa Ally Mbarouk Makakala na juzi tarehe 6 Septemba wameuawa watu wawili Elia Emmanuel Mbwane na Ramadhani John Mashimba.
Je, Serikali inawahakikishiaje usalama wa wakulima wa pale Tindiga lakini pia inawahakikishiaje usalama wananchi wa Tanzania ambapo suala la migogoro ya wakulima na wafugaji limeonekana kuwa kero kubwa sana hapa nchini? (Makofi)
Swali la pili, kwa kuwa Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ilikuja Tindiga na kutoa baadhi ya maagizo ambayo mpaka sasa hayajafanyiwa kazi na kupelekea vifo vya hao watu wawili vilivyotokea juzi.
Je, Naibu Waziri pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani wapo tayari kuambatana pamoja na mimi kuelekea Tindiga kuona hali halisi ya mauaji na hali ya kutotulia katika Jimbo la Mikumi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, kama Mheshimiwa Mbunge haridhiki na maelezo yangu nafikiri bado tuna fursa ya kuangalia suala hilo ili tuweze kupata maelezo mengine na ninamuahidi kwamba tukitoka hapa nitakaa naye tuone namna gani tunaweza tukapata taarifa ambazo zitatusaidia kuboresha hiyo ambayo tunayo ili tuweze kufanya yale ambayo ni ya muhimu kwa ajili ya kushughulikia mgogoro huo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tunafahamu mauaji ambayo yametokea Mheshimiwa Mbunge amewasiliana na sisi. Tunafahamu kwamba ni sehemu ya changamoto kubwa tuliyonayo nchi nzima ya migogoro ya wakulima na wafugaji. Ndiyo maana kama nilivyoeleza katika swali la awali Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara zingine ikiwepo Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na TAMISEMI tayari kuna timu ya Wizara hizo inafanya ground work kuja na mapendekezo ambayo yatatusaidia kuondoa migogoro tuliyo nayo. Kwa hiyo, naamini Mheshimiwa Mbunge akiwa na subira na katika muda ambao siyo mrefu tutafikia muafaka wa namna ya kusuluhisha matatizo haya.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili kwamba maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama hayajatekelezwa. Vilevile nipo tayari nikitoka hapa kuwasiliana na Mheshimiwa DC wa kule kujua ni kwa nini maagizo yale hayajatekelezwa, ikibidi kama anavyopendekeza mimi mwenyewe sitasita kuandamana naye kwenda Jimboni kwake kuangalia hali hii. Pamoja na kwamba tayari nafahamu aliyekuwa wakati huo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba tayari alishafika kwenye eneo hilo. Serikali hatutaki hii migogoro iendelee na pale panapotakiwa tufanye jambo lolote la kunusuru na kusuluhisha tutafanya hivyo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba siyo shida kwenda Jimboni kwake kuangalia hii hali. Nashukuru sana. (Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu sahihi aliyoyatoa. Niseme tu na mahali pote wasikie kwamba hakuna shamba lolote ambalo linafanana na thamani ya maisha ya mwanadamu, wala hakuna kundi lolote la mifugo ambalo linafanana na maisha ya mwanadamu. Kwa hiyo, hakuna mgogoro wowote ule ambao unaleta uhalali wa kuua mwanadamu.
Mheshimiwa Spika, kwa kutumia kigezo hiki nitoe maelekezo katika Mkoa husika na Wilaya husika kuwasaka wowote wale waliohusika na mauaji hayo na sehemu yoyote ile ambako watatumia vigezo vya mgogoro kuua watu, wakamatwe na wafikishwe kwenye mkono wa sheria. Kama watatumia kigezo cha mob nielekeze katika Kijiji husika ambacho watapoteza maisha ya mwanadamu, wakamate vijana wote wenye nguvu ambao wanaweza wakawa wawefanya hivyo ili kuweza kupekua na kuweza kupata wale waliofanya kazi hiyo. Kama Magereza hayatoshi wawaachie huru vibaka wote walioiba simu na vitu vidogo vidogo, wakamate wale wanaoua watu wawekwe ndani ili tuweze kukomesha utaratibu wa watu kuua wananchi wasiokuwa na hatia na kuwasababishia matatizo. (Makofi)
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa
kunipa nafasi ili nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Miundombinu ya mradi
wa umwagiliaji wa Bwawa la Dachi lililopo katika Kata ya Malolo liligharimu
takribani sh. 600,000,000 ambazo zilifadhiliwa na Shirika la JICA la Japan lakini
miundombinu hiyo imeharibika vibaya na imejengwa chini ya kiwango.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwashughulikia wale wote waliofanya
ubadhilifu huu na inachukua hatua gani ya kuokoa mradi huu ambao sasa Mto
Mwega umejaa mchanga na kuharibika na wananchi wakiwa wanategemea
sana bwawa hili kwa ajili ya umwagiliaji pale Malolo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,
kwanza nashukuru kwa kunipa taarifa kwamba kuna mradi wa umwagiliaji
umejengwa eneo la Malolo na kwamba mradi huo pengine umepata shida
kutokana na mafuriko au pengine kutokana na usanifu haukuwa sawasawa au
ujenzi haukufanyika vile inavyotakiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kitu tutakachofanya tutakwenda
kuchunguza kuona ni nini kilichopo na tukishachunguza kitu cha kwanza ni
kuhakikisha tunaboresha mradi huo ili uendelee kufanya kazi iliyotarajiwa. Baada
ya kufanya uchunguzi kama kuna tatizo lolote ambalo tutaliona kwamba lipo,
basi litashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na jitihada za Serikali za kukamilisha huu mradi wa World Bank, Mji wa Mikumi ni Mji wa kitalii na umekuwa ukipata wageni mbalimbali na idadi ya watu imeongezeka wamekaribia wakazi 30,000, lakini Mikumi kuna vyanzo vingi kama Iyovi, Madibila na pia Mto Muhanzi.
Je, Serikali haioni umuhimu wa kuweza kutumia
vyanzo vingine ili viweze kusaidiana na mradi huu ili iweze kusaidia wananchi wa Jimbo la Mikumi na kadhia hii?
Swali la pili, katika ziara ya Naibu Waiziri ulipokuja uliagiza watalaam waje kuangalia chanzo cha maji cha Sigareti pale Kata ya Ruaha ambapo kingeweza kusaidia Kata ya Ruaha na Rwembe, wameshafanya hivyo na kukuletea taarifa na imeonekana takribani shilingi bilioni mbili zinahitajika ili kuwezesha wananchi wa Ruaha waweze kupata mradi huo.
Je, Mheshimiwa Waziri unaweza kuwaahidi vipi wananchi wa Ruaha ambao sasa wanakutazama kwamba je, huu mradi utaingizwa katika Bajeti ya 2017/2018 ili uweze kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Mikumi kwa ujumla?
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyotaja kwamba ni kweli nilishawahi kutembelea Jimbo la Mikumi kwenda kuangalia miundombinu ya maji. Ni kweli tulienda na yeye mpaka Kijiji cha Ruaha na tukaona chanzo cha Segereti na tukaagiza. Kwa sababu kwa sasa hivi tuna utaratibu Wizara kwamba tunaweka fedha kila Halmashauri, basi kwa kutumia nafasi hili niagize ule mradi ambao tuliagiza kamba waufanyie mchakato wa kufanyiwa usanifu ukikamilika basi watumie fedha tutakazozitenga katika Bajeti ya mwaka 2017/2018.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia chanzo cha Madibira tayari tumeshamuagiza Mkurugenzi wa Maji wa Mamlaka ya Morogoro (MORUWASA) ambaye Aprili anatanganza tender, ifikapo Juni na Julai tayari atakuwa amempata mkandarasi kwa ajili ya kuboresha kile chanzo cha Madibira ambacho kina umbali wa kilometa 17 kutoka chanzo kuja mjini Mikumi na kazi zitakazofanyika ni pamoja na kwanza kuboresha chanzo chenyewe cha maji cha Madibira ili kiweze kupanuliwa kuongeza kiwango cha maji na kuweka mabomba mapya ambayo yataleta maji katika Mji wa Mikumi.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Katika ziara yake Naibu Waziri pale Wilayani Kilosa alitembelea bwawa la Kidete na alijionea jinsi ambavyo limekuwa likileta madhara makubwa ya mafuriko na kuharibu mpaka reli kwenye Wilaya yetu ya Kilosa. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa hili la Kidete ambalo ni muhimu kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni kweli kabisa nilitembelea hilo eneo na nikaenda kuona shida iliyoko katika lile bwawa. Palikuwa na mkataba lakini tayari Serikali imechukua hatua ya kuhakikisha kwamba sasa unafanyika usanifu upya na fedha ilishatengwa katika bajeti ya mwaka huu tunaokwenda nao. Kwa hiyo, wakati wowote tutatangaza tenda baada ya kukamilisha usanifu mpya ili tuweze kulijenga lile bwawa katika standard ile inayotakiwa isilete madhara tena kwa wananchi wa Kilosa.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nisikitishwe sana na majibu haya ya Serikali ambayo wamekuwa wakiyajibu mara kwa mara, kiukweli yanakatisha sana tamaa. Kwa sasa huu utaratibu wa Serikali wanaosema ni kifuta jasho kwa wananchi ambao wanakuwa wameuliwa na tembo au mazao yameharibiwa kiukweli haina uhalisia na haileti haki kwa wananchi ambao wamekaa kwenye mazingira hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii yote inatokana na sheria ya wanyamapori ambayo imeonekana kuwa na usumbufu na upungufu mkubwa sana. Ni lini Serikali itaileta sheria hii hapa Bungeni ili iweze kubadilishwa ili iweze kwenda na uhalisiana kurudisha fidia na hili neno la kifuta jasho libadilishwe iwe fidia iliyokuwa imetathiminiwa kutokana na matatizo ambayo wamepata wananchi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili juzi kuamkia jana katika Kijiji cha Kikwaraza pale Mikumi ambapo Mbunge wa Mikumi anaishi, simba alivamia zizi la mfugaji anaitwa Agrey Raphael na kuua ng’ombe mmoja pamoja na kujeruhi ng’ombe wawili.Sasa hayo matatizo na changamoto kama hizi zimekuwa nyingi sana kule Mikumi kwenye Kata kama Mikumi, Luhembe, Kidodi, Kilangali, pamoja na maeneo ya Mhenda. Je, Naibu Waziri yuko tayari kuambatana na mimi kuelekea kule mikumi ili akasikilize changamoto nyingi za wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu kutokana na matatizo kama haya ya wanyamapori kabla hawajaamua kuchukua sheria zao mikononi kwa kutumia silaha za jadi? Ahsante. (Makofi) [Maneno haya siyo sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii naomba….
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu iko sasa hivi inafanya kuiisha tunapitia upya sera na sheria pamoja na taratibu mbalimbali ambazo zinatumika katika kutoa hiki kifuta jasho na machozi, ni hivi karibuni tu tutaileta hii sheria hapa ndani Bungeni ili Bunge lako Tukufu liweze kushauri na liweze kuipitisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili la kuambatana naye, nataka nimwambie tu niko tayari mara baada ya shughuli za Bunge kukamilika, nitaambatana naye kwenda kuangalia maeneo hayo yote yalioathirika. Ahsante.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.
Moja kati ya changamoto kubwa za wasanii wa Tanzania ni kuibiwa kazi zao, lakini pia kutonufaika na kazi zao kwa sababu ya kazi hizo kutolindwa ipasavyo. Tunaona kuna upungufu mkubwa sana kwenye Sheria Namba 7 ya mwaka 1999, Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.
Je, Serikali haioni kwamba huu sasa ni muda muafaka wa kuileta sheria hii kwenye Bunge lako Tukufu tuweze kuibadilisha na kuirekebisha ili iweze kusaidia wasanii wa Tanzania waweze kupata haki zao, kwa sababu wengi wanakufa masikini, wanaibiwa kazi zao mtaani lakini wanaowaibia tunawajua?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Hili suala tayari COSOTA imeshaliona, hii ni Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki. Kwa kuanzia imeanza kufanya utaratibu wa kubadilisha kifungu namba 46. Kwa hiyo, mchakato huu unaendelea, tuwe na subira ili marekebisho yaweze kufanyika ikiwa ni pamoja na kanuni zake. Ahsante.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Matatizo yaliyopo katika Jimbo la Ludewa yanafanana sana na matatizo ambayo yapo katika Jimbo la Mikumi. Matatizo ya mtandao wa mawasiliano ya simu, hasa kwenye Kata za Vidunda, Muhenda, Uleling’ombe pamoja na Tindiga lakini pia Kata ya Masanze hasa kwenye vijiji vya Munisagala na Chabima. Je, ni lini Serikali italeta mawasiliano haya ya simu katika kata hizi za Jimbo la Mikumi. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilidhani jibu alilolitoa jana la kuikataa bajeti ni kwamba labda mwaka huu wote tusiangalie katika eneo la Mikumi. Nitaomba tukutane, pengine ile aliikataa siyo kutoka rohoni.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Bwawa la Kidete pale Kilosa ni bwawa ambalo kila mwaka linaleta maafa makubwa sana, reli inang’oka, wananchi wa Mabwelembwele, Masanze, Tindiga pamoja na Magomeni wamekuwa wakiathirika sana mafuriko makubwa. Mwaka 2017 nilipouliza Mheshimiwa Waziri alinijibu kwamba Serikali imeshatenga pesa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hili muhimu la Kidete.
Je, ni lini Serikali itapeleka pesa hizo ili ziweze kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Kilosa? Ahsante. (Makofi)
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la Kidete nimelitembelea, nikakuta topography jinsi ambavyo imekaa, kidogo ni tete, kwa sababu juu ya bwawa kuna reli, chini kuna kijiji. Ukijenga bwawa ukaweka tuta kubwa ni kwamba maji yatazamisha reli.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kutokana na changamoto hiyo, tumeunda timu ya wataalam ambao walianza kazi mwezi uliopita na Mheshimiwa Mbunge nitakuomba tu wiki hii, nina imani watakuwa wameshamaliza kazi hiyo ili niweze kukujibu ni nini sasa kinafuata baada ya kukamilisha huo usanifu? (Makofi)
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Awali ya yote naomba nitoe pole sana kwa familia za wasanii wenzangu, Jebby Mubarak na Agnes Gerald Masogange ambao wametangulia mbele za haki. Mungu awalaze mahali pema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali namba moja, pamoja na jitihada hizo tunazoziona za watu mmoja mmoja, wanariadha kuweza kufanya vizuri katika michezo mbalimbali, lakini imekuwa tabia ya Watanzania kupeleka timu mbaimbali kwenye mashindano mengine bila kuwaandaa.
Je, kwa nini sasa Serikali isiache kuwapeleka kwanza wanamichezo hao huko nje mpaka ihakikishe imewaandaa na kuweza kufanikiwa kuleta medali na kuitangaza vizuri Tanzania? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali namba mbili, changamoto kubwa ya wanamichezo wa Tanzania ni viwanja kukosa ubora na nadhani ile shilingi trilioni 1.5 ingeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa sana changamoto hiyo. Mara baada ya mfumo wa chama kimoja kusitishwa mwaka 1992 Chama cha Mapinduzi kimeonekana kuhodhi viwanja vikubwa karibu vyote vikubwa hapa nchini na kushindwa kuviendeleza…

MHE. JOSEPH L. HAULE: Je, hamuoni kwamba huu ni wakati muafaka sasa wa Chama cha Mapinduzi kurudisha viwanja vya michezo hivyo Serikalini ili viweze kutumika na Watanzania wote kwa ujumla? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nashukuru kwa maswali mazuri ambayo yameulizwa na kaka yangu Profesa Jay. Nikianza na swali lake la kwanza ambapo ametoa ushauri kwamba kwa nini Serikali haipeleki wanamichezo nje kwa ajili ya kwenda kufanya maandalizi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba ushauri ambao ameutoa ni mzuri lakini nachukua pia nafasi hii kuweza kumtoa hofu kwamba katika mwaka huu wa fedha 2017/2018 kwa sababu sisi kama nchi tunajua kabisa vijana wetu wa Serengeti Boys wanakabiliwa na mashindano makubwa na AFCON ambayo Tanzania itakuwa ni mwenyeji mwaka 2019. Kwa hiyo sisi kama Serikali kwa kushirikiana na TFF tuko kwenye mpango wa kuwachukua vijana wetu kuwapeleka Sweden kwa ajili ya kwenda kupata hayo mazoezi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake la pili ambapo amedai kwamba viwanja vingi vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi, niseme kwamba imekuwa ni Sera ya Michezo ya mwaka 1995 kuhamasisha wadau wote kuwa vyama vyote na taasisi zote vina hali ya kuweza kumiliki viwanja vya michezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, viwanja vyote ambavyo vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi vinamilikiwa kwa halali na ni haki yao na hakuna hata kiwanja kimoja ambacho kimeporwa na Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nachukua nafasi hii kuweza kuhamasisha Wabunge wote ambao mpo ndani ya Bunge hili, Halmashauri zote, wadau na taasisi zote kuhakikisha kwamba vinatenga maeneo kwa ajili ya michezo kwa sababu ni sera yetu ya mwaka 1995. Ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Ulaya kinatumika kwa wananchi wote wa Kata za Zombo, Muhenda pamoja na Ulaya, lakini kina upungufu mkubwa sana wa watumishi na hali mbaya sana ya miundombinu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itatupia macho kwenye Kituo cha Afya cha Ulaya ili wananchi wa pale kwenye Tarafa ya Ulaya waweze kupata tiba bora kwa mama na watoto, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE) Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya hicho Kituo cha Afya ambacho Mheshimiwa Mbunge anakitaja cha Ulaya sijapata fursa ya kukitembelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo ni ukweli usiopingika kwamba miongoni mwa mikoa ambayo imepata Vituo vya Afya vya kutosha katika awamu hizi ni pamoja na Mkoa wa Morogoro pamoja na Hospitali ya Wilaya. Ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba Vituo vya Afya vyote ambavyo vinafanya kazi kama Vituo vya Afya, lakini havina hadhi ya Vituo vya Afya tunaenda kuvikarabati na kuviboresha ili vifanane na hadhi ya Vituo vya Afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ni azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na yeye na pale alichombeza akaimba na wimbo nina amini hatutamsahau.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba uniruhusu niwape pole sana wenzetu wa Yanga kwa sababu msiba wa jirani yako ni msiba wa wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba asiwe na wasiwasi, naomba awe na subira mwaka 2018/2019 hii inakuja tutashughulikia suala lake la Ulaya.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.Nilishauliza mara kadhaa kuhusu barabara hii ya Dumila- Kilosa – Mikumi na Serikali ilikuwa ikitoa majibu haya haya kuhusu upembuzi yakinifu. Barabara hii ni muhimu sana na hata mwaka jana tulitengea bajeti kuhusu ujenzi wa kipande hiki cha kilometa 21 kutoka Ludewa kwenda Kilosa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ningependa nipate majibu ya Serikali, je, ni lini hasa wananchi wanataka kujua ni lini hasa kazi ya ujenzi wa barabara ya kipande hicho cha kilometa 21 Ludewa –Kilosa utakamilika na then tutaanza lini ujenzi wa kutoka pale Kilosa kuelekea Mikumi ili wananchi wa Mikumi waweze kufaidi matunda ya Serikali yao?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Mbunge amekuwa akisikia mara kwa mara kwamba upembuzi yakinifu tayari, usanifu wa kina tayari. Nimtaarifa tu kwamba hatua hizo mbili zilishafanyika, hatua inayofuata ni kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. Fedha ilikwisha tengwa na hivi karibuni tunaamini katika bajeti ya mwaka huu kipande hicho cha barabara kitaweza kujengwa ili tuwaunganishe watu wa Morogoro na Ludewa, ahsante.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Awali ya yote, nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kufanya ziara Jimboni kwangu Mikumi, pindi ambapo simba walivamia zizi la mwanakijiji wetu pale Kikwalaza na akaweza kuzungumza na wananchi. Pia alifanikiwa kwenda Ruhembe, bahati mbaya sana ni kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri hakuwasiliza wananchi bali alisikiliza haya ambayo anaambiwa na viongozi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza niseme tu, kama kweli tunaipenda nchi yetu, sisi tunajua kwamba kuwa na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi siyo laana bali ni baraka kutoka kwa Mungu, lakini ukweli ni kwamba wananchi wa Kata ya Ruhembe, Kijiji cha Kitete Msindazi na Kielezo wanateseka sana kwa sababu ya kunyimwa haki zao za msingi za kuishi maeneo yale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa Naibu Waziri, pamoja na ziara aliyoifanya, yale yote aliyoyazungumza kule hakuna hata kimoja kilichotekelezwa. Nimwombe asiwasikilize hawa wanaomwandikia hivi vitu, aje awasikilize wananchi wa Kata wa Ruhembe wamwambie A, B, C na vitu vingine vyote. Kwa hiyo, hiyo ndiyo rai yangu kwake kwamba namkaribisha tena Mikumi, azungumze na wananchi hawa viongozi wanaomwambia yote yamekamilika na kwamba kuna amani, wanafanyakazi yake iwe ngumu sana kwa kutokuwa na amani katika Kata yetu na Jimbo la Mikumi kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, sasa hivi wananchi wa Mikumi, napata ukakasi kusema kama wanapotea au wanachukuliwa na watu wasiojulikana, kuna watu wanatoka Usalama na TANAPA wananchi wa Mikumi wanakufa na wanapotea na wengine wanarudi wakiwa vilema kwa sababu tu wanaonekana kuchukuliwa katika hali ambayo haipo na tukiwatafuta katika Vituo vya Polisi hatuwapati, tunaambiwa wamepelekwa Dar es Salaam. Je, Serikali inasemaje kuhusu wananchi wa Mikumi wanaopotea? Mpaka sasa takribani wananchi 40 kutoka Kata za Muhenda, Ruhembe, Kidodi wamepotea hatujui wako wapi. Serikali inataka kutuambia nini kuhusu hawa ndugu zetu? Tumechoka kuzika nguo na ndugu zetu hatuwaoni? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph Leonard Haule, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa nimeshatembelea eneo hilo na ni kweli kabisa nilikaa na wananchi tukaweza kuzungumza na wakabainisha mambo mengi na tuliyawekea mkakati wa namna ya kuyatatua. Nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kipindi kati ya sasa na mwezi Septemba, tena wakati nakwenda Kilombero, nitapita kwenye eneo hilo ili tuweze kukutana na hao wananchi ili tuone kama kweli matatizo yao yanaendelea kuwepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu hao wananchi ambao anasema kwamba wanapotea bila sisi kujua, nadhani hizi taarifa kama Serikali hatunazo. Kama Mheshimiwa Mbunge anayo majina na anasema wananchi karibu 40 wote wamepotea, nadhani ni wakati muafaka tupatie hayo majina ili nasi Serikali tuweze kushirikiana na wananchi kubaini hao wananchi wote watakuwa wamekwenda wapi. Ni msimamo wetu kama Serikali kwamba kazi yetu ni kulinda wananchi na kuhakikisha wanaendelea kuishi vizuri na kufanya shughuli zao.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Awali ya yote, nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kufanya ziara Jimboni kwangu Mikumi, pindi ambapo simba walivamia zizi la mwanakijiji wetu pale Kikwalaza na akaweza kuzungumza na wananchi. Pia alifanikiwa kwenda Ruhembe, bahati mbaya sana ni kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri hakuwasiliza wananchi bali alisikiliza haya ambayo anaambiwa na viongozi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza niseme tu, kama kweli tunaipenda nchi yetu, sisi tunajua kwamba kuwa na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi siyo laana bali ni baraka kutoka kwa Mungu, lakini ukweli ni kwamba wananchi wa Kata ya Ruhembe, Kijiji cha Kitete Msindazi na Kielezo wanateseka sana kwa sababu ya kunyimwa haki zao za msingi za kuishi maeneo yale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa Naibu Waziri, pamoja na ziara aliyoifanya, yale yote aliyoyazungumza kule hakuna hata kimoja kilichotekelezwa. Nimwombe asiwasikilize hawa wanaomwandikia hivi vitu, aje awasikilize wananchi wa Kata wa Ruhembe wamwambie A, B, C na vitu vingine vyote. Kwa hiyo, hiyo ndiyo rai yangu kwake kwamba namkaribisha tena Mikumi, azungumze na wananchi hawa viongozi wanaomwambia yote yamekamilika na kwamba kuna amani, wanafanyakazi yake iwe ngumu sana kwa kutokuwa na amani katika Kata yetu na Jimbo la Mikumi kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, sasa hivi wananchi wa Mikumi, napata ukakasi kusema kama wanapotea au wanachukuliwa na watu wasiojulikana, kuna watu wanatoka Usalama na TANAPA wananchi wa Mikumi wanakufa na wanapotea na wengine wanarudi wakiwa vilema kwa sababu tu wanaonekana kuchukuliwa katika hali ambayo haipo na tukiwatafuta katika Vituo vya Polisi hatuwapati, tunaambiwa wamepelekwa Dar es Salaam. Je, Serikali inasemaje kuhusu wananchi wa Mikumi wanaopotea? Mpaka sasa takribani wananchi 40 kutoka Kata za Muhenda, Ruhembe, Kidodi wamepotea hatujui wako wapi. Serikali inataka kutuambia nini kuhusu hawa ndugu zetu? Tumechoka kuzika nguo na ndugu zetu hatuwaoni? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph Leonard Haule, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa nimeshatembelea eneo hilo na ni kweli kabisa nilikaa na wananchi tukaweza kuzungumza na wakabainisha mambo mengi na tuliyawekea mkakati wa namna ya kuyatatua. Nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kipindi kati ya sasa na mwezi Septemba, tena wakati nakwenda Kilombero, nitapita kwenye eneo hilo ili tuweze kukutana na hao wananchi ili tuone kama kweli matatizo yao yanaendelea kuwepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu hao wananchi ambao anasema kwamba wanapotea bila sisi kujua, nadhani hizi taarifa kama Serikali hatunazo. Kama Mheshimiwa Mbunge anayo majina na anasema wananchi karibu 40 wote wamepotea, nadhani ni wakati muafaka tupatie hayo majina ili nasi Serikali tuweze kushirikiana na wananchi kubaini hao wananchi wote watakuwa wamekwenda wapi. Ni msimamo wetu kama Serikali kwamba kazi yetu ni kulinda wananchi na kuhakikisha wanaendelea kuishi vizuri na kufanya shughuli zao.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi niulize swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Mikumi ni Jimbo la kitalii na kuna wawekezaji wengi sana wamejenga mahoteli kule katika Jimbo la Mikumi katika maeneo ya Kikwalaza, Tambukareli pamoja na kule Msimba, lakini mpaka leo wanatumia majenereta na hawana umeme. Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka umeme maeneo hayo ili kuwawezesha wawekezaji wetu waweze kuwekeza katika sekta hii muhimu ya utalii?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii, kama ambavyo nakumbuka naye Mheshimiwa Haule anakumbuka, Bunge lako hili hili aliuliza swali la msingi kuhusu upelekaji wa umeme katika Jimbo lake. Napenda nimthibitishie kwamba majibu tuliyotoa ya upelekaji wa umeme wa Awamu ya Tatu na kwa maeneo aliyotaja ambayo yanahusiana na masuala ya utalii, Serikali ya Awamu ya Tano italifanyia kazi. Namwomba aiunge mkono bajeti yetu leo, tuendelee kufanya kazi. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni juzi tu hapa tuliona kwamba barabara ya Dodoma-Morogoro ilipata tatizo pale Dumila na watu walipata tabu sana na kuzunguka kule Kilosa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwa na barabara mbadala na kutengeneza barabara ya lami ya kutoka Dumila-Kilosa mpaka Mikumi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa
Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbilinyi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu upo na barabara hii iko kwenye mpango wa kuboreshwa.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, asante sana. Kwanza nioneshe masikitiko yangu makubwa sana kwa Jimbo lenye chanzo kikubwa cha umeme kama Kidatu lakini pia ni Jimbo la Utalii kuwa na vijiji kama 57 lakini ni 16 tu ambavyo vina umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, ni kweli mkandarasi kweli State Grid yuko kule site na kwa muda mrefu ameonekana kuchimba mashimo na sasa hivi hajaonekana kwa sababu anasema kwamba ana tatizo la
nguzo. Je, ni lini maeneo haya ya Zombo, Ulaya, Muhenda, Tindiga, Vidunda, Uleling’ombe, Kilangali na Mwinsagala wataweza kupata umeme?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali na mbili, kwa kuwa kuna maeneo ambayo kuna nguzo na umeme umepita lakini maeneo hayo hayajapata umeme, mfano maeneo ya Ruaha Darajani, Kikwalaza, Mshimba lakini pia maeneo ya Ruhembe na Tambuka Reli, Kipekenya na maeneo ya Malolo. Je, ni lini serikali itawapatia umeme wananchi wa maeneo hayo kama ilivyofanya kwenye maeneo ya Nyanda za Juu Kusini.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Mheshimiwa Mbunge kwenye swali lake la kwanza la nyongeza amejielekezea katika kazi zinazoendelea katika Jimbo lake kupitia mkandarasi State. Amesema mkandarasi alionyesha kuna tatizo la nguzo, naomba nimtaarifu mkandarasi huyo nimewasiliana naye asubuhi hii na kwamba kweli kulikuwa na tatizo la nguzo. Lakini Serikali kupitia Mheshimiwa Waziri Mkuu na uongozi wa Mkoa wa Iringa ulifanya kikao kikubwa na ulifikia makubaliano na sasa wakandarasi wote nchi nzima wanapata nguzo na ninavyozungumza takribani nguzo 4000 zimeshaenda katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika eneo la Mkoa wa Morogoro.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kwamba mkandarasi yupo katika Mkoa wa Morogoro na anaendelea na kazi na Mheshimiwa Mbunge amekiri na kwa kweli kwa kuwa nguzo zimeruhusiwa na hivi asubuhi nilivyokuwa nawasiliana naye, mkandarasi ametoa taarifa ya kwamba anaendelea kwenye maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge umeyataja kwenye swali lako la msingi na kwamba pia alikuwa ameagiza mita takribani 3000 na karibu zinafika mwezi wa pili Dar es Salaam. Kwa hiyo, kazi ya uunganishaji katika vijiji hivyo itaendelea vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili umejielekeza katika maeneo ambapo kuna miundombinu ya umeme kwa mfano Ruaha Darajani, lakini wananchi hawajaunganishiwa umeme. Nataka nikutaarifu Mheshimiwa Mbunge Serikali yetu ya Awamu ya Tano imekuja na mradi mwingine wa ujazilizi awamu ya pili ambao utaanza Machi, 2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 197 na wafadhili wa Norway, Sweden na Serikali ya Ufaransa pamoja na Serikali ya Tanzania na mradi huu unaanza Machi kwa mikoa yote 26.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka nitoe wito kwa TANESCO na REA kubainisha vitongoji zaidi ya 1000 na vijiji ambavyo vimepitiwa na miundombinu ya umeme mkubwa lakini hawajaunganishiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nichukue fursa hii pia kutoa wito kwa wananchi wote ambao miradi imekamilika ya Densification Awamu ya Kwanza ya Mradi wa BTIP Iringa – Shinyanga na mradi wa Makambako – Songea kulipia shilingi 27,000 na kuunganishwa umeme. Kwa sababu taarifa ambazo tunazo inaonekana wananchi wa maeneo hayo wengi bado hawajalipia na miradi ile inakaribia kukamilika. Kwa hiyo, nitoe wito walipie mapema ili kuepuka gharama wakati miradi itakapokabidhiwa TANESCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni muda mrefu sana nimekuwa nikizungumzia suala la mgogoro kati ya Wanajeshi pale Mikumi na Kitongoji cha Vikweme ambao walihamishwa kwenye Hifadhi ya Mikumi mbugani kwenda kule kwenye Vitongoji vya Vikweme tangu mwaka 1963 lakini Jeshi wamevamia eneo hilo na kuwaondoa wananchi wale kwa maumivu makali sana. Kwa kuwa suala hili nimeliongea mara nyingi, je, Waziri yupo tayari baada ya Bunge hili tuweze kuongozana ili aweze kuwasikiliza wananchi wa Jimbo la Mikumi pale Vikweme ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu na hasa ikizingatiwa kwamba wananchi wengi wa Mikumi tunategemea Kitongoji hiki kufanya shughuli zetu za kilimo na kujiletea maendeleo.
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Haule, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli tumewahi kuzungumzia suala hili na kama nilivyosema awali maeneo mengi yana migogoro kati ya Jeshi na wananchi kuhusiana na masuala ya ardhi. Mimi nipo tayari kufanya hiyo ziara kama anavyoshauri Mheshimiwa Mbunge ili tukaangalie ni nani hasa mwenye haki katika eneo hilo na endapo itathibitika kwamba Jeshi linalazimika kulipa fidia kama nilivyosema, tutafanya hivyo.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nami niulize swali dogo la nyongeza. Kumekuwa na migogoro ya muda mrefu sana katika Jimbo la Mikumi, hasa kwenye Kata ya Kilangali kati ya wananchi na SumaGrow; Kata ya Masanze kati ya Miyombo Estate na wananchi; Kata ya Tindiga kati ya Mauzwi Estate na NARCO na wananchi lakini pia Kata ya Kisanga Estate na wananchi pamoja na WEDO na Stignati:-

Je, Serikali imejipanga vipi kumaliza migogoro hii ambayo ipo katika Jimbo la Mikumi ambayo kwa kweli inahatarisha sana maisha ya wananchi wa Jimbo la Mikumi?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, migogoro hii ameileta hapa na hatujajua wao wenyewe wamefikia wapi. Kwa sababu migogoro mingi Wizara inaingilia kati pale ambapo Halmashauri inakuwa imeshindwa. Mheshimiwa Mbunge amezungumza ni migogoro ya muda mrefu lakini katika ile migogoro ambayo tuko nayo mgogoro anaotaja hatuko nao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwahidi tu kwamba kama kuna migogoro kati ya wawekezaji na kata alizozitaja, basi tuko tayari kusaidiana nao kuitatua ili mradi tu tuweze kujua wao wenyewe wamefikia wapi. Kwa sababu mazungumzo lazima yaanzie kwenye eneo husika. Wizara haiwezi kuingia moja kwa moja mpaka ijue wapi wamekwama. Hatujalipokea na wakilileta tutalifanyia kazi.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Tatizo la Lulindi linafanana sana na Jimbo la Mikumi ambapo kwenye maeneo ya Vidunda, Uleli Ng’ombe, Kisanga, Tindiga na maeneo ya barabara ya kuu ya Tanzania; na Zambia maeneo ya Msimba, Mbamba pamoja na kwenye Hifadhi ya Mikumi, kuna tatizo kubwa sana la mawasiliano:-

Je, ni lini Serikali itawapatia mawasiliano wananchi wa Mikumi wa maeneo yao?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Mikumi lina changamoto moja ya kupeleka mawasiliano kwa uhakika, lile Jimbo liko linapakana sana na Hifadhi yetu ya Mikumi na utaratibu wa kuweka minara kule lazima upate kibali kutoka Wizara nyingine. Wasiwasi uliopo ni kwamba tukiweka mnara, watakaohudumia ule mnara watakuwa ni waaminifu wasilete hujuma. Kwa hiyo, tumekuwa tukipata changamoto mbalimbali za namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa eneo kubwa sana, wananchi wa Mikumi wanapata mawasiliano. Vijiji alivyovitaja, kimojawapo kinapata mawasiliano ya Halotel, isipokuwa nilipotembelea pale wananchi walitaka wapate na vodacom, kwa maana ya M-pesa na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashauri na kuwaeleza Waheshimiwa Wabunge kwamba lengo la Serikali kwa hatua hii, ni kuhakikisha tunapeleka mawasiliano maeneo yale ambayo hakuna mawasiliano kabisa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yale maeneo ambayo tayari yana mawasiliano yanataka option nyingine, watusubiri kidogo na ndiyo maana tunapeleka mawasiliano kule ambako hakuna mawasiliano ili Makampuni mengine yavutike kwenda kuwekeza pale, kwa sababu mwisho wa siku ni makampuni ambayo yanakwenda kupata faida na wananchi vilevile. Kwa hiyo, nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge...

MWENYEKITI: Ahsante.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu hayo ya Serikali, kwenye Kituo cha Afya cha Ulaya nilishauliza hapa mara nyingi kwamba Serikali itatusaidiaje maana ni kituo cha muda mrefu na kimeshachakaa na Serikali iliahidi kwamba itatupatia fedha za kuweza kukarabati kituo hichi cha Ulaya. Je, ni lini sasa Serikali italeta pesa kwenye kituo hiki cha Ulaya ambacho kimechakaa sana na ni kituo muhimu kinachituhudumia Kata za Ulaya, Muhenda, Zombo pamoja na Masanze?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Kituo cha Afya cha Malolo kinajengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na Mbunge na Halmashauri na sasa kimefikia kwenye kiwango cha lenta. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza nguvu za wananchi ambazo sasa hivi zimeonekana ili waweze kujipatia huduma katika Kituo cha Afya cha Malolo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Haule Joseph, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo katika swali lake la nyongeza anaongelea Kituo cha Afya cha Ulaya ambacho kimechakaa, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine wote, ni ukweli usiopingika kwamba vituo vya afya ambavyo vimepatiwa fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi vinaonekana viko bora kuliko vile ambavyo vilikuwa vya siku nyingi. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba vile vituo vya afya ambavyo vilijengwa miaka hiyo na hadhi yake haiendani na vituo vya afya vya sasa, iko katika utaratibu wa kuhakikisha kwamba vinakarabatiwa ili vilingane na hadhi ya sasa. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge aendelee kuiamini Serikali kama ambavyo tumeweza kupeleka fedha katika hivyo vituo vya afya na zahanati yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, anaongelea jitihada ambazo zinafanywa na halmashauri pamoja na nguvu yake mwenyewe nampongeza kwa sababu suala la afya linahusu jamii yote ikiwa ni pamoja na Waheshimiwa Wabunge. Pale ambapo wananchi wamejitoa kwa ajili ya kujenga vituo vya afya Serikali na sisi tunaunga mkono kwa sababu ndio azma ya Serikali nayo iko kwenye ilani yetu ya CCM.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nami napenda niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikisimama mara kwa mara nikimuomba Waziri atujibu ni lini wataleta pesa na kujenga barabara ya kilometa 142 kutoka Dumila – Kilosa mpaka Mikumi ambayo kwa sasa imejengwa kuanzia Dumila mpaka Ludewa na bado kilometa 21 Ludewa – Kilosa? Kila siku nimekuwa nikijibiwa kwamba tuko kwenye upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na vitu kama hivyo. Wananchi wa Kilosa wanataka kujua ni lini Serikali itaanza kujenga barabara hii muhimu kwa uchumi wao?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Haule, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara hii muhimu inayotoka Dumila - Kilosa, inapita maeneo ya Ulaya mpaka Mikumi, niseme tu kimsingi barabara hii imeanza kujengwa lakini tunaenda kwa awamu. Mheshimiwa Mbunge unafahamu eneo hili la Ludewa – Kilosa ambalo sasa tuna mpango wa kujenga kwa kiwango cha lami na katika bajeti inayokuja kipande hiki tutaanza kujenga ili tupunguze uelekeo wa kwenda Mikumi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nikuombe tu Mheshimiwa uvute subira, tumejipanga na tunaendelea kujenga kama unavyofahamu ili kuweza kuwaunganisha wananchi hawa wa Mikumi. Hii njia kwa kweli ni fupi, itapunguza gharama na muda lakini pia inapita maeneo muhimu ya uzalishaji na utalii kwenye maeneo yetu ya Mikumi. Ahsante.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, pamoja na ujenzi wa hospitali na Vituo vya Afya lakini bado kuna upungufu mkubwa sana wa watumishi wa afya hapa nchini. Je, Serikali haioni sasa huu ni muda muafaka wakati wanajenga Vituo vya Afya, lakini pia watoe ajira mpya kwa watumishi wa afya na pia walipe stahiki za wale watumishi wa afya wengine ili kuongeza morali na tija?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Jimbo la Mikumi lina jiografia mbaya sana na tuna Vituo vinne vya Afya vya Kidodi, Mikumi, Ulaya na Malolo ambacho wananchi wanajenga kwa nguvu zao wenyewe. Je, Serikali haioni sasa huu ni muda muafaka ili kuokoa Watanzania wa Mikumi tuweze kupatiwa magari ya wagonjwa kusaidia akina mama na watoto ambao wanapata matatizo katika maeneo hayo? Ahsante sana.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mheshimiwa Haule katika ziara kadhaa nilizofanya tulikuwa pamoja kule Jimboni kwake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mpango wa Serikali, kama tunavyofahamu kwamba Mheshimiwa Rais na Serikali kwa ujumla imefanya mchakato wa ujenzi wa Vituo vya Afya 352hivi karibuni, Hospitali zetu za Wilaya 67 na mwaka huu tumeongeza 27 mpya, jambo hili linataka human resources kwa ajili ya kuweza kufanya kazi vizuri.

Kwa hiyo, ni mpango wa Serikali tutaangalia nini kifanyike. Licha kwamba mwanzo tuliajiri takribani watumishi wasiopungua 11,000; wale wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu lakini tutaangalia nini kifanyike kwa ajili ya kuongeza idadi ya watumishi katika vituo vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Mikumi suala zima la kuongeza miundombinu, nikushukuru, lakini Mbunge hapa kwanza unge-appreciate kazi kubwa iliyofanyika pale Mikumi, nadhani na wewe unakumbuka, ilikuwa ni ya kusuasua sana. Serikali tumeenda tumefanya kazi kubwa na hivi sasa imekuwa ni miongoni mwa Kituo bora sana cha Afya katika eneo lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo tutaendelea kuangalia nini kifanyike kwa maeneo mbalimbali yenye changamoto kubwa, siyo Mikumi peke yake. Ni mpango wa Serikali kuangalia nchi nzima tunahakikisha wananchi wanaopata shida ya huduma ya afya sasa inakuwa ni historia. Ahsante sana.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasanii wa Tanzania changamoto yao kubwa sana na namba moja ambayo inawakabili ni wizi wa kazi zao. Tumekuwa tukiona kazi zao zikiuzwa kwa holela kwenye maeneo mbalimbali lakini Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, Na.7 ya mwaka 1999 imeonekana kuwa haina meno wala haiwasaidii wasani wa Tanzania. Je, ni lini Serikali italeta sheria hii hapa Bungeni ili tuweze kuifanyia mabadiliko ili wasanii wa Tanzania ambao wanaleta sifa kubwa kwa Tanzania kwa kupitia sanaa yao waweze kufaidika na kazi zao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Profesa Jay kwa swali nzuri la nyongeza kwa sababu yeye pia ni msanii, kwa hiyo, anatambua changamoto ambazo zinawakumba wasanii nchini Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kuna changamoto kubwa sana ya suala la wizi ya kazi za sanaa, lakini sisi kama Wizara tumechukua hatua kadhaa. Hatua mojawapo ni kuhakikisha kwamba tunawahamasisha wasanii waweze kusajili kazi yao COSOTA ili pale ambapo wanapata matatizo iwe rahisi kuweza kusaidiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile amezungumzia changamoto kubwa ya sheria, tukiri kwamba hii sheria ina upungufu lakini Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ipo kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara, kwa hiyo, kama Wizara ambacho tunafanya sasa hivi ni kuhakikisha kwamba kitengo hiki cha COSOTA kinahama kutoka Viwanda na Biashara kuja kwenye Wizara yetu ya Habari ili tuangalie ni namna gani ambavyo tutaifanyia marekebisho sheria hii. Ahsante.
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nisema kwa masikitiko makubwa sana Wilaya ya Kilosa ni moja kati ya Wilaya zinazoongoza kwa migogoro mikubwa sana ya mashamba na migogoro mikubwa sana kati ya wakulima na wafugaji kutokana na upungufu wa ardhi.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, katika Kata ya Tindiga kumekuwa na mgogoro mkubwa sana kati ya Kijiji cha Tindiga na NARCO ambao wamemega eneo la Tindiga na kuwapa wafugaji lakini kulikuwa na kesi tangu mwaka 2013 mpaka 2019 wananchi wa Kijiji cha Tindiga wameshinda lakini mpaka leo wanazuiwa kulima na ndiyo tunaowategemea kwa kilimo cha mpunga.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni kumetokea maafa makubwa sana akina mama wamebakwa na wakulima wamepigwa vibaya sana na kulazwa hospitali kwa sababu ya kuzuiwa kwenda kulima. Je, Serikali inatoa kauli gani kwa wananchi wa Tindiga ambao wameshinda kwenye Mahakama ya Ardhi ili warudishiwe ardhi yao? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali ilitoa mashamba kwa wawekezaji katika Kata ya Kisanga, Kata ya Masanze pia Sumargo pale Kilangale. Hata hivyo, hawa wawekezaji wameshindwa kutumia mashamba haya ipasavyo na kupoteza ajira kwa wananchi na Serikali inakosa mapato mengi kwa sababu yale mashamba ni pori na hayatumiki. Imeleta migogoro mikubwa sana pale Masanze mtu alipgwa risasi akafariki, pale Kisanga mwananchi alipigwa risasi akafariki, pale Sumargo, Kilangali migogoro ni mikubwa watu wanaumia sana. Wizara ya Ardhi mnatoa kauli gani kwa Wilaya ya Kilosa ili wananchi waweze kurudishiwa mamshamba haya na kuyaendeleza kwa kilimo ili kusaidia Taifa letu la Tanzania? (Makofi)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Haule, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, la kwanza juu ya wananchi wa Tindiga, wiki iliyopita niliongea na wananchi hawa waliletwa na Mheshimiwa Mbunge, nimekubaliana naye aniletee mimi barua na vielelezo hivyo vya kesi, maana mimi siwezi kujua yanayoendelea na kesi na mimi nina wanasheria, walete hizo hukumu za kesi kama kweli wameshinda mimi nitawasaidia ili wapate haki yao. Tulishaelewana na nafikiri alitaka hapa sasa wananchi wengi zaidi wasikie. Serikali lazima itekeleze uamuzi wa Mahakama na Serikali haiwezi kumwonea mtu. Kwa hiyo, fanyeni yale niliyowaelekeza leteni barua na vielelezo vile ili tuweze kuchukua hatua.

Mheshimiwa Spika, la pili, swali hili ni swali la msingi ambalo umeuliza. Katika mashamba ambayo yameshafutwa Mkoa wa Morogoro 15 yanatoka Wilaya ya Kilosa. Niliunda timu ya wizara, ilipokwenda kukagua mashamba yote ya Kilosa tukagundua kuna mashamba mengine mapya 23 ambayo yana sifa ya kufutwa pamoja na haya uliyoyataja.

Mheshimiwa Spika, sasa utaratibu wa kufuta hauanzii Wizarani unaanzia Wilaya ya Kilosa. Tulikuwa na timu ya hovyo pale wilayani Maafisa Ardhi waliokuwa wanafanya kazi ile pale wao sio Maafisa Ardhi walikuwa wamejivisha tu Uafisa Ardhi lakini hatukuwa na Afisa Ardhi. Kwa hiyo, tumefanya utaratibu tumeleta Maafisa Ardhi, kuna Afisa Ardhi mzuri sana tumemtoa kutoka Mkoa wa Mbeya tumempeleka pale sasa ndio wanaanza kazi ya utaratibu wa awali wa kisheria wa kusababisha haya mashamba yafutwe.

Mheshimiwa Spika, lazima notice ya wale wenye mashamba itolewe na Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ya Kilosa hamkuwa naye. Kwa hiyo, nimeelekeza huyo Afisa Ardhi aanze na mashamba haya. Hivi sasa ameshatoa notice ya siku 90 kwa wenye mashamba wajieleze kwanza hatua itapanda itafika kwangu tukiridhika na maelezo yao kwamba wanazo sifa za kufutiwa tutampalekea Mheshimiwa Rais kwa mujibu wa sheria.