Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Haroon Mulla Pirmohamed (1 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. HAROON M. PIRMOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa Ruaha na vijiji vinavyopatikana na vilivyomo ndani ya Hifadhi ya Ruaha umedumu takribani miaka tisa sasa tangu mwaka 2008. Hivi karibuni Serikali ilitoa maelekezo ya kushughulikia mgogoro wa mpaka huo ili uweze kuisha na wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilisha hatua ya kupokea maoni ya mapendekezo ya wananchi katika vijiji 333 na Shamba la Mifugo Usangu linalosimamiwa na NARCO ili kufanya marekebisho ya Tangazo la Serikali Na. 28 (GN 28 of 2008), ni lini Serikali itapitia maombi hayo na kufanya marekebisho ya mpaka huo ili kuachia maeneo ya makazi, ufugaji na kilimo na kutoa tangazo jipya la Serikali litakalomaliza mgogoro wa muda mrefu?