Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Esther Nicholus Matiko (62 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa nami niweze kuchangia kwenye bajeti hii ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kwanza kabisa kabla sijachangia nitoe masikitiko yangu kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano ambayo kwa kweli inajisifu kwamba ni Serikali ya Hapa Kazi Tu. Imezuia television isionyeshwe lakini yet tuko ndani tumejifungia sisi wenyewe, bado mnazuia taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani isisomwe. Inaonesha ni jinsi gani hamjiamini, hamjajipanga na hamjajua ni nini mnataka mlifanyie Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Polisi; kuna mambo makuu mengi sana ya kuyazungumzia na kwa sababu ni dakika kumi, naomba nianze na Jeshi la Magereza. Ni dhahiri kwamba kwenye Jeshi letu la Magereza sheria ambazo zinatumika sasa hivi ni zile ambazo zilikuwa zikitumika wakati wa ukoloni; ni sheria ambazo zimepitwa na wakati. Leo unaweza ukakuta Askari Magereza kwa bahati mbaya, mahabusu au mfungwa ametoroka, atapewa adhabu labda ndani ya miaka mitatu tuseme, ambayo adhabu moja ya mfungwa kutoroka anatakiwa akatwe mshahara wake, nusu ya mshahara au robo ya mshahara, anatakiwa ashushwe cheo, anatakiwa asiende masomoni kujiendeleza na hata ikitokea huyo aliyekimbia amekamtwa, bado huyu Askari Magereza atatakiwa atumikie hiyo adhabu kwa miaka yote ambayo amepangiwa. Hii ni dhuluma na haikubaliki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo mzima wa uendeshaji wa Jeshi la Magereza kiukweli unatakiwa ufumuliwe upya. Tunahitaji kufumuliwa upya kama walivyofanya kwenye idara nyingine. Kuna malalamiko mengi sana ambayo yamekuwa yakiendelea. Hata bila kufumba macho, ni dhahiri kwamba Commissioner General wa Prison amekuwa akilalamikiwa sana. Naomba kabisa mchunguze hayo malalamiko ambayo yako dhidi yake, myafanyie kazi. Kwa sababu tumekuwa tukizungumza, mnapuuzia, baada ya muda ukija kuchunguzwa, ripoti ya CAG inatoa yale ambayo tunayalalamikia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyakazi wote wa Umma tumekuwa tukijaza hizi fomu za maadili, mwachunguze mali wanazomiliki, mishahara wanayopewa ina-reflect uhalisia wa mali ambazo wanamiliki? Kuna ufisadi mkubwa sana ambao unaendelea kwa Viongozi Wakuu wa haya Majeshi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, makazi ya Askari ni duni sana. Mwaka 2015 wakati wa bajeti nilizungumza hapa na mkasema kwamba mlikuwa mmetenga kujenga zaidi ya makazi 9,000. Leo tunavyozungumza, Waziri umekuja unatuambia mnajenga makazi 4,000. Tunapenda kujua yale ya mwaka 2015, hayo makazi 9,000, yamejengwa kwa kiasi kipi? Leo ninavyozungumza, kule Tarime Askari Magereza makazi wanayoishi hata ukienda kumweka sungura, atalalamika kwa nini anaishi kwenye ile nyumba. Leo unamweka binadamu, tena Maaskari Magereza ambao wana familia, kinyumba ambacho kilijengwa mwaka 1942, enzi za ukoloni mpaka leo hujaboresha na zaidi kipindi hicho walikuwa wakikaa Askari Magereza wachache, leo wanakaa wengi kwenye kijumba hicho kimoja, wana familia na mnajua kuna mambo mengine ya staha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, unakuta saa nyingine Askari Magereza wanawajibika kujijengea wenyewe vijumba. Tunaomba mnapokuwa mnasema nyumba 4,000, basi wajalini wale ndugu zetu ambao wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba Serikali hii ya Hapa Kazi Tu inakwepa kuzungumzia Lugumi ya Jeshi la Polisi, lakini inasemekana kuna Lugumi nyingine kwenye Jeshi la Magereza. Inasemekana kwamba kuna fedha zilitolewa kwa ajili ya mfumo wa utambuzi wa ndugu zetu ambao wapo Magereza; wafungwa na mahabusu, wanaojulikana kama OMS (Offender Management System), ilitolewa ili hizi system ziweze kufungwa kwenye Magereza yote nchini, lakini inasemekana hadi leo hakuna system ambayo imefungwa kwenye hayo Magereza. Nataka kujua kama ni kweli, hizo fedha zimekwenda wapi? Au hii ndiyo ile dhana ya kuendeleza Lugumi ndani ya Jeshi la Polisi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, inasemekana pia kuna fedha zilitolewa kwa ajili ya kununua magari ndani ya Jeshi la Magereza ya kuwabeba mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na pia wale ambao unakuta wana-escort. Mheshimiwa Waziri amesema hapa kwamba watajitahidi kutenga fedha na kuna baadhi ya wilaya mmenunua, lakini inasemekana kwamba kuna fedha zilitengwa. Sasa nataka nijue, kama hizo fedha zilitengwa na mzabuni alikuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, zimeweza kununua hayo magari mangapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli zilitolewa, maana yake inasemekana zilitengeneza magari mabovu ambayo sasa hivi hayafanyi kazi na tunaendelea kuona kwamba Askari Polisi ndio wanasindikiza watu kwenda Mahakamani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambacho ni cha fedheha, ni uniform. Uniform mara ya mwisho kutolewa kwa hawa Maaskari Magereza, ambao nimefanya nao mazungumzo, ilikuwa ni 2009, mpaka leo hamjaweza kuwapa uniform.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hawa Maaskari Magereza, labda hata na wa Jeshi la Polisi, ukiwatazama na wengine wamekuja hapa Bungeni, wana uniform tofauti. Viatu vyao vinatofautiana, maana yake wanajinunulia, uniform zao ziko tofauti. Halafu Serikali ambayo inawatumia hawa ndugu zetu, tena vilivyo katika kuwakandamiza wapinzani, mnashindwa hata kuhakikisha kwamba mnawastahi na mavazi yao, angalau waonekane ni watanashati, mnawadhalilisha! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza, kama mmeshindwa kuleta uniform kwa hawa Askari, kwenye mshahara wao waongezeeni fedha za posho ya kununua uniform zao ambazo wataweza kununua uniform zenye kiwango cha juu. Maana inasemekana kuna mtu mmempa tenda ya ku-supply uniform; na ni mke wa kigogo wa Jeshi la Magereza. Anafanya kazi BOT, uniform zenyewe anazoleta ni za kiwango cha chini, yet hawa Maaskari wetu wanakwenda kununua vile vitambaa, wakifua siku mbili havina kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, najiuliza bado, hii Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha kwamba chombo hiki muhimu kwa mustakabali wa maisha ya Watanzania inawaboreshea makazi yao? Inawapa mazingira mazuri ya kufanya kazi? Siyo tu mnawatumia halafu mnawaacha wanaishi kama watumwa kwenye nchi yao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni ucheleweshaji wa malipo; mafao ya Askari wastaafu na Mheshimiwa Waziri nimekupa copy. Kuna baba, ni Askari mstaafu sasa hivi ana miaka 70, tena bila huruma, ametumikia Jeshi kwa zaidi ya miaka 32; kuanzia mwaka 1962 mpaka 1995, anaitwa Simon Mirumbe. Amekuwa akihangaikia mafao yake kuanzia 1995 mpaka leo 2016, mnamzungusha tu. Mmemtumia lakini mnashindwa kumpa mafao yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ifike wakati Serikali ya Chama cha Mapinduzi itambue umuhimu wa Jeshi hili la Polisi, msiwatumie tu, bali muwajali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni msongamano wa mahabusu kwenye Magereza yetu. Leo ukienda Tarime, lile Gereza limejengwa 1942, uwezo wake ulikuwa ni kubeba wafungwa na mahabusu 209, lakini kuna siku unakuta wapo zaidi ya 500 mle ndani. Miundombinu ni mibovu, choo hakitamaniki, watu wanabanana, magodoro yenyewe ni aah! Tumekuwa tukishauri humu ndani; kuna kesi nyingine hazihitaji hata kumpeleka mtu kwenye Gereza, lakini unakuta mnalundika. Leo ukienda Tarime, kufuatia uchaguzi wa Oktoba, kuna kesi za kisiasa watu wako mle zaidi ya mia, wakati mnajua kabisa ile ni hatarishi kwa afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, nataka kujua; na Mheshimiwa Ummy kama angekuwepo; unakuta mwanamke labda amekamatwa kwa bahati mbaya akiwa mjamzito, anapelekwa mahabusu Gerezani, inatokea anajifungua, yule mtoto aliyezaliwa naye anakuwa ni mfungwa au mahabusu kwenye lile Gereza. Nataka nijue Serikali mnajipanga vipi angalau miezi sita huyu mama muweze kum-excuse atoke Gerezani, aweze kumzaa mtoto wake ili mtoto asiathirike kwa yale… (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Aah, mmenibania eeh! (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia Wizara hii muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu kwenye maeneo makuu mawili, yaani nishati na madini. Naomba nianze na Sekta ya Madini ambayo tunajua kuwa, kuna Watanzania wamejiajiri kwenye sekta hii, lakini pia, kuna wawekezaji toka nje wamewekeza kwenye sekta hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu la Tarime Mjini limebahatika kuwa na migodi midogo kwenye Kata ya Kenyamanyori na Turwa. Wilaya ya Tarime tumebarikiwa kuwa na Mgodi wa North Mara ambao ni mkubwa na muwekezaji wa kutoka nje ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya uwekezaji wananchi walikuwa wakifanya uchimbaji mdogomdogo, lakini baada ya uwekezaji ule wamepata adha kubwa sana, hawana maeneo yaliyotengwa dhahiri kwa ajili ya kuwapa maeneo ya kuchimba bali wameendelea kuuawa pale wanapokuwa wameenda kuona chochote kwenye mabaki (vifusi).
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali na mgodi iliahidi ndani ya Bunge hili Tukufu wakati nilipotaka mkakati wa Serikali kutatua wimbi la mauaji ya Watanzania kwenye huo mgodi 2011, waliahidi kutenga maeneo pamoja na kumwaga vifusi vile kwenye maeneo ya wananchi, pamoja na ku-support vikundi mbalimbali ili vijishughulishe na ujasiriamali kuweza kukukuza uchumi.
Mheshimiwa Naibu Spika, haya yalisemwa na kurudiwa na Mheshimiwa Nagu, aliyekuwa Waziri wa Uwekezeaji, Mheshimiwa Wasira aliyekuwa Waziri wa Mahusiano na Uratibu na Mheshimiwa Ngeleja aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini. Ni vyema sasa Serikali ikatimiza haya kwa wananchi na Wilaya ya Tarime na Watanzania waishio Nyamongo na maeneo jirani na North Mara.
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Tarime kuna migodi ambayo wachimbaji wadogo wadogo wanashughulika na uchimbaji wa madini. Maeneo hayo ni Nyabhori na Kebaga, Kata ya Kenyamanyori na Mgodi mwingine ni ule wa Bajeti ambao upo mpakani mwa Turwa na Kenyamanyori. Kwa ajili ya kuboresha au kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji hawa wadogo ni muda muafaka Serikali kuhakikisha hizi ruzuku za zaidi ya bilioni 500 zinawanufaisha walengwa na sio matajiri wachache wanaojivisha joho la uchimbaji mdogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo wadogo ambazo naomba Serikali kujitahidi ndani ya bajeti ya mwaka huu waweze kupatiwa ruzuku, sambamba na vifaa muhimu vya kurahisisha uchimbaji. Changamoto ya kwanza ni juu ya teknolojia inayotumika kuchimba madini, ni ya kienyeji ambayo ni hatarishi sana kwa maisha yao; mfano kuchoronga miamba inabidi watumie nguvu nyingi badala ya morden equipments.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni changamoto ya maji. Aina ya uchimbaji ni underground ambapo unakuta water table ipo juu sana, hivyo inawawia vigumu kufanya shughuli za uchimbaji sababu ya maji na ikizingatiwa vitendea kazi vyao ni duni sana. Ni rai yangu sasa, Serikali itambue maeneo haya na kutoa ufadhili wake kwenye mashine za kuvutia maji kama vile motor, generator na waweze kutoa kwenye vikundi mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto nyingine ni miundombinu mibovu ya barabara kuelekea kwenye migodi hii. Nashauri Waziri akae na Wizara husika kuweza kushawishi ujenzi wa barabara angalau kwa ngazi ya changarawe ukizingatia migodi hii inachangia kwenye pato la Serikali kupitia leseni za uchimbaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine lenye changamoto kubwa ni juu ya kuweza kupata mitambo ambayo hupima udongo na miamba, ili kujua upatikanaji wa dhahabu au madini mengine. Maana kwa sasa wachimbaji wadogo wadogo wanajichimbia kienyeji na kwa kubahatisha tu na hivyo kujikuta wanapoteza nguvu kazi nyingi sana na haina ufanisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya Wilaya ya Tarime tumekuwa hatupatiwi sehemu ya mrahaba toka ACCACIA, kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa kutoa kiasi cha fedha ambacho hutumika kuleta maendeleo ya kijamii. Baadhi ya maeneo ya huduma za jamii ambazo ACCACIA wanapata ndani ya Mji wa Tarime ni Hospitali ya Mji, soko, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Uhamiaji, Stendi, Mahakama, hivyo kwa kuwa wafanyakazi wa ACCACIA wanapata huduma tajwa hapo juu ni dhahiri kuwa ACCACIA wana wajibu wa kuhakikisha Halmashauri yetu ya Mji wa Tarime inapata huduma muhimu za kijamii pamoja na mrabaha toka mgodi wa North Mara. Mji wa Tarime una ukosefu wa maji na barabara za mitaa ni mbovu mno.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mchana huu nichangie katika Sekta ya Nishati ya Umeme; Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa asilimia zaidi ya 70 hawana nishati ya umeme. Halmashauri ya Mji wa Tarime ina mitaa 88, ambapo kiuhalisia kuna kata nne ambazo zipo na vijiji na hamna nishati ya umeme kabisa. Kata hizi ni Ketare, Kenyamanyori, Nandoto, Nkende na baadhi ya maeneo ya Kata ya Turwa na Kata ya Nyamisangura.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilishapeleka barua kuelekeza maeneo yenye uhitaji mkubwa wa umeme, hivyo naomba kujua kama REA Phase III imeyafanyia kazi na ukizingatia Kata ya Kataer, Nyandoto na Kenyamanyori wanajihusisha sana na kilimo ambacho kitasaidia kwenye dhana nzima ya Tanzania ya Viwanda, tuweze kusindika mazao yetu, kufungua viwanda vidogo vidogo. Kata ya Nkende ndio yenye soko la Kimataifa ambalo linajengwa pale, pia kuna uwanja wa ndege ambao unatumiwa na watalii waendao Nyamongo na hata Viongozi wa Serikali na kisiasa, hivyo taa ni muhimu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia Kata ya Nkende ndiyo yenye Mnada wa Magera ambao Serikali imeahidi kuufufua. Pili, ni katika Kata hii ya Nkende ndiyo tuna machinjio ya kisasa, ofisi ya Uhamiaji inajengwa karibu na Mgena Airport na Remague East Africa Market, lakini pia wajasiriamali wadogo wadogo wanategemea nishati hii ya umeme ili kuendesha shughuli zao za kiuchumi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, ijulikane kuwa mahitaji muhimu ya kijamii, kama shule za sekondari na msingi, hospitali, vituo vya afya, zahanati, vituo vya polisi, viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao; hivyo, naomba sana Wizara hii itoe kipaumbele katika Halmashauri ya Mji wa Tarime ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Tarime. Hivyo nishati ya umeme ni ya muhimu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho naomba Wizara hii ichukue hatua ya kuhakikisha hakuna ukatikaji wa umeme mara kwa mara bila kutoa taarifa kwa mteja/wateja kitu ambacho husababisha uharibifu wa vifaa vinavyotumia umeme na kusababisha hasara kwa mlaji. Utolewe Waraka toka ngazi ya Wizara ukiamrisha uboreshaji wa utoaji wa nishati ya umeme bila kuleta madhara kwa mlaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha kwa kutoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha fedha za maendeleo zilizotengwa zitumike kwa ajili ya bajeti iliyotengwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu mbadala kwa wachimbaji wadogo wadogo, ili wapate elimu mbadala kwa uchimbaji wenye tija.
Mheshimiwa Naibu Spika, nawasilisha.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa sababu muda ni mchache mengi nitawakilisha kwa maandishi lakini kwa uchache huu niende kuzungumzia baadhi ya mambo kwenye Mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukirejea ukurasa wa 40 kipengele cha kwanza kabisa kimeainisha misingi na matarajio ya ukuaji wa uchumi. Kwenye kipengele cha kwanza kinasema kuendelea kuwepo kwa amani, usalama, utulivu na utengamano wa jamii ndani na pia nchi za jirani. Nafikiri hapa ingetakiwa ibadilishwe iandikwe kuimarishwa kwa amani, usalama, utulivu na mambo mengine kwa sababu sasa hivi ilivyo huwezi kusema kwamba Tanzania tuna usalama ilhali tukishuhudia wananchi wanatekwa, wanauawa, wengine viongozi wakubwa kabisa wanapigwa risasi nyumbani sehemu ambayo ni secured. Hatuwezi kusema kwamba tuna amani ilhali maisha ya Watanzania ni magumu sana. Wale wote ambao mfano wametolewa kwa vyeti fake na wale wengine wameambiwa ni darasa la saba hawajapewa pension, gratuity ya kuondoka leo useme kwamba kuna amani Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumeshuhudia na Mheshimiwa Msigwa ameomba Mwongozo hapa nchi jirani Kenya kwa yale ambayo yamejiri kwenye kuchomwa kwa vifaranga, ng’ombe kukamatwa na mambo mengine. Kwa hiyo, kipengele namba moja ukibadilishe kiseme, kutakuwepo na matarajio ya ukuaji wa uchumi iwapo kutaimarishwa amani, utulivu, usalama na mambo mengine lakini sio kwamba kuendelea kuwepo ilhali hivyo vitu hatuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine siku zote nasema hatuna uhalisia kwenye mipango yetu na bajeti ambazo tunazileta hapa. Tusipokuwa na uhalisia ni dhahiri hatutafika pale ambapo tunataka kufika kama nchi. Leo ukiangalia kwenye kitabu chako mwenyewe umeainisha bajeti ya maendeleo ya mwaka 2016/2017 ambayo ilikuwa ni shilingi trilioni 11.8 ilitekelezwa kwa asilimia 55 tu. Hii ya sasa hivi kwa quarter moja ya mwaka 2017/2018 imetekelezwa kwa asilimia 11, on average mpaka tunamaliza itakuwa asilimia 44 mpaka 50 au ikienda au ikienda zaidi tuseme 60. Sasa ikienda na trend hii ina maana tunapanga vitu bila kuangalia uhalisia, time frame, vipaumbele ni vipi, mwisho wa siku tunakuwa tunapoteza rasilimali za wananchi kukaa hapa tunajadili. Siku zote nashauri kwamba ni bora tuweke vitu ambavyo tunajua tutavifikia ndani ya muda kwa resources tulizonazo walau tunapokuwa tumekuja ku-discuss Mpango mnatuambia kwa mwaka uliopita tumeweza kufanya mambo ya maendeleo kwa asilimia 80 au hata 85, 90 sio kwa asilimia 44 au 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine na hiki naomba kabisa tuwe sober kwa nachoenda kukiongelea sasa hivi. Kwenye allocation ya kodi za wananchi, maana imechukua discussion nyingi hapa na watu wamekuwa na hisia tofauti.

Mimi natokea Kanda ya Ziwa lakini hili nalipinga na nalipinga with facts na sisi kama wawakilishi wa wananchi ambao tumetumwa hapa Bungeni tukalitafakari ili tuweze kuishauri Serikali vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunaambiwa ujenzi wa jengo la TRA Chato, ghorofa kubwa sana limejengwa kule. Leo tujiulize Chato kuna mzunguko gani mkubwa wa fedha, kuna biashara gani kubwa kule Chato mpaka twende tuwekeze ghorofa? Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya mapato gani kule Chato tukawekeze lile ghorofa la mamilioni ya kodi za Watanzania? Tutafakari kama Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni Uwanja wa Ndege wa Chato, kabisa. Mimi sipingi uwanja wa ndege kujengwa Chato lakini Uwanja wa Ndege wa Chato ulitakiwa kuwa ni chini ya kilometa moja ya run way.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo pamoja na kwamba kuna kukiukwa kwa Sheria ya Fedha za Umma ambayo tulipitisha hapa shilingi bilioni mbili, lakini naambiwa zimetumika zaidi ya shilingi bilioni 39, hiyo ni hoja lakini sio hoja kubwa sana kwangu, tujiulize sisi Watanzania na hawa ambao wanamshauri Rais…

T A A R I F A . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, inabidi nicheke kidogo. Wakati tunapitisha na kwenye kitabu chake cha Mpango wakati ule tunapitisha kwa ajili ya upembuzi yakinifu zile shilingi bilioni mbili walisema ule uwanja wa Chato unajengwa kwa ajili ya usafiri ndani ya Geita na mikoa jirani hawakusema otherwise.

TAARIFA . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu hajatoa taarifa ameuliza swali, nitamjibu kesho wakati wa kipindi cha maswali na majibu kama Waziri Kivuli wa eneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, point hapa ipo nimejibu kwamba wakati inakuwa allocated hapa ilikuwa ni uwanja kwa ajili ya usafiri ndani ya Geita na mikoa jirani. Hawakusema kwamba kwa ulinzi, usalama na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwa Mheshimiwa Jenista, ilikuwa ni shilingi bilioni mbili, ukiongeza shilingi bilioni 39 inakuwa ni shilingi bilioni 41, sijui ni sheria ipi hiyo? Pia reallocation yake tunataka tujue imekuwa reallocated kutoka kwenye kifungu kipi kuja kwenye hizo shilingi bilioni 39? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nimesema kwangu issue siyo sheria zaidi, lakini unaenda kuwekeza huo uwanja mkubwa pale Chato wa runway zaidi ya kilometa tatu ni ndege gani inaenda kutua pale kubwa hivyo? Hiyo ni misuse ya hela za walipa kodi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikajiuliza mara mbili, leo tunasema kwamba Serikali inahamia Dodoma, of which I support 100%; Makamu wa Rais anahamia Disemba, Mheshimiwa Rais tunaambiwa anahamia mwakani. Bunge la Kumi tulipitisha uwanja wa Msalato ujengwe mpaka leo haujajengwa, Rais akija hapa tunatarajia wakija wale Marais, like Trump akija hapa ana ndege ambayo ni Boeing 737 itatua hapa Dodoma au itaenda kutua Chato? Why don’t we rethink tukaja tukajenga kwenye uwanja wa Msalato maana itakuwa ni double cost kwa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wanakuja Marais ambao wanatumia ndege kubwa, Rais Magufuli anaondoka Dodoma kwenda kuwapokea Dar es Salaam maana haka ka-uwanja ka-Dodoma hakawezi kuwapokea. Kwa nini hizo hela tusingeweza kujenga hapa Msalato, kule Chato
tumjengee uwanja wa kuweza kutua ndege ya kawaida like Precision, Bombadier na ndege ya Serikali kuliko kujenga uwanja mkubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ndiyo hoja yangu kubwa au basi kama tunataka tuijenge Chato tungeweza kujenga hospitali kubwa kabisa ku-save maisha ya Watanzania kuliko ku-sink shilingi bilioni 39 kwenye uwanja ambao hautatumika au tungeweza kujenga Chuo Kikuu pale kama tunataka tuijenge ile Chato ikue vizuri, unlike tulivyofanya sasa hivi. (Makofi)

TAARIFA . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu yangu Mheshimiwa Innocent pale, mtani wangu, kwanza taarifa yake siipokei lakini pili, ngoja nimsamehe nilikuwa nampa dongo moja ila nimsamehe, niendelee kuchangia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Innocent nilimuona juzi wakati Rais amezuru kule, anapiga magoti kumuomba shilingi bilioni 30 za maji. Wajibu wako kama Mbunge ni kuisimamia Serikali hela za walipa kodi zije zifanye kazi kule, not to kneel down before the President ili uweze kuletewa mradi wa maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea, Chato bado, tumeona ujenzi wa traffic lights pale Chato, nikajiuliza hawa watu wanamuogopa Magufuli kwa nini wasimshauri vilivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini dhima kubwa ya hili, ukiangalia kuna miji mingi na ina high congestion ya magari leo mmeenda kujenga Chato na kuna picha niliona sitaki kuamini kama kweli ni ya kule lakini nilivyopita mimi Chato sikuona kama kuna congestion kubwa ya magari mnaweka traffic lights Chato, wanapita punda. Misuse of funds za walipa kodi wa Tanzania wakati tuna majengo ya shule hajajengwa, hospitali nyingi zinakosekana wamama wajawazito wanafariki hakuna huduma proper, mnaenda kujenga traffic lights za Chato. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo ndiyo the only way kwa kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda kama ingeenda vizuri, tungewekeza kwenye kilimo tungeweza kufikia hii ndoto ya Tanzania ya viwanda. Ukiangalia bajeti ya ruzuku ya mbolea na mbegu ya mwaka 2015/2016 tuliweza ku- allocate kwa kaya zaidi ya 900,000 lakini ukija 2016/2017 tume- allocate ruzuku ya mbolea na mbegu kwa kaya 370,000 tu. Leo tunasema tunaleta ukombozi kwa hawa Watanzania halafu wakilima wanataka kuuza mazao yao, mnawazuia badala ya kuwatafuta masoko. Mwaka 2015 kahawa Tarime ilikuwa inauzwa shilingi 2,000 kwa kilo leo ni shilingi 600 halafu tunasema nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpango na watu wako wanaokushauri naomba ukae uangalie vizuri ni jinsi gani tunaweza ku-move na haya ambayo tunakupa hapa kama Wabunge myafanyie kazi ili Tanzania tunayoitaka iweze kufikiwa. Nina imani kabisa kwa vivutio ambavyo Tanzania tumepewa, tungewekeza kwenye utalii kwa nchi hii tusingekuwa wategemezi tungeweza kujitosheleza kabisa. Tuna vivutio vingi vya kitalii ambavyo vingi havipatikani hata kwenye mataifa mengine lakini tume-underutilize, kwa nini? Ni kwa sababu priority zetu zinaenda kwa kinyume, we are thinking backward. Leo TTB ingepewa fedha za kutosha ingeweza kutangaza utalii wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungeweza kuiwezesha TTB kupitia Tourist Development Levy tukapeleka fedha nyingi ili sasa waweze kuvitangaza vivutio vyetu na kufanya wajibu wao kama inavyotakiwa. Leo unakuta TTB wakiomba fedha ili waweze kujiendesha wanapata chini ya asilimia 30, tunashindwa kuvitangaza vivutio vyetu. Ukiangalia tuna beaches nyingi sana, kuna nchi zingine zinajiendesha kwa vivutio vya utalii walivyonavyo ambavyo ni vichache ukilinganisha na Tanzania. Sisi Tanzania aliyeturoga nadhani alishafariki, tulishapewa laana ambayo haifutiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukae tujitafakari sisi kama Wabunge wa Bunge la Kumi na Moja tukiondoka tutakuwa tumeisaidia vipi nchi yetu. Ni wengi humu wanasafiri nchi mbalimbali ikiwemo Mawaziri, mnaposafiri huko mnajifunza nini ambacho mnakileta Tanzania ili tuweze kukitumia kuhakikisha kwamba nchi yetu ina-move? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Deni la Taifa. Nazungumzia deni la ndani, kuna wakandarasi ambao wanaidai Serikali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa sababu muda ni mchache mengi nitawakilisha kwa maandishi lakini kwa uchache huu niende kuzungumzia baadhi ya mambo kwenye Mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukirejea ukurasa wa 40 kipengele cha kwanza kabisa kimeainisha misingi na matarajio ya ukuaji wa uchumi. Kwenye kipengele cha kwanza kinasema kuendelea kuwepo kwa amani, usalama, utulivu na utengamano wa jamii ndani na pia nchi za jirani. Nafikiri hapa ingetakiwa ibadilishwe iandikwe kuimarishwa kwa amani, usalama, utulivu na mambo mengine kwa sababu sasa hivi ilivyo huwezi kusema kwamba Tanzania tuna usalama ilhali tukishuhudia wananchi wanatekwa, wanauawa, wengine viongozi wakubwa kabisa wanapigwa risasi nyumbani sehemu ambayo ni secured. Hatuwezi kusema kwamba tuna amani ilhali maisha ya Watanzania ni magumu sana. Wale wote ambao mfano wametolewa kwa vyeti fake na wale wengine wameambiwa ni darasa la saba hawajapewa pension, gratuity ya kuondoka leo useme kwamba kuna amani Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumeshuhudia na Mheshimiwa Msigwa ameomba Mwongozo hapa nchi jirani Kenya kwa yale ambayo yamejiri kwenye kuchomwa kwa vifaranga, ng’ombe kukamatwa na mambo mengine. Kwa hiyo, kipengele namba moja ukibadilishe kiseme, kutakuwepo na matarajio ya ukuaji wa uchumi iwapo kutaimarishwa amani, utulivu, usalama na mambo mengine lakini sio kwamba kuendelea kuwepo ilhali hivyo vitu hatuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine siku zote nasema hatuna uhalisia kwenye mipango yetu na bajeti ambazo tunazileta hapa. Tusipokuwa na uhalisia ni dhahiri hatutafika pale ambapo tunataka kufika kama nchi. Leo ukiangalia kwenye kitabu chako mwenyewe umeainisha bajeti ya maendeleo ya mwaka 2016/2017 ambayo ilikuwa ni shilingi trilioni 11.8 ilitekelezwa kwa asilimia 55 tu. Hii ya sasa hivi kwa quarter moja ya mwaka 2017/2018 imetekelezwa kwa asilimia 11, on average mpaka tunamaliza itakuwa asilimia 44 mpaka 50 au ikienda au ikienda zaidi tuseme 60. Sasa ikienda na trend hii ina maana tunapanga vitu bila kuangalia uhalisia, time frame, vipaumbele ni vipi, mwisho wa siku tunakuwa tunapoteza rasilimali za wananchi kukaa hapa tunajadili. Siku zote nashauri kwamba ni bora tuweke vitu ambavyo tunajua tutavifikia ndani ya muda kwa resources tulizonazo walau tunapokuwa tumekuja ku-discuss Mpango mnatuambia kwa mwaka uliopita tumeweza kufanya mambo ya maendeleo kwa asilimia 80 au hata 85, 90 sio kwa asilimia 44 au 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine na hiki naomba kabisa tuwe sober kwa nachoenda kukiongelea sasa hivi. Kwenye allocation ya kodi za wananchi, maana imechukua discussion nyingi hapa na watu wamekuwa na hisia tofauti.

Mimi natokea Kanda ya Ziwa lakini hili nalipinga na nalipinga with facts na sisi kama wawakilishi wa wananchi ambao tumetumwa hapa Bungeni tukalitafakari ili tuweze kuishauri Serikali vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunaambiwa ujenzi wa jengo la TRA Chato, ghorofa kubwa sana limejengwa kule. Leo tujiulize Chato kuna mzunguko gani mkubwa wa fedha, kuna biashara gani kubwa kule Chato mpaka twende tuwekeze ghorofa? Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya mapato gani kule Chato tukawekeze lile ghorofa la mamilioni ya kodi za Watanzania? Tutafakari kama Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni Uwanja wa Ndege wa Chato, kabisa. Mimi sipingi uwanja wa ndege kujengwa Chato lakini Uwanja wa Ndege wa Chato ulitakiwa kuwa ni chini ya kilometa moja ya run way.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo pamoja na kwamba kuna kukiukwa kwa Sheria ya Fedha za Umma ambayo tulipitisha hapa shilingi bilioni mbili, lakini naambiwa zimetumika zaidi ya shilingi bilioni 39, hiyo ni hoja lakini sio hoja kubwa sana kwangu, tujiulize sisi Watanzania na hawa ambao wanamshauri Rais…

T A A R I F A . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, inabidi nicheke kidogo. Wakati tunapitisha na kwenye kitabu chake cha Mpango wakati ule tunapitisha kwa ajili ya upembuzi yakinifu zile shilingi bilioni mbili walisema ule uwanja wa Chato unajengwa kwa ajili ya usafiri ndani ya Geita na mikoa jirani hawakusema otherwise.

TAARIFA . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu hajatoa taarifa ameuliza swali, nitamjibu kesho wakati wa kipindi cha maswali na majibu kama Waziri Kivuli wa eneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, point hapa ipo nimejibu kwamba wakati inakuwa allocated hapa ilikuwa ni uwanja kwa ajili ya usafiri ndani ya Geita na mikoa jirani. Hawakusema kwamba kwa ulinzi, usalama na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwa Mheshimiwa Jenista, ilikuwa ni shilingi bilioni mbili, ukiongeza shilingi bilioni 39 inakuwa ni shilingi bilioni 41, sijui ni sheria ipi hiyo? Pia reallocation yake tunataka tujue imekuwa reallocated kutoka kwenye kifungu kipi kuja kwenye hizo shilingi bilioni 39? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nimesema kwangu issue siyo sheria zaidi, lakini unaenda kuwekeza huo uwanja mkubwa pale Chato wa runway zaidi ya kilometa tatu ni ndege gani inaenda kutua pale kubwa hivyo? Hiyo ni misuse ya hela za walipa kodi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikajiuliza mara mbili, leo tunasema kwamba Serikali inahamia Dodoma, of which I support 100%; Makamu wa Rais anahamia Disemba, Mheshimiwa Rais tunaambiwa anahamia mwakani. Bunge la Kumi tulipitisha uwanja wa Msalato ujengwe mpaka leo haujajengwa, Rais akija hapa tunatarajia wakija wale Marais, like Trump akija hapa ana ndege ambayo ni Boeing 737 itatua hapa Dodoma au itaenda kutua Chato? Why don’t we rethink tukaja tukajenga kwenye uwanja wa Msalato maana itakuwa ni double cost kwa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wanakuja Marais ambao wanatumia ndege kubwa, Rais Magufuli anaondoka Dodoma kwenda kuwapokea Dar es Salaam maana haka ka-uwanja ka-Dodoma hakawezi kuwapokea. Kwa nini hizo hela tusingeweza kujenga hapa Msalato, kule Chato
tumjengee uwanja wa kuweza kutua ndege ya kawaida like Precision, Bombadier na ndege ya Serikali kuliko kujenga uwanja mkubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ndiyo hoja yangu kubwa au basi kama tunataka tuijenge Chato tungeweza kujenga hospitali kubwa kabisa ku-save maisha ya Watanzania kuliko ku-sink shilingi bilioni 39 kwenye uwanja ambao hautatumika au tungeweza kujenga Chuo Kikuu pale kama tunataka tuijenge ile Chato ikue vizuri, unlike tulivyofanya sasa hivi. (Makofi)

TAARIFA . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu yangu Mheshimiwa Innocent pale, mtani wangu, kwanza taarifa yake siipokei lakini pili, ngoja nimsamehe nilikuwa nampa dongo moja ila nimsamehe, niendelee kuchangia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Innocent nilimuona juzi wakati Rais amezuru kule, anapiga magoti kumuomba shilingi bilioni 30 za maji. Wajibu wako kama Mbunge ni kuisimamia Serikali hela za walipa kodi zije zifanye kazi kule, not to kneel down before the President ili uweze kuletewa mradi wa maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea, Chato bado, tumeona ujenzi wa traffic lights pale Chato, nikajiuliza hawa watu wanamuogopa Magufuli kwa nini wasimshauri vilivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini dhima kubwa ya hili, ukiangalia kuna miji mingi na ina high congestion ya magari leo mmeenda kujenga Chato na kuna picha niliona sitaki kuamini kama kweli ni ya kule lakini nilivyopita mimi Chato sikuona kama kuna congestion kubwa ya magari mnaweka traffic lights Chato, wanapita punda. Misuse of funds za walipa kodi wa Tanzania wakati tuna majengo ya shule hajajengwa, hospitali nyingi zinakosekana wamama wajawazito wanafariki hakuna huduma proper, mnaenda kujenga traffic lights za Chato. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo ndiyo the only way kwa kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda kama ingeenda vizuri, tungewekeza kwenye kilimo tungeweza kufikia hii ndoto ya Tanzania ya viwanda. Ukiangalia bajeti ya ruzuku ya mbolea na mbegu ya mwaka 2015/2016 tuliweza ku- allocate kwa kaya zaidi ya 900,000 lakini ukija 2016/2017 tume- allocate ruzuku ya mbolea na mbegu kwa kaya 370,000 tu. Leo tunasema tunaleta ukombozi kwa hawa Watanzania halafu wakilima wanataka kuuza mazao yao, mnawazuia badala ya kuwatafuta masoko. Mwaka 2015 kahawa Tarime ilikuwa inauzwa shilingi 2,000 kwa kilo leo ni shilingi 600 halafu tunasema nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpango na watu wako wanaokushauri naomba ukae uangalie vizuri ni jinsi gani tunaweza ku-move na haya ambayo tunakupa hapa kama Wabunge myafanyie kazi ili Tanzania tunayoitaka iweze kufikiwa. Nina imani kabisa kwa vivutio ambavyo Tanzania tumepewa, tungewekeza kwenye utalii kwa nchi hii tusingekuwa wategemezi tungeweza kujitosheleza kabisa. Tuna vivutio vingi vya kitalii ambavyo vingi havipatikani hata kwenye mataifa mengine lakini tume-underutilize, kwa nini? Ni kwa sababu priority zetu zinaenda kwa kinyume, we are thinking backward. Leo TTB ingepewa fedha za kutosha ingeweza kutangaza utalii wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungeweza kuiwezesha TTB kupitia Tourist Development Levy tukapeleka fedha nyingi ili sasa waweze kuvitangaza vivutio vyetu na kufanya wajibu wao kama inavyotakiwa. Leo unakuta TTB wakiomba fedha ili waweze kujiendesha wanapata chini ya asilimia 30, tunashindwa kuvitangaza vivutio vyetu. Ukiangalia tuna beaches nyingi sana, kuna nchi zingine zinajiendesha kwa vivutio vya utalii walivyonavyo ambavyo ni vichache ukilinganisha na Tanzania. Sisi Tanzania aliyeturoga nadhani alishafariki, tulishapewa laana ambayo haifutiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukae tujitafakari sisi kama Wabunge wa Bunge la Kumi na Moja tukiondoka tutakuwa tumeisaidia vipi nchi yetu. Ni wengi humu wanasafiri nchi mbalimbali ikiwemo Mawaziri, mnaposafiri huko mnajifunza nini ambacho mnakileta Tanzania ili tuweze kukitumia kuhakikisha kwamba nchi yetu ina-move? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Deni la Taifa. Nazungumzia deni la ndani, kuna wakandarasi ambao wanaidai Serikali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nakushukuru kwa kunipatia fursa hii kuweza kuchangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2016/2017.
Awali ya yote, nachukua fursa hii ya kipekee kabisa kuwashukuru wananchi wa Tarime Mjini, kwa mara ya kwanza tangu dunia iumbwe kuweza kuchagua mwanamke tena kutokea Chama cha Upinzani. Wameudhihirishia ulimwengu kwamba wamechagua mtu ambaye atawasemea na kuwatumikia na siyo jinsia. (Makofi)
Vilevile nawashukuru wananchi wa Mkoa wa Mara kwa kuonesha kwamba wana imani kubwa na UKAWA; na CHADEMA wote mtakumbuka kwamba Bunge ililopita alikuwepo Mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa, lakini sasa hivi tupo Wabunge wanne kutoka Mkoa wa Mara licha ya dhuluma nyingi nyingi, lakini nafikiri CCM mmeisoma namba kidogo kule. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa napenda kuchangia na nianze na utawala bora. Kwenye utawala bora, wakati wa uchaguzi yalijitokeza mambo mengi sana. Cha kusikitisha, hata Mheshimiwa Rais Magufuli alisema uchaguzi umeisha na mambo yameisha; lakini mpaka leo wale ambao wanaonekana walikuwa washabiki wa vyama vya upinzani, wameendelea kunyanyasika, wanakamatwa na wanabambikiwa kesi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naongelea hili nikizungumzia Jimbo langu la Tarime Mjini. Kuna wananchi wamebambikiwa kesi, wengine wamepewa murder case ya binadamu ambaye anaishi na ameenda akasema kabisa huyu mtu sijawahi kukosana naye na wala sijafa na nipo hai. Huyu anaitwa Charles Kitela Chacha na amepewa mashitaka ya murder mwenye PI No. 37/2015. Utawala bora uko wapi? Mtu ambaye wanasema ni Marehemu ameuawa anaitwa Wambura Ryoba Gucha, yupo hai wa Kijiji cha Turugeti, Tarime. Tunaomba muwe na utawala bora ili haki itendeke; na kama tutaenda kwenye demokrasia na uchaguzi muweze kupata haki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, Chama tawala kinasikitisha. Mnapoona wapinzani wameshinda, mnawawajibisha watendaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ninavyoongea, Tarime, Watendaji wanawajibishwa, walimu wanasumbuliwa, RPC amehamishwa, OCD amekuwa demoted kisa Mheshimiwa John Heche kashinda Tarime, Mheshimiwa Esther Matiko ameshinda Tarime; Halmashauri ya Mji wa Tarime upo CHADEMA; Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, upo CHADEMA. Utawala bora upo wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana hata watu wakisimama hapa wakaongea yanayotokea upande wa pili, nami nikipata muda baadaye nitazungumzia, mnabaki mnaona kwamba wanaongea ndivyo sivyo mjichunguze, mwitendee haki Tanzania. Tunataka amani, tusiimbe amani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine sasa nichangie kuhusu uchumi na viwanda. Tumekuwa tukishauri; Bunge lililopita nilikuwa Waziri Kivuli wa Mipango na kwa bahati nzuri sana ambaye ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Mpango alikuwa akituletea. Atakuwa ni shuhuda na amekidhihirisha hiki ambacho naenda kuongea kwamba mnapanga vitu bila uhalisia. Hiki kitu ambacho tunasema uchumi na viwanda hakiwezi kufanikiwa kama tunapanga vitu bila uhalisia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivyo? Tunajua kabisa ili tuweze kuwa na uchumi na viwanda ni lazima tuwe na barabara ili hata wale wazalishaji, wakulima waweze kusafirisha mazao yao na kufikisha kwenye viwanda. Lazima tuwe na reli imara, lazima tuwe na umeme, maji na vingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye barabara ukiangalia ukurasa wa 27 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mnatuambia kipengele cha pili ujenzi mpya wa barabara zenye urefu wa kilometa 5,427 na kukarabati barabara zenye urefu wa kilometa 1,055 kwa kiwango cha lami. Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mnaweza mkajenga kilometa 5,427 iwapo kwa miaka mitano mmetujengea kilometa 2,700.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna uhalisia gani? Ndani ya mwaka mtajenga Kilometa 5,400! Let’s be realistic! Ndiyo maana leo tutapoteza nguvu nyingi kuwashauri hapa; tutapoteza fedha nyingi za Watanzania, mnachokiandika hakioneshi uhalisia. Kwa hiyo, naomba kabisa, tuwe tunaonesha uhalisia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mmeainisha reli nyingi, nyingi! Mimi natokea Kanda ya Ziwa na ningependa kabisa reli ya kati iweze kukamilika ili tuweze kupunguza ajali. Siyo tu kukuza huu uchumi wa viwanda ambao mnasema; jana walisema hapa miundombinu ya barabara haichangii vifo, lakini kiuhalisia tunapoteza nguvu kazi ambazo tumezisomesha, wengine ni ndugu zetu ambao ni wajasiriamali wa kawaida, wanakufa barabarani kwa sababu ya barabara mbovu. Malori yanapita hapo hapo, ajali nyingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imarisheni reli ili tusafirishe kwa reli. Kwanza tunakuza uchumi lakini hatutapoteza Watanzania. Ninachokiona mmeainisha hapa, tutarudi hapa mwezi wa sita mwakani, mtaanza kusema hatukupata fedha na asilimia nyingi za maendeleo zilikuwa zinatoka kwa wahisani; na sijui sekta binafsi; tutaanza kuimba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bora mwandike mtajenga kilometa 300 za lami tutawaelewa, kuliko kutuandikia 5,400 halafu tunakuja hapa mwakani hamjafanya chochote. Tunapenda sana Watanzania tuwe na hiyo mnayosema uchumi wa viwanda; tunapenda kuona Watanzania wengi wakiwa kwenye uchumi wa kati na siyo wachache wapo juu, wachache ni masikini wa kutupwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuwe na uchumi wa viwanda nimeshataja. Kuhusu kilimo chetu; zaidi ya 70% Watanzania tunajishughulisha na kilimo, lakini kilimo ambacho hakina tija. Ile kauli mbiu ya kilimo kwanza tumeiimba, tumeicheza hakuna mafanikio. Mkisoma ripoti zenu zenyewe kuhusu kilimo inaainisha dhahiri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maji ni shida ingawa mmesema Mpango ulioisha umekamilisha kwa 68% vijijini na 95% mjini. Ndiyo maana nasema tuwe wakweli. Leo kule Tarime Mjini ukiyaona maji utafikiri ni ubuyu, tuje na uhalisia! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pensheni kwa wastaafu. Mwaka 2015 tulipitisha tukasema walipwe shilingi 100,000/=, lakini kuna watumishi tena Mapolisi ambao mnawatumia sana, wanalipwa shilingi 20,000/= mpaka leo. Sasa mlipokaa hapo mjiulize, hawa Watanzania wanaishi vipi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kampeni Mheshimiwa Magufuli alisema na hata kwenye Star TV mlikuwa mnarusha sana; ushuru wa kero kwa maana mboga mboga, matunda, mama ntilie na wengine wote mnaenda kuondoa. Leo Watanzania hawa wananyanyasika; na alisema pia mgambo watatafuta kazi nyingine. Mimi nasema mnisikilize na mwondoe wale mgambo kwenye Jimbo la Tarime Mjini. Watanzania wote, wamama, wababa, vijana wanaojitafutia wamachinga, mlisema ushuru mdogo mdogo mtaondoa. Tubuni vyanzo mbadala tusiwakamue hawa ambao wana kipato cha chini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu bure, mimi naomba mseme mmepunguza makali ya elimu, lakini siyo elimu bure.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu muda ni mchache, nimalizie kwa Zanzibar; ingawa watu walisimama hapa wakasema sisi wa Bara tusizungumzie ya Zanzibar. Kiukweli tujichunguze, kiuhalisia, tena nianze na Mheshimiwa King siku ile alisema kwamba maiti walipiga kura. Kama maiti walipiga kura, ajiulize na yeye huyo maiti alipiga kura tano. Yeye kama Mbunge wa Jamhuri amefuata nini hapa na yeye alipigiwa kura na maiti? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni sawa na kumwambia muislamu, umepika kitimoto, umechanganya na kuku, unamwambia achukue kuku, aache kitimoto, wakati ile supu yote imechanganyikana. Mmechambua kuku ambao ni wale Wabunge wa Jamhuri na Rais, mmeacha wale Wawakilishi kwamba ndio kitimoto. Jichunguzeni! Kama ni maiti alipiga kura, amepiga kote. Tutendee haki Watanzania wa Zanzibar, tusiingize nchi kwenye machafuko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ardhi. Mmeainisha mtapima ardhi, tunaomba mfanye hivyo. Ardhi imepimwa kwa 10% tu, kule Tarime Mjini tunahitaji mpime ardhi ili tupate thamani tuweze kukopa na kujishughulisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. Mheshimiwa Magufuli kwenye kampeni alisema atatoa shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji na Mtaa. Sijaona mmeainisha; naomba mwainishe, wananchi wa Tarime mimi nina Mitaa 81, ili tuanze kuzipata hizo shilingi milioni 50 kuanzia mwaka huu wa fedha, tuweze kunufaika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili na mimi niweze kutoa mchango wangu kwenye Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa.
Mheshimiwa Spika, naomba nianze kuchangia kwanza kwa kuangalia ni nini kimetekelezwa kwa Mpango wa Kwanza. Ukiangalia kiuhalisia Mpango wa Kwanza haujatekelezwa kwa asilimia 60 kama ambavyo mmeandika. Ni kwa nini nasema hivi? Mfano mdogo tu kwenye hotuba ya Waziri anatuambia kwamba maji vijijini yameenda kwa zaidi ya asilimia 72 kwamba wananchi wa vijijini zaidi ya milioni ishirini wamepata maji.
Mheshimiwa Spika, sasa mimi nikawa nauliza ni Tanzania ipi imepata maji safi na salama? Mkoa wa Mara, Wilaya ya Tarime, Mji wa Tarime siyo tu vijijini hata mjini hakuna maji. Ile Sera ya mwaka 2002 kwamba maji unapata ndani ya mita 400 ni ndoto. Kwa hiyo, kama takwimu zenyewe ndiyo hizi ni dhahiri mtakuja mtasema mmetimiza kwa asilimia 60 lakini kiuhalisia hakuna kitu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, leo mme-document hapa kwamba fedha za maendeleo sasa hivi zitakuwa zinaenda kwa asilimia 40 ya bajeti. Mkumbuke Mpango wa Kwanza tulisema asilimia 35, lakini mtu asimame aniambie kama Serikali hii na naomba sana msiwe mnasema Serikali ya safari hii ya Awamu ya Tano imedhamiria as if sasa hivi ni chama kingine, ni Chama hicho hicho cha Mapinduzi ndiyo mlikuwepo miaka yote…
MHE. ESTHER N. MATIKO: Msitake kutu-fake Watanzania mnakuja hapa mnasema ooh, sasa hivi tumedhamiria, nikiangalia cabinet iliyopo sasa hivi over sixty percent ni ile iliyokuwepo Awamu ya Nne. Mkumbuke kwamba hata Awamu ya Nne tulikuwa tukiongea hapa tukiwashauri, baba yangu Mheshimiwa Wasira alikuwa anakuja hapa anatubeza kwenye Mpango, nilikuwa Waziri Kivuli wa Mpango na bahati nzuri aliyekuwa kwenye Mpango ndiyo Waziri wa Fedha na Mpango sasa hivi. Halafu mkikaa mnasema sasa hivi hii Serikali ina dhamira ya dhati, come on, are you serious? Watu wale wale, chama kile kile tumekishauri, over sixty percent Mawaziri mliokuja madarakani ndiyo wale wale labda mmebadilishwa tu, ulikuwa Waziri wa Katiba na Sheria sasa hivi ni Waziri wa Afya, ulikuwa sijui wapi sasa hivi umeenda pale. (Kicheko)
Mheshimiwa Spika, sasa leo tukisema kwamba tulidhamiria kuimarisha miundombinu ya barabara ambayo ndiyo inaenda kuchochea uchumi wetu na mtu aka-document tukasema Rais, Mheshimiwa Magufuli ndiye aliyekuwa Waziri kipindi hicho na nakumbuka katika vitu ambavyo vilipewa kipaumbele ni ujenzi wa barabara, lakini ndiyo mmejenga kwa asilimia hamsini na tatu.
Mheshimiwa Spika, hivyo ambazo hatukuvipa kipaumbele sana asilimia 20, asilimia sijui ngapi! Asilimia tatu! Halafu tunaishia kuwa na mipango. Kwanza nilikuwa najiuliza, kuanzia jana na-postpone tu. Maana yake nasema nachangaia nini? Tunatoa ushauri, tunasema but nothing is going to be done. Tunachangia nini?
Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, naomba sana, tukisimama tuwe kama Wabunge, acha Mawaziri watakuja watajibu kama Serikali. Nashangaa Mbunge anasimama anatetea kweli! Kaka yangu wa Mkuranga, documents za Kambi ya Upinzani, tulicho-document kimetokana na alichokiandika Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Spika, sasa ukianza kusema, nikasema anajidai aah, sijui zimeongezeka 500. Ongeza hizo 500, zinakuwa ni 3000. Sasa 3000 kwa miaka mitano, leo unazitekeleza vipi?
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, taarifa!
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naomba nishauri na naomba...
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, taarifa!
SPIKA: Taarifa iko upande gani?
MBUNGE FULANI: CCM.
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Kulia kwako.
SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Mabula....
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, kwa heshima zote kabisa mdogo wangu katika hili Bunge, hajitambui. Ikumbukwe CCM ikichukua takwimu za Urais wanapataje, imeanzia 81% imeshuka mpaka Mheshimiwa Magufuli amepata 58%, tena questionable! Questionable! (Kicheko/Makofi)
Kingine, huyo huyo wakati Uenyekiti unabadilishwa badilishwa, wakati Mheshimiwa Mnyika anasema kwamba ule uongozi wa Mheshimiwa wa Kikwete ni dhaifu, ninyi mlisimama na kusema na kufedhehesha kila kitu! Leo yaani mnajikosoa ndani yenu wenyewe. Tunafurahi sana na wananchi wanawaona na wanasikia kwamba hamfai! Niendelee! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niendelee kwenye nishati ambacho ni kichochezi kwenye viwanda. Mpango uliopita, yaani mlikuwa mmedhamiria mnaleta Megawatt 2,780, lakini mpaka tunavyoongea miaka mitano ni Megawatt 496 tu. Hivi viwanda tunavyoongea tunaenda kuvipataje, kama nishati yenyewe bado ni goigoi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, leo kule kwetu Tarime ni wakulima na wafugaji. Tunahitaji hata viwanda, tuwe na umeme. Kwa mwendo huu, tutafikaje? Halafu tukiishauri Serikali hapa kwamba tuwe na vitu ambayo tukiviongea vina tija, watu wanaweka… nyie Wabunge, mmekuja kama Wabunge, wajibikeni kama Wabunge, acha Mawaziri watende. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, yaani kiuhalisia nikipitia sekta zote, kwenye elimu ndiyo kabisa! Siku ile Mheshimiwa Rais alisema hapa kwamba viwanda ambavyo anadhamiria na ambavyo vitaajiri Watanzania, vitatumia nguvu kazi zaidi kuliko teknolojia ya kisasa. Kwenye Mpango, matarajio yetu kwenye VETA tu hayajafikiwa kwa kiwango kikubwa sana. Sasa leo tuseme tuna Mpango mkakati upi ili uweze kutuaminisha kwamba hii dhamira ya dhati tuliyonayo tutafikia? Mimi mwenyewe natamani sana Tanzania tuweze kukua kiuchumi, wananchi wengi hawana ajira. Tuna rasilimali nyingi, lakini zilikuwa zinakumbatiwa tu na wachache huko, zinatumika vibaya.
Mheshimiwa Spika, sasa kama kweli hiyo awamu ya tano ina dhamira ya dhati na kwa sababu bajeti hii tunaenda kuongea mambo mengi Wizara mbalimbali, tutaenda kuipima kama ina dhamira ya dhati. Kweli kama ina dhamira ya dhati ya kuwasadia Watanzania, Mheshimiwa Waziri tunaomba hayo uliyoyaandika utuainishie kwamba tunamaanisha. Asilimia 40 zinaenda kwenye maendeleo, tumejizatiti vipi kwenye kodi?
Mheshimiwa Spika, mwaka 2015 wakati nachangia bajeti hapa nilimweleza mfano tu, Mama Sada. Nenda hapa kwenye supermarket moja Dodoma, umenunua vitu, hakupi ile risiti ya TRA, akaenda, akafuatilia akapata.
Mheshimiwa Spika, hawa Usalama wa Taifa, leo ukinunua vitu hawakupi risiti za TRA. Juzi tu nimenunua kitu Kariakoo Sh. 620,000/= nikawaambia wanipe risiti ya TRA, ooh, risiti ya TRA tukikupa inaenda zaidi ya hapo. Sasa si hii ndiyo bei umeweka kwenye duka lako? Ndiyo! Unajua aliniambia basi naomba nikupe sh. 100,000/= halafu sh. 520,000/= nikuandikie ya kawaida.
Mheshimiwa Spika, Usalama wa Taifa, ninyi kama Wizara mnadhibiti vipi hilo? Tunapoteza mapato mengi sana. Hii mnayosema sijui risiti za electronic, hazifanyi kazi, wanaziweka kando. Mtanzania akienda, anamwambia nitakupa hiki, fanya punguza, shell, yaani kote tunapoteza mapato and then mnakuja tu mme-document ma-paper; tupe sign mnakusanya vipi kodi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, haitoshi tu Mheshimiwa Rais kusimama kwenye TV, Tanzania lipa kodi. Mmeweka mechanism gani kuendeleza hii ya Mheshimiwa Rais anayosema kila siku kwenye TV kwamba kodi itakusanywa kweli? Wekeni watu waende kwenye maduka! Ajidai kama ananunua kifaa, aone kama atapewa hiyo risiti au atapewa lugha gani? Kamata, fanya vyote nchi nzima, watu walipe kodi, siyo kuwanyanyasa watu wadogo wadogo, wajasiriamali wenye vimbogamboga, wenye miradi midogo midogo ndio wanaoleta fedha kwa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilisema mwaka 2015 kwamba, worthiness ya mtu i-reflect ulipaji wa kodi yake. Sijui hata wamefanya nini? Mnatangaza watu wawe na TIN, sijui kila mtu awe na TIN: Je, kweli kila Mtanzania ana-TIN? Mimi kwa mfano, Esther Matiko, worthiness yangu ina-reflect nalipa kodi vipi? Do you trace that? Kama hamtaweza kukusanya mapato ya ndani na wafadhili wenyewe ndiyo hivyo, hii mipango, miaka mitano tunakuja hapa, patupu! Tena leo bora tunaambiwa zimepikwapikwa ziko asilimia 60. Tukija mwaka 2019 hapa tunaelekea 2020 tutaambiwa story zile zile.
Mheshimiwa Spika, nimalizie. Tuwe na nishati, tuboreshe miundombinu ya barabara kama mnataka hivi viwanda kuanzia kule kwa mkulima, barabara zipitike. Tuboreshe reli.
Mheshimiwa Spika, ukija kwenye Air Tanzania, aibu! National Carrier, aibu! Ukisafiri, ukaenda na hizi ndege, ukifika Nairobi, wanashuka watalii wote mnakuja Tanzania wachache. Wakishafika pale, ina maana zile hoteli za Kenya ndio wanafaidika. Wanaletwa na magari kuja kwenye mbuga zetu za Tanzania. Hata juzi niliona wanasema, hata daraja la Kigamboni ambalo mmelizindua jana, watasema liko Kenya. Mlima Kilimanjaro Kenya, mengine yote Kenya. We are not branding our Nation. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Samatta ni mchezaji sijui wa wapi huko, what are we doing? Tuwe serious! Tutafute vyanzo ambavyo vinatuletea mapato. Sekta ya Utalii, let„s have our National Career. Hatuna National Career! Ni wafanyakazi tu wamebaki na jengo pale city center tena ambalo lipo kwenye prime area, mliendeleze basi! Tunabaki tu na vijistori, tutaleta, tutaleta. (Kicheko)
Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa Jimbo langu la Tarime. Kwanza kabisa, naomba kabisa kipekee nimshukuru Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Najua kama wanavyojinafasi humu ndani, mkijivua kweli, ile ambayo tumekuwa tukiwashauri miaka yote, mnasema kelele za chura hazimnini sijui nini; sasa kweli mkiamua kufanya hivyo, siyo kama maigizo kwa sababu mnaona Mheshimiwa Magufuli anavyofanya, mtafika mbali.
Mheshimiwa Spika, ndugu yangu pale huwa anavaa zile scarf za Kitanzania na nini, kweli yule ni mzalendo sana. Amekuja Tarime, ameongea mambo mengi sana na Wanatarime.
Kama kweli hiyo dhamira itaenda kutendeka kama ni ya Serikali hii, rasilimali tulizonazo zikageuzwa kuwasaidia Watanzania, maana yake tumekuwa tukiongea, pale kuna Soko la Kimataifa, tumekuwa tukipiga kelele humu mimi na Mheshimiwa Nyambari, limechukua miaka mingi kumalizika, liko Lemagu; lile soko lingemalizika, ingekuwa ni kipato kikubwa sana kwa nchi yetu. Liko border pale! Mnachukua muda mwingi sana kumaliza lile soko. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wenzetu Kenya wanachukua hiyo opportunity, ukienda upande wa pili wa Kenya ni tofauti kabisa na Tanzania. Lile soko likikamilika, ule mnada ukafunguliwa, kipato ndani ya Mji wa Tarime, kipato ndani ya Wilaya ya Tarime kitaongezeka na Taifa linaenda kupata fedha ambazo leo zitatumika kusaidia hayo madawati na kujenga Maboma. Maana yake mmesema elimu bure, kule kwetu hakuna vipato. Havipo Tarime Mjini! Sasa mnahangaisha watu kujikusanya maskini wale wajenge viboma; watoto wanasoma 200 kwenye darasa moja. tupeni lile soko lifunguliwe, mnada ufunguliwe, kipato kiongezeke.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kipekee kabisa namshukuru ndugu yangu, kaka yangu pale, naomba na Mawaziri wengine, mmepewa ridhaa na Watanzania, mnatumikia nchi. Maana kuna mwingine nilisikia ooh, pale sijui CHADEMA, sijui CUF hatupeleki maendeleo. What?
Mheshimiwa Spika, hizi rasilimali ni za kwetu wote. Wale Watanzania wote wametuweka wote madarakani. Ninyi mmepewa ridhaa ya nchi, kuna wengine wamepewa ridhaa za Majimbo na Halmashauri. Tunatakiwa tuwatumikie wote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Nafikiri ushauri wangu mkiuzingatia, vichochezi vya kuanzisha viwanda, viwepo; nishati, miundombinu ya barabara na kilimo mkiboreshe, Sekta ya Elimu ili tuweze kupata hao watu ambao tunasema tunaenda kuwatumia, reli na usafiri wa anga. Ndoto ya Waziri wa Fedha na hii Mipango mnayotuletea, itatimia. Kinyume cha hapo, tutakuwa tunacheza vidogoli tu siku zote. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kwa ufupi tu kuhusiana na maombi yangu ya kupandisha hadhi Chuo cha Maendeleo ya Jamii (FDC) kilichopo Tarime Mjini kuwa VETA. Chuo hiki kwa sasa kinatoa huduma kwa wananchi wa Tarime nzima Rorya na Serengeti. Hivyo ili kuendana na azma ya Serikali ya Tanzania ya viwanda ni lazima vyuo vya ufundi viwe vingi. Tumekuwa tukiomba chuo hiki kuwa cha ufundi ili tuweze kukidhi hitaji la muda mrefu wa kuwa na chuo cha ufundi, tutashukuru sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni wimbi kubwa la walimu toka Kenya wanakuja kufundisha shule binafsi za Tarime. Hiyo tunaomba Wizara iingilie kati maana tunao Walimu wa kutosha kuweza kuajiriwa, hivyo vibali vinatolewaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, uboreshaji wa elimu kuanzia sera za elimu, mitaala yetu pamoja na miundombinu yetu, inatoa taswira pana ya nini tufanye kama Taifa kwa ufupi tu. Tarime tumejenga Maabara hatuna vifaa wala wataalam wa maabara, tuna uhaba wa Walimu wa Sayansi na ndiyo maana watoto wanafeli. Tusiangalie Quantity tuangalie Quality. if we need to have quality education then input lazima ziwe effective. Madaftari, vitabu, madawa, madawati, walimu wenye motivation, nyumba za walimu na posho ya ziada, posho ya pango, posho ya safari na usafiri, kupandishwa madaraja, chakula mashuleni, ukaguzi wa shule zetu na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi ni hayo, mengi yamechangiwa naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia hoja hii katika kuonesha ni jinsi gani sanaa na michezo inaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa. Leo hii Taifa lingehakikisha tuna viwanja vya kutosha kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mikoa na vyote ni vya kisasa, si tungekuza soka na michezo mingine kama ridhaa, basketball, volleyball, netball na mingine mingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, enzi zetu wakati tunasoma, michezo ilikuwa na hamasa na shule zote za msingi na sekondari zilikuwa na viwanja vya kutosha. Michezo mbalimbali ilikuwa ikichezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ni wakati sasa viwanja ambavyo vinahodhiwa na CCM virudi kwa Serikali ili viendelezwe na kuweza kuleta tija. Ni muhimu kwa sababu hivi vilijengwa enzi ya chama kimoja ambapo ni fedha za Watanzania zilitumika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kuiomba Serikali angalau watusaidie kuboresha uwanja wa Wilaya Tarime ambao upo pale Tarime Mjini, kwani umetelekezwa na kubaki kutumika kwenye mikutano ya hadhara badala ya michezo husika. Uwanja una sifa zote za kuweza kuchezwa ligi za daraja la kwanza na ukiboreshwa utasaidia sana kukuza uchumi. Hivyo, natoa rai yangu kwamba Serikali ishirikiane na Halmashauri ya Mji wa Tarime ambayo tayari wameshatenga fedha kiasi kidogo kwa ajili ya uboreshaji wa uwanja wa Serengeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni dhamira ya Halmashauri ya Mji wa Tarime kujenga shule ya michezo kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini. Hivyo tumeomba Serikali ione umuhimu wa sports accessory ziweze kuwepo nchi nzima na kwa wale walio tayari kama Tarime Mjini wapewe vipaumbele. Bila shule za michezo huwezi kukuza vipaji kuanzia shule za msingi hadi sekondari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, tuwekeze kwenye sanaa na wasanii wa kuigiza na kuimba nyimbo ambazo zitakuwa na tija kwao. Mfano, wanamuziki wetu wana vipaji vizuri sana lakini uhalisia wa maisha yao hayaakisi kipato ambacho Watanzania wengine wanavyopata nje ya nchi ni nyingi tofauti na wanazopata hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri tuwekeze kwenye tamaduni zetu ambazo zinaweza kuwa pia kumbukumbu ya tamaduni zetu. Siku hizi tamaduni zinapotea kabisa; ngoma za jadi zinapotea na mambo mengine ambayo yangekuwa kivutio kwa Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi naomba majibu, ni jinsi gani Serikali imejipanga katika hoja hii na nyingine?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuweza kunipa na mimi fursa hii niweze kuchangia kwenye bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Utawala Bora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia maeneo kadhaa kwa sababu dakika 10 ni chache sana. Nianze na suala zima la utawala bora na utawala bora wenyewe nitaanzia suala la kuwanyima fursa Watanzania kuweza kuona ni nini wawakilishi wao wanafanya Bungeni. Ni dhahiri kwamba tumesikiliza michango mingi sana na mingine kwa kweli inasikitisha, ukimwona Mbunge anasimama, anaunga mkono hoja hii dhalimu ya kupoka haki ya uhuru wa wananchi kuweza kujua wawakilishi wao wanafanya nini then unatakiwa ujiulize mara mbili mbili kwamba hata hao wananchi waliomleta huyu mwakilishi huku walifanya makosa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilisikitishwa na Mheshimiwa kijana kabisa Halima Bulembo, anasema tukionekana kwenye televisioni ni kwamba tunatafuta umaarufu. Nikasema labda nitembee kwenye hoja yake hiyo hiyo nimuelimishe kidogo huyu mdogo wangu. Akumbuke kwamba sisi wengine tuliweza kupata morale ya kutaka kuingia kwenye siasa baada ya kuwaona wanawake wenzetu akina Mama Abdallah, Anna Kilango, Halima Mdee na wengine na hata ukiwaona watu waliogombea Udiwani na Wenyeviti wa Mitaa wanapata inspiration wanapomwona Esther Matiko anachangia nini, fulani anachangia nini, wanaona kwamba hata sisi wanawake kumbe tunaweza tukiingia kwenye uwanda huu wa siasa. Sasa leo mwanamke kabisa anapiga vigelegele hiyo fifty fifty mnafika vipi? Yaani mnaungana na wanaume ambao wanaona hii ni njia pekee ya kuwakandamiza ninyi msifikie lengo lenu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wengine tuna malengo makubwa, kuna Mheshimiwa mwingine alichangia kaka yangu Chegeni anasema kwamba twende tukafanye kazi Jimboni. Mimi lengo langu siyo kulitumikia Jimbo la Tarime tu kuna siku nataka niwe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, ninachokiwakilisha hapa nataka Tanzania nzima itambue Esther Matiko anafanya nini kwa Taifa lake wala siyo Tarime tu.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Kwa hiyo, kama ninyi mna short vision ya Jimbo tu na mnaamua kuwanyima Watanzania haki zao, jitafakarini mara mbili na mkienda pale mnaapa kuitumikia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halafu mnaikiuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani alisema na Wabunge wengine wamechangia mkubali, msikubali suala hili liko wazi na nitaomba mpitie hii Katiba, tulipokuja tulipewa kibegi kina hivi vitu vyote msiende kuweka ndani ya uvungu pitieni hii Katiba. Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Fedha na wengine waliochangia juzi hapa mlikuja mkapotosha lakini ni dhahiri Rais hawezi kuhamisha fungu moja kwenda lingine bila idhini ya Bunge tunaopitisha hapa, Mwenyekiti wewe ni Mwanasheria unajua, ni Mfuko wa Dharura tu. Kasomeni vizuri kuanzia Ibara ya 135 mpaka 140, kama hamna Katiba nitawatolea copy niwape ili tuweze kumshauri Rais asivunje Katiba na sheria yetu ya nchi. Inawezekana kabisa Rais ana lengo zuri aje sasa watuletee statement ya reallocation tuipitishe, mwenye mamlaka hayo ni Waziri au ndiyo hiyo tunasema kwamba hamna instrument kwa hiyo Rais inapoka mamlaka ya Waziri wa Fedha na kufanya anachokifanya ninyi mnapiga makofi, haikubaliki! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie sasa, TAMISEMI na nachangia kwenye Jimbo langu, nimechangia Kitaifa narudi sasa kwenye Jimbo langu.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu bure ni sawa sawa na mgonjwa yuko ICU. Kuna siku nilisema tuseme tumepeleka unafuu kwa wananchi, tusiseme elimu bure. Kwa sababu leo utasema elimu bure lakini Serikali Kuu mnasema Halmashauri ndiyo ijenge maboma, ihangaike kupata madawati lakini hazina uwezo. Kwa mfano kwangu Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI pitia uone, kadri tunavyozidi kwenda mbele Halmshauri ya Mji wa Tarime kwa mwaka huu unaomalizika makusanyo ni shilingi milioni 300. Leo Halmashauri hiyo ijenge maboma ya shule za msingi za Tarime, ipeleke madawati na afanye na mambo mengine kwa fedha zipi? Walau mlitoa Waraka Na.5 wananchi walikuwa wameshaanza kujitolea mara tena Rais Magufuli akasema usichange labda upate kibali, wameacha, watoto wetu wanakosa mahali pa kusomea. Kama mnataka kutoa elimu bure jipangeni tunahitaji madarasa ya kutosha watoto wa Kitanzania wasome. Leo ukienda Tarime watoto zaidi ya 200 kwenye darasa, madarasa yenyewe hayapo. Walimu wanakaa kwenye miti, Tarime Mjini pale ofisi inatazamana na ofisi ya Chama cha Mapinduzi, walimu ofisi zao ni miti. Halafu mnakuja mnasema elimu ni bure. Mheshimiwa Cecilia Paresso hapa kasema do you have seven hundred billions kuweza kufanya elimu bure i-take off. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema hamna madawati, hamna madarasa, Sera ya Elimu inasema walau watoto 45 kwa darasa moja wanakaa zaidi ya 200. Walimu wenyewe hawawi-motivated, hawana nyumba, umesema umejenga nyumba 183; sijui 188 kwa sekondari, mimi najiuliza mwalimu apange mjini, achukue sijui ni pikipiki au gari aende kufundisha Kenyamanyori hiyo fedha ni ya kwake kwenye kamshahara kale unakompa hana motivation allowance yoyote ile halafu mtasema elimu bure inaenda kuwa elimu ambayo haina manufaa yaani bora amefika la saba au la kumi na mbili lakini anarudi kitaa hajapata elimu bora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili mtu afanye kazi vizuri lazima walau ufanye akili yake itulie yake, mwalimu anayekwenda kumfundisha mwanafunzi ni lazima awe ametuliza akili. Mwalimu hana nyumba na wenye vinyumba vyenyewe wakikaa wananyeshewa nilisema mwaka jana hapa, shule ya sekondari nyumba zao zinavuja wanahamisha vigodoro huku na huku halafu leo useme kwamba watoto wale wa maskini watafundishwa waelewe, hata siku moja. Tuwe na vitabu vya kutosha, tuwe na madawati, tuwe na madarasa ya kuweza kuhakikisha wanafunzi wanakaa walau 45 ili mimi mwalimu ninavyofundisha waweze kunielewa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye afya. Sera ya Afya inasema walau kila kijiji au mtaa wawe na zahanati, mmeonyesha mna zahanati 4,500 tangu uhuru mpaka sasa hivi bado kuna upungufu wa zahanati 8,043. Vituo vya afya mnavyo 488 upungufu wa 3,506 na mnajua Maazimio ya Abuja walau asilimia 15 ya bajeti ya Serikali iende kwenye afya tumekuwa tukiimba, you don’t do that. Leo mnasema mnaboresha afya, kama imewachukua miaka 50 tuna vituo vya afya 484 itatuchukuwa zaidi ya miaka 350 kutimiza hivi vituo vya afya vinavyohitajika, watu wetu wanakufa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano kwa Tarime kuna Zahanati ya Gamasara ambayo iko Kata ya Nyandoto inahudumia wananchi wa Kata ya Nyandoto kama kituo cha afya wakati ni zahanati, inahudumia wananchi wa kijiji cha Kongo na Ketere hiyo ni Wilaya ya Rorya na inahudumia wananchi wa Kewamamba na Nyagisya hiyo ni Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Jimbo la Vijijini). Zamani walau mlikuwa mnapeleka shilingi milioni nne kwenye Halmashauri ya Mji leo mnapeleka shilingi166,000 baada ya miezi mitatu, hawa Watanzania tunawapenda au tunachezea afya zao? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nije tena kwenye Hospitali ya Mji ambayo mliishusha hadhi kutoka Hospitali ya Wilaya mkaifanya Hospitali ya Mji na niliuza swali hapa nikasema ilitakiwa iwe Hospitali ya Rufaa maana inasaidia wananchi wa Rorya, Serengeti na Tarime kwa ujumla siyo mji tu, mnapeleka ruzuku ya shilingi milioni 51 halafu Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mnapeleka shilingi milioni 91 wakati mkijua kabisa kwamba ile Hospitali ya Mji iliyoko mjini inahudumia huko kote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, shilingi milioni 51 iweze kutibu Wilaya nzima maana kiuhalisia haitibu wananchi wa Mji wa Tarime tu. Ndiyo maana nasema hivi mna watendaji na watu wenu wanafanya kazi ku-check uhalisia? Halmashauri ya Wilaya ya Tarime haina hospitali, wanakuja kutibiwa kwenye Halmashauri ya Mji wa Tarime, kwa nini mnaweka allocation za kitoto namna hii? Mnachezea afya za Watanzania, tunaendelea kushuhudia wananchi wakifa, waoneeni huruma. Nipeni mwanga maana sioni na mniongezee dakika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo. Halmahsuri ya Mji wa Tarime tuna Mogabiri Extension Farm...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Nitachangia siku nyingine kwenye Wizara zingine, nina nondo nyingi sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuweza kunipatia fursa hii kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana ya Nishati na Madini.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kwamba Wizara hii ndiyo imeshikilia uchumi wa Tanzania, tukisema Tanzania ya viwanda ina maana Wizara hii ndiyo inatakiwa ifanye vema. Tukienda hata kwenye sekta ya afya, tumeshuhudia mikoani hasa katika Wilaya ya Tarime kwenye vituo vya afya ambavyo vipo kando kando ya mji wanawake wakienda kujifungua vituo hivi vinatumia tochi kuwazalisha wanawake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunategemea kwamba Wizara hii iweze kweli kuonesha kama ilivyosema kwenye hotuba yake kwamba asilimia zaidi 98 zimekwenda kwenye fedha za maendeleo na nje ya hizo 98 ambazo ni trilioni 1.54; trilioni 1.32 zinaenda kwenye nishati. Kwa hiyo, ni matumaini yangu kwamba itaenda kuwatendea haki Watanzania kwa kuwapatia nishati mbadala. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niende sasa kwenye madini; Halmashauri ya Mji wa Tarime au Wilaya ya Tarime imebarikiwa kuwa na madini pamoja na kwamba Profesa alisema dhahabu siyo kitu siku hizi, lakini bado tunaithamini dhahabu na tukiitumia vizuri inaweza ikatusaidia sana kukuza uchumi wa nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Tarime ina migodi midogo midogo ya Nyabori, Kebaga na Buguti. Hii migodi ya Kebaga, Nyabori na Buguti; mgodi wa Buguti bado ulikuwa na leseni ya Acacia ambao walisema inakwisha Disemba. Kwa hiyo, natumaini kwamba kama itakuwa imekwisha basi watapewa wachimbaji wadogo wadogo ambao tayari wapo field.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata mwanzoni mwa mwaka huu nilimwambia Profesa wakati ameweka ziara ya Tarime atembelee ule mgodi nafikiri nafasi haikumtosha. Hao wachimbaji wadogo wadogo wanapata changamoto nyingi sana na tukirejea Sera ya Wachimbaji Wadogo ya 2009 ambayo ilielekeza kwamba waweze kupatiwa mitaji kwa maana ya ruzuku ambayo wameonesha kwamba wanaitoa lakini ruzuku hizi ambazo wanazitoa hazifuati utaratibu au utaratibu wake ni mbovu.
Mheshimiwa Naibu Spika, walengwa siyo wale wachimbaji wadogo wadogo, wale ambao tunawa-target bali ni wajanja baadhi wanakuja wanajivisha umbrella ya wachimbaji wadogo wadogo, wana-benefit kwa hizi fedha na wale ambao ni targeted group hawapati. Kwa hiyo, ningependa sana utaratibu huu uweze kufuatiliwa vizuri, waweze kupata wale Watanzania ambao kweli ni wachimbaji wadogo wadogo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine tuna GST kwa maana ya Geological Survey of Tanzania (Mawakala wa Jiolojia) hawaendi kuhakikisha wanasaidiana na hawa wachimbaji wadogo wadogo kujua kwamba sehemu fulani kuna madini. Kwa mfano, sasa hivi wachimbaji wa Buguti na Nyabori ambao nimewaainisha hapa wanachimba kwa kubahatisha; kwanza wanatumia vifaa duni, wanatumia nguvu zaidi kuliko teknolojia ya kisasa; lakini wakifika chini wanakuta hakuna madini wanahama tena wanakwenda kwenye shimo lingine hivyo hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa hii GST ijielekeze kule iwasaidie hawa wachimbaji wadogo wadogo waweze kujua bayana kwamba nikichimba hapa nitakwenda kukutana na madini. Ukizingatia kwa mfano Buguti water table ipo juu sana, wanatumia vifaa duni, kutafuta jenereta na kuanza kutoa maji na kuchimba na hakuna umeme maeneo hayo yote ambayo nimeyaainisha, zile Kata hazina umeme kabisa. Hao wachimbaji kwanza hawajaweza ku-benefit na hiyo ruzuku wanajikongoja kwa kuchangishana vikundi vile, lakini wakichimba bado hawawezi kupata kinachostahili.
Mheshimiwa Naibu Spika, natambua kwamba huwa kuna Wakaguzi wa Madini ambao wanakagua teknolojia ya uchimbaji. Hawa watu hawawafikii hawa wachimbaji wadogo wadogo kwa kiasi kikubwa. Kwa hiyo, unakuta hawa wachimbaji hawapati ushauri mbadala kutoka kwa hawa wataalam wetu. Ningependa kuelekeza Wizara hii kama tumeamua kuwasaidia hawa wachimbaji wadogo wadogo tuhakikishe kwamba tunawafikia, tunashauriana nao, ikiwezekana tunawapatia elimu mbadala na tunawapatia na vifaa ili waweze kuchimba kwa teknolojia ya kisasa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kinachosikitisha zaidi kupitia uchimbaji mdogo mdogo ule uchenjuaji wa madini mineral processing mnaita, unakuta wanachukua yale madini, wanatia mercury ili kuweza ku-process na kupata ile dhahabu yenyewe; hii inawaua Watanzania kidogo kidogo, leo hata ukienda kwenye haya maeneo ya dhahabu au madini , utakuta kuna watu vipofu, maana yake haya madini yakiingia kwenye damu yana affect zile chromosome macho yataharibika. Unakuta watoto wanazaliwa wana vichwa vidogo, unakuta wengine ngozi zao ukiziona hazitamalaki. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika huu uchimbaji mdogo mdogo tusipowekeza vizuri, tukawapa kinu cha kufanya direct smelting mwisho wa siku tunawaua hawa Watanzania, baada ya muda mchache Watanzania wengi wanakufa kwa sababu wanatumia zile mercury. Leo ukienda Buguti, ukienda Kebaga, ukienda Nyabori unawakuta akinamama wengine hata ni wajawazito wanashika shika ile mercury, inawapa direct effect kwa kiumbe aliyepo tumboni ,lakini na yeye mwenyewe after five, ten years wanafariki dunia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, fanya research kwa wote nenda Geita, nenda Nyamongo, njoo kwenye hii migodi midogo midogo pale na Profesa unajua mercury effect yake, lakini wanatumia. Hivyo basi tuwawezeshe, tuwape modern instruments za kufanya hiyo process ya madini wasitumie mikono yao moja kwa moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Nyamongo kabla sijakwenda kwenye nishati. Nyamongo kwa kweli na naongea hii kama natokea Tarime, tumekuwa tukiongea huku kwa muda mrefu sana ule mgodi siyo neema kwa watu wa Tarime bali ni majonzi kwa watu wa Tarime na hata Watanzania wengine ambao wanafanya shughuli zao pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kwamba ukienda nchi za wengine kama kuna migodi ni neema, hivi leo kweli ukija Tarime huwezi ukaona reflection kwamba kuna mgodi ambao unatoa dhahabu ya kutosha kilometa kadhaa kutoka Tarime Mjini, hatuna barabara za lami, wamejitahidi ndani ya ile Kata ya Matongo pale ndiyo kuna shule wamejenga na kile kituo cha sungusungu, lakini hata ukienda hospitali ile ya mji ambayo mnaisema ambayo ndiyo inatoa huduma hata kwa asilimia kubwa kwa Wilaya nzima ya Tarime haioneshi uhalisia kwamba kuna mgodi upo kwenye hii Wilaya ya Tarime.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukiangalia huduma za jamii maji walikuwa wanatoa kwa kupeleka ile buldoza lidumu la maji lile, ina maana hawajawachimbia kuhakikishia kwamba wanawapa maji ambayo yapo salama. Kwa hiyo naomba sana kikubwa mwaka 2011 baada ya watu zaidi ya sita kuuawa Nyamongo aliyekuwa Waziri wa Nishati Mheshimiwa Ngeleja, Mama Nagu Mheshimiwa Waziri wa Uwekezaji na Mheshimiwa Wasira walikuja Nyamongo wakawaahidi wale Watanzania kwamba watawapa maeneo mbadala ya kuchimba.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile wakaongea na mgodi na wakawaahidi kwamba watachukua yale mawe wawe wanakuja kuwamwagia kwenye maeneo yao, maana wakienda kuokota mawe mnawapiga risasi. Wameshindwa kutimiza yale ambayo waliahidi, kwa sababu naamini Wizara hiyo ni institution hata kama ametoka yule Waziri amekuja mwingine, mnabukua ma-file mnaona mliahidi nini kwa wale Watanzania mkawatimizie. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee suala la nishati; Jimbo la Tarime Mjini au Wilaya ya Tarime kwa asilimia zaidi ya 70 wananchi wake hawana umeme. Leo tunavyoongea Mheshimiwa Profesa Muhongo, tumeshaleta mapendekezo yetu kupitia REA l pia na hizo njia nyingine za kuweka umeme kwa hawa Watanzania. Kama tunataka kukuza uchumi wetu tuhakikishe tunasaidia, mathalani Tarime Mjini Kata ya Nkende, Nyandoto, Kitale na Kenyamanyoli asilimia zaidi ya 98 hawana umeme. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano Nkende kuna soko tunalijenga la Afrika Mashariki hamna umeme, kuna uwanja wa ndege pale, kuna mnada wa Magena, lakini kuna machinjio ya kisasa Nkende na huduma zingine za jamii. Zaidi kwa upande wa pili wa Tarime ni Kenya; wenzetu Kenya ukija usiku ni taa zinawaka tu, ukija usiku upande wa Tanzania ni giza kama vile ni pori. Kwa hiyo, ningependa kuwaomba sana hizi trilioni 1.32 Tarime mtukumbuke, mtuletee hii nishati ya umeme, sisi ni wakulima, sisi ni wafugaji tuweze kusindika mazao yetu, tuweze kukuza uchumi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna Watanzania wengine ni wajasiriamali wadogo wadogo wamewekeza, leo mtu mwenye saloon kama hana umeme hawezi kumudu kununua jenereta, leo wale wafanyabiashara wadogo wadogo hawawezi kumudu bila umeme. Tukiwaza Tanzania ya viwanda, pia tuwaze Tanzania ya wajasiriamali wadogo wadogo ambao nishati ya umeme ndiyo mbadala wa kuweza kuwakomboa Watanzania. Tuwaze huduma za jamii kama shule, tuwaze huduma za jamii kama hospitali, tuwaze huduma za jamii zinginezo, magereza na vituo vya polisi bila umeme huko vijijini, hata hao wahalifu mnakwenda kuwaweka pamoja na Polisi mnategemea nini? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ningeomba sana Serikali hii ya CCM kupitia kwa Profesa Muhongo wawekeze na nina imani labda alikaa hawajampunja bajeti yake na akajiridhisha kabisa hii trilioni 1.32 inatosha kuhakikisha wanaleta umeme zaidi ya asilimia 70 kwa Watanzania ili tuweze kuondokana na umaskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Taifa lolote lile lenye nishati mbadala ya umeme utaona uchumi wake utaji-reflect kwa sababu umeme ndiyo kila kitu. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri atuangalie Tarime, Kata nilizozitaja za Kenyamanyoli na mgodi ukiwapelekea umeme hiyo migodi itaenda kufanya kazi bila kutumia jenereta. Apeleke umeme Kitale, Turo, Nyamisangula, Nyandoto na kwingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na mimi ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kweli kwa kuweza kunipa fursa hii ya kuweza kuchangia machache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kutoa opinion yangu kwa kile ambacho kinaendelea Bungeni, naona kama hatuitendei haki nafasi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanasimama, wanapongeza sana hili la darasa la saba walioajiriwa kabla ya 2004 kurudishwa. Kuna watendaji wengi na watendaji wengine kama hawa watendaji ambao wamerudishwa hospitalini, madereva ambao wameajiriwa mwaka 2004 mpaka sasa hivi ambao kosa lao si tu kuwa darasa la saba kwa sababu waliowaajiri ni Serikali hii hii, imewaondoa kazini, haitaki kuwalipa mafao ya kuwaachisha kazi, halafu leo unasimama mtu anasema tunaipongeza Serikali sikivu, sikivu what?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza wamefanya makosa hawa ambao wameajiriwa mwaka 2004 kurudi nyuma at the first place hawakutakiwa kutoka kazini, wanatakiwa tuwawajibishe kwa sababu kwa kuwaondoa kazini kuna Watanzania ambao wameathirika sana. Kuna Watanzania ambao wamekufa kwenye sekta ya afya, kuna Watanzania wengi ambao wameathirika halafu leo mnapiga makofi eti wamewarudisha watendaji kuanzia hapo kurudi nyuma, kwa kweli mimi nasikitika sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali iwajibike kuwalipa gratuity wale watendaji wote kwa maana waliokuwa katika hospitali na kwingine kote darasa la saba ambao iliwaajiri wenyewe na imewaondoa kazini. Kama hawana fedha wanajificha kwenye vyeti fake na utendaji kuwaondoa kazini waseme kwa sababu kitu kingine, wameondoa hawa watendaji makazini wameshindwa kuwa-replace ambao sasa wanasifa stahiki. Watu wanahangaika, mmewaondoa kwenye ajira hizi halafu mnashindwa kuwa-replace hapa inaonekana kabisa kwamba Serikali haina fedha ya kuwalipa hawa watu na ni dhambi sana watu wanakufa kuondolewa kwa ghafla makazini na kutokurudishwa kazini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye utawala bora nilisema sitachangia kabisa, lakini kwa sababu mimi ni mwanamke na ni mwanamama na najua uchungu wa kuzaa na kuona kijana wangu anapotea kwa mazingira ya kutatanisha, watu wanauawa kwa mazingira ya kutatanisha, watu wanalemazwa lakini ukiongea watu hawasikii. Nikasema katika Biblia kuna phrase moja inasema; “chozi la mwanamke lina thamani mbele ya Mwenyezi Mungu.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wale akina mama wote, mama yake Ben Saanane, mama yake Mawazo, mama yake huyu Diwani wa Kigoma, mama wa Watanzania wote waliopotea, mama yake watoto wote waliolemazwa na Serikali hii ambayo haitaki kuchukua hatua; mama yake wa Diwani wetu aliyeuawa pale Hananasif katika uchaguzi wa Kinondoni anapolia chozi lake Mwenyezi Mungu atakwenda kuyalipa hapa hapa. Na mimi naendelea kuungana nao hawa wanawake kulia chozi kwa sababu na mimi ni mwanamke najua uchungu wa kuzaa, najua thamani ya mtoto anakufa bila hatia, naendelea kulia na wanawake hakika Mungu atakwenda kutenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kuchangia, kwa sababu dakika ni chache nichangie kwenye TAMISEMI, Jimbo langu la Tarime.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiisoma hii hotuba ya Waziri anaeneleza kabisa kwamba upungufu wa madarasa kwa maana ya vyumba vya madarasa kwa mwaka Julai, 2017 mpaka Machi, 2018; kwanza nimpongeze, wanajitahidi pamoja na kwamba Serikali inashindwa kutambua kwamba TAMISEMI ilitakiwa kupewa fedha nyingi sana kwa sababu ndiyo inayobeba majukumu mengi. Kama ingeweza kutekelezewa vizuri basi maendeleo yangeonekana kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameeleza hapa kwamba yamejengwa madarasa 2,278 na hivi vyumba vimejengwa kwa asilimia 80 na Watanzania waliokuwa wanajichangisha. Upungufu ni 264,594, na vyumba tulivyonavyo sasa hivi ni 123,044. Miaka 57 ya Uhuru tume-manage kujenga madarasa 123,044 yamebaki 264,594 ukigawa kwa yale tu ambayo yamejengwa 2,278 inaonesha Chama cha Mapinduzi kitachukua miaka 116 kuweza kutatua matataizo ya vyumba vya madarasa Tanzania. Ikizingatiwa wanakuwa na matamko mengi mengi, wananchi wanakuwa wanajitolea ikiwemo wa kwangu wa Jimbo la Tarime Mjini wamejitolea sana, wamejenga mpaka kwenye lenter Serikali wanaendelea wanakamilisha…

T A A R I F A . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, huwa nasikitika sana halafu wajina wangu eti ana shule na yeye ana-own. Hiyo taarifa yako inani-support in actual sense. Tangu uhuru mpaka leo mmejenga 123,000 bado vyumba 264,594 ukijua kabisa population ya Tanzania inaongezeka, mmeleta elimu bure, mnasajili wanafunzi wengi na capacity yenu ya kujenga madarasa ni ndogo sana halafu tunaongea nini? Hivi nini ni kipaumbele chetu? Taifa ambalo haliwekezi kwenye elimu, mtafanya mengine yote lakini hatutaona uchumi ukijionesha. (Makofi/Viegelegele/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiendelea hapa hapa kwenye elimu ukija kwenye vyoo ni matatizo, na tunajua shule ambazo tunakuta hazina vyoo vya kutosha wanafungiwa wanafunzi wetu hawaendelei. Wananchi wanajitolea kwa asilimia kubwa ndiyo wanajenga hivi vyoo ambavyo wameweka hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna siku nilisema mwaka jana wakati nachangia ambapo mlisema mmefanya re- allocation ya shilingi bilioni 39 kwenda Chato. Nikasema kwanini hata msiangalie kipaumbele mkazipeleka kwenye elimu, mkazipeleka na kwenye afya ili angalau kutatua hizi changamoto ambazo tunaziona?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye elimu hapo hapo, walimu hawana nyumba za kuishi, na jana wakati wanajibu swali hapa wakasema wako nyumba zao binafsi au wamepanga. Mnawapa hiyo hela ya kupanga? Iko nje ya mishahara yao? Mwalimu anapanga kwa mshahara mdogo ule ule mnaomlipa, anasafiri kutoka sehemu “A” kwenda “B” kwa mshahara ule ule halafu unategemea matokeo yawe mazuri. Lazima tuhakikishe tunaweka vichochezi vya kutoa elimu nzuri kabla hatujaanza kusema kwamba tunatoa elimu bure ambayo haina tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa Tarime muweze kunikarabatia sekondari ya Tarime ambayo ni kongwe, imefunguliwa mwaka 1973, na ni sekondari ambayo ni ya high school tu na inachukua zaidi ya combination saba. Mheshimiwa Waziri nimeshakwambia sana. Vilevile kulikuwa kuna gari pale land cruiser mmeliondoa tunaomba lirejeshwe wanafunzi wale wanateseka sana. Pia nilileta maombi kwa tarime muweze kutupandishia hadhi sekondari ya Mogabiri kwa mwaka huu wa fedha unaoisha lakini pia tuna sekondari ya Nyandoto ili iwe ya kidato cha tano na cha sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraka haraka sana, Waziri unatambua kabisa tatizo tulilonalo kwenye Hospitali ya Wilaya na Mheshimiwa Kandege ulikuja na Waziri Mkuu mlijionea uhalisia. Hatuwezi kuwa tunapata basket fund ya shilingi milioni 11 Hospitali ya Wilaya wakati mnapeleka shilingi milioni 42 katika Kituo cha Afya cha Nyalwana hii si haki kabisa na ukizungatia kwenye Halmashauri yangu sijapata kituo cha afya pamoja na kwamba nahudumia Serengeti na Rorya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kwenye Mnada wa Magena. Ukiangalia kwenye hiki kitabu mapato ya Halmashauri yameshuka sana kutoka shilingi bilioni 1.1 kwa mwaka jana baada ya kuondoa mapato ya mabango na property tax kwa mwaka huu tumekusanya shilingi milioni 586 tu. Mkiturudishia Mnada wa Magena tutaweza kukusanya mapato mengi kwenye Halmashauri yetu. Hii story ya kusema kwamba Tarime sijui wizi wa ng’ombe kwanza mnatukebehi sana. Sasa hivi Tarime ni salama na ndiyo maana kuna Mkoa wa Kipolisi unaojitegemea wa Tarime-Rorya. Tunaomba kabisa ng’ombe wanatoka Serengeti haziendi Kirumi, ng’ombe wanaotoka Rorya hawaendi Kirumi wanapita moja kwa moja na wale ambao wananunuliwa kwenye Mnada wa Kirumi wanapitishwa Tarime kwa nini wasiibiwe? Tunahitaji Mnada wa Magena ufunguliwe ili uweze kutoa ajira kwa watanzania wa Tarime.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye halmashauri yangu wamekaimisha sana Wakuu wa Idara kitu ambacho kina- affect utendaji. Miaka inapita Wakuu wa Idara ndiyo wale wale naomba napo pia waweze kunibadilishia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba wa walimu wa sayansi. Tunasema Tanzania ya viwanda, uhaba wa walimu wa sayansi ni mkubwa sana, wananchi wakawa wanajichangisha ili kuwalipa walimu waweze kufundisha Rais akatoa tamko msichangishe, ipitie kwa Mkurugenzi. Wananchi wameacha, Serikali sasa hivi hakuna maabara wala vifaa, walimu wa sayansi hamna. Tunaomba kama mmeshindwa, kwa mfano Tarime tuko tayari kuchangisha na kuajiri walimu wa sayansi ili watoto wetu wasome vizuri. Tunaomba kabisa kama Serikali imeshindwa kutoa kipaumbele…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukru. Nami niweze kuchangia Wizara hii muhimu sana, Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji ni uhai lakini pia maji ni uchumi. Kwanza kabisa nianze na Jimbo langu la Tarime. Ukiangalia kitabu hiki page namba 175 ningependa kuja kupata ufafanuzi wa kina kwa sababu hizi fedha ambazo mmezi-allocate hapa na kusema miradi imekamilika kwa asilimia 100 ni vitu viwili tofauti. Pia page number 180 maji ambayo tunapata Tarime yanatokana na chanzo cha Bwawa la Nyanduruma. Bwawa hili ni tangu enzi za Mjerumani mpaka sasa hivi halijafanyika ukarabati wowote limetekelezwa, alipokuja Waziri Mkuu alielekeza na Katibu Mkuu ulikuja na timu yako, nashangaa kwenye kitabu bado mmeendelea kutenga shilingi milioni 300 ambazo mmekuwa mkizitenga miaka miwili au mitatu iliyopita bila kuzileta. Ningependa kuweza kupata ufafanuzi wa kina, ile timu iliyokuja iliweza kufanya utafiti upi na imeweza kushauri vipi ili lile bwawa liweze kutengenezwa kwa muda mfupi wakati tukisubiria chanzo kikuu ambacho nimekuwa nikipigia kelele hapa cha maji kutoka Ziwa Victoria ambayo itakuwa ni suluhisho kwa Wilaya ya Rorya, Tarime kwa maana ya Jimbo la Vijijini na Jimbo la Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji ya Ziwa Victoria ni sehemu fupi sana ambayo yanatolewa, Shirati Jimbo la Rorya ambayo inaweza ikaleta Rorya na Tarime lakini imekuwa ni kizungumkuti kwa Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi kuhakikisha kwamba inawaletea wananchi wa Tarime na Rorya maji ili waweze kufanya shughuli zao zingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nirudi kwenye hoja ambazo ni za kitaifa zaidi. Tumeshuhudia kabisa Serikali ya Chama cha Mapinduzi ikiwaambia Watanzania kwamba Sera ya Maji tutapata maji ndani ya mita 400 lakini Awamu hii ya Tano wakaja wakatuambia kwamba wanamtua mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi ni vitu viwili tofauti, wanaahidi hawatekelezi, wanapanga hawatekelezi na hii inajidhihirisha kwa hizi bajeti ambazo tumeweza kuziainisha. Bajeti ya mwaka 2015/2016 wlileta hapa Bungeni tukawatengea shilingi bilioni 485 lakini wakaweza kupeleka kwenye fedha za maendeleo shilingi bilioni 136 tu, ambayo ni sawasawa na asilimia 28. Ikaja mwaka 2016/2017 shilingi bilioni 913 wakapeleka shilingi bilioni 230 ambazo ni asilimia 25.7 tu. Mwaka 2017/2018 wakarudi tena wakaomba shilingi bilioni 623 lakini mpaka Machi ingawa Waziri ameendelea kusema zimekuja zingine, zilikuwa zimeenda asilimia 22 tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hoja hii utaona kabisa Serikali ya Chama cha Mapinduzi haina dhamira ya dhati ya kutatua tatizo la maji kwa Watanzania. Watanzania ambao, akina mama wanatembea usiku kutafuta maji, wanaliwa na mamba, wanaliwa na fisi, wanapata talaka, wanabakwa, wanapata magonjwa mbalimbali ya vichocho kwa sababu maji ni mabaya, watoto wetu chini ya miaka mitano wanafariki kwa sababu maji si safi na salama, leo Serikali ya Chama cha Mapinduzi inaendelea kuwahadaa Watanzania kwamba wana dhamira ya dhati ya kutatua tatizo la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili niweze kuungana na Mheshimiwa Mnyika ambapo jana alipendekeza tumalize michango yetu, leo jioni Wizara isihitimishe bali waende wahakikishe kwamba bajeti tuliyoitenga mwaka jana ambayo inamalizika Juni, iweze kupelekewa fedha walau ifikie asilimia 80 tutatue matatizo ya maji vijijini na mijini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi niliona Katibu Mkuu ametoa takwimu na hapa wamezirudia wakisema kwamba maji kwa vijijini asilimia 59 ingawa najua hii ni average, kuna vijiji havina maji kabisa, hata ukibaki kwenye asilimia 59 yenyewe na World Bank wamesema ni asilimia 50 utaona kabisa kwamba hamna ile dhamira ya dhati. Asilimia 59 hii ndiyo iliyokuwepo kwenye Awamu ya Nne mwishoni, sasa ndani ya miaka miwili na nusu, Serikali ya Chama cha Mapinduzi Awamu ya Tano haijafanya chochote bado ime- stuck kwenye asilimia 59. Huu ni uhalisia kwamba maji siyo kipaumbele, tunatenga billions of money lakini hawapeleki fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jana ndugu yangu Mheshimiwa Anna Gidarya alifanya analysis hapa kwamba kuna kijiji kimojawapo Hanang wananunua maji lita 200 kwa shilingi 7,000. Kwa shilingi 7,000 kwa mwaka unatumia shilingi milioni 2.5, pato la wastani la kila Mtanzania ni shilingi milioni 2.1. Ina maana huyu anatumia pato lake zaidi kwa asilimia 119 kununua maji tu, bado mahitaji mengine na maji ya vijijini siyo safi na salama, hayajawa treated kama maji ya mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili Taifa liendelee, lazima tuboreshe huduma za maji. Maji ni uchumi, bila maji hamna viwanda ambavyo mnasema Serikali ya viwanda. Maji ni uchumi, bila maji hamuwezi kujenga hizo barabara, bila maji hata magari tunayotumia hayawezi kwenda. Kwa hiyo, maji ni kila kitu. Taifa ambalo unataka liendelee lazima tuweze kuwekeza kwenye maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ni kuhusiana na ufisadi ambao wa kweli umekithiri kwenye miradi ya maji. Tunatenga bajeti zinakwenda kidogo lakini hata hiyo kidogo na yenyewe inafisadiwa na hatuoni hatua zikichukuliwa pamoja na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano mnasema mna-fight ufisadi, tunataka tuone kwa vitendo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano tu kwenye ripoti ya CAG anasema kuna mradi ulikuwa Geita ulikuwa ni wa shilingi bilioni 6.6 ambao ulisainiwa Mei, 2015 na ulikuwa ukamilike ndani ya mwaka mmoja, kati ya kampuni ya MSJC and Company Ltd. mpaka Novemba 2017 mradi haujakabidhiwa, fedha zilitolewa zote na zilikuwa za mfadhili (African Development Bank) hatua hazijachukuliwa, kitu cha ajabu wamefanya tu kumtoa Meneja wa Maji Geita, wamempeleka Wizarani. Kumhamisha kutoka eneo moja kumpeleka eneo lingine!

Mheshimiwa Naibu Spika, hii haikubaliki na katika mantiki hiyo tunajua kuna miradi mingi Tanzania nzima imefisadiwa, tunaomba kabisa, siyo Tume, tuunde Kamati Teule ya Bunge ambao ndiyo tunaisimamia Serikali ili tuweze kuhakikisha inapita kwenye miradi yote kuainisha ufisadi umesababishwa na akina nani ili hatua ziweze kuchukuliwa. Vinginevyo tukisema tuunde hii tume kama ambavyo wenzangu walisema awali, inaenda, inajadiliwa juu kwa juu hatujui wahusika ni akina nani, Bunge tunaisimamia Serikali tuweze kuunda Kamati Teule ya Bunge iende ipitie kama ambavyo imeshafanyika huko nyuma kwenye Nishati na Madini enzi za Jairo, tuliunda Kamati Teule ya Bunge ikaja na majibu hapa tukaweza kupata ufumbuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye maliasili na utalii tuliunda kuhusu ile operesheni tokomeza ikaja na majibu hapa tukapata ufumbuzi. Miradi ya ufisadi ya maji ambayo tunatumia kodi za wananchi maskini imekithiri ilhali Watanzania wakiendelea kufa kwa kukosa huduma bora ya maji. Tuunde Kamati Teule ya Bunge.

T A A R I F A . . .

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, at a time, we don’t need to waste time!

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni Bunge, linaisimaia Serikali, unavyoniambia Rais katoa kauli wakati nimetoka kusema hapa Mtendaji wa Geita amefanya kuhamishwa kupelekwa Wizarani, tafadhali sana, tusiwe tunapenda kuingiliana kwenye kuchangia kama unajua unatoa hoja ambayo haina mantiki, tuko serious hapa kufanya mambo ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ambayo inachukua muda mrefu bila kukamilika, ambayo inazidi kuongeza gharama kwa fedha za Watanzania walipa kodi maskini, utakuta miradi inachukua zaidi ya miaka saba haijakamilika na kuhakikisha kwamba shilingi yetu thamani yake inazidi kushuka kila siku ukilinganisha na dola, kwa hiyo gharama za mradi zinazidi kuwa kubwa zaidi na huu unakuwa ni mzigo kwa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano wa hii ni ule mradi wa Bwawa a Kidunda, Kimbiji na hata Mpera, umechukua miaka mingi sana, kwa nini Serikali inapoteza fedha za Watanzania kwa kuacha kukamilisha hii miradi?

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kusisitiza Serikali ya Chama cha Mapinduzi jana Wabunge wenzangu waliongea hapa mkawa mnawadhihaki, Serikali ya Chama cha Mapinduzi msiwekeze kwenye maendeleo ya vitu wekezeni kwenye maendeleo ya watu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa analysis ile ambayo mliisimamia jana mkatoa na miongozo hivi kwa akili ya kawaida kabisa vipaumbele vyetu ni vipi, kununua ndege ambayo only 5% of Tanzanians ndiyo wanatumia na kwa wengine is not even a basic need hiyo ni it’s a luxury need. Ni nini ambacho tunaanza nacho kama nilivyosema awali kwamba maji ni uchumi, unasema kwa sababu ya utalii ulete fedha. Hivi mtalii gani atakuja anaingia hotelini akifungua bomba linatoa maji kama chai ya rangi, wakati alipotoka unatumia tap water kunywa maji straight, tujiulize mara mbili tuboreshe kwanza kuhusu maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo unawekeza kwenye ndege asilimia tano ya Watanzania wanatumia, unaacha asilimia mia moja ambayo ni maji kila Mtanzania anahitaji, viumbe hai vinahitahi hayo maji, mimea inahitaji maji and then mnakuja mnalihadaa Taifa kwamba tumewekeza kwanza kwenye ndege ambazo zinaleta utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, hizo ndege ambazo zinaleta utalii let’s start with things ambazo tukiwawezesha Watanzania wetu hawataugua, watakuwa na afya, watafanya kazi, uchumi utapanda kuliko ilivyo sasa hivi and then automatically tutanunua hizo ndege tutajenga viwanda, tutafanya vitu vingine vyote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwenye maji. tumeshuhudia kwamba….

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kabla sijaanza kuchangia kwanza niweke rekodi maana naona Wabunge wa CCM wakisimama wanaanza kufanya reference kwa chaguzi ambazo zilifanyika 2015 kurudi nyuma. Tuingize kwenye rekodi tu kwamba Marais waliotangulia hawakuwahi kutamka bayana kwamba Wakurugenzi Watendaji ambao wameteuliwa na yeye wasipomtangaza mtu wa CCM watakuwa hawana kazi, hawajawahi kutamka bayana, lakini Rais Mheshimiwa Dkt. Magufuli ametamka bayana na amenukuliwa na vyombo vyote. Kwa hiyo tukisimama hapa tukiongea inabidi wakae wakemee, vinginevyo wataingiza nchi kwenye machafuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niingize kwenye rekodi kwamba Makatibu Mezani mnapunja sana muda wa upinzani. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Kweli hiyoo, kweli hiyoo.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti wa Chama ameongea chini ya dakika saba na hajawa interrupted, sisi tulikuwa tunamrekodi hapa tunaomba muwe fair kabisa maana yake wote tuna-deserve muda wa kuongea hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie hoja hii ambayo ni muhimu sana kwenye mustakabali wa nchi yetu. Tumekuwa…

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena kwa mujibu wa…

MWENYEKITI: Ni kuhusu utaratibu.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, umemkatalia Chief Whip hapa..

MWENYEKITI: Kwa mujibu wa kanuni gani Mheshimiwa?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena nirudie kwa mujibu wa kanuni ya 64 kwamba Mbunge hatatoa maneno ya uwongo katika Bunge. Ninalotaka kusema ni kwamba namwomba mchangiaji aliyekuwa anakaa sasa hivi kwa sababu anamzungumzia Mheshimiwa Rais ambaye tunaamini kwamba anaamini katika uchaguzi na kwa maneno hayo aliyozungumza yaingie kwenye rekodi, ningeshauri yasiingie kwenye rekodi wakati yeye hajaleta uthibitisho wa hayo maneno aliyozungumza Mheshimiwa Rais.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko, endelea kuchangia. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Tumekuwa tukishuhudia Mawaziri wanakuja wanaeleza wananchi kwamba uchumi wetu unakuwa kwa asilimia saba, yaani tumekuwa tukieleza uchumi wa nchi unakuwa kinadharia zaidi kuliko kiuhalisia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona kabisa taarifa ya Shirika la Fedha Duniani imesema bayana kwamba uchumi wetu unakuwa kwa asilimia nne. Uchumi kukua tunaupima vipi, moja ya kigezo ni kuangalia pia na kiwango cha umaskini cha watu wetu wananchi. Ukiangalia kiwango cha wananchi wa Tanzania awamu hii…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko, wewe ni Mbunge mzoefu sana ili ujenge hoja yako vizuri kuhusiana na ukuaji wa uchumi wa Tanzania kile kinachodaiwa na IMF ungelikuwa nacho hapa, unasema hiki hapa nakiweka hapa unaendelea kuchangia.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ulinde muda wangu ukitaka document…

MWENYEKITI: Narudia kama unayo just lay on the table, unaendelea kuchangia

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, I will lay it on the table right, I don’t have it now, but I will do that.

MWENYEKITI: Very good, ahsante.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuaji wa uchumi unapimwa pia kwa kuangalia umaskini wa wananchi wetu. Ukiangalia Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na kwamba sikatai lakini imejiegemeza sana kwenye maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu. Ukiangalia hata kwenye mpango hapa wameainisha bayana kabisa kwamba ili kuweza kufikia uchumi wa kati kichwa chao mojawapo watawekezwa kwenye maendeleo ya watu. Maendeleo ya watu namaanisha elimu, afya, maji, kuhakikisha wanawawezesha wananchi wao kiuchumi kupitia uwekezaji na vitu vingine lakini ukiangalia kiuhalisia Serikali inafanya kwa kiwango kidogo sana katika kuhakikisha kwamba inaweka maendeleo kwa wananchi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kwenye elimu, tumeshuhudia elimu yetu ambayo mmesema mnatoa elimu bure…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Nimeshakataa taarifa Waheshimiwa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia kwamba tumeendelea kuona watoto wetu wanasoma kwa kurundikana wanafunzi 200 wengine wanasoma kwenye miti. Tumeendelea kuona Walimu wakiwa wana-work load kubwa kinyume kabisa na uwiano wa mwanafunzi kwa Mwalimu. Tumeendelea kushuhudia ajira hazitolewi kwa Walimu. Tumeona juzi wametangaza ajira 4,000 tu lakini watanzania zaidi ya 91,300 wame-apply kwa ajira 4,000 tu ambazo zimetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia, ningeomba kuweka kwenye kumbukumbu, Mheshimiwa Waziri alivyoleta taarifa hapa angetuambia upungufu wa Walimu ni kiasi gani, lakini ameonyesha tu kwamba Walimu waliopo mwaka jana tumeajiri kiasi fulani, sasa hivi tunategemea kuajiri kiasi fulani. Tusipowekeza kwenye elimu, Taifa ambalo haliwekezi kwenye elimu kamwe halitakaa liendelee. Haya mambo tunayoyajenga sijui Stieglers Gorge, SGR, nimeenda juzi pale Kinyerezi naambiwa hata wale wanaokuja kufanya maintenance pale inabidi watoke nje kuja kufanya maintenance ya vifaa vile vya Kinyerezi, ina maana vikiharibika mitambo mingine ibebwe ipelekwe nje hii yote ni kazi, inabidi tuwekeze kwa watu wetu ili waweze kuja kuwa wanahudumia hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia statistically kwa Tarime tu mwaka jana nikiwa gerezani niliona watoto waliofaulu kwenda form one wengi wameachwa. Nilitarajia kuona Serikali ingewekeza kuhakikisha kwamba inamalizia maboma yote ambayo yamejengwa na wananchi. Kwa mfano Tarime wananchi walijitolea wakajenga maboma 40 kwa shule za sekondari na tukaandika kuja wizarani ili tuweze kupata fedha, hatukuweza kupata fedha za kumalizia maboma 40.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika halmashauri za Mkoa wa Mara Tarime Mji na Bunda Mji ambapo mapato yetu ni madogo sana hatukuweza kupata hata senti tano ya kumalizia maboma ili watoto wetu waweze kwenda sekondari na waweze kusoma. Kwa hiyo utanona kwamba kipaumbele cha Serikali ni kuwekeza kwenye vitu badala ya kwenye maendeleo ya watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia pia kwenye afya ni the same hata kama tumejenga vituo mia tatu na kitu. Nashukuru Nkende nimepata kituo kimoja, lakini bado tatizo halimaliziki, tunahitaji kuenga vituo vya afya, tunahitaji mahospitali yawe na dawa, vitendanishi na wataalam, waajiri Madaktari wa kutosha, tunahitaji kuona kwamba Mtanzania mfanyabiashara, mkulima wanakuwa na afya bora kuweza kufanya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kusema tu kwamba kwa Tarime Mji ile hospitali tunahudumia Rorya, Serengeti na wengine, lakini mnatupa fedha za basket fund kama vile ni watu wa Tarime Mji, watu 78,000. Tunaomba mkiwa mnatoa fedha muweze ku-consider kwamba tuna work load kubwa. Vilevile Daktari wa Kinywa na Meno wa Tarime alifariki lakini mpaka sasa hivi hatujapata replacement, wananchi wetu wanahangaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie vitambulisho vya wajasiriamali, wamevizungumzia pamoja na kwamba vimeathiri ushuru kwa maana ya kwa halmashauri zetu mapato yanapungua, lakini nataka nijue zaidi. Hivi vitambulisho tunaambiwa kwamba vimetengenezwa Ikulu, vimetengenezwa na Rais, nataka nijue vitambulisho hivi vimetengenezwa kutoka fungu gani, maana yake sina kumbukumbu kama tulishawahi kupitisha fungu hapa kwa ajili ya kwenda kutengeneza hivyo vitambulisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia je, hivi vitambulisho vimefuata Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na.7 ya mwaka 2011 na 2016? Je, walishindanisha tenda? Mzabuni ni nani aliyeshinda kutengeneza hivi maana yake mwisho wa siku atakuja atapita CAG, halafu itakuja Audit quarries tujue. Mbaya zaidi hivi vitambulisho ambavyo wanasema laki sita wanaovitoa ni Ma-DC ambao sio Maafisa Masuuli. Kwa hiyo, hii inaacha maswali mengi sana na wananchi wanasema badala ya Chama cha Mapinduzi kupeleka zile milioni 50 kama walivyoahidi kwa kila kijiji, ila sasa wameenda tena kuwakata wale maskini elfu 20 kujaza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kujua, je, hivi vitambulisho ni chaka ambalo linakusanya fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao au ni nini? Tunaomba watuondoe huo wasiwasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Tarime ni Mji ambao unakua, tunahitaji taa za barabarani, hata Mheshimiwa Rais alivyopita alisema mji ule unakua. Kama ambavyo wameweka Lamadi, tunaomba na Tarime nako waweze kutuwekea taa za barabarani. Uteuzi wa Wakurugenzi tumeukemea hapa na tutaendelea kuukemea kwa mujibu wa sheria inatakiwa angalau Mkurugenzi anayeteuliwa awe ametumikia kwenye utumishi wa umma angalau miaka mitano, lakini tumeshuhudia wakurugenzi wanaoteuliwa ni makada. Mfano wa juzi tu wa somebody Mhagama, alikuwa ni Katibu wa CCM kateuliwa kuwa Mkurugenzi, wanaziua halmashauri zetu kuleta watu ambao hawana, lazima tufanye succession plan kwenye halmashauri zetu. Wateue ma-DC ambao ni makada wao lakini kwenye kada ya Ukurugenzi, wazingatie sheria. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nami namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunijalia uzima na leo nasimama kuchangia maoni yangu kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ni Wizara muhimu sana kwa ustawi wa jamii yetu ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuzungumzia kwanza kabisa kuhusu Vitambulisho vya Taifa, maana yake leo asubuhi iliongelewa sana hapa Bungeni. Majibu ambayo Serikali imetoa asubuhi Bungeni ni majibu ambayo ni mepesi sana kwa Watanzania kuyasikia na hayana uhalisia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kabisa kwamba Serikali inadaiwa zaidi ya dola 30,000 za Kimarekani na Mkandarasi Alice ambaye amesitisha production ya hivi vitambulisho kuanzia Januari, 2019. Sasa haya mambo ambayo wamekuja hapa asubuhi wanaeleza ooh, watakwenda kutambuliwa kwa sababu ya usajili wa simu kwa kutumia namba, tutambue kwamba Watanzania wanahitaji vitambulisho vya Taifa, siyo kwa usajili wa simu tu. Kuna sehemu nyingi Watanzania wakienda wanaombwa vitambulisho vya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Serikali ituambie Bunge hili, ni lini itaenda kumlipa Mkandarasi huyu hizi takribani shilingi bilioni 69 ili Mkandarasi aendelee na production, aendelee kuandikisha Watanzania na wapate hivyo vitambulisho ambavyo ni muhimu? Mtueleze ni lini mtamlipa Mkandarasi huyu hizi shilingi bilioni 69. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo ndiyo maana tukikaa tunasema lazima Serikali iwe na vipaumbele. Mheshimiwa Waziri ameeleza hapa, mlikuwa na target ya kuandikisha Watanzania milioni 25, leo waliopata ni milioni nne tu. Mkandarasi amesitisha uzalishaji, Kisa, hamjalipa fedha; lakini fedha nyingine mnapeleka kwenye sehemu ambazo hata hazina tija kwa maendeleo ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nitaenda kuzungumzia Jeshi la Polisi; na hapa tukizungumzia Polisi, tunazungumzia wale ambao wanakiuka miiko na maadili ya kazi zao. Maana yake Wabunge wa CCM mkisimama huko mna generalize sijui mnafikiri nini. Tuko hapa kulisimamia Taifa, kulisimamia Jeshi la Polisi likienda kinyume. Nao wanatambua sisi ndiyo tunapigania maslahi yao hapa, lakini hatuwezi kuacha kuwasema wakienda kinyume. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unyanyasaji wa raia wanapokamatwa na Jeshi la Polisi; tumeshuhudia raia wanapigwa, wengine wanafariki. Juzi nimesikia Mwanga kuna kijana amefariki kwenye kituo cha Polisi. Yaani haiwezi kupita mwezi, miezi minne hatujasikia kuna raia amepigwa na Polisi, amefia Kituo cha Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hayo tu, nilipokuwa Segerea kuna mabinti walikuja wamekamatwa kwenye Vituo vya Polisi, wamebakwa, wameingiliwa kinyume na maumbile, wengine wameambukizwa magonjwa ya UKIMWI. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukizungumza hapa, tunataka Jeshi la Polisi liwawajibishe hawa Askari. Majina ya Maaskari nawajua na nilitaja kwamba Kituo cha Sitaki Shari, Kituo cha Kawe na Kituo cha Mabatini. Wanakaa na mabinti hawa zaidi ya mwezi, wiki tatu, miezi miwili wanawafanya kinyume na maumbile. Binti amekuja pale ameoza huku nyuma. Halafu tukizungumza, mnasema kwamba tuna…, come on! Lazima tusimamie hawa Polisi wasiende kinyume. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, kubambika kesi raia. Unamkamata raia kwa uzururaji, unampa amri robbery. Asipokuwa na fedha ya kukupa kitu kidogo, unambambika. Lazima tukemee hili ili Jeshi la Polisi, wananchi ambao ni walipa kodi ndiyo wanawalipa kuwepo; wanatakiwa wawalinde raia na usalama wao na siyo kuwageuza vinginevyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kabla sijaendelea hapo hapa katika kuwanyanyasa raia; tumekuwa tukisia matamko kwa kweli ambayo hata hayakemewi. RPC wa Dodoma, mwaka 2018 wakati nachangia nilimsema. Mwaka 2018 alisema kipigo cha mbwa koko; mwaka huu wakati ACT Wazalendo wanasema wataandamana, ambapo ni haki yao Kikatiba, akatoka kabisa confidently anaongea atawapiga mpaka wachakae. Kweli mnawachakaza Watanzania, maana yake mmewachakaza mpaka mnawaua. Kama hamkemei hili, mnafikiri ni sifa mnaua Watanzania, hakika hiyo laana itawarudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni mlundikano wa mahabusu kwenye Magereza yetu. Nashangaa Tanzania ni nchi ya ajabu. Nyie mnafurahia kuwalundika raia Gerezani, raia ambao wangekuwa ni wazalishaji kwenye Taifa letu, mnaweka mzigo kwenye Taifa kwa kuwalundika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Segerea unakuta zaidi ya asilimia 80 ni mahabusu, tena mahabusu kesi zao nyingine zinachekesha. Kuna kesi moja alikuwa ni mfanyakazi wa ndani, anatuhumiwa eti ameiba shilingi 800,000/=, tena ni mfanyakazi wa kigogo mkubwa sana Wizarani. Eti, akaenda kufuatwa Bukoba, ametoka Dar es Salaam; wamechukua gari Mwanza wamemfuata Bukoba ndani ndani huko, amekuja wamepandishwa ndege mpaka Dar es Salaam kwa shilingi 800,000/= mnasema kwamba mnasimamia matumizi ya walipa kodi masikini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima tukemee haya. Lazima tukemee haya. Watanzania wanaozea kule mahabusu Gerezani kwa kesi za kitoto sana. Wanakaa miaka mingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku hizi imekuja hii ya utakatishaji. Nikiwa Segerea kuna Watanzania vijana ambao wamejiajiri kwenye hizi Travel Agents, wanasemekana sijui wametakatisha shilingi milioni 10 za ATCL. Wamekamatwa vijana zaidi ya 11, wamesafirishwa kutoka Mwanza. Kuna mahakama kule! Usiku wamesafirishwa kutoka Mwanza na Maaskari wameletwa Segerea. Shilingi milioni 10 mnawaita watakatishaji, mnawanyima dhamana, vijana ambao ni wazalishaji zaidi ya 12 na kuna mama ana katoto ka miezi miwili. Yaani, basi, kama ni laana tunaipata kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sare za Magereza. Nimekuwa nikizungumza hili. Hawa Askari Magereza…

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa!

T A A R I F A

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa taarifa mzungumzaji, kusema kweli amtaje ambaye alitumia hiyo ndege na gari ili tumjue achukuliwa hatua za kisheria. Bila kumtaja haiwezekani. (Kicheko)

MWENYEKITI: Hiyo siyo taarifa. Endelea Mheshimiwa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema hao Maaskari ni wabaya tunataka tusafishe hili jeshi liwe jeshi ambalo linatumikia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu 2012 mpaka leo Askari wa Magereza hawajapewa uniform, wanajinunulia. This is a shame. Watu hawa wanawajibika kutunza watu mnaosema ni majambazi sugu, ni manani, wanaji-sacrifice wanawatunza, hata kuwapa uniform zao, hamna! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, tumekuwa tukiona majeshi yetu yanaingiliwa. Niliona hivi karibuni TISS wanatumika kukamata raia badala ya Polisi. Kwa hili I have the evidence. Hiki ni kuingilia mihimili mingine. Haya majeshi, TISS wanatakiwa wafanye kazi zao, Jeshi la Polisi lifanye kazi yake. Pia kuna malalamiko yalikuja na hata raia tuliona.

Mheshimiwa Rais alisema kabisa kwamba wakati anakwenda kukagua nyumba ambazo zinajengwa kule Ukonga na TBA ambazo Magereza hawahusiki kabisa, alitakiwa awawajibishe wale TBA, lakini kauli ya kusema CGP atatokana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kwa kweli ile kauli mpaka kesho sijui inamaanisha nini. Kwamba CGP wa Magereza atokane na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hii ina-demoralize hawa Askari wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kwa haraka haraka ni kuhusu Askari Magereza kutumia fedha zao za mfukoni kusafirisha mahabusu na wafungwa, kama wanatoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Hii fedheha kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Wekeni utaratibu wa kuweza kuwasafirisha hawa mahabusu na wafungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Askari wanatumia fedha zao halafu hamwalipi, inakuwa ni deni. Hii ni aibu. Askari hawa wanadai madeni ya likizo, hamwapi, wanadai na madai kibao. Mshahara hamjawapandishia, pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais alisema kwenye kampeni zake, akishinda ataongeza mishahara ili wasiwe wanauza vitumbua, wasiwe wanafanya mambo ya rushwa, kitu kimekuwa ni kunyume. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni mwaka wa nne tunaenda hamjapandisha mshahara, mnasubiri mwakani mpandishe; na hiyo itakuwa ni rushwa. Mlitakiwa mwapandishie kuanzia mwanzo, siyo msubiri ikifika mwakani sasa mnapandisha ili kuwasogeza karibu, maana yake kule kwetu huwa... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
MHE. ESTER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nami naenda kuchangia kwenye taarifa ya PIC na nikipata muda na Bajeti kidogo, lakini kwanza niwapongeze Wenyeviti wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza na hoja ya kutokukamilika kwa miradi, tutaona kwenye Shirika la NSSF kuna Mradi wa Holiday Inn na ule wa Dege kule Kigamboni, mpaka leo haujakamilika hatujui hatima yake na zile fedha ni za wanachama ambazo zinatakiwa ziweze kuwekeza kwa tija zaidi ili ziweze kuzalisha na kuweza kuwalipa wanachama ambao wamechangia kwenye huo Mfuko.

Mheshimiwa Mwenyeki, kingine nitagusia pia kwenye Shirika la Nyumba la Taifa, kwenye miradi mitatu kama ilivyoainishwa kwenye taarifa yetu ya PIC. Kwenye Mradi wa Mji wa Kawe tulitembelea pale Kamati yetu ya PIC mwaka juzi tukaelezwa na by then tukaambiwa kuna Watanzania ambao tayari walikuwa wameshatoa deposit kwa ajili ya kupanga na wengine kununua nyumba, kuanzia 2016 walikuwa wameshatoa deposit. Sasa tujiulize leo hao Watanzania ambao walitoa zile deposit zao, mradi haujakamilika that means hawajaweza kuhamia kwenye huo mradi. Sababu ambazo Serikali inatoa ni zile ambazo hazina tija kwa kweli na Serikali lazima iwe responsible kwa maamuzi ambayo imeyafanya ambayo yanaathiri miradi kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imesemwa hapa na jana imesemwa kweli, hivi kwa mtu gani ambaye anaweza akaona kwamba ni sawa kutoa bilioni 21kuliko kutoa kibali kuweza kukamilishwa kwa ule mradi ambao tunajua kabisa Shirika la NHC ni shirika ambalo linajiendesha kibiashara, wala Serikali haitakiwi kutoa dhamana ila inatakiwa itoe kibali na benki ndiyo wanatakiwa ku-assess business plan ya shirika husika kuona kwamba ni viable apewe mkopo, wakitoa mkopo for a certain period inaweza ikarejesha na wala siyo Serikali kuendelea kukatalia kibali, just kutoa tu kibali shirika likakope, hiyo haikubaliki na sisi kama Wabunge lazima tuazime sasa Serikali iweze kutoa kibali ili NHC iweze kukopa, iweze kumalizia ule mradi na Watanzania ambao wamesha-deposit waweze kuhamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli tutaonekana wendawazimu sana, kwa yeyote yule ambaye anaweza kupata hata ile view tu ya ule Mji wa Kawe ulikuwa si tu unaenda kukuza uchumi wa Tanzania, lakini unaenda kubadilisha taswira ya Tanzania kabisa kwa Jiji la Dar es Salaam. Sasa ukisema umeutelekeza kwa sababu mnahamia Dodoma, ni mambo ya ajabu sana, hata mwendawazimu hawezi kuyakubali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Morocco square ulikuwa umeshakamilika kwa asilimia 90 mwaka juzi, imebaki asilimia 10 nao umeachwa hizi asilimia kumi kwa miaka mitatu, unaachwa kukamilishwa. Hii siyo haki kabisa, mkandarasi anaendelea kulipwa asilimia 10 tu kukamilika kwa mradi, lazima Serikali iwajibike na ijue kabisa kwamba hii sekta ya ujenzi ndiyo sekta ya pili ambayo inachangia katika kutoa ajira Tanzania ukiacha ile ya kilimo, kwa hiyo ni lazima tujitoe zaidi kuhakikisha mambo yanasonga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kupungua kwa mitaji kwenye mashirika yetu, taarifa imefafanua vizuri sana. Hapa nitaenda kugusia Shirika la STAMICO, shirika hili tumelitwisha jukumu kubwa sana la kusimamia miradi mikubwa na ya kimkakati, linasimamia Stami Gold, Buhemba kule, inasimamia Kiwira, inasimamia utafiti wa madini, ununuzi wa madini bati, lakini shirika hili limeendelea kujiendesha kwa hasara, mtaji unapungua kila mwaka, matumizi ya shirika hili tumeona na kwenye ripoti ni zaidi on average 134 percent ya pato ghafi, ina maana linajiendesha kihasara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajiuliza kama Serikali imeamua kuwekeza kwa baadhi ya mashirika kama ambavyo wamewekeza kununua ndege nyingi tena kwa mabilioni mengi ya fedha, wamewekeza kwenye SGR trillions of money. Shirika la STAMICO ambalo ni muhimu sana na miradi ambayo wameipa Tanzanite One ipo STAMICO kwa nini wasitenge mtaji wake mpaka juzi ilikuwa bilioni 33. Kwa nini hata tusi-invest pale hata bilioni 200 tu tuone ijiendeshe sasa hivi na iweze kuendeleza hiyo miradi ya kimkakati, we have to start a balance, huwezi kupeleka materials kwenye SGR, sijui wanataka popularity ili Watanzania waone, unaacha shirika ambalo ni la muhimu sana ambalo umelipa majukumu makubwa sana. Kwa hiyo, naomba sana Serikali ione umuhimu wa kuipa hela STAMICO ili iweze kuendesha vizuri hiyo miradi yote ambayo imeelekezwa STAMICO. Tunaona STAMICO imerithi madeni ambayo yametoka kwenye baadhi ya hayo mashirika mengine ambayo yamehamia STAMICO, lakini Serikali haionyeshi njia ya ku- clear hayo madeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni ukosekanaji wa uwekezaji wa tija kutoka kwenye makampuni ya ubia tuliyonayo na hapa na-cite mfano wa TBC na Star Media, hii Star Media imekuwa ikijiendesha kwa hasara tangu ianze 2009 hapa Tanzania. Nakumbuka nilivyokuwa PIC Bunge la kumi tulihoji sana juu ya hii Star Media, lakini ukiangalia na ripoti yetu leo inaonyesha Star Media ilianza kwa mtaji wa milioni 238 ambayo ni takribani bilioni 547 za Kitanzania mwaka 2009. Walisema kwa business plan yao ikifika, ile business plan 2009 - 2014 wangeanza kutoa gawio kwa wanahisa lakini imekuwa kinyume ina-operate under loss, ripoti imeainisha kabisa, 2014 walipata loss ya bilioni 6.8; mwaka 2018 ilipata loss ya bilioni 19. Cha kushangaza mtaji mwaka 2009 ulikuwa bilioni 547, 2018 mtaji ni half wa bilioni 119, lakini bado tunaendelea kukumbatia Star Media kwamba ni shirika mbia na cha kushangaza hii Star Media ukitaka kuundwa hata Kamati Teule kufuatilia, unazuiliwa kwamba sijui kuna mambo nyeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliwaita Kamati ya PAC hawakutokeza, tunataka tujue kuna nini nyuma ya Star Media, fedha za Watanzania asilimia 35 tumewekeza pale kama wabia, tunataka kueleza Watanzania ni kwa nini huu mkataba hausitishwi ili tuweze kujua tuanze upya au tuachane nao? Huwezi kuwa na mbia ambaye ana-operate under loss. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine na mbaya zaidi Star Media, CAG walifanya ukaguzi 2014/2015; 2015 walivyotaka kufanya ukaguzi wakakataa kutoa nyaraka, lakini CAG aliainisha madudu zaidi ya 34 kwenye Star Media. Kwa hiyo tunaiomba sana Serikali kama hamna kitu nyuma ya pazia ambacho mnakijua, tunaomba huu mkataba uwe reviewed na uvunjwe kwa sababu tayari wameshavunja makubaliano kwenye MoU kwa kutoweza kutoa hiyo faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni hoja ya kuhusiana na kukaimu tumeona na tumeshuhudia watendaji wanakosa mamlaka kamili ya kufanya decision kwa sababu unamkuta mtendaji anakaimu zaidi ya miezi 30, sheria inasema miezi sita kama umemkaimisha miezi 30 ina maana huyu mtendaji anafaa kuidhinishwa ili aweze kufanya maamuzi kamili akijua yeye ni CEO wa kampuni fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia kuna madeni mengi sana Serikali inadaiwa na hayo mashirika au taasisi. Kwa mfano tumeona ALAF wanadai bilioni 3.94 kutoka TBA kuanzia 2017, TRA wanadaiwa VAT fund na ALAF ambayo ni mbia mwenza wa Serikali bilioni 15. Sasa nyie mnadaiwa VAT fund bilioni 15 na siyo ALAF tu hawa ata ma development partners nao wengi wanadai kwamba wanadai billions of money kutoka Serikalini. Halafu mkija hapa mnasema makubwa, rudisheni kwanza hiyo VAT fund kwa wanaohusika halafu ndiyo mje mtupe tathmini halali ya makusanyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anadai bilioni 15 mnategemea ata-operate vipi hii kampuni.

MHE. HALIMA MDEE: Wapigaji!

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, na hii ni kampuni moja tu, Serikali jamani tuache upigaji watu wanajua kwa sababu hamrudishi VAT funds.

MHE. HALIMA MDEE: Wanapiga kwa staha.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo AICC nayo inadai zaidi ya bilioni tatu kutoka Serikalini na mashirika lakini na taasisi nyingi sana zinadai wanapotoa huduma Serikalini hawalipwi. Msipowalipa hawa wanashindwa kujiendesha na kukosa ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine napongeza kabisa mashirika yanapotoa gawio lakini nasikitika kwa mashirika ambayo yanakuta yanaomba mitaji lakini na yenyewe yanatoa gawio kama STAMICO. STAMICO anajiendesha kwa hasara lakini tulishughudia ikitoa bilioni moja Serikali. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther malizia.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile vyuo vikuu na wengine eti wanatoa michango kama UDSM, UDOM, UCLAS, VETA ni kama vile tunaweka kahela halafu baadae tunakazungusha kwa mgongo wa nyuma kanarudi tena. Siyo sahihi ni kama unakunywa uji wa mgonjwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo pamoja na kwamba tuna-encourage watu watoe ile asilimia 15 ya michango na gawio lakini tuangalie zile ambazo zinatoa huduma per se. Kwa mfano UDSM au vyuo vikuu vingine ambavyo ndiyo vinatutolea, tunazalisha pale watu ambao wanakuja wataalam kwenye nchi yetu tena wenyewe wanataka tena waje pale watoe 15 percent na unajua Serikali ndiyo wanaleta hapa ndiyo tunawapitishia votes zao. Siyo haki ni kama vile tunacheza viini macho mbele ya macho ya watanzania, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia Wizara hii juu ya mambo muhimu matatu yanayohitajika ndani ya Wilaya ya Tarime na hasa Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Tarime kwa kiasi kikubwa haijapimwa. Mfano, Halmashauri ya Mji wa Tarime kwenye kata nane, ni kata mbili tu ndiyo zimepimwa. Hilo eneo lingine halijapimwa licha kuwa sasa hivi vijiji na vitongoji vyote vimekuwa mitaa na tuna idadi ya mitaa 81. Hivyo upangaji wa mitaa ni muhimu na uhitaji wa kupanga mitaa ni lazima ili tuweze kupima viwanja na kupandisha thamani ya ardhi yetu. Tunaweza kutumia ardhi ile ili kukopa katika taasisi za kifedha; vilevile mji ukipangwa vyema utavutia wawekezaji mbalimbali kuja katika Halmashauri yetu na kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kama vile viwanda, ufugaji, uwekezaji kwenye majengo ambapo tunahitaji strategic master planning ya mji wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa ni Kata ya Bomani kwa sababu tu ndiyo zimepimwa. Tunahitaji upimaji wa haraka kwenye Kata za Turwa, Nyamisangura, Nkende, Kenyemangori, Ketare na Nyandoto ziweze kupimwa ili kuweza kuruhusu utoaji mwingine wa huduma za kijamii kama umeme, barabara, shule, vituo vya afya, vituo vya biashara, maeneo ya viwanda na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama za upimaji wa ardhi ni ghali sana kwa Mtanzania wa kawaida kuweza kumudu, maana ni kuanzia shilingi milioni moja na kuendelea. Vilevile taratibu hizo zinachukua muda mrefu sana na zina mlolongo na urasimu. Hivyo tunaomba sana upimaji wa viwanja kwenye Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kipindi cha mwaka huu. Hii itaweza kupunguza kasi ya migogoro kama ule uliopo kwa wananchi wa Mtaa wa Mafarasini, Kata ya Bomani ambapo walipimiwa ardhi kwa ada (gharama) ya shilingi 20,000, shilingi 40,000, shilingi 70,000. Cha kushangaza baada ya muda Serikali inawaambia walipie tena upya gharama za kumiliki ardhi kuwa ni kuanzia shilingi 2,000,000 na kuwaambia kuwa wanaoshindwa kulipia gharama hizo watanyang‟anywa ardhi hizo na kupewa wenye uwezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili halikubaliki kwa maskini wale waliomilikishwa ardhi kwa kufuata sheria na walilipia. Iweje leo tena mnawapoka? Hadi sasa wananchi hawa wa Mafarasini wanashindwa/huogopa kuendeleza makazi yao kwa kuhofia kupokwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu nyingine ni juu ya waraka ambao umetoka Serikali Kuu (Wizarani) kwenda kwenye Halmashauri ya Mji ikitaka kutokutumia matumizi ya ardhi pale inapoona inafaa. Hili kiukweli limekuwa kikwazo kikubwa sana na ukizingatia Halmashauri yangu ni changa na hivi katika upangaji wa mji kuna maeneo yanaweza kubadilishwa matumizi ili yaweze kutumika katika shughuli za kijamii kama vile mashamba na hata viwanja vya michezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inarudisha nyuma maendeleo ya Tarime Mjini. Mfano Ofisi ya Mbunge iliandika barua kwenda Halmashauri ya Mji kuomba eneo ambalo litatumika kujenga maktaba ya umma ambayo itasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wetu. Vilevile kuongeza idadi ya Watanzania wanaosoma vitabu ili kupanua uelewa. Cha kushangaza na kwa masikitiko, Mkurugenzi wa Halmashauri wa Mji kasema kwamba Serikali imezuia ubadilishwaji wa matumizi ya ardhi. Hii inarudisha nyuma maendeleo ya Tarime Mjini. Naomba Wizara ione umuhimu wa kupatiwa eneo la kujenga maktaba ambayo ni muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ni tatizo sugu ni juu ya kucheleweshwa kwa malipo ya fidia kwa wananchi ambao ardhi yao imepokwa na JWTZ. Wananchi hawa walifanyiwa tathmini tangu mwaka 2012 hadi leo hawajalipwa na walizuiliwa kufanya shughuli za maendeleo tangu mwaka 2007 na wakapora hadi mkataba wa mnara wa Airtel, kinyume kabisa na sheria za nchi hii. Je, katika tathimini itakayofanywa tena itafidia mkataba wa mnara pamoja na uhalisia wa mali tangu mwaka 2007? Kutakuwa na riba?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nawataka Serikali imalize malipo ya Ranchi wa Ronsoti, Msati (Nyamisangura) Kenyambi (Nkende) na nyinginezo. Ni aibu kuwapoka wananchi ardhi kinyume na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 lakini mkashindwa kulipa fidia. Vilevile Serikali ione umuhimu sasa ya kuhakikisha Bodi ya Mifuko ya Fidia inaundwa mwaka huu ili tuepushe ucheleweshaji wa malipo ya fidia. Tunaomba NHC waje kuwekeza Tarime, maeneo tutawapatia ili kuweza kupunguza adha ya malazi na kukuza mandhari ya mji wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile fidia za wananchi wa Nyamoyo ambao walifanyia tathmini tangu mwaka 2011/2012 waweze kulipwa fidia zao maana waliondolewa na kwenda kutafuta makazi mengine ambapo ilibidi wakope fedha benki waweze kuanzisha makazi mengine. Hivyo wameshindwa kulipia mkopo na kubaki na adha kubwa sana. Hawa sasa ni wakazi wa mji wa Tarime, hivyo tufuate Sheria za Ardhi bila kunyanyasa Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inachukua muda mrefu kweli kurejesha retentions katika Halmashauri husika, mfano Halmashauri yangu ya Mji wa Tarime ambayo haina mapato ya kutosha. Hivyo hizo fedha za upimaji ardhi ni vyema ziwe zinapelekwa mapema kuliko kucheleweshwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kuwasilisha.
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nami naomba kuchangia Mpango wa Tatu wa Maendeleo. Ni dhahiri kwamba kitu na jambo la muhimu sana ambalo Serikali ingeanza nalo ni kushughulika na suala zima la mikopo ya Elimu ya Juu. Nimekuwa nikisema hili na nitarudia kusema tena kwa sababu tumeshuhudia wanufaika wa mikopo hii wanapata adha kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, tunajua kwamba Serikali inatakiwa kuwekeza kwenye elimu ambapo inatakiwa hata itoe elimu bure kwa watu wetu wa Vyuo Vikuu ili waweze kupata ujuzi ambao utaweza kutumika kwenye Sekta ya Umma, Sekta Binafsi na hata wengine waende nje kama ma-expert, kama vile ambavyo tunaleta watu kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, kwa jinsi ilivyo, Sheria ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Mwaka 2004 ambayo tuliifanyia marekebisho mwaka 2016 ni kandamizi. Hata kwenye ripoti ya CAG ametaja upungufu wa kisheria na kimfumo kwenye ukusanyaji wa haya madeni kwamba yanazidi uwezo ya walipaji. Tumependekeza na Waheshimiwa Wabunge wengi wameonyesha hii adha.

Mheshimiwa Spika, napenda kujielekeza na kuiomba Serikali ifanye marejeo; kufanya makato ya asilimia 15 ya mshahara ghafi wa huyu mfanyakazi ni kubwa sana. Tumesema mara nyingi hapa kwamba huyo mfanyakazi anakatwa asilimia 15 ya mshahara ghafi, anakatwa asilimia 10 ya mifuko ya jamii, anakatwa Pay As You Earn, anakatwa Bima, kuna wengine wana michango mingine, mwisho wa siku unakuta huyu mfanyakazi habaki na chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia ile penalty ya asilimia 10 ambayo ameiweka baada ya maturity ya miezi 24 ni kandamizi. Ambapo amesema mnufaika baada ya miaka miwili kama hana kazi anatakiwa atoe shilingi 100,000/=, short of that anakuwa na penalty ya asilimia 10. Hii mikopo tunaipitisha humu ndani inaenda, is a Revolving Fund; kwa nini muweke hizi tozo kama vile ni riba za mabenki? Isitoshe wameweka na six percent ya kutuza thamani ya fedha (retention). Huku kote ni kumkandamiza mnufaika ambaye ni huyu mtoto wa masikini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni rai yangu Serikali iangalie, hapa hatufanyi biashara, after all hii mikopo tunayotoa ni kodi zetu; hizi za Watanzania sisi masikini ambao tunatoa. Tuhakikishe: mosi, tunawapa Watanzania wote wenye hadhi ya kupata mikopo na wengi wao mayatima na bado wanafurahia masikini, wanapata hii mikopo. Hii mikopo iwe reduced kutoka 15 Percent ije kwenye single digit 5 mpaka 8 ili tuweze kuwasaidia hawa Watanzania masikini. Kwa hiyo, ije sheria hapa, tumesema na tumeomba, wasipoleta natangaza rasmi, ninaandaa Muswada Binafsi wa Sheria wa Mikopo ya Elimu ya Juu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ni kwenye Utawala Bora. Mmetaja hapa kwamba moja ya kiashiria cha utekelezaji wa mpango huu ni Utawala Bora. Hata hivyo ukiangalia kwenye Sheria ya Utakatishaji Fedha, kifungu namba 12, 13 na 14 vinatumika vibaya na vinakandamiza sana Watanzania hawa. Hasa tukichukulia mfano kifungu 12 (a) ambacho kinasema mtu yeyote ambaye atajihusisha na muamala ambao una viashiria vya utakatishaji wa fedha ama kwa kujua au kwa kutokujua anakuwa amekosa na anaenda jela.

Mheshimiwa Spika, ameeleza hapa Mheshimiwa Judith kwamba unakuta wengi wanakumbwa wanaenda bila dhamana. Inabidi tutambue kwamba uchumi wetu kwa Tanzania kwa asilimia kubwa unatumia fedha taslimu siyo cash less. Is not a cash less economy. Kwa hiyo, kama ni fedha taslimu, kwa mfano mtu anakuja kwangu, anataka kununua nyumba, ana hela zake, nitajuaje kama hizi hela anataka kutakatisha fedha haramu ambazo amepata somewhere else?

Mheshimiwa Spika, au tukichukulia mfano wa kule kwetu Kijijini Nyanchabakenyi, huyu mtu amepeleka ng’ombe zake kwenye miradi ya Kenya, Mabera kule kwenda kuuza ng’ombe zake 80, anarudi na mfuko wa milioni 100, ikitokea amekamatwa anaambiwa anatakatisha fedha. Kule tunajua kwenye minada hatuna mabenki wala mawakala, hatuwezi kufanya transaction huko, lazima azibebe na akiwa na knowledge aje sasa aziweke kwenye benki; asipokuwa na hiyo knowledge, ataenda kuweka ndani kama alivyosema Mheshimiwa Waziri kwamba watu watoe fedha ndani wazipeleke kwenye mabenki. Ila akikamatwa anakuwa liable kwa that.

Mheshimiwa Spika, kuna mfano mwingine ambayo ni hai. Nilivyokuwa Segerea, kuna wadada walikuwa kule, wamekuja kwa kosa la kutakatisha fedha miaka saba. Wawili; kulikuwa kuna mtu aliyekuwa ni mfanyakazi wa umma, sitamtaja, kumbe amechukua fedha ya mishahara hewa huko, ana girl friends amewaingizia kwenye account as normal transaction. Hao nao wakakamatwa, wamekaa Segerea seven good years, pamoja na mke wake kwamba wametakatisha fedha. Wameachiwa muda siyo mrefu kama miezi mitatu nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii sheria ni kandamizi sana, lazima ifanyiwe review ili tusiweze kuwanyanyasa hawa Watanzania, tuwe na utawala bora tuweze kutekeleza huu mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine ni kwenye Sera ya Fedha na mifumo ya kibenki. Tunajua kabisa kwamba utekelezaji wa mpango huu na ushiriki wa sekta binafsi kwa kiasi kikubwa katika Taifa letu hutegemea Sera ya Fedha na mipango na mifumo yetu ya kibenki. Sote tunajua riba za mikopo kwenye mabenki yetu ziko juu sana; sixteen percent, nyingine seventeen; hizi zimekuwa kandamizi ukilinganisha na nchi nyingine, unakuta ni less than ten; single digit; 3,4,5,6. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kikubwa kupitia Sera ya Fedha, Benki Kuu ilishusha kiwango cha dhamana kutoka 12% mpaka 6%. Cha ajabu mabenki yetu ya ndani yameshusha kutoka 17% mpaka 16.3% tu. Mbaya zaidi, hata kwenye mikopo ambayo ni risk free; kwa mfano, mikopo ya wafanyakazi ambayo marejesho yao yanatokana na mishahara, bado na wenyewe wanakatwa 16.5 percent to 17 percent. Huu ni ukandamizaji.

Mheshimiwa Spika, tunaomba sana, kama kweli tunataka utekelezaji wa mpango uende vizuri na kuweza kuhakikisha kwamba sekta binafsi inashiriki katika utekelezaji wa mpango huu, Serikali ihakikishe inaingilia kati na kuhakikisha kwamba viashiria vyote ambavyo vinapelekea kuwepo na hizi riba kubwa pamoja na kushushwa kiwango cha amani cha Benki Kuu kinapungua au mojawapo unakuta haya mabenki yanajiendesha, kuna gharama kubwa nyingine zinaweza kuepukika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunashuhudia pia utolewaji wa mikopo ambayo haifuati utaratibu, inayoongeza kiwango kikubwa cha mikopo chechefu ambayo wanashindwa kui- control, kwa sababu mzigo unakuja kwa Watanzania hawa wengine wa chini. Kwa hiyo, ili tuweze kuwa na sekta binafsi nyingi na shiriki, napenda Serikali iingilie kati kuhakikisha kwamba riba za mikopo ya mabenki zinaenda chini.

Mheshimiwa Spika, kingine ni usimamizi wa kodi. Tunajua kabisa kwamba haki ni wajibu. TRA wana wajibu wa kukusanya kodi, nasi wananchi tuna wajibu wa kulipa kodi, lakini kumekuwa na tatizo kubwa la muda mrefu. Malalamiko ya marejesho ya kodi ya ongezeko la dhamani, nina maana VAT. Kwa mfano, mwaka 2020 nilivyokuwa kwenye PAC, Kamati yangu ilitembea mashirika mbalimbali, madhalani ALAF; walikuwa wanalalamika wanaidai Serikali zaidi ya shilingi bilioni 17.

Mheshimiwa Spika, nilivyokuwa nashiriki kwenye Kamati ya UKIMWI, taasisi mbalimbali zilikuwa zinalalamika kuhusiana na hii VAT kurejeshwa; na wakienda kuomba, TRA wana-order kwenda kukagua ili kuona kama kuna kosa lolote waweze kufidia zile fedha zinazodaiwa za Kodi ya Ongezeko la Thamani. Wakikosa kupata kosa lolote, wanaendelea ku- delay. Ukienda kukumbushia, wanakuja tena kukagua. Kwa hiyo, inaenda kwenye cycle hiyo, wanakutafutia kosa ili kuweza kufidia hiyo tozo la Ongezeko la Thamani. Hiyo siyo haki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine ni hili sharti la moja ya tatu ya kodi ambayo umekadiriwa. Ikitokea Mtanzania amekadiriwa; na kuna cases umekadiriwa shilingi bilioni tisa, umeweka pingamizi kwamba mlivyokadiria sivyo, wanakwambia, toa moja ya tatu. Moja ya tatu ya bilioni tisa is almost bilioni tatu. Unazitoa wapi wakati unajua labda hukuwa liable kulipa tu; kulipa labda shilingi bilioni moja au shilingi milioni 500 umeandikiwa shilingi bilioni tisa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hizi zote lazima ziweze kufanywa review ili tuweze kuwa na harmonization ya wawekezaji, kuvutia wawekezaji wengi waje Tanzania. Kwa hali hii hatuwezi kuvutia wawekezaji kuja Tanzania. Pia wale ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi, hawatapata mvuto na mwamko wa kutaka kwenda kwenye sekta rasmi kama kuna bureaucracy hizi zinazoendelea katika mfumo wote wa kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine na cha mwisho ni hili la Bandari ya Bagamoyo, limeshika kasi sana kwenye mijadala na ambalo lina tija kwa Taifa letu. Nadhani kama Taifa tujiuleze na tutafakari. Tuangalie kama project ya Bagamoyo is it viable? Ina tija? Kama ina tija, ni nini cha kufanyika? Tusikae na kuji-bide; naangalia mijadala mingi inaenda, ooh masharti yalikuwa makubwa na vile.

Mheshimiwa Spika, kama Taifa lazima tuangalie, kama project ina tija, hatujabanwa kwamba twende na huyo mwekezaji. Tukiona project ina tija, tunaweza tukatangaza tenda tena, kama kuna mwekezaji ambaye anaweza kuja kutaka kuchukua ile bandari kwa manufaa mapana; au Serikali tukaenda through PPP kuweza kujenga ile bandari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine nimejaribu tu kuangalia, narudia tena kusema, bado sijafanya tafiti ya kutosha. Ukiangalia Bandari ya Dar es Salaam, kwa mwaka ina uwezo wa only seventeen million metric tons, tunajenga SGR. Bandari ya Dar es Salaam pale ilivyo haina uwezo wa kupanuka zaidi, lakini kule Bagamoyo already zimeshatumika twenty-seven billions za Watanzania kulipa fidia. Kupitia Special Economic Zone almost over thousand viwanda vinatakiwa vijengwe kule.

Mheshimiwa Spika, sasa tuangalie tija, tufanye cross benefit analysis; tukiona kama Taifa kuwekeza Bagamoyo kuna tija, twende, hatujafungwa na huyo mnayemwita the so called Mchina. Tuna wataalam wa kutosha, waende wafanye tafiti za kina kule Bagamoyo, tukijenga bandari kama Taifa, tunaenda kupata faida ipi? Je, masharti yaliyowekwa kwa huyo mwekezaji wa mwanzo ambayo mmesema ni magumu, tuyachambue tuone masharti ambayo ni rahisi, tunapotangaza tenda sisi ndio tunashikilia ni yupi mwekezaji ambaye anakuja na tija akiwekeza hapa kama Taifa tutanufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kinyume cha hapo, una mamlaka na Bunge lako hili. Kama mikataba ipo, kuna Kamati Maalum ya Miundombinu, unaweza ukai-task ikaenda kufanya kwa niaba ya Taifa letu kuona kama huo mradi ni viable kwa Taifa au la.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nami napenda kuchangia kwenye Wizara hii ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambayo ni wizara muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu. Nitajielekeza sana kwenye elimu na ni dhahiri kwamba kupitia elimu bila ada udahili wa wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari umeongezeka, lakini kunakosekana mpango mkakati wa kuhakikisha kwamba kunatolewa elimu bora. Nitaenda kuainisha baadhi ya maeneo. Tumeshuhudia kuwepo kwa uhaba wa Walimu ambazo ni inputs nzuri sana kuhakikisha kwamba tunatoa products au output ya vijana wetu wenye elimu bora. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uhaba wa Walimu mathalani kwa Mujibu wa BEST 2020, takriban walimu 50,000 kwa shule za msingi. Waliopo 191,000 na kitu na tunaambiwa hapa na waziri amesoma tuna wanafunzi milioni 11. Hasa unaweza ukaona Walimu waliopo wanaweza kukidhi kweli kufundisha kwa ikama inavyosema Mwalimu mmoja angalau kwa wanafunzi 45, unakuta wanaenda zaidi ya hapo. Tunajua kwamba kila mwaka au kila mwezi, kuna ambao wanafariki, wengine wanaacha kazi ya ualimu wanakwenda kwenye kazi zingine na huko nyuma waliondoa wa vyeti fake, lakini replacement katika kuhakikisha kwamba Serikali inakuja na mpango mkakati kuajiri Walimu wa kutosha ili kuweza kutatua changamoto ya Walimu haipo. Unakuta shule moja huko vijijini kuna Walimu sita, wawili, watano, wanafunzi 800 it’s quite unfair. Kwa hiyo hapa, niseme hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Walimu hao pia ni dhahiri kwamba Walimu pamoja na kwamba wanakuwa na workload kubwa sana, lakini wana mazingira magumu sana, sana. Hawana nyumba, haa kama wamesema wanajenga hapa, lakini Walimu wengi hawana nyumba, lakini mazingira ya kufundishia pia ni magumu, wengine wanakaa kwenye miti, hawana ofisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia hawajapandishwa madaraja na kulipwa mishahara kwa muda mrefu kwa kipindi cha miaka mitano yote, wanatoa wapi motisha. Nikawaza sana, hapo zamani Walimu walikuwa na hardship allowance 150,000 I think, kama yalivyo kwenye upande wa majeshi, tufikirie sasa Walimu ni kada moja muhimu ambayo inaelimisha wanafunzi wetu. Tufikirie kurudisha hii angalau kuweza kuwapa motisha Walimu wetu, tuwape kila mwezi, katikati ya mwezi na wenyewe waweze kupata ile 150,000 ambayo walikuwa wanapata as a flat rate ili kuwapa motisha zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kingine ambacho nazungumzia kama kichocheo cha kuhakikisha tunapata elimu bora; miundombinu ya kujifunzia wanafunzi wetu. Madarasa yameendelea kuwa na uhaba sana. lazima tuje na mpango mkakati, tusikae kwa kusubiria matakamko, maana hapa juzi kati niliona Ubungo huko shule moja sijui inaitwa King’ong’o, ilitokea tafrani fulani wakaandika katika mitandao na nini, hayati akatoa tamko, within a week or two tunaona shule imekamilika. Sasa lazima Wizara ije mpango mkakati iwekeze kuhakikisha inatatua tatizo la madarasa nchi nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukipitia ripoti ya CAG, ameainisha pale kabisa kwamba uhaba wa madarasa out of eleven million or so wanafunzi, zaidi ya wanafunzi milioni tano point something hawana madarasa, kwenye ripoti ya CAG imeonesha. Vile vile hata miundombinu ya vyoo, ripoti ya CAG again nai-quote, imeonesha kabisa kwamba takriban wanafunzi 6,150,000 hawana matundu ya vyoo. Sasa bila hivi unakuta shule zetu zingine zinapelekea kufungwa. Hatuwezi kukaa tukasema tunatoa elimu bora while hatuna mazingira wezeshi kuhakikisha kwamba hii elimu bora inapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, madawati, bado ni tatizo. Wanafunzi wanakaa kwenye mawe na hii ripoti ya CAG ime- quote walivyofanya ripoti ya ufanisi katika shule hizi, 1.1 wanafunzi wanakosa madawati. Tumesema elimu bila ada lakini unakuta wazazi wanachangishwa sana, anachangishwa kupeleka madawati, anachangishwa ajenge miundombinu ya darasa, ifike kwenye rental, anachangishwa hela ya mlinzi, anachangishwa 1,000 au 2,000 kuweza kulipwa Walimu wa ziada kufundisha wanafunzi wetu. So, it’s a burden, kama nchi lazima tujitoe. Wizara hii ikiamua kujitoa pamoja na Wizara ya Elimu tuwekeze, mbona kwenye uchukuzi tumeweza! Tunawekeza kule trillions of money, hebu sasa tuwekeze kwenye elimu, once and for all tuwe na Walimu wa kutosha, tuwe na madarasa ya kutosha, tuwe na maabara ya kutosha, tuwe na vyoo vya kutosha vyenye umeme, we are in science and technology era, tuwe na umeme kwenye mashule yetu, tuweze kuwa na computer and so called, tuweze kuwa na maji, vinginevyo hatutaweza ku-move popote kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine, kwenye elimu hapo hapo; ukiangalia NECTA kweli kupitia udahili huu, ukiangalia matokeo utasema ufaulu umeongezeka, lakini kiuhalisia ukiangalia tathmini ubora wa elimu unazidi kushuka. Ukiangalia watoto wanaofaulu kwa rank ya Division IV and Division. 0 ni wengi sana. Kuna tathmini imefanyika mathalani for last 10 years, Division 1 – 3 ni only 36%, the rest wanakuwa below that, sasa hatuwezi kukaa hapa tukasema tumejenga madarasa kweli, tume-enroll watu wengi shule ya msingi kupitia elimu bila ada lakini output out of it kama Taifa tunapata nini. Lazima tuangalie hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye quality assurance; udhibiti ubora wa elimu zetu, imekuwa ni kitendawili, bila kuwa na kitengo ambacho kinakuwa well equipped na human resources kwa maana Wadhibiti Ubora, kinakuwa well equipped na bajeti ya kutosha, hatuwezi kuwa na elimu bora. Nimejaribu kuangalia pale kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Wadhibiti Ubora by then walikuwa 1,081 tu, mahitajio yalikuwa 1,541, deficit ya 460. Hata hivyo Bunge hili Tukufu limekuwa likipitisha hapa fedha; 2018/2019 tulipitisha 1.5 billion, kwa ajili ya hii Idara ya Udhibiti Ubora, lakini hakuna hata senti tano ambayo ilikwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka 2020/2021 Bunge lako liliidhinisha billion 25 kwa ajili ya kuimarisha Idara hii ya Udhibiti Ubora, lakini mpaka Machi by then 2020 hakuna hata senti tano imekwenda out of this 25 bilion. Kwa hiyo, tumeidhinisha hapa, nothing is being done, kama hakuna Wadhibiti Ubora wa kwenda kuhakikisha kweli elimu inayotolewa ni bora, tunafanya mark time tu kama Taifa. Kwa hiyo tuhakikishe tunawapeleka Wadhibiti Ubora wa kutosha, tuhakikishe tunaweka bajeti ikipitishwa hapa inaenda, kuhakikisha kwamba wanapata miundombinu imara kwa maana ya magari na kila kitu kwenda kufanya ukaguzi huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, muda unaenda, lakini kingine ambacho nilisema nitagusia, ni hili suala la elimu jumuishi kwenye shule zetu. Limekuwa likiongelewa hapa nashukuru wame-quote, kwa hiyo shule zetu hizi lazima pia tuwe na miundombinu rafiki ambayo inawezesha wenzetu mathalani wenye ulemavu kuhakikisha kwamba na wao wanapata elimu stahiki. Kama tunajua tuna shule na zingine zinachangamana kwa mfano shule ya msingi pale Buhemba Tarime, inachangama na watu wenye ulemavu. Wengine wenye uono hafifu, usikivu na watu wenye ulemavu wa akili, unakuta wapo pale, lakini Serikali haipeleki Walimu wa kutosha, haipeleki miundombinu stahiki kwa hao watu ili na wenyewe waweze kupata elimu kama wenzao wanavyopata. Pia hata miundombinu hii tunayojenga, mathalani kwa watu wengine wenye ulemavu haina zile njia za kupita wao, kuhakikisha kwamba huyu mtu mwenye ulemavu anaweza kuwa-accept. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia katika shule za msingi na sekondari, watoto wa kike wengi wanaacha kwenda shule between four to five days mpaka six days wakiwa wameingia kwenye menstrual period, wanashindwa kuwa na usaidizi mathalani, anashindwa kuwa usaidizi na hili tumelipigia sana kelele Mheshimiwa Ummy Mwalimu anajua tangu akiwa Waziri wa Afya unajua. Tunataka kujua katika ile ruzuku ambayo inakwenda angalau waweze kutenga extra, waweze kuainisha, mathalani katika shule ya msingi wanajua watoto waliofikia umri wa kwenda kwenye hii kitu wako labda 200 au sekondari wako wangapi, waweze kupeleka extra katika hayo. Pia na hao watu wenye ulemavu waweze kuwa wanaongeza ku-catch hiyo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Dakika mbili Mheshimiwa Spika nimalizie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, dakika mbili tu. Katika hili la ruzuku ya 10,000 tumekuwa tunashuhudia inabaki 4,000 kama retention ambayo inatakiwa Serikali inunue vitabu, lakini for right four years haijawahi kupeleka hivyo vitabu na ukifanya calculation, nilikuwa nafanya haraka haraka hapa, kwa mwaka wanabakisha over 44 million, kwa miaka mitano karibu milioni 220. Tukienda mashuleni, tunaona bado kuna uhaba wa vitabu kwa hawa wanafunzi. Kwa hiyo kama Serikali wakibakisha hizo fedha wanaona ni ngumu kupeleka, bora ziende kule, Mwalimu husika aweze kuwajibika kuweza kununua hivyo vitabu kuliko kubaki huko Serikalini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuweza kunipatia fursa hii na mimi niweze kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza kwanza kwa kupitia utekelezaji wa bajeti ambayo tunatenga kwenye Wizara hii muhimu. Pamoja na unyeti na umuhimu wa Wizara hii kwa miaka yote tumekuwa tukitenga bajeti lakini haziendi kwa ukamilifu. Kwa mfano mwaka 2015/2016, Fungu 57 – Wizara ilitengewa shilingi bilioni 220 fedha ya maendeleo, lakini ilipokea shilingi bilioni 40 tu, sawa na asilimia 18; Fungu 38 – Ngome, tulitenga na kuidhinisha shilingi bilioni nane, hawakupokea chochote; Fungu 39 – JKT, tulitenga shilingi bilioni nne, hawakupokea chochote.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016/2017 zilitengwa shilingi bilioni 230 Fungu – 57 wakapokea shilingi bilioni 34 tu, sawasawa na asilimia 15; Fungu 38 tulitenga shilingi bilioni 10 wakapokea bilioni moja tu, sawa na asilimia kumi, za maendeleo hizi. Fungu 39 tulitenga bilioni nane wakapokea bilioni moja, sawa na asilimia 12.5.

Mheshimiwa Naibu Spika, 2019/2020 tulitenga shilingi bilioni 220 Fungu 57, shilingi bilioni nane Fungu 38 na shilingi bilioni sita Fungu 39. Lakini mpaka ile Machi hawakutoa taarifa yoyote kwenye hili. Lakini tumeona 2021/2022 utekelezaji wake nao unasuasua.

Mheshimiwa Naibu Spika, hizi ni fedha za maendeleo, na kwa nini nimeamua kufanya hii rejea; kwanza hata fedha ambazo tunapeleka ni ndogo sana. Ametoka kuchangia hapa Mheshimiwa Mwijage, Jeshi la Wananchi wa Tanzania na JKT kwa unyeti wake Jeshi la Wananchi wa Tanzania kulinda mipaka ya nchi dhidi ya adui kutoka nje, lakini pia Jeshi hili ni mbadala kwa nchi yetu pale ambapo inapata mkwamo kwenye sekta zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, inatakiwa Jeshi hili tuliwezeshe liweze kufanya tafiti za kina, liweze hata kufanya ugunduzi wa mambo mbalimbali, mengine ambayo hatuhitaji kuyajua ambayo yanaweza yakaisaidia nchi yetu kukwamuka kiuchumi. Lakini kwa fedha ambazo tunatenga ndogo na hatupeleki hatuwezi kufika popote.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii hili Jeshi haliwezi hata kujenga maabara ya kisasa yenye teknolojia za kisasa za kuweza kufanya huu utafiti na kuweza kujihakikishia kwamba kama nchi wanaweza ku-counter any crisis ambayo inakuwa imetokea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mathalani, dunia na sisi nchi tuko kwenye hili gonjwa la Covid-19. Kama kweli hili Jeshi tungekuwa tunaliwekeza, ndiyo maana hawa ndugu zetu wako pale kulinda mipaka ya nchi na vitu kama hivyo, yaani hawatumiki 24/7 kama ambavyo majeshi mengine yanafanya, lakini wangeweza kujiwekeza kwa kina kuweza hata kufanya tafiti za kina, wana madaktari wakaweza kugundua dawa ya Covid, wakaweza hata kugundua chanjo tukaachana na ma-debate ya kusema nchi za nje zinaleta chanjo ambazo zinaweza zikatuathiri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ikitokea Jeshi wakabobea kwenye sekta zote, mathalani siombei, unatokea mgomo wa madaktari nchi nzima, hawa wanajeshi wetu wanaweza waka-counter kuweza kuhakikisha kwamba Watanzania hawawezi kufariki pale ambapo wanaendelea kupata matibabu pale ambapo unatokea mgomo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine tunaona nchi kama Marekani, wanajeshi wale na nchi nyingine; mimi kuna kipindi nilikuwa nanunua blackberry wameandika research in motion. Zile ni tafiti ambazo zinafanyika na wanajeshi wa Kimarekani. Lakini pia kuna wanajeshi wa nchi mbalimbali, Mheshimiwa Mwijage hapa amelalamika kuhusu Nyumbu, sasa Nyumbu itawezaje kujikwamua wakati hata haipelekewi fedha za kutosha? Tunahitaji ku-invest kwenye Jeshi la Wananchi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapo hapo kwenye utekelezaji hafifu wa fedha za maendeleo, kunasababisha kuendelea kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na wananchi ambao wamechukuliwa ardhi ile. Imechukua miaka mingi sana, ni kwa sababu tunapitisha fedha hapa, kwenye vitabu ina- reflect kwamba wanakwenda kupeleka kulipa fidia, lakini miaka inakwenda wananchi hawalipwi fidia na tunajua ndugu zetu hawa wanajeshi, hawatakiwi mtu kukatiza kwenye kambi yao, ukikatiza unapewa adhabu kali sana, utalimishwa, utarukishwa kichura na vingine, ndiyo hivyo caliber ilivyo. Sasa unakuta wakati mwingine wamechukua maeneo ambayo yako kwenye maeneo ya raia ambako watakuwa wanapita.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano mgogoro ulioko Tarime wa Jeshi la Wananchi pamoja na wananchi wa Kenyambi na Bugosi wa Kata za Nkende na Nyamisangura, tumekuwa tukiongea hapa, wanajeshi walikuwa kwenye kambi yao Nyandoto lakini kuna kipindi yalitokea mafuriko wakakaribishwa huku ni kweli, kwa sababu walikuwa hawawezi kupita kipindi hicho hakukuwa na miundombinu, walivyokuja huku wakaamua kuchukua ile ardhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tangu Bunge la Kumi, mwaka 2010, nazungumzia hili suala; pale walipo ile kambi iko katikati ya mji kabisa. Kwa hiyo raia wakipita, kuna wengine wanapita wanakwenda Kata za Bumera au Susuni, kuna wakati wakikatiza pale raia wanachukuliwa wanapewa adhabu za kulima kwa sababu wamekatiza kwenye kambi. Tukasema basi kama wameamua kutwaa ile kambi wawalipe fidia stahiki hawa wananchi kwa wakati; ni zaidi ya miaka 17 sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya mwaka jana na mwaka juzi Serikali ilipitisha hapa ikasema inapeleka fidia, tayari wameshatenga fedha, nikshika mpaka na shilingi, ambaye sasa hivi ni Makamu wa Rais ikawa imeshapita wakasema wame-underestimate, wakaenda wakafanya re- evaluation ili watu wale walipwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini leo nimejaribu kupitia, Tarime haipo tena. Ina maana hawa wananchi wataendelea kuteseka, kukaa wamezuiliwa wasikate mti, choo kikibomoka wasijenge, hawafanyi maendeleo yoyote yale wapo tu kwenye kakiota, nyumba ikibomoka wasifanye chochote. This is not right! This isn’t right!

Mheshimiwa Naibu Spika, kama mmeamua kutwaa hata kwa mujibu wa sheria na kanuni za ardhi kama Jeshi limeamua kuchukua, which we respect, basi lipeni fidia. Short of that, Wanajeshi wale warudi kwenye kambi yao kule Nyandoto, after all iko mbali na mji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu nyingine ni kuhusu wastaafu wetu wanaotokana na Jeshi hili la Wananchi. Tumekuwa tukishuhudia wakishastaafu wanaishi maisha ya shida sana. Kwa sababu hata hiyo lump sum wanayopewa ya asilimia 25 kuna kipindi wanacheleweshewa wengine hawapewi kabisa, lakini hata wakiipata haikidhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunakubali wote kwamba Jeshi hili ni letu, kama vile ambavyo tunawatambua kada zingine kama Majaji na wengine, wakistaafu wanakuwa wanapata some percent, basi tuangalie hawa wanajeshi wetu wanapostaafu tuwape hata walau asilimia 20 ya mshahara wao wa mwanzo ili waendelee kujikimu na maisha wakiwa uraiani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukizingatia wanajeshi wakiwa kule kambini huwa wanapata vifaa vingi kwa ruzuku. Wameshazoea maisha hayo, wakija huku uraiani wanateseka sana. Lakini on top of that tuwakatie na bima ambayo anaweza akatibiwa muda wowote ule. Mwanajeshi akistaafu any time kuna crisis wanaweza wakawa-recall wakaingia pia kuendelea katika kunusuru nchi. Kwa hiyo, lazima tuwa- consider hata walau kwa asilimia 20, siyo asilimia 80 au 70 wanazopewa hao wengine, walau asilimia 20 ya mshahara ambao alikuwa akiupata wakati anastaafu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ripoti ya CAG ya mwezi Machi, 2021, ameainisha kwamba SUMA JKT kuna watumishi wanadai fedha, tena Idara ya Ulinzi. Mwaka 2018/2019 walikuwa wanadai milioni 208, mwaka 2019/2020 wakawa wanadai milioni 317, hela inazidi kuongezeka. Sasa kama Idara ya Ulinzi ambayo SUMA JKT wanapeleka kwenye private sector na hata kwenye mashirika ya umma, ina maana kule wanawalipa vizuri, kwa nini hawa watumishi ambao wanakwenda kufanya kazi ya ulinzi wasilipwe fedha zao?

Mheshimiwa Naibu Spika, yaani mimi nafanya kazi ya ulinzi unapokea fedha, lakini hunilipi. Unaweza hata ukashawishika ukajiingiza kwenye uhalifu, badala ya kulinda ukala njama ili uweze kuja kufanya uhalifu kwenye sehemu husika. Kwa hiyo, tunaomba mhakikishe msiwakope watumishi, hasa Idara ya Ulinzi jamani, kuwa kwenye lindo and then unamkopa, isn’t right. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine wamezungumza kwa kina hapa, ni kweli tunapeleka vijana wetu JKT, wanapewa mafunzo, lakini hawawezi kuwa absorbed wote kubaki kuajiriwa Jeshini, wa JKT na JKU. Sasa wasipochukuliwa wote Jeshini wengine wanarudi uraiani na unakuta wengine hawajapata mafunzo mbadala, hawezi akastahimili kukaa uraiani hana kazi, atashawishika. Ataingia kwenye magenge ambayo ni ya uhalifu na anajua, amejifunza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa wametoa ushauri mkubwa sana hapa, na mimi na-cement; Jeshi la Kujenga Taifa likiwezesha Tanzania ya viwanda ikawezekanika, tukipeleka fedha za kutosha tutaweza kuwa na kilimo chenye tija. Maana yake vijana wetu wakienda kule watajifunza, watawezeshwa, wakiwezeshwa ina maana tutakuwa na kilimo chenye tija, tutatoa raw material yataenda kwenye viwanda, viwanda vitakuwa vingi kwenye majimbo na mikoa; niliona siku ile Mheshimiwa Jafo anasema viwanda mia kila mkoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuwezeshe JKT isiishie tu kufanya mashamba machache, mimi naita mashamba darasa. Kukiwa na maonesho ya Nanenane wanakuja wametengeneza kweli furniture nzuri lakini wana viwanda all over the country, tumewawezesha hawa watu waweze kujenga nchi yetu kweli?

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nirudie tena, ukishasema taarifa mara moja unasimama. Ndiyo maana huwa naangalia mtu kasimama wapi. Mheshimiwa Mpembenwe.

T A A R I F A

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpe taarifa mzungumzaji kwamba point anazoziongea ni za msingi na zina maana sana za kusema kwamba tuweze kuwawezesha JKT na Jeshi kwa ujumla wake, lakini nataka tu nimpe taarifa mzungumzaji kwamba mfumo wetu wa bajeti ni cash budget system, tunakusanya halafu ndiyo tunatumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninamuomba tu mzungumzaji mimi na yeye na Wabunge wenzangu wengine wote humu ndani tuweze kushirikiana tuwe mabalozi wa kuweza kuhamasisha watu waweze kulipa kodi tukusanye ili Jeshi liweze kuwezeshwa. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, cash budget with priorities, kama tunaweza tuka-inject trillions of money kwenye Wizara ya Ujenzi tunashindwa nini kupeleka trillions of money kwenye hii Wizara ambayo tunaiita nyeti? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ni cash budgeting, yes, lakini tunatenga shilingi bilioni 220 na haziendi zinakwenda shilingi bilioni 30 wakati kwingine unakuta bajeti imeenda zaidi ya asilimia 100. Kwa hiyo we need to be serious na tusaidiande kama Wabunge, tukitenga shilingi bilioni 300 na ziende zote katika cash budgeting hiyo hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ninapenda kusahuri; tunasema ni Jeshi la Wananchi, sasa kama Jeshi la Wananchi liko pale kulinda mipaka ya nchi yetu ndhidi ya adui, lakini kama nilivyosema mwanzo, hii ya kuteua wanajeshi wetu wanakuja kwenye kupewa fursa au kuteuliwa kuwa watendaji Serikalini au Wakuu wa Mikoa, isn’t right. Civilian Government yaani utawala wa kiraia unamuingiza tena mwanajeshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, na huku sisi wengine tumeshazoea, ukimuona mwanajeshi kwanza you freeze, yaani nikiona DC mwanajeshi na wanavaa yale mavazi wakiwa kwenye hizi nafasi. Mimi ninashauri sana tuangalie wananjeshi tunawatumia, sijui nieleze vipi! Sasa ukishamuingiza mwanajeshi kwenye system Serikalini, tena wengine, kwa sababu DC na RC ni siasa, it’s a political thing. Yaani ukimuingiza kwenye siasa, it isn’t right.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Charles Mwijage.

T A A R I F A

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu hili la kutumia wanajeshi kwenye kazi mbalimbali, nataka nimpe taarifa Mheshimiwa Matiko kwamba Jeshi la Tanzania ni Jeshi la namna yake duniani. Ndipo unaweza kumkuta askari anakuja kuchumbia nyumbani kwako, mnacheza na mnakula wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi nyingine watu wakiona wanajeshi wanatupa kila kitu, hapa sivyo. Wewe ngoja kidogo tutoke nje uje uone nitakavyogongeana na majenerali wananipigia saluti. Sisi wanajeshi ni ndugu zetu, na ukimuona mwanajeshi maekwenda sehemu, jua kuna mambo. Ukimuona Kagera amewekwa nani, Mtwara amewekwa nani, fuatilia kuna mambo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther matiko, malizia mchango wako.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, napokea taarifa yake, lakini msisitizo wangu ni kwamba ukiwa Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa, unaingia kwenye Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya au ya Mkoa; this isn’t right, that’s where my point is, kwa sababu wengine tunawaweka mipakani huko.

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Tulieni jamani.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, anamalizia muda wake kwa hiyo taarifa moja tu ndiyo inayoruhusiwa hapo. Mheshimiwa Amar.

T A A R I F A

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nimpe taarifa mzungumzaji kwamba hao wanaoteuliwa kuwa Wakuu wa Mikoa, ma-DC, wanakuwa wameshastaafu tayari kutoka Jeshini. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, malizia mchango wako.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, wananimalizia muda wangu tu; Jenerali Mbuge amekwenda hapa, amestaafu lini? Do a bit of research kabla hujatoa taarifa. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba sana, wamezungumzia kuhusu nyumba za wanajeshi wetu; ni mbovu sana, dhoofuli hali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu
Spika, kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, kuna Kanuni inavunjwa, Mheshimiwa Jenista, Kanuni.

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba tu nimkumbushe Mheshimiwa Esther, Kanuni ya 71(h) ambayo inamzungumzia Mbunge kutokuzungumzia mwenendo wa Rais, Spika ama watu wengine wanaotoa haki.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nataka nimpeleke Mheshimiwa Esther kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ninaomba aende kwenye Ibara ya 36(2) ambayo inasema; Mheshimiwa Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka na watawajibika kuweka Sera na Idara na Taasisi za Serikali na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini akienda kwenye Ibara 34(4) inazungumzia pia madaraka ya Mheshimiwa Rais katika kufanya uteuzi. Kwa hiyo, sasa kama madaraka haya ya Rais katika kufanya uteuzi yamewekwa kwa mujibu wa Katiba nadhani si sahihi sana kwetu sisi Wabunge kuanza kuyazungumza madaraka ya Rais ya kufanya uteuzi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi hizi amepewa kwa mujibu wa Katiba na yeye katika Katiba hajafungwa amchague nani, amteue nani, amuache nani. Kwa hiyo, nilikuwa nafikiria kwa kuwa ni suala la kikanuni lakini ni suala la kikatiba haitakuwa sahihi sana sana kuanza kuzungumzia madaraka hayo ya Rais ndani ya Bunge lako Tukufu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, wakati akichangia Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko amesimama Mheshimiwa Jenista, akitoa maelezo kuhusu kanuni zetu namna ambavyo kwa namna moja au nyingine zinavunjwa na mchango wa Mheshimiwa Esther Matiko na ameweka maelezo yake kwenye eneo mojawapo ambalo Mheshimiwa Esther Matiko alikuwa anachangia, nalo eneo hilo linahusu wanajeshi kwenda kuwa sehemu ya Serikali huku uraiani na ametoa mifano ya namna wanavyoteuliwa kuwa Wakuu wa Mikoa na pengine Wilaya ama kuongoza vitengo mbalimbali ambavyo si vya kijeshi, lakini ni vya kiraia.

Waheshimiwa Wabunge, wakati akitusomea Mheshimiwa Jenista Kanuni ya 71(1)(a) ambayo inaelezea namna ambavyo tunakatazwa kufanya mambo kadha wa kadha hapo, lakini pia akatupeleka kwenye Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 36 na 34 kwamba Rais anapewa hayo mamlaka ya kuteua mtu yeyote ambaye yeye anaona anafaa kwenye nafasi fulani.

Sasa katika, wakati akichangia Mheshimiwa Esther hakuwa amejielekeza kwenye mamlaka ya Rais kuteua, lakini twende taratibu, hakuwa amejielekeza kwenye mamlaka ya Rais kuteua, lakini kwa sababu aliyokuwa anawazungumzia ni wateuliwa wa Rais basi Mheshimiwa Jenista ameona kwamba tukiwajadili wale wanaoteuliwa na Mheshimiwa Rais ni kama vile tunazungumzia mamlaka ya yule aliyeteua kama anayo mamlaka au hana. (Makofi)

Sasa wacha niliweke vizuri, mamlaka ya Mheshimiwa Rais kuteua hayawezi kuulizwa kwa namna hiyo kwa zile nafasi ambazo zinateuliwa kikatiba ama kisheria, Rais mamlaka yake hayaulizwi kwa sababu hata wale wanaompa ushauri hafungwi na huo ushauri yeye anaweza kufanya jambo ambalo ameruhusiwa kikatiba muda wowote. (Makofi)

Sasa hoja mahsusi ya hawa ndugu ambao wanateuliwa, hii si mara ya kwanza ikizungumzwa humu ndani. Sasa wacha niweke vizuri ili wanaochangia wengine waelewe mukhtadha wake.

Amesimama Mheshimiwa Mwijage hapa ameeleza kwa upande mmoja sababu maalum zinazoweza kumpelekea yule anayeteua na kwa mukhtadha huu Rais wetu kumteua mtu fulani kumpeleka sehemu fulani, anakuwa ana sababu na ameona mtu huyu ndiye anayefaa. Sasa kwa mukhtadha huo huwezi kusema kwa nini umempeleka huyu pale.

Lakini sasa, hoja ya Mheshimiwa Esther kwamba ukiwapeleka hawa wanajeshi wakaenda kuwa sehemu ya Kamati na ametaja mahsusi Kamati ya Siasa, lakini lazima unapozungumza Ukuu wa Mkoa usiuzungumze tu kwenye nafasi ndogo ya Kamati ya Siasa ya Mkoa ama Kamati ya Siasa ya Wilaya kwa Mkuu wa Wilaya, kwa sababu pia huyu ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenye huo Mkoa. (Makofi)

Kwa hiyo, wanapopelekwa huko maeneo ni kwamba huyu mwenye mamlaka ya uteuzi ameona kuna sababu. Kwa hiyo, ukichukulia tu hilo eneo ambalo wanaenda kuwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya na ukasema pengine haipo sawasawa hoja ya Mheshimiwa Jenista inasimama kwamba huwezi kuuliza yule anayeteua kama anaweza kumteua nani kwenye nafasi ipi.(Makofi)

Lakini sasa wanaenda pia kwenye nafasi nyingine ambazo siyo za kijeshi, lakini wanaenda wanajeshi na umetolewa mfano hapa anaweza kuwa Katibu Mkuu wa eneo fulani, Maliasili, sijui Mambo ya Nje, kwa hiyo hutegemea lile ambalo huyu mwenye mamlaka ya uteuzi ameona huyo ambaye ameteuliwa akasaidie kwenye hilo eneo. (Makofi)

Sasa kwa sababu limezungumzwa humu ndani na watu wengine huwa hawaelewi sana zile Kamati za Siasa zinafanya nini na kazi ya Mkuu wa Wilaya akiingia kwenye Kamati ya Siasa ya Wilaya kazi yake ni nini na akiingia kwenye Kamati ya Mkoa kwa maana ya Mkuu wa Mkoa kazi yake ni nini? Hiki ni Chama ambacho ndicho chenye Ilani ambayo inatekelezwa nchini. (Makofi)

Kwa hiyo, anavyoitwa kule ni kwenda kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwenye Mkoa wake au kwenye Wilaya yake. Sasa kwa sababu Wabunge wa CCM huwa hawalizungumzi hili kwa nini, kwa sababu wao ni sehemu ya hivyo vikao kwa hivyo wanaelewa majukumu ya huyu mtu ni yapi. (Makofi)

Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge na wananchi, wala wasiwe na wasiwasi kwa Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya ambaye ni mwanajeshi kwenda kuhudhuria hivyo vikao kwa sababu wanachoenda kukifanya kule ni kile ambacho ana kazi hiyo kikatiba kwa sababu nchi yetu imeweka utawala wa kidemokrasia lakini tunaongozwa na vyama vya siasa. (Makofi)

Kwa hiyo, chama cha siasa kilichopo madarakani kile kinachotekelezwa cha kwake lazima akawaambie wenye chama chao utekelezaji unaendaje. Kwa hiyo kule kwenye Kamati ya Siasa na Kamati ya Siasa ya Mkoa na Wilaya mukhtadha ni huo na nadhani kwa maelezo hayo nimeeleza kwa kirefu nadhani tumeelewana vizuri kuhusu hizi teuzi, lakini pia namna unavyoweza kuizungumzia humu ndani uteuzi ambao Mheshimiwa Rais ameufanya kikatiba au kuna teuzi ambazo hata pengine zinaweza kufanywa na mamlaka nyingine ambazo zimeruhusiwa kufanya hivyo. Nadhani hili limeeleweka tayari. (Makofi)

Mheshimiwa Esther Matiko malizia mchango wako.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nilikuwa namalizia kwenye makazi ya ndugu zetu. Ni dhahiri yapo duni sana sana, kwa hiyo, tunaomba Serikali iboreshe makazi ya hawa ndugu zetu, kwa sababu tusiishie tu kuwaambia jeshi letu lipo imara, lakini wawezeshwe basi hata wakiishi wajue kabisa kweli nchi yangu inanijali kama vile ambavyo naitumikia nchi yangu. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana ya Nishati.

Mheshimiwa Spika, nishati ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu kwa maana nishati ni uchumi bila nishati hamna utekelezaji wa Tanzania ya viwanda. Pia nishati ikiwepo inaimarisha usalama popote pale Tanzania hasa vijijini.

Mheshimiwa Spika, kama nchi au Taifa tuna Vision 2025 na tumeigawa katika miaka mitano mitano. Malengo ya Mpango wa Pili ya Maendeleo ya Taifa kwa Wizara hii ya Nishati target ilikuwa kuzalisha megawatt 4,915 kuanzia 2016/2017 mpaka 2020/2021 kutoka ile ambayo ilikuwepo ya 1,501. Nimenukuu kwenye hotuba ya Waziri mwenyewe anasema mpaka Aprili, 2021 tuna megawatt 1,605 kwa maana tofauti kwa miaka yote mitano hii tumeweza kuzalisha megawatt 104 tu. Katika malengo haya tulisema tutazalisha hizi megawatt zaidi ya 3,014 kwa kipindi cha miaka mitano ili iweze kutosheleza mahitaji ya ndani ya nchi na kuweza kuuza nje ya nchi. Sasa hatujafikia hayo malengo tumezalisha megawatt 401 tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nini kimepeleka hiki? Nimejaribu kupitia pia hotuba ya Mheshimiwa Waziri, Ibara ya 22 anaeleza bayana mathalani fedha tulizozitenga hapa 2020/ 2021 shilingi trilioni 2.17 mpaka Mei walikuwa wamepokea shilingi trilioni 1.3 tu ambayo ni asilimia 60, anakiri hapo.

Mheshimiwa Spika, kwa mwendo huu ndio maana tunashindwa kutekeleza mipango ya miaka mitano ambayo tulikuwa tumejiwekea kwa sababu haina uhalisia. Siku zote nimekuwa nikisema tuwe tunakuja na bajeti zenye uhalisia ili tunavyojipangia tuwe tunajua kabisa kwamba tuna kiasi fulani cha fedha tunakipa kipaumbele ili kutekeleza mradi A kama ni mradi wa Julius Nyerere Hydropower, LNG kwa maana gesi asilia tuweze kujua ni kiasi gani kinaenda na kiweze kutelekezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba tukifikia malengo ya kuuza umeme nje na kuzalisha kutosheleza Tanzania bado umeme wa Tanzania ni ghali sana. Mathalani, wenzetu wa Kagera wanalalamika kwamba hawajaunganishwa na Gridi ya Taifa lakini wanaponunua umeme kutoka Uganda kwa Sh.10 wanapata unit zaidi ya 80 lakini kwa category ile ile kwa Tanzania ukinunua umeme wa Sh.10,000 unapata unit 28. Kwa hiyo, kwanza umeme unavyouzwa kwa wananchi ni ghali sana, Serikali iangalie ni vipi inafanya standardization ya bei ili Watanzania wapate huduma hii, tunawapelekea lakini waweze ku-afford kununua kulinganisha na nchi zingine lakini tunapofikia wakati wa kuuza nje pia bei yetu ikiwa ghali sana hatuwezi kupata wateja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ambacho napenda kuzungumzia ni kutokuwepo na uhalisia wa takwimu ambao tunazitoa kwamba Watanzania wamefikiwa kwa kiasi gani. Nimesoma hotuba ya Waziri hapa anatuambia wameunganisha vijiji 10,312 kati ya vijiji 12,000 na zaidi, wanatuambia kwamba wameunganisha kwa asilimia 86. Wewe Spika umekalia Kiti jana na leo umeona kila Mbunge akisimama analalamika, Mbunge wa Mbinga Vijijini amesema ana vijiji 117 vimeunganisha 34, Mbunge wa Busanda jana amesema ana vijiji 83 vimeunganishwa 26 tu, nikizungumzia Mkoa wa Mara vijiji vilivyounganishwa ni chini ya asilimia 40. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa kila siku najiuliza hizi takwimu ambazo wanatuletea kwamba wameungnisha Tanzania kwa asilimia 86 zinatoka wapi? Wameenda mbali wakasema Watanzania milioni 47 wamefikiwa na nishati ya umeme. Wabunge tupo hapa tujiulize kule tunapotoka kwenye wilaya yako umepata umeme kwa asilimia 86? Hii kitu ni hatari sana tukitoa takwimu feki Wizara husika au Serikali ina relax hata wahisani hawawezi kutusaidia wanajua tuna-deficit kuwafikia Watanzania wote asilimia 13 tu which is a false, tutoe takwimu zenye uhalisia ili tuweze kupanga bayana kuhakikisha kwamba umeme unawafikia Watanzania wote kuliko hizi cooked data. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine hapo hapo napenda kushauri, tunapopitisha umeme tunasema tumepitisha kijiji fulani kwamba vijiji 10,000 ukiangalia miji 6, miji 10 kama ilivyo kwenye Sera ya Maji wanasema ndani ya mita 300 basi na sisi tuseme tunapopitisha huo umeme uwe ndani mita 400 au 300 au 200. Unapopitisha kwenye Kijiji A mtu yuko kilometa 8 au 10 unahesabu kwamba Kijiji cha Nyabilongo nipeleka umeme wakati ume-cover only ten percent or twenty percent. Hii siyo sawa tutakuwa tunajidanganya hatuwezi kulisaidia Taifa. Wana dhamira ya kweli na unyenyekevu kama wengine walivyosema, mimi mwenyewe nampongeza nikimfuata ni mnyenyekevu sana lakini tufikie target yetu, tuwafikie Watanzania kwa uhalisi sio kwa namba kwenye vitabu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ni uwiano wa mgawanyo wa fedha hizi. Wizara kweli inatengewa fedha na haziendi kwa uhalisia lakini hata zinazoenda basi tuweze kuangalia hii miradi yote iweze kupata kwa uwiano ili tuweze kutekeleza miradi hii kwa wakati vinginevyo inasababisha gharama kuwa kubwa. Mathalani katika hizi shilingi trilioni 2.3 za mwaka huu zaidi ya shilingi trilioni 1.44 zinakwenda kwenye Julius Nyerere Hydropower Project ambacho mimi na-support kwa sababu mradi ule ukiisha utasaidia sana kupatikana umeme nchini lakini pia unaangalia kwenye REA, tunapeleka shilingi bilioni 415 tu. Hizi takwimu zenu ndiyo zinasababisha mnapeleka fedha hizi, shilingi bilioni 415 haziwezi kwenda ku- cover maeneo yote na sasa hivi hii ni phase ya tatu. Tuangalie tukipeleka kwenye REA zaidi ya asilimia 70 au 65 ya Watanzania wataenda kupata umeme tuwekeze fedha huko kwa uwiano ambao unatoa uhalisia kuweza kutatua changamoto za nishati ya umeme kwenye maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine ni utekelezaji wa gesi asilia, kama nchi tukiamua kuwekeza kwa kasi kwenye mradi wa gesi asilia itasaidia sana. Kwenye hotuba yake amesema kwamba target ni kufikia nyumba 10,000 magari 700 na viwanda zaidi ya 20. Pia anasema by 2021 wamefikia nyumba 1,191 tu out of nyumba 10,000 ina maana kutoka nyumba 500 za mwaka 2020 mpaka nyumba 1,191 ni nyumba 691, kwa hizo 10,000 ina maana tutachukua zaidi ya miaka 20 kuzifikia kufikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuamue kuwekeza, ndio maana nikasema uwiano na vipaumbele ni muhimu. Tukiwekeza kwenye gesi asilia kwanza hata kwenye magari inaondoa hata environmental pollution, ukitumia petrol na diesel tunajua uchafuzi wa mazingira ambao unatokea. Tukiamua kuwekeza magari mengi Tanzania yakatumia hii gesi asilia tutakuwa tume-save matatizo ya kimazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa upande wa Tarime, nimekuwa nikiuliza sana na ndiyo maana nikirudi pale kwenye takwimu kwa mfano Tarime Mjini sijataka kwenda hata huko Susuni, Mwema na wapi, nilikuwa namwambia Mheshimiwa Waziri kila siku tangia Bunge la Kumi na Moja kuna kata sita hazina umeme akasema vinaisha by phase II lakini hata phase III bado umeme haujafika. Kwa mfano Kata ya Nyandoto, Mitaa ya Masulule, Nyagesese, Nyasebe, Kemonge, Itinunu Nyatenene hakuna umeme. Kata ya Kenyemanyori tunahitaji umeme Kebaga, Nyamitembe, Chila, Longa na Mwibari. Kata ya Nkende tunahitaji umeme Iteve, Mtulu, Lomoli, Kitale, Kirumi, Nyamitebe na Kalamoloni. Kata ya Ketale tunahitaji umeme Ntabulo, Binagi, Wigoronto, Nyagesese, Malulu Center, Nyamahisana, Tebakiri na Nyamihobo na Kata ya Tura tunahitaji umeme Gimenya na Kikogoo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini zaidi nilikuwa nikiongoelea hapa ndani tunavyoenda kuwekeza tuwekeza basi umeme uende kwenye taasisi; sekondari, vituo vya afya na zahanati ili mfano kwenye sekondari watoto wetu waweze kujisomea baada ya masomo ya kawaida. Mama anavyokwenda kujifungua pale kama hamna umeme wanatumia vitochi au vikarabai hivi hatutakiwa kuwa hapo. Tunapoenda kupeleka umeme priority namba moja iwe ni taasisi muhimu tuhakikishe kwamba zimefikiwa na umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie tu kwa kuwapongeza, wameainisha kwenye hotuba yao kwamba kuna viwanda hapa Tanzania vinazalisha vifaa ambavyo vinaenda kutumika kwenye miradi ya ujenzi ya umeme ambapo tumeweza ku- save zaidi ya shilingi bilioni 162, kwa hilo nawapongeza sana. Tuendelee kuwahamashisha watu wetu waweke ili kuzalisha hapa nchi kuliko kuagiza kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili na mimi nichangie kwenye Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kabla sijachangia nipende kuishukuru Serikali kwa kweli kwa kufungua mnada wa Magena uliopo Halmashauri ya Mji wa Tarime ambao ulifungwa tangu mwaka 1997, na tukawa tunakosa mapato mengi sana maana ule mnada una multiply effect. Nashukuru sana, na namshukuru sana Waziri wa Mifugo na Naibu wake; na hii inaenda kuongeza mapato kwenye Serikali Kuu pamoja na kwenye Halmashauri ya Mji wa Tarime. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitachangia bajeti hii kwa kweli ambayo kwa mbali imeonesha matumaini makubwa kwa Watanzania, hasa kada ya wafanyakazi. Japo wameweka tija kwa mbali sana lakini ni mwanga mzuri, ukizingatia miaka mitano yote tulikuwa hatujawakumbuka hawa wafanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshukuru Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa tozo ya asilimia sita, ambayo ilikuwa kwenye mikopo ya elimu ya juu. Kwa kweli imeenda kutoa unafuu mkubwa sana kwa wafanyakazi ambao walikuwa ni wanufaika wa mikopo hii ya elimu ya juu. Pia, kwenye kuondoa kodi kwenye cold rooms, Ibara ya 57 imeonesha, hii itachochea zaidi kilimo cha mboga mboga na matunda. Kwa hiyo nashukuru sana kwa hili na kwa kweli kwa hili wanastahili pongezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ukiangalia Ibara ya 73 wameonesha kwamba wameondoa faini kutoka shilingi 30,000/= mpaka kuja shilingi 10,000/=, ni jambo jema. Ningependa nishauri pia kuwa wafanye tathmini, kwamba faini isiwe kwenye uniformity, shilingi 30,000/= kwa gari za abiria, kwa gari binafsi na malori. Kama itawapendeza pia fanyeni tathmini ya kina ili muweze ku-charge kulingana na aina ya gari hizo ambazo nimezitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, wamepunguza faini kuwa shilingi 10,000/=, ni jambo zuri sana kwa sababu tunaajiri vijana wengi, lakini hapo hapo wameweka kodi ya kuingiza matairi mapya ya pikipiki, ambao ni ya hawa hawa vijana. Wameondoa kutoka asilimia 10 kwenda asilimia 25; ina maana hapo mnakuwa tena hamusaidii hawa vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ningeshauri muiangalie hii, kama mnaweza mkaiacha ikabaki pale pale asilimia 10; kwa sababu hatimaye watashindwa kununua haya matairi, watakuwa wanapewa adhabu ya matairi kuwa kipara barabarani na unakuta hizi shilingi 10,000 zinajirudia mara mbili mbili, na sasa unakuta haujasaidia chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, ningependa kuzungumzia kwa haraka tu Ibara za 45 na 46 ambazo zimezungumzia kuhusu madiwani, ambapo kwa kweli kwa muda mrefu ilikuwa ni kilio kwa. Vilevile mmeondoa, na kwamba mtakuwa mnawalipa posho ya mwisho wa mwezi kutoka Serikali Kuu kwa halmashauri ambazo zina kipato kidogo; na pale pale mmeeleza kwamba, mnafanya hivyo ili hawa madiwani wasipige magoti kwa wakurugenzi, lakini pia kuongeza ufanisi kwenye shughuli hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikawa najiuliza, kwamba kwa nini mnaweka double standard? Kuwa zile halmashauri 16 zenye vipato vya juu wenyewe waendelee kujilipa? Sasa kama wanaendelea kujilipa hamuoni kwamba inaweza ikatokea sehemu wakurugenzi wakaacha kuwalipa kwa makusudi ili waendelee tu kupiga magoti kwa wakurugenzi? kwa ajili kwamba wana mapato makubwa ili wawalipe. Kwa hiyo ningeomba hili mliangalie, muweke tu kwamba Serikali Kuu mtalipa kwa madiwani wote bila kujalisha kipato cha halmashauri husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia mmeweka kwamba ni mapato ya mwisho wa mwezi tu. Kuna halmashauri zingine kwa mfano Halmashauri ya Mji wa Tarime kuna kipindi tulikuwa tunakopa mpaka vile vikao vya madiwani vya kati kati hapo. Yaani vile vikao vile vinavyoendeshwa vinakopwa, sasa sijui hilo mnaliangalia kivipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusu nyasi bandia, ni jambo jema ambalo linaenda kuchochea sekta ya michezo Tanzania, lakini napingana na ninyi kuweka kwenye majiji tu. Naomba sana muondoe, muweke kwa yeyote atakayetaka kujenga viwanja kwa standard ya kuweka nyasi bandia, basi aweze kupata huo msamaha wa kuingiza nyasi bandia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Mkoa wa Mara, tuna kiwanja cha Karume pale Musoma Mjini. Pale si jiji lakini kile kiwanja kinatumika kwenye Ligi Kuu. Tukitaka kukiendeleza kuweka nyasi bandia tutashindwa maana mtataka tulipie kodi, ilhali Dar es Salaam na hizo halmashauri za majiji ambazo mmesema zina vipato vizuri wenyewe mnawapa msamaha. Hii naomba kwanza muitumie vizuri, Shinyanga pia inatumika, na kwingineko ambako si majiji. Kwa wekeni wazi iwe manispaa, iwe mji, iwe jiji, watakaokuwa tayari kujiendeleza kuweka nyasi bandia, basi wapate msamaha wa kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho kwa kweli naipongeza Serikali ni hili la kuona kwamba wapunguze muda wa mkataba kwa hawa askari polisi kutoka miaka 12 kuja miaka sita, na ikiwezekana mwende mpaka miaka mitatu kama ilivyo kwa JWTZ. Lakini hapa mmewasahau watu walio kwenye idara moja, askari magereza na askari zimamoto nao mikataba yao ni miaka 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa nao washushwe kama askari polisi, iwe miaka sita na baadaye huko muwashushe pia kuja miaka mitatu. Lakini pia, ukizingatia, kwa mfano maslahi yao, wako idara moja hawa. Askari polisi mwenye degree analipwa gross salary ya shilingi 860,000 anapewa asilimia 15 ya taaluma, anapewa na fedha ya makazi; lakini askari mwenzake aliye magereza mwenye degree analipwa shilingi 770,000 tu, hapewi asilimia 15 ya taaluma wala hapewi fedha za accommodation. Kwa hiyo naomba muweze kuwapa wawe na usawa kwa sababu wako kwenye Idara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusiana kwa kweli na tozo ambazo tumezi-introduce, Ibara ya 88 ya Sheria ya Posta na Mawasiliano, ambayo inaelekeza kukata kati ya shilingi 10/= mpaka shilingi 10,000/= kwenye hizi za mobile transaction. Fedha hizi zinaweza kufikia takribani trilioni moja na bilioni mia mbili hamsini na nne; na wakati unasoma hapa Mheshimiwa Waziri ulielekeza kwamba zinaenda kwenye sekta ya afya. Na ikizingatiwa sekta ya afya hatujawahi kufikia Azimio la Abuja, ambalo linatutaka tutenge asilimia 15 ya bajeti kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama hizi trilioni 1.25 zitaenda huko, na najua hizi fedha kwa hivi mlivyoziweka, lazima zitakuwa zinapatikana automatically. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ziweze kuwa ring-fenced na ihakikishwe kwamba kweli zinakwenda kwenye sekta ya afya kama ambavyo mmetueleza hapa, isiwe kwamba mnawakata Watanzania halafu baadaye hizi fedha haziendi. Tunahitaji, mathalani tukiamua kuwekeza kwenye miundombinu katika hii trilioni 1.234 tukichukua bilioni 800 tu tunaweza kujenga vituo vya afya 2,000 ambavyo hamjavijenga mpaka leo tangu tumepata uhuru wetu. Pia tukachukua bilioni 200 kupeleka kwenye vitendea kazi, dawa na vifaa tiba vingine. Vilevile, tukachukua labda bilioni 252 tukasema tunaweka kwenye zahanati ili kumalizia yale maboma tunaenda kutatua matatizo ya vifo vya mama na mtoto, matatizo ya Watanzania wakiugua kutembea umbali mrefu na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia, kwenye Ibara ya 88 hiyo hiyo kumeelekezwa fedha bilioni 322 kwenda TARURA ambazo zimeelekezwa zinaenda kuwa ring-fenced. Pia kuna bilioni 396 ambazo mmesema mmezielekeza kwenye maji. Mwaka huu wa fedha umepita zilienda tu bilioni 292. Sasa hivi bilioni 396 kama kweli zikienda kwenye maji, na kwa bajeti ya maendeleo waliyoomba ina maana kuna fedha zitabaki. Kwa hiyo tunatarajia miradi ya maji tukija hapa mwakani iwe imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 100; na zote hizi ziwe ring- fenced.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ukisoma Dhima nzima ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa; unasema ni kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu. Na ukisoma pia, Ilani ya CCM Ibara ya 8, mmesema mtazalisha ajira takribani milioni nane. Ukisoma Ibara ya 13 mnajenga Tanzania ya Viwanda, ukisoma Ibara ya 14 mmesema mtatambua na kuthamini sekta binafsi kama ndiyo inayochochea uchumi wa taifa letu. Pia Ibara ya 15 mmesema kwamba mtaendelea kutambua sekta binafsi kuwa ni engine ya kuchochea uchumi wa taifa letu na hivyo mtalinda na kuiendeleza hii sekta binafsi. Sasa, tunaratajia muweze kuyaishi haya mambo; lakini ni kinyume. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia sasa hivi viwanda vingi vimekufa wala hata havihuishwi. Vilevile kuna mazingira yasiyo rafiki kuweza kuvutia wawekezaji waje kuwekeza Tanzania. Sasa ili uweze kwenda na hii ambayo imeonyeshwa kwenye Ilani yenu ya CCM, ni wajibu sasa hivi, sera ya viwanda iweze kuwa attractive kwa investors ili waje kuendeleza viwanda vyetu hivi na vilevile muweze kuona vikwazo vilivyopo. Mathalani, kule kwetu Kanda ya Ziwa kuna viwanda vya pipi vilianzishwa. La Kairo ambaye alienda kuzindua Mheshimiwa Hayati na Jambo Sweet, Kenya ndio wana-supply pipi kutoka Kenya wanaleta huku kwa sababu wao hawana kodi kwa pipi ambazo wana-export. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Tanzania kuna asilimia 25 kama wana-import glucose na sukari kuja kutengeneza pipi hapa; lakini pia wana VAT, kwa hiyo wanashindwa ku- compete. Hivi viwanda vinakufa, na Mheshimiwa Magufuli alienda kuvifungua; Jambo Sweet na hiyo ya La Kairo, lakini sasa hivi vinakufa na ajira nyingi zinapotea na hatima yake hata hayo mapato na na vingine mnakosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nizungumzie kuhusu viwanda vya matrela. Tunajua tulikuwa na viwanda takribani 10 hapa Tanzania, sasa hivi vimebaki vitatu tu na hivyo vitatu vinasuasua. Kwa nini? Ni kwa sababu matrela yameagizwa kutoka nje, China, German na kwingineko hivyo hawa hapa ndani wanashindwa ku-compete kwa sababu kuingiza matrela mmeweka asilimia 10 tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili tulinde viwanda vyetu ili tupate na mapato nashauri tuweke asilimia 25, ili sasa kama watahitaji kuingiza hayo matrela yaweze ku-compete na viwanda vyetu hapa. Lakini hata hivi viwanda na vyenyewe tuvitunde, tuvisaidie, tuvipunguzie kodi. Tukitengeneza matrela hapa Tanzania tutazalisha ajira nyingi, tutapata SGL, tutapata pay as you earn na kodi zingine ambazo ni indirect zinapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la kushangaza sana. Ukiangalia Tanzania hatutengenezi magari, lakini import wameweka asilimia 25, matrela ambayo kuna Watanzania wanatengeneza asilimia 10. Nakuomba sana Mheshimiwa Mwigulu muirudishe, muweke asilimia 25, itaenda kuongeza mapato ya taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine mmeondoa msamaha kwenye taa za solar ilhali mnajua kabisa; mbali na hizi takwimu ambazo tunaziweka kwenye madaftari na kwenye vitabu Watanzania wengi kaya nyingi za vijijini hawana umeme, hawajafikiwa na umeme. Tunategemea taa za umeme wa jua, ambao bidhaa zao pamoja na kwamba huwa kuna msamaha wa kodi bado zilikuwa ziko juu sana. Sasa leo mnaondoa ilhali mnajua kabisa umeme haujamfikia kila Mtanzania kule vijijini kila kaya haina umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nashauri warudishe msamaha kwenye vifaa vya umeme wa jua ambavyo ni ghali sana ili kuweza kuwasaidia Watanzania ambao wamejiwekeza kule. Leo kuna saluni kuna mashine sijui za kusaga, watu wanasindika na nini. Mnavyoweka mnaua kabisa uchumi kule vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba waondoe kwanza mpaka pale ambapo watakapojihakikishia kwamba kila kaya kijijini ina umeme, ndio waweke sasa hii asilimia 25 ambayo wameileta ili kusema kwamba wapate uwiano sawa. Hivi ilivyo na msamaha uwiano wa bidhaa za umeme wa jua zilikuwa zipo juu sana, ukinunua bulb, wiring yake, ukinunua control unit panel zake, zote zipo juu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba sana, pump zinazotumia umeme wa solar nazo pia wazipe msamaha. Zinakwenda kuchochea umwagiliaji kwa watu wa greenhouses huko vijijini. Ukiwa na umeme wa solar unasaidia, lakini pia wanaofuga samaki and the like. Kwa hiyo naomba sana, Mheshimiwa Waziri aangalie hili ili tuweze kuchochea sekta ya kilimo na mifugo huko vijijini katika kuhakikisha kwamba tunachochea kwenye uchumi wa Taifa hili. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, tuhakikishe kwamba hii miradi ya kimkakati kwa kweli inamalizika on time kama SGR. SGR ikimalizika itasaidia sana kuchochea uchumi wa Taifa letu. Itasaidia sana na siyo tu kuchochea uchumi, itapunguza hata na ajira ambazo zinapatikana ambazo zinatokana kwa sababu ya malori makubwa kuchangamana na magari, mabasi na vitu vingine kama hivyo. Tukimaliza SGR kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza ina maana tunakwenda kukuza uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma transport economy itakwambia, moja ya vitu ambavyo vinasaidia na kuchochea kwenye uchumi, ni kuwa na miundombinu imara ya reli ambayo itasaidia kusafirisha. Kwa hiyo naomba sana, kama fedha tumezitenga hapa ziende tuweze kumaliza huu mradi kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie tu kwa kusema, maendeleo ya watu it includes elimu, maji, umeme na miundombinu ya barabara kutoka vijijini ambavyo ndio wanalima kuja huku mijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikushukuru kwa kunipa hizi dakika zangu za kuchangia. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nakushukuru kwa kunipatia fursa hii nami niweze kuchangia kwenye taarifa hizi mbili za Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nawapongeza Wenyeviti wetu wote kwa ripoti nzuri kabisa ambazo wamezi-table hapa. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti na nitaenda kujielekeza kwenye MSD, pale ambapo Kamati ya Bajeti tulitembelea tukagundua changamoto mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kabisa kwamba Taifa letu limekuwa likikumbwa na upungufu wa dawa kwenye hospitali na vituo mbalimbali vya kutolea huduma na suluhisho mojawapo ni haya ambayo nitaenda kuyasema, wala siyo yale ambayo Waziri alisema sijui kuondoa maduka ya dawa kwa mita 500. Unaweza kuondoa mpaka kilometa mbili, lakini bado kukawa na changamoto ya upungufu wa dawa, kama haya hayataweza kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mojawapo tumeshuhudia mlolongo wa utaratibu mzima wa ununuzi unachukua muda mrefu sana. Ni kwamba, mchakato wa zabuni tu unachukua miezi mitatu, baada ya pale kama unaagiza vitu kutoka nje itachukua miezi mitatu tena kufika baada ya kumaliza mchakato wa zabuni. Kama ni ndani ya nchi itachukua miezi miwili. Sasa ukijumlisha ni miezi mitano mpaka sita ili uweze kupata dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ili tuweze kuepukana na huu mlolongo mrefu nilikuwa nashauri: moja, tuhakikishe Serikali inapeleka fedha kwa miezi minne walau mfululizo ili kukabiliana na huu mchakato mzima uweze kuji-absorb ndani kwa ndani kuhakikisha kwamba tunakuwa na consistency ya ku-supply dawa kwenye vituo vyetu vya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ni kuhakikisha kwamba, walau tuweze kubadilisha sheria ili kwa dawa zile muhimu. Mchakato wa zabuni usichukue miezi mitatu, ungechukua hata mwezi mmoja kuhakikisha upatikanaji wa dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine, Sheria yetu ya Manunuzi ya Umma pia inatambua kwamba mzabuni mwenye gharama nafuu ndiye atakayepewa tenda, yaani bila kuangalia uhalisia wa bei ya gharama husika kwenye soko. Hii inasababisha baadhi ya wazabuni kuweza hata kula njama, just a syndicate.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano, labda nataka ni- supply let say, X-Ray machines nyingi kwenye hospitali fulani na ninajua kabisa na John anafanya biashara hiyo na mwingine; unaweza ukawa na syndicate tu. Bei halisi kwenye soko unakuta labda ni shilingi milioni 50 kwa X-Ray moja, lakini sisi tuka-bid; nikaweka shilingi milioni 100, John akaweka shilingi milioni 120, mwingine akaweka shilingi milioni 130. Mimi wa shilingi milioni 100 nikachukuliwa wakati kiuhalisia bado tume-inflate bei, imekuwa kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, MSD wakalalamika sana kwamba wamefanya tafiti na wamegundua kabisa, unapokuwa unachukua ile tender, pamoja na kwamba inaonekana ni the lowest bidder, lakini kwenye uhalisia kwenye market unakuta wame-inflate price. Unaweza ukanunua kwa shilingi milioni 120 wakati kwenye market unakuta kitu kinauzwa shilingi milioni 60.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nashauri pia tuangalie hili, tubadilishe Sheria ya Manunuzi ya Umma walauo iweze ku-accommodate kipengele kiongezeke pale kwamba, sawa ni the lowest bidder, lakini tuangalie na uhalisia wa bei kwenye soko inakuwa ni kiasi gani? Vinginevyo tutakuwa tunapeleka gharama kwa walaji ambao ni Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine, kuna huu mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao (Tanzania Electronic Procurement System). Huu mfumo una upungufu ambapo unasababisha gharama kwa MSD. Huu mfumo unatambua lugha mbili tu; Kiswahili na Kingereza. Sasa ukiangalia watengenezaji wakubwa wa vifaa hivi, kwa mfano, MRI, CT-Scan, sijui X-Ray, na kadhalia, kwa mfano, ni Spain, Russia, German and the alike. Wachina ambao hii lugha ya Kiingereza siyo lugha yao ya mwanzo ukiingia kwenye mifumo yao ya system; kwa hiyo, inasababisha mwanya kwa huyu MSD asiweze kununua straight from the manufacturer, inabidi anunue from the supplier ambaye ana- act kama an agent.

Mheshimiwa Naibu Spika, huyu supplier anaweza akanunua kwa sababu yeye mfumo unakubaliana; anajua Kiingereza na Kiswahili; ananunua kwa producer au manufacturer kitu ambacho tungeweza kukinunua sisi straight; let say kwa shilingi bilioni mbili, yeye anakuja anatuuzia kwa shilingi bilioni 2.5 au shilingi bilioni 2.8.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuangalie huu mfumo wetu tuurekebishe uweze ku-accommodate lugha zote ambazo tunajua kwamba tunanunua vifaa hivi vya hospitalini kuweza kupunguza gharama kinyume cha hapo tunatoa mwanya mkubwa na gharama kubwa kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine tulipotembelea pale tuliona kabisa kwamba kuna vifaa ambavyo vinatozwa kodi ya ongezeko la thamani na kodi ya maendeleo ya reli. Mathalani vifaa vya vifungashio vya madawa panadol, PVC unakuta vinatozwa kodi unakuta pia vinatozwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye vipuli ambavyo ni vipuli vya muhimu sana au kwenye mashine ya vitendanishi ambavyo vinasaidia mathalani kwenye kutoa huduma ya uchujaji wa damu dialysis. Hivi ukitoza hivyo unapelekea bei inakuwa kubwa sana na Watanzania wengi hawawezi waka-afford bei hizi za huduma ya uchujaji wa damu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilikuwa nashauri na ukitegemea Tanzania ili tuweze kuvutia wawekezaji nchi yetu ya Tanzania mojawapo ni kutoa hizi tax incentive. Kwa sababu vivutio vingine like umeme, ni shida bado kwetu hapa hatuna umeme ambao ni reliable muda wote ili wawekezaji waweze kuja achilia mbali hili taasisi ambayo ni ya Serikali. Maji pia ni shida miundombinu ya barabara na vingine vyote ni shida, sasa pale ambapo tunaona kuna umuhimu kwa maslahi ya Taifa kama hivi nilivyoeleza hapa hatuwezi kutoa exemption yaani tuondoe hii kodi ya ongezeko la thamani nah ii kodi ya maendeleo ya reli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mathalani kwa hawa wa Keko hawa MSD ambao wanasema ukiviweka hivyo inakuwa ni gharama sana sasa kwa kuanzia tuondoe hiyo tuone sasa tukishaondoa hii ambayo inaenda kupunguza gharama uzalishaji utaongezeka vipi kwa viwanda ambavyo ni vya Serikali. Tukishaona baada ya muda sasa tuweze kukaribisha na sekta binafsi kupitia PPP ili waweze kuingia na wenyewe kwa kufanya hivyo ina maana tutakuwa na viwanda vingi ambavyo vinazalisha madawa haya na tutaenda kupunguza ukosefu wa madawa kwenye vituo vya afya, kwenye hospitali na kuweza kuokoa maisha ya watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine kwa haraka haraka Mheshimiwa Naibu Spika na wewe ulikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje by then Ulinzi na Usalama, na tulikuwa na kikao Kamati ya Uongozi moja ya issue ambayo ilijitokeza zaidi ilikuwa ni fidia ambazo wanatakiwa walipwe watanzania wanaopisha maeneo kwa ajili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na katika Kamati ya Uongozi siku zile tuliazimia na Serikali ikasema kabisa inaenda kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa hivi yale maeneo yaliyoainishwa ya Viruti, sijui Kikombo, Nyabange na maeneo mengine ambayo pia yaliahidiwa kwamba yangeweza kutekelezwa by then mpaka kufikia muda huu ikiwepo Tarime ambayo kila siku nasimama naongea hapa tunaomba Serikali muweze kufanya fidia ili hawa wananchi Watanzania hawa waweze kuondoka kwenye hayo maeneo waende kwingine wakafanye shughuli za maendeleo wamekuwa wamekaa kama watumwa kwa muda mrefu sana mnafanya tathmini muda unapita muda unapita unarudi tena kufanya tathmini. Si sawa kabisa tunaomba kabisa kama vile ambavyo kamati imeainisha na kikao kilikaa Serikali iweze kupeleka fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa ni hili pendekezo la kuhakikisha kwamba tunaongeza fedha kwa ajili ya TARURA na hii imekuwa ni vilio sana hatuna muunganiko kwenye maeneo yetu huko si vijijini si mjini hata hapa Dodoma ukipita kwenye barabara hizi ambazo ziko under TARURA ni disaster. Sasa Serikali iweze kulichukua hii ihakikishe imeongeza hizo walau bilioni 111.3 kwa Kunzia kwa kuweka installment mwezi huu na mwezi ule ili uhakikishe kwamba tunaweza kurekebisha hizi barabara.

Lakini in future kama ambavyo Waziri wa TAMISEMI hapa juzi aliongea tuhakikishe kwamba haitokezi hii kitu muweze for cast muone kabisa kwamba huwa mvua ikitokea barabara zinaharibika kwa hiyo mtengeneze kwa kiwango ambacho kinakubalika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuweza kunipatia fursa nami kuchangia kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitajielekeza kwenye maeneo makuu mawili, ambayo migogoro ya ardhi pamoja na uwekezaji wa tija kwenye malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunatambua kwamba wananchi wanakuwa wanatwaliwa maeneo yao aidha na mwekezaji au na idara mbalimbali za Serikali. Tumeshuhudia, mathalani mimi tangu niko Bunge la Kumi hapa naongelea mgogoro wa ardhi kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na wananchi wa Bugoth na Kenyambi kule Tarime.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara ya mwisho Wizara ya Fedha iliandika barua kwenda kwa Halmashauri ya Mji wa Tarime Novemba 18 ikiwaeleza kwamba wameshapokea tathmini kutoka kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na kwamba wanaenda kutoa fedha takriban bilioni 2.5 kwa ajili ya maeneo ya Tarime, Usule kule Tabora na eneo la Nyangurunguru Mwanza; ambapo kwa Tarime ni takriban bilioni 1.6. hata hivyo mpaka leo, walienda wakafanya tathmini na uhakiki wa mwisho na wakawaambia kufikia Februari watakuwa wamepeleka hela.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kufuatilia kwa Katibu Mkuu Hazina na hata kwa mama yangu pale, Mheshimiwa Stergomena Tax, tukahakikishiwa kwamba kufikia Machi hela zitaenda, lakini mpaka leo wananchi wa Tarime, Bugosi na Kenyambi hawajapatiwa hela na wanapata adha kubwa. Kama mnavyowajua, wenzetu wa Jeshi la Wananchi, ukikatiza kwenye maeneo yale unapigwa unapewa adhabu kubwa. Ng’ombe wakijitokeza wakiingia wanapigwa faini kubwa, mpaka laki tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaomba, kwamba hawa Watanzania ambao wamezuiliwa kufanya uendelezaji wowote ule; kuanzia mwaka 2010 mpaka leo, walipwe fidia ili waende maeneo mengine wakafanye uzalishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, huwa ninasema hapa, kwamba kama wameshindwa kulipa fidia basi Jeshi hili lirudi kule Nyandoto ambako kulikuwa na kambi yake ili wale wananchi nao waendelee na uzalishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni kuhusu uwekezaji wa Barrick. Kuna maeneo ambayo walifanyia tathmini kule Nyamongo, maeneo ya Nyamichele na kwingineko. Kwa mfano Nyamichele pale zaidi ya wananchi 2,000 mpaka leo waliwakatia mazao yao wakaonesha kwamba wanaenda kuwalipa lakini hawajawalipa mpaka leo, wale wananchi wanasubiria hawajaweza kupata.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba, tunapokuwa tunatoa hizi ardhi basi tuhakikishe tunalipa fidia kwa stahiki kwa mujibu wa sheria inavyosema; msiendelee kuwatia umaskini, hawajiendelezi hamuwalipi hela wanakaa tu; ili waweze kwenda sehemu waweze kuzalisha na kuweza kuongeza tija kwenye taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine ni uwekezaji wa tija kwenye malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ambayo yanaanzia mwaka sifuri mpaka nane. Sote tunatambua kwamba mtoto hata ubongo wake unakuwa kwa asilimia 90 katika umri huu. Na nimesema niongelee hili hapa kwa sababu Ofisi ya Waziri Mkuu ndio waratibu na wasimamizi wa program jumuishi ya miaka mitano ambayo mmeianzisha, na ambayo ndiyo ya mama; sasa nikasema niongee na nitanabaishe changamoto ambazo tunakutana nazo na ni vipi tutazitekeleza. Tusiishie kuwa na document tu, tuna document nzuri tunai-document lakini kiuhalisia (in practiclal) unakuta haifanyiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunatambua kwamba watoto hawa umri wa miaka sifuri mpaka nane ni takriban milioni 16.5, ambao ni kama 30% ya population tuliyonayo. Katika program hii inaeleza kwamba kumsaidia mtoto katika kumlea, kumlinda, kumuhudumia kupata elimu bora ya awali, kuwa na afya bora, lishe bora kuhakikisha kwamba hadumai na mengineyo. Kuanzia kwanza mama akiwa mjamzito mpaka anazaliwa anafikisha miaka nane.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa Tanzania ni tofauti kabisa. Sote tunatambua kabisa kwamba kama Serikali ingefanya uwekezaji wa tija kwenye eneo hili ina maana umeshamjengea huyu mtoto foundation, tunakuwa na rasilimaliwatu yenye tija ambao wanaenda kulijenga taifa kwa baadaye. Tusipowekeza katika foundation ya umri huu ina maana tutaendelea kuwa na Taifa ambalo kwa kweli hatutaona hata huo uchumi unatamalaki. Tutajiegeza aidha kwa kutegemea ma-experts kutoka sehemu nyingine; kwamba, hatutakuwa na watu ambao ni analytical, watu ambao wamepevuka na ubongo wao umekuzwa vizuri, hawajadumaa, hawajashambuliwa na magonjwa mbalimbali, wamepata elimu ya awali vizuri na wanaweza kuwa hivyo. Kwa hiyo ni lazima tuwekeze.

Mheshimiwa Naibu Spika, tafiti mbalimbali zimefanyika na zinaonesha kwamba leo ukiwekeza dola moja kwa huyu mtoto au katika hizi program za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto faida yake au uzalishaji wake ni dola 17 za kimarekani. Lakini pia umeona kwa Watanzania zaidi ya asilimia 43 ya hao watoto hawafikii ukuaji timilifu, hawapati haya malezi kama yanavyotakikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshuhudia ukatili, mathalani nitatoa mfano kwenye ukatili tu, maana tunatakiwa tuwekeze kwenye lishe, elimu ya awali, kwenye kuhakikisha mtoto anahudumiwa vizuri na tuwekeze kwenye kumlinda; na naangalia hapa kwenye kumlinda na usalama wa huyu mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na matukio ya kikatili dhidi ya watoto kwenye taifa letu ambayo yamekuwa ni mwendelezo. Nita-site tu mfano ambao nimeshuhudia kwa wiki moja tu hii, na nitaanza jana kwenye Jimbo la Shinyanga Mjini la Waziri Patrobas pale. Kuna mtoto wa mwaka mmoja na miezi 18 amebakwa na baba wa kambo au baba yake mlezi. Amepelekwa hospitali Kambarage pale, wakapelekwa Government Hospital wakasema wakampa referral kwenda Bugando. Yule mtoto ameharibiwa kwa kutobolewa kote, mbele na nyuma. Inasikitisha sana! Inasikitisha sana! Mtoto wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja!

Mheshimiwa Naibu Spika, na haya matukio ni mengi, mengine yanakuwa reported mengine si reported. Kama taifa huyu mtoto hata akipona atakuwa affected kisaikolojia. Sasa wako wangapi kama hawa kwenye taifa letu? Tunachukua hatua gani dhidi ya haya yanayoendelea?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tena nilikuwa naangalia taarifa ya habari juzi kule Songea Shule ya Msingi Tembo Shujaa sijui kijana wa miaka 19 amebaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi zaidi ya nane, wadogo! Lakini kuna siku tulikuwa tunapata semina hapa, dada yangu Jesca hayupo leo, kule Iringa watoto wadogo wamelawitiwa na kubakwa! Sasa what are we doing? Mnafanya nini? Yaani tunafanya nini kama taifa? Kwa sababu hata hizi sheria tunazoziweka mimi naona kama vile zinakuwa loose. At a time unafikiri hata hao watu wawe wanahasiwa kabisa or even you remove that part ili jamii iweze kukaa vizuri, kwa sababu its unbecoming kabisa kwa taifa; its unbecoming.

Mheshimiwa NaibU Spika, kwa hiyo we end up documenting these things lakini hamna implementation so ever. Inaumiza sana! Inaumiza sana kama taifa; na kama mzazi kwa kweli naumia; kwa sababu pia nina watoto wadogo wa kiume na wa kike huwezi kujua huko wanafanyiwaje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia tumeshuhudia watoto hawa wananyanyasika wanauawa majumbani; yaani kuna mambo mengi sana. Mimi nafikiri tutafute approach nzuri ya kuhakikisha kwamba tunatatua hili tatizo. Tutafute the better approach.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri yafuatayo; moja; Serikali kama imedhamiria kutekeleza huu mpango itenge bajeti ya kutosha na katika hizi bajeti najua kuna settle means ziko huku katika kila Wizara ihakikishe ina kifungu kidogo cha bajeti kwenye Wizara husika; Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya TAMISEMI yenyewe pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi ya Teknolojia ili sasa tuweze kutekeleza kwa ukamilifu kwa kila mtu pale inapomgusa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine tuhakikishe basi kunakuwa na uratibu na usimamizi wenye tija kuhakikisha kwamba hawa watoto tunawalinda na wanakua kwa ktimilifu, yaani tusiishie ku-document ndugu zangu! naongea kwa ku-bold! Tukiishia ku-document hizi paper hatutafika popote pale tutakuwa na taifa ambalo limekuwa affected kisaikolojia, tutakuwa na taifa ambalo haliwezi kuzalisha kwa tija…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho dakika moja tu kwenye elimu ya awali ili watoto waweze kupata hizi elimu mbadala walimu ni wachache...

NAIBU SPIKA: Haya, sekunde moja.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nitaleta kwa maandishi ahsante sana.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa hizi dakika tano japo ni chache sana nitajitahidi kwenda katika point form. Kwanza kabisa niseme kwamba naunga mkono taarifa zote mbili za Kamati ya PAC na LAAC. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kikubwa nichangie kwanza kabisa kwenye misamaha ya kodi. Tumekuwa tukiongea kama Bunge na kuishauri Serikali kwamba walau misamaha ya kodi iwe angalau chini ya asilimia moja ya Pato la Taifa. Ukisoma taarifa ya PAC utaona kabisa wameainisha misamaha ya kodi isiyokuwa na tija kwenye Taifa letu na mbaya zaidi inatolewa kwenye makampuni mengine ambayo hayana leseni, mengine wanasema yameghushi. Sasa swali hapa ambalo tungetaka tujue hawa watu ambao wamepewa hizi fedha, Serikali imechukua hatua gani, wameshazirudisha na kwa wale watendaji ambao waliidhinisha hii misamaha ya kodi ilhali watu wameghushi nyaraka, leseni zime-expire na mambo mengine wamechukuliwa hatua gani? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine ni suala zima la madeni ya Serikali kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii. Siku Mheshimiwa Rais anaongea na wanahabari alisema kabisa kwamba mifuko hii inafilisika kikubwa ni kwa sababu wanasiasa na mbaya zaidi akasema Wabunge sisi ndiyo tunafilisi mifuko hii kwa sababu tumekopa. Kwenye ripoti hii ya PAC imeanisha kabisa zaidi ya shilingi trilioni 1.5 Serikali inadaiwa na Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tunavyoongea kuna wafanyakazi fedha zao hazijapelekwa kwenye mifuko husika, kwa mfano, Askari Magereza na Polisi na wafanyakazi wengine tangu mwezi wa nne mpaka sasa hivi makato yao hayajaenda kwenye mifuko husika. Sasa tunauliza ni kwa nini Hazina wasipeleke hizi fedha za michango kwenye mifuko husika? Yaani mnakopa kwenye michango ya wafanyakazi bado mnakopa kwenye uwekezaji halafu Rais anauambia umma kwamba Wabunge ndiyo wamefilisi mifuko ya jamii, is he serious? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine, tumekuwa tukilalamika kuhusu kukaimishwa kwa watendaji kwenye mashirika ya umma lakini pia imekithiri kwenye Halmashauri zetu. Ni wakati sasa Serikali ione umuhimu wa either kuwajiri watu wenye uwezo kwenye vitengo mbalimbali, kwa mfano kwenye Halmashauri yangu ya Mji wa Tarime mara nyingi nimekuwa nikimfuata Waziri husika, kuna watendaaji wanakaimu kule, ufanisi ni zero, Halmashauri inakuwa haiwezi ikafanya vizuri. Naomba kabisa Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ufanye juhudi na wale wengine ambao wanasimamia mashirika mbalimbali tusiwe tunakaimisha hizi nafasi inapunguza ufanisi wa kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, asilimia 20 za ruzuku ambazo zinatakiwa kwenda kwa Serikali za Mitaa na Vijiji. Tumekuwa hata tukiuliza maswali humu ndani, wale Wenyeviti wa Mitaa hawalipwi posho, unakuta hata hawana stationary kwa hiyo wanashindwa hata kufanya kazi. Fedha ambazo mnapeleka kule kwenye Halmashauri haziwafikii Serikali za Mitaa au za Vijiji. Tunaomba sasa Wizara husika muweze kuwa na ufuatiliaji kama ni ripoti inakuwa inatolewa kuhakikisha kwamba hizi asilimia 20 kweli zinatengwa au hazitengwi na kama hazitengwi ni kwa nini zisiende kule chini na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho kinahuzunisha zaidi ni zile asilimia kumi kwa ajili ya vijana na wanawake. Kikubwa hapa kinakuja unakuta Halmashauri haina mapato, fedha wanazokusanya wanapeleka sehemu zingine. Kwa hiyo, hii ipo tu kwenye makaratasi kwamba wanawake wanapewa asilimia tano na vijana wanapewa vijana asilimia tano lakini kiuhalisia hakuna. Mfano kwenye Halmashauri yangu ya Mji wa Tarime hiyo kitu haipo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo kubwa ni kwamba vyanzo vya mapato ni vichache, lakini kingine mnaelekeza kwamba fanya kitu fulani kwanza, kwa hiyo, priority ya kutoa fedha kwa ajili ya Mfuko huu kwa ajili ya vijana na wanawake haipo na hii inakuwa inayumbisha. Tunaomba sasa utiliwe mkazo kama nilivyopendekeza kwenye ruzuku ya asilimia 20 na kwenye hii ruzuku ya asilimia kumi ya vijana na wanawake napo Serikali kupitia Wizara husika wahakikishe wanawake na vijana wanaenda kunufaika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho nilitaka nizungumzie…
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Esther.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia Wizara hii muhimu kwa ujenzi wa uchumi wa nchi yetu. Nchi yoyote ile yenye miundombinu imara ya reli, barabara na anga, basi ni dhahiri uchumi wake huwa imara. Bila kuwa na miundombinu imara, kamwe hatutaweza kufikia Tanzania ya Viwanda kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano. Tuwe na barabara zenye kuwezesha usafirishaji wa malighafi kwenda viwandani na kuwezesha mazao kwenda sokoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji kuwa na reli imara itakayoweza kusafirisha mizigo na kupunguza uharibifu wa barabara zetu, lakini kuweza kusafirisha mizigo mingi kwa wakati mmoja, kusafirisha abiria kwa wingi na kwa muda mfupi. Vile vile tuwe na miundombinu ya anga imara ili tuweze kupokea ndege nyingi toka Mataifa mbalimbali hasa kwenye Majiji kama Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa niweke msisitizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma tuwekewe lami kwenye runways na hata kupanuliwe ikiwezekana. Uwanja wa Ndege wa Mugumu Serengeti, ni wakati muafaka ukamalizika ili kuweza kuinua uchumi wa Mara kwa kuongeza idadi ya watalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiwa bado kwenye dhamira ya kukuza utalii, ni vyema Serikali ikafanya tafiti za kina ni nini kilipelekea Shirika letu la ATCL kufanya vibaya toka kuwa na ndege kubwa zaidi ya kumi hadi kuwa na kandege ka kukodi? Sababu awamu hii Serikali imeamua kufufua ATCL kwa kununua ndege, basi ni vyema Menejimenti ya Shirika hili iweze kufumuliwa na kuundwa upya kwa kuweka wafanyakazi wenye weledi na dhamira ya kuendesha Shirika hili na kuona tunakuwa na National Carrier itakayoitangaza nchi yetu na hivyo kuongeza idadi ya watalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa lisilokuwa na ndege zake, basi daima uchumi utayumba. Ni dhamira yangu na nadhani matumaini ya Watanzania wengi akiwemo Mheshimiwa Rais kuona tunakuwa na ndege zetu na hivyo kukuza uchumi wetu. Angalizo ni kwamba tuzingatie kanuni, taratibu za manunuzi na kuepuka kununua ndege kwa cash money.
Mhesimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kwamba ujenzi wa barabara ya kuanzia Tarime Mjini kwenda Nyamwaga - Mto Mara hadi Ngorongoro, ijengwe kwa kiwango cha lami ili kuweza kurahisisha usafirishaji wa chakula kati ya Tarime na Wilaya ya Serengeti. Pia kukuza uchumi kupitia utalii, kwani watalii wengi hupitia Sirari kutoka Kenya na kupita njia hii kwenda Serengeti, Mbuga ambayo ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Jimbo langu la Tarime Mjini na hata Majimbo mengine, tunaomba TANROADs wanapojenga barabara, basi wawe wanaingia angalau mita 20, kama kanuni inavyoelekeza, maana Jimboni kwangu barabara unganishi na TANROADs zimekatika kwenye maungio na kusababisha adha kubwa sana kwa watumiaji. Pia na uchimbaji wa mitaro ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia hoja hii kwenye maeneo ya maliasili na utalii, elimu, kilimo, viwanda, afya na uchumi kwa ujumla.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa masikitiko makubwa kuona mpango huu haujaweka Sekta ya Maliasili na Utalii kama moja ya maeneo ya vipaumbele licha ya kwamba sekta hii huchangia zaidi kwenye kuingiza fedha za kigeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutolewa kwa maliasili na utalii katika vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo ya Taifa ni fedheha na masikitiko makubwa kuwa sekta hii haipo katika Mpango wa mwaka 2017/2018. Tunaomba Serikali itoe sababu za msingi, ni kwa nini Sekta ya Maliasili haipo ilhali ndiyo sekta iliyokuwa ikichangia kukuza uchumi wa ndani kwa miaka yote na ndiyo inayotoa ajira kwa vijana na haihitaji gharama kubwa sana za uendeshaji?
Mheshimiwa Naibu Spika, kupungua kwa watalii wanaoingia nchini na hali mbaya ya Sekta ya Utalii; mfano watalii wamepungua kwa 8% kutoka watalii 1,140,156 mwaka 2014 mpaka watalii 1,048,944 mwaka 2015 na bado hali inazidi kuwa mbaya kwani watalii wanazidi kupungua kila siku hasa baada ya uwepo wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma za Maliasili na Utalii. Pia kumekuwepo na upungufu wa idadi ya watalii wa hotelini 1,005,058 mwaka 2014 mpaka 969,986.
Mheshimiwa Naibu Spika, kupungua kwa mapato ya utalii kutoka dola milioni 1,982 mpaka 1,906; na hizi ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014/2015. Vile vile kwa wastani wa siku za kukaa watalii, zimepungua kutoka siku 12 mpaka kumi na kwa sasa hali imezidi kuwa mbaya zaidi baada ya kuwepo kwa VAT, maana Sekta ya Utalii imekuwa na mlundikano wa kodi nyingi sana takriban 32. Hizi zote zinaongeza gharama na kusababisha watalii kuona ni ghali sana kuja kupumzika na kujionea utalii wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kumekuwepo na matatizo makubwa kwenye Sekta ya Utalii yanayochangia kushuka kwa mapato yatokanayo na utalii. Mfano tu, ninavyoongea sasa, Mamlaka ya Ngorongoro imekataza wamiliki na magari binafsi yanayotoa huduma za kitalii kwa kutumia magari binafsi ambayo kimsingi yamesajiliwa kibiashara na yamekidhi vigezo vyote vya magari ya utalii ila tu siyo magari ya Kampuni, yawe ndiyo kama masharti ya leseni ya utalii inavyotaka. Kama barua yenye Kumbukumbu Namba NCAA/D/584/Vol.XIII/20, pamoja na barua TNP/HQ/L.10/22 iliyohusu zoezi la uhakiki wa leseni kwa makampuni yanayofanya shughuli za utalii.
Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa takriban magari 300 yamezuiwa kufanya kazi za kupeleka wageni ndani ya hifadhi. Makampuni yaliyokuwa yanafanya biashara kupitia magari haya tayari yalikuwa yana wageni ambao wanapaswa kwenda hifadhini, hivyo watalii wengi wanataabika ilhali tayari wameshatoa pesa zao na wanahitaji huduma. Hii ina athari ya moja kwa moja katika soko zima la utalii nchini ambalo mpaka sasa linakumbwa na changamoto lukuki.
Mheshimiwa Naibu Spika, natambua hitaji la kisheria katika kupata leseni ya utalii, lakini tujiulize, tunawasaidia vipi Watanzania hawa ambao wamejichanga na kupata fedha kidogo kwa ajili ya mtaji wa kuanzisha biashara hii?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, nichukue fursa hii kuishukuru Wizara kwa kuwa Waziri Profesa Maghembe na Watendaji wake waliweza kuona ni fursa nzuri za kuendelea kuwaajiri watu kwenye Sekta ya Utalii ya Usafirishaji kwa kulifanyia kazi pendekezo letu tulilolitoa wakati wa bajeti, ambapo tulipendekeza Serikali angalau iweke sharti la magari kuwa matano badala yake yamekuwa mawili au matatu. Kwa taarifa nilizonazo, ni kuwa magari matatu ndiyo hitajio. Hii ni hatua tatuzi kwa vijana maskini wa Kitanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, pendekezo langu ni kwamba, kufuatia barua ya Ngorongoro ni kuwa, Serikali ipate uhakika wa uwepo wa magari matatu katika kuanzisha biashara, iwe ni magari matatu bila kuwa na kigezo cha umiliki, bali ieleze kuwa kampuni ni lazima iwe na magari matatu, iwe ni magari ya kukodi au ya kibiashara lakini ni lazima kampuni ioneshe uwezo na uhakika wa magari hayo; na yabandikwe sticker. Msingi wa hoja hii ni kuwa siyo Watanzania wote wana uwezo wa kumiliki magari matatu yenye viwango elekezi, bali wanaweza kukodi magari yenye viwango elekezi na biashara hii ikaendelea na kutoa ajira na kukuza uchumi ndani ya nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kwenye sharti la leseni ya biashara (TALA License) hiyo kuna hitaji la kampuni kulipa dola 2,000 kwa makampuni ya ndani na dola 5,000 kwa makampuni ya nje, havijalishi idadi ya magari ambayo kampuni hiyo inamiliki.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini Serikali isihakikishe kuwa linalipa dola 100 kwa mwaka bila kujali idadi ya magari? Serikali itapata fedha nyingi zaidi kwa kuwa yapo makampuni yana magari zaidi ya 300 na yanalipa dola 2,000 na mengine yana magari matano na yanalipa kiasi sawa cha dola 2,000. Endapo kila kampuni italipa dola 100 kwa mwaka, ina maana kwamba kwa makampuni yenye magari 300 kwa mwaka watalipa dola 3,000 badala ya 2,000 kama ilivyo sasa. Hii itasaidia wafanyabiashara wadogo pia kuweza kumiliki magari yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nashauri hii Sekta ipewe kipaumbele. Tulishauri kuwa kodi ya ongezeko la thamani ni bomu kwa uchumi wetu na sasa athari imeanza kuonekana. Tuliwaiga Kenya, lakini wenzetu waliondoa hiyo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na nature ya utalii ya Kenya ni kama kwetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu mwingine ni juu ya zoezi zima la uhakiki wa wafanyakazi hewa ambalo limechukua muda mwingi, nalo linaendelea kuwaacha Watanzania wengi bila ajira na kwa wale waliokuwa wanasubiri ajira pamoja na wale walioajiriwa mwezi wa Nane, 2015 ambapo walisitishiwa ajira kupisha uhakiki tangu Februari, 2016 hadi leo hawapo kazini na hawalipwi mshahara. Unategemea hawa Watanzania wataishi vipi? Tunataka majibu kwenye hili maana Mheshimiwa Rais alisema akiwa BoT kuwa zoezi la uhakiki wa wafanyakazi hewa kuwa ni kati ya miezi miwili au mitatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kinachoonekana sasa ni dhahiri Serikali hii haina fedha ama inaelekea kufilisika na hivyo kuamua kwa makusudi kujificha chini ya kivuli cha uhakiki ili kuondoa aibu ya kutokuwa na fedha ya ajira mpya. Fedha za nyongeza kwenye kupandisha madaraja, kuongeza mishahara kwa mujibu wa Sheria na Mikataba, hakuna watumishi kwenda masomoni wakilipiwa na mwajiri wake. Tunaomba majibu katika hili, maana bila Walimu wenye motivation, Madaktari, Manesi na kadhalika, hii nchi tunaiweka kwenye bomb. Hatua stahiki zichukuliwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania ya viwanda bila mikakati ya elimu yenye kutoa elimu na wanafunzi wa kada mbalimbali ili waweze kwenda kwenye viwanda tarajia; bila mikopo kwa kada zote kwenye elimu ya juu ni bomb. Bila kuwekeza kwenye motisha za Walimu kama nyumba, ofisi, Transport Allowance and Hardship Allowance; pia bila kuwa na uhakika wa maji ni ndoto kuzungumzia Tanzania ya viwanda kama hakuna umeme, miundombinu imara ya barabara, kuwekeza katika kilimo chenye tija ili kiweze kutoa malighafi kwa ajili ya viwanda tarajiwa, itakuwa ni ndoto ya Abunuwasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ni juu ya kutokuwekwa asilimia za pato la Taifa kwenye Mpango wa Maendeleo, sababu na Sheria ya utekelezaji ya Mpango wa Maendeleo. Mpango wa mwaka 2011/2012 – 2015/2016 tuliazimia 35% ya pato la Taifa ziende kwenye Mpango wa Maendeleo lakini kwa sasa mpango hausemi chochote. Hii ni hatari sana maana tunaweza kukuta mpango huu ukitegemea wahisani zaidi, kitu ambacho ni hatari kama nchi tusipowekeza kwenye maendeleo yetu wenyewe.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ni juu ya umuhimu wa kuona review kwenye mdororo wa kutokuwa na mizigo Bandarini ambayo inatokana na tozo mbalimbali, wharfrage tunatoza dola 240 kwa futi 20 lakini wenzetu dola 70 na VAT on Transit na kadhalika.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru nami kuweza kupata fursa hii ili niweze kutoa maoni yangu kufuatia ripoti ya Kamati ya Bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nionyeshe masikitiko yangu ya kwamba katika ripoti hii ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ni robo moja tu ndiyo tumeletewa katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu. Tuko robo ya tatu sasa hivi kwa hiyo nilitarajia kabisa tungeweza kupata mpaka robo ya pili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/2017. Cha kusikitisha zaidi tunaona ni kwa kiasi gani bajeti hii haitekelezeki kama vile ambavyo tuliletewa hapa. Ikumbukwe wakati tumeleta hii bajeti mwanzoni nilisema kabisa kwamba hii bajeti haina uhalisia na nitashangaa sana kama hata itafikisha asilimia 70 ya utekelezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyoongea hivi leo, fedha za maendeleo hazijakwenda kwa kiasi kikubwa sana lakini zaidi madeni. Juzi wakati Waziri anatoa kuhusu hali ya madeni na hapa nisikitike kidogo kwa mwanafunzi wangu Stanslaus anasifia kwamba wanalipa sana madeni. Nizungumzie tu baadhi ya haya madeni ya Watanzania wa ndani ambao wanaidai Serikali na inapelekea hata hawa Watanzania wanauziwa mali zao na wengine wanajiua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taarifa aliyotoa Waziri mwenyewe hapa ndani anaeleza kabisa kwamba mathalani wakandarasi wanadai shilingi trilioni moja, bilioni moja na milioni mia nne na mpaka sasa hivi wamelipa tu shilingi bilioni 360. Wanaotoa huduma za ndani wanadai shilingi bilioni 237 na wamemaliza kulipa shilingi bilioni 11 tu. Wazabuni wanadai shilingi bilioni 900 na kwa mujibu wa taarifa ya Waziri ya tarehe 19 wamelipa shilingi bilioni 49 tu. Hivi tunavyoongea hawa watu wanaotoa huduma hospitalini, shuleni, majeshini wanasitisha kwa sababu Serikali mmeshindwa kuwalipa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti sasa ningependa kujua mkakati wa utekelezaji wa ulipaji madeni haya ukoje. Jana mnasema madai ya Walimu mnafanya uhakiki yaani sasa hivi Serikali inajificha kwenye kufanya uhakiki. Madeni ya pembejeo tunafanya uhakiki, madeni ya Walimu tunafanya uhakiki, madeni ya wazabuni mnafanya uhakiki, kuajiri watu mnafanya uhakiki, muwe wazi mseme Serikali haina fedha ili Watanzania wajue kwamba Serikali haina fedha, kama wanauziwa mali zao ni kwa sababu Serikali haitaki kuwalipa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho kinasababisha hata Serikali isipate mapato kama ilivyokuwa ime-project, tulisema hapa kuna kodi zingine mmeziweka ambazo hazina uhalisia, hazitekelezeki, kodi kwenye sekta ya utalii, kodi kwenye transit goods. Ikasikitisha zaidi Mheshimiwa Rais anasema kabisa ni bora aje mtalii mmoja lakini alipe kodi, waje watalii wachache walipe kodi kuliko kuacha tusiweke hizi kodi ili watalii waje wengi. Mtalii akija alikuwa analipa hiyo kodi, akilala hotelini analipa na sehemu zingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tungekuwa tumewekeza kimkakati kwenye utalii kuhakikisha tunakuwa na angalau watalii hata milioni tatu, milioni nne ingesaidia kwani ni sekta pekee ambayo inatoa ajira nyingi, ni sekta pekee ambayo ingekuwa inaingiza fedha za kigeni. Leo Tanzania tuna vivutio vingi sana, tuna utalii wa fukwe, ukilinganisha hata na Afrika Kusini tu, wenzetu on average wana watalii zaidi ya milioni 15 sisi Watanzania eti milioni moja, halafu tunakaa hapa tunafikiri nchi yetu itaenda, tuna utalii wa kila aina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda Afrika Kusini pale Soweto utakuta watu wamepanga foleni kuangalia sehemu aliyoisha Baba wa Taifa Mandela lakini hapa kwetu ukienda Butiama ambayo ni makumbusho ya Baba wa Taifa utashangaa. Uwanja wa ndege wa Musoma tumesema mturekebishie ili watalii waweze kwenda pale watu wanaenda kujenga Chato, ndiyo vipaumbele! Yaani badala uboreshe Musoma, uboreshe na kwa Baba wa Taifa ili watalii waje wengi kwenye makumbusho unaenda kujenga Chato! Vipaumbele vya nchi hii, inasikitisha sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuweke mkakati wa kuhakikisha angalau tunapata watalii milioni tatu, milioni nne, Taifa letu litasonga mbele. Tuna vivutio vingi sana, eti vi-table mountain vya South Africa, sisi tuna milima mingi tu hapa, tuna fukwe nyingi. Leo Brazil fukwe zao wanazitumia vizuri sisi Watanzania tupo tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, uwekezaji kwenye bahari kuu, wanasema Chenge report na vitu kama hivyo. Serikali ingeamua kujielekeza kutafuta wawekezaji kwenye uvuvi wa bahari kuu ingekuwa ni chanzo kingine kizuri tu ambacho kingeweza kutupatia mapato. Hii ina maana wale watu wavue wale samaki, tuwe tumejenga viwanda hapa hapa waweze ku-process hapa hapa itatoa ajira nyingi lakini pia tukisha-process na ku-pack tutasafirisha ina maana tutapata fedha za kigeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya yote hayaonekani kama ni chanzo, tunabaki kusubiria Watanzania wakamatwe kwa boda boda, matrafiki siku hizi wanakaa kwenye magari wanasema kabisa sijui mnawa-promote, leo nimekusanya shilingi bilioni moja kutokana na makosa ya barabarani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, siku hizi huko mikoani, walala hoi waendesha pikipiki wanakamatwa, Tarime mfano hata tumeona Mheshimiwa Lacairo wa Rorya analalamika, mtu ameajiriwa na kapikipiki kake unamwandikia faini Sh. 90,000 atoe wapi wakati mwisho wa siku anatakiwa apeleke Sh.10,000 kwa tajiri wake, akishindwa pikipiki inachukuliwa na magari hivyo hivyo. Yaani sasa hivi Serikali hii ya Awamu ya Tano chanzo kikuu cha mapato ni kupitia makosa ya barabarani, aibu! Kama Taifa tuwekeze kwenye bahari, viwanda viwe vikubwa, kama nilivyosema vichakate hapa hapa, ajira zitapatikana tutasafirisha nje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kingine cha mwisho ni kilimo. Zaidi ya Watanzania 80% wamewekeza kwenye kilimo lakini kilimo chetu hakina tija kwa sababu hata vichocheo vya kuhakikisha kilimo kina take over vyenyewe bado viko hoi. Huwa tunaimba hapa kuboresha miundombinu ya usafirishaji, kwa sababu mimi nikilima niko kule kijijini lazima niwe na barabara ambayo itanisababishia lori kubwa lifike niweze kusafirisha mazao yangu kutoka point A kwenda point B, barabara ni mbovu, hazijatengenezwa kabisa. Tunaona lami tu za kwenye highway, mkatengeneze na huko ambako ndiko wakulima wako wengi ili waweze kusafirisha mazao yao kutoka vijijini kuja mijini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine ni umeme. Kaka yangu hapa Profesa Muhongo alisema ame-invest kwa mwaka huu ni zaidi ya shilingi trilioni moja na bilioni mia ngapi kwamba tutaona umeme unawaka vijijini. Ni matarajio yangu kwamba tutaona umeme unawaka huko ili hao wakulima wanaolima waweze kusindika yale mazao yasiharibike, waweze kujenga viwanda vidogo vidogo kuviongezea thamani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tukiwa na umeme, tukiwa na miundombinu mizuri ya barabara, maji yakawa yanapatikana tutaweza kuona kweli tunasonga mbele vinginevyo hatutaweza kuwa na mapato kabisa. Tutakuja hapa tunatoa bajeti, mapato ni hayo unaelekeza kwenye vinywaji, unaelekeza kwenye vikodi vya utalii kwa hiyo watalii hawaji mnakosa, tuwe na watu ambao wamesomea mambo haya waweze kuishauri Serikali na kuleta bajeti ambayo inaakisi uhalisia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nimekuwa nawatetea sana hawa ndugu zangu wa Magereza. Naambiwa Askari Magereza wanaidai Serikali kuanzia mwaka 2012/2013, 2013/2014, 2015/2016 ndiyo nimesikia sasa hivi mmewapelekea ya 2015/2016 nataka kujua 2012/2013 na 2013/2014 ni lini mtaenda kuwalipa? Pia tuweze kujua fedha za kuweza kufidia yale maeneo ambayo mmechukua…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango wako.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa sababu ni dakika tano nitakwenda kuongea kwa kifupi sana. Kwanza kabisa naunga mkono ripoti za Kamati zote mbili, lakini zaidi naomba Serikali ifanyie kazi ripoti ya Kamati ya Uwekezaji kwa yale yote ambayo tumeshauri pale na ambayo tumeyaona field. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa haraka haraka nisisitize kwa yale ambayo tumeandika kwenye Kamati yetu. Ni kweli kabisa tumeona athari ambazo zinajitokeza kwa kutokuwa na bodi kwenye taasisi na mashirika ya umma. Taratibu zinataka kwamba mchakato wa kuweza kuwa na bodi baada ya ile nyingine kukaribia kuisha walau uanze miezi sita kabla, lakini tumeshuhudia Serikali hii taasisi zinakaa bila bodi zaidi ya miaka miwili hadi miaka mitatu. Na mfano tumetolea Bodi ya TANAPA, imekaa zaidi ya miaka mitatu tunaona kabisa ile kesi ya concession fee ilihukumiwa tarehe 12 Septemba, 2014, lakini Serikali ikaona ni bora Taifa liendelee kupoteza kila mwaka zaidi ya shilingi bilioni 10 kuliko kuunda Bodi ya TANAPA ambayo ingeweza kufanya maamuzi na kuweza kupata fedha ambazo ni takribani zaidi ya shilingi bilioni 20 zimepotea, ambazo zingeweza kwenda kujenga zahanati na vitu vingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kumekuwepo na watumishi kukaimu kwenye nafasi za watendaji wakuu kwenye mashirika yetu na taasisi kinyume kabisa na sheria inavyosema. Unakuta mtu amekaimu zaidi ya miaka miwili hadi mitatu, wakati inatakiwa ndani ya miezi sita mtu aweze kupatikana kwa nafasi husika. Hii inasababisha mashirika yetu, taasisi zetu zisiwe na ufanisi katika utendaji na tutaendelea kuona mashirika yakiwa yanajiendesha kihasara kwa sababu hatujaweza kutengeneza management ambayo kwanza kabisa imebobea na inajua ni nini inafanya. Ukimkaimisha mtu hawezi akafanya decision kwa sababu hajua kwanza ultimatum ya nafasi yake ile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusu madeni ambayo Serikali inadaiwa na hazi taasisi. Unakuta imepata huduma lakini inashindwa kulipa madeni haya. Kwenye Kamati tumeainisha; mfano ni madeni makubwa kutokana na mifuko ya hifadhi ya jamii, tumeona madeni takribani kwenye PSPF ukiyachukua yote kwenye categories zile tatu ni takribani shilingi trilioni 3.47 za wanachama. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, alikuja Naibu Waziri wa Fedha akatuahidi kwamba watatoa hati fungani ya takribani shilingi bilioni 290 ambayo ilikuwa ni deni linalotokana na miradi, lakini mpaka leo hawajaweza kutoa hiyo hati fungani, hawajaweza kulipa malimbikizo ya madeni ya mwajiri kwenda PSPF, hawajaweza kulipa takribani shilingi trilioni 1.7 ya yale madeni ambayo waliyachukua kwa wastaafu wale wa kabla ya mwaka 1999. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuishii hapo tu, Shirika kama DAWASCO ni shirika dogo sana, lakini unakuta linadai shilingi bilioni 16 kutoka kwenye Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hizi shilingi bilioni 16 zingeenda DAWASCO zingeweza kusaidia na kuboresha huduma ya maji Dar es Salaam na Pwani, lakini unakuta hawalipi wakiambiwa hawalipi kwa sababu ni Jeshi basi linaendelea tu wanapata huduma. Ifike wakati hizi taasisi kama hazilipi na zenyewe zikatiwe maji, haiwezekani Mtanzania anashindwa kulipa 20,000 mnamkatia maji, lakini taasisi ya Umma inadaiwa mpaka shilingi bilioni 16 hamuwakatii maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni uonevu na Mtanzania wa kawaida akisikia anashangaa sana, yaani akishindwa kulipa bili ya maji ya shilingi 10,000, 20,000 anakatiwa maji lakini unakuta mnadai zaidi ya shilingi bilioni 16 na bado huduma ya maji inaenda. TANESCO wanawadai, TSN wanadai, LAPF wanadai, Serikali mnadaiwa madeni mengi sana. Tuweze kulipa haya mashirika ili yaweze kujiendesha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine kwa haraka haraka kabisa, wakati tumepitia kwenye hizi taasisi tumegundua kwamba hizi taasisi zinajiendesha kihasara. Tatizo lingine ni kwamba fedha wanazozipata wanazitumia kwenye matumizi ya kawaida badala ya uwekezaji. Kwa mfano, kama ilivyoainishwa kwenye baadhi ya mashirika; tumeona NSSF walitumia zaidi ya asilimia 17 kinyume kabisa na vile ambavyo matakwa yanataka asilimia 10 kwa mwaka wa fedha 2015/2016; lakini pia kamati imeainisha AICC na mashirika mengine. STAMICO inajiendesha kwa hasara, wanaweza wakawa wanakopa benki wanakuja wanajitumia kwenye matumizi ya kawaida ambayo ni kinyume kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kuhusu mikataba ambayo mashirika yetu yanaingia, taasisi zetu zinaingia hasa zikiwa kwenye ubia na wawekezaji wengine. Hii imekuwa inalipeleka taifa letu kwenye shimo siku zote. Na ninashindwa kuelewa wataalam wetu ni kwamba tunakuwa hatujui ni nini tunafanya au hatuna uzalendo wa kutosha. Kwenye taarifa yetu umetolewa mfano wa mkataba wa Mlimani City; kwamba sisi tunakubali kuingia mkataba wa kupata gawio la asilimia 10 ya faida na tunasema kwamba tunaingia mkataba mpaka baada ya miaka 50 ndipo tunaweza tukapata ile mali, na ukiangalia ubora wa yale majengo ya Mlimani City ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, ni dhahiri kabisa ndani ya miaka 50 tutakuwa tunapata mabua. Yaani wale wawekezaji watafaidika wataondoka sisi wakitupa asilimia 10 tu, Taifa…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante,
Sheria ya Fedha ya Mwaka 2019
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba niweze kutoa mchango wangu kwenye Muswada huu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2019. Ni dhahiri wote tunakubali kwamba tunahitaji kodi ili iweze kwenda kujenga miundombinu mbalimbali kama hospitali, barabara na mengine, lakini lazima tuwe na muundo ambao unakusanya kodi zenye tija na kutoka source ambazo zina uhalisia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nchi kodi inaweza kuwa ni mojawapo lakini tuna vyanzo vingi sana ambavyo tungeweza kupata mapato mbadala na kutoku-rely kwenye baadhi ya kodi kwa kweli ambazo hazistahili kuwa kodi. Naomba kwenye marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147, Serikali inapendekeza kifungu cha 7 chenye HS code 6703.00.00, 6704.11.00, 6704.19.00, 6704.20.00 na 6704.90.00 ambazo ni nywele bandia, bandia kope bandia, yaani na Waziri kabisa anasema kwamba lengo la kuweka hii kodi ni kuhakikisha kwamba tunapata mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa na kama ilivyokuwa imependekezwa awali na nasikitika bado Serikali inang’ang’ania hizi kama chanzo, huwezi ukasema leo unaweka asilimia 10 kwa viwanda vya ndani vinavyozalisha hizi nywele bandia na asilimia 25 kwa wale ambao wana- import ili uweze kuongeza mapato. Siyo chanzo halisia, hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wewe mwenyewe umependeza na hujaweka nywele bandia. Mheshimiwa Grace Kiwelu hapa, Mheshimiwa Dkt Sware, Mheshimiwa Mary Mwanjelwa, Mheshimiwa Salome na wengine wote, sasa Watanzania akinamama tukiamua kwenda hivyo, tusiweke hizo nywele bandia, hiki chanzo siyo halisia, kabisa. Tunapita hapo tutapoteza muda, tutapitisha, tutafanya kila kitu, mwisho wa siku tutakuja hapa haya mapato hayapo, ndiyo yale wana-project bilioni kadhaa, wakija uhalisia makusanyo chini ya asilimia 37.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, bado nasisitiza kabisa hiki kiondolewe chote hiki kifungu cha 7 chenye HS code 6703.00.00, HS code 6704.11.00, 6704.19.00, 6704.20.00 na 6704.90.00, wakiondoe ni aibu kwanza. Hii wanaenda kusababisha wajasiriamali akinamama ambao wamewekeza kwenye saloons na hivi vitu vingine waweze kuyumba. Sasa kama ni Serikali ya wanyonge…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko kuna taarifa, Mheshimiwa Getere

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba nimpe mdogo wangu Esther kwamba kwamba habari ya nywele gharama za kutoa nywele hazihusiki na wanawake zinahusika na wanaume. Sisi wanaume siyo wanawake…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ester Bulaya, naona umesimama.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, hicho alichokisema kaka yangu ambaye baada ya Jimbo kuachiwa kaenda kule kijijini, ni udhalilishaji wa wanawake, si kweli kwamba wanawake au kila mwanamke anategemea mwanaume ili apendeze, huo ni udhalilishaji, afute kauli yake. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tusikilizane, Mheshimiwa Getere amesimama akitaka kumpa taarifa Mheshimiwa Esther Matiko, kuhusu nani wanunuzi wa vifaa bandia ama nywele bandia ama kope bandia na vitu vyote vilivyoandikwa kwenye hicho alichokuwa anachangia Mheshimiwa Esther Matiko, kwamba hata hivyo wanunuzi wa hivi vitu ni wanaume na amesimama Mheshimiwa Ester Bulaya akisema kwamba kwa kusema hivyo Mheshimiwa Getere anadhalilisha wanawake.

WABUNGE FULANI: Ndiyo.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nimepata fursa ya kusikiliza nadhani michango yote ya hotuba ya Mheshimiwa Waziri kabla hatujahitimisha jana. Hata hivyo, nilisikia humu ndani sisi wenyewe wanawake na kama kuna mtu hakusikia ataenda akafuatilie Taarifa Rasmi za Bunge, humu ndani alisimama mwanamke akisema kwamba…

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Nani?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Haonga nimesimama unazungumza.

Kwa hiyo, alichangia kana kwamba hoja hii namna inavyopelekwa mbele tusiisisitize sana kwamba tunalipishwa kodi wanawake kwa sababu kulikuwa na mchango wa namna hiyo. Huyu alivyosimama akasema hii kodi huwezi kusema tunalipishwa wanawake kwa sababu na wanaume wanahusika kwenye kununua. Sasa alipokuwa anazungumza mwanamke huyu sikuona popote ambapo tulisimama kuonyesha kwamba ule ulikuwa ni udhalilishaji. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, sasa nimesimama hapa ili niweke vizuri, michango yetu anapochangia mwanamke kama na yeye anadhalilisha basi na yeye aambiwe hivyo na pia anapochangia mwanaume kama anadhalilisha na yeye aambiwe hivyo. Maana yake nini? Ni hivi yale maneno tunayoweza kuyasema mtaani huko tusiyaweke hapa ndani kwa sababu watu wengi walioko hapa ndani lakini pia hata huko nje, tunavyozungumzia hamsini hamsini siyo hamsini tu ya kuingia humu ndani ni hamsini na mambo mengine ikiwa ni pamoja na kujinunulia nywele na kulipa ada za watoto na mambo kama hayo.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, tusifike mahali tukaona wanaume ndiyo lazima watuhudumie, tuna uwezo wa kujihudumia wenyewe lakini ni pamoja na sisi wenyewe wanawake kulikubali hilo. Kwa sababu isitokee mwanamke anachangia kwa namna tofauti tukaona ni sawa lakini mwanaume akizungumza tukaona ni tofauti. Kwa hiyo, wanawake na wanaume kwenye jamii yetu tunatofautiana, wapo wanawake wanaotegemea wanaume lakini wapo wanaume wanaotegemea wanawake, tunategemeana.

Mheshimiwa Esther Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuru, muda wangu, nilikuwa nimeongea dakika moja tu. Hujaniuliza kama napokea taarifa au naiacha.

NAIBU SPIKA: Kwa sababu haikuwa taarifa, kwa hiyo, endelea na mchango wako.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ila siku nyingine Wabunge kama hawa wasiwe wanaingia Bungeni. Kama umenisikiliza kuanzia mwanzo nimesema hiki siyo chanzo halisia cha kodi, you can not rely on this. Halafu unatuaibisha sana watu Mara ndugu yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee, kwa hiyo, bado nasisitiza kwamba hii kodi iondolewe kabisa. Mapendekezo yangu hii kodi yote iondelewe kwa vifungu vyote ambavyo nimetaja, kwanza siyo halisia lakini pili inaweza ikaweka ugumu kwa wale wa akina mama ambao wamejiwekeza kwenye ujasiriamali wa salon na vitu vingine kama hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ni Sehemu ya Nne, amendment of Income Tax Act, Cap 332. Katika marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, kifungu cha 9, Serikali pia inapendekeza kiongezwe kipengele (d) kwenye kipengele cha (a)(iii) ambapo pamoja na mengine yote kuhusiana na taulo za kike mmesema mtaweka hiyo exemption kwa makampuni for two years kwa corporate income tax lakini pia kuna sheria ambayo iliondoa import duty of which makampuni hayajaelezwa, ni mawili tu ndiyo yamepata kupata msamaha wa kuingiza bila huo ushuru wa bidhaa. Kikubwa hapa taulo za kike pamoja na hizi measure ambazo mmezionyesha hapa hazitasaidia kupunguza hapa bado nasisitiza kwamba Kodi ya Ongezeko la Thamani iondolewe kwenye taulo za kike kama vile ambavyo tulifanya mwaka wa fedha uliopita. Hii itamsaidia siyo tu mwanamke wa Kitanzania, tulilenga pia kuwasaidia watoto wetu ambao ni wanafunzi wanashindwa kwenda shule wakiwa kwenye siku zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, excuses ambazo Serikali ilitoa hapa kwamba ikiweka VAT haina athari kwenye bei ya mlaji haina mashiko. Kama Serikali mnatakiwa kusimamia kuhakikisha kwamba ushuru umeondolewa huu wa VAT lakini wale wauzaji na wasambazaji wapunguze bei, it can be done, nyie Serikali vingapi mmevisimamia na Waraka zinatoka na wauzaji wanafuatilia, why not this? Kwa hiyo, naendelea kusisitiza kabisa Serikali muangalie suala hili kwa jicho la kipekee kuhakikisha mnamsaidia siyo tu mwanamke wa Kitanzania bali na wale mabinti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kabisa jana nilisikitika Mheshimiwa Naibu Waziri anasema kwamba mojawapo ya factor ya kuondoa hii, kwanza baada ya kuondolewa kuna baadhi ya Wabunge hapa walizunguka wakawa wanapongezwa na nchi za nje, kwa hiyo, ikawa ni factor mojawapo ya kurudisha kodi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiki kitu ni cha ajabu sana yaani wakienda nje wakawa proud of kwamba Serikali yetu imeondoa kodi ni sifa kwa Serikali na wala siyo chanzo cha ku-penalize watu hawa. Hii ni ajabu sana kwa sababu Mtanzania akipewa tuzo huko nje ni sifa kwa Serikali yake. Kwa hiyo, naomba kabisa hii kodi iweze kuondolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ni marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Fedha, clause ya 39(5).

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Muda wangu ndiyo kwanza kengele ilikuwa imegonga.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, usiuzungumzie sana muda kwa sababu kengele ya kwanza imeshagonga hapa. Mheshimiwa Waitara.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuru naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Esther Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini, mwanamke wa Mara kwamba sisi watu wa Mara tunasikitika sana tunapokuwa tunazungumzia mambo ya pedi na nywele. Kule kwetu haya mambo ni aibu kuyazungumza.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nimpe taarifa kwamba…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko malizia mchango wako.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, sema muda umeenda lakini nasikitika kama na wewe ni mmoja wa watu kutoka Mara kwamba mwanamke wa Mara hastahili kupata pedi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu hiki cha 39(5) kinasema kwamba biashara inavyoanzishwa hawa wafanyabiashara wapya wanapata ahirisho la kulipa kodi kwa miezi sita wanakuja kulipa baadaye. Mimi nasema hii haisaidii, napendekeza Serikali itoe msamaha kabisa kwa miezi sita ya mwanzo wakati biashara inaanzishwa ule mwezi wa saba ndiyo hawa wafanyabiashara waweze kutozwa kodi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukisema unafanya ahirisho la muda kwamba unampa muda wakati anaanzisha ile biashara suppose inafika mwezi wa sita au wa saba huyu mtu anashindwa kuendesha biashara ile ndiyo utaanza kuona mnakimbizana mnamkamatia mali zake maana biashara imekufa wakati anatakiwa alipe malimbikizo. Kwa hiyo, nina-propose wapewe tax holiday kama tunavyowapa makampuni ya nje yanayokuja hapa nchini, ya six month kuanzia mwezi wa saba ndiyo waanze kutozwa kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa Serikali imeleta kifungu kingine ambacho kinaingiza kwenye sheria na kanuni kwamba sasa mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya vitambulisho vya wajasiriamali ni Waziri. Kwanza nashukuru limekuja lakini nasikitikia kwamba vitambulisho vilishasambazwa kitambo na ma-DC na Wakuu wa Mikoa leo ndiyo mnatuletea kipengele hiki kuingiza kwenye kanuni na sheria kwamba Wizara sasa iweze kusimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hapa hapo tunaenda kumtoza huyu majasiriamali kitambulisho Sh.20,000 wakati huo huo makampuni ambayo mapato yao turnover ni shilingi milioni 4 kwa mwaka hawatozwi chochote. Kwa hiyo, tuna nia ya dhati ya kumsaidia Mtanzania maskini au tunafanya tu? Unamsamehe mtu wa shilingi milioni 4 asilipe chochote unaenda kumdai mama ntilie mtaji wake Sh.15,000 au Sh.30,000 unampa kitambulisho cha Sh.20,000. Kwa hiyo, hii nayo kwanza tuitafakari mara mbili mbili ikiwezekana iondolewe kabisa. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa hii niweze kuchangia. kwanza kabisa, naunga mkono ripoti za Kamati zote mbili lakini nitajielekeza sana kwenye suala la elimu kama ambavyo tunajua elimu ya Tanzania iko ICU.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda kushauri baadhi ya maeneo ambayo Serikali inatakiwa iyafanyie kazi ili walau tuweze kuwa na elimu iliyo bora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki ya Dunia ilishauri ili Taifa liweze kuwa na elimu bora walau tuweze kuwekeza 5% ya Pato la Taifa. Ukiangalia nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wenzetu wamewekeza vya kutosha. Kwa mfano, Kenya wamewekeza 6% ya pato la Taifa, Rwanda wamewekeza 5%, Uganda wamewekeza 4%, Burundi wamewekeza 3% lakini sisi Tanzania tumewekeza 1% tu ya Pato la Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutashikana uchawi hapa, Wakuu wa Mikoa watawafukuza walimu kama tulivyosikia Mtwara, wanasiasa wataingilia, watawaghadhibu walimu lakini uhalisia ni kwamba hatujawekeza vya kutosha kwenye elimu ya Watanzania. Kama Taifa lazima tuwekeze vya kutosha. Kamati hapa imesema tunatenga fedha lakini haziendi.
Kwa hiyo, naomba kabisa Waheshimiwa Wabunge tuazimie na kwenye bajeti ya 2017/2018 tuhakikishe walau tunatenga 3% ya Pato la Taifa kwenye elimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kushauri Rais aone kwamba ni wakati muafaka sasa wa kuunda tume ya kuweza kuchunguza hali ya elimu nchini ili waje na mbadala wa nini kifanyike kuweza kufufua elimu yetu. Pia ni wakati sasa Waziri aweze kuteua Wajumbe wa Baraza la Kumshauri kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1978 na marekebisho yake ya mwaka 1995 ambao watakuwa wanamshauri Waziri kitaalamu maana tumekuwa tukishuhudia sasa hivi Mawaziri wanatoka tu na matamko. Kwa hiyo, tunaomba kabisa aunde lile Baraza liweze kumshauri kitaalam ni vipi tuweze kusonga mbele katika elimu yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuwathamini walimu, mimi ni mwalimu. Walimu wasipokuwa na motisha hatuwezi kuwa na elimu bora. Imeelezwa hapa kwa mujibu wa takwimu za CWT ni zaidi ya shilingi trilioni 1.06 walimu wanadai. Wale ambao wamerekebishiwa mishahara ni walimu 5,000, walimu 80,000 bado hawajarekebishiwa mishahara wanadai zaidi ya shilingi bilioni 300, kuna wale walimu ambao wamestaafu takriban 6,000 wanadai zaidi ya shilingi bilioni 480 na kuna wanaodai madeni ya likizo ambayo hata bado hayajaboreshwa. Malengo ya BRN walisema walimu waweze kulipwa madeni yao ndani ya siku 90, sasa ni kwa nini Serikali inachukua muda mrefu sana?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu kwa Wote (Universal Secondary Education). Kwa maoni yangu nashauri sera hii tusiitekeleze sasa hivi kwa sababu Serikali haijajiandaa. Kwa mfano, ukisema elimu ya msingi iishie darasa la sita na waendelee kwenda sekondari kwa wote, tumejenga sekondari zipi za kuweza ku-absorb hawa watoto wanaotoka shule ya msingi na kuendelea moja kwa moja, bado hatujajiandaa! Ni dhahiri sasa tuweze kujiandaa kwanza kama nchi, kwa baadaye ndiyo tuweze kutekeleza hii Sera ya Elimu kwa Wote.
Kwa hiyo, iendelee watoto kujiandikisha shule wakiwa na miaka saba na elimu ya msingi iendelee kuwa darasa la saba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni wanasiasa kuingilia masuala ya kitaalam ya walimu. Utakuta Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa anajaziwa mafuta eti anaenda kukagua shule wakati huo huo wakaguzi ambao ni wataalam wanakagua kwa 30% tu na wanasema hawana fedha za kuweza kuwazungusha kukagua shule. Sasa hawa Wakuu wa Wilaya na Mikoa wengine hata hawana utaalamu huo, wako busy wanajaziwa mafuta kuzunguka kukagua shule. Tusiingilie kabisa kwenye masuala ya kitaalamu tupeleke fedha kwa wakaguzi waweze kukagua na kutoa mapendekezo ya kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni kwenye afya kuhusu Taifa la vijana kuteketea na viroba. Kamati hapa imesema na mimi Jimboni kwangu kabisa waliniambia nilete Hoja Binafsi. Hivi viroba na sasa hivi hali imekuwa ngumu vijana asubuhi tu na mmewakataza wasiende kwenye bar mpaka saa kumi, kwa hiyo, wenyewe wakiamka tu asubuhi na pikipiki zao wamekamatwa na polisi na wengine kazi ngumu ngumu wanakunywa viroba vile. Viroba kwanza havina standard! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimboni kwangu nilivyokuwa nimekwenda baada ya hii likizo fupi tumezika vijana zaidi ya wanne na wananchi wamenituma kama Bunge tuazimie viroba vifutwe Tanzania, visizalishwe wala visiingizwe Tanzania.
Kwa hiyo, naunga mkono kabisa mapendekezo ya Kamati kuhusiana na viroba viweze kupotea kabisa vinginevyo tunateketeza Taifa letu, vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa wanateketea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine na cha mwisho ni kuhusu dawa za kulevya, zimezungumzwa kwa upana wake. Kama Taifa tujiulize ni kwa nini tumekuwa tukiimba, hatutekelezi. Kabla ya mwaka 2010 hata sijawa Mbunge tunaona kuna ma-champions walikuwa humu wakizungumzia dawa za kulevya na wengine wakataja kabisa, Marehemu Amina alitaja baadhi ya watu hapa. Tukaja Bunge la Kumi wengine tukawa Wabunge, Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, Mheshimiwa Bulaya, Mheshimiwa Jenista, Mheshimiwa Rais Kikwete akasema ana orodha….
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuweza kunipatia fursa hii nami niweze kuchangia kwenye hotuba ya Waziri Mkuu. Naomba Waheshimiwa Wabunge kama tunatambua ni nini wananchi wametutuma kufanya kwenye Bunge hili Tukufu, basi tuwatendee haki kwa kufanya yale ambayo wametutuma kufanya na kutokujitoa ufahamu na kufanya kinyume na ambavyo tumetumwa na wananchi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hotuba ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni na ninaomba Waheshimiwa Wabunge msome hotuba zote pamoja na kwamba mtakuwa mnayo mengine kichwani, lakini hotuba ya Upinzani kwa kweli imeeleza mengi na mazuri kwa Taifa letu, tuweze kuishauri vema Serikali ili tuweze kusonga mbele kama nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016 nilisema kabisa wakati wa bajeti imepitishwa na niliandika kwenye mtandao wa Bunge, nikasema hii bajeti ikitekelezwa hata kwa asilimia
70 tu, nikatwe kichwa changu. Mbunge mmoja, ndugu yangu Mheshimiwa Chegeni akaingia inbox akaniambia unamaanisha nini? Sasa napenda nimwambie nilichokimaanisha ndiyo tunachokiona leo, kwamba mpaka leo bajeti ya maendeleo hata asilimia 40 hatujafika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nishauri kwamba kuliko kuja na bajeti ambazo hazina uhalisia, kama mpaka leo hatujafika asilimia 40, ile bajeti ya mwaka jana, tuchukue nusu yake ndiyo tuilete. Tulete bajeti ambazo zinatekelezeka. Tusiandike matumaini kwenye makaratasi mwisho wa siku hata asilimia 50 tu hamfikishi. Tuwe na uhalisia ili hata unapokuwa umeelezwa kwamba mathalan Mkoa wa Mara Jimbo la Tarime Mjini kwenye maendeleo kwa mwaka wa
fedha 2017/2018 tutaleta shilingi bilioni moja, basi na hiyo shilingi bilioni moja tuweze kuitekeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo ningezungumzia tuliondoa duty free kwa majeshi kwa maana Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi, Askari wa Uhamiaji, Askari wa Majini na Magereza. Cha ajabu mpaka leo kumekuwa na double standard. Kuna wengine wameshalipwa mara mbili, kwa maana ya kila mwezi laki, laki; wameshalipwa shilingi laki sita. Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Askari Polisi, lakini Askari wa Uhamiaji, Majini na Magereza mpaka leo hawajalipwa. Ndugu zangu, tunataka kujua ni kwa nini kunakuwa na double standard?
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba kabisa Mheshimiwa Waziri Mkuu awaangalie ndugu zetu Magereza, wamekuwa wakionewa sana. Unakuta Askari Magereza ana degree lakini bado analipwa mshahara kama yule askari wa kidato cha nne. Leo mnawalipa hawa wengine, lakini hawa Askari Magereza niliowatja mpaka leo hamjawalipa. Wale watu ni muhimu sana na ikizingatiwa kuna watu mnawapeleka kwa kesi za kubambikwa kule Magereza. Hawa watu wakiamua kugoma, wale watu waliopo magerezani kule kutakuwa hakukaliki. Kwanza mngekuwa mnatumia busara zaidi, mngewalipa wale kabla hata hamjawalipa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Naomba mzingatie hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna madeni wanadai ya mwaka 2012/2013; 2013/2014 mpaka leo hawajalipwa. Leo mfungwa akitoroka, hawa ndugu zetu wanapewa adhabu kutokwenda masomoni, wanapewa adhabu ya kukatwa fedha, maisha wanayoishi ni duni na kipato chao ni duni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Waziri husika tunaomba hawa ndugu zetu muazingatie na wenyewe waweze kupata hiyo package ambayo mliiondoa ya duty free nao waweze kupata stahiki zao kama mnavyowapa Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba ya Waziri Mkuu ametanabaisha kwamba wamejitahidi sana katika kuwawezesha wananchi, lakini ukisoma ameainisha kwamba kuna shilingi bilioni moja sijui pointi ngapi wamewapa vijana kwa mfuko wa vijana na shilingi bilioni 4.6 kupitia
Halmashauri, kwamba ndiyo hapo wamewezesha wananchi. Hatuko serious na Serikali hampo serious. Mlituambia mmetenga milioni 50 kwa kila kijiji au mtaa, mpaka leo mtuambie mmetekeleza vipi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Waziri Mkuu akija akasema kwamba Halmashauri zimejitahidi kupeleka 4.6 billion kuwezesha wananchi ilhali mkijua kuna Halmashauri nyingine hazina kipato cha kutosha, mathalan Halmashauri ya Mji wa Tarime, tumejitahidi, hapo zamani walikuwa hata
hawatoi hela. Kwa mwaka huu, tumejitahidi tumetoa ten million. Ten million only; leo mnasema tunaweza kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itekeleze ile ahadi yao ya shilingi milioni 50 kila mtaa na kijiji; tumehamasisha wananchi wameunda vikundi mbalimbali na SACCOS tunazihitaji hizo shilingi milioni 50. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye elimu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, ndugu yangu amesema kabisa tumejitahidi kutoa elimu bure na vitu kama hivyo. Ni dhahiri baada ya kuja hii elimu bure sijui, wakasema kwamba usipopeleka motto, unafungwa; kweli tumeandikisha watoto wengi sana mashuleni, lakini hatuangalii idadi. Tunatakiwa tuangalie quality ya ile elimu ambayo tunaitoa. Leo mmesajili wanafunzi wengi, lakini walimu wanadai madeni mengi na
hamjawapa mazingira mazuri ya kuwafanya wafundishe watoto wetu waweze kuelewa, hawana motisha yoyote ile, leo mnategemea kutakuwa na ufaulu mzuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mmesema mmerekebisha madawati. Sawa, madawati kwanza kuna sehemu nyingine bado hayajatosheleza, madarasa hayatoshi. Wananchi wanajenga, Serikali inashindwa kwenda kuezeka, vitabu hamna pamoja na kwamba TWAWEZA jana wamesema ratio ni moja kwa tatu, lakini mimi kwangu darasa la kwanza na la pili ni moja kwa tano; darasa la tatu mpaka la saba, kitabu kimoja; wanafunzi 50 mpaka wanafunzi 100. Hapo tunategemea elimu bure itatoka wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwe serious, kama tunataka tutoe elimu ambayo ni nzuri kwa wanafunzi wetu, elimu bora, tuwekeze na walimu wawe na motisha, wapewe fedha stahiki, walipwe madeni yao na wawe na mazingira mazuri ya kufundishia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee afya. Hospitali ya Mji wa Tarime mmeandika kwamba bado ni Hospitali ya Wilaya ya Tarime, lakini mnaleta OC na basket fund ambazo zinatumika idadi ya wananchi wa Mji wa Tarime, wakati kiuhalisia wanahudumia wananchi wa Wilaya nzima ya
Tarime, watumishi mmepunguza idadi wakati wanahudumia wananchi wa Wilaya nzima ya Tarime, wengine wanatoka Rorya na wengine Serengeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwepo na vigezo stahiki. Kama mnaona ni vyema hospitali ile iwe ya Wilaya, basi tunaomba OC na basket funds zije kwa idadi ya wananchi wa Wilaya ya Tarime na siyo idadi ya wananchi wa Mji wa Tarime. Mnawapa kazi kubwa watumishi, unakuta
daktari anafanya masaa zaidi ya 30 wakati alitakiwa awe kazini kwa saa nane tu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye maji. Kuna mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ambao usanifu ulishafanyika na Benki ya Maendeleo ya Ufaransa wapo tayari ku-sponsor huo mradi ambao unaanzia Shirati, Ingili Juu, Utegi, Tarime mpaka Sirari. Kuanzia mwaka 2011 watu
wamefanya design mpaka leo haujatekelezwa. Napenda kujua ili kutatua tatizo la maji Tarime, ni lini huu mradi utaanza kufanya kazi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, fidia ya ardhi ya wananchi ambao Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamechukua. Nimekuwa nikiimba sana hapa Bungeni na Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba unisikilize katika hili.
Mheshimiwa Mama Ritta Kabati mwache Waziri Mkuu anisikilize, maana nimekuwa nikiimba hii kuanzia mwaka 2007. Jeshi la Wananchi wa Tanzania limechukua maeneo ya wananchi wa Nyandoto, Nyamisangula na Nkende mpaka leo hawajalipwa. (Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji). MWENYEKITI: Ahsante,
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kwenye Wizara hii muhimu kwa maslahi ya Watanzania na uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuanza kwa kusikitika juu ya kipaumbele kidogo kinachopewa kwa Wizara hii muhimu sana. Mfano bajeti ya Wizara hii imetekelezwa kama asilimia 25.8 tu kwa bajeti za maendeleo kwenye Sekta ya Afya. Pia kwenye Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni asilimia 5.65 tu ya bajeti ya maendeleo. Hii ni aibu sana kwa kweli kwa nchi. Hivi kwa mwendo huu tutafika kweli?

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya maendeleo ni shilingi bilioni 5.8 tu, lakini Serikali inashindwa kutimiza hili. Kwa mwendo huu tutafikia Abuja Declaration ya kutenga angalau asilimia 15 ya bajeti kuu? Imekuwa ni kinyume kabisa! Kwanza katika kutenga; pili, katika kutekeleza hata kile kidogo kilichotengwa. Tanzania ya Viwanda itafikia wapi kama hatuwekezi kwenye afya ambapo tutakuwa tumewekeza kwenye rasilimali watu (Human Capital Investment) na tukifanya hivi tutakuwa na skilled labour?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili litawezekana tu kwa kuwekeza kwenye lishe (nutrition). Nchi yetu kwa sasa ina tatizo kubwa la malnutrition, stunting, wasting, hivi vinapelekea udumavu wa mwili (physical development) na udumavu wa akili (cognitive development). Tukiwa na Taifa la wadumavu daima hatutaweza kufika popote kama Taifa la Tanzania ya viwanda. Ni ndoto!

Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia nzima kwa sasa wameamua kuwekeza kwenye lishe ili kuweza kuzalisha rasilimali watu na kukuza uchumi. Tukiwekeza kwenye lishe, tutapunguza vifo vya mama na mtoto, maana mtoto mwenye malnutrition huweza kupata maambukizi ya magonjwa kama vile pneumonia, kuhara, Malaria, utapiamlo na hata kupelekea kifo na ukiangalia idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano, bado ni tatizo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ni jukumu letu sisi kuwekeza kwenye lishe kwa kufanya yafuatayo:-

(1) Kuhakikisha tuna Maafisa wa Lishe kuanzia ngazi ya Kijiji, Mtaa, Kata na Wilaya ili waweze kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi. Maana zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania, cha kushangaza, mikoa yenye idadi kubwa ya watu wenye udumavu ni ile inayolima mazao mbalimbali ila hawana elimu ya lishe bora kwa afya bora;

(2) Kuhakikisha tunakuwa na vipeperushi vinavyotoa elimu juu ya umuhimu wa lishe na ni nini lishe bora ili wananchi wa vijijini na kaya maskini wajue ni jinsi gani wanapata mlo kamili wenye lishe bora?;

(3) Kuweza kutoa ruzuku kwenye viwanda vinavyozalisha chakula ili waweke virutubishi kwenye packages zao;

(4) Kuwekeza, kutoa Supplement Bills hasa kwa akinamama wajawazito wasiokuwa na uwezo wa kupata hivi vidonge vyenye madini ya chuma na vitamins;

(5) Kuweza kuwa na miundombinu imara ya maji, hospitali, zahanati na vituo vya afya; na

(6) Kuepusha mimba za utotoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijikite kwenye utatuzi wa huduma ya afya kwenye Jimbo la Tarime Mjini. Kwanza kabisa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Wizara ilituahidi tutapata vituo vinne vya afya, maana kwa sasa hatuna kituo cha afya hata kimoja. Hivyo naomba sana mtupatie hivi vituo vya afya ili kutatua tatizo la huduma za afya Jimboni kwangu, maana sasa ni tegemeo la Hospitali ya Mji ambayo nayo inahudumia Wilaya nzima na hata Wilaya jirani kama Serengeti na Rorya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni kuhusu mzigo mkubwa wa Hospitali ya Mji wa Tarime ambayo bado inasomeka kama Hospitali ya Wilaya, lakini basket fund na OC zinakuja kwa kuzingatia idadi ya watu na Mji wa Tarime na siyo Wilaya nzima. Hii inapelekea upungufu wa Watumishi, mfano hili la vyeti feki limeondoka na Madaktari wawili, hivyo tumebaki hoi na inaweza kupelekea vifo vingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru tumepata Madaktari watatu; wale wa Kenya lakini tumeondokewa na wawili, hivyo tatizo la uhaba lipo pale pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri hatua za haraka zichukuliwe ili tupate hao Madaktari, Manesi na Wahudumu wengine wa Afya. Pili, Hospitali yetu itambulike kwa idadi ya watu wa Wilaya ya Tarime na siyo Mji wa Tarime ili kuwe na uhalisia wa huduma ya afya inayotolewa, maana kule Halmashauri ya Wilaya haina Hospitali. Tunaomba sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, JWTZ kupora ardhi ya wananchi wa Kenyambi, Kata ya Nkende na Bugosi, Kata ya Nyamisangura, zilizopo Halmashauri ya Mji wa Tarime. Napenda kuchangia kwa kifupi sana kwenye Wizara hii hasa katika suala zima la Jeshi la Wananchi la Tanzania kuchukua ardhi ya wananchi kinyume cha Sheria ya Ardhi na kulipa fidia stahiki na kwa muda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Igaga Mike kuwa JWTZ wana eneo lao ambalo ni kambi lililopo Kata ya Nyandoto ambayo lipo nje ya Mji, lakini kwa makusudi kabisa waliamua kujitwalia kwa nguvu eneo walilokaribishwa kwa muda kupisha uharibifu wa miundombinu ya daraja iliyosababisha kukatika kwa mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa miundombinu hiyo ilishakamilika, lakini JWTZ wamegoma kuhama badala yake wameendelea kuongeza maeneo ya wananchi na hii inaleta sintofahamu na inaweza kusababisha uvunjifu wa amani, maana wananchi wangu wamezuiwa kufanya shughuli zozote za maendeleo kwa miaka yote hii. Nimekuwa nalizungumzia hili tangu 2010 na kupangwa kwenye kila fedha za bajeti ya maendeleo kwamba watalipa fidia, lakini hamna hatua zozote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wangu waliweza kuunda Kamati na kufika hadi kwa Waziri kuelezea matatizo yanayowakumba kwa ardhi yao kuchukuliwa na wanajeshi bila kufanyika malipo ya fidia ili waweza kwenda kutafuta makazi mengine ama kama fidia imeshindikana kulipwa, basi Wanajeshi warudishe ardhi ya wananchi wangu ambayo wameendelea kujitwalia kila kukicha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Tarime wangependa kujua ni kwa nini Serikali ya CCM kwa makusudi imeshindwa kurudisha ardhi ya wananchi hawa na ikizingatiwa Halmashauri ya Mji wa Tarime ina changamoto kubwa ya ardhi na hawa Wanajeshi wamekuja katikati ya Mji kuchukua maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ardhi kwa mila za Wakurya ni kitu kinachothaminiwa, Serikali itakumbuka vita nyingi za koo hutokana na migogoro ya ardhi. Hivyo, tunaomba ardhi yetu irudishwe na kwa kweli, wanajeshi warudi kambini kwao ambalo ni eneo kubwa waliloshindwa kulipia ada ya ardhi kwa miaka yote hiyo na kulitelekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, kuwepo kwa Wanajeshi kwenye hizi Kata za uvamizi kumesababisha matatizo mengi kama vile kunyanyasa wananchi wanaotumia barabara inayopita kwenye mitaa ya Bugosi na Kenyambi eneo walilochukua. Vilevile kuna kipindi wananchi wakifuatilia nyagabona za ng’ombe Wanajeshi huwazuia na kuruhusu mwanya wa wizi wa ng’ombe na hili hufanywa na baadhi ya Maafisa wasio waaminifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa vyombo vya moto hasa bodaboda ambao hupewa adhabu kali bila kuzingatia kuwa yale ni maeneo ya umma na si Kambi ya Jeshi na ndiyo maana tunashauri warudi kwenye kambi yao Nyandoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizari ya Maji na Umwagiliaji
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuweza kunipatia fursa na mimi nichangie kwenye Wizara hii muhimu sana kwa maisha ya Watanzania na hasa kwa sisi wahanga ambao ni wanawake ambao tunatembea kilomita nyingi kutafuta maji licha ya Sera ya Maji kusema kwamba tutakuwa tunapata maji ndani ya mita 400.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kabisa zaidi ya asilimia 80 ya Wabunge waliopo humu ndani watakubaliana na ukweli kwamba maji imekuwa ni tatizo na inapelekea tunakuwa na vifo vingi. Mwanamke akienda hospitalini kujifungua bila maji kwa kweli sidhani hata kama zoezi litaweza kukamilika kama inavyotakiwa na katika hali ya usafi na afya. Zaidi mtakubaliana na mimi kwamba watoto wetu wa kike wengine wanarudi majumbani kutoka shuleni au hawaendi kabisa kwa sababu ya kukosa maji hasa wakiwa kwenye zile siku zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na kulaani wale Wabunge waliosema kwamba tusiongeze fedha. Ni ajabu sana kuona kwamba fedha za maendeleo zilizokwenda kwenye sekta hii ya maji ni asilimia 19 tu ilhali kwenye sekta ya ujenzi fedha zilienda zaidi ya asilimia 100 tulizozipanga kwenye bajeti iliyopita. Kwa hiyo, naomba sana Serikali kwa mapendekezo ambayo tumeyatoa hapa Bungeni tuongeze kutoka shilingi 50 mpaka shilingi 100 kwa sababu hizi fedha zipo ring-fenced, tuziongeze zifikie hapo tuweze kutatua matatizo ya maji vijijini na mijini pia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nirudi sasa kwenye Jimbo langu la Tarime. Tarime tuna Hospitali ya Wilaya na kuna kipindi tunakosa maji kabisa, wagonjwa wakienda pale inakuwa shida na mtafutano. Tuna Gereza la Tarime linahitaji maji na lina shida kubwa sana, tuna taasisi zingine mbalimbali zahanati na vitu kama hivyo vina tatizo hili la maji. Katika Mji wangu wa Tarime licha ya kwamba ni mjini ni chini ya asilimia kumi tu ya wakazi wa Tarime ndio wanapata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati najaribu kupitia hiki kitabu kwa kweli nimesikitika sana. Nimekisoma na kugundua katika miji mikuu ambayo imepata maji Tarime haipo licha ya kwamba nilishauliza maswali mengi sana hapa ndani na Waziri akaniahidi kabisa kwenye bajeti hii atakwenda kutenga fedha na kuhakikisha kwamba anatatua tatizo la maji Tarime. Nikasema kwa mfano mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda mpaka Tarime na Sirari tayari mwaka 2012 walishafanya upembuzi yakinifu na Benki ya Maendeleo ya Ufaransa ilishajitolea kufadhili mradi huu na Waziri akaniahidi kwamba watatenga bajeti, nimeangalia sijaona.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Tarime wanateseka na maji. Wanapoteza muda mwingi ambao wangeenda kufanya shughuli za kimaendeleo kutafuta maji.Akinamama wajawazito wanatembea kilomita nyingi kutafuta maji. Kwa hiyo, naomba sana mnisaidie kwa kuweka fedha ili kutatua tatizo la maji katika Mji wa Tarime. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tarime pia tuna Bwawa la Nyanduruma, lile bwawa ni la enzi za Mjerumani lakini mpaka leo hii halijaboreshwa. Napenda sana Serikali muwekeze fedha pale kwani bwawa lile tukiliboresha zaidi litakwenda kutoa mtandao wa maji ambayo yataenea kwenye Mji wa Tarime na kusaidia kutatua tatizo la maji wakati tukisubiria maji ambayo yatatoka Ziwa Viktoria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, linguine, kuna mradi ambao ulikuwa ni msaada kwenye Kata ya Nyandoto, mradi wa Kemangeumekamilika lakini bado hamjaleta fedha kuweza kuweka sasa mtandao wa maji kuwafikia wananchi. Tenki limeshajengwa, tunahitaji kupata fedha ili kuweka network ili wananchi wa Tarime waweze kupata maji. Nishauri hii sio kwa Tarime tu hata huko kingine unakuta wakati mwingine tuna visima vya asili ambavyo tukiviboresha vinaweza kusaidia kutatua tatizo la maji kwa muda mfupi wakati tukisubiria mjipange kwa mipango ambayo inatekelezeka kwa kutumika kwa muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe sana Wabunge tukatae hii bajeti...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa Esther Matiko.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa mchango wangu kwenye maeneo matatu muhimu. Nikianza na umuhimu wa kulinda amani, utulivu na mshikamano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameeleza kuwa kuna amani nchini ilhali hakuna amani kwa sasa. Hakuna utulivu kwenye Taifa letu maana kila kukicha matukio ya maonevu yanayofanywa na vyombo vya dola ya kuvunja haki za msingi kwa raia wake. Tunashuhudia mauaji yakiendelea kwa kasi nchini, utekaji pamoja na watendaji wa Serikali kutishiwa hata kushindwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na weledi wa kazi yake bali wanasubiria kauli kutoka juu. Jambo hili linalirudisha Taifa letu nyuma. Taifa linakuwa la woga, wanahifadhi chuki na mawazo mbadala moyoni badala ya kuyatoa ili yasaidie kuijenga nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia unyanyasaji wa dhahiri wa Vyama vya Upinzani huku Msajili wa Vyama vya Siasa anafumbia macho na zaidi anatumika kukandamiza Upinzani. Mfano kwenye Hotuba Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kabisa kuwa Vyama vya Siasa vimeruhusiwa kunadi sera zao na itikadi ili kupata wanachama, kitu ambacho ni uongo kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu anajua fika kuwa watendaji, polisi na hata Ofisi ya Usajili wa Vyama vya Siasa anaifumbia macho kauli batili inayoenda kinyume na Sheria na Kanuni za Vyama Vingi na Katiba ya nchi yetu; huku tukishuhudia Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi akiendelea na mikutano ya hadhara na kupokea wanachama huku mtendaji wa Chama cha Mapinduzi (Katibu Mwenezi), ndugu Humphrey Polepole, akiendelea kufanya mikutano ya hadhara na kuvinanga vyama vingine huku wakipandikiza chuki. Leo hii kusema kuwa wawakilishi tu ndio wafanye mikutano ilihali inafahamika fika kuwa tuna vyama ambavyo havina uwakilishi wa Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji Sasa hivi vyama vitatangaza vipi hizo sera zake na itikadi zao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia pia jinsi fedha za Watanzania maskini zikitumika vibaya, hasa kwa chaguzi ambazo zinarudiwa kupitia minada ya viongozi wa wananchi kununuliwa na kusababisha si tu upotevu wa fedha bali mauaji na ulemavu kwa raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Mheshimiwa Waziri Mkuu anasema bila aibu kuwa CCM wameshinda Majimbo yote na kata 58 huku CHADEMA wakishinda moja tu? Eti CCM wameshinda kwa kishindo ilhali anajua hujuma inayofanywa na vyombo vya dola, Tume ya Uchaguzi na Wakurugenzi ambao ni makada wa CCM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia jinsi Jeshi la Polisi linavyojigeuza Tume ya Uchaguzi na kubandika matokeo ya uchaguzi kinyume na taratibu, wakishuhudia watendaji wakibadili ballot box na kuondoka nalo mbele ya RPC Kinondoni na pale Magomeni. Hapa hatuwezi kuwa na uchaguzi huru na hivyo hakuna amani wala mshikamano.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuweza kunipatia nami fursa kuchangia bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ambayo ni muhimu sana kwa ulinzi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa masikitiko makubwa kwamba tunakaa hapa tunapitisha bajeti ambazo hazina uhalisia na hatimaye utekelezaji wake unakuwa ni wa kusuasua. Waziri wakati anawasilisha bajeti yake hapa ameainisha bayana kwamba fedha za maendeleo ambazo zilikuwa ni shilingi bilioni 248 zimetolewa asilimia 14.5 tu ambazo ni sawa na shilingi bilioni 35.9

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii kuna wazabuni wengi sana wanaidai Serikali ambao wametoa huduma kwenye Jeshi letu la JKT pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hawa wazabuni wamekopa fedha kwenye benki, wanafilisiwa na wengine wanafariki kwa sababu ya pressure. Nilikuwa naomba Serikali tunapokuja hapa tunatenga hizi bajeti hasa za maendeleo ziwe na uhalisia ili ziweze kwenda kukidhi mahitaji kwa muda wa mwaka nzima kama tunavyokuwa tumepanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine napenda kuzungumzia fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya kupima, kuthamini na kulipa fidia kwa yale maeneo ambayo Jeshi imeyatoa kwa wananchi, tena wakati mwingine bila kufuata Sheria za Ardhi. Katika hili nitajikita zaidi katika eneo ambalo Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamejitwalia kule Tarime katika kata ya Nyamisangura na kata ya Nkende ambapo kwa kweli kila mwaka ninakuwa ninasimama hapa naelezea, na Mheshimiwa Waziri amekuwa akiniambia kwamba wanakuja kumaliza kuwalipa fidia. Mwaka jana tulitenga shilingi bilioni 27.7 Mheshimiwa Waziri ameeleza hapa na wote tunaona kwamba haikutolewa hata shilingi 1,000 kwenda kufanya hii kazi; shilingi bilioni 27.7 hata shilingi 1,000 haijatolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nilikuwa nashauri, kwa sababu wanajeshi kwa mfano kwa Tarime kile kosi kilipewa eneo kubwa sana Kata ya Nyandoto; tunaomba waondoke kwa sababu mmeshindwa kulipa kwa miaka yote hii kuanzia mwaka 2008, tunaomba hawa wanajeshi warudi kwenye maeneo yao kule Nyandoto eneo ni kubwa sana ni pori kubwa kuliko kuja kuchangamana na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi yao iko kule Nyandoto ya kikosi cha 28KJ warudi kule, wakakae kule ili waweze kulinda vizuri dhidi ya mipaka ya Nchi yetu kwa upande wa Kenya. Huku kwenye kata ya Nyamisangura na Nkende wanachangamana sana na wananchi na mmeshindwa kulipa. Kwa hiyo naomba leo Mheshimiwa Waziri uniambie either mnatulipa kwa kipindi cha bajeti ya mwaka huu au mwende mkawaombe wale wanajeshi waondoke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanachokifanya sasa hivi kwanza wanakodisha yale maeneo kwa raia yaani wamepoka maeneo ya wananchi halafu wanakodisha kwa kufanya biashara, zaidi ni maslahi ya watu binafsi kule. Naomba uje na wewe mwenyewe Tarime ukae na wataalam wako tulimalize suala hili. Mimi binafsi kama mwakilishi inaniuma sana ninapoona wananchi wanakaa kwa miaka mingi bila kufanya shughuli za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, wale ndugu zetu wanajeshi ambao wanakwenda kusoma nje ya nchi mnachelewesha kuwapelekea fedha za kijimu, wanakuwa wanateseka sana. Kwa hiyo, naomba kabisa wakati mnapanga bajeti muweze kuzingatia mjue kwamba mnapeleka wanajeshi wangapi kusoma nje ya nchi muwapelekee fedha za kujikimu ili wamalize mafunzo yao wakiwa na utulivu wa akili na kurudi Tanzania kuweza kulinda nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wanajeshi ambao unakuta wanatumwa kwenda kulinda amani kwenye nchi zingine; Kambi za Tanzania za wale wanajeshi wetu wanaokwenda kukaa kule ni mbovu, hazina hadhi ukilinganisha na kambi za nchi zingine ambazo wameenda kulinda amani kwenye sehemu husika.

Tunaomba wakati mnawatuma wanajeshi wetu kwenda kulinda amani huko basi na wenyewe muwape hadhi, wawe na makambi mazuri kama wale wengine ambao wametoka nchi zingine. Ukienda ukiangalia kambi za wanajeshi kule zinatia fedheha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mwisho nimalizie kwenye top up allowance. Wanajeshi mara ya mwisho wamelipwa hizi top up allowance ni mwaka wa jana mwezi wa tatu. Sasa hivi ni zaidi ya mwaka hamuwalipi hizi stahiki zao. Tunarudi pale pale, tunapopanga bajeti zetu tupange bajeti yenye uhalisia, tujue kwamba katika Wizara hii tuna mahitaji haya na haya. Tuweze kutimiza yale mahitaji ambayo ni ya muhimu, kwa mfano hii top up allowance ni hitajio ambalo mtu anapokuwa anafanya kazi anajua kabisa anatakiwa alipwe. Sasa inapita mwaka bila kuwalipa; na ndiyo maana hotuba ya kambi rasmi ya Upinzania imejikita zaidi kuelezea matatizo na maslahi ya wanajeshi wetu.

Kwa hiyo, naomba kipekee kabisa; Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeelezea kwa kina sana, dakika tano ni chache kuchambua, naomba Mheshimiwa Waziri uifanyie kazi yale yote ambayo yamebainishwa kwenye Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni yafanyiwe kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kuhusu wanajeshi wetu wastaafu na wale ambao unakuta wameaga dunia. Ni dhahiri na mimi mwenyewe nina ndugu ambao wengine waliaga dunia na wengine ni wastaafu wanakuwa wanaangahika sana kupata mafao yao; naomba muwatendee haki. Hawa ndugu unakuta wametumikia nchi hii kwa uaminifu zaidi, lakini ikija kwenye mafao inakuwa wanatendewa ndivyo sivyo, nashukuru.
Makadirio ya na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia angalau dakika tano ili niweze kuchangia kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya dakika tano yale ya kitaifa nitayaandika kwa maandishi, naomba nijielekeze kwenye Halmashauri ya Mji wa Tarime. Kwanza niwapongeze kwa kuanzisha Kanda ya Simiyu ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma ya hati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kiasi kikubwa sana ardhi yetu haijapimwa. Kwa hiyo ningependa niiombe Wizara iweze kuzingatia haya ambayo nitayasema ili waweze kuharakisha na kuhakikisha kwamba tunapata upimaji kwa kiwango kikubwa sana ambapo tukipima ardhi yetu inaongeza thamani na hata wale wananchi wanaweza kuitumia kuweza kukopa na vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna upungufu mkubwa sana wa wafanyakazi, hatuna Afisa Mipango Miji, tuna surveyor mmoja tu, hatuna Maafisa Wasaidizi wa Ardhi. Kwa hiyo naomba Wizara, kuna vijana wawili ambao wametoka Chuo cha Tabora wameletwa pale kwenye Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa ajili ya ile kazi ya mfumo wa kodi wa ardhi na walikuja kwa mkataba na mkataba unakaribia kwisha; naomba kabisa Mheshimiwa Waziri waweze kuwaajiri wale vijana wabaki katika Halmashauri ya Mji wa Tarime ili kupunguza hii adha ya wafanyakazi na kurahisisha upimaji wa ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ukosefu wa vifaa vya upimaji. Halmashauri ya Mji wa Tarime tunakodisha vifaa kutoka katika Halmashauri zingine kuja kufanya upimaji. Kwa hiyo naomba Wizara iweze kutupatia angalau set moja ya vifaa vya upimaji, kwa mfano differential GPS au hata total stations, tukipata set moja ya hivyo itaturahisishia upimaji katika Halmashauri ya Mji wa Tarime na tuache kukodi kutoka kwenye Halmashauri nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, ningeomba Wizara iweze kutusaidia fedha ili tuweze kuandaa Master Plan kwa sababu Halmashauri ya Mji wa Tarime hatuna fedha za kutosha. Tukiandaa Master Plan itatusaidia, maana kuna miradi mingine tunaikosa, kwa mfano ya World Bank, kama hatuna Master Plan hatuwezi kupata hiyo misaada. Kwa hiyo, Wizara ione kwamba ni muhimu sana kutusaidia tuweze kupata. Halmashauri nyingi sana zinakosa miradi ya World Bank. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo awali kulikuwa na Mfuko ambao ulikuwa unaitwa Plot Development Revolving Fund (PDRF), tulikuwa tunaomba uweze kurejeshwa. Watukopeshe fedha tuweze kuzitumia kupima viwanja ambapo itarahisisha; maana yake kama nilivyosema awali, unakuta Halmashauri zingine hazina fedha za kutosha. Kupitia huo mfuko tunaweza tutakopa fedha, tukapima na kuweza kulipa fidia kwenye viwanja na itasaidia sana kuweza kuweka mji wetu uwe vizuri na hata Bunda nao wana changamoto kama hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho kwa kweli ningependa Wizara ya Ardhi iweze kuingilia ni mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Tarime wanaotoka Kata ya Nyamisangura na Nkende kwa maana ya Bugosi na Kenyambi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Jeshi la Wananchi wa Tanzania walichukua ile ardhi kinyume kabisa na sheria za ardhi; lakini mbaya zaidi tumeshuhudia zaidi ya miaka kumi hawapati fedha za kulipa fidia. Mheshimiwa Waziri ningependa kabisa na kipindi kile cha Wizara ya Ulinzi alisema atakuja Tarime, aje na Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi ili aangalie uhalisia, wale wanajeshi warudi kule kwenye kambi yao na wananchi waweze kurudishiwa ardhi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kwa kweli na mimi nichukue fursa hii kuwapongeza National Housing, wanajitahidi sana na wanastahili pongezi. Tunaona ni wapi wametoka na wapi walipo kwa sasa hivi. Kuna changamoto ambazo zipo na tumekuwa tukiziongea ambazo kama Wizara au Serikali wakizifanyia kazi tutaweza kupata zile nyumba ambazo tunasema za bei nafuu. Kwa sasa hivi walivyo ni kazi kwa kweli maana Serikali hawawapi ruzuku, wanajiendesha zaidi kama kibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna changamoto zingine ambazo tumekuwa tukiongea kwenye kupata ile miundombinu ya kwenda kwenye makazi husika; waweze kupata urahisi kwa hapo maji, umeme na miundombinu ya barabara ambayo itaenda kuwarahisishia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa ndugu zangu wa Mbarali na wenyewe wana mgogoro wa ardhi kati ya hifadhi na wananchi wale wakulima wa Mbarali. Mwaka 2007 walienda wakachukua vijiji 21, sasa hivi tena Serikali imeenda imeongeza beacon inachukua Vijiji 32 yaani wale wa Vijiji 21 walihamia kwenye Vijiji vingine na sasa hivi wanaondolewa tena. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri naomba awazingatie na hao watu wa Mbarali nao waweze kupata haki yao ili hatimaye tuondoe hii migogoro ambayo unakuta kwa kweli haina tija na inakatisha tamaa; na tukizingatia wakati wa uchaguzi Chama Cha Mapinduzi kiliahidi kwamba watawajengea barabara ya lami sasa msiwahamishe hapo hawa wananchi. Ahsante sana
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia Wizara hii muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu. Kwanza kabisa nianze kuzungumzia changamoto za elimu kwenye jimbo langu la Tarime Mjini. Licha ya Tarime kuwa mjini lakini tuna shule moja ya kidato cha tano na sita (A-Level) ambayo ipo tangu miaka ya 1960, na shule hii ni ya wavulana tu. Hivyo tunaomba ombi letu ambalo limekuwa ni la muda mrefu lipatiwe ufumbuzi kwa kupandisha shule za Nyamisangura na Mogabiri kuwa na A-Level kwa kuwa miundombinu yake inakidhi vigezo na pia tuna walimu wa kutosha wa kufundisha masomo ya A-Level. Tunaomba Serikali ione umuhimu wa kuanzisha hizi shule ili kutoa fursa. Kuna watoto wetu wa kike ambao humaliza na kukosa fursa za masomo ya A-Level. Limekuwa ni ombi la muda mrefu tunaomba lifanyiwe kazi mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Halmashauri ya Mji wa Tarime tuna changamoto za shule za msingi, kitu ambacho kinapelekea uhafifu na ubora wa elimu kwa sababu ya mazingira mabaya ya kufundishia na kujifunzia. Kumekuwa na uhaba mkubwa wa madarasa licha ya juhudi za wananchi pamoja na mimi Mbunge wao ambapo nimeweza kujenga maboma kadhaa, lakini Serikali inashindwa kuweza kukamilisha majengo yake ili yaweze kutumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Elimu inaelekeza kuwa na ratio ya wanafunzi 45 kwa darasa, lakini jimboni kwangu uwiano wa mwanafunzi kwa darasa ni darasa moja kwa wanafunzi 120 au 150 au 200. Hii haikubaliki na ni aibu kwa nchi yetu kwani ni dhahiri hapo kutakuwa hakuna mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi.

Naomba sana Serikali ilete fedha ili kuweza kumalizia maboma na kupunguza adha ya madarasa jimboni kwangu na hivyo kutoa elimu bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ni kuhusiana na uhaba wa nyumba za walimu ambapo walimu wanapanga nyumba mbali na shule zao kitu ambacho kinafifisha ufundishaji kwani walimu wanachelewa kurudi au kuja shuleni hasa kipindi cha mvua. Hii ni aibu na Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema walimu wawe na nyumba shuleni. Naomba Serikali ielekeze kwenye nyumba za walimu ili kuweza kutoa ufanisi kwenye kufundisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika jimbo langu kuna uhaba wa ofisi za walimu ambapo inapelekea walimu kukaa nje, chini ya miti hasa shule za Sabasaba, Azimio pamoja na Mapinduzi. Wengine kugeuza madarasa kuwa ofisi huku wakiwa hawana samani au makabati ya kuhifadhia vitabu. Kwa kweli hali ni mbaya sana, tunaomba Serikali ione haja ya kuboresha mazingira ya walimu ya kuandaliwa, kufundishia na kuishi. Hizi zitatoa motisha kwani walimu wana matatizo mengi sana kama vile madeni, kutokupandishwa madaraja, malimbikizo ya fedha za likizo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni kuhusiana na mahitaji au vifaa vya kufundishia. Kuna uhaba mkubwa sana wa vitabu kwenye jimbo langu, yaani uwiano wa kitabu ni 1:100, hii inaleta ugumu sana kwa mwanafunzi kuelewa. Inatakiwa kuwa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja, lakini sasa ni kitabu kimoja kwa wanafunzi 100 au 150; hii ni mbaya sana. Sasa cha kusikitisha ni juu ya vitabu vilivyogawiwa hivi karibuni kwa darasa la pili na la tatu, takribani 13,680,981 hivi vitabu vina makosa. Tunaenda kujenga Taifa la wajinga, maana mtoto huamini alichofundishwa au kusoma kwenye kitabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Wizara ione umuhimu wa kuweka nishati ya umeme kwenye shule zote ili kurahisisha ufundishaji na kutoa fursa ya wanafunzi kujisomea.

Pia tuweze kuboresha miundombinu ya vyoo kwenye shule zetu kwa ili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kupunguza magonjwa kwa walimu na wanafunzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni juu ya elimu bure ambayo kwa kiasi kikubwa haijatoa nafuu kwa mwananchi na zaidi ime-affect, maana wazazi wamegoma kutoa michango ya chakula, hata wengine kwenye ujenzi. Lakini pia bado wazazi wanaochangishwa fedha za kulipa walimu wa sayansi wa kujitolea michango ni mingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nichangie Kitaifa juu ya nini kifanyike ili kuboresha elimu ya Tanzania na kujenga Taifa lenye watu walioelimika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kuomba Serikali ilipe madeni yote ambayo walimu wanadai, fedha za likizo, kupandishwa madaraja na stahili zote ikiwepo kuongezewa mishahara. Hii itatoa motisha na hamasa kwa walimu wetu na hivyo kuwa na ufundishaji bora na hivyo kuwa na elimu bora kwa wanafunzi wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa Serikali ione umuhimu wa kuhakikisha makundi mawili, kwa maana ya wale wasiojiweza pamoja na watoto wa kike wapewe kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni makundi muhimu sana ambayo yamekuwa sidelined. Vilevile tuwe na uwajibikaji kwenye elimu ya watoto wetu na hii ni kwa wadau wote maana ya wazazi na walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa Serikali iwekeze kwenye majengo. Kwenye kitabu cha Mheshimiwa Waziri anaonyesha ni madarasa 2,000 tu yatajengwa kati ya madarasa 158,674. Hii inaonesha dhahiri Serikali bado haijadhamiria kuondoa tatizo la msongamano mashuleni kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya madarasa kwa sababu kwa speed hii itachukua miaka 79 kuweza kutatua tatizo la madarasa/msongamano. Pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo 200,000 (Best 2016).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naomba vifaa vya maabara jimboni kwangu maana majengo mengi yamekamilika lakini hatuna vifaa na wataalamu wa maabara hadi majengo yanageuzwa kuwa madarasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia sekta hii ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu, ukizingatia zaidi ya Watanzania asilimia 80 ni wakulima na wafugaji na ukizingatia kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kilimo chenye tija hatutapata malighafi kwa ajili ya viwanda bila kuboresha sekta ya mifugo hakuna njia tutakuwa na viwanda vya kuchakata nyama, ngozi, kwato, pembe na kutoa bidhaa za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni sekta ya uvuvi, Tanzania ni kati ya nchi iliyojaliwa maziwa, bahari, mito na mabwawa ambayo tukiwekeza basi uchumi wa nchi yetu utakuwa ni wenye tija. Kama nchi tunahitaji kuwekeza kwenye uvuvi wa kisasa, kuna teknolojia za ku-fence maeneo muhimu kwenye ziwa au bahari ambapo baada ya muda huwezi vuna samaki wengi na kuweza kuwachakata na kutoa mazao mengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nizungumzie issue ya mnada wa Magena ambao ulifungwa bila sababu za msingi zaidi ya kisiasa. Nashukuru niliweza kuuliza swali humu ndani ambalo lilisababisha aliyekuwa Waziri Mheshimiwa Mwigulu Nchemba pamoja na Watendaji wake wa Wizara waliweza kufika Tarime na tukawa na vikao pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ambapo baadaye tulienda eneo la mnada na wakaongea na wananchi na kuwaahidi kuwa ule mnada utafunguliwa, maana hauhitaji gharama kuufungua, miundombinu yote ipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni takriban mwaka sasa tunaomba ule mnada ufunguliwe ili kuokoa pato la bure linalopotea kwa njia za panya ambapo ng’ombe wengi hupelekwa ng’ambo ya pili upande wa Kenya kwa maelfu. Tulikumbushana kuwa mnada wa Butiama/Kinesi uwepo lakini ule ambao upo mpakani ni wa muhimu sana, utatoa ajira nyingi kwa wananchi wa Tarime na hivyo kukuza uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba wakati wa kuhitimisha niweze kupata jibu la hili, yale maazimio walioelezwa wananchi juu ya ufunguzi wa ule mnada yatatimia, wananchi wana imani na Serikali ya Awamu ya Tano, watatimiza hayo ya kukuza uchumi wa viwanda kwa kufungua ajira mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni kuhusiana na Chuo cha Kilimo kilichopo Tarime (Tarime Extensions Centre) kimetelekezwa kabisa wakati ni chuo ambacho kama Serikali ingewekeza tungekuwa tunatoa si tu wataalam bali Mabwana Shamba wengi ambao wangeweza kutembelea na kutoa elimu juu ya kilimo cha kisasa na ukizingatia Wilaya ya Tarime ina udongo ambao unastawi mahindi, ndizi, mihogo, mtama, alizeti, tikitimaji, ulezi, viazi vitamu, viazi mbatata, kahawa, chai zao linalochipukia, vitunguu na kadhalika. Tukiwekeza vema kwenye kilimo chenye tija Tarime tutakuza uchumi imara na viwanda vingi vitajengwa kwa ajili ya kusindika mazao haya na kuongeza thamani, viwanda vya biscuits na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba Serikali ione ni muhimu wakafanya tafiti za kina juu ya zao la bangi na kuona kama inaweza kuwa zao la biashara kwani kuna nchi hununua na kutengeneza bidhaa zinazotumika hospitalini. Pia hivi karibuni tuliona ndugu Keluch wa nchini Kenya aliweza tumia marijuana (mirungi) na kugeuza toka dawa ya kulevya na kutengeneza vinywaji mbalimbali kama wines (mvinyo), juice, maziwa ya mtindi (yoghurt) na kadhalika. Hivyo wataalam wa madawa ya kulevya pamoja na chakula na wale wa dawa za binadamu wafanye tafiti ya kina ili kuona madhara ambayo kama zao hili likiwa processed hayana direct effect, maana hili ni moja ya zao lenye uchumi mkubwa kuliko hata tumbaku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kuhusiana na zao la kahawa na kushuka kwa bei ya kahawa jambo ambalo linakatisha tamaa wakulima. Vilevile usimamizi juu ya kilimo cha miwa huko Jimbo la Tarime Vijijini.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia juu ya udhibiti wa vifaa vya usambazaji wa maji (water supply accessories) na madawa ya kutibu maji (water treatment). Inabidi tujiulize, ni nani anadhibiti ubora na bei ya vifaa hivi na madawa ya kutibu maji? Je, Wizara inajua kinachoendelea? Je, kuna chombo chochote kinachoshughulikia hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, uharibifu wa miundomibinu huchangiwa na kukosekana kwa taarifa sahihi za ubora. Kwa kuwa soko ni huria na wakandarasi wanatafuta faida, hivyo ni wazi watakimbilia cheap price ili kupata faida kubwa at the end.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuhusu madawa ya kutibu maji, je, Wizara ina mechanism gani ya kujiridhisha kuwa mamlaka zote zinazosambaza maji nchini zinawajibika kutibu maji ili kutunza afya na uhai wa Watanzania?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni chombo gani ndani ya Wizara chenye jukumu la kuhakikisha udhibiti wa upatikanaji wa madawa ya kutibu, kusambaza na kupanga bei? Kuliacha soko liamue juu ya bei ya vifaa vya usambazaji maji na madawa ya kutibu maji bila udhibiti, kutaendelea kulitia hasara Taifa kwa kuwa na miundombinu isiyo na ubora.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kukosekana kwa uhakika kuhusu usalama wa Watanzania wote wanaotumia maji kwani hakuna uhakika kama nguvu ya soko inaweza kuratibu upatikanaji wa madawa yenye ubora na kwa bei sahihi ya soko. Hali hiyo pia husababisha kila mamlaka kujipangia bei yake ya huduma ili kufidia gharama zisizothibitika za madawa na vifaa. Kwa mfano, Wizara ya Afya inadhibiti usambazaji na bei kupitia MSD.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Natambua kwamba leo ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani. Napenda kutumia fursa hii kuweza kuwakumbuka wale wote ambao waliweza kupoteza maisha kwa sababu ya kazi yao ya uandishi kama ndugu Mwangosi ambaye aliuawa na Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ndugu yetu Azori ambaye mpaka sasa hivi amepotea hatujui yuko wapi; na wengine wote Ansbert Ngurumo sasa hivi yuko uhamishoni kwa sababu ya shughuli ya Uandishi wa Habari na wengine wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tuko kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani na nafikiri tumekuwa tukishuhudia baadhi ya Maafisa ndani ya Jeshi la Polisi, tena wakubwa kabisa wakisema maneno kinyume kabisa cha weledi unavyowataka ndani ya Jeshi la Polisi na hekima kabisa hawana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inafedhehesha sana kwamba Jeshi la Polisi ambalo kazi ni kulinda raia na mali zao, wamegeuka kuwaona raia kama mbwa koko ndani ya nchi yangu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa kifungu cha
(32) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinawataka Jeshi la Polisi kumfikisha mtuhumiwa Mahakamani ndani ya saa 24. Tumeendelea kushuhudia Jeshi la Polisi ama kwa makusudi au kwa kile wanachokiita maagizo kutoka juu; na sijui ni juu wapi siku hizi kwenye Awamu hii ya Tano, kitu kikifanyika, tunasubiri maelekezo kutoka juu. Sijui ni sheria ipi ambayo wameitunga ambayo haijaletwa Bungeni hapa kuthibishwa kwamba kuna maelekezo yanatakiwa yatoke juu ili Jeshi la Polisi litende kazi kwa mujibu wa weledi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipokuwa Gerezani nilikutana na binti anaitwa Salma Ramadhani ambaye alifutiwa mashtaka yake baada ya kukaa miaka minne Gerezani na Mheshimiwa Hakimu Mwijage akatoa ruling kwamba huyo dada asikamatwe na wenzake watatu; lakini alivyotoka tu, akakamatwa baada ya siku mbili akarudishwa Kisutu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yule Hakimu Mwijage akasema, “nimesema huyu mtu asikamatwe mpaka apate kibali cha Mahakama Kuu.” Polisi walimkamata akaenda na wenzake wakaa Kituo cha Kawe zaidi ya miezi nane ndani ya Kituo cha Kawe. Ukaguzi ukiwa unapita, wanawachukua wanakuja wanawaweka pale Kisutu, hawawaingizi ndani ya zile chamber, baadaye wanawarudisha. Hawa Watanzania ndani ya miezi nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua hawa Maaskari ambao kuwaweka Watanzania zaidi ya miezi nane kituoni mpaka sasa hivi bado wako nao, watueleze hizi ni sheria za wapi? Ni mambo mengi sana yanatendeka kinyume. Nina muda mchache sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Magereza kuna wastaafu ambao wamestaafu mwaka 2017, mpaka leo hawajawalipa stahiki zao hata fedha za kubeba mizigo hawajawapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kuna magari 950 mwaka 2012 ambayo yaliidhinishwa kwamba yanunuliwe na yasambazwe nchi nzima kwa ajili ya kubebea mahabusu kwenda Mahakamani. Mpaka leo hayo magari hayajulikani yameota mbawa za wapi. Sasa kwa sababu Awamu ya Tano mna-fight ufisadi, tunataka mliambie Bunge hili, hayo magari yameota mbawa za wapi? Kama yamenunuliwa, yako wapi? Maana yake tunashuhudia ndugu zetu ambao wako Magereza wanabebwa kwenye makarandinga kupelekwa Mahakamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho napenda kuzungumzia kwa haraka haraka, tunaomba waweke vifaa vya kisasa kuweza kuwakagua wale watu ambao wanaingia Magereza. Kinachofanyika sasa hivi ni udhalilishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, mwana mama anakuja anataka aingie gerezani, ana-bleed anaambiwa kama ana-bleed anabidi aruke kichurachura kumchunguza kama ana kitu ameweka ndani au wanamwingiza mkono. Huu ni udhalilishaji, haukubaliki. Nunueni vifaa vya kisasa vya kuweza kuwapima na kujua kama ana kitu, vina- detect. Naomba wanunue vifaa vya kisasa ambavyo ni vya bei rahisi sana, wasidhalilishe Watanzania. Wanunue vifaa vya kisasa waweze kufunga, waweze kukaguliwa wakati wanatoka na wakati wanataka kwenda Mahakamani na wakati wanaingia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Magereza imepitwa na wakati, tunaomba ifanyiwe marekebisho. Leo utashuhudia Askari Magereza ana masters lakini analipwa kama mtu wa Form Four. Pia kuna mengine mengi ambayo yanatendeka kwenye Jeshi la Magereza ambayo ni kinyume. Leo wafungwa hawa uniform. Unakuta wakati mwingine Askari anatoa jezi yake anampa mfungwa. Ni aibu! Wao kama wamepeleka wafungwa, wawahudumie, hawana uniform kabisa. Wanawapa adhabu Maaskari Magereza. Unakuta eti mfungwa ameweka kilemba kimeandika tu “mfungwa” huku hana sare.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kusema kwamba wanatumia nguvu nyingi sana, fedha za Watanzania maskini; wakati wa Ukuta ndiyo tuliona watu wanafanya demonstration na Askari, wakati wa Mange Kimambi tukaona watu wanafanya demonstration ya Askari wajulikane kama wanafanya mazoezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasiharibu fedha za Watanzania maskini kwa kutembeza Maaskari na magari ya washa washa, hizo fedha wapeleke kwenye mahospitali, hizo fedha wangezi-convert zingeweza kujenga shule. Watoto wanasoma 200 kwenye darasa moja. Leo anaweza akajitokeza mtu amekaa sijui Canada akasema anaanzisha maandamano Tanzania, halafu Serikali inakuwa iko tete.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia matamko ya IGP, (Maneno haya siyo sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge) tumeshuhudia matamko ya Mheshimiwa Waziri pale, tukamshuhudia Rais, tukamshuhudia Mkuu wa Majeshi, just a single lady who is sitting in the USA, wanawatetemesha, wanatumia rasilimali zetu vibaya. Wana hofu gani Serikali ya Awamu ya Tano ya Chama cha Mapinduzi?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii ili nami niweze kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu lakini zaidi kwa maendeleo ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, kwenye page yake ya 2, Waziri anakiri kwamba maji yana mchango mkubwa kwa maisha ya watu, kwa maendeleo ya uchumi na jamii. Kinachoshangaza Serikali haioneshi kuipa kipaumbele Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia hata bajeti ambazo tunapitisha hapa, bajeti ya mwaka 2018/2019 tulipitisha shilingi bilioni 673 lakini kwenye hotuba Waziri anasema mpaka Aprili zimeenda shilingi bilioni 344 ambayo ni sawasawa na asilimia 51 tu na hizi zote ukiangalia sanasana zimetoka kwenye Mfuko wa Maji. Watanzania tumekuwa tukihangaika na maji, wengine wanapoteza maisha wakienda kutafuta maji wanaliwa na mamba, akina mama wengine wanabakwa na ndoa zinaharibika lakini haya yote Serikali haioni ni muda muafaka sasa wa kuweza kuwekeza kwenye Wizara hii muhimu sana kwa maendeleo ya watu. Waziri ameendelea kukiri kwamba kiasi cha mtu anachotumia maji kimepungua kutoka zaidi ya 7,600 mpaka 2300 lakini hamna mkakati ambao unawekwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niombe Wabunge, pamoja na kusema kwamba tupitishe hili Azimio la shilingi 50, sasa tuitake Serikali kama vile ambavyo inafanya kwenye Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, inapeleka hela hata ambazo zingine hatujapitisha hapa Bungeni iweze kuipa kipaumbele Wizara ya Maji ili once and for all tuwekeze kwenye miundombinu ya maji vijijini na mijini, tu-solve hili tatizo ili sasa huu Mfuko ambao tunaupigania ubaki kufanya maintenance ya ile miundombinu ambayo tumeweka vinginevyo hatuwezi kufikia hata uchumi wa viwanda bila maji. Naomba kabisa kama Bunge tuitake Serikali sasa ije kwanza na bajeti yenye uhalisia ambayo imesheheni kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine nataka kuzungumzia kuhusu takwimu ambazo Waziri anatoa za Watanzania wanaopata maji. Vijijini mnatuambia asilimia 64 na wanasema wanazi-drive hizi kwa kuangalia zile center za kuchota maji, sijui ni vijiji vipi hivi.

Mheshimiwa Spika, mimi vijiji ambavyo nimepitia Tanzania hata kama mnafanya kwa average, sijaona vijiji ambavyo unaweza uka-generalize ukasema Watanzania kwa sasa wanapata maji kwa asilimia 64 na target mwaka 2020 mnataka muwe mmefikisha maji vijijini kwa asiimia 95. Tunavyoongea kufikia mwaka 2020 tuna mwaka mmoja tu lakini mnaweza mkaona uhalisia Wabunge wakisimama adha za maji wanazosema Majimboni kwao. Sasa hii asilimia 95 vijijini tutaifikia kweli au tumekuja hapa tunaongea tuna- document inapita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi mijini mnasema kwenye miji ni asilimia 64, mimi kwangu pale Tarime na nimekuwa nikisimama nalalamika pamoja na kwamba ndiyo Makao Makuu ya Wilaya ya Tarime lakini ni kata mbili tu ambazo zina maji kati ya kata nane na hizo kata mbili sio wananchi wote ambao wameunganishiwa. Tunataka Serikali ituambie mikakati ambayo ina dhamira ya dhati ya kutekeleza Sera ya Maji ya Mtanzania kupata maji ndani ya mita 400. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, narudia kusema tukiamua kuwekeza kwenye maendeleo ya watu inawezekana. Kama vile ambavyo Serikali ya Magufuli/CCM mmeamua kuwekeza kwenye miundombinu ambayo ni maendeleo ya vitu na tunaona kweli mmewekeza kwa zaidi ya asilimia ambayo tumepitisha hapa hivyo hivyo tupeleke kwenye maji ili tutatue na tutekeleze Sera ya Maji kwa ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie sasa kuhusiana na Jimbo langu la Tarime. Tuna miradi mingi ya maji; kuna mradi wa Gamasala ambao umekwama ungeweza kusaidia kule Nyandoto. Waziri, Mheshimiwa Kamwelwe alienda akaona na nimeuliza swali hapa ukasema sasa fedha zimepatikana lakini mpaka sasa hivi navyoongea mkandarasi bado hajapelekewa fedha. Mheshimiwa Waziri unapokuja ku- windup naomba mtuambie ule Mradi wa Gamasala unaenda kukamilika lini na ni lini mkandarasi atarudi site?

Mheshimiwa Spika, kingine ni kuhusu Bwawa la Nyanduma. Mmekuwa mkitenga shilingi milioni 300 na nashukuru na hapa mmetenga tena lakini mnatenga shilingi milioni 300 kwanza hazikidhi haja lakini tutashukuru zikija zitaweza kufanya ukarabati wa kuhakikisha kwamba wananchi wa Tarime hawapati yale maji ambayo wanayapata sasa hivi ambayo ni mchafu, unaweza ukafikiri ni ubuyu, chai ya maziwa imewekwa pale. Kwa hiyo, hizi shilingi milioni 300 ambazo mmezitenga hapa tungependa kujua sasa hivi mtazileta au itakuwa kama kila mwaka zinavyotokea kwenye kitabu lakini haziji? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia nishukuru, nimeona mmetenga zaidi ya shilingi bilioni 600 ingawa hazijanyambulishwa ambazo zitakuja Tarime, napenda kujua hizi zinaenda kwenye nyanja zipi, nimejaribu kutafuta sijaona. Maana najua tunawadai visima 23 ambavyo vipo tangu mwaka 2017/2018 na 2018/2019 lakini hazijaenda mpaka leo.

Mheshimiwa Spika, pia niliuliza swali hapa ukanihakikishia kwamba umewaambia DDCA waende maana wanasubiria fedha, ukasema umeagiza waende mara moja, imepita takribani sasa hivi mwezi sijawaona kule Tarime. Napenda nihakikishiwe hawa DDCA wanaenda lini maana ulisema fedha zimeshapatikana ili sasa zile kata za pembezoni za Nyandoto, Nkende, Kenyemanyori na Kitale waweze kupata maji wakati huo sasa tukisubiria Mradi wa Ziwa Victoria ambao nao pia nashukuru mmeuweka hapa kwa zile fedha za India.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, wakati tunasubiria huo mradi mkubwa kutoka Ziwa Victoria ambao utapeleka maji Rorya na Tarime, nitake kujua hivi visima 23 ni lini vinaenda kuchimbwa maana vipo tangu mwaka uliopita na uliniahidi. Kwa hiyo, mkitufanyia hayo walau zile taasisi mbalimbali ambazo zipo ndani ya Mji wa Tarime kuna magereza, hospitali na biashara nyingi maana Tarime ni mji ambao unakua wataweza kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, samahani, nataka kujua maana tusije tukasahaulishwa, Wabunge wote tunajua msisimko ambao tulikuwa nao Bunge la bajeti lililopita la mwaka 2018/ 2019. Kulionekana kuna ufisadi mkubwa sana, hata mimi mwenyewe nilisimama nikataja ufisadi ule wa mkandarasi kule Geita. Hata siku zile Mheshimiwa Eng. Kamwelwe akasema kwa kweli mimi naogopa hata msinipe tena hela mpaka tuhakikishe huu ufisadi ambao mmeutaja hapo umefanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tujue sasa kabla hatujawapa hizi hela ambazo Mheshimiwa Kamwelwe aliogopa kuzipokea, ule ufisadi wote ambao tuliutaja kwenye miradi mbalimbali ya maji hapa nchini mmechukua hatua zipi ili sasa muweze kutuaminisha sisi kwamba tunaweza kuweka fedha nyingi kwenye hii Wizara na zisipate ubadhirifu wowote ule. Kinyume na hapo hatuwezi kuja tu tunakaa hapa tunapitisha fedha zinaenda, zinatumika vibaya, leo ukikagua miradi mingi maji hayatoki, lakini fedha zinaenda tu, hii itakuwa siyo ufanisi wa Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kumalizia kwa kusisitiza kabisa na kwa nia ya dhati kabisa kwamba kama nchi maji ni mojawapo ya kichocheo cha maendeleo. Bila maji wananchi watakuwa wanapoteza muda mwingi kuliko kufanya kazi zao za shughuli za maendeleo. Bila maji safi na salama, tunakunywa maji watoto wetu wanapata vichocho. Ukishapata kichocho ina maana unaipelekea Serikali gharama kubwa ya kuweza kumtibu huyu mwananchi, kwanza anaacha kufanya kazi lakini pia inakuwa ni gharama kwenye hospitali zetu ambazo pia tunajua hazina madawa ya kukidhi mahitaji. Kwa hiyo, mwananchi asipopata tiba mbadala pia ina maana tunampumzisha kwa amani. Tukiwekeza kwenye maji tutaenda kuondoa haya yote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuishia hapo lakini naunga mkono hoja ya upinzani, yale yote ambayo yamewekwa mle tuyachukue na tuyafanyie kazi na michango yote ya Wabunge ambayo ina tija tuifanyie kazi kwa maendeleo ya taifa letu, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia Wizara kwa kugusia vitu vichache, lakini muhimu sana. Ni kweli kwamba Tanzania tumeingia Mkataba wa Abuja (Abuja Declaration) ya kutenga walau 15% ya bajeti yote kwenye afya, lakini miaka yote tumekuwa tukitenga fedha chini ya 10% na bado hatutekelezi hata hii asilimia ndogo tuliyotenga.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuizungumzia kwa takwimu sehemu mojawapo ya bajeti ya afya ambayo ni kuzuia vifo vya mama na mtoto, lakini katika bajeti ya mwaka 2017/2018 kwenye mradi wa kupunguza vifo vya akina mama zilitengwa jumla ya shilingi bilioni 12 ambazo zote ni fedha za ndani; kwenye ukurasa wa 179 kwenye jedwali la mchanganuo wa fedha za miradi ya maendeleo halijaonesha mchanganuo ni kiasi gani ambacho kilipokelewa katika kutekeleza mradi huu ikizingatiwa kwenda 2017/2018 fedha za ndani ambazo zilipaswa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa Wizara hii ilikuwa 42.8% ya fedha za ndani na zilizopelekewa zilikuwa 19% tu ya fedha iliyoidhinishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka unaokuja wa fedha 2018/2019 mradi wa kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi umeongezewa bajeti kwa 0.82% na hivyo kufikia shilingi bilioni 12.2 tu. Je, Wizara imezingatia masuala au vigezo gani katika ongezeko hilo ukilinganisha na ukubwa wa tatizo la vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi nchini?

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mradi wa kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi umetengewa shilingi bilioni 12.2 na katika malengo ya utekelezaji wake kwa mwaka 2018/2019 karibu 50% ya kiasi chote kilichotengwa imeelekezwa katika kukamilisha malipo ya mchango wa Serikali katika First Health Rehabilitation Project uliokuwa wa ukarabati mkubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kutokana na mradi huu kuchukua fedha nyingi ambazo ni takribani shilingi bilioni sita karibu 50% kutoka kwenye kiasi kilichotengwa kwa mradi wa kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kujua mradi huu wa First Health Rehabilitation umesaidia au utasaidia kwa kiwango gani kupunguza vifo vya akina mama ukilinganisha na kiasi kikubwa cha pesa zilizoelekezwa huko?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwingine kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bajeti ya miradi ya maendeleo imeshuka kutoka kiasi cha shilingi bilioni 785.8 (785,805,952,000) kwa mwaka 2017/2018 mpaka shilingi 561,813,998,998 kwa mwaka 2018/2019 ambayo ni sawa na 28.50%. Nataka nijue Wizara ina maelezo gani kuhusu punguzo hili ukiangalia kwamba kutoka bajeti ya mwaka 2017/2018 ni 49% kati ya bajeti iliyopangwa ndio zilizopelekewa katika kutekeleza miradi ya maendeleo hii inamaanisha kuna miradi mingi bado haijateakelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kujua Serikali imejipangaje katika kutekeleza miradi iliyopangwa kwa mwaka uliopita na kuendeleza miradi iliyopangwa kwa mwaka huu kwa punguzo hili la bajeti ya miradi ya maendeleo?

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya maendeleo kwa mwaka 2018/2019 imepunguza utegemezi wa fedha za nje katika bajeti ya mradi wa maendeleo yenye kiasi cha shilingi 561,813,998,998 fedha toka vyanzo vya nje ni shilingi 184,959,998,998; je, Wizara imejipangaje katika ukusanyaji wa mapato ya fedha za ndani ili kukamilisha utekelezaji wa mradi wa maendeleo kwa kuzingatia mwaka 2017/2018 fedha za ndani zilizokusanywa kutoka bajeti ya maendeleo iliyopokelewa ni shilingi 385,771,297,343 zilikuwa ni shilingi 64,756,206 sawa na 19% na fedha za nje zilikuwa shilingi 34,015,208,137.12 sawa na 71% zilizoidhinishwa. Hii ina maana kwamba fedha maendeleo zinatoka nje.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wizara hii muhimu niwatakie masuala yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Israel, sera yetu ya mambo ya nje siku na katika Awamu zote Nne zilizotangulia, zilikuwa rafiki wa kweli wa Israel na Palestine. Awamu ya Tano imefungua Ubalozi kwa mbwembwe zote Israel. Je, wanajua mlivyoikwaza the Arab World!

Mheshimiwa Naibu Spika,Morocco/Western Sahara, awamu hii imefungua Ubalozi Algeria. Hii ni sawa, lakini wakati huo huo wanafunga ndoa ya rafiki na unafiki na Morocco. Algeria ndiyo mtetezi wa Sahara Magharibi. Mbinu zetu za ukombozi zimeishia wapi? Morocco ilikuja mwaka jana na kuweka mikataba 21, iko wapi sasa? Waziri atueleze mikataba yote imefika wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua hamna kitu, Mfalme wa Morocco alikuja kwa nia ya kuishawishi Serikali iunge mkono azimio la ombi la Morocco kurejea AU na siyo vinginevyo. Mengine yote yalikuwa danganya toto. Mbaya zaidi ukikutana na watu wa Morocco utasikia Dkt. Mahiga mtu wetu, Dkt. Mahiga mtu wetu. Sasa hapa ni Dkt. Mahiga au ni Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, ushiriki hafifu wa nchi katika mikutano ya kimataifa na kimkakati. Safari za nje kwa Mheshimiwa Rais kuzikatisha amechemsha, Watanzania sasa lazima tumlazimishe Mheshimiwa Rais kuhudhuria mikutano muhimu. Mwaka huu tumlazamishe aende UN akahutubie Umoja wa Mataifa tufurahi kwa kuwakilisha nchi yetu na kupata fursa mbalimbali. Haiwezekani Mheshimiwa Rais awe ametembelea Rwanda na Uganda tu miaka yote hii, tukiuliza tunaambiwa ni kubana matumizi, hapana! Siyo kweli. Ikulu na Wizara ituambie tu ukweli, kuna tatizo gani? Je ni lugha? Kama ni lugha si atumie Kiswahili tu kwanza atakuwa anakuza na kuitangaza lugha yetu. Je, ni afya? Je, ni usalama wake anahofia au ni majukumu? Katika haya yote sioni sababu labda kama ni ya kiafya.

Mheshimiwa Naibu Spika, msiba wa Winnie Mandela, kwenye msiba huu katika nchi yenye mahusiano mazuri ni sisi tangu enzi hizo hatukuweza kupeleka mwakilishi. Ajabu nchi zote za SADC zilituma wawakilishi, sisi Tanzania hatukwenda! Hii ni aibu sana!

Mheshimiwa Naibu Spika, je, kuna economic diplomacy tena nchini? Ipi! Hakuna economic diplomacy, sasa kuna diplomasia ya miundombinu tu, ambayo ni diplomasia ya barabara na Bombadier!

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi amesikika akisema kuwa kwenye vikao mbalimbali inapofika zamu ya Tanzania kuongea basi watu wote walikuwa wanaacha kwenda hata chooni, walikuwa na shauku ya kusikiliza. Sasa ni kinyume chake, sasa hawana shauku na kwa kweli hakuna cha kusikiliza. Tumefika hapo? We are a laughing stock! Gone are the good days. Inachosha sana leo Bungeni tumeshangilia nafasi walizopata wenzetu kwenye Bunge la Africa (PAP). Tumeshuhudia si Mheshimiwa Rais tu haudhurii bali hata Mawaziri na mbaya zaidi Wabunge katika mikutano ya jimbo ambayo ni calendar meeting, hii sio sawa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kwa kifupi sana juu ya Wizara hii ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi na maendeleo ya nchi yetu. Taifa lenye watu wasioelimika daima halitakaa liendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukiendelea kushuhudia anguko la elimu licha ya Serikali kujitahidi kutoa elimu bure. Tumeendelea kushuhudia quantity na siyo quality kwenye elimu yetu. Kuzidi kuongeza usajili wa wanafunzi bila kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia ni sawa na kazi bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumeshuhudia upungufu wa walimu na kushuhudia uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu ukiwa 1:50 na shule za awali 1:1159. Hata ije miujiza gani hapa hamna ufaulu. Vilevile uhaba ni mkubwa sana kwenye upungufu wa walimu na masomo ya sayansi hasa biology, physics, chemistry na mathematics na ukizingatia tunasema Tanzania ya viwanda bila kuwa na msingi imara ya sayansi tangu shule ya msingi na maabara ni kazi bure. Cha kusikitisha zaidi walimu tulionao wengi wamekata tamaa kwa sababu mbalimbali kama kutokuwepo kwa motisha, kutopandishwa madaraja, mishahara duni, mazingira duni ya kazi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule nyingi za Serikali hazina miundombinu imara ya kufundishia mfano madarasa, vyoo, maabara, nyumba za walimu, ofisi za walimu na kadhalika. Hizi ndiyo sababu kubwa ukilinganisha na shule za binafsi ambapo wao uwiano kati ya mwanafunzi na mwalimu ni ya kuridhisha, idadi ya wanafunzi darasani ni chini ya 40, maabara za kisasa, maktaba na idadi ya walimu ni wa kutosha. Ni wakati muafaka sasa tuwe na mjadala mpana kama Taifa juu ya hatma ya elimu yetu na nini kifanyike na hili lifanyike mapema sana. Bila hivi tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu huku tukifurahia idadi kubwa ya kusajili wanafunzi na ufaulu duni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa ufupi naomba kukarabatiwa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tarime (TFDC) ili kiweze kutoa elimu yenye tija ikizingatiwa kinahudumia Tarime, Rorya na Serengeti na ikiwezekana kijengwe VETA. Katika bajeti ya mwaka huu imeainisha vyuo 20 vitakarabatiwa na ama kuongezewa majengo.

Naomba sana Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Tarime nacho kiingie kwenye ukarabati wa majengo na karakana zake ambazo zimechoka na majengo mengine hayajakamilika. Hili nimekuwa nikiliulizia sana, hivyo, naomba sana katika hivyo vyuo 20 na cha Tarime kiwemo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu ukarabati wa shule kongwe ya Tarime ambayo ina michepuo zaidi ya saba na inachukua wanafunzi toka nchi nzima na ni shule ya A-Level tu kwani miundombinu yake imechakaa sana ni ya tangu mwaka 1973, hii siyo sawa kabisa. Vilevile tupewe gari la wagonjwa na ile Land Cruiser iliyochukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni kuboreshwa kwa Chuo cha Ualimu Tarime. Naomba pamoja na uboreshaji huo ikiwezekana kibadilishwe na kuwa chuo kikuu hasa ikizingatiwa ukanda ule hatuna chuo kikuu ili kuboresha elimu na kuweza kuchukua wanafunzi wengi wanaokosa udahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kuhusu uhitaji wa shule ya wasichana Jimboni kwangu ukizingatia jamii ya Wakurya awali tulikuwa nyuma katika kusomesha watoto wa kike. Kwa kuzingatia pia Mkoa wa Mara tupo tano bora kwa idadi ya mimba za utotoni na kuacha shule kwa watoto wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Jimbo langu (Halmashauri ya Mji wa Tarime) hatuna high school ya wasichana au hata mchanganyiko, bali tunayo high school moja tu ya Tarime ambayo ni wanaume tu siyo mchanganyiko, hivyo inatoa fursa kwa wavulana tu ambao wanatoka shule za kata mchanganyiko na hivyo kuacha wasichana. Kwa kuzingatia haya, naomba sana Serikali itupe fedha za kujenga high school ya wasichana maana tayari tuna uwanja pale Tagota, Kata ya Kenyamanyoni. Pia tunatarajia kupata fedha za Mogabiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo naomba sana Halmashauri ya Mji, tunahitaji fedha kwa ajili ya high school ya wasichana tu ili tuwe na uwiano wa high school ya Tarime ambayo nayo ni chakavu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba majibu na utekelezaji.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye elimu bado nilisahau kuhusu msongamano wa wanafunzi na kwa makusudi kabisa wananchi wa Tarime pamoja na wadau mbalimbali tumeamua kujenga shule nyingi za msingi, mbili za sekondari, lakini cha kusikitisha Shule ya Msingi Rebu ilikuwa ikitumiwa na Shule ya Msingi Buguti pamoja na Shule ya Msingi Mturu, ambapo tumejenga shule Bufuti na imekamilika, tumejenga shule ya Mturu kwa ushirikiano wa Mitaa ya Uwanja wa Ndege na Mkuyuni ambapo tulijenga vyumba sita na ofisi hadi usawa wa renta, lakini Mkurugenzi amesimamisha ujenzi kwa sababu zisizo na msingi. Wakati Waziri Mkuu amekuja alisema DC ashughulikie hiyo shule, tunaomba sana tupate suluhisho ili wanafunzi wetu wasisome zaidi ya 120-200 kwa darasa au wengine kukaa chini ya mti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuondoa ukaimishaji wa idara zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime ili kuweza kuweka ufanisi wa kazi na kuleta maendeleo ndani ya halmashauri ya mji. Tupate rasilimali watu wenye uweledi na wanaomudu kazi zao. Tusibebane kwa maslahi ya watu wachache bali tuangalie Taifa. Halmashauri ndio wasimamizi wa miradi mbalimbali kutoka wizara zingine. Hivyo watendaji wazembe ni msiba kwa halmashauri na maendeleo hayatakuwepo. Mfano ni Idara ya Maji, miradi yote ya maji tulikosa kwa uzembe, Idara ya Mipango ndio ime-paralyze kabisa, idara zingine zimekwisha, si sawa. Tunaomba waajiriwe kama wanafaa au watafutwe wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyingine ni fedha za jengo la utawala hatujapewa hata senti tano. Tunaomba review ifanyike ili na sisi tuweze kujenga jengo letu la kukamilika kuliko pale tulipo ili hata mandhari ya mji wetu yawe mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni mnada wa Magena, tunaomba sana Wizara hii ifanye follow up na Wizara ya Mifugo ili ule mnada ufunguliwe na kuwe chanzo cha mapato kuliko kupotea kwa kupeleka mnada wa mpakani kwa nchi ya Kenya (Mabara). Kwa nini sisi Magena isifunguliwe kwa makubaliano ya kikao cha 2016 kilichojumuisha Mheshimiwa Mwigulu, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Kamati ya Ulinzi na Usalama; wananchi na kuridhia kuwa minada yote ifanye kazi maana Magena ni wa mpakani na ule wa Kinimi Check point ni wa upili. Hii yote italeta tija ya mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia Wizara hii muhimu kwa ustawi wa Taifa letu, Wizara ambayo Serikali ikiwekeza kimkakati na kuhakikisha inapeleka fedha za maendeleo kama zinavyopitishwa na Bunge basi Watanzania zaidi ya 10% ambao wamejiajiri moja kwa moja kwenye sekta hii wataweza kuinuliwa kuliko hali ilivyo sasa ambapo tumeendelea kushuhudia wafugaji wakihangaika vilevile wavuvi na wafanyabiashara wa samaki na dagaa wamekuwa wakinyanyasika sana.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya CCM ni kweli haina dhamira ya dhati kwenye maendeleo ya watu bali vitu ambavyo Watanzania chini ya 5% ndiyo wanatumia, mathalani ndege ambazo zimenunuliwa kwa fedha taslimu. Ikumbukwe mwaka 2017/2018 Bunge lilipitisha kiasi cha shilingi bilioni nne kama fedha za maendeleo lakini kwa taarifa za Waziri kwenye kitabu cha hotuba anasema hadi Aprili, 2018 Wizara haikupokea fedha yoyote kwa ajili ya maendeleo licha ya Wizara kukusanya zaidi ya shilingi bilioni nane kwenye tozo ya chapa za ng’ombe tu.

Mheshimiwa Spika, hivi kwa nini tunapoteza muda na fedha za Watanzania walipa kodi maskini kukaa vikao vya bajeti ambavyo hata asilimia moja ya utekelezaji inakosekana? Hii ni aibu kubwa sana kwenye mhimili huu muhimu sana katika kuisimamia na kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Spika, baada ya mchango huo, naomba kuongelea umuhimu wa kuufungua mnada wa mpakani wa Magena uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime. Naomba sasa kuikumbusha kwa mara ya nne Serikali juu ya umuhimu wa kuufungua Mnada wa Magena ambao ulifungwa bila sababu za msingi mwaka 1997 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wizi wa mifugo. Sababu hii ilitolewa tarehe 9/4/2018 wakati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akijibu swali langu nilipotaka kujua ni lini Serikali itaufungua mnada wa mpakani wa Magena. Kwa masikitiko Serikali ilirudia majibu ya ukaririsho kuwa mnada ulifungwa mwaka 1997 kwa ajili ya wizi wa mifugo. Ukweli ni kwamba kuna nia ovu na wananchi wa Tarime na nia hiyo imetawaliwa zaidi na utashi wa kisiasa badala ya maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2011 nimekuwa nikiiomba Serikali kuufungua Mnada wa Magena nikitambua fika mnada ule upo kimkakati na ufunguaji wake ungeweza kutoa fursa nyingi sana kwa wananchi wa Tarime na kupelekea kukua kwa uchumi kwani sekta mbalimbali zingenufaika (mulitiplier effect). Majibu ya Serikali ya tarehe 9/4/2018 yalijaa fedheha kwa wananchi wangu wa Tarime kwani mnada kupelekwa Kirumi bado ng’ombe wanaonunuliwa Kirumi hupitishwa Tarime kwenda Kenya kwenye Mnada wa Maabara na kupelekea upotevu wa fedha za Tanzania kwani wanaopeleka ng’ombe Kenya hufanya manunuzi ya mahitaji huko huko na kutoa fursa za ajira Kenya.

Mheshimiwa Spika, lakini tujiulize zaidi hapa Tarime wanaposema tangu mwaka 1997 hadi 2018 yaani miaka 21 baadae bado wimbo ni sababu ya wizi wa ng’ombe? Serikali inasahau kuwa Tarime bado kuna Mnada wa Mtana na Randa mbona hao ng’ombe hawaibiwi? Serikali inasahau kuwa tuna Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya na kuwa Mnada wa Kirumi kwanza siyo wa mpakani, lakini pia upo Mkoa wa Kipolisi wa Mara.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii hii haijui kwamba mwaka 2016 baada ya kuuliza swali Bungeni aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mheshimiwa Mwigulu aliweza kufika Tarime na watendaji wa Wizara ambapo tulikaa kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime na maazimio ya kikao ilikuwa ni kuufungua Mnada wa Magena baada ya kujiridhisha na mazingira ya sasa na hivyo kupangwa siku za Mnada wa Kirumi uwe mara mbili kwa wiki na ule wa Magena nao mara mbili kwa wiki ila siku tofauti. Baada ya hapo tuliweza kutembelea eneo la mnada na kujionea miundombinu iliyopo kuwa inakidhi kuanza mnada mara moja. Mheshimiwa Waziri
pamoja na DC Luoga waliongea na wananchi na kuwahakikishia ufunguzi wa mnada huo.

Mheshimiwa Spika, nimeandika haya kuweka kumbukumbu sawa maana nilishtushwa na majibu ya mwaka 2018 wakirejea maamuzi ya mwaka1997 ilhali kuna maamuzi ya mwaka 2016 yanayosubiri utekelezaji tu. Naomba Serikali ione ni kiasi gani tunapoteza fursa kwa kutoufungua mnada ule kwani Mnada wa Kirumi kamwe hauwezi kuwa mbadala wa Mnada wa Magena badala yake tutaendelea kuifaidisha Kenya.

Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba ng’ombe zinazotoka Wilaya ya Serengeti haziendi Kirumi zinaenda moja kwa moja Kenya kupitia Tarime. Ng’ombe zinazotoka Rorya kwa asilimia kubwa zinaenda Kenya moja kwa moja kupitia Tarime. Ng’ombe zinazotoka Kirumi zinapita Tarime kwenda Kenya.

Mheshimiwa Spika, naendelea kuiomba Serikali hii ya CCM ifungue mnada huu wa kimkakati wa Magena ili uweze kuwa stop center ya minada hiyo mingine na uweze kuliingizia Taifa fedha ambazo sasa zinapotea kwa kupeleka ng’ombe kwenye mnada wa mpakani wa Kenya ilhali Tanzania tuna mnada wa mpakani lakini tumeufunga kwa sababu za kisiasa. Tunataka kuona watu wa Kenya wanakuja kufuata mifugo Tanzania na kuweza kuacha fedha za kigeni kwetu na siyo sisi kuwapelekea mifugo.

Mheshimiwa Spika, labda Serikali haijui Kenya wanategemea sana ng’ombe (mifugo) wa Tanzania na hivyo huu mnada ukifunguliwa utakuza uchumi wa wananchi wangu wa Tarime, Halmashauri tutapata mapato na Serikali Kuu pia itapata mapato na zaidi kasi ya ukuaji wa Mji wa Tarime itaongezeka na fursa za uwekezaji nazo zitaongezeka na hatimaye maendeleo. Zaidi ule usumbufu wanaoupata wafanyabiashara wa Tanzania wakati wanavusha mifugo kwenda Kenya utakuwa umepunguzwa. Naomba Wizara inipe majibu ni lini na kwa uharaka mnada ule utafunguliwa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia kwenye Wizara ya TAMISEMI ambayo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya nchi yetu. Maana ndio Wizara inayoratibu utendaji wa Wizara nyingine kwenye ngazi ya halmashauri na tawala za mikoa, lakini tumekuwa tukishuhudia baadhi ya utendaji usioridhisha na hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo katika halmashauri zetu na Taifa kwa ujumla. Ni Wizara ambayo inahitaji kupewa kipaumbele na kuhakikisha bajeti tunazoziweka zinatolewa zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, halmashauri zetu zina rasilimali watu wenye uwezo na kazi walizopewa au wanawekwa tu kwa itikadi za vyama ili kulinda maslahi ya Chama cha Mapinduzi, Chama Tawala. Maana tumeona watendaji wengi wanakaa kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi na sio wananchi wote kwa ujumla bila kujali vyama vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukishuhudia kuporomoka kwa elimu yetu huku ikichangiwa na mambo mengi. Mojawapo ni uhaba wa madarasa, vyoo, nyumba za Walimu, maabara zisizo na vifaa vya maabara, ofisi za Walimu, kupandishwa madaraja Walimu ili waweze kuwa na motisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hotuba ya Waziri ukurasa wa 38 ameonesha kuwa tuna vyumba vya madarasa 123,044 ambapo kwa mwaka wa fedha 2,278, idadi ambayo ni ndogo sana na bado imeonesha changamoto ya upungufu wa madarasa kuwa ni 264,594. Kwa kasi hii tunahitaji miaka 116 ili kujenga hii na ikumbukwe tunavyosonga mbele population inaongezeka na idadi ya ya vyumba vilivyojengwa mwaka 2017/2018 havitajengwa kwa miaka ijayo kwa kuwa wananchi wamepunguza kasi ama wameacha kuchanga kufuatia kauli tata za viongozi. Mheshimiwa Rais alisema hamna michango mara Mawaziri wakasema ichangiwe kupitia DED. Leo hii tunaendelea kushuhudia wanafunzi wakisoma hadi 200 kwenye darasa moja, kinyume na sera ya elimu kwa darasa moja kuwa na wanafunzi 45, lakini hata idadi ya Walimu kwa wanafunzi, wanafunzi kwa kitabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeendelea kushuhudia jitihada za wananchi kama wale wa Jimboni kwangu Tarime Mjini wakijitolea sana kujenga madarasa na shule, lakini wanazuiliwa kuendelea kwa sababu za mgogoro wa ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana Mheshimiwa Waziri husika afike Shule ya Msingi Mturu iliyopo Uwanja wa Ndege Tarime Mjini ambao walikuwa wameshajenga madarasa sita na ofisi, lakini wamezuiliwa kwa sababu zisizo za msingi kwa sababu mmiliki wa lile eneo hana shida na ni mtu binafsi ambaye alipata eneo kinyume cha taratibu, lakini pia alishindwa kuendeleza kwa zaidi ya miaka thelathini. Tunaomba sana, tumejitahidi sana na wananchi wangu wana ari kubwa ya kujenga vyumba vya madarasa, vyoo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna upungufu wa Walimu, nyumba za Walimu wanakaa mbali na wanaishi mbali na shule na wanatumia fedha zao kwa nauli na makazi, lakini wakati wa mvua wanashindwa kufika. Kingine ni motisha kwa Walimu hawa haipo kabisa, wanafundisha katika mazingira magumu sana; kutopandishwa madaraja, madeni ya likizo, nyumba za kulala, na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa sekta ya afya tuna changamoto juu ya hospitali ya wilaya inayohudumia Wilaya tatu, Serengeti, Rorya na Tarime Halmashauri ya Wilaya, lakini unapofikia muda wa mgawo hii hospitali inakuwa treated kama hospitali ya mji inayohudumia wakazi wa Tarime Mjini tu. Mortuary yetu ni ndogo sana, Basket Fund tumepata shilingi milioni 11, wakati Kituo cha Nyarwana wanapata shilingi milioni 42. Hii si sawa na hata Waziri nilimweleza hili. Tunaomba sana watuongezee fedha pamoja na vifaa pamoja na Wauguzi. Hili ni tatizo kubwa sana na linasababisha upungufu wa dawa kwa sababu ya kupewa dawa ndogo kwa idadi ya halmashauri ya mji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni vituo vya afya katika mgawo wa shilingi milioni 500 sikupata, kwenye shilingi milioni 400 hatukupata, pamoja na kwamba tuliomba, hii si sawa kabisa. Tunahitaji ku-upgrade zahanati ya Magena kuwa Kituo cha Afya, Zahanati ya Gamasara kuwa Kituo cha Afya na kile kituo ambacho Kata ya Kenyamayoni wananchi wameanza kujenga, lakini hatujapata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana waangalie jiografia ya utoaji huduma, bado hizo zahanati zinatoa huduma kwa Kata za Jimbo la Rorya na Tarime Vijijini, mfano Gamasara, Nkerege inatoa huduma Kata za Tarime Vijijini.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia Wizara hii kwenye maeneo makuu mawili; mosi, ulipaji wa fidia kwa wakati na kwa wananchi wote waliopo kwenye maeneo yaliyochukuliwana na Mgodi wa Acacia North Mara. Maana kuna baadhi ya nyumba hazijafanyiwa tathmini kabisa na yapo maeneo ya operesheni za mgodi. Hivyo, Waziri anapokuja kuhitimisha atueleze hatua zilizochukuliwa kwa hizi familia na lini wanalipwa sanjari na wengine wanaosubiri malipo tangu mwaka 2009.

Mheshimiwa Spika, baadhi ya hizo familia zilizopatwa na madhara kutokana na operesheni kama vile vumbi, mishtuko wakati wa blasting, kubomoka kwa nyumba; mfano ni Simon Mikulabe, Max, Ibrahim, Max, Prisca Chacha, Chacha Ihande, Abel Max, Mwita Tall, Amos Atendo, Mwita Nyamhanga, Chacha Tall John, Mwikabe Bina, Amos Atendo Nyankobe, Mhere Wagi na wengine.

Mheshimiwa Spika, kuna baadhi waliachwa kwenye zoezi la uthamini No. 20 ndani ya buffer zone kwa sababu mbalimbali kama vile kutokuwepo wakati wa tathmini (safarini), wengine walikuwa gerezani. Raia hawa wameshafika mgodini na kuongea na uongozi wa mgodi juu ya uthamini. Hata hivyo mgodi wanasema Serikali inasitisha uthamini hadi itakapotoa kibali tena. Tunaomba kauli ya Serikali juu ya hatua ya hizi familia zilizopo ndani ya buffer zone.

Mheshimiwa Spika, vilevile ninataka kujua, katika ile faini waliyotozwa Acacia dhidi ya uchafuzi wa mazingira Wananyamongo wanafaidika vipi kwa kupewa fidia hasa wale walioathirika na uchafuzi wa mazingira?

Mheshimiwa Spika, pili ni kuhusu Mgodi wa Kabanga ulioko katika Mji wa Tarime ambao wachimbaji wadogowadogo wamekuwa wakipata matatizo mengi kwa kunyanyaswa na watu wenye fedha (kama Mzungu) na hata wengine kupelekwa gerezani wakati wanachimba kwenye maeneo yao halali.

Mheshimiwa Spika, hili jambo nilishalifikisha Wizarani kipindi Mheshimiwa Kairuki akiwa Waziri na hata kwa Kamishna wa Madini wa Kanda yetu na mkoani wanajua. Hili eneo la Kabanga inasemekana leseni ni ya Barrick, kwa muda mrefu tumeomba iweze kufutwa na leseni zipewe kwa wachimbaji wadogowadogo ili wafanye uchimbaji wao kwa uhuru zaidi bila kubugudhiwa. Pale kuna wajane wananyanyasika sana. Pale kuna mkandarasi tu ndiye ana leseni na hiyo ya Barrick. Wanakabanga tunapenda kujua kama leseni ya Barrick imeshafutwa ama bado na kama imefutwa kwa nini leseni hawajagaiwa wale wachimbaji wadogo wadogo.

Mheshimiwa Spika, pili, mkishawapa leseni watakuwa wmaepata sifa ya kupewa ruzuku ili wajiendeleze kwenye Sekta ya Uchimbaji na kufaidika na rasilimali zilizopo kwenye maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kuchangia hoja hii naomba kutoa shukrani kwa matumaini yanayoanza kuonekana kwa kwanza, kukarabatiwa kwa FDC ya Tarime. Hiki chuo kinasaidia wanafunzi toka Tarime, Rorya na hata baadhi ya kata za mpakani za Serengeti, hivyo ni bora kile chuo kingefanywa kuwa chuo cha VETA. Pia napenda kushauri baada ya ukarabati basi viweze kupatiwa vifaa vya kisasa vya kujifunzia, karakana ya kisasa na vifaa vingine. Hii itaongeza ufanisi kwenye utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi wetu na wakufunzi kwa ujumla. Vyuo hivi vya Maendeleo ya Wananchi vikitoa mafunzo yenye tija vitasaidia sana kutoa vijana watakaosaidia katika soko la ajira na huduma kwa Taifa letu kwani wengi watajiajiri na kuajiri Watanzania wengi. Ikumbukwe huchukuliwa vijana waliokosa udahili wa form one na wale ambao wanakosa udahili wa form five. Ikizingatiwa changamoto za nafasi hizo sanjari na ufaulu wa wanafunzi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ningependa kujua status ya ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Tarime ambayo ni ya kidato cha tano na cha sita tu na ina mikondo mingi sana. Kwa kweli, ni shule ya tangu mwaka 1970, hivyo inahitaji kukarabatiwa na kuwa na hadhi ya aina yake maana shule za hivi ni chache sana Tanzania na lazima tuweke mazingira mazuri kwa wanafunzi ya kujifunzia. Pia, shule hii haina gari la dharura, mfano, mtoto akiugua. Tulikuwa na gari aina ya Land Cruiser, lakini lilichukuliwa kwa mazingira ya kutatanisha na hadi leo halijarudishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri alitembelea jimboni kwangu na kuahidi kutupatia fedha kwa ajili ya kujenga shule ya bweni kwa watoto wa kike. Tayari tuna eneo kwenye kata mbili, ningependa kujua kama mwaka huu wa fedha tumetengewa fedha za kuanza ujenzi na ni kiasi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, tuna shule mbili za kata ambazo zipo tayari na miundombinu ya kuwa high school mchanganyiko. Tumeomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ambayo ni shule ya Mogabini na ile ya Nyandoto. Je, lini tutapata hizo fedha, tumeshuhudia Halmashauri nyingine zinapata na sisi Halmashauri ya Mji tunakosa, ilhali tuna mapato ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika kusimamia elimu ya msingi na sekondari lazima tuboreshe mazingira ya kujifunzia kama vile madawati, madarasa, vitabu, maabara, maktaba, motisha kwa Walimu wetu kama vile kuwapunguzia workload kwa kuajiri Walimu wa kutosha, ili waendane na uwiano pendekezwa, wapewe malipo ya ziada. Unakuta Walimu watatu shule nzima mlundikano wa wanafunzi zaidi ya wanafunzi 200 au 150. Walimu wapandishwe mshahara, walipwe posho ya nyumba kama hawana nyumba katika maeneo ya shule, maana upungufu wa nyumba za Walimu ni zaidi ya 80%, walipwe madeni yao ya likizo na wapandishwe madaraja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa ni kuhusu mikopo ya elimu ya juu; wanafunzi wengi wanaachwa kwa kigezo cha kuwa, alisoma private, lakini pia kuna wengine wamesoma shule za kawaida, lakini wanakosa fursa ya kusoma, hii si sawa na inajenga matabaka kwenye jamii. Ikizingatiwa huu ni mkopo. Ni muda sasa Serikali itenge fedha za kutosha kuwapa mikopo Watanzania wote wenye sifa. Maana Rais wakati wa kampeni 2015 aliahidi akiwa Tabora kuwa, kila Mtanzania mwenye sifa ataenda chuoni.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia hoja hii muhimu kwa mustakabali wa afya za wananchi wa Tarime. Kwanza niombe Wizara izingatie maoni yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hasa maeneo ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 kufanyiwa marekebisho ili kuweza kumlinda mtoto wa kike, maana ilivyo sasa inakinzana na sheria nyingine zinazomlinda mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni kuhusu hospitali yangu ya Mji wa Tarime ambayo ina hadhi ya kuwa Hospitali ya Mkoa wa Tarime/Rorya au kuifanya angalau hospitali ya wilaya. Tunakuwa treated kama vile hospitali inahudumia wananchi wa Tarime Mjini tu ilhali tunahudumia na wananchi wote toka Tarime Vijijini, Serengeti, baadhi ya maeneo ya Rorya na wengine wanatoka nchi jirani ya Kenya, lakini fedha tunazopokea za basket fund ni ndogo sana pamoja na stahiki nyingi za kuwezesha utolewaji wa huduma bora ya afya kama vile idadi ya Wauguzi/Wauguzi Wasaidizi inatolewa kwa idadi ya population ya Mji wa Tarime. Hii sio haki na inasababisha utolewaji wa huduma duni za afya na hatimaye kusababisha umauti.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna upungufu mkubwa wa Madaktari uliopelekea mosi na uchukuliwaji na ugawaji wa basket fund kwa kuzingatia idadi ndogo kuliko uhalisia; zoezi la vyeti feki; kustaafu na vifo. Tuna upungufu mkubwa sana. Wahudumu hawa, Madaktari wanafanya kazi kwa muda mrefu sana bila mapumziko na stahiki zao haziridhishi. Niiombe Serikali na juzi nilisema Bungeni kuwa tuna shida na Daktari wa Meno baada ya aliyekuwepo kufariki kwa ajali mwaka jana. Niombe sana suala hili lipewe kipaumbele maana sasa wananchi wanapata shida sana. Serikali ilichukulie kama jambo la dharura ili kuokoa afya ya kinywa na meno kwa wananchi wa Tarime.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia Wizara hii iweze kujenga utamaduni wa kutembelea magereza ili kujua manyanyaso wanayoyapata wanawake hawa wawapo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi (vituoni), wengi wanabakwa na kudhalilishwa kijinsia. Pia waweze kuona ni jinsi gani wanawake maskini wanavyoonewa na kukosa misaada ya kisheria. Wengi wanakamatwa kwa makosa ya wanaume zao, wengine wana kesi za kudhaminika ila wapo, tena wengine wapo na watoto wadogo/wachanga, wengine ni mabinti wadogo sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitendo cha Jeshi la Polisi kubaka/kuingilia kinyume wanawake tena mabinti ni kinyume kabisa na sheria na kanuni za kazi. Huu udhalilishaji ni lazima Wizara iufanyie kazi ili kulinda utu wa mwanamke.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni wakati sasa Serikali itenge fedha kwa ajili ya kitengo cha lishe. Serikali ya Awamu ya Tano haijawahi kutenga fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ni mahitaji ya ambulance kwenye Kituo cha Afya cha Magena (Nkende) na kile cha Kenyamanyori. Upanuzi wa zahanati ile ya Nkongore Kenyamanyori na Ganasara (Nyandoto) kuwa Kituo cha Afya, ni muhimu sana na sisi tupate fedha za kukarabati na kupandisha hadhi ili ziweze kutoa huduma stahiki. Natambua huwa kuna fedha zinakuja tuweze kupatiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, cha kusikitisha mwaka huu wa fedha, yaani 2019/2020 hakuna bajeti ya uzazi na mpango (family planning). Ningependa kujua ni kwa nini hamna au ni kufuatia kauli ya Rais.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara lazima itoe elimu juu ya ugonjwa wa ini (hepatitis), magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, kuwekeza kwenye kutoa elimu juu ya UKIMWI (HIV). Muhimu kuwekeza kwenye lishe, chanjo, vitamini kwa mama na watoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia hoja hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu, hasa kwenye transport economy. Muda umefika sasa Serikali kuhakikisha inajenga ama kukarabati viwanja vya ndege katika Wilaya zote nchini. Kama bajeti hairuhusu, lazima ihakikishe basi mikoa yote ya nchi yetu ina viwanja vya ndege ambavyo vina hadhi za kupokea ndege za abiria ili kuweza kuharakisha safari toka sehemu moja ya nchi kwenda nyingine.

Mheshimiwa Spika, mfano, Mkoa wa Mara ni mkoa wenye fursa nyingi za kibiashara kama vile samaki toka Ziwa Victoria, biashara ya utalii maana tuna mbuga pale, tuna migodi na zaidi tuna kumbukumbu ya Baba wa Taida ambapo Mataifa mbalimbali wangependa kutembelea na kuweza kuingiza fedha kwenye mkoa wetu pamoja na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, imekuwa ni aibu kwa kweli kuona mkoa ambao ametoka Baba wa Taifa hili na Rais wa Kwanza hadi leo hatuna uwanja wa ndege wenye hadhi na ambao ungepitika kwa maana ya ndege kutua muda wote. Nakumbuka kuna mwaka tulishashindwa kutua pale sababu ya mvua na uwanja ule runway yake siyo ya lami na ilikuwa ni Kumbukumbu ya Kifo cha Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikiongelea huu uwanja tangu Bunge la Kumi. Tunaomba sasa fedha ziende ili wale wananchi walipwe fidia na hatimaye uwanja ukarabatiwe na kupanuliwa ili wananchi wa Mara waweze kurahisishiwa usafiri wa kutoka sehemu mbalimbali za nchi kama ndege za Precision Bombadier na hata Dream Liner kutua. Naomba sana Mheshimiwa Waziri wakati wa majumuisho atueleze wananchi wa Mara juu ya hatua ya uwanja wa Mara, Musoma.

Mheshimiwa Spika, noamba pia kuzungumzia kuhusu usikivu hafifu wa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo Wilaya ya Tanze na hasa Jimbo la Tarime Mjini maeneo ya Mofabiri, Nkende ambapo Mheshimiwa Naibu Waziri alifika na kuahidi kushughulikia hasa Kata ya Ketave, Nbende, Ngendoto na Kuyananyori. Vilevile Jimbo la Tarime Vijijini hasa maeneo ya Mpabani, Sirari na kule Nyamundu, ni muhimu sasa hili lishughulikiwe maana tunapata Safaricom ya Kenya.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu round about iliyopo Tarime Mjini ambayo ni junction ya kwenda Sirari, Nyamagana, Mwanza na Soko Kuu. Ile round about inasababisha ajali nyingi sana na hasa kwa wageni maana sehemu ni finyu sana kuweza kuruhusu mzunguko wa magari hasa makubwa (kama lori na mabasi). Pia ukifika unashindwa kujua unaanzia wapi wala unaelekea wapi. Tumeshazungumzia sana hili kwenye Road Boad tangu mwaka 2017 na TANROADS Mara iliahidi kulishughulikia.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kuondolewa ile round about na kuwekwa taa za barabarani ili ziweze kuongoza magari pale kama ile ya Mwenge inavyoruhusu magari ya kutoka Kawe/Lugalo, Mikocheni kwenda Ubungo na kwenda Posta (hii junction ndiyo mfano). Hizi taa zitasaidia kuondoa ajali nyingi sana zinazopoteza maisha ya Watanzania lakini pia zitasaidia kupandisha hadhi Mji wa Tarime ambao unakua kwa kasi sana na upo jirani na nchi ya Kenya.

Mheshimiwa Spika, vilevile tunaendelea kupata adha ya mtaro hasa kwenye barabara ya Nyamwaga kujaa hasa mvua inaponyesha, mitaro midogo haikidhi haja kabisa. Vilevile, maungio ya barabara za TANROADS kuingia kwenye mitaa zinaachwa bila maingilio kwa barabara nyingine, kukatika kwa mawasiliano kati ya barabara za TANROADS na zile za TARURA.

Mheshimiwa Spika, naomba sana kujengewa daraja la Nyandogo linalounganisha watu wa Kata ya Nyandogo na Bunera pamoja na ukarabati au upanuzi wa daraja la Movi linaloenda uwanja wa ndege wa Magena.

Mheshimiwa Spika, mwisho ni kuhusu ATCL. Kwanza kabisa ieleweke kuwa naunga mkono uboreshaji wa Shirika la Ndege, ambapo kimekuwa ni kilio changu cha muda mrefu na tunatumia fedha za walipa kodi kulifufua. Naishauri Serikali kuiacha Menejimenti ya ATCL iwe huru kujiendesha kibiashara.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani imeshauri vyema. Ili Shirika liwe na ufanisi, Serikali haina budi kuwaacha menejimenti waweze kupanga na kulisimamia Shirika, maana wao ndiyo wana utaalam wa biashara hii ya ndege kuliko sasa wanavyoingiliwa kibiashara, hili Shirika kuendeshwa kisiasa na siyo kibiashara. Ona wenzetu wa KQ, Ethiopia, Emirate, Shirika lolote la operation, mawasiliano na mengineyo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia Wizara hii muhimu kwa ulinzi wa mipaka ya nchi yetu dhidi ya adui wa nje, Jeshi la Wananchi la Tanzania lipo kuhakikisha linamlinda Mtanzania dhidi ya mataifa mengine na pale kunakuwa na utawala dhalimu basi Jeshi hushika hatamu. Ni kwa masikitiko makubwa Awamu hii ya Tano tumeshuhudia wanajeshi wakishushwa hadhi hadi kufikia kusafisha Jiji la Dar es Salaam, kupiga picha zilizo na mantiki wala taswira nzuri na Wakuu wa Mikoa hasa wa Dar es Salaam. Enzi nakuwa niliamini wanajeshi ni watu wenye mosi, kujitokeza kwa nadra sana mbele ya umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sote tunakumbuka hata wakati wa operation UKUTA ya CHADEMA tulishuhudia wanajeshi nao wakijiandaa kukabiliana na raia ilhali Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ipo kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, na kama kuna uhalifu wowote ichukue hatua. Hii ni sawa kuona Jeshi la Wananchi likifanya mambo kwa matakwa ya mtawala na hili limedhihirishwa dhahiri kwa kauli aliyoitoa Mkuu wa Majeshi Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Ofisi za Serikali kuwa wanafuatilia kauli za uchochezi na viashiria vyake na kuwa wapo tayari kuvidhibiti. Hii si sawa na wala si kazi ya JWTZ. Na hili linabidi likemewe kwa nguvu zote na kila mzalendo anayelitakia mema Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuchangia kwenye hilo napenda sana Mheshimiwa Waziri atuambie wananchi wa Bugosi na Kenyambi ni lini watalipwa fidia zao stahiki kwa sababu wanajeshi walivamia lile eneo inasemekana ni baada ya kuvutiwa na mnara ambao Ndugu Thobias Ghati alikuwa ameingia mkataba na Kampuni ya Vodacom huku wakiacha kambi yao iliyopo Kata ya Nyandoto ambayo mosi ipo nje ya mji na mahali stahiki kwa wao kukaa maana miundombinu ya barabara na madaraja sasa imeimalika si kama awali. Lakini kama wameshindwa kulipa fidia kwa wakati wananchi wangu wanaomba wanajeshi wawapishe na warudi kwenye kambi yao, maana hili nimekuwa naliongelea tangu Bunge la Kumi na kila siku Waziri anaeleza watalipa mwaka wa fedha uliopo lakini hawalipi mwaka wa tisa huu sasa nikilisemea hili bila utekelezaji wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hivi wananchi hawa wamewakosea nini Serikali ya Chama cha Mapinduzi tangu mwaka 2008 wanashindwa kuyaendeleza maeneo wala kufanya shughuli za maendeleo maana wamezuiwa, hii si haki kabisa. Jana Tarehe 15 Mei, 2019 Waziri akijibu swali la Mheshimiwa Masoud alisema zile shilingi bilioni 20 zilizotengwa na Bunge tayari wananchi waliofanyiwa tathmini wamelipwa shilingi bilioni tatu, nauliza Tarime tulishafanyiwa tathmini kwa zaidi ya mara tatu bila malipo na hata juzi walikuwa huko, ni lini sasa tutalipwa? Naomba kupewa majibu yanayokidhi haja na yenye matumaini kwa wananchi wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niombe wanajeshi hao waliovamia maeneo ya Bugosi na Kenyambi ambayo yapo katikati ya mji basi iwapo mtalipa fidia wasizidi kujiongezea maeneo maana Tarime Mji hatuna maeneo ya kutosha na inakuwa na muingiliano mkubwa kati ya Jeshi na raia. Mwisho wa siku kwa principle za Jeshi unakuta wananchi wangu wanapitia dhoruba nyingi na mateso ya kijeshi pale wanapotumia public services zilizopo kwenye maeneo waliochukua na kibaya zaidi mnachelewesha fidia huku wanajeshi wamewazuia wananchi kuendeleza maeneo yao ila wao wanakodisha hayo maeneo waliopoka kwa raia na fedha wanazichukua, hii si sawa na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Kama kiongozi nimekuwa nikiwasihi wananchi wavumilie lakini uvumilivu una mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati muafaka sasa Waziri utuhakikishie, kumbuka hata wale wananchi waliokuja mwaka juzi kukuona toka Tarime wengine ni wazee wanafariki kabla ya kupata haki yao si sawa kabisa. Mwisho naomba kujua kama Wizara inapata mapato ya ule mnara uliopo Bugosi ambao ulikuwa na mkataba kati ya Ndugu Thobias Ghati na Vodacom na baada ya wanajeshi kujichukulia maeneo yale waliamuru Vodacom walipe Mkuu wa Kikosi cha Makoko kinyume na sheria maana bado yule mwananchi hajafidiwa, hivyo ule mkataba ulitakiwa kuendelea mpaka pale watakapolipa fidia. Maana hapa si sawa na kuamuru mojawapo ya nyumba yenye wapangaji kuwa wale wapangaji walilipe Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Ndugu Thobias Ghati tunapenda kujua hizo fedha za mnara zimekuwa zikija Wizarani na kama ndivyo ni kiasi gani cha fedha kwa miaka yote hiyo? Na kama haziji ni hatua gani itachukuliwa sambamba na ukaguzi wa kina kwenye hilo suala la mnara?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ndio maombi na mchango wangu kwa leo ambayo ni Jeshi la kulinda mipaka ya nchi na sio kuingilia mambo ya ndani ya nchi. Pili fidia kwa wananchi wangu wa Mtaa wa Kenyambi, Kata ya Nkende na Bugosi Kata ya Nyamisangura pamoja na mapato ya mnara uliopo kwenye eneo la Ndugu Thobias Ghati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia hoja iliyo mezani ambayo tukiamua kama nchi kuwekeza kwenye sekta ya kilimo na uvuvi tutapata faida kubwa kwa kukuza uchumi wa wananchi wetu na pia Pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa bajeti zinazotengwa kwenye Wizara hii ni ndogo sana na haziendi zote na kwa wakati. Leo tunaona idadi ya kupeleka nyama nje ya nchi ni sawa na kiwango ambacho tunaingiza nyama kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, hapa ni kwamba sisi tunapoteza maana tuna mifugo mingi; hivyo ili tukawe mosi tuanzishe viwanda vingi vya kusindika nyama na kuchakata byproducts nyingine kama vile ngozi, kwato, pembe etc. Ili sasa tuweze kumudu kuhudumia soko la ndani na kuondoa uingizwaji wa nyama kutoka nje ya nchi. Pia tunaongeza idadi ya kupeleka nyama na mazao (By-products) nyingine za mifugo nje ya nchi. Hii itakuza sana uchumi wa nchi maana tunakuwa na foreign currencies nyingi kuliko ilivyo sasa.

Mheshimiwa Spika, ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na mazingira mazuri kwa wawekezaji kwenye sekta ya mifugo na uvuvi. Kwa mfano kwa kutafuta masoko, kuondoa tozo, ushuru kwenye bidhaa hizi hasa zile ambazo hazitoshi na nchi wananchama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mfano export levy kwenye ngozi.

Mheshimiwa Spika, hii inachangia sana kuua soko la ngozi na Watanazania wengi wameathirika na hapa Tanzania hamna viwanva vya kutosha ku- absorb ngozi zote. Tozo hii iwe discouraged kabisa kwenye uwekezaji kwenye ngozi; na sasa ngozi nyingi zinaharibika kwenye maghala. Ngozi mwaka 2015 ilikuwa imeanza shilingi 20,000 lakini sasa ni shilingi 1,000, tena wanakubembeleza ununue.

Mheshimiwa Spika, wakati awali ilikuwa unaweka booking na payment in advance, hii ni mbaya sana, inabidi Serikali ijue kuwa siku hizi kuna teknolojia ambayo mataifa kama China wana uwezo wa kutengeneza products equivalent na ngozi bila kutumia ngozi za wanyama (Artificial leather). Sasa with artificial leather na bado kuna hizo tozo za export levy ni dhahiri hizo ngozi zetu zitaendelea kuoza kwenye maghala. Hivyo naishauri Serikali waone umuhimu wa kuondoa hii tozo ya kusafisha.

Mheshimiwa Spika, kwenye upande wa uvuvi pia mazao yetu kama samaki na dagaa pamoja byproducts za daa (vyakula vya kuku) haviuziki kwenye masoko ya nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Congo n. k. Kuna export levy ya 80.16 kwa kila kilo moja ya dagaa, hii inasababisha bidhaa za dagaa zinazotoka Tanzania kuwa ghali sana na hivyo kusababisha bidhaa zetu kutouzika kabisa. kwa mfano mfanyabiashara wa Tanzania tozo na ushuru mbalimbali kwa tani 10 inagharimu takribani shilingi 4,800,000 lakini yule wa Uganda anagharimu shilingi 800,000. Sasa hapa utaona ni jinsi gani bidhaa zetu hazina thamani hata soko nyuma. Maana ni ghali sana hivyo hujikuta hawauzi bidhaa/dagaa zao.

Mheshimiwa Spika, mbaya zaidi Serikali inatoza hii tozo hata kwenye dagaa/chakula cha kuku kwenda miji ya pembezoni; mfano Mbeya, Tunduru, Sirari, Ruvuma etc; nao wanalipa nao export levy. Hii si sawa maana hawa ni Watanzania na hili linasababisha dagaa kuuzwa kwa bei kubwa sana. Nashauri Serikali kuondoa hii tozo ili bidhaa zetu ziwe sindanishi. Hii ni muhimu sana katika kukuza sekta ya uchumi na kuwapa unafuu wafanyabishara wa dagaa.

Mheshimiwa Spika, mwisho ni kuhusu kufunguliwa kwa Mnada wa Magena ambao umekuwa ukiuliza maswali hapa na kueleza umuhimu wa mnada ule ambao ungetoa fursa kwa wananchi wa Tarime na kukuza uchumi wa nchi yetu na ule Tarime.

Mheshimiwa Spika, upande wa pili, Kenya, wana Mnada wa Maabera ambao ambao upo mpakanikabisa, chini ya kilometa tatu. Hawa wanapata faida na tunakuza uchumi wao. Mheshimiwa Mwigulu alipokuwa Waziri mwaka 2016 yeye na watendaji walifika na kutembelea Mnada wa Kirumi na ule wa Magena ambao miundombinu ipo. Huu mnada tulikubaliana ufunguliwe siku moja baada ya ule wa Kirumi ili tuweze pata faida.

Pili, ilivyo sasa mifugo ya Rorya, Serengeti na Tarime inaenda maabera Kenya moja kwa moja; na ilivyo sasa kuna mianya mingi ya rushwa na upotevu wa mapato.

Mheshimiwa Spika, mnada ule ulifungwa kwa sababu ya wizi mwaka 1997. Hata hivyo wote ni mashahili, hali Tarime sasa ni shwari, mifugo inapita kutoka mikoa mingine kwenda Kenya badala ya kuuziwa pale Magena. Hii ni fursa tunayoichezea Watanzania. Ijulikane tu kuwa Kenya wanategemea ng’ombe kutoka Tanzania; inashangaza tunapoteza fursa kwa mambo ya kisiasa na si. Kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, pia alikuja Mheshimiwa Waziri Tizeba na watendaji wakaahidi kuufungua lakini nashangaa kuna nini nyuma ya pazia.

Mheshimiwa Spika, hata alivyokuja Mheshimiwa Rais Julai 2018 alielekezwa mnada wa Magena aufunguliwe. Nashangaa hata amri ya Mheshimiwa Rais inapuuzwa! Wananchi wa Tarime tungependa kujua kwa nini miradi hii inapotezewa? Hata jengo la mazao ya kimataifa la Remegwe limetelekezwa. Naomba tujulishwe hatua ya mnada wa Magena maana muhtasari upo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa hii nami kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Rais. Kwanza kabisa napenda kutoa pole kwa familia ya Mzee Waheke kwa kifo cha mzee Waheke, lakini pia kwa familia ya Mzee Mantago kwa kifo cha bibi yetu mpendwa Bhoke ambaye amefariki muda mchache katika hospitali ya Benjamin Mkapa. Mwenyezi Mungu azilaze roho hizi mahali pema peponi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitajielekeza tu kwenye hotuba ya Rais ukurasa wa 66 ambao amezungumzia kuhusu elimu. Kama Taifa tunatakiwa kuwekeza kwenye elimu. Ukiangalia tulivyo sasa, elimu ya msingi, sekondari na hata vyuo vikuu bado tuna changamoto kubwa sana na ili tuweze kuwa na elimu bora na kupata wataalam wa fani mbalimbali ambao wamebobea na kuweza kupunguza umaskini katika Taifa letu na hapo kukuza uchumi, lazima Serikali itoe kipaumbele kwenye elimu. Leo ukiangalia miundombinu bado iko dhofli-hali. Tuna shule watoto wanakaa chini ya miti. Watoto wanakaa kwenye mawe, Walimu ofisi zao ni kwenye miti, leo hatuna madawati, vitabu vya kutosha; Walimu badala ya kupata motisha, wengi hawana mishahara wala hawana nyumba. Sasa haya yote tusipoyaboresha hatutakuwa na watu ambao wameelimika na Taifa lililoelimika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uchache sana hapo nashauri Serikali itatue tatizo la upungufu wa walimu mashuleni. Serikali iliondoa walimu wengi sana kupitia vyeti fake lakini haikuweza kufanya replacement na walikuwa tayari kwenye payroll.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata kabla walimu wa vyeti fake hawajaondolewa tulikuwa tuna upungufu mkubwa sana wa walimu. Unakuta shule ina mwalimu mmoja au walimu wawili, unategemea watoto wafaulu katika shule hii? Nashauri kwanza Serikali iharakishe ku-replace wale wote ambao walitolewa kwa vyeti fake maana kuna Watanzania wengi mtaani ambao wana sifa za kuwa walimu wawaajiri lakini pia kuajiri walimu kwa ajili ya shule hizi ambazo hazina walimu wa kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye vyuo vikuu amesema anaongeza bajeti ya wanufaika wa mikopo ya vyuo vikuu, ni jambo jema sana. Hata kwenye kampeni yake 2015 alisema hatakubali kuona mtoto wa Kitanzania ambaye ana sifa za kwenda chuo kikuu anakaa bila kupata mkopo. Sasa kupata mikopo ni jambo moja na jema lakini hawa wanufaika wa mikopo hii badaye wanakuja kukaa kwenye kaa la moto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona Sheria ile ya 2004 na marekebisho ya 2016 makato ni makubwa sana. Huyu Mtanzania unamkata asilimia 15 ya mshahara wake baada ya miaka miwili tu baada ya kuhitimu kama ameajiriwa na kama hajaajiriwa atatakiwa kulipa Sh.100,000/= bila kujali anazipata wapi; unamkata asilimia 6 ya kulinda thamani ya fedha; unakatwa asilimia 10 iwapo amechelewesha kama penalty; na anakatwa asilimia 1 ya kusimamia ule mkopo. Mtu huyu anakatwa makato mengine mengi; kuna NSSF hapo asilimia 10, bima, Pay As You Earn ambayo tunaipigia kelele, kodi ya wafanyakazi ni kubwa sana haijawahi kurudi hata kwenye single digit, huyu Mtanzania atabaki na shilingi ngapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, bado hapo mtu huyu anatakiwa akope, hata sisi Wabunge tumekuja hapa tumekopa yaani ule mshahara wetu sisi tumekopea. Sasa huyu mfanyakazi ambaye ana mlolongo mwingi wa makato naye atataka kukopa ili aweze kujinufaisha, atakuwa anabaki na shilingi ngapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niliuliza swali hapa na Waziri hakunijibu kifasaha ingawa alisema tunaweka hivi ili makusanyo yawe mazuri, tumekusanya asilimia 46. I think tatizo ni recovery system ili hii mikopo iweze kurejeshwa na siyo kuongeza rate ambazo zinazababisha makato kuongezeka. Kama Taifa in fact ilitakiwa tuwekeze kupata wajuzi wa fani mbalimbali at the level of university. Tena tungekuwa tunawapa mikopo kwamba warejeshe tu bila hizo riba nyingine na tuwape muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi unakuta wengi, hasa ambao hawajaajiriwa, wanajificha, hawezi akafungua hata account, anaogopa. Sasa hivi mtu anajifanyia biashara zake au anaweza akaingia tu mkataba wa ajira siyo za Serikalini ili nisigundulike nisije kukatwa hayo makato ambayo mmeyaweka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya kwanza yanasababisha moja, hata benki zetu zinashindwa kupata hawa wateja, kwa sababu, nikiamua kujificha hata akaunti sitafungua. Pili, hata nyie Serikali kwa kufanya hivyo mnakosa mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili marejesho ya-boost kutoka asilimia 46 tupunguze ije 8 hata tano, watakuwa wengi ambao wanaleta marejesho haya na watoto wetu wengine wengi wataweza kufaidika. Naomba sana Serikali mlichukue hili mlifanyie kazi, it is a burden to these people wanaokopa ambao ni watoto wa kimaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nami napenda kuchangia kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambayo ni muhimu sana.

Kabla sijaanza kuchangia, napenda kujua kwa kweli hatima ya vijana wawili; Wilson Thomas na Richard Kayanda ambao walipotea wakati wanatoka nyumbani kwangu; walikuwa kwenye timu yangu ya kampeni siku tarehe 26 mwezi wa Kumi, mpaka leo hawajulikani walipo. Hawa vijana wana wake zao, wana watoto wadogo na ndiyo walikuwa tegemeo kwenye familia. Mheshimiwa Waziri unalifahamu hili, IGP analifahamu, RPC analifahamu, OCD analifahamu, DC analifahamu; tungependa kujua hatima ya hawa ndugu, kama wameshafariki mtuambie tuweke matanga; na kama wapo gerezani tuweze kwenda kuwatembelea tuwaone. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niendelee sasa. Ukisoma hotuba au ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu waliotoa Machi, 2021 wameonyesha ni jinsi gani Jeshi la Polisi linakiuka Haki za Binadamu na wakaainisha baadhi ya mambo ikiwepo raia kufia mikononi mwa Jeshi la Polisi, pia ukamataji usiokuwa na staha; na huu ninaweza nikakiri kwamba ni mimi mhanga mmojawapo.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2020 mwezi wa Kumi nilivamiwa na Jeshi la Polisi, wakaja kunikamata na video ilizunguka sana. Tena Jeshi la Polisi wanaume, wakati mwanamke anatakiwa akamatwe na Polisi wa kike. Mbaya zaidi, kijana yule Polisi alionekana kabisa akinipapasa kwenye makalio. Kwa hiyo, ni wengi sana wanafanyiwa hii kero. Unapoenda kukamata una-harass kitu ambacho ni kinyume cha haki za binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tunashuhudia watuhumiwa wanapokua kwenye Jeshi la Polisi vituoni wanapigwa na kuteswa. Kuna baadhi ya Polisi wanawatesa wakiwalazimisha wakiri makosa ambayo hawajayatenda na ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu imeainisha haya. Kwa hiyo, Waziri naomba myafanyie kazi ili sasa Jeshi la Polisi, isiwe Police Force kama ilivyo, liweze kuwa ni Jeshi ambalo linatoa huduma kwa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa spika, kitu kingine ni jinsi ambavyo watuhumiwa kwa maana ya wafungwa na mahabusu wanavyokaguliwa kwenye Magereza yetu. Juzi wakati Mheshimiwa Ole-Sendeka anaongea kwa machungu sana kuhusu Mererani, kwamba watu wanakaguliwa uchi, ikanikumbusha sana wakati niko Segerea. Mnavyoingia pale, mnavuliwa nguo zote, mnaambiwa mnakaguliwa na hata kama mama yuko kwenye siku zake, utaruka kichurachura ili waone kama una kitu umeficha huku chini. Mwaka 2020 nilizungumzia hili jambo hapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukipiga picha, siku hizi wanakamata hata familia. Leo unamkamata baba ana mkwelima wake, labda mkwelima ana shemeji yake pale, wakifika Gerezani wanavuliwa nguo zote wanabaki uchi wote! Uchi kabisa wa mnyama, anakalishwa kwenye ndoo analazimishwa kwamba ajisaidie haja kubwa ili waone kama kuna kitu ameingia nacho Gerezani. Nadhani hii ni kinyume kabisa na haki za binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru Waziri Mkuu juzi alitoa kauli hapa kwamba wataenda kuangalia, ikiwezekana waweke mashine. Tuwe na modern tools za ku-screen, mahabusu akipita au akiingia anakuwa screened tu, kama kuna kitu ameweka tumboni kitaonekana, kuliko wanavyofanya sasa hivi. Ni udhalilishaji. Yaani kila unapotoka kwenda Mahakamani, ukirudi lazima uvue nguo zako zote, ukaguliwe, ni udhalilishaji sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine kwenye NIDA, vitambulisho vya Taifa ni muhimu sana. Mosi, vingeweza kuwa ni pato hata kwa Taifa letu. Tunajua kwamba makampuni mbalimbali yanatumia kama data na wanalipa, bima, ukienda benki, ukienda kwenye simu, lakini pia hata Watanzania wengi hasa walivyosema ukiwa na simu ni lazima usajili kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa, wengi walihangaika sana. Utakuta hata mwingine anamsajilia ndugu yake.

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Pili wa Maendeleo uliainisha kwamba kufikia Juni, 2021 tutakuwa tumeandikisha na kutoa vitambulisho kwa Watanzania milioni 21, kitu ambacho kimekuwa kinyume. Hata leo hapa Mheshimiwa Waziri anakiri tumeshamaliza Mpango wa Pili, kwamba ni milioni saba tu ndiyo wana vitambulisho. Pamoja na kwamba kulikuwa na kanuni ya 7(1) inaelekeza wale Maafisa Uandikishaji wanapoandikisha wahakikishe wanatoa vitambulisho ndani ya miezi sita. Mheshimiwa Waziri amesema hapa kuna watu wana namba, ambao ni zaidi ya milioni 18. Hao kwa mujibu wa hii Kanuni walitakiwa wawe na vitambulisho, lakini hawana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine, ukisoma ripoti ya CAG amesema haya yote yamefanyika kwa sababu ya upungufu wa rasilimaliwatu na fedha. Ukiangalia mwaka wa fedha 2016/2017 waliweza kuandikisha 4% tu ya lengo ambalo lilikuwa limewekwa. Kwa hiyo, utaona kwamba hatutoi kipaumbele. Hii inasikitisha. Kama tunaweza tukahuisha na wapiga kura wakapata kadi zao, tunashindwa nini kwenye hiki kitu muhimu sana ambapo Kitambulisho cha Taifa unatembea nacho kila sehemu! Nimesema, kwa hicho kitambulisho unapata mapato kama Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine CAG ripoti imeonyesha kulikuwa hakuna viashiria ambavyo vingeweza kufuatilia ufanisi wa hii kazi, lakini mbaya zaidi kadi zaidi ya 427,000 ziliweza kuharibika ambazo is worth shilingi bilioni 3,400. Sasa shilingi bilioni 3,400 zimeharibika ambazo hata ukisema ujenge madarasa ya shilingi milioni ishirini ishirini ni zaidi ya madarasa 170 watoto wetu wangeacha kukaa kwenye miti, lakini
zimeharibika. Kwa hiyo, naomba sana tuone umuhimu wa NIDA, watu wapewe Vitambulisho vyao vya Taifa. Kwanza hata inaweza kupunguza uhalifu, maana unaweza uka-m- trace mtu popote pale. Pia hata kwenye haya mambo ya Loan Board wanaweza waka-trace wakajua ni vipi watakupata; na sehemu nyingine zote Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Spika, kingine, napenda kuongelea kuhusu maslahi ya hawa Askari Magereza na Askari wengine kwa kweli. Hawa watu wanafanya kazi. Mimi nazungumzia Magereza kwa sababu nimeishi nao. Namshukuru Mungu nilivyoenda Gerezani miezi minne ile, nimeweza kujifunza mengi sana. Askari Magereza leo, mwenye degree analipwa shilingi 770,000/= lakini hapewi asilimia 15 za taaluma kama wanavyopewa wenzao Askari Polisi. Kwa mfano, Askari Polisi mwenye degree analipwa shilingi 860,000/=, anapewa asilimia 15 ya taaluma ambayo ni shilingi 129,000/=, anapewa shilingi 61,000/= ya pango, lakini wenzao huku hawapati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mbaya zaidi hawa watu hawajapandishwa vyeo kwa takribani ya miaka sita. Hakuna ajira ambazo zimefanyika kwenye Jeshi la Magereza na kwingine kote. Tunajua kuna watu wanakufa, watu wanaacha kazi, kuna watu wanalemaa na mambo mengine mengi, sasa tusipoajiri kwenye hii kada tunasababisha utendaji kazi kuwa na udumavu kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine, uniform, nimelipigia sana kelele hili. Hawa maaskari wanajinunulia wenyewe. Fedha zilitoka mathalani, naambiwa fedha zilitoka kidogo wakaambiwa wanunue baret, lakini ni wajibu wa Serikali kuhakikisha yule Askari anapewa kama ni baret, anapewa shati, anapewa mkanda, suruali, sketi, kiatu everything! Sasa wamekuwa wakijinunulia muda wote. Sasa kama ni hivyo kwamba Serikali inashindwa kuwanunulia, basi waweke package kwenye mshahara wao ili wakiwa wanapata na wawaelekeze ni wapi wanaenda kununua. Ukiwa-align hapa utakuta kila Askari ana-uniform yake tofauti tofauti. Huu pia ni udhalilishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho ni kwenye zimamoto. Lazima tujue kama Taifa majanga ya moto yameongezeka. Umeme wenyewe unakatikakatika kila mara, mengine yanatokea ni hitilafu tu; mtoto amewasha kiberiti, pasi ya umeme na nini; lakini ukiangalia kiuhalisia, hatuna magari ya zimamoto kwenye Majimbo na Wilaya, achilia mbali ofisi. Hapa Mheshimiwa Waziri amesema anajenga Chamwino, kwa sababu hapa kuna Ikulu, lakini huko ukienda wilayani ukikuta gari, ni lile dogo ambalo halina capacity. Kwa mfano, lile gari lililoko Tarime, ikitokea dharura yoyote haliwezi kwenda Mori ichote maji irudi. Kwa hiyo, badala ya kununua magari ya washa washa, tununue magari ya zimamoto.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana (Makofi)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuweza kunipatia fursa hii kuchangia kwenye Wizara muhimu sana na mtambuka.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji ni uhai, lakini zaidi maji ni uchumi. Bila maji hatutaweza kuwa na viwanda ambavyo tunaimba “Tanzania ya Viwanda.” Bila maji hatuwezi kuwa na kilimo chenye tija wala ufugaji; bila maji, wamesema wengi hapa kwamba, afya za Watanzania zitatetereka na itaenda kuigharimu Taifa kuweza kugharimia hawa Watanzania ambao watakuwa wameugua, lakini pia wataacha kufanya kazi za maendeleo kwenye nchi yetu. Bila maji pia tumeshuhudia ndoa nyingi zikiharibika na watu wetu wakiliwa na mamba, watoto wetu wa shule wakipoteza muda mwingi kwenda kutafuta maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa ulijiwekea malengo ambayo yalikuwa kwamba kufikia mwaka 2021 kwa maana ya baada ya miaka mitano, maji vijijini yawe yamepatikana kwa asilimia 85 na maji mijini yawe yamepatikana kwa asilimia 90, lakini kwa taarifa ya Waziri ambayo ameitoa hapa ni kwamba maji sasa ni asilimia 72.3 vijijini ambapo pia siyo kiuhalisia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Mpango wameainisha, kwa kipindi chote cha miaka mitano kufikia Desemba, 2020 walikuwa wametekeleza miradi 1,423 ambayo ilikuwa na vituo au visima 131,370. Katika vituo hivyo au visima, ni 86,000 tu vilikuwa vinatoa maji na vituo au visima 44,590 havitoi maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hayo yote yanatokea mosi, fedha tunazopeleka hazina usimamizi na ufuatiliaji wa kina, unakuta fedha za Watanzania masikini zinapotea tu. Zaidi walishindwa kufikia malengo kwa kuwa bajeti tunazotenga haziendi kiuhalisia. Hata ukiangalia bajeti ya 2020/2021, tulitenga shilingi bilioni 705 hapa, lakini Waziri anakiri kwenye ibara ya 22 kwamba mpaka Aprili, 2021 zimeenda shilingi bilioni 376 tu, ambayo ni asilimia 53; ndani ya miezi kumi, bado miezi miwili tu utaona kabisa dhahiri kwamba hawataenda kutekeleza kama ambavyo wamepanga. Kwa hiyo, hata hapa tunaweza tukawa tunakaa, Wabunge tunafurahia tumepewa miradi kadhaa kwenye maeneo yetu, lakini kiuhalisia haitaenda kutekelezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapo hapo kwenye ubadhilifu wa miradi yetu hii ya maji; na tumekuwa tukiongea hapa kwa kweli, kuanzia Bunge la Kumi, Bunge la Kumi na Moja na Bunge hili la Kumi na Mbili Wabunge wanasimama wanalalamika fedha zinazopotea. Mheshimiwa Waziri


ameainisha hapa kwamba kuna miradi 85 ilibidi irudiwe tena. Nitachukua michache tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia kwenye Kiambatanisho Na. 2, mfano ameainisha Mradi wa Ntomoko, Kondoa huko Dodoma zilitumika shilingi bilioni 2.2, lakini tena kuuhuisha, wametumia shilingi bilioni 2.2 na kitu, asilimia 100. Ukienda kule Mombo, Mbuyuni kuna mradi ulikuwa umeshatumia shilingi milioni 400 ukawa haufanyi kazi. Ili kuuhuisha, imebidi tena watumie shilingi milioni 300, asilimia 85.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda Arusha huko Karatu Remote, kulikuwa na bwawa linajengwa huko, lilitumia shilingi milioni 124 likawa halijafikia kufanya kazi. Ili kulihuisha lifanye kazi, ikabidi watumie tena shilingi milioni 204, asilimia 165. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujua, hawa watu waliofanya huu ubadhirifu wamechukuliwa hatua gani? Tumeshaomba hapa, Wizara ifanye ukaguzi wa kina kwenye miradi yote ili tuweze kujua ni miradi mingapi imetumia kiasi gani cha fedha ya Watanzania masikini na haifanyi kazi na hao watu wamechukuliwa hatua gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine, naenda kwenye miji 28 ambayo na Tarime ilikuwemo. Ni dhahiri hii miji 28 ingekuja ingeweza kutusaidia sana. Kuna fununu kwamba kuna baadhi ya miji itaenda kuondolewa ikiwepo Tarime, Mafinga, Songea na kwingine. Zile dola 460, mwaka 2020 aliongea Mheshimiwa Kitwanga hapa kwa machungu sana, akaelezea kwamba hizi dola 460 zingeweza kutosha miji hata 54; na akaelezea kwamba kuna harufu harufu ya upotevu wa fedha kwenye hii kitu. Sasa badala ya 28, wanataka wapunguze irudi 24.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa DPR ya sasa hivi; kwa maana ya mapitio ya kina ya mradi huu kwa sasa, wanaonyesha kwamba hata mtandao wa maji wanaenda kuupunguza kutoka kilometa 5,751 kwenda 711. Capacity wanaipunguza kutoka 98,450 wanapeleka 48,150. Sasa unajiuliza, kama wanapunguza haya yote, tulitarajia basi gharama ingeenda kuwa kinyume na hapo, badala ya dola 460, ziwe dola 225. Tujiulize nyingine zinaenda wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Tarime mathalani, ukisema ugawanye tu, huwezi ukatumia dola milioni 16.2 ambayo ni shilingi bilioni 38. Tarime pale; kutoka Rorya kuja Tarime ambao watanufaika na wananchi wa Rorya karibia zaidi ya Kata 11, siyo zaidi ya shilingi bilioni 16 tu. Kwa hiyo, tunaomba sana. Kila nikiongea namkumbuka Mheshimiwa Kitwanga mwaka 2020 alivyokuwa akilalamika. Tuna wataalam wetu, tuna ma-engineer wetu, tuna technician wetu hapa hapa Tanzania. Kama WAPCOS tunaona ni shida, basi ufanyike uchunguzi wa kina tena. Hata Bunge lako kupitia hii Kamati ya Maji, muunde Tume ipitie huu mradi. Hizi hela ni nyingi sana. Ni mkopo ambao Watanzania masikini wataenda kuulipa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuhakikishe kwamba, tunaenda na ile review ya mwanzo na siyo ya sasa hivi ambayo wanasema wanaenda kupunguza baadhi ya miji ili iweze kutumika effectively kuhakikisha kwamba siyo tu miji 28, ikiwezekana na miji mpaka 54. Hata hii 28 yenyewe, 24 ambayo itabahatika kupata, mtandao wa maji nao wameupunguza sana. Kama ilikuwa wakamilishe kwa Tarime nzima Kata nane, sasa hivi watajikuta labda wanakamilisha Kata mbili au tatu. Haiwezekani kabisa, kuna harufu ile ile ya uendelevu wa ubadhilifu wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri anajitahidi sana, anapita huko kuhakikisha kwamba miradi inahuishwa, lakini sasa bila kung’oa mizizi ya ubadhirifu wa fedha kwenye Wizara hii, tutaendelea kulia na fedha za Watanzania masikini zitaendelea kupotea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa Tarime, vile visima 23 mmechimba visima vinane lakini maji yanatoka kwenye visima sita. Mradi wa Gibaso hautoi maji kule Tarime Vijijini na mradi wa Mwema hautoi maji ambao ulitumia fedha nyingi sana. Tunaomba sana, sana uweze kupitiwa na hawa ambao wanawajibika kupoteza hizi fedha waweze kuchukuliwa hatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, muda ni mchache sana, lakini napenda kuchangia kwenye Wizara hii ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ambayo ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba Tanzania tumebarikiwa madini ukiacha madini, kuna maliasili na utalii lakini kilimo kwa maana kilimo chenyewe, mifugo na uvuvi. Natambua kabisa Rais wetu Mama Samia amewachangua Waziri na Naibu Waziri strategically, Waziri anatoka kwenye jamii ya wafugaji na Naibu Waziri anatoka kwenye jamii ya uvuvi.

Kwa hiyo, tunatarajia kuona matokeo chanja na dhamira ya dhati ya mama alivyokuwa anahutubia Bunge hapa lime-reflect kwenye bajeti ya mwaka huu ambapo ametenga kweli fedha za maendeleo shilingi bilioni 99 sasa kutenga ni kitu kimoja na utekelezaji ni kitu kingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa bajeti umekuwa ukisausua mathalani mwaka 2016/2017 bajeti ilitengwa lakini zilienda asilimia 3.25 mwaka 2018/2019 bilioni nne lakini hawakwenda chochote kile na 2018/2019 ilienda asilimia 39 tu. Bajeti ya maendeleo ikitelezwa vizuri ina maana Wizara hii itaenda kufanya tafiti za kina kuweza kugundua fursa mbalimbali, kuweza kugundua mbegu mbadala matharani kwa kuwa na ufugaji wa tija. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maana yake najua Tanzania tuna ufugaji wa asili na huu wa ranchi ambao huu nao unasuasua, ufugaji wa asili wapo wale ambao wapo awalimi wanafuga tu na wengine tunalima na kufuga kwa maana ya agropastoral kama sisi hapa Wakurya tunafuga na kulima. Sasa mkiweza kugundua kwa kiwango kikubwa ambacho cha mifugo tulichonacho lakini tija ni ndogo sana na ukafanya tafiti ya kina kuweza kugundua tatizo ni nini, tutaenda mbali.

Mheshimiwa Spika, ufugaji na uvuvi ni sekta ambayo ikiwekezwa kwa kina kabisa tutaenda kupata pato kubwa sana Taifa na shilingi bilioni 23 kwa maana mifugo shilingi bilioni 10 na uvuvi shilingi bilioni 13 mmepeleka shilingi bilioni 11 tu. Lakini makusanyo ni shilingi bilioni 51; sasa mnakusanya shilingi shilingi bilioni 51 mnashindwa vipi kuwekeza shilingi bilioni 23 ili tija iongezeke maradufu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kama hata Kamati ilivyoshauri kwamba wadau mbalimbali wanalalamika kuwa sera, sheria na kanuni zimepitwa na wakati, ifanyike review twende na ufugaji wa kisasa. Hata kama Ranchi ya Taifa ambayo ni asilimia tano ya uwekezaji katika mifugo tuliyonayo nayo inasuasua yaani capacity ni ng’ombe 80,000 mpaka 90,000 mpaka sasa ranchi zetu za Taifa kulingana na takwimu zilizopo 12,000 na … ni bora tufanye ugawaji mzuri wa ardhi, tutafute na tuvutie wawekezaji, tutoke kuwekeza kwa government iende kwenye sekta binafsi. Wawekezaji waje wengi ili sasa hata tuweze kupata na masoko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia kwenye mazao ya mifugo, nyama tuna viwanda 25 lakini capacity yake ni kuweza kuchakata kilo 627,000. Lakini sasa hivi wanafanya under capacity, kilo 81,000 tu. Tatizo ni nini; labda teknolojia imepitwa na wakati, labda kuna factors nyingi, lakini tukiwekeza tukafanya tafiti tutagundua na tuweze kuwekeza kwa kina. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini hata tunapopeleka nje, yaani tuna-export tani 2,000 na tuna-import tani 2,000. Lakini tunazozi-export zinakuwa na bei ndogo kuliko zile ambazo tuna-import sisi, what is this? Tuangalie ubora wa nyama zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata ukija kwenye zao la ngozi utaona ngozi zetu za kondoo, ng’ombe, mbuzi, hazipati market huko nje na sababu ni nyingi. Tumesema hata upigaji chapa, maeneo ya machinjio, makaro yenyewe na kila kitu, ni wakati hata wa kuwekeza kuhakikisha kwamba walau katika kila Wilaya au Majimbo yanakuwa na machinjio ya kisasa kama ambavyo mmewekeza kule Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye maziwa sasa ndiyo unaweza ukalia, yaani hapa ninyi mna-document kwamba tunazalisha maziwa bilioni 2.7 kwa mwaka na target ni kufika bilioni nne, lakini uchakataji wa maziwa ambayo yanazalishwa ni two percent. Na mbaya zaidi kwa mfano mwaka 2018/2019 Serikali mmetoa vibali 417 vya kuingiza maziwa kutoka nje ambapo zilitumika zaidi ya bilioni 22 na kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi bilioni 22 na kitu zingetumika kuboresha viwanda vya Tanzania na kujenga viwanda vingine ili waweze kuchukua haya maziwa tungeweza kutoa fedha nyingi kwa hawa wafugaji na kutoa ajira nyingi hapa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mnada wa Magena kabla sijasahau; pale Magena tuna mnada wa kimkakati ambao ng’ombe wengi wamekwenda Kenya kutoka Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara. Na tukifanya mnada ule wa Magena pale tutapunguza wizi wa mifugo kutoka pale Tarime.

Mheshimiwa Spika, wewe ni mwenyeji pale, unajua, ng’ombe wanatoka Rorya, Serengeti kuja pale wanakwenda Maabera, Kenya, lakini sasa hivi ukiuza ng’ombe kule unachukua hela za Kenya, inabidi ubadilishe upate hela za Tanzania. Lakini ukipeleka ng’ombe umetoka Simiyu au Mara kupeleka Kenya, ikifika jioni ng’ombe wa laki saba utauza laki tatu kwa sababu uko Kenya ili uweze kurudi Tanzania. Tunapoteza fedha nyingi sana za mapato. Tunaomba Serikali ifungue ule mnada wa Magena kwa maslahi mapana ya uchumi wa Wanatarime, Mara na Taifa kwa ujumla. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nitaandika mchango wa maandishi, muda ni mchache sana. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nami kuchangia Wizara hii muhimu katika uchumi wa Taifa letu. Kama nchi tumejiwekea malengo kwamba tufikie watalii milioni tano lakini ukiangalia trend kuanzia hata mwaka 2016 kwa takwimu za Wizara yenyewe walikuwa na watalii milioni 1.28; mwaka 2017 wakawa milioni 1.3; wakaja milioni 1.5; na sasa hivi 2020 waka-drop mpaka 620,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba sisi ni wa pili kwa vivutio vingi duniani, lakini hatujaweza kuvitumia vizuri kuhakikisha kwamba utalii unatuingizia fedha nyingi za kigeni. Sasa nitakwenda kushauri machache tu kwa sababu ya uchache wa muda, kama Taifa na hili tumekuwa tukilisema, tuhakikishe katika balozi zetu tunaweka Maafisa Utalii ambao wanaujua utalii per se, ambao wanajua vivutio vyote tulivyonavyo Tanzania. Wakiwa kule kwenye zile nchi, watatumika kutangaza utalii wetu katika maeneo mbalimbali kwenye nchi husika. Hii itaenda kuongeza utalii na watu kutembelea nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine utalii wa ndani kama sisi Watanzania tunakuwa mpaka unamaliza chuo, unaenda, wengine wanaenda mpaka nchi za nje, lakini hawajui hata vivutio tulivyonavyo Tanzania. Kwa hiyo tuki-promote utalii wa ndani kuhakikisha kwamba entry fee inakuwa ni ndogo, Mtanzania wa kawaida akiingia pale, basi hata yale mahoteli yawe accommodated kwa hawa Watanzania. Unakuta mahoteli ya mle ndani bei zao ni juu sana dola 200, 300 mpaka 1,000 huko, Mtanzania wa kawaida hawezi ku-afford kwenda pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, inatakiwa hata wanafunzi wetu wa Shule za Msingi, Sekondari wanapata fursa ya kwenda kule, wanajifunza ili wanapokuwa wakubwa baadaye wakienda nchi za huko wanatangaza. Wakija watalii wa nchi zingine hapa kama ni watalii wa kibiashara wakikutana na mimi Esther Matiko nakuta nimeshajifunza, najua mbuga zetu, najua vivutio vyote, kwa hiyo nikiongea naye, akitoka akienda huko nje atatangaza na utalii utaongezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ni kuweza kuboresha miundombinu ya barabara hasa kwenye maeneo ambayo yako mipakani ili hata watalii ambapo wako nchi za jirani wanavyotaka kuja huku waweze kuwa vizuri, mathalani kule Tarime, tunapokea watalii ambao unakuta wameingia nchi ya Kenya, wanatoka Nairobi wanaingia Sirari, lakini wakishafika pale Tarime kwenda Serengeti, barabara ni mbovu na tumekuwa tukiongea kwa muda mrefu, irekebishwe ile barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Marais wote wa Awamu ya Tatu, ya Nne na ya Tano waliahidi kutengeza barabara ile. Barabara tukitengeneza kwa kiwango cha lami watalii wakitoka kule ni wengi sana kuingia Serengeti tunaweza kukuza uchumi wetu. Serengeti imetajwa kuwa ni mbuga ya kwanza duniani na hata kwa Taifa letu ndio inaongoza kuleta mapato kwenye nchi yetu. Kwa hiyo ile barabara lazima iwekewe lami na maeneo mengine hata zile barabara za ndani ya mbunga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya uchache wa muda, niendelee kuzungumzia mgogoro wa hifadhi na wananchi wetu. Tumekuwa tukizungumza hili Watanzania wetu wanauawa na hawa maaskari game mathalani kule Tarime, kuna Watanzania wameuawa Manga wa Kijiji cha Kenyamusabi; kuna ndugu John wa Kijiji cha Nyandage; kuna ndugu Mangenyi wa Kijiji cha Kegonga; hawa walikuwa ni wakulima tu wako mpakani. Ikasikika tu risasi wamepigwa wananchi wale hawajaonekana mpaka leo, lakini kuna wengine ni wafugaji zikasikika tena risasi ng’ombe hawajaonekana na hao wananachi hawajaonekana mpaka leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sio Tarime tu, Mbunge wa Mbarali alisimama juzi kati hapa akawa na statement na wananchi wengi hapa kama hatuwezi tukathamini wanyama huku tukawa tumewaua ndugu zetu, ichukuliwe hatua stahiki, kama askari game walinde hifadhi vizuri, wakiwakamata wawapeleke kwenye sheria, Mheshimiwa Waziri na Katibu Mkuu wake na Naibu Waziri najua haw ani watu ambao hawataki kuona haya mambo yanatokea, lakini watendaji kule chini wanafanya ndivyo sivyo. Hii haikubaliki kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ni vile wanavyotaifisha ng’ombe. Hata wakienda mahakamani, mahakama ikaruhusu kwamba hawa watu warudishiwe ng’ombe wao, bado hawarudishiwi. Mathalani kuna Ndugu Hamisi wa Chato alinitafuta sana, ng’ombe wake walikamatwa kwenye Pori la Kigosi huko Kibondo mwaka 2018, walikuwa ng’ombe 420, lakini hawa askari wakasema walikuwa ng’ombe 216, wale wakawapekeleka mahakamani wakasema walipe tozo ya shilingi 500,000 wale ndugu wakalipa, lakini hawakurudishiwa ng’ombe wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, wale watu wakaendelea kufuatilia.wakakata rufaa kwenda mkoa wakashindwa, kwenda Kanda ya Tabora wakashindwa, wakawa wanaamuriwa warudishiwe ng’ombe wao, wakashindwa kurudishiwa. Wakampigia aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Kigwangala, walivyopiga simu kule wakaitwa wakapewa ng’ombe 73 tu. Hii ni dhuluma, kama wanaweza wakawakamata Watanzania wengine wakasema ni uhujumu uchumi, ina maana na wao wanafanya uhujumi uchumi dhidi ya Watanzania. Kama yule mtu tangu mwaka 2018 alikamatiwa ng’ombe wake 420, waka-declare wenyewe ni ng’ombe 216, yet wanaipa ngombe 73 wengine wanaenda wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii haikubaliki, mpaka hukumu tatu zote na wakiomba nitazi-table hapo, tunaomba hii ni just a single case study, wako wengi sana wamezungumza hapa. Kuna juzi kati nilimwona hata yule wa Longido kule alikuwa analia, yule baba na familia yake, ng’ombe wanataifishwa, tuna sheria tumejitungia ng’ombe wakiingia wapige faini inajulikana, kwa nini wanawataifisha, yet hawawarudishii ng’ombe wao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa matumizi bora ya ardhi; kuweza kuondokana na hii sijui mara mara ng’ombe wametaifishwa, wananchi wanauawa, sijui tembo wanaingia kwa raia, sasa hivi hifadhi tulizokuwa nazo kama tunataka tuzichukue kwa matumizi bora ya ardhi tutenge, lijulikane kabisa hili eneo ni kwa ajili ya hifadhi, hili eneo halitakiwa kuwepo, ili hata vile vijiji ambavyo vipo kwenye hifadhi basi Wizara iweze ku-declare waondoe wale wananchi, kuliko hiki wanachowafanyia wanawaua.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni bora ijulikane, kama wameamua kuondoa hivyo vijiji zibaki hifadhi waondolewe, wawape alternatives ardhi waende wakakae. Hatuwezi kuvumilia kama nchi kuona Watanzania wanauawa. Nina majina zaidi ya Watanzania 30 ndani ya Mkoa wa Mara ambao wameuawa kwenye ile Mbunga ya Serengeti, hatuwezi kukubali kitu kama hiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa Bunda, Serengeti na Jimbo la Tarime Vijijini haikubaliki. Kwa hiyo tunaomba sana Waziri na watendaji wote hawa askari game ukinikamata kama nimeenda kinyume, nichukue nipeleke kwenye vyombo vya sheria, why are you killing our people? Ni Tanzania pekee ambapo mtu anaweza akauawa then inachukuliwa easy tu, yaani maisha ya Mtanzania hayana thamani dhidi ya tembo, fisi, simba na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii is unbecoming kabisa, hatuwezi tukathamini wanyama dhidi ya Watanzania. Naomba sana naongea very bitterly, tunataka tujue hatma ya hawa Watanzania wa Tarime. Kama waliwauwa watupe maiti tuzike, tunasubiria kama wapo hai, wako wapi wapelekwe kwenye vyombo vya sheria ili ndugu wale waweze kujua, hawa walikuwa ni baba wa familia, walikuwa ni baba ambao wanatunza wazazi wao. Ahsante. (Makofi)
Hoja ya Dharura kuhusu Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nami nimesimama kuunga hoja ya Mheshimiwa Eng. Ezra. Kama Taifa ni lazima tuwekeze kwenye elimu, in a serious way we need to invest in human capital. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama Taifa na sisi ni lazima tuzalishe wataalam wa kuweza kuwauza nje, kama vile tunaona mataifa mengine madaktari wanatoka huko India, sijui China na kwingineko, ma-engineer, kama Taifa lazima tutengeneze wataalam na sisi ambao tunaweza tukawauza nje na ndiyo tunaweza kufikia huo uchumi wa kati ambao tunaufukuzia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi kwa kweli nashangaa sana. Nashangaa kwa nini, tunapata hii crisis, kila mwaka unakuta watoto wanaopata hii mikopo ni wachache wengine wanaachwa na Serikali inakuja inaona kabisa, hai- assume inakuwa imesha-project kwamba, kwa bajeti hii ambayo tunaomba pamoja na makusanyo ambayo tutakuwa tumechukua, kama ilivyosema mwaka jana imekusanya asilimia 78 tunao uhakika kulingana na trend ya ufaulu wa hawa wanafunzi, kwa sababu lazima mnaangalia trend, mwaka jana 2020 form six walimaliza hawa, katika hawa waliomaliza walio-qualify kwa mikopo, let say walikuwa ni 60%. 2021 you have that trend, kwa kufuatana na hiyo trend mnakuwa mnajua kabisa 2022 tutaweza kupata wahusika wambao wanaweza wakaomba in the likeliness kama asimia hizi na bajeti ambayo tumeomba ni hii.

Mheshimiwa Spika, sasa nikataka nijue Serikali inafanya tafiti ya kina kujua uhitaji halisi wa watoto hawa wa Kitanzania ambao unakuta wengi wao wamesomeshwa kwa shida sana. Kuna wengine wanafanya kuchangishiwa wakati wanaenda shule, unamchangishia akiwa sekondari, high school, unachangishiwa na wanakijiji na wengine, wakifika huko wanashindwa kupata mikopo wanabaki mtaani. Mama hawezi ku-afford hata 200,000/= leave alone hizo 5,000,000/= alizosema Mheshimiwa Ezra hapa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nikataka nijue Mheshimiwa mwenye hoja, Mheshimiwa Ezra, katika maazimio yake mojawapo, nimesema kuanzia mwanzo, tuwekeze katika elimu tuweze kuwa na vyanzo mbadala. Tuwe na chanzo mbadala kabisa na hiki chanzo tuki-ring fence kama tatizo ni hela hazitoki, kiwe ring fenced kama inavyokuwa kwenye REA, tunajua kabisa hii ni kwa ajili ya elimu ya juu, mikopo. Iwekwe kama tunajua itapatikana sehemu gani tutakuwa tunapata kiasi fulani kama ilivyo kwenye REA, ili sasa watoto wetu wote wanaofaulu wanakuwa na sifa waweze Kwenda Chuo Kikuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili huko nyuma, mpaka Mheshimiwa Tendega hapa ananiambia na yeye alinufaika, wazazi wetu walivyokuwa wanafika CHUO Kikuu walikuwa wanasomeshwa bure. Kama tunaona hapa tunaacha Watanzania wengi wa kimaskini nje na itakuwa ni motisha, wanaopata daraja la kwanza Serikali si tunawekeza kwenye elimu na ndio maana imewekwa kwenye kasma ya maendeleo, wanaopata daraja la kwanza tuwasomeshe bure, siyo mkopo, hao wengine sasa ndiyo tuwape huo mkopo. Hii itatoa motisha sana I am telling you, watafaulu kama nyuma waliweza wazazi wetu wamesoma bure, why not now? Tunaweza kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama tunaweza kuwekeza tukatoa fedha tukajenga barabara, tukajenga maji, tuone human capital na yenyewe ni asset. Ni kitu muhimu sana cha kuweza kuwekeza kwenye Taifa, kama tunavyosema tunawezekeza kwenye barabara, kwenye maji, human capital ni kitu muhimu sana kwenye Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa wale wanaopata division one wasomeshwe na Serikali, wanaopata division one unaweza ukasema hata division one ya kufikia point fulani ambayo itachagiza sana. Let say kama mnataka muweke kwenye sayansi, wanaopata division one at this point wanasomeshwa bure, itachagiza sana bila kubagua amesoma private, amesoma public, sijui amesomeshwa nan ani kwa sababu amefikisha hizo sifa basi aweze kupata huo mkopo, na hao wengine ambao wanafuata sasa ndiyo labda waweze kukopeshwa.

Mheshimiwa Spika, simu ni nyingi, malalamiko ni mengi, Watanzania masikini kabisa watoto wao wamefaulu vizuri na wako nyumbani hawawezi Kwenda shule. Ni kitu ambacho ni cha muhimu sana na cha uharaka kuweza kufanyiwa kazi. Baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kwenye sekta hii muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu kiuchumi na usalama. Tumeshuhudia shughuli nyingi za maendeleo zikikwama kwa ajili ya ukosefu wa nishati. Akina mama wajawazito wanapoteza maisha pale wanapojifungulia kwenye zahanati/vituo vya afya ambavyo havina umeme na wanatumia torch kuzalishiwa. Kwenye hospitali kubwa ambazo hazina generator ikiwa mgonjwa anafanyiwa operation na umeme ukakatika basi kuna vifo vya mama na watoto hutokea ikiwa ni pamoja na wagonjwa wengine wenye kufanyiwa operation.

Mheshimiwa Spika, umeme unasaidia uchumi wa nchi yetu kwani wananchi wetu wataweza kujishughulisha na uchakataji wa mazao ghafi, viwanda mbalimbali vikubwa na vidogo vitaanzishwa, wafanyabiashara wa chini, kati na juu wote watafaidika. Lakini muhimu kuliko yote ni usalama kwa raia, maana mwanga, hasa vijijini utasaidia sana kupunguza uhalifu.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huu naomba Waziri na Naibu Waziri ambao wamekuwa mara kadhaa wakizunguka kufuatilia utekelezaji wa miradi, hasa ule wa REA, lakini maeneo mengi ya Mji wa Tarime hayana umeme. Mji wa Tarime una kata nane, lakini umeme ni chini ya asilimia 40. Umeme upo Kata ya Bomani kwa asilimia zaidi ya 90, Kata ya Nyamisangura ina umeme kwa asilimia 50 tu, Kata ya Nyandoto ni kwa asilimia 20, Kata ya Kenyamanyori ni chini ya asilimia 20. Maeneo ya Kogete, Tagotha, Mubali, Kenyamanyori Cnetre, Lobasa, Kebaga Mining, Makao, Nyamitende, havina umeme. Kata ya Katare nayo ina umeme chini ya asilimia 30, maeneo ya Nkongore yenye zahanati, shule ya msingi na sekondari havina umeme. Kata ya Nkende nayo haina umeme kwa zaidi ya asilimia 70 za wakazi wake, maeneo ya Magena yenye Kituo cha Afya na shule ya msingi, Katare, Itebe, Nyamihito, Nyamitende, Kata ya Nyandoto, maeneo ya Kewoje, Nyagisesa wanapojenga Mji Mpya na nyumba za Askari Polisi na Kanda Maalum Tarime/Rorya.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba Mji wa Tarime ndio Makao Makuu ya Wilaya ya Tarime, ni mji wa kimkakati maana upo mpakani. Wenzetu upande wa Kenya umeme unawaka vyema na kutoa mandhari nzuri wakati wa usiku ilhali upande wa Tanzania Mji wa Tarime ni giza totoro. Ni vyema Serikali ikatoa kipaumbele kwenye miji kama Tarime iliyokaa kimkakati. Nitaomba commitment ya Serikali maana REA inapita kwenye baadhi ya maeneo tu kwenye kijiji na kata na si wakazi wote. Hii inaleta mtafaruku mkubwa na wananchi wanahisi kubaguliwa. Ni rai yangu Serikali kuhakikisha Mji wa Tarime kata zote nane za Nkende, Nyandoto, Katare, Turwa, maeneo ya Buguti, Nyamisangura, Bomani, Kenyamanyori na Sabasaba wapatiwe either umeme wa REA, hasa kata za pembezoni, densification, na umeme wa TANESCO.

Mheshimiwa Spika, kwa haya machache, lakini ya umuhimu naomba kuwasilisha, lakini bila kusahau mradi wa Kinyerezi ambao kwa kweli Serikali ikiwekeza vyema itasaidia sana kupunguza kero ya umeme. Ila nishauri Serikali kupeleka wataalam nje ili waweze kuwa na ujuzi kwenye uendeshaji wa mradi wa Kinyerezi, na pia utengenezaji wa mitambo inapoharibika au kui-service kuliko sasa kuipeleka mitambo Marekani kwa ajili ya service.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuendelea kutoa chanzo cha mapato ambacho kitasaidia kukuza mapato ya Serikali na kuondokana na utegemezi wa kodi ambazo hazina uhalisia mfano wa kodi za nywele bandia.

Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunajua kuwa Sekta ya Utalii ni moja ya Sekta zinazochangia kwenye Pato la Taifa lakini ukweli ni kwamba hatujatumia rasilimali za utalii tulizonazo na kuwekeza ili tupate mapato ambayo kwa kweli yangesaidia kupunguza kodi kwenye maeneo mengine kama taulo za kie, nywele bandia, punguzo la PAYE kwa wafanyakazi, vitambulisho vya wafanyabiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye mchango wangu wa kuongea nilieleza kidogo kwenye uwekezaji wa utalii wa fukwe (beach tourism), utalii wa meli (cruising tourism) na utalii wa mikutano, matukio (Mice tourism). Haya mambo hatujayaona na kuwekeza ili kuweza kukuza uchumi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna fukwe nyingi sana za bahari kuanzia Mtwara, Dar es Salaam, Tanga, fukwe za ziwa, fukwe za visiwa. Tunahitaji kufanya classification za fukwe zetu ili tujue fukwe zenye mchanga, miamba na kdahalika, lakini pia tunaweza kutengeneza artificial beaches kwenye maeneo ambayo bado hayajatumika (beach resort). Mfano kule Bagamoyo (SES). Pale tukijenga beach resort yenye facility zote. Kule Kigamboni tunaweza kujenga connection center zenye hadhi za Kimataifa kwa Tanzania hatuna kwakweli zaidi ya ile AICC iliyojengwa na Mwalimu Nyerere. Tunahitaji Mataifa mbalimbali waweze kuvutika kuja Tanzania maana tuna uwanja wa ndege wa kisasa, tuna ndege, tujenge connection center kama za Barcelona, Rwanda na kwingineko. Tuwe na modern pitch ambazo zina accommodate michezo yote na ambazo wakati mwingine inageuka kuwa concert hall. Hapo kwa kweli tutaongeza idadi ya watalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile ni wakati wa kuhakikisha convention center zetu ziwe hotel zenye sifa za kuweza kukalika/kupokea Marais wa nchi mbalimbali. Leo tuna Mkutano wa SADC lakini Jiji la Dar es Salaam sio tu halina uwezo wa kupokea ugeni huo lakini ukweli hoteli zenye sifa ya kufikia Marais ni hotel ya Hyatt tu ambayo hoteli hii ilikuwa ni ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ni wakati sasa wa kuwekeza kwenye theme parks, najua wengi wetu tumesafiri nchi mbalimbali hata watendaji na tumeona ni jinsi gani hizi theme parks zilivyo. Tunaweza wekeza theme park katika Majiji kama Dar es Salaam pale pande game reserve ijengwe theme park, kule Mbeya pia pawe na theme park, Mwanza napo tuwe na theme park na Arusha. Hapa tunaweza kuongea na Disney ili waweze kuja kuwekeza kupitia PPP. Hakika hili likijengwa litasaidia kukuza uchumi na kuongeza mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile ili kuweza kurahisisha usafiri kipindi watalii wamekuja na kuweza kutembelea vivutio mbalimbali, hivyo ni vyema tufanye cruising terminal (cruise terminal). Mfano SGR na uwanja wa ndege terminal III vinahitaji kiunganishi cha Dar es Salaam, cruise terminal kama ile ya Kai Fan ya Hong Kong. Ijengwe pia Mtwara Cruise terminal, Tanga cruise terminal, hakika itasaidia mtalii anaenda Mtwara, Lindi kuona malikale under water experience, kule Mafia wakija Dar es Salaam wanashuka kirahisi na kuungana na SGR kuelekea Mikumi na kwingineko. Leo fukwe za Saadan ukilinganisha na Costa Rica, Mtwara na Seychelles, Dar es Salaam, Durban/Cape town. Walikuja hapa watalii walishindwa kutumia kamba, wengine ni wazee na ni aibu.