Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Hamidu Hassan Bobali (69 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupata majibu kuhusu suala la mjusi (mabaki yake) ambayo yalichukuliwa Tendegu katika Jimbo la Mchinga na kupelekwa Ujerumani, naomba kupata majibu ya hoja zangu hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inanufaika na nini kutokana na mjusi huyo kuhifadhiwa huko. Mheshimiwa Waziri hii hauoni kwamba suala hili linatuletea fedheha kubwa Watanzania kwa kuonekana kwamba hatujali na kuthamini rasilimali na maliasili za nchi yetu? Kwa nini rasilimali kubwa na ya kihistoria kama hii imebaki Ujerumani bila sisi kama Taifa kunufaika kwa chochote? Kumekuwa na kauli tata kuhusu manufaa ya mjusi huyu kutokana na suala hili pia kuihusisha Wizara ya Mambo ya Nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa anayofanya katika Wizara hii muhimu lakini anaifanya peke yake bila hata kuwa na Naibu Waziri wa kumsaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuonesha malalamiko yangu juu ya kukosekana kwa soko la uhakika la zao la ufuta. Namwomba Mheshimiwa Waziri aliangalie suala hili ili tupate soko la uhakika la zao la ufuta, wakulima waweze kupata fedha stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu suala la kuwezesha wakulima wa chumvi kupata uwezeshaji wa kupata mkopo wa mashine ya kusindika chumvi ili kuinuna kipato chao. Naomba Mheshimiwa Waziri aweze kuwaunganisha wakulima hao wa chumvi na SIDO ili SIDO iwapatie mashine hizo hata kwa mkopo ili tuweze kufungua kiwanda cha kusindika chumvi hivyo wakulima hao waweze kujiongezea kipato zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutambua miaka michache iliyopita kulikuwa na taarifa ya uwepo wa Kiwanda cha Simenti pale Mchinga. Taarifa za kiwanda hicho zilikuwepo tangu wakati Jimbo la Mchinga linaongozwa na Mheshimiwa Mudhihir Mohamed Mudhihir lakini hadi sasa hatuna taarifa zozote kutoka katika mamlaka husika. Tunaomba kujulishwa kiwanda hiki kimefikia wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu hatua ya viwanda vya LNG. Tunasikia kuwa kuna watu wanataka kuhujumu jambo hili, je, taarifa hizi ni kweli au la?

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu viwanda vya korosho ambavyo vimebinafsishwa lakini watu waliovichukua wanavigeuza kuwa ni maghala tu badala ya kuvitumia kwa ajili ya kuongeza thamani ya korosho kwa kuzibangua. Mheshimiwa Waziri tunaomba wale wote waliochukua viwanda vyetu vya mtama, Nachingwea, Newala na kadhalika wanyang’anywe na viwanda hivyo wapewe watu ambao watavitumia kwa lengo lililokusudiwa.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru kwa kunipa fursa hii ili nami niweze kuchangia hotuba hii ya Waziri wa Fedha kuhusu Mpango wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze na suala zima la kilimo na ningegusia moja kwa moja mlinganisho uliopo kwenye kilimo na uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kuwa na uchumi wa kati, hatuwezi kuwa na uchumi wa viwanda kama hatutawekeza ipasavyo kwenye kilimo. Viwanda vyote ambavyo tunavikusudia vinahitaji malighafi kutoka kwa wakulima, wakulima hawa lazima tuwawezeshe ili waweze kuzalisha kisasa na waweze kuzalisha kwa tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozalisha ili uchumi uweze kukua hautakua kwa maneno mazuri tutakayokuwa tunayazungumza, wala hautakua kwa kauli mbiu nzuri, kama hivi sasa tunasema uchumi wa viwanda. Tuzungumze Watanzania wote uchumi wa viwanda, havitapatikana viwanda kama hakuna mikakati kwa sababu kauli mbiu nzuri za namna hii zilishawahi kupatikana huko nyuma kwamba kilimo uti wa mgongo na kauli mbiu nyingine, kulikuwa na kauli mbiu nyingi sana katika kilimo, lakini mwisho wa siku bado kilimo chetu kimeendelea kubaki kuwa kilimo cha kutumia jembe la mkono na kilimo kile cha kizamani primitive way. Kwa hiyo, hatuwezi kuendelea kwa kutumia kaulimbiu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri nakushukuru unanisikiliza kwa makini nataka niseme jambo moja, katika suala la korosho ambalo ni zao ambalo kwa sasa linatuingizia kama Taifa kipato kizuri, tunahitaji tuwekeze kwenye viwanda ili korosho zetu tuweze kuzibangua hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia takwimu ambazo yuko mzungumzaji alikuwa anasema hapa na nilijaribu kum-crush kwamba siyo takwimu sahihi. Tanzania kwa kusaidia tu na kuweka sawa, Tanzania mwaka jana tulizalisha tani 250,000 za korosho na ni nchi miongoni mwa wazalishaji wakubwa tu wa korosho na kwa bahati nzuri korosho ya Tanzania ni moja ya korosho bora duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kwenye mitandao wameandika kabisa best cashewnuts producers ni Tanzania na Mozambique. Ni korosho tamu, zenye mafuta na ni korosho ambazo zinapendwa sana. Kwenye soko la dunia zikifika korosho za Tanzania na Msumbiji zingine zinasubiri ili ziweze kuuzwa. Sasa nini ninachokusudia kusema? Ninachokusudia kusema ni kwamba, hii thamani ya korosho ya sasa shilingi 3,900 mpaka shilingi 4,000 bado haikidhi haja wala haifikii kiwango ambacho wakulima wanapaswa kukipata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, nimejaribu kuangalia leo soko la dunia bei ya korosho ghafi ni shilingi ngapi, ni kuanzia dola tano mpaka dola 13 lakini korosho iliyobanguliwa yaani zile cashewnuts canals nilizokuwa nazisema mara ya kwanza, leo zinacheza kwenye dola 25 mpaka dola 29. Ni korosho ambazo tayari zimeshakuwa processed, maana yake ni zaidi ya shilingi milioni 50 lakini huko mbali. Katika soko la ndani pekee hivi sasa korosho iliyobanguliwa ukifika pale Mtwara inauzwa kati ya shilingi 25,000 na shilingi 30,000 maana yake ni zaidi ya dola 12 mpaka dola 15. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokusudia kusema ni kwamba kama tuna mipango iliyokuwa madhubuti, tunaweza tukabangua korosho zetu, tukategemea soko la ndani na soko la nje, tukapata kipato kikubwa zaidi. Ndiyo maana wasioelewa ukiingia leo kwenye mtandao ukatafuta kujua wauzaji wa korosho kwenye soko la dunia hautaiona Tanzania, you will never see it! Utaona tu pale Brazil, utaiona India, utaiona Vietnam, utaiona Ivory Coast, utaiona Canada, kwa sababu wao siyo kwamba wana mikorosho mingi bali wao wana viwanda ambavyo wana-process korosho zao na wanaweza kuzipeleka kwenye soko la dunia, bali Tanzania ni wazalishaji lakini hatupeleki korosho zetu kwenye soko la dunia, we are not recorded anywhere kwamba tunauza korosho kwenye soko la dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ninaomba sana hivi ni viwanda ambavyo tunavipoteza, tungeweza kuwekeza kwenye korosho kwa kuweka vile viwanda, kuvifufua vilivyopo, tungeweza kupata kipato kikubwa. Wanatushinda Msumbiji ambao wamepigana vita miaka mingi, leo Msumbiji wanabangua more than 80 percent ya korosho zao, sisi hatujafikia hata asilimia 20, maana yake bado tuko chini kwenye suala la ubanguaji wa korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo Mheshimiwa Waziri naomba sana mpango tunapopanga kwamba tunataka kwenda kwenye uchumi wa kati na uchumi wa viwanda basi tuhakikishe kwamba tunakuwa na mipango madhubuti lakini siyo maneno matamu yanayoweza kusikika na kufurahisha wasikilizaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ninataka nilichangie ni suala la miradi mikubwa ambayo ilizungumzwa kwenye mpango wa mwaka jana. Mheshimiwa Waziri tunakumbuka kwamba mwaka jana kwenye hotuba yako ya mpango ulizungumzia suala la mradi wa gesi wa Lindi (Liquidfied Natural Gas) nataka kujua umefikia wapi? Taarifa zilizopo mpaka sasa ambazo wananchi wa Lindi, Wabunge na wawakilishi wa wananchi tunajua kwamba ule mradi ndiyo umekufa kifo cha mende, sasa tunataka tujue kwamba mradi ule umekufa au umeendelea na kama unaendelea umefikia wapi, kwa sababu taarifa tulizonazo ambazo inawezekana isiwe rasmi ni kwamba wale jamaa Wentworth Resources na wenzao wameshafunga hata ofisi zao pale London, kwamba shughuli za kuendelea ku-negotiate na ile miradi imeishia wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kama siyo hiyo njoo ututoe hofu, kwa sababu wale wananchi walifanyiwa tathmini ya kutaka kulipwa fedha zao, watu wameacha kuendeleza mashamba yao, watu wameacha kuendeleza nyumba zao, basi njoo tuambie watalipwa lini na mradi ni lini utaanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachangia kwenye hotuba ya mpango kwa sababu mradi huu ni moja ya miradi mikubwa inawezekana Watanzania hawajui, Mheshimiwa waziri uje utueleze, mradi huu ni mkubwa kama unavyoonekana mradi wa standard gauge, ni mradi mkubwa sana ambao utatumia trillions of shillings, kama tutaupata utatusaidia sana katika kukuza kipato na pato letu la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilitaka niseme ni suala la kuwekeza kwenye uvuvi. Mheshimiwa Waziri katika hotuba hii nimejaribu kuangalia uvuvi namna ulivyouzungumza it is just like a minor issue. Kuna nchi ambazo zinaendesha bajeti zao kwa kutegemea uvuvi tu, na sisi Mwenyezi Mungu ametujalia tuna bahari kuanzia Tanga mpaka unafika Mtwara, bahari ambayo ina samaki wengi na sasa Watanzania wameacha kupiga mabomu, kuua samaki kwa kutumia mabomu na samaki leo wako wengi sana. Mimi miezi miwili hapa niliyokuwa Jimboni pale Mchinga tumekula samaki wengine kama ingekuwa ni binadamu tungeona mpaka mvi, samaki waliozeeka tayari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni kiashiria kwamba samaki wako wengi lakini uwezo wa wavuvi wetu kwenda kuvua kwenye Bahari Kuu imekuwa ni changamoto. Leo Mheshimiwa Waziri anatambua kwamba mapato pekee tunayoyapata kutoka kwenye uvuvi wa Bahari Kuu ni kutegemea leseni tu, kama tunategemea leseni wakati meli moja ya uvuvi na ninamuona hapa Naibu Waziri wa Uvuvi anajua ni mtaalam, meli moja ya uvuvi ikienda pale Bahari Kuu wana uwezo wa kuvua samaki kwa siku mbili wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni moja, bilioni mbili. Lakini sisi tunachukua ushuru wa shilingi milioni 30, milioni 40 na tunafikiria kwamba ndiyo inatosha kabisa!

Mheshimiwa Waziri kama kuna jambo ambalo tunapaswa tuliwekee msingi na msisitizo ni kuwekeza katika bandari ya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiwekeza katika bandari ya uvuvi tutapata mapato makubwa, kwanza wale wavuaji wataleta samaki wao bandarini tutawa-charge ile kodi, lakini pia kutakuwa na viwanda vya uchakataji ambavyo vitaajiri vijana wengi. Jambo hili liendane sambamba na kuwawezesha wavuvi wetu wa ndani waweze kuwa na capacity ya kwenda kuvua kwenye Bahari Kuu, kwenye kina kirefu cha maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo Mheshimiwa Waziri suala la uvuvi halipaswi kuwa ni suala ambalo linazungumzwa kana kwamba ni suala la utani au kama suala dogo. Uvuvi ni sawa na madini, uvuvi ni sawa na kilimo na uvuvi ni sawa na kitu kingine kama tutawekeza vizuri tunaweza tukapata pesa nzuri na itakayotosheleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la kilimo. Suala la uhakika wa bei ya mazao ya wakulima. Mwaka jana tulisisitiza sana na tuliona Waziri Mkuu wa India alikuja hapa akasaini mkataba na Serikali ya Tanzania juu ya suala la zao la mbaazi, lakini jambo hili linakwenda sambamba na uzalishaji wa zao la ufuta. Nimesikia hapa kwenye taarifa kwamba ufuta sasa umepanda kutoka tani 2,000 na mpaka kufika tani 8,000, lakini wakulima wa ufuta wenyewe hawajui uhakika wa soko la mazao yao. Tunaendelea pale pale kwamba kwenye vichwa vyetu tumejijenga na mentality kwamba mazao ya kuyasafirisha na kupeleka nje ya nchi, kuwatafuta Wahindi wako wapi ili tuwasafirishie, kuwatafuta Wavietnam wako wapi tukawauzie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tusiwe na mipango mikakati kwamba huu ufuta uwe processed ndani ya nchi, tukawa tunakula mafuta ya ufuta, na imethibitishwa na madaktari kwamba mafuta ya ufuta ni miongoni mwa mafuta mafuta mazuri ambayo hayana lehemu nyingi.
Tunaweza tukaondoa magonjwa ya pressure at the same time tutakuwa tunaongeza kipato cha wakulima na pato letu la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine Mheshimiwa Waziri ni kuhusu suala la uwekezaji kwenye sekta ya afya. Hatuwezi kuwa na rasilimali watu ambao watakuwa more productive kwenye nchi kama afya zao zitakuwa ni zenye utata. Hivi sasa nilikuwa nasoma hapa ripoti ya ongezeko la ugonjwa wa saratani nchini (cancer), taarifa kutoka Hospitali yetu ya Ocean Road ni kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ambayo kiwango kikubwa cha wagonjwa wa kansa wamekuwa wakiongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jirani zetu wa Uganda walikuwa wametuzidi miaka fulani hapa, wameweka mikakati mambo yamekuwa mazuri tumewazidi sisi sasa, Kenya na wenyewe mambo wameweka vizuri kidogo tumewazidi. Katika huu Ukanda wa Afrika Mashariki Tanzania ndiyo tuna orodha kubwa, tuna percentage kubwa ya watu kuugua saratani kuliko nchi yoyote nyingine. Sasa Mheshimiwa Waziri jambo hili ni baya, kwa sababu ugonjwa huu kwanza unatisha jamii lakini pia ni ugonjwa ambao matibabu yake ni very expensive. Kwa hiyo, tunahitaji kuwekeza kama Taifa kuhakikisha kwamba tunatengeneza mechanism nzuri za kufanya prevention ya ugonjwa ama kutoa elimu, ama kuhamasisha jamii kuachana na baadhi ya vyakula au na vitu vingine ili tuwe na jamii ambayo itakuwa na afya njema iweze kuwa productive kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo suala la afya lisiwe tu suala la kulipigia ngonjera kuja kusema tumewekeza dawa kiasi gani, linahitaji kuwekewa mikakati kuhakikisha kwamba tunapambana madhubuti kabisa na huu ugonjwa wa saratani ambao kwa sasa unatishia kwa kiwango kikubwa sana maisha ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa fursa hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwanza niendelee kumwombea Mbunge Mwenzangu Ndugu yangu Mheshimiwa Kasuku Samsoni Bilago safari yake anayokwenda Mwenyezi Mungu ampokee na amuweke mahali pema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri anisikilize. Mwaka jana nilimpongeza humu ndani ya Bunge kwa kazi aliyoifanya pale Mchinga ya kuamua kumnyang’anya yule mtu ambaye alituibia ardhi yetu zaidi ya hekta 4,000 na kuzirudisha Serikalini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nataka nimwambie kwamba lile jambo kuna Watendaji wa Serikali waliopo ndani ya Mkoa wetu wa Lindi halikuwafurahisha. Huwezi kuamini kwamba mwaka jana mwezi Machi, Mheshimiwa Rais alifika Mchinga akaoneshwa vile Vituo vya Afya viwili ambavyo alijenga yule jamaa pale Mchinga na Ruvu, akatoa agizo kwamba ndani ya mwezi mmoja viwe vimefunguliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka nimwambie Mheshimiwa Waziri mpaka sasa hivi tumepata mfadhili amekubali atatuletea vifaa tiba vyote. Hivi sasa ninavyosema viko baharini vinaelea vitafika mwezi wa Tisa, lakini lile eneo tumezuiwa tusilitumie, tumezuiwa zile Zahanati tusizitumie, tumezuiwa kila kitu pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuna vitu vinaletwa na mfadhili lakini Serikali ya Mkoa na Serikali ya Wilaya tena iliagizwa na Mheshimiwa Rais kwamba walishughulikie jambo lile ili tupate funguo, mpaka sasa hivi yule jamaa funguo amezi-withhold, hataki kuzitoa, Mkoa ule una Mkuu wa Mkoa, una Mkuu wa Wilaya na una watendaji wote wa Serikali lakini wanashindwa namna ya kufungua zile Zahanati

Mheshmiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Waziri nataka nimwambie jambo lile halikuwafurahisha. Tulikwenda kwenye kikao cha RCC, Kiongozi ninayemheshimu sana wa mkoa anasema kwamba kuna utaratibu ambao haukufuatwa vizuri, kwa hiyo jamaa amegoma kutoa funguo. Yeye kama Mkuu wa Mkoa, kama kiongozi wa mkoa anachukua hatua gani kulazimisha ama kuhakikisha kwamba zile funguo tunazipata na yule jamaa lile eno letu anatuachia. Maana inakuwa ni kana kwamba lile eneo bado analo yeye. Kama tunashindwa kuvitumia vitu ambavyo yeye alivijenga na tukamnyang’anya, sasa inaonekana kwamba sisi wenyewe kwenye Mkoa ndio tuna matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri, kama alitoa amri ambayo haikuwa na document, hakufanya documentation, naomba aiandikie Serikali ya Mkoa yale maagizo yake, kwa sababu inaonekana kwamba wao wanaona just business as usual. Sasa namwomba sana Mheshimiwa Waziri alichukulie jambo hilo kwa umuhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusu tatizo la mipaka kati ya vijiji, kati ya halmashauri na halmashauri, kati ya kata na kata. Mheshimiwa Waziri huwezi kuamini kwamba Wilaya ya Lindi ambayo mimi ndiko ninakotokea; sisi tuna migogoro mizito kwanza ndani ya Wilaya kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Manispaa ya Lindi DC. Pia tuna mgogoro wa kati ya Lindi DC na Wilaya ya Ruangwa. Sasa naomba sana Mheshimiwa Waziri jambo hili la migogoro ya mipaka walichukue, walifanyie kazi, waje mpime.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachonishangaza mimi Ruangwa ilikuwa sehemu ya Wilaya ya Lindi, wao wametoka mbavuni kwetu wakachukua eneo lao wakaondoka. Sasa leo na wao wanakuja wanasogea wanachukua baadhi ya maeneo yetu tena ya Lindi DC wanasema ya kwao. Kuna mgogoro mzito, hata pale ambapo mimi napasema kila siku kuna mjusi alichukuliwa leo watu wa Ruangwa wamesogea kabisa na tusipokuwa makini mwakani tutakuja kuambiwa yule mjusi amechukuliwa Ruangwa. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba sana hii migogoro aje atutatulie, aje aseme kwamba mpaka wa Wilaya umepita humu na GN inasoma hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna migogoro ya kwenye kata huko, hiyo ndiyo mingi, lakini kwanza angalau tuanze na hii ya Wilaya. Huwezi kuamini kwamba watu wa Manispaa maeneo ambayo tuliyowapa juzi tu ili wakidhi vigezo kuwa Manispaa leo wanakwenda wanatunyang’anya. Wao wameanzisha mkakati wao wa kuhakikisha watu wanalima korosho wanauza maeneo yao, wanawapa wenye fedha walime mashamba makubwa ya mikorosho. Sasa wamegawa maeneo yamekwisha wanakuja kuchukua na maeneo yetu ya Lindi Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri atume watu wake, waje Lindi, waje watutatulie migogoro iliyopo kati ya Lindi Manispaa, Lindi DC, na watu wa Wilaya ya Ruangwa kwa sehemu ndogo. Naamini hata huu mgogoro wa Ruangwa hata Waziri Mkuu sijiu kama anaufahamu labda kwa sababu yupo bize na mambo mengine ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri aje atatulie hili, kwa sababu tatizo la migogoro ya ardhi Lindi sasa hivi, viongozi tunaowaamini kwamba wanaweza kuwa ma-referee wao ndio part and parcel ya hii migogoro; kwa sababu nao wamejichukilia hayo maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hao watu wa Manispaa watu ambao wamegawa maeneo, hao ambao tunawategemea kwamba wangesimama katikati ndio waliochukua hayo maeneo. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri hili ni tatizo. Sasa ukienda ukawaambia hili eneo la Lindi DC na hili la Manispaa hawakuelewi kwa sababu wao ni wanufaika wa hayo mambo. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri aliangalie kwa umakini sana suala la migogoro ya ardhi kwa sababu linaleta shida.

Mheshimiwa Mweyekiti, jambo la tatu, ni suala la upatikanaji wa hati ya umiliki wa ardhi. Jana nilimsikiliza vizuri sana Mheshimiwa Waziri, akasema kwamba wameongeza upatikanaji wa hati ndani ya miezi sita, sijui miezi mingapi, lakini mchakato huu bado ni mkubwa sana, bado mchakato ni mrefu. Mimi naishi Dar es Salaam, tupo pale kwenye mtaa wetu kule Chamazi, tumefanya application tangu mwaka jana mpaka leo hatujapata hati, tunahangaika na suala la hati na tuko watu wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri akija akisema kwamba tumeongeza na mimi naamini si suala la kwangu; na nilimwona wakati anazunguka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, aliona namna ya watu wanavyomjalia, alikuwa anafanya kazi mpaka saa sita usiku, ni ushahidi kwamba kuna tatizo kubwa kwenye mfumo wa Wizara yake, kuna tatizo kubwa kwa walio chini ya Wizara yake, kwamba wao ndio wanategemewa waipunguze hii migogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ukiona kwamba Mheshimiwa Waziri anakwenda anapokelewa na zaidi ya watu 1000 au 2000 which means walio chini yake hawawajibiki vizuri. Kwa hiyo hili liwe changamoto kwa Mheshimiwa Waziri, lisiwe suala la Kanda ya Ziwa na maeneo
mengine tuu, hata akija Lindi na Mtwara tatizo litakuwa ni hilo hilo, kwamba kunakuwa na ucheleweshaji mkubwa, mtu anaomba hati, basi namna ya kuja kuipata zaidi ya miaka miwili au miaka mitatu hili nalo ni tatizo sana. Kwa hiyo namwomba Mheshimiwa Waziri suala la upatikanaji wa hati za ardhi liwe ni suala ambalo ni haki ya Mtanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, ziko hati zinaitwa Hati za Kimila. Sisi Halmashauri yetu ya Wilaya ya Lindi, kwa kutumia MKURABITA na sisi wenyewe tumeomba baadhi ya maeneo tupatiwe Hati za Kimila. Hata hivyo, hapa tunapomweleza Mheshimiwa Waziri hakuna hata kijiji kimoja ambacho kimeanza kutoa Hati za Kimila.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mahitaji makubwa sana kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara sasa hivi ardhi ikawa inamilikishwa na kwa sababu mbili; kwanza kwa potentiality ya maeneo yale, kugundulika kwa gesi kumeongeza au kume-attract watu wengi kuja kumiliki ardhi kule. Sasa hawa watu leo wasipokuwa na Hati zao, ni rahisi kuja kunyang’anywa, ni rahisi kuja kurubuniwa na watu wenye vijisenti wakachukua maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina ushahidi mkubwa, katika eneo ambalo linakwenda kujengwa mradi wa LNG, pale Likong’o mpaka ukija pale Geza eneo ambalo lipo kwenye jimbo langu; maeneo yale tayari wale watu wamiliki wa asili wote walishaondolewa. Wale wamiliki wa asili wameondolewa na waliopo sasa hivi ukienda ukiangalia majina yao hakuna hata mtu mmoja ambaye ni mwenyeji wa Mchinga, hakuna mtu ambaye ni mwenyeji wa maeneo yale. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri suala la upatikanaji wa Hati za Kimila kwa Lindi na Mtwara liwe priority kwa sababu ya potentiality ya maeneo yale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017 MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru kwa kunipa fursa hii adhimu. Pia niwashukuru wananchi wa Jimbo la Mchinga, Mkoa wa Lindi, kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi kuwa Mbunge wao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kueleza huzuni kubwa niliyonayo kwamba Diwani wa Kata ya Kimwani, Jimbo la Muleba Kusini kupitia Chama cha Wananchi CUF jana ameuawa akiwa nyumbani kwake kwa kukatwakatwa mapanga. Tunashukuru Jeshi la Polisi tayari limekwishamkamata mgombea wa CCM ambaye alishindwa na tunaamini haki itatendeka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatengeneza mipango ya kwenda kutatua changamoto za wananchi, lakini wenzetu mliopo madarakani hamkubali kushindwa. This is very shameful to our country. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati naanza kuchangia mapendekezo haya, niyakumbuke maneno ya Profesa mmoja Mchumi wa Uingereza lakini kwa bahati mbaya anafundisha mpira. Wiki iliyopita timu yake ilicheza na timu nyingine na kwa bahati timu yake ndiyo nilikuwa naishabikia. Baada ya matokeo timu yake ikawa imefungwa, anahojiwa na Waandishi wa Habari anasema, we had good attitude and fantastic spirit despite the result. Anasema attitude ni nzuri, spirit ni fantastic lakini matokeo ni mabovu, wamefungwa. Ndiyo hili ninaloliona siku zote Tanzania tunapanga mipango mizuri, mipango ambayo inapoletwa ndani ya Bunge inapata sifa kubwa kwamba ni mipango mizuri na inatoa dalili ya matumaini kwa Tanzania lakini matokeo siku zote yamekuwa ni mabovu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Tano, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, asije mwisho wa siku akalalamika kama alivyolalamika kocha wangu mimi kwamba good attitude and fantastic spirit despite the result na ili yasimkute haya aangalie anatumia mfumo gani kuwapata Watendaji Serikalini na wasaidizi wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni tumesikia ametumbua majipu kwa Mabalozi. Hatuwezi kustaajabu kuona Mabalozi wetu wanafanya kazi chini ya kiwango, wanachukuliwa makada wa CCM walioangushwa kwenye Ubunge, wananchi wamewakataa, ndiyo wanakwenda kuwa Mabalozi, utatumbua tu. Napenda Mheshimiwa Magufuli asije akashindwa, aangalie mfumo wake wa kuwapata wasaidizi na watendaji wake ili mipango mizuri hii tunayoipanga iweze kuwa na tija kwa Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, natokea Lindi, tuna changamoto kubwa Lindi ya misitu yetu kuvamiwa, sijui niwaite majangili wa misitu au niwaite watu gani. Mkoa wa Lindi ulikuwa ni miongoni mwa mikoa yenye hifadhi kubwa ya misitu, Hifadhi ya Selous iko kule lakini tuna hifadhi kubwa ya misitu ambayo wananchi na Serikali kwa nia nzuri kabisa tuliamua kui-conserve kwa manufaa ya Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sisi Mkoa wetu wa Lindi unapatikana katika hali ya kitropiki ambapo mvua zetu tunategemea misitu na bahari. Waziri wa Muungano anayeshughulikia misitu naomba asikilize hili, kuna uvunaji wa kupita kiwango wa misitu ambao unawahusisha vigogo wa Serikali. Ndiyo maana mimi kama Mbunge na Wabunge wenzangu tumekuwa tukilalamika, tumekuwa tukiwaeleza Wakuu wa Wilaya, tumekuwa tukimueleza Mkurugenzi, kila siku misitu iliyohifadhiwa na Serikali inaisha na ukikamata mbao unakuta zimegongwa, tunapata shida. Hatuwezi kutengeneza mipango ya maendeleo wakati rasilimali na maliasili hii tunaiacha ipotee hivihivi tu. Hawa watu hawalipi kodi na hata wakilipa kodi wanafanya over harvesting (wanavuna zaidi).
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri wa Maliasili ulichukue hilo, very serious. Tuna shida misitu Lindi inaisha, inapotea, mmeleta ng‟ombe wengi wasiokuwa na idadi lakini hiyo ni nafuu, tumeweza kuwa-accommodate, hatuna migogoro ya wafugaji na wakulima, shida yetu kuna majangili wa kukata misitu hovyo. Kuna msitu mkubwa wa hifadhi katika Jimbo la Mchinga, Msitu wa Nkangala unavunwa, Mkurugenzi anajua, Mkuu wa Wilaya anajua, Mkuu wa Mkoa anajua, naomba mchukue tahadhari katika hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la uvuvi, mimi nashangaa kwelikweli. Jimbo la Mchinga ama Mkoa wa Lindi umepakana na Bahari ya Hindi, inafikia wakati samaki wanazeeka na kufa wakaja tu kuokotwa ufukweni hivi, maana yake kwamba ile bahari watu hawajavua na wavuvi hawajawezeshwa. Staajabu yenyewe kubwa iliyopo maeneo yote ambayo bahari imepitia ndiyo kuna watu maskini kwelikweli. Bahari badala ya kuwa ni faraja au kitega uchumi muhimu imegeuka kuwa laana kwani walio karibu na bahari wote ni maskini. This is very shameful.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wenzetu wanatumia bahari tu uchumi wao umekuwa mkubwa sisi watu tuliokuwa karibu na bahari ndiyo maskini. Kwa bahati mbaya mnapopanga hii mipango, pangeni na namna ya kuwasaidia wavuvi, msipowasaidia ndiyo wanatumia zana haramu za uvuvi. Watu wanapiga mabomu, wanatumia makokoro na kadhalika, hatuwasaidii, tunabakia kulalamika tu kwamba achene uvuvi haramu, hawataacha kwa sababau hawana alternative.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri suala hili mlichukue, wakati mnakwenda kutengeneza huo mpango ambao mtau-submit tena, wekeni nguvu kwenye suala la uvuvi. Nilishukuru kweli, kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais, ukurasa wa 23 aliweka msisitizo kwa suala la uvuvi, alisema kwamba viwanda, uvuvi na kilimo ni ajenda yake. Naomba tuone kwa vitendo wakati mtakapo-submit Mpango wa Miaka Mitano au wa mwaka mmoja, tuone mmewekeza nguvu kubwa katika suala la uvuvi. (Makofi)
Mheshimiwa mwenyekiti, suala la viwanda, Mkoa wa Lindi na Mtwara imejaliwa. Imekuwa nyuma kimaisha kwa muda mrefu, uchumi wetu umekuwa wa chini sana lakini Mwenyezi Mungu ametuletea neema ya gesi ambayo ni utajiri na ni umeme pia. Tunashukuru Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo pamoja na REA wamejitahidi vijiji vingi hivi sasa vinapata umeme Lindi na Mtwara. Mie nashukuru Jimboni kwangu zaidi ya 80 % ya vijiji vimepata miradi ya REA. Naomba tu Mheshimiwa Muhongo unimalizie vile vijiji kumi na tano vilivyobakia ili Jimbo zima liwe linawaka umeme. Haitakuwa upendeleo maana umeme unatoka kwetu, gesi ipo kwetu, tukiwa na umeme namna hii ni jambo la kheri na ndiyo wananchi watapunguza kelele ya gesi ibaki na mambo kama hayo. Tumelalamika, watu wakapigwa, tukaelimishwa tukaelewa, bomba limejengwa, sasa hivi tunalilinda, tuwekeeni umeme katika kila kijiji ili tuone sasa kumbe manufaa ya gesi ni haya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala hili liendane na viwanda. Tuna rasilimali nyingi, tuna maliasili nyingi, Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo anajua, kuna madini mengi yako Lindi. Jimbo la Mchinga kuna madini mengi ya kutengeneza cement na vitu vingine ninyi wenyewe mnajua. Wasaidieni wachimbaji wadogowadogo waweze kupata mitaji ili wao waweze kuchimba. Tusiwaachie hao watu wanaanzisha viwanda, yeye ndio ameanzisha kiwanda, yeye ndio awe ana-transport minerals, tusifanye hivyo tutashindwa kutoa fursa kwa wananchi maskini hawa. Naomba nishauri hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ili mipango yetu yote iende vizuri tunahitaji tuwe na amani. Tunahitaji tuwe na amani ya kweli siyo amani inayozungumzwazungumzwa tu. Tunalalamika kuhusu suala la Zanzibar, Bukoba watu wanauana.
MWENYEKITI: Muda wako umekwisha Mheshimiwa.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa nasimama kwa mara ya kwanza katika hotuba ya bajeti, nawashukuru kwa dhati kabisa wananchi wa Jimbo la Mchinga kwa kuniamini, kwa kunichagua kwa kura nyingi sana na hatimaye kuwa Mbunge wao, Mbunge jirani kabisa na Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, itoshe kuwashukuru na kuwapongeza Wabunge wenzangu wote waliozungumzia suala la korosho. Namshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Ghasia, leo naona amepiga hoja nzuri hapa. Namshukuru sana Mheshimiwa Chikota, Mheshimiwa Cecil Mwambe, Mheshimiwa Katani na wengine, wamejenga hoja za kimsingi kuhusu zao la korosho. Kiukweli kabisa, zao la korosho ni miongoni mwa mazao yanayoliingizia Taifa hili fedha nyingi, lakini inaonekana kama tunacheza nalo, bado tunacheza! Inaonekana kama we are not Serious kwenye zao la korosho. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Mwigulu Nchemba awe mtu wa kwanza kuwafuta machozi wakulima wa korosho. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie alipoishia Mheshimiwa Hawa Ghasia kwenye suala la uvuvi na matumizi makubwa ya nguvu za dola katika kupambana na uvuvi haramu wakati uwekezaji tunaowekeza kwenye kuwasaidia wavuvi ni mdogo mno. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na-declare interest kwamba, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimo. Wakati wa Vikao vya Kamati na Mheshimiwa Waziri jana wakati anawasilisha hoja yake alieleza mikakati ya namna wanavyopanga kushirikiana na jeshi kwenda kuzuia uvuvi haramu. Nataka nimkumbushe Mheshimiwa Waziri, mwaka 1997 na 1998 Serikali hii ilitumia jeshi, lakini leo uvuvi haramu bado unaendelea. Tusiangalie tulipoangukia, tuangalie tulipojikwaa! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya jeshi hayatatusaidia, badala yake tunakwenda kuwaumiza wavuvi, wananchi wetu watapigwa, watadhalilishwa na haya yote yana ushahidi wa kutosha. Niwashauri Waheshimiwa, kama mnataka kutumia jeshi, hakikisheni mnaandaa Leseni za Uvuvi za Mbao, kwa sababu zitakuwa haziharibiki, wavuvi wanakwenda baharini wakiwa na leseni zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, najua mwaka 1997/1998, mimi mwenyewe nikiwa mvuvi ilikuwa ukienda baharini unaambiwa onesha leseni yako! Leseni ni karatasi. Mimi nakwenda kuzamia, navua pweza kwa kutumia kioo kuzamia baharini. Nibebe leseni kule chini ya bahari si itaharibika! Kwa hiyo, niwashauri kama mmeweka mkakati wa kutumia jeshi, please andaeni leseni za mbao, hazitaharibika, tutakwenda nazo baharini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mjiandae pia kupokea watu majeruhi wengi kwa sababu najua wavuvi wengi watapigwa, watadhalilishwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, liko suala hapa ameliongea Mheshimiwa Ghasia; suala la wavuvi kukata leseni, nikiwa Lindi Vijijini pale Mchinga nakata leseni; nikitoka, nikienda Kilwa, nakata leseni; katika nchi moja, mkoa mmoja mnatutenganisha! Yaani Lindi Vijijini nikitoka hatua kumi kwenda Kilwa, natakiwa nikate leseni nyingine! This is very shameful! Wavuvi wanapata wapi hii fedha? Msitutenganishe kimikoa na kiwilaya jamani! Nawaomba sana, tunaishi kindugu; kama ni wilaya kwa wilaya mtu anatakiwa akate leseni, tunawaumiza sana wavuvi wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la ufuta. Mheshimiwa Mwigulu nchi yetu wewe unajua ni nchi ya tatu kwa kulima ufuta mwingi duniani. Ni nchi ya kwanza kwa kulima ufuta mwingi Afrika. Unajua! Mkoa wa Lindi ndiyo Mkoa unaolima ufuta mwingi kuliko mikoa yote Tanzania, unajua! Hivi sasa ninavyokwambia, tayari wanunuzi wa ufuta, hao wanaoitwa Choma Choma, wako Lindi wananunua ufuta.
Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa hatujui ni mamlaka gani inayoweza kutangaza bei elekezi ya zao la ufuta. Mpaka hivi sasa tunapoongea, ufuta unanunuliwa kwa sh. 1,300/=, sh. 1,800/=, kwa decision ya mnunuzi. Serikali iko kimya, Mkuu wa Wilaya yupo kule, Mkuu wa Mkoa yupo kule! Naomba Mheshimiwa Waziri, toeni tamko, bei ya ufuta mwaka huu ni shilingi ngapi? Mtuambie! Watu wanauza sh. 1,300/=, sh. 1,800/=, kwa kweli tunawaumiza sana wakulima wa ufuta. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwenye suala la mifugo. Mkoa wa Lindi mmepeleka ng‟ombe wengi, wafugaji wengi; tulitegemea kungekuwa na mpango mzuri kabisa wa kupanga matumizi bora ya ardhi; wakulima wakae wapi, walime wapi na mifugo ifugiwe eneo gani. Nasikitika sana, najua Wizara iliomba shilingi bilioni tatu za kupanga matumizi bora ya ardhi, mmepewa shilingi milioni 25.
Naomba Waheshimiwa Wabunge tuhakikishe Wizara hii inapewa hizi fedha, shilngi bilioni tatu. Shilingi milioni 25 hawawezi kupanga hawa matumizi bora ya ardhi, ku-demarcate maeneo kwa ajili ya wafugaji na wakulima. Otherwise migogoro ya wakulima na wafugaji itaendelea, haitakwisha na tutaendelea kuishuhudia kila siku Kilombero na maeneo mengine. Hata kule Lindi ambako ni wastarabu sana, lakini kuna viashiria vyote kwamba kama hali hii itaendelea na kwenyewe tutaanza kuweka kwenye eneo la kimgogoro!
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, naomba take this issue very serious, hakikisheni mnapata fedha za kutosha mfanye demarcation ya maeneo kati ya wakulima na wafugaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie tu, nasikitika sana na Mheshimiwa Nape hapa hayupo, ni Mbunge mwenzangu kwenye Halmashauri moja kwenye wilaya moja; nasikitika, najenga hoja hapa za wavuvi hawanioni, hawanisikii; najenga hoja hapa za wakulima hawanioni, hawanisikii na Watanzania wanatulalamikia!
Mheshimiwa Naibu Spika, siungi mkono hoja!
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kama kuna kosa kubwa mtalifanya ni kuviweka vyuo vya walimu chini ya NACTE. Kwanza jambo hili litashusha nidhamu za walimu tarajali, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabli wa elimu nchini. Pia jambo hili litafanya sekta hii muhimu ya utoaji wa mafunzo kwa walimu kusimamiwa na watu ambao hawana ujuzi wala uzoefu katika masuala ya mafunzo ya walimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni suala la kudharau mafunzo kwa vitendo kwa walimu tarajali. Kazi ya walimu inadharaulika, wanafunzi walimu mnawapa shilingi 2,000 wanapokwenda BTP, ili wakanunue nini? Sekta ya elimu ni sekta muhimu na lazima Serikali ioneshe seriousness katika kuratibu, kusimamia na kuongoza sekta hii.
Mheshimiwa Waziri, jambo lingine ni Idara ya Ukaguzi. Hivi kwa nini Idara hii haiwezeshwi kipesa iweze kufanya kazi ya kusimamia utoaji wa elimu na kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa. Tafadhali sana wezesheni Idara ya Ukaguzi ili ifanye kazi yake ipasavyo. Jambo hili ni muhimu sana, ahsante
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nianze kwa kusema kwamba binafsi sina mashaka na uwezo, dhamira na nia ya Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii. Ukimtazama usoni unaona kabisa huruma aliyonayo kwa Watanzania, kwa hiyo, sina mashaka kwamba anaweza kuitendea haki huko mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yupo mtunzi mmoja wa vitabu maarufu sana, anaitwa Mudhihir Mohamed Mudhihir, aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo ninaloliongoza mimi sasa, ametunga kitabu kinaitwa Mwele Bin Taaban. Dibaji ya kitabu hiki imeandikwa na Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe. Maudhui yaliyopo ndani ya kitabu hiki ya Mwele Bin Taaban naona kama yanafanana na uhalisia uliopo katika nchi yetu hususan namna bajeti ya Wizara ya Afya mwaka huu ilivyopangiwa fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 9 ya Katiba yetu (i), kinasema kwamba utajiri na rasilimali za nchi hii zitawekezwa kwenye kuhakikisha kwamba zinaondoa matatizo ya umaskini, maradhi na ujinga. Maradhi yanagusa Wizara ya Afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa takwimu zinaonyesha kila mwaka Watanzania tunaongezeka kwa idadi ya watu 1,000,000, Wizara ya Afya badala ya kuongezewa pesa yenyewe ndiyo inapunguziwa. Mwaka huu imepunguziwa shilingi bilioni 18 kutoka kwenye bajeti ya mwaka jana wakati wale watu 1,000,000 wameendelea kuongezeka, matatizo ya afya yameendelea kuongezeka, uwezo wa kuyatatua kwa fedha hizi naamini hakuna. Dada yangu hapa ameongea vizuri na nilikuwa namtazama usoni nikiona kabisa dhamira yake, lakini fedha huna dada! Kwa bajeti hii inaashiria kabisa kwamba you are going to fail, business itakuwa vilevile, business as usual. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitolea mfano Hospitali ya Rufaa ya Mtwara ya Ligula, mwaka jana mlitenga shilingi bilioni mbili, mwaka huu tena mmetenga shilingi bilioni mbili, nikuulize shilingi bilioni mbili za mwaka jana umepeleka shilingi ngapi, aibu! Mwaka huu tena mmetenga shilingi bilioni 2, najua ni ku-copy na ku-paste tu, pesa hizi haziendi. Kama mwaka jana mlitenga na hamkupeleka, mwaka huu hiyohiyo tu, hamtapeleka fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Mkoa ya Sokoine - Lindi, aibu! Hospitali ile haina chumba wala sehemu ya watu waliowasindikiza wagonjwa kuweza kupumzika. Kwa hiyo, kuna mtu anapeleka mgonjwa wake akifika pale akikaa yeye mwenyewe kesho anageuka kuwa mgonjwa kwa sababu ataugua malaria, atang‟atwa na mbu usiku kwa hiyo badala ya kusindikiza mgonjwa na mwenyewe anakuwa mgojwa, otherwise asimame usiku mzima. Hakuna sehemu ya kupumzika watu wanaopeleka wagonjwa Hospitali ya Mkoa ya Sokoine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nigusie suala la Kituo cha Afya Kitomanga kilichopo kwenye Jimbo la Mchinga. Ndiyo maana nasema this government is it serious? Pale Kitomanga kuna kituo cha afya, kwenye Jimbo langu la Mchinga, mmepeleka vifaa tiba kama X-ray, mashine za CT-Scan, mmepeleka vifaa vingi na kile kituo cha afya lengo lake ilikuwa mkifanye Hospitali ya Wilaya, huu ni mwaka wa nne, vifaa vile vinaharibika, vinaliwa na panya, ni aibu! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi wa tatu mwaka huu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya alitembelea pale badala ya kutoa majibu kwamba ni lini kituo hiki kitapandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya amekwenda kufanya issue kuwa too much complicated watu wamekata tamaa. Ameongea na wananchi pale anawaambia kwa namna taratibu na sheria zilivyo, kituo hiki kuja kuwa hospitali itatuchukua muda mrefu, vifaa vile mlipeleka ili iweje? Pia katika maeneo yale watu hawana hospitali ya karibu kwa hiyo wanaendelea kuteseka. Namuomba Mheshimiwa Waziri wakati anakuja kuhitimisha hoja yake hapa aje anipe majibu ni lini mtakipandisha Kituo cha Afya Kitomanga kuwa Hospitali ya Wilaya? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nigusie suala la wazee. Nimemsikia Mheshimiwa Waziri anasema kwamba Serikali ina mpango wa kuleta Bill of Right hapa ili Sheria ya Wazee iweze kupitishwa. Sera ya Wazee imepitishwa mwaka 2003 mpaka leo haina sheria. Kinachokuja kutokea Maafisa wa Maendeleo wa Jamii kwenye Wilaya huko kazi wanayoijua wao ni ku-deal na wanawake na vijana tu kundi la wazee limesahaulika, hii ndiyo reality.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata haya mambo yanayozungumzwa kwamba kutakuwa na fedha shilingi milioni 50 za Magufuli za kila kijiji, Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wanahamasisha vijana, wanahamasisha wanawake waanzishe vikundi vya ujasiriamali wawapatie fedha, wazee wanaachwa. Ni kwa sababu hawana sheria, kungekuwa na sheria haya yasingetokea. Ukiangalia sera ya wazee ni sera nzuri, yenye lengo zuri la kuwatetea wazee, unfortunately kwa sababu hakuna sheria basi ndiyo hivyo mambo yanakwenda tu, business as usual, wazee wetu wanataabika. Lililo baya sisi wote ni wazee watarajiwa ikiwa tutafika, kwa hiyo, lazima tuhakikishe tunatengeneza mazingira na sisi miaka 20 mbele ikija tukiwa wazee mambo haya yawe vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kidogo suala la Mfuko wa CHF (Mfuko wa Afya ya Jamii). Mimi jimboni kwangu ndani ya Halmashauri yetu na Mheshimiwa Nape tuko Halmashauri moja, sisi tumekubaliana kwamba tutahamasisha wananchi wetu wote wajiunge na mkakati ilikuwa wakati huu wa msimu wa ufuta wananchi wote wakate kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii. Unfortunately tumesitisha na nimewaambia wananchi wangu wasijiunge kwa sababu wanaibiwa bure tu. Mtu anakata kadi kwenye zahanati ya Kilolambwani akienda Mvuleni, kilometa tatu tu anaambiwa hutambuliki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia dawa, Halmashauri wanatumia fedha za Mfuko wa Afya ya Jamii kwenye matumizi yao. Kwa hiyo, mtu amekata kadi anakwenda hospitali hana dawa. Wanasema Mheshimiwa sasa hii haja ya kukata kadi inatokea wapi, bora twende tulipe shilingi 5,000. Kwa hiyo, kama kuna hoja ambayo Mheshimiwa Waziri anatakiwa ai-address ni hii issue ya Mfuko wa Afya ya Jamii. Wananchi wameitikia sana, mimi nimewasimamisha jimboni kwangu nimewaambia never, mpaka mimi niseme, msijiunge kwa sababu mnaibiwa na mnaibiwa kwa sababu mtu anakata hapa, kilometa tatu anaambiwa hutambuliki lakini pia dawa hakuna, kwa hiyo, anafanana na mtu ambaye hana kadi hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie suala moja kwa haraka haraka sana linalohusu pia mambo ya wazee. Sera ya Wazee inasema wazi kwamba wazee na watoto watatibiwa bure, lakini kwa masikitiko makubwa sana, mwezi wa 12 nilipoteza wazee zaidi ya watatu kutoka Jimboni kwangu pale Sokoine. Wazee wale walifariki kwa sababu tu ya kukosa matibabu ya operesheni ya mshipa ngiri eti hawana fedha. Iliniuma sana na inaendelea kuniuma, kama sera inaweka wazi kwamba wazee wanatibiwa bure kwa nini mzee anakwenda hospitali hapati matibabu kwa kigezo tu kwamba hana fedha? Tuwe na huruma na wazee wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nianze kwa kumwombea msanii Kinyambe ambaye masaa machache yaliyopita ameingia kaburini. Mwenyezi Mungu amrehemu, ampeleke peponi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisikitishwa wakati Mheshimiwa Waziri anawasilisha hapa, nilidhani angeweza kumtaja msanii huyu. Ni miongoni mwa wasanii maarufu kwa vicheko waliokuwa wanakonga nyoyo za Watanzania, lakini kwa masikitiko Mheshimiwa Waziri amemsahau. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kuipongeza sana tena sana timu yangu niipendayo Dar es Salaam Young African kwa kutangazwa kuwa mabigwa wa kihistoria wa mpira wa miguu wa Tanzania kwa mara ya 26. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwombe Mheshimiwa Waziri, najua fedha hakuna, najua bajeti yake fedha hamna, Mheshimiwa leo hapa sigongi, leo nakushauri tu brother, tunatoka Halmashauri moja. Mimi na wewe ni Wabunge wa Halmashauri moja. Mheshimiwa Waziri angalau kesho tu, Yanga watakuwa wanakabidhiwa kombe lao, TBC iwe live Watanzania waone. Angalau kesho tu, yes! Yanga watakuwa wanacheza pale Dar es Salaam na Ndanda, baadaye siku inayofuatia wataruka ndege kwenda Angola kuliwakilisha Taifa hili kwenye mashindano ya Kimataifa kwa kuwa wao ni wa Kimataifa. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana juzi yalipokuwa yanaulizwa maswali hapa kuhusu bei ya ndege hapa jana, mimi nilikuwa naumia sana kwa sababu timu yangu ya Yanga inaumia sana. Ndani ya nchi inasafiri kwa ndege, nje ya nchi kwa ndege, sasa bei za ndege mkishusha zitatupa ahueni watu wa Yanga. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maneno hayo machache ya utangulizi, nataka nimshauri Mheshimiwa Waziri juu ya mambo machache yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri mwaka 1992 mwandishi mashuhuri wa vitabu, Mohamed Said Abdulla, ni Mtanzania mwenye asili ya Zanzibar aliandika kitabu kimoja kinaitwa duniani kuna watu. Angalau nisome tu aya moja ya ukurasa wa kwanza wa kitabu chake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitabu kinaanza; “Ilikuwa kiasi cha saa moja unusu usiku, Kassim alipanda ngazi pana zilizotandikwa zulia au blanketi nene zinazoongoza kufikia ghorofa akaayo baba yake Hakimu Marijani.”
Mheshimiwa Nape, wewe ni sawa na Kassim. Tumekutandikia zulia upande uende kwa Mheshimiwa Magufuli, Baba Marijani ukamweleze shida zetu. Shida ya Watanzania, wanataka kuwaona Wabunge wao wakijenga hoja, wakiwasilisha hoja zao, nenda kamweleze Baba Marijani. Umri wako ni kijana sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Abdulla anaendelea, anawataja watu maarufu, watu wanaopata umaarufu, kuna wengine wanapata umaarufu kwa kupongezwa, wengine wanapata umaarufu kwa kuzomewa, wengine wanapata umaarufu kwa watu tu kuwachukiza, brother hili jambo limewachukiza sana Watanzania. Miongoni mwa watu wanaochukiwa, mimi inaniuma, wewe ni kaka yangu, Wabunge wawili wa Halmashuri ya Wilaya ya Lindi, tunakaa kiti hiki na hiki, nikiona unaandikwa vibaya brother inaniuma. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili nenda kamwambie baba, pita kwenye zulia kamwambie Marijani, Watanzania wanataka kuona Bunge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naombe tena nimshauri brother, miaka ya nyuma aliyekuwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kipenzi chetu, Mzee wetu Mwinyi, aliwahi kuita timu ya Taifa sawa na kichwa cha mwendawazimu. Mheshimiwa Waziri naomba, Mzee Mwinyi bado yuko hai, twende tukampigie magoti, ile kauli aitengue. Ile kauli Mzee wetu ajirudi, inawezekana ikawa ndiyo sababu ya timu yetu ya Taifa haifanyi vizuri. Kwa nini timu yetu kila ikijaribu inapigwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nadhani siyo tu ile kauli ya Mheshimiwa Rais, pamoja na kwamba ilikuwa inatupa changamoto, leo mmeelezwa hapa, tumebakiwa na mechi mbili za timu ya Taifa, Mheshimiwa Waziri ulipokuwa unasoma hapa, nilifikiri angalau utaitaja timu ya Taifa. Tukiwafunga Misri brother, tuna-qualify. Tukiwafunga Misri tukienda Nigeria kule, tukienda kutoa sare, tuna-qualify.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mkakati gani wa kuisaidia timu ya Taifa? Vijana wetu wanapenda sana mpira. Na wewe mwenyewe Mheshimiwa Waziri nakupongeza, kila nikienda pale Taifa tunakutana, Chamazi pale tunakutana. Nakupongeza sana, unajaribu sana kwenda uwanjani. Hivi huoni kwamba Watanzania wanapenda sana soka? Kama wanapenda soka hivi jiulize kwa mapenzi yale waliyonayo, timu ikifungwa inakuwaje? Wanaumia sana.
Mheshimiwa Waziri katika hili nakuomba sana, isaidieni timu ya Taifa ivuke hapa, tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nigusie masafa ya TBC. Kama bahati mbaya vile, Lindi inapatikana hii redio ya TBC. Maana ni bahati mbaya, lakini mmezima mitambo ya analog. Lindi leo tupo kwenye digital, hiyo Star Media Lindi haipatikani. Kama sijui unajua ama hujui! Na wewe ni Mbunge kutoka Lindi. King‟amuzi cha Startimes Lindi hakifanyi kazi; ni ving‟amuzi vya Azam na Zuku ndiyo vinafanya kazi. Hawa watu wote wana uwezo wa kulipia?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini msipeleke hiyo Star Media angalau mtu akiwa na kantena kake na kadhalika, analipia shilingi 5,000 mambo yanakwenda? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ni masikitiko makubwa. Mkoa kama wa Lindi ni wa siku nyingi, una mitambo ya TBC pale ipo, lakini hawapati, Star Media haipatikani Lindi, watu wanaangalia Azam na Zuku tu. Watu wale wa vijijini kule Jimboni kwangu Mchinga huyu bwana ananikumbusha hapa, Liwale ndiyo kabisa. Lindi yote brother.Wewe wa Liwale kule ndiyo pole yako kabisa. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie suala la wasanii. Brother watu wanakusema sana kuwa unampenda sana Diamond. Aah, mimi si nakueleza! Nilikwambia leo nakushauri tu brother. Wasanii wetu ni kweli wana changamoto nyingi, lakini pia kuna haja ya kuangalia maadili ya kazi zao kabla hazijatoka. Leo tunakuja kuzuia chura, tayari ameshaingia mtaani. Chura yupo mtaani anarukaruka kwenye maji, anazuiwa chura, mimi nina kijana wangu pale ana miaka mitano, ukifika tu anakwambia baba chura anarukaruka. Tayari wameshamwona chura.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tengenezeni mechanism ya kuhakikisha kwamba hizi kazi za wasanii haziingii mtaani bila kupitia kwenu. Leo mpaka jamii imeanza kulalamika ndio chura kaanza kuzuiwa. Sasa ndugu yangu, kuna akina chura wengi, maadili yetu yanamomonyoka na jamii inaharibika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna suala la ngoma za asili, sijui mnalipa kipaumbele kwa namna gani? Sisi kwetu kule kuna Sindimba. Muda siyo mrefu tutaanza kuagiza watu waje kucheza kule, maana vijana wale wadogo wadogo hawajui kabisa. Ngoma zile za asili, jadi zile mmezisahau kabisa. Nikiangalia bajeti hii uliyopewa brother, huwezi ku-function. Naona dhamira yako ya kutaka kusaidia, wewe ni kijana, una dhamira nzuri, lakini shida yangu ni bajeti. Pita kwenye zulia alilolisema Mohamed Abdulla, ukamshauri Rais akuongezee bajeti hii. Hali ni mbaya Mheshimiwa. Hayo tu leo brother!
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nianze kwa kutoa ushauri wangu kwa Mheshimiwa Waziri wa Nishati. Kwanza nimpongeze kwa jambo moja anaingia kwenye historia Profesa Muhongo ya kutenga bajeti ya maendeleo ya asilimia 94. Wenzake na Wizara zao tulizozipitisha hapa tumeona Wizara zingine maendeleo asilimia 50, wengine asilimia 40, wengine asilimia 60; yeye ametenga asilimia 94, dhamira ya kuiwasha Tanzania kwa umeme inaonekana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tena nimshauri Mheshimiwa Muhongo kama Mbunge ninayetokea Mkoa wa Lindi, kuna suala hapa Wabunge wa Mkoa wa Lindi hawajalielewa vizuri na mimi nimwombe kama kuna uwezekano afanye kikao na Wabunge wa Mkoa wa Lindi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna huu mradi mwema sana, mradi wa LNG ambao unakwenda kufanyika pale Likong‟o kilometa tatu tu kutoka kwenye Jimbo langu. Wabunge hawajauelewa vizuri na ndiyo maana unaona alipokuwa anachangia hapa Mbunge wa Lindi Mjini alikuwa anasema kiwanda hakijengwi wakati LNG siyo issue ya kiwanda, LNG inakwenda kuchochea viwanda. Sasa nilichokiona hapa kuna tatizo la uelewa kwamba huu uelewa wa Wabunge kwanza ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi, fanya kikao na sisi utueleweshe vizuri kabisa. Hii complication unayoiona kwetu Wabunge kwa wananchi huko ndiyo hawaelewi kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kila siku napigiwa simu naambiwa Mheshimiwa Mbunge tunaelezwa kwamba sasa Jimbo letu la Mchinga linahamishwa linapelekwa Lindi Mjini. Suala la mradi LNG nawaambia hicho kitu hakipo mbona mimi sijui, sasa mkilihamisha Jimbo la Mchinga kupeleka Lindi Mjini maana yake mimi Mbunge ndiyo basi! Kwa hiyo, hili ni jambo ambalo huko chini halieleweki. Sasa naona shida kama na Wabunge na sisi hatulielewi vizuri, naomba Mheshimiwa Waziri atenge muda tu hata nusu saa akutane na Wabunge wa Mkoa wa Lindi, ateleweshe vizuri tuweze kulifahamu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nichangie kuhusu suala la usambazaji wa gesi kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara, dhamira njema naiona kwa Mheshimiwa Waziri. Mradi wa usambazaji wa gesi kwa ajili ya matumizi ya majumbani na kwenye vipuri, nimeona wameelezea Miji mitatu ya Kilwa, Lindi Mjini na Mtwara. Mradi ule unagharimu karibu dola milioni kumi karibu shilingi bilioni 22 lakini kwa mwaka huu wametenga shilingi milioni 700, nataka tu kujua kutoka kwa Mheshimiwa Waziri hizi milioni 700 walizozitenga mwaka huu za nini? Kwenda kufanya impact assessment au kufanya evaluation maana hizo ndiyo terminologies tulizozizoea, hizi milioni 700 ni za nini?
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kujibu hapa aniambie, huu mradi wameuandika vizuri kabisa hapa na kwa takwimu kama mwenzangu alivyotangulia kusema Profesa yupo vizuri sana kwenye takwimu, kwa hiyo, ameainisha vizuri kwamba mradi utagharimu shilingi bilioni 22, lakini mwaka huu wametenga milioni 700 za nini hizi milioni 700? Kwa hiyo, naomba majibu katika hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimboni kwangu kumebakia vijiji 15 kupata umeme; umeme wa REA phase I na phase II umebakisha vijiji 15, kwa Lindi na Mtwara kubaki na vijiji 15 siyo privilege kwa sababu tuna umeme mwingi unapotea tu, bado ni suala la usambazaji tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, karibu megawatt 30 Waziri unajua zinapotea kila siku kwamba hazitumiki, sasa namwomba Mheshimiwa Waziri mradi wa REA phase III animalizie vijiji vilivyobakia katika Jimbo la Mchinga vyote vipate umeme kwa sababu ametengeneza fitna kubwa kuonekana vijiji vingine vina umeme na vijiji vingine havina umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sana Mheshimiwa Waziri Kijiji cha Dimba, Ruvu, Namtamba, Mputwa, Kiwawa, Luchemi, Luhoma, Micheye, Mihandara, Lihimilo na Mkongo, vijiji hivi naomba sana vipatiwe umeme. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto nyingine iliyopo Mheshimiwa Waziri hivi sasa ninapoongea kuna vijiji vimepata mradi wa REA phase II. Jambo la ajabu ni kwamba unakuta nguzo zilizopo pale kijijini ni nguzo tatu nne; kijiji kikubwa ambacho vijiji vingine ni Makao Makuu ya Kata, Makao Makuu ya Tarafa, unakuta wanapewa nguzo tatu au nne ndiyo za usambazaji! Kuna shida kubwa sana, unakuta kijiji kizima chenye wakazi karibu 3,000 au 4000 wanapewa nguzo tatu nne, nani atapata umeme? Kwa hiyo, jambo hilo linaleta changamoto kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tatizo kubwa pale Kitomanga, tatizo kubwa Lutamba, Milola, Mvuleni kuna tatizo kubwa, wamepeleka umeme sawa upo lakini wananchi wanautazama tu, kwa sababu kuna nguzo tatu tu ambazo zimepelekwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo ni kwamba hivi sasa ninapoongea nina wananchi kule karibu 200 wamekamilisha taratibu zote za kuingiziwa umeme mpaka sasa huu karibu mwezi wa tatu umeme hawajapata. Nimewahi kuuliza changamoto ni nini? Nguzo ipo karibu wamelipia wamemaliza, wamefanya wiring, kuna shida kubwa watu karibu 200 Mvuleni, Lutamba, Milola, Mchinga, Maloo na Kilolambwani watu wamelipia wanasubiri umeme, umeme hawapati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri atueleze tatizo ni nini, mita zimekwisha au LUKU hizo ndiyo shida, tatizo ni nini? Watu wamelipia na wamekamilisha taratibu zote lakini umeme hawapati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalo kwa kweli limenipa shida sana ni kuhusu Mchinga. Mchinga ambapo ndiyo Makao Makuu ya Jimbo pale palipata umeme kabla ya hizi program za REA, ndiyo kilikuwa Kijiji pekee, Mchinga na Vijji viwili. Vijiji pekee vya pale katika Jimbo zima vilikuwa na umeme kabla ya kuingia program ya REA, ilipokuja kwenye program ya REA Mchinga haikuwa included. Kilichokuja kutokea ni kwamba ule umeme ambao ulikuwa nguzo tatu, nne pale za awali REA ilikwenda imeiacha kabisa Mchinga hivyo watu wa Mchinga leo hawanufaiki na REA na badala yake kuna madai makubwa ya watu kupatiwa umeme na Mchinga ni sehemu kubwa ina vivutio vingi vya uwekezaji lakini shida ni kwamba umeme hakuna. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie na suala la madini ya gypsum, naomba tu Mheshimiwa Waziri anisikilize, Mheshimiwa Waziri hapo anayemsemesha Waziri kidogo namwomba dakika moja tu Waziri anisikilize. (Makofi/ Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba kuna suala la gypsum, Jimbo la Mchinga ni miongoni mwa Majimbo au maeneo ambayo yana gypsum quality. Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri aliniunganisha na watendaji wake, nilimletea sample ikapimwa ikaonekana the best gypsum inatoka pale Mchinga, ipo na majibu yapo pale Wizarani kwamba ile gypsum ambayo nimeipeleka one among the best gypsum in Tanzania, ipo pale. Shida iliyokuwepo ni kwamba hivi sasa ninavyoongea kuna maeneo ya vitalu ambavyo tayari vimeshasajiliwa watu zaidi ya 200 wamesajili mimi siwajui, wananchi wenyewe hawawajui. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mkurugenzi wa Madini wa Kanda ya Kusini Ndugu Mtwampaka, kwa sababu niliunganishwa naye, aliniletea orodha ya watu ambao wana certificates karibu 200 za kumili ile migodi. Nilipokwenda kuwahoji wanakijiji hakuna hata mgodi mmoja ambao wananchi wanajua. Hawa watu wenyewe hawajulikani, wako kwenye maandishi tu. Nataka kujua Mheshimiwa Waziri, kuna taratibu gani zinafuatwa ili mtu kupata certificate ya kumiliki eneo la uchimbaji wa madini ama hii migodi ya gypsum.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna shida kubwa Mchinga, nikwambie Mheshimiwa Waziri, kama hili litaendelea hawa waliochukua certificates wajue tu kwa Mchinga ni nullified, yaani mimi nikiongea kule kazi imekwisha. Kwa hiyo, kama wataendelea kujificha, Mbunge siwajui, Mkurugenzi wa Halmashauri hawajui, wananchi hawawajui, wajue hizo certificates zao ni za mfukoni, hazita-function Mchinga. Nahitaji watu wote ambao wana certificates za kumiliki maeneo ya uchimbaji waje tuwaone, wasijifiche, waje tuwaone.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna shida ya watu kutoka TPDC, hili nilishakueleza Mheshimiwa Waziri, wanakwenda Mchinga kuchukua maeneo, wanakwenda ku-lease wanakatia hati za ardhi kwa sababu tu Mchinga kunaonekana kuna potentiality ya gesi na gypsum. Hili namhakikishia Mheshimiwa Waziri hakuna mtu kutoka TPDC atakayepata eneo Mchinga, ninayeongea ndiye Mbunge wa Jimbo la Mchinga, ndiyo mwisho, ndiyo final say pale. Hakuna mtu ambaye atakwenda kuwadhulumu watu wa Mchinga.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutatua kero na changamoto nyingi zilizopo katika Sekta ya Nishati na Madini nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizo namwomba Mheshimiwa Waziri au nimkumbushe ahadi yake ya kuvipatia umeme vijiji vifuatavyo vilivyopo katika Jimbo la Mchinga ambavyo ni:-
Vijiji vya Dimba, Ruvu, Namtamba, Ruchemi, Michee, Kiware, Mputwa, Lihimilo, Namkongo Matapwa na Mnyangara. Mheshimiwa Waziri vijiji hivi ni miongoni mwa vijiji vilivyopo Jimboni ambavyo havijapata umeme kupitia mradi wa umeme vijijini REA. Nakumbuka hoja hii kwakuwa tayari tulishawahi kuzungumza na Mheshimiwa Waziri kuhusu suala hili la umeme mara kadhaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ni kuhusu suala la madini, Mheshimiwa Waziri kwanza nimpongeze kwa juhudi zake mahsusi za kunisaidia juu ya suala la wanakijiji wenyewe kuunda vikundi ili waombe hati za wachimbaji wa madini gypsum na kupeleka sokoni kama vile katika kiwanda cha cement Dangote. Mheshimiwa Waziri pamoja na msaada wake huo kwangu bado kuna haja ya Wizara yake kufanya juhudi za maksudi kuhakikisha kuwa maeneo yote yaliyopo Jimboni yanayohusishwa na upatikanaji wa gesi, mafuta na madini yamepimwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na uvamizi mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali kuja kurubuni wapiga kura wangu kwa kununua maeneo yenye madini kwa kiasi kidogo cha fedha. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri Wizara yake ifanye mkakati maalum na kukutana na wananchi wa Jimbo hili ili kuhakikisha kuwa maeneo yote yanayotiliwa mashaka kuwa yamo madini yapimwe ili kuwaokoa wananchi kutokana na kasi kubwa ya watu kutoka mbali kuja kuchukua maeneo haya kwa kuwapa fedha kidogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia TANESCO ihakikishe zoezi la upatikanaji wa mita za LUKU na kuunganishiwa kwa umeme kwa wananchi ambao wapo vijijini, wameshakidhi vigezo vya kupatiwa umeme. Jimboni kwangu kuna kaya zaidi ya 200 ambazo zimekamilisha taratibu zote za kuingiza umeme lakini kumekuwa na delay kubwa kwa TANESCO Lindi kuwaingizia umeme wananchi hawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza, niombe tu Mheshimiwa Waziri anisikilize kwa makini kwenye suala hili ambalo nataka nilizungumze sasa hivi. Niunge mkono hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwenye kipengele cha mabaki ya mjusi ambayo yapo Ujerumani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna tatizo hapa, kuna mabaki ya mjusi ambayo yalichukuliwa katika eneo la Tendenguru, Jimbo la Mchinga ambako mimi ndiyo Mbunge wao, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kupelekwa Ujerumani. Dinosaur huyu ndiyo mjusi mkubwa kuwahi kuishi katika dunia hii tuliyonayo, anatengeneza historia kubwa kwa nchi yetu. Mungu hakufanya makosa mjusi huyu kupatikana katika ardhi ya Tanzania, unfortunately alichukuliwa akapelekwa Ujerumani. Hivi sasa ninavyowaambia mabaki yake yapo pale Ujerumani, watalii maelfu kwa maelfu wanakwenda kuangalia pale Serikali ya Ujerumani inapata pesa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi kifupi nilichokuwa Mbunge wa Jimbo la Mchinga nimekwenda Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambako nilielekezwa kwamba wao ndiyo wanalishughulikia suala hilo. Mheshimiwa Waziri jioni nitamletea barua niliyojibiwa na Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, majibu yake yanasikitisha Mheshimiwa Waziri. Hapa kwa sababu Mnadhimu alikuwa amesema kwamba nichangie jioni ningekuwa nayo hapa lakini jioni nitaileta. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mazingira ya kusikitisha na ambayo sikutarajia Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ananijibu kwamba mpaka sasa Serikali inafanya calculation kujua huyu mjusi anaingiza kiasi gani kwa mwaka, this is very shameful. Mwaka 1907 alipochukuliwa, Tanzania imepata uhuru mwaka 1961 mpaka hivi sasa hatujui mjusi huyu anaingiza kiasi gani Ujerumani, this is very shameful. Ananijibu kwamba Wizara inaendelea kuhakikisha inafanya calculation kujua kwa mwaka inapata shilingi ngapi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mazingira mengine ya kusikitisha wiki mbili mbele wananitumia tena barua nyingine ya majibu wakijibu barua yangu hiyo moja, imepata barua mbili za majibu kwamba sasa Serikali ya Tanzania imeshirikiana na Serikali ya Ujerumani kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo ndiyo Wizara hii kwamba waanzishe ushirikiano na mahusiano ya utunzaji wa mambo ya kale. Hii ina maana kwamba mahusiano yatatengenezwa kati ya Ujerumani na Tanzania ili kuhakikisha kwamba Tanzania inanufaika kutokana na mjusi yule. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili la aibu. Alikuwepo Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mheshimiwa Mudhihir Mohamed Mudhihir, alizungumza sana juu ya suala la mjusi mpaka amemaliza kipindi chake hakuna majibu. Haya mama Fatma Mikidadi akapewa jina kabisa kwamba mama mjusi, Mbunge wa Viti Maalum amezungumza mpaka mkambatiza jina la mama mjusi, chwee majibu hakuna. Bi. Riziki Lulida miaka kumi huu sasa mwaka wa 11 anazungumzia suala hilo la mjusi majibu hakuna. Mimi Mbunge wa Jimbo la Mchinga leo nazungumza suala la mjusi na nitatoka hivi miaka mitano chwee majibu hakuna. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie Mheshimiwa Waziri jambo moja, kama kuna suala ambalo lilinipa Ubunge na mkimuuliza Mbunge niliyemtoa Mtanda atawaambia wananchi hawataki kusikia juu ya suala lolote kuhusu mjusi, wananchi wa Jimbo la Mchinga hawaitaki CCM kwa sababu ya suala la mjusi, nawaambia kabisa. Mheshimiwa Magufuli Rais wetu wakati yupo kwenye kampeni alivyofika Mchinga aliwekewa mabango bring back our dinosaur.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Magufuli kwenye mkutano pale Nangalu, waliokuwa wanatembea na mgombea wa Urais watawaambia, Mheshimiwa Nape angekuwepo angesema hapa, alisema pale Nangalu kwamba najua tunapoteza fedha za mjusi huyu hatutaweza kumrejesha lakini nitahakikisha kwamba fedha za mjusi zinarudi katika Serikali ya Tanzania na kuletwa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kuja kutatua kero ndogondogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa mgombea wa Urais ambaye sasa ndiye Rais kwa hii ahadi yake aliyowaahidi wana Mchinga wanaisemaje? Ahadi aliyowaahidi Watanzania kwamba pesa za mjusi zitapatikana inakuwaje? Inakuwaje sisi Tanzania hatuthamini mali zetu kwa nini? Kwani Mungu mwenyewe alivyoamua huyu mjusi apatikane Tanzania unadhani alifanya makosa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Waziri atakapokuja kufanya majumuisho ya hoja suala la mjusi alizungumzie. Namwambia kabisa Waziri asipozungumza juu ya suala hili nakamata mshahara wake, tunahitaji majibu ya kutosha juu ya masuala ya mjusi. Kwanza atakuwa anatunasua sisi kutokana na aibu, wenzetu watu wa Kenya wakitangaza Mlima Kilimanjaro, mnalalamika leo watu wa Kenya wala hawasemi kwamba mjusi anatoka kwao wamekubali kwamba mjusi anatoka Tanzania, anatoka huko huko kwetu lakini wao kuchukua kwamba huyu ni wa kwetu hawataki, tatizo nini? Kama kuna mtu anapata maslahi ndiyo anatukwamisha wamtaje kwamba labda kuna mtu anapata maslahi juu ya hili ili watu tujue. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusu suala la ndovu kuvamia kwenye Jimbo langu la Mchinga. Kwanza Mheshimiwa Waziri nimpongeze sana mzee wangu ametusaidia vya kutosha, Serikali yake imehakikisha kwamba kila ndovu wanapovamia mashamba ya wakulima wangu wanakuja kuwafukuza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Jimbo la Mchinga wastaarabu sana, ndovu wanatembea kwenye vijiji vyangu vile yaani kama mbuzi tu na wanakotoka mbali. Kutoka Selou kuja Mchinga ni zaidi ya kilometa 180, wanakuja wanakaa kule siku 20 - 30 lakini hakuna tembo amepigwa au hawaendi, wale wananchi wakichukua hasira baadaye wakaamua kuwapiga watawalaumu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri amenisaidia sana kila walipokuwa wanakuja alikuwa anapeleka askari kwa hili namshukuru na kumpongeza lakini isiishie pale. Yale mashamba ekari 183 za wananchi wale ambazo wamelima kipindi chote cha miezi sita (6), akinamama maskini wale, watu maskini wale, mtu amelima shamba lake la mihogo lote limeliwa na tembo, leo wanakuja kuniuliza Mheshimiwa Mbunge unatusaidiaje? Siyo mimi ni ninyi Serikali mnawasaidiaje wananchi wa Jimbo la Mchinga kutokana na chakula chao kuliwa? Naomba ifanyike tathmini haraka ili wananchi wa Jimbo la Mchinga walipwe fidia kutokana na mazao yaliyoliwa na tembo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema Mnadhimu kwamba ilikuwa nichangie jioni, lakini nakushukuru hayo ndiyo maamuzi ya Kiti. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Waziri naomba anisikilize kwa makini ili nimshauri, ingawa tuko wachache huku lakini tuna ushauri mzuri kweli, huko usione wingi huo, hakuna kitu watakachokushauri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwenye hiki kitabu cha Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 112 ameelezea malengo ya Wizara yake. Kwenye lengo namba tatu, anasema kuendelea kusimamia, kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa mikataba, naishia hapo hapo kwa sababu nina dakika tano. Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana na wamesaini mikataba kwamba kila nchi itakuwa na Wizara maalumu inayoshughulikia Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kenya wana Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki na wana Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje; Uganda hali kadhalika; Rwanda hali kadhalika na sisi Rais Kikwete alikuwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Waziri wa Afrika Mashariki. Ndiyo, Mheshimiwa Mwakyembe anasikitika nini, alikuwa Waziri wa Afrika Mashariki. Mwanasheria Mkuu wa Serikali hajui kama kuna mkataba wa Afrika Mashariki kwamba lazima kuwe na Waziri Maalum anayehusika na mambo ya Afrika Mashariki au huyu Mwanasheria anamshauri nini Rais sasa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, naomba nilirejeshe kwa sababu Mheshimiwa Waziri ndiye anayehusika, suala la mabaki ya mjusi wa Tendegulu yaliyopo Ujerumani. Aibu! Watu wa Ethiopia walikuwa na mnara wao ulikaa Italia miaka 68, wameurejesha. Leo tuna mabaki ya mjusi yamechukuliwa Tanzania ninyi mnakaa hapa kuja kusifia tu, tani 70, sijui alikuwa na urefu wa mita 60, Tanzania tunanufaika na nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeandika barua nimewaletea kwenye Wizara hii, Makatibu Wakuu walichonijibu sikielewi, mara mpaka leo wanafanya calculation, hawajui Tanzania inanufaika na nini. Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kujibu hapa aje atuambie Tanzania inanufaika na nini na mabaki ya mjusi wa Tendegulu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani mjusi huyu mkubwa anaijengea historia Ujerumani, yuko pale Hamburg, watalii wanakwenda kuangalia wanaingiza pesa Ujerumani, leo alikotoka mjusi maji ya kunywa hawana, barabara hakuna, Wazungu wanakwenda pale Tendegulu tunawabeba mgongoni. Mheshimiwa naomba majibu na niliwaambia wananchi wangu na Mheshimiwa Magufuli alisema wakati wa kampeni alipokuwa Jimbo la Mchinga kwamba atashughulikia suala hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiona Waziri anashindwa kulishughulikia nitawachukua wananchi 112,000 wa Jimbo la Mchinga, nitampelekea Mheshimiwa Magufuli awajibu alichowaahidi wakati wa uchaguzi. Haiwezekani kama Taifa tunakaa tu, vitu vyetu viko nje vinawanufaisha watu wengine, sisi wenyewe tuko bwerere tunafurahifurahi tu hapa. Tunaomba majibu, mabaki ya mjusi wa Tendegulu tunayapata na kama hatuyapati tunanufaika na nini? Tunaomba majibu juu ya hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka nizungumzie ni suala la Chuo cha Diplomasia. Limezungumzwa sana. Hiki chuo wamekitelekeza au hiki chuo sasa hivi kazi yake ni nini? Miaka mitatu Chuo cha Diplomasia hawapeleki bajeti ya maendeleo na ni chuo ambacho kina-train wanadiplomasia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshauri Waziri na nivishauri vyama, kuna umuhimu wagombea wa Urais waanze kupitia pale kwa sababu tunaingia kwenye matatizo ya kidiplomasia kwa sababu viongozi wetu wengine hawajui hata maana ya diplomasia ni nini. Ndiyo maana leo unakuta tunazuia hela za MCC shilingi trilioni moja, kiongozi mkubwa wa nchi anasema yeye haoni kama ni tatizo. Mheshimiwa Waziri nataka atakapokuja hapa atuambie tumewakosea nini, tatizo nini, diplomasia yetu imeyumba kwa kiasi gani mpaka pesa za MCC zimezuiwa, aje ajibu hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, muda tu, lakini nilitaka nimshauri mambo mengi. Nakushukuru.
Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuweza kuchangia juu ya mkataba huu wa EPA.
Mheshimiwa Spika kwanza nieleze msimamo wangu. Msimamo wangu mimi binafsi, serikali isiusaini huu mkataba. Ninazo sababu za msingi za kusema lakini pia nina maangalizo mengi kwa Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wakati tunahitaji kusaini mkataba huu au tunautazama mkataba huu, kuna haja ya kuangalia Mkataba wa Cotonou (Cotonou Agreement) ambao tulisaini.
Mheshimiwa Spika, ukisoma faida ambazo nchi za Afrika tumezipata kwa kusaini Mkataba wa Cotonou, unaona kwamba tulipata faida moja wapo kubwa ilikuwa ni kwamba tuliweza kuingiza bidhaa zetu katika soko la Ulaya na tukaweza kuokoa zaidi ya Euro billion 1.4 ambayo ilikuwa ni duty and tariff ambayo kama si mkataba ule hizi pesa maana yake tulitakiwa tuzilipe.
Mheshimiwa Spika, tunaposema EPA kwetu sisi haitufai kwa sasa ni kwa sababu moja kubwa. Wenzetu wameweka kifungu cha import duty kuwa free, tujiulize kwetu sisi kama Taifa tuna bidhaa ambazi zinakidhi viwango kuingia kwenye soko la Ulaya? Hili ni swali la msingi sana na je, wenzetu wa Ulaya wanazo bidhaa ambazo zinaweza kuingia zikakidhi vigezo katika soko letu la Tanzania? Hili ni swali la msingi sana la kujiuliza.
Mheshimiwa Spika, lakini pia tujiulize, ikiwa tutaondoa ushuru kwa bidhaa zinazoingia, tutapoteza mapato ya kiwango gani katika bandari yetu ambapo tunategemea import kwa kiwango kikubwa kutoka kwenye hayo mataifa ambayo leo tunaingia nayo mkataba. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la msingi kuangalia; tunawalaumu wenzetu Kenya kwamba wameharakia, Kenya wenzetu wameandaa facilities na wana bidhaa za kwenda kuuza Ulaya, tayari wanazo. Suala sio kuwalaumu, suala tunatakiwa na sisi tujiandae ili tuweze kuwa na bidhaa zitakazofikia viwango vya kuviuza Ulaya. Kwa hiyo, angalizo ninalolitoa mimi, si tu tunawalaumu Kenya, ni kweli, hatuwezi ku–compete na wenzetu lakini tujione kwamba tumechelewa kwasababu ya uzembe wetu sisi wenyewe. Tumeshindwa kujipanga.
Leo tunakuja kuwalalamikia wenzetu, tuwaache wenzetu waende lakini sisi kama Taifa nasema kwa maslahi mapana ya Taifa hili hatuwezi leo kuusaini kwasababu hatuwezi kushindana nao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Tanzania tuna sifa ya kusaini mikataba mingi. Ukisoma mikataba, Lome Convention, Cotonou convention - tulisaini lakini maeneo mengi ya vifungu ambavyo tulikubaliana navyo vingi tukashindwa kuvitekeleza, na kimoja wapo cha kifungu ambacho tulisaini kwenye Cotonou Convention ilikuwa ni suala la impunity pamoja na rule of law ambavyo hivi vyote vilikuwepo kwenye Cotonou Agreement, tulishindwa kama Taifa kuvitekeleza, sisi wenyewe.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, wakati mwingine tunaposaini mikataba sisi wenyewe tunakuwa hatujajitengenezea mazingira ya kuweza kuendana na mkataba husika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi kwa niaba yangu na nashukuru sana kwamba hata chama changu, Chama cha Wananchi CUF kimetuagiza kwamba huu mkataba tuukatae. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, chama chetu kimefanya analysis ya kutosha, na mara nyingi chama chetu kimekuwa na watu makini na tukifanya misimamo mizuri. Mkataba huu, msimamo wa chama chetu tunaukataa.
Kwa hiyo tunaomba Serikali, Mkataba wa Cotonou usiusaini kwa sababu tumechelewa, wenzetu wametuacha sana. Jukumu pekee ambalo tunapaswa kulifanya ni sisi kujipanga kwa sababu wenzetu duniani wanakimbia, tusiendelee kutambaa, ndilo suala la msingi la kulifanya.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ibara ya 63 ya Katiba yetu, kazi tunayofanya hapa ni kazi ya Kikatiba. Naomba nimalizie kwa kutoa wito, ipo mikataba pia ambayo kama Taifa tumesaini ambayo yenyewe ina mpact kubwa kwenye nchi yetu ikiwemo na Mikataba ya Gesi na Madini.
Mheshimiwa Spika, tengeneza jina, tunaomba mikataba hiyo ya gesi tuilete ndani ya Bunge na yenyewe tuje kuijadili kwa sababu inakwenda kugusa maslahi mapana ya Taifa letu. Nakushukuru kwa kunipa fursa hii.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii adhimu na mimi niweze kuchangia taarifa hizi mbili za oversight committee ya PAC na LAAC.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaingia ndani kwenye kuona madudu makubwa ambayo yameainishwa na Mdhibiti pamoja na viongozi wa hizi Kamati, niungane na wenzangu na mimi kuzungumzia juu ya weledi mdogo walionao Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli ambao uko dhahiri kwamba kama kuna jambo ambalo Halmashauri zetu zitakwama ni kuwa na watendaji dhaifu, ni kuwa na Wakurugenzi ambao hawajui walifanyalo. Na jana hapa wakati Mheshimiwa Waziri wa Habari anajibu baadhi ya hoja nilistaajabu sana aliposema kwamba walioteuliwa ndio watakaokuwa watekelezaji wazuri wa Ilani ya CCM. Kama CCM imekaa ikiwategemea Wakurugenzi wa aina ile ninawathibitishia mnakwenda kushindwa. Kama aina ya Wakurugenzi tulionao ndio mnaowategemea kufanikisha Ilani ya Chama cha Mapinduzi wanakwenda kushindwa muda mfupi ujao.
Mheshimiwa Naibu Spika, aina ya Wakurugenzi tulionao hawajui walitendalo na Mheshimiwa Waziri mimi nakuambia tuna Wakurugenzi ambao wanafanya mambo ya ajabu kweli kweli kwenye Halmashauri. Baraza la Madiwani linakaa likapitisha maamuzi yake, Mkurugenzi anabeba document anampelekea Mkuu wa Wilaya anakwenda kumwambia hebu pitia haya sahihi kweli haya? Yaani Mkuu wa Wilaya sasa ndiye anayefanya maamuzi kwa niaba ya Halmashauri. Kwa hiyo, tumekuwa na Wakurugenzi ambao hawajui walifanyalo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nawaomba katika namna ya kuwasaidia na kuzisaidia Halmashauri zetu, Serikali ihakikishe inatoa mafunzo kwa Wakurugenzi hawa mliowateua from nowhere. Mfumo wa utendaji wa kazi Serikalini unajulikana na unatambulika, huwezi kumtoa mtu kutoka huko kwenye NGO ukampeleka kwenye taasisi kubwa kama Halmashauri, ni shida. Mmetengeneza matatizo makubwa kwenye Halmashauri zetu.
T A A R I F A...
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, hajanipa taarifa alikuwa anachangia, kwa hiyo obvious siwezi kuikubali na mimi ninachokichangia ninachangia kwa mujibu wa taarifa hii iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, kwamba asilimia 60 ya Wakurugenzi waliokutana nao wameonyesha udhaifu kwamba hawajui walitendalo, ndiyo taarifa inavyosema. Hatuchangii kwa mujibu wa mtu, hapa ninachozungumza tunachangia Taarifa za Kamati. Kwa hiyo, ukisema ukitoa taarifa maana yake unampa taarifa Mwenyekiti wa Kamati aliyewasilisha hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika kwa hiyo niendelee kusisitiza kuna haja ya kuwapa mafunzo, kuna haja ya kuwapa semina ili watende vile mtakavyo, ili watende kwa mujibu wa sheria na ili tupate manufaa na mafanikio kwenye Halmashauri zetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la TIB (Tanzania Investment Bank), ukisoma Taarifa ya Mkaguzi ukasoma na Taarifa ya Kamati ya PAC inaonesha kwamba Tanzania Investment Bank imetoa mikopo zaidi ya shilingi bilioni 64 kwa watu ambao hata kuwataja hawataki. Taarifa ya Kamati inaeleza kwamba hata Mwenyekiti wa Bodi alivyoitwa kwenye Kamati aje aeleze kwamba hizi shilingi bilioni 64 imewakopesha akina nani ameshindwa kuwataja na katika masikitiko yangu makubwa Mwenyekiti wa Bodi juzi alikuja hapa kutueleza mambo ya EPA, namheshimu sana Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi, akaonesha kwamba ni mzalendo sana. Kama ana kiwango hicho cha uzalendo kinachomshinda kutaja hawa waliokopeshwa bilioni 64 ni nini? Na taarifa inaonesha kwamba wao wamefungua kesi 21 kuwashtaki watu, akina nani? Wanapata ukakasi gani kuwataja hawa waliowakopesha shilingi bilioni 64? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii tuombe, kama Mwenyekiti wa Bodi anashindwa kutaja au kama Mtendaji Mkuu wa hii Benki anashindwa kuwataja, rungu lako la Bunge lifanye kazi ili hawa waliokopeshwa shilingi bilioni 64 ambao hawatajiki waje waelezwe ndani ya Bunge humu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nichangie juu ya suala la misamaha ya kodi kwenye uingizaji wa mafuta. Mheshimiwa Waziri wa Fedha anatafuta sana pesa kwenye kodi. Taarifa ya Mkaguzi inaeleza kwamba mwaka 2012/2013 Geita Gold Mines na Resolute Tanzania Limited walipatiwa msamaha wa kodi ya mafuta, lakini wao ule msamaha wakautumia nje ya mizania, nje kabisa ya utaratibu wakahamisha yale mafuta kwenda kupeleka kwenye kampuni nyingine. Zaidi ya bilioni 22 zinaoneshwa hapa kwamba watu wa Geita Gold Mines walihamisha kodi ile ya mafuta kwenda kuipa kampuni nyingine yale mafuta, jambo ambalo ni kinyume kabisa na Tamko la Serikali Namba 480 la mwaka 2002.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunahitaji hizi bilioni 22 ambazo zilitolewa, ambazo zilikuwa ni kodi ya msamaha kwa Geita Gold Mines pamoja na Resolute Tanzania Limited, fedha hizi zipatikane, Waziri wa Fedha ulisikie hili, ulifanyie kazi ili kodi iweze kurudi kwa Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine naomba nichangie juu ya ucheleweshaji wa fedha kutoka Hazina kwenda Halmashauri na kwenda Wizarani. Kumekuwa na tabia iliyozoeleka kwamba Hazina inasubiri robo ya mwisho ya mwaka wa fedha ndipo hupeleka fedha nyingi kwenye Halmashauri, ama inasubiri robo ya mwisho wa mwaka kupeleka fedha nyingi Wizarani, matokeo yake nini kitatokea? Miradi ya maendeleo iliyokuwa inatekelezwa inaongezeka riba na Serikali inapata hasara kubwa kwa kuwa imechelewesha malipo ya wakandarasi. Lakini jambo la pili, fedha nyingi zinapelekwa katika Halmashauri katika kipindi ambacho muda wa utekelezaji unakuwa unakaribia kwisha kabla ya mwaka wa fedha kuisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma report inaonesha wazi kwamba katika mwaka wa fedha 2012/2013 zaidi ya shilingi trilioni 1.8, fedha ya maendeleo haikupelekwa, zaidi ya asilimia 38. Lakini pia ripoti inaonyesha kwamba zaidi ya Shilingi bilioni 19 zilipelekwa katika kipindi cha mwisho kabisa cha robo ya mwaka, fedha za OC na fedha zile hazikutumika. Katika mazingira kama haya tunatengeneza mwanya wa watendaji wetu wa Halmashauri wafanye vitendo ambavyo siwezi kusema kama ni wizi, isipokuwa si vizuri kwa mujibu wa sheria za fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine Serikali imepunguza sana uwekezaji wake kwenye baadhi ya taasisi. Ukisoma ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeonesha kwamba uwekezaji wa Serikali katika Shirika la TAZARA hisa zake zimepungua sana. Serikali imepunguza hisa nyingi katika Benki ya NBC, lakini pia hata katika mashirika mengine ambayo hapo awali yalikuwa na hisa nyingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, kupungua kwa hisa za Serikali katika TAZARA ina-reflect nini? Serikali imekuwa na uwekezaji mdogo katika hili shirika la reli ambalo tuna-share na watu wa Zambia. Kama Serikali ya Tanzania haipeleki fedha za kutosha TAZARA which means kama wenzetu wa Zambia kama wataendelea kuwekeza katika hili shirika mwisho wa siku hawa watu wa Zambia watakuwa wanamiliki hisa nyingi TAZARA kuliko vile ambavyo sisi Watanzania tunamiliki hisa maeneo hayo. Ni jambo la aibu sana shirika la reli ambalo tunalimiki kwa pamoja, tumelianzisha kwa pamoja sisi Watanzai kuwa nyuma katika kupeleka fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ni la msingi sana lazima tulizungumzie ni suala la Halmashauri na fedha za vyanzo vilivyofutwa. Halmashauri zetu zinajulikana kwamba kuna vyanzo Serikali imevifuta katika kumpunguzia mzigo mlipa kodi kule ndani ya Halmashauri, hili jambo lilikuwa jema sana na sisi tulidhani kwamba ili Halmashauri ziweze kujiendesha kwa ufanisi Serikali mngekuwa mnapeleka pesa kwa wakati. Lakini leo hii tuhojiane humu ni Halmashauri gani imepata pesa kutoka Serikalini au kutoka Hazina katika vyanzo vilivyofutwa na Serikali? Inatoa justification kwamba Serikali mnahatarisha uhai wa Halmashauri zetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya Halmashauri huko ni mbaya na ubaya huu umechochewa kwa kiwango kikubwa kabisa na kufuta baadhi ya vyanzo ambavyo vilikuwa vinatusaidia kwenye Halmashauri kuendesha Halmashauri zetu. Mmevifuta, kufanya compensation mpaka sasa hamfanyi, pesa hampeleki. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwahiyo ni jambo ambalo Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Waziri wa TAMISEMI wanatakiwa kutazama, kwa sababu Halmashauri zinakufa na Halmashauri zikifa ita-justify kwamba performance yako siyo nzuri Mheshimiwa Waziri wa Fedha, haitakuwa jambo jema kwako Halmashauri kufa kwa kikwazo tu kwamba Waziri wa Fedha hapeleki fedha kwenye Halmashauri kutokana na vyanzo vilivyokufa.
Kwa hiyo mimi niombe sana, Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI wewe unajua, unazunguka kwenye Halmashauri unajua kwamba Halmashauri zote zina vilio vya juu ya fedha za vyanzo vilivyofutwa, kwa hiyo ni jambo la msingi wewe kumbana Waziri wa Fedha aweze kupeleka hizo fedha katika Halmashauri zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho la kumalizia, naona muda umekaribia sana, kwamba Mkaguzi na Taarifa za Kamati zinaonesha wazi, Mkaguzi fungu la pesa alilotengewa ni dogo kiasi kwamba halimuwezeshi kufanyakazi yake ipasavyo, na cha ajabu ni kwamba kwa mujibu wa bajeti inaonesha kwamba mtapeleka fedha shilingi milioni sijui 50 katika kila kijiji, ingawa kwenye bajeti hazionekani lakini wenyewe mnasema bado maana yake hayo maneno mnayarudia kwamba mtapeleka hizo fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama mnapeleka fedha vijijini maana yake kwamba mnapanua wigo wa kazi za Mkaguzi kutoka kwenye central government kwenda mpaka kwenye local government mpaka kwenye village level, kwa sababu popote zilipo fedha za Serikali Mkaguzi ana wajibu wa kwenda kuzikagua. Ikiwa hamjamtengea fungu la kutosha huyu Mkaguzi hizi kazi ataifanyaje?
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi napata wasiwasi kwamba tunakuwa na Serikali ya aina gani ambayo inaogopa kivuli chake yenyewe, Serikali inayoogopa kukaguliwa, Serikali inayopambana na rushwa kwamba mnajionesha, mnaji-brand kwamba nyie mnapambana na rushwa lakini kumuwezesha Mkaguzi kwenda kukagua hamtaki, tutajuaje weledi wenu wa kupambana na rushwa? Mimi napata wasiwasi kwamba inawezekana mnatumia kumminya huyu Mkaguzi asiende kuwakagua ili udhaifu wenu na aina ya ufisadi mwingine mnaotengeneza huko sisi tusije tukaujua. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninaomba sana, ninaomba sana, ikiwa Serikali inampango wa kumfunga kama ni midomo au kama ni miguu huyu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali asiende kukagua fedha za Serikali mnajikaanga kwa mafuta yenu ninyi wenyewe.
Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumze mambo mawili tu kwa kuwa mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji nataka nichangie kwenye maeneo mawili muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala la Mfuko wa Maji, nashukuru Waziri wa Fedha yupo, fedha pekee ambazo Wizara hii inapata ni fedha za Mfuko wa Maji peke yake. Ukiacha fedha za Mfuko wa Maji, Wizara ya Maji haipati fedha za maendeleo ya miradi ya maji kutoka Serikalini. Kwa hiyo, tunaomba ufafanuzi na tunaomba suala hili Waziri wa Fedha alieleze Bunge hili kwa nini fedha za maendeleo ambazo tulizipitisha kwenye Bunge hili la Bajeti haziendi kwenye Wizara ya Maji ukiacha na fedha za Mfuko wa Maji ambazo ni shilingi 50, tunachangia huko tunaponunua mafuta.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili; suala la Bandari ya Uvuvi. Tangu Bunge la Kumi, Wabunge hapa walikuwa wanapiga kelele suala la Bandari ya Uvuvi, tunapoteza fedha nyingi sana katika nchi hii kwa kukosa Bandari ya Uvuvi, nimesikitika sana. Nimestaajabu kuona Wajapani wametoa fedha kujenga Bandari ya Uvuvi eti inakwenda kujengwa Chato!
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bandari ya Uvuvi ikajengwe Chato wakati tuna maeneo kwenye Bahari Kuu tunapoteza fedha nyingi wavuvi wanakuja kuvua wanashindwa kutua Tanzania kwa sababu hatuna Bandari ya Uvuvi. Kwa nini Bandari ya Uvuvi msifikirie kuipeleka Mtwara, kwa nini msifikirie kuipeleka Tanga, kwa nini msifikirie Bagamoyo, Bandari ya Uvuvi ukaweke Chato kwa samaki gani walioko Chato ili tukajenge bandari kubwa ya uvuvi na kwa kiwango gani cha fedha ambazo tunapoteza kwenye Ziwa Victoria? Kwa nini tusifikirie kujenga Bandari ya Uvuvi kwenye Bahari ya Hindi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu hili suala kwa kweli linatia doa Serikali yenu. Bandari ya Uvuvi imekuwa ikidaiwa sana humu ndani na tunapoteza fedha nyingi kwenye Bahari Kuu, kwa sababu ya kukosa Bandari ya Uvuvi, leo Bandari ya Uvuvi inaenda kujengwa Chato, fedha waliyotoa Wajapani ni jambo la hatari na ni jambo ambalo kwa kweli linafedhehesha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo nataka nizungumzie ni suala la migogoro ya wakulima na wafugaji. Mheshimiwa Mchengerwa amezungumza hapa na mimi ni Mjumbe wa Kamati. Kwa kweli mwenyewe pia sikufurahishwa sana na taarifa tuliyoiandika kuileta hapa juu ya migogoro ya wakulima na wafugaji. Migogoro hii haipungui, inaongezeka. Mheshimiwa Waziri, tunahitaji migogoro ya wakulima na wafugaji ipungue, badala ya kila siku inaongezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ina makakati gani wa kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji ili suala hili liwe historia? Vifo vinaongezeka, migogoro inaongezeka, hata maeneo yale ambayo kulikuwa hakuna migogoro ya wakulima na wafugaji kama Lindi hivi sasa na kwenyewe kumeshaanza kuwa plotted ni maeneo ya migogoro. Tunaomba Wizara iwe serious, mnapoamua kumaliza changamoto za wakulima na wafugaji...
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Bobali.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza niunge mkono hoja za Kamati. Kamati imeeleza mambo mengi na ya msingi, isipokuwa tatizo ni moja, kwamba hizi hoja ambazo Kamati wanazieleza katika Bunge hili la Taarifa za Kamati kwa mwaka mmoja, Kamati hizi hizi zingekuwa zinajenga hoja kama hivi wakati wa bajeti nadhani tungekuwa tuko mbali sana. Lakini inapofika wakati wa bajeti Kamati zote zinajigeuza, badala ya kusimamia na kuishauri Serikali kama ambavyo leo imefanya, zinajigeuza zinakuwa caucas ya vyama, hii ndiyo inakuwa changamoto kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukipitia taarifa ya Kamati, imejitosheleza kwa kiwango kikubwa ingawa yako maeneo mimi binafsi ningetaka kupata ufafanuzi zaidi. Kwa mfano kwenye ukurasa wa 33 wa Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii, ukurasa wa 33 kipengele (b) anasema, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kuna ufisadi mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Mwenyekiti wa Kamati angeeleza aina ya ufisadi huu anayotaja kwenye ukurasa wa 33 ni ufisadi wa nini. Ni kiwango gani cha fedha ambacho yeye anafikiria kwamba watu wamechukua, wameiba na wameiba katika mradi upi. Kwa hiyo, ukiangalia hii taarifa iliyoandikwa hapa katika ukurasa wa 33 haijitoshelezi, imesema tu kwamba, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kuna ufisadi. Kwa hiyo, naomba Mwenyekiti wa Kamati utakapokuja kuhitimisha hoja yako uje na maelezo kwamba ufisadi huu ulioueleza katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ni ufisadi wa aina gani ili Bunge na Watanzania tuweze kufahamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusu suala la ongezeko la ugonjwa wa kansa. Ukisoma taarifa za Wizara, ukiingia kwenye website ya Wizara ya Afya, ukasoma taarifa inaumiza sana kwamba ugonjwa wa kansa unaenea kwa kiwango kikubwa kabisa. Taarifa zilizopo kwa mujibu wa WHO ambayo taarifa yao waliitoa mwaka 2002 ni kwamba kila mwaka zaidi ya watu 21,000 Tanzania wanapata ugonjwa wa kansa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine taarifa inaeleza kwamba ugonjwa wa kansa za uzazi takribani wanawake 7,515 wanapata ugonjwa wa kansa ya uzazi na kati ya hao 6,009 wanafariki kila mwaka kutokana na kansa ya uzazi. Kwa hiyo, ningetaka kujua na Kamati ingetueleza wao kwa kuwa wanaisimamia na kuishauri Serikali, Serikali ina mkakati gani wa kupambana na ugonjwa huu ambao kwa sasa unaenea kwa kasi kubwa kabisa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma taarifa za kansa namna unavyoenea na namna unavyosababisha vifo ni jambo ambalo linasikitisha sana kuona hatua ambazo Serikali wanazichukua. Lakini kinachosikitisha zaidi ni kuona kwamba hata hiyo Hospitali yenyewe ya Ocean Road katika bajeti ya mwaka 2016/2017 kile kiwango cha pesa ambacho ilitengewa hiyo pesa haikupelekwa, kiwango kilichopelekwa ni kidogo sana. Kwa hiyo, inaonesha kwamba dhamira ya Serikali ya kupambana na ugonjwa huu ambao ni hatari sana ni ndogo sana, lakini WHO wana-estimate kwamba tunakoelekea zaidi ya asilimia 25 ya Watanzania tuko hatarini kupata kansa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba karibu kwenye Watanzania wanne, mmoja yuko hatarini. Ni jambo la hatari na ni jambo very serious, tunahitaji Kamati kwa kuwa ndio inaisimamia Serikali ije itueleze wapi Serikali imekwama katika kuhakikisha inapambana na ugonjwa huu wa kansa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu Uganda naona wamechukua hatua kubwa kabisa na si vibaya Waziri akaenda akajifunza kwa zile measures ambazo Uganda wamezionesha na namna wanavyopambana imeonesha kwamba is a serious issue na national problem na Rais ame-declare kabisa kwamba kansa ni tatizo la Taifa na wameamua kupambana nalo. Sidhani kama Tanzania tumefikia kwenye level ya namna hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la ugonjwa wa UKIMWI. Sisi tunaotoka vijijini siku hizi ugonjwa huu ni kana kwamba umehama mjini umekwenda vijijini. Hali ya maambukizi vijijini ni makubwa kuliko hata mijini mimi nasema. Ukienda kule vijijini, mimi natokea Lindi, ukienda Lindi vijijini kabisa ukielezwa idadi ya watu wanaotumia dawa kule vijijini kabisa, inasikitisha sana. Inaonesha dhahiri kwamba inawezekana kuna tatizo kubwa la elimu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huu ambayo wanayo wananchi wa vijijini?
Kwa hiyo, mimi naomba Kamati, kwasababu, ninyi ndio wenye hoja mtueleze pia, kwamba katika ushauri wenu kwa Serikali, Serikali wana mkakati gani wa kuongeza utoaji wa elimu vijijini? Suala la ugonjwa wa UKIMWI sasahivi limekuwa kubwa vijijini kuliko mijini; na hii ni kwa sababu, wananchi kule vijijini wamezoea kuishi maisha yao yale ya kawaida. Inasikitisha sana, ukiwa kwenye vikao vya Halmashauri ukapewa takwimu za ugonjwa wa UKIMWI katika Halmashauri inasikitisha na inatisha sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi binafsi nimeshiriki Vikao vya Kamati ya UKIMWI juzi juzi tu kwenye Halmashauri yetu ya Wilaya ya Lindi, taarifa iliyopo ni mbaya sana. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba hili ulichukue kwamba hali ya maambukizi ya UKIMWI vijijini sasa hivi ni kubwa zaidi kuliko hata mijini. Sijui kama takwimu zako zinasemaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa nilizungumzie ni suala la Bodi ya Mikopo. Tulizungumza hapa wakati wa bajeti kwamba bajeti hii ni ndogo, lakini pia, utaratibu unaotumika kupima vigezo vya nani apate na nani akose bado ni utaratibu ambao hauridhishi. Kwa hiyo, tunaomba, Kamati muendelee kuishauri na kuisisitiza Serikali kwamba katika mwaka na ninadhani Kamati mngekuja na orodha ama idadi kwamba ni wanafunzi wangapi ambao walistahili kupata mikopo lakini wamekosa katika mwaka wa masomo 2016/2017. Idadi ni kubwa na waliokosa wengi ni maskini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda vijijini unawakuta watu ambao walifaulu kwa division one, division two, lakini wanatoka kwenye familia maskini wako vijijini wamekosa mkopo. Kwa hiyo, Kamati tunaomba mngekuja na takwimu walao mkatueleza kwamba kukosekana kwa mikopo kumeathiri kiwango gani cha vijana wetu wa Kitanzania katika mwaka wa masomo wa 2016/2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naona muda wangu umekwisha, nakushukuru na ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupata ufafanuzi wa lini uwanja wa ndege wa Lindi utakarabatiwa na kutoa huduma za ndege kama ilivyokuwa kwa hapo awali? Uwanja huu ni miongoni mwa viwanja vya ndege vya zamani hapa nchini lakini pia ni uwanja mkubwa wenye barabara nyingi za kurushia ndege. Uwanja huu umechakaa sana kiasi cha kufanya ndege kuacha kutua jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa Lindi ikizingatiwa kuwa hivi sasa Lindi iko mbioni kuanza mradi wa LNG hivyo kuna haja ya kuboresha uwanja huu ili kurahisisha usafirishaji kwa njia ya anga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusu ombi la Mfuko wa Maafa ulio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuweza kusaidia katika maeneo mbalimbali ya jimboni kwangu ambapo miundombinu ya madaraja yamebomolewa na mafuriko yaliyotokea mwezi wa tatu mwaka huu wa 2017. Madaraja na barabara zilizoharibiwa na mafuriko ni barabara ya Mkwajuni - Namkongo; barabara ya Milola - Nangaru; pamoja na barabara ya Kitomanga - Mvuleni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiukweli kabisa barabara hizo zimeharibika sana na fedha kidogo zinazotolewa na mfuko wa barabara haziwezi kujenga madaraja hayo yote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba sana mfuko wako wa maafa usaidie kujenga walau madaraja yaliyopo katika barabara tajwa hapo juu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya niweze kusimama leo kuchangia kwenye Bajeti ya Ofisi ya Rais.
Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na mkanganyiko kwamba watu wanasema tusimtaje Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya TAMISEMI iko chini ya Rais, Ofisi ya Utawala Bora iko chini ya Rais. Wizara tunazozijadili leo zinafanya kazi chini ya Rais. Kwa hiyo,
kutomtaja Rais maana yake hatujadili kabisa hizi Wizara.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutuzuia tusiseme, tuishie kwenye kusifia, mimi Mbunge wa Jimbo la Mchinga wananchi hawakunituma nije kusifia hapa. Wananchi wamenituma nije kueleza kero zinazowakabili. Katiba yetu ya nchi imetoa mamlaka ya kazi za Bunge, sasa nashangaa
kama kuna mtu anakuja anasema nyie mnaponda tu. Tusifie! Aah, sisi tuliochaguliwa bwana hatusifii, tunakuja kueleza kero za wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze suala la utawala wa sheria. Nchi yetu inafuata utaratibu; tuna Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Mheshimiwa Waziri Simbachawene, kuna Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya, Vijiji; hizi Serikali nasi tuliamua kutumia mfumo wa D by D, lakini leo vyanzo vya mapato kwenye Halmashauri zetu tumevihamisha tumepeleka Serikali Kuu. Property Tax ambayo kwenye taarifa
yako mwenyewe umeeleza kwamba haijakusanywa.
Mheshimiwa Naibu Spika, makadirio ilikuwa zikusanywe shilingi bilioni 29, zimekusanywa shilingi bilioni nne; nami naamini itakuwa sijui Kinondoni tu. Haijakusanywa kwa sababu hizi shughuli zinahitaji zifanywe na Halmashauri wenyewe. Tunapoteza mapato mengi, mmejilimbikizia kila kitu mmepeleka TRA, mwisho wa siku Halmashauri zetu zitashindwa kufanya kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri kwa kuwa tumeamua kufuata mfumo huu wa D by D, hizi Serikali ni Serikali zilizopo kwa mujibu wa Katiba, tuzipe mamlaka zikusanye mapato zenyewe, hii Property Tax ni muhimu sana. Jana nilikuwa nafuatilia, nilikuwa najaribu
kuangalia kusoma mifumo ya nchi mbalimbali. Nimeangalia India, Thailand na nchi nyingine ambazo tunafanana nazo.
Hakuna nchi ambayo imechukua Property tax kwenye Halmashauri inapeleka kwenye Central Government, ni sisi tu na sijui kwa malengo gani?
Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri, naomba sana hili mliangalie. Isiwe kila mpango unaoletwa na Waziri wa Fedha iwe unau-copy na kuu-paste na kuuchukua, mwisho wa siku wewe ndio utalaumiwa. Halmashauri zikifa, wewe ndio utabeba huu msala. Mheshimiwa Mpango ataendelea na
kazi yake ya kukusanya mapato TRA.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka niliunganishie hapo hapo, kumekuwa na tabia isiyoridhisha ya Wakuu wa Wilaya kuziondoa Madarakani Serikali za Vijiji. Imefikia hatua leo Serikali za Vijiji wale Wenyeviti wakisikia Mkuu wa Wilaya anakuja, hawaendi kwenye
Mkutano, kwa sababu wanajua wakienda, wanatumbuliwa. Sasa tunataka tujue ni sheria ipi inampa Mamlaka Mkuu wa Wilaya kuondoa Serikali halali ya Kijiji iliyochaguliwa na wananchi?
Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo mifano mizuri mingine hapa Dodoma. Mkuu wa Wilaya Dodoma katangaza tu, Mwenyekiti hapa ondoka! Kwa hiyo, tunahitaji ufafanuzi; haya ni maagizo ya Mheshimiwa Rais? Kwa sababu hizi Wizara ziko chini ya Rais. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la kuajiri Watumishi wa Idara ya Afya. Kwenye Jimbo langu zipo zahanati nne, zimejengwa, zimekamilika. Hazijafunguliwa kwa sababu hazina wahudumu wa afya. Kwa bahati nzuri, Mheshimiwa Rais alikuja mwezi wa Tatu Lindi, alisimama Mchinga, akaelezwa na wananchi kwamba kero yetu kubwa hapa ni wahudumu wa afya. Mheshimiwa Rais akamwachia
lile suala Mganga Mkuu wa Mkoa, akamwambia shughulikia hilo. Mganga Mkuu wa Mkoa anawatoa wapi? Kila tukiangalia kwenye Halmashauri yetu, hakuna mtu ambaye anaweza kutoka kituo kimoja kwenda kwenye kituo kingine, kwa sababu hata hivyo vituo vyenyewe vina uhaba mkubwa wa watumishi hao.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba sana Mheshimiwa Waziri, hili alichukulie kwa uzito wake. Tunahitaji Watumishi wa Idara wa Afya waende wakahudumie wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la TASAF. Nashukuru Mheshimiwa Waziri ameeleza kwamba upo mpango wa wa kuongeza vijiji vingine. Jambo hili litatusaidia sana. TASAF sasa hivi imekuwa hata kwetu wanasiasa siasa yetu imekuwa ngumu. Kwa mfano, mimi Jimbo langu lina Tarafa nne. Katika Jimbo lenye Tarafa nne, Tarafa mbili zinanufaika, Tarafa mbili hazinufaiki, inatuwia shida na wananchi hawajui; wanachofikiri wao ni kwamba wewe ndio Mbunge, unaamua kwamba hapa wapate hapa wasipate.
Kwa hiyo, naomba sana mtusaidie, vile vijiji ambavyo havijapata hii miradi ya TASAF pelekeni na kama inashindikana, basi bora tuondoke wote tukose wote, kwa sababu haileti maana kwamba wengine wanapata; wana sifa zile zile na wengine wanakosa. Nashauri sana Mheshimiwa
Waziri hili alichukulie very seriously kwa sababu ni suala la kisiasa na linatuharibia siasa huko na sisi wote ni wanasiasa hapa.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ni muhimu nataka nilizungumzie ni suala la utendaji mbovu usioridhisha wa Wakurugenzi. Watu wamesema hapa, lakini inaonekana kama masihara. Jamani sisi wenzenu, nafikiri hata mwenzangu Mheshimiwa Nape wa Halmashauri moja naye anawezakuja kusema hapa. Wenzenu tuna shida. Tulikuwa tunavumilia lakini sasa tunasema, wenzenu tuna shida. Yaani unamtoa mtu, sijui alikuwepo Afisa nani sijui kwenye Kata huko unakuja kumfanya Mkurugenzi katika Halmashauri kubwa kama ilivyo Halmashauri yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri yetu ni kubwa kuliko Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi, zina eneo kubwa!
Unatuletea mtu ambaye ukisoma hivi vitabu, katika Mkoa mzima wa Lindi, internal collection iliyo chini kuliko zote ni Halmashauri yetu ya Wilaya ya Lindi. Ndiyo Halmashauri yenye population kubwa na Halmashauri ambayo ni kubwa. Tatizo ni utendaji usioridhisha wa hao watu mliowateua mkatuletea. Kwa hiyo, tunaomba sana, kama kuna haja ya kubadilisha, tubadilishieni, lakini kama hamna haja ya kufanya hivyo, tunaomba basi muwape mafunzo, kwa sababu wanatuletea umaskini; badala ya kwenda mbele sasa, tunarudi nyuma. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho, nilimwandikia jana Mheshimiwa Simbachawene, nami namwamini kwamba hilo, nililomwandikia atalifanyia kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la Walimu, nilipoona taarifa kwamba kumeajiriwa Walimu nilipata faraja sana hususan Walimu wa sayansi. Katika Jimbo langu kuna shule za sekondari saba, nimepata Walimu katika shule za sekondari mbili; Shule ya Mvuleni na Shule ya Rutamu; shule ambazo zina matatizo makubwa zimekosa Walimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, siyo tu shule yangu au Halmashauri yetu, Mkoa wa Lindi mnajua matokeo ya mtihani uliopita yalikuwa mabaya; tumekuwa kwenye tatu bora na hatupendi kuwa hivyo. Katika jambo ambalo linatuuma ni sisi kuwa wa mwisho na ni Mkoa uliotoa Waziri Mkuu; lakini moja ya sababu ambayo imepelekea Mkoa wetu kuwa katika kiwango cha mwisho cha ufaulu ni kwa sababu ya idadi ndogo ya Walimu.
Waheshimiwa Mawaziri wanajua historia ya Lindi, hili halifichiki. Zamani watu walikuwa wanagoma kuja kule. Siku hizi wanakuja kwa sababu kuna mambo mazuri; kuna miradi ya gesi, korosho ziko juu, kila kitu kipo. Kwa hiyo, waleteni, hawagomi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilipoona kwamba mmetangaza ajira, nikajua mtatufanyia affirmative action kwa sababu mkoa wetu uko chini, tunahitaji mtusaidie. Kama mtaajiri tena, naomba sana, shule zilizopo katika eneo langu la Jimbo la Mchinga zina uhaba mkubwa
wa Walimu. Shule ya Sekondari Mchinga ambayo ni kubwa, inafaulisha kidogo wastani, lakini ina uhaba wa Walimu wa Sayansi; Shule ya Sekondari ya Mvuleni nimepelekewa mmoja, mahitaji ilikuwa ni Walimu watano; Milola na shule nyingine zote zina uhaba mkubwa wa Walimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa nakushukuru. Kwa kuwa muda wenyewe mdogo nianze na suala la uwanja wa ndege wa Lindi. Kwa masikitiko makubwa nimepitia kitabu cha maendeleo ukurasa wa 134 mpaka 136 ambapo vimeorodheshwa viwanja vya ndege ambavyo Serikali imevitengea fedha kwa ajili ya kuviendeleza. Kwa masikitiko makubwa uwanja wa ndege wa Lindi umeachwa. Sijui umeachwa kwa kuwa mmeusahau au hamuutaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja ule tangu Mheshimiwa Rais aliyetoka madarakani aondoke hatujaona tena ndege kwa sababu Mheshimiwa Salma hapa alikuwa anatua pale kama Mke wa Rais, tangu yeye ametoka madarakani uwanja wa ndege wa Lindi haujatumika tena na ni uwanja wa kihistoria, ni uwanja wa muda mrefu. Naishangaa Serikali kuna mradi mkubwa wa LNG ambao unataka kufanyika takribani kilomita moja tu kutoka uwanja wa ndege. Hao Wazungu wanaotaka kuja watakuja kwa magari? Ama watakuja kwa usafiri gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nataka atakapokuja kuhitimisha, siku moja hapa Mheshimiwa Naibu Waziri wakati anajibu maswali alieleza kwamba uwanja wa ndege wa Lindi utafanyiwa upembuzi yakinifu na pesa itatengwa, leo nimedhihirisha kwamba taarifa alizozitoa Mheshimiwa Naibu Waziri siyo za kweli, ni taarifa za uwongo, uwanja wa ndege wa Lindi mmeusahau, hamuutaki. Kwa nini hamtaki kutenga fedha kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Lindi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni suala la fedha za maendeleo ya barabara, nimemweleza Mheshimiwa Waziri, haiwezekani Mkoa mkubwa kama Mkoa wa Lindi mnautengea shilingi bilioni 800, kuna mikoa mingine midogo mnaitengea shilingi trilioni mbili tena ni mikoa ambayo tayari imeendelea. Leo Mkoa wa Lindi ambao miundombinu yake ya barabara bado ni mibovu, haijaendelea, mnautengea shilingi bilioni 800. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie mfano Mkoa wa Kilimanjaro, mmeutengea shilingi trilioni 2.2, Mkoa wa Lindi mnautengea shilingi bilioni 800 kwa sababu gani? Mheshimiwa Waziri tunaomba maelezo Mkoa wa Lindi ni mkubwa sana, mkoa ambao haujaendelea au kwa sababu ni Kusini? Au mnaona gere kwa sababu korosho inalipa sasa? Tunaomba sana Mheshimiwa Waziri kwa kuwa kuna korosho na inahitaji kusafirishwa, korosho hailimwi mjini Korosho inalimwa vijijini, lazima isafirishwe ipelekwe huko bandarini Mtwara ipelekwe Dar es Salaam, tunaomba miundombinu ya barabara ijengwe katika mkoa wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inasikitisha kwa sababu Majimbo nane, Majimbo yote saba hayajatengewa fedha, Jimbo moja tu la Mheshimiwa Waziri Mkuu ndiyo limepata fedha, hili jambo ni la hatari, Majimbo yetu wengine hayana fedha, yamekuwa hayana kitu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri aje atueleze kwa nini Mchinga haijatengewa fedha, kwa nini Liwale haijatengewa fedha, kwa nini Kilwa haina fedha, kwa nini Mtama haina fedha, kwa nini Nachingwea haina fedha, tunahitaji majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la ubovu wa barabara ya kutoka Somanga kwenda Nangurukuru. Hii barabara imejengwa miaka michache iliyopita, leo hii ukipita katika eneo lile barabara ni mbovu, inathibitisha kwamba imejengwa chini ya kiwango. Eneo hili sasa hivi la Nangurukuru kumekuwa na uharamia, majambazi wanakaa, wanateka watu na sababu, kipande kile cha barabara ni kibovu. Kwa nini Serikali inatumia fedha nyingi lakini barabara zinadumu kwa muda mfupi? Kuna harufu ya nini? Kuna harufu ya ufisadi au kuna harufu gani? Kwa sababu haiwezekani barabara iliyojengwa miaka miwili au miaka mitatu iliyopita leo barabara mbovu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiwa unatembea kutoka Lindi ukifika kipande cha Nangurukuru unasahau kama upo kwenye lami, ni mashimo kwenda mbele. Tunaomba sana majibu ya kina juu ya barabara hususan kipande cha kutoka Nangurukuru kwenda Somanga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la kumalizia ni suala la alama za (X) ambazo mmeziweka kwenye nyumba zetu katika eneo hili la barabara. Tunataka majibu (X) zile za kijani mwisho wake lini? Kama mmeshindwa kulipa tuwaambie wananchi waziendeleze nyumba zao. Mnawawekea alama za (X) hawaendelezi nyumba. Leo ukiingia Jimboni kwangu kuanzia Mkwajuni, Kitomanga, Kilangala, Mchinga mpaka unafika Mto Mkavu kote kuna alama za (X) za kijani. Watu wale hawaendelezi nyumba zao mpaka leo kumekuwa hakuna maendeleo tunahitaji maelezo hizi (X) mwisho wake lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi; Mheshimiwa Waziri kwa masikitiko makubwa sana Mkoa wa Lindi mwaka huu mmeupatia fedha chache kuliko uhalisia wa miundombinu iliyopo. Kwa nini Lindi, mkoa mkubwa kwa eneo tena bado miundombinu yake bado haijaimarika, unatengewa fedha chache kuliko mkoa wenye eneo dogo kama vile Kilimanjaro ambao umetengewa kiasi cha fedha zaidi ya trilioni 2.2 wakati Mkoa wa Lindi mmeutengea fedha chache kiasi cha shilingi bilioni 800 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Jimbo la Mchinga ambalo mimi ni Mbunge wake halijatengewa fedha hata senti moja katika fedha za maendeleo, kwa nini mgao wa rasilimali za nchi hii hauzingatii usawa kwa sehemu yote ya nchi hii? Naomba maelezo ya kina juu ya swali hili.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme kwamba Mheshimiwa Waziri mwaka jana nilieleza hapa kwenye bajeti zipo zahanati tano jimboni kwangu zimejengwa, zimekamilika ila hazijafunguliwa kwa sababu hakuna wahudumu, lile tatizo limeendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mazingira mengine nimshukuru sana Waziri wa Ardhi, jana amefanya kazi kubwa, tena inahusu na Wizara yako Mheshimiwa Ummy.

Mheshimiwa Lukuvi namshukuru jana ameweza kumnyang’anya eneo mtu mmoja ambaye anapenda sana kuibaiba sana maeneo ya watu. Aliwahi kuiba eneo akamkabidhi Mkuu wa Mkoa Makonda pale Dar es Salaam, Mheshimiwa Lukuvi akamnyang’anya, jana tena kaenda kumnyang’anya hekari 4000, ambazo alitaka kuwaibia wananchi wa Jimbo la Mchinga katika kijiji cha Ruvu na kijiji cha Mchinga, kwa hiyo namshukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, njia aliyoitumia alijenga zahanati mbili, moja Mchinga na moja Ruvu. Kila alipokuwa anaambiwa azikabidhi akawa hataki kuzikabidhi, akamtumia Afisa Mipango Miji wakaenda wakaghushi hati ya kumiliki ardhi, alipoona Mheshimiwa Lukuvi anakomaa naye wakaamua kusita, kwa hiyo zile zahanati mbili ambazo jana lile eneo amenyang’ anywa, Mheshimiwa Ummy nafikiri sasa hivi muagize Mkuu wa Mkoa tuzichukue sisi. Tumemnyang’anya eneo lakini zile zahanati ziwe kwetu, kama hataki kabisa basi akavunje haraka iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la upatikanaji wa dawa. Mheshimiwa Waziri siyo kila taarifa wanayokuletea watendaji wako uiandike na ui-copy kama ilivyo. Nimekisoma hiki kitabu, nimejiridhisha kwamba hii taarifa uliyoisoma jana haukuipitia labda kabla haujaja Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hali ya upatikanaji wa dawa Mkoa wa Lindi ukurasa 126, wameeleza kwamba Mkoa wa Lindi umepata dawa kwa asilimia 70. Lindi ina Halmashauri sita, ukienda kwenye upatikanaji wa dawa kwa Halmashauri, Halmashauri ya Kilwa asilimia 77, Lindi DC asilimia 80, Lindi MC asilimia 84, Liwale asilimia 88, Nachingwea asilimia 81, Ruangwa asilimia 86, ukitafuta wastani ni wastani wa asilimia karibu 83. Lakini huku kwenye Mkoa umetuandikia kwamba tumepata dawa kwa asilimia 70, ukitazama kwenye mgao wa Halmashauri asilimia wastani wake ni asilimia 83. Mlifanya mahesabu? Ndiyo maana nikasema wakati umeletewa hii taarifa haukuipitia, kwa hiyo, najua kwamba asilimia ya dawa tuliyopata Mkoa wa Lindi ni asilimia ndogo kuliko Mikoa yote. Hii inasikitisha, mmetusahau kwenye walimu, mmetusahau kwenye madaktari, mnaendelea tena kutusahau kwenye dawa. Ninaomba sana hali ya upatikanaji wa dawa katika Mkoa wetu wa Lindi siyo mzuri, naomba muongeze hiyo kasi ya kutuletea dawa katika Mkoa wetu wa Lindi. (Makofi)

Suala lingine ni suala la vifo vya akina mama hususan wanaokwenda kujifungua. Mheshimiwa Waziri wewe ni mwanamke, nilifikiri kwamba katika jambo ambalo utalipigania kwa dhati kabisa ya moyo wako, uache legacy, kila siku kina mama 30 nchi hii wanafariki wakiwa wanajifungua. Umeikuta hali hiyo hivi sasa mwaka wa pili hali ipo hivyo hivyo, utaondoka miaka mitano, hali ikiwa hivyo utaacha historia gani! Akina mama watakukumbuka kwa lipi? Tunaomba sana na nimewasikia Wabunge hapa wanakusifia sana na mimi pia mwaka jana nilikusifia, lakini nimegundua haya maneno mazuri ni kwa ajili ya asili yako tu ya kutoka Tanga, watu wa Tanga mnajua vizuri Kiswahili, mnaongea vizuri, tunahitaji ufanisi na utendaji, tunataka tuone uache legacy kwenye hii Wizara. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa nimesema Tanga tu, maneno yale mazuri kwa sababu ya Tanga. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana tunahitaji matendo, ninataka mtu ambaye ana-perform na ndiyo maana nilisema mara ya kwanza, nimempongeza sana Mheshimiwa Lukuvi tumempelekea tatizo la ardhi, mtu anataka kunyang’anya watu ekari 4000 katika mazingira ya wizi tu, watu wa Serikali mpo, huyu Azimio Housing Estate kwa nini hii kampuni na yenyewe msiifungie kabisa? Kila siku anafikiria kuiba maeneo tu ya watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee tena kumshauri Mheshimiwa Waziri, hatuhitaji maneno mengi kwenye vitabu hivi, tunahitaji action, tunahitaji utekelezaji. Bajeti yako inapungua umechukua mechanism gani kuishauri Serikali ikuongezee bajeti, usiwe unakubali tu unaletewa bajeti ndogo na wewe unakubali. Hii shilingi trilioni 1.1 haikutoshi, matatizo ya afya ya nchi hii ni makubwa kuliko kiwango cha pesa. Inawezekana hata hii shilingi trilioni moja usiipate yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu suala la magari ya wagonjwa niliona wakati fulani Mikoa ile ya Mwanza wapi kule, watu wanapewa magari ya kubeba wagonjwa, kwetu huku mbona hatuletewi? Mimi katika vituo vyangu vitatu, Kitomanga, Lutamba na pale Milola magari yake yote yamechakaa na sasa hivi hayafanyi kazi, yamekufanya kabisa yote, lakini wenzetu tumeona mnawapatia magari, je mna mpango gani na sisi kutupatia magari ya wagonjwa? Hii distribution of resources uwe sawa, hii keki ya Taifa tuigawane sawa, tunaposhindwa kutenda haki katika mgawanyo wa hii keki ya Taifa tunasababisha matatizo na wengine tutakuwa tunajihisi wanyonge. Sasa binadamu anapojihisi mnyonge ni tatizo kubwa sana, nisingependa katika Taifa hili wengine tujione wanyonge na wengine wawe siyo wanyonge.

Kwa hiyo, naomba sana hakikisha katika bajeti hii unatupatia gari la wagonjwa japo moja katika Halmashauri yetu na specifically liende kwenye Jimbo la Mchinga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la vyeti fake limeathiri sana Halmashauri yetu. Ziko zahanati mbili zimefungwa hivi sasa ninavyokuambia kwa sababu watumishi wake wote wameonekana wana vyeti fake. Namuomba sana Mheshimiwa Waziri uchukue initiative za haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hotuba ya Kambi ya Upinzani.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuitumikia nchi yetu. Mheshimiwa Waziri nikuombe sana ukiangalie kituo cha afya Kitomanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kituo hiki hivi sasa kinafanya kazi kubwa kama hospitali ya Wilaya lakini uwezo wake ni wa kituo cha afya. Changamoto kubwa iliyopo katika kituo kile ni uchache wa vitanda, kutokamilika kwa jengo la x-ray pamoja na kuchakaa kwa gari la wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali sana nakuomba utuokoe kwa kutupatia gari la wagonjwa katika kituo cha afya Kitomanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni kuhusu vyoo katika shule za msingi. Nakumbuka mwaka jana nilikueleza changamoto ya vyoo iliyopo katika shule nyingi za msingi zilizopo Jimboni kwangu. Changamoto hii zinawaathiri sana wasichana wawapo shuleni. Nakumbuka uliniahidi kutupatia fedha kwa ajili ya kujenga vyoo kadhaa katika baadhi ya shule za msingi ukataja kuwa upo mradi Wizarani kwako ambao ungeweza kutusaidia katika baadhi ya shule. Ahadi yako ile bado hadi sasa hajalitekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu fedha kidogo ya dawa zinazoletwa katika Mkoa wetu wa Lindi. Mheshimiwa Waziri nakuomba uipitie taarifa yako uliyoisoma hapa Bungeni, utagundua kuwa Mkoa wa Lindi umepata asilimia 70 tu ya fedha mliyoitenga mwaka wa fedha 2016/2017 tatizo ni nini? Lindi ni Mkoa ambao wakazi wake wengi ni maskini wenye kipato cha chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu kukosekana kwa Sheria ya Wazee ambayo inapaswa kwenda sambamba na Sera ya Wazee ya mwaka 2003. Je, ni lini Serikali italeta Bungeni Muswada wa Sheria ili sera hii itungiwe sheria yake?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nianze kuchangia Wizara hii kwa kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa wa Uwaziri katika Wizara hii. Pamoja na pongezi hizo, natambua kuwa majukumu yaliyopo katika Wizara hii ni makubwa mno kutokana na ukweli kwamba Wizara hii inagusa furaha za Watanzania wengi kupitia michezo.

Mheshimiwa Spika, kwanza nishauri kufanya marekebisho katika kanuni za ligi kuu ya Vodacom kwa kuondosha kanuni inayoipa timu iliyoshindwa uwanjani ushindi eti kwa kigezo cha timu shindani kumchezesha mchezaji mwenye kadi za njano tatu. Kanuni hii imepitwa
na wakati na nchi nyingi duniani wameiboresha kwa kubakisha point kwa timu iliyoshinda na ile timu ilivyotumia mchezaji mwenye kadi tatu za njano huadhibiwa kwa kutozwa faini na mchezaji husika kupigwa faini pia.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri jambo lingine ni lugha ya Kiswahili; lugha hii ni miongoni mwa urithi ambao tuliopo leo tumerithi na hatuna budi na sisi kurithisha kizazi kijacho. Lugha ya Kiswahili ni alama muhimu isiyo na shaka kabisa kuwa inalitangaza Taifa letu. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri kuandaa mipango madhubuti ya kukilinda na kukienzi Kiswahili kwani Serikali haijengi chuo maalum cha kufundisha Kiswahili pekee. Chuo hiki kitafanya kazi kubwa ya kukienzi Kiswahili kwa kufundisha masomo mahususi yanayohusu Kiswahili tu.

Mheshimiwa Spika, kwa nini Kiswahili kisitumike kama lugha ya kufundishia na kujifunzia kwa elimu ya sekondari na vyuo hapa nchini. Kitendo cha kuendelea kukitumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika masomo ya elimu ya juu ni kuendelea kuwa watumwa wa kikoloni. Nashauri lugha ya Kiswahili iwe ndio lugha rasmi ya kufundishia na kujifunzia katika masomo ya elimu ya juu.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu uozo uliopo TFF na Vyama vya Mpira vya Mikoa na Wilaya. TFF imetawaliwa na watu wanaosimamia maslahi yao binafsi badala ya mpira wa miguu. Kwa nini kila kukicha utasikia stori za magari ya Timu ya Taifa kuzuiwa hotelini au TRA. Hizi habari za TFF kudaiwa na TRA pamoja na hoteli ambazo timu zetu zinaweka kambi ni dalili za wazi kuwa TFF wana upungufu katika utendaji kazi wao. Mfumo wa usimba na uyanga uliokithiri pale TFF ni adui kwa maendeleo ya soka nchini.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kutorushwa mubashara kwa matangazo ya Bunge. Jambo hili ni kinyume kabisa na katiba ya nchi yetu inayotoa haki ya Watanzania kupata taarifa na habari hususan za Bunge ambapo wawakilishi wao wanawasemea wao lakini kwa bahati
mbaya wananchi hawaoni jinsi wawakilishi wao wanavyofanya kazi walizowatuma.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri jambo lingine ni kuhusu Ciber Crime Act. Sheria hii imekuwa ikitekelezwa kwa wananchi ambao wana mlengo mmoja tu wa kisiasa (Wapinzani). Katika wingi wa vijana waliowahi kushtakiwa na kuhukumiwa wote ni aidha CHADEMA au CUF, kwa nini vijana wa CCM ambao kila kukicha wanaendelea kutoa maneno ya kejeli na matusi kwa viongozi wa upinzani lakini hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Tunaomba Serikali iache kutekeleza usimamizi wa sheria ya mtandao kwa ubaguzi wa itikadi za kisiasa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuendelea kunipa afya njema hadi leo na kuweza kuwatumikia wapiga kura wangu wa Jimbo la Mchinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuendelea kuorodhesha na kuweka kumbukumbu juu ya matatizo makubwa ambayo wakulima wanakutana nayo kutokana na adha kubwa wanayosababishiwa na tembo, ambao wanatoka mbali katika Mbuga au Hifadhi ya Selous. Mfano, mwaka jana pekee zaidi ya ekari 100 za mazao ya kilimo zililiwa, lakini hakuna hatua yoyote ambayo Wizara yako imeichukua hadi sasa.

Mheshimiwa Waziri, naomba sasa kile kiasi kidogo (kifuta jasho) kiwafikie wakulima wote, lakini mwaka huu ndio kuna tembo wamefunguliwa mlango, wamekuja tembo zaidi ya 20 hadi hivi sasa tembo bado wapo Jimboni wanaendelea kusababisha hasara kubwa kwa mazao ya wakulima. Namuomba sana Mheshimiwa Waziri jambo hili ulifanyie kazi, ukimya wako katika jambo hili unanikatisha tamaa pia unawaumiza sana wapiga kura wangu.

Mheshimiwa Waziri jambo lingine ni kuhusu ahadi yako ya kuwapatia huduma ya maji wananchi wa Tendegura sehemu ambayo mjusi mkubwa dinosaur alipochukuliwa na kupelekwa Ujerumani. Ombi letu kubwa ni kuhakikisha kuwa eneo lile lipatiwe maji na barabara ili watalii wale wanaokwenda kule waweze kupata barabara nzuri na pia huduma za maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo naomba kufahamu ni kwa nini basi Wizara yako haitaki hata kulitangaza eneo lile kuwa ni miongoni mwa maeneo muhimu ya utalii ili wazungu na watalii wengine waweze kuja kufanya utalii hivyo Mkoa na Taifa kuweza kupata kipato kinachotokana na utalii huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza nasikitika kwamba nitachangia huu mchango wakati Waziri wa Fedha hayupo na hata Naibu wake hayupo, kwa hiyo, mambo mengi ambayo nitayasema hapa wao hawatayasikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba awafikishie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kilimo. Kiukweli kabisa naunga mkono hotuba yetu ya Kamati yetu ya Kilimo. Waheshimiwa Wabunge mtakuwa mashahidi, hii Kamati katika Bunge hili la bajeti tumekuja na hotuba ambazo ni very constructive. Tumefanya hivyo kwenye Wizara ya Maji na leo tumerudia tena. Nampongeza zana Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Mary Nagu kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziri, hebu ajaribu kuchukua ile hotuba ile ya Kamati yetu tunafanya kazi pamoja, aiangalie. Tumeshauri vitu vya msingi sana kwa maslahi ya Taifa. Shida ninayoiona ambayo siku zote tunaeleza kwenye Kamati, Mheshimiwa Waziri hauna fedha. Hapewi pesa! Watu wanasema zaidi ya 75% ya Watanzania ni wakulima. Haifanani na fedha ambayo anaipata na ndiyo maana nikasema Waziri wa Fedha labda angekuwepo angetusikiliza.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wengi wanalalamika humu ndani, kwa nini hii Wizara haipewi fedha inazotengewa? Kwa nini Wizara ya kilimo ambayo ndiyo tunasema uti wa mgongo wa Taifa letu, fedha zinazotengewa tunapata pungufu? Mheshimiwa Waziri, sijui kama kuna Wizara ambayo imepata fedha chache kuliko hii!

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunavyochangia hapa tujue kwamba tunachangia kwa hotuba nzuri ya Waziri na kwa maneno mazuri aliyotuambia, lakini in reality hii Wizara haijapata fedha. Mwenyekiti wetu amesema hapa, fedha ya development ni asilimia 3.8; ni jambo la aibu sana! Sasa kama tunapata fedha ndogo kiasi hicho, tunadhani haya mambo tuliyoyazungumza yatafanikiwaje.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Jenista amfikishie Mheshimiwa Waziri wa Fedha; tumemkosea nini Watanzania; ambapo 75% ya Watanzania ni wakulima? Kwa nini hapeleki fedha kwenye Wizara ya Kilimo? Hilo ndio jambo langu la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, katika hotuba yetu ya Kamati tumezungumzia suala la bulk procurement ya mbolea. Kama kuna mtu yeyote aliyejiandaa kupinga huu mfumo, sisi kama Wajumbe wa Kamati, nami nasema huyo mtu kwa kweli labda ana maslahi yake mengine lakini siyo maslahi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mbolea linajulikana namna lilivyokuwa na utata, lakini jambo hili sisi pale Kilwa kunajengwa Kiwanda cha Mbolea. Kwa hiyo, tunahitaji na hawa ambao leo wanapinga, ndio hao hao wanafanya mipango ya kuhujumu kile Kiwanda cha Mbolea. Kwa hiyo, jambo hili linabeba maslahi ya Taifa, linabea maslahi mapana kabisa ya nchi yetu. Naomba jambo hili lianze haraka, mbolea ianze kuagizwa kwa mfumo huo; litakuja kutusaidia kama Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaposimama kwenye maslahi ya Taifa, haya mambo ya itikadi zetu na mambo mengine tunaweka pembeni kwa sababu tunajenga nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nizungumze pale alipoishia jirani yangu ndugu yangu Mheshimiwa Dau; amelalamika sana kuhusu masuala ya uvuvi. Kwenye fikra yangu nafikiri hii Wizara kubwa kwa sababu hata kwenye matamshi yake inaitwa Wizara ya Kilimo, Mifugo, yaani huo uvuvi wenyewe ndiyo umetamkwa mwishoni kabisa “na Uvuvi;” yaani as if ni supplementary, yaani uvuvi ni kama additional. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachoamini ni kwamba kuna nchi kadhaa duniani zimepiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kutegemea uvuvi na tunayo mifano mingi katika hili. Sasa Mheshimiwa Waziri hebu angalia namna gani unatoa kipaumbele kwenye sekta ya uvuvi, leo tuna uvuvi wa bahari kuu, kuna nchi zinaendesha nchi zao kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu tu. Wapo wazungumzaji wamesema hapa kwamba lipo eneo kama Lindi na Mtwara ni kama ni virgin sea, bahari ambayo haijatumika kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna mifano mingine, kulikuwa na samaki walikamatwa hapa, walikuwa wanaitwa samaki wa Magufuli, wakati ule Mheshimiwa Rais alikuwa Waziri wa Uvuvi. Wale samaki walikamatwa walivuliwa siku tatu tu walipokwenda kuuzwa thamani yake ilikuwa zaidi ya bilioni tatu, kwa mtu ambaye tulimpa leseni ya shilingi milioni 800 kwa mwaka kuvua.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili liangaliwe. Tukitegemea kupata mapato ya uvuvi wa bahari kuu kwa kutegemea leseni, we are very wrong na hatutaendelea. Tuwekeze sisi wenyewe, tuwawezeshe wavuvi wetu wa ndani waweze kuwa na uwezo wa kuvua bahari kuu. Tuna samaki wengi kule. Vile vile jambo hili liende sambamba na ujenzi wa bandari ya uvuvi, ili hata hawa wavuvi ambao leo tunawapa leseni, wakishavua waweze kushushia mzigo wao hapa Tanzania tuweze kukusanya kodi. Jambo hili kila siku tunalisema.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bahari kuna lasilimali nyingi. Leo ukitoka Tanga mpaka Mtwara watu walio karibu na bahari kwa bahati mbaya ndio maskini, yaani nchi hii ukikaa karibu na bahari wewe ndio kama umepigwa laana; wewe ndio maskini; wakati bahari ni utajiri. Leo
tunajua kuna mikoa mingi nchi hii wanategemea uvuvi, ukiwemo na Mkoa anaotoka Mheshimiwa Waziri; hawa wavuvi tunawasaidiaje?

Mheshimiwa Naibu Spika, leo uvuvi tumeuweka ni kama additional, kama supplementary. Naomba sana, Katibu Mkuu wa Wizara namfahamu, ni mtu mzuri, ni mchapakazi, wamwezeshe, wampe pesa! Hawezi kufanya kazi! Hili nalalamika tena kwa Waziri wa Fedha, leo Sekta ya Uvuvi imeachwa kabisa. Ukiangalia mafungu, fedha walizozipata ni as if sisi nchi hii hatuna wavuvi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba sana suala hili tulizingatie kwa umakini mkubwa sana, litatusaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais aliyepita alianzisha harakati za ujenzi wa bandari ya uvuvi, nataka kujua wameishia wapi? Tunataka tupate majibu ya kutosha kwamba ile bandari ya uvuvi iliyokuwa inataka kujengwa, mpaka leo imefikia wapi? Naamini kuna hatua kadhaa zilishachukuliwa, sasa je, wao ndio wameacha kabisa au wanaendelea? Mheshimiwa Waziri, naomba atakapokuja aje kunijibu hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la NFRA. Suala la chakula ni jambo muhimu sana. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo haina chakula na hatuwezi kuwa na watu ambao watakuwa wanafanya kazi vizuri kama chakula hakuna. Mwaka huu tumeingia kwenye matatizo makubwa, wengine wanasema kuna njaa, wengine hakuna njaa, wengine kumekuwa na shida. Pia, hebu tujipime kama nchi; hifadhi yetu ya chakula ina kiasi gani cha chakula cha kuweza kutulisha? Kumekuwa na majanga mengi sasa hivi yanatokea kama ukame. Unaona Mkoa wa Dodoma uko na ukame mwaka huu na mikoa mingine. Uzalishaji wetu wa chakula umekuwa mdogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, NFRA hawaipi kabisa kipaumbele. Nawaambia, ukitokea mwaka mmoja hapa kama Wabunge wangekuwa wanajua kwamba ingetokea Mwenyezi Mungu akatupiga gharika hapa miezi mitatu; siyo jambo la kuombea na siombei na leo siku ya Ijumaa, Mwenyezi Mungu hili jambo atuepushie.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikitokea miezi mitatu tu nchi hii ikaingia njaa, nchi hii tunaparaganyika kabisa, kwa sababu hifadhi yetu ya chakula haiwezi kukidhi haja hata ya miezi miwili kulisha nchi hii. Leo mwaka 2017/2018 bajeti iliyopita NFRA ilitengewa shilingi bilioni 18 iweze kununua mahindi na nafaka. Mpaka hivi sasa tunapozungumza, mmeipa shilingi bilioni tisa tu. Yaani ni nusu ya fedha ambayo tumeitengea. Hata hii tulilalamikia kwamba ilikuwa ni fedha ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakupa mfano, mwaka 2014/2015, wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, Serikali ilitenga shilingi bilioni 109,656 kwa ajili ya NFRA, lakini ilitoa zaidi ya asilimia 110; Serikali ilitoa shilingi bilioni 111. 9. Leo mwaka 2016/2017 tunatoa bilioni tisa, are we serious? Hatuoni kwamba kuna mabadiliko ya tabianchi? Hatuoni kwamba hali ya uzalishaji wa chakula inapungua? Kwamba tumeifanyaje hiyo NFRA? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri, suala la chakula; chakula ni siasa, food is politics, food is life; chakula ni maisha pia. Kwa hiyo, tusicheze na jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie jambo la mwisho, naona muda unakwenda. Mheshimiwa Esther, naomba kidogo Mheshimiwa Waziri wa Maliasili anisikilize na Mheshimiwa Waziri wa Kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jana nilisema pale Wizarani kwamba sisi tunafanya kazi kubwa kuwahimiza wakulima waweze kulima ili baadaye wajinasue na matatizo yao ikiwepo kuondoa njaa. Leo ndovu (maana nikisema tembo kuna watu wengine nawakwaza) mpaka hivi sasa ninavyokwambia, tangu juzi nimeomba Mwongozo hapa, mpaka hivi sasa wameshakula zaidi ya ekari 45 za wakulima. Mwaka 2016 zililiwa ekari 183, hakuna hatua iliyochukuliwa.

Hivi sasa ninapowaambia, hao ndovu wako Mchinga wanatembea tu kama mbuzi. Kwa hiyo, nasema na mwaka 2016 nilisema hapa, msituone wapole, nasi tunawaachia kwa sababu sisi tunajua kwamba ndovu ni rasilimali ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkulima ni mtu mnyonge. Ikifika siku akachoka, akaamua kufanya hicho anachokiweza, tusije tukalaumiana. Lazima tuliseme hilo! Haiwezekani mtu ambaye mwaka 2016 ameliwa ekari 183 hakuna hatua iliyochukuliwa. Naibu Waziri wa Maliasili amekwenda anasema kwamba tutawaletea hiyo laki moja kwa kila ekari, tangu mwaka 2016 amekwenda, mpaka leo hakuna hatua iliyochukuliwa. Leo hao hao ndovu wanakula tena!

Mheshimiwa Naibu Spika, ndovu wanatoka mbali sana, sisi hatujapakana na hifadhi, wamekuja kwa sababu ya mazingira mazuri tuliyonayo kwamba tuna misitu ya asili, tuna maeneo yana maji na bahari. Wakifika wanakaa msituni, usiku wanakwenda kula kwenye mashamba ya watu, mchana wanakwenda kupata upepo wa bahari, ndiyo mazingira yaliyowavutia! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema very serious, juzi nimeomba Mwongozo hapa lakini mpaka sasa hakuna hatua iliyochukuliwa Mheshimiwa Waziri. Nazungumza kwenye Wizara hii kwa sababu wale watu watakapoishiwa chakula, watapeleka tena. Juzi walipeleka tani 500 kwa sababu chakula kimekwisha. Nikienda tena kuwaomba tani 1,000 wasininyime kwa sababu ndovu ambaye anawatunza Mheshimiwa Waziri wa Maliasili wanakula vyakula vya wakulima wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza nianze kwa kusema kwamba katika hotuba ya Kambi ya Upinzani niliweka utafiti kadhaa uliofanywa na TWAWEZA na sisi tunawaamini TWAWEZA kwamba ni Taasisi iliyosajiliwa na inachokifanya nadhani Serikali wanajua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina wasiwasi kwamba tumeendelea kurudia kosa ambalo mwaka 2016 tulilifanya la kuendelea kutenga fedha nyingi za nje tukitegemea kwamba tuzipeleke kwenye miradi ya maji vijijini, fedha ambazo hazitoki. Ukisoma randama, inaonyesha kwamba katika hizi shilingi bilioni 623 za maendeleo zilizotengwa mwaka huu, shilingi bilioni 214 zinategemewa kuwa ni fedha za wahisani. Kwa bahati mbaya, kati ya hizo 214 shilingi bilioni 130 zinakwenda kwenye miradi ya maji vijijini. Wasiwasi wangu ni kwamba, tutaendelea kufanya kosa lile lile, Waheshimiwa Wabunge watakuja hapa mwakani kulalamika kwa sababu fedha hizi hazitatoka na miradi ya maji vijijini itakwama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wazungumzaji waliopita wamesema, kwamba kulikuwa na haja leo Mheshimiwa Waziri wa Fedha awepo, namwona Naibu Waziri wa Fedha yupo. Atakapokuja kuchangia aseme, kwa nini fedha za mwaka 2016 za Wahisani hazikutoka? Unakuta mradi ambao Wahisani waliahidi shilingi bilioni 41 wametoa shilingi bilioni moja; ni kana kwamba wanatutania, huu ni mzaha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili lazima tuliweke wazi, kwamba hizi fedha shilingi bilioni 214 za Wahisani ambazo mnazitegemea, ni fedha ambazo mimi naziona kama kiini macho, sizitegemei kupatikana. Lazima Serikali ije na maelezo, kwa nini fedha za Wahisani hazitoki? Isiwe tunaishia tu kwamba tunapanga tunazitumaini shilingi bilioni 200 zitakuja, halafu hazitoki na Serikali haiji na maelezo kwamba kwa nini hatukupata fedha kutoka kwa Wahisani?

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwamba sh.50/= iongezeke ili fedha za Mfuko wa Maji uweze kuongezeka. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Maji, tumetembelea miradi mingi. Hizi fedha asilimia 19.8 zinazosemwa, kati ya hizo, zaidi ya 8% mpaka 9% ni fedha za Mfuko wa Maji. Kwa hiyo, kama siyo Mfuko wa Maji kuwa na fedha, leo tungekuwa tunazungumza chini ya asilimia 10 ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hii. Kwa hiyo, tunahitaji fedha iongezeke ili angalau mwakani bajeti iwe imetekelezwa kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie miradi ya skimu za umwagiliaji. Mheshimiwa Waziri aje atueleze, kuna skimu nyingi nchi hii, karibu kila Halmashari. Zilianzishwa mwaka 2014/2015, 2015/2016 na 2016/2017, fedha zimeliwa. Mfano mzuri ni Skimu ya Umwagiliaji Narunyu pale Kiwalala kwenye Halmashauri yetu, shilingi milioni 600 imeliwa, halafu Mkandarasi anasema kwamba Designer alikosea. Kwa hiyo, hizi shilingi milioni 600 zimeliwa, nani ana-compensate?

Mheshimiwa Naibu Spika, kilio hiki hakipo Lindi Vijijini tu, kipo karibu nchi nzima. Aje na maelezo, kuna miradi mingi na kwenye hotuba ya kambi tumeorodhosha. Aje atujibu kwa nini miradi ya umwagiliaji imetafuna fedha za Watanzania halafu imeishia katikati na hakuna maelezo? Atueleze, hao waliohusika na wizi huu wamewajibikaje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie suala la Bonde la Rufiji. Nasikitika sana, leo nchi hii tunalia na njaa. Bonde la Rufiji lina maji the whole season. Ukipita pale unakutana na maji, yapo. Bonde liko zuri, kwa hiyo, katika kilimo cha mwagiliaji kwa nini hatulitumii? Leo tunalalamika kwamba tuna njaa, wenzetu, jirani zetu hapo South Sudani wana vita, wenzetu Wakenya wanahitaji chakula, Ethiopia wanataka chakula; tunashindwa kutumia chanzo ambacho tungeweza kukitumia kama pato letu la Taifa? Lingeongeza pato; lakini pia leo tusingekuwa na malalamiko kwamba chakula hakuna nchi hii. Tungekuwa na chakula ambacho tungeweza kusaidia hata Mataifa mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba maelezo ya kina. Kwa nini bonde la Rufiji halitumiki? Sisi tunaopita pale kila siku kwenda Lindi na kurudi, tunajisikia aibu. Mwaka 2016 nilisema hapa, wale RUBADA; kitu kinachoitwa RUBADA, kama kuna watu wanaofilisi nchi hii, wale wanaongoza, kwa sababu hakuna wanachokifanya. Wako pale, sasa hivi wamekuwa kama madalali wa kuuza ardhi, madalali wa kuingiza mifugo; ng’ombe kuingia pale, hakuna zaidi ya hilo. Kwa hiyo, naomba maelezo ya kina juu ya suala hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kwa mwaka huu naomba niwatakie Waheshimiwa wote heri ya mwaka mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na suala la Halmashauri na Uongozi kwenye halmashauri na kikubwa nitaomba, usikivu wa Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI, kwamba kama kuna changamoto kubwa ambazo taarifa ya Kamati imeziainisha, kukusanya mapato madogo, kutopeleka fedha za asilimia 10 na mengine. Changamoto kubwa tuliyonayo ni aina ya Wakurugenzi tulionao kwenye Halmashauri zetu. Uwezo na utendaji kazi wa Wakurugenzi wa nchi hii kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kama utaamua kufanya assessment ya kupima performance ya Wakurugenzi wako ni sehemu kubwa ya watu wanaokuangusha wewe na wanaoingusha Serikali kwa sababu ya uwezo wao. Hii imetokana na namna walivyopatikana, kama ingekuwa Wakurugenzi walipatikana kwenye mfumo ule wa kawaida wa Watumishi wa Umma huu upungufu mwingine usingekuwepo leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, jambo ambalo nataka niliseme kama kuna jambo ambalo nilifikiria ningeliona kwenye taarifa ya Kamati na hii ni challenge kwa Kamati ya LAAC kwamba Kamati ingekuja na mapendekezo ya kushauri Bunge, liishauri Serikali namna ya upatikanaji wa Wakurugenzi, Wakurugenzi walioteuliwa na Mheshimiwa Rais wengi uwezo wao wa ufanyaji kazi ni mdogo hauendani na majukumu yaliyopo kwenye Halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda ukamhoji Mkurugenzi namna anavyofanya kazi wewe mwenyewe unajiuliza kwamba huyu hivi tangu lini amekuwa Mtumishi wa Umma. Huko kwenye Halmashauri kuna migogoro mikubwa kati ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwa sababu Wakuu wa Idara wana-perform vizuri kuliko Wakurugenzi. Haya wote mnayashuhudia kama Waheshimiwa Wabunge mnashiriki kwenye vikao vya Halmashauri vya Madiwani kwenye Mabaraza kule wote mtakuwa mashahidi. Aina ya Wakurugenzi wetu ni wana-perform vibaya mno. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tulitakiwa tuanzie hapa, siku moja nilipokuwa namsikia Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI anasema tutajenga viwanda 100 kwenye kila Mkoa nilikuwa najiuliza kwamba hao watu wenyewe wa kusimamia wako wapi. Yaani jambo moja ambalo lili-click kwenye kichwa changu hao watu wenyewe wa kusimamia wako wapi. Pale kwangu kuna watu wametaka kuja kuanzisha viwanda tangu mwaka jana mwezi wa Tisa mpaka leo kupewa ardhi tu ile watu watatu, wanataka kuja kuanzisha viwanda vya kuchakata muhogo mpaka leo watu watatu Mkurugenzi ukimuuliza anasema sijui kitu gani hakijakamilika najua ni kwa sababu ya performance uwezo walionao ni mdogo kweli. Hilo jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusu suala la miradi ya maji hususani ile ya vijiji 10 kwenye kila Halmashauri pamoja na miradi ya umwagiliaji. Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi kama kuna jambo ambalo nchi hii Serikali imepata hasara kubwa ni kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji kwenye Halmashauri na nafikiri more than 70% ya ile miundombinu sasa haifanyi kazi. Kamati ilitakiwa ije na ripoti ituambie kila halmashauri ni halmashauri gani angalau imefikia 50% hakuna, angalau kama kuna miradi ilianzishwa vijiji 10 ya maji ambayo imeweza kuitekelezeka kwa asilimia 50 kwenye Halmashauri hakuna. Huu ni uthibitisho kwamba kuna fedha zimetumika vibaya na kuna fedha zililiwa vibaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni la msingi sana kwenye Halmashauri na hili nilivyokuwa nalifikiria nikaona kwamba, kama kuna uwezekano labda wale Wakuu wa Idara ya Maji labda waondoke kuwa monitored na TAMISEMI ili wawe moja kwa moja kwenye Wizara ya Maji ama watoke Wizara ya Maji waende moja kwa moja TAMISEMI. Hapa naona kuna-contradiction namna mnavyofanya kazi, inawezekana namna ya upelekaji wa maagizo yanakwenda yanawachanga wale watu, kwamba Wizara ya Maji wanaweza kusema hivi TAMISEMI ikasema, ikapelekea kukawa na shida kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, naamini kuna miradi mingi ya maji ilianzishwa tena kwa lengo jema na Serikali kule kwenye halmashauri miradi ile haifanyi kazi. Halafu hakuna continuation hakuna mwendelezo leo unaweza ukakuta limeanzishwa hili kesho lile halijakamilika linaenda kuanzishwa lingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mradi pale ulijengwa na TAMISEMI tena lambo la kunyweshea mifugo, ulijengwa uligharimu karibu milioni mia mbili haujakamilika, haufanyi kazi tumeenda mwaka huu kwenye bajeti ya halmashauri unaenda kuanzishwa tena mradi mwingine ambapo hata huu wa kwanza haujakamilika. Sijui kama TAMISEMI wanajua, sijui hiyo Wizara yenyewe ya Mifugo inajua kwa sababu naona kama mambo yanajichanganya changanya tu. Hilo jambo lingine ambalo ni la msingi sana nilitaka nilizungumzie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu katika ukurasa wa 65 wa kitabu cha LAAC Kamati inaomba Bunge kuazimia kuunda Kamati Maalum ya Bunge itakayochunguza sababu na chanzo cha tatizo la miradi ya maji kutotekelezwa. Ndiyo hili nilikuwa nalisema kwamba, kama Bunge litaona inafaa naunga mkono hoja hii kwamba Bunge liunde Kamati ipitie kwenye kila Halmashauri, ikachunguze ni miradi mingapi ya maji ilianzishwa ile ya vijiji 10 pamoja na umwagiliaji iliyoanzishwa na TAMISEMI, tuone mingapi inafanya kazi na mingapi haifanyi kazi. Katika hii tutagundua madudu mengi kweli kweli kwa sababu Halmashauri nyingi hazijatekeleza vizuri hili suala. Kwa hiyo, naomba niunge mkono hili suala la kuunda Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni Halmashauri kutokupewa pesa kwa wakati, wakati mwingine haya yote tunayasema kwamba Wakurugenzi hawafanyi kazi, uwezo wao mdogo ni kweli, lakini jambo lingine kwamba hizo fedha zenyewe za kufanyia kazi wanazipata wapi. Unakwenda kwenye halmashauri leo mwezi huu tupo karibu kwenye quarter ya tatu unakuta fedha za development kutoka kwenye Serikali Kuu labda wamepata asilimia 15, asilimia 20 unajiuliza sasa huyu Mkurugenzi hapa anafanya kazi gani kwa sababu upatikanaji wa fedha kutoka Serikali Kuu ni kikwazo na Mheshimiwa Waziri wa Fedha bahati yupo hapa alieleze Bunge tatizo ni nini. Leo kwenye Halmashauri tunapitisha bajeti kwa ajili ya Mwaka wa Fedha 2018/2019, fedha za mwaka 2017/2018 hazipo, fedha za maendeleo hazipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine linalokwamisha maendeleo kwenye Halmashauri zetu ni Serikali Kuu kutopeleka fedha kwenye halmashauri zetu.

Jambo hili ni hatari linaua moja kwa moja Halmashauri ya Wilaya. Leo tunalaumu fedha za asilimia 10 haziendi, halmashauri inapewa maagizo ya kutumia fedha hizi za ndani kwenye kuajiri watumishi. Nimesikia hapa leo mmoja wa Waziri anajibu kwamba halmashauri itumie fedha za ndani kuajiri watumishi. Fedha hizi ambazo zingepaswa kupelekwa kule kwa vijana zile asilimia 10 kwa wanawake na walemavu, leo Waziri anakuja kusimama anatolea agizo waajiri watumishi

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, jambo lingine ambalo linakwamisha ni suala la fedha kutoka Serikalini ziende kwenye halmashauri na jambo hili pia linapelekea halmashauri kuwa na mzigo mkubwa kwa sababu hata yale mapato yetu ya ndani ambayo asilimia 60 tumepanga kupeleka kwenye maendeleo, tunaondosha tunapeleka kwenye maeneo ambayo yalipaswa yagharamiwe na fedha za Serikali Kuu. Kwa hiyo, hili ni jambo la msingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka nilimalizie ni kuhusu suala la Halmashauri kukosa mapato ya ndani kadri tulivyopanga. Unakuta tumepanga tukusanye labda milioni 300 kutoka kwenye mazao ya wakulima kwa mfano mbaazi. Halmashauri yetu sisi ambayo mbaazi ni chanzo kikubwa cha mapato tunashindwa kukusanya ule ushuru kwa sababu mbaazi imekosa soko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama kuna jambo ambalo lingine ni la msingi sana ni Serikali kujielekeza katika kutafuta masoko ya mazao ya wakulima kwa sababu mazao yakikosa soko halmashauri hazipati pesa za kujiendesha. Kwa hiyo, leo mbaazi inauzwa mpaka Sh.150, Sh.200 halmashauri hii itatoza ushuru wa shilingi ngapi kwa mkulima ili ipate mapato yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, jambo la Serikali kutafuta masoko sio jambo la blaa blaa linalohitaji majibu mepesi ni jambo la lazima kwa sababu Serikali ipo kwa ajili ya wananchi na wananchi lazima watafutiwe masoko na Serikali iwahudumie wananchi wake, lisiwe jambo sasa la kuja hapa fulani amesema hivi, hili Lindi hawataki, tunahitaji majibu ya kweli kwamba mtu akilima mbaazi zake apate soko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru kwa dhati kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia hotuba ya bajeti ya Wizara hizi mbili; Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Utumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kwa kazi kubwa anayoifanya. Kiukweli amethibitisha kwamba anaweza, ingawa Wizara hii ina changamoto nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa Wabunge wote hapa leo ukiwauliza kama kweli tunahudhuria kwenye vikao vyetu vile vya Halmashauri vya Madiwani, hakuna mtu ambaye halalamiki juu ya fedha kutoka Hazina kutopelekwa Halmashauri. Kama kuna Mbunge hapa leo anaweza akatuthibitishia kwamba fedha wanapelekewa kwa wakati na kadri zilivyopagwa basi labda hiyo ni Halmashauri ya nchi nyingine haipo Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo haliko kwingine, tatizo liko kwa Wizara ya Fedha, tatizo analo Mheshimiwa Dokta Mpango. Kwa nini fedha za miradi mikubwa yote, Mheshimiwa Dokta Mpango, anazo, kwa nini fedha za Halmashauri ambako ndiko waliko wananchi, ndiko wanakohudumiwa wananchi wa chini, fedha hana kwa nini? Tunapokwenda kwenye vikao vya Halmashauri, Wakurugenzi tukiwabana wanatuambia ninyi ndiyo mnatoka Bungeni na ninyi ndiyo mko na Waziri wa Fedha huko, muulizeni kwa nini haleti fedha. Kwa hiyo, mtu mmoja ambaye labda anaweza kukwamisha Wizara ya TAMISEMI isifanye kazi vizuri ni Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa sababu hapeleki fedha Halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, ni suala la watumishi, Ofisi ya Utumishi, Mwenyekiti wangu wa Kamati ameeleza hapa kwamba mwaka huu Wizara inayoongozwa na Mzee wangu, Mheshimiwa Kapteni Mkuchika, bajeti yake imepungua kwa shilingi bilioni 152 kutoka kwenye bajeti ya mwaka jana na hii ndiyo Wizara inayoajiri, hii ndiyo Wizara inayosimamia Utumishi wa Umma nchi hii. Sasa tunataka Mheshimiwa Waziri atueleze, hiki kiasi kilichopungua cha bilioni 152 maana yake ni nini? Kwamba shughuli za kuajiri hazitafanyika tena, kwamba hakuna ajira mpya, kwamba hakuna promosheni? Maana suala la kuongezwa mshahara nadhani Watumishi wa Umma sasa hivi wameshalisahau, limeshaondoka kwenye utamaduni wa kawaida. Hata hivyo, hata kuajiri hamtaajiri kama shilingi bilioni 152 mnaiondoa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, napata shida nikisikiliza kwamba Rais anasema mwaka huu tutaajiri, napata shida ukisikia Viongozi wa Serikali wanasema tutaajiri watumishi wa afya, unapokuja kusoma vitabu vya bajeti unakutana na fedha zimepungua kwa bilioni 152, napata shida kuamini kwamba haya yanayosemwa kweli yatatekelezwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kwenye TAMISEMI, nizungumzie suala la zahanati. Kwenye Halmashauri zetu tumejenga zahanati nyingi. Mheshimiwa Waziri, zahanati zimekamilika na nyingine zinabomoka, zimechakaa, zimekaa miaka minne, mitano, hazifunguliwi kwa sababu hazina watumishi. Sasa naomba kujua, nini mpango wake wa kutafuta watumishi wa idara za afya ili waende wakafungue zahanati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimboni kwangu kuna zahanati tano zimekamilika, mbili Mheshimiwa Rais alipokuja mwaka jana mwezi wa Tatu alitoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa kwamba hakikisha ndani ya miezi miwili ziwe zimefunguliwa, mpaka sasa zile zahanati hazijafunguliwa. Naomba Mheshimiwa Waziri amfikishie salamu Mheshimiwa Rais kwamba zile zahanati mbili zilizojengwa na mfadhili pale Mchinga na Ruvu ambazo Mheshimiwa Rais alitoa order zifunguliwe ndani ya miezi miwili, hazijafunguliwa, naomba ampelekee salamu hizo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya TAMISEMI, nimesikitishwa sana kuona kwamba Mawaziri wanatoa order kupeleka kwa Wakurugenzi na Wakurugenzi hawatekelezi, hili jambo linaumiza sana na wala siyo jambo la kushabikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka juzi 2016 humu wakati tunachangia bajeti tulisema kitendo cha Wakurugenzi kuwa wateule wa Rais italeta contradiction kwenye Utumishi wa Umma, tulisema humu na mkichukua Hansard mtaona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mkurugenzi hamuheshimu Mheshimiwa Waziri kwa sababu yeye aliyemteuwa ni Rais na Waziri kateuliwa na Rais na inawezekana ndani ya Chama yeye ni kada mkubwa anawadhifa mkubwa kuliko Mheshimiwa Waziri. Kwa hiyo anaona kwamba mimi ni kada mkubwa na mimi nimeteuliwa na Rais huyo huyo aliyemteua yeye inakuwaje katika mazingira ya kawaida Mkurugenzi anapelekewa order na Mheshimiwa Waziri na hatekelezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa eti Mheshimiwa Waziri ambaye amedharauliwa kaka yangu Mheshimiwa Kigwangalla, sisi tunakutetea wewe ili ufanye kazi vizuri na wewe unakuja kutetea ulivyodharauliwa! Wabunge hatupendi kuona Waheshimiwa Mawaziri mnadhalilishwa hatupendi kuona mnatoa order ambazo Wakuu wa Mikoa ama Wakurugenzi hawataki kuzitii. (Makofi)

Najua kwamba najadili bajeti za Ofisi ya Rais, Mheshimiwa Mpango hili nalielekeza moja kwa moja, Waislamu mwezi huu tunaita mwezi wa Rajab, tuko kwenye mwezi wa mfungo kumi, tunakaribia kabisa kuingia kwenye mwezi Mtukufu wa Ramadhan kufunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuulize Mheshimiwa Mpango, hivi Serikali hii itashindwa kuongoza, mtashindwa kukusanya kodi ikiwa tu mmeachia tende ziingie bure ikiwa tu tende peke yake mtaziruhusu ziingie bila kodi mtashindwa kuongoza Serikali? Kenya tende zinaingia free, Mozambique tende zinaingia free, Zanzibar wana mwaka wa saba tende free, huku Bara tende zinatozwa kodi! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme inawezekana hamtuelewi tukisema kwamba, moja ya nguzo kubwa kabisa za Uislam ni kufunga na tunapofunga kuna sunna na kuna mambo ya faradhi. Jambo kubwa katika sunna katika funga ya Ramadhan ni Muislam kufungua kwa kutumia tende, leo tende mnaitoza kodi, hivi Kenya na wenyewe hawatozi kodi tende, Mozambique hawatozi kodi tende, Zanzibar hawatozi kodi tende na ninyi hapa jamani hamuoni aibu au ndiyo yale aliyosema bwege Waislamu hawana wa kuwasemea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuwa mchangiaji wa mwanzo katika kipindi hiki cha jioni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajadili bajeti ya Wizara ambayo inachukua takribani theluthi moja ya bajeti yetu ya nchi. Kwa hiyo, tunavyojadili bajeti ya Wizara hii kwanza ni vizuri ingependeza tukaondoa ushabiki tulionao badala yake tukachukua dhima na kazi yetu kama Bunge ya kuishauri na kuisimamia Serikali kwa sababu ni Wizara ambayo inatengewa fedha nyingi za kodi za walipa kodi wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la barabara zetu kujengwa na kuharibika mara kwa mara. Ni jambo la aibu sana kwamba barabara za nchi hii zinapojengwa kila ukifika wakati wa masika zinaharibika, kana kwamba wakandarasi wanaojenga barabara za Tanzania hawajui kama Tanzania inapata mvua kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inatia hasira wakati mwingine ukiona kwamba barabara za Tanzania zilizojengwa kwa kiwango cha lami, ukifika wakati wa masika mvua zikinyesha basi zinabadilika na balaa lake katikati ya barabara utakuta madimbwi ya maji, kitu kinachopelekea kuchangia ajali mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi juzi nilikuwa nasafiri natoka Lindi nakuja Dar es Salaam, barabara ambayo imejengwa si zaidi ya miaka sita, miaka mitano iliyopita sasa hivi karibu barabara nzima inahitaji repair. Ni barabara ambayo nadhani imejengwa mwishoni kabisa mwa kipindi
cha Rais Kikwete, lakini ukipita sasa hivi ukitembea bila kuwa na tahadhali ni jambo la hatari sana. Sasa nashangaa kwamba tunapojenga barabara zetu hivi hakuna chombo kinachodhibiti ubora wa ujenzi wa barabara hasa hizi barabara za lami?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hakuna chombo nashauri, kwa kuwa tunatumia bilions of money kwenye suala la ujenzi wa barabara za lami, nashauri Bunge kama kuna nafasi ya kuunda Kamati Bunge lingeweza kuunda Kamati ya kuchunguza mikataba ya barabara hasa hizi trunk road ambazo zimejengwa ni barabara kubwa na zina umuhimu mkubwa katika uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiingii akilini kuona barabara ya Lindi - Dar es Salam imejengwa juzi, leo hii barabara nzima ina viraka na kwa kweli ni barabara ambayo inatia kichefuchefu kabisa ukiwa unatembea kwenye ile barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni suala la ufufuaji wa shirika la ndege. Tunapaswa tuelewane humu kwamba hakuna mtu ambaye anakataa au anapinga shirika la ndege lisifufuliwe hakuna. Tunachopenda kushauri ni namna na njia inayotumika kulifufua shirika la ndege. Mathalani nyie wote mashahidi na Naibu Mawaziri wapo hapa wanasoma ripoti za IATA (Shirika la Ndege la Duniani) mnaona nini kinachoendelea kwenye mashirika ya ndege mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa takwimu zilizopo kwa mwaka mmoja mashirika ya ndege duniani yanapata hasara ya dola za Kimarekani bilioni nane kwa mwaka. Kwa Afrika pekee mwaka uliopita mashirika ya ndege yalipata hasara ya dola milioni 600, kwa Afrika pekee. Sasa ikiwa hali ndio hii tunapokwenda kulifufua shirika letu la ndege lazima tuwe na tahadhari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tahadhari mojawapo wako Wabunge wamechangia hapa walikuwa wanahoji kwamba hivi inakuwaje tuna ndege ambazo zinasafiri ndani ya nchi tu lakini wateja wetu wako mikoani tuna viwanja vya ndege havina taa, ndege hazitui usiku. Ni kana kwamba wakati tunanunua ndege tulijua labda tutasafiri kwenye viwanja vya kimataifa vya nje ya nchi, lakini najua kusudio la kununua bombadia zitumike ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama tumenunua ili zitumike ndani, kwa nini zaidi ya viwanja vya ndege zaidi ya asilimia 70 viwanja vya ndege nchi hii havina taa za usiku. Ndege zinapumzika, Mzee Zungu alikuwa anasema hapa ndege sio chombo kinachohitaji kupumzika, kwamba kimefanya kazi mchana usiku kipumzike hapana ndege zinasafiri wakati wote mchana, asubuhi, jioni, usiku, alfajiri wakati wote na nyie wote mnasafiri ni mashahidi mnajua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa inakuwaje ndege za Tanzania zinafanya kazi asubuhi, zinafanya kazi mchana ikifika usiku zinapumzika ni kama mabasi ya abiria vile, kwamba ikifika saa sita usiku basi yaache kusafirisha abiria labda wanaogopa kutekwa mimi sijui. Kama kweli tumekusudia kufufua shirika la ndege, jambo la kwanza lilipaswa kujenga miundombinu, tulitakiwa tujenge miundombinu ambayo itaendana na ufufuaji wa Shirika la Ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitawapeni mfano, wote mnasafiri, ukifika Ethiopia pale Addis Ababa pale Bole International Airport jambo la kwanza utakaloliona ule uwanja wa ndege umezungukwa na hoteli kubwa za kifahari. Hii maana yake ni nini? Ni kwamba wanatoa picha kwamba Ethiopia Airlines inachangia kwa kiasi kikubwa sana biashara ya utalii na biashara ya hoteli ndio jibu wanalotoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi shirika letu la ndege hatuna hoteli ambazo ni nzuri tumezijenga ama zipo tumezi- attract, pia ndege zenyewe zinasafiri kuanzia saa 12 asubuhi mwisho saa 12 jioni maana yake ni kwamba tunatoa huduma kama huduma ya zahanati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukianza kufanya upembuzi yakinifu na tukaondoa ushabiki tukapima tunachokiingiza kwenye shirika letu la ndege tutakuwa tunapata hasara kubwa sana mimi sijawahi kuona shirika la ndege ambalo hili leo tunataka tulifufue, liwe linafanya kazi wakati wa mchana tu, tutapata hasara kubwa sana. Kwa hiyo, lazima tuchukue precaution kubwa kwamba kwa kuwa tunetenga pesa nyingi za walipa kodi wa Tanzania, basi haya mengine yaendane ili tuweze kupata faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida ya mashirika ya ndege siku hizi watu hawaangalii tiketi , hawaangalii collection yatransport,ukiangalia huko hakuna Shirika la Ndege linazalisha pote, hata hiyo unayosikia Emirate unasikia Dubai Air, unayosikia Quatar Airlines, hawaangalii fedha ya tiketi wanaangalia income inayopatikana kutokana na sekta zingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa kuwa Shirika la Ndege ni catalyst ya maendeleo, iwe inachangia maendeleo kwenye sekta ya utalii, iwe inachangia maendeleo kwenye sekta zingine, ndio kinachoangaliwa, huangalii tiketi za ndege, hakuna shirika la ndege linapata faida kwa kuangalia tiketi, hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka nizungumzie ni suala la upandishaji wa barabara zetu, mimi nina barabara pale jimboni kwangu, ina miaka kadhaa tunaiombea ipande lakini sijaona hapa inapandishwa. Naomba sana barabara yetu ya Chikonji - Nangalu kwenda Milola ina urefu wa zaidi ya kilometa 100, waipandishe, watu wa TARURA hawaiwezi na nature ya ile barabara angekuwepo Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa yeye ni shuhuda mkubwa sana kwa sababu wakati mwingine anaitumia kwenda kwake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nature ya ile barabara ni lazima iingie TANROAD ndio inawezekana ikafanyiwa marekebisho lakini hivi sasa inafika wakati kwamba tumeitumia season, kuna wakati hatuwezi kuitumia kabisa kwa sababu kuna madaraja makubwa yamekatika na inahitaji ukarabati mkubwa fedha za TARURA haiwezi kabisa kujenga ile barabara, kwa hiyo naomba hilo jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nimepitia bajeti ya ukarabati wa hizi barabara za TANROAD ukiangalia hii bajeti na nimepitia vizuri sana kwa mikoa, mkoa ambao umepunjwa sana kuliko yoye ni Mkoa wa Tabora na bahati nimewasikia Wabunge wa Tabora wakisemea jambo hili, lakini mkoa uliofuatia ni Mkoa wa Lindi, yaani sisi Lindi tuna kilometa za barabara TANROAD kilometa 629 lakini kwa bahati mbaya tumepewa shilingi milioni 800.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo linasikitisha sana kwamba ukiangalia mikoa mingine ambayo wana kilometa 400, wana kilometa 300, wanapewa fedha nyingi, sisi wenye kilometa 600 tunapewa shilingi milioni 800. Jamani mtuangalie na sisi Lindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo inayosemwa korosho, ufuta inahitaji ipite kwenye barabara, inahitaji isafirishwe. Kwa mazingira haya tuliyonayo hivi sasa maana yake ni kwamba utafika wakati tutashindwa kusafirisha mazao yetu ya biashara na huo uchumi unaosemwa hautaweza kukua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, ni suala la mitandao, tunao Mfuko wa Mawasiliano, hebu na sisi tuleteeni, nimeona kwenye ripoti yao nimepata angalau vijiji viwili pale jimboni kwangu, lakini uhalisia ni kwamba zaidi ya vijiji 15 vinahitaji kupata minara ambayo itawezesha wananchi kupata mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana waingize kwenye record zao Vijiji kama vya Mputwa, Kiwawa, Namkongo, Nyamnyangala, Kijiweni, Mvuleni na Ruvu; hivi vijiji waviingize kwenye orodha ili viweze kupata fedha ya Mfuko huu na sisi tuweze kujengewa minara ili na sisi tuwe tunaishi katika Tanzania hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuweza kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watanzania wote wana haki ya kushtaki ama kushtakiwa isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jambo linaloshangaza, mwanafunzi yupo kwenye kiwango cha elimu ya juu anafanya masomo yake ya degree ya kwanza university anashtakiwa, prospectus ya chuo yaani kanuni ya uongozaji wa chuo inazuia mwanafunzi yule asiendelee na masomo, ni jambo la kushangaza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya chuo kikuu ni tertiary education na tafsiri yake ni third level education, ni elimu ya ngazi ya tatu. Amepita elimu ya msingi, elimu ya sekondari, university education level ni elimu ya watu wazima. Wanaosoma pale sio lazima wawe vijana, wengine ni watu wazima; wengine wanashtaki na wengine wanashtakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Elimu, jambo la mwanafunzi Abdul Nondo kuwa ameshtakiwa na chuo kikamsimamisha masomo, it is contrary to human rights, very contrary. Kama prospectus ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inasema hivyo, prospectus ya namna hiyo haifai na sheria hiyo inapaswa ifutwe. Ni sheria isiyokwenda na wakati lakini pia inanyima na inazuia haki za binadamu lakini pia inakwenda kinyume na Katiba yetu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaoa fursa ya mtu kushtaki na kushtakiwa. Sasa hivi ni kweli wanafunzi wote waliopo vyuo vikuu aliyekuwa na kesi mahakamani ni Abdul Nondo peke yake? Hivi ni kweli? Kwa hiyo, kama sheria za chuo zinasema hivyo, sheria hii hebu ifuteni, inawatia aibu, vinginevyo mtuambie kwamba jambo hili mmelichukulia kisiasa.

T A A R I F A . . .

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na taarifa yake nimeipokea kwa msisitizo kabisa.

Jambo hili linakichafua Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tuseme ukweli, to be sincerely, hadhi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inashuka kwa sababu mnataka kuwaingiza kwenye siasa. Hata hapo UDSM tukifanya leo sensa ya wanafunzi wangapi wenye kesi mahakamani hawatapungua hata wanafunzi 20, 30 lakini aliyeonekana mwenye makosa ni mmoja tu, this is quite unfair. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, kama ingekuwa vyuo vikuu vinafanya mtihani wa pamoja kama ilivyokuwa elimu ya sekondari, vyuo vikuu vya Serikali vingekuwa vinashindwa kama ambavyo shule za sekondari za Serikali zinashindwa dhidi ya shule binafsi. Pamoja na mambo mengine yanayochangia ni hizi kanuni na sheria zilizopo kwenye vyuo, hizi prospectus za chuo Mheshimiwa Waziri jaribuni kuzipitia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo mimi nimesoma pale. Hivi unakwendaje kwenye chuo unakuta kuna mchepuo au fani wanafunzi wanasoma, chuo cha Serikali miaka mitatu wanahitimu, wakienda Serikalini wanaambiwa hii haitambuliki, yaani chuo cha Serikali lakini mtu amehitimu anaambiwa haitambuliki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere watu wamesoma faculties zaidi ya tatu, lakini mwisho wa siku wanaambiwa hizi hazitambuliki. Sasa chuo cha Serikali inakuwaje wanasomesha kitu ambacho hakitambuliki? Jambo hili na lenyewe ni la aibu sana. Mheshimiwa Waziri nitakuja kukupa orodha ya hizo faculties ambazo wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wamezisoma, leo mtaani huko wakiomba ajira wanaambiwa kwamba hizi hazipo kwenye system ya Lawson na huwezi kuajiriwa, ni jambo la aibu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo langu la Mchinga lina shule nyingi za sekondari. Shule ya Sekondari ya Mchinga sasa ni kongwe inafanya vizuri sana, ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri, tumeomba muipandishe hadhi iwe shule ya A-Level. Naomba sasa Mheshimiwa Waziri mwaka huu uje unithibitishie kwamba ile shule mtaitengea fedha. Shida yetu sisi ni mabweni tu, mkitupatia mabweni shule itapanda hadhi, ina walimu wa kutosha, ina walimu wengi wenye degree, ina wanafunzi wengi, lakini pia catchment area yake ina shule nyingi ambazo wanaweza wakai-feed shule ya sekondari Mchinga ikaweza kuwa shule ya A-Level na ikaweza kufanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni jambo la kuhamisha walimu kuwatoa shule za sekondari kuwapeleka shule za msingi. Jambo hili sio baya kwamba kama dhamira ni hiyo sio mbaya, tatizo ni namna linavyotekelezwa. Leo mwalimu aliyesomea kufundisha wanafunzi wa sekondari anakwenda kupelekwa akafundishe wanafunzi wa darasa la kwanza, darasa la pili bila kumfanyia orientation, jambo hili haliwezi kuwa na tija. Walimu wenyewe wana frustrations za kutosha, information yenyewe haijatolewa vizuri, namna ilivyochukuliwa na Wakurugenzi kule chini Mkurugenzi huyu analitekeleza kivyake, Mkurugenzi mwingine anatekeleza kivyake, wengine wamepewa fedha ya uhamisho…

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme kwamba Mheshimiwa Waziri amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuzungunguka kwenye Mikoa yetu kufuatilia shida ya maji na Mheshimiwa Naibu Waziri kwa hilo tu mnalifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingekuwa kwamba kama Wabunge tunakubaliana mimi ningetoa hoja ama mtu yeyote atoe hoja kwamba Wizara hii tusiipitishe mpaka Waziri wa Fedha aje kutoa commitment ndani ya Bunge kwamba kwa nini fedha za miradi ya maeneleo hazipelekwi kwenye Wizara ya Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani ya chama kinachoongoza, Chama cha Mapinduzi, hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa wakati anazindua Bunge aliongea kwa msisitizo kwamba anakusudia kuhakikisha kwamba anamtua mama wa Kitanzania ndoo kichwani na Watanzania walimfuatilia na wakamshangilia tukadhani kwamba yale yanayoongelewa tutakuja kuyaona sasa kwenye utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa nipate majibu yafuatayo na wa kutujibu upande wa Serikali ambao ninyi ndiyo mmepewa dhamana na wananchi, upande wa Chama cha Mapinduzi, mtueleze sekta ya maji mmeipa kipaumbele cha ngapi kwenye vipaumbele vyenu. Haiwezekani kwamba Watanzania waliopo vijijini mpaka leo wanaopata maji ni asilimia 56 pekee, haiwezekani, hizi asilimia 44 wanaishije? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko miradi ilianzishwa na World Bank na World Bank wakati wanaanzisha mradi walitoa fedha dola za Kimarekani bilioni 1.4, miaka saba ya utekelezaji wake shida ya maji iko palepale. Hili linatokana na kwamba kulikuwa na usimamizi mbovu wa miradi mingi ya maji iliyokuwa inatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukawa tunapambana na individuals, kuamini kwamba labda Waziri hafanyi kazi, Naibu Waziri hafanyi kazi ama Katibu Mkuu hafanyi kazi, tatizo ambalo linapelekea Watanzania kukosa maji ni mfumo na inawezekana hakuna political will waliyonayo Chama Tawala ya kutatua matatizo ya maji, inawezekana hakuna political will. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa nane na wa tisa inaelezea upatikanaji wa maji vijijini na mijini. Takwimu hizi ambazo Mheshimiwa Waziri amezisoma zina-contradict sana na uhalisia. Lakini pia hata hizi takwimu zenyewe zinajikanganyakanganya ukizisoma na ukazipitia ukafanya calculation kidogo zina tofauti. Kwa mfano, upatikanaji wa vyanzo vya maji kwa Jiji la Dar es Salaam unaonesha kwamba kwa sasa umeshuka kutoka asilimia 85 mpaka asilimia 76, lakini upatikanaji wa vyanzo vya maji siyo upatikanaji wa maji kwa wananchi kwa sababu haya maji yanahitaji usambazaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ukienda ukaangalia namna mtandao wa maji ulivyosambazwa na vyanzo vya maji vilivyopo ni tofauti, na ndiyo maana leo ukifanya mahesabu wakazi wa Dar es Salaam anaopata huduma ya maji, waliounganishiwa kwa huduma ya bomba hawafiki hata robo ya wakazi wa Dar es Salaam. Hili ndilo tatizo, unaweza ukaona kwamba kwenye takwimu tunasema kwamba watu wengi wa Dar es Salaam wanapata huduma kumbe wanaopata huduma ni wachache, walio wengi tunaishi Dar es Salaam, tunatumia maji ambayo mengine siyo salama ni yale maji ya kuchimba wenyewe. Ukifanya research Dar es Salaam watu wengi wamechimba maji chini, yale maji ambayo siyo salama sana lakini mtandao wa maji wa Ruvu Chini, Ruvu Juu na vyanzo vyote vya Dar es Salaam, bado havijawafikia wakazi wengi wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda maeneo ya Temeke, Mbagala huko Chamazi, Kigamboni na maeneo mengi, ukienda ukiangalia mtandao wa maji Dar es Salaam unaona kabisa kwamba maji hayawajafikia, sisi tunaishi Dar es Salaam karibu wote hapa tuna makazi yetu Dar es Salaam tunajua. Kwa hiyo, hizi takiwmu zenyewe ambazo Mheshimiwa Waziri amezisema kidogo zina mashaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nirudi upande wa Wizara ya Fedha na labda Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, hivi Serikali ina diplomatic complication na wahisani tunajiuliza? Ukisoma hotuba ya bajeti ya mwaka 2017 na ya mwaka huu, fedha ambazo wahisani walihaidi kuzitoa hazijatolewa mpaka sasa. Sasa wakati mwingine unajieleza inawezekana Bunge linapaswa kufahamishwa kama kuna matatizo ya kiplomasia baina ya Tanzania na wahizani wetu tuelezwe ili tujue kwamba kinachoendelea kumbe hatupati fedha za wahisani kwa sababu tumenasanasa hapa ili Bunge lichukue hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana wakati tunajadili bajeti hapa ilielezwa kulikuwepo na dola milioni 503 na wako Wabunge waliishabikia kwamba fedha hamuioni kuna dola milioni 503 ipo, mpaka leo mbona haionekani kwenye utekelezaji wala kwenye kitabu humu hakuna. Hiyo dola milioni 503 iliyokuwa imesemwa mwaka jana na tukaambiwa kwamba Waziri wa India alishakuja na ametia sahihi sasa kilichokwama ni wapi, tumenasa wapi ili dola milioni 503 ili iweze kwenda kukamilisha miradi yetu ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ukiangalia Wabunge tunaweza tukasemaa sana hapa, lakini jambo la maji kwa sasa, kwa upatikanaji wa fedha za maendeleo wa asilimia 22 nilidhani Wabunge leo tungesimama pamoja tukasema tunahitaji commitment ya Serikali ama taarifa ya Serikali very intense watuleleze ndani ya Bunge kwamba kwa nini Wizara ya Maji haipewi fedha za maendeleo, haingii akilini kuona Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inapewa asilimia 0.85. Sasa hii mishahara ambayo inalipwa wafanyakazi, wanalipwa ili wafanye kazi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, unaweza kuona kwamba tatizo watu wengi wanaweza kusema kwamba kuna tatizo labda kwenye utendaji tunaweza tuka-deal na personalities, tunaweza tukaona kwamba Katibu Mkuu labda tatizo, ama Waziri tatizo ama Naibu Waziri, kumbe tatizo ni mfumo kwamba fedha hazitolewi labda Waziri wa Fedha anakipaumbele chake yeye tofauti na kipaumbele ambacho vimetajwa kwenye ilani ya chama chenu ama kile kipaumbele ambacho Mheshimiwa Rais alikitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji maelekezo ya kina mje kutueleza namuona Naibu Waziri wa Fedha yupo, jambo la maji ni jambo tete, huko vijijini tunakotoka Watanzania wana shida kubwa ya maji na hili tatizo linapelekea kuwa na tatizo lingine la magonjwa ya mlipuko, kwa sababu maji wanayopata Watanzania ni maji ambayo siyo maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukaongea sana hapa tukajenga hoja tunavyoweza kujenga. Lakini suala linabaki palepale kama Waziri amepewa asilimia 22 ya fedha za maendeleo afanye nini, hiyo asilimia 22 tunaigombania hapa na unajua likitokea swali hapa la Wizara ya Maji, Wabunge wote tunasisima humu kila mtu ana shida ya maji, lakini asilimia 22 ikafanye nini! Wewe mwenyewe leo umeelezea suala la maji Ilala na maeneo mengine, lakini pia kuna haja kubwa ya kuipitia mikataba ya karandasi za maji ambazo zilitolewa pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna shida kubwa upo mradi wa maji uko pale Longido, nilikuwa kwenye Kamati ya maji tuliutembelea mwaka huu una shida kubwa Mkandarasi yupo amepewa fedha zaidi ya asilimia 80 amelaza mabomba tu hakuna kinachofanyika. Kwa bahati mbaya watendaji wa Wizara yako ambao ndiyo waliingia mkataba wanautoa sasa wanataka kujivua baada ya kuona wanaenda kukwama wanawapelekea watu wa Arusha Water Supply ili wakausimamie. Kwa hiyo, mwisho wa siku mtakuja kuona kwamba kumbe usimamizi mbovu umepatikana Arusha Water Supply Agency kumbe tatizo ni Wizara yako. Hivyo, kuna tatizo kubwa pia la kuingia mikataba

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kwa nini taasisi za Serikali hazilipi ankara za maji, huu ni mtihani mwingine. Nikiwa Kamati ya Maji tulitembelea katika Mamlaka ya Maji pale Moshi tulikuta Chuo cha Polisi cha Moshi kinadaiwa shilingi milioni 900, RPC wa Moshi anadaiwa shilingi milioni 300 anaambiwa kwamba sasa tukufungie mita za prepaid anakataa anagoma. Sasa unaweza kuona kwamba kumbe tatizo linalokwamisha maji wakati mwingine maeneo ya mijini ni taasisi za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiwa Arusha yule Mtendaji Mkuu wa Idara ya Maji Arusha aliieleza Kamati kuwa kama Serikali inaweza ikalipa madeni yake yote, yeye hahitaji ruzuku kutoka Wizarani kwako, inakuwaje sasa Idara za Serikali zinatengewa bajeti tunaidhinisha humu kwenye Bunge, bajeti inakwenda wanatumia huduma za maji hawataki kulipa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo siyo tu kwamba mfumo wenyewe haupeleki fedha kwenye Wizara ya Maji, pia hata mfumo hautaki kuzisimamia Taasisi na Idara za Serikali zikaweza kulipa bill zake ili wananchi wakaweza kupata huduma za maji. Hii nayo ni changamoto nyingine Mheshimiwa Waziri unakutana nayo.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nimeona kwenye kitabu chako hapa kuna uchimbaji wa visima vya DDCA nami nimekuomba, Mheshimiwa Waziri naomba vile visima uviweze kuvikamilisha ili wananchi wa Jimbo la Mchinga wapate huduma ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme kwamba Mheshimiwa Waziri amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuzungunguka kwenye Mikoa yetu kufuatilia shida ya maji na Mheshimiwa Naibu Waziri kwa hilo tu mnalifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingekuwa kwamba kama Wabunge tunakubaliana mimi ningetoa hoja ama mtu yeyote atoe hoja kwamba Wizara hii tusiipitishe mpaka Waziri wa Fedha aje kutoa commitment ndani ya Bunge kwamba kwa nini fedha za miradi ya maeneleo hazipelekwi kwenye Wizara ya Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani ya chama kinachoongoza, Chama cha Mapinduzi, hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa wakati anazindua Bunge aliongea kwa msisitizo kwamba anakusudia kuhakikisha kwamba anamtua mama wa Kitanzania ndoo kichwani na Watanzania walimfuatilia na wakamshangilia tukadhani kwamba yale yanayoongelewa tutakuja kuyaona sasa kwenye utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa nipate majibu yafuatayo na wa kutujibu upande wa Serikali ambao ninyi ndiyo mmepewa dhamana na wananchi, upande wa Chama cha Mapinduzi, mtueleze sekta ya maji mmeipa kipaumbele cha ngapi kwenye vipaumbele vyenu. Haiwezekani kwamba Watanzania waliopo vijijini mpaka leo wanaopata maji ni asilimia 56 pekee, haiwezekani, hizi asilimia 44 wanaishije? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko miradi ilianzishwa na World Bank na World Bank wakati wanaanzisha mradi walitoa fedha dola za Kimarekani bilioni 1.4, miaka saba ya utekelezaji wake shida ya maji iko palepale. Hili linatokana na kwamba kulikuwa na usimamizi mbovu wa miradi mingi ya maji iliyokuwa inatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukawa tunapambana na individuals, kuamini kwamba labda Waziri hafanyi kazi, Naibu Waziri hafanyi kazi ama Katibu Mkuu hafanyi kazi, tatizo ambalo linapelekea Watanzania kukosa maji ni mfumo na inawezekana hakuna political will waliyonayo Chama Tawala ya kutatua matatizo ya maji, inawezekana hakuna political will. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa nane na wa tisa inaelezea upatikanaji wa maji vijijini na mijini. Takwimu hizi ambazo Mheshimiwa Waziri amezisoma zina-contradict sana na uhalisia. Lakini pia hata hizi takwimu zenyewe zinajikanganyakanganya ukizisoma na ukazipitia ukafanya calculation kidogo zina tofauti. Kwa mfano, upatikanaji wa vyanzo vya maji kwa Jiji la Dar es Salaam unaonesha kwamba kwa sasa umeshuka kutoka asilimia 85 mpaka asilimia 76, lakini upatikanaji wa vyanzo vya maji siyo upatikanaji wa maji kwa wananchi kwa sababu haya maji yanahitaji usambazaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ukienda ukaangalia namna mtandao wa maji ulivyosambazwa na vyanzo vya maji vilivyopo ni tofauti, na ndiyo maana leo ukifanya mahesabu wakazi wa Dar es Salaam anaopata huduma ya maji, waliounganishiwa kwa huduma ya bomba hawafiki hata robo ya wakazi wa Dar es Salaam. Hili ndilo tatizo, unaweza ukaona kwamba kwenye takwimu tunasema kwamba watu wengi wa Dar es Salaam wanapata huduma kumbe wanaopata huduma ni wachache, walio wengi tunaishi Dar es Salaam, tunatumia maji ambayo mengine siyo salama ni yale maji ya kuchimba wenyewe. Ukifanya research Dar es Salaam watu wengi wamechimba maji chini, yale maji ambayo siyo salama sana lakini mtandao wa maji wa Ruvu Chini, Ruvu Juu na vyanzo vyote vya Dar es Salaam, bado havijawafikia wakazi wengi wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda maeneo ya Temeke, Mbagala huko Chamazi, Kigamboni na maeneo mengi, ukienda ukiangalia mtandao wa maji Dar es Salaam unaona kabisa kwamba maji hayawajafikia, sisi tunaishi Dar es Salaam karibu wote hapa tuna makazi yetu Dar es Salaam tunajua. Kwa hiyo, hizi takiwmu zenyewe ambazo Mheshimiwa Waziri amezisema kidogo zina mashaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nirudi upande wa Wizara ya Fedha na labda Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, hivi Serikali ina diplomatic complication na wahisani tunajiuliza? Ukisoma hotuba ya bajeti ya mwaka 2017 na ya mwaka huu, fedha ambazo wahisani walihaidi kuzitoa hazijatolewa mpaka sasa. Sasa wakati mwingine unajieleza inawezekana Bunge linapaswa kufahamishwa kama kuna matatizo ya kiplomasia baina ya Tanzania na wahizani wetu tuelezwe ili tujue kwamba kinachoendelea kumbe hatupati fedha za wahisani kwa sababu tumenasanasa hapa ili Bunge lichukue hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana wakati tunajadili bajeti hapa ilielezwa kulikuwepo na dola milioni 503 na wako Wabunge waliishabikia kwamba fedha hamuioni kuna dola milioni 503 ipo, mpaka leo mbona haionekani kwenye utekelezaji wala kwenye kitabu humu hakuna. Hiyo dola milioni 503 iliyokuwa imesemwa mwaka jana na tukaambiwa kwamba Waziri wa India alishakuja na ametia sahihi sasa kilichokwama ni wapi, tumenasa wapi ili dola milioni 503 ili iweze kwenda kukamilisha miradi yetu ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ukiangalia Wabunge tunaweza tukasemaa sana hapa, lakini jambo la maji kwa sasa, kwa upatikanaji wa fedha za maendeleo wa asilimia 22 nilidhani Wabunge leo tungesimama pamoja tukasema tunahitaji commitment ya Serikali ama taarifa ya Serikali very intense watuleleze ndani ya Bunge kwamba kwa nini Wizara ya Maji haipewi fedha za maendeleo, haingii akilini kuona Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inapewa asilimia 0.85. Sasa hii mishahara ambayo inalipwa wafanyakazi, wanalipwa ili wafanye kazi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, unaweza kuona kwamba tatizo watu wengi wanaweza kusema kwamba kuna tatizo labda kwenye utendaji tunaweza tuka-deal na personalities, tunaweza tukaona kwamba Katibu Mkuu labda tatizo, ama Waziri tatizo ama Naibu Waziri, kumbe tatizo ni mfumo kwamba fedha hazitolewi labda Waziri wa Fedha anakipaumbele chake yeye tofauti na kipaumbele ambacho vimetajwa kwenye ilani ya chama chenu ama kile kipaumbele ambacho Mheshimiwa Rais alikitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji maelekezo ya kina mje kutueleza namuona Naibu Waziri wa Fedha yupo, jambo la maji ni jambo tete, huko vijijini tunakotoka Watanzania wana shida kubwa ya maji na hili tatizo linapelekea kuwa na tatizo lingine la magonjwa ya mlipuko, kwa sababu maji wanayopata Watanzania ni maji ambayo siyo maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukaongea sana hapa tukajenga hoja tunavyoweza kujenga. Lakini suala linabaki palepale kama Waziri amepewa asilimia 22 ya fedha za maendeleo afanye nini, hiyo asilimia 22 tunaigombania hapa na unajua likitokea swali hapa la Wizara ya Maji, Wabunge wote tunasisima humu kila mtu ana shida ya maji, lakini asilimia 22 ikafanye nini! Wewe mwenyewe leo umeelezea suala la maji Ilala na maeneo mengine, lakini pia kuna haja kubwa ya kuipitia mikataba ya karandasi za maji ambazo zilitolewa pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna shida kubwa upo mradi wa maji uko pale Longido, nilikuwa kwenye Kamati ya maji tuliutembelea mwaka huu una shida kubwa Mkandarasi yupo amepewa fedha zaidi ya asilimia 80 amelaza mabomba tu hakuna kinachofanyika. Kwa bahati mbaya watendaji wa Wizara yako ambao ndiyo waliingia mkataba wanautoa sasa wanataka kujivua baada ya kuona wanaenda kukwama wanawapelekea watu wa Arusha Water Supply ili wakausimamie. Kwa hiyo, mwisho wa siku mtakuja kuona kwamba kumbe usimamizi mbovu umepatikana Arusha Water Supply Agency kumbe tatizo ni Wizara yako. Hivyo, kuna tatizo kubwa pia la kuingia mikataba

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kwa nini taasisi za Serikali hazilipi ankara za maji, huu ni mtihani mwingine. Nikiwa Kamati ya Maji tulitembelea katika Mamlaka ya Maji pale Moshi tulikuta Chuo cha Polisi cha Moshi kinadaiwa shilingi milioni 900, RPC wa Moshi anadaiwa shilingi milioni 300 anaambiwa kwamba sasa tukufungie mita za prepaid anakataa anagoma. Sasa unaweza kuona kwamba kumbe tatizo linalokwamisha maji wakati mwingine maeneo ya mijini ni taasisi za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiwa Arusha yule Mtendaji Mkuu wa Idara ya Maji Arusha aliieleza Kamati kuwa kama Serikali inaweza ikalipa madeni yake yote, yeye hahitaji ruzuku kutoka Wizarani kwako, inakuwaje sasa Idara za Serikali zinatengewa bajeti tunaidhinisha humu kwenye Bunge, bajeti inakwenda wanatumia huduma za maji hawataki kulipa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo siyo tu kwamba mfumo wenyewe haupeleki fedha kwenye Wizara ya Maji, pia hata mfumo hautaki kuzisimamia Taasisi na Idara za Serikali zikaweza kulipa bill zake ili wananchi wakaweza kupata huduma za maji. Hii nayo ni changamoto nyingine Mheshimiwa Waziri unakutana nayo.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nimeona kwenye kitabu chako hapa kuna uchimbaji wa visima vya DDCA nami nimekuomba, Mheshimiwa Waziri naomba vile visima uviweze kuvikamilisha ili wananchi wa Jimbo la Mchinga wapate huduma ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Wapo wazungumzaji wamenitangulia wamechukua baadhi ya hoja zangu, lakini naweza nikaongezea kidogo. Nianzie pale alipoishia mzee wangu, Mheshimiwa Bulembo.

Mheshimiwa Spika, ndani ya Bunge, Wabunge walio wengi ni Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, pia Serikali inayoongoza ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Wakati wa utengenezaji wa bajeti viko vitu vinaangaliwa, inaangaliwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, inaangaliwa hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati anazindua Bunge lako, lakini pia unaangaliwa Mpango wa Miaka Mitano wa Taifa.

Mheshimiwa Spika, jana nimeangalia kwa makini sana, nimeipitia kwa mara ya kwanza Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Nimeona kumbe ilani imeandika vizuri sana juu ya uendelezaji wa sekta ya uvuvi na mifugo. Jana hiyo hiyo nikapitia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, lakini pia nikasikiliza na clip ya Mheshimiwa Rais wakati anazindua Bunge lako mwezi Novemba, 2015.

Mheshimiwa Spika, yaliyoandikwa kwenye Ilani ya CCM, yaliyoandikwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na aliyoyasema Mheshimiwa Rais, hayajatekelezwa yote kwenye sekta ya uvuvi na mifugo. Hayajatekelezwa! Bajeti imepata asilimia sifuri ya maendeleo kwa mwaka 2017 au mwaka huu tulionao, 2018. Maana yake ni kwamba sekta ya uvuvi na sekta ya mifugo ndiyo basi tena, imekwenda kuzimu. Waswahili wanasema imekwenda kuzimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna ukanda wa bahari wa kilometa1,400 kuanzia Mtwara mpaka unafika Tanga. Kwa maajabu makubwa kabisa, ni Tanzania pekee ambako wavuvi ndio maskini. Katika maeneo nchi tulizopakana nazo, ukienda katika visiwa vya Mauritius, ukienda Seychelles na maeneo mengine, Zanzibar tu inawezekana huu umaskini wa Zanzibar labda tumewaambukiza sisi. Hata maeneo ya Comoro, wale wavuvi sio masikini kama wavuvi wa Tanzania. Leo wavuvi wa Tanzania ndio wamekuwa na laana ya kuwa maskini jambo ambalo kwa kweli linasababishwa na usimamizi mbovu na sera mbovu za chama kinachoongoza, lazima tuseme ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jana nimekutana na wavuvi kutoka upande wa Kanda wa Ziwa, wana malalamiko makubwa. Wanalalamika kwamba sasa hivi wamezuiwa kabisa kuvua. Hoja iliyoletwa mezani kwako ya kuunda Tume, naomba sana uiunge mkono. Kuna haja ya kubwa sana ya kuchunguza. Najua umeunda Tume ya Kuchunguza Uvuvi. Kuna haja kubwa sana ya kuangalia operesheni inayofanywa kwenye maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Maftaha amezungumzia hapa kwamba kule Mtwara kuna kijana amepigwa risasi. Kwa bahati mbaya yule kijana mimi namfahamu, amepigwa risasi ya kisogoni na hawa watu ambao wanasema wanapambana na uvuvi haramu. Nataka nikuhakikishie uvuvi wa mabomu haupo Mtwara, haupo Lindi, sasa hivi watu wameacha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zamani tulikuwa hatupati samaki, nami niliwaambia, nilikuwa Mjumbe wa Kamati ya Kilimo. Nilimwambia Mheshimiwa Mpina, kama kuna jambo mlitusaidia na wananchi wameelewa, wameacha kupiga mabomu, niliwaambia kwenye Kamati. Wakati fulani nilimwambia Mheshimiwa Ulega alikuwa Mjumbe mwenzetu wa Kamati. Nilisema operation hizi za kwenda kupambana na uvuvi haramu, msipokuwa makini, mnakwenda kuua Watanzania wasiokuwa na hatia. Leo yametokea, watu wamepigwa risasi. Leo pale Jimboni kwangu Mchinga, vijana wa maeneo ya Ruvu, Mchinga na Kijiweni hawana shughuli nyingine zaidi ya uvuvi. Wakienda wanakutana na askari, wanawatisha, watu wanaacha uvuvi wanarudi. Tunawaongezea umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, suala la kwenda kuchunguza kilichoendelea kwenye operation hii inayoitwa tokomeza ni jambo muhimu na isifanyike kwenye ukanda wa ziwa tu, ufanyike pia maeneo ya Mtwara, maeneo ya Lindi na maeneo ya Kilwa kwa sababu pia watu wamedhurika kwa kiwango kikubwa sana na hii operesheni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni ufugaji, sisi watu wa Mkoa wa Lindi na Wilaya tatu siyo Wilaya zote. Mkoa wa Lindi kwenye maeneo mengine walikataa kupokea mifugo wakati wanahamishwa kutoka Ihefu, lakini Wilaya ya Lindi ambako mimi ndiko ninakotoka, Wilaya ya Kilwa na Liwale tulikubali. Tulikubali kwa sababu maeneo ya kuwaweka wafugaji tunayo. Kwa bahati mbaya walipoletwa ni kama tu tumewa-damp, hawajaendelezwa.

Mheshimiwa Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Nishati
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Waziri, Naibu Waziri na Mkurugenzi wa TPDC kwa kukubali ushauri wangu wakati tunapitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kuna ushauri niliutoa nawashukuru mmetusaidia hususani kwa wananchi wangu pale Kilangala kuweza kunufaika na mkuza. Mheshimiwa Waziri nakuomba tu kwamba yale tuliyoyaanza na Mkurugenzi wa TPDC nafikiri ananisikia basi tuyamalizie ili kile tulichokubaliana wananchi sasa wakione ili wapate moyo ule ambao walikuwa nao siku ile tulipokuwa tunakubaliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hoja mbili ama tatu, kwanza nataka nihoji Wizara. Mwaka 2013, Rais wa Marekani Barack Obama alikuja Tanzania na kuzindua Initiative iliyoitwa Power Africa. Sababu iliyofanya aje kuzindua Power Africa, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo wananchi wengi hawapati huduma za umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi ambazo ziko Sub- Saharan Africa, asilimia 76 ya wananchi tunaoishi katika Jangwa la Sahara hatupati umeme na Power Africa ilikuja kuzinduliwa Tanzania, ilikuwa ni mpango wa miaka mitano chini ya ufadhili wa African Development Bank na partners wengine. Sasa miaka mitano imefika, tunaomba ndani ya Bunge iletwe tathmini ama Waziri wakati anajibu atuambie tathmini ya programu ya Power Africa imeishia wapi? Je, fedha ambazo zilikuwa zimeahidiwa zimepatikana ama hazijapatikana? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu taarifa tulizonazo Mheshimiwa Waziri Power Africa alipoondoka Rais Kikwete na Power Africa imeondoka Tanzania. Ndiyo taarifa tulizo nazo na imeondoka kwa sababu tumefeli kwenye Diplomasia ya Kiuchumi. Wafadhili waliokuwa wanafadhili miradi ile ya Power Africa wengi wao wame-withdraw fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hili siyo sahihi wakati Waziri anakuja kuhitimisha aje atueleze kwa sababu takwimu tunazo. Wamarekani ndiyo walikuwa wachangiaji pamoja na partners wao, wao sasa hivi hawatoi fedha na tunajua sababu kubwa na ugomvi mkubwa wa Marekani na Serikali iliyopo sasa madarakani ni hii Sheria ya Mtandao, sheria hizi ambazo zinakinzana kabisa na demokrasia ya wakati huu. Sasa fedha hizi kama kweli zilikuwa zinakwenda au zimetolewa basi tunahitaji tathmini ya Power Africa imeishia wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie suala la gesi. Gesi imegundulika maeneo ya Kusini mwa Tanzania lakini kiwango ambacho kimepatikana ni kikubwa mno. Nashauri kama inawezekana hatuna hata sababu ya kwenda kwenye Stiegler’s Gorge, hatuna. Kwa kiwango cha gesi tulichonacho unaweza kupatikana umeme wa kutosha tukatumia kwenye viwanda na kwenye majumba yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi ya Qatar inatumia gesi. Rasilimali kubwa iliyofanya Qatar leo wafike pale walipofikia ni gesi. Mheshimiwa Rais Kikwete wakati yuko Mtwara anatushawishi wananchi wa Kusini tukubali mradi wa bomba la gesi alisema Tanzania itabadilika itakuwa Qatar ya Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais Kikwete alikuwa Rais aliyetokana na Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye aliyetuahidi kwamba tutakuwa Qatar ya Afrika. Rais John Magufuli naye ni Rais anayetokana na Chama cha Mapinduzi amekuja anaachana na ule mradi wa bomba la gesi, anaachana na miradi yote ya gesi, je, mmeshatufikisha kwenye Qatar ya Afrika? Kama tumefika kwenye ile level ya kuitwa Qatar ya Afrika basi tuelezeni. Tunachokishuhudia ni umeme shida na kiwango cha upatikanaji wa umeme vijijini bado ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna biashara ya gesi ambayo nimemwona Waziri juzi anaizungumzia kwamba inataka kuanza Mtwara na Dar es Salaam, ni biashara nzuri sana. Mwaka jana hapa tulitenga fedha kwenye bajeti kwamba pamoja na maeneo mengine ambayo gesi itasambazwa majumbani ni Lindi. Nakumbuka ilitengwa shilingi bilioni moja kwenye bajeti iliyopita kwa ajili ya kutengeneza miundombinu Lindi. Leo Waziri anakwenda kuzindua anaanza kusema kwamba Dar es Salaam na Mtwara wataanza kutumia gesi majumbani mbona Lindi haipo? Lindi tuna gesi ya kutosha lakini sijaona imetajwa. Sasa Waziri hebu atueleze kwamba wametutoa au sisi tutakuwa watu wa kufuatia baadaye? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu suala la REA. Mheshimiwa Waziri wakandarasi wengi wa REA wanalalamika kwamba Waziri amekuwa kama anawafanyia harassment. Leo Waziri anasema mnakwenda kuzindua mradi, vifaa wanatakiwa waende wakavichukue TANESCO, wakaviazime, wakati mwingine kuna miradi mnaizindua haijakamili ili mradi tu ionekane kwamba REA inafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna tatizo Wizara ya Fedha ambako Bunge zima tunajua kwamba mambo ya nchi hii hayaendi kwa sababu tatizo liko Hazina na Wizara ya Fedha. Hakuna Mbunge ambaye hajui, hakuna mwananchi ambaye hajui kwamba kama Waziri Mpango ndiyo Waziri wa Fedha na ataendelea kuwepo katika miaka mitano yote ya Rais Magufuli, nchi hii haitakwenda kwa sababu ameshindwa kumshauri Rais. Mimi leo ukiniambia nitaje Waziri aliyefeli zaidi nchi hii ni Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Philip Mpango, hili halifichiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Wizara ya Kilimo wamelalamika fedha, kwenye Wizara ya Maji wamelalamika fedha, TAMISEMI wamelalamika fedha, kwenye umeme tunajua Waziri hasemi tu kwa sababu ya uwajibikaji wa pamoja lakini naye pia shida yake ni fedha. Ndiyo maana wakandarasi wamesaini mikataba zaidi ya miezi tisa mpaka sasa hamjawapa fedha.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuweza kutimiza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na Sunnah ya sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze suala la korosho. Nimefuatilia mjadala wa asubuhi ulivyokuwa unaendelea na namna watu walivyokuwa wanataka kulipotosha jambo hili.

Mimi nilikuwa Lindi nimerudi jana, athari za pesa za export levy kutopeleka Bodi ya Korosho wataziona mwaka huu kwenye mapato ya korosho. Kwa sababu naamini labda Mheshimiwa Dkt. Mpango anachotaka ni asikie kwamba korosho zimeshuka uzalishaji atafurahi labla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka nimwambie Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dkt. Mpango kwamba Bodi ya Korosho mwaka huu imeshindwa kutoa sulphur yenye ruzuku, hawajatoa hata mfuko mmoja. Mpaka sasa, nainapozungumza humu ndani ya Bunge sasa hivi mfuko mmoja wa sulphur unauzwa Sh.70,000 kutoka Sh.30,000 ya mwaka jana. Hivi ninavyoongea ndani ya Bunge chupa ya dawa ya viuatilifu ambayo ilikuwa inanunuliwa Sh.15,000 sasa hivi inauzwa Sh.51,000 wakulima wanakopeshwa kwa riba kubwa, yako makampuni nimeyakuta yako Jimboni yanakopesha wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dkt. Mpango anachokitaka ni kwamba mazao yote yafe na korosho ife jibu litapatikana mwezi wa Kumi wala siyo mbali, korosho itakufa ili afurahi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu walitaka kutupotosha hapa kwamba export levy siyo fedha wakulima. Tunasema fedha ya wakulima kwa sababu korosho zimelimwa na wakulima, fedha ile kwa mujibu wa sheria asilimia 65 inakwenda kwenye maeneo yaliyolima korosho. Maana yake ni kwamba ile fedha ndiyo iliyokuwa inatumika kutengeneza ama kuandaa miche. Wataalam wa Hazina wapo pale wananisikia wamekwenda kule wamezunguka Lindi na Mtwara kwenda kuangalia wale watu waliokuwa wanaandaa miche na walikuwa wanasema wanakwenda kufanya tathmini, wamefanya tathmini wamemaliza wanawalipa lini, wale watu wanalipwa lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoongea hapa kuna watu leo nyumba zao zimewekwa bond na benki, Bodi ya Korosho iliingia mikataba na wazalisha miche, mpaka sasa hakuna. Nimezungumza na wale watu ambao walichukua tender Jimboni kwangu, nilikutana nao juzi, nikazungumza nao wanalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dkt. Mpango anatakaje, tuache kulima korosho, atuambie? Anayesema kwamba asilimia 65 siyo fedha ya wakulima maana yake ni nini? Fedha hii ndiyo ilikuwa inafanya utafiti, wakumbuke kwamba Kituo cha Utafiti cha Naliendele ndiyo miongoni mwa vituo bora vya utafiti vya korosho Barani Afrika, imepata na tuzo, wao ndiyo wamefanya utafiti wa korosho wamepeleka korosho Nigeria, wamefanya utafiti wa korosho wamepeleka korosho Gambia, wamepeleka korosho Ivory Coast, jana nimewaona watu wa Naliendelea wanalalamika hawajapata fedha ya maendeleo hata shilingi kumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umezuka ugonjwa wa mikorosho, wote wameona Waziri wa Kilimo alikuwa anahangaika hapa na Naibu wake, umezuka ugonjwa mikorosho inakauka kule Liwale, wanashindwa kufanya utafiti hawa hawana fedha hata shilingi tano, sasa kuna mtu anasisima anasema fedha za export levy siyo za wakulima ili iweje, mikorosho ife?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dkt. Mpango nimemsikia Mwenyekiti wangu wa Wabunge wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Bwege ametangaza maandamano waandae Magereza watatufunga. Kama wameandaa Askari kuja kutukamata kutupiga watatupiga ikitokea mpaka tarehe Mosi tunatoka hapa fedha bilioni 200 hawajapeleka, tunakwenda kuandamana tunadai fedha zetu tutafunga barabara, hatutakubali kwa sababu ni fedha zetu, ni fedha za wananchi, wanataka kuua zao la korosho tubaki kuwa maskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dkt. Mpango ni Mchumi, Mchumi wa aina gani ambaye hafanyi affirmative action kwa watu maskini. Ninachojua Serikali kunapokuwa na gap kubwa la maendeleo baina ya walionacho na wasionacho, hawa wasionacho wanafanyiwa affirmative action. Watu wa Mikao ya Lindi na Mtwara mara nyingi tumekuwa maskini, kiwango cha umaskini Lindi na Mtwara ni kikubwa, kitu pekee kingeweza kutusaidia ni zao la korosho, leo wanataka kuliua! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili hatukubali kabisa, it is nosense to remain here wakati korosho wanataka kuiua, hatutakubali kubaki Bungeni wakati korosho wanataka kuiua hatukubali, kwa sababu ndiyo njia pekee ya kutokea wananchi wa Lindi na Mtwara. Huu mjadala ulioletwa wa kutaka kuja kubadilisha sheria, wanataka kuja kubadilisha sheria ili pesa hizo wazichukue, wakae nazo, wapange lini tuwapelekee na lini tusiwapeleke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoongea kama labla hawajui sasa hivi kuna maeneo korosho zimeanza kuokotwa. Mimi mwenyewe ni mkulima wa korosho ninasema hilo, nimekwenda shambani kwangu nimekuta korosho zimeanza, tayari, mpaka leo Bodi hawana hata mfuko mmoja wa sulphur hizi korosho watazipata wapi, shilingi trilioni 1.3 ya fedha ya korosho kama ya mwaka jana wataipata wapi? Mheshimiwa Dkt. Mpango huu ni uchumi wa aina gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka tuseme labda watatuelewa, kwamba katika suala la korosho fedha shilingi bilioni 210 ambazo zimebaki zilikuwa bilioni 210, shilingi bilioni kumi mmepeleka, bado bilioni 200 fedha hii Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dkt. Mpango apeleke. Apeleka kabisa wakulima wa korosho hatumwelewi na hatutamwelewa maisha yote. Hii habari tunaongea mchana wengine mpaka usiku tukilala tunaota kwenye ndoto, hii habari siyo ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wangekuwa wanajua huko wakulima wanasemaje wala wasingekaa hapa wakasema, kwa sababu ninachokiona kama wakishindwa kabisa wajue kwamba hicho Chama chenu ndiyo kinakufa Kusini na we are very serious! Watu wa Lindi tuna historia ya kufanya hivyo. Nawaomba sana hili jambo wali-take very serious. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nimesikia suala la Gaming Board, hii Bodi ya Michezo ya kubahatisha pia nimeona namna wanavyotaka kuongeza tax. Ukiwasikiliza wadau wa michezo ya kubahatisha wanasema wanachokipata wao ni 1.4 percent. Sasa hivi wanataka kuwaongezea kodi ya mashine kutoka Sh.32,000 mpaka kufika Sh.100,000 kwa mashine moja. Nimekutana na Taasisi moja wanasema wao wana mashine 1,550 kwa mwezi wanalipa kodi shilingi milioni 49. Leo wakiwaongezea kodi ya Sh.100,000 maana yake michezo yenyewe itakwisha watashindwa kabisa hata kupata hiyo kodi yenyewe. Sasa hivi kupata kidogo ambacho wanakipata kila mwezi, TRA wanakusanya na kukosa kabisa lipi ni jema? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hii kama hawajui sasa hivi wamebatizwa jina badala ya kuwa ‘Hapa Kazi Tu’ wameitwa ‘Hapa Kodi Tu’. Wamekuwa ni watu wa kodi tu!

T A A R I F A . . .

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeipokea taarifa, sijatetea kamali. Maana yake ukisema hivyo unasema kwamba watendaji wote kila mtu ana dini yake hapa ndani, maana yake tusifanye shughuli za Kiserikali hilo jambo halipo. Ninachokisema kwamba kama tunaamua ku-discourage, tu-discourage totally kwamba Tanzania hatutaki michezo ya kubahatisha. Kama tunaamua iwepo kwa ajili ya kutengeneza ajira za vijana, basi tuamue kwamba iwepo na itozwe kodi inayostahiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho najua muda umekimbia sana, bajeti discipline. Mheshimiwa Dkt. Mpango tunaweza tukapanga fedha nyingi sana hapa, je, nidhamu ya utoaji wa fedha iko wapi? Changamoto ya Serikali tangia Mheshimiwa Dkt. Mpango umekuwa Waziri ni nidhamu ya bajeti. Bajeti discipline ni ndogo, kinachopangwa na Bunge sicho kinachoenda kufanyika. Leo wanaweza wakapanga shilingi fulani ziende huku hata fedha ambazo zimekuwa ring fenced wanazitumia kwenye matumizi mengine. Nidhamu ya kibajeti haipo na hili ndiyo tatizo kubwa ambalo linawapata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini hii bajeti wanaosema inawezekana ikawa bajeti hewa ni kweli. Ukisoma kitabu cha bajeti inaonesha mapato ya ndani yatakuwa trilioni 18, maana yake ni kwamba kila mwezi watakuwa mnakusanya 1.5 trilioni, ukipiga mahesabu matumizi ya kulipa deni pamoja na watumishi wa umma ndo hiyo 1.5 trilioni, fedha za maendeleo ziko wapi au ndiyo wanakwenda kukopa kwenye hiyo mikopo ya kibiashara ambayo inasababisha riba kubwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na discipline ya kibajeti lakini changamoto nyingine walionayo ni kwamba namna ya matumizi ya fedha, sioni kama kuna dalili ya fedha za ndani zitatumika kwenye miradi ya maendeleo na kusipokuwa na fedha za ndani kwenye miradi ya maendeleo tukategemea wahisani na mikopo tu, mpaka Mheshimiwa Magufuli anatoka nchi hii ataacha deni kubwa kabisa ambalo litakuwa siyo himilivu na halitalipika na Rais ajae atakuta mzigo mkubwa kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Madini
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza niendelee na kumuombea Kaka na ndugu yangu na Mbunge mwenzetu ambaye leo ameingia kaburini, Mheshimiwa Bilago, Mwenyezi Mungu ampokee na amlaze mahali pema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri na Naibu Mawaziri wote watatu bado ni wapya na huu ni mwaka wao wa kwanza, kwa hiyo, leo sitakuwa na malalamiko mengi ya kuwashutumu na kuwalaumu, nataka niwashauri. Personality zao nawafahamu namna walivyo na namna wanavyoweza kukimbia kwa sababu bado ni vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la leseni za uchimbaji wa madini na utaratibu wa namna zinavyotolewa. Mwaka jana na mwaka juzi nililalamika kwamba kuna watu wamechukua leseni wakisema kwamba wanakwenda kuchimba au kuchukua gypsum kwenye eneo la Jimbo la Mchinga hasa katika Kijiji cha Mchinga. Watu hawa leseni wanazo kutoka Wizarani lakini Serikali ya Kijiji, Kata na Halmashauri hazijui. Zipo leseni 15 ambazo zimechukuliwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya gypsum katika eneo la Mchinga lakini Serikali ya Kijiji na Halmashauri hazijui. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujua utaratibu ukoje, wakati ule Kamishna wa Kanda wa Madini alikuwa Ndugu yangu Benjamin Mchwampaka na baadaye akaletwa hapa akaja kuwa Kamishna Mkuu na sasa sijui yuko wapi, nilimwambia na suala hili akawa analijua na bahati alinipa ushirikiano wa kunipatia na addresses za wale wahusika na ni kweli kabisa alikiri kwamba hao watu wana leseni na wamechukulia leseni pale eneo la Mchinga. Nataka kujua sasa, utaratibu gani unatumika wa mtu akaenda kwenye eneo ‘A’ akaomba leseni akapewa, wakati wahusika wa pale hawajui? Kwa hiyo, hii ni changamoto kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni suala la mineral cutter. Hapa katika viwanja vya Bunge kuna watu ambao wanatuonesha namna tasnia ya madini inavyofanya kazi, tumekwenda kutembelea pale, jana mimi nimetembelea. Wale wanaohusika na suala la ukataji wa madini, nimekwenda kuangalia ile mineral cutter yenyewe kwa saa moja sijui ni gramu ngapi, ni kitu kidogo kabisa ambacho kinakatwa kwa kutumia saa moja na wakatuambia nchi yetu hazifiki hata mashine 200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asubuhi nimemsikia mchangiaji mmoja na mimi naunga mkono, hivi kwa nini Wizara isifikirie kununua mashine nyingi za kukata madini ili utaratibu wa ukataji wa madini ukawa unaharakishwa? Nimesikia kwamba kuna watu wanasimama foleni muda mrefu wakisubiri madini yao yawe yanakatwa kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, lakini mjue kwamba madini ni fedha, tena fedha kwelikweli siyo ya masihara, madini ni fedha. Kama mtu anakaa na mzigo wa madini wa nusu kilo au kilo moja akisubiri kukata, hivi mtu huyo anashindwa kwenda kufanya mipango huko mipakani akavuka akaondoka nayo? Badala ya kuwa tunafikiria kwamba Serikali itakuwa inapata fedha kumbe tutakuwa tunapoteza mapato ya Serikali. Kwa hiyo, kama kuna jambo la makusudi mnapaswa kulifanya ni kuhakikisha kwamba hizi mashine za kukatia madini zinakuwa nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, tuwa- train watu wetu. Sekta ya madini ni muhimu kweli, ingeweza hata kuendesha nchi hii peke yake. Kama tutaweza kuweka udhibiti mzuri kwenye madini tunaweza kwenda Tanzania kwa kutegemea sekta ya madini. Chuo cha Madini mkitengee fedha za kutosha tu-train watu, tufanye kama ilivyo kwenye kilimo, kuna ma-Extension Officer mpaka kwenye Kata, ninyi mngeanzia hata kwenye Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Halmashauri kama za kwetu kule Lindi, Ruangwa, ukitaka huduma ya madini unakwenda Kanda. Hivi kwa nini kwenye level ya Halmashauri hakuna watu wenu? Changamoto iliyopo ni kwamba huko kwenye Halmashauri, sifikirii kwamba hakuna Halmashauri ambayo siyo wadau wa madini, mchanga upo huko, kuna gypsum na kuna madini mengine ambayo yanapatikana katika maeneo hayo, kwa nini sasa Wizara isi-train watu wa kutosha, tutumie chuo chetu wenyewe, mkawa mmeajiri Maafisa Madini kwenye ngazi za Halmashauri, wangekuwa wanatusaidia sana kufanya hizi kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda nyumba zinazojengwa nchi hii Halmashauri zinakusanya mapato kwenye mchanga lakini Wizara sijui kama mmepata shilingi ngapi kwenye madini ya mchanga. Hapa nimesoma kitabu cha Kamati wanasema mpaka Machi mmepata asilimia 3 za maendeleo, lakini fedha zipo kama mngeweza kuwa na watu kuanzia kwenye ngazi zile za Halmashauri naamini mapato yangekuwa yanakusanywa na mngekuwa mnaweza kujiendesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ni suala la STAMICO, limezungumzwa hapa kwamba STAMICO inaitia hasara nchi hii na ni kweli kabisa. Nikifikiria taarifa ambayo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyokuwa imeundwa na Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Doto ambaye sasa hivi ni Naibu Waziri wa Wizara hiyohiyo, ilionekana STAMICO haina tija kwa Taifa. Nashangaa Waziri, nilitegemea leo angekuja na hatua madhubuti ama kutuambia kwamba anaifanyia restructuring ya Management au mfumo wenyewe anautengeneza upya au anaamua kuiweka pembeni kuja na taasisi nyingine ambayo itakuja kusimamia masuala haya kwa sababu imekuwa ikilaumiwa maeneo mengi. Sasa na lenyewe hili ni jambo la kuliangalia sana kwa sababu kila mtu anayesimama analalamikia STAMICO, nadhani kama haina tija ni bora kuachana nayo kuona namna nyingine ya kufanya. Huu ni ushauri wangu mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, mimi binafsi nimetoka maeneo ya Lindi na Mchinga kule, tuna madini ya chumvi. Sasa hivi kumekuwa na utaratibu wa chumvi kuongezewa madini joto na wale wakulima wa chumvi wanalalamika sana kwamba upatikanaji wenyewe wa hayo madini joto ni changamoto, lakini siyo upatikanaji tu, wanachokilalamikia kingine pia ni gharama. Sasa nataka kujua, hawa wakulima wa chumvi ni wadogo kama walivyo wachimbaji wadogo wadogo, mna utaratibu gani wa kuwasaidia? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeelezwa kwamba mkulima wa chumvi aliyeko Mchinga anayelima katika lile eneo la Namdima analazimika naye pia aende Mtwara akapate hayo madini joto kwa Kamishna wa Madini wa Kanda. Kuna utaratibu gani wa kuweza kusaidia? Kama nilivyosema kwamba watu wa Madini kwa nini wasikae kwenye Halmashauri, kwa nini msi-decentralise haya mambo ya madini yakawa yanashughulikiwa kwenye ngazi za Halmashauri au walau ngazi ya Mkoa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kumalizia, Wilaya ya Lindi pamoja na Wilaya ya Kilwa tuna deposit nyingi sana ya gypsum. Naomba sana muandae utaratibu kwa sababu wale watu wanaosomba madini ya gypsum wanatumia barabara hizi ambazo zinatengenezwa na TARURA, baada ya miezi mitatu au sita TARURA wanatumia pesa kuzitengeneza baadaye wao wanatumia magari makubwa wanapita mule wanaharibu zile barabara. Kuna utaratibu gani wa kufanya compensation? Kwa sababu kwenye Halmashauri tunaamini kwamba hawa wanaochimba madini ya gypsum wanapaswa walipe fidia ya barabara kwa sababu wanaziharibu na magari wanayotumia ni makubwa, kinyume na utaratibu na uwezo wa zile barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana mtoe maelezo magari yote makubwa ambayo yanabeba gypsum, kwa mfano eneo la kutoka Kilanjelanje pale Kilwa kuingia kule ndani kuna magari mengi makubwa ya tani 18, 30 yanabeba gypsum katika barabara hizi za TARURA wanatusababishia barabara kuharibika ndani ya muda mfupi sana. Kwa hiyo, tunaomba Waheshimiwa Mawaziri kama kuna chochote ambacho wanapaswa wakitoe kama fidia mtueleze ili nasi tuendelee kuwadai. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, nawatakia kila la kheri Mawaziri watatu wa Wizara hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na juhudi kubwa ambazo zimefanywa lakini bado kuna mambo kadhaa yanahitaji umakini mkubwa wakati wa utekelezaji wake ili kuruhusu sekta hii kukua zaidi na kulipatia Taifa pato kubwa na stahiki. Naomba kushauri mambo muhimu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara iongeze bajeti katika Chuo chetu cha Madini pamoja na kuhakikisha kwamba kunakuwa na wataalam wa madini na wanaandaliwa kikamilifu ili kukidhi haja ya kupata pato la kutosha katika sekta ya madini hapa nchini. Je, Wizara inashindwa kuandaa wataalam wengi zaidi na kuwa na Maafisa wa Madini angalau kwenye kila tarafa katika nchi hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu imejaliwa kuwa na deposit ya kutosha ya madini, ukiacha yale ya vito vya thamani, lakini yapo pia madini ya chumvi, mchanga, gypsum ambayo yametapakaa kila sehemu ya nchi yetu. Namna bora ya kuwa na uratibu mzuri wa sekta hii ni kuwa na maafisa wake katika ngazi za chini za utawala. Sekta ya madini imekuwa centralised mno, ikiwa tatizo ni uchache wa wataalam basi dawa yake ni kuanda wataalam zaidi kupitia chuo chetu cha madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu utaratibu wa kukata madini hapa hapa nchini. Jambo hili ni jema sana na likifanywa kwa weledi mkubwa litaipatia nchi mapato makubwa sana. Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba hizo mashine zenyewe za kukatia madini hapa nchini ni chache mno na bado zinatumia teknolojia ya zamani kidogo. Jambo hili linasababisha kuwa na foleni kubwa katika maeneo ya kukatia madini na kuongeza kasi ya utoroshaji wa madini hivyo Serikali kupoteza mapato yake mengi. Jambo hili ni jema, kama nilivyotangulia kusema hapo awali, lakini linahitaji perfect and gradual changes na si haraka haraka tu, bila kuimarisha mifumo yetu ya ndani katika kuliratibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kutoipatia fedha za maendeleo Wizara hii. Kiwango cha asilimia 3 pekee cha fedha za maendeleo ni kidogo mno kwa mustakabali wa maendeleo ya sekta hii muhimu. Wizara inapaswa kuwa na mkakati maalum na mahsusi wa kuhakikisha kuwa fedha za bajeti zilizopitishwa na Bunge zinapatikana ili sekta hii ijikwamue. Wizara ishirikiane na halmashauri za wilaya nchini katika kuhakikisha kuwa machimbo yake ya madini na mchanga yanatambuliwa na kuratibiwa vizuri ili mapato yake yawe registered vizuri na yafike kila sehemu inayohusika kwa mujibu wa Sheria ya Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho ni kuhusu zoezi la utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini ya mchanga na gypsum. Madini haya yapo maeneo mengi ya nchi yetu, watu wengi wanatamani kufanya biashara ya madini haya, lakini utaratibu wa kupata leseni bado ni mrefu. Tunaomba leseni za uchimbaji wa madini haya ziwe zinapatikana katika ngazi ya halmashauri.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia na kunijalia mimi jioni ya leo kupata fursa ya kuweza kushauri machache ambayo yanaweza, kama mtaamua kuyasikiliza na kuyafanyia kazi yanaweza kutusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninalo swali moja kwa Mheshimiwa Dkt. Mpango. Naomba tu kwanza Mheshimiwa Mpango anijibu atakapokuja kwenye kufanya majumuisho, ama atujibu Watanzania, kilio kikubwa cha Watanzania ni kwamba watu hawana fedha mifukoni, yaani mifukoni fedha hakuna, kwenye mabenki fedha hakuna, kwanza tunataka tujue fedha ziko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, kinachoshangaza zaidi, mie sio mchumi mtatusaiia nyie wachumi, kinachoshangaza zaidi kwamba fedha mfukoni hakuna, benki hakuna fedha, halafu kuna mfumuko wa bei, sasa kiuchumi hii inakuwaje? Yaani fedha, purchasing power ya watu imepungua mifukoni, lakini pia kwenye benki watu hawana pesa, halafu kunakuwa na price flactuation, hii inakuwaje kwenye uchumi? Kwa kawaida watu wanapokuwa na fedha nyingi mifukoni ndio panapotokea na hiyo boom, sasa inakuwaje kwamba watu hawana fedha, halafu kumekuwa na mfumuko wa bei?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tusaidie na watu hawana fedha kweli kweli, hawana fedha kabisa na sio watu tu hata makampuni tunashuhudia sasa TTCL juzi wametangaza kupunguza wafanyakazi 500, TBL huko ndio watu wako hoi kabisa na makampuni mengine tunajua namna hali ilivyo, sasa hilo ni swali langu la kwanza Mheshimiwa Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili wakati nachangia ninaomba niishauri Serikali, tumeisahau sana sekta ya gesi na tumeisahau bila kujua kwa nini tunafanya hivi, wakati Serikali hii hii ndio iliyowaahidi Watanzania kwamba, itaibadili Mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa Qatar ya Afrika, lakini pia Serikali hii hii ilituaminisha Watanzania kwamba kwa kupitia uchumi wa gesi tutakuwa na umeme wa uhakika, tutakuwa na viwanda vingi vya mbolea, tutakuwa na viwanda vya menthol, kutakuwa na viwanda vya Liquified Natural Gas pale Lindi, tutakuwa na vitu vingi, tuliahidiwa na Serikali hii hii, leo tumefikia wapi kwenye gesi? Tunaomba maelezo Mheshimiwa Mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asubuhi nilikuwa nasoma taarifa kwenye mtandao mmoja, Hydro-carbons Technology Limited ambao ndio wanatoa sana taarifa za gesi. Russia ambao ndio leading na super power wa gesi duniani ambao wana cubic litre karibu milioni 47,000 wao ndio wanaouza umeme karibu 60% ya umeme wa Ulaya unatoka Russia na hili mnalifahamu, lakini sisi umeme wa gesi Watanzania hatuutaki tunaona sijui kwamba una gharama, tunaachana na umeme wa gesi tunaenda kwenye maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu ambalo ni jambo la hatari sana, nilikuwa nafuatilia taarifa kwenye mtandao, sisi mpaka sasa ni nchi ya 22 kwa kuwa na reserve nyingi ya gesi, kwa taarifa zilizopo mpaka Januari, 2017 ni nchi ya 22 duniani. Msumbiji ni nchi ya 15 na mkumbuke gesi ya Tanzania iko kwenye eneo moja na gesi ya Msumbiji, ni pale Ruvuma Basin ambayo wenzetu tayari sasahivi wameshagundua na wanaitumia karibu milioni mbili cubic litres hizo kwenye trillion huko, hata mahesabu yake sijui, 2,100,086 sisi tuko kwenye milioni 1,068,000 wakati sisi tunagundua gesi, Msumbiji walikuwa bado hawajaanza matumizi ya gesi. Kwa hiyo, wana-extract gesi nyingi ambayo gesi ni kitu kinachohama, probably watakuwa wanaichukua gesi hata hii ambayo sisi ingekuwa tungeweza kui-extract kwenye eneo la Tanzania. Mwisho wa siku tutakuja kujikuta kwamba, gesi yote ya Ruvuma Basin imetumika Msumbiji, sisi hatuna gesi ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mpango hili liangalie sana, gesi ile pale Msimbati pale, Mnazi Bay, iko mpakani kabisa kati ya Tanzania na Msumbiji na wenzetu mpaka sasa wana plant za LNG tatu ambazo wana- export gas sasa hivi, sisi hatuna hata moja. Kulikuwa na mpango wa kujenga mitambo ya LNG pale Lindi, pale Likong’o na mpakani kabisa kwenye eneo la jimbo langu na watu mmekwenda, mmefanya tathmini kwamba mnataka kulipa fedha bilioni tano mkatuambia kwenye mpango wa mwaka juzi, wa mwaka jana kwamba mmetenga, mpaka leo hata mtu mmoja hamjamlipa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tuambieni mtakapokuja kujibu kwamba, mnaachana kabisa na mipango ya gesi, mnaachana kabisa na mipango ya LNG ili tuweze kujua kwa sababu kule Lindi na Mtwara tunaishi kwa matumaini tukijua LNG itakuja kumbe kitu chenyewe hakipo kabisa. Kwa hiyo, naomba hili tuliweke wazi na kila mtu alifahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2013 wakati watu wa Lindi na Mtwara walipofanya riot kuikumbusha Serikali juu ya majukumu ya wao kunufaika na gesi na mnakumbuka tarehe 16 Mei, TPDC walifanya press conference kuwajulisha umma namna gani wananchi wa Lindi na Mtwara watanufaika na ugunduzi wa gesi kule Lindi na Mtwara. Ndugu zangu, Mheshimiwa Mpango, ninachotaka nikueleze yale waliyoyasema TPDC jambo moja la uhakika ambalo sasa lipo ni moja tu kwamba umeme wa uhakika upo, lakini mengine yote mmetudanganya hayapo kabisa.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mpango hili tunapolisema naomba uli-take very serious na ninaona lazima tuseme kwamba tukiidharau gesi, si tukiidharau, gesi ni kimiminika kinachohama, Msumbiji wataitumia na mwisho wa siku sisi tutakuja kuvuna mabua kama alivyosema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanasema sana mbishi Mheshimiwa Mpango, haambiliki, lakini ndio tunasema hivyo. Tuliongea humu kwenye korosho na wengine tulisema kabisa kwamba ikifika mwezi wa 10 majibu yatapatikana hapa na mwezi wa 10 majibu yamepatikana ni kwa sababu hii hii ya kueleza mkatudharau. Sasa ukichukua ule msemo wa Kiswahili kwamba kama husikii la muadhini hautasikia la mchoteamaji, basi sawa tutaendelea hivyo hivyo, lakini naamini madhara yake yanatugusa sisi Watanzania wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, mimi nilitaka kujua sera ya uwekezaji ya Tanzania sasa hivi wapi tumekwama? Juzi nimeona taarifa imetolewa kwamba usalama wa biashara Tanzania tumeshuka kutoka 137, aliyoisema hata mama yangu hapa Mheshimiwa Ruth Mollel, sasa hivi tuko 144. Hali ya ufanyaji wa biashara, usalama wa biashara Tanzania tuko nafasi ya 144 duniani, tunaendelea kuporomoka, tatizo ni nini? Kwamba kadri siku zinavyokwenda sisi kibiashara tunashuka, tumekwama wapi Mheshimiwa Mpango?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kengele imepigwa, jambo la mwisho Mheshimiwa Mpango ni suala la korosho. Korosho ni moja ya giant cash crop in this country na inatuingizia fedha kubwa. Mwaka jana imeingiza 1.3 trillion katika nchi hii, sio kitu kidogo cha kukidharau ni jambo kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mpango tunakata kujua, tumesikia Mheshimiwa Rais amesema kwamba zingeweza kununuliwa, hebu tupe assurance watu wa Lindi na Mtwara; na nimemsikia Waziri anasema eti minada hii ni ya awali, sijui ile sheria haijasomwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, minada ya korosho Lindi inaanza tarehe 1 Oktoba, leo tuko tarehe 7 Novemba, ukituambia ni minada ya awali unatudanganya. Miaka yote korosho tunaanza kuuza tarehe 1 Oktoba, leo hili jambo sio la kawaida, lazima tuseme ukweli ndugu zangu, tuseme kwamba, kuna tatizo lipo na tuwaambie Watanzania kuna tatizo moja, mbili, tatu na solution ni hii. Mkituambia solution kwamba, jeshi litabangua hata kwa meno it is not a solution, tunaona kama mnatutania. Mtuambie what is a way forward, solution ya korosho iko wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda kule Lindi watu wananyanyaswa, korosho zinabaguliwa, korosho ambazo mwaka jana zilikuwa zinaonekana ni super leo watu hawazitaki na zina content za kutosha kwa sababu wanajua hatuna soko la uhakika mtu anakwenda anasema content ya korosho hii ndogo. Mheshimiwa Mpango tunaomba majibu ya uhakika korosho yetu lini tutauza na soko likoje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii kuchangia. Niseme kwamba nimezipitia hizi taarifa za Kamati zote mbili; Kamati ya Bajeti na Kamati ya PIC. Niseme wazi kabisa kwamba ninawapongeza sana Wajumbe wa PIC kwa kazi kubwa waliyoifanya na wameleta taarifa ambayo iko very heavy, nawashukuru sana na nawapongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka kuchangia jambo moja tu kwenye mjadala huu leo na jambo lenyewe si lingine ni korosho. Mimi nilitegemea Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti angetueleza kwamba hizi fedha ambazo Serikali wanatumia kununua korosho zimetoka kwenye kifungu gani, angeanzia hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, wakulima wamecheleweshewa fedha zao sana, hiyo haitoshi tumesikia juzi Serikali imeuza korosho tani laki moja. Binafsi nilimfuata Waziri nikaenda kumpongeza kwamba sasa najua wakulima watapata fedha zao. Cha ajabu korosho tani laki moja imeuzwa kwa mujibu wa maelezo ya Waziri wa Katiba, nilikuwa namuangalia, Serikali imeingiza shilingi bilioni 418 kwa tani laki moja. Kwa mahesabu ya kawaida itakuwa Serikali imeuza korosho kwa shilingi 4,180.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama Serikali imeuza shilingi 4,180 Serikali ije itueleze mnaendelea kulipa grade one shilingi 3,300 kwa faida hii kubwa mliyoipata, hilo moja. La pili…

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa ya kwanza hiyo.

T A A R I F A

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, nimeikubali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha ajabu zaidi mimi nilimfuatilia Mheshimiwa Rais wakati anatangaza uamuzi wa kwenda kununua korosho alisema atanunua korosho za Watanzania wote kwa shilingi 3,300 hakuna kauli nyingine iliyotolewa na kiongozi yeyote mwingine kubatilisha bei hii.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Kuchauka, Mheshimiwa Bobali.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sikubaliani nayo taarifa aliyonipa Mheshimiwa Kuchauka kwa sababu moja, Serikali ilikwenda kwenye Kamati ya Kilimo ikakiri kwamba korosho gharama yake ilivyo sasa ukijumlisha hizo zote ni shilingi 3,800; Serikali tena kwa taarifa yake yenyewe kabisa iliyo rasmi imekiri gharama ya korosho ni shilingi 3,800 ukijumlisha gharama hizo zote ambazo Mheshimiwa Kuchauka amezisema. Sasa kama mmeuza shilingi 4,180 tunataka kauli mtuambie hii iliyoongezeka mtawarudishia wakulima? Hilo moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, sasa hivi ninapozungumza wakulima wanalipwa shilingi 2,640 hawalipwi tena shilingi 3,300…(Makofi)

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais alisema korosho itakuwa…

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kuhusu Utararibu.

MWENYEKITI: Haya Kuhusu Utaratibu.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima sasa hivi wanalipwa shilingi 2,640; kama kuna Waziri ama Mbunge anasema nasema uongo akathibitisha kwamba mimi nasema uongo, nipo radhi kujiuzuru Ubunge kama unaweza kuthibitisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mimi ninayoyasema kwamba wakulima hawalipwi shilingi 2,640 na anaweza kunithibitishia, nitajiuzuru Ubunge. Wakulima wanalipwa shilingi 2,640 Rais alisema wakulima wote watalipwa shilingi 3,300 kwa kuingiziwa moja kwa moja. Ni tamko gani la Serikali limetolewa na kiongozi yeyote wa Serikali likabadilisha bei hii? (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kunipa nafasi hii. Nitaongea kiungwana sana katika hoja zangu nitaziwasilisha na nakusudia kuzungumzia mambo mawili tu. Zanzibar ilipata uhuru tarehe 10 Disemba, 1963 lakini baada ya kupata Uhuru wananchi wa Zanzibar wakaona haitoshi…

T A A R I F A

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea. Zanzibar ilipata Uhuru tarehe 10 Disemba, 1963 ikafanya Mapinduzi tarehe 12 Januari, 1964. Nazungumzia Uhuru, independence and revolution are two different things. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mataifa ambayo wakati wanatawaliwa na Wakoloni walifanya mambo makubwa ya kuwaletea maendeleo ya kujenga barabara, miundombinu ya viwanja vya ndege kama vile South Africa na Angola lakini wananchi wa nchi hizo wakaona haitoshi kwa sababu hawakuwa huru. Kwa hiyo, kwa kuwa Mheshimiwa Profesa Kabudi yupo na yeye ni mtaalamu wa historia na sheria anajua hili kwamba kitu kinachoitwa uhuru ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kabudi wakati anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tulikuwa tunafuatilia sana hotuba zake nzuri, alikuwa anatufundisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyo pamoja na umuhimu wa Katiba Mpya. Mwenyezi Mungu amejalia sasa ndiyo umefungwa kengele, wewe ndiyo Waziri wa Katiba na Sheria wa nchi hii, ule mchakato wa Katiba Mpya umekwama wapi Mheshimiwa Profesa Kabudi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa ma- champion wa nchi hii wa kuhakikisha kwamba nchi inapata uhuru ni wewe. Mheshimiwa Profesa Kabudi utaandika historia kubwa sana ikiwa yale uliyokuwa unayasema, unayapigania wakati uko nje na sasa wewe ndiyo Waziri wa Katiba na Sheria ukiweza kuyatekeleza utaacha historia kubwa sana kwenye nchi hii. Vinginevyo the vice versa is true kwamba kumbe ulichokuwa unakisema haukiamini kama utashindwa kutelekeleza ukitoka kwenye nafasi yako bila kuwa na Katiba Mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo ambalo nilikuwa nataka niseme kwa sababu namuona Mheshimiwa Profesa Kabudi yupo hapa ili ajue kwamba ana dhima hiyo ya kuhakisha nchi yetu inapata Katiba Mpya. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee kwa sababu siyo kila taarifa unaweza ukaijibu.

Mheshimiwa mwenyekiti, ukisoma taarifa ya Kamati ya Katiba na Sheria, ukurasa wa 39 - 40 inazungumzia juu ya uwepo wa Mfuko wa Taifa wa Vijana ambao pia nimemsikia vizuri Makamu Mwenyekiti wa Kamati hii akisema kwamba 2016/2017 ulitengewa shilingi bilioni 1 na 2017/2018 wakapewa shilingi bilioni 2. Mimi bado si muhenga, bado nipo kwenye kundi la vijana lakini Mfuko huu siujui. Mheshimiwa Mhagama hizi fedha mnapeleka wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo ya Kamati nayaunga mkono kwamba inatakiwa kwenda kufanya ufuatiliaji juu ya fedha za vijana zilipopelekwa. Nasema hivyo kwa sababu moja Mheshimiwa Mhagama, kuna Mfuko wa Uwezeshaji wa Rais na unajulikana na upo nchi nzima, hata ukija Lindi pale ofisi zao zipo. Huu Mfuko wa Vijana ulio chini ya Waziri Mkuu, mbona hatuufahamu?

T A A R I F A

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimtoe wasiwasi, Halmashuri yetu ina Wabunge wawili, mimi na Mheshimiwa Nape. Wewe muulize tu, sijawahi kukosa kuhudhuria kikao chochote cha Baraza la Madiwani, hata vikao Kamati za Fedha, nikiwa Dodoma nawahi kwenda Lindi. Kwa hiyo, hatuna wasiwasi, tunahudhuria.

MWENYEKITI: Hata kipindi cha korosho?

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Ndiyo, hata kipindi cha korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachokisema ni kwamba ukifika Lindi leo ukimuuliza kijana Mfuko wa Uwezeshaji wa Rais unajulikana. Mimi sijaongea from nowhere, hiki ndicho kilichoandikwa na Kamati kwamba hizi fedha Kamati inaomba kwenda kuvifuatilia hivyo vikundi vilivyopewa fedha. Sasa mimi kuunga mkono hoja ya Kamati inakuwa kosa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachosema ni kwamba Kamati yenyewe wameweka wasiwasi kwamba kuna umuhimu wa kufuatilia. Mimi naunga mkono Mheshimiwa Mchengerwa fuatilieni kwa sababu wanasema hapa kuna SACCOS zimekopeshwa, mimi Mbunge kutoka…

T A A R I F A

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni muungwana, nimelelewa kiungwana na naheshimu sana watu wote, nakushukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza nianze kwa shukrani na kupongeza hatua ya Serikali ya kutatua tatizo la umeme kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kiukweli kabisa mimi nimekaa kule karibu miezi miwili sikuwahi kushuhudia hata siku moja umeme ukiwa umekatika tena kijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sambasamba na hilo, naomba Mheshimiwa Waziri wa Nishati atusaidie, najua Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja mwezi Februari katika Mkoa wa Lindi na alisema kwamba mkandarasi wa State Grid anafanya kazi zake taratibu sana, yuko very slow. Ni kweli kabisa katika Jimbo la Mchinga nakotoka mimi katika kipindi chote cha Phase II na III huyu mkandarasi hajawahi kabisa kuonekana. Viko vijiji ambavyo vimeingia kwenye mradi lakini miaka yote tangia 2016 mpaka leo 2019 hajawahi kuleta hata nguzo moja.

Kwa hiyo, naomba jambo hili lichukuliwe kwa kipaumbele sana kwa sababu hivi vijiji viliingia kwenye mradi na tulishawaeleza wananchi na wananchi wamejiandaa kwa siku zote kusubiri umeme lakini umeme haufiki. Kwa bahati mbaya sana wakienda kwenye vijiji jirani ambako umeme unafika wanaukuta na haukatiki. Tuna umeme wa uhakika sana lakini kuna vijiji ambavyo havijapata hiyo stahiki ya umeme…

T A A R I F A

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Haya taarifa.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Nataka nimpe taarifa mzungumzaji, huyu State Grid anayemzungumza hatufahi kabisa kwa Mkoa wa Lindi kwa sababu mimi kwenye Jimbo langu la Liwale ameweza kuwasha umeme katika vijiji viwili kwa muda wa miaka miwili sasa. Kwa hiyo, huyo mkandarasi hatufai.

SPIKA: Unaipokea taarifa hiyo Mheshimiwa Bobali?

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nimeipokea taarifa hiyo. Ni kweli Waheshimiwa Wabunge wote wa Mkoa wa Lindi tunamlalamikia mkandarasi huyu na hata Naibu Waziri, Mheshimiwa Subira Mgalu alikuja na yeye akamlalamikia.

Mimi nafikiri ifike wakati hatua zichukuliwe kwa sababu kama mkandarasi yuko site miaka mitatu hajawahi kwenda hata kwenye kijiji kimoja kupeleka nguzo mkandarasi huyo hafai, lakini siku zote yupo, ukifika Lindi pale Mkoani unamkuta, ana makabrasha yake, kubwa analokuambia sijalipwa, lakini taarifa za Serikali zinasema kwamba amelipwa. Naomba sana Serikali walichukue hili jambo huyu mkandarasi kwa kweli hatufai kabisa watubadilishie watupatie mkandarasi mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nishukuru pia juzi nimemsikia Mheshimiwa Rais akiwa Mkoani Mtwara ametupongeza Wabunge wa Mkoa wa Lindi na Mtwara namna tulivyosimamia na namna tulivyolisemea zao la korosho. Nashukuru kwa sababu Mheshimiwa Rais ame-recognize juhudi yetu ambayo tulikuwa tunaifanya ndani ya Bunge na sisi tunashukuru na tunapongeza kwa hatua zilizochukuliwa na Serikali kulipa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo hili la mwaka huu liwe fundisho kwetu wote. Kwenye suala la korosho kuna changamoto nyingi sana. Nafikiri Mheshimiwa Rais mwenyewe amejionea na zingine amekuwa akishangaa kama zinatokea katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wako watu wengi wamekatwa fedha zao, mtu badala ya kulipwa ile fedha yake halali analipwa anakatwa Sh.300. Yako maagizo mengine Mheshimiwa Rais ameyatoa lakini nachosisitiza jambo lililotukuta kwenye msimu wa korosho uliopita liwe fundisho kwetu sote. Jambo hili kwa kweli limetupotezea fedha nyingi. Mimi nashukuru kwamba Mheshimiwa Rais ame- recognize na ametambua juhudi zetu namna Wabunge tulivyolisemea zao la korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sambasamba na hilo kuna zao la ufuta, ndiyo ile hoja ya uwekezaji ambayo imezungumzwa na Waheshimiwa Wabunge wengi hapa, ufuta unalimwa kwa wingi sana Mkoa wa Lindi. Ukizungumza na matajiri wanasema ule ufuta wa Lindi ambao kwa jina unaitwa Lindi White ni ufuta bora sana kwa sababu una mafuta mengi. Mafuta ya ufuta ni miongoni mwa mafuta bora na ni mazuri yanatumiwa na watu wenye fedha zao. Hapa Tanzania sidhani kama tuna kiwanda cha kukamua mafuta ya ufuta. Ufuta wote ambao unazalishwa kwenye nchi hii unasafirishwa kupelekwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa naposema tayari wakulima wanakaribia muda wa mavuno, najua tayari matajiri wameshajiandaa kuja kuchukua ufuta, tunapoteza fedha nyingi sana za kigeni kuagiza mafuta ya kupikia, kwa nini tusifanye mpango ufuta unaozalishwa ukawa umewekewa utaratibu pale Lindi tukapata kiwanda cha kukamua mafuta, tukaongeza ajira, kuna tatizo kubwa la ajira ingesaidia pia kupunguza tatizo la ajira la vijana. Kwa hiyo, hili jambo la uwekezaji ni muhimu sana na nashukuru umekuwa ukisimama zaidi ya mara mbili kulisisitiza. Jambo hili linahitaji lichukuliwe kwa tahadhari kubwa sana kwa misingi ya kutaka kupata maendeleo kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, nitoe rai pia viongozi wetu, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wasifanye harassment kwa wawekezaji. Kuna jambo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika moja ya Mikoa ya Kusini mwa Tanzania, Mkuu wa Mkoa anaonekana anaweka ndani mwekezaji, anachukuliwa anasekwa mule, mambo kama haya yanaharibu taswira nzima ya uwekezaji na mtu mwingine ambaye alikuwa ana nia ya kutaka kuja Tanzania hawezi kuja. Kwa hiyo, jambo hili lazima lichukuliwe kama ni sensitive na iwe ni ajenda ya Taifa kwamba tunakwenda kwenye kuvutia wawekezaji, sheria zibadilishwe, miongozo iwekwe sawa ili wawekezaji warahisishiwe namna gani wanaweza wakaja wakafanya shughuli zao vizuri kabisa lakini bila kubuguziwa, kuwekwa ndani saa 24 na kadhalika. Mambo haya kwa kweli yanatutia doa wote.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuweza kuchangia hoja ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Nataka nianze na hoja ya vijana wa bodaboda wa pale Mchinga kutakiwa kuwa na kitambulisho cha Sh.20,000, hivi vitambulisho vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais. Nataka kupata majibu kwamba huu ndio utaratibu? Mimi nimesoma ule Waraka unaoainisha ni watu gani wanapaswa wachangie ile Sh.20,000, sijaona sehemu ya bodaboda. Kwa Mchinga pekee bodaboda baada ya kuwa na leseni wanatakiwa pia wawe na kitambulisho cha Sh.20,000.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri akija aje atueleze kwamba haya ni maelekezo yanafanyika kwa ajili ya kukusanya kodi na ikiwa kama bodaboda wanatakiwa wachangie Sh.20,000, je, madereva wa gari taxi kwa nini nao wasilipe? Kwa hiyo, hili jambo nataka nipate majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nakubali kama wenzangu wanavyokubali kwamba Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri na kubwa ya kulinda raia na mali zetu tulizonazo lakini yapo mapungufu lazima tuyaseme na Jeshi la Polisi wayachukue waweze kuyafanyia kazi yabadilike. Dhamira ya mtu inapimwa kwa maneno na vitendo, wakati mwingine unaweza ukachafuka kwa ajili ya maneno yako tu.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano anapotokea Polisi akasema nitawapiga na kuwachakaza, hili neno linaudhi lakini pia halina tafsiri njema kwa raia ambao umeapa utakwenda kuwalinda wao na mali zao. Kwa nini usitumie lugha nyingine ambayo inaweza ikatumika kuzuia lakini pia wewe ukaonekana kwamba dhamira yako ni njema katika kulifanikisha jambo lile.

SPIKA: Kwa mfano Bobali, hebu mfundishe lugha ya kutumia, asemeje?

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, kwa mfano tu aseme maandamano haya yamezuiwa na msiandamane, inatosha. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

SPIKA: Sasa huyo anayesema hivyo ni Mwenyekiti wa Mtaa au askari huyo? (Kicheko)

Endelea Mheshimiwa Bobali.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

SPIKA: Askari ni askari tu, kama umepita JKT hutashangaa hivi vitu.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru lakini katika tamaduni za kawaida kabisa Polisi walioapa kulinda raia na mali zao si vyema kuwatisha kwamba watawapiga na watawachakaza, si vyema kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi yako mambo Jeshi la Polisi lazima tuyaseme wamefanya vizuri. Kwa mfano, katika jambo la kupambana na ujambazi, kiwango cha ujambazi kimepungua, hili ni jambo la kupongeza, wanafanya kazi nzuri sana lakini yako mambo yanatia doa Jeshi la Polisi. Kwa mfano, very recently Jimbo la Mchinga kulikuwa na uchaguzi, Diwani mmoja alikuwa amefariki mwezi Machi, kwa hiyo, uchaguzi ukatangazwa.

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi wakiwa kwenye gari ya polisi, wakiwa na silaha zao wamekwenda nyumbani kwa mgombea wa Chama cha CUF kumlazimisha asaini barua kwamba yeye anajitoa. Jeshi la Polisi usiku wamemvamia nyumbani kwake. Bahati nzuri tulijua kabla hawajakwenda tukamwambia toka akakimbia. Sasa Mheshimiwa Waziri, haya ndiyo majukumu ya Jeshi la Polisi? Tena wakiwa wameambatana na msimamizi wa uchaguzi, unakwenda nyumbani unamwambia saini hapa kwamba unajitoa halafu baadaye wanatangaza kwamba wamepita bila kupingwa, this is not fair. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri mambo kama haya yanatia doa Jeshi la Polisi. Tukikaa nao hawa Polisi wakati mwingine ni rafiki zetu wanatuambia kabisa jamani eeh sisi tunaambiwa. Sasa ni nani anayewaambia Jeshi la Polisi kufanya kazi hii? Ukija utuambie kwamba wewe Waziri ndiyo umewaambia kwa sababu tunakuona muda wote unashika Ilani ya CCM unatembea nayo …

SPIKA: Mheshimiwa Bobali, tukikutaka utuletee hao Askari waliokwambia haya unayoyasema humu utaweza kuwaleta?

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, mimi natekeleza jukumu langu la kumfahamisha Mheshimiwa Waziri.

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

SPIKA: Unatekeleza jukumu lako lakini hupaswi kutudanganya kama Bunge, hili ni Bunge.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, sidanganyi.

SPIKA: Kwa hiyo, kama ulipewa taarifa hizo inconfidence basi ni vizuri ukae nazo inconfidence, as long as unaziweka hapa maana yake uko tayari kutuletea hao Askari waliosema hayo na kama hauko tayari kuleta hao Askari maana yake wewe uko tayari kuwa liable kwa unayoyasema. Yaani lazima upime kama kiongozi kuna habari unapewa kwa matumizi yako mradi umeamua kuyaanika hapa maana yake uko tayari kusimama nayo.

Sikukatazi kusema endelea mradi uwe tayari kwa hayo naku-caution tu.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nimekuelewa ila nachosema tunakokwenda kwenye mwaka wa uchaguzi huu Serikali za Mitaa, jeshi letu litumike kwenye kutulinda na kuhakikisha kwamba vyama vyote vinatendewa haki. Hilo ndiyo hoja yangu, nimekuelewa.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ni kwenye suala la uhamiaji. Pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji lakini kuna jambo lina dosari. Kumekuwa na wahubiri especially wa Kiislamu wamekuwa wakija miaka mingi hapa wanapita kwenye maeneo yetu wanakuja kuhubiri hasa karibu na mwezi huu wa Ramadhani. Mheshimiwa Waziri anajua kwamba wako wahubiri mwaka jana waliondolewa hapa nchini kwa kupewa warrant ya saa 24, ikawa shida sana. Sasa hivi kumekuwa na shida nyingine wahubiri wakiomba visa inakuwa shida sana wakati mwingine mpaka hata ule muda wenyewe uliokusudiwa kwamba twende tukaelimishe au tukaseme hili unapita.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri jambo hili mliangalie. Tunajua kwamba mnaangalia mambo ya ugaidi na kadhalika lakini wako wahubiri mkiangalia records zao wamekuwa wakija kwenye nchi hii miaka yote. Kwa mfano, mimi toka nimekuwa na akili timamu wako watu nimewahi kuwaona wanapita maeneo yetu wanakuja wanahubiri wale Wapakistani lakini sasa hivi wakiomba visa kuja Tanzania inakuwa shida sana. Sasa Mheshimiwa Waziri wakati mwingine mnapozuia watu hebu tazameni na records zao kwamba hawa wana record gani zilizopita?

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze na hoja ya matokeo ya kidato cha nne na darasa la saba na namna yanavyo-reflect uhalisia. Mheshimiwa Waziri atakubaliana na mimi, matokeo ya kidato cha nne, ya mwaka 2017 nitaitaja Mikoa nane ya mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanga ilishika nafasi ya 24, Ruvuma ilishika nafasi ya 25, Mjini Magharibi nafasi ya 26, Lindi nafasi ya 27, Kusini Pemba nafasi ya 28, Kaskazini Pemba nafasi ya 29, Kusini Unguja nafasi ya 30, Kaskazini Unguja nafasi ya 31. 2018 Tanga 24, Mtwara 25, Mjini Magharibi 26, Lindi 27, Kusini Pemba 28, Kaskazini Pemba 29, Kusini Unguja 30 na Kaskazini Unguja 31.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri amejifunza nini kwenye matokeo haya? Mikoa ni ile ile na kwa bahati mbaya mikoa yenyewe iko kwenye Ukanda mmoja, Ukanda wa Pwani. Tunapozungumzia inclusive education lazima iambatane na inclusive performance ambayo itakuja kuleta inclusive development. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa ukanda mmoja, watu wanafanya vizuri ukanda mwingine watu hawafanyi vizuri, tunakwenda kutengeneza matabaka katika Taifa letu. Mheshimiwa Waziri wa Elimu lazima aipitie Sera ya Elimu, lazima matokeo haya yamfundishe jambo, kwa nini Lindi kila siku wanakuwa wa mwisho? Kwa nini Kusini Unguja kila siku wanakuwa wa mwisho? Kwa nini Tanga kila siku na mikoa yenyewe yote iko kwenye Ukanda wa Pwani? Mimi siamini kama watu wanaokaa Ukanda wa Pwani, hawana akili, siamini kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viko vigezo vingi vya kupima kwamba uelewa wao ni mkubwa na performance zao katika maeneo mengine ni mzuri. Hawa watoto wa pwani sio kwamba hawapendi elimu, kuna watu wanakuja na majibu mepesi kabisa, watu wa pwani hawapendi elimu, hawapendi kusoma, sio kweli. Wanasoma, ukiwapeleka madrasa mtoto amesoma juzuu thelathini, amehifadhi, anaweza akasoma Quran vizuri, kwa nini ashindwe kusoma kitu alichofundishwa kwa Kiswahili? Yaani mtu anaweza kutafsiri Kiarabu alichofundishwa, lakini eti kujibu methali ya haba na haba, hujaza kibaba, anafeli? Kuna namna lazima tutafakari na tujiulize, tusiwe na majibu mepesi, jambo hili ni kubwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine amezungumza Mheshimiwa Mbatia, inawezekana Kilimanjaro wanaonekana nafasi ya kwanza kwa sababu ya idadi ya shule za private, nadhani kama Serikali inataka wajitathimini waone performance ya shule za Serikali, watoe matokeo ya shule za Serikali peke yake kwanza, halafu wawe na matokeo ya shule za Private.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lindi mathalani, Lindi shule za private hazifiki hata sita, ina maana hii competition inayokwenda, inakwenda Canossa na shule zingine zinakwenda kupambanishwa na shule hizi za kayumba zilizopo Lindi. Hakuna shule za private Lindi, sidhani kama Kaskazini Pemba au Kusini Pemba kuna shule za private. Kwa hiyo mtai-label hii mikoa kama ni mikoa ya mwisho kila siku, kumbe hawapambani shule za Serikali na shule za Serikali, wanapambana shule za Serikali na shule za private.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni hoja very sensitive, Mheshimiwa Waziri ajaribu kuiangalia, lazima tuwe na inclusive education ili tuweze kuja kuwa na inclusive development, vinginevyo tutatengeneza matabaka ambayo wakati mwingine yanaweza kuja kuleta matatizo, haiwezekani kila siku Mikoa ya Pemba ndiyo ya mwisho. Bahati mbaya sana, panapotokea matokea ya kuwa wa mwisho, wanaoathirika ni Maafisa Elimu wa Mikoa, utasikia kila siku, Afisa Elimu wa Mkoa Lindi kabadilishwa, Afisa Elimu wa Mkoa sijui Mtwara kabadilishwa, Afisa Elimu Mkoa wa Tanga anabadilishwa na sio kubadilishwa, wakati mwingine kwenye mikutano hii ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, na wakati mwingine wanadhalilishwa pia. Sasa inawezekana unamlaumu huyu, kumbe yeye shule zake ni sa Serikali tupu. Anapambanishwa na maeneo ambako kuna shule nyingi za private. Hili ni jambo, ni jambo ambalo linahitaji tafakuri ya kina, na lazima waliangalie kwa umakini mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni juu ya hadhi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere; hivi karibuni Mheshimiwa Waziri Mkuu, alitembelea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, nami ni mhitimu wa kile chuo na Mheshimiwa Waziri niliona aliambatana naye na Mheshimiwa Waziri Mkuu akatoa maagizo kwamba kile chuo kipandishwe hadhi ya kuwa Chuo Kikuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wiki moja baadaye ndani ya Bunge hili hili, mimi nikauliza swali lile lile, likajibiwa na Mheshimiwa Naibu Waziri, akasema kwa sasa Serikali haina mpango wa kukipandisha hadhi Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ni-contrary na kile alichokieleza Mheshimiwa Waziri Mkuu pale chuoni siku ile walipokwenda, sasa wanafanyaje kazi Mawaziri? Huku Mheshimiwa Waziri Mkuu anaagiza, kuwe na Chuo Kikuu kipandishwe hadhi, huku majibu ya Serikali ndani ya Bunge kwamba kwa wakati huu hakuna, lakini Mheshimiwa Waziri, hoja yangu ni nini? Hoja yangu kwanza ni kuthamini mchango wa Muasisi wa Taifa hili juu ya Sekta ya Elimu, kwanza hiki Chuo ndiyo chuo cha kwanza kabisa cha wazalendo kujengwa na wazalendo katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, wenzetu kwenye Mataifa ya wenzetu, Baba zao wa Mataifa yao, wale Waasisi wa Mataifa wote, wamepewa majina ya Vyuo Vikuu. Ukienda Kenya leo, unakuta Kenyata University, ukienda South Africa kuna Nelson Mandela University, ukienda Ghana unakuta Kwame Nkurumah University, kwa nini Tanzania hakuna Mwalimu Nyerere University, kuna shida gani, kwani kuna ukakasi gani? Elimu inayotolewa ni ile ile, kuna ukakasi gani wa kukipandisha hadhi Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuwa University?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi nimeona katika ukurasa wa 184 mwaka huu wanaenda kutoa na Shahada za Uzamili, sasa kama wamefikia mpaka hatua ya kutoa Shahada za Uzamili? Kwa nini wanapata ukakasi wa kukipandisha hadhi chuo hiki kuwa Chuo Kikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, mwaka juzi, mwaka jana na mwaka huu nasema, juu ya shule ya Sekondari ya Mchinga na Mheshimiwa Maftaha alitoa ushahidi hapa, shule ina vigezo, ina madarasa mengi, ina Walimu wengi, Walimu karibu asilimia 95 ni graduates, kuna shida gani kuipandisha hadhi ya kuwa high school? Jimbo la Mchinga hakuna shule ya high school hata moja, shule zote za sekondari zinazalisha watu wanaokwenda high school wanakwenda nje ya maeneo yale na wakati mwingine wengine wanaachwa wanakosa nafasi kwa sababu ya uhaba wa shule za A-level.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri aliangalie sana, mwaka huu tumeanza mchakato wa kujenga mabweni na nina hakika mpaka mwakani tutamaliza, wananchi wamehamasika sana, hebu waiweke kwenye mpango shule hii kuifanya ni miongoni mwa shule za high school itatusaidia sana kuondoa gharama za vijana wanaokwenda maeneo ya mbali kwenda kusoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa mnafiki kama sitasema kuhusu Walimu, mimi mwenyewe nimefundisha miaka mingi najua maisha ya Walimu bado yana changamoto, mishaharara wanayopata ni midogo, lakini pia suala la upandishaji wa daraja. Walimu wamekaa wanatega masikio kusikia kesho Mheshimiwa Rais atasema nini, lakini kama hakuna itaenda vilevile, itapita bila bila tu kama hakuna chochote, wana-demoralize watu na matokeo yake performance inakuwa ndogo kwa sababu Walimu wana matatizo mengi kabisa, wengi tulikuwa Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba nianze na suala la minazi; kwetu sisi watu wa Mwambao wa Bahari ya Hindi nazi ni chakula, lakini pia inatumika kupamba miji yetu. Ukifika Lindi, Kilwa, Bagamoyo, Pangani na maeneo mengine, miji inapendeza kwa kuwa na minazi. Minazi inakufa; mwaka jana nilizungumza humu na bahati nzuri wakati fulani dada yangu pale, Mheshimiwa Dkt. Mwanjelwa, wakati akiwa Naibu Waziri wa Kilimo nilizungumza naye nikiwa jimboni kumwonesha masikitiko makubwa ya wananchi ambavyo mashamba yao ya minazi yanakufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi Wizara ya Kilimo na hili nalo linawashinda? Yapo maeneo ambayo nitakutajia, kwa mfano jimboni kwangu minazi sasa imekufa kabisa. maeneo yale ya Kilangala, Mchinga, Milola, Lutamba, maeneo ya Sinde, lakini hata Kilwa kwa Mheshimiwa Ngombale hapa ukifika Miteja, nenda Kisiju, minazi imekufa, nenda kule Mafia, ukienda Pangani minazi inakufa. Hili nalo linawashinda? Naomba Mheshimiwa Waziri aje na jibu. Waende wakafanye utafiti tujue minazi hii inakufa kwa sababu gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ufuta; Mkoa wa Lindi ni wakulima wazuri sana wa ufuta na ufuta wetu ni ufuta mzuri, una mafuta mazuri, mengi. Wananchi baada ya dhoruba kubwa tuliyopigwa kwenye korosho, mategemeo yetu yalibakia kwenye ufuta, tunaanza kutaka kukata tamaa. Kuna jambo limeingizwa katika mfumo wa ununuzi wa ufuta, jambo hili linakwenda kuwaumiza wananchi wakulima wa ufuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na matajiri wale kutakiwa kukata vibali kulipa leseni zote, wameandikiwa barua na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa walipe shilingi milioni mbili ya kuchangia Mwenge. Suala la kuchangia Mwenge walilifanya liwe kwenye biashara? Hivi kuna mfanyabiashara gani atalipa shilingi milioni mbili, milioni mbili hii asiihamishie kwa wananchi? Kwa hiyo kuja kuzima Mwenge Lindi mwaka huu wanakwenda kuwatoza wananchi kulipia Mwenge?

Mheshimiwa Mwenyekiti, this is not fair. Jambo hili lazima Mheshimiwa Waziri ulitolee maelezo na ni kwamba hatutakubali, Mheshimiwa Waziri lazima uwe ukweli, kwamba sisi tutawaambia wananchi wasikubali na hawatauza ufuta wenyewe kwa sababu kwenye korosho watu wana vidonda vikubwa na nitavisema hapa. Sasa wakitaka kuturudisha na huku kwenye ufuta haya mambo kwa kweli Mheshimiwa Waziri wayaangalie vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barua aliyoandika Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwaandikia matajiri wanaokwenda kununua ufuta ambao msimu utafunguliwa tarehe 25, mwezi huu, ile barua suala la kuwaambia walipe shilingi milioni mbili mchango wa Mwenge ufe. Hebu imagine kukiwa na matajiri 50 watachangia milioni 100, milioni 100 hii inahamia kwa wakulima, inahamia kwa halmashauri, na mfumo wenyewe mwaka huu tunakwenda kuuza kwa mfumo wa mnada. Kwa hiyo lazima hii tozo itahamia kwa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, kuhusu korosho; Bunge lako hili tarehe 14, Mwezi Novemba, lilipitisha Azimio la Kuunga Mkono Serikali Kununua Korosho, humu ndani mwaka jana na tukapongeza lile jambo. Leo ukiwaambia Wabunge wanaotoka maeneo yanayolima korosho tulete orodha ya wananchi ambao bado hawajalipwa, orodha hapa tutasoma majina siku nzima. Watu wengi hawajalipwa. Mimi mwenyewe nimeuza korosho zangu, katika milioni 30 nimelipwa milioni tatu, milioni 27 nitalipwa lini, sijui. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa ninavyoongea, nimetoka jimboni juzi, tayari mikorosho imeanza, msimu wa palizi umeanza na tayari kuna baadhi ya mikorosho imeshaanza kutaka kuonesha kutaka kuzaa. Kama jimboni kwangu wananchi hawajasafisha kabisa na kilio chao kikubwa watu hawajalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Mtwara kuliwekwa centre ya kulipa wakulima; wakulima walikuwa wanapiga simu pale Mtwara. Sasa hivi nasikia ile centre imefungwa kabisa, kwahiyo matumaini kwamba tutalipwa hayapo; na kwa Lindi tumeombwa radhi na Mkuu wa Mkoa kwamba tunawaombeni radhi wakulima wa korosho. Sasa hii inamaanisha nini? Mimi nawaambia, suala la korosho kwetu sisi ndiyo maisha yetu. Leo madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ninakotoka mimi wana miezi sita hawajalipwa posho, wana miezi sita; wanakwenda wanafanya vikao ile posho yao ya mwezi hawajalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendeshaje halmashauri hizi? Halmashauri yetu mpaka leo makusanyo yake mpaka sasa ni asilimia 20, sasa tutatatuaje changamoto za wananchi endapo fedha za ushuru wa korosho hazitapelekwa halmashauri? Kwahiyo hili suala la korosho tusilifanyie siasa kwa mtindo huo maana kila siku tunaambiwa maneno. Jana nimeona Mheshimiwa Waziri wa Biashara anatuambia watu wa Lindi na Mtwara tunazaana sana kwasababu tunakula korosho; huu ni mzaha. Tulipeni fedha zetu, walipeni wakulima wa korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais amekuja Mtwara akasema fedha zitapelekwa bilioni 58, alivyotoka pesa zimepelekwa bilioni 18. Kwa utaratibu huu zitakwisha lini kulipwa? Wengine tuliongea humu ndani ya Bunge kuhusu suala hili tukatolewa humu Bungeni; kwamba huku tunakokwenda siko. Tukapiga na vigelegele, hivi hata Bunge halitaki kujua hatua ambayo Serikali imechukua? Mimi napendekeza kama itakufaa Bunge liunde tume iende ikachunguze, kwenye korosho kuna mambo makubwa, watu hawajalipwa, watu wametiwa umasikini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nakushauri jambo linguine; kwa kuwa msimu umeanza, basi nendeni Benki mkawakopee hawa watu basi walau waweze kufanya palizi; au mkawape bondi waweze kukopesheka. Mtu ana hela zake milioni 30, milioni 20, milioni 10 anashindwa milioni moja ya kufanya palizi shamba lake; nendeni mkawawekee bondi basi Benki waweze kuwakopesha ili kilimo kiendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumza suala la korosho tunazungumza maisha yetu. Baadaye mtakuja kutuambia hapa watu wa Lindi na Mtwara tunafeli; watu hawasomi kwasababu wana-frustrations nyingi ikiwemo na ya korosho. Mtoto akienda shuleni hawezi akafanya vizuri wakati nyumbani baba analalamika hajalipwa korosho. Jambo hili Bunge lazima liingilie kati, Serikali inaonesha wazi kwamba imeshindwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia jioni ya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kusema kwamba tunachangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa ambao fedha zake zinatokana na kodi za wananchi bila kujali hao wananchi wapo kwenye vyama gani vya kisiasa ama wao ni wafuasi wa kundi lolote lakini wote ili mradi ni Watanzania tunchangia kodi na ndiyo fedha hizi ambazo zinatumika kugharamia miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa yako maelezo yanasemwa na wako watu wanzunguka kwenye majimbo yetu kwenda kusema maendeleo hayapatikani kwa sababu kuna Mbunge wa Upinzani kwamba Seriakli ya Rais Magufuli haipeleki miradi ya Maendeleo kwenye Majimbo ya Upinzani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili linapaswa Mheshimiwa Waziri wa Fedha ulikemee kwa sababu ni kinyume kabisa na Katiba na Sheria lakini pia nadhani ni kinyuma hata na matakwa na Rais Magufuli kwamba yeye siye aliyeagiza watu wapite kwenye majimbo yetu waseme kwamba maendeleo hayaji kwa sababu mechagua Wapinzani. Ni jambo ambalo kidogo ukilisikiliza linaleta fadhaa kuona watu wenye uelewa wa kiwango hicho wanasema maneno hayo.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali upokee taarifa!

T A A R I F A

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa Taarifa mzungumzaji. Anachokisema si sahihi. Kuna vituo vya afya viwili vimejengwa Mchinga na Mchinga ni Jimbo la Upinzani.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali unasema maendeleo hayapelekwi, anasema kuna vituo vya afya viwili. Karibu bilioni moja imeletwa kwako.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuelewa na nadhani kaka yangu Mheshimiwa Kuchauka hakunielea nilichokisema. Kwanza, tumepata kituo kimoja cha afya sio viwili lakini hakunielewa. Nilichosema ni, wako watu wanazunguka na tukisema hivi wengine tunawaweka bracket, wengine tunawaheshimu sana. Inawezekana wengine wako ndani humu wanasema kwamba hapa hayaji maendeleo, Rais hapeleki maendeleo kwenye Jimbo la Upinzani ndiyo maana sisi tumeishia hapo hapo tu kwa hiyo hili Waziri wa Fedha alitolee ufafanuzi. Aliseme kwamba jambo hili si mkakati wa Rais na ni kwa sababu yako mambo yamefanywa ndani ya kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano yamefanywa ndani ya Jimbo la Mchinga. Yanapaswa hayo, wanaokwenda huko waseme kwamba pale limefanyika, kituo cha afya milioni 420 zimepelekwa.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali taarifa pokea.

T A A R I F A

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nilitaka nimpe kaka yangu ambaye ni mstaarabu sana na ninamuheshimu mno lakini nilitaka tu nikupe taarifa kwamba wakati nikiwa CHADEMA nilipata bilioni 52.3 kwa ajili ya lami. Nimepata bilioni 1.8 kwa ajili ya maji, nimepata milioni 250 kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya, nimepata milioni 751 kwa ajili ya maji sehemu nyingine na zaidi ya milioni 800 kwa ajili ya elimu. Kwa hiyo, nikupe tu taarifa kwamba hilo sio suala la Waziri wa Fedha, ni suala lako na watu wanaofanya siasa ndani ya eneo ako. Ahsante sana.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, naomba niendelee. Nimepokea Taarifa yake nadhani ameongezea tu kile nilichokuwa nakisema…

Mheshimiwa Mwenyekiti…

MWENYEKITI: Anamaanisha ni vigumu sana kwa Waziri wa Fedha kuzungumzia hilo jambo. Hajui nani aliyesema, wapi, ilikuwakuwaje sasa yeye atoe statement yaani ataanzia wapi? Lakini endelea tu kutoa mchango.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nakushukuru, nianze na mradi wa LNG mradi. Mradi wa kufua umeme na nimesoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri wakati anawasilisha ukurasa wa 20. Amezungumzia ni sehemu ya Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunatoka Lindi. Lindi kwa sasa nafikiri ndiyo Mkoa maskini zaidi kuliko yote Tanzania kwa mujibu wa taarifa zilizopo. Kipato chetu ni kidogo, hali ya udumavu umekuwa ni mkubwa sana na hata matokeo yetu ya shule yamekuwa mabaya sana, bahati mbaya sana miaka mitano tunaburuza mkia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Fedha inapaswa ifanye affirmative action kwa maeneo kama haya ili kutusaidia ili na sisi vijana wa Lindi wapate ajira kwenye miradi ambayo itakuwa inatekelezwa na Serikali kwenye maeneo yetu na hakuna mradi mkubwa ambao ungetekelezwa ungesaidia sana kama mradi wa LNG.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma taarifa ya Mheshimiwa Waziri anasema suala la kufanya tathmini ya malipo ya watu wanaopaswa kuondoka pale limekamilika lakini shida iliyopo ni suala la kimkataba kati ya wawekezaji na Serikali. Wakati nachangia bajeti ya Wizara ya Nishati wakati wa Bajeti nilishauri kitu. Hii mikataba hizi negotiations zimechukua muda mrefu sana. Kama inawezekana kwanini Wizara ya Fedha isitume wataalam kwenda kujifunza kwenye maeneo ya nchi za kiafrika am bapo miradi kama hii inatekelezwa ili i-fast track hiyo negotiation inayofanyika baina ya Serikali na wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muda mrefu sasa mashamba ya watu hayaendelezwi. wananchi wanshindwa kuziendeleza nyumba zao wakisubiri mradi uweze kuja ku- take off lakini mpaka sasa zaidi ya miaka sita au saba mradi haufanyi kazi. Sasa nilikuwa napendekeza Waziri Mheshimiwa Dkt Mpango tunaomba jambo hili mli-fast track kwa sababu kwanza litaleta kodi kubwa kwa Serikali, litatuletea mapato ndani ya nchi lakini pia ni mradi mkubwa wa kielelezo. Leo tukisoma hapa Taarifa ya Mpango, miradi yote ile mikubwa ya kielelezo tunaona inaelekezwa kwenye mikoa ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Mikoa ya Kati hakuna mradi mkubwa wa kielelezo unaokwenda kusini zaidi ya huu mradi wa umeme wa Nyerere na ambao utatekelezwa katika nchi yote sio kwamba utakwenda moja kwa moja Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Mpango ni kweli, naona unasikitika. Ukiangalia kitabu hiki, mradi mkubwa ambao unakwenda direct Kusini ni mradi wa LNG pamoja na mradi wa kiwanda cha gesi cha Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba sisi ni maskini ndiyo maana nilizungumza kwamba…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali, maneno yako haya yana ukweli wowote?

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, yana ukweli.

MWENYEKITI: Haya sema, hebu toa mifano kwamba miradi sijui inaelekea wapi, inaelekea wapi haielekei huko kwenu.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumzia miradi ya kielelezo ambayo imezungumzwa kwenye hotuba.

MWENYEKITI: Si useme mradi fulani na fulani.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano mradi wa reli ya kisasa ambao unatumia pesa nyingi, ukiangalia miradi ukifanya calculation…

MWENNYEKITI: Kwa hiyo ukichukulia mradi kwa mfano wa reli ya kati kukata nchi wewe unaona kama ni ubaguzi dhidi ya Kusini?

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapana! Nilikuwa naendelea, kwa mfano, kuna mradi umesemwa humu wa reli…

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Samahani kuna taarifa Mheshimiwa Waziri tafadhali.

T A A R I F A

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa Taarifa mzungumzaji kwamba tunajenga Bandari Mtwara kwa bilioni 147, tunajenga uwanja wa ndege mpya pale Mtwara, tunajenga barabara ya Mtara – Mivata na karibu tutajenga barabara kutoka pale Mivata kwenda mpaka Masasi kwa zaidi ya kilometa 160. Niliona nikupe taarifa hiyo hayo maneno unayoongea sio kweli.

MWENYEKITI: Ndiyo maana nikakustua kidogo. Unajua kuwa na concept za kama vile kuna ubaguzi baguzi hivi wakati hakuna na haya ni maendeleo ya nchi, maana reli haiwezi kupita angani, lazima ipite mahali fulani. Endelea tu Mheshimiwa.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nakushukuru. Naomba niendelee na uzuri taarifa niliyopewa imezungumza kabisa ni Mtwara, nami nimesema natoka Lindi na Lindi ni Mkoa masikini katika orodha Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango anajua ni Mkoa wa mwisho kabisa. Mradi mkubwa uliotajwa kwa Lindi ni mradi huu wa LNG ndiyo maana nimeusisitiza. Mwishoni nilikuwa nataka niseme kwamba kuna mradi hata wa reli umetajwa kwenye Mpango kutoka Mtwara kwenda Mbambabay. Nilikuwa nataka niseme mwishoni, lakini ameniwahi Mheshimiwa Waziri. Sasa labda nikumbushe kwamba upo kwenye Mpango, lakini yote inazungumzia Mkoa wa Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukizungumza Mkoa wa Lindi specifically, hakuna mradi mkubwa uliotajwa zaidi ya mradi LNG na ndiyo maana naomba ufanyiwe fast tracking. Naomba sana mradi huu kwa sababu ungegusa direct kabisa maisha ya watu wa Mkoa wa Lindi.

MHE. JOSEPH KASHEKU MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa, Mheshimiwa Musukuma nilikuona.

T A A R I F A

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba Kiti chako kilinde hizi kauli zinazozungumzwa na mchangiaji. Tukianza kuzungumza watu masikini; moja ya Jimbo masikini ni Jimbo langu la Geita ambalo miaka yote Serikali imekuwa ikikusanya pato kubwa sana kwenye dhahabu inayotoka Geita, lakini ukienda Geita leo hakuna lami hata robo, hatuna maji ya bomba hata theluthi kwenye Jimbo langu. Juzi tu tumemwona Mheshimiwa Rais anazunguka Mkoa wa Lindi akiporomosha maahadi na kufungua miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa haya maneno anayoyazungumza Mheshimiwa, naomba Kiti chako kimwambie ayaondoe kwa sababu yanatugawa sisi ambao wengine tumechangia mapato makubwa kwenye Taifa hili lakini hatujawahi kuwa na hiyo hata miradi ambayo Mheshimiwa Rais kafungua juzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Serikali ya Awamu ya Tano, Lindi haiwezi kuwa masikini tena kwa ahadi tulizozisikia na ziara iliyofanywa pale; iko ni Mikoa ambayo ni masikini. Sisi Geita ni masikini lakini kwao Mwalongo ni Mkoa wa tatu na hauna dhahabu na hauna kitu chochote. Tukianza kutajana hapa tunajenga chuki na tutaligawa Bunge kwa watu ambao hatujafaidika na hiyo miradi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali, labla uliona kidogo nilijaribu kuingia ingia, anachokisema Mheshimiwa ni kitu cha msingi. Sisi ni viongozi wa Kitaifa, kwamba kuchaguliwa kwangu Kongwa kuja hapa au ninyi kwa madirisha mliyoingia nayo, ni namna ya kupatika kwenu. Katika nchi yetu tumeamua kwamba tupatikane kwa taratibu hizi tulizopatikana, wengine Viti Maalum, wengine Jimbo hili, zile categories zetu za kupatikana kwetu.

Tukishafika hapa, sisi ni viongozi wa Kitaifa. Haisadii sana kama kila anayesimama atakuwa anapanda mbegu za kibaguzi kuonesha kwake ni masikini, kwake ni nini; factors za umasikini ni nyingi, hazitokani na Serikali peke yake. Tusingekuwa Bungeni huko, tungekaa nje tungeanza kuambiana. Mimi mwenyewe nimeishi Lindi, ningeweza kukwambia baadhi ya mambo ya umasikini, hili nalo Serikali! Kwani watu wa Kongwa ni tajiri? Ni masikini, na kadhalika.

Kwa hiyo, concepts hizi za kwamba kuna ubaguzi na nini, hizi fikra siyo sahihi. Kama ndiyo mnawahutubia watu wenu namna hiyo, mtazidi kuwachelewesha. Tusonge mbele, twende mbele kama nchi. Wewe jenga hoja yako ya mradi wa LNG, nasi tunaunga mkono wote. Tutapinga kwa sababu gani? LNG ina faida kubwa katika uchumi wa nchi. Sasa LNG utaiweka Kongwa? Si lazima iwekwe Mtwara bwana au Lindi ambako na gesi iko huko huko na kadhalika! (Makofi)

Kwa hiyo, tuisaidie Serikali katika namna ya kuweka mambo vizuri kwenda mbele, lakini hii ya ubaguzi baguzi kila wakati kwamba kuna hiki, kuna kile unless kweli unaona kuna ubaguzi hatukatai, lakini kama haupo haisaidii sana kupanda mbegu za kibaguzi. Inaleta tu sentiments, hata kwa wengine unaona watu wanaanza kuwaza kwamba dhahabu yetu na kadhalika. Kweli raslimali za Taifa siku zote sera yetu ni kwamba zinakuwa katika chungu kimoja, tuna-share wote, hata korosho ile nasi tunapatapata mnyepe mnyepe huko kidogo, na kadhalika.

Mheshimiwa Bobali, endelea tu.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima yako nimeamua niifute kabisa ile, naona iondolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumzia jambo la pili ambalo ni Sekta ya Uvuvi. Tuna eneo kubwa la bahari ambalo kama wavuvi wangekuwa wanawezeshwa na ni Mheshimiwa Ghasia amezungumzia hapa, tungeweza kuongeza kipato cha wananchi kwa kutumia Sekta hii ya Uvuvi. Niseme, wakati Waziri wa Uvuvi akiwa Mheshimiwa Dkt. Magufuli ambaye sasa hivi ni Rais wa nchi, wavuvi waliwezeshwa kwa kupewa boti, mashine na vifaa; vyavu za kuvulia. Ulikuwa ni mpango madhubuti wa kuwawezesha wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nahoji leo, ule mpango uko wapi sasa hivi? Watu walihamasishwa waache kutumia uvuvi wa mabomu; na kwa kiwango kikubwa kabisa watu wameacha sasa hivi utumiaji wa mabomu, umekufa kabisa, haupo. Bahati mbaya sasa mabomu hayatumiki, lakini leo ukienda kijijini kule huli samaki, kwa sababu hawana alternative. Nyavu tunajua namna ilivyo. Nyavu ambazo wanaweza kuzinunua na kuzifikia ni hizi za bei ya chini ambazo nyingi zimekatazwa kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri Mpango hebu tengenezeni mfumo maalum wa kusaidia wavuvi; na siyo wavuvi wa ukanda wa bahari tu, hata wavuvi waliopo kwenye maeneo ya mito, ziwa na wenyewe pia. Kwa mfano, kwenye Sekta ya Kilimo kuna Taasisi nyingi sana zinazosaidia kilimo, ukianza kuzihesabu hapa, zaidi ya tano, sita, zote zina-deal na wakulima; lakini kwenye uvuvi huoni hizo Taasisi ambazo zimeanzishwa na Serikali. Zinasaidia moja kwa moja wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukiulizia hizi boti ambazo zimepewa ruzuku ya Serikali tunazipataje? Ukimwuliza hapa ndugu yangu Mheshimiwa Ulega atakwambia fuata utaratibu huu, mimi nilishawahi kuzungumza nao, utaratibu wake ni mrefu mno, mlolongo wake ambao kwa mwananchi wa kawaida, aliyeko Mchinga, Ruvu, Lushungi na kwingineko hawezi kufikia; na tumejaribu mara kadhaa, imeshindikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekeza kwenye Sekta ya Uvuvi kiwekwe kitengo maalum ambacho kitakuwa kinasaidia wavuvi hata kwa kutoa subsidiaries kwa wavuvi ambao watakuwa wanataka kununua aidha boti, ama injini za boti ama nyavu zile kubwa za kuvua baharini. Vinginevyo samaki wapo baharini kule, wamebakia wengi, watakuja wavuvi kutoka nje na meli zao, watapata vibali, watakwenda kuwavua, wataondoka. Sisi hapa hatutakula samaki wazuri kwa sababu wavuvi wetu hawana capacity ya kuweza kuvua vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo nilitaka nilichangie ni suala la fedha za TARURA. Miradi ya maendeleo ya TARURA na Waheshimiwa Wabunge wengi wamechangia hapa, kwamba kweli inapatikana asilimia 30 ni ndogo; na kwa bahati mimi ni Mjumbe wa Kamati ya TAMISEMI na Utawala ya Bunge ambayo inasimamia hiyo TARURA. Shida kubwa, ukikutana na watu wa TARURA, ni kwamba siyo kutengwa tu ile asilimia 30, shida nyingine ni kwamba hiyo asilimia 30 yenyewe haipelekwi. Yaani utakuta barabara imetengewa shilingi milioni 100 au milioni 150 ambayo inapaswa ipelekwe, lakini mpaka mwaka wa fedha unamalizika, fedha ile haikupelekwa, labda imepelekwa asilimia 40 au asilimia 50. Kwa hiyo, jambo hili na lenyewe ni la muhimu sana. Ufuta, korosho, zabibu na vitu vingine vinalimwa huko vijiji ambako vinahitaji usafiri wa uhakika. Sasa kama TARURA ingekuwa inawezeshwa, yule sungura mdogo wa asilimia 30 ambaye amepangiwa kwa mujibu wa sheria, wangekuwa wanapata kwa uhakika. Nadhani barabara nyingi za vijijini zingekuwa zimetatuliwa ile changamo ambazo zipo kwa sasa hivi ambayo nyingi hazipitiki zingekuwa zimeweza kuondolewa changamoto hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii adhimu niweze kuchangia taarifa ya Kamati hizi mbili. Nitajikita zaidi kwenye Kamati ya Kilimo, Kamati ambayo nilidumu kwa takriban miaka miwili na nusu.

Mheshimiwa Spika, nianzie na suala la korosho. Msimu uliopita huu wa 2019 hakukuwa na malalamiko mengi ya wakulima wa korosho kucheleweshewa kulipwa fedha zao, ingawa bei ime-drop tofauti na msimu uliopita ule wa 2018, lakini malipo yalikwenda kwa haraka. Changamoto ni msimu wa 2018.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri yupo hapa, anajua, wako wakulima mpaka leo wanadai fedha zao. Mpaka sasa nilitegemea taarifa ya Kamati inge-include kwamba ni kwa kiwango gani ama ni kiasi gani ambacho wakulima bado wanadai hawajapatiwa fedha zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakumbuka taarifa ya mwaka 2019 ya Kamati hii ya Kilimo ilielezea na iliitaka Serikali kuhakikisha wanakamilisha malipo ya wakulima kwa wakati. Kwa hiyo, naomba sana Wizara ihakikishe kwamba deni la msimu wa 2018 wanalimaliza. Taarifa zilizopo ni kwamba information ambayo Waziri anayo, ile amount ambayo wakulima walikuwa wanadai na Serikali ikatoa, namshukuru Mheshimiwa Rais alitoa zile fedha, lakini zile information inaonekana hazikuwa sahihi, kuna fedha nyingi zaidi ya shilingi bilioni 10 ambazo hawa wakulima waliachwa, hawakuwa included. Kwa hiyo, hii ndiyo leo ukienda pale Mtwara unakuta wakulima wa korosho siku zote wanaenda Mtwara, wanarudi wanaambiwa tutawalipa pesa ikipatikana.

Mheshimiwa Spika, imefikia hatua wakulima waliouza korosho 2019 wamekatwa fedha zao wakiambiwa kwamba tuliwalipa shilingi 3,300/= mwaka 2019 kwahiyo tunazikata hizi fedha kwenda kuwalipa wakulima wengine ambao hawajalipwa, lakini mpaka sasa malipo hayajafanyika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana, kwa kuwa Waziri yupo, Naibu Waziri yupo, wajitahidi kuhakikisha wanakamilisha kulipa deni la mwaka 2018. Kuna wakulima wengi ninaowafahamu, wapo wanadai na kila siku wamekuwa wakisumbuka kwenda Mtwara kufuatilia fedha zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo zao la nazi, nimekuwa nikisema sana hapa zaidi ya mara mbili mara tatu. Zao hili liko hatarini kupotea na ni zao ambalo kwa mikoa ya Pwani wale Waswahili tunaotokea Pwani ni kama identity yetu. Identity ya miji yetu, inapendezesha miji yetu lakini pia ni kwa wapenzi wa chakula ambacho kimeungwa na nazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unajua, utafiti unahitajika kufanyika kwenye zao la nazi. Minazi mingi sasa hivi ukienda Kisiju imekufa, hukuti ile minazi ya zamani sasa hivi. Ukienda Pangani, the same story, ukienda Lindi minazi mingi pale eneo la Ng‟apa ambalo ndilo eneo linategemewa kutoa nazi nyingi, inakufa na nimekuwa nikisema mara nyingi sana. Kuna wakati nilizungumza na Mheshimiwa Naibu Waziri pale ambaye sasa hivi yuko Utumishi wa Umma nilimwambia niko Jimboni nimewakuta wakulima wanalia minazi inakufa. No research tujue kwamba kitu gani kinapelekea minazi kufa ili ufanyike utafiti tuweze kutibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama ujuavyo, mtu wa Pwani akila ubwabwa au wali ule bila nazi, hauendi kabisa. Tunaomba sana ufanyike utafiti wa kina ili ijulikane tatizo ni nini?

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, mvua zinanyesha, kwa hiyo, ilikuwa ni wakati muafaka sasa hivi wananchi kuhakikisha wanavuna maji. Maji ya mvua yangeweza kutumika kwenye kilimo cha umwagiliaji lakini pia hata matumizi ya kawaida. Wakiulizwa swali hapa Wizara ya Maji, unakuta kila Mbunge anasimama kuonyesha kwamba kwake kuna shida ya maji. Mwaka 2019 tulipitisha Sheria ya Maji hapa. Sheria ile inataka uvunaji wa maji, mtu akivuna lita 20,000 awe analipa kodi. Ukiangalia lita 20,000 ni kidogo sana kwa matumizi.

Mheshimwa Spika, nilifikiria Kamati ingekuja na mapendekezo, kwa sababu haya niliyaona nikiwa Mjumbe wa Kamati hii, wananchi na wadau walikuja kulalamikia kwamba sheria hii inaweza ikakwaza watu wenye malengo ya kutaka kuvuna maji ya mvua. Mvua Mwenyezi Mungu ametujalia kama mwaka huu mvua ipo ya kutosha sana, lakini shida ni hiyo kwamba sheria inataka ukishafikisha kutaka kuvuna lita 20,000 ambayo ni maji kidogo sana, uweze kulipa kodi, uitolee taarifa Wizarani na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napendekeza sheria hii ingefanyiwa marekebisho. Kamati ingekuja na mapendekezo sheria hii kuifanyia marekebisho kuongeza wigo na ku-encourage watu waweze kuvuna maji ya mvua ili tupunguze hili tatizo la watu kulalamikia maji, maji maji.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, niliamua nichangie kwenye Sekta hii ya Kilimo. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati Kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu, leo nami nasherekea kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa, natimiza umri wa miaka kadhaa. Kwa hiyo nakushukuru kupata fursa hii, lakini pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa umri alionijalia.

Mheshimiwa Spika, nianze suala la Uhamiaji hususan kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara. Mpaka kati ya Msumbiji na Tanzania sielewe kuna tatizo gani? Kuna ndugu zetu; ukienda Mtwara kuna watu wanahitwa Wamakonde. Hawa Wamakonde wapo kwenye nchi mbili; wanaotoka Msumbiji na wengine waliopo huku ng‟ambo, Tanzania.

Mheshimiwa Spika, unakuta unapofika wakati wa uchaguzi wa Msumbiji hawa watu wanaletewa masanduku na wanapiga kura kuchagua Rais wa Msumbiji, halikadhalika watu hawa hawa ukienda unakuta wamejiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, sasa jambo hili ni hatari sana. Namshukuru Afisa Uhamiaji wakati ule wa mchakato wa Serikali za Mitaa, Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Lindi tulishirikiana naye vizuri sana na kuna baadhi walikwenda wakawaondoa kwenye list ya watu waliojiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kujua kwamba walishiriki kwenye uchaguzi wa Msumbiji. Kwa bahati mbaya, watu wale waliondolewa kwenye daftari la kupiga kura za Serikali za Mitaa lakini wapo wengine kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba jambo hili lifuatiliwe, hususan Waziri wa Mambo ya Ndani, namheshimu sana kaka yangu Komredi Simbachawene, hayupo lakini jambo hili ni muhimu sana kuhusu suala la uhamiaji. Unajuwa sasa hivi pale mpakani kati ya Mtwara na Msumbiji hali siyo nzuri sana, kumetokea mauaji hivi karibuni, lakini nafikiri kama kuna uholelaholela wa namna ya watu kupita pale, mwingiliano umekuwa wa kawaida sana, yaani huwezi kujuwa kama mtu anavuka anaenda upande wa pili; anaenda Msumbiji au anaingia Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na uholela mkubwa sana, inafikia hatua tuliona wakati fulani hapa mwaka uliopita 2019, kuna ndugu zetu kule Tandahimba walipoteza maisha na sijajuwa kama wale watu walishakamatwa au namna gani, lakini ni kwa sababu ya ule mwingiliano. Waziri wa Ulinzi, yupo anafahamu kwamba kuna watu wa Tanzania wanalima Msumbiji na kuna watu wa Msumbiji wanalima Tanzania.

Mheshimiwa Spika, sasa lile suala la mpaka pale, namwomba Mheshimiwa Waziri alichukulie kwa umakini na kwa uzito mkubwa sana. Kumekuwa na uholela sana katika mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji kwenye kile kipande cha kule Mkoani Mtwara.

Mheshimiwa Spika, Jambo lingine, pale Jimbo la Mchinga kuna Gereza moja linaitwa Kingurugundwa. Ni Gereza maarufu sana, wale wafungwa watukutu ndio wanapelekwa pale. Kwenye kadhia hii ya mafuriko yaliyotokea Mkoa wa Lindi, hili Gereza sasa hivi kama liko kisiwani vile; na wako mahabusu pale wanatakiwa wapelekwe Mahakamani, lakni takribani sasa karibu wiki ya pili inashindikana.

Mheshimiwa Spika, hata yale maji yakiondoka, barabara ya kutoka pale barabara kubwa kwenye eneo la Mkwajuni kwenda pale Kingulugundwa almost too kilometers, ni ngumu kulifikia. Kwa hiyo, naomba hili Gereza kwa sababu la umuhimu wake huo na haliko mbali kutoka barabara kuu, lakini wamekuwa wakipata shida sana ya usafiri, namna ya kusafirisha watuhumiwa au mahabusu kuwapeleka Mahakamani na hata wale Askari wenyewe, huduma zile za kiusafiri zimekuwa ngumu sana.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, kumekuwa na malalamiko mengi kwa wananchi ukisikiliza juu ya traffic kubambikia kesi madereva. Jambo hili nalo ni kero kwenye jamii. Tunajadili suala la mambo ya ndani ya nchi, tunaangalia viashiria ambavyo vinaweza vikaleta shida kwenye nchi; suala la ma-traffic kubambikia kesi madereva limekuwa kubwa na wakati wengine hata sisi wengine linatukuta.

Mheshimiwa Spika, unamkuta traffic anakwambia ume-over speed, ukimwambia nionyeshe gari, wengine hawataki na akikuonyesha unakuta siyo gari yako kabisa. Kwa hiyo, hili limekuwa ni tatizo na wamekuwa watu wakibambikiwa na madereva wanalalamika sana kwamba kwa nini tunabambikiwa kesi namna hii? Inaonekana kama ni kitega uchumi cha kukusanya fedha, jambo ambalo kwa kweli siyo nzuri sana. Naelezwa hapa, wakati wengine wanakaa porini wanajificha kwa ajili ya kuchukuwa hizo picha.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nataka nizungumzie ni kuhusu suala la matamko yanayotolewa na baadhi ya viongovi wa Vyama vya Siasa. Taifa hili letu wote na tunapenda tuendelee na amani hii iliyokuwepo, lakini panapotokea viongozi wanatoa matamko ya kuashiria kama ni uchochezi, wakitoa upande fulani hawashughulikiwi, huoni hata wameitwa Polisi, wakitoa upande mwingine wanaitwa. Jambo hili kwa ustawi wa Taifa letu siyo jema sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeona juzi huko Arusha Mwenyekiti wa UVCCM ametoa tamko baya sana. Nilifikiri angalau angewahi kuitwa akahojiwa.

SPIKA: Mheshimiwa Bobali, unajua watu wengine wala huna haja ya kupoteza muda. Niko na wewe, sikupingi, yaani wako watu, wewe hebu endelea na mengine tu.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nashukuru Mheshimiwa Spika.

SPIKA: Kwa sababu ni matamko ambayo hakuna anayekubaliana nayo hata robo. Hakuna! Kwa hiyo, tutakuwa kama tunakuza kitu ambacho… mmh!

Nafikiri sisi kama Wabunge, tuko above that.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Okay.

SPIKA: Huo ndiyo ulikuwa ushauri wangu, ahsante.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nashukuru.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho nilitaka niongelee dogo tu. Kwa kuwa tunazungumza Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na furaha kwenye nchi; kuna jambo ambalo linaendelea sasa hivi hasa kwenye mitandao ya kijamii, watu wanalalamika sana juu ya upendeleo wanaopewa timu ya samba. (Kicheko/Makofi)

Eeeh, ndiyo! Marefaree, nilikuwa naomba…

SPIKA: Mheshimiwa Bobali ngoja nikae vizuri. Ngoja nikae sawa sawa, unaweza ukaendelea Mheeshimiwa Bobali. (Kicheko/Makofi)

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tendency ya watu watu kulalamika. Mambo haya, wakati timu fulani inapendelewa kulikuwa na viti vilivunjwa pale na wengine walirusha viti pale Uwanja wa Taifa. Ni jambo baya sana. Sasa hili lazima likemewe na Waziri wa Mambo ya Ndani lazima ahakikishe kuna amani. Sisi wote tunapenda furaha.

Mheshimiwa Spika, jana nimelala sikufurahi kabisa kwa sababu siyo Yanga ilifungwa, sikufurahi kwa sababu Timu ya Polisi walichofanyiwa jana is not fair. Kwa hiyo, jambo hili sasa imeonekana kama tabia inataka kukua na wananchi tuna mambo mengi ya kufurahia. Wengine tunapenda mpira, kwa hiyo...

SPIKA: Kuna taarifa unapewa, sijui! (Kicheko)

MBUNGE FULANI: Aah, hapana Mheshimiwa Spika! (Kicheko)

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, kuna taarifa bwana!

T A A R I F A

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wao walipokuwa wanachangia bila kibali, sisi tulikuwa hatusemi. sasa inawauma, wakae watulie tu, ubingwa ni wetu. (Kicheko)

SPIKA: Pokea hiyo taarifa Mheshimiwa Bobali.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nimeipokea, nakushukuru sana. Ahsante sana.
Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Wabunge wenzangu wa Chama cha CUF, naomba niseme kwamba sisi tunaliunga mkono Azimio hili. Tunaliunga mkono sehemu hii ya Selous kuchukuliwa kufanywa kuwa ni hifadhi na kiukweli yapo mafanikio ama faida ambazo zitaonekana hapo baadaye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mimi ni Mbunge ninayetoka Mkoa wa Lindi, naomba nieleze machache ambayo Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha hoja anaweza akawa na majibu. Kwanza, ifahamike mbuga ya Selous inachukua asilimia 38 ya Mkoa wa Lindi. Mkoa wenye ukubwa wa square kilometer 67,000 asilimia 38, zaidi ya square kilometer 24,000 ni Msitu wa Hifadhi wa Selous.

Mheshimiwa Spika, jambo la kupandisha hadhi sisi kama Mkoa wa Lindi utaathiri moja kwa moja, inawezekana athari zikawa za faida (positive) ama negative. Nataka nihoji mambo kadhaa, sasa hivi ukiwa unatembea unatoka Nangurukuru Kilwa unaelekea Liwale hasa muda wa asubuhi, ajabu sana utakutana na malori yanabeba magogo yanayotoka kwenye Selous, tena malori yenyewe hata plate number hayana, yaani yale malori ya zamani, yaliyochakaa na ni mengi. Mimi nimefanya ziara hivi karibuni nimekutana na malori mengi yanakata miti nikastaajabu hii ni kwa mujibu wa vibali ambavyo vimetolewa ama imekuwaje.

Mheshimiwa Spika, pia wafugaji sasa, ukitoka eneo linalopakana kati ya Kilwa na Liwale, maeneo ya Zinga unaelekea Liwale kumekuwa na uvamizi mkubwa wa wafugaji, ng’ombe wako wengi, kule msituni kuna ng’ombe wengi na kuna ukataji hovyo wa miti katika eneo lile. Sasa tunakupandisha hadhi swali linakuja hawa wafugaji ambao wamevamia kwa kiwango kikubwa, wafugaji wengi Mkoa wa Lindi wako Liwale na unapozungumza Selous Mkoa wa Lindi unazungumzia Wilaya za Liwale na Kilwa na Halmashauri ya Lindi Vijijini ya kwetu sisi, hawa wafugaji mtawapeleka wapi, ni wengi mno na wana mifugo mingi kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Lindi ambayo ina eneo kubwa la Selous na nimeangalia ramani ya eneo ambalo linachukuliwa kupelekwa Selous, tuna vivutio vingi kabisa ambavyo kupandishwa hadhi kwa pori hili kunaweza kukaunganisha utalii wa Kusini especially utalii wa Lindi. Mfano, tunao mji mzuri wenye historia, Mji wa Kilwa Kisiwani ambao ni kivutio kizuri kabisa cha watalii na inafanya vizuri sasa hivi ukiangalia ile channel yetu ya Tanzania Safari huwezi kuangalia siku mbili kama hujaona inaonyeshwa Kilwa Kisiwani. Nadhani upandishaji wa hadhi wa pori hili unaweza ukaunganisha sasa utalii ukaenda moja kwa moja kwenye Mji wa Kilwa Kisiwani na fukwe nzuri zilizopo katika Pwani ya Kusini maeneo ya Lindi mpaka Mtwara hasa eneo la Mikindani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia mimi nina hakika kwamba jambo hili ili liwe jema sana hizi fedha za REGROW ambazo zinataja Southern Circuit ya utalii ziguse na Mkoa wa Lindi, hazitugusi. Hili ni swali Mheshimiwa Waziri kwako. Fedha za Southern Circuit zinakwenda Mkoa wa Morogoro, Iringa na Njombe, ni fedha zilizosababishwa na Selous, sisi ambao tunachangia kilometa za mraba 24,000 kwa nini fedha hizi hazitugusi? Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha ajibu na swali hili fedha za REGROW sisi watu wa Lindi tunazikosaje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimesema tunaunga mkono jambo hili lakini liendane na uboreshaji wa miundombinu ya barabara. Barabara ya kutoka Nangurukuru kwenda Liwale zile kilometa 230 ni ya vumbi. Kwa hiyo, watalii watakwendaje ikiwa ile barabara haipitiki? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mnaweza mkastaajabu, Lindi tumepakana na Mkoa wa Morogoro kule kwa Mheshimiwa Mlinga, watu wanatoka Liwale wanakwenda Mahenge wanatembea kwa miguu wanatumia zaidi ya siku 5, 6 na wanasindikizwa na wale askari wanyamapori. Naomba upandishaji wa hadhi wa msitu huu uendane na ujenzi wa miundombinu ili na sisi watu wa Lindi tuweze kunufaika na hifadhi ya Nyerere. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wenzangu wote na mimi tunaunga mkono Azimio hili. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza nichukue fursa hii kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kufanya social cooperate responsibility yeye akishirikiana na Mkurugenzi wa TPDC, namshukuru sana engineer Kapulya wamewasaidia wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri anafanya kazi nzuri. Katika Mkoa wa Lindi tatizo la umeme sasa hivi katika maeneo mengi limekwisha na nilisema mwaka jana sisi Lindi na Mtwara tulikuwa tuna shida sana ya umeme, lakini walivyotuingiza kwenye grid ya Taifa wamepunguza ile changamoto ya umeme, sasa hivi unaweza kwenda kukaa kijiji kule uka-relax kwa kuwa umeme utakuwa unaupata.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri juzi alikuwepo Lindi na tulizungumza, kuna yule Mkandarasi State Grid sasa hivi ameanza kufanya kazi, lakini katika Majimbo manane ya Mkoa wa Lindi Majimbo ya wenzangu yote yamepelekewa nguzo na kazi inafanyika. Jimbo la Mchinga tu ndiko ambako hata nguzo moja haijapelekwa. Sasa Mheshimiwa Waziri hili analiweza walau leo tu amwagize kwamba walau zile nguzo zipelekwe pale tuwe na imani. Viko vijiji vimeingia kwenye REA awamu III, phase one Vijiji vya Ruvu na Dimba na nimeshampelekea mara nyingi sana Mheshimiwa Waziri na haviko mbali na ulikopita umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaomba sana Mheshimiwa Waziri hivi vijiji na namshukuru sana Meneja wa TANESCO wa Mkoa ndugu yangu Makota, kama tulivyoongea wakati ule mwezi uliopita alikwenda mpaka kwenye vile vijiji akafanya survey na baadaye nadhani alileta taarifa kwamba yale maeneo hayahitaji nguzo nyingi ili kupelekwa umeme. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri naomba sana na mimi nione kwamba katika maeneo yale ya Ruvu na Dimba nguzo zinapelekwa ili wananchi wale waweze kupata umeme. Ni vijiji ambavyo viko pembezoni mwa bahari, ni wale wavuvi wamejenga nyumba nzuri, wakiweka na umeme pale mambo yataenda vizuri sana. Kama pale Ruvu pana ile bandari ndogo inatumika, bila umeme kwa kweli ni changamoto kidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nishauri mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la mradi wa gesi wa LNG, nisipouzungumza huu mimi natoka Lindi, natoka Jimbo la Mchinga ambako ndiyo eneo kabisa mahususi sisi pale na Lindi Mjini mradi huu utatekelezwa. Mradi huu wa LNG kwanza utakuwa na faida kubwa kwa Taifa, utakuwa na faida kubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi na wananchi wa Mkoa wa Mtwara na utakuwa ndiyo mradi mkubwa kabisa kuliko miradi yote katika Afrika Mashariki. Mradi wenye uwekezaji wa dola bilioni 30 siyo mradi mdogo ni zaidi ya trilioni 69.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu ukizungumza na wawekezaji, juzi nilikutana nao Lindi, wao wanaonesha kwamba hata kesho wako tayari, Wizara wanaonesha hawana tatizo. Baada ya ku-study huu mchezo, maana kila siku ukiuliza huku unaambiwa hivi, nimegundua tatizo lipo kwenye taasisi ama sekta moja inaitwa Government Negotiation Team, Timu ya Uatanishi/Mapatano ya Serikali inaonesha kwa sababu hata kwenye kitabu cha Waziri kwenye ukurasa wa 93 alipozungumzia huu mradi amezungumzia kwamba mwaka huu bado utaendelea na majadiliano kati ya Serikali na Wawekezaji. Sasa ninachopata shida ni kwamba, wawekezaji wanaonesha wako tayari Serikali wako tayari, kwa nini kwa miaka minne sasa hii negotiation team bado haijamaliza kujadiliana na wawekezaji kujua kwamba Serikali itapata hiki na wao watachukua hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, LNG sisi hatuanzi huu mradi, siyo kwamba Tanzania tunaanza, ziko nchi ambazo tayari wana hii miradi. Nitatoa mfano, Algeria, wameanzisha mradi wao LNG ulianza mwaka 1964. Tangu mwaka 1964 hivi hii Government Negotiation Team inashindwa kusafiri kwenda Algeria kwenda kujifunza wenzetu walikubalianaje, Serikali inanufaikaje na sisi Tanzania tutawezaje kuwekeza kwenye huu mradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Msumbiji wana Mradi wa LNG, Angola wana Mradi wa LNG, Egypt wana Mradi wa LNG, sisi hatuanzi. Kama kuna tatizo wanaona kwamba labda inawezekana Serikali itaingia hasara, twende tukajifunze kwa hawa wenzetu, hawa ni Waafrika wenzetu. Bahati mbaya sana makampuni yenyewe yanayokuja kuwekeza hapa ndiyo hayo hayo ambayo yako Namibia na Egypt, Shells Equinor, Camel ndiyo hayo hayo kwa sababu haya ndiyo makampuni yanaongoza duniani kwa uwekezaji kwenye gesi. Napata ukakasi sana mradi mkubwa kama huu kila mwaka tunauchezea na gesi ipo tu pale baharini katujaalia Mwenyezi Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tumegundua gesi sambamba na Msumbiji, wenzetu Msumbiji wameanza kunufaika na gesi wanaumeme wa uhakika, maendeleo yao yanakwenda kwa haraka sana, sasa hivi wameshatuacha. Tuna mfano mzuri wa kuutazama Uingereza na Norway waligundua gesi mwaka mmoja. Norway wamenufaika sana na gesi, Uingereza mpaka sasa hawajanufaika chochote na gesi. Ukisoma kwenye vitabu vyao wanasema hata wao hawajui kwanini hawajanufaika na gesi, lakini wamegundua mwaka mmoja na wako jirani pale Norway wame-advance sana, wameendelea kwa kutumia gesi, sasa na sisi tukichelewa wenzetu Mozambique wataendelea watatuacha sisi tutaendelea kukaa kila siku Government Negotiation Team haijamaliza kazi, tunaendelea kuwa maskini wakati siyo watu maskini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo gesi hii ametupa Mwenyezi Mungu ipo pale kwenye visima, Zafarani na maeneo mengine, tuitumie. Kama kuna tatizo wanaliona kwenye makubaliano, basi waende wakajifunze hayo maeneo mengine wenzetu walifanyaje ili huu mradi uweze kuondoka. Sisi tumekaa tunausubiria pale Mchinga, tumejaribu kujipanga ukifika tufanye nini hatuna shida, wananchi tutawapokea hao wawekezaji,watakaa vizuri na eneo wameshaandaa kulipa fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, angalia, mwaka jana kwenye bajeti ya...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia Sera za Elimu hapa nchini. Mheshimiwa Waziri nianze kwa kukuomba kukipatia fedha za maendeleo Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kiweze kukamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa lililoanza kujengwa miaka minne iliyopita. Mheshimiwa Waziri Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere zamani Kivukoni ni chuo kinachobeba historia kubwa ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni chuo cha kwanza kujengwa na Watanzania wenyewe tena kabla ya kupata uhuru. Chuo kile kimesaidia sana kuwaandaa viongozi wa nchi jirani kama vile Jocob Zuma, Rais wa Afrika Kusini. Mheshimimiwa Waziri jambo lingine ni kuhusu kuzisimamia na kuziangalia kwa karibu mno shule binafsi. Utaratibu wa shule binafsi ni mzuri sana tena sana, umesaidia kwa kiwango kikubwa mno kupungua kwa watoto waliokuwa wanakwenda nchi jirani kutafuta elimu bora. Hivyo umuhimu wake ni mkubwa mno, lakini kuna haja ya kuziangalia mara mbili zaidi hususani katika mambo muhimu mawili; kwanza ni kuhusu suala la ada kuwa kubwa mno na pili, huduma ya chakula kinachotolewa shuleni; kwa nini shule nyingi za binafsi hususani za Dar es Salaam hazitoi chakula kwa wanafunzi hasa zile shule za kutwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa watoto wadogo kuchukua pesa kwa wazazi wao ili wanunue chakula si mzuri hata kidogo na unapelekea watoto wetu kula vyakula visivyoeleweka, lakini pia ni chanzo cha kuwafundisha watoto tabia mbaya ya kupenda pesa wangali wadogo. Mheshimiwa Waziri naomba Wizara yako itoe maelekezo kwa shule zote binafsi zile za kutwa kuhakikisha zinawapatia chakula watoto wadogo wawapo shuleni badala ya kuwaambia wazazi watoe pesa kuwapatia watoto wakanunue wenyewe chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni uchache wa vyuo vya elimu ya juu na ufundi katika Mkoa wetu wa Lindi. Mkoa wetu wa Lindi una vyuo viwili tu ambavyo ni VETA Lindi na Chuo cha Utabibu. Naomba Serikali ilete vyuo zaidi Lindi kwani ardhi ya kujenga vyuo ipo na usafiri hivi sasa umeimarika hivyo kuharakisha mawasiliano. Nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na matukio kadhaa hapa nchini ya wananchi kuokota mabomu ambayo yalikuwa ardhini tangu wakati wa Vita ya Majimaji na Vita vya Dunia. Mifano ni mingi, lakini kwa Mkoa wa Lindi maeneo ya Mahiwa, Kiwalala na Ndanda yamekuwa yakitokea mara kwa mara .

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Jeshi lifanye utafiti wa kutosha hususan katika maeneo yote ambayo Vita vya Majimaji vilipigana pamoja, Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia. Wanajeshi wa Ujeremani katika maeneo mengi walizika silaha zao ardhini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali suala hili mlipe uzito unaostahili mfanye utafiti wa kutosha ili kuepusha madhara zaidi. Mifano mizuri ni maeneo ambayo Wajerumani walikuwa na mashamba ya mkonge na baadhi ya sehemu ya ngome zao. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba ufafanuzi kuhusu miradi mingi ya umwagiliaji iliyoanzishwa katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini, kwani haijakamilika na hivyo kupelekea fedha nyingi za walipa kodi kuwa zimetumika lakini hakuna matunda yaliyopatikana. Mifano ni mingi sana, lakini kwa sasa naomba kupata maelezo juu ya skimu mbili zilizopo katika Halmashauri yetu ya Lindi DC.

Mheshimiwa Naibu Spika, Skimu ya Kinyope iliyopo katika Jimbo langu ambayo ilikusudiwa kumwagilia hekari 400, lakini hadi sasa mradi unaonesha kuwa umekamilika ilhali bado, mradi ule haujatatua changamoto zilizopo pale, badala yake imeongeza maji kuwa yanamwagika hovyo katika mashamba ya wakulima, jambo ambalo linapelekea kilimo kuwa kigumu.

Mheshimiwa Naibu Spika, skimu ya pili, ni ile ya Narunya iliyopo katika Kata ya Kiwalalu, Jimbo la Mtama ambapo shilingi milioni 600 zimetumika, lakini hadi leo hakuna kinachoendelea na badala yake maelezo yanayotolewa ni kwamba designer alikosea. Sasa Je, nini hatima ya mradi ule?

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, ni vile visima viwili ambavyo vilichimbwa Jimboni kwangu Mchinga na Wakala wa Serikali wa Uchimbaji na Visima (DDCA). Naomba tafadhali miundombinu ya visima vile vikamilishwe. Pia naomba kupatiwa visima vingine viwili katika Vijiji vya Maloo na Makumba. Vijiji hivi vina shida kubwa sana ya maji. Wananchi wa vijiji hivyo wanatembea zaidi ya kilometa tano kufuata maji. Tafadhali sana naomba Mheshimiwa Waziri anipatie maji katika vijiji hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu, ni kuhusu kutotumika kwa bonde la Mto Rufiji ambalo ni very potential kwa kilimo cha umwagiliaji, lakini bonde lile halitumiki kabisa. Hawa watu wa RUBADA hawafanyi juhudi yoyote kuhakikisha kuwa kilimo cha umwagiliaji kinashika kasi katika bonde la Mto Rufiji.

Mheshimiwa Naibu Spika, tafadhali sana, naomba Mheshimiwa Waziri achukue juhudi za makusudi kuhakikisha kuwa bonde hili linatumika ipasavyo ili tuondokane na taarifa za njaa katika Taifa ambalo lina ardhi ya kutosha na maji mengi yanayoweza kutumika katika kilimo cha umwagiliaji.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamuomba sana tena sana Mheshimiwa Waziri, waichukue barabara ya Chikonji – Nangani kwenda Milola iingie kwenye barabara za TANROADS. Ni barabara kubwa na muhimu sana kwa uchumi wa wakazi wa Jimbo la Mchinga na Lindi Mjini. TARURA hawawezi kujenga barabara hii ina madaraja mengi na makubwa hivyo kuachia TARURA si sawa hata kidogo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (The Mwalimu Nyerere Memorial Academy) kilichopo Kigamboni Dar es Salaam kuna faculty (fani) ambazo watu wamesomea lakini huko kwenye soko la ajira wanaambiwa faculty hizo hazitambuliki katika mfumo wa ajira (caurdon). Nakutajia faculty hizo ni Politics And Management of Social Development na Gender and Development (GD).

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali naomba sana ufafanuzi wa jambo hili kwa kuwa ni kilio cha wahitimu wengi ambao hivi sasa wapo mtaani zaidi ya miaka mitatu bila ya kupata ajira Serikalini. Mheshimiwa Waziri, jambo hili ni aibu kwa Serikali kwa kuwa chuo hiki ni cha Serikali na miongoni mwa vyuo vikongwe hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kubwa ni kwamba chuo hiki hakijakamilika kwa jengo la hosteli la ghorofa tatu, ambalo limeanza kujengwa zaidi ya mika mitano sasa. Jengo hili lilikusudiwa kuwa hostel ya wanafunzi wa shahada ya pili (Masters Degree Students Hostel) mwaka huu nimeona mmetenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya Development Project. Sasa je, hii bilioni moja ndiyo inakwenda hapo au sehemu nyingine tofauti?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali, namuomba sana Mheshimiwa Waziri, tupatieni fedha ya mabweni katika Shule ya Sekondari Mchinga ili shule iweze kupandishwa hadhi kuwa ya A-Level. Shule ni kubwa, ipo sehemu nzuri na imezungukwa na shule nyingi za sekondari hivyo catchment area yake ni kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba Mheshimiwa Waziri, nitumie lugha ya sanifu ya kiswahili, chonde chonde, itazameni Mchinga sekondari, muipatie mabweni ili shule iweze kupanda hadhi hiyo. Shukrani sana.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianze kwanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Maliasili kwa juhudi kubwa ambazo Wizara yako imezichukua katika kuhakikisha kuwa tembo wa nchi hii wanalindwa na kubaki salama. Ombi langu kwako tafadhali naomba juhudi hizo za kupambana na ujangili zisiendeshwe kwa kukiuka haki za binadamu na dhuluma dhidi ya mali za wananchi kama vile ng’ombe.

Mheshimiwa Spika, nimesikitishwa sana na kitendo cha kuacha hata kulitambua na kutaja mabaki ya mijusi yaliyopo Ujerumani ambayo yalichukuliwa jimboni kwangu. Mheshimiwa Waziri katika ukurasa wa 6, 7, 8, 9, 10 na 11 wa kitabu chako, umezungumzia namna ya uendelezaji wa Mali Kale. Mheshimiwa Waziri imekuwaje uache hata kutambua tu kwamba kuna hayo mabaki yalichukuliwa na kupelekwa katika makumbusho ya Mali Kale kule Ujerumani. Kutokana na hali hiyo nimejiuliza maswali matano yafuatayo ambayo nimekosa majibu hivyo naomba majibu kutoka kwako:-

(a) Je, suala la mjusi huyo haulitambui?

(b) Serikali imeshindwa kabisa kulipatia muafaka suala hili?

(c) Serikali haina utashi wa kisiasa kurudisha na kutunza rasilimali hiyo ya kale?

(d) Majibu ambayo Serikali imekuwa ikiyatoa hapa Bungeni mara kwa mara kuhusu mijusi yote ni ya uongo?

(e) Serikali haitaki kuliendeleza eneo lile ambalo taarifa zinaonesha kuwa yapo mabaki mengine chini ya ardhi?

Mheshimiwa Spika, kama kuna suala ambalo Serikali ya CCM inaonesha udhaifu mkubwa katika kulinda rasilimali na maliasili ya nchi zetu ni huku kufeli kwenu kwa kushindwa kurudisha nchini mabaki yale, kushindwa kuliendeleza suala lile na au hata namna ambavyo nchi haipati kitu chochote kutokana na mabaki yale ya mijusi. Jambo hili linafedhehesha sana na kukianika Chama cha Mapinduzi kwani ni dhaifu katika kulinda, kutetea na kuhifadhi rasilimnali na maliasili za nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, nakuomba basi uutangazie umma wa Tanzania kwamba Serikali imeshindwa kulipigania suala hili. Mnashindwa hata kuchonga barabara inayokwenda katika lile bonde ambalo watalii wamekuwa wakienda mara kwa mara kila mwaka. Shame to you guys.

Mheshimiwa Spika, kutokana na longo longo ya Serikali katika jambo hili, wananchi wa Mchinga tunaona ni dhana ile ile ya vitendo vya makusudi ya Serikali kudharau, kutothamini na kutojali vitu vya thamani vilivyopo Kusini hususan Mkoa wa Lindi na Mtwara.

Mheshimiwa Spika, ninaandika haya kwa uchungu mkubwa nikiwiwa na namna ambavyo Serikali inaacha kutumia mali kale hii katika ku-promote eneo husika, kukosa pesa za kigeni lakini pia kushindwa kujivunia rasilimali hii muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu. Ahsante.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa sana naomba nimjulishe Mheshimiwa Waziri kwamba baba yangu Mzee Mohamed Said Bobali amestaafu utumishi wa umma tangu mwaka 2010 lakini hadi leo hii bado hajalipwa pensheni yake. Mzee huyu aliajiriwa na Idara ya Ujenzi na baadae akahamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, hivyo kahamishwa na Mfuko wake wa Pensheni tangu mwaka huo, Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali za Mitaa na Hazina wamekuwa wakishindana ni nani anapaswa kumlipa mafao yake? Jambo hili ni kinyume kabisa na haki za binadamu na haki za wafanyakazi kama zinavyoelezwa na ILO.

Mheshimiwa Waziri, naomba sana Wizara yako ifanye intervention juu ya jambo la mzee huyu kwani linamsababishia stress na manung’uniko sana. Si vyema Serikali ije ilipe mirathi ili hali mhusika aliwahi kustaafu salama, salmini.

Kuhusu tozo kubwa za kuingiza fedha kutoka nje ya nchi; Mheshimiwa Waziri Jumuiya ya Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora) ni moja ya kundi muhimu sana katika uwekezaji humu nchini ikiwa Serikali itaweka taratibu rafiki za kuvutia kundi hili kuja kuwekeza nchini. Moja ya kikwazo kikubwa ambacho wamekuwa wakikisema ni tozo wanayotozwa wanapotaka kuingiza fedha nchini jambo linalopelekea wao kuanza kuwekeza nchi nyingine tofauti na Tanzania.

Mheshimiwa Waziri, kwa nini msiweke utaratibu mahsusi ili kuwavutia watu hawa kurudisha nyumbani mitaji yao kwa wao kuja kuwekeza hapa nchini. Hali ilivyo pia inachangia watu kuingiza fedha kwa njia zisizo halali hivyo kuikosesha Serikali mapato yake.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kwa kuyasema mambo matatu muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Polisi Mchinga, bado kina changamoto nyingi ingawa kimekitajwa katika ukurasa wa kumi wa kitabu cha hotuba. Kituo kile kimejengwa tangu mwaka 2002, lakini hadi leo bado hakijakamilika; Askari wamehamia pale lakini hawana nyumba hata moja ya kuishi. Hivyo wanaishi Lindi Mjini na wanalazimika kuja asubuhi na jioni kurudi Lindi. inapofika wakati wa usiku ikitokea dharura ya kuhitajika huduma za Kipolisi wananchi hawawezi kupata huduma hiyo. Naomba Ofisi ya Mheshimiwa Waziri itenge fedha za angalau nyumba tatu za kuishi Askari pale Mchinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusu Kituo cha Polisi Rutamba. Kituo hiki pia kipo Jimbo la Mchinga. Kituo hiki kinakabiliwa na changamoto kubwa ya makazi ya Askari, hakuna nyumba za makazi ya Polisi, lakini pia jengo lenyewe la kituo limechakaa na halikidhi haja ya kuwa Kituo cha Polisi. Naomba watutengee pesa za kujenga jengo la Kituo cha Polisi Rutamba pamoja na nyumba za Askari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ni kwamba, magari ya Polisi Lindi (Wilaya) yote yamechakaa, hivyo yanaharibika mara kwa mara. Askari Polisi hamwapi OC, hivyo mara kwa mara wamekuwa wakitusumbua sisi Wabunge tuwape fedha za matengenezo ya magari yao pamoja na mafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuuliza Mheshimiwa Waziri, kwa nini wanawatesa hivi Askari na kulidhalilisha Jeshi wakiacha mafao yao ambayo bado machache? Hata magari yao ya kufanyia kazi nayo ni shida pia. Waone aibu, watengeneze magari ya Askari, ya Ofisi ya OCD Lindi pamoja na kupewa mafuta yatakayowezesha kutekeleza majukumu yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu kubwa kwa Mheshimiwa Waziri wa Mazingira ni namna Wizara inavyoachia mifugo hasa ng’ombe kuharibu mazingira yetu kwa kiwango kikubwa. Mkoa wa Lindi ni moja ya mhanga mkubwa wa hali hii; mifugo inaingia bila kuzingatia uwezo wa mazingira yaliyopo katika eneo husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Lindi ipo hatarini kugeuka jangwa. Jimbo langu la Mchinga ni kielelezo cha hoja hii. Wafugaji wanavamia maeneo yote oevu ya Jimbo la Mchinga kama vile bonde la Mbwenkulu na eneo la bonde la Mkoa lililopo katika Kata za Mvuleni na Kitomanga. Wizara lazima ishirikiane na Wizara ya Mifugo katika kupanga maeneo mbalimbali hapa nchini. Uchungaji holela wa mifugo yetu utapelekea kuligeuza Taifa letu kuwa jangwa siku chache zijazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu ya pili ni kuhusu miti adimu ya mikoko na mkakati wa nchi wa upandaji mikoko. Kutokana na umuhimu wa miti hii, Serikali inapaswa kuongeza juhudi katika kuilinda na kuongeza miti ya mikoko.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri, Olympic ni maarufu sana duniani kwa sasa. Ni michezo inayoendeshwa kwa ukwasi mkubwa wa fedha na hivyo Mataifa yanayoandaa yamekuwa yakijizolea mamilioni na mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa nini Serikali haifikirii kujenga kituo cha michezo ya Olympic (Olympic Centre) katika moja ya fukwe zetu tulizojaliwa na Mungu kama vile ufukwe wa Kijiweni uliopo Mchinga Lindi?

Mheshimiwa Spika, Serikali ioneshe nia hiyo kwanza, kisha itafute wachezaji ambao wataingia ubia na Serikali katika kufanikisha jambo hilo muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Sekta ya michezo nchini.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni TBC kugeuzwa kuwa chombo cha chama badala ya kuwa chombo cha habari cha Taifa. Imefahamika kuwa duniani kote Television ya Taifa inafanya kazi kwa karibu na Serikali iliyopo madarakani, lakini TBC inavuka mipaka na hivyo kuondoa kabisa ladha ya kuendelea kuitazama na hamu ya kuipenda. Jambo hili halina afya njema kwa mustakabali wa Taifa linalokusudia kupiga hatua ya maendeleo na kufikia uchumi wa kati. Ujumbe wangu, TBC iache kushabikia siasa za mrengo mmoja pekee, inapoteza watazamaji na wasikilizaji wake kila kukicha.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu ni wazo la Serikali kuandaa mashindano maalum ya Insha yanayohusu Lugha ya Kiswahili ili kuongeza hamasa na hulka ya vijana wetu kuipenda, kuithamini na kuienzi lugha yetu hii. Mheshimiwa Waziri, mashindano haya yanaweza kuanzia ngazi za Shule za Msingi hadi Chuo Kikuu. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Elimu kwanza naomba kukujulisha kuwa binafsi ni mhitimu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere zamani kivukoni. Mheshimiwa Waziri hebu tusaidie kutatua hoja hii, hivi karibuni Mheshimiwa Waziri Mkuu alitembelea Chuo cha MNMA akiwa ameongozana na wewe Waziri na kukuagiza kuwa wizara ifanye mchakato wa kukipandisha hadhi chuo hiki na kuwa chuo kikuu. Je, mmefikia wapi hadi leo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku mbili tu baada ya agizo lile la Waziri Mkuu, nikauliza swali la msingi hapa Bungeni kuhusu hoja hiyo hiyo ya kupandisha hadhi chuo hiki lakini majibu ya wizara yako yalionyesha kutokubaliana na hoja ya kukipandisha hadhi chuo hiki na kuwa chuo kikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nadhani ni muda muafaka sasa chuo hiki kipewe hadhi ya kuwa chuo kikuu ili kuendeleza fikra pevu za hayati Mwalimu Nyerere. Nchi za wenzetu waasisi wa mataifa yao wamewaenzi kwa kuvipa majina ya vyuo vyao mfano mzuri ni Nelson Mandela University, Kwame Nkurumah University , Kenyatta Universtity, MOI University etc. naomba chuo hiki kwa umuhimu wake kipandishwe hadhi kuwa chuo kikuu.

Jambo la pili ni shule ya Sekonari Mchinga kupandihswa hadhi na kuwa shule ya kidato cha tano na sita. Wilaya yetu ina shule moja tu ya kidato cha V na VI nayo ni Maliwa Sekondari iliyopo Jimbo la Mtama. Lakini Jimbo la mchinga halina shule ya kidato cha V na VI hata moja. Tafadhali ninaomba wizara itusaidie kwa kutenga fedha za nyumba za walimu na sisi tutajenga mabweni ili shule hii ipandishwe na kuwa ya kidato cha tano na sita. Ahsante.
Muswada wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini wa Mwaka 2016
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Na mimi niungane na baadhi ya wazungumzaji hapa kwamba sheria hii ni nzuri na dhamira inaonekana ni nzuri na ukisoma maelezo ya Waziri wakati anatoa hoja pia uchanganuzi wake ni mzuri. Napata shida katika baadhi ya maeneo tu ambayo ningeomba sasa nichangie ama nimshauri Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, inaonekana hii sheria kama inakwenda kuwa mother law; inatengeneza contradiction na baadhi ya sheria nyingine. Kwa mfano, wakati Waziri anawasilisha, alizungumzia suala la fidia ambalo kimsingi kabisa ni kweli watu wanakandamizwa, wananyonywa, lakini pia hii nchi ina Sheria ya Fidia. Sasa sijui hii sheria inawezaje kwenda ku-cut across na Sheria ya Fidia ambayo tunayo kwenye nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia umezungumzia suala la ndoa, ni jambo jema kwamba kuna tendency ya wanaume kuwadhulumu wanawake, lakini huko kwenye sheria huko kuna mambo haya ya Sheria za Mirathi na Sheria za Dini ambazo zinaongoza masuala mazima ya ndoa, naona pia inaweza kutengeneza contradiction. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nishauri jambo lingine. Katika definition ya property ambayo Kamati ilishauri na mimi pia ningeweza kushauri kwamba tuongeze baadhi ya maneno kwa sababu siyo tu nyumba na majengo ambazo watu wanadhulumiwa, leo watu wanadhulumiwa hata mashamba yao yanaliwa na tembo, lakini thamani inayofanyika ni thamani dhalili kabisa kwa wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimboni kwangu hivi sasa tembo wamekula vyakula vya wakulima, wamemaliza mashamba, sasa hivi wanaingia kwenye kuharibu mikorosho. Sasa mtu anaharibiwa shamba lake la mikorosho ekari 10, ekari 15, halafu anakwenda kulipwa shilingi 100,000, this is unfair. Kwa hiyo, naomba kama kuna uwezekano, definition ya property iongezeke na haya mengine, uharibifu unaofanywa na tembo nchini kwetu, pia iingie huko ili nao wafanyiwe tathmini au uthamini na hawa wathamini tunaokwenda kuwatungia sheria. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naomba decentralization ya huyu mtu anayeitwa Mthamini, isiwe makazi yake yanaendelea kuwa mjini; sisi watu tunaotoka kwenye majimbo ya vijijini na wananchi wangu wa pale Mchinga akitaka kukutana na Mthamini, aende Lindi na akifika kule wakati mwingine pia anaweza akamwambia mimi sina mafuta ya kujia huko Mchinga. Kwa hiyo, ni kwamba kuwe na decentralization. Hawa watu wawe wanapatikana kwenye ngazi za Halmashauri, wawe wa kutosha ili waweze kwenda vijijini ambako Watanzania wengi ndiko waliko; kusiwe tena na urasimu kwamba sina mafuta, ama nashindwa kuja kwa sababu ya umbali na mambo mengine. Tufanye decentralization ya uhakika, wasiwe centralized, ni jambo la msingi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningeweza kushauri ama kuchangia, naona hapa kwenye kifungu cha 52 cha compensation kweli mmeweka kwamba kutakuwa na riba, lakini inaonesha kwamba ule ukomo ni zaidi ya miaka mitatu, ukiangalia vile vipindi vya miezi sita, sita ni zaidi ya miaka mitatu, bado hatuondoi tatizo la watu ambao watakuwa wanachukua mali zao hawa wananchi iwe Serikali ama wawekezaji ku-delay kwenye kulipa. Kipindi cha miaka mitatu ni kikubwa sana na mtu anaweza akaamua tu kwamba uwezo wa kulipa riba ninao, kwa hiyo, anaweza kukaa, akachelewa na baadaye sheria inasema kwamba lile eneo linaweza likarudi kwa mwenyewe. Tayari tumeshamharibia malengo yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa yeye anakuwa ameshajiandaa kwamba hili eneo limeshafanyiwa uthamini, nitalipwa. Unapokuja ukasema kwamba sasa kwa sababu ameshindwa kukidhi vigezo, tunalirudisha tena, bado changamoto iko pale pale kwamba badala ya kuwa tumemwondolea shida na kero huyu mwananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine ambalo nimeona Mheshimiwa Waziri kama litampa mamlaka kubwa sana, kuna kifungu kilitakiwa kuwepo kwenye sheria, naona siyo vyema kukipeleka kwenye regulation kama mlivyopendekeza, kwamba kuna mambo ya msingi ambayo yalipaswa yawe kwenye sheria yenyewe. Ukisoma kifungu cha 49 na kifungu cha 52(6) kinaeleza kwamba baadhi ya vitu ambavyo vitafanyiwa uthamini, maelezo yake yatatolewa na regulations za Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini vitu hivi vyote visingetajwa kwenye sheria badala ya kusubiri Mheshimiwa Waziri sasa kwenye mwongozo wake hivyo vitu avitaje kwenye mwongozo? Ni vema kwa sababu haya mambo yanahusu maisha, property za watu na za wananchi, ni vizuri yangewekwa kwenye sheria ikabaki ni utaratibu wa kisheria, siyo tena utaratibu wa kikanuni kwamba tusubiri kanuni za Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine niendelee tu kusema kwamba sheria imechelewa, kuna contradiction kubwa ya namna watu wanavyolipwa, mkanganyiko mkubwa upo. Sisi kule Lindi tuna miradi ya LNG ambayo Mheshimiwa Waziri hapa alikuwa anajibu swali, leo unakuta kuna contradiction TPDC wanasema wao wanalipa kiwango hiki, Manispaa wanalipa kiwango hiki, kumekuwa na contradiction kubwa. Contradiction hii inachelewesha baadhi ya miradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati wakati anajibu hapa alishindwa kueleza sijui kwa sababu haijui ama ni kwa sababu ya muda, kwamba pamoja na mambo mengine ambayo mradi wa LNG unaweza ukawa unacheleweshwa pale Likong‟o ni kwamba uthamini unaofanywa, wananchi bado wanaendelea kugomea kwa sababu kile kiwango kinacholipwa wao wanakiona ni kidogo zaidi, lakini pia TPDC wana kiwango chao, Manispaa wana kiwango chao. Kwa hiyo, ni vyema kama hii sheria ingekuwa imewahi ingekuwa labda ni mwarobaini kwa haya ambayo leo yanakwamisha kuendelea kwa miradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niseme kwamba sheria kama ilivyo ina malengo mazuri, wasiwasi wangu ni kwenye usimamizi, kwa sababu shida ya nchi hii siyo tu kuwa na sheria nzuri, usimamizi wenyewe wa sheria ni changamoto. Kwa hiyo, kama kutakuwa na usimamizi mzuri, kutakuwa na political management nzuri ambayo imejipanga kuja kutatua kero za wananchi, tunaweza tukapiga hatua kwa namna moja ama nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuchangia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie baadhi ya vipengele vichache tu kwenye muswada huu na niseme kwamba, nitachangia moja kwa moja kwenye huu Muswada wa Maabara ya Mkemia Mkuu (The Government Chemist Laboratory Act, 2016).
Mheshimiwa Naibu Spika, binafsi nimekuwa so much impressed na muswada huu na namna ulivyokuwa presented, nimeusoma kwa makini ni muswada mzuri. Ningeweza kusema labda umechelewa kwa sababu kuna matukio mengi ambayo kama sheria ingekuwepo yangekuwa yamefanyiwa kazi mapema.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama ilivyo kawaida dosari hazikosekani, naomba niweke mapendekezo kwenye baadhi ya maeneo. Mfano, nashauri sheria tunayotunga iwe na meno zaidi hasa katika masuala yanayohusu national interest, kwa mfano, Mkemia Mkuu tukimpa mamlaka ya kwa final say kwenye kuamua baadhi ya maeneo, mfano, kuna timu ya mpira ya Serengeti boys ambayo kigezo chake cha kucheza ni lazima uwe under 17, lazima uwe chini ya umri wa miaka 17 na tuna experience Tanzania ilishawahi ku-qualify kwenye mashindano ya Afrika lakini tukatolewa kwa sababu tulichezesha vijeba yaani watu ambao wamezidi umri. Hivi sasa tunavyozungumza Congo na nchi nyingine pia wametolewa na Afrika kwa sababu wamechezesha watu ambao wana umri mkubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wazo langu ninachofikiria kwamba yale mambo ambayo yanagusa national interest, ambayo yanahitaji kidhibiti cha umri yaani mtu ili ashiriki kuliwakilisha Taifa anahitaji awe na umri wa miaka kadhaa, Mkemia Mkuu awe na final say ya kusema kwamba huyu ana-qualify ama huyu ha-qualify. Kwa sababu tumpe mandate ya kupima umri wa kujua kwamba huyu ni kweli ana umri huu. Na ni jambo unaweza kuona kama kibwagizo lakini lina-cost wakati mwingine maslahi ya Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia wakati nafuatilia hotuba ya Mheshimiwa Waziri wakati anawasilisha hapa, alisema kwamba sheria hii haitakwenda ku-affect sheria zingine; haitakwenda kufuta wala kurekebisha sheria zingine. Kidogo nataka maelezo ya kina kutoka kwa Waziri utakapokuja kwa sababu najua kwamba Mkemia Mkuu yupo lakini alikuwa anafanya kazi kama Wakala wa Serikali. Lakini kipindi chote hiki alikuwa anafanya kazi chini ya sheria mbalimbali zingine,kwa mfano, Traffic Road Act, Plant Protection Act, Mining Act; hizi zote na zingine zilikuwa zinampa nguvu huyu Mkemia Mkuu kutekeleza wajibu wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo Mkemia Mkuu tunakwenda kumtungia sheria yake peke yake, sheria hizi ambazo tayari zimeshakuwa documented, zimeshaandikwa, zenyewe hazitakuwa affected na maandishi haya na sheria hii ya Mkemia Mkuu, nataka clarification atakapokuja kusema, kwa sababu leo ukienda kuangalia Traffic Road Act wakati unavyopata ajali yapo maeneo ambayo yanaainishwa kabisa kwamba inatakiwa procedure zake iende kwa Mkemia Mkuu akathibitishe hili na hili. Leo tunakwenda kutunga sheria hii ambayo yenyewe itakuwa ni independent, unaposema kwamba haitaenda ku-affect hizi sheria zingine maana yake ni nini? Kwamba zile sheria zingine ambazo zimeshakuwa documented tunakwenda kuzifuta au inakuwaje. Kwa hiyo, nataka nipate maelezo tu kidogo hapo kutoka kwa Waziri utakapokuja ku-finalize. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na jambo lingine ambalo ningeweza ku-suggest kwenye suala la vinasaba. Kumekuwa na changamoto kubwa sana ya watu wanapohitaji huduma hizi za vinasaba husani kupima kujua kwamba huyu mtoto wa kwangu au sio wa kwangu na namna nyingine, watu wanachukuliwa vipomo. Mfano mimi natokea Jimbo la Vijijini kule Lindi, Mchinga; mtu anaambiwa bwana vipimo vyako tunavipeleka Dar es Salaam, sijui tunavipeleka wapi kumekuwa na shida.
Mheshimiwa Naibu Spika, sheria iainishe wazi kwamba ofisi ya Mkemia Mkuu itakuwa decentralized haitakuwa centralized katika makao makuu sijui ya Kanda ama Dar es Salaam ama Dodoma kama sasa hivi inavyokuwa ili huduma hii iwarahisishie zaidi watu kule chini kwa sababu mahitaji ni makubwa, lakini tatizo lililopo ni suala tu kwamba ni huo upatikanaji wa huduma yenyewe na aina ya watu wenyewe kwamba mtu anahisi kwamba vinachukuliwa vinasaba vinapelekwa Dar es Salaam, vinakwenda kufanyiwa wakati mwingine majibu unayoyapata sio ya kwangu, kuna hiyo shida. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano sasa hivi kuna shida kubwa hasa kwenye vipimo pia vya baadhi ya magonjwa mahospitalini; kwa mfano ukiwa Lindi kuna baadhi ya magojwa yakipimwa inatakiwa majibu yake mpaka yaende Dar es Salaam yakafanyiwe vipimo ndio yarudishwe Lindi.
Sasa ningeomba tu-decentralize hii Ofisi ya Mkemia Mkuu ili watu wapate huduma wakiwa huko kwenye maeneo yao ikiwezekana kwenye ngazi ya Halmashauri ama Wilaya. Hizo ndio hoja ambazo nilikuwa nataka nizichangie, nilihisi kwamba kwa hivi sasa ni jambo ambalo ni la msingi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni hayo tu sikuwa na mengi lakini nimeona ni ya msingi sana niweze kuongezea katika michango ya waheshimiwa Wabunge. Nakushukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba niongezee pale alipoishia Mheshimiwa Zitto Kabwe kwenye kutoa ushuhuda wa watu ambao walikuja kuibuka kuwa wanahabari nguli kwa kupata tu uzoefu kwa kuajiriwa wakiwa si wanahabari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, humu ndani tunaye Mbunge mwenzetu Mheshimiwa Juma Selemani Nkamia. Mheshimiwa Juma Nkamia mwenyewe anaweza kutoa ushahidi, aliajiriwa TBC akiwa hajasomea uandishi wa habari. Mheshimiwa Juma Nkamia aliajiriwa TBC kwa kuonekana ana uwezo wa kutangaza mpira kabla hajasomea uandishi wa habari na baadaye Mheshimiwa Nkamia akaja kuwa miongoni mwa waandishi wa habari nguli kabisa nchini ambao ni mafundi wa kutangaza mpira. Leo mnakuja kufunga vipaji visije vikaonekana, sijui mna dhamira gani! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wa Awamu ya Kwanza alipoingia madarakani alikuwa na kazi kubwa kabisa ya kurekebisha sheria ambazo zilikuwa zina element ya kikoloni ambazo zilikuwa ndani yake kuna ufashisti, za kuwatesa Watanzania. Kinachoendelea hivi sasa ni kuturudishia sheria ambazo ndani yake kuna element ya kikoloni, kuwafunga midomo Watanzania wasiseme, kuwafunga midomo Watanzania wasiongee na kuwafunga masikio wasisikie, ndicho kinachoendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, sasa mambo yanakuwa dhahiri kabisa. Ni wazi kabisa haya yanayosemwa yanatufanya tuamini, unapokuja kusema mwanahabari na mwandishi wa habari ni vitu viwili tofauti nina mashaka na uelewa wa kiswahili wa ndugu yangu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea; tunachokifanya hapa ni kutaka kulisaidia Taifa na tunatoa hoja ya kutaka kulisaidia Taifa. Unapotunga sheria ukampa mamlaka Msajili yeye awe anatoa leseni; ukiangalia kifungu cha 5(e), Msajili kazi yake ni kusajili lakini kwa mujibu wa mapendekezo haya Msajili atakuwa anasajili na kutoa leseni. Kifungu hiki kinakwenda kuji-contradict na sheria nyingine. Vyombo vya habari ni biashara kama ilivyo biashara nyingine na biashara zinasajiliwa na zinatolewa leseni huko kwenye Halmashauri za Miji, Halmashauri za Wilaya pamoja na Manispaa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakwenda ku-contradict na sheria nyingine za utoaji wa leseni. Kifungu hiki na chenyewe hakifai kuwepo kwa sababu kinakwena kuji-contradict na sheria ya utoaji wa leseni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka nilizungumzie, tunatunga Sheria ya Upatikanaji wa Habari tukiwa tunakumbukumbu kuwa mwaka 2015 ilipitishwa Sheria ya Cyber Crime humu ndani ya Bunge, sheria ambayo imewaathiri Watanzania kiuchumi. Ni nani hajui kwamba MCC waliondoa fedha mojawapo ya sababu ikiwemo Sheria ya CyberCrime? Nani hajui humu ndani? Cyber Crime Act imetufanya MCC waondoe pesa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na jana wakati Waziri anahitimisha alisema kwamba fedha za wafadhili kutoka nje tumepata asilimia moja. Tunatunga sheria ambazo zinakwenda kuji-contradict na zinakwenda kuathiri diplomasia yetu ya kiuchumi na ya kisiasa na Mataifa makubwa. Na kunakuwa na contradiction mtu anasema hahitaji misaada hahitaji utegemezi, lakini unaacha kutegemea Marekani unakwenda kutegemea Morocco, nalo hili pia ni tatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wamarekani kwa sababu ya sheria hizi za habari tunazopitisha humu, wanatoa miradi yao, kwamba wanaacha kuisaidia Tanzania, tunasema basi ninyi Wa-Morocco njooni mtujengee uwanja na mtujengee msikiti! Tunatunga sheria leo mwaka 2016, na mtapitisha kwa sababu Rais ameshasema ataisaini, lakini athari yake inakwenda kuwaathiri Watanzania moja kwa moja.
Watanzania ambao leo wanajua kwamba sheria inapitishwa kukiwa na mizongwe ya ninyi kupewa shilingi milioni 10 ili muweze kuipitisha, watu wanajua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia, sheria inatao mamlaka makubwa kwa Waziri kufanya accreditation kwa vyombo vya habari pamoja na director kwa wanahabari. Lakini mimi naomba kuuliza hivi mwenyewe huyu Waziri na yeye ana taaluma ya habari? Waziri na Naibu Waziri wana taaluma hiyo ya habari? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana isiwe mtu leo amesomea engineering anaenda kupewa Uwaziri wa Habari aka-aprove maombi ya wanahabari kwa mujibu wa sheria wakati wewe mwenyewe siyo mwanahabari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe nimalizie jambo moja, baharini kuna viumbe wengi sana lakini kiumbe kimoja ambaye ninakipenda sana kumtolea mfano ni pweza. Pweza unapomchukua akiwa hai ukimleta nchi kavu ukimgusisha na moto badala ya mikia yake kuipeleka mbali yeye ndiyo anakumbatia. Tofauti sana na viumbe wengine binadamu wakigusa moto anatoa, pweza akigusa moto anakumbatia, watu wanatoka maeneo ya Pwani wananielewa. (Makofi)
Mheshimiwa Waziri, Waziri, sheria hii ni moto, na wewe kwa kutaka sifa kuwa Waziri ndiyo umeikumbatia. Umeikumbatia na watu wote wanajua kwamba pamoja na mambo mengine umeshindwa kumshauri vizuri Rais katika suala la kutunga sheria za habari na haya yote yanayotokea kwenye sekta ya habari tatizo ni wewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa Mwaka 2017
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.Kwanza nielekeze masikitiko yangu kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sijui anajisikiaje kama miezi miwili iliyopita alileta Muswada hapa na ukapitishwa na Bunge leo anauleta tena kuja kuurekebisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, wapo Waheshimiwa Wabunge wenzetu waliteuliwa kuwa Mawaziri miaka iliyopita wakakosea kidogo inawezekana walishauriwa vibaya na Wanasheria leo wako matatani. Kwa nini huyu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na yeye asiwajibishwe? Ameiaibisha Serikali lakini unaleta Sheria ambazo zinakuja kuja ku-contradict na Sheria zingine ambazo zinakuja baadaye. Naamini Sheria hizi zote ambazo zinaletwa huku zinapitia mezani kwako, unazipitia…..

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bobali zungumza na Kiti.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naamini kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali anazipitia. Wiki iliyopita hapa tulikuwa tunapitisha Songwe Convention na ibara ya 13(3) ilikuwa ina-contradict na Sheria ambayo tuliipitisha hapa miezi mwili iliyopita ya sovereignty of state. Sheria ile Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati anai- present hapa aliitetea sana akasema na huu ndiyo utaratibu mzuri wa kulinda rasilimali na Maliasili za nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ikaletwa hapa Songwe Convention tukaipitisha lakini ndani yake ina Ibara ya 13(3) inayosema kwamba usuluhishi utakwenda kufanywa na SADC, halikadhalika leo imekuja kuwa tena vile. Kwa hiyo kwangu naona kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajitathmini kwa namna gani anaishauri Serikali.

Mheshimiwa MNaibu Spika, nikubaliane sana na pendekezo la kuifuta RUBADA. Mimi nikiwa kama Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwenye Wizara ya Maji mwaka jana kwenye hotuba yangu niliizungumzia, mwaka huu nikaizungumzia; hata juzi wakati nasoma maoni na mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kuhusu Songwe convention nilizungumzia namna gani RUBADA inalitia hasara Taifa hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, badala ya kufanya majukumu yake RUBADA ikawa madalali watu wengi wameongea. Sisi ambao tunapita mara kwa mara pale Rufiji kwenda Lindi na kurudi tunapatwa na wivu kuona namna tunavyoshindwa kulitumia bonde la Rufiji ili kuleta tija kwa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bonde lina maji, lina ardhi yenye rutuba inayostawi mzao mbalimbali lakini inafika wakati leo nchi hii tunalalamika kwamba nchi ina njaa, hakuna chakula na wale waliolima maeneo mengine wakapata wanazuiwa wasiuze kwa ajili ya kuogopa kwamba chakula ni kichache wakati tuna bonde zuri la Rufiji lina maji, lina kila kitu. Hawa watu waliendeleze hili bonde lakini badala yake ukienda pale sasa hivi hukuti miwa, hukuti Mpunga, huoni mahindi, utaona ng’ombe wengi wamezagaa kwenye lile bonde ndiyo kitu pekee ambacho nafikiri unaweza kukiona. Kwa hiyo hili naunga mkono.

Mheshimiwa Naibu Spika, naona hapa kuna marekebisho ya Sheria ya Petroli na Madini. Najiuliza na wakati mwingine napata shida labda inawezekana haya yanaletwa leo kutokana na hizi shughuli zilizofanyika mwezi mmoja, miezi mwili, mambo ya makinikia, mambo haya ya hizi Tume za Mheshimiwa Spika na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, inawezekana leo akatokea mtu akaja akatuambia makapi ya mpunga ni dawa tutakuja kutungia Sheria hapa as if kwamba hatu-predict au hatuwezi ku-focus mbele, tunakwenda kwa matukio, Mheshimiwa Rais akitoa order ya namna hii inaletwa sheria kuja kubadilishwa, Mheshimiwa Rais akitoa order nyingine italetwa sheria tena kuja kubadilishwa. Kwa hiyo tunakwenda kulingana na namna ambavyo matukio yanavyotuongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu mzuri wa Taifa ambalo tunataka kuendelea ni utaratibu wa ku-focus mbele, tutunge sheria ambazo zita-survive miaka 20, miaka 50 au miaka 100.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru, ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya TAMISEMI na Utawala, namshukuru Mwenyezi Mungu miongoni mwa Wabunge ambao tumekuwa tumeujadili huu Muswada kwa muda mrefu ni sisi Wajumbe. Tumepata fursa ya kupata mafunzo, semina lakini pia tumekuwa na Mwanasheria Mkuu kwa mara kadhaa tukijadili juu ya Muswada huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niunge mkono Hotuba ya Mwenyekiti wangu wa Kamati aliyoisoma hapa leo asubuhi. Pia niunge mkono baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliyosema, sifikirii kama kuna mtu ambaye anapinga hoja ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi yetu, sifikirii. Kinachoelezwa hapa ni namna ya kuboresha na wakati mwingine ni challenge tunai-challenge Serikali juu ya uendeshaji wa jambo hili kwamba kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma ni njia ipi inatumika ni mfumo gani umetumika ndio kinachofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hotuba ya Mheshimiwa Waziri na Hotuba ya Kamati tume-refer sana kuhamishwa kwa Mji wa Lagos kwenda Abuja mwaka 1991. Hata sisi wakati wa Semina Wanasheria wa Serikali walipokuwa wanakuja walikuwa wanaelezea tu habari ya Abuja tarehe 12 Desemba, 1991 kutoka Lagos kwenda Abuja maelezo yalikuwa hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba ni-challenge upande wa Serikali kama kweli tumeamua kuiga mfumo wa Nigeria, lazima kuna maswali mawili tujiuliuze, wenzetu Nigeria wakati Rais Ibrahim Babangida anahamisha Makao Makuu kutoka Lagos kwenda Abuja alisema hivi Lagos ni economic capital ya West Africa. Imekuwa congested ina mambo mengi ya kiuchumi yanayofanyika, sasa naomba tujiulize Dar es Salaam ni economic capital ya Tanzania pekee ama ya ukanda wote ya Afrika Mashariki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili alilolisema Babangida ni kwamba anahitaji kwenda Abuja kwa sababu ya kiusalama ili Serikali ipate fursa ya kukaa kwenye sehemu iliyotulia waratibu vizuri mambo ya kiusalama. Nataka kujua kwamba Dodoma na yenyewe imekuwa ni center ya usalama wa nchi yetu tumejipanga kihivyo ama tumeamua kuja, Mbunge mmoja amesema hapa kwamba Mheshimiwa Tundu Lissu kapigwa risasi Dodoma na mpaka sasa hata aliyepiga hajulikani hata mtu kuwa suspected hayupo. Sasa je, na hili nalo tunalichukuliaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la tatu capital city inaweza ikawa na mambo mawili economic capital and political capital, kwamba kama Dodoma inakuja kuwa capital city inakuwa pia capital city ya kiuchumi au ya kisiasa pekee? Kama tunaamua kuja kiuchumi na kisiasa tuliweke waz.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunaamua tunakuja kisiasa tufanye hivi naomba nishauri kama Dar es Salaam itaendelea kuwa economic capital ya Tanzania kuna haja gani leo Wizara ya Viwanda na Biashara kuhamia Dodoma, kuna haja gani? Kuna haja gani leo Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kuhamia Dodoma kwa nini zisibaki Dar es Salaam kuendelea kuratibu mambo ya kiuchumi na mambo ya Mahusiano ya Kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya Nigeria wamefanya sio Wizara zote zipo Abuja, Wizara zingine zipo Lagos kuratibu masuala ya kibiashara kwa sababu Lagos ni Centre of Economics. Wizara ya Viwanda inahitaji ibakie Dar es Salaam, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Wizara zingine mfano Wizara ya Uchukuzi, inahitaji kubaki Dar es Salaam, iendelee ku-manage airpot zetu na bandari zetu, lakini Wizara ya Uchukuzi inakuja Dodoma, kule bandari anaratibu nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima tuweze mikakati kwamba kama tunakuja Dodoma, tujue kwamba tunakuja as a political capital siyo economic capital. Economic Capital itaendelea kubaki kuwa Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani inawezekana ni kwenye maneno kuna tofauti, lakini kwenye utekelezaji naona kama mnafanya hivyo kwamba wanaendelea kuifanya Dar es Salaam kuwa ni economic capital. Wanajenga interchange, flyover, standard gauge railway Dar es Salaam. Maana yake ni kwamba Dar es Salaam is still an economic capital na wanaitambua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama hilo ndiyo jibu, lazima tuliweke sawa kwamba tunakuja Dodoma as a political capital, not as an economic capital. Capital City yoyote lazima iwe na element mbili, kuwa Capital City ya kisiasa na ya kiuchumi. Kwa hiyo, naomba kaka yangu Mheshimiwa Jafo atakapokuja kujibu hizi hoja, atujibu kwamba tunakuja full tukiwa economic and political ili Watanzania waweze kuelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, unaposema capital city, sisi kwenye Kamati tulikuwa tunajadili, hivi Dar es Salaam ilikuwa Capital City, kulikuwa na sheria iliyoitambua? Jibu ni kwamba hakuna, lakini ilikuwa Capital City kwa sababu moja. Ikulu ya nchi iko Dar es Salaam. Unapozungumza Capital City, unazungumzia State House ndiyo kipaumbele namba moja. (MakofI)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nilikuwa natamani mtu wa kwanza kuhamia Dodoma angekuwa Mheshimiwa Rais kabla hata ya Mawaziri. State House ndiyo element inayo- identify kwamba hapa ndiyo Capital City ya nchi. Huwezi leo kwenda Nigeria tunakosema ukakuta Ikulu iko Lagos.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata huyo Ibrahim Babangida mwaka 1991 alianza kuhama yeye ndiyo Wizara zikaanza kumfuata. Sasa sisi tunaanza Wizara, Idara, Ikulu iko Dar es Salaam. Hii kwanza ni gharama, mnasafiri sana Waheshimiwa Mawaziri kwenda huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, haya ni mambo ya msingi sana lazima tuyazingatie. Kwa hiyo, tusisifie kwa Waziri Mkuu kuhamia, Waziri Mkuu ni kitu kimoja. Ikulu ya nchi inapaswa iwepo hapa na mtu wa kwanza aliyepaswa kuja Dodoma ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyosema, sisi hatupingi Muswada huu wala hatupingi sheria hii ya Dodoma kuwa Capital City. Tunachokifanya ni kutoa challenge na tungependa kuona Serikali wakizifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la muhimu sana, tunahamia Dodoma kuja kuwa Capital City, yako mambo ya msingi ya kuyaangalia na sisi kwenye Kamati tuli- raise hiyo issue. Issue hii ya Muungano ndugu zangu nawaambia siyo issue ndogo, ni kubwa kabisa. Hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunapoamua kuwa Capital City ya nchi lazima partner states, pande zote mbili za nchi ziwe consulted na ziamue. Wala siyo suala la kihistoria kwamba mwaka 1973 watu walikuwa consulted, hapana. Hatutungi sheria hapa leo kwa sababu ya hotuba ya Baba wa Taifa mwaka 1973, tunatunga sheria kwa sababu ya hotuba ya Rais wa Awamu hii. Kwa hiyo, yeye ndio alipaswa kuwa- consult upande wa Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu aje atueleze kwa upande wa Zanzibar wamefanya negotiation, wamekubaliana kwa kiwango gani? Kwa sababu jambo hili liko kwenye mkataba wa Muungano. Kama liko kwenye mkataba wa makubaliano yao kwamba Makao Makuu yatakuwa Dar es Salaam, leo wanapohama kwenda Dodoma, wamewashirikisha? Wamewauliza? Wameafikiana? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, yangu yalikuwa hayo.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza).
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nitajikita kwenye eneo moja la mabadiliko ya kodi (Property Tax) kwenye Serikali za Mitaa. Niliposoma hii amendment kifungu cha 11, kidogo nimepata shock, sijaelewa, labda Mwanasheria Mkuu ama Waziri atatufafanulia. Inasema, in the case of City Council, Municipal Council and Town Council areas; na ikaongezewa kifungu cha District Council areas.

Mheshimiwa Spika, kwenye Halmashauri za Vijijini wakati mwingine unakuta Makao Makuu ya Halmashauri zile yako kwenye Makao Makuu ya Mikoa. Nitatolea mfano, Halmashauri yetu sisi ya Lindi Vijiji, Makao Makuu yetu yako Lindi Mjini pale. Kwa hiyo, ukiweka eneo la Halmashauri ya Wilaya, maana yake ni vijiji vyote vya Jimbo la Mchinga na vijiji vyote vya Jimbo la Mtama.

Mheshimiwa Spika, sasa nataka kupata ufafanuzi, kinachokusudiwa hapa kwenda kutozwa kodi katika hizi nyumba, ni zile nyumba mpaka za vijijini au zile Makao Makuu ya pale ilipo Halmashauri? Nimetolea mfano huu kwa sababu ya kesi hiyo kwamba ziko halmashauri ambazo Makao Makuu yake yako maeneo ya mijini.

Mheshimiwa Spika, kuna jambo limezungumzwa kuhusu suala la utunzi wa sheria hii ya bajeti ya tarehe 21 Juni, 2017. Haya leo ambayo tunaona ni mabadiliko makubwa kabisa, nami niseme ukweli, kistaarabu kabisa kwamba Mheshimiwa Mpango tulikushauri mwaka 2017 na mwaka 2018, umekuja nayo umeyafanya. Sisi kama Bunge, bila kujali kwamba hawa Wapinzani ama hawa ni Chama Tawala, tuna haja pia ya kujipongeza kwamba ushauri wetu umepokelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nashukuru. Pia Mheshimiwa Waziri alipaswa ku-admit kwa kazi kubwa tuliyofanya Waheshimiwa Wabunge kwenye kushauri hili. Kwa kuwa ushauri huo ameupokea, wakati mwingine anapokuja kwenye Bajeti, asisite pia kusikiliza ushauri wa Waheshimiwa Wabunge. Tuepuke hii aibu ya leo tunatunga sheria, kesho kutwa inakuja kufanyiwa amendment. Imekuwa ni trend ya Bunge la sasa kuwa tunafanya amendments nyingi sana ya sheria ambazo hazijadumu kwa muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hili nalo nadhani kiti chako italiona kwamba marekebisho mengi ya shera yanayoletwa ni sheria hizi ambayo tumetunga kwenye Bunge hili la 11. Ina maana kwamba wakati tunatunga hatukuangalia ama hatuku-consult wadau.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa na interest na eneo la Serikali la Mitaa, naomba sana ufafanuzi kwa sababu suala lililopo huko, watu wanajua kwamba sasa ni nyumba zote, vijijini na kwenyewe wataenda kutoza hiyo kodi ya shilingi 10,000/=. Tungepata ufafanuzi ili leo tukiondoka tukawaambie. Kwa mfano, wale wananchi wangu wa Mchinga, Kilolambwani, Melola na wapi ambako ni maeneo tu ya Halmashauri ya Vijijini basi wajue kwamba wao hawahusiki juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira wa Mwaka 2018
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Asubuhi nimewasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani, mengi ambayo nimeyapendekeza nadhani Serikali itakuwa wameyaona na sasa nataka ni-summarize kwenye hoja chache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali kwa kuleta Muswada huu wa Sheria. Huu Muswada utafanya kupunguza idadi ya sheria zinazoshughulika na maji. Mpaka sasa Mheshimiwa Mwenyekiti kuna sheria kumi ndani ya nchi hii zinazoshughulika na maji; nitazitaja haraka haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009, kuna Sheria ya Ardhi Na.4 ya mwaka 1999, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na.20 ya mwaka 2004, Sheria ya Misitu Na.14 ya mwaka 2002, Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji Na.4 ya mwaka 2013, Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na.12 ya mwaka 2009; hii inafutwa na sheria hii, Sheria ya DAWASA Na. 20 ya mwaka 2001 na hii inafutwa, Sheria ya EWURA Na.11 ya mwaka 2001 na hii inafutwa, Sheria ya Serikali za Mitaa na Sheria ya Afya kwa Jamii Na.1 ya mwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninachotaka kusema nini, ninachotaka kusema kwamba kumekuwa na sheria nyingi zinazohusika na masuala ya maji. Mheshimiwa Komu amesema kuna Sheria Na.12 ya mwaka 2009, hii ilipaswa iwe accommodated ingefutwa na sheria hii kama ambavyo mmeifuta Sheria Na.11 ya mwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, haya malalamiko wanayoyasema Waheshimiwa Wabunge, kwamba ukichimba kisima ukawa unavuna ama ukawa unavuna maji ya mvua lita 20,000 bado wapo kwenye Sheria Na.12 ya mwaka 2009; huko ndiko kuna adhabu kubwa kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ninadhani kwa sababu tu Serikali haijaamua kufuata ile sheria vinginevyo takriban watu wote wa Tanzania nusu wangekuwa wako magerezani kwa sababu kuna hukumu kubwa, lakini pia ni sheria ambayo kwa kweli haiendani na wakati tulionao. Kwa hiyo, hilo jambo moja

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Waheshimiwa Wabunge wengi wamechangia juu ya tafsiri ya neno misuse of water hili neno misuse of water (matumizi mabaya ya maji) ni vizuri lingekuwa limefafanuliwa, tena ndani ya sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimeleta amendment na nime-define kabisa. Ninaomba suala la maji ni suala ambalo halihitaji kuleta tena itikadi, ni suala ambalo linawahudumia Watanzania wote, hili halihitaji itikadi, tuliweke hapa, kwa sababu tusipoliweka neno misuse of water watu wengi watakwenda kuhukumiwa ama tutachochea rushwa kwenye utekelezaji wa hii sheria.

Mhesimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninaomba sana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati mpo hapo mliangalie, kwa sababu tumeleta amendments ili tuweze kuli- accommodate. Waheshimwia Wabunge wengi mmesikia wanalilalamikia, kwamba ni neno ambalo lipo kana kwamba sky is limit, yaani mtu anaweza kukaa kwa maono yake akasema umetumia vibaya maji. Kwa hiyo ni vizuri tukaliweka kwa sababu ni jambo ambalo ni dhana sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, Waheshimiwa Wabunge waliochangia wakati wa asubuhi wameeleza kwamba mpaka sasa upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 58, upatikanaji wa mijini ni asilimia 78, malengo ya Taifa ifikapo mwaka 2020 vijijini kuwe na upatikanaji wa maji wa asilimia 85 na asilimia 95 mijini. Sasa hapa ninaongezea hoja yangu, ile Sheria Na.12. Kama Sheria ya Rasilimali za Maji itaendelea kuwa vilevile hili lengo halitafikiwa. Kwa sababu kwanza Sheria Na.12 ya mwaka 2009 inazuia hata watu kuvuna maji kwa wingi na kuweza ku-supply kwa watu wengine. Kwa hiyo, hili lengo mliloliweka, kwa sababu hii sheria ina-deal na ku-supply maji hai-deal na namna ya upatikanaji wa maji; sheria inayohusika na upatikanaji wa maji ni Sheria Na.12 ya mwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali liangalieni hili, nalo lingekuwa ni vyema mkali-accommodate, lakini kwa kuwa mmechelewa ni vyema mkaleta hata amendment, vinginevyo hili lengo tulilojiwekea la 2020 kuwa na asilimia 85 na asilimia 95 haliwezi kufikiwa ikiwa mpaka sasa tuko asilimia 58.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo sisi tumeliona, kwanza nishukuru hata mapendekezo mengi ambayo tumeyatoa na amendments ambazo tumezi-move nyingi Serikali mmeziangalia. Hata hivyo kuna changamoto nyingine ambayo kama Kamati tumeiona ni kwenye suala zima la Mfuko wa Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TARURA wanafanya vizuri kwa sababu sheria imeainisha kabisa, hawa watachukua fedha za Mfuko wa Barabara asilimia 30 na hawa watachukua fedha asilimia 70. Kwa hiyo, mgawanyo wa umeoneshwa kwenye sheria. Mimi nilidhani sheria hii ingeweka kabisa mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Zitto ameeleza hapa asubuhi, ukisoma ripoti ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maji fedha nyingi ya Mfuko wa Maji inatumika mijini, na hiki ndicho chanzo ambacho kina uhakika, hakuna chanzo chochote kwenye Wizara ya Maji chenye uhakika kama siyo fedha ya Mfuko wa Maji, hakuna. Vyanzo vingine vyote upatikanaji wa fedha mpaka sasa ni asilimia 10, 12 na 14; lakini chanzo madhubuti ni Mfuko wa Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa kuwa tunakusudia kupeleka maji vijijini ni vema sheria ingeweka wazi kwamba hizi fedha za Mfuko wa Maji basi asilimia 50 ziende vijijini asilimia 50 ziende mijini, lakini kuachia loophole, tunafahamu miradi mingi ya mijini ni miradi mikubwa inayotumia fedha nyingi. kwa hiyo kama tutaendelea kuachia hivi itakuwa vijijini tunapeleka petty cash, mradi wa shilingi milioni 10/milioni 12 unatengenezwa mradi mmoja, mjini unagharimu shilingi bilioni 50. Kwa hiyo Mheshimiwa Mwenyekiti, hili tulitaka tuliweke wazi…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Serikali Mtandao wa Mwaka 2019
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, mchango wangu nimeugawa katika maeneo mawili makubwa, kwanza nitazungumza kama Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI ambao ndiyo tulikuwa na jukumu la kujadiliana na Serikali juu ya namna bora ya kuufanya huu Muswada uje kuwa Sheria nzuri. Lakini pia nitakuja kuchangia sasa kama Mbunge wa kawaida ili nione michango yangu Serikali inaweza kui-accommodate.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri wa WIzara hii kwa ushirikiano mkubwa waliotupa Wajumbe wa Kamati wakati tunajadili Muswada huu. Kwa mara ya kwanza katika historia ya kuwepo Bungeni nimeshuhudia Serikali ikikubali mapendekezo ya Kamati zaidi ya asilimia 90, mapendekezo na schedules of amendment ambazo Kamati tulikuwa tumeziona tukajadiliana nao Serikali ikazi-accommodate. Kwa hiyo tunashukuru sana Mheshimiwa Waziri na timu yake na Katibu Mkuu Dkt. Laurian Ndumbaro kwa kazi nzuri ambayo wamifanya lakini pia nimpongeze Mtendaji Mkuu wa huu Uwakala Dkt. Bakari Jabiri na yeye kwa ushirikiano mzuri ambao alikuwa anatupa Wajumbe kwenye Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa ujumla uelewa wangu wa kawaida na maelezo ya kutosha yaliyoletwa na Serikali kwenye Kamati yamenifanya niamini kwamba sisi tumechelewa kuingia kwenye e-government. Nimesema hivyo kwa sababu lengo la Serikali mtandao pamoja na mambo mengine pia ni kurahisisha utoaji wa huduma lakini pia kukwepa kwepa mambo ya bureaucracy ikiwemo pia ku-save gharama ambazo unnecessary kabisa. Kwa hiyo, maoni yangu kwa kawaida na maelezo ya Serikali na namna tulivyoupitia na kuujadili tulipata wadau waliofanya utafiti wa kutosha juu ya mambo ya e- government yamenifanya niamini kwamba tulichelewa, tulihitaji kuwa mbali zaidi wakati huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija sasa kuchangia kawaida kama Mbunge, yako mambo ambayo ningeweza kuyashauri na ningeomba Serikali wayaangalie inawezekana isiwe sehemu ya sheria wanaweza wasi-accommodate kwenye sheria leo lakini wayaangalie kwenye mustakabali wa Taifa letu. Jambo la kwanza, Mheshimiwa Waziri wakati anawasilisha, hotuba yake asubuhi, ameeleza kwenye ukurasa wake wa mwisho amesema sehemu ya 11 inapendekeza kufanya marekebisho katika sheria mbalimbali yanayotokana na kutungwa kwa sheria ya Serikali Mtandao na sheria zenyewe ambazo zinaombewa kufanyiwa marekebisho ni sheria ya miamala, electronic namba 13 ya mwaka 2015 na Sheria ya Ununuzi wa Umma Namba 7 ya mwaka 2011.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa napendekeza hapa, sheria nyingine ambayo ilipaswa pia iwe accommodated ni sheria ya uchaguzi, National Election Act ili tunakokwenda huko tuachane kabisa kuwa na chaguzi ambazo zinatumia makaratasi na pia chaguzi ambazo zinalaumiwa kwamba inawezekana kumefanyika election leakages. Sasa tukiwa na Serikali mtandao, usiishie tu kwenye kupeleka taarifa za watendaji wa vijiji, kata kwenda halmashauri na kwenda Serikali. Twende mbali hata zoezi la upigaji wa kura especially uchaguzi mkuu lipigwe kwa kutumia vifaa vya electronic. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nalisema hili with authority, nchi ya kwanza ambayo hata sisi Kamati tumei-refer kwenye ukurasa wa 6 wa hotuba yetu ni nchi ya Denmark ambayo inatajwa kuwa ndiyo imefika mbali kwenye masuala ya e- government kuliko nchi zote Duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nenda mafanikio ya Denmark, mafanikio ya kwanza ya Denmark ni nchi ambayo haina rushwa, ndiyo nchi yenye kiwango kidogo cha rushwa duniani kuliko nchi zote lakini la pili inatajwa kuwa ndiyo nchi yenye demokrasia na nchi ambayo hakuna ubadhilifu kwenye uchaguzi kwa sababu hata upigaji kura Denmark wanatumia mfumo wa e-government na nimeushuhudia kwa macho yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ningeomba pamoja na mambo mengine, hili liwe accommodated ili tunapkwenda uchaguzi unapofika tupige kura, mpiga kura anaenda pale badala ya kwenda kujaza kwenye makaratasi mtu anakwenda anagonga kidole, tiki ikitiki pale anaondoka, kura zinahesabiwa, ndani ya saa mbili mshindi anajulikana na hii itakuwa imetusaidia sana na e-Government itakuwa ina maana sana na malalamiko mengi yataondolewa kwamba watu wanashinda kwa kuiba na kufanya forgery. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine la muhimu, Serikali iangalie uwezekano wa kuwapatia laptop watendaji wa vijiji na watendaji wa Kata ili kurahisisha utendaji kazi wakati wa e-government na hili liwe kwa kuanzia Ofisi ya TAMISEMI kwa sababu Ofisi ya Rais TAMISEMI ina watendaji wengi kuanzia huko chini kwenye mitaa, vijiji, inashindikana, tuwape walau laptop mojamoja watendaji wa vijiji na wa Kata ili e-Government iwe na maana isiwe tena b ado tumeingia kwenye e-Government bado m akaratasi yanatumika, tuanzie kule chini kwenye vijiji na kwenye Kata itakuwa inaleta tija sana sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya je tunazo kompyuta za kutosha au smart phone za kutosha kuweza kutumia, ndugu zan gu e-Government haihitaji, sio lazima uwe na kompyuta, uwe na simu kwa mtu wa kawaida za smart phone. Hata ukifanya ukitumia simu ya tochi, kwa namna ya mafunzo tuliyoyapata sisi na uelewa tuliojengewa hata simu ya tochi inaweza ikaendesha e-Government isipokuwa inahitaji uelewa. Watu wajengewe uelewa, waeleweshwe papatikane semina za kutosha jambo hili linaweza likatusaidia sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)