Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Lucy Thomas Mayenga (16 total)

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia leo kusimama hapa na kwa kweli nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa sababu hiki ni kipindi changu cha tatu ndani ya Bunge, namshukuru sana Mwenyezi Mungu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri na nimpongeze kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya na Baraza la Mawaziri. Watu wamekuwa wanafanya kazi vya kutosha, wanapiga kazi ambayo inasifika sana na kila mtu kwa kweli anaona utendaji wao, ingawa kuna wengine wamezidi zaidi, wengine viwango vyao ni vya juu sana. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuzungumzia kuhusu suala la makato ya kwenye kiinua mgongo. Hapa Mheshimiwa Waziri wa Fedha amegusa pabaya kwa Waheshimiwa Wabunge. Hata hivyo, nafahamu kwamba una busara sana, kwa hiyo utafikiria tena upya ili angalau mambo yakae vizuri sina haja ya kueleza zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza bajeti hii ni bajeti ambayo ina kila sababu ya kutuonesha na kutupa imani kwamba huko mbele tunakokwenda pako vizuri sana. Naisifu kwa sababu angalau imetuonesha na inatupa picha kwamba huko mbele yale ambayo tunayafikiria yameanza kidogo kuja.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na suala zima la uchumi wa viwanda. Tunapozungumzia suala zima la uchumi wa viwanda, najiuliza, kwamba tunazungumza kuhusu suala la uchumi wa viwanda je, tuko tayari? Kwa sababu tunaweza tukakaa tukazungumza mambo mazuri sana na tukawa na mipango mizuri sana, tukapiga makofi hapa tukawa na sifa nyingi sana lakini tusipofunga mikanda na kusema kwamba hapa sasa tumeamua kufanya kazi vya kutosha, haya masuala yataishia kwenye makaratasi na utekelezaji wake utakuwa ni mgumu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu lipo jambo moja ambalo sijapata picha sawasawa, suala hilo ni la Inter-Ministerial Coordination. Wizara hii na Serikali hii kwa ujumla kwenye suala hili la uchumi wa viwanda, Wizara ya Kilimo inashirikiana vipi na Wizara ya Elimu, Wizara ya Nishati, Wizara ya Maji na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu tunapozungumzia uchumi wa viwanda, huu ni uchumi na ni biashara ambayo ni mkakati wa muda wa kati na muda mrefu. Sisi wengine siyo wafanyabiashara wakubwa, lakini angalau tunajaribu jaribu kidogo. Kwa hiyo, ninapozungumzia hivi ni kwa sababu tukisema kwamba tunazungumzia viwanda lazima tujiulize, Wizara ya Elimu imejiandaa kwa kiwango gani? Wizara ya Maji licha ya kwamba Tanzania ni Taifa ambalo ni la tatu duniani kwa wingi wa maji, imejiandaa kwa kiwango gani ili kuweza ku-facilitate? Kwa sababu kiwanda bila maji ni kitu ambacho hakiwezi kwenda. Wizara ya Kilimo imejiandaaje? Wizara ya Nishati imejiandaaje?
Mheshimiwa Naibu Spika, tusipokuwa makini tutajikuta kwamba watu wanakuja, wanasema sisi ni wawekezaji tunataka kuwekeza, mimi nataka kuja kuwekeza labda pengine kwa wananchi wangu wa Shinyanga kule, nataka nifungue kiwanda cha kitu fulani, lakini akikaa anaanza kwanza kujiuliza wakati anafanya due-diligence, hivi maji hapa nitayapataje? Anajiuliza hivi umeme bei yake na upo kwa kiwango gani? anajiuliza hivi kwa mfano, kama nikifanikiwa kama endapo nitawekeza kwenye kilimo, masoko yako wapi? Anajiuliza hivi, hapa nikifungua kiwanda human resource nitaitoa wapi? Kwa hiyo, haya ni maswali ambayo inatakiwa kama Serikali kwa ujumla wetu tujiulize kwa pamoja ili tuweze kuwa wote na kauli moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu sisi kama Watanzania, wapo Watanzania ambao tunafanya kazi vizuri sana, lakini wapo watu ambao wamezoea business as usual. Wao kazi yao mtu anaingia ofisini, tunaona hata kwenye ofisi na taasisi za Serikali, mtu anaingia asubuhi saa mbili anatoka saa tisa, uvivu na ile kukaa tu kwa kujiona kwamba mimi sina tatizo lolote yaani mtu anakaa tu ile laissez-faire imekuwa ni tatizo letu. Kwa hiyo, hatuna budi sisi kama Viongozi na Wanasiasa tuseme kwamba tumejiandaa vipi kwenye hili suala.
Mheshimiwa Naibu Spika, mfano tu mdogo nitolee, National Housing ni Shirika letu la Umma, lakini siyo wawekezaji, National Housing, wanajenga nyumba za Serikali wanaziuza, Wabunge tumekuwa mara nyingi sana tunapiga kelele kwamba nyumba hizi bei yake ni kubwa sana, lakini ukikaa na National Housing wanakwambia kwamba tunapokaa wakati tunaanza hii project ya kuanza kujenga nyumba sehemu, tunajikuta kwamba maji mimi mwenyewe National Housing ndiyo nivute, umeme mimi mwenyewe ndiyo nikae nifanye hizo jitihada, kwa hiyo unajikuta ile pesa ambayo unaiweka pale ni kubwa sana kiasi ambacho baadaye inabidi irudi kwa mlaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalo nataka kuzungumzia ni kuhusu suala zima la mifumo yetu pia. Mifumo yetu na system yetu ya nchi ya kuchukulia mambo, lazima tubadilishe pia sheria zetu za kazi kabla ya kuanza kukaribisha hawa wawekezaji. Sheria ya Kazi iliyopo sasa hivi inatakiwa iwe fair kwa mwajiri pamoja na mwajiriwa. Hivi sasa unakuta Sheria ya Kazi ime-base zaidi kwa yule mwajiriwa kiasi kwamba anajiona kama Mungu mtu, sasa nini kinachotokea?
Mheshimiwa Naibu Spika, kinachotokea sasa ni kwamba, watu wanafanya kazi, mtu anajua kwamba kwa mfano, mimi kama labda nafanya kazi kwenye shirika lolote labda pengine tigo, airtel na kadhalika, anaweza mwingine aka-misbehave, mwingine anafikia kiwango hata cha kuiba lakini haya mashirika na haya makampuni, hiki naomba Serikali kwa kweli tujitahidi sana, tuwe makini sana, tukae tujiulize na ikiwezekana tuunde timu ya kuangalia hawa wawekezaji tu tulionao hapa, sasa hivi kabla ya kuwakaribisha hawa wengine kwenye uchumi wa viwanda, wana matatizo gani? Maana kinachotokea sasa hivi, mtu anaiba airtel au anaiba tigo kwa mfano au anaiba sehemu nyingine yoyote lakini kinachotokea ni kwamba lile shirika au hiyo ofisi wanamchukua yule mtu wanamwambia tu naomba u-resign.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kutoa mchango wangu. Nianze kwa kutoa shukrani zangu nyingi sana kwa Waheshimiwa Wabunge wote walioko katika Bunge hili kwa support kubwa waliyonipa na hatimaye sasa
nimekuwa Mrs. Jamal, ahsanteni sana. Haya makofi naomba yaendelee mpaka mwisho najua kuna sehemu yatagoma. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe pongezi za dhati sana Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Jenista Mhagama na Naibu wake Mheshimiwa Mavunde, wanafanya kazi nzuri sana na kazi kubwa sana. Leo nimesimama hapa, kwanza kwa kweli nina hasira kwa sababu kuna baadhi ya vitu ambavyo havijanifurahisha hata kidogo na kuna baadhi ya vitu ambavyo nikiviangalia unamwangalia mtu halafu unasema; hivi huyu anategemea nini? Unakosa majibu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa nafasi ya kipekee nimpe pongezi zangu za dhati sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa sana ambayo anaifanya yeye pamoja na Baraza lake la Mawaziri, wanafanya kazi kubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi ambayo asilimia 32 ya mapato ya ndani yanakwenda kulipa madeni, katika nchi ambayo malimbikizo ya madeni yapo asilimia sita, katika nchi ambayo Mheshimiwa Rais anapozunguka au Waziri Mkuu au Mawaziri wanapozunguka Rais anaanza kuombwa kuanzia vidonge kwenye hospitali mpaka kwenye ndege watu wanalalamika, Rais huyu kwa kazi hizi anazozifanya kwa kipindi hiki kifupi alichofanya kazi, anastahili pongezi kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukakaa hapa kukaanza kuongea kirahisi rahisi kwamba Rais huyu amefanya hivi, Rais huyu hafai, Rais huyu sijui amefanya hivi ni rahisi sana kuongea namna hiyo, lakini Wabunge baadhi wamezungumza; hivi sisi Waheshimiwa Wabunge maana nianze hata na mimi mwenyewe kwa sababu nipo humu ndani; katika kipindi hiki cha 2016 mpaka sasa hivi mmefanya nini kwenye Majimbo yenu? Hivi kila mtu akisema akae hapa aanze kuulizwa orodhesha ulichokifanya atasema amefanya nini? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema makofi yaendelee najua yatagoma; mimi nimekaa hapa Bungeni kwa kipindi cha miaka 12 kuanzia mwaka 2005 mpaka leo hii niliingia hapa Bungeni nikiwa mdogo sana. Naomba kutoa tahadhari kubwa sana kwa Wabunge ambao ni wapya na hasa Waheshimiwa Wabunge ambao ni vijana. Wako watu ambao ni Genuine kabisa kutoka pande zote mbili; kutoka upinzani na pia na huku. Kuna watu ambao wakiongea unajua kabisa huyu anaongea ni kwa kutoka kwenye dhamira yake lakini kwa experience yangu kuna watu nimeshuhudia tangu nimeingia hapa Bungeni miaka 12 hii kuna watu wananunuliwa na ni Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wana interest zao nyuma, mambo yao yameharibika, wanakuja hapa wanataka kutuvuruga. Kuna mtu anakuja hapa anasimama kwa sababu mume wake alikuwa fisadi ameondolewa kwenye madaraka anasimama hapa anataka kutuvuruga.
Kuna mtu anakuja anasimama hapa kwa sababu alikuwa anapewa pesa na mafisadi, mambo yamekuwa magumu anakuja hapa anataka kutuvuruga, kila saa Serikali mbaya, Rais mbaya, sijui vitu gani vibaya; tunaomba samahanini sana hayo maneno yenu mnyamaze mkaongee huko barabarani. Hapa tunataka tukae tuongee masuala ya maana, masuala ya wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeishi Rwanda kwa kipindi cha miaka kadhaa siwezi kusema ni miaka mingapi na kule walikuwa wanajua mimi ni Mnyarwanda. Nimeishi uswahilini ya Rwanda na nimeishi Masaki ya Rwanda; watu ambao ni viongozi wanakuwa wazalendo, kuna mambo ambayo ni ya msingi, mtu anakaa nazungumza kwa ajili ya nchi yao. Watu wanakaa wana-discuss issues ambazo ni za maana leo hii tumekuwa viongozi ni mambo ya Twitter, sijui Whatsapp, meseji za kipumbavu pumbavu ni aibu kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, inatakiwa tutumie muda ambao huu tunao kukaa, kufanya mambo ambayo ni ya maana. Kwa nini hatukai tukashauriana kwamba jamani hebu tufundishane ujasiriamali tunafanyaje, hebu jamani twende tukamfuate Mheshimiwa Waziri wa Fedha, jamani Mheshimiwa hebu tusaidie, tunataka tujiunge Wabunge 20 tufungue kiwanda, Mheshimiwa Waziri wa viwanda hebu tusaidie Wabunge 50 tunataka tukae tuweke mitaji yetu, tunataka tufanye biashara ya maana, matokeo yake watu mnakaa mnaanza kuchanganyikiwa, mnakuwa hamna hela mkitoka hapa maisha magumu, mmekaa wengine hapa mnapiga makelele, mnapata hizo nguvu kwa sababu mpo
ndani ya vyama vyenu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inatakiwa watu muweze kukaa kila mtu amekuja hapa kwa nguvu yake na kila mtu amekuja hapa kwa moyo wake na anajua yeye mwenyewe nini kilichomleta. Sasa msikae hapa mnaanza ku-insight other Members of Parliament to turn against the Government hii ni adabu mbaya, mbaya, mbaya kupita kiasi. Kama mna mambo yenu huko pembeni nendeni mkayamalize, kama mna jambo lenu huko pembeni nendeni mkakae mkaongee huko, lakini siyo mnakuja hapa eti Bunge zima likae liongee mambo ya ajabu ajabu…
Taarifa....
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokisema nilisema kwamba, katika kipindi ambacho nimekaa hapa Bungeni nimeshuhudia Wabunge wa aina hiyo wapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu afikishe salamu zetu kwa Mheshimiwa Rais aende akamwambie kwamba tuko nyuma yake, tunajua kazi kubwa ambazo anazifanya, tunajua Serikali hii kazi kubwa ambayo inaifanya na tuko nyuma yake kwa njia yoyote ile. Hatuwezi kunyamazishwa lakini ninachoweza kuwaambia, hawa ambao wanaweza kupambana naye, yupo mpaka 2025 ambao wanadhani kwamba 2020 ni mwisho, they are very wrong na wanajidanganya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuwaambia hata baadhi ya Wabunge ambao tuko huku kwenye Chama chetu, kila siku nasema na kuna mtu mmoja nimeshawahi kumwambia; You cannot win the fight with your Boss, you are messing up with the very wrong person katika Awamu hii
ya Tano. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwepo hapa Bungeni, kipindi cha uchaguzi uliopita, wote tulikuwepo hapa labda hawa wengine wageni ambao hawakuwepo lakini walikuwa wanafuatilia. Baadhi ya Wabunge tulikuwa tunaona tabia za ajabu ajabu walizozifanya ukiwa humu ndani, watu na heshima zao. Mimi nimeingia hapa kwa mara ya kwanza ulikuwa unamwona Mheshimiwa Mbunge unadhani kwa sababu ya umri wake ni mtu mzima, ‘shikamoo Mheshimiwa’ baadaye unakuja kukaa baada ya mwaka mmoja, baada ya miaka miwili, unasema kumbe hata ‘mambo’ hastahili kwa sababu ya jinsi vitu anavyovifanya vya aibu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wote tunajua na wala siyo siri, tulikuwa tumekaa hapa, watu wakati wa uchaguzi, makundi yaliyokuwepo, sasa mimi nasema hivi; kama yale makundi yalikuwepo, kama ni masuala ya interest nyingine ambazo tunazo tuachane na hizo biashara sasa hivi tukae tujenge nchi yetu. Tukae tufanye kazi, tukae tuanze kuangalia maendeleo ya nchi yetu yanakwendaje, wengine hapa kwanza hata muda wenyewe wa kuuliza maswali hatuna kwa sababu unawaza biashara tu sasa unamshangaa mtu mwingine kila saa amekaa ‘Serikali hii sijui imefanya hizi’ mimi nasemaga hivi hawa watu wanatoa wapi muda? Mwisho mtakosa Ubunge mrudi nyumbani kule maisha yaanze kuwa magumu, shauri zenu. Ndiyo ukweli wenyewe si nyie mnajijua? Niliwaambieni haya makofi yatafika mwisho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata siku moja Simba Wazungu wana msemo kwamba; “The lion does not turn around when a small Dog barks” Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu wala msihangaike na hawa watu ambao wanapiga makelele ya ajabu ajabu, maneno ya ajabu ajabu, wanasema vitu vya ajabu ajabu, ninyi kaeni, fanyeni kazi mwendelee kuwepo kwenye mstari na tuko pamoja, tunaowaunga mkono ndani ya hili Bunge ni wengi zaidi kuliko hawa wachache ambao wanapiga makelele. Tuwaache waendelee kupiga makelele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nataka niseme; watakuja siku moja kula matapishi yao, wapo watu ambao tumewashuhudia leo mtu anasema hivi kesho anakuja unamshangaa huyo huyo anasimama Serikali hii nzuri sana. Unashangaa haya maneno ametolea wapi, watakuja kurudi
kula matapishi yao lakini wakati huo tutakuwa tayari tumeshawajua.
Mheshimimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nina hasira sana. Naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante sana kwa kunipatia nafasi hii, ninakushukuru sana. Nianze kwa kum-quote Profesa mmoja wa Kenya ambaye anaitwa Patrice Lumumba, yeye alisema kwamba; “Magufuli is the real deal.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wangu kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya kiasi ambacho amewafanya mpaka baadhi ya watu wameanza kuchanganyikiwa, wanahisi kama Mheshimiwa Magufuli amekaa miaka saba, wakati ndio kwanza ana mwaka mmoja na nusu. Na ninapenda kuwaambia kwamba hii ni mpaka 2025. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi kubwa ambayo leo hii nimeamua kusimama hapa, kwanza ni utendaji wake, lakini vilevile ni jinsi ambavyo ameshughulikia suala hili la makinikia. Suala hili la makinikia wananchi wangu, kwa mimi ambaye natokea Mkoa wa Shinyanga, wamenituma wanasema kwamba, katika vitu ambavyo utazungumza usiache kuelezea furaha kubwa tuliyokuwanayo sisi kwa jinsi ambavyo Rais ameweza kutusaidia, walau kuonyesha njia ambayo tunajua sasa tutafaidika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nimesoma magazeti, kuna gazeti moja nikasoma limeandika kwamba, kuna utafiti wa TWAWEZA, wanasema kwamba sijui umaarufu wa Mheshimiwa Rais Magufuli umeporomoka kwa sababu anapendwa na watu wa kada ya chini! Mimi nilikuwa nataka niseme jambo moja, wala hajakosea kwa sababu asilimia kubwa ya Watanzania ni maskini wale ambao ndio wanachukua asilimia kubwa asilimia 70. Kwa hiyo, kwa Rais kukubalika kwa watu asilimia 70 na kupingwa au kutokukubalika kwa ile asilimia 30 mimi naona ni jambo zuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa mtu yeyote, kiongozi yeyote ambaye unajua unachokifanya hiki ndicho ambacho kinatakiwa kufanyika. Wewe hutakiwi upendwe na watu wachache ambao tena wengi mara nyingi wanakuwa ni mafisadi au wanakuwa ni watu ambao umewagusa kwa namna moja au nyingine, inatakiwa wewe upendwe na wale watu ambao ndio wengi.

Kwa hiyo, kwa Rais kukubaliwa na watu wa kada hii ya chini ndio hasa kitu ambacho tunakiunga mkono na kwa kweli, ndio kinaonyesha kwambam Rais wetu yuko imara sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara ya mwisho wakati nachangia…

TAARIFA ...

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu yeyote mwenye akili timamu lazima apokee hiyo taarifa. Ni ukweli kabisa utafiti umefanyika between mwezi wa tatu na mwezi tano na ndiyo kipindi masuala ya vyeti fake yamesemwa masuala ya mafisadi yamesemwa kwahiyo hawa wenzetu hii asilimia 30 tunawajua ni wakina nani na hawa wa Makinikia na wao pia tunawajua na wenyewe pia wanajijua na wengine wako humu humu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwenye kuzungumzia suala hili la makinikia mimi nina ushauri mdogo. Mtanisamehe sauti yangu kidogo inakwaruza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala hili la Makinikia mimi nilikuwa na ushauri kidogo biashara hii ni biashara kubwa sana, ninampongeza sana sana Profesa Mruma na pamoja na Profesa Osoro. Profesa Mruma nimekuwa naye kwenye board ya Williamson Diamond kwa kipindi cha miaka kama nane, kwa hiyo biashara hii ya diamond ninaifahamu kwa kiwango cha chake. Biashara hii inaitwa holding business. Biashara hii hata ikija kutokea duniani leo hii dhahabu zote zikaisha almasi zote zitakaisha kwenye mashino yetu aidha Afrika au sehemu nyingine yoyote. Of course sana sana ni Afrika. Biashara hii bado itaendelea kufanyika kutokana na nature ya hii biashara jinsi ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu nilikuwa naomba kushauri kwamba amekuja huyu CEO wa Barrick, lakini inatakiwa sisi kama Tanzania tukae naye. Mimi ambacho naomba kushauri naomba kwamba timu yetu ya Tanzania tufanye upembuzi mzuri sana wa watu wa kukaa na huyu mtu. Hawa wenzetu ni wazoefu sana wa hizi biashara ni tycoon wa hizi biashara, ni biashara ambazo zina pesa nyingi sana lakini wenzetu wame-deal na hivi vitu maeneo mbalimbali kupita kiasi zaidi yetu sisi. Kwahiyo, lazima kwenye kuchagua watu wa kukaa nao meza moja lazima tuchague watu ambao vichwa vyao viko sawa sawa kikweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwenye suala hili la makinikia mimi nilikuwa naomba kuuliza Wizara ya Fedha, miaka ya nyuma BOT walitoa wayver kwa makampuni yote ya madini ambayo wanachimba hapa Tanzania ambayo yanatoka nje kwamba mnaruhusiwa kuweka pesa zenu nje. Ile wayver ilitolewa wakati ule Gavana akiwa Dkt. Balali mpaka sasa hivi wayver ile haijarudishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu kubwa ya haya makampuni walisema kwamba sisi tunataka tuweke pesa zetu huku nje kwa sababu hapa Tanzania hakuna mabenki ambayo ni international, lakini vile vile na sisi ambao ni wafanyabiashara ya hizi biashara. Sisi mikopo yetu tunaitoa huko nje. Sasa hawa watu sasa hivi international bank zipo nyingi hapa Tanzania. Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa kweli mimi nitaomba jibu hapo baadaye utakapokuja kuhitimisha uje utuambie ni sababu zipi zilizofanya mpaka leo hiki kitu kimekuwa kimya hakisemwi kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu kama tunavyoelewa kwamba pesa hizi zilikuwa zinawekwa hapa Tanzania, sisi Tanzania hapa tumekuwa tunalalamika bei ya dola imekuwa kubwa wafanyakabiashara wanalalamika. Pesa hizi zikiwa zinawekwa hapa tutafaidika hata mzunguko wetu wa pesa, urari wa biashara utaweza kuonekana na mzunguko wetu wa pesa itakuwa ni rahisi zaidi kwa sababu hata dola itachuka at least ita-stabilize vizuri kuliko ilivyo sasa hivi. Nilikuwa naomba jambo hili liweze kuliangalia kwa macho makali zaidi na kwa kweli ulifanyie kazi kwa haraka sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine ambalo nilikuwa nataka nizungumzie. Kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake dada yangu Dkt. Ashantu wanafanya kazi nzuri sana ni watu ambao siyo waongeaji sana lakini kwa kazi wanapiga vizuri sana. Mmefanyaka kazi nzuri sana bajeti ni nzuri sana kusema za ukweli. Huwezi kuwa mtu mwenye akili timamu ukasema bajeti hii ina matatizo ina dosari za hapa na pale kwa sababu ni ile tu kwamba hatuwezi kumaliza matatizo yote kwa mara moja. Lakini hatuwezi kusema kwamba bajeti hii mbaya, bajeti hii ni nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba kwenye suala zima la kuwasaidia wajasiriamali wadogo tusiishie tu kwenye masuala ya administrative pamoja na facilitation, mimi nilikuwa naomba tu tujikite zaidi kwenye jinsi ya kuwasaidia hawa wajasiriamali wadogo.

Mheshimiwa Waziri nilikuwa naomba kukuambia ujaribu kumulika pale Airport - TRA ya kwako. Kuna matatizo makubwa sana wakati tumekaa tunazungumzia habari za kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, Mheshimiwa Waziri wafanya biashara hawa wadogo wako akina mama, wako vijana wanaangaika wanakwenda nchi mbalimbali kuja kuleta bidhaa. Wanafanyabiashara ambazo mitaji yao ni dola 20000/30000 siyo pesa nyingi, lakini mtu analeta mzigo akifika pale airport anapata usumbufu wa hatari. Inakuwa inamkatisha mtu tamaa mpaka anaona kwa nini nimeanza kwenda. Anapata visa anamaliza anatoka anakenda huko nje kwenda kufanya hiyo biashara lakini akiingia hapa Tanzania anapata usumbufu kupita kiasi na rushwa pale imezidi. Mimi nakuambia kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho ambalo nilikuwa nataka nilizungumzie, Wizara ya Afya, uchumi ni afya, Wizara ya Afya nilikuwa naomba nitoe wazo Bunge hili liunde Kamati ya kushughulikia suala zima la Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeoza, haifai na kama ikiwezekana Mheshimiwa Rais na angekuwepo hapa leo Mheshimiwa Waziri Mkuu, nadhani ningempa message kwa sababu yeye alijua jinsi ya kuzungumzia angeifuta kabisa. Ofisi ya Mkemia Mkuu inatakiwa ifanye control ya chemicals ambazo zinaingia Tanzania jambo ambalo hawafanyi hata kidogo. Kuna kampuni inaitwa TECHNO imeiingiza chemical kampuni moja tu. Imeingiza chemical ambazo ni nyingi wanaulizwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali hawajui hata idadi ya Chemicals ambazo zimeingizwa hapa Tanzania. Kemikali hizi zinatumika hospitalini, kwenye mashule yetu, wanafunzi wanakwenda kufundishwa kwa ma-chemicals ambazo zime expire, wanafunzi wanakwenda kufundishwa kwa chemicals ambazo nyingine siyo zenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitu kama hivi tukiendelea kukaa tukivinyamazia, Mheshimiwa Waziri Mkuu alifanya ziara kwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akakutana na hili jambo linatia aibu nasikitika tu kwamba sikupata nafasi ya kulizungumza kwa urefu wakati wa Wizara Afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia leo kusimama hapa na kwa kweli kutoa mchango wangu wa mawazo kwenye Wizara hii. Kwanza kabla sijaanza, niseme ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya yangu ya Shinyanga Mjini kwenye Jimbo letu la pale Shinyanga Mjini, Mheshimiwa Waziri naomba achukue hili suala na shida hii kubwa ambayo tunayo; tuna tatizo kubwa sana la uchakavu mkubwa wa Kituo chetu cha Polisi pale Shinyanga Mjini. Vilevile tuna tatizo kubwa sana la uhaba wa magari; kuna Wilaya mbili za Kipolisi, Ushetu pamoja na Msalala, hazina magari ya Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba nianze. Kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza sana Rais wangu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa sana ambayo amekuwa akiifanya. Nalipongeza sana Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya. Naomba niseme yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa IGP na Makamanda wake, watulie wala wasiwe na wasiwasi. Waendelee kuchapa kazi. Kazi wanazozifanya zinaonekana, mambo mema wanayoyafanya yanaonekana. Hatuwezi ku- compromise kwenye suala zima la usalama. Hii nchi watu walikuwa wamezoea kudeka, kufanya mambo ya ajabu na kuropoka maneno ya ajabu kila siku na kutukana hovyo kwenye mikutano. Lazima ifike wakati tushikishwe adabu. (Makofi)

Vyama vyote vya Siasa, ukiwa CCM, ukiwa chama chochote lazima ufike wakati ujue kwamba nchi lazima ifike wakati itawalike. Isiwe kwamba watu wanakuwa huru kiasi ambacho mtu anakaa ana uwezo wa kuamka leo asubuhi akafanya anachotaka, ana uwezo wa kukaa mchana akafanya anachotaka, lazima ajue kwamba nikifanya jambo lolote nikiwa na azma mbaya, nitashughulikiwa. Hiyo ndio Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu mpaka wamefikia kusema kwamba Jeshi la Polisi ni wapiga debe wa CCM; watu wanasahau. Ndiyo kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge aliyetoka kuzungumza hapa kwamba yanapokuwa masuala mema, pale tunapokaa tunalindiwa mali zetu na usalama wetu, tunaona hivi vyombo vya ulinzi na usalama kwamba ni vizuri sana. Pale inapokuja sasa kwamba na sisi tunashughulikiwa kwa mambo yetu ambayo tumeyafanya mabaya, tunaanza kuona Jeshi la Polisi ni baya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Polisi sio wote ni wabaya, sio wote wanafanya kazi zao kinyume na sheria na utaratibu, wapo watu wengine baadhi ambao tunaona na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tusione kwamba Polisi wote hawafai, Polisi wote sijui wameoza. Kwanza hali ya usalama iliyopo sasa hivi, uhalifu ulivyopungua, sasa hivi inaonesha kabisa kwamba Jeshi letu la Polisi na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza RPC wa Dodoma, licha ya haya maneno ambayo watu wanasema sijui amesema hivi, lakini mimi nampongeza. Nampongeza RPC wangu wa Mkoa wangu wa Shinyanga, nampongeza pia sana RPC wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana. Kwa ujumla ni mfumo mzima ndani ya Jeshi la Polisi wanafanya kazi nzuri, lakini yote haya, lazima na sisi tukiwa kama Watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa, tofauti zetu za kiitikadi, lazima tujiulize, kwa nini nchi yetu imekuwa na chokochoko namna hii? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini mambo mengi sana sasa hivi yamekuwa yakisemwa na kumekuwa na chokochoko namna hii? Tena mpaka imefikia kiwango watu wa nje sasa wanaanza kuingilia uhuru wetu na mwenendo wetu wa nchi. Lazima tujiulize, yote haya yanasababishwa na kazi nzuri ambayo anaifanya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ambayo anaifanya, kwa namna yoyote ile hakuna mtu ambaye anaweza akakaa akafurahia. Wawekezaji kwenye Sekta ya Madini huko watu wamebanwa, wameshikwa pabaya; wakiangalia sijui watumishi hewa, wameshikwa pabaya; mafisadi, watu walikuwa wamekaa wamejiachia, wanakula pesa, wanafanya mambo ya ajabu, wameshikwa pabaya. Kwa hiyo, lazima tujue kwamba vita hii tuliokuwa nayo ni vita kubwa kuliko ambavyo tunaweza kufikiria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tu asubuhi Mheshimiwa Lema hapa amezungumza, aliuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhusu suala zima la matatizo ya mafuta ghafi ambayo yamezuiliwa huko bandarini. Hilo suala lina makorokoro mengi sana huko ndani. Namshukuru Mheshimiwa Lema hata kwa kuuliza lile swali. Sasa watu kama hawa ambao wamekuwa wakishughulikiwa lazima wao wenyewe kwa wenyewe watakuwa wanapiga makelele. Mwaka jana Mheshimiwa Rais alisema, wewe ukiwa kama mwanaume, unafanya biashara halali, ikifika mwezi wa Sita wewe utakuwa ni mwanaume kweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alikuwa anasema namna ile kwa sababu hawa watu ambao wameguswa pabaya na wengi wetu na hata hawa wengine wa upande wa pili wanawajua na wengine wengi wao ambao wanawajua, wanajua kwamba baadhi yao wafadhili wao. Lazima ifike wakati na wao wawe wazalendo kutoka mioyoni mwao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ukiona kwamba jambo hili ni baya, tuangalie hatima zetu za huko mbele, tusiangalie tu leo; tuangalie wajukuu na watoto wetu na ndugu zetu hao wengine wa baadaye. Tusikae tu kuangalia kwamba eti tumekaa, mara mambo yamekuwa yanaibuka ovyo, mara sijui hivi na hivi na hivi; lazima tujue kabisa kwamba hawa wafadhili wetu itafika mwisho sisi tutaondoka, lakini maisha ya Watanzania yanaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata wakiendelea kusema, mimi nimezoea. Waseme wee, wakichoka wananyamaza, mimi naendelea. Watulie misumari iingie. (Makofi)

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge kwa muda mrefu wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala zima…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa mwenyekiti, licha ya changamoto nyingi ambazo Jeshi la Polisi limekuwa linazo, lakini kazi kubwa ambayo imekuwa ikifanyika imekuwa inaonesha kabisa kwamba nchi hii, kinachotakiwa kimsingi ni dhamira ambayo iko kwa viongozi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ambalo nataka nizungumzie, nataka nizungumzie Wizara hii ya Mambo ya Ndani. Nailaumu Wizara hii ya Mambo ya Ndani. Nampongeza sana Kamishna wa Uhamiaji, mwanamke, Kamishna Anna Makakala, anafanya kazi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamishna wa Uhamiaji anafanya kazi kubwa na nzuri sana. Kamishna huyu amekuwa anashughulikia masuala ya uhamiaji haramu, lakini yako mambo na matatizo ambayo yamekuwa yakijitokeza. Kuna taarifa kwamba wapo wahamiaji ambao wamekuwa wakiingizwa hapa Tanzania na watu ambao hawana uzalendo na nchi yetu; wahamiaji hawa haramu wamekuwa wakifa kwenye magari; wahamiaji hawa haramu wamekuwa wakitupwa na wale watu ambao wanaingiza kinyume na sheria; wanawatupa kwenye mito, bahari na kadhalika, lakini Wizara hii ipo kimya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwigulu, matokeo yake sasa imekuwa ni kwamba Serikali na sisi ambao tupo Chama cha Mapinduzi tumekuwa tunalaumiwa kwamba watu hawa sijui wanakufa, sijui wanauawa na kadhalika. Kwa nini Serikali hamsemi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mnapokaa mnanyamaza kimya inafanya kwamba kile ambacho kinaendelea kufanyika sasa hivi, watu wanatumia sana mitandao hii ya kijamii, taarifa ambazo zinapelekwa kule siyo zote ni za kweli.

KUHUSU UTARATIBU . . .

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ripoti ya CAG, naomba Mheshimiwa Waitara akaichukue, atulie kichwa chake kiwe sober, aisome yote ataelewa ninachokisema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumzia kuhusu Wizara hii ya Mambo ya Ndani. Naomba kuanzia sasa hivi Wizara hii iamke. Iwe inatoa taarifa bila kumwonea mtu aibu. Matukio ambayo yanatokea, changamoto ambazo zinaendelea; ninafahamu kwamba endapo kama mtu ameuawa aidha kisiasa au hata kama siyo kisiasa, kwa sababu yapo mambo mengi ambayo yanafanyika, jinsi mwendelezo wa huo uchunguzi unavyoendelea, wawe wanatoa taarifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nafahamu kwamba hawawezi kusema kila kitu, lakini wawe wanasema kwamba angalau tumemkamata mtu na mambo haya yanaendelea. Kwa sababu yapo mambo ambayo yanasemwa kisiasa wakati kiuhalisia hata kwenye vyama vyetu vya siasa kuna mambo mabaya tunafanyiana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi, kuwa mwanachama wa CUF, kuwa mwanachama wa CHADEMA, kuwa mwanachama wa chama chochote haina maana ya kwamba huwezi kuwa na matatizo yako mengine ya kijamii. Haina maana kwamba wewe kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa au wewe kuwa kiongozi wa Chama cha Siasa, basi ni mtakatifu kwamba ikitokea kuna chochote ambacho kimetokea dhidi yako maana yake ni kwamba umefanywa au jambo hilo limefanywa na mpinzani wako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Wizara hii waamke. Wamekuwa wananyamazia sana haya matukio. Matokeo yake Serikali imekuwa ikisemwa na ikihusishwa kwa mambo mengine ambayo hata hayapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili Mheshimiwa Waziri kwa kweli endapo kama ataendelea kunyamaza namna hii wakati anajua kabisa kwamba haya mambo yapo mengine ambayo yanafanyika kinyume na utaratibu; naomba watu watajane na watu watajwe kwamba huyu amehusika na huyu amehusika kwa moja, mbili, tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii walau na mimi ya kuweza kutoa mchango wangu katika Wizara hii ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kutoa pongezi nyingi sana kwa Waziri huyu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, pamoja timu nzima katika Wizara ya Viwanda, Katibu Mkuu, Watendaji wote FCC,TBS,TRA na wengine wote huko chini ninawapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nianze tu yaani kwa kusema maneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana Wizara hii ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ukianza Waziri pamoja na watendaji wako ichukuliwe kwa umuhimu wa kipekee, mtoke nje. Jana iligusiwa kidogo na Mheshimiwa Spika wetu, na mimi kitu ambacho nimekuwa nikikifikiria sana Wizara hii kuna baadhi ya watendaji kule chini ambao vitu vingi sana wanavifanyia mezani, hawajui on the ground, kwenye hali halisi kule mambo jinsi yalivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi ninaomba na biashara ni ushindani na baishara msingi mkubwa wa biashara ni connection. Kwa hiyo, Waziri wetu pamoja na watendaji wote, Wakurugenzi yaani mimi nitafurahi sana endapo kama nitaanza kusikia Mkurugenzi wa FCC,
Mkurugenzi wa TBS wamekwenda huku na huku, wasikae ofisini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi kazi zao si kazi za kusubiri tu kwamba mtu amefanya makosa ndipo aje huku kuja kmshughulia, inatakiwa na wao waende on the ground, waende kule kujifunza. Ninasema hivyo kwa sababu gani, kuna nchi jirani zawenzetu ambazo tunapakananazo, haiwezwekani sisi tukawa na urataibu mwingine nchi za wenzetu zikawa na utaratibu mwingine, Serikali inakosa mapato. Mfanyabiashara yoyote duniani hata kama mtu mkiwa mama ntilie nia yake anataka apate faida na sio tu faida akipa upenyo wa kuongeza faida kubwa yeye kwake ndiyo anaona ndiyo mafanikio ya baishara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokaa kuzungumzia uchumi, uchumi ni biashara, hauwezi kutenganisha uchumi na baishara. Sasa basi nikupe tu mfano kwa mfano sisi kama Watanzania kwa wezetu ambao ni wafanyabiashara kuna bidhaa ambazo kwa nchi za wenzetu kule kwao ni zero tariff. Lakini hapa kwetu tumeziwekea tariff, lazima na sisi tuweze kuangalia kwa nini wale wenzetu kule wamefanya hivyo ili nasi huku tuweze ku-react haraka. Kwa sababu kwa mfanyabiashara ambaye anajua biashara ataona kwamba nikiingiza Tanzania nitapata hasara, kwa hiyo atakachokifanya ataenda kukimbilie kuingiza huko jirani kwenye nchi za wezetu jirani ambako kule zinaingia kwa bei ya chini alafu baadae zitakuja kuigia huku Tanzania. Kwa hiyo mimi nilikuwa naomba sana Serikali iweze kuangalia kuhusu hili suala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ninapongeza sana hii Wizara na ninampongeza sana Mheshimwa Rais. Hata leo hapa tunavyozungumza ni miaka takribani miaka miwili na wala si miaka mingi sana, lakini wamefanya kazi kubwa sana wanajitahidi sana. Mheshimiwa Waziri usijali baadhi ya madongo unayopigwa pamoja na wenzako, madongo hayo unayopigwa mimi huwa wakati huwa najiuliza natamani na huwa mara nyingi sana nasema kwamba natamani yaani huwa wakati mwingine nasema kwamba ndiyo maana sasa nailewa baadhi ya nchi duniani viongozi waliopita kwenye nafasi mbalimbali kama Mawaziri, Makatibu Wakuu na kadhalika kuna baadhi ya nchi huku Mawaziri walikuwa wanapigwa mawe na wanafanyiwa hivi kwa sababu ya mambo waliyofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hi inapata matatizo mengi sana na Serikali hii imekuwa ikipata mataizo mengi sana kwa sababu ya system ambayo ilikuwa imeoza iliyopita. Nitoe mfano, utaratibu wa TRA wa zamani maana na mimi si mfanyabiashara mkubwa, lakini walao nakaakaa karibu karibu na wafanyabiashara, utaratibu wa TRA wa zamani ilikuwa ni kwamba mtu lazima utoe rushwa ili mambo yaende, ilikuwa ni kwamba lazima utoe rushwa huku na huku ndipo mambo yako yaende. Sasa basi mfanyabiashara/mtu yoyote ambaye anataka biashara yake na apate faida alikuwa anaona kwamba huo ndiyo utaratibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa sababu huo ndio utaratibu wafanyabiashara walikuwa wanalazimika kufanya vitu ambavyo vilikuwa wakati mwingine ni kinyume na maadaili.

Sasa ninachoiomba Serikali kwa sasa hivi tujaribu kukaa chini kuangalia, hawa wafanyabiashara si watu wa mataifa mengine, baadhi yao ni Watanzania wenzetu. Hata kama mtu akiwa pengine labda ana rangi tofauti lakini bado pia ni Mtanzania mwenzetu, wapo hapa Tanzania wanataka kuendelea kufanya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tusiendelee na yale mambo ya kukaa kuangalia yaani wao ni kwamba kama sheria imekaa, kama kanuni na taratibu tumekaa, tumesema kwamba hawa watu walifanya mambo mabaya tukae nao, najua kwamba Serikali kamba imekaa nao imewasikiliza, imeweza kuangalia kwamba wewe ulikwepa kodi mwaka fulani, lakini baada ya hapo tujiulize huyu mtu anaendelea na biashara au haendelei? Kama anaendelea Serikali iweze kumwangalia kwa macho mawili na kwa ukaribu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile isichukuliwe sasa kwamba mfanyabiashara kwa sababu miaka ile ya nyuma alikuwa labda pengine inasemekana kwamba aliwahi kukutwa tuhuma za kufanya jambo fulani, kwa sasa hivi anaendelea kuzibiwa kwa asilimia 100. Tusiendelee kufanya namna hivyo sisi tunachotaka hizi kodi zitusaidie kwenye nchi yetu nchi yetu ili nchi ipate pesa. Hawa wafanyabiashara hawajakimbia nchi, wapo wengine ambao si wazalendo wameamua kukimbia nchi, lakini hawa wafanyabiashara kama walikuwa na madeni yao kaeni nao huko mkubaliane nao kwamba watalipaje hizo pesa walipe Serikali ipate pesa. Lakini tusiendelee kusema kwamba wafanyabiashara fulani, kwa mfano labda Lucy Mayenga huyu inasemekana kwamba alikuwa anafanya jambo fulani basi ndo anakuwa ameharibika kiasi kwamba mpaka sasa hivi hata akiingiza mizigo yake anapata usumbufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiendelea kufanya namna hiyo biashara za watu zitakufa, kodi ambazo sisi kama Serikali tumekuwa tukifikiria kuendelea kuzipata hatutaendelea kuzipa kama inavyotakiwa. Pamoja na hayo ninataka kwamba Serikali iendelee kufanya utaratibu kama inavyotakiwa. Kinachotokea sasa hivi kwa hilo ambalo linaendelea ni nini, kwa mfano mimi kama mfanyabiashara nina kampuni yangu inaitwa X inaonekana kwamba labda inasakwama sana kutokana na mambo ambayo labda pengine nilifanya huko nyuma, labda pengine tumekaa chini tumekubaliana kwamba jamani nilikuwa nadaiwa nitalipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anaamua sasa, kwa mfano Mheshimiwa Waziri nikupe mfano mmoja, mfano tu mdogo TIN Number mpaka mwendesha boda boda anayo. Mimi nikileta leo hii makontena kumi kwa ajili kampuni yangu ninyi kama Serikali mtu akija akanikanidiria makadirio ya juu natafuta watu wa bodaboda kumi kila mtu pale na TIN Number yake anaingia ule mzigo kama vile kwamba ule mzigo ni wa kwake. Kwa maana hiyo sasa Serikali itakosa income tax na itakosa VAT return. Kwa hiyo, lazima tukae tuangalie, biashara ni vitu lazima wakati wewe unafikiria (a) uangalie (b), (c) na (d). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niongezee tu hapo; kama sisi tunafahamu Serikalini kwamba asilimia 30 ya pato la Taifa linatokana na wafanyabiashara wakati na wadogo lazima tuangalie kwamba tunawezaje kuweka mazingira mazuri. Mheshimiwa Rais amekaa na wafanyabiashara, uamuzi wa Mheshimiwa Rais kukaa na wafanyabiashara si uamuzi mdogo. Ameamua kukaa na wafanyabiashara kwa sababu anachotaka haya mambo na malalamiko anataka kwamba watu wakae tuanze upya, kazi zianze kufanyika upya na mabo yakae yawe sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabla sijagongewa kengele ninachoomba kusema, ninaomba kusema ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara, ninaomba na sisi wanasiasa kwa ujumla na hasa sisi Wabunge tusiwe madalali wa wafanyabiashara. Sisi kwenye Kamati yetu tulikuwa na Mheshimiwa Munde Tambwe, tumekaa kuna baadhi ya vitu tulikuwa tumekaa tukasema hivi hatuvikubali. Kuna mtu mmoja ambaye alikuwa ni mfanyabiashara anadiriki mpaka kiwango cha kuongea lugha mbaya na bahati yake ni kwamba sisi hatukuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliwahi kusema kwamba kwenye mambo ya msingi, mambo ya uchumi mambo ya kulitakia mema Taifa letu lazima sisi wana siasa tuanze kwanza, hata kama ukiongea uongee yale ambayo unaona kabisa kwamba haya ni mambo ya ukweli ili kuweza kulisaidia Taifa letu. Tusikae tu kwa sababu sisi tuna interest, una interest zako binafsi huko pembeni unataka watu wote wakukubalie waseme ndiyo, for what? Ni kitu ambacho hakiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho kabisa kabla sijagongewa kengele, shilingi bilioni kumi na tatu za kulipa fidia Liganga na Mchuchuma Mheshimiwa Waziri nilikuwa naomba hizi pesa ni nyingi sana. Kabla ya kulipa hizi pesa bajeti yako ikishapita nenda kajiridhidhishe uangalie pesa hizi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake kwa kazi nzuri wanazozifanya licha ya changamoto kubwa na nyingi zilizopo kwenye Wizara yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa heshima na taadhima Mheshimiwa Waziri apokee ushauri wangu kuhusu suala la kuwapa offer madaktari na timu yote ya madaktari hao kutoka Marekani ambao walifanya kazi kubwa kuwasaidia watoto wetu wa Kitanzania katika ajali iliyohusisha wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya Lucky Vincent. Mheshimiwa Waziri, madaktari hawa walikuwa wamekuja Tanzania kwenye programu tofauti lakini wakiwa nchini waliona nia ya kwenda kutembelea vivutio vyetu ambapo walikutana na ajali hiyo eneo la Karatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, timu hii ilifanya kazi kubwa ya kuwasitiri watoto wetu ambao walifariki lakini waliendelea pia kuwasaidia waliojeruhiwa kwa kuwapeleka nchini Marekani kwa ajili ya matibabu. Huu ni moyo wa kipekee, kwani ilibidi wakatishe safari yao kutokana na tukio hilo. Naiomba Wizara licha ya ukweli kwamba madaktari hawa wana uwezo, lakini sisi kama Watanzania tuna njia nyingi za kuwashukuru kutokana na kitendo hicho, na kwa kuwa walionesha nia ya kutaka kwenda kwenye vivutio vyetu naona itakuwa ni jambo jema kama tukitambua mchango wao kwa kuwapa offer hiyo ya kuja bure kwenye vivutio vyetu popote watakapotaka kutembelea. Kama ikikupendeza basi tuwape offer ya muda mrefu ili waweze kujipanga na kuamua siku watakazotaka wao wenyewe.

Mheshimiwa Waziri, hiyo itasaidia kuonesha shukrani yetu lakini pia itasaidia kuendelea kutangaza utalii wetu hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nafasi ya kipekee, naomba kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mkuu wa Majeshi na watendaji wote wa Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwapongeza sana sana wanajeshi wote walioshiriki katika operesheni ya Kibiti. Kazi hii waliyoifanya ilikuwa ni nzuri sana na ya kutukuka. Wanajeshi hawa wanastahili pongezi za dhati sana kwani walijitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujua wanajeshi hawa walishalipwa stahili zao zote? Je, kiwango kilicholipwa kinafanana na kile cha wenzao wa TISS pamoja na Polisi? Nashauri Jeshi kuangalia na kufanya tathmini ya malipo yote waliyolipwa pamoja na stahili zao kama zilikuwa zinalingana na wenzao wa taasisi nyingine nilizozitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza lakini hili naomba lifanyiwe kazi. Ahsante sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana kwa kunipatia nafasi hii walau na mimi niweze kutoa mawazo yangu kwenye mpango huu ambao umeletwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuipongeza Serikali kwa mpango huu mzuri. Naomba kumpa moyo sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake. Haya maneno mengine ambayo yanasemwa uyazoee tu kwa sababu leo wanasema, kesho wanasifia, ndivyo walivyo baadhi ya watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kupoteza muda nimpongeze sana kwa nafasi ya kipekee Mheshimiwa Waziri wetu Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu ni mtendaji mkuu, ni kiongozi wa shughuli za Serikali ndani ya Bunge. Anafanya kazi nzuri sana, anafanya kazi kubwa sana na mimi napenda sana style ambayo huwa inakuwa ya kimya kimya, tunakupongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Taifa leo tunajadili mpango lakini yapo mambo ambayo mbele huko tunaona mwanga mkubwa sana na wa kijani. Hata hivyo, mafanikio haya yatakamilika endapo na sisi wenyewe kama Taifa tutakaa katika mstari na kufanya yale mambo ambayo kweli tunajua kabisa yatatufikisha kule tunapotaka kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivyo? Mipango ambayo tumekuwa tunajiwekea kuanzia 2011 - 2016 na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2020-2025, tumekuwa tunajinasibu na tunasema kwamba tunataka tuwe Taifa la uchumi wa katika by 2020-2025. Hata hivyo, mimi nikiwa mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara ninajiuliza jambo moja, hivi kweli tupo tayari? Ninajiuliza hivi kweli Serikali ipo pamoja? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu sioni inter-connection kati ya Wizara na Wizara. Kuna tatizo kubwa sana kwamba tumejinasibu sasa hivi kwamba tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda lakini ukiangalia Wizara hii inafanya jambo pekee yake na hii inafanya jambo peke yake. Kwa utaratibu huu hatuwezi kufikia malengo na matokeo yake viongozi hawa wakubwa, Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Waziri Mkuu tutakuwa tunawapa kazi kubwa sana, watakuwa kama vile ni Mawaziri wa Wizira zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano moja, kuna Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), mimi mpaka nawaonea huruma wale watendaji wa TIC kwa sababu yapo mambo ambayo yanatakiwa kufanywa na Serikali. Jamani, tunajinasibu kwamba tuwe na uchumi wa viwanda lakini tunashughulikia yale matatizo ambayo tunaona kabisa kwamba yanatukwamisha huko ambako tunataka kwenda? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitolee to mfano, TIC iko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, kwanza naomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa heshima kubwa itolewe chini ya Wizara hii. Kwenye nchi za wenzetu ambazo zimeendelea kituo hiki huwa kinakuwa chini ya Ofisi ya Rais au Ofisi Waziri Mkuu. Zamani kituo hiki kilikuwa chini ya Ofisi ya Rais, baadaye kikatolewa kikapelekewa chini ya Ofisi ya Waziri lakini baadaye kimepelekwa chini ya Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale watu kazi yao ni kuratibu mamlaka zote za Serikali kwenye masuala yote yanayohusu uwekezaji. Hata hivyo, kama tunavyojua watendaji tulio nao Serikalini ni kweli wana mawazo yale ya uwekezaji? Zipo sheria kwa mfano Sheria za Uhamiaji mwekezaji akiwa ametoka nje ameingia hapa Tanzania ameleta mtaji wake mkubwa anakuja kuwekeza sheria inasema akiwa mwekezaji mkubwa kwa class A atapata kibali cha kuishi hapa kwa kipindi cha miaka 10. Akiwa kama ni mfanyakazi, labda ni mtaalam anapewea kibali cha miaka miwili, lakini kibali cha Uhamiaji kile cha ukaazi wa hapa, anatakiwa arudi kule kwao aje a-apply tena miaka miwili mingine baadaye tena arudi kwao aje apply mwaka mmoja. Hivi kweli mtu anakuja kuwekeza pesa zake nyingi, hii haipo sawasawa hata kidogo. Mimi nimekuja kuleta pesa zangu halafu ninyi mnaanza kuniambia eti kibali kikiisha inabidi uondoke, mbona ni vitu vidogo vidogo! Hawa watu ambao wapo kwenye Serikali kwa nini hawashughulikii vitu kama hivi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria nyingine ni Sheria ya Kazi. Wote tunajua kwamba kama wewe ni mwekezaji umekuja hapa Tanzania maana yake ni kwamba unataka kuleta wataalam. Hata kama mimi Lucy Mayenga nataka kufungua ofisi, nataka nitafute mtaalam toka nje, nikimtafuta yule mtu kuja kumleta hapa, kwanza lazima tukubaliane kwa mfanyabiashara au kwa mwekezaji yeyote suala la kumleta mtaalam kutoka nje si kwamba wanapenda sana wakati mwingine ni kutokana na mazingira. Ndiyo maana nimefurahi sana kwamba michango mingi ya Waheshimiwa Wabunge wanasema tuongeze uwekezaji na tuongeze usimamizi mkuu kwenye mafunzo ya ufundi. Hawa watu wakati mwingine wanaleta mtu si kwa maana pengine labda hapa anaweza kukosa mtu lakini sisi tunajali sana masuala ya vyeti na elimu za makaratasi, wenzetu wakati mwingine wanajali pia uzoefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unakuta Sheria ya Kazi mtu amekuja hapa kama mwekezaji lakini wakati huo huo, naomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha ujaribu kuliangalia hili na uzuri Mheshimiwa Prof. Ndalichako, Waziri ambaye namwamini sana, naomba ulifanyie kazi jambo hili, vibali vya walimu wa international schools ambao wanatoka nje naomba Serikali ianze kuangalia sasa hivi havipo katika utaratibu ambao unaeleweka. Sasa mwekezaji amekuja mnamwambia karibu lakini hajui ampeleke mtoto wake shule ipi? Wenzetu hawa wanajali sana familia, hicho tu peke yake kinaweza kikamfanya akasema siwezi kukaa hapa kwa sababu elimu ya watoto wangu haipo sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za Ardhi huko ndiyo kabisa! Mtu anakuja kama mwekezaji kutafuta eneo kwa ajili ya kuwekeza inamchukua takribani mwezi mzima wanazunguka tu kwa kuwa hatuna data base ya ardhi kwa ajili ya uwekazaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria nyingine ni Sheria za Kodi. Ni lazima kama Taifa tuwe predictable. Haiwezekani kila mwaka tukikaa hapa tunakuwa na Public Finance Act, leo tunabadilisha hili, kesho linakaa hivi. Mwekezaji na mfanyabiashara yoyote anataka kuwa na uhakika na kodi anayolipa kwamba leo nalipa kodi hii, kesho nalipa hii, kesho kutwa nalipa hii siyo kwamba leo analipa hii lakini hajui kesho atalipa nini, ni vitu vigumu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, naomba kama Taifa na sisi kama Wabunge tukubaliane jambo moja, kuwa Mzungu au mtu anayetoka nje aidha ni Balozi au ni Mzungu mtaalam wa jambo lolote umekuja hapa tuheshimiane, hii ni nchi huru. Naiomba sana Serikali, mtu yeyote ambaye atakuja hapa akienda kinyume na utaratibu wa Taifa letu aondolewe saa 24. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo ya kusema kwamba eti kwa sababu ni Mzungu, eti kwa sababu ni hivi, tunataka wale ambao watakuja wawe na malengo mema na sisi. Wawe na malengo mema kwamba mtu anakuja anasaidia, ni mdau kweli wa maendeleo. Siyo mtu anakuja anapiga blabla, mara anakwenda chini kwa chini anafanya mambo mengine, wengine wanajiingiza kwenye mambo ya siasa, tutakufukuza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la mwisho kabisa, nampongeza sana Mheshimiwa Rais wangu, ni Rais ambaye kwa nafasi ya kipekee na naomba kwenye hili baadhi ya Mawaziri tuweze kukaa na kutega masikio yetu vizuri kuhusu utendaji wa Mheshimiwa Rais wetu. Wizara jamani acheni mambo ya kupeleka matatizo ya ndani ya Wizara zenu kwa Mheshimiwa Rais yashughulikieni ninyi wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ahsante sana, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii nami niweze kutoa mchango wangu kwenye taarifa hii ya Kamati. Naomba kwa nafasi ya kipekee, kwanza kabisa nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya katika suala zima la kusimamia Sekta ya Madini hapa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kikao ambacho amekifanya tarehe 22 Januari, kwa uamuzi aliouchukua kuongea na wadau kusikiliza matatizo yao. Vile vile, tumeweza kuona kwamba Mheshimiwa Rais anaumia sana na suala zima la kutaka
wananchi wake tuwe na maisha mema, kiasi ambacho amekuwa akiingilia hata hizi sekta nyingine licha ya kwamba yeye ni Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi hizi ninazisema, lakini vile vile Mheshimiwa Rais wetu ni msikivu sana. Nilisimama hapa kwenye Bunge la mwezi Tisa, nikaomba kwamba Mheshimiwa Rais aweze kusaidia kuhamisha TIC kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais na baada ya wiki moja alifanya hivyo. Namshukuru sana na ninampongeza sana, kwa sababu kwa uamuzi huo sasa ina maana tutakuwa tunaanza kuzungumza lugha moja kwenye masuala mazima ya uchumi na hasa kwa kutegemea kituo chetu cha uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 31wa taarifa hii ya Kamati, inasema hivi, naomba kunukuu: “Hadi sasa mchango wa Sekta ya Madini ni asilimia 4.8.” Taarifa hii inasema kwamba, “Wizara ya Madini pamoja na Tume ya Madini inapaswa kuendelea na usimazi na udhibiti wa utoroshwaji wa madini yote nchini kwa kuimarisha ulinzi kwa maeneo yenye migodi mikubwa na ya kati.”

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe wazo langu na ushauri. Ninaomba Serikali, niseme wazi kwamba siyo Tume ya Madini wala siyo Wizara yenye uwezo wa kudhibiti utoroshwaji wa madini hapa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini nasema namna hiyo? Kwa sababu biashara ya madini kwanza kabisa inafanana sana na madawa ya kulevywa. Nasema hivyo kwa sababu ni biashara ambayo inahusisha pesa nyingi sana; ni biashara ambayo crime yake huwa ni very organized kiasi ambacho Tume ya Madini au Wizara peke yake haitakuwa na uwezo wa kufanya control.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu ni nini? Naomba Serikali iweze kuunda Mamlaka ya Udhibiti wa utoroshwaji wa madini hapa Tanzania, pamoja na usimamizi wa kodi. Kwa sababu lazima tujiulize, hawa watu kwa nini wanatorosha madini? Maana kutorosha madini ni suala lingine na kuweza kuwadhibiti ni suala lingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye biashara hii ya madini, kuna kodi nyingi sana. Hizi kodi ndizo zinazofanya watu hawa waweze kutorosha. Kuna VAT, Withholding Tax, kuna vitu vingi, kuna Service Levy, kuna vitu vingi sana kama inspection fees na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na haya, mtu anaona akipata madini, kuliko aende Serikalini kulipa kodi zote hizo, bora kutorosha. Kwa binadamu yeyote kwenye suala linalohusu pesa, tutalaumiana, tutafukuzana, tutafanyiana kila aina ya vitu, lakini inabidi nasi, hasa Serikali, tuweze kubadilika jinsi ya kuweza ku-deal na watu wanaofanya biashara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mbaya zaidi, yapo mambo ambayo tunafanya kama maamuzi lakini baadaye yanakuja kututokea puani. Suala la ku-declare dhahabu umeitoa wapi? Huu ni uamuzi ambao siyo wa busara. Naomba suala hili Serikali iweze kuangalia upya. Kwa sababu kama tunavyofahamu kule kwetu Shinyanga na maeneo mengine huko Usukumani, mtu amepata dhahabu yake, anakwenda Serikalini ili aweze kukadiriwa kodi. Akifika kule, anaanza kuhojiwa kwanza utueleze ulipoitoa hii dhahabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, huu utaratibu kwa kweli naomba Serikali iangalie upya, kwa sababu mtu huyu huyu akitoka hapo, akivuka border tu pale Sirari akapita Kenya, anaenda kuisajili kama dhahabu ambayo imetoka Kenya. Wenzetu wanamaliza hapa, wanakwenda kuuza nje kama vile dhahabu ambayo imetoka Kenya. Matokeo yake Tanzania kuna madini mengi sana, migodi mingi sana lakini ukiangalia takwimu za uuzaji wa dhahabu nje, zinasikitisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana nasisitiza sana uundwaji wa hii mamlaka. Ninafahamu kwamba mamlaka hii itafanya kazi kama ilivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevywa ili tuweze kupata mafanikio makubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, tuweze kuangalia mashine zetu (scanners) kwenye maeneo ya Airport, Bandarini na na kadhalika, zina uwezo kiasi gani? Watu wanatorosha madini. Hata juzi kuna mshiriki mmoja wa kile kikao cha Mheshimiwa Rais, aliweza kusema jinsi wanavyotorosha madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba ku-declare interest, mimi nimekuwa Mjumbe wa Williamson Diamond for nine years, kwa hiyo, najua kinachofanyika. Ukichukua dhahabu ukafunga na hizi karatasi za sigara, ukaweka katikati sponge ya nusu inchi au ya inchi moja, hakuna mashine ina-detect.

Mheshimiwa Naibu Spika, hawa watu wamekuwa wakifanya hivi. Vile vile, lazima tuweze kuangalia kwamba kama watu hawa wanaweza kuwa na mbinu kama hizi, ingawa wengine taarifa zinapelekwa wanakamatwa: Je, Serikali inachukua hatua gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie kuhusu Serikali kununua dhahabu. Naomba Serikali kabla haijafikia uamuzi wa kununua dhahabu, iweze kukaa chini na kupitia mfumo mzima, tangu mtu anavyoanza kuchimba dhahabu mpaka kufikia kwenye mauzo. Nasema hivyo kwa sababu wachimbaji wadogo, tujiulize, pesa wanatoa wapi? Watu hawa siyo mitaji yao, mitaji inatoka Uarabuni, India na kadhalika. Wanapokuja kupata fedha ndiyo wanaingiza kwenye biashara hii. Wakiingiza kwenye biashara hii hawawezi kuuza dhahabu Serikalini hata mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababu watu hawa sasa hivi pesa zinaingia, ingawa tuna Sheria ya Money Laundering, ndiyo maana nimesema kwamba Serikali lazima ikae ijipange sana. Hata hii Mamlaka ya Kudhibiti Utoroshaji wa Madini naomba sana ihusishe vyombo vya ulinzi na usalama, ihusishe wataalam kwa maana ya Maprofesa na kadhalika, vile vile ihusishe wale ambao ni wachimbaji local kabisa, ili muunganiko wao huu, wale ambao ni wako kabisa, waweze kutoa experience wa kile ambacho wanakifanya on the ground. Tusikae kutegemea tu kwamba ni wataalam peke yao watakaa chini, wao watakuwa wanafanya experience ya makaratasi wakati on the ground mambo ni tofauti.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuangalie pia airports zetu jinsi zilivyojengwa. Maofisi ya Maafisa katika airports zetu. Unaingia kwenye Ofisi ya Afisa wa Airport, una uwezo wa kutoka kwenye ndege ukapita kwenye Ofisi ya Afisa bila kupita kwenye scanner. Naomba Airport ya Mwanza iangaliwe na airport nyingine zote ziangaliwe. Hii ndiyo mianya ambayo inasababisha madini yetu yanatoroshwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala lingine Mheshimiwa Heche alikuwa analizungumzia hapa kwamba tunafaa kuongoza au hatufai, naomba kumwambia Mheshimiwa Heche, yeye mwenyewe anapumulia mashine, hali yake ni mbaya sana. Akae tu avumilie, milango tulishaifunga. Yeye mwenyewe alishakaa akasema anataka kurudi huku lakini mambo yamekuwa magumu. Asubiri ikifika mwakani, aende nyumbani kwake apumzike. Maana kuna watu wakikaa, kila siku Serikali haifanyi kazi, Serikali haifanyi hivi; Serikali inajitahidi, lakini ninyi wenyewe mkikaa, mna matatizo lukuki! Hayo matatizo yenu ambayo yanasababisha mpaka mnafikia hapo mlipo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii angalau nami niweze kuchangia kwenye Wizara hii, ingawa bahati mbaya dakika hizi tano ni chache sana, lakini sina budi kutumia muda huo huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilisimama hapa mara ya mwisho wakati nikizungumza kwenye Wizara hii ya Viwanda na Biashara nikatoa wazo kwamba Mheshimiwa Rais na Serikali kwa ujumla iweze kuihamisha TIC kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na kuihamishia aidha kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais. Ninaomba kwa heshima na taadhima nithibitishe kwamba, Mheshimiwa Rais ni msikivu, ninafahamu kwamba vyombo vyake vimesikia na wamepima wameona kwamba, wazo hilo lililkuwa ni zuri. Ninajua kwamba vyombo vyake vitakuwa vilishafanyia kazi kabla hata sijazungumza na ndiyo maana TIC imehamishwa. Ninampongeza sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo TIC imehamishwa, bado Wizara inatakiwa sasa ifanye haraka na kwa mkakati maalum kuweza kuleta Sheria ya TIC mpya hapa Bungeni. Sheria Namba 26 ya Mwaka 1997 imepitwa na wakati. Yaani miaka imekuwa ni mingi mno kiasi kwamba mabadiliko yanayoendelea sasa hivi duniani hayaendani na hii sheria. Hata hivyo, sheria hiyo ikiwepo itasaidia kurekebisha vitu vingi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna vitu vingi ambavyo vimezungumzwa na Wabunge kwenye Bunge hili kwamba kuna masuala ya tozo, masuala sijui ya taasisi mbalimbali ambazo zinashughulikia biashara pamoja na uwekezaji. Sheria hii endapo kama ikiletwa, itaweza kurekebisha mambo haya; mambo ya OSHA watu wanalalamika, mambo ya sijui NEMC na kadhalika, kwa hiyo, mambo mengi yataweza kurekebishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile uratibu wa masuala mazima ya uwekezaji angalau yataweza kufanywa na chombo kimoja, maana sasa hivi ni vile kila mtu mkubwa. Kila taasisi inajiona kwamba kubwa. Kila mtu, leo anakuja anasimama anasema hivi, mwingine kesho anakuja anasimama anasema hivi. Kwa hiyo, sheria hii ikiletwa, itaweza kusaidia ili mambo yakae sawasawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mara ya mwisho nilizungumzia kuhusu habari ya vibali vya kazi pamoja na ukaazi. Mheshimiwa Waziri, yapo masuala mengine hayatakiwi labda mpaka mtu mkae mtafute mwezi mzima muweze kuyafanyia kazi. Hili suala la vibali vya kazi halijakaa sawa sawa katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani sheria hiyo hiyo ya mwaka 1997 inasema kwamba, mwekezaji akija, kwenye sheria imeandikwa kwamba anaruhusiwa kupewa watu watano. Kwa hiyo, huku sheria inasema aruhusiwe kupewa watu watano, lakini akishafika wale watu watano hapewi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala tunaonekana hatuwezi kuaminika. Huu ni uwekezaji, lazima ifike wakati tuone kwamba sisi kama nchi ndiyo tuna shida na wawekezaji na siyo kwamba wawekezaji wana shida na sisi. Tukiwa na mtazamo wa kusema kwamba wawekezaji wana shida na sisi, hatuwezi kufika. Nami nilikuwa naomba Wizara ya Uwekezaji, Wizara ya Viwanda na Biashara inabidi mkimbie maana sasa hivi naona bado mnatembea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nizungumzie kuhusu suala zima la wafanyabiashara. Baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisimama hapa wanazungumzia kwa mfano, kuna hoja ambayo inasemwa na wafanyabiashara sitaki kusema ni wapi; kwamba, kuna mafuta yamekamatwa, yamewekwa huko, meli zimekaa miezi saba. Kama unaulizwa document, TRA kosa lake ni nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, tusije tukaja tukakaa mara nyingi tukawa tunaweka mzigo mkubwa sana kwa TRA. Hakuna mfanyabiashara na wala hakuna mkusanya kodi ambaye anapendwa, lazima na sisi tuweze kujiangalia tumekosea wapi? Kama unaambiwa lete kibali original, hamna mfanyabiashara ambaye unaleta mzigo unakosa kibali original, haipo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, naomba kumpongeza sana sana Mheshimiwa Rais wangu. Naomba kumwambia maneno yafuatayo: Miradi yoyote ile ambayo inaletwa katika nchi yetu kama haina maslahi au haina tija, naomba kusema kwamba waizuie huko huko wala hata isiendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu gani? Tuna imani kubwa, tunaomuunga mkono katika nchi hii na katika Bunge hili tuko wengi. Kwa hiyo, miradi kama inaonekana kwamba ina hitilafu, kwa msimamo aliouonesha Rais wetu; kwanza cha kwanza kabisa hakuna mtu mwenye information katika hii nchi kama Rais wetu. Rais ndio mtu wa kwanza mwenye information za uhakika kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa hiyo, akikaa akasema kwamba suala hili haliko sawa sawa, mjue kwamba haliko sawa sawa. Sasa tukikaa tena hapa mtu akasimama akasema unajua suala hili sijui limekaa hivi, mwisho tutakuja kuvunjiana heshima. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuweza kuchangia leo humu Bungeni.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, nianze kumshukuru Mungu kwa kunijalia leo kuongea hapa ikiwa ni kipindi changu cha nne. Pia niwashukuru walionileta hapa, wapiga kura wangu wa Mkoa wa Shinyanga nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwape pole Wabunge wote, nafahamu kwa mujibu wa Kanuni pole zilishatolewa lakini kuna kitu kinaniambia kwamba nirudie kuwapa pole Wabunge wote kwa msiba mkubwa uliotokea wa kiongozi wetu Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba kuchangia Wizara hii ya TAMISEMI. Kwanza kabisa, naomba kumpogeza Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu sina shaka naye, najua ni mfuatiliaji, ni mtu wa vitendo zaidi na nafahamu kwamba yale yote ambayo sisi kama Wabunge tuna kiu nayo ana uwezo nayo. Hongera sana Mheshimiwa Ummy. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini maendeleo yoyote yale kwenye Wizara hii ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa hayataweza kufikiwa ikiwa hakutakuwa na umoja na mshikamano kuanzia juu mpaka chini, kwenye ngazi za Mikoa maana Wizara hii inagusa kuanzia Mikoa, Wilaya mpaka kule chini kabisa kwenye Kijiji. Lipo jambo ambalo jana Mheshimiwa Rais amelisema, kwa nafsi yangu siwezi kuliacha likapita kimya kimya. Mheshimiwa Rais alisema kwamba humu ndani Bungeni mwenendo wetu lazima tuuangalie. Kauli ile unaweza kuiona kama ndogo fulani hivi lakini vipo vitu ambavyo vinatusababishia humu ndani kukosa umoja na mshikamano.

Mheshimiwa Spika, nafahamu kwamba wapo watu tena ni wengi, ambao mtu akipinga anapinga kutoka moyoni na mtu akiunga mkono bila kungalia vyama, kuna mtu anaweza akawa yupo chama kingine wala siyo CCM, lakini akisema jambo akikosoa au akipinga anapinga kutoka moyoni. Mimi naomba niwaelezee Waheshimiwa Wabunge kuhusu uzoefu wangu wa humu ndani, kidogo tu, miaka niliyokaa wala sio mingi kiasi hicho. Mimi ambacho nakiona lipo kundi la watu ambalo wao wanataka wamchomoe Mheshimiwa Samia kutoka kwenye utawala wa Magufuli kama vile hakuwepo. Kundi hili kazi yake wanakaa, wengine wanamsifia kwa nia njema kweli kama kumsifia lakini wengine wanamsifia kwa maana ya kudhoofisha legacy ya Magufuli. Jambo hilo hatuwezi kulikubali hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini lipo kundi lingine ambalo wao tunatofautiana yaani kila siku tangu Magufuli alivyokuwa yupo madarakani wao ni kumpinga Magufuli. Leo mtu yule yule anasimama anasema, Mheshimiwa Samia nakupongeza sana bora umekuja wewe na mtu yule hata alivyokuwa Magufuli alikuwa anapinga sana leo ukimpongeza Mheshimiwa Samia kuna ajenda za siri. Mimi naomba kusema mkakati wenu tunaujua na mfunge midomo yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais wetu Samia na hapa naomba pia niseme inatakiwa sisi tusimame kwa nguvu moja kwa haya mambo ambayo yanayotokea na tuseme hapana. Lazima tumuunge mkono Rais wetu kwa vitendo na siyo kumuunga mkono kwa kuzungumza humu ndani Bungeni, tumuunge mkono hata huko nje ambako tunatoka. Hiki kinachofanyika ni kumchonganisha Rais wetu Samia na umati wa watu kule nyuma. Mheshimiwa Rais Magufuli alikuwa na watu wake ambao walikuwa wanampenda na kumtegemea leo unaposimama unasema kwamba wewe ulikuwa unampinga Magufuli halafu unaamua makusudi kabisa kwa mkakati ambao mmekaa huko uchochoroni mmeupanga mnaanza kusema kwamba sisi tulikuwa tunampinga Magufuli tuanze kumsifia Samia sio jambo la sawasawa. Huu mkakati naomba niwaambie utafeli kwa sababu Mheshimiwa Samia hana kundi hata moja, Mheshimiwa Samia hajajiunga na mtu yeyote, Mheshimiwa Samia nafasi aliyonayo ni Mwenyezi Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu gani? Mambo kama haya yaliwahi kutokea mwaka 2016/2017 wapo watu ambao ndiyo hawahawa yaani kila siku ni hawa hawa, kwanza najiuliza hivi ninyi ni akina nani kwa sababu kila siku huwa ni hawa hawa wenye maneno, makelele. Mimi nilikuwa natamani siku moja nimwambie Rais hata Mheshimiwa Samia kwamba hawa watu wakipewa vyeo siku wakiondolewa mtuambie sababu.

Nasema hivi kwa sababu wakati mwingine mtu anafanya mambo ya ajabu lakini mkija kuangalia mambo yake huko mengine yanatia aibu na yalikuwa ni mabaya lakini ukisamama hapa sasa hili ni Bunge jipya Wabunge wengine wapya wanatuuliza sisi ambao kidogo wa zamani jamani Mheshimiwa Mbunge …

SPIKA: Mheshimwa Lucy sasa turudi kwenye bajeti. (Makofi/Vigelegele)

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ujumbe umefika na umekuwa delivered. Cha msingi ni kwamba naomba sisi tuache hayo mambo ya ajabu, tukae kwenye mstari tumuunge mkono Rais wetu kwa asilimia 100 na kwa vitendo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu TAMISEMI, kama nilivyoeleza hapo awali najua uwezo wa Mheshimiwa Waziri wetu. Ripoti ya CAG imeeleza bayana kwamba yapo mambo ambayo yamekuwa yakifanyika huko kwa Wakurugenzi bila kusema ni wa maeneo gani lakini kwa kweli hayaridhishi. Naomba Mheshimiwa Waziri ashuke kule chini aende akafanye kazi hii kwa vitendo. Kwa kuwa najua kwa uwezo wako utafanya kazi hii kwa vitendo, ile field aliyokuwa anaifanya alipokuwa Wizara ya Afya naomba aende pia field kwenye Wizara hii kwa sababu yapo maeneo ambayo watu wanalalamika sana, matatizo ni mengi, watu wanajichukulia sheria mkononi. Utawala huu kwenye Serikali za Mitaa kuna baadhi ya maeneo huko vijijini kwenye kata na kadhalika na hasa kwenye Mabaraza ya Ardhi, naomba Wizara hii ya TAMISEMI iweze kuwa na mkakati maalumu yale mambo ambayo yanazungumzwa kwenye masuala ya ardhi na kadhalika ambayo yanahusu Wizara hii yaweze kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile kwa kuwa Waziri ametoka Wizara ya Afya najua Wizara hii ya TAMISEMI inahusika pia mambo ya afya, naomba afuatilie kuhusu matumizi ya pesa za Serikali zinazoshushwa kule chini. Pesa nyingi sana zinashushwa kule chini lakini tija inaonekana kwa kiwango fulani cha kawaida lakini kwa kiwango kikubwa upigaji unaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nianze kwa kushukuru kwa kunipatia nafasi hii, ninajisikia furaha na fahari kubwa leo kwa mara ya kwanza katika miaka yangu yote ambayo nimekaa Bungeni ninasimama hapa kuchangia Wizara hii ikiwa chini ya Amiri Jeshi Mkuu mwanamke. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba Watanzania wote kwa ujumla wetu tumpatie zawadi kubwa moja tu Mheshimiwa Amiri Jeshi MKuu, ni tulitaje jina lake kwa wema popote tulipo ili aweze kupata moyo wa kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze sana Jeshi letu, Jeshi hili limetuheshimisha watanzania kwa muda mrefu sana jeshi hili limekuwa likifanya kazi nyingi sana, licha ya kazi ambazo ziko kwenye Katiba yetu kisheria, lakini limekuwa likifanya kazi nyingi sana kwenye jamii yetu kwa maana hiyo na limekuwa likituheshimisha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sio tu kwenye nchi yetu, Jeshi hili limekuwa likifanya kazi kubwa sana na zipo kihistoria, zipo nchi ambazo haziwezi kuelezea mafanikio waliyonayo ya uhuru wao bila kutaja mchango wa Jeshi la Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya maeneo mbalimbali katika nchi hii au nje ya Tanzania yamekuwa yana matatizo kadhaa, lakini Jeshi hili limekuwa likienda, matatizo yao yanakwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kwa kifupi kuhusu suala zima la mchango wa jeshi letu katika operation za amani duniani, jeshi hili limekuwa likishiriki katika operation za amani katika nchi mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa kama ambavyo tunafahamu wapo Lebanon, wapo Darfur, wapo Congo na kadhalika. Kazi wanayoifanya kule ni kubwa sana na kwa kweli mimi ningeomba jeshi hili kazi hii iendelee kwa sababu inawapa exposure na ni faida kwao pia kiuchumi kutokana na posho wanazozipata. Lakini pia vilevile jeshi hili wanajeshi hawa wanapokwenda kule wanakuwa pia na nafasi ya kujipima uwezo wao pamoja na majeshi mengine ya nchi mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwasababu kazi hii inafanywa chini ya Umoja wa Mataifa, kuendelea kwa jeshi letu kuaminika kwa wanajeshi kupelekwa huko kwa kweli ni sifa kubwa sana na wanastahili pongezi kubwa sana. Lakini kwenye hili mimi nilikuwa naomba, ninaomba Mkuu wa Majeshi Mabeyo, kaka yangu kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri sana. Mimi nilikuwa naomba kwenye operation hizi idadi ya wanawake iongezwe, wanawake wanaweza, leo tumeona akinamama…. (Makofi)

MHE. RIDHIWANI M. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, pale wamechafuka mabegani, akina mama wanaweza. Kwa hiyo mimi nilikuwa naomba kwamba kwenye…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lucy Mayenga, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete.

T A A R I F A

MHE. RIDHIWANI M. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naomba nimpe taarifa tu dada yangu tunapo mu-address Mkuu wa Majeshi hatumwiti kwa jina lake, yule anaitwa General Mabeyo. Ahsante sana. (Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Haya sasa kwa sababu Mheshimiwa Lucy Mayenga anachangia Kiswahili basi ni Jenerali. (Makofi)

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaipokea taarifa hiyo kwa mikono miwili kabisa Jenerali Mabeyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini baada ya kazi hizi ambazo zimekuwa zikifanywa nje ya Tanzania pamoja na hapa kwetu Tanzania, sina budi kutoa pongezi kwa jeshi letu kwa kazi kubwa sana ambayo wameifanya Kibiti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niwapongeze kwa sababu kazi ile kwenye masuala ya kivita, mimi sijawahi kuwa mwanajeshi wala sijawahi kuwa askari, lakini ninafahamu kwamba conventional war ni tofauti sana na gorilla war; aina ya mapigano na hali iliyokuwepo kule Kibiti, ilikuwa inafanana sana na gorilla war; humjui adui yako lakini kazi iliyofanyika ni kazi kubwa sana na ninaomba kwenye hili pia ili na sisi Tanzania tuendelee kuwa na amani kwa sababu inavyoelezwa ni kwamba wale magaidi wametoka sasa kwa upande wa Tanzania wamehamia kwa majirani zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Tanzania na Msumbiji au na hizi nchi zingine ambazo tuko nazo majirani Tanzania na Msumbiji hasa ambako ndio inasemekana kwamba wamekwenda kule tuko karibu sana. Kwa hiyo, ina maana kwamba na sisi tusipojiimarisha wasije tena wakaona kama tumelala lala wakarudi. Nilikuwa naomba tuongeze msimamo, tuongeze kazi, tuongeze nguvu kama ambavyo ilivyo. Na kwenye hili, ninaomba niendelee kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuteua watu ambao wakiwepo kwenye maeneo kama haya strategically wataweza kutusaidia. Kwa sababu hawa ni watu ambao wana mafunzo ya hali ya juu wanajua wanachokwenda kukifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe pongezi zangu kwa kulingana na seniority ya wanajeshi naomba niwapongeze sana Jeshi la Nchi Kavu, naomba niwapongeze sana Jeshi la Anga, naomba nipongeze sana Jeshi la Wanamaji pamoja na JKT, kwa kazi hii kubwa ambayo walikuwa wameifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini licha ya kuelezea kwamba wanajeshi hawa wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana, mimi niwaombe with due respect kwamba kuna kitu ambacho kilikuwa kinatolewa kwa wanajeshi wetu kama motisha, kwa maana ya yale maduka ambayo yalikuwa yana duty free ya Jeshi. Lakini pia vilevile, mess ambazo zilikuwa zinaendeshwa katika utaratibu wa duty free kwa maana ya vinywaji na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hawa wanajeshi wanapokuwa wanakaa pamoja kwenye maeneo kama haya ya mess na kadhalika wanakuwa na cohesion lakini pia hii ni organizational culture, dunia nzima hivi vitu vipo. Sasa mimi nilikuwa naomba tukikaa tukasema kwamba labda pengine kuna either kubana matumizi au kwa njia moja au nyingine ile hali ambayo ilisababisha tukaondoa hivi vitu, mimi nilikuwa naomba tufanye tathmini kama ilikuwa kuna dosari dosari, ubadhirifu na kadhalika kwenye vitu kama hivi tujaribu kuangalia tena upya ili kama ikiwezekana tuweze kuwarudishia kwasababu hivi ndio vitu ambavyo vinawapa motisha wanajeshi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ninafahamu kwamba jeshi letu limekuwa likitoa huduma mbalimbali kwa wananchi wetu, hasa katika maeneo ambayo yamekuwa yakikabiliwa na majanga lakini pia vile vile yamekuwa yakikabiliwa na matatizo mbalimbali wakati wa dharura.

Nilikuwa naomba kutoa ombi Mheshimiwa Waziri wetu wa Ulinzi Mheshimiwa Kwandikwa ambaye anafanya kazi nzuri sana, nilikuwa ninaomba Mheshimiwa Waziri wetu na ninafahamu kwamba ni msikivu uweze kutusaidia katika Mkoa wetu wa Shinyanga yapo maeneo katika Wilaya mbalimbali Wilaya ya Kishapu, Wilaya ya Shinyanga Mjini, Wilaya ya Kahama, Majimbo yote pamoja na kwako Ushetu, kumekuwa kuna matatizo mengi sana sana sana, pia Wilaya ya Shinyanga Mjini na kadhalika kumekuwa kuna matatizo ya uharibifu mkubwa wa miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu kwamba masuala ya miundombinu yako kwenye Wizara ya miundombinu, lakini tunajua pia kwamba mchakato wa ujenzi wa madaraja kwenye maeneo mbalimbali huwa sio kitu cha mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nakuomba sana Mheshimiwa Waziri uweze kutusaidia uwepo wa madaraja kwa mfano kwa kwetu Shinyanga Mjini kuna Upongoji ambayo linaunganisha Ndala na Masekelo kuja Shinyanga Mjini, kuna Ibinza Mata ambayo inakwenda Kitangiri, kuna Uzogole kwenda Bugwandege, kuna Old Shinyanga kwenda Mwamalili na kadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wetu wamekuwa wakipata shida, nilikuwa naomba haya madaraja ya muda ambayo mnayo basi muweze kukaa chini kuweza kuangalia ni jinsi gani mnaweza kuja kutusaidia. Ndugu zangu kwenye maeneo haya ambayo nimeelezea hali huwa ni mbaya, wananchi wanasombwa na maji, magari yanasombwa na maji, hali huwa inakuwa mbaya sana. Kwa hiyo, nilikuwa nakuomba sana Mheshimiwa Waziri muweze kuliangalia hilo na ninafahamu kabisa kwamba hili ukilikalia vizuri litawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la mwisho nilikuwa nataka kuzungumzia kuhusu suala zima la teknolojia. Wote tunafahamu kwamba, dunia inabadilika naomba tu kuelezea kwa kifupi, kuna kitu kinaitwa high tech. warfare naomba kuuliza, are we ready?

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo ahsanteni sana kwa kunisikiliza. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuweza kuchangia Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kabisa kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu Mama yetu mama Samia Suluhu kwa kweli kwa jinsi alivyoweza kubadilisha taswira ya biashara katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokaa, watu wanapokaa kila kona kuzungumzia masuala ya kipato au kuweza kulalamikia kipato, hakuna njia yoyote inayoweza kusaidia wananchi hawa wakaja kuridhika zaidi ya biashara. Ninasema hivyo kwa sababu biashara zote duniani utakuta inagusa kilimo, biashara zote duniani utakuta inagusa mambo ya Liganga, Mchuchuma, biashara zote duniani kuna sehemu ambapo mwananchi atafaidika kwa njia moja au nyingine.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ambacho wasiwasi wangu, ambacho nakiona ni kwamba mitazamo ambayo wanakuwa nayo viongozi wetu wakubwa na hasa niseme Marais wetu na hawa viongozi wengine wakubwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wakikaa kuongea na wafanyabiashara, wakikaa kuongea kisiasa, ni vitu havifanani kabisa na mawazo ambayo yapo huku chini kwa watendaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninachokiona ni tatizo la sisi Watanzania hasa huku kwenye watendaji tubadilishe mindset na siyo kitu kingine. Tumekaa kwa muda mrefu sana tunazungumzia changamoto zilizopo kwenye biashara, baada ya hizi changamoto wakasema tuje na kitu kinaitwa blueprint, lakini blueprint hii ni karatasi, blueprint hii ni kitu ambacho kimeandikwa, kinataka mtu aje sasa aseme kwamba hiki tutakitekeleza kwa aina gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine hata kwenye kuchukua hizi hatua tuwe basi tunachukua hizi hatua haraka haraka, niwapeni mfano, kwa mfano, sheria zetu sisi hapa Tanzania kwa muda mrefu hazifungamani, yaani sheria za kodi na sheria za kibiashara zipo tofauti sana. Mtu akija hapa kwa mfano mtu akitoka popote una mtaji wako hata wa dola laki moja, dola laki mbili, ukisema nataka kwenda kufanya biashara fulani, yaani mchakato jinsi utakavyokuwa na jinsi utakavyosumbuliwa kwenye hicho ambacho unakifanya mpaka unakata tamaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini yote haya viongozi na watendaji Serikalini huko wanayajua kwa nini hawachukui hatua? Ndiyo maana ninasema kwamba viongozi wanaweza wakawa na mawazo mazuri sana, lakini huku chini lazima tubadilike.

Mheshimiwa mwenyekiti, nitoe tu mfano wa mambo kama mawili, matatu hapa Tanzania kuna viwanda viwili tu vya mabati, viwanda hivi ndivyo ambavyo vinafanya kazi ya kuzalisha mabati hapa Tanzania, lakini wafanyabiashara ambao wana mawazo au wanamitaji ya kufanya biashara hii wapo wengi sana. Sasa kinachofanyika ni kwamba kunakuwa na kama kautaratibu kaku-monopoly biashara, mtu anakuja anakaa anakwenda kuongea na watu anaowajua mwenyewe huko akienda kuongea nao ninyi ambao mnataka kufanya hiyo biashara kila mkijitahidi kufanya mnashindwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ndiyo maana nimesema tubadilishe mindset, sasa matokeo yake wafanyabiashara hivi sasa wameamua badala ya kuzalisha bidhaa hapa Tanzania wanaamua kwenda Kenya na Uganda kwa sababu kule walipi kitu, wanakuja wanaingiza hapa Tanzania ndiyo wanafanya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda hivi tunavyokaa kupiga makelele viwanda vitawezaje kuanzishwa kwa utaratibu huu. Kodi hizi kwa nini haziwi na mwingiliano yaani kwamba tukisema kwamba tunamfutia kodi hii, import duty, tukisema tunafuta import duty tunaacha VAT tufanye haya mambo kwa sababu ya kuweza kusaidia watu waanzishe viwanda na mambo mengine yaendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, mtu leo hii ukisema kwamba mimi nataka nifanye biashara, mfano labda kama dawa za minyoo, dawa za mifugo, nataka niingize hapa Tanzania, ukiwa na kiwanda hapa Tanzania ile dawa ni ghali kuliko ambayo inatoka nje kwa sababu ya changamoto ya kodi, sasa mtu anafikiria mimi namtaji wangu hakuna mfanyabiashara ambaye hataki faida. Mimi ninamtaji wangu nasema nataka nifanye biashara ya aina fulani halafu nikipiga mahesabu naona kwamba kuanzisha kiwanda hapa Tanzania, najiona kwamba kiwanda kile sawa kuna faida kitaingiza, kitaajiri watu na kadhalika, lakini faida yangu itakuwa ndogo tofauti na ile faida ambayo utaipata kwa kuagiza kutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana changamoto licha ya kwamba sijui kuna mazingira biashara, jamani wawekezaji mje mfungue viwanda, siyo rahisi mtu kuja kuanzisha kiwanda hapa Tanzania kwa mazingira haya yaliyopo ya hizi sheria, kanuni, taratibu na haya masuala ya kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile sheria hizi hizi leo mimi nimekaa nataka nianzishe kwa mfano labda kiwanda, mimi naomba niwaulize Wizara hii ya Viwanda na Biashara hivi hivi viwanda tu vilivyopo wanavitembelea kwenda kuangalia kinachozalishwa? Kwa sababu huku chini kwa wananachi mwananchi leo hii, Mheshimiwa Subira amesema pale kwamba kuna viwanda vingi sana kwenye Mkoa wa Pwani, kuna viwanda vya tiles na kadhalika. Lakini zile bidhaa ambazo zinazalishwa kwenye hivi viwanda wakati hawa wawekezaji wanakuja, walikuwa wanaamini kwamba watumiaji wa bidhaa hizi mtu analenga soko la lile eneo ambalo anaanzisha ile biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kinachofanyika kwenye Wizara hii ya Viwanda na Biashara hawaendi kukagua hizo bidhaa, wala kwenda kuangalia nini kinaendelea kwenye uzalishaji, wala kwenda kuthibitisha kwamba hiki kinachozalishwa kina ubora, hivi mnafanya nini ofisini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachotokea sasa watu wanakuja wanaanzisha biashara, wakianzisha biashara, mtu anaanzisha biashara let’s say kiwanda cha tiles, wanunuzi wanakosekana kwa sababu mnunuzi anaangalia quality, akishaangalia quality anasema hivi hapa nilipo nikinunua box moja la bidhaa labda let’s say ya tiles za Tanzania na tiles za China nikiongeza shilingi 10,000 tu, napata hii ya China ambayo fundi anamthibitishia kwamba bora ununue hii itadumu zaidi kuliko hii ambayo inatengenezwa Tanzania. What is this? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Wizara ya Viwanda na Biashara haiendi kuangalia ubora wa bidhaa ambazo zinazalishwa? Hii ni hatari kubwa sana kwa sababu mwisho wa siku hivi viwanda vita-collapse, watu watakaa wanasema karibuni tutawahamasisha kwa njia nyingi sana, Mheshimiwa Mama Samia ameweka mazingira mazuri sana. Lakini kama sisi wenyewe hatutakuwa serious kwenda kuangalia mambo ambayo yanafanyika huko, tusikae mwishowe Mbunge mmoja hapa ameelezea, hapa Tanzania tatizo letu ni kama vile kila mtu yaani kwamba elimu ni huyu, wa elimu ndio kinamuhusu peke yake, huyu mwingine wa maji kinamuhusu peke yake, kwenye viwanda huku mambo ya fedha, mambo ya kodi ni mwingine yaani hatushirikiani, hakuna co- ordination. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo tukiendelea kuyafanya namna hii tutakuwa tunaongea, viongozi wetu watakuwa wanahubiri haya mambo sana, wananchi wetu watakuwa wanalalamika kwamba pesa hatuna mifukoni, wakati sisi ambao tuko kwenye nafasi hizi za kufanya utendaji huu wa kuthibitisha na ni vitu vya kukaa tu na watu tukawasikiliza na kuthibitisha. Mwisho wake tumekaa hapa tukazungumza sheria ya TIC, na namshukuru sana Mheshimiwa Rais pia ali-mention hili, mtu anakuja na mtaji wake anasema kwamba, mimi nimekuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana tunamkaribisha mwekezaji, tunamuambia kwamba ukija Tanzania utaingiza wafanyakazi moja, mbili, tatu na kadhalika, lakini huku unampa unamnyang’anya kwa mlango wa nyuma. Sheria ya TIC na yenyewe pia kwanza ni ya muda mrefu sana mwaka 1972 inatakiwa kubadilishwa, lakini mpaka leo ni mambo yale ya Serikali mambo yanakwenda hivi na nini tunatumia muda mrefu sana. Mtu anakuja na mtaji wake, mimi nina mtaji wangu wa dola 500,000 au dola 1,000,000 nimekuja hapa Tanzania baada ya kufika hapa nakaa naanza kuwekeza kwenye masuala labda pengine kwenye biashara fulani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema kwamba kwa mimi kwa pesa yangu namuamini dada yangu Esther huyu akinisimamia hapa, yaani hatakuwa na mambo ya ajabu ajabu, namuamini aidha ndugu yangu au ni mtendaji wangu. Halafu sheria inakuambia kwamba umeshafika umeshawekeza mtaji wako, lakini inabidi kwa kweli hapa kwasababu kuna mtanzania mwingine ana elimu kama hiyo kwa nini huyu asifanye. Mwisho, vitu vingine mtu anaangalia kwamba, yeye na huyu mtu wana historia gani, wana ukaribu gani, wako pamoja kwa kiasi gani, uaminifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwentekiti, mwisho, lakini naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kutoa na mimi mchango wangu.

Meshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu na kumpongeza kwa kazi nzuri ambazo anaendelea nazo, na kwa kweli kimsingi kwenye hili nimpongeze sana kwa hatua ambao Mheshimiwa Rais ameichukua ya kuteua wakuu wa Wilaya kutoka kwenye makundi mbali mbali, hongera sana. (Makofi)

Meshimiwa Naibu Spika, hizi siasa wakati mwengine huwa zinatufanya kama vile tunakuwa na hamaki hamaki halafu baadaye tunarudi kwenye mstari. Nilikuwa naomba tu kumwambia ndugu yangu Mheshimiwa Halima Mdee, kwamba kati ya mambo licha ya kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ilikuwa anaelezea kwamba si mambo yote yalikuwa perfect kwamba mambo mengine yalikuwa na dosari, mimi nakubaliana nae. Lakini nataka nimwambie kubwa zaidi ambalo hatakiwi kulisahau, kwamba perfect kuliko yote ni wao kuendelea kuwepo hapa Bungeni. (Makofi)

Meshimiwa Naibu Spika, ninaomba kumpongeza Waziri huyu wa Fedha, kaka yangu Mwigulu, Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa wizara hii, kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana. Bajeti hii ni bajeti ambayo kwa kweli wananchi wengi wanaipokea positive, ambacho wanakitaka na tatizo kubwa la wananchi; Mheshimiwa Waziri wa Fedha alisema kwamba Watanzania tufunge mikanda. Mimi nilikuwa naomba kumwambia Mheshimiwa Waziri, kwamba Watanzania hawana tatizo la kufunga mikanda, matatizo yao yapo kwenye maeneo mawilili tu. Ni kwamba wananchi wafunge mikanda lakini kinachopatikana kitumike kule ambako kunatakiwa kutumika. (Makofi)

Meshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwengine wa pili, ni kwamba wananchi wanasema wapo tayari kufunga mikanda lakini kusiendelee kuwepo na mianya ya upotevu wa pesa katika maeneo mbali mbali. Kwa hiyo hayo yakienda sawa sawa kwa kweli Watanzania hawana wasi wasi na wapo tayari kufunga mikanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo mimi ningependa kushauri hapo, zipo njia ambazo Serikali imesema inataka kuongeza matumizi ikiwemo utaratibu mzima wa kupata fedha kwa njia ya kodi, kwenye simu, kwenye majengo na kadhalika. Sasa mimi naomba kuuliza, hivi tangu siku ile bajeti imesomwa hapa ni nini kinaendelea huko chini kwa watendaji wetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu tusipoangalia, Mungu atajaalia, najua kesho bajeti hii itapita. Tusipoangalia tunaweza kujikuta hapa tumekaa tumepanga vizuri lakini baadaye kutakuwa na kero kubwa sana kule chini kwa wananchi. Nilikuwa naomba Wizara zote za Serikali katika maeneo yote ambayo Wizara zote zitaguswa, na hasa pia kwa wananchi wale ambao watakuwa ni wamiliki wa nyumba (wenye nyumba), Serikali iweze kuwa na utaratibu wa haraka na utaratibu mzito sana na wenye kutilia mkazo ili kwamba mambo kule yaweze kwenda sawa sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninasema hivyo kwa sababu, ninajua watendaji wetu walivyo. Mpaka sasa hivi kule chini baadhi ya watendaji kwenye baadhi ya maeneo kumeanza ile kama kuamka amka wameanza kukimbizana kimbizana, hatuna data base ya vitu vingi. Sasa hivi hata ukiuliza tuna nyumba ngapi kwenye maeneo fulani watu bado hawana. Sasa vitu kama hivyo kama huna data ya vitu ufuatiliaji wake na utekelezaji wake utakuwa ni ule wa kukamatana, kushikana na kadhalika, Itasababisha chaos nyingi sana. Ndiyo mana nasema kwamba wenye nyumba, na ndiyo mana nasema Wizara nyengine zote tufanye kazi kwa pamoja kuhakikisha mambo haya mengine hayawezi kutokea.

Meshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo nataka niliseme, kwenye kurasa wa 117 wa hotuba unasema, kwamba nchi yetu baada ya kuingia kwenye nchi ya uchumi wa kati wa chini, itaifanya nchi yetu kutakiwa kujiendesha kiuchumi bila ya kutegemea kwa kiwango kikubwa misaada na mikopo yenye masharti nafuu, ambayo hupewa nchi zenye kipato cha chini.

Meshimiwa Naibu Spika, hili nilikuwa naomba niseme, kwamba humu ndani tangu watu wameanza kuchangia hakuna mbunge ambaye hajasimama au ambaye hawezi kusema kwamba kwake kuna matatizo ya maji. Hata kama hajasema maji, kwenye masuala ya pembejeo, na kama hatasema embejeo atazungumzia masuala ya barabara na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu inahitaji pesa, sasa tunapataje pesa hizo? Mimi nilikuwa naomba tuwe na njia mbili. Mheshimiwa Rais wetu ameanza vizuri sana, kwamba tusijifungie, ameanza kufungua; na kwe kweli niwapeni Habari njema, hata sasa hivi baadhi ya wafanyabiashara Kariakoo wanasema tunamshukuru Rais wetu, mambo yamebadilika. (Makofi)

Meshimiwa Naibu Spika, sasa kwa kusema hivyo, kama nchi yetu inatakiwa pesa, ziko pesa ambazo zitapatikana, kwa maana ya Serikali kutafuta pesa kwa kutumia vyanzo mbalimbali, lakini ziko pesa nyengine ambazo zitapatikana kwa hizi nafasi ambazo Serikali imeachia ili watu waweze kufanya shughuli zao kama kawaida, kwa kuwawezesha wananchi. Sasa mimi nilikuwa naomba kuishauri Serikali. Yapo mashirika ya wenzetu hapa duniani ambayo yanatoa mikopo kwa riba nafuu.

Nilikuwa naomba Serikali yetu, najua sasa kwamba sasa hivi imejifungua, kuna mashirika ya kiarabu bila ya kujali masuala ya itikadi za dini, twende tukajaribu kuangalia huko kwa wenzetu wana mashirika ambayo yanatoa misaada kwa riba nafuu sana sana. Kwa sababu tunachokitaka, hata kama watu watasema kwa sababu nyengine zozote, tunachokitaka hatuangalii mambo mengine sisi tunaangalia ni jinsi gani tutaweza kuwasaidia wananchi wetu.

Meshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuwawezesha wananchi kiuchumi. Mimi nilikuwa naomba Watanzania na watu wengine ndugu zangu tusiwachukie wanfanya biashara, tusiwachukie wafanyabiashara kwa sababu mfanya biashara au mtu mmoja akipata ile chain ikishuka mpaka chini watu wengi wananufaika na mfanyabiashara huyo na kwa hiyo uchumi wa watu utakuwa mzuri kuanzia chini mpaka juu.

Meshimiwa Naibu Spika, ninasema hivyo kwa sababu ninaomba sana Serikali tuweze kubadilisha utaratibu wetu wa jinsi ya kufanya kazi, tuwawezeshe Watanzania. Hivi kuna ubaya gani kwa Mtanzania mtu ametoka huko nje amekuja hapa kuwekeza, wakati wa tender evaluation, tukasema kwamba tunataka walau mtu akitoka nje awe walau na Mtanzania. Kwasababu kwa kufanya vile na tukiwapa masharti hayo yataweza kuwasaidia na Watanzania wenzetu. Kuna wakandarasi, kuna watu wanauwezo mkubwa sana wa kufanya hizo kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sasa hivi hebu niulize, Stiegler’s Gorge Mtanzania anafanya kazi pale? Najuwa watu watasema wapo lakini anafanya kazi gani? Huku kwenye daraja la Kigongo Busisi jiulizeni Mtanzania anafanya kazi gani? Tukiangalia kwenye maeneo mengine, hata hilo daraja la Tanzanite, pale Salender Bridge, tuangalie Watanzania wanafanya shughuli gani? (Makofi)

Meshimiwa Naibu Spika, tukiwawezesha wananchi kiuchumi, itasaidia Watanzania hao wakiingia huko kupata si tu fedha pia na ujuzi. Siku nyengine Serikali hata ikisema inataka kufanya mradi mkubwa watu wa kufanya kazi hizo watakuwa wameshaingia, wamepata uzoefu na wao wanashiki kuendeleza shughuli mbali mbali za uchumi wa nchi yetu.

Meshimiwa Naibu Spika, tukiendeleza kusema wawekezaji wanakuja mtu anakuja na mitambo yake na ucjuzi wake anafanya, Mtanzania kazi yake iwe kupeleka cement na kupeleka kokoto, hatuwezi kuwawezesha Watanzania kiuchimi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee suala linguine, kwa sababu ya muda, suala la ranch za taifa. Ninaomba kuishauri Serikali, ninafahamu kwamba kuna baadhi ya ranch za taifa, bado hatufanyi vizuri. Lakini na ninaomba niseme hivi, hata hizi dhahabu na madini mengine yote haya; kuna wakati Mwalimu Nyerere alisema tuache kwanza mpaka pale tutakapokuwa tayari. Si kila ardhi kwenye hii nchi ni lazima itumike kwa ajili ya matumizi mengine yeyote. Mimi nilikuwa naomba hata, kama hizi ranch hazifanyi vizuri lakini tuwe makini sana sana, hatuwezi kujua zitatusaidia lini na kwenye jambo gani. (Makofi)

Meshimiwa Naibu Spika, lingine nizungumzie suala zima la biashara. Kama ambavyo nimesema kwamba wananchi wawezeshwe kiuchumi; Wizara ya Viwanda na Biashara, unajua wakati mwengine kuna mambo yanakuwa yanafanyika watu wengine wanakaa wanapanga mambo makubwa halafu huku nje wapo ambao wanakuwa kama hawapo, yaani kama tunachokiongea wao hakiwahusu. Ninasema hivyo kwasababu, kama tumekaa tumesema kwamba tukae tujiandae kiuchumi tuwe na bajeti tutafute pesa, tupate pesa kwenye kodi na kadhalika.

Meshimiwa Naibu Spika, ninafahamu kaka yangu Waziri wa Viwanda na Bisahara unafanya kazi nzuri sana pamoja na Naibu wake. Wizara ya Kilimo kaka yangu Waziri wa kilimo pamoja na kaka yangu Bashe wanafanya kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mashirika pale Wizara ya Viwanda, kama CAMARTEC, wapo pale, hivi mimi naomba kuuliza wanafanya nini? CAMARTEC kimsingi ukiangalia kwenye muundo wao, mimi nimeusoma, wanatakiwa waje na ubunifu kusaidia maendeleo katika sekta mbali mbali za kilimo na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kule vijijini wananchi mpaka leo wanatumia majembe ya mkono, na wao wapo, majembe ya mkono yapo, hata kuwasikia huwasikii. kuna TANTRADE ambao kimsingi wanatakiwa wawawezeshe wafanyabiashara wa ndani na nje, lakini leo hii TANTRADE Mama Samia au Waziri aende pale Kariakoo aende akaangali jinsi gani biashara zinafanyika, kwenda tu kuangalia hawaendi, wanafanya nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna TIRDO, kuna SIDO. Walau SIDO wanajitahidi, wanafanya kazi mambo yanaonekana, kuna TEMDO, lakini kuna hizi taasisi nyengine ambazo ukiwauliza mnafanya nini hawajui wanachokifanya na wapo wanapata mishahara kwa pesa za Serikali. Nilikuwa naomba Wizara hii ya Viwanda na Biashara, waweze kuamka, hivi vishirika shirika na viataasisi taasisi hivi, Serikali iweze kuviangalia waliundwa kwa sababu ya nini, ili tukijua waliundwa kwasababu ya nini tutajua kama wanafanya kazi na wanastahili kuwepo au wanakula kodi za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingine ambayo naomba sana, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara aweze kuangalia ni BRELA. Waziri wa Viwanda na Biashara, katika kitu ambacho kitamfanya aonekane kwamba amefanya kazi kwenye Wizara hii au hajafanya kazi ni BRELA, naomba sana afungue macho aende akaangalie BRELA nje na ndani. Najua kama yupo atakuwa ananisikia au hata kama hayupo najua akipata hii habari atajua kwamba imekaakaaje.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, ni kwenye Sekta nzima ya Maji. Pesa zote zinazokwenda kwenye Sekta ya Maji zaidi ya nusu hazifanyi kinachotakiwa.

Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Maji kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kufumua ma-engineer wa maji kwenye Wizara ya Maji kwa sababu ambacho kilikuwa kinafanyika ni kitu ambacho kwa kweli kinasikitisha sana. Haiwezekani wewe ukawa huko Wizarani, halafu una mtandao wa wizi kuanzia kule juu Wizarani mpaka kule chini kabisa. Wananchi wanalalamika kuhusu upungufu wa maji, mabomba yamepasuka na kadhalika halafu wewe umekaa umepumzika tu.

Naomba sana Mawaziri hawa, Waziri wa Maji, Waziri wa Viwanda, Waziri wa Fedha, Waziri wa Kilimo waendelee kufanya kazi ya kuangalia watu ambao wanawazunguka Wizarani, kwa sababu inawezekana tunaweza tukakaa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Mambo ni mengi, muda mchache. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi ya kusimama hapa. Lingine kwa kweli leo ni siku ambayo nina amani sana na furaha kubwa, kwa sababu naichangia Wizara ambayo inaonesha kwamba watu wapo serious. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sisi ambao ni Wabunge Mawaziri wote hawa tunawaona, tunajua kila mtu utendaji wake ulivyo. Vipo vitu ambavyo kuna Waziri anaongea, hata maswali wananchi wanatutuma, tunakuja hapa tunauliza, Waziri akidanganya tunajua, Waziri akifanya siasa tunajua na Mawaziri ambao wapo serious pia tunajua. Wizara hii ya Kilimo ni Wizara ambayo ipo na watu serious kupita mfano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina Wizara zangu chache; Wizara ya Kilimo, Wizara ya Madini, nyingine siwezi kuzisema leo lakini hizo naamini kwamba zipo na watu serious na lazima niwapongeze watu hawa kwa sababu kazi kubwa na hali halisi ya maisha ya wananchi wetu inajulikana. Wananchi wetu wana shida sana kule, vipo vitu vingine tukikaa kupongezana na kusifiana sana mambo kule yatakuwa hayaendi. Mwaka 2025 itafika wakati sasa tunakaa tunaanza kutafutana, tunabembeleza, tunapiga magoti tunaonekana kwenye magazeti haipendezi. Kwa hiyo, kwa Mawaziri ambao wanafanya kazi vya kutosha na kwa kiwango cha juu, ni lazima tuwapongeze. (Makofi)

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

T A A R I F A

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nakubaliana na dada yangu Lucy Mayenga kwamba ni kweli mawaziri hawa vijana wanafanya kazi, lakini jukumu letu kama Bunge ni kuhakikisha Wizara ya Fedha tunaibana ili wawapelekee hawa Mawaziri fedha wakabadilishe maisha ya watanzania ambao asilimia 80 ni wakulima. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mayenga unapokea taarifa?

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Taarifa hiyo si mbaya, naipongeza kwa sababu pesa ndiyo kila kitu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia Mheshimiwa Rais wetu, kwa kweli huyu mama anafanya kazi kubwa sana, nasema hivi kwa sababu hata kwenye Wizara hii tumeona kiwango cha pesa bajeti ya Wizara hii kwa mara ya kwanza imefika shilingi bilioni 751 haijapata kutokea. Kwanza ameonesha kuwathamini sana wakulima, lakini amewaheshimisha… (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mayenga imefika bilioni 700, bilioni weka takwimu vizuri.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema bilioni 751.

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sawa. Imetoka bilioni 200 mpaka bilioni 751, lakini Mheshimiwa Rais pamoja na Wizara hii wameweza kupandisha, yapo maeneo ambayo tunajua kabisa kwamba ukiyagusa, kama tunavyojua kwamba kilimo kinamgusa mwananchi kwa asilimia 100. Maeneo ya utafiti, maeneo ya hawa ndugu zetu Maafisa Ugani, maeneo ya maendeleo yote katika Sekta ya Elimu yamepandishwa kwa kiwango kikubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitolea mfano kwenye utafiti; kutoka bilioni 7.0 mpaka bilioni 11.6; kwenye huduma za ugani bajeti imepanda kutoka milioni 603 mpaka bilioni 11.5; kwenye umwagiliaji kutoka bilioni 17 mpaka bilioni 51; ni mabadiliko makubwa sana na kwa kweli kwenye hili tunampongeza sana Mheshimiwa Rais, nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii Naibu na Watendaji wote. Kama ingekuwa kuna uwezo Waziri mmoja na watendaji wake na hii timu ya Wizara ya Kilimo kuhudumia Wizara mbili, kuna Wizara ningependekeza kama iende huko pia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimpongeze mama yangu Mwenyekiti wa Kamati hii. Ni mama ambaye amekuwa anafanya ziara kwa vitendo na kwa kweli Kamati hii imekuwa ikifanya kazi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo matamko mengi sana ya historia ya kilimo katika nchi yetu, imeanza kwa mambo mengi sana. Awamu ya Kwanza naya Nne wao walijikita kwenye masuala mazima ya uzalishaji; Awamu ya Pili na Tatu wao walijikita kwenye Muundo wa Taasisi pamoja na mifumo mizima ya kilimo; Awamu ya Tano iliyopita ilijikita kwenye kuboresha masuala mazima ya kuongeza thamani ya mazao, uzalishaji lakini na pia vilevile kuweka miundombinu bora kwa ajili ya kusaidia kilimo chetu katika mazao ambayo yanapatikana yaweze kusafirishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mambo ambayo nataka niyazungumzie, tunazungumza kwamba kwenye sekta hii, zipo pesa nyingi sana. Wizara hii Mheshimiwa Waziri kaka yangu Bashe amepewa fedha nyingi sana na fedha hizi naomba awe mkali sana. Nasema hivi kwa sababu moja kati ya tatizo kubwa sana ambalo limekuwa likitokea hapa nchini kwetu, ni kwamba bado baadhi ya watu ni kama wanataka ku-test test mitambo hivi, bado hawaamini kwamba kula fedha ya Serikali ni kosa na unaweza kuchukuliwa hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Serikali au Wizara hii ijitahidi sana kusimamia pesa hizi kwa sababu kule kwa wananchi kilimo ni kinachukua asilimia 70 ya Watanzania. Kwa hiyo, bila fedha hizi kusimamiwa ipasavyo maendeleo na yale matokeo ambayo tunahitaji hatutayapata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo nataka kuzungumzia, kuna Miradi ya Umwagiliaji katika Wilaya yangu ya Kishapu, ipo Miradi ya Umwagiliaji katika Kata za Mwadui, Lohumbo Itilima na Talaga, kuna skimu za umwagiliaji. Naomba Mheshimiwa Waziri kwa unyenyekevu mkubwa, ikiwezekana tuweze kupata fedha pale. Katika skimu ya Umwagiliaji ya NIDA ambayo ilikuja mwaka 2020, namshukuru sana Wazii alikuja pale Shinyanga Vijijini baada ya kelele nyingi sana za kaka yangu Mheshimiwa Ahmed, Mbunge wa Jimbo, alikuja akasikiliza shida zetu na akatuelewa na nimpongeze na nimshukuru kwamba ametupatia fedha kwa ajili ya skimu hiyo ya umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia atusaidie skimu ya umwagiliaji ya kwenye Kata Uhendele ambayo ipo kwenye Manispaa ya Kahama Mjini. Kuna Mheshimiwa Diwani wetu pale anaitwa Justin Sita amekuwa akipiga kelele kila mara kwenye kila kikao kwamba mradi huu uweze kupata fedha, naomba Mheshimiwa Waziri atusaidie. Miradi hii endapo kama itafanikiwa, itasaidia akinamama. Watu wanategemea miradi hii ikifanikiwa maji yale yaweze kulisha mifugo pamoja na akinamama waweze kupata maji kwa ajili ya matumizi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho; naomba kusema hivi, naomba tumpe Mheshimiwa Rais wetu muda. Mheshimiwa Rais wetu ameingia katika kipindi ambacho kina changamoto nyingi sana, endapo sisi wanasiasa tutakuwa tunakaa katika kila kitu kwa kuangalia dosari, kuangalia hapa amefanya hivi, kwa kuangalia kukosoa, hatuwezi kumpa moyo Mheshimiwa Rais wetu. Tumpe muda tukae, kama ambavyo tulikuwa tumeanza mwezi Januari, Februari, Machi mpaka Aprili maneno yalikuwa mengi mengi, lakini juzi amekuja amefanya jambo la maana, maneno yamekuwa mengi ndivyo Watanzania walivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana kumpa moyo Mheshimiwa Rais, afanye kazi, ameingia kipindi kigumu, kipindi ambacho kina matatizo mengi, matatizo ya vita ya Urusi, UVIKO na mengine mengi, lakini naomba nimpe moyo, tupo pamoja naye hata kama kuna wanasiasa ambao tunawasikia wanaongeaongea vitu ambavyo havieleweki, sisi tupo pamoja naye na naomba wanasiasa hao washindwe na walegee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wa Mwaka 2017
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia hii nafasi. Vilevile ninaomba kwa nafasi ya pekee nichukue nafasi hii kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ambaye kwa kweli kwa kiwango kikubwa yeye ndiye aliyesababisha mpaka leo hii Tanzania kwenye vita hii tumeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze pia Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa msimamo mkubwa alionao dhidi ya vita hii. Vile vile kwa nafasi na upendeleo wa kipekee nimpongeze Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Kamishana Siang’a, ninampongeza sana. Ninampongeza sana kwa sababu anafanya kazi na amefanya kazi kubwa sana, ndani ya muda mfupi na katika mazingira magumu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamishna huyu ndiye yule ambaye alikataa rushwa ya shilingi milioni 800. Kwa kweli ni kitu ambacho kwanza ni nadra maana hata katika hali ya kawaida unaona kabisa kwamba kama ni mtu ambaye si mzalendo na hauna uzalendo wa dhati kutoka moyoni mwako, ni kitu ambacho ni kigumu sana, kwa hiyo ninampongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ninampongeza kwa sababu alifanya kazi hii katika mazingira magumu sana ya sheria; alifanya kazi hii katika mazingira ambayo sheria hii ilikuwa haitumiki Zanzibar, katika mazingira ya sheria ambayo yalikuwa hayaruhusu mamlaka hii kumiliki silaha, mazingira ambayo hata yeye mwenyewe kuweza kutaifisha na kufanya mambo mengine yote ili kuweza kukabiliana na hawa wauzaji wa dawa za kulevya ilikuwa haiwezekan lakini aliweza kupambana na hatimaye sasa hivi kwa kweli watu wanasema kwamba misuli imekaza lakini kwa hawa wauzaji wa dawa za kulevya imekaza zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niingie kwenye suala hili la dawa za kulevya kwa upande wa Zanzibar. Mimi nilikuwa ninategemea kwamba leo Wazanzibari wote wangekuwa na kauli moja kwamba sheria hii wanaiunga mkono kwa asilimia 100 bila kusita. Nasema hivyo kwa sababu matatizo haya ya madawa ya kulevya athari zake ukiachilia mbali athari za kijamii kwa maana ya kwamba maradhi na nyingine lakini ina athari kubwa sana kwenye masuala ya uchumi…

T A A R I F A . . .

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, yeye alikuwa ni sehemu ya Wazanzibari, lakini hasa nilikuwa nimem-target Mheshimiwa Ally Saleh kwa sababu naye pia ni Mzanzibari. Kwa hiyo, kwa wale ambao wanaunga mkono sheria hii tupo pamoja, lakini kwa wale ambao hawaungi mkono kwa sababu pia wewe unaweza ukawa ni mmojawapo, lakini kuna wenzenu pia hawauingi mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sitaki kusema mengi lakini ninachotaka kusemea ni kwamba hata kama tunaunga mkono sisi viongozi na sisi ambao ni Wabunge Wazanzibari tuliopo humu ndani, ninaomba sasa maana yake nilikuwa sitaki kusema lakini ninaomba kwenda mbele zaidi. Ninaomba tufanye kazi ya ziada kwa tume ya kudhibiti na kupamba na madawa ya kulevya Zanzibar. Imeunda zaidi ya miaka kumi, lakini mpaka sasa hivi haijakamata hata kilo tano, naishia hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala haya ya madawa ya kulevya yana athari nyingi sana. Zipo nchi ambazo zimekuwa zikifadhiliwa kutokana na athari hizi za dawa za kulevya zimeingia kwenye matatizo makubwa sana kisiasa, kiuchumi na nyingine pia zimepinduliwa. Nchi kama Nicaragua, Panama, Mexico na kadhalika na wengi pia mnajua historia hizo, wapo katika hali ngumu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo vita hii ninaomba wote tuwe na kauli moja kwa sababu vita hii inahusu kuanzia wale wadogo ambao ni watumiaji lakini hata na sisi pia wakubwa. Kwa sababu ambao wamekuwa wakikamatwa mara nyingi huko wanasemwa sana, lakini bado miongoni mwetu kuna watu ambao baadhi yao wapo katika nafasi mbalimbali, si lazima wawe Wabunge ni watu ambao wapo katika nafasi kubwa lakini wamejiingiza kwenye biashara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ninaomba kupongeza sana sheria hii na kwa kweli ninaomba serikali kwenye utekelezaji wa sheria hii isimuangalie mtu usoni, awe mtoto wa mkubwa, awe mwenyewe ni mkubwa awe sijui ni nani, tuangalie na tuweze kuchukua hatua zinazostahili. Haiwezekani watu walikuwa wamefikia kiwango cha kuingiza katika nchi yetu mpaka tons as if ni unga wa mahindi, haiwezekani. Kwa hiyo, sheria hii ikate kotekote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikiliza kuhusu taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu suala la kifungu cha dhamana kwamba ile kupunguza gramu. Ili mtu alewe kutokana na unga anatakiwa atumie 0.01 gramu ya unga ndipo analewa. Sheria iliyopita ilikuwa ni kwamba mtu akikamatwa na madawa ya kulevya haya ya viwandani, heroin au cocaine ikiwa ni chini ya gramu 200 anapata dhamana, sasa nini kilichokuwa kinafanyika?

Mheshimiwa Naibu Spika, kilichokuwa kinafanyika ni kwamba wafanyabiashara walikuwa gramu 200 anazigawa kwa watu tofauti tofauti, kwa sababu anajua kwamba akikamatwa na gramu 200 au zaidi mtu mmoja itakuwa ni matatizo. Gramu 200 anaweza kutengeneza, gramu moja ya dawa za kulevya inatengeneza kete 100 kwa maana hiyo gramu 200 ni zaidi ya kete 20,000…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)