Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Raphael Michael Japhary (25 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nipo lakini hukuniambia mapema.
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Naitwa Japhary Michael, Mbunge wa Jimbo Moshi Mjini. Nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi wa Moshi Mjini ambao wamenichagua kwa kura nyingi sana pamoja na Madiwani wangu kuongoza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nina mambo machache ya kuchangia katika hotuba ya Mheshimiwa Rais. Kabla ya hayo, nataka nitoe observation yangu niliyoiona katika kuchangia huku. Ukiangalia ndani ya Bunge hili utadhani kama vile Serikali tunayoizungumzia leo
imeanguka jana, haikuwepo katika nchi hii kwa hiyo, matatizo yaliyopo hawahusiki nayo. Kwa bahati nzuri kwa zaidi ya miaka 50, Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa matatizo ya Taifa hili kwa vyovyote vile yanawagusa kwa kiwango cha kutosha kabisa. Kwa hiyo, naona kama vile
kuna watu wanaomba toba, sasa ni wajibu wa wanaoombwa toba kukubali au kukataa.
(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende moja kwa moja kwenye hotoba ya Rais pale anapozungumzia habari ya ushirikiano wa Serikali yake na Halmashauri. Nimekuwa Diwani na nimekuwa Meya kwa miaka kumi sasa hivi. Tunapoelekea niiombe sana Serikali ijitahidi kuishi
katika dhana ya decentralization, ya kupeleka madaraka kwa wananchi, izipe mamlaka ya kutosha Halmashauri za Wilaya, Majiji na Manispaa kama sheria inavyosema kwamba madaraka yatatoka kwa wananchi. Hali inavyoendelea, Halmashauri zimekuwa zikiongozwa kwa miongozo, waraka, maagizo na kusababisha leo hii watendaji wengi wa Halmashauri na Madiwani wanakosa creativity (ubunifu). Kwa hiyo, wanajikuta siku zote wataishi kwa maagizo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri wa TAMISEMI na matokeo yake kiukweli
mambo mengi yanaenda ndivyo sivyo. Kama tunataka wananchi watumikiwe vizuri na ndivyo alivyoelekeza Mheshimiwa Rais, ni vizuri mamlaka zile zipewe power inayostahili ambayo itaweza kuwafanya waweze kuzitumia rasilimali za Taifa vizuri na kuzifanya ziwe na ufanisi na tija kwa wananchi wa taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hata maslahi ya Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa, huwezi kumwambia Mwenyekiti wa Mtaa hana chochote lakini anaitwa Mheshimiwa, ndiye anatakiwa apokee watu waliogombana kwenye ndoa zao, ndiye anatakiwa apokee kila tatizo halafu hapati chochote ambacho kimeelekezwa na Serikali, mnaziachia Halmashauri ziamue zenyewe wakati hazina hata uwezo wa kujiendesha zenyewe. Ni vizuri Serikali iliangalie hili kwa ndani sana namna gani itasaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kujiendesha vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangie suala la utalii. Jimbo naloongoza lipo karibu sana na Mlima Kilimanjaro. Kama tunataka kuuendeleza utalii ili tuweze kukuza uchumi wa nchi hii ambapo tunafikiri kuwa na mawanda mapana katika viwanda, ni vizuri tujitahidi
kuuboresha utalii na hasa tuutumie vizuri Mlima Kilimanjaro.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Uwanja wa Ndege wa Moshi umekuwa kama gofu lakini hautumiki vizuri. Uwanja huu ungeweza kusaidia watalii wanapotoka kwao waje moja kwa moja pale na uongeze mapato na uchumi wa Mji wa Moshi lakini pia ungesababisha Mji wa Moshi
ukue kwa haraka. Mji wa Moshi umekuwa kwa taratibu mno kama vile siyo Mji Mkongwe na wa zamani. Naomba sana Serikali ilione hili kwa mapana yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la rushwa na ufisadi ambalo limezungumzwa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais na kwa sauti kubwa sana. Naomba kwa dhati kabisa, katika Bunge lililopita wakati linamaliza muda wake, Mheshimiwa Halima Mdee, alileta kwenye
Bunge hili Tukufu hoja ya udanganyifu uliofanywa na taasisi fulani kupitia RITA wa kughushi saini za marehemu na wakabadilisha Bodi ya Wadhamini wa taasisi hiyo ili wapore eneo ambalo Halmashauri ya Manisapaa ya Moshi imelikalia zaidi ya miaka 20. Hoja hiyo imekuja hapa lakini Mbunge aliyeleta hoja ile hakupewa majibu na leo watu wale wamebarikiwa, wamekabidhiwa udhamini wa ile taasisi na tayari kiwanja kile kimeshachukuliwa na hiyo taasisi na kimeuzwa kwa watu wengine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunapozungumza habari ya ufisadi, lazima tumsaidie Rais, seriously. Tukizungumza mambo kama hatuko seriously tutakuwa tunazungumza mambo yaleyale, kwa sura zilezile na matokeo yatakuwa ni yaleyale. Kwa hiyo, ni lazima tuwe na
jitihada za kutosha kwa yale ambayo tunataka kuiaminisha jamii.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la hali ya watu wa chini ambalo kimsingi ukiliangalia kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais limeongelewa kwa mapana yake na amelenga zaidi huko, hali ilivyo na kwa namna utekelezaji wake unavyoendelea watu wa chini siyo muda mrefu
wataichukia Serikali. Kwa sababu inaonekana kiukweli, kumekuwa na matamko mengi ambayo yanawaumiza watu wa chini. Ni lazima tukubaliane kuna mambo ya msingi ambayo hatuna nafasi ya kuyafumbia macho, hatuwezi kufumbia macho uhalifu wa aina yoyote katika
Taifa hili wa ufisadi na rushwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, kuna mambo yanahitaji huruma ya kawaida tu hasa ikizingatiwa kuwa Serikali ni ileile kwa muda wa miaka 50 na mambo mengine mmeyasimamia ninyi leo mnapokwenda bila jicho la ubinadamu mnawafanya wananchi
wasiwaelewe na hasa wa hali ya chini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, unapokwenda ukavunja nyumba ya mwananchi wa hali ya chini ambaye pato lake ni la chini mno wakati miaka 50 amekaa katika eneo hilo ndani ya utawala wa chama hichohicho, ni hatari sana. Ni lazima tujitahidi kuwa watu wenye huruma, wenye ubinadamu kama ambavyo hotuba ya Mheshimiwa Rais imejaribu kuonesha kwamba tujielekeze huko, tuwahurumie hawa watu wa chini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini namna gani tunaweza kuwasaidia watu wa chini kama Wamachinga na wachuuzi mbalimbali, lazima tuone kwamba hakuna Taifa lolote duniani watu wamekuwa matajiri bila kuanza katika hiyo primitive accumulation lazima tujitahidi kuona
tunawasaidiaje watu hawa. Alichotuagiza Rais ni kwamba watendaji wabadilishe spirit na attitude zao, wawe na tabia ya kuwa wabunifu ni namna gani watengeneze mazingira rafiki kwa hawa watu wa chini kuweza kusaidiwa na sio wawe watu wa kuwabugudhi na kuwaumiza,
ni lazima hilo lifanyike kwa nguvu zote.
Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri anapokwenda kuongea na wananchi akaongea kibabe ni hatari wakati akienda kuomba anaomba kiungwana na kama binadamu. Namna mnavyoomba kura ni namna hiyohiyo mnatakiwa muwatumikie wananchi ili waone kwamba
siku zote mko nao.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuishauri Serikali, lazima sisi wanasiasa maana Mawaziri hamvui vazi la siasa ninyi bado ni wanasiasa, mnapozungumza na wananchi…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Japhary muda wako umekwisha, tafadhali naomba ukae.
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kushukuru kwa kupata nafasi hii ya kuchangia. Pia niipongeze sana hotuba ya msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa namna ambavyo ipo katika mtazamo wa kuisaidia Serikali kuboresha mpango wake wa kuifanya Tanzania ya viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nina maeneo machache ya kutoa mchango wangu. Mpango wa kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda ni mwema na maombi yetu sote tufikie hapo. Lakini mashaka yangu mimi ni sababu zilizotusababisha tukashindwa kufikia hapo siku za nyuma. Kwa sababu miaka ya 80 tulikuwa tunaenda vizuri, ni kizungumkuti gani kilituingia mpaka tukaamua kuruhusu mipango isiyo mizuri ambayo imelifikisha Taifa hapa mpaka leo ndiyo tunaanza kutafakari namna ya kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Hofu yangu ni kwamba inawezekana mpango huu wa Serikali ukawa ni mpango unaosikika vizuri masikioni lakini bado ukawa na shida katika utekelezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni nini ambavyo tunavikosa katika Taifa hili? Ukiangalia Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi kama vile Serikali imeanguka leo, haikuwepo tangu huko nyuma, kama vile ni chama kipya kimeanza kutawala Taifa hili wala sio Chama cha Mapinduzi kilichokuwa kinatawala. Kwa hiyo, hakuna muunganiko kati ya mfumo wa Serikali iliyopita na mfumo wa Serikali inayofuata sasa ambao ungesaidia kujua ni mabaya yapi mnayaacha, ni mazuri yapi mnayapokea. Matokeo yake kila mtu anakuja na mtazamo kama vile anataka kuizaa Tanzania leo wakati Tanzania ina miaka 50 tangu imeitwa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hofu yangu kubwa ni consistency ya government. Hiyo ndiyo inanipa mashaka kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutofikia hii mipango yote ambayo tumeipanga. Mimi ukiniuliza leo ningekuambia kilichokosekana katika Serikali zilizopita, ya Awamu ya Tatu na ya Nne ni dhamira na uzalendo kwa viongozi waliopewa dhamana, ndicho ambacho ningekujibu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa msingi huo kama Rais wetu kweli ana dhamira na kama Waziri wa Viwanda leo alivyotoa hotuba yake kweli ndiyo dhamira yake hivyo ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anaambukiza hiyo dhamira kwa watu wote wanaomzunguka ili Tanzania ifike hapo inapotaka kufika kuwa Tanzania ya viwanda. Kama hatutaweza kuibadilisha culture ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi zilizopo katika Taifa hili hizi zitakuwa ni nyimbo na ngojera ambazo zitaimbwa kila mwaka na hatufiki popote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nachoshauri ni kwamba Serikali ijiandae katika hilo, kwanza kwa kubadilisha utamaduni wa watendaji wetu wa kuliibia na kuliumiza Taifa ili kidogo tunachokipata sasa tukielekeze kwenye maendeleo. Nina hakika tukifanya hivyo tunaweze kufika mahali fulani.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa utangulizi huo, nataka niongelee suala la wafanyabiashara kama wenzangu waliotangulia walivyosema. Taifa hili bado halijaonyesha kiukweli, kama maneno nitakayotumia siyo mazuri sana lakini nadhani hivyo kwamba Taifa hili bado halijaonyesha kiukweli kwamba lina haja ya kuwasaidia wafanyabiashara wake wa ndani, bado halijaonyesha kwa dhati. Ndiyo haya unasikia mambo ya kodi watu wanapoingiza mali lakini hata wafanyabiashara wa ndani mazingira yao waliowekewa vikwazo vyao vimekuwa ni vingi sana kiasi kwamba uwezo wa wafanyabiashara hawa kufanya kazi yao vizuri wakawa ni sehemu ya wawekezaji muhimu katika Taifa hili umekuwa ni mdogo sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wakati tumejikuta tunathamini wawekezaji wa nje kuliko wa ndani, siyo jambo baya lakini siyo vizuri kushindwa kuwatengenezea fursa na mipango mizuri wafanyabishara wa ndani ili waweze kuwa wawekezaji ambao wana uhakika kuliko wawekezaji wa nje na watakaohakikishia Taifa hili kubaki na pato lake la ndani na uchumi wake kukua kwa haraka sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, rai yangu kwa Serikali ni vizuri tuhakikishe tunaondoa vikwazo kwa wafanyabiashara wetu wa ndani, tozo zimekuwa nyingi mno. Leo ukiuliza hivi ni kwa nini bado corporate tax ni kubwa kwa wafanyabiashara hakuna majibu ambayo ni ya msingi sana. Ukiuliza kwa nini VAT bado ni kubwa kwa wafanyabiashara hakuna jibu ambalo ni la msingi sana. Kanuni mojawapo ya kodi ni kuwa na compliance ili mfanyabiashara aweze kulipa kodi hiyo. Sasa leo kodi inatumika kumfilisi mfanyabiashara, anaingia kwenye uchumi kesho, kesho kutwa anafilisiwa na kodi na anafilisiwa na Watanzania wenzake halafu mnakwenda kufikiri kuwaneemesha watu wa nje waje kuwekeza wakati mnashindwa kuwawezesha wafanyabiashara wa ndani wakafanya vizuri maana yake ni kwamba hamsaidii wafanyabiashara wenu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo pamoja na jitihada ya kuvutia wawekezaji wa nje ni vizuri tusaidie wafanyabiashara wetu wa ndani ili wafanye biashara zao vizuri. Hebu tuangalieni tax regime yetu kama ipo sawa sawa na inawasaidia wafanyabiashara wa ndani? Kodi ya Taifa hili imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara. Leo katika nchi hii mfanyabiashara akimuona mtu wa TRA ni afadhali amuone simba kwa jinsi ambavyo muda wote anafikiri kufilisiwa. Bahati mbaya Serikali inajenga taswira hasi kwa wafanyabiashara kwamba wote ni wizi, ndiyo inavyoonekana hivyo, hakuna wakati maafisa wa TRA wamekuwa tayari kuamini taarifa halisi za wafanyabiashara na ndiyo maana leo unasikia gari inanunuliwa nje shilingi dola 500 inakuja kuchajiwa kodi ya dola 2,000 kwa sababu ya kutoamini wafanyabiashara. Nadhani ni muhimu sana kuangalia eneo hili kama tuna dhamira ya kuwafanya wafanyabiashara hao wawekeze katika sekta ya viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niongelee suala la sekta isiyo rasmi. Kama Mheshimiwa Waziri alivyoonyesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha anasaidia viwanda vidogo, vidogo sana na vya kati na wafanyabiashara wadogo sana na wa kati, ni lazima sekta hii ipewe kipaumbele. Kipaumbele nachozungumzia siyo kwa maneno ya kisiasa, siyo kwa kuzungumzia habari ya asilimia tano ya Halmashauri kwa akina mama ambayo haipatikani, ni lazima tujenge mkakati rasmi wa kuhakikisha kwamba tunatengeneza mazingira ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo katika Taifa hili Mheshimiwa Rais anasema wafanyabiashara wadogo wasibugudhiwe, wasisumbuliwe katika Halmashauri zao lakini huko chini Wakurugenzi wanasumbua wafanyabiashara hao. Ni lini wafanyabiashara hawa wataweza kwenda mbele? Rais anatoa maagizo, huko chini maagizo ni mengine. Rais anaagiza kwamba watu watengewe maeneo ya kufanyia biashara, hakuna maeneo ya kufanyia biashara kila siku watu hawa wanaishi kama swala anayemuogopa simba katika Taifa hili. Hatuwezi kupeleka Taifa hili mbele, ile sekta ni muhimu sana na ina uwezo ikitumika vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nimekuwa Meya katika Halmashauri yangu najua ikitumika vizuri ina uwezo wa kulitoa Taifa hili hapa kulipeleka mahali pengine na wana uwezo hao kuwekeza vizuri katika eneo la viwanda. Kwa hiyo, ni vizuri mtengeneze mkakati thabiti wa kuwasaidia hawa watu kule chini. Toeni maelekezo kwa Wakurugenzi wawe creative, wabuni namna gani wawasaidie wale wafanyabiashara rather than kuwapiga na kuwasumbua katika maeneo yao wanayofanyia biashara ili nao waishi kama Watanzania wengine na wapate faida ya matunda haya tunayotaka kuyafikia ya lengo la kuwa na Tanzania mpya ya viwanda. Nilidhani hiyo sekta ni muhimu sana na muione kama engine muhimu sana inayoweza kutusaidia kufika tunapotaka kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nizungumzie kidogo kwenye suala la forward and backward linkage ya sekta zetu. Bado tuna tatizo kama wengi walivyosema la kilimo, ni vizuri tuone sasa kwamba kama tunataka kweli kufika kwenye viwanda pamoja na matatizo hayo huko nyuma ambayo tunaweza tukayarekebisha, lakini ki ukweli ni lazima tukiinue kilimo chetu kiwe ni kilimo chenye sura ya viwanda. Kama hatutafanikiwa hili bado tutaimba tu viwanda na hatutafikia lengo. Bila kumung‟unya maneno…
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha hoja yangu, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vya Moshi Mjini na Kilimanjaro kwa ujumla ambavyo vimefanywa maghala na vingine havifanyi kazi kwa ufanisi. Naishauri Serikali itekeleze ahadi ya Rais wakati wa kampeni kuwanyang‟anya wawekezaji ambao hawajaweza kutimiza malengo ya awali yaliyotarajiwa katika viwanda vilivyobinafsishwa. Mahusiano ya kisekta ni muhimu sana (forward and backward interlinkage). Naishauri Serikali iwekeze katika Agro Processing Industries (value added) ambavyo vitaongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo. Pia nishati lazima iwe ya uhakika na ya bei rahisi ili viwanda vyetu vizalishe kwa bei nafuu kwa maana ya kuwa cost effective.
Vilevile ni lazima miundombinu ya reli iimarishwe ili iweze kubeba mizigo ya viwandani. Hatuwezi kutegemea barabara katika kusafirisha mizigo ya viwandani. Aidha, lazima Serikali iimarishe taasisi za kifedha financial institutions ili ziweze kutoa mitaji kwa wawekezaji wadogo, wakubwa na wa kati. Mikopo ikiwa na riba kubwa haiwezi kusaidia wawekezaji ndani wala wa nje. Nashauri Serikali iwe na mkakati wa kuacha kukopa mikopo mikubwa kwenye taasisi za fedha ili wawekezaji binafsi waweze kukopa kwa riba nafuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, masoko ni muhimu sana katika kuhakikisha uwepo wa viwanda, nashauri mambo yafuatayo katika masoko:-
(a) Serikali ifanye jitihada za kuimarisha soko la ndani kwa kuongeza fursa za vipato kwa wananchi. Mataifa yanayokua kwa kasi kiuchumi kama China, India na mengineyo yamefanikiwa kuimarisha soko la ndani hivyo bidhaa zao wanazozalisha zinapata walaji wa ndani ya nchi na ziada ndio inauzwa nje. Kuimarika kwa soko la ndani kunavihakikishia viwanda uhakika wa kupata faida kwa bidhaa zinazozalishwa. Mojawapo ya mkakati wa kusaidia soko la ndani ni kuongeza uwezo wa kununua (purchasing power) kwa wananchi kwa kuhakikisha vipato vizuri vya mtu mmoja mmoja na wananchi kwa ujumla.
(b) Masoko ya nje lazima yatafutwe kwa kuanzia nchi jirani. Jambo hili litafanyika kwa kujifunza vizuri bidhaa ambazo tunaweza kushindana na jirani zetu. Pia ni vizuri wananchi wetu wasaidiwe jinsi ya kuingia kwenye ushindani na wananchi wenzetu katika masoko mbalimbali ya nchi jirani.
(c) Masoko yataimarishwa kwa kuziimarisha sekta za utalii, madini na Halmashauri zetu na sekta binafsi. Sekta ya utalii imekuwa kwa haraka katika nchi yetu, hivyo ni vizuri ikatumika katika kutoa ajira ambazo zitaongeza kipato cha wananchi na baadaye kupanua soko la ndani. Pia sekta ya utalii itafanya hivyo hivyo.
Aidha, Serikali ikizitumia Halmashauri zetu vizuri kwa kuimarisha sekta ya wajasiriamali wadogo wadogo kwa maana sekta isiyo rasmi itatengeneza kundi la watu wenye mitaji ambao wanaweza kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo, viwanda vya kati na hata baadaye wanaweza kuunganisha mitaji na kuwekeza kwenye viwanda vikubwa. Zaidi ya hayo sekta binafsi inatakiwa itengenezewe mazingira rafiki ya kufanya shughuli zake ili iweze kuajiri wananchi wengi zaidi hivyo kuongeza kipato cha wananchi na kwa maana hiyo kuongeza nguvu ya kununua yaani purchasing power.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali lazima iwekeze katika teknolojia kwa kuimarisha mifumo yetu ya elimu na vyuo vya sayansi na ufundi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata fursa hii na namshukuru Mbunge mwenzangu kwa kunipa fursa hii ya kuchangia dakika zake tano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo mawili tu, la kwanza ni suala linaloendelea hapa Bungeni mara kwa mara, Wabunge wengi wakichangia na hasa wa maeneo ya Kusini wanajaribu kuonesha kwamba Kaskazini kumeendelea sana. Sasa hofu yangu dhana hiyo inaweza ikapoteza mwelekeo wa Serikali katika kupanga keki ya Taifa, kwa kuamini kwamba Kaskazini kumeendelea kweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukizungumzia Kanda ya Kaskazini unazungumzia Tanga, ukienda kwenye Majimbo ya Tanga kuhusu barabara utapata shida, sasa ikioneshwa kwamba Kaskazini kumeendelea, maana yake ni kwamba hayo Majimbo yote yana barabara nzuri za lami, yanapitika vizuri, kitu ambacho siyo kweli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukienda Manyara ni Kaskazini, maeneo ya Wamasai, hayapitiki; kwa hiyo, hoja ya kwamba Kaskazini kumeendelea pia siyo ya ukweli kama inavyozungumzwa hapa Bungeni. Ni jambo jema kufikiri kwamba kama kuna maeneo hayajaunganishwa mkoa kwa mkoa likatekelezwa hilo, kwa sababu ni sera ya Serikali. Yale ambayo yalishaunganishwa mkoa kwa mkoa yaunganishwe wilaya kwa wilaya, yale ambayo Wilaya zilishamalizika yataunganishwa Kata kwa Kata na hatuwezi kwa pamoja katika nchi hii, kuendelea kwa kiwango cha aina moja kwa wakati mmoja, tunapogawa resources za Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima tukubaliane tu kwamba kwenye Bunge hili, sote katika nchi hii kama walipa kodi na wachangiaji wa Pato la Taifa tunapaswa kugawana keki ya Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda Kaskazini reli ya Tanga mpaka Arusha, hapa ni wimbo, ukijiuliza ni kwa nini reli hiyo mpaka sasa iko katika hali ile, wala kabla hatujafikia upembuzi yakinifu bado ile reli ingefaa kutumika na ikainua sana uchumi wa Kanda ya Kaskazini. Hata hivyo, reli ile mpaka sasa haifanyi kazi, lakini bado kuna dhana kwamba Kaskazini kumeendelea. Ukienda kule Kilimanjaro ukienda Upareni utasikitika, bado unaambiwa Kilimanjaro kumeendelea au Kaskazini kumeendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme hilo ili kuweka rekodi sawa, kwamba Taifa hili lina uhitaji unaofanana katika mahitaji yote ya barabara, mahitaji ya reli na mahitaji mengine yoyote yanayohusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri alivyoleta bajeti yake, ni lazima aiangalie Kaskazini kama anavyoiangalia Kusini na Magharibi na Mashariki mwa Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niongee suala la pili kuhusu TRL na RAHCO. Mpaka mwaka 2002, Shirika la Reli (TRC) lilikuwa na uwezo wa kufanya kazi yake vizuri. Mpaka mwaka 2002 Shirika la TRC lilikuwa na vichwa 68, mpaka mwaka 2002 Shirika la TRC lilikuwa na mabehewa 1,500 mpaka mwaka 2002 Shirika la TRC lilikuwa na uwezo wa kusafirisha tani 1,500,000; kwa hiyo, mgawanyiko kati ya TRC na RAHCO, ndiyo umeleta shida katika Shirika la Reli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ni makosa ya Serikali kuingia kwenye mkataba ambao haukuwa mzuri, kati yake na kampuni ya wenzetu wa India, ndiyo uliosababisha hali hii iliyojitokeza. Sasa rai yangu kwa Serikali, ni lazima hapa leo tutoke na azimio katika Bunge lako Tukufu la kuunganisha RAHCO na TRL, ni lazima tutoke na tamko hilo, vinginevyo maeneo mengi yaliyokuwa yakifanya vizuri kipindi cha TRC yatakuwa ni magofu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, TRC ilikuwa na karakana nzuri, ilikuwa inahudumia reli yake vizuri, lakini leo maeneo yote hayo hayafanyi vizuri kwa sababu ya TRL kunyimwa nguvu na Shirika la RAHCO ambalo ukiangalia kwa nini lipo hupati majibu yaliyokamilika. TRL haina uwezo wa kukopa, kwa sababu haina dhamana, lakini TRL ndiyo inayoangalia mabehewa yake, vichwa vyake na reli kwa wakati mwingine, naomba sana, muunganishe TRL na RAHCO.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea hapo alipoishia mchangiaji aliyepita ambaye amenipa muda wake wa dakika tano, naomba niongelee mambo machache sana ya Jimbo langu la Moshi Mjini katika suala la nishati. Napenda kuongelea kwenye upande wa nishati mbadala kama ilivyoandikwa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri katika page ya 60 na Serikali imeonyesha kwamba, imepitia maeneo ambayo wanadhani kwamba, wanaweza wakawekeza kwenye umeme wa upepo na umeme wa jua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani ni mpango mzuri, lakini sijui kwa nini umechelewa kiasi hiki kwa Taifa letu la Tanzania. Pamoja na yote hayo, nataka nisisitize kidogo kwenye suala la matumizi ya takataka zetu, miji yetu mingi inazalisha takataka nyingi, lakini Serikali haijawa tayari kuwa na matumizi bora ya takataka hizi na matokeo yake tumekuwa tukizalisha maradhi ya kila siku na kuharibu mazingira kila wakati, wakati tunaweza tuka-control hiyo situation.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukulia mfano Manispaa ya Moshi; Manispaa ya Moshi tuna mradi wa kutumia jalala letu ambalo ni semi-land fill ambalo lina uwezo wa kuzalisha methane gas ambayo inaweza ikatumika kupunguza sana matatizo ya nishati ya umeme katika mji wetu wa Moshi. Bahati nzuri tumeshafanya feasibility study na bahati nzuri tumeshapata ushirikiano wa wenzetu wa mji dada wa Tubingen, Ujerumani kwa hiyo, tuko katika hatua nzuri ya kutekeleza mradi huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachohitaji ni msukumo wa Serikali katika hili kwa sababu, haionekani kama vile Serikali imeweka mkazo katika eneo hili. Kwa hiyo, tunahitaji msukumo wa Serikali katika hili, ili wale watu wa Ujerumani watusaidie kufikia malengo yetu kwa sababu tayari tumeshatumia fedha za own source katika kutekeleza mradi huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, tunahitaji committment ya Serikali kwamba, wenzetu wa Ujerumani wametuambia kama tuki-raise cost ya mradi, wao wako tayari ku-raise 80% na sisi tu-raise 20%. Uwezo wa halmashauri kufanya kazi hii ni mdogo, lakini tunaamini kama Wizara itaji-commit itatusaidia sisi kupata 20% ili huo mradi utekelezwe mapema zaidi. Namwomba Mheshimiwa Waziri, aifanye Moshi pilot area ya mradi wa methane gas ambayo itasaidia sana kuzalisha umeme ili maeneo mengine yaige katika nchi hii ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna suala lenye shida katika Manispaa yangu ya Moshi katika Jengo la Stand kuhusu suala la umeme. Wananchi wanaomiliki vibanda katika Jengo la Stand yetu Kuu, jengo ambalo ni mali ya Manispaa, wametaka kuwekewa LUKU, lakini TANESCO wamekataa kuwafungia LUKU wakisema kwamba, mpaka wapate kibali cha Waziri. Sasa wale wananchi hawako tayari kuletewa bili na landlord ambaye ni manispaa. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri atoe kibali, ili wananchi wale wa Manispaa ya Moshi wafungiwe zile LUKU ili waweze kuendesha shughuli zao kirahisi kuliko kupata usumbufu usio wa lazima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu ni suala la biogas. Ukiangalia page ya 28 ya hotuba hii, biogas imeonekana kuelekezwa zaidi maeneo ya vijijini kupitia mradi wa REA na miradi mingine. Hata hiyo 3.2 billion iliyotengwa inaonesha ni kwa maeneo ya vijijini, lakini maeneo ya mjini watu wanafanya zero grazing, kwa hiyo, wanapata resources ambazo zinafaa kwa biogas na hitaji muhimu sana la wananchi, ili kupunguza matumizi ya kuni na ya mkaa ambayo siku zote tumekuwa tukikimbizana na tunagombana na wananchi kwa sababu, wanatumia mkaa na kuni na wengine mpaka tunawafunga.
Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa hiyo, naomba maeneo ya mjini ikiwemo Manispaa ya Moshi mradi huu uwe considered kufika katika eneo hili ili wananchi wangu wa Manispaa ya Moshi nao wafaidike na mradi huu wa Serikali. Naamini tukilitekeleza hili tutaweza kukabiliana na hali halisi ya uchafuzi wa mazingira. Bado naamini, Serikali yetu haijawekeza vizuri katika solid waste management ambayo ni teknolojia itakayosaidia sana maendeleo ya nishati katika dunia tunayoishi leo. Ukienda Nchi za Ulaya…
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa kwa mchango wako.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko ya waendesha utalii wa ndani (local investors) kuhusu gharama kubwa ya leseni yashughulikiwe. Waendesha utalii wa ndani wanaoomba leseni TALA kwa uwekezaji wa ndani iwe dola za Kimarekani 500 badala ya dola 2,000. Hii itasababisha Serikali kupata mapato zaidi kwa vile mzunguko wa fedha utabaki ndani tofauti na sasa ambapo fedha nyingi zinabaki nje kutokana na kampuni nyingi za kitalii kumilikiwa kwa ubia na wageni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maslahi ya waongoza watalii na wapagazi bado ni duni sana, mikataba yao ni mibovu na mazingira yao ya kufanyia kazi ni magumu. Serikali ni vyema isimamie Sheria ya mwaka 2008 iliyotangazwa katika GN mwaka 2008 ambapo pamoja na mambo mengine sheria hiyo itasimamia usajili wa waongoza watalii na kuwapatia leseni; ambapo mapato yataongezeka kwa Serikali kuwa na takwimu za waongoza watalii. Kuwe na waongoza watalii wanaokidhi vigezo na kuongezeka kwa watalii kwa kuwa huduma itakayotolewa itakuwa ina ubora na inakidhi viwango vya utalii wa ushindani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kukomesha wageni ambao wanafanya kazi ya kuongoza watalii, Serikali inaelewa kwamba ni kinyume cha sheria kwa wageni kuongoza watalii. Aidha, kumekuwa na volunteers ambao wanaingia nchini na kuingiza watalii kwa kuwalaza katika malazi bubu, hali hii huchangia kudumaza utendaji wa hoteli zetu katika Mji wa Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mpango wa kuboresha njia za kupandia Mlima Kilimanjaro, mfano ni njia ya Machame, ni vyema kukawa na namna bora ya KINAPA kutengeneza tent za kulia (mess tent) zinazofanana ili kutunza mazingira kuliko kuacha kila muendesha biashara ya utalii akajenga tent lake la kulia. Hivyo, nashauri njia ya Machame katika camp ya Machame Hut patengenezwe uniformity plan ya kujenga ma-tent yanayofanana na yenye kiwango kizuri kinachovutia kwa ajili ya wageni kupata chakula. Machame Hut iwe kama pilot na njia nyingine zitafuata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuongeza mapato kwa kuagiza TRA wawe na maafisa wao ambao watakaa kwenye lango la mlima kukagua tax clearance za wenye makampuni ya utalii ili kulinganisha taarifa za usajili wa makampuni hayo na uhalisia wa kodi wanazolipa. Tatizo kubwa lililopo ni kwamba makampuni yanakuwa na leseni lakini yanakuwa ni makampuni ya nje yanayotumia baadhi ya waongoza watalii kujificha katika hicho kivuli chao na hivyo kukwepa kodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utalii wa Mlima Kilimanjaro kwenda sambamba na hali ya uchumi ya wananchi wa Kilimanjaro, hususan wananchi wa Manispaa ya Moshi. Nashauri Serikali kuona jinsi ambavyo itakubali ombi la Manispaa ya Moshi kuwa Jiji kwa vile ni ahadi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa wananchi wa Moshi, jambo ambalo lilisababisha Manispaa ya Moshi kuanza mchakato wa kuhamasisha maeneo ya vijiji na kata jirani ili wakubali wazo la Manispaa ya Moshi kupanukia katika maeneo yao. Jambo la kusikitisha baada ya mchakato huo uliotumia fedha za ndani za Halmashauri, Serikali haijaleta majibu mazuri ya kuridhisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu wa Manispaa ya Moshi kuwa Jiji ni kuinua thamani ya mlima ambapo watalii wataiona Moshi kama Jiji la Mlima Kilimanjaro, hivyo kusaidia kuongeza idadi ya watalii wanaofika Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla na hatimaye kuhamasisha watu kuwekeza kwenye miundombinu ya utalii na hivyo kukuza uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao umeanguka kwa kiwango kikubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja wa ndege wa Moshi ni lazima uboreshwe. Hoja kwamba Kilimanjaro kuna uwanja wa KIA haitendei haki utalii wa Mlima Kilimanjaro ambapo uwanja wa Moshi ungetumika vizuri ungeweza kupokea ndege ndogo kutoka Mbuga za Serengeti na mbuga nyingine za wanyama za Kanda ya Kaskazini. Aidha, uwanja wa ndege wa Moshi unaweza kupokea ndege ndogo moja kwa moja kutoka Kenya, vilevile unaweza kusaidia kupokea helkopta za uokoaji katika Mlima Kilimanjaro kwa wale watalii wanaopata shida za afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utalii wa utamaduni unaweza kufanyika Moshi kwa kujenga Jumba la Makumbusho (Museum) ambalo litatunza historia ya watu wa Mkoa wa Kilimanjaro, hivyo kutumika kama eneo la kuvutia watalii kabla na baada ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Aidha, Msitu wa Rau katika Manispaa ya Moshi unafaa kutumika kama eneo la kivutio cha watalii kwa vile lina aina za miti ambayo haipatikani maeneo mengi duniani. Hivyo, ni vizuri ikawa kama recreational centre.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi, hii na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya na kuweza kuchangia katika hoja hizi za Kamati hizi mbili za PAC na LAAC.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitajikita kwenye Kamati ya Serikali za Mitaa na ninaunga mkono hoja zote ambazo zimeibuliwa na Kamati ya LAAC kwamba ni hoja za msingi zinazoonyesha baadhi ya matatizo ambayo yapo kwenye utendaji wa Halmashauri zetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nilikuwa naomba pia mindset za Wabunge zibadilike kidogo. The way tunavyokwenda tunataka kuipeleka Serikali inapotaka kwa mtazamo wangu. Lengo la Serikali ni kuua Serikali za Mitaa, ndilo lengo la Serikali. Tunapojaribu kwenda tunataka kuwathibitishia kwamba Halmashari hazina uwezo wa kutimiza wajibu wake jambo ambalo si la kweli kabisa. Halmashauri zetu zina uwezo wa kutimiza wajibu wake. Kama tutarudi nyuma, reform iliyofanyika mwaka 1998 mpaka 2008 ilikuwa ina lengo la kuzifanya Halmashauri ziwe na uwezo wa kujitegemea zaidi jambo ambalo Serikali ya Awamu ya Tano hailitaki kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja za Kamati zinasema Halmashauri hazina uwezo wa kukusanya fedha vizuri, zinakusanya kutoka wapi? Vyanzo muhimu vya mapato vimechukuliwa na Serikali Kuu. Sasa Halmashauri zinakusanya kutoka wapi? Mimi naamini bado Serikali ya Awamu ya Tano haina dhamira ya dhati ya kuzisaidia Halmashauri, ina dhamira ya kupora madaraka ya wananchi kuyarudisha kwenye central government. Mimi ndiyo ninachokiona katika mawazo yangu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi naomba, la kwanza kubwa kuliko lote Wabunge wailazimishe Serikali itambue wajibu wa Serikali za Mitaa na dhamira ya kuanzishwa kwa Serikali za mitaa za kupeleka madaraka kwa wananchi.
Tukifanikiwa kuifahamu hiyo dhana vizuri, na nimuombe Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI awaite Wenyeviti wa Halmashauri na Mameya wakae na Wabunge, kila mmoja azungumze matatizo ya Halmashauri ili Wabunge watambue vizuri matatizo ya Halmashuri ili wakijadili hapa ndani waelewe vizuri kwamba Halmashuri zina matatizo gani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu inawezekana hata sisi baadhi ya Wabunge hatufahamu vizuri matatizo ya Halmashauri ndiyo maana tunapelekea kuzilaumu Halmashauri kama vile wao ni wakosaji kuliko Serikali Kuu. Kwa hili la kwanza nilikuwa naomba kama Waziri mwenye dhamana anaona inafaa na itampendeza basi afanye hivyo kwa manufaa na malengo mazima ya kusaidia Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunazungumzia habari ya Wakurugenzi. Ukizungumzia Wizara nyingi kama Wizara ya Ujenzi utasikia wanakuambia tunataka tupate ma-CEO wazuri watakaoimarisha shirika la ndege, watakaoimarisha bandari, wengine mpaka tumewatoa nje. Lakini ni maajabu kwamba Wakurugenzi tunawachukua kutokana na itikadi zao za kisiasa tunawapeleka kwenye Halmashauri, kitu ambacho ni contrary kabisa na dhana ya uboreshwaji wa Serikali za mitaa tuliofanya 1998 mpaka 2008. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la uboreshwaji ni kwamba Wakurugenzi watafutwe watu wenye uwezo na ndiyo maana wakatakwa wasiusike na mambo ya kisiasa. Lakini leo Mheshimiwa Waziri wa Habari anatuambia kwamba Serikali imepeleka watu wa kutekeleza ajenda, watu wa kutekeleza ajenda ni Wakuu wa Wilaya. Watu wa kutekeleza ajenda ni Wakuu wa Mikoa, watu wa kutekeleza ajenda si Wakurugenzi wala Makatibu Tawala.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa unapopeleka hawa watu wa kutekeleza ajenda Wakurugenzi ni nani atakayesaidia Halmashauri zifanye kazi? Unapopeleka mtu kwa sababu unamfahamu kwa uzuri, haiba yake kwa namna anavyovyaa au kwa sababu ni rafiki yako, utafanyaje hizo Halmashauri zifanye kazi? Kila siku Taarifa za Kamati zitakuwa na madudu yasiyoisha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mmeona mwaka 2013/2014 kulikuwa na taarifa za hati safi za Halmashauri zaidi ya 133, 2014/2015 zaidi ya asilimia 68 ya Halmashauri zina hati chafu, ni kwa sababu gani, kwa sababu mmepeleka watu gani wenye uwezo wa kusimamia hizo Halmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo rai yangu kwa Serikali kama tunataka kuisaidia nchi hii lazima tuzisaidie Serikali za Mitaa. Kama tunataka kuua nchi hii tubaki na kauli na maneno yasiyoisha ya kisiasa tuue Serikali za Mitaa, ndio mtazamo wangu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tufike mahali ambapo tunawachagua Wakurugenzi kwa vigezo. Kama ni lazima sana tubadilishe Sheria Namba 7 na Namba 8 hapa ili tupeleke Wakurugenzi ambao wamechaguliwa kwa vigezo, si Wakurugenzi wanaopelekwa kwa sababu ya kujuana. Ukiangalia wakurugenzi waliopelekwa katika Halmashauri leo kuna watu wanaowatetea hapa. Kuna Wakuu wa Idara wenye uwezo kabisa lakini hawakuchaguliwa kuwa Wakurugenzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninajua ni mamlaka ya Rais na mimi sitaki kubishana na mamlaka ya Rais lakini Rais ashauriwe vizuri. Anachagua akina nani wa kwenda kwenye Halmashauri? Leo mnazungumzia habari ya ubovu wa mwaka 2014/2015 sasa mtaona madudu mwaka wa 2016/2017, ndio mtakaoona madudu kwa watu mliowapeleka Halmashauri. Naomba hilo suala lichukuliwe katika uzito wake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna suala la Halmashuri, kama nilivyosema kwamba mnasema halikusanyi vyanzo vya mapato. Tumekuja kwenye Bunge la Bajeti hapa mmechukua chanzo muhimu sana cha Halmashauri cha kodi ya majengo na mmetudanganya hapa ndani ya Bunge kwamba chanzo kile mmeshakikusanya mtakuwa mnakusanya kama vile mnavyokusanya asilimia 30 ya land rent na mtarejesha. Tunapozungumza leo hakuna shilingi moja imerejeshwa, Halmsahauri zinafanyaje kazi? Mtakuja kuzilaumu kila siku kwenye Taarifa za LAAC na LAAC yenyewe ndiyo hiyo hata fedha hamuipi, hamumpi Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Mahesabu ya Serikali fedha kwa sababu hamtaki Halmashauri zifanye kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba vyanzo ambavyo ni vya lazima, kwa sasa hivi kuna mpango kwa mujibu wa sheria tuliyopitisha, inawezekana hata mkachukua service levy katika Halmashauri, Halmashauri zitajiendesha na nini? Kwa hiyo naomba vyanzo vya Halmashauri viachwe, halafu tuwapime Wakurugenzi na Watendaji wa Halmashauri kwa uwezo wao. Tuwaongezee manpower, tuwaongezee namna ya kukusanya vizuri, TRA hawana uwezo wa kukusanya mapato yote katika nchi hii kama mnavyotaka kuwapa hiyo burden ambayo hawaiwezi. Mapato ya bandari hawawezi kukusanya, mapato ya utalii hawawezi kukusanya, mnataka kuwaongezea mapato ya Halmashauri ya sababu gani? Nilikuwa naomba Serikali iliangalie hilo kwa makini sana kama mnataka kuzilaumu Halmashauri kwamba hazina uwezo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za miradi ya maendeleo haziendi, hazipo. Angalau kule nyuma tulikuwa tunapata asilimia nane, asilimia tano, leo hazipo mpaka tunavyozungumza karibu nusu ya kwanza inakwisha, hakuna fedha za mradi wa maendeleo. Leo kuna hoja yetu ya Kamati inasema miradi mingine inachukua muda kukamilika, itakamilikaje kwa muda kama fedha haziendi? Miradi inakamilikaje kwa muda wakati fedha hampeleki? Miradi mingine mingi inategemea fedha za Serikali kuu, haziendi! Itakamilikaje? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna hoja ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwamba hati nyingi chafu zimesababishwa na Halmashauri kutokuwa na taarifa sahihi ya mali zake iliyonazo.
Sasa mimi nashauri Serikali na nakushauri Mheshimiwa Waziri, zisukume Halmashauri zote zitengeneze database, zifahamu wapi zinakusanya mapato, zifahamu mali zake iliyonazo (inventory) zake ili hiyo hoja ya ukaguzi isijirudie tena. Na ili zifanye hivyo ni lazima zitenge fedha ya kutosha kwenye bajeti katika kitengo cha takwimu. Bila ya kutenga fedha za kutosha katika kitengo hawatafanikiwa, hizi hoja za ukaguzi zitaendelea na bado Halmashauri zitapata hati chafu, zenye mashaka ambazo sio za lazima.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la kukaimu, kwamba ni mojawapo ya sababu ambazo zinazifanya Halmashauri zisifanye vizuri. Kamati imeonesha kwamba Serikali inachelewa kupeleka permanent employer’s katika Halmashauri, hilo ni tatizo la kwanza ambalo Serikali inatakiwa ikabiliane nalo.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, Wakurugenzi wetu tunaowachagua hawakai maofisini kufanya kazi zao, wanakaimisha nafasi zao kila siku. Mkurugenzi anakaimisha nafasi yake kikao cha Kamati ya Fedha hayupo, yupo kwenye Kamati ya Siasa ya CCM anakuwa anapeleka taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, sasa utafanyaje kazi? Mkurugenzi hakai. Leo ameitwa na Mkuu wa Mkoa asubuhi, Mkurugenzi anaripoti kwa Mkuu wa Mkoa asubuhi, kwa Mkuu wa Wilaya jioni. Halafu hawezi kukaa kwenye Halmashauri, atafanyaje kazi zake?
Sasa matokeo yake sio tu kwamba kukaimisha kwa maana hiyo ya kwamba Serikali haijapeleka hao waajiriwa wa kudumu lakini hata Wakurugenzi wenyewe hawakai kwenye Halmashauri zao kufanya wajibu wao. Matokeo yake Mkurugenzi muda wote anapata taarifa zake za utekelezaji kupitia kwa watu wa kukaimu tu, kwa hiyo hapati taarifa ambazo ni sahihi, hapati namna ya kupambana na madiwani wake ili ajue namna ambavyo anaweka madiwani wake sawasawa ili wapeleke Halmashauri mbele. (Makofi)
Kwa hiyo ni lazima utoe agizo, Wakurugenzi wasimamie vikao vyote wanavyovisimamia katika Halmashauri unless kuwe na strong reason. Lakini kila Mkurugenzi kikao cha Baraza anakuwa yeye, kikao cha Kamati ya Fedha anakuwa yeye, kikao cha Afya na Uchumi anakuwa yeye, kikao cha Mipango Miji anakuwa yeye ili apate taarifa halisi kama Katibu halisi wa Baraza. Otherwise kila siku watakuwa wanaletewa taarifa za uongo na hata kujibu kwenye Kamati hawawezi kujibu wanapoitwa kwenye vikao.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nataka nizungumzie suala la internal auditors ambalo limezungumzwa kama tatizo pia kwenye Taarifa ya Kamati.
Mheshimiwa Naibu Spika, internal auditors tulionao ni kweli kwamba wanafanya kazi chini ya Mkurugenzi, na kwa misingi hiyo wataripoti according kwa matakwa ya Mkurugenzi kwa sababu hawana fedha wakipewa fedha kidogo wataripoti kadri Mkurugenzi anavyotaka. Sasa usipopeleka Mkurugenzi ambaye ni mahiri ukapeleka Mkurugenzi mla rushwa, Mkurugenzi asiye na mtazamo, asiyefahamu kwamba Halmashauri ni sehemu yake kwa vyovyote vile internal auditors hawezi kumsaidia Mkurugenzi na Halmashauri lazima ifanye vibaya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini wakati mwingine internal auditors wanaweza wakawa wanasaidiana kuharibu Halmashauri kwa sababu wakati mwingine wanaweza wakatumiwa vibaya na hata madiwani ambao hamtaki kuwapa mafunzo. Mmeamua sasa hivi kwamba Madiwani hawapati mafunzo, Diwani hawezi kwenda hata kwenye Halmashauri nyingine kujifunza mpaka Mkuu wa Mkoa atake.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hizi Halmashauri mnapozibana namna hii, zinapokuwa na intervention ya Mkoa namna hii, Wakuu wa Mikoa wanaingilia Halmashauri, Wakuu wa Wilaya wanaingilia Halmashauri, kila mmoja na kauli yake, mnapelekaje Halmashauri? Halmashauri kwa mujibu wa Katiba yetu ni Serikali ambayo ni ndani ya Serikali Kuu, na zina utaratibu wake. Wajibu wa Mkoa ni kutoa ushauri, wajibu wa Wilaya ni kutoa ushauri, si kuziingilia Halmashauri. Leo Wakuu wa Mikoa, Wilaya wanaziingilia Halmashauri kama ni vyombo vyao vya pale ofisini, kama ni Idara katika ofisi zao. Zinawezaje zikafanya kazi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunalalamika hapa bure tu kuhusu Halmashauri. Wanaoua Halmashauri hapa ni Serikali Kuu, anayeua ni Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa. (Makofi)
Kwa hiyo kama tunataka kuzisaidia Halmashauri, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa asaidiwe, aelimishwe, zifanyeni Halmashauri zilizo na creativity, watu wawe wabunifu, watu wawe na uwezo wa kujituma, watu waweze na kubuni mikakati yao halafu wasaidieni. Saidieni Halmashauri katika dhana ya PPP zifanye kazi vizuri na hizi hoja za ukaguzi yatapungua sana. Lakini bila kuzisaidia hizi hoja za ukaguzi yatakuja kila siku mpaka mtachanganyikiwa hapa Bungeni tu. Wabunge mtawalaumu Madiwani Bure, mtawalaumu Wakurugenzi bure lakini tatizo liko kwenye central government, ndio mtazamo wangu na mimi nashauri Serikali ilichukue katika uzito wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama muda wangu haujaisha nilikuwa naomba sana tuyatilie uzito mawazo ya wenzetu kwamba CAG apewe fedha ya kutosha, Kamati ya LAAC ipewe fedha ya kutosha, iende kwenye Halmashauri ifanye ukaguzi wa kutosha, itatusaidia sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ya PAC ipewe pia fedha za kutosha. Tuzisaidieni hizi Kamati kama overside committees zetu ziweze kutusaidia kujua Halmashauri zilivyo na kujua na sisi tulivyo ili tusaidiane katika kuhakikisha kwamba nchi hii inakwenda mbele. Bila kusaidiana sisi Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, mtakaa mkitoa maagizo; ni kweli kabisa kwa mujibu wa taarifa ya Kamati Halmashauri nyingi zimekuwa zikibadilisha matumizi yake kutokana na maelekezo ya Serikali Kuu, kutokana na maelekezo ya Mkuu wa Mkoa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, watu wana mpango wao wanaambiwa kuanzia leo mnajenga maabara, fedha zinatoka wapi? Hawaambiwi. Lazima Mkurugenzi afanye hivyo maana ni muoga atafanye? Asipofanya vizuri atatumbuliwa. Madawati yameagizwa anafanya nini? Asipofanya hivyo anatumbuliwa, hata akifanya akija kwenye hoja ya ukaguzi inampiga, anatumbuliwa. Wakurugenzi hawana hata mahali pa kupumulia wakati mwingine kwasababu mnawaumiza. Wakuu wa Idara hawana mahali pa kupumulia, ni waoga kwa sababu wanakwenda pale wakitishwa na mambo ya itikadi. Tuacheni mambo ya itikadi tuamueni kupeleka hili Taifa mbele ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie tena kuipongeza Kamati, imefanya kazi yake vizuri na nadhani tuna umuhimu wa kuchukulia uzito matatizo waliyoyaona lakini Serikali itimize wajibu wake ili twende mbele. Ahsante sana kwa kunisikiliza.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchangia kuhusu Annual Motor Vehicle License. Nashauri Serikali katika Mpango wake iangalie namna ya kurekebisha sheria hii ili isiwaumize wanaomiliki vyombo vya moto na wale wanaouza vyombo vya moto. Aidha, Serikali iweke katika Mpango wake namna ya kusamehe malimbikizo ya kodi hiyo kwa watu waliouza vyombo vya moto kama pikipiki halafu waliouziwa hawakubadilisha umiliki.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza na mimi nizipongeze Kamati zote kwa uwasilishaji mzuri, lakini ntajikita kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuongelea kidogo suala la asilimia 10 ya vijana na akinamama. Suala hili limekuwa mara nyingi likiongelewa na Waheshimiwa Wabunge wakilalamika kwamba fedha zile hazipatikani katika halmashauri. Kwa hili kidogo nitofautiane na mawazo ya Kamati, kwamba iletwe sheria Bungeni ya kuzilazimisha halmashauri zitenge fedha hii. Halmashauri zetu hazina fedha za kuendesha shughuli zake za kila siku, leo tukipanga kuzitengenezea sheria ya kuzilazimisha zitenge fedha hii maana yake tunataka kuzimaliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema Kamati ingeshauri Serikali ihakikishe Fedha za Matumizi ya Kawaida (OC) zinapatikana katika halmashauri zetu ili fedha za OC zikipatikana zisaidie zile fedha za ndani zinazokusanywa kupangwa katika asilimia tano ya vijana na asilimia tano ya akinamama, lakini kulazimisha halmashauri kupata maziwa ya kulisha halmashauri zao mpaka ipatikane damu ni vigumu sana. Kwa hiyo, naomba hili kKmati kidogo iliangalie katika sura nyingine pamoja na maoni mazuri ya Kamati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi halmashauri zina wajibu mwingine mkubwa wa kutenga fedha katika Mfuko wa Watu Wenye Ulemavu katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017. Yote hiyo ni wajibu wa halmashauri na hizo fedha ni lazima zitengwe, lakini halmashauri hazina uwezo wa kujiendesha. Vyanzo vya halmashauri vingi vimechukuliwa na Serikali Kuu, halmashauri zinajiendesha vipi? Utaratibu wa makusanyo ya halmashauri wenyewe umebadilika mno kutokana na maelekezo ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa Bunge la Bajeti tulishauri hapa, katika maeneo ya manispaa na majiji yale makusanyo yaliyokuwa yanafanywa na mawakala yaliyofanyiwa tathmini na Benki ya Dunia kwa miaka zaidi ya 10 yasibadilishwe utaratibu wake kwa sababu Halmashauri nyingi zitadhoofika katika makusanyo ya mapato, lakini kwa bahati mbaya, wakati mwingine kwa kiburi cha wakubwa, mlikataa kusikiliza. Leo halmashauri nyingi zimeshindwa kutumia mawakala katika kukusanya fedha katika mpango wenu wa kutumia commission, halmashauri zinajiendesha vipi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tusije tukakaa hapa tukizilaumu halmashauri tukiwalaumu Wakurugenzi bure wakati sisi wenyewe ndio tumewabana tukashindwa kuwafanya waweze kutimiza wajibu wao, Wabunge ni sehemu ya Madiwani, ni vizuri mjue shida ambazo Wakurugenzi na Madiwani wanazo katika Halmashauri zenu ili mkizungumza muwe mnaelekeza, maana wakati mwingine Serikali inavua majukumu yake na lawama zake inataka kuzihamishia kwenye halmashauri peke yake. Kwa hiyo, nadhani kwamba kwa hili Kamati ingeangalia vizuri na Serikali ni vizuri ikaangalia vizuri namna ya kuziboresha na kuimarisha Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bado mimi naendelea kusisitiza kwamba dhamira ya Serikali Kuu katika kuimarisha Serikali za Mitaa bado haijawa nzuri sana, ni vizuri Serikali Kuu iangalie mtazamo wake na dhamira yake ya kuimarisha Serikali za mitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la mdororo wa elimu pamoja na dhamira ya Serikali ya kutoa elimu, sijui bure ama bila malipo – maana mpaka sasa sielewi terminology halisi ni ipi, ni elimu bure ama ni elimu bila malipo. Nashauri kwamba miundombinu sio mizuri, lakini hata kama tukiimarisha miundombinu ya elimu ni vizuri tuangalie namna ya kuzisaidia shule za Serikali. Shule za Serikali hazifanyi vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Kilimanjaro kwa mfano, tulikuwa tuna utaratibu wa kuwalisha watoto chakula wakati wa mchana shuleni, chakula cha kawaida kabisa, lakini wazazi walikuwa wanalazimishwa kutoa michango kwa ajili ya kuhakikisha watoto wao wanakula shuleni. Baada ya tamko la Serikali la elimu bure mindset za wazazi na wananchi zikaamini kwamba sasa hawapaswi tena kuchangia chochote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni vizuri mkaainisha, mkitamka elimu bure mmedhamiria nini? Inawezekana mmedhamiria ada, kwamba wazazi hawatalipa ada ile ya sh. 20,000 katika shule za kutwa na shilingi 70,000 katika shule za mabweni, maana shule za msingi hazikuwa na ada. Ni vizuri mka-specify mnazungumzia nini katika suala la elimu bure ama elimu bila malipo ili wananchi waelewe Serikali hasa ni nini ambacho haichangii na wananchi wanapaswa kuchangia nini ili watimize wajibu wao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya nchi hii ilikuwa ya ujamaa na kujitegemea, bado mmeandika kwenye Katiba kwamba iko hivyo kwa sasa. Wananchi mindsets zao ni hivyo hivyo kwamba nchi hii ni ya ujamaa na kujitegemea, kwa hiyo huduma zote zinatolewa na Serikali. Wananchi ndio tulikuwa tunawabadilisha kidogo wafahamu kwamba na wao wana wajibu wa kuchangia baadhi ya huduma. Leo mnakuja na propaganda za kisiasa za elimu bure, matokeo yake mnawabadilisha wananchi wanatoka walipokuwa wanakwenda mbele mnawarudisha nyuma bila kuwa na fallback position kwamba mnawasaidiaje katika hatua hizo. Kwa hiyo, ndugu zangu nafikiri Waheshimiwa Wabunge waliangalie hili kwa mapana ili waone namna ya kulisaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la utawala bora. Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, tukiwalaumu tunawaonea bure kwa sababu nimeona hata spirit ya Waziri wa Ofisi ya Rais ,TAMISEMI, ndiyo hiyo hiyo ya udikteta fulani na ndiyo maana anaweza akasema ni halali Wakuu wa Mikoa kufanya wanachoweza kufanya kusumbua viongozi wenzao katika maeneo mbalimbali, sasa inaonekana maelekezo ya nini wafanye Wakuu wa Mikoa yametoka juu, si maamuzi yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nashauri sana kwamba ni vizuri ninyi viongozi wa juu mbadilike, badilisheni mwelekeo wenu. Serikali ya Awamu ya Nne ilikuwepo, ya Awamu ya Tatu ilikuwepo, Wakuu wa Mikoa kweli hawakuwa hivyo, walikuwepo wala Katiba haijabadilika, wajibu wao baina yao na Halmashauri unaeleweka na wanaujua, ni kwa nini Serikali ya Awamu ya Tano Wakuu wa Mikoa ndiyo wabadilike, wamezaliwa upya, wameanguka kutoka mbinguni? Kwa nini waende kukamata watu, wakamate Walimu, wakamate Madaktari, wawaweke ndani kama wanaweka ng‟ombe na mbuzi na ninyi mnaangalia mnaona jambo la kawaida? Kwa nini mnaondoa ule moyo wa wafanyakazi na watumishi kufanya kazi katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri Ofisi ya Rais, TAMISEMI ikaliangalia hili jambo kwa uzito wake ili wafanyakazi wale wafanye kazi kwa moyo. Wafanyakazi na watumishi katika maeneo mbalimbali hawana moyo kwa sababu ya maelekezo mnayowapa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, wamepoteza mwelekeo wa wajibu wao kabisa, sasa hivi wamekwenda kuvuruga kabisa mikoa na wilaya zao na halmashauri, kwa hiyo ni jambo la msingi sana kuliangalia katika uzito wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la rushwa. Rushwa imekuwa ni utamaduni katika nchi hii kwa muda mrefu, lakini inavyoonekana kuna jitihada ambazo inaonekana zinafanyika ambazo huwezi kukwepa kuziona kwamba ni za muhimu, lakini jitihada hizi zinafanywa na mtu mmoja; inakuwa ni one man show kwamba anayeweza kupambana na rushwa ni mtu mmoja, ni Mheshimiwa Rais. Hajaweza kuimarisha mifumo yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante na naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kwa kuanza niipongeze sana Hotuba ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na ningeomba basi Serikali ichukue yale mazuri yote ambayo inaona yanaweza yakaisaidia Serikali kufanya kazi zake vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwenye Hotuba ya Waziri Mkuu nichangie suala la demokrasia. Hotuba ya Waziri Mkuu inaonesha kwamba, hali ya demokrasia katika nchi yetu inaboreshwa, lakini ningependa Serikali ijitathmini kama kweli Taifa hili sasa linasimamia misingi ya demokrasia. Ni vizuri ijitathmini kwa makini kwa sababu, kuna kila viashiria vya kuporomoka kwa misingi ya demokrasia katika nchi yetu,
kila viashiria vya kukosekana kwa uhuru wa habari, viashiria vya kukosekana kwa utawala unaofuata sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni vizuri Serikali ikajitathmini kwa sababu hata yote yaliyokuwa yanatokea asubuhi hii, yanalalamikiwa na Waheshimiwa Wabunge, ni kuonesha namna ambavyo misingi ya utawala bora katika Taifa hili imeshaanza kupotea.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wananchi wanapiga kelele kuhusu marekebisho ya Katiba walikuwa wanaona kwamba wana haki bado ambazo hazijakaa sawasawa katika dhana nzima na muktadha wa demokrasia katika nchi hii, lakini angalau kipindi hicho walipokuwa wakipiga kelele hali ilikuwa ni nafuu kidogo, lakini leo hali imekuwa mbaya zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inatuonesha kwamba kuna kuboreshwa kwa hali ya demokrasia na misingi yake katika nchi hii. Naendelea kusisitiza ni vizuri Serikali ijitathmini sana katika suala hili. Haiwezekani leo tuseme kuna misingi ya demokrasia katika nchi hii wakati vyama vya siasa haviruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara, likiwa ni jukumu lake la msingi kabisa la kisheria na Serikali imekaa kimya na viongozi wakubwa wa nchi hii wanaunga mkono jambo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, inakuwaje Serikali isijiamini kiasi kwamba leo inakuwa sawa na kumfunga adui yako minyororo mikononi kwenye mti ukampiga kadri unavyoweza halafu ukajisifu kwamba unafanya vizuri. Kwa sababu kama leo unazuia vyama vingine visifanye kazi ya siasa, halafu kuna mtu mmoja peke yake kwa sababu ni Mwenyekiti wa chama kimoja cha nchi hii, kwa kutumia kofia yake aliyonayo ya mamlaka yake anaweza akazunguka nchi nzima akijaribu kuzungumza yale ambayo anatenda yeye, hatakiwi ajibiwe, hatakiwi akosolewe, ni Taifa la namna gani? Demokrasia inakuwa iko wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi leo Mheshimiwa Rais anatupa Kauli Mbiu ya HAPA KAZI TU; kwa nini Rais asijue kwamba kazi ya Wanasiasa ni kufanya siasa? Kwa nini hajui kwamba viongozi wa vyama vya siasa wajibu wao, kuanzia kiongozi wa tawi mpaka Taifa ni kufanya siasa? Kwa nini umpangie kiongozi wa kisiasa kufanya vikao vya ndani tu? Kwa nini nchi hii wanasiasa wanaoruhusiwa kufanya kazi wawe ni Wabunge tu, lakini viongozi waliopewa kazi ya kisiasa, Makatibu, Wenyeviti na Viongozi wengine wazuiwe kufanya kazi zao za kisiasa kwa sababu ya kuogopa vivuli vyetu wenyewe?
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri Serikali ijitathmini kama kweli nchi hii inatimiza misingi ya demokrasia. Kama inajiangalia vizuri, vyama vya siasa viruhusiwe kutimiza wajibu wake wa kufanya kazi za kisiasa kwa sababu chama cha siasa ni lazima kinadi sera zake, ni lazima kinadi falsafa yake, ni lazima vinadi itikadi zao, kikiwemo Chama cha Mapinduzi ambacho kinatakiwa kitetee Serikali yake. Vyama vya Upinzani viikosoe Serikali ili Serikali ijitathmini na ijitazame kama iko sawasawa. Sasa kama vitu hivyo haviruhusiwi katika Taifa hili demokrasia iko wapi ndani ya Taifa hili? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani si sahihi Mheshimiwa Waziri Mkuu kusema kwamba misingi ya demokrasia katika Taifa hili inatekelezwa; labda atwambie tumerudisha nchi hii nyuma miaka 40 sasa, jambo ambalo si jema na sio lenye afya katika Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nijiulize, Serikali inajipimaje kwa wananchi wake wa kawaida kama haitaki kusikia kutoka kwingine? Haitaki kusikia wananchi wanasema nini. Mnasubiri tafiti za kitaalam ambazo mara nyingine zinatolewa kwa woga wala haziwezi kuwapa picha nzuri ya namna ambavyo Taifa lipo, lakini hamjui wananchi wa chini wanasema nini kuhusu ninyi; mtawajua kama mtaruhusu wing hii ya pili ifanye kazi yake ya kisiasa vizuri, mtasikia malalamiko ya wananchi na mtajua mmekosea wapi na mjirekebishe wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani Serikali inapaswa kutimiza wajibu wake vizuri katika kuhakikisha kwamba inasimamia misingi ya demokrasia katika Taifa hili ili tusije tukaliingiza Taifa hili katika matatizo. Nchi hii yetu sote; tumezaliwa hapa na tutafia hapa, tunapaswa kuipigania katika nyanja zote ili tuhakikishe kwamba wote tunaishi maisha ya furaha katika Taifa la Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la usalama wa kiuchumi katika nchi hii. Wananchi wanaumia. Taarifa ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inasema kwamba hali ya uchumi na usalama wake uko vizuri. Lakini leo wafanyabiashara hawana uhakika na biashara zako; wafanyabiashara hawajui kwamba kesho kutatoka tamko gani na nani atazungumza nini. Wakulima vile vile hawajui kwamba wanaishi maisha gani yenye uhakika na wafugaji vile vile.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini leo Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inatuonesha kwamba kuna utulivu wa kiuchumi. Leo benki hazikopeshi kwa sababu hazina uwezo wa kukopesha; tunaambiwa kwamba benki zina mitaji na zipo vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri Serikali pia katika eneo hili ijiangalie na iangalie vizuri kwamba tulipokuwa na tulipo pana tofauti gani, na kwa nini kulikuwa na hali nzuri ya watu kukopa na kukopesheka na kulikuwa na utulivu wa kufanya kazi. Leo maafisa wa TRA hujui ni wakati gani watafilisi mwananchi, leo hawajui ni wakati gani benki itafilisi wananchi kwa sababu wananchi hawana uwezo wa kulipa. Sasa katika sura hii tunaendeshaje hii nchi na huu uchumi wa viwanda tutaupata kwa namna gani? Ni lazima Serikali ijipime sana katika eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la utalii; Mkoa wa Kilimanjaro umebahatika kupata Mlima Kilimanjaro. Mlima ambao ndio unaowakilisha Taifa hili katika sura ya vivutio vya utalii ambavyo vina heshima duniani.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeomba Mkoa wa Kilimanjaro Mji wetu wa Moshi upate hadhi ya kuwa Jiji. Nadhani Serikali ingetusikia kilio chetu; haiwezekani Mkoa ambao una kivutio cha utalii ambacho ndio kinachochangia pato kubwa katika sekta ya utalii kuliko kivutio kingine
chochote kile ishindwe kupata Jiji kama yalivyo Majiji mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali isikie kilio chetu cha kufanya Mji wa Moshi uwe Jiji ili tuweze kuongeza shughuli za utalii katika Mkoa wa Kilimanjaro ili tuweze kuongeza watalii na kuongeza pato la Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia nilikuwa naomba Serikali isikie kilio chetu cha kukarabati uwanja wa ndege wa Moshi, uwanja ambao umejengwa tangu wakati wa malkia. Lakini leo imekuwa ni kazi kweli kukarabatiwa mpaka umekuwa ni gofu; eneo lile sasa lipo katika mazingira hatarishi na inawezekana hata watu wakalivamia. Kama lingejengwa ni eneo ambalo lingeinua sana utalii kwani ni uwanja wenye
uwezo wa kujiendesha wenyewe. Nilikuwa naomba Serikali itazame kama ina dhamira kweli ya kuinua utalii katika taifa hili na kuinua pato la taifa kupitia utalii na pia kusaidia wananchi wa Kilimanjaro kujiinua katika uchumi wao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie suala la viwanda. Viwanda vingi vya Moshi vimekufa, na ni vile ambavyo vilibinafsishwa kwa sera mbovu ya ubinafsishaji ambayo imeumiza sana uchumi wa viwanda katika Taifa hili. Sasa naiomba Serikali isimame katika maneno yake,
kwamba kwa muda mfupi uwezekanavyo viwanda ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa na waliobinafsishiwa wakashindwa kuvifanyia kazi basi wanyang’anywe kama hawawezi kuendelea kuviendeleza na kama wanaweza kuviendeleza waviendeleze ili wananchi wapate ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu viwanda zaidi ya kumi na tano Mkoa wa Kilimanjaro vimekufa lakini tunalalamika hakuna ajira; tunaanza kufikiri ajira za kupitia kwenye mifuko ya vijana na akinamama ya Halmashauri, tunawaza kufikia ajira kupitia Mfuko wa Taifa wa Ajira wa Vijana lakini tuna viwanda ambavyo vipo, vilikuwa vinatengeneza ajira leo vimekufa na Serikali haioneshi jitihada zozote za kuhakikisha ajira zinapatikana. Naomba viwanda vile vifanyiwe kazi, vifunguliwe mapema ili viweze kufanya kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii, na mimi naomba kidogo nichangie kwenye Wizara hii ya Elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia kwenye suala la elimu bure ama elimu bila malipo. Sera hii ni sera nzuri kwa maana ya kuwasaidia Watanzania wengi ambao watoto wao walikuwa hawajaandikishwa mashuleni, kama Kambi ya Upinzani ilivyotoa hotuba yake ni hii ni sera inayohitaji tathmini ya hali ya juu ili kuwa na manufaa katika Taifa, vinginevyo inaweza ikawa ni sera yenye matatizo ambayo baadae tutakuja hapa Bungeni kuanza kusutana wenyewe kwa wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafikiri kwamba ni lazima tuangalie namna gani tunapokea mapendekezo ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuangalia miundombinu ya elimu yetu, kuangalia majengo yetu ya utawala, kuangalia ikama ya walimu wetu katika kuhakikisha kwamba watoto

wanaoandikishwa wanapata elimu bora. Shida ya mfumo huu ni kwamba sasa unasababisha elimu iwe katika ubora wa hali ya chini sana na lengo siyo kuwa na mfumo ambao utaturudisha katika elimu ambayo haina ushindani. Ni lazima kuwe na ushindani kati ya elimu inayotolewa na private school na elimu inayotolewa na shule zetu za umma. Sasa ushindani huo haupo kwa sasa. Kwa upande wa shule zetu za umma na shule za private bado dhana si kuwasaidia wazazi wapeleke watoto wao katika shule za umma, dhana inawafanya wazazi sasa wapeleke watoto katika shule za private. Kwa hiyo, wasio na uwezo bado hawasaidiwi katika huu mfumo tulionao. Ni vizuri sana tuangalie huu mfumo kwa upana wake wa kutosha ili uwe na faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uelewa wangu hata huko nyuma kinachoendelea sasa kilikuwa kinafanyika, kwa sababu kilichoondolewa hapa kwa upande shule za msingi ni ada ya kuandikisha wanafunzi shuleni ambayo ndiyo ilikuwa kikwazo. Kwa mfano, sekondari ni ada ya shilingi 20,000 ama 70,000 lakini kwa upande wa tuition ilikuwa inabebwa na Serikali mlichokitangaza ni kuondoa michango ambayo wazazi walikuwa tayari wanalipa matokeo, yake wazazi wameamua ku-relax hawataki kulipia michango watoto wao. Sasa hivi mmezilazimisha Halmashauri zianze kukamata wazazi na kuwapeleka polisi kuanza kuwafungulia kesi na bahati mbaya kwa sababu hamkuwa na transitional period, hamkujiandaa vizuri namna gani baada ya kutangaza huu utaratibu mtahakikisha kwamba ni namna gani Halmashauri zinawabana wazazi, sasa wanatumia Sheria ya Ustawi wa Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kw ahiyo ni rai yangu kwako Mheshimiwa Waziri, kwa sababu ni sera, zielekezeni Halmashauri zianzishe by-laws ambayo itawalazimisha wazazi waweze kulipia watoto wao na kama hawawalipii waweze kuadhibiwa kwa Sheria za Halmashauri zisizozidi shilingi 50,000 kuliko sasa kuwapeleka Polisi unnecessarily. Kwa hiyo nilikuwa nafikiri ni jambo la msingi sana kuliangalia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie habari ya maslahi ya walimu. Kwanza walimu wana madeni mengi wanaidai Serikali kama Kambi ya Upinzani ilivyoonesha, ambapo bado kuna zaidi ya shilingi bilioni 138 wanadai hawajalipwa. Hiyo inaondoa moral yao ya kutimiza wajibu wao wa kuelimisha watoto wetu, hivi hapa katika Serikali ambayo ina miaka zaidi ya 55 bado tunapaswa ku-debate habari ya maslahi ya walimu ya madeni yao badala ya kufikiri kwamba ualimu ingetakiwa iwe ni rear professional ambayo tunatakiwa watu watu wanaokuwa Walimu tuwalipe vizuri. Leo ualimu umekuwa kama ni ile ajira ambayo inatupiwa watu walioshindwa ndiyo mtu anakuwa mwalimu, haiwezekani! Hatuwezi kulea Taifa ambalo wanaopaswa kuelimisha watoto wetu ndiyo tunaifanya ni professional ya mwisho kabisa, mtu akipata division four ndiyo anakuwa mwalimu. Division zero aliyefeli ndiyo anakuwa mwalimu lazima tubadilishe huu mtazamo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunataka kuwa na elimu bora lazima tutenge maslahi ya kutosha kwa walimu. Kwahiyo nilikuwa nadhani……….

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia kwenye Wizara ya Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuna hoja ambayo imekuwa-raised kwamba inawezekana ndoto yetu ya kufikia Tanzania ya viwanda ina mashaka makubwa. Lakini imeonekana kama vile ni uchokozi ambao upande mwingine haukuutaka. Lengo la Kambi ya Upinzani kuonyesha wasiwasi wetu kwa dhana hii kufikiwa, ni vizuri Serikali ikalichukulia hili kama changamoto na isiwe ni sababu ya kuanza kuleta malumbano yasiyo ya lazima.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1967 Tanzania ilishaanza hatua hizo za kujijenga katika dhana mzima ya Industrial Revolution na bahati mbaya tulienda na dhana hiyo tukiwa na mtu ambaye ni dedicated ambaye alikuwa Rais wetu wa Kwanza wa nchi hii. Hata hivyo mwaka 1996 dhana ile tuliiua wenyewe. Na bahati nzuri mwaka 1996 kwa lengo hilo la ubinafsishaji tulikuwa na dhamira kwamba tunaweza tuka-develop zaidi kama tutakuwa tume-adopt vizuri dhana ya ubinafshaji ambayo bahati mbaya hatukuweza kuifanyia kazi vizuri. Sasa wasiwasi wetu ni kwamba kama Sustainable Industrial Development Policy ya tangu mwaka 1996 mpaka leo haijaweza kufanya kazi vizuri, nini miujiza ya kuifanya kwa miaka mitano? Ndio wasiwasi wetu. Sasa nafiki ni vizuri tungeichukua kama changomoto muhimu sana Serikali ilituweze kuifanyiakazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa kipindi hicho vikwazo vilivyokuwa vinakabili sekta ya viwanda ndiyo ambavyo viko sasa, tangu 1996. Wachambuzi waliokuwa wanatunga hii Sera ya Sustainable Industrial Development Policy waliona kwamba tuna vikwazo vya unfavorable legal and regulatory framework ambazo zilikuwa ni kikwazo kimojawapo, limited access of SMEs to finance, cha pili; cha tatu kilikuwa infective and poor coordinated institutional support framework; vitu ambavyo mpaka leo tunavizungumza kwamba ni tatizo katika nchi hii.

Sasa lazima tuone kwamba tuna mahali ambapo panatukwamisha na kwa pamoja tufikiri namna gani tunatoka hapa kwenda mbele ili tufikie hiyo ndoto ya Tanzania ya viwanda. Kwa hiyo ni vizuri mkaichukua kwa uzito wake hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la pili ambalo linafanya tuone mashaka ya viwanda ni soko letu la ndani. Tuna soko la ndani la kiwango gani. Nini uwezo wa watu wetu kununua katika soko letu la ndani, purchasing power yetu. Ukizingatia kwamba viwanda anavyovihubiri Mheshimiwa Waziri ni viwanda vidogo sana vyenye kuajiri mtu mmoja mpaka watu watano; viwanda vidogo vinavyofuatia vyenye kuajiri watu watano mpaka watu 49 na viwanda vya kati vyenye kuajiri watu 49 mpaka 99.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda hivi vinatengemea sana soko la ndani, soko ambalo hatuna kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano imechukua fedha zote ambazo zilikuwa za Serikali ikaziamishia Benki Kuu na ni sawa tu na hadithi ile ya mtu aliyechukua rupia akaifukia chini ya ardhi. Haiwezekani uchukue fedha zile ambazo zilikuwa kwenye mzunguko uzipeleke benki ukiamini ndio uwekezaji.

Kwa hiyo, matokeo yake tumepunguza sana mzunguko wa fedha katika uchumi wetu, tumepungusa uwezo wa uwekezaji katika uchumi wetu na kwa misingi hiyo purchasing power ya watu imepungua, sasa kwa hawa watu wanaozalisha wanakwenda kumuuzia nani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio leo tunaambiwa kwamba kuna hata soko la kuuzia bidhaa za kiwanda cha bidhaa za kupambana na malaria zimekosa soko kwa sababu hatuna soko la ndani. Sasa tunafikiaje haya malengo? Hili ndilo suala la msingi la kujadili kwa pamoja ili tuone tunavyoweza kufikia lengo la kuwa na Tanzania ya viwanda. Kwa hiyo ni vizuri tukayachukua haya masuala kwa uzito wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, wafanyabiashara wa ndani kama wengi walivyosema hawana mazingira rafiki ya kibiashara, kuna vitu vingi vya kuwakwaza, ni lazima tuviangalie, tuwapende wafanyabiashara wa ndani. Wafanyabiashara wa ndani tunawaumiza, tunaonekana kama hatuna haja nao, tunaonekana kuvutia zaidi wafanyabiashara wa nje ambao hata wenyewe hatuna vivutio vya kutosha vya kuwavutia.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni vizuri tuone namna gani tunajiweka vizuri katika maeneo hayo ili tufikie katika dhana ya Tanzania ya Viwanda. Kila mtu anaona uthubutu wa kufikia hiyo dhamira ya kuwa na Tanzania ya Viwanda iliyoonyeshwa na Serikali hii, lakini lazima sasa tuone tunafikaje katika hatua hiyo kwa pamoja wote kama Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la Mkoa wa Kilimanjaro. Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa na viwanda zaidi ya 15, leo hakuna kiwanda kinachofanya kazi ukiondoa Kiwanda cha Bonite peke yake. Sasa nataka Mheshimiwa Waziri aniambie ni lini atahakikisha Kiwanda cha Madawa ya Mimea kinafanya kazi? Kiwanda kile kimewekeza fedha za Watanzania nyingi mno za mikopo lakini kiwanda kile hakuna siku kimefanya kazi na Watanzania wanadaiwa madeni kutokana na fedha ambazo Serikali hii ilikopa lakini kiwanda kimekuwa pale ni white elephant haifanyi kazi yoyote mpaka leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri aniasaidie ni lini kiwanda kile kitafanya kazi? Ni lini Kiwanda cha Machine Tools kitafanya kazi? Kiwanda ambacho katika zama za Mwalimu Nyerere kilikuwa ni kiwanda mama kama vilivyokuwa viwanda vya chuma vya Tanga. Kama ninavyozungumzia Liganga na Mchuchuma, lakini leo kiwanda kile hakifanyi kazi, na ni kiwanda ambacho kilikuwa ni cha tatu katika Afrika, lakini leo hakifanyi kazi; na mnaimba Tanzania ya viwanda, mnafikiaje hilo lengo la kufika Tanzania ya viwanda kama kiwanda mama hamuwezi kukifanya kikafanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nilikuwa najiuliza kiwanda cha magunia Mheshimiwa Waziri umeorodhesha kwenye hotuba yako Kilimanjaro viwanda vimebinafsishwa havifanyi kazi. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais ameonesha dhamira kwamba anataka Tanzania ya viwanda, kuna kigugumizi gani cha kuwanyang’anya wale watu viwanda ambao hawavifanyii kazi? Nini kigugumizi cha Serikali? Kwa nini hapo mnakosa uthubutu wa kufanya maamuzi magumu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama watu wamechukua viwanda tangu mwaka 1996 mpaka leo hawavifanyii kazi, ni kwa nini mnapata vigugumizi ya kuchukua vile viwanda? Kiwanda cha Magunia kilichokuwa kikiajiri watu wa Kilimanjaro leo hakifanyi kazi, kimekuwa godown la kuwekea bidhaa, kwanini tunawalea hawa watu na nyie mnaona ni jambo la kawaida. Bahati mbaya kuliko vitu vyote Serikali yenu haifanyi kazi kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wa Moshi tumegundua kwamba hamtaki kufufua vile viwanda. Tumeanzisha mipango yetu ya kujiendeleza wenyewe, tumetaka kujenga stendi ya kisasa pale ya kushindana na soko letu lakini mpaka leo Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI hataki kutupa kibali, kwa nini? Kwa sababu ni eneo la upinzani ama sababu ni nini? Tumeomba kwamba Moshi iwe Jiji ina sifa zote, lakini leo tunanyimwa kwa nini? Sasa mtakuzaje huu uchumi na mnafikaje Tanzania ya viwanda? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilikuwa nafikiri ni vizuri kama kuna lengo la kufikia Tanzania ya viwanda tuone tunafikaje huko, lakini kuanza kuhujumiana kwa sababu za kisiasa ni jambo la ajabu sana. Kama hamtaki huu mfumo wa vyama vingi vya siasa futeni ili wengine tukafanye biashara zetu zingine kwa sababu hatuwezi kuja hapa kuwawakilisha wananchi, tujenge mawazo ambayo ni constructive halafu myakatae unnecessary bila sababu yoyote ya kimsingi, kwa nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa natamani sana nione mlivyo-link katika suala la kufikia Tanzania ya viwanda, namna gani mnamsaidia Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Bashe amewaambia na Mheshimiwa Zitto amewaambia; namna gani mnamsaidia Rais ili ndoto yake itimie. Otherwise mtazungumza kama ilivyozungumzwa tangu mwaka 1967, mtazungumza kama ilivyozungumzwa tangu 1996 mpaka leo na mtazungumza mpaka miaka mingine 40 ijayo mbele hamuwezi kufikia Tanzania ya viwanda. Hatutaki kwamba mfike hapo, hii nchi ya kwetu wote, tunataka tu-achieve lengo la kuwa na Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lazima na nyie mheshimu mawazo ya watu wengine muone kwamba wanaweza wakafanya. Lengo la viongozi ni kuwa wabunifu, ziacheni Halmashauri Madiwani wabuni mipango yao na muwape support Madiwani. Acheni kule chini wafanyabiashara wafanye biashara zao vizuri, waacheni wamachinga wa-develop ili dhana ya SME ifanyike. Sasa msipoyafanya haya mnaifikiaje Tanzania ya viwanda? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimependa kuyaonesha haya kwamba Kilimanjaro tuna shida. Kiwanda cha Ngozi leo kinazalisha kidogo; Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira itusaidie kuhakikisha kwamba kile kiwanda kinatumia teknolojia ya kisasa; watu pale wanaumia kwa harufu ya kile kiwanda. Sasa hatutaki kifungwe kwa sababu hatuna viwanda, lakini tunataka kilazimishwe kuzalishwa ka teknolojia ya kisasa ili kulinda afya za watu wa Moshi maana kuna watu pale wanapata maradhi, mtawalipa na nini na mtawafidia kwa kitu gani kwa roho za? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilikuwa naomba sana ichukuliwe kwamba lengo letu ni jema na ni la msingi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunakuwa na Tanzania ya Viwanda kweli.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naomba niunge mkono maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu hoja ya bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo napenda kulizungumza hapa ni ambalo limekuwa likinadiwa sana katika bajeti hii kwamba hii bajeti ni ya kihistoria. Na mimi nimepita kwenye hii bajeti kwa kadri ilivyowezekana nikitazama hiyo historia ya hii bajeti, bahati mbaya sijaweza kuona, labda Mheshimiwa Waziri atanishawishi wakati ana- wind up kunionesha jinsi hii bajeti ilivyo ya kihistoria kwa sababu mimi nilivyoiona hii bajeti ni tegemezi kama zilivyo bajeti nyingine zote ambazo zimepita katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inategemea kukusanya shilingi trilioni 19.9 mapato ya ndani, takribani na inategemea kutumia kutumia shilingi trilioni 19.7 mapato ya ndani kwa matumizi ya kawaida. Sasa najaribu kujiuliza tofauti yake na bajeti zingine ni nini kwa sababu bado asilimia 38 ya bajeti hii inategemea mikopo ama misaada kutika nje. Kwa hiyo, nilikuwa najaribu kutafuta huo uhistoria na mimi siuoni! Naomba sana kushawishiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika shilingi trilioni 11 za maendeleo pesa yenye uhakika wa kupatikana katika bajeti hii ni mikopo ya ndani ya shilingi trilioni 6.1 mikopo ya shilingi trilioni 5.56 tunategemea kutoka wa wahisani au washirika wa maendeleo ama mikopo kutoka nje. Katika kitabu hiki cha Mheshimiwa Waziri anakiri kwamba, mahusiano yetu na washirika wa maendeleo sio mazuri na ndio maana imeundwa timu ya pamoja ya kutoa ushirikiano wa namna gani tume huru inaweza ikasaidia namna ya kujenga mahusiano na washirika wetu wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini mahusiano yetu sio mazuri wakati yalikuwa mazuri wakati wa Mheshimiwa Mkapa mpaka tukafutiwa madeni? Ni kwa nini mahusiano yetu sio mazuri wakati wa Mheshimiwa Kikwete mpaka tulikuwa na International PR? Kwa nini kwa sasa hivi mahusiano yasiwe mazuri? Ni lazima Serikali ingetakiwa ijiangalie mmekosea wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo mlilokosea ni la wazi kabisa, wanazungumza kila siku. Mmekiuka misingi ya demokrasia katika nchi hii, mmekiuka misingi ya utawala bora, mmezuia uhuru wa vyombo vya habari, mmetengeneza sheria mbovu za mitandao, ni vitu vya wazi. Sasa mnatafuta kitu gani cha kuzungumza na hao mnaowaita mabeberu ambao angalau wana-good governance kuliko sisi Watanzania ambao sio mabeberu? Kwa hiyo, nilikuwa natamani nipate sababu ya kwa nini bajeti hii inaitwa bajeti ya kihistoria, ambayo ni bajeti tegemezi kama zilivyo bajeti nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili, bajeti hii haina uhalisia, sio realistic. Kwa sababu, najaribu kuangalia ni namna gani tutapata shilingi trilioni 17.1 kwenye mapato ya ndani wakati tunakwenda kukopa sisi, kama Serikali, kwenye benki za ndani zaidi ya shilingi trilioni sita. Kwa misingi hiyo tunazuia private sector kukopa, hiyo private sector inaposhindwa kukopa italipaje kodi kwa Serikali, ili tupate mapato ya shilingi trilioni 17.1? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini biashara zinafungwa, makampuni yanondoka kwenye biashara tunakuja kuambiana hapa kwamba, kuna makampuni 200,000 yameongezwa katika kujiandikisha kwenye biashara. Sasa najiuliza swali…

TAARIFA ....

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa mujibu wa Kanuni, Serikali ndio ilitakiwa ithibitishe kwamba ninayosema siyo ukweli, lakini naomba twende kwenye ukurasa wa 41 mpaka 42. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ulinde muda wangu, Mheshimiwa Waziri anasema; Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018 Serikali itaendelea kupanua soko la fedha na mambo mengine, lakini 42 anasema; katika jitihada za Serikali kutaka kuimarisha ushirikiano kati yake na washirika wa maendeleo na kuhakikisha fedha zinazoahidiwa zinatolewa kwa wakati, Serikali na washirika wa maendeleo walitafuta washauri elekezi huru, timu hiyo iliongozwa na Dkt. Donald P. Kebaruka aliyekuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Washauri Elekezi walipewa kazi ya kutathmini na kutoa mapendekezo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na washirika wa maendeleo na muundo wa utoaji fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikasema kwa namna ya lugha yoyote itakayofaa kutumika, kama ni kuimarisha, what so ever mimi sina ubishani katika hilo, hoja yangu ni kwa nini sasa nchi ambayo tumekuwa na uhusiano na hawa washirika siku zote mpaka madeni yakafutwa na Paris Club wakati wa Mheshimiwa Mkapa, mpaka tukawa na mahusiano makubwa ya kusifika wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, kumeingia kitu gani Serikali ya Awamu ya Tano? Ndiyo hoja yangu ya msingi ninayotaka kuuliza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo hoja ina ukakasi, Serikali itabidi mniwie radhi, lakini ndicho kilichoandikwa hapa ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka tu kujua kama yanaimarishwa, yanaimarishwa kwa sababu gani? Nilichokuwa najaribu kusema ni kwamba hata bajeti yenyewe kama nilivyosema sio ya uhalisia kwa sababu hiyo ya kwanza niliyosema kwamba, haiwezekani Serikali mkope kwenye benki za ndani, halafu wafanyabiashara watakopa wapi? Mnajua kabisa kwamba Serikali ina uhakika wa security zake kukopeshwa kuliko wafanyabiashara, private sector. Kwa misingi hiyo kusinyaa kwa private sector haionekani kodi mtapatia wapi ya shilingi trilioni 17. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia biashara nyingi kama nilivyosema zimefungwa, lakini hata matumizi yenyewe ya mashine za EFD bado kabisa hatujaweza kuhamasisha kwa kiasi cha kutosha katika mikoa yote katika nchi hii. Inaonekana hizi mashine za EFD zinakuwa so selective kwa sababu ukienda Kilimanjaro hizi mashine zinatumika mno kuliko kawaida. Kiduka cha shilingi milioni 14 lazima kiwe na mashine ya EFD, lakini njoo katika maeneo mengine ya nchi hii, hazitumiki! Tena hao ndio wanalalamika sana kwamba, hawana maendeleo, lakini hawataki kutumia mashine za EFD. Kwa hiyo, ni lazima haya mambo yafanyiwe kazi kama tunataka kuhakikisha kwamba tunapata hiyo shilingi trilioni
17. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata wigo wa walipa kodi (tax base), Mheshimiwa Waziri hajaonesha hata kwamba, labda kwenye taarifa atuambie ni walipa kodi wangapi wa makampuni? Walipa kodi wangapi binafsi? Na walipa kodi wangapi ambao ni wa kawaida ili tufahamu kwamba hivi tunatengeneza tax base yetu kupitia wapi, ili tujue uwe…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE.RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata fursa hii ya kuchangia. Awali ya yote kwanza niunge mkono maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mpango wa maendeleo, na nishauri kwamba Serikali ijitahidi kuzingatia yale ambayo yatakuwa yanaweza kusaidia kuboresha Mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nilitaka nizungumzie suala la makusanyo ya Halmashauri, kama ambavyo Mpango unaonesha, kwamba una lengo la kukusanya shilingi bilioni 847.7 kwa mwaka 2018/2019. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi napata mashaka sana kuhusu Mpango huu wa Serikali kama kweli unaweza kutekelezeka, kwa sababu mwaka 2017/2018 malengo yetu ni kukusanya shilingi bilioni 687.3, lakini bahati mbaya vyanzo vyote vingi vya Halmashauli vile vikubwa vimechukuliwa. Maeneo ya Halmashauri za Wilaya, ushuru wa mazao umechukuliwa kwa kiwango kikubwa na kwa bahati mbaya mkuu wetu wa nchi anapopita anawashauri wananchi kwamba kuanzia asubuhi mpaka jioni wasafirishe tani moja moja mpaka jioni, watakuwa wamekwisha kamilisha lengo la kusafirisha tani moja moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba Halmashauri za Wilaya ukusanyaji wa mapato kupitia kwenye mazao utakuwa mdogo sana, lakini kwenye Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji ukusanyaji wa proper tax, ukusanyaji wa kodi za matangazo kwa maana ya posters na billboards utakuwa umeshuka kwa sababu tayari kodi hizi zinakusanywa na TRA. Sasa napata mashaka ni namna gani tutaweza kufikia lengo la hii shilingi bilioni 847.7 kwa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kujibu basi atuoneshe mpango mkakati wa kuhakikisha tunafikia malengo ya kupata hii shilingi bilioni 847.7 katika halmashauli zetu ili tuweze kufikia malengo ya mapato ya ndani ya nchi yetu tunayo tarajia. Vilevile katika eneo hili la halmashauri utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2017/2018 uko katika kiwango cha chini sana katika Halmashauri zetu nyingi. Miradi mingi ya maendeleo fedha hazijaja, sasa nilikuwa naomba wakati Mheshimiwa Waziri atakapojibu atusaidie ni kwa namna gani watazisaidia Halmashauri ili zitekeleze miradi yake ya maendeleo kwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri Mheshimiwa Waziri akatuambia katika mpango wake, nini malengo yake hasa kuhusu Halmashauri, malengo ya ukweli kabisa kuhusu Halmashauri na dhamira ya Serikali hasa kuhusu Halmashauri. Kwamba dhamira ni kuzifanya Halmashauri ziwepo ama dhamira ni kuziua Halmashauri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima haya mambo yawekwe bayana ili tuelewe maana inavyoonekana Serikali ya Awamu ya Tano dhamira yake kubwa ni kuziua Halmashauri. Unapoondoa uwezo wa Halmashauri kukusanya maana yake unazifanya zisiwe na mapato. Na kama unazinyima mapato, maana yake unazinyima uwezo wa kujiendesha. Leo Halmashauri nyingine hazina uwezo wa kulipa hata posho za Madiwani, sasa zitajiendesha namna gani? Ni vizuri Serikali ituoneshe kiukweli kabisa kwamba dhamira yenu hasa nini? Dhamira yenu kwamba Halmashauri ziwepo kama ilivyokuwa mpango wa awamu, dhamira ni kuziuwa Halmashauri? Ili kama ni kuziua Halmashauri tuondokane na Halmashauri, tuachane na mzigo wa kuwa na Madiwani ambao hawana kazi, kuwa na Wakurugenzi ambao hawana kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ndiyo maana maana leo katika halmashauri zetu utakuta wanao-dictate mipango ya Halmashauri sasa wanakuwa ni Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa kwa sababu power ya Halmashauri imeondoka kwa sababu hawana fedha hawana chochote na inaonekana dhamira ya Serikali Kuu ni kuziua Halmashauri. Kwa hiyo niombe, kama mpango bado ni kuziboresha Halmashauri basi turudi katika mpango wetu, tuonyenyeshe ambavyo tutaziboresha na kuzisitawisha halmashauri zetu ili ziweze kujitegemea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika malengo tulikuwa tumejipangia kwamba angalau Halmashauri zetu nchini zijitegemee kuanzia kwa kiwango cha chini asilimia 35 mpaka asilimia 50, ili zimpunguzie Mheshimiwa Raisi na Serikali mzigo wa majukumu madogo madogo, yale ya chini na Serikali ijihusishe na majukumu makubwa kama ya reli na ndege, lakini mambo ya vituo vya afya, zahanati, shule za msingi yashughulikiwe na Halmashauri kwa kiwango cha kutosha. Mheshimiwa Waziri naomba sana uonyeshe jinsi ambavyo umepanga kujielekeza katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo ambalo mpango huu unaelekeza kwamba utapunguza umaskini wa wananchi utaendelea na jambo ambalo likizungumzwa mara kwa mara katika mipango yetu ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka Mheshimiwa Waziri atuambie kama kweli mpango wa Serikali ni kupunguza umaskini wa Watanzania, na leo tunapata ujasiri wa kubomoa nyumba za wananchi bila huruma, nyumba ambazo wananchi wamejenga wengine kwa utaratibu, lakini tunazibomoa kwa kisingizio kwamba ziko katika hifadhi ya reli na hifadhi ya reli ni mita 30 kuna nyumba ambazo zipo nje ya mita 30, zimeishi katika maeneo hayo zaidi ya miaka 50, leo tunawabomolea wale wananchi hivi dhamira yetu ya kupunguza umaskini wa hao wananchi iko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo ambayo wananchi wana vibali vyote vya ujenzi, taratibu za kubadilisha matumizi ya maeneo hayo zimefanyika, lakini leo wananchi wale wanaambiwa walifika maeneo hayo baada ya mpango reli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimefuatilia mpango wa ramani ya reli, hawana ramani ambayo imepitishwa na Wizara ya Ardhi, wananchi wana eneo ambalo limepitishwa na Wizara ya Ardhi na Serikali ni moja. Wizara ya Ardhi ni moja, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi yote ni Serikali, sasa inakuwaje leo watu waliopewa ruhusa na Wizara ya Ardhi wavunjiwe maeneo yao bila kulipwa fidia wakiambiwa kwamba wamevamia maeneo? Hivi inakuwaje eneo ambalo watu wamepewa kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi hii waambiwe wamevamia hayo maeneo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Waziri kama ana dhamira ya kupunguza umaskini wa Watanzania awasaidie watu wanaovunjiwa nyumba zao wakati wametimiza masharti yote na wana hatimiliki za maeneo ambayo wanayomiliki ili wananchi wawe salama na wawe na mioyo yenye furaha yenye amani. Kama ni dhamira kufanya nchi iwe yenye utulivu basi tuwafanye wananchi wetu pia wawe na mioyo yenye utulivu na tuwasidie wananchi hawa ambao ni maskini ambao wamejenga hizi nyumba kwa hali ngumu sana, leo wanavunjiwa kirahisi kama vile hizo nyumba zimeanguka kutoka mbinguni. Naomba sana Serikali ilione hii kwa uzito wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la mikopo ya elimu ya juu. Hotuba ya Kambi ya Upinzani imejaribu kuzungumzia suala la mikopo ya elimu ya juu. Ni vizuri Serikali ibainishe inaweza kukopesha wanafunzi wasome ama haiwezi? Ni vizuri tuweke bayana, kwa sababu kama tunahitaji kuwasaidia wanafunzi na wanafunzi hawa ni watoto wa maskini, maskini tunaowafahamu wana-qualify kukopeshwa lakini hawakopeshwi kwa sababu Serikali haina uwezo, inaonekana kuna ubaguzi kwa sababu kuna ambao wanakopeshwa na ambao hawakopeshwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili kuondoa hii hali ya ubaguzi ama tuondoe mikopo ama kama tunatoa mikopo tutoe mokopo kwa watu wanaostahili kupewa mikopo kama jukumu la Serikali ya nchi hii. Na kwa sababu ni kweli kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ilijitanabaisha kwamba wananchi wenye kuhitajiwa kukopa watakopeshwa wote bila mmoja kukosekana basi Serikali itimize wajibu wake huo vya kutosha ili wanafunzi wasikose haki yao ya msingi ya elimu ambayo ni haki ya Kikatiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana katika Mpango huu Mheshimiwa Waziri atujibu ni wakati gani watamaliza tatizo la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu bila kuonesha aina yoyote ya ubaguzi kama inavyoendelea sasa hivi? (Makofi)

Kuhusu suala la utalii, hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni imeonesha jinsi ambavyo VAT kuwekwa katika utalii ilivyoathiri utalii katika nchi hii. Malengo yetu ni kuifanya nchi hii ishindane na nchi nyingine katika utalii, bahati nzuri nchi yetu ina vivutio vingi vya utalii, tunategemea kwamba tungekuwa tuko katika hatua ya juu sana katika utalii. Ni vizuri pia Mheshimiwa Waziri akatueleza ni watalii kiasi gani ambao wameingia kipindi hiki ukilinganisha mwaka uliopita, na ni mpango gani uliopo katika Serikali hii kuingiza watalii zaidi kipindi cha mwaka 2018/2019? Tushindane na nchi ambazo zina vivutio kama vya kwetu, haiwezekani nchi ambazo hazina vivutio kuliko vya kwetu zitushinde katika kuingiza idadi kubwa ya watalii katika nchi hii. Kwa hiyo ni vizuri tuangalie sana mfumo wa kodi katika eneo la utalii ili itusaidie katika kuongeza idadi ya watalii katika nchi yetu na ukizingatia kwamba Mlima Kilimanjaro ni moja wapo wa vitega uchumi muhimu sana katika nchi yetu, ni vizuri tuone jinsi ambavyo tunaweza kuutumia ule mlima kutuingizia mapato ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka pia niongelee suala la mfumo wa kodi. Mheshimiwa Waziri kwenye mpango wake ameonyesha kwamba angalau wananchi wameonesha ku- comply kulipa kodi, ameonesha kuwa wananchi wengi wameingia kwenye mfumo wa EFD machine. Ni kweli, sasa ni wakati wa mpango wetu Mheshimiwa Waziri uoneshe namna gani tunaangalia upya sera ya kodi na mfumo wa kodi ili sera hii ya kodi na mfumo wa kodi ifanye kodi ilipike kwa wafanyabiashara vizuri zaidi. Kwa sababu kodi ikilipika vizuri maana yake ni kwamba watu wengi watakuwa wanafanya biashara na uchumi wetu utapanuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kodi tulionayo sasa hivi hailipiki ndiyo maana watu wengi inabidi waingie kwenye mfumo wa rushwa ili wakwepe kulipa kodi. Kwa hiyo, watu wengi wanakwepa kodi kwa sababu ya viwango vya kodi kuwa vikubwa pamoja na mfumo wa kodi kuwa mgumu. Kwa hiyo tuangalie kwa kiwango cha kutosha mfumo wetu wa kodi ili kodi yetu ya nchi hii ilipike na wafanyabiashara wapate nafuu katika kufanya biashara zao. Ili wasifunge biashara zao kama ambavyo wanafunga sasa, ili wasigombane na TRA kama wanavyogombana na TRA sasa, tuwafanye watu wa-comply kulipa kodi wenyewe na Mheshimiwa Waziri unafahamu kodi nzuri ni ile inayolipika. Sasa kama kodi hailipiki maana yeke hiyo kodi inapoteza ule uzuri wake, naomba Mheshimiwa Waziri hilo lifanyiwe kazi kiasi cha kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la viwanda. Suala la viwanda katika nchi hii tunalolizungumza ni jambo bora; ni jambo la msingi kuifanya nchi hii kuwa ya viwanda. Hata hivyo tunazungumzia viwanda vya vyerehani vitatu, vinne, vitano ndivyo tunavyovipigia kelele, lakini kuna viwanda vimebinafsishwa katika nchi hii, tumeendelea kusema viwanda vile virudishwe kwa watu ambao wana uwezo wa kuviendesha, lakini havirejeshwi mpaka sasa hivi. Watu wamekalia viwanda vimekuwa magofu halafu tunaendelea kupiga kelele viwanda vidodo vidogo. Sawa, hata hivyo ni viwanda, lakini hivi viwanda vikubwa lazima vifanyiwe kazi, virejeshwe katika uendeshaji. Viwanda havifanyi kazi, vimekufa na vilikuwa viwanda vyetu vya kodi ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama waliopewa wameshindwa kuviendesha wavirejeshe kwa wanaoweza kuviendesha. Kilimanjaro viwanda vingi vimelala kwa sababu tu watu wamevichukua na haviendeshwi. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri utusaidie katika mpango wako, nini mpango wa Serikali katika kuhakikisha kwamba viwanda vilivyobinafsishwa vinarejeshwa kwa watu wanye uweza kuviendesha kama wale waliokuwa wamepewa wameshindwa kuviendesha ili vifanye kazi viongeze ajira kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho nataka kuongea katika siku ya leo ni suala la sekta binafsi. Serikali inakuwa kama inajinadi kwamba ina dhamira ya kusaidia sekta binafsi lakini katika uhalisia tunaonekana hatuna dhamira ya kusidia sekta binafsi. Leo tunavyozungumza sekta binafsi haikopesheki, benki haziwezi kukopesha sekta binafsi, na watu wengi wa sekta binafsi wanafunga biashara zao kama hotuba ya Kambi ya Upinzani ilivyosema. Hatujafanya tathimini ya kutosha ni kwa nini watu binafsi wafunge biashara zao? Hatujafanya utafiti wa kutosha ni kwa nini leo benki haziwezi kukopesha sekta binafsi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatujafanya utafiti wa kutosha ni kwanini benki zishindwe kukopesha. Mheshimiwa Waziri ni lazima mpango wako utuoneshe ni namna gani mmejipanga kuhakikisha kwamba mnasaidia sekta binafsi na mnazisaidia benki zikopeshe sekta binafsi. Hatuna sababu ya kujenga ugomvi na benki zetu, hatuna sababu ya kujenga ugomvi na sekta binafsi kwa sababu sekta abinafsi ndiyo chachu muhimu sana yakuinua uchumi wetu. Huko nyuma Serikali ilishajitoa kufanya biashara, leo Serikali mnakuja sana katika kufanya biashara. Sasa wakati mnakuja kwa kasi isaidieni sekta binafsi kwa sababu ndiyo inayoinua uchumi katika dunia hii. Mheshimiwa Waziri mpango wa Serikali utusaidie sekta binafsi ili sekta hizo binafsi zisaidie malengo ya Serikali ya kufikia uchumi wa viwanda, malengo ya Serikali ya kuinua uchumi wa nchi hii, malengo ya Serikali ya kuondoa umaskini wa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha, ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii ya kuishauri Serikali katika Hotuba ya Bajeti ya Mwaka 2018/2019. Mwaka wa fedha 2016/2017, nilipokuwa nachangia Hotuba ya Bajeti, nilisema kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ilivyokuja na malengo yake inaonekana kama vile si Serikali ya CCM iliyokuwa inaongoza nchi hii kwa miaka yote. Nikasema kwamba kama watakwenda na spirit hiyo basi kutakuwa na mabadiliko tutakayoweza kuyaona.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa sababu niliamini kwamba watu wanaoiongoza Serikali ya Awamu ya Tano ni wale wale ambao wameongoza nchi hii kwa miaka yote tuliyonayo ya uhuru wa nchi hii, niliamini kwamba kusingekuwa na mabadiliko makubwa kama ambavyo inaonekana leo. Kwamba baada ya miaka mitatu bado hali ya maisha ya Watanzania yamezidi kuwa magumu sana, watu wameendelea kuishi katika shida na matatizo ambayo walikuwa wametegemea kwamba yangemalizwa katika Serikali hii ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii imeendelea kuwa un- popular kwa wananchi kwa siku zinavyoendelea kuliko hata ilivyokuwa huko nyuma. Kama hali hii itaendelea, kama uchaguzi utakuwa huru na haki 2020 nafasi yenu ya kushinda ni ndogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, angalau katika bajeti hii kuna harufu ya kuonesha kwamba kuna mambo wanataka kuyashughulikia ambayo ni ya msingi sana kwa jamii na hasa katika eneo la kodi. Jambo ambalo tumelizungumza sana kama Kambi Rasmi ya Upinzani lakini wakati wote mmekuwa hamko tayari kusikiliza; na imekuwa ndio traditional ya Serikali hii. Kwamba kama jambo Mheshimiwa Rais hataamka alizungumze alitilie uzito basi wengine wakilishauri utekelezaji wake unakuwa ni mgumu sana.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu Mheshimiwa Rais alikaa na wafanyabiashara angalau ukiangalia bajeti hii kuna vitu unaanza kuviona angalau vinaanza kutekelezwa. Hata hivyo, naona kama muda umechelewa sana wa kujenga confidence ya wafanyabiashara na wananchi kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, nashauri mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, la kwanza, Serikali ya Awamu ya Tano ijaribu kuondoa hofu wanayokuwa nayo wafanyabiashara na wawekezaji katika nchi hii; hakuna kabisa confidence ya kuwekeza. Mtu anapowekeza katika nchi hii uhakika wake wa kufanya biashara yake mpaka ifike mwisho umekuwa ni mgumu sana. Hana uhakika kwamba kesho kutaamka na nini, keshokutwa kutakuwepo na nini. Imekuwa kama vile kufanya biashara katika nchi hii ni kitendo kiovu. Mfanyabiashara anakuwa anaandamwa kwa kiwango ambacho ni cha kutisha, wala kufanya biashara tena katika nchi hii siyo baraka.

Mheshimiwa Spika, sasa nadhani ni vizuri Serikali ibadilishe huo mtazamo, ifanye kwamba wafanyabiashara ni sehemu ya wadau muhimu sana katika Taifa hili na hasa kwa Serikali ambayo inategemea kodi. Iwafanye wafanyabiashara kuwa ni watu ambao ni kama ng’ombe unaowakamua ambao kimsingi unapaswa kuwalisha majani ili upate maziwa kuliko kufika mahali ambapo wafanyabiashara wanaonekana kama ni maadui katika Taifa.

Mheshimiwa Spika, mtazamo kwamba wafanyabiashara wote ni wakwepa kodi si sahihi, wako wachache ambao wanaokwepa kodi lakini wafanyabiashara wengi katika nchi hii ya Tanzania hasa Watanzania kwa tabia zao na malezi yao hawapendi kusumbuana na Serikali katika suala la kodi; wanahitaji tu maelekezo sahihi, uongozi bora wa namna ambavyo wataongozwa katika kulipa kodi.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri, kama ambavyo leo tunaleta Tax Amnesty katika maeneo mbalimbali, sheria za namna ambavyo tunafikiri kwamba riba na faini ambazo zimejilimbikiza angalau ziangaliwe. Tuangalie pia utaratibu ambapo kama mfanyabiashara amefanyiwa auditing na akaonekana kodi yake ni kiasi fulani apewe muda wa kuilipa taratibu. Haiwezekani mfanyabiashara apewe kodi ya milioni mia moja umtake alipe wakati huo huo, anaipatia wapi hiyo fedha? Unless awe ni mwizi. Apewe muda taratibu hata wa miaka miwili, mitatu alipe hiyo fedha taratibu huku akiwezeshwa kuendelea kufanya biashara ili aweze kuisaidia Serikali na kuweza kusaidia mambo mengine ya maendeleo ya nchi hii yaende.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nafikiri ni vizuri sana Mheshimiwa Waziri akaliangalia hilo. Kukawa kuna roho ya huruma ambayo anatakiwa awe nayo na hasa kwa watu ambao wame-comply kulipa. Wale ambao wanakataa kulipa ndio waadhibiwe, lakini mtu amepewa demand note leo, baada ya siku mbili anafungiwa biashara yake, akaunti zake zinaanza kufungwa, fedha yote inachukuliwa na TRA, huyu mtu ana mikopo ya benki, ataendeleaje na biashara? Matokeo yake mambo yafuatayo yanatokea; wafanyabiashara wanakufa kwa presha, wanafilisiwa na matokeo yake na ninyi hampati chochote katika Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni vizuri sana tuangalie namna gani; kwa sababu Taifa hili la Tanzania hakuna njia nyingine ya kuishi zaidi ya kukaa vizuri na wafanyabiashara na wawekezaji, maana hawafanyi biashara wao, wanataka kujitahiditahidi kuanza kuingia kwenye biashara ambako kimsingi tulishatoka huko. Automatically naona kama wameshindwa na hawataweza kabisa kwa sababu tulishatoka huko kwa karne ya sasa hivi. Sasa watu ambao wanaweza kuwasaidia ni wafanyabiashara na wawekezaji, wasaidieni hao watu. Nadhani hilo ni eneo la kwanza la muhimu sana, naishauri Serikali iliangalie kwa makini.

Mheshimiwa Spika, kwenye hotuba hii wamesema mojawapo ya shida inayowasumbua ni sekta isiyo rasmi. Naamini bajeti hii waliyonayo TRA wana uwezo wa kukusanya kabisa hizi fedha, naamini kabisa, lakini inahitaji umakini katika kusimamia hili. Sekta isiyo rasmi lazima waigawanye katika makundi, sekta isiyo rasmi wanapoizungumzia kwamba ni Wamachinga tu siyo maana yake. Kuna watu ambao wana maeneo kabisa wana-settlement vizuri, wako mahali pazuri, wanafanya biashara zao lakini hawajaingizwa kwenye mfumo wa kodi.

Mheshimiwa Spika, tatizo kubwa tulilonalo ni kwamba tuna wafanyakazi wachache wa TRA ambao hawawezi kuwafikia hao wafanyabiashara na wa bahati mbaya hawaoni umuhimu wa wajibu wa halmashauri zenu, hawataki kuzitumia halmashauri zao. Wangetumia halmashauri zao vizuri wakaamini kwamba halmashauri ni chombo muhimu cha kuwasaidia zingewasaidia ku-trap hawa wafanyabiashara ambao wapo na hawana leseni lakini wanafanya biashara, wamejificha kwenye kivuli cha kutokuwa wafanyabiashara wasio rasmi, leo wangekuwa wameweza kuongeza mapato yenu.

Mheshimiwa Spika, sasa ushauri wangu kwa Serikali waongeze wafanyakazi wa TRA, kwa sababu ni investment. Kumwongeza mfanyakazi wa TRA si sawa na kumwajiri Mwalimu. Ni investment ya haraka ambayo pesa yako ipo ili waweze kufikia walipa kodi wengi. Sasa matokeo yake wanabaki na walipa kodi wachache ambao kila wakiamka ndio hao wanapambana nao.

Mheshimiwa Spika, walio wengi wamewaacha wako barabarani na bahati mbaya wamejifunika kwenye kigezo kwamba wao hawajafikia kwenye pato la mauzo ghafi ya milioni 20 kwa mwaka, kwa hiyo wanabaki hapo hapo wao hawaguswi, wala hawapo kwenye VAT, hawapo popote wapo tu. Siku zote wamezidi kuwapotezea mapato na wao hawawezi kulisukuma hilo. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri aongeze wafanyakazi wa TRA ili wafikie walipa kodi wengi ili waweze kufikia haya malengo waliyotarajia.

Mheshimiwa Spika, suala la tatu ni suala la halmashauri. Mheshimiwa Waziri a-revisit uamuzi wa kuchukua vyanzo vya mapato vya halmashauri. Watajidanganya sana wakiendelea kuamini kwamba vyanzo vya mapato vya halmashauri vitasaidia Serikali Kuu. Serikali Kuu wana vyanzo vingi, wazifanye halmashauri ziweze kukusanya mapato ili zitoe huduma kwa wale watu wa chini, watu wengi wako chini.

Mheshimiwa Spika, Rais atakuwa na nafasi na wao ya kupanga mambo ya Bomberdier, mambo ya reli na mambo mengine kwa sababu ya fedha zao za Serikali Kuu, lakini waache halmashauri zikusanye fedha kwa mambo yale ya maji, afya, elimu na kadhalika. Kama watajidanganya kwamba walioanza huko nyuma walikuwa hawaelewi wakaona wao wanaelewa zaidi wakaanza kuturudisha kwenye centralization wanapotea katika mwelekeo. Nishasema hili narudia kulisema hili, hakuna kosa kubwa wanalolifanya Serikali ya Awamu ya Tano kama kuua halmashauri, kama kuua Serikali za Mitaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bahati nzuri katika nchi ambayo ina muundo mzuri wa Serikali za Mitaa, Tanzania ni mojawapo, lakini bahati mbaya katika nchi ambayo haitimizi wajibu wake vizuri kwenye Serikali za Mitaa, Serikali ya Awamu ya Tano ni ya kwanza. Sasa ni vizuri waone ni namna gani wanavirudisha vyanzo vya halmashauri ili ziweze kutengeneza barabara zake, halmashauri zitengeneze vituo vya afya, zitengeneze zahanati. Sasa wasipofanya hivyo kila pesa wakitaka tupige magoti kuwaomba mpaka lini?

Mheshimiwa Spika, haya yalikuwa maoni yangu na ushauri wangu kwa Serikali. Nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia. Nami nichukue fursa hii kupongeza kazi kubwa ambayo Mheshimiwa Waziri anafanya, Waziri wa TAMISEMI na Naibu Mawaziri wake. Naamini kwamba ana Naibu mzuri ambaye amebobea kwenye mambo ya Serikali za Mitaa, huenda anaweza akamsaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pamoja na hayo yote niliyosema ya kumpongeza Waziri, pamoja na jitihada ambazo Waziri anaonekana kufanya, lakini nina hofu kwamba, dhamira ya Serikali hii ya Awamu ya Tano ni kutengeneza Serikali za Mitaa dhaifu, kufanya Halmashauri zetu ziwe dhaifu na kwenda kinyume kabisa na dhamira ya maboresho ya Serikali za Mitaa yaliyofanywa tangu 1998 mpaka mwaka 2014 na Serikali ya Awamu ya Tatu na Serikali ya Awamu ya Nne. Kwa sababu theory zote zinaonesha kwamba, Serikali zote ambazo zinataka kufanya kazi kama zinavyotaka huwa zinahakikisha kwamba Serikali za Mitaa zinakuwa dhaifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana leo sote tuko hapa tunalalamika jinsi ambavyo Wakuu wa Mikoa wanaweza wakaziingilia Serikali za Halmashauri. Tunalalamika jinsi ambavyo Wakuu wa Wilaya wanaweza wakaziingilia Halmashauri kwa sababu ya dhamira inayoonekana yenye mwelekeo wa kufanya yale mawazo yote ambayo yaliwekezwa fedha nyingi sana ya kufanya maboresho ambayo yangezipa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa ni mamkala kamili katika maamuzi katika rasilimali yanakuwa hayana nia njema katika Serikali hii ya Awamu ya Tano, kwa maoni yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ushauri wangu kwa Mheshimiwa Waziri ili aweze kufanya kazi yake vizuri ni lazima ajielekeze sana katika kujenga Serikali za Mitaa imara. Tukijenga Serikali za Mitaa imara hata hii dhana kubwa kwa Waheshimiwa Wabunge wengi kwamba kila wakati tunadhani kitu tunatakiwa tuombe Serikali Kuu. Barabara za vijijini tuombe kwenye Serikali Kuu, barabara za mitaani tuombe Serikali Kuu itapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndio ilikuwa dhamira halisi ya kuimarisha Serikali za Mitaa. Kuzifanya ziwe na maamuzi sahihi ziwe na rasilimali za kutosha rasilimali watu na rasilimali fedha jambo ambalo kwa Serikali hii inaonekana siyo jambo la mkazo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri urejee sana katika hilo la kufanya maboresho yale ya Serikali za Mitaa yaliyozalisha sera ya D by D yafanyiwe kazi za kutosha ili kufanya mahusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa yawe ni ya ushirika na siyo ya Baba na Mtoto. Kwa hali ilivyo hapa sasa hivi hapa ni kwamba Serikali Kuu inakuwa ni baba, Serikali za Mitaa zinakuwa ni mtoto, kwa hiyo mtoto ni kulalamika kwa Serikali Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la maboresho lilikuwa kuzifanya Serikali za Mitaa ziwe na autonomy ili ziweze kujitegemea vizuri. Mheshimiwa Waziri naomba sana ajitahidi katika hilo, ni vizuri akaweka sheria itakayozipa uimara, itakayotengeneza taasisi imara ya Serikali za Mitaa itakayoweza kujiendesha ili tuondoe huu mfumo wa watu kutegemea kila saa kuja kuomba, kupiga magoti hapa na ndiyo maana imefika mahala ambapo inaonekana sasa hivi katika nchi hii bila kuvunja heshima na hadhi ya Mheshimiwa Rais na ikionekana kwamba sasa fedha ya nchi hii ni fedha ya Mheshimiwa Rais na siyo fedha ya walipa kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba sasa hivi kila mtu anamshukuru Rais amempelekea hiki, amempelekea kile, amempelekea kile wakati Rais amechaguliwa na wananchi wote kama mtumishi wa wananchi na mabosi wake ni wananchi wanaolipa kodi ili awatumikie. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nadhani kwamba ni eneo muhimu sana la kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili; kumekuwa na malalamiko makubwa sana ya kuhusu Mfuko wa Vijana na Akinamama. Mara nyingi kumekuwa na hoja hizi kwamba fedha hazikusanywi lakini kubwa zaidi ni kwamba hata hizo zinazokusanywa kidogo hizo zinazopatikana zinatumiwaje. Kwa sababu fedha zile zinaingia Hazina, namwomba Mheshimiwa Waziri ajitahidi kuwe na akaunti maalum ya Mfuko wa Akinamama na Mfuko wa Vijana ile asilimia 10 iingie kwenye hiyo akaunti, kwa sababu ule mfuko ni revolving ili zikitoka kwa wakopeshwaji zirejeshwe kwenye mfuko ule, lakini hela ile ikitoka kwa wakopeshwaji inarejea kwenye Mfuko Mkuu wa Halmashauri, bado inaingia kwenye matumizi mengine ya Halmashauri, kwa hiyo haieleweki ni fedha zipi zimetoka kwa ajili ya bajeti na ni fedha zipi zimerejeshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni vizuri aelekeze Halmashauri ziwe na mfuko maalum na aushauri Mheshimiwa Rais akubali kuwa na Mfuko maalum kwa ajili ya fedha hizi za Mfuko wa Vijana na Mfuko wa Akinamama ili sasa mwisho wa siku tuweze baada ya muda tuwe tumetengeneza fedha ya kutosha kwenye hizi akaunti na baada ya miaka kadhaa tukazipa viwango maalum Halmashauri, mwisho wa siku tusizipelekee tena fedha ili zile fedha ziwe kwa ajili ya maendeleo, kwa ajili ya vijana na kwa ajili ya akinamama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ni vizuri ajitahidi sana na hili kwa sababu zile fedha kwa sasa hivi hapa hazijulikani zinapoingia kwenye matumizi ya kawaida ni wakati zinaitwa za vijana ni wakati zinaitwa za akinamama, ni wakati gani zinaitwa za matumizi ya Halmashauri. Kwa hiyo, nafikiri ni jambo la muhimu sana kwa Mheshimiwa Waziri kuliangalia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha zilizokuwa zinatengwa za retention asilimia 30 za ardhi ambazo leo hazirejeshwi katika Halmashauri na Mheshimiwa Waziri anajua katika nchi hii kila Halmashauri ardhi ndiyo rasilimali yake kubwa. Ile asilimia 30 ilikuwa inasaidia sana Halmashauri kujiendesha leo zile hela hazirejeshwi, ni vizuri angeshauriana na Wizara ya Ardhi zile fedha asilimia 30 zikarejeshwa katika Halmashauri, zikasaidia mambo ya Halmashauri yakaenda. Kwa sababu mambo ya Halmashauri hayaendi na watakuwa wanazi- commit Halmashauri wakati hazina uwezo wa kupata fedha na vyanzo vyote wamevichukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii spirit ya kuchukua vyanzo vya Halmashauri ni vema Mheshimiwa Waziri akamshauri Mheshimiwa Rais ambaye ni Waziri akaiondoa. Serikali Kuu ina maeneo mengi ya mapato makubwa tu ina bandari na maeneo mengi. Haya maeneo ambayo ndiyo Halmashauri kwa mujibu wa makubaliano ya maboresho ya Serikali za Mitaa yaachwe yabaki katika Halmashauri ili yaweze kusaidia Halmashauri. Kwa hiyo, naomba asilimia 30 ya Halmashauri iachwe irejee katika Halmashauri ibaki katika Halmashauri isaidie Halmashauri kuliko kuichukua wakaipeleka Serikali Kuu asilimia 30 ya kodi ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la posho ya Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji. Hebu tusifanye wale watu kama vile wao sio miongozi mwa watu ambao ni muhimu katika Taifa hili. Wale watu tunategemea kuwatumia katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi hii. Hata wao wanawatumia katika sera mbalimbali, maelekezo mbalimbali na makusanyo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale watu ni vizuri waelekeze Halmashauri zitenge zile fedha angalau Sh.20,000/= mpaka Sh.50,000/= kwa ajili ya Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji ili waweze kufanya mambo yao. Tumewafanya wale watu wamekuwa kama ni watu ambao hawana mtu wa kuwasaidia. Wamekuwa watu ambao ni ombaomba, wamekuwa wakiishi kwa majamvi ili watu wagombane wapate fedha, lakini wale watu ni watu ambao wamechaguliwa kwa mujibu wa sheria wanapaswa kusaidiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba wale Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji watengewe fedha kwa ajili ya mambo yao.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia. Nami nichukue fursa hii kupongeza kazi kubwa ambayo Mheshimiwa Waziri anafanya, Waziri wa TAMISEMI na Naibu Mawaziri wake. Naamini kwamba ana Naibu mzuri ambaye amebobea kwenye mambo ya Serikali za Mitaa, huenda anaweza akamsaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pamoja na hayo yote niliyosema ya kumpongeza Waziri, pamoja na jitihada ambazo Waziri anaonekana kufanya, lakini nina hofu kwamba, dhamira ya Serikali hii ya Awamu ya Tano ni kutengeneza Serikali za Mitaa dhaifu, kufanya Halmashauri zetu ziwe dhaifu na kwenda kinyume kabisa na dhamira ya maboresho ya Serikali za Mitaa yaliyofanywa tangu 1998 mpaka mwaka 2014 na Serikali ya Awamu ya Tatu na Serikali ya Awamu ya Nne. Kwa sababu theory zote zinaonesha kwamba, Serikali zote ambazo zinataka kufanya kazi kama zinavyotaka huwa zinahakikisha kwamba Serikali za Mitaa zinakuwa dhaifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana leo sote tuko hapa tunalalamika jinsi ambavyo Wakuu wa Mikoa wanaweza wakaziingilia Serikali za Halmashauri. Tunalalamika jinsi ambavyo Wakuu wa Wilaya wanaweza wakaziingilia Halmashauri kwa sababu ya dhamira inayoonekana yenye mwelekeo wa kufanya yale mawazo yote ambayo yaliwekezwa fedha nyingi sana ya kufanya maboresho ambayo yangezipa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa ni mamkala kamili katika maamuzi katika rasilimali yanakuwa hayana nia njema katika Serikali hii ya Awamu ya Tano, kwa maoni yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ushauri wangu kwa Mheshimiwa Waziri ili aweze kufanya kazi yake vizuri ni lazima ajielekeze sana katika kujenga Serikali za Mitaa imara. Tukijenga Serikali za Mitaa imara hata hii dhana kubwa kwa Waheshimiwa Wabunge wengi kwamba kila wakati tunadhani kitu tunatakiwa tuombe Serikali Kuu. Barabara za vijijini tuombe kwenye Serikali Kuu, barabara za mitaani tuombe Serikali Kuu itapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndio ilikuwa dhamira halisi ya kuimarisha Serikali za Mitaa. Kuzifanya ziwe na maamuzi sahihi ziwe na rasilimali za kutosha rasilimali watu na rasilimali fedha jambo ambalo kwa Serikali hii inaonekana siyo jambo la mkazo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri urejee sana katika hilo la kufanya maboresho yale ya Serikali za Mitaa yaliyozalisha sera ya D by D yafanyiwe kazi za kutosha ili kufanya mahusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa yawe ni ya ushirika na siyo ya Baba na Mtoto. Kwa hali ilivyo hapa sasa hivi hapa ni kwamba Serikali Kuu inakuwa ni baba, Serikali za Mitaa zinakuwa ni mtoto, kwa hiyo mtoto ni kulalamika kwa Serikali Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la maboresho lilikuwa kuzifanya Serikali za Mitaa ziwe na autonomy ili ziweze kujitegemea vizuri. Mheshimiwa Waziri naomba sana ajitahidi katika hilo, ni vizuri akaweka sheria itakayozipa uimara, itakayotengeneza taasisi imara ya Serikali za Mitaa itakayoweza kujiendesha ili tuondoe huu mfumo wa watu kutegemea kila saa kuja kuomba, kupiga magoti hapa na ndiyo maana imefika mahala ambapo inaonekana sasa hivi katika nchi hii bila kuvunja heshima na hadhi ya Mheshimiwa Rais na ikionekana kwamba sasa fedha ya nchi hii ni fedha ya Mheshimiwa Rais na siyo fedha ya walipa kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamba sasa hivi kila mtu anamshukuru Rais amempelekea hiki, amempelekea kile, amempelekea kile wakati Rais amechaguliwa na wananchi wote kama mtumishi wa wananchi na mabosi wake ni wananchi wanaolipa kodi ili awatumikie. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nadhani kwamba ni eneo muhimu sana la kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili; kumekuwa na malalamiko makubwa sana ya kuhusu Mfuko wa Vijana na Akinamama. Mara nyingi kumekuwa na hoja hizi kwamba fedha hazikusanywi lakini kubwa zaidi ni kwamba hata hizo zinazokusanywa kidogo hizo zinazopatikana zinatumiwaje. Kwa sababu fedha zile zinaingia Hazina, namwomba Mheshimiwa Waziri ajitahidi kuwe na akaunti maalum ya Mfuko wa Akinamama na Mfuko wa Vijana ile asilimia 10 iingie kwenye hiyo akaunti, kwa sababu ule mfuko ni revolving ili zikitoka kwa wakopeshwaji zirejeshwe kwenye mfuko ule, lakini hela ile ikitoka kwa wakopeshwaji inarejea kwenye Mfuko Mkuu wa Halmashauri, bado inaingia kwenye matumizi mengine ya Halmashauri, kwa hiyo haieleweki ni fedha zipi zimetoka kwa ajili ya bajeti na ni fedha zipi zimerejeshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni vizuri aelekeze Halmashauri ziwe na mfuko maalum na aushauri Mheshimiwa Rais akubali kuwa na Mfuko maalum kwa ajili ya fedha hizi za Mfuko wa Vijana na Mfuko wa Akinamama ili sasa mwisho wa siku tuweze baada ya muda tuwe tumetengeneza fedha ya kutosha kwenye hizi akaunti na baada ya miaka kadhaa tukazipa viwango maalum Halmashauri, mwisho wa siku tusizipelekee tena fedha ili zile fedha ziwe kwa ajili ya maendeleo, kwa ajili ya vijana na kwa ajili ya akinamama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ni vizuri ajitahidi sana na hili kwa sababu zile fedha kwa sasa hivi hapa hazijulikani zinapoingia kwenye matumizi ya kawaida ni wakati zinaitwa za vijana ni wakati zinaitwa za akinamama, ni wakati gani zinaitwa za matumizi ya Halmashauri. Kwa hiyo, nafikiri ni jambo la muhimu sana kwa Mheshimiwa Waziri kuliangalia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha zilizokuwa zinatengwa za retention asilimia 30 za ardhi ambazo leo hazirejeshwi katika Halmashauri na Mheshimiwa Waziri anajua katika nchi hii kila Halmashauri ardhi ndiyo rasilimali yake kubwa. Ile asilimia 30 ilikuwa inasaidia sana Halmashauri kujiendesha leo zile hela hazirejeshwi, ni vizuri angeshauriana na Wizara ya Ardhi zile fedha asilimia 30 zikarejeshwa katika Halmashauri, zikasaidia mambo ya Halmashauri yakaenda. Kwa sababu mambo ya Halmashauri hayaendi na watakuwa wanazi- commit Halmashauri wakati hazina uwezo wa kupata fedha na vyanzo vyote wamevichukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii spirit ya kuchukua vyanzo vya Halmashauri ni vema Mheshimiwa Waziri akamshauri Mheshimiwa Rais ambaye ni Waziri akaiondoa. Serikali Kuu ina maeneo mengi ya mapato makubwa tu ina bandari na maeneo mengi. Haya maeneo ambayo ndiyo Halmashauri kwa mujibu wa makubaliano ya maboresho ya Serikali za Mitaa yaachwe yabaki katika Halmashauri ili yaweze kusaidia Halmashauri. Kwa hiyo, naomba asilimia 30 ya Halmashauri iachwe irejee katika Halmashauri ibaki katika Halmashauri isaidie Halmashauri kuliko kuichukua wakaipeleka Serikali Kuu asilimia 30 ya kodi ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la posho ya Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji. Hebu tusifanye wale watu kama vile wao sio miongozi mwa watu ambao ni muhimu katika Taifa hili. Wale watu tunategemea kuwatumia katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi hii. Hata wao wanawatumia katika sera mbalimbali, maelekezo mbalimbali na makusanyo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale watu ni vizuri waelekeze Halmashauri zitenge zile fedha angalau Sh.20,000/= mpaka Sh.50,000/= kwa ajili ya Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji ili waweze kufanya mambo yao. Tumewafanya wale watu wamekuwa kama ni watu ambao hawana mtu wa kuwasaidia. Wamekuwa watu ambao ni ombaomba, wamekuwa wakiishi kwa majamvi ili watu wagombane wapate fedha, lakini wale watu ni watu ambao wamechaguliwa kwa mujibu wa sheria wanapaswa kusaidiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba wale Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji watengewe fedha kwa ajili ya mambo yao.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Makadirio ya Bajeti ya Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Jambo la kwanza ninalotaka kuishauri Serikali, ni suala la mapato ya Serikali ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwekezaji katika sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maoni yangu, mojawapo ya eneo ambalo limekuwa ni kikwazo cha kuimarisha sekta binafsi katika nchi hii, ni viwango vya kodi katika nchi yetu. Viwango vyetu vimekuwa ni kichocheo kikubwa cha kufanya wafanyabiashara wengi na wawekezaji wengi wakwepe kodi. Bahati nzuri nimeshaona jitihada zinazofanyika kusukuma hili suala la kupunguza viwango vya kodi. Nilikuwa naiomba Serikali ilifanye jambo hili kwa haraka iwezekanavyo ili iweze kuwa kichocheo cha wananchi kulipa kodi na kwa maana hiyo kuwekeza kwa kiwango kinachoridhisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kodi katika nchi hii imekuwa kama ni silaha ya kuadhibu baadhi ya watu ambao inawezekana wakawa na maoni tofauti au wakawa na mitazamo tofauti na Serikali hii. Sasa badala ya kodi kuwa sehemu ya kichocheo cha kuhakikisha kwamba nchi yetu inapata mapato ya kuendelea na kuweza kujiendeleza vizuri, kodi imekuwa sasa ni sehemu ya kuonyesha kwamba kama mtu ametofautiana na Serikali au ametofautiana na mtu yeyote katika Serikali, basi inakuwa kama ni adhabu, kwa sababu viwango vyake vimekuwa vikubwa, kwa hiyo, vinamfanya kila mtu akikutana na mtu wa TRA, aone ni afadhali angekutana na simba kuliko kukutana na mtu wa TRA.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani ni vizuri tuvirekebishe viwango vyetu vya kodi ili vilipike na visiwe ni kichocheo cha kuwa kama adhabu kwa watu wengine ambao wanaonekana kwamba wanapingana na mitazamo fulani na fikra fulani za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili katika suala hili hili la uwekezaji, ni namna ambavyo kodi imekuwa ikilipwa na kundi fulani la watu wachache katika nchi hii. Bahati nzuri nimesikia Mheshimiwa Rais juzi akitoa takwimu kwamba mpaka sasa hivi tunavyozungumza Tanzania ina watu wasiozidi 2,700,000 kati ya watu milioni 55 ambao ni walipa kodi. Maana yake bado tuna kundi kubwa la watu ambao bado wako nje ambao hawalipi kodi. Inawezekana hatujafanya jitihada kubwa za kuwafanya hawa watu waingie.

Mheshimiwa Naibu Spika, rai yangu ni kwamba, kwa sababu kuna huo msisitizo wa Mheshimiwa Rais ni vizuri tuhakikishe kuwa tunasukuma ili watu wengi zaidi waingizwe kwenye utaratibu wa kulipa kodi ili tupunguze mzigo huu kwa watu wachache ambao sasa imefanywa kodi kuwa kama adhabu kwa watu fulani katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nizungumzie suala la vitambulisho vya wajasiriamali wadogo. Kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu amedhani kwamba mpango huu utasaidia makusanyo ya mapato katika Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika na Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kuwaambia kuwa vitambulisho hivi kwa sasa tena siyo msaada kwa Halmashauri zetu bali ni tatizo kwa Halmashauri zetu kuhusu suala la mapato. Kwa sababu wazo la vitambulisho vya wajasiriamali wadogo lilipokuwa limetolewa na Mheshimiwa Rais nilidhani lilikuwa limetazama Wamachinga wanaozunguka barabarani na mitaani, lakini leo tunavyozungumza, vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo vimeenda mpaka masokoni kwenye ambavyo ni vitega uchumi vya Halmashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wafanyabiashara wadogo wadogo walioko kwenye masoko, leo nao wanapaswa kupewa vitambulisho vya Mheshimiwa Rais. Kwa misingi hiyo, ina maana kwamba hata mapato yaliyokuwa yakipatikana kwenye masoko yetu, leo hayapatikani kwa ajili ya kuendesha Halmashauri, masoko hayana utaratibu sahihi wa kufanyiwa usafi. Kwa hiyo, mwisho wa siku zoezi hili linaweza likasababisha uchafu katika maeneo yetu mengi na masoko yetu mengi na Halmashauri zetu nyingi kukosa mapato na pia kushindwa kusafisha maeneo yao muhimu sana katika Halmashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni vizuri suala hili liangaliwe. Pamoja na nia yake njema ya kusaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kwa maana ya Wamachinga, wale wanaotembea na vitu kichwani ili watambulike, ili wasibugudhiwe, lakini ni lazima tuone namna gani mpango huu unaendelea kuzibakishia Halmashauri mapato ili dhamira hii ambayo Mheshimiwa Waziri Mkuu ameonyesha kwenye hotuba yake kwamba lengo ni kusaidia Halmashauri zipate mapato badala ya kuathirika kuhusu mapato yake. Kwa sababu kwa hali ilivyo sasa hivi hapa, mpango huu unaziathiri sana Halmashauri nyingi ambazo zilikuwa zinatumia baadhi ya maeneo kama masoko kama sehemu ya vyanzo vyake vya mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kwamba hali ya demokrasia nchini anaona inaimarika. Inawezekana hali inaimarika kwa mtazamo wa tawala, lakini kwa uhalisia na kama wote mnamwogopa Mungu, hali ya demokrasia katika nchi hii imekuwa mbaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipokuwa tupo kwenye Serikali ya Awamu ya Nne na zilizokuwa nyuma yake hali ilikuwa angalau ni nzuri hata kama ilikuwa na matatizo kidogo kidogo kuliko hali ilivyo sasa. Kwa kujidanganya kwamba hali ya demokrasia katika nchi hii inaimarika, kujidanganya kwamba chaguzi zilikuwa huru na haki, ni kujidanganya sisi wenyewe kama vile hatuoni. Kimsingi ni kwamba hali ya demokrasia katika nchi hii imekuwa ni mbaya zaidi kuliko wakati wowote mwingine katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri, tungejitathmini vizuri bila kuwa na ushabiki wa kisiasa. Katika Taifa hili hatuna ubaguzi wa kidini, hatuna ubaguzi wa kikabila, lakini tumekuwa na ubaguzi mkubwa sana wa kiitikadi. Leo kuna watu ambao katika nchi hii, kwa kuwa katika itikadi tofauti na Chama Tawala wanaonekana kama vile sio watu wenye haki na Taifa la Tanzania. Wanaonekana kwamba hawastahili kukaa Tanzania. Tumejikuta tunatengeneza mbegu ambayo mwisho wa siku itakuwa ni tatizo kubwa katika Taifa hili na inaweza ikaliumiza sana Taifa hili kwa kubaguana kiitikadi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi wote ni Watanzania tuonane kwamba tuna haki ya kuishi Tanzania na kufaidi rasilimali za Watanzania. Leo tunavyozungumza hapa, Serikali yenyewe mtazamo wake ni kwamba kimaendeleo inaweza ikadhani kwamba kupeleka maendeleo maeneo yaliyochagua CCM ni sahihi zaidi kuliko kupeleka maendeleo maeneo yaliyochagua Upinzani, wakati Upinzani uko kwa misingi ya Katiba ya nchi hii, tumekubaliana wenyewe kwamba lazima Vyama vya Siasa viwepo na wananchi wana haki ya kuchagua anayeona anafaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri tuheshimu haya mambo tuliyokubaliana kwa mujibu wa Katiba yetu ya nchi hii, kuliko kuanza kubaguana kwa misingi tuliyojiwekea wenyewe. Tunatengeneza kizazi ambacho kitakuwa ni cha ubaguzi kisichopendana bila sababu yoyote ya kimsingi. Kazi yote aliyoifanya Mwalimu Nyerere na wenzake katika nchi hii mwisho wa siku itaishia mahali pasipojulikana. Ni vizuri turudishe umoja wetu, itikadi iwe kichocheo cha maendeleo isiwe sababu ya kubaguana baina yetu sisi wenyewe kwa wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kutoa rai yangu kwa Serikali kwamba hebu rudini nyuma tazameni kwamba hivi tuko katika mstari sahihi? Hivi kweli ni sahihi kusema kwamba demokrasia imeimarika?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru kwa kupata nafasi hii ya kuchangia. Naomba nichangie hotuba zetu mbili za Kambi ya Rasmi za Upinzani naeneo kubwa ambalo nataka nichangie la kwanza, ni kuhusu kanuni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Katika hotuba Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI, ukurasa 17, kifungu cha 18, imeonesha kwamba kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zimeshakamilika lakini jambo la kushangaza ni kwamba tarehe 1, 2 na 3 Aprili, wadau wa vyama vya siasa na NGO’s na Asasi Zisizo za Kiserikali waliitwa kwa ajili ya kutoa maoni yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 4 Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokuwa anahutubia Bunge hili alisema kwamba tayari kanuni zimekamika wakati wadau waliitwa kwa ajili ya kutengeneza rasimu. Sasa tunachojiuliza hapa nikwamba wadau waliitwa kufanya nini, kwa sababu haiwezekani tarehe 1-3wadau waitwe halafu tarehe 4 Aprili, kanuni zionekane kuwa zimeshakuwa tayari wakati waliitwa kwa ajili ya kuandaa rasimu. Sasa rai yetu, tunaomba Mheshimiwa Waziri wakati anahitimisha hotuba yake atusaidie kupata nakala zile za kanuni ya uchaguzi ili tuone kama mawazo na maoni ya wadau yamechukuliwa kwa kiwango gani ili kufanya uchaguzi huu uwe ni uchaguzi ambao ni huru, utakaofanya kila mtu aliyeshiriki aone ametendewa haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninalotaka kuzungumza kuhusu kujenga taasisi kuliko kujenga mtu katika nchi yetu. Tulidhani kwamba ni vizuri katika nchi yetu tuhakikishe kwamba taasisi zetu zinakuwa imara kwa sababu watu wanapita, lakini taasisi zitaendelea kubaki. Lazima tuwe na taasisi ambazo zinahakikisha kwamba watendaji wanaoteuliwa katika nchi hii wanateuliwa kwa sababu ya uwezo wao na sio kwa sababu ya uswahiba wao na viongozi wa juu. Hawateuliwi kwa sababu wana mahusiano yoyote na viongozi wa juu bali kwa sababu wana maadili ya kuweza kuwasaidia Watanzania, taasisi zetu lazima zioneshe hivyo. Pia taasisi zetu lazima zioneshe kwamba kiongozi wa nchi hii ni mlinzi wa fedha za wananchi na sio mwenye fedha za wananchi. Kwa sababu hali ilivyo sasa walipakodi ni wananchi, lakini fedha inaonekana inayokusanywa katika nchi ni fedha ya kiongozi wa nchi. Kwa misingi hiyo ana uwezo wakuamua anavyotaka kuipeleka, ana uwezo wa kutembea nayohata kwenye maboksi akagawa barabarani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunadhani ni vizuri tujenge mfumo ambao utafanya kiongozi wa nchi afahamu fedha aliyonayo ni fedha ya wananchi kwa hiyo kila mwananchi katika nchi hii ana haki ya kupata maendeleo kwa kadri ya mchango wake.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. MAULID S. A. MTULIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na heshima yangu kubwa kwa kaka yangu Mheshimiwa Mbunge, nataka nimpe taarifa kwamba kiongozi wa nchi yetu anatambua fedha zote ni fedha za wananchi na ndio maana bajeti ya nchi inaletwa hapa kila mwaka na ndio maana tupo hapa ndani ya miezi mitatu kujadili bajeti ya nchi. Kwa hiyo,asipotoshe umma kwamba kiongozi anasema pesani za kwake, pesa za wananchi, ndio maana Wabunge tupo hapa. Taarifa hiyo nampa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Japhary.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema ni kwamba nasema tutengeneze mfumo katika Taifa letu utakaowafanya viongozi wote watambue kwamba fedha za nchi sio za kwao ila ni za walipakodi. Kwa hiyo wana haki ya kuwapelekea wananchi maendeleo kwa kadri wanavyostahili na sio kwa kadri ya utashi wake na sijazungumzia kiongozi wa nchi aliyepo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni vizuri mifumo hii ikawepo ili iheshimu demokrasia. Ndani ya nchi yetu hii leo demokrasia haipo, na kila wakati ukisema demokrasia haipolinaonekana hili ni suala la upande mmoja,lakini leo Mungu angeweza akageuza kibao, upande huo ukawa upande huu, halafu kwa mifumo hii hii tuliyonayo, Tume za Uchaguzi tulizonazo na mazingira haya tulionayo, upande huo ungelalamika kuliko upande huu.

T A A R I F A

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Nimpe Taarifa muongeaji pamoja na kwamba wenzetu wakiambiwa kwamba ipo siku moja inaweza kugeuka wanakataa, lakini katika Qurani Tukufu ipo aya inayosema hivi;Innama amruhu idha arada shay-an an yakuula lahu kun fayakuun (hakika Mwenyezi Mungu jambo analolitaka huliamrisha na kuwa).Sasa msijidanganye kwamba haiwezekani ipo siku, ipo siku.

MWENYEKITI:Mheshimiwa Japhary, huyo anachanganya.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni muumini mkubwa sana wa Mungu na kwa bahati mbaya wana siasa wanajitoa kwenye uelewa wa kumwamini Mungu, kwa taarifa iliyotolewa na Mheshimiwa Mbunge naipokea kwa mikono miwili, kwamba kilichowaweka huko mkatawala ndicho kitakachoweza kuwaweka watu hawa huko wakatawala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi ambao tunatakiwa tuujenge kwenye Taifa hili ni wote tutambue kwamba tunapaswa kuliona Taifa hili kama letu wote pamoja. Akitawala huyu aheshimu wengine anaowatawala. Sasa bahati mbaya katika Taifa hili imeonekana kwamba kuna upande ambao hili Taifa ni la kwao wengine sio Watanzania yaani tunaonekana tupo Tanzania kwa bahati mbaya tu lakini si kwamba nasi tuna haki ya kuwa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninachosema kwamba ni vizuri tutengeneze mfumo ambao utaheshimu haya, demokrasia iwe part ya maisha yetu. Haiwezekani leo Mheshimiwa katika Taifa hili CCM wanafanya mikutano ya hadhara ya ndani, wanafanya maandamo, wanalindwa lakini kila siku Wapinzani wanaandamwa ndani ya Taifa moja na Wapinzani hawajavunja sheria kwa sababu hawajawaWapinzani kwa sababu wametaka kuwa hivyo bali katiba imewaruhusu kuwa hivyo. Vyama vingi vya siasa vimeruhusiwa na Katiba ya nchi yetu. Hivyo,ni wajibu wetu sote sisi tuheshimiane kwa sababuKatiba inaruhusu kuwe kwetu sisi na kuwepo kwenu nyie.

Mheshimiwa Mwenyekiti,Katiba inakuwepo ili sisi tuwakosoe nyie na sio tuwasifu nyie, hatupo hapa kwa ajili ya kuwasifu, ingekuwa kuwasifu tungekuwa upande wenu. Tupo upande huu ili tuwakosoe ili siye tuwe kioo kwenu ili mfanye vizuri, mnatulazimisha tukae Bungeni kuwasifu inaonekana as if kuwakosoa ni kumchukia Rais, si kweli. Hatumchukii Rais bali tunatimiza wajibu wetu wa kuwakosoa, tunam-shape Rais aweze kuongoza vizuri, ndio maana ya kuwa huku. Sasa ninyi mnadhani kumkosoa Rais ni kumkosea adabu Rais, si kweli na ubaya zaidi mnamfanya Rais ahisi kwamba sisi tuna ugomvi na yeye, tuna chuki na yeye, baadala ya kumsaidia kwamba hawa ni wenzako wanaku- shape ukae vizuri. Kwa hiyo nadhani mfumo mzuri wa utawala ndani ya nchi hii utatufanya tukae vizuri. Kwa hiyo,hiyo ndio rai yangu kwaWaheshimiwa viongozi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la tatu, nataka nizungumze suala la TARURA, Bunge lako Tukufu liliridhia kuanzishwa kwaTARURAkatika nchi hii, lakini TARURA malengo yake ya msingi kama yalivyofikiriwa hayawezi kuwa msaada sasa kama TARURA haitaangaliwa vinginevyo. Sasa hivi Wakala wa Ujenzi wa Barabara Vijiji na Mjini hajawa msaada sana wa kuhakikisha barabara zetu zinakuwa kama zilivyokuwa zimetegemewa ni vizuri Mheshimiwa Waziri tuone namna gani tunahakikisha kwamba moja tunapeleka bajeti ya kutosha kwenye wakala huyu ili afanye vizuri kwenye barabara zetu,otherwise barabara ni mbaya zaidi kuliko hata wakati zikisimamiwa na Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri wakati Halmashauri zikisimamia barabara zilikuwa zinauwezo wa kutenga fedha kwenye Kamati zao za dharura zikahakikisha barabara zao zinatengezwa. TARURA hawana hiyo fedha mpaka wasubiri fedha kutoka kwenye Mfuko Mkuu, matokeo yake wanashindwa kufanya kazi yao inayotarajiwa. Barabara nyingi zinakuwa mbovuna yakitokea majanga ya mafuriko na mambo mengine inakuwa vigumu sana barabara zetu kutengenezwa kwa hiyo hali inakuwa ni mbaya zaidi. Ni vizuri tuongeze bajeti ya kutosha nani vizuri tutafute vyanzo vingine kwa TARURA ili waweze kuhakikisha kwamba wanasimamia zoezi hili vizuri na malengo ya Wabunge kuomba agency hii iundwe yawe na maana. Kwa hiyo, nashauri sana tuangalie hili katika uzito wake wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti,la pili, katika TARURAni vizuri tuone jinsi gani Madiwani wanashirikishwa, Madiwani wanakuwa kama sio sehemu ya Halmashauri husika wala miji husika, matokeo yake maamuzi ya watendaji wa TARURAyanakuwa ni wao wenyewe. Sasa tuangalie sheria yetu itafanyaje Madiwani washirikishwe ndani ya TARURA hata kama angalau Kamati za Fedha zipewe taarifa ya namna gani TARURAinaendelea na pia TARURA iheshimu vipaumbele vya Halmashauri. Ingesaidia sana suala la kuzisaidia mamlaka hizi kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho ni D by D kumekuwa na hoja nyingi sana kwa upande huu zaidi kwamba Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya wamekuwa wakigombana na Halmashauri, lakini kama mfumo huu D by D Policy yake ingezingatiwa vizuri Wakuu wa Mikoa wakaelewa vizuri na ndio maana nikasema ni vizuri hata wanaochaguliwa, wachaguliwe kwa ethics zao, wachaguliwe kwa uwezo wao na sio kwa ukada wao, leo hii migogoro isingekuwa inaendelea katika Halmashauri zetu. Ipo hivi kwa sababu viongozi wetu wengi wa Mikoa na Wilaya wameshindwa kufuata maadili yao, wamekwenda kwa ukada, wamekwenda kwa ajili ya kuwaumiza Wapinzani au kuumiza watu waliopo chini yao. Matokeo yake imekuwa vurugu kila siku mpaka kila siku…

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Japhary.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL:Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi hii ya kuchangia katika Wizara hii ya Viwanda. Nafikiri tatizo tulilonalo katika nchi yetu ni viongozi wetu wengi na Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi muda mrefu kuishi kwa kaulimbiu bila kuwa na utekelezaji. Kwa sababu tangu awamu zilizopita zote kuacha Awamu hii ya Tano, ukiangalia mtazamo wa viongozi wakuu ilikuwa ni Tanzania ya viwanda, wala wazo hili halijaanza sasa kwa Awamu ya Tano, lakini suala ni kwamba je, katika muda wote huo ni kwa kiwango gani tumefikia kwenye malengo ambayo tumekuwa tukiyazungumza; ni utayari gani uliopo juu ya viongozi wetu wanaopewa hizo dhamana za kutekeleza hayo? Ndilo swali ambalo tunatakiwa wote tujiulize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana wakati mwingine viongozi wetu wakuu wana mawazo mazuri sana ya kutupeleka mahali, lakini inawezekana wasaidizi wao ama hawako tayari au hawana uelewa juu ya dhamira za viongozi wakuu wanazokuwa nazo juu ya safari tunayotakiwa twende. Kwa hiyo kuna haja ya kubadilisha sana mawazo na mitazamo yetu ili tufikie hapa tunapotarajia kupafikia. Vinginevyo dhana hii ya Tanzania ya viwanda itakuwa inakuwa ni wimbo tu kama ambavyo zimekuwa ni nyimbo tangu baada ya Serikali ya Awamu ya Kwanza katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani lilikuwa jambo jema tu kwamba Serikali ya Awamu ya Tano kwa sababu imeamua kufikia malengo ya kuwa na Tanzania ya viwanda, kufikia uchumi wa kati, basi ingerudi pale ambapo mwaka 1985 Mwalimu Nyerere aliachia wakati anaacha nchi hii. Kwa sababu miaka hiyo tayari mwelekeo wa namna gani tunatakiwa tujenge Taifa la viwanda ulishaonekana katika nchi hii. Bahati mbaya Serikali hii hii ya Chama cha Mapinduzi, viongozi waliofuata baada ya Mwalimu wakaamua kuondoa yale matumaini yote ambayo yalikuwa yamewekwa kwa Watanzania juu ya kujenga Tanzania ya viwanda. Tumerudisha wazo hilo sasa kwa Awamu hii ya Tano, je, sisi wasaidizi wa Rais tuko tayari katika kufikia malengo hayo ama tunajaribu kumwonesha Rais kwamba tuna dhamira wakati hatuna dhamira hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri unajaribu kutafakari, je, kweli tuna hiyo dhamira; tumedhamiria kufika Tanzania ya viwanda? Kwa hiyo haya ni maswali ambayo sote tunatakiwa tujiulize kwa pamoja na nafikiri kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi wanatakiwa wajiangalie sana, tusipende kuishi kwa kauli mbiu ambazo tunazi-take by event, kwa matukio na hatuzifanyii kazi. Tusifanye suala la viwanda kama suala la zimamoto, tudhamirie kweli kwamba tunajenga Tanzania ya viwanda kwa sababu ni ukweli kwamba ndiyo kichocheo cha maendeleo ya Taifa hili kwa sasa na kwa siku zijazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kitabu hiki cha bajeti, ukiangalia trend ya bajeti ya Wizara ya Viwanda mwaka 2017/2018, 2018/2019 na hata 2019/2020, unaona kabisa kwamba bajeti iliyotengwa inaonesha kwamba Serikali ina dhamira ya ku-facilitate ukuaji wa viwanda katika nchi hii na ukuaji wa biashara katika nchi hii. Hata hivyo, tofauti yake ni kwamba ukiangalia maneno ya viongozi wa Serikali, maneno hata ya kiongozi wetu mkuu, inaonekana kama vile Serikali imeamua sasa kufanya biashara yenyewe, imeamua kuendesha viwanda yenyewe, imeamua ku- centralize hivi vitu badala ya mfumo ambao tulishazoea kwamba tunategemea kuimarisha Private Sector.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa matokeo yake Serikali inachukua majukumu mazito sana. Ukiangalia bajeti hii ina fedha ndogo sana lakini hushangai kwa bajeti ndogo kwa sababu dhamira ya kweli ya Serikali ilikuwa ni kusaidia kuhakikisha mazingira mazuri ya biashara katika nchi hii, mazingira mazuri ya uwekezaji katika nchi hii, mazingira mazuri ya uwepo wa viwanda katika nchi hii, lakini ukweli halisi ulioko kwenye utendaji, Serikali inaonesha wananchi kwamba yenyewe ndiyo inataka ifanye kazi ya biashara, ifanye kazi ya kujenga viwanda na vitu vingine kama hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo inaonekana kwamba wana-discourage sekta binafsi, hawataki kui-encourage sekta binafsi, ndiyo maana kila anayenyanyuka hapa anasema kuna vikwazo vingi sana kwa wafanyabiashara ambao ni ukweli ulio halisi. Leo Wabunge hapa wanalalamika kuhusu hivi vi-regulator vingi ambavyo vimekuwepo vinavyotoza wafanyabiashara. Sasa swali langu najiuliza, kama Serikali wanasikia haya Wabunge wanayolalamika, hao regulators wote kama TFDA, TBS na nyingine nyingi zimewekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, kwa nini Waziri asifanye kazi rahisi tu mpaka leo aambiwe ajiuzulu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri alete sheria hapa viunganishe hivi vitu, waambiwe Wabunge wabadilishe sheria, kwa sababu hivi tunavyozungumza viko kwa mujibu wa sheria; TFDA wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, TBS kwa mujibu wa sheria, OSHA kwa mujibu wa sheria. Bahati mbaya bado hawajaanza kutufunga, wakianza kutufunga ndiyo tutajua kwamba wapo kwa mujibu wa sheria mlizotunga ninyi wenyewe, sasa hivi bado wanatupiga tu penati, wanatuadhibu, sheria zinaruhusu watufunge, sasa siku wakianza kuwafunga hapa ndiyo tutaona kelele zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo cha msingi, Serikali walete mapendekezo hapa au hoja, Wabunge wajadili, waone namna gani wanawapunguzia wafanyabiashara hizi adha. Vinginevyo watu wa OSHA watalalamikiwa wakati wanaangalia sheria; TRA watalalamikiwa wakati wanaangalia sheria na wengine wote watalalamikiwa wakati sheria mmetunga wenyewe hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo TRA wangefanya kazi kwa mujibu wa sheria ilivyo kila mtu huku ndani angekuwa amefungwa kama ni mfanyabiashara. Kwa hiyo watu wanasema TRA ni wabaya sana, lakini ukiniuliza nitakwambia TRA hawajawa wabaya kwa sababu bado hawajafunga watu, bado wanakudai fedha zao ambazo hujalipa, penati kama hujalipa au umechelewa kwa muda, lakini kama unataka kufanya kazi kama ilivyo watafunga hata watu wengine hapa ndani, kila siku watu watafungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nafikiri kwa sababu wanaolalamika ni Wabunge na ndio wanaomwelekeza Mheshimiwa Waziri, ni rahisi tu; alete sheria hapa zibadilishwe ziweze kusaidia nchi yetu iende mbele na tuweze kukuza viwanda vyetu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli kwamba kufanya biashara katika Tanzania ni adhabu kubwa sana. Wakati naingia kama Mbunge hapa nilikuwa nafikiri labda Wabunge humu ndani hawajui ugumu huu, lakini baadaye nikagundua viongozi wengi walikataa biashara wakaamua kuwa wakulima na kule kwenye kilimo wamejifichia huko, wana mamilioni ya pesa kibao lakini wamejifichia huko. Sasa mateso yote yako kwa wafanyabiashara, yaani ukiamua kufanya biashara wewe katika nchi hii ni umenunua mateso makubwa sana katika Taifa hili, kwa nini? Kwa sababu siku zote wamekuwa wakiwa na perception ya kupata kodi, kupata fedha, lakini hawataki kumlea huyo ng’ombe ambaye wanamkamua ili wapate hiyo kodi, hawataki kabisa, yaani Serikali inafikiri kodi tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumzia katika Taifa hili biashara zimefungwa nyingi halafu watu tumekaa kimya na kuna majibu yanakuja kwamba biashara zilizofungwa ni watu ambao wanakwepa kodi, as if hao sio Watanzania. Walishaenda wakaonana nao, wakafahamu kwa nini wamefunga hizo biashara? Kwa nini wafikiri tu kwamba ni kwa sababu wamekwepa kodi, kwa nini wafikiri kitu kimoja tu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunavyozungumza kila kukicha biashara zinafungwa. Inawezekana hazijafika milioni, lakini ukweli unabaki kwamba kuna biashara kadhaa zimefungwa katika Taifa hili, zimefungwa kwa nini? Kwa sababu ya mfumo usio rafiki kwa wafanyabiashara wa nchi hii. Je, Waziri na Wizara yake wamewasaidiaje wafanyabiashara? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapokaa hapa kama watetezi tusiwafanye wafanyabiashara kama watu wasiotuhusu. Tuna tatizo kubwa la nchi hii kuamini kwamba wafanyabiashara wote ni mabepari, wafanyabiashara wote wanakwepa kodi, which is not true. Kuna wafanyabiashara wanalipa kodi, mfumo wetu wa kodi ndiyo sio mzuri. Sasa tuwasaidie wafanyabiashara hawa na ndiyo kazi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuwasaidia wafanyabiashara. Kwa hiyo naomba Mheshimiwa Waziri ili aweze kuacha legacy asaidie wafanyabiashara, asimwachie jukumu hili Mheshimiwa Rais peke yake. Rais mpaka aamke, akishaamka na wao ndiyo wanaamka, haiwezekani, hatuwezi kuendesha Serikali ambayo Rais ndio everything. Rais ana wasaidizi wake, Urais ni taasisi, lazima asaidiwe na je, wanamsaidia inavyostahili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tusipoweka dhamira ya kutosha, leo tunazungumzia habari ya viwanda karibu 4,000 na kitu ambavyo vimekua katika nchi hii. Hata kama hivyo viwanda tunasema ni vya vyerehani, ni vya nini, lakini kwa mujibu wa kanuni ni viwanda vidogo. Wajibu wetu, je, tuna mkakati gani wa kuinua hawa wawekezaji wa viwanda wadogowadogo wawe wawekezaji wakubwa wa viwanda; wajibu huo tumejipangaje nao? Kwa sababu leo Wachina tunaozungumza miaka ya 2000 ukienda kwao kule Guangzhou ilikuwa watu wanazalisha bidhaa zao, chaki mtu anazalisha kwenye kibanda cha nyumbani, lakini leo Wachina hao hao wamekuwa ni mabilionea katika nchi zao. Je, sisi tunajiandaa vipi kuwa-empower hawa wafanyabiashara wadogowadogo wawe wafanyabiashara wakubwa ndani ya nchi yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama tunataka kufikia malengo ya kuwa Tanzania ya viwanda, tuna kazi kubwa ya kufanya na tudhamirie, tuwe na viongozi wabunifu, waliodhamiria kulipeleka Taifa hili mbele. Kama viongozi watabaki kuishi maisha yaleyale waliyozoea kumdanganya Rais kwamba wanafanya wakati hawafanyi ili wapate Uwaziri, wapate Naibu Uwaziri, wapate Ukatibu Mkuu, nchi hii hatuendi popote na kila siku tutakuwa na wimbo wa Tanzania ya viwanda ambayo hatutaifikia na itakuja Serikali nyingine na wao wamesema wanataka kutawala miaka mia moja, watatawala miaka mia moja wakiwa wanaishi katika Tanzania ambayo sio ya viwanda wala sio ya kilimo, itakuwa Tanzania… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Japhary.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hayo ndiyo yalikuwa maombi yangu, naomba kushauri, nashukuru sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia bajeti hii ya Serikali ya mwaka 2019/2020. Mchango wangu kwa Serikali ni kwamba tuna kipindi cha miaka minne tangu tumepewa dhamana kwa upande wa Chama cha Mapinduzi kuongoza nchi hii, nilitaka kupata tafakari ya Serikali kwamba je, kwa miaka minne hiki walicho-achieve ndiyo yalikuwa matarajio ya Watanzania? Na ninajaribu kutafakarisha Serikali kwa sababu naamini mwaka 2015 wakati wa kampeni za kuogombea kila upande ulikuwa na movement zake for change. CHADEMA walikuwa na movement for change na upande wa CCM walikuwa na Magufuli for change. Maana yake nikwamba wananchi walikuwa na matumaini makubwa sana ya mabadiliko makubwa ya maisha yao katika nchi hii.

Mheshimiwa Spika, sasa nilifikiri kwamba labda Serikali itafakari baada ya miaka minne yale matatizo ya wananchi yametatuliwa na yametatuliwa kwa kiwango gani? Nadhani tungetafakari hili kwa undani tungejipima vizuri zaidi. Hapa tunabishana kati ya maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu ambayo kwa ujumla yote ni muhimu katika nchi yetu. Lakini wananchi walipokuwa wanakimbizana na sisi barabara zilikuwa hazijengwi? Wananchi walipokuwa wanakimbizana na sisi reli zilikuwa hazijengwi? Ndege zilikuwa hazipo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa haya maswali tukitafakari tutajua hitaji kubwa la wananchi katika nchi hii ilikuwa kuondokana na umaskini walionao. Je, katika miaka yetu minne tumeweza kuondoa umaskini Watanzania walio nao? Hayo ndio nafikiri maswali ya msingi ya kuuliza. Hivi sisi tunataka tushukudie nini?

Mheshimiwa Spika, nadhani sisi Watanzania hasa Chama cha Mapinduzi tunakuwa wagumu kuamini kuliko hata tomaso alivyokuwa ameamini ufufuko wa Yesu. Kwa nini kwa sababu Watanzania wote tuliopo hapa tunafahamu kabisa ndugu zetu ni maskini, wana maisha ya dhiki, wana matatizo, wote Wabunge hapa tuliopo hapa ndani tunajua kwamba tuna matatizo makubwa ya dependence ya watu wetu, kwa sababu hawana uwezo na tuna uhakika kwamba dependence imeongezeka halafu tunaambia uchumi unakuwa kwa 7% kwa hiyo articulate hali yetu ya maisha ya Watanzania na tunapongezana kabisa yaani mnapongezana as if your doing so well, hamtaki kukubali kwamba Taifa limerudi nyuma mno maisha ya watanzania yamezidi kudidimia.

Mheshimiwa Spika, lazima tujipime kwamba hivi mwaka 2015 maisha ya Watanzania yalivyokuwa ya huko kijiji na miaka minne sasa maisha yalivyo. Hivi mazuri yakikuwa wakati gani yalikuwa mazuri kipindi hicho au kipindi hiki? Ndicho kipimo cha maendeleo ya wananchi. Sasa nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri anisaidia ni mtu mwenye weledi mkubwa sana na ni mbobezi wa masuala ya uchumi anisaidie na Naibu wake Waziri nawaamini kabisa kwa uwezo wao, sina mashaka nao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda waniambie ni kwa nini wamechagua mtazamo wa uchumi uliofungika kwa maana ya contractionary economic policy and in ward looking policy kuliko kuangalia expansionary policy uchumi unaoangalia nje zaidi. Tafakuri yangu inaniambia tunapotazama uchumi wa ndani tukaangalia kodi zetu za ndani na mapato mengine yasiyo ya kodi ya ndani kama chanzo cha ku-finance miradi ya maendeleo tunazidi kuumiza watu wetu. Tunaweza tukawa na mawazo bora sana ya kusaidia miradi mikubwa ya nchi hii, ya kusaidia maendeleo ya nchi hii lakini tukaosa approach bora ya kui- finance miradi hiyo hayo ndio mawazo nafikiri hayo ndio mawazo ya Kambi ya Upinzani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani haijawahi kufikiri kwamba kuna ubaya wa kujenga reli, Kambi ya Upinzani haijawahi kufikiri kama kuna ubaya wa kuwekeza kwenye ndege, Kambi ya Upinzani haijawahi kufikiri kwamba kuna ubaya wa kuwekeza kwenye miundombinu yoyote ile. Lakini tunadhani tunachofautiana Mheshimiwa Waziri katika approch ni namna gani tu-finance hii mipango ili wananchi wetu wa chini wasiteseke. Sasa problem tuliyonayo ni kwamba tunabishana hapa tu kwamba labda kuna watu wanaopinga haya mambo, which is not true. Wote tunakubali kwamba lazima wananchi waendelee, lakini approach zetu zikoje katika suala la mitazamo ya kiuchumi, sasa nyie ni wabobezi wakubwa mliopewa dhamana hii kubwa, ni vizuri Mheshimiwa Waziri na mimi ungeniambia ni kwa nini ume- opt kwenye mawazo ya uchumi uliofungika ya kubana uchumi zaidi kuliko kufungua uchumi, nadhani unge-opt kwenye approach ya kufungua uchumi leo hotuba yako Mheshimiwa Waziri ingekuwa inaonesha namna gani uta- attract FDI - Foreign Direct Investment katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, hotuba hii ingeonyesha hivi kama solution, labda hotuba leo ingeonesha namna gani uta- incorporate PPP - Public Private Partnership ambayo ingeweza kusaidia, lakini kwenye mpango wenu mnaonekana sana kwamba mna-discourage PPP, mna- discourage uwekezaji kutoka nje. Mnaamini kwamba through hizi Kodi ambazo mnaumiza wafanyabiashara, mnaumiza wafanyakazi zinaweza zikawasaidia kwenda mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwangu mimi naamini kwa Kambi ya Upinzani hatuamini kwamba mko kwenye mtazamo sahihi, ndiyo ninachofikiri hicho na kimsingi hapa ndipo tunapopata tatizo hapa, kigugumizi kwa sababu watu hasa tunabishana, hivi wananchi wanapata maendeleo ama ni wanataka vitu?

Wananchi wanataka vitu maendeleo ya vitu, lakini wanachotaka maendeleo yao pia. Hawataki vitu tu, wanataka wapate uhakika wa huduma za afya, wanataka wapate uhakika wa huduma za maji, wanataka uhakika wa kipato cha kulisha familia zao, wanataka wapate uhakika kusomesha watoto wao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hamuwezi kusema mme-achieve economically while people are suffering, na mnakusanya Kodi mnazitumia kwa expense ya maisha ya Watanzania kwa sacrifice ya maisha ya Watanzania, haiwezekani, kwa hiyo ni lazima Mheshimiwa Waziri kwa uwezo wako na kwa ubobezi wenu mtazame hili kwa upana wake, na hili nafikiri siyo jambo la kubishana sana ni jambo la kutazama namna gani tunahakikisha miradi ya maendeleo inafanyika lakini namna gani tunahakikisha kwamba watu wetu wanapata huduma wanazostahili na vipato vyao vinakuwa, ili na wananchi nao wa-feel huu uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unapowekeza kwenye standard gauge unafanya jambo jema, lakini mradi utakapo toa matokea baadaye sana je kwa sasa hivi Mwananchi huyu wa Tanzania aendelee, amefunga mikanda for fifty years, hajapata mabadiliko, amepata matumaini kwamba baada ya kuingia Serikali hii atapata mabadiliko, ataongeza kipato chake, as we are talking leo mfanyakazi hajaongezewa mshahara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninapozungumzia leo...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, watu wanapunguzwa kazi, tunapozungumzia leo biashara zinafungwa, ninapozungumzia leo matatizo ni mengi makubwa katika nchi hii, lakini sisi tukikaa hapa kwenye Bunge hili tunapongezana kwamba tunafanya vizuri katika uchumi huu, tunahitaji philosophy za kitaalam sana tuchanganyane huku ndani, lakini wananchi...(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Japhary.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, philosophy, kwa hiyo ninadhani ni wakati wa kutafakari...

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

SPIKA: Eti! Ni ya pili tayari.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, ya kwanza.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

SPIKA: No, alianza na dakika 35.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, ya kwanza.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

SPIKA: Tayari ni dakika kumi. (Makofi)

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, Ya kwanza.

SPIKA: Wala hujaonewa kabisa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, nimeonewa kwa kweli.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

SPIKA: Tayari, tayari dakika kumi.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali itoe msamaha kwa wafanyabiashara wote wa magari na pikipiki ambao waliuza vyombo hivyo vya moto lakini wanunuzi hawakubadilisha majina. Natoa ushauri huo kwa sababu mbili kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, Sheria ya Annual Motor Vehicle License haimlazimishi muuzaji kulazimisha mnunuzi kufanya mabadiliko ya umiliki. Sheria inampa mnunuzi siku saba mpaka thelathini za kufanya mabadiliko ya mmiliki (Transfer of Ownership), hivyo hata asipofanya mabadiliko ya umiliki hakuna namna ambavyo muuzaji anaweza kufahamu kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hiyo inafanya vyombo vingi vya moto kubaki na majina ya wauzaji kwenda muda mrefu, hivyo kusababisha wafanyabiashara wa magari na pikipiki kudaiwa madeni makubwa kupitia TIN zao. Mheshimiwa Waziri, akitaka kuwasaidia wafanyabiashara hao, ni jambo la busara kutoa msamaha wa madeni wanayodaiwa ili wasifilisiwe na TRA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, madeni hayo yamekuwa ya muda mrefu sana kutokana na Mamlaka ya TRA kutokumbusha wafanyabiashara wa magari na pikipiki kwamba wanabeba jukumu la kulipa Motor Vehicle License kwa vyombo ambavyo walikwishauza, lakini wanunuzi hawakubadilisha umiliki wake. Makampuni mengi yameshafanyiwa ukaguzi zaidi ya mara moja na wakalipa kodi ya Serikali. Nadhani siyo jambo la afya sana kuwabebesha wafanyabiashara hao mzigo huo mkubwa wa deni ambao siyo wa kwao moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi wa hoja yangu ni kwamba Serikali ni lazima ijenge mazingira rafiki kwa wafanyabiashara kwa vile ndiyo wateja wao. Hivyo, kutokana na ukweli kwamba kuna eneo ambalo mamlaka yenyewe ya TRA ilijisahau kuwakumbusha wafanyabiashara wajibu wao katika kufuatilia mabadiliko ya umiliki wa vyombo vya moto kwa wanunuzi, ni vema Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa mamlaka aliyonayo akaona busara ya kutoa msamaha wa madeni hayo makubwa wanayodaiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri aelewe kwamba madeni mengine yana miaka 10 au zaidi, hivyo ni vigumu sana kwa wafanyabiashara kuweza kulipa madeni hayo. Nashauri Mheshimiwa Waziri atoe msamaha wa hayo madeni ya Motor Vehicle Licence ili waanze ukurasa mpya na wafanyabiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri mambo mawili muhimu katika suala la mashine za EFD. Kwanza, kuna maeneo mengi katika mikoa ya nchi hii ambayo hayajalazimishwa kutumia EFD machine. Mikoa kama ya Dodoma na mingineyo, biashara nyingi kubwa hazina EFD machine wakati Mkoa kama wa Kilimanjaro biashara ndogo tu zinatumia EFD machine. Naishauri Serikali ihakikishe EFDs machine zinatumika sawasawa na kwa haki nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, EFDs machine zinaharibika mara kwa mara, hivyo kuwafanya wafanyabiashara wabebe mizigo mikubwa katika kuzirekebisha au kufanyia matengenezo; na gharama za matengenezo ni kubwa kuanzia kati ya Sh.50,000/= mpaka Sh.150,000/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Hospitali ya Wilaya katika Manispaa ya Moshi. Manispaa ya Moshi ina mahitaji makubwa sana ya Hospitali ya Wilaya kwa vile Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi imezidiwa na wagonjwa na Hospitali ya KCMC pia imezidiwa na wagonjwa. Hospitali zote hizi mbili zinahudumia wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali nje ya Manispaa ya Moshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Moshi ina eneo ambalo imelitenga kwa ajili ya ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya. Hivyo, ni matumaini yangu kwamba Serikali italifanyia kazi ombi langu kwa niaba ya wananchi wa Moshi Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupandishwa hadhi vituo vitatu vya zahanati kuwa vituo vya afya. Manispaa ya Moshi imeleta maombi ya muda mrefu Serikalini ya kupandisha hadhi zahanati tatu za Shirimatunda, Msaranga na Longuo B. Maombi hayo ni muhimu sana kwa vile idadi ya watu inaongezeka kila siku katika Manispaa ya Moshi. Kutokana na ongezeko hilo, mahitaji ya huduma ya matibabu yanaongezeka kwa kasi. Naomba Serikali ipandishe hadhi zahanati tajwa hapo juu kuwa vituo vya afya ili kuwasaidia wananchi kupata huduma kirahisi zaidi na kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa niaba ya wananchi wa Manispaa ya Moshi, Serikali itenge fedha kwa ajili ya kuboresha kituo cha afya kimoja katika Manispaa ya Moshi ili kutoa huduma bora kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vya Mkoa wa Kilimanjaro vilivyobinafsishwa bado havijaanza kufanya kazi kama ambavyo Serikali imekuwa ikiagiza. Mji wa Moshi katika miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa miaka ya 90 ulikuwa una viwanda vikubwa zaidi ya 12 ikiwa ni pamoja na viwanda vya watu binafsi. Viwanda hivyo ni pamoja na viwanda vya magunia, ngozi, mbao, nguo, pipi, vibiriti, karatasi na kadhalika. Hali ilivyo sasa ni tofauti kabisa kwa vile viwanda vyote hivyo vimekufa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Serikali ipitie upya kanzidata ya viwanda katika Mkoa wa Kilimanjaro ili ione ni namna gani inaweza kufufua viwanda vilivyokufa katika Mji wa Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla. Kufufuliwa kwa viwanda hivyo kutachochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla. Pia, kutaongeza ajira na mambo mengine kama hayo. Aidha, ni vizuri Wizara ikawatafuta wawekezaji binafsi ambao viwanda vyao vimekufa ili kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikishana namna bora ya kuvifufua.

Mheshimiwa Naibu Spika, uimarishaji wa soko la ndani. Dhamira ya Serikali ya kujenga Tanzania ya Viwanda itafikiwa iwapo tutaimarisha soko la ndani. Soko la ndani ndilo litakalohakikisha mauzo ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani. Wajibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ni kutoa msukumo na motisha kwa wafanyabiashara wa Tanzania ili biashara zao ziimarike ambapo wataweza kuajiri wafanyakazi wengi sana, hivyo kuongeza kipato cha Watanzania na kwa maana hiyo kuongeza nguvu ya soko (purchasing power).

Mheshimiwa Naibu Spika, soko la ndani ndilo linaweza kufanya wawekezaji wa kiwango cha kati na cha chini kuimarika na baadaye kuwa wawekezaji wakubwa watakaouza nje. Soko la ndani ndilo linaweza kukuza kidogokidogo viwango vya bidhaa zetu zinazozalishwa na kuziingiza kwenye ushindani wa soko la nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kodi ya Huduma (Service Levy). Sheria ya Kodi hii ya Huduma lazima ibadilishwe ili iweze kulipika. Utaratibu wa sasa ambapo kodi hii inalipwa kwa kigezo cha mauzo ghafi siyo utaratibu wenye tija kwa wafanyabiashara na kwa Taifa kwa ujumla. Utaratibu huu unaweza ukafilisi wafanyabiashara kama ukitekelezwa kama ulivyo. Hivyo, ushauri wangu ni kwamba kodi hii itozwe katika faida na kama haifai kutozwa katika faida itozwe kwa viwango kulingana na madaraja ya biashara.
Muswada wa Sheria ya Reli wa Mwaka 2017
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia. Pamoja na hoja zangu nyingi kwamba zinaangua alipopita mchangiaji aliyetangulia.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, ninaunga mkono hoja ya kuunganisha Shirika la TRL na RAHCO, jambo ambalo tumelipigia kelele kwa muda mrefu na nashukuru Mungu kwamba leo limetekelezwa; linaweza likachangia katika ubora wa huduma ya shirika la Reli lenyewe kwa maana ya iliyokuwa TRL lakini na kwa maana miundombinu ya reli yenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu kubwa ambayo naiomba Serikali iangalie kwa makini ni hoja ya ubomoaji. Maeneo mengi wananchi wamekaa kwa muda mrefu, kama walivyotangulia kusema wengine, Serikali ikiwa inawaangalia, mamlaka mbalimbali zikiwa zinawaangalia. Pamoja na kwamba kuna sheria ambazo pia zinawaruhusu wanapokaa muda mrefu kuwa na haki hiyo ya kuwa katika maeneo hayo, lakini watumishi wa RAHCO walikuwepo, wameangalia watu wakijenga structures mbalimbali katika hifadhi ya reli lakini hawakuchukua hatua. Leo wananchi wale wanaadhibiwa kwa kuvunjiwa nyumba zao, wananchi maskini ambao hawana uwezo na Mtanzania kujenga nyumba sio jambo jepesi, leo anavunjiwa kirahisi, lakini wale waliosababisha hiyo adha hawajaonesha kuchukuliwa hatua yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni vizuri Serikali ikatazama kwanza namna gani inaweza ikatumia busara kuwasaidia hawa wananchi waliojenga hizo nyumba angalau kwa kufikiri kuwapa fidia ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha mbele ya safari. Ni ukweli kwamba ni lazima maeneo hayo ya hifadhi ya reli yabaki yakiwa wazi, lakini wananchi waliojenga kwa sababu waliachiwa wakajenga, basi wafikiriwe jinsi ya kutoa fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hata wale maafisa wa Serikali ambao hawakutimiza wajibu wao basi wachukuliwa hatua stahili ili angalau mambo haya yasijirudie tena. Kama tutaacha kuwachukulia hatua maana yake wataendelea kuona ni jambo la kawaida na yatakuwa ni maisha ya kawaida kwa watumishi wengine ambao wapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kubwa zaidi ni kwamba kuna watu ambao wako kwenye maeneo tayari kihalali kwa sababu wana hatimiliki na wamepitia mchakato wote wa kubadilisha maeneo hayo. Pale Moshi kuna eneo ambalo sasa hivi ninavyoongea kuna vurugu iko pale, watu 48 wameathirika, wamewekewa alama ya “X” eneo ambalo haliko kwenye hifadhi ya reli, lakini inasemekana huko nyuma ilikuwa ni eneo la reli, miaka zaidi ya sabini iliyopita. Mamlaka ya Serikali za Mitaa ilishaomba mabadiliko ya matumizi ya eneo lile na wakakubaliwa na Wizara ya Ardhi, watu wamepimiwa, wamepewa vibali vya ujenzi, leo hivi wanaambiwa kwamba hata eneo ambalo lilikuwa la halmashauri, ina hatimiliki, nalo limewekwa alama ya “X” , ni la kuvunjwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa unajaribu kujiuliza Serikali inafanyaje kazi? Mimi naamini kabisa kwamba Wizara ya Ardhi ina records za ardhi za maeneo yote, ramani zote, haiwezi kutoa kibali cha mabadiliko ya matumizi ya eneo kama eneo hilo lina hati nyingine mpaka libatilishe ile hati. Sasa ilikuaje watu wapewe hati juu ya hati nyingine kama hali iko hivyo?

Kwa hiyo, nadhani Serikali ina haja ya kujitathmini kwa kuyaangalia maeneo na kuyavunja kwa vigezo mbalimbali si kwa kigezo kimoja. Kwamba kila mtu aangaliwe ni namna gani aliingia katika eneo na namna gani anapaswa kusaidiwa ili angalau wananchi wasipate sana hasara kutokana na uamuzi huu wa Serikali wa kuvunja maeneo ambayo yalikuwa ni maeneo ya reli na mojawapo naomba Mheshimiwa Waziri anisaidie sana eneo la Mji wa Moshi kwa sababu mji ule wanaovunjiwa hawapo kwenye hifadhi ya reli.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la abiria ambao bahati mbaya wanakuwa wamecheleweshewa safari yao na Shirika la Reli ni lazima liangaliwe. Kama tunataka kuliingiza shirika hili kwenye ushindani ni lazima liwe tayari kuwafidia abiria ambao kwa uzembe wao ndio wamewachelewesha. Kama abiria wanapaswa kusafiri saa tano asubuhi, wasafiri, na kama hawasafiri kwa sababu wamecheleweshwa na Shirika la Reli basi wafidiwe. Wafidiwe gharama ya malazi, wafidiwe gharama ya chakula, kwa sababu huo ni uzembe wa Shirika la Reli.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa wananchi wanapokuwa wamecheleweshwa halafu wakapata adhabu ni kulidumaza Shirika la Reli na kuliacha lisiwe katika ushindani. Ni lazima shirika hili liwe la kibiashara na liingie katika ushindani kama mashirika mengine. Na shirika hili hatutegemei abiria wake wawe ni watu wa ndani tu, hata wa nje wanaweza wakasafiri, watalii wanaweza wakatumia reli kusafiri. Sasa kama hatuna sheria za kimataifa za namna ya kuwahudumia abiria maana yake tutakuwa hatuko kibiashara na shirika linaweza likapata pia shida ya kufa tena mbele ya safari. Kwa hiyo ni vizuri tujitahidi tutoe huduma nzuri na ya kutosha kwa abiria.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la tiketi; tiketi wanasema kwamba kama umepakia treni sehemu ambayo siyo bila tiketi unapaswa kulipa penalt ya asilimia 100. Lakini lazima tuangalie jiografia ya nchi yetu; maeneo mengi inapopita treni ni maeneo ya vijijini sana ambako ni mbali kutoka kwenye stesheni zetu.

Sasa kama mwananchi anataka kusafiri na eneo analotakiwa aende akakate tiketi ni mbali sana ambapo gharama yake ni kubwa na akapanda kwenye treni ambapo ameweza kupanda, kumpiga faini ya asilimia 100 ni kuwaumiza wananchi wa Tanzania ambao ni maskini, na wanaopanda treni ni watu wa vijijini. Ni vizuri tuangalie hiyo, kwamba kwa nini isiwe asilimia 50 ili iwe affordable kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ni suala la haki ya wafanyakazi. Kuna malalamiko kama wenzangu walivyosema, ya iliyokuwa TRC huko nyuma mpaka leo hayajafanyiwa kazi vizuri, tunabadilisha sasa hivi hapa tunarudi tena kwenye TRC, sasa tuangalie namna gani tunakabiliana na suala la wafanyakazi ili lisije likawa na shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nashukuru sana, naomba kuwasilisha.