Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Freeman Aikaeli Mbowe (8 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi nchangie hoja ya wizara hii. Nitachangia masuala machache sana, na suala la kwanza ambalo ningependa nimuombe kabisa Mheshimiwa Waziri aelewe, nitazuia mshahara wake; ni suala linalohusu uwanja wa ndege wa KIA. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala limezungumzwa Bunge la Nane, Bunge la Tisa, Bunge la Kumi, leo tuko Bunge la 11. Nimeshasimama katika Bunge hili zaidi ya mara kumi nazungumza suala la KIA, lakini mimi sielewi Serikali yetu inafikiri nini na inataka nini, na sijajua ni nani hasa beneficiary wa ule uwanja wa ndege wa KIA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa faida ya wale wapya nitatoa historia kidogo tu kwa muda mfupi sana. Uwanja huu mliubinafsisha mwaka 1997 kwa kipindi cha miaka 25 kwa gharama ya dola 1,000 kwa mwaka. Mkamkabidhi mwekezaji eneo la kilometa za mraba 110, mkamkabidhi na uwanja mzima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumelalamika kuhusu ule mkataba wa KIA kwamba ardhi mliyoikabidhi kwa huyo mwekezaji ilikuwa ni ardhi iliyogusa Wilaya mbili; Wilaya ya Hai na Wilaya ya Arumeru katika Mkoa wa Arusha. Ni ardhi ambayo imegusa kata sita na vijiji 12. Sasa uwanja wa ndege ule umetumika kama vile hauna mwenyewe. Tumelalamika, tumeunda tume tumekwenda na Mawaziri KIA, lakini bado kuna sintofahamu haieleweki kuhusiana na uwanja ule; hatimaye Serikali ikakiri kwamba uwanja ule una matatizo, mkataba una matatizo; mwaka 2009 Serikali ikavunja ule mkataba.
Baada ya Serikali kuvunja mkataba wakadai kwamba wamerejesha uwanja wa Kimataifa wa KIA katika miliki ya Serikali. Lakini Serikali ikatoa kauli kwamba asilimia 90 ya masharti ya mkataba hayakutekelezwa, lakini kitu cha ajabu mkataba ulipovunjwa Serikali ikailipa fidia kampuni ambayo ilitakiwa kuwekeza pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yakalipwa mamilioni ya dola; na wakati wamiliki hao wanaendesha ule uwanja Serikali ilikopa kutoka kwenye European Development Bank zaidi ya dola milioni nne ambazo tunalipa Watanzania wote. Mimi najiuliza viongozi wetu wako wapi, yaani wanafikiri nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kichekezo kikubwa kuliko vyote ni hiki; baada ya ule uwanja kuwa umerejeshwa Serikalini, Serikali ikamuachia yule yule aliyekuwa anauendesha ule uwanja kazi ya kuuendesha ule uwanja. Ukiiuliza Serikali leo au hata Waziri, uwanja wa Kimataifa wa KIA unaingizia Serikali hii shilingi ngapi hawezi kukuambia jibu ambalo linaeleweka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na uwanja huu ambao mwekezaji yule yule wa KADCO ameachiwa, tunaambiwa inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100, viwanja vyote vya ndege nchi hii vinaongozwa na Taasisi inayoitwa Tanzania Airport Authority. Kama uwanja ni asilimia 100 mali ya Serikali ni kwa nini mnawaachia watu binafsi wanauendesha? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na watu hao hao ndio wale ambao walishindwa kutekeleza asilimia 90 ya masharti ya mkataba. Sasa leo uwanja wa ndege wa KIA unatumia eneo la kilometa za mraba, nimesema umetengewa eneo la kilometa za mraba 110. Umegusa watu, makabila mbalimbali na eneo lile waliishi Wamasai kabla hata ya Uhuru wa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachofanyika pale sio uendelezaji wa uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro, ni watu ndani ya Serikali wanaweka mikakati ya ku-grab ile land inayozunguka uwanja wa KIA. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitawapa takwimu ambazo mtaona miujiza ya Tanzania. Mojawapo ya viwanja ambavyo viko bize sana duniani ni uwanja Heathrow nchini Uingereza, (London Heathrow) ambao una terminal one, terminal two, terminal three, terminal four na wanakwenda terminal five and six.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja wa Heathrow London umejengwa katika eneo la hekta 1,227. Lakini uwanja wa KIA uki-compare na Heathrow, London eti Serikali inasema uwanja ule unahitaji hekta 11,085. Uwanja wa Heathrow kwa mwaka mmoja una handle flight na hizi ni data za mwaka 2014, 500,000. Uwanja wa KIA kwa mwaka mzima una handle flight 7,800.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja Heathrow kwa mwaka mzima unapitisha passengers milioni 75, uwanja wa KIA comparatively unapitisha abiria 820,000. Uwanja huo wa Heathrow unaotumia hekta 1,200 unapitisha tani 1,420,000 za cargo lakini uwanja wa KIA unapitisha tani 3,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunasema vijiji vinavyozunguka uwanja ule, vijiji vya Mtakuja, Tindigani, Sanya Station, Rundugai, Chemka, Majengo katika Jimbo la Arumeru, Samaria, Malulu na Maroroni upande Arumeru, haya maeneo yanatakiwa Serikali iweke mpango chini yarejeshwe kwa wananchi, wananchi waishi kwa amani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja wa KIA hauhitaji kilometa za mraba 110 kwa ajili ya kujenga uwanja haiwezekani, ni matumizi mabaya ya ardhi na wizi wa ardhi ya wananchi na mnajua kabisa mikoa ya Kaskazini ardhi ni tatizo kubwa kweli kweli. Hilo ni jambo la kwanza ambalo ningependa sana kulizungumza kuhusiana na mpango wa KADCO.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, barabara. Kuna barabara moja inajengwa, kwanza Waheshimiwa Wabunge nieleze jambo moja hapa. Kuna dhana ambayo inajengeka kwamba kuna barabara zinajengwa sana Kilimanjaro au pengine Kaskazini, ni kweli na napenda nikiri kuna mikoa yenye uhaba mkubwa wa barabara na ni lazima tupige sana kelele ili tupate barabara za kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hata huku Kilimanjaro hali sio shwari mnavyofikiria na naomba nitoe takwimu kwa Jimbo langu kwa mfano; barabara ya kwanza ya lami ilijengwa mwaka 1966, barabara ya kilometa 12, kwa miaka 40 haikujengwa barabara nyingine. Barabara iliyofuata kujengwa ilijengwa wakati ya awamu ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alitoa ahadi ya kujenga barabara inayoitwa Kwa Sadala - Masama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hiyo imejengwa tangu mwaka 2010, kilometa hizo 12.5 hazijakamilika mpaka leo. Sasa kama tunaweza kujenga kilometa 12.5 kwa miaka sita ni dhahiri kwamba wajenzi (contractors) wanalipwa fidia kubwa kwa ajili ya interest kwa sababu ya kukaa site kwa muda mrefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi niiombe Serikali kwamba wamechukulia suala la ujenzi infrastructure kama priority ni jambo jema kwenye uchumi, lakini absorption capacity inanitia wasiwasi kidogo. Kwa idadi ya fedha iliyopelekwa katika Wizara hii, kwa idadi ya miradi ambayo itatakiwa kutekelezwa katika Wizara hii, ni lazima Serikali na Wizara hii iangalie uwezo wake wa kuweza ku-absorb kiwango hiki cha fedha otherwise mnaweza mkatoa room kubwa sana ya ubadhilifu na wizi wa fedha kupitia miradi mbalimbali ambayo inategemewa kujengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kulizungumza kwa haraka sana ni reli ya kaskazini. Ni kweli reli ni kitu muhimu kwa nchi nzima kila mahali, nina-understand, lakini hii reli ya northern line tusiipuuze kwa muda mrefu kwa sababu hata kidogo kilichobakia pale kitapotea. Kwa hiyo, naungana Waheshimiwa Wabunge wa Tanga katika kilio chao, kwamba tunapofikira reli tusifikirie tu central line, tuiimarishe central line, tuimarishe TAZARA, tujenge reli ya kusini na vilevile northern line ambayo tayari ilikuwepo tusiipoteze ile reli kwa sababu itakuja kutugharimu fedha nyingi sana kuijenga wa mara nyingine.
Makadirio ya na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Na mimi nafikiri nisiwe mchawi, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Lukuvi na Naibu wake. Kwa kweli ni Wizara ambayo inafanya kazi bila itikadi za kisiasa, inasimamia wajibu wake vizuri. Mheshimiwa Waziri sifa unazopewa wewe na Naibu wako zinawastahili pamoja na Wizara yako yote, endeleeni kufanya kazi na tutawapa ushirikiano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo manne tu ya kuzungumza siku ya leo na yote naelekeza katika Jimbo langu la Hai. Kwanza, japo nafahamu ni suala linalohusu Wakala wa Barabara yaani TANROADS lakini kwa sababu linagusa ardhi nalizungumza ili Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, na nina hakika Mheshimiwa Profesa Mbarawa yuko hapa naye atanisikiliza, kwa pamoja mnaweza mkaona mnaweza kutupa vipi watu wa Hai ufumbuzi wa tatizo hili ambalo ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hili linahusu barabara ya Kilimanjaro Machine Tools - Machame Girls’. Barabara yenye urefu wa kilometa 26, barabara ambayo ilijengwa wakati wa ukoloni na ni barabara kuu inayohudumia eneo lote la Machame lenye wakazi zaidi ya 200,000. TANROADS wame-declare kupanua wigo wa barabara hii na waka- declare kwamba eneo la mita 60 linahitajika liwe reserved kwa ajili ya barabara. Sasa sisi hatuna tatizo na ulazima wa kupanua na kuimarisha miundombinu yetu ya barabara. Ni kweli sheria hizi inawezekana kuna sheria ambazo zinasimamia mambo haya, lakini sheria hizi zinatungwa na Bunge na tukitunga sheria mara nyingi tunatunga sheria kwa kuangalia nchi nzima bila kuangalia mazingira mahsusi ya eneo moja baada ya jingine.

Mheshimiwa MWenyekiti, kwa eneo la Kilimanjaro ambako makazi yana watu wengi sana, mashamba hakuna. Watu wenye miaka 50 kushuka chini hawana ardhi, kuchukua eneo la barabara ya mita 60 ambayo inakwenda kwenye forest pamoja na Kilimanjaro Gate (Machame gate) kwenda kwenye National Park ni eneo kubwa sana. Tutambue kwamba kuna wakazi wamekaa kwenye maeneo haya kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na kupanua barabara kwa upana huu maana yake ni kwamba tutabomoa misikiti, shule, makanisa, makaburi, tutapoteza kabisa flow ya Mto Weruweru, tutakata mashamba ya wananchi, hili ni jambo lenye ugomvi mkubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upanuzi huu unazungumziwa kufanyika bila kulipa fidia. Ningependa kuishauri Serikali katika kutekeleza sheria lazima tuangalie mazingira ya maeneo na historia ya maeneo. Hii barabara ni muhimu ndiyo, lakini haijengwi reli, wala hatutegemei kwamba kweli mita zote 60 zitatumika katika kuipanua barabara hii, kwa sababu inakwenda ndani kwa kilometa 13 tu kuanzia maeneo ambayo wanakaa wakazi unaanza kukuta Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana Serikali, Waziri wa Barabara, Waziri anayeshughulika na mambo ya miundombinu pamoja na Waziri wa Ardhi tutafute ufumbuzi na ikiwezekana tafadhali m-visit Wilaya ya Hai, mkaangalie hali halisi ninayoizungumzia mahali hapa, muelewe namna ambavyo vijiji vya Nshara, kijiji cha Uduru, Warisinde, Warindoo na Foo katika Kata ya Machame Kaskazini mpaka kwenye Mronga na Mkuu wote hawa wanaathiriwa. Kwa hiyo ni jambo ambao kwa kweli linawakwaza sana wananchi. Bomoabomoa hii japo mnaona ni kilometa 13 kwa Hai, inagusa zaidi ya wananchi 6,000, zaidi ya kaya 800 zinaguswa katika jambo hili bila kuzungumzia hizo taasisi ambazo nimezizungumzia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo ni jambo la kwanza ambalo ningependa kushauri Serikali na ningeomba sana Waziri katika majibu yako, na pengine niombe Waziri Mheshimiwa Mbarawa na timu yake nao vilevile pengine washirikiane katika kutupa ufumbuzi, tungependa tumalize hili tatizo bila kuleta mgogoro wa ziada na usumbufu usio wa lazima sana kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili Mheshimiwa Waziri ni kuhusu hali nzima ya ardhi katika Mkoa wa Kilimanjaro. Tatizo kubwa la Mkoa wa Kilimanjaro ni ardhi. Tuna uhaba mkubwa sana wa ardhi, nitakiri kwamba ni Mkoa ambao idadi ya wakazi kwa kilometa za mraba ni kubwa kuliko kijiji chochote katika Afrika Mashariki na ya Kati.

Tunapozungumzia Kilimanjaro, kilomita moja ya mraba sehemu za milimani zina watu kuanzia, ikipungua sana ni 650 mpaka 1,800 per square kilometer, hii density ni kubwa kuliko eneo lolote katika Afrika ya Mashariki na Kati. Watu wenye umri wa miaka 50 kushuka hawana ardhi kabisa sasa hivi na watu wameendelea kujenga, population imeendelea ku-increase kwa rate ya 1.9 people per annum ambayo siyo kubwa sana ukilinganisha na maeneo mengine ya nchi, lakini kwamba kuna tatizo kubwa la ardhi ambayo inahitaji special management hili ni la lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo namuomba Waziri wa Ardhi mfanye land auditing ya Mkoa wa Kilimanjaro, siyo Hai peke yake, Mkoa mzima wa Kilimanjaro. Kwa sababu katika maeneo mengine sasa watu wamejenga nyumba mpaka kumekuwa squatters, kuna squatter za vijijini. Sasa siyo kawaida sana kukuta squatter vijijini, kuna squatter za vijijini, kuna shida ya kupitisha huduma za barabara hizi feeder roads, kuna tatizo kubwa sana ambalo linahitaji kwa kweli kufanyiwa intervention. Ningeomba Serikali Kuu ifanye intervention na kama kawaida Mheshimiwa Waziri nakukaribisha ili uje na wengine kuangalia mnaweza kufanya jambo gani katika kutatua tatizo hili la wakazi wa Hai. (Makofi)

Jambo la tatu nizungumzie mashamba ya ushirika. Huko miaka ya nyuma wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Nyerere alitaifisha mashamba makubwa yaliyokuwa ya wawekezaji wa kizungu na akakabidhi kwa vijiji kadhaa vya Wilaya ya Hai na maeneo mengine ya Mkoa wa Kilimanjaro. Baadae yale mashamba yakahamishwa kupelekwa kwenye Vyama ya Msingi vya Ushirika, lakini baada ya Sheria ya Ushirika kubadilishwa yale mashamba hayakuwa tena miliki za vijiji yakawa ni washirika wale wanaushirika ambao ni kundi katika kijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mashamba yame-hold uchumi mkubwa sana wa Wilaya ya Hai na katika Mkoa mzima wa Kilimanjaro. Ni ombi langu Mheshimiwa Waziri wa Kilimo na Waziri wa Ardhi mje tuyafanyie tathmini mashamba haya. Hivi kweli kuna economic value tunayopata kwenye mashamba yale ama yanatumika tu bila kutengeneza kile ambacho kilikusudiwa. Kama ni lazima tubadilishe matumizi yake yaweze kurejeshwa kwa wananchi, yaweze kuwa na tija zaidi katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro hasa ukizingatia namna ambavyo ardhi imekuwa ni jambo adimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mashamba makubwa yamekodishiwa watu, hawalipi katika Vyama vya msingi vya Ushirika, wananchi hawafaidi chochote wakati wananchi wengine wa kawaida hawapati hata robo eka ya kulima. Kwa hiyo ni jambo ambalo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi, ningeomba sana Waziri hili uliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo ningependa kulizungumzia liko pale pale katika masuala ya ardhi ni kuhusu mgogoro wa KIA. Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu anisikilize vizuri kwa sababu Waziri Mkuu hili jambo amelisikiliza kwa muda mrefu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba Mkuu unisikilize sana katika hili unisaidie vilevile. Mheshimiwa Waziri Mkuu, unakumbuka bado mgogoro wa KIA tumeushughulikia, nakushukuru sana kwa effort yote uliyofanya, lakini bado hatujapata ufumbuzi, kwa sababu lile eneo la mgogoro wa KADCO uwanja wa Kilimanjaro wa KIA umegusa maeneo ya wananchi wa vijiji vitano vya upande wa Wilaya ya Hai na vijiji kadhaa katika Wilaya ya Arumeru kwa ndugu yangu hapa Mheshimiwa Nassari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji vya Hai kama Mtakuja, Tindigani, Sanya Station, Rudugai, Chemka vimeathirika, kwa kipindi chote hiki chenye mgogoro wananchi wamenyimwa kufanya shughuli zozote za maendeleo katika maeneo yao mpaka mgogoro huu utakapotatuliwa.

Kwa hiyo, kuchelewa kutatua mgogoro huu na kuwapa wale wananchi haki ya kuendelea kuishi katika maeneo yao kunakwaza sana maendeleo na ujenzi wa huduma za kijamii kama shule, barabara, miundombinu nyingine, umeme, maji na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri wa Fedha ningeomba sana tusaidiane tumalize tatizo hili, kwa sababu kuna suala la mgogoro wa ardhi na kuna suala la KIA. Suala la KIA hilo ni suala lingine na Waziri Mbarawa naye amekuwa anashughulika na Waziri Mkuu, nawashukuru sana, lakini ardhi kwa wale wananchi waliozunguka eneo hili inakuwa ni tatizo kubwa kweli kweli. Kwa miaka kadhaa sasa wananchi hawawezi kufanya chochote wamekaa kwenye vijiji vyao, hawaruhusiwi kujenga, kupanua mashamba, hawaruhusiwi kufanya chochote cha maendeleo ya kudumu. Sasa jambo hili ni gumu kidogo hasa inapogusa wananchi wengi sana katika Wilaya ya Arumeru na Wilaya ya Hai ambayo wote wanagusa eneo la KIA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu nikuombe ile juhudi uliyokuwa umeianza uimalizie, Waziri Mbarawa atusaidie tumalizie jambo hili na Waziri Lukuvi nae vilevile aje tuwa-relieve hawa wananchi. Kama tutaendelea na mazungumzo kuhusu uwanja wa KIA tuendelee, kuhusu uwekezaji wa uwanja wa KIA na KADCO tuache wananchi katika maeneo yao waweze kufanya shughuli zao za maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina imani Waziri Mkuu umelifanyia kazi vema jambo hili na nina hakika ukiamua wewe na Mheshimiwa Lukuvi na Mheshimiwa Mbarawa mlimalize tatizo hili, mnao uwezo wa kulimaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuruni sana na nawatakia kheri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, maombi maalum ya barabara. Jimbo la Hai liko katika maporomoko ya Mlima Kilimanjaro, ardhi yake ni alluvial, ambayo huwa tope kali na zito lenye utelezi mkali na hatari hata kwa mvua kidogo sana. Barabara za lami hakika siyo anasa, hasa ukitia maanani hali ya miinuko na mabonde makubwa yaliyopo; barabara ya Kwa Sadala - Masama - Machame Junction ni muhimu sana sasa ikamilishwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara za mji wa Hai ambao ni makao makuu ya Wilaya nazo zinahitaji sana lami. Mji huu sasa unawakazi zaidi ya 60,000 na haujawahi kupata hata kilometa moja ya lami, ukiacha barabara kuu inayotoka Moshi kwenda Arusha inayopita katikati ya mji huu; tunaomba angalau kilometa kumi za lami katika mji huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Bomang‟ombe - Rundugai - Longoi - Kikavu Chini - TPC - Moshi, ni barabara muhimu iliyo ukanda wa tambarare. Ni eneo linalokumbwa na mafuriko mara kwa mara na miundombinu ya changarawe husombwa na hivyo kulazimika kujengwa kila mwaka. Barabara hii ina urefu wa kilometa 27, naomba sana iingizwe kwenye orodha ya barabara za kufanyiwa angalau upembuzi yakinifu kwa mwaka 2016/2017.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Na mimi nafikiri nisiwe mchawi, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Lukuvi na Naibu wake. Kwa kweli ni Wizara ambayo inafanya kazi bila itikadi za kisiasa, inasimamia wajibu wake vizuri. Mheshimiwa Waziri sifa unazopewa wewe na Naibu wako zinawastahili pamoja na Wizara yako yote, endeleeni kufanya kazi na tutawapa ushirikiano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo manne tu ya kuzungumza siku ya leo na yote naelekeza katika Jimbo langu la Hai. Kwanza, japo nafahamu ni suala linalohusu Wakala wa Barabara yaani TANROADS lakini kwa sababu linagusa ardhi nalizungumza ili Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, na nina hakika Mheshimiwa Profesa Mbarawa yuko hapa naye atanisikiliza, kwa pamoja mnaweza mkaona mnaweza kutupa vipi watu wa Hai ufumbuzi wa tatizo hili ambalo ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hili linahusu barabara ya Kilimanjaro Machine Tools - Machame Girls’. Barabara yenye urefu wa kilometa 26, barabara ambayo ilijengwa wakati wa ukoloni na ni barabara kuu inayohudumia eneo lote la Machame lenye wakazi zaidi ya 200,000. TANROADS wame-declare kupanua wigo wa barabara hii na waka- declare kwamba eneo la mita 60 linahitajika liwe reserved kwa ajili ya barabara. Sasa sisi hatuna tatizo na ulazima wa kupanua na kuimarisha miundombinu yetu ya barabara. Ni kweli sheria hizi inawezekana kuna sheria ambazo zinasimamia mambo haya, lakini sheria hizi zinatungwa na Bunge na tukitunga sheria mara nyingi tunatunga sheria kwa kuangalia nchi nzima bila kuangalia mazingira mahsusi ya eneo moja baada ya jingine.

Mheshimiwa MWenyekiti, kwa eneo la Kilimanjaro ambako makazi yana watu wengi sana, mashamba hakuna. Watu wenye miaka 50 kushuka chini hawana ardhi, kuchukua eneo la barabara ya mita 60 ambayo inakwenda kwenye forest pamoja na Kilimanjaro Gate (Machame gate) kwenda kwenye National Park ni eneo kubwa sana. Tutambue kwamba kuna wakazi wamekaa kwenye maeneo haya kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na kupanua barabara kwa upana huu maana yake ni kwamba tutabomoa misikiti, shule, makanisa, makaburi, tutapoteza kabisa flow ya Mto Weruweru, tutakata mashamba ya wananchi, hili ni jambo lenye ugomvi mkubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upanuzi huu unazungumziwa kufanyika bila kulipa fidia. Ningependa kuishauri Serikali katika kutekeleza sheria lazima tuangalie mazingira ya maeneo na historia ya maeneo. Hii barabara ni muhimu ndiyo, lakini haijengwi reli, wala hatutegemei kwamba kweli mita zote 60 zitatumika katika kuipanua barabara hii, kwa sababu inakwenda ndani kwa kilometa 13 tu kuanzia maeneo ambayo wanakaa wakazi unaanza kukuta Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana Serikali, Waziri wa Barabara, Waziri anayeshughulika na mambo ya miundombinu pamoja na Waziri wa Ardhi tutafute ufumbuzi na ikiwezekana tafadhali m-visit Wilaya ya Hai, mkaangalie hali halisi ninayoizungumzia mahali hapa, muelewe namna ambavyo vijiji vya Nshara, kijiji cha Uduru, Warisinde, Warindoo na Foo katika Kata ya Machame Kaskazini mpaka kwenye Mronga na Mkuu wote hawa wanaathiriwa. Kwa hiyo ni jambo ambao kwa kweli linawakwaza sana wananchi. Bomoabomoa hii japo mnaona ni kilometa 13 kwa Hai, inagusa zaidi ya wananchi 6,000, zaidi ya kaya 800 zinaguswa katika jambo hili bila kuzungumzia hizo taasisi ambazo nimezizungumzia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo ni jambo la kwanza ambalo ningependa kushauri Serikali na ningeomba sana Waziri katika majibu yako, na pengine niombe Waziri Mheshimiwa Mbarawa na timu yake nao vilevile pengine washirikiane katika kutupa ufumbuzi, tungependa tumalize hili tatizo bila kuleta mgogoro wa ziada na usumbufu usio wa lazima sana kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili Mheshimiwa Waziri ni kuhusu hali nzima ya ardhi katika Mkoa wa Kilimanjaro. Tatizo kubwa la Mkoa wa Kilimanjaro ni ardhi. Tuna uhaba mkubwa sana wa ardhi, nitakiri kwamba ni Mkoa ambao idadi ya wakazi kwa kilometa za mraba ni kubwa kuliko kijiji chochote katika Afrika Mashariki na ya Kati.

Tunapozungumzia Kilimanjaro, kilomita moja ya mraba sehemu za milimani zina watu kuanzia, ikipungua sana ni 650 mpaka 1,800 per square kilometer, hii density ni kubwa kuliko eneo lolote katika Afrika ya Mashariki na Kati. Watu wenye umri wa miaka 50 kushuka hawana ardhi kabisa sasa hivi na watu wameendelea kujenga, population imeendelea ku-increase kwa rate ya 1.9 people per annum ambayo siyo kubwa sana ukilinganisha na maeneo mengine ya nchi, lakini kwamba kuna tatizo kubwa la ardhi ambayo inahitaji special management hili ni la lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo namuomba Waziri wa Ardhi mfanye land auditing ya Mkoa wa Kilimanjaro, siyo Hai peke yake, Mkoa mzima wa Kilimanjaro. Kwa sababu katika maeneo mengine sasa watu wamejenga nyumba mpaka kumekuwa squatters, kuna squatter za vijijini. Sasa siyo kawaida sana kukuta squatter vijijini, kuna squatter za vijijini, kuna shida ya kupitisha huduma za barabara hizi feeder roads, kuna tatizo kubwa sana ambalo linahitaji kwa kweli kufanyiwa intervention. Ningeomba Serikali Kuu ifanye intervention na kama kawaida Mheshimiwa Waziri nakukaribisha ili uje na wengine kuangalia mnaweza kufanya jambo gani katika kutatua tatizo hili la wakazi wa Hai. (Makofi)

Jambo la tatu nizungumzie mashamba ya ushirika. Huko miaka ya nyuma wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Nyerere alitaifisha mashamba makubwa yaliyokuwa ya wawekezaji wa kizungu na akakabidhi kwa vijiji kadhaa vya Wilaya ya Hai na maeneo mengine ya Mkoa wa Kilimanjaro. Baadae yale mashamba yakahamishwa kupelekwa kwenye Vyama ya Msingi vya Ushirika, lakini baada ya Sheria ya Ushirika kubadilishwa yale mashamba hayakuwa tena miliki za vijiji yakawa ni washirika wale wanaushirika ambao ni kundi katika kijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mashamba yame-hold uchumi mkubwa sana wa Wilaya ya Hai na katika Mkoa mzima wa Kilimanjaro. Ni ombi langu Mheshimiwa Waziri wa Kilimo na Waziri wa Ardhi mje tuyafanyie tathmini mashamba haya. Hivi kweli kuna economic value tunayopata kwenye mashamba yale ama yanatumika tu bila kutengeneza kile ambacho kilikusudiwa. Kama ni lazima tubadilishe matumizi yake yaweze kurejeshwa kwa wananchi, yaweze kuwa na tija zaidi katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro hasa ukizingatia namna ambavyo ardhi imekuwa ni jambo adimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mashamba makubwa yamekodishiwa watu, hawalipi katika Vyama vya msingi vya Ushirika, wananchi hawafaidi chochote wakati wananchi wengine wa kawaida hawapati hata robo eka ya kulima. Kwa hiyo ni jambo ambalo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi, ningeomba sana Waziri hili uliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo ningependa kulizungumzia liko pale pale katika masuala ya ardhi ni kuhusu mgogoro wa KIA. Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu anisikilize vizuri kwa sababu Waziri Mkuu hili jambo amelisikiliza kwa muda mrefu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba Mkuu unisikilize sana katika hili unisaidie vilevile. Mheshimiwa Waziri Mkuu, unakumbuka bado mgogoro wa KIA tumeushughulikia, nakushukuru sana kwa effort yote uliyofanya, lakini bado hatujapata ufumbuzi, kwa sababu lile eneo la mgogoro wa KADCO uwanja wa Kilimanjaro wa KIA umegusa maeneo ya wananchi wa vijiji vitano vya upande wa Wilaya ya Hai na vijiji kadhaa katika Wilaya ya Arumeru kwa ndugu yangu hapa Mheshimiwa Nassari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji vya Hai kama Mtakuja, Tindigani, Sanya Station, Rudugai, Chemka vimeathirika, kwa kipindi chote hiki chenye mgogoro wananchi wamenyimwa kufanya shughuli zozote za maendeleo katika maeneo yao mpaka mgogoro huu utakapotatuliwa.

Kwa hiyo, kuchelewa kutatua mgogoro huu na kuwapa wale wananchi haki ya kuendelea kuishi katika maeneo yao kunakwaza sana maendeleo na ujenzi wa huduma za kijamii kama shule, barabara, miundombinu nyingine, umeme, maji na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri wa Fedha ningeomba sana tusaidiane tumalize tatizo hili, kwa sababu kuna suala la mgogoro wa ardhi na kuna suala la KIA. Suala la KIA hilo ni suala lingine na Waziri Mbarawa naye amekuwa anashughulika na Waziri Mkuu, nawashukuru sana, lakini ardhi kwa wale wananchi waliozunguka eneo hili inakuwa ni tatizo kubwa kweli kweli. Kwa miaka kadhaa sasa wananchi hawawezi kufanya chochote wamekaa kwenye vijiji vyao, hawaruhusiwi kujenga, kupanua mashamba, hawaruhusiwi kufanya chochote cha maendeleo ya kudumu. Sasa jambo hili ni gumu kidogo hasa inapogusa wananchi wengi sana katika Wilaya ya Arumeru na Wilaya ya Hai ambayo wote wanagusa eneo la KIA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu nikuombe ile juhudi uliyokuwa umeianza uimalizie, Waziri Mbarawa atusaidie tumalizie jambo hili na Waziri Lukuvi nae vilevile aje tuwa-relieve hawa wananchi. Kama tutaendelea na mazungumzo kuhusu uwanja wa KIA tuendelee, kuhusu uwekezaji wa uwanja wa KIA na KADCO tuache wananchi katika maeneo yao waweze kufanya shughuli zao za maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina imani Waziri Mkuu umelifanyia kazi vema jambo hili na nina hakika ukiamua wewe na Mheshimiwa Lukuvi na Mheshimiwa Mbarawa mlimalize tatizo hili, mnao uwezo wa kulimaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuruni sana na nawatakia kheri.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi leo nichangie kidogo mambo machache ya msingi ambayo nafikiri ni vyema tukakumbushana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mazingira ya kawaida, ya namna utawala wa nchi yetu ulivyo Chama cha Mapinduzi kina dhamana kubwa kwa sababu ndicho chama kilichozalisha Serikali. Lakini wakati wa uchaguzi, wakati tayari imeshatoka ilani ni Chama cha Mapinduzi tulisikia kauli yenye ukakasi, badala ya kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi mkaona raha sana kujiita Serikali ya Magufuli. Juzi katika ziara ya Mheshimiwa Rais amerudia kauli hiyo akisema CCM kuna majizi, kwenye vyama vya siasa kuna majizi alichanganya vyama vyote, vyote vya upinzani na chama chake akasema ndio sababu yeye anasema Serikali ni ya kwake. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunajiuliza hivi tuna Serikali ya Chama cha Mapinduzi, chama kinachosimamia Serikali yake ama tuna Serikali ya mtu, anajisimamia mwenyewe. Napata wakati mgumu sana ninaposikia Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, Wabunge wenzetu wanajirasibu Serikali yetu ameshawaambia Serikali ni yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimesikia michango ya Waheshimiwa Wabunge wote wa pande zote mbili nimshukuru sana Mheshimiwa Bashe na Mheshimiwa Serukamba wamekuwa honesty na hatutaisaidia nchi hii kwa kuwa wanafiki, tutaisaidia nchi hii, tutaisaidia Serikali yetu, tutawasaidia wananchi wetu wote kwa kuwa wakweli, kuwa critical kwenye mambo ambayo tunafikiri ni ya lazima, tupongeze pale ambapo tunafikiri kuna haki ya kupongeza tuko tayari kupongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wakati tunapokosea tusipoikemea Serikali, tusipoiambia Serikali ukweli na wale wanao-criticize wanaonekana wana stahili ya kufa, wale wanaikosoa Serikali wanaonekana wana stahili ya kuumizwa, hatutafika. Chama cha Mapinduzi, chama chochote cha siasa kikifikia hatua ya kutokutaka ushauri, kikifikia hatua ya kuweka pamba masikioni kutokusikiliza watu wanasema nini, chama hicho hata kingekuwa kina nguvu kiasi gani za kijeshi lazima kitakufa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahiyo, naomba Chama cha Mapinduzi kifanye wajibu wake, mtanisamaehe, nimefuatilizia ndani ya vikao vya Chama cha Mapinduzi kama hata mambo haya yanajadiliwa kwenye vikao vya chama. Lazima tuambiane ukweli ninyi mna dhamana kuliko sisi, sisi ni wapinzani lakini ninyi ndio watu ambao mmepewa dhamana ya nchi hii maumivu yanapotokea kwa wananchi nyinyi mko responsible kuanzia Rais ninyi Mawaziri, Wabunge wa Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninachokiuliza ni kwamba tuna mfumo upi? mmesimama wapi kwenye msingi wa kiitikadi? Ninachokiona kinachofanyika kwa juhudi sana ni kujaribu kulirejesha Taifa hili kwenye ujamaa. Ndugu zangu policy za ujamaa zinapendeza sana na ni tamu sana kuzizungumza, lakini ukweli wa uhalisia wa hali halisi ya binadamu inakwambia tukijaribu kung’ang’ania siasa za kijamaa we are bound to fail. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefanya makusudi nika- tweet asubuhi jana asubuhi nikizungumzia kuhusu suala la mahusiano ya Serikali na private sector. Nika-tweet halafu nione reaction ya watu watasemaje. Wakajitokeza watu wengi wakisema wapinzani mnajifanya ninyi mna mawazo mazuri sana, lakini nilichokuwa nakisema hatutajenga uchumi wa nchi hii kwa kutumia bunduki, hatutajenga uchumi wanchi hii kwa kutumia ubabe na vitisho, ni lazima Serikali itambue kwamba private sector ndio injini ya economy na Serikali ni bodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili gari liende linahitaji engine linahitaji matairi linahitaji bodi, bodi ni Serikali, matairi ni Serikali, engine ni private sector. Hakuna Taifa lolote limeendelea duniani kwa kuipuuza private sector, hakuna Taifa lolote limeendelea duniani kwa ku-disturb private sector, hakuna Taifa lolote limeendelea duniani kwa kufikiria private sector ni wezi tu. Kufanya biashara katika nchi hii chini ya Awamu ya Tano ni kiama, wafanyabiashara wote wa ndani na wa nje wanalia, Mheshimiwa Mpango tumemwambia kwenye Kamati ya Bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamwona Rais anahimiza viwanda unashangaa hivi Watanzania mnajua tumeanza sera ya industrialization lini? Soma historia ya industrialization process in Tanzania na challenge zake. Hakuna kipindi ambacho tunakabiliwa na tatizo kubwa kama kipindi hiki kwenye masuala ya uwekezaji kwenye upande wa viwanda, kwa sababu tunaandika paper nyingi, tuna-policy document nyingi, tatizo letu kubwa ni utekelezaji. Tunapanga mipango mingi ambayo hatuitekelezi sio awamu hii peke yake kuanzia awamu nyingi zilizopita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasoma maandiko ya wasomi wetu fulani wanasema; policy is crafted in Tanzania, modified in Uganda, implemented in Kenya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani Watanzania ni wazuri sana wa ku-craft policies, ndio nilikuwa nasema ukiangali policy mbalimbali ambazo zinazungumzia suala la viwanda nchini linasema nini, kwa miaka 10, 15 iliyopita tumekuwa na Industrial Development Policy, tumekuwa na Vision 2025 najaribu ku-define na kutoa ile frame work tumekuwa na kitu kinachoitwa Tanzania Integrated Industrial Development Strategy ya 2025. Tumekuwa na Mini-Tiger Plan ya 2020, tumekuwa na plan hizi za miaka mitano, mitano zipo tatu ambazo Mheshimiwa Mpango utakuwa unazijua, tuna National Trade Policy, tuna Small Medium Enterprises Development Policy ya 2003. Sasa ukiangalia policy zote hizo zinazungumza kitu kimoja na hakuna hata moja unaweza kusema imekamilika kwa asilimia 10 ama 15. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza habari ya kilimo kwanza tumezungumza haya mambo ya agrarian revolution tunazungumza mageuzi ya viwanda ya kilimo imezungumzwa sana chini ya Kilimo Kwanza, Kilimo Kwanza jamani leo kimeishia wapi? Tumetumia fedha chungu mzima, watu wamefanya plan chungu mzima where is consistency katika planning ya nchi haipo. Leo Rais anahimiza viwanda ili Tanzania by 2025 iwe nchi yenye uchumi wa kati. Nchi yenye uchumi wa kati ambayo inaweza ikaitwa ni industrialized country lazima viwanda vya kuzalisha yaani manufacturing na processing viweze kuchangia angalau asilimia 40 ya GDP. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, industrial hiyo Tanzania inachangangia less than 5% of the GDP, lakini tunajiuliza vilevile hivi viwanda vinavyohimizwa vijengwe soko liko wapi? Huwezi ukajenga uchumi wa viwanda kwa kutegemea soko lako la ndani ni lazima the biggest part of your production iende katika masoko ya jirani na ndio sababu wenzetu wa Asia walivyokuwa na ile Asia Mini Tiger Plan ya Asia ya Southern Eastern ya Asia na Vietnam walifungua kwanza mipaka yao, wakatengeneza National integration policies ili kwamba product inayotoka Tanzania inaweza ikauzwa Kenya, ya Kenya ikaenda Uganda lakini ukiangalia mahusiano yetu namna tunavyojenga mahusiano Afrika Mashariki actually leo tunafunga mipaka hatufungui mipaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoma vifaranga, tunauza ng’ombe za watu, tunaharibu mahusiano yetu, katika misingi kama hiyo tunategemea tutawezaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna suala la utawala bora hili jambo tunalizungumza wenzetu mnaliona kama ni utani hili jambo sio utani, hali ya nchi yetu leo kiusalama, ukizungumza leo unashatakiwa, ukichambua uchumi leo unashitakiwa, sisi wapinzani tufanye nini huo ndio wajibu wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatoa takwimu za uongo, Benki Kuu inatoa takwimu zinazotofautiana na Wizara ya Fedha na watu wa takwimu kila mmoja anatoa takwimu zake pengine ili kuilinda Serikali. Ndugu zangu ninachowambia ni kwamba kama tusipojipa ujasiri wa kuikosoa Serikali pale ambapo inabidi, tukaacha kuunda sheria ndogo ndogo za kudhibitiana humu ndani, za kudhibitiana nje ya Bunge tukawazuia Watanzania wasiongee, msiba utatuumbua, msiba utaumbua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali yetu ya uchumi ni ngumu na uchumi sio fly over wala uchumi sio ndege sita, uchumi ni kipato cha wananchi wa kawaida waweze kuboresha maisha yao kutoka pale walipo kwenda maisha bora zaidi. Watanzania wanazidi kuwa maskini na kundi dogo la watu ndilo ambalo linaweza kuona faida ya kukua kwa uchumi wa Taifa hili. Kukua tunakoambiwa kwa uchumi haku-reflect kwenye maisha ya wananchi, wananchi wanazidi kuwa maskini kila siku hili jambo tukilisema wenzetu mnaona labda sisi ni wachokozi, lakini ukweli ni kwamba yako mambo mengi yanaendelea nchi hii leo kama hamkumwambia Rais hamumsaidii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia na rafiki yangu Ndassa, ndugu yangu rafiki akizungumza suala la ukanda nakubaliana naye 100%; lugha ya kuanza kusema kanda hii kanda ile sio nzuri. Vilevile hebu tujipe ujasiri wa kufikiria chanzo cha maneno hayo ni nini? Kwa nini maneno hayo hayakuzungumzwa miaka minne iliyopita, hayakuzungumzwa miaka mitatu iliyopita, kuna mambo ambayo lazima tufike mahali tuelezane ili tuishi kama Taifa la Watanzania kila mmoja akionekana ana haki katika Taifa hili, tuache kuwa na double standard. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ni chama cha siasa tuna wanachama nchi nzima, tungependa tuwe kama Watanzania, tusingependa tuanze kunyoosheana vidole huyu ni kabila fulani, huyu ni dini fulani, huyu ni rangi fulani sio lugha inayopendeza. Lakini yako mambo yanayofanyika katika nchi yetu leo ambayo yanabagua baadhi ya watu wanaonekana wao wanakuwa disenfranchised, haya yasipozungumzwa misiba itakuja kutuumbua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mengine mumwambie bwana mkubwa kwamba unapofanya mambo mengine tenda haki pande zote, tutampongeza tutamsifu, lakini unapokuwa kwamba wewe haki hiyo labda unaipeleka mahali fulani na ukanda mmoja unawanyima. Niseme mfano mmoja ambao ni dhahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchaguzi unazalisha viongozi kutoka maeneo mbalimbali na watu wote wana haki ya kuchagua na kihistoria katika nchi yetu viongozi waliotangulia Marais wetu waliotangulia walihakikisha kwamba hata nafasi za uteuzi katika Serikali, katika mashirika, katika taasisi za umma zinagawiwa kwa Watanzania kwa wote kwa kadri iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo sio hali inayofanyika leo katika nchi hii na mkitaka nilete takwimu nitaleta takwimu za appointment zote za bwana mkubwa tangu ameingia madarakani kwamba kuna baadhi ya watu na baadhi ya mikoa ambayo makusudi kabisa imekuwa disenfranchised. Huu ni ukweli ambao ni lazima tuuseme mambo haya hayapendezi kwa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukija kwenye mambo ya msingi sana Awamu ya Nne ya Serikali iliyopita tulizungumza uchumi wa gesi, ukiangalia kwenye Mpango wote huu uchumi wa gesi ni kama vile umesahaulika hivi ni chama kilekile ama ni chama kingine? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimekwenda ukanda wa kusini kutembelea hiyo miundominu ya gesi ni mambo ya aibu, ni mambo ya kulia, tumejenga bomba la gesi kutoka Kusini kuja Dar es Salaam…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)
TAARIFA YA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE KUHUSU SHAURI LA KUDHARAU NA KUDHALILISHA BUNGE LINALOMKABILI NDUGU PROF. MUSSA ASSAD, MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nitazungumza kwa kifupi sana kwa sababu natambua kwamba Azimio ambalo mnakusudia kulipitisha mahali hapa mmeshalifanyia maamuzi na historia ambayo mnaiandika leo itawahukumu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge mnajipa utukufu na utukufu ni wa Mungu peke yake. Mnataka kuwaziba Watanzania midomo, watu wasiseme, watu wasi-comment wakati sisi hapa Bungeni tunafanya maamuzi yanayowaathiri Watanzania. Tunataka kupoka haki za msingi za watu kwa sababu sisi tuna mamlaka ya kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba ninukuu Katiba ya nchi yetu kuhusu haki na uhuru wa mawazo. Ibara ya 18 ya Katiba inasema nini? Inasema hivi:

“(a) Kila mtu akiwemo CAG, kila mtu, ana uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake.

(b) anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi. (Makofi)

(c) anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa…”

T A A R I F A

MHE. GOOLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbowe kuna taarifa, Mheshimiwa Mlinga.

MHE. GOOLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpe taarifa Mheshimiwa Freeman Mbowe anayezungumza kuwa kifungu ambacho ananakili kuwa kila mtu ana haki ya kutoa taarifa na kupokea taarifa, Profesa Assad siyo mtu kama watu wengine, Profesa Assad ni kiongozi mkubwa katika taasisi kubwa katika nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbowe unaipokea taarifa hiyo?

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, hii taarifa naipokeaje? Mimi naona niiache tu wala nisi- comment kuhusu taarifa hiyo na haya ndiyo mambo ya kufanya utani kuhusu mambo ya msingi ya nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele cha (c) kinasema nini? Kinasema: “anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake.

(d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu ya jamii.” (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huo ndiyo msingi wa Katiba na Katiba ni sheria mama. Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge haiwezi ikavunja Katiba ya nchi. Kifungu ambacho kimemtia hatiani Profesa Assad kinavunja Katiba ya nchi, hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili na naomba iingie vilevile kwenye record za Bunge kwamba katika siku za usoni tunapounda hizi Kamati za Maadili kama tuna nia njema na nchi yetu tuangalie kwa makini composition ya Kamati za Maadili. Kwa sababu composition ya Kamati ya Maadili leo haiwezi ikafanya justice kwa vyama vya upinzani au kwa watu ambao wanaonekana pengine wanaikwaza Serikali. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. BONIFACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Kamati hii ya Maadili...

MHE. BONIFACE M. GETERE: Taarifa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hiyo itakuwa ni taarifa ya mwisho, Mheshimiwa Getere.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. BONIFACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kutoa taarifa kwa Mheshimiwa Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumpa mtu adhabu au kwa nidhamu aliyoifanya kumpa adhabu hiyo siyo kwamba unakwenda kumtesa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. BONIFACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, leo ningeona Bunge au upande mwingine wa Bunge wangekuwa jasiri kama msingi wa CAG uliopo sasa hivi ulikuwa ni kuzungumzia shilingi trilioni 1.5.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. BONIFACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, kama Kamati ya PAC na CAG mwenyewe amekubali kwamba matumizi ya shilingi trilioni 1.5 hayana matatizo yoyote katika nchi hoja ya kuja kusema kwamba Bunge ni dhaifu inatoka wapi?

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. BONIFACE M. GETERE: Angekuwa jasiri kama angekubali mambo yote kwamba matumizi ya shilingi trilioni
1.5 ni hovyo na sasa yeye hawezi kukubali hoja hiyo. Ameleta matumizi ya shilingi trilioni 1.5 kwamba yako sawa, udhaifu wa Bunge unatoka wapi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbowe unaipokea taarifa hiyo?

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, napokea nini hapo? Yaani kuna nini cha kupokea hapo? Maana sijui Mheshimiwa Mbunge, aaah, nafikiri niachane naye. Naomba tu unilindie muda wangu, mimi hiyo taarifa siipokei kwa sababu hata sielewi anataka kusema nini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nazungumzia composition ya Kamati ya Maadili, ushauri wangu kwa Bunge na kwa Mheshimiwa Spika na Wabunge wote, tukitaka maadili ya Bunge yasimamiwe sawasawa kwa haki, uangaliwe uwezekano wa kufanya balance kwa members wa Kamati ya Maadili. Mkiendelea kuiongoza hii Kamati ya Maadili mnavyoipeleka leo, perception ya umma na nasisitiza, perception ya umma inaona Kamati ya Maadili ni Kamati ya Chama na maamuzi yanafanyika nje ya Bunge watu huku pengine tunakuwa tunaelekeza tu maelekezo tuliyopewa. Caucus ya Chama ndiyo inafanya maamuzi kwa niaba ya Bunge and this is dangerous, tuna-set precedent ambayo ni mbaya zaidi na zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama mnafikiri ni Profesa Assad mwenyewe anaona Bunge hili ni dhaifu ruhusuni Bunge live. Hamtaweza kuwazuia Watanzania kuliona Bunge ni dhaifu kama tutatunga sheria ambazo zinawaumiza wananchi na kama tutafanya maamuzi ambayo yanawaumiza wananchi na kama tutaendelea kuzuia uwazi na ukweli na transparency katika shughuli za Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ya CAG tuna-deal na matawi tunaacha ku-deal na tatizo la msingi. Hoja ya shilingi trilioni 1.5 ambayo imekwenda mpaka shilingi trilioni 2.4 haijapata majibu ya kuridhisha katika Bunge hili na huo ndiyo mtazamo wa nchi. Mnamkaanga Profesa Assad anayeisaidia nchi hii kuokoa mabilioni na matrilioni ya fedha kwa sababu ametumia neno dhaifu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Hebu niulize...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbowe kengele ilishagonga hapa.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, muda wangu walinipotezea sana.

NAIBU SPIKA: Mimi hapa mbele sina saa, saa iko kwa wataalam wangu na wanasema muda umekwisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuwa mchangiaji mchana huu, nami nitazungumza mambo mawili tu ya msingi.

Mheshimiwa Spika, mwaka huu au kwa kipindi hiki tunakabiliwa na mambo mawili makubwa sana katika nchi yetu, janga la maambukizi ya virusi vya Corona na baadaye mwaka huu Uchaguzi Mkuu na haya ni mambo mawili makuu sana katika Taifa.

Mheshimiwa Spika, kwanza nizungumze suala la Corona. Nazungumza kama mtu ambaye kwa bahati mbaya nime-experience tatizo hili katika familia yangu. Kwa hiyo, nalizungumza kama mtu ambaye nina uhakika na ninachokizungumza ni nini. Kwa sababu nilikuwa katika isolation mpaka leo nilipotoka rasmi, namshukuru Mungu kwa hilo, ninapenda nishirikishe viongozi na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kitu ambacho nafikiri pengine hatujakipa uzito wa kutosha katika kukabiliana na janga la Corona.

Mheshimiwa Spika, hili tatizo ni realy, wala Watanzania wasifikiri kwamba hili tatizo linaweza likazuiwa na mipaka ya nchi yetu. Kwa hiyo, ni wajibu kabisa wa Serikali na wadau wengine wote kushirikiana katika kuhakikisha jambo hili linapewa uzito unaostahili kama ambavyo Mataifa mengine ambayo yame-experience tatizo hili yanavyopitia.

Mheshimiwa Spika, mbali na tahadhari mbalimbali ambazo zimetolewa na Serikali bado kuna uzembe mkubwa sana miongoni mwetu, aidha kwa kujua ama kutokujua, ama kufikiri tatizo liko mbali na haliko mikononi mwetu. Kwa upande wa Serikali, naomba nishauri kitu kimoja; itakuwa ni dhana ya bahati mbaya sana kufikiria jambo hili ni kazi ya Serikali peke yake. Jambo hili ni lazima lishirikishe wadau wote, lakini kwa vyovyote itakavyokuwa, lazima Serikali i-take a leading role na Serikali nina hakika ina wajibu wa ku-take a leading role. Hili ni jambo ambalo linahusu taasisi binafsi, sekta binafsi, Mashirika ya Umma, nyumba zetu za imani na ibada, tunahitaji effort ya Kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri mkubwa ambao napenda kuutoa katika Bunge lako ni kuunda a National Taskforce ambayo itasimamia masuala yote yanayohusu Corona. Serikali iongeze hii taskforce, lakini ishirikishe wadau wengine, wanazuoni, madaktari, hospitali binafsi na taasisi mbalimbali za nchi ili jambo hili lipewe uzito wa Kitaifa. Lisiachiwe Serikali peke yake kwa sababu Serikali ni sehemu ya uongozi, lakini kuna wadau wengine huku nje ambao ili nao wakielimika wanaweza wakajua na wakaisaidia Serikali katika kufikia malengo yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili tatizo la Corona ni kubwa sana na watu wengine mpaka sasa hivi wanaliona kwamba kwetu halijawa kubwa kwa sababu pengine watu wengi wakaathirika na wakapata maafa, lakini ukweli maafa ya Corona tayari yameshaingia katika uchumi wetu. Nilitegemea sana katika bajeti ya mwaka huu Serikali ingekuja na mpango maalum kabisa wa kibajeti na kutoa taarifa katika Bunge hili kwamba hivi tuna athari kiasi gani za kiuchumi zinazotokana na janga la Corona? Ukiangalia mipango ya Serikali mpaka sasa hivi, labda yatabadilika baadaye, bado mipango iko kama business as usual, bajeti ziko pale pale, hatuja-foresee kushuka kwa mapato makubwa sana ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, Sekta ya Utalii ambayo ni sekta inayoingiza mapato makubwa ya fedha za kigeni, hii sekta imeanguka kabisa, yaani hii kwa asilimia 99. Hoteli zimefungwa, kampuni za tour zimefungwa, facilities zote za kitalii zimefungwa, mashirika ya ndege ya Kitaifa na Kimataifa haya-operate. Hali hii haita-recover baada ya wiki mbili, hili anguko la kibiashara kwenye upande wa utalii, impact yake ni mwaka mzima, kwa sababu wageni wame- cancel booking mpaka Desemba, mpaka new year. Kwa hiyo hili siyo jambo la leo au kesho. Ni lazima Serikali iweze ku- foresee haya mambo.

Mheshimiwa Spika, tunapojadiliana bajeti hapa, mpaka sasa hivi katika bajeti za nchi utaona kwa kiwango kikubwa sana utekelezaji wa mipango mingi ya Serikali ulikwama njiani kwa sababu ya mapato kuwa kidogo. Sasa bado tunakwenda kuangusha mapato zaidi.

Mheshimiwa Spika, biashara zinaanguka, foreign direct investments sasa hivi zitakuwa almost suspended kwa mwaka mwingine mmoja, misaada kutoka nchi mbalimbali ambazo zilikuwa zinatusaidia nina hakika zitapunguza misaada kwa sababu ya hali yao wenyewe katika nchi zao; uwekezaji wa ndani vilevile sasa hivi umeingia katika mashaka makubwa; uagizaji wa bidhaa kutoka nchi za nje ambao unachangia kwa kiwango kikubwa sana mapato ya Serikali, unaanguka; mashirika na makampuni mengi yatafunga kazi na wafanyakazi watakuwa retrenched, lakini sijaona hili jambo likichukuliwa uzito wa kutosha kwenye bajeti yetu ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kama tunaendelea na kufanya mipango yetu ya bajeti vile vile kama vile hakuna tatizo lililotokea, wakati tuna-expect mapato ya Serikali yataweza kupungua almost by 40% katika kipindi cha miezi sita ijayo, tunawezaje kutekeleza bajeti zetu za kiserikali? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili ni jambo ambalo nilitamani sana Mheshimiwa Waziri Mkuu atusaidie, Mheshimiwa Waziri wa Fedha atusaidie tuwe na mipango ya pamoja na wala tusione aibu katika kukabiliana na janga la Corona. Ni vyema tukajiandaa mapema kwa kutafuta mitigation factors gani zifanyike ili kujaribu kupunguza hili tatizo.

Mheshimiwa Spika, inawezekana tukalazimika kuacha baadhi ya miradi yetu mikubwa ambayo tunaipenda. Tunaipenda sana na tungetamani ikamilike, lakini inawezekana kabisa kabisa tukashindwa ku-fund miradi hii kwa sababu mapato ya Serikali ni lazima yatashuka. Kama tunadanganyana kwamba mapato ya Serikali hayatashuka, siyo kosa la mtu yeyote, ni kosa la ugonjwa huu na ni lazima tukabiliane na hali hiyo.

Mheshimiwa Spika, wakati huo huo tukichukua tahadhari hizo, ni lazima tuongeze fungu kubwa la fedha kwenda katika facilities mbalimbali zinazotoa huduma kwa wananchi hasa mambo ya kiafya. Kuwaambia watu wanawe tu mikono; tunaona information ambazo ni contradictory. Wakuu wa Mikoa wanatoa matamko mbalimbali na maelekezo mbalimbali, watu waendelee kukusanyika na kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, sasa tunajiuliza, Serikali mbona inakuwa na kauli mbili mbili! Kuna mikusanyiko tunaiona kwamba haifai, siyo ya lazima kwa tafsiri ya Serikali, lakini kuna mikusanyiko ya ghafla, Wakuu wa Mikoa wenyewe wanafanya majumuiko ya watu, wanakusanya watu, wanahutubia watu, wanawaambia watu Corona iko mbali. Haya ni mambo ya hatari. Sasa Serikali inasema nini? Tumsikilize nani?

Mheshimiwa Spika, natamani tumsikilize Mheshimiwa Rais wa nchi, ningetamani tumsikilieze Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mheshimiwa Waziri wa Afya. Hawa ndio mamlaka ambazo tumeambiwa zitatoa kauli kuhusiana na ugonjwa wa Corona. Sasa kila Mkuu wa Mkoa na kila Mkuu wa Wilaya anakazana kutafuta kutoa maelezo katika maeneo yake. Mimi nafikiri hii nchi tukienda hivi huu ugonjwa utatupeleka mahali pabaya sana.

Mheshimwa Spika, katika hili la Corona, ni bora tujiandae hata kama tunaona janga liko mbali ili janga likifika tukute tumejiandaa kuliko kutokujiandaa tukafikiri liko mbali halafu likafika, litakuwa fedhea kwa nchi. Na lazima tujifunze kwa nchi za wenzetu, jamani sisi hatuishi wkenye mipaka na siyo vibaya kujifunza kwa wenzetu siyo siri hili tatizo limekumba dunia, hebu angalieni wenzetu wa Rwanda wanafanya nini, tuangalie wenzetu wa Kenya wanafanya nini, hawa wenzetu siyo wajinga na mipaka yetu sisi ni ya jamiii hiyo moja Kenya na Tanzania jamii ni hiyo hiyo moja na Uganda na Rwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nitake nisisite kwamba hili jambo linahitajiwa kuundiwa national task force tuanze kuangalia athari za kiuchumi, athari za kijamii, tufanye nini tuache nini, hatuwezi kuendelea na mipango yote kama tunavyofanya siku zote hiki ni kipindi cha prioritize, yaani tuamue priority za Taifa katika kipindi hiki cha corona ni nini, lazima tu suspend baadhi ya mipango ya Serikali ili kuwezesha kukabaliana na tatizo ambalo linajitokeza.

Mheshimwa Spika, jambo la pili ningependa nizungumze kuhusiana na uchaguzi, leo tuna kama miezi tu actual process za uchaguzi zimeasha, lakini ukiangalia tumekuwa tunadai kwa muda mrefu sana, jamani tutengenezeeni maridhiano katika nchi tutengeneze Tume huru ya Uchaguzi. Uchaguzi ni process na hii process ni ndefu, uwandikishaji ni sehemu ya process, upatikanaji vifaa ni sehemu ya process, kurekebisha Sheria bali tunavyokidhi na matatizo ni sehemu ya process, lakini siye umekuwa tunadai minimum reform kwa sababu moja tu, kwamba tunaamini kwamba ili nchi iweze kuendelea vizuri, lazima ipate viongozi wanaopatikana kwa misingi ya kidemokrasia, tunaimani kwamba wawakilishi wananchi lazima wapatikane kwa misingi ya kidemokrasia. Ili jambo linahitaji political will wala siyo kushindana kupiga kelele. (Makofi)

Mheshimwa Spika, nimemwandikia Mheshimiwa Rais, tumesema mara nyingi tumezungumza mara nyingi katika forum mbalimbali, kwamba jamani tunaposema tunataka minimum reforms, marekebisho machache ya Sheria kwa sababu mtakumbuka 2015 wakati mchakato huu wa Katiba mpya unashindikana makubaliano na Mheshimiwa Rais wakati ule Mheshimiwa Jakaya Kikwete yalikuwa tuende basi angalau kwenye minimum reform mpaka tutakapomaliza mchakato mzima wa Katiba. Bahati mbaya ile process haijarudia mpaka leo.

Kifungu namba 74 na namba 75 katika Katiba yetu vinahitaji marekebisho machache, na haya mambo kama kuna political will upande wa Serikali haya mambo yanawezekana, tukaenda kwenye uchaguzi watu tumeridhiana, tumekubaliana, uchaguzi haki akichaguliwa huyo, akichaguliwa yule basi tupate viongozi ambao wamepatikana kwa ridhaa ya wananchi na siyo kwa giliba za mifumo ya kiuchaguzi. (Makofi)

Mheshimwa Spika, sasa Katiba ina matatizo yake mapungufu, ambayo marekebisho yake ya kufanya kwa sabau zamani minimum reforms ni machache, kifungu cha 74 na 75, halafu kuna masuala ya Sheria za uchaguzi tumeainisha Sheria mbalimbali tumeshapeleka taarifa hizi Serikalini bwana mkubwa mwenyewe kwamba kuna maeneo mbalimbali yana criminalize process zima ya uchaguzi. Kuna watu wengine wanaenguliwa kwenye process ya uchaguzi kwa sababu tu eti amekosea kuweka nukta hapa vitu kama hivyo ambavyo vinavuruga ile dhana ya kupaya viongozi bora.

Mheshimwa Spika, kwa hiyo, tunachosema sisi ni kama tunahitaji hizi minimum reform zifanyike, na nina hakika bado huo muda tunao, hata Bunge hili kabla halijaifa, kama kuna willingness na political will ya kutafuta mwafaka katika Taifa, kutafuta amani ya kudumu na maridhiano katika Taifa haya mambo bado yanaweza kufanya siyo mambo magumu ya kuhitaji bajeti maalum hapana, ni mambo ambayo yanawezekana, tumeainisha mambo chungu mzima katika Sheria ya uchaguzi na Katiba ambayo yanafaa kufanyiwa reforms ili kuwezesha jambo hili kufanyika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niungane na wenzangu kuchangia katika hoja hii ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Utumishi na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanzia hapo ambapo amemalizia Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe, kuzungumzia hoja ya utoaji haki katika Taifa na hilo suala amelizungumza vilevile Mheshimiwa Mama Tibaijuka. Nalizungumza kama mhanga ambaye nimekaa Magereza kwa siku 104 na Mheshimiwa Matiko na fursa ile ya kuishi Magereza imetupa nafasi kubwa sana ya kujua hali halisi ya nchi yetu. Imetupa nafasi ya kujua hali halisi sisi Wabunge tunapotunga sheria tunafikiri sheria hizi hazituhusu, kwa hiyo, tunatunga sheria nyingine ambazo ni ngumu na mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umekuwa ni utamaduni wa Serikali kugeuza kesi za money laundering kama chanzo cha mapato ya Serikali, yaani inaonekana kama kesi za money laundering ni mkakati mpya wa kukuza mapato ya Serikali. Watu wanakamatwa, uchunguzi unaendelea miezi sita au mwaka mzima, Magereza za Dar es Salaam zimejaa mahabusu zaidi ya 5,000 ambao kesi zao zinaendelea hawapewi haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wamekaa ndani miaka mitatu, wengine wamekaa miaka minne, kesi zao wengine hawazijui. Sasa tunalundika Magereza zetu kwa watu ambao kwa kweli walistahili kuwa nje kwa misingi ya dhamana. Utamaduni huu unaharibu investment climate ya nchi kwa sababu watu wanaokamatwa wanatoka kwenye Makampuni na Mashirika makubwa ambayo yanatoa mapato makubwa kwa Serikali yetu. Lazima Serikali iangalie namna ya ku-leverage haya mambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema kweli tukasimamia sheria na kukawa na haki katika Taifa, lakini upande wa pili tujue athari zake kwa uchumi wa nchi. Sasa tunakamata watu na watu wengine mnaowakamata, wanaoshtakiwa kwa makosa mbalimbali ya rushwa ni watu ambao wako katika miradi ambayo iko chini ya PPP. Leo Mkurugenzi na mke wake na viongozi wengine wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam wako mahabusu kwa kesi za money laundering na huyu mtu ni mbia wenu, mngeweza mkakaa nao kwenye Vikao vya Bodi mkamaliza mambo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiendelea na utamaduni huu, ni nani atakuwa na confidence ya kuwekeza na Serikali wakati Serikali yenyewe inawaweka ndani wabia wake? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema nilizungumze hilo. Waheshimiwa Wabunge, tunatunga sheria nyingine ambazo zinawaumiza sana watu. Kuna watu kule wamekutwa na msokoto mmoja wa bangi, siungi mkono hoja ya bangi, lakini wanafungwa miaka 30. Kuna watu wamekutwa na mirungi kifurushi kimoja wanafungwa miaka 30. Ukienda Kenya, mirungi ni biashara halali. Hebu tujiangalie katika sehemu ya dunia, tuko wapi katika kusimamia mambo haya ili kuhakikisha kwamba tunapotunga sheria, tusitunge kwa ushabiki, tutambue kwamba zinawaumiza sana watu na Bunge linalaaniwa sana katika Magereza zetu zote kwa sababu halisimamii utoaji wa haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoka hapo, nizungumze suala la utawala la bora, yote haya nayazungumza katika mwamvuli wa utawala bora. Mheshimiwa Mkuchika wewe ni Waziri mzoefu sana, mnajua kwamba Vyama vya Siasa vimeruhusiwa kufanya kazi katika nchi hii katika misingi ambayo ni ya kweli kabisa. Jambo hili limezungumzwa na wengi, mimi kama Kiongozi wa Upinzani nilizungumze kulisisitiza. Ukiulizwa Serikalini, hivi mmezuia kazi za Vyama vya Siasa, kwa sheria gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mnaona sifa kutangaza kwamba tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwishoni mwa mwaka huu; mnaona sifa kusema tutashinda uchaguzi wa mwaka ujao, wakati mnazuia Vyama vya Siasa visifanye kazi zake za Kikatiba. Hivi vyama ambavyo havina Wabunge, havina Madiwani, vitajitanua vipi? Vitaeleza vipi sera yake viweze kushiriki uchaguzi wa mwaka ujao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maisha ya siasa ni maisha yetu ya kila siku. Mnazuia Mikutano halafu mnakuwa proud kwamba tunawashinda Wapinzani. Mnaogopa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hofu hii, unaiona hofu katika Taifa, watu wanaogopa. Leo nimekutana na msafara wa Mheshimiwa Rais, nimeogopa, nini kinaendelea nchi hii? Ni lazima Rais wetu alindwe, nakubali; na sipuuzi kabisa umuhimu wa ulinzi wa msafara wa Rais, lakini ukiangalia uzito wa ulinzi wa ule unaona kwamba hata hawa wanaomchunga Rais wanagundua kwamba kuna tatizo mahali. Kwa hiyo, ulinzi unawekwa wa ziada sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, msururu wa magari karibu 80, helikopta ziko angani. Sasa unajiuliza, ile nchi yetu ya amani na utulivu tumegeuka tena! Kile kisiwa chetu cha amani na utulivu kinakuwaje sasa? Tulizoea kuona viongozi wetu wakiwa huru, wakiwa wana-mix na watu wetu bila hofu yoyote, lakini kwa namna mambo yanavyokwenda sasa, tunaona kuna tatizo kubwa la msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaitaka Serikali na Mheshimiwa Waziri atupe kauli, ruhusuni tukafanye kazi ya siasa. Msiwe marefarii na wakati huo huo mkawa wachezaji. Mnatufunga mikono halafu mnaringa hapa! Ruhusuni tufanye mikutano ya siasa, tukutane kwenye majukwaa ya wananchi tukaone haki iko wapi? Hilo ni jambo moja ambalo ningependa sana kulizungumza kwa sababu naona tuna- restrict sana democracy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huo nizungumzie Tume Huru ya Uchaguzi. Hoja ya Tume Huru ya Uchaguzi imezungumzwa kwenye Bunge hili tangu mfumo wa Vyama Vingi umerudi kwa mara ya pili mwaka 1992, hakuna mwaka unapita Tume Huru haizungumzwi. Mnaogopa Tume Huru ya kazi gani? Tume Huru ndiyo inatupa misingi ya utawala bora, tunapata viongozi ambao wametokana na utashi wa wananchi, kila kiongozi anayeingia ndani ya Bunge hili ajione yuko proud, akiwa wa CCM au wa Upinzani ajione yuko proud kwamba amechaguliwa katika uchaguzi ambao ulikuwa huru na haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mnakwenda kwenye uchaguzi na Tume yenu, Mheshimiwa Rais ambaye naye mdau; kuna conflict of interest hapa, anamchagua Mwenyekiti wa Tume, anachagua Makamishna, anawachagua Watendaji wake, anachagua Wakurugenzi ambao wanatokana na Chama cha Siasa, kitu ambacho Sheria ya Utumishi wa Umma inakataza. Hatuheshimu tena sheria wala katiba yetu, tunalipeleka Taifa hili wapi? (Makofi)

Mheshimwia Mwenyekiti, sisi tunapendekeza very strongly kwamba ni wakati muafaka sasa, kama tunataka amani sustainable katika Taifa hili, tutafakari suala la kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi. Tusisubiri tuingie kwenye machafuko kama Mataifa mengine, halafu tukajiona kwamba tumeingia kwenye machafuko kwa sababu hatukujua tunafanya nini? Ningependa... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)