Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Dr. Godwin Oloyce Mollel (256 total)

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza naomba niulize, je, Wizara hawaoni kwamba sababu mojawapo inayoweza kusababisha malalamiko au kutotekelezeka kwa sera hii ni ile hali ya kuzi-upgrade hii vituo vyetu vya afya na zahanati zetu? Kwa mfano katika Manispaa ya Iringa, hospitali yetu ya Frelimo ilipandishwa hadhi kuwa hospitali ya Manispaa tangu mwaka 2013 lakini mpaka sasa inapokea mgao kama kituo cha afya. Katika hospitali ile tuna takribani akina mama 300 mpaka 350 wanaojifungua pale kila mwezi. Unaweza ukaona hiyo inachangia kwa sababu mahitaji ya watu wanaokuja pale yanakuwa makubwa kuliko mgao wanaoupata.

SPIKA: Yaani Mheshimiwa Hospitali ya Frelimo pale kila siku kumi wanajifungua?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Ndiyo.

SPIKA: Endelea na swali lako Mheshimiwa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, kwa sababu hospitali yetu ya Frelimo, kwanza tulikuwa na Hospitali ya Wilaya imepandishwa hadhi na kuwa hospitali ya rufaa, kwa hiyo, wilaya tumepewa ile iliyokuwa kituo cha afya Frelimo kuwa hospitali ya wilaya. Kwa hiyo, ile hospitali yetu iliyokuwa ya wilaya imekuwa hospitali ya rufaa, hivyo, wagonjwa wengi sana wamekuwa wakienda pale na kwa kuwa bado tunapata mgao kama kituo cha afya imesababisha sasa wagonjwa wengi kuwepo pale na akina mama wengi wanaojifungua kukosa ile huduma bure. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka, tangu 2013 jamani kwamba na sisi Iringa tupewe mgao kama hospitali ya Wilaya?

SPIKA: Ahsante sana, swali la pili fupi.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, swali la pili, niombe tena Serikali ione, je, hii migao inayokuwa inakinzana yaani unaipandisha hospitali hadhi halafu unaipa mgao wa kile kiwango cha awali, hawaoni hiyo inaweza kuwa ni sababu mojawapo ya malalamiko kwamba Sera hii haitekelezeki?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza alivyouliza swali lake ni suala ambalo tunahitaji tufuatilie tujue specifically kwamba kwenye hospitali yake mgao wake uko kwa namna gani.

Nikitoka hapa Mheshimiwa Mbunge tutakaa pamoja tuangalie ukweli wa hilo unalosema. Nimekwenda Hospitali ya Mbozi, wanatumia shilingi milioni 415 kwa mwaka kutibu kinamama na watoto, kwa hizi huduma zinazotolewa bure lakini wanapata OC kutoka Serikalini shilingi milioni 485 kwa mwaka, maana yake ukitoa hizo huduma wanabaki na zaidi ya shilingi milioni 60 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya matumizi kwa huduma hizi ambazo zinatolewa bure.

Mheshimiwa Spika, hata ukienda Hospitali ya Mkoa wa Mbeya wamepewa dawa za shilingi milioni 53 pamoja na kuhudumia akina mama wakauza wakapata shilingi milioni 157 lakini mwisho wa siku wakaenda kununua dawa za shilingi milioni 29 maana yake ni chini hata ya dawa walizoziuza. Kwa hiyo, kimsingi ukiangalia tunahitaji tupate ushirikiano kwa Wabunge na viongozi wote ili tuhakikishe haya mambo tunaweza tukaya-solve kwa pamoja kwa sababu mengi ni ya kitendaji kule chini.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, lakini tunaenda kwenye bima ya afya kwa wote haya mambo yataweza kutatulika kwa urahisi zaidi.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kundi kubwa la watu wenye ulemavu wana vipato duni na hivyo inawapelekea kushindwa kumudu gharama za matibabu. Je, Serikali inaonaje ikiwatambua kama ilivyofanya kwa wazee na kuwapatia vitambulisho vya huduma za afya bila malipo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, swali la Mheshimiwa Mbunge ni swali nzuri sana, lakini kwa sababu tunaenda kuleta Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, naamini wakati wa mjadala haya maswali yote na kuwahudumia watu wa namna hiyo tutaweza kupata namna ya kufanya. Ahsante.
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza, mgao wa fedha wa kununulia dawa kwa mwaka huu wa fedha zimeenda mara moja tu katika vituo vyetu vya afya na zahanati zetu na isitoshe fedha hizo zinakatwa juu kwa kwa juu kwenda kulipia deni sugu lililopo Bohari ya Dawa. Swali langu kwa Serikali, je, Serikali inamkakati gani kuhakikisha deni linalipwa na dawa zinapatikana katika zahanati na vituo vyetu vya afya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, nataka kujua Serikali inampango gani kuhakikisha kwamba mgao wa fedha wa kununulia dawa haukatwi juu kwa juu kwenda kulipia deni hilo. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO:-Mheshimiwa Spika,…

SPIKA: Mheshimiwa Waziri amesimama, Mheshimiwa Waziri, sijui mlivyokubaliana lakini tuanze na lile la kwanza.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, yes.

SPIKA: Aliuliza kwa nini dawa za shinikizo la damu hazitolewi katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya na wewe umejibu vizuri kwamba sasa hivi hata watu wenye Shahada za Udaktari sasa wanapangwa kwenye vituo vya afya, kwa hiyo mmekubali kwamba sasa dawa za shinikizo la damu zitatolewa katika vituo vya afya au bado hamjakubali?

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, msisitizo uliowekwa nikwamba dawa za shinikizo la damu zinatolewa kulingana na zinavyofanya kazi, lakini na athari zake. Kwa sababu kuna dawa ambazo zinaenda kugusa moyo moja kwa moja na kuna dawa ambazo hazigusi moyo. Sasa utoaji wake unazingatia utaalam na uwezo wa wataalam wenyewe. Kwa hiyo, wakati tunaamuliwa ndiyo maana sasa utaona wakati kunadawa sasa hivi mpaka sasa zinatolewa kwenye zahanati, vituo vya afya, lakini inakwenda mpaka kufika rufaa.

Mheshimiwa Spika, kuna dawa zingine haziwezi kutolewa huko kulingana na utaalam ulioko katika sehemu husika. Kwa hiyo, sasa tunakwenda kuboresha kushuka chini kuhakikisha sasa wataalam ambao walikuwa wanapatikana tu katika hospitali za wilaya na za mikoa wanaanza kushuka chini sasa kuwepo kwenye maeneo hayo. Pia kuna mwongozo mpya ambao umetengenezwa ambao utaenda sasa kusaidia hizo dawa ziweze kupatikana kila mahali, ndicho ambacho tulimaanisha.

Mheshimiwa Spika, kwenye swali lake la nyongeza, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Hawa Mchafu kwa sababu katika meseji nyingi ambazo nimekuwa nikirushiwa na Waziri na ambazo nilikuwa nazipata, tumepata meseji zake sana zinazokwenda kwenye service delivery. Bado narudi pale pale kwamba tunahitaji, ukiangalia nilieleza na nikasema kwamba umeona nimetoa mfano wa hospitali, nitoe Hospitali ya Katavi, tumekwenda Hospitali ya Katavi nao wamepewa dawa zenye thamani ya milioni 41, lakini wakauza hizo dawa pamoja na kuhudumia akinamama na watoto wakapata milioni 112, mwisho wa siku wakaenda kununua dawa za milioni…

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri swali alilouliza Mheshimiwa Hawa Mchafu kama la nyongeza ni national problem.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Yes.

SPIKA: Hela zinakatwa juu kwa juu…

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, sawa, nakuja hapo. Kwa hiyo ukiangalia dawa za milioni 22 maana yake amenunua chini ya pesa aliyopata MSD, kwa maana hiyo ni kwamba utakuta utekelezaji kule chini kuna uwezekano wa hospitali zetu kuuza dawa na kupata pesa ya kutosha kupeleka kule na kuweza kuhudumia wananchi. Sasa…
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa muda mrefu kwenye kundi hili la watu wenye matatizo ya akili baadhi yao wamekuwa wakipata matatizo ya kisheria na kuweza kuchukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kufungwa, lakini kwa sababu tiba hii na ugunduzi wa watu wa aina hii huwa inachukua muda mrefu sana, kwa maana ya kwamba, mtu anakuwa na matatizo ya akili, lakini uthibitisho kwamba, huyu anakuwa na matatizo ya akili unachukua muda mrefu. Je, Serikali sasa iko tayari kwa kundi hili maalum kwa matatizo haya waliyonayo wakaongeza muda wa jinsi ya kuwahudumia watu hawa, hasa wafungwa, lakini zaidi waweze kuwa na kitengo maalum cha kuhudumia watu hawa, ili badala ya kuteseka muda mrefu kwenye jela na mahabusu, basi waweze kupata huduma mapema ili kuweza kuchukuliwa hatua mapema?
WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa la nyongeza, lakini naomba kuongezea kidogo pale mwanzo kwenye vyanzo vya sababu zinazosababisha ugonjwa wa afya ya akili, ili ikibidi na sisi wenyewe tuwe mabalozi wa kuweza kudhibiti hivi vyanzo maana vingine ni vya kawaida kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, zimetajwa sababu za kibaolojia ambazo ni vinasaba vile ambavyo mtu amekuwa ameumbwa navyo. Unaweza ukawa unavyo lakini usifikie stage ya kuweza kupata huu ugonjwa kutokana na mazingira unayoishi nayo katika jamii yako na wewe mwenyewe yanavyokuandaa kupata au kutokupata. Naweza nikatoa mifano hai hapa kuhusu matumizi ya vilevi kupita kiasi mfano bangi au pombe kupita kiasi, kama mwili wako katika maumbile yake unavyo vile vinasaba unaweza ukajikuta unaangukia kwenye ugonjwa wa kukosa akili. Kwa hiyo, inabidi jamii yetu tunakokwenda huko tuishi vizuri, matumizi ya kila kitu ni kwa kiasi, yasije yakakusindikiza kwenye kupata ugonjwa huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tuna watu wanawafanyia wenzao ukatili. Ukatili ukianza kufanyika kwenye maisha ya binadamu katika hatua zake zote siyo jambo jema. Sisi kama Waheshimiwa Wabunge ni mabalozi wazuri wakuweza kukemea vitendo vya ukatili maana vinaweza vikawapeleka kupata msongo hatimaye kupata ugonjwa huu wakawa hatari kwenye taifa letu na kwenye jamii yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna masuala jinsi gani mwanadamu anachukulia maisha yake, zile changamoto, watu wanasema wana ugumu wa maisha, hili nalo ni suala la kukaa na jamii iweze kuchukulia positive changamoto mbalimbali na siyo kujiwekea msongo wa mawazo kufika huko kusikotakiwa. Dunia imeendelea sana nayo ni shida kwa watoto wetu wanapoangalia.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala lile lingine la pili naomba nilipokee, kweli umuhimu huo upo. Tutajipanga kama Wizara kuona jinsi gani tunatoa huduma hiyo ya kuharakisha hayo mashauri yaishe yanayotokana na afya ya akili. Ahsante.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza, kabla sijauliza kwanza nikushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri nimekuwa nikikusumbua sana kwa masuala ya afya, Mkoa wetu wa Iringa na wakati wote upo tayari. Naomba sasa nikuulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kukosekana kwa kipimo hiki katika hospitali yetu ya Mkoa wa Iringa kumefanya wagonjwa wetu kupata matatizo makubwa na mateso makubwa kwa sababu ni lazima kwanza waje wafanye kipimo Hospitali ya Mkapa au Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam. Kwa wagonjwa wasio na uwezo wamekuwa wakipata mateso na kusababisha vifo vingi sana katika mkoa wetu wa Iringa.

Je, Serikali sasa iko tayari kuhamasisha sekta binafsi kwa kutumia miradi ya PPP ili iweze kufunga katika hospitali zetu kwa sehemu ambazo hakuna mashine hizo?

Mheshimiwa Spika, swali letu la pili, kwa kuwa kumekuwa na mfumo usio mzuri kati ya MSD, hospitali na vituo vyetu vya afya kuletewa madawa yasiyoombwa na kuacha yale ambayo wanayaomba. Je, Mheshimiwa Waziri anaweza akalizungumziaje suala hili la madawa katika hospitali zetu na vituo vya afya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa sababu si tu amekuwa akieleza matatizo ya afya yaliyoko kwenye Mkoa wa Iringa, lakini vilevile amekuwa akiyazungumzia matatizo ya watumishi wa Mkoa wa Iringa.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu tunaenda kwenye utaratibu wa bima ya afya kwa wote, lakini Serikali ina utaratibu wa PPP. Sasa kwa kuunganisha hayo kwa sababu utaratibu wa PPP unahitaji umakini wake kutekeleza tusubiri wakati tutaona jinsi ya kufanya namna tuweze kuona namna gani ya kushirikiana na private sector ili kufunga mashine hizo kwenye hospitali zetu, lakini ieleweke tu kwamba Serikali bado ina mpango huo wa kufunga kwenye hospitali zote, na sasa hapa tulipo kuna mashine mbili ziko njia kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni kwamba ameuliza kuhusu MSD, nalichukua wazo lake, ni wazo nzuri ambalo sasa Meneja wa MSD ataenda kulifanyia kazi kuhakikisha mawazo yake haya mazuri yanafanyiwa kazi kuhakikisha vinavyoagizwa ndivyo hivyo vinavyopelekwa kule. Lakini tunawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na ma- DMO wote (Waganga Wakuu wa Wilaya) wahakikishe wanaweka takwimu sahihi za magonjwa ili wanapokuwa wanaagiza wafamasia waagize vitu kwa uhitaji wa hospitali husika bila kuagiza kwa namna nyingine tofauti.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, ndani ya wiki hii tuhakikishe tutatimiza ile ahadi yetu ambayo ilivunjika, twende Iringa tukakae pamoja, tujenge uelewa wa pamoja tuje tutatue matatizo ambayo Wabunge wote wa Mkoa wa Iringa wamekuwa wakizungumzia dawa hasa na vilevile na Mbunge wa Iringa Mjini, ahsante sana. (Makofi)
MHE. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu yenye matumaini kutoka kwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Kabla sijauliza, napenda kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Shinyanga hasa wanawake walioweza kunichagua na chama changu kuniteua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza la nyongeza; kwa kuwa ili hospitali iweze kukamilika na kuanza kufanya kazi ni lazima miundombinu yote iwepo kama maabara, X-Ray na mortuary. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba majengo mengine na miundombinu mingine inakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa tumeanza kuona jitihada nzuri za Wizara ya Afya katika kudhibiti wizi wa madawa na ubadhirifu wa madawa: Je, nini mkakati endelevu wa Serikali kuhakikisha kwamba wizi wa dawa unadhibitiwa na dawa zinapatikana muda wote? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, Mheshimiwa Mnzava ameuliza kuhusu majengo mengine. Kwa bajeti ya mwaka huu 2021 Serikali imetenga shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya majengo mengine ambayo ameyataja.

Vilevile imetenga shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko. Kwa maana kwa bajeti mwaka huu tunaokwenda kuanza, kuna shilingi bilioni 6.4 ambazo zinaenda kuelekezwa kwenye hospitali husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, ameuliza ni kwa namna gani tunaenda kudhibiti wizi wa madawa kwenye hospitali zetu. Kwanza, niseme tu kwamba tumepita na tumegundua kwamba watumishi wengi wa Wizara ya Afya wanafanya kazi nzuri sana lakini kuna wachache ambao wanafanya haya mambo ya ubadhirifu. Vile vile tumegundua kwamba wabadhirifu wamekuwa wakienda Mahakamani aidha, wanaishinda Serikali au kesi zinachukua muda mrefu. Kwa hiyo, tunaenda kimkakati sana kuhakikisha kwamba yeyote atakayepatikana hachomoki, ni lazima awajibike.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, baada ya miezi miwili, mtaanza kuona mkakati wa Wizara wa kuhakikisha moja kwa moja hayo mambo yamefutika, kwa sababu watu wako chini kuhakikisha kwamba tukianza kufanya hiyo kazi hakuna atakayechomoka na tunamaliza hilo tatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nichukue nafasi hii kuipongeza Wizara ya Afya kwa kazi nzuri chini ya Mheshimiwa Dkt. Gwajima, lakini hivi karibuni Mheshimiwa Dkt. Mollel alifanya kazi nzuri pale Mount Meru Hospitali kwa ajili ya kurudisha zile fedha ambazo alitozwa yule mama ambaye alikuwa ametoka kujifungua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Hospitali ya Kitete Tabora bado inatoza fedha kwa akinamama ambao wamejifungua normal delivery na ushahidi upo. Je, msimamo wa Serikali ukoje ukizingatia katazo ambalo alilitoa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa Songwe na hiyo Sera ya Afya ambayo ametoka kuitamka Mheshimiwa Naibu Waziri? Nini msimamo wa Serikali kuhusu kuendelea kutozwa akina mama hao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; akinamama ambao wanashindwa kutoa hizo fedha ambazo zinaanzia Sh.30,000/= mpaka Sh.50,000/= katika normal delivery, huwa wanazuiliwa pale Hospitali ya Kitete Tabora Manispaa. Je, Serikali ina msimamo gani kuhusu wale akinamama ambao bado wanazuiliwa na watoto wao wachanga, hakuna kutoka mpaka watoe fedha hizo ambazo ni za kujifungulia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake huo mzuri kwa ukaribu kwenye eneo hili la Huduma ya Mama na Mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, msimamo wa Serikali bado ni ule ule wa kisera na miongozo na maelekezo ya Serikali, kama ambavyo nilishasema kwamba Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa sera hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini msimamo wa Serikali? Ukienda kwenye hospitali ambayo Mheshimiwa Mbunge anasema, mapato yao kwa mwezi huu wa Januari, 2021 ni shilingi milioni 73; mapato kutokana na Bima ni shilingi milioni 133, lakini Serikali imepeleka OC ya shilingi milioni 54 kwa mwezi wa Januari, 2021. Maana yake mapato yao kwa mwezi ni shilingi milioni 260. Ukitoa na matumizi ya akinamama na watoto, hizi za kutoa bure, ni milioni 13 point, ndiyo matumizi yao kwa mwezi Januari, 2021. Maana yake ukitoa matumizi mengineyo ni shilingi milioni 134, ukija ukijumlisha, wanabakia kuingia mwezi huu wa Februari, 2021 na shilingi milioni 120. Kwa maana nyingine hakukuwa na sababu yoyote ya kum-charge mama na watoto pesa yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ikipeleka OC ya shilingi milioni 54 kwenye hospitali hiyo kila mwezi, maana yake imeshawalipia hawa akinamama. Ukiondoa shilingi milioni 13 ina maana imebaki fedha nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaondoka pamoja na Mheshimiwa Mbunge kwenda Kitete, tukae site pamoja tupige hesabu na tuone. Tutakubaliana pamoja, tutakuja na way forward. (Makofi)
MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwanza naipongeza sana Serikali kwa kuweza kuweka mkakati madhubuti…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa uliza swali.

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa mapambano dhidi ya malaria nchini Tanzania yalianza toka mwaka 1890; na wengi tunafahamu kwamba suala la malaria linatokana na mbu; kwa vile tunacho kiwanda kinachozalisha dawa ya viuadudu ambayo inamaliza kabisa mazalia ya mbu: Je, Serikali haioni kwamba umefika wakati wa kuzitaka Halmashauri kutenga bajeti katika bajeti zao ili kuweza kununua dawa hizi kila Halmashauri iweze kudhibiti malaria kupitia kila Halmashauri? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa wenzetu toka nje ya nchi wanakithamini sana na kuona umuhimu wa kiwanda hiki na dawa hii inayozalishwa Tanzania: Je, Serikali kupitia Wizara hii inatoa elimu gani kwa wananchi kuhusiana na suala la dawa zinazozalishwa na kiwanda hiki kilichoko Kibaha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Maida kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni namna gani tutakitumia kiwanda ambacho kiko Kibaha kuweza kushirikiana nacho kumaliza tatizo la malaria? Hili tunalichukua. Vile vile ndani ya swali la kwanza ameuliza Halmashauri itafanyaje? Tutaenda kushirikiana na TAMISEMI na hasa kwa sababu kuna tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kule Halmashauri zinazotokana na masuala ya afya, fedha hizo zinaweza zikatumika asilimia fulani, vile vile kusaidia kugharamia eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili linaonekana linahusu elimu. Nafikiri kwenye strategic ya mwaka 2021 – 2025 kwa kweli tutakwenda kuwekeza kwenye eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelishauri. Tunachukua ushauri wake na tutaenda kuufanyia kazi kwa nguvu zote kabisa.
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo. Swali la kwanza; je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka watumishi wengi zaidi katika Mkoa wa Tanga, hasa ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Tanga ndio mkoa wenye halmashauri nyingi zaidi nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; utoaji wa huduma za afya kwa vituo vya Serikali unakabiliwa na changamoto nyingi tukilinganisha na vituo binafsi. Je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha huduma zinaboreshwa kwenye vituo vya Serikali ili kuongeza mapato ya Serikali? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ajira 12,476, Serikali inaenda kuelekeza kwenye maeneo kama aliyoyataja ndio kipaumbele kitakuwa, ukiangalia Mikoa kama Kigoma, Mtwara, Songwe na mingine ambayo kwa kweli ni mikubwa, lakini kuna upungufu mkubwa zaidi, itakuwa ndio priority ya Serikali. Kwa hiyo, tunachukua ushauri wake na utaenda kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile swali lake la pili ameuliza kwamba, alitumia neno mapato kwenye eneo upande wa Serikali. Ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba, ukiangalia kwenye vituo vyetu vya Serikali, hasa ukiangalia kwenye eneo la bima tu, ukiangalia kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge utaona. Tukichukua hata zahanati tu, tuliwahi kuchukua moja, kwenye zahanati tu ya kawaida ambayo wanalipwa bima kidogo ukilinganisha na mkoani, unakuta wanaingiza milioni 84 kwa mwaka, lakini Serikalini wanaingiza 420, lakini ukigawa kwa idadi ya watumishi Serikalini tulijua walikuwa 187 huku kwenye private walikuwa 17, lakini utakuta kwa mwaka wanaingiza shilingi 5,300,000/=, lakini huku serikalini tena mkoani wanaolipwa zaidi wanaingiza shilingi 2,000,000/=

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunafikiri kuna umuhimu wa kwenda kufanya kazi kuhakikisha productivity ya watu wetu inaongezeka. Tukiongeza kwenye eneo la productivity maana yake hata kuna mahali ambapo prpductivity ndio inasababisha ionekane kwamba kuna upungufu, lakini upungufu sio halisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna eneo la watumishi; tutaenda kuchukua modal ya Wizara ya elimu. Wizara ya elimu wameshirikiana vizuri sana na private sector kwamba, private sector wana shule, lakini na Serikali ina shule, lakini wamekuwa wanashirikiana vizuri sana bila kuwepo anayenyonya upande huu. Hivyo, kwenye afya tutaenda kudhibiti hasa kwenye eneo la kwamba, unakuta kuna watumishi wakati wa kufanya kazi Serikalini wako eneo la private sector wakati wameajiriwa ndani ya Serikali. Nalo hilo litaenda kufanyiwa kazi kwa nguvu na litatusaidia sana kuweka mambo sawa. Ahsante. (Makofi)
MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Je, lini Serikali itafanya ukarabati mkubwa kwenye majengo mengine yaliyo chakavu zaidi katika Hospitali hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; uchakavu wa majengo ya hospitali hiyo yanakwenda sambamba pamoja na uchakavu wa vifaa tiba, ikiwemo ultra sound, Mashine ya kufulia na vifaa vingine. Je, Serikali haioni umuhimu wa kununua vifaa hivyo katika hospitali hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa sababu nilikuwa naongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ananiambia alimtembelea juzi kabla ya kuja Bungeni. Kama alivyotembea amejionea yeye mwenyewe kwanza jengo ambalo limejengwa hilo la magonjwa ya dharura, lakini alijionea ukarabati mzuri uliofanyika kwa mapato ya ndani kwenye magonjwa yanayoambukiza ambayo sasa wagonjwa wenye matatizo ya kupumua wamelazwa mle ndani na Serikali inaendelea na ukarabati wa majengo mengine kwa mtindo ambao sasa jengo ambalo linamalizika mwezi Oktoba umefanyika.

Mheshimiwa Spika, pia akumbuke kwamba pamoja na hilo kwa juhudi za Wabunge wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mheshimiwa Jenista Mhagama, walianzisha mchakato wa kupata hospitali mpya kabisa ya mkoa, ambapo kule Mwenge - Mshindo wameweza kupata heka 276 kwa ajili ya kujenga hospitali mpya ya mkoa. Waziri wa Afya alituma watu wa kwenda kuangalia eneo, lakini ikaonekana kuna watu sita walitakiwa kufidiwa na ikafanyika tathmini ikaonekana inatakiwa milioni 700 kwa ajili ya kufidia. Sasa Waziri wa Afya ameagiza hebu tuhakiki hiyo milioni 700 kwa watu sita kwa nyumba za udongo ni nini. Kwa hiyo, mimi na Mheshimiwa Mbunge tutakwenda kuangalia tujihakikishie hilo ili sasa tuanze michakato ya kupata Hospitali mpya kabisa ya Mkoa wa Ruvuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu vifaa tiba; Mheshimiwa Mbunge atakumbuka, Bunge lililopita alikuja akilalamika kuhusu x-ray yao iliyoharibika ambayo ilikuwa ina shida ya battery na ilikuwa imeagizwa nje na imeshafika sasa na x-ray inafanya kazi. Tunampongeza sana Mbunge kwa juhudi zake hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ameshapeleka milioni 348 MSD, zipo cash pale ambazo ni fedha, tukimaliza hapa tukutane mimi na Mheshimiwa Mbunge ili tuwasiliane na Uongozi wa Hospitali na Mkoa ili tuweze kupanga kulingana na mahitaji anayoyasema…

SPIKA: Ahsante sana.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, lakini Rais wetu amepeleka direct kwenye akaunti yao milioni 110, nayo hiyo haijapangiwa chochote, kwa hiyo tunaweza vilevile kupanga kuelekeza kwenye maeneo anayoyasema.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, nashukuru ahsante.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, pia kuna milioni 130 kwa ajili ya Kiwanda cha Majitiba, kwa hiyo kazi inaendelea vizuri.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na Mungu akubariki.
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa kumekuwa na changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa dawa katika zahanati zetu na vituo vya afya. Je, Serikali ina mpango gani wa kuyaruhusu maduka ya dawa ambayo yamesajiliwa kutoa huduma ya upatikanaji wa dawa ambazo wagonjwa wameandikiwa kupitia Bima ya Afya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Serikali ina mpango gani wa kuanzisha upatikanaji wa Bima za Afya kwa wajasiriamali wadogo na wananchi wenye vipato duni kulipia Bima za Afya kwa awamu lakini vile vile kuendelea kupata matibabu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuuliza swali ambalo ni muhimu sana hasa kwa mustakabali wa afya ya Watanzania. Swali la kwanza, Serikali ina mpango gani wa kuruhusu maduka yanayouza dawa kutumia bima. Mpango huo upo na una utaratibu wake ili kuweza kuruhusiwa kufanya hivyo. Kwa hiyo, kimsingi mpango huo upo labda kama kuna eneo la kuboresha na kuongeza ufuatiliaji zaidi ili kuhakikisha kwamba yanafika sehemu nyingi. Hilo tutaenda kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni kuhusu wajasiriamali wadogo na kuhakikisha watu wanapata bima ya afya. Sisi tunachofikiri leo kwa sababu kwenye bajeti hii tunaenda kujadili Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, tuko tayari kupokea mawazo yenu na kupokea namna nyingi ambazo tunaweza tukaboresha hii huduma.

Hata hivyo, tunawashauri kwa sasa kuna hicho kitita ambacho kinatumika kwa wajasiriamali ambao hawajajisajili kwenye makundi maalum ambayo yanaangalia umri, ukubwa wa familia na kadhalika, tunamwomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuwahamasisha wajiunge kwa hilo, lakini wazo lake la kwamba tunafanyaje waweze kujiunga kidogo kidogo nalo hilo ni wazo tunalolichukua, wakati tunajadili huu muswada mpya wa sheria tuone tunalifanyaje na wakati hata mwingine kwenye simu na vitu vingine ili wazo lako ambalo ni zuri liweze kutekelezeka. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. MARTHA N. GWAU: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, la kwanza. Je, ni mamlaka gani hasa inayosimamia uingizaji wa zebaki nchini?

Mheshimiwa Spika, lakini kingine, Serikali iko tayari kutenga fedha kwa ajili ya kwenda kutoa elimu ya madhara ya kemikali hiyo ya zebaki kwa wananchi wanaojihusisha na uchimbaji wa madini, hususan Mkoa wangu wa Singida, Ikungi na Wilaya ya Iramba? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, kwanza swali lake la kwanza ni mamlaka gani inayohusika na kusimamia uingizaji wa kemikali hizi nchini:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema kwenye swali la msingi, ni Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini ili tuweze kufanikiwa kwenye hili ni suala ambalo linahitaji kushirikisha mamlaka mbalimbali. Kwa hiyo, kikubwa ni kwamba, kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mamlaka mbalimbali ambazo zinahusika zitashirikishwa, ili kuhakikisha kunakuwepo na udhibiti wa kina.

Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili. Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu suala hilo:-

Mheshimiwa Spika, ni swali zuri, na nafikiri iko tayari na kwa sababu tunahitaji kwakweli kutoa elimu pamoja na kudhibiti kwa maana ya kuwasajili watu kama hao wanaoingiza, lakini vilevile kuna umuhimu wa ufuatiliaji, ili zebaki isiweze kuingia kwa njia za panya. Lakini wakati huohuo kwenda kutoa elimu hasa kwenye maeneo ya madini ambayo wanachimba dhahabu, kwenye makaa ya mawe ambao wanahitaji kutumia zebaki. Wakati huohuo kwenye hospitali zetu ambazo vilevile zenaki inatumika, kuhakikisha kwamba, wakati wa ku-despose hivyo vitu vinakuwa disposed vizuri. Vilevile kuwajulisha wananchi namna nzuri ya kutumia, lakini kununua vifaa ambavyo wakati wachimba madini wanapokuwa wanatumia basi kuwe na mashine na vifaa maalum ambavyo vinasababisha hivyo vitu visiweze kutoka na kuingia kwenye jamii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nafikiri swali lake Serikali iko tayari na nafikiri kwa ajili ya kufanya hatua hiyo fedha zinahitajika.
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ilianza kama zahanati mnamo mwaka 1920 ikapandishwa daraja ikawa Kituo cha Afya mwaka 1922, ikapandishwa daraja ikawa Hospitali ya Mkoa mwaka 1956, mwaka 2011 ikapanda daraja kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Hospitali hii inahudumia Wilaya zote saba za Mkoa wa Kilimanjaro, lakini ina upungufu wa Madaktari Bingwa hususani upande wa wanawake.

Je, Serikali inasema nini kuhusu kuongeza madaktari bingwa wa Hospitali hii kwa sababu huduma stahiki wananchi wa Kilimanjaro hawazipati kutokana na ukosefu wa madaktari na madaktari bingwa?

Kutokana na miundombinu hii iliyoanza tangu mwaka 1920 ni kweli kabisa hospitali ile imechoka, mazingira…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa uliza swali.

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati na kujenga majengo ambayo yana hadhi ya kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake mzuri sana hasa kwenye eneo la hospitali hiyo, lakini kwa ufuatiliaji wake mzuri hasa kwenye huduma ya akina mama na watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni kuhusu Madaktari Bingwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Mawenzi hospitali hiyo mpaka sasa ina ma-specialist, tisa lakini specifically idara anayoisema Mheshimiwa Mbunge ambayo inahitajika kuwa na Madaktari Bingwa wanne ina Daktari Bingwa mmoja. Kwa hiyo, ninamuahidi Mheshimiwa Mbunge wakati tunajipanga kwa mwaka huu kwa maana ya ajira za mwaka huu Hospitali ya Mawenzi itakuwa mojawapo ya hospitali za kipumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sivyo tu kwamba kuna ma-specialist tisa, lakini kuna baadhi ya Idara kama Idara ya Mifupa ambayo haifanyi vizuri sana, tutaenda kufanya kazi kubwa kwenye kuboresha hasa kuweka kwenye vifaa, lakini kuelekeza utawala wa hospitali ili usimamie vizuri eneo hili liwe kufanya kupunguza rufaa kwenda KCMC.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pilli ni kuhusu miundombinu kwamba hospitali ni ya muda mrefu na kuna majengo ambayo yamechakaa na mengine kabisa hayafai kutumika. Ni kweli kama Mheshimiwa Mbunge anavyosema na baada yeye kuja Wizarani, Mheshimiwa Waziri wa Afya alituma timu wiki mbili zilizopita, wameshakwenda Mawenzi na sasa wako kwenye hali ya kuangalia yale majengo ambayo hayafai kabisa na michoro imeanza kuchorwa ili kuja na mawazo ya namna gani tunaweza kuboresha hospitali hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Lakini kuna suala la ardhi pembeni ya Hospitali ya Mawenzi kuna ardhi ya Manispaa ambayo tunaweza tukafikiria namna ya kushirikiana na Manispaa kama inawezekana, lakini ukiangalia ramani yamwaka 1959 Hospitali ya Mawenzi na ukiangalia mabadiliko ya 2009 utaona kuna maeneo fulani ya hospitali hiyo ambayo vilevile hayaonekani kwenye ramani nayo yatashughulikiwa kuhakikisha sasa tunaenda kuja na mkakati ambao hospitali hiyo itaboreshwa vizuri sana, ahsante sana.
(Makofi)
MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kama alivyoainisha Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa upande wa figo, kama Taifa tumepiga hatua kubwa sana pia kwa kutumia wataalam wetu wa ndani.

Hata hivyo, utakubaliana nami kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo kisukari, moyo na figo. Sasa swali langu la kwanza, kwa Serikali, ni lini mchakato huu wa kuandaa huu Muswada utakamilika kama alivyoonesha sasa hivi tunatumia utaratibu wa Kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini sasa Muswada huu utaletwa hapa Bungeni ili kutupa nafasi sisi ambao tuko tayari kuchangia viungo vyetu kama vile figo tuweze kufanya hivyo? Sheria hii itaruhusu sasa wale wenzetu ambao wanafikia mwisho wa maisha yao wataweza kuchangia viungo vyao kama vile figo na moyo ili kuwasaidia Watanzania wenzetu wenye uhitaji wa viungo hivyo waweze kuboresha afya zao na kuendelea kujenga Taifa letu. Nashukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia sana huduma za watu wake wa Iringa. Amekuwa akiwasiliana na sisi sana, hasa wagonjwa wake wanapokuwa Bugando, Muhimbili, KCMC na kwingine amekuwa akifuatilia kwa karibu sana. nadhani ndiko alikojifunzia kwamba, haya matatizo yanatakiwa yashughulikiwe haraka sana kwasababu, yanasumbua wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake ni kwamba, ni lini?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwasababu kama nilivyosema kwamba, tuko sasa kwenye hatua ya kukusanya maoni ya wadau. Kwa hiyo, kwenye Bunge la mwezi wa tisa tutaleta muswada kwa ajili ya kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini niliombe Bunge lako Tukufu kwamba, suala sio kwamba tu sisi kuja na sheria ya kuweza kuruhusu upandikizaji na kuvuna viungo. Suala ni kwamba, ni kwa nini imeongezeka tatizo la watu kuharibika figo na matatizo ya moyo, hilo ndio swali kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe Wabunge wenzangu kwa sababu sauti zao zinafika mbali na zinaheshimiwa na wananchi zile za taratibu za kuzuia matatizo ya figo, za kuzuia kupata magonjwa ya moyo. Tutakapokuja Wizara na mkakati na mtaona wakati wa corona tulikuwa na mkakati mzuri ambao mmetusaidia endeleeni kutuunga mkono ili kuzuia watu wasipate haya matatizo.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, KFW Germany wamekuwa wakitoa huduma hiyo tangu mwaka 2013 mpaka 2018 mwishoni Mkoani Tanga, lakini 2019 mwanzoni ndipo walisitisha huduma zile na kuweza kupeleka mikoa mingine. Naomba kujua sababu gani imesababisha KFW Germany kuacha kutoa huduma ile ya mama na mtoto Mkoani Tanga na kuhamishia sehemu nyingine?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Mwaka 2017 Serikali kwa mara ya kwanza ilianzisha upasuaji kwa watoto wenye upungufu wa usikivu nchini Tanzania, yaani wanafanyiwa upasuaji na wanapata mashine ambayo ni cochlear implant surgery machine, lakini accessories ama spare parts za mashine hizo zimekuwa ni ghali sana kwa wananchi wa kawaida kuweza kuzi-afford. Betri moja la mashine ile ambayo ni rechargeable ni zaidi ya laki tano, lakini ukienda kwenye…

NAIBU SPIKA: Swali Mheshimiwa.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba, Serikali sasa ione haja ya kuvigiza vifaa hivyo nchini na wananchi waweze kununua kupitia Serikali, ili kuweza kushusha bei ya ununuzi kwasababu India ni rahisi sana. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali yake mawili kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni kwamba, kwa nini, sababu iliyofanya ule mkataba ukavunjika wa elfu mbili maana mkataba ule ulikuwa ni wa kipindi maalum 2012 ambao umeanza kama anavyosema 2013 na mpaka 2018, lakini nafikiri anauliza sababu iliyofanya:-

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu ya kwanza ambayo sisi tunaijua ilikuwa ni mkataba wa wakati maalum, lakini nimuombe Mheshimiwa Mbunge tutafuatilia vizuri zaidi kwasababu inawezekana kulikuwa na uwezekano wa kuongeza mkataba na ukaweza kusitishwa. Tutaenda kufuatilia pamoja na yeye ili tujue na nitampa taarifa kwamba, ni nini kama kuna uwezekano wa kufanya lolote tuweze kufanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kufuatia hilo najua amekuwa akipata shida sana na umekuwa ukija wizarani kwa ajili ya akinamama wa Mkoa wa Tanga kuchajiwa hela. Mimi na wewe tutatafuta muda tuende tukaangalie tatizo liko wapi tulishughulikie haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali lake la pili lilikuwa ni suala la upandikizaji wa viungo, watu wenye shida ya usikivu, upandikizaji ili waweze kusikia:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikwambie kwamba, Serikali yetu ukweli watu walikuwa wanapelekwa nchi za nje kwenda kuweza kupandikizwa hivyo viungo na walikuwa wanatumia zaidi ya milioni 100 kwa mtu mmoja. Lakini sasa Tanzania vimeshanunuliwa vifaa na upandikizaji huo umeanza kwenye hospitali yetu ya Muhimbili na ndicho anachozungumzia Mheshimiwa ambayo bado ni changamoto kwasababu, kununua tu vifaa vyenyewe ni zaidi ya milioni 40 ili kuweza kumpandikiza mtu huyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaenda vilevile kuja na Muswada wa kupanga gharama za vifaa tiba na dawa hatuna muongozo wa kudhibiti bei za vifaa hivyo, mtu anajiamulia tu kuuza bei anayoitaka. Lakini kwasababu Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan alitoa bilioni 80 juzi kwa ajili ya kununua vifaa tiba tutaenda kuzingatia kwenye eneo hilo tuhakikishe Muhimbili wana vifaa hivyo kupitia MSD.
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, mbele ya Rais kwa maana ya Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mheshimiwa Waziri Ummy alituhakikishia kwamba itakapofika mwezi Julai, 2020 hospitali hiyo itakuwa imekamilika. Serikali inasema nini kwa Wanakatavi kutokana na ahadi hizi zisizotekelezeka? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili Mkoa wa Katavi umbali kutoka Katavi ikitokezea amepatikana mgonjwa, anahitaji tiba na madaktari bingwa ama umpeleke Mbeya, Mwanza au Dar es Salaam. Umbali huu ukiwa salama na katika mazingira ya amani unaweza ukaenda bila matatizo, lakini ukiwa katika hali ya mahtuti, umbali unakuwa ni mrefu zaidi. Serikali inasemaje katika namna ya kuwanusuru Wanakatavi kuja na suala zima la dharura nikizingatia yapo maeneo mengine hospitali zimejengwa kwa fedha ambayo ni zaidi ya hiyo bilioni tisa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji mkubwa sana wa hali ya afya ya Mkoa wake na Wabunge wa Mkoa huo kwa sababu wamekuwa wakija Wizarani na nakumbuka alikuja pamoja na Wabunge wenzake. Waziri wa Afya alinituma nikaja Mkoani kwao, ni kweli kama Mbunge anavyosema kwa rufaa tu pale kwao wanatumia shilingi milioni 250 kwa mwaka kwa ajili ya ambulance tu kupeleka watu rufaa. Kwa hiyo, anachosema ni kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza anasema hospitali hiyo iliahidiwa kumalizika mwaka jana na bahati mbaya haijafanyika kama ahadi ilivyokuwepo. Kama unakumbuka tulikwenda Wizarani na tayari Waziri wa Afya ameunda timu na imechunguza sababu ambazo zimesababisha hizi hospitali zichelewe na sababu hiyo utaletewa Mheshimiwa Mbunge. Vilevile tumeshatengeneza strategy ambayo kwa uhakika kabisa Januari, 2022 hospitali hiyo inakwenda kumalizika ili kuondoa wananchi katika adha hiyo ambayo tayari ulishakwenda kunionesha Mkoani kwako.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili umezungumzia umbali, tulipokwenda mkoani kwako ulielezea suala la ramani ambayo mlitaka hasa kwenda kwenye hospitali za kanda. Ile ramani ambayo ulikuwa unaizungumzia Mheshimiwa Mbunge, tayari Waziri ameshakaa na timu yake na hata yale mapendekezo yenu ya kupunguza rufaa hasa kuelekea kwa hospitali za kanda inatafutiwa suluhisho na itafanyiwa kazi vizuri kama ambavyo mlitegemea ifanyike Wabunge wa Mkoa wenu. Ahsante. (Makofi)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini sasa Serikali italeta mashine za CT-scan na MRI kwa ajili ya Hospitali za Mikoa hususan Mkoa wa Manyara kwa kuwa gharama ni kubwa za wagonjwa wa magonjwa makuu kwenda kwenye Hospitali za kKnda? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kutoka Mbulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama anavyosema hata kwenye bajeti ya mwaka huu Serikali imejipanga, siyo tu kuweka CT-Scan kwenye hospitali za kanda, bali pia kwenye hospitali za mikoa. Tayari Hospitali ya Mkoa kama Mwananyamala; na sasa hivi tunavyozungumza nilikuwa naongea na Meneja wa MSD, kuna CT-Scan mbili ambazo ziko njiani kwa ajili ya kufunga kwenye hospitali mbili za mikoa; na jinsi fedha zitakavyokuwa zinapatikana, Serikali itahakikisha kwamba hospitali zote za mikoa zinapata CT-Scan na hasa tutazingatia umbali kutoka CT-Scan moja kwenda nyingine ili kuhakikisha kwamba zinawekwa kwenye angle ambazo zitapunguzia wananchi adha ya kwenda mbali kufuata CT-Scan.
MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, napenda kuishukuru Serikali kwa ujenzi na swali langu la nyongeza ni kwamba, kwa kuwa ujenzi huu umechukua muda mrefu na kwa kuwa wananchi wa Mkoa wa Katavi bado wanaisubiri kwa hamu sana hiyo Hospitali ya Mkoa. Je, Serikali inatoa commitment gani kutoa pesa zilizobaki bilioni 5.8 kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa hii hospitali? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa Mkoa wa Katavi tumejenga vituo vingi sana vya afya, lakini pia tunazo hospitali tatu tumejenga kwenye Wilaya zetu tatu za Mkoa wa Katavi pamoja na zahanati. Je, Serikali ina mkakati gani wa kutuletea vifaa tiba kama vile vifaa vya upasuaji, ultrasound na kadhalika kwa ajili wananchi wakati wakiwa wanasubiri hiyo hospitali iishe waweze kuhudumiwa kwenye vituo vya afya pamoja na hizo hospitali? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwapongeze Wabunge wote wa Mkoa wa Katavi, kwa kweli wamekuwa wakifuatilia suala la afya kwenye mkoa wao kwa kina sana na nawaelewa sana kwa sababu ni mojawapo ya mikoa ambayo ni migumu kufikika.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ni kwamba ni lini sasa Serikali kwenye hospitali ambazo zimejengwa itapeleka vifaa tiba. Kama ambavyo Wabunge wanajua Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa bilioni 80 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba. Kwenye hizo bilioni 80 mojawapo ya vipaumbele ambavyo tayari tumeviweka ni hospitali ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja hapa. Kwa hiyo, kwa uhakika kabisa tutafanya hivyo. (Makofi)
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida imechukua muda mrefu sana kukamilika. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha ujenzi wa hospitali hiyo ili wananchi waweze kupata huduma nzuri za afya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumeeleza kwenye Hospitali ya Mkoa ya Katavi, kwa ujumla kwenye Hospitali zetu za Mikoa kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi, Serikali kwenye bajeti ya mwaka huu imetengwa bilioni 57 ambapo kwenye bajeti hiyo mojawapo ya hospitali ambayo imetengewa bajeti ni Hospitali ya Mkoa wa Singida.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge baada tu ya bajeti hii sasa tunaenda kuanza kazi hiyo. Naomba mimi na yeye tupange kwenda kwenye Hospitali ya Mkoa wa Singida tuangalie mambo mengi kwa sababu vilevile kuna suala la wao kutoka kwenye ile hospitali ya mjini kuhamia kwenye hiyo hospitali inayojengwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata nafasi. Ningependa kujua ni lini Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe iliyopo Vwawa Ilembo itakamilika kwa sababu ilikuwa ianze kufanya kazi mwaka 2020? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge anakumbuka yeye alikuja akanieleza suala hilo na nilikwenda kwenye ile hospitali. Ninachotaka kumwambia jengo la OPD na maabara limeshakwisha lakini sasa jengo ambalo liko kwenye level ya msingi linajengwa ni jengo la wazazi ambalo nalo linaendelea na Waziri Mkuu alikuwa amepanga ziara ya kwenda kuzindua hayo majengo mawili.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwenye bilioni 80 iko kwenye bajeti ya kuweka vifaa kwenye hilo jengo la wagonjwa wa nje. Kwa hiyo, mara tu baada ya Bunge hili ratiba ile ya Waziri Mkuu ya kwenda kulizindua itakamilika na kazi itaanza kwenye hospitali wakati majengo mengine yanaendelea kuingizwa kwenye bajeti. (Makofi)
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali hii ni ya Rufaa ya Mkoa na ukisoma vitabu vya bajeti kwenye mwaka uliokwisha ilikuwa inahudumia wagonjwa karibu 75,000; mwaka huu ambao tunaumalizia wameongezeka wamefikia 96,000 na ni ongezeko la karibu asilimia 13. Lakini pia vitu vya kawaida kabisa kama nyuzi za kushona, kama giving set, vitu vya kawaida kabisa kwa ajili ya huduma ya akinamama havipatikani na ni Hospitali ya Rufaa.

Je, Serikali inatoa commitment gani kuhakikisha vitu hivi vya kawaida kabisa vinapatikana wakati tunasubiri ukamilishaji wa jengo hilo la mama na mtoto?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge Priscus Tarimo kwa jinsi ambavyo anafuatilia kwa umakini sio tu hospitali yetu ya Mawenzi, lakini na Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya KCMC hasa kwenye maeneo ya miundombinu, lakini kwenye kuwatetea na kufuatilia maslahi ya watumishi wa hospitali zetu hizi zote mbili.

Swali lake ni kwamba ni lini Serikali itahakikisha kwamba vifaa vinapatikana, ametaja nyuzi na vitu vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo huko nyuma mmesikia Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan mwezi wa pili alitoa shilingi bilioni 43 kwa ajili ya vifaa tiba na dawa, lakini mwezi wan ne alitoa shilingi bilioni 80 kwa hiyo, ukijumlisha ni kama shilingi bilioni 123 zimetolewa kwa ajili ya eneo hilo la huduma ya tiba. Kikubwa ni kwamba ndani ya mwezi mmoja vifaa hivyo vitakuwa vimefika kwa sababu vimenunuliwa viwandani na hilo tatizo litakwenda kuisha na hospitali yetu itakuwa na vifaa vyote ambavyo vinahitajika. (Makofi)
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali nyingi za Halmashauri zimebaki bila kumalizika na kwa bahati mbaya Serikali imekuwa na tabia ya kupeleka fedha na mwisho wa bajeti inazichukua. Jimbo la Mbulu Vijijini hospitali imefikia asilimia 95 kumalizika.

Je, ni lini Serikali itarudisha shilingi milioni 300 ilizozichukua ili hospitali ile iweze kumalizika?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tatizo ambalo amelizungumzia Mheshimiwa Mbunge Massay limetokea kwenye Wilaya nyingi hapa nchini, hata ikiweko Wilaya yetu ya Siha.

Mimi ninachoweza kumwambia Mheshimiwa Mbunge tukimaliza hapa, hebu tutoke mimi na wewe twende Hazina tuangalie ni nini kimetokea na waweze kusuluhisha hilo tatizo liweze kufanyiwa kazi na fedha hizo zipatikane kazi hiyo imalizike ambayo ni asilimia tano imebaki ili hiyo hospitali ianze.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa hii nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Mbozi lenye wakazi 300,000 halina hospitali, linategemea vituo viwili vya afya kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wake, lakini katika hivyo vituo viwili vya afya cha Itaka na Isansa havina vyumba vya kulaza wagonjwa, havina wodi za kulaza wagonjwa. Sasa pamoja na kwamba tuna madaktari wazuri wa kufanya upasuaji mkubwa katika hivyo vituo vya afya wananchi wanakosa huduma kwa sababu hawana vyumba vya kulaza wagonjwa.

Sasa nini mkakati wa Serikali wa kujenga wodi za kulaza wagonjwa kwenye hivyo vituo vya afya viwili vya Itaka na Isansa ambavyo vinategemewa katika Jimbo la Mbozi? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa Mheshimiwa Mbunge ni kweli kwenye Hospitali yake ya Wilaya ya Mbozi kwanza miundombinu ni michache, lakini sasa hivi ndio inatumika kama Hospitali ya Mkoa na sasa tumeshamalizia majengo ya Hospitali yao ya Mkoa. Kwa hiyo, mzigo ulioko kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mbozi ambao ilikuwa inaubeba kama Hospitali ya Mkoa sasa utahamia kwenye hospitali ya mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni kweli kwamba ili kuboresha huduma na kupunguza adha ya wananchi kufuata huduma mbali ni vizuri vituo vya afya viweze kusimamiwa. Kwa hiyo, mimi nafikiri Mheshimiwa Mbunge ni tukitoka hapa Bungeni tukae mimi na wewe, ili uweze kuleta vituo vya afya ambavyo umevifikiri tuangalie kama tayari tumeviingiza kwenye bajeti, kama hatujaingiza tutaweza kuingiza kupitia Global Fund ili viweze kufanyiwa utekelezaji.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii na mimi narejea kwenye lile swali la msingi la Hospitali ya Mawenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Hospitali ya Mawenzi ilipandishwa hadhi ikawa Hospitali ya Rufaa na kule Moshi hakuna Hospitali ya Wilaya. Ni lini Serikali itatujengea Hospitali ya Wilaya ili iweze kuhudumia watu wa Jimbo la Moshi Vijijini, Jimbo la Vunjo na Manispaa ya Moshi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu swali la Mheshimiwa ndugu yetu, Profesa Mbunge wa Moshi Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Wilaya ya Moshi Vijijini haina hospitali ya wilaya na ndio maana hata baadhi ya ambulance kwa ombi la Mbunge ambazo zilikuwepo pale Mawenzi zimetolewa zikapelekwa kwenye vituo vya Moshi Vijijini ili kusaidia wananchi kutokana na hiyo adha ambayo anaisema.

Mimi nafikiri Mheshimiwa Mbunge kuna umuhimu wa kukaa sasa na kuangalia jiografia ya Moshi Vijijini kwa sababu ukiiangalia jiografia yake kwanza ni milimani, lakini imezunguka Mji wa Moshi Mjini; muangalie sehemu nzuri kijiografia ambayo inafaa halafu hatua stahiki zianze kufuata sasa kuanzia kwenye Halmashauri yenu kuja Mkoani - RCC, ili iweze kufika TAMISEMI na mwisho wa siku kazi hiyo iweze kufanyika.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri; nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ugonjwa hautasubiri mpaka mpango huu mzuri wa bima ya afya kwa wote ukamilike, na kwa kuwa miongozo ambayo inatolewa na Serikali kiuhalisia haizingatii na watendaji; ni nini kauli ya Serikali kwa watendaji hawa?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia ikumbukwe kwamba wakati wa Bajeti ya Wizara hii ya Afya, Mheshimiwa Waziri wakati akihitimisha hotuba ya bajeti yake alisema kwamba Serikali imeandaa utaratibu mzuri wa matibabu kwa wazee, ambapo alisema kwamba zitaandaliwa tisheti nzuri ambazo zitahamasisha utoaji wa huduma bora kwa wazee.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Serikali inaonaje mpango huu mzuri ukawajumuisha na watu wenye ulemavu?

Kwa mfano kama tisheti hizi zitaandikwa mzee kwanza, basi iwe mzee kwanza na mtu mwenye ulemavu, lakini pia kama itaandikwa kwamba tuwajali wazee basi tuwajali wazee na watu wenye ulemavu.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL). Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kusema kwamba ni kweli kama Mheshimiwa Mbunge anavyosema, kwamba ugonjwa na matatizo hayasubiri mswada kutengenezwa. Lakini kama ambavyo unajua kwamba kwa sasa kwenye hospitali zetu; na kwenye eneo hilo anachotaka kujua Mheshimiwa Mbunge ni tamko gani linatolewa. Kwa sababu kwa kweli pamoja na kuwepo na sheria na vitu, vingine inawezekana kuna maeneo ambayo haizingatiwi maelekezo ya Serikali kwa mambo ambayo kwa sasa yapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mimi niseme na nitoe ari kwamba, kwanza agizo, Waganga Wakuu wa Mikoa na Ma-DMO wanapokuwa wanazunguka; cha kwanza kwenye CCP zetu na kwenye supervision zao wahakikishe kwamba wamekagua na kuhakikisha kwamba hizi haki zimezingatiwa. Pia kuwaomba kupitia TAMISEMI Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala kusimamia suala hilo ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ni kuhusu suala la kuunganisha huduma za watu wenye ulemavu pamoja na huduma za wazee. Kama ambavyo tayari Mheshimiwa Waziri ameshazindua hili suala la tisheti na kuzindua huo mkakati wa kuweza kuboresha huduma za wazee kama ambavyo mmeona kwenye vyomba vya Habari; tunachukuwa wazo lake kwamba hilo suala liende kuunganishwa pamoja na suala la watu wenye ulemavu.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Serikali inawaambia nini wananchi hasa wazee wenye kadi za Bima ya Afya pindi wanapokwenda kupata huduma na kujibiwa dawa wakanunue madukani; nini majibu ya Serikali juu ya hili?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kutokana na ongezeko kubwa la zahanati vijijini changamoto kubwa ni upatikanaji wa dawa, vifaa tiba kwa maana ya vipimo na waganga. Nini kauli ya Serikali katika kuhakikisha vifaa hivi vinapatikana bila usumbufu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Spika, ni kweli concern ya Mbunge anayoisema ndiyo concern kubwa ambayo imeonekana kwenye eneo la CHF ambayo wananchi wengi wamekuwa wakienda na wakifika kwenye kituo wanakutana na tatizo hilo la upatikanaji wa dawa pamoja na daktari kumwandikia na CHF ni kwamba haiwezi kumsaidia mtu huyu kupata kwenye maduka mengine dawa zaidi ya kwenye kituo husika.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana sasa hivi Serikali umesikia moja; Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni 123 kwa ajili ya kuboresha eneo la dawa, maana yake sasa wakienda vituoni watakutana na dawa. Lakini umemsikia Waziri wetu kwa sababu suala la upatikanaji wa dawa vituoni ni zaidi tu ya fedha zenyewe kupatikana ndiyo maana umemsikia Waziri wetu wa Afya pamoja na Waziri wa TAMISEMI wameanza kufanya kazi kubwa sana kwenye eneo la uadilifu kuhakikisha kuna accountability kwenye eneo zima la dawa. Kwa hiyo hilo ndilo jibu la swali lako la kwanza.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili ni upatikanaji vilevile wa dawa na vifaa tiba vituoni; nalo linajibiwa na swali la kwanza kwa sababu tukishakuwa na shilingi bilioni 123 ambayo Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ameshazitoa kimsingi tutakuwa tumetatua hilo tatizo. Lakini vilevile sasa tunapokwenda kwenye Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote maana yake hata tukiingia watu wote wakapata bima ya afya inayofanana na hizi ambazo wafanyakazi wa Serikali wanazo hata kama watakosa dawa kwenye kituo chake, kuna maduka ya dawa ambayo yanatumia Bima ya Afya ambayo ni hii kubwa ya Taifa kwa hiyo tatizo hilo la dawa litaondoka.
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, kwa sababu Mheshimiwa Waziri katika jibu lake amesema kwamba wanaruhusu kuwahakiki wazee na kwa sababu mfumo wa kuhakiki wazee haujawa rasmi, mmewaachia Halmashauri na ndiyo unakwamisha wazee wengi kutokupata huduma hii kwa kigezo cha kutokusajiliwa.

Ni nini hatua ya ziada ya Serikali kuhakikisha wazee wote wanasajiliwa katika muda ambao umepangwa ili wapate haki yao ya matibabu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL):
Mheshimiwa Spika, labda nijibu swali zuri la Mheshimiwa Mbunge, moja; nachukua concern yake kwa sababu ameonesha kuna tatizo kwenye eneo zima la utambuzi wa wazee. Kwa hiyo tutaenda kukaa kuona ni namna gani tunaweza kuboresha hilo eneo hasa la utambuzi wa kujua ni nani mzee na nani siyo mzee.

Lakini kwa sababu tunakwenda, suala hapa ni tiba ni ku-access tiba tunapokwenda kwenye Muswaada wa Bima ya Afya kwa Wote kimsingi hilo litakuwa lipo contained kwenye utaratibu mzima, kwa hiyo, halitakuwa tatizo.
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakini nina swali la nyongeza.

Kwa kuwa hospitali ile ni kongwe na mpaka sasa hivi kwenye Hospitali ya Ligula Mtwara haina x-ray machine, lakini katika suala hilo la kutokuwa na x-ray machine huduma za theatre kwa ujumla wake hazipo.

Je, ni lini Serikali sasa itaamua kututengenezea masuala mazima ambayo yanahusu package hiyo ya x-ray machine pamoja na jengo la theatre? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, je, ni lini Serikali itaratibu suala zima la kutuletea Madaktari Bingwa ambapo tunashida ya Madaktari Bingwa wa Watoto, Madaktari Bingwa wa Koo ambao vifo vinasababisha kuwa vikubwa sana kwenye hospitali yetu? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge, kaka yangu Hassan Tenga kwa ufuatiliaji wake wa kina sana kwa suala zima la Hospitali ya Mkoa, lakini sio tu Hospitali ya Mkoa, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwenye Wilaya yake.

Swali lake la kwanza ni lini hospitali hiyo itapata x-ray, lakini pamoja na vifaa vya theatre. Kama ambavyo nimekuwa nikisema hapa Rais wetu miezi michache iliyopita alitoa shilingi bilioni 123 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na dawa na hospitali yake hiyo ipo kwenye bajeti kwa ajili ya vifaa husika ambavyo ameulizia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili analoulizia ni suala ambalo mimi na yeye kama ambavyo nimemuomba la madaktari kupelekwa kwenye hospitali yake; na ni ukweli kwamba kuna tatizo la madaktari kwenye maeneo mengi tu sio eneo la kwake na kuna makakati huo sasa wa ajira mpya ambazo zinakuja tunamfikiria lakini mimi na yeye kama tulivyopanga tutakwenda kwenye hospitali yake kufuatilia Hospitali ya Mkoa tutakwenda pamoja tutaona tatizo ni kubwa kiasi gani tuone tunafanya nini kuhamisha sehemu nyingine ili madaktari waweze kusaidia eneo hilo.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niulize Hospitali ya Wilaya ya Hai imekuwa na changamoto kubwa sana ya majengo mpaka ninivyozungumza hatuna jengo la mama na mtoto, hatuna jengo la pharmacy, hatuja jengo la maabara kakini pia work way za kuwasiliana kwenye majengo haya hatuna.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutujengea majengo haya? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze kaka yangu Saashisha Mafuwe kwa kazi kubwa ambayo anaifanya kwenye Wilaya ya Hai hasa kwenye kufuatilia miundombinu tu sio tu ya Hospitali ya Wilaya, lakini zahanati zake lakini vituo vya afya na Hospitali ya Machame ambayo ni DDH, ni ya kanisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kuna kazi kubwa sana inafanywa na Waziri wa Afya Mheshimiwa Dorothy Gwajima pamoja na Waziri wa TAMISEMI dada yetu Ummy Mwalimu ya kuhakikisha tunapata resources kupita sources zingine ili tuweze kukamilisha miradi kama hiyo ambayo anaisema ambayo inawezekana haijaingia kwenye bajeti kubwa ambayo sasa tumeipitisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Saashisha tukitoka hapa twende pamoja, tuangalie mkakati huo wa Mawaziri wetu wawili tuone ni namna gani inaweza kufanyika kupitia Global Fund, ahsante sana. (Makofi)
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana; kwa kuwa Serikali imeendelea na ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mandewa, nataka kujua tu ni nili itakamilisha ukarabati huo ili kuondoa adha inayojitokeza katika suala la kupata huduma ya afya katika Mkoa wa Singida? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tulishakwisha kusema hapa kwa bajeti ya mwaka 2021/2022 zimetengwa zaidi ya shilingi bilioni 57 kwa ajili ya kufanya ukarabati na ujenzi katika hospitali mbalimbali za rufaa hapa nchini hospitali aliyoitaja Mheshimiwa hapa ni mojawapo ya hospitali ambayo ipo kwenye mpango huo.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu Hospitali ya Rufaa ya Ligula tuna ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Kusini Mtwara ambao naishukuru Serikali imekamilisha kwa awamu ya kwanza; je, Serikali imejipangaje kuanza ujenzi awamu ya pili ya hospitali hiyo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo amekuwa karibu sana kufuatilia ujenzi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Kanda nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwenye bajeti ya mwaka huu ni moja wapo ya hospitali ambazo zimetengewa fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi na kumalizia baadhi ya unit ambazo ilikuwa hazijamaliziwa, ni hospitali aliyoitaja.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la x-ray katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Ligula mimi niliuliza hilo swali Bunge lililopita Naibu Waziri wakati ule Mheshimiwa Ndugulile aliniambie x-ray machine ya Mkoa wa Mtwara ipo bandarini, leo majibu ya Naibu Waziri anaongea as if hakuja kitu kabisa. Mimi nataka tu kujua ile x-ray yetu ambayo tuliambiwa ipo bandarini ime-evaporate au vipi? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze dada yangu mpambanaji kwa swali lake zuri ambalo linahusu wananchi; moja ni kwamba anasema kwamba x-ray hiyo ilikuwa ipo bandarini na mpaka sasa haijafika kwenye eneo husika. Nikuombe dada yangu tukimaliza maswali hapa twende mimi na wewe tukakae pale tufuatilie hiyo x-ray na tuweke utaratibu iweze kufika mapema inapotakiwa, ahsante sana.
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; nafahamu kwamba utaratibu wa kuomba fedha kwa awamu ya kwanza ya ukarabati umeshakamilika. Swali langu langu kwa Serikali: Je, ni lini fedha hizo zitatolewa ili ukarabati uanze?

Swali la pili: Je, Serikali ina mpango gani wa ziada kuhakikisha kwamba ukarabati wa majengo haya chakavu ya Milembe unakamilika katika awamu hii na awamu ijayo ya mwaka wa fedha?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O MOLLEL): Mheshimiwa Spika, kama ambavyo amesema Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kwamba kuna utaratibu ambao tayari umefanyika, lakini wakati utaratibu huo umefanyika imeonekana kwamba kwa kweli unahitajika ukarabati mkubwa sana na vile vile baadhi ya majengo kubomolewa na kujengwa upya, kwa hiyo, ikahitajika kufanyika tathmini kwa sababu fedha nyingi zitahitajika zaidi.

Mheshimiwa Spika, mara tu baada ya huu upembuzi kufanyika, kwanza kazi ambayo ilikuwa inaendelea itaendelea kufanyika, lakini tunahitaji ifanyike kazi kubwa zaidi kwa maana ya kuingia kwenye bajeti ya mwaka kesho 2022 ili ujenzi mkubwa ufanyike na ukitambua kwamba pale Mirembe inaenda kuwa taasisi kamili, sasa iko kwenye wakati wa kuunda muundo. Maa yake kutakuwa na ongezeko la kibajeti na wataweza sasa kuandika proposal zao binafsi ili kufanya research na pengine ile taasisi kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Ahsante.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Sisi Kusini nadhani magonjwa haya kwa sababu ya korosho hayapo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya aliwahi kutembelea kusini. Katika ziara yake, tulimpa maombi ya kusaidiwa kukarabati kituo cha afya kikongwe kuliko vyote katika Jimbo la Mtama ambacho kinahudumia zaidi ya kata sita na ahadi hiyo ilitolewa. Sasa nataka kujua ni lini tutapata fedha ili tusaidie kuboresha huduma katika eneo hili?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nape, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli kama ambavyo amesema tulikwenda na vilevile baada ya hapo aliandika barua kwa Mheshimiwa Waziri wa Afya na Mheshimiwa Waziri wa Afya aliwasiliana na TAMISEMI. Nataka kumhakikishia kwamba kituo hicho kimeingizwa kwenye bajeti na kimetengewa shilingi milioni 500 na baada ya fedha kupatikana kazi itaanza. Nami baada ya kumaliza Bunge, twende pamoja ili tusisitize na mambo mengine ambayo tuliyapanga wakati ule kuyafanya. (Makofi)
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli Hospitali hiyo ya kanda imeanza kutoa huduma, lakini lengo la Hospitali ya Kanda ni kutoa huduma za rufaa. Huduma hizo hazijaanza kwa sababu hakuna vifaa na hakuna madaktari bingwa. Sasa swali langu: Ni lini vifaa na madaktari bingwa wataletwa katika hospitali hiyo kwa sababu hiyo ndiyo shida yetu sisi watu wa kusini hususan Mkoa wa Mtwara? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Ukiangalia mazingira ya nje ya hospitali ile, bado yapo shaghalabaghala, ni lini yatawekwa katika mandhari ambayo inaendana na mandhari ya hospitali? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri sana; na kweli mawazo mazuri aliyoyatoa ndiyo mwelekeo wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwanza hospitali hiyo imeanza na ni kweli bado watumishi hawajafikia idadi aliyoisema. Tumegawa uanziswaji wa hiyo hospitali. Ukiangalia hospitali yenyewe sasa ina umri wa mwezi mmoja na siku nane, lakini tumegawa uanzishwaji wake kwa phase tatu, maana yake tumeanza phase ya pili ambayo sasa wanaenda kuwekwa watumishi.

Mheshimiwa Spika, tayari Serikali imetenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya hospotali hiyo na tayari shilingi bilioni tatu zimeingia kwa ajili ya kununua CT-Scan na MRA. Kuna specialist mmoja na mwezi ujao wanapelekwa 4 ili wafikie 5. Mpaka mwezi wa Pili ambapo tutaenda kwenye Phase ya tatu ya uanzishwaji wa hospitali, tutakuwa na watumishi 217. Kwa hiyo, Mheshimiwa ukitembelea mwazi wa tatu utakuta imeanza kama ulivyotaka wewe.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ni kuhusu mazingira ya Hospitali. Kweli nimeyaona na mimi wakati jiwe la msingi linawekwa, bado mazingira yaliyozunguka siyo safi. Wakati tunaendela kwenye phase hizi, tunaendelea kuhakikisha vile vile na usafi unafanywa.

Mheshimiwa Spika, OC imetengewa shilingi milioni 600. Kwa hiyo, watatumia kwa ajili ya kuhakikisha mambo mengine yanakuwa sawa na kufikia lengo ambalo Wana- Mtwara wangetegemea kuona.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika nashukuru. Nami napenda kuiuliza Serikali: Ni lini itaimarisha utoaji wa huduma kwa magonjwa yale ambayo yalikuwa hayapewi kipaombele; magonjwa ya kitropiki, kwa maana ya neglected tropic diseases kwenye hospitali hii ya Kanda ya Kusini? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Spika, kwanza ukisikia tunaanzisha specialists mbalimbali, tunazungumzia magonjwa yote hayo. Ukisikia tunasema tunaongeza watumishi, ni kwa kuzingatia hayo. Ndiyo maanda unaona sasa kuzunguka nchi nzima, utaona kila Mkoa sasa unafanya wahamasa kuhusu magonjwa ambayo ameyazungumzia. Juzi Arusha nilimwakilisha Waziri wa Afya kwenye kuzindua swala hilo kitaifa. Ahsante. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba nimwulize maswali mawili madogo ya nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kwenye jibu la msingi Mheshimiwa Naibu Waziri amezingatia eneo moja tu la uchimbaji wa dhahabu: Je, Serikali ina mpango gani wa kubadili matumizi ya zebaki inayotumika katika vifaa vya afya ikiwemo katika ujazaji wa jino?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili: Je, zebaki inayotumika katika huduma za afya kama vile kipima joto kwa maana ya thermometer ama wakati wa kujaza jino kwa maana ya amalgam, ina athari gani zinapotumiwa na binadamu; na je, athari hizo zinapatikana baada ya muda gani? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili mazuri ya Mheshimiwa Mbunge mwenzangu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, matumizi ya vitu vyenye mercury kwenye kutibu meno; moja, kwa mercury ipo dozi maalum ambayo kuna mahali inapofikia ndiyo inaweza kuleta athari. Hata hivyo ni kweli kwamba kuna baadhi ya watu wakizibwa meno kwa kutumia amalgam hiyo yenye mercury, wengine wanapata allergy.

Kwa hiyo, wakati mwingine watu wanaweza wakafikiri ni madhara ya mercury, lakini ni allergy kwa sababu kuna watu wenye allergy na baadhi ya mambo. Mpaka sasa, kwa kutibu meno, inatumika na haijaonesha madhara ambayo unadhani yanatokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna options mbalimbali za kutumia na utafiti unaendelea kuona namna ya kupata kitu chenye strength ile ile ambayo amalgam ilikuwa inafanya ili waweze kuitoa, lakini kwa kweli mpaka sasa kitiba haina shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, amezungumzia thermometer na vifaa vingine vya tiba ambavyo vina mercury, tunafanyaje? Kikubwa ambacho mpaka sasa hata kwenye madini kinafanyika, kwenye vifaa vyote vya tiba na hata dawa, suala kubwa hapa, ni kwa namna gani unafanya disposing na control mechanism zinavyohaibika na zile thermometer unazi-dispose kwa namna gani? Ndiyo maana kuna utaratibu maalum wa namna ya ku-dispose vifaa tiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaendelea na utaratibu wa kuhakikisha thermometer na vifaa vingine vyote vinavyotumia mercury vinakuwa under control na vikiharibika ile disposing mechanism inafuatwa ili kutunza mazingira na kutunza afya ya binadamu. Ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa matumizi ya zebaki, hasa Kanda ya Ziwa, sehemu ambazo wanachimba madini imekuwa ikisababisha ongezeko la wagonjwa wa Kansa ya Shingo ya Uzazi: Je, Serikali imeshafanya utafiti kuthibitisha kwamba zebaki ndiyo chanzo cha ongezeko la magonjwa ya kansa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba hata ukienda Ocean Road imeonekana kwamba wagonjwa wengi wenye matatizo ya kansa wanatokea Kanda ya Ziwa. Hayati Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Magufuli aliwahi kuagiza ufanyike utafiti ambao bado majibu yake hayajaja ili kuthibitisha nini hasa chanzo cha tatizo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachofanyika kwa sasa ni kwamba kwanza kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha kansa ya kizazi. Kwa hiyo, hatuwezi kusema specifically ni hilo. Kikubwa, tunashirikina na Wizara ya Madini kupitia taasisi yake kuhakikisha sasa wanapochenjua madini, wale wachimbaji wadogo na wakubwa kunakuwepo na control ya kutosha kuhakikisha kwamba haiendi kwenye mazingira na vilevile haiendi kufika maeneo ambayo binadamu wanatumia maji na vitu vingine. Hilo ndiyo tunaendelea nalo kwa sasa.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijauliza maswali yangu ya nyongeza, siafiki takwimu za Serikali kwa sababu Covid ilisambaa nchi nzima na kwa watu 725 ukigawanya tu kwa mikoa 31 maana yake kila mkoa wamekufa watu 23 ambayo haina mantiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kama nchi tulisimamisha mwaka mzima, Machi, 2020 mpaka Machi, 2021 kutoa takwimu. Kwa hiyo, hizi taarifa za takwimu siyo za ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa maswali yangu ya nyongeza mawili; la kwanza, moja kati ya changamoto kubwa ilikuwa ni upimaji, kwa sababu ilikuwa lazima upime ndiyo ujue huyu mtu amekufa na Covid ama hajafa na Covid; sasa Mheshimiwa Waziri ameeleza vizuri sana juu ya mkopo wa shilingi bilioni 466 toka IMF, lakini hivi vitu alivyoviainisha hapa hakuna hata sentensi moja inayozungumzia ujenzi wa maabara ama uwepo wa maabara kwa ajili ya kupima Covid ama virusi vingine vinavyoashiria ama vinavyofanania na hivyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka aniambie, kwa sababu tunaishi na Covid-19 na virusi vinavyofanania na hivyo vitakuja, ni fedha kiasi gani katika mkopo huu wa shilingi bilioni 466 tutapeleka kwenye eneo la maabara specifically; na siyo hizi maabara sijui X-Ray, hizo zinatoa viashiria tu, kwamba kuna homa ya mapafu? Hilo ni la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusiana na dawa, nili-intend hapa kuuliza, tiba za asili za Tanzania kwa kiwango kikubwa sana zimechangia kutibu madhara yanayotokana na Covid. Imesaidia sana; na hizi ni fursa kwa watu wa tiba za asili kwa nchi, kwa ukanda na dunia: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka Serikali iniambie, mpaka sasa, kwa sababu kila siku mnajibu mnafanya tafiti, mmeshagundua ni tiba gani za asili ambazo ni sahihi kwa Watanzania watakaopata maradhi ama Virusi vya Covid ili wakiugua tujue protocol ya matibabu ni hii; na siyo sasa hivi kila mtu anakunywa kivyake mpaka tunakunywa sumu? Ni lini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimwambie tu rafiki yangu kwamba hii ni sayansi. Kama ni sayansi, inahitaji akili kubwa kuweza kuyaona hayo na siyo hisia za kwenye ma-corridor. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu kwamba Bugando, Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia amepeleka vifaa vya maabara vya kupima Corona vyenye thamani ya shilingi bilioni nne na mlinisikia nikisema. Kibong’oto ambayo ndiyo taasisi yetu ya magonjwa ambukizi, imepelekewa vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni sita na maabara inajengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 14. Maabara yetu ya Taifa nayo inayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujue virus siyo mdudu mpya. Ni mdudu mpya kwenye genetic makeup lakini sayansi ni ile ile. Kwa hiyo, maabara ni zile zile, mashine ndiyo zimetofautiana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni kuhusu tiba ya asili. Kwanza hatujaacha tiba ya asili. Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 1.2 imeenda NIMR kwa ajili ya kuchakata dawa zetu zilizoonekana kwamba zinatusaidia na kuziweka vizuri. Vilevile kwenye fedha hizi ambazo nilikuwa nazitaja, shilingi bilioni 466, imetengwa shilingi bilioni tatu kwa ajili ya utafiti ule mkubwa na mgumu kwa ajili ya kuja na chanjo yetu ya Kitanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hapa ninachoweza kumwambia Mheshimiwa, haya ya kisayansi huwa ni magumu, nawaachia wanasayansi. Unahitaji super computing system kubwa kuziona; hii siyo ngwini yaani, unajua. Kwa hiyo tulia. (Makofi)
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nami pamoja na majibu mazuri kabisa ya Daktari msomi, mwanasayansi Mheshimiwa Mollel, nina swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huko nyuma tulikuwa tunaona Serikali ikishiriki katika kampeni mbalimbali tunapokuwa na magonjwa haya ya mlipuko na magonjwa mengine. Kwa mfano tuliwahi kuwa na kampeni ya kutokomeza Malaria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kufahamu, ni upi mpango wa Serikali kutumia wasanii wetu katika kuhamasisha, lakini pia kutoa elimu zaidi kwa wananchi hasa makundi ya vijana katika kupambana na Ugonjwa huu wa Uviko-19? Kwa sababu tunaona katika awamu hii kama wasanii hawajatumika sana katika eneo hili? Ni upi mpango wa Serikali?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la Mheshimiwa Mbunge ni muhimu sana; na kweli kwa kutumia wasanii wanaweza wakatufikishia vizuri sana ujumbe, lakini kikubwa ambacho kinaendelea sasa hivi ni kuhakikisha kwamba badala ya kutumia wasanii kutoka juu, tunapeleka kabisa huduma iende ikafanyike na jamii yenyewe kule chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeonekana kwamba, ukiangalia fedha tulizonazo, ukitumia sana wasanii hawa wakubwa, ambao bado tunaendelea kuwatumia na tutawatumia jinsi watakapohitajika, lakini kwa kupeleka kule chini huduma inafika kwa urahisi zaidi kwa lugha inayoeleweka na watu wa jamii iliyoko eneo husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana tumesema tutakwenda kule na tukifika kule Umasaini tutawatumia wasanii walioko kule, lakini tutatumia redio na lugha zilizoko kule ili waweze kupata kirahisi na ili ujumbe ufike. Ila hatuna lengo la kuwaacha wasanii, isipokuwa tunatafuta namna ya kutumia hela kidogo kwa kufanya kazi kubwa zaidi. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Wakati Mheshimiwa Waziri anajibu maswali ya nyongeza, alisema wamefanikiwa kupeleka vifaa vya maabara kwenye maeneo mawili. Nchi yetu ukichanganya na Zanzibar ina mikoa 31, kwa Bara ni 26: Je, hamwoni kwamba hiki ni kikazi kiduchu kwa tatizo kubwa ambalo limetukumba la Covid? Ni lini mtahakikisha hizo maabara zinakuwepo nchi nzima na siyo hizi mbili ambazo zimetokana na pesa ya mkopo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo niliyoyasema ni mifano tu. Nataka nimweleweshe Mheshimiwa Mbunge kwamba toka Uhuru tumekuwa na CT- Scan mbili tu kwenye nchi hii, kwenye hospitali za mikoa mbili tu, lakini amekuja leo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, tunakwenda kupata 29 ambazo zina gharama kubwa kuliko mashine za kupima Corona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachotaka tu kumhakikishia ni kwamba tuna uwezo huo, mpaka leo tunapoongea hivi Mount Meru Hospital wanapima, Mbeya wanapima, kila mahali tutafikiwa. Kwa hiyo, usiogope, kazi inapigwa. Sisi tuendelee kusherehekea, karibuni upande huu kumenoga. (Kicheko/Makofi)
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu ya Serikali yaliyotolewa hapa, bado kuna tatizo kubwa, hasa kwenye vituo vyetu vya afya, huduma hii imekuwa ngumu sana kwani akinamama wanapokwenda kujifungua wameendelea kutozwa hela na watoto chini ya miaka mitano wanapokwenda pia kupata huduma wameendelea kutozwa fedha. Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ni nini hasa kinakwamisha huduma hii au sera hii isitekelezwe?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; katika vituo vyetu vya afya kumekuwa na upungufu mkubwa sana wa dawa na vifaa tiba. Je, Serikali ina mkakati gani sasa kuhakikisha kwamba vifaa tiba na dawa zinapatikana katika vituo vyetu vya afya ili watoto wetu na akinamama wanapokwenda kujifungua waweze kupata huduma hiyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Spika, nilijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Regina Ndege kwamba kwa kweli tumeshafanya uchunguzi wa kutosha na kujua kwamba tatizo hilo lipo, ndiyo maana straight forward tumetaka kuwaelekeza wanaohusika kufanya kazi yao. Hata kwenye presentation ya semina iliyofanywa jana kwa Wabunge wote na Wizara ya Afya tulionesha kwamba exemption ile ya akinamama na watoto inachukua asilimia 0.1 mpaka 10.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo maeneo ambayo ni 0.1 ni maeneo yale ambayo kwa kweli unakuta akinamama walitakiwa kupewa hiyo huduma bure na hawapewi; tutakwenda kuboresha kwa nguvu kuhakikisha kwamba huduma inapatikana. Ndiyo maana tumeleta vilevile kwenu ili tushirikiane kwa pamoja ili kuweza kutatua tatizo hilo.

La pili, kwenye eneo la dawa; kwenye eneo hili, Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan alishatoa bilioni 16 na najua Kamati inakwenda siku ya Jumapili, kimejengwa kiwanda kule Njombe ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vidonge vyote vya kutosha nchi nzima kwa siku mbili tu na kimeshafika asilimia 98 kukamilika.

Mheshimiwa Spika, tayari Rais wetu, mama Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya bilioni 185 kwa ajili ya kununua dawa. Tukijumlisha na uelewa ambao jana tulipeana Wabunge wa kusimamia upotevu wa dawa, wanaweza kuona tuna items zaidi ya 400 za dawa, lakini tumechunguza tu items 20 ndani ya mwaka mmoja kuna upotevu wa bilioni 83. Maana yake tukishirikiana kwa pamoja sisi na viongozi tuliotaja hapa huko mbele tutaweza kufika hatua nzuri na dawa zikapatikana kwenye maeneo yetu. Ahsante sana.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nami niulize swali dogo la nyongeza: -

Mheshimiwa Spika, wewe ni shahidi; hii sera ni ya muda mrefu na haitekelezeki. Wabunge mnajua kwenye majimbo yetu, akinamama wajawazito, wazee na watoto chini ya miaka mitano hakuna matibabu bure. Sasa Mheshimiwa Waziri anasema atatoa miongozo, kama hakuna kitu cha kumbana mambo ni yaleyale.

Je, kwa nini kusiwe na sheria kwamba ni lazima akinamama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wazee wapate matibabu bure ili wazee wasiweke tiba ya kisaikolojia tena, wakienda hospitali wapate matibabu bure? Sera imekuwepo haitekelezeki, leteni sheria kama mna dhamira njema.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL): Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge na ndiyo maana umekuwa mkali sana kwenye suala zima la bima ya afya kwa wote. Nataka kukuhakikishia tukienda kutekeleza agizo lako la suala la bima ya afya kwa wote, haya mambo yatakuwa ni historia. Kwa wakati huu miongozo iliyopo tutaendelea kuifuatilia na kusisitiza, lakini Mheshimiwa Ester Bulaya aendelee kushirikiana na sisi ili tuweze kufanya hilo litekelezeke. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa kwa sasa wagonjwa wote wa akili katika Hospitali za Temeke, Mwananyamala na Amana, wanapelekwa katika Hospitali ya Muhimbili, lakini jengo hilo la wagonjwa wa akili la Hospitali ya Muhimbili halijafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu kiasi kwamba, mwananchi wa kawaida kuingia kwenye ile wodi unaogopa. Sasa napenda niiulize Serikali.

Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati jengo la wagonjwa wa akili katika Hospitali ya Muhimbili, ili Madaktari wetu waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na wagonjwa waishi katika mazingira mazuri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa, takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kwamba, kuanzia mwaka 2020 kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa akili duniani na hasa vijana kuanzia miaka 15 mpaka miaka 35 na hiyo inatokana na matatizo na changamoto mbalimbali za kimaisha. Haya yameanza kujitokeza katika nchi yetu ya Tanzania, watu wameanza kuuana ovyo na matendo ambayo sio ya kibinadamu yanatendeka sana, tunapata hizo taarifa. Je, Serikali haioni haja sasa ya kujenga hospitali maalum ya wagonjwa wa akili badala ya kuwa Mirembe, Dodoma peke yake? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mbunge kwa ufuatiliaji mzuri sana anaoufanya kwa kufuatilia masuala ya afya ya watu wanaoishi kwenye Mkoa wa Dar-es-Salaam, tunampongeza sana Mheshimiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama Mheshimiwa Mbunge anavyosema kwamba, kweli jengo lile liko chakavu pale Muhimbili, lakini kwa mwaka huu tu, hii miezi miwili iliyopita, hospitali ya Muhimbili Rais wetu amepeleka bilioni 16 pale, lakini ilitengwa zaidi zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya kukarabati jengo lile, lakini kwa sababu ya matatizo ya corona na kulikuwa na umuhimu wa kuhakikisha baadhi ya expenses zilizoongezeka wangebeba wananchi wenyewe ingeleta shida, fedha zile zilielekezwa upande huu, lakini ameshatoa maelekezo Waziri wa Afya juzi alivyotembelea Muhimbili na sasa hiyo kazi inaenda kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani. Swali lake la pili amezungumzia kwamba, kuna matatizo ya akili yameongezeka duniani, lakini vilevile hapa nchini kwetu Tanzania. Ni kweli, yameongezeka, suala sio kuongeza idadi ya hospitali, lakini ni kuangalia visababishi ambavyo vinasababisha watu kupata matatizo hayo viweze kutatuliwa. Vilevile sio tu kujenga hospitali maalum kwa ajili ya hiyo, lakini ni ku-integrate hizi huduma kwenye huduma nyingine mpaka kushuka chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wetu ameshaelekeza kwamba, hospitali zote zianze na nilianza na Kigoma kama uliangalia kwenye vyombo vya habari, kulikuwa na wataalam wa afya ya akili na wale wataalam wa afya ya akili tukaanza kuelekeza kwamba, waanze sasa kutengewa bajeti na zile ofisi zao zipewe bajeti ya kutosha ili waweze kufanya kazi zao na kushuka chini mpaka kwenye vituo vya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata unapoona CT-Scan zimesambazwa kwenye hospitali zote za mkoa, wakati mwingine wagonjwa wa akili wamekuwa wakitibiwa kwa kuangalia dalili zao tu, lakini sasa tunataka kwenda kuwaangalia kabisa, kwa sababu wanaweza wote kuonesha dalili zinazofanana, lakini visababishi vikawa tofauti. Kwa hiyo, sasa tunaenda kwenye level ya kupiga CT scan za ubongo ili kila mmoja aweze kutibiwa kwa namna ambavyo ana tatizo lake. Ahsante sana.
MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, tatizo la afya ya akili hata katika Mkoa wetu wa Iringa limekuwa kubwa sana na changamoto kubwa kabisa ya tatizo hili ni kwamba, bei ya dawa iko juu sana, sana. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba, dawa zinakuwa na bei ndogo au kuondoa kabisa, ili waweze kupatiwa bure kama yalivyo magonjwa mengine?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya, naomba nijibu swali lake la nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kwanza dawa za wagonjwa wa akili zinatolewa bure na tayari Serikali imeshapeleka kwenye maeneo yote watu wa kufanya hivyo. Kama kuna mahali wanawauzia kwa Mkoa wa Iringa, nitalifanyia kazi ili kuona namna ya kufanya. Nalipokea ili tuweze kulifanyia kazi. Wote tutaona kwamba Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ameshaunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, mojawapo ya kazi ni kuhakikisha, ile Wizara itakaposimama kwenye eneo lake tutapunguza sana mambo yanayosababisha yanayoongezea idadi ya watu wenye matatizo ya akili kwenye jamii.

Kwa hiyo, kikweli nachukua wazo la Mheshimiwa la dawa, lakini tutaenda kulifuatilia zaidi na kwenda Iringa kuimarisha zaidi hicho kitengo ambacho umekizungumzia hasa kwenye eneo la dawa.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nikiri kabisa kwamba, Wizara ya Afya kwa kweli, kwa upande wetu Jimbo la Hai wanatutendea haki, lakini naomba niulize swali. Hospitali yetu ya Wilaya ya Hai ni chakavu sana na watumishi wanapata tabu kweli kutoa huduma pale. Walk ways zimekuwa chakavu, hatuna jengo la mama na mtoto, hatuna jengo la pharmacy, kiufupi hospitali hii ni chakavu na Naibu Waziri anaifahamu vizuri. Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati katika hospitali yetu ya Wilaya ya Hai?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Hai kwa jinsi ambavyo anapambana na matatizo ya watu wa Hai. Kwenye hospitali hiyo ya Hai Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan amepeleka milioni 220, amepeleka 300, akapeleka tena milioni 90 kwa ajili ya kujenga nyumba ya watumishi, hata hivyo, nakubaliana na yeye kwamba, kwa kweli hospitali hiyo ni chakavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipita mimi na yeye na kikubwa tuliongea na DMO pale kwamba, sasa waanze kuweka kwenye mchakato wa bajeti ya mwaka huu ili itakapofika fedha zimepatikana basi liweze kutekelezeka kulingana na taratibu za fedha.
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kama ilivyoelezwa hapo awali kwamba, kumekuwa na ongezeko la matatizo ya akili na tunafahamu ongezeko la matatizo ya akili ni pamoja na kukosekana kwa watu wa ushauri na unasihi. Je, ni nini mkakati wa Serikali katika kuhakikisha inaongeza Maafisa Ustawi wa Jamii mpaka ngazi ya kata? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge alivyosema. Tunachukua hilo wazo, lakini katika sehemu nyingi kuna Maafisa Ustawi wa Jamii, bahati mbaya tu tukienda kwenye wilaya zetu wamepewa kufanya kazi nyingine, unakuta wengine ni Watendaji wa Vijiji au wengine wanafanya shughuli nyingine ambazo sio za ustawi wa jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kikubwa kwanza tutaenda kusimamia waliopo kwanza wafanye kazi ambayo walitakiwa kuifanya na wawezeshwe kufanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa sababu tumefika kwenye level ya mkoa kupeleka wataalam hawa wanaoshughulikia masuala ya akili, basi tutashusha kwenye wilaya ikiwezekana kwenye vituo vya afya jinsi bajeti itakavyoruhusu. Ahsante sana.
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Rufaa ya Kitete, kama neno rufaa linavyoonesha, ndio hospitali tegemezi kwa Mkoa wa Tabora. Hospitali ile inahitaji Madaktari Bingwa wasiopungua nane na kama alivyojibu Mheshimiwa Waziri kwamba, kuna Madaktari watatu, ingawa mimi nafahamu kuna Madaktari Bingwa wawili yani kama ilivyo jibu lake la msingi, kwa watoto na akinamama; hatuna Madaktari wa upasuaji, hatuna Madaktari wa mifupa, hata physician hawapo kwa hiyo, hatuna Madaktari wengi na hii ni hospitali ya rufaa. Niseme namshukuru sana Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, kwa kutupa shilingi hizo bilioni 10.5 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya dharura pamoja na majengo ya watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, baada ya Mheshimiwa Rais kutoa fedha zote hizo na majengo tayari yamekamilika, hayana Madaktari Bingwa kwa muda mrefu, Wizara ya Afya hamuoni mnaanza kudidimiza hata juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kutoleta madaktari bingwa katika majengo hayo mazuri ambayo yanajengwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa, sehemu zingine kuna Madaktari Bingwa wengi sana, ikiwemo Dar-es-Salaam. Na kwa kuwa, Madaktari wengi hawaendi kwenye mikoa mingine kama Tabora kwa sababu ya vivutio. Je, Wizara imejipangaje kuweka vivutio kwa madaktari hawa bingwa ili waweze kuvutiwa kufanya kazi sehemu kama Tabora Mjini? ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja amesema Madaktari ni wawili sio watatu; mimi ninachoweza kumwambia mpaka mwisho wa mwaka huu maana yake wanaenda kuongezeka Madaktari sita. Wanapoongezeka maana yake watakuwa, tulitegemea wawe tisa, lakini maana yake unasema watakuwa nane, lakini nataka kukuhakikishia watakuwa tisa mpaka tunapofika mwisho wa mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, specifically ametaja baadhi ya magonjwa na matatizo yanayowasumbua zaidi kwenye eneo lao; tayari Waziri wa Afya ameshaelekeza upembuzi yakinifu ufanyike nchi nzima kujua maeneo yenye Madaktari wengi kuliko mahitaji halisi, ili kuweza kuwapeleka katika yale maeneo ya pembezoni ambayo yana uhitaji zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia amezungumzia suala zima la kwamba, la watumishi kwa ujumla kwamba, majengo yanakwenda kwisha na wakati mwingine majengo yanakuwa mazuri, lakini ndani yake hakuna watumishi wa kufanya kazi hiyo; lakini nimwombe Mheshimiwa Mbunge suala la watumishi wa afya kuwa wachache sio suala tu la Tabora peke yake ni suala la nchi nzima na ni tatizo ambalo hata wanapokwenda shuleni kuwa recruited wanakuwa vilevile wachache, kwa hiyo kwenye soko kuwapata aina ya kada unayotaka wakati mwingine ni changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme kwamba tumechukua; na hata wakati fedha hizi shilingi trillion 1.3 ambazo Mheshimiwa Rais wetu ameipa Sekta ya Afya shilingi bilioni 495, alielekeza kwamba wakati ujenzi huu unaendelea, vile vile tukae na TAMISEMI na kwa wakati huo huo tukae na Wizara ya Utumishi kujipanga kuhakikisha majengo yanapoisha na ujenzi huo unapoisha, watumishi wanapatikana wa kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mwakasaka usiogope jinsi fedha na ikama inavyotoka. Tutahakikisha kila mahali kunakuwepo na watumishi wanaoweza kutoa huduma. Pia tunapunguza hilo tatizo kwa kuhakikisha vilevile madaktari bingwa walioko Dar es Salaam na mikoani wanaweza wakachukua wale wagonjwa wanaotakiwa kupelekwa rufaa Dar es Salaam au kwingine au kuletwa Benjamin, wakawafuata huko huko Kitete na kutibiwa huko huko ili kupunguza wananchi kuja Benjamin au kwenda Dar es Salaam. Ahsante sana.
MHE. HUMPHREY H. POLEPOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani; na ni lini itaanza kuwezesha majaribio ya kitabibu au kwa Kiingereza wanaita clinical trials kwa bidhaa za mimea dawa ambazo zimesajiliwa na Baraza la Tiba Asili na mbadala na tayari
zinatumika kwa uhiyari wa wagonjwa kama over the counter drugs na zimeonyesha ufanisi mkubwa katika kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mfumo wa upumuaji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri. Labda nimwambie tu siyo kwamba ni lini itaenda kuanza, imekuwa ikifanya hivyo; na taasisi yetu ya NIMR na kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnakumbuka kwenye fedha hizi ambazo zimetoka, shilingi trilioni 1.3, katika fedha hizo, shilingi bilioni 6.1 zilitengwa kwa ajili ya eneo hilo la tafiti ikiwepo na suala la tiba asili. Kama mnakumbuka hapa Bungeni, niliwahi kusema kwamba kuna kipindi Mheshimiwa Rais wetu alipeleka shilingi bilioni 1.2 pale NIMR kwa ajili ya kufanya mambo kama hayo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyaulizia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli Rais wetu ameielekeza Wizara kwamba tuwekeze nguvu nyingi sana kwenye eneo hili la kufanya tafiti za madawa yetu ya asili kwa sababu yametusaidia sana kipindi kile ambapo tunapitia wakati mgumu kwenye Corona wakati hakuna anayejua suluhu ni nini kwenye tatizo hili. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza namshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia shilingi 1,500,000,000 tukajenga Hospitali ya Halmashauri. Sasa hospitali hii inafanya clinic ya watoto pake yake, haina vifaa tiba na hasa madaktari bingwa.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuleta vifaa tiba ili hospitali ile ifanye kazi kama ilivyokusudiwa na Serikali?
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake mzuri wa masuala ya wilaya yake. Labda nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba suala siyo fedha za kununua bidhaa hizo, tayari Rais wetu ametoa fedha na sasa ni mchakato wa manunuzi unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, nikimaliza muda wa maswali njoo tukae pamoja ili ueleze specifically na tuwasiliane na DMO wako ili aweze kutuletea list specifically kinachotakiwa ili kiweze kwenda kununuliwa na kufanyika haraka ili upate huduma hiyo. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nasikitika sana kwa majibu haya yaliyotolewa na Serikali. Kipindi cha miaka minne toka mwaka 2018 mpaka leo Serikali inazungumzia suala la tathmini, inazungumzia suala la upembuzi yakinifu, miaka minne! Wananchi wa Simiyu wamechoka na hizi danadana za Serikali, leo tunataka tuambiwe nini sababu zilizozuia mradi huu kujengwa ili tujue, kwa sababu huwezi kutuambia hadi miaka minne unazungumzia tathmini, unazungumzia upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni nchi yetu imekuwa ikiagiza bidhaa za nguo kutoka nje ya nchi kutokana na ukosefu wa viwanda kama hivi, tunaagiza bidhaa za nguo kutoka nje tunatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za nguo nje ya nchi. Lakini pia wananchi wa Tanzania wanateseka kwa kukosa soko zuri la pamba kwa sababu ndani ya nchi hakuna viwanda na kugeuka kuwa soko la wakulima wa nchi zingine kwa kununua bidhaa zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ajira zetu tunazi-export kila leo; Serikali ituambie ni lini Serikali itachukizwa na mambo haya na kuingia kwenye uwekezaji wa viwanda vya pamba ili wakulima wa pamba waweze kupata bei nzuri na tuweze kunufaika na valua addition la zao la pamba? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mbunge kwa swali lake zuri la nyongeza na ni kweli akisikitika ana haki ya kusikitika, lakini kiukweli ilikuwa ni lazima taasisi yetu ya TIRDO ifanye upembuzi yakinifu wa kuhakikisha kwamba kinachokwenda kufanyika je, kinaweza kuleta manufaa tarajiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile ikumbukwe kwamba kuna mifuko kama mitano ambayo ilikuwa ichangie kwenye ujenzi huo; kwa maana ilikuwa kwanza ni kuhakikisha hii mifuko inakubaliana na module operant pamoja na kufanya hayo mambo mengine, lakini kimsingi ilionekana vilevile katika upembuzi yakinifu ndiyo maana utaona upembuzi wa kwanza ulionesha tunahitaji shilingi bilioni 59.4 kujenga. Lakini wakati wakifanya mchakato wakaona kwamba kuna uwezekano wa kuokoa hizo shilingi bilioni 51.

Sasa labda Mheshimiwa anasema ni lini tutamalizana na jambo hilo, labda Mheshimiwa Mbunge nikuombe kitu kimoja kabla ya tarehe 15 Machi, 2022 tayari kitaitishwa kile kikao ambacho kitaelezea muafaka wa hili jambo na Mheshimiwa Mbunge tutawaalika Wabunge wa Mkoa wa Simiyu ili tuweze kukubaliana way forward kwa pamoja.
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na pia nashukuru kwa majibu sana ya Serikali. Naendelea kuipongeza Serikali kwa juhudi inazofanya kuhakikisha kwamba upatikanaji wa dawa unakuwa ni mzuri. Pia naishukuru Serikali, inajitahidi kuhakikisha kwamba wazee wanapata vitambulisho vya kupata dawa bure na pia wanaendelea kupata vitambulisho vingine. Hata hivyo nina swali la nyongeza kwa Serikali.

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba wazee wanaendelea kupata stahiki za dawa kwa mwendelezo mzuri bila usumbufu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi anavyofuatilia matatizo ya akina mama wa Mkoa wa Pwani kwa ukaribu sana hasa kwenye mahospitali yetu; vile vile kwa jinsi ambavyo anafuatilia watoto wa kike kule mashuleni, niliona procedure yake nzuri sana inayofuatilia kwa karibu sana watoto wakike wa Mkoa wa Pwani.

Mheshimiwa Spika, kwanza niseme kama tulivyosema, mmeona Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 338.8, shilingi bilioni 495 na umeona shilingi bilioni 18. Kwa kipindi cha miezi tisa tu zimekwenda zaidi ya shilingi bilioni 846. Maana yake ni nini? Shida siyo fedha, ni kujipanga.

Mheshimiwa Spika, kikubwa Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Bashungwa wameshatoa maelekezo kwa ma- RMO wote na ma-DMO wote kuhakikisha kila hospitali na kila kituo cha afya na zahanati, wana dirisha la wazee kwenye hospitali zao na kunakuwepo na daktari na mtu maalum wa kuwahudumia wazee. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile kuhakikisha kwamba kunakuwepo na dawa eneo husika na wazee wapate vitambulisho vyao kwa sababu kuna utaratibu wa wazee kupata vitambulisho vyao. Pia tumeshawaelekeza MSD, vituo vyetu vikiomba dawa wapeleke ndani ya siku tatu dawa ziwe zimefika kituoni na kama hawana item hizo, ndani ya masaa 24 wawe wamewaruhusu vituo vinunue dawa kwa sababu imeonekana vituo vinakuwa na fedha za basket fund, na own source lakini wanashindwa kununua dawa kwa sababu hawajapewa ruhusa ya kufanya hivyo kama taratibu zinavyotaka na MSD. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu masuri ya Serikali, ninalo swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itaiwezesha hospitali zote za kanda kutoa huduma ya tiba ya kansa kwa asilimia 100?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi ambavyo anahangaika na matatizo ya wananchi na akinamama wa Kagera, lakini jinsi ambavyo anashirikiana na Wabunge wa majimbo kwa kuwafuata kwenye viti vyao na kuwauliza mambo ambayo wanaweza wakafuatilia kwa pamoja. Hili linaonesha ni kwa nini umeaminika miaka iliyopita na sasa unaendelea kuaminika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda niseme tu kwamba Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, amenunua kifaa chenye thamani ya shilingi bilioni 18 ambacho ni kifaa pekee kwa Afrika Mashariki kwa sasa na viko vitano tu kwa Afrika ambacho kina uwezo wa kusaidia kupima kansa na kiko Ocean Road na kinazalisha mionzi ambayo ilikuwa tunaenda kuchukua Afrika Kusini. Kwa maana hiyo sasa mionzi iliyokuwa inachukuliwa Afrika Kusini hata nchi za Afrika Mashariki sasa watakuwa wanachukua hapa Ocean Road.

Mheshimiwa Spika, lakini hiyo haijatosha kwa Kanda ya Ziwa; kwa Kanda ya Ziwa tayari Serikali imepeleka shilingi bilioni 7.4 kwa ajili ya kuboresha miundombinu pale na kununua vifaa ili kuweza kutoa huduma pale kwa asilimia 100, KCMC imeshapelekwa shilingi bilioni sita kwa ajili hiyo na kwa upande wa Kanda ya Mbeya sasa hivi tukio kwenye hatua, inatakiwa ufanyike ujenzi kujenga kituo kimoja ambacho kinashughulikia kansa kwa eneo lote. Tayari michoro imeshachorwa na sasa tathmini inafanyika ili kujua sasa ni shilingi ngapi itumike hiyo kazi ianze mapema. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kutokana na kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukizwa yanayosababishwa na ulaji wa vyakula, kwa mfano cancer na viriba tumbo: Je, Serikali haioni kwamba TBS imeshindwa kudhibiti ubora wa vyakula?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Kwa kuwa TBS inadhibiti ubora wa vitu vingi ikiwemo petroli, magari, matairi, chemicals na vitu vingine: Je, Serikali haioni kwa unyeti wa chakula ikaweza kutenganishwa na vitu hivi vingine? Ahsnate. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Neema Mgaya kwa sababu tu ushauri wake hauishii kwenye kutushauri kupitia maswali, lakini amekuwa ni mdau mzuri sana wa Wizara ya Afya katika kutoa ushauri hasa kwenye kuboresha afya za Watanzania. Swali lake la kwanza anadhani sisi hatuoni kwamba kutokana na matatizo ya cancer pamoja na viriba tumbo, inawezekana ikawa ni vigumu kusimamia eneo hilo kama haya mambo yataendelea kubaki TBS. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza moja, hili ni suala la kisheria. Lilikuja Bungeni na ikaonekana sababu za kuweza kuhamisha hizi shughuli ziweze kupelekwa TBS badala ya kubaki Wizara ya Afya. Sasa, wazo lake ni zuri kwa sababu kweli kama ambavyo hata wiki iliyopita na inaonekana masuala ya cancer yamekuwa yakisumbua watu, lakini kuna umuhimu wa masuala ya chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakwenda kujadiliana na Wizara ya Afya na tuko tayari kupokea maelezo na kujadiliana na Wizara ya Viwanda, ambayo ni Wizara husika. Tukiona kuna umuhimu wa kuhamisha, basi tutarudi Bungeni kwa ajili ya kufanya hilo ambalo amelisema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kwamba anadhani vile vile kule TBS wanafanya mambo mengi mengine hayahusiani kabisa na afya. Hata hivyo, nimwambie tu, hata petroli yenyewe ina-impact vile vile kwenye afya. Kwa hiyo, usipoangalia vizuri unaweza ukahamisha kila kitu ukaleta afya. Kwa sababu, petroli ukienda kwa maana ya mazingira na mambo mengine bado yanarudi pale pale kumuumiza binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachoweza kusema, wazo lake ni zuri, lakini ni suala la kisheria na Bunge lilikaa likapitisha, tutaendelea kukusanya maoni ya wadau, tutashirikiana na Wizara ambayo inahusika na masuala hayo. Kukionekana kuna uhitaji wa kurudi Bungeni kubadilisha sheria na mambo hayo yaje Wizara ya Afya, tuko tayari kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli input ya Mheshimiwa Mbunge ni muhimu kwa sababu tuna changamoto kubwa sana sasa hivi kwenye masuala mazima ya afya. Mimi nalichukua kama wazo, tunakwenda kuanza kufanyia kazi. Nafikiri na mimi kuna umuhimu wa kuanza kutafakari kama anavyofikiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza nakiri kwamba nimekuwa mtumishi wa TFDA kwa miaka kumi. Niseme, kuhamisha bidhaa za chakula na vipodozi kumekinzana na dhana nzima duniani ya udhibiti wa bidhaa hizo. Ukiangalia nchi zote duniani; uende Marekani bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba, zote zinadhibitiwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, duniani pote ndivyo ilivyo, lakini TFDA imekuwa ni kioo katika East Africa. Wamefundisha Rwanda, wamefundisha hadi Tanzania Visiwani leo tuna ZFDA. Kwa hiyo, kuhamisha kwenda kwenye Bureau of Standards ni jambo ambalo kidunia wanatushangaa. Je, ni lini sasa Serikali italeta sheria hapa ibadilishwe ili hizi bidhaa zidhibitiwe kulingana na matakwa ya kikanda na kimataifa? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri. Kwanza amesema ni practice ya kidunia na pia amesema kwamba TFDA ni mfano kwa East Africa. Nataka kumwambia, ni ya kwanza kwa Afrika nzima. Ndiyo sasa hivi inaongoza kwa Afrika nzima kwa zile standards za kidunia. Kwa hiyo, kwa Afrika ni ya mfano, hata nchi zilizoendelea kuliko sisi tumewapita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi mimi kama ambavyo nimejibu swali la msingi, naona kuna element hapo, lakini kwa sababu walioamua kubadilisha ilikuwa ni suala la kisheria na Bunge likaleta hapa Sheria Na. 8 ya Fedha ilivyobadilishwa ndiyo uamuzi ukafanyika, kwa hiyo, kabla ya kusema tutafanya nini, naomba mtupe muda wa kufanya uchambuzi wa kina kwa kushirikiana na Wizara husika ili tulete maamuzi hapa tusije tukaingilia mambo ambayo yanaweza yasitekelezeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tunaelewa concern yenu Wabunge, tunaelewa concern ya swali la msingi. Tutaendelea kulichungulia vizuri na kushirikiana na wadau husika ili tuweze kuona tuendeje. (Makofi)
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nataka niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukumu ya TFDA ikiwa ni pamoja na Baraza la Wafamasia ni udhibiti wa dawa. Sasa hivi kumekuwa na tatizo kubwa sana la uuzaji wa dawa holela ikiwa ni pamoja na hizi dawa zinaitwa P2. Nini mkakati wa Serikali wa kudhibiti uuzaji holela wa dawa katika maduka bila kuzingatia misingi na matumizi ya dawa hizo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ameeleza kwamba kuna uuzaji wa dawa kwa namna holela. Kikubwa wala hilo halihitaji kusema tunajipangaje. Hilo liko wazi, zipo hizo taasisi, yupo Mfamasia wa Serikali, ipo Pharmacy Council, wapo TMDA ambao ndiyo wanahusika kufanya hiyo kazi. Straight forward ni kwamba hatutaki kuliona hilo. Waanze kusimamia miongozo na sheria na taratibu za kusimamia masuala mazima ya dawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kimsingi ni agizo tu linatoka hapa kwamba inatakiwa hili analolisema Mbunge lisiweze kuonekana tena likitokea kama lipo. Tutakwenda kulifuatilia kama lipo, wanaofanya hivyo watawajibika na vile vile tutaenda kusimamia sheria kama ambavyo ilishapitishwa na Bunge. (Makofi)
MHE. MICHAEL M. KEMBAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nimshukuru na nimpongeze Waziri kwa majibu yake mazuri ambayo yametolewa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia 45 ya Watanzania wanatumia tiba asili. Tunashuhudia waganga wa tiba asili wakiwapa watumiaji kwa vifungashio ambavyo siyo salama. Vilevile tunaona wanatumia vikombe kupima dawa na mengine ambayo sijayataja. Ningependa kujua, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba dawa wananchi wanazotumia ni salama na vilevile zinasajiliwa kwa ajili ya matumizi sahihi ya wananchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nijibu swali la Mheshimiwa Kembaki kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, alichojaribu kusema ni kwamba asilimia 45 ya Watanzania wanatumia hizi dawa za asili ambayo ni kweli. Pia anajaribu kuonesha kwamba wakati mwingine zinafungwa kwenye vifungashio ambavyo siyo salama. Anataka kujua tunafanyaje ili kuhakikisha sasa hizi dawa zinaweza kuwafikia Watanzania zikiwa salama?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tuna taasisi yetu ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambayo kazi yake moja kwa moja ni kwa ajili ya kupima usalama wa dawa hizo; lakini kuwapa maelekezo ni namna gani wanaweza wakazipaki na kufikisha kwa wananchi zikiwa salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakiri ukweli kwamba kwa kipindi hiki cha corona kumekuwa na dawa mbalimbali na mambo mengi ambayo yanaleta shida. Hata hivyo, Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan kama nilivyosema nyuma hapa, alishatoa shilingi bilioni 1.2; na leo nimetoka ofisini, imeenda tena shilingi bilioni 1.2, kwa maana ya shilingi bilioni 2.4 kwenye eneo hili la tiba asili kwa ajili ya kwenda kujenga uwezo kwa hawa watu wetu wazalishaji wa tiba ya asili, lakini kujengea taasisi zetu uwezo wa kuangalia hizo tiba asili zinazotolewa.

Je, zina hivyo vitu ambavyo vinaweza kutibu ugonjwa wenyewe unaosemekana? Pia itaenda kununua mashine za kupima na mambo mengine ya kusaidia utafiti na kupima usalama wa dawa hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali imejiwekeza kwenye hilo. Majibu mengine kutokana na hii shilingi bilioni 1.2 ambayo imetoka leo, nayo tutawaletea majibu yake kwa sababu tunaenda kuangalia dawa nyingine 56 ambazo zilikuwa zinatumika wakati huu wa corona. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. HUMPHREY H. POLEPOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nchi za Uingereza, Denmark, Sweden na Norway zimeamua kuachana kabisa na masharti kichefuchefu dhidi ya ugonjwa wa Corona; na kuamua kuishi na ugonjwa wa Corona kama magonjwa mengine. Nini kauli ya Serikali kuhusu mwelekeo huu mpya Kimataifa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli ya Serikali, ninachokiona ni kwamba Sweden na nchi zilizotajwa zimeamua kusimama kwenye msimamo wa Tanzania toka mwanzo. Kauli ya Tanzania ni moja tu kwamba sisi kama Tanzania tutaendelea kuhakikisha tunakuwa makini katika kufuata zile taratibu zote ambazo WHO wamezielekeza. Pia tutaendelea kufuata zile taratibu ambazo ni local, zinazotokana na watu wetu na nchi yetu ambazo tulishazifuata toka mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huo tutaendelea kulinda mipaka yetu na kuwapima watu wanaoingia na wanaotoka kuhakikisha watu wetu ndani ni salama. Pia tuwahakikishie usalama wenzetu waliopo huko duniani wakija kwetu, nasi tukienda kwao ili tuweze kuitengeneza dunia salama kwa kufanya kazi kwa pamoja. Kwa sababu tukiwa wote salama, wote tutakuwa salama; mmoja asipokuwa salama, wote hatutakuwa salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, lakini niseme, dunia siku moja itafika mahali ikubali mwelekeo wa Tanzania toka mwanzo ulikuwa ni sahihi. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Madawa ya asilia ni kweli kama Watanzania tulikuwa tunayatumia siku za nyuma mpaka sasa. Ila kwa sasa kumekuwa na matangazo mengi sana kwenye vyombo vya habari, wakielezea kwamba wanatibu magonjwa sugu ya figo na magonjwa mengineyo ambayo ni hatarishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina kauli gani ya kukataza matangazo hayo kwa kuwa hayana tafiti sahihi kwa wananchi na wamepoteza fedha nyingi sana kwa kununua dawa hizo na zisitibu chochote? Tunaomba kauli ya Serikali kwa watu kama hao. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nampongeza kwa swali lake zuri, kweli kwamba kumekuwa na matangazo hayo. Ila ukisikia Serikali na Taasisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na TMDA tena inapunguziwa kazi; na hata Wizara ya Afya kwa kutumia wadau wengine, kwa kweli lengo ni moja kusaidia hawa watu ambao ni wabunifu wetu wanaohangaika huku na huku kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali hawakatishwi tamaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuhakikisha tunawadhibiti ili wasiweze kufanya kitu ambacho kinaweza kikapelekea madhara kwa watu; na ndiyo maana leo kwenye Wizara ya Afya kuna Kurugenzi ya Tiba Asili. Moja ya kazi yake, pamoja na ku-facilitate waweze kuzalisha hiki wanachokifiki, lakini ni kuwa-control kuhakikisha wanachokifanya mwisho wa siku hakiwi holela. Tutakwenda kuongeza nguvu hapo kama Mheshimiwa Mbunge alivyoshauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge ukienda Wilaya ya Meru, najua kuna watu wasiokuwa na uelewa walivuruga. Kuna Hospitali ilikuwa inaitwa MOMELA ilikuwa unapimwa vipimo vingine vyote vya kidaktari; unapimwa Ultra-Sound, unapimwa damu kama kawaida, lakini ukifika duka la dawa, unapata dawa za tiba za asili. Tunataka tufike hapo, kwamba ifike mahali tuna dawa ambazo tunajua zinatibu ugonjwa, tuna dawa za kisasa na tiba asili. Vilevile uweze kufuata taratibu zote za kuhakikisha usalama. Huko ndiko tunakoelekea.

Mheshiiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunachukua wazo lako na tunaongeza nguvu kwenye eneo hilo. (Makofi)
MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa jibu zuri la Serikali, lakini kutokana na umuhimu wa hospitali hii ya Kanda ambayo inajumuisha mikoa mitatu; Kigoma, Katavi na Tabora; nataka majibu ambayo yataweza kutuonesha Wana-Kanda ya Magharibi ni lini hasa hospitali hii itaanza kujengwa kutokana na kwamba eneo lilishatengwa kama ambavyo amesema na katika Kata ya Magili kwa hekari 200? Hii itasaidia wananchi wasianze kufanya shughuli za maendeleo kwa kuzingatia ni muda mrefu mchakato huu walishasema utafanyika lakini bado haujafanyika.

Je, Serikali inaweza kutueleza ni lini hasa kazi hii inaweza ikafanyika? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ambavyo nimeshaeleza kwenye swali la msingi kuhusu tathmini; kwanza fedha za kwanza ambazo makadirio ya kuanza, kwa sababu ni fedha ambazo hazitamaliza, lakini zimeshatengwa shilingi bilioni 10 za kuanza, lakini kazi inayofanyika ni kuangalia kwenye mikoa hiyo kuhusu umbali, kwa sababu hatuangalii tu Hospitali ya Kanda kwamba tunaweka Magharibi au wapi, tunaangalia ni mikoa ipi na ni mkoa upi upo mbali na facilities kama hizo?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, ukiangalia kutoka Tabora kuja Benjamin Mkapa ni Kilomita ngapi? Tabora kuja hospitali nyingine ya Kanda ni Kilomita ngapi? Hii itasaidia tuweze kuamua eneo sahihi ambalo huduma itawasogelea wananchi walio wengi na tuangalie eneo ambalo vile vile huduma nyingine ziko mbali na wananchi ambazo wengine wako karibu nazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, upembuzi bado unafanyika ili kutambua eneo ambalo hospitali itaenda kuwekwa kwa kutumia busara kusogezea huduma wananchi walio wengi zaidi. Ahsante.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa. Shida ya kujengewa hospitali katika Kanda ya Magharibi inafanana kabisa na shida tuliyonayo Wilaya ya Moshi.

Je, ni lini Serikali itatujengea Hospitali ya Wilaya ya Moshi kwa sababu tayari tumeshapata eneo la ekari 38? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge. Mimi mwenyewe nimetembelea eneo hilo ambalo anasema limetengwa, nimeliona. Kikubwa ni kwamba tutashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI ili kwenye bajeti ya mwaka huu tuweze kuona ni namna gani utekelezaji wa hilo hitaji lao litafanyika. (Makofi)
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwetu kule Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Rungwe kuna hospitali kubwa sana ambayo ilikuwa ikiwatibu watu wenye ugonjwa wa ukoma na watu kutoka nchi mbalimbali walikuwa wakitibiwa ikiwa ni pamoja na Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda na Malawi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hospitali ile, ukoma ulifungwa rasmi mwaka 2002. Majengo yale ni hospitali kubwa ambayo ina wodi ya wanaume, wanawake na watoto, ina mochwari, bwalo, jiko kubwa, mpaka machine ya kuchomea takataka na Makanisa yapo pale, pia heka zaidi ya 100 ziko pale, lakini yamekaa bila kufanyiwa kazi yoyote: -

Je, Serikali ina mpango gani na majengo yale? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kujibu swali zuri la Mheshimiwa Mbunge, ameeleza kwamba kuna hospitali yenye facilities hizo. Sasa niweke tu vizuri kwamba suala la ukoma, bado tunaenda kuongeza nguvu kwa sababu tunataka mwaka 2030 ukoma uwe umeisha kabisa Tanzania. Ila wazo lake hilo ambalo anasema kuna facility hiyo ambayo inaweza kutumika kwa namna nyingine; baada ya Bunge tarehe 24, nitakuwepo Njombe, nitapitia Songwe kuangalia Hospitali ya Mkoa wa Songwe halafu tutaenda pamoja kutembelea hilo eneo na watalaam ili tuweze kuamua kwa kuangalia mazingira halisi na kuleta majibu ambayo yatakuwa sahihi kulingana na hali halisi ya kule. (Makofi)
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini majengo yale ni zaidi ya miaka 10 sasa yamekaa hayana matumizi yo yote. Swali la kwanza; je, MUHAS lini wanaanza huo upanuzi wao wa hayo maeneo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa nini wasiwaazime Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo yale majengo yakatumika kwa Hospitali ya Wilaya ili mradi majengo yale yapate kutumika, yasiendelee kuharibika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anawakilisha wananchi wa Bagamoyo. Ameuliza swali ni lini wataanza kufanya upanuzi na kuyatumia, nafikiri yanatumika wakati wote lakini nitakwenda tutembelee mimi na yeye na tuweze kuwasiliana na utawala wa MUHAS ili tuweke mkakati mzuri wa kuhakikisha wanashirikiana ofisi ya Mbunge na wananchi wa Bagamoyo na Chuo cha MUHAS.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ninachoweza kumwambia ndugu yangu ni kwamba, kikubwa kwa wananchi wa Bagamoyo, Chuo Kikuu kila Mbunge hapa angetamani Chuo Kikuu kiwepo ndani ya Jimbo lake. Chuo Kikuu kuwepo ndani ya Jimbo lako ni fursa kubwa sana. Kwa hiyo, kikubwa mimi na yeye tutakachokifanya ni kujenga uhusiano na Hospitali ya Wilaya na Chuo Kikuu cha MUHAS ili waweze kushirikiana na kufanya kazi pamoja na kufufua yale majengo ili hospitali ya Mheshimiwa iweze kupanuka, lakini manufaa ya watumishi yapatikane. Kwa upande wa hospitali ya wilaya lakini manufaa yanayotokana na Chuo Kikuu yapatikane kwa watu wa Bagamoyo. Tutakwenda kusisita umuhimu wa mahusiano. Ahsante.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Singida Mjini hatuna Hospitali ya Wilaya na ipo ahadi ya Serikali ya kukabidhi majengo ya Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa Hospitali ya Wilaya. Sasa nataka kujua ni lini ahadi hii itatekelezwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge, swali lake, kama lifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza alivyo na taarifa na tulivyotembelea mimi na yeye kwenye hospitali yake ya mkoa juzi, tumeona majengo ambayo yanajengwa hospitali mpya ya Mkoa wa Singida. Siyo muda mrefu mpaka mwezi Julai majengo yale yanakwenda kukamilika na hospitali ya mkoa itaondolewa kwenye eneo iliyokuwepo halafu na kuwaachia wilaya hiyo iendelee kutumia hospitali iliyoko pale. (Makofi)
MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kuuliza Chuo cha MUHAS kimedahili wanafunzi wengi sana kiasi kwamba wanafundishwa somo hilo hilo kwa session mbili kwa siku. Je, Serikali inaonaje sasa ikachukua hatua ya haraka sana kuhakikisha kwamba haya majengo ambayo yanamilikiwa na Serikali yakatumika haraka ili wanafunzi wakayatumia ili kuweza kupunguza hiyo changamoto?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nahato, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza niseme kwamba ndiyo maana nikamwambia Mheshimiwa Mbunge aliyeuliza swali la msingi uwepo wa majengo yale kule Bagamoyo ni fursa kwake; na sababu mojawapo ni hilo analolisema Mheshimiwa Mbunge kwamba wanafunzi sasa wamerundikana pale Muhimbili na somo lilelile linaingia darasa hilo hilo mara mbili na wanafunzi wa session tofauti, lakini darasa lilelile.

Kwa hiyo, kimsingi tutakwenda kufanya haraka na tutakwenda kushauriana kwenye bajeti ya mwaka 2022/2023, fedha ziweze kuwekwa kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kuweza kukarabati majengo yaliyopo Bagamoyo na haya Mlonganzila iweze kutumika ili wanafunzi wa MUHAS waweze kufundishwa kwa wakati mmoja.
MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante; kwa kuwa kuna ucheleweshaji mkubwa wa malipo ya watu wanaomiliki maduka hayo na hospitali.

Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuweka njia nzuri ya kuwafanya wamiliki wa maduka yale waweze ku-invest au kuingia katika uwekezaji huu wa kutoa huduma?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa mfumo uliokuwepo kabla wa kuandika karatasi na kujaza fomu za kawaida umekuwa ukichelewesha hayo malipo ambayo imekuwa ni sababu mojawapo ya wamiliki wengi wa vituo na maduka kusita kujiunga na Bima ya Afya, lakini sasa bima ya afya imeshatengeneza mfumo mtandao ambapo sasa malipo hayo yanaweza moja kwa moja yakaingizwa kwenye mtandao siku hiyo na akaweza kulipa mapema kila baada ya mwisho wa mwezi.

Kwa hiyo, tunaielekeza Bima ya Afya sasa waweze kufikisha hiyo huduma Zanzibar mara moja ili hilo tatizo liweze kuondolewa. (Makofi)
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kutoa maswali yangu mawili ya nyongeza.

Kwa kuchelewa kuonekana TB Serikali ina mkakati gani ili kuepukana na masuala ya maambukizi? (Makofi)

Je, kuna mpango gani wa kutoa elimu kwa umma juu ya ugonjwa huu kwa kupitia warsha, semina au kongamano? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mwantumu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza anasema kwa sababu ugonjwa wa TB unachelewa kuonekana Serikali ina mpango gani wa kusaidia wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ni utafiti, tayari nchi yetu kwa kushirikiana na vyuo vikuu mbalimbali duniani umefanyika utafiti kwenye Hospitali ya Kibong’oto iliyoko Wilayani Siha ambao ulitizama vinasaba vya TB ambavyo huko nyuma TB ilichelewa kugundulika sana kwa sababu wakati mwingine ukipima unamuona mtu ana TB, lakini ni TB mfu, sasa imegundulika kupitia Hospitali yetu ya Kibong’oto technic ambayo inatumia RNA kwa kutumia watafiti wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ni kwenye kutambua haraka, sasa hivi kuna vipimo ambavyo vimegundulika madaktari wazalendo wa Kitanzania kwa kushirikiana na Wamarekani wamegundua vinaweza kutambua mapema vimelea. Lakini ya pili, tunapeleka huduma chini sasa kwa bajeti ya mwaka huu kuna vituo 1,859 vinakwenda kuwezeshwa kuweza kupima, kuna ambulance na x-ray digital ambazo ni movable zinakwenda kuzungushwa kwenye nchi nzima ambavyo kila mkoa itakuwa na ya kwake kwa ajili kuzunguka kwenye jamii kusaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, amesema warsha na kutoa semina, sasa hivi Serikali imenunua malori ambayo ni hospitali inayotembea ambayo ina x- ray yenye artificial inteligency ambayo inatembea kila mkoa na kutoa semina na kwenda kwa kongamano, kila mikutano na kuitisha wananchi, kupima pale pale na tiba kutolewa eneo lile lile. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Ninamshukuru kwanza majibu ya Mheshimiwa Waziri lakini changamoto kubwa kuna baadhi ya Vijiji, Kata hakuna hospitali wala vipimo, sasa sijui anawasaidiaje wazazi ambao wanazaa watoto wachanga ambao wapo katika vijiji ambavyo hakuna hata hospitali yenye vipimo kama hivyo?

Swali langu la pili, kuna watoto ambao wanazaliwa na sickle cell wamekuwa wakipata mateso makubwa sana, damu kupungua mwilini, lakini sasa hivi tunaona kwamba hatupatiwi dawa bure katika hospitali zetu. Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba wanawasaidia watoto wanaozaliwa na sickle cell?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo.

Moja ni suala la kwamba kuna watoto ambao vituo haviko kule, ndiyo maana kuna juhudi kubwa ambayo Rais wetu anafanya kwenye masuala ya kujenga vituo vya afya kila mahali katika nchi yetu na ndiyo maana pia tunasisitiza kila mama mjamzito aweze kujifungulia kwenye zahanati au kituo cha afya ili utambuzi uweze kufanyika na kumpa mtoto tiba stahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili linalohusu suala la selimundu maana yake sickle cell ni kweli kuna tatizo hilo katika nchi, lakini imeshachukuliwa hatua sasa na dawa ya kuweza kuwasaidia hawa watoto imeshawekwa package yake kwa ajili ya kununuliwa na MSD na kusambaza kwenye vituo vyetu na kuweka utaratibu maalum, kwa kushirikiana vilevile na Serikali ya Marekani tayari vilevile imetengenezwa program maalum ambayo inashughulikia watoto wenye matatizo hayo. Ahsante sana.
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kunipa nafasi na mimi kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, tafiti zimefanyika Kitaifa, Je, ni maeneo gani ambayo yanaonyesha baada ya kufanya tafiti kwamba zoezi hili liko kwa wingi nchini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi tunachoweza kumwambia Mheshimiwa Mbunge ni kwamba katika kila watoto 20 mmoja anakutwa na tatizo hilo, maeneo yote ya nchi wamekuwa wapatikana watoto kama hao kwa sababu matatizo mengine yanatokana na maambukizi au wakati mwingine inaweza kuwa mama ana damu aina fulani na mtoto ana damu aina fulani ambayo wakati mwingine ikichanganyikana inasababisha tatizo hilo. Wakati mwingine inatokana kwamba wakati mtoto yuko tumboni kwa mama anakuwa na damu nyingi, chembechembe nyekundu nyingi za damu, kwa sababu tumboni kwa mama anatumia hewa oxygen ambayo ni ile ya mama, kwa hiyo ni lazima awe na chembe chembe nyingi za damu.

Kwa hiyo, akitoka nje akizaliwa baada ya saa 24 zile chembechembe nyekundu zinaanza kuondoka kwa maana ya kupasuka zinapoanza kuondoka sasa inasababisha hilo tatizo lakini ni la kawaida kwa sababu anapofika sehemu yenye oxygen nyingi basi chembe chembe zile nyekundu hazihitajiki inabidi ziondoke. Hivyo ni kwamba, kila mahali hilo tatizo linaonekana, jambo la msingi ni kujua katika kila watoto 20 mmoja anaonekana ana hilo tatizo.(Makofi)
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti mbalimbali na majarida mbalimbali yanaonyesha bado vifo vinavyotokana na uzazi vinazidi kuongezeka. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba inapunguza vifo hivyo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba vifo vinavyotokana na wazazi vipo lakini vinapungua kwa kila wakati. Suala zima la mkakati wa kuendelea kupunguza zaidi ndiyo maana umeona Rais wetu ameelekeza tutumie shilingi bilioni 23 kujenga wodi maalum kwa ajili ya watoto njiti, kwa sababu vifo vya watoto wachanga vinachangiwa asilimia 48 na watoto njiti wanaozaliwa.

Vilevile kwenye suala la akinamama ukiona tunasogeza vituo sana, kumekuwepo na tozo kwa ajili ya kuchangisha kuhakikisha tunajenga vituo kule sehemu ambazo hakuna vituo vya afya ni kuhakikisha wale akinamama ambao wanashindwa kujifungua, basi vituo vinavyoweza kufanya huduma ya dharura na kuokoa maisha ya akinamama vinapatikana hivyo ukiona hela nyingi zinaelekezwa kwenye vituo vya afya, zahanati lakini kwenye kuboresha huduma za afya dawa, ndiyo hatua ambazo zinatumika kuhakikisha tunapunguza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhakikishie kwenye nchi yetu vifo vya akinamama na watoto vinaendelea kupungua. Ahsante.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ninashukuru sana kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutujengea jengo kubwa sana la zaidi ya bilioni 11 pale Mkoani Mbeya hospitali ya Meta.

Mheshimiwa Rais alizindua jengo hilo pindi alipofika mkoa wa Mbeya, hali imekuwa mbaya sana wanawake bado wanatumia jengo la zamani kujifungulia. Ni lini Serikali italeta vifaa hata angalau vitanda 100 ili wakinamama wanusurike kulala wanne wanne kwenye wodi ya zamani? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Rais wetu alikwenda akafungua jengo kubwa sana la akinamama pale Mbeya Meta, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Mkoa wa Mbeya ni kati ya Mikoa yenye hali nzuri sana ya afya ukilinganisha na sehemu zingine. Kwa maana ya kwamba ukiangalia hospitali ya Mkoa kuna ujenzi mkubwa sana unafanyika wa zaidi ya bilioni 21 na unaujua, pia ukienda kwenye hospitali ya Rufaa pale umeona jengo lililojengwa. Rais wetu alipoondoka alielekeza kwamba shilingi bilioni 2.1 zielekezwe pale kwa ajili ya kuhakikisha jengo hilo linawekwa vifaa na tayari vifaa vimenunuliwa kwa hiyo ndani ya miezi miwili zitakuwa zimefikishwa pale na kufanyia kazi. (Makofi)
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini bado nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; wakati huwa tunasubiri madaktari waliokwenda kusoma lakini pia bado ile hospitali ni chakavu, na miundombinu yake imechoka; na wakati huo tuna eneo ambalo lilipimea na limefanyiwa usanifu.

Je, ni lini sasa Serikali itaanza ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili wakati huwa tuna changamoto za madaktari inalazimika wagonjwa kuwasafirisha kuwapeleka rufaa ya Mbeya.

Je, ni lini Serikali itaongeza magari kwenye hospitali ya Rufaa Mkoa wa Rukwa ikiwemo na ambulance? ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge Bupe Mwakang’ata kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza la kwamba wameshatenga eneo na kwamba ni lini Serikali itaanza ujenzi kwenye eneo jipya ambalo hospitali ya mkoa inataka kujengwa. Kwenye bajeti kwa mwaka huu imetengwa Bilioni tatu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali hiyo, pamoja na Shilingi milioni mia tisa kwa ajili ya kufanya ukarabati kwenye eneo lile ambalo sasa hivi bado majengo yake ni chakavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kwamba sasa hivi wagonjwa wanapekekwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, kwa maana ya rufaa wanapokuwa wanashida. Umeona idadi ya madaktari bingwa waliopo kwenye hospitali yako ya Mkoa. Maana yake ni nini, wanaopeleka rufaa Mbeya ni wale ambao wanahitaji kutibia kwenye hospitali ya level ya Kanda. Lakini tanategemea kwa idadi hii ya madaktari tulionao ambao sasa hivi katika hao watano waliopo shuleni watatu watamaliza mwezi ya kumi mwakani. Maana yake ni kwamba tutaongeza idadi ya madaktari bingwa na hata rufaa nayo itapungua, ili ifikie kwamba wale wanaohitajika kanda ndio waende lakini wa level ya mkoa ibadi pale pale mkoani. Ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ahsante, namshukuru Naibu Waziri wa Afya kwa majibu yake.

Kwa kuwa, umesema kwamba Wizara imekwishafanya ufuatiliaji wa hivyo vifo na sababu zake. Moja ya sababu ni kutokana na matatizo ya dawa za ganzi (nusu kaputi).

Je, kuna watumishi wa kutosha wa kutoa dawa za nusu kaputi katika vituo vyetu vya afya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa mwaka 2021 ni asilimia 4.1 ya akina mama walipoteza maisha baada tu ya kujifungua kwa oparesheni. Je, kuna utafiti wowote ambao Wizara imeufanya ili kubaini sasa ni dawa gani ambazo zinasababisha akina mama wanapoteza maisha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja, anauliza kama tuna uhakika wa kuwa na wataalam wa kutoa dawa ya nusu kaputi kwenye nchi. Juzi mlimsikia Mheshimiwa Waziri wa Afya akieleza kuhusu mkakati wa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ametoa Shilingi Bilioni Nane kwa ajili ya kusomesha wataalam 524 kwa mwaka huu. Mojawapo wa eneo lililoangaliwa ni eneo hilo ambalo kwa kweli kuanzia kwenye hospitali zetu za Wilaya kushuka chini kumekuwepo na watalaam wachache lakini kwa wanaomaliza chuo mwaka huu tutaenda kupunguza hilo tatizo kwa kiasi kikubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili baada ya uchunguzi wetu kwamba imegundulika nini na tunatakiwa kufanya nini kwenye eneo hilo la kupunguza vifo vya akina mama. Moja, ndiyo maana unaona kuna eneo hili la kusomesha, imefanyika kazi kubwa sana, lakini baada ya Serikali yetu kutoa zile fedha za tozo, vituo vya afya 238 vimejengwa kwa mwaka huu tu peke yake. Pia mwaka huu ambulance 663 zinaenda kununuliwa, nazo mnajua zitakavyokwenda kuweza kupunguza kwenye eneo hilo suala la vifo vya akina mama na watoto.

Mheshimiwa Spika, labda nimalize kwa kumjibu namna hiyo.
MHE. IDRISSA JUMA ABDUL-HAFAR: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Pamoja na majibu haya ya Mheshimiwa Waziri, lakini kumekuwa na ongezeko la malazi ya kisukari, malazi ya moyo pamoja na kansa kwa watoto walio chini ya miaka mitano na hata watoto kwa mujibu sheria za nchi zetu walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Je, Serikali haioni sasa iwe na utaratibu maalum wa kuhudumia kwa asilimia mia moja matibabu ya malazi yasiyoambukiza kwa watoto wote walio chini ya miaka 18? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli suala la kuhudumia watoto chini ya miaka mitano ni suala ambalo kiutaratibu wanatakiwa kupata huduma bure, bila malipo yoyote. Ni kweli kwamba kumekuwa na changamoto ya kwamba wanahitaji huduma lakini baadhi ya dawa zinakosekana. Pia, tuna mzigo mkubwa kweli wa magonjwa hayo yasiyoambukiza, ndiyo maana tunaleta Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote wenye lengo la kusababisha sasa matatizo anayoyataja Mheshimiwa Mbunge yaweze kusuluhishwa.

Mheshimiwa Spika, ukiona uwekezaji mkubwa ambavyo umewekezwa kwenye miundombinu, vifaa tiba na tunaona mwaka huu kuna bilioni 10.7 zinaenda kutumika ni kwa ajili ya kuhakikisha wale wasiojiweza pia wanapata huduma bila malipo.
MHE. MARIAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza ni gharama sana. Je, Serikali wanasaidia vipi wananchi kwenye gharama hizi?

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwa mwaka mmoja, Serikali inatumia bilioni 670 kwa exemption yaani kwa maana na hasa asilimia kubwa ya fedha hizo zinaelekea kwenye kuwasaidia hawa wenzetu ambao wana matatizo ya magonjwa yasiyoambukiza, zinatumika hizo fedha kwa ajili ya exemption.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Muswada wa Bima ya Afya, unakuja hapa ndani, hilo ndiyo litakuwa suluhisho na mnajua pamoja na kwamba tuna Muswada wa Bima ya Afya, Rais wetu ametenga bilioni 149.77 kwa ajili ya kuwapatia bima wale wasiojiweza. Kwa hiyo, mikakati ndiyo hiyo ya kwenda kuboresha na kuhakikisha watu wanapata huduma.
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu hayo ya Serikali. Swali la kwanza; kwa kuwa magonjwa yasiyoambukiza ni tatizo kubwa katika Mkoa wa Lindi. Je, ni lini sasa watapeleka specialist hao wa internal medicine? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, ni lini Waziri atakwenda Mkoa wa Lindi pale Hospitali ya Sokoine kwenda kuona hali halisi ya ukosefu wa Madaktari hao na kadhia wanayopata wananchi? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ni lini Serikali sasa itapeleka Daktari huyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge tukae naye pamoja tuwasiliane na Afisa Utumishi na Wizara ya Utumishi tuone ni lini watakamilisha mchakato huo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, ameniuliza kwamba ni lini tutakwenda Lindi ili kwenda kuona matatizo yanayoendelea pale. Namuahidi Mheshimiwa Mbunge mara tu tukimaliza Bunge, tutashirikiana na yeye na Mbunge mwingine wa Mkoa wa Lindi twende huko. Ahsante.
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Hospitali ya Mkoa wa Katavi inao upungufu mkubwa sana wa Madaktari Bingwa akiwemo Physician na Daktari Bingwa wa Watoto, pia Mkoa mzima Daktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake yupo mmoja tu.

Je, ni lini Serikali itapeleka Madaktari Bingwa katika Mkoa wa Katavi?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge, kwanza hospitali yao ni mpya inayojengwa sasa, lakini ni kweli kwamba siyo tu kwa Mkoa wa Katavi bali upungufu wa Madaktari Bingwa uko karibu nchi nzima, ndiyo maana unaona kuna mkakati unaofanywa kuongeza Madaktari Bingwa. Nitashirikiana na Mheshimiwa Mbunge tuangalie la kufanya. Kwa sababu najua kuna Daktari wa Watoto aliyekuwepo pale alipelekwa Songwe, sasa tutaona ni nini kinafanyika ili kurekebisha hayo yaliyotokea. Ahsante.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Natambua kwamba kila hospitali ya Wilaya inayo shida ya kupata Madaktari Bingwa na upatikanaji wake kidogo unakuwa ni mgumu. Pia kuna Halmashauri zinakuwa na uwezo wa kusomesha Madaktari Bingwa, mojawapo ikiwa ni hospitali yangu. Sheria ya Utumishi inasema tukimsomesha at least afanye Miezi 36 ndiyo aweze kuhama. Sasa kwa sisi ambao tumepeleka Madaktari wakapata huo Ubingwa, halafu wakarudi ndani ya wiki moja wakahamishwa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri anasemaje kuhusu hilo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwenye hili suala la Madaktari Bingwa siyo tu kwa hospitali za Wilaya hata za Mikoa kuna baadhi ya Mikoa ukimpeleka Daktari Bingwa ana-resign anakwenda sehemu nyingine. Tulichokubaliana ni kwamba kama ni Wilaya au Mkoa ametokea pale Daktari kwenda kusomea Ubingwa, anapewa mkataba maalum wa kufanya kazi na Halmashauri au Mkoa huo kwa muda wa Miaka mitano bila kuhama. Kwa hiyo, hilo likianza kutekelezwa na tumeanza kutekeleza huo mkakati ili kuzuia wasihame tena, hivyo, nafikiri hiyo itasaidia sana. Mheshimiwa Musukuma hebu uje kwangu tuone kilichotokea kwenye eneo lako ili tuone kwa yule mliyemsomesha kama tunaweza kufanya lolote. (Makofi)
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, tatizo lililopo katika Hospitali ya Mkoa wa Lindi Sokoine ni sawa kabisa na tatizo lililopo katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Ligula, kukosekana kwa Daktari wa magonjwa ya ndani pamoja na mifupa. Je, Serikali ina kauli gani kutuletea, ingawa tunajua tunayo hospitali ya Rufaa lakini hii ni kuhusu ya Mkoa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimemwelewa Mheshimiwa kwa sababu sijaiangalia vizuri kama ya Mtwara lakini kwa kweli wana bahati moja kwamba, wana hospitali ya Mkoa ambayo ina baadhi ya specialists lakini haijafika hata kilometa moja kutoka Hospitali ya Mkoa kuna Hospitali ya Kanda, ambayo nayo ina Mabingwa. Kwa hiyo, mimi na wewe tutakuja tuangalie specifically tatizo ni nini ili tushirikiane na Mheshimiwa Waziri tuone tunafanya nini.
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada za Serikali, lakini hali bado ni mbaya.

Je, Serikali ina mkakati gani wa dharura wa kutatua changamoto hiyo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo Mheshimiwa Waziri wa Afya alieleza juzi hapa Bungeni, ni kwamba tunaendelea kuangalia sasa ikama ya madaktari kwenye hospitali zote za mikoa kwenye nchi yetu na kuwaangalia mabingwa kote waliko, tukiona na kuangalia hali ilivyo pale Hospitali ya Mkoa wa Iringa ili kuweza kuwahamisha maeneo mengine ambayo yamezidi na kupeleka kule Iringa.

Mheshimiwa Spika, lakini kuna masomo yanayoendelea miezi mitatu mitatu kwa ajili ya super specialists kwa hiyo tutawaondoa nao kwenye eneo hili na kuwasomesha kwa muda mfupi na kuwarudisha kwenye eneo hilo.
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona.

Mheshimiwa Spika, changamoto iliyopo katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa inafanana kabisa na changamoto iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara. Je, ni lini Serikali itakwenda kutatua changamoto hii ya uhaba wa madaktari, hasa kwa magonjwa ya wanawake na watoto katika hospitali hiyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi anavyofuatilia mambo ya mkoa wake, na nakumbuka alikuja Wizarani kwa ajili ya hilo. Ninamuomba Mheshimiwa Mbunge tukutane wakati wa haya mapitio ya kuwahamisha tuone tunaweza kufanya nini kwenye eneo la mkoa wake.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa watoto njiti hao wana haki kabisa kama alivyosema mwenye kutujibia maswali kutoka Serikalini.

Ni kwa nini sasa basi Serikali hailipi gharama ya mtoto huyo wakati ambapo yuko hospitali na inalazimu wazazi kulipa mpaka milioni tano ikiwemo Muhimbili Hospital? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, niseme kwanza moja kwa mwaka huu kwenye bajeti zimetengwa bajeti ya kujenga vituo vya watoto njiti 100, lakini katika module yetu ya kawaida pamoja kwamba hakuna sheria ambayo imetunga kwamba unampa mama huyu likizo, lakini kuna utaratibu wa ndani umekuwa ukifanyika wakati wote ambapo mama akitokea namna hiyo madaktari wanaandika na anapewa huduma.

Mheshimiwa Spika, lakini kwenye suala lako la kusema kwamba Serikali kwa nini hawalipii, kwenye mfuko wa bima kweli kulikuwa na changamoto hiyo kwamba anatokea mtoto njiti, lakini anatakiwa afanyiwe hivyo, lakini inaandikwa na sasa hivi tumeshaondoa hiyo na watoto njiti wanalipiwa na watoto chini ya miaka mitano huwa wanalipiwa bure kama sio bima. Kwenye mfuko wa bima ndio kulikuwa na shida na hiyo shida imeshamalizwa sasa hivi, watoto njiti wanahudumiwa kama kawaida.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, mtoto njiti akizaliwa pale Muhimbili Hospital, anatakiwa alelewe mpaka afika ule umri ambao sasa mimba ingekuwa term na mtoto azaliwe na wengi wanakuwa na complication, lakini suala alilojibu Naibu Waziri mimi mwenyewe nilishafikisha kwake maombi ya kufadhili mtoto njiti ambaye alipitishwa kwangu na anaijua hiyo kesi ilifika mpaka shilingi milioni tano, ni watoto wa kawaida pamoja na hata wale waliokuwa kwenye insurance kama alivyoeleza yeye. Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli alishanifikishia, mara nyingi kuna wenzetu kulikuwa na shida kweli Muhimbili, watoto wakipata matatizo si watoto tu hata wazee na watu wengine imekuwa kwamba wanakuwa-charged hasa hao watoto chini ya miaka mitano. Lakini tulipiga simu kwa sababu ni suala kisheria na halikuwa exempted na sasa tumeweka mfumo ambao hayo mambo hayajitokezi tena. Ahsante.
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa nakushukuru sana lakini pia nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na changamoto kubwa sana ya vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kujifungulia akina mama katika Mkoa wa Mara.

Je, Serikali inawahakikishiaje wananchi na akina mama wa Mkoa wa Mara kwamba endapo italeta vifaa tiba hivyo hospitali pamoja na Vituo vya Afya vya Mkoa wa Mara vitapata vitanda kwa ajili ya kuondoa tatizo hilo?

Swali la pili; je, Serikali imejipanga vipi kuthibiti wizi wa dawa nchini?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa sababu siyo mara ya kwanza kufika Wizarani akizungumzia Hospitali yake ya Mkoa wa Mara. Lakini nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwa sababu yeye anajua kwa sasa tayari vifaa vyenye thamani ya bilioni tatu zimeshapelekwa Mkoa wa Mara na hapa tunapoongea tayari CT Scan ipo pale Mkoani Mara na Digital Xray inangojea tu jengo liishe ili kazi ianze.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie kuwa hospitali ya Mkoa wa Mara tumeshakubaliana ndani ya Wizara na Waziri wa Afya ameshatoa maelekezo tarehe 12 na Mkoa wamekubaliana na maelekezo ya tarehe 12 Disemba hospitali hiyo inaenda kuanza na watumishi watahama kwenye hospitali waliokuwepo ili wahamie kwenye hospitali ya Mkoa.

Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili la suala kuwa tumejipangaje kudhibiti wizi wa dawa. Moja, tumetengeneza mfumo ambao MSD sasa wataweza ku- track dawa kuanzia zinapotoka Taifani mpaka zinapofika kituoni. Wakati huo huo kama Wabunge mnakumbuka tulikuja hapa kwenu na kuwaonesha mianya ambayo inapotea dawa zinapofika kwenye Wilaya zetu na Mikoa yetu. Ushirikishwaji huo sio kwamba tulikuwa tunasema wizi wa dawa, lakini tulitaka kumleta kila mtu on board tujue wote ili tuweze kushirikiana kusimamia na sasa kule kwenye zahanati zetu, vituo vyetu vya afya, hospitali zetu za Wilaya tunashirikisha jamii na Waziri wa Afya ameshatoa maelekezo kwamba dawa ikitoka MSD inapofika Wilayani, Mkuu wa Wilaya ajue, Mkurugenzi ajue, lakini Mbunge apewe copy ili wote pamoja na zile Kamati za Afya za zahanati, za vituo vya afya na Wilaya wajue dawa iliyoingia ili kwa pamoja tushirikiane kulinda huu ubadhirifu ambao umekuwa ukitokea kwenye nchi yetu.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa pale Musoma Mjini hatuna Hospitali ya Wilaya na nimekuwa nikiomba mara nyingi Serikali iweze kutukabidhi ile hospitali iliyopo ambayo ni ya Mkoa na imeahidi kwa muda mrefu.

Napenda kujua ni lini sasa rasmi Serikali itatukabidhi ile hospitali iwe Hospitali ya Manispaa ya Musoma ili huduma bora zaidi ziweze kupatikana kwa watu wetu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo nimesema ni tarehe 12 Disemba, 2022 wanaanza kuhama kwenda kwenye hospitali mpya halafu mnakabidhiwa Hospitali ya Wilaya na ibaki kutumika namna hiyo.
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete bado ina upungufu mkubwa wa dawa, je, Serikali imejipangaje kuhakikisha inapunguza tatizo hilo la upungufu wa dawa katika Hospitali ya Kitete?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwa sababu kwa asilimia na kwa rekodi ambazo zimetoka MSD kwa sasa upatikanaji wa dawa ni asilimia 78 maana yake tuna upungufu wa asilimia 22. Moja ya namna ya kufanya ni kuchukua mapato ya ndani ambayo Hospitali ya Kitete inapata itumie kununua dawa palepale Tabora kama hazitakuwepo pale MSD.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante, Hospitali ya Kanda ya Mtwara bado inaupungufu mkubwa katika kuikamilisha kiujenzi, lakini pia vifaa tiba. Lakini Kanda yote ya Kusini inaitegemea hospitali hiyo kwa muda mrefu.

Sasa ni lini hospitali hiyo itakamilika ili kuwaondolea adha wananchi wa Kusini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza niseme kwamba kwa kweli Hospitali ile ya Kanda ya Mtwara ni mojawapo ya hospitali nchini ambayo imejengwa kwa majengo ya kisasa mno. Lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, pamoja na kazi kubwa ambayo imefanyika pale, mwaka huu wametengewa shilingi bilioni tano kwa ajili ya kuendelea na ujenzi ili kukamilisha mambo ambayo Mheshimiwa Mbunge anasema hayajakamilika. Niendelee kumpongeza Mheshimiwa Mbunge, kwa namna anavyofatilia shughuli za Mkoa wake.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umbali wa kutoka Morogoro Mjini mpaka Mikumi ni kilometa 120 na kutoka Mikumi mpaka Iringa ni kilometa 190, kuna ajali nyingi sana ambazo zinatokea katika kipande hiki na wanategemea sana huduma katika Kituo cha Afya na Hospitali hii ya Mtakatifu Kizito pale Mikumi.

(a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka watalaam wa huduma wa utengamao na physiotherapy pale Mikumi? (Makofi)

(b) Je, Serikali haioni wakati umefika sasa kuokoa maisha ya Watanzania wengi kuanzisha centre of excellence ya wataalam wa mifupa kwa ajili ya kujifunza pale Mikumi? Naomba kuwasilisha. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yake mawili moja la kuongeza watalaam. Moja, kwenye eneo la kuongeza watalaam suala tu siyo kuongeza watalaam lakini ni kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, lakini uchukuzi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunapunguza mambo ambayo yanapelekea ajali zitokee kwenye maeneo hayo, pia kuhamasisha elimu ya magonjwa yasiyoambukiza ili kupunguza idadi ya watu hao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na yeye kwamba Mkoa wa Morogoro ukiangalia wanahitajika watalaam 30 na kwa mwaka huu wanaenda kuongezwa watalaam tisa maana yake katika hawa tisa tutaona ni namna gani tunaweza kuhakikisha tunaongeza watalaam kwenye eneo ambalo yeye amelitaja. Lakini kuangalia vizuri zaidi data zilizotumika kuamua wanahitajika Mkoa wa Morogoro hawa 30 kuangalia kama ilitumika data za wakati gani ili kama kunahitajika kuongeza basi tuwaongeze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine la wataalam wa mifupa na vitu vingine tunaenda kufikiria kwenye ajira ambazo amesema Mheshimiwa Waziri wa Utumishi ni 32,000 basi tutaenda kulizingatia eneo hilo wakati tukipata hivyo vibali. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kupata nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa huduma ya utengemao na mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwa wagonjwa wanaopata matatizo yanayohusika na viungo, na kwakuwa Wilaya nzima ya Mwanga kuanzia Hospitali ya Wilaya mpaka vituo vyake vya afya hatuna matalaam hata mmoja wa huduma hiyo.

Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya kutupatia physiotherapist katika Wilaya ya Mwanga hasa ukizingatia ahadi ya Mheshimiwa Waziri wa Utumishi juu ya ajira lukuki zinazokuja kwa ajili ya afya. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kuwapigania wananchi wa Mwanga, lakini yeye mwenyewe anajua sasa Rais wetu amepeleka fedha pale Mwanga kwa ajili ya kujenga Idara ya Dharura na ujenzi unaendelea. Wakati ujenzi unakamilika na kuweka vifaa na ajira 32,000 ambazo zimetokea hayo mambo yatakwenda kuzingatiwa kuhakikisha tunapomaliza huduma ya magonjwa ya dharura na watalaam wa aina hiyo uliowasema wanakuwepo vilevile kwenye eneo hilo. (Makofi)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, hospitali ya Mji wa Tarime inahudumia zaidi ya wananchi wa Wilaya tatu na imekuwa ina uhaba wa watumishi wa afya wakiwemo watalaam wa utengamao na mazoezi ya viungo.

Je, ni lini sasa Serikali itatuletea watalaam hawa wa utengemao na mazoezi ya viungo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri, lakini nitamuomba Mheshimiwa Mbunge mimi na yeye tutashirikiana kuangalia kwa maana ya data za Wilaya hiyo na sehemu hizo, kwanza kwasababu amesema hospitali inatumiwa na Wilaya tatu, tutaangalia kuona tatizo lipo wapi.

Moja; kama kuna maeneo ambayo inaweza ikafanyika kwenye Wilaya husika wapelekwe kwenye Wilaya husika, lakini kwenye ajira ambazo zinakwenda kutokea tutaenda kuzingatia kwa kuangalia data za eneo husika na utumishi watakapotuletea kibali hayo yatazingatiwa. (Makofi)
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga siyo tu kwamba haina Daktari hata mmoja wa masuala ya viungo, lakini haina Daktari hata mmoja wa macho, meno na radiojia na anesthesia.

Je, Serikali inatuahidi nini katika kupata watalaamu hawa.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mbunge nampongeza sana jinsi ambavyo amekuwa na mchango mzuri sana hasa kwenye eneo la lishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuambie majibu ni yale yale kwamba kwenye ajira 32,000 pia tutachukua kwa kushirikiana na yeye lakini tutawauliza watalaam wa eneo husika kwa kuangalia load ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya mtengamao kwenye eneo alilolitaja ili tuweze kuamua mapema na kupeleka mahitaji Utumishi ili kuweza kupata hao watalaamu ambao Mheshimiwa anawataja.
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba kuuliza swali la nyongeza kwa Mheshimiwa Naibu Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri ulikuja Sengerema nikaalika mkutano mkubwa sana na ukaahidi katika kituo cha Busisi kukipa vifaa, leo mwaka unakwisha unaniandalia kitu gani huko Jimboni kwangu. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimjibu Kaka yangu Mheshimiwa Tabasam ni kweli nimekwenda kwenye eneo husika, tulifanya pamoja naye mkutano wa wananchi na tuliahidi mbele ya wananchi, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa kushirikiana na wenzangu wa TAMISEMI, tayari Kituo cha Afya cha Busisi kipo kwenye maombi ya dharura ambayo sasa yanaenda kutekelezwa mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tayari imeshaingizwa kwenye mpango na fedha zinaenda kupelekwa kwa ajili ya kufanya kazi tuliyokubaliana siku ile kwenye mkutano. (Makofi)
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kupata nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa vile bado tuna upungufu mkubwa wa wataalam wa mazoezitiba na utengamao: -

Je, hawaoni sababu ya kuanzisha course hii kwenye vyuo kama UDOM ambapo inachukua watu wengi ili angalau tupate wahitimu wa taaluma hiyo kwa wingi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Mbunge, Dkt. Kaijage kwa namna anavyoshirikiana na Wizara ya Afya kwa karibu hasa kwenye kushughulikia huduma ya mama na mtoto kwenye Mkoa wa Pwani. Vilevile nimwambie tu kwamba, siyo tu Chuo Kikuu cha UDOM, kuna mkakati wa vyuo zaidi ya vitano sasa tunaongeanao na kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kuanzisha kada hizi ili kusaidia kupunguza upungufu wa wataalam kwenye soko la ajira. Ahsante sana.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri. Niliomba kujua dawa ambazo zinasababisha akinamama kufa kutokana na ganzi; naomba sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya ifanye utafiti ili tuweze kubaini ni dawa zipi ambazo zinasababisha wanawake wajawazito baada ya kujifungua wafariki? Kwa sababu hapa ametoa sababu nyingine, siyo zile dawa ambazo ilikuwa ni swali langu la msingi. Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda nimsaidie Mheshimiwa Mbunge kwamba leo mimi niliyesimama hapa huwa nikitumia flagyl nachubuka, lakini mimi kutumia flagyl na kuchubuka, haimaanishi flagyl inachubua watu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anatakiwa kujua kwamba vifo vya akina mama vimepungua kwa zaidi ya nusu kutokana na upasuaji unaofanyika na kutumia ganzi hizi hizi. Maana yake ni nini? Ganzi ambazo tunazozitumia leo hapa Bungeni, tuna Wabunge wengi wamefanyiwa operesheni na wametumia dawa hizi hizi na wako salama. Maana yake ni nini? Tumesema kuna sababu za vinasaba na kuna sababu nyingi ambazo zipo; sasa hizo haziwezi kufanya tukaleta taharuki kwenye nchi.

Mheshimiwa Spika, sisi madaktari huwa ni watu ambao tuna miiko na tunaapa na tuna maadili ya taaluma. Sasa ni muhimu sana unapouliza swali uhakikishe kwamba huvuki ile mipaka ya kitaaluma na miiko kwa sababu kimsingi labda kama angetaka nimweleze ninaposema DNA maana yake nini; ninaposema ganzi, maana yake ni nini? Kwa sababu kuna ganzi ukipigwa hapa kwenye mgongo inasababisha mtu kutokupumua. Kuna procedure za kufanya. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nakuomba tuonane kama wanataaluma ili tuweze kusaidiana nawe uelewe jambo linafanyikaje?
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Je, ni lini Serikali itapeleka mashine ya kupimia saratani ya matiti katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Iringa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nafikiri Mheshimiwa Mbunge hilo ni hitaji la msingi kwa sababu mashine hiyo iko kwenye Hospitali ya Kanda ya Mbeya, lakini ni vizuri ikapatikana kwenye hospitali ya Mkoa wa Iringa. Basi mimi na wewe tuje tukae tushirikiane na wenzetu ili tuone ni namna gani tunaweza tukaweka utaratibu wa mashine hiyo kupatikana kwa sababu fedha zipo.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, hospitali ya Halmashauri ya Ushetu imekamilika ujenzi wake, lakini wananchi bado wanatembea zaidi ya kilometa 80 kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Je, ni lini Serikali italeta vifaa tiba katika hospitali hiyo ili wananchi hawa waanze kupata matibu karibu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza priority ambayo Mheshimiwa Waziri wa Afya ameelekeza sasa hivi ni kuhakikisha hospitali zote zile ambazo zimeshajengwa vituo vya afya, zahanati na hospitali za Wilaya na majenzi yote, kuhakikisha sasa vifaa tiba vinaenda kununuliwa. Kama ambavyo nilisema jana sasa hivi shida siyo fedha kwa sababu Rais wetu kama nilivyosema tayari alishapeleka shilingi bilioni 333.8 na tayari kila mwezi kuna utaratibu wa kupeleka shilingi bilioni 15 MSD. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge kwanza nitumie fursa hii kwa kushirikiana na wenzangu wa TAMISEMI kwamba RMO asimamie kwanza OPD kwenye hiyo hospitali ianze, kwa sababu inawezekana kuanza OPD mapema na kujipanga kwa ajili ya kuanza wakati tunangojea vifaa vya kuhakikisha hospitali hii inaenda kufanya kazi kama full flagged kama hospitali ya Wilaya. (Makofi)
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, hospitali ya Wilaya ya Tanganyika imekamilika kila kitu, tatizo lililopo ni ukosefu wa vifaa tiba ambavyo vinapelekea huduma ya upasuaji kukosekana katika hospitali hiyo.

Je, ni lini itakamilisha kuleta vifaa tiba ambavyo vimebaki katika hospitali hiyo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza hospitali hiyo tuliitembelea na nilitegemea Mheshimiwa Mbunge kwanza angeshukuru kwa Digital X-Ray ambayo tayari tuliikabidhi pale siku ile, yeye hakuwepo lakini Mkuu wa Wilaya alipokea kwa niaba yake.

SPIKA: Ngoja Mheshimiwa Naibu Waziri subiri kidogo, Waheshimiwa Wabunge nilishatoa maelekezo hapa kwa hiyo usimuweke Mbunge mazingira kwamba yeye hatambui huo mchango uliotolewa, anatambua mchango ni kwa sababu maswali lazima yawe mafupi, kwa hivyo anaenda moja kwa moja kwenye swali na wewe nenda moja kwa moja kwenye jibu la swali alilouliza. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni ukweli anachokisema Mbunge kulikuwa na vifaa vya Shilingi Milioni 507 vilitakiwa zipelekwe vimepelekwa vifaa vya Shilingi Milioni
203 vitaenda kumaliziwa mwaka huu kuhakikisha vimepelekwa vilivyobakia.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Je, ni lini zile mashine ulizokuja kukagua mwaka jana ukaniahidi baada mwezi utaleta Wataalam wa dialysis zitaanza kufanya kazi katika Hospitali ya Mkoa ya Iringa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nalipokea swali lake na kwa sababu tulienda wawili tukalitembelea eneo, naomba tukutane tukae pamoja tuhakikishe hiyo kazi inaanza mara moja.
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, asante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itakamilisha taratibu za manunuzi ya mashine ya CT-Scan ambapo na tunategemea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi itapata mojawapo?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachosema Mheshimiwa Mbunge na tayari CT-Scan yao iko kwenye manunuzi kabla ya mwezi Juni itakuwa imefika ST-Scan ya hospitali ambayo Mheshimiwa Mbunge anaisema.
MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tatizo la MSD kutokuleta dawa kwa wakati katika Mkoa wa Kigoma, hata wakileta wanaleta chini ya asilimia 50.

Je, nini kauli ya Serikali katika kutatua changamoto hii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachosema Mheshimiwa Mbunge na kama nilivyosema jana na nimerudia leo kwamba shida siyo fedha ni pale MSD Idara ya Manunuzi kumekuwa na tatizo ambalo Wabunge mmekuwa mkielezea.

Mheshimiwa Spika, siyo Kigoma tu nilikwenda Mkoa wa Lindi waliomba madawa 102 lakini ziko item 55 wakapewa Tano, kwa hiyo kuna tatizo kwenye eneo la manunuzi na ndilo ambalo mmekuwa mkizungumzia.

Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na wenzetu tutaenda kulishughulikia. (Makofi)
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa majibu haya, dah, hadi maswali ya nyongeza yanakuwa na utata. Kwa ruksa yako nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri wakati Serikali inaendelea na mchakato wa kuboresha huduma za afya nchini; katika Jimbo la Kilombero chini ya Kanisa Katoliki imejengwa Hospitali kubwa sana ya Kansa. Hospitali hiyo mpaka leo haijafunguliwa. Baba Askofu anaomba Viongozi Wakuu wa nchi yetu wakafungue Hospitali hiyo. Mheshimiwa Waziri ana majibu gani?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. St. Francis Hospital ni hospitali ya kanda, inatibu zaidi ya mikoa 10. Gharama zimekuwa kubwa na wananchi wanalalamikia kwa sababu Serikali imeondoa ruzuku iliyokuwa inatoa zamani: -

Je, Waziri anaweza kusema chochote kwamba wanaweza kukaa na Uongozi wa St. Francis Hospitali ya Ifakara ili kuzungumza namna ya kurejesha ruzuku ya awali?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza amezungumzia hospitali ambayo imefunguliwa, mimi na yeye tutakwenda Kilombero kuiangalia hospitali hiyo na kukagua halafu tuje tushauri mamlaka husika ili taratibu anazozisema ziweze kuchukuliwa hatua.

Mheshimiwa Spika, pili, suala la ile ruzuku ambayo alikuwa anaipata, nafikiri hata juzi tulikuwa tunazungumza hapa na Mheshimiwa Jenista Mhagama kuhusu hata masuala ya watumishi na mambo mengi. Nalo hili tunaenda kulifikiria kwenye bajeti hii na wakati wa bajeti tutawajibu.
MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi kuuliza swali la nyongeza. Serikali ilianzisha ujenzi wa hosteli kwenye Chuo cha Uuguzi pale Tukuyu mwaka 2008. Ujenzi umekamilika, umefikia hatua ya kufanya finishing tu yaani kuweka madirisha na milango, wanafunzi 150 wanakaa nje ya chuo. Je, ni mpango gani wa Serikali kuhakikisha kwamba majengo yale yanakamilika na wanafunzi wale 150 wanaingia kukaa chuoni? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwantona kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo amesema Mheshimiwa Mbunge labda nimwambie tu kwa mwaka huu kwa ajili ya umaliziaji vyuo kama hivi ambavyo vimekaribia kufanyiwa finishing ili watoto waingie ndani, zimetengwa around bilioni 2.7 kumalizia vyuo ambavyo viko 17 vinavyotakiwa kumaliziwa nchi nzima. Kwa hiyo kitamaliziwa kabla ya mwezi wa 12 kila kitu kitakuwa kimekaa vizuri.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Jimbo la Lushoto wananchi pamoja na Serikali yao wamejenga vituo vya afya pamoja na zahanati, lakini kumekuwa na changamoto kubwa sana za nyumba za watumishi. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za watumishi katika Wilaya ya Lushoto?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shekilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo swali la msingi lilieleza kwamba kwa mwaka huu wa fedha zinaenda kujengwa nyumba 300. Naomba tukae na Mheshimiwa Mbunge tuangalie katika hizi 300 kama Lushoto eneo analolizungumzia limeguswa kama halijaguswa, tuone mapema tunaweza tukafanya nini ili hilo litekelezeke.
MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri katika Wizara hii. Niombe na kuishauri Serikali ifanye hivyo kwa Mikoa yote ya Tanzania nzima ukizingatia wanawake wenzetu na wao wanatakiwa wazae katika uzazi salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la nyongeza liko hivi, Mkoa wa Mara, ni kati ya Mikoa yenye changamoto yenye uhitaji huu wa vyumba vya kujifungulia wanawake wenzetu wenye uhitaji maalum.

Je, Serikali ina mpango gani wa kwenda kujenga vyumba hivyo katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara ukizingatia ni Mkoa special alikotoka muasisi wa Taifa hili Baba yetu Mwalimu Julius Nyerere?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza maelekezo ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan hasa alipokuwa anatusisitiza kuhusu eneo la kupunguza vifo vya akina Mama na Watoto mojawapo ni eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala siyo kujenga maeneo maalum kwa ajili ya wao kujifungulia, lakini ni suala la ndani ya ramani yenyewe na huduma yenyewe ambayo akina mama wengine wote wanapata huduma ndani humo kuhakikisha kwamba kuna usaidizi mazingira infrastructure inawasaidia wao kuweza kupata huduma hiyo. Lakini kunakuwepo na vifaa ambavyo vinaweza vikawasaidia wenzetu wenye mahitaji maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kwa niaba ya Waziri wa Afya kwa kushirikiana na wenzetu wa TAMISEMI kwamba sasa Waganga Wakuu wa Mikoa yote wanapokwenda kufanya usimamizi shirikishi eneo hilo liwe sehemu yao ya hadidu rejea ya kufuatilia kuhakikisha kila Wilaya, kuhakikisha kila Kituo cha Afya kila Zahanati wamezingatia hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zahanati zilizojengwa miaka ya 2000 vyumba vyake havikidhi hadhi ya kujifungulia kinamama kwa kuwa ni vidogo na vingine ni mfano wa corridor limewekwa pazia tu.

Je, Serikali haioni haja zahanati hizo za zamani kukajengwa wodi ya akina Mama ili kuendana na sera ya afya ya kinamama baada ya kujifungua wapumzike Saa 24? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ndiyo maana nimesema Serikali imeanza na imegundua tatizo hilo kwamba lipo na ndiyo maana kumekuwa na marekebisho yanayoendelea kwenye vituo mbalimbali. Nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika harakati za kupunguza vifo vya akina Mama na Watoto hayo anayoyasema yamezingatiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaona kuna fungu maalum kwa kushirikiana na wenzetu wa TAMISEMI, limekuwa likipelekwa kwa ajili ya kujenga hayo maeneo ya akina Mama kwa ajili ya kujifungulia.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Kwa kuwa, changamoto kubwa kabisa inayokabili watu wenye ulemavu wanapokwenda hospitali hasa ni mawasiliano kati ya Daktari na mgonjwa, kwa sababu ulemavu unatofautiana.

Je, nini mkakati wa kuhakikisha kwamba Madaktari wanaelewa lugha za watu wenye ulemavu, kwa sababu wengine wanaongea kwa ishara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme Mheshimiwa kwa kweli ameelezea suala siyo tu kusema ulemavu lakini ni wenzetu wenye mahitaji maalum kwa sababu kila mmoja ana mahitaji yake tofauti ukilinganisha na mwenzake. Na anasema mojawapo ya sehemu ni kwenye mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli kwa mfano kwenye hospitali ya Kanda ya Mkoa wa Mbeya tayari tumeanza process ya kuweka wale watu wanaoweza kutafsiri lugha kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum, tunaendelea sasa ku-roll out kuingia kila mahali. Lakini kwa kweli kuna shida kubwa hasa kupata watu wale wenye uwezo wa kufafanua lugha, kufafanua na mambo mengine hasa inapofika maeneo ya kitiba. Lakini Serikali inawekeza eneo hilo nguvu kuhakikisha hao watu wanapata huduma hiyo.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa sera ya Taifa ya Afya inatamka kuwa kila Kijiji kinastahili kuwa zahanati, kila Kata inastahili kuwa na kituo cha afya, na kila Wilaya inastahili kuwa na hospitali ya Wilaya.

Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha vijiji 22 vilivyopo katika Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, ambavyo havina zanahanti wala kituo cha afya vinafikiwa na huduma hii?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema na inakumbukwa kwenye Bunge hili yalishatoka maelekezo kwa maana kwa Halmashauri zetu kwamba watenge bajeti wao wenyewe kwa maana ya kujenga zahanati kulingana na mapato yao, lakini bado Serikali inafikiria namna ya kufanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelekezo yalishatoka kwamba utaenda utajenga kituo cha afya kwenye Kata lakini ukweli ukiangalia idadi ya watu eneo husika na mahitaji ya kituo cha afya kile kituo cha afya inakuwa kama kinatumika chini ya kiwango. Ndiyo maana tumekwenda kwenye kusema kila Tarafa ipate kituo cha afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachukua mawazo ya Mheshimiwa Mbunge hasa ulipozungumzia Longido kwa sababu ukizungumzia Longido ni karibia mara 2.5 ya Mkoa wa Kilimanjaro. Kwa hiyo, kwa kuangalia Longido specifically tunaweza tukakaa kwa pamoja na tuone ni namna gani tunaweza kufanya kwa approach hiyo ili tuweze ku-treat kila eneo kulingana na changamoto za eneo husika bila ku-generalize. (Makofi)
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya kuwatambua watoto ambao wamezaliwa na ulemavu katika hatua za awali kutokana na uelewa usiokuwa wakutosha kwa wale ambao wanazalisha yaani Manesi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza elimu hiyo kwa kasi hasa vijijini ili mtoto atambuliwe katika hatua za awali kabisa na kuweza kusaidiwa kwa mfano kwenye mtindio wa ubongo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anachokisema Mbunge, lakini nimuondoe wasiwasi, uelewa kwa manesi ni mkubwa, lakini kumekuwa kukitokea maeneo machache ambayo kweli watoto wanachelewa kutambuliwa hasa kwa mfano wa wenye autism na matatizo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri tutaendelea kuhakikisha elimu inakwenda na utaona sasa hivi kuna taasisi ambazo zinahamasaisha hayo maeneo ambayo kwa kweli yamekuwa na changamoto. Ukiona Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ametenganisha Wizara ya Afya na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, ni kwa sababu vile kuna masuala mengine ni ya kijamii na sasa kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii tutahakikisha kwenye eneo la jamii sasa hata wale ambao wanaoweza jamii ikashirikiana na sisi kuwatambua kwa sababu bado tuna tatizo vilevile, kuna watu wanaozalia majumbani na wakati mwingine wasifike kwenye vituo vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kushirikiana wote kwa pamoja ninahakika tutaweza kutatua hayo matatizo na Mbunge uwe mmojawapo wa balozi wetu kuhakikisha eneo hilo linafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali zetu nyingi katika Mkoa wa Arusha hususan zile zilizoko kwenye Wilaya za pembezoni zina uhaba mkubwa wa vifaa vya kujifungulia kinamama.

Je, Serikali ina mikakati gani ya kuhakikisha vifaa hivi vinapatikana na vinatolewa bure kwa akina mama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna maeneo yenye changamoto. Lakini Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kama ambavyo nimekwishaeleza hapa Bungeni hapo kabla ameshatoa Shilingi Bilioni 333.8 na kila mwezi imekuwa ikitoka Bilioni 15.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kumekuwa na shida kwenye eneo la manunuzi kuhakikisha kwamba zile fedha zinanunuliwa vitu na kuhakikisha zinafika eneo husika. Tutaenda kulitatua hilo na kuhakikisha tunatekeleza kama alivyosema. Kwa sababu sasa hivi tatizo siyo fedha, tatizo ni kasi ya kuhakikisha vifaa vinafika eneo husika. Ahsante sana.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza naipongeza Serikali kwa kutenga hiyo shilingi bilioni 2.04 kwa bajeti ijayo kujenga maeneo ya kusubiria wagonjwa, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza, changamoto ya watu kukosa sehemu za kusubiria wagonjwa inaikumba hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam za Temeke, Amana na Mwananyamala. Maeneo ambayo yametengwa ni madogo sana kiasi kwamba idadi ya watu ni wengi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kupanua maeneo ya watu kukaa wanaosubiria wagonjwa katika hospital hizo za Mkoa wa Dar es Salaam?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa changamoto ya watu kukosa sehemu za kusubiria wagonjwa inaikumba hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hali ambayo imesababisha taharuki, wananchi wanaokuwa kule ndani ni wengi lakini hawana sehemu maalum za kukaa, kusubiria kupata huduma na kusubiria kuona wagonjwa.

Je, Serikali inatoa kauli gani kwa wananchi wake ili waondokane na kadhia hiyo ya kufukuzwa hovyo hovyo na Askari Mgambo kule ndani ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa hospitali ya Mwananyamala na hospitali ya Temeke wametenga kwenye bajeti ya mwaka huu kabla ya Juni watakuwa wamejenga maeneo hayo, lakini hospitali ya Muhimbili hiyo kadhia inatokana na kazi hiyo anayoisema Mheshimiwa Mbunge kwamba wamefunga pale OPD wanafanya renovation kujenga vizuri, lakini kujenga hiyo sehemu ya kungojea na kuna maeneo mengine ambayo yamefungwa kazi hiyo anayoisema Mbunge ikifanyika, kwa hiyo ndani ya miezi mitatu hiyo kadhia itakuwa imeondoka. Ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mimi nishukuru kwamba Serikali imeona hii changamoto kwa sababu katika Mkoa wetu wa Iringa hili tatizo ni kubwa sana, hasa kwenye hospitali yetu ya Mkoa wa Iringa wananchi wanasubiria kwenye magereza, kwa sababu hakuna kabisa eneo lakini pia katika Wilaya ya Kilolo Mufindi hakuna maeneo ya kusubiria wagonjwa.

Mheshimiwa Spika, lakini mimi nilikuwa naomba labda niulize. Je, ni kwanini Serikali pengine iingie sasa ubia? Kwa sababu iko haja kuwepo hata na hosteli wale wanaosubiria wagonjwa wanalala nje kabisa kwa sababu ya matatizo ya sehemu za kusubiria wagonjwa wetu? Ahsante (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge, nimemuelewa. Anachokizungumzia ni kwamba Hospitali yao ya Mkoa wa Iringa iko kwenye eneo dogo na upande mwingine wapo Magereza, ambao kumekuwa na mjadala mkubwa. Kwamba wataka hospitali ile ihamishwe ipelekwe sehemu nyingine kwenye eneo ambalo ni kubwa.

Mheshimiwa Spika, lakini investment iliyofanyika kwenye eneo lile ni kubwa sana kiasi kwamba ukihamisha harakaharaka utadororesha huduma za tiba. Sasa nimuombe Mheshimiwa Mbunge wakati Mkuu wa Mkoa na Wizara tukijadiliana kabla maamuzi hayo hayajafanyika atupe Subira, kwa sababu kuna mambo ya muhimu kwanza yanafikiriwa kati ya TAMISEMI lakini pia na sisi Wizara ya Afya na masuala yote ya tiba ili tuweze kufanya huo uamuzi.
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Spika, pale Muhimbili miaka ya nyuma katika bustani (gardens) zinazozunguka na zingine zilizo ndani kulikuwa na street lights lakini vilevile kulikuwa na sehemu za kupumzika kwa wagonjwa; badala ya kukaa kwenye wodi muda wote huwa wanatoka kupata fresh air huduma zile hazipo.

Je, ni lini Serikali inatarajia kuzirudisha huduma zile?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, bado naendelea kuwasisitiza Waheshimiwa Wabunge, hizo sehemu zipo na sasa zinafanyiwa renovation ambayo ndio inayoleta shida ambazo wabunge wa Dar es Salaam wanaziona. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge avumilie kwa muda mfupi sana, renovation inayoendelea itakamilika, na hata hayo ya nje yatakuwa yameongezeka zile sehemu za kupumzikia.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali namba moja, upungufu wa damu unaotokana na kukosekana madini chuma unatajwa kuwa chanzo kikuu cha udumavu wa kimo na akili nchini, tatizo ambalo linapelekea Taifa kuwa na watu wasioweza kubuni na wasioweza kujifunza. Je, ni nini mkakati wa Serikali wa kutatua changamoto hii kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali langu la pili, tafiti zinaonesha kwamba asilimia 47 ya wanawake walio katika umri wa kubeba ujauzito wana tatizo la upungufu wa damu na asilimia 57 kwa wanawake wajazito mtawalia. Sasa ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba wasichana wanakuwa na damu sahihi ili kuandaliwa kuwa kinamama wenye afya imara na uwezo wa kuhimili kubeba ujauzito? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Engineer Ulenge, kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia afya ya watoto na mama na nimeona jinsi anavyoshirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Tanga katika kufuatilia mambo hayo katika Wilaya za Mkoa wa Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu maswali yake mawili ambayo kimsingi kwa kweli ni kama swali moja limetenganishwa. Ninachoweza kusema, kwanza Rais wetu Dokta Samia Suluhu Hassan alishazindua Mkakati wa Lishe wa Taifa na kama mnakumbuka aliwasainisha Wakuu wa Mikoa yote kwa ajili ya masuala ya lishe na lishe hiyo sio kwa ajili ya watoto ni kwa ajili ya kila mtu na ambayo kinamama ni sehemu ya wanaotakiwa kufanya hivyo. Maana yake tukizingatia taratibu za lishe hatutakutana na mambo kama haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kwamba wakinamama sasa ambao wamefika umri ambao ni wa kubeba mimba na ambao wanajitayarisha, tunafikiri Waheshimiwa Wabunge Mtusaidie kwamba suala la kubeba mimba lisiwe suala la dharura. Kama unataka kubeba mimba, basi unahitajika kujitayarisha na tunashauri waweze kuchukua folic acid. Tunawashauri watumie vidonge vya folic acid na mambo mengine, vitamin kimsingi ukijitayarisha namna hiyo ukibeba mimba hutakuna na upungufu wa damu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia amesema issue ya kimo, uzito na mambo mengine. Ni kweli kwamba suala hili linasababisha pia udumavu wa akili na inatuletea hasara kubwa kwa sababu lina uhusiano na maendeleo yetu, kwamba tusipozingatia haya tunaenda kuwa na kizazi ambacho hakiwezi ku - compete kwenye soko la ajira hakiwezi kuwa innovative na ndiyo maana unaweza kushangaa Tanzania tuna profesa mzuri wa uchumi anakuelezea kupata hela lakini yeye mwenyewe hana hela hayo ndiyo matatizo yanayotokana na mambo kama haya. Ahsante. (Makofi)
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa. Zaidi ya asilimia 25 ya kinamama ambao wamekwisha jifungua tayari wana upungufu mkubwa wa damu na hivyo kusababisha kuongezeka kwa idadi kubwa ya kinamama waliokwisha jifungua tayari.

Je, Serikali haioni haja sasa ya kuanzisha program maalum ya kuwafuatilia kinamama hawa na kuwasaidia ili kupunguza idadi ya vifo hivi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana naye kwamba wakinamama hawa wanapojifungua wanatakiwa kufatiliwa. Ndiyo maana utaona kinamama wakishajifungua kwanza anaenda kliniki akiwa mjamzito, afya yake inafuatiliwa mpaka anapojifungua lakini anakuwa anaenda kliniki na mtoto wakati wote. Kwa hiyo, tutaenda kuendelea kusisitiza kwamba wanapokuja sio tu kumwangalia mtoto na afya ya kinamama iendelee kufatilliwa lakini pia niwaombe hili ni suala la kijamii naendelea kusisitiza Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Kila mtu, suala la lishe na huduma ya mama na mtoto iwe ni ajenda yetu ya kudumu, ahsante sana.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ningeomba niweke wazi swali langu lililenga kichaa cha mbwa na kwa sababu kwangu Urambo watu 21 waliumwa na mbwa mwaka jana mwaka 2022 na kati ya hao 21 walioumwa na mbwa 12 walifariki ndio maana nikauliza swali hili. Je, Serikali ina mkakati gani wa kukabiliana na kichaa cha mbwa kwa kushirikiana na Wizara nyingine? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia, mtu anaeyeumwa na mbwa mwenye kichaa anatakiwa achomwe sindano tano, na sindano moja ni elfu 30,000. Sindano ya kwanza inabidi alipe 35,000 kwa ajili ya ile ada ya kujiandikisha, sasa wengi wanashindwa kulipa 155,000. Je, Serikali inasemaje kuhusu kupunguza gharama za matibabu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu katika hao wagonjwa wake 21, wengi kabisa amekuwa akija kwangu na akihangaika kuhakikisha wanapata tiba. Nimwambie Mheshimiwa Mbunge sisi na Wizara ya Mifugo tutaendelea kushirikiana kuhakikisha kwanza, sio tu uwepo wa tiba kwa ajili ya watakao kuwa wameumwa lakini mbwa wetu kuhakikisha wanakuwa wanachanjwa na nitumie fursa hii kuwaomba Wakuu wa Wilaya na Wilaya zetu ma DMO kuhakikisha wanashirikiana na wenzetu kuhakikisha mbwa walioko mtaani wanatafuta solutions lakini pia kuhakikisha wenye mbwa wanakwenda kuchanja mbwa wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini amezungumzia suala la gharama 155,000; Waheshimiwa Wabunge ndiyo maana kila wakati hapa tunakuja na Muswada Bima ya Afya kwa wote, leo hapa nilipokaa kwenye kiti change hapa, nina wabunge zaidi ya watatu mmoja anadaiwa milioni tisa mwingine anadaiwa milioni sita na mwingine milioni 4.8, anatakiwa kulipa na wagonjwa wa jimbo lake wameshindwa kulipa. Maana yake ninashukuru tumefanikiwa kuwasaidia Wabunge lakini tunaweza kuwasaidia wangapi? Ndiyo maana wakati wote tunasema na tusisitiza na nitumie fursa hii kuwaomba Wabunge wenzangu kama tunataka kuondokana na matatizo haya ni lazima wote kwa pamoja tukubaliane kwamba suala la bima ya afya kwa watu wote ni la msingi sana ili tuweze kuondokana na hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, nitumie fursa hii kuwaomba Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuwa mtu yeyote akiumwa na mbwa cha kwanza sisi tunachotaka ni kuokolewa kwa maisha, wasifikirie hela wamtibu mtu ndio suala la fedha lifuate. Waache tabia ya kuwanyima watu tiba eti kwa sababu hawana fedha. Pia MSD, niwaagize MSD kwamba kuanzia sasa hatutategemea kusikia hospitali yoyote mgonjwa amekwenda na hakuna dawa za kusaidia watu walioumwa na mbwa. Tunataka dawa zote za magonjwa ambayo sio magonjwa ambayo yanaoneka kila wakati ziwepo, lakini dawa za kichaa cha mbwa ziwepo kwenye kila hospitali na watu wakiumwa wapewa priority ya kutibiwa mapema, ahsante sana.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini nilitaka kujua ni mpango upi wa kupunguza kabisa gharama hasa za mama mjamzito anapojifungua kwa operesheni, ambapo Temeke tunalipa laki mbili kwa operesheni na Vituo vya Afya ni shilingi laki moja; je, mpango huo ukoje wa kupunguza kabisa gharama hii?

Swali la pili; je, kuna mkakakti gani wa kufanya ili sasa Serikali itoe vifaa vile ambavyo akina mama tunapokwenda kujifungua tunaambiwa tununue pamba viwembe vile na kadhalika.

Je, Serikali ina mpango mkakati gani sasa wa kuweka vile vifaa ndani ya hospitali zote ili tusiweze kununua. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza kwa jinsi ambavyo anafuatilia masuala haya kwa ukaribu kwenye Jimbo lake. Niseme tu kwamba suala ni la kisera kwamba mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano hawatakiwi kulipishwa. Ninaomba Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa tuweze kushirikiana pamoja kusimamia hili takwa la kisera.

Mheshimiwa Naibu Spika, Dar es salaam kwa kweli nilitembea kwenye baadhi ya vituo vya afya na hospitali za Wilaya nilichogundua ni kwamba, unaweza ukakuta Kituo cha Afya kinapata wagonjwa wengi kuliko hata baadhi ya hospitali za Wilaya. Kwa hiyo, wakati mwingine mgao wanaoupata MSD unakuwa mdogo kiasi kwamba wanaishiwa mapema kulingana na idadi ya watu, hata kwa mwaka ni zaidi ya 160,000 watoto wanazaliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, maana yake ni nini? Kwamba mgao wanaoupata MSD ni mdogo ukilinganisha na idadi ya watu, kwa hiyo tutakwenda sisi kama MSD kufanya kuhakikisha inatolewa mgao wa dawa na vifaa kulingana na idadi ya watu na siyo kuangalia kituo, aidha ni kituo cha afya au na ku-generalize.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tu mkakati ndiyo huo, kwamba tukiweza kwa Dar es Salaam ambapo unakuta kituo cha afya kinapata wagonjwa kuliko hata baadhi ya Hospitali za Wilaya sehemu nyingine, tukienda kuwapa vifaa kulingana na idadi ya wagonjwa badala ya kuangalia ni status gani hospitali inayo, maana yake hawatakuwa tena na huo upungufu na pale MSD zimenunuliwa kit za kutosha kwa ajili ya akina mama kujifungua. Hivyo hilo tatizo litaenda kuisha, nafikiri shida kwako ni idadi ya watu kwa hiyo kinachopelekwa kinakuwa kidogo sana. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mhesimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba niulize maswali madogo mawili. Kwa kuwa katika majibu ya msingi amesema matibabu ya wototo njiti hayatozwi, lakini kwa kuwa mpaka sasa huduma hizo zinatozwa;

Je, Serikali iko tayari kurejesha fedha ambazo wazazi waliojifungua watoto njiti walizitoa?

Kwa sababu ninayo madai ya mama anayedaiwa milioni moja na laki nane katika Hospitali ya Muhimbili.

Mhesimiwa Naibu Spika, kwa kuwa watoto njiti wamekuwa na changamoto mbali mbali za kiafya zinazowakosesha pengine kuendelea kuishi vema sawa sawa na watoto wengine;

Je, Serikali iko tayari kufanya mapitio ya likizo ya uzazi kwa wazazi wanaojifungua watoto njiti?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mhesimiwa Naibu Spika, nijibu maswali yake mawili kama ifuatavyo: -

Mhesimiwa Naibu Spika, moja; nitoe agizo kwa hospitali zote lakini vile vile mfuko wetu wa bima ya afya, kwamba suala la watoto njiti kama ni mama amejifungua na mtoto njiti au wakati wowote bima ya afya iweze kumuhudimia kama ni mwenye bima ya afya. Kuhusu kwamba wakizaliwa kwenye hospitali zetu zote watibiwe bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa Hokororo amesema je Serikali iko tayari kwa sababu ana ushahidi wa hospitali ambayo wanatoza. Ninakuomba Mheshimiwa Mbunge nikishakaa uje unionyeshe halafu tufuatilie nini kilichotokea. Siwezi kukuambia kwamba zitarudishwa lakini tutampata anayefanya hivyo na tuweze kumpa maelekezo mazuri, ili suala hilo lisijitokeze tena.

Mhesimiwa Naibu Spika, lakini la pili, suala la sheria ya likizo, hilo sasa ni la kisheria sio suala la Wizara ya Afya, lakini nimeshasikia kuna harakati hizo zinaendelea na kuna majadiliano ndani ya Serikali kuona hilo linafanyikaje. Tungojee hayo majadiliano ndani ya Serikali halafu yakifikia muafaka tunaweza tukajua ni nini kitakachofanyika. Kwa sababu hilo si suala la Wizara ya Afya pekee yake, hilo linahitaji masuala mengi kama vile utumishi, Wizara ya Katiba na mambo mengine.
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika Tanzania, ugonjwa huu wa fistula ni ugonjwa ambao unasumbua sana.

Je, ni hospitali ngapi au zipi zenye wataalamu wa kutibu ugonjwa wa fistula zilizoko nchini ukiondoa Hospitali ya CCBRT?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Ukiangalia sana ukizingatia haki za binadamu huu ugonjwa huwezi kumsafirisha mgonjwa kukiwa katika magari ya kawaida.

Je, Serikali imejipangaje kutoa usafiri maalum kwa ajili ya watu hao na namna ya kujikimu ili kutoka sehemu moja na kwenda nyingine ukizingatia waliowengi hali zao ni duni?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze kwa kufuatilia haya mambo ambayo kwa kweli yanawasumbua akina mama wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameuliza ni hospitali ngapi; hospitali zetu zote za mikoa, kanda na taifa zinatoa huduma hiyo. Kumekuwepo kila wakati sasa hivi madaktari kutoka Hospitali ya Muhimbili na hospitali zetu za kanda wakienda kwenye hospitali za mikoa yetu ili kuendelea kuongeza nguvu na ujuzi kwa hospitali zetu za mikoa ili huduma hii iweze kutolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali lake la pili; nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge; moja tuna mkakati kwamba magari yanapita kuhamasisha mtaani. Pia akipatikana mgonjwa yeyote huwa ambulance inamfuata na kupelekewa sehemu husika. Hata hivyo, ninajua kwamba kwenye eneo hilo bado hatujajiimarisha vizuri. Hivyo, tunachukua wazo lako ili tuweze kulifanyia karibu kwa kushirikiana na hospitali zetu za wilaya ili akina mama wale wakionekana waweze kupelekwa bila kupitia mabasi ya kawaida, waende kwa kutumia gari za Serikali.
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Tunajua ugonjwa huu unawasumbua akina mama wengi sana wakati wa kujifungua.

Je, Serikali haioni haja sasa ya kuongeza huduma za tija kwenye Hospitali za Mikoa ya Kusini?
NAIBI WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali inaongeza, na unapozungumzia kusini ndio maana kuna Hospitali ya Kanda ya Mtwara Kusini kule, ambayo kwa kweli inajengewa uwezo mkubwa kama hospitali zingine za kanda. Moja kutoa huduma lakini pia kujenga uwezo kwa hospitali za upande huu kwa chini ili waweze kutoa huduma hiyo. Pia kwa muda wa miaka hii miwili vimejengwa vituo 862; na kati ya hivyo 421 vimewekewa sehemu za kupasua akina mama ili kuwanusuru na hili jambo. Tutaendelea kufanya hivyo ili kuweza kuwanusuru akina mama. Kwa hiyo kuna mkakati wa nchi nzima si suala la Kusini peke yake.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kama ilivyo ugonjwa wa fistula pia maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado ni janga kwenye nchi yetu, lakini inaonekana kama Serikali imelegalega katika kutoa elimu. Mimi nataka kujua;

Je, ni nini mkakati wa Serikali kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya UKIMWI kwa wananchi wetu wa Tanzania?
NAIBI WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nadhani anachosema, Serikali haijalegalega lakini ni strategy tu zimebadilika kwa ku-approach kulingana na hatua ambazo tumefikia. Kwa sababu ukiangalia hali ya maambukizi sasa hivi imeshuka sana na hali ya maambukizi ni makubwa kwa makundi maaulum na nguvu zinaelekezwa kwenye makundi maalum kuhakikisha hali hiyo inadhibitiwa.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Licha ya majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili madogo. Swali la kwanza; licha ya mpango mzuri na unaoendelea wa upanuzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro lakini kuna mpango wa kujenga Hospitali ya kisasa ya Rufaa ya Mkoa wa Hospitali ya Morogoro.

Je, ni lini ujenzi huu utaanza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika Kituo cha Mafiga Manispaa ya Morogoro wanawake wengi wajawazito wanapenda sana kujifungulia kwenye kituo hicho lakini tatizo mojawapo linalojitokeza kituo hiko hakina jengo la upasuaji.

Je, kuna mpango gani wa kuweka jengo la upasuaji katika Kituo hicho cha Mafiga? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Mheshimiwa Mbunge nikupongeze. Unakumbuka ulikuja na ukaniambia na tulikwenda hospitali ya mkoa na uliona miundombinu na uwekezaji mkubwa ambao umefanyika kwenye hospitali yenu ya mkoa. Najua lengo lenu, pamoja na upanuzi unaozungumziwa kwenye eneo hili la hospitali mnahitaji kujenga hospitali nyingine eneo lingine. Mimi nikuombe, kama nilivyosema hapa, majadiliano yanayoendelea kati ya Wizara na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro tukiyamaliza basi tutakaa pamoja ili tuweze kwenda forward tukiwa pamoja. Kwa sababu sasa hivi nikikupa majibu inawezekana huo mchakato wa kimkoa wakawa na mawazo mengine tofauti na hayo ambayo wewe unayo. Kwa hiyo tutashirikiana kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili unazungumzia kwamba pale kwa akina mama hakuna jengo la upasuaji. Mheshimiwa Mbunge naomba nikimaliza hili swali tukae mimi na wewe tukae na TAMISEMI tuweke mkakati wa pamoja tuhakikishe hicho unachokisema kinaenda kutokea.
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Naomba nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali anayoiongoza kwa kutupatia fedha za kumalizia jengo la mtoto katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Hospitali ya Mawenzi. Tangu alipoitembelea Octoba 2021 fedha zimekuwa zikija na fedha za UVIKO zimekuja, na sasa jengo lile linamalizika. Sasa swali langu ni;

Je, ni lini Serikali itaanza mpango wa kuitengeneza master plan ya hospitali ile upya ili kuondoa yale majengo ya zamani na kuweka majengo mapya ya ghorofa yanayoendana na hospitali za kisasa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimwambie Mbunge Rais wetu Daktari Samia Suluhu Hassan alipotembelea pale Hospitali ya Mawenzi yeye aliomba mambo kadhaa na mambo hayo Rais wetu ameshatoa hela. Aliomba bilioni sita ya kumalizia jengo la mama na mtoto na tayari bilioni sita zimekwenda. Pia aliomba CT-Scan, tayari imekwenda, aliomba bilioni 1.3 kwa ajili ya emergency department imeshajengwa na bilioni 1.3 imekwenda, na jana zimekwenda bilioni moja kwa ajili ya kuendeleza kazi ambayo unasema kwamba kubomoa yale majengo ya zamani na kunyanyua mengine ambayo yatafanya ile hospitali iwe vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna moja tu ambalo tunaenda kutekeleza kabla ya Juni mwaka huu ambalo ulimwomba Mheshimiwa Rais; la ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha gesi tiba, hilo litaenda kutekelezwa kabla ya Juni na kazi itaenda pale vizuri sana. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie kazi uliyomwomba Rais inaendelea kufanyika na ahadi amezitekeleza takriban zote. (Makofi)
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoani Rukwa kwa sababu tayari uwanja ulishapatikana na ufundi sanifu ulishafanyiwa. Je, ni lini Serikali sasa itaanza ujenzi wa hospitali hiyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namwelewa anachosema na usanifu ni kweli umefanyika kama Mheshimiwa Mbunge anavyosema. Kwanza nimpongeze kwamba anafatilia masuala mazima ya afya ya hopsitali yao ya mkoa. Kwa mwaka huu zimetengwa bilioni 5.5 kwa ajili ya hospitali anayosema na usanifu anaouzungumzia unaenda kufanyika.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwanza nishukuru na niipongeze Serikali kwa jitihada inayofanyika kwa ajili ya kuendeleza hospitali hii.

Mheshimiwa Spika, hospitali hii ni tegemeo kubwa sana kwa watu wa Kanda ya Kusini ambao wanalazimika kutembea umbali wa kilometa 1,200 kwa mfano kutokea Mbamba Bay mpaka Dar es Salaam kufuata hizi huduma kutokana na pale kutokuwa na huduma kamilifu. Hospitali hii haina ambulance, haina gari ya Mkurugenzi, haina chumba cha kuhifadhia maiti, hospitali hii OC yake ni ndogo sana lakini ndiyo Hospitali ya Kanda.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka jicho la kipekee katika hospitali hii? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili; sambamba na hilo watumishi pia wako wachache, lakini tayari kumeshakuwa na msongamano na pia kupunguza msongamano ambao pia unaelekea katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Je, ni lini Serikali itaongeza idadi wa watumishi ili kuondoa hadha hii ambayo imeendelea huko? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kumpongeza Mbunge kwa namna ambavyo anafatilia masuala ya huduma kwenye kanda yake, lakini pia tumepokea barua yake kuhusu vifaa vinavyohitajika na Wilaya yake, pamoja na mambo mengine.

Mheshimiwa Spika, lakinio niseme kwamba moja kwanza ieleweke kwamba hospitali hii ya kanda ni hospitali ambayo sasa ndiyo inaenda kufikisha miaka miwili toka izinduliwe na Makamu wa Rais na kwa kibali cha mwaka huu tumepeleka kuomba kuajiri watumishi 111; lakini kwa sasa wako watumishi 166.

Mheshimiwa Spika, lakini pia amezungumzia suala la ambulance; kwa hospitali hii ya kwenu katika ambulance 727 ambazo Rais wetu ametoa fedha kwa ajili ya kununua ambulance iko kwa ajili ya hospitali hii ya kwenu.

Mheshimiwa Spika, lakini amezungumzia suala la mortuary na mengine; shilingi bilioni 4.4 ambazo ninazungumzia hapa tayari manunuzi yameanza kufanyika kwa ajili ya ujenzi wa mortuary, ujenzi wa nyumba za wanyafakazi, umaliziaji wa maabara lakini umaliziaji wa jengo la mama na mtoto.

Kwa hiyo, nataka nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hospitali hii itaenda kuwa ni nzuri na unajua we mwenyewe kwamba katika hospitali zote za kanda nchini hospitali hiyo ndiyo ina majengo mazuri kuliko hospitali yoyote, ahsante sana.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana; kwa kuwa Singida Mjini hatuna Hospitali ya Wilaya na kwakuwa Wizara ya Afya ilikuwa tayari kutukabidhi Hospitali ya Mkoa kwa maana ya yale majengo ya Mkoa ili tuanzishe Hospitali ya Wilaya. Sasa nataka kujua ni lini mtatukabidhi hayo majengo ya Mkoa tuweze kuanzisha Hospitali ya Wilaya? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli anaposema Mheshimiwa Mbunge Hospitali ya Mkoa iko sasa hivi kwenye eneo ambalo Hospitali ya Wilaya ndiyo inatakiwa iwepo na sasa kuna majengo mengine ambayo yanaendelea kujengwa kwenye eneo lingine. Lakini Mheshimiwa Mbunge ni kweli tuna majengo yanamaliziwa siyo muda mrefu ili Hospitali ya Mkoa iweze kuhama lakini nikuhakikishie tuna shida hiyo kule Geita, pale kwako tutahama polepole kwa sababu ukiama ghafla haraka haraka unaweza ukavuruga shughuli za tiba kwenye eneo lako, ili tusikuharibie siasa yako kabla ya mwaka 2025 tunamalizia majengo, tutahama polepole, lakini tutahakikisha kwamba hatutavuruga shughuli zako, cha msingi wape ushirikiano lile lile eneo na mshirikiane kwa pamoja kuweza kutoa huduma. (Makofi)
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwanza tunaishukuru sana Serikali kwa hatua iliyofikia katika hospitali yetu ya Kanda ya Kusini, lakini tumekuwa na changamoto kubwa sana ya Madaktari Bingwa. Je, ni lini sasa Serikali itatuletea Madaktari Bingwa katika hospitali yetu hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba hospitali ile inahitaji Madaktari Bingwa. Kuna Madaktari Bingwa, lakini Madaktari Bingwa kwa kiwango kinachohitajika kwa Hospitali ya Kanda bado hawajafikia hicho kiwango. Sasa upembuzi yakinifu unafanyika kuweza kuainisha maeneo mengine ili kuamisha na kupeleka kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Spika hivyo hata hivyo cha kwanza tulikuwa tunangojea kukamilisha baadhi ya miundombinu hapa karibuni ndiyo CT-scan imekwenda na MRI mashine, sasa hata ukiwahamisha wataalam wa kibingwa wanaweza wakapata vifaa vya kufanyia kazi ndiyo maana hawajaweza kupelekwa mapema katika eneo hilo.
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, natambua kwamba watoto ambao wanazidi miaka mitano na wengi wao ni wale ambao wana Selimundu wamekuwa wakitozwa fedha katika hospitali ikiwemo hospital za Serikali.

Swali la kwanza, je, kwa kuwa hadi sasa Serikali inagharamia dawa za magonjwa kama UKIMWI, kifua kikuu na ukoma; kwa nini Serikali isiingize kwenye bajeti matibabu ya Selimundu kwa wagonjwa wa Selimundu ambao ni wachache kwenye bajeti ijayo kuanzia mwezi Julai?

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa dawa zinazotibu Selimundu ikiwemo hii dawa inayoitwa hydroxyurea zimekuwa hazipatikani kwenye Wilaya nyingi ikiwemo Sikonge hali ambayo wagonjwa wanalazima kusafiri kwenda sehemu za mbali kama Mwanza au Dar es Salaam; kwa nini dawa hizi zisiletwe kwenye Wilaya ili zipatikane katika Wilaya kuondoa usumbufu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia hili suala kwa ukaribu, lakini swali lake la kwanza kwamba ni kwa nini tusitenge bajeti?

Mheshimiwa Spika, Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amefika mbali kwenye hili kwamba sasa kuna tiba ambayo inafanya gene editing kwa kutumia CRISPR-CAS9 technology ambayo ameshatafuta shilingi bilioni 11.5 kwa ajili ya kuanza, siyo tu kutibu kwa kupeleka dawa, lakini sasa kwenda kwenye genetic makeup ya mtu na kufanya diting ili kuweza kumtibu huyu mtu moja kwa moja na tiba hiyo siyo muda mrefu itaanza.

Mheshimiwa Spika, pia tutaona kwenye baadhi hospitali zetu za mikoa sasa zimeanza kutenga asilimia 10 ya bajeti yao mapato yao ya bima kuwasaidia watu hawa na ndiyo maana wakati wote tumekuwa tukiwasisitiza ninyi Wabunge tukikubaliana kwamba tutafika kwenye Bima ya Afya kwa Wote ni moja ya suluhisho hili la kutatua hili tatizo.

Hivyo Mheshimiwa Mbunge nakubaliana na wewe ni wazo zuri kutenga kwenye Bajeti.
MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, ninashukuru majibu ya Mheshimiwa Waziri ila nina swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa, wapo watalii wanaokuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta matibabu na tunao waganga wa jadi ambao wanaweza kutibu COVID kama vile Mheshimiwa Shekilindi. Swali langu ni kwamba Serikali ina mpango gani kwanza kuwawezesha waganga wa jadi kama hawa wenye ujuzi wa hali ya juu na kuwatangaza pia ili Pato la Taifa liongezeke? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nafikiri kama nimelisikia ni kwa namna gani tunaweza tukawasaidia waganga wa asili. Moja ni kwamba na kwa sababu kuna ushirikiano kweli na Wizara ya Maliasili kwa sababu baadhi ya vitu ambavyo vinatumika na watu wetu kama mizizi na vingine vipo kwenye maeneo ya maliasili.

Mheshimiwa Spika, kikubwa ni kwamba tunaanza kuiweka rasmi na kuna tafiti zinazofanyika kuthibitisha hivyo vitu ambavyo waganga wa asili lakini tunajenga ukaribu na Wizara ya Maliasili kwenda kwa pamoja ili tuweze kuwasaidia. (Makofi)
MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza, pamoja na kwamba huduma hizi za Wazee za kutibiwa bure zinatolewa kwenye hospitali zetu, lakini tunaona wazee wetu wanapofika kwenye hivi vituo wanakosa dawa za muhimu wakati mwingine wanapata usumbufu mkubwa kulingana na umri wao. Sasa Serikali inayo mkakati gani kuhakikisha kwamba endapo dawa zinakosekana wazee hawa wanafanyiwa utaratibu maalum wa kutafutiwa dawa hizo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lingine ni kwamba tunao utaratibu ambao umekuwa ukisemwa na Serikali wa Bima ya Afya kwa wote. Je, ni lini sasa Serikali inaenda kukamilisha utaratibu huu ili wananchi wote, wazee na wengine waweze kupata huduma hii muhimu kwenye hospitali zao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge. Moja ni kama wazee wakifika mahali, dawa haiko hospitalini ni utaratibu gani umewekwa kuhakikisha kwamba wanapata dawa bila kusumbuliwa.

Mheshimiwa Spika, kikubwa ni kwamba kuhakikisha hakuna dawa inayokosekana kwenye hospitali zetu hicho ndiyo cha kwanza. Lakini sasa hivi tunaelekeza maduka ya Bima ya Afya ambayo yako kwenye maeneo yetu ya hospitali ambayo yanaendeshwa kama private yaweze vilevile kutoa huduma hiyo kwa wazee bila kuwa-charge wakati mchakato wa bima ya afya unakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia suala la Bima ya Afya kwa watu wote kama alivyoelezea Waziri wa Afya hapa hivi karibuni kwamba tayari limeshafika kwenye Baraza la Mawaziri na michakato mingine ya Serikali.

Sasa Serikali imeshauri lirudi Bungeni lakini lirudi vilevile kwenye chama, kwa maana linatakiwa lije kwetu sisi Wabunge, likija kwetu Wabunge tuliangalie kwa makini yake kwa sababu kupitisha ni jambo moja, lakini je litakuwa na athari gani wakati wa utekelezaji. Hilo nalo tunaenda kulifanya na likirudi litaingia kwenye Kamati ya Huduma za Jamii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge ushauri wenu sana ni muhimu wakati wa utekelezaji wake na kuangalia mambo yote ili wakati wa utekelezaji Wabunge vilevile tusiweze kulaumiwa kule na wananchi. Kwa hiyo, likirudi ushauri wenu unategemewa zaidi ili tuweze kuikamilisha mara moja. (Makofi)
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu hayo ya Serikali lakini bado kuna changamoto kubwa sana ya wazee kupata huduma ya afya kwenye vituo vyetu vya afya, hususan hospitali zetu za rufaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niiombe Serikali kuna changamoto kubwa sana, umefika wakati wa kutoa tamko rasmi kabisa kwamba wazee hawa watibiwe bure na ikionekana kuna changamoto yoyote kwenye hiyo hospitali hatua zichukuliwe mapema.

Je, Serikali inatoa tamko gani sasa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Mheshimiwa Mbunge ameielezea vizuri na tunapokea ushauri wake, Waziri wa Afya kwa kushirikiana na Waziri wa TAMISEMI, watatoa maelekezo mahususi kwa maandishi kwa ajili ya hilo kutekelezwa kama inavyotakiwa. (Makofi)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Tatizo la huduma bure kwa wazee, akina Mama na Watoto limekuwa ni changamoto kubwa sana katika nchi yetu, na kwa kuwa wote tulioko hapa ni wazee watarajiwa leo, kesho, keshokutwa na mtondo go.

Je, Serikali haioni kuwa ni wakati muafaka wa kutoa waraka wa wazi kwa ajili ya jambo hili la huduma katika makundi niliyoyataja?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi tunapokea ushauri wa Mbunge na labda niseme tu kidogo kwamba, kwa mfano tunazungumzia tu wazee walioko kwenye mfumo ambao ni wastaafu 149,000 ukiwaangalia sasa hivi kwa mwaka tu wanatumia Bilioni 61 kwenye kupata huduma za afya ambayo ni asilimia 82 tu wao ndiyo wagonjwa. Kwa maana hiyo, ukizungumzia wazee wote kwenye nchi nzima nalo ni tatizo kubwa na nakubaliana naye kwamba inahitajika hela nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi kama ambavyo nimesema swali la kwanza la msingi tutashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI ili kuhakikisha kwamba hayo mambo yanafuatiliwa kwa ukaribu lakini tunawaomba wenzangu Wabunge na sisi tufatilie kwa karibu kuhusu wanavyohudumiwa wazee na mkiona kwamba hawahudumiwi tupaze sauti kwa pamoja, lakini sisi tutaelekeza sheria na kusimamia na kuwaadhibu ambao wanaacha kutekeleza maelekezo ya Serikali.(Makofi)
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wazee wa Mkoani Kagera walipewa vitambulisho ambavyo vinawaruhusu kwenda kupata matibabu bure. Lakini vitambulisho vile havitambuliki pale ambapo wanakwenda kwenye hospitali au vituo vya afya. Vilevile wakiandikiwa dawa, huwa wanaandikiwa dawa ambazo bado wanaambiwa hawawezi wakapewa pale hospitali au kituo cha afya, inabidi wakanunue nje.

Je, Serikali ina mpango gani kudhibiti hayo maeneo mawili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisikia ni Mzee mwenye kitambulisho chake, maana yake ni mzee ambaye tayari ameshatimiza vigezo vyote ambavyo vinatakiwa apate huduma. Kwa hiyo, kimsingi anatakiwa apate huduma. Lakini kuna hilo tatizo sasa kwamba anapewa huduma lakini anapofika dirisha la dawa, dawa inayohihitajika kupata haipatikani haipo kwenye dirisha la dawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mmesikia hapa nyuma tukiwa tunazungumza masuala ya MSD na upatikanaji wa madawa kwenye vituo vyetu. Nguvu nyingi sasa tunaelekeza kuhakikisha hakuna dawa inayokosekana kwenye vituo vyetu ili wazee wetu waliotimiza vigezo wakienda kwenye dirisha la dawa wapate dawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Jumamosi tulikuwa na Wabunge wenzetu wa Kamati ya Huduma za Jamii, kwa ajili ya Muswada wa Bima ya Afya kwa wote. Sasa tutaenda kutoa semina kwa Wabunge wote likija Bungeni basi tulisimamie hilo kwa sababu ndiyo litakuwa suluhu la kudumu. (Makofi)
MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa huduma hizi za Bima ya Afya upatikanaji wa dawa kwa upande wa Zanzibar zimekuwa za chini sana.

Je, ni lini Serikali itaenda kuboresha huduma hizo ili watu wapate dawa katika hali ambayo itakuwa ni ya kawaida?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe tu Mbunge, wakati wa sisi kupitisha Muswada wetu wa Bima ya Afya kwa watu wote, wote kwa pamoja tushirikiane kuweka input nzuri ambayo mwisho wa siku italeta suluhu ya kuduma bila tena kuona wazee wanarudi kule kule ambako hatukupenda warudi. (Makofi)
MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jawabu zuri la Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; Magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza kwa kweli yanaongezeka kila uchao. Kwa mfano, kuanzia mwaka 2016 kulikuwa na wagonjwa takribani milioni nne na kumi na nane elfu, lakini kufika mwaka 2020 kumekuwa na wagonjwa wasiopungua milioni nne na laki nane. Magonjwa haya yanagharimu Serikali kupitia Wizara ya Afya takribani asilimia 20 ya bajeti yake na vifo takribani asilimia 33 ya vifo vyote. Je, Mheshimiwa Waziri haoni kwamba, wakati sasa umefika magonjwa haya kuyaundia Tume Maalum ambayo itayashughulikia kama vile TACAIDS?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; miongoni mwa magonjwa haya yasiyoambukiza ni saratani ambayo nayo inaua watu wengi sana na pia inagharimu pesa nyingi sana kwa kuagiza dawa kutoka nje. Je, Waziri haoni wakati sasa umefika wa kuwa na kiwanda ambacho kitazalisha mionzi tiba?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumjibu swali lake la kwanza Mheshimiwa Mbunge anashauri kwamba tuanzishe tume kama ya TACAIDS kwa sababu magonjwa haya yanaonesha kila mwaka yanaongezeka na yanakuwa ni tatizo kubwa kwenye nchi yetu. Tutalifanyia upembuzi yakinifu wazo lake, lakini kikubwa ni kwamba ni sisi kuongeza nguvu zaidi kwenye kuelimishana hasa haya magonjwa yasiyoambukiza, namna life style na mambo mengine ili kupunguza idadi ya watu ambao wanapata matatizo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuongeza bajeti na kubwa zaidi kwenye eneo hili ili elimu iwafikie watu wengi lakini watu wengi zaidi wapate huduma bila bughudha yoyote. Maana yake ukianzisha taasisi wakati mwingine tunarudi kule kule, fedha nyingi zinaishia kwenye masuala ya utawala badala ya kumfikia mgonjwa husika. Kwa hiyo nafikiri ni kuongeza nguvu katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ambalo kimsingi linaonyesha ni namna gani Serikali ilivyo serious kwenye eneo hili, ni suala alilosema kwamba kiwanda cha kutengeneza mionzi dawa. Kiwanda cha kutengeneza mionzi dawa kama tulivyosema hapa kwa Afrika ni nchi nne tu zilikuwa na uwezo na kiwanda hicho na sasa Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ndani ya mwaka mmoja amewezesha na tayari hicho kiwanda kipo na mwezi wa sita kinaenda kuanza kazi rasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi na ukiangalia maana yake ni nini? Sisi kwa Afrika sasa Rais wetu ametufikisha mahali, katika nchi tano ambazo zina kiwanda cha kuzalisha mionzi dawa na sisi tuko. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge nafikiri eneo hilo linaenda vizuri na hatuna haja ya kutengeneza taasisi. Unajua watu wetu kwenye masuala ya utawala fedha nyingi badala ya kwenda kwa mgonjwa zinaweza zikaishia kwenye masuala ya utawala.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuweza kuuliza swali la nyongeza. Nataka kufahamu nini mkakati wa Serikali wa kupeleka dawa za magonjwa yasiyoambukiza katika ngazi ya zahanati?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali moja ilikuwa ni kupatikana vile vitu ambavyo huduma hiyo inaweza ikafanyika na mmeona sasa hivi kwamba karibia kila jimbo kila mahali kuna ujenzi unaoendelea kwa ujenzi wa vituo vya afya, zahanati na mambo mengine. Kikubwa sasa hivi na kwa ajira iliyopo sasa hivi utaona sasa hivi Madaktari wenye level ya digrii sasa hivi wameshafikishwa mpaka vituo vya afya na dawa hizo zinaenda kutolewa kwa ukaribu zaidi. Kwa hiyo Serikali ina mkakati kuwa, tunapomaliza hivi vituo wakati tunaweka vifaa, tunaweka madawa, lakini wataalam watapelekwa wenye uwezo wa kuwatibu watu wenye matatizo hayo.
MHE. FAHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa maradhi yasiyoambukiza kama sukari na presha, ushatumia dawa kwa muda mrefu au uliugua kwa muda mrefu, lakini kila ukienda kupima inaonekana normal kwa sababu unatumia dawa kwa wakati. Je, inaweza kupunguza dawa kutumia ili niepushe kupata maradhi mengine wakati tayari maradhi haya yako normal?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge ambalo ni lizuri. Nafikiri nisingetoa ushauri wa kijumla kwa sababu kila mtu anakuwa na hali halisi anapofika kwa Daktari. Nashauri jambo lolote unalotaka kufanya inapofikia mahali una shida ya presha au sukari, usiamue kijumlajumla, amua baada ya kufika kituo cha afya, kupewa vipimo na Daktari mwenyewe kwenye eneo hilo na kukushauri.
MHE. KABULA E. SHITOBELO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, je, sasa Serikali imeshafanya utafiti kujua ni watumishi wangapi watawapeleka, na je, kwenye hizi ajira mpya watapeleka watumishi wangapi kwa ujumla? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake specific kwa Mkoa wa Mwanza kwamba tutapeleka watumishi wangapi, labda tu nimwambie kwamba inajulikana kwamba kwenye level ya zahanati wanahitajika watumishi wangapi, kwenye level ya kituo cha afya inahitajika watumishi wa wangapi kwenye level ya hospitali ya wilaya wanahitajika watumishi wangapi mpaka tunapofika Taifa. Lakini kama kawaida kutokana na bajeti na uwezo wa Serikali imekuwa si rahisi kuhakikisha tunawapata wote kwa wakati mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Serikali ilitangaza juzi ajira 32,000 nimuombe Mheshimiwa Mbunge ili nisije nikamwambia data ambazo si sahihi tuje tukae tuangalie specifically Mkoa wa Mwanza kwenye ajira hizi wanapata watumishi wangapi kwenye eneo hilo.
STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kujua. Pamoja na maandalizi ya vifaa kwenye vituo vinavyojengwa, tunavyo takribani vituo vinne ambavyo vimeshakamilika; kule Igoma, Fumagila, Bulale pamoja na Nyegezi;

Ni lini sasa Serikali itakuwa tayari kupeleka vifaa kwenye vitu hivi ambavyo vipo tayari na kuanza kutoa huduma? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele sasa cha Wizara ya Afya na Waziri wa Afya ameshaelekeza wataalam wote, kwamba vituo vingi sasa vimeshakamilika na ujenzi wa kwa kiasi kikubwa sasa umeshafanyika.

Sasa kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha kuwa vituo ambavyo vipo tayari vinaanza kazi na kuhakikisha vina vifaa na watumishi. Kwa hiyo ndani ya mwaka huu kabla ya mwezi wa 10 vituo vyote vitakuwa vimepata vifaa tiba na vitakuwa vimeanza na wataalam watakuwa site. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itaanza kutupa mrejesho wa vifo vya uzazi vinavyotokana na uzembe ili tuweze kuwa na imani kwamba Serikali inafuatilia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kila kifo kinachotokea cha mama anayejifungua huwa kinajadiliwa. Sasa, anasema kwamba ni lini wataanza kutupa mrejesho; kwakweli ni kazi yetu pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwetu Mheshimiwa Waziri wa Afya ameshaelekeza, na kwamba tumegundua watu kama Red Cross wana mtandao mkubwa sana kutoka taifa mpaka tunafika kwenye vitongoji vyetu na ni mtandao wa kijamii. Tunafikiri kwamba tukiwashirikisha hao, tunataka sasa, kama ilivyo elimu, kwenye vituo vyetu vya afya na zahanati zetu kuwepo na ownership wa kijamii, kwamba kila tatizo linapotokea liwepo wanajamii wanajadili inajulikana kwenye jamii na information zinaenda vizuri kwenye jamii. Kwa namna hiyo tutaweza kupunguza vifo vya akina mama

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vile vile sisi wanaume tunahitaji kuwa na ownership ya ujauzito wa akina mama tangu mama anavyobeba mimba tuweze kushirikiana na mama mpaka siku anapojifungua. Tukifanya hivyo nayo itatusaidia vizuri sana kwasababu kila baba anapenda kujisifia mtoto wake ambaye anafaulu vizuri shuleni, lakini kufaulu kwa mtoto vizuri shuleni kunaendana vilevile na kuanza kutunza mimba toka siku mimba inavyobebwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo akinababa kama tunapenda watoto wafanya vizuri shuleni wawe brilliant kwenye maisha tuanze na mimba siku mama anapobeba ujauzito. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna hiyo suala la afya litakuwa sio suala la wataalam wa Afya peke yao, litakuwa suala la kijamii. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Takwimu zinaonesha Watanzania takribani milioni kumi na tano, sawasawa na asilimia 34.2 ni maskini kabisa.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuleta Muswada wa Bima ya Afya kwa kadri ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais ili akina mama wajawazito waweze kupata huduma ya afya na kupunguza vifo vyao?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jibu swali zuri la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba, kama mnavyojua Wabunge, tayari kwenye Kamati ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii tumewaelezea na tumewafafanulia hatua tulizozifikia kwenye suala zima la bima ya afya. Na nafikiri Bunge zima limeshaelekeza sisi Wabunge tuna uchaguzi. Kwa sababu ukiangalia mtu anaweza akasubiri akaacha kuweka luku kwenye nyumba yake umeme usiwepo na akasubiri kesho lakini akiugua haiwezi kusubiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anaweza akaamka akiwa na afya yake kufuata maji mbali zaidi, lakini afya hawezi hata iliyopo ndani ya nyumba yake hawezi.

Kwa hiyo ni uchaguzi wetu, tutakapoleta Mswada tuamue tunapata vyanzo gani ambavyo vitatusaidia kuweza kuweka kwenye mfuko wa afya; tupate bilioni 149.77 ambazo zitatusaidia na kuwasaidia wale Watanzania wasioweza kujilipia mfuko wa mima ili sasa tufikie hatua ya sisi kuanzisha bima ya afya kwa wote. Ahsante sana Wabunge. (Makofi)
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Kwanza ninasikitika sana kwa majibu ya Serikali ya jumla namna hii, kwa sababu mpaka naleta swali hili tayari nilikuwa nafahamu kwamba kuna mapungufu ya Wakufunzi pamoja na vifaa vya kufundishia. Wakati wanafunzi wakiwa 24 ndiyo fedha zilipelekwa, leo kuna wanafunzi zaidi ya 280 hakuna walimu, walimu ni hao unaowasema hawa 11 hao wakufunzi ndiyo waliyopo. Ninaomba nipate commitment ya Serikali, ni lini mtapeleka wakufunzi ili chuo hichi kiweze kufanya vizuri kama vilivyo vyuo vingine? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, hizi Maabara zinafanyiwa ukarabati lakini mpaka sasa hata vifaa vya kufundishia kwenye hizi Maabara bado hazijaenda Mheshimiwa Naibu Waziri. Hebu naomba mnipe majibu halisi watu wa Tabora wasikie, ni lini mtapeleka fedha ili vifaa vipelekwe na wanafunzi hawa waweze kupata mafunzo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kukipenda chuo chake. Pamoja na swali lake hili Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini aliandika barua, nimuombe sasa specifically mimi na yeye tukishamaliza hapa, tukishamaliza leo Bunge hili na tukamaliza bajeti yetu, tuende mimi pamoja na yeye akathibitishe hivi vyote ambavyo nimemwambia hapa.

Tutakwenda mimi na wewe, najua ulikwenda ukakuta hayo matatizo na hukurudi tena, baada ya wewe kuuliza hili swali Mheshimiwa Waziri wa Afya alielekeza na kazi imefanyika. Twende pamoja ili usimamie hizi fedha ambazo zimeshapelekwa uhakikishe zimefanya kazi ambayo wewe ulitegemea. (Makofi)
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana Serikali kwa majibu mazuri na mipango mizuri na mikakati mizuri kwa ajili ya Bima ya Afya kwa watu wote. Naomba niulize swali langu la nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tunafahamu kwamba watu wenye ulemavu ni watu ambao hawajiwezi wengine. Je, Serikali haioni haja sasa ya kuweka dirisha maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu kama vile kwa Wazee?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Kwa kuwa Bima ya Afya mara nyingine vipimo vingine havifanyiki. Je, Serikali haioni haja sasa kwamba vipimo vya Kansa ya Saratani ya Ngozi viweze kufanyika bure katika hizo Bima ambazo mnaziandaa kuja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, moja amesema kuwa na dirisha maalum kwa ajili ya watu wenye Ulemavu. Hili ni wazo zuri sana tunalichukua, vilevile pamoja na kuwa na dirisha lakini ni katika kila infrastructure ya hospitali kwenye wodi na kila mahali kuwepo na sehemu ambazo ni maalum zinazowezesha watu wenye ulemavu kuweza kupata huduma kirahisi kama wanavyopata watu wengine.

Meshimiwa Spika, nimeona vilevile amezungumzia na watu wenye ulemavu wa ngozi. Sasa hivi kwa mfano kwenye Hospitali ya Kanda ya KCMC wamepelekwa watu kutoka Hospitali mbalimbali za Mikoa. Moja kujifunza kwa ajili ya kuzalisha dawa maalum kwa ajili ya wale watu wenye ulemavu wa ngozi hasa ile screening ile ya kujipaka kwa ajili ya kuzia miale ya jua. Kwa hiyo, hayo yanaboreshwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni suala la kwamba kuna baadhi ya mahitaji ambayo ya kitiba ambayo wanahitaji baadhi ya Walemavu ambayo hayapo kwenye Mfuko wa Bima ya Afya. Mheshimiwa Mbunge kwa sababu tunaenda kuboresha kuja na Muswada wa Bima ya Afya kwa watu wote, ni wakati wa muafaka wa sisi kuhakikisha kwamba vitu vyote hivyo vimeingia kwenye utaratibu. Lakini wakati kabla hatujafikia hilo la Sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya, naomba mimi na wewe tukae unianishie hayo mambo maalum ili Mheshimiwa Waziri wa Afya aweze kuyafanyia kazi mapema, ahsante. (Makofi)
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Spika, ahsante, nakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa Serikali ilikuwa na mpango wa Bima za Afya kwa wote, je, ni hatua ipi imefikiwa ili kupata Bima hizo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, hatua zilizofikiwa. Kwanza zimefikiwa hatua zote za kitaalam, tuko kwenye hatua ambayo nafikiri uliona Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Waziri wa Afya alileta ushauri wake na akawaleza Wabunge hatua tuliyofikia ambavyo Wabunge mmetoa input muhimu na mmeturuhusu tuendelee na mchakato.

Kwa hiyo, hatua ambayo tunaendelea sasa ni zile hatua ambazo kwa kweli inatakiwa maoni yenu Wabunge nasi pamoja Serikali na Wabunge tuweze kulisukuma na Muswada huo uje mapema Bungeni. Kikubwa tunategemea mchango wenu mzuri ili mwisho wa siku tukishapitisha basi pasiwepo na kasoro ambazo tutaziona baadae.(Makofi)
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Sambamba na Bima kwa Walemavu umezuka ugonjwa kwa wanawake wanaojifungua watoto ambao wana mgongo wazi, hasa kule Mkoa wa Mbeya kwenye Hospitali ya Rufaa pale wanachaji fedha kuanzia 500,000 mpaka 1,000,000. Je, Serikali ina mpango gani kuwasaidia kuwapunguzia mzigo wa kulipa gharama hizo wanawake wanaojifungua watoto wa mgongo wazi? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa wa Waziri wa Afya alishaelekeza na ameshasema mara nyingi kwamba akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano wanatakiwa wapate huduma bure, hilo ni la kwanza. Lakini ninyi ni mashahidi Waheshimiwa Wabunge jinsi ambavyo Serikali imeendelea kuboresha infrastructure kwa miaka sasa mingi sasa hivi tunaenda ndani ya miezi miwili hakutakuwepo na hospitali ya Mkoa haina na CT scan na vile vifaa ambavyo vitatusaidia kufanya operation zile ambazo zinahitaji utaalam wa juu kama hizo. Kwa hiyo kikubwa ni kwamba tutaboresha hiyo, ili iwe inaenda sambamba na suala la watoto njiti. Kwa hiyo watoto njiti na hao wanaozaliwa na malformation mbalimbali imewekwa utaratibu na ma-specialist wanapelekwa kwenye maeneo kwa ajili ya kuhakikisha hilo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge mkikutana na matatizo specific kwa sababu binaadam ndiyo wale wale mnatuambia mimi na Waziri na hata information kutoka popote zinafanyiwa kazi kwa wakati wake. Ahsante. (Makofi)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushuru. Kuna utafiti ulifanywa na Jumuiya ya Viongozi wa Dini kuhusiana na mambo ya Bima ambao unaonyesha takribani Watanzania milioni 15 hawana uwezo wa kabisa wa kujikatia hii Bima ya Afya.

Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuweza kuwakatia hawa Watanzania Milioni 15 waweze kupata matibabu wakati huo wakisubiria Bima ya Afya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali zuri la Mbunge. Kwanza, moja kupanga ni kuchagua na tunaopitisha bajeti ni sisi, kwa hiyo kikubwa tayari Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu imejulikana kweli kwamba kuna asilimia 28 ya watu ambao hawawezi kujilipia, Rais wetu ameshakubali itengwe kila mwaka bilioni 149.77 kwa ajili ya kuwahudumia watu hao ambao unasema.

Mheshimiwa Spika, wakati tunapanga nikuambie tu ni rahisi sana kungojea wewe LUKU iingie kwenye nyumba ukaacha kuwa na giza lakini ukiugua haisubiri. Kikubwa tunachowaambia wakati wa kupanga na kuamua vipaumbele tukate kodi wapi hasa kwenye Bima ni wakati wa sisi Wabunge kuchagua tunaelekea upande gani.

Mheshimiwa Spika, ahsanteni sana. (Makofi)
MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimia Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi nyingine.

Mheshimiwa Spika, hospitali za Wilaya za Mkoa wa Ruvuma pamoja na vituo vyake vya afya vina changamoto kubwa ya magari ya kubebea wagonjwa, kutoka kwenye vituo vya afya kwenda kwenye hospitali za Wilaya au kwenda hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Serikali ina mpango gani wa kupeleka magari ya kubebea wagonjwa katika vituo hivi vya afya au hospitali zake za Wilaya Mkoa wa Ruvuma? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mhehsimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwamba anafuatilia vizuri sana masuala yanayoendelea kwenye Wilaya zao kwa kushirikiana na Wabunge.

Mheshimiwa Spika, unaona kwamba kuna magari ya kubebea wagonjwa zaidi ya 727 maana yake ni kwamba hakuna Wilaya ambayo itakosa gari. Tutashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI kuyatizama yale maeneo specific yenye uhitaji maalum ambayo yanahitaji kupewa magari zaidi ya moja na nadhani eneo lake la Mkoa wa Rukwa ni mojawapo ya hiyo mikoa Lindi, Mtwara, Kigoma na sehemu zingine ili tuone ni namna gani tunatatua hilo tatizo kwa wakati ambao tumeusema hapa.
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mahitaji ya watumishi wa afya nchi nzima ni 336,453; waliopo ni 114,582 sawa na asilimia 34 tu na pungufu ni 221,946 upungufu huu ni mkubwa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuajiri watumishi hawa ili kunusuru afya za Watanzania?

Swali la pili, Serikali haioni umuhimu wa kutengeneza database ili kutambua wahudumu wote wanaojitolea ili wakati wa ajira waweze kupewa kipaumbele? Ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Swali la pili: Serikali haioni umuhimu wa kutengeneza database ili kutambua wahudumu wote wanaojitolea ili wakati wa ajira waweze kupewa kipaumbele? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza ni upungufu. Ni kweli tuna upungufu kwenye Sekta ya Afya na unachangiwa na mambo mengi. Wakati mwingine katika Hospitali ya Wilaya tumeweka idadi ya watumishi, Hospitali ya Mkoa tumeweka idadi ya watumishi, na Hospitali ya Kanda hivyo hivyo. Pamoja na hivyo, utakuta kwa mfano Hospitali ya Mawenzi wana watumishi 400 lakini pale Mwananyamala hospitali, wanaona wagonjwa 500 kwa siku; ukienda pale Mnazi Mmoja Dar es Salaam ambayo ni ya Wilaya wana watumishi 170 wanaona wagonjwa 700 mpaka 800 kwa siku. Maana yake ni nini?

Mheshimiwa Spika, tukienda kwenye eneo la kuangalia ni watu wangapi hospitali husika inaona wagonjwa kwa siku na tukaweza kupeleka watumishi kulingana na mzigo ulioko kwenye eneo, hata huo upungufu anaousema Mheshimiwa Mbunge haupo.

Mheshimiwa Spika, tulikwenda Wilaya moja kule Shinyanga wakasema wana upungufu katika Hospitali ya Wilaya. Nilipowauliza, wakasema tuko 37. Ni kweli ukiwasikia Hospitali ya Wilaya wako 37, utasema kwamba ni wachache sana, lakini nikawauliza mnaona wagonjwa wangapi kwa siku? Wakaniambia tunaona wagonjwa 13. Unaweza ukaona kwamba kuna umuhimu wa kufikiria. Hilo moja, ni kwamba linatakiwa lifanyiwe kazi, kuangalia hali halisi na kupeleka watumishi kulingana na mzigo.

Mheshimiwa Spika, la pili, lile la kuweka database, ndicho nilichokisema hapa, tutashirikiana na wenzetu wa Utumishi kuona namna nzuri tutakayofanya na kuweka database kama alivyoshauri Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kuwatambua wakati wa ajira wapewe kipaumbele. Hilo ni wazo zuri sana, tunalichukua na tunakupongeza Mheshimiwa Mbunge.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, napenda kumshukuru sana Waziri kwa majibu yake mazuri. Nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Busega na Wilaya Itirima tuna hospitali nzuri sana za wilaya, tatizo ni moja majengo ni mazuri na yanapenda hatuna watumishi wa kutosha. Kwa hiyo hospitali zile hazina hadhi ya kuitwa hospitali ya wilaya kwa sababu watumishi hawatoshi;

Je ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha ili na wananchi wa kule wafaidike?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge jinsi anavyofuatilia masuala ya afya kwenye mkoa wake kwa kushirikiana na Wabunge wa majimbo. Kama ambavyo nimesema kwamba kwa mwaka huu tunategemea kupata watumishi takribani 12,000 hivi. Tutaendelea kushirikiana na wenzetu wa TAMISEMI ili tuweze kuona ni namna gani tunaweza kupeleka watumishi maeneo hayo ili wananchi waweze kupata huduma kulingana na ukubwa wa hospitali yenyewe.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ina changamoto kubwa sana ya watumishi kada ya elimu na afya;

Je, ni lini Serikali itapeleka watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ili kuondoa changamoto iliyopo hasa ukizingatia Ukerewe ni kisiwa ambacho kimejitenga na wananchi wake wanapata shida sana?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kuuliza swali zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si tu suala la watumishi kwenye Kisiwa cha Ukerewe, tumeamua kama Wizara ya Afya tuchukulie Ukerewe kama kanda maalum; na ndiyo maana Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe sasa inaenda kupewa hadhi kama hospitali ya mkoa. Maana yake ni kwamba sasa yenyewe haitaenda kupata watumishi na vilevile vifaa tiba na mambo mengine kama hospitali ya wilaya bali inaenda kupata kama hospitali ya mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunajua kwamba kuna visiwa mbalimbali; ukisema umemaliza kijiji kimoja kumbe kijiji hicho kina visiwa mbalimbali. Maana yake ni kwamba ukizungumzia zahanati hutaenda kufikiria Ukerewe ukasema kijiji ukadhani umemaliza. Tunatamani kila kisiwa kiwe na zahanati yake kwa ajili ya logistic zilizopo kule. Kwa hiyo tunachukua tutashirikiana na wewe Mbunge na Mbunge wa Jimbo tuhakikishe tumefikia azma yenu ambayo mnaitamani.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante, nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza, nashukuru kwa majibu yaliyotolewa.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Katika Hospitali yetu ya Mkoa wa Iringa imefungwa mashine ya CT-scan na inatoa huduma kwa wagonjwa wote isipokuwa wagonjwa wa bima ya afya kwa sababu NHIF wameshindwa kutoa kibali cha wagonjwa kupata huduma hizo. Swali langu ni kwa nini hawataki kutoa kibali?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; gari ya chanjo ya Manispaa ya Iringa ni ya mwaka 1998, imekwenda zaidi ya kilometa 380,000 na zaidi na hatuna gari, gari imechakaa kabisa. Ni lini tutapata gari hiyo ili wananchi waendelee kupata huduma za chanjo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kusema kwamba Rais wetu alipopokea nchi kwenye Tanzania nzima ni hospitali mbili tu za mikoa zilikuwa na CT-scan na kwa sasa hospitali zote za mikoa zimepelekewa CT-scan na zimebaki nne za ziada maana yake Rais wetu amefanya kazi kubwa mno. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tusingefurahi mtu yeyote awakoseshe Watanzania hiyo huduma ambayo Rais wao amepeleka. Kwa hiyo, niseme tu kwa niaba ya Waziri wa Afya nimuagize DG wa Bima kwamba mpaka kesho saa mbili watu wa Iringa ambao wanastahili kupata huduma na waliotimiza vigezo waanze kupata huduma.

Mheshimiwa Spika, swali lako la pili ni kwamba gari; tumezungumzia hapa tukasema zimenunuliwa Ambulance zaidi ya 727 maana yake hata Iringa itaenda kupata gari na tutaenda kuwekeza kwenye eneo hilo ambalo unasema ambalo ni muhimu sana la chanjo.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, ni lini bima ya afya watasajili vituo vipya vya afya kikiwemo cha Ng’uluhe, Ruaha Mbuyuni, Ilula pamoja na Nyalungu ili waweze kuanza kupata huduma watu kupitia mfuko wa bima ya afya?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge ninachoweza kukwambia ni kwamba ninakuomba tukae chini leta vituo vyako ambavyo havijasajiliwa tutizame vigezo, vikikidhi vigezo zianze kusajiliwa na huduma itolewe.
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, mwaka jana Bunge la Bajeti kama hili niliuliza swali kama hili hili na Mheshimiwa Naibu Waziri Dkt. Mollel mwenyewe aliniahidi mwaka jana kwamba ifikapo mwezi Novemba, mwaka jana wangekuwa wametuletea Madaktari Bingwa pale Kitete kwa sababu kuna upungufu wa Madaktari Bingwa wasiopungua 11.

Je, ahadi hiyo wale wananchi wa Tabora Mjini na especially kwa hiyo Hospitali yetu ya Kitete lini watapelekewa hao Madaktari Bingwa ambao niliahidiwa mwaka jana?

Swali la pili, hospitali ya Kitete ambayo ndiyo Hospitali yetu ya Rufaa ina upungufu mkubwa wa vifaa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa zikiwemo oxygen cylinders kwa wale wenye mahitaji maalum ya kupumua na vitu vinavyofanana na hilo.

Je, ni lini Serikali itatusaidia vifaa hivyo katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Kitete? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Mheshimiwa Mbunge aliuliza swali kama hili na Mheshimiwa Waziri wa Afya alielekeza kwamba wakati tunasomesha hawa, Madaktari wengine watafute sehemu zingine ili wapelekwe na ilishafanyika upembuzi yakinifu na wamepatikana Madaktari wa kusambazwa siyo tu Kitete ni maeneo mengi ya nchi ambayo kuna tatizo kama hili la Tabora.

Mheshimiwa Spika, sasa tupo kwenye stage ya kutafuta fedha kwa ajili ya uhamisho ili waweze kupelekwa kwenye maeneo yale, kwa kweli tumefikia karibia hatua za mwisho ili jambo hili liweze kutekelezwa ambalo ulitaka lifanyike.

Mheshimiwa Spika, swali lako la pili, kwanza ninakupongeza wewe na Wabunge wa Tabora kwa sababu mmepigana, lakini Rais wetu kwa mwaka huu kwa miaka yake hii miwili zimepelekwa Bilioni 13 kwenye hospitali yenu ya Mkoa. Maana yake unapozungumzia oxygen, kimejengwa kiwanda cha kuzalisha oxygen chenye thamani ya milioni 800 na sasa imeshawekwa miundombinu yote jengo limejengwa, kiwanda kimejengwa na imebaki tu filling pump ambayo mpaka tarehe 25 itakuwa imekamilika ili oxygen iweze kupatikana kwa ajili ya watu wetu wa Kitete.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Moja ya kisababishi kikubwa cha matumizi holela ya dawa za binadamu ni kukosekana kwa wafamasia kwenye vituo vya ngazi ya chini, kwa maana ya zahanati.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kusambaza wafamasia kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; matumizi ya dawa holela yanaambatana au yanaenda sambamba na utengenezaji na usambazaji wa dawa holela. Hivi karibuni tumeshuhudia TMDA wamekamata watu mbalimbali wakiwa wanafanya shughuli hizo.

Je, Serikali sasa ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba, mambo hayo yanasitishwa na hayatokei tena kwa afya ya binadamu, Mtanzania?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge. Kwanza nimpongeze kwa sababu, swali lake ni muhimu sana na limekuja kwa wakati muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza linasema ni kwa namna gani tunaweza tukahakikisha kwamba, vituo vyetu vya afya na zahanati kuna wafamasia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuwahakikishia kwamba, wafamasia, lakini tunaweza tukachukua wale waliosomea dawa, certificates na diploma. Tutashirikiana na wenzetu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ili kuona kila wakati ni namna gani tutapunguza hilo gape kwa kuajiri watu wa namna hiyo ili kuweza kusimamia dawa vizuri kule chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali lake la pili ni kuhusu kwamba, kunakuwepo na utengenezaji holela wa dawa, kwa maana unamaanisha dawa ambazo ni fake: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza moja inaeleweka kabisa kwamba, tunayo taasisi yetu ya TMDA na inafanya kazi nzuri ya kuhakikisha hayo mambo hayatokei. Kikubwa tunaendelea, tunapoelimisha yote haya, elimu hiyo kwa jamii kwamba, watoe taarifa, tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha tunadhibiti hawa wahalifu wanaofanya kazi hiyo, na kwamba wakipatikana wanapewa adhabu kubwa ambayo itawafanya wasirudie tena.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa zoezi la ukaguzi wa ubora wa dawa linafanyika katika vituo vya wauza dawa nchini, kitendo ambacho kinaleta hasara kubwa kwa wafanyabiashara hawa;

Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa ubora wa dawa katika hatua za mwanzo kwenye viwanda ili wafanyabiashara wasipate hasara?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, moja ni kwamba, kwenye kudhibiti suala la dawa na wafanyabiashara ya dawa wenzetu wakati mwingine wanaangalia kutengeneza faida kuliko usalama wetu sisi watumiaji. Kwa hiyo suala la wao kuendelea kusimamiwa kwa nguvu na kuhakikisha kwamba wanafuata taratibu ni lazima tuwasimamie namna hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tumekuwa na mjadala wa kuhakikisha sasa badala ya kuwepo na wafamasia kwenye maduka ya dawa ambao wanaweka vyeti vyao, tubadilishe hiyo sheria iwe sasa mfamasia anaajiriwa kwenye duka husika na anakuweko pale kuhakikisha usalama unakuweko, na hasa kazi ya ukaguzi inakuwepo kwa mambo ambayo hayaendani na utaratibu yanazuiliwa mapema.
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, kuna dawa ambazo zinanunuliwa bila cheti cha daktari, (over the counter medication) na kuna dawa zile ambazo ni lazima uwe na cheti cha daktari, ili uweze kununua, (prescription medication).

Je, Serikali inafanya jitihada gani na ina mikakati gani thabiti ya kuhakikisha kwamba, zile dawa ambazo zinahitaji cheti cha daktari hazinunuliwi over the counter? Yani, hazinunuliwi bila cheti cha daktari; na hasa kwa sababu, dawa za aina hii zinatumika na wale wenye uraibu wa dawa za kulevya?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Katimba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni mambo ambayo tunakuwa tunaelimisha. Katika elimu hii tunayoitoa ni kuhakikisha kwamba watu wetu hawafanyi hivyo. Ukimsikia Mbunge mwenzetu akisema kuna baadhi ya maduka ya dawa ambayo tumekuwa tunawafungia na wamekuwa wakipewa adhabu mbalimbali, ni kwa sababu ya makosa kama hayo na kuna utaratibu wa kusimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nataka kukuhakikishia tukienda sasahivi kuhakikisha kwamba maduka ambayo wafamasia waliopo wanaweka vyeti vyao badala ya kuweka cheti sasa wanaajiriwa wafamasia kwenye eneo husika, tutaondokana na matatizo kama hayo. Hii ni kwa sababu kwenye site atakuwepo mtaalamu wa dawa, atakuwepo na nesi ambaye ana utaalamu huo wa kuuza dawa na mambo mengine ambayo yatazuia hicho. Kwa sababu, hata kama ni duka la chini kabisa ni lazima anayeuza pale anajua dawa. Kwa hiyo, hayo matatizo yanadhibitika.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kutoa huduma ya afya bure kwa wafungwa, lakini kwa kuwa Waziri amekiri kwamba, suluhisho la matatizo yote ya afya ni kupitishwa kwa muswada wa bima ya afya;

Je, changamoto wanazokutananazo kwa sasa wafungwa juu ya huduma za afya, Serikali haioni haja ya kukaa na kupitia utaratibu ambao imeuweka kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge, lakini nianze kwa kusema kwanza ni wakati muafaka sisi Wabunge na sisi viongozi wote kujirudi na kutafakari kwa makini muswada wa bima ya afya kwa watu wote, moja hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa leo tu ukienda pale Mirembe wako wafungwa wa namna hiyo zaidi ya 270 na wanahudumiwa na wanapewa tiba bure na Serikali. Lakini pia, kweli kumekuwepo maeneo kama unavyosema Mheshimiwa Mbunge ambayo wakati mwingine akifika mfungwa anatakiwa kupewa huduma, anapewa zote bure, lakini kuna dawa inakosekana, saa nyingine ndugu anatafutwa kununua hiyo dawa iliyokosekana. Waziri wa Afya ameshatoa maelekezo kuhakikisha kwa kutumia watu wetu wa ustawi wa jamii mfungwa huyo anapitia kwenye utaratibu hata kwenye mapato ya ndani mfungwa huyo anatafutiwa dawa wakati tukishirikisna na Wizara ya Mambo ya Ndani kuona tunafanya nini, ili hilo tatizo lisiwepo.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Wakati tunasubiri Musawada wa Bima ya Afya kwa wote.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba, watu wenye ulemavu wanapata bima ya afya wasio na uwezo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kumuomba Mbunge mimi nayeye ili tusisubiri muswada wa bima ya afya, tuusukume kwa pamoja tuhakikishe unatokea. Lakini pia, ukweli ni kwamba kila hospitali yetu anakuwepo mtu wa ustawi wa jamii. Kazi yake ni kuhakikisha watu wa namna hiyo wanashughulikiwa na wanapata huduma. Hao walemavu hakuna ambaye hana uwezo ambaye amekosa huduma.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi.

Je, sasa Serikali ni lini itasaidia hospitali za Mikoa nazo kutoa huduma hii ya saratani, kwa sababu sasa hivi inatolewa katika Hospitali za Kanda tu na hospitali kubwa kama ile KCMC, Bugando na Ocean Road tu?

Swali la pili, kwa kuwa magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa ukiwemo ugonjwa wa kisukari, pressure pamoja na magonjwa mengine; Je Serikali sasa ina mkakati gani wa kutoa elimu ya kutosha hasa Wilayani ambako wagonjwa hawa ndiyo wanakotokea ili kuondoa rufaa nyingi kwa ajili ya hospitali kubwa kama Muhimbili?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ndiyo maana Serikali sasa hivi, Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha na amehakikisha hospital zote za Mikoa zina CT scan, maana yake sasa kwenye hospitali zetu za Mikoa wanaweza kucheki na kugundua mapema saratani kabla haijakua.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna mkakati mahsusi wa kuwasomesha Wataalam kwa ajili ya kuwapeleka ngazi za Mikoa na kuweza kutoa huduma hiyo. Kwa sasa tunapima lakini tunashirikiana kwa kutumia telemedicine ili kuwasiliana na hospitali zetu za Kanda na Mikoa.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kunipa fursa ya kuweza kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, saratani ya kizazi pamoja na saratani ya matiti imekuwa ni tatizo kubwa sana kwa wanawake. Je, nini mkakati wa Serikali wa kufanya utafiti wa kina ili kujua chanzo cha saratani hii ili iweze kuzuiwa badala ya kutibu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ndiyo maana umesikia kuna kampeni zinazoendelea kule shuleni na kwingine kuhakikisha kwamba watoto wanapata chanjo hasa watoto wadogo na wasichana, vilevile tunahamasisha sana kupima.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachukua ushauri wako na tutaendelea kufanya utafiti na kuona changamoto zinazosababisha mambo haya yaongezeke kila siku.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri. Vile vile nitoe masikitiko yangu makubwa sana kwa haya majibu aliyotoa, kwa sababu mchakato huu wa kuhamisha gereza ili hospitali iweze kufanya kazi vizuri siyo wa leo wala wa jana, ni wa muda mrefu sana; je, huu mchakato ni lini utakamilika? Kwa sababu haya majibu nimekuwa nikipatiwa muda mrefu, naomba leo anipe jibu, lakini siyo la mchakato tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Kwa niaba ya akina mama wa Mkoa wa Iringa naomba kumpongeza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama, Dkt. Mwakalebela. Kwa kweli anawatendea haki akina mama, na vifo vya watoto vimepungua; lakini tunayo changamoto ya muda mrefu sana kwa Daktari Bigwa wa Upasuaji wa Mifupa. Wananchi wa Iringa wanapata ajali nyingi sana, hata jana kuna ajali pale Kitonga imetokea; hili tatizo tumeshalileta muda mrefu Serikali, lakini hatupatiwi Daktari, wananchi wanapata shida kuja Dodoma au kwenda Dar es Salaam: Je, ni lini sasa huyu Daktari Bingwa wa Upasuaji atakuja katika Mkoa wetu wa Iringa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi anavyofuatilia huduma za afya, siyo tu kwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, lakini kwa Wilaya zake za Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza ni mchakato utaisha lini? Namwomba Mheshimiwa Mbunge, mimi na yeye twende pamoja Wizarani na tutamwonyesha mchakato ulipofikia na tutaendelea kwa pamoja tuumalize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizungumzia Hospitali ya Mkoa, siyo suala la majengo tu, ni suala la skills zilizopo pale na teknolojia iliyosimikwa kwenye hospitali. Kwa hiyo, ni kazi. Ukisema uchomoe hiyo teknolojia haraka ukahamisha, utavuruga huduma za afya kwenye mkoa. Kwa hiyo, ndiyo maana mambo mengi yanachelewa pamoja na mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusu Daktari Bingwa wa Mifupa, kama alivyosema Mheshimiwa Waziri wa Afya, Bunge liliopita, kwa hospitali yetu ya Iringa kwa mchakato unaoendelea sasa hivi ndani ya Wizara kuhamisha madaktari, Iringa wanahitaji kupelekewa Daktari wa Mifupa, Daktari wa ENT na Daktari wa Neurologist. Kwa hiyo, tumelipokea na litafanyiwa kazi mara moja. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Hospitali ya Manyamanyama inatoa huduma kwa wananchi wa zaidi ya Mkoa wa Mara pale Bunda Mjini, lakini wana changamoto ya nyumba ya watumishi wa afya. Ni lini sasa mtatupatia nyumba mbili ya watumishi wa afya katika Hospitali ya Manyamanyama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimwambie Mbunge hongera kwa swali lake zuri, nawakumbuka watu wake huko Bunda. Nimwambie tu kwamba kwa nafasi zilizotolewa zaidi ya 21,000 tutashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI tuone ni namna gani tunaweza tukatatua hilo tatizo mapema zaidi kwenye nafasi zilizotoka sasa.
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante. Namshukuru Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa sababu swali langu ni swali la kiutumishi, je, Serikali inafahamu tofauti ya kati ya Vyama vya Wafanyakazi ambavyo vinatetea maslahi ya Utumishi na Vyama vya Kitaaluma kwenye kada husika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; linakuja suala zima la uhuishwaji wa maslahi ya kiutumishi je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kuwa unashirikisha Vyama vya Wafanyakazi ambavyo vimesajiliwa kisheria kutimiza maslahi ya wafanyakazi ili kuepusha sintofahamu ambayo imetokea kwa uhuishwaji wa mwaka jana 2022 kutangazwa kwamba Daktari Bingwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge Alice siyo tu kwa kufuatilia masuala ya Watumishi na Madaktari Bingwa, lakini kwa kazi kubwa ambayo anaifanya kusaidia wenzetu wa Mkoa wa Pwani haswa kwenye maeneo ya afya na masuala ya akinamama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema katika swali lake la kwanza, je, tunafahamu tofauti ya vyama na vile vya kitaaluma. Ndiyo tunafahamu kuna Vyama vya Wafanyakazi lakini kuna vya Kitaluuma kama ambayo mimi na yeye tupo cha Madaktari cha Tanganyika tunafahamu tofauti ya hivyo viwili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile swali lake la pili kwamba je, wakati wa kuamua haya tunawashirikisha. Ndiyo maana imechelewa ni kwamba baada ya kutengeneza ile draft na kuona matatizo ambayo na wewe umeyaona hasa tunapofika kuna Madaktari super specialist ambao sasa kwenye muundo hawatambuliki, kuna watu walioongeza elimu kama manesi wengine wameongeza elimu lakini haifiki kwenye muundo, tulivyoyaona hayo tumemaliza sisi kama Wizara. Sasa tunataka tushirikishe hivyo vyama vyote, tukishashirikisha sasa, wakishakubali wote tunapeleka utumishi sasa kitu ambacho ni shirikishi na kimekubalika na pande zote.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Dar es Salaam imekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa siku hadi siku na idadi kubwa ya wagonjwa ambayo inaongezeka hapo ni akina mama wenye matatizo ya kansa ya kizazi: Je, Serikali haioni haja sasa kuwasaidia akina mama hawa kufungua vituo vya kansa katika hospitali za kanda na mikoa ili kupunguza gharama za usafiri kwa akina mama hao na mahitaji muhimu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Serikali imeonesha kwamba kuna huduma za awali za uchunguzi wa kansa katika hospitali mbalimbali: Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuziunganisha huduma za uchunguzi wa awali za kansa katika kliniki zetu za mama na mtoto ili mama apate huduma hiyo kabla na baada ya uzazi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya ya kufuatilia eneo hili la afya ya akina mama. Nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake la kwanza kwamba Serikali yetu imejipanga, ndiyo maana mmetusikia hapa tukisema Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kwa mwaka huu tu shilingi bilioni 290.9 kwa ajili ya kuleta vifaa tiba. Kwa hiyo, kwenye hospitali zetu za kanda na mikoa, vifaa vile vitasaidia kuchunguza, lakini kwenye kanda wanatibiwa kabisa. Kwa hiyo, hiyo huduma imepelekwa, kanda watatoa, mikoa watatoa. Tuliona juzi madaktari waliokuwepo hapa, kazi yao mojawapo ni kwenda kuhakikisha wanatambua mambo hayo.

Mheshimiwa Spika, kwenye maana ya kufika kule wilayani, labda nikwambie tu, tunalichukua, tunaliongezea nguvu lakini wenzetu waliokuja hapa pia mojawapo ya kazi yao ni kukutana na akina mama mpaka kwenye vituo vyetu na zahanati, wakiendelea kuhakikisha kwamba mojawapo ya jambo la kuzingatia ni kuangalia hiyo saratani ya kizazi, ahsante.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Kumekuwa na Waganga wa Jadi na wa Asili ambao wamekuwa wakibaini kwamba wao wanatibu kansa mbalimbali: Nini kauli ya Serikali kuhusiana na waganga hao ambao wamekuwa wakiwapa wagonjwa taarifa ambazo siyo sahihi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kauli yetu ni moja tu kwamba, yeyote atakayeibuka akiwa na jambo hilo, moja, tunatuma watu wetu wa Mkemia Mkuu, lakini taasisi ya tiba asili kuhakikisha na kukiangalia kile anachokisema kama ni kweli. Tunapogundua siyo tiba, tunamzuia kufanya hivyo na tunamtia moyo wa kuendelea kufanya utafiti na kufikiria namna ya kutatua kwa pamoja kwa kushirikiana na sisi. (Makofi)
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwa kuwa swali la msingi linauliza kuhusu ongezeko la kansa, mimi nilitaka kufahamu: Je, Serikali imefikia wapi katika kufanya tafiti kwenye mikoa ya kanda ya ziwa na suala zima la ongezeko kubwa la magonjwa ya kansa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, hatua tuliyoifikia tayari tumeshachukua sample kwa watu mbalimbali zaidi ya 700, na sasa ziko kwenye maabara kwa ajili ya kuchambua kwenye level ya genetics ili kuona hasa ni nini tatizo linalosababisha hali hiyo kule kanda ya ziwa.
MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.

Je, Serikali imejipangaje katika kupunguza gharama za huduma hii ya dialyisis, kwani kwa sasa ni shilingi 200,000 hadi shilingi 350,000 kwa mgonjwa anapoenda kuhudumiwa kwa mara moja?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kutokana na majibu ya Serikali, napenda kufahamu, ni utaratibu upi mgonjwa ambaye ana kipato kidogo afuate ili aweze kupata msamaha wa huduma hii ya usafishaji wa figo? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge, lakini niseme, moja ni kwamba kwenye bajeti hii ambayo tunaiwasilisha sasa, mpaka jana tulikuwa tunakaa kuangalia maeneo mawili. Waziri wetu ameangalia kwenye eneo la mama na mtoto na eneo hili, na tumegundua kuna uwezekano badala ya tiba hii kuwa shilingi 350,000, inawezekana kabisa mtu akatibiwa kwa shilingi 90,000 hadi shilingi 150,000. Kwa hiyo, tuna mpango huo wa kushusha gharama hizi.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni kwamba, mtu afuate utaratibu gani? Moja, akishakuwa na barua ya Mtendaji wake wa Kata, hiyo inatosha kumfanya aweze kupewa exemption, ndivyo utaratibu unavyosema.
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Je, ni lini Serikali itaanzisha huduma hii ya usafishaji figo katika Mkoa wetu wa Katavi?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwenye hospitali yao mpya ya Mkoa wa Katavi tayari vifaa vimenunuliwa, sasa hivi wako kwenye finishing ya aneo ambalo linatakiwa hivyo vifaa visimikwe halafu huduma hii itaanza mara moja kwenye mkoa wenu wa Katavi. Hata CT- Scan ambayo Rais wetu ameinunua imeshafika.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Bugando ni Hospitali ya Kanda, kutokuwa na watumishi wa kutosha kunaathiri utendaji kazi na hivyo kusababisha vifo vingi sana; na kwa kuwa Bugando inahudumia mikoa ya Kanda ya Kati, mikoa ya Kanda ya Magharibi na mikoa ya Kanda ya Ziwa: Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kulipa umuhimu suala hili ili kuweza kupata watumishi wa kutosha na kuweza kuondokana na tatizo lililopo la vifo vingi vya wananchi wetu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza tunapokea maombi yake, na tutaenda kuyachakata kwa sababu Hospitali ya Bugando kwa siku inapata wagonjwa 1,200 mpaka 1,500 na unaona idadi ya watumishi hapa ni 1,930. Sasa tutaenda kuchakata tuone tutakachoweza kufanya, lakini mwaka 2022 walipewa watumishi 367. Kwa hiyo, tutaendelea. Kwa kuimarisha Hospitali ya Kanda ya Chato na kuimarisha hospitali yetu ya mkoa iliyopo pale na hospitali za wilaya, foleni itapungua kwenye eneo la Bugando na itawezekana sasa kumaliza hili tatizo la watumishi na msongamano uliopo pale.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza. Bukoba Government Referral Hospital haijafikia hadhi ya kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera. Hata Mheshimiwa Waziri wa Afya alisimama hapa na yeye mwenyewe akakiri kwamba ile hospitali bado haijafikia ile hadhi, na mkatuahidi kwamba mtatuletea fedha kusudi tuweze kujenga hospitali nyingine au kukarabati ile ifikie hadhi hiyo: Je, ni lini Serikali italeta fedha za kutosha kuweza kutuhakikishia kwamba wanatujengea hospitali yenye hadhi ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mkoa wa Kagera uko mpakani na unapakana na nchi kadhaa. Kwa hiyo, yakitokea magonjwa ya mlipuko ni rahisi kuingia Mkoa wa Kagera kwa sababu magonjwa hayana mipaka. Kwa kuwa juzi juzi uliingia mgonjwa mbaya sana wa Marburg na mkaona Wizara na Mkoa walivyokuwa wanahangaika kutafuta mahali pa kuweka wale watu waliokuwa wamechangamana na wagonjwa, kwa sababu hakuna isolation centers ikabidi wawaweke mpaka kwenye mahoteli na hayo mahoteli yakafungwa yakawa hayatoi huduma kwa wakati huo: Je, ni lini sasa Serikali itaujengea Mkoa wa Kagera Isolation center? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufatiliaje wake makini wa masuala ya afya ya Mkoa wake wa Kagera. Pia nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea, hata mwaka huu inatarajia kupeleka zaidi ya shilingi bilioni nne kwa ajili ya kuendelea kuboresha hospitali yao ya Mkoa. Vile vile nimhakikishie kwamba hospitali ya Mkoa wa Kagera ni sawa na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, level yake ni moja, lakini tutaendelea kuwaongezea wataalam na vitu vingine ambavyo vimepungua kwenye hospitali yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, Mheshimiwa Mushashu anazungumzia suala la ugonjwa wa Marburg. Nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tumeshapata heka 90 ndani ya Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kujenga hiyo isolation center. Wakati huo tunapojenga isolation center tunahitaji tafakuri ya kina, kwa sababu ninyi Wabunge wa Mkoa wa Kagera mnajua kuna mwenzetu, Dkt. Mahona Ndulu wakati akihudumia wagonjwa wa Marburg alipata matatizo ya figo na moyo ambapo ilihitaji awepo kwenye sehemu ambazo hizo huduma zitakuwepo. Wakati tunatafakari hayo, tutaendelea kuona namna gani tutaitumia hiyo sehemu ya heka 90.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza Wabunge wa Mkoa wa Kagera kwa nia yao ya kwenda kumpongeza daktari huyo.
MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu hayo mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, kwa kuwa tathimini iliyofanywa na Wizara Novemba 2021 ilibaini kwamba jumla ya bilioni 83 za bidhaa za dawa pamoja na bidhaa za afya zilikuwa zimeibiwa.

Je, Serikali ilichukua hatua gani na imechukua hatua gani kwa hao watumishi ambao wamefanya ubadhilifu wa dawa hizo kwa ajili ya wananchi kwa ajili ya kutolea huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa, uwezo wa Bohari ya Dawa (MSD) kusambaza dawa pamoja na bidhaa nyingine za afya ni asilimia 59 tu. Hii inatokana na malimbikizo ya madeni ambayo ni zaidi ya bilioni 259, lakini pia mtaji wa bilioni 593. Je, Serikali inatoa tamko gani kumaliza matatizo haya, ili kuiwezesha taasisi yetu ya MSD kuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza dawa pamoja na bidhaa nyingine za afya kwa maslahi ya wananchi wetu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimshukuru Mbunge mwenzangu kwa swali lake zuri, lakini swali la kwanza ni kwamba, wamechukuliwa hatua gani wale walioonekana kufanya ubadhiriru wa bilioni 83. Moja, sisi kama wataalam wa Wizara ya Afya tulifanya kazi yetu na kuona kwamba, kuna dalili za upotevu wa bilioni 83.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi yetu iliyofuata ni kukabidhi kwenye taasisi yetu ya TAKUKURU ambayo ina wataalam wa kujua sasa ili kufuata sheria na taratibu na haki za watumishi wa umma, tumepeleka kule wanafanya uchunguzi. Miezi miwili iliyopita walituambia kwamba, wako kwenye hatua za mwisho sasa kuweza kubaini specifically ni nani kafanya nini na ni nini kimefanyika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua. Hilo ni swali lake la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni kweli kwamba, Waheshimiwa Wabunge fedha wanazopitisha hapa bilioni 200 kwa ajili ya vifaa tiba na dawa ni fedha za vituo vyetu kwenye majimbo yetu. Maana yake tukipitisha hapa kwenye bajeti tunapitisha pesa kwa ajili ya vituo vyetu. Vituo vyetu vikipata pesa zinapelekwa MSD, maana yake ni nini? MSD tulitegemea i- operate kama bohari ya dawa, lakini ina-operate kama procurement entity.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hilo la kwamba, wapewe mtaji, nafikiri liliibuka wakati wa bajeti yetu na Wizara ya Fedha wamelichukua na wiki iliyopita tulikutana kujadili kuona namna gani MSD wanaweza wakapatiwa mtaji, ili sasa tukiwapitishia fedha hapa Bungeni, basi vituo vyetu vikiomba dawa MSD wakutwe tayari walishanunua dawa hizo. Hilo ni suala la kulichukua tu ili kuondoa ucheleweshaji uliopo.
MHE. JEREMIAH M. AMSABI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya mwaka jana tulipata bahati ya kupita naye katika baadhi ya zahanati zetu Wilayani Serengeti alishuhudia upungufu mkubwa wa dawa na vifaa tiba. Sasa je, ni lini na kuna mpango gani wa kuhakikisha uwepo wa dawa na vifaa tiba vya kutosha katika zahanati ya Kemgesi, Maburi, Busawe, Nyansulula, Mbalibari, Koleli, Rubanda, Kituo cha Afya Nata na Zahanati ya Rigita? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tulikuwa naye pamoja Serengeti, tuliona hilo tatizo. Sasa namwagiza DMO wa Serengeti leo aandike mahitaji ya hiyo hospitali na wiki hii watapata dawa.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza nachukua nafasi kwa kuipongeza Serikali kwa kujengwa kwa hospitali za mMikoa;

Je, ni lini Hospitali hizo za Mikoa zitaanza huduma za dialysis?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali langu la pili. Kwa kuwa Serikali imekiri kwamba gharama za matibabu ziko juu;

Je, nini kauli ya Serikali juu ya kuwasaidia wale wananchi masikini ambao hawana uwezo wa kukidhi gharama hizo za matibabu?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge, kwa namna ambavyo anashirikiana na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Manyara kufutilia shughuli mbalimbali za afya katika mkoa huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza linahusu huduma kwenye hospitali zetu za mikoa. Kati ya bilioni 290.9 ambazo Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu amezileta zimetumika kununua vifaa kwa ajili ya dialysis kwa hospitali zote za mikoa. Na hata Mkoa wako wa Manyara vifaa tayari vimefika na nategemea mpaka sasa kazi hiyo imeanza na watu wanapata huduma pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili linahusu suala la gharama. Ni kweli ni gharama kubwa sana kwenye eneo la kutibu figo, na nilisema juzi hapa. Tunafikiri kwamba bei yake inaweza ikashuka kuanzia tisini hadi 150,000, hapo inawezekana kushusha. Lakini kuna utaratibu wa exemption kwa watu ambao wananshindwa kulipa. Kama yuko kule Manyara kwenye kata yake akiwa na barua ya mtendaji wake wa kata, akifika hospitali anastahili kutibiwa bure.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa matibabu ya ugonjwa wa figo nchini yakemkuwa na gharama kubwa sana na kwa kuwa bima ya afya kwa sasa haitoi huduma ya ugonjwa huu; je, ni utaratibu upi mbadala wa Serikali ili kusaidia kundi la wananchi wa ngazi za chini kwa sababu ugonjwa huu unawakabili rika mbalimbali nchini?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, labda nimwambie kaka yangu kwamba bima ya afya inatoa huduma hiyo, ndio maana katika presentation tuliyowasomea Wabunge, utaona eneo linalotumia fedha nyingi kwenye eneo la bima ni eneo hilo, lakini liawezekana Mbunge anamaanisha Bima ya Afya ya CHF ambayo ndio iko kwenye majimbo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ile bima ya afya ya CHF na tulitaka tuitafute namna ya kuiboresha iweze kuwapa wananchi manufaa mazuri zaidi. Kama ambavyo nimesema kwenye maswali ya nyongeza, kwamba utaratibu ni ule ule. Niendelee kusisitiza Waheshimiwa Wabunge wenzangu, tuendelee kuwa mabalozi wazuri wa bima ya afya kwa watu wote kwa sababu ndipo tutakapoweza kupata suluhisho la kudumu kwa matatizo haya.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafsi niulize swali dogo la nyongeza. Huu ugonjwa wa figo, ugonjwa ambao unatesa sana, kuanzia sasa hivi mpaka watoto wadogo sana; lakini gharama za matibabu ni kubwa sana. Wakati sasa hivi bima haijaanza kwa nini wasiondoe gharama kwa ugonjwa huu tu, Kwa sababu watu wengi wanakufa kwa sababu ya kukosa pesa ya matibabu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mlisikia juzi kwenye bajeti yetu kwamba Rais wetu ametoa bilioni tano kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiojiweza kwenye eneo hili la matatizo ya figo na mengine. Lakini bado tuna utaratibu mzuri sana kama nchi wa kuweza kuwapa exemption wale ambao hawajiwezi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nafikiri kikubwa ambacho naendelea kukuomba Mheshimiwa Mbunge uwe balozi mzuri wa bima ya afya kwa wote kwa sababu ni suluhisho la kudumu kwenye matatizo haya. Tuna magonjwa mengine hapa ni asilimia 15, hii ni asilimia saba, wanateseka sana watanzania. Kwa hiyo mimi ninachosema tuwe mabaloozi wazuiri wa bima ya afya kwa wote tutapata suluhisho la kudumu kwenye tatizo hili.
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa takwimu za Bohari ya Madawa, sasa hivi upatikanaji wa dawa ni asilimia zaidi ya 80, lakini ukienda kwenye uhalisia, hicho kitu ni tofauti kabisa. Kumekuwa na shida kubwa ya dawa sijui tatizo ni nini? Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili ni kwamba, sasa kumekuwa na tatizo sugu kabisa kwenye hospitali zetu nyingi; wagonjwa kila wanapokuwa wameandikiwa dawa nyingi huwa wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya watu binafsi: Je, Serikali ina mpango gani wakutatua tatizo hili la wagonjwa kila mala kuandikiwa kwenda kununua dawa katika maduka ya watu binafsi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza amesema kwenye takwimu za Bohari ya Dawa upatikanaji wa dawa ni asilimia 80, lakini ukienda kwenye uhalisia unakuta kuna jambo tofauti. Labda nimwambie Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kwamba ukiangalia kwenye hospitali zetu za Taifa mpaka hospitali zetu za mikoa, upatikanaji wa dawa ni asilimia 97, kwa sababu wanatumia dawa zinazotoka Bohari ya Dawa na pia wanatumia mapato ya ndani kununua dawa wenyewe. Kwa hiyo, asilimia yao ni kubwa kuliko hata ile ambayo ipo Bohari ya Dawa. Pia kwenye hospitali zetu za wilaya, ni kweli kwamba sasa upatikanaji wa dawa kwa sasa ni asilimia 68, maana yake kuna asilimia 32 ya watu ambao bado wanakosa dawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ni shahidi kwamba ukilinganisha mwaka jana 2022 na sasa kuna ongezeko la upatikanaji wa dawa. Kama ambavyo sasa MSD inaenda kupata mtaji kutoka Serikalini ili waweze kununua dawa mapema, sasa hilo tatizo litaisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Mheshimiwa Mbunge amesema kuna tatizo sugu la wananchi kukosa dawa na wanatakiwa kununua kwenye maduka ya watu binafsi. Hilo hilo linajibu, kwa sababu kama ndani ya hospitali zetu za wilaya na vituo vyetu kwenye hospitali za mikoa kwenda Taifa ni asilimia 97, maana yake kuna upungufu wa asilimia tatu. Ukija kwenye hospitali zetu za wilaya kushuka chini asilimia 32, kwa hiyo, ni lazima watanunua.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumwambia Mheshimiwa Mbunge, kwa mkakati ambao umewekwa hapa na Serikali kwa maana ya kutoa mtaji MSD, tutaenda kutatua hilo tatizo kama ambavyo anategemea litatuliwe. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Hospitali ya Rufaa Njombe, tunaishukuru Serikali kwanza kwa kuleta vifaa tiba na kuweza kuiboresha, lakini bado wananchi katika Mkoa wa Njombe wana matatizo makubwa sana ya uhitaji wa kusafishwa damu na bado inawabidi wasafiri: Ni lini Serikali italeta mashine ya kusaidia kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika Hospitari ya Rufaa ya Njombe?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimemsikiliza, kama vile anasema suala la upatikanaji wa damu, lakini nilichomwelewa anamaanisha kusafisha figo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeagiza hospitali zote za mikoa, na vifaa vipo kwa ajili ya kuweka majengo ya kusafisha damu. Kwa sababu hospitali yetu ni mpya, namwomba Mheshimiwa Mbunge tufanye mawasiliano tujue jengo kwa ajili ya kusafisha damu, kwa maana ya kutibu wagonjwa wa figo, lipo kwenye hatua gani ya ujenzi ili vifaa viweze kwenda kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Hospitali ya Selian imekuwa ni hospitali ambayo inatoa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa Arusha, lakini hospitali hii imekuwa inapitia changamoto nyingi: Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuisaidia hospitali hii ya Selian kama ambavyo imekuwa ikisaidia hospitali nyingine? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Hospitali ya Selian kwa maana ya ALMC inapitia katika changamoto ambapo tumeona wanafika mahali wanakaa mpaka miezi minne hawajalipa mishahara, na walishaleta maombi yao Serikalini kwa ajili ya kusaidiwa kwenye baadhi ya mambo ili waweze kujikwamua kwenye hali hiyo. Serikali imeshaunda timu, na timu imeenda kwenye hospitali hiyo, wamefanya uchunguzi ili kujua ni matatizo gani ambayo yanaikumba hospitali hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshayaona matatizo, kuna mengine tumewaambia warekebishe na watupe Subira kwani kuna mchakato unaendelea ndani ya Wizara zetu ili tujue tutafanya nini. (Makofi)
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa Halmashauri ya Msalala tumekamirisha ujenzi wa vituo vya afya viwili na zahanati 24: Nini mkakati wa dharura wa Serikali wa kuhakikisha kwamba wanapeleka vifaa tiba ili zahanati hizi na vituo vya afya vianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi na Mheshimiwa Mbunge, tumetembelea vituo hivyo na nimeona kweli kuna tatizo hilo. Namwomba Mheshimiwa Mbunge aje tukae pamoja, tumpigie DMO wake ili aweze kutuma list ya vifaa ambavyo tulikuwa tumeona havipo tupeleke MSD ili aweze kupata vifaa. (Makofi)
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Tatizo la madawa nchini linaweza kwisha iwapo tu Serikali itaamua kutoa fedha za mtaji ambazo Bohari Kuu ya Dawa Nchini (MSD) wameomba. Wameomba takribani shilingi bilioni 200.

Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, anaweza kutuhakikishia Wabunge kwamba Serikali ipo tayari kutoa hizo fedha za mtaji ili kumaliza tatizo la usambazaji wa dawa hapa nchini kwenye vituo vyetu vya afya na zahanati?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, hilo lilikuwa ni mjadala mkubwa sana hapa ndani ya Bunge wakati wa bajeti. Nawashukuru ninyi Wabunge kwamba mlilipitisha hilo na Serikali ipo tayari, ndiyo maana wakati wa bajeti, Waziri wa Afya na Waziri wa Fedha walikiri kwamba hilo litaenda kufanyiwa kazi.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Changamoto hii ya ukosefu wa dawa imetugharimu sana kwa wananchi: Je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuweka alama dawa za Serikali ili kudhibiti upotevu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kuweka alama limekuwa ni endelevu na dawa zote za MSD zimekuwa na alama. Ninachoweza kumwomba Mheshimiwa Mbunge, kwenye Baraza la Madiwani suala la dawa na vifaa tiba liwe ni ajenda ya kudumu. Pia nawaomba Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hilo liwe ni ajenda ya kudumu, kwa sababu ni ukweli kwamba upungufu mkubwa unasababishwa na matumizi mabaya ya fedha yanayopatikana baada ya kuuza huduma na dawa zenyewe, na pia baadhi ya dawa kuibiwa kwenye vituo vyetu.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi nami niulize swali dogo la nyongeza. Kumekuwa na changamoto katika maeneo mbalimbali nchini. Aidha, hospitali ina vifaa tiba vya kutosha, haina wataalam; au ina wataalam, haina vifaa tiba: Serikali haioni haja sasa yakupeleka hivyo vikaenda sambamba ili kutumia fedha hizi vizuri za walipa kodi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu anakubaliana kwamba kuna wakati watumishi wamekuwepo lakini kunakuwa nashida ya vifaa tiba na wakati mwengine kunakuwepo na vifaa tiba, lakini hakuna watumishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, na kama kuna hilo tatizo kwenye jimbo lake la hiyo irregularity, aniletee tuone jinsi ya kulitatua kwa pamoja.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Tumejenga vituo vya afya viwili vya Hydom na Eshkesh, havina vifaa tiba na mmetuletea madaktari: Je, lini mnapeleka vifaa tiba ili wananchi wapate huduma ya utabibu?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimeshasema hapa, Rais wetu ameshatoa kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa vituo vyote ambavyo vimeisha. Namwomba Mheshimiwa Mbunge, nikitoka hapa, tutakaa pamoja naye tujue ni vifaa gani vinahitajika ili tuweze kuweka utaratibu wa kuvipeleka kwenye eneo lake. (Makofi)
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ina uhaba mkubwa wa madaktari: Je, Serikali ina mpango gani kuongeza madaktari katika hospitali hii ambayo inahudumia zaidi ya mikoa mitatu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru nafikiri anachomaanisha Mheshimiwa Mbunge, ni upungufu wa madaktari bingwa. Ni kweli kwenye hospitali yetu ya Mount Meru na siyo Mount Meru peke yake, hospitali nyingi kuna upungufu wa madaktari bingwa. Ndiyo maana Rais wetu ametoa shilingi bilioni tisa kwa ajili ya kusomesha madaktari bingwa. Mmesikia Dkt. Samia Suluhu Hassan Scholarship ambayo inaendelea na tunaendelea namna hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mount Meru wana madaktari ambao wapo shuleni ambao pia wamesomeshwa kuanzia miaka miwili iliyopita, kwa maana hao wakimaliza shule, upungufu huo ambao upo Mount Meru utapungua.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Mkansila, tunashukuru Serikali ilituletea fedha na Kituo cha Afya cha Masamakati, wewe mwenyewe Mheshimiwa Naibu Waziri, ulituhamasisha pale tukajenga kwa nguvu za wananchi na fedha ya Halmashauri: Je, ni lini Serikali italeta fedha ya kumalizia vituo hivi vya afya viwili?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumekwenda na Mheshimiwa Mbunge, tukakuta wananchi wanaohitaji zahanati, tuliwaomba na tukawahamasisha pamoja na yeye ili waweze kuanza wakati Serikali inakuja nyuma. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hapa, kabla ya mwezi wa Tatu mwakani 2023, kazi hiyo itakuwa imeisha. (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kituo cha Afya Mkoga, kimejengwa kwa nguvu za wananchi na Mfuko wa Jimbo, tumefikia hatua ya boma: Je, Serikali inawezaje kutusaidia ili tumalizie kwa sababu tunahitaji sana huduma kwa eneo lile? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo Serikali imekuwa ikitoa fedha shilingi milioni hamsini hamsini kwa ajili ya kumalizia vituo kama hivyo, navyo tutaenda kuviangalia na tutahakikisha na kituo chake kinakuwepo kwenye orodha ya vituo ambavyo vitamaliziwa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni je, Serikali inatoa ushirikiano gani kwa vituo vya afya vinavyomilikiwa na sekta binafsi hususan Makanisa ili viweze kutoa huduma kwa wananchi wanaotegemea sana hivi vituo kwa bei nafuu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwepo na utaratibu wa Serikali kushirikiana na hivyo vituo kwa mikataba maalum. Kama Mheshimiwa Mbunge anakumbuka hata kwenye jimbo lake kuna kituo ambacho kuna ushirikiano kama huo, naomba kama kuna Kituo ambacho amekiona kinategemewa sana na wananchi na vituo vingine vipo mbali na anahitaji hilo, angeleta ili kupita kwenye mchakato ikionekana inafaa na ikikidhi vigezo, basi Serikali itatafakari la kufanya. (Makofi)
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Waziri, je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Buy Lava Off Taking Agreement unasainiwa ili kuiwezesha Wizara ya Afya kununua dawa zinazotengenezwa na kiwanda hiki ili kutokomeza malaria nchini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, ninataka kujua sasa ni lini kiwanda hiki kitalipa deni linalodaiwa na TANESCO ili waweze kurudishiwa umeme na kuhakikisha kazi ya uzalishaji wa dawa ya viuadudu inaendelea kwa kasi ile ile? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Afya pamoja na Waziri wa Viwanda wameunda taskforce ambayo inashungulikia kiwanda hiki kiweze kupata ithibati na hiyo mikataba kuweza kusainiwa. Wiki ijayo tunakutana kwa ajili ya kuona ni namna gani tunaweza kwenda mbele na tatizo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia swali lako la pili la suala la umeme nafikiri mojawapo ya ajenda kwenye hicho kikao itakuwa pamoja na hili suala la umeme tutalitatua kwa pamoja. Nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge hili suala litashughulikiwa na litapata suluhu muda si mrefu. (Makofi)
MHE. STELLA A. IKUPA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, ili kuendelea kutokemeza malaria nchini, pamoja na majibu mazuri yaliyotolewa hapa, Serikali inaonaje ikajielekeza pia kutuhamasisha sisi wananchi kufanya fumigation kwenye makazi yetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza swali lake hilo liko straight, kwanza nimuombe awe balozi wa kwanza na niwaombe Wabunge mliopo hapa mtusaidie kuhamasisha na tunalichukua kama alivyolisema, tunaenda kutekeleza. (Makofi)
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi, naomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri, je, Serikali ina mpango gani wa kutambua, kwa sababu hii teknolojia ya viuadudu ni teknolojia ya kuangamiza mbu. Mbu ni kiumbe aliyeumbwa na Mungu kuishi duniani.

Je, Serikali imefanya mkakati gani kwamba teknolojia hii ikitamalaki mbu wote watakuwa wamekwisha yaani hatutakuwa na mbu. Je, Serikali imeshafanya utafiti kutambua umuhimu wa mbu kuwepo duniani?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli anachosema Mheshimiwa Nyongo, anazungumzia kweli unapomuondoa kiumbe yoyote ndani ya ikolojia kuna madhara yake kwenye ikolojia. Kwa sababu sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakifanya hilo na wakatokomeza mbu wanaoeneza malaria na haijawahi kutokea tatizo kwenye ikolojia ambalo limeweza kuleta madhara ya kibinadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri aendelee kuiamini hii sayansi inayoenda kutumika kwa sababu moja, sisi tunaenda kumtegea mbu pale ambapo anazaliwa kwa maana ya kumuondoa pale ambapo anazaliana, lakini anapokosekana hapa ndiyo tunatumia alichosema dada yangu Mheshimiwa Ikupa kwa maana ya kunyunyuzia.

Mheshimiwa Naibu Spika, anaposhindikana eneo hilo tunatumia net, tunaenda kutumia hizo mbinu zote. Nataka kumhakikishia kwamba kitakachoenda, ndiyo maana tunataka ipate ithibati kupitia Shirika la Afya Duniani kwa maana ya WHO ili kuhakikisha hayo mambo yote unayoyasema ya ikolojia na mambo mengine yamezingatiwa, ahsante.
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, suala hili ni suala la muda mrefu kiwanda hiki kutonunuliwa dawa hizi. Serikali imekuwa ikiziomba halmashauri zetu ziweze kununua dawa hizi ili kutokomeza malaria kwenye Majimbo na Mikoa yetu ya Tanzania.

Je, ninyi kama Wizara mna mpango gani wa kutoa waraka maaalum ili angalau halmashauri zetu ziweze kununua hizi dawa na tuweze kutokomeza malaria nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa maana anaonekana kwamba anatamani hili litokee kwa nguvu. Kwa hiyo, tayari ni balozi wetu. Ninachosema ni juzi Waziri wa TAMISEMI alikuwa na Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote na Wakuu wa Mikoa. Mojawapo ya makubaliano ni kwamba wahakikishe wameweka fedha kwa ajili ya afua ya lishe, pia wahakikishe wameweka fedha kwa ajili ya kununua viuddudu wa kutokomeza malaria.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hilo linafanyika na la kuandika waraka tutaenda kushirikiana na wenzetu wa TAMISEMI tutaandika waraka maalumu kuhakikisha mambo haya yanatokomezwa.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nilikuwa kwenye swali hilo hilo. Mlihakikisha kwamba Halmashauri zetu zinanunua dawa kutoka kwenye hicho kiwanda, lakini naona NBS walipojenga hiki kiwanda ilikuwa ni makusudi maalum kabisa kwamba fedha hizi zirudi ndani ya shirika lile.

Je, sasa hamuoni ipo haja Serikali itoe mamlaka zaidi ili tuweze kununua dawa kutoka kwenye Manispaa zetu kutoka kwenye hiki kiwanda ili kiwanda hiki kiendelee kujiendesha kwa sababu sasa hivi naona kama kiwanda chenyewe hakipo tena? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, ukiona tumeomba shilingi bilioni 129.1 kwa maana tunaomba fedha maalumu kutoka Wizara ya Fedha, hiki ni kikao ambacho Waziri Mkuu mwenyewe amekisimamia na ameki-push ili haya mambo yatokee.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, alikaa mwenyewe kikao na kuelekeza tulifanye hili na pia kwa maana ya ushauri wenu pia uandikwe waraka kuhakikisha kwenye CCHP za halmashauri inawekwa bajeti kwa ajili hiyo. Tukifanya hayo yote tutaenda kufakinikiwa.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; kwa kuwa tafiti zinaonyesha magonjwa yasiyoambukizwa yanakua kila siku; je, Serikali haioni haja sasa ya kuanzisha mchakato wa kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia Magonjwa Yasiyoambukizwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tuna Hospitali ya Kilimatinde inayoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali na Kanisa la Anglikana, lakini hospitali hii haifanyi vizuri; je, nini mkakati wa Serikali wa kuiboresha hospitali hii iweze kusaidia katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza la kwamba magonjwa haya ya kuambukizwa yanaongezeka, ni kweli yanaongeza na hasa Kusini mwa Afrika yanaongezeka sana. Sasa hata ukiangalia leo kwenye UKIMWI, wewe ni shahidi tunatoka kwenye suala la kuuangalia UKIMWI peke yake kama UKIMWI, lakini tunaangalia magonjwa kwa ujumla na data zinaonyesha kwamba unapomchukua mgonjwa wa matatizo ya UKIMWI ukaangalia suala la pressure wakati huohuo sukari na ukatibu yote kwa pamoja, matokeo yanakuwa mazuri kuliko unapotibu ugonjwa mmoja na kumwangalia kama ugonjwa mmoja.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nafikiri pamoja pia na kuanzisha Taasisi kama alivyoshauri Mheshimiwa Mbunge ambayo itashughulikia hilo moja, tunaweza tukatumia fedha nyingi ambazo bora tu hizo fedha tungepeleka kuenga vituo vya afya kule kwenye jimbo lako.

Kwa hiyo, nafikiri Mheshimiwa Mbunge aendelee kukubaliana na Serikali kwa namna hii ambayo itatumia rasilimali vizuri, lakini wakati huo huo mgonjwa huyo akaangaliwa kwa ujumla wake, kwa sababu mgonjwa anapokuja huwezi tu kusema ni mgonjwa wa pressure au mgonjwa sukari unamwangalia kwa ujumla wake kuanzia saikolojia na mambo mengine ambayo yanafuatana na hilo. Kwa hiyo tukiyaangalia kwa pamoja namna hiyo tutapata matokeo mazuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la hospitali hiyo ambayo Serikali iko pamoja na Kanisa. Mheshimiwa Mbunge mwenyewe ni shahidi kwenye hii hospitali kwamba Serikali imepeleka watumishi, lakini vilevile Serikali inatoa dawa, pia wanapewa ile asilimia ya basket fund kwa maana ya kuboresha mambo yao. Sasa ninachofikiri kama Serikali imefanya yote hayo na bado Mheshimiwa Mbunge kama mwakilishi wa wananchi bado wananchi wake wanalalamika kwamba huduma inayotolewa bado ni ya chini maana yake inawezekana kuna suala sasa la kiutawala.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Mbunge, Manyoni Mashariki ni karibu hapa, saa nne zinatutosha mimi na yeye twende site, tukae kwa saa nne tuangalie mambo mengi ili tuweze kuhukumu kwa haki na kutoa maamuzi ya kuboresha hiyo hospitali kwa namna ambayo tutakuwa tuko site, ahsante.
MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa kuwa Serikali ina mapango wa kitaifa wa kupambana na haya magonjwa yasiyoambukizwa; je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha sasa tunashuka chini sasa kwenye ngazi ya Kata na Vijiji ambako kuna uhitaji mkubwa ili hawa wananchi waweze kufikiwa na huduma hizo? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, moja ya mkakati ni kuwa Serikali inaendelea kutoa hamasa kuhusu magonjwa haya na mmekuwa mkiona kwenye tv zetu. Pia kama ambavyo tumesema hapa Wizara ya Afya inatengeneza miongozo na mojawapo ya miongozo kwenye eneo la dawa, kwenye eneo la kutoa elimu na eneo la tiba. Kwa hiyo, tutaanza kushuka mpaka level ya zahanati na kwa mwaka huu tunaenda kusajili hawa watu wa afya jamii ambao watafanya hiyo kazi kwenye kufika kwenye vitongoji vyetu. Kwa hiyo ni wazo zuri na tunakwenda kutekeleza kwa nmna hiyo.
MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza maswali mawili ya ziada.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Swali langu la kwanza kwa kuwa Madaktari Bingwa 2,098 wako katika sekta ya umma na Madaktari Bingwa 371 wako katika sekta binafsi; je, Serikali inawapatia marupurupu gani Madaktari Bingwa hao ili kulinda ajira zao wasiende sekta binafsi au nje ya nchi? (Makofi)

Swali langu la pili; Je, Serikali ina mpango gani wa kuweza kutambua taaluma bobezi ambazo huwa zinasomewa kwa muda mrefu, waweze kutambua bobezi hizo na kuweka mishahara mikubwa ili kuhamasisha watu waweze kusomea ubobezi huo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mawili mazuri.

Moja kwanza mpaka sasa kama ambavyo umeona hapa asilimia 75 ya Madaktari wako Serikalini na mpaka sasa Madaktari wengi na watumishi wengi wanapenda zaidi kufanyia kazi Serikalini, maana yake ni kwamba Serikalini kuna uhakika zaidi na incentive nyingi zaidi kuliko kwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kama unavyojua kwamba Serikali inatoa incentive, mmemsikia Waziri wa Afya akisema kwamba tunatakiwa Madaktari wetu wamekuwa wakikimbia kwenye private sector wakati wa jioni wamekuwa wanafanya kazi, kwa hiyo sasa wameruhusiwa ndani ya hospitali zetu za umma wafanye private clinic humo humo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niweke vizuri pamoja na hayo yote ambayo Serikali inafanya bado tunafikiri tunahitaji wawe umma lakini pia wawe private sector, kwa hiyo pande zote mbili Madaktari wetu tungefurahi wakafanya kazi sehemu zote, wawe private sector wengine wawe public sector. Tungefurahi wafanye kote kwa sababu kote wanamhudumia Mtanzania yuleyule.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ni Je, Serikali inafanya nini kwa wale wanaosoma muda mrefu. Mheshimiwa Waziri wa Afya alipeleka hilo tatizo kwa Mheshimiwa Rais wetu. Mheshimiwa Rais wetu na ameshatoa maelekezo tukae na utumishi ili kujadili kuona Madaktari ambao wanasoma muda mrefu ni kwa namna gani utumishi wakaweka incentive au kuongeza mshahara kulingana na ule muda wanaosoma ili wengi wavutiwe kusoma masomo hayo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais wetu ameshatoa maelekeo ya kutatua tatizo hilo. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu gani unafanyika kuwapeleka Madaktari Bingwa kama wakiwa wamehamishwa, kwa sababu Mkoa wetu wa Iringa sasa ni karibu mwaka wa tatu Daktari Bingwa wa Mifupa amehamishwa na hatujampata na kuna ajali nyingi sana. Je, ni lini sasa tutampata katika hospitali ya Mkoa wa Iringa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nalichikua tatizo lake kama alivyolisema kuona tunalishughulikiaje, lakini jana Mheshimiwa Waziri wa Afya ameelekeza Idara ya Utumishi wakishirikiana na Idara yetu ta IT na kuwasiliana na Utumishi ili tuwe tunaweza kuona kwenye mfumo jinsi ambavyo watumishi wa afya wamegawanyika maeneo mbalimbali na hiyo itaturahisishia kuona ni namna gani, maeneo gani ambayo yana upungufu, ni maeneo gani wamezidi watumishi kwa namna hiyo tutakuwa tunapanga kwa kujua vizuri wamezidi wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nakubaliana na wewe kwamba Madaktari Bingwa wengi wako Dar es Salaam, wako kwenye Miji mikubwa na Waziri ameshatoa maelekezo kuona namna gani iyo Mikoa ya mbali wanapelekwa hao Madaktari Bingwa. (Makofi)
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza swali moja dogo la nyongeza lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itafanya mapitio upya ya Sheria Na. 263 ya Mwaka 2015 ili kuongeza fidia na pensheni kwa watumishi hao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, tatizo hili ni kubwa ambalo linapelekea kwamba Madaktari na Manesi pindi inapotokea magonjwa ya mlipuko wanakosa ari na moyo wa kufanya kazi kutokana na fidia ndogo ambayo wanaipata. Je, Serikali imefanya utafiti wa kina juu ya tatizo kubwa namna hii? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake amabalo kwa kweli linalenga kuboresha huduma lakini kuwatia ari watumishi wa afya. Kwanza, ameuliza kwamba ni lini Serikali itakaa na kujadili ni namna gani tunaweza kuboresha hili. Hili suala linahitaji siyo Wizara ya Afya peke yake linahitaji Wizara mbalimbali za sekta husika kulingana na tatizo lilivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi niwaombe Wabunge kwa sababu mmelisema hili hapa, basi tutaenda kufanya mawasiliano na kukaa na wenzetu na Serikali ikitokea mjadala ndani ya Serikali ikionekana kuna uhitaji huo basi italetwa hapa Bungeni kwa ajili ya kubadilisha, lakini turuhusu kwanza likatazamwe na wataalam ili tuone linaweza kufanywajwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili kwamba watumishi wengi wanaogopa kufanya kazi kwenye maeneo yao, kwa sababu wanaogopa kupata matatizo. Mimi nikwambie tu kwanza nitumie fursa hii kuwapongeza watumishi wa afya Tanzania, tulipata tatizo Kagera watumishi wetu hawakutazama kuna hatari gani wakati watu wengine wanakimbia kwenye majanga wao walikimbilia kwenye eneo la tatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania Waziri wetu wa Afya alikwenda Marekani juzi kwenye Umoja wa Mataifa walimpongeza kwa kushangaa ni kwa namna gani ndani ya siku 78 Tanzania imeweza ku-control Marburg. Maana yake hizi ni juhudi za watumishi wetu hawa ambao wana moyo, wana nia njema ya kuwahudumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, mnajua wakati wa corona kila mtu alikuwa anakimbia, kila mtu anaogopa kwenda hospitalini lakini watumishi wetu walikimbia na wakafanya na umeona kilichotokea Tanzania na vifo vingi havikuwepo Tanzania kama maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hawa watumishi kwa kweli pamoja na mazingira mengine na matatizo mengine, wanafanya kazi nzuri sana na wana moyo mzuri. Kwa hiyo, nikuambie tu hawaogopi lakini kwa ukweli halisi hebu tukayaangalie haya mengine ambayo umeyasema hapa yaonekane kama kuna sababu ya kufanya hivyo tuende nayo na kuboresha zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais wetu amekuwa akimuelekeza Waziri wetu. Kwa mfano, kuna kijana aliyepata shida kule Kagera na Mheshimiwa Rais wetu alielekeza na yule kijana alipewa zaidi ya Shilingi Milioni Kumi, kama incentive tu kupitia masemo wa Mheshimiwa Rais wetu na sasa hivi amaepewa shilingi 10,000,000 yake na anaendelea na shughuli zingine za Kisheria na haki zake za Kisheria bado anaendelea kuzipata. Kwa hiyo, tutaendelea kuwatia moyo kwa namna hiyo, lakini nikuambie tu kwamba Watumishi wana ari sana. (Makofi)

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama kwanza kumshuruku Mheshimiwa Naibu Waziri kwa maelezo mazuri, pia nimesimama kumshukuru Mheshimiwa Jacqueline Msongozi kwa swali lake. Nimesimama kwa sababu kipaumbele cha kwanza cha Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupambana na magonjwa hatarishi na magonjwa ya mlipuko ni kuwalinda watumishi wa afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatufanyi kitu chochote. Kwanza tunatoa training kwa watumishi wa afya jinsi gani ya kuhudumia wagonjwa wa magonjwa ya mlipuko. Pili, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anatuwezesha kutoa vifaa kinga vya kutosha kwa ajili ya watumishi wa afya, lakini pale kutakapotokea changamoto amesema vizuri Naibu Waziri Serikali inafanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya mtumishi wa afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana Kagera tulikuwa na mtumishi Daktari mmoja alipata maambukizi ya Marburg kwa sababu ya kumhudumia mgonjwa, tulipeleka dialysis mashine Kagera, tumepeleka Madaktari Bingwa Saba na Wauguzi Bingwa na leo Daktari yule tumeweza kuokoa maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimesimama kwanza kuwashukuru watumishi wa afya. Watumishi wetu wa afya siyo waoga, hawajawahi kukimbia wagonjwa. Pili, nimesimama kuwahakikishia Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia itatoa kipaumbele cha kuwalinda watumishi wa afya katika kupambana na magonjwa ya mlipuko na magonjwa hatarishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama ili kuweza kuwatia moyo watumishi wa afya, hatujawahi kuona Watumishi wa Afya wamekimbia wagonjwa Tanzania.
MHE. ABDUL-HAFAR IDRISSA JUMA: Mheshimiwa Spika nashukuru, nina swali moja la nyongeza.

Je, Serikali imeshapeleka elimu kwa Wakuu wa Shule na Kamati za Shule hasa shule za Serikali zilizoko vijijini kwamba ipo huduma hii ya afya kwa watoto na inaweza kupatikana kupitia shule? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, anasema kama Serikali imeshapeleka. Ni kweli tumeshaanza kupeleka na kwa sababu suala la elimu ni endelevu, tunaendelea kupeleka, lakini pia nilitumie Bunge lako tukufu, nawaomba Wabunge kwenye mikutano yetu ya kwenye Wilaya zetu, tuendelee kuwasisitiza wananchi na watu wengine na Serikali ya Wilaya na watu wengine kuhakikisha wanahamasisha hili na kuwapa taarifa wazazi, tufanye hilo kwa pamoja.

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, wakati tunasubiri mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, Serikali inatumia utaratibu gani kuwapatia matibabu watu wenye ulemavu wasiokuwa na uwezo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kuna utaratibu wa kutoa matibabu bure kwa watu wasio na uwezo wa kujilipia. Kwenye eneo lake la kata yake, akishapata barua ya Katibu Kata akienda hospitali na kuna watu wa Maendeleo ya Jamii kwenye kila hospitali yetu, ambao wanashughulikia mambo hayo na wanaweza kumsaidia na akapata huduma bure kama hana uwezo wa kujilipia.
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza. La kwanza, kwa kuwa sasa Serikali imekiri kwamba kuna tatizo kubwa la upungufu wa madawa kwenye zahanati;

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapa wazee bima maalum ya afya ambayo inaweza ikawasaidia kupata dawa katika maduka ya watu binafsi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa sasa kuna mmomonyoko wa maadili miongoni mwetu kijamii wazee wakiwa wanaenda hospitali wengi hawawapishi katika zile foleni wanawaacha wazee wanapata shida.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kila hospitali inakuwa na madirisha maalum ya wazee kupata huduma haraka?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake hili muhimu sana kwa ajili ya afya za wazee wetu. Kwanza nianze kwa kumwambia Mheshimiwa Mbunge, moja tuliposema tunakuja na Bima ya Afya kwa Wote, ndilo lilikuwa suluhisho la hili jambo, na unajua kwamba kwenye Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote tulikuwa na kipengele cha kuwalipia watu wasio na uwezo, kwamba wanakuwa na bima ya afya, maana yake na kuwa wazee wako sehemu ya hili. Lakini suala la kusema kwamba wapate bima maalum ili wakikosa ndani ya hospitali zetu dawa waweze kupata kwenye maduka binafsi; mimi nafikiri cha msingi hapa ni hospitali zetu, kwa maana ya vituo vya afya, hospitali za wilaya na zahanati zetu ziwe na dawa zote ambazo zinaweza kuwasaidia wazee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mikakati imefanyika; nafikiri Mheshimiwa Mbunge unajua jinsi ambavyo sasa hivi dawa zikifika kuna kamati za vijiji za kupokea dawa, Waheshimiwa Wabunge wanapewa ripoti na kila mtu anashiriki kwenye mchakato huu. Nina hakika hakutakuwepo na upungufu mkubwa na wazee watapata dawa zao.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niulize swali la nyongeza fupi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Vunjo kuna vituo vya afya vinne tu licha ya kwamba tuna kata 16. Na hivi vituo vya afya vikiwemo Unyika Msae, Marangu Head Quarter ambacho ni kipya, Kilua Vunjo na Kahe havina uwezo wa kutoa huduma ya upasuaji, hususan kwa wanawake ambao ni wajawazito na hivyo wanalazimika kupewa rufaa kwenda kwenye hospitali za Mawenzi ambapo ni mabli au KCMC ambapo pia kuna usumbufu mkubwa;

Je, ni lini Serikali itatoa vifaa na madaktari ili vituo hivi viweze kutoa huduma hiyo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Serikali ya Doctor Samia Suluhu Hassan ilipopeleka vituo vya afya kule kwa kweli lengo lake ni kufika mahali vile vile viweze kufanya upasuaji waweze kuwasaidia akina mama kule kule badala ya kuwapeleka mbali kama hospitali ya Mkoa anavyosema Mheshimiwa. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge kama suala ni ukosefu tutakuja kuangalia vituo vyako specifically kama theater ipo na vitu vingine vipo. Kama ni ukosefu wa vifaa tutashirikiana na wenzetu TAMISEMI tuone namna vitakavyoweza kupatikana ili huduma hiyo iweze kutolewa.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, ninapenda kujua;

Je, ni kwa nini sasa sera hii haitekelezeki kikamilifu, kwa sababu wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano bado wanalipishwa kwenye suala zima la afya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; wazee zaidi ya miaka 60 bado pia wanatozwa pesa wanapokwenda kutibiwa;

Je, kwa nini sera hii haitekelezeki?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anashirikiana na Waheshimiwa Wabunge wa mkoa wake kufuatilia masuala muhimu ya afya katika mkoa wake.

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, ni kwa nini sera hii haitekelezwi kwa asilimia 100 kama ilivyozungumzika. Ni kama maeneo mengine, wote tunajua kuna kipindi tulipitia kwenye shida ya upungufu wa dawa, kwa hiyo kunapokuwa na upungufu wa dawa na vifaa tiba basi linaathirika eneo hili kama yanavyoathirika maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, lakini pia unakumbuka hapa wakati wa bajeti yetu mlizungumzia suala la mtaji kwa MSD. Sasa maana yake MSD ikishapata mtaji badala ya kutegemea fedha kutoka kwenye vituo, basi sasa ule mnyororo wa upatikanaji wa dawa hautakatika tena kama ambavyo umekuwa ukikatika, na sasa tutaweza kuhakikisha kwamba sasa dawa zitakuwa zinapatikana wakati wote na vifaa tiba vinapatikana wakati wote, na akina mama wanaweza kupata huduma kama ambavyo inatajwa na sera. Tumeshaainisha, Mheshimiwa Waziri ameunda tume imeonesha kwamba tunahitaji bilioni 167 kuweza kuhudumia wananchi katika eneo hili.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu wazee linafanana na hili lingine. Kwanza niseme tu kwamba tumeagiza kila kituo cha afya, kila zahanati, kila hospitali kuwepo na dirisha la wazee. Na tunawaomba wenzetu wakuu wa wilaya na wakurugenzi wasimamie eneo hili la akina mama na eneo la wazee kuhakikisha hili takwa la kisera linatekelezwa ipasavyo, ahsante. (Makofi)
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu ya Serikali. Nina swali la nyongeza. Kwa kuwa utoaji wa Mimba siyo kitu kizuri na kinahatarisha maisha ya wasichana: Je, elimu hiyo ambayo mmeitoa, imetolewa kwa kiwango gani au katika mikoa mingapi ya nchi yetu ya Tanzania? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba elimu ni mchakato endelevu na ni mchakato ambao watoto wanapata mashuleni, lakini kila akina mama wanapohudhuria kliniki tunawapa elimu na vile vile, kuna vipindi mbalimbali vinavyotolewa kwenye tv ambavyo vinawafikia wananchi. Kwa hiyo, kimsingi hakuna Mkoa wala wilaya ambayo elimu hiyo haijatolewa.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Kwa kuwa, Serikali imeshaongeza vifaatiba na dawa kwa zaidi ya asilimia 100 kwenye Zahanati na Vituo vya afya. Ni lini sasa watatoa hadhi kwenye vituo hivyo ili viweze kutoa huduma zote za Bima ya Afya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Serikali inatambua kwamba yapo maeneo ambayo bado huduma hizi hazijafika na amesema ipo mikakati ya Serikali kwa ajili ya kufikisha huduma hizo. Ningependa kujua sasa ni ipi mikakati hiyo ya Serikali ili kuhakikisha kwamba Watumishi kwa maana ya rasilimaliwatu wanaongezeka, vifaatiba pamoja na miundombinu inaimarika? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake ambalo ni strategic kwa ajili ya kuboresha huduma za afya. Swali lake la kwanza kwamba ni lini vituo hivyo vitapewa vibali vya kusajili? Mheshimiwa Mbunge ni kwamba vituo vyote, zahanati, vituo vya afya ambavyo vimesajiliwa ni kwamba Bima wanatakiwa wawaruhusu pia kutumia dawa hizi ambazo ziko kwenye mwongozo wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge kama kuna zahanati au kituo cha afya chochote ambacho hakijasajiliwa nawaagiza Bima ya Afya wapitie nchi nzima wahakikishe vituo vyote ambavyo vimetimiza hivi vigezo basi viwe vimesajiliwa na kutoa huduma hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kuhusu kufikiwa vituo vingine. Moja, tunajua mwaka huu vifaa vingi sana vimenunuliwa na viko njiani vinakuja, kwa hiyo, vitasambazwa kwenye vituo vyetu lakini kwenye bajeti ya mwaka huu tunakwena ku–cover hivyo vituo na ajira zitaendelea kufanyika kila mwaka unaokuja kuhakikisha tunawafikia wote.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa dawa ya kisukari kwa wagonjwa wa sukari imekuwa ni changamoto sna kwenye vituo hivi vya afya mpakla waende Wilayani. Je, Serikali sasa haioni umuhimu wa ku-review utaratibu huu ili kwenye level za Vituo vya Afya pia waweze kupata?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo ambalo lilikuwa linaleta malalamiko mengi hasa kwenye zahanati na vituo vya afya hasa kwa wazee wetu wagonjwa wa kisukari na presha ni eneo hili ambalo Mheshimiwa Mbunge amesema. Ukiona hapa tumeongeza dawa kwa kiasi hiki ni moja wapo ya dawa hizi za sukari na presha kuhakikisha sasa hiyo shida iliyokuwepo huko nyuma haitatokea tena.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru sana na nashukuru pia majibu ya Serikali nimeyasikia. Lakini wananchi wapokata Bima ya Afya wanajua wameweka akiba kwa ajili ya matibabu pale wanapoumwa kumekuwa na utofauti wanapokwenda hospitalini kupata huduma wanaambiwa bima yako daraja lake huwezi kupata dawa hizi, huwezi kupata huduma hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuwapa elimu mapema kabla hawajakata bima ili kujua kwamba bima yake anaweza kupata matibabu gani kwenye eneo lipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa NHIF na Serikali mmekili kwamba bado kuna changamoto na changamoto hizo na CAG naye amezungumza usimamizi mbovu pamoja na taarifa za uongo zinapotolewa. Ni upi mkakati wa Serikali wa kumaliza changamoto hizi ili kurudisha dhana ile kwa Serikali kuliko hivi sasa wananchi wanaamini hatuna maana tena ya kuwa na Bima ya Afya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri lakini naomba tu nimwambie kwamba kwenye eneo la NHIF hakuna madaraja labda akiwa amechanganya kati ya NHIF na CHF. Kwenye CHF ndiyo kuna madaraja kwa maana kuna kutibiwa kwenye kunafikia level fulani hutibiwi level fulani na mambo mengine kama hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana tulikuja na mkakati wakati wa kuja na Muswada wa Bima ya Afya kwa watu wote tulikuja na mkakati thabiti wa kuboresha eneo la CHF pamoja kwamba tunayo Bima ya Afya kwa wote. Lakini tuone kwa uwezo pili hicho kwa sababu hatufuti CHF lakini tukaja na makakati wa kuboresha ili kuondoa madaraja ambayo Mheshimiwa Mbunge anayazungumzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nataka kukuhakikishia kwamba matatizo watu wako wa Nkasi wanayoyapata kutokana na hayo mambo tukikubaliana pamoja kwamba baada ya muda tutakuja na Muswada wa Bima ya Afya kwa wote tutaweza kutoa hilo tatizo. (Makofi)
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kujua, hivi karibuni kumekuwa na utata sana wa Bima ya Afya CHF kwa wananchi wa vijijini. Hii bima imefutwa au ipo? Nini tamko la Serikali? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, bima hii haijafutwa na tunashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI ambao ndiyo wanasimamia eneo hili la CHF ili kuona katika kipindi hiki cha mpito ambacho kuna haya matatizo ambayo Wabunge mnayazungumzia tunaboreshaje pamoja sisi na TAMISEMI tuone ni namna gani tunaiboresha ili kuondoa matatizo yayosemwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo kuna wenzetu ambao wanafadhili eneo hili kuna Taasisi inafadhili eneo hili wanasaidia kwenye matangazo wanasaidia kwenye kuhamasisha, tunataka tukae nao pamoja tuone namna gani badala ya kufanya matangazo, kufanya warsha na tamasha warudishe hizo fedha waende kuboresha kwenye eneo la kitita ili wananchi kuweza kuondokana na tatizo hili. (Makofi)
MHE. ENG. EZRA J. CHILEWESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza. Hospitali ya Wilaya Biharamulo tulianza kutoa huduma tarehe 13 Januari, tukapata usajili tarehe 20 Februari. Lakini mpaka sasa tangu tume-apply maombi kwa ajili ya kutoa Huduma za NHIF kwenye hospitali yetu hatujapata kibali wala hatujapata majibu kutoka NHIF. Ni nini kauli ya Serikali juu ya wakazi wa Biharamulo wanaotumia hospitali ile kwa sababu wamekosa haki yao ili hali wanazo kadi na wana kila kitu kinachohusu NHIF. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimeanza kumjua Mheshimiwa Mbunge kwa yeye kupigania hii hospitali yake. Kwa hiyo, kwa kweli sisi kama Serikali hatutakubali kazi uliyofanya kwa nguvu kubwa kwa miaka miwili wananchi wasiweze kupata huduma. Kwa hiyo, namwagiza Mkurugenzi wa NHIF Taifa nampa siku tatu Hospitali yako ya Biharamulo ipate Mfuko wa NHIF.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana niliuliza kwamba kwa kuwa na nyinyi Serikali mmekiri kwamba kuna changamoto kwenye aina ya Bima hiyo ya CHF kwamba mkakati wa Serikali ni upi wakumaliza changamoto hizo ili kuondoa hii dhana ambayo wananchi wanayo sasa kuona hakuna haja ya kuwa na Bima ya Afya wanapoenda kwenye huduma. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, anachosema Mheshimiwa Aida nimekwenda pamoja na yeye kwenye jimbo lake nimeona hilo tatizo na wananchi wamekuwa lalamika. Kwanza nikupongeze Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi ulivyo karibu na nilivyopita kule nilikuwa nashangaa ulishindaje kule kwa ile structure? Nikajua hapo sasa hivi kwa kweli wewe ni mwanamke wa shoka kwa ushindi uliyopata pale Nkasi. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niseme tu kwamba, tumesema hapa moja nimeeleza kwa swali alilosema mwenzetu Mbunge pale kwamba kwakweli kwa sasa tunashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI ambao wanasimamia eneo hilo kwamba tuone kwa kipindi hiki cha mpito ambao bado Muswada wa Bima ya Afya kwa wote haujaja tunakaaje tuweze kuboresha eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni kwa sababu kuna taasisi ambayo ina support eneo hili na Waziri wa Afya ameishawaita tuone tunakaaje waweze kukaa. Fedha wanazotumia kwenye warsha, matangazo na nini wanaweza kuboresha hicho kitita wakati tunangojea Muswada wa Bima ya Afya kwa wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata mimi mwenyewe eneo hilo la CHF sithubutu kulipigania kule jimboni kwangu. Kwa sababu ukipigania halitoi matokeo unayotegemea lakini naamini kwa ushirikiano wetu na TAMISEMI tumeweka mkakati mzuri sana ambao tutaboresha eneo hilo baada ya muda siyo mrefu.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa duniani kwa sasa, watu zaidi ya 28 wanakufa kila sekunde kwa sababu ya magonjwa yasiyoambukiza na kwa sababu Tanzania kwa sasa kisababishi kikubwa cha vifo Tanzania ni magonjwa yasiyoambukiza. Kwa nini Serikali isitoe fedha za kutosha ili wananchi waweze kupata elimu, wajue visababishi, wajue na namna ya kujikinga kwa sababu haya magonjwa yanaweza kuzuilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, tumbaku ni zao la biashara ndani ya Tanzania, lakini tumbaku hiyo hiyo ni kisababishi kikubwa kinacholeta magonjwa yasiyoambukiza kama kansa, stroke, presha na kisukari. Je, ni lini Serikali itawawezesha wakulima wa tumbaku nchini ikawapa mazao mbadala, wakawatafutia na masoko ili kusudi waondokane na hiki kilimo ambacho kinaathiri afya zao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kuja na swali hili zuri ambalo ni eneo kwa kweli ambalo Mheshimiwa Waziri wa Afya ameliwekea msisitizo wa nguvu sana kwa sababu ndiyo tatizo kubwa kwa sasa kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza; kwanza Serikali imeweka fedha nyingi kwa sababu ukiona kwenye miundombinu, lakini ukiona manunuzi ya CT scan na mambo mengine, lakini Wabunge wamemwona Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan hapa karibuni alisaini mikataba na Wakuu wa Mikoa kwenye eneo hili la lishe. Pia wameona viongozi mbalimbali wakishiriki katika matamasha makubwa. Kwa hiyo fedha tulizotaja hapa ni fedha tu kwa ajili ya hamasa, lakini hatujazungumzia kwa ujumla dawa na sehemu zingine mtambuka ambazo fedha zimewekezwa kwa ajili ya eneo hilo. Kwa hiyo kuna fedha za kutosha na tutaendelea kuona ni namna gani tutasisitiza eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu tumbaku; kupanga ni kuchagua, ni ukweli kabisa kama ambavyo Mbunge anasema tumbaku ina madhara mengi, siyo tumbaku tu pekeyake pamoja na kelele zinazopigwa mitaani pamoja na mambo mengine mengi ambayo tunayatumia. Sasa Mheshimiwa Mbunge pamoja na ukweli huu wa kwamba tunahitaji kutafuta zao mbadala wa tumbaku, naomba nisiseme lolote hapa kwa sababu linahusu Wizara zote na taratibu zetu na maslahi ya wananchi, tutashirikiana na Wizara husika na tuone ni namna gani tunaweza kufanya, lakini kweli kuna tatizo hili na siyo tumbaku peke yake kuna mambo mengi yanayosababisha tatizo hilo. (Makofi)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali; je, mpango ukoje kwa Bima ya Afya kwa Wote kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa hawa wa magonjwa yasiyoambukiza?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa bima ya afya ulikuja hapa kwa ajili ya sisi kuja na Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuweza kabisa kuboresha mambo mengi ambayo yangeweza kusaidia pamoja na eneo hili tunaloliona. Kwa hiyo kikubwa mimi na wewe tuendelee kushirikiana kuona ni namna gani tunapambana kupeleka Muswada wetu wa Bima ya Afya kwa Wote uweze kurudi na iwe ajenda ya Mbunge ya kudumu na ajenda ya kudumu ya Wabunge ili wananchi waweze kupata huduma tukija na mpango wa Bima ya Afya kwa Wote. (Makofi)
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kumekuwa na tabia wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza wakienda kwenye dispensary na vituo vya afya hawapewi dawa za magonjwa ya kuambukiza kama presha. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha inatoa dawa kwa wagonjwa wetu hata huku kwenye ngazi ya dispensary na vituo vya afya?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli anachokisema Mheshimiwa Mbunge tulikuwa na tatizo hili, lakini kama Wabunge wanakumbuka juzi nilijibu swali kwamba kwenye eneo la dispensary zimeongezeka dawa zinazotolewa kutoka 243 mpaka 459, maana yake madawa hayo ya presha, sukari yameongezwa kwenye level ya dispensary, kwa hiyo tatizo hilo halitakuwepo tena. (Makofi)
MHE. PROF. SHUKRANI E. MANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kukamilika na kuanza kutumika kwa jengo hilo kunaifanya Hospitali ya Kanda ya Mbeya kuongeza uwezo na ufanisi hata hivyo kuongeza pia viatanda kutoka 600 hadi 800.

Je, ni lini Serikali itakapoifanya Hospitali ya Kanda ya Mbeya kupata hadhi ya taasisi kama ilivyo MOI, JKCI na nyinginezo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mchakato huo unaendelea wa kuifanya hospitali hiyo kuwa taasisi na bado tunaendelea mjadala, Wizara ya Afya, Wizara ya Fedha na Utumishi kuona namna gani tunaweza kufikia hatua hiyo, ili nayo Mbeya iweze kuwa taasisi kama ambavyo hospitali nyingine za Kanda zinakuwa. (Makofi)

MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; je, ni lini Serikali itatekeleza maombi ya kibali cha mabadiliko ya mishahara katika hospitali ya KCMC ambacho wameomba tangu mwaka 2011?

Swali la pili; kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi katika Hospitali hii, je, Serikali imejipanga vipi kuweza kutatua changamoto hiyo, ikizingatiwa hospitali hii ni ya Kanda?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyoshirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro na namna ambavyo anafanya kazi yake. Swali lake la kwanza kuhusu ni lini Serikali itafanya maombi yale ya kupandisha hadhi na kuongeza mishahara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu swali la kwanza la kuhusu Mbeya Mbeya pamoja na KCMC ni hospitali ambazo ziko kwenye mchakato ambao kuna mjadala kati ya Wizara ya Afya, Wizara ya Fedha na Utumishi kwa ajili ya kufikia kiwango hicho ambacho Mheshimiwa Mbunge unakitaja. Wiki hii tumepanga tufanye kikao na utumishi ili tuweze kuona ni namna gani tunaweza kujikwamua na kusaidia vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ni suala la upungufu wa watumishi. Kama ambavyo nimesema kuna watumishi 905 ambao wanalipiwa na Serikali, lakini wao wenyewe wanalipa kwa mapato yao ya ndani zaidi ya watumishi 400. Maana yake ukiangalia wanao watumishi karibu 1,300 sasa huo upungufu labda tutaenda kuangalia upungufu umetokana na nini. Inawezekana huko nyuma kweli kulikuwa na upungufu unaoletwa na hospitali yetu ya Mawenzi ilikuwa haifanyi vizuri, sasa hospitali yetu ya Mawenzi sasa inafanya vizuri kwa hiyo, wagonjwa wengi watazuiliwa Mawenzi, wataenda wale wanaohitaji kwenda kwenye Hospitali ya Kanda kwa hiyo, huo upungufu unaweza usionekane. (Makofi)
MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa zoezi hili ni endelevu, je, Serikali imejipangaje sasa kuhakikisha kwamba wanafunzi ambao hawajasajiliwa wanasajiliwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Pili; kwa kuwa utekelezaji wa zoezi hili si kwa takwa ama kwa mujibu wa sheria. Je, Serikali sasa ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba sheria hii inawekwa kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanasajiliwa katika Bima ya Afya? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri.

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ni nini tutafanya ili kusajili wanafunzi wengi zaidi, kikubwa ni kuendelea kuhamasishana kuwaomba wakuu wa shule na wazazi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu wote kwa pamoja tuone umuhimu wa watoto wetu kuwa na bima ya afya kwa sababu ugonjwa hauji kwa kusema, ugonjwa unakuja kwa ghafla na vizuri kujipanga wakati wote, hilo ni moja.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu mpango gani, kwa sababu hili suala haliko kisheria, tunafanya nini. Mheshimiwa Mbunge ni kwamba ndiyo maana Serikali ilikuja na Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ili kulifanya hili jambo liwe sasa la kisheria. Kikubwa ambacho nawomba Watanzania, nawaomba ninyi Wabunge tuendelee kuelewa na kupigana kwa pamoja kuhakikisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote unarudi hapa ili tuweze kufanya hili suala la kisheria kwa sababu masuala ya afya ni muhimu na afya ni uchumi wa nchi. (Makofi)
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza; kwa kuwa kwenye jibu la msingi Waziri ametuambia chanzo ni upungufu wa chembechembe nyekundu kwenye mwili wa mtoto. Sasa je, tunamshauri nini mama mjamzito ili kuondokana na tatizo hili? (Makofi)

Swali langu la pili; mtoto akishazaliwa na akagundulika ana tatizo hili la manjano, wataalam wetu huwashauri wazazi kuwaanika watoto juani. Ni, lini tiba ya ugonjwa huu itapatikana ili kuondokana na changamoto kubwa ya wazazi wanaokumbana na ugonjwa huu wa manjano, baadhi wanapoteza maisha na hatimaye kupunguza nguvu kazi ya Taifa letu? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge. Swali lake la kwanza anasema kwamba tumesema chanzo ni upungufu, siyo upungufu, wakati mwingine watoto wanapokuwa wamezaliwa halafu wanakuwa na chembechembe nyingi za damu ambazo alitoka nazo tumboni zinapokuwa zinasafishwa kunakuwepo sasa na bilirubin ambayo inasababisha hiyo hali ya umanjano kwamba sasa hicho ndiyo kinachotokea. Wakati mwingine kwa sababu ini la mtoto anapozaliwa ndani ya siku 14 anakuwa bado ini lake halijakua vya kutosha, kwa hiyo, uwezo wa kubadilisha ile kitu kinachosabisha umanjano haina uwezo wa kutosha ndiyo maana unaona huo umanjano, kwa hiyo, ni kitu cha kawaida. Ikitokea kama tulivyosema ndani ya masaa 24 basi ni tatizo tunalifuatilia na kujua. Hata hivyo ikitokea baada ya masaa 24 ni muhimu vilevile wataalam kumuangalia.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ni suala la kwamba watoto wanaanikwa juani. Nimuambie tu Mheshimiwa Mbunge, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshafanya revolution kubwa sana, ndiyo maana umeona trilioni 1.3 imefanya mabadiliko makubwa sana ya tiba ya afya. Leo unaona vifaa vingi sana vimesambazwa kwenye maeneo yetu na vituo vyetu vya afya, utaona kuna vifaa maalum vya kuwaweka watoto ambavyo vinatoa mionzi maalum kwa ajili ya kuondoa hilo tatizo. Kwa hiyo, watoto wetu kwa revolution aliyoifanya Dkt. Samia Suluhu Hassan mpaka kwenye vituo vyetu na zahanati sasa vifaatiba vinaenda kununuliwa na hili tatizo litaondoka. (Makofi)
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Ninaomba kuuliza, je, Serikali imejipanga vipi kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa rheumatic heart disease ambao unaonekana unaongezeka kwa kasi kubwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kikubwa ambacho naweza kumwambia Mheshimiwa Mbunge moja ni elimu, watu kuangalia afya zao kila wakati na kupata tiba stahiki mapema, ndiyo maana unaona leo, hata Taasisi yetu ya Jakaya Kikwete keshokutwa inakwenda Pemba kwenda kabisa kule vijijini kuhakikisha watu wanafanyiwa uchunguzi na kuhakikisha haya matatizo yanagundulika mapema na watu kupata tiba stahiki mapema. (Makofi)
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa.

Je, Serikali ina mpango gani kusaidia wagonjwa wanaohitaji viungo bandia kama vile miguu bandia, kwani gharama zake ziko juu sana kwa mgonjwa wa kawaida. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, alichokisema Mheshimiwa Ndakidemi ni kweli na kuna tatizo hilo na ndiyo maana bado tulikuwa tunasisitiza, mwarobaini wa tatizo hili la uwezo wa kulipia tiba ni Bima ya Afya kwa wote hilo ndiyo la kwanza. Kumekuwepo na utaratibu wa Serikali kusaida Watanzania wasiojiweza, wale ambao watathibitika hawana uwezo wa kujilipia basi kuna utaratibu unakwenda kwa Mtendaji wako wa Kata anaandika barua na kuna social welfare kwenye hospitali zetu wanazipitia basi anapata exemption anaweza kuhudumiwa. (Makofi)
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nichuke nafasi hii kuipongeza Serikali kwa majibu mazuri, lakini pia nina maswali yangu mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikinunua dawa MSD na inapokosa inanunua kwa mshitiri; je, Serikali inamkaguaje mshitiri ili kuwa na dawa za kutosha pale inapokosekana MSD?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; ni hatua gani zinachukuliwa kwa watoa huduma wa vituo vya afya ambao wanathibitika na upotevu wa madawa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mazuri ambayo yanalenga kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma. Ni kweli kama anavyosema Mbunge kwamba, wakati mwingine inapokuwa MSD hakuna dawa, basi watu wetu wanapewa OS na wanakwenda kununua kwa mshitiri, lakini kuna mikoa ambayo wamemweka mshitiri ambaye ni mmoja na wataalam wetu hawaruhusiwi kunua dawa nje ya yule mshitiri. Kwa hiyo, anapokuwa amekosa MSD, anafika kwa mshitiri, naye mshitiri akiwa hana dawa, kwa hiyo, inafika mahali watu wetu wanateseka hawana dawa na huku fedha wanazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii na hili swali la Mheshimiwa Mbunge kuagiza kwamba, kwanza tusilazimishe hospitali zetu kununua kwa mtu fulani dawa. Ni kwamba tutengeneze biashara huria, duka lolote lenye dawa ambalo limetimiza vigezo, watu wetu waweze kununua kwenye duka lolote la dawa bila kulazimishwa kununua kwa mtu fulani. Kwa sababu nayo hiyo ni aina ya ufisadi mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumwambia Mheshimiwa Mbunge, hakika tutakapokuwa tunapita, tutashirikiana naye kushughulikia suala hilo, kwa sababu ukiona mtu mmoja analazimishwa kwenye mkoa mmoja kwamba yeye ndio auze dawa, hiyo ni aina mwingine wa ufisadi na tutausimamia na ku-control.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusu tunafanya nini kwa wale wanaobainika kwamba wameiba dawa, kwa kweli kuna sheria na taratibu za utumishi wa umma. Kama unavyojua, nasi ni Wabunge ambao tunatunga sheria hapa, kuna baadhi ya sheria tumetunga ambapo mwizi anakuibia mara moja, lakini ikifika mahali wakati wa kumshughulikia mwizi ambaye una hakika kwamba ameiba, inabidi ufuate taratibu na sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inabidi tutafakari kwa kina namna gani tutawashughulikia watu ambao wanafanya ufisadi kwa sababu wakati mwingine sheria zinawalinda sana.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini majibu haya ni tamko la sera, ni miongozo ya Serikali, lakini bado huko vijijini akina mama wajawazito wanaendelea kuagizwa kwenda na vifaa vya kujifungulia.

Je, Serikali inatoa tamko gani, kwamba hawa akina mama watakapokosa huduma hizi wachukue hatua gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba Serikali imeimarisha huduma na wanawake walio wengi vijijini wanapata hizo huduma.

Je, Serikali ipo tayari sasa kutuletea sheria (kwa sababu haya yote ni matamko na miongozo) Bungeni kwa ajili ya kusimamia huduma hizi za mama na mtoto ziweze kutolewa bure? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake hili zuri ambao ni ukweli unaogusa maisha ya akina mama wetu kila siku. Swali lake la kwanza kuhusu je, wanapokosa huduma tunafanyaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niwaambie tu kwamba, sheria hiyo ipo. Nitoe tamko kwamba suala la akina mama kupata huduma, mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano ni bure. Pia ni ukweli kwamba kile kipindi ambacho tulikuwa tunapitia kwenye upungufu wa vifaa tiba, pamekuwa pakitokea changamoto hizi ambazo amezisema hapa Mheshimiwa Mbunge. Kama ambavyo nimeeleza kwenye swali la kwanza linalohusu upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kutoka kwa Mheshimiwa Halamga, tukiweza kusimamia yale ambayo nimeyasema hapa, nataka kuwahakikishia kwamba suala la akina mama kununua vifaa na vitu vingine havitawezekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba tu Waheshimiwa Wabunge, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wote kwa pamoja tushikamane kuhakikisha kwenye Kamati zetu za Ulinzi na Usalama, suala la upatikanaji wa dawa na huduma za afya liwe ni ajenda ya kudumu ili tuijadili. Kwa sababu kwa kweli ikikosekana dawa, huduma zikiwa mbaya, watu watakufa. Kwa hiyo, pia ni suala la kiusalama, wote tulijadili kila wakati na kuhakikisha tunalisimamia kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili la kwamba tutunge sheria ya kusimamia hili la akina mama kupata huduma, naomba nilichukue tukalitafakari tuone namna ya kufanya, lakini ninaamini Mheshimiwa Mbunge tukikubaliana pamoja sisi Wabunge na Watanzania wote, tukaja na Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, tunakuwa tumepata mwarobaini wa suala hilo. Maana yake kila mama atakapokuwa na bima yake ya afya, kila familia itakapokuwa na bima yake ya afya, basi matatizo haya mengine yatakuwa yameisha, ahsante.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu haya ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, zaidi ya asilimia 70 ya vifo vya watoto vya chini ya miaka mitano, vinatokea kati ya umri wa miaka sifuri hadi mwaka mmojal; je, Serikali haioni haja sasa kuweka mikakati mahsusi na kuwekeza kwa watoto wa umri huo mwaka sifuri hadi mmoja ili kupunguza vifo hivi?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, katika Mkoa wangu wa Arusha moja ya sababu ambayo inapelekea vifo vya watoto wa chini ya mwaka mmoja ni ukosefu wa mashine za kuhifadhi watoto njiti; je, ni lini Serikali itapeleka vifaa hivi katika Hospitali zote za Mkoa wa Arusha? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge hasa kwa jinsi ambavyo anafanya ziara zake kwenye maeneo magumu hasa kwenye maeneo ya Mkoa wa Arusha yasiyofikika. Ni kweli anajua haya matatizo yapo, lakini umeona tulikotoka na mimi nimtoe tu Mheshimiwa Mbunge wasiwasi kwa sababu Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa sana katika eneo hili, kwa maana ya kuweka vifaa na mambo mengine na mmeona tulikotoka mambo makubwa kama CT Scan tulikuwanazo tatu nchi nzima lakini leo tuna zaidi ya 50, MRA mbili lakini leo tuna zaidi ya 19 kwa maana hili nalo ni dogo.

Mheshimiwa Spika, anachokisema Mheshimiwa Mbunge hapa ni kuongeza hiyo huduma. Kwa mwaka huu sasa tunaenda kujenga mia moja maana yake kwa swali lake la kwanza kwamba hilo la maeneo kufikika, maana yake zinajengwa mia moja, maeneo ya Mkoa wa Arusha ni maeneo ambayo pia hivi vituo 100 vinaenda kujengwa kwenye maeneo ambayo hayana.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni suala la kuweka vifaa vya kusaidia hao watoto ambao wanazaliwa kwa uzito mdogo. Ukijenga vituo mia moja na equipments zake zinawekwa kule ndani kwa hiyo hilo tatizo litakwenda kutoka na hakutakuwa na tatizo hilo tena.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, licha ya vifo vya watoto wachanga vilevile kuna tatizo kubwa la wazee kwa sababu hawana uwezo wa kulipa gharama na hata vile vitambulisho vinavyotolewa na Halmashauri wengi wa wazee huwa wanapata usumbufu.

Je, ni lini sasa Serikali itatoa bima za afya kwa ajili ya wazee ili waendelee kupata huduma nzuri?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, suala hili la wazee kuwa na vitambulisho lakini hawapati huduma limekuwa likitokana na upungufu wa dawa na vifaa tiba ambapo hata Mbunge ni shahidi kwa sasa masuala ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vyetu umeongezeka. Kwa hiyo, hili sasa limeshatatuliwa kwa asilimia 78 kwenye vituo vyetu na hospitali zetu. Hivyo tutaendelea kuongeza mpaka zifike asilimia 100.

Mheshimiwa Spika, pili, suala ambalo linaweza likatusaidia sisi kuondokana na hili tatizo moja kwa moja, ni sisi Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwamba ni lazima twende kwenye suala la Muswada wa Bima kwa Wote na ndilo suluhisho la kudumu kwa hilo. Lakini wakati huo kabla hatujafikia kwenye suala la Bima ya Afya kwa Wote kuna utaratibu wa kwamba mtu/mzee anayeshindwa kulipa kabisa na anayepata shida tunaweza tukatumia kwa maana ya kupata barua na mambo mengine, lakini sheria zetu vilevile zinatoa room kwa watendaji wetu kuwaaandikia barua na kupata huduma.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkoa wa Kagera una maambukizi makubwa ya Malaria, ni namba tatu kwa maambukizi makubwa Kitaifa na kwa kuwa Wilaya ya Ngara ndiyo inayoongoza katika maambukizi ya Malaria Mkoani Kagera. Je, ni lini sasa Serikali itatusaidia kufanya unyunyiziaji wa viuatilifu (Indoor Residual Spraying) katika Wilaya ya Ngara ili kupunguza maambukizi ya Malaria?

Swali la pili, kwa kuwa zipo nchi duniani ambazo tayari zimeshatokomeza kabisa Malaria. Je, ni lini Tanzania tumelenga ni mwaka gani tutakuwa tumefikia zero Malaria, kwa maana ya kutokomeza kabisa Malaria? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ni kuhusu Mkoa wa Kagera. Ni kweli kwamba Mkoa wa Kagera ni Mkoa wa tatu una asilimia 18 ukiongozwa na Tabora wenye asilimia 23 ukifuata Mtwara. Ni kweli Ngara inaongoza na tulikwenda na tunao ushirikiano na wenzetu wa Rwanda katika kutokomeza na tumeshajenga vituo upande wa Tanzania na upande wa Ngara kwa ajili ya kuweka utaratibu.

Mheshimiwa Spika, moja ni huu ambao amesema kunyunyuzia hiyo dawa, lakini tunafikiria kwa sababu Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati anazindua Malaria Council alielekeza kwamba tuandike Wizara ya Fedha tuoneshe tunahitaji shilingi ngapi kwa ajili ya kununua zile dawa za kuua viluilui na tayari tumeshafanya na tumewasilisha Wizara ya Fedha bilioni 22 kwa ajili ya nchi nzima na mojawapo Ngara kwa maana ya Mkoa wa Kagera ikiwepo ni sehemu ya kufanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu ni lini tutaweza kutokomeza Malaria. Kwanza nikuhakikishie kabisa kuna Mikoa zaidi ya tisa sasa ni chini ya asilimia moja Malaria kwenye nchi yetu, na Mikoa mingi sana imeshuka. Kwa hiyo, tunadhani mpaka 202030 nchi yetu nayo itafikia kwenye kiwango cha hizo nchi nyingine. (Makofi)
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, Mheshimiwa Mariam Kisangi ana maswali mawili ya nyongeza.

Swali lake la kwanza linasema; ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam kumekuwa kuna ucheleweshwaji wa upatikanaji wa kadi za bima za afya yaani toka tarehe mtu analipia mpaka kuja kuipata ile kadi inaweza kuchukua hata miezi sita. Nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba kadi hizi zinapatikana kwa wakati? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili; linasema kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo wagonjwa ambao wanahitaji huduma ya kuzisafisha hizi. Nini kauli ya Serikali kuruhusu wagonjwa hawa kuwa na Bima za Afya hata kama ni zile za vifurushi vikubwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda nijibu maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, moja; ni ucheleweshaji wa bima ya afya ukilipia; ni ukweli kwamba umewekwa utaratibu kwamba toka unapolipia basi upate bima yako baada ya miezi mitatu na lengo lilikuwa ni moja tu kwamba watu wengi wakiwa na afya, wakiwa salama, wanakuwa hawana tabia ya kujiunga na bima watu wakadhani kwamba ni vizuri mtu akajiunga wakati hana ugonjwa wowote ili kulinda mfuko huo.

Lakini hili la miezi sita kwakweli nilakushughulikia kwamba tulishughulikie mapema ili watu wapate ndani ya muda uliopo. Lakini sasa wakati muswada unakuja hapa ambao sisi Wabunge ndiyo tutakaojadili basi tujadili tuone tunatakiwa upate kwa wakati gani na tutaweka utaratibu mzuri ambao hautaleta matatizo ambayo sasa mnayaona.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusu wenzetu wenye matatizo ya figo; moja ni kwamba sisi wote tushirikiane kwa sababu suala moja ni kuhakikisha kwamba watu hawafiki mahali wanapata matatizo hayo ya figo, lakini ikitokea sasa wamepata basi kwa kweli Serikali inajitahidi.

Moja; ilikuwa kufanya dialysis kwa mara moja ni shilingi 380,000 lakini sasa hivi imeshuka mpaka shilingi 120,000 lakini bado ni gharama kubwa. Tutaendelea kuona namna ya kufanya ili hao watu wapungukiwe na mzigo kwa sababu kwanza wengi hawana uwezo wa kufanyakazi na wengine hawana kazi. (Makofi)
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwakuwa suala la huduma ya mama na mtoto imekuwa na changamoto kubwa.

Je, ni kwanini sasa Serikali isiweke kanuni inayosimamia Sera ya Huduma ya Mama na Mtoto? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali nyeti na la msingi la Mheshimiwa Mbunge ni kwamba kwanza tukishaleta Sheria ya Bima ya Afya kwa wote tutakuwa tumemaliza mambo mengine yote mimi ninachomuomba Mheshimiwa Mbunge kwasababu tayari tumekuja kwenu na mmeona mchakato wetu unaoendelea wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na unaendelea kwa sasa ikifika hapa Bungeni tuhakikishe tumetengeza sheria nzuri, utaratibu mzuri nataka kuwahakikishia haya matatizo yanayojitokeza kila siku tutakuwa tumeyatafutia suluhisho la kudumu.
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa kuna sheria inayo guide mama wajawazito na wagonjwa kwaajili ya kutibiwa. Je, nini upande wa pili wa Serikali kuhusiana na vituo vya afya ambavyo hakuna jengo la mama na mtoto mfano Kata ya Wazo ambapo kunatokea vifo vingi kutokana na kukosekana kwa jengo hilo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Mheshimiwa Mbunge ni shahidi hapa kwamba kwa mwaka huu katika historia ya Tanzania kuliko wakati wote fedha nyingi zimepelekwa kwenye eneo la afya naniukweli kwamba hatutaweza kumaliza vyote kwa wakati mmoja lakini kwakweli hoja yako Mheshimiwa Mbunge niyamsingi, kimsingi basi shirikiana na halmashauri yako na hata leo tuandike vizuri tuhakikishe tunashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI iingie kwenye utaratibu na kama haijawahi kuingia kwenye utaratibu tuanze sasa mchakato litekelezeke lakini kwa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wala usipate wasiwasi na hilo.

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Wananchi wa Jimbo la Ushetu kwa kutumia nguvu zao wameweza kukamilisha zahanati saba; Zahanati ya Butibu, Zahanati ya Itumbo, Itebere, Makongoro, Manungu, Bugera na Misayo ambayo ni Zahanati tumeipa kwa jina la Eliasi Kwandikwa ambayo imejengwa kwa msaada wa Kampuni GTI na hiyo zahanati yenyewe tayari inavifaa tiba. Lakini sasa ni lini Serikali inatuletea vifaatiba na watumishi kwenye zahanati hizi ili wananchi waweze kupata matibabu yao maeneo ya karibu badala ya kuendelea kwenda zaidi ya kilometa 80 kupata matibabu.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwanza mimi na yeye ili tufanye mambo ambayo yanatekelezeka ametaja zahanati zenye tatizo cha kwanza awasiliane na Mganga Mkuu wa Wilaya yake kupitia Mkurugenzi ili walete mahitaji husika wa eneo hilo mimi na yeye tushughulikie hilo liweze kufanyika nanimuambie tu Mheshimiwa Mbunge pamoja na fedha ambayo Mheshimiwa Rais wetu ameshazipeleka MSD lakini kwenye manunuzi ya juzi ya fedha zile za UVIKO kununua vifaatiba kama X-Ray, CT Scan Serikali ime-save yaani imepata salio baada ya kununua kwa bei rahisi ime-save zaidi ya bilioni 17 na zote zinaelekezwa kwenye kununua vifaatiba na madawa kwaajili ya vituo vinavyoanzishwa.

MHE: AGNES HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru pamoja na majibu ya Serikali naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Je, ni sheria ipi kati ya hizo sheria 30 inayosimamia wanawake wajawazito wakati wa kujifungua wanaopata huduma zisizoridhisha? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na swali la pili; je, sheria hizo zinaruhusu malipo ya fidia kwa wagonjwa wanaopata huduma zisizoridhisha au zisizo na ubora zinazopelekea athari za kiafya au hata kifo? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nijibu swali la Mheshimiwa Agness Hokororo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze kwa namna ambavyo anafuatilia namna wananchi wanavyotolewa huduma za afya katika eneo lake. Ni kweli kwamba kumekuwepo na mambo anayoyasema kwa maana ya huduma ya mama na mtoto lakini si tu sheria, sheria za nchi yetu, utaratibu wa nchi yetu na kanuni za Wizara ya Afya zinataka mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano wapate huduma bure lakini sasa tunapokuja kujibiwa vibaya, kujibiwa kwa masuala ya fedheha maana yake kuna sheria za kiutumishi ambazo zipo zimeonyesha watu wanaofanya mambo yanayofanana na hayo lakini kuna sheria za maadili ya kitaaluma ambayo mara nyingi anapopatikana mtu ambaye amekuwa akijibu vibaya akifanya nini wakati mwingine anapitishwa kwanza kwenye sheria za maadili ya kitaaluma anawajibika lakini anaachiwa vilevile sheria za kiutumishi zichukue mkondo wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge kama mdau mkubwa kwenye eneo hilo endelea kutusaidia na kutusaidia kutengeneza ushahidi wa kutosha kuwapata watu wa namna hiyo ili waweze kushughulikiwa kulingana na taratibu na sheria, ahsante.

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vituo vyetu vya afya kwenye Jimbo letu la Vunjo kuna uhaba mkubwa wa wahudumu lakini pia kuna wahudumu ambao wanataka kujitolea ili wasaidie na wenyewe wamesomea mambo hayo hayo ya ukunga nakadhalika na unesi lakini hawana kazi. Je, Wizara haioni umuhimu wa kuweka utaratibu wa kuwaruhusu hawa ambao wanataka wajitolee kusaidia kutoa huduma bure hata kama watalipwa kidogo na wananchi ili waweze kuchukuliwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza anachokisema Kimei ni kweli kipo na nimetembelea jimbo lake tumeliona hilo na ameshakieleza mara nyingi lakini sasa Mheshimiwa Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu alishaelekeza na tayari utaratibu, muongozo wa ajira ya kujitolea umeshatengenezwa kwa level ya Hospitali za Mikoa na kwenda juu. Sasa tunashirikiana na amesema atashirikiana na Mheshimiwa Bashungwa ili kutengeneza na utaratibu kwa kushuka chini tuone tunafanyaje hilo liweze kutekelezeka kwa urahisi lakini ni jambo jema sana kwasababu hata kwenye shule zetu tumeona kwamba kuna walimu wengi wanajitolea na wanasaidia sana watoto nayo kwenye afya tungetamani tuwe na jambo kama hilo lakini tulitafakari kwa kina kabla ya kutekeleza.

MHE. CONCHESTA LEONCE RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Nchi yetu ni kutoa Huduma ya Afya bure kwa wazee lakini sera hii imekuwa haitekelezeki kwasababu hakuna sheria. Je, ni lini Serikali itatunga sheria ili kumbana mpeleka huduma na mtoa huduma ili sera hii iweze kutekelezwa sawasawa kwa wazee? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, anachokisema Mbunge kipo sidhani kama tatizo ni sheria tatizo ni kwamba wazee kweli wamewekewa dirisha lao lakini wanapoandikiwa prescription na madaktari na baadhi ya vipimo wanapofika kwenye kufanya vipimo au kuchukua dawa wanakosa dawa husika na hilo ndiyo maana tunazungumzia suala la usimamizi wa dawa kwenye vituo vyetu na kuhakikisha dawa zipo kwenye vituo vyetu ambalo kwaweli kama Wizara ya Afya na TAMISEMI sisi wenyewe huku juu hatutaweza tunawaomba Waheshimiwa Wabunge, Baraza la Madiwani na Wakuu wa Wilaya wasimamie kwasababu kuna fedha nyingi zinakuja za Basket Fund na mambo mengine ambayo usimamizi ukifanyika tutapunguza tatizo kwa zaidi ya asilimia 80 lakini Mheshimiwa Mbunge tukishapitisha Muswada wa Bima ya Afya kwa watu wote maana yake kimsingi suala hilo tena alihitaji sheria suala hilo ni kwamba tutakuwa tumelitatua moja kwa moja, ahsante sana.
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Je, Mheshimiwa Waziri uko tayari kuambatana na mimi ili ukaweze kunidhibitishia mradi huu utakamilika mwaka huu wa fedha? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kutokana na changamoto nyingi wanawake wanazozipitia kipindi wanachokuwa wajawazito; Je, Serikali haioni haja kushusha huduma hii Wilayani ili tuweze kupata huduma hii kwa Mkoa wa Shinyanga kwa Watoto Njiti? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Santiel Erick Kirumba Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, moja niko tayari kuandamana naye kwenda Shinyanga na nitafurahi tukiwa wawili tu peke yetu. Ahsante. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni kwamba Je, Serikali haioni kuna umuhimu wa kupeleka kwenye hospitali za Wilaya huduma hizi. Kwenye bajeti yetu Mheshimiwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema kwamba, kwa mwaka huu unaokuja wa fedha tunaenda kujenga sehemu za Watoto Njiti 100 na siyo tu kwenye hospitali za Wilaya na kwenye Vituo vya Afya. Kwa hiyo, fedha zimeshapatikana sasa imebaki kuwasiliana na Waziri wa TAMISEMI ili kupanga sehemu za vipaumbele vya kuanza na kwa jiografia ya Mkoa wa Shinyanga ni mojawapo ya maeneo yataenda kufaidika na huu ujenzi. Ahsante sana.
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Hospitali ya Mkoa ya Tumbwi siyo kwamba inahudumia watu wa Pwani tu na wale wapita njia. Kitengo cha Watoto Njiti kweli kipo lakini uboreshaji ni pamoja na vifaa tiba. Watoto wanazaliwa pale lakini inabidi wakimbizwe.

Je, ni lini Serikali pamoja na kuboresha kitengo cha Watoto Njiti na vifaa tiba vitaboreshwa lini?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dokta Kaijage kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwamba Hospitali ya Tumbwi ni mojawapo kweli kuna eneo la Watoto Njiti lakini hospitali inazidiwa. Katika Bilioni 59.3 ambazo zimetengwa kwa ajili ya uboreshaji, Hospitali ya Mkoa wa Tumbi ipo mojawapo na eneo ambalo limetengewa hela kwa ajili ya kulipanua na kuongezea vitanda ni eneo hilo la Watoto Njiti. (Makofi)
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, Serikali haioni haja ya kumjumuisha mtoto njiti kwenye Bima ya Mama yake ili pindi anapozaliwa aweze kupata huduma hiyo na kumwondolea Mama mwenye mtoto njiti adha ya kuanza kufanya usajili wa mtoto kwenye Bima ya Afya?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, swali aliloliuliza Mbunge ni swali muhimu sana na nitumie fursa hii kumwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bima ya Afya kwamba suala la kuhudumia mtoto njiti ambaye mama yake ana bima yake ya afya lisiwe mjadala. Mtoto njiti akizaliwa na huduma yake inakuwa ni automatic. Vilevile kwa sababu tunakwenda kwenye suala la bima ya afya kwa watu wote Wabunge wote tukumbuke hayo mambo tuhakikishe sasa tutaweka kwenye sheria ijayo iweze kufanyika vizuri zaidi. (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Katika Hospitali yetu ya Mkoa wa Iringa tuna kitengo cha Watoto Njiti na tuna upungufu mkubwa wa mashine na dawa inaitwa Lung surfactant ambayo dozi moja inauzwa Shilingi Laki Tano na mtoto ili a-survive anahitaji dozi tatu. Serikali ina mpango gani kuangalia kwamba dawa hizi angalau zinawekewa ruzuku ili kupunguza gharama hiyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, moja kwanza sioy dawa kuwekewa ruzuku kwa taratibu na sheria na taratibu za Wizara ya Afya ni kwamba huduma ya mtoto chini ya miaka Mitano including hawo Watoto Njiti na Mama na Mtoto ni bure. Kwa maana kwamba tunaposema mlitupitishia bilioni 200 kwa ajili ya kununua dawa na vifaatiba. Hilo eneo tutakwenda kulielekeza nguvu nyingi kuhakikisha kwamba Watoto njiti hawawezi kukutana na matatizo hayo.
MHE. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Hospitali ya Kahama inahudumia watu kutoka pembezoni kwa maana ya Mikoa ya Tabora pamoja na Geita. Je, ni lini Serikali itaboresha kituo cha Watoto njiti pale Hospitali ya Kahama?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nijibu swali la Mheshimiwa hapa, ukisikia Serikali inasema inajenga vituo vya afya kwa kila Tarafa na kazi ile imeendelea kufanyika kupitia TAMISEMI ni kwenda kupunguza wagonjwa ambao sasa wanaenda kurundikana kwenye hospitali moja kama ilivyo Kahama.

Mheshimiwa Spika, mimi nafikiri Mbunge ni muhimu tukatembelea hospitali hiyo inawezekana tukikaa mle ndani tutaona tu maeneo ambayo tunaweza tukaweka sehemu ya Watoto njiti, ibaki kazi ya kuleta vifaa na kuvipachika na Watoto waweze kupata huduma.
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa Serikali imetueleza kwamba wana mpango wa kujenga vituo 100 vya Watoto Njiti hapa nchini; Je, sisi ni miongoni mwa watu tutakaofaidika Jimbo letu la Mchinga kwa kituo hicho?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wao ni wafaidika na Wilaya yake ni sehemu ambayo inafaidika, kuna utaratibu ambao unatumika hata ndani ya miezi miwili ijayo kuna vifaa vinapelekwa kwenye Jimbo lake kwa ajili ya huduma ya Watoto Njiti.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Ni dhahiri kwamba viko visababishi ambavyo vinapelekea mama kujifungua mtoto njiti ikiwemo mahitaji ya lishe. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inaimarisha huduma za lishe kwa akina mama wajawazito ili waweze kufikisha full term yaani mtoto azaliwe ndani ya umri anaotakiwa kuzaliwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu ameshaelekeza, kumekuwepo na makongamano mengi, kumekuwepo na semina nyingi ambazo zinazungumzia suala zima la lishe. Sasa badala ya kufanya makongamano na semina fedha hizo zitaelekezwa kununua vitamini ambazo zina multiple vitamin na akina mama wajawazito wote wanapewa hizo vitamin. Lakini niendelee kuwaomba Wabunge wa kike na wa kiume mojawapo ya sababu za Watoto Njiti ni stress. Sisi wote tunapofika mahali kina mama wajawazito wanakuwepo tuhakikishe mazingira yao ya kufanya kazi lakini sisi wanaume tuwe karibu nao ili kuondokana na mambo mengine yanayoweza kuzuilika yanayosababisha uwepo wa Watoto Njiti.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Swali langu nilikaa nikafikiri kwamba ultrasound machine pamoja na x-rays ni muhimu sana kwenye suala zima la Watoto Njiti. Kwa hiyo nilitaka nimuulize Waziri kwamba ni lini watepeleka ultrasound machine na x-ray katika kituo cha Afya Himo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mimi na yeye nikimaliza haya maswali kama kituo chake hakina ultrasound tukae chini ili tuweze kuelekeza MSD wapeleke mara moja ultrasound kwenye eneo lake. Pia suala la x-ray kuna fedha zile ambazo Waziri wa Afya amesema zimeokolewa tumefanikiwa vilevile kupata x-ray 33 za ziada, kwa hiyo katika hiyo ziada tutaona tunaelekeza maeneo gani baada ya watalaam kuchakata na kuona vipaumbele.(Makofi)
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Tunayo changamoto kubwa sana katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo Mkoani Tabora ya chumba ama kitengo maalum kwa ajili ya Watoto Njiti. Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha kitengo hiki ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo hivi sasa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Katika hospitali ambazo zimetengewa fedha kwa mwaka huu wa fedha Bilioni 59.3 mojawapo ni hospitali ya Kitete. Kwa maana hiyo eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge unalisema tutaenda kulingalia kwa umakini zaidi. Pia maeneo ya kutembelea inawezekana tatizo siyo sehemu ya kuweka Watoto Njiti lakini maamuzi katika kupanga vyumba inawezekana tunahitaji tu vifaa. Tutaenda kuangalia kwa pamoja Mheshimiwa Mbunge halafu tuone tunafanya nini kama ni uhitaji wa vifaa tutaweka vifaa mapema. (Makofi)
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa ni ahadi ya CCM ya kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara hizi ambazo siyo za Muungano. Je, Wizara ya Afya inashirikianaje na Wizara ya Afya ya Zanzibar kwenye kutatua changamoto hizi za Watoto Njiti? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, anachokisema Mbunge ni kweli na nimejaribu kutembelea baadhi ya maeneo upande wa Taifa letu upande wa Visiwani ni kweli kunahitajika maboresho makubwa sana kwenye huduma za afya. Jana Mheshimiwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alikuwa anajadiliana na baadhi ya wadau ili kuona ni namna gani hawa wadau ambao wanatoa huduma huku upande wa Bara waweze kwenda upande wa pili wa visiwani na kuweza kuboresha miundombinu ya afya badala ya kupeleka fedha kwenye maeneo hayo. Tayari AMREF wamekubali kuelekea upande huo wa pili kwa ajili ya kuboresha maeneo unayosema Mheshimiwa Mbunge.
MHE. KABULA E. SHITOBELO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mkoa wa Mwanza una hospitali na vituo ambavyo bado havijapata huduma hii ya chumba cha mtoto njiti.

Je, Serikali lini itakamilisha kutuwekea vyumba maalum kwa mtoto njiti?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli anavyosema lakini kwenye hospitali ya Sekou-Toure ya Mkoa wa Mwanza ujenzi mkubwa sana unaendelea, suala ni kwenda kuamua na kuweka vifaa kwenye eneo hilo ili watoto waweze kupata huduma. Nafikiri anazungumzia Mkoa mzima kwa ujumla na hasa maeneo ya visiwani. Kwa mfano, Ukerewe ambako ni Visiwani sasa hospitali ya Wilaya ile inaenda kujengwa kwa level ya hospitali ya Mkoa ili mambo yote ya Rufaa ya Mkoa yaweze kutolewa huko huko Visiwani. Kwa hiyo, tutaendelea kufanya ziara na kugundua matatizo mbalimbali kwenye maeneo na kuelekeza fedha kadri ya mahitaji ya maeneo husika. (Makofi)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwanza swali hili lilikuwa limeulizwa kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu niliuliza mimi mwenyewe na ninakushukuru kiti chako kuamua Wizara ijibu na leo amekuja kuleta majibu.

Nina maswali madogo mawili ya nyongeza, swali la kwanza, kwa kuwa sasa Halmashauri ya Mji wa Mbulu haina jokofu kwa muda wa mwaka mmoja au zaidi ya mwaka sasa, na kwa mapato yetu ya ndani hatuwezi kununua jokofu hilo linalohitaji takriban Milioni 70.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutununulia hilo jokofu ili hospitali ya Mbulu ipate huduma hiyo na kuondoa adha hiyo kwa wananchi?

Swali la pili, kwa kuwa kumeonekana kuna gharama kubwa sana ya uagizaji wa dawa na vifaatiba nchini kupitia Wakala wa MSD Serikali haioni kuwa ni wakati muafaka wa kutazama gharama hizo ili kuona namna mbadala ya kupunguza gharama kwa Serikali na kutoa huduma hiyo kwa Umma?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Kwanza ninampongeza kwa ufuatiliaji wake makini wa hili suala kwa ajili ya Wilaya yake. Kwanza ameshafika Wizarani na nimhakikishie kwamba majokofu yameshafika MSD siku tatu zilizopita, kwa hiyo mpaka mwisho wa wiki itakuwa jokofu la kubeba miili 12 litakuwa limefika Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya kuelekea kwenye hospitali yake ya Wilaya.

Swali lake la pili ni suala la gharama ya bei ya MSD kuwa ni ghali. Kwanza nimwambie MSD ni Shirika la Serikali na kweli huko nyuma kulikuwa na tatizo hilo lakini halipo sasa hivi, ndiyo maana Rais wetu Samia Suluhu Hassan ametoa fedha na tumejenga viwanda kule Idofi ambavyo vinazalisha dawa pamoja na gloves ukienda sasa hivi MSD ukilinganisha na bei zilizopo mtaani, MSD ni bei rahisi kuliko ilivyo mtaani. Kwa hiyo, hilo tatizo limesha tatuliwa na linaendelea kufanyiwa kazi zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako niseme tu moja kwenye eneo hili la mortuary, Mbunge wa Meru amejenga yeye mwenyewe mortuary kwa asilimia 80 kwa fedha zake na niipongeze Halmashauri yake ikachangia asilimia 20 iliyobaki na katika majokofu yanayokuja, jokofu lako linakuja na Mbunge wa Makete.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ninapozungumzia tiba ya macho, pua na koo, nazungumzia ongezeko la mabubu na viziwi nchini. Sasa kwa kuwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la mabubu na viziwi nchini ambalo limesababisha Serikali kupeleka ruzuku kwa wanafunzi kutoka bilioni 3.6 mwaka 2018/2019 mpaka bilioni 6.3 mwaka 2021/2022. Je, Serikali haioni haja ya kupeleka vifaa vya kupima usikivu kwenye hospitali za wilaya ili kila mtoto anapozaliwa aweze kupimwa usikivu ili kupunguza tatizo la ububu na uziwi nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa, tangu mwaka 2016/2017, Serikali ilianzisha upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu nchini. Je, ni juhudi gani zimefanyika kuongeza vitengo vya speech therapy katika hospitali zetu, ili kuondosha tatizo la mabubu na viziwi nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja anaulizia ni kwa namna gani Serikali itajipanga kupeleka vifaa tiba kwenye level ya wilaya. Tunapokea ushauri wake na sio tu kwenye eneo la kupeleka vifaa kwa ajili ya kupima watu wenye matatizo hayo, lakini ni ku-include kwenye package ya mama anayejifungua, wakati anajifungua basi mtoto aweze kuhakikishwa kwamba amechunguzwa vitu vyote kiasi kwamba, hata wakati anahudhuria clinic kuna uchunguzi kama huo ili kuwatambua mapema na kuwasaidia.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kwamba, toka 2016 kulikuwa na operation za kuweka vipandikizi kwa wale watu ambao wana shida ya usikivu; tunapokea ushauri wake na bado tunasema hivyohivyo kama kwenye issue ya suala zima la watoto wadogo, vilevile tutapeleka kwa kuanzia kwenye level za mikoa kuhakikisha operations kama hizo zinaweza kufanyika na watu wao kupata huduma, lakini vilevile kwa watu ambao tayari wana tatizo hilo tunatengeneza utaratibu wa kuwasaidia hasa wanapokuja hospitali, watu wanaoweza kufafanua zile lugha za ishara na mambo mengine, ili waweze kupata huduma kama watu wengine. Ahsante sana.
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kituo cha Afya cha Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga Mjini ambacho ni tegemeo kubwa sana kwa wananchi na hasa akinamama kwa kuwa kinazalisha akinamama takribani 330 kwa mwezi, kinakabiliwa na tatizo kubwa sana la ukosefu wa generator. Kiasi cha shilingi milioni 290 ambayo ilitolewa katika mpango wa Serikali kuboresha vituo vya afya ilitolewa na ikakabidhiwa MSD, vifaa tiba vingi vimekuja kasoro generator, wananchi wanalalamika. Je, ni lini generator litakuja kama sehemu ya vifaa-tiba katika Kituo hicho cha Afya cha Kambarage? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nimetembelea hicho kituo na nimekuta Mheshimiwa Mbunge alichangia milioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa hicho kituo, lakini ninachoweza kusema ni tukishamaliza maswali hapa, tukutane mimi na yeye, tutashirikiana na mwenzangu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ili tuweze kuhakikisha kwamba, vifaa hivyo vinafika kwa sababu, kama fedha zimepelekwa, basi ni kupeleka kile ambacho kinatakiwa kufanyika. Tukae mimi na yeye tuhakikishe generator limeenda.
MHE. JUMA USONGE HAMAD: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; kwa kuwa utaratibu wa kutoa msamaha kwa wazee umekuwa na mlolongo mrefu, lakini wazee hao wanakatishwa tamaa wanapopata hizo huduma.

Je, ni ipi kauli ya Serikali ya kupunguza mlolongo huo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, toka Bunge hili kuanza tumekuwa tumesikia sana hizi kauli za kusema kwamba inakuja Bima ya Afya kwa Wote.

Je, ni nili hasa Serikali italeta Muswada wa Bima ya Bure kwa Wote? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja la kwanza; suala la ukiritimba kwenye msamaha kwa wazee na kuwahudumia wazee. Kwanza nitumie fursa hii kutoa agizo kwa Waganga wote Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya kwamba suala la tiba kwa wazee siyo tu kwamba ni bure lakini vilevile wanatakiwa wawe na dirisha lao. Kwa hiyo, hatutegemei tena kusikia haya malalamiko ya kwamba wazee wanapata mlolongo mrefu wa kupata tiba. Lakini Waganga Wakuu wa Wilaya wahakikishe vilevile wazee wamepata vile vitambulisho vyao.

Mheshimiwa Spika, la pili, kwamba ni lini sasa Muswada huu utakamilika, Mheshimiwa Mbunge hili nisije nikalidanganya Bunge ninachoomba tutalishughulikia na mapema sana tunaweza tukaja kukuambia ni nini kitakachofanyika kabla Bunge hili halijaisha. Lakini kwa sasa ukinipa tarehe specific inaihusu organ mbalimbali za Serikali ili hilo liweze kuja hapa Bungeni, naomba nilifuatilie kwa uhakika zaidi. (Makofi)
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa pale mkoani Rukwa kwa sababu tayari eneo limetengwa, lakini Serikali bado haijaanza ujenzi. Ni lini Serikali itaanza ujenzi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwenye bajeti ya mwaka huu imepangiwa kwa ajili ya kufanya ujenzi kwenye eneo ambalo amelitaja.
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Je, Mheshimiwa Waziri uko tayari kuambatana na mimi ili ukaweze kunidhibitishia mradi huu utakamilika mwaka huu wa fedha? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kutokana na changamoto nyingi wanawake wanazozipitia kipindi wanachokuwa wajawazito; Je, Serikali haioni haja kushusha huduma hii Wilayani ili tuweze kupata huduma hii kwa Mkoa wa Shinyanga kwa Watoto Njiti? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Santiel Erick Kirumba Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja niko tayari kuandamana naye kwenda Shinyanga na nitafurahi tukiwa wawili tu peke yetu. Ahsante. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni kwamba Je, Serikali haioni kuna umuhimu wa kupeleka kwenye hospitali za Wilaya huduma hizi. Kwenye bajeti yetu Mheshimiwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema kwamba, kwa mwaka huu unaokuja wa fedha tunaenda kujenga sehemu za Watoto Njiti 100 na siyo tu kwenye hospitali za Wilaya na kwenye Vituo vya Afya. Kwa hiyo, fedha zimeshapatikana sasa imebaki kuwasiliana na Waziri wa TAMISEMI ili kupanga sehemu za vipaumbele vya kuanza na kwa jiografia ya Mkoa wa Shinyanga ni mojawapo ya maeneo yataenda kufaidika na huu ujenzi. Ahsante sana.
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Hospitali ya Mkoa ya Tumbwi siyo kwamba inahudumia watu wa Pwani tu na wale wapita njia. Kitengo cha Watoto Njiti kweli kipo lakini uboreshaji ni pamoja na vifaa tiba. Watoto wanazaliwa pale lakini inabidi wakimbizwe.

Je, ni lini Serikali pamoja na kuboresha kitengo cha Watoto Njiti na vifaa tiba vitaboreshwa lini?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dokta Kaijage kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwamba Hospitali ya Tumbwi ni mojawapo kweli kuna eneo la Watoto Njiti lakini hospitali inazidiwa. Katika Bilioni 59.3 ambazo zimetengwa kwa ajili ya uboreshaji, Hospitali ya Mkoa wa Tumbi ipo mojawapo na eneo ambalo limetengewa hela kwa ajili ya kulipanua na kuongezea vitanda ni eneo hilo la Watoto Njiti. (Makofi)
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, Serikali haioni haja ya kumjumuisha mtoto njiti kwenye Bima ya Mama yake ili pindi anapozaliwa aweze kupata huduma hiyo na kumwondolea Mama mwenye mtoto njiti adha ya kuanza kufanya usajili wa mtoto kwenye Bima ya Afya?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, swali aliloliuliza Mbunge ni swali muhimu sana na nitumie fursa hii kumwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bima ya Afya kwamba suala la kuhudumia mtoto njiti ambaye mama yake ana bima yake ya afya lisiwe mjadala. Mtoto njiti akizaliwa na huduma yake inakuwa ni automatic. Vilevile kwa sababu tunakwenda kwenye suala la bima ya afya kwa watu wote Wabunge wote tukumbuke hayo mambo tuhakikishe sasa tutaweka kwenye sheria ijayo iweze kufanyika vizuri zaidi. (Makofi)

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Katika Hospitali yetu ya Mkoa wa Iringa tuna kitengo cha Watoto Njiti na tuna upungufu mkubwa wa mashine na dawa inaitwa Lung surfactant ambayo dozi moja inauzwa Shilingi Laki Tano na mtoto ili a-survive anahitaji dozi tatu. Serikali ina mpango gani kuangalia kwamba dawa hizi angalau zinawekewa ruzuku ili kupunguza gharama hiyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, moja kwanza sioy dawa kuwekewa ruzuku kwa taratibu na sheria na taratibu za Wizara ya Afya ni kwamba huduma ya mtoto chini ya miaka Mitano including hawo Watoto Njiti na Mama na Mtoto ni bure. Kwa maana kwamba tunaposema mlitupitishia bilioni 200 kwa ajili ya kununua dawa na vifaatiba. Hilo eneo tutakwenda kulielekeza nguvu nyingi kuhakikisha kwamba Watoto njiti hawawezi kukutana na matatizo hayo.

MHE. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Hospitali ya Kahama inahudumia watu kutoka pembezoni kwa maana ya Mikoa ya Tabora pamoja na Geita. Je, ni lini Serikali itaboresha kituo cha Watoto njiti pale Hospitali ya Kahama?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nijibu swali la Mheshimiwa hapa, ukisikia Serikali inasema inajenga vituo vya afya kwa kila Tarafa na kazi ile imeendelea kufanyika kupitia TAMISEMI ni kwenda kupunguza wagonjwa ambao sasa wanaenda kurundikana kwenye hospitali moja kama ilivyo Kahama.

Mheshimiwa Spika, mimi nafikiri Mbunge ni muhimu tukatembelea hospitali hiyo inawezekana tukikaa mle ndani tutaona tu maeneo ambayo tunaweza tukaweka sehemu ya Watoto njiti, ibaki kazi ya kuleta vifaa na kuvipachika na Watoto waweze kupata huduma.

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa Serikali imetueleza kwamba wana mpango wa kujenga vituo 100 vya Watoto Njiti hapa nchini; Je, sisi ni miongoni mwa watu tutakaofaidika Jimbo letu la Mchinga kwa kituo hicho?

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wao ni wafaidika na Wilaya yake ni sehemu ambayo inafaidika, kuna utaratibu ambao unatumika hata ndani ya miezi miwili ijayo kuna vifaa vinapelekwa kwenye Jimbo lake kwa ajili ya huduma ya Watoto Njiti.

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Ni dhahiri kwamba viko visababishi ambavyo vinapelekea mama kujifungua mtoto njiti ikiwemo mahitaji ya lishe. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inaimarisha huduma za lishe kwa akina mama wajawazito ili waweze kufikisha full term yaani mtoto azaliwe ndani ya umri anaotakiwa kuzaliwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu ameshaelekeza, kumekuwepo na makongamano mengi, kumekuwepo na semina nyingi ambazo zinazungumzia suala zima la lishe. Sasa badala ya kufanya makongamano na semina fedha hizo zitaelekezwa kununua vitamini ambazo zina multiple vitamin na akina mama wajawazito wote wanapewa hizo vitamin. Lakini niendelee kuwaomba Wabunge wa kike na wa kiume mojawapo ya sababu za Watoto Njiti ni stress. Sisi wote tunapofika mahali kina mama wajawazito wanakuwepo tuhakikishe mazingira yao ya kufanya kazi lakini sisi wanaume tuwe karibu nao ili kuondokana na mambo mengine yanayoweza kuzuilika yanayosababisha uwepo wa Watoto Njiti.

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Swali langu nilikaa nikafikiri kwamba ultrasound machine pamoja na x-rays ni muhimu sana kwenye suala zima la Watoto Njiti. Kwa hiyo nilitaka nimuulize Waziri kwamba ni lini watepeleka ultrasound machine na x-ray katika kituo cha Afya Himo?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mimi na yeye nikimaliza haya maswali kama kituo chake hakina ultrasound tukae chini ili tuweze kuelekeza MSD wapeleke mara moja ultrasound kwenye eneo lake. Pia suala la x-ray kuna fedha zile ambazo Waziri wa Afya amesema zimeokolewa tumefanikiwa vilevile kupata x-ray 33 za ziada, kwa hiyo katika hiyo ziada tutaona tunaelekeza maeneo gani baada ya watalaam kuchakata na kuona vipaumbele.(Makofi)

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Tunayo changamoto kubwa sana katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo Mkoani Tabora ya chumba ama kitengo maalum kwa ajili ya Watoto Njiti. Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha kitengo hiki ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo hivi sasa?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Katika hospitali ambazo zimetengewa fedha kwa mwaka huu wa fedha Bilioni 59.3 mojawapo ni hospitali ya Kitete. Kwa maana hiyo eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge unalisema tutaenda kulingalia kwa umakini zaidi. Pia maeneo ya kutembelea inawezekana tatizo siyo sehemu ya kuweka Watoto Njiti lakini maamuzi katika kupanga vyumba inawezekana tunahitaji tu vifaa. Tutaenda kuangalia kwa pamoja Mheshimiwa Mbunge halafu tuone tunafanya nini kama ni uhitaji wa vifaa tutaweka vifaa mapema. (Makofi)
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa ni ahadi ya CCM ya kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara hizi ambazo siyo za Muungano. Je, Wizara ya Afya inashirikianaje na Wizara ya Afya ya Zanzibar kwenye kutatua changamoto hizi za Watoto Njiti? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, anachokisema Mbunge ni kweli na nimejaribu kutembelea baadhi ya maeneo upande wa Taifa letu upande wa Visiwani ni kweli kunahitajika maboresho makubwa sana kwenye huduma za afya. Jana Mheshimiwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alikuwa anajadiliana na baadhi ya wadau ili kuona ni namna gani hawa wadau ambao wanatoa huduma huku upande wa Bara waweze kwenda upande wa pili wa visiwani na kuweza kuboresha miundombinu ya afya badala ya kupeleka fedha kwenye maeneo hayo. Tayari AMREF wamekubali kuelekea upande huo wa pili kwa ajili ya kuboresha maeneo unayosema Mheshimiwa Mbunge.

MHE. KABULA E. SHITOBELO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mkoa wa Mwanza una hospitali na vituo ambavyo bado havijapata huduma hii ya chumba cha mtoto njiti.

Je, Serikali lini itakamilisha kutuwekea vyumba maalum kwa mtoto njiti?
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli anavyosema lakini kwenye hospitali ya Sekou-Toure ya Mkoa wa Mwanza ujenzi mkubwa sana unaendelea, suala ni kwenda kuamua na kuweka vifaa kwenye eneo hilo ili watoto waweze kupata huduma. Nafikiri anazungumzia Mkoa mzima kwa ujumla na hasa maeneo ya visiwani. Kwa mfano, Ukerewe ambako ni Visiwani sasa hospitali ya Wilaya ile inaenda kujengwa kwa level ya hospitali ya Mkoa ili mambo yote ya Rufaa ya Mkoa yaweze kutolewa huko huko Visiwani. Kwa hiyo, tutaendelea kufanya ziara na kugundua matatizo mbalimbali kwenye maeneo na kuelekeza fedha kadri ya mahitaji ya maeneo husika. (Makofi)