Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA (K.n.y MHE. SAVELINA S. MWIJAGE) aliuliza:- Pamoja na Serikali kuwa na mipango mizuri kwa wananchi wake lakini mipango hiyo baadhi yake haitekelezwi; wakulima wengi nchini wanalima bila ya kuwa na elimu ya kilimo na hivyo kushindwa kulima baadhi ya mazao ya biashara na chakula kama vile ndizi, kahawa, mahindi, maharage, karanga na kadhalika:- (a) Je, Serikali itawasaidiaje wakulima hao ili wanufaike na kilimo pamoja na mazao yao kwa chakula na biashara? (b) Je, Serikali ina mipango gani juu ya utoaji wa elimu kwa wakulima ili wafaidike na kilimo chao?

Supplementary Question 1

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa sababu kubwa ya ukosefu wa elimu kwa wakulima ni uchache wa Maafisa Ugani. Je, Serikali ina mpango gani wa kuajiri Maafisa Ugani kwa kila kijiji? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa kuwa wakulima wa kahawa hupeleka kahawa zao nchi jirani kufuata bei nzuri. Je, Serikali ina mpango gani kuongeza bei ya kahawa ili wananchi hawa wasipeleke nchi jirani?

Name

Dr. Charles John Tizeba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Answer

WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama nilivyojibu katika swali la msingi kwamba tuna upungufu wa Maafisa Ugani 6,022, hii ni idadi kubwa. Vilevile kama nilivyosema katika jibu langu la msingi ni kwamba Serikali inasomesha Maafisa Ugani hawa zaidi sasa katika vyuo vyetu ili kukabiliana na huu uhaba ambao upo na vibali vya kuwaajiri vinaendelea kutolewa. Kwa hivyo, hivyo hivyo tunakwenda kukabiliana na huo upungufu na nina uhakika baada ya miaka michache ijayo kama nia ilivyo ya Serikali na Mheshimiwa Mbunge, kila kijiji kitakuwa na Maafisa Ugani wanaotakiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la kahawa kuruhusiwa kuuzwa nje ya nchi, nikijibu swali lililotangulia nimesema kwamba kahawa hatutakubali iende nje kwa sababu tunavyo viwanda vya kuhudumiwa hapa hapa nchini. Hii kahawa bei yake itakuwa nzuri tukiondokana na msururu wa kodi hizo ndogo ndogo zilizopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, zao la kahawa leo tunapozungumza hapa lina kodi 26, ni kodi nyingi sana na ndiyo maana tunafanya sasa uchambuzi ndani ya Serikali ili kuona hizo kodi ambazo kwa kweli zinastahili kuondolewa, ziondolewe ili kuwapa wakulima unafuu. Kwa sababu kodi zikitozwa wanunuzi hawalipi wao, zinahamishiwa kwa muuzaji wa kahawa ambaye ni mkulima. Kwa hivyo, tukizipunguza hata kwa wanunuzi na watu wengine, mwisho wa siku atakayenufaika ni mkulima kwa sababu kodi hizo zitakuwa zimepungua na bei ya kahawa zitakuwa zimepanda.

Name

Omary Tebweta Mgumba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini Mashariki

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA (K.n.y MHE. SAVELINA S. MWIJAGE) aliuliza:- Pamoja na Serikali kuwa na mipango mizuri kwa wananchi wake lakini mipango hiyo baadhi yake haitekelezwi; wakulima wengi nchini wanalima bila ya kuwa na elimu ya kilimo na hivyo kushindwa kulima baadhi ya mazao ya biashara na chakula kama vile ndizi, kahawa, mahindi, maharage, karanga na kadhalika:- (a) Je, Serikali itawasaidiaje wakulima hao ili wanufaike na kilimo pamoja na mazao yao kwa chakula na biashara? (b) Je, Serikali ina mipango gani juu ya utoaji wa elimu kwa wakulima ili wafaidike na kilimo chao?

Supplementary Question 2

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mazao mengi ya biashara tunategemea sana soko la nje ambalo lina ushindani mkubwa kuzingatia nchi nyingi zinalima mazao hayo na wakati mwingine wakulima wanalima kutokana na mazoea. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Kitengo cha Utafiti wa Masoko hayo ili kujua mahitaji halisi ya soko la dunia kuliko kama sasa ufuta umeshuka mpaka Sh.1,500 kutoka bei ya mwaka jana ya Sh. 3,000? Nataka kujua tu Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Kitengo hicho cha Utafiti wa Masoko Ulimwenguni ili kutoa habari nchini kwa wakulima kulima mazao kutokana mahitaji ya soko badala ya kulima mazao kwa mazoea.

Name

Dr. Charles John Tizeba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Answer

WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mazao yetu mengi kwa sasa bado yanategemea masoko ya nchi za nje, lakini naomba nimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kwamba takribani kila zao kubwa la biashara linalo Bodi na hizo zina Vitengo vya Utafiti wa Masoko. Kwa hivyo, labda tu tutumie nafasi hii kuvikumbusha hivyo vitengo kwamba wanao wajibu wa kufanya huo utafiti na kufikisha habari wanayoipata kwa wakulima.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo hapa ninaloliona ni pale ambapo bodi na hivyo vitengo wanapokuwa na habari kuhusu soko kuanguka au kupanda wakaacha kufikisha habari hiyo kwa wadau wao ambao ni wakulima. Kwa hivyo, niwakumbushe tu katika bodi na taasisi hizi zinazohusika na utafiti wahakikishe kwamba hicho wanachokibaini na kukijua kuhusu masoko ya haya mazao basi kwa haraka iwezekanavyo wafikishe habari hiyo kwa wahusika kwa maana ya wakulima na wafanyabiashara wa mazao hayo.