Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mussa Ramadhani Sima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mjini

Primary Question

MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza:- Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Malengo ya Dira ya Taifa 2025, inaeleza kwamba ifikapo mwaka 2025 Tanzania itakuwa na uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda. (a) Je, Serikali imeweka mkakati gani wa kuinua wananchi wa tabaka la kati (middle class) kuweza kujitegemea? (b) Je, ni kampuni ngapi zilizowekeza nchini na Serikali ina hisa kiasi gani kwenye kampuni hizo?

Supplementary Question 1

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri niulize maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa Singida mjini kwa asilimia kubwa ya wakazi wanajishungulisha na biashara za mazao hususani biashara ya vitunguu. Serikali ina mpango gani sasa wa kujenga Soko la Kimataifa la Vitunguu pale Misuna ambalo linawahusisha mpaka wenyeji wa nchi za Afrika Mashariki na Kati?
Swali la pili, kwa kuwa Serikali imeonyesha ina hisa nyingi kwenye Makampuni ya Umma, je Serikali ina mpango gani wa kuongeza hisa lakini pia hold share na kuongeza uzalishaji katika makampuni hayo? Ahsante.

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

HARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Sima kwa anavyoshughulikia masuala ya masoko na viwanda hapo Singida, hakuna asiyejua kwamba Singida ni wakulima wa vitunguu na wakulima maarufu sana wa zao la alizeti. Serikali inachofanya pamoja na mambo mengine ni kuhakikisha kwamba sasa hivi inawasiliana na Halmashauri ya Singida ili kuona sasa zao la vitunguu linapewa kipaumbele na kuanzisha soko la kati.
Mheshimiwa Naibu Spika, umuhimu wa Singida pamoja na mambo mengine hadi sasa kwa kilimo cha vitunguu pamoja na alizeti nadhani ni Mkoa unaongoza kwa Tanzania kwa sasa ukifuatiwa na Mkoa wa Iringa. Hivyo Serikali inaona kuna umuhimu kweli wa kuanzisha soko la Kimataifa kama ambavyo tumeanzisha masoko mengine mipakani kwa ajili ya kuimarisha mazao ambayo yanalimwa hapa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la Mheshimiwa Mbunge ni kuhusiana na hisa za Serikali. Ni kweli kabisa Serikali ina miliki hisa katika makampuni mengi sana. Kwa sasa hivi kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi Serikali ina hisa katika makampuni 61 na katika makampuni yale asilimia kubwa ya hisa za Serikali ni chini ya 50. Kama mnavyotambua tuna asilimia kwa sasa hivi kwa mfano Tanzania Oxygen tuna asilimia 9.59, ukienda Kilombero Sugar tuna asilimia 25, ukienda Tanelec tuna asilimia 30. Lakini hata ukienda kwenye makampuni mengine kama migodi Mwadui tuna asilimia 25.
Mheshimiwa Naibu Spika, upo mkakati wa kuongeza za Serikali katika mipango ya kimkakati, mipango ya kimakakati kwa mfano mathalani kwa sasa hivi viwanda vyetu vya nguo kama Urafiki Serikali ina asilimia 49. Serikali inajaribu kuangalia uwezekano wa kuongeza hisa zake ili iweze kuwa na maamuzi ya uzalishaji katika viwanda vile.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikiongeza suala lingine kuhusu uongezaji wa hisa katika kuweka asilimia za Serikali, katika mipango na miradi na viwanda vya kimkakati kama viwanda vya chuma cha Liganga, kama viwanda vya Kiwira, Serikali inaona kuwa na asilimia nyingi ili iweze kuwa na uwekezaji yenyewe kama ambavyo inaweza kufanya kwa maendeleo ya wananchi wake.