Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. DAVID E. SILINDE (K.n.y MHE. FRANK G. MWAKAJOKA) aliuliza:- (a) Je, Serikali ina Mpango gani wa kugenga Kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya hapa Tunduma ili kuendana na ongezeko la watu na wageni wanaoingia nchini? (b) Je, Serikali haioni vema ujenzi wa kituo hicho uende sambamba na ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu kwa Polisi wetu ambao wana shida kubwa ya makazi? SPIKA: Sasa Mheshimiwa Silinde wewe Tunduma si ulishaondoka, majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu, Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Hamad Yussuf Masauni. (Kicheko)

Supplementary Question 1

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba kuna changamoto katika ujenzi wa nyumba za Polisi pamoja na vituo. Sasa swali langu ni je, kwenye Polisi kuna kitengo cha Usalama Barabarani yaani Trafiki, ambacho kimekuwa kikikusanya fedha nyingi, almost kwenye bajeti huwa tunatenga ni zaidi ya bilioni 10 kwa mwaka.
Je, ni kwa nini sasa Serikalli isiamue kuruhusu Polisi kutumia fedha zinazotokana na Polisi wa barabarani kwa ajili ya kuondoa kero ya ujenzi wa nyumba za polisi, pamoja na Vituo vya Polisi katika Wilaya zote nchini?
Swali la pili, katika majibu ya Mheshimiwa Waziri, amesema Serikali inatajarijiwa kukopa kutoka Benki ya Exim China; je, haijatueleza ni kiwango gani mnatarajia kukopa na namna ambavyo mtalipa, kwa sababu suala la Polisi siyo miradi ya maendeleo? Ahsante sana.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI YA WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna fedha ambazo zinakusanywa kupitia faini ambazo zinakusanywa na Trafiki, lakini fedha hizi hazirudi Polisi, zinakwenda Hazina. Kwa hiyo, wazo lake Mheshimiwa Mbunge, nadhani siyo wazo baya labda tunaweza tukalitafakari pamoja kwa baadaye tuone jinsi gani ya kufanya.
Hata hivyo, Polisi ina mikakati mizuri tu ya kuweza kujenga nyumba za ziada kwa ajili ya kutatua changamoto hizo. Nimezungumza mradi wa ujenzi wa nyumba 4,138 hii ikiwa ni awamu ya kwanza, lakini kuna mradi ambao utaweza kuhakikisha kwamba tunahitaji nyumba 3,500 kwa mwaka, kwa maana nyumba 35,000 hadi kufikia mwaka 2025. Hiyo ni mikakati ya muda mirefu.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili, ambapo ameuliza huu mkopo wa Exim Bank ya China, mkopo huu unakadiriwa kufikia shilingi bilioni 500 ambao ni mkopo kutoka Serikali ya Exim Bank ya China ambao vilevile utalipwa na Serikali kulingana na kusainiwa kwa memorundum of understanding. Kwa hiyo, niseme tu kwamba taratibu zitakapokamilika, mkopo huu utakapokuwa tayari ujenzi utaanza mara moja na changamoto ya nyumba inaweza kupungua kwa sehemu kubwa sana.

Name

Khatib Said Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Konde

Primary Question

MHE. DAVID E. SILINDE (K.n.y MHE. FRANK G. MWAKAJOKA) aliuliza:- (a) Je, Serikali ina Mpango gani wa kugenga Kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya hapa Tunduma ili kuendana na ongezeko la watu na wageni wanaoingia nchini? (b) Je, Serikali haioni vema ujenzi wa kituo hicho uende sambamba na ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu kwa Polisi wetu ambao wana shida kubwa ya makazi? SPIKA: Sasa Mheshimiwa Silinde wewe Tunduma si ulishaondoka, majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu, Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Hamad Yussuf Masauni. (Kicheko)

Supplementary Question 2

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mwaka 2012 katika Bunge hili niliuliza swali kama hili linalohusiana na Askari wa Jimbo la Konde kuendelea kukaa kwenye magofu yaliyoachwa na Mkoloni. Nataka Mheshimiwa Waziri, unijibu kati ya Mpango huo unaokuja, Jimbo la Konde kujengewa Askari nyumba hizo umo au haumo, kama haumo ni kwa nini?Mpango huo unaokuja, Jimbo la Konde kujengewa Askari nyumba hizo umo au haumo, kama haumo ni kwa nini?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI YA WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, programu hizi za ujenzi wa nyumba za Askari zinapofanyika zinaangalia maeneo yote ya pande za Muungano. Kwa mfano, mtakumbuka kwamba tulikuwa tuna mradi ambao haujakamilika hata hivyo wa ujenzi wa nyumba kupitia NSSF, kulikuwa kuna nyumba zilizojengwa pia Zanzibar ikiwemo Pemba. Katika mradi huo ambao utatarajiwa kujenga nyumba 4,136 kati ya nyumba hizo nyumba 150 zitajengwa Pemba.
Kwa hiyo, nataka nimtoe wasiwasi tu Mheshimiwa Khatib, kwamba labda baadaye tuonane tuone Konde ni ngapi lakini kati ya nyumba hizo nyumba 150 zitajengwa Pemba. Hata hivyo, huu mradi nimeuzungumza wa muda mrefu wa nyumba 3,500 kila mwaka kufikia 2025, pia utazingatia mahitaji ya sehemu zote. Huu mradi wa nyumba 4,136 utaanza mikoa 17 kwanza baadaye tutamalizia mikoa mingine.