Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU D. HAJI aliuliza:- Vijana ndiyo nguvu kazi ya kutegemea katika Taifa hili na ulimwenguni kote. Kwa bahati mbaya, vijana wetu wengi wameathirika sana na madawa ya kulevya kiasi kwamba, badala ya kuwa nguvu kazi, imekuwa ni mzigo mkubwa kwa familia zao na Taifa kwa ujumla. Je, Serikali imejipanga vipi kuona inawanusuru vijana katika janga hili?

Supplementary Question 1

MHE. MWANTUMU D. HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri aliyoyasema Mheshimiwa Waziri, naomba niongeze swali langu la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kuna Askari Polisi ambao kwa maksudi wanafumbia macho masuala ya biashara za madawa ya kulevya katika kuhakikisha mipango ya Serikali ya kudhibiti madawa ya kulevya inafikiwa. Je, kutakuwa na utaratibu gani wa kuwadhibiti Askari ambao hawaendi na kasi ya kupambana na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya? (Makofi)

Name

Dr. Abdallah Saleh Possi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

MHE. DKT. ABDALLAH S. POSSI - NAIBU WAZIRI, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU: Mheshimiwa Spika, labda niseme tu kutokuchukua hatua kuzuia uhalifu ni kosa la jinai kisheria. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge, Wabunge wote au mwananchi yeyote mwenye taarifa kuhusu Askari ambaye kwa maksudi kabisa hajatimiza wajibu wake, aviarifu vyombo husika na Askari huyo atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria. (Makofi)