Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Frank George Mwakajoka

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. SALUM MWINYI REHANI (K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJADI) aliuliza:- Hapo kwanza Maafisa Uhamiaji wetu walikuwa wakipelekwa kwenye Balozi zetu kufanya kazi ya kutoa viza kwa wageni wanaotaka kuja Tanzania lakini hivi sasa Maafisa hao hawafanyi tena kazi hiyo na badala yake kazi hizo zinafanywa na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na hutoa viza hata kwa waombaji wasiotakiwa kupewa:- (a) Je, kwa nini Maafisa hao wa Uhamiaji waliondolewa kwenye Balozi hizo? (b) Je, ni sahihi kwa Maafisa wa Mambo ya Nje kufanya kazi za kutoa viza kwa wageni?

Supplementary Question 1

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wetu wanavyokwenda katika nchi ya Zambia hasa katika Jimbo la Copperbelt wamekuwa wanakamatwa wakiwa stand na wanapelekwa gerezani bila kupelekwa Mahakamani. Je, Serikali inasema nini kuhusiana na jambo hili kwa sababu kuna vijana wengi sana ambao wako magereza na hawajapelekwa Mahakamani mpaka sasa hivi? Ahsante.

Name

Dr. Susan Alphonce Kolimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili nalipokea na Wizara yangu pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani tutalifanyia kazi, ahsante.

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Primary Question

MHE. SALUM MWINYI REHANI (K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJADI) aliuliza:- Hapo kwanza Maafisa Uhamiaji wetu walikuwa wakipelekwa kwenye Balozi zetu kufanya kazi ya kutoa viza kwa wageni wanaotaka kuja Tanzania lakini hivi sasa Maafisa hao hawafanyi tena kazi hiyo na badala yake kazi hizo zinafanywa na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na hutoa viza hata kwa waombaji wasiotakiwa kupewa:- (a) Je, kwa nini Maafisa hao wa Uhamiaji waliondolewa kwenye Balozi hizo? (b) Je, ni sahihi kwa Maafisa wa Mambo ya Nje kufanya kazi za kutoa viza kwa wageni?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Pamoja na hawa professional staff kutofanya kazi zinazopaswa katika Balozi zetu, mimi nilitaka kujua tu effectiveness ya commercial attaché wetu katika balozi hizo kwa sababu wako dormant. Kiujumla nataka kujua suala zima la utalii pamoja na uwekezaji katika kuongeza pato la Taifa na vilevile kuitangaza nchi linashughulikiwa vipi na Balozi zetu? Naomba majibu.

Name

Dr. Susan Alphonce Kolimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza za Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, amelisema kwa ujumla kwamba kama kuna watu wanapelekwa ambao siyo taaluma yao wanafanya hawafanyi kazi vizuri lakini vilevile amesema kwamba baadhi ya Maafisa huwa hawatekelezi kazi zao vizuri. Kama anavyojua hii ni Wizara mpya, sasa hivi kuna mpango wa kuwaangalia hawa Maafisa wote na kupima utendaji kazi wao na wale ambao wataonekana hawatekelezi kazi zao vizuri tutawarudisha na kuwapeleka wale ambao wanastahiki.