Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI aliuliza:- (a) Je, Serikali inasafirisha nje ya nchi mbao na magogo kiasi gani kwa mwaka? (b) Je, ni nchi gani inaongoza kwa kununua mbao na magogo kutoka Tanzania? (c) Je, ni fedha za kigeni kiasi gani zimepatikana kutokana na mauzo ya magogo na mbao nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka 2010 - 2015?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Kumekuwa na uvunaji holela wa mikoko katika eneo la Rufiji na mikoko hii ikiwa inasafirishwa kwenda Zanzibar kwa kutumia bandari bubu. Je, Serikali inajua kuhusu suala hili na je, itachukua hatua gani?
Swali la pili, kumekuwa kuna uvunaji na utoaji holela wa mbao au mazao ya misitu katika maeneo ambayo hayana hata hiyo management plan au strategy ya uvunaji wa rasilimali hii. Je, Serikali ina mpango gani kupambana na hii hali? Ahsante.

Name

Eng. Ramo Matala Makani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya maliasili na utalii kwa ujumla viko vitendo ambavyo kwa ujumla wake vinaitwa ujangili na ujangili hauishii kwa wanyamapori tu peke yake na bidhaa zao, ujangili pia unahusisha bidhaa za misitu na misitu yenyewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vitendo vyote ambavyo vimekuwa vikifanyika vya ujangili ni kinyume cha sheria na Wizara au Serikali kwa ujumla imejipanga vizuri zaidi sasa hivi kuweza kudhibiti vitendo vyote vya ujangili kwa kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yanayohusika, kuboresha vikosi vya askari na kuwawezesha askari kuwa na vitendea kazi bora zaidi katika kufuatilia vitendo vya ujangili na kuchukua hatua mara moja.